Search This Blog

Monday, 19 December 2022

QUEEN MONICA (2) - 1

 



IMEANDIKWA NA PATRICK CK

SEASON 2

Simulizi : Queen Monica (2)

Sehemu Ya Kwanza (1)

ILIPOISHIA SEASON 1 “ Mheshimiwa rais kwa hili ulilolifanya hujanitendea haki hata kidogo.Ulipaswa kunitaarifu kwanza ili nithibitishe ushiriki wangu kabla ya kuutangazia umma.” Akasema Monica akanyamaza na kuendelea “ Hata hivyo,tayari umenifunga mikono na siwezi tena kusema hapana.Nitahudhuria kongamano hilo” “ Ahsante sana Monica.Nashukuru mno.Hii ni heshima kubwa umenipa” “ Lini linafanyika kongamano hilo? Akauliza Monica “ Linaanza kesho.Kwa hiyo jioni ya leo nitatuma ndege yangu binafsi kuja kukuchukua hapo Dar es salaam” akasema David Zumo.Ukimya ukatanda tena baada ya muda Monica akasema “Sawa David” “Ahsante Monica.Nitawasiliana nawe baadae mchana wa leo” akasema David na kukata simu “Dah ! Kweli David amedhamiria kufanya kila awezalo kutafuta ukaribu na mimi.Amenibana katika kona na nisingeweza kusema hapana.Hili ni jaribu kubwa na taratibu najiona kama vile ninaelekea kuanguka.Ninapoisikia sauti ya David nahisi kutetemeka kwa ndani.Nahisi amefanya hili makusudi kabisa ili apate nafasi ya kuwa na mimi.Lakini hata hivyo hii ni nafasi yangu pia ya kumsoma na kumfahamu vizuri ni mtu wa aina gani hasa.Ngoja niende Congo kwa sababu naona kuna nguvu kubwa inanitaka niende kuonana na David “ akawaza na kuoga akajiandaa akatoka kuelekea ofisini kwake.Njiani bado kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi na hata alipofika ofisini kwake alishindwa kufanya kazi yoyote.Kikubwa alichokuwa anakiwaza ni safari ya kwenda Congo. ENDELEA SEASON 2....................... “Any word from Monica? Akauliza mzee benedict akiwa mezani na mkewe wakipata kifungua kinywa “Sijawasiliana naye toka asubuhi.Nimeambiwa kwamba aliamka alfajiri akaondoka.Nahisi aliwahi hospitali kumjulia hali Yule rafiki yake aliyepigwa risasi” akajibu Jane “Ulivyomuona unadhani anaweza kukubali kuolewa na David Zumo? Akauliza mzee Ben “ Siwezi kujua anawaza nini na atatoa jibu gani lakini nakuhakikishia nitafanya kila niwezalo na lazima Monica atakubali kuolewa na David ila Ben...” Janet akasita kidogo.Ben akamkazia macho “Makubaliano yetu yabaki vile vile kama tulivyokualiana .Monica hatalifahamu suala hili katika maisha yake yote na familia yetu itabaki na amani.Monica will remain your daughter forever” akasema Jane. “Mimi sina tatizo kabisa katika hilo lakini wasi wasi wangu ni kwako kama utaweza kuitunza siri hii na hutamueleza Ernest kama Monica ni mwanae.” Janet akatabasamu na kusema “Naomba uniamini Ben.Siwezi kwenda kinyume na makubaliano yetu.Sintomueleza chochote.Hii itabaki ni siri yetu mimi na wewe pekee” akasema Janet akamtazama Ben usoni na kuuliza “Are you still angry with him? “Nani? “Ernest” Ben akanywa chai akaweka kikombe chini na kumtazama mke wake kwa makini kwa sekunde kadhaa halafu akasema “No ! I’m not” “Good.Nafurahi kusikia hivyo” akasema Jane “Ninyi ni marafiki mmetoka mbali na hamtakiwi kugombana katika umri huu.Makosa yamekwisha fanyika na hatutakiwi kuangalia mambo ya nyuma.Tuelekeze nguvu zetu katika mambo makubwa ya msingi yaliyoko mbele yetu .” akasema Janet “ Hicho ndicho kikubwa tunachopaswa kukifanya” akasema Ben na kuinuka “Naelekea ofisini kama utapata taarifa zozote toka kwa Monica utanijulisha” “Sawa Darling” akajibu Janet,Ben akaondoka “Mwanamke muongo mkubwa huyu.Bado anakutana kwa siri na Ernest.Nina uhakika lazima atamueleza ukweli kuhusiana na Monica.Ernest akifahamu kama Monica ni mwanae atafanya kila awezalo kumchukua na hilo ndilo jambo ambalo sitaki litokee.Monica ataendelea kuwa mwanangu daima.” Akawaza Ben Muda mfupi baada ya benedict kuondoka,mkewe Janet naye akaondoka na moja kwa moja akaelekea ofisini kwa Monica “Naomba Monica akubali ombi la David ili amani iwepo ndani mwetu kwani bila kufanya hivyo hili bomu litalipuka na kutujeruhi sote.Lazima nifanye kila ninaloweza kuhakikisha Monica anakubali kuolewa na David.Mimi mwenyewe ndiye niliyechafua hali ya hewa kwa hiyo lazima nifanye jitihada za kuisafisha.” Akawaza Janet akiwa njiani kuelekea ofisini kwa Monica Aliwasili ofisini kwa Monica na kumkuta akiwa amejiegemeza kitini hakuwa na hamu ya kufanya kazi.Mezani kulikuwa na pakiti la biskuti “ mama karibu sana” akasema Monica na kumkaribisha mama yake ofisini kwake “Ahante Monica.Samahani kwa kuja bila taarifa” “Usijali mama karibu sana ni muda mrefu hujafika hapa ofisini kwangu” akasema Monica.Bi Janet akalishika lile pakiti la biskuti na kumtazama mwanae “Nakufahamu vizuri Monica.Unapenda kutumia biskuti hizi pale unapokuwa na mawazo mengi.Pole sana nina imani ni kuhusu lile suala tulilokueleza jana.” Akasema Bi Janet “ Ni kweli mama kichwa changu kimejawa mawazo mengi.Suala lile linaninyima amani kabisa.” Akasema Monica “ Pole Monica lakini suala hilo hilo ndilo limenileta hapa kwako .Nataka tuzungumze kama mama na mwana.Nataka niwe muwazi kwako na wewe ufunguke kwangu.It’s a serious talk between you and me” akasema Janet.Monica akamtazama halafu akainuka na kusema “Twende bustanini” Walitoka ofisini wakaelekea bustanini.Ilikuwa ni bustani nzuri iliyotengenzwa kwa ustadi mkubwa “Monica wewe ni mwanangu” akaanzisha maongezi bi Janet “Nimekukuza mimi na ninakufahamu vizuri kuliko mtu mwingine yeyote.Ninafahamu msimamo wako kuhusiana na masuala ya mahusiano na ninafahamu unahitaji mwanaume wa namna gani.Ni jambo zuri kuwa na mpenzi Yule mwenye sifa unazozitaka lakini Monica mambo yamebadilika sana zama hizi.Nafahamu wapo wanaume wengi tu wanakupenda kwa dhati ya mioyo yao lakini wengi wamekosa sifa unazozitaka” akanyamaza na baada ya sekunde kadhaa akaendelea “Mwanangu kama nilivyokueleza awali kwamba maisha yamebadilika sana siku hizi na hivyo kutufanya tusiegemee sana katika masuala ya vigezo au sifa bali tunachoangalia kikubwa ni moyo wa mtu na nia ya dhati .Ukisema usubiri mtu mwenye vigezo unavyotaka utasubiri sana na usimpate.Nikupe mfano wangu mimi ,baba yangu alikuwa ni tajiri mkubwa na niliishi maisha ya kitajiri mno,nilisoma shule nzuri na nilikuwa na ndoto nyingi kubwa za kutimiza maishani lakini kila kitu kilibadilika pale nilipokutana na baba yako” akanyamaza kidogo kisha akaendelea “ndoto yangu ilikuwa ni kumpata mwanaume tajiri,mzuri wa sura,mwenye elimu ya kutosha .Nilitaka mwanaume mwenye kufanana na hali yangu na msimamo wangu haukuyumba.Niliwakataa vijana wengi toka familia kubwa walionitaka kimapenzi lakini msimamo wangu ulitetereka pale nilipokutana na baba yako.Hakuwa akitoka katika familia kubwa yenye uwezo na alikuwa anasoma shule ya kawaida .Nilikutana naye wakati shule zetu zilipokutana katika bonanza la michezo.Alivutiwa nami na bila kujali utofauti wa hali zetu za kimaisha kwa ujasiri mkubwa alinipenda akanifuata akanitongoza.Nilishangazwa mno na ujasiri wake nikajikuta nikimpenda.Ni hicho tu kimoja kiichonivutia kwake na kunifanya nilegeze msimamo wangu na kuingia katika mapenzi kwa mara ya kwanza na katika mapenzi hayo kwa bahati mbaya nikapata ujauzito nikatakiwa na familia yangu nikaitoe mimba hiyo lakini nilikataa.Baba yangu akanitaka nichague maisha mazuri aliyoniandalia au Benedict nami kwa ujasiri nikamchagua baba yako na nikafukuzwa nyumbani.Ndoto zangu za maisha nilizokuwa nazo zikaishia hapo lakini angalia mahala niliko hivi sasa,nimetimiza kila kile nilichokuwa nakihitaji.Sijawahi kuwaelezeni historia hii lakini nimeona nikueleze leo ili ufahamu namna maisha yanavyoweza kubadilika” Bi Janet akanyamaza na kwa mbali sura ya Monica ikaonyesha tabasamu “That’s a very interesting story.Sikufahamu historia yenu “ akasema Monica “Ni safari ndefu na haikuwa rahisi lakini tumesimama imara na hadi sasa tumekuwa wazee.Huu ni mfano nimekupa kukufundisha kwamba usiiache nafasi hii iliyojitokeza.Ni nadra sana kwa nafasi kama hizi kutokea zama hizi.Inawezekana David hana vigezo vya mwanaume unayemuhitaji katika maisha yako lakini unachopaswa kuangalia ni moyo wake na dhamira yake ya dhati ya kutaka kukuoa.Monica mimi kama mama yako nakushauri nafasi hii usiikatae.Wanawake wenzako nafasi kama hizi wanaziota ndotoni.Kwa hiyo Monica nakushauri ulipokee ombi la David kwa mikono miwili kwani ni jambo lenye faida nyingi kubwa kwako na kwetu pia kama familia na hata nchi kwa ujumla.Ukiolewa na David utakuwa mke wa bilionea mkubwa duniani,utakuwa mtu mkubwa na mwenye nguvu,utafanya mambo mengi yale ambayo umekuwa ukiota kuyafanya ,utatimiza ndoto zako zote.Dakika utakayotamka neno nakubali basi maisha yako yatabadilika .Ukiolewa na David utaumiliki utajiri wake wote,utafungua viwanda vikubwa hapa nchini na utaleta ajira kwa maelfu ya vijana .Kwa kuwa lengo lako la muda mrefu ni kuisaidia jamii masikini na yenye uhitaji basi hii ndiyo fursa unayotakiwa kuitumia.Inawezekana Mungu anataka kukutumia ili uwasaidie watu wake wenye uhitaji kwa hiyo isikie sauti yake ndani mwako na ukubali ombi la David.Mimi kama mama yako,kama rafiki yako,kama msiri wako,sina maneno mengine mazuri zaidi ya kukushawishi kuhusu suala hili,nimekueleza mengi ,ni juu yako sasa kupima na kufanya maamuzi sahihi.” Akasema bi Janet akachukua glasi ya maji akanywa Monica naye akachukua pakiti lake la biskuti akatoa moja na kutafuna,kila mmoja alionekana kuwaza lake.Mwishowe Monica akauvunja ukimya “Mama nimekusikiliza kwa makini na nimefurahi pia kusikia japo kwa ufupi kuhusu historia yenu wewe na baba.Kwa ufupi ni kwamba usiku wa leo sikuweza kupata usingizi kutokana na mawazo mengi niliyokuwa nayo na kubwa zaidi ilikuwa ni suala hili .Baada ya tafakari ya kina nimeamua kulipa nafasi jambo hili” “ Wow ! that’s good my princess” akasema bi janet “Kuamua kulipa nafasi suala ili si kukubali ombi la David bali nataka nipate wasaa wa kutosha kutafakari,kumfahamu David ni mtu wa aina gani na mwisho nitoe maamuzi.Nina msimamo wangu kuhusiana na mwanaume wa maisha yangu na sibabaishwi na jina au utajiri wa mtu na hata nilipotajiwa kuhusu David Zumo sikustuka sana kwa sababu ninaufuata moyo wangu hata hivyo nimeona hakuna sababu ya kutoa maamuzi ya haraka kuhusu suala hili kwani inawezekana David akawa ni mtu mzuri wa kunifaa .Naombeni mnipe muda wa kutosha ,nataka nijenge kwanza mahusiano mazuri na David na baadae nitatoa jibu langu.Kwa hiyo mama jioni ya leo ninakwenda Congo nimealikwa na David kutoa mada katika kongamano la umoja wa vijana wa Congo.” “Usinitanie Monica.Mara hii David amekwisha kupa mwaliko?? Bi Janet akapatwa na mshangao “Ndiyo mama,leo nakwenda Congo.David amenipigia simu asubuhi na kuniomba niende na nimekubali japokuwa najua anataka kutumia kigezo hicho kutengeneza ukaribu na mimi.Hicho ndicho kitu ambacho ninakitaka hata mimi kuwa karibu naye ili nimfahamu vizuri.” “Monica mwanangu Mungu anakuongoza na ndiyo maana mambo yako yanakwenda vizuri.Jiulize imewezekanaje kwa David Zumo kuwaacha wanawake hawa wote duniani na kukuona wewe pekee ? Haya ni maongozi ya Mungu.Please promise me that when you come back you’ll give us a good answer” “Mama siwezi kukuahidi chochote kwa sasa kwa sababu bado moyo wangu hauna hisia zozote kwa David “ “Nimekuelewa Monica.Vipi masuala ya usafiri? Tayari umekwisha fanya utaratibu wa kupata tiketi ya ndege? Kama bado nina rafiki yangu anaweza akakusaidia kupata nafasi katika ndege inayoondoka kila siku jioni kwenda Congo.Ngoja nimpigie sim...” “hakuna haja mama” Monica akamkatisha mama yake ambaye tayari alikuwa ameanza kutafuta namba za simu za huyo rafiki yake. “David anatuma ndege yake binafsi kuja kunichukua “akasema “Mungu akutangulie mwanangu na mambo yako yote yakafanikiwe.Nitamtaarifu baba yako kuhusu jambo hili na nina hakika atafurahi sana.Basi mimi ngoja nikuache ukajiandae tutakutana uwanja wa ndege mimi na baba yako tutakuja kukuaga” akasema Bi Janet akaagana na mwanae akaondoka “Hata mimi sina haja ya kuendelea kukaa hapa ngoja niondoke nikajiandae kwa safari ya jioni.Hii itakuwa ni safari ya kimya kimya sitaki mtu yeyote zaidi ya wazazi wangu ajue kama ninasafiri.” Akawaza Monica ****************** Ni saa sita na dakika kumi na nane za mchana ,rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest Mkasa akiwa ofisini kwake ,mara akaingia msaidizi wake wa karibu mzee Mukasha akiwa na faili mkononi. “ Karibu Mukasha.Umefanikiwa kupata chochote ? “Ndiyo mheshimiwa rais.NImeipata faili lake lakini kuna mambo mengine nimeyagundua kuhusu Austin January na kubwa zaidi ni kuhusiana na mdogo wake ambaye amefungwa nchini China baada ya kukamatwa na dawa za kulevya.” Akasema Mukasha “Thank you Mukasha.Thank you so much.Hii ni taarifa nzuri sana.Saa ngapi atapiga simu? Mukasha akaitazama saa yake ya mkononi na kusema “Kwa mujibu wa Mr Boaz alisema Austin atapiga baada ya saa moja na kwa mujibu wa saa yangu zimebaki dakika kumi tu muda huo utimie” “Good.Twende chumba cha faragha tukaisubiri simu yake kule.Sitaki mtu yeyote ajue tunaongea nini” akasema Ernest wakatoka wakaelekea katika chumba cha maongezi ya faragha.Ernest akaanza kulipitia faili lile lenye nyaraka mbali mbali zinazomuhusu Austin January. “Mukasha una uhakika Austin atapiga simu? Akauliza Ernest baada ya kumaliza kuzipitia nyaraka zile “Atapiga mheshimiwa.Tuendelee kusubiri kidogo” akasema Mukasha “Nina wasi wasi sana kama atapiga “ “Usiwe na wasi wasi mheshimiwa rais atap..” Kabla Mukasha hajamalizia sentensi yake ikapigwa simu katika kompyuta iliyokuwa mbele ya rais ,bila kuchelewa akabonyeza kitufe cha kupokelea na katika kompyuta alionekana kijana mmoja mtanashati sana akiwa katika ofisi nzuri .Alikuwa ametulia na hakuonekana kuwa na chembe ya wasi wasi “Shikamoo mheshimiwa rais,naitwa Austin january” akasema Austin “Marahaba Austin,habari za huko? Maisha yanakwendaje? “Habari nzuri na maisha mazuri mheshimiwa rais,sijui nyie hapo Tanzania” “Sisi pia tunaendelea vizuri ,Tanzania iko salama” akasema Ernest. “Nafurahi kusikia hivyo mheshimiwa rais.Nimeelekezwa na mkuu wangu kuwa una maongezi na mimi.Naomba twende moja kwa moja katika kile unachohitaji kuongea nami.”akasema Austin.Ernest akakohoa kidogo na kusema “Kwanza nashukuru sana Austin kwa kukubali kuzungumza nami.Bila kupoteza muda utaniwia radhi kama nitazungumza mambo ambayo pengine hukupanga kuyasikia.” “ Endelea tu mheshimiwa rais” akasema Austin “ Austin ni mara ya kwanza mimi na wewe tunazungumza.Sikuwa nimekufahamu hapo kabla hadi hivi karibuni nilipoelezwa kuhusiana na historia yako na nini kilikutokea.Nilipoingia madarakani nilielezwa kuhusiana na tukio lililokupata wewe na wenzako ambalo lilitokea mwaka mmoja kabla sijaingia madarakani.Taarifa niliyopewa haikuwa kamili na haikuzungumza chochote kuhusu wewe kushiriki katika operesheni ile ya kwenda kuwakomboa madereva wa kitanzania waliotekwa nchini Somalia.Namshukuru sana mmoja wa wasaidizi wangu wa karibu ambaye amenifumbua macho na kunieleza ukweli halisi wa tukio hilo.Baada ya kuufahamu ukweli ndipo nilipoanza mchakato wa kukutafuta.Haikuwa kazi rahisi kwa mr Boaz kukubali ombi langu la kutaka kuonana nawe lakini baada ya majadiliano marefu nashukuru akanielewa .” akanyamaza na Austin akasema “ Mheshimiwa rais,pamoja na kuombwa na Boaz ambaye mimi namuita baba lakini haikuwa rahisi kwangu kukubali kuzungumza nawe hata hivyo baada ya kunieleza kwamba una jambo la muhimu la kuzungumza nami nikakubali kukusikiliza kwa hiyo mzee wangu naomba tuokoe muda na tujielekeze katika suala la msingi unalotaka kunieleza” akasema Austin “Nitakueleza Austin usijali.Nilianza kwanza na utangulizi.Kwa ufupi tu ni kwamba nimekutafuta kwa jambo moja kubwa.Ninataka urejee Tanzania” akasema Ernest na wote wakabaki kimya.Baada ya muda Austin akatoa kicheko kidogo na kusema “Me ??..Tanzania??Hahahahaha...That’s impossible Mr President.Jambo hilo haliwezekani kabisa” “Kwa nini isiwezekane Austin? “Do you real want to know? Kuna watu wachache walionifanya nikaichukia nchi yangu.I sacrificed my life for the country I real love.Mara kadhaa nimenusurika kifo nikifanya kazi za nchi yangu. Haikuwa rahisi kupenya katika maeneno yanayomilikiwa na Alshabaab lakini nilipenya na kufanikiwa kugundua mahala walikofichwa watu wetu na nikakiongoza kikosi maalum kwenda kuwakomboa lakini pamoja na hayo yote niliyoyafanya bado malipo yake ni kutaka kuuawa.Mheshimiwa rais umenitonesha kidonda ambacho tayari kimekwisha pona “ akasema Austin na tayari sura yake ilibadilika “Samahani sana Austin kwa kuirudisha tena kumbu kumbu hii katika kichwa chako lakini pamoja na hayo narejea tena kukuomba Austin kwama nakuhitaji urejee Tanzania .Kunak......” “Stop mr President!! Akasema Austin “Naomba ufahamu kabla hujaendelea mimi si raia wa Tanzania kwa sasa.Tayari nimechukua uraia wa nchi nyingine.Huku nina maisha mazuri na nimekwisha achana na kazi zangu za zamani.Tafadhali mheshimiwa rais ninaomba mniache niishi maisha yangu.Sihitaji bughudha kwa sasa.Kama hakuna lingine mzee naomba tumalize niendelee na shughuli zangu.”akasema Austin “Austin naomba tafadhali usiondoke kwanza.Kuna jambo nataka tuongee.Pamoja na mambo yote yaliyotokea na kupelekea ubadili uraia lakini wewe bado ni mtanzania.Uraia huo ni karatasi tu lakini mwili wako una damu ya Tanzania.Umezaliwa hapa,wazazi wako waliishi hapa,ndugu zako wako hapa so you belong here.This is your home.I beg you my son please come back home.” Akasema Ernest “mheshimiwa rais naomba usipoteze muda wako kwa kujaribu kunishawishi nirejee .Nimekwisha sema Tanzania sirudi tena so save your time” akasema Austin.Ernest akashusha pumzi na kusema “ Austin hapa mbele yangu ninalo faili lenye mambo yote yanayokuhusu wewe.Taarifa zako nyingi ziko humu.Usiniulize nimezipataje kwani mimi ni rais wa nchi na ninaweza kupata taarifa za mtu yeyote Yule ninayemtaka.” Akasema Ernest na Austin akaonekana kustuka kidogo. “Austin pole sana kwa kuwapoteza wazazi wako wote wawili .Baada ya wazazi wako kufariki kwa ajali ya ndege wewe ulibaki na jukumu la kumlea mdogo wako Linda.Baada ya tukio lile la Somalia ulitoweka na kumuacha Linda katika wakati mgumu sana.Alianza kushirikiana na magenge ya vijana wahuni na baadae alianza kujishughulisha na biashara ya dawa za kulevya.” “Oh my God !!..akasema Austin na sura yake ikabadilika “Austin you abandoned you sister.Kwa hiyo usistuke kwa mabadiliko ya tabia ya mdogo wako” “ Hapana sikumtelekeza Linda.Sikutaka kumueleza mahala nilipo kwa ajili ya usalama wake.Kama angefahamu mahala nilipo asingekuwa hai hadi leo hii.Hata hivyo nilimuachia mali nyingi,utajiri wote wa wazazi waliotuachia alibaki nao.Mali zangu zote alibaki nazo.Hakupaswa kujiingiza katika mambo hayo machafu” akasema Austin na kuinamisha kichwa.Alionekana kuchomwa sana na suala lile. Austin !! akaita rais na Austin akainua kichwa. “ taarifa hii najua imekuumiza lakini naomba upige moyo konde kwa hili nitakalokwambia ambalo naamini litakuumiza zaidi” “ Don’t tell me she’s dead” akasema Austin” “ Hapana Austin mdogo wako hajafariki yuko hai bado lakini kwa taarifa tulizonazo ni kwamba Linda kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka kumi na tano nchini China baada ya kukamatwa akijaribu kuingiza dawa za kulevya nchini humo.” “ Ouh my God!! Akasema Austin na kuinamisha kichwa “ I know it hurt Austin but you have to be strong.Sasa nisikilize kwa makini Austin.Ninao uwezo wa kumuondoa ndugu yako toka katika kifungo hicho anachokitumikia” akasema Austin “ Please help her Mr President” akasema Austin na macho yake yalionekana kulengwa na machozi “ Kama nilivyokueleza kuwa uwezo wa kumsaidia ninao lakini nitafanya hivyo pale tu nawe utakapokubali kunisaidia” Austin akafikiri kidogo na kusema “ Unahitaji nikusaidie nini ? “ Come back home.Kuna kazi ambayo nataka kukupa.Ni kazi binafsi na ambayo nina uhakika ni wewe pekee unayeweza kuifanya kikamilifu.Nakuahidi kukupatia ulinzi na chochote kile utakachohitaji.Ni juu yako sasa kuamua ni kitu gani hasa unakihitaji” Austin akafikiri kwa muda na kusema “ Mheshimiwa rais sina cha kuamua kwani tayari umekwiswha nifunga mikono .Nitakuja Dar es salaam kuifanya kazi yako kwa ajili ya kumsaidia mdogo wangu lakini naomba uniahidi kuwa baada ya kazi yako kukamilika utaniacha niondoke zangu nikaendelee na maisha yangu” “ Nakuahidi hivyo Austin.Mara tu kazi yangu itakapokamilika utakwenda kuendelea na maisha yako” “ Ahsante mheshmiwa rais.Lini unanihitaji Tanzania ? Lini mchakato wa kumtoa dada yangu gerezani utaanza?Ningependa nitakapoanza kazi yako tayari dada yangu awe ametoka gerezani au anakaribia kutoka.Kitukingine ambacho nataka nikubaliane nawe ni kwamba baada ya kutoka gerezani sitaki Linda arejee Tanzania nataka umtafutie makazi katika nchi nyingine akaishi maisha mazuri.Huko afunguliwe biashara au atafutiwe kazi nzuri aifanye.Tunakubaliana katika hilo? Akauliza Austin “ Hilo ni suala dogo sana kwangu Austin.Ninakuahidi kufanya kama unavyotaka.Kuhusu lini ninakuhitaji Tanzania,ninakuhitaji haraka sana.Nitatuma ndege sasa hivi ije ikuchuke ili hadi usiku wa leo uwe umefika hapa Dar es salam.” “ Sawa mheshimiwa rais.Nitakuja Tanzania” “ Austin nashukuru sana kwa kunikubalia ombi langu .Nakuahidi kila nilichokuahidi nitakitekeleza.” “ Mr President I’m doing this for my sister so you don’t have to thank me .Kama si yeye katu nisingekuja Tanzania” Pamoja na hayo bado nakushukuru pia Austin” “Mheshimiwa rais naomba nikukumbushe kuwa ujio wangu Tanzania ni siri kati yangu nawe.Watu waliotaka kuniua wakati ule bado wapo na wana nguvu kwa hiyo wakifahamu kuwa niko nchini lazima maisha yangu yatakuwa hatarini .Nadhani umenielewa.” “ Nimekuelewa Austin na niko makini sana kwa hilo.Usihofu utakuwa salama” “ Ahsante mheshimiwa rais” “ Ahsante Austin utataarifiwa na msaidizi wangu mara tu ndege itakapowasili hapo afrika kusini.” Akasema Ernest na kuagana na Austin. “ Thank you Mukasha .Wewe ndiye uliyefanya hili jambo likafanikiwa” “ Ahsante mheshimiwa rais” akajibu Mukasha huku naye akitabasamu “ By the way Mr President nimesikia ukimuahidi Austin kumsaidia kumtoa mdogo wake gerezani.Are you going to do that? Akauliza Mukasha “ Im a man of my words so Yes I’m going to do that.NItamsaidia mdogo wake Austin kutoka gerezani, kwa sasa jambo ninalolihitaji ni kuonana na balozi wa China hapa nchini jioni ya leo kwa hiyo andaa kikao .Halafu jioni ya leo pia nataka kuonana na mkuu wa magereza.Vikao vyote hivi ni vya siri na vitafanyikia pale hotelini kwangu.Jambo lingine ambalo nataka ulifanye ni kuandaa makazi ya Austin kwa muda wote atakaokuwa hapa nchini.Ninayo nyumba yangu kule Mikinda ambayo ilikuwa imekodishwa na ubalozi wa Denmark lakini kwa sasa haikaliwi na mtu baada ya balozi kuondoka .Ni nyumba nzuri ya kisasa ambayo naamini itamfaa.Ina ghorofa mbili,ina nafasi ya kutosha ,ina kila kitu ndani,bwawa la kuogelea ,chumba cha mazoezi na hata mfumo wake wa usalama ni mkubwa na wa kisasa.Nitahitaji vile vile gari tatu za kifahari zikae mle ndani ambazo Austin atazitumia.Nitampigia simu Hussein magari, tutachukua magari hayo kwake.Yeye huuza magari mazuri mapya na ya kisasa.Vitu vingine anavyovihitaji atakuja kutueleza pindi akifika huku” akasema rais na kuongozana na Mukasha wakatoka ndani ya kile chumba. ***************** Hali ya Dr Marcelo iliwaridhisha madaktari kuwa hakuhitajika tena kuwa katika kile chumba cha wagonjwa walio katika hatari.Maendeleo yake yalitia moyo sana na hivyo akatolewa na kupelekwa katika chumba kingine. Mchana huu ndani ya chumba walikuwemo baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliokuja kumjulia hali.Miongoni mwa watu waliokuwemi mle chumbani alikuwamo Daniel.Pamoja na Dr Marcelo kuonyesha maendeleo mazuri lakini bado hakuwa anaweza kuzungumza chochote .Madkatari waliendelea na uchunguzi wa kubaini kitu gani kilichosababisha Dr Marcelo akashindwa kuzungumza licha ya hali yake kuendelea vizuri.Aliweza kusikia kila pale alipoitwa na hata kutabasamu lakini hakuweza kuongea. Muda uliowekwa kwa ajili ya kuwatazama wagonjwa ulikaribia kumalizika hivyo wengi wa waliokuja kuwatembelea wagonjwa walianza kuondoka.Watu walipopungua mle chumbani Dr Marcelo akamfanyia ishara Daniel asogee karibu.Katika meza iliyokuwa karibu na kitanda kulikuwa na kijitabu kidogo na kalamu akaomba apatiwe akachana karatasi na kuandika “ Monica yuko wapi? Daniel naye akaandika “Amechelewa mchana huu atakuja jioni” Dr Marcelo akaichukua karatasi na kuandika “ Wasiliana naye mwambie namuhitaji sasa hivi afike hapa hospitali” Baada ya Daniel kuusoma ujumbe ule wa Marcelo akatoka akachukua simu yake kwa lengo la kumpigia Monica lakini kabla hajapiga Julieth dada wa Marcelo akatokea. “ Marcelo anahitaji nini? Akauliza Julieth na Daniel akampatia ile karatasi aisome ,akasogea pemeni na kumpigia simu Monica “ Hallow Daniel habari yako? Akasema Monica “Nzuri Monica.Uko wapi mida hii? Mbona hujafika hospitali kumtazama Marcelo? “ Nimeshindwa kufika mchana huu nimepata safari ya dharura hivyo niko katika maandalizi.Anaendeleaje? “ Maendeleo yake si mabaya ila bado hajaweza kuzungumza.Madaktari wanahisi labda ni tatizo la kisaikolojia na wanashauri kwamba awe karibu na watu wake wa karibu muda mwingi hii inaweza kumsaidia akaweza kuzungumza tena.Nimewasiliana naye muda mfupi uliopita kwa njia ya maandishi na amenisisitiza kwamba anahitaji sana kukuona sasa hivi.” Akasema Daniel.Monica akatafakari kidogo halafu akasema “ Daniel bado uko hapo hospitali? “ Ndiyo bado niko hapa” “ Sawa ninakuja hapo muda si mrefu” akasema Monica Mara tu alipomaliza kuzungumza na Daniel ,akavaa haraka haraka akaingia garini na kuondoka kuelekea hospitali.Aliwasili hospitali na kukuta tayari muda wa kutazama wagonjwa umekwisha,akashuka garini na kuelekea moja kwa moja katika chumba alimohamishiwa Marcelo.Nje ya chumba hicho akamkuta Daniel akimsubiri. “ Ahsante kwa kuja Monica.Marcelo anakuhitaji sana”akasema Daniel. “ Vipi maendeleo yake? “ Ni kama vile nilivyokueleza simuni “ akasema Daniel na kuufungua mlango wakaingia ndani .Uso wa Dr Marcelo ukajenga tabasamu baada ya kumuona Monica.Julieth na Daniel wakatazamana wakatabasamu “ How are you Marcelo? Akauliza Monica huku akisogea karibu na kitanda cha Dr Marcelo ambaye alimtazama bila kutamka chochote. “ Usijali Marcelo utapona tu.” Akasema Monica huku akionekana kulengwa na machozi.Dr Marcelo akamfanyia ishara Daniel ampatie kalamu na karatasi akaandika ujumbe Fulani na kumpatia Monica. “ Soma kwa siri” ndivyo kichwa cha ujumbe ule kilivyosomeka.Baada ya kichwa kile ujumbe ukaendelea. “ Monica fanya lolote uwezalo unitoe hapa hospitali kwani ninataka kuuawa.One of them visited me last night.Please do it quick and don’t let anybody know.You are my only hope.” Haraka haraka Monica akaukunja ujumbe ule na kuuweka katika mfuko wa suruali halafu akatabasamu na kusema “ Usijali Marcelo ,kesho nitakuletea vitu vyote ulivyoagiza ila nataka nitakapokuja kesho uwe tayari unaongea” Marcelo akatabasamu .Monica hakutaka kukaa sana pale hospiali kwani alihitaji kupata muda wa kujiandaa kwa safari ya jioni.Akaagana na Marcelo na kutoka.Mara tu alipotoka nje Julieth dada wa Marcelo akamfuata. “ Marcelo alikwambia ana hitaji nini? Akauliza “ Kuna baadhi ya vitu ameniagiza,nitamletea kesho” “ Jamani kwa nini amekusumbua namna hii? Nipe mimi hiyo orodha ya hivyo vitu nikavitafute” akasema Julieth “ Usijali Julieth nitavitafuta na kuvileta mwenyewe kesho” akajibu Monica na kuondoka kuelekea maegesho akaingia katika gari lake.Akaitoa karatasi ile yenye ujumbe alioandika Marcelo akarudia kuusoma na akahisi kijasho kikimtoka.Akawasha gari na kuondoka “ Sitaki kuamini eti Dr Marcelo amepatwa na tatizo la akili hadi akaandika ujumbe huu.Nina hakika lazima kuna kitu kinachoendelea.Lazima jambo hili ni la kweli lakini nani hao wanaotaka kumuua na kwa nini? Akajiuliza “ One of them visited me last night” akakumbuka moja ya sentensi katika ujumbe ule. “ Inaonekana Marcelo anawafahamu watu hao wanaotaka kumuua lakini kwa nini hawaweki wazi kwa vyombo vya usalama wawashughulikie? Kwa nini hataki mtu mwingine yeyote ajue kuhusu watu hao wanaotaka kumuua? Ninahisi kuna jambo kubwa linaloendelea hapa na ndiyo maana hataki kuliweka wazi suala hili hata kwa ndugu zake.Nadhani suala hili ni kubwa zaidi ya ninavyofikiria .Nitafanya nini sasa kumsaidia ? Nitamuondoaje pale hospitali? Au nikatoe taarifa polisi? Monica akaendelea kujiuliza maswali mengi “ Hapana sitakiwi kuwashirikisha polisi katika hili.Kama angehitaji msaada wa jeshi la polisi angenieleza lakini amesema kwamba hataki mtu mwingine yeyote afahamu kuhusu suala hili.Ameniamini mimi peke yangu na amekiri mimi ndiye tumaini lake.I must find a way to help him.Najua ni jambo gumu na la hatari lakini lazima nitafute namna ya kumsaidia.He’s my friend and I cant just let him die” Monica alifika nyumbani kwake na kuendelea na zoezi la kujiandaa kwa ajili ya safari. “ Laiti ningekuwa sijampa uhakika David kuwa nitakwenda Congo ningeahirisha safari hii ili nipate muda wa kushughulikia suala la Marcelo lakini kwa sasa siwezi tena kuahirisha kwani tayari ndege iko angani ikija kunichukua.Ngoja niende Congo nitakaporejea nitalishughulikia suala hili.Naomba Mungu Marcelo awe salama hadi hapo nitakapokuwa nimrejea toka Congo” akawaza Monica ege linalotajwa kuwa kubwa kuliko zote zinazotumiwa na marais wa afrika linalomilikiwa na rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo David Zumo tayari lilikwishatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumchukua mwanamke mrembo kuliko wote Afrika ,Monica Benedict Mwamsole. Ilipotimu saa kumi na moja za jioni ,gari ya Monica ikawasili pale uwanjani.Ndani ya gari alikuwa peke yake kwani hakutaka watu wafahamu kama anasafiri .Tayari wazazi wake walikwisha wasili kitambo na walikuwa wakimsubiri yeye ili wamuage .Walitumia kama dakika kumi hivi wakibadilishana hili na lile na kumpa Baraka zao wakimtakia safari njema.Monica akaingia katika jengo la uwanja kwa ajili ya taratibu za safari .Alipokamilisha taratibu zote akaenda kuagana na wazazi wake kisha akaongozana na wahudumu wanne wa dege hilo waliovalia nadhifu kabisa kuingia ndegeni “ Ama kweli David amedhamiria.Kutuma dege kubwa kama hili kwa ajili ya tu ya kuja kunichukua mimi si kitu kidogo.” Akawaza Monica wakati akipanda ngazi kuingia ndegeni “ Karibu sana mama Monica” Monica akasalimiwa na Jean Pierre Muyeye “ Jean Pierre Muyeye!! Akasema Monica kwa furaha Pierre akampeleka Monica katika sehemu mbalimbali za ndege ile akamtambulisha kwa marubani na wahudumu wengine halafu akampeleka katika chumba maalum cha rais.Saa kumi na moja na nusu dege likapaa na safari ya kuelekea Kinshasa ikaanza.Ndani ya ndege wahudumu wachangamfu walijitahidi kumuhudumia Monica kwa kila alichokihitaji na kuufanya uso wake usikauke kwa tabasamu “ Nimepanda ndege nyingi lakini sijawahi kupanda ndege nzuri ya kifahari kama hii.Kweli David ni tajiri mkubwa.Yeye ni rais pekee Afrika anayemiliki ndege yake binafsi tena kubwa kama hii ambayo inafanana kwa kila kitu na ndege ya rais wa marekani.” Akawaza Monica na uso wake haukukauka tabasamu “ Endapo nitakubali kuolewa na David ndege hii pia itakuwa ya kwangu na nitaipanda muda wowote kwenda sehemu yoyote ninayotaka kwenda.This is life.Kama alivyonishauri mama misimamo mingine haina maana sana kitu kikubwa ni kuangalia moyo na dhamira ya mtu.David ameonyesha wazi kwamba ananipenda .Kwa maisha kama haya mwanamke gani anaweza kukataa ombi la kuolewa na mtu kama David Zumo?Nitachekwa hadi na ndege mwitu nikisema hapana” akawaza Monica akiwa ndani ya chumba cha kifahari cha David Zumo ndani ya ndege hii kubwa Mr Jing wang Zhu,karibu sana .Nimefurahi kukutana nawe jioni hii ya leo” Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akaanzisha mazungumzo baada ya kukutana na balozi wa China nchini Tanzania katika hoteli yake.Tayari kiza kimekwisha tanda angani na kwa mujibu wa saa ilionyesha mida hiyo ilipata saa moja na na dakika saba za jioni. “ Mheshimiwa rais hata mimi nimefurahi sana kukutana nawe jioni ya leo.Nilikuwa na miadi ya kukutana na wageni jioni hii lakini baada ya kupata ujumbe wa kutaka kuonana nawe imenilazimu kuvunja miadi hiyo na kuja kukusikiliza.Naamini kuna jambo la muhimu la kujadili” akasema Jing wang Zhu “ Ni kweli mheshimiwa balozi.Kuna suala la msingi ambalo limenifanya nitake kuonana nawe jioni ya leo” Ernest akanyamaza kidogo baada ya sekunde kadhaa akaendelea “ Mheshimiwa balozi sitaki nitumie muda wako mwingi kuelezea kuhusu mahusiano mazuri ya kindugu baina ya nchi zetu mbili.Mahusiano yetu yamekuwa makubwa sana katika Nyanja zote za kiuchumi na kidiplomasia .Mahusiano hayo mazuri ndiyo msingi wa maongezi yetu usiku huu” akasema Ernest. “ Nakusikliza mheshimiwa rais” akasema Jing “ Kuna raia wangu mmoja anatumikia kifungo cha miaka kumi na tano katika gereza moja nchini China kwa kosa la kujaribu kuingiza madawa ya kulevya nchini China.Ninamuhitaji msichana huyo na ninataka nimkomboe kwa hiyo nimekuita jioni hii ili tujadiliane namna ya kuweza kulifanikisha suala hili” akasema Ernest.Balozi Jing wang akavua miwani yake akachukua kitambaa akafikicha macho na kusema “ Mheshmiwa rais,nadhani unafahamu sheria za China kuhusu watu wanaokutwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya zilivyo kali.Serikali ya China haina masihara katika suala hili na mfanya biashara wa dawa za kulevya sisi tunamchukulia kama muuaji na ndiyo maana wengi wao wanauawa na wengine kutumikia kifungo kirefu gerezani.Kwa hiyo mheshimiwa rais suala hilo unalolihitaji naweza kusema ni gumu sana kwangu Watu kama hao ni hatari mno kwa watu wa China na hatuna huruma nao hata kidogo” akasema Jing wang Zhu “ Mheshimiwa balozi,nafahamu ugumu wa jambo hili na ndiyo maana hapo awali nilitangulia kuelezea kuhusu mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi zetu mbili China na Tanzania.Suala hili linaweza kumalizwa kirafiki tu bila kuathiri uhusiano wetu mzuri.Msichana huyu ninamuhitaji sana arejee Tanzania na kwa ajili yake niko tayari kufanya mabadilishano kati yake na raia kumi wa China waliofungwa hapa nchini.Kuna raia nane wamefungwa miaka hamsini kila mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali ,wengine wawili wamehukumiwa kunyongwa kwa kosa la mauaji.Nitawaachia hawa wote kwa ajili ya kumpata huyo mtanzania mmoja” akasema Ernest “ Mheshimiwa rais ninaiona nia yako ya dhati ya kutaka kumkomboa mtu wako huyo na ndiyo maana uko tayari kuwaacha watu hao wengi waliohukumiwa hapa Tanzania.Pamoja na utayari huo lakini suala hili siwezi kulitolea maamuzi hapa.Ninaomba nilichukue na niliwasilishe kwa wakuu wangu na watakachokiamua nitakujulisha.Ninakuahidi kufanya kila linalowezekana ili jambo hili lifanikiwe” akasema balozi Jing wang Zhu Maongezi kati ya balozi Jing wang Zhu na rais Ernest Mukasa yaliwapeleka hadi saa mbili na nusu za usiku kisha wakaagana balozi akaondoka zake.Baada ya balozi kuondoka mzee Mukasha akamfuata rais “ How did it go mr Mresident? Akauliza “ Mambo yamekwenda vizuri sana.Tumekuwa na mazungumzo mazuri amelipokea suala langu na ameniomba nimpe muda awasiliane kwanza na viongozi wake halafu atanipa jibu.Nina uhakika mkubwa kwa ombi langu kukubaliwa kwani mimi na rais wa China ni marafiki sana.Sasa nahitaji kuzungumza na mkuu wa magereza.Naomba umruhusu aje nionane naye tafadhali.” Akasema rais na kamishna jenerali wa magereza Elimeleck Akwisa akaingia KINSHASA –DRC Saa mbili na nusu juu ya alama dege la kifahari aina ya Boeing 747 mali ya rais David Zumo ikatua katioka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kinshasa.Usiku huu jiji la Kinshasa lilikuwa linang’aa na kupendeza ukitokea angani. “ Sikujua kama jiji la Kinshasa linapendeza hivi ukilitazama kutokea angani.Hii ni kazi ya David Zumo.Amelibadilisha mno jiji hili na kuwa mojawapo ya majiji yanayovutia zaidi Afrika “ akawaza Monica akilishuhudia jiji la Kinshasa akiwa ndegeni Dege lilitua na kusimama,Monica akawashukuru marubani na wahudumu kwa kumfikisha salama kisha akaonozana na Pierre Muyeye kushuka ngazi. Alipomaliza kushuka ngazi Monica akapokewa na watoto wawili wadogo waliomkabidhi maua akainama na kuwakumbatia akawabusu halafu Muyeye akamuongoza walikokuwa wamesimama watu zaidi ya ishirini “Monica kutana na Pauline Zumo mke wa rais David Zumo.Hapa Congo anajulikana kama Malkia.” Muyeye akamtambulisha Monica kwa Pauline.Nusura maua aliyokuwa ameyashika Monica yamponyoke kwa mstuko.Hakuwa ametegemea kabisa kama mke wa David Zumo angeweza kuja kumpokea pale uwanja wa ndege.Pauline alikuwa ni mwanamke mrembo na usiku huu alikuwa aking’aa kwa vito vya thamani alivyovaa . “ Monica karibu sana Congo.Karibu sana Kinshasa.Jisikie nyumbani” akasema Pauline huku akitabasamu.Monica naye akatabasamu wakaongea mawili matatu kila mmoja akimsifia mwenzake kwa namna alivyopendeza halafu Pauline akaanza kumtambulisha Monica kwa watu aliokuwa ameongozana nao pale uwanjani.Baada ya hapo wakaingia katika gari la kifahari wakaondoka pale uwanjani.Ulinzi ulikuwa ni mkali sana.Ndani ya gari Monica na Pauline walikuwa wanaongea mambo kadhaa na kucheka.Kwa muda huu mfupi walitokea kuzoeana kama watu wanaofahamiana kwa muda mrefu Msafara ule uliwasili katika jumba moja kubwa la kifahari lililowaka taa nyingi za kupendeza.walinzi wawili wakafungua milango ya gari lile la kifahari walimokuwamo akina Monica ,wakashuka.Pauline akamuogoza Monica kuingia ndani ya jumba lile lililokuwa na uzuri wa kipekee sana.Walikwenda hadi ghorofa ya pili kulikokuwa na sebule kubwa iliyosheheni samani za gharama kubwa “ Nimeingia katika sebule nyingi kubwa na nzuri laini sijawahi kuingia katika sebule nzuri kama hii.Ina uzuri usioweza kuelezeka.” Akawaza Monica “ Monica karibu sana hapa ni sehemu ambayo wageni muhimu wa rais hufikia.Si sehemu kubwa sana ila tumejaribu kuifanya iwe ya kupendeza.Ni imani yangu utapafurahia mahala hapa.” Akasema Pauline. “ Wahudumu wapo hapa kwa saa ishirini na nne na kazi yao ni moja tu,kukuhudumia.Wapo wapishi ambao watakupikia chakula chochote ukitakacho,kuna saluni humu ndani na wapo wahudumu maalum watakaokuremba kwa staili yoyote ile uitakayo.Ulinzi upo wa kutosha na wa uhakika..Monica nimefurahi sana kuonana nawe ana kwa ana .Narudia tena kuwapongeza wale waliokutaja kuwa ni mrembo kuliko wote Afrika ,hawakukosea.Una uzuri wa ajabu sana” akasema Pauline na wote wakacheka “ Ahsante Pauline lakini hata wewe ni mrembo pia” akasema Monica “ Nakubali mimi ni mzuri lakini kwako sifiki hata robo.Monica umebarikiwa uzuri wa kipekee “ akasema Pauline halafu akamuomba Monica waongozane kwenda katika chumba cha chakula Katika chumba cha chakula walikuwemo wahudumu waliovalia nadhifu ,wakiwa wamesimama kwa adabu tayari kabisa kutoa huduma ya chakula kwa Pauline na mgeni wake.Monica akawasalimu wahudumu wale halafu wakaketi katika meza kubwa yenye viti kumi na mbili .Vyombo vyote vilivyotumika kwa chakula vilikuwa vya dhahabu.Uzuri wa jumba hili ulimsisimua mno Monica. “ Kweli huyu ndiye tajiri wa Afrika.Pamoja na kukulia katika utajiri lakini sijawahi hata mara moja kula kwa kutumia sahani au kijiko vyote vya dhahabu.Haya ni maisha ya kifahari mno.” Akawaza Monica wakati wakiendelea kupata chakula Walipomaliza kula Pauline akampeleka Monica katika chumba ambacho angelala kilichokuwa katika ghorofa ya tatu.Kilikuwa ni chumba kikubwa kilichosheheni samani za gharama kubwa “ Monica hiki ni chumba ambacho utalala.Sifahamu unapendelea vitu gani katika chumba chako cha kulala lakini nimejitahidi kukiweka kifanane na hadhi ya malkia wa afrika.Kama kuna mapungufu yoyote utanijulisha” akasema Pauline “Pauline ahsante sana.Hiki ni chumba kizuri mno .Nimekipenda sana” akasema Monica na Pauline akatabasamu “ Ahante Monica kama umekipenda .Naomba nikuache upumzike .Kesho saa nne asubuhi nitakuja kukuchukua tutakwenda sehemu kupata chakula cha mchana pamoja na maongezi kidogo” akasema Pauline halafu akamuelekeza Monica mambo kadhaa ya mle chumbani ,akaondoka “ Haya yanayonitokea mbona naona kama ni ndoto?Mambo yamekuwa tofauti sana na nilivyotegemea.Nimealikwa na David Zumo kuhudhuria kongamano la vijana ambalo alidai linaanza kesho lakini kesho Pauline amesema kwamba atanichukua twende mahala tukapate chakula cha mchana na maongezi kidogo.Mhh !! haya ngoja nisubiri nione nini kinachoendelea hapa.hata hivyo nimempenda Pauline,ni mwanamke mkarimu sana.kwa namna alivyonipokea sina hakika kama anafahamu chochote kuhusu mambo anayotaka kuyafanya mume wake.Sina hakika kama anafahamu mume wake anataka kunioa.Baada ya kuonana na Pauline nadhani sintakubaliana tena na ombi la David.Siwezi kuingilia ndoa ya Pauline na kuiharibu furaha aliyonayo.Sitaki kuibomoa ndoa yake.Sitaki kumuumiza .Kwa namna sisi wanawake tulivyo pindi akigundua kitu anachotaka kukifanya mume wake urafiki wetu utatoweka na tutakuwa maadui.Sitaki jambo hilo initokee.Kama ni utajiri na mali hata mimi ninaweza kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia vipawa ambavyo Mungu amenijalia na nikaupata.” Akawaza Monica baada ya Pauline kuondoka.Mara akamkumbuka Dr Marcelo “ Masikini Dr Marcelo sijui anaendeleaje hivi sasa..Mpaka sasa bado sijapata njia ya kuweza kumsaidia kumtoa pale hospitali. Naomba aendelee kuwa salama hadi hapo nitakaporejea Dar es salaam ili nitafute namna ya kufanya kumuokoa dhidi ya watu wanaotaka kumuua.Najua ni suala la hatari but I’m too involved now and I must help him” akawaza huku akijiandaa kwenda kuoga. DAR ES SALAAM – TANZANIA Inakaribia saa tano za usiku,bado rais Ernest Mkasa alikuwa hotelini akiwa na mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Magereza .Walikuwa na maongezi ya kina sana.Wakiwa bado katika maongezi akaingia Mukasha na kumnong’oneza rais jambo na kutoka “ Kamishna nimepata dharura kidogo nalazimika kwenda sehemu Fulani.Nakushukuru sana kwa kufika na kwa kunielewa.Nitawasiliana nawe tena muda wowote nitakapopata jibu toka kwa balozi wa China.Naomba nikukumbushe kuwa mambo haya tuliyoyazungumza ni ya siri kubwa na jitahidi asifahamu mtu mwingine yeyote.” “ Mheshimiwa rais usiwe na wasi wasi kabisa ,mambo yote yatafanyika kwa siri sana na hakuna yeyote atakayejua.Mheshimiwa rais ahsante sana naomba sasa niende ili nikupe muda wa kuendelea na majukumu mengine.” Akasema mkuu wa magereza na kusimama akampa mkono rais wakaagana.Baada ya mkuu wa magereza kuondoka Ernest akamuita mlinzi wake mkuu “ Evans kuna sehemu nataka kwenda usiku huu lakini sihitaji kwenda na msafara au walinzi zaidi yako kwani sitaki kufahamika.Ninataka nitumie gari la kawaida ambalo si rahisi kwa mtu yeyote kuhisi kuwa rais anaweza akalitumia.Najua taratibu haziko hivyo lakini ninalotaka kufanya ni la muhimu mno” “ Sawa mheshimiwa rais naomba unipe dakika kumi nifanye maandalizi” akasema Evans na kutoka.Ernest akaingia chumba cha kulala akafungua kabati na kuchagua mavazi ya kuvaa .Alichagua suruari ya jeans ya bluu na shati zuri halafu akavaa koti jeusi ,kofia na miwani myeusi.Shingoni akavaa mkufu mkubwa wa dhahabu.Mwisho kabisa akaweka ndevu za bandia kidevuni na haikuwa rahisi kumtambua kuwa ni rais Ernest Mkasa.Akajitazama katika kioo na kutabasamu “Kwa muonekano huu hata mke wangu hawezi kunitambua.” Akawaza Ernest halafu akampigia simu Mukasha akamtaarifu kuwa yuko tayari.Baada ya dakika mbili Mukasha na Evans wakaingia mle chumbani “ Mzee tayari kila kitu kimekamilika na tunaweza kuondoka.Tutapita upande huu wa nyuma na kwenda hadi katika maegesho ya VIP 2.Hakuna mtu yeyote upande ule atakayekutambua “ akasema Evans “ Evans sitaki gari zaidi ya mbili” akasema Ernest “ “ Ndiyo mzee kuna gari mbili tu.Moja utapanda wewe na mzee Mukasaha na nyingine nitakuwepo mimi na walinzi wengine wawili.Mheshimiwa rais pamoja na kwamba safari hii ni ya kibinafsi lakini lazima uwe na ulizi wa kutosha kwa hiyo tutakuwa walinzi watatu” “ Sawa Evans.Tunaweza kuondoka” akasema Ernest na kumgeukia Mukasaha “ Tutawahi kabla ya ndege haijatua? “ Ndiyo mzee.Ndege itatua baada ya dakika ishirini toka sasa kwa hiyo tutawahi.Usiku huu magari yamepungua sana barabarani” akasema Mukasha.Walitoka ndani ya kile chumba wakapita upande wa nyuma hadi mahala zilikoegeshwa gari mbili .Evans akamfungulia rais mlango katika gari la nyuma akaingia pamoja na Mukasha halafu yeye na walinzi wawili wakaingia katika gari la mbele wakaondoka pale hotelini.Mukasha ndiye aliyekuwa akiendesha gari lile alimopanda rais “ Kila kitu tayari kimekaa sawa kilichobaki kwa sasa ni kusubiri jibu la kutoka China ili mchakato wa mabadilishano uweze kufanyika mara moja” Ernest akamueleza Mukasha wakiwa garini “ That’s good Mr President” akajibu Mukasha na safari ikaendelea kimya kimya.Waliwasili uwanja wa ndege dakika nne kabla ya muda wa ndege waliyoisubiri kuwasili. “ Tumewahi mheshimiwa rais.Ndege inatagemewa kuwasili ndani ya dakika chache zijazo” akasema Mukasha Hatimaye ndege waliyokuwa wanaisubiri ikawasili katika muda ule ule uliopangwa.Hii ilikuwa ni ndege maalum ya rais yenye kasi ya aina yake iliyotumwa na rais kwenda Afrika ya kusini kumchukua Austin January na kumleta Dare s salaam.Tayari Mukasha na mlinzi mmoja walikwisha ingia ndani ya uwanja kwa ajili ya kumpokea Austin.Mlango ukafunguliwa na Austina akiwa ameambatana na wanausalama wawili waliotumwa kumfuata Afrika ya kusini wakashuka na kupokewa na Mukasha halafu akamuongoza kutoka nje ya uwanja moja kwa moja hadi katika gari alimo rais akamfungulia Austin mlango na kumtaka aingie.Mizigo ya Austin ikaingizwa katika gari la walinzi na bila kupoteza hata dakika moja wakaondoka pale uwanjani. “ Hallow Austin “ akasema Ernest na kuivua kofia aliyokuwa ameivaa,akatoa miwani na zile ndevu za bandia “ Mr President !! Austin akashangaa.Alipoingia mle garini hakuwa amemtazama vizuri mtu aliyekuwa amekaa pembeni yake na wala hawakusalimiana. “ Pole na safari Austin,Karibu tena Tanzani” “ Mr President what are you doing here? Samahani sikujua kama ni wewe.Umebadilika sana” akasema Austin “ Nimefanya hivi ili niweze kuja kukupokea mimi mwenyewe na nihakikishe kama kweli umefika Tanzania.Wewe ni mtu muhimu sana” “ Ahsante mheshimiwa rais” akasema Austin na kugeuza shingo kutazama nje .Alionekana kutokuhitaji maongezi. “ Nimefurahi Austin amefika salama.Anaonekana ni kijana mahiri sana.Hana maongezi mengi.Anaonekana ni mtu wa kazi tu.Huyu atanifaa sana kunifanyia kazi zangu za siri.Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha haondoki tena Tanzania ili nimuajiri kwa ajili ya kazi zangu.Nimesoma faili lake,amepata mafunzo ya hali ya juu sana ya ujasusi .Amepata mafunzo nchini Israel,Marekani,China na hata japan.Amepata pia mafunzo nchini Iran na Iraq kuhusiana na mitandao ya kigaidi na namna wanavyofanya kazi zao.Amefanya pia mafunzo ya kupambana na magaidi akiwa na vikosi vya Marekani nchini Afghanistani na ameiva sana katika kupambana na magaidi.Anazifahamu mbinu nyingi wanazotumia magaidi na ndiyo maana aliweza hata kufahamu mahala walikofichwa Watanzania waliotekwa na kundi la Alshabaab nchini Somalia na akakiongoza kikosi maalum kwenda kuwakomboa.Taifa linapaswa kujivunia kuwa na mtu kama huyu lakini nashangaa kwa nini alitaka kuuawa? Inawezekana aligusa maslahi ya watu Fulani na ndiyo maana akaonekana ni mtu mbaya na hivyo akatakiwa afe.Suala lake ni kubwa na ndiyo maana limefanywa siri.” Akawaza Ernest na kugeuza shingo akamtazama Austin “ Anaonekana bado ana hasira na Tanzania na kama isingekuwa mdogo wake katu asingekubali kuja .Kijana huyu ni hazina kubwa kwa taifa hili na nitamlinda.Anatakiwa kulindwa kama mboni ya jicho.” Akaendelea kuwaza Ernest.Safari ikaendelea kimya kimya Walifika Mikinda iliko nyumba ya Ernest ambako ndiko Austin atakapoishi.Ni nyumba nzuri ya ghorofa mbili iliyozungukwa na ukuta mrefu imara .Milango ya gari ikafunguliwa Ernest na Austin wakashuka “ Karibu ndani Austin” Ernest akamkaribisha ndani Austin. “ Austin hapa ndipo utakapoishi.Hii ni nyumba yangu na miezi michache iliyopita alikuwa akiishi balozi wa Denmark hapa nchini.Ni nyumba kubwa ya ghorofa mbili.Ina mfumo wa kisasa wa ulinzi .Nitaongeza vile vile walinzi watatu wa kukulinda.Kesho asubuhi watakuja wafanyaazi wawili mmoja kwa ajili ya kukupikia na mwingine kwa ajili ya kazi nyingine za ndani kufua n.k.Hapo nje kuna gari tatu za kisasa ambazo utazitumia.Kama kuna chochote kingine utakachokihitaji utanijulisha.” Akasema Ernest.Ukapita ukimya mfupi Ernest akasema “ Kama hutajali naomba nikuzungushe katika sehemu mbali mbali za jumba hili uzifahamu” Walizunguka sehemu mbali mbali za jumba lile na sehemu ya mwisho ikawa katika chumba cha kulala.Kilikuwa ni chumba kizuri kikubwa kilichochukua sehemu kubwa ya ghorofa ya pili.Mle chumbani wakaketi katika sofa nzuri nyeupe “ Austin umeiona nyumba imekuridhisha? Naomba uwe muwazi kama haijakuridhisha nieleze ili nikutafutie nyumba nyingine mimi nina nyumba nyingi.” Akasema Ernest na kutoa mkebe katika koti akaufungua na kutoa sigara kubwa akaiweka mdomoni halafu akatoa nyingine na kutaka kumpa Austin “ Cigar ?... akamuuliza Austin endapo angehitaji “ No thanks.” Akajibu Austin.Ernest akawasha sigara yake na kuvuta mikupuo kadhaa “ Mzee kuna mambo mawili ambayo nataka niyaweke wazi kwako” akasema Austin “ Karibu” akasema Ernest “ Kwanza nataka mifumo yote ya usalama katika nyumba hii itolewe, na wala sihitaji mtu yeyote wa kunilinda.Nitaweka mifumo yangu mwenyewe ninayoiamini.Sihitaji pia mfanyakazi , kazi zote nitafanya mwenyewe.Jambo la pili nataka kufahamu kuhusu mchakato wa kuachiwa huru dada yangu umefikia wapi.Sintoifanya kazi yako yoyote hadi hapo nitakapohakikisha kweli dada yangu ameachiwa huru.” Akasema Austin.Ernest akavuta mkupuo mkubwa na kupuliza moshi mwingi hewani na kusema “ Tukianzia na suala hilo la pili,tayari mchakato umekwisha anza na uko katika hatua nzuri.Tayari nimekwisha zungumza na mamlaka za China na ninachosubiri ni jibu toka kwao muda wowote kwa hiyo usiwe na wasi wasi Austin niamini na kila kitu kitakwenda vizuri.Kuhusu usalama hilo ni jukumu langu kukulinda kwani ndiye niliyekuleta hapa.Maadui zako bado wapo na wakifahamu kuwa upo hai na umerudi Tanzania watasuka mipango ya kutaka kukuangamiza tena .Sitaki jambo hilo litokee na ndiyo maana ninataka kuimarisha ulinzi kila mahala ulipo.Niruhusu nitumie nguvu niliyo nayo kukulinda Austin” “ Ahsante mheshimiwa rais,sijamaanisha kuutoa mfumo huu wa usalama hapa ndani basi nikae bila kujilinda la hasha ,nitaweka mfumo wangu wa ulinzi ninaouamini zaidi” akasema Austin “ sawa Austin uko huru kufanya chochote utakachojiskia kufanya lakini usisite kuomba msaada wowote utakaohitaji muda wowote” akasema Ernest “ Ahsante mheshimiwa rais.Kwa sasa mimi na wewe nadhani hatuna chochote cha kuongea .Tutazungumza pale dada yangu atakapokuwa ametoka gerezani .Naomba nikutakie usiku mwema mheshimiwa rais” akasema Austin na kuinuka akampa mkono Ernest wakatoka mle chumbani wakashuka chini.Ernest akawachukua watu wake wakaondoka “ mambo yamekwendaje mheshimiwa rais? Akauliza Mukasha “ Mambo bado.Mchakato wa kumtoa gerezani mdogo wake ukikamilika ndipo tunaweza kuzungumza lakini kwa sasa amekataa tusizungumze chochote.” Akasema Ernest na kuegemea kiti “ Toka nimekuwa rais nimekuwa karibu sana na hawa watu wa usalama wa taifa lakini sijawahi kukutana na mtu kama Austin.Nitahakikisha haondoki Tanzania ” akawaza Ernest “ Im back again.Back to Tanzania” akawaza Austin akiwa amekaa kibarazani akitazama mataa ya jiji la Dar es salaam “ Niliapa kutokurudi tena Tanzania lakini nimevunja kiapo changu na nimerejea tena.Sina namna nyingine ya kufanya kumsaidia dada yangu atoke gerezani zaidi ya kukubali kuifanya kazi ya rais.Masikini Linda kwa nini aliamua kujiingiza katika biashara hizo haramu wakati alikuwa na utajiri mkubwa ambao ungemuwezeha kuendesha maisha yake kwa miaka mingi bila hata kufanya kazi? Lakini yote haya yamesababishwa na mimi kutokuwepo.laiti kama ningekuwepo karibu naye asingejiingiza katika mambo kama haya.Lazima nifanye kila lililo ndani ya uwezo wangu kumsaidia.Siwezi kujilaumu sana kwa sababu sikuwa na namna nyingine ya kufanya kwa wakati ule zaidi ya kutoweka.Nisingeweza kurejea Tanzania na wala nisingeweza kumueleza Linda mahala nilipo kwa ajili ya usalama wake.Angefahamu mahala nilipo ningemuweka katika hatari kubwa.” Akawaza Austin “ Akifanikiwa kutoka gerezani sitaki arejee tena Tanzania.Nataka akaishi mbali ambako ataanza maisha mapya .Nitamsaidia kuanzisha biashara kubwa na ataishi maisha mazuri.Nikimaliza kazi ya rais nitaondoka na sintarejea tena Tanzania na nitafanya mipango ya kuungana na dada yangu tena.” Akawaza Austin na kumbu kumbu nyingi zikaanza kumjia kichwani “ I loved this country with all my heart lakini kwa sasa ninaichukia .Ninaichukia Tanzania kwa sababu ya YA 20 watu wachache walioiuza nchi hii na kuitumbukiza katika mambo machafu ya laana .Kwa mfano hivi sasa kuna mswaada unaotaka kuwasilishwa bungeni ambao unataka kutambua haki za wapenzi wa jinsia moja na utoaji mimba. 


ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog