Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

SAYARI YA KIFO - 2

 










Simulizi : Sayari Ya Kifo

Sehemu Ya Pili (2)







Kituo cha Polisi cha Oysterbay, unazuka ubishi kati ya askari wawili, mmoja akitaka kumsaidia mtuhumiwa moja alietaka kuwajulisha nduguze juu ya kuwepo kwake pale lakini mwingine aligoma na kumwambia hiyo sio sheria.



Ubishi ukawa mzozo, kila mmoja akiona kama sheria inavunjwa kwa makusudi na mwenzie

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ni haki yake kuwajulisha watu wake juu ya uwepo wake sehemu kama hii, huwezi kujua huenda ndugu zake huko walipo wanamtafuta na wala hawajui ni wapi alipo,” alisema askari mmoja na mwenzie akamjibu



“Siku zote watu wanaotafutwa huwa wanaanza kutoa taarifa Polisi kisha ndio huenda wapi huko Sijui mahospitalini na sehemu nyingine, hivyo haina haja ya kusumbuka, kwanza mtu mwenyewe ana wiki humu, angekuwa ni muhimu angekuwa anatafutwa na tungejua,” afande huyu alikuwa ni muongeaji kuliko mwenzie na hivyo alimzidi kwenye maongezi na ikamlazimu Yule mwingine anyamaze.



Inspekta Jitu alikuwa kwenye mwendo wa kasi akitumia pikipiki ya jeshi la Polisi, safari yake alilenga kuelekea eneo la Bunju ambapo mwili wa Allen ulikutwa ukiwa umeuawa.



Pamoja na kuuawa, baadhi ya vitu vyake muhimu vilichukuliwa, kuonesha kuwa kuna jambo lingine nyuma ya pazia, sio tu mauaji ya kisasi, maana mauaji ya kisasi mara nyingi wauaji huwa hawachukui chochote.



Sasa pamoja na kuchukua uhai wake, walichukua Pasport ya marehemu, Leseni ya udereva, kiasi cha fedha alichokuwa nacho ambacho hakieleweki ni kiasi gani na zaidi ya yote, wakaiba na gari ya marehemu aina ya Lexus.



Hapo ndio vichwa viliwauma mno jeshi la Polisi hasa baada ya kuikuta alama ya V kwenye shavu la kulia la marehemu.



Kingine kilicho wachanganya zaidi ni ile hali ya Kelvin kutokuonekana na kubadili matumizi ya gari, kila wakati yeye hupenda kutumia gari, ila siku hiyo kwake wanasema ametoka na pikipiki, kitu ambacho kichwa cha Inspekta Jitu kiligoma kabisa kulikubali hilo.



Akiwa na mwendo wa kasi kuliko ule wa awali kichwa chake kilizidi kujenga maswali hadi anafika pale kwenye eneo lile ulipookotwa mwili wa Marehemu Allen, alikuwa hajapata majibu.





Alishuka na kuzunguka kidogo hapo kisha akaelekea jirani na hapo ambapo kuna nyumba tu watu wanaishi, akagonga na baada ya dakika kadhaa mlango ulifunguliwa na kukaribishwa ndani.



Aliingia na kuketi kisha kujitambulisha pasina hata kutoa kitambulisho chake, aliefungua mlango alikuwa ni bi mkubwa, alishtuka sana baada ya kujua Jitu ni askari, lakini akamtuliza na kumuuliza kama aliona maiti iliokutwa pale.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bi mkubwa akasema aliiona ndio baada ya kuitwa na wajukuu zake ambao wao walisikia kelele na kutoka nje kwenda kusikiliza kuna nini na ndipo waliporudi na kumueleza kwamba kuna maiti ipo nje, hivyo nae akatoka kwenda kushuhudia.



“Je unaweza kuitambua maiti ile uliyoiona hapo nje?” aliuliza Jitu na bi mkubwa akakataa kuwa haitambui.



“Kuna hata mmoja kati ya watu wa humu ndani alieona tukio lenyewe?” aliuliza tena Jitu.



“Hapana kwa kweli, maana sote tulikuwa ndani tukitatazama marudio ya Maisha + hadi tuliposhituliwa na kelele ndio wajukuu zangu wakatoka,” alieleza bi mkubwa huyo na hapo Jitu akaona hawezi kupata la msingi, akaaga na kutoka hadi nje ambapo alielekea ilipo pikipiki yake na kupanda kusogea mbele.



Eneo hilo ilipopatikana maiti ya Allen, palikuwa ni kwenye uwanja wa mpira wa miguu, ambao wala haukuwa na kingo yoyote, ulikuwa wazi sana, kitu kinacho changanya ni ile hali ya mwili ule kutelekezwa pale muda wa jioni ambao ni muda wa watu kuwepo hapo huku wakicheza mpira.



Alilizunguka zunguka kidogo eneo hilo na akafika kwenye kona moja ya uwanja na kukuta kama kijiwe cha vijana na aliposimama tu, walionekana kuingiwa na mashaka.



Lakini kutokana nauvaaji wake, hawakuweza kumjua kama ni Polisi lakini ilionekana kama vile wamehisi kuwa huyo ni askari, wakawa wakimtazama wakati anawasogelea huku wao wakiwa na tahadhari ya kutaka kukimbia.



Alianza kuwaonesha sura ya amani tu akiwa anasogea kwa miguu, pikipiki akiwa ameipaki mita kadhaa. Aliwasalimu na kuwaomba kuketi kwa dakika mbili tatu aongee nao kidogo.



Walisogea na kumpa nafasi ya kuketi pale kwenye Kigogo cha mnazi walipoketi wao. Akajitambulisha kwa jina la uongo na kuwaomba msamaha kidogo kwa swali ambalo atawauliza.



“Sina nia mbaya ndugu zangu, ninachotaka ni kujua tu…” akawajenga kiurafiki hadi wakawa upande wake ndio akawachomekea kama kuna yeyote alieona lile tukio pale la mauaji.



Kwa kuwa tayari alikuwa ametumia muda wake mwingi kuwajenga kiujamaa, mmoja alisema kwa kujiamini kabisa



“Blaza, Yule hajauawa hapa, itakuwa amekuja kutupwa tu, we mwenyewe kama uliiona ile maiti, inaonesha kabisa alikuwa ameisha kufa kitambo tu Yule, pale yaani umeletwa mzoga tu,” alisema mmoja na mwingine akadakia;



“We si uliona hata ile gari ilivyokuja? Mwendo wa kawaida tu na ikakaa kidogo hapo kwa madakika, ilipoondoka ndio tukamuona jamaa kama kakaa ameegamia mti huku sigara ikiwa mkononi, dah! Kama ni wauaji basi hao jamaa ni hatari sana!” kauli ile ikaufanya moyo wa Inspekta Jitu upige mshindo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Ina maana kumbe aliletwa hapa na gari? Ni gari gani hiyo? Je hapa alipofikishwa na kutelekezwa hapo, hakukuwa na mtu jirani?” hayo ndio yalikuwa ni maswali yake ambayo yalijirejea kichwani mwake na kushindwa kuuuliza, kwani hakutaka kujulikana kama yeye ni Polisi.



Maswali yanapokuwa mengi, husababisha kuzusha maswali mengine kwa unao wauliza, akawashukuru na kutoa noti moja ya shilingi elfu kumi na kuwapa wagawane.



Walimshukuru huyo na kumuona kama vile ni mwokozi kwao, hawakujua ni kiasi gani wao wamemsaidia yeye huku akiwakariri sura zao, akilini mwake tayari alikuwa amejiongeza kivingine.



Alipotokomea mbele kidogo akasimama na kutoa simu, akapiga kituo cha Usalama Bunju na kuomba msaada wa askari wawili. Akawaelekeza alipo na wakamuahidi kufika eneo hilo mara moja.

*****



Inspekta Kalindimya aliwasili nyumbani kwa Allen na kukaribishwa akikuta kuna kundi la watu ambao walionekana kuwa na majonzi makubwa. Aliwapa pole wale waliokuwepo nje na kuelekea ndani ambapo alikutana na Merina.



Merina alipomuona tu Inspekta akaanza kulia na kumwambia Inspekta

“Afande, mume wangu mie Allen!” kitendo cha kumuita afande, kilikuwa ni kosa kubwa mno, hilo aliliona yeye tu Inspekta, maana pale haikujulikana kuna watu wangapi na wazuri ni wapi na wabaya wao ni kina nani.



Akamsogelea kwa haraka asizidi kumwaga ubuyu, na kumkumbatia akimpoza na kumwambia atulie na kuomba kuongea nae kwa faragha. Merina wala hakubisha, lakini alikuwa yupo hoi kwa kilio.



Alihama nae pale na kwenda chumbani na huko akamwambia kuwa asipende kumuita jina la kazi yake kwani hawajui pale kuna nani ambae sio mzuri kwao, Merina akaomba msamaha na kukiri kuwa hatorudia tena.



Inspekta akamuuliza utaratibu wa mazishi, Merina akamwambia watazika siku ya Jumamosi saa tisa mchana kwenye makaburi ya Kinondoni. Inspekta akamuaga na kumuahidi atarejea tena japo hajui ni lini wala wakati gani.







Akatoka nje na kuja kuungana na wale wafiwa waliokuwa nje, hapo aliweza kumuona mtu mmoja akijipendekeza sana kwake kwa kujichekesha chekesha na kumpa mkono.



Inspekta kwanza wala hakumtilia shaka lakini ule ukarimu wake wa ghafla ndio uliomtia shaka yeye na kuamua kuwa nae makini, maana jamaa alifika na kujitambulisha jina, ishara ya kuwa Inspekta nae ajitambulishe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Kitu hicho Inspekta wala hakukifanya, bali alichofanya ni kumpotezea kwa kumpa tabasamu la kawaida na kumwambia;



“Nashukuru sana kukufahamu Moses, nafikiri mi naweza kwenda sasa, maana muda hauniruhusu tena kuendelea kuwepo hapa,” alisema huku akitazama saa yake na kumkwepa kijanja kwa kumpa mkono mtu mmoja aliefika muda ule na kuwasalimia aliowakuta.



Kisha akajichanganya haraka haraka kwa watu wengine na kumuacha Yule kijana akiendelea kusalimiana na watu wanaozidi kufurika, yeye akaelekea kwenye gari yake na kuingia.



Ilikuwa ni Tinted, akaiwasha na kutulia akiwa anakula kipupwe huku akimtazama kwa umakini Yule kijana ambae alionekana kama anamtafuta kila sehemu kwa kugeuza shingo huku na kule pasina kumuona.



Mwisho akamuona akikimbia kuelekea ilipo barabara kuu ambayo ilipita hatua kama mia tatu hivi kutoka walipo watu wa msiba, ndio hapo nae akaondoa gari kwa kuelekea upande wa pili akimuacha Moses kaelekea upande mwingine.

**********



Nyumbani kwa Inspekta Kalindimya, Zuwena alipogeuka ili kuchukua mafuta katika kuendeleza mapishi yake, ndio akaona karatasi ikiwa pale chini na ikiwa imekandamizwa na kalamu, ishara kuwa kuna mtu aliingia pasina yeye kumuona.



Alisogelea ile karatasi na kuitazama kwa jicho la hofu na kisha akanyanyua shingo kuangalia mle jikoni, hakuona mtu mwingine zaidi yake mwenyewe, akatoka na kuelekea Dinning Room, kisha Sitting room, kote hakukuwa na mtu.



Akarudi na kuinyanyua karatasi ile na kuisoma, ilikuwa imeandikwakwa lugha ya Kispaniola, iliandikwa ‘La Mujer Di Mi Vida’ ikimaanisha ‘Mwanamke wa Maisha yangu’ mwisho kukawa kuna kiss.



Zuwena alitabasamu na kuikumbatia ile karatasi kifuani mwake, kwani sasa alijua ni nani alieiandika, aliendelea kuikumbatia hivyo hivyo akiwa ameegamia ukuta na macho kafumba.



Hisia za kimapenzi zilikuwa juu sana, alihisi kama yupo na Inspekta, alishtuliwa na harufu kali ya kitu kuungua ndio ikamfanya afumbue macho na kusogelea jiko la gesi ambalo alikuwa akilitumia na kuipua mboga aliyokuwa akichemsha.



Akatoka jikoni na kuelekea chumbani akidhani mumewe yupo ndani, huko akamkosa na kumtafuta nyumba nzima akiamini amejificha, lakini hakumuona hadi alipokwenda kuchungulia nje na kukubali kweli huyo mtu hayupo mle ndani, maana hakuiona gari, kitu ambacho aliamini ni ishara ya mumewe kuwepo hapo.



Akarejea jikoni na kuendelea na mapishi yake huku akijiuliza huyo mwanaume aliingia saa ngapi mle ndani hadi hakumuona. Akapanga nae ipo siku atamlipa tu kwa wakati wake.

*****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Askari wawili walifika jirani na uwanja wa shule ya Bunju, sehemu ambayo Inspekta Alikuwa akiwasubiri. Walipofika na kumuona, akawaambia sababu ya kuwaita kwao.



Aliwapa jukumu la kwenda pale na kuwakamata wale vijana, hususan Yule ambae alionekana kama vile aanajua mengi kuliko wenzie, Yule alieona tangu gari ikifika.



“Kuna mmoja pale amevaa jezi ya Brazil, huyo ndio hasa nimtakae, wale wengine si muhimu sana, sawa wazee?” alitoa amri ambayo ilipokelewa bila kupingwa.



“Lakini tumieni akili yenu bila kuathiri mahusiano mema ambayo nimeyaanzisha na jamii, unajua habari zote zinatoka kwa wananchi, msifanye watuogope na kushindwa kutoa msaada pindi tunapouitaji, sawa wakuu?” aliwapa nasaha za mwisho kabla hawajaingia kwenye gari ya kazi na kuondoka, nae akaelekea kituoni Bunju kwenda kuwasubiri.



Inspekta sasa alikuwa ameiacha barabara ndogo na alikua ameingia barabara kuu kwa ajili ya kurejea nyumbani kwake, akakumbuka kumpigia Jitu na kumuuliza maendeleo, Jitu akamueleza mchakato wake kuwa kuna kijana anataka kumkamata huyo aliona tukio lote la kule Bunju.



“Basi sawa, mi narejea nyumbani, kwa maelezo zaidi nafikiri itakuwa ni kesho kazini hiyo, ama kuna lolote?”



“Hapana mkuu, mengine yote kesho,” wakamalizana.



Inspekta Kalindimya akarudisha simu yake kwenye Dashboard na kuendelea na safari ya kurejea nyumbani kwake haraka kumuwahi mkewe ambae alimuacha akiwa anapika.





Askari wale walifika pale na kuwavamia vijana waliokuwa wamekaa wakipiga story, kwa kuwa hii ya sasa ilikuwa ni ya kuwashtukiza, hawakuweza kushtuka hadi gari iliposimama miguuni pao na ghafla wakaona askari wenye sare wakishuka garini.



Waliwasalimia kibabe tu kisha mmoja wao akauliza kuwa Yule mtu aliekuja na pikipiki na wakakaa nae alifuata nini pale na yupo wapi?



Wale vijana wakatazamana, kisha mmoja akajibu wao hawamfahamu na alikaa nao wakapiga story na alipochoka akaondoka.

Endelea;



“Ameelekea wapi?” aliuliza Yule askari mwingine na kijana mwingine akajibu kuwa ahawajui kaenda wapi ila alielekea upande huu, hapo akamuonesha upande wa kaskazini ya eneo lile walilokaa.



Afande Yule wa kwanza akamgeukia aliekuwa amevaa jezi ya Brazil ambae muda wote alikuwa kimya na kumkanyaga mguuni kisha akamsemesha;



“We ndio hutaki kujibu maswali yetu eti? Ama wewe ndio unajuana nae na ndio aliekufuata hapa?” kijana sasa akapanua mdomo na kusema;



“Afande, mi nimeona mshikaji anakujibu ndio maana nikakaa kimya lakini mimi simjui kabisa huyo msela, yeye ameibuka tu hapa maskani na kuanza kupiga story, sasa si unajua sisi ni wana nini? Tukaunga tu mastory ya Town,” maneno aliyotumia, askari wakajidai hawamuelewi na kutazamana kisha wakaulizana kama wanamuelewa.



“Afande mi hata simuelewi, inawezekana huyu ndio akawa anajua ni nini Yule jamaa alifuata hapa, sasa huyu inabidi twende nae, nyie wengine bakieni,” alisema moja huku akimtaka jamaa anyanyuke.



Kijana kidogo aliweka kaubishi, lakini kwa kuwa hana uwezo wa kubishana na chombo cha Dola, hata wenzie wakamshauri tu yeye anyanyuke aende wao wanakuja nyuma.



Kumbe hakukuwa na hata mmoja ambae alikuwa tayari kumfuata huko, bali walichokuwa wakitaka ni yeye aondoke tu eneo hilo nao wapate nafasi ya kupotea kabisa, maana waliona pale si sehemu salama tena.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakamnyanyua msobemsobe na kumuingiza garini kisha wakandoa gari kwa kasi na kuwaacha wale waliosalia kila mmoja akipotelea anapo pajua mwenyewe, hakuna kitu walichokuwa wakikiogopa kama Polisi, maana wengi wao walikuwa ni mateja.



Zuwena alimaliza kupika na sasa alikuwa akipanga meza kwa ajili ya kumsubiri muewe arudi na kupumzika kabla hajaingia kuoga na kisha wakae mezani na kupata chakula.



Nje akasikia sauti ya muungurumo wa gari, akachungulia kwenye pazia na kumuona mumewe, basi nae akatabasamu na kuelekea mlango mkubwa wa nje na kuufungua kisha akachomeka funguo kwa nje na kurudi ndani haraka.



Akaelekea chumbani na kuiweka simu yake Kitandani, kisha akatoka tena na kuelekea jikoni ambapo alifunga mlango. Aliporudi kwenye pazia kuchungulia, akamuona mumewe akikagua gari kama vitasa vyote vimefunga.



Inspekta aliporidhika tu akiwa ana funguo ya gari mkononi, akaingiza mkono wa kulia mfukoni na kutoa funguo ya mlango mkubwa, ajabu alipotaka kudumkiza funguo yake, akakutana na funguo nyingine, alipoitazama akagundua ni funguo ya mkewe, akishangaa.



Akawa anaitoa huku akijiuliza kuna nini? Na kwanini funguo iwe nje? Akaizungusha kufungua, akishangaa tena kugundua kwamba mlango upo wazi, yaani haujafungwa.



Akaingia ndani na kuita kwa sauti kubwa ilio na mashaka kwa mbali, maana lile tendo la kuikuta funguo ikiwa nje na mlango ukiwa wazi, haikuwa salama kwake, kutokana na kazi yake, amekuwa na madui wengi, hivyo amani haipo kwa asilimia mia moja.



“Honey...” kama mara tatu hivi huku akimtafuta, lakini wapi! Hakumuona na wala hakuitikiwa hadi alipopata wazo la kupiga simu ambayo ikaitia chumbani, akapata ahueni kidogo na kuelekea huko chumbani.



Ilikuwa ni mshtuko baada ya kuikuta simu ya mkewe ikiwa kitandani inaita na mtu hayupo, akajiuliza ni wapi alipoenda huyu mwanamke usiku ule?



“Tangu lini tabia ya kutoka bila kuaga imeanza humu ndani? Na wapi ameiga tabia ya kutoka na kuacha simu? Sasa dawa yake ni moja tu!” alijisemea moyoni huku tayari hasira zikiwa zimempanda.



Aliona kama vile amedharaulika hivi, mkewe kutoka bila kumuaga? Tena nyumba akiwa ameiacha wazi? Basi akasogea mlangoni na kufunga mlango mkubwa kwa ndani, akaenda na ule wa uwani kuukagua, akaukuta wenyewe umefungwa.



Kwa ghadhabu akasema tuone anaingilia wapi huo muda atakaorudi. Mawazo mchanganyiko yakamtawala, ina maana ameshindwa hata kunitonya ‘Beep’ ama kunitumia Arafa ‘Sms’ kama anatoka? Hii ni dharau kubwa sana.



Akarejea hadi kwenye TV na kuwasha, akaelekea pembeni ya Sittingroom, kuna eneo dogo walilitenga kama maktaba, wameweka meza moja na viti viwili, Computer na vitabu kadhaa.



Akachukua kitabu kimoja na kurejea nacho kwenye sofa na kuketi akitazama TV, siku hiyo hakutaka hata kubadili mavazi, alikaa tu akiamini atagongewa tu mlango muda wowote na Zuwena.



Ajabu hiyo TV aliyoiwasha, wala hakuitazama akawa ameshika kitabu mkononi, nacho hata hakuwa na mpango nacho, ilikuwa ni kama amechanganyikiwa hivi, hata hajui ni nini afanye.



Akasikia sauti kama vyombo vimegongana jikoni, akaweka kitabu chini na kuelekea huko, sasa akili ilimbadilika, akahisi huenda mkewe ametekwa labda na watu Fulani na wengine wamebaki humu kwake.



Kwa tahadhari kubwa akausogelea mlango wa Jikoni na kuusukuma mara moja kwa nguvu na kukuta hakuna mtu bali yalikuwa ni mawenge tu ya kumkosa mkewe, ndio yalimyumbisha.



Akashusha pumzi kwa nguvu na kurejea kwenye sofa na kukishika tena kitabu chake, akiwa anaanza kufunua kitabu tu…

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Akafunikwa paji lake la uso kwa vitanga laini vya mikono, vitanga ambavyo alivijua mara moja kuwa ni vya mkewe, presha ikamshuka hasa baada ya kugundua kuwa mtu aliekuwa anategemea kwamba hayupo, kumbe yupo nae ndani.



“Baby ujue hivyo tunaweza kuuana bure kwa magonjwa ya mishtuko,” aliongea taratibu Inspekta ambae wala hakusumbuka kuitoa mikono ya mkewe kwenye uso wake, hatimae Zuwena mwenye ndio aakaitoa na kumbusu mumewe shingoni.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog