Simulizi : Sayari Ya Kifo
Sehemu Ya Nne (4)
Hiyo ndio ilionekana kama hospitali iliokuwa ipo karibu zaidi kutoka eneo hilo la tukio. Kuondoka kwao na utulivu wa eneo hilo ndio kukampa nafasi nzuri kwa Yule askari aliebaki pale kuanza kutafuta msaada.
Alianza kuwajulisha wenzake, akianza na namba ya simu ya Inspekta Jitu ambae ndio aliwapa amri hiyo na kumuelezea tukio lote kiufupi tu lakini lilikuwa likieleweka.
Jitu aliekuwa akiishi maeneo ya Mwenge, akawapigia askari waliokuwa doria waende kutoa msaada wa haraka kwa mwenzao kisha ndio akamjulisha Inspekta Kalindimya.
Habari ile ilimshitua sana Inspekta ambae alikuwa nje ya geti la nyumbani kwake akitaka kuingia ndani baada ya kutoka kituoni. Kwa kuwa alikuwa ameishafika nyumbani kwake, hakuona umuhimu wa kutoka tena kurejea ofisini kwake.
“Jitu nenda kaungane nao usiku huuhuu, japo nina maswali mengi mno ya kuuliza ila nahisi kesho tutaongea zaidi, jambo la msingi, fuatilia jambo hili na unijulishe kila hatua,”
“Sawa mkuu!” alitika Jitu kwa sauti ambayo unaweza kudhani kuwa hajalala kabisa, kumbe aliamshwa tu na simu ilipoita.
“Wajulishe Patrol kuwa waikamate hiyo gari popote itakapo onekana, pia nawe ushughulike na pikipiki, ila usisumbuliwe na Plate namba, kwani nyingi ni bandia, ili kumpata muhusika, wewe deal na Chasis namba na Engine namba ili kumjua mmiliki wa pikipiki hiyo, haya yote jitahidi kuyafanya kesho asubuhi kabla ya saa tano tuwe tumepata majibu, sawa Afande?”
“Ndio Mkuu,” akaitikia na kujiandaa kuondoka kuelekea eneo la ajali na kisha aende kituoni hata kama ni alfajiri, ili tu akirudi kwake awe na namba zote za pikipiki anazo zihitaji.
Sasa ndio Inspekta akaingia ndani ya nyumba yake na kupaki gari, akafungua mlango wa nyumba na kuzama ndani mwake. Akashangaa kumkuta mkewe akiwa amelala sofani japo alikuwa amemuacha chumbani.
Alihama chumbani na kwenda kulala sofani akiwa anatazama CD yao ya harusi, inaonesha kama ni mtu aliekosa usingizi, hivyo akatoka na kwenda kutazama TV sitting room.
Roho ilimuuma sana Inspekta Kalindimya. Kutokana na jinsi alivyomuacha mkewe akiwa na majonzi, sasa anarudi anamkuta akiwa amelala sofani na hali ubaridi ukiwa ni mkali, aliumia sana moyoni.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mapenzi makubwa ya mkewe aliyaona hapo, hivyo kwa sasa hakutaka kumsumbua tena, akaenda chumbani na kuchukua Blanket na kuja kumfunika vizuri kisha nae akakaa chini sakafuni huku akiegamia sofa na kuanza kuipitia tena ile CD ya harusi yao.
Bahati mbaya nae akapitiwa na usingizi akiwa ameketi hapo…
Hakudhamiria kulala pale, bali alikuwa anataka kuvutia tu muda wa kuangalia angalia cd ya harusi yao kama kumbukumbu kisha akianza kuusikia usingizi, amnyanyue mkewe waende ndani kulala.
Lakini haikuwa hivyo, akiwa yupo deep na kutazama ile CD akiwa na tabasamu usoni, nae akapitiwa na usingizi mzito, hakuanza kwa kusinzia, bali alilala kabisa.
Wa kwanza kushtuka alikuwa ni Zuwena, ambae alishangaa kuona TV ikiwa ipo on huku CD ikiendelea kuonyesha picha ya harusi yao, alipojiangalia akashangaa kuona akiwa amejifunika Blanket na hali wakati akiwa anajilaza wala hakuwa hata na khanga.
Akajigeuza na kumuona mumewe akiwa amelala akiwa ameegemea kochi ambalo yeye amelalia, hapo sasa ndio akapata picha. Kuwa ni mumewe ndie aliefanya hivyo.
Huruma ikamuingia Zuwena na akanyanyuka toka pale alipolala na kwenda kuketi pembeni ya mume wake na kumlalia mapajani huku akijikunyata. Mlazo wa kichwa kwenye mapaja ya Inspekta ndio ukamfanya ashtuke na kufumbua macho.
Aliponyanyua macho yake yakakutana na macho ya kipenzi mkewe yakimtazama kwa Mawadda, jicho ambalo aliona dhahiri lilikuwa ni jicho la huruma kwake, akamtazama kwa mapenzi makubwa na kujikuta akitabasamu na kusema
“Pole mke wangu kwa kukuacha peke yako,”
“Usijali mume nawe pole kwa ishtighali nyingi unazokutana nazo,” kila mmoja kutoka pale alipo, akajikuta amenyanyuka na kukumbatiana na mwenzie, kwa takriban sekunde tano hivi kisha wakaachiana.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuna aliemsemesha mwenzie neno lolote lile, bali wote kwa pamoja walinyanyuka na kuelekea chumbani kwenda kuumalizia usiku wao huku kila mmoja akionesha mapenzi makubwa kwa mwenzie.
**********
Saa 12 za asubuhi wakati Inspekta Kalindimya akiwa amejidamka na anafanya mazoezi ndani ya uwa wa nyumba yake, mkewe alikua amesimama dirishani akimtazama mumewe akijinyonga nyonga kwa mazoezi ya kimapigano kama vile Tae Kwon Du na Tai Chi.
Jinsi alivyokuwa akijirusha na kujikunja kunja ilikuwa ni burudani sana kwa aliekuwa akimtazama, maana kuna wakati ilikuwa ni kama anafanya vitu ambavyo haviwezekani katika hali ya kawaida.
Wakiwa kila mmoja mawazo yamezama sehemu yake, simu ya Inspakta Kalindimya iliita na kwa kuwa ilikuwa pembeni ya mkewe Zuhura, aliitazama na kuinyanyua huku akimuita mumewe aliekuwa amewekwa busy na mazoezi.
“Nani aliepiga simu mke wangu?” aliuliza kama mtu ambae anaona anapotezewa hali yake ya mazoezi ambayo sasa ilikuwa imechemsha damu.
“Ni Jitu huyu mume wangu,” kisha ili kuisaidia simu ile isikatike kwa kuwa ilikuwa imeita kwa muda mrefu na mumewe nae alikuwa mbali kidogo, ikamlazimu Zuwena apokee simu ile na kumsalimia Jitu huku akimtaka radhi na kumwambia mumewe anasogea kuelekea hapa alipo yeye na simu.
“Shem, Inspekta alikuwa mbali lakini sasa anasogea, niliipokea ili tu isikatike, samahani lakini,” alisema kwa dhati kabisa ya moyo wake na ni kweli hicho ndio alichokifanya kwa nia hiyo tu na si vingine.
“Aah Shem lake, hofu ya nini nawe ni mke wangu tu? Ni vema kwanza kusabahiana nawe asubuhi kama hivi, lakini umeamka salama?” kabla hajajibu zaidi ya kusema ameamka salama, Inspakta akawa amefika, Zuwena akampa simu na kusimama pembeni.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walisalimiana na baada ya muda kidogo Jitu akamwambia Inspekta kuwa Yule askari mwenzao aliepigwa risasi usiku uliopita, anaendelea vizuri maana ile risasi haikuleta madhara yoyote mwilini.
“Kivipi yaani? Risasi ilimkosa ama alikuwa na bullet Proof?”
“Alivaa Bullet mkuu, hivyo niliwaacha pale kama saa tisa uaiku hivi akiwa anawekewa maji kwa sababu alizimia kutokana na kuangushwa na uzito wa risasi kama ujuavyo mkuu, akaangukia kingo ya barabara na kujipiga kichwani, ndio alipo potezea fahamu hapo,”
“Ok! Sasa upo wapi?” Jitu akajibu kuwa muda ule yeye yupo mitaani tu akielekea tena Mwananyamala kuangalia kama anaweza kuambulia lolote. Wakapanga wakutane kwenye ofisi yao itakapotimu saa mbili na nusu asubuhi.
Muda huo wao wakiongea na simu, tayari Zuwena alikuwa ameisha potelea zake jikoni kuandaa kifungua kinywa, alipomaliza kungea na simu, Inspekta akaelekea moja kwa moja maliwatoni na kukuta kila kitu kikiwa kimeandaliwa na mkewe.
Dakika zisizozidi 10 akawa tayari juu ya meza kwa ajili ya kufungua kinywa. Chai iliandaliwa na kuanza kunywa taratibu huku wakiongea na mkewe kwa madaha na tabasamu usoni.
Kila mtu alionesha mapenzi, hakika walionekana ni watu wanaojitamini mno, hadi muda wa kutoka Inspekta ulipowadia, Zuwena akaendea funguo ya gari ndani na kuja kumpa mumewe.
Lakini alipoipokea tu, Zuwena akaiomba tena na ubishi mdogo ukaanza. Inspekta akahoji ye anataka ufunguo wa nini? Zuwena nae badala ya kujibu akauliza kwani ye hatakiwi kuushika huo ufunguo wa gari yao?
“Hapana baby, we unaruhusiwa tu kuushika, hata kuuhifadhi, lakini kumbuka wewe ndio umeniletea, sasa niambie sababu ni nini?”
Mi sababu sikwambii na kiukweli tu nataka ufunguo wa gari Hubby…” kila mmoja akawa hataki kukubaliana na mwenzie.
Wa kwanza kukubali yaishe akawa ni Inspekta ambae akautwaa kwa mkono wa kulia huo ufunguo aliokuwa ameushika kwa mkono wa kushoto na kumpa Zuwena ambae akatabasamu na kumsogelea mumewe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akambusu na kisha akamshika mkono na kumwambia watoke nje hadi garini. Walipofika nje, Zuwena akamwambia Inspekta leo ni zamu yake kumfungulia mlango, Inspekta katabasamu na kwenda kufungua geti.
Zuwena tayari muda huo alikuwa ndani ya gari akiichemsha Injini tayari kwa ajili ya matumizi ya siku hiyo, geti lilipofunguliwa, akaitoa gari na kwenda nayo hadi nje akapaki nje.
Inspekta akalirudishia geti na kuelekea garini ambapo alimkuta Mkewe amesimama nje ya gari akiwa na tabasamu huku akimwambia sio kila siku anatakiwa asumbuke kutoa gari, siku zingine anatolewa tu.
Wakakumbatiana na kukiss kisha wakaagana, Inspekta akaingia ndani ya gari na Zuwena akaelekea ndani kwa ajili ya shughuli zake ndogondogo za ndani ya nyumba yake.
Safari ya Inspekta Kalindimya iliishia ofisini kwake na akamkuta tayari Jitu akiwa hapo akiwa na makaratasi mkononi kama mtu ambae amechanganyikiwa vile, akawa anasonya kila saa, mara kashika karatasi hii, mara kaishika ile.
Akitupa hii, basi jua anaokota ile, kazi ikawa ni hiyo tu hadi Inspekta alivyoingia, Jitu hakuwa hata na habari, alikuwa ameshughulishwa na makaratasi yale mikononi mwake.
Inspekta Kalindimya ndio akamsemesha na kumuuliza kulikoni? Ndio Jitu akashtuka na kusimama wima kumsalimia mkuu wake, kisha akamwambia kuna jambo linamchanganya kichwa pale alipo.
“Jambo lipi linaloanza kukusumbua asubuhi kabisa ilhali ndio pamekucha?”
“Mkuu ni kuhusu ile habari ya jana ya kutekwa kwa Kelvin,”
“Mh! Kuna kipi?”
“Jana ile ile usiku nilianza uchunguzi rasmi kuhusiana na tukio lile na kwa kuanzia nikachukua ile pikipiki na kuifanyia ukaguzi wa dharula, sasa majibu niliyo yapata ndio pasua kichwa kamanda,”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yapoje hayo majibu?” aliuliza huku akimtazama. Nae Jitu wala hakujibu kitu, bali alinyanyua karatasi zake kama tano hivi na kumpatia boss wake kimyakimya, aliona kama akiongea atamchanganya tu.
“Mkuu, shika tu mwenyewe usome, maana mi naona kama vile inanichanganya tu,” kauli ile akaandamana na mikono ya Inspekta kuppokea karatasi toka kwenye mikono ya Jitu.
Taratibu Inspekta akaanza kuzifunua, mwanzo alionesha kuchukulia kawaida tu, wakati wote huo Jitu alikuwa akimtazama yeye, Inspekta akanyanyua shingo na kumtazama Jitu, hivyo walikutanisha macho yao.
“Inspekta Jitu, kama sielewi hivi, ina maana zile Plate namba za ile pikipiki aina ya Boxer 150, ni feki si ndio?”
“Ndio mkuu, Plate namba zile ni za Bajaj, ina maana zimefojiwa kuwa hapo kwenye Boxer,”
“Sawa, na Chasis namba inasoma kuwa mwenye pikipiki ni mtu tofauti na Injini namba?”
“Haswaa kiongozi, ina maana Injini imebadilishwa, hiyo Injini mmili ni mwingine na Chasis anamiliki mwingine,”
“Doh! Hii sasa kazi na kibaya zaidi hata kadi inayo onekana kwenye pikipiki hiyo majina yake hayafanani kabisa na majina mengine yaliyopatikana kwenye vielelezo vingine.”
“Ndio maana umenikuta najikuna kichwa hapa mkuu, maana pikipiki moja inamilikiwa na watu wanne huku kila mmoja akimiliki sehemu ya pikipiki na si pikipiki yote, hii haijawahi kutokea kwa kweli.”
“Je umejaribu kufuatilia waliotajwa humo ni watu wa wapi na wana taarifa zipi?”
“Ndio mkuu, hiyo karatasi ya mwisho ndio inaonesha majibu ya maswali yako,” alisema kwa kujiamini kabisa Jitu huku akimuonesha Inspekta.
Tena kwa umakini mkubwa Inspekta akrejesha macho yake, ilionesha kwamba mwenye Chasis ya ile pikipiki aliwahi kuleta taarifa ya kuibwa kwa pikipiki yake kama miezi mitatu iliopita.
Sambamba na huyo, Yule ambae jina lake linasomwa kwenye Injini, tayari ana RB kutokana na upotevu wa pikipiki yake huko mkoani Tanga, na kadi inayo onekana pale, ni ya pikipiki aina ya SANLG ambayo iliibwa huko Kahama mkoani Shinyanga.
Mmiliki tu wa Bajaji ndio yupo Jijini Dar Es Salaam huku bajaj yake ikiwa ni nzima na Inaendelea kufanya kazi kama kawaida, nae anasema hajawahi kudondosha plate namba wala hajaibiwa pikipiki.
“Mkuu mimi ninachoweza kukiona hapa ni kuwa, kila kitu kimefojiwa, na kwenye suala hili la pikipiki hii, hatuwezi kupata msaada wowote,” aliongea Jitu.
Walichoka, Inspekta akasema hapo kazi wanayo. Akachukua peni na kutaka kuandika kitu, alkini akajikuta amesahau na kuiuam peni kwenye kizibo huku akitafakari.
Huyu mtu alijipanga saa ngapi hadi kufanya jambo hili? Ina maana huyu mtekaji alijua kuwa muda huo Kelvin atakuwa hapo? Walitambua vipi kuwa muda ule Yule mtu atakuwa barabarani? Ama watekaji walipiga kambi Bunju?
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maswali yalikosa majibu na akaamua sasa kumshirikisha mwenzie jitu.
Maswali yalikosa majibu na akaamua sasa kumshirikisha mwenzie jitu ambae nae alisema hana jibu ila tu sasa waongeze njia za kuwasaidia kuwatia nguvuni kabla hata huyo Kelvin nae hajauawa.
Kama mtu aliekumbuka kitu hivi, akamtazama Inspekta Jitu na kumuuliza kuhusu gari iliyotumika kumteka Kelvin ni ya aina gani?
Jitu akasema yeye hana jibu, maana hakukumbuka kuhoji hilo, bali akamtuma askari mmoja amuite mmoja wa ewale askari waliovamiwa usiku uliopita kwa ajili ya kuja kuhojiwa.
Dakika chache mbele akawa amefika na kukakamaa kwa ajili ya kutoa saluti kisha akaoneshwa kiti na kuketi. Maswali yakaanza, hakuna ambacho kilikua kinaandikwa, maana yalikuwa ni maswali ya kawaida tu.
Inspekta akamuuliza kama anaikumbuka gari ambayo ilimteka Kelvin ni ya aina gari na ipoje?
Askari huyo akawaambia aina ya gari ile iliyomteka Kelvin ni Land Cruiser VG ya rangi ya Bluu na ilikuwa na watu kama sio watato basi wanne hivi na wote walikuwa wamevalia suti za rangi ya Bluu.
Inspekta Jitu akamuuliza kama anaikumbuka plate namba? Inspekta Kalindimya akamuwahi na kumwambia kuanzia sasa wasizamishe zaidi akili zao kwenye suala la Plate namba, bali wapambane kitofauti ili wafikie malengo.
“Kama kwenye pikipiki tu wameweza kufanya hivyo, huko kwenye gari unafikiri itkuwaje? Pale hakuna hata kimoja cha halali zaidi ya kuijua gari yenyewe,” alimaliza Inspekta Kalindimya.
“Ni kweli mkuu, sasa hapo tunafanyeje?”
“Ok! Nenda kitengo, waambie kuwa unaihitaji gari hiyo aina ya Land Cruiser VG rangi tajwa, hata kama zipo mia, watutajie zote zilipo na wamiliki wake pia, sawa?”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa mkuu,”
“Tena basi waambie watueleze kati ya hizo kama kuna yeyote ina rekodi ya uhalifu, basi mapema tu watuambie na anwani ya makazi ya mmiliki wa gari hiyo,”
Aliongea huku akitazama saa yake ikiwa ni karibia saa nne asubuhi, muda ambao alipanga kwenda hospitali ya Mwananyamala kumuona kijana ambae alifikishwa huko akiwa amepigwa risasi ya mguu.
*********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment