Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

SAYARI YA KIFO - 5

 









    Simulizi : Sayari Ya Kifo

    Sehemu Ya Tano (5)









    Kitengo, ni idara maalum iliopewa jina hilo kwa kuwa ilikuwa ni idara nyeti ambayo imekuwa ikishughulikia yale mambo ambayo yanahatarisha usalama wa nchi ama viongozi na hata usalama wa raia.



    Ndani ya Kitengo, kulikuwa na watu maalum ambao walifanya kazi ya kupeleleza na kung’amua mambo mbalimbali hata yale yaliyokuwa nje ya nchi, wakifanya yote hayo kwa faida ya Taifa lao.



    Walikuwa ni watu ambao hawalali, muda wote wapo macho, kila wakati wakiangalia usalama, tayari kufa kwa ajili ya Taifa lao.



    Hivyo hata Jitu alipofika na kuwaeleza shida yake walimuambia awape nusu saa tu watakuwa wamemkamilishia, kwani wao waliweza kuingia mtandao wowote hapa nchini na kupata habari waitakayo.



    Hivyo kazi ile wala haikuwa kubwa kwao, cha msingi walichohitaji ilikuwa ni muda tu ambao ndio huo walimuomba Inspekta Jitu awape.

    *******



    Inspekta aliwasili hospitali ya Mwananyamala na kwenda moja kwa moja wodini kama alivyopata maelekezo toka mapokezi ya Jeshi, hivyo akaelekea hadi alipo kijana huyo.



    Hakuwa peke yake, pembeni yake alikuwepo nesi mmoja hivi, lakini wakiwa wamesimama mbele ya kitanda cha huyo mgonjwa aliemfuata, mtu mwingine ambae nae ni mgonjwa, akamuita Yule nesi, akaenda kumsikiliza.



    Inspekta akamsogelea huyu aliemfuata na kumkuta akiwa amelala usingizi, mguu ulikua umefungwa kwa juu ukiwa umenyooka, alimsoma jina na kukuta anaitwa Raymond Joseph ambae umri wake ulikua ni mdogo sana.



    Hakuwa yupo katikati ya usingizi, bali alikuwa amefumba tu macho yake. Hivyo wakati Inspekta akigeuza geuza kile cheti pale kitandani, akamsikia na kufumbua macho akidhani huenda labda ni daktari anapita kuwajulia hali.



    Lakini hamadi, alipofunua macho anakutana na mtu amevaa suti, mtu ambae alionesha kuwa si daktari, bali ni mtu mmoja muhimu ambae yupo mbele yake.



    Hakuwa na uwezo wa kukaa, ila Inspekta alivyoona Raymond kafumbua macho, akamsogelea akiwa na sura ya utakatifu na kumpa pole kwanza hata kabla ya salamu.



    Raymond aliitika akiwa na ishara ya maumivu, ndio baada ya hapo Inspekta akajitambulisha na kumuomba kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kufanikisha kuwatia mbaroni hao waliomkosea.



    Muitikio wa Ray japo ni mwanzo tu lakini Inspekta aliutilia shaka, alihisi kama kuna jambo. Yakaanza maswali madogomadogo ambayo Ray hakuona affect yake. Kwani yalikuwa ni ya kawaida mno.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Inspekta alitaka kujua anapoishi, anaishi na nani, anafanya kazi gani? Hayo yote aliyajibu kwa uharaka tu hadi pale walipofika kwenye hatua ya kutaka kujua ni nani aliemfanyia vile?



    Hapo ndio kitete kilipomvaa Raymond, alimjua fika mtu aliemfanyia vile, lakini je amtaje? Mbona mtu huyo amemuonya kuwa atamfanyia kitu kibaya kuliko hicho iwapo atagundua kuwa amemtaja kituoni ama kwa askari.



    Moyo ukamuingia nyongo, akaogopa na kusema hamjui, lakini kauli yake ilipingana na sura yake. Maana waungwana husema macho yanaongea haraka kuliko ambavyo mwenye macho anaweza kunena.





    Hilo Inspekta alilitambua, hii kwake haikuwa kazi ya kwanza, ameisha fanya nyingi mno kiasi ambacho mtu akiwa anamdanganya basi mara moja humng’amua, na hapa ndio kilichotokea.



    Akamuuliza tena kama anamtambua aliemfanyia vile? Sasa alikuwa akimtazama machoni, Ray akakwepesha macho na kuangalia pembeni, Inspekta akanyanyuka pale alipokuwa ameketi na kumsogelea zaidi Ray.



    “Ray ninatambua fika kuwa unamjua kabisa aliekufanyia hivi, nasi tuna imani kabisa unatuficha, lakini tambua kwamba, sisi hapa tupo kwa ajili yako wewe na si kwa ajili nyingine yeyote, tafadhali sema wala usiogope,”



    Bado kauli zile laini hazikuweza kumfanya Ray ataje, kitu ambacho kilimuudhi Inspekta, sasa akiwa na sura ya tabasamu usoni, moyoni alikuwa na ghadhabu, akamwambia hapa kitandani kama hutasema ni nani aliekufanyia hivi, utalala na pingu muda wote.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliposikia suala la Pingu tu, Ray akaingiwa hofu, akauliza kwa hofuhofu hivyohivyo kuwa yeye ndio amekosewa, sasa iweje tena yeye ndio apigwe pingu?



    Inspekta akamjibu kuwa atampiga pingu kwa kuwa anashirikiana na majambazi katika kuficha ukweli ambao yeye anaujua.



    “Na ole wako ukipigwa pingu hapa, ina maana ipo siku utakuja kuchukuliwa na kupelekwa mahabusu ukiwa hata hujapona, na shuruba za huko mimi nazijua, we umewahi kwenda mahabusu ama umewahi kufungwa jela?”



    “Ndio afande mimi niliwahi kukamatwa kwa kosa la kufanya biashara sehemu ambayo haijaruhusiwa, nikawekwa ndani wiki mbili ndio nikawekewa dhamana na wenzangu,”



    “Ok! Ulipapenda sana kule?”

    “Hapana afande, sitamani hata kupakumbuka bwana mkubwa,”



    “Sasa jiandae kwenda tena kwa wiki mbili tena ukiwa mgonjwa kutokana na kuficha ukweli ambao unaweza kukusaidia hata wewe mwenyewe, ama nawe unahusika?”



    “Hapana afande, sasa nitahusika vipi tena halafu nami niumie?

    “Labda itakuwa mmezurumiana huko?”

    “Hapana afande, amini kuwa mimi siwafahamu walionipiga risasi!”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Inspekta akatazama saa na kunyanyuka, bila kugeuka kumtazama Ray akasema



    "Ray ninakupa nafasi moja tu ya mwisho, sitataka kulaumiwa baadae, uamuzi nitakaoufanya baada ya sasa utakuweka mahala pabaya mno, fanya maamuzi sahihi sasa kabla hujaingia matatizoni,” kauli ya Inspekta ilikuwa ya kiume sana.



    Alikuwa anamaanisha kile anachokisema, alidhamiria kumfunga pingu pale kitandani ili kumsubiria atakapopona amvundike ndani.



    Ray sasa nae akaona mabadiliko, lakini kila alipoikumbuka ile kauli ya kundi la Chidi, alijiona kama anapumulia pua moja.



    Alikumbuka jinsi Mkono wa Willy ulipochomoka kutoka kwenye koti alilokuwa amevaa, haukutoka na Bastola kama ambavyo Ray alidhania, bali ulitoka na kibunda cha noti na kumuwekea kifuani huku akimpiga piga kwa mkono wake kwenye shavu kwa vikofi laini, akanyayuka na kumwambia



    “Ole wako useme lolote kuhusu jambo hili, utakufa kimyakimya nyoko wewe,” akageuka na kumuacha Ray ambae alikuwa hajiamini kama ameachwa hai, kalala chini anatikisa kichwa kukubaliana na hilo.



    Kama risasi maneno hayo yalijirudia kichwani mwake na kumpa wakati mgumu sana, Hapo ndio ikawa kazi, majambazi yamemuonya asiseme, Serikali inamlazimisha ataje, akashindwa kujua ni wapi asimamie, lakini alikua akiogopa sana jela wakati huohuo aliona yeye bado ni mdogo sana kufa.



    Akabaki njiapanda, taratibu machozi yakaanza kujidhihirisha, maana alijitahidi mno kuyabana yasitoke lakini ikafikia hatua sasa ni lazima yachomoke tu.



    Sasa ndio Inspekta Kalindimya akamgeukia na kumwambia;

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Muda niliokupa wa kujifikiria sasa umeisha rasmi,” alipomaliza kuongea na kuanza kupiga hatua moja tu mbele, Ray akamuita huku akilia na kumuomba arudi pale kitandani.



    Inspekta alirudi na safari hii hakukaa bali alisimama na Ray akamtaka radhi na kumwambia kuwa waliompiga risasi ni watu ambao hawajui.



    “Kwa hiyo ndio umenirudisha kwa ajili ya kuja kuniambia huo upuuzi?”

    “Hapana Afande, bali wamenitishia maisha yangu, nikisema kuhusu wao maisha yangu yatakuwa shakani mkuu, usalama wa maisha yangu unanilazimu mimi kunyamaza kimya,” aliongea akilia.



    “Kunyamaza kimya hakuwezi kukusaidia wewe wala hakuisaidii jamii iliokuzunguka, raia mwema hutoa tarifa mbaya ili zishughulikiwe mapema, kwani mwisho wake huwa mbaya mno, kesho wanaweza kukurudia hao watu, utasema jeshi la Polisi ni baya na ilhali ni wewe ndio hukutoa ushirikiano nao?”



    Afande aliendelea kuhoji na Ray akajitetea kuwa jeshi linapaswa kulinda raia hasa walio kwenye wakati mgumu kama wake, badala ya kutishwa na kuwekewa vikwazo lukuki.



    “Kijana, jeshi la Polisi ni usalama wa Raia na mali zao, lakini kama wewe umetishiwa na hujalitaarifu jeshi, labda nikuulize wewe sasa, hilo jeshi lenyewe litajuaje kama kuna sehemu raia ametishiwa maisha? Kukaa kimya ni tatizo,”



    Kisha Ray akadakia

    “Marehemu baba aliwahi kuniambia ‘Anyamazae amesalimika’ hivyo afande, mi nimekubali kuwaacha tu waende zao madhali wameniacha hai, nitapona tu, wao achana nao,” alisema Ray kwa kuomboleza



    “Ok niachane nao ili waende wakawadhuru watu wengine eti? Wewe huna jipya, nafikiri Keko inakustahili sana, ahsante kwa muda wako, anakuja sasa hivi askari ambae atakuwepo hapa kwa ajili yako,” afande akaanza kuondoka.







    “Afande ni Chidi na Wenzie ndio walinipiga risasi…” kauli hiyo ikamfanya ghafla afande asimame na kugeuka nyuma akamtazama Ray aliekuwa akimtazama akiwa amekunja uso machozi yakimtoka kwa uchungu akiamini kuwa tayari ameisha yaweka rehani maisha yake.



    “Chidi yupi huyo unaemzungumzia wewe?” Inspekta Kalindimya sasa aliuliza huku akimrudia Ray pale kitandani alipo. Alipomfikia alivuta shuka kidogo pale kitandani na kuketi.



    “Afande ninamjua kwa jina hilo tu,” kwa mara nyingine tena Ray akadanganya, lakini hilo wala halikumsumbua, alichotaka kujua kwanza ni nani alietenda jambo lile.



    “Ok! Ray, kupitia hiyo kauli yako ulioniambia sasa hivi, inaonekana unamjua sana huyo Chidi, hivyo ninataka nami nimjue pia, nakuhakikishia usalama na uache woga wowote, upo sehemu salama kabisa, mazungumzo yetu yatabaki kuwa ni siri yetu tu baina ya mimi nawe, sawa?” aliongea kwa upole Inspekta.



    Sasa Ray akaitika, alihisi kuwa haya ni kama maji ambayo ameisha yavulia nguo, alilazimika tu kuyaoga.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Inspekta sasa akamuomba amuhadithie kwa urefu tangu ilivyotokea hadi kuwa vile. Ray sasa alikua tayari, akamuhadithia, ila alipofika kwenye gari, rangi ya gari ndio ikamchanganya Inspekta.



    “Unasema gari ilikuwa ina rangi hizo, je ukiiona leo unaweza kuijua hiyo gari?”

    “Ndio, naweza kabisa, ila siwezi kuwa huru iwapo Chidi atakuwepo, ameahidi kuniua afande, hapa sasa mimi sina amani, hata Sijui nikitoka hapa nitaenda wapi!?”



    Sauti ya Ray ilikuwa ni yahuzuni sana, Inspekta akamuhakikishia ulinzi wa uhakika huku akimwambia kabla hajatoka pale hospitali, wao watakuwa wamewatia nguvuni.



    “Hapa utalindwa muda wote, na ukitoka hapa utakuwa ni Ray mpya hakutakuwa na mtu yeyote atakaekusumbua, maana Chidi tutakua nae ndani ya mikono ta dola ila wewe tutakuhitaji tu kwenye ushahidi, sawa Ray?”



    Kidogo ile kauli ilimpa tahfiif Ray na sasa akatikisa kichwa kukubali huku akigeuka kuangalia huku na kule kutazama kama kuna mtu yeyote anawasikiliza mazungumzo yao.



    Aliridhika kuwa hakuna mtu kisha akarejesha macho yake kwa Inspekta Kalindimya aliekuwa akiandika vitu Fulani kwenye Diary yake, alipomaliza kuandika akanyanyuka na kumuaga Ray akimwambia kuanzia muda ule kutakuwa na ulinzi kwenye kile chumba alicho yeye.



    “Utakuwa peke yako muda wote ndani ya chumba hiki ila nje muda wote watakuwepo askari wawili watakaokuwa wakipishana katika kukulinda, ondoa hofu na ukipata shaka yoyote wajuze hao askari wao wanajua nini watafanya, sawa?” alimaliza Inspekta huku akirejesha kalamu na diary yake mfukoni.



    “Sawa afande,” nae akajibu huku akijiegamiza kitandani kuanza kuupumzisha mwili wake.

    **********



    Masaa mawili mbele, Jitu alikuwa kwenye lift akishuka kutoka kwenye ofisi maalum ya Kitengo, tayari mkononi alikuwa na majibu toka kwao na alidhamiria kwenda nayo moja kwa moja ofisini kwake ili wayafanyie kazi sambamba na mkuu wake wa kazi.



    Aliingia ofisini kwake na kuwasiliana na Inspekta ambae alimwambia ampe dakika chache tu atakuwa amewasili eneo hilo kwani yu njiani akitokea hospitali ya Mwana Nyamala.



    Haikuchukua muda mrefu sana ikawa tayari wamekutana ofisini, tayari Jitu alikuwa ameisha anza kupitia majibu ya watu wa Kitengo. Alipigwa mno na butwaa mara tu alipoanza kusoma majibu yale.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Inspekta akamgutusha kwa kumsalimia, Jitu akanyanyua sura na kukutanisha na sura ya Inspekta ambae alimuuliza kunani? Mbona amepigwa na butwaa kiasi kile?



    “Inspekta haya mambo yanashangaza sana kwa kweli, huyu Muuaji ni mtu mmoja hatari mno, tena anajua vema kujipanga, lakini pia naweza kusema anachokifanya chochote kile hakibahatishi,”



    “Maelezo ni mengi mno, lakini swali bado lipo pale pale, Jitu kuna nini ndani ya taarifa hiyo ambacho kimekutoa macho kiasi kikubwa kiasi hicho?” aliuliza tena huku sasa akijongea.



    Jitu sasa akaegamia kiti na kumwambia mkuu wake kuwa gari aina Land Cruiser VG bila kujali rangi zake, zipo nne tu hapa nchini, na katika hizo gari, bahati mbaya hakuna hata moja ya rangi tajwa kwa hapa nchini.



    “Hivyo hii gari, inatumika ndivyo sivyo hapa nchini, hilo tayari kwanza ni kosa ambalo linalazimika sasa kuwasiliana na watu wa Mamlaka ya Kodi, walishughulikie,”



    “Hapana si suala la kulishughulikia tu, bali ni gari ambalo linapaswa kukamatwa haraka iwezekanavyo Jitu, inashangaza sana hali hii, dah!” kauli ya Inspekta ikamfanya muda uleule Jitu ashike simu ya mezani na kumpigia Kamanda wa kikosi cha usalama wa Barabarani.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kaka Mo Mpina, kwanza pole na kazi nyingi ziznazokuzunguka hapo ofisini kwako…” baada ya salamu ambayo haikuwa na utani mwingi siku hiyo, Jitu akaendelea



    “Pili kuna gari inatakiwa ikamatwe popote itakapo onekana hapa Jijini Dar Es Salaam hata kama ni nje ya Jiji iwapo itakuwa imetoka, itapendeza zaidi ikiwa ni leo hiihii, gari hiyo imekuwa ikitumika kufanya uhalifu sana hapa Jijini,”



    “Sasa Inspekta Jitu hujanipa namba za gari, hujanitajia aina ya gari na hata fununu zozote kuhusu gari hiyo hujasema, tunaikamataje sasa mkuu?”



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog