Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

TSSI 01 PRISONER - 1

 




IMEANDIKWA NA : RAMADHANI K KAONEKA



*********************************************************************************



Simulizi : TSS 01 Prisoner

Sehemu Ya Kwanza (1)





Kama zilivyo siku nyengine zilizopita, hata hii ilikuwa ndio vivo hivyo. Ila hii ilitofautiana matukio na ya jana na ya juzi na zilizopita. Pengine huenda ikawa yanafanana, lakini haiwezikuwa sawa na ya siku zilizopita. Jua halikuwa kali sana tofauti na siku zilizopita. Siku hii jua lilikuwa la wastani kidogo na wingu lililochagizwa na mawingu ya bluu na utando mweupe. Pilika pilika za watu zilikuwepo kama siku iliyopita. Wale waliobarikiwa vipando vya matairi manne, walikuwa ndani ya vipando vyao wakielekea wanapopajua wao. Wale waliobarikiwa vipando vya matairi mawili nao pia walikuwa juu ya vipando vyao wakielekea panapo wahusu. Na wale wenzangu na mimi tuliobarikiwa usafiri wa ‘HamzahKannon’ yani usafiri wa miguu walikuwa katika njia wakielekea huko wanapoenda. Ilimradi tu jiji lichangamke mchana huo.



Katika uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K Nyerere. Watu walipishana, hawa wakiwa wanaingia na hawa wakiwa wanatoka na wapo pia wale waliokuwa wakitega tax zao kwaajili ya kujipatia chochote kitu kwa kuwapeleka wageni ama wasafiri wanaowasili katika uwanja huo pale wanapopataka. Katika sehemu iliyotengwa kwajili ya kuwasubiria wasafiri wanaoshuka kwenye ndege zinazowasili uwanjani hapo. Kulionekana vijana wawili wenye jinsia tofauti wakiwa wanatokea sehemu ya ukaguzi. Wakiume alikuwa amevaa suruali ya jinzi, juu akiwa amevaa shati la mikono mirefu na chini akiwa amevaa raba nyeusi, kichwani akiwa na nywele nyingi zilizochongwa kiufundi huku kwenye macho akiwa amevaaa miwani ya jua. Mkononi aliburuza begi jeusi huku mkono mwengine akining'iniza begi jengine dogo la mkono mmoja mgongoni mwake.



Yule wakike alivalia jinzi iliyombana na kulifanya umbo lake maridhawa kwa chini lijichore vyema na umbile zuri lenye kumtamanisha kila amuangaliae. Juu alivalia shati la mikono mirefu na chini alivalia na raba zilizoendana rangi na lile shati alilovaa. Kichwani nywele zake za asili akibana kwa nyuma na kumfanya apendeze sana. Kwenye macho alivalia miwani ya jua iliyomtoa bomba sana.

Walikuwa wapo kileo zaidi.

Vijana hawa walikuwa ni Hemedy na Hilda waliokuwa wakitoka kwenye mafunzo ya ujasusi kiserikali baada ya kuondoka miaka sita iliyopita na sasa walirejea nchini wakiwa wamebadilika sana kiumri, kimwili, kiakili na kimapigano pia kutokana na mafunzo waliyokuwa wakiyapata huko walikokwenda.

Pengine walibadilika zaidi ya hivyo!.



Walikuja kupokelewa na kijana mmoja aliekuwa amevalia suti safi na kuwaongoza kuwapeleka kwenye gari lililokuwa limepaki sehemu ya kuegesha magari. Wakaingia humo na safari ikaanza. Walienda hadi katika jengo moja refu lililokuwa katikati ya mji. Jengo hilo lilikuwa ni hotel lakini kwa upande mwengine ndipo ambapo ofisi za TSSI zilipo.



Walishuka kwenye gari na kuingia ndani humo. Walipofika mapokezi walinyoosha zilipo lifti na kupanda kuelekea flow za juu. Huko walionyeshwa vyumba viwili vilivyokuwa karibu na kuambiwa na huyo mtu kuwa ndio vyumba watakavyo vitumia kwa siku hiyo kabla ya kupewa maelekezo mengine kesho yake. Kila mmoja akaingia kwenye chumba chake wakimuacha mtu aliewaleta akiondoka hapo.



Nusu saa mbele. Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K Nyerere. Walionekana vijana wawili wenye jinsia tofauti, ila walifanana kwa kila kitu, bilashaka ni mapacha. Wakiume alivalia ‘track' nyeusi na juu alivalia fulana kubwa za kukata mikono zile wanazovaa wachezaji wa mchezo wa kikapu ‘Basketball' na juu alivaaa kofia aina ya cape na kwenye sikio lake moja aliweka hereni, chini kabisa alivaa raba aina ya ‘All Star' za rangi nyekundu mkononi akiwa amening'iniza begi la kushika.



Yule wakike alivalia kama alivyovalia yule wakiume, track na fulana za michezo ya kikapu, ila kichwani alivalia kofia aina ya mzula lililoacha nywele zake ndefu hadi mabegani zionekane. Aaa! Zilikuwa ni nywele za kuunga. Na chini akivalia raba aina ya ‘All Star' na akiwa amening'iniza begi kama lile ambalo analo yule wa kiume. Walisimama ghafla na kuonekana kama wanajadiliana jambo fulani.



“We must relived now. Hakuna kupumzika”



Yule wakiume aliongea hivyo na yule wa kike alionekana kumuunga mkono kwa hicho alichokisema. Walienda katika dirisha la mapokezi na kutaka kukata tiketi nyengine kwaajili ya safari. Hapo walifanya itfaki zote zilizotakiwa na kwenda kusubiri ndege kwaajili ya safari nyengine ya kuelekea katika mkoa wa Tanga. Hawakutaka kupumzika hata kidogo. Walitaka wafike katika mji huo siku hiyo hiyo.



Baada ya nusu saa walienda kupanda ndege hiyo ndogo ambayo iliwapeleka katika mji huo wao na abiria wengine. Iliwachukua saa moja na nusu kuwa angani na ndege hiyo ikatua katika uwanja wa ndege Majani Mapana. Kisha hapo wakatoka ndani ya uwanja huo na kupokewa na kijana mmoja alionekana akiwasubiria kwa muda mrefu. Wakapakia kwenye na gari na safari ya kuondoka hapo uwanjani ikaanza.



“How about journey?" (Vip kuhusu safari?) Kijana huyo aliwauliza huku akiwa anaendesha chombo hicho.



“Aagh!! Paskali unadhani labda tumesahau kiswahili" Kijana wa kiume aliongea kumuambia yule dereva aliemuita kwa jina la Paskali.



“Hahaha!! Ila kwa miaka mliyoondoka hadi sasa mnapaswa kabisa kufundishwa tena lugha hii, hahaha" Paskali aliongea pasi na kuwaangalia hao watu waliokuwa siti za nyuma za gari hilo.



“Ni kweli, ila hiyo ni kwa watu ambao sio wazalendo na lugha yao ndio wanaweza wakaisahau na kuishika lugha ngeni tu wakiicha lugha yao ikipotea vichwani mwao" Kijana wa kiume aliongea.



“Hata ‘sister' pia hapo hajaisahau lugha yake, au yeye sio mzalendo?" Paskali aliongea huku akiwatazama kupitia kioo kilichokuwa juu yake kwa mbele.



“Paskali unadhani mimi ni mjinga kiasi gani hadi niisahau lugha yangu? Kwanza naazaje. Nawezaje kuisahau wakati kila siku nilikuwa nikiongea na baba lugha hii.. Siwezi kuisahau lugha yangu bwana!" Kijana wa kike aliongea huku akiwa anaangalia mazingira ya nje.



“Dah! Halafu wadogo zangu nimewasahau majina yenu mnajua, maana mmeondoka kitambo sana, mlikuwa wadogo wa miaka saba sijui sita ile hadi leo hii mmekuwa watu wazima. Lazima majina yenu niyasahau" Paskali aliongea.



“Ni lazima utusahau Paskali wala mimi sikulaumu kwa hilo kwasababu hata umri wako pia ushaenda sana. Mimi naitwa Ata na huyu dada yangu anaitw...." Ata kama alivyojitambulisha alikatishwa na sauti ya Paskali.



“Atu!. Hahaha! Majina yenu yamefanana fanana, ulivyonitajia lako tu nikalikumbuka na la ‘sister' hapo" Paskali aliongea hivyo huku akiliingiza gari kwenye nyumba ya aliewahi kuwa tajiri mkubwa katika mji huo wa Tanga anaeitwa Mr Bakari Heneni. Ila kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo chake cha maisha kwa makosa ya kuua watu kwa makusudi na akiteka watoto wadogo kwaajili ya kufunga madawa ya kulevya na kuuza madawa hayo. Waliingia katika jumba hilo na kuliweka gari katika sehemu maalumu ya kuegeshea magari.



Kisha watu hao wakashuka na kuangaza angaza macho kwenye mandhari ya nyumba hiyo ambayo waliondoka hapo wakiwa na miaka saba pekee. Wakaongozwa kuingia ndani na Paskali aliewatambulisha watu hao kwa walinzi wawili waliokuwa wanailinda nyumba hiyo. Wakaingia sebuleni na Paskali alienda kuwaletea vinywaji na kuwapa kila mmoja chake huku akiwa na chake.



“Hivi Paskali, Baba anaendeleaje huko gerezani?" Ata aliuliza.



“Dah! Wadogo zangu nisiwafiche, mkuu hali yake kule sio nzuri kabisa, yani mkimuona sidhani kama mtaweza kumtambua haraka haraka" Paskali aliongea.



“Kwani ana miaka mingapi gerezani hadi sasa?" Atu aliuliza.



“Miaka kumi na tano gerezani, ila imembadilisha sana, anaonekana ni mzee hata wa miaka tisini huko. Dah! Anatia huruma sana.. Halafu aliwahi kuniambia kuwa mkirudi niwachukue mkamuone" Paskali aliongea.



“Baba yangu hawezi kuishi jela hadi kifo chake hata kidogo. Nilazima nifanye kitu awe huru" Ata aliongea.



“Kivipi? Utafanya nini wakati amehukumiwa kufungo cha maisha. Sawa ninaweza nikasema ukakate rufaa ukidai ameonewa kwa makosa hayo. Au adhabu hiyo haikumfaa. Lakini amekiri mwenyewe mahakamani kuwa makosa yote hayo ni yake ndipo akahukumiwa kifungo cha maisha. Sasa wewe unasema lazima awe huru, hapo nashindwa kukuelewa mdogo wangu" Paskali aliongea.



“Unajua nini Paskali. Ni lazima nitumie njia ya aina yoyote ile, hata kuua lakini awe huru" Ata alionyesha msisitizo.



“Sasa utamuua nani wakati baba yako yupo gerezani? Askari? Mkuu wa gereza? Au nani sasa?" Paskali alimuuliza.



“Yoyote yule atakaeleta pingamizi, ni lazima afe ili baba yangu atoke gerezani"



Paskali alishangaa sana kusikia hivyo, akamuangalia Atu kuona yeye amelipokeaje hilo swala na kukuta akiwa na tabasamu ishara ya kuwa yupo pamoja na kaka yake. Ikambidi amuulize ili kuthibitisha hilo.



“I am a be a strain on my brother, ni lazima baba awe huru kwa njia yoyote ile, hata kufa mtu pia sawa" Atu aliongea hivyo huku akinywa kinywaji kilichomo ndani ya glasi aliyoishika.



“Sikilizeni wadogo zangu niwaambie. Hilo swala la kumtoa mkuu gerezani hata mimi naliunga mkono, ila inabidi tutumie akili nyingi kwasababu pale ni gerezani na kuna ulinzi mkali, na kama tukiingia hovyo hovyo basi ujue na sisi tutaenda kuungana nae kifungoni" Paskali aliongea.



“Akili lazima itumike, lakini sidhani kama kuna askari ataeweza kunibabaisha nchi hii. My father he must be come out in jail" Ata aliongea hivyo huku akinyanyuka kwenye sofa alilokaa.



“Where are you going?" Atu alimuuliza.



“I want to rest, nimechoka sana na safari"



“Sasa si ungekula kwanza?" Paskali aliongea.



“Nitakula baadae, acha nikapumzike kwanza" Ata alijibu hivyo huku akiinua begi lake na kupandisha ngazi kuelekea flow ya juu akiwaacha hawa wa chini wakimuangalia tu.



* * * *



Jijini Daresalam siku iliyofuata. Hemedy na Hilda walikuja kuchukuliwa katika vyumba vyao walivyopewa siku iliyopita na kuongozwa kupelekwa chini kabisa ya hilo jengo. Huko baada ya kutoka katika lifti. Walienda sehemu ambayo kama hutotazama vizuri huwezi kujua kwamba hapo kuna mlango. Kwanza utatazama vizuri ili iweje? Ili iwe vipi? Labda kama ikiwa umetumwa kuja kuchunguza hilo jengo, tena pia awe makini sana ndio anaweza akang'amua hicho kitu. Sehemu hiyo ilikuwa ni ukutaka kabisa, ila kuna kibonyezo kidogo cha rangi hiyo hiyo iliyopakwa hapo ukutani. Huyo aliewaongoza alikiminya na ukuta huo ukajiachia kwa upande wa kushoto kujivuta kushoto na upande wa kulia ukajivuta kulia. Katikati pakawa na njia iliyoingia ndani zaidi.



Hilo halikuwashangaza sana Hemedy na Hilda kwasababu walijua hiyo ni moja kati ya ulinzi wa kitengo hicho. Wakaingia wote na ule ukuta ukajifunga wenyewe na wao wakaanza kushuka na ngazi zilizoenda chini ya jengo hilo. Huko Hemedy na Hilda walishangazwa sana na mandhari ya humo ndani. Kulikuwa na watu waliokuwa wakipishana, wote wakiwa na sare moja tu za nguo za suti, si wanawake wala wanaume. Humo ndani kulikuwa na vyumba vingi vilivyokuwa vimetenganishwa na kordo ndefu. Watu hao walionekana wakiendelea na kazi zao kutokana na vyumba hivyo kuwa ni vya vioo vigumu vyenye rangi ya bluu.



Walipita huku wakiwa wanashangaa shangaa mandhari ya humo ndani. “Kweli hii ni TSSI" Hemedy alijiwazia huku akiwa na tabasamu usoni mwake kwa anayo yaona. Waliendelea kutembea hadi wakafika sehemu kuna uwazi mkubwa kama wa mita hamsini. Hapo pia wakavuka na mbele kidogo wakaingia kwenye ujia mmoja uliwapeleka hadi katika vyumba vyengine, ila hivi vilikuwa na vioo vyeusi ambavyo wa nje huwezi kuona ndani ila wa ndani anawaona wanje.



“Waoh! Zaka umepotea sana" mwanamke mmoja aliekuwa ndani ya chumba fulani kama mapokezi alimuambia kijana aliekuwa akiwaongoza Hemedy na Hilda baada ya kufika karibu yao.



“Mishe nyingi Stela. Ila si uko poa kabisa?" Zaka aliongea na kuuliza.



“Safi tu, ila sio vizuri hivyo, wote tunafanya kazi humu humu halafu tusionane......" akatulia na kuwaangalia wakina Hemedy. Kisha akasema. “Hao ndio watu ambao Mkuu alikuambia ukawachukue?"



“Ndio" alijibu.



“Basi aliniambia ukija nao niwaambie waingie ofisini moja kwa moja" aliongea dada huyo huku akiwa macho yake hayabanduki kwenye uso wa Hemedy.



“Sawa....." akawageukia na kuwaambia. “Mi safari yangu ndio imeishia hapa, nyie nendeni kwenye ule mlango na mkifika fungueni tu bila kubisha hodi kwasababu mtakuwa tayari mmeonekana" Zaka aliwalekeza na wao wakaanza kupiga hatua kuelekea huko.



“Mmmh!! Hawa ndio hao TSSI wenyewe?" Stela alimuuliza Zaka.



“Sijui ila nahisi watakuwa ndio, si unajua kitengo hichi kila kitu ni siri kwahiyo siwezi jua" Zaka alijibu.



“Mkaka mwenyewe ana sura nzuri, sidhani kama hizi kazi ataziweza" Stela aliongea hivyo na kumfanya Zaka acheke sana.



“Stela subiri nikuambie kitu. Usimtafsiri mtu kwa kumuangalia usoni au umbile lake lilivyo. Unaweza ukamuona mtu anasura ya upole lakini ndio akawa anamiliki roho mbaya na chafu. Lakini unaweza ukamuona mtu ana sura ngumu na mbaya lakini ndio mwenye moyo safi na mwema. Kwahiyo usimtafsiri mtu kwa kumuangalia usoni"



“Ni kweli lakini..."



Walipofika pale mlangoni, Hemedy akajaribu kuchunguza haraka haraka kama kutakuwa na kamera yoyote ya ulinzi ila akaambulia patupu. Akanyonga kitasa na wakaingia ndani. Huko walimkuta Mr Kaoneka akiwa amekaa na vijana watatu mmoja akiwa ni wakike. Wakasalimia na wakapewa ishara wakae kwenye viti viwili vilivyokuwa havina watu. Ni dhahiri kwamba humo ndani palipangwa kwaajili ya watu sita tu. Maana hapakuwa na kiti chengine kilichobakia baada ya watu hao kukaa.



“Karibuni TSSI... Tanzania Secret Service Investigation. Kitengo cha serikali cha siri sana cha kipelelezi kuliko vitengo vyote. Tulikuwa tukimingoja nyie mje ili tuanza kujuana na kupangiana nafasi kulingana na mafunzo mlioenda kuyachukua huko ughaibuni kwa miaka sita. Najua hamjuani na hata hivyo pia tulitaka msijuane na ndio maana tuko hapa ili mjuane. Mtaanza kujitambulisha wenyewe majina ili mjuane kuanzia sasa maana mtafanya kazi kwa pamoja. Ok anzia kulia kwangu kujitambulisha" Mr Kaoneka aliongea na kumfanya mtu aliekaa upande wake wa kulia aanze kujitambulisha.



“Naitwa Feysal Mzaham kutoka Zanzibar, nipo hapa kwaajili ya kukitumikia kitengo cha TSSI, Asanteni" aliongea huyo kijana aliejitambulisha kwa jina la Feysal kwa lafudhi ya kufifia ya kizanzibari.



“Naitwa Trace Daniel kutoka Daresalam, nipo hapa kwaajili ya kukifanyia kazi kitengo cha TSSI, asanteni"



“Naitwa Faustin Dickson kutokea Arusha, nipo hapa kwaajili ya kukilinda kitengo cha TSSI, asanteni"



“Naitwa Hilda Ganjo kutokea Tanga, nipo hapa kwaajili ya kuitumikia TSSI, asanteni"



“Naitwa Hemedy Bhachu kutokea Tanga, nipo hapa kwaajili ya kulilinda Taifa langu chini ya kitengo cha TSSI, asanteni"



Walipomaliza wote kujitambulisha, akafuatia Mr Kaoneka na yeye kujitambulisha.



“Naitwa Hussein Kaoneka kutokea Tanga, nipo hapa kama Mkuu wa kitengo hichi cha kulinda Taifa TSSI." Alipomaliza kujitambulisha na yeye. Akaongea kitu ambacho vijana hao walikuwa wakikisubiria tangu muda wote na kila mmoja alikuwa na hamu ya kukisikia..







“Ok. Sasa ni wakati wa kumipanga kwa nafasi kutoka wa kwanza hadi wa tano. Nasafi hizo sio kwamba nimezichagua mimi kuwapa nyie. Hapana. Ila nafasi hizo namipa kutokana na juhudi zenu mlizozionyesha mkiwa mafunzoni.. Acha sasa nianze kumipanga. Wa kwanza kabisa ambae ndie atakuwa ni kiongozi wenu katika ‘mission’ yoyote ni Hemedy Bhachu. Huyu atakuwa ndio TSSI 01 na wapili ni Faustin Dickson. Huyu ndie atakuwa ndio TSSI 02. Na watatu atakuwa ni Hilda Ganjo. Huyu atakuwa ndie TSSI 03. Na wanne ni Trace Daniel. Huyu atakuwa ndie TSSI 04. NA Feysal Mzaham atakuwa ndie TSSI 05. Feysal nimempa namba hii kutokana na yeye kazi yake kubwa itakuwa ni kuwapa ulinzi kwa malekezo kwa njia ya kompyuta. Feysal amebobea na amefuzu kwenye masuala ya kucheza na kompyuta kila sekta, yani amesomea IT. Nitamkabidhi ofisi yake punde tukitoka hapa.



Trace yeye atakuwa ndio tabibu wenu kwasababu yeye ana taaluma ya udaktari. Kwahiyo kama pakiwa na tatizo lolote kuhusu kutibiwa inabidi Trace ahusike. Faustini yeye ni ‘engineer’ wa kutengeneza magari, pikipiki na chopa vyenye uwezo wa kipekee kwaajili ya ‘mission' yoyote. Nadhani wakati mnaingia katika hili jengo kuna sehemu mlipita kulikuwa na sehemu kubwa iliyoachwa pasi na kuwa na kitu chochote. Basi sehemu ile itakuwa ndio sehemu ya Faustin kwaajili ya matengenezo hayo.



Hilda na wewe utakuwa msaada Mkubwa wa Hemedy pale anapoenda katika ‘mission'. Wewe ndie utakae toa msaada kwake kabla ya kuongezwa nguvu pale itakapo hitajika. Nadhani hadi hapo mmenielewa na kila mmoja ameijua kazi yake inayo muhusu. Nyote nyie ofisi zenu zipo humu humu ndani ya hili jengo. Na tukitoka hapa kila mmoja nitampeleka sehemu yake". Akatulia kidogo huku akiwa anatembeza macho kwa kila sura zilizopo hapo ndani. Kisha akaendelea baada ya kuona vijana hao wakiwa makini kumsililiza yeye.



“Hakuna ambae amelazimishwa kujiunga na kitengo hichi. Nyote mmekubali kwa moyo mmoja kukifanyia kazi kitengo hichi ambacho ni cha siri sana hata viongozi wakubwa wakiserikali hawakijui zaidi ya Raisi tu. Kwahiyo kama ambavyo mmeamua kufanya kazi kwa moyo mmoja kulilinda Taifa lenu. Basi ndivyo ambavyo ataadhibiwa kwa adhabu kali kama sio kuuliwa kabisa ambae atakiuka na kutoa siri za kitengo au hata kuhasi kitengo. Sidhani kama hicho kitu kitakuja kutokea kwenu. Naamini mtakuwa waaminifu kukitumikia kitengo hichi mpaka vifo vyenu.



Mtalipwa mshahara mzuri na kila mmoja atapewa nyumba ya kuishi na gari kwajili ya matembezi yenu. Kwasasa tunaenda kumionyesha ofisi zenu zilipo na kila mmoja ataanza kufanya kazi kuanzia sasa japokuwa hakuna kazi mtakazo zifanya. Ok. Inukeni twendeni" Mr Kaoneka aliongea hivyo na vijana hao wakainuka na kutoka nje ya chumba hicho. Huko walitembezwa kwenye vyumba vyengine kabla ya kupelekwa kwenye ofisi zao. Waliingia katika vyumba mbali mbali na kujionea wenyewe jinsi kitengo hicho kilivyokuwa kikubwa.



“Hiki chumba ni kwaajili ya kuwatesa na kuwapa adhabu mateka au wahalifu mtakao wakamata" Mr Kaoneka aliwaambia huku akiwaonyesha vifaa mbalimbali kwaajili ya kutesea. Chumba hicho kilitisha kwa kukiangalia maana kilikuwa na vifaa hatari vyenye ncha kali na vya kukata. Walikizunguka chumba hicho huku Mkuu wao akizidi kuwapa maelekezo. Wakatoka humo na kuingia katika chumba chengine.



“Hiki ni chumba chako au ofisi yako Trace. Kuna vifaa vya kitabibu, kuna kompyuta ile pale ya kufanyia kazi. Kompyuta ile imeunganishwa na kompyuta sita za TSSI yani ya kila mmoja wetu hapa. Kwahiyo kama utafanya kazi na ukataka kutoa majibu au maekezo yoyote. Unatuma tu kwa njia ya ujumbe na tutazipata wote. Nafikiri itakuwa umeshanielewa" alipomaliza kutoa maelekezo hayo. Wakazungukazunguka humo kuangalia hiki na kile, kisha wakatoka na kuingia katika chumba au ofisi nyengine.



“Feysal, hii ndio itakuwa ni ofisi yako. Utafanya kazi hapa, kama unavyoona kila kitu kipo hapa, embu angalia vizuri" wakaangalia kila sehemu humo ndani. Muda wote huo Feysal alikua akitabasamu tu kwa kuviona hivyo vitu humo ndani. Akaenda kwenye kompyuta moja na kuanza kuiminyaminya ikiwa imezimwa na kupelekea wenzake wacheke kwa kituko hicho.



“Inavyoelekea unapenda sana kucheza na hivyo vifaaa?" Faustin alimuuliza huku akiwa anatabasamu.



“Saaanaaaa! Yani napenda kinyama, ukiniwekea chakula na hivi vyombo mi nachukua hivi vyombo" Feysal aliongea huku akijinyanyua pale alipokaa akichezea kompyuta iliyozimwa. Wakatembea tembea kwenye chumba hicho. Kisha wakatoka na kuingia kwenye chumba chengine.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Chumba hiki ndio itakuwa ni ofisi ya Hemedy na Hilda. Chumba hiki kimegawanywa vyumba viwili. Hiki cha kwanza ni cha Hilda na hicho huko ndani ni cha Hemedy. Vyumba hivi ndio vitakuwa ni ofisi zenu" wakazunguka kuangalia mandhari ya humo ndani kisha wakatoka na kuenda katika ile sehemu iliyokuwa wazi. Ila sasa hapakuwa wazi kama mwanzo. Palikuwa na mitambo mingi ya kiufundi na kila aina ya vikorokoro vya ki ‘Mechanical'.



“Uuhuuuh!! Yeahh!" Faustin alipiga kelele baada ya kuviona hivyo vitu huku akiruka kama mchezaji wa mpira wa miguu anapofunga goli. Kitendo hicho kilipelekea wenzake wacheke sana.



“Naona mzee wa ‘mechanical' umefurahi ile mbaya kuona mamitambo yako yametulia hapo yanakusubiri wewe tu" Feysal alimtania.



“We acha tu, sikutegemea kama nitakutana na hivi vitu" Faustini aliongea hivyo huku akikagua kagua hiyo mitambo iliyokuweko hapo.



“Faustini wewe ofisi yako nii hii hapa, na kule kwenye kile chumba ndio kuna kila kitu. We chumba chako kidogo ni chatofauti. Chumba chako wewe ni kikubwa sana tofauti na hivi vya hawa wengine... Embu twendeni tukakione" Mr Kaoneka akaanza kupiga hatua kukifuata hicho chumba huku hao vijana wakimfuata kwa nyuma. Walipofika huko walishuhudi mitambo kidogo ila ni mikubwa yenye uwezo mkubwa tofauti na ya kule nje. Mitambo hii imeunganishwa unganishwa kwa kutumia umeme. Hapo Faustini pia alishangaa baada Kuona mingi haijui.



“Fau najua mitambo hii ni mipya machoni mwako. Ila hii ni mikubwa na nirahisi sana kutumia. Kwahilo usijali. Kesho mtakapo kuja rasmi kuanza kazi humu. Utakutana na mwalimu atake kuelekeza kidogo na wewe utaelewa kwasababu sio migumu sana kwenye kutumia ila ina nguvu kubwa kuliko unavyodhani. Kutokana na mitambo hiyo, una weza kutengeneza hata bomu kama ukiamua” walipomaliza wakaondoka humo na kuenda katika kile chumba cha mwanzo walichokuwemo na kila mmoj akachukua nafasi yake.



“Nadhani kila mmoja ameshaona ofisi yake ilipo. Kilichobakia hapa ni kila mmoja kumpeleka katika nyumba yake ambayo ni ya kitengo hiki. Hizo nyumba ambazo mmepewa zipo kiulinzi zaidi, namaanisha kuna milango na silaha kila pande ambavyo hamtoonyeshwa na mtu yoyote ila kwa vile nyie ni watu wa ki ‘intelligence' mtagundua wenyewe bila kuonyeshwa. Una ruhusiwa silaha hizo kuziamisha na kuweka sehemu ambayo wewe mwenyewe utaona inafaa" akatoa viboksi vidogo vidogo vitano na kuviweka juu ya meza. Kisha akasema.



“Kwenye hivi viboksi ndani yake kuna simu, simu hizi pia zipo kiulinzi zaidi. Naamini mtakapoanza kuzitumia mtajua kila kitu kwasababu huko mafunzoni mmefundishwa vitu vyote hivyo. Kwahiyo sina shaka na hilo. Ok kila mmoja achukue la kwake" alipoongea hivyo kila mmoja akachukua boksi moja lililokuwa juu ya hiyo meza na kutulia.



“Kwenye hizo simu ndani yake kuna laini. Hampaswi kubadilisha line kwasababu hizo line zitatufanya tujue uelekeo wa wapi mtumiaji alipo, ila hata kama hizo laini zikitolewa pia tutajua kwasababu hizo simu zimeunganishwa na kompyuta ambayo ataitumia Feysal. Ok, kwa leo tumemaliza, nendeni hapo nje, mkifika mtakutana na watu wa tano wanamisubiria na kila mmoja ataondoka na wakakwe kupelekwa huko kwenye hizo nyumba zenu" Walinyanyuka wote watano huku wakimuacha mkuu wao akiwa anawaangalia na wakatoka nje na kukuta kuna watu watano wakiwasubiri wao. Kila mmoja akaondoka na wake kupelekwa huko kwenye nyumba walizopewa. Chaajabu. Hawakuweza kuona tena ile mitambo ambayo wametoka kuiangalia muda si mrefu. Ile sehemu ilikuwa iko vile vile na uwazi wake pasi na kuwa na kitu chochote kile. Wakatoka huku wakiwa na mshangao wao.



* * * *



Tanga. Majira ya saa kumi jioni. Paskali na ndugu wawili mapacha. Walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuenda sehemu iliyokuwa kuna magari mengi yamepaki ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Wakaingia kwenye gari moja na kutoka ndani humo.



“Yani kule palivunjwa na serikali baada ya kugundulika ile ngome, sasa hivi kumebaki gofu tu, tena gofu lenyewe lina mamiti ndani yaliyojiotea" Paskali aliongea hivyo huku akiwa nyuma ya usukani akiutendea haki ipasavyo.



“Kwani kule hakuna watu wanaoishi kwa sasa?" Atu aliumuuliza.



“Hapana, hakuna watu wanaoishi. Raia wote waliondolewa na serikali wakidai wanataka kutengeneza bandari lakini hadi sasa kumepita miaka mingi hakuna dalili ya aina yoyote kutengenezwa hicho kitu"



“Kwani ilikuaje kuaje hadi hiyo ngome ikavamiwa wakati hakuna watu wanaoishi kule kusema kwamba wao ndio wameutoa huo mchongo kwa polisi?" Ata alimuuliza.



“Kule kulivamiwa ghafla tu na polisi wakaanza mashambulizi. Haikujulikana hadi sasa ni nani alieichoma ile ngome hadi ikaja kuvamiwa. Ila nahisi ni polisi wenyewe wameamua kufuatilia baada ya kuona watoto wengi wanapotea mitaani.. Hata hivyo niliwahi kumshauri mkuu kuwa tusiwateke watoto wengi kwa wakati mmoja, nikamuambia njia hiyo itafanya polisi kulivalia njuga hilo swala, ila yeye akatumia ukubwa wake kujifanya kujua vingi, mi nikamuacha" Paskali alisema.



“Baba nae amekamatwa kwenye hiyo ngome au yeye alikamatiwa wapi?" Atu alimuuliza.



“Mkuu yeye siku hiyo alikuwepo nyumbani tu, ndio akapigiwa simu na kuambiwa kuwa ngome imevamiwa na wao tayari wameshazidiwa kwahiyo wanahitaji msaada. Sijua mkuu aliwajibu nini, ila nilimuona tu akitoka na mlinzi mmoja na kuondoka na gari pale nyumbani. Ila baadae tukapata taarifa kuwa wameshikwa maeneo ya Sabasaba wakiwahi uwanja wa ndege kutaka kutoroka. Ndio hapo waliposhikiwa na kupelekwa mahakamani"



“Dah! Najisikia uchungu sana kuona baba yangu yupo gerezani halafu mimi uwezo wa kumtoa ninao" Ata aliongea kwa uchungu sana.



“Msijali wadogo zangu, twendeni kwanza tukaiangalie hiyo ngome ilivyo kwa sasa kisha ndio tutapanga ni jinsi gani tutamtoa mkuu gerezani" Paskali aliongea hivyo huku akiongeza mwendo wa gari kuwahi huko palipo kuwa na ngome ya Mr Bakari Haneini. (Wale waliosoma kisa cha UHASAMA wanaijua hiyo historia).



Baada ya dakika kadhaa wakawa wamefika na kushuka hapo na kuanza kuangalia vizuri hayo mabakibaki ya hilo jengo. Kulikuwa na pori kubwa huku miti miti ikilizunguka hilo jengo na kufanya litishe hata kulisogelea. Kuna baadhi ya ukuta ilikuwa imevunjika na kuanguka chini kabisa huku mengine ikitoa nyufa kuashiria muda wowote ule itaanguka

Ilitisha!.

Wakalizunguka hilo jengo mbele nyuma na waliporidhika, wakarudi kwenye gari na safari ya kurudi mjini ikaanza.



“Ok, tunafanye ili kumtoa mkuu gerezani kule" Paskali aliongea wakati wakiwa wameshafika kwenye mjengo wao na hapo wakiwa sebuleni.



“Baba lazima atoke kwa njia yoyote kule jela. Hawezi kukaa gerezani wakati wanae tunauwezo wa kumtoa" Ata aliongea.



“Unajua Ata wewe unaongea lakini husemi ni kwanjia ipi tutamtoa" Paskali aliongea.



“Labda mimi nishauri, twendeni kwanza tukamuangalie halafu tumjulishe kuwa tunataka kumtoa gerezani. Kisha hapo ndio tujue ni kwanjia gani anatoka" Atu aliongea.



“Safi kabisa, hapo Atu umeongea, inabidi tuende tukamuone halafu pia tutayasoma mazingira ya kule gerezani, ili hata kama tukakapoamua kumtorosha, basi tunamtorosha tukiwa na uhakika wa tukifanyacho, tusibahatishe mambo" Paskali aliongea.



“Kwani siku maalumu ha kuwaona wafungwa ni lini?" Ata alimuuliza.



“Jumapili ndio siku ya kuwaona wafungwa" Paskal alijibu.



“Basi inabidi jumapili hii tuende" Ata aliongea na kuungwa mkono na wenzake. Kisha hapo wakaendelea na maongezi mengine ambayo hayakuwa na ulazima wa kuyaandika hapa.



* *



Siku tatu mbele. Walikuwa ndani ya gari wakielekea gereza la Maweni kuenda kumuangalia baba yao na kujua ni jinsi gani ya kumtorosha jela. Nusu saa ilitosha kuwafikisha kwenye gereza hilo. Wakaingia katika lango la gereza na kuenda kupaki gari sehemu husika baada ya ukaguzi wa gari. Kisha Ata na Atu walishuka wakimuacha Paskali garini. Walienda hadi ndani ya gereza hilo na kuomba kuonana na baba yao. Wakaambiwa wataje jina la huyo baba yao na kulitaja. Askari huyo alishangaa sana, maama mtu huyo anaedaiwa kuwa ni baba wa watoto hao. Hakuwahi kuwaona hata siku moja kuja kumtembela huyo baba yao.



Lakini kwavile yeye kazi yake sio hiyo ya kuhoji kile kinachomtatiza. Akawaelekeza sehemu ya kumsubiria mtu huyo na yeye akaenda kumleta. Mr Bakari Hanein aliewahi kuwa tajiri mkubwa katika mkoa huo. Alikuwa amechoka sana na kuonekana na kama mzee wa miaka themanini au tisini kwa jinsi alivyo. Wote walijikuta wakilia kwa uchungu baada ya kutoonana kwa miaka ishirini sasa. Baba yao hakuwa yule waliemuacha kipindi wao wakiondoka hapa nchini. Wala hakuwa yule waliekuwa wakiwasiliana nae kwenye mitandano kwa njia ya kuonana. Huyu alikuwa ni mzee aliechoka sana hata kuonekana ana sura ya kizee tofauti na umri wake.

Ili wasikitisha!.

Ili waumiza!.



“Aroo nyie mkienderea kuria hapo, na muda ukiisha mjue mtaondoka na huyu baba yenu nitamrudisha ndani bila ya kuongea nae chochote. Alaah!!" Askari aliewasimamia alibwata kwa gadhabu baada ya kuona watu hao wakilia tu bila kuongea chochote. Ikabidi wanyamaze na kuanza kuongea huku wakiwa na huzuni nyingi. Waliongea kidogo tu na kuwasilisha kile walichopanga.



“Baba inabidi utoke humu gerezani, sio sehemu sahihi ya wewe kuwepo, kwa hiyo miaka uliyokaa inatosha kabisa, inabidi uwe huru" Ata aliongea kwa sauti ndogo sana ili huyo askari aliewasimamia asisikie.



“Lakini mimi nimeua na nimekiri hivyo mwenyewe mahakamani na ushahidi pia ulikuwepo, siwezi kutoka hata kama mkikata rufaa" Mr Haneni aliongea.



“Baba hapa hapakatwi rufaa wala nini. Utatoka kwa njia yoyote ile" Ata aliongea.



“Kwahiyo mnataka kunitorosha? Kwasababu hakuna njia nyengine zaidi ya hiyo" Mr Hanein aliuliza kwa taharuki.



“Ndio baba hakuna njia nyengine zaidi ya hiyo. Tunakuomba sana uibariki njia hiyo" Ata aliongea.



“Sawa. Ila inabidi kuna mtu mnitoroshe nae, kwasababu nimetokea kuzoeana nae sana" Hanein aliongea.



“Ni nani huyo?" Ata aliuliza.



“Ni kijana mdogo ila anaakili nyingi, naamini hata kama tukifanikiwa kutoroka atatufaa kwenye kazi zetu. Anaitwa MRUTU" Mr Haneni aliongea.









“Sawa hakuna shida, kama unaona anafaa basi na yeye tutaondoka nae" Ata alisema.



“Ni lini ndio mmepanga mje kututoa humu ndani?" Mr Hanein aliwauliza.



“Tukija mara ya pili tutakuja na mpango thabiti wa kumitoa humu ndani, chakufanya wewe ongea na huyo mtu umpange kabisa ili hiyo siku tukakayokuja, kazi iwe rahisi" Ata aliongea.



“Arooh, muda mazungumozo umeisha, kwahiyo mnatakiwa muondoke, kama bado mnamazungumuzo nae mtakuja siku nyengine" Askari aliekuwa amewasimamia aliwaambia na kuanza kumtoa Mr Hanein hapo kumrudisha vyumbani. Watoto wake walibaki wakisikitika huku wakimuonea huruma baba yao. Hapo ndio mori wa kumtoa ndipo ulipoongezeka. Wakajiapiza kimya kimya kwamba ni lazima baba yao atoke humo ndani kwa namna yoyote ile.



Wakatoka na kumfuata Paskali aliekuwa kwenye gari akiwasubiri wao. Wakaingia kwenye gari na safari ya kuondoka hapo ikaanza.



“Haki ya Mungu naapa lazima baba yangu atoke gerezani" Ata aliongea hivyo wakati wakiwa ndani ya gari wakirudi mjini.



“Dah! Baba yangu hali yake ndio iko vile? My Brother tupo pamoja, baba hawezi kuteseka wakati sisi wanae tupo" Atu aliongea.



“Mmeishuhudia hali ya mkuu ilivyo eeeh, basi vile ndivyo anavyoteseka kila siku" Paskal aliongea hivyo na kimya kikachukua nafasi ndani ya gari. Kila mmoja akawa anawaza lake. Kisha Paskali akaongea.



“Kwanjia ipi tutamtoa mkuu kule gerezani?" Paskal aliwauliza.



“Paskali subiri kwanza tufike nyumbani tutajua nini chakufanya" Ata aliongea na kimya kikachukua nafasi tena.



* * * *



Jijini Daresalam katika jengo la Hotel ilipo ofisi ya TSSI. Mr Kaoneka alikuwa ofisini kwake akiwa anaminyaminya kompyuta yake. Simu yake ya mkononi iliita, akaacha kuminyaminya kompyuta na kuiangalia hiyo simu. Kisha akaipokea haraka baada ya kuona jina la aliepiga.



“Ndio kiongozi" alianza kuongea hivyo.



“Mr Kaoneka njoo Ikulu muda huu” Mtu wa upande wa pili aliongea.



“Sawa kiongozi nakuja” baada ya kuongea hivyo, simu ilikatwa na Mr Kaoneka akazima kompyuta na kutoka hapo chumbani. Akatoka na kuanza kutembea na kuondoka humo ndani. Akapita njia anazozijua yeye na kutoka nje ya Hotel hiyo lakini sio kwa kule wanapoingilia wateja. Huku alipotokea yeye kulikuwa ni nyuma ya jengo hilo. Kisha akaingia kwenye gari lake na kuondoka hapo.



Baada ya dakika kadhaa, akawa amefika nje ya geti la Ikulu. Geti likafunguliwa na yeye akaingiza gari ndani na kwenda kulipaki sehemu maalumu. Akashuka na kuanza kupiga hatua kuingia ndani ya jengo hilo linalolindwa kwa ulinzi mkali kupita maelezo. Kamera za ulinzi zilikuwapo kila mahali hadi chooni achilia mbali walinzi makini waliokuwa wakilinda hilo jengo masaa ishirini na nne.



Aliendelea kupiga hatua kuingia ndani ya jengo hilo, aliingia kona hii na kutokea hii na mwisho wa safari yake ilikuwa ni katika mlango wa chumba kimoja wapo. Akaufungua na kuingia humo ndani. Akakuta chumba kitupu, akaenda kwenye kiti kimoja na kukaa hapo akimsubiri aliemuita hapo.



“Oooh! Karibu Mr Kaoneka, mtu makini kwenye mambo yake ambae hajapata kutokea kama yeye katika serikali" Raisi Alex Kileo aliongea baada ya kutokea katika mlango mwengine tofauti na ule aliongia nao Mr Kaoneka. Akakaa kwenye kiti chengine na kusema.



“Mtu makini mwenye kutumia akili kwenye mambo yake bila ya kutumia nguvu nyingi. Raisi wa awamu ya pili hakukosea kabisa kukufanya wewe ukiongoze kitengo hiki cha siri. Enhe niambie TSSI na vijana wake wanasemaje" Raisi Alex Kileo aliongea.



“Muheshimiwa TSSI iko vyema kuanzia sasa na kila kijana nimempanga kwenye nafasi yake na sasa tunasubiria oda yoyote kutoka kwako" Mr Kaoneka aliongea.



“Unajua wiki mbili zilizopita nilikuwa nchini Namibia kwenye ziara maalumu, na nimerudi jana tu, sasa ndio nikaona leo nikuite hapa ujekuniambia nini kinaendelea TSSI"



“Kila kitu kiko sawa, vijana wanaonekana wana mori wa kufanya kazi muda wowote"



“Hivi ni nani kati yao ambae ni TSSI 01?"



“Ni Hemedy. Yule kijana nimesoma ripoti zake toka kwa walimu wake huko. Yani alikuwa na bidii katika mazoezi na ana upeo mzuri na ubongo mwepesi wa kufikiria jambo. Ripoti imeonyesha ameshika nafasi ya tatu kati ya wanafunzi wote walioenda kujifunza mambo hayo"



“Unamaanisha wanafunzi wakila bara?" Rais Alex Kileo alimuliza kwa mshangao.



“Ndio"



* * * *



Majira ambayo mkuu wa nchi akiongea na Mr Kaoneka kuhusu TSSI. Ndio Muda ambao watu wale watatu wanafika kwenye nyumba yao. Wakaegesha gari sehemu maalumu na wote wakashuka na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Walipofika sebuleni, kila mmoja akachukua nafasi kwenye sofa na maongezi yakaanza tena.



“Hadi sasa nyie mmewaza nini juu ya kumtoa mkuu jela?" Paskal aliwauliza.



“Mi naona tukafanye uvamizi pale gerezani" Ata aliongea kauli iliyopingwa na wenzake wote.



“Hahaha! Ata pale ni gerezani sio kiwanda au nyumba ya mtu ile ukadhani ulinzi utakuwa ni wa kubabaisha. Hapana. Ata mimi sikuungi mkono hata kidogo. Tukafanye uvamizi gerezani?" Paskal aliongea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“My Brother hata mimi sikuungi mkono kwa hilo. Ile sehemu ina ulinzi mkali na walinzi wake wanailinda kwa silaha kali masaa ishirini na nne. Tutafute tu njia nyengine" Atu aliongea.



“Ok, hiyo njia nyengine ni ipi sasa?" Ata aliuliza. Atu alinyanyuka na kupanda ngazi kuelekea flow ya juu akiwaacha wenzake wakimuangalia pasi na kujua ni kipi kilichomfanya kuondoka hapo. Baada ya dakika moja alirudi tena mkononi akiwa ameshika ki boksi kidogo. Akakifungua na kutoa kidonge kimoja kidogo kama ‘priton' na kukishika na viganja vyake viwili cha shahada na dole gumba.



“Hiki ni kidonge kidogo sana, ila kina madhara makubwa endapo mtu atakimeza. Madhara yake yatatokea baada ya mtu kukimeza na asipopata dawa yake ambayo ni hii (akatoka kichupa kijidogo humo humo kwenye hicho kiboksi na kuwaonyesha) ndani ya masaa ishirini na nne baada ya mtu kukimeza, basi atakufa kwa kukakamaa kwasababu kidonge hiki kinaenda kukausha damu yote" alipofika hapo akatulia kidogo na kuwaangalia wenzake na kuona wanaumakini na yeye. Akaendelea.



“Inabidi baba atoke kwa njia hii" aliongea hivyo na kutulia kimya akitegea swali lolote kutoka kwa hao wanaomsikiliza.



“Sijakuelewa Atu, umesema baba inabidi atoke kwa njia hiyo. Kivipi?" Ata alimuuliza.



“Brother baba tutampa hiki kidonge akimeze, baada ya hapo atapata madhara yake na ndio hapo watakapo mpeleka hospitali ya pale pale gerezani. Ila hospital hiyo hawatoweza kuona ugonjwa wowote kutokana na hiki kidonge hakionyeshi maradhi ila madhara yake yataonekana. Bilashaka watampeleka hospitali ya mkoa baada ya hospitali hiyo kushindwa. Sasa hapo watakapo mpeleka huko hospitali, sisi tutakuwa njiani tukilitega hilo gari. Najua hawatompeleka kwa ulinzi mkubwa kwasababu makosa aliyofungiwa nayo sio makubwa sana. Sasa sisi hapo hapo tutaliteka hilo gari, kama ni kuua askari wote tunaua halafu tunaondoka na mtu wetu" Makofi yalipigwa baada ya Atu kumaliza kutoa huo mpango. Wakajikuta wakiuunga mkono moja kwa moja. Halafu akamalizia. “Halafu tukishaondoka na baba tunampa hii dawa na atapona baada ya nusu saa kuinywa"



“Atu huo mpango wako my sister nimeuunga mkono, inabidi itumike njia hiyo. Ila sasa baba alisema kuna mtu pia anahitaji atoroshwe nae" Ata aliongea.



“Ni nani huyo?" Paskali aliuliza.



“Aagh! Ni mtu tu katutajia jina lake sijui alisema anaitwa nani. Aagha! Jina lake limenitoka ila baba alisema tumtoreshe nae" Ata aliongea.



“Tena tukimpa hiki kidonge tutamuambia akimeza majira ya jioni hapo watampeleka Hospital majira ya usiku, kwahiyo hapo kazi itakuwa nyepesi zaidi" Atu aliongea.



“Basi tukienda jumapili tutamueleza huu mpango" Paskali aliongea.



“Hivi wewe hivi vidonge na hiyo dawa umevitolea wapi?" Ata alimuuliza.



“Brother hivi nilipewa na teacher wakati tunataka kuondoka, sijui alinipea vya nini ila ndio hivyo tu alinipa"



“Sawa tuachaneni na hayo kwanza. Mchana huu tutakula nini?" Ata aliuliza.



“Sister si yupo? Atapika tu" Paskal aliongea.



“Hahahaha huyo hata uji hajui unavyopikwa. Labda umuambie mambo ya ‘martial arts’ lakini sio kupika. Anaweza akatuunguzia hadi chai huyo" Ata aliongea hivyo na kumfanya Atu achukue glasi ya dongo ya kunywea juisi iliyokuwa karibu na meza alipokaa na kuirusha kwa ghafla kumuendea Ata usoni. Ila Ata aliiona na kuiwahi kuizuia na mkono, hapo hapo nae akairusha kumuendea Atu ya uso vile vile. Lakini mwanadada huyo aliyumbisha kichwa kuenda kulia na kufanya glasi hiyo ipite sentimita chake liliposikio lake na kwenda kugonga ukutani na kupasuka vipande vipande.



“Haaaaa!!" Paskali alimaka kwa taharuki kwa kuona hilo jambo. Ila Ata na Atu wao walitabasamu tu pasi na kujali taharuki la Paskali.



* *



Siku iliyofuata gereza la Maweni. Saa saba mchana wakati wafungwa wakiwa wanakula. Haneni na Mrutu aliekuwa amechoka kimwili kwa maisha ya jela kwahiyo miaka aliobarikiwa kuwepo humo. Ilitosha kabisa kuufanya mwili wake kuwa dhohofu hali. Walikuwa wamekaa chini wanakula taratibu chakula walichopewa. Haneni akaanzisha maongezi.



“Mrutu hujachoka tu kuishi humu gerezani?" Mr Haneni aliongea hivyo huku akikata tonge la ugali na kulichomvya kwenye bakula lililojaa mchuzi wa maharage ambayo hayajaungwa huku maharage yenyewe yakiwa machache kwenye mchuzi huo.



“Haneni hata kama nikisema nimechoka haitosaidia kitu. Kumbuka nimehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kushiriki mauaji ya familia ya kaka yangu achilia mbali kudhulumu mali zake. Sasa hapo ni kipi cha kujipa moyo eti kwamba ipo siku nitakuja kutoka humu" Mrutu alipoongea hivyo, akanyanyua bakuli lililokuwa na mchuzi wa maharage na kuligida mdomoni kwa pafu moja baada ya kuona chuzi hilo ni jingi kuliko ugali.



“Hivi kama ikitokea ukapata nafasi ya kutoroka humu gerezani, unaweza ukaitendea haki hiyo nafasi?" Mr Hanein alimuuliza.



“Mmmh!! Hiyo kwanza ngumu kutoroka katika jela hii yenye ulinzi mkali, pili nikitoroka sitoishi kwa amani huko uraiani" Mrutu aliongea.



“Mbona nilivyokuuliza na unavyo nijibu ni tofauti? Nimekuuliza ikitokea nafasi ya kutoroka humu utaitendea haki au laa! Au hutaki kutoka humu?"



“Mimi kutoroka humu ndanii! Dah! Ila kama ikitokea hiyo nafasi nitatoroka tu kwasababu nishayachoka maisha ya humu"



“Basi jiandae tutatoroka muda si mrefu humu ndani" Mrutu alishtuka baada ya kusikia kauli hiyo. Akabaki akimuangalia huyo mzee anaesema hivyo.



“Sijakuelewa Haneni, unasema tutatoroka muda si mrefu?"



“Ndio nilazima tutoroke humu siku si nyingi, na ishu hii usijaribu hata kutaka kumuambia mfungwa yoyote achilia mbali askari. Kwasababu kufanya hivyo ni kuukwamisha huu mpango na itapelekea tupate adhabu kali. Kwahiyo usijaribu kumuambia mtu yoyote, baki nayo moyoni"



“Sawa. hiyo siku ya kutoroka ni lini?"



“Usijali. Hiyo siku ikifika nitakuambia" Mr Hanein aliongea hivyo huku akinyanyuka hapo alipokaa na kujikung'uta vumbi lililokuwa limeganda kwenye nguo yake na kifungwa upande wa makalioni. Kitendo hicho kilimfanya Mrutu awahi kuziba bakuli zake zenye chakula kutokana na vumbi hilo huku akinung'unika. Mr Hanein aliondoka hapo na kupotelea ndani ya gereza hilo huku akimuacha Mrutu akifikiria huo mpango wa utorokaji gerezani.



“Hivi ni kweli ni sahihi kutoroka gerezani Au ni kujitafutia matatizo tu kwa polisi? Maana mimi nimehukumiwa kifungo cha maisha, nikisema nitoroke na huko uraiani nitaishi vipi? Nitaishi wapi? Je siku nikikamatwa si nitahukumiwa kunyongwa mimi? Mmh! Hii ni hatari" wakati akiwa anaendelea kuwaza mwenyewe, mbele yake palipita askari aliekuwa mkononi ameshika kirungu. Mrutu akaacha kula na kumsimamisha yule askari. Askari akasimama. Mrutu akainuka na kumfuata yule askari.



“Arooh sema shida yako haraka, nina mambo mengi ya kufanya" Askari huyo alikoroma baada ya kumuona Mrutu akiwa anajing'atang'ata kuongea. Baada ya kukoromewa hivyo. Ikambidi ajikaze aseme kile ambacho alikikusudia kumuambia huyo askari.... Askari alikumbwa na taharuki na kupigwa na butwaa baada ya kusikia maneno ya Mrutu. Akabaki kumuangalia mara mbili mbili mfungwa huyo pasi na kuelewa amfanye nini.









“Ndio afande, si hata wewe mwenyewe unaona nguo zangu zilivyoisha. Kwahiyo nilikuwa naomba kama kuna nguo nyengine zozote unipatie" Mrutu aliongea kwa kulalamika baada ya kuona askari huyo akiwa amechukia kwa kumuambia hivyo.



“Unadharau eee? Huna adabu eee? Unahitaji adhabu eee?" Askari huyo aliongea huku akipigapiga kurungu chake kwenye kiganja chake.



“Hapana Afande, ila nimekuambia hivyo kwasababu hii nguo imeshaisha kwahiyo nahitaji nyengine"



“Kwani unanguo hiyo hiyo moja tu?" Askari huyo aliuliza huku akiwa amekaza sura kama anakunywa dawa chungu ya muarubaini.



“Hata hiyo nyengine pia imeisha, ipo kama hii tu"



“Nani aliekuambia kuwa mimi nasimamia masuala hayo? Au unanichora tu?"



“Hapana afande sikuchori ila nilikuwa najaribu kukuambia nikidhani labda utanisaidia, ila samahani kwa hilo"



“Pumbavu wewe, mfungwa mmoja, haya potea haraka kabla kirungu hiki hakija uadhibu mwili wako. Alaaa!!" Mrutu aliondoka hapo haraka haraka baada ya kuona ombi lake limepita kushoto kwa askari huyo.



“Kwanza sina muda mrefu nitatoroka, mxxxyuuuc!" akamalizia na msonyo huku akikaa chini kumalizia chakula chake.



* * * *



Siku ya kuwaona wafungwa gerezani ilifika. Paskal na mapacha wawili walipanda kwenye gari kwaajili ya kwenda gerezani kwenda kumuona Mr Hanein. Safari hii walimpelekea na chakula maana walijua ni muda mrefu hakuwahi kula chakula kizuri. Kama kawaida. Walipofika kwenye lango la kuingilia, gari lao lilikaguliwa kwanza ndipo wakaruhusiwa kuingia. Wakapaki gari sehemu na mapacha wawili wakashuka huku wakimuacha Paskal kwenye gari. Wao wakaongoza njia kwenda mapokezi. Wakaeleza shida yao na kuambiwa wasubiri sehemu maalumu.



Wakaletewa mtu wao waliemtaka. Safari hii hakuna ambae alielia pindi walipoonana. Waliishia kutabasamu tu. Labda ni kwavile walijua mtu huyo muda si mrefu atatoka au ni kwavile walishaonana mara ya kwanza. Kwanza kabla ya kumpa kile chakula walichokuja nacho. Askari aliwaamuru wakionje wao kwanza kabla hajakula mfungwa. Hii ni kwa usalama zaidi. Baada ya kukionja na kuonekana hakina madhara. Ndipo akakichukua baba yao na kuanza kula.



Walimsubiri alipomaliza kula ndipo wakaanza kumueleza mipango yao waliyoipanga. Walimueleza mwanzo mwisho jinsi walivyopanga. Mwanzo Mr Hanein alikataa maana hiyo ni njia hatari zaidi. Kutoroshwa kwa kupitia ugonjwa. Ugonjwa wenyewe ni kumeza kidonge chenye sumu kali. Kisha hapo achukuliwe apelekwe hospital ya gereza, halafu hapo achukuliwe tena apelekwe hospital ya mkoa, ndipo njiani waje kulivamia hilo gari ambalo atakueko yeye na huyo anaetaka kutoroka nae.



Ilikuwa ni njia ngumu kuikubali maana kifo kilikuwa wazi wazi. Je kama wasipofanikisha kuwatorosha hiyo siku? Sindoitakuwa mwisho wao kwa kufa kifo kibaya cha kukaushwa damu yote na mwili kukakamaa kama mbuzi wa kubanikwa alimaarufu kama ‘ndafu'. Alikataa mwanzo ila baada ya ushawishi wa wanae akakubali na kuwaachia wafanye vile wanavyoona wao ni sawa.



Hapo wakafurahi na kumpenyezea kwa siri kubwa sana baba yao hivyo vidonge na kumuambia kuwa vidonge hivyo ndio hivyo atakavyo vimeza yeye na huyo mwenzake. Wakamuambia na muda ambao utakuwa ni mzuri kwaajili ya kuvimeza na wakamuambia hiyo kazi itafanyika usiku kwasababu wanaamini lazima watapelekwa hospital ya mkoa usiku baada ya kushindikana kwenye hospital ya gereza.



“Najua mmepanga kweli kunitoa humu ndani kwa njia yoyote ile ilimradi niwe huru.. Kuna mtu anaitwa Mr Tanganyika. (mtu huyu tutakuja kumuona kwenye riwaya inayofuata na mambo yake). Huyu mtu nikiwapa mawasiliano yake naamini atatia nguvu kwa hili. Naamini atakubali kuwasaidia kwa namna yoyote ile. Yeye hayupo Tanga. Yupo Morogoro huko" Mr Hanein aliwaambia hao wanae wapekee wenye mpango wa kumtoa yeye gerezani.



“Tutampataje huyo mtu?" Atu alimuuliza.



“Nendeni katika chumba changu kwenye droo ambayo ipo pembeni ya kabati. Sijui kama imeiamishwa au laa. Ila naamini itakuwa ipo pale pale, na kama itakuwa imehamishwa hiyo droo. Basi mtamuuliza kwa uzuri Paskal maana yeye ndie niliemuachia kila kitu wakati mimi nipo gerezani.. Kwenye hiyo droo, kuna kijitabu ambacho nimezihizfadhi namba nyingi sana za watu wangu na pia namba ya huyo ndipo ilimo.. Mkiipata jaribuni kuipiga na kama isipopatikana basi nyuma kabisa ya hicho kijitabu, kuna ‘Email' pia zipo. Kwahiyo mtaangalia jina la huyo mtu na mkilipata basi mtamtumia ujumbe na mumualekeze kuwa nyie ni watoto wangu. Hawezi kuwajua kwa sura ila kwa majina yenu naamini atayakumbuka. Kwasababu zamani amewaacha nyie mkiwa wadogo sana. Mr Tanganyika lazima atawapa msaada wowote akisikia mnataka kunitoa humu" alihitimisha maelekezo yake.



“Sawa baba tumekuelewa. Hayo mawasiliano tutaanza kuyafanya leo baada ya kufika nyumbani. Naamini hiyo kazi itafanyika jumanne kwahiyo nyie mntakiwa mvimeze hivyo vidonge siku hiyo jioni.. Lakini mnatakiwa mvimeze kwa pamoja na huyo mfungwa mwengine pia umpange kabisa ili hiyo siku mpango uende kama ulivyopangwa" Ata aliongea.



“Sawa wanangu nimewaelewa, nitafanya kama hivyo mlivyosema, na nina wahakikishia kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa"



“Sasa baba acha sisi tuondoke tukaanze muchakato sasa hivi ya kuukamilisha huu mpango" Ata aliongea.



“Sawa wanangu, tutakutana jumanne"



Walitoka sehemu hiyo na kutoka nje, walienda kuingia kwenye gari lao na safari ya kutoka hapo gerezani ikaanza. Dakika ishirini na tano zikatosha kuwafikisha kwenye nyumba yao. Walipofika wakashuka kwenye gari na kuingia ndani ya mjengo huo hadi sebuleni.



“Amesema kuna mtu anaitwa Mr Tanganyika ndie ambae atakaetia nguvu katika hili?" Paskal aliwauliza.



“Yeah. Na amesema mawasiliano yake tutayapata chumbani kwake. Embu twendeni tukaangalie" wakatoka hapo sebuleni na kuenda katika chumba cha baba yao na kuingia humo. Macho yao yalituwa katika droo iliyokuwa pembeni ya kabati kubwa la nguo. Wakaiendea na kuifungua. Ilikuwa na vumbi jingi kiasi kwamba mende na buibui walifanya ndio makazi yao humo.



Ilishangaza sana maana hakukuwa na tundu ama tobo lililowawezesha kuingia humo ndani. Ila walikuwepo na kufanya ndio makazi yao. Ikabidi watoe uchafu uchafu wote humo ndani, kisha ndio wakaanza kutafuta hicho kijitabu walichoambiwa. Haikuwapa tabu sana kukiona kwasababu kwenye droo hiyo hapakuwa na vitu vingi.



Wakakichukua na kurudi nacho sebuleni. Kisha hapo wakaanza kuitafuta namba iliyoandikwa jina waliloambiwa na baba yao. Walilipata na kujaribu kuipiga namba hiyo. Ila jibu walilopatiwa ni kuwa namba hiyo haikuwa ikitumika tena. Hapo wakachoka. Na kuanza kuona mafanikio ya kumpata mtu huyo ni madogo. Wakafungua nyuma ya kijitabu hicho na kukutana na ‘email' nyingi. Wakazisoma na kuipata wanayoitaka.



Wakachukua ‘laptop' na kuiingiza ‘email' hiyo. Wakatuma ujumbe na kusubiri kwa dakika kumi. Kimya!. Wakazidi kuchoka. Hapo wakajipa moyo huenda ikawa mtu huyo hayupo hewani kwa muda huo. Wakaandika ujumbe mrefu wa kujitambulisha wao ni wakina nani na wanataka nini. Kisha wakautuma. Ila kabla hawajaizima, pakaingia ujumbe. Wakaufungua na kuusoma.



‘Mmesema nyie ni watoto wa Mr Bakari. Embu nitumieni picha zenu nione' Ujembe ulisomeka hivyo. Wakaandika neno ‘Ok' na kulituma. Kisha Atu akaiendea picha moja iliyokuwa ukutani. Iliyoonyesha taswira za watu wa nne. Mr Hanein, Mke wake na vitoto viwili vidogo ambavyo vilikuwa vimepakatwa. Cha kiume kilipakatwa na mama na kike kilipakatwa na baba. Alifanya hivyo kwakujua kwamba, kwasababu mtu huyo aliwaacha wao wakiwa wadogo, basi lazima wakimtumia hiyo picha ataikumbuku tu. Kisha akaipiga picha kwenye simu yake picha hiyo na kuiingiza kwenye ‘laptop' kwa njia ya ‘Bluetooth' kisha wakamtumia. Baada ya hapo ukaingia ujumbe.



‘Sawa. Mlikuwa mnataka nini kutoka kwangu?' Ujumbe ulisomeka hivyo. Wakaeleza shida yao kama vile walivyoambiwa na baba yao.



‘Ok. Nitamipatia Chopa ambayo ndani yake kutakuwa na wanaume wa kazi watatu watakao wasaidia hiyo kazi. Kisha hapo mkishakamilisha hiyo kazi. Mtaenda Pongwe. Kule kuna nyumba yangu ya siri. Nyumba hiyo mtaitumia muda wote hadi pale mtakapo amua muondoke wenyewe.. Nimefurahi sana kuona mnataka kumsaidia baba yenu kutoka gerezani. Mr Hanein hakukosea kabisa kuwapeleka kwenye mafunzo ya ujasusi... Embu nitumieni na picha zenu za umri huo mliokuwa nao' Ujumbe ulimalizika hivyo.



Wakatuma picha zao tatu wakiwa sehemu tofauti tofauti na mavazi tofauti tofauti. Na kwachini wakaandika ujumbe.



‘Tutapajuaje kwenye hiyo nyumba yako huko Pongwe?'



‘Mmekuwa sana wanagu. Na kuhusu kupajua huko kwenye hiyo nyumba. Hawa vijana nitakao watuma huko ndio watakuja na ramani itakayo wafikisha huko. Kwahiyo nyie msijali'



‘Lakini Mr Tanganyika. Sisi huku hatuna silaha zozote'



‘Msijali kuhusu hilo. Hao vijana watakuja nazo za kutosha tu'



‘Sawa tumekuelewa'



Wakamaliza kutumiana ujumbe. Furaha yao iliongezeka baada ya kujua kuwa msaada umepatikana. Hapo wakaiona kazi ikiwa rahisi kabisa. Wakawa na shauku kubwa ha kufika hiyo siku ya tukio ili wamtoe baba yao kifungoni.



“Kazi imeisha" Ata aliongea hivyo huku akiinuka kwenye sofa alilokaa na kupandisha ngazi kwenda flow ya juu ya nyumba hiyo.



* * * *



Siku ya tukio ilifika. Siku hii baada ya kutoka kwenye kazi za gereza ikiwa ni moja ya adhabu zinazopatikana gerezani. Wakapanda kwenye gari kuelekea gerezani wakitokea kwenye kazi. Hapo Mr Hanein alimsogelea Mrutu na kuanza kumuambia kwa sauti ya chini.



“Leo ndio ile siku ya kutoroka" Mr Hanein alimuambia Mrutu kwa sauti ya chini kabisa waliojisikia wao wenyewe wawili tu.



“Kivipi. Sijakuelewa" Mrutu alimuuliza. Hapo Mr Hanein aliingiza mkono wake kwenye nguo yake yakifungwa kwenye mfuko na kutoka na kidonge kimoja, kisha akamkabidhi Mrutu na kumuambia.



“Tukifika tu gerezani, wakati tukiwa tunashuka kwenye gari kwaajili ya kuhesabiwa namba. Kimeze hicho kidonge"



“Hapana. Kwanza hiki kidonge ni cha nini?" Mrutu alimuuliza kwa wasiwasi.



“Huo ni mpango mmoja wapo wa kutufanya tuondoke jela. Kwahiyo fanya hivyo" Mrutu akabaki kuduwaa tu asielewe ni kwa kivipi hicho kidonge kiwe ni moja ya mpango wa kutoroka gerezani. Akakiangalia vizuri na kukitia mfukoni mwake.



Mr Hanein hakutaka kumuambia kuwa hicho kidonge ni cha sumu. Maana alijua anaweza akamtisha mtu huyo na kupelekea kutokimeza na kuharibu mpango wao. Kwahiyo alitaka akimeze pasi na kujua kuwa kidongo hicho ni cha sumu kali yenye kukausha damu na kuuwa ndani ya masaa ishirini na nne ikiwa hujapatiwa dawa yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya dakika kadhaa. Wakawa wamefika gerezani. Wakashushwa kwenye gari huku wakiwa wanahesabiwa namba. Wakwanza kushuka alikuwa ni Mr Hanein. Akahesabiwa namba na alipofika mbele kidogo akakimeza kile kidonge. Mrutu alipoona mtu huyo amekimeza kidonge alichokuwa nacho. Na yeye akakimeza chake. Kisha akashuka na kuhesabiwa namba.



Dakika mbili hazikuisha. Wote wakaanguka chini na kuanza kupapatika kama kuku aliechinjwa na kuachiwa. Askari na wafungwa wengine wakashangaa kwa tukio hilo. Ikabidi askari mmoja apige firimbi kuwaita wenzake. Walipofika wakawachukua watu hao haraka na kuwapeleka katika hospital ya hapo gerezani. Wakalazwa kwenye vitanda vya kitabibu na kuanza kuchekiwa kwanza ni kipi kilichowafanya kuwa katika hali hiyo.



“Mmmh! Dokta Mugiso wala mimi sioni tatizo lolote kwa watu hawa" Mtu mmoja alievaa mavazi ya kitabibu alimuambia mwenzake alievaa kama yeye.



“Embu nipishe mimi niwaangalie" Dokta Mugiso akawasogelea watu hao na kuanza kuwapima.



“Duh! Tatizo halionekani kweli. Lakini hali zao zinazidi kuwa mbaya. Si unaoana wanavyotoka mapovu midomoni mwao"



“Basi itabidi Dokta tuwaambie askari wawapeleke hospotal ya mkoa maana hali zao zinazidi kuwa mbaya"



“Hapana. Hawa watu watabaki hapa hapa na tutawahudimia na watapona tu. Subiri tuendelee na kuchunguza tatizo" Dokta Mugiso alipinga wazo la mwenzake na kuendelea kuchunguza tatizo. Hakujua kwamba watu hao wamemeza vidonge ambavyo havina dawa zaidi ya dawa ambayo ni yake pekeake. Yeye alidhani ni ugonjwa tu wakawaida. Akaendelea na uchunguzi wake wa kitabibu.







“LAKINI Dokta, si unaona hali zao zinazidi kuwa mbaya hivi? Halafu sasa chaajabu ugonjwa wenyewe hauonekani, watakufa hawa!" Dokta ambae hatujalijua jina lake, alimuambia Dokta Mugisu kwa mashaka na wasiwasi mwingi baada ya kuona hali za hao wafungwa zina zidi kuwa mbaya.



“Dah! Basi nenda kawaite wale askari waje" Dok. Mugisu alimuambia yule Dokta mwengine, nae akatoka humo na kuenda nje. Baada ya dakika moja akarudi na askari mmoja.



“Afande naona hali za hawa watu zinazidi kuwa mbaya kila muda unapokwenda mbele. Kwahiyo hapa cha kufanya ni kuwahamisha Hospital na kuwapeleka katika hospital ya mkoa haraka sana kwajili ya matibabu" Dok. Mugisu alisema.



“Kwani wanasumbuliwa na nini hao? Maana imekuwa ni ghafla tu wameanguka chini" Askari alimuuliza.



“Huwezi amini Afande, vipimo vyote vinaonyesha hawana tatizo kabisa. Lakini sasa chaajabu hali zao zinazidi kuwa mbaya" Dk. Mugiso alimuambia.



“Basi subirini nakuja sasa hivi" aliongea Afande huyo na kutoka katika chumba hicho. Baada ya dakika tano, alirejea tena.



“Ok. Inabidi wapelekwe katika gari inayo wasubiri hapo nje kwaajili ya kwenda hospital, na mmoja kati yenu ataongozana nasi" aliongea askari huyo na kuwaita askari wawili waje kusaidia kuvisukuma hivyo vitanda. Wakawatoa na kuwaingiza katika gari maalumu kwajili hiyo. Wakaingia askari wawili ndani ya gari lililo wabeba wagonjwa huku askari wengine wanne wenye silaha wakiingia katika gari nyengine aina ya ‘defender' kwaajili ya kuusindikiza msafara huo. Majira hayo yalikuwa ni saa moja za usiku. Magari hayo yalitoka huku yakipiga ving'ora vya kuomba njia barabarani.



Huku njiani. Mapacha wawili na vijana wawili waliotumwa kuongeza nguvu. Walikuwa wapo pembeni kidogo ya njia. Walikuwa wakitega msafara huo ili kutimiza adhama yao waliyoipanga. Mbali kidogo waliipaki Chopa yao wakisubiri watimize kazi yao na kuondoka mahala hapo haraka. Mikononi mwao walikuwa wameshika silaha kali kali kwaajili ya mashambulizi ya ghafla. Kwambali walisikia ving'ora wakajua msafara huo ndio unakaribia kufika.



Atu akatoka kwenye maficho akiwa peku huku kichwani nywele zikiwa timtim na nguo zake alizovaa baadhi ya sehemu zikiwa zimechanika. Akaanza kurusha mikono kama mtu aliechanganyikiwa huku miguu yake akiipigapiga chini, akiwa anazunguka zunguka katikati ya barabara huku akiwa analia. Hiyo ilikuwa ni katika moja ya mipango yao.



Dereva wa gari lililowabeba wagonjwa, ndio wakwanza kumuona msichana huyo akiwa katikakati ya barabara. Akafunga breki za gari na kufanya gari lililokuwa nyuma yao kwaajili ya ulinzi pia lisimame. Atu pale barabani aliendelea kuwa katika hali ile ile pasi na kuyajali yale magari yaliyosimama kwaajili yake.



Akashuka askari mmoja aliekuwa na bunduki mkononi mwake na kumfuta dereva wa gari ya mbele yao kumuuliza kulikoni mbona amesimamisha gari barabarani. Alipofika, akaonyeshwa msichana alieonekana kuchanganyikiwa kama ambae amepatwa na tatizo. Askari huyo akaanza kupiga hatua kumfuata mwanamke huyo huku akifuatiwa na askari mwengine kutoka katika gari la nyuma, naye pia akiwa na bunduki mkononi mwake.



“We dada mbona hivyo tena barabarani usiku huu, una nini?" askari mmoja alimuuliza huku akiwa anazidi kumsogelea.



“Vibaka" Atu alijibu hivyo huku akiendelea kulia na kupigapiga miguu yake pale barabarani. Askari hao wakamsogelea kabisa na kumtuliza.



“Embu tulia dada. Hao vibaka wapo wapi?" Askari mmoja alimuuliza huku akimshika mikono silaha yake akiiweka begani. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa. Bilashaka alienda kuwahadithia askari wenzake waliotangulia mbele za haki kwa kosa la kumuamini mwanamke huyo akidhani labda ndio kama wale wengine.



Yule askari mwengine alikuwa amepoteza umakini kabisa, akawa na yeye anamshangaa mwanamke huyo... Atu aliwaonyesha kwa kidole sehemu ambayo alikuwa amejificha Ata huku wale vijana wengine wakiwa tayari wameshazunguuka kulifuata lile gari la nyuma waliloshuka askari hao. Kipindi hicho kwenye gari kulibakia askari wawili kwenye bodi ya gari na mwengine ambae ni dereva.



Wale askari waliokuwa wamezubaishwa na Atu. Walizidi kuzubaa. Wakawa wanaenda kule walipoelekezwa na mwanamke huyo. Ghafla walidondoka chini baada ya kupigwa risasi zilizotoka huko walipoelekezwa. Wakalala chini huku roho zao zikiachana na mwili kwa maumivu ya risasi. Dereva wa gari lililobeba wagonjwa. Muda wote alikuwa kaduwaa tu asielewa nini kinaendelea hapo.



Atu akaokota bunduki moja za wale askari waliokuwa wafu muda huo na kumpiga risasi ya kichwa dereva na kuondoka na uhai wake papo hapo. Kule kwenye ‘defender' ya gereza. Wale askari wawili waliobaki nyuma, walishuka hai hai baada ya kusikia milio ya risasi. Lakini bahati ya kuishi haikuwa kwao. Walikutana na risasi nyingi zilizozama kwenye miili yao na kufa papo hapo wakiwa wanataka kuwaokoa wenzao.



Kwenye msafara huo pakabakia watu sita wenye roho zao. Walibakia askari wawili waliokuwa ndani ya gari la wagonjwa na Dokta na wagonjwa. Huku kwenye lile ‘defender' paki bakia askari dereva. Wale askari wawili kwenye gari la wagonjwa, hawakujua wafanye nini ili kujiokoa. Mikononi mwao walishika bastola ndogo. Wakafungua mlango ili kujihami. Ila ile wanafungua mlango tu. Wakakutana na risasi zilizozama kwenye vufua vyao na kuwafanya warudishwe ndani kwa msukomo wa hizo risasi.



Dokta alipiga yowe la hofu baada ya kuwaona askari hao wakirudi ndani lakini sio kama walivyotoka. Safari hii walirudi wakiwa hawana uhai tena.. Yule dereva wa lile ‘defender' alipigwa na kitako cha bunduki na kuzimia humo humo garini kabla hajashushiwa mvua ya risasi na kufia humo humo kwenye gari.



Atu na wale vijana wengine wawili. Walienda kuvitoa vitanda ambavyo juu yake walilazwa watu wao wanaowataka. Dokta kipindi hichi alikuwa akitetemeka kwa uoga huku akiwa amejikunyata kwenye kingo za gari hilo.



“Na huyu daktari tumfanyeje?" Jamaa mmoja kati ya wale wawili waliokuja kutoa nguvu kwenye tukio hilo aliuliza.



“Huyo afe tu, hakutakiwi kubakie hata punje ya ushahidi" Atu aliongea hivyo na kummiminia risasi.



Wakawachukua watu wao na kuondoka nao haraka kuelekea kule walipopaki chopa lao. Huku nyuma Ata alitega mabomu kwenye magari hayo, akaiikusanya ile miili ya wale askari na kuingiza ndani ya lile ‘defender' kisha akaondoka hapo kuwawahi wenzake. Alipofika akapakia haraka na chopa hilo likaanza kupaa angani kuondoka maeneo hayo. Huku chini kwenye zile gari. Mlipuko mkubwa ulitokea na kuzisambaratisha zile gari na kubaki moto tu ukiwa unateketeza mabaki ya magari hayo.

Kazi ikawa rahisi!.



“Atu wape hiyo dawa kabisa kabla hali zao hazija kuwa mbaya zaidi" Ata aliongea hivyo. Atu akatoa kile kichupa na kukifungua. Akawafumbua midomo watu hao na kuwanywesha hiyo dawa. Alipohakikisha wamemeza kabisa. Akawaacha wapumzike.



“Ulisema watapata nafuu baada ya muda gani?" Ata alimuuliza.



“Nusu saa mbele" Atu alijibu huku akikifunga kichupa hicho.



Baada ya mwendo wa muda mfupi. Wakatua chopa hilo ndani ya jumba moja lililokuwa na eneo kubwa huko Pongwe. Jumba hilo ndio hilo la Mr Tanganyika alilowapa watu hao kwaajili ya matumizi yao. Baada ya kutua chopa hilo kwenye sehemu yenye uwazi mkubwa kwenye jumba hilo. Wakawashusha wagonjwa hao na kuwaingiza ndani kwenye chumba kimoja wapo. Wakawalaza kwenye vitanda na wao wakatoka kwenda kwenye sebule ya nyumba hiyo.



* *



Huku kwenye eneo la tukio. Askari wenye silaha kali walikuwa wameshajaa kwa ajili ya kuweka ulinzi na kuchunguza chanzo cha tukio hilo. IGP Taure ambae tulianza kumjua akiwa na cheo cha Koplo kwenye riwaya iliyopewa jina la ‘UHASAMA'. alifika pia kama kiongozi katila jeshi la polisi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mkuu, tumepata maganda ya risasi tu zilizotumika kwenye tukio hili" askari huyo aliongea hivyo huku akimkabidhi IGP Taure maganda ya risasi. Akayapokea na kuyaangalia kwa kumulika na tochi yake.



“Hakuna chengine kilichopatikana ambacho kitasaidia katika upelelezi wa hili tukio?" alimuuliza huku akimkabidhi askari huyo maganda hayo ya risasi.



“Hakuna mkuu zaidi ya haya maganda tu"



“Ok, utaniletea hayo maganda ofisini kwangu kesho asubuhi" Wakati huo akaja askari mwengine mbio mbio hadi hapo na kuwapa taarifa.



“Mkuu. Kwenye lile ‘defender' kuna miili ya watu iliyoungua vibaya sana kwa kuchomwa na moto. Twendeni mkaone" alisema askari huyo na kuwafanya IGP Taure na yule askari mwengine kuenda huko. Walipofika huko waliona miili ya watu iliyokuwa kwenye bodi la gari hilo ikiwa imeungua vibaya sana. Hawakuweza kuitambua kwasababu hata nguo za kiaskari magereza walizovaa askari hao zilikuwa tayari zimeteketea kwa moto huku zikiiacha miili hiyo ikiwa dhalili na kuungua vibaya sana.



Mkuu wa gereza ama kwa cheo chake cha Kamishna . Alifika hapo akiongozana na ‘defender' moja iliyokuwa nyuma ya gari lake aliekuwa akiendeshwa na dereva wake. Walipofika hapo moja kwa moja akashuka na kuenda sehemu waliposimama askari wakiangalia miili hiyo. Akatoa salamu na wale waliokuwa chini yake ki cheo wakampigia salut za heshima. Kisha na yeye akaonyeshwa miili hiyo.



“Hii ni miili ya askari wangu!" alihamaki Kamishana huyo baada ya kuiona miili ya askari wake magereza waliokuwa wakiwasindikiza wafungwa wagonjwa hospital. IGP Taure akamvuta pembeni na kumuambia.



“Hili tukio ni la kupangwa. Sio ajali wala bahati mbaya hii. Hili tukio ni la kuwatorosha hao wafungwa wagonjwa" IGP alimuambia.



“Kwanini umeongea hivyo?" Kamishna alimuuliza.



“Kwasababu miili ya hao wafungwa haijapatikana na katika maelezo niliyoyapata kutoka kwa askari wako waliowahi kufika hapa, ni kwamba, wagonjwa hao hawakuwa wakijiweza hata kuinuka. Sasa unadhani ni kwanini wao wasiungue katika huu moto?" IGP aliongea.



“Ni kweli usemayo, kwasababu kama ingekuwa ni ajali ya kawaida, basi wale askari wangu wasingekuwa wamejikusanya sehemu moja eti waungue wote" Kamishna aliongea.



“Kwanza hii haiwezi kuwa ni ajali kwasababu kila nikiangalia mazingira ya ajali yenyewe hata siyaoni. Halafu pili, kumekutwa maganda ya risasi eneo hili. Kuna askari nimempa akae nayo halafu kesho aniletee kituoni kwangu tuyafanyie uchunguzi"



“Hakuna shaka Afande. Naamini kila kitu kinaenda sawa kikiwa chini yako" Kamishna aliongea.



“Usijali Afande, tutapeana taarifa itakavyokuwa"



Waliondoka na kwenda eneo la tukio na kwenda kuangalia angalia. Kisha viongozi hao wakaondoka hapo huku wakiwaachia maagizo askari waliobakia ya kuondoka na hayo mabaki ya magari yalioungua moto na maiti hizo kuzipeleka hospital muda huo...



* *



Kule kwenye jumba walilokuwemo watu wale waliotoka kufanya uvamizi wa ghafla. Walikuwa wapo sebuleni mwa nyumba hiyo wakijadili hili na lile juu ya mpango wao. Walikuwa wakijipongeza kwa kazi waliyotoka kuifanya muda mfupi uliopita. Hawakuwa na wasiwasi kwasababu walijua kuwa hawakuacha kitu chochote nyuma kitakacho wafanya polisi wapate pa kuanzia upelelezi wao.



Wakawa wana uhakika wa kile walichokifanya. Wakiwa wanaendelea na maongezi. Ata aliinuka kwajili ya kuenda kuwaangalia wagonjwa wao katika chumba walicho walaza. Ghafala alipiga kelele za kuwaita wenzake waliokuwa sebuleni na kuwafanya waende mbio mbio kwenye chumba hicho. Walipofika macho waliyotoa pima kwa walichokishuhudia humo ndani..







WALIWAKUTA watu hao wakiwa wamenyanyuka kwenye vitanda walivyo lalishwa huku wakiwa wana kohoa sana kiasi kwamba wanatoka damu za midomoni. Atu alitoka hapo mbio kwenda nje ya chumba hicho na aliporudi alikuwa ameshika chupa mbili za maji safi. Akawapangua wenzake na kuwafuata wale wagonjwa na kuwapa kila mmoja chupa yake kisha akawaambia wasukutue na kutema hizo damu kisha wanywe maji hayo na wao wakafanya hivyo.



“Msiogope ilitakiwa iwe vile ili watoe ile sumu ya vile vidonge. Ila kwa hapa sasa ni salama" Atu aliwaambia. Wakasaidiana kuwainua watu hao na kuwapeleka sebuleni.



“Baba mnajisikiaje kwa sasa?" Ata aliwauliza.



“Afadhali sasa.." akatulia na kuyaangalia mazingira ya hapo kisha akawauliza. “Hapa ni wapi?"



“Hapa tupo katika nyumba ya Mr Tanganyika" Ata alijibu.



“Kwahiyo hapa tupo morogoro!?" Aliuliza kwa hamaki.



“Hapana baba, hii ni nyumba yake iliyokuwa maeneo ya Pongwe ndio ambayo ametupatia kwa kazi hii" Ata alijibu.



“Ooohps!, Njaa" Mr Hanein aliongea. Watu wote humo walielewa. Ila sasa hakukuwa na chakula chochote na wala hakukuwa na mpikaji.



“Nilazima iwe hivyo" Atu aliongea huku akiinuka kwenye sofa alilokaa na kuanza kuufuata mlango wa kutokea humo.



“Unakwenda wapi wewe?" Ata alimuuliza.



“Humu ndani hakuna chakula wala mpikaji. Acha nikanunue chakula huko juu" Atu aliongea hivyo na kutoka humo ndani. Alilazimika kwenda na gari maana palikuwa na umbali kidogo kutoka hapo hadi sehemu wanapouza vyakula. Baada ya muda alirudi na mfuko mkubwa wa nailoni uliokuwa na vyakula vingi vya kutosha ndani yake. Alipofika sebuleni, akawagaia kila mmoja mfuko wake wenye chakula, kisha kila mmoja akaanza kula baada ya kunawa.



Walitumia muda kidogo kumaliza kula. Kisha wakaanza kuongea na kujadili jambo hilo lililotoka kufanyika masaa mawili yaliyopita. Mwisho Mr Hanein aliomba kuongea na Mr Tanganyika Kwaajili ya kumshukuru kwa kumpa msaada. Kwavile namba zake za simu walikuwa nazo ambazo amewapa yeye mwenyewe. Wakazipiga na kumpa simu baba yao baada ya kuanza kuita upande wa pili.



“Tanganyika!" Mr Hanein alianza kuongea baada ya simu kupokelewa.



“Hanein!" mtu wa upande wa pili nae akaita. Hapo pakafuatia vicheko kwa hao watu wawili kwa furaha.



“Siamini ndugu yangu kama umetoka gerezani" Mr Tanganyika alisikika akiongea.



“Ndugu yangu nimetoka baada ya kukaa gerezani kwa miaka mingi. Ila nashukuru sana kwa msaada wako kwa kufanikisha hili"



“Usijali, wewe ni ndugu yangu kabisa kwahiyo msaada ni lazima kaka.. Haya nambie unamipango gani sasa baada ya kutoka gerezani?"



“Tena kaka naomba msaada wako kwa hili pia. Nina mpango wa kuifanya serikali ya Tanga ijutie kunifunga jela kwa miaka mingi kiasi hichi. Nilikuwa nakuomba unipatie vijana kama kumi hivi wa kazi nataka niingie rasmi kwenye maangamizi ya mji huu. Maana serikali yake imeniulia ngome yangu na kunisababishia hasara kubwa ya kupoteza mizigo yangu ya madawa ya kulevya, pia wakaniulia na vijana wangu wote wa kazi. Kwahiyo ndugu yangu naomba msaada kwa hilo"



“Hahahahahahah!! Mr Hanein naona unataka kurudi kwa kishindo kikuu sana. Nilikuambia ndugu yangu kuwa kama mimi ukajifanya kujiamini sana. Sasa umeona yaliyokukuta. Ila sio mbaya. Nitakutumia vijana ishirini na silaha nyingi kama zawadi ya ule wema wako ulionifanyia kipindi kile"



“Sawa ndugu yangu. Nategemea msaada wako kwa sasa"



“Usijali. Halafu hiyo nyumba nadhani unaijua vizuri. Kule chini kuna baadhi ya silaha nimeziacha. Mtaanza kutumia hizo kabla hizi nyengine hazija kuja huko"



Waliendelea na maongezi yao hadi pale walipoona inatosha. Simu ikakatwa na Mr Hanein akawataka watu hao wamfuate. Akawaongoza hadi katika chumba kimoja wapo. Huko alibinya swichi moja iliyokuwa ukutani na kitanda kilichopo humo ndani kikajisogeza chenyewe pembeni na kubakia uwazi mtupu. Akaisogelea ile sehemu iliyokuwa imebaki tupu baada ya kitanda kusogea chenyewe.



Hapo napo akabonyeza sehemu na uwazi huo ukaachia kwa kurudi juu kidogo na pakaonekana kama vile mfuniko hivi. Mfuniko huo baada ya kurudi juu, ukajivuta kwa pembeni na kuacha tundu kubwa lililokuwa na ngazi za kushuka chini. Hapo akawapa ishara na yeye akaingia humo ndani huku akifuatiwa na hao wanaomfuata.



Huko chini Mr Hanein alibonyeza swichi iliyokuwa ukutani kabla hajamaliza ngazi zote kushuka chini, na humo ndani paka pata nuru ya mwanga baada ya taa kuwaka na kuliondoka giza nene lililokuwa limetawala humo ndani. Palikuwa panatisha humo ndani. Utando wa buibui, panya, mende na wadudu wengine kama hao walipafanya ndio makazi yao kwa muda mrefu.



Wakawa wana kazi ya kupangua pangua nyuzi za buibui zilizotanda humo. Lilikuwa ni eneo kubwa lenye vitu vichache lakini vya kazi kazi. Nikimaanisha, kulikuwa na mavyuma ya kufanyia mazoezi na vyumba vitatu vilivyokuwa humo ndani. Wakaanza kutembelea vyumba hivyo. Humo walikuta silaha nyingi zikiwa zimetapakaa tu bila mpangilio maalumu.



Kwenye chumba cha tatu, humo hapakuwa na vitu vingi. Palikuwa na vioo pembe zote nne za ukuta. Vioo ambavyo vilikuwa vimewekwa mwanzo wa ukuta hadi mwisho wa ukuta. Mr Haneni aliviendea vioo hivyo na kuanza kuviminyaminya. Ghafla kioo kimoja kikajifungua na kuacha uwazi mkubwa ambayo mtu anaweza akaingia kwa kuinama.



“Mmeona huu uwazi. Huu ni mlango ambao kama sio mchunguzi mzuri wala huwezi kujua. Mlango huu ili kuufungua inabidi ukibinyebinye hiki kioo mara tatu sehemu hii" akawaonyesha. Na kuendelea. “Ukibinya mara hizo tatu sehemu hii, hiki kioo kina jifungua chenyewe na kuuacha huu uwazi. Uwazi huu ni njia ambayo unapita kwenye hili bomba na kutokea kwenye barabara kuu. Kwahiyo kama itakuwa siku tumevamiwa basi tutatimia njia hii kutorokea" alipomaliza hapo, akakirudishia kile kioo kikajitia ‘Lock' na kugeuka kuwaangalia.



“Sasa baba hiki kioo si kina vunjika tu hata kwa kukipiga ngumi?" Ata alimuuliza.



“Hahahah! Embu jaribu tuone kama kitavunjika" Mr Hanein aliongea. Ata akakifuata na kukipiga ngumi legevu na kuona kikiwa ngangari. Akaambiwa akaze mkono na apige ngumi yenye nguvu nyingi na yeye akafanya hivyo. Alipiga ngumi zaidi ya tatu lakini kioo hiko hata kutoa ufa hakikutoa.



“Vioo hivi vimetengenezwa na madini magumu ya ‘Aluminium' yaliotoka huko urusi. Kwahiyo usije ukaona kisa ukikiangalia unajiona ukadhani ni kama vile vyengine. Hapana, hivi viko tofauti sana. Risasi moja haiwezi kutoboa hapa zaidi itaacha ufa tu. Labda zipigwe mbili na kuendelea ndio panaweza kutoboka.. Ok, twendeni juu kule" alipowaambia hivyo, akatoka chumbani humo na kujongea kuzifuata zile ngazi huku akifuatiwa na wale vijana. Wakapanda wote juu na kurudishia kitanda sehemu ile ile na wao wakatoka kuenda sebuleni.



“Wanangu tumeamua kurudi katika kazi zetu kwa kasi kubwa. Nataka kwanza tulipize kisasi kwa walichonifanyia kuniweka ndani miaka yoto hiyo" Mr Hanein aliongea.



“Tunaanza kukilipizia wapi na kwa nani?" Ata alimuuliza.



“Yule hakimu alienihukumu ndio wakwanza kufa. Halafu anafuatia yule askari alienikamata, nae pia anakufa. Kisha tunamalizia kwa mkuu wa lile gereza nililofungwa" Mr Hanein aliongea.



“Sawa. Hao wote unataarifa zao muhimu?" Atu alimuuliza.



“Kuhusu taarifa zao ninazo za yule mkuu wa gereza tu. Hao wengine sina ila watapatikana kutokana na uweledi wenu wa kijasusi mliojifunzia huko mlipotoka"



“Kazi rahisi sana hiyo baba.. Tukiimaliza hiyo hakuna nyengine inayofuata?" Atu alimuuliza.



“Tutajua baada ya kuimaliza hii.. Kwasasa twendeni tukapumzike" Mr Hanein aliongea hivyo na kila mmoja akainuka na kuingia kwenye chumba chake. Halikuwapa tabu swala hilo kwasababu jumba hilo lilikuwa na vyumba vingi vya kutosha.



* * * *



Katika nyumba moja jijini Daresalam. Wapenzi wawili walikuwa wamelala katika kitanda ghali kilichoamua kuvumilia uzito wao usiku kucha. Hata hivyo kingefanya nini wakati kimetengenezwa kwaajili hiyo? Mwanaume aliinuka taratibu ili asimbughudhi mwenza wake asubuhi hiyo. Aliposhuka kabisa chini ya kitanda. Akalivuta shuka lililokuwepo hapo kitandani na kumfunika nalo kuanzia unyayoni hadi kwenye mabega. Kisha akamalizia na busu la kwenye paji la uso la binti huyo na yeye akatoka nje ya chumba hicho.



Alikwenda sebuleni na kukaa kwenye sofa. Kisha akainuka na kuiendea luninga bapa, akaiwasha na kurudi kwenye sofa akiwa amekamata rimoti. Akawa anakazi ya kubadilisha chaneli hadi pale alipokutana na chaneli moja ikitoa habari. Akaacha hapo na kumsikiliza vizuri huyo mtangazaji anaetoa habari hiyo.



“........wafungwa hao, wametoroshwa wakiwa wanapelekwa hospitali baada ya kukumbwa na ugonjwa ambao haukutambulika kwenye hospital ya gereza. Wavamizi hao, walivamia magari mawili yaliyokuwa yakiongozana kuwapeleka wafungwa hao katika hospitali ya mkoa. Waliwaua askari magereza na daktari mmoja waliokuwa wakiwapeleka wafungwa hao hospitali. Kwa majina ya wafungwa hao ni Bakari Hanein na mwenzake Mru..." Ghafla luninga ikazimika.



“Honey twende bwana tukalale, mbona umeondoka kitandani asubuhi hivi?" Alikuwa ni Hilda ama TSSI 03 kwa jina la kazi yake ndio ameizima luninga hiyo baada ya kuachwa na TSSI 01 ama Hemedy kitandani pekeake.



“Lakini kuna habari nilikuwa naifuatilia hapa" Hemedy aliongea kwa kulalamika.



“Achana nayo watafuatilia wenyewe huko. Twende ndani mimi bado nina usingizi" Hilda aliongea hivyo na kumfanya Hemedy amuangalie kwa jicho la matamanio. Alikuwa amevaa gauni jepesi liliayaacha maungo yake yaonekane vizuri. Hemedy aligandisha macho yake kwenye mwili huo pasi na kuangalia sehemu nyengine. Funda kubwa la mate likapita kwenye koo lake. Hilda alimfuata pale alipokaa, akamuinua na kuongoza njia ya kurudi chumba huku akiwa anamvuta kwa mkono wake mmoja. TSSI 01 bila kupenda akawa anafuata nyuma.



* * * *



Jijini Tanga asubuhi hiyo. Ilimkuta IGP Taure ofisini kwake akiyachambua kwa umakini maganda hayo ya risasi aliyoletewa asubuhi hiyo na askari alieyaokota jana kwenye tukio la kutoroshwa kwa wafungwa. Aliyaangalia kwa muda na kugundua kitu.



“Haya maganda yapo ya aina mbili. Haya ya mwanzo sina shaka nayo, haya ni ya bunduki za askari magereza. Sasa haya mengine ndio hayo ya hao wavamizi" aliongea mwenyewe huku akiwa bado anayaangalia vizuri.



“Hao watu walipanga kuifanya ile kazi kwa umakini sana ndio maana hawakutaka kuacha ushahidi wowote nyuma. Lakini watapatikana tu" IGP aliongea hivyo na kuyaweka maganda hayo kwenye kiboksi na kuyahifadhi kwenye droo yake, kisha akainua mkonga wa simu yake ya mezani na kuvuta vuta namba kadhaa kwenye kinobu, kisha simu hiyo akaiweka sikioni.



* *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Katika jumba la Pongwe walipofanya ndio makazi yao kwasasa huku wakimuacha Paskal akilinda nyumba iliyokuwa Raskazon. Asubuhi hii iliwakuta wakijadili ni jinsi gani ya kuanza mipango yao waliyoipanga jana. Kila mmoja alitoa wazo lake hadi pale palipopatikana muafaka kwa hilo.



“Sasa wewe Atu nenda kwenye ile nyumba ya kule Raskazon ukaangalie kama utaipata" Mr Hanein alimuambia.



“Kwanini tusimpigie simu Paskal aangalie kama ipo?" Atu alitoa wazo lake.



“Kumbuka wewe na Paskal wewe ndio mwenye uwaledi mkubwa katika kazi hizi. Kwahiyo nenda wewe"



Atu hakuwa na tena cha kupinga, akainuka na kutoka nje, akaingia kwenye gari na safari ya kuenda kwenye nyumba yao iliyoko Raskazon ikaanza. Ilimchukua dakika arobaini na tano akawa amefika nje ya nyumba hiyo. Wakati akiwa anataka kuingiza gari ndani ya nyumba hiyo. Gari ya polisi iliyosheheni askari wengi wenye bunduki ilifunga breki nje ya geti hilo. Atu akashtuka. Hakujua askari hao wamefuata nini kwenye nyumba hiyo. Akajiweka tayari kwa chochote kitakachotokea..







ASKARI wale wakashuka kwenye gari lao na kuingia ndani ya nyumba hiyo, wakati huo Atu alikuwa ndio anashuka kwenye gari lake baada ya kuliweka kwenye maegesho ya magari ya humo ndani. Wale askari walimfuata Atu pale aliposimama.



“Habari yako dada" Askari mmoja mwenye cheo cha Inspekta alimsalimu.



“Salama tu" Atu alijibu huku akiwa hana wasiwasi hata punje. Alijua kwa uwezo wake alionao anaweza akawadhibiti askari hao kwa muda mfupi na kupotea hapo haraka.



“Wewe ni mmoja wa humu ndani?" Inspekta alimuuliza.



“Yeah, ni mmoja wa humu ndani... Mnashida gani kwani?" Atu aliwauliza.



“Sawa. Sisi ni askari polisi" akamtolea kitambulisho. Atu akakipokea na kukiangalia, kisha akamrudishia kitambulisho chake. “Tumekuja kusachi nyumba hii kwasababu mmliki wa nyumba hii ametoroka ama ametoroshwa jana wakati akitolewa gerezani akipelekwa hospitali yeye na mwenzake. Kwahiyo tunaomba tuchunguze nyumba hii maaana tunawasiwasi huenda ikawa wapo humu" Inspekta aliongea.



“Kibali kipo wapi?" Atu aliwauliza.



“Hiki hapa" Inspekta alimtolea kibali na kukisoma. Kisha akawaruhusu wafanye wanachotaka. Askari hao wakagawanyika kuingia vyumbani kwenye nyumba hiyo. Wakatafuta kila kona. Kila sehemu. Kila pahali. Wakafunua kila kitu. Kwauhakika zaidi wakafunua hadi vijiko vilivyokuwa vimefunikwa lakini hawakuwaona watu hao wanaowatafuta. Baada ya kutafuta sana. Wakarudi wote mikono mitupu hadi pale nje alipokuwa amesimama Inspekta na Atu.



“Mkuu hamna kitu" askari mmoja aliongea.



“Samahani dada, kwani kwenye hii nyumba unahusika vipi?" Inspekta alimuuliza Atu.



“Mwenye hii nyumba ni baba yangu" Atu alijibu bila hofu yoyote.



“Bakari Hanein wewe ni baba yako?" Inspekta alimuuliza.



“Yeah, ni baba yangu. Tena baba yangu mzazi" Atu alijibu.



“Unataarifa gani kuhusu yeye?" Inspekta alimuuliza.



“Taarifa niliyonayo ni kwamba yupo gerezani kwa sasa akitumikia kifungo chake cha maisha kwa kosa la mauwaji na uuzaji wa dawa za kulevya.. Kwani kuna nini Afande" Atu aliongea.



“Baba yako ametoroka jana na mwenzake wakati wakipelekwa hospitali na hadi sasa jeshi la polisi linamtafuta kwa udi na uvumba na akipatikana hukumu yake ni ya kunyongwa tu, kwasababu amesababisha vifo vya askari magereza na daktari mmoja huku wakiyaunguza kwa makusudi magari ya serikali" Inspekta aliongea. Aliongea hivyo akiwa na maana yake, alitaka kuona mwanamke huyo atakua katika hali gani baada ya kumpa taarifa hizi.



“Sawa. Hakuna shaka" Atu alijibu na kuanza kupiga hatua kuondoka hapo akimuacha Inspekta huyo akiduwaa tu huku akimuangalia. Inspekta alitikisa kichwa kwenda juu na chini. Kisha akawaamuru askari wake waondoke eneo hilo baada ya kukosa walichokifuata.



Atu aliingia ndani ya nyumba hiyo. Moja kwa moja akaenda katika chumba alichokuwa akilala baba yake na kuiendea ile droo ambayo siku kadhaa nyuma waliifungua kwajili ya kuchukua kijitabu chenye namba. Hapo alikusanya baadhi ya makaratasi yaliyokuwepo humo ndani na kuyatia kwenye mkoba wake aliokuja nao. Kisha hapo akaondoka ndani humo na kwenda kupanda kwenye gari lake alilokuja nalo. Akaanza kuliondoa mdogo mdogo kwenye maegesho kulifuata geti la kutokea kwenye nyumba hiyo. Alipofika karibu na geti, akamuita mlinzi mmoja na huyo akaja hadi pale alipo.



“Paskal ameenda wapi?" Atu alimuuliza.



“Madam hatujui. Yeye alitoka bila kutuambia chochote" Alijibu mlinzi huyo.



“Sawa. Hakikisheni ulinzi unakuwepo kwenye nyumba hii na msimruhusu mtu ambae hamumjui kuingia humu ndani" Atu alipoongea hivyo. Akapandisha kioo cha gari na kuondoka kwenye nyumba hiyo.



Wale askari waliotumwa kuja kuchunguza nyumba ya Mr Hanein. Walifika kituoni na kila mmoja akaenda katika sehemu yake ya kazi huku Inspekta akielekea ilipo ofisi ya IGP Taure. Alipofika, alipiga salut na kukaa kwenye kiti.



“Mkuu, tumeenda kwenye ile nyumba tumeangalia kote lakini watu wetu hawapo. Lakini kuna binti tumemkuta mimi namtilia shaka kidogo" Inspekta aliongea.



“Kivipi?" IGP Taure alimuuliza.



“Kwanza uongeaji wake. Anaonekana kujiamini sana tofauti na vile nilivyodhani mimi. Pili majibu yake ni kama mtu asiekuwa na wasiwasi ama kuwa na mshtuko kwa kutoroka wale watu. Maana nilimuuliza kuwa yeye anahusika vipi na ile nyumba, alichoniambia yeye kuwa ni mtoto wa Hanein. Nikamuuliza tena ana taarifa gani kuhusu baba yake, alichojibu yeye ni kwamba, baba yake yupo gerezani akitumikia kifungo chake. Mimi nikampa taarifa ya kwamba baba yake ametoroka na anatafutwa na jeshi la polisi na akipatikana basi hukumu yake ni kunyongwa. Lakini jibu alilonipa alisema kuwa hakuna shaka. Sasa majibu yake na uongeaji wake vimenitia wasiwasi sana" Inspekta aliongea.



“Kivipi?" IGP alimuuliza.



“Wasiwasi wangu ni kwamba, huenda ikawa anajua kivyovyote vile wale wafungwa walipo"



“Sawa nimekuelewa. Nenda nitakuita baadae kidogo" Inspekta aliinuka na kupiga salut kisha akaondoka humo akimuacha IGP Taure akikuna kichwa.



Atu alifika katika jumba lao na kuweka gari kwenye maegesho. Kisha yeye akashuka na kuingia ndani ya jumba hilo, akawakuta wenzake wakiwa wamekaa sebuleni wakimgojea yeye. Alipofika akampelekea baba yake yale makaratasi baada ya kuyatoa kwenye mkoba wake. Yeye akarudi kukaa kwenye sofa na wote wakawa wana muangalia Mr Hanein.



“Safi, haya ndio yenyewe" Aliongea hivyo huku akiyakunja vizuri.



“Paskal yupo kule?"Mr Hanein alimuuliza.



“Hapana, nimeambiwa ametoka" Atu alijibu.



“Basi mpigie simu aje. Si anapajua huku?" Mr Hanein alimuuliza.



“Ndio" Atu alijibu huku akiitoa simu yake. Akaitafuta namba ya Paskal, alipoipata akampigia na kumumbia kuwa Mkuu wake anamuita. Akakata simu na kusema.



“Nyumbani kwako palikuja askari, wakataka kuchunguza ile nyumba eti wanadai huenda ikawa nyie mpo mule. Mimi nikawaruhusu wafanye wanavyotaka ila waliambulia patupu na kuondoka zao" Atu aliongea hivyo na kuwafanya wenzake wote kumuangalia yeye.



“Hawajakuambia chochote au kukuuliza chochote?" Mr Hanein alimuuliza.



“Wametishia tu, eti oooh tutampata na tukimpata ni kumnyonga yeye na huyo mwenzake"



“Hahahahh! Wanachekesha sana. Wataanzia wapi kunipata, naona sasa kwavile mwanzo walifanikiwa kunipata, sasa wanadhani na wakati huu pia watanipata.. Atu, kazi ndio inaanza leo. Nenda katika ile mahakama waliyonihukumu. Nenda kawaulize aliewahi kuwa hakimu wa mahakama ile anaishi wapi. Anaitwa Nasra Mpito. Sina haja ya kukuelekeza sana ni mbinu gani utumie, ila naamini mwenyewe utajua nini ufanye hadi upajue anapoishi. Huyo nataka awe wakwanza kufa kabla ya hawa wengine kufuatia" Mr Hanein aliongea.



Mr Hanein alidhamiria kufanya mabaya katika mji huo wa Tanga kama mwenyewe alivyosema kwa madai eti ya kulipa kisasi kwa alichofanyiwa na serikali kwa kumfunga ndani kifungo cha maisha. Aliwaza kuichanganya serikali. Wakati wakiwa wanaendelea na mazungumzo. Paskal alifika na yeye akajumuika na wenzake. Mr Hanein alitumia muda huo kumtambulisha Mrutu kwa watu hao.



“Huyu ndio yule mtu niliesema mnitoroshe nae. Anaitwa Mrutu" Akamgeukia Mrutu na kumuambia. “Mrutu, wale pale mapacha ni wanangu kabisa, na wale vijana wawili wametumwa na rafiki yangu mmoja kuja kutoa msaada wa sisi kutoroshwa kule gerezani, yule pale mmoja ni mfanyakazi wangu tangu miaka hiyo nipo uraiani hadi sasa nipo uraiani tena... Nadhani tutafanya kazi wote kwa pamoja" Mr Hanein alimaliza.



“Ndio niko tayari" Mrutu aliongea.



“Basi sawa... Kuanzia sasa kule nyumbani hakuna mtu kuenda. Wote makazi yetu yatakuwa hapa. Maana kule askari wameshaanza kuenda... Paskal kama kule kuna vitu vyako vya kuhamisha basi nenda sasa kavilete, maana sasa maisha yetu yatakuwa ni huku tu hadi pale tutakapo amua kuhama"



“Sawa mkuu, nimekuelewa" Paskali alijibu.



“Na wewe Atu nenda sasa kule mahakamani ukafanye mpango wa kujua ni wapi anaishi hakimu Nasra Mpito, kisha umpeleke walipokuwa babu yake na bibi yake leo leo"



“Usijali baba nitakuletea majibu hivi karibuni" Atu aliongea huku akiinuka kwenye sofa alilokaa. Paskali nae alifanya hivyo hivyo. Wakatoka wote nje na kila mmoja akaingia kwenye gari lake na safari ya kurudi mjini ikaanza.



Walipofika. Atu yeye akaelekea mahakama ya Chumbageni huku Paskali akielekea katika nyumba ya Mr Hanein. Alipofika, akakusanya kila kilicho chake cha muhimu na kutoka nje. Aliwapa maagizo walinzi na kuwaambia kuwa asiruhusu mtu yoyote kuingia ndani ya nyumba hiyo hadi pale watakapo rudi kwa muda usiojulikana kisha akaondoka kurudi kule kwenye lile jumba.



Kule mahakamani. Atu alifika na kukuta watu wachache tu mahakamani hapo. Akamfuata mwanamke mmoja aliekuwa amekaa nje ya mahakama hiyo akichezea simu yake. Na kumuuliza iwapo yeye anajua ama anahusika kwa chochote kwenye mahakama hiyo, ila mwanamke huyo akajibu hapana na kumuelekeza kwa mtu ambaye aliona anaweza kumsaidia kwa lolote. Atu akashukuru na kuenda kwa yule mtu mwengine.



“Za saa hizi kaka yangu?" Atu alisalimia kwa sauti ya upole na yenye shida fulani ndani yake. Mwanaume yule alielewa na kujibu salamu hiyo.



“Nilikuwa namuulizia Mama mmoja aliewahi kuwa hakimu katika mahakama hii anaitwa Nasra Mpito, sijui nimemkuta?" Atu aliongea hivyo huku akiangaza angaza macho yake huku na huko.



“Unamjua ukimuona?" Kijana huyo alimuuliza.



“Kiukweli kaka yangu hata simjui, ila nimeambiwa kuwa nikifika hapa niweza elekezwa hata kwake" Atu alijibu.



“Sawa. Yule mama hivi sasa amestaafu na yupo nyumbani tu. Na kuhusu anapokaa ni mtaa wa Mikanjuni nyumba namba 1109. Nadhani kama utakuwa ni mjuzi mzuri wa namba za nyumba hutoweza kupotea" Kijana yule alimuelekeza bila kujua dhamira ya huyo anaemulekeza.



“Asante kaka yangu kwa msaada wako. Acha mimi niende sasa" Atu alishukuru na kuondoka hapo. Akaingia kwenye gari na safari ya kwenda mtaa wa Mikanjuini ikaanza. Hakupajua ila alifika kwa kuulizia ulizia mtaa huo ulipo. Alipofika sasa akawa anakazi ya kuitafuta nyumba yenye namba hiyo. Ilimpa tabu kidogo kwasababu nyumba nyengine zilikuwa na mageti kwahiyo hakuweza kuziona namba zake. Ikambidi aulizie tu wadhifa wa huyo mama na jina lake. Hapo ndipo alipoelekezwa na kufika hadi kwenye nyumba moja yenye rangi nyeupe na geti jeusi. Akabisha hodi na kutokea mtu mwenye sare za walinzi.



“Nikusaidie nini dada angu?" aliuliza mlinzi huyo.



“Aaaa! Nilikuwa namuuliza mama Mpito sijui nimemkuta?" Atu aliongea.



“Unashida nae gani?" Mlinzi alimuuliza huku akiwa ana mkagua msichana huyo kuanzia juu hadi chini.



“Ni shida binafsi tu... Samahani kaka yangu, kama yupo naomba nikaonane nae maana ni muhimu sana"



“Subiri" Mlinzi aliongea na kufunga geti hilo akimuacha Atu kwa nje. Baada ya dakika moja alirudi na kumruhusi Atu aingie ndani bila kujua amemkaribisha izraeli kuju kutoa roho ya bosi wake.



Atu aliingia ndani ya nyumba hiyo. Akawa anaangaza angaza macho yake kwenye mandhari ya nyumba hiyo huku akiufuata mlango wa kuingia ndani. Alipofika alifungua mlango huo na macho yake yakatua kwa kipande cha mama kilichokuwa kimebweteka kwenye sofa moja wapo kati ya mengi yaliyokuwa hapo sebuleni. Akaachia tabasamu na kwenda kukaa kwenye sofa jengine lililokuwa limeangaliana na lile alilokaa yule mama mnene..







Atu alikaa kwenye sofa kimya bila kuongea chochote huku akitabasamu. Mama huyo wala hakuwa bado akimuelewa mgeni huyo, maana aliingia bila salamu wala kuongea chochote tena akajikaribisha kwenye sofa bila ya kukaribishwa. Mama huyo akabaki kumuangalia kwa mshangao hadi pale alipo nyanyua mdomo wake kuongea.



“Samahani mama. Wewe ndio mwenye jina la Nasra Mpito?" Atu alimuuliza huku bado tabasamu halijamtoka usoni.



“Yeah, ni mimi, kwani wewe ni nani na unataka nini?" Mama huyo alimuuliza.



“Mimi ni msaidizi halali wa malaika mtoa roho na nimeifuata roho yako maana muda wa kukaa kwenye mwili huo mnene umeisha" Atu aliongea na kumfanya mama huyo atabasamu tu, bilashaka alijua ni masihara tu ya mtu huyo japokuwa hamjui.



“Mwanangu embu sema kilichokuleta, mimi sikujui, lakini nakushangaa unaniletea masihara"



“Sawa. Subiri nifanye kilichonileta" Atu alivaa ‘gloves' kwenye mikono yake, kisha akainuka na kumfuata yule mama pale alipokaa. Alipofika akampiga kofi la uso lililomfanya mama huyo agugumie kimya kimya. Kisha akawahi kumziba mdomo asipige kelele. Akakaa karibu yake na kumuambia.



“Nadhani hadi hapa ushajua kwamba sipo katika utani. Haya tulia kimya niitoe roho yako kwa utaratibu kabisa bila usumbufu wowote" Mama huyo wasiwasi ukaanza kumshika. Akajua kuwa hakukuwa na utani kama yeye alivyodhani. Akabaki akitetemeka tu pasi na kufanya chochote.



“Kwa...kwani nimefanya nini mwana...nangu" Mama huyo aliongea kwa kitetemeshi kikubwa.



“Anhaaa! Halafu nilisahau kukuambia kosa lako linalokupeleka kuzimu.. Ni kwamba, umemhukumu mtu kifungo cha maisha pasi na huruma, kwahiyo na mimi leo nakuhukumu kifo cha maisha pasi na huruma.. Utaenda kuishi na wafu wenzako hadi pale utakapopata uwezo wa kutoroka kuzimu. Nakutakia safari njema, kanisalimie wote huko" Atu alipoongea hivyo. Akampiga pigo moja matata la nyuma ya shingo kisha pigo lile lile akalirudia kwenye koromeo. Sidhani mama huyo kwamba alipata hata nafasi ya kutubu dhambi zake. Alikodoa macho mbele ili asipotee njia ya kwenda kuzimu. Uhai ukamtoka huku akiwa bado anautamani.

Akafa!.



Atu alimuegemeza kwenye sofa alilokaa na kuvua ‘gloves' alizovaa, akazitia kwenye mkoba wake aliokuja nao na kuondoka ndani humo huku akiwa anatabasamu. Alifika kwa mlinzi na kumuaga kisha akaondoka huku akimuacha mlinzi akimkodolea macho ya tamaa kwa zile nguo alizovaa.



Atu alifika kwenye lile jumba na kuingiza gari ndani. Akashuka na kuingia ndani humo na kumkuta kaka yake Ata akikatakata mboga za majani aina ya ‘spinach' huku Mrutu akikatakata nyama.



“Sasa hivi tumepata mpishi wewe si hujui kupika" Ata aliongea huku akiwa anatabasamu akiendelea kukatakata mboga hizo.



“Mpishi ni nani?" Atu aliuliza.



“Broo Mrutu hapa"



“Baba kwanza yupo wapi?" Atu aliuliza.



“Baba kalala huko ndani"



“Basi baadae" Atu aliongea hivyo huku akipiga hatua kuenda kwenye kordo inayoelekea vyumbani. Huko alipotelea kwenye chumba kimoja wapo.



Kule nyumbani kwa yule marehemu hakimu Nasra Mpito. Mfadhaiko ulimkumba mlinzi baada ya kuingia sebuleni akimfuata bosi wake kumpelekea barua aliyopewa na mtu aliekuja getini. Yowe la hofu lilimtoka na barua kumuanguka mkononi mwake baada ya kuenda kumtingisha mama yule pale kwenye sofa mara baada ya kumuita sana pasi na kuitikiwa. Alipiga makelele ya woga na hofu akiomba msaada kwa majirani. Hata basi alimaliza kuita hao majirani vizuri? Muda huo huo nae akakata moto.



Kuja kushtuka alijikuta akiwa katika mazingira tofauti na yale aliyoyazoea. Hewa safi iliyotoka katika mashine za kupoza joto huku akiwa amelalia kitanda kilichotandikwa kwa mashuka safi meupe. Akazidi kushangaa mazingira hayo baada ya kuangaza angaza macho yake ndani humo. ‘Inamaana nilikufa na hapa nipo mbinguni ama? Hapana. Kwanini nife haraka namna hii? Lakini huenda ikawa kweli, si unaona hata mazingira ya hapa yalivyo, duniani hakuna hewa hii'.



Alijiuliza maswali mwenyewe na kujijibu mwenyewe hadi pale alipoingia msichana mmoja mrembo mwenye mavazi meupe ya kidaktari. Aliachia tabasamu baada ya kumuona mgonjwa huyo ameinuka. ‘Mama weee! nipo mbinguni kweli, si unaona hata malaika huyu hapo ananifuata, sijui anataka nini?' aliendelea kumtumbulia macho daktari huyo wakike hadi pale alipomsogelea karibu kabisa. Kisha akachomoa visikilizia mapigo ya moyo akitaka kumuwekea mlinzi kifuani ili ajue mapigo yake ya moyo kwasasa yanaendaje.



“Mama weeeeee!! Usiniue tena, nisamehee. Sirudiii tena kufaaa. Niachee!" Mlinzi alipiga mayowe ya hofu baada ya kumuona daktari huyo akipeleka kifaa hicho kifuani mwake. Daktari alirudi nyuma kwa hamaniko baada ya kusikia mayowe ya mtu huyo. Muda huo huo akaingia yule Inspekta alieongoza msafara wa kuenda kuipigasachi nyumba ya Mr Hanein. Aliingia hai hai baada ya kusikia kelele humo chumbani.



“Kuna nini Dokta?" Aliuliza huku akimuangalia yule mlinzi pale kitandani alivyo gwaya.



“Amenishtua sana, nahisi bado kumbukumbu zake hazijakaa sawa" Daktari aliongea huku akikiminyaminya kifaa kile pasi na kujua kama anafanya hivyo huku akimuangalia mgonjwa huyo.



“Broo, vipi hali yako sasa?" Inspekta alimuuliza yule mlinzi huku akimsogelea pale kitandani.



“Kwani hapa nipo wapi?" Mlinzi aliongea huku akitaka kuinuka, ila Inspekta aliwahi kumzuia.



“Tulia kaka, hapa upo hospitali kwahiyo usiwe na hofu" Inspekta alimjibu na kumtuliza. Ila alimuachia maswali mengi sana mlinzi kichwani mwake. ‘Hospitali? Nimefikaje fikaje? Na nimefuata nini? Kwani nini kimetokea?' alijiuliza mwenyewe maswali hayo. Akatuliza akili yake na kuanza kukumbuka kila kilichotokea muda uliopita.



“Jamani bosi mimi amemuua bosi wangu, mimi nitafanya kazi gani tena ikiwa bosi amekufaaa" Mlinzi alianza kulia kama mtoto mdogo baada ya kukumbuka kilichotokea.



“Embu nyamaza kulia na unieleze imekuaje kuaje hadi kifo kikamkuta yule mama" Inspekta aliongea.



“Kulikuja msichana mmoja pale nyumbani, akidai anataka kuonana na mama, mi nikamruhusu aingie baada ya mama kutoa ruhusa. Sijui walikuwa wanaongea kitu gani, ila baada ya muda yule mwanamke akaondoka. Sasa akaja mtu mwengine, huyu alileta barua akasema nimpe mama. Mi nikaondoka getini na kuingia ndani ili kumpelekea mama ile barua, ila nilipofika nikamkuta mama amekaa kwenye sofa huku akiwa macho ameyatumbua kuagalia mbele tu bila kupepesa. Nikaona nikamtingishe pale alipo lakini mama akanguka chini kabisa baada ya kumtingisha... Haki ya mungu afande mimi sijaua ni yule mwanamke ndio kaua" Mlinzi aliongea kwa uoga, akijua kabisa jela itamuhusu kwa kesi ambayo sio yake.



“Najua kuwa haujamuua wewe.. Embu nielezee muonekano wa huyo mwanamke" Inspekta alimtoa hofu na kumuomba amuelezee muonekano wa huyo muuaji.



“Ni mrefu kidogo mweupe, alivaa sketi fupi nyekundu iliyoishia magotini, na juu alivaa shati jeusi na chini alivaa viatu vya wazi vyeupe, na usoni alivaa miwani nyeusi. Afande huyo ndie aliemuua mama lakini sio mimi afande" Mlinzi bado alikuwa na hofu ya kufungwa jela pamoja na kutolewa wasiwasi na Inspekta. Wakati huo Inspekta alikuwa katika mawazo yaliyomrudisha nyumbani kwa Mr Hanein alipokwenda kufanya uchunguzi asubuhi hiyo, alikutana na mwanamke kama huyo anaelezewa na mlinzi. Kibaya zaidi, hata mavazi aliyoambiwa ndio hayo hayo aliyomuona nayo yule mwanamke asubuhi.



“Acha kwanza kwa sasa upumzike, baadae ama siku nyengine nitarudi tena kuja kunipa ushirikiano wako hadi tumpate huyo muuaji" Inspekta aliongea hivyo huku akijitoa karibu na mlinzi.



“Hata hivyo Afande, huyu anaweza kuruhusiwa leo leo kwasababu alipata mshtuko tu kwa kile alichokiona, ila hana tatizo jengine lolote" Daktari aliongea.



“Hakuna shaka Dokta. Huyu mimi nitamtafuta nikiwa na shida nae, acha kwanza niende kituoni kwasasa"



Inspekta aliondoka hapo na kuelekea kituoni kwake. Alipofika aliingia katika ofisi ya mkuu wake na kumpa taarifa hizo.



“Mkuu yule mwanamke mimi nilikuwa na mashaka nae tangu asubuhi nilipomuona, na nina uhakika yeye ndie aliefanya mauaji ya yule mama hakimu kutokana na maelezo aliyonipa yule mlinzi" Inspekta aliongea.



“Umesema ni mtoto wa Mr Hanein?" IGP Taure alimuuliza.



“Ndio mkuu kwa yale maelezo yake aliyonipa baada ya kumuuliza"



“Umegundua chochote kutokana na hicho kifo cha yule hakimu?"



“Hapana"



“Yule hakimu ndie alie muhukumu Mr Hanein kwenda jela kwa makosa yake. Sasa bilashaka atakuwa amefanya kisasi kwa ile hukumu aliyopewa na yule hakimu. Ndio maana akamtuma mwanae kwenda kumuua. Si jana tu ndio ametoroka jela na leo hii Hakimu alie muhukumu ameuliwa. Sasa unadhani kama sio kisasi ni nini?" IGP aliongea.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mmmh! Itakuwa kweli"



“Sasa basi, fanya haraka, chukua askari wakutosha wenye silaha muende kwenye ile nyumba ya Mr Hanein na yoyote mtakae mkuta mchukueni mje nae hapa"



“Yes Sir" alipiga salut na kutoka ndani humo.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog