Simulizi : TSS 01 Prisoner
Sehemu Ya Pili (2)
Majira ambayo IGP Taure anatoa agizo kwa Inspekta kuwahi haraka kwenye nyumba ya Mr Hanein. Ndio muda ambao Atu anampa taarifa za kifo cha Nasra Mpito baba yake. Majira haya walikuwa wapo kwenye meza kubwa huku juu ya hiyo meza pakijaa mabakuli yaliyokuwa na vyakula ndani yake. Kila mmoja alikuwa anakula kwa nafasi yake.
“Lakini umekumbuka kutoacha ushahidi wowote?" Mr Hanein alimuuliza.
“Wakati namsafirisha kuzimu nilikuwa nimevaa ‘gloves' kwahiyo sikuacha alama yoyote kwenye mwili wake"
“Basi watamtafuta muuaji hadi wachoke" Mr Hanein aliongea hivyo huku akitabasamu.
“Nafanya kazi hii kwa waledi mkubwa baba... Lakiniii...!" Akawa kama kuna kitu amekikumbuka. Akatoka mezani hapo na kuuendea mkoba wake, akapekua pekua na kukosa anachokitafuta.
“Unatafuta nini?" Mr Hanein alimuuliza.
“Picha. Kuna picha yangu niliichukua kule nyumbani lakini nashangaa kwenye mkoba siioni.....Aagh! Nimeiacha kwenye ile droo nilipochukua zile karatasi kule nyumbani" Atu aliongea.
“Sasa tatizo nini? Mbona unawasiwasi hivyo?" Ata alimuuliza.
“Nahofia askari wanaweza kwenda kule kufanya uchunguzi na kuichukua ile picha wakaitumia kunitafuta nayo"
“Sasa watakutafuta kwani wamejua kuwa wewe ndio uliyefanya mauaji ya huyo hakimu?" Ata alimuuliza.
“Braza, mi ndio najua nilichokifanya, ngoja nikaichukue" Atu aliongea hivyo, kisha akatoka nje na kupanda kwenye gari na safari kuenda kwenye ile nyumba ikaanza.
Wakati Atu akiondoka hapo kuelekea kwenye nyumba yao iliyoko Raskazon kwenda kuichukua picha yake ili ukosekane kabisa ushahidi wa kumtafuta yeye. Ndio muda huo askari walitumwa kwenda kumtafuta alieshukiwa kuwa ni muuaji wa hakimu Nasra Mpito ndio wanafika. Walinzi walishaangaa baada ya kuwaona askari hao wamerudi tena kwa mara ya pili, ila walitulia baada ya kuonyeshwa kibali cha kuipigasachi nyumba hiyo.
Safari hii Inspekta aliingia na yeye vyumbani kwenda kusachi. Walizunguka nyumba nzima bila ya kumuona waliemfuata. Inspekta wakati akikipiga sachi chumba cha Mr Hanein. Kwenye droo alikutana na picha moja iliyokuwa imewekwa juu ya hiyo droo. Akaifuata na kuingalia. Akagundua kuwa mwenye taswira kwenye hiyo picha, ndie huyo huyo anaeshukiwa kufanya mauaji ya hakimu. Picha ile ilimuonyesha Atu akiwa katika pozi zuri la kike huku nyuma yake kukiwa na majengo makubwa ya maghorofa.
“Hii picha haikupigwa nchi hii" Inspekta aliongea pekeake huku akiiangalia vizuri picha ile. Akaichukua na kuondoka nayo. Akatoka nje na kukuta askari wengine wakimsubiri yeye. Akawaambia waondoke hapo na hao walinzi wa nyumba hiyo. Walinzi walichukuliwa na kutiwa ndani ya gari la polisi bila kujua kosa lao ni nini.. Muda huo huo wakaona geti likijifungua lenyewe na gari moja aina ya Noah yenye rangi nyeusi likiingi humo ndani. Askari hao wakawa wanaitazama gari hilo waone nani atakae shuka humo.
LILE GARI lienda kupaki mbele kidogo ya geti, akashuka kijana mmoja. Inspekta akamfuata hadi pale aliposimama yule mtu akiwa anashangaashangaa kuona askari wapo ndani ya nyumba hiyo.
“Salama Afande?" alianza kusalimia yule kijana.
“Salama. Nani wewe?" Inspekta alimuuliza.
“Braza Paskal aliniagizia asubuhi nimletee vitu vyake hivi hapa" Yule kijana akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kutoa mifuko miwili mikubwa na kuenda mbele ya yule Inspekta. “Hivi ni vyakula, huwa anakawaida ya kuniagizia nimletee na leo pia nimemletea” Kijana huyo aliongea lakini alikuwa na hofu kidogo ya kuongea na askari ana kwa ana.
“Huyo Paskal yupo wapi?" Inspekta alimuuliza.
“Sijui, ila nahisi atakuwa yupo humu ndani, maana aliniagizia nimletee hapa"
“Sawa. Inabidi tuondoke wote kuelekea kituoni sasa hivi"
“Afande mbona sielewi? Nina kosa gani hadi mtake kunipeleka kituoni?. Mime tumwa tu nilete hii mizigo lakini sihusiki na chochote humu ndani. Kweli tena Afande" Kijana huyo aliongea kwa kulalamika huku jasho la uso likimtoka.
“Sawa huna kosa, lakini twende kituoni" Akawageukia wale askari na kumuita mmoja aje kuendesha gari la huyo kijana huku yeye akipakizwa kwenye gari la polisi. Akawafuata wale walinzi wa nyumba hiyo na kuwauliza.
“Hivi nyie hili geti linajiendeshaje. Maana tumeona likijifungua lenyewe wakati huyu mtu akiingia na hili gari" Inspekta aliwauliza.
“Afande hili geti ni ‘automatic'. Limewekwa ‘sense' kwa magari maalumu yanayojulikana humu ndani" alijibu mlinzi mmoja.
“Kwahiyo kama pakija gari lisilo husika haliwezi kufunguka lenyewe?" Inspekta alimuuliza.
“Ndio afande"
“Je kama akija mtu pia hatoweza kufungua?"
“Tukiachana na magari yaliyowekwa ‘sense' kwenye hili geti. Vitu vyengine vyote lazima ufungue kwa ndani"
“Basi twendeni" Inspekta aliingia kwenye gari la polisi na safari ya kuenda kituoni ikaanza.
Atu alipaki gari lake mbali kidogo na nyumba yao baada ya kushuhudia gari la polisi likiwa nje ya nyumba hiyo. Akajua moja kwa moja kwamba wamemfuata yeye. Alikaa hapo hadi pale alipoona askari hao wakiondoka huku wakiongozana na gari nyengine nyuma yao. Alimuona yule Inspekta aliekutana nae asubuhi akiwa viti vya mbele kwenye gari la polisi. Alishuhudia walinzi wakiwa ndani ya gari la polisi. Akajua wamechukuliwa wakatoe maelezo yoyote. Akacheka na kushuka ndani ya gari lake. Alipanga kuingia ndani ya nyumba hiyo bila gari. Ila alipokumbuka kuwa itakuwa ni ngumu kwake kuingia bila gari. Akapanda tena na kuigeuza gari kuelekea kwenye ile nyumba yao.
“Nikikutana na askari yoyote mle ndani halali yangu"
Aliongea mwenyewe na kulifuata geti la nyumba hiyo. Alipofika karibu tu, geti likajifungua lenyewe na yeye akaingiza gari ndani huku geti likijifunga. Akashuka kwenye gari na kuangazaangaza humo ndani kama kuna askari yoyote alieachwa. Ila akaona pako salama. Akipiga hatu za haraka haraka kuingia ndani ya nyumba hiyo. Moja kwa moja hadi katika chumba cha baba yake na kuiendea droo ambayo juu yake alisahau picha yake. Ila hakuiona. Akatafuta humo ndani, pia hakuiona. Akatoka sebuleni na kuangalia na hapo pia hakuiona.
“Wameichukua!" Alijiongelea mwenyewe. Akatoka ndani humo na kupanda kwenye gari lake safari ya kurudi kule kwenye lile jumba ikaanza.
Zile gari zilifika kituoni na wale walinzi na yule kijana mwengine wakashushwa na kuingizwa kwenye selo. Inspekta alienda kwenye ofisi ta IGP Taure na kuingia. Alipiga salut ya heshima na kumpa taarifa.
“Sawa. Nenda kawahoji mmoja mmoja kisha uniletee taarifa watakazo kuambia"
Inspekta alipiga salut na kutoka humo ndani. Akaenda kumchukua mlinzi mmoja na kwenda nae kwenye chumba cha mahojiano. Akamsihi kumuambia ukweli wote anaoujua yeye na mlinzi huyo akaapa kuongea ukweli.
“Unaitwa nani?" Inspekta alimuuliza.
“Mgawa Seba" alijibu mlinzi huyo.
“Unamiaka mingapi tangia uanze kulinda pale?"
“Mi tatu Afande"
“Unamjua vipi huyu mwanamke kwenye hii piacha?" Inspekta alimtolea ile picha.
“Afande sisi tulitambulishwa tu kuwa ni mtoto wa bosi mkubwa"
“Bosi mkubwa ndio nani?"
“Ni Mr Bakari Hanein"
“Unataarifa zozote za huyo bosi mkubwa?"
“Hapana afande"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ok. Na huyu mwanamke umeanza kumjulia lini?"
“Ni wiki tatu tu zilizopita ndio alikuja pale nyumbani yeye na pacha wake wa kiume"
“Wametokea wapi?"
“Tulivyoambiwa kuwa wametokea Marekani"
“Wameenda wapi wenye ile nyumba?"
“Wote waliondoka asubuhi na sijui wameelekea wapi. Ila bosi Paskali alituambia tulinde nyumba yeye hajui ni muda gani atarudi huko alipoenda"
“Unahakika kwenye haya maelezo uliyoyatoa haujaongea uongo hata moja? Maana naenda kumchukua mwenzako na yeye pia nimuhoji. Sasa ole wako atoe maelezo mengine tofauti na haya ndio utajua kwanini maji hayanywewi na puani"
“Kweli afande sijadanganya chochote hapo"
Akamtoa huyo kumrudisha selo, kisha akamchukua yule mwengine na kuenda nae kumuhoji. Maelezo aliyoyatoa yalifanana na ya yule wa mwanzo labda hapa walitofautiana majina tu. Akamrudisha na huyo kisha akamchukua yule kijana, nae akatoa maelezo yake akidai anaonewa tu kwa kosa ambalo wala halijui. Alipoona hana jipya. Akamrudisha selo na yeye akaenda kwenye ofisi ya IGP Taure. Akamuelezea yote na IGP akamuambia awaruhusu watu hao waende. Akapiga salut na kutoka.
“Sasa wewe hapo utawapeleka hawa wenzako kule na wewe utaendelea na safari zako. Haya nendeni" Watu hao wakaondoka kituoni hapo.
Atu alipofika katika lile jumba. Akaingia na kuwakuta wenzake wamemaliza kula. Akakaa kwenye sofa huku akiwaangalia watu hao waliokuwa wakimuangalia yeye.
“Ile picha wameichukua na wameenda kusachi ile nyumba kama nilivyotabiri. Nina wasiwasi huenda ikawa wameshajua kuwa mimi ndio muuaji wa yule hakimu" Atu aliongea.
“Kwanini umehisi hivyo?" Ata alimuuliza.
“Brother. Kama sio hivyo sasa kule nyumbani wamefuata nini mara ya pili? Tena leo leo tu" Atu alisema.
“Kwahiyo sasa tunafanyaje?" Ata aliuliza.
“Lazima yule mlinzi wa nyumba ya yule hakimu afe na yule askari anaefuatilia hii kesi afe. Hakuna tena namna nyengine zaidi ya hiyo" Atu aliongea.
“Hata hivyo pia ni sawa ili kuupoteza ushahidi" Mr Hanein aliongea. Halafu akaendelea. “Atu ukimaliza kuwaua hao watu wako, utapumzika na wale watu wangu waliobakia watauliwa na Ata"
“Sawa hakuna shaka" Ata aliitikia.
“Lini ama saa ngapi utaenda kufanya hayo mauaji?" Mr Hanein alimuuliza.
“Nataka nipoteze ushahidi kabla mambo hayajawa magumu. Naenda kuwaangamiza leo leo. Naaza na yule mlinzi halafu yule askari nitajua pakumpata" Atu aliongea.
“Kuwa makini" Mr Hanein aliongea.
“Acha kwanza nikalale baadae nipate muda mzuri wa kufanya nilichopanga" Atu aliongea hivyo na kuelekea kwenye chumba chake.
Majira ya saa kumi na moja jioni. Inspekta aliitwa kwenye ofisi ya IGP Taure. Alienda na kumsikiliza mkuu wake ni kipi anataka kumuambia.
“Unajua Inspekta hizi kesi zitatupotezea sifa zetu kwa wakuu. Maana ni jana tu wafungwa wawili wametoroka na kuuwa askari magereza nane na daktari mmoja. Na leo asubuhi pakafanyika mauwaji ya hakimu Nasra Mpito. Sasa hapa ninapokuambia wakubwa huko juu wamechachamaa wanataka maelezo ya kina kuhusiana na haya matukio yaliyofululiza. Kamanda Magambo amenipigia simu sasa hivi akitaka maelezo kuhusu haya matukio. Nashkuru mungu nimemchengachenga akaniambia ananipa siku mbili za kumpa maelezo ya kina akidai na yeye anasumbuliwa na wakubwa zake huku juu" Akamuangalia Inspekta machoni na kumuambia. “Sasa na mimi kama mkubwa wako. Ni lazima nikusumbue uifanye hii kazi kwakina na kesho nataka meelezo mazuri. Hata kama usipompata huyo muuaji. Lakini uwe tayari umeshajua taarifa muhimu kuhusu yeye. Sitaki kuonekana mzembe na wakubwa zangu"
“Sawa mkuu nimekuelewa. Nitajitahidi kwa uwezo wangu hadi huyu muuaji apatikane na wale wafungwa pia wapatikane" Inspekta alijibu kwa ukakamavu.
“Ok. Unaweza kwenda sasa" IGP Taure alimuambia.
“Yes Sir" akapiga salut na kutoka ndani humo.
Kichwa kilimuuma ghafla kwa mawazo na majukumu aliyopewa ayatafutie ufumbuzi kwa muda mfupi. Sawa alikuwa na mashaka na yule mwanamke aliekutana nae nyumbani kwa Mr Hanein akidai ni mtoto wa mzee huyo. Swali Je atampata wapi? Akatoka kituoni hapo na kuingia kwenye gari lake binafsi na kuenda nyumbani kwake kwanza. Alipofika akapitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake akimuacha mke wake sebuleni hamuelewi anatatizo gani lililomsababishia kumpita bila kumsalimia.
Akaamua amfuate mume wake huko huko chumbani alipoingia. Hata pale alipofika hakupata maelezo yoyote zaidi ya kuambiwa amuache kwanza hadi pale atakapo tuliza akili vizuri. Akatoka chumbani humo kwa hali ya unyonge huku akimuacha Inspekta huyo akiwa amejilaza kitandani chali miguu ikimning'inia chini.
“Hizi kesi zitanipelekea kuchanganyikiwa sasa. Muda wenyewe niliopewa ni mdogo. Aagh! Hata sielewi nifanye nini?" alijiongelea mwenyewe huku akiwa macho ameyafumba. Akaingiza mkono mfukoni na kuitoa picha ya Atu aliyoichukuwa kwenye nyumba ya Mr Hanein. Akaiangalia kwa muda. “Itabidi leo nimfuate mlinzi anihakikishie kuwa huyu mwanamke kwenye picha ndie alifanya mauaji ama sie" Alijiwazia mwenyewe na kuona hapo ndipo atakapo pata uhakika zaidi kama aliefanya mauaji ya hakimu ndie huyo ama sie. Akalipitisha wazo hilo na kujikuta akipitiwa na usingizi hapo hapo.
* *
Majira ya saa nne na nusu usiku. Atu alikuwa yupo nje ya nyumba ya hakimu alietoka kufanya mauaji yake siku hiyo asubuhi. Nyumba ilikuwa kimya kiasi kwamba unawezadhani hakuna mtu humo ndani. Ila taa zilizokuwa zikiwaka ndio zilidhihirisha kuwa ndani humo kuna mtu au watu. Atu akaona kugonga geti italeta wasiwasi kwa waliokuwepo ndani humo. Akaangaza macho yake kwenye ukuta wa fensi ya nyumba hiyo. “Yes” alijisemea mwenyewe baada ya kuona ukuta huo ni rahisi kurukika. Akarudi nyuma kuvuta kasi, kisha akaja mbio na kutanguliza mguu mmoja kweye ukuta huo huku mikono yake ikishikilia juu ya ukuta huo. Akaji ‘push’ kwenda juu na akawa yupo juu ya ukuta huo. Akaangalia mandhari ya humo ndani na kukuta yapo salama. Akaruka chini kwa ustadi mzuri kabisa usioleta kishindo chochote.
Akanyata hadi dirishani na kuchungulia ndani. Akamuona mlinzi akiwa amekaa kwenye sofa huku akiwa ana pangapanga nguo kwenye begi. Akarudi hadi kwenye mlango wa kuingilia humo sebuleni na kugonga. Mlinzi kule ndani alishangaa. Inakuaje geti lisigongwe halafu uje kugongwa mlango wa kuingilia ndani humo? Akaona hayo ni maajabu. Mlango ukaendelea kugongwa pasi na mgongaji kutoa sauti ya hodi. Ikambidi aulize kwa sauti ni nani huyo anaegonga? Akajibiwa kuwa ni jirani yake. Alaaa!! Jirani wa vipi huyu usiku usiku? Na je ameingiaje wakati geti nimelifunga? Alijiuliza maswali hayo pasi na kuwa na jibu.
Ikambidi aulize shida ya huyo jirani. Akaambiwa afungue tu mlango atajua. Bila kujua chochote, akauendea mlango na kuufungua. Alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia muuaji wa bosi wake akiwa amemjia na yeye. Akajua zake zimefika sasa. Atu akamsukumizia na ndani kisha na yeye akaingia.
Huku nje ya nyumba hiyo. Inspekta ndio alikuwa anapaki gari lake nje ya uzio wa nyumba hiyo. Shida yake ilikuwa ni kumuuliza mlinzi kuwa huyo mwanamke kwenye ile picha ndio huyo aliefanya mauaji ya mama hakimu au sie. Kuna kitu kilimshangaza wakati anashuka kwenye gari lake. Pembeni ya nyumba hiyo. Palipaki gari. Gari hiyo ni kama vile alikuwa akiifananisha hivi. Ikambidi aisogelee kwa karibu hapo ndipo alipojidhihirishia kuwa hakuwa akiifananisha hiyo gari. Gari hii ndio ile aliyoiyona asubuhi kwenye nyumba ya Mr Hanein akishuka mwanamke ambae kwa sasa anamshukia kuwa ni muuaji wa mama hakimu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaisogelea kwa umakini mkubwa huku bastola yake ikiwa mikononi mwake tayari kwa chochote kitakachotokea.“Ndio ni hii hii” alijisemea mwenyewe baada ya kuiona kwa umakini kabisa. Akaisogelea kwa mwendo wa tahadhari. Akachungulia kwenye vioo na kukuta gari ikiwa tupu. Akajua moja kwa moja muuaji yule amekuja kufanya mauaji ya mlinzi wa nyumba hiyo ili kupoteza ushahidi kabisa. Akarudi hadi pale kwenye ile nyumba. Akawa anawaza ni vipi ataingia. Akawaza kugonga geti, lakini alijua kufanya hivyo ni kumshitua muaji alieko ndani kujiandaa. Akapanga kuruka ukuta. Hilo likapita. Akauruka ukuta huo na sekunde hiyo hiyo akawa ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Sasa akawa ananyata kuuendea mlango huku bastola yake ikiwa ipo tayari kwa lolote.
Vijana hao wawili wenye malengo tofauti waliokuwa nyumbani kwa marehemu Hakimu. Mmoja akiwa na lengo la kumuondoa mlinzi wa nyumba hiyo duniani ili kupoteza ushahidi. Ilhali huyu mwengine akiwa na lengo na kupata uhakika kutoka kwa mlinzi huyo huyo wa nyumba hiyo. Akiwa na picha ya aliemshuku kuwa ndie muuaji wa Mama hakimu. Walipata urahisi wa kuwamo ndani humo kutokana na msiba wa marehemu huyo haukuwa ukifanyika hapo nyumbani kwake. Badala yake ulifanyika huko nyumbani kwao Sahare na nyumba hiyo aliachiwa mlinzi ailinde kwa siku hiyo na siku inayofuata ndipo mipango mengine ipangwe.
Akalisogelea dirisha ambalo mwanzo Atu pia alifika hapo. Akachungulia kwa ndani na kumuona mwanamke yule yule anaemtafuta akimalizia kumuua mlinzi wa nyumba hiyo. Bila kuchelewa aliwahi mlangoni na kuufungua kwa pupa kisha akazama ndani bastola yake mkononi akiwa amemuelekezea Atu.
“Mwanamke tulia hivyo hivyo. Ukithubutu hata kutingishika basi ujue utaukosa uhai wako" Atu alikuwa tayari ameshammaliza mlinzi. Akainua mikono juu na kutulia vile vile.
“Haya geuka nyuma taratibu" Atu akageuka na kukutana na yule askari ambae ameanza kumjulia siku hiyo hiyo asubuhi.
“Umemuua mama hakimu, ukaona haitoshi ili kupoteza ushahidi kabisa, ukaamua uje kumuua na huyu mlinzi. Na bilashaka huenda ikawa wewe ndie uliewatorosha wale wafungwa. Sasa leo siku yako imefika na nitapandishwa cheo nikikupeleka muuaji wewe. Pumbavu! Haya lala chini mikono ikiwa umeiweka nyuma ya mgongo" Atu akafanya kama alivyoambiwa. Hakuwa na wasiwasi hata kidogo. Alijua kuwa huyo askari kuna sehemu tu atajichanganya na ndio hapo sasa atakapo muonyesha kazi. Akawa anaisubiri.
Inspekta alitoa pingu mfukoni mwake. Na kumuendea Atu alielala kifudifudi pale chini. Alienda huku bastola yake ikiwa mkononi. Atu kipindi hicho mikono yake alikuwa ameiweka mbalimbali kiasi kwamba haikuweza kufungwa pingu hadi iwe karibu karibu.
Inspekta alifanya kosa ambalo sidhani kama alipata wasaa wa kulijutia. Kitendo cha kuuvuta mkono mmoja wa Atu kuuleta kwa huu mwengine ili aweze kufunga pingu, kilimgharimu bila yeye kujua kama kingemgharimu. Akiwa anauleta mkono wa kushoto wa Atu kuuendea wakulia ili afunge pingu. Mkono wa kulia wa Atu ulichomoka ghafla hadi kwenye korodani za Inspekta na kupiga ngumi moja hafifu kutokana na vile alivyo lala pale chini lakini yenye maumivu sehemu hiyo.
Inspekta alijikuta akiuachia ule mkono mwengine wa Atu na kujishika sehemu hiyo huku yowe na la maumivu likimtoka. Atu akajivuta kwa mbele na kumpiga teke la uso vile vile akiwa bado yupo chini. Teke hilo lilimfanya Inspekta kuitupa bastola yake mbali huku na yeye akisogezwa nyuma kwa msukumo wa hilo teke. Atu akainuka pale alipolala na kukaa kimapigano. Inspekata nae alikaa sawa na kujipanga kwa ajili ya kupambana na huyo mwanamke ambae kwa sasa alijua kuwa ni hatari.
Inspekta akawa anaiangalia bastola yake iliyokuwa mita chache alipo yeye. Atu alijua kuwa Inspekta anataka kuiwahi bastola ili amdhibiti. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Inspekta alitoka mbio kuiwahi bastola yake lakini mkono wake wa kulia ambao ndio ulikuwa anataka auokotee nao, ulipigwa teke kisha hapo akapigwa teke la kifua. Atu akarudi nyuma kidogo na kumuacha Inspekta akigugumia kwa maumivu.
“Nimegundua kuwa na pambana na mtu ambae sio ‘level' zangu kabisa. Naona kama vile nakuonea tu. Sikupaswa hata kukugusa ngumi yangu. Askari gani umepumbaa namna hii. Yani unazidiwa na raia wa kawaida tena wa kike? Sasa unafaida gani ya kuwa mwanaume" Atu aliongea maneno ya kuudhi ili mradi azidi kumpandisha hasira askari huyo. Na kweli alifanikiwa. Inspekta baada ya kuona amedharauliwa vya kutosha. Akamuendea binti huyo mbio mbio na mapigo ya hasira.
Atu alimkwepa na kumpiga teke la nguvu la mgongo na kumfanya askari huyo kuenda kuuvamia ukuta. Atu pale pale alimfuata na kumpiga ngumi nyingi sana na za haraka za mgongo kisha akamalizia na ngumi moja ya shingo. Akakishika kichwa cha Inspekta ambae kwa wakati huo alikuwa amelegea kwa mapigo hayo na kukipigiza kwenye ukuta mara nne na kupelekea Inspekta aende chini taratibu. Hakuwa na nguvu tena za kuinuka. Akabaki kufinyafinya macho huku damu nyingi za uso zikimtoka.
“Hujakosea kabisa kusema kwamba mimi ndio nimewatorosha wale wafungwa, na mimi ndie nilie muua yule mama, na mimi ndie nilie muua mlinzi wa nyumba hii, na mimi ndie ninae kutorosha na wewe kukupeleka kuzimu sasa hivi. Na unabahati sana, maana nilipanga nikutafute ila umekuja mwenyewe. Sasa nisalimie wote huko unakoenda. Halafu usisahau kuwaekea nafasi wenzako wengine ambao watafuatia baada ya wewe” Atu alimuongelea huku akiwa amemshika kichwa. Baada ya kuongea hivyo. Alipenyeza vidole vyake viwili upende wa pembeni ya shingo. Akabinya kwa ndani kisha akavizunguusha halafu akavivuta kwa nje. Hadi hapo shuhuli ya Inspekta ikwa imeishia hapo.
Atu alimsachi mifukoni mwake, akakuta simu, funguo za gari na ile picha yake. Akatabasamu na kuichukuwa picha yake. Akainuka hapo. Akaziangalia maiti hizo mbili. Ya Inspekta na Mlinzi. Akapiga hatua kuondoka ndani humo. Akaruka ukuta na kupotea mahala hapo na gari lake.
Kazi ikawa imekwisha hivyo.
* * * *
Siku iliyofuata habari zilizoenea kote ni kuhusu vifo mfululizo vilivyotokea kwa siku mbili mfululizo. Raia waliitupia lawama serikali na kudai kuwa haifanyi kazi yake ipasavyo. Amani ilivurugika kwa muda katika mkoa huo wa Tanga. Viongozi wa kiserikali wa mkoa huo walizidi kuchanganyikiwa kwa matukio hayo. Wakawa wanahaha huku na huko kuwashurutisha askari wao kufanya jitihada za kuwatafuta wauaji kabla mambo hayo hayajafika ngazi za juu serikalini.
IGP Taure alichanganyikiwa kwa taarifa hizo za kuuliwa kijana wake na mlinzi ambae alitakiwa kuwa kama shahidi wa kifo cha mama hakimu. Kila mara simu yake ya ofisi iliita, na hao waliokuwa wakimpigia walikuwa ni wakuu wake wakimlaumu na kumuona mzembe kwa matukio hayo kutokea mfululizo. Wakuu hao wakidai kuwa na wao wanalaumiwa na wakubwa zao.
IGP Taure alichanganyikiwa, hakuelewa afanye nini ili kutatua matatizo hayo. Akaona sasa kama si kuvuliwa vyeo basi ni kufukuzwa kazi kabisa kwa kuonekana kama vile hafanyi kazi yoyote. Kwa hakika alichanganyikiwa kupita maelezo. Akainuka kwenye kiti alichokaa, na kutoka humo ofisini kwake. Akapotelea huko nje.
Katika jumba la kule Pongwe, ilikuwa ni shangwe na furaha baada ya kufanikiwa kuwauimiza vichwa jeshi la polisi. Mr Hanein aliona sasa huo ndio muda wa kulipa kisasi kwa kile alichofanyiwa. Akawaita vijana wake wote na kukaa nao sebuleni wapange ni jinsi gani ya kuzidi kuichanganya serikali.
“Sasa Ata nataka hivi vifo viongozane ili wazidi kuchanganyikiwa. Leo nimeangalia taarifa ya habari asubuhi. Eti mkuu wa polisi wa jeshi la Tanga, amesema raia wasiwe na wasiwasi hili jambo litapatiwa ufumbuzi muda si mrefu. Sasa nataka jeshi la polisi lionekane halina maana kwa raia. Nataka leo afe mmoja wapo kati ya mkuu wa gereza au yule askari alienikamata" Mr Hanein aliongea.
“Nitaanza na huyo askari kisha nitafuatia mkuu wa gereza. Cha muhimu ni kunipa taarifa zake, wapi anapatikana au nifanye nini ili kumpata" Ata aliongea.
“Sawa. Kipindi kile wakati ananikamata, alikuwa na cheo cha Koplo. Ila kwasasa bilashaka atakuwa amepanda cheo. Alikuwa akiitwa Koplo Taure. Huyo ndie ambae amenikamata mimi" Mr Hanein aliongea. Mrutu baada ya kusikia jina la Koplo Taure, akamkumbuka. Hapo akaongea kitu kilichofanya Mr Hanein aone hajafanya makosa kutoroka na mtu huyo gerezani.
“Huyo askari mimi napajua alipokuwa akikaa kipindi hicho kabla sijaenda jela. Lakini sasa sijui kama atakuwa amehama au la!" Mrutu aliongea.
“Hakuna shaka nitanzia hapo hapo kumtafuta" Ata aliongea. Mrutu alichukua wasaa huo kumuelekeza Ata mahala alipokuwa akikaa IGP Taure kipindi hicho akiwa na cheo cha Koplo. Japokuwa ilikuwa ni ngumu kwa Ata kupajua kwasababu yeye ni muda mrefu sana aliondoka nchini. Ila kwa uwezo aliokuwa nao haikuwa ngumu sana kupajua, hata hivyo angeulizia iwapo asingepaelewa. Mrutu akamuambia mtaa aliokuwa akiishi na muonekano wa nyumba aliokuwa akikaa. Hakuijua namba ya nyumba hiyo. Aliamini kwa miaka sita aliyokaa jela. Hata kama patakuwa pamebadilika, basi itakuwa sio sana.
“Usijali broo Mrutu. Kwahayo maelezo uliyonipa yatosha kabisa mimi kufika katika hiyo nyumba" Ata aliongea.
“Hiyo kazi nataka ifanyike leo. Nataka kesho vyombo vya habari vitangaze kifo cha yule askari" Mr Hanein aliongea.
“Basi acha mimi nikaifuatilie hiyo nyumba sasa hivi, ili baade niwe na uhakika wa kazi nitakayo ifanya" Ata aliongea huku akisimama.
“Kuwa makini" Mr Hanein alimtahadharisha.
“Usijali baba" Ata akatoka ndani humo na kuenda kuingia kwenye gari na safari ya kuenda mjini ikaanza.
Dakika arobaini mbele, alisimamisha gari lake nje ya nyumba moja yenye rangi ya khaki na geti kubwa jeusi. Nyumba hii ndio nyumba ambayo IGP Taure alikuwa amepanga kipindi hicho kabla hajaamia katika nyumba yake. Ata akashuka na kuangalia huku na huko. Kisha akaaza kulisogelea geti la nyumba hiyo. Akagonga hodi mara tatu kisha akatulia baada ya kusikia hatua za mtu zikisogea kwenye geti hilo kwa ndani.
“Za saa hizi dada?" Ata alisalimia huku akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Salama tu" mwanamke huyo alijibu. Kisha akamuangalia Ata kwa sekunde kadhaa. Akasema. “Sijui nikusaidie nini?"
“Ninashida na mwenye nyumba hii" Ata alijibu.
“We ni nani?" Mwanamke huyo alimuuliza huku akiwa anamchunguza vizuri.
“Niliwahi kusikia kwamba mwenye nyumba hii ana nyumba za kupangisha. Kwahiyo na mimi nilikuwa nataka nyumba ya kupangisha"
“Subiri nakuja" Aliongea mwanamke huyo na kuingia ndani. Baada ya dakika moja alirudi na kumkaribisha Ata ndani. Waliongozana hadi sebuleni na hapo akaonekana mwanamke mtu mzima akiwa amekaa kwenye sofa. Ata akamsalimia na kueleza shida yake.
“Nyumba umepata. Zipo mbili ambazo zimebakia. Kwahiyo ni wewe tu" Mama huyo alijibu.
“Sawa mama nimekuelewa. Aaaa nimekuja kupata uhakika kama nyumba nitapata, ila kesho nitakuja kuziona mama yangu" Ata aliongea.
“Sawa, hakuna shaka, wewe ukiwa tayari njoo tu mimi ndio mwenye nyumba hizi, hata hii unayoiona pia niyakwangu. Ila kuna kipindi flani pia niliipangisha kwa askari mmoja" Mama huyo aliongea kitu ambacho Ata alitaka amuulize kwa mitego ila aliongea na kufanya kazi ya Ata iwe rahisi sana.
“Dah! Mama nimekumbuka kitu. Unajua huyo askari mimi ni baba yangu mdogo. Kaka yake alipokufa ambae ni baba yangu mimi mzazi. Mimi nikachukuliwa na mjomba angu. Ilikuwa zamani sana. Asa ndio nimerudi ila naikumbuka sana hii nyumba kwamba ndio ambayo alikuwa akiishi baba yangu mdogo. Sasa naomba unisaidie kupajua kwake ili niweze kuenda. Dah! Akiniona atafurahi sana maana alikuwa akinipenda kweli" Ata aliongea huku usoni mwake pakiwa na tabasamu kubwa.
“Yule askari alikuwa ampole sana. Ni miaka minne tu iliyopita ndio alihama hapa. Ila sasa alipohamia mimi sipajui. Ila kuna kijana mmoja hapa mtaani yeye na wenzake ndio walimuhamisha na huko kwake. Labda nikuitie yeye ndie atakupeleka anapoishi" Ata kusikia hivyo alifurahi kwa nje na ndani maana alijua kazi ya kumpata huyo askari imetimia. Mama huyo akamtuma yule mwanamke alienda kumfungulia geti Ata akamuite huyo mtu. Mwanamke huyo akatoka akiwaacha Ata na huyo Mama wakiongea. Aliporudi alikuwa ameongozana na kijana mmoja mwenye miaka kati ya kumi na nane hadi ishirini.
Mama huyo akamueleza kijana shida ya Ata na kijana akajibu anapajua na yupo tayari kumpeleka. Ata akashukuru na kumuaga mama huyo na kutoka na kijana. Wakaingia kwenye gari la Ata na safari ya kwenda nyumbani kwa IGP Taure ikaanza. Iliwachukua dakika ishirini kufika nje ya nyumba hiyo. Kijana akamuambia kuwa hapo ndio nyumbani kwa huyo askari anaemtafuta. Ata akaiangalia vizuri hiyo nyumba. Akamshukuru yule kijana kisha akampa elfu kumi na tano. Akamuambia elefu tano achukue boda boda halafu inayobakia iwe kama ya usumbufu. Kijana akafurahi na kushuka ndani ya gari na kutokomea zake.
Ata akaiangalia vizuri hiyo nyumba kwa kuichunguza. Kisha akawasha gari na kuondoka hapo.
* *
Katika chumba kimoja palikuwa na watu sita walionekana kuwa na wadhfa flani serikalini. Walikuwa katika chumba hicho wakijadili hali inayoendelea kutishia amani kwa raia kwa siku hizo mbili mfululizo. Walikuwa wakijadili ni jinsi gani wataieupuka hiyo aibu inayoenda kuikumba au tayari imeshaikumba jeshi la polisi. Walijadili pasi na kupata muafaka unaotakiwa. Mwisho kabisa wakamuachia maagizo IGP Taure. Maagizo hayo yalimfanya afisa huyo kichwa kumuuma huku mke wake ambae pia ni askari polisi akimuonea huruma. Kikao kikafungwa na kila mmoja akaondoka hapo.
IGP Taure alirudi ofisini kwake akiwa na mawazo mengi kupita kawaida. Akajikuta akililaza kichwa chake juu ya meza iliyokuwa mbele yake baada ya kukaa kwenye kiti. Hapo akawa anawaza hili na lile. Akawaza ni jinsi gani atayatimiza hayo maagizo aliyoachiwa. Aliendelea kuwa katika hali hiyo hadi pale alipopitiwa na usingizi kabisa hapo hapo.
Majira ya saa tatu usiku ndio muda ambao alishtuka katika lindi la usingizi lilichanganyikana na mawazo. Akajishangaa kuwa hapo hadi muda huo. Akainuka haraka na kuanza kutoka hapo kuelekea nje. Muda ambao IGP Taure anashtuka kutoka usingizini. Ndio muda ambao Ata alikuwa yupo nje ya nyumba ya IGP Taure akiwaza ni jinsi gani ataingia humo ndani kwenda kufanya mauaji.
Ata aliuangalia ukuta huo ulivyo. Akauona ugumu wa kuruka hapo. Ukuta ulikuwa ni mrefu usio wezekana kupandika kirahisi. Akaona hakuna namna zaidi ya kuingilia na getini. Akaliendea geti. Alipofika hapo. Akaliangalia na kisha akainua mkono wake ili agonge, ila akaghairisha. Akaona kufanya hivyo ni kuwatia wasiwasi waliomo ndani. Akaanza kuuzunguka ukuta huo. Bahati ikawa kwake baada ya kuona mti wa mpera mkubwa uliokuwa nyuma ya ukuta huo.
Giza pia lilimficha. Akaundandia mti huo na kupanda hadi juu. Hapo akaambaa na tawi lililokuwa limeelekea karibu na ukuta huo. Mwisho akaachana na tawi na kuhamia juu ya ukuta. Akaangalia mandhari ya ndani akaona kumepoa sana. Taa za humo ndani zilipambana na giza. Akatua chini kwa ustadi mzuri kiasi kwamba hakutoa kishindo kikubwa. Akaanza kunyata na ukuta wa nyumba sio ukuta wa fensi tena. Hapo akaona kivuli katika chumba kimoja wapo cha mtu kama ambae anaebadilisha nguo hivi. Akapita mbio kuelekea na mlango wa nyuma wa nyumba hiyo.
Kule chumbani. Alikuwa ni mke wa IGP. ASP Jesca ndie aliekuwa akibadilisha nguo akivaa nguo za kulalia baada ya kutoka kuoga. Kivuli cha mtu akipita mbio alikiona. Akajua kuna hatari maana sio kawaida. Akaiendea droo yake na kuivuta kwa mbele. Akachukua bastola na kumsubiri huyo mvamizi aje waonane.
Ata alifanikiwa kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma, sasa akawa ananyata kukiendea kile chumba ambacho kwa nje aliona kivuli cha mtu. Akiwa katika harakati za kukitafuta hicho chumba. Alishutukia akiwekwa chini ya ulinzi na kushurutishwa kutulia hivyo hivyo pasi na kuleta fujo.
“We ni nani unaeingia katika nyumba za watu kwa kuvamia?" Sauti ya kike iliyozoea kuwashurutisha na kuwahoji maswali wahalifu ili muuliza.
“Samahani mama sikuja kuiondoa roho yako. Naomba uniache nifanye kile ninachokitaka halafu niondoke kwasababu sipendi kutoa uhai wa mtu ikiwa siku zake bado hazijafika" Ata aliongea hivyo huku akiwa hana wasiwasi hata kidogo. Sio kwamba hakujua kuwa amewekwa chini ya ulinzi na mtu alieshika bastola kumuelekezea yeye? La hasha! Alijua vizuri ila sijui ni kipi kilichomfanya kujiamini namna ile.
“We unasemaje!?" ASP Jesca aling'aka kwa mshangao.
“Ndio hivyo mama. Cha muhimu ni kuniambia mume wako yupo wapi ili niitoe roho yake kisha niondoke. Kama na wewe unataka kufa subiri nitakutafutia siku yako ila usinilazimishe nikuue sasa" Ata aliongea maneno hayo yaliyomfanya mama huyo azidi kuchanganyikiwa. Maana hakujua ni kiasi gani mtu huyo amejiamini kiasi kwamba anaongea bila kuwa na hofo yoyote.
“Wewe ni nani?" ASP Jesca alimuuliza.
“Mimi ni msaidizi halali wa malaika mtoa roho za watu na nimekuja hapa kwaajili ya kuitoa roho ya IGP Taure. Nadhani itakuwa vizuri ukinipa msaada wa kujua wapi alipo mtu huyo. Au kama vipi acha nimtafute mwenyewe" Ata aliongea hivyo kisha akaanza kupiga hatua kwenda mbele bila kujali kama anaweza kudhuriwa na hiyo bastola alioelekezewa. ASP Jesca alimkemea kwa sauti asimame. Ata akasima kisha akamuangalia, ikawa ni uso kwa uso sasa.
Ata akaanza kupiga hatua kumfuata mama huyo huku akiwa na tabasamu usoni mwake. ASP Jesca akaiondoka usalama bastola yake akiwa anataka kuminya ‘trigger' ili amfyatulie risasi mvamizi huyo. Kwa wepesi usio wa kawaida. Ata aliupiga teke la nguvu mkono wa ASP Jesca na bastola ikarushwa mbali nae. Akampiga ngumi mbili za uso mama huyo na kumfanya arudi nyuma huku akiwa mikono yake ipo kwenye uso.
“Nilikuambia mama ila sio mbaya ngoja nikutangulize wewe kuzimu ili ukamuwekee makazi mume wako ambae atakufuata muda si mrefu huko utakapofikia” Ata aliongea hivyo na kumfuata ASP Jesca aliekuwa sasa amesimama akijiandaa kukabiliana na mvamizi.
ASP Jesca alimuendea na mapigo ya haraka lakini yote Ata aliyaona kisha akamzawadia ngumi mbili za mbavu. Ngumi hizo zilimfanya ASP Jesca kuuegemea ukuta huku akigugumia kwa maumivu. Akajiweka tena sawa kwaajili ya mpambano. Sasa akaja na mapigo ya kurusha mateke ya haraka haraka. Nguo ya kulalia ilimuwezesha kufanya hivyo. Ilikuwa ni nguo nyepesi yenye mtindo wa suruali. Mateke hayo yote yalikosa lengo baada ya kuhepwa na Ata kwa ustadi mzuri.
“Naona najidhalilisha tu kupigana na kiumbe ambacho hakijafikia uwezo wangu hata robo ya robo. Subiri nikuteketeze mara moja"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ata alipoongea hivyo, alimfuata mama huyo kwa pigo moja la kareti lililompeleka hadi chini. Hapo akamfuata tena na kumshushia ngumi tatu za kifua zilizomfanya ASP Jesca kucheua damu. Akammalizia na ngumi moja ya shingo iliyoukatisha kabisa uhai wa askari huyo. Akasonya kwa nguvu na kuondoka hapo. Akaanza kupitia chumba kimoja baada ya kingine lakini kote hakuona mtu. Wakati akiwa anatokeza sebuleni akaangalie na huko. Alishtukia ngumi moja tu ya uso iliyomfanya kurudi nyuma huku akiuziba uso wake na viganja vyake vya mikono.
Alikuwa ni IGP Taure ndie aliemzawadia ngumi hiyo. Ata akajiweka sawa kwajili ya mpambano na askari huyo huku IGP Taure akiwa tayari kwa mpambano. Ata alimuendea mbio mbio kwa mapigo ya karate ila yote IGP aliyaona na kumkwepa. Wakati Ata akiwa hewani baada ya kukwepwa mapigo yake. Alimzawadia teke la mgongo IGP lililompeleka kuukumbatia ukuta huku Ata akitua chini. Wote wakajiweka sawa.
IGP Taure akamuendea Ata huku akirusha ngumi nyingi. Ata alizikwepa zote na kumpiga makonde mawili ya kifua ulipo moyo IGP yaliyomfanya ajishike sehemu hiyo huku akikohoa sana. Hakuweza tena kuendelea kupambana. Akajikuta akikaa chini huku akimuangalia Ata. Ata alimfuata pale alipokaa chini akiwa hajiwezi tena kwa pigo hilo alilopatiwa. Alimuinamia na kumshika kidevu.
“IGP Taure sijui unajua kwanini muda si mrefu unaenda kufa? Ila acha ni kujulishe. Ni hivi. Unakufa kwasababu ulimkamata Mr Hanein na kumsababishia kifungo cha maisha jela. Ila sasa yeye yupo uraiani huku wewe ukienda kukitumikia kifo chako cha maisha ukiwa kuzimu. Wape salamu wote waambie sio wote wanaokufa kwa ahadi zao bali wengine wanakufa kwa ujinga wao" Ata alipomaliza kumuambia hivyo. Alimpiga ngumi ya shingo iliomfanya IGP kutoa mguno hafifu kisha akailaza shingo yake kwenye bega lake la kushoto.
Ata alitoka mbio hapo baada ya kusikia hatua za mtu akija humo ndani mbio kutokea nje. Akatoka kuufuata mlango wa nyuma aliyoingilia nao na kupotelea huko kwa kuruka ukuta.
Kule sebuleni mlinzi aliingia mbio na kumkuta IGP Taure akiwa amekaa chini huku shingo yake ameilaza begani kwake. Akamfuata hadi pale na kumtingisha lakini aliona mtu huyo akilegea kila akimtingisha. Akaangalia mapigo yake ya moyo na kukuta yapo chini sana. Akatoka mbio kuifuata korido ya kuingia vyumbani kwania ya kumuita ASP Jesca lakini aliukuta mwili wake ukiwa upo katikati ya korido ukiwa umelala. Akazidi kuchanganyikiwa. Nao akausikiliza mapigo ya moyo na kukuta yamesimama kuashiria amekufa. Akatoa simu huku akiwa bado na kitete na kupiga mahala, akaongea kidogo huku akiwa anatetemeka kisha akakata simu na kurudi sebuleni.
* *
Siku iliyofuata habari kubwa iliyozagaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni kuhusu kifo cha ASP Jesca huku ikitangazwa hali mbaya aliyokuwa nayo IGP Taure. Viongozi wa jeshi la polisi walizidi kuchanganyikiwa baada ya vifo hivyo mfululizo kutokea. Wakakaa kikao tena kujadili hilo swala na kumteua askari mmoja kwaajili ya kulifuatilia hilo swala.
“Ninawasiwasi hii itakuwa inasababishwa na Mr Hanein. Haiwezekana vifo hivi vitokee tangu atoroke yeye. Tena kwa kufuatana" alisema afisa mmoja kwenye kikao hicho na wenzake wakamuunga mkono japokuwa hawakuwa na uhakika na wazo hilo.
Hapo akaongezwa askari mwengine kwaajili ya kusaidiana na yule mwengine kwaajili ya kulifumbua tatizo hilo. Kikao kikafungwa huku kila askari akiondoka akiwa amenyongea kwa kuona sasa jeshi la polisi linaingizwa katika aibu kubwa sana.
Kule kwenye lile jumba la maficho yao. Kulikuwa kuna kikao kimewekwa baada ya kupata taarifa kuwa mtu waliemkusudia sie aliekufa. Mr Hanein alikuwa akimlaumu Ata kwa kufanya mauaji kwa mtu ambae hakuwa sahihi huku akimuambia kuwa hamlaumu kwavile amefanya mauaji ya ASP Jesca bali alikuwa akimlaumu kwa kutofanya mauaji ya IGP Taure.
“Lakini baba mimi nilihakikisha na yeye pia amekufa" Ata aliongea kwa malalamiko.
“Sasa kama umehakikisha amekufa mbona taarifa zina sema kuwa yupo hospitali hali yake ikiwa ni mbaya?" Mr Hanein alimuliza.
“Lakini pia sio mbaya hata kwa kifo cha huyo mke wake pia nimekifurahia kwasababu kimezidi kuwachanganya polisi na watajuta. Sasa kabla ya yote, nataka na yule mkuu wa gereza nae afe leo leo ili wazidi kuchanganyikiwa. Nitakupa maelekezo ya wapi pakumpata ili uifanye hiyo kazi" Mr Hanein aliongea. Akamgeukia Paskali na kumuambia.
“Paskal utaongozana na Ata kwasababu yeye mitaa ya huu mji haijui. Nitakuelekeza mtaa uliokuwa na nyumba ya mkuu wa gereza kisha utaenda na Ata hadi huko. Yeye atafanya kazi yake kisha mtarudi nyote" Mr Hanein aliongea.
“Sawa" aliitikia na Mr Hanein alianza kumuelekeza mtaa aliokuwa akiishi huyo wanaemtaka, baada ya maelekezo Paskal akakiri kupafahamu na muda huo huo wakaondoka kwenda kufanya mauaji ya mkuu wa gereza.
Iliwachukua dakika hamsini kufika nje ya nyumba ya mkuu wa gereza. Paskal alipaki gari mbali kidogo na nyumba hiyo akimuacha Ata akishuka na kuifuata nyumba hiyo. Alipofika getini, akagonga geti na kufunguliwa na mtu aliekuwa na sare za kiaskari. Hata kabla hajauliza shida aliyokuwa nayo huyo mgeni. Akashtukia akipigwa teke la kifua lililompeleka chini ndani ya geti hilo. Ata aliingia ndani haraka na kufunga geti kisha akamuwahi yule askari hata kabla hajainuka pale chini. Akaupindisha mshipa mmoja wa shingo na kumfanya askari huyo kupoteza fahamu hapo hapo.
Akauendea mlango wa kuingilia ndani huku akiwa na umakini mkubwa. Alipofika mlangoni wakati akiwa anataka kuufungua mlango. Ghafla aliona mlango ukifunguliwa kwa ndani. Akajibanza pembeni ya mlango hapo akatokeza mama wa makamo. Akamvuta haraka na kumkaba shingo. Kisha akamfanya kama alivyomfanya askari aliekuwa getini. Mama huyo nae akalegea. Ata akamuachia akenda chini taratibu. Akamuegemeza kwenye ukuta huku akiwa hana fahamu.
Akauendea mlango na kuzama ndani kwa kasi. Hapo akamkuta Kamishna ambae ndie aliekuwa mkuu wa gereza akiwa amekaa kwenye sofa akiangalia luninga iliyokuwa mbele yake. Kamishna alishtuka na kunyanyuka kwa haraka baada ya kumuona mtu huyo alieingia kwa ghafla hapo sebuleni. Kamishna kabla hajakaa sawa alishtukia akipigwa teke la tumbo lililompelekea kukaa kwenye sofa bila kupenda. Akataka kuinuka tena lakini alijikuta akipokea ngumi nyingi za kifua na tatu za uso zilizomuacha na wenge kubwa.
Hapo Ata hakutaka kuchelewa. Akampiga ngumi ya kidevu aliyoipiga kwa chini na kumfanya Kamishna agugumie huku shingo yake akiinua juu. Hapo Ata alimpiga konzi la nguvu kwenye koo. Hakika pigo hilo lilitosha kuuondoka uhai wa Kamishna. Alibaki akitoa macho huku mikono yake akiinua kutaka kulishika shingo lake kwa maumivu hayo. Lakini mikono ilishindwa na kujikuta akiiachia chini huku uhai ukimtoka.
Kazi ikawa rahisi kabisa!.
Ata aliondoka hapo akiacha kifo cha Kamishna huku akiwazimisha mke wa Kamishana na askari aliekuwa getini. Alitoka na kulifuata gari alilokuja nalo na kuingia humo. Akavua ‘gloves' alizovaa mikononi na kuzitupia siti za nyuma.
“Tayari?" Paskal alimuuliza huku akiwa haamini kama tayari ameshatekeleza kifo cha Kamishna kwa muda mfupi hivyo. Ata alimjibu kwa kichwa kisha akaangalia nje ya gari hilo. Paskal alimuangalia kwa mshangao na kutoamini uwezo wa mtu huyo. Akawasha gari na kuondoka hapo.
* *
Taarifa za kifo cha Kamishna wa gereza ziliwachanganya zaidi wakuu wa polisi na kujikuta wakitoa machozi ya uchungu kwa vifo hivyo mfululizo. RPC Shehiza aliwaita tena kikao wakuu wenzake kwaajili ya kuwapa taarifa aliyoipokea hivi punde baada ya kutangazwa kifo cha Kamishna. Askari hao wa vyeo vya juu walienda tena katika chumba wanachofanyia mikutano yao na kumkuta RPC Shehiza akiwa anawasubiri huku akiwa ana mfadhaiko usoni mwake. Ni siku hiyo hiyo asubuhi walitoka katika chumba hicho hicho wakijadili kifo cha ASP Jesca na hali mbaya ya IGP Taure na majira hayo walikutana tena kupokea taarifa zilizomfikia RPC Shehiza. Kila mmoja akachukua nafasi yake na kukaa kimya huku kwenye nyuso zao pakiwa na huzuni kubwa sana.
“Tumekutana tena kwa mara ya pili kwa siku ya leo tukijadili vifo vya maaskari vinavyotokea mfululizo" RPC Shehiza akawaangalia askari hao na kuwakuta wakiwa na nyuso za huzuni huku wote wakimuangali yeye. Akaendelea
“Lakini sasa tumekutana tena kwaajili ya kuwapa taarifa iliyotoka ngazi za juu kabisa serikalini. Na taarifa yenyewe ni kuwa tuachane kabisa kufuatilia chanzo cha vifo hivi na tusithubutu kuwatuma askari wetu kufuatilia haya mambo" RPC Shehiza aliongea hivyo na kuwafanya askari wote waliokuwa humo ndani kumuangalia kwa mshangao mkubwa sana huku wakiwa hawaamini taarifa hiyo. Wakabaki wakimtumbulia macho huku mioyo yao ikienda mbio kwa hofu.
Eeee lazima wawe na hofu na hata zaidi ya hofu pia.
“Lakini hii inawezekana vipi?" Afisa mmoja aliuliza kwa hamaniko.
“Ninavyo waambia sasa hivi, hii taarifa imetoka ngazi za juu kwamba tuachane na hizi kesi za mauaji tusifuatilie tena. Kumedaiwa kwamba sisi hatuna kazi yoyote zaidi ya kukaa tu na kushuhudia vifo vya maaskari wenzetu huku wafungwa wakitoroka gerezani. Jamani hii si aibu hii? Mimi nilijua tu kwamba tutaonekana hatufanyi kazi yoyote na ndio hivi sasa ilivyo kuwa" RPC Shehiza aliongea.
“Kwahiyo sasa hizi kesi nani atakae zifuatilia kama sisi tumeambiwa tuziache?" Afisa yule yule wa mwanzo aliulia tena.
“Kwa hapo sijajua ila agizo nililopewa ni hilo"
Wakaendelea kujadili huko kuachishwa kufuatilia vifo vya maaskari wenzao. Wakabaki hawaelewi nini wafanye. Wakakuna vichwa. Walikuwa na hofu si mchezo kwakuona pia wanaweza kuachishwa kazi ikiwa wameshindwa kupata ufumbuzi juu kumpata muuaji au wauaji wa maafisa wa jeshi la polisi. Kikao kikafungwa na Kila mmoja akainuka hapo na kutoka huku hofu bado wakiwa nazo. Walihofia kuitwa tena kikao chengine cha kuachishwa kazi.
* * * *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jijini Daresalam Ikulu katika chumba walichozoea kukutana Raisi na Mr Kaoneka. Ndani humo watu hao walikuwepo wakionekana wakijadili swala ambalo walilianzia muda si mrefu kulijadili.
“Ilinibidi kuwazuia kufuatilia zile kesi maana naona kila siku wanazidi kuuliwa tu halafu hao wengine wamekaa kwenye maofisi yao" Raisi Alex Kileo aliongea.
“Kwahiyo unataka TSSI iingie kazini kwa mara ya kwanza kwenda kufuatilia hivyo vifo?" Mr Kaonekana alimuuliza.
“Ndiyo. Hata hivyo pia tunawajaribu na hiyo kazi yao ya kwanza ili hata baadae pakitokea kazi kubwa ya kuifuatilia tutakuwa tumejua uwezo wao. Hivi vifo vinaweza vikafuatiliwa na mpelelezi wa kawaida na pia akajua chanzo chake. Ila mimi nataka nijue uwezo wa kitengo chako ndio maana nikazuia hilo ili wafanye wao"
“Nimekuelewa, hata mimi nakuunga mkono kwa hilo Kiongozi"
“Basi ongea na vijana wako waifanye hii kazi haraka sana kabla raia hawaja kuwa na hofu zaidi kwa haya matukio"
Baada ya maongezi hayo mafupi. Mr Kaoneka aliondoka Ikulu na kwenda katika ofisi za TSSI kuwapa jukumu hilo vijana wake. Alipofika, aliwaita ofisini kwake na wao wakaenda kumsikiliza mkuu wao.
“Nadhani nyote mmesikia hayo machafuko yalioko huko jijini Tanga ya kuuliwa kwa askari kila siku. Sasa Raisi ametoa agizo la kitengo hiki kutafuta ufumbuzi chanzo cha matukio hayo na nani muuaji au wauaji. Na mimi kama mkuu wenu sina budi kuwaachia nyie vijana wangu kuifanya hiyo kazi. Naamini kwa uweledi wenu mliokuwa nao hii kazi wala haitochukua zaidi ya wiki mbili itakuwa ameshapatikana muuaji au wauaji" Mr Kaoneka aliongea hivyo kisha akawaangalia vijana wake na kuona kila mmoja akiwa katika usikivu mkubwa wa kumsikiliza. Akaendelea.
“TSSI 01 Hemedy Bhachu utaenda huko kuafuatilia chanzo cha vifo vya maaskari. Kama kutahitajika msaada TSSI 03 Hilda Ganjo atakufuata, na hawa wengine watakuwa nyuma yako kwa namna yoyote kuhakikisha kazi inakuwa rahisi kwako. Nadhani hadi hapo tumeelewana" Mr Kaoneka alitoa maelekezo. Hilda akataka kuongea kitu ila akasita. Akabaki kumuangalia TSSI 01 ambae yeye macho yake yalikuwa kwa Mr Kaonekana.
“Ndio mkuu tumekuelewa. Na ni lini naenda huko?" TSSI 01 Hemedy Bhachu alimuuliza.
“Sio lazima mniite mkuu, niiteni Father tu hiyo itapendeza kuficha wajihi wangu mbele za watu. Na kuhusu kuenda huko, utaenda kesho asubuhi na usafiri wa basi" Mr Kaoneka alimuambia. Kisha akaongeza.
“Na kuhusu vifaa vya kazi, utaenda hapo nje kwa Stela atakukabidhi. Nadhani hadi hapa kila kitu kitaenda sawa. TSSI 01 usikubali kukitia aibu kitengo chako kwa hii kazi nyepesi kabisa ambayo hata mimi kama naamua basi haichukui hata wiki hao wauaji washapatikana. Nategemea ufanisi mkubwa katika hii kazi"
“Usijali father hii ni kazi ya kawaida sana na wala sitegemei kuishindwa" TSSI 01 alijibu na kupelekea mkuu wake kutabasamu.
“Ok. Tumemaliza hapa. Kila mmoja aende akapumzike na kesho nyie wanne nitawahitaji hapa huku huyu mwenzenu akienda huko.... Nendeni" Waliinuka na kutoka katika chumba hicho. Hemedy alienda katika ofisi ya yule mwanadada Stela kwenda kukabidhiwa vifaa vya kazi.
“Naona mlikuwa na maongezi na babu yenu huko ndani" Stela aliongea huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake baada ya Hemedy kufika hapo.
“Si unajua mzee yule kesha zeeka kwahiyo majukumu yote anatuachia sisi wajukuu zake..... Halafu nimefuata mzigo wangu nataka kusafiri"
“Oooh! Nalijua hilo japo sijajua wapi unaenda" Stela aliongea huku akiinama chini. Alipoinuka alikuwa ameshika kibegi kidogo. Akampa kupitia uwazi ulioachwa kwenye kioo kilichowatenganisha. TSSI 01 akakipokea na kukifungua. Akachungulia kidogo na kukifunga vile vile.
“Ni safari ya ghafla ambayo imetokea" alijibu huku akiondoka hapo na kibegi chake mkononi akimuacha Stela akimtolea macho tu huku tabasamu likiwa usoni mwake.
TSSI 01 alitoka nje ya hoteli hiyo ambayo ndipo zilipo ofisi za TSSI, akaliendea gari moja lililokuwa limepaki kwenye maegesho ya magari kwenye hoteli hiyo. Akaingia ndani yake na kumkuta TSSI 03 akimsubiria.
“Huko Tanga unaenda pekeako?" Hilda alimuuliza huku akiliondoa gari hilo kwenye maegesho kufuata uelekeo wa getini.
“Ni mkuu ndie ametaka" Hemedy alijibu na kupelekea kimya kitawale humo ndani. Wakaondoka hapo kuelekea wanapopajua wao.
* * * *
Siku iliyofuata jijini Tanga majira ya saa sita mchana. Mzee Ganjo mstaafu wa jeshi la polisi alikuwa yupo stendi ya mabasi Kange akiwa amekaa kwenye mabenchi yaliyokuwepo eneo hilo. Kila mara alikuwa akiangalia saa yake iliyokuwa mkononi mwake wa kushoto huku akichezesha funguo za gari kwa kidole chake cha shahada cha mkono wa kulia.
Basi moja la abiria la kampuni ya Tashrifu liliingia stendi hapo. Mzee Ganjo aliinuka akilifuata hadi pale liliposimama. Abiria mmoja mmoja alianza kushuka kwenye basi hilo. Mzee Ganjo aliachia tabasamu baada ya kumuona Hemedy akishuka kwenye gari hilo. Akampokea mizigo michache aliyoibeba na kumuongoza hadi alipopaki gari lake wakaingia humo. Hapo wakaulizana habari za siku nyingi ambazo hawakuonana kipindi chote.
“Hilda yeye hatokuja?" Mzee Ganjo alimuuliza huku akiwa na umakini kwenye usukani.
“Hapana, yeye ni kama msaidizi wangu kwahiyo kama nitahitaji msaada basi atakuja yeye"
“Sawa..." Akatulia kidogo na kuendelea. “Biashara zako zinaendelea vizuri na sasa unamafanikio makubwa sana, una hela nyingi mwanangu maana hela zote nilikuwa nikiziweka benki"
“Inamaana wewe hukuwa ukitumia?" Hemedy alimuuliza kwa mshangao.
“Nitatumiaje wakati sio mali zangu"
“Aagh! Baba mbona hivyo? Kwani kunanini kama ingekuwa ukitumia? Haya mimi kijana hela zote hizo nyingi nitazipeleka wapi?.. Kwahiyo unataka kuniambia miaka yote sita ulikuwa ukiziweka tu benki?"
“Tukiachana na hizo biashara zako, hata mimi ninazangu, sasa nani atakaetumia hela zangu ikiwa mimi natumia hela zako?"
Hemedy akatulia kimya huku akiwa anaangalia tu nje ya gari hilo. Kwa swali hilo hakuwa tena na cha kuongea. Akabaki kimya tu. Safari ikaishia katika nyumba yake iliyokuwa maeneo ya Donge. Nyumba ambayo alikuwa akiishi na wazazi wake. Mzee Ganjo alimuacha hapo huku akimuambia kuwa atakuja kijana muda si mrefu kumletea gari kwaajili ya kazi iliyomleta huko. Akashukuru na kuingia ndani ya nyumba hiyo.
Nyumba ilikuwa imepoa vibaya sana japokuwa haikuwa chafu kutokana na Mzee Ganjo alikuwa akimpa kazi mtu kuifanyia usafi miaka yote hiyo. TSSI 01 aliangalia mandhari ya nyumba hiyo baada ya kuiacha kwa miaka sita sasa. Akatembea taratibu huku akiangalia huku na huko. Mambo mengi aliyakumbuka. Alimkumbuka mfanyakazi wao ambae yeye alimchukulia kama kaka yake. Aliwakumbuka wazazi wake waliouliwa kwa wivu wa mali tu. (ambao wamesoma kisa kilichopewa jina UHASMA wanalijua hilo).
Chozi la huzuni likamtoka, akalifuta na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Huko aliikuta sebule ikiwa iko vile vile kama alivyoiacha miaka sita iliyopita. Akaangaza macho na hapo. Kisha akapandisha ngazi na kuenda katika flow ya pili ya nyumba hiyo. Akaingia katika chumba ambacho zamani wazazi wake ndio walikuwa wakilala, akaweka mizigo yake humo. Ikasikika kengele ya getini ikilia. Akainuka na kutoka nje, huko akakuta kuna kijana amekuja na gari. Akaambiwa kuwa hiyo gari ndio hiyo aliyotumwa amletee. Akafungua geti na gari hilo likaingizwa ndani. Kijana akaondoka na Hemedy akaingia ndani baada ya kufunga geti.
* *
Kule kwenye jumba la maficho ya kundi la Mr Hanein. Walikuwa na kikao wakijadili ni jinsi gani wataendeleza mipango yao baada ya kufanikisha kuwaua watu alioweka kisasi nao.
“Lakini mimi bado sijaridhika nataka na huyu IGP pia afe maana yeye ndie alienikamata mimi si mke wake" Mr Hanein aliongea.
“Kwahiyo ulitaka na yeye pia afe?" Ata alimuuliza.
“Ndio, akifa na yeye nafsi yangu itaridhika"
“Basi nitaenda kumuulia kule kule hospitali" Ata aliongea.
“Hapana hutoenda wewe tena, acha sasa hivi aende Atu" Mr Hanein alipinga na kumfanya Ata aone kama amedharauliwa kutumwa dada yake kwenda kumuua IGP.
“Kwanini nisiende mimi baba na aende Atu?" Ata aliuliza kwa ghadhabu kidogo.
“Inabidi aende Atu kwasababu ukienda wewe atakugundua mapema ukimkuta yupo macho tofauti na Atu" Mr Hanein aliongea.
“Kumbuka baba tumefanana sana kwahiyo hata kama akienda yeye itakuwa ni vile vile tu" Ata aliongea huku akitabasamu.
“Najua sana kama mmefanana lakini lazima achanganyikiwe akiona muuaji amemfuata kwa jinsia nyengine. Sasa ule muda atakao changanyikiwa ndio muda ambao Atu atammaliza"
“Hapo nimekuelewa. Ila sasa Atu hamjui kwa sura yule askari, itakuaje akienda kule?" Ata aliuliza.
“Kumbuka nyie mna weledi mkubwa sana wa masuala ya kijasusi, kwahiyo naamini ukimuelekeza kidogo tu atamjua"
* *
Majira ya jioni TSSI 01 alipanga kuenda hospitali kwenda kumjulia hali IGP Taure na kumchukua maelezo ili apate pa kuanzia katika kazi yake. Akaondoka kwake hadi hospitali. Alipofika akapaki gari kwenye maegesho na kuzama ndani ya hospitali hiyo. Moja kwa moja akaenda mapokezi kwenda kuulizia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati TSSI 01 akienda mapokezi kuulizia chumba alicholazwa IGP Taure ndio muda ambao Atu akiwa katika mavazi ya kidaktari na kisahani kilichojaa dawa akiuendea mlango ambao ndio wa chumba alicholazwa IGP. Nje ya mlango huo kulikuwa na askari wawili waliokuwa wameweka ulinzi hapo katika chumba hicho. Atu akiwa katika mavazi ya kidaktari huku macho yake yakiwa ndani ya miwani ndogo yenye vioo vyeupe. Mikononi akiwa ameshika sahani iliyokuwa na dawa. Alifika hadi pale mlangoni na kuwaomba askari wale kuingia kwenda kumpatia dawa IGP.
Askari hawakujua nia ya msichana huyo aliejifanya kuwa ni Daktari. Wakamruhusu na Atu akaingia ndani ya chumba hicho. Muda huo huo TSSI 01 Hemedy Bhachu nae alikuja hadi hapo, akawa anataka kuingia ndani ya chumba hicho. Ila askari hao wakamgomea na kumuambia kuwa chumba hicho hakiruhusiwi kuingia watu wakawaida. TSSI 01 akawatolea kitambulisho feki kilichomtambulisha kuwa ni askari mwenye cheo cha Inspekta. Walishangaa sana tena kushangaa kuliko kukubwa. Maana hakuna askari mwenye nywele nyingi kichwani na hawajawahi kuona kitu kama hicho. Ila kwa vile kitambulisho kimeonyesha kuwa mtu huyo ni askari tena aliewazidi cheo. Walisaluti na kumpisha kuingia humo ndani.
“Ooh! Samahani Dokta" Hemedy aliongea hivyo baada ya kuingia ndani ya chumba hicho na kumkuta Atu akiwa amesimama na kisahani chake cha dawa. Kitanda kikiwa kitupu bila mtu. Atu alimuangalia bila kuongea chochote. Ikabidi Hemedy amuulize.
“Huyu mgonjwa yupo wapi?"
“We ni nani?" Atu nae alimuuliza.
“Mi ni askari" aliongea huku akitoa kitambulisho. Atu alishangaa sana kama walivyoshangaa wale askari pale nje. Ni vipi askari awe na nywele nyingi kiasi hicho kichwani? Akajua kuna namna tu kwa mtu huyo.
“Anhaa! Basi afande ngoja mimi niende, nitarudi sasa hivi, maana kuna mgonjwa mwengine nahitaji kwenda kumpa dawa saa hii. Sasa naona huyu anachelewa sana kutoka huko chooni" Atu aliongea huku akiwa na tabasamu. Akaweka kile kisahani cha dawa juu ya meza iliyopo pembeni ya kitanda na kutoka humo. Uwezo wa kumuua IGP huko huko chooni alikuwa anao, ila sasa IGP alifunga mlango kwa ndani kwahiyo hakuweza kufungua, ndio maana akawa anamsubiria atoke ili atimize kilichomleta hapo.
Muda kidogo IGP Taure alitoka chooni huku maji yakimtiririka kumaanisha alitoka kuoga. Alipomuona Hemedy alifurahi sana na kwenda kukumbatiana nae. Kisha wakaka kitandani na kuanza kuongea.
“Hivi ulikuwa wapi siku zote hizo. Namuuliza mzee Ganjo ananiambia sijui mmeenda kusoma huko" IGP aliongea.
“Ndio tulienda kusoma nchi za nje" Hemedy alimuambia.
“Kwahiyo hata kuniaga pia mliona tabu mkaamua muondoke tu hivi hivi?"
“Hapana ila ilikuwa dharura tu. Halafu kuna Daktari sijui ni nesi yule, alikuja hapa alikuwa anataka kukupa dawa ila ameondoka baada ya kuona unachelewa sana kutoka huko chooni. Ila amesema atarudi na dawa zenyewe kaziacha zile pale" Hemedy alimuambia na kumfanya IGP ashangae.
“Weee! Nimetoka kunywa dawa nusu saa iliyopita, sasa hizo dawa nyengine zatokea wapi? Na huyo nesi ni nani?" IGP aliongea huku mshangao ukiwa pamoja nae.
“Sasa unaniuliza mimi nitajuaje afande?" Hemedy alimuuliza huku akiwa na tabasamu. IGP aliinuka pale kitandani na kukiendea kile kisahani kilichokuwa na viboksi vidogo vidogo vya dawa na kuvifungua. Akakumbwa na taharuki, hakukuwa na dawa kwenye hivyo viboksi, vilikuwa vitupu tu. Akarudi na kumuonyesha Hemedy Bhachu, nae pia akashangaa.
“Nini maana yake hii?" TSSI 01 alimuuliza.
“Kwani huyo nesi aliekuja kuleta hivi vitu alikuwa katika muonekano gani. Yani alikuajekuaje?" IGP alimuuliza.
“Alikuwa katika mavazi ya kidaktari. Kwani vipi afande?" TSSI 01 alimuuliza huku akikaa vizuri kumuangalia IGP.
“Hapana hii haiwezekani" akatulia kidogo, akawa kama anafikiria kitu. “Inspekta aliwahi kuniambia kuwa muuaji wapo mapacha, na yeye aliuwawa na wakike, sasa nahisi huyu ndie yule aliemuua Inspekta na mama hakimu" IGP ni kama vile alikuwa akijiongelea mwenyewe. Akamgeukia Hemedy na kumuambia. “Sikiliza Hemedy. Hawa wauaji wapo mapacha wakike na wakiume kwa maelezo aliyonipa askari wangu ambae kwa sasa ni marehemu na ameuliwa na wakike. Kwa maelezo ya mke wa Kamishna, alisema walivamiwa na mwanaume mmoja na huyo ndie alitekeleza mauaji ya kamishna. Tukamuita askari wetu mwenye weledi mzuri wa kuchora picha kwa maelezo achukue maelezo kwa yule mke wa kamishna ya jinsi ya huyo muuaji alivyo. Akatuchorea picha ya muuaji na wanayo askari wangu. Na mtu aliechorwa kwenye hiyo picha ndie huyo huyo alienivamia mimi na kumuua mke wangu huku akinijeruhi. Sasa naomba tumuite tena umueleze muonekana wa huyo nesi alieingia humu ndani halafu tuangalie kama kutakuwa na uwiano wa hizo sura ama laa" IGP Aliongea na kunyanyuka hapo kitandani, akatoka nje ya chumba hicho na kuongea na wale askari waliokuwa nje wamesimama mlango. Kisha akarudi tena ndani.
“Sasa afande unasema hao wauaji wapo mapacha na mapacha wanaweza kufanana au wasifanane. Huyo aliemuua Kamishna na kukujeruhi wewe ni wakiume. Na huyo aliemuua askari wako na huyo mama hakimu ni wakike. Je kama hao wauaji sio hao mapacha, utajuaje?" TSSI 01 alimuuliza.
“Subiri kwanza huyo askari aje halafu umuelezee muonekano wa huyo nesi, baada ya hapo ndio tutajua" akamuangalia Hemedy machoni na kumuambia. “Unajua kwanini mimi namuhisi huyo nesi ni katika hao mapacha. Tangu niletwe hapa hospitali, anae nihudumia mimi ni Daktari wa kiume, huyo ndie anaenikumbusha kila unapofika muda wa dawa na isitoshe dawa zangu zipo humu humu ndani. Zile pale kwenye kile kikabati. Sasa huyo nesi alikuwa anataka kuniletea dawa zipi? Tena pia hajaleta dawa, ni viboksi tu vya dawa. Kwanini nisimuhisi kwamba yeye ni mmoja katika hao mapacha?" IGP Taure alimfafanulia vizuri TSSI 01. Muda huo bado hajajua kwamba huyo aliekaa nae sio yule aliekuwa nae miaka sita iliyopita. Huyu wa sasa ni mpelelezi katika kitengo cha siri. TSSI 01 akayachuja hayo maelezo na kukuta yana tija ndani yake. Muda huo huo akaingia askari humo ndani. Akapiga saluti na kutulia.
“Afande kuna mtu nahitaji umchore kwa kusikiliza maelezo ya huyu mtu hapa"
“Sawa mkuu" askari huyo akatoa karatasi nyeupe na kalamu ya penseli katika kibegi chake. Akavuta droo iliyokuwa hapo hapo ndani na kuweka juu yake karatasi na ile penseli. Akatoka nje na aliporudi alikuwa na kiti. Akakaa tayari kusikiliza muonekano wa huyo anaetaka kuchorwa. Ni kitendo kilichochokuwa nusu saa tu mchoro ukawa umekamilika. Akampatia IGP ile karatasi yenye mchoro. IGP alishtuka na kupayuka kwa nguvu huku akiwa anauangalia ule mchoro.
“Ndio huyu huyu! Embu afande toa ule mchoro mwengine halafu tuufananishe" IGP alimuambia yule askari huku yeye macho yake yakiwa katika ule mchoro wa Atu akiwa katika mavazi ya kidaktari. Askari akatoa mchoro mwengine kwenye kile kibegi chake na kumpa IGP.
“Sasa si umeamini maneno yangu Hemedy. Si unaona walivyofanana hawa watu? Hawa ndio wauaji na huyu alikuja hapa kwa lengo la kuniua na mimi" TSSI 01 akazichukua picha na kuziangalia kwa umakini. Akatikisa kichwa huku tabasamu likimtoka usoni mwake. Akaona sasa kazi iliyomleta inaenda kuisha muda si mrefu baada ya kuwajua wauaji. Akaomba azipige kopi zile picha ili na yeye awe nazo. Hapo alimshangaza IGP ikabidi amuulize.
“Hizo picha wewe wazitaka za nini? Kwani wewe bado ni askari? Na utakuaje askari wakati huna muonekano wa kiaskari" IGP alimuuliza kwa mshangao. TSSI 01 akabaki kumuangalia machoni IGP. IGP kama vile alimuelewa. Akamruhusu yule askari kuondoka ila zile picha akaziacha.
“Mimi ni mpelelezi namba moja katika kitengo cha siri kinachoitwa. TSSI. Tanzania Secret Service Intelligence. TSSI 01 na nimekuja huku kuja kuchunguza hivi vifo vya maaskari vinavyotokea" IGP alipigwa na butwaa huku akimuangalia kijana huyo huku mshangao ukionekana waziwazi usoni mwake. TSSI 01 akamtolea na kitambulisho chake halali cha kazi, akamuonyesha.
“I..inamaana Hemedy umekuwa mpelelezi mwenye namba hiyo ya kwanza?" IGP alimuuliza huku akiwa ametahayari kwa taarifa hiyo. Akamuangalia usoni kisha macho yake akayarudisha kwenye kile kitambulisho ambacho kwa sasa amekishika mkononi akikiangalia angalia. Hemedy aliishia kutabasamu tu.
“Na Hilda nae, pia ni kama wewe?" IGP alimuuliza huku akimuangalia usoni.
“Ndio, ila yeye ni namba tatu. Yani ni TSSI 03" IGP akazidi kushangaa kwa taarifa hizo. Akamrudishia kitambulisho chake na kumuuliza.
“Kwahiyo umetumwa kuja kufuatilia chanzo cha matukio yanayotukia katika mji huu?"
“Ndio. Nina hitaji ushirikiano wako ili kuimaliza hii kazi mapema" TSSI 01 Aliongea.
“Sawa, hakuna shaka na hizo picha pia kama unataka kwenda nazo kupiga kopi pia sawa. Wote tupo kwaajili ya kulilinda taifa letu" IGP Taure aliongea.
“Sasa afande acha mimi nikazitoe kopi hizi picha, nakurudishia sasa hivi ‘original' zake" TSSI 01 alitoka ndani ya chumba hicho na kupotelea huko nje akimuacha IGP Taure akilifikiria hilo swala alilotoka kuambiwa hivi punde. Baada ya dakika kumi. TSSI 01 aliingia humo na kumkabidhi zilepicha halisi na kubaki na zile kopi. Akamuaga IGP na kuondoka hapo.
Akaenda kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye gari lake. Akalitoa ndani ya hospitali na kuliingiza barabarani. Wakati akiwa barabarani, aliona kuna gari nyuma yake linamfuata. Akacheka kimoyo moyo na kuendelea na safari yake bila ya kuwa na wasiwasi wowote. Atu ndie aliekuwa akimfuatilia TSSI 01. Na kilichomfanya kugundulika mapema, ni ile kutoijua mitaa ya mji huo. Kwahiyo hakuwa na budi kumfuatilia kwa ukaribu zaidi ili asiachwe.
Hemedy Bhachu alifika nyumbani kwake na kupaki gari nje ya geti. Akashuka kuliendea geti, akalifungua na kuingiza gari ndani. Kisha akarudi tena kulifunga geti. Kabla hajafunga geti. Alichungulia nje na kuliona gari lililokuwa likimfuata likigeuza kuondoka.
“Mtego umenasa. Kama usipo wapata wote wawili, basi utampata mmoja wapo" Akatabasamu na kufunga geti. Akaapiga hatua kuuendea mlango wa nyumba hiyo. Akiwa bado anatembea. Akazitao zile picha kisha akaziangalia vizuri.
“Haina haja ya kubaki na picha ambazo hazina maana kwasababu wenye picha hizi punde tu watajileta wenyewe" Akazichana zile picha na kuzitupa kwenye bustani. Kisha akaendea na safari ya kuingia ndani ya nyumba yake.
Atu alirudi kwenye lile jumba la maficho. Akashuka kwenye gari na kuingia ndani. Akawakuta wote wapo sebuleni wakimsubiri yeye awape taarifa. Kabla hajaongea kitu. Moja kwa moja akaenda kwenye friji lililopo hapo hapo sebuleni na kuchukua maji kisha akaenda nayo kwenye sofa na kukaa. Akapiga tafu moja na kuwaangalia wenzake na kuona wote wapo makini kumuangalia yeye.
“Naona hizi kesi serikali wameamua kumpa mtu makini kuzifuatilia. Lakini hawezi kuwa makini mbele ya vichwa viwili vilivyotoka kwenye damu ya Bakari Hanein" Atu aliongea na kutulia kimya. Akawaangalia na kuwaona wote wapo kimya kumsikiliza yeye. Ni kama vile hawakumuelewa, au walimuelewa ila walitaka maelezo zaidi. Akaendelea.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wakati nipo katika chumba alicholazwa yule askari nikimsubiria atokea chooni" akawaangalia tena kwenye nyuso zao. Kisha akaendelea. “Nilikuwa na uwezo wa kumuulia kule kule chooni ila bahati nzuri kwake alikuwa amefunga mlango kwa ndani. Sikuwa na budi kumsubiri, ndipo akaingia mtu aliejitambulisha kama askari lakini alifeli kunidanganya kwasababu mimi nina akili zaidi yake. Askari gani katika nchii hii alieruhusiwa kuwa na nywele nyingi? Tena nyingi ambazo unauwezo hata wa kuzisuka? Alifeli kunidanganya. Mimi nikaona niondoke pale chumbani kwa kisingizio kuwa kuna mgonjwa mwengine ninahitajika kumpelekea dawa. Ila baada ya kutoka pale. Nikaenda kwenye gari langu na kumsubiria yule mtu hadi pale alipotoka. Na hivi ninavyowaambieni huyo mtu ambae mimi nilipomsoma machoni niligundua sio wa kawaida. Yani anauweledi wowote katika masuala ya kijasusi. Nilimfuatilia nyuma nyuma hadi nikapajua anapoishi. Kwahiyo nimerudi hapa nikiwa sijatekeleza mauji ya yule askari lakini nimepata kitu chengine" Atu alimaliza kutoa maelezo kuhusu huyo mtu anaesema hana akili zaidi yake tena amefeli kumdanganya. Ila hakujua uwezo wa huyo mtu anaemsema amejidanganya kumdanganya yeye. Hakujua. Hakujua uwezo na akili alizonazo TSSI 01. Ndio atajuaje wakati alimuona kwa mara moja tu? Tena akiwa katika hali ambayo yeye alihisi ni ya kawaida. Hakujua.
Na labda angejua!!
“Sawa. Nakupongeza kwa kupiga hatua uliyoipiga ya kumgundua huyo mtu unaedai sio wa kawaida. Maana tumemjua sisi kabla yeye hajatujua. Na siku ambayo atatujua ndio sikua ambayo atamjua malaika mtoa roho ana sura gani" Mr Hanein aliongea. Kisha akamuuliza swali. “Unafikiria nini hadi sasa?"
“Ni lazima wote wawili wafe. Ataanza yule askari ili kupoteza ushahidi kabisa. Kisha atafuatia huyu aliejivika uaskari" Atu aliongea.
“Sawa. Wewe utaenda kumtembelea huyo aliejivika uaskari na Ata atamfuata yule askari" Mr Hanein aliongea. Lakini majukumu hayo Ata aliona kama vile amedharauliwa kuambiwa akamuue IGP Taure wakati ni mgonjwa. Yeye alitaka akapambane na huyo alieingilia haya mambo.
“Baba acha mimi nikakutane na huyo aliejivika uaskari, Atu yeye aende kwa yule askari" Ata alito wazo lake.
“Hapana. Wewe humjui huyo mtu kisura wala hapo anapoishi. Kwahiyo wewe utaenda kwa yule askari na Atu tamfuata huyo mwengine" Mr Hanein alimuambia.
“Lakini mbona Atu alimfuata yule askari pasi na kumjua? Alimfuata kwa malekezo yangu tu na akafika. Sasa iweje mimi nisimpate huyo mtu mwengine?" Atu aliongea kwa sauti ya hasira na ghadhabu ndani yake. Kisha hakutaka kusubiri jibu lolote. Akaondoka kuelekea vyumbani akiwaacha wote hapo wakimuangalia kwa macho ya taharuki huku vinywa vyao vikiwa wazi kwa mshangao.
* *
Majira ya saa sita usiku. Katika hospitali aliyolazwa IGP Taure. Alionekana mtu akiuvizia mlango wa chumba alicholazwa IGP. Sasa hapakuwa na askari yoyote mlangoni alielinda chumba hicho. Mtu huyo alikuwa ni Ata. Akauendea mlango na kunyonga kitasa. Mlango ukakubali kufunguka. Akazama ndani na kuufunga malango kwa ndani ili alieko nje asiweze kuufungua. Akatupa macho kitandani na kukuta mwili wa mtu ukiwa umelala juu ya kitanda umefunikwa shuka mwanzo mwisho. Akajua sasa kazi imekuwa nyepesi. Akachomoa bastola yake na kuufuata mwili ule taratibu huku akiwa makini. Alipofika kabla hajaupiga risasi. Akataka kuhakikisha je anaetaka kumuua ndie huyo anaemtaka?.
Akapigwa na butwa huku umakini wote aliokuwa nao ukimuondoka baada ya kufunua shuka na kukuta mtu aliemtarajia sie. TSSI 01 Hemedy Bhachu ndie aliekuwa ndani ya shuka zito la hospitali akiwa ameweka mtego kama vile alivyodhani kuwa utawanasa wote au mmoja wapo k
“Ooh! Samahani Dokta" Hemedy aliongea hivyo baada ya kuingia ndani ya chumba hicho na kumkuta Atu akiwa amesimama na kisahani chake cha dawa. Kitanda kikiwa kitupu bila mtu. Atu alimuangalia bila kuongea chochote. Ikabidi Hemedy amuulize.
“Huyu mgonjwa yupo wapi?"
“We ni nani?" Atu nae alimuuliza.
“Mi ni askari" aliongea huku akitoa kitambulisho. Atu alishangaa sana kama walivyoshangaa wale askari pale nje. Ni vipi askari awe na nywele nyingi kiasi hicho kichwani? Akajua kuna namna tu kwa mtu huyo.
“Anhaa! Basi afande ngoja mimi niende, nitarudi sasa hivi, maana kuna mgonjwa mwengine nahitaji kwenda kumpa dawa saa hii. Sasa naona huyu anachelewa sana kutoka huko chooni" Atu aliongea huku akiwa na tabasamu. Akaweka kile kisahani cha dawa juu ya meza iliyopo pembeni ya kitanda na kutoka humo. Uwezo wa kumuua IGP huko huko chooni alikuwa anao, ila sasa IGP alifunga mlango kwa ndani kwahiyo hakuweza kufungua, ndio maana akawa anamsubiria atoke ili atimize kilichomleta hapo.
Muda kidogo IGP Taure alitoka chooni huku maji yakimtiririka kumaanisha alitoka kuoga. Alipomuona Hemedy alifurahi sana na kwenda kukumbatiana nae. Kisha wakaka kitandani na kuanza kuongea.
“Hivi ulikuwa wapi siku zote hizo. Namuuliza mzee Ganjo ananiambia sijui mmeenda kusoma huko" IGP aliongea.
“Ndio tulienda kusoma nchi za nje" Hemedy alimuambia.
“Kwahiyo hata kuniaga pia mliona tabu mkaamua muondoke tu hivi hivi?"
“Hapana ila ilikuwa dharura tu. Halafu kuna Daktari sijui ni nesi yule, alikuja hapa alikuwa anataka kukupa dawa ila ameondoka baada ya kuona unachelewa sana kutoka huko chooni. Ila amesema atarudi na dawa zenyewe kaziacha zile pale" Hemedy alimuambia na kumfanya IGP ashangae.
“Weee! Nimetoka kunywa dawa nusu saa iliyopita, sasa hizo dawa nyengine zatokea wapi? Na huyo nesi ni nani?" IGP aliongea huku mshangao ukiwa pamoja nae.
“Sasa unaniuliza mimi nitajuaje afande?" Hemedy alimuuliza huku akiwa na tabasamu. IGP aliinuka pale kitandani na kukiendea kile kisahani kilichokuwa na viboksi vidogo vidogo vya dawa na kuvifungua. Akakumbwa na taharuki, hakukuwa na dawa kwenye hivyo viboksi, vilikuwa vitupu tu. Akarudi na kumuonyesha Hemedy Bhachu, nae pia akashangaa.
“Nini maana yake hii?" TSSI 01 alimuuliza.
“Kwani huyo nesi aliekuja kuleta hivi vitu alikuwa katika muonekano gani. Yani alikuajekuaje?" IGP alimuuliza.
“Alikuwa katika mavazi ya kidaktari. Kwani vipi afande?" TSSI 01 alimuuliza huku akikaa vizuri kumuangalia IGP.
“Hapana hii haiwezekani" akatulia kidogo, akawa kama anafikiria kitu. “Inspekta aliwahi kuniambia kuwa muuaji wapo mapacha, na yeye aliuwawa na wakike, sasa nahisi huyu ndie yule aliemuua Inspekta na mama hakimu" IGP ni kama vile alikuwa akijiongelea mwenyewe. Akamgeukia Hemedy na kumuambia. “Sikiliza Hemedy. Hawa wauaji wapo mapacha wakike na wakiume kwa maelezo aliyonipa askari wangu ambae kwa sasa ni marehemu na ameuliwa na wakike. Kwa maelezo ya mke wa Kamishna, alisema walivamiwa na mwanaume mmoja na huyo ndie alitekeleza mauaji ya kamishna. Tukamuita askari wetu mwenye weledi mzuri wa kuchora picha kwa maelezo achukue maelezo kwa yule mke wa kamishna ya jinsi ya huyo muuaji alivyo. Akatuchorea picha ya muuaji na wanayo askari wangu. Na mtu aliechorwa kwenye hiyo picha ndie huyo huyo alienivamia mimi na kumuua mke wangu huku akinijeruhi. Sasa naomba tumuite tena umueleze muonekana wa huyo nesi alieingia humu ndani halafu tuangalie kama kutakuwa na uwiano wa hizo sura ama laa" IGP Aliongea na kunyanyuka hapo kitandani, akatoka nje ya chumba hicho na kuongea na wale askari waliokuwa nje wamesimama mlango. Kisha akarudi tena ndani.
“Sasa afande unasema hao wauaji wapo mapacha na mapacha wanaweza kufanana au wasifanane. Huyo aliemuua Kamishna na kukujeruhi wewe ni wakiume. Na huyo aliemuua askari wako na huyo mama hakimu ni wakike. Je kama hao wauaji sio hao mapacha, utajuaje?" TSSI 01 alimuuliza.
“Subiri kwanza huyo askari aje halafu umuelezee muonekano wa huyo nesi, baada ya hapo ndio tutajua" akamuangalia Hemedy machoni na kumuambia. “Unajua kwanini mimi namuhisi huyo nesi ni katika hao mapacha. Tangu niletwe hapa hospitali, anae nihudumia mimi ni Daktari wa kiume, huyo ndie anaenikumbusha kila unapofika muda wa dawa na isitoshe dawa zangu zipo humu humu ndani. Zile pale kwenye kile kikabati. Sasa huyo nesi alikuwa anataka kuniletea dawa zipi? Tena pia hajaleta dawa, ni viboksi tu vya dawa. Kwanini nisimuhisi kwamba yeye ni mmoja katika hao mapacha?" IGP Taure alimfafanulia vizuri TSSI 01. Muda huo bado hajajua kwamba huyo aliekaa nae sio yule aliekuwa nae miaka sita iliyopita. Huyu wa sasa ni mpelelezi katika kitengo cha siri. TSSI 01 akayachuja hayo maelezo na kukuta yana tija ndani yake. Muda huo huo akaingia askari humo ndani. Akapiga saluti na kutulia.
“Afande kuna mtu nahitaji umchore kwa kusikiliza maelezo ya huyu mtu hapa"
“Sawa mkuu" askari huyo akatoa karatasi nyeupe na kalamu ya penseli katika kibegi chake. Akavuta droo iliyokuwa hapo hapo ndani na kuweka juu yake karatasi na ile penseli. Akatoka nje na aliporudi alikuwa na kiti. Akakaa tayari kusikiliza muonekano wa huyo anaetaka kuchorwa. Ni kitendo kilichochokuwa nusu saa tu mchoro ukawa umekamilika. Akampatia IGP ile karatasi yenye mchoro. IGP alishtuka na kupayuka kwa nguvu huku akiwa anauangalia ule mchoro.
“Ndio huyu huyu! Embu afande toa ule mchoro mwengine halafu tuufananishe" IGP alimuambia yule askari huku yeye macho yake yakiwa katika ule mchoro wa Atu akiwa katika mavazi ya kidaktari. Askari akatoa mchoro mwengine kwenye kile kibegi chake na kumpa IGP.
“Sasa si umeamini maneno yangu Hemedy. Si unaona walivyofanana hawa watu? Hawa ndio wauaji na huyu alikuja hapa kwa lengo la kuniua na mimi" TSSI 01 akazichukua picha na kuziangalia kwa umakini. Akatikisa kichwa huku tabasamu likimtoka usoni mwake. Akaona sasa kazi iliyomleta inaenda kuisha muda si mrefu baada ya kuwajua wauaji. Akaomba azipige kopi zile picha ili na yeye awe nazo. Hapo alimshangaza IGP ikabidi amuulize.
“Hizo picha wewe wazitaka za nini? Kwani wewe bado ni askari? Na utakuaje askari wakati huna muonekano wa kiaskari" IGP alimuuliza kwa mshangao. TSSI 01 akabaki kumuangalia machoni IGP. IGP kama vile alimuelewa. Akamruhusu yule askari kuondoka ila zile picha akaziacha.
“Mimi ni mpelelezi namba moja katika kitengo cha siri kinachoitwa. TSSI. Tanzania Secret Service Intelligence. TSSI 01 na nimekuja huku kuja kuchunguza hivi vifo vya maaskari vinavyotokea" IGP alipigwa na butwaa huku akimuangalia kijana huyo huku mshangao ukionekana waziwazi usoni mwake. TSSI 01 akamtolea na kitambulisho chake halali cha kazi, akamuonyesha.
“I..inamaana Hemedy umekuwa mpelelezi mwenye namba hiyo ya kwanza?" IGP alimuuliza huku akiwa ametahayari kwa taarifa hiyo. Akamuangalia usoni kisha macho yake akayarudisha kwenye kile kitambulisho ambacho kwa sasa amekishika mkononi akikiangalia angalia. Hemedy aliishia kutabasamu tu.
“Na Hilda nae, pia ni kama wewe?" IGP alimuuliza huku akimuangalia usoni.
“Ndio, ila yeye ni namba tatu. Yani ni TSSI 03" IGP akazidi kushangaa kwa taarifa hizo. Akamrudishia kitambulisho chake na kumuuliza.
“Kwahiyo umetumwa kuja kufuatilia chanzo cha matukio yanayotukia katika mji huu?"
“Ndio. Nina hitaji ushirikiano wako ili kuimaliza hii kazi mapema" TSSI 01 Aliongea.
“Sawa, hakuna shaka na hizo picha pia kama unataka kwenda nazo kupiga kopi pia sawa. Wote tupo kwaajili ya kulilinda taifa letu" IGP Taure aliongea.
“Sasa afande acha mimi nikazitoe kopi hizi picha, nakurudishia sasa hivi ‘original' zake" TSSI 01 alitoka ndani ya chumba hicho na kupotelea huko nje akimuacha IGP Taure akilifikiria hilo swala alilotoka kuambiwa hivi punde. Baada ya dakika kumi. TSSI 01 aliingia humo na kumkabidhi zilepicha halisi na kubaki na zile kopi. Akamuaga IGP na kuondoka hapo.
Akaenda kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye gari lake. Akalitoa ndani ya hospitali na kuliingiza barabarani. Wakati akiwa barabarani, aliona kuna gari nyuma yake linamfuata. Akacheka kimoyo moyo na kuendelea na safari yake bila ya kuwa na wasiwasi wowote. Atu ndie aliekuwa akimfuatilia TSSI 01. Na kilichomfanya kugundulika mapema, ni ile kutoijua mitaa ya mji huo. Kwahiyo hakuwa na budi kumfuatilia kwa ukaribu zaidi ili asiachwe.
Hemedy Bhachu alifika nyumbani kwake na kupaki gari nje ya geti. Akashuka kuliendea geti, akalifungua na kuingiza gari ndani. Kisha akarudi tena kulifunga geti. Kabla hajafunga geti. Alichungulia nje na kuliona gari lililokuwa likimfuata likigeuza kuondoka.
“Mtego umenasa. Kama usipo wapata wote wawili, basi utampata mmoja wapo" Akatabasamu na kufunga geti. Akaapiga hatua kuuendea mlango wa nyumba hiyo. Akiwa bado anatembea. Akazitao zile picha kisha akaziangalia vizuri.
“Haina haja ya kubaki na picha ambazo hazina maana kwasababu wenye picha hizi punde tu watajileta wenyewe" Akazichana zile picha na kuzitupa kwenye bustani. Kisha akaendea na safari ya kuingia ndani ya nyumba yake.
Atu alirudi kwenye lile jumba la maficho. Akashuka kwenye gari na kuingia ndani. Akawakuta wote wapo sebuleni wakimsubiri yeye awape taarifa. Kabla hajaongea kitu. Moja kwa moja akaenda kwenye friji lililopo hapo hapo sebuleni na kuchukua maji kisha akaenda nayo kwenye sofa na kukaa. Akapiga tafu moja na kuwaangalia wenzake na kuona wote wapo makini kumuangalia yeye.
“Naona hizi kesi serikali wameamua kumpa mtu makini kuzifuatilia. Lakini hawezi kuwa makini mbele ya vichwa viwili vilivyotoka kwenye damu ya Bakari Hanein" Atu aliongea na kutulia kimya. Akawaangalia na kuwaona wote wapo kimya kumsikiliza yeye. Ni kama vile hawakumuelewa, au walimuelewa ila walitaka maelezo zaidi. Akaendelea.
“Wakati nipo katika chumba alicholazwa yule askari nikimsubiria atokea chooni" akawaangalia tena kwenye nyuso zao. Kisha akaendelea. “Nilikuwa na uwezo wa kumuulia kule kule chooni ila bahati nzuri kwake alikuwa amefunga mlango kwa ndani. Sikuwa na budi kumsubiri, ndipo akaingia mtu aliejitambulisha kama askari lakini alifeli kunidanganya kwasababu mimi nina akili zaidi yake. Askari gani katika nchii hii alieruhusiwa kuwa na nywele nyingi? Tena nyingi ambazo unauwezo hata wa kuzisuka? Alifeli kunidanganya. Mimi nikaona niondoke pale chumbani kwa kisingizio kuwa kuna mgonjwa mwengine ninahitajika kumpelekea dawa. Ila baada ya kutoka pale. Nikaenda kwenye gari langu na kumsubiria yule mtu hadi pale alipotoka. Na hivi ninavyowaambieni huyo mtu ambae mimi nilipomsoma machoni niligundua sio wa kawaida. Yani anauweledi wowote katika masuala ya kijasusi. Nilimfuatilia nyuma nyuma hadi nikapajua anapoishi. Kwahiyo nimerudi hapa nikiwa sijatekeleza mauji ya yule askari lakini nimepata kitu chengine" Atu alimaliza kutoa maelezo kuhusu huyo mtu anaesema hana akili zaidi yake tena amefeli kumdanganya. Ila hakujua uwezo wa huyo mtu anaemsema amejidanganya kumdanganya yeye. Hakujua. Hakujua uwezo na akili alizonazo TSSI 01. Ndio atajuaje wakati alimuona kwa mara moja tu? Tena akiwa katika hali ambayo yeye alihisi ni ya kawaida. Hakujua.
Na labda angejua!!
“Sawa. Nakupongeza kwa kupiga hatua uliyoipiga ya kumgundua huyo mtu unaedai sio wa kawaida. Maana tumemjua sisi kabla yeye hajatujua. Na siku ambayo atatujua ndio sikua ambayo atamjua malaika mtoa roho ana sura gani" Mr Hanein aliongea. Kisha akamuuliza swali. “Unafikiria nini hadi sasa?"
“Ni lazima wote wawili wafe. Ataanza yule askari ili kupoteza ushahidi kabisa. Kisha atafuatia huyu aliejivika uaskari" Atu aliongea.
“Sawa. Wewe utaenda kumtembelea huyo aliejivika uaskari na Ata atamfuata yule askari" Mr Hanein aliongea. Lakini majukumu hayo Ata aliona kama vile amedharauliwa kuambiwa akamuue IGP Taure wakati ni mgonjwa. Yeye alitaka akapambane na huyo alieingilia haya mambo.
“Baba acha mimi nikakutane na huyo aliejivika uaskari, Atu yeye aende kwa yule askari" Ata alito wazo lake.
“Hapana. Wewe humjui huyo mtu kisura wala hapo anapoishi. Kwahiyo wewe utaenda kwa yule askari na Atu tamfuata huyo mwengine" Mr Hanein alimuambia.
“Lakini mbona Atu alimfuata yule askari pasi na kumjua? Alimfuata kwa malekezo yangu tu na akafika. Sasa iweje mimi nisimpate huyo mtu mwengine?" Atu aliongea kwa sauti ya hasira na ghadhabu ndani yake. Kisha hakutaka kusubiri jibu lolote. Akaondoka kuelekea vyumbani akiwaacha wote hapo wakimuangalia kwa macho ya taharuki huku vinywa vyao vikiwa wazi kwa mshangao.
* *
Majira ya saa sita usiku. Katika hospitali aliyolazwa IGP Taure. Alionekana mtu akiuvizia mlango wa chumba alicholazwa IGP. Sasa hapakuwa na askari yoyote mlangoni alielinda chumba hicho. Mtu huyo alikuwa ni Ata. Akauendea mlango na kunyonga kitasa. Mlango ukakubali kufunguka. Akazama ndani na kuufunga malango kwa ndani ili alieko nje asiweze kuufungua. Akatupa macho kitandani na kukuta mwili wa mtu ukiwa umelala juu ya kitanda umefunikwa shuka mwanzo mwisho. Akajua sasa kazi imekuwa nyepesi. Akachomoa bastola yake na kuufuata mwili ule taratibu huku akiwa makini. Alipofika kabla hajaupiga risasi. Akataka kuhakikisha je anaetaka kumuua ndie huyo anaemtaka?.
Akapigwa na butwa huku umakini wote aliokuwa nao ukimuondoka baada ya kufunua shuka na kukuta mtu aliemtarajia sie. TSSI 01 Hemedy Bhachu ndie aliekuwa ndani ya shuka zito la hospitali akiwa ameweka mtego kama vile alivyodhani kuwa utawanasa wote au mmoja wapo katika hao mapacha wauaji.cha wauaji.
ENDELEA.
Ata alikuwa bado ameduwaa baada ya kumkuta mtu sie aliemfuata. TSSI 01 muda huo alikuwa anatabasamu tu akimsubiria Ata afanye chochote ili mchezo uanze humo ndani. Ata akaona akiendelea kuzubaa mambo yanaweza yakaharibika. Akarudi nyuma kidogo na kuiondoa usalama bastola yake tayari kumfyatulia risasi TSSI 01. TSSI 01 alilikusanya lileshuka na kumrushia nalo usoni kisha yeye akahama haraka pale kitandani. Risasi mbili zilienda kuchimba ukutani sentimita chache tu TSSI 01 alipokuwepo kabla haja hama. Ata muda huo alikuwa akihangaika kulitoa shuka hilo lililoziba uso wake baada ya kuachia risasi mbili ambazo hazikutoa mlio kutokana na bastola aliyoishika kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti.
TSSI 01 ALIMFUATA Ata pale alipokuwa akibabaika kulitoa lileshuka usoni mwake. Akampiga ngumi tatu za uso. Kisha akalivingirisha lileshuka shingoni mwa Ata kwa staili ya kumkaba. Ata alipiga kelele huku akiuinua mkono wake wenye bastola kuelekeza nyuma ili ampige risasi TSSI 01 aliekuwa nyuma yake akimkaba kwa lile shuka. Hemedy Bhachu aliusoma mchezo anaotaka kuufanya Ata. Akaushika mkono wa Ata wenye bastola na kuuviringirisha huku mkono wake mwengine ukizidi kulikaza lile shuka shingoni mwa adui yake.
Ata aliuachia mkono wake mmoja uliokuwa umeng'ang'ania kulitoa shuka lililo kaba shingo lake na kumpiga kifuti cha mbavu TSSI 01. Hapo alimuweza, maana Hemedy Bhachu alirudi nyuma, lakini hakurudi hivi hivi, alirudi na bastola aliyokuwa ameishika Ata. Akamnyooshe kipindi hicho Ata ndio alikuwa amefanikiwa kuliondoa shuka usoni mwake. Macho yake yalipokuwa huru, akakutana na bastola iliyoelekezwa kwake. Bastola yake mwenyewe.
Akagwaya!.
Akabaki ametulia hivyo hivyo huku akitweta kwa nguvu kama mtu alietoka kuokoka kufumaniwa na mke wa mtu. TSSI 01 alikuwa anatabasamu huku akiwa amemnyooshea bastola Ata. Akamuamrisha akaekitandani nae Ata akakaa. TSSI 01 vile vile akiwa amemnyooshea bastola Ata. Alitoa pingu na kumfuata kwa uangalifu mkubwa pale kitandani. Mkono mmoja wa Ata ukafungwa pingu pamoja na chuma cha kitanda. Ata akawa amedhibitika.
“Utanisamehe kwa kukuotea. Ila leo sikupanga kupigana na wewe. Nia yangu ilikuwa nikujue tu na tayari nishakujua. Ila naamini ipo siku tutakutana na hapo tutaonyeshana uwezo mimi na wewe nani mkali" TSSI 01 alimuambia.
“Naitwa Hemedy Bhachu kutoka kitengo cha siri cha kipelelezi na nimekuja hapa kwaajili yenu" Alipoongea hivyo. Akairusha bastola mbali kidogo na alipo Ata. Kisha akamuambia.
“Naomba niwe shemeji yako kwa dada yako maana leo nimemuona katika chumba hiki hiki amenivutia sana. Nitamuoa siku nitakayo kutana nae ila kwa sasa jua kwamba mimi ni shemeji yako" Ata alighadhibika kwa maneno hayo. Akatamani patokee muujiza pingu ikatike ili apambane na huyo mtu anaeongea maneno ya kejeli mbele yake. Ila hicho hakikuwezekana.
“Naenda shemeji. Sijakudhuru kwa chochote kwasababu wewe ni shemeji yangu. Ila nakuacha hapa hapa kesho asubuhi nitarudi tena. Nikikukuta basi jua ndio mwisho wako.. Lala salama" TSSI 01 aliongea hivyo na kutoka chumbani humo akimuacha Ata akitafuta jinsi ya kujitoa katika chumba hicho.
* *
Majira ya saa kumi na mbili asubuhi. Katika chumba alichokuwa amelazwa IGP Taure kilikuwa kina watu watatu ndani yake. Mstaafu wa jeshi la polisi Mzee Ganjo, IGP Taure na TSSI 01 Hemedy Bhachu.
“Sasa kwanini hukumdhibiti vizuri tukampata muuaji, au kwanini hukupiga simu usiku ule ule akaja kuchukuliwa na askari?" IGP Taure alimuuliza TSSI 01 kwa kulalamika kwa kitendo cha kumpa nafasi Ata kutoroka usiku ule ule.
“Hapana afande, hawa watu hatujajua wapo wangapi japokuwa wawili tumeshawajua. Sasa kama tungemkamata huyu hao wengine wangekuwa makini zaidi ili kujilinda wasikamatwe na kutafuta mbinu za kumuokoa mwenzao. Lakini hapa lazima watanitafuta mimi na kutaka kuniua, sasa hapo ndipo tutakapojua wapo wangapi na wapi wameweka makazi yao" TSSI 01 Alimuambia.
“Inavyoelelea alitoroka kwa kuikata hii pingu kwa risasi. Si mnaona kipande chengine cha pingu hakipo kimebaki hichi kilichofungwa kwenye chuma" Mzee Ganjo aliwaambia huku akikishika shika kipande cha pingu kilichobaki kwenye mchuma wa kitanda sehemu ambayo amefungwa pingu jana usiku Ata.
“Nilimtupia bastola pembeni kidogo ili ajiokoe mwenyewe. Sikutaka kumdhibiti jana ile ile japokuwa uwezo huo nilikuwa ninao. Nilitaka tu nimjue" TSSI 01 aliongea.
“Sawa. Sasa huyu mmoja tayari ushamjua na huyo mwengine je utafanya nini ili umjue?" Mzee Ganjo alimuuliza.
“Huyo wa kike nilikutana nae jana humu humu chumbani....." Akamuhadithia ilivyokuwa.
“Halafu hawa mapacha ni watoto wa Mr Hanein" IGP Taure aliongea kitu kilichowafanya wenzake wamuangalie kwa mshangao.
“Kwanini umesema hivyo?" Mzee Ganjo alimuuliza.
“Kwa maelezo ya askari niliemtuma aifuatilie kesi ya kutoroka kwa wale wafungwa wawili mmoja wapo akiwa ni huyo Mr Hanein ndie alienipa taarifa hizo baada siku ya pili ya tukio kuenda katika nyumba ya Mr Hanein. Alimkuta huyo mtoto wa wakike na akajitambulisha kuwa ni mtoto wa mzee huyo" IGP Taure aliwaambia.
“Kwahiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa watoto hawa ndio waliofanya mpango wa kumtorosha baba yao?" Mzee Ganjo alimuuliza.
“Hata mimi nimehisi hivyo" IGP Taure alijibu.
“Na huyo mwenzake alietoroka nae ni nani?" TSSI 01 Aliwauliza. Wote wawili wakamuangalia yeye usoni. TSSI 01 Hemedy Bhachu akawa haelewi nini kilicho wafanya watu hao wamuangalie bila kumjibu hilo swali. Baada ya dakika moja. Mzee Ganjo alimuambia.
“Ni Baba yako mdogo Mrutu ndie alietoroshwa na Mr Hanein" Mzee Ganjo alimuambia. Mshtuko wa TSSI 01 ulionekana dhahiri baada ya taarifa hiyo. Akabaki mdomo wazi huku akiwaangalie wazee hao kwenye nyuso zao akidhani labda watakuwa wanamtania tu. Lakini alikutana na sura zilizoonyesha uhakika wataarifa hiyo.
“Inamaana huyo mwengine ni bamdogo ndie alie toroka na Mr Hanein?" TSSI 01 aliwauliza utafikiri hakusikia hiyo taarifa.
“Ndio. Na hadi sasa hawajulikani walipo" IGP Taure aliongea. Hemedy akabaki amegwaya kwa taarifa hiyo. Hakua akiamini kwamba baba yake mdogo anaweza kufanya kitendo kama hicho. Wakatoka katika chumba hicho wakiwapisha wafanya usafi kusafisha chumba.
* *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kule kwenye lile jumba maficho Kange. Kulikuwa na kikao kama wafanyavyo kila siku wanapotoka kuuwa.
“Uwezo wa kunikamata alikuwa anao japokuwa sio kwa asilimia zote" Ata aliongea huku akiushikashika mkono wake sehemu ambayo alifungwa pingu jana kwenye kitanda cha hospitali. Na muda huu kile kipande kilichobaki kwenye mkono wake baada ya kuikata pingu na bastola hakipo tena baada ya kutolewa na funguo walizokuwa nazo.
“Sasa kwanini usinge muua kabla. Umesubiri hadi yote hayo yamekutokea" Mr Hanein aliongea.
“Sikutaka kumuua kwanza bila ya kuhakikisha kama ndie ama laa! Ila vile kujifunika shuka mwili mzima kumbe ulikuwa ni mtego wake" Ata aliongea.
“Uwezo wake wa kupigana upo vipi?" Atu alimuuliza.
“Anaonekana wa kawaida sana, ila ndio vile tu aliniotea lakini asinge fua dafu" Ata alijitapa.
“Basi huyo mtu anatakiwa afe haraka maana anaweza kuwa ni kikwazo kwetu" Mr Hanein aliongea.
“Alijitambulisha hadi jina lake. Anadai anaitwa Hemedy Bhachu sijui kutoka kitengo gani cha siri cha kipelelezi huko serikalini. Lakini hana lolote wala sio wa kumuhofia sana" Ata alisema. Lakini alimshitua sana Mrutu baada ya kulitaja jina la huyo mpelelezi alietumwa kuja kufuatilia hizo kesi. Akajua sasa mwanae ameingia sehemu mbaya.
“Hata kama, ila inabidi afe" Atu alisema.
“Atu utaenda leo katika nyumba yake ukafanye mauaji yake" Mr Hanein aliongea.
“Baba mimi nitaenda, bado namtamani huyu mtu" Ata aliongea.
“Ata, acha Atu aende yeye" Mr Hanein aliongea.
“Lakini baba mbona kila ninapotaka kufanya kazi unaniwekea kipingamizi?" Ata alimuuliza kwa hasira baba yake.
“Embu kumbuka jana uling'ang'ania unataka uende nyumbani kwake huyo mtu. Lakini matokeo yake ukaenda kukutana naye kule hospitali. Acha Atu nae aende" Mr Hanein aliongea kwa kubembeleza.
“Baba mimi yule mtu ndio namjua vizuri, sasa kwanini unataka kumtuma Atu wakati mimi nipo?" Ata alimuuliza.
“Kumbe Ata tabia yako ya ubishi bado hujaiacha? Mbona lakini unakuwa mbishi namna hii?" Mr Hanein nae alipandisha baada ya kuona sasa sikio linataka kuzidi kichwa.
“Sio hivyo baba ila nilikuwa najaribu kuwaelewesha tu" Ata alishuka sauti na kuwa mpole baada ya kuona baba yake amekasirika.
“Haya basi ataenda Atu" Mr Hanein alitoa uamuzi wa mwisho ambao Ata hakuwa na budi kuukabali japokuwa kishingo upande. Sio kwamba Ata alikuwa anabishana kwasababu anataka akamuue yeye Hemedy Bhachu. La hashaa! Ila alihofia vile vitisho alivyopewa kuwa siku Hemedy atakapokutana na dada yake, basi ndio siku atakayo muoa. Sasa alihofia dada yake kuolewa na alietangaza kumuoa. Akataka kuwaambia vitisho hivyo. Ila akasita, akabaki kumuangalia tu dada yake.
IGP Taure na TSSI 01 walipotoka hospitali. Waliongozana kuelekea kituoni huku wakimuacha Mzee Ganjo akirudi nyumbani kwake. Walipofika waliingia ndani ya ofisi ya IGP baada ya Hemedy kusalimiana na askari kadhaa aliofahamiana nao miaka sita iliyopita wakati akiwa anafanya kazi kituo hicho hicho.
Walipoingia ndani ya ofisi. IGP alimuonyesha mafaili ambayo yalikuwa na kesi za mauaji ya askari yaliyotokea hivi siku zilipopita. TSSI 01 alipitia faili maja baada ya jengine kisha akamuangalia IGP kwa mshangao mkubwa na kumuuliza.
“Hata Afande Jesca nae pia walimuua?"
“Ndio Hemedy, mke wangu walimuua baada ya kunikosa mimi, na nilipoingia ndani ya nyumba ndipo nilipokutana na huyo muuaji. Akani jeruhi na kuondoka. Bilashaka alikusudia kuniua ila ndio hivyo baada ya kuona nimelegea akadhani tayari ameshaniua. Na hizi taarifa za kufa kwa mke wangu nilizipata wakati nikiwa hospitali" IGP Taure alimuambia huku huzuni ikiwa nae. TSSI 01 aliyarudia tena yale mafaili kuyaangalia.
“Nakubaliana na wewe kwamba hawa mapacha wameshiriki kwa namna moja ama nyingine kumtorosha Mr Hanein jela kutokana na haya maelezo ya huyo askari wako uliempa hii kazi....." TSSI 01 akayarudisha yale mafaili kwa IGP.
“Ila muda si mrefu watapatikana wote" akamalizia kusema hivyo.
“Lazima wapatikane kwasababu kumeletwa mpelelezi namba moja kuja kupeleleza haya matukio" IGP aliongea huku akitabasamu.
“Sasa sijui nikuite baba au afande? Lakini mimi nitaendelea kukuita vile vile anko kama vile nilivyokuwa nakuita kipindi kile... Anko acha mimi niende nyumbani saa hii. Tutakutana kesho ama baadae" TSSI 01 aliongea na kutoka katika ofisi hiyo. Akapanda kwenye gari lake na kuondoka hapo.
* *
Majira ya usiku TSSI 01 alikuwa nyumbani kwake sebuleni akiangalia muvi ya kibongo ya kipelelezi inayoitwa MEMORY CARD iliyochezwa kwa umahiri mkubwa huku muhusika mkuu akiwa ni Sajent Minja. Stori ya muvi hiyo ilitungwa na mtunzi mahiri Alex Kileo. Stori hiyo ilimpa umaarufu sana baada ya kuchezwa vizuri na kuuzwa Afrika Mashariki nzima.
Wakati yeye akiendelea kuangalia muvi hiyo kali. Huku nje Atu alikuwa akiruka ukuta kuingia ndani ya nyumba hiyo. Alinyata hadi dirishani na kumkuta mlengwa wake yupo hana hata habari kwamba nyumba yake imevamiwa. Akatoa bastola yake na kuuendea mlango. Akaufungua. Ila ukakataa kuashiria umefungwa kwa funguo. Akatoa funguo zake na kujaribu moja moja, ya nne ikakubali. Mlango ukafunguka. Haraka akamnyooshe bastola TSSI 01 aliekuwa amejilaza kwenye sofa akiangalia luninga, ila sasa hivi alikuwa akiangaliana na mdomo wa bastola.
“Ohooo! Mpenzi umekuja? Karibu ukae" TSSI 01 aliongea hivyo huku akimuangakia Atu aliekuwa amemnyooshea yeye bastola. Hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo kwa kitendo hicho cha kunyooshewa bastola na Atu.
“Sijaja kuzungumza na wewe" Atu aliongea huku akiwa bado amemnyooshea bastola.
“Kumbe ndio umekuja tufunge ndoa? Kaka yako nilimpa hizo salamu naona umekuja, lakini sasa umekuja pekeako bila kuja nae. Au na yeye atakuja?” TSSI 01 aliongea hivyo. Kisha badala ya kujilaza kwenye sofa, akakaa kumuangalia Atu.
“Nahisi unadhani nimekuja kwaajili ya matani hapa. Subiri nifanye kilichonileta" Atu aliongea hivyo. Kisha akaitoa usalama bastola yake tayari kufyatua risasi kumuendea TSSI 01. Ila alikatishwa na sauti ya TSSI 01.
“Subiri kwanza kabla hujaniua mimi kwa kutumia hiyo bastola yako. Basi ujue utaanza kufa wewe kwa bomu lilokuwa nyuma ya huo mlango ulioingilia. Labda ulizuie hilo bomu kisha ndio uniue mimi" akaangalia saa iliyokuwa ukutani na kusema. “Zimebaki sekunde nane ili lilipuke. Sasa nakushauri zuia kwanza hilo bomu kisha ndio uniue mimi" TSSI 01 aliongea hivyo na kumfanya Atu ageuke haraka nyuma yake kuangalia hilo bomu.
KOSA. tena kosa kubwa ambalo ni lakizembe. TSSI 01 aliichukua glasi iliyokuwa chini ya sofa alilokaa ambayo alikuwa akinywa shurubati iliyosindikiza muvi ile anayoiangalia. Kisha akairusha kwa ustadi nzuri ikaenda kuupiga mkono wa Atu ule ambao ulikuwa umeshika bastola. Bastola ikaenda pembeni huku Atu akiugulia maumivu ya kupigwa na hiyo glasi ambayo kwa sasa ilikuwa ni vipande vipande pale chini baada ya kusambaratika sakafuni.
Akataka kuiokota bastola ila alikutana na teke kali la kidevu lilomrusha mbali huku likimuacha akitoa damu nyingi mdomoni. TSSI 01 aliiokota ile bastola na kuzitoa risasi. Kisha akaiweka pembeni. Muda huo Atu alikuwa amesimama tayari kwa mpambano. Atu alimuendea TSSI 01 kwa mapigo ya karate ambayo mengi aliyahepa ila moja lilimpata la kifua na kumfanya TSSI 01 Kurudi nyuma kidogo. Akaangalia sehemu lilepigo lilipotua, akapangusa kisha akamuangalia Atu kwa tabasamu.
“Mimi nilidhani basi umekuja tufunge ndoa, kumbe umekuja kupigana?"
Atu hakutaka kuongea chochote, ila badala yake akamuendea TSSI 01 kwa kasi huku akirusha ngumi ambazo alizirusha kiufundi sana. TSSI 01 ngumi hizo zikambabaisha kidogo ila alifanikiwa kuzikwepa kisha akampiga teke la mbavu lililomfanya Atu akunje sura kwa maumivu kwa sekunde chache kisha akakaa sawa tena kwaajili ya mapigano.
“Unajua leo sipo katika kupigana kabisa, ila naona unanilazimisha nifanye hivyo kwako. Acha nikudhibiti halafu nikuachie nyumba pekeako maana naona unataka kunibughudhi na nyumba yangu"
TSSI 01 Hemedy Bhachu alimfuata kwa pigo la tik taka ila Atu aliliona na kuinama kidogo. Hivyo ndivyo ilikuwa TSSI 01 anavyotaka. Akiwa kule kule hewani, alimpiga mateke mawili ya haraka. Moja la shingo akamalizia na la mgongo. Atu akaenda chini huku akitanguliza mikono huku TSSI 01 akijigeuza haraka baada ya kumpa shambulio hilo adui yake. Atu pale chini alikuwa akijilazimisha kuinuka ila kwa mapigo yale ilikuwa kama vile mlevi alieanguka katika matope. Aliinuka kidogo na kurudi chini baada ya mikono yake kumsaliti.
“Pole sana mpenzi ila yote umeyataka wewe. Acha nikuache upumzike kesho nitarudi. Na nikikukuta basi ujue utakuwa mke wangu halali. Pumzika kwa amani" TSSI 01 aliondoka hapo huku akimuacha Atu akimuangalia kwa hasira nyingi huku damu za mdomoni zikimtoka. Alifunga mlango kwa nje na kutokomea zake.
* *
Majira ya asubuhi TSSI 01 alirudi nyumbani kwake. Aliingia kwa uangalifu maana alijua mtu aliemuacha jana hakuwa wa mchezo. Alipoufikia mlango wa kuingia ndani ya nyumba. Akatia ufunguo kisha akaufungua mlango kabisa na yeye akawahi kubana pembeni nje ya mlango akisikilizia kama kuna shambulizi lolote linaweza kutokea. KIMYA!. akachungulia na kukuta sebule ikiwa tupu. Akaingia ndani na kuangazaangaza macho yake hapo sebuleni na kukuta iko vile vile kama alivyoiacha jana. Ila kitu kimoja tu ndio hakikukuwepo.
Adui yake hakuwepo mahala alipomuacha jana akigaagaa kwa maumivu. Akapanda ngazi na kuenda katika chumba cha kuongozea kamera na kuiendea kompyuta iliyokuwa ikionyesha matukio yote. Akatafuta video ya siku ya jana na kuirudisha masaa saba nyuma. Hapo ndipo video hiyo ilipoanza kuonyesha Atu akiwa kalala chini huku yeye akiufungua mlango na kutoka nje. Akaona baada ya yeye kutoka Atu akijiinua pale chini kwa taabu sana. Akaichukua bastola yake na kuzitia zile risasi ambazo TSSI 01 alizitoa kwenye bastola. Baada ya hapo video ikamuonyesha Atu akiuendea mlango huku akiwa anachechemea. Akajaribu kuufungua ila akaoma umefungwa kwa nje. Akautia mkono wake mfukoni na kutoka na funguo akafungua mlango na kutoka ndani humo. TSSI 01 alitabasamu na kuiweka kompyuta hiyo iendeleee kufanya kazi yake.
“Kumbe hakufanya chochote kitakachokuwa hatari kwa afya yangu" aliongea hivyo huku akiuendea mlango wa kutokea ndani humo. Ila akageuza macho yake haraka kule ilipo kompyuta na kuona ikionyesha sebuleni kuna mgeni ameingia. Akatoka ndani humo na kushuka chini. Hapo akatabasamu alipofika na kusalimiana na huyo mgeni aliengia.
“Jana usiku nilipokea ugeni wa yule pacha wa kike" TSSI 01 alimuambia IGP Taure aliekuwa amekaa kwenye sofa sebuleni hapo.
“Weee!! Alifuata nini huku na kapajuaje?" IGP Taure alimuuliza kwa hamaki huku akimuangalia kwa umakini Hemedy Bhachu.
“Juzi nilipotoka pale hospitali niliongozana nae nyuma nyuma akidhani labda mimi sikumjua ndipo nikafika nae hadi hapa" TSSI 01 alijibu huku akitabasamu wakati IGP Taure akiwa na kwenye mshangao.
“Kumbe ulijua kuwa unafuatwa kwanini umekubali akapajua hapa kwako. Huoni kama hiyo inaweza kuwa ni hatari?" IGP Taure alimuuliza.
“Haiwezi kuwa hatari kwasababu hii ipo katika mpango wangu" TSSI 01 alimuambia.
“Enhee! Ilikuaje hiyo jana alipokuja huyo mtu?" TSSI 01 alimuhadithia ilivyokuwa.
“Haaa! Sasa kwanini huwadhibiti? Au unataka wazidi kuleta maafa kwenye mji huu?" IGP alimuuliza kwa hamaniko na mshangao. Hakuelewa mtu huyu yupo vipi. Maana alikuwa na uwezo wa kuwadhibiti wote wawili lakini chaajabu anawapa nafasi ya kutoroka.
“Anko najua nini nichokifanya. Na wala usiwe na wasiwasi ya kuleta maafa tena kwasababu kwasasa hawatakuwa na mpango wa kufanya hivyo, badala yake watahangaika kunitafuta mimi" TSSI 01 alimuambia.
“Na vipi kuhusiana na wale wafungwa wawili kutoroka gerezani, na hilo pia unalishuhulikia wewe ama?"
“Inaonekana hawa watu wamehusika pia katika hilo. Kwahiyo itakuwa napiga ndege wawili kwa jiwe moja"
“Mbona hii ‘mission’ umekuja pekeako, au ndio utaratibu wa kazi zenu?"
“Huo ndio utaratibu, halafu hata hivyo pia imeonekana ni rahisi. Vinginevyo, Hilda ndie msaidizi wangu"
“Hii ni ‘mission’ ya ngapi kuifanya?"
“Ndio ya kwanza"
TSSI 01 alichukua simu yake na kuipokea baada ya kuona ikiita. Aliongea kwa dakika kadhaa kisha simu ikakatwa. Alikuwa akiongea na Hilda akimuuliza kuhusu hali yake na maendeleo ya kazi. Baada ya hapo alifanya usafi hapo sebuleni kuondoa vipande vipande vya glasi aliyoirusha jana kumpiga nayo adui yake baada ya kumnyooshea bastola. Akafuta na zile damu chache zilizokuwa pale sakafuni.
* *
“Baba yule mtu sio wa kumuendea hovyo hovyo. Inahitaji kama akifuatwa basi watu wawe wamejipanga" Atu alimuambia baba yake hivyo baada ya kuwahadithia kilichomkuta kwa TSSI 01.
“Na ndio maana jana nikasema niende mimi kwasababu nililijua hilo" Ata aliongea.
“Kwahiyo nyie mnashauri vipi? Kwasababu nilazima afe kivyovyote vile. Anavyoonekana ni kikwazo kwenye mambo yetu na mimi bado kabisa sijaanza kufanya lolote kwa yote niliyoyapanga" Mr Hanein aliongea.
“Itabidi tumteke tumlete humu aje kufia humu humu" Kijana mmoja kati ya wale wawili walioletwa kuja kutoa msaada aliongea.
“Atatekwaje?" Mr Hanein alimuuliza.
“Nitakwenda na huyu mwenzangu. Mtu mmoja hawezi kutushinda wote wawili" Yule jamaa aliongea. Kisha wazo hilo likaungwa mkono na yule mwenzake.
“Sawa. Basi inabidi nyie muwape muongozo hawa wenzenu wajue wapi pa kunzia" Mr Hanein aliongea kuwaambia wanae.
Baada ya mpango huo kupitishwa. Wakawapa maelekezo ya wapi pa kumpata. Bahati mmoja kati ya wale wawili ni nwenyeji katika jiji hilo. Kwahiyo haikuwapa tabu kupajua. Zoezi hilo lilipokamilika. Ukasubiriwa muda ili litendeke.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Majira ya saa saba mchana. TSSI 01 alikuwa nyumbani kwake akiwasiliana na kitengo chake ili kuwapa taarifa ya alipofikia katika ‘mission’ hiyo. Baada ya kuwasiliana nao. Akatoka nje na kupanda kwenye gari lake. Akatoka hapo na kwenda nyumbani kwa Mzee Ganjo. Huko alikaa nusu saa na kuondoka hapo.
Safari yake iliishia Mkwabi SuperMakert. Huko alienda kununua vitu vya nyumbani kwake. Alifanya manunuzi kwa dakika ishirini, kisha akatoka na mfuko mkubwa uliokuwa na vitu alivyo nunua ndani yake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment