Simulizi : I Died To Save The President
Sehemu Ya Nne (4)
I DIED TO SAVE MY PRESIDENT
Saa kumi na mbili na dakika sita iliwakuta akina Elvis nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakiwa wamefika kumpokea Omola anayetokea nchini Afrika kusini.Ndani ya gari alikuwemo Steve,Vicky na Elvis ambaye kwa jioni hii alitumia ule mtindo wake wa kujibadili mwonekano kwa kuongeza ndevu bandia na kuvaa kofia ya mzunguko na miwani.Haikuwa rahisi kumtambua kama ni Elvis.Steve na Vicky wakashuka garini na kwenda katika sehemu ya kusubiri abiria wanaowasili Elvis akabaki garini Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ambayo hufanya safari zake kutoka Dar es salaam na Johanesburg ilitua na abiria wakashuka miongoni mwao akiwemo Omola.Alikamilisha taratibu za uhamiaji na kuruhusiwa kuingia nchini.Vicky ambaye ndiye aliyekuwa akimfahamu alielekeza macho yake katika mlango wanakotokea abiria na mara akamuona Omola akiwa amevaa suti nyeusi akamfuata "Mhh!! akaguna Steve baada ya kumuona Vicky akisalimiana na Omola Operesheni hii mbona inanikutanisha na visura namna hii.Nilidhani Vicky ni mzuri kupita wote lakini huyu Omola ni kiboko.Ana uzuri wa aina yake" akawaza Steve "Omola huyu ni mwenzangu anaitwa Steve na vile vile kuna mwingine yupo garini utamfahamu anaitwa Elvis" Vicky akafanya utambulisho "Karibu sana Tanzania Omola" akasema Steve "Ahsante sana Steve.Nashukuru kukufahamu" akasema Omola kwa sauti laini iliyopenya masikioni mwa Steve kama kinanda.Steve akakokota mabegi mawili ya Omola hadi katika gari akamfungulia mlango na Omola akaingia garini "Omola huyu ndiye Elvis niliyekuambia kwamba utamkuta garini.Huyu ndiye kiongozi wetu mimi na Steve.Elvis huyu ndiye Omola Otola" "Omola nafurahi kukutana nawe.karibu sana Tanzania" akasema Elvis "Ahsante sana nimekwisha karibia" akasema Omola na Vicky aliyekuwa katika usukani akaondoa gari.Tayari kiza kilikwisha ingia na moja kwa moja wakaelekea Maasai 5 star hoteli . ************* Graca na Winnie walibaki nyumbani peke yao baada ya akina Elvis kuondoka kwenda kumpokea Omola. "Siamini kama ile ndoto yangu leo imetimia.Elvis amekubali kuwa mpenzi wangu!! akawaza Graca akiwa jikoni akiandaa chakula cha usiku "Ninajiona mwenye furaha kuliko wanawake wote wa dunia hii.Kumpata mwanaume kama Elvis si jambo dogo.Ni mwanaume mwenye kila aina ya sifa nzuri.Ni mzuri wa sura,ana roho nzuri,anajali na zaidi sana kitandani amehitimu shahada ya uzamivu.Mchaka mchaka alionikimbiza leo sijawahi kuuona.Siwezi kukubali Elvis anitoke mikononi mwangu.Leo amenionjesha asali lazima nichonge mzinga.Lazima nihakikishe baada ya operesheni hii kumalizika mimi na yeye tunakuwa pamoja.Lazima awe wangu milel........." Graca akaondolewa mawazoni na sauti ya Winnie aliyemuita " Unasemaje Winne? "Graca mimi ninaondoka siwezi kuendelea kukaa ndani ya jengo hili kama mtumwa.Watu hawa ni wabaya sana na siwezi kuwaamini hata kidogo" "Unaondoka?!!Graca akashangaa "Ndiyo ninaondoka zangu" Hapana usifanye hivyo Winnie.Subiri hadi dada yako atakaporudi ndipo ufanye maamuzi ya kuondoka" "Siwezi kumsubri kwani dada hawezi kuniruhusu kuondoka hapa.Hii ni nafasi nimepata lazima niitumie vyema.Nisipoondoka sasa siwezi kuondoka tena.Siwezi kukaa humu nikifugwa kama kuku nikizuiwa hata kutumia simu yangu.Siyawezi maisha ya namna hii.Kuishi ndani ya nyumba hii ni zaidi ya kuishi gerezani" "Winnie sikushauri uondoke kwani huko nje si salama kwenu.Dada yako amekubali mje kuishi hapa kwa sababu za kiusalama hivyo utakapotoka hapa utahatarisha maisha yako mwenyewe.Tafadhali subiri hadi watakaporejea na kama kuna tatizo lolote uwaeleze watakusikia na kukusaidia kuliko kuchukua maamuzi ya kuondoka" "I don’t care.Litakalonipata na linipate ila nikiwa nje ya nyumba hii.Kwanza dada amenificha siku zote kuhusu kazi anazofanya na jana tu ameua mtu.Sitaki kuwa karibu naye nitakwenda kutafuta maisha yangu mwenyewe.Graca tafadhali naomba ukanifungulie geti niende zangu" akasema Winnie.Graca hakumjibu kitu akabaki akimtazama "Graca naomba ukanifungulie geti niende zangu" "Hapana Winnie siwezi kukufungulia na kukuacha uondoke.Ni hatari huko nje si salama kwako"akasema Graca na winnie akatoa kisu akakunja sura "Nenda kanifungulie geti Graca ama sivyo nitakumaliza.Tuepushe shari.Nifungulie geti niende zangu" akasema Winnie huku akimsogelea Graca.Kwa nguvu Graca akamsukuma Winnie akaanguka chini halafu akatoka mbio akaenda chumbani kwake akajifungia.Winnie akainuka akachukua sanduku lake na kutoka akaelekea getini akapanda juu ya pipa kuu kuu akalirusha begi lake nje akapanda geti na kuanza kushuka taratibu akajiachia na kuanguka kama furushi.Alichubuka mguuni,hakujali akasimama na kuchukua begi lake akaondoka "Kamwe siwezi kukaa nyumba moja na hawa mashetani.Huu ni wakati wa kulipiza kisasi kwa ukatili walionifanyia.Walinichoma na umeme wakati sijawakosea chochote.Kama haitoshi walitakakuanza kunibandua kucha zangu.Hawa jamaa ni makatili mno na dada hapaswi kabisa kuwaamini.They are monsters!! akawaza Winnie akiwa na hasira kali http://deusdeditmahunda.blogspot.com/**************** Vicky aliegesha gari nje ya Maasai 5 star hoteli.Steve ndiye aliyetangulia kushuka akahakiki usalama halafu wengine wote wakashuka na kuelekea ndani.Tayari chumba cha Omola kilikwisha andaliwa na hivyo akapelekwa moja kwa moja katika chumba chake.Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye kujitosheleza.Kulikuwa na sebule kwa ajili ya maongezi na kupumzika vile vile kukawa na chumba cha chakula bila kusahau bafu na choo.Kwa kuwa wote hawakuwa wamepata chakula cha usiku ikawalazimu kuagiza chakula na kutokana na umahiri wa wapishi wa hoteli hii ndani ya muda mfupi chakula kikawa tayari na kuandaliwa wakaanza kula.Kulikuwa na maongezi na utani wa hapa na pale na Steve ndiye aliyekuwa mzungumzaji mkubwa sana pale mezani.Alikuwa anataka kumsoma Omola ni mtu wa aina gani. "Ninajaribu kumuingiza katika darubini yangu lakini haingii.Sikati tamaa nitamuingiza tu katika kumi na nane zangu"akawaza steve Kisha kula wakaenda sebuleni kwa ajili ya mazungumzo. "Omola kwa niaba ya wenzangu napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kukubali ombi langu la kuja Tanzania.Hili halikuwa ombi langu peke yangu bali letu sote unaotuona hapa tukiongozwa na Elvis"Vicky akaanzisha maongezi na kumpa ishara Elvis aendelee "Kama alivyosema Vicky,wazo la kukuomba uje Tanzania ni la kwetu sote na imetulazmu kufanya hivyo kutokana na operesheni nzito inayotukabili.Mimi na mwenzangu Steve tunafanya kazi katika shirika la ujasusi Tanzania.Tumegundua uwepo wa mtandao unaojishughulisha na biashara haramu ya silaha na waasi wanaopigana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Huu ni mtandao mkubwa na unaohusisha watu wakubwa waliomo katika serikali za Tanzania na Congo.Tumeanza uchunguzi wa kuwabaini watu waliomo katika mtandano huo na tayari kuna watu tunawafahamu lakini tunataka kuuchimba mtandao huu hadi mzizi wake na kisha kuwahakikisha wale wote wanaofanya biashara hii haramu wanafikishwa mbele ya sheria.Miongoni mwa watu ambao tumekwisha wafahamu kuwa wanahusika na biashara hii ni ni mtu mmoja anaitwa brigedia Frank huyu ni mwanajeshi na mwingine anaitwa Pascal ambaye ameuawa jana.Kuna mwingine ambaye tunahisi anaweza kuwa na mahusiano na mtandao huu lakini bado hatuna uhakika naye na huyo ndiye tunayetaka kumchunguza.Huyu ni makamu wa rais wa Tanzania"Elvis akanyamaza kidogo halafu akaendelea "Kazi ambayo tunataka utusaidie kuifanya ni kumchunguza makamu wa rais.Tunataka tufahamu kama ana muunganiko na mtandao unaofanya biashara ya silaha na waasi wa Congo.Tayari mipango imekwisha andaliwa ya wewe kumchunguza.Utajifanya ni mwandishi wa habari za mazingira kutoka nje ya nchi.Utatafuta chombo chochote cha habari kikubwa cha nje ya nchi kinachofahamika tutatengeneza kitambulisho kikionyesha unatoka katika chombo hicho.Kila kitu kimekwisha andaliwa na kesho asubuhi utaianza kazi yako kwa kukutanishwa na makamu wa rais” akasema Elvis “Tunafahamu hili si jambo jepesi lakini tumekwisha chukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha kwamba unakuwa salama.Wewe ni mzoefu katika hizi kazi na tuna uhakika utafanya kila uwezalo kuhakikisha kwamba unapata kile tunachokihitaji kutoka kwa makamu wa rais” akasema Elvis “Nimekusikia Elvis lakini nataka nifahamu mmefahamu vipi kama makamu wa rais anaweza kuwa na mahusiano na mtandao huo wa kuuza silaha?Kuna kitu chochote kilichowafanya muhisi hivyo? Ndiyo.Kuna mambo ambayo yanatufanya tuhisi makamu wa rais anahusiana na mtandao huu wa kuuza silaha.Kwanza kwa kumtumia mkurugenzi wetu aliagiza mimi niuawe kwa kisingizio kwamba nimeingia mahala ambako siruhusiwi kufika.Alidai nimevuka mipaka yangu.Hilo lilitokea baada ya kugundua kuhusu uwepo wa mtandao unaojihusisha na biashara ya silaha.Ili niweze kufanya uchunguzi wangu vizuri ilinilazimu kughushi kifo changu na mpaka hivi sasa wanaamini tayari nimekufa.Haikuishia hapo makamu wa rais akamtaka tena mkurugenzi wetu ahakikishe Pascal ambaye ni mmoja wa vinara wa biashara hiyo ya silaha anauawa.Hakutoa sababu yoyote kwa nini auawe na jana huyo jamaa akauawa.Vicky alishiriki katika tukio hilo na akafahamika kwamba alishiriki na makamu wa rais akamtaka mkurugenzi ahakikishe Vicky anauawa.Kwa bahati nzuri mkurugenzi wetu yuko upande wetu na kila linapotokea suala kama hilo anatushirikisha na tulipopata taarifa hizo tukawahi nyumbani kwahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Vicky na kumuokoa kutoka kwa mtu ambaye alitumwa kwenda kumteka.Matukio hayo yanatufanya tuamini kuwa makamu wa rais anajihusisha na mtandao huu mkubwa wa uuzaji silaha.Tunaamini kuna watu wakubwa katika mtandao huu na makamu wa rais anaweza kuwa mmoja wao hivyo tunataka tupate uhakika.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Kuna mtu moja ambaye naye tunamtafuta ambaye anaonekana ni kiongozi wa mtandao huu anaitwa Deusdedith MM.Katika nyaraka tulizozipata huyu amekuwa akiwasiliana na Brigedia Frank na kumpa maelekezo.Vicky amewahi kumchunguza mtu huyu lakini hakufanikiwa.Ni mtu anayejua sana kujificha na tukifanikiwa kumpata huyu tutakuwa tumefanikiwa sana katika operesheni hii.Huyu anaishi nje ya nchi na anaonekana ndiye anayeongoza mtandao huu akiwa nje ya nchi.Tunataka kuchunguza kama huyu Deus ana mawasiliano pia na makamu wa rais” akasema Elvis “Elvis ahsante kwa maelezo yako ambayo yamenifumbua macho kuhusiana na kile mlichoniitia hapa.Kabla ya yote napenda kuwashukuru kwa mapokezi mazuri na ninapenda kuwahakikishia kwamba nimekubali kwa moyo mmoja kuja kuungana nanyi na kuwasaidia katika kazi yenu.Aliponipigia simu Vicky nilikuwa katika operesheni fulani na nikashindwa kukataa kuja kumsaidia kwani mimi na yeye ni marafiki wakubwa sana na tumekuwa tukisaidiana katika mambo mbali mbali.Kazi hizi ni za kusaidiana huwezi kufanya peke yako na hata mimi siku moja nitakuja kuwaomba msaada wenu na nina hakika hamtanitupa” akasema Omola “Uko sahihi kabisa Omola.Tunashukuru sana kwa kuacha shughuli zako na kuja kutusaidia.Huu ni mwanzo mpya wa mashirikiano makubwa baina yetu na muda wowote utakapohitaji msaada sisi tuko tayari kukusaidia” akasema Elvis “Ahsante sana.Nina waahidi kwamba nitafanya kazi mtakayonitaka niifanye kwa weledi mkubwa na nitafanikiwa kupata kile mnachokihitaji.Kwa pamoja tutahakikisha tunaufagiamtandao huu wa kuuza silaha ambao kupitia kwao mamia ya watu wasio na hatia wamepoteza maisha.Katika maelezo yako Elvis nimekiona kitu fulani na ninaomba mniruhusu nitoe mawazo yangu kama itafaa” “Karibu” akasema Elvis “Nionavyo mimi inawezekana makamu wa rais hana uhusika wa moja kwa moja katika biashara hii ya silaha lakini kuna watu wanamtumia katika kufankisha mambo yao hasa hili la kuua watu ambao wanaonekana ni kikwazo kwao kwa sababu yeye ana nguvu.Wanatumia ofisi yake kufanikisha mambo yao.Kuna huyu mtu umemtaja hapa ambaye ni kinara wa biashara hii ya silaha anaitwa Frank nadhani tungeanza kwanza kuchunguza mahusiano yake na makamu wa rais na kama tukigundua kwamba kuna mahusiano yoyote kati yake na makamu wa rais itatusaidia sana katika uchunguzi wetu.Huyu Frank ni mtu wa kuchunguzwa sana kwa kila kitu na kwa kupitia yeye tutaweza kuufahamu mtandao wake wote.Kuna mipango yoyote mmeiweka ya kumchunguza huyu mtu? Akauliza Omola “Mipango ipo na hata usiku wa leo baada ya kutoka hapa tunakwenda mahala ambako tutapata mambo ambayo yatatusaidia kumfahamu zaidi Frank na mtandao wake.Tunaye mtoto wake ambaye ndiye anayetusaidia katika kupata taarifa za baba yake.Usiku wa leo atatupeleka mahala ambako tutaweza kupata mambo mengi zaidi kuhusiana na Frank na mt………………” Elvis akanyamaza baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni Meshack Jumbo “Mkurugenzi anapiga” akasema na kuipokea “Hallo mzee” “Elvis habari za jioni?Vipi maendeleo yenu? “Tunaendelea vyema mzee.Tuko na Omola tayari amewasili na tuko hapa katika hoteli aliyofikia tunapanga mikakati” Good.Nimeshindwa kuja jioni hii nimebanwa sana na majukumu mengine.Utanijulisha kila kitu kinavyokwenda.Ulinipigia na kuniomba nikusaidie kuhakiki kuhusiana na kifo cha Joseph Mballa mpenzi wa Juliana.Nimefuatilia polisi na wanasema kwamba jalada la mauaji hayo lilifunguliwa lakini hakuna anayejua liliko ama uchunguzi huo uliishia wapi.Kwa ufupi ni kwamba hakukuwa na uchunguzi wowote kuhusiana na kifo hicho” “Inashangaza sana.Kwa nini mauaji ya kinyama namna hii yafanyike bila kufanyika uchunguzi? Akauliza Hii inatuonyesha kwamba kuna kitu hakiko sawa katika mauaji yale.Naamini kwa jibu hili kuna kitu mtakipata ambacho kitawasaidia katika uchunguzi wenu.Kama kuna kitu chochote kile mnahitaji msaada wangu nijulisheni mara moja" "Ahsante sana mzee.Tutawasiliana baaade nitakujulisha mahala tulikofikia kwani usiku huu kuna sehemu tunakwenda ambako tunaweza kupata mambo mengi kuhusiana na Frank na mtandao wake" akasema Elvis na kuagana na Meshack.Elvis akamgeukia Steve ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya Mkurugenzi anadai kwamba hakuna uchunguzi wowote uliowahi kufanyika kuhusiana na kifo cha Joseph.Hata jalada la uchunguzi lililofunguliwa halijulikani lilipo,limepotea" akasema Elvis "Joseph ni nani? akauliza Vicky "Kuna mtu wetu wa karibu sana anaitwa Juliana ambaye ametuomba tumsaidie kufanya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya mpenzi wake pia mdogo wake ambao waliuawa kikatili lakini mpaka sasa hakuna muuaji yeyote aliyepatikana.Taarifa za kutoka polisi hazionyeshi kama kuna uchunguzi wowote uliowahi kufanyika kuhusiana na mauaji hayo.Haya yanaonekana ni mauaji ya kulipiza kisasi.Kitu tunachoweza kukifanya kwa sasa ni kumchuguza mama yake Juliana ili tufahamu anajihusisha na biashara gani haramu na watu gani anaohusiana nao katika biashara hizo na vile vile tuchunguze mahusiano kati yake na wazazi wa Joseph.Tuchunguze pia familia ya Joseph ni familia ya aina gani?Wanajishughulisha na mambo yapi?Tukipata majibu ya maswali haya tutapata picha au kufafahamu nani waliofanya mauaji hayo.Steve ulisema mama yake Juliana anaitwa nani? akauliza Elvis "Anaitwa Elizabeth Mlabwa Mwakyusa" akajibu Steve Omola kwa taarifa alizotupa Vicky ni kwamba wewe ni mdukuaji hatari sana.Naomba utusaidie kumtafuta huyu mwanamama anaitwa Elizabeth Mlilo Mwakyusa.Mwanae ametuambia kwamba huyu mama anajihusisha na biashara haramu lakini hana uhakika ni biashara gani hivyo tunataka tumfanyie uchunguzi.Tunahisi chanzo cha mauaji hayo ni huyu mama au biashara nazoshughulika nazo"akasema Elvis "Anahusiana kwa namna yoyote na mtandao wa kuuza silaha? akauliza Vicky "Hatuna uhakika bado ila tunataka kumfahamu vyema ili tutakapomaliza suala hili la silahabasi tumsaidie Juliana kuwatafuta waliomuua mpenzi wake na mdogo wake." akajibu Elvis Omola akaenda katika chumba cha kulala akafungua moja ya sanduku lake na kutoa kompyuta akarejea sebuleni akaiwasha kisha akaanza kazi ya kumtafuta Elizabeth.Wote walikuwa kimya wakimsubiri amalize shughuli yake ambayo ilimchukua zaidi ya dakika tano "Nimeshindwa kumpata huyo Elizabeth labda ningeweza kuipata picha yake ingeweza kutusadia.Inaonekana huyu mama anatumia jina lingine tofauti na hilo.Watu wa namna hii ambao hutumia majina tofauti tofauti mara nyingi si watu wazuri.Kuna mambo mengi wanayaficha"akasema Omola. "Steve mpigie simu Juliana mwambie akutumie picha ya mama yake" akasema Elvis na Steve akawasiliana na Juliana na bila kuchelewa akamtumia picha ya Elizabeth.Omola akaiingiza katika programu yake na kuanza kuifanyia kazi baada ya dakika nne zikatokea picha nne zinazofanana na Elizabeth "Nimeingia katika kompyuta za shirika la ujasusi la Uingereza ambako mmesema kwamba huyu mama anaishi na nimemtafuta kwa kutumia picha hii tuliyotumiwa.Majibu yanaonyesha kuwa huyu mama anahisiwa kujihusisha na magenge ya Mafia yanayojishughulisha na biashara haramu japo mpaka sasa bado hakuna ushahidi wowote wa kuweza kumtia hatiani kwa tuhuma hizo.Inasemekana anamiliki makasino makubwa katika nchi za Afrika kusini,Uingereza,Italia na Urusi.Ni katika makasino hayo magenge hayo ya mafia hufanyia shughuli zao" "Juliana yuko sahihi kabisa kuhisi kuwa mama yake anajihusisha na biashara haramu na hata mawazo yetu kuwa mauaji ya mwanae Godson yametokana na biashara haramu anazofanya ni sahihi.Magenge ya kimafia hii ndiyo aina yake ya mauaji.Kama tayari Uingereza wamekwisha mtilia shaka huyu mama basi ni mtu hatari na hili si suala dogo wala la kufanyia mzaha hata kidogo.Ni suala zito.Tusubiri kwanza hadi tutakapomaliza suala hilila mtandao wa silaha halafu tutaanza kulishughulikia hilo suala.Ahsante Omola kwa msaada huo mkubwa" akasema Elvis.Waliendelea na majadiliano na ilipofika saa nne kasorobo Elvis akawataka waondoke wakaendelee na mambo mengine wamuache Omola apumzike kwa ajili ya kuanza shughuli yake kesho "Elvis nimekuja hapa kikazi hivyo ninaomba kuongozana nanyi huko mnakoenda" akaomba OmolaOmola umechoka kwa safari ndefu na kesho utakuwa na kazi nyingine hivyo endelea kupumzika na sisi tutaimaliza kazi hii tunayokwenda kuifanya" "Tafadhali naomba na mimi niongozane nanyi huko mnakoenda.Nitaboreka sana nikibaki hapa peke yangu wakati wenzangu wanakwenda kupambana.Niruhusuni niongozane nanyi tafadhali" akazidi kuomba Omola "Ok fine.Jiandae twende" akasema Elvis na wote wakaingia garini wakaondoka ******************* Winnie alitembea haraka haraka na kwa tahadhari kubwa huku akiangaza kila upande kuona kama kuna mtu anamfuatilia.Hakuna aliyemjali kwani kila mmoja alikuwa na mambo yake.Baada ya mwendo wa dakika kumi na tano akatokea katika baa kulikokuwa na taksi zimeegeshwa.Akamfuata dereva taksi mmoja na kumuelekeza ampeleke nyumbani kwao "Leo ni mwisho wa wale mashetani.Dada pia lazima aachane na kazi hizi za hatari.Ana pesa nyingi sana kwa nini aendelee kufanya kazi kama hizi?Kwa nini ameingia katika uuaji? Sikutegemea kabisa kama dada Vicky anaweza kujihusisha na mambo kama haya.Kama aliamua kujiingiza katika masuala haya wakati hana fedha hivi sasa tayari ni tajiri anapaswa aachane na kazi hizi.Haipendezi hata kidogo pamoja na utajiri wake wote lakini hivi sasa anaishi kama ndege.Hana amani na kila wakati anahisi anatafutwa kuuawa.Mimi pia nimeingizwa katika maisha hayo ya kukimbia kimbia.Siwezi kukubali kuishi maisha kama ya kunguru.Nitafanya kile niwezalo kwanza kumsaidia dada na pili kulipiza kisasi kwa wale jamaa walionitesa hasa yule aliyenichoma na umeme bila huruma.Kitendo kile kila nikikumbuka kinaniumiza mno.Sikuwa nimewafanyia jambo lolote baya hadi wanitese kiasi kile.Huu utakuwa mwisho wao na mwisho wa dada kufanya kazi zake hizi za hatari" akawaza Winnie akiwa garini na kumkumbuka Graca "Namshangaa sana yule Graca kwa kukubali kukaa mle ndani kama mateka.Anaishi kama mfungwa hatoki nje anajifungua tu ndani.Amenieleza historia ya maisha yake inasikitisha amepitia mambo mengi magumu lakini hawa jamaa wanazidisha ugumu zaidi katika maisha yake.Wanamtumia tu na hawatamsaidia kwa lolote.Halafu nimegundua kitu,Graca na yule jamaa Elvis wana mahusiano ya kimapenzi kwani mchana wa leo wameitana na kujifungua chumbani kwa takribani saa nzima na Graca aliporejea alikuwa amechoka akaoga na kulala.Yule jamaa ana tabia chafu sana.Lazima nimuokoe Graca naye atoke katika mikono ya wale jamaa ambao hawatamsaidia lolote zaidi ya kumuharibia maisha yake.Wale jamaa ni wanyama sana ninawachukia mno na leo utakuwa mwisho wao" akaendelea kuwaza Winnie Alifikishwa nyumbani kwao akamlipa dereva na kuingia ndani ambako mtumishi wao wa ndani alifurahi sana kumuona.Winnie hakutaka maongezi naye akaenda chumbani kwake akajifungia halafu akawasha simu yake na kuziandika namba za simu za Frank alizozitoa katika simu ya dada yake akapiga simu ikaita na kupokewa na sauti nzito "Hallow" ikasema sauti nzito ya mwanaume "Hallow nazungumza na nani tafadhali?akauliza Winnie "Wewe umempigia nani? akauliza mtu yule kwa sauti kali kidogo "Ninataka kuzungumza na brigedia Frank." "Ndiye mimi.Wewe ni nani? "Naitwa Winnie.Ni mdogo wake Vicky nadhani unamfahamu" "Ndiyo ninamfahamu.Unataka nini Winnie? "Nahitaji kukuona mzee" kuniona?!! Frank akashangaa 'Ndiyo mzee nahitaji kukuona" "Kuna nini? Nani kakutuma unitafute,Vicky? "Hakuna aliyenituma bali nimelazimika mimi mwenyewe kukutafuta.Nina jambo kubwa ambalo nahitaji kukueleza wewe mwenyewe ana kwa ana" "Jambo gani hilo?Huwezi kunieleza katika simu hadi tuonane? "Ni kuhusiana na dada yangu vile vile mwanao Graca" "Graca?!! Frank akastuka "Ndiyo" "Umemfahamuje Graca?Umejuaje kama ni http://deusdeditmahunda.blogspot.com/mwanangu?Nimeonana naye na ninafahamu mahala alipo" akasema Winnie na kupitia spika ya simu Frank akasikika akivuta pumzi ndefu "Uko wapi sasa hivi? akauliza "Niko nyumbani kwetu" "Mimi niko msibani sasa hivi.Ninakuja hapo nyumbani kwenu muda si mrefu.Vicky yuko hapo? "Hapana usije hapa nyumbani ni hatari hapafai kwani ninaamini hivi sasa watakuwa wananitafuta na sehemu ya kwanza kuja watakuja hapa nyumbani.Nielekeze nikufuate wapi? "Toka hapo nyumbani nenda hadi Ashanti Club halafu subiri hapo nitakupa maelekezo" akasema Frank na kukata simu "Wale mashetani lazima walipe uovu wao.Walinitesa sana na kitendo kile hakiwezi kuachwa hivi hivi.They must pay !! akawaza Winnie huku akitoka chumbani kwake akaenda chumbani kwa dada yake akachukua funguo ya moja wapo ya magari akatoka kuelekea Ashanti Club kama alivyoelekezwa na Frank "Dada atanilaumu sana kwa hiki ninachokifanya lakini ni kwa faida yake mwenyewe.Wale jamaa anaoshirikiana nao si watu wazuri hata kidogo.Anapaswa kuachana nao kabisa na aachane na shughuli hizi za kipelelezi.Ninataka pia kumsaidia Graca aweze kutoka ndani ya nyumba ile anamofungwa na kugeuzwa mtumwa wa ngono.Wale jamaa watamuharibia maisha yake" akawaza Winnie akionekana kuwa na uso uliojaa hasira kali Alifika Ashanti Club moja wapo ya kumbi kubwa za burudani na usiku huu kulikuwa na onyesho la bendi,akaelekea maegesho halafu akampigia simu Frank. "Tayari nimefika hapa Ashanti" "Good.Washa na kuzima taa kubwa mara tatu" akaelekeza Frank na Winnie akafanya kama alivyoelekezwa "Good.Usitoke garini hadi nitakapokupa maelekezo" akasema Frank na kukata simu.Baada ya dakika nane hivi akampiga simu "Kuna mtu atakuja kugonga kioo cha gari,shuka mfuate.Usimuulize chochote" Hazikupita dakika mbili akatokea mtu akagonga kioo cha gari na kugeuka,Winnie akafungua mlango wa gari na kutoka akamfuata hadi katika gari aina ya Prado lenye rangi nyeusi wakaingia na ndipo Winnie akastuka baada ya kuitambua sura ya yule mtu. "You ?!!! akauliza kwa mshangao.Yule mtu alikuwa ni Obi yule aliyewavamia mchana nyumbani kwao No questions please !! akasema yule jamaa kwa sauti kali "Huyu jamaa ndiye yule aliyetuvamia mchana wa leo.Ana mahusiano na Frank? Au ndiye Frank mwenyewe? akajiuliza akiwa na woga mkubwa "Unanipeleka wapi? akauliza "Nimekwisha kwambia kwamba sitaki maswali!! akasema Obi Walifika Tarakea Supermarket akakata kona wakaingia hapo "Usitoke ndani ya gari.Unahitaji nikuletee nini? "Nothing" akajibu Winnie na Obi akashuka garini akaingia ndani.Alikaa humo ndani kwa dakika kumi na Winnie akastuka baada ya mlango kufunguliwa ghafla Obi akaingia garini akamrushia pakiti ya chokolate akawasha gari na kuondoka.Hawakusimama kokote hadi walipofika katika jumba moja kubwa wakafunguliwa geti wakaingia.Obi akamtaka Winnie ashuke wakaingia ndani "Wewe ndiye Frank? akauliza winnie "Hii ni mara ya mwisho ninakuonya kwamba sitaki maswali" akasema Obi na kuchukua simu yake akamjulisha Frank kuwa tayari wamefika.Baada ya dakika kumi Frank akawasili *******************
Akina Elvis waliwasili katika makazi yao wakiwa wameongozana na Omola.Steve akashuka na kwenda kubonyeza kengele ya getini na zikapita dakika tatu bila mtu kujitokeza kuja kufungua geti.Akabonyeza tena wakasubiri kwa muda bila mtu yeyote kutokea. "Yawezekana Graca amelala kiasi cha kutokusikia kengele ikilia? akauliza Steve "Si kawaida ya Graca kupitiwa na usingizi kiasi hiki hasa tusipokuwepo.Mara nyingi huwa macho hadi pale turudipo" akasema Elvis na kumtaka Steve apande ukuta aingie ndani akafungue geti.Haraka haraka Steve akapanda kama paka na kurukia ndani akafungua geti wakaingia ndani.Kulikua na ukimya mkubwa mle ndani na walipojaribu kufungua mlango wa sebuleni ulikuwa umefungwa.Elvis akagonga mlango lakini hakukusikika hata nyayo za mtu akitembea ndani "Huu si usingizi wa kawaida.Graca hana kawaida ya kulala namna hii" akasema Elvis na kutoa vitu fulani mithili ya funguo akaufungua mlango ule wa sebuleni wakaingia ndani. "Graca ! akaita Elvis lakini hakujibiwa "Graca ! akaita tena lakini bado kukawa kimya Steve akatoa bastora yake kwani walihisi hatari.Kwa tahadhari kubwa wakaelekea katika mlango wa chumba cha Graca ambacho kilikuwa kimezimwa taa "Graca ! akaita Elvis na taratibu kukasikika sauti ya funguo ikichomekwa katika kitasa na mlango ukafunguliwa "Uuuph ! Elvis akashusha pumzi baada ya kumuona Graca "Umetupa wasi wasi sana Graca tayari tulikwisha anza kuhisi hatari.Imekuaje leo umepitiwa na usingizi kiasi hicho? akauliza Elvis "Sikuwa nimelala,nilikuwa nimejificha nikiogopa" "Kuogopa?Unaogopa nini wakati nimekwisha kuhakikishia kwamba nyumba hii ni salama? Nimeogopa labda Winnie anaweza akawaeleza watu kuhusiana na sisi kuwepo hapa" "Winnie?akauliza Vicky "Ndiyo Winnie ameondoka" Watu wote wakatazamana.Walipatwa na mshangao "Ameondokaje? "Mlipoondoka tu naye akasema anaondoka hawezi kuendelea kukaa humu ndani kama mfungwa" "Kwa nini ukamuacha akaondoka Graca? akauliza Vicky "Alinitishia kunichoma kisu ili nimfungulie geti lakini sikuwa tayari nikamsukuma akaanguka na mmi nikakimbia hadi chumbani nikajifungia.Nilipotoka baadae hakuwepo.Inawezekana alipanda ukuta akaruka nje kwani geti halikufunguliwa" "Jamani mdogo wangu !! akasema Vicky kwa wasi wasi "Tulia Vicky usihofu.Tutafanya kila tuwezalo kumpata Winnie" akasema Elvis "Elvis watu wanaonitafuta wakimpata Winnie watamtumia kama fimbo ya kunichapia kwani watanilazimisha nifanye kile wakitakacho.Tafadhali Elvis nisaidieni nimpate mdogo wangu" "Nini kimetokea hapa? akauliza Omola ambaye hafahamu kiswahili sawa sawa.Elvis akamsimulia kile kilikuwa kimetokeaHilo si tatizo tunaweza kufuatilia na kujua mahala alipo.Naomba namba zake za simu" akasema Omola na kuiwasha kompyuta yake akafungua programu fulani na baada ya muda ukaonekana mduara mwekundu "Nimempata ! akasema Omola huku akitabasamu na wote wakamsogelea "Hapa ndipo alipo kwa sasa" akasema Omola na kubonyeza bonyeza zaidi na kompyuta ikamuelekeza mahala alipo Winnie "Ahsante sana Omola.Endelea kumfuatilia Winnie na baada ya kutoka huko mahala tunakotaka kwenda usiku huu tutamfuata huko aliko na kumchukua" akasema Elvis akaelekea chumbani kwake na kurejea akiwa na sanduku la silaha aliloletewa na Meshack Jumbo akaliweka mezani na kuwaacha wenzake wakichagua silaha yeye akamtaka Graca wakazungumze pembeni "Graca muda ndio huu wa kutimiza ile ahadi yako.Usihofu utakuwa salama.Sote tumejiweka tayari kukulinda wewe pekee hivyo ndoa hofu na endapo tukipata jambo lolote la kutusaidia katika uchunguzi wetu tutakuwa tumerahisisha sana kazi na utakuwa huru muda si mrefu" akasema Elvis "Elvis mimi sina tatizo nitawapeleka mahala ambako mtafahamu mambo mengi kuhusu baba na mambo yake anayoyafanya lakini naomba uniahidi tena kwamba ile ahadi yako ya kuwa na mimi utaitimiza" "Usiogope Graca nimekwisha kuahidi kukupa kila unachokihitaji.Nimekudhihirishia hilo mchana wa leo na tutaendelea kufurahi kila siku kila pale utakapohitaji" akasema Elvis "Ahsante sana Elvis.Ninakupenda mno zaidi ya ninavyoweza kukueleza.Naomba usiuvunje moyo wangu" akasema Graca na kumbusu Elvis "It's time.Jiandae tuondoke" akasema Elvis Dakika tano baadae wote walikuwa tayari na safari ikaanza.Ni Graca pekee aliyefahamu mahala walikokuwa wanaelekea WINNIE NDUGU MDOGO WAKE VICKY ANAKUTANA NA BRIGEDIA FRANK,ANATAKA KUMUELEZA NINI?WAKATI HUO HUO GRACA ANAWAPELEKA AKINA ELVIS MAHALA ANAKOPAFAHAMU YEYE ILI KUPATA MAMBO MUHIMU YANAYOHUSIANA NA BABA YAKE JE WATAFANIKIWA KUPATA WANACHOKITAFUTA? MCHAKATO WA MAPINDUZI UNASHIKA KASI WANASIASA TAYARI WAMETANGAZA KUFANYIKA KWA MKUTANO WA HADHARA BILA KIBALI KWA LENGO LA KUANZISHA VURUGU KUBWA JE WATAFANIKIWA LENGO LAO? JULIANA ANAAMUA LIWALO NA LIWE LAZIMA WAUAJI WA MPENZI WAKE NA MDOGO WAKE WAJULIKANE,JE WATAFANIKIWA KUWAPATA?MAMA YAKE ATAGUNDUA? MAJIBU YA MASWALI HAYA NA MENGINE MENGI USIKOSE SEHEMU YA MWISHO YA SIMULIZI HII
Usiogope Graca nimekwisha kuahidi kukupa kila unachokihitaji.Nimekudhihirishia hilo mchana wa leo na tutaendelea kufurahi kila siku kila pale utakapohitaji" akasema Elvis "Ahsante sana Elvis.Ninakupenda mno zaidi ya ninavyoweza kukueleza.Naomba usiuvunje moyo wangu" akasema Graca na kumbusu Elvis "It's time.Jiandae tuondoke" akasema Elvis Dakika tano baadae wote walikuwa tayari na safari ikaanza.Ni Graca pekee aliyefahamu mahala walikokuwa wanaelekea ENDELEA..............................Obi una hakika hakuna yeyote aliyekuwa anamfuatilia huyu msichana wakati unamleta hapa? akauliza Frank baada ya kuwasili mahala alipomuelekeza Obi ampeleke Winnie "Hakuna mkuu.Nimekuwa makini sana kuhakikiha hakuna yeyote anayemfuatilia.Nimechukua kila aina ya tahadhari kabla ya kufika hapa na kujiridhisha kuwa hakuna hatari yoyote"akasema Obi "Unamuonaje huyu msichana? Anasema ukweli au ametumwa kama mtego?kwa sababu simuamini tena Vicky" akasema Frank "Kwa namna nilivyomchunguza anaonekana kweli ana shida ya kuonana nawe.Sina hakika sana kama ametumwa" akasema Obi "Kabla sijaenda kuzungumza naye nataka ukahakikishe kwamba hana kifaa chochote cha kuweza kunasa au kurusha maongezi yangu naye.Siku hizi teknolojia imekua kubwa, nina wasi wasi yawezekana amefungwa kifaa maalum cha kunasa mazungumzo yetu.Nenda kamchunguze umuhakiki kama hana kifaa chochote.Hata simu yake pia ichukue na uizime kabisa hadi nitakapomaliza mazungumzo naye" akasema Frank na Obi akarejea sebuleni aliko Winnie. "Frank yuko wapi? akauliza Winnie "Inuka! akaamuru Obi "Unataka kunipeleka wapi? akauliza Winnie "Stand up!! akasema Obi kwa ukali na Winnie akasimama na Obi akaanza kumpapasa kuona kama kuna kifaa chochote amekivaa kinachoweza kunasa maongezi yake na Frank.Winnie hakupendezwa na kitendo kile akamsukuma Obi "Sikiliza we msichana,ukitaka mambo yako yafanikiwe usiwe na kiburi.Niache nifanye kazi yangu ama sivyo hautapata unachokitaka" akasema Obi na kuendelea kumkagua Winnie.Alipohakikisha hakuna kifaa chochote alichokuwa nacho akaichukua simu yake halafu akamfuata Frank "She's clean.Hana kitu chochote kibaya na simu yake hii hapa nimeichukua" akasema Obi na kumkabidhi Frank simu ya Winnie "Thanks.Hakikisha eneo hili ni salama wakati ninakwenda kuzungumza na huyu msichana" akasema Frank na kuingia ndani.Winnie alipomuona Frank akiingia mle ndani akaogopa na kusimama "Winfrida tafadhali keti" akasema Frank "Shikamoo" akasema Winnie kwa uoga "Marahaba.Hujambo Winnie? "Sijambo" "Winnie nina mambo mengi ya kufanya hivyo fanya haraka nieleze kile unachotaka kunieleza" akasema Frank "Wewe ndiye Frank? "Ndiye mimi.Una wasi wasi? "Hapana umefanana na mwanao Graca" "Haya nieleze kilichokuleta hapa" akasema Frank ambaye alionekana kutokutaka mazungumzo marefu "Mzee kama nilivyojitambulisha simuni kuwa ninaitwa Winnie mimi ni mdogo wake Vicky.Nimelazimika kuja kukuona kwa ajili ya kuzungumza nawe mambo mawili makubwa" akanyamaza akamtazama Frank aliyekuwa amemkazia macho akimtazama kwa makini sana halafu akaendelea "Jambo la kwanza ni kuhusiana na dada yangu Vicky.Kabla sijasema lolote nataka kufahamu kitu kimoja.Huyu jamaa aliyenileta hapa alituvamia asubuhi nyumbani,wewe ndiye uliyemtuma? Frank akatabasamu kidogo halafu akasema "Winnie tafadhali naomba usipoteze wakati wangu.Nieleze kile ambacho umeniitia hapa.Huruhusiwi kuuliza chochote! akasema Frank aliyeonekana kukasirishwa na swali lile la Winnie "Samahani mzee.Kitu cha kwanza ambacho kimenileta hapa ni kuhusiana na dada yangu Vicky.Amenieleza kwamba unamtafuta umuue na baada ya kumuona huyu jamaa aliyetuvamia asubuhi yuko hapa ninaamini ni kweli unamtafuta dada umuue.Kwa nini unataka kumuua dada yangu?akauliza Winnie "Nani kakwambia ninamtafuta dada yako? Frank akauliza "Dada mwenyewe amenieleza hivyo" "Amekudanganya.Vicky ni rafiki na mtu wangu wa karibu sana kwa nini nimtafute au nitume mtu akamteke? akauliza Frank "Kwa nini hutaki kunileza ukweli Frank?Ninafahamu kila kitu kinachoendelea kati yako na dada na ndiyo maana niko hapa kutafuta suluhu" akasema Winnie na Frank akatabasamu Nimeupenda ujasiri wako.Nini unakifahamu kuhusu mimi na dada yako? "Everything" akajibu Winnie na Frank akavuta pumzi ndefu "Ok tell me everything you know" akasema Frank "Nitakwambia kila kitu ila na mimi kuna sharti moja nataka litekelezwe" "Winnie nadhani haufahamu unazungumza na nani.Unazungumza na mtu mkubwa na si mwanafunzi mwenzako hivyo jaribu kuwa na adabu na ueleze kile kilichokuleta hapa.Wewe si wa kunipa mimi sharti lolote.Dada yako mwenyewe ananifahamu vyema mimi ni nani na ananiheshimu.Nakupa nafasi ya mwisho uweze kueleza kile kilichokuleta hapa"akasema Frank Frank nimesema hivyo kwa sababu ninayo mambo ambayo hutaamini nikikueleza na ambayo yatakuwa na msaada mkubwa sana kwako.Siwezi kukueleza mambo hayo muhimu bila na mimi kutimiziwa kile ninachokitaka" "Unahitaji nini? akauliza Frank baada ya kufikiri kidogo "Ninahitaji umuache dada yangu.Acha kumfuata na umuache afanye shughuli zake kwa amani.Leave her alone! akasema Winnie na Frank akaangua kicheko "Umenifanya nicheke Winnie ila naomba nikufahamishe kitu kimoja"akanyamaza na kumtazama "Vicky ni rafiki yangu na mtu wangu wa karibu sana lakini kuna jambo amelifanya ambalo limeniudhi na kunifanya nimsake kila kona ili anieleze kwa nini amefanya vile,hivyo basi siwezi kumuacha hivi hivi hadi atakaponieleza ukweli"akasema Frank "Nafahamu unachomtafutia dada ni kuhusiana na kifo cha Pascal" akasema Winnie na Frank akamtazama kwa makini akashindwa aseme nini.Baada ya muda akauliza "Unamfahamu Pascal?Umefahamuje kuhusu kifo chake? "Nilikwambia kwamba nina fahamu kila kitu hivyo tulia nisikilize"akasema Winnie na kunyamaza kidogo kisha akaendelea "Unamuhusisha dada na kifo cha Pascal.Ni kweli yeye ndiye aliyemuita pale hotelini"akanyamaza tena na kumtazama Frank ambaye alikaa vizuri ili kumsikiliza Winnie kwa makini "Endelea Winnie" akasema Frank "Dada hakufanya vile kwa kupenda bali alilazimishwa kufanya vile.Alitekwa na watu fulani ambao walimlazimisha afanye wanavyotaka na kama angekataa basi wangenidhuru mimi.Nadhani unafahamu kuwa dada anajihusisha na mambo ya ukahaba hivyo mmoja wa watu hao alijifanya kumtaka kimapenzi na ndipo walipomteka na kumlazimisha amuite Pascal pale hotelini.Kwa kutumia simu ya dada walinipigia simu na kunidanganya kuwa dada amepata ajali na anahitaji kuniona nikawaelekeza nyumbani mahala nilipo akaja mmoja wao http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kunichukua na kumbe hakukuwa na ajali yoyote aliyoipata dada bali walitaka kunitumia kumlazimisha dada afanye vile watakavyo.Kwa kuwa dada yangu ananipenda sana hakuwa na na njia nyingine zaidi ya kukubali matakwa ya wale jamaa ambao kitu kikubwa walichokuwa wanakihitaji ni kumpata Pascal.Walifahamu kuwa Pascal na dada ni marafiki hivyo wakamtaka dada ampigie simu na kumtaka afike pale hotelini na dada akafanya hivyo akawasiliana na Pascal na kumtaka afike pale hotelini" akanyamaza na kumtazama tena Frank halafu akaendelea "Pascal alifika pale hotelini na wakafanikiwa kumuweka chini ya ulinzi lakini kabla hawajamfanya chochote dada akataka kupambana nao wale jamaa na Pascal naye akaitumia nafasi hiyo kupambana nao lakini wakawazidi nguvu na katika mapambano hayo Pascal akapigwa risasi akafa.Tukachukuliwa mimi na dada na kupelekwa sehemu fulani wakaanza kumtesa dada wakimtaka awaeleze mahala ulipo.Dada aligoma kusema chochote na ndipo wakatisihia kunitesa endapo hatawaeleza.Bado dada alikuwa mgumu kuwaeleza chochote na ndipo walipoanza kunitesa ili kumlazmisha dada afanye wanavyotaka.Walinitesa sana kwa kunichoma na umeme na walipoona bado dada amekuwa mgumu wakataka kuanza kunibandua kucha za vidole ndipo dada akawaomba wasifanye hivyo atawaeleza wanachokitaka.Akawadanganya kwamba atawasaidia ili waweze kukupata.Akawaeleza kuwa anayo namba maalum ambayo huwa anawasiliana nawe na ambayo iko chumbani kwake na kulipopambazuka wakatupeleka nyumbani.Dada akiwa katika harakati za kutafuta namna ya kutoroka akatuvamia yule jamaa ambaye naamini ulimtuma na hapo yakatokea ,mapigano kati yake na m,moja wa wale jamaa anayeitwa Steve na mtu wako aliposhindwa akakimbia.Steve akaturejesha tena kule katika nyumba yao na dada akawaahidi kwamba atawapeleka mahala ambako anaamini watakupata na usiku huu wamemchukua kuelekea huko.Kwa bahati nzuri walisahau kufunga mlango na mimi nikatoroka" akasema Winnie na Frank akavuta pumzi ndefu akamtazama Winnie kwa macho makali yaliyojaa hasira "Nani amekutuma uje unieleze mambo haya?! akauliza kwa ukali "Nimekwisha kueleza kwamba hakuna mtu yeyote aliyenituma bali nimekuja mimi mwenyewe ili kutafuta msaada kwa dada yangu.Frank,dada yangu hana kosa alitumiwa na hawa jamaa ili kumpata Pascal na kwa sasa wamegeuka wanakutafuta wewe.Hivi tuongeavyo wameelekea mahala ambako dada amewapeleka ambako wanaamini watakupata.Nimekuja kukueleza haya yote ili kutafuta msaada.Kwanza kumukoa dada yagu kutoka katika mikono ya wale jamaa na pili kuhakikisha wale jamaa wanapatikana" "Who are they? Unaweza kuwaelezea muonekano wao? "Watu hao wako wawili tu na majina yao ni Steve na Elvis" Mstuko alioupata Frank ulikuwa mkubwa sana.Alihisi mwili ukimtetemeka "Rudia tena umesema majina yao ni akina nani? "Mmoja anaitwa Steve.Huyu ndiye aliyekuja kunichukua nyumbani.Mwingine anaitwa Elvis na huyu ndiye aliyekuwa ananitesa akimlazmisha dada afanye wanachokitaka.Ni mtu mkatili sana" akasema Winnie "No! it's not true.Haweze kuwa ni Elvis yule ambaye tulimuua.Huyu atakuwa ni Elvis mwingine kabisa" akawaza Frank "Frank" akaita Winnie baada ya kumuona Frank amebadilika ghafla "Ninahitaji sana msaada wako kumuokoa dada kutoka katika mikono ya wale jamaa ambao hawana mpango wa kumuachia huru.Wataendelea kumtumia ili kufanikisha mipango yao mbali mbali na mwisho watamuua" "Nni hasa ambacho hawa jamaa wanakitafuta?Unaweza kufahamu ? "Nilivyowasikia wale jamaa walikuwa wanaongelea masuala ya silaha lakini sikujua ni silaha zipi hizo ila inaonekana wanachokitafuta ni kuhusiana na masuala hayo ya silaha.Kwa sasa wameelekeza nguvu zao katika kukusaka wewe" akasema Winnie na kuzidi kumstua Frank "Oh my God! akasema Frank kwa sauti ndogo "Winnie una uhakika mtu huyo ambaye alikutesa anaitwa Elvis? "Ndiyo anaitwa Elvis" akasema Winnie na Frank akainuka na kuanza kuzunguka zunguka mle sebuleni akiwa ameinamisha kichwa chake alionekana kuzama katika mawazo mazito "Najaribu kutaka kumuamini huyu sichana lakini ninashindwa kwani Elvis ni mfu.Tayari tumemzika na hakuna namna yoyote anayoweza kurudi.Lakini swali lingine ni je kama Winnie hasemi kweli amefahamuje masuala haya ya silaha?Hata Vicky mwenyewe hafahamu chochote kuhusiana na masuala ya biashara ya silaha.Mtu pekee ambaye aligundua kuhusu biasharaya silaha ni Elvis ambaye amekwisha fariki hawa wengine ni akina nani ambao wanaanza kunifuatilia?Yawezekana wakawa ni washirika wa Elvis?I'm confused na sijui niamini kipi" akawaza Frank akionekana kweli kuchanganyikiwa.Akamtazama Winnie na kuuliza "Kwenye simu ulisema unamfahamu Graca?Umemfahamuje?Unafahamu mahala aliko? "Ndiyo ninafahamu mahala aliko Graca.Yuko na hawa jamaa wawili anaishi nao ndani ya nyumba yao.Nilimkuta humo na akanieleza historia yake yote.Amenieleza kila kitu kilichomtokea mateso uliyompatia ukimtaka arejeshe begi lenye kompyuta yako ambayo iliibwa ofisini kwako.Kwa ujumla amenieleza kilakitu hadi alivyokutana na Elvis afrika kusini akamtoa katika hospitali ya magonjwa ya akili na hadi walivyofika hapa Tanzania.Amenieleza mambo mengi sana kuhusu yeye na hata matarajio ya maisha yake.Ameahidiwa mambo mengi na Elvis.Kingine cha kusikitisha zaidi ni kwamba Elvis na Graca wana mahusiano ya kimapenzi.Graca anaishi ndani ya nyumba ile kama mtumwa wa ngono" Frank alipandwa na hasira kali baada ya maelezo yale ya Winnie na kuibinua meza.Winnie akaogopa na kutetemeka baada ya Frank kumsogelea.Macho yake yaliwaka hasira "Winnie haya unayonieleza hakikisha ni ya kweli kwani endapo unanieleza uongo naapa nitakukata kichwa.Nitazame vizuri machoni mimi sina huruma hata kidogo kwa yeyote anayenidanganya!! akasema Frank "Frank nakueleza mambo ya kweli kabisa na si uongo" akasema Winnie na Frank akavuta pumzi ndefu haraka haraka "Nisikilize!! akasema "Huyo Graca ni mwanangu lakini amenifanyia mambo mabaya sana yeye na mama yake kiasi kwamba ninajuta kuwa na mtoto kama yeye.Simuhesabu kama mwanangu bali kama adui yangu kwa mambo aliyonifanyia endapo nitampata adhabu yake ni kifo! Kama una hakika kweli umemuona nipeleka mahala hapo alipo ninamuhitaji sana huyu mtoto!! akasema Frank kwa hasira akionekana kuchanganyikiwa "Frank sikudanganyi.Ni kweli Graca yupo nimemuona na ninaweza kukupeleka mahala alipo.Unapaswa kumuondoa kutoka katika jumba lile kwani wale jamaa si watu wazuri hata kidogo.Mambo wanayomfanyia si mazuri.Graca bado ni mwanao na unapaswa kumsaidia japo amekukosea.. "No!! Frank akamkatisha Winnie "Graca siwezi kumsamehe hata kidogo.Aliwahi kuwa mwanangu lakini kwa sasa ni adui yangu,tena adui mkubwa na nitamfanya kama vile ninavyowafanya maadui zangu,I kill them!! akasema Frank kwa hasira na mara akahisi kama miguu inaisha nguvu akaketi sofani na kuinamisha kichwa "Elvis !! akasema kwa sauti ndogo "Graca alitoroshwa hospitali na Elvis na akampatia kompyuta yangu na Elvis akafahamu kuhusu biashara ya silaha na kuanza kutufuatilia.Tukafanikiwa kumuua na amezikwa kaburini huyu Elvis ambaye Winnie anamtaja ni Elvis yupi? I'm totaly confused" akawaza Frank "Suala hili si la kupuuzia hata kidogo lazima nifanye uchunguzi wa haraka sana.Kwanza ni kuhakikisha ninampata Vicky yeye ndiye atakayeweza kunipa majibu ya suala hili.Anamfahamu Elvis vizuri kuliko huyu Winnie.Yawezekana kuna mtu amejipa jina la Elvis ili kumuenzi rafiki yao" akawaza Frank na kumtazama Winnie "Winne nakushukuru sana kwa taarifa hizi ulizonipa.Ni taarifa nyeti mno na ambazo nilikuwa nazihitaji sana hasa kuhusiana na Graca ambaye sikujua ni wapi ningeweza kumpata.Ninachokitaka ni kunipeleka huko mahala waliko ili nikamuokoe dada yako na Graca" akasema Frank Frank nitakupeleka huko ila nataka kwanza unihakikishie kwamba dada yangu atakuwa huru na hautamfuatilia tena" akasema Winnie "Kama nilivyokueleza Winnie kwamba dada yako ni rafiki yangu sana na sina atizo naye.Ni bahati mbaya tu sikuwa nikifahamu kilichojificha nyuma ya pazia.Maelezo yako yamenipa picha ya nani hasa ninayepaswa kumtafuta kuhusiana na kifo cha Pascal hivyo sina shida tena na Vicky.Atakuwa huru" akasema Frank "Nitashukuru kama ukitimiza ahadi yako"akasema Winnie "Mimi si mkatili hadi pale unaponichokoza.Vicky ni rafiki yangu and I don't hurt my friends.Naomba tafadhali unisubiri hapa ili twende huko mahala waliko akina Vicky" akasema Frank Yule mtu wako alichukua simu yangu.Naweza kuipata? akauliza Winnie na Frank akatoa simu mfukoni mwake akampa "Dada yako au mtu mwngine yeyote akikupigia simu usipokee hadi uniulize.Umenielewa?" akasema Frank "Nimekuelewa Frank" akasema Winnie na Frank akatoka akamfuata Obi "Obi kuna kazi kubwa imejitokeza.Nahitaji vijana sita au kumi kwa haraka kuna kazi ya kufanya usiku huu" "Kazi gani mkuu? akauliza Obi "Yule mwanamke niliyekutuma ukamteke asubuhi tayari nimefahamu mahala alipo.Winnie amenielekeza mahala alipo na si yeye peke yake bali pia mwanangu Graca naye yuko hapo.Nahitaji kwenda kuwachukua kutoka mahala wanaposhikiliwa" "Nani wanawashikilia?akauliza Obi "Winnie anasema kuna watu wawili wanawashikilia Vicky na Graca hivyo andaa kikosi ili tukavamie mahala hapo na kuwachukua Vicky na Graca haraka sana" akasema Frank lakini Obi akaonyesha shaka kidogo na kuuliza "Mkuu unamuamini huyu msichana? "Ninamuamini.Kuna mambo amenieleza ambayo yamenifanya nimuamini" "Nina wasiwasi asiwe anatumiwa kama mtego" "Tutajua huko huko kama anatumiwa au vipi ila lazima tukavamie mahala hapo na kuwachukua akina Vicky.Tafadhali andaa vijana wanaoweza kazi kwani sitaki uzembe kama uliofanyika asubuhi.Safari hii hata mimi mwenyewe nitakuwepo kuhakikisha kila ktu kinakwenda vyema" akasema Frank na kurejea ndani "Ninaandaa vijana kwa ajili ya kwenda huko aliko Vicky.Wakati wanajiandaa nataka uniambie kuhusu Elvis.Yukoje?akauliza Frank.Winnie akafikiri kidogo na "Elvis ukimtazama amefanana sana na yule mcheza mpira wa kikapu mahiri wa timu ya Golden state warriors ya marekani anaitwa Stephen Curry.He's very handsome sipati namna ya kumuelezea vizuri ila ukiipata pcha ya Stephe utakuwa umepata picha halisi ya Elvis kwani wamefanana sana" akasema Winnie na Frank akahisi kibaridi kinapenya mwilini mwake "This cant be!! akasema kwa sauti Unasemaje Frank? akauliza Winnie na Frank hakumjibu kitu akainuka akatoka "Winnie anachokiongea ni cha kweli kabisa.Elvis amefanana sana na yule mchezaji mpira wa kikapu wa Marekani.Lakini mbona Elvis tayari amefariki dunia?Huyu Elvis gani aliyejitokeza tena?Ni mzimu?akajiuliza Frank na kusimama akaegemea ukuta "Siamini sana katika mambo haya ya imani za mizimu lakini yawezekana kuna mambo yanaongelewa yakawa kweli kuhusu mzimu wa mtu kurudi.Inawezekana Elvis huyo anayeonekana sasa hivi akawa ni mzimu umerudi kututafuta.Jibu nitalipata usiku wa leo kama ni binadamu au ni mzimu " akawaza na kumfuata Obi "Obi vijana wako tayari? Ndiyo mkuu nimepata vijana saba na wote wako tayari.Tutawapitia sehemu fulani.Wewe uko tayari? "Niko tayari lakini itanilazimu kupita kwanza nyumbani kwangu kuchukua silaha kisha tuelekee huko ambako naamini kutakuwa na mapambano" akasema Frank akamfuata Winnie na kumtaka waondoke. "Wale mashetani leo ndiyo mwisho wao.Nashukuru Frank ameniamini kwa namna picha nilivyoipanga.Kwa sasa dada yuko huru kwani nimemuondoa katika sakata lile la mauaji ya Pascal na mzigo wote nimewatupia wale jamaa.Nina hasira nao sana na roho yangu itakuwa na amani nitakapowaona nao wakiteseka kwa unyama walionifanyia.Siwezi kusahau nilivyochomwa na umeme bila kosa lolote.Dada naye huu ni mwisho wake kufanya kazi hizi za upelelezi.Anatakiwa ajikite zaidi katika biashara na kuachana na shughuli hizi hatarishi ambazo zinatufanya sote kuishi maisha magumu" akawaza Winnie wakiwa garini wakielekea nyumbani kwa Frank kwenda kuchukua silaha akijiandaa kuelekea kwa akina Elvis.Bado picha ya Elvis iliendelea kuzunguka kichwani kwake ************** "Simu ya Winnie imezimwa" Omola akawataarifu akina Elvis wakiwa garini. "Vicky mahala hapo alipo mdogo wako unapafahamu? akauliza Elvis Hapana sipafahamu na wala sijawahi fika" "Sawa.Omola endelea kumfuatilia endapo atawasha simu yake ili tukimaliza huku tujue mahala aliko tumfuate" akasema Elvis na safari ikaendelea kimya kimya.Graca aliyekuwa amekaa mbele na Steve alikuwa akitoa maelekezo ya sehemu ya kwenda. "Graca una hakika na huku tunakoelekea? akauliza Steve baada ya kuona wanazidi kuelekea nje ya mji "Ndiyo nina uhakika.Japo ni muda mrefu sijafika huku lakini napakumbuka sana"akasema Graca "Huku ni wapi?Frank ana nyumba huku?akauliza Elvis "Huku ni shambani kwake.Kuna nyumba kubwa sana huku ameijenga na chini ya nyumba hiyo kuna ofisi yake ya siri na vile vile kuna ghala ambalo huhifadhi vitu vyake mbali mbali" "Umefahamuje kuhusu nyumba hiyo ya siri aliyoijenga chini?Umewahi kuingia?akauliza Elvis "Wakati ule ananitesa na kunitaka nirejeshe kompyuta yake aliwahi kunileta huku akanifungia huko chini na kuniacha kwa siku mbili.Nilihisi upweke mkubwa sana na woga mwingi kwani ni sehemu yenye kiza kikubwa.Aliniacha bila chakula wala maji kwa siku mbili na akaja kunifungulia akanitaka nimueleze ilipo kompyuta yake lakini bado sikuwa tayari kumueleza mahala ilipo.Alipokuja aliwasha taa na ndipo nikafanikiwa kuona ofisi yake ya siri.Ndani ya ofisi hiyo kuna mlango ambao ukiufungua unaingia katika ghala kubwa ambalo huhifadhi vitu vyake" akasema Graca Dah! Pole sana Graca.Sikujua kama Frank ni mkatili kiasi hiki.Hata hivyo wewe ni jasiri sana" akasema Vicky "Ahsante sana Vicky.Unanionaje ninaweza kufaa kuwa mpelelezi? akauliza Graca "Unafaa sana kwani kazi hii inahitaji mtu jasiri asiyekata tamaa wala kulegea hata akiteswa vipi.Kama unapenda kuifanya kazi hii utafaa sana"akasema Vicky "Graca ana maisha mengine mazuri baada ya operesheni hii kumalizika na si kuingia katika kazi hizi za hatari" akasema Elvis na Graca akatabasamu "Graca tupe picha pana zaidi ya mahala hapo.Je pana walinzi? akauliza Elvis Walinzi wapo.Kuna nyumba tatu amejenga wanazoishi walinzi wanaolinda nyumba kubwa" "Tutawezaje kuingia humo ndani hadi katika ofisi yake ya siri? "Tutayaacha magari kijijini halafu tutatembea kwa miguu si umbali mrefu sana kutoka hapo kijijini.Tutazunguka upande wa mashariki ambako kuna bwawa la samaki na mashine ya kufua umeme wa maji kwani kuna mto unapita hapo karibu.Tukipita huko ni njia rahisi kidogo ya kukwepa kupita karibu na nyumba za walinzi" akasema Graca "Nimepata wazo.Kama kuna umeme wa nguvu za maji basi tutazima umeme kwa muda ili tuweze kupata nafasi ya kuingia ndani.Mimi na Steve,tutatangulia ndani,Vicky na Omola mtabaki pale katika mashine ya maji kulinda usalama.Baada ya sisi kuingia ndani tutawajulisha na mtawasha umeme.Nina uhakika mkubwa kuwa umeme utakapozima lazima walinzi watakuja kuangalia kama kuna tatizo.Yeyote atakayefika eneo hilo mzimisheni haraka sana.Endapo mtaona kuna hatari yoyote basi mtujulishe haraka sana" akasema Elvis "Graca unahakika baba yako huhifadhi nyaraka zake za siri huku? akauliza Steve "Toka mama alipoinia katika ofisi yake na kuiba kompyuta baba hakutaka tena kuhifadhi vitu vake vya siri katika ofisi yake iliyopo nyumbani akahamishia kila kitu huku shambani.Nina uhakika lazima kuna kitu kitapatikana kuhusiana na biashara zake au mtandao wake" akasema Graca na safari ikaendelea hadi walipofika kijiji chaMsolali.Walikipita kijiji kidogo halafu Graca akaelekeza kuwa waache gari hapo na watembee kwa miguu.Gari likaegeshwa chini ya mkorosho halafu wakaanza kutembea kwa miguu.Kiza kilikuwa kinene na kwa mbali taa zilionekana na Graca akawaeleza mahala pale panapowaka taa ndipo shambani kwa baba yake.Walitembea kwa dakika kumi na tano wakipita katika majani marefu na hatimaye wakafika katika uzio wa seng'enge "Huu ndio uzio wa shamba letu " akasema Graca na kwa kutumia mkasi mgumu seng'enge ikakatwa wakaingia shambani.Kila mmoja alikuwa na bastora mkononi tayari kukabiliana na lolote isipokuwa Graca.Walitembea kwa tahadhari na baada ya dakika sita wakatokeza katika bwawa kubwa la samaki Hapa ni bwawani na ukishuka kule chini kuna mashine ya umeme" akasema Graca akiwaelekeza akina Elvis "Ninakwenda kuchunguza kama kuna mtu yeyote kule halafu nitawajulisha" akasema Steve na kuanza kutembea kwa tahadhari kubwa akishuka mahala iliko mashine ya kufua umeme wa maji.Baada ya dakika nne akarejea na kuwajulisha kuwa hakukuwa na mtu yeyote mahala pale.Wote wakashuka kuelekea katika mashine ile.Mlango haukuwa umefungwa Elvis akausukuma wakaingia ndani.Steve pekee ndiye aliyebaki nje akilinda usalama. "Kazi inaanza" akasema Elvis na kuzima mashine ya umeme.Eneo lote kukawa giza na kwa haraka wakiongozwa na Graca wakaanza kutembea kuelekea katika jumba kubwa.Mbwa walisikika wakibweka.Mara ghafla wakasikika watu wakizungumza wakielekea kule katika mashine wakiwa wamewasha tochi za simu zao.Haraka akina Elvis wakarukia ndani ya mtaro wa maji wakajificha "Hii mashine tumueleze bosi alete mafundi waitazame ina matatizo gani.kwani ni mara ya pili sasa inazima" akasema mmoja wao wakitembea kwa kasi kueleka katika mashine ya umeme.Walipopita akina Elvis wakatoka mtaroni.Elvis akapiga piga sikioni alikoweka kifaa cha kuwawezesha kuwasiliana halafu akasema kwa sauti ndogo "Vicky,Vicky do you copy" "Nakupata Elvis" "Kuna watu wawili wanakuja huko katika mashineUsijali Elvis watakutana nasi" "Wangejua wanachokwenda kukutana nacho huko waendako wangegeuza na kurejea walikotoka" akasema Elvis huku wakitembea taratibu kwa tahadhari kuelekea katika nyumba wakiongozwa na Graca.Walifika katika bustani iliyokuwa na miti mingi ya maua na sanamu kadhaa za wanyama "Kuna mlango wa kuigilia ndani uko upande huu wa nyuma" akasema Graca. "Steve ninakwenda kuufungua mlango.Cover me" akasema Elvis na kutoka kwa tahadhari katika ile bustani akatembea kwa kunyata huku Steve akiwa makini kuhakikisha hakuna hatari yoyote eneo lile.Elvis akafuata maelekezo ya Graca na kutokea katika kibaraza cha nyuma.Akaangaza angaza kama kuna mtu yeyote maeneo yale lakini kulikuwa kimya kabisa.Akatoa pochi ndogo katika begi alilobeba iliyokuwa na vifaa fulani vidogo na kuanza kuufungua mlango.Kwa sekunde chache akafanikiwa kuufungua halafu akamtaarifu Steve ambaye naye akiwa na Graca wakamfuata na wote wakaingia ndani.Bado eneo lote lilikuwa giza. "Vicky unanisikia? akauliza Elvis baada ya kufanikiwa kuingia ndani "Ninakupata Elvis,huku kila kitu inakwenda vyema na wale jamaa wawili tumekwisha walaza usingizi wa muda.Tayari mko ndani? "We're in.Washeni mashine" akasema Elvis na baada ya dakika mbili umeme ukawaka.Ndani hakukuwa na taa iliyowashwa ila kulikuwa na mwanga mdogo kutokana na taa zilizokuwa zikiwaka nje Graca tuelekeze tunaelekea wapi?akauliza Elvis "Tunaelekea katika chumba cha kulala cha baba na humo kuna mlango wa kuingilia katika chumba cha chini" akasema Graca na kuwaongoza akina Elvis kuelekea sebuleni halafu wakaelekea katika chumba cha baba yake cha kulala.Elvis akatumia funguo bandia na kuufungua mlango wakaingia katika chumba cha kulala.Kulikuwa giza.Elvis akatoa tochi ndogo katika begi lake na kuiwasha. "Tunapita huku katika chumba cha nguo" akasema Graca na wakaingia katika chumba cha kuadilishia nguo kilichosheheni nguo nyingi. "Nyuma ya kabati kubwa kuna mlango.Sukumeni hili kabati" akasema Graca.Elvis na Steven wakalisukuma kabati na kweli wakakuta kuna mlango nyuma yake "Huo ndio mlango wa kuingilia katika chumba cha chini" akasema Graca.Elvis akaumulika na kugundua ulikuwa unafunguliwa kwa namba . "Tumekwama.Mlango huu unafunguliwa kwa namba maalum.Unaweza kuzikumbuka namba za kufungulia mlango?Elvis akauliza "Hapana sizifahamu.Wakati ule baba aliponileta hakukuwa na huu mlango wenye namba" akasema Graca.Elvis akafikiri kwa muda halafu akapiga sikioni "Vicky ,Vicky unanipata? "Ninakupata Elvis" "Good.Tumefanikiwa kuupata mlango wa kuingilia ndani lakini kuna tatizo limejitokeza.Mlango huu unafunguliwa kwa namba kabati na kweli wakakuta kuna mlango nyuma yake "Huo ndio mlango wa kuingilia katika chumba cha chini" akasema Graca.Elvis akaumulika na kugundua ulikuwa unafunguliwa kwa namba . "Tumekwama.Mlango huu unafunguliwa kwa namba maalum.Unaweza kuzikumbuka namba za kufungulia mlango?Elvis akauliza "Hapana sizifahamu.Wakati ule baba aliponileta hakukuwa na huu mlango wenye namba" akasema Graca.Elvis akafikiri kwa muda halafu akapiga sikioni "Vicky ,Vicky unanipata? "Ninakupata Elvis" "Good.Tumefanikiwa kuupata mlango wa kuingilia ndani lakini kuna tatizo limejitokeza.Mlango huu unafunguliwa kwa namba maalum.Nitahitaji kumtumia Omola katika kuufungua mlango huu kwani uliniambia kuwa ni mtaalamu wa mambo haya.Steve anakuja huko kumchukua wewe utabaki hapo ukihakiki usalama,hivyo zimeni umeme" akasema Elvis na kisha Steve akatoka kwenda kumchukua Omola "Baba yako amejihami sana.Naamini kuna mambo mengi ya muhimu anayaficha huku na ndiyo maana akaweka mlango wa namna hii" akasema Elvis wakati wakimsubiri Steve na Omola "Baba naweza kumfananisha na gaidi kutokana na roho yake ya kikatili.Kwake kutoa roho ya mtu ni kitu kidogo sana" akasema Graca "Usihofu haya yote yanakwenda kumalizika muda si mrefu.Utakuwa na amani tena" akasema Elvis Naomba iwe hivyo.Nimechoka kuishi maisha ya ndege" akasema Graca.Zilipita dakika kumi na mbili na Steve akarejea akiwa na Omola "Huko nje salama? akauliza Elvis "Usihofu.Huko nje ni salama kabisa.Hakuna mtu yeyote anayezunguka maeneo haya na inaonekana watu wa hapa hawaelewi kinachoendelea.Hawajui kama wamevamiwa" "Good." akasema Elvis na kumgeukia Omola "Omola imekuwa vizuri umeongozana nasi.Tunahitaji msaada wako katika kuufungua huu mlango" akasema Elvis na Omola akachukua tochi ndogo akaumulika halafu akatafuta katika kompyuta yake aina ya kitasa kile na kuanza kutafuta namba za siri.Baada ya dakika mbili kompyuta ikamonyesha namna ya kubadili namba za siri za kufungulia mlango ule.Akaanza kufuata taratibu za kufungua mlango ule na baada ya kumaliza kuingiza namba alizoelekezwa na kompyuta yake taa ndogo ya kijani ikawaka na mlango ukafunguka "Ahsante sana Omola" akasema Elvis akiwa wa kwanza kuingia ndani na kumulika akaziona ngazi za kushuka na wote wakashuka kuelekea chini "Vicky,tayari tumeingia tunaelekea chini" akasema Elvis akimjulisha Vicky "Elvis mawasiliano si mazuri baada ya kuingia huko chini.Sikupati vizuri" akasema Vicky lakini Elvis naye hakuweza kumpata sawa sawa.
Baada ya kutoka nyumbani kwa brigedia Frank kuchukua silaha waliwapitia vijana ambao Obi alikuwa amewaandaa waliokuwa na gari lao kisha wakaongozana kuelekea kwa akina Elvis.Walikuwa wamejianda kwa mapambano wakiwa na silaha kali.Watatu kati ya vijana hawa wamewahi kupitia jeshi na wakafukuzwa kutokanana utovu wa nidhamu.Wote walikuwa ni wajuzi sana katika kutumia silaha na walikuwa na genge lao la kufanya uhalifu wa kutumia silaha.Wengine watano walikuwa na uzoefu pia katika mambo ya uhalifu na hata kutumia silaha. "Ninaomba hiki anachonieleza Winnie kuhusu Elvis kisiwe kweli.Nataka kwanza nithibitishe ni Elvis yupi huyo anayemtaja wakati Elvis amekwisha zikwa?Ni mzimu wake ndio umerudi kutusumbua? akajiuliza "Nafsi yangu inakataa kabisa na haiamini katika mambo hayo ya mizimu.Yawezekana kuna mtu mwingine anajiita Elvis na si Elvis yule tuliyemuua.Lakini mbona wasifu alionielezea Winnie unafanana kabisa na wasifu wa Elvis? Hili suala naona linataka kunipasua kichwa changu lakini nitapata majibu muda si mrefu.Usiku huu wa leo kwa namna yoyote ile lazima nimpate Vicky kwani yeye ndiye anayeweza kunithibitishia kuhusu huyo mtu anayejiita Elvis" akaendelea kuwaza Frank Japokuwa Winnie alipita maeneo yale usiku lakini aliweza kukumbuka vyema mahala ilipo nyumba ya akina Elvis na hatimaye wakawasili katika nyumba ile Ni pale kwenye lile geti" akaelekeza Winnie na gari zikasimama "Una hakika ni hapa?akauliza Frank "Nina uhakika Frank ni hapa" akasema Winnie "Nataka uwe na uhakika Winnie .Una hakika ni hapa?Frank akauliza tena "Nina uhakika ni hapa.Siwezi kupotea" akasema Winnie "Good.Obi wapange vijana wako ili muweze kuingia ndani mimi nitakuwa pale mbele nikiangalia namna zoezi linavyokwenda na endapo kutakuwa na tatizo lolote nitatoa msaada" akasema Frank na Obi akashuka.Frank akaenda kuegesha gari mita kadhaa kutoka geti la kuingilia katika nyumba ile akaichukua bunduki yake kubwa akaiandaa kwa ajili ya lolote ambalo lingeweza kutokea "Winnie utakuwa umenisaidia sana kama kweli tukifanikiwa kuwapata hao jamaa pamoja na Graca.Ninakuahidi baada ya kuwapata hao jamaa basi dada yako atakuwa huru na sintamfuatilia tena.Lakini endapo unanidanganya utanisamehe kwa kile nitakachokufanyia" akasema Frank ambaye kwa wakati huu sura yake ilionyesha ukatili mkubwa "Ninakuambia ukweli Frank siwezi kukudanganya.Ninafanya hivi ili kumsaidia dada yangu aweze kuachiwa na hawa jamaa" akasema Winnie kwa kujiamini Obi na vijana watano wakafanikiwa kuruka ukuta na kuingia ndani bila kelele.Walikuwa ni wazoefu sana wa mambo kama haya hivyo kuingia mle ndani iliwachukua muda mfupi tu.Kabla ya kufanya lolote wakatulia kwa dakika mbili wakihakiki usalama na baada ya kuhakikisha http://deusdeditmahunda.blogspot.com/eneo lile ni shwari na hakuna mtu yeyote pale nje Obi akatoa maelekezo kwa vijana watatu watawanyike kuizunguka nyumba ile kisha yeye na wale vijana wawili waliobaki wakanyata kuusogelea mlango.Taa za ndani zilikuwa zinawaka na waliamini lazima kuna watu ndani ila hawakusikia sauti ya mtu akiongea.Kwa kutumia funguo bandia wakafungua mlango na kuingia sebuleni ambako kulikuwa kimya kabisa.Taratibu wakafuata varanda kuelekea vyumbani.Walipita vyumba vyote lakini hakukuwa na mtu.Hii ikawashangaza sana. "Where are they? akauliza Obi lakini vijana wake wakabaki kimya Let's search again.Safari hii tuwe waangalifu sana kutafuta yawezekana kuna mlango wa siri wamepita watu hawa na kwenda kujificha" akasema Obi na upekuzi ukaanza upya.Walipekua sana lakini hawakuambulia kitu.Huku akitokwa na jasho akampigia simu Frank "Frank hakuna mtu humu ndani" "Nini?! akauliza Frank kwa mshangao "Hakuna mtu humu ndani" "No ! Search again.They must be there!! akasema kwa ukali "Mzee tumerudia kupekua mara mbili lakini hakuna mtu yeyote humu ndani ila kunaonekana kuna watu walikuwepo humu muda si mrefu sana kabla ya sisi kuwasili" "Damn it !! akasema kwa hasira na kupiga usukani halafu akamgeukia Winnie "Watu wako hawapo humo ndani.Unanidanganya? akauliza Frank kwa ukali "Hapana Frank sikudanganyi.Watu hawa wanaishi humu ndani" akasema Winnie akionekana kuogopa "Kama wanaishi humu wako wapi?Wamejificha wapi? "Sifahamu ila wanaishi humu"akasema Winnie "Get out of the car ! akaamuru Frank na Winnie akafungua mlango wa gari akashuka. "Obi nifungulie geti ninakuja humo ndani" akasema Frank na mlango mdogo wa geti ukafuguliwa akamshika mkono Winnie akamuingiza ndani "Frank nilikwambia huyu msichana si wa kumuamini kwani hakuna mtu yeyote humu ndani" akasema Obi "Nilikwisha mtahadharisha kuwa mimi ni mtu mbaya sana nikidanganywa na nitamtoa uhai hapa hapa!! akasema Frank akiwa amewaka hasira "Mna hakika hakuna mtu yeyote humu ndani?akamuuliza Obi "Tumepekua mara mbili na hakuna mtu yeyote humu ndani" "Hakuna mlango wa siri ambao hawa jamaa wameutumia kukimbia baada ya kugundua uwepo wetu? "Hakuna mzee.Tumetafuta sana hakuna mlango wowote wa siri"akasema Obi na Frank akamgeukia Winnie akamtaka apige magoti halafu akatoa bastora yake "Ninakupa nafasi ya mwisho ya kunieleza ukweli.Nani alikutuma uje unieleze ongo huu?Ukishindwa kunijibu ninakutoa uhai wako sasa hivi!! akafoka Frank "Please dont kill me I'm telling the truth!! akasema Winnie huku akilia "Mkuu huyu msichana ni muongo kabisa.Huu ni mtego tumewekewa.Tuondokeni haraka sana hapa kabla hatujavamia.Nilikuwa na wasi wasi naye muda mrefu" akasema Obi "Hata mimi sikuwa nikimuamini kabisa hasa kwa namna alivyonitafuta na kunipata.Nimebadili mawazohHatutamuua kwani anatumiwa na watu wanaonifahamu vyema hivyo itakuwa rahisi kwangu kuwafahamu kwa kumtumia yeye.Mfungeni tunaondoka naye" akasema Frank kwa hasira "Frank please I'm telling the truth!! naomba uniamini tafadhali!! akalia Winnie lakini haraka haraka akafungwa mikono kwa kamba "Frank tafadhali naomba uniamini.Ninachokueleza ni kitu cha kweli kabisa.Sijakudanganya" Winnie akaendelea kulia "Winnie nilikutahadharisha kuwa sitaki kudanganywa lakini hukusikia ukanidanganya.Siwezi kukusamehe kwa hilo lazima nikuue!! Kitakachokuokoa ni pale utakaponieleza ukweli" "Ninakueleza ukweli Frank kwa nini hutaki kuniamini? akauliza Winnie "Mpelekeni katika gari ,sitaki kumuona mbele ya macho yangu" akasema Frank na kwa haraka Winnie akatolewa mle ndani akabebwa juu juu hadi katika gari la Frank "Nini kinaendelea hapa Frank?Obi akauliza na Frank akainamisha kichwa kwa muda akifikiri halafu akasema "I'm confused.Yule msichana anaweza kuwa anasema kweli kwani kuna maneno alinieleza ambayo yananifanya kidogo nimuamini.Hatutaondoka hapa sasa hivi hadi tuhakikishe ni nani anaishi katika nyumba hii.Tusikate tamaa mapema"akasema Frank "Mkuu huu unaweza kuwa ni mtego.Huyu msichana anaweza kuwa ametumika kukuwekea mtego.Kumbuka Pascal ameuawa na hatujui nani kamuua hivyo nawe pia unaweza kuwa katika orodha ya wanaotafutwa wauae.Nakushauri tuondoke hapa si mahala pazuri kwetu" akasema Obi "No! Hatuondoki hapa.Waelekeze vijana wako wajipange kukabiliana na shambulio lolote ambalo litatokea hapa.Nataka niwafahamu hao watu wanaonitafuta ni akina nani." akasema Frank na Obi akatoka kwenda kuwapanga vijana wake "Sintatoa mguu wangu ndani ya hii nyumba hadi nipate uhakika kuhusu huyo Elvis.Mambo niliyoambiwa na Winnie yamenichanganya mno na hasa baada ya kusikia jina Elvis likitajwa tena.Kila nikilifikiria jina hili ninaishiwa nguvu kab............" Frank akatolewa mwazoni baada ya ujumbe kuingia katika simu yake.Ujumbe huu ulikuwa na mlio wa tofauti na ule wa jumbe nyingine zinapoingia.Haraka haraka akaitoa simu na kuusoma ujumbe ule "Hongera.Nambayako ya siri imefanikiwa kubadilishwa"ndivyo ulivyosomeka ujumbe ule.Ndani ya sekunde chache akajikuta akiloa jasho mwilini What ?!! akasema kwa sauti "This cant be!! Nini hiki kinanitokea?Nani kabadilis.........." akawaza na haraka haraka akazitafuta namba za simu za msimamizi wake mkuu wa shamba ambaye ndiye mwenye funguo za kuingilia mle ndani ya nyumba lakini simu yake haikuwa ikipatikana.Miguu ikamtetemeka "No ! No ! No !akasema huku akitoka nje kwa kasi na kumfuata Obi "Obi tuondoke haraka sana kuna jambo limetokea"akasema Frank "Nini kimetokea mkuu? akauliza Obi kwa mshangao "Wakusanye vijana wote tuwahi haraka sana nyumba yangu imevamiwa! akasema huku midomo ikimtetemeka kwa hasira.Haraka haraka Obi akawakusanya vijana wake wakaingia katika gari na kuondoka kwa kasi akimfuata Frank aliyekuwa akiendesha gari kama mwendawazimu kuwahi shambani kwake "Ni nani hawa waliovamia nyumba yangu na kuingia katika katika ofisi yangu?Hawa lazima watakuwa ni ni hawa watu wanaonifuatilia.lazima watakuwa ni kundi la Elvis na wenzake.Wamefahamuje kama nina ofisi kule shambani ambako ninahifadhi mambo yangu nyeti? akajiuliza "Winnie anasema kwamba Vicky aliwahidi kuwapeleka hao jamaa mahala ambako ana uhakika kwamba wanaweza wakanipata.Vicky niliwahi kumpeleka katika nyumba yangu ya shambani na kumficha kule.Yawezekana ni yeye ndiye aliyewapeleka hao jamaa kama alivyosema Winnie? Ukiacha Vicky mwingine ambaye anafahamu kuhusiana na nyumba yangu ya shambani ni Graca.Tena hyu anafahamu kama kuna ofisi ya siri iliyoko chini ya nyumba kwani niliwahi kumfungia kule wakati ule nikimtisha anirejeshee kompyuta yangu.Kama kweli Graca anaishi na akina Elvis kama basi kuna uwezekano mkubwa huu ni muendelezo wa jitihada zao za kuhakikisha kwamba wanafahamu kila ninachokifanya na hasa kuhusu biashara ya silaha.Naamini ni yeye ndiye aliyewaelekeza wenzake kuhusu ofisi yangu ya siri kwani Vicky hafahamu chochote kuhusu ofisi hii.Kwa nini lakini mwanangu wa kumzaa ananifanyia haya?Haogopi kupambana nami?Ninaanza kuhisi Vicky na akina Graca wote ni kundi moja na wameungana ili kupambana nami,nahisi hata huyu Winnie ametumwa kwa lengo la kuja kwangu ili kunipotezea muda na kuwapa nafasi hao watu pamoja na dada yake kuvamia nyumba yangu.Huyu nitamtumia katika kuwatafuta Vicky na wenzake hadi niwapate.Haya yote yanatokea kwa sababu nilimpuuza Pascal alipotoa wazo la kumuua Vicky mapema.Hata madam Elizabeth alipotoa maelekezo nimuue Vicky sikutekeleza kwa vile tayari nilimuhitaji Vicky kingono na hizi ndizo athari zake.Sipaswi kumlaumu mtu kwa haya yanayonikuta.Nimeharibu mimi mwenyewe na sasa natakiwa kupambana kuhakikisha ninarekebisha hii hali haraka sana na nitarekebisha baada tu ya kuhakikisha nimewapata hao watu kwa haraka sana.Kabla ya kufika asubuhi kesho lazima niwe nimewapata Vicky na kundi lake lote"Kichwa cha Frank kikajaa mawazo mengi sana ******************* Graca aliwaongoza akina Elvis hadi katika ofisi ya baba yake aliyoijenga chini ya ardhi. "Hii ndiyo ofisi ya baba" akasema Graca "Steve pitia kwa haraka na uchukue chochote kinachoweza kutufaa katika uchunguzi wetu.Graca ulisema kuna sehemu pia huwa anahifadhi vitu vyake ni wapi? akauliza Elvis "Ni katika mlango ule pale" akaelekeza Graca na Elvis akaenda kuutazama ule mlango nao pia ulikuwa unafunguliwa kwa namba maalum. "Huyu jamaa amejidhatiti sana kiusalama.Si rahisi kuingia huku mahala anakohifadhi mambo yake." akasema Elvis huku akivua begi lake na kutoa kitu flani akakipachika katika mlango halafu akabonyeza kitufe katika kidude hicho na namba nyekundu zikaonekana zikihesabu kuanzia kumi na ilipofika sifuri kidude kile kikalipuka ingawa hakikutoa mlipuko mkubwa wenye madhara na mlango ukafunguka "Huku tuko chini ya ardhi hivyo hakuna anayeweza kusikia sauti hii ya mlipuko huko juu" akasema Elvis na kuusukuma mlango wakaingia katika chumba kimoja kikubwa sana kama ukumbi wa mikutano wenye kuweza kuchukua watu zaidi ya mia tano. What is this place" akawaza Elvis .Akiwa na tochi wakafanikiwa kupata sehemu ya kuwashia taa na kukawa na mwangaza wa kutosha.Kulikuwa na maboksi ya mbao yamepangwa vizuri "Nini wanahifadhi humu? akauliza Omola.Elvis akashusha moja ya boksi lile la mbao na kutoa mfuniko wake akakutana na jozi za viatu vya kiume "Viatu? Elvis akashangaa.Akashusha boksi lingine akalifungua na kukuta limejaa jozi za viatu.Wote wakazidi kushangaa.Akashusha lingine la tatu na kukuta kuna viatu. "Frank anafanya biashara ya viatu?Elvis akamuuliza Graca "Hata mimi nimeshangaa.Ameianza lini biashara hii" Graca naye akashangaa Hainiingii akilini Frank afiche jozi za viatu katika sehemu kama hii yenye ulinzi mkubwa.Milango yote ya hapa inafunguliwa kwa namba maalum na haiwezekani akatumia gharama kubwa kutengeneza sehemu kama hii kwa ajili ya kuhifadhi vitu kama viatu" akasema Elvis na kumgeukia Graca "Graca una fahamu kama baba yako anajihusisha na biashara ya viatu? "Hapana sifahamu chochote kuhusiana na baba kujihusisha na biashara ya viatu" akasema Graca "Tuendelee kupekua yawezekana tukakabaini vitu vingine.Siamini kabisa kama Frank anatumia sehemu hii kuficha viatu" akasema Elvis na kuanza kushusha makasha na kuyafungua na yote yalijaa viatu.Alishusha zaidi ya maboksi ishirini lakini yote yalikuwa na viatu.Jasho lilimtiririka kutokana na zoezi lile "Inaonekana maboksi haya yote yana viatu.Nilitegemea sehemu kama hii angeweza kuhifadhi silaha au vitu vingine lakini kumejaa maboksi ya viatu" akasema Elvis na wote wakatazamana.Elvis akaendelea kuchunguza lakini hakufanikiwa kupata aina yoyote ya silaha "Twende tukamuone Steve kama kuna kitu chochote amekipata cha kuweza kutusaidia" akasema Elvis wakatoka na kuingia katika ofisi walikomuacha Steve "Steve kuna kitu chochote umekipata? akauliza Elvis "Kuna hii bahasha nimeipata katika droo ya kati ina nyaraka za kutolea mizigo bandarini.Nyaraka zinaonyesha kuna kontena kumi na nane zimeingia nchini mwezi uliopita kutoka nje ya nchi.Vingi ya vitu vilivyomo humu ni risiti mbali mbali za malipo lakini nimekuta kompyuta ndogo katika moja ya droo" akasema Steve "Vizuri.Huko ndani kuna chumba kikubwa kama bohari la kuhifadhia mizigo na tumekuta kuna shehena kubwa ya viatu" "Viatu?Hakuna silaha hata moja?Steve akashangaa "Hata mimi nilitegemea tungeweza kukuta silaha lakini tumekutana na jozi za viatu" akasema Elvis na kumgeukia Graca "Graca kuna sehemu nyingine ambayo unadhani unaweza kutupeleka na tukapata nyaraka zaidi kuhusu baba yako na mtandao wake? akauliza Elvis Hapa ndipo ninapopafahamu kuwa anaficha mambo yake ya siri.Kama mkikosa hapa kupata kitu cha kuwasaidia sifahamu tena sehemu nyingine" akasema Graca "Ahsante hata hivyo umetusaidia sana.Steve chukua hivyo ulivyofanilkiwa kuvipata tuondokeni kabla hawajatugundua kuwa tuko hapa" akasema Elvis kisha wakaanza kutoka.Walipotoka chini Elvis akapiga piga sikio na kumuita Vicky "Vicky unanipata? 'Ninakupata Elvis.Mpo salama? "Salama kabisa Vicky.Tumekwisha maliza kazi hapa na tunaondoka.Uko salama? hakuna hatari yoyote? "Niko salama kabisa na hakuna hatari yoyote" "Good.Zima mashine ili tuweze kutoka" akasema Elvis na hazikupita sekunde thelathni umeme ukakatika na kwa haraka wakatoka mle ndani na kuelekea iliko mashine ya umeme mahala walikomuacha Vicky "Pole sana kwa kukuacha peke yako" akasema Elvis baada ya kufika mahala aliko Vicky "Mmefanikiwa kupata chochote? "Si haba kuna vitu vichache tumevipata na tunakwenda kuvifanyia uchunguzi tuone kama vinaweza kutusaidia.Washa ueme kisha tupotee maeneo haya" akasema Elvis na mashine ikawashwa kisha wakaondoka wakifuata ile njia waliyojia ******************* Frank na vijana wake waliwasili shambani wakiwa katika mwendo mkali sana.Walipofika katika geti la walinzi Frank akashuka na kumkuta mlinzi mmoja tu "Wenzako wako wapi?akauliza "Wamekwenda kutazama mashine ya umeme ina matatizo" "Matatizo?Frank akauliza "Ndiyo bosi.Umeme umekuwa unazima mara kwa mara usiku huu hivyo wakaenda kutazama kama kuna tatizo na hawajarejea" "Tatizo hilo limeanza lini? akauliza "Limeanza usiku huu" "Mbona nawapigia simu zao hawapatikani?Wamekwenda bila simu? "Wamekwenda nazo bosi" "Kuna mtu yeyote amekuja hapa usiku wa leo? "Hapana bosi hakuna mtu yeyote aliyekuja hapa" Una hakika? "Ndiyo bosi hakuna yeyote aliyefika hapa"akajibu yule mlinzi Frank akaingia haraka katika gari lake na kuingia shambani akiendesha kwa kasi ya ajabu.Alisimamisha gari nje ya nyumba akashuka na kumtaka Obi awaelekeze vijana wake wazunguke nyumba kukagua kama kuna mtu yeyote halafu yeye Obi na kijana mmoja wakaingia ndani.Waliingia kwa tahadhari kubwa sana.Nyumba ilikuwa kimya kabisa.walipita sebuleni ,wakakagua vyumba vingine vya kulala hakukuwa na mtu yeyote na wakati wakiendelea kukagua mmoja wa vijana wa Obi akamuita na kumuonyesha mlango wa nyuma ulikuwa wazi.Obi akamuita Frank na kumuonyesha ule mlango "Yawezekana Marwa aliufungua mlango huu wakati akitafuta chanzo cha umeme kukatika mara kwa mara" akasema Frank na kuchukua simu akampigia Marwa mlinzi wake mkuu pale shambani lakini bado simu yake haikupatikana "Mbona simu yake haipatikani? akajiuliza halafu akaendelea na zoezi la kukagua nyumba.Chumba cha mwisho kukagua kilikuwa ni chumba chake cha kulala.Aliingia kwa wasiwasi mkubwa na kila kitu kilionekana kiko sawa.Hakuna kitu kilichoguswa "Where are you bastard!! akasema kwa sauti ndogo na kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo na kabati lililouziba mlango wa kuingilia katika nyumba ya chini lilionekana kutokuguswa,akalisogelea taratibu kulichunguza lakini lilionekana kama vile alivyoliacha akashusha pumzi Naona kila kitu kiko sawa.Hakuna kitu chocotekilichoguswa.Kama kila kitu kiko sawa kwa nini basi nikatumiwa ule ujumbe nikijulishwa kuwa namba ya siri ya kufungulia mlango 34DN imebadilishwa?akawaza halafu akamtaka Obi na kijana wake watoke wakaendelee kufanya uchunguzi nje na mle chumbani akabaki peke yake.Akalisogeza pembeni kabati na kuingiza namba za siri za kufungulia mlango na hapo ndipo akili zilipotaka kumruka.Mlango uligoma kufunguka na jibu alilopewa ni kwamba namba aliyoingiza si sahihi.Akaingiza tena namba zile lakini zikakataa na ukatolewa ujumbe wa onyo kuwa amebakisha nafasi moja tu ya kujaribu kuufungua mlango ule kabla ya king'ora cha hatari kulia.Frank akasimama akashika kiuno alihisi miguu inamuisha nguvu "Nani huyu aliyethubutu kunifanyia kitu kama hiki? Amewezaje kubadili namba za siri? akajiuliza halafu akampigia simu Obi na kumtaka aende chumbani kwake mara moja.Obi akakimbia na kwenda chumbani "Obi kuna tatizo limetokea.Kuna watu walikuwa humu chumbani" "Wamechukua kitu gani?Walinzi hawakufanikiwa kuwaona ?akauliza Obi na Frank akaegemea ukuta kwani miguu yake alihisi ikiisha nguvu "Tukiwa kule mahala alikotupeleka Winnie,nilitumiwa ujumbe katika simu yangu kwamba namba ya siri ya kufungulia mlango wangu wa kuingia katika chumba cha siri ninakohifadhi vitu vyangu vya siri imebadilishwa na ndiyo maana nikataka kuja hapa haraka na kweli namba imebadilishwa" "Ni nani hao wanaokufuatilia mkuu? "Kuna watu fulani wanafuatilia sana mambo yangu" "Unawafahamu? "Ninawafahamu na wengine ni watu wangu wa karibu." "Tunawafanya nini?Nipe maelekezo" akasema Obi "Tutawatafuta na kuwapata lakini kwanza ni kuufungua mlango huu kufahamu nini hasa walichokuja kukitafuta humu ndani" Frank akamchukua Obi hadi stoo wakachukua vifaa vya kuwawezesha kutoboa tundu kazi na kazi ya kuutoboa ukuta ikaanza.Obi alichukua dakika ishirini kuweza kutoboa tundu katika ukuta lililowazewezesha kupita.Frank akashuka ngazi huku akikimbia na Obi akimfuata nyuma.Moja kwa moja Frank akaelekea katika ofisi yake.Akasimama na kushika kichwa.Vitu vilitawanya na ilionekana kulikuwa na upekuzi mkubwa . "I swear I'm going to kill them!!!..I'm going to kill...!!!! akasema kwa hasira na kuanza kuokota karatasi mbalimbali zilizokuwa zimetupwa chini "Nani hawa waliofanya kitu hiki mkuu? akauliza Obi lakini Frank akujibu kitu alikuwa anafungua droo za kabati haraka haraka na kutazama ndani. "Oh my God!! akasema akiwa amekata tamaa "Nini bosi kuna kitu cha muhimu wamechukua?akauliza Obi "My laptop!! akasema Frank na kukaa juu ya meza Ndani ya kompyuta hiyo kuna mambo yoyote ya muhimu ulikuwa umeyahifadi? "Kuna mambo ya muhimu sana na nyeti ambayo sikutaka mtu yeyote ayafahamu" akasema Frank kwa masikitiko "Ni akina nani hawa waliokufanyia hivi?akauliza "Wamecheza na petroli kwenye moto na wataijua nguvu yangu.!!!! akasema kwa hasira Frank "Wote waliohusika katika jambo hili wao na familia zao hakuna atakayesalimika.Kila walilolitenda la kuvamia makazi yangu ni tangazo la vita na ninaapa nitawafyeka hadi kizazi chao.Sintakuwa na huruma kabisa katika hili" akasema Frank "Mungu atanisamehe kwa hiki ninachokwenda kukifanya kwa wote waliofanya ujinga huu!! akasema Frank na kuusukuma mlango unaoingia katika chumba cha kuhifadhi vitu vyake ambao ulikuwa umepigwa na kilipuzi na ukawa wazi akakuta makasha ya mbao yaliyojaa viatu yakiwa yamesambazwa. "Walikuwa wanatafuta nini hasa mkuu hadi wakapekua namna hii? akauliza Obi "Stop asking question Obi.Jiandae kwa kazi.Safari hii sitaki makosa.Sitaki mahojiano nataka kifanyike kitu kimoja tu.Kutoa rho ya kila nitakayekuelekeza.Mungu atanisamehe kwa hili" akasema Frank "sawa bosi ninasubiri kauli yako"akasema Obi "Nimekwisha kwambia kwamba jiandae kwa kazi kubwa.Roho za watu wengi zitaondoka katika hili lakini kabla ya yote namtaka Winnie hapa ndani.Mleteni haraka sana" akasema Frank na biakatka baada ya dakika tano akarejea akiwa na Winnie.Frank akamtaka Obi amfungue awe huru na kumuamuru atoke mle ndani "Winnie nimekuita hapa kwa mara ya mwisho kwani una dakika chache sana za kuendelea kuivuta pumzi" akanyamaza na kumtazama Winnie aliyekuwa akitetemeka kwa woga "Hii ni ofisi yangu ya siri ambayo huhifadhi nyaraka zangu za siri.Muda mfupi uliopita imevamiwa na watu wasiojulikana na unajionea mwenyewe mambo waliyoyafanya.Wamepekua kila mahala wamevuruga ofisi yangu na wamechukua kila walichoona kinawafaa wakaondoka.Hili ni tangazo la vita kati yangu na wao" akanyamaza akavuta pumzi ndefu halafu akaendeleaNinaamini kabisa kwamba miongoni mwa hao jamaa waliofanya uchokozi huu ni dada yako Vicky na kwa kitendo hiki nimeamua kulipiza kisasi kibaya sana kwao.Mimi huwa sichezewi kiasi hiki.Huu ni uchokozi uliovuka mipaka na nitawafanyia kitu kibaya mno.Nitawateketeza wao na familia zao.Nitakiondoa kizazi chao hapa duniani.Mungu atanisamehe kwa hili ninalokwenda kulifanya."akasema kwa hasira "Frank please dont kill me!! Winnie akalia huku mwili wote ukimtetemeka kwa woga.Frank alikuwa amekasirika mno. "Kuna kitu kimoja tu ambacho kinaweza kukuokoa Winnie na kunifanya nibadili adhabu yangu kwako.Nataka unieleze ukweli ni wapi alipo dada yako?Ukinieleza hilo nakuahidi nitakuacha huru.Mimi ni mtu ninayetembea katika maneno yangu hivyo nikisema nitakuacha huru amini nitakuacha huru.Winnie wewe bado msichana mdogo na una mambo mengi bado ya kufanya katika maisha,una ndoto nyingi za kutimiza na unayapenda maisha yako lakini utayatimiza hayo yote endapo tu utanieleza ukweli.Chaguo ni lako aidha unieleze ukweli uendelee kuishi au nikutoe roho.Ninakupa sekunde sitini za kuamua hatima ya maisha yako"akasema Frank "Frank sifahamu mahala pengine ninapoweza kumpata dada kwa wakati huu zaidi ya pale nilipowapeleka.Tafadhali naomba usiniue Frank nakuomba sana"akalia Winnie "Thirty seconds!! akasema Frank "Frank please I'm telling the truth!! akazidi kulia Winnie "Ten seconds!! akasema Frank "Frank nakuomba tafadhali!! akalia Winnie "Five seconds!! akasema Frank na Winnie akaongeza kulia akiomba Frank asimuue "Two Seconds!! akasema Frank na kutoa bastora akamlenga Winnie "Nimekupa nafasi ya kufanya uchaguzi kuhusu maisha yako nawe umechagua kufa.Kwa heri Winnie" akasema Frank na bila huruma akaachia risasi tatu kutoka katika bastora yake zilizomkosa Winnie na kuvunja kioo cha kabati Winnie akaanguka kwa woga "Una bahati ninahitaji bado kukutumia vinginevyo ningeweza kukutoa uhai"akawaza Frank akiwa amewaka kwa hasira.Akamuita Obi Toa hii takataka nenda kaifunge garini bado nitahitaji kumtumia" akasema Frank "Mkuu kuna taarifa nimepewa na vijana waliokuwa wanazunguka nyumba kwamba wameokota miili ya watu wawili karibu na mashine ya kufua umeme wakiwa hawana fahamu" "Wako wapi hao watu? akauliza Frank "Wameletwa wako hapo nje" akajibu Obi halafu wakatoka haraka kwenda kuwatazama watu wale ni akina nani "Oh my God ! Ni akina Marwa.Are they still breating?akauliza Frank kwa masikitiko "Wanaonekana bado wanapumua japo kwa mali" akasema Obi na Frank akaagiza wapakiwe garini ili wawakimbize hospitali.Akawataka vijana watatu wabaki pale nyumbani wakilinda yeye na wengine wote wakaingia katika magari na kuondoka kuwahi hospitali kuokoa maisha ya akina Marwa "Ninarudia tena kwamba hakuna aliyeshiriki katika unyama huu atabaki salama.Swali linalonila akili ni je watu hawa ni akina nani na kitu gani wanakitafuta kwangu? Lakini mkosi wote huu umeletwa na Graca na mama yake.Kama asingeiiba kompyuta yangu haya yote yasingejulikana.Nilikuwa na mipango naye mizuri sana ya kumjengea maisha bora lakini akapuuza hayo yote na akachagua kushirikiana na akina Elvis" Mara tu alipokumbuka Elvis akahisi mwili wote unamsisimka "Bado sijapata jibu kuhuus huyu Elvis ambaye Winnie amemtaja kuwa ni mmoja wa watu waliomteka Vicky.Kama ni kweli huyu Elvis ametokea wapi wakati Elvis ninayemfahamu aliyekuwa akinifuatilia amekwisha uawa?Kuna Elvis wawili katika idara ya ujasusi? Au kuna mtumwinine amejipa jina la Elvis ?akajiuliza "Jambo hili linazidi kunichanganya lakini nitapata majibu pale tu nitakapofanikiwa kumpata Vicky.Yeye ndiye anayeweza kunihakikishia ni Elvis yupi ambaye Winnie amemtaja"akaendelea kuwaza Frank. Waliwafikisha akina Marwa hospitali na kwa haraka wakapatiwa huduma.Wakati wakiendelea kuhudumiwa Frank akawataka akina Obi waondoke kwani walikuwa na mambo mengi ya kufanya kwa usiku ule Tunaelekea wapi mkuu? akauliza Obi "Nahitaji kumuhoji zaidi Winnie.Nikimpata dada yake nitakuwanimepata jibu la kila kilichotokea usiku huu.Ni yeye pekee anayeweza kunisaidia kumpata Vicky.Turejee kule mahala tulikokwenda mwanzo" akasema Frank wakaondoka pale hospitali kurejea tena katika makazi ya akina Elvis
Baada ya kutoka shambani kwa Frank,akina Elvis walirejea katika makazi yao.Mara tu walipofika wakastushwa na kukuta mlango mdogo katika geti la nyumba yao ukiwa wazi Winnie amerejea? akauliza Vicky lakini hakuna aliyemjibu kila mmoja akatoa bastora yake,wakashuka garini na kuingia ndani kwa tahadhari kubwa.Walizunguka nyumba yote lakini hawakuona dalili zozote za kuwepo mtu "Kote kuko salama" akasema Steve kisha wakaingia ndani na kukuta sebuleni si kama walivyopaacha "Some one was here" akasema Elvis na kwa tahadhari wakaanza kuzungukia vyumba vyote wakakuta milango yote iko wazi "Yawezekana ni Winnie aliamua kurudi na alipotukosa akaondoka tena" akasema Vicky "Hapana si winnie.Kuna watu wengine wamekuja hapa wakati hatupo na inaonekana kuna kituwalikuwa wanakitafuta.Tutaufahamu ukweli" akasema Elvis na kuchukua kadi ndogo ya kuhifadhia kumbu kumbu katika kamera ndogo za siri alizozifunga na wote wakaenda sebuleni akaiweka kadi ile katika kompyuta na kuanza kutazama toka muda ule walipoondoka pale nyumbani.Hakukuwa na mtu yeyote aliyeonekana katika kamera hadi zilipopita dakika hamsini ndipo kamera iliyoelekezwa getini ikaonyesha watu sita wakiruka ukuta na kuingia ndani "Hawa hapa" akasema Elvis na kurudisha nyuma kidogo wakaanza kuwafuatilia.Hawakuwa wameziba nyuso zao mmoja wao akasogelea mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni ndipo Vicky akamtambua "Nimemkumbuka mtu huyu.Ni yule aliyetuvamia nyumbani asubuhi.Amenifuata hadi huku? akasema na Steve akamtazama akathibitisha kuwa ndiye.Kamera iliyokuwa sebuleni ikawaonyesha wale jamaa wakifuata korido kuelekea vyumbani ambako hakukuwa na kamera nyingine iliyofungwa.Baada ya muda wakarejea sebuleni na yule kiongozi akatoa simu akazungumza na mtu fulani na kutoka na baada ya dakika kama tatu hivi akarejea akiwa ameongozana na watu ambao waliwawafanya wote mle ndani wapatwe na mshangao "Baba!! akasema Graca "Winnie? akasema Vicky "Sasa picha limekolea.Winnie na Frank? Wamekutana wapi?Wanafahamiana?akauliza Elvis akimtazama Vicky "Frank na Winnie wanafahamiana? akauliza Elvis Hapana hawafahamiani.Sijawahi kumtambulisha Frank kwa Winnie hata mara moja.Makutano yetu yote huwa ni nje ya nyumbani.Hata mimi nashangaa wamekutana wapi?akasema Vicky na katika kumbukumbu ya kamera ikaonekana Winnie akiwa amepigishwa magoti na Frank aliyekuwa amefura hasira akamnyooshea bastora na ilionekana kuna kitu alikuwa anamuuliza.Winnie akalia akiomba na Frank akaachia risasi zilizovunja kioo cha kabati na Winnie akaanguka chini na baada ya muda akafungwa mikono na kutolewa nje.Vicky akashindwa kujizuia akatokwa na machozi "Jamani mdogo wangu" akasema "Stop crying Vicky!! akasema Elvis.Kamera ilimuonyesha Frank akiwa sebuleni na baadae akaitoa simu yake akasoma ujumbe kisha akatoka mbio na kamera ya nje ikamuonyesha akitoka nje ya geti.Hawakuonekana tena "Walikuja hapa kutufuata sisi.Tayari wamekwisha tufahamu mahala tulipo na ndiyo maana wakaja na kikosi wamejiandaa kwa mapambano" akasema Elvis "Lakini wamefahamuje kuhusu sisi? Wamempataje Winnie?akauliza Vicky "Winnie ndiye anayepaswa kujibu swali hilo.Kupitia kwake tutafahamu ni vipi ameweza kukutana na akina Frank" "Elvis tafadhali nawaomba tufanye kila lililo ndani ya uwezo wetu kumuokoa mdogo wangu.I won't forgive myself if anything bad happens to her!! akasema Vicky huku macho yake yamejaa machozi We'll do everything we can but right now we have to get out of here.Tuchukue kila kinachotufaa tuondoke kwani mahala hapa si salama tena.Tayari tumegundulika" akasema Elvis "Tunakwenda wapi? Steve akauliza "Tutajua baada ya kutoka hapa" akasema Elvis na kuchukua smu yake akampigia Meshack Jumbo akamjulisha kilichotokea na kumuahidi kumpigia tena simu baadae.Akachukua kompyuta ya Frank aliyopewa na Graca na kila kilicho chake akavipeleka garini.Zoezi hilo halikuchukua muda mrefu wakafunga nyumba na kuondoka "Tunaelekea wapi? akauliza VickyBado sifahamu lakini tuondoke kwanza hapa kisha tutapata sehemu ya kwenda" akasema Elvis "Ninayo nyumba yangu ambayo imekamilika ninataka kuitumia kwa biashara ya kupangisha.Iko sehemu tulivu.Tunaweza kuhamishia makazi ya muda hapo" akasema Vicky "Winnie anapafahamu mahala hapo?Elvis akauliza "Hapana hapafahamu" "Good.Tupeleke hapo tuweke makazi ya muda" akasema Elvis na kumgeukia Omola "Omola endelea kumfuatilia Winnie ili tufahamu mahala alipo" akasema na Omola akawasha kompyuta yake na kusema "Simu yake bado imezimwa" "Endelea kumfuatilia na kama kuna chochote utakigundua utujulishe" akasema Elvis na safari ikaendelea.Garini kila mmoja alikuwa kimya akiwaza lake.Kitendo cha Frank kugundua mahala walipo kiliwastua sana "Steve alinionya kuhusu kuwakaribisha akina Vicky pale nyumbani lakini kinapuuzia na hiki ndicho kilichotokea.Pamoja na kumuonya Winnie hakutaka kutusikia akakimbia na sasa amesababisha madhara.Amekamatwa na akina Frank ameteswa na amewaonyesha mahala ulipo.Ni vipi endapo atawaeleza kuwa bado niko hai? akajiuliza na kuhisi joto la ghafla licha ya gari kuwa na kipoza hewa "Kama wakigundua niko hai kila kitu kitaharibika na nitawaweka katika hatari watu watu wengi akiwamo mke wangu Patricia.Natakiwa kuchukua hatua za haraka sana za kumnusuru Patricia.Anatakiwa ahame haraka sana kwa akina Juliana na atafutiwe makazi mengine na hata ikiwezekana ahamishiwe nje ya nchi kwa muda hado hapo mambo yatakapotulia.Nitazungumza na mkurugenzi baadae kuhusu jambo hili lakini kesho asubuhi lazima Patricia aondoke haraka sana pale kwa akina Juliana" akaendelea kuwaza Walifika katika nyumba ya Vicky ambayo tayari ilikwisha kamilika na ilikuwa ikisubiri mpangaji. "Nyumba nzuri sana hii.Hongera Vicky"akasema Steve mara tu walipoingia ndani.Ilikuwa imekamilika na ilikuwa na kila kitu ndani "Nyumba hii nina mpango wa kukodisha raia wa kigeni ambao wanakuja kufanya kazi Tanzania na ndiyo maana nimeweka kila kitu ndani.Karibuni jisikieni nyumbani" akasema Vicky "Ahsante Vicky tumekwisha karibia lakini hatuna muda wa kupumzika tunaendelea na kazi.Hakuna kulala leo"akasema Elvis.Saa ilionyesha ni saa nane kasoro dakika ishirini na mbili "Zoezi letu limekwenda vizuri licha ya hili lililojitokeza la Frank kugundua makazi yetu ila nawasihi msiogope .Tuko salama na hakuna kitakachotokea tukashindwa kukidhibiti.Tumepata nyaraka kadhaa kutoka kule kwa Frank pamoja na komputa yake ambavyo tunaamini vinaweza kutusaidia kupata mambo ya muhimu kuhusu mtandao wao wa kuuza silaha.Steve weka kila kitu mezani tuanze kupitia nyaraka hizo_Omola wewe utaikagua kompyuta hii ya Frank na kama kuna kituchochote cha maana utatujulisha" akasema Elvis na Steve akaweka mezani bahasha ile yenye nyaraka mbalimbali na Elvis akamgawia Steve na Vicky kila mmoja nyaraka zake azipitie.Baada ya muda Steve akasema "Elvis ulisema ndani ya kile chumba mlikuta kuna shehena ya viatu? "Ndiyo kuna shehena kubwa ya viatu" "Basi hapa nina nyaraka zinazoonyesha kuwa wiki tatu zilizopita kuna kontena kumi na nane za viatu zilitolewa bandarini.Kontena hizi zote zinakwenda kwa kampuni ya Pendeza Co.Ltd" "Thats's interesting.Inawezekana labda mzigo hupo wa viatu ndiyo ule tumekuta katika kile chumba cha siri cha Frank?akauliza Hapo ndipo tunapaswa kuchunguza"akasema Steve "Tuichunguze kwanza kampuni hii ya Pendeza Co.Ltd tumfahamu mmiliki wake ni nani na kama Frank ana uhusika wowote katika kampuni hii" akasema "Guys I got something" akasema Omola aliyekuwa akiipekua kompyuta ya Frank,wote wakamsogelea "Nini umekipata? akauliza "Kuna barua pepe nimefanikiwa kuzipata.Barua pepe hizi ni nakala ambazo mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya McLolien anaitwa Shanon blank alikuwa anawasiliana na mtu anaitwa Patrice Lwibombe.Mawasiliano yao ni kwa lugha ya kifaransa.Katika mawasiliano hayo Shanon anamlalamikia Patrice kwa kuchelewesha malipo ya mzigo waliopewa.Patrice akamuhakikishia Shanon kuwa kabla ya wiki kumalizika watalipa pesa yote.Akaendelea kujitetea kwamba makusanyo hayakuwa mazuri kutokana na mapambano makali ya vikosi vya Serikali ya Congo vikisaidiana na vile vya kutoka umoja wa Afrika na kuwarudisha nyuma kidogo.Shanon amemuahidi Patrice kwamba watakapolipa deni lao basi watatumiwa mzigo mkubwa haraka sana.Frank ametumiwa nakala za mawasiliano hayo wiki moja iliyopita" akasema Omola "Finaly we got them" akasema Elvis kwa furaha. "Subiri kidogo Elvis" akasema Steve "Maelezo haya ya Shanon yametoa picha fulani.Nyaraka hizi za kutolea mzigo bandarini zinaonyesha kwamba zile kontena za viatu zilitumwa na kampuni ya McLorien .Tayari picha imeanza kujitokeza"akasema Steve "Ni kweli Steve picha imeanza kujitokeza na kueleweka.Hii kampuni ya McLorien ndio waliotuma mzigo ule wa viatu kwa kampuni ya Pendeza Co.Ltd.Mmiliki wake Shanon Blank ana mawasiliano na Frank na katika mawasiliano hayo tunaona akiwasiliana na Patrice ambaye hakuna shaka kwamba ana mahusiano na kundi la waasi kwani amekiri kwamba wamechelewa kulipa fedha kwa sababu ya mapambano makali na vikosi vya serikali na vile vya umoja wa Afrika.Tunaona Shanon anamsisitiza Patrice alipe deni lao na halafu watumiwe mzigo mwingine ambao ninaamini ni silaha.Kwa hiyo sasa tuna kampuni mbili ambazo tunapaswa kuzichunguza.Kwanza ni hii Pendeza na pili ni hii McLorien.Tunapaswa kuifahamu vyema kampuni hii ya McLorien na vile vile tumfahamu huyu Patrice ni nani na yuko wapi.Tunatakiwa kufahamu ni namna gani silaha zinaingia hapa nchini?Omola anza kufanya uchunguzi wa kampuni hii ya McLorien tufahamu mmiliki wake ni nani na inajishughulisha na nini? Vile vile fuatilia huyu Patrice ni nani na yuko wapi?akasema Elvis na Omola akaenda kuketi mezani kuendelea na kazi aliyopewa "Wakati Omola akiendelea na uchunguzi wa kampuni ya McLorien sisi tutaendelea kuichunguza kampuni ya Pendeza.Tutamtumia Mkurugenzi kwani yeye anao uwezo wa kuingia katika mtandao wa taasisi yoyote.Nataka atusaidie kuingia katika mtandao wa wakala wa kusajili biashara na makampuni ili tuifahamu vyema kampuni hii ya Pendeza iko wapi na mmiliki wake ni nani?akasema Elvis na kisha akatoa simu na kuzungumza na Meshack Jumbo "Mkurugenzi kuna jambo tunahitaji msaada wako" akasema Elvis "Jambo gani Elvis?Mko wapi sasa hivi? "Tumepata hifadhi sehemu fulani salama"akasema Elvis na ukimya mfupi ukapita akaendelea "Kama nilivyokueleza kuwa tumetoka katika nyumba ya Frank iliyoko shambani kwake na kule tumeingia katika ofisi yake ya siri iliyoko chini ya nyumba.Ndani ya ofisi hiyo tumefanikiwa kupata nyaraka kadhaa pamoja na kompyuta ndogo ambavyo tumekwisha anza kuvifanyia uchunguzi.Ndani ya ofisi hiyo ya siri kuna chumba kikubwa ambacho kinatumika katika kuhifadhi vitu na tumekuta kuna shehena kubwa ya viatu.Katika nyaraka tulizozipata katika ofisi hiyo ya Frank zipo zinazoonyesha kuwa kuna mzigo wa kontena kumi na nane umetolewa bandarini wiki nne zilizopita ambazo zinaonyesha ni mzigo wa viatu.Kontena hizo zinaonekana kutumwa na kampuni inaitwa McLorien na kampuni iliyotumiwa mzigo huo hapa Tanzania inaitwa Pendeza Co.Ltd.Katika komputa tuliyoichukua katika ofisi hiyo tumefanikiwa kupata nakala za barua pepe ambazo Frank ametumiwa na mtu moja anaitwa Shanon Blank ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya McLorien ambaye alikuwa akiwasiliana na mtu anaitwa Patrice Lwibombe.Shanon anamuuliza Patrice kuhusu kuchelewa kuwasilisha malipo baada ya kukabidhiwa mzigo na Patrice akaahidi kulipa haraka sana pesa hizo huku akijitetea kwamba wameshindwa kulipa kwa wakati kutokana na mapambano kuwa makali kati yao na vikosi vya serikali vikisaidiwa na vile vya umoja wa Afrika" "Ouh hizo ni habari njema sana.Tayari tumepata mwanga.Huyu Patrice lazima ana mahusiano na waasi ambao wanauziwa silaha na akina Frank"akasema Meshack Jumbo "Ndiyo mzee.Tayari tumekwisha anza uchunguzi kuhusiana na kampuni hii ya McLorien pamoja na kumfahamu huyu Patrice ni nani,yuko wapi na anajishughulisha na nini.Msaada tunaohitaji toka kwako ni kuichunguza kampuni ya Pendeza Co.Ltd ya hapa Tanzania ili tumfahamu miliki wake kwani kampuni hii ina mashirikiano na kampuni ya McLorien ambao tunaamini wana mashrikiano ya kibiashara na Patrice ambaye tunaamini anahusiana na waasi wanaopigana na serikali ya Congo.Tunaomba utusaidie kuingia katika mtandao wa msajili wa viwanda na baishara Tanzania ili tufahamu mmiliki wa kampuni hii ya Pendeza Co.Ltd"akasema Elvis "Sawa Elvis nipe dakika tano halafu nitakupa majibu.Ninachowataka kuanzia sasa mnapaswa muwe makini sana kwani hali imebadilika na kwa hiki kilichotokea usiku huu kinaonyesha wazi kwamba hali si salama kwetu.Tunatajiwa kufanya haraka sana kulimaliza suala hili kabla ya akina Frank hawajagundua kwamba uko hai"akasema Meshack na kumtaka Elvis amsubiri kwa dakika kadhaa ili aweze kumpa majibu ya kuhusiana na kampuni ya Pendeza Co.Ltd "Elvis nini tunafanya kumpata Winnie? akauliza Vicky ambaye alionekana kuwa mbali sana kimawazo. "Vicky kwa sasa tujielekeze kwanza katika mambo ya msingi na baadae tutaangalia namna ya kumtafuta Winnie ambaye hatufahamu mahala alipo.Usihofu Vicky tutafanya kila tuwezalo kumpata mdogo wako" akasema Elvis "Elvis we need to do something quick.Tukichelewa wale jamaa wataweza kumuua.Tumeona kwenye kamera mambo aliyofanyiwa.Nawaombeni jamani tufanye haraka tukamuokoe" akasema Vicky huku macho yake yamejaa machozi. "Winnie ameyatafuta mwenye haya yote yaliyompata.Kiburi chake kimempomnza kwani hakutaka kuamini kama alikuwa katika mikono salama na badla yake akaamua kuondoka na sasa ametuongezea kazi nyingine.Tumalize kwanza mambo mhimu ndipo tushughulike na hawa watu wenye viburi" akasema Steve na maneno yale yakamkera sana Vicky "Steve ungekuwa mahala pangu kamwe usingethubutu kutamka maneno kama hayo.Winnie ni mdogo wangu wa damu na siwezi kuwa na amani kama hatapatikana akiwa mzima.Wale jamaa wanaweza wakamuua wakati wowote.Please we have to save her" akasema Vicky "Vicky vumilia kidogo tupate majibu ya uchunguzi wetu halafu tutashughulikia suala la mdogo wako"akasema Elvis "Elvis they are going to kill her !! akasema Vicky huku akilia "Niamini Vicky hawataweza kumuua kwani watamtumia yeye ili kuweza kutupata.Kama si hivyo tayari wangeweza kumuua.Naamini Winnie ndiye aliyewaelekeza mahala pale tulipokuwa na uliona katika kumbu kumbu ile ya kamera namna walivyokasirika walipokuta hakuna mtu na ndiyo maana wakamtishia kumuua ili aseme mahala uliko.Niamini tafadhali kwamba tutampata Winnie akiwa mzima.I give you my word" akasema Elvis "Elvis ninakuamini lakini muda tunaoupoteza hapa wale jamaa wanaweza wakamfanya kitu kibaya mdogo wangu." akasema VickyVicky umekwisha hakikishiwa kwamba mdogo wako atakapatikana akiwa mzima sasa hofu ya nini? Tuache tufanye kazi na tukimaliza tutashughulikia suala la mdogo wako" akasema Steve na Vicky akamtazama kwa jicho la chuki "Ninyi ndio mliosababisha haya yote yakatokea.Kama msingenihusisha katika kifo cha Pascal tusingefika hapa tulipofika.Haya yote yameanza baada ya kunilazimisha nishiriki katika kumuua Pascal.Kabla ya hapo maisha yangu yalikuwa na amani na nilikuwa nikiishi na kufanya kazi zangu kwa amani bila matatizo yoyote lakini nilipoanza kushirikiana nanyi ndipo matatizo yote yalipoanza.Kama hamtaki kunisaidia kumtafuta mdogo wangu siendelei kushirikiana nanyi tena.I'm out of the team"akasema Vicky kwa hasira "Kama unataka kufanya ujinga kama aliofanya mdogo wako hadi akakamatwa na akina Frank be our guest!! akasema Steve kwa ukali "Please stop !! akafoka Elvis "Mkitaka tufanikiwe katika hili tunalolifanya mnatakiwa muache mambo ya kitoto na wote muelekeze akili zenu katika jambo zito la maana lililoko mbele yetu.Tuna jukumu zito sana ambalo tunapaswa kulikamilisha na mchango wa kila mmoja wetu aliyeko hapa unahitajika sana.I'm a leader here and you'll all listen to what I say.If anybody of you dont want to listen to me or follow my directions,is allowed to leave right now!!akasema Elvis na kuwatazama Steve na Vicky kwa macho makali "I'm sorry Elvis" akasema Steve "Hakuna anayetaka kuondoka? akauliza Elvis lakini hakuna aliyemjibu "Kama hakuna anayetaka kuondoka basi acheni mambo ya kijinga na tufanye kazi.Vicky nimekwisha kueleza kwamba tutafanya kila tuwezalo kumpata mdogo wako lakini hatuwezi kuacha kazi hii muhimu iliyoko mezani na kuanza kuzunguka kumtafuta Winnie ambaye hatufahamu yuko wapi.Nimekuahidi kufanya kila tuwezalo kumpata na ninaomba uniamini.Kama umeshindwa kuniamini basi ninakupo uhuru uende http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ukamtafute wewe mwenyewe lakini kama unataka mdogo wako apatikane akiwa mzima nisikilize ninachokuambia.Unanielewa Vicky?! akauliza Elvis na Vicky akatikisa kichwa kukubaliana naye Good.Lets get back to work" akasema Elvis "Omola kuna chochote umekipata? akauliza "Nipe dakika chache kuna kitu nakifuatilia " akajibu Omola "Wakati tukisubiri kupata majibu kutoka kwa mkurugenzi tutafakari namna akina Frank walivyoweza kumpata Winnie." "Yawezekana walimpigia simu na kumtaka waonane" akasema Steve "Wanafahamu njia nyepesi ya kumpata Vicky ni kwa kumtumia Winnie na ndiyo maana wakawekeza nguvu katika kumsaka.Mkumbuke mtandao huu ni mkubwa na wanaweza wakafanya jambo lolote" akasema Steve "Kuna jambo moja linanipa wasiwasi kidogo lakini sina hakika kama linaweza kuwa na mahusiano na hiki kilichotokea" akasema Graca ambaye toka walipofika hapa amekuwa kimya "Katika uchunguzi hata jambo dogo sana linaweza kuwa na msaada mkubwa.Tueleze hicho kinachokupa wasi wasi" akasema Elvis "Tukiwa chumbani nilimueleza Winnie historia ya maisha yangu na akashangaa sana.Akaniuliza maswali mengi kuhusiana na baba yangu" "Maswali gani aliyauliza? akauliza Elvis "Alitaka kufahamu nyumbani kwetu,na kwa namna alivyokuwa anauliza maswali yake ni kama vile alikuwa anatafuta njia nyepesi ya kuweza kuonana na baba.Mimi sikumtilia maanani na nikamueleza kila kitu nikiamini mimi na yeye sote tuko katika boti moja.Nilipomuona akiwa na baba nikakumbuka maswali yale aliyokuwa ananiuliza kuhusiana na baba." akasema Graca "Graca unahisi kwamba Winnie alikwenda mwenyewe kwa Frank?akauliza Elvis "Exactly!! akasema Graca "Wait" akasema Vicky "Kuna kitu hata mimi nimekikumbuka kuhusiana na hiki anachokisema Graca.Jana niliporejea kutoka kuonana na rais,Elvis alinitaka nizungumze na Winnie na nimsihi atulie kwani hali hii ni kwa muda tu na baadae maisha yetu yatarejea kama kawaida.Nilimuita chumbani nikamuelewesha akanielewa na ninakumbuka aliniuliza kama ninamfahamu Frank nikamwambia kwamba Frank ni rafiki yangu.Sikujua kwa nini aliniuliza swali lile lakini sasa ninaanza kupata picha ya swali lake.Kuna uwezekano mkubwa kwamba Winnie alikwenda kumfuata Frank yeye mwenyewe" "Lakini kwa nini afanye hivyo? Kwa nini akamtafute Frank wakati tayari Graca amekwisha msimulia kila kitu kuhusiana naye na anafahamu kuwa ndiye anayewawinda?Steve akauliza "Hayo ni mawazo yangu tu lakini majibu yote anayo yeye mwenyewe Winnie.Tukimpata atatupa majibu namna alivyok................." Vicky akanyamaza baada ya simu ya Elvis kuita,alikuwa ni Meshack Jumbo,Elvis akaipokea haraka haraka "Elvis nimefuatilia ile kampuni kama ulivyonitaka na nimepata majibu.Kampuni hii imesajiliwa hapa Tanzania na mmiliki wake anaitwa Irene mwabukusi.Mmiliki wake ni moja tu na Frank hajaorodhshwa kokote kama mmiliki wa kampuni hii.Nadhani mtu wa kumchunguza hapa ni huyo Irene kujua namna anavyoshiriana na Frank" akasema Meshack "Ahsante sana mzee kwa msaada huo mkubwa.Tutakujulisha nini tutakipata kutoka kwa Irene" akasema Elvis "Kitu kingine Elvis,tayari nimekwisha anza kufuatilia nyumba niliyokwambia kwamba Patricia ataishi baada ya kumuondoa kwa akina Juliana na kesho nitakamilisha kila kitu kishaPatricia ahamie hapo.Usihofu kila kitu kitakwenda vyema.Nitawasiliana nanyi mchana kujua mlikofikia na kuwajulisha ni wapi nimefikia.Ninachowaomba vijana wangu jitahidini sana kuwa waangalifu hasa wakati huu ambao Frank na watu wake wanamtafuta sana Vicky" Usijali mzee tuko makini" akajibu Elvis na kukata simu akawageukia wenzake "Mzee anasema kwamba mmiliki wa kampuni ya Pendeza Co.Ltd anaitwa Irene Mwabukusi.Anadai Frank hahuski chochote na kampuni hii hivyo kazi yetu sasa ni kumsaka huyo Irene na tukimpata tumuhoji tufahamu uhusianao wake na Frank na mahusiano yake na kampuni ya McLorien.Steven kesho asubuhi itakuwa ni kazi yako ya kwanza kumtafuta Irene na kuhakikishe kabla ya saa nne asubuhi umekwisha mpata na kupata majibu toka kwake." "Sawa Elvis.Katika nyaraka hizi kumeelekezwa mahala zilipo ofisi za kampuni hiyo ya Pendeza.Itakuwa rahisi kwangu kumpata" "Good.Omola yeye ataanza kazi yake kesho ya kumchunguza makamu wa rais.Mimi na Vicky tutashughulikia suala la Winnie.Gracayeye ataendelea kupumzika" akasema Elvis na kumgeukia Omola "Omola kuna chocte mpaka sasa hivi? "Kwa taarifa nilizofanikiwa kuzipata kutoka katika mtandao ni kwamba kampuni hii ya McLorien imesajiliwa nchini Marekani.Ni kampuni mama ambayo ndani yake kuna benki na makampuni mengine mbali mbali.Hakuna taarifa nyingi za kutuwezesha kuifahamu kampuni hii kiundani hata hivyo nimewasiliana kwa barua pepe na rafiki yangu mmoja aliyeko nchini Marekani ili anisaidie kupata taarifa za kuhusiana na kampuni hii ya McLorien.Kwa kuwa tayari imeingia katika mikono yetu lazima ichunguzwe hadi mzizi wake.Kesho tutapata jibu kuhusiana na hii kampuni" akasema Omola "Sawa Omola ahsante kwa kazi nzuri.Tunaitegemea sana taarifa hiyo ya kuhusiana na hii kampuni.Vipi kuhusu Winnie unaweza kumtafuta tena na kujua mahala alipo?akauliza Elvis "Bado simu yake imezimwa" akajibu Omola baada ya kubofya kompyuta yake "Hakuna tatizo kesho tutamsaka na kumpata.Ni usiku mwingi tayari na ni wakati wa kupumzisha miili yetu kujiandaa kwa siku ya kesho ambayo itakuwa ni ndefu sana.Ahsanteni nyote kwa ushirkiano mkubwa na tumeweza kufanikiwa kupata mambo ya kutusaidia katika uchunguzi wetu.Steve utampeleka Omola hotelini kwake akapumzike kwani kesho asubuhi anatakiwa kuanza shughuli iliyomleta hapa Tanzania" akasema Elvis na kuagana na Omola akangia garini na Steve akamrejesha hotelini alikofikia "Vicky naendelea kukusihi kwamba usiwe na wasi wasi hata kidogo tutampata Wema.Kwa sasa hawataweza kumuua kwani wanaamini yeye ndiye njia pekee ya kuweza kuwafikisha kwako japo mateso atayapata"Elvis akamwamia Vcky "Elvis moyo wangu umekosa amani kabisa kwa hawa jama kumshikilia mdogo wangu.Ni vipi kama watamtesa na akawaeleza kwamba mimi ni mpelelezi?Sitaki siri hii ijulikane.Elvis we have to do whatever we can to get her back.Can you promise me that? Elvis akamtazama Vicky usoni na kusema "I give you my word we'll get her back alive" "Thank you" akasema Vicky "Ni wakati wa kwenda kupumzika tuelekeze vyumba vyetu vya kulala" "Nyumba hii haina vyumba vingi kama ile mliyokuwa mnaitumia ila vilivyopo vitatutosha." akasema Vicky na kumuongoza Elvis hadi katika chumba watakamolala halafu yeye na Graca wakaelekea katika chumba kingine.Mara tu walipoingia chumbani wakijiandaa kupumzika Graca akamwambia Vicky kuwa kuna kitu anataka azungumze na Elvis akamfuata chumbani kwake akagonga mlango na Elvis akafungua "Graca,karibu ndani" akasema Elvis na kumkaribisa Graca ndani "Elvis nimekuja kukuaga mpenzi wangu.Siwezi kulala bila kukubusu" akasema Graca na kumsogelea Elvis akamkumbatia na kumbusu. "Graca kama nilivyokuleza kwamba unatakiwa uwe makini sana watu humu ndani wasifahamu kama mimi na wewe tunakutana.Hii ni siri yetu.Umenielewa? "Nimekuelewa Elvis lakini wakati mwingine ninashindwa kujizuia kwa mfano usiku huu sijui kama ningepata usingizi bila kukubusu.Ninakupenda sana Elvis zaidi ya unavyoweza kufikiri" akasema Graca akiwa bado amemkumbatia Elvis.Taratibu Elvis akaitoa mikono yake na kusema "Graca nakushukuru sana kwa msaada wako uliotusaidia siku ya leo.Nina imani kubwa kwamba yale yote tuliyofanikiwa kuyagundua ofisini kwa baba yako usiku wa leo yatakuwa na manufaa makubwa sana katika uchunguzi wetu" Ahsante sana Elvis.Nimejitolea kufanya lolote lile kwa ajili yako.Ngoja nirejee chumbani Vicky asinisubiri sana.I love you" akasema Graca na kumbusu tena Elvis kisha akatoka kurejea chumbani kwao "Kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo Graca anavyozidi kuchanganyikiwa juu yangu.Sikupaswa kabisa kufanya naye mapenzi lakini sikuwa na namna nyingine ya kuweza kupata taarifa muhimu tuliyoihitaji mno.Hili si suala la kupuuzia na kulichukulia kirasirahisi kwani Graca tayari anaamini nimekubali toka moyoni kuwa naye.Ni vipi atakapogundua kwamba nilimdanganya ili niweze kupata taarifa toka kwake? Hata hivyo sitakiwi kuumizwa na jambo kama hili wakati katika mto na kuanza kutafakari jukumu zito lililo mbele yao
Frank,Obi na vijana walioongozana nao wakarejea tena katika makazi ya akina Elvis na kukuta mlango mdogo wa geti waliouacha wazi ukiwa umefungwa. "Mlango huu tuliuacha wazi lakini umefungwa.Hii inaonyesha hawa jamaa tayari wamekwisha rejea na wako ndani" akasema Obi "Wapange vijana haraka sana muingie ndani na muwe waangalifu sana.Jitahidini kuwadhibiti ninawahitaji wote wakiwa hai" akasema Frank na Obi akawapa maelekezo ya kufanya vijana wake halafu yeye na vijana wanne wakarukia ndani na baada ya kuhakikisha kuko shwari wakaelekea katika mlango wa kuingilia sebuleni wakachungulia ndani hakukuwa na dalili zozote za mtu licha ya taa kuwaka.Akajaribu kukinyonga kitasa mlango ulikuwa umefungwa kwa funguo.Akawafanyia ishara vijana wake wakae tayari akatoa funguo bandia na kuufungua ule mlango na kisha akaingia sebuleni akifuatiwa na vijana wawili .Walikagua nyumba yote lakini hakukuwa na mtu,akampigia simu Frank "Mkuu hakuna mtu ila inaonekana walikuwa hapa muda si mrefu kwani wamechukua vitu vyao na kuondoka.Hakuna nguo wala mabegi tuliyoyakuta wakati ule" "Damn it !! akasema kwa hasira Frank huku akiupiga usukani kwa mikono yake.Akaegemea kiti na kuzama mawazoni "Sijawahi endeshwa na mtu yeyote kama hivi sasa ninavyoendeshwa na hawa jamaa.Lakini sikati tamaa lazima watapatikana tu.Mimi huwa sichezewi kiasi hiki.Watauona moto wangu" akawaza Frank halafu akamgeukia Winnie aliyekuwa amefungwa mikono kiti cha nyuma "Winnie ninakupa nafasi ya mwisho ya kunionyesha mahala alipo dada yako" akasema "Frank nakuomba mzee uniamini ninalokwambia.Dada na hao jamaa niliokueleza wanaishi katika nyumba hii.Tuendelee kusubiri lazima watarudi" akasema Winnie.Frank akatafakari halafu akatoa simu katika droo ya gari na kumfungua Winnie mikono akampa ile simu "Simu yako hii nataka uiwashe na uwasiliane na dada yako mwambie kwamba uko hapa na akufuate mara moja" akaamuru.Winnie akawasha simu ile na kuzitafuta namba za Vicky akapiga lakini simu ya Vicky haikuwa ikipatikana.Akapiga tena jibu likawa lile lile simu ya Vicky haipatikani "Endelea kujaribu kupiga kila baada ya dakika kumi.Leo tutaendelea kukaa hapa hapa hadi asubuhi.Lazima tuwasubiri" akasema Frank na kumpigia simu Obi akamtaka atoke mle ndani na kuwapanga vijana pale nje wawasubiri akina Elvis "Uzima wako ni pale dada yako atakapopatikana lakini kama ukishindwa kusaidia katika kumpata basi jihesabu wewe tayari ni mfu" akasema Frank "Frank nakuomba tafadhali usiniue.Kama ningejua mahala ambako dada anaweza kupatikana ningewaeleza lakini sijui.Ninafahamu mahala hapa kwani hata mimi nilikuwa nimefungiwa hapa" akasema Winnie " Salama yako ni kama watarejea hapa lakini kama wasipoonekana ninasikitika kwamba sintaendelea kukuacha hai tena" akasema Frank Masaa yalizidi kusonga bila ya akina Elvis kuonekana pale nyumbani.Taratibu kukaanza kupambazuka na Obi akamfuata Frank ambaye hakufunga ukope wake akisubiri akina Elvis warejee "Mkuu kumeanza kupambazuka na hawa jamaa hawajareea hadi muda huu tufanye nini? akauliza Onbi "Tuondokeni ili watu wasije wakapatwa na wasi wasi wakitukuta hapa ila waache vijana wawili waendelee kuchunguza na pindi wakiwaona akina Elvis wamerejea basi watujulishe mara moja.Huyu msichana mtandoka naye.Hakikisheni mmempa kila aina ya mateso ili aseme ukweli wake ni nani walimtuma kwetu?Kama hata baada ya kuteswa ataendelea kuwa mgumu wa kusema,kill her"akasema Frank huku akimtazama Winnie kwa macho yaliyojaa hasira "Sawa mkuu" akasema Obi na kumshusha Winnie kutoka katika gari la Frank akampakia katika gari lao wakaondoka zao ********************* Siku mpya ilianza na habari kubwa iliyoliamsha taifa asubuhi hii ni onyo la jeshi la polisi likiwaonya wafuasi wa vyama vya upinzani wasithubutu kuhudhuria mkutano ulioitishwa na viongozi wao kwani haukuwa na kibali.Hii ni habari kubwa iliyoandikwa karibu na magazeti yote na kutangazwa na vituo vyote vya redio na runinga.Wakati habari hii ikitangazwa Elvis na Steve tayari walikwisha amka na walikuwa sebuleni wakitazama taarifa ya habari kufuatilia kilichokuwa kinaendelea nchini. "Hakuna jipya haya yote ni ya wanasiasa.Tuwaachie mambo yao na sisi tuendelee na yetu.Nadhani ni wakati wa kwenda kuanza kumfatilia Irene Mwabukusi.Nimefikiria na nimeona itabidi twende wote katika kazi hii.Irene ana mahusiano na akina Frank na hatujui yawezekana naye akawemo katika mtandao wao na hivyo akawa ni mtu mwenye ulinzi au yawezekana Frank akatuma watu kwenda kumuua endapo atagundua kwamba tumezipata nyaraka zile za kutolea mzigo bandarini.Watu hawa ni rahisi sana kuua ili mambo yao yasijulikane" akasema Elvis "Are you sure?Steven akauliza "Yes I'm sure.Siwezi kukuacha ukaenda huko peke yako ni hatari sana.Wasiliana na Samira kama tayari amekwisha fika kumchukua Omola kumpeleka ikulu.Mimi ngoja nikajiandae kwani siwezi kutoka bila kubadili mwonekano wangu" akasema Elvis na kutoka akarejea chumbani kwake akajiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda kuanza kazi. "Ouh ! hakika unajua kujibadilisha mwonekano.Hakuna yeyote atakayekutambua kwa mwonekano huo" akasema Steve aliyeingia chumbani wakati Elvis akijiandaa. "Vipi samira umewasiliana naye? "Ndiyo.Yuko njiani hivi sasa akielekea hotelini kwa Omola" Good.Inabidi tuzungumze pia na Omola.Piga simu hotelini wakuunganishe naye.Halafu itabidi tutafute simu nyngine tatu kwa ajili ya Omola,Vicky na Graca ili iwe rahisi kuwasiliana" akasema Elvis na Steve akapiga simu hotelini kwa Omola akaunganishwa naye "Hallo Steve habari yako?Elvis na wengine wote hawajambo? "Wote wazima kabisa.Vipi wewe hali yako"akauliza Steve na kuiweka simu katika sauti kubwa ili Elvis naye aweze kusikia mazungumzo yale "Hali yangu ni nzuri kabisa.Imekuwa vizuri umewahi kunipigia kwani nilikuwa na mpango wa kuwapigia kuwajulisha kuwa ile simu ya mdogo wake Vicky imewashwa lakini inaonekana amekuwa akizungushwa sehemu mbali mbali .Mpaka sasa bado wako katika mzunguko." akasema "Hallow Omola,Elvis hapa ninaongea" akasema Elvis "habari yako Elvis." "Nzuri Omola.Kwa kuwa unakwenda ikulu asubuhi hii tutahitaji kuipata hiyo kompyuta yako ili tuendelee kumfuatilia Winnie na kufahamu mahala aliko.Jioni ya leo tutakutana ili utupe mrejesho wa kazi yako ya leo" "Sawa Elvis.Mtaipataje?Mnakuja huku hotelini kuichukua?akauliza "Ndiyo tunakuja hapo muda si mrefu.Tusubiri" akasema Elvis na kukata simu "Hizi ni habari njema kwa Vicky.Inabidi afahamishwe ili aweze kupata moyo kwamba mdogo wake bado yuko hai" akasema Elvis na kumalizia kupakia silaha zake katika kibegi kidogo wakatoka na kuelekea katika chumba walimolala Vicky na Graca,akagonga mlango na Graca akaufungua.Macho yake yalionekana bado amelemewa na usingizi. "Elvis,karibuni.Habari za asubhi?akasema Graca huku akiyafikicha macho yake "Umeamkaje?Akauliza Elvis "Nimeamka vizuri." "Nahitaji kuzungumza na Vicky" "Vicky?! Graca akashangaa "Ndiyo" "Hakuwaaga?Graca akauliza na akina Elvis wakatazamana "Hapana.Ameondoka? "Vicky ameondoka alfajiri akasema kuna sehemu anakwenda.Mimi nilikuwa na usingizi sikumtilia maanani nikajua atawajulisha." Where is she?akauliza Elvis na kutoka nje wakalikuta gari lao lipo ila geti lilikuwa wazi "Inawezekana labda amekwenda mahala kutafuta mahitaji ya hapa nyumbani.Anyway atakaporejea mwambie sisi tumetoka na asitoke atusubiri hadi tutakaporejea"akasema Elvis "Mnakwenda wapi? "Tunakwenda kufuatilia taarifa muhimu kuhusiana na zile nyaraka tulizozipata jana ofisini kwa Frank.Usihofu utakuwa salama.Hakuna anayefahamu mahala hapa ila uwe makini.Mtu yeyote akigonga geti usimfungulie kwanza hakikisha umechungulia na kumfahamu ni nani.Hatutakawia sana" akasema Elvis "Sawa Elvis .Halafu humu ndani hakuna chochote cha kuandaa"Nadhani Vicky amekwenda kushughulikia hilo lakini tutakapokuwa tunarejea tutapita supermarket na kununua mahitaji yote yanayohitajika" akasema Elvis kisha wakaingia garini na kuondoka "She's very beautifull"akasema Steve kwa utani "Steve mambo hayo huu si wakati wake.Tuna mambo makubwa ya kujadili .,Kwa sasa tujiulize Vicky amekwenda wapi?Mbona hajatujulisha kama anatoka?akauliza Elvis "Hata mimi nimeshangaa ila yawezekana ameona asitusumbue kutokana na uchovu wa jana"akasema Steve aliyekuwa katika usukani "Lakini utaratibu wetu hauko hivyo.Tuko katika kipindi cha hatari kubwa na alipaswa atujulishe kuwa anatoka na anakwenda wapi.Nitamkanya asirudie tena kitendo hiki cha kuondoka bila kuaga wenzake" akasema Elvis "Vicky na mdogo wake wanafanana tabia.Wote ni wabishi sana" "Ubishi wao hauna manufaa yoyote kwetu zaidi ya kutuweka katika matatizo.Tazama alichokifanya Winnie.Ameondoka kwa kiburi lakini ametua katika mikono ya akina Frank"akasema Elvis na safari ikaendelea kuelekea hotelini kwa Omola.Walisimama katika duka la kuuza simu Steve akashuka na kwenda kununua simu tatu pamoja na laini zake akarejea garini wakaendelea na safari. Walifika Maasai Hoteli alikofikia Omola Steve akashuka na kumfuata Omola chumbani kwake.Samira tayari alikwisha fika na alikuwa chumbani na Omola "Oh Samira kumbe tayari umefika"akasema Steve "Nimewahi sana kama ulivyonielekeza." "Ahsante sana." akasema Steve na kumgeukia Omola "Omola huyu atakayekuwa dereva wako wa leo na siku zote anaitwa Samira ni mpenzi wangu hivyo jisikie amani uko katika mikono salama"akasema Steve na Omola akatabasamu "Nafurahi kukutanana naye Samira ni mrembo sana.Una bahati sana kumpata mrembo kama huyu" akasema Omola halafu akachukua kompyuta yake na kumkabidhi Steve na kumuelekeza namna programu ile inavyofanya kaziHii programu ni mpya kabisa na CIA ndiyo shirika la kwanza la ujasusi duniani kuanza kuitumia programu hii .Japo zipo programu nyingine kama hii ambazo zinaendelea kutumika lakini hii ni mwisho wa yote.Ni programu ya kisasa mno" akasema Omola na kuendelea kumuelekeza Steve mambo kadhaa kuhusiana na programu ile "Ahsante Omola tutaonana jioni.Tutakuja kukuchukua hapa hapa.Nadhani kila kitu kuhusiana na Ikulu Vicky amekwisha kuelekeza"akasema Steve "Ndiyo Steve kila kitu nimekwisa elekezwa na hakuna tatizo lolote.Mambo yote yatakwenda sawa" "Nakutakia kila la heri" akasema Steve na kuanza kupiga hatua kuondoka halafu akakumbuka kitu "Nimesahau.Hii hapa ni simu yako ambayo utakuwa unaitumia ukiwa hapa Tanzania.Ndani ya simu hii kuna muda wa maongezi wa kutohja na kuna namba zetu Elvis,ya kwangu na Vicky.Muda wowote ukitaka kuwasiliana nasi usisite kufanya hivyo" akasema Steve na kumkabidhi Omola simu kisha akaondoka.Alirejea garini alikomuacha Elvis "Sasa mambo yamekaa vizuri.Kompyuta ya Omola hii hapa" akasema Steve na kumkabidhi Elvis kompyuta ile na kumuelekeza kuhusiana na programu ile inayotumika kumfuatilia Winnie. "Kwa mujibu wa programu hii kwa sasa wako katika mtaa wa viwandani na anaonekana anaendelea na safari.Kwa mwendo anaokwenda nao inaonyesha yuko katika gari.Anakwenda wapi huku?Anyway tuendelee kumfuatilia tutajua mwisho wake.Twende tukamtafute kwanza Irene" akasema Elvis na Steve akaondoa gari huku Elvis akiendelea kumfuatilia Winnie "Wamesimama.Nayafahamu maeneo haya ni maeneo ya viwanda na si maeneo ya makazi"akasema Elvis Steve alifuata maelekezo yaliyokuwepo katika nyaraka zile za kutolea mzigo bandarini kuhusu mahala ilipo kampuni ya Pendeza Co.Ltd na kufika bila taabu. "We're here" akasema Steve akimwambia Elvis ambaye bado alikuwa ameelekeza akili yake yote katika kompyuta akimfuatilia Winnie "Good.Ni duka kubwa na zuri" akasema Elvis akilikodolea macho duka lililokuwa mbele yao likiwa na maandishi makubwa Pendeza Co.Ltd wakaenda katika maegesho Elvis mimi ninashuka na kuingia ndani wewe baki hapa hapa ndani ya gari.Nitamaliza kila kitu mwenyewe.Kama ukiona hatari yoyote huku nje nitaarifu haraka sana" akasema Steve na kushuka akaangaza angaza kama ilivyo kawaida ya majasusi kuhakiki usalama halafu akaanza kupiga hatua kuelekea ndani.Tayari duka limekwisha funguliwa na hakukuwa na wateja wengi asubuhi hii.Mle ndani akawakuta akina dada watatu wamesimama wakipeana michapo,akawasogelea "Habari zenu akina dada" akawasalimu kwa uchangamfu mkubwa "habari nzuri kaka,habari yako" "Nzuri kabisa.Nawaona na nyie mko vizuri.Sura zenu zinanionyesha hivyo" akasema na wale akina dada wakatabasamu na kufurahia uchangamfu wake "Karibu kaka .Tukusaidie nini?akauliza dada mmoja baada ya kumuona Steve kama si mnunuzi "Nina shida na madam Irene. Nimemkuta au nimewahi sana?akauliza huku akiwatolea tabasamu "Bosi aje saa hizi?Umewahi sana." "Saa ngapi anaweza kuja? "Kuanzia saa nne ndio muda wake.Ila yupo msaidizi wake unaweza kumuona huyo naye akakusaidia shida yako" akasema mmoja wa wale akina dada "Hapana nina shida na madam Irene pekee.Nitakuja tena baadae kwani maagizo niliyopewa ni kwamba nionane naye mwenyewe" akasema Steve na kuwaaga wale akina dada akaanza kupiga hatua kuondoka.Alipokaribia kufika mlangoni akageuka na kurudi "Naombeni mnielekeze kwake ili nimfuate huko huko" akasema Steve na kuelekezwa nyumbani kwa Irene.Akaondoka na kurejea garini "Irene bado hajafika hapa ila nimeelekezwa nyumbani kwake.Twende tumfuate kwani wanasema huwa anachelewa sana kufika hapa" akasema Steve huku akiwasha gari wakaondoka maeneo yale "Kuna maendeleo yoyote kwa Winnie? akauliza "Inaonekana amesimama.Hili ni eneo la viwanda na sijui anatafuta nini huku.Tumalizane kwanza na Irene halafu tutaenda kumtafuta Winnie" akasema Elvis Walifika katika nyumba Steve aliyoelekezwa kuwa ni nyumbani kwa Irene Mwabukusi.Ilikuwa ni nyumba kubwa ya ghorofa moja. "Ni hapa tumefika.Jumba lenyewe linaonyesha ni mtu anayejiweza sana" akasema Steve na kuendesha gari taratibu hadi karibu na geti akashuka na kwenda kubonyeza kengele ya geti.Baada ya dakika moja dirisha dogo lililokuwa pembeni ya geti likafunguliwa na msichana mmoja akajitokeza. "Karibu.Nikusaidie nini? "ahsante sana.Nahitaji kuonana na madam Irene" "Una miadi naye? "Hapana sina miadi naye ila nina shida naye ya dharura nimemfuata ofisini kwake nikaelekezwa kumfuata hapa nyumbani" "Nimwambie unaitwa nani? Walifika katika nyumba Steve aliyoelekezwa kuwa ni nyumbani kwa Irene Mwabukusi.Ilikuwa ni nyumba kubwa ya ghorofa moja. "Ni hapa tumefika.Jumba lenyewe linaonyesha ni mtu anayejiweza sana" akasema Steve na kuendesha gari taratibu hadi karibu na geti akashuka na kwenda kubonyeza kengele ya geti.Baada ya dakika moja dirisha dogo lililokuwa pembeni ya geti likafunguliwa na msichana mmoja akajitokeza. "Karibu.Nikusaidie nini? "ahsante sana.Nahitaji kuonana na madam Irene" "Una miadi naye? "Hapana sina miadi naye ila nina shida naye ya dharura nimemfuata ofisini kwake nikaelekezwa kumfuata hapa nyumbani" "Nimwambie unaitwa nani? Mwambie Lukas ninatoka kampuni ya kusafirisha mizigo ya Shamsi " akasema Steve na yule msichana akaondoka na baada ya dakika tatu akarejea na kufungua geti na akawakaribisha ndani akina Steve.Walikaribishwa katika sebule nzuri sana yenye samani za kupendeza. "Karibuni .Mama amesema mumsubiri hapa atakuja muda si mrefu" akasema yule msichana na kuondoka akawaacha akina Elvis peke yao "Kuna watu hapa duniani hawafahamu nini maana ya shida wanaishi kama vile wako katika sayari nyingine" akasema Steve kwa sauti ndogo wakiwa pale sebuleni wakimsubiri Irene lakini Elvis hakumjibu kitu macho yake yalikuwa katika kompyuta akiendelea kumfuatilia Winnie.Baada ya dakika tano mama mmoja mnene mwenye umri wa kati ya miaka arobaini hadi arobaini na tano akatokea.Kwa mavazi aliyokuwa amevaa ilionyesha wazi kuwa alikuwa amekwisha jiandaa tayari kwa kutoka kwenda katika shughuli zake. "Karibuni" akasema yule mama .Steve na Elvis wakasimama kumsalimu "Madam Irene shikamoo."akasema Steve huku akimfuata na kumpa mkono kana kwamba wanafahamiana hali iliyomfanya Irene naye atabasamu na kufurahia uchangamfu ule wa Steve "Habari nzuri sana .Karibuni" akasema huku akipeana mkono pia na Elvis halafu wote wakaketi "Samahani kwa kukusumbua madam Irene tumefika dukani wakatuambia kwamba utachelewa kufika ikabidi tukufuate hapa nyumbani" akasema http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Steve "Karibuni sana ila sina hakika kama tunafahamiana.Mmeseam mnatokea kampuni gani?akauliza Irene "Hapana hatufahamiani ila tumekutafuta kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara.Sisi tuna kampuni yetu ya usafirishaji ....." akasema Elvis na kuinuka akachomoa makaratasi kutoka katika mfuko wa koti na kumfuata Irene pale alipokuwa amekaa kwa dhumuni la kumuonyesha zile karatasi.Mara tu alipoketi kitini akainua koti lake na bastora ikaonekana.Irene akastuka sana na kugeuka haraka na Steve naye akainua koti lake ikaonekana bastora na akamfanyia ishara ya kukaa kimya.Macho yakamtoka pima.Kwa sauti ndogo Elvis akamwambia "Usipige kelele wala kutaharuki,inuka na tuongozane hadi katika gari.Ukithubutu kupiga kelele au kufanya chochote tunakufumua kichwa chako.Now let's go!! akaamuru Elvis huku akisimama na Irene naye akasimama,Steve akaichukua kompyuta yao wakaanza kuondoka mle ndani.Walitembea kana kwamba hakuna tatizo lolote.Sura ya Steve ilionyesha tabasamu muda wote na hakuna yeyote ambaye angehisi kuwa Irene alikuwa ametekwa.Walifika katika gari la akina Elvis Steve akamfungulia mlango wa nyuma akaingia kisha nao wakaingia garini na kuondoka. ********************** I have to do anythng I can to get Winnie back.Hawa jamaa akina Elvis hawana uchungu kama nilio nao mimi na ndiyo maana hawaonyeshi juhudi zozote za kutaka kumtafuta Winnie.Siwezi kumuacha ndugu yangu wa damu akiendelea kuteswa bila kufanya jitihada zozote za kumuokoa.I must do something" akawaza Vicky baada ya kuondoka katika nyumba walikohamia.Alikuwa anatembea kwa miguu na kwa mbali akaiona piki piki inakuja,akapunga mkono na piki piki ile ikasimama akamuelekeza dereva ampeleke katika kituo cha taksi.Dereva akaendesha kwa mwendo wa kasi na kwa muda wa dakika nane wakafika katika kituo cha taksi akashuka na kuchukua taksi iliyompeleka moja kwa moja nyumbani kwake.Kitu cha kwanza alipofika nyumbani ni kuuliza walinzi kama Winnie amefika pale akaelezwa kwamba hajafika akaingia ndani haraka haraka na kuwasha simu yake akazitafuta namba za Frank na kumpigia. "Vicky!! ikasema sauti ya Frank kwa mshangao "Frank where are you?akauliza Vicky "Where are you? Frank naye akauliza "Niko hapa nyumbani kwangu.Frank we need to talk" "We need to talk?Frank akauliza "Yes we need to talk"akasema Vicky na Frank akavuta pumzi ndefu akauliza "What do you want? "I want Winnie back!! Badala ya kujibu Frank akaangua kicheko kisha akasema You want me to free Winnie,surrender yourself to me and I'll let her go" akasema Frank "Where are you now? "You want to kill me too?akauliza Frank "Frank I only want Winnie, nothing else" "If you want Winnie back stay where you are" akasema Frank na kukata simu Vicky alihisi kutetemeka kwa ndani,alikuwa anaogopa "Mwili unanitetemeka kwa woga lakini sina namna nyingine lazima nifanye hivi ili Winnie awe huru.Ni bora kama nikiteswa mimi kuliko Winnie hana kosa lolote.Sijui nini kitatokea akina Elvis wakigundua kwamba nimefanya hivi,lakini wao ndio chanzo cha haya yote.Kama wasingeniingiza katika mpango wao wa kumuua Pascal haya yote yasingenikuta.Nadhani ni wakati muafaka wa kuachana na hizi kazi na kuendelea na shughuli zangu nyingine.Kuendelea kuzifanya ni kuendelea kumuweka hatarini ndugu yangu Winnie" akawaza Vicky. Mara tu alipomaliza kuzungumza na Vicky simuni,Frank akampigia Obi "Obi nimepigiwa simu muda si mrefu na Vicky anataka kujisalimisha ili kumuokoa mdogo wake" "Unamuamini?akauliza Obi "Bado sijamuamini yawezekana huu ukawa ni mtego wanataka kuutumia hivyo waache vijana wawili hapo mlipo waendele kumchunga Winnie halafu wewe na wengine wote mjipange kwenda kumchukua Vicky nyumbani kwake.Nataka apotezwe fahamu ili asifahamu mahala anakopelekwa.Chukueni kila aina ya tahadhari ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu yeyote anayewafuatilia kwani kuna uwezekano mkubwa watu hawa wanaomtumia wakamtanguliza kama chambo ili waweze kunipata kirahisi kama walivyofanya kwa Pascal.Umenielewa Obi? "Nimekuelewa mzee" "Vipi kuhusu wale vijana tuliowaacha katika ile nymba kuna ripoti yoyote wametuma? "Nimezungumza nao muda si mrefu na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika pale nyumbani" "Ok sawa wasiondoke waendelee kubaki hapo hapo ili tujue ni nani anaishi hapo" akasema Frank na kukata simu akainuka na kwenda kuchukua chupa ya mvinyo akaimimina katika glasi na kuanza kunywa huku uso ake ukiwa umejaa hasira Hatimaye umekuja mwenyewe.Wewe ndiye mwenye majibu ya maswali yangu yote.Sipati picha mateso nitakayokupa Vicky" akawaza huku akiendelea kugugumia mvinyo kwa fujo *********************** Imekuwa ni kawaida ya Patricia kutokupata usingizi usiku na badala yake huanza kupata usingizi mida ya alfajiri.Akiwa katika usingizi mzito asubuhu akasikia simu yake ikiita,akajiinua kivivu na kuichukua akatazama mpigaji alikuwa ni Meshack Jumbo.Haraka haraka akaipokea "Shikamoo mzee Jumbo" Marahaba Patricia,habari za asubuhi? "Nzuri kabisa mzee wangu" "Patricia nimekupigia kukujulisha kuwa leo hii utahama hapo kwa akina Juliana.Kuna nyumba nimekutafutia maeneo ya Peninsula ni nzuri ambayo utaishi hapo kwa muda wakati tunakutafutia makazi ya kudumu.Tumeona tukuondoe hapo kwani panaonekana si mahala salama kwa wewe kuendelea kuishi hasa kwa wakati huu ambao tunafanya uchunguzi wa lile suala la Juliana.Ninakwenda kukamilisha taratibu za malipo asubuhi hiyo na jioni ya leo kila kitu kitakuwa tayari kwa wewe kuhamia hapo"akasema Meshack "Mzee Jumbo nakushukuru sana kwa kunijali.Hata hivyo nakuomba usisumbuke mzee wangu kutafuta nyumba kwani kuna sehemu nitakwenda kuishi yenye usalama zaidi.Rais na mke wake wameniomba nikaishi nao ikulu hadi hapo nitakapokuwa nimeweza kujitegemea tena.Wale wazee wananipenda sana na wananichukulia kama sehemu ya familia yao hivyo usihofu kuhusu mimi mzee Jumbo nitakuwa salama" "Hilo ni jambo zuri sana wamelifanya kwani pale ikulu kuna ulinzi na usalama wa kutosha sana.Hata hivyo bado nitaendelea kufuatilia nyumba hii ili pale utakapoondoka ikulu uweze kuwa na sehemu ya kuanzia.Patricia najua wewe ni mgumu sana kukubali vitu hasa kutoka kwa watu wenye mahusiano na Elvis lakini nakuomba usikatae hili ninalotaka kulifanya kwa ajili yako.Elvis nilimpenda kama mwanangu na kwa sasa hayupo tena na jukumu la kukulea ninalibeba mimi hivyo ninaanza kwa kukutafutia makazi.Muda wowote ukichoka kuishi ikulu utakwenda kuishi katika hiyo nyumba niliyokutafutia" "Ahsante sana mzee Jumbo.Ninashukuru kwa hilo" akajibu Patricia huku akitabasamu "Ni lini unahamia Ikulu? "Nimepanga kwenda ikulu baada ya msiba wa hapa kumalizika.Nataka nishiriki nao katika mazishi ya baba yao ndipo niondoke.Ni watu wema sana kwangu hivyo siwezi kuondoka kabla msiba haujamalizika" "Patricia ninakushauri ufanye haraka sana kwenda ikulu kwani kuna viashiria vinatuonyesha mahala hapo si salama kwa wewe kuendelea kuwepo hivyo itakuwa vyema kama utahamia ikulu leo hii hii.Hata ukiwa kule utaendelea kuwatembelea na kuungana nao katika msiba lakini kitendo cha kuendelea kuishi hapo si salama" "Mzee Jumbo ahsante sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi japo Juliana atasikitika sana kama nikiondoka na kumuacha peke yake" "Hautamuacha peke yake Patricia bado utakuwa na muda wa kwenda kuungana nao katika msiba tunachohitaji sisi ni kukuondoa tu hapo" "Nimekuelewa mzee wangu.Nitafanya kama ulivyoelekeza nitawasiliana na mama mke wa rais nitamjulisha kuwa nitahamia kwao leo" "Good.Thank you very much.Usimweleze mtu yeyote hata Juliana kuwa unaondoka kwao kwa sababu za kiusalama.Waeleze kwamba rais amesisistiza uende ukaishi nao na wewe huwezi kumkatalia" akasema Meshack Jumbo akaagana na Patricia "Analolisema Meshack ni jambo la kweli.Familia hii ya akina Juliana inaonekana inawindwa sana na mimi kuendelea kuishi hapa kunaweza kuniweka matatani.Ngoja niondoke zangu nikaishi ikulu sitaki tena matatizo zai......."Patricia akatolewa mawazoni na simu ya Dr Washington "Habari za asubuhi Dr Washington" "Habari yangu nzuri,hofu yangu kwako.Umeamka salama? "Nimeamka salama kabisa." "Ni hicho pekee ninachohitaji kukisikia kutoka katika mdomo wako kwamba unaendelea vyema" akasema Dr Washington na halafu ukimya ukapita "Patricia utanisamehe kwa hili lakini nina hamu sana ya kukuona.Nafahamu bado una machungu mazito ya kifo cha mumeo lakini naomba kama utaniruhusu nikutembelee nije nikujulie hali.Nataka nikufariji ana kwa ana.Toka yalipotokea matatizo haya hatujaonana na hii inanipa wakati mgumu sana hata katika kutenda kazi zangu.Kila wakati picha yako inakuja kichwani kwangu.Nahitaji nikuone Patricia,tafadhali nielekeze mahala ulipo ili nikutembelee" akasema Dr Washington.Patricia akavuta pumzi ndefu na kusema "Dr Washington hata mimi nimekukumbuka sana na ningependa kuonana nawe ila mazingira niliyomo kwa sasa hayaruhusu mimi na wewe kuonana.Tuendelee kuwasiliana simuni na siku moja tutaonana tena" akasema Patricia Nimekuelewa Patricia ila bado nina swali moja.Utarudi tena kazini?akauliza Dr Washington na Patricia akachukua muda kidogo kujibu "Bado sijajua nini nitakifanya kama nitarejea tena kazini au vipi.Nitakujulisha maamuzi nitakayochukukua kwani maisha yangu tayari yamebadilika sana na hayatakuwa kama yale niliyoishi wakati niko na mume wangu.Dr Washington ahsante kwa kunijulia hali tutawasiliana siku nyingine" akasema Patricia na kukata simu tayari machozi yalikuwa yanamtoka "Machozi haya ya kumlilia Elvis hayatakauka kamwe.Elvis alikuwa ni sehemu kubwa ya maisha yangu.Kuna nyakati ninaomba utokee muujiza na nimuone tena mume wangu mbele yangu lakini haiwezekani.Elvis is gone.Kuna nyakati hata mimi ninatamani kama ningekufa ili nikaungane na mume wangu huko aliko kwani naamini maisha yangu yatakuwa magumu sana bila yeye" akawaza Patricia na kujilaza tena kitandani ********************* Dr Makwa Tusangira na waziri mkuu mstaafu David walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa kwani Dr Makwa alilala hapa nyumbani kwa David kwa hofu ya kukamatwa na polisi baada ya kutangaza kufanyika kwa mkutano wa hadhara uliopigwa marufuku na jeshi la polisi.Wakiwa mezani wakiendelea kupata kifungua kinywa pamoja na maongezi mbalimbali simu ya Dr Makwa ikaita akaipokea haraka haraka.Akazungumza kwa dakika zaidi ya kumi na mtu aliyempigia halafu wakaagana huku uso wake ukiwa na tabasamu kubwa " Nilikuwa nazungmuza na familia yangu tayari wamevuka mpaka wa Namanga na wameingia Kenya.Ni hao tu waliokuwa wananipa wasi wasi.Ahsante sana David kwa msaada wako mkubwa wa kuiondoa familia yangu.Sitaki ipate misuko suko ya aina yoyote" akasema Dr Makwa "Dr Makwa siku zote familia huwekwa mbele.Ningekushangaa sana kama ungeacha familia yako hapa Tanzania wakati unafahamu fika kuwa machafuko makubwa yanakwenda kutokea.Leo inazinduliwa rasmi safari ya kuelekea ikulu.Hakikisha tafadhali kila kitu kinakwenda vizuri hatuhitaji uzembe wa aina yoyote ile" "Usihofu David kila kitu kinakwenda vyema na hakuna uzembe wowote utakaotokea.Tumejipanga vizuri.Frank alifanya vyema sana kuhakikisha tunapokea pesa jana na zimetusaidia mno katika maandalizi na matunda yake utayaona" akasema Dr Makwa kisha wakaendelea na mikakati mingine huku simu ya Dr Makwa ikiita kila wakati akiwasiliana na watu mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya mipango yao **************** Steve aliendesha gari hadi karibu na daraja ambalo ujenzi wake ulikuwa umesimama akaegesha pembeni. "I'm going out.Endelea naye" akasema Steve na kushuka akafungua mfuniko wa injini na kujifanya anatengeneza "Irene naomba nisikilize kwa makini sana.Hatuna tatizo nawe ila kuna mambo tunataka kuyafahamu kutoka kwako hivyo nakuomba uwe mkweli kwa kila nitakachokuuliza." akasema Elvis "Ninyi ni akina nani?Mnataka nini?Niambieni ni kiasi gani cha pesa mnahitaji niwalipe but please don't hurt me" akasema Irene huku macho yake yakilengwa na machozi "Hatuhitaji pesa Irene ila tunachohitaji ni taarifa.Wewe ndiye mmiliki wa kampuni ya Pendeza Co.Ltd? "Ndiyo.Hiyo ni kampuni yangu" akajibu Irene Unaimiliki wewe mwenyewe kwa asilimia mia moja au kuna mtu mwingine unashirikiana naye? "Hii ni kampuni yangu kwa asilimia mia moja.Hakuna mtu mwingine ninayeshirikiana naye" "Are you sure? "Yes I'm sure" "Irene ninarudia tena kuuliza kwamba kuna mtu yeyote unayeshirikiana naye katika kumiliki kampuni hii? "Hakuna mtu mwingine,mmiliki ni mimi peke yangu" "Unaifahamu kampuni inaitwa McLorien? "Ndiyo ninaifahamu.Hao ni washirika wangu wa biashara .Wanatuuzia mzigo wa nguo na vatu kutoka Marekani na Ulaya" "Mara ya mwisho ilikuwa lini kupokea mzigo kutoka kwao? Ni miezi kadhaa imepita" "Mingapi? "Miezi kama mitano au sita hivi" "Hakuna mzigo wowote umepokea kutoka katika kampuni hii wiki tatu zilizopita? "Hapana hakuna mzigo wowote tumepokea" "Are you sure? "Yes I'm sure" akajibu Irene kwa kujiamini "Good.Unamfahamu Frank?akauliza Elvis na swali lile likamstua Irene akababaika "Frank?..akauliza "Frank yupi?akauliza tena "Brigedia Frank" Irene akawaza halafu akasema "Hapana simfahamu mtu huyo" "Are you sure?Elvis akauliza Yes I'm sure"akajibu Irene.Elvis akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema "Irene wewe ni dada yangu na nilikuonya toka awali kwamba unieleze ukweli mtupu kwa yale nitakayokuuliza lakini wewe unanidanganya.Umeniudhi kwa kuniambia uongo na mimi huchuia sana mtu anaponieleza uongo" "Sijakudanganya kaka yangu simfahamu mtu huyo anaitwa brigedia Frank"akasema Irene.Elvis akashusha kioo cha gari na kumuita Steve akamtaka aingie garini waondoke "Mnanipeleka wapi? "Nilikupa nafasi ukaichezea sasa ni wakati wetu wa kuutafuta ukweli kwa kutumia nguvu.Hatukutaka kutumia njia hii lakini umetulazimisha" Mtaniumiza bure kaka zangu mimi simfahamu huyo Frank nawaomba mniamini tafadhali"akasema Irene.Steve akawasha gari wakaondoka.Mara tu walipoingia barabarani Elvis akatoa karatasi mfukoni akazikunjua na kumuonyesha Irene "Hizi ni nyaraka za kutolea mzigo bandarini ambazo zinaonyesha kuwa wiki tatu zilizopita umepokea mzigo wa viatu kutoka kwa kampuni ya McLorien" Irene macho yakamtoka mdomo ikamtetemeka hakujua aseme nini.Nyaraka zile zilieleza kila kitu "Umekataa kwamba hujapokea mzigo wowote kutoka kwa kampuni ya Mclorien kwa miezi mitano au sita lakini nyaraka zinaonyesha umepokea mzigo wiki tatu zilizopita.kwa nini umetudanganya? akauliza Elvis na Irene akamtazama kwa woga akasema "Samahani kaka..Samahani sana.Naombeni tuzungumze" "Mazungumzo ni kutueleza ukweli tu.Unamfahamu Frank? "Hapana simjui Fr....."kabla hajamalizia sentensi yake Steve aliyekuwa katika usukani akageuka kwa kasi ya ajabu na kumnasa kibao kikali usoni "Don't lie to us !! akasema na kuendelea kuendesha "Jamani naombeni msiniumize simfahamu Frank"akasema Irene "Nyaraka hizi tumezitoa katika ofisi yake.Kwa nini usimfahamu?Tueleze haraka mahusiano ya Frank na kampuni yako"akasema Elvis Nimekwisha waeleza kaka zangu kwamba simfahamu kabisa huyo Frank!! akasema Irene "Unazidi kunipa hasira Irene.Ninakupa nafasi ya mwisho utueleze unamfahamu Frank? akauliza Elvis "Jamani naombeni mniamini kwamba simfahamu Frank" akasema Irene. "Steve naomba vifaa vyangu" akasema Elvis na Steve akafungua droo ya gari na kumrushia kiboksi kidogo akakifungua akatoa koleo ndogo na kuukamata kwa nguvu mkono wa Irena akakibana kidole kwa koleo na Irene akapiga kelele kwa maumivu makali aliyoyapata "Tell me the truth! akasema Elvis lakini Irene aliendelea kulia.Elvis akamnasa kibao kikali halafu akaukamata tena mkono wake na kukibana kidole kingine kwa koleo lakini bado Irene aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutokumfahamu Frank.Elvis akazidi kukasirika akamshika kwa nguvu na kumlaza katika kiti halafu akachukua kisu kidogo "Ninakwenda kuliondoa jicho la kwanza na kama utaendelea kuwa mbishi nitaliondoa jicho la pili.Akasema na kumkandamiza Irene kichwa na kukipeleka kisu sehemu ya chini ya jicho na Irene akaanza kuhisi kitu chenye nya kali kikiichana ngozi yake "Basi !! basi !! nitawaeleza ukweli!! Usinimize tafadhali nitakueleza kila kitu!! akasema Irene na Elvis akamuachia.Tayari damu ilikwisha anza kutoka sehemu ya chini ya jicho la kulia.Irene akavuta pumzi haraka haraka hakuamini kilichotaka kumtokea. "Nataka majibu haraka sana" akasema Elvis.Wakati haya yakitokea gari lilikuwa katika mwendo mkali na hakuna yeyote aliyeweza kuona kilichokuwa kinaendelea ndani kwani vioo vyote vilikuwa na rangi nyeusi halafu Steve alifungua mziki kwa sauti kubwa. "Irene naomba usinipotezee muda wangu.Nipe majibu haraka sana"akasema Elvis "Nitakueleza kaka angu ila naomba msiniumize.Nitawaeleza kila kitu"akasema Irene na kumtazama Elvis kwa woga halafu akaendelea "Frank ndiye mmiliki wa kampuni hii ya Pendeza Co.Ltd" akasema na kunyamaza kidogo akafuta damu na kuendelea Hakutaka kujulikana kama anamiliki hii kampuni hivyo akanitumia mimi ili niwe kama mmiliki wake lakini ukweli yeye ndiye mwenye kampuni.Frank hajihusishi na lolote katika kampuni hii zaidi ya kuagiza mzigo na kutukabidhi." "Frank ndiye huagiza mzigo? "Ndiyo.Mimi humpelekea orodha ya bidhaa tunazozihitaji na yeye huagiza kutoka nje na baadae huja kutukabidhi kwa ajili ya kuuza" "Wiki tatu zilizopita kontena zaidi ya kumi za viatu zimetolewa bandarini.Mmeupokea mzigo huo?akauliza Elvis na Irene akababaika "Irene answer me!! akafoka Elvis "Tulipokea jozi chache za viatu kwani bado havijapakuliwa katika makontena.Upakuzi utakapokamilika basi tutaupata mzigo wote" akasema Irene "Mnasubiri upakuzi?Mnapakulia wapi mzigo wenu mkiutoa bandarini? "Mzigo unapokuja ni Frank ambaye hushughulikia kila kitu na kisha huenda kuupakua na ndipo hutuletea kwa ajili ya kuuza.Mahala anapopakulia hata mimi sipafahamu na sijawahi kumuuliza kwani shida yangu mimi ni kupata mzigo pekee.Wakati mwingine mzigo huwa unakuja kwa ajili ya maduka yetu yaliyoko nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Burundi." "Mna maduka mengine Congo na Burundi? "Ndiyo tuna maduka mengine mawili makubwa nchini Congo na Burundi" akasema Irene. Namna gani huwa mnayatoa makontena yenu bandarini? akauliza Elvis na Irene akabaki kimya "Irene usitake kuniudhi tena.Nitakuondoa jicho lako sasa hivi"akasema Elvis kwa ukali na Irene huku akionyesha woga mkubwa akasema "Frank ndiye anayesimamia utoaji wa makontena bandarini lakini ninavyofahamu kuna watu huwa wanatusaidia katika utoajia makontena hayo" "Mnapotoa makontena hayo hupita katika mtambo maalum wa kuchunguza na kuoa kilichomo ndani? akauliza Steve "Hapana hayapiti huko" "Kwa nini?akauliza Elvis na Irene akabaki kimya "Kwa nini?akauliza tena lakini Irene akabaki kimya Irene nataka majibu.Kwa nini makontena yenu hayapiti katika ukaguzi?akauliza Elvis lakini Irene hakufumbua mdomo wake.Kufumba na kufumbua akajikuta amenaswa kofi kali sana lililomuangusha kitini na damu ikaanza kutoka mdomoni.Elvis akamkandamiza tena kichwa na kukipeleka kisu jichoni "Wait !!! wait !!.akasema Irene "Irene tafadhali naomba usicheze nami kabisa.!! Answer my questions !! akasema Elvis "Mizigo yetu haipiti katika ukaguzi kwa sababu Frank hudai kuna mizigo yake huwa anaipakia ndani ya mzigo huo wa nguo au viatu ambayo hataki ijulikane na ndiyo maana mizigo haipiti katika ukaguzi" "Ni mzigo gani huwa anaupakia ndani ya makontena hayo ya viatu? Hajawahi kunieleza.Hiyo ni siri yake mwenyewe na ndiyo maana hushughulikia mizigo yote yeye mwenyewe" "Nani mshirika wake mkubwa katika biashara zake ukiacha wewe? "Frank ana marafiki wengi wakubwa anaoshirikiana nao katika mambo mbali mbali lakini katika biashara hii ni mimi pekee ninayeshirikiana naye" "Nani unayemfahamu ambaye anashirikiana naye kwa karibu zaidi? "Ni Pascal ambaye ameuawa juzi" "hakuna mwingine? "Frank anafahamiana na watu wengi hivyo sijui yupi anashirikiana naye katika jambo gani ila huyo Pascal ndiye muda mwingi walikuwa wote.Huyo ndiye rafiki yake kubwa ninayemfahamu"akasema Irene.Elvis akamtazama kwa muda halafu akasema "Tutakuacha uende zako ila usimweleze Frank chochote juu yetu sisi.Ukifanya hivyo you'll die.Umenielewa Irene? akauliza Elvis "Nimewaelewa na nitafanya kama mlivyonielekeza,sintamwambia Frank" akasema Irene na Elvis akamuelekeza Steve aegeshe gari karibu na hoteli 66.Palikuwa na taksi nyingi pale Steve akashuka "Get out of the car.Chukua taksi na uende nyumbani!! akasema Elvis.Irene akashuka kwa woga Steve tayari alikwisha mtafutia gari akamfungulia mlango na kumtaka dereva ampeleke Irene mahala atakapomuelekeza na dereva wa taksi akamuuliza Irene mahala anakotaka apelekwe akamuelekeza wakaondoka.Steve alipohakikisha taksi ile imepotea kabisa akaingia garini kisha nao wakaondoka "Kwa nini umemuacha aende?Steve akauliza "Hana msaada tena kwetu.Tayari amekwisha tueleza kile tunachokitafuta hivyo hakuna haja ya kuendelea kumshikilia.Kwa maelezo yake ni wazi ndani ya makontena hayo ndimo hupakiwa silaha ndiyo maana hayapiti katika ukaguzi.Hapa inaonyesha kuna mtandao uko bandarini na ndiyo maana imekuwa rahisi kwao kutoa mizigo yao bila wasiwasi wala kukaguliwa.Hizi ni taarifa nzuri sana tumezipata.Makontena hayo huja kama mzigo wa nguo na viatu kisha hutolewa bandarini na halafu husafirishwa kwenda Congo na Burundi kama viatu na huko ndiko huuziwa waasi.Haya ni mafanikio makubwa sana tumeyapata lakini bado tunahitaji kuchimba zaidi na kufahamu Frank anashirikiana na akina nani katika biashara hii?Lengo ni kuhakikisha mtandao wote tunaung'oa.Hakuna atakayesalia"akasema Elvis "Nakubaliana nawe Elvis kwamba sasa tumepata picha ya kueleweka kuhusiana na biashara ya silaha anayoifanya Frank.Nguvu kubwa sasa tuielekeze katika kumchunguza Frank ili tuufahamu watu anaoshirikiana nao" "Tunapaswa kufanya uchunguzi pia bandarini kujiridhisha namna makontena hayo yanavyotolewa na tufahamu ni akina nani wanahusika katika jambo hilo.Vile vile tusubiri taarifa kutoka kwa Omola ili tufahamu kuhusiana na kampuni ya McLorien.Irene nimemuachia huru makusudi kabisa kwani naamini atamueleza Frank na akipata taarifa hizi atastuka sana na ataanza kutafuta namna ya kujihami na sisi tutampata kirahisi.Kwa sasa tuendelee kukusanya vielelezo kuhusiana na hii biashara.Bado hatuna ushahidi wa kutosha kwamba ndani ya makontena hayo kuna silaha" akasema Elvis "Nimekupata vyema Elvis.Vipi kuhusu Winnie?akauliza Steve "Oh tumemsahau kabisa Winnie" akasema Elvis na kuichukua kompyuta "Bado inaonyesha yuko pale pale.Tuelekee eneo la mtaa wa viwanda.Huko ndiko aliko" "Anafanya nini huko? akauliza Steve "Yawezekana amefichwa huko kwani wale jamaa hawataweza kumuachia hadi wahakikishe wamempata dada yake"akasema Elvis na gari likasimama katika taa kabla ya kuingia katika barabara ya Chaguso.
Vicky alitoka chumbani kwake baada mlango wa sebuleni kugongwa akaenda kuufungua akakutana na mlinzi "Kuna watu wanakuuliza mama"akasema yule mlinzi "Waruhusu waingie ndani"akasema Vicky na mlinzi yule akaenda kuwafungulia geti wakaingia ndani.Kutoka ndani ya gari wakashuka watu wanne wakiongozwa na Obi.Vicky akahisi woga "Hallo Vicky.Tumekutana tena.Uko tayari?akauliza Obi "Mnanipeleka wapi? "Unakotakiwa kwenda.Kama uko tayari ingia garini tuondoke" akasema Obi na Vicky akaongozana nao hadi katika gari lao akaingia na kuondoka.Mara tu walipovuka geti Obi ambaye alikuwa amekaa kiti cha nyuma pamoja na Vicky akamuomba kijana aliyekuwa amekaa mbele ampatie vifaa vyake "Mnataka kunifanya nini? akauliza Vicky kwa wasi wasi "Relax Vicky.This is just a procedure.Hutakiwi kufahamu mahala unakoelekea hivyo naomba usiwe mbishi" akasema Obi na kutoa sindano katika mkoba ule akavuta dawa fulani katika kichupa na kumchoma Vicky katika .Hazikuisha sekunde thelathini Vicky akalala usingizi mzito_Obi akatoa simu na kumpigia Frank "Mkuu tayari tunaye Vicky" "Good.Fanyeni kama nilivyowaelekeza hakikisheni mnachukua kila aina ya tahadhari kwani watu wanaomtumia wana mbinu nyingi"akasema Frank "Tuko makini sana.Tutakujulisha tukifika" akasema Obi na kukata simu.Walikuwa makini sana katika kuangalia kama kuna mtu yeyote aliyekuwa anawafuata nyuma.Walikwenda hadi katika nyumba moja maeneo ya Mijiwe na kuingia ndani.Haraka haraka Vicky akashushwa na kupakiwa katika gari lingine ambalo lilipita katika geti la nyuma na kupita katika njia iliyokuwemo shambani halafu wakatokea katika barabara kubwa wakaendelea na safari "Kama walikuwa wanatufuatilia kwa namna yoyote ile hapa tumewalamba chenga ya mwili" akasema Obi huku akicheka. Waliendelea na safari hadi katika nyumba ambayo Winnie aliletwa usiku wa jana wakaingia na Vicky akapelekwa katika chumba akafungwa pingu miguu na mikono kisha akamchoma sindano nyingine na wakaamuacha azinduke.Obi akamjulisha Frank kuwa tayari wamekwishamfikisha Vicky sehemu husika "Good Job Obi.Sasa jipeni muda wa kuchunguza kama hakuna yeyote anayemfuatilia mimi niko njiani ninakuja hapo"akasema Frank ****************** Jina mtaa wa viwanda lilitokana na eneo hilo kutengwa maalum kwa ajili ya viwanda.Kulikuwa na viwanda vikubwa zaidi ya kumi vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbali mbali za ujenzi.Kulikuwa na majengo makubwa makubwa na mengine yalizungushiwa ukuta mkubwa.Steve aliendesha gari taratibu huku Elvis akitumia programu ile katika kompyuta kutafuta mahala alipo Winnie. "Ni maeneo haya hapa" akasema Elvis baada ya kufika katika eneo la kilichokuwa kiwanda cha saruji ambacho kwa sasa hakifanyi kazi.Mwekezaji wa kiwanda hiki alishindwa kukiendeleza akakitelekeza na kung'oa mashine zote muhimu na kubaki magofu.Elvis na Steve wakashuka garini na kuangaza angaza.Watu waliokuwa njiani hawakuwa wengi kutokana na muda huo wengi kuwa makazini. "Programu inatuonyesha ni eneo hili la kushoto ambako kuna hiki kiwanda cha saruji" akasema Elvis Ukuta uliozunguka kiwanda hiki ulibomoka bomoka na hivyo kupafanya kuwa ni sehemu ambayo vijana hupenda kujificha na kuvuta bangi.Doria za mara kwa mara za polisi ndizo ziliowakimbiza vijana hao eneo hili na kuondoa kitisho kilichokabili raia hasa wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi katika viwanda vilivyoko eneo hili waliokuwa wakiporwa fedha na mali zao kila uchao. Steve na Elvis wakaambaa na ukuta wakakuta sehemu iliyoanguka wakaingia ndani.Walitembea kwa tahadari kubwa wakipita majengo kadhaa yaliyotelekezwa bila kukutana na mtu yeyote na mara wakatokea katika jengo kubwa la ghorofa moja ambalo lilionekana kama awali lilitumika kama ofisi ingawa kwa sasa hakukuwa na madirisha wala milango.Lilibaki gofu.Steve aliyekuwa ametangulia mbele akasimama na kumsukuma Elvis arejee nyuma "Kuna nini? akauliza Elvis "Kuna mtu amejificha pembeni ya lile jengo anavuta sigara" akasema Steve "Good.Zunguka kwa nyuma mimi nitamuwahi kwa mbele" akasema Elvis na Steve akanyata akapita pembeni ya mtambo mmoja mkubwa uliotelekezwa pembeni ya jengo lile bila kuonekana akazunguka nyuma ya lile jengo akaruka dirisha na kuingia ndani akaanza kupanda ngazi kuelekea juu alikokuwa yule jamaa akivuta sigara.Elvis akamuona Steve akipanda ngazi taratbu naye akaiweka sawa bastora yake iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti.Yule jamaa alikuwa ameegemea ukuta akivuta sigara akionekana kujisahau kabisa.Mara akastuliwa na sauti ya kitu kama jiwe lililoanguka nyuma yake.Akaitupa sigara na haraka akageuka nyuma kutazama kuna nini lakini hakuona chochote "Peter ! akaita lakini hakujibiwa.Haraka haraka akatumia ngazi zilizokuwa nje akaanza kushuka haraka haraka lakini kabla hajafika cini akatokea Elvis na kumtaka asimame alipo.Yule jamaa kwa woga akageuka na kutaka kurudi juu lakini akakutana na Steve akiwa na bastora.Kwa ujasiri na wepesi wa aina yake akaitoa bastora kwa lengo la kupambana na akina Steve lakini Elvis tayari alikwisha kiona kitendo kile na hakumpa nafasi kwani kwa shabaha ya aina yake akaupiga risasi mbili mkono ule uliokuwa umeshika bastora akaanguka chini.Steve akamuwahi na kumvuta juu akamuingiza ndani.Elvis akaangaza kila upande na hakuona mtu yeyote.Akapanda ngazi haraka haraka akamfuata Steve kule juu "Tuambie wewe ni nani na unafanya nini hapa? akauliza Steve "Jamani naombeni msiniue.." "Hatutakuua kama utatueleza wewe ni nani na unafanya nini hapa? akauliza Elvis lakini yule jamaa hakujibu kitu alikuwa anagugumia kwa maumivu huku damu nyingi ikiendelea kutoka katika jeraha. Elvis akamkanyaga katika jeraha la yule jamaa ambaye alipiga ukelele mkubwa wa maumivu. "Beka !! ikasikika sauti ikiita.Elvis akamuinamia yule jamaa "Huyo ni nani anakuita?akauliza kwa sauti ndogo "Ni mwenzangu tuko naye hapa" akajibu yule jamaa Muite aje hapa haraka sana lakini usimueleze kama tuko hapa" akasema Elvis na kumnyooshea bastora. "Peter njoo huku! akasema yule jamaa kwa sauti iliyojaa maumivu.Steve na Elvis wakajificha na mara Peter akaingia mle ndani "Peter kimbiaaaaa!!! akasema Beka na Peter akataka kugeuka akimbie lakini Steve akacheza vizuri na bastora yake na kumpiga risasi mbili za mgongo akaanguka chini,akamuwahi na kuichukua bastora yake.Akamgeuza akamtazama lakini alikuwa katika dakika zake za mwisho. "Can he make it? Elvis akauliza "No he won't" akasema Steve "Mwenzako roho yake inachukuliwa na ziraili muda huu nawe utamfuata muda si mrefu endapo hautatueleza ninyi ni akina nani na mnafanya nini hapa?Kwa nini mna silaha? "Msiniue jamani.Sisi tuko hapa tumepewa kazi ya kufanya" "Kazi gani na nani kawapa kazi hiyo? "Kuna mtu tunamlinda hapa.Tumepewa kazi na Obi" "Yuko wapi huyo mtu mnayemlinda?Kafanya nini?akauliza Steve "Ni msichana na hatujui kafanya nini.Sisi tumepewa kazi ya kumlinda.Obi ndiye anayefahamu kafanya nini" "Inuka haraka tupeleke mahala alipo huyo msichana" akasema Elvis na Steve akamshika mkono akamuinua yule jamaa ambaye akawapeleka katika chumba walimomfungia mtu ambaye walikuwa wanamlinda.Msichana mmoja aliyechafuka damu akiwa ameinamisha kichwa alikuwa amefungwa kamba katika kiti.Haikuhitaji nguvu kubwa kugundua kwamba yule msichana alikuwa ameteswa sana "Winnie !! akaita Elvis na kwa taabu Winnie akainua kichwa.Hakuwa na nguvu kabisa.Elvis akamgeukia yule jamaa na kumtandika ngumi iliyompeleka hadi chini. "Mnawezaje kufanya ukatili huu kwa msichana huyu asiye na kosa lolote? akasema kwa ukali Elvis na Steve akaanza kumfungua Winnie kamba alizofungwa "Nisaidieni jamani mnipeleke hospitali."akalia yule jamaa ambaye jeraha lake liliendelea kutoa damu. "Elvis !! akasema Winnie kwa sauti dhaifu baada ya kufunguliwa Winnie you'll be fine" akasema Elvis na kumuinua Winnie akaanza kushuka naye chini. "Jamani nitakufa nipelekeni hospitali" akalia yule jamaa.Steve akamtazama kwa hasira na kuchomoa bastora yake "You'll go to hospital in hell!! akasema na kuachia risasi nne na kuuondoa uhai wa yule jamaa "Hizi ni salamu kwa hao wanaowatuma mpambane na watu msiowafahamu" akasema na kushuka ngazi haraka haraka kumfuata Elvis "Umemuacha yule jamaa? "I killed him" "Good" akasema Elvis wakitembea haraka haraka hadi walipofika katika gari lao .Kulikuwa na watu wachache wakipita barabarani lakini hawakuwajali wakampakia Winnie na kuondoka eneo lile "Wamemtesa sana"akasema Steve "Winnie hakupaswa kupitia haya yote aliyoyapitia.Mateso haya ni makubwa sana kwake.Hakustahili" akasema Elvis "Naamini kwa haya yaliyomkuta atakuwa amejifunza akiambiwa asifanye kitu fulani basi atii.Kama angesikia tuliyomweleza yasingemkuta haya yaliyomkuta.Nini kinafuata baada ya hapa? akauliza Steve "Kwa sasa tumshughulikie Winnie hali yake iboreke halafu tusubiri taarifa kutoka kwa Omola"akasema Elvis na kumpigia simu Dr Philip akamuelekeza mahala walikohamia na kumtaka afike haraka sana ***************** Samira na Omola waliwasili ikulu na hawakupata taabu katika kuingia kwani taarifa za kuwasili kwa Omola tayari zilikuwepo.Wasaidizi wa rais wakamjulisha Omola kwamba rais hataweza kuonana naye kwa muda ule kwani alikuwa katika kikao muhimu hivyo alitoa maelekezo kwamba atakapofika apelekwe moja kwa moja kwa makamu wa rais ambaye tayari amekwisha zungumza naye.Omola na wasaidizi wale wa rais wakaelekea moja kwa moja hadi katika ofisi ya makamu wa rais ambako ilimlazimu Omola kusubiri kwani tayari makamu wa rais alikuwa na mazungumzo na watendaji kadhaa wa ofisi yake.Saa nne na nusu ndipo makamu wa rais alipomaliza mazungumzo na watendaji wake na akataarifiwa kwamba Omola tayari amekwisha wasili akaelekeza aingie ofisini kwake. "Karibu sana" akasema makamu wa rais akimkaribisha Omola.Uso wa Dr Shafi ulionyesha tabasamu baada ya kumuona mrembo yule ambaye kwa wajihi alioutengeneza alionekana kweli mwandishi wa habari "Nashukuru sana mheshimiwa makamu wa rais"akajibu Omola "Naitwa Omola Otola ni mwandishi wa habari za mazingira.Ninafanya kazi na shirika lisilo la kiserikali ambalo kazi yake ni kutunza na kuhifadhi mazingira.Katika shirika letu kuna kitengo cha habari za mazingira na tuna jarida la mazingira litokalo kila mwezi hivyo tunazunguka sehemu mbalimbali duniani kutafuta habari za mazingira na kuziandika katika jarida letu.Kikubwa tunachoangalia katika nchi tunazozitembelea ni namna wanavyotunza na kuhifadhi mazingira.Ni mara ya kwanza tunafika Tanzania kuandika habari za mazingira.Katika Afrika ni nchi ya kwanza kuitembelea na tumeamua kuandika habari za Tanzania katika jarida letu kwa sababu ni nchi inayokua kwa kasi kiuchumi.Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la shughuli mbali mbali za kiuchumi hususan viwanda na katika shughuli hizi za kiuchumi uchafuzi wa mazingira hauwezi kukosekana hivyo ni muhimu kujua namna serikali ya Tanzania inavyokabiliana na suala la uchafuzi wa mazingira,namna inavyotunza mazingira ya fukwe,namna inavyotunza na kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji.Kwa ujumla tunataka kufahamuu mazingira kwa upana wake hapa Tanzania" akasema Omola "Omola ninashukuru sana kukufahamu.Mheshimiwa rais amenipigia simu na kuniueleza kwamba utakuja kuonana nami hivyo nikupe ushirikiano.Ni kweli ofisi yangu ndiyo inayoshughulika na masuala yote ya mazingira na nitakueleza kwa upana wake kuhusiana na mazingira kwa ujumla.Utaniwia radhi kwani kwa sasa ninahitaji kupata mapumziko kidogo halafu tutapata wasaa wa kuzungumza utaniuliza maswali na mimi nitakujibu na nitakuelekeza pia kwa watu wangu wanaohusika na mazingira na utapata mambo mengi kupitia kwao.Kama hutojali naomba tuongozane kupata chai" akasema makamu wa rais na Omola hakujivunga akakubali wakaongozana na Dr Shafi kupata chai. "Karibu sana Tanzania Omola.Ni mara yako ya kwanza kufika Tanzania?akauliza Dr Shafi "Ndiyo mheshimiwa makamu wa rais.Ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania.Ni nchi nzuri nimeipenda.Nimekuwa nikizisikia sifa zake kwa muda mrefu na leo nimefurahi kuwa hapa.Nimekutana na watu wakarimu sana kama vile nilivyokuwa nikisikia kwamba waTanzania ni watu wakarimu mno.Kikubwa kilichonifurahisha ni namna serikali ya Tanzania inavyojitahidi kuupaisha uchumi wake.Hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania katika kuinua uchumi zinazaa matunda na sasa uchumi wa Tanzania ni moja ya chumi za mfano barani Afrika na duniani kwa ukuaji wakehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ wa kasi"akasema Omola na Dr Shafi akatabasamu "Ni kweli Omola,uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa sana kwani hii ni mipango ya serikai kwamba kabla ya kufika 2025 Tanzania iwe imeingia katika uchumi wa kati na kwa namna uchumi unavyoendelea tunaamini tutafika lengo hilo" akasema Dr Shafi wakaendelea na mazungumzo mengine na wakati wakiendelea kupata chai makamu wa rais akafuatwa na kujulishwa kwamba kuna waziri amekuja anahitaji kuzungumza naye.Dr Shafi akamtaka radhi Omola kwamba amepatwa na dharura na akamuomba aendelee kumsubiri amalize mazunumzo yake na waziri aliyemtembelea.Baada ya Dr Shafi kuondoka Omola akapata nafasi na kumpigia simu Elvis Omola mambo yanakwendaje huko? akauliza Elvis baada ya kupokea simu "Tayari nimeonana na makamu wa rais na muda mfupi uliopita nimekuwa naye ila hatujafanya mazungumzo yoyote amepata dharura kuna waziri amekuja ana mazungumzo naye ila akimaliza tutazungumza" "Vipi kuhusiana na ile taarifa ile kuhusiana na kampuni ya McLorien ambayo uliahidiwa kuipata leo? akauliza Elvis "Oh! Ahsante kwa kunikumbusha.Nipe muda kidogo niwasiliane na mtu wangu kama ana taarifa zozote amezipata kuhusu hiyo kampuni"akasema Omola na kukata simu akachukua kijitabu kidogo kutoka katika mkoba wake akazitafuta namna fulani nakupiga akazungumza kwa dakika moja na kukata simu halafu akampigia Elvis "Elvis mtu wangu amenijulisha kwamba tayari amekwisha nitumia taarifa katika barua pepe yangu.Nitakapokuja jioni tutaifungua tujue nini amekipata kuhusiana na kampuni hiyo ya McLorien" "Sawa Omola.kazi njema.Kama kuna msaada wowote unauhiaji nijulishe tafadhali" akasema Elvis akaagana na Omola na kukata simu na Omola akaendelea kumsubiri makamu wa rais hadi alipomaliza kikao na waziri kisha akamuita Omola ofisini kwake wakaanza mazungumzo.Makamu wa raia akampa Omola muhtasari wa hali ya mazingira ulivyo hapa nchini na akamueleza namna wanavyoshughulikia suala la uharibifu wa mazingira.Ulikuwa ni muhtsari mrefu na wakati akiendelea Omola akaomba samahani kwani kifaa kile kidogo alichokuwa anakitumia kurekodia kilionyesha kujaa.Akafungua mkoba wake na kukiminya kichupa kidogo mithili ya kichupa cha uturi halafu akachukua kifaa kingine cha kurekodia akakiweka mezani akaendelea kumrekodi makamu wa rais.Sekunde chache makamu wa rais akaanza kupiga chafya. "Oh sorry" akasema Dr Shafi na kutoa kitambaa mfukoni "Tunaweza kuendelea" akasema lakini ghafla akaanza tena kupiga chafya mfululizo "Excuse me" akasema na kuinuka akaelekea katika mlango mdogo ulioonekana kama maliwato.Kwa muda wote ambao alikuwa amekaa na makamu wa rais aliweza kumsoma vizuri na kugundua kwamba alikuwa anatumia kalamu nyekundu ambayo aliitoa katika mfuko wake wa koti.Kwa kasi ya ajabu akafungua mkoba wake na kutoa kitu fulani kidogo na kukiweka ndani ya kalamu ile aliyokuwa anaitumia makamu wa rais halafu akatoa kitu fulani kama kichupa cha dawa akakiweka puani kama vile anavuta hewa ya kile kilichokuwamo ndani ya ile chupa kisha akatoa tena kichupa kile mithili ya kichupa cha uturi na kukipuliza karibu na meza ya makamu wa rais.Baada ya muda kidogo makamu wa rais akarejea "Samahani sana Omola.Nimepatwa na hii chafya ya ghafla" akasema makamu wa rais na ,mara tu alipoketi akaanza tena kupiga chafya mfululizo. "Pole sana mheshimiwa makamu wa rais"akasema Omola Usijali Omola.Naomba samahani sana kwa hali hii iliyonitokea" akasema makamu wa rais na kuinuka akaingia tena maliwato_Omola akaiona mezani simu ya mkononi akaichukua na kuifungua akatoa kadi ndogo ya kuhifadhia kumbu kumbu iliyokuwamo na kuingiza kadi yake halafu akabonyeza namba kadhaa na programu fulani ikaingia katika ile simu ya makamu wa rais.Haraka haraka akaitoa ile kadi yake na kuirejesha ile ya makamu wa rais na kuiweka simu mahala ilipokuwa.Kitendo kile kilichukua muda mfupi sana.Sekunde chache tu baada ya kuirejesha simu,mlango ukafunguliwa na makamu wa rais akarejea. "Omola utanisamehe sana ninaona hali yangu imebadilika ghafla hivyo ninahitaji kuonana na daktari wangu mapema.Nadhani itakuwa vyema kama tukiendelea na mazungumzo zaidi kesho" "Sawa mhesimiwa,nitakuja tena kesho.Pole sana" akasema Omola na kutoka.Bado Samira alikuwa garini akimsubiri wakaondoka ******************* Frank aliwasili katika nyumba alikopelekwa Vicky,akawakuta vijana wa Obi wakiwa wameimarisha ulinzi "Kazi nzuri Obi.Mna hakika hakuna yeyote aliyekuwa anawafuatilia?akauliza Frank "Hapana mkuu hakuna yeyote aliyetufuatilia" "Are you sure Obi? akauliza Frank Ndiyo mkuu.Tumechukua kila aina ya tahadhari hadi kufika hapa.Nimewatuma vijana wamefanya uchunguzi wa eneo lote kuzunguka hapa hakuna hatari yoyote" "Vipi kuhusu Vicky, mmemchunguza hajafungwa kifaa chochote cha kurekodi mazungumzo? akauliza Frank "Hana kifaa chochote tumemfanyia uchunguzi wa kutosha" "Good.Where is she?akauliza Frank na Obi akampeleka katika chumba alimokuwamo Vicky.Mlango ukafunguliwa na taa ikawashwa Vicky tayari alikwisha zinduka. "Hallow Vicky.Dunia imekuwa ndogo sana hatimaye tumeonana tena" akasema Frank huku akitabasamu "Winnie yuko wapi? Not so fast pretty lady.Tunakwenda taratibu hatua kwa hatua.Mimi nawe tuna mazungumzo marefu sana siku ya leo" akasema Frank na kumuita Obi akamtaka amfungue Vicky pingu alizokuwa amefungwa. "Samahani sana Vcky kwa kukuleta hapa kwa staili hii lakini imenibid kufanya hivi kwa ajili ya tahadhari" "I'm so dissapointed with you Frank.Kwa nini umenifanyia hivi?Kwa nini ukamtuma huyu mtu wako kuja kututeka?Kwa nini umemteka mdogo wangu na kumpa mateso? Nijibu Frank kwa nini umenifanyia haya?Dont you trust me anymore?akasema Vicky huku akilengwa na machozi "Ninakuamini Vicky lakini kwa mambo yaliyotokea ndani ya siku mbili hizi nimepata mkanganyiko na sina hakika kama nitakuamini tena" akasema Frank "Kitu gani kinakufanya usiniamini? "Ninataka unishawishi nikuamini tena.Nataka unieleze kwa nini ulimuua Pascal?Nimeumia sana kujua kamba umeshiriki katika kifo chake.Tuanzie hapo nieleze kitu gani kimekufanya umuue Pascal? akauliza Frank na macho yake yakaanza kubadilika na kujaa ukatili "Una hakika ni mimi ndiye niliyemuua Pascal?Kwa nini unanihusisha na jambo kama hili?Mimi ninawezaje kumuua mtu wangu wa karibu?Wewe na Pascal ni watu wangu wa karibu na hata mimi nimeumizwa vile vile na kifo chake.Tafadhali nakuomba usinihusishe na jambo kama hilo.Mimi si muuaji.Nilikubali kumuua kanali Norman kutokana na fedha nzuri aliiniahidi Deus lakini mimi si muuaji.I'm not a kiler" akasema Vicky.Frank akainuka na kumsogelea "Vicky tell me the trust.Kwa nini ulimuua Pascal? "Frank please I'm not a killer" akasema Vicky "C'mon Vicky tell me the truth why you killed him? Who sent you to kill him?akauliza Frank huku akipiga kitanda kwa mikono,tayari hasira zilianza kumpanda "Frank mambo haya yote umeyatoa wapi?Aliyekwambia kwamba mimi nimemuua Pascal amekudananya.Siwezi kufanya jambo kama hilo.I'm not a killer like you" akasema Vicky.Frank akamtazama kwa hasira Vicky naomba unisikilize vyema.Frank huyu unayezungumza naye hapa si Frank yule ambaye umemzoea.I'm real Frank the killer! Hivyo nakupa angalizo kuwa makini sana unapozungumza nami.Nipe majibu ya maswali yangu ninayokuuliza or else I'll destroy you.Dont force me to do that. I'm asking again why you killed Pascal and who sent you? "Frank nimekwisha kueleza kwamba sihusiki na jambo hilo.Naomba unieleze kwa nini unamshikilia mdogo wangu?Where is she? "Vicky please I dont want to destroy you my dear.Tell me the trut.I swear I'll understand and let you go.Ninaamini huwezi kufanya jambo kama hili wewe mwenyewe lazima kuna mtu amekutuma na huyo ndiye ninayetaka kumjua.Huyo ndiye ninayemuhitaji" akasema Frank "Frank nakuomba tusiendelee kupoteza muda wakati unafahamu fika kwamba sijahusika na siwezi kujihusisha na jambo kama hilo.Naomba usiyachoshe masikio yangu kwa jambo hilo.Nataka nimone Winnie" akasema Vicky "C'mon Vicky.Usitake kulifanya suala hili likawa gumu zaidi .Tell me the truth!! akafoka Frank "There is no truth!! Vicky naye akafoka.Frank akamtazama kwa hasira halafu akasema "Nisikilize vyema.Usijidanganye kwamba sifahamu ulichokianya.Ninajua kila kitu.Tayari nimefuatilia na nimegundua wewe ndiye uliyempigia simu Pascal ukamuita aje kule hotelini na huko ukamuua.Nani alikutuma ufanye hivyo? akauliza Frank.Maneno yale ya Frank yakamstua Vicky lakini akajikaza ili Frank asigundue. "Thats not true.Sijawasiliana na Pascal kabla ya kifo chake" akasema Vicky na kuzidi kumpamdisha hasira Frank akamnasa kofi kali "Yes you called him !!!akafoka Frank "If you don't tell me the trruth I swear I'm going to destroy you and Winnie!! Vicky aliyekuwa ameanguka kitandani kufuatia kofi kali la Frank akainuka aliposikia jina Winnie likitajwa "Dont dare touch her!!! akasema Vicky "Kama hutanieleza ukweli nani alikutuma umuue pascal nitamuua Winnie tena mbele ya macho yako.Ninakupa nafasi ya mwisho .Niambie ukweli !! "Frank tafadhali nakuonya usimguse mdogo wangu.Cheza na mimi utakavyo lakini si Winnie.Uliyekuwa unanitafuta ni mimi na si Winnie.Yeye hahusiani kwa lolote na wewe ndiyo maana nimejileta kwako ili umuachie Winnie.Please let her go!! akasema Vicky "Uhai wa Winnie uko mikononi mwako.Wewe ndiye utakayeamua kumuua au kumuacha hai.Kama utanieleza ukweli Winnie ataendelea kuwa hai lakini kama utanificha nitaanza kwanza kumtoa uhai Winnie na wewe utafuata tena kwa mateso makali mno" "Ni ukweli upi unautaka Frank? Tell me everything.Niambie nani kakutuma umuue Pascal?Nani unashirikiana nao? "Nimekwisha kwambia hakuna mtu yeyote aliyenituma na wala ninayeshirikiana naye" "Where is Elvis?!!! akauliza Frank kwa ukali "Elvis?!! Vicky akashangaa "Ni nani huyo Elvis?akauliza "Usijifanye humjui Elvis.Yule jamaa aliyekufuata akaanza kukuchunguza kuhusiana na kifo cha kanali Norman" "That man is dead!.Isn't he? Tena wewe mwenyewe ndiye uliyeniambia kwamba mmemuua sasa iweje uniulize yuko wapi wakati unafahamu mahala alipo?akauliza Vicky "Vicky unajifanya mjanja sana siyo?Kwa taarifa yako tayari Winnie ametueleza kila kitu.Ametuelezakuhusu Elvis na mwenzake Steve ambao waliwateka na kukulazimisha uwaonyeshe mahala nilipo.Kwa nini hutaki kunieleza ukweli kuwa ni wao ndio waliokutumia ili kumpata Pascal?Kwa nini unanificha jambo hilo wakati tayari ninalifahamu?akauliza Frank na Vicky akatoa kicheko "Do you believe her?akauliza "Winnie amekudanganya" "Hapana hajanidanganya.Alifahamu kwamba ninakutafuta kwa ajili ya kufahamu kwa nini ulishiriki katika mauaji ya Pascal na akanieleza kwamba wewe huhusiki bali ulilazimishwa kumuita Pascal hotelini.Alinieleza kila kitu ili niweze kukuacha huru kwani ana wasiwasi wale jamaa wanaokushikilia wanaweza wakakuua. Alinitaka nikuokoe kutoka katika mikono ya hao jamaa aliowataja kwa majina ya Elvis na Steve.Kama haitoshi alinieleza pia kwamba katika nyumba hiyo mliyokuwa mnashikiliwa yupo pia mwanangu Graca ambaye alitoroshwa na Elvis kutoka afrika ya kusini.Nilimtaka akanionyeshe mahala hapo mnaposhikiliwa tukaenda na hatukukuta mtu yeyote.Ninataka kuwafahamu hao jamaa ni akina nani?Kwa nini wananitafuta?Ninavyofahamu ni kwamba Elvis aliyemtorosha Graca kutoka Afrika kusini tayari amefariki dunia nataka kujua ni Elvis yupi huyo aliyekuwa anakushikilia?Ninahitaji sana kuwafahamu hawa jamaa ni akina nani na wako wapi.Sina shida yoyote na wewe Vicky.Ninakuomba tafadhali nieleze ukweli kuhusu hawa jamaa ninawahitaji sana" akasema Frank Frank narudia tena kukueleza kwamba Winnie amekudanganya.Nashangaa mambo haya yote aliyokueleza ameyatoa wapi.Hakuna mtu yeyote aliyetuteka zaidi ya yule aliyekuja kutaka kututeka nyumbani ambaye ninaamini wewe ulimtuma ukiamini kwamba nimehusika katika kumuua Pascal.This is a big lie.Hakuna Elvis wala Steve ninaowafahamu.It's a lie" akasema Vicky "Vicky tafadhali huu si wakati wa utani.Nieleze ukweli tafadhali." akasema Frank "Ukweli upi unaouhitaji Frank?Nimekueleza kila kitu kwamba Winnie alikudanganya" "Hapana.Hakunidanganya.Sina mahusiano yoyote na Winnie na sina hakika kama ananifahamu lakini alinipigia simu akahitaji kuonana nami na tulipoonana akanieleza haya yote akiomba nikusaidie kwani uko katika matatizo" akasema Frank na kumtazama Vicky kwa hasira halafu akauliza "Where were you last night? "Last night? akauliza Vicky "Ndiyo ulikuwa wapi? "Hayo ni masuala yangu binafsi ambayo hutakiwi kuyafahamu"akasema Vicky "I need to know Vicky.Kwa mujibu wa Winnie uliwaahidi hao jamaa kwamba utawapeleka mahala ambako unaamini wanaweza kunipata na jana usiku nikiwa katika nyumba ambayo Winnie alinipeleka akidai ndiko mlikokuwa mnashikiliwa nikataarifiwa kwamba kuna watu wamevamia katika nyumba yangu ya shambani na wakaingia katika ofisi yangu ninamohifadhi mambo yangu ya siri wakachukua kila walichoona kina wafaa.Ninaamini waliofanya http://deusdeditmahunda.blogspot.com/hivyo ni hao jamaa waliokuwa wanakushikilia na ninaamini wewe ndiye uliyewapeleka huko kwani uliwaahidi kufanya hivyo.Vicky ninarudia tena kukuomba kwa mara ya mwisho hawa watu ni akina nani na wanataka nini kwangu?Ninataka kujua huyo mtu anayeitwa Elvis ni yupi? "Frank sitaki kuendelea kuzungumza tena masuala hayo ambayo nimekwisha kueleza kwamba si ya kweli.Tafadhali nionyeshe alipo Winnie!!Let her go!! akasema Vicky huku akihisi mwili unamtetemeka kwa ndani.Frank akazidi kumtazama kwa hasira "Vicky sikutaka kukufanyia hivi lakini umenilazimisha wewe mwenyewe nikuharibu and I'll destroy you!! akasema na kutoka akamkuta Obi amesimama nje ya mlango "Obi huyu mwanamke bado mgumu kusema chochote.Sikutaka kumtesa lakini amenilazmisha kufanya hivyo.Ninataka umfunge na twende naye kule aliko mdogo wake.Nitamtesa na atasema kila kitu na hata ikibidi kumuua mdogo wake nitafanya hivyo.Leo lazima niupate ukweli!! akasema Frank na Obi akaingia ndani ya kile chumba akamfunga Vicky kitambaa usoni,akamfunga pingu za mikono akamtoa mle ndani na kumfungia katika buti ya gari wakaondoka kuelekea mahala walikomuacha Winnie ****************Elvis na Steve walimpitia Dr Philip mahala walikopanga wakutane wakaelekea moja kwa moja katika makazi yao mapya.Elvis akamueleza kila kitu kilichotokea na mahala walipofikia katika uchunguzi wao "Poor girl.Ameingia katika matatizo ambayo hakuyategemea.Hakupaswa kufanyiwa ukatili wa namna hii.Watu hawa wana roho za kinyama sana"akasema Dr Philip huku akimuangalia Winnie namna alivyochafuka kwa damu "Ni watu makatili sana lakini siku zao zinahesabika.Tayari tumepata mwangaza mkubwa kuhusiana nao na nina uhakika muda si mrefu sana tutakuwa tumepata taarifa kamili za kuhusiana na mtandao wao" akasema Elvis na safari ikaendelea hadi walipofika katika makazi yao.Haraka Winnie akashushwa na kuingizwa ndani Dr Philip akaanza kumuhudumia.Wakati Winnie akiendelea kuhudumiwa Elvis akamuita pembeni Graca "Vicky hajarejea?akamuuliza "Hapana hajarejea"akajibu Graca na taarifa ile ikamshangaza sana Elvis.Steve akatoka haraka kwenda kununua mahitaji kwani hawakuwa wamepitia sehemu yoyote wakiwahi kumpatia huduma Winnie "Vicky amekwenda wapi?Kwa nini hakuaga tujue anakwenda wapi? akajiuliza Elvis na kutolewa mawazoni baada ya simu yake kuita.Mpigaji alikuwa Omola "Omola mambo yanakwendaje?akauliza Elvis "Mambo yanakwenda vizuri.Tayari nimeondoka kwa makamu wa rais na ninaelekea hotelini.Naomba aje mtu kunichukua" akasema Omola na muda huo huo Elvis akampigia simu Steve akamtaka akamchukue Omola hotelini kwake. "Anaendeleaje?Elvis akauliza baada ya kuingia katika chumba alimo Winnie "Anaendelea vyema.Tumuache apumzike na akiamka ataendelea kutumia dawa za kumsaidia kutuliza maumivu.Amepata michubuko kwa nje lakini haionyeshi kama ameumizwa kwa ndani hivyo dawa hizi zitamsaidia" akasema Dr Philip na kwa kuwa alimaliza kazi yake aliyoitiwa akaagana na akina Elvis akaondoka.Hakuwa amekuja na gari hivyo ikamlazimu kutembea kwa miguu kutafuta taksi.Wakati akiwasubiri akina Omola,Elvis akaenda kujipumzisha chumbani kwake Vicky amekwenda wapi?Kwa nini akaondoka kimya kimya bila kuaga?Staili yake ya kuondoka inanipa mashaka sana hata hivyo ngoja tuendelee kumsubiri.Kingine kinachoniumiza kichwa ni namna gani akina Frank walivyoweza kumpata Winnie?Amewaeleza mambo gani?Atatueleza kila kitu atakapoamka.Imekuwa ni jambo zuri kumshirikisha Omola katika operesheni hii kwani bila yeye tusingeweza kumpata Winnie kwa haraka namna hii..." Elvis akatolewa mawazoni baada ya mlango wake kufunguliwa akaingia Graca "Elvis poleni sana na hongereni kwa kufanikiwa kumpata Winnie" akasema Graca na kukaa karibu na Elvis "Tumewahi kumpata kabla ya wale jamaa hawajamuumiza sana" Vipi kuhusu zile nyaraka tulizozipata jana ofisini kwa baba,kuna maendeleo yoyote yamepatikana? "Nyaraka zile ni muhimu sana na uchunguzi wake unaendelea.Zimetusaidia tumepiga hatua kubwa na tumepata mwangaza kuhusiana na biashara hii ya silaha.Tumefanikiwa kumpata Irene mwabukusi ambaye nyaraka zinaonyesha ndiye mmiliki wa kampuni ya Pendeza Co.Ltd .Irene amekiri kwamba kampuni ya Pendeza ni kampuni ya Frank lakini yeye ndiye msimamizi mkuu.Mizigo imekuwa inatumwa kutoka kampuni ya McLorien kuja katika kampuni ya Pendeza na muagizaji mkuu wa mizigo hiyo ni David.Ikifika Tanzania mizigo hiyo hutolea bila kufanyiwa ukaguzi na kisha David huipeleka mahala ambako hutoa silaha na kisha hupeleka mali katika maduka yake.Irene anadai kwamba Pendeza Co.Ltd iko pia katika nchi za Congo na Burundi.Tunahisi kuwa David anatumia kampuni hii ya Pendeza kupitishia mizigo ya silaha.Tunataka tuichunguze pia kampuni ya McLorien ambayo inaonekana ndiyo inayotuma mizigo kwa kampuni ya Pendeza.Tunamsubiri Omola ambaye aliomba msaada kwa wenzake wamsaidie kuichunguza kampuni hii ya McLorien na tayari amekwisha tumiwa majibu katika barua pepe akifika ataifungua na tutajua nini wamekipata kuhusiana na kampuni hii.Graca mambo yanakwenda vizuri usiwe na hofu tutahakikisha yeyote anayejihusisha na mtandao huu anafikishwa mbele ya sheria" Sina cha kusema Elvis,ninawaombea wewe na wenzako mfanikiwe katika suala hili ili na mimi niweze kuwa huru kwani bila baba na mtandao wake kumalizwa nitaendelea kuishi maisha kama ya ndege ya kujificha ficha.Lakini kwa kuwa niko nawe karibu siogopi tena.Elvis nakuomba usiivunje ahadi uliyonipa kwani ukifanya hivyo utauvunja moyo wangu vipande.Nimepitia mengi magumu,nimepita katika giza nene na sasa nimeanza kuona mwangaza katika maisha yangu hivyo sihitaji kuumizwa tena.Lizingatie hilo" akasema Graca na kumbusu Elvis akaelekea chumbani kwake "Graca anasema kweli,amepitia mengi magumu na hapaswi kuumizwa tena na mimi nimekwisha muahidi kwamba nitakuwa naye kimapenzi na tayari amechanganyikiwa juu yangu.Nitafanya nini wakati bado ninampenda Patricia?Ngoja niyaweke pembeni masuala haya ya wanawake nimalize kwanza masuala muhimu kisha nitajua nini cha kufanya." akawaza Elvis "Nina uhakika mkubwa kwamba Frank anaitumia kampuni hii ya Pendeza kupitishia silaha.Ndani ya makontena hayo yanayotumwa ninaamini ndimo silaha hupakiwa na ndiyo maana makontena hayo hutolewa bila kufanyiwa ukaguzi wowote ili kuficha kile kilichomo ndani yake.Frank huyapeleka katika shamba lake na kule hupakua silaha na kisha huzisafirisha kwenda nchini Congo.Tayari mwanga huo nimeupata lakini bado nahitaji ushahidi zaidi.Nahitaji kuwafahamu wote waliomo katika mtandao huu" akaendelea kuwaza Elvis **************** Frank na Obi wakiwa na vijana wao wakawasili eneo la viwanda ambako Winnie alikua amepelekwa.Baada ya kufika katika jengo alimokuwamo Winnie,Vicky akashushwa toka katika buti ya gari na kufunguliwa kitambaa. "Hapa ni wapi? akauliza huku akitetemeka "Quiety!! akasema Frank na kumtaka Vicky apandishwe ghorofani.Vijana wawii wakamshika Vicky na kuanza kumpandisha juu Frank na Obi wakiwa wametangulia mbele.Obi akamuongoza Frank katika chumba alimokuwa amefungiwa Winnie lakini wote wakapatwa na mshangao mkubwa sana baada ya kukuta chumba kitupu na kamba alizofungiwa zilikuwa zimekatwa na kutupwa "beka!!!! akaita Obi lakini hakujibiwa "Peter !!! akaita tena lakini akajibiwa na ukimya mkubwa "Somehing is wrong ! akasema Obi kwa sauto ndogo na kutoka haraka mle chumbani "Obi nini kimetokea?Wako wapi vijana?Winnie yuko wapi? akauliza Frank akimfuata Obi nyuma.Ghafla Obi akasimama kama mtu aliyekutana na kitu cha kutisha akahisi miguu inamuisha nguvu akapiga magoti na kushika kichwa "Oh my God!! akasema Obi na mara Frank naye akaingia mle ndani ya kile chumba na kuwakuta vijana wawili wakiwa wamekufa kwa kupigwa risasi Who did this !!! akasema Frank kwa mshangao na kwa hasira akamfata Vicky akamuwekea bastora kichwani "Utanieleza wapi walipo watu uliowasaidia kumuua Pascal? akasema na kumshika Vicky nywele akampeleka katika chumba kile walichouawa wale vijana wawili "You see this?!akauliza "Waliofanya hivi ni hao wenzako unaoshirikiana nao.Ukitaka nikuache hai nieleze wako wapi? "Winnie yuko wapi? Siwezi kusema chochote bila kumuona Winnie.Show me Winnie and I'll tell you everything" akasema Vicky Frank akapandwa na hasira akamrushia ngumi nzito iliyompeleka chini akamkalia juu na kuanza kumporomoshea makonde Mkuu imetosha.Utamuumiza huyu na tutakosa kila kitu" akasema Obi na kumvuta Frank ambaye alikuwa amepandwa na hasira isiyo kifani.Uso wa Vicky uliloa damu na mara simu ya Frank ikaita.Akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa ni Irene akasogea pembeni "Irene" akasema baada ya kuipokea "Frank where are you? I need to see you !! akasema Irene "Kuna tatizo Irene? akauliza Frank "Chochote unachokifanya achana nacho nakuhitaji hapa nyumbani sasa hivi.Kuna jambo la msingi sana" "Irene ni jambo gani hilo?Huwezi kunieleza simuni? "Frank believe me acha kila unachokifanya na uje hapa nyumabani ninakusubiri.Usipuuze tafadhali"akasisitiza Irene.Frank akazama katika tafakari "Frank !! akaita Irene "I'm coming there" akasema Frank na kumtaka Obi wazungumze "Obi kuna dharura imejitokea ninahitajika sehemu fulani.Take care of everything here.Mrudisheni Vicky na hakikisha anaongea.Do everything you can to make her tell us everything!! akasema Frank na kuondoka haraka haraka akionekana kuchanganyikiwa "Bastard !! akapiga usukani wa gari baada ya kukumbuka miili ya wale vijana wawili waliouawa na Winnie kutoweka "Nani huyu aliyefanya haya?Amefahamuje kama Winnie yuko pale? Winnie alikuwa ni muhimu sana kwetu kwani bila yeye Vicky hawezi kutueleza jambo lolote.I'm back to square one.Watu hawa tayari wanaonekana kunifuatilia kila mahala,na wanafahamu kila ninachokifanya.I must find them immediately!! akawaza akiendesha gari kuelekea nyumbani kwa Irene "I think Winnie and Vicky are playing a game with me.Kauli zao zinakinzana.Winnie anadai kwamba walikuwa wametekwa na watu ambao amewataja kwa majina na mmoja wa watu waliotajwa ni Elvis lakini Vicky amekana kutekwa na watu hao.Winnie ametupeleka hadi mahala walikokuwa wanashikiliwa lakini hatukukuta mtu yeyote mahala hapo na tukiwa hapo ofisi yangu shambani ikavamiwa na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeonekana akiingia ndani ya nyumba hiyo.Leo tena Vicky amejitokeza na kukana kila kile alichokisema Winnie na kama haitoshi Winnie akatoroka.What kind of game are they playing?How could I be such a fool?!! How could I let them fool me like this?! akawaza na kuupiga usukani kwa hasira "Vicky atanieleza kila kitu leo.Nitampa kila aina ya mateso hadi atakaponieleza ukwe.." Frank akatolewa mawazoni baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni David "Hallow David" akasema Frank " Hallo Frank.Habari za leo?Vipi maendeleo yako ? "Ninaendelea vyema.Vipi wewe? "Hata mimi ninaendelea vyema.Nimekupigia kukujulia hali kwani toka asubuhi sijaipata simu yako.Tuko katika hatua kubwa sana hivi sasa tunapaswa kuwa na mawasiliano ya karibu na kupeana taarifa za mara kwa mara juu ya kile kinachoendelea kujiri.Dr Makwa amelala nyumbani kwangu kwa kuhofia kukamatwa na amekuwa akiwasiliana na wenzake kuhusiana na kinachoendelea na taarifa anazoendelea kupokea ni kwamba kila kitu kinakwenda vyema na maandalizi yanaendelea ya mkutano wa leo.Jioni ya leo lazima tuwe na kikao tujadili kuhusu mambo yalivyokwenda na kinachoendelea.Baada ya mkutano wa leo tutapata picha kamili ya namna operesheni yetu inavyokwenda" akasema David "Sawa David.Tutakutana jioni ili tupeane taarifa zaidi kuhusu operesheni hii" akasema Frank "Frank are you ok today?akauliza David "Why?Frank naye akauliza "Unaonekana hauko sawa.Vipi kuhusu mazishi ya pascal? Ni kweli siko sawa David kuna jambo fulani linaniumiza kichwa sana.Kuhusu Pascal bado sijapata taarifa kamili ni lini anazikwa.Nitapita msibani baadae kupata taarifa kisha nitakujulisha" "Frank umesema kwamba kuna jambo linakuumiza kichwa.Ni jambo lipi?Linahusiana na hili suala letu?Kama linahusiana na sisi liweke wazi tulifanyie kazi haraka.Hatutaki kikwazo chochote kwa sasa" "Ni suala binafsi ninaweza kulishughulikia" "Sawa Frank tutawasiliana baadae"akasema David na kukata simu "Sijui kwa nini nimeanza kumchukia David.Huyu jamaa ninahisi anaweza akahusika pia katika kifo cha Pascal.Lakini suala ili la kifo cha Pascal bado lina ukakasi.Winnie aliwataja Elvis na Steve kwamba walimteka Vicky na kumlazimisha kumuita Pascal pale hotelini kisha wakamuua.Madam Elizabeh naye akadai kwamba yeye ndiye aliyemuua Pascal.Ninaposhindwa kupata jibu ni je madam Elizabeth ameshirikiana na hao akina Steve?Nilimuuliza kuhusu kushirikiana na Vicky na akadai kwamba ndiyo alishirikiana na Vicky ..oh gosh I'm confused.Ngoja niliendee taratibu hili suala nikiliendea kwa pupa litanichanganya.Mwenye majibu yote juu ya suala hili ni Vicky.Nina uhakika nikimtesa atanieleza ukweli wote kama kweli alitumwa na madam Elizabeth au vipi.Kama kweli alimtuma nitachunguza nijue Pascal alifanya jambo gani hadi akauawa?akaendelea kuwaza.
David alipomaliza kuzungumza na Frank simuni akazitafuta namba za simu za makamu wa rais akampigia "Hallow David" akasema Dr Shaf "Dr Shafi habari yako.Vipi mbona sauti yako haitoki vizuri leo? "NImepatwa na mafua ya ghafla ila tayari nimepata dawa na ninaendelea na kazi zangu.Kuna taarifa zozote mpya? "Nimetaka tu kukujulia hali na kukujulisha kuwa leo ndiyo mambo yanaanza rasmi.Maandalizi ya mkutano yanaendelea na kila kitu kimekamilika.Dr makwa ninaye hapa nyumbani kwangu toka jana na viongozi wengine wote wa vyama vya siasa wako katika sehemu zao wamejificha wakisubiri muda ufike ili wajitokeze na mambo yaanze rasmi.Dr Shafi nitakuwa nikikujulisha kila hatua tunayopiga ninachokusisitiza tu usiwe na wasiwasi kila kitu kimepangwa vizuri na kila jambo litakwenda kama vile tunavokusudia" "Hizo ni taarifa njema sana David.Mimi sina wasiwasi nawe hata kidogo kwani najua mahala ulipo hapaharibiki kitu.Endelea kunijulisha kila kitu kinavyoendelea ila nashauri umakini mkubwa unatakiwa hasa katika hatua hii.Polisi wanawawinda sana hawa wanasiasa na endapo watafanikiwa kumkamata hata mmoja wao basi wanaweza wakamtesa na akaeleza kwamba wewe ndiye uliyekuwa nyuma ya mpango huu wa maandamano na vurugu.Ikifika hapo kila kitu kitakuwa kimeharbika hivyo viongozi hawa wa siasa wawe makini mno" Hilo nimekwisha liona na nimezungumza nao na tumewekeana mikakati na kutokana na mipango yetu ilivyoandaliwa hakutakuwa na tatizo lolote.Nitawasiliana nawe tena jioni ya leo kukujulisha mambo yanavyokwenda" "Nawatakia kila la heri na mafanikio" akasema Dr Shafi na kukata simu "Sasa ngoja niende katika msiba nyumbani kwa madam Elizabeth nikamjulishe mambo yanavyokwenda.Mambo yote tayari yanakwenda vyema ninachosubiri ni muda tu ufike ili tujue mbivu na mbichi"akawaza David na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda msibani nyumbani kwa Elizabeth ****************** Steve alirejea katika makazi yao akiwa ameambatana na Omola "Karibu sana Omola"akasema Elvis "Ahsante sana Elvis.Nashukuru kila kitu kinakwenda vyema kwa upande wagu.Vipi hapa kwenu mambo yanakwendaje?akauliza Omola na kabla Elvis hajajibu kitu akatokea Steve akiwa na chupa ya mvinyo akiwa na glasi tatu akamimina na kuwapatia Elvis na Omola.Kila mmoja akanywa funda moja halafu Elvis akasema "Kwa upande wetu mambo yamekwenda vizuri.Kwanza kabla ya yote nataka nikushukuru sana kwani ile programu yako imetusaidia tumeweza kumpata Winnie japo alikuwa ameumizwa lakini tayari amekwisha shughulikiwa na anaendelea vyema" akasema Elvis na kumtazama Omola aliyekuwa anatabasamu "Tukiachana na hilo,tumefanikiwa pia kumpata Irene Mwabukusi mmiliki wa kampuni ya Pendeza.Baada ya kumuhoji amekiri kwamba mwenye kampuni ile ni brigedia Frank lakini alimtumia yeye kuanzisha na kuisimamia kwa kuwa yeye hataki kujulikana kama anamiliki kampuni" akasema Elvis na kumueleza Omola kila kitu walichoelezwa na Irene mwabukusi.Omola akanywa funda la mvinyo na kusema "Haya ni mafanikio makubwa yamepatikana ndani ya kipindi kifupi.Ninyi ni wachapa kazi hodari sana ninafurahi kukutana na kufanya kazi nanyi.Nimeipenda timu yenu" akasema na wote wakatabasamu Mpaka hapa tayari mwanga umepatikana.Kama kampuni hii ni ya Frank basi anatumia kama mwavuli wa kumkinga na biashara hii haramu ya silaha anayoifanya.Watu hawa wanazo mbinu nyingi za kufanikisha biashara yao.Ni mtandao mrefu na ndiyo maana hata mizigo yao inatoka bandarini bila hata ya kukaguliwa.Tuendelee kuchunguza na tutaupata ukweli wote" akasema Omola na kumimina tena mvinyo katika glasi akanywa halafu akaendelea "Nimefanikiwa kuonana na makamu wa rais.Nashukuru Vicky amefanya kazi nzuri na sikupata taabu yoyote kuingia ikulu kwani taarifa zangu tayari zilikuwepo hivyo nikapata urahisi wa kuonana na makamu wa rais.Sijamuona Vicky yuko wapi? akauliza Omola.Vicky ameondoka asubuhi na mpaka sasa hajarejea.Kinachonipa wasiwasi hakumuaga mtu yeyote anakwenda wapi" "Aliondoka bila kumuaga mtu yeyote? "Ndiyo.Aliondoka wakati bado tumelala na mpaka sasa hajarejea.Msiwe na wasi wasi Vicky atakuwa salama,anajua kujilinda,tuendelee na kazi.Tupe maelezo ya kazi yako ya leo" akasema Elvis "Sikuonana na rais ila wasaidizi wake walipewa maelekezo walinipeleke kwa makamu wa rais na nikafanikiwa kuonana naye.Makamu wa rais bado ni kijana na na anaonekana ni msomi mzuri.Nilijitambulisha kwake kumbe tayari taarifa zangu alikuwa nazo,aliambiwa na rais.Tulikunywa chai pamoja na kisha nikapata wasaa wa kuzungumza naye kuhusu masuala ya mazingira.Wakati nikiendelea kumuuliza maswali huku nikimrekodi nikafungua mkoba wangu na kubonyeza chupa ya dawa isiyokua na harufu ambayo humfanya mtu kupatwa na mafua ya ghafla na makamu wa rais akapatwa na chafya ya ghafla.Dawa hii haikuniathiri mimi kwani tayari nilikuwa nimepaka dawa fulani puani ambayo huzuia kuathiriwa na hii dawa pindi unapoipuliza sehemu.Dr Shafi alitoka na kuingia maliwato na mimi nikapata nafasi ya kufanya utundu wangu.Nilichomeka kifaa fulani kidogo katika kalamu yake ambacho kitarekodi mazungumzo yake yote.Nilingiza pia proramu fulani katika simu yake ambayo itatuwezesha kunasa mawasiliano yake yote ya simu.Kwa kuwa alikuwa anapiga chafya mfululizo aliniomba radhi kwamba hataweza kuendelea na mazungumzo yetu na akanitaka niende tena kesho.Hapo ndipo nilipoishia siku ya leo" akasema Omola na kuinua glasi akanywa tena funda lingine la mvinyo "Hongera sana Omola umefanya kazi kubwa na nzuri.Yale maneno yote aliyotueleza Vicky sasa nimeyaamini.Kuhusu kifaa hicho ulichokiweka katika kalamu ya makamu wa rais tutawezaje kupata taarifa zake?Itakulazimu tena kwenda kupata kalamu hiyo na kukipata hicho kifaa ili kusikia mambo kiliyorekodi? "Hatuhitajitena kuipata hiyo kalamu kwani kifaa hicho ninaweza kukiongoza kwa kutumia kompyuta yangu.Tutapata kila kitu hapa hapa"akasema Omola na Steve akainuka akampatia kompyuta yake "Kwanza tuanze na majibu ya ule uchunuzi niliowaomba wenzangu wanisaidie kuichunguza kampuni ya McLorien.Kama nilivyowaleza kwamba majibu tayari yametumwa katika akaunti yangu ya barua pepe" akasema Omola huku vidole vyake vikicheza na vitufe vya kompyuta yake na mara akaifungua akaunti yake ya barua pepe akazikuta barua pepe kadhaa lakini aliyokuwa anaihitaji kwa wakati huo ni moja tu akaitafuta akaipata akaifungua na kuanza kuisoma.Alipomaliza akawageukia akina Elvis "Kwa mujibu wa wenzangu walionisaida kupata taarifa za kampuni ya McLorien ni kwamba kampuni hiyo imesajiliwa nchini Marekani na inajishughulisha namasuala ya mavazi na urembo.Inajulikana sana kwa uuzaji wa nguo nzuri na viatu vya bei nafuu sana.Mmiliki wa kampuni hii anaitwa Shanon Blank jina ambalo tulilikuta katika mawasiliano ya barua pepe kati yake na Patrice Lwibombe.Kwa bahati nzuri wamenitumia pia na picha ya mmiliki wa kampuni hiyo na hiyo kidogo imenistua" akasema Omola na kuwataka akina Elvis wasogee ili waweze kuishuhudia picha hiyo ya Shanon Blank "Is this true?akauliza Steve kwa mshangao "Huyu si Elizabeth mama yake Juliana? akauliza "Picha aliyotutumia Juliana ya mama yake na hii zinaonyesha ni watu wanaofanana sana lakini bado hatuwezi kuwa na uhakika kama huyu ni mama yake Juliana.Tufanye kwanza uchunguzi"akasema Elvis "Sioni sababu ya kufanya uchunguzi wakati hata kwa macho unaona kabisa huyu ni Elizabeth mama yake Juliana.Believe me Elvis"akasema Steve "Steve unaweza kuwa sahihi lakini tujiridhishe kwanza kama ni kweli ni yeye.Huyu anaitwa Shanon Blank na mama yake Juliana anaita Elizabeth je ni mtu yule yule lakini ana majina tofauti?Kama ni kweli kwa nini awe na majina tofauti?hayo ni mambo ambayo tunapaswa kuyatafutia majibu japo sura ni kweli inaonyesha ni ya mama yake Juliana ingawa katika picha hii amekuwa mweupe zaidi" "Elvis ukumbuke pia kwamba tulijaribu kumtafuta kwa jina lile alilotuambia Juliana la Elizabeth lakini hatukuweza kumpata.Hii inaonyesha kwamba hatumii jina hilo na yawezekana akawa anatumia jina hili la Shanon Blank.Kumbuka Juliana alisema kwamba mama yake amekuwa anajiusisha na biashara haramu na hii ni staili ya watu wanaojihusisha na biashara hizi haramu mara nyingi hawatumii majina yao halisi.Yawezekana jina lake halisi ni Elizabeth lakini akabadilisha na kujiita Shanon.Unasemaje kuhusu hilo Elvis?akauliza Steve "Kwa hili tulazimika kumuhitaji Juliana.Mpigie simu tukutane naye"akasema Elvis mara Omola aliyekuwa anacheza na kompyuta yake akawageukia "Nimeingiza picha hizi mbili katika programu yangu na matokeo yanaonyesha kuwa huyu ni mtu mmoja.Anachokisema Steve ni kitu cha kweli.Elizabeth ndiye huyu Shanon" akasema Omola "Hapa tunahitaji msaada wa Juliana ili tuweze kumfahamu mama yake kwa undani"akasema Elvis "Una hakika atakubali kutupa taarifa za mama yake?Yuko tayari mama yake achunguzwe?akauliza Omola "Juliana yuko tayari mama yake achunguzwe kwani ni yeye aliyetupa taarifa kwamba anahisi mama yake anajihusisha na biashara haramu na akatutaka tuchunguze jambo hilo.Vile vile lazima atupe ushirikiano kwa sababu ametuomba tumsaidie kufanya uchunguzi kwa watu waliomuua mpenzi wake vile vile mdogo wake." akasema Elvis na Steve aliyekuwa amesogea pembeni akiongea na simu akarejea Nimempata Juliana na nimemuomba tukutane amekubali.Ninakwenda kuonana naye mara moja" akasema Steve "Huwezi kwenda peke yako,tutakwenda sote" "Are you sure Elvis? "Yes.Hataweza kuniona mimi nitabaki garini na wewe utakwenda kuzungumza naye katika gari lake na utamtaka athibitishe kama huyu anayeonekana katika picha ni mama yake.Omola atakutumia picha hizi katika simu ili Juliana aweze kuziona.Sisi tumethibitisha kuwa ni yeye kupitia programu ya Omola lakini tunahitaji na yeye athibitishe kweli huyu ni mama yake.Akithibitisha kuwa ni mama yake tutahiaji atusaidie kuchunguza pasi za kusafiria za mama yake ili tulifahamu jina lake halisi ni nani.Ni jambo gumu kidogo lakini litakuwa na msaada mkubwa kwetu.Kama kweli ana nia ya dhati ya kutaka kumfahamu vyema mama yake na biashara anazozifanya basi huu ni wakati wake.Tunahitaji msaada wake sana"akasema Elvis "Wakati mkienda huko mimi nitaendelea kufuatilia kifaa kile ambacho nimekitega katika kalamu ya makamu wa rais nifuatilie maongezi yake.Sifahamu kiswahili laiti Vicky angekuwepo angenisaidia kujua kile anachokizungumza makamu wa rais" akasema Omola "Usijali Omola yupo Graca hapa atakusadia kujua kile kinachoongelewa" akasema Elvis na kumuita Graca akamtaka amsaidie Omola kufahamu kile kinachozungumzwa katika mazungumzo ambayo kifaa alichokitega katika ofisi ya nakamu wa rais kitayanasa.Bila kupoteza muda Elvis na Steve wakaingia garini na kuondoka kwenda kukutana na Juliana "Kama Juliana atathibitisha kweli huyu ni mama yake basi jambo hili litakuwa pana sana"akasema Elvis "Mimi sina shaka kabisa kuwa huyu ni Elizabeth lakini ni vyema tukathibitisha kwa kumtumia mwanae Juliana"akasema Steve na Elvis akaendelea kuzichunguza picha zile mbili zilizowekwa katika simu ya Steve "Umemuonaje Omola?akauliza Steve huku akitabasamu "Not now Steve.Tuko katikati ya jambo zito masuala ya wanawake yaweke kwanza pembeni" akasema Elvis na safari ikaendelea ******************* http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Frank aliwasili nyumbani kwa Irene,akapokewa na mtumishi wa ndani akamkaribisha sebuleni.Baada ya dakika tano Irene akatokea akiwa amefunga plasta chini ya jicho na uso wake ulionekana kuvimba.Mkononi pia alikuwa amefunga bandeji "Irene nini kimetokea?Umepata ajali? "Ni bora kama ningepata ajali."akasema Irene huku akikaa sofani "Irene nieleze umepatwa na tatiuzo gani?Umenistua sana uliponipigia simu nikaacha kila kitu na kuja kukuona" akasema Frank.Irene akamtazama Frank kwa makini sana kwa sekunde kadhaa halafu akasema "Frank nataka leo unieleze ukweli" Ukweli gani Irene?Kabla ya yote nieleze nini kimekupata? "Frank nataka kufahamu unajihusisha na mambo gani?akauliza Irene na Frank akastuka sana "Sielewi unamaanisha nini Irene unapouliza swali kama hilo wakati unafahamu kabisa mambo ninayojihusisha nayo.Unaifahamu kazi yangu na unazifahamu pia biashara zangu"akasema Frank "Frank chochote kile unachojishughulisha nacho ambacho si kizuri nakuomba ukiache haraka sana"akasema Irene.Frank akasimama na kumtazama kwa macho makali "Irene unanishangaza sana kwa haya maneno yako" "Usishangae Frank na wala sina lengo ya kuyachimba maisha yako na kufahamu kila unachokifanya lakini nakueleza ukweli kwamba uko katika hatari kubwa" "Hatari?! akauliza Frank kwa mshangao "Ndiyo uko katika hatari kubwa" "Irene tafadhali sitaki uendelee kunizunguka,nieleze ukweli kwani umekuwa unazungumza mambo ambayo siyaelewi" Irene akameza mate na kusema "Nimefuatwa na watu wawili hapa nyumbani asubuhi ya leo.Niliwakaribisha ndani nikijua ni wateja wamekuja kuzungumza nami masuala ya biashara lakini ikawa tofauti wote wawili walikuwa na bastora na wakaniamuru niongozane nao kimya kimya bila kutoa ukelele wowote" "Oh my God! what happened then?Who are they?Siwafahamu na sijawahi kuwaona lakini wao wananifahamu na walifika hadi dukani kwangu asubuhi wakaambiwa sijafika ndiyo maana wakanifuata huku nyumbani"akasema Iene na Frank akagonganisha mikono yake kwa hasira "Walikupeleka wapi?Walikuw wamnataka nini? "Niliingia katika gari lao na wakaanza kuniuliza maswali.Waliniuliza kwamba kampuni ya pendeza ni ya nani?Nikawajibu ni ya kwangu lakini hawakuamini wakaanza kunitesa humo humo ndani ya gari.Waliniuliza tena mahusiano yangu na wewe nikawajibu sikufahamu na hapo ndipo walipotaka kunitoa jicho kwa kutumia kisu ikanilazimu kuwaeleza ukweli" Jesus Chris !! akasema Frank kwa sauti ndogo akiwa amesimama ameshika kiuno "Uliwaeleza mambo gani?akauliza "Kila kitu kuhusiana na kampuni.Niliwaeleza kwamba wewe ndiye mmiliki wa kampuni na umeniweka mimi kama msimamizi wake.Waliniuliza pia namna tunavyoagiza mizigo yetu nikawaeleza" "Kwa nini Irene umewaeleza kila kitu?Hukuweza uvumilia mateso?akauliza Frank kwa ukali "Frank I'm sorry nilivumilia sana lakini ikafika mahala nikashindwa kuendelea kuvumilia zaidi ikanilazimu kuwaeleza kile walichokuwa wanakitaka.Isitoshe inaonekana tayari walikuwa wanafahamu kila kitu kwani walikuwa na nyaraka za kutolea mzigo bandarini ambazo wanadai walizipata toka kwako hivyo ikanilazimu kuwaeleza ukweli wote.I'm sorry Frank" akasema Irene na Frank akaonekana kuchanganyikiwa akaanza kuzunguka zunguka mle sebuleni halafu akasimama na kuuliza "Nini kingine walikuuliza? "Walitaka kufahamu kuhusiana na kampuni ya McLorien." "Oh my gosh !akasema Frank akizidi kuchanganyikiwa "Uliwajibu nini? "Niliwajibu kwamba kampuni ya McLorien ndiyo ambayo hutuuzia bidhaa tunazouza katika maduka yetu" Frank akavuta pumzi ndefu na kuketi sofani "who are those people?Kwa nini wanakuchunguza?akauliza Irene Irene samahani sana kwa kukuingiza katika matatizo haya.Pole kwa yote yaliyokupata kwa ajili yangu.Watu hawa siwafahamu lakini ninaamini lazima watakuwa wametumwa na mahasimu wangu wa biashara.Kuna watu ninahasimiana nao katika mambo yetu ya biaahsra na ndiyo hao wananichunguza na kwa taarifa ulizowapa wamepata kitu kikubwa sana" "I'm sory Frank sikuwa na namna nyingine ya kufanya.Kama nisingewaeleza ukweli wangeweza kuniua wale jamaa.Nisamehe sana Frank sikujua chochote" "Usijali Irene hilo si kosa lako lakini watu hawa sintawaruhusu waendelee na kutaka kunihujmu.Nitawaonyesha kazi.Unaweza kunieleza wasifu wa watu hao? Mmoja alikuwa na mwili uliojengeka na ndiye alikuwa dereva wa gari na mwingne alikuwa mwembamba wastani na mrefu kidogo ila alikuwa na ndevu nyingi na alikuwa amevaa kofia na miwani.Huyu ndiye aliyekuwa ananitesa" akasema Irene na Frank akaitafuta picha ya mcheza mpira wa kikapu wa Marekani Stephe curry na kumuonyesha Irene "Mmoja wao anaweza kufanana na huyu jamaa pichani? "Hapana hakuna anayefanana naye.Kidogo labda yule mwenye madevu mengi anaweza kulingana naye mwili lakini sura hawafanani kabisa" "Who are they?!! akajiuliza Frank "Frank mimi na wewe ni watu tunaoheshimiana na kuaminiana sana.Nataka nikuombe fanya kila uwezavyo kuwatafuta wale jamaakwani wanaonekana ni watu hatari na wanakufahamu vyema.Kama wameweza kupata hadi nyaraka zile za mizigo basi tayari wanafahamu mambo yako mengi.Watu hawa ni hatari na si wa kuwapuuza.Please don't mess with them.Kama unao uwezo wa kuwadhibiti fanya hivyo angalia bado mapema watu hawa wanakusaka kila kona" akasema Irene "Ahsnate sana Irene kwa taarifa hizi.Hapa nyumbani kwako hakuna kamera za ulinzi? "Hakuna kamera hapa nyumbani" "Sawa.Nitakufungia kamera za ulinzi hapa nyumbani na kukuwekea walinzi wa kukulinda wewe na famlia yako.Nakuahidi watu wale hawatarejea tena hapa kukutisha kwani nitawasaka kila kona na kuhakikisha nimewapata.Pole sana Irene ila nakuomba uwe muangalifu sana kuanzia sasa" akasema Frank huku akiinuka "Irene inanilazimu kuondoka natakiwa kuanza kuwasaka hawa jamaa haraka sana kwani ni watu hatari mno kwangu.Kama kuna hatari yoyote unahisi nijulishe hataka sana" akasema Frank akaagana na Irene akaelekea katika gari lake "Aaaaaghhh!!! akapiga ukelele wa hasira Frank huku akiupiga usukani kama kawaida yake awapo na hasira "What's happening to me?Why now?? akajiuliza na kuwasha gari akaondoka "Yote haya yaliyotokea na yanayoendelea kutokea yamesabishwa na Graca.Kama asingeiba kompyuta yangu na kuanza kushirikiana na akina Elvis haya yote yasingekuwepo.Mpaka hapa nina uhakika kwamba watu hawa wanaoendelea kunifuatilia ni mtandao wa Elvis.Inawezekana Elvis alikuwa anashirikiana na wenzake katika kunichunguza na hata baada ya yeye kufa hao wenzake wanaendelea na uchunguzi wao.Ninawafahamu hawa jamaa hawatalala hadi wahakikishe wamenichunguza na kunifahamu kiundani.Mpaka sasa tayari wamefahamu kuhusiana na biashara ya silaha na kila uchao wanazidi kunichiba zaidi wakitafuta ushahidi zaidi.I wont let them go far.Hapa walipofika panatosha sana" akawaza "Wanasema watoto ni baraka kutoka kwa Mungu lakini kwangu imekuwa tofauti si baraka tena bali ni laana.Graca ni laana kwangu na amenisababishia matatizo makubwa.Nitahakikisha ninamsaka na kumtia mikononi na ninaapa nitamkata kiungo kimoja baada ya kingine.Nitampa mateso makali ambayo hajawahi kuyashuhudia" akawaza na kusimamisha gari pembeni akachukua simu na kumpigia Elizabeth "Frank unasemaje?akauliza Elizabeth baada ya kuipokea simu "Habari yako madam Elizabeth?akauliza Frank "Frank nilikukanya usinipigie simu nilikuwa na maana yangu.Kwa nini umepuuza agizo langu? "Madam kuna jambo limejitokeza I need to talk to you"akasema Frank.Elizabeth akasikika akivuta pumzi ndefu "Jambo gani limetokea? "Madam siwezi kukueleza simuni.Naomba nije nikuone tafadhali" akasema Frank na Elizabeth akamruhusu aende nyumbani kwake Kwa hapa lilipofika hili suala siwezi kulikabili peke yangu,ninahitaji msaada kutoka kwa Elizabeth.Hili suala limekwisha kuwa kubwa na ili kulimaliza nguvu kubwa inahitajika" akawaza Frank akampigia simu Obi "Mmekwisha anza kumtesa Vicky?Amefunguka lolote? "Bado hatujaanza mkuu,tunashughulikia namna ya kuihifadhi miili ya wenzetu ndipo tuanze lile zoezi la Vicky" "C'mon Obi !! fanya haraka sana uanze kumuhoji huyo mwanamke.Hali si nzuri hata kidogo.Ikiwezekana waachie vijana wako waendelee na zoezi la kuwahifadhi hao wenzenu na wewe ushughulike na suala la Vicky.Nataka nitakapopiga tena simu nikute tayari kuna taarifa umezipata kutoka kwa Vicky!! Mkuu hawa waliofariki mimi ndiye kiongozi wao hivyo lazima nishiriki hadi mwisho kuwahifadhi.Siwezi kuliacha jambo hili kwa mtu mwinvine.Nitakapomaliza nitaifanya kazi yako lakini kama unaona ninachelewa unaweza ukatafuta watu wengine wakakusaidia" Frank akatafakari na kusema "Samahani Obi,kichwa changu kimevurugika kabisa kwa sasa kwani mambo mengi mazito yananizunguka.Endelea na taratibu zako ila nakuomba ujitahidi ufanye kila linalowezekana kumuhoji Vicky kwani ana taarifa muhimu ninazozihitaji mno" "Sawa mkuu" akajibu Obi na kukata simu *************** Flaviana beauty salon ndipo mahala Juliana na Steve walipanga wakutane.Alifika katika maegesho ya saluni hii kubwa akashuka na kwenda katika duka lililokuwa pembeni akanunua pakiti za Chokolate na kurejea garini akaendelea kumsubiri Steve.Mara simu yake ikaita alikuwa ni Steve "Hallow Steve" "Juliana mimi tayari nimefika hapa mahala tulikopanga tukutane.Wewe uko wapi? "Mimi tayari nimefika kama ronbo saa iliyopita." akasema Juliana "Ok good.Usishuke garini nielekeze gari lako lilipo nitakufuata" akasema Steve na Juliana akamuelekeza aina ya gari lake na kukata simu Elvis na Steven wakafika katika maegesho.Steve akaweka sikioni kifaa cha kuwawezesha kuwasiliana "Testing one two three,one two three..." akasema Steve akijaribu kifaa kile kama kinafanya kazi "Good lucky brother" akasema Elvis wakati Steve akishuka na kuelekea katika gari la Juliana.Elvis alibaki garini akiangalia kila kilichokuwa kinaendelea pale.Alitaka kuhakiki usalama wa Steve. Steve alilitambua gari la Juliana akafungua mlango na kuingia ndani. "Habari ya mchana Steve" akasema Juliana huku akimpatia Steve pakiti ya chocolate Steve akatabasamu "Samahani sana Juliana nimekuvurugia ratiba zako mchana huu" akasema SteveUsijali Steve.Tunaendelea na maandalizi ya mazishi ya baba hivyo sikuwa na kazi kubwa sana nyumbani" "Ahsante kwa kufika.Kuna jambo tumelipata ambalo tunahitaji msaada wako" "Mimi niko tayari kutoa kila aina ya msaada muda wowote mkihitaji hivyo msisite kila pale mtakapohitaji msaada wangu" "Thank you" akasema Steve halafu akaitoa simu yake ya mkononi na kufungua sehemu ya kuifadhi picha "Nataka uzitambue picha hizi mbili"akasema Steve na kumpatia simu Juliana ambaye alitabasamu na kusema "Huyu ni mama yangu"akasema Juliana "Are you sure? "Yes I'm sure.Huyu ni mama" Steve mwambie akuthibitishie kwa mara nyingine kama kweli huyo ni mama yake" Elvis aliyekuwa anafuatilia mazungumzo ya Steve na Juliana akamuelekeza Steve bila Juliana kujua "Hii ni picha ya kwanza ambayo ulitutumia na hii ni picha ya pili ambayo tumeipata sisi.Nataka kwa mara nyingine tena unithibitishie kwamba huyu ni mama yako" akasema Steve "Steve mbona huniamini?Huyu ni mama yangu.Ninamfahamu kuliko ninyi hivyo niamini ninaposema kwamba huyu ni mama yangu japo kuna utofauti mdogo katika picha hizi mbili lakini amini huyu ni mama" 'Thank you so much" akasema Steve na kuiweka simu mfukoni Nini kinaendelea?Kuna chochote mmekipata katika uchunguzi wenu?akauliza Juliana "Ndiyo kuna jambo tumelipata.Tumegundua kwamba mama yako anamiliki kampuni inaitwa McLorien iliyosajiliwa nchni marekani na anatumia jina la Shanon Blank.Unaifahamu kampuni hii? "Mc What? akauliza Juliana "McLorien"akajibu Steve "Hapana siifahamu hiyo kampuni.Ni mara yangu ya kwanza ninasikia kwamba mama anamiliki kampuni hiyo.Ninafahamu ana biashara zake nchini marekani na anafanya kwa ubia na mtu mmoja anaitwa Joe Gregory.Niliwahi kusikia kwamba wanataka kuanzisha biashara ya mitumba kutoka Marekani na kuiuza katika nchi za Afrika lakini sifahamu chochote kuhusiana na kampuni hiyo ya McLorien." "Joe Gregory? akauliza tena kwa sauti ili Elvis aweze kusikia vyema "Ndiyo anaitwa Joe Gregory.Huyu ninamfahamu ni tajiri na inasemekana ana makampuni kadhaa nchini Marekani na ndiye mshirika mkubwa wa mama katika biashara nchini Marekani" akasema Juliana. "Jina halisi la mama yako ni nani? akauliza Steve "Mimi ninamfahamu kwa jina la Elizabeth"akajibu Juliana "Hili jina Shanon Blank kalitoa wapi?Kwa nini asitumie jina lake halisi la Elizabeth? akauliza Steve "Hata mimi ninashangaa.Kama nilivyowaeleza awali kwamba mama anajihusisha na mambo ambayo si mazuri ndiyo maana nikawaomba mnisaidie kumchunguza" Tunaendelea kumchunguza ila na wewe tunakuomba utusaidie jambo moja" "Sema chochote Steve mmi niko tayari kuwasaidia" "Tunataka kulifahamu jina halisi la mama yako.Tusaidie kuchunguza kwa nini hatumii jina lake halisi na je ana majina mengine tofauti na hili la Shanon Blank?Unaweza kutusaidia kwa hilo? "Bila shaka.Kuna mtu mmoja ambaye naamini anaweza akanipa taarifa zote za mama.Huyu ni Robert ambaye ni mlinzi wa mama na ni mtu ambaye mama anamuamini mno.Siri zake nyingi huyu anazifahamu" "Unadhani anaweza kukubali kukueleza siri za mama yako? "Sina hakika sana lakini ngoja nijaribu kwani huyu jamaa amekuwa ananitaka sana kimapenzi lakini sijawahi kumkubalia.Nitamwambia kwamba nimekubali ombi lake na nitamdanganya kwamba atakapokuja Tanzania wakati wakileta maiti ya baba nitampa anachokihitaji"akasema Juliana "Muda gani nitegemee jibu ? "Nitazungumza naye na atakachonieleza nitakupa jibu" "Ahsante sana Juliana kwa ushirikiano wako mkubwa" "Muda wowote mimi niko tayari kutoa kila aina ya msaada kwani nataka watu hawa walioiandama familia yetu wajulikane na wafikishwe katika mkono wa sheria" "Steve muulize kuhusu Patricia" Elvis akamwambia Steve "Nakuhakikishia Juliana kwamba wote walioshiriki katika mauaji hayo siku zao zinahesabika.By the way how's Patricia?Patricia anaendelea vyema.She's deeply hurt but she's very strong.Anajitahidi kwa kila namna awezavyo kuweza kukabiliana na ukweli kuwa Elvis hayupo tena.Ni jeraha kubwa amelipata ambalo litachukua muda kupona lakini ninaamini siku moja litapona na maisha yataendelea kama kawaida.Sisi tulio karibu naye tunajitahidi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kumsaidia ili aweze kukivuka kipindi hiki kigumu kwake.She'll be fine.Halafu kabla sijasahau leo Patricia atahama pale nyumbani anahamia ikulu.Rais na mke wake wamemuomba akaishi nao hadi hapo atakapokuwa tayari kuishi mwenyewe.Patricia ana nyota ya kupendwa na watu.Rais na mke wake wanampenda na wanamchukulia kama sehemu ya familia yao" akasema Juliana "Juliana ahsante sana kwa muda wako.Tutaendelea kuwasiliana.Usiache kunijulisha tafadhali majibu utakayoyapata" akasema Steve na kushuka garini akarejea katika gari lao "Nadhani umesikia kila kitu tulichozungumza na Juliana"akasema Steve "I heard everything.." akasema Elvis huku akiwa ameeleza macho yake katika gari moja jeusi 'Unaliona lile gari jeusi karibu na gari la Juliana? akauliza Elvis na wakati huo Juliana alikuwa anaondoka "NImeliona.Kuna nini? "Ninahisi gari lile linamfuata Juliana.Nimelichunguza kuna mtu yumo mle ndani na wakati wewe unazungumza na Juliana alikuwa anafungua dirisha na kutoa kichwa anachungulia na kuna wakati akashuka akajifanya anatengene......."akanyamaza Elvis baada ya gari lile nalo kuanza kondoka baada ya Juliana kuwasha gari na kuanza kuondoka "Juliana anaondoka naye anaondoka.Yule jamaa lazima anamfuatilia" akasema Elvis "Twende tumfuate tumjue ni nani? "Au ni mlinzi wa Juliana?akauliza Steve "Mpigie Juliana muulize kama ana walinzi"akasema Elvis na Steve akampigia simu Juliana "Hallo Juliana samahani kwa usumbufu.Ninataka kufahamu jambo moja je unao walinzi wanaokulinda kile sehemu uendako?akauliza Walinzi?akauliza Juliana na kucheka kidogo "Sina walinzi,mlinzi wangu pekee ni Mungu" "Ahsante sana."akajibu Steve na kukata simu "Juliana anadai hana walinzi" "Kama si mlinzi wake basi tufanye zoezi moja dogo tupate uhakika kama kweli anamfuatilia Juliana ama vipi.Mwambie Juliana aingie barabara ya Ndovu" akasema Elvis na Steve akampigia simu Juliana akamtaka aingie barabara ya Ndovu.Alipokata kuingia barabara ya ndovu lile gari nalo likakata na kuendelea kumfuata "Bado anamfuata.Mwambie aende moja moja Uchumi supermarket" akasema Elvis na Steve akampa maelekezo Juliana http://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Steve nini kinaendelea?akauliza Juliana kwa wasi wasi "Usiwe na wasi wasi Juliana ninataka kuhakikisha kuwa uko salama"akasema Steve na kukata simu Juliana akafuata maelekezo aliyopewa hadi alipofika Uchumi supermarket akaingia na kwenda katika maegesho lile gari nalo likakata kona na kuingia hapo supermarket "Mpaka hapa tuna uhakika yule jamaa anamfuatilia Juliana" akasema Elvis "Nimefika tayari.Nifanye nini?akauliza Juliana "Shuka ingia ndani kununua kitu chochote" akasema Steve na Juliana akashuka akaingia ndani ya supermarket.Yule jamaa naye akafungua mlango akashuka akajifanya anakwenda kununua maji halafu akarejea garini. "It's our chance.Let's go get him" akasema Elvis na wote wakashuka wakatembea kwa tahadhari kulifuata lile gari.Elvis akagonga kioo cha dirisha na yule jamaa aliyekuwamo mle ndani akashusha kioo na wakati huo huo Steve akafungua mlango na kuingia ndani kwa kasi ya aina yake akamtolea bastora "Shhh!!! akamfanyia ishara asitoe ukelele "Shuka taratibu nifuate" akasema Elvis na yule jamaa akashuka na kuongozana na Elvis katika gari lao.Steve akabaki katika gari la yule jamaa akipekua kama kuna kitu chochote cha kumfaa halafu akatoka na kurejea garini,wakawasha gari na kuondoka "Tell Juliana to go home" akasema Elvis na Steve akampigia simu Juliana Juliana you are free to go home now" akasema Steve "Steve kuna tatizo gani? "Tutazungumza baadae ila kwa sasa unaweza kwenda nyumbani" akasema Steve na kukata simu.Yule jamaa alikuwa amekaa kiti cha nyuma na Elvis aliyekuwa anaichezea bastora yake.Ndani ya muda mfupi tayari alikuwa ameloa jasho "Jamani mnanipeleka wapi?Ninyi ni akina nani?akauliza lakini hakuna aliyemjibu.Steve aliyekuwa katika usukani akamrushia Elvis simu ya yule jamaa akaifungua na kuikagua akakutana na picha ambazo zilimstua kidogo.Juliana akiwa na Patricia na Meshack Jumbo. "Kwa nini unamfuatilia Juliana?Nani kakutuma umfuatilie?akauliza Elvis Simfahamu Juliana" akasema yule jamaa.Elvis akamnasa kibao kikali halafu akamuonyeha picha ya Juliana akiwa na Meshack Jumbo na Patricia "Hii picha umeitoa wapi?Nani kakutuma umpige picha Juliana? Yule jamaa akabaki kimya "Usiponijibu utakuwa ni mwisho wako leo!! akasema Elvis huku akimtazama yule jamaa kwa macho makali "Steve naomba zana zangu" akasema Elvis na Steve akamrushia kiboksi kidogo chenye vifaa akatoa koleo dogo na kukibana kidole cha mwisho cha yule cha jamaa kwa nguvu akapiga kelele kubwa. "Nani kakutuma umfuatlie Juliana? akauliza tena Elvis kwa ukali lakini yule jamaa hakujibu This is not working.Ngoja nikufundishe adabu.Ninawapenda sana watu kama ninyi" akasema Elvis halafu akamshika yule jamaa mikono na kumfunga kwa kamba halafu kwa kutumia ile kolea akaishika korodani na kuiminya.Yule jamaa akapiga kelele kubwa "Ni madam!!...akasema na Elvis akamuachia "Nani kakutuma umfuatilie Juliana? akauliza Elvis "Ni madam Elizabeth" "Elizabeth ni nani? "Ni mama yake Juliana.Alinitaka nimfuatilie Juliana kila anakokwenda na nimpige picha kila anayekutana naye" akasema yule jamaa. "Lini umeanza kumfuatilia? "NImeanza jana"akasema yule jamaa.Elvis akamtazama na kusema Ninakupa onyo kwamba kuanzia sasa acha kumfuatilia Juliana.Safari hii nitakuacha hai lakini nikigundua kwamba unaendelea na mchezo wako wa kumfuatilia nitakuondoa uume wako.Umenisikia!! akauliza Elvis huku akimsindikiza na kofi kali "Nimekusikia kaka" "Good.Usimweleze chochote huyo tajiri wako anayekutuma umfuatilie Juliana kama umekutana na sisi.Ukithubutu kufanya hivyo tutajua na tutakutafuta na kukuua.JIna lako nani? "Duma" "Duma nadhani tumeelewana" "Nimekuelewa kaka sintarudia tena" akasema Duma.Elvis akamtaka Steve asimamishe gari na kumtaka Duma ashuke.Alikuwa katika maumivu makali sana hivyo mara tu aliposhuka garini akajitupa katika nyasi pembeni ya barabara na akina Steve wakaendelea na safari yao "Elizabeth tayari ameanza kuhisi kitu kuhusu Juliana na ndiyo maana ameweka mtu wa kumfuatilia kwa bahati mbaya mtu mwenyewe aliyepewa kazi hii hana ujuzi wowote wa kumfuatilia mtu.Nimemuonea huruma yule kijana ni njaa tu ndiyo inawapelekea wakafanya kazi za namna hii" "Si njaa Elvis ni uvivu.Ziko fursa nyingi ambazo wangeweza kuzitumia kujitengeneza maisha mazuri lakini wanapenda mteremko"akasema Steve "Hata hivyo ameipata tamu yake na hatathubutu tena kumfuatilia Juliana.By the way nimefurahi kusikia Patricia anahamia ikulu leo.Ni muhimu sana kuondoka pale kwa akina Juliana.Tuachane na hilo,turudi katika kazi.Picha inaendelea kujitengeneza na sasa amejitokeza Elizabeth ambaye bado hatufahamu jina lake halisi ni nani.Huyu mama kwa jina lolote lile analolitumia tayari tuna uhakika kuwa anahusiana na Frank na anahusika pia katika biashara ya silaha kwani ndiye aliyekuwa anawasiliana na Patrice. Tunaanza kupata picha mtandao huu ulivyo mkubwa lakini pamoja na haya yote tuliyoyapata we have to dig deeper.Lazima tuutafute mtandao wote na kuusafisha.Tutachimba hadi ule mzizi wa mwisho hata kama ni mdogo au mkubwa kiasi gani.Narudia tena kuweka ahadi kwamba hakuna mwenye kuhusika na mtandao huu atabaki salama" akasema Elvis "Itabidi nizungumze na Juliana nimweleze awe makini sana kwa sasa kwani mama yake tayari ameanza kumfuatilia.Amekwisha anza kumtilia shaka na hasa baada ya kutumiwa picha Juliana na Patricia wakiwa na Meshack Jumbo" akasema Steve "Kwa picha ilivyo inaonyesha huyu Elizabeth au Shanon ndiye kiongozi au anayo nafasi kubwa katika mtandao huu wa kuuza silaha.Vile vile kuna mtu wa tatu amejitokeza hapa ambaye Juliana amemtaja Joe Gregory.Huyu naye kama ni mshirika wake lazima tumfanyie uchunguzi inawezekana naye akawa anahusika pia katika biashara hii ya silaha.Vile vile kuna huyu mtu naitwa Patrice lazima naye tumfahamu kwani huyu aidha ni mmoja wa viongozi katika kikundi hiki cha waasi au ni kiungo baina ya waasi na akina Frank.Tukimpata huyu tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana" akasema Elvis.Waliendelea na safari yao huku wakijadiliana mambo mbalimbali hadi walipofika katika makazi yao. "Mambo yanakwendaje hapa? akauliza Elvis "Hapa kila kitu kinakwenda vyema.Nashukuru nimerejea salama" akasema Omola "Mmemtazama Winnie anaendeleaje? "Hakuna aliyekwenda huko kumtazama toka mlipoondoka" akajibu Graca na Elvis akaenda katika chumba alimokuwa amelazwa Winnie akafungua mlango na kumkuta Winnie bado amelala,akarejea sebuleni "bado amelala ila anaendelea vyema." akasema Elvis na kuketi sofani "Kuna lolote mmefanikiwa kulipata kutoka kwa makamu wa rais?akauliza Ndiyo kuna jambo tumelipata.Graca amenisaidia sana kuweza kufahamu maongezi yaliyorekodiwa na ile programu niliyoiweka katika simu ya makamu wa rais.Kwa mujibu wa Graca mengi ni mazungumzo ya kikazi lakini tumefanikiwa kunasa mazungumzo ya simu kati ya makamu wa rais na mtu aliyemtaja kwa jina la David" akasema Omola na kubonyeza rekodi ile ya mazungumzo ya Dr Shafi "Hallow David" akasema Dr Shaf "Dr Shafi habari yako.Vipi mbona sauti yako hitoki vizuri leo? "Nimepatwa na mafua ya ghafla ila tayari nimepata dawa na ninaendelea na kazi zangu.Kuna taarifa zozote mpya? "Nimetaka tu kukujulia hali na kukujulisha kuwa leo ndiyo mambo yanaanza rasmi.Maandaliz ya mkutano yanaendelea na kila kitu kimekamilika.Dr Makwa ninaye hapa nyumbani kwangu toka jana na viongozi wengine wote wa vyama vya siasa wako katika sehemu zao wamejificha wakisubiri muda ufike ili wajitokeze na mambo yaanze rasmi.Dr Shafi nitakuwa nikikujulkisha kila hatua tunayopiga ninachokusisitiza tu usiwe na wasiwasi kila kitu kimepangwa vizuri na kila jambo litakwenda kama vile tunavyokusudia" "Hizo ni taarifa njema sana David.Mimi sina wasiwasi nawe hata kidogo kwani najua mahala ulipo hapaharibiki kitu.Endelea kunijulisha kila kitu kinavyoendelea ila nakushauri umakini mkubwa unatakiwa hasa katika hatua hii.Polisi wanawawinda sana hawa wanasiasa na endapo watafanikiwa kumkamata hata mmoja wao basi wanaweza wakamtesa na akaeleza kwamba wewe ndiye uliyekuwa nyuma ya mpango huu wa maandamano na vurugu.Ikifika hapo kila kitu kitakuwa kimeharibika hivyo viongozi hawa wa siasa wawe makini mno" "Hilo nimekwisha liona na nimezungumza nao na tumewekeana mikakati na kutokana na mipango yetu ilivyoandaliwa hakutakuwa na tatizo lolote.Nitawasiliana nawe tena jioni ya leo kukujulisha mambo yanavyokwenda" "Nawatakia kila la heri na mafanikio" akasema Dr Shafi na kukata simu Elvis akavuta pumzi ndefu na kurudia kusikiliza tena rekodi ile kwa mara ya pili. Dr Shafi anazungumza na David kuhusiana na mkutano ulioandaliwa na viongozi wa vyama vya siasa.David anasikika akimtaja Dr Makwa kuwa amelala nyumbani kwake akiogopa kukamatwa na polisi.Dr Makwa ni kiongozi wa chama kikubwa cha siasa hapa nchini."akasema Elvis na kunyamaza kidogo halafu akasema "Katika taarifa ya habari leo asubuhi nimemsikia mkuu wa jeshi la polisi nchini akitoa onyo kuhusu mkutano wa hadhara ulioandaliwa na vyama vya siasa uliopigwa marufuku na jeshi la polisi.Baada ya kuyasikia mazungumzo haya ya Dr Shafi na David ninashawishika kuamini kwamba Dr Shafi na huyo David wako nyuma ya huu mkutano ulioandaliwa leo na wanasiasa wa vyama vya upinzani.Kinachonishangaza ni kwamba Dr Shafi yuko katika chama tawala iweje ashirikiane na wakuu wa vyama pinzani kwa siri?Kuna nini kinaendelea hapa?David ni nani? akauliza Elvis "Jamani kuna jambo linaendelea hapa na taa nyekundu imeniwakia tayari.Japo tuna masuala mengi makubwa yanatukabili lakini tusilipuuze suala hili.Wakati tunaendelea kumchunguza makamu wa rais kuhusiana na uhusika wake katika mtandao wa silaha tuendelee pia kumchunguza mahusiano yake na wanasiasa wa vyama pinzani tujue kuna kitu gani kinaendelea kati yao?Mazungumzo haya tuliyoyasikia yanaashiria kuna jambo ambalo si zuri"akasema Elvis "Elvis play that record again" akasema Steve na Elvis akaicheza tena ile rekodi.Steve akasikiliza kwa makini Play again" akasema na kuisikiliza tena "Kuna kitu umekigundua Steve?akauliza Elvis "Elvis kuna jambo ambalo sikuwa nimelitilia maanani sana lakini baada ya kusikia mazungumzo haya nimeanza kuliona kama lina maana" "Jambo gani? "Kwanza kabla ya yote naomba nipate hii sauti ya David.Tunahitaji kufahamu ni David yupi.Sauti hii si ngeni kwangu lakini tunahitaji kupata uhakika" "Hata mimi hii sauti si ngeni kwangu.Unahisi umewahi kuisikia mahala?akauliza Elvis "Elvis ninaomba dakika chache tutafahamu kuhusu sauti hii" akasema Steve na kuichukua simu yake ambayo tayari Omola alikwisha muwekeakipande cha sauti ya David.Akatoka nje na kumpigia simu Samira "Summer baby" akasema Steve baada ya Samira kupokea simu "Hello my love.Vipi maendeleo yako? "Ninaendelea vyema Samira.Ahsante sana kwa msaada wako mkubwa kwa kumpeleka Omola kwa makamu wa rais" "Usijali Steve.Muda wowote ukiwa na jambo lolote niko tayari kukusaidia.Vipi kuhusu kazi zako zinakwendaje? "Kazi zangu zinakwenda vyema ila ninahitaji msaada wako tena" "Sema Steve unahitaji msaada gani? "Kuna faili nakutumia lifungue halafu sikiliza sauti hiyo na kama utaweza kuitambua niambie ni sautiya nani?Tafadhali nisaidie sana katika hilo ni muhimu sana" "Sawa Steve" akajibu Samira na Steve akamtumia lile faili lenye sauti ya David.Baada ya dakika moja Samira akapiga simu "Umeisikia sauti hiyo?Unaweza kuitambua?akauliza Steve "Hii ni sauti ya David." "Are you sure?Steve akauliza "yes I'm sure.Kuna nini kwani?Hii rekodi umeitoa wapi?akauliza Samira akionekana kuwa na wasi wasi kidogo "Ahsante sana Samira kwa msaada wako huu mkubwa.Nitazungumza nawe baadae" akasema Steve na kukata simu akarejea sebuleni "Nimethibitisha sauti hii iliyokuwa inazungumza na makamu wa rais ni sauio ya waziri mkuu mstaafu David Sichoma" "Exactly! akasema Elvis "Sauti hii si ngeni kwangu na nilikuwa najiuliza ni wapi nimewahi kuisikia.David na makamu wa rais wako nyuma ya mkutano huu unaotarajiwa kufanyika leo na Dr Makwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani amelala nyumbani kwa David.Kuna kitu gani hawa jamaa wanakipanga dhidi ya serikali?Hainiingii akilini watu wakubwa kama hawa,makamu wa rais na waziri mkuu mstaafu washirikiane na viongozi hawa wa vyama vya siasa kuandaa mkutano wa hadhara.Ndugu zangu hapa kuna kitu kinachoendelea ambacho hatuna budi kukifahamu" akasema Elvis "Awali niliwaeleza kwamba kuna jambo ambalo sikuwa nimelitilia maanani lakini kwa sasa ninauona umuhimu wake" akasema Steve na kunyamaza akamtazama Elvis na kusema "Elvis sikuwa nimekueleza kuhusu suala hili kwani ni suala binafsi lakini kwa hapa tulipofika nalazimika kuweka wazi kila kitu" "Ni jambo gani hilo Steve? "Samira ana mahusiano na waziri mkuu mstaafu David Sichoma" "Wow ! akasema Elvis na wote wakawa kimya wakitazamana "Nilipotoka kizuizini nimewakuta wakiwa katika mahusiano na David ndiye anayemgharamia Samira kwa kila kitu.Kwa kuwa Samira ananipenda sana alinieleza ukweli kwamba yuko na David kwa sababu ya fedha zake na si kwa mapenzi.Nilimtaka Samira aachane na David ili mimi na yeye tuyaanze maisha mapya lakini akakataa kwa madai kwamba hawezi kuachana ghafla na David kwani amemuahidi mambo mengi.Kikubwa ambacho ninakiona kwa sasa kina umuhimu ni pale aliponiambia kwamba David ana mipango ya kuwa rais wa Tanzania na amemuahidi mambo mengi makubwa endapo atakuwa rais na ndiyo maana Samira hataki kuachana naye.Mazngumzo yake na makamu wa rais yamenifanya nione kauli hii ina umuhmu mkubwa kwetu" "Ahante Steve kwa jambo hilo.Kauli hiyo ni nzito sana.David ni waziri mkuu mstaafu amekwisha achana na mambo ya uongozi lakini kwa kauli hiyo anaonyesha kwamba bado ana mipango ya kutaka urais.Ataupataje huo urais?Hilo ni swali ambalo tunapaswa kujiuliza.Je anataka kuhama chama na kujiunga na chama cha upinzani na ndiyo maana anashirikiana nao?Kama ndiyo kwa nini basi asijitokeze na kutangaza wazi kukihama chama chake na kujiunga na upinzani?Kwa nini anaongoza harakari zake chini kwa chini na hataki ajulikane?akauliza Elvis "Elvis ninashauri wakati tunaendelea na suala la akina Frank basi tuendele pia kumchunguza David na hapa tunaweza kumtumia Samira kumchunguza kwani ni wapenzi na David hajui kama Samira ana mahusiano na mimi.Unaonaje suala hilo? "Ni wazo jema.Utazungumza na Samira uone kama atakubali kutusaidia kwa hilo" akasema Elvis "Ktu kingine ambacho tunapaswa kukumbuka ni kwamba makamu wa rais ndiye alitoa amri ya mimi kuuawa,na vile vile akatoa amri Pascal auawe na hata Vicky pia ni yeye aliyetoa amri auawe.Tunapaswa tufahamu kwa nini alitoa maelekezo watu hawa wauae?Bado nina imani Dr Shafi lazima atakuwa anahusiana na mtandao wa akina Frank kwani haya yote yalianza baada ya mimi kuipata kompyuta ya Frank na kufahamu kuhusu biashara ya silaha.Tutafute kitu kitakachotupa ushahidi kwamba Dr Shafi anahusiana na akina Frank" akasema Elvis "Kesho nitarejea tena kuendelea na mazungumzo naye na kumchunguza zaidi.Vile vile bado tunaendelea kufuatilia mazungumzo yake yote ya simu na kila baada ya nusu saa tutakuwa tunaangalia mazungumzo yaliyorekodiwa hivyo msiwe na wasi wasi tutapata kila tunachokihitaji" akasema Omola Ahsante Omola.Tuliweke hilo pembeni na tuendele na uchunguzi wetu.Kuna mtu amejitokeza anaitwa Joe Gregory.Kwa mujbu wa Juliana ni kwamba huyu ni mshirika mkubwa wa mama yake wa biashara nchini Marekani.Mchunguze huyu naye ili ufahamu ni mtu wa namna gani vle vile tuanze kumtafuta Patrice." "Nina ushauri"akasema Omola "Karibu" akasema Elvis "Nashauri kwa sasa tuelekeze nguvu katika kumchunguza Elizabeth au Shanon au vyovyote vile anavyojiita.Tunaweza kupata taarifa nyingi za kutusaidia kutoka kwake.Nitahitaji kuipata simu au kompyuta yake niifanyie uchunguzi na tutaweza kupata mambo mengi ya kutusaidia.Ninawashauri ndugu zangu tukitaka kumpata huyu Patrice na kumfahamu ni nani basi tuwekeze nguvu kubwa katika kumchunguza Elizabeth.Nina uhakika mkubwa lazima anawasiliana na Patrice" akasema Omola "Hilo ni wazo zuri japo tutakuwa tumemuweka Juliana katika hatari kubwa na hasa kwa wakati huu ambao mama yake tayari amekwisha anza kumtilia mashaka kufuatiwa kutumiwa picha akiwa na Meshack Jumbo" akasema Steve "Ni kweli yuko katika hatari lakini hatuna namna lazima atusaidie kuweza kumchunguza mama yake.Ninaamini atakubali kufanya hivyo kwani hata yeye anahitaji kumfahamu mama yake na mambo yake ya siri anayoyafanya.Naamini tukimuomba atakubali kutusaidia" akasema Elvis "Sawa Elvis.Nitazungumza naye" Nitalazimika kwenda nawe wakati unazungumza naye kuna mambo ambayo nitapenda kumuelekeza" akasema Omola "Vipi kuhusu Joe Gregory?Umekwisha anza kumchunguza? akauliza Elvis "Nimemtumia barua pepe rafiki yangu wa nchini Marekani anisaidie kupata taarifa zake.Atanipa majibu ndani ya muda mfupi " akajibu Omola "Guys msimame kidogo mpate chochote cha kuweka tumboni.Toka asubuhi mmekuwa mkifanya kazi na mmesahau kabisa kama miili yenu nayo inahitaji kuhudumiwa" akasema Graca aliyeingia pale sebuleni akiwa na sinia lenye mabakuli ya supu "You are so fast Graca" akasema Omola akichukua bakuli lake la supu na kila mmoja akachukua lake.Wakati wakiendelea kupata supu ukasikikamlio katika kompyuta ya Omola akaangalia na kusema "Majibu yamekuja" Omola akaifungua barua pepe ile akaisoma "Tumekipata tulichokuwa tunakihitaji" akasema Omola "Kwa mujibu wa taarifa nilizozipata kuhusu Joe Gregory ni kwamba huyu ni mwanajeshi mstaafu na kwa sasa anajishughulisha na biashara mbali mbali.Amewekeza katika biashara za migahawa,anamiliki pia meli kubwa za mizigo,kwa ujumla Joe ni mtu tajiri.Ukiwataja matajiri wa Marekani na Joe huwezi kukosa kumtaja" akasema Omola akameza mate na kuendelea "Masuala ya utajiri wake sisi hayatuhusu lakini kuna hili moja ambalo naamini linatuhusu sana sisi.Joe anamiliki kiwanza cha kutengeneza bunduki kubwa na ndogo.Katika kiwanda hicho anatengeneza bunduki za kawaida na hata zile za kivita.Kwa maelezo haya tayari tunapata jibu kwamba Elizabeth anapata silaha kutoka kwa Joe ambazo huja kuziuza kwa waasi.Inawezekana vile vile kwamba silaha nyingine zinakuja kufanyiwa majaribio kwa waasi ili kujua ubora wake" "Oh Ahsante Mungu" akasema Elvis "Picha inazidi kujiunganisha na muda si mrefu tutapata picha kamili nani na nani wamo katika mtandao huu wa biashara ya silaha.Nani wanafaidika kutokana na damu isiyo na hatia ya wananchi wa Congo inayomwagwa na waasi wanaouziwa silaha na mtandao huu wa akina Frank.Watu hawa tuliowafahamu si peke yao bado kuna wengine ambao lazima tuendelee kuwatafuta na kuwafahamu.Wote lazima walipe uovu wao.Huko waliko wafahamu kuwa siku zao zinahesabika.Kama alivyoshauri Omola nguvu kubwa kwa sasa tuielekeze katika kumchunguza Elizabeth ili tuweze kumfahamu huyu Patrice ni nani hasa yuko wapi na mahusiano yake na waasi wa Congo.Vile vile tuendelee kumchunguza makamu wa rais tujue kama naye anahuska katika mtandao huu.Wakati huo huo David naye aendelee kuchunguzwa kama tulivyokubaliana.Hatuhitaji kupoteza muda mpigie simu Juliana muulize kama amefanikiwa yale tuliyomuomba atusaidie na vile vile na umjulishe kuwa tunahitaji kuonana naye tena" akasema Elvis na Steve akampigia simu Juliana akamuomba waonane.Steve na Omola wakaingia garini wakaondoka kwenda kuonana na Juliana "Bado natafakari kwa nini David na Dr Shafi wahusike katika mkutano wa vyama vya siasa vya upinzani na kibaya zaidi ni kwamba licha ya kwamba mkutano huu umepigwa marufuku lakini bado wanaendelea kuufadhili ufanyike.Kuna kitu gani wanakitafuta hawa viongozi?Je wanataka kujiunga na vama vya upinzani?Kama ni hivyo kwa nini wasijiunge kwa uwazi kuliko kufadhili mikutano kama hii ambayo ni wazi itasababisha vurugu?Steve anadai kwamba David ana dhamira ya kuwania urais,je hizi ni harakati zake ameanza za kutaka kujirudisha katika siasa kwa kufadhili mkutano huu wa leo?akajiuliza Elvis akiwa sebuleni peke yake baada ya akina Steve kuondoka
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment