Search This Blog

Saturday 5 November 2022

I DIED TO SAVE THE PRESIDENT - 3

 





    Simulizi : I Died To Save The President

    Sehemu Ya Tatu (3)



    I DIED TO SAVE MY PRESIDENT





    No !! this is not true.You?!! akasema Pascal kwa mshangao midomo ikimtetemeka "It's true Pascal.It’s me Elvis.Mimi ni halisi na wala si mzimu kwa hiyo usiifanye akili yako ione kama vile uko ndotoni" akasema Elvis na kuinua glasi ya mvinyo iliyokuwa mezani akanywa "Nadhani sasa hauna wasi wasi tena.Mimi ni halisi kwani mzimu hauli wala kunywa lakini mimi nimekunywa mvinyo mbele yako" “You are dead !! akasema Pascal "No I'm not." akasema Elvis na uso wa Pascal ukaonekana kuloa jasho.Ghafla macho yake akayaelekeza mlangoni "Vic........" kabla hajamaliza sentensi yake mara risasi mfululilzo kutoka katika bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti zikamiminika kichwani kwa Pascal na kumuodoa uhai pale pale.Elvis na Steve kila mmoja akaruka upande wake kujinusuru.Vicky alisimama akiwa na bastora mkononi ikifuka moshi.Kwa haraka na kwa shabaha ya aina yake Elvis akaulenga mkono wa Vicky uliokuwa na bastora ikaanguka chini.Wakati Vicky akiwa chini akigugumia kwa maumvi makali Steve akaruka na kumuwahi akamnyooshea bastora .Elvis akaenda kumtazama Pascal tayari hakuwa na uhai.Kichwa chake kilifumuliwa kwa risasi. "Can he make it? Steve akauliza "No he's gone" akasema Elvis na kumfuata Vicky pale chini "What have you done?!! akauliza lakini Vicky hakujibu kitu.Alikuwa anagugumia kwa maumivu makali ya risasi "Kill me you bastard!! akasema kwa ukali. "We cant kill you.We need you” akasema Elvis na kwa haraka akalifungua sanduku alilokuja nalo lililokuwa na vifaa mbali mbali akachukua dawa na kuivuta katika bomba la sindano kisha akamchoma Vicky karibu na mahala alipopigwa risasi na kumfanya asihisi maumivu makali pamoja na kuzuia damu isiendelee kutoka. “Steve kila kitu kimeharibika we have to get out of here now lakini kabla hatujaondoka lazima tuhakikishe tumepaacha salama mahala hapa. Mlaze Pascal hapa mahala damu ya Vicky ilipomwagika ili zichanganyike halafu hakikisha hakuna mahala ulikoacha alama zako za vidole.Pangusa kila sehemu haraka haraka" akasema Elvis na kumuinua Vicky akampeleka bafuni akamuamuru aoage aondoe damu iliyotapakaa mwilini.Wakati Elvis na Vicky wakiwa bafuni Steve akaanza kufuta alama za vidole katika sehemu zote ambazo aliamini amezishika kwani hakuwa amevaa kitu chochte mkononi tofauti na Elvis aliyekuwa amevaa glovu.Baada ya kuoga na kujifuta damu Elvis akalifunga jeraha la Vicky halafu akamtaka avae koti la Steve ili jeraha lile la risasi lisionekane "We're going out.Utakuwa kimya na kufuata maelekezo yetu.You'll smile like nothing happened.Ukienda kinyume na sisi kwa namna yoyote ile you are finished.Kichwa chako nitakifumua kwa risasi kama ulivyomuua Pascal.Umenielewa !! akauliza Elvis kwa ukali "Nimekuelewa lakini naombeni mnipeleke hospitali " akasema Vicky.Elvis na Steve wakatazamana "Everything ok? Can we go now? Elvis akauliza "Tunaweza kuondoka.Kila kitu kiko sawa." akasema Steve wakazima taa na kutoka mle chumbani.Elvis alikuwa amemshika kiuno Vicky wakionekana kama wapenzi.Steve alikuwa nyuma yao hatua kadhaa akiangalia kwa makini kama kuna hatari yoyote nyuma yao.Walishuka kwa kutumia lifti halafu wakaingia katika ukumbi wa chakula na kutoka wakaelekea maegesho ya magari.Hakuna yeyote aliyewatilia shaka au kuwa na wasi wasi nao.Kwa upande wa Elvis ilikuwa vigumu kutambulikahasa kutokana na vitu bandia alivyokuwa amevaa na kuubadili kabisa mwonekano wake. Vicky akaingizwa katika gari la Elvis na kukaa kiti cha pembeni na kwa tahadhari mikono yake ikafungwa pingu zile alizokuwa amefungwa Pascal na kuondoka mahala pale huku Steve akiwa nyuma yao kuhakikisha wanakuwa salama.Baada ya kuingia barabarani Elvis akampigia simu Dr Philip na kumtaka wakutane nyumbani kwake haraka sana usiku ule kuna dharura imetokea halafu akampigia simu Meshack Jumbo na kumtaka pia afike nyumbani kwake usiku ule kuna jambo limetokea. Elvis akageuza shingo na kumtazama Vicky ambaye uso wake ulikuwa mkavu sana na hakuonyesha hata chembe ya wasi wasi kana kwamba hakuna kilichokuwa kimetokea muda mfupi uliopita "Who is this woman? Siamini kama ni kahaba kwa namna alivyoweza kuitumia silaha kwa wepesi ule.Hakuna kati yetu aliyekuwa na mawazo kama angeweza kufanya kitu kama kile na akaitumia fursa wakati sisi tukiwa tumeelekeza akili zetu kwa Pasal akachukua bastora na kumuua.Bastora ile aliitoa wapi? Ni ya kwake? Kwa nini akamuua Pascal? akajiuliza Elvis huku akiongeza mwendo wa gari Ukimtazama alivyo na kitendo alichokifanya hawaendani kabisa.Hakuna atakayeamini akiambiwa kwamba mwanamke huyu ametoka kutoa uhai wa mtu kikatili muda mfupi uliopita.Huyu ni mwanamke hatari na kuna mambo mengi tutayafahamu kupitia kwake.Lazima ipo sababu iliyopelekea akamuua Pascal.Huu ni mwanzo tutafahamu mambo mengi yaliyojificha.Nimekwisha weka ahadi kwamba hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe.Tutawaangusha wote waliomo katika mtandao haramu wa kuuza silaha kwa waasi wa Congo DRC.Je na huyu mwanamke naye ni mmoja wa watu waliomo katika mtandao huo? akajiuliza Elvis na kulipita gari lililokuwa mbele yake "Ninahisi hata huyu naye ni moja wao kwa sababu kwa mujibu wa barua pepe nilizozikuta katika kompyuta ya Frank,mtu anayejiita Deusdedith MM alitoa maelekezo kwamba kahaba huyu atumike katika mauaji ya kanali Norman.Kuna uwezekano mkubwa mwanamke huyu naye akawa ni mmoja wao au akawa ni muuaji anayetumiwa na watu hawa kuua kimya kimya.Inashangaza sana kahaba kuwa na utajiri mkubwa kama alionao huyu Vicky.Atatueleza kila kitu" akawaza Elvis na kujitazama tena Vicky ambaye alikuwa ameegemea kitini akionekana kupitiwa na kijiusingizi. Waliwasili katika makazi yao na Graca akawafungulia geti.Vicky akashushwa na kuingizwa katika moja wapo ya chumba kilichokuwa kimeandaliwa akalazwa kitandani na kufungwa pingu mkono wake wa kushoto na miguuni katika kitanda cha chuma. "Please take me to hospital" akasema Vicky "Hapa uko hospitali usihofu" akasema Elvis na kutoka mle chumbani akaufunga mlango "Elvis nimefurahi umerejea salama.Kila kitu kimekwenda vizuri? akauliza Graca Kila kitu kiko sawa Graca.Nenda chumbani ukapumzike sisi bado tunaendelea na kazi" akasema Elvis na Graca akaenda kupumzika chumbani kwake "Good job Steve" akasema Elvis huku akichukua glasi ya maji "Elvis kilichotokea pale ninaona kama filamu.Bado najaribu kutafakari lakini inaniwia vigumu kuamini kama kweli Vicky ndiye aliyefanya kitendo kile na kwa wepesi ule" akasema Steve "Ni kweli ni kitu ambacho kinashangaza sana.Hatukuwa tumetegemea kama Vicky angeweza kufanya kitendo cha namna ile na ndiyo maana hatukuwa tumeelekeza macho yetu kwake na akatumia mwanya huo kufanya alichokifanya.Swali ambalo tunapaswa tulitafutie jibu ni kwa nini amemuua Pascal?lazima ipo sababu iliyomfanya akamuua Pascal.Alifahamu kuwa tutamfanyia mahojiano Pascal na kuna mambo tutayafahamu hivyo akaamua kumuua ili tusiweze kumuhoji.Tumemkosa Pascal lakini tumempata mtu ambaye naamini ni muhimu sana atakayetusaidia kupata majibu ya maswali yetu"akasema Elvis "Mwanamke yule ni hatari sana.Angeweza hata kutumaliza sote" akasema Steve "Nahisi lengo lake lilikuwa hilo kutumaliza sote kwani bastora yake bado ilikuwa na risasi za kutosha na kama tusingekuwa makini angeweza kutumaliza na kutokomea zake.Siku zote nimekuwa nikikufundisha Steve usiwaamni sana wanawake hasa hawa wenye uzuri wa kimalaika.Wanaweza kuwa hatari kuliko hata shetani.Mtazame Vicky huwezi hata kuhisi kama amewahi kuigusa hata silaha lakini ndani ya sekunde chache ameweza kuutoa uhai wa mtu kikatili.Anaonekana ni mzoefu sana katika mambo……" Elvis akanyamaza baada ya kengele ya getini kulia Steve akaenda kwa tahadhari kubwa na kumkuta ni Dr Philip karibu sana Dr Philip" akasema Steve baada ya Philip kushuka garini "Nimeitika wito kwa haraka Elvis.Is everything ok here? akauliza Dr Philip baada ya kuingia ndani "Kazi imeanza Dr Philip na kuna mtu anahitaji huduma yako ya haraka amepigwa risasi mkononi" akasema Elvis na kumsimulia Dr Philip kilichotokea.Bila kupoteza muda Philip na Elvis wakaenda katika chumba alimo Vicky.Dr Philip akalitazama jeraha la Vicky kisha akaelekeza afunguliwe na baadhi ya vitu viandaliwe ili aweze kumfanyia upasuaji wa mkono.Meza kubwa ya chakula ikaletwa mle chumbani na kuwekwa godoro juu yake Vicky akalazwa na kuchomwa sindano ya kuondoa maumivu kisha Dr Philip akaanza kuufanyia upasuaji mkono ule kuondoa risasi.Lilikuwa ni zoezi la dakika thelathini halafu akashona jeraha na kumchoma Vicky Sindano nyingine.Wakiwa katika hatua za mwisho mlango ukafunguliwa na Meshack Jumbo akiwa na Steve wakaingia "Karibu sana mzee"akasema Elvis na kumuacha Dr Pilip na Steve mle chumbani akaongozana na Meshack kuelekea sebuleni "Elvis habari za hapa? mambo yanakwendaje? Nilikuwa na siku ndefu iliyokabiliwa na mambo mengi na ndiyo maana sikuweza tena kurejea hapa.Ila nilihudhuria kikao cha mwisho cha kuhitimisha msiba na..." "Tayarini ninafahamu kila kitu kilichotokea mzee.Doreen naye alikuwepo na amenieleza kila kitu"akasema Elvis "Vizuri kama tayari unazo taarifa.Alichokifanya Patricia kimesikitisha wengi.Inaonekana kuna mambo mengi aliyokuwa anafanyiwa na ndugu zako hadi akaamua kuchukua uamuzi ule mgumu .Tuachane na hayo ninataka kufahamu kinachoendelea hapa.Yule mwanamke mle ndani ni nani na kafanya nini? akauliza Meshack na Elvishttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ akamsimulia kila kitu kilichotokea usiku ule. "Elvis nimesisimkwa mwili kusikia kitu alichokifanya yule mwanamama.Mmekwisha mfahamu ni nani? "Hapana bado.kwanza tunamtibu kumuondoa risasi halafu tutamfanyia mahojiano tumfahamu ni nani ila lazima ni mtu hatari na ni mzoefu wa silaha kwa namna alivyoweza kumuua Pascal.Alimlenga risasi za kichwa na lengo likiwa ni kumuua kwa haraka ili tusiweze kupata chochote kutoka kwake" "Kwa mtazamo wangu mtandao wa hili genge ni mkubwa na kuna uwezekano hata huyu mwanamke naye akawa ni mmoja wao." akasema Meshack "Kwa mujibu wa barua pepe nilizozipata kutoka katika kompyuta ya Frank iliyoibwa na Graca,mtu anayeitwa Deusdedith MM anaonekana kutoa maelekezo mengi kwa Frank na ambaye anaonekana ndiye kiongozi wao alimuelekeza Frank amtumie Vicky katika mauaji ya kanali Norman kwa hiyo basi huyu mwanamke ni muhimu sana kwetu kwani anafahamu mambo mengi kuhusiana na mtandao huu .Ni yeye ambaye anamfahamu Deusdedith MM na atatuongoza kujua mahala alipo.Kuna uwezekano pia mwanamke huyu akawa ni muuaji anayetumiwa na akina Frank kuua watu kimya kimya kwa kutumia uzuri wake.Tutayafahamu haya yote ndani ya kipindi kifupi.Zama zake tayari zimekwisha" akasema Elvis "Mimi ngoja niwasiliane na makamu wa rais nimjulishe kwamba tayari Pascal ameuawa kama alivyoagiza" akasema Meshack na kumpigia simu makamu wa rais akamjulisha kwamba tayari Pascal ameuawa. "Kazi nzuri sana Meshack .Hizi ni taarifa njema kabisa.Kesho ule mzigo niliokuahidi utaletwa ofisini kwako" akasema makamu wa rais Dr Shafi na kuagana na Meshack "kwa nini makamu wa rais atake Pascal auawe? Elvis akaulizaHilo ni swali ambalo tunapaswa kulitafutia majibu.Alitaka wewe uuawe kwa sababu tayari ulikwishaingia katika anga za vigogo lakini huyu Pascal sijafahamu yeye alifanya nini hadi ikaamriwa auawe" akasema Meshack "Pascal na Frank ni marafiki wakubwa na bishara ya silaha wanaifanya kwa pamoja.Inawezekana makamu wa rais ni mmoja wa washirika wa mtandao huu na ndiyo maana kila pale maslahi yao yanapoguswa anatumia nguvu yake kuondoa vikwazo.Kama ni hivyo kwa nini Pascal atakiwe kuuawa wakati ni mwenzao. Je Frank anaweza kumtoa kafara swahiba wake mkubwa kama Pascal? kama jibu ni ndiyo basi lazima kuna jambo kuwa limetokea kati yao kwa maana hiyo lazima kumchunguza pia Frank kujua kama kuna jambo lolote limetokea kati yake na Pascal lakini kabla ya hayo yote lazima kwanza tuufahamu ukubwa wa mtandao huu na tuwajue wahusika wote kisha tuanze kuubomoa hatua kwa hatua.Hakuna atakayesalia hata mmoja" akasema Elvis. "Mara nyingi viongozi wakubwa kama hawa wanaposhiriki katika magenge kama haya yenye kufanya biashara haramu huwa hawajihusishi moja kwa moja bali uhusika wao huwa wa siri na inawezekana kukawa na ugumu wa kuthibitisha kama makamu wa rais ni mmoja wa wahusika.Inawezekana akawa si mmoja wao ila kuna kitu anakipata kutoka kwa wakuu wa mtandao huu na akawa akiwasaidia kutekeleza maagizo yao mbali mbali.Haya yote yanawezekana na yanatakiwa yachunguzwe." "Usemayo ni ya kweli kabisa mzee na tutayafanyia kazi ili kuufahamu ukweli.Ahadi yangu ni ile ile siku zote kwamba kaika suala hili hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe.Yeyote anayehusika katika biashara hii akiwa hapa nchini lazima atajulikana na hatua stahiki zitachukuliwa" akasema Elvis.









    Brigedia Frank kwaju akiwa katika chumba chake cha kusomea akipitia nyaraka zake mbali mbali mara simu yake ikaita na mpigaji alikuwa ni David,akaipokea haraka haraka "Mheshimia rais" akasema Frank kwa utani "Frank kuna taarifa yoyote umeipata kuhusu Pascal? "Pascal? Frank akauliza kwa mshangao "Ndiyo.Una taarifa zozote juu yake? Pascal nimewasiliana naye usiku huu na kumtaka afike nyumbani kwangu.Akiwa njiani kuja huku akaniambia kwamba atachelewa kidogo amepata dharura kuna mtu amempigia simu anahitaji kuonana naye.Niko hapa nyumbani nikimsubiri.Kuna taarifa gani kuhusu Pascal? akauliza Frank kwa wasi wasi "Nimepokea taarifa muda si mrefu kwamba Pasal ameuawa" Frank akakaa kimya kwa zaidi ya sekunde thalathini halafu akasema “David mimi nawe ni watu tunaoheshimiana mno na hatuna utani wa aina yoyote.Tafadhali usiingize utani katika suala kama hili" Huu si utani Frank.Ni kweli Pascal ameuawa usiku huu hotelini Samawati beach hotel" "Samawati beach hotel?!! Alikwenda kutafuta nini huko? "Hakuna anayefahamu alikuwa anafanya nini huko." "Ahsante kwa taarifa David.Ninaelekea huko sasa hivi nitakupigia simu baadae" akasema Frank na kukata simu.Alihisi miguu yake imeisha nguvu akavuta pumzi ndefu na kuketi kitini "Pascal is dead?!! akasema kwa sauti na kutikisa kichwa "Thats not true.Ngoja niende huko nikahakikishe kama taarifa hizi ni za kweli" akawaza Frank na kutoka kwa haraka sana akaingia garini akaondoka kwa kasi kuelekea Samawati beach hotel. "Nahisi taarifa hizi zinataka kunipa uchizi.Ni vipi endapo ni taarifa za kweli na Pascal akawa kweli amefariki? akajiuliza akiwa garini "Pascal nimezungumza naye usiku huu kweli anaweza kuwa amefariki dunia? kama kweli amekufa nani kamuua? akajiuliza Frank na kuchukua simu yake akazitafuta namba za simu za Pascal akampigia lakini simu yake haikuwa ikipatikana. "Simu yake haipatikani.Wasi wasi unazidi kunijaa yawezekana kweli akawa ameuawa.lakini ni nani ambaye amefanya kitendo kama hiki?Naomba jambo hili lisiwe kweli .Naomba walau awe amejeruhiwa ila awe mzima kwani ni mtu muhimu sana kwangu.Ni rafiki yangu mkubwa na ninamtegemea katika mambo mengi.Kama kweli amekufa litakuwa ni pigo kubwa mno kwangu" Kichwa cha Frank kilijaa mawazo mengi.Alijaribu tena na tena kupiga namba za simu za Pascal bila mafanikio. Aliwasili Samawati beach hotel na kukuta kundi kubwa la watu nje ya hoteli.Mapigo ya moyo yakaanza kwenda haraka haraka.Akasimamisha gari akashuka na kutembea haraka haraka akajiunga na kundi lile la watu waliokua nje ya hoteli.Kulikuwa na gari nne za askari polisi. "Ndugu kuna nini kimetokea hapa? Frank akamuuliza mtu mmoja aliyekaa pembeni yake "Kuna tukio la mauaji limetokea hapa hotelini.Nasikia kuna mtu ameuawa hapa ndani usiku huu" "Maiti yake imekwisha tolewa ? "Bado polisi wanaendelea na uchunguzi wao huko chumbani na watakapomaliza wataondoka na mwili wa marehemu.Binadamu wamekuwa katili sana siku hizi.Yaani mtu anathubutu kutoa uhai mapema namna hii?akasema yule jamaa Wauaji wenyewe wamekamatwa? akauliza "Sifahamu chochote,sisi tumekuja hapa kwa ajili ya kupata chakula na ndipo tukaona polisi wakiingia hapa kwa kasi na baada ya muda tukajulishwa kuwa kuna mauaji yamefanyika" akasema yule jamaa na kuzidi kummaliza nguvu Frank "David hawezi kunidanganya.lazima itakuwa kweli Pascal ameuawa.lakini nani amemuua na kwa nini? Hakuwahi kunieleza kama ana adui yeyote anayemuwinda amtoe uhai.Hata hivyo inaonekana tukio hili ni mpango uliondaliwa kitaalamu sana bila Pascal kufahamu .Alikuwa njini kuja kwangu lakini akanipigia simu na kuniambia kwamba atachelewa kidogo kuna mahala anakwenda kuna mtu anakwenda kumuona kwa dharura.Huyo mtu aliyempigia simu na kumtaka aje hapa hotelini waonane naamini ndiye aliyemuua au anahusika katika mpango wa mauaji" Frank akatolewa mawazoni baada ya polisi kutoka katika mlango mkubwa wakiwa wamebeba mwili wa mtu katika machela ukiwa umefunikwa shuka wakaupakia katika gari lao na kuondoka haraka eneo lile.Pamoja na ujasiri wake lakini Frank akajikuta akibubujikwa na machozi na kwa haraka akaondoka eneo lile akaenda katika gari lake na kuegemea usukani akilia. "Who ever did this must pay!!.Nitamsaka kila kona ya dunia hii lazima nimpate na alipe kwa kitendo hiki cha kikatili.Pascal alikuwa mtu muhimu mno kwangu na aliyemuua ameniondolea kiungo muhimu. Nani huyo amethubutu kufanya jambo hili ? Nitamsaka mtu huyo hadi nihakikishe nimempata na nitamondoa kiungo kimoja baada ya kingine.”Frank akazama katika mawazo mazito. "Kuna namna moja ya kumpata muuaji wa Pascal.Natakiwa kumfahamu mtu aliyempigia simu na kumtaka waonane hapa hotelini ni nani.Nikimfahamu huyo nitakuwa nimempata muuaji wa Pascal.Lazima nifanye haraka sana kumfahamu mtu huyo ili nijue sababu za kumuua." akawaza Frank na kuchukua simu yake. "Kuna wazo linanijia yawezekana labda ni wale wanasiasa akina Makwa ndio waliofanya hivi baada ya kuona anaanza kuwafuatilia.Lakini nitapata jibu muda mfupi ujao." akawaza huku akizitafuta namba fulani na kupiga,simu ikapokelewa "hallow Imelda habari yako.? akasema Frank "habari nzuri Frank umenisusa sana siku hizi.hata salamu hakunaSijakususa mrembo ni kutingwa na mambo mengi ndiyo maana nimeshindwa hata kuwasiliana nawe.Vipi maendeleo yako? "Ninaendelea vyema Frank" "Nafurahi kusikia hivyo.Vipi ile nyumba yako umekwisha maliza? “Nimefanikiwa kuezeka kwa sasa nahangaika na milango na madirisha" "Basi usihofu Imelda nitakusaidia kiasi cha pesa uweze kuipata hiyo milango na madirisha umalizie nyumba yako.Unahitaji shilingi ngapi? "ninataji kama milioni tano hivi" "Nitakutumia fedha hizo" "Real?! "Kweli kabisa.Sijawahi kukudanganya Imelda" "Nakuamini Frank .Ahadi zako ni za kweli kabisa. Nashukuru umetokea kwa wakati muafaka ambao nilikuwa nahitaji sana msaada" "Hili si tatizo kubwa kwangu ningekwisha kutatulia muda mrefu shida yako hutaki kututafuta watu kama sisi na unakimbilia kwa hawa vijana wasio na chochote.Tuachane na hayo kuna kitu naomba unisaidie.Uko kazini mida hii? "Ndiyo niko zamu ya usiku.Kitu gani unahitaji Frank? akauliza Imelda Nitakutumia namba fulani ambayo nataka unisaidie kutazama simu ya mwisho iliyompigia na kama kuna uwezekano nipate hata mazungumzo yao" "Mhh..!! akasema Imelda "Tafadhali Imelda ni muhimu sana kwangu.Nisaidie tafadhali" "Hilo ni suala gumu kidogo kwangu kwani nimehamishwa kitengo kwa hivi sasa lakini ngoja nione kama ninaweza kufanikiwa" akasema Imelda "Nashukuru sana Imelda ." akasema Frank na kukata simu halafu haraka haraka akamtumia Imelda kiasi che pesa alichokuwa anakihitaji na milimi moja ya ziada.Baada ya sekunde kadhaa toka atume pesa ile Imelda akampigia simu "Oh Frank sijui nikushukuruje kwa msaada huu mkubwa " “Usijali Imelda mambo hayo ni madogo sana kwetu.Ukiwa na shida yoyote tafadhali usisite kunitafuta nitakusaidia" "Ahsante sana Frank.Nitumie hiyo namba ili niifanyie kazi mara moja" akasema Imelda na kukata simu "Siku zote ukitaka mambo yaende haraka haraka penyeza rupia.Pesa haijawahi kushindwa sehemu yoyote ile" akawaza huku akiziandika namba za Pascal katika meseji na kumtumia Imelda halafu akawasha gari akaondoka kwa mwendo wa taratibu.Akachukua simu na kumpigia David "David ni kweli Pascal amefariki.Nimetoka eneo la tukio" "Nani lakini aliyefanya unyama huo?David akauliza "Bado haijulikani lakini huu ni mpango maalum uliopangwa kitaalamu.Uliponieleza kile alichokifanya kwa Dr Makwa nilimpigia simu na kumtaka tuonane ili nimkanye asirudie tena.Akiwa njiani kuja kwangu akapigiwa simu na mtu na kumtaka waonane akanipigia na kunijulisha kwamba atachelewa kidogo kuna mtu anakwenda kuonana naye na nilikuwa naendelea kumsubiri hadi uliponipigia simu na kunijulishakuwa ameuawa.Mtu huyo aliyemuita waonane naamini ndiye aliyemuua na tayari nimekwisha anza jitihada za kuhakikisha ninamfahamu haraka sana" akasema Frank "Frank jitahidi umfahamu mtu huyo ili tujue sababu ya kumuua Pascal.Lazima mtu huyo au kikundi hicho cha watu watakuwa na sababu fulani ya kumuua" akasema David na ukapita muda kidogo halafu Frank akauliza "David I want you to be honnest with me." akasema na kunyamaza "Honnest with you? David akashangaaKama unahusika katika kifo hiki cha Pascal tafadhali naomba unieleze mapema ili tuyamalize na nisiendelee na uchunguzi wangu" "Frank kitu gani kimekuingia kichwani hadi ukafikiria jambo kama hilo?Kwa nini unahisi naweza kuhusika katika kifo cha Pascal? "Nakumbuka jana katika maongezi yetu uliweka wazi chukio zako kwake na kutaka nimuondoe katika timu.Kwa maneno yale ya jana kuhusu Pascal yeyote angeweza kuhisi kuwa unahusika katika kifo chake cha ghafla" "Frank mimi na wewe tumefahamiana kwa muda mrefu na unafahamu kabisa kwamba siwezi kufanya jambo kama hilo.Ni kweli sikupendezwa na tabia ya Pascal na nikakuomba tumuondoe katika timu lakini ukagoma ukadai utazungumza naye.Sikuwa na tatizo tena baada ya kuniahidi kwamba utazungumza naye na kumuelewesha namna mambo yanavyokwenda.I wanted him out of the team but not to kill him.Kama ningehitaji kumuua ningefanya hivyo kimya kimya bila kukueleza.Nakuomba ndugu yangu ondoa hofu kabisa mimi siwezi kushiriki http://deusdeditmahunda.blogspot.com/katika jambo la namna hiyo.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kufanya uchunguzi na kubaini ni nani hasa aliyemuua?Mimi nitashirikiana nawe bega kwa bega hadi tumbaini muuaji" akasema David "Ahsante David na samahani kwa kukuhisi vibaya.Kwa sasa akili yangu naona haifanyi kazi vyema ila nitaendelea na uchunguzi wangu na nitakutaarifu itakachokibaini" "Ahsante sana.Nijulishe tafadhali kila hatua unayoichukua"akasema David na kukata simu "Sijui ninawaza wapi hadi nikamuhusisha David na kifo hiki cha Pascal.Yawezekana ni maneno ya jana aliyoyazungumza ndiyo yaliyonifanya niwe na hisia kwamba anaweza kuwa anahusika katika kifo hiki.Ngoja nisubiri taarifa kutoka kwa Imelda halafu nitajua wapi pa kuanzia.Mabalaa yanazidi kuniandama.Likitoka hili linakuja hili.Wakati ambao tuko karibu na mafanikio ndipo linaponikumba jambo baya kama hili.Dah ! imeniumiza sana.Aliyemuua Pascal ameniweza kweli kweli" akawaza Frank akiwa katika mwendo mkali na mara simu yake ikaita akatazama mpigaji alikuwa ni Imelda ikamlazimu kusimamisha gari pembeni ili aweze kuzungumza naye. "Imelda kuna lolote umefanikiwa kulipata? akauliza Frank “Ndiyo Frank.namba ile ya simu uliyonipa imesajiliwa kwa jina la Pascal Evarist Situmwa.Namba ya mwisho kumpigia ni namba iliyosajiliwa kwa jina la Victoria Boaz Tamile." Frank akashusha pumzi na baada ya sekunde chache akauliza "Imelda are you sure? "Ndiyo Frank nina uhakika .Nimepata hiyo kutoka katika kumbu kumbu zetu" "Ahsante sana."akasema Frank na kukata simu.Mapigo ya moyo wake yalianza kumuenda mbio "Vicky?!! Akajiuliza huku akitikisa kichwa "Namba ya Vicky ndiyo ya mwisho kumpigia Pascal kwa usiku huu.Kama ndivyo basi Vicky ndiye aliyemtaka Pascal waonane hotelini? Kwa nini alitakawakaonane hotelini?Kwa nini Pascal hakunieleza kama anakwenda kuonan ana Vicky hotelini? Frank akajiuliza maswali mengi haraka haraka na kuhisi kichwa kinagonga kwa nguvu. "Ninaanza kuhisi yawezekana Vicky akawa ameshiriki katika mpango wa kumuua Pascal japo wazo hili silipi uzito mkubwa .Kama ni hivyo kwa nini? akajiuliza na kuchukua simu akazitafuta namba za simu za Vicky akapiga lakini simu haikuwa ikipatikana.Akawasha gari na kuondoka "Mbona hili jambo linazidi kunichanganya? Ni kweli Vicky anaweza kushiriki katika mauaji ya Pascal?Kwa nini afanye hivyo wakati yeye pia ni mtu wetu wa karibu?Bado inaniwia ugumu kuamini kama kweli Vicky naye anashiriki katika mauaji haya.Ngoja niende hotelini kwake nitamsaka kila mahal usiku wa leo hadi nimpate.Vile vile kuna ulazima wa kuchunguza pia kule hotelini kama Vicky alionekana pale.Kama alikuwa pale basi hakutakuwa na shaka yeye ndiye aliyemuua au alishiriki katika mpango wa mauaji" akawaza Frank David alikuwa kama mtu aliyemwagiwa maji baada ya kuzungumza na Frank simuni.Aliingiwa na woga. "Hili suala naona litachukua sura mpya kwani huyu Frank akifanya uchunguzi wake anaweza akagundua kwamba ninahusika na kifo cha Pascal na mimi na yeye tutaingia katika uadui mkubwa.Tukifikia hatua hiyo kila kitu kitaharibika na tutakosa kila kitu.Sitaki hilo litokee kabla hatujachota yale matrilioni.I must do something" akawaza David na kuchukua simu akazitafuta namba za simu za Elizabetha na kumpigia.Simu iliita na kukatika bila kupokelewa,akapiga tena safari hii ikapokelewa "Unasemaje David usiku huu? akauliza Elizabeth "Madam Elizabeth samahani sana kwa kukusumbua usiku huu ambao naamini utakuwa umepumzikaNiko kwenye kikao kujadili mazishi ya mume wangu" "Madam ninahitaji msaada wako ndiyo maana nimekupigia" "Sema unahitaji msaada gani? "Kuna rafiki yake Frank anaitwa Pascal ambaye pia yupo katika timu ya peresheni mapinduzi.Kijana huyu anafanya kazi idara ya usalama wa taifa" "Ninamfahamu Pascal japo sijawahi kuonana naye ana kwa ana" "Huyo Pascal tulikuwa naye katika timu inayoandaa mapinduzi .Nilimuona ni kikwazo katika kufanikisha mipango yetu kwani haniamini na amekuwa anahoji kila jambo ninaloliwasilisha na asubuhi ya leo alimfata mmoja wa wanasiasa ambao tunawategemea sana katika kuanzisha vurugu na kumuhoji maswali.Sikufurahishwa na jambo hilo ikanilazimu nifanye mipango ya kumuondoa haraka sana.Usiku huu ameuawa lakini tayari Frank amekwisha anza kuwa na wasi wasi kwamba ninahusika na ameanza uchunguzi" "Unahitaji mimi nifanye nini? akauliza Elizabeth "You are the only one who can stop him.Mzuie asiendelee na uchunguzi wake" "Sawa nitafanya hivyo lakini nitahitaji maelezo ya kina kwa nini umefikia maamuzi ya kumuua huyo kijana ambaye alikuwa anamsaidia sana Frank katika biashara ya silaha” “I beg you madam Elizabeth do anything to stop him”akasema David “I’ll stop him” "Ahsante sana madam kwa msaada huo" "David wakati mwingine usikurupuke kumuua mtu bila kuwa na utafiti wa kutosha kama kifo chake hakina madhara baadae.Unadhani Frak akijua umehusika katika kifo cha rafiki yake atakuacha salama? Fikiri mara mbili mbili kabla hujafanya jambo" "Nimekuelewa madam" akasema David na simu ikakatwa Nilidhani kumshirikisha David katika mpango huu wa mapinduzi kungekuwa na manufaa makubwa kwetu lakini imekuwa ni mzigo mzito kuubeba" akawaza Elizabeth na kuzitafuta namba za simu za Frank akampigia. "Madam Elizabeth!! akasema Frank kwa mshangao.Hakuamini kuziona namba za Elizabeth. "Frank habari yako" "Habari nzuri madam.Mbona umekuja kimya kimya?Hakuna aliyeniambia kama unakuja Tanzania” "Nimekuja kwa dharura kwa ajili ya mazishi ya Deus" "Deus amefariki?!! akauliza Frank kwa mshangao Ndiyo" "Amefariki lini?mbona sijataarifiwa? "Hujataarifiwa kwa sababu ni masuala ya kifamilia zaidi na si lazima ujulishwe ila tuko katika maandalizi ya mazishi atazikwa hapa Tanzania" "Madam uko wapi mida hii nije nikuone ?Msiba uko wapi? "Kwa sasa kinachoendelea ni vikao vya maandalizi na utajulishwa kila kitu pindi taratibu zitakapokuwa tayari ila kwa usiku huu nimekupigia simu kukuelekeza jambo moja la muhimu" "Nakusikiliza madam" akasema Frank kwa adabu Usifanye uchunguzi wowote kuhusiana na kifo cha Pascal" "What?!!! "Umenisikia vyema.Usifanye uchunguzi wowote kuhusiana na kifo cha Pascal.Umenielewa? "Madam umenichanganya kidogo.Umefahamuje kuhusu jambo hili?Kwa nini nisifanye uchunguzi? "Frank toka lini umeanza kumuhoji mkuu wako?If I say stop I mean it.Sitaki maswali yoyote.Achana na uchunguzi wowote kuhusiana na kifo cha Pascal.!! "madam I'm sorry to ask this.are you behind this? "You want to know? Yes I'm behind this.I'm watching you Frank so dont try to desobey me!! akasema Elizabeth na kukata simu.Frank aliyekuwa njiani kuelekea hotelini kwa Vicky akabaki amepigwa na butwaa asijue la kufanya "Whats going on? Mambo gani haya yanaendelea?Madam Elizabeth yupo hapa nchini toka lini?Deus is dead? How come I wasn’t informed? Frank akajiuliza maswali mfululizo akakosa majibu "I'm confused right now.Ngoja nikapumzishe kichwa changu kwani naona kila muda unavyozidi kwenda ndivyo ninazidi kuchanganyikiwa na akili kushindwa kufanya kazi yake"akawaza Frank na kuwasha gari akaondoka kuelekea nyumbani kwake.









    Inakaribia saa sita za usiku Elizabeth na Juliana wakiwa garini wakitoka katika kikao cha ndugu ambacho walifikia muafaka kuhusiana na mazishi ya Deus mume wa Elizabeth. "Juliana kuna jambo ninalifikiria kuhusu yule rafiki yako Patricia" "Jambo gani mama? "Ninataka nimuweke awe msimamizi wa miradi yetu mbali mbali.Kwa sasa baada ya kufiwa na mumewe atakuwa katika upweke mkubwa.Kwa kuwa tunamiradi sehemu mbali mbali duniani atakuwa akisafiri mara kwa mara na hii itamsaidia sana katika kusahau machungu ya kifo cha mumewe.Unaonaje kuhusu wazo hili? "Wazo lako ni zuri mama lakini hapana.Sitaki Patricia ahusishwe kwa namna yoyote katika miradi ya familia yetu.Kwanza yule ni msomi mzuri na ana kazi yake.Amesomea udaktari na hana elimu ya biashara.Hatafuti kazi kwani anaweza kujimudu kutokana na kazi yake anayoifanya na hana shida ya kutafuta kazi nyingine.Pili miradi ya familia yetu imekuwa na mabalaa mengi” sura ya Elizabeth ikabadilika.Juliana akaendelea “Sintasahau kifo cha Godson.Alipoteza uhai baada ya kumshirikisha katika miradi ya familia.Godson alikuwa msomi na mwenye kazi nzuri sana lakini mkamshawishi aachane na kazi aliyokuwa anaifanya asimamie miradi ya familia lakni matokeo yake ni kukatwa pumzi kikatili namna ile.Patricia amepitia mambo mengi sana na sitaki kumuongezea matatizo mengine"akasema Juliana "Juliana tafadhali usinikumbushe kuhusu Godson.Mpaka leo kidonda kilichotokana na kifo chake hakijapona."akasema Elizabeth Sote bado tunatibu majeraha yaliyosababishwa na kifo cha Godson.Patricia ni muhimu sana kwangu hivyo sitaki kuongeza tena kidonda kingine" "Juliana tafadhali naomba unielewe sina leno baya na Patricia bali ninatafuta msaidizi.Wewe umekwisha kataa kusimamia miradi ya familia.Mdogo wako Sekela naye yuko masomoni na kwa sasa baada ya baba yako kufariki nimebaki peke yangu hivyo nahitaji msaidizi ambaye ni mtu wa karibu na familia yetu.Patricia anafaa sana"akasema Elizabeth "mama tafadhali kama unahitaji mtu wa kufanya shughuli zako tafuta mtu mwingine na si Patricia.I dont want to involve her in your dirty business"akasema Juliana na Elizabeth akastuka na kumtazama kwa macho makali "What you've just said? akauliza Elizabeth kwa ukali "I dont want Patricia to be involved in your dirty businesses" akasema Juliana.Elizabeth aliyekuwa katika usukani akalazimika kupunguza mwendo wa gari na kuegesha kandoni mwa barabara halafu akainamisha kichwa chini . “Kuna nini mama mbona tumesimama? akauliza Juliana.Elizabeth akavuta pumzi ndefu na kusema "Sikutegemea kabisa kusikia neno kama hilo likitoka kinywani mwako my dear daughter" akasema Elizabeth huku akimtazama Juliana kwa macho makali “Unathubutuje kutoa kauli kama hiyo Juliana? akauliza Elizabeth "Kwani si kweli mama?Mimi ni mtu mzima ninaelewa mambo mengi japo sijawahi kukueleza chochote kuhusiana na mambo mnayoyafanya wewe na baba lakini ninafahamu kuwa kuna mambo machafu mnayafanya na ndiyo maana sitaki kushiriki katika biashara zetu" akasema Juliana huku akilengwa na machozi "Kila siku taswira ya Godson inanijia namna alivyoshambuliwa na mwili wake kuharibiwa kwa risasi.Yalikuwa ni mauaji ya kinyama sana.Japo hamtaki kusema lakini ukweli ni kwamba yalisababishwa na mambo yenu ya siri" Elizabeth akavuta pumzi ndefu na kuwasha gari wakaendelea na safari kimya kmya hadi walipofka nyumbani.Mara tu Juliana aliposhuka mama yake akamuita "Juliana we need to talk!! "Mama nimechoka tutazungumza siku nyingine" "Hakuna siku nyingine.We need to talk now! akasema Elizabeth kwa ukali.Juliana hakutaka malumbano na mama yake wakaongozana hadi katika chumba cha maongezi.Elizabeth akamtazama Juliana kwa muda halafu akasema "Arlight .Its true,me and your father we have some dirty business"akanyamaza na baada ya sekunde chache akaendelea "You are who you are, because of the dirt businesses me and your father are doing.Ni kwa sababu ya biashara hizo unazozita haramu,umeishi maisha mazuri,umesoma vizuri na umejulikana.Mimi na baba yako hatukuwa na maisha haya mnayoishi ninyi.Tumehangaika na kujiingiza katika mambo mengine mabaya kwa ajili yenu hivyo unapaswa kuwa na shukrani kwa maisha haya unayoyaishi leo.Hujawahi kukosa kitu chochote unachokihitaji katika maisha yako nini kingine unakihitaji?Ninataka leo iwe ni mwanzo na mwisho kusikia unalitamka neno kama hilo.Nataka uwe kimya na uendelee kuyafurahia maisha.Niambie chochote unachokihitaji nitakupatia lakini usithubutu kutaka kuingia katika mambo yangu.Sitaki kukupoteza kama nilivyompoteza Godson." akasema Elizabeth kwa ukali na Juliana akawa kimya "Unafahamu ni hatari ngapi mimi na baba yako tumezipita ili ninyi muwe salama na muishi maisha ya kifahari kama haya?akauliza Elizabeth halafu akavua gauni alilovaa na kumuonyesha Juliana makovu kumi na moja ya risasi mwilini . "Huu ni ushahidi kwamba nimepitia magumu mengi hadi kufika hapa nilipo.Nilitegemea ungenishukuru kwa mambo haya yote niliyowafanyia lakini badala yake umenibeza.Kama mtoto wangu wa kwanza sikutegemea kabisa kama siku moja ungeweza kutamka maneno kama yale" "I'm sorry mother" akasema Juliana "Juliana nakubali I'm not a perfect mother lakini ninaweza kujivunia kwamba kwa asilimia kubwa wanangu nimehakikisha wanapata maisha bora.Siku moja utaelewa kwamba haya yoteninayoyafanya ni kwa ajili yenu,utanitafuta unishukuru lakini utakuwa umekwisha chelewa.Siaki kukuingiza katika mambo yangu ila nataka ufurahie maisha wewe na mdogo wako.Tazama baba yako ameondoka,mimi mwenyewe hakuna ajuaye pengine muda wowote ninaweza kuondoka pia hivyo ninajitahidi kuwawekea misingi mizuri ili kwamba hata nikifa leo muendele kuwa na maisha mazuri wewe na mdogo wako.Kuna mambo mazuri ninayaandaa kwa ajili yako.Nataka nikuibie siri ila naomba uufunge mdomo wako na usimwambie mtu yeyote.Skutaka kukueleza lakini imenilazmu nikueleze ili ujue kwamba mimi silali nikiwaza mambo mazuri kwa ajili yako"akasema Elizabeth na kunyamaza kwa muda halafu akasema "David kuna jambo alikuja kunieleza.Kuna mpango unaendelea wa kumuondoa rais wa sasa madarakani na yeye David ataapishwa kuwa rais wa mpito na akishafanikiwa kuwa rais atakuteua uwe waziri wa maliasili na utalii.Jambo hilo tumekwisha lijadili na tumekubaliana .Nilitaka iwe suprise kwako lakini umenilazimisha nikueleze kabla ya wakati" Juliana akamtazama mama yake akakosa neno la kusema.Uso wake ukajenga tabasamu "Say something Juliana"akasema Elizabeth "What can I say mother? Nimekosa neno la kusema ila nimepokea taarifa hiyo kwa mstuko kwani mimi sina uzoefu wowote na mambo ya siasa.Nitawezaje kuimudu nafasi kubwa kama hiyo?Halafu naomba ufafanuzi kuhusu hilo jambo la kumuondoa madarakani rais kwani kwa ninavyofahamu mimi rais huchaguliwa kila baada ya miaka mitano na rais aliyepo madarakani hajamaliza kipindi chake cha pili cha miaka mitano wanamuondoaje?Wanataka kumuua?akauliza Juliana akionyesha kuwa na wasi wasi mkubwa "Hapana hakuna mapinduzi yoyote au kumuua rais wa sasa.Kwa maelezo aliyonipa David ni kwamba kuna mchakato unaendelea ndani ya chama chake wa kumuondoa rais madarakani kwa kushindwa kumudu vyema majukumu yake.Chama hakiridhishwi na uongozi wake hivyo wanataka kumtoa na kumuweka mtu mwingine kwa muda na mtu huyo tayari ameandaliwa ni David.Pindi akipata urais na wewe utangia katika baraza la mawaziri.Huu ni mwanzo wa safari yako ya kuwa mwanamke mwenye nguvu na utakapoingia katika nafasi kubwa ndipo utakapoelewa mimi ninafanya nini.Usihofu kwamba hufahamu siasa.Si kila waziri au mbunge anaifahamu vyema siasa.Kila kitu utakifahamu huko huko mbele ya safari.Hukupaswa kulifahamu hili kwa sasa lakini kwa kuwa umekwisha lifahamu anza kufanya maandalizi.Si muda mrefu sana utakuwa mheshimiwa.Hizi zote ni juhudi zangu za kuhakikisha unakuwa na maisha mazuri na mafanikio makubwa.Juliana mimi na wewe hatupaswi kuwa na tofauti.Tunapaswa kuwa kitu kimoja.Umechoka sana Juliana nenda kapumzike tutazungumza mambo mengi baada ya mazishi" Juliana akaondoka na moja kwa moja akaelekea chumbani kwa Patricia akagonga mlango. Patricia ambaye hakuwa na usingizi akainuka na kwenda kuufungua mlango “Dada Juliana karibu” “Ahsante Patricia.Samahani kwa kukusumbua usiku huu.Tayari ulikwisha lala? Akauliza Juliana “Hapana dada.Sina usingizi.Ahsante sana kwa ule mvinyo ulioniletea umenisaidia sana.Vipi huko utokako mambo yamekwendaje?akauliza Patricia.Juliana akamimina mvinyo katika glasi akanywa funda kubwa kisha akasema Huko mambo yamekwenda vizuri na tumefikia makubaliano.Mazishi ni jumanne ijayo.Msiba utakuwa hapa nyumbani na kesho kutwa jumatatu mwili utawasili na siku ya jumanne tutazika.Kuanzia kesho hapa nyumbani patakuwa ni mahala penye heka heka nyingi za maandalizi” “Imekuwa vyema mmefikia makubaliano”akasema Patricia “Ni kweli Patricia imekuwa vyema kwani hata wao hawakuwa wakielewana lakini kwa msiba huu umewaleta pamoja na wamemaliza tofauti zao” akasema Juliana na ukimya ukatanda.Patricia akasema Dada Juliana kuna jambo nataka nikueleze.” Juliana akainua kichwa na kumtazama Patricia “Nimepigiwa simu na mke wa rais akanijulisha kwamba wamejadiliana na rais na wamekubaliana kwamba niende nikaishi nao ikulu kwa muda hadi hapo nitakapokuwa tayari kuanza shughuli zangu.Nimefikiria nimeona ni jambo jema hivyo baada ya mazishi ya baba nitakwenda kuishi ikulu.Nakuomba usinielewe vibaya kwani hata hapa ni nyumbani na ninapata kila ninachokhitaji lakini wale wazee wameniomba sana nikaishi nao na nimeshindwa kukataa” Hakuna tatizo kuhusu hilo Patricia.Hayo ni maamuzi yako lakini siku zote kumbuka kuwa hapa ni nyumbani kwako na milango iko wazi kwako muda wowote” Akasema Juliana.Ukapita ukimya kisha Patricia akauliza “Dada Juliana baada ya mazishi ya baba utaondoka tena kurejea huko ulikokuwa? “Hapana sintaondoka tena.I’m back for good.This time I wont run again” akasema Juliana “ Run?!! Akauliza Patricia “ Patricia kuna mambo mengi yalinikuta na kunifanya nikakimbia nchi.Sikuondoka kwa kupenda.Ninapenda sana nyumbani lakini nililazimika kuondoka bila kupenda” Nini kilitokea dada Juliana? akauliza Patricia.Juliana akaichukua chupa ya mvinyo akaitingisha halafu akagugumia mvinyo wote uliobaki “Wewe ni mdogo wangu na nitakueleza,ila yote nitakayokueleza yabaki katika kifua chako.Hatakiwi mtu mwingine yeyote kuyafahamu” “Usiwe na wasi wasi nami Juliana” akasema Patricia.Juliana akavuta kumbu kumbu halafu akasema “Sikuwahi kukuonyesha mpenzi wangu wakati ule lakini nilikuwa na mpenzi anaitwa Jose.Tulipendana mno na tulikuwa na mipango mingi sana ya maisha yetu ya usoni.Ni mwanaume pekee ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote na hadi leo hii bado ninaamini kwamba hatatokea mwingine kama yeye.Jose alikuwa ni mtoto wa kigogo mmoja wa serikali na familia yao walikuwa wenye kujiweza sana kifedha kama sisi.” Akanyamaza kwa sekunde kadhaa na kuendelea “Yuko wapi kwa hivi sasa? Mliachana? Akauliza Patricia “Mapenzi yetu yalikuwa mazito sana na tusingeweza kuachana.Aliuawa” “Aliuawa? Nani alimuua? “Mpaka leo sifahamu ni nani walimuua Jose lakini alikatwa shingo na kichwa kikatenganishwa na mwili kishamwili wake ukaenda kuwekwa katika geti la nyumbani kwa wazazi wake na pembeni yake kukiwa na barua ya onyo kwamba nitakayefuata ni mimi.Kwa haraka sana wazazi wangu wakanikimbiza na kwenda kunificha nje ya nchi ambako nimeishi toka wakati ule na sijawahi kurejea Tanzania.Msiba wa baba umenirejesha tena hapa na ndiyo maana ninasema kwamba safari hii siwezi kukimbia tena.Nimechoka kuishi nchi za watu.Kama ni kuniua waniue tu siwezi kuogopa tena”akasema Juliana akionekana kuwa na hasira na uchungu mwingi “Pole sana Juliana.Ninajiona nimepitia matatizo lakini kumbe ya kwako ni mazito kuliko yangu.Pole sana.Ni nani hao waliomuua Jose? Walifanikiwa kukamatwa? “Mpaka leo imebaki ni fumbo gumu kufumbuliwa” “Hakuna aliyewahi kukamatwa kuhusiana na mauaji hayo? Akauliza Patricia “Hakuna aliyewahi kukamatwa.Hii inaniumiza mno.” “Kuna kitu kinanishangaza sana dada Juliana" akasema Patricia "Kitu gani Patricia? "Ulisema kwamba Godson aliuawa kwa kupigwa risasi nyingi na watu wasiojulikana na mpaka leo watu hao hawajawahi kukamatwa.Kama haitoshi na mpenzi wako Jose naye aliuawa kikatili na mpaka leo hii wauaji wake hawajawahi kukamatwa.Wewe mwenyewe ulichukuliwa na kwenda kufichwa nje ya nchi na hiyo ndiyo salama yako kwani vinginevyo na wewe ungekwisha uawa.Hudhani kama kuna watu wanailenga familia yenu?Haya yanaonekana ni mauaji ya kulipiza kisasi.Mmewahi kulifikisha suala hili katika vyombo husika? akauliza Patricia "Patricia uko sahihi kabisa.Ni wazi wauaji hawa wana lengo baya na familia yetu.Mdogo wangu wa mwisho aliwahi kunusurika kuuliwa kwa risasi na ndiyo maana ikawalazimu wazazi kumtafutia walinzi wa kuongozana naye kila sehemu .Ni majanga matupu katika familia yetu.Matukio haya yote yanapotokea wazazi husema wanashughulikia lakini mpaka leo hakuna majibu yoyote ya nani waliofanya mauaji haya mabaya .Jambo hili limekuwa linaniumiza sana kwa miaka mingi na ndiyo maana safari hii sitaki kukimbia nataka nibaki hapa hapa nchini ili niwafahamu watu hao ni akina nani na sababu ya kuiandama familia yetu? "I’m going to help you" akasema Patricia "Patricia no! Dont involve yourself in this" akasema Juliana "Juliana wewe ni dada yangu umenisadia mambo mengi kwa wakati ule ambao nilikuwa na shida sana na mpaka sasa bado uko nami.Ninao wajibu wa kukusaidia pia" "Patricia nauthamini sana mchango wako lakini katika hili hapana.Sitaki ujihusishe nalo.Ni jambo la hatari kubwa.Tayari una matatizo mengi yanayokukabili kwa sasa na sitaki uongeze matatizo.Nimekueleza tu kama mdogo wangu ili uwe na picha ya masahibu ninayoyapitia" "Juliana tafadhali naomba ukubali nikusaidie dada yangu"Patricia akasisitiza "Unataka kunisaidia vipi Patricia? "Ninaweza kukuunganisha na watu ambao wanauwezo wa kufanya uchunguzi na kuwabaini wauaji.Ninafahamiana na rafiki zake Elvis na nikiwaomba wataniskiliza.Hata bosi wao mzee Meshack Jumbo ninafahamiana naye na ni mtu mwema.Amekuwa nami toka msiba ulipotokea na hadi jana katika kikao cha familia alikuwepo nikimuomba anisaidie kuhusu suala hili hawezi kukataa" akasema Patricia na Juliana akainamisha kichwa akazama mawazoni "Juliana" akaita Paricia "Unasemaje kuhusu wazo hilo? "Wazo hilo si baya lakini..." "Mbona una wasi wasi dada Juliana?akauliza Patricia.Juliana akafikiri kidogo na kusema Kuna tatizo lipo Patricia." "Tatizo gani? "Japo sina bado uthibitiso au ushahidi wa kutosha wa kuhusiana na hili lakini ninahisi wazazi wangu ni chanzo cha haya yaliyotokea.Nahisi kuna mambo wanajihusisha nayo kuna uwezekano familia yetu inalengwa na mahasimu wao wa kibiashara ndiyo maana tunauawa kama kuku.Endapo nitakubali kuruhusu uchunguzi ufanywe kuna uwezekano yakaibuka mambo mengine kuhusu familia yangu.Sitaki jambo hilo litokee" akasema Juliana "Juliana usiogope katik akuipigania haki.Ndugu yako Godson na mpenzi wako Joseph waliuawa kikatili na wewe mwenyewe ukanusurika.Una uhaika gani kama hao wauaji wamekwisha acha kukusaka? Uko tayari kuwaacha wauaji hawa waendelee kutamba na kuwafanya muishi kwa hofu kana kwamba hakuna vyombo vya kuwasaidia? Tafadhali usikubali kuwaacha hivi hivi.Pambana hadi haki ipatikane. na wote waliohusika katika mauaji haya watiwe nguvuni.Kama usipowapata watu waliofanya mauaji haya basi hata wewe hautakuwa na amani na bado utaendelea kuwa hatarini.Wakifahamu umerudi lazima watakusaka na kukuua.Usihofu kama kuna mambo yataibuka yanayowahusu wazazi wako kama wanahusika kwa namna yoyote na kusababisha vifo hivyo lazima nao wapate haki yao.Hili ni jambo gumu sana kwa wengi lakini mimi ushauri wangu kwako ni huo dada yangu ila kama unaona hakuna ulazima wa kutafuta haki na kuwaacha wauaji hao waendelee kutamba basi hakuna haja ya kufanya uchunguzi lakini kama unataka kuufahamu ukweli na kuwajua wauaji ili na wewe uendelee kuwa salama kubali nikusaidie na ukweli uwekwe bayana.Piga moyo konde fumba macho na uitafute haki hata kama itakubidi kuwaigiza wazazi wako katika matatizo lakini kama wanahusika kwa namna moja au nyingine sheria lazima ichukue nafasi.Hii ni kutafuta haki kwa wale waliouawa bila hatia" akasema Patricia "I'm confused Patricia and I dont know what to do.Ninataka sana kuwafahamu wauaji hawa na kuona haki ikitendeka lakini kwa upande mwingine ninahofia kuhusu familia yangu.Ninaweza kuwaingiza katika matatizo makubwa kitu ambacho sitaki kukifanya" "Unahisi ni mambo gani mabaya ambayo wazazi wako wanashiriki usiyotaka yajulikane ?Patricia akauliza "I'm not sure yet but I know they are doing dirty businesses.Godson aliuawa baada ya kuanza kushiriki katika biashara za familia.Alikuwa na kazi yake nzuri sana na yenye mshahara mkubwa ila wazazi wakamshauri aachane na kazi hiyo ili asimamie miradi ya familia na ndipo alipouawa kikatili.Siku kadhaa kabla ya kifo chake aliwahi kunieleza kwamba kwa namna yoyote ile nisithubutu kujiingiza katika miradi ya familia.Hakunifafanulia kwa kina kwa nini aliniambia vile ila ninaamini kuna mambo aliyaona na ndiyo maana akanitaka nisijihusishe kabisa katika biashara zile"akasema Juliana "Juliana mapema uliniambia kwamba mpaka sasa bado hujapata mbadala wa mpenzi wako Jose.Ulimpenda kwa dhati ya moyo wako.Kama kweli unampenda kiasi hicho ni wakati sasa wa kupambana kwa ajili yake na mdogo wako Godson.Ni wakati wa kuhakikisha haki inapatikana.Pambana kwa ajili yao.Elvis amenifundisha jambo kubwa sana siku zote unapaswa kupambana kwa ajili ya yule unayempenda.Elvis aliwahi kudiriki hata kukorofishana na mama yake mzazi kwa sababu yangu. Wewe pia unapaswa kupambana kwa ajili ya wale uwapendao ambao walinyimwa haki yao ya kuishi na hivyo kukunyima wewe furaha ya maisha yako.Kama Jose asingeuawa hivi sasa ungekuwa na furaha na amani wala usingeikimbia nchi.Unapombana kwa ajili ya haki unapaswa kufumba macho na kuhakiksha wale wote waliohusika wanatiwa nguvuni hata kama ni watu wa muhimu kwako."akasema Patricia.Juliana akainuka akazunguka zunguka mle chumbani na baada ya dakika tano akaketi "Patricia umeniambia maneno mazito sana leo hii na macho yangu yamefumbuka,ule woga umekwisha.Naomba unikutanishe na huyo mtu unayesema anaweza akanisaidia" akasema Juliana "Are you sure ?Patricia akauliza Yes.I want to find justice.Siwezi kuliacha jambo hili likaishia hewani.Potelea mbali litakalotokea" "Vizuri.Kesho ni jumamosi siku ya mapumziko nitampigia simu mzee Meshack asubuhi na kumuomba tuonane na nitamuomba tukutane naye” akasema Patricia "Ahsante sana Patricia.Sasa ngoja nikuache ulale tutaonana hiyo asubuhi" akasema Juliana na kuondoka akaelekea chumbani kwake "Aliyoyasema Patricia ni mambo ya kweli kabisa.Ni wakati sasa wa kuutafuta ukweli wa nani aliwaua mpenzi wangu Joseph na mdogo wangu Godson.Nilifikiria muda mrefu kulichunguza suala hili nikaogopa,nashukuru Patricia amenipa moyo na sasa nataka kuwafahamu wauaji waliomuua Godson na Jose.Mama hatafurahi akilifahamu jambo hili lakini sina namna nyingine ya kufanya lazima niwajue watu hao ni akina nani kwani hata mimi walitaka kuniua.Kama si wazazi kunikimbiza nje ya nchi lazima na mimi wangekwisha niua.Halafu nimekumbuka jambo huu ni wakati pia wa kufahamu mambo ambayo mama anayafanya .Ninaamini kuna mambo haramu anayafanya ila ni hodari sana wa kuyaficha hivyo ni wakati wa kufanya uchunguzi na kuyajua.Amekiri mwenyewe kwamba ni kweli kuna mambo haramu anayafanya kakini hakutaka kuniweka wazi.Ni wakati wa kumuondoa katika biashara hizo haramu.Nililazimika kumkubalia yote aliyoniambia likiwamo la eti kutaka kunichagua kuwa waziri wa maliasili na utalii.Siwezi kukubali uteuzi kama huu utakaofanywa na genge lao ili wanitumie katika mambo yao haramu" akawaza Juliana. *****************



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Dr Philip alipomaliza kazi yake aliaga na kuondoka kwani alikuwa na kazi nyingine ya upasuaji kwa usiku ule katika hospitali ambako hufanyia kazi kwa muda wa ziada.Meshack Jumbo naye alikuwa amechoka sana hivyo naye akaomba andoke kwenda kupumzika "Umefanya kazi nzuri sana leo Steve" akasema Elvis "Ahsante.Ni muda mrefu nilikuwa nimezikosa kadhia kama hizi lakini taratibu nitarejea katika ubora wangu" "Good.Hatuna muda wa kulala, ni wakati wa kuanza kumchunguza Vicky tufahamu kwa nini alimuua Pascal.Baadae atakapoamka tutamfanyia mahojiano lakini kwa sasa tuchunguze kila kitu chake.Tuchunguze simu yake anawasiliana na akina nani na tuchunguze kila alichonacho hata kama ni kidogo kiasi gani kitatusaidia kuweza kumfahamu vizuri" akasema Elvis.Steve akaufungua mkoba wa Vicky na kumwaga mezani kila kilichokuwemo katika mkoba wa Vicky na kukuta kuna vitu vichache kama kadi za benki,heleni mikufu na vitu vingine vidogo vidogo vya urembo. "Hakuna chochote cha maana hapa" akasema Steve "Hizi kadi za benki tutazichunguza pia na kufahamu kuna kiasi gani katika akaunti yake na kujua fedha hizo anapokea kutoka wapi.Zinaweza kutusaidia kuufahamu mtandao wake.Kwa sasa tuichunguze simu yake ili tuone kama kuna kitu tunaweza kukipata" akasema Elvis na simu yake ikaingizwa katika kifaa fulani ambacho kiliunganishwa na kompyuta kisha wakaanza kuchunguza.Baada ya dakika kadhaa za uchunguzi Elvis akasema "Hakuna kitu kikubwa cha kutuwezesha kumfahamu Vicky kwani inaonekana simu hii anaitumia sana kibiashara.Kuna kitu kimoja ambacho kinaweza kutusadia kumfungua na akatupa taarifa zozote tuzitakazo.Ni kwa kuitumia familia yake.Tuchunguze tujue kama ana watoto au ndugu au hata wazazi wake na tukimpatammoja wao basi atakuwa tayari kutueleza kila kile tunachokihitaji. Kuna picha fulani nimeziona humu katika simu ambazo zinamuonyesha Vicky akiwa na msichana fulani wamefanana sana.Fungua faili la picha" akasema Elvis na Steve akalifungua faili la picha na ndani ya faili hilo kulikuwa na faili lingine limeandikwa W.Bday.Wakalifungua faili hilo ambalo lilikuwa na picha zaidi ya mia moja.Walipitia picha hizo kisha Elvis akasema "Keki ina maandishi yanasomeka Happy birthday Winnie ikimaanisha msichana huyu ambaye alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa anaitwaWinnie.Picha nyingi zinaonyesha Winnie akiwa na Vicky.Wawili hawa wana ukaribu mkubwa.Inawezekana ni mtu na mdogo wake au ni ndugu" "Nakubaliana nawe Elvis kuna uwezekano wawili hawa wakawa ni ndugu kwani hata sura zao zinafanana japo Vicky amekuwa mweupe sana."akasema Steve.Elvis akaichukua picha moja ya Winnie akaikata kiufundi na kubakisha sehemu ya kichwa pekee halafu akaiweka picha ile katika programu ya kufananisha picha.Picha zilipita haraka haraka sana na baada ya nusu dakika programu ikasimama na kuonyesha majibu.Ilitoa picha mbali mbali za Winnie ambazoalikuwa ameziweka katika mitandao "Wasichana hawa huwa wanaweka taarifa zao nyingi katika mitandao na wakati mwingine hata namba zao za simu." akasema Elvis na kuufungua ukurasa wa facebook wa Winnie na kuanza kupitia taarifa zake.Jina lake katika ukurasa huu liliandikwa queen Winnie.Aliweka picha nyingi na katika taarifa zake aliweka pia namba zake za simu na mwaka aliozaliwa.Alikuwa na miaka ishirini na nne. "Kama watakuwa na mahusiano basi lazima huyu atakuwa ni mdogo wake kwani kwa umri wa Vicky huyu Winnie hawezi kuwa mwanae." akasema Steve "Tunachotakiwa kukifanya ni kufahamu mahala alipo na kumpata usiku huu huu na kumuweka tayari ili Vicky atakapoleta ukaidi au ugumu wa kutupa taarifa basi tumtumie huyu Winnie.Mpigie simu kwa kutumia simu ya Vicky na jifanye wewe ni daktari.Mdanganye kuwa Vicky amepata ajali na anataka kumuona halafu muulize mahala aliko ili umfuate.Ataamini kuwa ni kweli na tutamfuata kwenda kumchukua" akasema Elvis na bila kupoteza muda akaziandika namba za simu za Winnie walizozitoa mtandaoni na baada ya kupiga likatokea jina Winnie.Simu ikaita na kukatika bila kupokelewa akapiga tena na safari hii ikapokelewa "hallow dada samahani kwa kuchelewa kupokea simu nilikuwa usingizini" "Hallow Winie"akasema Steve "Wewe ni nani? akauliza Winnie kwa mstuko mkubwa "Naitwa Dr Bakari kutoka hospitali ya Samaria.Nimeelekezwa na dada yako anaitwa Vicky kuwa nikupigie simu.Amepata ajali ndogo ya gari na amelazwa hapa hospitalini kwetu" "Amepata ajali?! Winnie akastuka "Ndiyo amalazwa hapa hospitaliOh my God ! anaendeleaje? "Ni mzima kabisa amepata majeraha kidogo na tumemlaza kwa muda hapa hospitali " "Thank you God! akasema Winnie na kushusha pumzi "Vicky amenituma kuwa anahitaji kukuona kuna mambo anataka akuelekeze ya muhimu sana.Uko wapi mida hii? "Niko nyumbani" "Nielekeze nyumba yenu ilipo ili nikufuate hapo mara moja" akasema Steve na Winnie akamuelekeza kila kitu "Vizuri Winnie ninakuja hapo sasa hivi kukuchukua ili uje umtazame dada yako.Kingine anachosisitiza ni kwamba usimweleze mtu yeyote kuwa amepata ajali hadi mtakapoonana” "Dr Bakari una hakika dada yangu ni mzima? "Vick ni mzima kabisa usihofu.Amepata majeraha madogo madogo kama nilivyokueleza.Jiandae ninakuja hapo kukuchukua sasa hivi" akasema Steve na kukata simu "Umefanya vizuri.Sasa wewe nenda kamchukue Winnie mimi nitabaki hapa nataka nianze kumuhoji Vicky ili hadi utakaporejea kama hajasema chochote basi tujue namna ya kufanya"akasema Elvis na bila kupoteza muda Steve akaondoka kwenda kumchukua Winnie.Elvis akaelekea katika chumba alimoVicky akaufungua mlango na kumkuta Vcky amekaa kitandani.Elvis akavuta kiti karibu yake na kuketi wakatazamana halafu akasema "Unajisikiaje Vicky? akauliza lakini Vicky hakumjibu kitu "Unaendelaje Vicky? akauliza tena "Unataka niendelee vipi? Vicky akauliza kwa ukali "Usiwe na hasira Vicky.Kuwa mtulivu na kila kitu kitakwenda vizuri.We're not bad people.I'm sorry for what happened hatukuwa na lengo la kukuumiza kwani wewe si yule tuliyekuwa tunakuhitaji lakini nililazimika kukupiga risasi ya mkono kufuatia kitendo ulichokifanya ambacho hakuna kati yetu aliyetegemea kama ungekifanya" akasema Elvis na kutulia kidogo akamtazama Vicky aliyekuwa anamtazama kwa macho yaliyojaa hasira "Kufuatia kiendo kile ulichokifanya nina maswali machache ambayo ninataka unijibu kwa ufasaha mkubwa.Endapo utanijibu vizuri utanishawishi nikuachie huru uende zako lakini endapo utakuwa kiburi na kukataa kunijibu maswaliyangu utanipa hasira na utakuwa ni mwisho wako wa kuliona jua .Nitakupeleka kuishi mahala penye giza hadi kifo chako.Utauona mwanga mara tatu tu kwa siku na utafungwa miguu na mikono kwa minyororo.Sitaki nikufanyie hivyo mrembo kama wewe hivyo nakuomba unijibu maswali yangu" Vicky akabetua midomo na kusonya kwa dharau "Wewe kama nani wa kunitaka mimi nikujibu maswali yako? Hunijui na bado unataka nikujibu maswali.Save your time you idiot mimi siwezi kukujibu mtu kama wewe! akasema Vicky kwa dharau "Huyu mwanamke ni mtu mjanja sana na anajibu hivi kwa ajili ya kunipandisha hasira kwani anajua mtu ukiwa na hasira huwezi kufikiri sawa sawa na anaweza akapata upenyo wa kutoroka" akawaza Elvis Kwa nini ulimuua Pascal? Elvis akauliza. "Sina muda mchafu wa kukujibu chawa kama wewe.Wewe ndiye unayetakiwa unijibu kwa nini unamuhitaji Pascal? akauliza Vicky na kumfanya Elvis ainuke kitini akamsogelea Vicky "Nisikilze vizuri Vicky kwa sasa wewe hauna uwezo wowote wa kuniuliza maswali.Nakuomba usiendelee kupoteza muda wangu nijibu maswali yangu ninayokuuliza ama sivyo utanilazimisha nitumie nguvu jambo ambalo silitaki" akasema Elvis "Nimekwisha kueleza kwamba sina muda wa kujibu swali la taka taka kama wewe.Huna uwezo wa kunihoji mimi na kitendo hiki ulichokifanya cha kunishikilia na kuniweka mimi hapa utakijutia kwa maisha yako yote hadi siku unaingia kaburini" akasema Vicky kwa kujiamini sana.Hakuonekana kuwa na wasi wasi hata chembe. "Vicky narudia tena kukusisitiza kwamba sitaki kutumia nguvu kukulazimisha unijibu mawali yangu.Naomba unijibu bila jeuri na tutakwenda sawa lakini endapo utakuwa kiburi utanibadilisha na nitakuwa mtu mwingine kabisa.Tafadhali nakuomba usinilazimishe nikabadilika utaomba ugeuke hewa upotee.Jibu swali langu tafadhali"akasema Elvis na Vicky akatoa kicheko kidogo cha dharau na kusema " Sikiliza handsome boy mimi sitishiki na hayo maneno yako.Sikulazimishi unifungue lakini utajutia kilichokufanya ukanileta hapa." "Soon that handsome will be a monster please dont push me to change into a monster" akasema Elvis "I'm a monster too.Monsters dont hurt each other"akasema Vicky huku akicheka "Please dont try me Vicky" akasema Elvis "Go to hell handsome" akasema Vicky na Elvis akamtazama kwa hasira. Umeniudhi sana Vicky kwa kiburi chako.Endelea kupumzika nitarudi tena baadae kidogo na nina hakika wakati huo tutaelewana" akasema Elvis na kutoka mle chumbani akiwa amefura kwa hasira "Who is this woman?Kwa nini anajiamini namna hii? Vicky huyu ni tofauti na yule Vicky kahaba.Kuna mambo mengi ya kufahamu kutoka kwa huyu mwanamke.Kabla ya jogoo kuwika alfajiri lazima tutakuwa tumekwishamfahamu ni nani.Ngoja nimsubri Steve arejee na mdogo wake na ndipo atakapotufahamu sisi ni akina nani" akawaza Elvis na kuingia chumbani kwake na kuanza kuandaa zana zake za kutesea *************** Steve aliwasili katika nyumba aliyoelekezwa na Winnie.Lilikuwa ni jumba kubwa la ghorofa.Alipokaribia getini akamulikwa na tochi yenye mwanga mkali na mlinzi ,akapunguza mwendo na kusimamisha gari.Mlinzi yule aliyekuwa amevaa sare za kampuni ya ulinzi na aliyekuwa na bunduki mkononi akalisogelea gari la Steve ambaye alishusha kioo na kumsabahi yule mlinzi kwa adabu. Steve akajitambulisha kwamba ni mgeni wa Winnie na ili kumthibitishia mlinzi yule analolisema ni la kweli akachukua simu yake na kumpigia Winnie akamjulisha kuwa tayari amekwisha fika yuko pale nje.Mlinzi yule hakuamini alikuwa amesimama imara ameshika bunduki yake hadi aliposikia geti likifunguliwa na Winnie akatoka. "Aunt huyu ni mgeni wako?akauliza "Ndiyo" akajibu Winnie na Steve aliyekuwa amevalia nadhifu akashuka akamfungulia Winnie mlango wa gari akaingia kisha wakaondoka "Nimestuka sana kwa taarifa ulizonipa kuhusu dada Vicky.Anaendeleaje?Kama nilivyokueleza simuni kwamba hali yake ni nzuri anaendelea vyema kabisa.Amepata majeraha madogomadogo" "Alikuwa amelewa? "Hapana hakuwa amelewa.Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba yeye ndiye aliyegongwa na gari lingine.Usihofu Winnie hali ya dada yako ni nzuri na kesho asubuhi ataruhusiwa kutoka hospitali" akasema Steve na ukimya ukatanda garini "Vicky ni nani kwako? Akauliza Steve "Vicky ni dada yangu.Wazazi wetu wamekwisha fariki na yeye ndiye baba na mama yangu.Tumezaliwa wawili tu" "Oh nilihisi hivyo kwani amenisisitiza sana akitaka nikupeleke akuone ili aweze kukutoa hofu kwani alihisi ungestuka sana kama ungezipata taarifa kutoka kwa watu wengine" akasema Steve na safari ikaendelea kimya kimya.Barabarani magari hayakuwa mengi sana usiku huu "Unafanya kazi gani Winnie? "Mimi bado mwanafunzi.Ninasomea udaktari niko mwaka wa tatu" "Hongera sana" akasema Steve na hakutaka tena mazungumzo akihofu pengine Winnie angeweza kumuuliza maswali ambayo angeshindwa kuyajibu "Winnie tunapitia sehemu fulani kuna dawa nataka kuzichukua ili twende nazo hospitali" akasema Steve "hakuna tatizo" akajibu Winnie.Steve akaliongoza gari kuelekea katika makazi yao "She's very pretty.Hapa ametoka kuamka na anaonekana mremo hivi je akijiremba si atakuwa malaika.Ana uzuri wa kipekee sana lakini uzuri wote huu unakwenda kuharibika .Mpaka kesho asubuhi hatakuwa anatazamika labda dada yake aamue kutueleza ukweli.Wakati mwingine inaumiza kuwaumiza watu wasio na hatia yoyote lakini hakuna namna lazima tutumie kila aina ya mbinu hadi Vicky afunguke." akawaza Steve na kuanza kukumbuka mambo aliyoyafanya na Vicky usiku ule kule hotelini "Vicky tayari alikwisha ukubali mziki wangu.Nilimfanyia mambo makubwa ndani ya kipindi kifupi na akachanganyikiwa hadi kukiri kwamba hajakutana na mwanaume ninayejua mapenzi kama mimi.Hakujua kama nilikuwa kazini.Aliamini kweli mimi ni bilionea kutoka nje ya nchi.Shukrani za kipekee zimwendee Samira ambaye aliandaa mpango huu hadi nikafanikiwa kukutana na Vicky japo nimevunja ahadi niliyompa kwamba sintafanya mapenzi na Vicky.Ningewezaje kumuacha malaika yule hivi hivi? "akawaza Steve na kwa mbali akatabasamu "Pamoja na uzuri wake lakini mwanamke yule ni hatari sana.Kitendo alichokifanya cha kumuua Pascal kwa haraka namna ile kinanifanya niamini yule si mwanamke wa kawaida.Ni jambazi? Kwa nini anatembea na bastora?Nilifanya makosa sana kutomchunguza kwanza kabla ya kukimbilia kufanya ngono.Lakini sipaswi kujilaumu kwani sote tulijua yule ni kahaba tu.Baada ya kuishika bastora na kumuua ndipo sote tukapata akili kuwa Vicky ni zaidi ya kahaba.Kabla ya mapambazuko lazima tumfahamu yeye ni nani na kwa nini akamuua Pascal” akaendelea kuwaza Steve huku akiendesha gari kwa kasi kwa sabau maeneo haya hakukuwa na magari mengi usiku huu. Walifika katika makazi yao akabonyeza kengele ya geti na Elvis akatoka akawafungulia mlango wakaingia ndani "Winnie kama hutajali naomba uingie ndani upate walau maji wakati ninapakia mzigo" akasema Steve na kumfungulia Winnie mlango wakaeleka sebuleni.Mara tu walipoingia sebuleni sura ya Winnie ikapatwa na mstuko mkubwa alipoiona bastoa ikiwa mezani,akataka kugeuka ili akimbie lakini nyuma yake alikuwepo Steve akamshika mkono na kumuamuru akae kitini kisha akaichukua simu ya Winnie akaizima kabisa "Tafadhali jamani naomba msiniue!! akasema Winnie huku akitetemeka kwa woga. "Relax Winnie.We're not bad people and we're not going to hurt you" akasema Elvis "Mnataka nini kwangu ?Msiniue jamani dada yangu ana pesa na atawapa kiasi chochote mnachokihitaji.Tafadhali msinuie" akasema Winnie huku macho yake yamejaa machozi "Winnie nimekuleta kuja kumuona dada yako na muda si mrefu utakwenda kuonana naye na mtazungumza.Usiwe na wasi wasi wowote.Baada tu ya kuonana naye nitakurejesha nyumbani kwenu" akasema Steve halafu yeye na Elvis wakasogea pembeni "Kuna chochote umekipata toka kwa Vicky?Steve akauliza "Hapana sikufanikiwa kupata chochote.Yule mwanamke ni jeuri sana.Steve ninahisi huyu mwanamke ni tofauti sana na tunavyomchukulia kama kahaba.Kuna kitu zaidi ya ukahaba na kuna mambo mengi anayafahamu ambayo lazima tuyajue kwa kumtumia mdogo wake.Endelea kumchunga Winnie mimi ninarejea tena chumbani kabla ya kumuingiza Winnie" akasema Elvis na kurejea chumbani alimo Vicky ambaye alikuwa amejilaza kitandani.Mlango ulipofunguliwa akainuka na kukaa "Umekuja kunifungua? akauliza "Hapana hautafunguliwa Vicky hadi kiburi chako kitakapokwisha.Sikiliza Vicky awali nilipokuja nilikuuliza kirafiki sana na kutaka unieleze wewe ni nani na kwa nini ulimuua Pascal lakini ukawa kiburi ukagoma kujibu swali langu.Kwa kitendo kile uliniudhi na kunilazimisha nitumie nguvu kupata kile ninachokihitaji" "Are you going to hurt me? akauliza Vicky huku akitoa kicheko cha dharau "No" akajibu Elvis I'm not gong to hurt you but your sister Winnie " Sura ya Vicky ikabadilika akapandwa na hasira zilizochanganyika na mstuko,akamtazama Elvis kwa macho yaliyojaa hasira "Umesema nini wewe ng'ombe?akauliza Vicky "Nadhani umenisikia vizuri.Mmi sina shida ya kukuumiza wewe.Nitaanza na mdo wako Winnie.Tayari yuko hapa ndani " "You are kiddng.This is a joke" akasema Vicky kwa ukali "Its not a joke.Winnie tunaye hapa ndani na utashuhudia namna nitakavyomtesa .Utashuhudia machugu atakayoyapata.She's so young and pretty.Kwa nini uache ateseke? Kwa nini umuumize? Just tell me what I want and we'l let her go.Hata mimi sipendi kumuumiza mtoto mzuri kama yule lakini ukinilazimisha nitamuingiza katika mateso makali na atakuchukia kwa kushindwa kumsaidia.Ni wewe pekee ambaye unaweza kumuokoa kutika katika dhaama inayomkabili.Nakupa dakika moja kuamua hatima ya mdogo wako" akasema Elvis na kuanza kuhesabu sekunde katika saa yake hadi ilipotimia dakika moja "Tayari dakika moja.Naamini umekwisha fanya maamuzi kuhusu mdogo wako" "Go to hell! Sina ndugu anaiwa Winnie.Kama ulidhani kwa kufanya ujinga huo unaweza kunipata umekosea sana.Wewe bado ni chawa tu.Nakupa ,saa mbili uweze kunifungua niende zangu" akasema Vicky "Nakupa nafasi ya mwisho Vicky.Tafadhali naomba msaidie mdogo wako.She dont deserve this" akasema Elvis. Kwa nini una kichwa kigumu kuelewa wewe kobe?Nimekwambia sina ndugu mwenye jina hilo na kama ulidhani kwa kutumia njia hiyo unaweza ukanipata umekosea sana.Narudia tena kukusisitiza kwamba muda unakwenda na usiponiachia yatakufika makubwa sana.Bado saa moja na dakika arobaini za mimi kukaa humu ndani.Naomba ulizingatie hilo" akasema Vicky.Elvis akamtazama halafu akatoka "I have no choice.Amenilazimisha nifanye jambo ambalo sikuwa nimetaka kulifanya.Huyu mwanamke ni jeuri sana lakini leo amekutana na jeuri zaidi yake na atasema tu kila kitu" akawaza Elvis na kuingia chumbani kwake akachukua vifaa vyake vya kutesea na kuvipeleka chumbani alimo Vicky akaviweka mezani na bila kusema chochote akatoka na kuelekea sebuleni "Steve it’s time." akamwambia Steve. Winnie inuka twende ukamuone dada yako"akasema Steve "Mnanipeleka wapi? Tafadhali nawaomba msiniue jamani,dada yangu atawapa kiasi chochote cha pesa mtakachokihitaji" akasema Winnie huku akilia na kumlazimu Steve kumtolea bastora "Kaa kimya na ufuate kila utakachoamriwa kukifanya.Umenisikia Winnie? akasema Steve kisha akamshika Winnie mkono wakaelekea chumbani alimo Vicky.Elvis ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia halafu akafuata Winnie na nyuma yake alikuwepo Steve Winnie ?!!! akasema Vicky kwa mshangao "Dada !! Winnie naye akashangaa na kutaka kumkimbilia dada yake lakini Steve akamzuia "Dada yangu amefanya nini? akauliza Winnie huku akilia baada ya kumuona dada yake akiwa amefungwa mkono na mguu kwa pingu.Elvis akamfanyia ishara Steve amruhusu Winnie akasalimiane na dada yake akamuachia wakakumbatiana huku wote machozi yakiwatoka "Wamekuumiza kokote? akauliza Vicky "Hapana hawajaniumiza" "Wamewezaje kukupata Winnie? Wamenipigia simu kwa kutmia simu yako na kunieleza kwamba umepata ajali huko hospitali na unataka kunioa hivyo nikawaelekeza nyumbani wakaja kunichukua.Who are these people?Kwa nini wamekufunga? akauliza Winnie na Vicky akafuta machozi.Elvis akashika Winnie na kumvuta pembeni "Vicky nadhani sasa umeamini kwamba mimi sisemi uongo.Nataka uniambie huyu ni nani?Ulisema kwamba hauna ndugu yako anaitwa Winnie.Nataka utamke mbele yake ni kweli hauna ndugu yako anaitwa Winnie? akauliza Elvis "Nawaonya msijaribu kumgusa mdogo wangu!!Ninaapa nitawafanyia kitu kibaya sana endapo mtamfanya chochote mdogo wangu.Shida yenu ni mimi kwa hiyo mdogo wangu hahusiki na chochote.Muacheni haraka sana aende zake" akasema "Ahsante sana Vicky kwa kukiri kuwa Winnie ni mdogo wako.Ninakupa nafasi ya mwisho Vicky ya kumsaidia mdogo wako.Una dakika tano za kutafakari na kufanya maamuzi" akasema Elvis na kisha akamtoa Winnie mle chumbani "Nini kinaendelea hapa? Dada yangu amefanya nini?Naombeni mumfungue tafadhali.Kama ni fedha mnahitaji atawapa anazo za kutosha" akalia Winnie, Winnie tunafahamu kuwa unampenda sana dada yako na ninaomba nikuhakikishie tena kuwa sisi si watu wabaya na tutamuachia dada yako ila kuna mambo tunahitaji kuyafahamu.Unaweza kutusaidia kutuambia dada yako anajishughulisha na nini? akauliza Elvis "Dada ni mfanya bashara " "Anafanya biashara gani? Steve akauliza "Anafanya biashara ya hoteli na ana maduka ya nguo na urembo" "Hakuna mambo mengine anayafanya kwa siri nyuma ya hizo biashara? Kama unafahamu tueleze tafadhali kwani utakuwa umemsaidia sana dada yako kipenzi" "Ninachokifahamu ni kwamba amekuwa akitoka na wanaume mbali mbali kiasi cha watu kumuita kahaba" "Una hakika hakuna jambo lingne unalolifahamu kuhusu dada yako? "Ukiacha hayo niliyowaelezeni hakuna kingine ninachokifahamu" akajibu Winnie "Are you sure?Steve akauliza "yes I'm sure" akajibu Winnie "Kwa ufupi tu ni kwamba dada yako yuko hapa kwa sababu amefanya jambo kubwa usiku huu.Amempiga risasi na kumuua mtu ambaye ni hatari kwa taifa.Tumemleta hapa ili kumhoji na kufahamu sababu za kumuua mtu yule ambaye tulitegemea kupata taarifa nyeti sana kutoka kwake?Dada yako amekuwa mgumu sana kutupa ushirikiano na ndiyo maana tumelazimika kukuleta hapa ili utusadie kumshawishi afunguke na atupe sababu za kumuua yule mtu"akasema Elvis "Dada yangu ameua mtu? akauliza Wnnie kwa mshangao "Ndyo.Umewahi kumuona akiwa na bastora? "Ndiyo nafahamu kuwa anayo bastora lakini aliniambia ni kwa ajili ya kujilinda" "Ukiiona bastora hiyo unaweza kuifahamu?







    Ndiyo nimewahi kuiona mara moja" akasema Winnie na Seve akaileta bastora ya Vicky "Hii si bastora ya dada.Niliyomuona nayo haikuwa kubwa hivi.Yenyewe ilikuwa ndogo" "Bastora hii ndiyo aliyoitumia kutoa uhai wa mtu" "Bado siamini kama dada yangu amefikia hatua ya kutoa uhai wa mtu.Yawezekana labda mtu huyo alikuwa na lengo baya la kutaka kumdhuru.Kwani ninyi ni akina nani? Ni polisi?" "Sisi ni watu tunaosughulika na usalama wa nchi na mtu ambaye dada yako amemuua alikuwa na taarifa muhimu sana kwa usalama wa nchi"Kwa hiyo nini mtamfanya dada yangu?Mtampeleka mahakamani? "Itategemea na ushirikiano wake kwetu.Kama akiendelea kuwa na kiburi itatulazimu kumkabidhi katika vyombo husika na atapelekwa mahakamani ambako atashtakiwa kwa makosa ya mauaji ya kuhatarisha usalama wa nchi.Kama jambo hili likifika huko basi dada yako hutamuona tena" "Tafadhali nawaomba msimfikishe dada yangu huko.Tafadhalini nawaomba mnisaidie mimi kwani ninamtegemea yeye kwa kila kitu.Wazazi wetu wote wamekwisha fariki na yeye ndiye baba na mama yangu kwa sasa." "Winnie tutakusaidia endapo tu utakuwa tayari kwenda kuzungumza na dada yao na kumshawishi atueleze kile tunachokitaka.Ukifanikiwa kumshawishi,suala hili litamalizika na dada yako atakuwa salama.Can you do that? "Ndiyo ninaweza kufanya.Nipeni dakika kadhaa nizungumze naye" "Tunakupa dakika tano zitumie vyema .Jitahdi ndani ya muda huo umshawishi akubali kutueleza kile tunachokihitaji.Kama akiendelea kuwa kiburi basi tutachukua hatua nyingine"akasema Elvis na kumpeleka Winnie chumbani alimo Vicky akamfungulia mlango na kuwaacha wazungumze . "Dada nimepewa dakika chache sana za kuzungumza nawe.Nina dakika tano hivyo naomba tujielekeze katika masuala ya msingi."akasema Winnie na Vicky akashangaa "Wamekueleza nini hawa jamaa? akauliza Vicky kwa wasi wasi "Everything.Wamenieleza kila kitu kilichotokea usiku wa leo.Je ni kweli umeua mtu? akauliza Winnie "Winnie listen to me.You dont have to trust these people.Right now you have to help me get ot of here.Dont believe them" akasema Vicky "There is no way you are going to get out of here.Just answer me is it true or not that you killed someone? "Winnie I'm your sister and you should be on my side and believe me not them" "Dada ninachohitaji kusikia kutoka kwako ni jibu la ndiyo au hapana.I want to help you so tell me the truth." Vicky akamtazama mdogo wake kwa hasira "Wamekufanya nini hadi unashindwa kuniamini mimi dada yako na badala yake unachagua kuwasikia hao mashetani? "Dada watu hawa wako kazini kwa hiyo wajibu wanachokuuliza.Kwa nini umemuua huyo mtu? "Winnie I love you so much but today you've dissaponited me.How come you dont trust me? "Dada unalifanya jambo hili liwe gumu hata kwangu pia.Wewe ndiye baba na mama yangu hivyo nakuomba usilifanye suala hili likachukua sura mpya.Bado nakuhitaji sana.Limalize suala hili hapa hapa lisifike mbali zaidi.Wajibu kwa nini umemuua huyo mtu na hicho ndicho wanachotaka kukisikia.Kama huwezi kufanya hivyo kwa ajili yako do it for me.I still need you" "Get out of here now!! akafoka Vicky "dada please!!! "Nimesema toka nje!! akasema Vicky kwa ukali na Winnie hakuwa na njia nyingine zaidi ya kuufungua mlango akatoka na kuwakuta Steve na Elvis nje ya mlango "Tafadh...................." akataka kusema kitu Winnie Elvis akamzuia "Tumesikia kila kitu.Ahsante kwa kujaribu" akasema Elvis na kuingia chumbani "Muda wa kucheza umekwisha sasa ni wakati wa kazi.Tumekupa muda wa kutosha lakini umeupoteza na hatuna tena muda mwingine wa kupoteza" akasema Elvis na kumtaka Steve amfunge kamba Winnie "Dont touch her!! akafoka Vicky lakini Steve kwa kutumia mikono yake yenye nguvu akamfunga Winnie katika kitu halafu akamfunga kitu fulani mdomoni cha kumzuia kutoa sauti.Macho yalijaa machozi.Steve akamwamgia ndoo ya maji na Elvis akakichomeka kifaa fulani katika umeme na kugusanisha ncha, cheche zikatoka.Vicky akapiga ukelele na kutaka kutoka pale kitandani lakini mkono mmoja na miguu vilikuwa vimefungwa kwa pingu na hakuwa na uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kupiga kelele akiwataka akina Elvis wasimtese Winnie "You have ten seconds to help her!! Elvis akamwambia lakini bado Vicky alikuwa mbishi akiendelea kutukana "I dont have a choice" akasema Elvis na kumgusisha Winnie zile waya za umeme na kumtetemesha.Vicky akafumba macho asikione kitendo kile namna mdogo wake alivyokuwa anateswa. "Help her tell us the trusth!! akasema Elvis lakini Vicky alikuwa analia tu na kuomba mdogo wake asiendelee kuteswa. "One more time!! akasema Elvis na kumchoma tena Winnie kwa umeme.Hakuweza kutoa kelele kutokana na kile kitu alichokuwa amefungwa mdomoni ila alipata mateso makali sana. "Unaturuhusu tuendelee? Elvis akamuuliza Vicky ambaye hakujibu kitu machozi yakimtoka "This is not working" akasema Elvis na kumtaka Steven amfungue Winnie halafu akachukua kifaa kidogo kinaitwa koleo na kisu kidogo "Unataka kufanya nini? akauliza Vicky "Ninamuondoa kucha zake zote bila ganzi nikianzia na kucha za mikononi na baadae mguuni.Kama utakuwa mbishi nitaondoa pia jino moja baada ya lingine na sina hakika kama mpaka wakati huo mdogo wako atakuwa bado mzima kwani maumvu atakayoyapata ni makubwa mno." "stop.Please stop !akasema Vicky "Are you ready now? akauliza Elvis "Nitawaeleza kila kitu mnachokitaka lakini msiendelee kumtesa mdogo wangu" akasema Vicky "Tell us" akasema Elvis.Vicky akavuta pumzi ndefu na kusema "Sina ujanja i have to tell you” akasema huku akihema kwa kasi “I'm a deep undercover agent" akasema Vicky na Elvis na Steve wakatazama "Undercover agent? Elvis akauliza "Ndiyo.Please take Winnie out of here first" akasema Vicky na Steve akamchukua Winnie akampeleka chumbani kwa Graca "Now we can talk.Tufafa nulie wewe ni nani na kazi zako ni zipi? "Naitwa Vicky.Mimi ni mfanya biashara maarufu hapa jijini lakini pia ninajishuhulisha na kazi ya ukahaba ambayo imenifanya nijulikane sana lakini ukahaba wangu mimi si wa kujipanga barabarani na kusubiri wateja bali ni kwa sababui maalum.Ninao wateja wangu maalum na wengi wao ni viongozi wakubwa serikalini watu maarufu matajiri na kiwango changu ninachowatoza ni kikubwa sana.Ninawatoza kuanzia milioni tano nakuendelea kwa usiku mmoja. Kazi hii ya ukahaba ninaifanya lakini nikiwa na kazi nyingine nyuma yake” “Vicky hatutaki kusikia kuhusu kazi yako ya ukahaba.Tueleze kile tunachotaka kukisikia”akafoka Elvis “Mimi ni jasusi wa siri sana ambaye ninafanya kazi maalum na kuripoti moja kwa moja kwa rais.Nilichukuliwa na rais na kupelekwa katika mafunzo nchi mbali mbali kwa siri na kuhitimu halafu nikaja kuanza kufanya kazi aliyotaka niifanye." KAZI GANI VICKY AMEPEWA NA RAIS AIFANYE? KWA NINI KAMUUA PASCAL? MPENZI MSOMAJI TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA SIMULIZI HII







    Mimi ni jasusi wa siri sana ambaye ninafanya kazi maalum na kuripoti moja kwa moja kwa rais.Nilichukuliwa na rais na kupelekwa katika mafunzo nchi mbali mbali kwa siri na kuhitimu halafu nikaja kuanza kufanya kazi aliyotaka niifanye." ENDELEA……………………………… "Tueleze kwa ufasaha umefahamiana vipi na rais hadi akakuchukua na kukupeleka mafunzoni.Ni mafunzo gani uliyapitia na kazi gani ambayo unaifanya hivi sasa? akauliza Elvis Awali kabla ya kuingia katika shughuli hizi nilikuwa na kijisehemu kidogo ninauza vinywaji.Baba moja namfahamu kwa jina moja tu la Gidioni alikuwa ni mteja wangu sana na kila siku lazima afike kupata kinywaji,alivutiwa nami na tukaanza kutoka.Baadae akanipa mtaji nikafungua baa kubwa ambayo ilijipatia umaarufu na wateja wengi na hapo ndipo nilipoanza kujulikana.Siku moja mzee Gidion alinieleza kwamba kuna mtu mmoja mzito anahitaji kuonana nami.Sikujua ni nani huyo mtu,jioni akanipeleka katika jengo fulani la ghorofa tukaingia ndani na kupanda hadi ghorofa ya sita na nikagundua kwamba ile ni klabu ya viongozi wakubwa na watu wazito.Tuliingia katika chumba fulani na nikastuka kumuona rais wa Tanzania mle ndani.Sikuwa nimetegemea kama siku moja ningekutana na rais wa nchi ana kwa ana.Rais Dastan Mkobolwa akanikaribisha vizuri na kwa upendo mkubwa na alinisihi nisiogope.Alinieleza kwamba kuna kazi anataka kunipa.Baada ya uchunguzi wa muda mrefu ameniona ninafaa kuifanya kazi yake.Alinieleza kwamba kabla ya kuifanya kazi hiyo lazima kwanza nikapate mafunzo nje ya nchi na nitakapokuwa tayari basi nitaanza rasmi kuifanya kazi hiyo.Alinielezea faida ambazo nitazipata endapo nitakubali kuifanya kazi yake na kwa sababu nilikuwa na hamu na mafanikio makubwa nikakubali bila kujua ni kazi gani rais anataka kunipa" Vicky akanyamaza kwa muda halafu akaendelea "Niliondoka nchini na kwenda nchini Ujerumani nikiwa sielewi ninakwenda kujifunza nini.Nilipokewa katika uwanja wa ndege na mtu maalum na kupelekwa katika chuo fulani cha mafunzo ya ujasusi.Nilianza mafunzo japo yalikuwa magumu lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo nilivyojikuta nikiyamudu na kuyapenda mafunzo yale.Baada ya kutoka Ujerumani nikaenda nchini Ufaransa nikajifunza tena kwa muda wa mwaka mzima na halafu nikaenda nchini Uingereza kujifunza tena kwa miezi sita.Baada ya hapo nikarejea nyumbani na ndipo rais akanipa kazi” akanyamza tena kidogo na baada ya muda akaendelea Mara tu alipochaguliwa,rais Dastan na http://deusdeditmahunda.blogspot.com/wakuu wenzake wa nchi za Afrika Mashariki kwa pamoja walikutana na wakuu wa umoja wa ulaya na kujadili kwa kina kuhusiana na biashara iliyoanza kushika kasi barani afrika ya kuuza binadamu kama watumwa.Kila nchi ilitakiwa kuunda kikosi maalum chenye watu waliopata mafunzo makubwa ya namna ya kubaini na kukabiliana na mtandao wa watu wanaofanya biashara hii haramu ya kusafirisha na kuuza binadamu kikosi ambacho kitafadhiliwa na umoja wa ulaya.Hapa Tanzania kiliteuliwa kikosi cha watu sita kwa ajili ya kuendesha zoezi la kubaini mtandao wa watu wanaojishuhusisha na biashara ya binadamu.Watatu kati yetu tayari wamekwisha fariki dunia na tumebaki watu watatu.Ofisi yetu iliunganishwa na ofisi nyingine kama hizi katika nchi nyingine za bara la Afrika kwa lengo la kupeana taarifa lakini baada ya wenzetu watatu kufariki dunia ikabainika kwamba kuna viongozi katika baadhi ya nchi wanafanya hujuma ili kikosi hiki kishindwe kufanya kazi zake na baadhi yetu kuuawa kwani wana mahusiano na watu wanaofanya biashara hii na kuna faida wanazipata hivyo mtandao wa kikosi hiki ukavunjika na kila nchi ikaanza kujitegemea yenyewe.Baada ya hilo kutokea wenzangu wawili wakapelekwa katika idara ya usalama wa taifa na mimi nikapewa kazi nyingine.Rais alinitaka nifanye uchunguzi kuhusiana na mtandao unaofanya biashara ya kuuza silaha.Alipata tetesi kwamba waasi wanaopambana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo wanapata silaha zao kutokea Tanzania.Alitaka kujiridhisha na tetesi hizi kama ni za kweli na kama ni kweli niwabaini watu hao ni akina nani" akanyamaza.Elvis na Steve wakatazamana na halafu Elvis akampa ishara Steven ya kumfungua pingu Vicky. “Thank you” akasema Vicky baada ya kufunguliwa "Endelea" akasema Elvis.Vicky akaomba maji akanywa kulainisha koo halafu akaendelea "Nilianza kufanya uchunguzi wangu kuubaini mtandao huu unaojishughulisha na biashara ya silaha lakini mpaka sasa bado sijafanikiwa kuubaini.Watu hawa ni makini sana na wanafahamu kuwa biashara wanaoifanya ni haramu hivyo wanachukua kila tahadhari ya kuhakikisha hawafahamiki na mpaka leo bado sijafanikiwa kuwafahamu.Wakati nikiendelea na uchunguzi huo nimekuwa pia nikifanya kazi mbali mbali anazonipa rais.Naweza kusema kwamba nimekuwa mpelelezi maalum wa rais.Ili kufanikisha baadhi ya kazi ambazo nimekuwa nikipewa na rais imenilazimu kujigeuza kahaba.Kupitia kazi yangu ya ukahaba nimekuwa nikitembea na watu mbali mbali hasa viongozi wa serikali ninaotakiwa kuwachunguza.Nimekuwa nikipata taarifa mbali mbali toka kwao na kumpatia rais.Kwa kifupi hiyo ndiyo kazi ninayoifanya pembeni ya biashara zangu.Vipi kuhusu ninyi,who are you?akauliza Vicky "Ahsante Vicky kwa kujitambulisha.Tumefurahi kukufahamu kwani utakuwa na msaada mkubwa kwetu zaidi ya tulivyotarajia"akasema Elvis na kunyamaza kidogo halafu akaendelea Mimi naitwa Elvis tarimo na yule mwenzangu anaitwa Steve Kinke sote tunafanya kazi katika idara ya ujasusi" "Good to hear .But Elvis you are supposed to be dead" "I'm not dead” "Ilitokeaje hadi ukafanikiwa kumuaminisha kila mtu kuwa umefariki?akauliza Vicky "Tusipoteze muda tafadhali katika hilo,tujielekeze katika mambo ya msingi.Labda nianze na maelezo mafupi ili tuelewane vizuri" akasema Elvis "Kuna msichana mmoja anaitwa Graca ambaye ni mtoto wa mtu mmoja anaitwa brigedia Frank Kwaju.Huyu msichana alikuwa katika hospitali ya magonjwa ya akili nchini Afrika kusini na nilimtorosha nikamleta hapa Tanzania kutokana na kuwa na taarifa nyeti sana kuhusiana na baba yake. Graca aliwahi kupewa kompyuta na mama yake ambayo aliiba kutoka katika ofisi ya nyumbani ya Frank na kumtaka akaifiche sehemu salama.Kompyuta hiyo ilileta mtafaruku mkubwa sana baina ya wazazi wake na siku chache baadae mama yake akafariki katika ajali tata.Kilichoendelea hapo ni mtafaruku baina ya Frank na mwanae Graca.Frank alimpa vitisho vingi sana akimtaka arejeshe kompyuta hiyo.Pamoja na masahibu mengi yaliyomkuta lakini Graca hakuwahi kuirejesha kompyuta ile kwa Frank bali aliificha sehemu salama.Nimefanikiwa kuipata kompyuta hiyo yenye siri nyingi za Frank.Baada ya kupitia mafaili yaliyomo katika kompyuta hiyo nimegundua kwamba Frank akishirikiana na Pascal Situmwa wanashiriki katika biashara haramu ya silaha.Wanawauzia silaha waasi wanaopambana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo" "Real?! akauliza Vicky kwa mshangao mkubwa "Nilipopekua mawasiliano yake nikakuta kuna maelekezo amekuwa akipokea kutoka kwa mtu anayejiita Deusdedith MM.Huyu amekuwa akimpa maelekezo mengi na inaonekana ni mtu mwenye sauti katika mtandao huu.Katika moja ya mawasiliano yao Deusdedith MM amemuelekeza Frank kwamba akutumie wewe katika kumuua kanali Norman.Hii inakufanya uwe mtu muhimu sana kwetu kwani tayari unashirikiana na watu tunaowachunguza.Nataka tuanzie hapo.Deusdedith MM ni nani? akauliza Elvis.Vicky akavuta pumzi ndefu na kusema "Nilipoanza uchunguzi kuhusiana na mtandao wa biashara ya silaha ilinichukua muda mrefu hadi kubaini kwamba kuna mtu anaitwa Deusdedith MM ambaye anahusika na mtandao huu.Huyu ni mfanya biashara mkubwa na tajiri mwenye makazi yake nchini Uingereza na vile vile ana makazi afrika ya kusini.Ilinilazimu kuanza kumfuatilia ili kuubaini ukweli.Niligundua huyu jamaa anapenda sana kwenda katika makasino na ikanilazimu kuishi Afrika kusini kwa muda nikimuwinda.Nilijifanya kahaba katika moja ya kasino analolimiliki na nikafanikiwa kumuweka karibu.Alinipenda zaidi alipogundua kwamba ninatokea Tanzania.Mimi na yeye tukawa na mahusiano ya siri huku nikiendelea kumchunguza" "Uligundua nini katika uchunguzi wako?akauliza Elvis "Deus ni mtu makini sana na anafahamu kujificha.Katika uchunguzi wangu wote sikuwahi kubaini chochote kuhusiana na yeye kuhusika katika biashara ya silaha.Nilizifahamu biashara zake za halali kama vile maduka makubwa ya kuuza magari ya kifahari Dubai.Nchini uingereza ana duka la bidhaa za asili za Afrika na kasino.Anazo biashara nyingine pia nchini Afrika kusini,Urusi na Italia.Vile vile anazo biashara za siri lakini anajua mno kuzificha na sikuwahi kufanikiwa kuzifahamu" "Stupid" akawaza Elvis "Deus alininitaka nirejee Tanzania kuna kazi anataka kunipa ambayo nikiikamilisha atanilipa feda nyingi sana.Nilikubali kurejea Tanzania kuifanya kazi yake na baada ya miezi miwili toka nirejee Tanzania alinifuata Frank na kunieleza kwamba amepewa maelekezo na Deus aje anione anipe kazi.Alinieleza kwamba kuna mtu anahitajika kuuawa ambaye ni kanali Norman.Sikuweza kukataa kwani nilitaka bado kuendelea kuwa karibu na Deus.Nilianza ukaribu na Norman na muda ulipofika ikanilazimu kumuua.Nilipoikamilisha shughuli hiyo Deus alinilipa fedha nyingi sana na kunitaka nisiendelee tena na kazi ya ukahaba na wala nisirejee tena Afrika kusini bali nianzishe biashara hapa hapa Tanzania na ndipo nikaamua kujenga ile hoteli.Huo ndio ulikuwa mwisho wa mawasiliano yangu na Deus kwani hakupatikana tena katika namba za simu wala katika barua pepe.Aliuza biashara zake zote nchini Afrika kusini.Deus ni mtu mmoja makini sana na anajua kujificha.Baada ya kumpoteza Deus ilinilazimu kuanza kujenga mahusiano na akina Frank ili niwachunguze kwani niliamini lazima watakuwa na mahusianona Deus lakini kila nilipojitahidi kujiweka karibu nao walinikwepa kabisa lakini sikukata tamaa nikaendelea kuwachuguza hadi pale ulipojitokeza na kuanza kunichunguza ukijiita Robin.Niliwaeleza kwamba kuna mtu ananichunguza ili kujiweka karibu zaidi nao, wakanipeleka mafichoni katika shamba la Frank nikaishi huko kwa siku chache hadi nilipoambiwa kwamba umekufa" "Nini umekigundua kutoka kwa akina Frank? Elvis akauliza "Sijagundua chochote bado japo ninafamu kuna mambo wanayafanya kwa siri na wana mahusiano na Deus" "Wewe ni mpelelezi wa aina gani uliyeshindwa hata kuwachuguza panya wadogo kama Frank na mwenzake?akauliza Steve kwa ukali "Taratibu Steve" akasema Elvis "It's not easy like you think.These peole are very smart.Wanajihami kwa kila namna wawezavyo hivyo ni ngumu kuwapata kirahisi" "Umefanya kazi nzuri Vicky japo hujaweza kufika mwisho lakini hapa ulipofika ni pakubwa.Kuna jambo nataka kulifahamu.Kwa nini ulimuua Pascal? akauliza Elvis "Kama nilivyosema kwamba ulipoanza kunichunguza niliwaeleza akina Frank na wakanieleza kwamba wewe ni mtu wa usalama na wakanipeleka mafichoni katika shamba la Frank.Nikiwa kule nilisikia mazungumzo yao Pascal akimshinikiza Frank waniue kwani tayati nimekwisha kuwa hatari kwao lakini Frank alikataa kwa vile alikuwa ananihitaji kingono.Mlipotaka nimuite Pascal pale hotelini nilijua mtampeleka kumuhoji na kwa vile mtandao wao ni mrefu angeweza kuachiwa na kama angeachiwa huru basi lazima angeniua ndiyo maana nikamuua"akasema Vicky "Maelezo yako bado hayajajibu swali kwa nini ulimuua Pascal?Sababu ulizotoa hazijitoshelezi kabisa.Tushawishi tukuamini kwamba yale yote uliyotueleza ni ya kweli" akasema Elvis "Yote niliyowaeleza ni ya kweli kabisa.Pascal alikuwa ni mtu anayeniwinda aniue na ile ilikuwa ni nafasi yangu nzuri ya kumuwahi" "Hukufikiri kwamba kitendo kile kinaweza kukuweka hatarini na hata kukuharibia kabisa maisha yako? "Hilo haliwezi kutokea kwa sababu nina ngao kubwa.Rais asingeweza kukubali niingie katika matatizo ndiyo maana sikusita kumuua Pascal.Nisingefanya hivyo angeniwahi kwani alikuwa na mpango huo" akasema Vicky "Ulifanya kosa kubwa sana kumuua Pascal kwani alikuwa ni mtu muhimu sana kwetu na angeweza kutupa taarifa nyingi za kutusaidia katika uchunguzi wetu.Hata hivyo umezungumzia kuhusu akina Pascal kuwa na mtandao mkubwa,unataarifa zozote kuhusiana na mtandao wao? "Ninafahamu wanao mtandao mrefu lakini bado sijafanikiwa kuubaini" What kind of agent are you?Mbona kila kitu hujafanikiwa? akauliza Steve kwa ukali "Steve taratibu,usiwe na hasira"akasema Elvis na kumtaka Steve watoke nje ya kile chumba wazungumze "Elvis this woman il lying to us" akasema Steve "Nisikilize Steve" "Tumeianza operesheni yetu na huyu Vicky anazo taarifa zinazoweza kutusaidia hivyo tumsikilize na kuna mambo tunaweza kuyapata toka kwake ambayo yanaweza yakatusaidia" "I don't believe her.Kwa nini kila kitu hafanikiwi?Do you believe her? Yes I do believe her.She's telling te truth" akajibu Elvis "Nakuomba tumuhoji taratibu ili atueleze kila kitu anachokifahamu.Niachie mimi nitazungumza naye" akasema Elvis kisha wakarejea ndani "Vicky nieleze tena kuhusu huyu Deusdedith MM namna unavyomfahamu.Ni mtu wa aina gani? Ana familia?Anapendelea vitu gani? "Kama nilivyokueleza awali kwamba Deus ni mtu anayejua sana kujificha.Tabia zake haziweki wazi hivyo ni vigumu sana kumfahamu ni mtu wa namna gani.Ninachoweza kusema ni mtu anayebadilika badilika kama kinyonga.Unaweza ukadhani havuti sigara lakini ukamkuta anavuta,naweza kusema ni mtu mwenye kubadilika kila mara.Kuhusu familia anayo familia lakini sikubahatika kuifahamu wala mke wake sijawahi kumuona.Ni watu wanaojificha sana.Nimewapa maelezo mengi kuhusu mimi ni zamu yenu sasa kunijibu na mimi kwa nini mlikuwa mnamtaka Pascal? akauliza Vicky "Tulimhitaji Pascal kwa mambo mawili.Kwanza kumuokoa na pili kupata taarifa za muhimu kutoka kwake zitakazotusaidia kuubaini mtandao unaojishughulisha na uuzaji wa silaha " "Mlitaka kumuokoa? Ndiyo.Pascal alikuwa anatakiwa kuuawa" "Nani walitaka kumuua? "Bado hatuna taarifa za kutosha ni nani walitaka kumuua na tulikuwa katika kuwatafuta watu hao ila tunahisi ni watu anaofanya nao biashara" akasema Elvis "Mshirika wake mkubwa ni Frank kama ni wenzake wanataka kumuua basi lazima Frank atakuwa analifahamu jambo hilo" akasema Vick "Vicky limekuwa jambo zuri tumekutana wote tukiwa na lengo moja.Sote tunautafuta mtandao wa kuuza silaha.Ninakuomba uungane nasi katika kuusaka mtandao huu na kuufutilia mbali" akasema Elvis "Hata mimi nimefurahi kukutana nanyi na nina uhakika mkubwa kwamba kama tukishirikiana na kuunganisha nguvu tutafanikiwa kuusambaratisha mtandao huu ambao peke yangu nimejitahidi kuutafuta bila mafanikio.Ninyi wenzangu mnaonekana mnao uzoefu mkubwa sana katika masuala haya tofauti na mimi.Naamini nitapata fursa nzuri ya kujifunza kutoka kwenu" "Usemayo ni ya kweli Vicky,mtandao kama huu hauwezi ukapambana nao mtu mmoja,mnapaswa kunganisha nguvu.Utakuwa ni msaada mkubwa sana kwetu.Karibu kwenye timu" akasema Elvis "Ahsante sana Elvis" "Naamini utatusamehe kuhusu mdogo wako Winnie lakini hatukuwa na namna ya kukufanya ufunguke zaidi ya kumtumia yeye.Ni kwa sababu yake tumeweza kugundua kwamba nawe ni mwenzetu lakini bila kufanya vile usingeweza kufunguka na tungeendelea kutesana hadi asbuhi"akasema Elvis "Kabla hatujaendelea mbele naomba niwaweke wazi jambo moja.Mimi ninayo timu yangu ambayo wananifuatlia kila mahala ninapokwenda kwa kutumia vifaa maalum.Hata sasa wanajua kuwa niko hapa na kwa mujibu wa taratibu zetu kila baada ya saa sita natakiwa kubonyeza namba fulani katika simu yangu kuwataarifu wenzagu kuwa niko salama na nikichelewa kufanya hivyo basi wataamni niko katika hatari na watavamia.Sitaki wavamie hapa hivyo naomba simu yangu niwasiliane nao kwa sababu saa inanionyesha kuwa muda wangu wa kubonyeza namba umekaribia" akasema Vicky.Elvis akamfanyia ishara Steve ailete simu ya Vicky ili aweze kubonyeza namba "Ahsante Elvis .Wewe unaonekana ni mtu mwenye kuelewa haraka sana tofauti na huyu mwenzako Steve.Mpaka sasa anaonekana bado hajanikubali na haniamini kabisa" "Binadamu tuko tofauti sana na Steve ndivyo alivyo huwa hamuamini mtu haraka haraka.Mvumilie kwa maneno na maswali yake lakini atakuelewa tu" "What about you.Do you believe me? Do you trust me?Vicky akauliza,Elvis akamtazama akatabasamu kwa mbali na kusema "Sina sababu ya kutokukuamini wakati macho yako yananionyesha kwamba unasema ukweli,ila nikigundua kwamba kuna udanganyifu wowote nakuhakikishia utajuta kunifahamu.Mimi ni mtu mbaya sana ninapodanganywa" "I can see both angel and devil in your eyes.Kuna nyakati unakuwa malaika lakini kuna nyakati unakuwa shetani.Hata hivyo you are not a bad person" akasema Vicky na mlango ukafunguliwa akaingia Steve akiwa na simu ya Vicky akampatia kisha akaziandika namba fulani katika simu yake na kuiweka pembeni "Sasa tunaweza kuendelea"akasema "Lengo letu kuu bado ni lile lile kuutafuta na kuusambaratisha mtandao wote wa watu wanaofanya biashara ya kuuza silaha kwa waasi wa Congo.Mtandao huu ni mkubwa na unawahusisha watu walioko hapa Tanzania,Congo na hata nje ya nchi.Tunaanza kwanza na hawa waliopo Tanzania kwa sababu silaha zote zinapitia hapa.Tutawasambaratisha wote na hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe.Hakuna anaeshiba kwa fedha za mauzo ya silaha atabaki salama.Wote lazima wakutane na mkono wa sheria.Hii ni ahadi yangu na ni lengo letu sote hivyo tuhakikishe tunalitimiza.Vicky wewe tutakutumia sana katika kupata taarifa mbali mbali.Unatakiwa kumuweka Frank katika himaya yako na kisha upate taarifa za muhimu kutoka kwake.Naamini hili utalitekeleza vyema kwani liko ndani ya uwezo wako.Frank ndiye kinara wa biashara hii ambaye tunamfahamu hadi sasa na kupitia huyo tutaufahamu mtandao wote unaohusika na biashara hii hivyo unapaswa kuwa karibu naye sana"akasema Elvis "Frank ni dhaifu sana kwangu na ninao uwezo wa kumfanya chochote" akasema Vicky "Good.Utautumia udhaifu huo ili kuweza kutusaidia kupata taarifa za muhimu kuhusu watu anaoshirikiana nao katika biashara hiyo ya silaha.Hakikisha umekutana naye kesho na ufanye kila uwezalo uipate simu yake na ndani ya muda mfupi utaingiza namba fulani nitakazokupatia katika simu yake ambazo zitatuwezesha kupata mawasiliano yake yote.Tutajua anawasiliana na nani na wanaongea kuhusu nini.Tunaweza kufanikiwa kunasa jambo kupitia mawasiliano yake" "Hilo ni wazo zuri lakini watu hawa ni makini sana na wanajua kuficha mambo yao hata hivyo nitafanya kama ulivyoniagiza" "Jambo lingine tunataka kumchunguza pia makamu wa rais Dr Shafi ambaye tunahisi anaweza kuwa anahusiana na mtandao huu.Makamu wa rais ndiye aliyetoa amri mimi niuawe na ndiye aliyetoa maelekezo Pascal auawe pia."akasema Elvis Makamu wa rais?!! Vicky akashangaa 'Ndiyo.Mimi sifahamiani naye hata kidogo lakini alitoa maelekezo niuawe.Lazima kuna jambo kwani hawezi akatoa maelekezo kama yale kama hakuna sababu ya msingi .Lazima kuna mahala nimemgusa na ndiyo maana akaamua kutumia nguvu yake ili kuniondoa.Nina hisi lazima atakuwa na mashirikiano na akina Frank japo kwa siri sana.Huyu naye anapaswa kuchunguzwa pia" akasema Elvis "Nimestuka sana kusikia kuwa ni makamu wa rais ndiye aliyetoa maelekezo ya kuuawa wewe na Pascal.Kama unavyosema lazima kuna sababu kubwa.Sina mahusiano yoyote na makamu wa rais lakini tunaweza kutafuta namna ya kumchunguza" akasema Vicky na kuinamisha kichwa akafikiri kwa muda na kusema "Ofisi ya makamu wa rais ndiyo inayojishughulisha na masuala yote ya mazingira.Tumtafute mwanamke mmoja mrembo sana ambaye atajifanya ni mwandishi wa habari za mazingira kutoka nje ya nchi na ambaye mipango itafanyika ili aweze kukutanishwa na makamu wa rais.Nitazungumza na rais na kumtaka amuunganishe huyo mwanamke na makamu wa rais na tutamtumia katika kumchunguza.Ninaye rafiki yangu ambaye tunaweza kumtumia katika shughuli hiyo ambaye tulikuwa naye mafunzoni anaitwa Omola Otola.She's pretty like me but she's a professional hacker.Hakuna mtandao asioweza kuudukua.Kwa sasa anafanya kazi zake nchini Afrika kusini akiwa na kampuni fulani ya uchunguzi akichunguza mtandao wa biashara ya pembe za ndovu.Nitamuomba aje atusaidie katika shughuli hii kama mtaridhia lakini atahitaji malipo makubwa.Atalipiwa tiketi ya ndege ya kuja na kurudi mara atakapomaliza kazi yake,hoteli nzuri atakakofikia kwa muda wote atakaokuwa hapa nchini na malipo yake ya kufanya kazi.Japo malipo yake ni makubwa lakini ni mtu sahihi tunayeweza kumtumia katika kuifanikisha kazi yetu.Kupitia kwake tunaweza kupata taarifa zote tunazozihiaji kuhusu makamu wa rais" akasema Vicky "Una mawazo mazuri kama ilivyo sura yako" akasema Steve na kutabasamu "Ni wazo zuri sana hilo Vicky.Kuhusu gharama usihofu tutamlipa kiasi chochote atakachokihitaji,pesa si tatizo.Tena itakuwa vyema kuongeza mtu mwingine katika timu yetu kwani tunahitaji sana mtaalamu wa teknolojia.Sote tunaweza kucheza na kompyuta lakini tukimpata mtaalamu zaidi ambaye ana ufundi wa hali ya juu wa kucheza na mitandao itakuwa vyema zaidi." "So can I call her right now? akauliza Vicky "Ndiyo" akajibu Elvis na Vicky akachukua simu yake akazitafuta namba fulani akapiga.Akazungumnza kwa takribani dakika ishirini halafu akakata simu "Omola ana kazi nzito sasa hivi lakini nimemuomba sana aje anisaidie.Ni rafiki yangu mkubwa na amesema atanipa jibu kabla ya saa tatu kesho asubuhi kama atakuwa na uwezo wa kuja au vipi.Tuombe akubali" "Ok good.Tutasubiri hadi muda huo na kama akishindwa kuja basi tutatafuta namna nyingine"akasema Elvis na wakaendelea na kupanga mikakati mingine namna ya kufanikisha jukumu lile hadi mshale wa saa ulipoonyesha ni saa kumi na moja na dakika nane. "Umekuwa ni usiku mrefu sana.Kwa sasa baada ya kuwa kitu kimoja mnaweza mkaturuhusu mimi na Winnie tukapumzike nyumbani ili niweze kujiandaa kwa kazi kubwa inayotukabili? akauliza Vicky "Hakuna shaka mnaweza kwenda kupumzika.Mtatumia mojawapo ya magari tuliyonayo hapa ila tukutane saa nne za asubuhi kwa mipango zaidi.Halafu kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kukizingatia ni kwamba usithubutu kumueleza rais kwamba kuna watu unashirikiana nao au hata kutaja jina langu kwani mke wangu ni daktari wa mke wa rais na wanafahamu kuwa nimekufa.Wakijua niko hai inaweza kuvuruga mambo yote.Kwa taarifa yako hata mke wangu hajui kama niko hai"akasema Elvis "Mkeo hajui kama uko hai?! akashangaa Vicky "Ndiyo hafahamu chochote kama niko hai" "Dah huu ni uongo mkubwa sana lakini katika kazi hizi kuna nyakati inabidi kutumia mbinu kama hizi ili kufanikisha mambo muhimu" akasema Vicky na mlango ukafunguliwa akaingia Steve akiwa amemshika mkono Winnie ambaye alikuwa analia "Tafadhali usilie Winnie" akasema Elvis "Mnataka kunitesa tena? akauliza Winnie "Hapana Winnie.Yale mambo yamekwisha na hautateswa tena" akasema Vicky "Winnie I'm sorry for what happned.Halikuwa lengo letu kukuumiza lakini ilitulazimu kufanya vile ili kumfanya dada yako atupe taarifa fulani muhimu.Kwa sasa tumekwisha elewana na tumekuwa kitu kimoja" akasema Elvis "You are all monsters!! akasema Winnie kwa hasira Nataka kwenda nyumbani!! akasema Winnie " Guys we have to go now.Tutaonana hiyo baadae" akasema Vicky kisha wakaelekezwa gari la kutumia wakaondoka. "Imekuaje ukamuamini yule kahaba haraka namna hii hata ukamjumuisha katika timu? akauliza Steve baada ya akina Vicky kuondoka "Macho yake yananionyesha kuwa anachokiongea ni cha kweli na halafu atakuwa na msaada mkubwa kwetu.Ni mwanamke mwenye kufikiri haraka haraka sana na anazo mbinu nyingi za kufanikisha mambo.Katika operesheni kama hii mwanamke kama Vicky ni muhimu mno kuwa naye" "Elvis wewe ni kiongozi wangu na sikupingi katika maamuzi yako ila suala la ka Vicky katika mpango huu bado linanipa mashaka sana.Ni mapema mno kumuamini"akasema Steve "It's not a mistake Steve.Haikuwa rahisi hata kwangu kumuamini lakini moyo wangu umenituma nimuamini na ninakuomba nawe umshirikishumuamini.Atatusaidia sana katika mambo mengi.Tupumzike kidogo kwani usiku umekuwa mrefu sana lakini wenye mafanikio"akasema Elvis na kila mmoja akaenda chumbani kwake kupumzika







    Safari ya Vicky na mdogo wake Winnie ilikuwa ya kimya kimya na njia nzima Winnie alikuwa anadondosha machozi "Nyamaza kulia Winnie"akasema Vicky "Vicky naomba usinisemeshe kabisa.Sitaki kuisikia sauti yako! akasema Winnie kwa ukali "Nafahamu umekasirika sana Winnie kwa mambo yaliyotokea usiku wa leo lakini nakuahidi tukifika nyumbani nitakueleza kila kitu" "Sitaki kusikia chochote kutoka kwako.What kind of sister are you?Unawezaje kuwaacha wale jamaa wanitese namna ile kwa kunichoma na umeme huku ukiangalia? Vicky akameza mate,alionekana kuumizwa sana na kauli ile ya Winnie "Winnie I'm sorry !!akasema na kwa mbali akalengwa na machozi "Sorry?! akauliza Winnie. "Winnie hatuwezi kuzungumza suala hili barabarani.Tutazungumza tukifika nyumbani ni suala pana sana ila kitu kimoja tu ambacho nataka ukifahamu ni kwamba I love you so much and I wont let anybody hurt you" akasema Vicky na safari ikaendelea *************** Saa kumi na mbili na dakika nane za asubuhi Patricia akaamka na kitu cha kwanza alichokifanya ni kuwasha simu yake na jumbe nyingi zikaingia toka kwa watu mbali mbali.Hakujishughulisha nazo akazitafuta namba za Doren akampigia na kumjulia hali halafu akamuuliza endapo anazo namba za Meshack Jumbo "Meshack Jumbo?!! Doreen akashangaa "Ndiyo.Yule bosi wake na Elvis tuliyekuwa naye msibani" "Kuna tatizo gani Patricia? akauliza Doreen kwa wasi wasi "Ninahitaji kuonana naye ni suala binafsi" akasema Patricia na Doreen akampatia namba za Meshack Jumbo "Ahsante Doreen tutawasiliana baadae.Nitakuelekeza mahala nilipo ili uje tuwe wote kwa sababu na hapa pia wana msiba wamefiwa na baba yao" akasema Patricia wakaagana.Patricia hakupoteza muda akampigia Meshack "Hallow" ikasema sauti ya upande wa pili "Shikamoo mzee" akasema Patricia "Marahaba.Nani mwenzangu? "Ni mimi Patricia mke wa Elvis" "oh Patricia.Habari yako? Vipi maendeleo yako?"Ninaendelea vizuri mzee.Nakushukuru sana kwa msaada wako mkubwa kwa wakati wote wa msiba wa Elvis" akasema Patricia na kuhisi analengwa na machozi "Usijali Patricia.Elvis alikuwa kijana wangu niliyempenda sana." "Mzee samahani nimekusumbua asubuhi hii.Ninahitaji kukuona baadae kidogo nina shida ya muhimu sana na ni wewe tu unayeweza kunisaidia kuitatua shida hiyo" akasema Patricia "Usijali Patricia muda wowote utakaokuwa na shida nitakuwa tayari kukusaidia.Unataka tuonane saa ngapi na wapi? Nataka tuonane asubuhi hii mahala utanielekeza mwenyewe" akasema Patricia na kisha mzee Jumbo akamuelekeza mahala mbako alitaka wakutane halafu wakaagana "Lazima nimsaidie Juliana ili aweze kuwapata wale waliomuua mdogo wake Godson.Mimi na yeye sote tuko katika jahazi moja la kufiwa na wapendwa wetu.Ninataka waliomuulia mpenzi na mdogo wake wakamatwe kwa sababu ninafahamu machunguya kufiwa na umpendaye.Japo ni muda sasa umepita lakini machungu ya kufiwa huwa hayasahauliki na hayazoelezi.Ni kidonda kisichopona.Mimi pia ninataka waliomuua mume wangu nao pia wakamatwe na wafikishwe mbele ya sheria" akawaza Patricia na kusikia sauti za watu wakizungumza akafungua pazia akaona mafundi wakiwa katika harakati za kujenga hema kwa ajili ya waombolezaji watakaoanza kufika mapema asubuhi "Patricia anahitaji nini hadi akataka tuonane asubuhi hii? au kuna fununu tayari amekwisha zipata kuhusiana na kifo cha Elvis? akawaza Meshack Jumbo halafu akachukua simu yake na kuzitafuta namba mpya za Elvis akampigia "Mzee shikamoo"akasema Elvis baada ya kupokea simu Marahaba Elvis.Habari za asubuhi? Vipi maendeleo yenu hapo? "Tunaendelea vyema mzee.Usiku ulikuwa mrefu sana lakini kuna mafanikio tumeyapata,tutazungumza utakapofika huku baadae" "Vizuri sana.Nitafka huko lakini kuna jambo lililonifanya nikupigie asubuhi hii.Patricia kanipigia simu muda si mrefu na amenitaka tuonane asubuhi ya leo tuzungumze" "Patricia?! Ana tatizo gani?akauliza Elvis ambaye kila akisikia jina patricia likitajwa hustuka sana "Hajanieleza ni tatizo gani ila amesema kwamba ana tatizo na mimi ndiye mwenye uwezo wa kumsaidia tatizo lake" akasema Meshack.Elvis akavuta pumzi ndefu "Sawa mzee.Utanijulisha mara utakapoonana naye" "Sawa Elvis.Nikitoka kuonana naye nitakuja huko" akasema Meshack na kukata simu ****************** Tayari kujua kimeanza kuchomoza na tayari mafundi walikwisha wasili nyumbani kwa Elizabeth na kuanza kufanya maandalizi ya kujenga mahema kwa ajili ya waombolezaji watakaofika msibani.Elizabethakiwa amezama katika maongezi na mtu kwenye simu kengele ya mlangoni ikalia akaenda kuufungua mlango akakutana na msaidizi wake Rosemary na ikamlazimu Elizabeth kumuomba mtu aliyekuwa anazungumza naye kumsubiri kidogo "Rose karibu" "Ahsante madam.Samahani sikujua kama uko simuni." "It's ok.Nilikuwa nazungumza na watu walioko Uingereza kwa ajili ya taratibu za kusafirisha mwili.Huko nje kila kitu kinakwenda sawa?maandalizi yamekwisha anza? "Ndiyo madam.Kila kitu tayari kinakwenda vizuri.Viti vimewasili na hata mpambaji tayari amekwisha anza kazi" "Good" "Madam kuna mtu amekuja anahitaji kukuona" "Ni nani? Hujamueleza kwamba huwa sionani na watu asubuhi namna hii? "Walinzi walimueleza hivyo lakini akasisitiza kwamba ni muhimu akaonana nawe ndipo waliponiita nikaongea naye na akasema kwamba anahitaji sana kuonana nawe asubuhi ya leo" "Ni nani huyo anayesisitiza kutaka kuonana nami asubuhi namna hii? "Ni Brigedia Frank" Elizabeth akafikiri kwa muda na kusema Ok.let him in" akasema Elizabeth na kuingia chumbani kwake kujiandaa kwani alikuwa katika vazi la kulalia.Akatoka chumbani na kuelekea seuleni akakutana na Frank ambaye alisimama kwa adabu alipomuona Elizabeh akamsalimia "Madam Elizabeth" akasema Frank "Frank.Karibu sana" "Ahsante madam" akasema Frank "Vipi mbona asubuhi namna hii? Kwema huko utokako?akauliza Elizabeth "Huko kwema madam lakini si kwema sana.Kwanza kabisa utanisamehe kwa kukusumbua asubuhi namna hii.Nafahamu huu si utaratibu wako lakini imenilazimu kuja mida hii kwani nisingeweza kupata nafasi ya kuonana nawe baadae tukazungumza kutokanana kutingwa sana na shughuli za msiba.Kabla sijaeleza kilkichonileta hapa,niruhusu nikupe pole nyingi sana kwa msiba uliokupata.Nilistuka sana uliponiambia kwamba Sir Deus amefariki dunia.Sikuwa na taarifa hizo na nikashangaa kwa nimi madam ulinitenga hukunijulisha kuwa bosi wangu amefariki dunia"akasema Frank "Wengi bado hawafahamu kama Frank amefariki dunia.Tumewajulisha watu wachache tu kuhusiana na kifo hiki.Nimefanya hivi kwa sababu maalum kwa hiyo usihofu.Kuondoka kwa Deus hakutaathiri chochote,kila kitu kitaendelea kama kawaida kwa sababu mimi nipo.Mimi ndiye mkuu kwa sasa" "Nimekuelewa madam" "Tuachane na hayo.Nini kimekusibu asubuhi yote hii?Sikuwa nimepanga kuonana nawe leo hadi pale nitakapomaliza msiba ndipo ningekutana nawe na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu mambo mbali mbali" "Madam utanisamehe kwa kuvuruga ratiba zako lakini nimeshindwa kabisa kupata usingizi hivyo ikanilazimu kuja kukuona ana kwa ana" Nini kimekukosesha usingizi? akauliza Elizabeth "Kwanza ni taarifa za kifo cha Deus na pili ni jambo lililotokea jana usiku" "Frank nilikupigia simu na kukujulisha kuwa usifanye chochote kuhusiana na kifo cha Pascal ambaye ameuawa kwa sababu maalum na mimi ndiye niliyeagiza jambo hilo lifanyike kwa hiyo sitaki maswali kuhusu jambo hilo"akasema Elizabeth "Madam Elizabeth ninakuhesimu sana na sitaki kukukosea adabu lakini ninahitaji kueleweshwa japo kidogo nini hasa kilichopelekea Pascal akauawa?Alifanya jambo gani baya?Ninamfahamu Pascal nimekuwa naye katika biashara yetu kwa muda mrefu na amekuwa msaidizi wangu mzuri.Toka nilipomfahamu hadi sasa sijaona tatizo lake.Utendaji kazi wake ni mzuri na zaidi ya yote amekuwa ni chanzo kizuri sana cha taarifa kwetu na mara nyingi nimekuwa nikikueleza kuhusiana na kazi nzuri anayoifanya.Mambo haya ndiyo yanayonisukuma kutaka kujua ni kwa nini ameuawa?tafadhafali madam"akasema Frank "Frank unanifahamu vyema mimi huwa sipendi ubishani.Nimekwisha kupa maelekezo kwamba suala la Pascal ni suala langu mwenyewe na uachane nalo.Tafadhali nakuomba usiendelee na hili suala!! akasema Elizabeth akionekna kuwa mkali kidogo "Sawa madam nimekusikia lakini ninaomba nikupe maelezo kidogo kama utaniruhusu" "Go ahead" akasema Elizabeth "Nilikueleza kuhusiana na Elvis kufahamu biashara yetu na kuanza kutuchunguza.Alifahamu pia kuhusu Victoria kwamba tulimtumia kumuua Norman na akaanza kumchunguza.Ulitoa maelekezo kwamba niusafishe uchafu huo na kuwaua wote wawili Elvis na Vicky.Elvis tayari amekwisha fariki na amezikwa ila Vicky bado sijamuua ninamtengenezea mazingira na muda wowote nitamkata pumzi.Jana usiku nilimpigia simu Pascal na kumtaka afike nyumbani kwangu kwa ajili ya mazungumzo muhimu na akaniambia kwamba yuko njiani anakuja.Wakati nikimsubiri akanipigia simu na kunijulisha kuwa amepigiwa simu na mtu fulani na kumtaka waonane hivyo akanieleza kuwa atachelewa kufika kwangu ili akaonane na huyo mtu.Baaae nikapigiwa simu na David akanijulisha kuwa Pascal amefariki dunia.Amepigwa risasi.Nilikwenda eneo la tukio na kujiridhisha kuwa ni kweli amefariki dunia" "Frank mbona unaanza kunihutubia?Nina mambo mengi sana siku ya leo hivyo nakuomba kama huna cha maana cha kunieleza usubiri hadi siku yako nitakapokuita kwa mazungumzo rasmi"akasema Elizabeth "Madam naomba unipe dakika mbili tu nimaliziehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ nilichotaka kukisema" "Be quick!! akasema Elizabeth "Thank you.Kabla hujanizuia kufanya chochote kuhusiana na kifo cha Pascal nilifanya uchunguzi mdogo nikagundua kwamba mtu wa mwisho kuwasiliana na Pascal alikuwa ni Vicky ambaye naamini ndiye aliyemtaka waonane pale hotelini.Nataka nifahamu je ulimtumia Vicky katika kumuua Pascal? akauliza Pascal na Elizabeth akastuka "Vicky? "Ndiyo.Ulimtuma amuue Pascal? Swali lile likambabaisha Elizabeth.Akafikiri kidogo kisha akasema "Ndiyo nilimtumia" "Inanishangaza kidogo madam kwa nini umtumie mtu ambaye umekwisha toa maelekezo auawe?Umebatilisha kauli yako na Vicky hauawi tena?Halafu mbona hujanijulisha kuwa kwa sasa umeamua kumtumia Vicky ili nisiendelee na mipango yangu niliyoipanga ya kumuua? Frank kuna mambo mengi yua kuzungumza mimi na wewe lakini ni hapo baadae nitakapokamilisha mazishi ya mume wangu.Kwa sasa nakuomba nenda kaendelee na masuala mengine kuhusiana na operesheni mapinduzi.Bado sijasikia tamko la wanasiasa.Nini wanasubiri? "Leo Dr Makwa Tusangira na viongozi wenzake wa vyama vya upinzani wanakutana na waandishi wa habari na kuwatangazia wanachama wao wakutane kesho katika viwanja jamhuri kwa ajili ya mkutano wa hadhara.Bado hawajapewa kibali cha kufanya mkutano lakini watakaidi amri hiyo ili kupata chanzo cha vurugu.Tayari maandalizi ya awali yamefanyika na leo hii ninawafanyia mpango wa fedha ili wapate kiasi cha kuanzia.Mambo mengine yote yanakwenda vizuri.Kila kitu kinategemea vurugu zitakazoanzishwa na wanasiasa hapo kesho.Wanajeshi wote wako tayari na leo hii nitafanya kazi ya kushughukia malipo yao na watakachobaki wanasubiri ni wakati ufike waweze kuchukua nchi" "Good.Kazi inakwenda vyema lakini bado naona kuna mianya ya uzembe katika baadhi ya sehemu.Nitakapokutana nawe tutarekebishana kwani sitaki uzembe wa aina yoyote utokee katika operesheni hii muhimu sana.Uzembe wowote hata mdogo unaweza ukasababisha mipango yetu ikashindwa kufanikiwa" akasema Elizabeth Wakati Elizabeth na Frank wakiendelea na mazungumzo yao,Juliana na Patricia walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na Meshack Jumbo. "Juliana are you sure you want to do this? akauliza Patricia kabla hawajatoka chumbani "Patricia hakuna haja ya kurudia rudia kujibu swali hilo.Umeniuliza jana na nilikujibu.Twende tuondoke tukaonane na huyo mzee" akasema Juliana wakatoka na walipopita sebuleni wakawakuta Frank na Elizabeth katika mazungumzo.Wakasalimiana "Mama ninatoka kidogo na Patricia kuna sehemu tunakwenda ila hatutakawia sana"akasema Juliana "Mnakwenda wapi? "Kuna mahala tunakwenda.Tutazungumza baadae" akasema Juliana na kumshika mkono Patricia wakaondoka hakutaka maneno mengi na mama yake.Mara tu walipotoka,Elizabeth naye akamuomba Frank amsubiri akaelekea chumbani kwake na kuchukua simu akazitafuta namba fulani akapiga "Duma,kuna kazi nataka uifanye ya haraka.Juliana na mwenzake wanaingia garini wanaondoka kuna mahala wanakwenda.Follow them.Fuatilia wamekwenda wapi na kuonana na nani.Nataka picha za mtu wanayekwenda kuonana naye" akasema Elizabeth halafu akarejea sebuleni alikomuacha Frank "Umemuona yule mwanamke aliyeongozana na Juliana? "Ndiyo nimemuona"akajibu Frank "Anaitwa Patricia ni mke wa Elvis" "Ni huyu? akauliza Frank kwa mshangao "Ndiyo" "Amefikaje hapa? Ni rafiki na Juliana na ndiye aliyemchukua akamleta hapa ili aweze kupumzika" "madam kukaa na mtu kama huyu ndani ni hatari kubwa.What are you going to do with her? "Hutakiwi kunifundisha kazi Frank mimi ninajua zaidi yako hivyo nafahamu nini nifanye.Nadhani tumemaliza .Una lingine?akauliza Elizabeth "Hapana sina madam.Yalikuwa ni hayo tu"akasema Frank "Mazishi ni wiki ijayo.Jiandae baada ya mazishi tutakuwa na kikao kizito mimi na wewe" akasema Elizabeth wakaagana na Frank akaondoka Bado hainiingii kabisa akilini eti madam Elizabeth amemtumia Vicky katika mauaji ya Pascal.Cha kushangaza nilipomueleza kwamba Vicky ndiye mtu wa mwisho kuzungumza na Frank simuni na ndiye aliyemtaka waonane pale hotelini,Elizabeth alistuka na akababaika kujibu na baadae akasema kwamba yeye ndiye aliyemtuma.Hili nalikataa kabisa kwa sababu alikwisha toa maelekezo kwamba Vicky auawe sasa iweje aamue kushirikiana na adui yake?Mimi ni mwerevu na hawezi kunidaganya chochote.Hapa lazima kuna kitu kinaendelea.Kwanza sina hakika kama kweli madam Elizabeth anahusika katika kifo ca Pascal.Hamfahamu Pascal japo ninashirikiana naye katika biashara ya silaha sasa iweje amuue mtu ambaye hamjui.Kwa kosa lipi? Taa nyekundu inaniwakia hapa lazima kuna kitu kinaendelea na siwezi kufumba macho hadi nifahamu nini hasa sababu na nani waliomuua Pascal? Nisipofahamu chanzo cha mauaji ya Pascal hata mimi naweza kuwa niko hatarini bila kujifahamu kwani Pascal alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana.Nitachunguza kwa siri na lazima nifahamu waliofanya mauaji haya.Mtu pekee ambaye anaweza akaniongoza katika kuutafuta ukweli ni Vicky.Huyu alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza na Pascal na lazima kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo hiki.Akipatikana akiteswa ataeleza kila kitu" akawaza Frank na kutoa simu yake akazitafuta namba za Vicky akapiga,simu ikaita na baada ya muda ikapokelewa "Hallo Frank"akasema Vicky baada ya kupokea simu "Habari yako Vicky.Usingepokea simu yako au ingekuwa haipatikani ningejua tayari nawe umapatwa na matatizo.Are you ok? akauliza Frank "Yes I'm ok. Vipi kuhusu wewe uko salama? "Niko salama.Nimekutafuta sana kuanzia jana usiku lakini hukuwa ukipatikana,uko wapi?Umekwisha pata taarifa za jambo lililotokea jana usiku? akauliza Frank "Ndiyo nimesoma katika mitandao ya kijamii kuwa Pascal ameuawa.Nimesikitika sana.Nani hasa waliomuua na kwa nini? "Mpaka sasa hakuna anayefahamu nini hasa kilichotokea na kupeleka kifo chake ila hali si nzuri hata kidogo.Uko wapi mida hii? "Niko nyumbani" "Ok sawa nitakuomba tuonane baadae mchana ili tuweze kuzungumza kuhusu suala hili kwani linatuhusu sote.Sisi tulikuwa ni washirika wakubwa wa Pascal na yawezekana na sisi tukawa hatarini pia.Tukutane tujadili kwa kina suala hili na tutafute namna ya kujilinda" "Kwa mchana wa leo sintaweza kupata nafasi nitakuwa na mteja wangu wa muhimu sana labda kesho ninaweza kupata nafasi.Nitaomba unijulishe taratibu za msiba na mazishi.Ukinikosa hewani nitumie ujumbe mfupi nitakapowasha simu nitaupata" "Vicky samahani si kwamba ninaingilia ratiba zako lakini Pascal alikuwa ni mtu wetu sote na hata ulipopatwa na tatizo la kufuatwa na yule jamaa aliyetangulia mbele za haki tulisimama wote kuhakikisha unakuwa salama,huwezi ukaahirisha japo kwa siku moja tu ratiba zako ili tuweze kujadili suala hili muhimu na vile vile kuhudhuria msibani?Tunapaswa kuchukua hatua za haraka kujilinda kwani hatujui bado ni nani aliyemuua Pascal na kwa nini?Tafadhali nakuomba" "Frank kwa leo haitawezekana.Mimi ninakwenda kwa ratiba na kwa mujibu wa ratiba yangu ya leo sintapata nafasi hadi kesho.Usijali nitakapopata wakati tutaonana na kujadili.Nijuze tafadhali kila kitakachoendelea kujiri" akasema Vicky na kukata simu kabla Frank hajatamka neno lolote "bastard !!! akasema kwa hasira na kuitupa simu pembeni Anafahamu alichokifanya na ndiyo maana hataki kuonana nami.Nitampata tu kahaba mkubwa yule.Lazima nimuweke katika himaya yangu na atajuta kwa nini ulikuja duniani.Ni heri angezaliwa mti kuliko kuzaliwa mwanadamu.Nitamtesa na utaeleza kila kitu" akawaza Frank na kupekua simu yake akatafuta jina limeandikwa Obi akapiga "Heshima yako Afande" ikasema sauti ya upande wa pili "Obi habari yako? "Nzuri kabisa mkuu" "Obi uko wapi sasa hivi? "Ninajiandaa kulala afande.Nimefika nyumbani muda si mrefu nimekuwa na kazi usiku kuchaUsilale Obi.Kuna kazi nataka kukupa.Nitakulipa vizuri" "Mkuu kwa leo nimechoka sana labda kesho" "Hapana Obi,kazi hiyo haiwezi kusubiri.Nataka leo hii hii tena ifanyike kuanzia asubuhi ya leo" akasema Frank "Uko wapi mkuu? Obi akauliza "Niko njiani ninakuja hapo kwako naomba unisubiri tafadhali" akasema Frank "Sawa ninakusubiri" akasema Obi na kukata simu Baada ya Frank kuondoka Elizabeh akampigia simu David ambaye bado alikuwa kitandani.Alipoona jina la Elizabeth katika kioo cha simu akakurupuka na kutoka chumbani "Habari za asubuhi madam Elizabeth? akasema David "David we have problem" "A problem?! "Ndiyo.Frank ametoka hapa muda si mrefu" "Frank? "Ndiyo.Amekuja asubuhi sana na nilikuwa na mazungumzo naye marefu kidogo.Anadai kwamba kabla sijamzuia asifanye chochote kuhusu kifo cha Pascal tayari alikwisha anza kufanya uchunguzi wake na aligundua kwamba yule kahaba Vicky anahusika na kifo cha Pascal kwani ndiye aliyempigia simu na kumtaka waonane hotelini ambako Pascal alikwenda kuuawa.Imenilazimu kukubali kwamba mimi ndiye niliyemtuma Vicky afanye mauaji yale ya Pascal.Frank bado hajaridhika na lazima atafanya uchunguzi kwa siri na anaweza akabaini kwamba unahusika katika kifo cha rafiki yake na hii inaweza kusababisha mipango yetu ikashindwa kufanikiwa.Kwa sasa naamini kitu pakee anachokilenga ni kumpata Vicky.Atatumia kila mbinu kumpata na akifanikiwa atamtesa hadi aufahamu ukweli.Atagundua kwamba mimi sikumtuma Vicky na hapa mimi na yeye tutaingia katika mgogoro kitu ambacho sitaki kitokee hasa kwa wakati huu.Ningeweza kumuondoa Frank lakini bado ninahitaji kumtumia katika mambo yangu hivyo mtu pekee ambaye tunapaswa kumuondoa hapa tena kwa haraka ni Vicky.Akitoweka huyu kahaba Frank hataweza kupata taarifa anazozihitaji hivyo fanya kila uwezalo,tumia kila mbinu huyu mwanamke leo hii atoweke.Lakini nina swali moja kwako" "Uliza madam" "Wewe si ndiye uliyefanya mipango ya kumuua Pascal? "Ndiyo madam" "Vicky ulimshirikisha katika mauaji hayo? "Hapana madam.Mimi niliomba msaada kutoka kwa mwenzangu ambaye ana rasilimali watu wa kuweza kuifanya hiyo kazi na sikufahamu chochote kuhusu Vicky.Kwanza simfahamu huyo mwanamke na wala sijawahi kumuona.Hata mimi nimeshangaa kwa taarifa kwamba anahusika katika kifo cha Pascal"akasema David "Naweza kumfahamu ni nani huyo uliyeshirikiana naye katika kumuondoa Pascal?akauliza Elizabeth "Madam naomba ibaki kuwa siri yangu" "David jana tu nilikupa somo kuhusu utii.Mimi ni kiongozi wako na unapaswa unijibu kila ninachokuuliza.Mbona mimi nilikueleza siri yangu kuwa nilifanya mipango ya kumuua mume wangu?Naomba unieleza tafadhali ni nani huyo mnashirikiana naye?akauliza Elizabeth na David akasita kidogo halafu akasema "Ni makamu wa rais.Madam naomba ufahamu kuwa makamu wa rais Dr Shafi nayeni mwenzetu katika operesheni mapinduzi.Kuna mipango ambayo tumeipanga mara tu nitakapoingia ikulu na ndiyo maana akakubali kushirikiana nasi" "Good.Unajua sana kupanga safu yako ya ushindi.Ningeshangaa sana kama katika mapinduzi haya usingemshirikisha kiongozi yeyote mkubwa.Hata hivyo bado nina swali.Kama uliomba msaada kutoka kwa makamu wa rais ili Pascal auawe kimya kimya Vicky ameingiaje katika sakata hili? "Madam,sina hakika kama kweli Vicky anahusika katika kumuua Pascal.Yawezekana Pascal na Vicky walikuwa na mahusiano yao na wakapanga wakutane hapo hotelini na kwa bahati mbaya Pascal akauawa" akasema David "David naomba unisikilize.Mimi nimekuwa katika magenge ya kimafia toka nikiwa msichana nilipokuwa na mahusiano na Deus hadi leo hii.Ninafahamu mambo mengi kuhusu wapelelezi,ninafahamu mbinu zao na ninafahamu namna ya kuwakwepa.Sina hakika bado lakini kuna kitu kinaniambia kwamba yawezekana huyu Vicky akawa ni miongoni mwao" "Una maanisha Vicky ni mpelelezi?! Akauliza David "Ndiyo.Uwezekano huo upo.Wapelelezi wanazo mbinu nyingi za kupata taarifa kutoka kwa watu mbali mbali" "Hapana madam,sina hakika kama inaweza kuwa kweli.Vicky hawezi kuwa mpelelezi" "Hiyo nimekupa kama tahadhari tu ila fanya kila lililo ndani ya uwezo wako na Vicky apatikane.Asiuawe kwanza ili apelekwe mahala akahojiwe na tumfahamu ni nani.Nataka hadi kufikia jioni ya leo nipate taarifa kwamba suala hili limetekelezwa kikamilifu na tayari tunamfahamu huyu Vicky ni nani" akasema Elizabeth "Sawa madam nitalitekeleza hilo kama ulivyoagiza" akasema David na simu ikakatwa "Mambo haya mbona yanaanza kunichanganya kichwa changu?Huyu Vicky ameingiaje tena katika sakata hili la Pascal?Lakini naamini hizi ni hisia tu za Frank na Vicky hahusiki na chochote katika kifo hicho cha Pascal.Waliotekeleza kifo hicho ni watu wa usalama wa taifa.Hata hivyo ngoja nifanye kama alivyonielekeza.Lakini mambo haya ya kuua ua watu yataendelea hadi lini?Nilianza na Elvis akafuata Pascal na sasa anafuata Vicky.Natakiwa kuwa makini sana pale ninapotakiwa kutekeleza mauaji haya" akawaza na kuzitafuta namba za makamu wa rais akampigia "habari za asubuhi Dr Shafi?akasema David baada ya Dr Shafi kupokea simu "Habari nzuri.Umeamkaje? "Nimeamka salama kabisa.Samahani sana kwa usumbufu asubuhi hii" "Bila samahani David" "Ahsante sana.Nimekupigia tena Dr Safi kuomba msaada wako.Nina shida nyingine.Tafadhali naomba usinichoke" "Usihofu David,tatizo lolote ulilonalo nimekwisa kuahidi kukutatulia.Unahitaji nikusaidie nini safari ii? "Kuna mambo yamejitokeza kwa yule mtu niliyekuomba msaada wa kumlaza usingizi jana ambayo yanahitaji kushugulikiwa haraka sana.Imegundulika kwamba Pascal alipigiwa simu na mwanamke mmoja kahaba anaitwa Vicky na kumtaka wakutane hotelini na huko ndiko alikokwenda kuuawa.Huyu kahaba tayari anaanza kuhisiwa kuhusika na mauaji hayo na kuna hatari anaweza akakamatwa na kutoa siri" "Hilo lisikuogopeshe David.Hakuna uchunguzi wowote utakaofanyika kuhusiana na kifo kile na tayari nimekwisha toa maelekzo kwa jeshi la polisi wasifanye uchunguzi wowote waachie suala hilo idara ya usalama wa taifa hivyo hakuna yeyote atakayekwenda kinyume na maagizo hayo niliyoyatoa" "Ahsante sana kwa hilo Dr Shafi lakini wanaofuatilia suala hili si polisi bali ni rafiki wa karibu na Pascal na kwa hivi sasa wanamuwinda wampate Vicky" "Watu hao ni akina ani? Tunapaswa kuwaondoa haraka sana." "Tutalazimika kuwaondoa endapo wataendelea na kihere here chao lakini kabla ya yote nataka kufahamu kuhusu huyu Vicky je ni mpelelezi? Anafanya kazi idara ya usalama wa taifa?akauliza David "Idara ya usalama wa taifa iko chini ya ofisi yangu lakini si wafanyakazi wote wa idara hii ninawafahamu.Ninaowajua ni viongozi wao.Unapoomba msaada wa kumuondoa mtu fulani mimi huwa nina mkabidhi jukumu hilo mkuu wa idara ya ujasusi anaitwa Meshack Jumbo na yeye hutoa maelekezo kwa vijana wake na mambo yakikamilika hunijulisha.Siwezi kufahamu kama huyo Vicky naye ni mmoja wa watu wake au vipi hadi hapo nitakapomuuliza" "Ahsante sana Dr Shafi.Basi ninamuhitaji huyo Vicky.Awe ni usalama wa taifa au siyo ila ninamuhitaji kwa ajili ya kumfanyia mahojiano.Huyu naye nataka aondoke lakini kabla ya kuondoka kuna mambo napaswa kuyafamu kutoka kwake hivyo natakiwa kumpata akiwa hai na baada ya kumuhoji nitamkabidhi kwa wahusika ili waweze kumuondoa" "Sawa David.Nitatoa maelekezo jambo hilo lifanyiwe kazi.Vipi kuhusu mambo yetu yanakwendaje? "Kila kitu kinakwenda vyema.Maandalizi yanaendelea na baadae leo wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani watakutana na waandishi wa habari na watatangaza kufanyika kwa mkutano wao kesho na hapo ndipo tunapopatafuta.Safari yetu ya kuelekea ikulu itaanzia hapo" akasema David "Sawa David usiache kunijulisha kila kinachoendelea na hata kama kuna yeyote unayeona ni kikwazo katika kukwamisha jambo hili nieleze tu na mimi nitamkata kauli haraka sana.Nitawasiliana nawe baadae mara tu jambo hili litakapokamilika" akasema Dr Shafi na kuagana na David.Hakupoteza muda akampigia simu Meshack "Dr Shafi habari za asubuhi? akasema Meshack Jumbo baada ya kupokea simu "Meshack Jumbo,habari ni nzuri sana.Vipi umeamka salama? Nimeamka salama kabisa" "Nafurahi kusikia hivyo.Mzigo wako niliokuahidi utawasili saa sita mchana wa leo" "ahsante sana Dr Shafi" "Hata hivyo kuna kazi nataka ifanyike leo.kwanza kabla ya kazi naomba nikuulize unamfahamu Vicky? "Vicky? "Ndiyo" "Vicky yupi Dr Shafi? "Una Vicky wangapi katika idara yako? "Sina mtu yeyote anayeitwa Vicky katika idara yangu" "Are you sure? "yes I'm sure" "Nani waliotekeleza mpango wa jana wa kumuondoa Pascal? Nina vijana fulani ambao huwa ninawatumia kwa shughuli kama hizo ndio waliotekeleza huo mpango" "Kwa taarifa nilizonazo kuna mwanamke mmoja anaitwa Vicky ambaye anafanya biashara ya ukahaba anadaiwa kushiriki katika mauaji hayo.Inasemekana kuwa ndiye aliyempigia simu Pascal na kumtaka wakutane hotelini na huko hotelini Pascal akaenda kuuawa.Una taarifa zozote kuhusu huyo mwanamke? "Sina taarifa zozote Dr Shaf.Mimi hutoa kazi kwa vijana wangu na ninachohitaji ni kupewa taarifa kwamba kazi imetekelezwa na kumalizika bila kuhoji ni kwa namna gani wametekeleza.Tulitaka Pasal afe na ameariki.Yawezekana labda vijana wangu walionahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ njia nyepesi ya kumpata Pascal ni kwa kumumia huyo Vicky" "Hata mimi ninahisi hivyo lakini kwa kuwa tayari amekwisha anza kuhisiwa kuhusika katika mauaji hayo huyo mwanamke ayari ni hatari kweu hivyo anapasswa aondolewe haraka sana lakini kabla ya kuondolewa anapaswa ahojiwe.Kuna mtu anataka kumuhoji hivyo naaka akamatwe na awekwe sehemu fulani kwa ajiliya kuhojiwa kisha nitaarifiwe.Nataka jambo hili lifanyike leo hii" "sawa Dr Shafi nimekuelewa.Nitafanya hivyo na nitakujulisha pindi tukimpata huyo mwanamke" "Ahante sana Meshack.Uwe na siku njema" "Ahsante Dr Shafi" akasema Meshack na kukata simu "Sarakasi zimeanza.Tayari Vicky amekwisha fahamika kuwa alishiriki katika mauaji ya Pascal.Ngoja nimjulishe Elvis kuhusu jambo hili haraka" akawaza Meshack na kumpigia simu Elvis "Mzee tayari umeonana na Patricia ? akauliza Elvis baada ya kupokea simu "Nilikuwa najiandaa niondoke lakini nikapokea simu kutoka kwa makamu wa rais Dr Shafi" Anataka nini Dr Shafi? "Wanamtafuta Vicky wanataka akamatwe akahojiwe kuhusiana na kifo cha Pascal na baadae auliwe.Bado uko naye hapo nyumbani? "Hapana amekwisha ondoka.Mzee kuhusu Vicky ninataka tuzungumze mara utakapokuja huku lakini nadhani nikupe maelezo kidogo.Jana tumemfanyia mahojiano kwa usiku mzima na tumegundua kwamba Vicky ni mpelelezi anayejificha chini ya mwamvuli wa ukahaba.Anatumia njia hii kwa ajili ya kupata taarifa muhimu kutoka kwa watu mbali mbali hususan viongozi wa serikali.Anafanya kazi za siri za rais na kwa sasa amepewa kazi ya kuchunguza kuhusiana na mtandao wa biashara haramu ya silaha.Rais pia amekwisha pata tetesi kuhusu uwepo wa biashara hii na anamtumia Vicky kuchunguza.Imekuwa ni jambo jema sana kwetu kumpata kwani sote tuna lengo moja na tayari tumeungana tumekuwa timu moja." "Real?!! akauliza Meshack "Ndiyo mzee" "Dah ! sikulitegemea kabisa hili.Yuko wapi hivi sasa? bado yuko hapo nyumbani kwako? "Hapana hayuko hapa amerejea nyumbani kwake.Atakuja hapa baadae" Elvis call her right now.She's in danger.Anatakiwa awepo sehemu salama na kwa sasa sehemu salama ni hapo kwako" "sawa mzee ngoja nimjulishe" "Mimi nitakuja huko baada ya kukutana na Patricia na nitakujuza kilichojiri" akasema Meshack na kukata simu.Elvis hakupoteza muda akampigia Vicky lakini simu ya Vicky haikuwa ikipatikana.Akapiga tena haikupatikana.Akarudia zaidi ya mara tano lakini simu ilikuwa imezimwa "C'mon Vicky kwa nini unazima simu? akajisemea na kuwaza kwa sekunde kadhaa halafu akaenda chumbani kwa Steve akaufungua mlango bila kubisha hodi na kwa kasi ya iana yake Steve akakurupuka na kuchukua bastora iliyokuwa pembeni "It's me Elvis don't shoot!! ikamlazimu Elvis ajitambulishe haraka "Next time knock the door.!! akasema Steve huku akiirudisha bastora yake chini ya mto "Sorry brother nilidhani umelala ndiyo maana nikaingia wangu wangu bila hodi" "Kuna tatizo lolote? akauliza Steve "Ndiyo kuna tatizo.Muda mfupi uliopita nimetoka kuzungumza na mkurugenzi.Amesema kwamba amepigiwa simu na makamu wa rais asubuhi hii na akamueleza kwamba tayari Vicky amekwisha julikana kuwa anahusika katika kifo cha Pascal hivyo anatafutwa" "Oh my god! akasema Steve "Mkurugenzi amepewa maagizo ya kuhakikisha kwamba Vicky anakamatwa na kuweka sehemu salama kwa ajili ya kuhojiwa kisha auawe.We have to save her.Nimempigia simu yake haipatikani inaonekana amezima simu" "Kwa hiyo tunafanyaje? "Kwa kuwa nyumbani kwake unapafahamu,unatakiwa kwenda kumchukua yeye na mdogo wake.Wote watakuja kuishi hapa ambako watakuwa salama" "Are you sure? akauliza Steve Steve hatuna namna nyingine ya kufanya.We must save them.Tunamuhtaji sana Vicky na tukizembea wanaweza wakamuua.Jiandae uende huko haraka sana ukamchukue" akasema Elvis na Steve akainuka akaingia bafuni kujimwagia maji ****************







    Mawenzi complex ni jengo la ghorofa ishirini na mbili lililoko katikati ya jiji.Ni jengo lenye biashara nyingi na muda mwingi huwa limesheni watu wanaokwenda kufanya manunuzi katika maduka mbali mbali yaliyojazana katika jengo hili.Ghorofa ya sita ndani ya jengo hili kuna hoteli nzuri sana inaitwa Kibo.Ni katika hoteli hii ndipo Meshack Jumbo alikuwa anakutana na Patricia.Watu hawakuwa wengi sana asubuhi hii,Meshack akaangaza angaza na kwa mbali akamuona Patricia amekaa mezani na mwanamke mwingine akawafuata.Wote wakasimama na kumsalimu kisha wakaketi "Samahani nimechelewa kidogo" "Hakuna tatizo mzee"akasema Patricia "Unaendeleaje Patricia? "Ninashukuru Mungu kaniamsha salama siku ya leo." "Jana uliwahi sana kuondoka msibani na hatukupata nafasi ya kuzungumza.Nilitaka tuzungumze kuhusiana na mirathi ya marehemu" akasema Meshack "Mzee Jumbo utanisamehe sana mzee wangu labda kwa kuonekana mkaidi lakini kitu chochote kinachohusiana na Elvis nataka akabidhiwe mama yake.Sitaki kujihusisha tena na mali au kitu chochote cha Elvis" "Patricia jana msibani umeelezea kwa nini umefanya maamuzi haya ya kurejesha mali zote ulizochuma na mumeo kwa mama mkwe wako,nimekuelewa lakini unapaswa kujifikiria na wewe mwenyewe pia.Maisha hayasimami yanaendelea,itakuchukua muda kuanza kujijenga upya.Nakushauri Patricia fuatilia mirathi hii na itakusaidia kuweza kuyaanza upya maisha yako.Wewe ni mke halali wa Elvis na hii mirathi ni haki yako"akasema Meshack Jumbo "Mzee Meshack ,mimi na Elvis tulipendana upendo ambao siwezi kuuelezea kwa maneno.Ulikuwa ni zaidi ya upendo.Nikuweke wazi mzee wangu kwamba mimi sina uwezo wa kuzaa mtoto na Elvis alilifahamu hilo na akanipenda kama nilivyo.Hata siku moja hakuwahi kusononeka kwa kukosa mtoto na hata pale nilipomtaka akazae na mwanamke mwingine hakuwa tayari kufanya hivyo kwa sababu ya upendo wake mkubwa kwangu.Upande wa ndugu zake walininyanyasa mno kwa kukosa mtoto.Ninaposema nilinyanyasika nielewe mzee wangu.Kibaya zaidi kiongozi wa manyanyaso hayo alikuwa ni mama mkwe wangu.Nimetukanwa matusi ya kila aina.Nimeitwa kila jina baya.Kwa ujumla nimetendewa mambo mabaya sana ambayo siwezi kuyasahau lakini upendo nilioupata toka kwa Elvis ulinifanya niyavumilie yote.Kwa sasa baada ya Elvis kuondoka sitaki tena kuendelea kunyanyasika,nataka niishi kwa amani.Yule aliyekuwa anaupooza moyo wangu kwa neno lake moja tu hayupo tena.Sitaki kuendelea kuumia ndiyo maana nimewarejeshea kila kitu cha mtoto wao ili nibaki salama.Hiyo mirathi watafuatilia wenyewe.Nataka niwaonyeshe kwamba sikumpenda Elvis kwa sababu ya mali.Nadhani umenielewa mzee Meshack" "Nimekuelewa Patricia ila ninataka nikuombe kitu kimoja.Elvis alikuwa ni kijana wangu niliyempenda sana na wewe pia ni binti yangu hivyo kama una tatizo lolote lile tafadhali naomba unieleze.Umenielewa Patricia? "Nimekuelewa mzee,ahsante sana kwa ushirikiano wako mkubwa" Kwa sasa unaishi wapi?akauliza Meshack "Oh samahani mzee Meshack nimesahau kufanya utambulisho.Huyu anaitwa Juliana ni dada yangu na kwa sasa ninaishi kwao" "Nafurahi kukufahamu Juliana.Mimi naitwa Meshack Jumbo.Elvis aliyekuwa mume wa Patricia mimi ndiye mkuu wake wa kazi" "Nashukuru kukufahamu mzee Meshack Jumbo" akasema Juliana. "Mzee Jumbo nafahamu wewe ni mtu mwenye shughuli nyingi hivyo hatutaki kukupotezea wakati.Ngoja nijielekeze moja kwa moja katika kile nilichokuitia" akasema Patricia na Meshack akatikisa kichwa kumkubalia "Kama nilivyokutambulisha huyu hapa anaitwa Juliana ,kazi yake ni mwanamitindo.Ni mtu maarufu sana hapa Tanzania nina hakika unaweza kumfahamu.Kwa muda mrefu amekuwa nje ya nchi na sasa amerejea nyumbani.Ana tatizo kubwa linamkabili na anahitaji msaada wa kulitatua.Aliponieleza tatizo lake nikaamua kumsaidia kwa kumuunganisha kwako nikiamini lazima atapata msaada anaohitaji"akasema Patricia "Patricia kwa heshima yako na Elvis ninakuahidi kumsaidia Juliana kama suala lake litakuwa ndani ya uwezo wangu.Hata kama litakuwa nje ya uwezo wangu nitatafuta namna ya kumsaidia"akasema Meshack "Ahsante sana mzee Meshack.Kabla sijampa nafasi Juliana aeleze mwenyewe tatizo lake kuna maendeleo yoyote katika kuwatafuta watu waliomuua Elvis? akauliza Patricia "Uchunguzi tayari unaendelea na hatutalala usingizi hadi tuhakikishe wale wote waliohusika katika kifo cha Elvis wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria.Nakuomba ondoa hofu kabisa kwani kazi hii inafanywa kwa kasi kubwa.Watu wote wameumizwa na kifo cha Elvis na ndiyo maana wanafanya kila wawezalo kuwapata wauaji.Nitakuwa nikikutaarifu kila pale tunapopiga hatua fulani" "Ahsante sana mzee" akasema Patricia na kumtazama Juliana "Juliana karibu mueleze mzee Meshack tatizo lako" akasema Patricia "Kwanza kabisa napenda nikushukuru mzee kwa kukubali kuja kuonana nasi.Najua una mambo mengi ya kufanya lakini umeahirisha na kutenga muda wako kuja kukutana nasi.Nashukuru sana kwa hilo". "Usijali Juliana mimi nipo kwa ajili yenu" "Kama alivyosema Patricia mimi ni mwanamitindo ambaye nilikuwa ninafanya shughuli zangu za mitindo hapa nyumbani Tanzania lakini baadae nikaenda nje ya nchi.Ilinilazimu kuondoka hapa nchini bila kutaka kwa ajili ya kuokoa maisha yangu" akanyamaza kidogo kisha akaendelea "Samahani kama nimeanzia mbali sana kutoa maelezo yangu" "Hapana usijali Juliana ni vizuri kutoa maelezo marefu ili niweze kupata picha halisi ya tatizo lako" "Ahsante.Wazazi wangu wote ni wafanya biashara na kwa muda mrefu hawako hapa nchini wanaishi nchini Afrika kusini na Uingereza ambako kote huko wanamiliki biashara mbali mbali.Tumezaliwa watatu tu,mimi nikiwa wa kwanza halafu Godson na yupo mwingine wa mwisho.Mimi na Godson ndiyo tuliokuwa tukiishi hapa Tanzania wakati mdogo wetu wa mwisho alikuwa akiishi nje ya nchi na wazazi.Nilikuwa na rafiki wa kiume ambaye tulipendana sana aliitwa Joseph na tulikuwa na mipango mingi ya usoni kuhusu mahusiano na maisha yetu kwa ujumla.Mahusiano yetu yalidumu kwa miaka takribani mitano hadi pale alipotolewa uhai kikatili" akanyamaza kwa sekunde chache na kuendelea "Nakumbuka ilikuwa ni asubuhi ya saa tatu siku ya jumanne nilipopigiwa simu na dada wa Jose akanitaarifu kwamba Joseph ameuawa na watu wasiojulikana na maiti yake kutelekezwa katika geti la nyumba ya wazazi wake.Ilikuwa ni taarifa mbaya sana kuwahi kuipokea katika maisha yangu.Haikuishia hapo bali kulikuwa na barua iliyoeleza kwamba mimi ndiye nitakayefuatia.Kwa haraka sana wazazi wangu wakafanya mpango nikaondoka nchini na kwenda kujificha nchi za nje.Nimekuwa nikihama hama nchi na mwishowe nikaamua kuishi na wazazi nchini Uingereza ambako ninaishi hadi baba alipofariki hivi majuzi ndipo tumelazimika kurejea Tanzania kwa mazishi.Toka yalipotokea mauaji yale hadi leo hii sijawahi kusikia mtu yeyote kukamatwa kuhusiana na mauaji yale" akanyamaza kidogpo halafu akaendelea "Nikiwa nje ya nchi huku nikiamini kwamba mambo yamemalizika,mdogo wangu Godson naye aliuawa na watu wasiojulikana nchini Afrika kusini.Taarifa ya daktari aliyefanyia uchunguzi mwili wake inasema kwamba walikuta risasi zisizopungua hamsini katika mwili wake.Yalikua ni mauaji ya kinyama sana"akanyamaza na kuinamisha kichwa "Pole sana.Kweli yalikuwa mauaji ya kikatili mno.Ni nani hao walioifanya unyama huo?Tayari wamekwisha kamatwa? akauliza Meshack Hapana mzee.Hakuna aliyewahi kukamatwa hadi leo hii." "Inashangaza sana kwa nini watu wafanye unyama huu mkubwa na wasipatikane" akasema Meshack "Kweli inashangaza sana na watu hawa hawakuishia hapo bali walitaka hata kumuua mdogo wangu wa mwisho kwa kumpiga risasi lakini madaktari waliwahi kuokoa maisha yake baada ya kukimbizwa hospitalini.Hivi sasa anatembea na walinzi kila aendako" "Pole sana Juliana kwa mikasa hiyo mizito" "Ahsante sana mzee.Maisha yangu yamekosa amani na furaha.Kila wakati ninaishi kwa hofu kama ndege nikiogopa kuuawa.Nimerejea hapa nchini kwa ajili ya mazishi ya baba aliyefariki katika ajali ya ndege na baada ya kukutana na ndugu yangu Patricia nikamsimulia masahibu yaliyonikuta na akanishauri kwamba nipambane kuwasaka waliofanya mauaji yale ya Joseph na mdgo wangu Godson.Nimechoka kuishi nje ya nchi mzee Meshack na ninataka kuishi hapa nchini kwa amani nifanye mambo ninayoyapenda lakini siwezi kufanya hivyo bila kwanza kuwa na uhakika kuwa wale waliokuwa wananitafuta waniue hawapo tena.Patricia akaniahidi kuniunganisha nawe ili niweze kukuomba unisaidie" "NImekusikia Juliana.Unahitaji msaada gani? "Nahitaji kuwafahamu hawa wanoiandama familia yetu ni akina nani na kwa nini wakawaua mpenzi wangu na mdogo wangu?Kwa nini na mimi wakaniwinda waniue? Mimi sina uwezo wa kufanya uchunguzi ila ninyi wenye taaluma na uzoefu wa mambo haya mnaweza mkanisaidia kuwapata watu hawa waovu.Sintakuwa na amani katika maisha yangu hadi pale nitakapopata taarifa kwamba wale wauaji wanaoiandama familia yetu wamekamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.Niko tayari kutoa kiasi chochote cha malipo kugharamia uchunguzi huu ili wauaji hawa wajulikane." akasema Juliana na ukimya mfupi ukapita "Katika matuko haya yote mawili hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kukamatwa akihusishwa na mauaji hayo?akauliza Meshack "Mpaka leo hakuna hata mtu hata mmoja aliyewahi kukamatwa"Juliana akajibu " Matukio haya yote mliyaripoti katika vyombo husika n a uchunguzi ukafanyika? "Sina hakika kama uchunguzi ulifanyika kwani kila tukio lilipotokea wazazi walisema kwamba watalishughulikia lakini hakuna mrejesho wowote kutoka kwao kama kuna uchunguzo wowote unafanyika au vipi" "Hujawahi kuwauliza kama kuna uchunguzi wowote umewahi kufanyika kuwabaini waliofanya mauaji haya? "Nimewauliza mara nyingi na kila mara jibu lao ni hilo kwamba niwaachie wao wanalishughulikia" akasema Juliana. "Mahusiano ya aliyewahi kuwa mpenzi wako Joseph na wazazi wako yalikuaje?Walimfahamu na kumkubali uwe naye? "Familia ya Joseph na famila yetu ni marafiki wa muda mrefu na ndiyo maana ilikuwa rahisi kwetu kuwa wapenzi kutokana na ukaribu uliokuwepo baina ya familia zetu mbili hata hivyo wazazi wangu hawakuonekana kumpenda Joseph.Siogopi kusema kuwa mama hakumpenda Joseph na si mara moja aliwahi kunieleza kwamba nisiendelee naye lakini haikuwa rahisi kwangu kwa kuwa ndiye mwanaume niliyemchagua" "mama yako alikueleza sababu za kukutaka uachane na Joseph? "Sababu alizozitoa hazikuwa na uzito wowote.Alidai kwamba Joseph hawezi kunifanya niwe na furaha kwa kuwa ni mtu mwenye wanawake wengi na alikuwa ananipotezea wakati wangu.Hii ilikuwa ni sababu nyepesi mno na ilikosa mashiko kwani ninamfahamu vyema Joseph toka tukiwa wadogo hakuwa na tabia hiyo" Meshack akafikiri kidogo halafu akamtazama Juliana vizuri machoni "Unadhani mamayako alikuwa anamchukia Joseph? " Hakuwahi kunionyesha wazi wazi kama anamchukia" "Umewahi kuonana na wazazi wa Joseph toka mtoto wao alipofariki dunia?akauliza Meshack "Niliondoka Tanzania mara tu Joseph alipozikwa na sikuwahi kurejea tena hadi hivi sasa hivyo wazazi wa Joseph sijawahi kuonana nao" "Familia ya Joseph walikuchukuliaje?Walikukubali uwe na mtoto wao? "Wazazi wake na familia yao kwa ujumla hawakuwa na tatizo lolote nami na walinipenda sana" Mzee Meshack akatafakari kwa muda na kusema "Juliana ahsante kwa kwa maelezo uliyonipa na ninapenda kukuweka wazi kwamba hapa kuna kitu ninakiona kabla hata ya uchunguzi kufanyika.Mauaji haya yanaonyesha ni mauaji ya kisasi.Ninachokuomba usihofu tena endelea kuwa mtulivu kwani suala hili tayari limefika sehemu husika na nitakusaidia.Ninaongoza idara yenye watu wenye ujuzi wa hali ya juu wa kushughulika na mambo kama hayo na ninakuhakishia kwamba kama watu hao bado wako hai lazima watajulikana na wewe utaendelea kuishi maisha yako kwa furaha na amani.Nitawateua vijana watakaolishughulikia suala hili na watakuja kukuona mtazungumza na nitakomba uwaeleze kwa kirefu zaidi kila kitu ili wapate sehemu ya kuanzia uchunguzi wao" "Ahsante mzee Meshack.Sijui niseme neno gani zuri kwa msaada huu mkubwa ambao sikuutegemea.Itanigharimu kiasi gani ili nijiandae?akauliza Juliana na Meshack akatabasamu Patricia ni binti yangu na ndiye aliyekuleta kwangu hivyo kuanzia sasa nawe pia ni binti yangu kwa hiyo suala hili ninalifanya kama la nyumbani na hakuna hata senti moja utakayotakiwa kutoa labda kama utaamua kutoa kiasi chochote utakachoona kwa vijana wale watakaokuwa wanalichunguza hili suala ili kuwasaidia katika mizunguko yao mbalimbali wakati wakifuatilia hili jambo" "Ninakushukuru sana mzee wangu na nitakuombea kwa Mungu akupe umri mrefu ili uendelee kuwasaidia watu kama sisi" "Amina" akasema Meshack na kisha wakaendelea na maongezi kidogo halafu wakaagana na kuondoka









    Baada ya kuachana na akina Patricia,Meshack Jumbo akaelekea moja kwa moja katika makazi ya Elvis ambako alikaribishwa na Graca na baada ya muda mfupi Elvis akatoka wakasalimiana "karibu mzee" "Ahsante Elvis.Poleni kwa shughuli ya usiku kucha" "Ahsante mzee" akajibu Elvis "Umekutana na Patricia? "Ndiyo nimeonana naye" "Anaendeleaje? Ni rahsi sana kusema anaendelea vyema kwa kumtazama lakini hatuwezi kujua ndani ya moyo wake maumivu anayokutana nayo ila yule mwanamke ni jasiri sana.Anajitahidi kukubaliana na hali halisi ilivyo ili maisha yaende mbele" "dah ! Nimemuumiza mno Patricia.Maisha yake hayatakuwa sawa tena"akasema Elvis "Nilijaribu kumgusia kuhusu suala la kufungua mirathi lakini amekataa kabisa na ameelekeza suala hilo aachiwe mama yako.Ni jambo gani baya ambalo ndugu zako walimfanyia na kumfanya asihitaji kitu chochote cha kwako? Ninaamini kuna mambo alikuwa anafanyiwa na ndugu zangu ila hakuwa ananieleza.Nafahamu manyanyaso aliyokuwa anayapata toka kwa ndugu zangu wakitaka mtoto lakini inaonekana kuna mengi zaidi alikuwa ananificha.Natamani hata leo hii niibuke na kumchukua mke wangu twende mbali tukaishi.Inaniumizz mno anavyoteseka" "Usihofu Elvis na wala usiwe na wazo hilo la kuitaka kuibuka kwani utafanya mambo yawe magumu zaidi.Mimi nipo na nitahakikisha Patricia anakuwa na maisha mazuri yenye furaha" Elvis akazama kidogo katika tafakari halafu akaulizaMzee sifahamu operesheni hii itachukua muda gani.Ni vipi kama Patricia ataamua kuwa na mwanaume mwingine? "Elvis kijana wangu naomba nikuweke wazi bila kukuficha kwamba matumaini ya wewe na Patricia kurudiana ni asilimia ndogo mno au naweza kusema kwamba safari yenu imeishia hapa.Hakuna namna unayoweza ukajitokeza tena kwa Patricia na kudai kwamba hukuwa umekufa.She'll never trust you again.Kwa sasa weka pembeni mawazo kuhusu Patricia I need you to focus in your mission.Mambo ya kuhusu Patricia yatajulikana baada ya operesheni kumalizika.Umenielewa Elvis? akauliza Meshack "Nimekuelewa mzee" "Good.Nipe taarifa za jana usiku" akasema Meshack na Elvis akamsimulia kila kitu kuhusu Vicky "Do you trust her? akauliza Meshack baada ya kuhadihiwa kila kilichotokea "yes I do trust her"akajibu Elvis "Vizuri kama umemuamini na unaona anaweza kuwa na msaada kwetu mimi sina tatizo.Mjumuishe katika timu yetu,wewe ndiye nahodha wa jahazi hili hivyo siwezi kukuingilia katika kuliongoza ninachoweza kufanya mimi ni kutoa tu ushauri.Umekwisha wasiliana na Steve kama tayari amefika numbani kwa Vicky? "Amenipigia simu dakika chache kabla hujafika hapa na kunijulisha kuwa anaweza akachelewa kufika kwa Vicky kwani njia aliyopita kuna ajali imetokea hivyo gari zimesimama na foleni ni ndefu sana" " Anatakiwa kufanya kila awezalo ili kumuwahi Vicky.She's in danger.Nimepewa maagizo na makamu wa rais kwamba akamatwe na awekwe sehemu fulani kuna mtu anataka kumuhoji na baada ya hapo auawe kwani tayari amekwisha anza kuwa tishio kwao"Amefahamuje kama Vicky alikuwepo eneo la tukio wakati Pascal anauawa? akauliza Elvis "Hata mimi nashangaa.Kwanza aliponipigia aliniuliza kama ninamfahamu Vicky nikamuuliza ni Vicky yupi anayemzungumzia akanifafanulia kwamba kuna mwanamke anaitwa Vicky ambaye anahusishwa na kifo cha Pascal akataka kujua kama Vicky ni mtu wangu ambaye nilimtumia katika kumuua Pascal nikamweleza kwamba simfahamu huyo Vicky ila yawezekana alitumiwa na vijana wangu ili kuweza kumpata pascal kirahisi ndipo akasema kwamba anataka Vicky apatikane ahojiwe na baadae auawe kwani tayari ni mtu hatari kwao." "Vicky ndiye aliyempigia simu Pascal na kumuomba waonane pale hotelini yawezekana wamefanya uchunguzi wa mawasiliano ya Pascal na wakagundua kwamba Vicky ndiye aliyemtaka Pascal afike pale hotelini na akauawa.Kinachonishangaza ni kwamba hawa jamaa walitaka pascal auawe sasa wana wasiwasi gani tena? "Wasi wasi wao ni kuhusu huyo Vicky kuhusika katika kifo cha Pascal"akajibu Meshack "Vicky ni mshirika wa Frank na Pascal na ndiye walimtumia kumuua kanali Norman.Kwa nini sasa wawe na wasiwasi?Anyway tuliache kwanza suala hili tutajadiliana na Vicky pale atakapofika hapa.Patricia alikuwa na shida gani? akauliza Elvis "Patricia hakuwa na tatizo lolote kubwa,alitaka tu kufahamu kama tayari uchunguzi wa kuwabaini wale waliosababisha kifo cha mumewe umekwisha anza nikamuhakikishia kwamba uchunguzi mkali unaendelea hivi sasa" "Only that? akauliza Elvis kwa mshangao "Haikuishia hapo.Patricia alikuwa ameongozana na dada yake anaitwa Juliana" "Ninamfahamu Juliana ni mtu wa karibu sana naye na kwa sasa ndiye aliyemchukua anaishi kwao"akasema Elvis "Huyo Juliana ndiye aliyekuwa na tatizo na Patricia alimleta kwangu kwa ajili ya kumpatia msaada "Ana tatizo gani Juliana? akauliza Elvis na Meshack akamueleza kila kitu alichoelezwa na Juliana "Oh my God!! akasema Elvis baada ya Meshack kumaliza kumsimulia mkasa wa Juliana "Elvis,mbona umestuka?akauliza Meshack "Sijastuka mzee ila ninapatwa na wasi wasi mkubwa kwa Patricia kuendelea kuishi pale.Yuko katika hatari.Kuna kila sababu ya kuamini kwamba familia hii ya akina Juliana inawindwa na mtu au kikundi cha watu na hivyo kumfanya mke wangu awe katika hatari kubwa endapo kuna lolote litatokea.Meshack we have to get her out of there.Patricia hatakiwi kuendelea kukaa pale kwa akina Juliana ni sehemu hatari sana kwake" "Hata mimi nimeliona hilo na nitajaribu kumueleza Patricia ili aweze kuondoka na kutafuta sehemu nyingne ya kuishi.Nitamtafutia makazi mengine.Kuna nyumba zinapangishwa kule maeneo ya Peninsula nitamfanyia mpango ili aweze kupata nyumba moja aishi kwa wakati ambao tunaangalia namna ya kumtafutia nyumba yake mwenyewe ili maisha yake yaweze kuendelea kama kawaida" "Ahsante sana kwa hilo mzee naomba lifanyike kwa haraka" "Nitalitekeleza hilo usijali." "Good.Sasa umeamua nini kuusu suala hili la Juliana? "Bado sijaamua chochote kwa sasa kwani bado kuna kazi kubwa inatukabili mbele yetu hivyo sitaki kuchanganya mambo.Tumalize kwanza suala hili la mtandao wa silaha halafu tutamsaidia Juliana.Au wewe unasemaje?akauliza Meshack "Wazo lako si baya mzee.Tuna suala kubwa mbele yetu lakini hata hivyo bado tunaweza kumsaidia Juliana pia.Tunaweza kuzungumza naye na kupata picha halisi ya suala lake na pale tutakapokuwa tumemaliza operesheni yetu tuanze kulifuatilia suala lake.Steve na Vicky wanaweza wakamuhoji Juliana ili tuone ni wapi pa kuanzia.Nataka ukaribu na Juliana ili iwe raisi kwetu kujua maendeleo ya Patricia" "Elvis huoni kama tutakuwa tunaongeza kazi nyingine hasa kwa wakati huu ambao tunakabiliwa na jukumu zito ambalo ndilo kwanza limeanza kushughulikiwa?Ninao vijana wengi pale ofisini ninaweza kuwapa kazi hiyo wakaifanya na ninyi mkaendelea na kazi moja ya kuufumua mtandao huu wa kuuza silaha" Hapana mzee tuachie sisi suala hili tutalifanya wenyewe.Juliana ni mtu wa karibu sana na Patrcia hivyo suala lake linapaswa kushughulikiwa kwa uzito mkubwa sana.Ni mtu ambaye anaweza kumsaidia sana Patricia na hata baadae operesheni itakapokuwa imekwisha anaweza akanisaidia kurejesha tena mahusiano na Patricia.Usijali mzee tutajipanga kufanya kazi zote mbili" "Una hakika Elvis? "Ndiyo mzee ondoa hofu" "Sawa.Nataka kufahamu kuhusu namna mlivyojipanga kuiendesha operesheni hii ya kuubaini mtandao wa akina Frank" Kwanza tunataka kuwachunguza Frank na makamu wa rais.Kupitia hawa wawili tunaweza kuufahamu ukubwa mtandao wote wa kuuza silaha.Tayari Vicky amekwisha zungumza na rafiki yake yuko nchini Afrika kusini na amemuomba aje atusadie na tunasubiri jibu lake na endapo akikubali nitakufahamisha mara moja.Anaitwa Omola Otola.Atajifanya ni mwandishi wa habari za mazingira na kwa kuwa ofisi ya makamu wa rais ndiyo inashughulika na mazingira itakuwa rahisi sana kumchunguza Dr Shafi.Vicky atazungumza na rais na kumjulisha kwamba anataka kumchunguza makamu wa rais na rais atafanya mpango ili kuwe na ukaribu kati ya makamu wa rais na Omola.Vicky yeye atamchunguza Frank kwani wana ukaribu mkubwa.Kupitia wawili hawa kuna mambo tutayafahamu kuhusu mtandao huu mkubwa.Kuna mtu ambaye anaonekana ni kinara katika huu mtandao anaitwa Deusdedith ambaye Vicky amewahi kuwa na ukaribu naye na kumchunguza lakini hakuwahi kuambulia chohiote kwani ni mtu makini sana anayejua kujificha.Huyu naye tunamtafuta na tuna imani tukimchunguza Frank tutafahamu mengi kuhusu Deus.Ndani ya muda mfupi ujao kutakuwa na hatua kubwa imepigwa katikakuwabaini watu hawa na na namna wanavyofanya biashara yao ya silaha" "Ni mpango mzuri ila nina ushauri mdogo.Huyu Vicky kama anaripoti kwa rais asithubutu kuweka wazi kwamba anashirikiana nanyi.Hili ni suala la siri sana" "Tumekwisha liona hilo na kumuonya asithubutu kufanya hivyo" akasema Elvis "Good.Nimeridhiswa na mpango huo.Fanyeni kila muwezalo kuikamilisha operesheni hii muhimu sana kwa taifa letu.Muda wowote kama kuna lolote ambalo mtahitaji,mnijulishe na mimi nitakikishaninalifanikisha.Nitakuja tena jioni ya leo ili kwa pamoja tujadiliane namna ya kulishughulikia suala la Juliana.Kuhusu Patricia nitashughulikia nyumba kama nilivyokuahidi ili aweze kuondoka pale kwa akina Juliana.Mambo yote haya tutakuja kufahamishana jioni nimefikia wapi" "Ninashukuru sana mzee" akasema Elvis na mzee Meshack Jumbo akaondoka kwenda kuendelea na majukumu mengine "Patricia kuendelea kukaa kwa akina Juliana ni hatari kubwa kwake na kama ningekuwa na uwezo ningekwenda sasa hivi kumtoa lakini ngoja nifuate ushauri wa mkurugenzi.Mimi ndiye chanzo cha Patricia kuingiakatika hatari hii.Kama nisingefanya jambo hili la kudanganya kifo changu haya yote yasingemkuta.Kuna nyakati najiona sijafanya jambo sahihi lakini nikikumbuka namna ndugu zetu wanavyouliwa na waasi wanaopata silaha kutoka kwa akina Frank najiona nimefanya kitu sahihi.Frank na genge lake ndio waliosbabisha haya na ninaapa lazima watalipa" akawaza Elvis na kuchukua simu akampigia Steve.Simu ikaita kidogo na kukatwa.Akajaribu tena kupiga haikuwa ikipatikana.Elvis akaingiwa na wasiwasi Hatimaye askari wa usalama barabarani walimaliza kupima kufuatia ajali iliyokuwa imetokea, magari yaliyokuwa yamegongana yakaondolewa na gari zikaanza kwenda.Ulikuwa ni msururu mrefu sana wa magari yaliyokuwa yamekwama katika barabara hii nahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Steve akiwa ni mmoja wao akielekea nyumbani kwa Vicky.Kila wakati alikuwa anatazama saa yake na tayari ilikwisha fika saa tatu na dakika kumi na nane "Ningejua kama yangetokea haya nisingepita barabara hii.Nilitakiwa kuwahi sana nyumbani kwa Vicky.Ajali ile imenichelewesha sana na nisingeweza kuondoka na kulitelekeza gari barabarani lingeleta usumbufu kwa wengine na hata kuibiwa.Nitajitahidi kupita barabara za vichochoro ili nifike kwa haraka.Kama kuna hatari yoyote itakuwa imetokea siwezi kujilaumu sana kwani sikuwa na namna nyingine ya kunifikisha kwa haraka" akawaza Steve na kutolewa mawazoni baada ya simu yake kuita .Akatazama mpigaji alikuwa Samira.Kwa kuwa gari lilikuwa linakwenda taratibu kutokana na wingi wa magari akaipokea "Hallow baby summer" "Steve kulikoni hadi mida hii hujanipigia simu?Umenogewa na Vicky? Si hivyo mpenzi wangu ni kutingwa tu na kazi.Hivi sasa niko barabarani nitakupigia baadae tutazungumza" "Sawa Steve je ulifanikiwa kupata ulichokuwa unahitaji? "Nilifanikiwa na Vicky niliachana naye usiku ule ule" "Kweli? "Kweli kabisa Samira" "Niambie uliitimiza ahadi uliyonipa? akauliza Samira "Ahadi ipi Samira? "Tulikubaliana kwamba hautafanya mapenzi na Vicky" "Ouh! Usihofu kabisa kuhusu hilo baby summer.Mimi shida yangu ilikuwa ni taarifa tu na si mapenzi.Kama ni mapenzi ninayapata kwako tu kwani hakuna wa kufikia kiwango chako.Nitawasiliana nawe baadae kidogo nitakapokuwa nimetulia kwa sasa niko barabarani" akasema Steve ana kuagana na Samira "Nilimuahidi Samira kwamba nisingefanya chochote na Vicky lakini sikuitimiza ahadi hiyo.Samira mwenyewe anafahamu ugonjwa wangu ni wanawake wazuri sasa ningewezaje kumuacha mrembo kama Vicky?Daah ! mwanamke yule ni mjuzi sana kitandani na ukichanganya na uzuri wake ndo balaa kabisa utajiona kama uko anga za mbali.Japo tulifanya kwa muda mfupi lakini nilipata raha ya ajabu sana.Baada ya mambo kumalizika lazima nitafute wasaa niweze kujivinjari naye tena kiumbe yule asiyeisha utamu" akawaza Steve na kutabasamu "Elvis amekuwa ananiusia kila mara kwamba siku zote nisiwaamimi wanawake wazuri kwani wanaweza kunitoa uhai na hii ndivyo ilivyotokea kwa Vicky.Katu huwezi kudhani kuwa ni mpelelezi.Watu wanamchukulia kama kahaba kumbe mwenzao yupo kazini.Vigogo wanampapatikia huku wakimwaga mahela yao kumpata hawajui kama anawachunguza. Safari hii kifaranga katua katika miguu ya mwewe.Nitachagua nimlie angani au ardhini" akawaza Steve huku akitabasamu kwa mbali. Ilmchukua takribani saa moja kufika nyumbani kwa Vicky.Hakukuwa na mlinzi nje akapiga honi ili kumstua afungue geti lakini zikapita dakika mbili bila mlinzi au mtu yeyote kutoka.Steve akafungua mlango wa gari na kushuka akatemea taratibu na kwa tahadhari hadi getini akachungulia katika dirisha dogo la chumba cha walinzi lakini hakukuwa na mtu.Akatazama kila upande kuona kama kuna mtu maeneo yale ya karibu,hakukuwa na mtu aliyemtilia maanani zaidi ya wapita njia.Akausukuma mlango mdogo wa geti ukafunguka haukuwa umefungwa akaingia ndani taratibu na kwa tahadhari kubwa.Nyumba ilikuwa kimya na hakukuwa na dalili za kuwepo mtu.Ndani aliyaona magari mawili.Moja ni lile ambalo Vicky aliondoka nalo na halafu kukawa na gari lingine jeupe. "Vicky aliondoka na lile gari letu hii ina maana kuwa yupo ndani.Yawezekana amepumzika na hataki usumbufu hata hivyo huu ukimya mbona kama si wa kawaida?Hakuna mlinzi wala mtu yeyote humu ndani? akawaza Steve na kusogea taratibu hadi katika gari la kwanza jeupe lililokuwa na vioo vyeusi akachungulia ndani hakukuwa na mtu akatembea taratibu kuelekea katika mlango mkuu wa kuingilia sebuleni.Kabla hajafika mlangoni akasikia sauti ikiuliza kwa ukali "Una hakika hakuna wengine humo ndani? "Hakuna mkuu nimepitia vyumba vyote hakuna mwingine ni hawa tu" ikajibu sauti nyingine "Sawa.Nenda nje kahakikishe hakuna anayeingia humu ndani.Mimi nitamalizana na hawa.Una hakika wote umewafunga vizuri? "Ndiyo mkuu wote wamefungwa vizuri" "Good.Nenda nje" ikasema ile sauti kali na haraka sana Steve akajibanza pembeni ya mtungi mkubwa wa maua ambao haukuwa mbali sana na mlango na taratibu akaitoa bastora yake kwani alikwisha ng'amua hatari iliyopo.Katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni kijana mmoja aliyevaa fulana nyeupe na suruali ya jeans ya rangi ya bluu na koti la rangi ya kahawia akatoka akiwa ameshika bastora mkononi.Usoni alikuwa amevaa miwani myeusi na kichwani alikuwa na kofia nyeusi pia.Aliangaza pande zote kuhakiki usalama kisha akaanza kupiga hatua kwa tahadhari kuelekea getini.Alipita katika chungu alichokuwa amejibanza Steve na alipompita kama hatua nne simu ya Steve ikaita,kwa haraka sana akaikata na kuizima kabisa.Yule kijana alistuka aliposikia mlio ule wa simu akageuka na kukutana na kitu ambacho hakuwa amekitegemea.Alikuwa anatazamana na mtu mwenye sura yenye kuonyesha hamu ya kutoa roho ya mtu.Steve akaweka kidole mdomoni ishara ya kumtaka yule jamaa anyamaze kimya halafu akamfanyia ishara atupe chini bastora yake na kisha aanze kutembea kuelekea getini.Yule kijana hakuwa mbishi akaitupa chini bastora yake akaanza kupiga hatua kuelekea getini.Steve akaiokota bastora ya yule jamaa na kuifutika kiunoni na kumfuata nyuma akiwa katika tahadhari kubwa,akamuamuru aingie katika kile chumba kidogo cha walinzi na kumtaka apige magoti Brother naonba usiniue mimi sifahamu chochote"akajitetea yule kijana "Ninyi ni akina nani na mmefuata nini hapa?Steve akauliza "Mimi sifahamu chochote brother naomba uniamini" akasema yule kijana na Steve akiwa katika sura inayotisha akaiweka sawa bastora yake na kumlenga yule jamaa kichwani "Kijana naomba unitazame vizuri machoni sina muda wa kupoteza na mimi kazi yangu ni kuua hivyo usiponijibu kwa ufasaha ninachokuuliza nitausambaratisha ubongo wako.Nakupa sekunde tano unieleze ninyi ni akina nani na mnatafuta nini hapa? "Nitakueleza brother tafadhali naomba usinidhuru" akasema yule kijana kwa woga "Kama nilivyokwambia mimi sifahamu chochote nimechukuliwa na Obi ameniambia kwamba kuna kazi ya kufanya na tukaja hapa.Hajanieleza chochote zaidi ya kuvamia hapa na kuwakusanya watu wote sebuleni ambako ndiko aliko yeye na mimi amenitoa kuja kuangalia ulinzi" "Mko wangapi? "Tuko wawili tu mimi na Obi" akasema yule kijana "Nani kawatuma? Sifahamu chochote brother.Obi ndiye anayefahamu kila kit......" hakumaliza sentensi yake Steve akampiga teke kali lililomrusha hadi ukutani akajibamiza na kutoa mguno wa maumivu.Akamfuata pale chini alipokuwa ameangukia akivuja damu mdomoni akampiga teke lingine kali la uso na yule kijana akapoteza fahamu "Nina hasira sana nanyi,tena una bahati nina haraka ya kwenda ndani kumuokoa Vicky vinginevyo ningekumwaga ubongo wako" akasema Steve kwa hasira na kutembea kwa tahadhari kuelekea sebuleni.Alinyata na kuukaribia mlango na kuangaza kila upande kuhakiki kuwa hakuna mtu mwingine. "Nahitaji kujua namna walivyokaa huko ndani ili nijue namna ya kumkabili huyo shetani ndani" akawaza Steve na kusogea kuelekea katika dirisha.Akachungulia ndani na mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni Vicky akiwa amefungwa mikono kwa nyuma amepiga magoti. "Nieleze unashirikiana na akina nani?sauti kali ya yule jamaa kule ndani ikauliza lakini Vicky hakujibu kitu na yule jamaa akamsogelea na kumpiga teke kali lililompeleka hadi chini.Steve alikiona kitendo kile akauma meno kwa hasira Huyu jamaa hana habari kama ziraili yuko hapa nje akisubiri kuichukua roho yake" akawaza Steve na kuanza kuusogelea mlango.Wakati akinyata kuelekea mlanoni akagonga kopo. "Gabi !! akaita yule jamaa aliyeko ndani lakini hakujibiwa "Mambo yameharibika" akawaza Steve na kujiweka tayari. "Gabi !! yule jamaa akaita tena na aliposikia kimya akatoka taratibu ili kuchungulia na ghafla akapigwa teke kali la uso lililomrusha ndani.Kwa wepesi wa aina yake Obi akajigeuza na kuruka sarakasi halafu akatua chini kwa ufundi mkubwa na kuachia risasi kuelekea mlangoni alikokuwa amesimama Steve.Risasi toka katika bastora ya Obi ikamchubua Steve begani na kumuangusha.Obi akasimama lakini kabla hajafanya chochote Vicky kwa kutumia miguu yake akajigeuza na kumkata mtama akaanguka.Steve akasimama ili kumuendea Obi pale chini alipoangushwa lakini Obi alikuwa mwespi sana alimuona na akaiwahi bastora yake akaachia risasi mfululizo.Kwa jicho kali kama tai Steve alikiona kidole cha Obi kikiizinga bastora hivyo akaruka katika korido na kunusuru maisha yake,akaingia katika chumba cha chakula.Obi akainuka haraka haraka na kutoka kwa kasi ya mshale akakimbia Steve!! akaita Vicky kwa sauti kubwa na baada ya muda Steve aliyekuwa amechafuka damu akajitokeza. "Are you ok? Steve akamuuliza Vicky "Amekimbia,go after him !! akasema Vicky na Steve akatoka nje na kuliona gari jeupe likimalizika kutoka getini.Akakimbia hadi katika kibanda cha walinzi lakini yule jamaa aliyekuwa amempoteza fahamu hakuwemo. "Bastard !! akasema kwa hasira halafu akarejea ndani "We lost them.Wamekimbia" akasema huku akianza kuwafungua Vicky na wenzake waliokuwa wamefungwa mikono kwa nyuma "Nyote mko salama.Hawajawaumiza? akauliza Steve "Hapana hawajatuumiza.Umefika kwa wakati muafaka sana kwani alikuwa anaanza kunihoji.Ahsante sana Steve kwa kutuokoa.Umejuaje kama niko katika hatari? akauliza Vicky "Vicky tutazungumza kuhusu hilo lakini nataka kufahamu yule jamaa ni nani?Unamfahamu?Steve akauliza "Hapana simfahamu.Ni mara ya kwanza leo kumuona.Nikiwa chumbani ninajipumzisha mlango wangu ukagongwa nilipokwenda kuufungua nikajikuta nikitazamana na bastora hivyo sikuwa na ujanja tena zaidi ya kufuata walivyotaka wale jamaa" "Vicky hatuna muda wa kupoteza.Jiandaeni chukueni baadhi ya vitu vyenu vichache tunaondoka" "Tunakwenda wapi? akauliza Vicky "At our place.Hapa si sehemu salama kwenu kwa sasa"akasema Steve na kutoka nje Vicky na Winnie wakainuka wakaelekea chumbani.Steve akamtazama kwa hasira mlinzi aliyekuwa amekaa chini akitafakari.Alikuwa ameloa jasho mwili mzima.Tukio lile lilimuogopesha mno.Inaonekana hajawahi kukumbana na tukio kama lile. "Na wewe mni mlinzi wa aina gani?Ilikuaje ukakamatwa kirahisi na wale jamaa?Hujapitia mafunzo maalum ya kujihami?akauliza Steve kwa ukali "Nimepitia mafunzo kaka lakini wale jamaa ni wataalamu sana kwa namna walivyoweza kunidhibiti hata mimi nashangaa" "Natamani nikuchape vibao kwa uzembe huu mkubwa ulioufanya.Wewe umewekwa hapa ili kuwalinda hawa watu lakini wavamizi wamevamia kana kwamba hakuna mlinzi. Hufai kabisa kufanya kazi hii.Kumlinda mtu unayatoa maisha yako kwa ajili yake.Unatakiwa kupambana hata ikibidi kupoteza maisha kumuokoa mtu unayemlinda kuliko kukubali kukamatwa kizembe namna hii!! akasema Steve kwa ukali "Nisamehe brother.Naomba taarifa hizi zisifike kwa wakuu wangu.Nitajitahidi sana kuwa makini katika kazi" akajitetea yule mlinzi ambaye miguu yake ilikosa nguvu.Steve akamtaka ainuke haraka atoke mle sebuleni "Dada yule jamaa aliyetuvamia ni nani? Naomba unijibu ama sivyo sintaondoka hapa"akasema Winnie wakiwa chumbani kwa Vicky "Winnie tuko katika hatari kubwa hivi sasa na hawa jamaa wananitafuta kufuatia tukio lililotokea jana" "Unakiri kuwa jana umeua mtu? Kwa nini?Unajihusisha na mambo gani mabaya dada?Huoni kuwa unaniweka katika matatizo makubwa hata mimi?akauliza Winnie .Vicky akamshika mkono akamketisha kitandani "Hatuna muda wa kutosha lakini itanilazimu nikueleze japo kwa ufupi na ninakuomba uniamini na ufuate yale nitakayokuelekeza"akasema Vicky halafu akavuta pumzi ndefu "Mimi ni mpelelezi" "What? akauliza Winnie kwa mshangao "Shhhhhh!! Vicky akamfanyia ishara anyamazeMimi ni mpelelezi wa siri.Sikuwahi kukueleza kuhusu jambo hili kwa ajili ya usalama wako.Kwa sasa kuna jambo ninalichunguza na ndiyo maana yakatokea yale yaliyotokea jana na hawa jamaa kuanza kunifuatailia.tayari wanafahamu kuwa nimehusika katika kifo cha Pascal na wanaanza kunitafuta.Wanataka kujua kwa nini ndiyo maana wakamtuma yule jamaa kutuvamia lakini imekuwa bahati Steve amefika kwa wakati akatuokoa.Tupatapo nafasi nitakueleza zaidi kila kitu na kwa nini ninaifanya kazi hii.kwa sasa nakuomba ujiandae tuondoke kwani hapa si salama sana kwetu kwa sasa" akasema Vicky "Kwa nini ukanificha hukunieleza muda huu wote kama wewe ni mpelelezi?Huniamini hadi ukanificha?Winnie akauliza "Winnie sikukueleza chochote kuhusiana na jambo hili kwa ajili ya kukulinda.Sikutaka kukuingiza katika hatari.Naomba tuokoe muda Winnie,jiandae tuondoke" akasema Vicky "Tunakwenda wapi?Huko tuendako hao jamaa hawataweza kutufuata?Winnie akauliza "Winnie naomba uniamini dada yao nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kukulinda na kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakaye hatarisha maisha yako.Naomba unielewe" "Huyu jamaa aliyekuja kutuokoa ni mmoja wa wale jamaa waliokuwa wananichoma na umeme jana.Anataka kutupeleka wapi? " Winnie tutaongea vizuri baadae.Jiandae tuondoke"akasema Vicky na Winnie akatoka kwa shingo upande "Yule mtu ni nani na katumwa na nani?Yawezekana tayari wamekwisha fahamu kama nilishiriki katika kifo cha Pascal na sasa wanaanza kunisaka.Hii si vita ndogo”akawaza Vicky "Namshukuru sana Steve kwa kutokea kwa wakati na kutuokoa.Nilikuwa sina ujanja tayari nilikuwa nimenaswa.Lakini Steve alifahamuje kama niko katika matatizo?akajiuliza "Nisipoteze muda ngoja niongozane na Steve na nitapata ufafanuzi kutoka kwao kuhusu tukio hili la leo.Kwa sasa nahitaji sana kuwa karibu na akina Elvis kwani peke yangu siwezi kujilinda,tayari nimeanza kuwindwa na si mimi peke yangu bali na familia yangu hasa mdogo wangu Winnie.Nani lakini wananiwinda? akajiuliza na kuendelea kupakia nguo na baadhi ya vitu vichache katika sanduku na alipokuwa tayari akamfuata Winnie akamsaidia kuchukua baadhi ya vitu vyake vichache wakaondoka na kuwaacha nyumbani mlinzi pamoja na mtumishi wa ndani ambaye Vicky alimtaka aende mapumzikoni kwa wiki mbili na asimueleze mtu yeyote kile kilichotokea pale nyumbani







    Nyumbani kwa Elizabeth hakukuwa na watu wengi kwani msiba wa mumewe Deus ulihusisha ndugu na watu wengine wachache wa karibu na familia hasa wafanya biashara wakubwa. Elizabeth akiwa amekaa na baadhi ya wafanya biashara waliokuja kumfariji,simu yake ikaita akatazama mpigaji alikuwa ni Duma kijana aliyemtuma kuwafuatilia Juliana na Patricia ,akaomba samahani kisha akaelekea ndani na kumpigia Duma "Nipe ripoti" akasema Elizabeth "Madam nimewafuata Juliana na mwenzake kama ulivyonitaka.Walipotoka hapo walielekea moja kwa moja Mawenzi Complex na pale wakaingia Kibo Restaurant na na baada ya muda akatokea mzee mmoja hivi ambaye nahisi ndiye waliyekuwa wakimsubiri.Sikuweza kunasa mazungumzo yao ila kuna picha nimezichukua nitakutumia" akasema Duma Nini kiliendelea baada ya kukutana na huyo mzee? "Kwa namna walivyokuwa wakiiongea inaonekana walikuwa na mazungumzo nyeti sana na walipomaliza yule mzee akaondoka zake na akina Juliana wakaenda makaburini.Sifahamu walikwenda kutafuta nini kule na baada ya kutoka makaburini wakaelekea saloon ambako wako hadi sasa ninaendelea kuwafuatilia" "Good Job.Nitumie hizo picha sasa hivi" akasema Elizabeth na Duma akamtumia picha alizowapiga akina Juliana.Akazifungua na picha ya kwanza ikamstua sana Meshack jumbo!!! akasema Elizabeth kwa suti ndogo akiwa katika mshangao "Namfahamu Meshack Jumbo ni mkuu wa idara ya ujasusi.Wamefahamiana vipi na Juliana?Mambo gani walikuwa wanaongea? akajiuliza halafu akatabasamu "Nimepata jibu.Huyu alikuwa ni mkuu wa kazi wa Elvis mume wa Patricia na nina hakika hapa alikuwa na mazungumzo na Patricia na si Juliana.Hata hivyo Juliana hapaswi kuwa na ukaribu na watu kama hawa ambao ni hatari kwetu.Lazima nitafute namna ya kumuweka mbali na Patricia kwani kama wakiendelea kuwa karibu basi atakuwa akikutana mara kwa mara na hawa wapelelezi ambao wako karibu na Patricia.Suluhu pekee ni Patricia aondoke hapa nyumbani haraka sana.Sitaki aendelee tena kuwa na ukaribu na Juliana kwa sababu anafahamiana na wapelelezi wengi na iko siku huyu Meshack au mpelelezi mwingine yeyote anaweza kuja hapa nyumbani kumsalimu Patricia na akaanza kuchunguza mambo yasiyomuhusu”akawaza Elizabeth. "Dah ! Tayari nilikwisha anza kupatwa na wasi wasi mkubwa kumuona Juliana na Meshack Jumbo" akawaza Elizabeth na kutoka chumbani na kuelekea waliko waombolezaji ****************** Ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Sahare ulijaa waandishi wa habari walioitika wito wa viongozi wa vyama vya siasa waliowataka waandishi wa habari kufika katika hoteli hiyo kwa ajili ya mkutano maalum.Saa tano kasoro dakika mbili Dr Makwa Tusangira na wenyeviti wenzake wa vyama vya upinzani wakawasili katika chumba cha mikutano na ukumbi ukawa kimya .Dr Makwa ambaye ndiye kiongozi wa jopo lile la viongozi wa vyama vya siasa akasimama na kuwasalimu waandishi wa habari "Habari za asubuhi ndugu waandishi wa habari.Kwa niaba ya wenzangu wote walioko hapa mbele ninapenda nitoe shukrani zangu nyingi kwenu kwa kuitika wito wetu na kufika kwa wingi sana.Hatukutegemea kama mngeitika kwa wingi namna hii"akanyamaza halafu akafungua kitabu chake alichoandika yale ambayo alitaka kuwaeleza waandishi,akasoma kidogo na kusema "Ndugu zangu waandishi wa habari,walioko mbele yenu pamoja nami ni wenyeviti wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu na uwakilishi bungeni.Karibu vyama vyote vya siasa vilivyo na usajili wa kudmu hapa nchini kiongozi au mwakilishi wake yuko hapa.Huu ni muunganiko mkubwa wa vyama vya siasa na tumeamua kuwa kitu kimoja ili tuwe na nguvu moja katika kupigania zile hoja zetu za msingi kwa maendeleo ya nchi yetu Tanzania" akanyamaza akasoma kidogo halafu akaendelea "Ndugu waandishi wa habari,tumewaiteni hapa siku hii ya leo ili kupitia kwenu wafuasi wetu wa vyama vya upinzani na watanzania wote hasa wale wapenda maendeleo waweze kupata kile ambacho tumekusudia kiwafikie.Kikubwa tulichowaitia hapa ni kuwafahamisha wafuasi wetu kuhusiana na mkutano mkubwa tuliowatangazia kuwa utafanyia siku yakesho.Tumewasilisha taarifa mapema kwa jeshi la polisi kuwaomba waturuhusu tufanye mkutano wetu wa hadhara siku ya kesho lakini bila sababu za msingi jeshi la polisi wametukatalia tusifanye kufanya hivyo.Tumetuma wawakilishi kwenda kwa viongozi wa juu wa jeshi la polisi kuomba tufanye mkutano wetu wa hadhara lakini bado tumenyimwa na hakuna sababu yoyote kubwa ya msingi iliyotolewa kwa nini tunazuiwa kufanya mkutano wetu kwa amani.Huu ni ukandamizaji mkubwa wa demokrasia unaoendelea hapa nchini kwetu"akanyamaza kidogo halafu akaendelea Kupitia kwenu ndugu waandishi wa habari tunapenda kuwataarifu wafuasi wetu kuwa licha ya jeshi la polisi kutuzuia tusifanye mkutano wa hadhara lakini siku ya kesho wafike kwa wingi sana katika viwanja vya jamhuri ambako tutafanya mkutano wetu mkubwa wa hadhara na viongozi wote wa vyama vya siasa hapa nchini watahudhuria.Katika mkutano huo tutaeleza dhumuni letu la kuunda umoja huu wa vyama vya siasa vya upinzani na nini hasa shabaha yetu.Njooni siku ya kesho mje msikilize namna nchi yenu inavyouzwa,namna rasilimali zenu zinavyofilisiwa na wajanja wachache ambao wanatumia kila aina ya nguvu waliyonayo kuhakikisha kwamba wananchi hawafahamishwi kuhusu mambo maovu wanayoyafanya.Wakati umefika sasa wa kuweka wazi mambo yote tunayofanyiwa watanzania.Wakati umefika wa kukomesha unyoyaji huu mkubwa wa rasilimali zetu. Nawasihi msiogope tujitokezeni kwa wingi sana katika mkutano wa kesho ambapo mambo makubwa ya kitaifa yatajadiliwa"akanyamaza na kuwatazama waandishi wa habari na kuendelea "Nawasihi tena wafuasi wetu na wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii msiache kuja kesho tuanze pamoja safari ya ukombozi wa nchi yetu.Hatutaogopa mabomu au risasi za polisi.Hatutafanya fujo bali tutafanya mkutano wetu kwa amani na utulivu mkubwa.Nawaomba vyombo vya dola wasiwazuie wananchi kuhudhuria mkutano wetu kwani tutahakikisha hawafanyi vurugu bali wanakaa kwa amani wakiwasikiliza viongozi wao" “Ndugu zangu waandishi wa habari kwa leo ni hayo tu machache niliyowaitia hapa naamini nyote tutakutana kesho katika viwanja vya jamhuri.Naomba mfike kwa wingi sana kuna mambo mengi mtayasikia siku ya kesho ili muweze kuwahabarisha wananchi.Kwa kuwa muda mfupi ujao tutakuwa na kikao na hawa wakuu hakutakuwa na maswali kutoka kwenu bali tutapanga tena mkutano mwingine ambako mtapata fursa ya kuuliza mawali yenu ila kwa leo mtatuwia radhi kwani muda si rafiki kwetu.Ahsanteni sana kwa kuja na ninawatakia kila la heri katika shughuli zenu za kila siku.Mungu awabariki sana" akamaliza Dr Makwa na wenzake wote wakasimama wakatokea mlango wa nyuma na kuwaacha waandihsi wa habari waliokuwa na kiu kubwa ya kutaka kuuliza maswali Mara tu baada ya kumaliza mkutano ule na waandishi wa habari Dr Makwa akampigia simu David "David kila kitu kimekwenda vizuri.Tumemaliza kikao na waandishi wa habari na sasa tunaingia katika kikao cha ndani.Ninakukumbusha kuhusu zile fedha ziwe tayari leo hii kwani mambo yameanza kupamba moto.Tayari tumekwisha tangaza mgogoro na serikali" "Kazi nzuri Dr Makwa.Usijali kuhusu fedha.Suala hilo linashughulikiwa na mpaka badae kila kitu kitakuwa tayari" akasema David ambaye naye baada ya kukata simu akampigia Dr Shafi "Dr Shafi kila kitu kinakwenda vizuri.Muda mfupi uliopita Dr Makwa ametangaza mkutano wa hadhara kesho licha ya polisi kupiga marufuku mkutano huo na hapo ndipo safari yetu itakapoanzia.Nimeona nikujulishe namna mambo yanavyokwenda" "Ahsante sana kwa taarifa David.Nina imani kila kitu kitakwenda kama tunavyotarajia.Endelea kunihabarisha kila hatua inapopigwa"akasema Dr Shafi wakaendelea na mazungumzo mengine **************** Steve aliwasili katika makazi yao akiwa ameongozana na Vickyna mdogo wake Winnie.Akawakaribisha ndani "Dada siwezi kukaa hapa" akasema Winnie baada ya Steve kutoka kwenda kumuita Elvis "Winnie tafadhali hii ni....."kabla hajamaliza sentensi yake Elvis akatokea "Karibuni sana" akasema Elvis "Dada sitaki kukaa hapa.Sitaki kumuona huyu jamaa ambaye jana amenichoma na umeme !! I dont want to be near this monster!! akasema Winnie kwa ukali "Steve mpeleke Winnie kwa Graca" akasema Elvis na Steve akamchukua Winnie akampeleka chumbani kwa Graca halafu akarejea sebuleni "Nilikupigia simu lakini ikakatwa na haikupatikana tena.What happened? akauliza Elvis.Steve akamuelezea kila kitu kilichotokea "Ninashukuru sana kwa Steve kufika kwa wakati kwani bila yeye sijui yule jamaa angetufanya nini kwani tayari sikuwa na ujanja wa kujinasua"akasema Vicky "Huyo jamaa unamfahamu?Umewahi kumuona? "Hapana simfahamu na ni mara yangu ya kwanza kumuona" "Nini hasa alichokuwa anakitafuta? Swali pekee aliloniuliza ni akina nani ninashirikiana nao?Kabla sijamjibu chochote akatokea Steve ambaye aliweza kupambana naye akatuokoa lakini kwa bahati mbaya akafanikiwa kumjeruhi Steve kwa risasi begani na akakimbia"akasema Vicky "That man was a professional" akasema Steve huku akivua shati lake na Elvis akalikagua jeraha alilojeruhiwa na Obi "kwa bahati nzuri risasi haikuweza kuingia ndani ilikwaruza kwa nje.Pole sana" akasema Elvis "Ilikuaje hadi huyo jamaa akafanikiwa kuingia ndani na kuwawekeni chini ya ulinzi?Hakuna walinzi nyumbani kwako? "Kama alivyosema Steve huyo jamaa ni mzoefu sana kwani akiwa na mwenzake mmoja walifanikiwa kumdhibiti mlinzi mmoja aliyekuwepo getini halafu wakaingia ndani wakamdhibiti msichana wa kazi na kumfuata Winnie chumbani kwake kwani kwa muda huo sote tulikuwa tumelala kutokana na uchovu wa jana usiku,wakamtumia msichana wa kazi kugonga mlango wangu na akaniita hivyo sikuwa na wasi wasi na nilipofungua tu nikajikuta nikitazamana na bastora wakanikamata wakanifunga mikono na sote tukawekwa sebuleni na yule jamaa akaanza kunihoji ,kwa habati nzuri akatokea Steve na kutuokoa.Mlifahamuje kama tuko katika hatari?akauliza Vicky "Nilipigiwa simu na mkurugenzi wetu akaniambia kwamba amepewa maelekezo na makamu wa rais ukamatwe ukahojiwe kisha uuawe.Tayari wanazo taarifa kwamba umeshiriki katika mauaji ya Pascal .Wewe ni mmoja wa watu unaoshirikiana nao na walipogundua kwamba umeshiriki katika mauaji ya Pascal wamestuka na wanataka kujua kwa nini umeshiriki katika tukio lile na ndiyo maana maelekezo ya makamu wa rais ni kukuteka wakuhoji na uwataje wale wote ulioshirikiana nao katika kifo cha Pascal halafu wakuue.Baada ya kupokea maelekezo hayo kutoka kwa mkurugenzi wetu nikapiga simu yako ili nikutahadharise lakini haikuwa ikipatikana ndipo nilipomtuma Steve haraka sana akufuate.Nilipatwa na wasi wasi baada ya kumpigia simu ya Steve ikaita na kukatika halafu haikupatikana tena" "Kuna simu ilipigwa wakati nikiwa nje nikimvizia kijana aliyekuwa na yule jamaa na nikaizima haraka na sikukumbuka kuiwasha tena" akasema Steve "Imekuwa vyema kuwa Steve alifika kwa wakati na kuzima jaribio hilo la http://deusdeditmahunda.blogspot.com/hao wavamizi.Lazima mfahamu kuwa hivi sasa mnawindwa ila ninawahakikishia kuwa hapa mtakuwa salama.Tuliweke kwanza hilo pembeni.Umewasiliana na Omola? "Bado sijawasiliana naye nilikuwa nimezima simu" akasema Vicky na kuwasha simu yake akazitafuta namba za Omola na kupiga "Vicky nimekutafuta simuni lakini hukuwa ukipatikana” akasema Omola “Nilikuwa katika kazi iliyonilazimu nizime simu.Vipi umeamua nini? “Nimeweka vizuri ratiba yangu na nitakuja Tanzania ila kwa wiki moja tu.Kama kazi unayotaka nikusaidie itachukuazaidi ya wiki moja utanisamehe sintaweza" "Asante sana Omola.Kazi yenyewe haitazidi wiki moja.Nashukuru sana kwa siku hizo chache ulizojitolea kuja kunisaida.Lini unategemea kuja Tanzania? "Nitaondoka saa tisa alasiri na saa kumi na mbili za jioni nitawasili Dar es salaam.Nitakujulisha nitakapoanza safari" "Ahsante sana Omola.Nikutakie safari njema"akasema Vicky "Omola amekubali kuja Tanzania kutusadia japo ametoa sharti kwamba ana nafasi ya wiki moja tu" Hata siku hizo saba zinatosha sana.Atakuwa ametusaidia mambo mengi ndani ya siku hizo chache.Anatakiwa kuandaliwa hoteli nzuri atakayokaa kwa muda wa siku hizo zote atakazokuwa hapa nchini.Aandaliwe gari zuri na kila chochote kitakachomfaa" "Sawa nitalishughulikia hilo suala" akasema Vicky.Baada ya ukimya mfupi akauliza " Kwa sasa nini kinachoendelea? "Kitu ambacho unatakiwa ukifanye kwa sasa ni kuonana na rais kuanza maandalizi ya kumuunganisha Omola na makamu wa rais.Rais anapaswa afahamu kuhusu mpango wa kumtumia Omola kumchunguza Dr Shafi na yeye ndiye aandae mazingira ya Omola na Dr Shafi kukutana.Sisi tunaendelea kuandaa mikakati ya kumchunguza Frank.Unadhani rais anaweza kukubali kuonana nawe? “Rais hawezi kukataa kuonana nami.Nitamjulisha kuwa ninahitaji kumuona.Hata hivyo nina wazo moja Elvis,kama tayari mnafahamu na mnao ushahidi usio na shaka kuwa Frank anajihusiaha na biashara hii ya silaha kwa nini basi asikamatwe ateswe na ataje wote anaoshirikiana nao? "Kweli hatuna shaka kuhusu Frank kujihusisha na biashara hii ya silaha lakini hatuwezi kufanya hivyo, kumkamata na kumtesa ili atuonyeshe mtandao wake.Hata kama tukimkamata tukamtesa hataweza kutueleza kuhusu mtandao wake kwani watu kama hawa wamekula yamini ya kutokusema siri zao na yuko radhi afe kuliko kutoa siri hivyo hataweza kutusaidia kwa lolote hata kama tukimpa mateso ya aina gani.Alikuwa tayari kumuua mtoto wake ili kuilinda siri hii hivyo hataweza kabisa kutamka chochote hata akiteswa.Tunachotakiwa kufanya ni kumchunguza na hatimaye kuubaini mtandao wake wote na tuung'oe hadi mizizi yake.Usihofu Vicky tutawapata tu japo inaweza kuchukua muda kidogo lakini lazima tutawapata" "Sawa Elvis mimi ngoja niwasiliane na rais niombe kuonana naye" akasema Vicky "Vicky kumbuka unapozungumza na rais usimueleze chochote kuhusu kushirikiana nasi.Mueleze kwamba mpango huu unaufanya wewe peke yako na haushirikiani na yeyote" "Nimekuelewa Elvis nitafanya hivyo.Ni wapi chumba changu? Steve akampeleka Vicky katika chumba atakachokitumia halafu akarejea sebuleni "Elvis kama tusingewahi tungeweza kumpoteza Vicky kwani yule jamaa aliyetumwa kumteka ni mtaalamu sana.Anaweza kucheza na silaha na hata karate pia.Kama nisingekuwa makini angeweza kuniua"akasema Steve "Pole Steve.Tuliweke kwanza pembeni suala hilo la Vicky kwani tayari tumekwisha muondoa katika hatari.Mkurugenzi alikuwepo hapa na kuna jambo alikuja kunieleza" "Jambo gani Elvis? "Ameonana na Patricia asubuhi hii wakazungumza lakini Patricia hakuwa na tatizo lolote bali rafiki yake anaitwa Juliana.Huyu Juliana ni mwanamitindo maarufu sana hapa nchini lakini kwa muda mrefu amekuwa akiishi nje ya nchi na sasa amerejea nchini.Juliana ana tatizo na anahitaji msaada" akasema Elvis na kisha akamsimulia Steve tatizo la Juliana "Elvis kwa maelezo hayo uliyonipa ninapata picha kwamba haya ni mauaji ya visasi.Kuna kila sababu ya kuamini kuwa wanaofanya mauaji yale aidha wana kisasi na Juliana au wana kisasi na familia yao" "Hata mimi nilimweleza hivyo mkurugenzi.Pamoja na kwamba tuna shughuli kubwa mbele yetu lakini lazima tumsaidia pia Juliana.Tumuhoji na atueleze kwa kina zaidi na tutaweza kubaini namna ya kumsaidia" "Juliana tutampataje? Mkurugenzi atatuunganisha naye.Kwa mchana huu wakati tunamsubiri Omola,Vicky anafanya mpango wa kuonana na rais hivyo nawe itumie nafasi hii kuzungumza na Juliana.Mimi nitazungumza na Graca na kumuhoji zaidi ili nione kama ataweza kutusaidia namna nyingine ya kumchunguza zaidi baba yake" akasema Elvis halafu akampigia simu Meshack Jumbo akamjulisha kuwa Steve anataka kwenda kuonana na Juliana na Meshack akawaomba wasubiri ili awasiliane na Juliana.Vicky akarejea sebuleni "Nimezungumza na rais na amekubali kuonana nami ila amesema niwahi kabla ya saa saba kwani kwa muda huo anategemea kuwa na wageni muhimu hivyo natakiwa kuwahi" "Sawa Vicky,jiandae uende ikulu kuonana na rais.Utatumia moja wapo ya gari hapo nje.Steve kuna kazi anaenda kuifanya angeweza kukusindikiza na kuhakikisha unakuwa salama" "Usihofu Elvis nitakuwa salama.Ninaweza kujilinda.Ni kwa bahati mbaya tu yule jamaa aliniwahi lakini asingeniweza hata kidogo.Ngoja nikajiandae nielekee ikulu kuonana na rais" akasema Vicky na kwenda chumbani kwake kujiandaa.Baada ya dakika nne Meshack Jumbo akapiga simu "Nimewasiliana na Juliana ameniambia kwamba kwa sasa yuko saluni lakini ameelekeza sehemu ya kukutana na Steve" akasema Meshack na kumuelekeza Steve mahala ambako atakutana na Juliana akamtumia pia namba zake za simu ili akifika sehemu hiyo awasiliane naye Steve na Vicky baada ya kujiandaa kila mmoja akaondoka kwenda kushughulkikia jukumu alilopewa na pale nyumbani wakabaki Elvis Graca na Winnie "Nadhani ni muda muafaka wa kuongea na Graca.Anaweza kutusaidia kupata namna ya kumchunguza zaidi baba yake.Yeye anamfahamu vizuri zaidi kuliko mtu yeyote" akawaza Elvis na kuelekea chumbani kwa Graca akabisha hodi,Graca akaufungua mlango "Elvis karibu ndani" akasema Graca na Elvis akaingia mle chumbani,Winnie alipomuona akajifunika na mto. “Winnie" akaita Elvis lakini Winnie hakujibu kitu "Elvis kwa sasa Winnie hayuko tayari kuzungumza nawe lolote.Mpe muda muache apumzike na atakapokuwa tayari mtazungumza" akasema Graca "Sawa Graca ila lengo langu ni kutaka kumuelewesha tu hali halisi ilivyo.Hata hivyo nitazingatia ushauri wako na nitasubiri hadi hapo atakapokuwa ametulia ili nizungumze naye" "Sawa Elvis"Graca tunaweza kuzungumza kidogo? akasema Elvis "Hakuna tatizo" akasema Graca kisha wakatoka wakaenda kukaa katika viti vya kupumzikia pembeni ya bwawa la kuogelea. "Mambo yanakwendaje Elvis?Huyu Winnie na mama yake ni akina nani na kwa nini wako hapa? akauliza Graca "Samahani kwa kutokufahamisha Graca ila hawa ni wenzetu tutaishi nao hapa nyumbani kwa muda wakati tukiendelea na operesheni yetu.Vicky mama yake Winnie ni mpelelezi na ameungana nasi ili kutusaidia katika kazi yetu na kwa kuwa hivi sasa wako katika hatari tumeona itakuwa vyema endapo watakaa nasi hapa nyumbani ili kuhakikisha usalama wao hasa Winnie" "Nimefuarahi kusikia hivyo.Vicky ni mwanamke mrembo sana.Kumbe hata mimi ninafaa kuwa mpelelezi.Kama Vicky mwanamke mrembo namna hii ameweza hata mimi nitaiweza" akasema Graca "Graca sikuzuii kuipenda hii kazi lakini sikushauri utake kuifanya.Ni kazi yenye hatari nyingi.Ona maisha yangu yalivyo hivi sasa.Kama ningekuwa katika kazi nyingine nisingekuwa na maisha haya hivi sasa.Ni kazi nzuri lakini lazima ukubali kwamba hautakuwa na maisha ya kawaida.Ukitaka kuifanya kazi hii ujiandae kwa hilo" akasema Elvis "Ninaipenda hii kazi japo bado sijafikiria kuifanya ila nitazingatia ushauri wako.Vipi kuhusu uchunguzi unaendeleaje? akauliza Graca "Uchunguzi wa kuubaini mtandao wa baba yako umeanza japo hatujapiga hatua kubwa bado lakini kuna mambo tayari tumeyagundua.Kwanza naomba ufahamu kuwa Pascal yule mshirika mkubwa wa baba yako amefariki dunia usiku wa kuamkia leo" "Pascal !! "Ndiyo.Yule alikuwa ni mshirika mkubwa na mtu muhimu sana katika uchunguzi wetu lakini amefariki jana kwa bahati mbaya wakati tukiwa katika harakati za kumpata ili tumuhoji.Hata hivyo kifo chake hakiwezi kutuzuia kuendelea mbele.Uchunguzi unaendelea na hivi tuongeavyo Steve na Vicky wote wametawanyika katika majukumu niliyowapa" "Natamani kusikia baba amekamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.Ni mtu mkatili sana yule,mambo aliyotufanyia mimi na mama ni mabaya mno na mengine siwezi kueleza.Itakuwa ni sherehe kubwa kwangu siku nitakapomshuhudia akiwa katika pingu" akasema Graca akionekana kuwa na hasira za wazi juu ya baba yake Hilo litafanyika Graca na baba yako pamoja na wenzake wote anaoshirikiana nao katika biashara yake haramu watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria" "Naingoja kwa hamu sana siku hiyo.Nataka nimuone baba yangu akiwa kizimbani akijibu tuhuma zinazomkabili na mimi nitasimama kama shahidi.Nitaeleza uovu wake wote alioufanya" akasema Graca "Graca narudia tena kukuhakikishia kwamba hilo litafanyika lakini nahitaji msaada wako zaidi” "Sema Elvis unauhitaji msaada gani?Niko tayari kukusaidia kwa lolote ambalol iko ndani ya uwezo wangu”akasema Graca "Tunafahamu baba yako ni kinara katika biashara hii ya silaha lakini hatuwezi kumkamata yeye peke yake bali lengo letu ni kuuondoa kabisa mtandao wote unaojishughulisha na biashara hii.Ili tuufahamu mtandao wote lazima tumfanyie baba yako uchunguzi wa kina.Nataka utusaidie ni kwa namna gani tunaweza kumchunguza zaidi baba yako?Kuna mahala unadhani tunaweza kupata nyaraka au ushahidi wowote wa kuweza kutusadia?Kuna mtu yeyote unayemfahamu ambaye unadhani anaweza akatusaidia kupata taarifa za uhakika kuhusu Frank na mtandao wake?Nafahamu umetusaidia sana na hadi hapa tulipofika ni kwa sababu yako lakini bado nahitaji msaada wako zaidi.Kama kuna lolote ambalo unaona linaweza kutusaidia kupata taarifa za kutosha kuhusu baba yako na mtandao wake nisaidie tafadhali" akasema Elvis.Graca akatabasamu "Nilifahamu iko siku utakuja kuniomba kitu kama hicho na nilikuwa naisubiri sana siku kama hii.Ni wakati wangu wa kutimiza kile nilichokuwa nakitaka" akawaza Graca "Unasemaje Graca kuhusu ombi langu hilo?Unaweza ukatusaidia?Elvis akauliza Elvis I'm not comfortable here.Twende tukazungumzie suala hili ndani.Twende chumbani kwako" akasema Graca kisha wakainuka wakaelekea chumbani kwa Elvis "Haya nieleze Graca unachotaka kunieleza" akasema Elvis "Elvis ninaweza kukusaidia kupata taarifa muhimu kuhusu baba.Kuna sehemu anahifadhi taarifa zake za siri.Nitakusaidia kukupeleka mahala hapo ambako nina imani utapata mambo mengi yatakayokusaidia" "Ahsante sana Graca.Nakuhakikishia kuwa nitakulinda kwa kila namna niwezavyo" akasema Elvis huku naye akitabasamu "Hata hivyo" akasema Graca na Elvis akamtazama kwa makini "I need something in exchange.Kuna kitu nakihitaji kutoka kwako na tafadhali usiseme hapana kwani ni muhimu mno kwangu" akasema Graca "Graca nakuhakikishia kitu chochote utakachokihitaji utakipata hata kama sina nitahakikisha unakipata" akasema Elvis kwa kujiamini "Are you sure?Graca akauliza "Yes I'm sure" "Good"akasema Graca halafu akakaa kimya kama vile anaogopa kusema kile anachokihitaji" "Sema Graca unahitaji nini? Nimekuwa katika hospitali ya magonjwa ya akili kwa muda mrefu sasa na katika muda huo wote sijawahi kuwa na furaha.Ninataka sasa kuanza kuishi kama wenzangu.Nataka niwe na furaha nifurahi kama wenzangu.Ili furaha yangu ikamilike ninahitaji mtu wa kunipa raha za dunia na kunifanya niwe na furaha kila sekunde" "Graca usihofu.Sisi tuko hapa na tutakusadia kwa kila hali kuhakikisha kwamba unakuwa na furaha tele katika maisha yako.Ahadi yangu kwako siku zote ni kufanya uso wako uwe na tabasamu"akasema Elvis "Nalifahamu hilo na ninawashukuru sana nyote kwa namna mlivyojitolea kunitunza na kunilinda.Hata hivyo ninaposema kwamba nahitaji mtu wa kunipa raha za dunia namaanisha nahitaji kuwa na mpenzi.Nahisi nataka kuingia tena katika mapenzi.Nahitaji mpenzi na hicho tu ndicho ambacho ninakihitaji kwa sasa" "Graca siwezi kukuzuia jambo hilo lakini nadhani huu si wakati wake .Mambo yako yakishakaa vizuri basi utakuwa na nafasi pana zaidi ya kuchagua mpenzi umtakaye.Ninakushauri kwa sasa uliweke pembeni suala hilo.Sisi tupo hapa tutahakiksha unakuwa na maisha mazuri na hapo ndipo utakapokuwa na uhuru wa kuchagua mwanaume umtakaye" akasema Elvis "Elvis sina haja ya kusubiri kwa muda mrefu wakati tayari nimekwisha zama mapenzini" "Umezama mapenzini? Mbona sikuelewi Graca? akauliza Elvis "Ndio Elvis.I'm in love with you" akasema Graca na maneno yale yakamstua sana Elvis akamtazama Graca kwa mshangao.Wakatazamana kwa dakika moja Graca akasema "Hukutegemea kusikia kitu kama hiki kutoka kwangu Elvis lakini huo ndio ukweli.Ninakupenda sana na wewe ndiye mwanaume pekee ambaye nakuhitaji katika maisha yangu.Elvis naomba tafadhali usinielwe vibaya,hata mimi sikutegemea kabisa kitu kama hiki kunitokea.Nimejikuta tu nikikupenda bila sababu.Moyo wangu umekuridhia wewe.Najua kiumri hatulingani lakini hiyo si hoja bado tunaweza kuwa wapenzi.Naamini haitakuwa rahisi kurejeana tena na mkeo Patricia hivyo mimi niko hapa nitakupa kila aina ya huduma unayoikosa kutoka kwa mkeo Pat......" "Graca please stop" akasema Elvis na kujikuta ameshika kichwa "Tafadhali naomba usirudie tena kutamka maneno kama hayo" "Elvis nafahamu ni vigumu sana kwako kunikubalia ombi langu lakini naomba ufahamu kwa ni kweli ninakupenda na ninahitaji kuwa na wewe.Ukilikubali hilo nitakupeleka mahala ambako utapata kila kitu unachokihitaji.Fikiri kuhusu hilo halafu utanijibu" akasema Graca na kusimama ili aondoke "Graca naomba ukae tafadhali" akasema Elvis na Graca akaketi "Graca huu si wakati wa utani.Tuko vitani tunapambana na mtandao mkubwa wenye nguvu.Watu hao ni makatili na wasio na hata chembe ya huruma.Nimejitoa mhanga kupambana nao na kuhakikisha ninaufutilia mbali mtandao wao hivyo nahitaji msaada mkubwa kutoka kwenu.Unadhani ni jambo rahisi kuamua kuwadanganya watu ninaowapenda kuwa nimekufa?Unadhani ninafurahi mateso anayoyapata mke wangu Patricia?Nimewaumiza watu wengi sana lakini si makusudi bali kwa ajili ya kupata nafasi nzuri ya kuusafisha mtandao huu wote ambao unauza silaha zinazotumiwa na waasi kuua watu huko mashariki ya Congo.Wewe pia ni mmoja wa waathirika wa mandao huu kwani baba yako ambaye ni kinara wa biashra hii ya kuuza silaha amekutesa sana hadi kukupeleka katika hospitali ile ya magonjwa ya akili.Nimefanya haya wa ajili yenu ninyi wote mnaomizwa na mtandao huu.Nataka niwakomboe ili muwe huru hivyo nahitaji sana ushirikiano mkubwa kutoka kwenu.Jambo unalolihitaji ni gumu kukutekelezea kwa sababu kwanza mimi ni mume wa mtu na ninampenda sana mke wangu Patricia.Pili wewe ni kama mdogo wangu hivyo siwezi kuwa na mahusiano na mtu mwenye umri wa mdogo wangu.Naomba tusilifanye suala hili liwe gumu Graca nieleze kile unachokifahamu kuhusu baba yako ili tuweze kuufutilia mbali mtandao wake na hatimaye wewe na wote mlioteseka kwa uwepo wao muweze kupumua na hata wewe uweze kuwa huru na kufanya chochote ukitakachoikiwamo kumtafuta mpenzi atakayekufaa.Tafadhali sana Graca" akasema Elvis "Elvs utanisamehe sana hata mimi sikutaka kuyatamka maneno haya ila nimeshindwa kuvumilia.Moyo wangu unateseka na kuumia kwa namna ninavyokupenda.Siwezi kueleza ni kwa namna gani umeweza kuingia moyoni mwangu na kung'ang'ania kiasi hiki.Nakupenda sana Elvis na ndio maana niko tayari kufanya lolote hata la hatari kwa ajili yako.Nataka ufanikiwe katika operesheni hii,nataka uuondoe mtandao huu wote wa baba lakini hata mimi ninataka mahitaji yangu yatimie pia na hitaji langu pekee ni kuwa nawe.Hata kama si kwa maisha yote basi kwa wakati huu ambao tuko hapa naomba tafadhali tuwe wote.Umri wetu isiwe kigezo cha mimi na wewe kutokuwa wapenzi.Nakubali umenizidi umri lakini bado tunaweza kuwa na mahusiano yenye furaha.Elvis si rahisi kwangu kukutamkia maneno kama haya mtu kama wewe ambaye umenisaidia kwa mengi na bado nahitaji msaada wako ila nimeshindwa kujizuia na kuamua kukueleza kweli japo naamini unaweza ukaniona kama mgonjwa wa akili lakini mimi ni mzima wa afya na sina tatizo lolote la kiakili.Naliongea hili nikiwa na akili zangu timamu" akasema Graca halafu akainuka Elvis lifikirie saula hilo na utakapokuwa tayari unijulishe" akasema Graca na kuondoka akimuacha Elvis haamini alichokisikia kutoka kwa Graca "Ama kweli haya ni maajabu ya Musa.Graca!! akasema na kuinuka akatikisa kichwa " Sikutegemea kabisa kusikia maneno kama yale kutoka kwa Graca.Sura yake haifanani kabisa na maneno aliyoyatamka.Eti anataka mimi na yeye tuwe wapenzi!! Nini kimemuingia Graca hadi akatamka maneno kama yale.Anawezaje kunipenda mtu kama mimi ambaye kwanza hatulingani kiumri,pili mimi nina mke wangu ambaye siachi kueleza namna ninavyompenda.Sikutegemea kabisa jambo kama hili" akawaza Elvis " Nataka ufanikiwe katika operesheni hii,nataka uuondoe mtandao huu wote wa baba lakini hata mimi ninataka mahitaji yangu yatimie pia na hitaji langu pekee ni kuwa nawe.Hata kama si kwa maisha yote basi kwa wakati huu ambao tuko hapa naomba tafadhali tuwe wote.Umri wetu isiwe kigezo cha mimi na wewe kutokuwa wapenzi.Nakubali umenizidi umri lakini bado tunaweza kuwa na mahusiano yenye furaha."maneno haya ya Graca yakaendelea kujirudia kichwani kwa Elvis Dah ! nahisi huyu Graca bado atakuwa na matatizo ya akili.Maneno kama haya hayawezi kutoka kwa mtu mwenye akili zake timamu.Lakini…....” akawaza Elvis na kusita kidogo “Graca hana matatizo ya akili na nilipomtazama machoni alionyesha wazi kumaanisha kile alichokisema yaani ananitaka kimapenzi.Oh my God nitafanya nini?Nahitaji sana msaada wake na yupo tayari kunisaidia ila ametoa sharti kwamba ili nisaidie lazima nimkubalie tuwe na mahusiano ya kimapenzi.Nitawezaje kuwa na mahusiano na mtu mwenye umri wa mdogo wangu?Kwa nini kila wakati wanawake huniweka katika majaribu makubwa.Kwanza alianza Doreen ambaye ni wazi ananitaka na anafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa ninakuwa na mahusiano naye japo nimejaribu kumkwepa lakini bado ni king’ang’anizi.Nimefanikiwa kumuondoa hapa na kumuweka mbali ila naamini atarejea tena na kabla hilo sijalimaliza anaibu ka tena Graca na jambo lake.Kwa nini wananifanyia hivi hawa wanawake? Akajiuliza Elvis “Graca hakupaswa kunifanyia hivi wakati anafahamu kabisa kwamba jambo hili ninalolifanya ni kwa faida yake mwenyewe.Kwa mateso makubwa aliyoyapitia kutoka kwa baba yake alipaswa kunipa ushirikiano mkubwakuhakikisha kwamba ninaufyeka mtandao wa baba yake asiye na huruma hata chembe lakini anaonekana amekwisha sahau ukatili wote wa baba yake na sasa anataka kutumia nafasi hii kufanya mambo ambayo hayatamletea faida yoyote” Akaendelea kuwaza Elvis “Nifanyaje kumshawishi Graca anieleze mahala ninakoweza kupata taarifa zaidi kuhusu mtandao wa baba yake bila kumkubalia ombi lake? Akajiuliza Elvis na kutoka akaenda kukaa nje “Huwaogopi hawa jamaa? Winnie akamuuliza Graca aliporejea chumbani kwake Siwaogopi.Kwa nini wewe unawaogopa? “Ni watu makatili sana hawa hasa huyu jamaa aliyekuja kukuita muda mfupi uliopita” “Elvis? “Simfahamu jina lake lakini ni mkatili sana yule.Alinichoma na umeme kama mimi si binadamu na sikuwa nimemfanyia kosa lolote.Siwezi kusahau mateso niliyoyapata kwa usiku wa jana” akasema Winnie huku akionekana kulengwa na machozi “Sikiliza Winnie hawa jamaa si watu wabaya hata kidogo.Ni watu wema sana lakini wanapokuwa kazini huwa wanabadilika na ndiyo maana wanaonekana wakatili” Who are they? “Hawa ni wapelelezi”akajibu Graca “Vipi kuhusu wewe imekuaje ukafika hapa?Umekutaka wapi na hawa jamaa?Nawe pia ni mpelelezi?Winnie akauliza “Hapana mimi si mpelelezi” akasema Graca na kumsimulia Winnie kila kitu kuhusiana na maisha yake historia iliyomshangaza sana Winnie “Sikujua kama umepitia mambo mengi namna hiyo.Pole sana Graca.Huyo baba yako anaonekana ni mtu mkatili sana.Ni mtu wa namna gani huyu anayeweza kumfanyia ukatili huu mtoto wake wa kumzaa mwenyewe?akauliza Winnie na Graca akamuelekeza mahala anapoishi baba yake “kwa hiyo una mpango gani na maisha yako ya mbele? “Kwa sasa ninamsubiri Elvis amalize operesheni yake na atanisaidia kwenda kuishi nchi ya mbali ambako nitakuwa salama na hakuna ambaye atatishia tena maisha yangu” akasema Graca “Hilo ni wazo zuri lakini unawaamini hawa jamaa kama watakusaidia kuyaanza upya maisha yako? “Ninawaamini hawa jamaa hasa Elvis.Amepitia mambo mengi na mazito kwa ajili yangu na hawezi kuniangusha hata kidogo” akasema Graca na mlango ukagongwa akaufungua na kukutana na Elvis “Graca nakuomba tuzungumze”akasema Elvis kisha Graca akatoka wakaenda chumbani kwa Elvis “Graca nimetafakari kuhusu lile suala uliloniambia lakini jibu langu ni hapana.Siwezi kufanya au kuwa na mahusiano nawe.Wewe ni mdogo wangu na ninafanya haya yote kwa sababu yako na wengine wale wanaoteseka kutokana na silaha zinazouzwa na mtandao wa baba yako.Please don’t make this hard for me.Nahitaji sana msaada wako ili niweze kuumaliza mtandao huu na wewe uwe huru.Ukiwa huru utaweza kumpata mwanaume wa hadhi yako ambaye utampenda kuliko wote lakini mimi haitawezekana”akasema Elvis “Elvis nimekwisha weka wazi kwako kwamba ninahitaji sana uumalize mtandao huu tena haraka iwezekanavyo lakini nimepatwa na huu ugonjwa wa kukupenda ambao hauna dawa zaidi ya wewe kunikubalia kuwa na mahusiano nami hata kwa kipindi hiki ambacho tutakuwa hapa wote.Elvis mwili wote unawaka moto kila pale ninapokuwaza.I need you darling.I need you to hold me in your strong arms.Please kiss me…” akasema Graca na kufumba macho na kumbusu Elvis.









    Graca nini hasa unakihitaji.Unanihitaji niwe mpenzi wako au una hamu ya kufanya mapenzi? “Vyote.Nina miaka mingi sijawahi kufanya mapenzi na hapa nilipo mwili wangu wote unawaka kwa tamaa na mwanaume pekee ambaye ninamtaka aniweke katika mikono yake ni wewe pekee.Utanisamehe Elvis mimi ninapopenda huwa ninakuwa kama kichaa hivyo nakuhitaji sasa na siku zote” Akasema Graca na kuanza kukipapasa kifua cha Elvis “Not so fast Graca.Nenda kwanza chumbani kwako nitakupa jibu baadae” “Nakuhakikishia tena Elvis kwamba ukinipaninachokihitaji,nitakupeleka mahala ambako utapata kila unachokihitaji” akasema Graca na kumbusu Elvis halafu akatoka mle chumbani. “Please help me Lord” akasema Elvis na kuchukua simu akampigia Steve “Steve tayari umefika eneo la makutano? Umekwisha onana na Juliana? Akauliza Elvis “Tayari nimekwisha fika lakini Juliana bado hajafika ninaendelea kumsubiri atafika muda si mrefu” “Good.Kuna jambo limetokea hapa na ninahitaji ushauri wako” “Jambo gani Elvis? “Ulipoondoka nimezungumza na Graca na kumuuliza kama kuna jambo lolote analifahamu linaloweza kutusaida kuufahamu mtandao wa baba yake akanieleza kwamba kuna sehemu anaifahamu ambako tunaweza kupata tunachokihitaji” “That’s good.Amefanya vizuri sana” “Hata hivyo kuna ugumu kidogo katika hilo” “Ugumu gani tena?Ni mahala pasipoingilika?Yeye atuelekeze sisi tutakwenda kuingia na kuchukua tunachokitaka” “Si hivyo Steve.Graca ametoa sharti ambalo nikilitimiza basi atanipeleka huko mahala” “Sharti gani ametoa? “Anataka niwe mpenzi wake” “Eti nini?Anataka niwe mpenzi wake” “Hapana anatania huyo” “Si utani Elvis.Anamaanisha anachokisema.Anataka niwe mpenzi wake ili anipeleke hiyo sehemu ambako anadai tunaweza kupata kila tunachokihitaji” “Shetani gani kamuingia huyu mtoto? “Steve nimekupigia unipe ushauri wako kwani nimeshindwa kufanya maamuzi.Tunahitaji kupata taarifa lakini siwezi kufanya au kuwa na mahusiano na mtu ambaye ninamuona kama mdogo wangu” akasema Elvis.Ukimya mfupi ukapita Steve akasema “Hata mimi umeniweka katika wakati mgumu lakini hivi ndivyo ningefanya kama ningekuwa mahala pako” “Nakusikiliza” akasema Elvis “Tunahitaji sana taarifa na mara zote tunapokuwa katika kutafuta taarifa muhimu za kutusaidia katika operesheni zetu mbalimbali huwa tunafumba macho na kufanya lolote lile ambalo litawezekana ili kuzipata.Wakati mwingine tunalazimika hata kutoa uhai wa watu ili kupata taarifa.Kwa kuwa Graca ametaka mwenyewe iwe hivyo mkubalie.Mpe anachokitaka ili naye atupe anachokitaka.Najua kwako itakuwa vigumu lakini hatuna namna Elvis.Taarifa aliyonayo Graca inaweza kuwa na msaada mkubwa kwetu.Operesheni hii ni ya muda mfupi na unaweza kukubali kuwa naye na kumpatia anachokitaka na pale tutakapomaliza operesheni yetu basi kila mmoja ataendelea na maisha yake” “Steve....” “Elvis tayari nafahamu unachotaka kukisema lakini naomba uusikilize ushauri wangu.Mpe anachokitaka na yeye atupe taarifa.Isitoshe kale kabinti kazuri sana hakana tatizo lolote na hata yeye ana hisia kama wengine.Laiti angeniambia mimi hivyo nisingejiuliza mara mbili muda huo huo ningemtembezea mjeledi.Elvis naona Juliana anapiga simu nadhani amekwisha fika.Zingatia ushauri huo” “Sawa Steve.Ahsante kwa ushauri” akasema Elvis na kukata simu “Steve anachukulia jambo hili kirahisi sana.Laiti angekuwepo mahala pangu angeweza kuuona ugumu ninaoupata.Hata hivyo hatuna namna zaidi ya kumtimizia anachokitaka.Ouh gosh ! kama nikifanya hivi itakuwa ni mara ya pili ninamsaliti Patricia.Mara ya kwanza nilifanya na Doreen na sasa atakuwa ni Graca.Sikuwahi kuhisi kama siku moja nitamsaliti mke wangu lakini operesheni hii imenifanya nisaliti kiapo changu.Siku nikimuweka mikononi Frank atajuta kuzaliwa kwani yeye na wenzake ndiyo chanzo cha haya yote yanayonitokea”akawaza Elvis na kukumbuka kitu “Patricia naye aliwahi kunisaliti na mwanaume fulani na niliwashuhudia kwa macho yangu wakitoka hotelini na baadae akakiri kwa Doreen kuwa alilala na yule mwanaume.Yeye ndiye aliyeanza kusaliti kiapo chetu cha ndoa.Ni vipi kama ataendeleza mahusiano na yule jamaa akiamini mimi tayari nimekufa?Aaaghhh!! Elvis akajikuta amepandwa na hasira za ghafla. “Sitakiwi kabisa kuyapa nafasi mawazo kama haya.Ngoja nijielekeze zaidi katika operesheni yangu” akawaza na kutoka akaenda chumbani kwa Graca akagonga mlango na kumuita Graca.Mara tu walipofika chumbani Elvis akamuinua na kumuweka mikononi.Graca alikuwa mwepesi sana “Nitakutimizia kile ambacho unakitaka ili uweze kunipa na mimi kile ninachokihitaji” “Real? You are my boyfriend now?akauliza Graca “Ndiyo nimekubali ila kutakuwa na masharti” “I don’t care” akasema Graca na kumkumbatia Elvis kwa nguvu na kuanza kumporomoshea mabusu.Taratibu Elvis akajikuta ikulu kunaanza kufukuta akamuweka Graca kitandani na kuvua nguo kisha mtanange ukaanza. Kilikuwa ni kipute cha saa moja na nusu.Licha ya umri wao kuwa tofauti lakini Graca alionekana kuwa fundi zaidi lakini Elvis naye alionyesha umahiri kwani alimpeleka mizunguko miwili bila kupumzika na hadi mzunguko wa pili unamalizika Graca alikuwa hoi akajitupa pembeni “Tuendelee? Elvis akauliza.Huku akihema kwa kasi Graca akasema “Hapana imetosha.Nilikuwa na hamu sana lakini nimetosheka.Ile kiu yangu yote ya miaka kadhaa bila kukutana na mwanaume imekatwa.Sikufanya makosa kukupenda Elvis kwani wewe ni wa kipekee sana.Una pumzi kama Duma” akasema Graca “Graca jambo hili ni la siri yetu na hatakiwi mtu mwingine yeyote humu ndani kufahamu.Hivyo inuka uende chumbani kwako kabla Vicky na Steve hawajarudi.Kabla hujaondoka tayari nimekutimizia ulichokuwa unakitaka na sasa ni wakati wako kunipa na mimi kile ninachokihitaji” akasema Elvis “Ahsante Elvis.Sikutegemea kabisa kukupata ila nakuomba samahani kwa kutumia njia hii kukulazimisha jambo hili lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya.Kuhusu ile ahadi yangu usijali nitakupeleka sehemu ambako utapata kile unachokihitaji.Usiku wa leo nitakupeleka huko” “Ni wapi huko? “Usihofu Elvis,naomba uniamini” akasema Graca na kumbusu Elvis akatoka mle chumbani “Wanasema usidharau udogo wa reli kwani inabeba kitu kikubwa kama treni.Usemi huu nimeuthibitisha kwa Graca licha ya umbo lake lakini mambo yake ni mazito.Amenionyesha mambo ambayo sikuwa nimeyategemea kabisa kuwa anaweza kuyafanya.Hata mimi nimemkimbiza mchaka mchaka hadi akaomba kupumzika.Sijisifu kwa hiki nilichokifanya kwani ni kosa lakini ni katika kutafuta taarifa muhimu.Ninachoogopa nimemuonjesha asali na atataka kuchonga mzinga.Baada ya kupata taarifa ile ninayohitaji nitaanza kumuweka mbali ili kuzuia jambo hili lisiendelee zaidi” akawaza Elvis *************** Juliana aliwasili mahala alipomuelekeza Steve wakutane.Alikuwa ameongozana na Patricia. “Karibuni sana” akasema Steve akiwakaribisha Juliana na Patricia “Ahsante sana.Samahani kwa kuchelewaBila samahani.Wasema ni afadhali kuchelewa kuliko kukosa kabisa kufika” akasema Steve.Muhudumu akafika wakaagiza vinywaji na maongezi yakaanza “Nadhani ni mara yetu ya kwanza kuonana.Mimi naitwa Steve Kinke.Nimetumwa na mkurugenzi Meshack Jumbo kufuatia mazungumzo yenu asubuhi ya leo” akasema Steve “Tunafurahi kukutana nawe Steve.Mimi naitwa Juliana na huyu mwenzangu anaitwa Patricia ambaye mum……” “Ninamfahamu Patricia.Pole sana kwa matatizo yaliyokupata.Elvis ni rafiki yangu mkubwa na mimi ndiye niliyekuwa naye wakati shambulio lile linatokea na nikafanikiwa kuwamaliza wale jamaa wote lakini mwenzangu akapoteza maisha.Ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba mimi na wenzangu tutafanya kila linalowezekana hadi tuhakikishe tunawapata wale wote waliosababisha kifo cha Elvis.Msiba huu ni wetu sote na sote tumeumizwa sana.Elvis was like a brother to me” akasema Steve na kwa mbali macho ya Patricia yakaonekana na machozi. “Nimekuja kuonana nawe Juliana kufuatia mazungumzo yako na mkurugenzi asubuhi ya leo” akasema Steve Ndiyo tumekutana na Meshack Jumbo asubuhi ya leo na kuna masuala tumeyazungumza” “Mimi ndiye aliyenikabidhi suala hilo nilishughulikie hivyo nataka unieleze kwa kina kuhusu yale yote uliyomueleza ili nione wapi pa kuanzia.Usiogope nieleze kila kitu hata kile ambacho hujawahi kumueleza mtu yeyote http://deusdeditmahunda.blogspot.com/nieleze mimi na kinaweza kunisaidia katika uchunguzi wangu” akasema “Steve nakushukuru sana kwa kuja na kuubeba mzigo huu nilioubeba kwa miaka mingi.Ninauita ni mzigo kwa kuwa nimeubeba kwa miaka kadhaa moyoni mwangu bila kuona sehemu ya kuutua” Akanyamaza kidogo na kuendelea “Tumezaliwa watoto watatu katika familia yetu.Mimi nikiwa mtoto wa kwanza halafu akafuata mwingine anaitwa Godson na yupo mwingine wa mwisho.Wazazi wetu ni wafanya biashara.Awali baba alikuwa akifaya kazi katika shirika moja la kimataifa lakini baadae akaacha kazi na kuendelea na biashara.Kwa muda mrefu wazazi wetu hawakuwa wakiishi hapa Tanzania bali walikuwa Afrika kusini na hapa Tanzania nilikuwepo mimi na mdogo wangu Godson.Kazi yangu mimi ni mitindo.Nilikuwa na kampuni yangu ya mitindo lakini baada ya kuondoka nchini imekufa” Akanyamaza akameza mate na kuendelea “Nilikuwa na mpenzi wangu anaitwa Joseph mtoto wa mfanya biashara mmoja mkubwa hapa nchini.Tulipendana sana na tulikuwa na mipango mingi ya maisha lakini siku moja nilipigiwa simu na na mdogo wake Jose akanijulisha kuwa mpenzi wangu ameuawa kinyama kwa kuchinjwa.Kichwa kilitenganishiwa na kiwiliwili na kisha mwili wake ukaenda kutupwa katika geti la nyumba yao.Pembeni ya mwili huo kuliokotwa kijikaratasi kikieleza kuwa bado mimi wakimaanisha kwamba mimi ndiye nitakayefuatakuuawa baada ya mpenzi wangu.Wazazi wangu walichukua hatua za haraka sana kuniondoa hapa nchini na kunipeleka nje ya nchi ambako nimeishi hadi sasa niliporudi nyumbani kumzika baba” “Pole sana.Baba yako naye amefariki! “Ndiyo amefariki na sasa taratibu zinafanywa ili wiki ijayo tumpumzishe” “Endelea” akasema Steve akimsikiliza Juliana kwa makini sana “Vifo viliendelea kuiandama familia yetu.Miaka michache baadae mdogo wangu Godson naye aliuawa kinyama sana.Wakati huo alikuwa akisimamia miradi ya familia na aliuawa kwa kuigwa risasi zaidi ya hamsini mwilini mwake.Yalikuwa ni mauaji ya kikatili sana.Mdogo wangu wa mwisho naye aliwahi kupigwa risasi lakini kwa bahati nzuri akapona na kwa sasa anatembea na walinzi kila aendako.Mambo haya yameniumiza mno kwa miaka mingi na linaloniumiza zaidi ni kwamba hadi leo hii hakuna aliyewahi kupatikana kuhusika na mauaji hayo.Nimerudi nyumbani lakini sina amani nikihofu labda wale wauaji wataendelea kunifuata na kuniua kama walivyoahidi wakati ule walipomuua Joseph na ndiyo maana nikaonana na mzee Meshack nikamuomba anisadie kuchunguza na kuwabaini watu waliofanya mauaji haya kwa familia yangu.Ninakuomba Steve mfanye kila muwezalo ili niweze kuwafahamu watu hawa na kwa nini wameiandama familia yangu namna hii? Akasema Juliana "Pole sana Juliana kwanza kwa kuondokewa na baba yako na pili kwa masahibu yaliyokupata ya kufiwa na mpenzi wako vile vile kaka yako.Napenda kukuahidi kwamba mimi na wenzangu tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba watu waliofanya mauaji haya wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria.Huu ni unyama uliopitiliza na sisi maisha yetu tumeyatoa kwa ajili ya kupambana na watu kama hawa.Narudia tena kukuahidi kwamba kwa namna yoyote ile lazima tuwajue watu hawa na tufahamu lengo la kufanya mauaji haya"akasema Steve "Ahsante sana Steve.Nitashukuru mno kwani jambo hili limenitesa kwa miaka mingi.Sielewi ni kwa nini watu hawa walinijumuisha na mimi katika orodha ya watu wanaotaka kuwaua kwa sababu kwanza siwajui na vile vile sijawahi kuwa na ugomvi na mtu yeyote" "Usijali Juliana kila kitu kitajulikana.Nataka kufahamu je yalipotokea mauaji ya mpenzi wako Joseph suala hili lilifikishwa katika vyombo vya uchunguzi?Kuna ripoti yoyote wamewahi kuwapa kuhusiana na uchunguzi wa vifo hivi?akauliza Steve "Kuhusu uchunguzi sifahamu chochote kwani baada tu ya mazishi nikaondolewa hapa nchini na kupelekwa nje ya nchi" "Hukuwahi kuwauliza wazazi wako kuhusiana na uchunguzi wa suala lile na kama wauaji wamepatikana? "Nimewauliza lakini jibu lao siku zote ni kuwa nisijali suala linashughulikiwa.Hata yalipotokea mauaji ya Godson hakukuwa na uchunguzi wowote uliofanyika na mpaka leo hii hakuna mtu yeyote aliyewahi kukamatwa kuhusiana na mauaji haya"akasema Juliana.Steve akamtazama kwa makini machoni halafu akasema "Nitahitaji kuonana na mama yako nimuulize maswali kadhaa kuhusiana na matukio haya mawili" "Hapana Steve usithubutu kufanya hivyo.Sitaki kabisa mama afahamu kuwa ninachunguza kuhusu mauaji ya Godson na Joseph.Ninafanya jambo hili kwa siri bila yeye kufahamu chochote" "Juliana nadhani kuna kitu hakijakaa sawa hapa.Kwa nni unafanya jambo hili kwa kificho bila wazazi wako kufahamu?Kuna sababu yoyote inayokupelekea ukafanya hivi?akauliza Steve Swali lile likambabaisha kidogo Juliana akageuka na kumtazama Patricia. "Tell him everything" akasema Patricia "Juliana kama nilivyokueleza toka awali kwamba nieleze kila kitu hata kama ni kidogo sana kinaweza kunisadia katika kufahamu chanzo cha mauji na baadae kuwabaini wauaji.Usiogope tafadhali nieleze kila unachoona kinaweza kuwa na msaada katika uchunguzi wa jambo hili" akasema Steve na Patricia akainamisha kichwa akafikiri kwa muda halafu akasema "Kuna suala ambalo linaihusu sana familia yangu.Kama nilivyokueleza kuwa wazazi wangu ni wafanya biashara wakubwa,wanamiliki biashara kadhaa kubwa kubwa ambazo nyingine ninazifahamu na nyingine sizifahamu.Ninahisi kuna biashara ambazo si nzuri wanazifanya ambazo haziko wazi.Sina uhakika sana wa hilo lakini ninaamini kuna biashara ambazo si halali wanazifanya" "Kitu gani kimekufanya uhisi kuna biashara ambazo si za kawaida zinafanywa na wazazi wako? Steve akauliza "Mdogo wangu Godson aliachishwa kazi na kutakiwa awe msimamizi mkuu wa biashara zote za familia.Nakumbuka aliwahi kunieleza kuwa nisijihusishe kabisa na biashara za familia.Hili lilikuwa ni angalizo kwangu na nilipomtaka anifafanulie akasema atanieleza kila kitu akipata nafasi na wiki mbili baadae akauawa kinyama alipigwa risasi zaidi ya hamsini mwilini mwake.Sina ushahidi wa moja kwa moja lakini nina imani kabisa kuwa my parents are involved in dirty business.Hii ni sababu mimi na ndugu zangu tunaishi kwa mashaka na wasi wasi mkubwa.Tumekosa amani kabisa" akasema Juliana "Ahsante sana Juliana kwa taarifa hizi ambazo ni muhimu sana kwetu.Tutazifanyia kazi na kupata majibu.Maelezo hayo yamenipa mwangaza kuwa yawezekana kuna watu ambao wanahasimiana na wazazi wako katika biashara na ndiyo maana ninyi mmekuwa walengwa.Mama yako anaitwa nani? "Mama anaitwa Elizabeth Mlabwa Mwakyusa" "Kuna biashara yoyote ambayo amewahi kuisajili hapa Tanzania? "Hapana hajawahi kufungua biashara yoyote hapa Tanzania.Biashara zake zote ziko Afrika kusini ,Uingereza,talia ,India,marekani na hata Urusi" "Ouh kumbe amewekeza sana" "Ndiyo amewekeza sana sehemu mbali mbali lakini makazi yake ni nchini Uingereza"akajibuJuliana na Steve akaendela kumuuliza maswali mengine ili kulifahamu kwa kina zaidi tatizo lile la Juliana.Aliporidhika wakaagana na kuondoka "Namuonea huruma sana Patricia kwa mateso ya moyo aliyonayo lakini Elvis hakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutumia njia hii.Kuhusu Juliana kweli ana tatizo kubwa.Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka mauaji haya ni ya kulipiza kisasi.Kama alivyosema mwenyewe kuwa wazazi wake wanajihusisha na biashara haramu inawezekana kabisa kuwa wauaji walifanya vile ili kulipa kisasi.Ninashawishika kuamini kuwa ni mauaji ya kulipiza kisasi.Tutaanza kwanza kwa kuchunguza biashara za wazazi wake na halafu tutachunguza pia watu anaoshirikiana nao lengo ni kufahamu ni biashara gani haramu wanazozifanya.Kwa sasa ngoja niende kwa Samira.Nahitaji sana kuiona sura ya kimwana yule" akawaza Steve ****************** Brigedia Frank akiwa katika benki ya Arab Commericial bank akishughulikia fedha kwa ajili ya akina Dr Makwa akapigiwa simu na Obi mtu aliyemtuma kwenda kumteka Vicky.Hakuweza kuipokea simu akiwa mle benki na alipomaliza shughuli zake akatoka na kumpigia "Obi nipe habari.Kazi imekamilika? akauliza Frank "Mkuu kazi haikwenda vizuri" "Kwa nini Obi?akauliza Frank akianza kupandwa na hasira "Mkuu nilivamiwa na mtu mmoja hatari sana na anaonekna ana mafunzo ya hali ya juu mno.Tumepambana ila nilifanikiwa kumjeruhi kidogo kwa risasi na nilipopata upenyo ikanilazimu kukimbia. " "Unasemaje Obi?Umesindwa kumteka yule mwanamke? "Mkuu nilifanikiwa kumpata yule mwanamke na watu wote waliomo ndani mwake akiwamo mlinzi wa getini lakini ghafla akatokea mtu mmoja akiwa na bastora na ambaye anaonekana kuwa na utaalamu mkubwa sana wa kupigana na tukaanza kupambana.Kama nisingetoroka baada ya kupata ule mwanya ninaamini wangeweza kunidhibiti na kunitesa sana.Hata Vicky anaonekana kuwa na mafunzo mazuri sana ya kujihami kwani pamoja na kumfunga mikono kwa nyuma lakini aliweza kuungana na yule jamaa kupambana nami.Sikutegemea kama mwanamke yule angeweza kuwa na uwezo mkubwa kiasi kile" akasema Obi "Obi yuo failed me!! Yule mwanamke alikuwa muhimu sana kwangu.!! akasema Frank kwa ukali "Kwa hiyo tufanye nini mzee? "Umenirudisha nyuma sana Obi.Ngoja nifikiri namna ya kufanya halafu nitakujulisha"akasema Frank na kukata simu kwa hasira "Huyu mwanamke ana maisha marefu kama paka.Hata hivyo asidhani kuwa ameshinda nitamsaka kila kona hadi nihakikishe nimempata.Lazima aeleze nani alimtuma amuue Pascal? akawaza Frank *************** Saa tisa za alasiri Vicky akarejea katika makazi ya ElvisMambo yamekwendaje huko ulikoenda? Akauliza Elvis “Mambo yamekwenda vyema kabisa.Nimekutana na rais nimemuelezea kwa kina mpango wangu wa kutaka kumchunguza makamu wa rais.Alistuka sana na kuniuliza mara mbili mbili kama nina uhakika na kile ninachotaka kukifanya nikamueleza kwamba sina ushahidi bado wa moja kwa moja ila nina wasi wasi makamu wa rais anahusiana na watu wanaofanya biashara haramu ya silaha.Rais akanielewa na kuniuliza namna ambavyo ninataka kufanya uchunguzi wangu nikamueleza kwamba kuna mtu ninataka kumpandikiza kama mwandishi wa habari wa kimataifa wa mazingira na yeye rais ndiye anayetakiwa kuhakikisha mwandishi huyo anakuwa karibu na makamu wa rais.Amekubali kufanya hivyo na kesho asubuhi Omola atakwenda kuonana na rais na ataanza kazi mara moja” akasema Vicky “ Good.Tayari umekwisha fanya maandalizi ya mahala atakapofikia Omola? “Tayari nimekwisha andaa chumba Maasai 5 star hotel.Nadhani unaifahamu hii ni moja ya hoteli kubwa hapa nchini” “Good.Anapaswa vile vile awe na gari zuri na dereva wa kumpeleka kila sehemu anakotaka kwenda.Tutazungumza na Steve ataliweka hilo sawa.Steve mtoto wa mjini hashindwi na kitu chochote” akasema Elvis “Yah.Nini kinaendelea hivi sasa wakati tunamsubiri Omola awasili jioni ya leo?akauliza Vicky “Kwa sasa endelea kupumzika hadi hiyo jioni ila kuna kitu nataka kukuomba.Kaa na mdogo wako na umueleweshe kwamba hapa mko sehemu salama na asihofu.Sisi siyo watu wabaya na tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba mnakuwa salama na wael wote wenye kuwafanya muishi kwa wasiwasi tutahakikisha tunawabaini na kuwafagia.Mwambie awe huru na ajisikie nyumbani na endapo akihitaji kitu chochote asisite kunieleza ila muonye kwamba hatakiwi kutumia simu yake au hata kumuelekeza mtu yeyote mahala mlipo.Hawa watu hawataacha kuwatafuta hadi wahakikishe wamewapata.” “Sawa Elvis ngoja nikaonane naye nimuelweshe japo tayari nimekwisha muelewesha lakini anaonekana ni mgumu kuelewa” akasema Vicky na kuinuka akaanza kupiga hatua akasimama na kugeuka akamtazama Elvis “Elvis nakosa neno zuri la kukushukuru kwa msaada mkubwa uliotusaidia leo hii.Kama usingemtuma Steve aje haraka kuokoa maisha yetu sijui nini kingetokea.Ahsante sana” akasema Vicky huku akitabasamu Usijali Vicky,tutafanya kila kitu kuhakikisha mnakuwa salama” akasema Elvis na Vicky akaondoka kuelekea chumbani kwa Graca aliko mdogo wake Winnie akamchukua na kwenda naye chumbani kwake “Umeshindaje Winnie.Kila kitu kimekwenda vizuri? Umekula ? “Dada tafadhali naomba uniondoe katika gereza hili.I’m not happy here,I’m not free.Nimeshindwa hata kula leo.Nakuomba dada nipeleke sehemu yoyote nikajifiche lakini si hapa”akasema Winnie “Winnie sikiliza mdogo wangu,kama nilivyokueleza kuwa dada yako ninafanya kazi ya upelelezi na kwa sasa kuna suala la muhimu sana ambalo mimi na hawa akina Elvis tunashirikiana kulichunguza.Yule jamaa aliyetuvamia pale nyumbani asubuhi ametumwa na watu ambao tunawachunguza na kama asingetokea Steve kuja kutuokoa sijui hivi sasa tungekuwa wapi.Hapa ni sehemu salama Winnie nakuomba vumilia kwa muda mfupi na kazi yetu ikikamilika basi tutaondoka hapa na kurejea nyumbani kwatu ila kwa sasa tutaendelea kukaa hapa mahala ambako hawa jamaa wanaonitafuta hawapafahamu”akasema Vicky “Dada kwa nini ukaamua kushirikiana na hawa jamaa? They’re monsters.Si watu wazuri hata kidogo.Kumbuka walikuumiza mkono na wakakufunga kwa pingu miguu na mikono kama mhalifu na walivyo wanyama wakakuacha ushuhudie namna wanavyonichoma kwa umeme.Siwezi kusahau kitu kile hata kidogo.Mambo kama yale nimekuwa nayaona katika filamu na sikutegemea kama siku moja na mimi nitachomwa na umeme.Dada siwezi kukubali kukaa hapa”akasema Winnie “Winnie narudia tena kukuomba kwamba vumilia kwa muda mfupi tumalize operesheni yetu na kisha tutarejea nyumbani kwetu.Siwezi kukutoa hapa kwani nitahatarisha maisha yako.Watu wanaonitafuta wakikupata watakutumia kuhakikisha kwamba wananipata na huo utakuwa ni mwisho wangu” “Ni akina nani hao wanaokutafuta? Umewafanya nini?Akauliza Winnie “Ni hadithi ndefu Winnie na mambo haya ya kiusalama huwezi kuyaelewa” “Nitaelewa dada nieleze tafadhali na mimi nifahamu ni akina nani hao wanaokutafuta na kwa nini? Akauliza Winnie “Kuna watu ambao wanafanya biashara ya silaha.Wana wauzia silaha waasi wanaopigana na serikali ya Congo na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia.Mtandao huu ni mkubwa na unahusisha watu wazito na hata viongozi wa serikali lakini kinara ni mtu mmoja anaitwa Frank Kwaju huyu ni mwanajeshi ana cheo cha brigedia” “Umesema Frank Kwaju? Baba yake Graca? Akauliza Winnie “Unamfahamu? “Graca amenieleza historia yake na akanitajia baba yake anaitwa brigedia Frank kwaju” “Ndiye huyo.Frank anaye rafiki yake ambaye wanashirikiana katika biashara hii anaitwa Pascal ambaye ndiye niliyemuua jana na akina Frank wanafahamu kuwa nimehusika katika kifo cha Pascal na ndiyo maana wananisaka.Kwa bahati nzuri nimekutana na hawa akina Elvis nao wanachunguza suala hilo hilo hivyo tumeuganisha nguvu ili tuweze kuusaka mtandao huu na kuikomesha biashara haramu ya silaha.Hiyo ndiyo hali halisi ilivyo” “Huyo Frank unafahamiana naye? “Ndiyo.Ili kumchunguza nililazimika kujiweka karibu nao na tukawa marafiki lakini mpaka sasa hawafahamu kama mimi ni mpelelezi”akasema “Sawa dada nimekuelewa.kama unawaamini hawa jamaa basi hakuna tatizo mimi nitavumilia hadi hapo utakapokuwa umemaliza kazi yako” Ahsante.Jambo lingine utalazimika kuzima simu yako.Watu hawa wanaweza wakafahamu mahala ulipo kwa kufuatilia simu yako” “Dada maisha yangu yatakuaje bila kutumia simu? “Ni kwa muda tu Winnie na halafu maisha yetu yatarejea kama kawaida.Nitakutafutia laini nyingine ya simu ambayo utakuwa ukiitumia kwa muda” akasema Vicky “Hakuna tatizo dada.Umechoka sana nenda kaoge upumzike.You need anything? Whysky? Akauliza Winnie na Vicky akatabasamu ‘Thank you so much Winnie.Nitahitaji mvinyo ili nipumzishe kichwa kwa muda kwani jioni kuna mahali tunakwenda” “Mtatoka jioni? “Ndiyo tutatoka kidogo,kuna sehemu muhimu tunakwenda”akasema Vicky na Winnie akatoka kwenda kuchukua mvinyo.Aliporejea akakuta dada yake yuko bafuni anaoga haraka haraka akafungua mkoba wa Vicky akatoa simu na kutoka nayo akaiwasha na kutafuta namba ya Frank.Kulikuwa na namba nne zimeandikwa Frank akachagua namba moja imeandikwa Br.Frank.Haraka haraka akaiandika katika kiganja cha mkono kisha akaizima simu ya dada yake na kuirudisha mkobani halafu akaondoka akarejea chumbani kwa Graca ambaye kwa sasa alikuwa amelala fofofo. *************** Saa kumi na moja za jioni Steve akarejea katika makazi yao.Mathew ndiye aliyemfungulia geti kwani Graca alikuwa bado amelala kufuatia gwaride alilochezeshwa na Elvis “Graca yuko wapi? Akauliza Steve mara tu baada ya kushuka garini “Graca yuko chumbani amelala” “Kabla ya yote niambie je uliamua nini kuhusiana na lile suala ulilonieleza?Steve akauliza Nilifuata ushauri wako.Nilimpa alichokuwa anakihitaji.Nimefanya hivyo kwa ajili ya kupata taarifa za muhimu but in record I don’t like it” akasema Elvis wakielekea katika viti vya kupumzika katika bwawa la kuogelea “You did great Elvis.Hupaswi kumlaumu Graca kwani ni binadamu mwenye hisia kama wengine na usisahau ameishi kwa muda mrefu hospitali na kwa muda huo wote hajakutana na mwanaume.Kwa sasa ana amani na anahitaji mtu wa kumkuna na akaona aitumie nafasi hii kutimiza haja zake.Amekueleza nini baada ya kumpa alichokuwa anakitaka? Akauliza SteveHajanieleza chochote bado,ila amesema baadae kuna mahala atanipeleka ambako tutapata majibu ya maswali yetu” akasema Elvis “Do you trust her? “Yes I do.Yeye ndiye anayemfahamu vyema baba yake kuliko sisi hivyo lazima tumuamini.Si muda mrefu kutoka sasa Omola atakuja,tutakwenda kumpokea na kisha tutampeleka moja kwa moja katika hoteli ambayo Vicky ameiandaa ,tutakuwa na mazungumzo naye kuhusiana na kazi tunayotaka aifanye halafu tutamuacha apumzike na sisi tutaenda kumchukua Graca atatupeleka huko mahala alikoahidi.Vipi huko ulikokwenda?Umefanikiwa kuonana na Juliana?akauliza Elvis “Ndiyo nimeonana na Juliana.Hakuwa peke yake bali na Patricia” “How’s my wife? Akauliza Elvis "I can say she’s fine but down dep she's deeply hurt.Ameumizwa mno na kifo chako Elvis.Anyway tuyaache hay she'll be fine" akasema Steve " I hope so.Juliana amekueleza tatizo lake kwa undani?akauliza Elvis "Tumezungumza kwa kirefu kuhusiana na tatizo lake na amefunguka mambo mengi kuhusu vifo vya mdogo wake na mpenzi wake.Kikubwa nilichokipata katika maelezo yake ni kwamba mauaji haya yanaonekana kuwa ni mauaji yanayoilenga familia yao.Linaonekana ni jambo la kulipiza kisasi"akasema Steve "Hata mimi nilipoelezwa suala hili na mkurugenzi mara moja nilijua haya ni mauaji ya kisasi.Swali la kujiuliza je ni akina nani hao ambao wanalipiza kisasi kwa familia yao na kwa nini?akauliza Elvis "Kuna jambo ambalo Juliana ameniambia hata mimi likanipa mwanga mkubwa.Hakuwa akitaka kulisema lakini baada ya kumbana akajikuta hana namna ya kufanya zaidi ya kunieleza japo hana uhakika bado lakini anahisi kuwa wazazi wake wanajihusisha na biashara haramu.Anadai kwamba wazazi wake wanamiliki biashara katika nchi mbalimbali lakini anachoamini kuna jambo limejificha nyuma ya biashara hizo.Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa mdogo wake kabla ya kuuawa alikuwa akisimamia miradi ya familia yao na kuna siku aliwahi kumueleza kwamba asithubutu kujiingiza katika miradi ya familia.Hakupata nafasi ya kumfafanulia kwa kina kwa nini alimwambia vile akapigwa risasi na kufa.Hii inanipa picha kwamba kweli mauaji haya ni ya kulipiza kisasi na inawezekana waliofanya mauaji haya ni washirika wao wa kibiashara.Kinachonipa uhakika mkubwa kwamba mauaji haya ni ya kisasi inaonekana kila yanapotokea hakuna uchunguzi wowote unaofanyika kubaini wauaji.Nilitaka kufahamu kutoka wa Juliana kama kuna uchunguzi wowote ulifanyika alipouawa mpenzi wake Joseph lakini akasema kwamba hana uhakika kwani baada tu ya mazishi yeye akaondolewa na kupelekwa mafichoni nje ya nchi.Hata alipouawa mdogo wake Godson bado hakukuwa na uchunguzi wowote uliofanyika hivyo kutoa taswira kwamba kuna jambo linafichwa lisijulikane.Mambo kama haya hufanywa na magenge ya watu hatari kama vile wauza dawa za kulevya n.k.Ninashawishika kuamini kwamba yawezekana wazazi wa Juliana wanajihusisha na biashara hii ya dawa za kulevya au katika magenge makubwa yanayofanya biashara mbalimbali haramu"akasema Steve "Inabidi tumfanyie mahojiano mama yake,itatusaidia kuweza kupata jambo la kutusaidia katika uchunguzi" "Juliana amekataa kabisa tusifanye hivyo kwani anafanya uchunguzi huu bila ya mama yake kufahamu” akasema Steve "Inaonekana Juliana hamuamini kabisa mama yake na hadi ameamua kufanya jambo hili kimya kimya.Tutamsaidia kuwabaini waliofanya mauaji ya mpenzi na mdogo wake na kama wazazi wake watakuwa wanahusika kwa namna yoyote nao pia watafikishwa mbele ya sheria.Kitu cha kwanza ambacho tunapaswa kukifahamu ni je mauaji yale yalipotokea yaliripotiwa polisi na kufunguliwa jalada la uchunguzi?Kama jalada lilifunguliwa uchunguzi ulifanyika?Baada ya kufahamu kuhusu kilichoendelea katika uchunguzi huo kama ulifanyika tutawatafuta wazazi au familia ya Joseph na kuwahoji" "Kwa mujibu wa Juliana ni kwamba wazazi wa Joseph hawaishi tena hapa nchiniwanaishi nje ya nchi ila hafahamu wanaishi nchi gani" “Dah ! kweli hapa kuna utata mkubwa hata hivyo hatuwezi kushindwa.Tutatumia kila aina ya mbinu kuwapata wauaji" akasema Elvis na kuchukua simu "Mkurugenzi ndiye atakayefuatilia polisi kufahamu kama kuna uchunguzi wowote uliwahi kufanyika kuhusiana na mauaji ya Joseph" akasema na kumpigia Meshack Jumbo "Hallow Elvis" akasema Meshack Jumbo "Mkurugenzi kuna jambo tunahitaji msaada wako.Steve ametoka kuzungumza na Juliana kama ulivyoelekeza na tunaanza kulishughulikia suala lake.Tunaanza kwa kuchunguza kifo cha mpenzi wake Joseph Mballa.Tunataka kujua kama yalipofanyika mauaji yale kuna jalada lolote la uchunguzi wa kifo chake lilifunguliwa?Na kama lilifunguliwa walifikia wapi katika uchunguzi wao?Tunaomba ulifanyie kazi hilo suala na kisha utatupa majibu" akasema Elvis na kukata simu "Alikoenda Vicky amefanikiwa?Steve akauliza "Ndiyo amefanikiwa na kila kitu kimekwenda sawa.Rais amekubali kumuunganisha Omola na Dr Shafi hivyo ni jukumu letu kumuwezesha Omola kufanya kazi yake kwa wepesi.Tunatakiwa kupata gari zuri ambalo atakuwa akilitumia pamoja na dereva wa kumuendesha,kuhusu hoteli tayari Vicky amemtafutia hoteli nzuri ya hadhi ya juu" "Kuhusu gari hakuna tatizo kwani nitamuomba Samira atusaidie hata kumuendesha kwani yeye ana gari zuri sana la kifahari" "Unataka kumuhusisha Samira katika suala hili? "Ndiyo Elvis.Tayari yeye anafahamu kinachoendelea na isitoshe ni mtu ambaye hawezi kunikatalia chochote nikimuomba" "Good kama hutakuwa umemsumbua"akasema Elvis. So Elvis tell me how was she?akauliza Steve huku akitabasamu "Nani? Elvis naye akauliza "Graca.How was she on bed? "C'mon Steve sitaki tuongelee suala hilo.Nimekwisha fanya kosa na sitaki kulikumbuka tena.Sikuwa nimetegemea kufanya mapenzi na msichana ambaye kiumri ni sawa na mdogo wangu.Nimemkosea sana Patricia" akasema Elvis "Usijilaumu sana Elvis kwani hukuwa na namna nyingine ya kufanya.Tazama mimi nimelazimika kulala na Vicky ili kumpata Pascal.Japokuwa tumemkosa lakini tumefanikiwa kumpata Vicky ambaye amekuwa ni msaada mubwa kwetu" akasema Steve na Elvis akainamisha kichwa akiwaza halafu akainua kichwa akamtazama Steve "Steve kuna jambo linanichoma moyo sana kila nikilikumbuka" "Jambo gani ? "Niliporejea kutoka afrika kusini na nikafanikiwa kuipata kompyuta ya Frank na kugundua kwamba ana mashirikiano na Vicky nilianza kumfuatilia Vicky na nikaweka miadi ya kukutana naye hotelini kwake.Nilipotoka kuonana naye nikamshudia Patricia akitoka hotelini akiwa na mwanaume.Nilimtuma Doreen akamchunguze na akakiri kwamba ni kweli ametembea nje ya ndoa na yule mwanaume ambaye ni daktari.Suala hili linaniumiza kichwa sana kwani nina uhakika huyo daktari anaweza akaanzisha mahusiano na mke wangu wakiamini nimekufa.Nashindwa nifanye nini Steve"akasema Elvis. "Elvis kwa sasa hata mimi siwezi kukushauri chochote kuhusu suala hilo lakini ninachokuomba liondoe katika mawazo yako.Akili zetu tuzielekeze katika suala lililoko mbele yetu na litakapokwisha basi tutageukia masuala mengine" akasema Steve "Sawa tujiandae kwa ajili ya kwenda kumpokea Omola kwani muda unakwenda sana" akasema Elvis



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog