Search This Blog

Saturday 5 November 2022

I DIED TO SAVE THE PRESIDENT - 2

 






Simulizi : I Died To Save The President

Sehemu Ya Pili (2)



I DIED TO SAVE MY PRESIDENT



wapi ilipo kompyuta yake.Elvis naomba usiniache hapa.take me anywhere safe.Ni mara yanguya kwanza kukuona lakini I feel safe around.macho yako yananifanya nikuamini” akasema Graca huku macho yake yakilengwa na machozi “ Nitakusaidia Graca.Nitakuondoa hapa na kukupeleka sehemu salama kabisa ambako si baba yako wala yeyote anayekutafuta atakupata.Lakini kabla ya kufanya hivyo kuna jambo nataka kulifahamu toka kwako.Nataka kufahamu ndani ya hilo begi kulikuwa na kitu gani cha muhimu kiasi cha kupelekea baba yako kufanya haya yote aliyoyafanya?Kompyuta hiyo uliyoichukua ilikuwa na jambo gani na iko wapi kwa sasa? Graca akamtazama Elvis na kusema “Siwezi kukueleza chochote kwa sasa hivi hadi hapo nitakapohakikisha kwamba niko sehemu salama.Take me somewhere safe and I will tell you everythingI know na nitakueleza kompyuta hiyo iko wapi” akasema Graca “ Graca ninaelewa hofu yako lakini naomba uniamini na uniambie kuhusiana na ulichokigunuda kwa baba yako.Tafadhali naomba ushirikiane nani.Usiniogope mimi si mtu mbaya” akasema Elvis “ Elvis najua umefunga safari ndefu kuja huku kuonana na mimi kwa nia njema kabisa na kama nilivyokueleza awali kwamba ninakuamini na niko tayari kukueleza kila kitu lakini kwa sasa siwezi kukueleza jambo lolote ninalolifahamu hadi hapo nitakapohakikisha kwamba niko salama.Mkoba ule na kilichomo ndani yake ndiyo kinga yangu kwa sasa kwa hiyo fanya nilivyokuelekeza na nitakueleza kila unachokitaka” akasema Graca “ Graca !!... Elvis akataka kusema kitu lakini Graca akamzuia “ Elvis hakuna chochote utakachoniambia kitakachoweza kuubadili msimamo wangu.Ninazo taarifa nyeti sana ambazo ninaamini zitakuwa ni za msaada mkubwa sana kwako lakini siwezi kukueleza hadi hapo nitakapohakikisha kwamba niko salama” akasemaGraca.Elvis akamtazama kwa makini usoni na kuamini kile alichokisema Graca “ She’s telling the truth.hawezi kunieleza chochote bila kufanya anavyotaka” akawaza Elvis na kusema “Nimekuelewa Graca.Naomba unipe muda kidogo niangalie namna ya kufanya.I promise you I’ll get you out of here.”akasema Elvis.Bila kusema chochote Graca akainuka na kutembea taratibu kuelekea ndani.Elvis akamtazama namna alivyokuwa akitembea kwa unyonge akamuonea huruma sana lazima nimsaidie.Siwezi kumuacha hapa akiendelea kuteseka.Akawaza Elvis halafu akaelekea katika meza waliyokuwa wamekaa Bongan na Dr Susan “ Tayari mmekwisha ongea? Umefanikiwa kupata ulichokuwa unakihitaji? Akauliza Bongani “ Bongani mambo si rahisi kama nilivyitegemea" akasema Elvis “ Nini kimetokea Elvis,Graca hajakupa ushirikiano? ” akauliza Bongani.Elvis akamvuta pembeni kidogo ili waongee.Akamweleza kila kitu alichoongea na Graca “kwa hiyo mambo yako namna hiyo Bongani.Graca kuna jambo kubwa analifahamu kuhusiana na baba yake lakini hayuko tayari kuliweka wazi bila kwanza kuwa na uhakika wa usalama wa maisha yake” akasemaElvis “ kwa hiyo tutafanya nini Elvis ili tuweze kuzipata taarifa hizo toka kwa Graca?akauliza Bongani “hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kufanya vile anavyotaka yaani kumpeleka sehemu salama.Bongani naomba unisaidie katika hili ili niweze kumuondoa Graca hapa hospitali.Pamoja na kuwa na kitu cha muhimu ninachokihitaji lakini nimeguswa sana na mateso ya binti huyu,ameteseka kiasi cha kutosha na siko tayari kumuacha akiendelea kuteseka hapa.Tafadhali naomba unisaidie” Bongani akafikiri kwa muda na kusema “ Hata mimi nimeguswa sana na histora ya huyu binti na nitakusaidia ili tuweze kumtoa hapa.Ninachotaka kufahamu ni kuhusu usalama wa maisha yake endapo tutafanikiwa kumuondoa hapa.Una hakika atakuwa salama?akauliza Bongani.Elvis akawaza kidogo na kusema “Bongani suala la usalama wa Graca lina changamoto nyingi lakini hilo ni jukumu langu ambalo sina budi kulibeba na nitahakikisha kwamba anakuwa salama.Nitamlinda dhidi ya yeyote mwenye nia ya kumdhuru” “Bongani akainama akafikri kidogo na kusema “ sawa Elvis .Nitakusaidia,naomba unipe muda wa dakika kama kumi nikaongee na Dr Susan nione kama anaweza akatusaidia” “ una hakika atatusaidia? Akauliza Elvis “ Nina uhakika lakini hatuna budi kujaribu.Nina mahusiano naye mazuri.Tuliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi wakati tukiwa chuo kikuu na mpaka sasa bado tuna mahusiano mazuri” akasema Bongani na kuelekea katika ofisi ya Dr Susan “Nahisi kuna suala zito sana ambalo liko nyuma ya pazia kiasi kwamba Frank alikuwa tayari hata kutaka kumuua mwanae kwa ajili ya kulificha.Lazima nilifahamu suala hilo .Nitamsaidia Graca kwa namna yoyote ile nitakayoweza na nitamuondoa hapa.Nitamlinda dhidi ya yeyote yule anayetishia maisha yake.”akawaza Elvis Bongani alitumia zaidi ya dakika kumi na tano kuongea na Dr Susan kumuelezea kuhusiana na tatizo la Graca.Hadi anamaliza kumueleza Dr Susan alikuwa anahisi baridi.Alionekana kuzama katika mawazo mengi “ Siku zote nilijua lazima kuna jambo haliko sawa kwa Graca.Sikutaka kuharakisha kumuuliza nini kilichokuwa kinamsumbua na ndiyo maana nikajenga ukaribu mkubwa kati yangu naye ili siku moja aweze kunieleza tatizo lake.Namuoenea huruma sana binti huyu kwa mateso makubwa aliyonayo.Huu ni mtihani mkubwa kwangu lakini lazim animsaidie” Dr Susan akiwa katika mawazo mengi mara akastuliwa na Bongani “ Dr Susan !!... Akainua kichwa na kumtazama Bongani “Unasemaje Bongan? Akauliza “ natumani umenisikia na kunielewa.Nini mawazo yako? Akaulizia Bongani .Dr Susan akavuta pumzi ndefu na kusema “Bongani nashindwa niseme nini lakini naomba nikiri kwamba nimegswa mno na historia nzima ya Graca.Siku zote nilikuwa nikifahamu kwamba Graca ana tatizo kubwa linalomsumbua tofauti na ugonjwa wa akili lakini sikuweza kumshawishi anieleze tatizo lake.Maelezo uliyonipa yamenistua mno”akasema Dr Susan “ Dr Susna sote tumeguswa na tatizo la Graca na ndiyo maana tunatafuta namna ya kumsaidia na mtu pekee ambaye tunamtegemea kwa sasa ni wewe” akasema Bongani .Dr Susan akaonekana kuzama mawazoni halafu akakohoa kidogo na kusema “ Una hakika kwamba Elvis ana nia ya dhati kumsaidia Graca na si mmoja wa watu wa baba yake ambaye anataka kumchukua na kwenda kumdhuru? Bongani akatabasamu na kusemaElvis anafanya kazi kama ninayofanya mimi na lengo lake ni kumsaidia Graca hivyo nakuomba usiwe na hofu naye hata kdogo” akasema Bongani.Dr Susan akaegemea kti chake akatazama juu kwa sekunde kadhaa na kusema “ Nitamsaidia.Ninakuamini sana na nina hakika baada ya kutoka hapa Graca atakuwa katika mikono salama” “ Ahsante sana Dr Susan .Ahsante sana kwa msaada wako” akasema Bongani kwa furaha. “Tutafanya hivi.Graca nitaondoka naye mimi katika gari langu.Hataondoka na kitu chochote hapa kila kitu chake atakiacha hapa ili kutoleta udadisi pindi itakapobainika kwambaametoweka.Baada ya kama dakika kumi nitakapoondoka ninyi mtafuata kwa nyuma.Nitawasubiri pale kwa Pamela Thambo”akasemaDr Susna naBongani akatoka mle ofisini kwa Dr Susan akamfuata Elvis “ What happened? amekubali kutusuaidia?akauliza Elvis kwa wai wasi mara tu alipomuona Bongani “ Ndiyo! Amekubali kutusaidia” akasema Bongani “ Thank you Lord! Akasema Elvis huku akiinua mikono kumshukuru Mungu.Bongani akamueleza Elvis namna mpango utakavyokuwa kisha wakaelekea katika kantini ya hospitali hapo wakaagiza vinywaji baridi.Wakati wakiendelea na vinwyaji mara ikapita gari ya Dr Susan ikafunguliwa geti na kutoka bila kukaguliwa . Dakika kumi baada ya Dr Susan kutoka Bongani na Elvis nao wakaelekea lilipo gari lao,wakaingia na kuondoka.Katika lango kuu walikaguliwa na kuruhusiwa kupita wakaondoka. ****************** Katika nyumba kubwa iliyokuwa na utulivu mkubwa,Bongani ,Elvis na Graca walikuwa wamekaa wakijaribu kuangalia ni kwa namna gani Elvis na Graca watakavyoweza kurejea Tanzania salama.Graca alionekana mchovu sana hali iliyomlazimu alale sofani na kuwaacha Bongani na Elvis wakiendelea kujadiliana “ Kuna njia nyingi za kuweza kuwaondoa hapa na kuwarudisha Tanzania lakini tunahitaji kupata usafiri wa haraka wa kuweza kuwaondoa hapa leo hii .Hamtakiwi kulala hapa leo” akasema Bongani “ Hilo ni jambo la msingi sana .Kwa hali ilivyo hatutakiwi kulala hapa leo.Tutawezaje basi kupata usafiri wa haraka wa kutuondoa hapa? “ akauliza Elvis .Bongani akainama akafikiri kidogo na kusema “ Usihofu kuhusu suala hilo Elvis.Ni jukumu langu kuhakikisha kwamba unapata usafiri na unaondoka hapa salama.Ngoja kwanza niwasiliane na washirika wangu kadhaa nione namna watakavyoweza kunisaidia” akasema Bongani kisha akainuka na kuelekea chumbani .Elvis akamtazama Graca aliyekuwa amelala sofani .Graca akageuza shingo na kugonganisha macho na Elvis ,akatabasamu kidogo na kwa sauti ndogo akauliza “ Mbona unanitazama hivyo? Elvis akainuka na kwenda kukaa katika sofa lililokuwa pembeni ya Graca “ Unajisikiaje Graca? Akauliza “ Ninajisikia vizuri tu.Ni yale madawa waliyokuwa wakinichoma ndiyo yanayonifanya nionekane naumwa sana lakini mimi siumwi” akasema Pole sana Graca.Kuna kitu chochote unahitaji kwa sasa? “Elvis Kwa sasa Ninachohitaji ni kwenda sehemu salama” “ Usihofu Graca.Nimeibeba dhamana hiyo ya usalama wako na nitahakikisha unakuwa salama na hakuna atakayekudhuru” “ Nitashukuru sana kwa hilo Elvis….” Akasema Graca na mara Bongani akaingia pale sebuleni “ Vipi kuna mafanikio yoyote ? akauliza Elvis “ Ndiyo.Kunaweza kuwa na uwezekano.Nimewasiliana na mmoja wa rafiki zangu amenidokeza kwamba kuna ndege ya jeshi inaondoka usiku wa leo kuelekea Zambia.Nimewasiliana na mmoja wa makamanda wa jeshi amenitaka nionane naye sasa hivi.Ngoja nikaonane naye nimsikilize ni mtu ambaye nina hakika anaweza akanisaidia” akasema Bongani “ Ahsante sana Bongani kwa msaada wako huu mkubwa.Ninaomba Mungu ufanikiwe ili tuweze kuondoka hapa” akasema Elvis “ Usihofu Elvis.Ngoja nikaonane na huyu mkuu nitarejea baada ya muda mfupi” akasema Bongani na kutoka. “ Huyu rafiki yako ana roho nzuri sana.Ni nadra sana katika dunia ya sasa kumpata mtu ambaye anaweza akakuhangaikia kama huyu.” Akasema Graca baada ya Bongani kuondoka.Elvis akatabasamu na kusema Anaitwa Bongani.Naye anafanya kazi kama ninayoifanya mimi na vile vile ni rafiki yangu sana.Ni jadi yetu kusaidiana tunapokuwa na matatizo na hata yeye akija Tanzania na akiwa na tatizo ni jukumu langu kuhakiksha kwamba nimemsaidia kwa kila namna.Hivyo ndivyo tunavyofanya kazi” akasema Elvis “ Natamani na mimi siku moja ningefanya kazi kama yako” akasema Graca “ Unaipenda kazi hii? Akauliza Elvis “ Ndiyo nimetokea kuipenda sana” akasema Graca “ Kwa nini unaipenda kazi hii? “ Mambo yaliyonikuta ndiyo yananifanya niipende na na nitake kufanya kazi kama yako.Nataka nipambane na watu makatili wasio na hata chembe ya huruma kwa binadamu wenzao.Vile vile nataka nilipe kisasi kwa baba yangu pamoja na washirika wake kwa kusababisha maisha yangu yawe namna hii.Unawezaje kunisaidia ili niweze kuifanya kazi hii? akauliza Graca Elvis akavuta pumzi ndefu akamtazama Graca ambaye hakuonyesha kama alikua akitania “ Graca naomba unisikilize mdogo wangu .Kwanza kabisa naomba ufahamu kwamba kuna maisha mazuri zaidi yanayokusubiri pale utakapokuwa huru na unastahili maisha mazuri.Umri wako bado unaruhusu wewe kuendelea na masomo na baadae ukaishi maisha yale ambayo umekuwa ukiyaota kwa siku nyingi hivyo naomba uondoe kabisa kichwani mwako wazo la kutaka kufanya kazi kama hii.Kazi hii ni ngumu mno na ina mambo mazito ndani yake .Inahitaji mtu mwenye roho ngumu kama ya paka.Mara tu uingiapo katika kazi hii hutakuwa na maisha ya kawaida tena kwani muda wote unakuwa umezungukwa na maadui ambao dhamira zao si njema hata kidogo na walio tayari kuua muda wowote .Kazi hii inakuweka katika hatari muda wote.Wengi wetu tumeingia katika kazi hii bila kufahamu tunakwenda kukutana na mambo gani na kwa sasa tumekwisha zoea na kuiona ni ya kawaida lakini naomba nikuhakikishie kwamba hii si kazi rahisi kuifanya na wala usiitamani.Niko tayati kukusaidia kwa kila namna niwezavyo kuyajenga maisha yao lakini si kukusaidia ili uingie katika kazi hii.Umenielewa Graca? Akaulizia Elvis “ Nimekuelewa Elvis japokuwa bado moyo wangu unataka sana kuifanya kazi hii ili niweze kuufutilia mbali mtandao wote wa baba” akasema Graca na kuzidi kumvutia zaidi Elvis “ Mtandao upi Graca? Baba yako ana mtandao unaoshughulika na nini? Akauliza Elvis “ Usiwe na haraka Elvis.Utafahamu kila kitu ila naomba ufuate makubaliano yetu .Nipeleke sehemu salama na nitakueleza kila kitu ninachokifahamu” akasema Graca “ Sawa nitahakikisha unakuwa salama.Ninahitaji sana taarifa zako” “ Usijali Elvis,nitakueleza kila kitu,” akasema Graca halafu ghafla akaonekana kama kuna kitu anakiwaza “ Elvis kuna kitu ambacho nilisahau kukwambia” “ Kitu gani Graca? “ Kuna watu wawili pale hospitali wamekuwa wakinichunguza.Kuna mpishi mmoja pamoja na mlinzi.Watu hawa wamekuwa wakinifuatilia sana na nina hakika watakuwa wanalipwa na baba ili wanichunguze nyendo zangu.Japokuwa sina hakika sana lakini kwa namna walivyokuwa wakinifuatilia nina hisi lazima watakuwa wamepewa kazi ya kunichunguza” akasema Graca “ Usijali kuhusu hao watu.Hata kama wamewekwa na baba yako kukuchunguza hawana uwezo wa kupambana na mimi.Usihofu kitu ukiwa na mimi” akasema Elvis “ Ahsante sana Elvis” akasema Graca na kimya kifupi kikapita Ilipita saa moja na dakika ishirini Bongani akarejea “ Hallow Elvis.Mko salama wote? “ Tuko salama.Mambo yamekwendaje huko? Mambo yamekwenda vizuri sana .Kuna ndege ya jeshi inayowapeleka wanajeshi kwenye mazoezi nchini Zambia na tayari nimekwisha ongea na kiongozi wa kikosi hicho na amenikubalia kuwachukua na ninyi.Hakukuwa na ugumu wowote kwani wakuu wengi wa jeshi ni marafiki zangu.Pale Lusaka nimekwisha wasiliana na mtu mmoja anaitwa Stanley Chiteta.Huyu ni rafiki yangu mkubwa na ni mfanyakazi wa idara ya usalama wa taifa ya Zambia.Yeye ndiye atakayewapeleka hadi katika mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji wa Tunduma na tokea pale hamtakuwa na wasi wasi tena mtakuwa mmekwisha ingia nchini kwenu na mtatafuta usafiri wa kuelekea Dar es salaam.Stanley ni mzoefu na nina hakika atakuwa ni msaada mkubwa kwenu” akasema Bongani “ Bongani sina namna ya kukushukuru kwa msaada wako huu mkubwa uliotusaidia.” Akasema Elvis .Bongani akatabasamu na kusema “ Usijali Elvis ni jukumu langu kukusaidia na nimefanya kile ninachopaswa kukifanya .Kwa kuwa hatuna muda wa kutosha ni wakati sasa wa kujiandaa kwa safari.” Akasema Bongani na kumpatia Graca mfuko uliokuwa na nguo na vitu vingine mbali mbali alivyomnunulia.Graca akaingia chumbani kujiandaa na baada ya kuwa tayari safari ya kuelekea uwaja wa ndege wa jeshi ikaanza DAR ES SALAAM – TANZANIA Ni saa moja za jioni ,kiza tayari kimetanda angani,Patricia na Doreen rafiki yake wamekaa katika kibaraza nyumbani kwa Doreen wakiongea.Walionekana kuzama katika maongezi mazito “ Kwa hiyo Doreen maisha yangu yanazidi kuwa magumu siku hadi siku.Umeona wewe mwenyewe ujumbe ninaotumiwa katika simu na ndugu za Elvis.Wanayafanya maisha yangu yawe magumu sana.Hakuna mtu anayejali upendo mkubwa uliopo kati yangu na Elvis.Wao wanachotaka ni mtoto tu” akasema Patricia kwa uchungu.Doreen akamtazama akamuonea huruma rafiki yake “ Pole sana Patricia .Ninafahamu ni kiasi gani unaumizwa na suala hili na kama nilivyokueleza toka awali kwamba niko tayari kukusaidia katika jambo hili.Sipendi kukuona ukiumia namna hii” Akasema Doreen “ Doreen nashukuru sana kwa kukubali kunisaidia ingawa najua haikuwa rahisi kukubali kufanya jambo kama hili lakini tutafanya nini tena wakati mpango wetu ulishindikana? Akasema Patricia .Kimya kikatanda kila mmoja alikuwa anawaza lake.Ni Doreen ndiye aliyeuvunja ukimya Patricia naomba usikate tamaa ndugu yangu. Ni kweli tulijaribu ikashindikana lakini hatupaswi kukata tamaa .Tunapaswa kufikiri namna nyingine tutakayoweza kufanya ili kumfanya Elvis akubaliane na wazo letu” akasema Doreen “ Doreen unionavyo hapa tayari nimekwisha fikiri sana na ninatumai akili yangu imefikia kiwango chake cha mwisho cha kufikiri na bado sijapata jibu” akasema kwa uchungu Patricia.Doreen akamshika bega na kumwambia “ Patricia its too early to give up.Nina hakika lazima tutapata njia ya kufanya .Kitu cha msingi ni kujaribu kutuliza akili na kuja na mpango mpya.Nina hakika tutafanikiwa “ akasema Doreen “ Doreen sina shaka nawe hata kidogo najua uko tayari kunisadia lakini tatizo liko kwa Elvis.Ananipenda kupindukia na hayuko tayari kufanya jambo kama hili tunalolipanga.Suala la kumuomba azae na mwanamke mwingine kwake yeye ni sawa na usaliti kwangu kwa hiyo hataki kabisa kulisikia.Nimechanganyikiwa Doreen na sijui tutafanya nini na ndugu za Elvis ndo hao wanadai mtoto kila leo” akasema Patricia “ Unaonaje endapo tutakaa naye na kuongea naye kwa pamoja kuhusiana na suala hili pengine anaweza akatuelewa” Akasema Doreen Elvis ni mtu mwenye msimamo mkali sana na akisema hapana katika jambo Fulani basi huwa ni vigumu sana kumbadili.Sina hakika kama hata tukimueleza ukweli anaweza akatuelewa.Mpango ule ulioshindikana ulikuwa mzuri sana” akasema Patricia “ Pamoja na hayo Patricia ni mapema mno kukata tamaa.Bado kuna njia nyingi tu tunaweza kufanya ili kumfanya Elvis akubaliane nasi” Akasema Doreen Patricia akamtazama na kuonyesha wasi wasi “ Unazungumzia njia gani Doreen? Kama unazungumzia masuala ya waganga mimi siko tayari kwa hilo.Ni bora niendelee kuteseka kuliko kwenda kwa waganga” Doreen akacheka na kusema “ Hapana Patricia.Mimi si muumini wa masuala hayo na tangu utoto wangu siamini kabisa katika mambo hayo ya waganga.Nilikuwa namaanisha kutafuta njia nyingine za kuweza kulifanikisha jambo hili hata kama Elvis hataki kuliko kukata tamaa” akasema Doreen “ Hilo ndilo jambo la msingi ambao tunapaswa kulifanya kwa sasa.Ngoja kwanza niende nikapumzishe kichwa ili nije na wazo jipya.” Akasema Patricia huku akinyanyua mkoba wake na kupiga hatua kuelekea lilipo gari lake Sikuwahi kuota kama siku moja nitakuwa na wakati mgumu kama nilionao hivi sasa. Kuna wakati ninajuta hata kuolewa .Ningekuwa peke yangu haya yote yasingenitokea.Anyaway ninampenda Elvis na nitalipigania penzi letu kwa gharama zozote zile” akawaza Patricia ******************** Ni shamba lenye ekari zaidi ya kumi lililoko njekidogo ya jiji la dar es salaam.Ndani ya shamba hilo lililosheheni mazao mbalimbali kulikuwa pia na mifugo kama vile kuku,ng’ombe n.k.Kati kati ya shamba lile kuwa kulikuwa na jumba kubwa la kifahari la ghorofa tatu.Hili ni shamba linalomilikiwa na Brigedia jenerali Frank kwaju.Jioni hii ukimya mzito ulitawala kulizunguka jumba hili.Ni milio ya mifugo tu ndiyo iliyokuwa ikisikika .Hakukuwa na zile pita pita za kila siku za wafanyakazi Saa mbili na dakika tatu za usiku,gari tatu zikawasili katika geti la kuingilia shambani hapo.Geti kubwa likafunguliwa na walinzi na kisha gari zile zikaikamata barabara iliyokuwa inaelekea moja kwa moja katikati ya shamba liliko jumba lile kubwa lililozungukwa na ukuta mkubwa na nyaya za umeme juu yake.Geti likafunguliwa na gari zikaingia Watu kumi wakashuka toka katika zile gari wakiongozwa na Brigedia jenereli Frank halafu wakalekea ndani katika ukumhi wa siri wa mikutano ulioko ndani ya jumba lile.Ukumbi tayari ulikwisha andaliwa maalum kwa ajili ya kikao hiki kizito kinachotaratiwa kufanyika usiku huu.Baada ya kama dakika ishirini toka akina Frank wawasili pale numbani,zikawasili gari mbili na akashuka waziri mkuu mstaafu Daud Sichoma akiwa ameongozana na watu wengine watano wakapokelewa na Brigedia Frank na kupelekwa katika ukumbi wa mikutano ambako wajumbe wote waliokuwa wakitakiwa katika kikao kile walikwisha wasili na aliyekuwa akisubiriwa ni Mheshimiwa Daudi Sichoma na ujumbe wake.Mara tu walipoingia katika chumba cha mikutano,watu wote wakasimama kuonyesha heshima kwa wgeni waliowasili.Daudi na ujumbe wake wakaonyeshwa viti wakaketi na bila kupoteza wakati mwenyekiti wa kikao kile brigedia Frank akafungua kikao.Kwanza alianza kwa kufanya utambulisho.Baada ya wajumbe kufahamiana kwa majina na sehemu watokako Frank akaendelea “ Ndugu wajumbe nadhani ni wakati sasa wa kuwatambulisha wageni wetu wakuu waliotufanya tukusanyike hapa usiki huu.Wageni wetu watasimama na kujitambulisha wao ni akina nani na kisha tutaendelea na kile kilichotuleta” akasema Frank na kuwaomba wageni wale wawili wasimame mmoja mmoja na kujitambulisha “ naitwa Mustapha Al jamal”akaanza kujitambulisha mgeni wa kwanza “ Mimi ni raia wa Iran na ni mmiliki wa wa kampuni moja kubwa ya mafuta katika mashariki ya kati.Kwa sababu za kiusalaam naomba nisiitaje kampuni yangu hadi hapo mbeleni” akamaliza kujitambulisha ndugu Mustapha na kumpa nafasi mwenzake aliyeambatana naye “ Mimi naitwa Alhafidh Sadiq.Na mimi kama mwenzangu aliyetangulia ni mmiliki wa kampuni kadhaa kubwa za mafuta katika eneo la mashariki ya kati.Vile vile kama alivyofanya mwenzangu nisingependa na mimi kuziweka wazi kampuni zangu” akasema Alhafidh “ Ahsanteni sana wageni wetu kwa kujitambulisha.Sisi ni wenzenu na tumefurahi sana kuwa nanyi hapa kwa usiku huu”akasema Frank akameza mate na kuendelea “ Ndugu wajumbe baada ya kuwafahamu wagheni wetu naomba sasa tuendelee na kikao chetu.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea “ Wageni wetu hawa wamekuja na jambo zito sana ambalo utekelezaji wake unatuhitaji sana sisi.Endapo jambo hili likifanikiwa basi sisi sote pamoja wao tutafaidika sana.Kwa hiyo basi sitaki kuchukua muda mwingi kwani muongeaji mkuu yupo na ndiye atakayetueleza kila kitu.Karibu ndugu Alhafidh ili uweze kutueleza nini hasa kilichowaleta hapa Tanzania” akasema Frank.Alhafidh akaweka sawa koo lake akafungua faili lililokuwa mbele yake akaisoma karatasi ya kwanza kana kwamba kuna mambo anajikumbusha halafu akasema “ Ndugu zangu ni furaha kubwa kwetu kukutana nanyi usiku huu.Kwa niaba ya mwenzangu napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru nyote kwa kuacha shughuli zenu na kuja kutusikiliza.Napenda kuwahakikishia kwamba hamtajutia kufika kwenu hapa usiku huu kwani suala tulilowaitia hapa ni lenye manufaa makubwa kwenu na kwetu pia.Brigedia jeneral Frank ni rafiki yangu sana wa muda mrefu.Tumefahamiana katika shughuli zetu za kibiashara na ninyi nyote aliowachagua kuhuddhuria kikao hiki nina imani ni watu makini na anaowaakini hivyo natumaini mazungumzo yetu yatakwenda vizuri” Alhafidh akanyamza kidogo akameza mate na kuendelea “ Nadhani ninyi nyote hapa mnafahamu hali halisi ya eneo zima la masharaiki ya kati inavyoendelea hivi sasa.Katika kila taarifa ya habari inayotangazwa duniani hakukosekani taarifa kuhusiana na mashariki ya kati.Lakini nini hasa kiini cha machafuko yote katika eneo hili la mashariki ya kati?.Chanzo chote cha machafuko ni nchi za Marekani na washirika wake.Nchi hizi za magharibi zimekuwa zikiendesha chochoko dhidi ya serikali za mashariki ya kati na hivyo kusababisha machafuko kusambaa katika eneo zima la masharikiya kati.Lakini naomba nyote mjiulize kwa nini mashariki ya kati? Kwa nini nchi za magharibi zinachochea migogoro na mifarakano mashariki ya kati? Jibu hapa ni jepesi sana.Ni kwa sababu ya utajiri mkubwa wa mafuta ulioko katika eneo hili.Migogoro hii inapotokea wanaofaidika ni Marekani na washirika wake kwani hujitokeza na kuingilia kati huku wakibeba na kujiwekea akiba kubwa ya mafuta katika nchi zao huku wakiwaacha maelfu ya watu wasio na hatia wakiuana.Suala hili limeamsha hasira na chuki kubwa dhidi ya marekani na washirika wake na ndiyo maana mnasikia kila mara vinaibuka vikundi mbalimbali vya kigaidi ambavo vingi adui yake mkubwa ni Marekani na washirika wake.Hii ni sababu kubwa iliyopeleka Marekani kuanza kujitoa taratibu katika siasa za mashariki ya kati na kuanza kupunguza utegemezi wa mafuta toka mashariki ya kati .Kwa hivi sasa marekani imeongeza juhudi katika kuzalisha mafuta ya ndani ikiwemo mafuta yatokanayo na mimea .Wamewekeza katika teknolojia mpya ili watengeneze magari na mitambo visivyohitaji mafuta mengi.” Alhafidh akanyamaza kidogo halafu akaendelea. “ Baada ya utafiti wa miaka mingi kuhusiana na uwepo wa mafuta na gesi katika bahari kuu nchini Tanzania na kulitolewa taarifa iliyoushangaza ulimwengu.Kumegunduliwa kiasi kikubwa cha mafuta nchini Tanzania ambacho kinasemekena ni kikubwa kuliko hata kilekinachoweza kupatikaana eneo zima la mashariki ya kati.Huu ni ugunduzi mkubwa sana kuwahi kufanyika katika miaka ya hivi karibuni.Ugunduzi huu unaifanya Tanzania kuingia katika ulimwengu mpya kwani mataifa yote makubwa hivi sasa yameelekeza macho yao nchini Tanzania.Uchumi wa Tanzania utapaa kwa kasi kubwa na ndani ya muda mfupi ujao nchi yenu itaingia katika nchi tajiri duniani” Alhafidh akatulia na kuwatazama wajumbe ambao wote walikuwa wakitabasamu kutokana na taarifa ile “ Rais wa marekani amemaliza ziara ya siku nne nchini Tanzania ikiwa ni ziara ndefu kuwahi kufanywa na rais wa marekani katika taifa moja husan haya ya bara la Afrika.Ninathubutu kusema kwamba hii imekua ni ziara yenye mafanikio makubwa sana kwa marekani.Mambomengi mazuri yamefanyika katika ziara hiyo ikiwa ni pamoja na kuzindua miradi mikubwa ya nishati ,reli na maji,Pamoja na mambo hayo makubwa huku watanzania walio wengi wanaamni ni neema kubwa wameipata lakini nataka mjiulize kwa nini iwe sasa? Kwanini rais wa marekani aitembelee Tanzania sasa tena ikiwa ni ziara ndefu kuwahi kufanywa na kiongozi yoyote wa taifa la marekani katika nchi yoyote ya afrika? Jibu hapa ni rahisi tu.Nikwa sababu ya neema kubwa ya mafuta na gesi iliyogunduliwa Tanzania..Sababu ya pili ni kujiimarisha kijeshi kwa kujenga kambi yake hapa Tanzania ili kuendeleza mapambano dhidi ya wale wote wenye kupambana na taifa hili bila kuchoka na hasa vikundo vya kigaidi kama vile Alqaeda,alshabaab,Boko haram, n.k ambavyo vimekuwa vikijimarisha sana kwa siku za karibuni” Alhafish akanyamaza kidogo na kuwatazama wajumbe wa kikao kile ambao wote walikuwa kimya kabisa wakimsikiliza kisha akaendelea “ Kama nilivyowafahamisha kwamba ziara hii ya rais wa Marekani nchini Tanzania ilikuwa ni kwa sababu maalum zenye manufaa kwa taifa hilo.Ukiacha sababu za kiusalama ,kubwa lililomleta hapa ni suala la mafuta na gesi.Mtakumbuka awali niliwaeleza kwamba kwa sasa Marekani wanapunguza utegemezi wa mafuta ya mashariki ya kati na na kuifanya itegemee mafuta yake ya ndani.Ugunduzi huu wa kiwango kikubwa cha mafuta na gesi nchini Tanzania umeifanya Marekani ianze kitolea macho tanzania nchi ambayo imekuwa ikipokea misaada mingi toka Marekani.Katika ziara hii ya rais wa Marekani kumesainiwa mikataba kadhaa mikubwa baina ya serikali ya tanzania na wawekezaji wakubwa wa mafuta na gesi toka Marekani.Katika mikataba hiyo Serikali ya Tanzania imeyaruhusu makampuni makubwa ya marekani kufanya uwekezaji mkubwa katka sekta ya mafuta na gesi Tanzania.Hii ina maana moja kubwa kwamba makampuni ya kimarekani ndiyo yatakayoliongoza soko la mafuta duniani .Marekani haitakuwa tena na tatizo la mafuta na haitahitaji tena mafuta toka mashariki ya kati.Washirika wa Marekani pia au nchi zile kubwa zinazoongoza http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kwa viwanda duniani hazitakuwwa tena na wasi wasi kuhusiana na suala la mafuta na gesi ,watahamia katika mafuta yatokayo Tanzania.Bei ya mafuta duniani itaporomoka na hali hii itayalazimisha makampuni ya mafuta ya mashariki ya kati kupunguza bei ya mafuta ili kuendana na bei itakayokuwepo katika soko la dunia.Kushuka kwa bei ya mafuta kwa nchi za mashariki ya kati inamaanisha kwamba hata uchumi wa nchi hizi lazima utaporomoka kwa sababu uchumi wao unategemea sana biashara ya mafuta.Lengo kuu la Marekani ni kuhakikisha kwamba uchumi wa nchi za mashariki ya kati unazorota kutokana na kudorora kwa biashara ya mafuta” akanyamaza akanywa maji kidogo kisha akaendelea. “Nadhani hadi hivi sasa kuna picha ambayo tayari mmekwisha ipata kuhusiana na ziara ya rais wa Mareani” akasema Alhafidhi na wajumbe wote wakatikisa vichwa ishara kwamba wanakubaliana naye.Akatabasamu halafu akaendelea “ Suala hili limekuwa likiumiza vichwa sana makampuni makubwa ya mafuta ya masharki ya Kati na hata serikali zao kwa ujumla.Ni suala linalohusu maslahi mapana ya mataifa haya ambayo uchumi wake unategemea mafuta.Hatutaki makampuni yetu yatetereke kutokana na kuyumba kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.Hatutaki uchumi wa mataifa yetu uzorote kutokana na kuyumba kwa bei ya mafuta .Vita vya wenyewe kwa wenyewe katika eneo zima la mashariki ya kati vimesababisha chumi za mataifa haya zilizokuwa zikikua kwa kasi kuzozorota .Endapo litaatokea tena baa hilo la kuporomoka kwa bei ya mafuta mataifa haya yatakuwa yakichungulia katika lindi kubwa la umasikini kwani chumi zao hazitaweza kustawi kamwe.Ni kutokana na hali hiyo kumekuwa na mazungumzo ya kina kati ya serikali za mashariki ya kati na makampuni makubwa ya mafuta ya wazawa wa mashiriki ya kati.katika mazungumzo hayo yote suala la Marekani kuendesha sekta ya mafuta ya Tanzania limepingwa vikali.Hatuko tayati na hatutakuwa tayari kuiacha Marekani itawale sekta hii nyeti sana ambayo ndiyo hasa uchumi wetu sisi watu wa mashariki ya kati.Narudia tena kwamba hatuko tayari na wala hatuwakuwa tayari kuiacha Marekani itawale sekta ya mafuta ya dunia.Kwa maana hiyo basi tumefikia uamuzi wa kuusimamisha na kuuzima kabisa mpango wa marekani wa kuidhibiti sekta ya mafuta duniani.” Alhafidh akatoa kitambaa na kujifuta jasho halafu akanywa maji kidogona kuendelea. “ Serikali ya Tanzania tayari imekwisha sainiana mikataba mikubwa na makampuni ya kimarekani na hivyoo suala hilo kwa sasa lipo kisheria .Hakuna namna tunayoweza kufanya ili kutengua mikataba hiyo mikubwa sana.Kuna njia moja tu ambayo tunaweza kuifanya ili kulimaliza suala hili” Alhafidh akanyamaza na kuziangalia nyuso za wajumbe waliokuwa kimya wakimsikiliza.Akanyanyua glasi ya maji na kupiga funda moja akaiweka chini akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililokuwa likimtoka usoni licha ya ukumbi ule mdogo kuwa na kiyoyozi.Hii ilitokaa na uzito wa suala walilokuwa wakiliongelea “ Ndugu wajumbe njia pekee ya kuweza kulipatia ufumbuzi suala hili ni kwa kuiangusha serikali iliyoko madarakani” Kimya kizito kikatanda mle ndani.Sura za wajumbe zilionyesha mabadiliko ya ghafla.Minong’ono ya chini kwa chini ikasikika.Mara Daudi Sichoma akasimama na kumuelekezea macho Brigedia Frank huku midomo yake ikitetemeka “ What is this Frank? Hiki ndicho kitu cha muhimu ulichoniitia? I cant believe this !!!....akasema Daudi kwa ukali .wajumbe wengine wanne wakasimama wakionyesha kustushwa na kauli ile.Hali ilibadikika mle chumbani ikamlazimu Brigedia Frank asimame. Please calm down guys.Nawaombeni mtulie na tusikilizane.Mr David tafadhali naomba ukae chini na tusikilizane”akasema Frank na wale wajumbe waliokuwa wamesimama wakiongozwa na Daudi Sichoma wakaketi na ukimya ukatawala mle ndani .Frank alipohakikisha wajumbe wote wametulia kaendelea “ Ninauona mstuko mkubwa katika nyuso zenu.Nilitegemea kitu kama hiki kutokea.Hii si taarifa nyepesi hata kidogo.Ni taarifa nzito na yenye kustusha lakini nyote niliowachagua kuhudhuria kikao hiki ninauhakika mkubwa kwamba hizi ni taarifa njema sana kwenu.Naomba msiwe na jazba na twende taratibu tutaelewana” akasema Frank “Frank kuiangusha serikali si suala rahisi hata kidogo kama unavyodhani” akasema David Sichoma .Frak akatabasamu na kusema “ Ninafahamu unachokimaanisha David lakini nina uhakika mkubwa hakuna kitakacho shindikana.Nime………”kabla Frank hajaendelea zaidi Daudi Sichoma akamkatisha “Frank you know nothing .Suala ulilolileta ni suala lisilowezekana kabisa” akasema Daudi “ Unaweza kuwa sahihi David kwamba sijawahi kuwa katika serikali lakini ninafahamu kila kinachoendelea serikalini.Ninawafahamu viongozi wakubwa serikalini.Ninaifahamu seriali nje na ndani.Daudi Sichoma ninakufahamu vyema umewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini na hatimaye ukafanikiwa kwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Nafahamu ndoto yako kubwa ilikuwa ni kuwa rais wa Tanzania lakini kwa bahati mbaya ndoto yako hiyo haikuwezekana kutimia kwa sababu watu ndani ya serikali waliligundua hilo na hawakuwa tayari kukuona ukishika nafasi ya urais na ndiyo maana walianza kukuandama kwa mambo mengi na hatimaye kukuzushia kashfa kubwa na ukaondolewa katika nafasi yako ya uwaziri mkuu.Ninafahamu madai yale yaliyotolewa dhidi yako kuhusiana na kashfa ile hayakuwa ya kweli na zilikuwa ni njama za kisisasa na kuhakikisha unapotea kabisa katika ulingo wa siasa.Lengo lao limefanikiwa kwani wamefanikiwa kabisa kukuondoa katika ulingo wa siasa.Hausikiki tena viywani mwa watu.Umekwisha sahaulika kabisa na ndoto yako ya urais imepotea.Najua unajitahidi sana kutaka kujirudisha katika medani za siasa lakini wabaya wako hawataki kukupa tena nafasi.Vikwazo vimekuwa vingi na wamepambana hadi kuhakikisha kwamba umaarufu wako unapotea.This is your last chacne to make your dream come true.Ni wakati wako wa kuitengeneza njia ya kuingia katika lile jumba jeupe.” Frank akanyamaza akamtazama Daudi Sichoma aliyekuwa kimya akimsikiliza halafu akawageukia wajumbe wengine “Nyote niliowaita hapa nafahamu ni wenye kuhitaji sana nafasi za uongozi na mpango huu wa kuiangusha serikali ndio mpango pekee utakaowawezesha na kuwahakikishia nafasi za uongozi.Kuiangusha serikali iliyoko madarakani ni jambo zito ambalo haliwezi kufanywa na sisi pekee yetuliomo humu chumbani .Huu ni mchakato mrefu na jumuishi nikimaanisha kwamba ni mchakato unaohusisha watu wengi lakini wenye lengo na nia moja.Sisi sote tulioko hapa ndio tutakaoratibu mchakato mzima wa mapinduzi haya.Naombeni ndugu zangu msikate tamaa.Tunaweza kulifanya jambo hili.Mkumbuke pia tunayo sapoti ya kutosha toka kwa washirika wetu katika suala hili.Tayari zimekwisha tengwa shilingi Trilioni sita kwa ajili tu ya kufanikisha jambo hili.Pamoja na fedha lakini washirika wetu watatusaidia pia katika ila kitu tunachokihitaji”akasema Frank na kunyamaza tena akawatazama wajumbe wale.daudi sichoma akakohoa kidogo na kusema “ Kidogo sasa ninaanza kukuelewa Frank.Mpango huu si mbaya kama nilivyokuwa ninaufukiria isipokuwa ni mpango mzito wenye kuhitaji mikakati mizito pia .Lazima tuvihusishe vyombo vya ulinzi na usalama hususani jeshi na idara ya usalama wa taifa,wanasiasa na wadau wengine watakaoonekana kuhitajika.Mimi niko tayari kushirikiana nanyi katika mpango huu lakini kwa makubaliano maalum” akasema Daudi Sichoma “ Ahsante sana Daud kwa maamuzi yako .Kwa kuwa bado tuna mchakato mrefu mbele yetu nina imani kwamba tutafikia makubaliano unayohitaji” akasema Frank na kuwageukia wajumbe wengine “ Ndugu zangu kati yenu kuna yeyote mwenye mawazo tofauti? Kuna yeyote mwenye duku duku au maoni yoyote kuhusiana na mpango huu? Akauliza Frank.Kabla mtu yeyote hajajibu,simu ya Frank ikaita,akastuka baada ya kuona watu wote wanamtazama “ Samahani ndugu zangu kwa kutoizima simu yangu katika kikao kizito kama hiki” akasema Frank huku akitoa simu yake kwa lengo la kuizima lakini mara tu alipotazama jina la mpigaji akastuka.Jina lilisomeka kama hospitali Graca “ Samahani jamani naomba niipokee simu hii ni muhimu sana” akasema Frank na kutoka nje ya kile chumba “Hallow” akasema Frank “ Hallow Frank habari za Dar es salaam? Ikasema sauti ya upande wa pili



Habari ni nzuri nani mwenzangu? Akauliza Frank “Ninaitwa Dr Susan napiga simu toka katika hospitali na magonjwa ya akili anakotibiwa mwanao Graca.” “ Oh! Dr Susan.Nimestushwa sana na simu yako usiku huu.Kwema huko? Akauliza “ Huku si kwema.Kuna jambo limetokea mchana wa leo”akasema Dr Susan na kuzidi kumtia hofu Frank “ Jambo gani limetokea? Mbona unanipa hofu namna hiyo?akauliza Frank “ Graca amepotea na mpaka sasa hivi hatujui yuko wapi” “ What ?!!...Frank akahamaki “ Nakutaarifu kwamba mwanao Graca ametoweka mchana wa leo na mpaka muda huu hajaonekana.Juhudi za kumtafuta zinaendelea tukishirikiana na vyombo vya usalama” “ Dr Susan jambo hili limetokeaje?hakukuwa na ulinzi hapo hospitali hadi mwanangu akatoroka? Akauliza Frank “ Badohakuna anayefahamu nini kilitokea hadi Graca akatoweka.Tumewachia jukumu hili vyombo vya usalama vichunguze .Usiwe na hofu tunalishughulikia suala hili kwa karibu sana na tunaamini Graca hatakuwa mbali na hapa” “ Dr Susan bado maelezo yako hayajitoshelezi? Nieleze kwa ufasaha mwanagu amepoteaje wakati hapo hospitali kuna ulinzi na wagonjwa wote wanakuwa chini ya uangalizi maalum? Akauliza Frank kwa ukali “ Tukio hili hata sisi limetustua sana.Awali tulidhani yuko katika maeneo ya hapa hospitali lakini saa moja za jioni wakati tunapitia wagonjwa wote ili kuhakikisha wako wote Graca pekee ambaye hakuonekana.Tulianza juhudi za kumsaka kila kona ya hospitali lakini hakuonekana ikatulazimu kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama na tayari wamekwisha fika na wanaendelea na zoezi la kumtafuta.Nitawasiliana nawe kila mara nitakapopata ripoti toka kwao.Nakuhakikishia kwamba tunafanya kila linalowzekana kuhakikisha Graca anapatikana kwani ni mgonjwa na anahitaji matibabu.Picha yake itasambazwa katika kila kona na watu watatusaidia kumtafuta.Tahadhari imekwisha tolewa pia kwa wote wanaoishi jirani na hospitali kwamba kuna mgonjwa ametoweka hospitali kwa hiyo watakapomuona watoe taarifa haraka sana hapa hospitali au katika kituo chochote cha polisi.Ninahakika mpaka kesho asubuhi tutakuwa na taarifa nzuri zenye kutia matumaini” akasema Dr Susan “ Ok ! Ahsante sana Dr Susan kwa taarifa japokuwa ni taarifa zenye kustusha sana.Naomba unipe taarifa kila hatua inayofikiwa” akasema Frank usijali Frank.Nitawasiliana nawe kila mara kukupa taarifa” akasema Dr Susan na kukata simu.BadoFrank aliendeelea kutazama juu akiwa na mawazo mengi “ Hii imetokeaje?Graca amepoteaje? Amewezaje kutoroka pale hospitali wakati kuna ulinzi mkali? Akajiuliza Frank halafu akachukua simu yake na kuzitafuta namba Fulani akapiga “hallow Bonny.” akasema Frank baada ya simu kupokelewa “Hallow Frank”ikajibu sauti ya upande wa pili “Bonny hebu nieleze nini kimetokea? Ninakulipa fedha nyingi kila mwezi wewe na mwenzako kwa ajili ya kumlinda mwanangu imekuaje leo ninapokea taarifa kwamba amepotea? Akauliza Frank kwa ukali “ Frank utaniwia radhi lakini nilikuwa katika hatua za kukutaarifu kilichotokea.Ni kweli Graca ametoweka na sote tumeshirikiana kumtafuta bila mafanikio.Kuna kitu kilitokea ambacho nakiunganisha na tukio hili la kutoweka kwa Graca” “ Nini kilitokea ? akauliza Frank “ Mchana wa leo kuna watu wawili walifika hapa na mmoja wao akawa akiongea na Graca bustanini.Nilifanikwia kupata picha yake toka kwa mbali nitakutumia muda si mrefu ili uweze kumuona mtu huyo ni nani na kama unamfahamu ama vipi.Baadae watu hao waliondoka na walifanyiwa ukaguzi getini ila hawakuwa na kitu chochote .Tunachoshindwa kuelewa ni kwamba Graca ametoweka vipi? Kuna uzio mkubwa na hawezi kuruka.Kama ni hivyo amewezaje kutoweka? Lakini wasiwasi wangu upo kwa wale jamaa wawili.Lazima kuna kitu wanakifahamu kuhusu kupotea kwa Graca”akasema Bony “Nitume picha za watu hao haraka”akasema Frank na baada ya dakika moja picha zikaingia.Akaziangalia picha zile na kuhsi kwa mbali kijashi kinamtoka. “Mungu wangu …..Elvis!!..akasema Frank kwa sauti ndogo ya mshangao.Kwa dakika mbili alibaki anaziangalia picha zile katika simu yake na mara akakumbuka kwamba kuna kikao kinachoendelea akakurupuka na kurejea kikaoni Kikao kiliendelea hadi ilipotimu saa tisa za usiku ndipo kilipomalizika kwa makubaliano kwamba siku itakayofuata wakutane tena nyumbani kwa Daudi Sichoma kwa ajili ya mikakati zaidi.Wajumbe wakaagana na kutawanyika.Frank na Pascal Situmwa wakawapeleleka akina Alhafidh hotelini walikofikia kisha wakaagana nao kwa miadi ya kuonana tena asubuhi kabla hawajaelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kuondoka nchini “Pascal we need to talk” akasema Frank wakati wakishuka ngazi za hoteli kuelekea katika maegesho ya magari.Pascal akaonekana kustuka kidogo akageuka na kumtazama Frank akagundua kuna kitu hakikuwa sawa. “ Frank are you ok?akauliza Pascal “ No ! I’m not ok”akajibu Frank “ Nini kimetokea Frank? Toka ulipotoka mle kikaoni ukaenda kuongea na simu kuna kitu nilikigundua.Haukuwa sawa kabisa.Whats wrong? Akauliza Pascal “ Pascal tuna tatizo” akasema taratibu Frank huku akiufungua mlango wa gari akaliwasha wakaondoka.Mara tu walipotoka katika geti la hoteli Pascal akauliza “ Frank kuna tatizo gani? Fran akavuta pumzi ndefu na kusema “ Graca ametoroka hospitali na hajulikani alipo” “ Graca !! ametoweka vipi?Hospitali hiyo haina ulinzi? Akauliza pascal “ Ulinzi upo tena mkali sana” “ sasa ametoroka vipi kama kuna ulinzi?.akauliza pascal.Frank akapunguza mwendo wa gari akachukua simu yake na kumuonyesha Pascal “ Elvis Tarimo” akasema Frank “ Elvis !!!!!..Pascal akastuka “ Unamfahamu vizuri Elvis? “Ndiyo ninamfahamu vizuri.Ni mfanyakazi wa idara ya ujasusi ya taifa.Inasmekana ni mmoja kati ya watu tegemeo sana katika idara yake.Elvis anahusiana nini na kupotea kwa Graca?akauliza Pascal “ Elvis alionekana akiongea na Graca na baadae jioni Graca hakuonekana tena” Sura ya pascal ikaonyesha uoga mkubwa.Safari ikaendelea kimya kimya.Pascal alionekana kuwa na mawazo mengi sana “ Pascal unawaza nini? Akauliza Frank baada ya kumuona Pascal akiwa amezama katika lindi la mawazo “ Frank we have a problem” akasema Pascal “ yes I know that we have a problem” Akasema Pascal “ Ninavyomfahamu Elvis mpaka afikie hatua ya kwenda kuonana na Graca basi lazima kuna jambo amekwisha linusa.Something is not right ” akasema Pascal “ Ninachojiuliza ni kwamba kwa nini akaongee na Graca ?Nina wasi was kuna jambo ameligundua kuhusiana na nyaraka zile zilizokuwamo katika komputa ile aliyoiba Graca na mama yake.Graca ni mtoto wangu lakini nilifanya kosa kubwa sana kumuacha hai mpaka sasa hivi” akasema Frank “Una hakika Elvis anaweza kuwa amezipata nyaraka hizo? Akauliza Pascal Sina hakika kama atakuwa amezipata kwa sababu kama tayari angekuwa nazo basi asingesumbuka kwenda kuonana na Graca.Ninachohisi mimi ni kwamba kuna kitu atakuwa anakihisi au kuna fununu fulani anazo na ndiyo maana anafanya uchunguzi.Kama nyaraka zile angekuwa nazo mikononi toka zilipopotea basi tungekuwa tunaongea mambo mengine hivi sasa”akasema Frank “So what are we going to do? Akauliza Pascal “ Tunatakiwa tukabiliane na suala hili haraka sana.Kwanza tunatakiwa kuhakikisha kwamba Graca anapatikana na vile vile tunatakiwia kumdhibiti Elvis.Tunatakiwa tufahamu ni kitu gani anakijua kuhusiana na sisi” akasema Frank.Pascal akazama tena mawazoni “ Frank unakumbuka niliwahi kukwambia kwamba pochi yangu ndogo iliyokuwa na kumbu kumbu zangu muhimu iliwahi kupotea pale nyumani kwangu? “Ndiyo nakumbuka.Nadhani msichana yulealiyeiiba aliuawa” “Ndiyo .Niliwatuma vijana wangu wamzimishe kabisa kwani niliamini lazima kuna mtu alimtuma aniibie pochi ile.Kuna jambo ambalo nimelikumbuka sasa hivi” “Jambo gani Pascal? “Ni hivi majuzi tu kuna mtu alingia pale nyumbani kwangu lakini hakuiba kitu chochote.Alionekana wakati akitoka kwa hiyo vijana hawakuweza kumjua ni nani.Ninaanza kuhisi kwamba huenda mtu huyu naye alitumwa kuja kuchunguza kitu pale kwangu.Nina wasiwasi kwamba huenda tukawa tumejulikana mambo yetu na hivyo wanaendelea kutuchunguza na kukusanya ushahidi wakutosha.Nadhani hata Elvis kwenda kuonana na Graca ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea.Elvis anataka kupata taarifa toka kwa Graca.Endapo kuna mambo ambayo Graca anayafahamu kuhusu sisi hatasita kumweleza Elvis.Kwa sasa nina uhakika mkubwa kwamba ni Elvis ndiye aliyemtorosha Graca.Swali la kujiuliza ni je wako wapi? Akasema Pascal. Yule mtoto nina hakika tayari atakuwa anafahamu mambo mengi kuhusiana na sisi na ninahisihatasita kumweleza Elvis kila kitu anachokifahamu.Kumuacha hai lilikuwa kosa kubwa sana”akasema Frank “Pascal una hakika yule msichana alikufa? Pascal akastuka kwa swali lile.hakuwa amelitegemea “ Ndiyo nina hakika .kwani vipi? “ I’m just Curious” “Vijana niliowatuma waifanye kazi ile walinihakikishia kwamba wamemuua na kumtupa bonde la mpunga” “ Ulifanya kosa kuwaamini na kuwaacha wakaifanya kazi ile peke yao.Ulitakiwa uwepo na uhakikishe kwamba ni kweli amekata pumzi” “ Mbona unaonyesha wasi wasi Frank? “ Kuna kitu ninakihisi.Naomba kesho ulifanyie uchunguzi suala hili kama ni kweli alikufa ama vipi” akasema Frank “ Vijana walinihakikshia kwamba yule binti amefariki na wakamtupa lakini ushauri wako si mbaya.Ninafahamiana na wakuu wa polisi wa vituo karibu vyote hapa jijini.Nitawasiliana nao ili nijue kama katika tarehe ile kuna maiti yoyote iliokotwa.Mpaka kesho saa nne tayari tutakuwa na jibu” “Good”akasema Frank na kukanyaga pedeli ya mafuta gari ikaongeza mwendo kuelekea nyumbani kwa Pascal “ Pascal kesho asubuhi kitu cha kwanza unachotakiwa kukifuatilia ni iwapo Elvis yupo hapa nchini au hayupo.Kama hayupo tutapata uhakika kwamba ni kweli alikwenda afrika ya kusini kuonana na Graca.Baada ya hapo tunatakiwa tufahamu pia kama alitumwa afrika ya kusini kikazi .Kama alitumwa kikazi alitumwa kazi gani?Lazima tuchukue tahadhali za mapema na hasa katika wakati huu mbao tunakabiliwa na mpango mzito mbele yetu.Elvis mtu yeyote hatakiwi kuwa kizingiti kwetu.Yeyote yule ambaye ataonekana kama hatari kwetu tutamuondoa haraka sana” akasema Frank “ Kesho ni siku yetu ngumu sana.Tuna mambo mengi ya kufanya .Kesho ni mwanzo wa harakati mpya”akasema Pascal huku akishuka garini wakaagana Frank akaendelea na safari kuelekea kwake “ Elvis tarimo !!.. akasema Frank kwa sauti ndogo “ Huyu kijana bado hajanifahamu mimi ni nani.I swear nitamkata kauli sekunde chache nikigundua kwamba amekuwa akinifuatilia mambo yangu.Safari hii ameingia sehemu mbaya sana” akawaza Frank akiwa njiani kuelekea kwake. ******************** Saa tatu za usiku ndege ye jeshi la afrika kusini iliyokua ikiwapeleka wanajeshi wa afriak kusini katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi nchini Zambia ikatua katika uwanja wa ndege wa kijeshi uliopo nje kidogo ya jiji la Lusaka.Ndani ya ndege hiyo walikuwamo pia Elvis na Graca.Ilikuwa ni safari ngumu kwa Graca kwani hakuwahi kusafiri na ndege za kijeshi ila kwa Elvis ilikuwa ni moja ya safari zake za kawaida Ndege ilisimama lango likafunguliwa na wanajeshi wakashuka.Kiongozi wa msafara ule Meja Tsemaleke Suso akawaongoza Elvis na Graca hadi katika gari dogo la jeshi wakapanda.Wanajeshi wengine wakaingia katika katika gari kubwa na safari ya kuelekea katika kambi ya kijeshi ikaanza.Baada ya kukatisha mitaa kadhaa ya mji wa Lusaka hatimaye Meja Tsemaleke akamuamuru dereva wa lile gari walilopanda akina Elvis asimamishe gari katika mtaa Fulani wenye maduka mengi akashuka na kuwaomba akina Elvis nao washuke “ kwa mujibu wa maelekezo niliyopewa na Bongani ni kwamba niwafikishe hapa na toka hapa kuna mtu ambaye atawachukua na kuendelea na safari yenu” akasema Meja Tsemaleke “ Ahsante sana Meja kwa msaada wako huu mkubwa” akasema Elvis huku akipeana mkono na MejaTsemaleke wakaagana akarejea garini wakaendelea na safari yao Elvis na Graca walisimama pale mahala waliposhuswa nje ya duka moja lililokuwalimefungwa.Huu ni mtaa wa maduka na bado maduka kadhaa pamoja na sehemu za kuuzia vyakula na vinywaji yalikuwa wazi.Graca alionekana kuwa na wawi wasi mwingi “ Nini kinaendelea baada ya hapa? Akauliza “ Usiwe na wasi wasi Graca tutafika tu Tanzania” akasema Elvis na baada ya kama dakika tano mlango wa gari lililokuwa limeegeshwa mita chache toka pale walipokuwa wamesimama akashuka mtu mmoja aliyekuwa amevaa kofia nyeusi ya duara na koti refu jeusi.Mtu yule alisimama nje ya gari lake akaangaza angaza pande zote kisha akaanza kutembea taratibu kuwafuata akina Elvis “ Hallow” akawasalimu “ Hallo” akajibu Elvis Elvis? Yule jamaa akauliza “ Stanley? Elvis naye akauliza.Yule jamaa akaitika kwa kichwa kisha wakashikana mikono wakasalimiana halafu akawaongoza hadi katika gari lake wakaingia lakini kabla hawajaondoka akamgeukia Elvis “ Elvis Maelekezo niliyopewa ni kuwafikisha mpakani mwa Tanzania na Zambia na kuhakikisha mnafika salama nchini kwenu.Niko sahihi?” akasema Stanley “ Uko sahihi Stanley.Hilo ndilo hitaji letu kubwa” akajibu Elvis na Stanley ambaye alionekana ni mtu asiyependa maongezi mengi akawasha gari na kuondoka “ Stanley samahani naweza kutumia simu yako kupiga Tanzania? Akasema Elvis .Bila kujibu kitu Stanley akampatia Elvis simu yake.Elvis akaandika namba alizotaka kupiga na kubonyeza kitufe cha kupigia simu ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa “ Hallo “ ikajibu sauti tamu ya kike upande wa pili “ Hallow Doreen..” akasema Elvis “ Elvis !! Doreen akastuka “ Ndiyo Doreen” akasema Elvis na kumsikia Doreen akishusha pumzi “ Patricia aliniambia kwamba umesafiri kwenda afrika ya kusini mbona unanipigia na namba ya simu ya Zambia? Akauliza Doreen “ Ndiyo nilikwenda afrika ya kusini lakini kwa sasa niko Zambia” akajibu Elvis na kimya kifupi kikapita “ Doreen are you there? Akauliza Elvis “ I’m here Elvis” Good.Doreen unakumbuka uliniambia kwamba uko tayari kunisaidia kwa jambo lolote ? “ Ndiyo nakumbuka Elvis .Unataka nikusaidie kwa jambo gani? Sema chochote niko tayari” akasema Doreen “ Naomba kesho alfajiri na mapema uchukue gari lako lile jipya na uanze safari ya kuelekea jijini Mbeya.Nitakupigia simu nikiwa Mbeya na kukujulisha mahala nilipo” akasema Elvis .Doreen akabaki kimya “ Doreen are you there? Akauliza Elvis “ I’m here Elvis” akajibu Doreen “ Umenielewa nilichokuomba? I real need your help right now” akasema Elvis Baada ya kimya cha sekunde kadhaa Doreen akasema “ Ok Elvis nitakusaidia.Kwako sina uwezo wa kusema hapana” akajibu Doreen.Uso wa Elvis ukapambwa na tabasamu baada ya jibu lile la Doreen. “ Ahsante sana Doreen.Ahsante sana.Tafadhali naomba usimweleze chochote Patricia.Nitakupigia simu kesho nikiwa Mbeya na kukupa maelekezo mahala nitakapokuwa” akasema Elvis “ Usijali Elvis japokuwa umenistukiza sana lakini nitajitahidi kufanya kama ulivyoniomba.Ila tafadhali naomba unihakikishie kwamba uko salama na hakuna tatizo lolote” akasema Doreen “ Niko salama Doreen usihofu chochote” akasema Elvis na kukata simu akamrudishia Stanley simu yake.Hawakuongea kitu chochote safari ikaendelea kwa kasi kuelekea Tunduma mji uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia *********************** Ilikuwa ni safari ndefu kutokana na umbali mrefu uliopo kati ya Lusaka na Tunduma .Kutoka Lusaka hadi Tunduma ni umbali wa kilometa 1022.Stanley ambaye alionekana kwa mahiri mno katika usukani aliendesha gari kwa kasi na umakini mkubwa.Graca kutokana na uchovu aliokuwa nao kwa safari ndefu ilimlazimu alale katika kiti cha nyuma Saa mbili za asubuhi walikaribia mji wa Tunduma.Stanley akaachana na barabara kuu akachepuka katika barabara ya vumbi ambayo ilionyesha haikuwa ikipitwa sana ma magari.Aliendesha taratibu kutokana na barabara ile kujaa mashimo mengi.Baada ya mwendo wa kama dakika ishirini katika barabara ile akasimamisha gari na kutoa simu akampigia mtu Fulani wakaongea halafu safari ikaendelea.Dakika kama kumi hivi akasimisha gari chini ya mti mmoja mkubwa akashuka na kutoa simu yake akawasiliana na mtu na baada ya kama dakika tano hivi wakatokea watu wawili wakiwa na piki piki.Stanley akasalimiana nao wakaongea kidogo halafu akatoa fedha katika pochi yake na kuwahesabia na kurejea garini alikowaacha akina Elvis “ Elvis hawa jamaa wa piki piki ndio watakaowaingiza Tanzania ,Ni wazozefu sana wa njia hizi za vichochoroni kwa hiyo msiwe na wasi wasi hata kidogo.Kitu ninawachowaomba ni kwamba msiwaulize chochote na wala msitake kufahamu chochote toka kwao.Watawapeleka sehemu mnakotaka kwenda na baada ya hapo mtatafuta usafiri wa kuwafikisha Dar es salaam.Poleni sana kwa safari ndefu” akasema Stanley “ Stanley sina neno kubwa la kuweza kukushukuru kwa msaada huu ya kusema ahsante sana. Tunashukuru umetufikisha hapa salama na ninakutakia safari njema ya kurejea Lusaka “ akasema Elvis huku akimpa mkono wakaagana na kuelekea katika piki piki wakapanda na safari ya kuelekea Tunduma ikaanza. Dakika thelathini baadae waliwasili katika mji wa Tunduma mji wenye pilika pilika nyingi sana za kibiashara.Elvis akawaomba wale vijana wawapeleke katika stendi ya magari yaendayo mjini Mbeya na kuagana na vijana wale .Pale stendi kulikuwa na watu wengi na Elvis hakutaka wapande gari lenye watu wengi hivyo akakodisha gari ndogo aina ya Noah ili iwapeleke Mbeya. Saa saba za mchana wakawasili jijini Mbeya, jiji zuri na lenye kuvutia sana.Dereva wa lile gari walilokodi alilifahamu vyema sana jiji la Mbeya hivyo akawapeleka katika hoteli nzuri ambako walichukua vyumba viwili .Kwa kutumia simu ya pale hotelini Elvis akawasiliana na Doreen aliyekuwa safarini kuelekea Mbeya na kumfahamisha mahala walikofikia.







**************** Pamoja na kurejea nyumbani saa kumi alfajiri lakini Pascal alishindwa kabisa kupata usingizi .Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi sana lakini mawili makubwa yaliyokuwa yakimsumbua kichwa ni mpango ule wa kuiangusha serikali na pili ni taarifa za kuonekana kwa Elvis akiwa na Graca nchini afrika ya kusini.Hizi ni taarifa zilizomstua sana kwani anafahamu vizuri Elvis mpaka akaonane na Graca lazima kuna kitu ambacho alikuwa anakifuatilia “ Damn !! akasema Pascal kwa hasira na kuinua glasi ya mvinyo akanywa Hadi kunapambazuka bado alikuwa macho.Akaoga na kuelekea kazini.Akiwa njiani aliwasiliana na Arafa mmoja wa wafanyakazi wa idara ya ujasusi anakofanya kazi Elvis “ Hallow Pascal” akasema Arafa baada ya kupokea simu “ hallow Arafa uko wapi sasa hivi? Akauliza Pascal “ Ninaelekea kazini Pascal.wewe uko wapi? “ Hata mimi ninaeleka kazini.” “ Kulikoni Pascal leo umenipigia simu asubuhi namna hii? Akauliza Arafa “ Nilitaka kuja ofisini kwenu leo hii lakini sintaweza kwa hiyo ninahitaji msaada wako” “ Msaada gani Pascal? “ Ninahitaji kuonana na Elvis.Kuna taarifa ninataka kumpa lakini kuna mtu aliniambia kwamba Elvis hayupo.Sina uhaika sana na jibu hilo kwa hiyo naomba unisaidie kuthibitha kama ni kweli hayupo.Kama yupo usimweleze chochote nitaarifu nitamtafuta mimi mwenyewe kwa wakati wangu” akadanganya Pascal “Hauna mawasiliano na Elvis? Akauliza Arafa “ Hapana sina .Elvis ni mtu ambaye sijazoeana naye kiasi cha kuwa na mawasilino naye japokuwa tunafahamiana.” Akasema Pascal .Arafa akafikiri kidogo kisha akasema “ OK nitakutaarifu nikifika ofisini” akasema Arafa na kukata simu “ Leo lazima nipate uhakika kuhusu Elvis kuonekana afrika ya kusini.Huyu mtu ananiweka tumbo joto sana.Elvis ni mtu hatari na lazima tumdhibiti mapema” akawaza Pascal Alifika ofisini kwao na alionekana ni mwenye mawazo mengi .Aliendelea na kazi na saa tatu na robo Arafa akampigia simu “ Halow Arafa” akasemahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Pascal “ Pascal ni kweli Elvis hayupo yuko nje ya mkoa kikazi” “ Amekwenda mkoa gani na atarudi lini? “ Siwezi kujua yuko wapi na anafanya nini na atarudi lini kwani kiwango change si cha kufahamu mambo kama hayo.Atakaporejea nitakufahamisha mara moja” “Ahsante sana Arafa .Naomba unitaarifu atakaporejea ila tafadhali naomba usimfahamishe chochote kama nilikuwa namtafuta” “ usijali Pascal” akajibu Arafa na kukata simu “ Kwa sasa nina uhakika kwamba Elvis amekwenda nchini Afrika ya kusini na si nje ya mkoa kama alivyoniambia Arafa.Lakini kwa nini akaenda kuonana na Graca? Hili ndilo swali la kutafutiamajibu haraka sana” akawaza Pascal na kutoka nje ya jengo akampigia simu Brigedia Frank “ hallow Pascal “ akasema Frank “ Frank tayari nimepata uhakika kwamba Elvis ana safari ya kikazi lakini mtu aliyenipa taarifa hizo hakuweza kunieleza amekwenda wapi na ni kazi gani amekwenda kufanya.Mpaka hapa hakuna shaka kwamba ni kweli Elvis alikwenda Afrika ya kusini.” Akasema Pascal halafu kimya kifupi kikapita Frank akasema “Kinachoniumiza kichwa ni kwamba kwa nini alikwenda kuonana na Graca? Nina hakika kuna kitu anakitafuta.Ni kitu gani basi alikuwa anakitafuta kwa Graca?Amempeleka wapi Graca? Mpaka hivi sasa sijapokea taarifa zozote kuhusiana na zoezi la kumtafuta mwanangu” Frank hata mimi jambo hilo limekuwa linaniumiza sana kichwa changu.Tunatakiwa tutafute jibu la haraka sana la swali hili” akasema Pascal “ OK vizuri.Bado uko ofsini? Akauliza Frank “ Ninajiandaa kuondoka ili kuwahi kikao cha leo mchana “ Good.Kikao cha leo mchana ni muhimu sana kwani ndicho kitakachotupa muelekeo mzima wa mkakati wetu .Wageni wetu tayari nimewasindikiza wameondoka .Utanipitia hapa nyumbani ili tuongozane wote kuelekea kikaoni” akasema Frank “ Ok Frank nakuja sasa hivi” akasema Pascal ***************** Jumba la kifahari la aliyewahi kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Daudi sichoma lilizungukwa na bustani iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa,iliyosheheni miti mizuri na maua ya kupendeza. Ndege wazuri wa kila rangi waliruka katika miti yenye maua mazuri na kuzidi kuifanya bustani ile iwe na mandhari ya kipekee sana.Daudi Sichoma ni mmoja kati ya viongozi wanaosemekana kujilimbikizia utajiri mkubwa sana ndani na nje ya nchi.Alimiliki mahoteli makubwa ndani na nje ya nchi,pia anamiliki shirika la ndege na vile vile ana hisa nyingi katika makampuni mengi makubwa ya ndani na nje ya nchi.Kiwango cha utajiri wake kimebaki kuwa siri kutokana na kumiliki miradi mingine mingi kwa siri Eneo litakalotumika kwa ajili ya kikao liliandaliwa vizuri sana katikati ya bustani hii nzuri.Kabla ya kukaa katika meza ya kikao kulikuwa na sehemu iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya wajumbe kupata chakula kabla ya kuanza kwa kikao. Mpaka saa saba mchana karibu wajumbe wote waliotakiwa kuhudhuria kikao kile tayari walikwisha wasili.Daudi akawaongoza wajumbe wale hadi katika sehemu kulikoandaliwa chakula na wajumbe wakaanza kujipatia mlo wa mchana.Kilikuwa ni chakula kizuri kilichoandaliwa na wapishi mahiri waliotoka katika mojawapo ya hoteli anayomiliki Daudi.Baada ya chakula wajumbe wakaelekea sehemu kulikokuwa kumeandaliwa kwa ajili ya kikao.Eneo lote lilikuwa kimya sana. Ni milio tu ya ndege iliyokuwa ikisikika katika bustani ile.Brigedia Frank ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kikao kile akafungua kikao kwa kuwashuku wajumbekwa kufika kwao “ napenda niwataarifu kwamba wale wageni wetu tuliokuwa nao jana wameondoka leo asubuhi kurejea makwao na majukumu yote ya ule mpango yako juu yetu kwa hiyo hatuna muda wa kupoteza tunatakiwa tuanze mara moja mikakati ya kutekeleza mpango huu mkubwa.wao tutakuwa tukiwatumia mihutasari ya kila kikao tunachokifanya na utekelezaji wa kila jambo.Fedha zitawekwa katika akaunti maalum na kila pale tutakapokuwa tukihitaji fedha hatutakuwa na upungufu wowote.Ndugu zangu hiki ni kikao cha chetu cha kwanza cha kuweka mikakati ya kuelekea Tanzania mpya.Mnakaribishwa kwa mawazo tukianza na mheshimiwa Daudi ambaye ana uzoefu mkubwa wa kuwepo serikalini na atatusaidia sana kimawazo” akasema Brigedia Frank .Daudi sichoma akatabasamu na kukohoa kidogo akasema “ Awali ya yote napenda kuwashukuru nyote kwa kufika kwenu.Namshukuru sana Frank kwa uamuzi wake wa kunishirikisha katika mpango huu muhimu.Nasema ni mpango muhimu kwa taifa letu kwani endapo utafanikiwa basi utaleta neema kwa watanzania na maisha yao yataboreka tofauti na hali ilivyo sasa.Sote tuliwasikia akina Alhafidh na maelezo waliyotupatia .Ukiyachambua kwa undani maelezo yale utagundua kwamba kuna kila ulazima wa kuiondoa kwa lazima serikali iliyopo madarakani.Hatuwezi kuiondoa kwa njia za kdemokrasia bali kwa kufanya mapinduzi.” Akasema Daudi na kunyamaza kidogo kisha akaendelea “ Tukirejea maelezo ya Alhafidh tunagundua kwamba mipango yote inayofanyika hivi sasa kuhusiana na uwekezaji mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi inalenga katika kuwanufaisha viongozi walioko madarakani.Hakuna hata mpango mmoja utakaowanufaisha wananchi wa hali ya chini.Kitu cha pili ni kwamba viongozi hawa wanataka kuipeleka Tanzania katika machafuko kwa sababu endapo marekani watajenga kituo chao cha kijeshi hapa nchini basi Tanzania itakuwa ni moja ya shabaha za magaidi.Nchi haitakuwa salama tena.Tunatakiwa tuhakikishe kwamba hilo halitokei kwa kuja na mikakati mizito sana ambayo itakuwa na faida kwa watanzania na hata tutakapofanikiwa kuiangusha serikali basi watanzania watuamini kwamba tuna nia ya dhati ya kufanya mageuzi makubwa ya maisha yao.Endapo kila mtanzania ataiona na kufurahia faida ya kuwa na gesi na mafuta nchini Tanzania basi mapinduzi tutakayoyafanya yatakuwa na manufaa na watanzania watatupenda na kutuunga mkono.Makampuni ya kiarabu tutayapa udhibiti wa biashara ya mafuta na yatatuletea faida kubwa sana na tutahakikisha kila mwananchi wa nchi hii mkubwa kwa mdogo wanafaidika nayo.Tutakuza uchumi tutaboresha maisha ya mwananchi mmoja moja na kila raia wanchi hii atakuwa na uso wenye tabasamu.Hiyo ndiyo ndoto yangu ya muda mrefu sana ya kumfanya Mtanzania afurahi kuwapo Tanzania” akasema Daudi na wajumbe wote wakampigia makofi kumuunga mkono David akaendelea “ Ndoto yangu ya miaka mingi ni kuwa rais wa nchi hii.Lengo si kutaka kutafuta utajiri au umaarufu au kuabudiwa lakini lengo langu kubwa ni kutaka kumfanya kila raia wa nchi hii awe na furaha ,ayamudu maisha yake ,watoto wetu wasome na ajira zipatikane.Hayo yote yanawezekana tu kwa kuwa na koongozi jasiri kama mimi.Nyote mnafahamu mambo niliyoyafanya na kuleta mabadiliko katika jamii .Ni mambo hayo niliyoyafanya ndiyo yanayofanya nikawa na maadui wengi kisiasa na nikaondolewa madarakani.Pamoja na kuondolewa katika nafasi yangu ya uwaziri mkuu bado wameendelea kunifuata fata na kuhakikisha kwamba wananizika kabisa na kwa hilo naweza kusema kwamba wamefanikiwa kwani sionekani tena katika medani za siasa.Ninamshukuru Frak kwa kunishirikisha tena kaika mpango huu ambao nina hakika lazima utafanikiwa.” Wajumbe wakapiga makofi halafu akaendelea “ Naomba niweke wazi kwenu kwamba kama ilivyo ndoto yangu ya muda mrefu na endapo mpango huu utafanikiwa basi naombeni mimi niwe rais.Naomba tukubaliane toka awali kwamba tukifakiwa mimi ndiye nitakayekuwa rais” Daudi akasema na kuwatazama wajumbe .Kimya kifupi kikapita Frank akasema “ Mimi sina kipingamizi na hilo.Nafahamu wananchi wengi bado wanakuhitaji sana ili uwaongoze.wewe ndiye utakayekuwa rais wetu” Wajumbe wengine nao wakaungana na Frank na wote wakakubaliana kwamba endapo mapinduzi yatafanyka basi Daudi awe ndiye rais “ Ahsanteni sana ndugu zangu kwa kunikubalia ombi langu.Kwa sasa nitatoa ushirikiano wa kila namna ili kufanikisha mpango huu”akasema Daudi huku akitabasamu na wajumbe wakampigia makofi “ Ndugu zangu kuiangusha serikalini ni mpango mpana sana na wa siri kubwa.Ili tufanikiwe kuna watu ambao lazima uwe nishirikishi .kwanza kabisa lazima tutafute uungwaji mkono toka kwa makamanda wa vikosi vya jeshi ambao watatengeneza mtandao wa askari watakaofanya uasi.Jeshi litaipindua serikali na kukabidhi madaraka kwa mtandao wetu kwa maana hiyo lazaima tupate makamanda wa jeshi ambao watakuwa tayari kushirikiana nasi.Pili tunatakiwa kuchochea uhasama mkubwa na chuki kwa raia dhidi ya serikali yao.Tunatakiwa tulete aina Fulani ya machafuko ambapo jeshi la polisi litalazimika kutumia nguvu kubwa katika kuyatuliza na kusababisha vifo na katika machafuko hayo sisi yatakuwa na faida kwetu .Serikali itaonekana imeshindwa kuwalinda raia wake na inakiuka haki za binadamu na hivyo wananchi hawatakuwa na imani nayo tena.Tanzaniaitachafuka katika jumuia ya kimataifa na hiyo itakuwa ni sababu nyingine ya kutosha kabisa kwa sisi kufanya mapinduzi.Tutakapoingia madarakani ndani ya kipindi kifupi tutarejesha halali ya amani na hivyo wananchi watakuwa na imani na matumaini makubwa na sisi.Katika kipengele hiki tutawatumia wanasiasa wa vyama vya upinzani.Hawa watapandikiza chuki kwa katika jamii kwamba serikali imewazuia mafuta wa marekani na hivyo kuongoza maandamano na migomo isiyo na kikomo kuishinikiza serikali iliyoko madarakani kuachia ngazi.Migomo na maandamano hayo yataandamana na vurugu na hivyo kuilazimisha serikali kutumia nguvu kubwa.Tutawawezesha wanasiasa hawa kifedha na watazunguka nchi nzima kuifanya kampeni hii”David akanyamaza wajumbe wakampigia makofi kwa mawazo yake mazuri. Kisha wakaendelea “ wanasiana hawa wanachokipigania wa watanzania bali maslahi yao binafsi kwa hiyo kwa kutumia ushawishi wa fedha tutaviunganisha vyama vyote vya upinzani hiyo itaturahishishia kutimiza lengo letu.Mimi nitawaita viongozi hao wa vyama vya siasa vya upinzani na kufanya nao mkutano wa siri.Nitawashawishi na watakubaliana nami.Sintawaeleza kuhusiana na mpango wetu wa kuiangusha serkali lakini nitawahakikishia kwamba endapo watafanya kampeni hiyo na serikali iliyoko madarakani ikaondolewa basi mimi nitagombea urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani.Baada ya mapinduzi viongozi hawa wa vyama vya siasa tutawapatia nyadhifa mbalimbali katika serikali ikiwa ni njia ya kuwafunga midomo”akanyamaza akainua glasi yake ya maji akanywa na kuendelea “ Kipengele cha tatu ambacho tunatakiwa kukifanya ni kuwashirikisha baadhi ya viongozi kadhaa kutoka serikali kuu,idara ya usalama wa taifa.Jeshi la polisi na sehemu yoyote ambayo tutayaona ina manufaa.kwa upande wa serikali kuu kuna mtu ambaye tunaweza kumtumia.Makamu wa rais ndugu Shafi Abdulkhareem Omari.Mzee huyu hana maelewano mazuri na rais na si mara moja kumetokea mikwaruzano.Mzee huyu atatufaa sana na atatusaidia katika mambo mengi.Baada ya mapinduzi mzee huyu ataendelea na wadhifa wake wa makamu wa rais” akanyamaza tena na kuwatazama wajumbe halafu akaendelea “ hayo ndiyo mambo matatu makubwa ambayo tunatakiwa kuyafanya iwapo tunataka mpango wetu ufanikiwe,Jeshi, wanasiana na viongozi wachache wa serikali na idara za usalama .Tukifanikiwa kuzidhibiti sehemu hizo basi tujue kwamba mpango wetu utafanikiwa asilimia mia moja .Kwa upande wangu mimi nitashughulika na viongozi wa vyama vya siasa na kuwaweka chini na watanisikiliza.Nitashughulika pia na makamu wa rais pamoja na vongozi wengine.Wote hawa nina hakika ya kuwashawishi na wakajiunga nasi.Upande wa jeshi na sehemu nyingine itakayoonekana kuwa na umuhimu zitashughulikuwa na watu wengine” akamaliza kutoa maoni yake Daudi .wajumbe wakampigia makofi “ Ahsnte sana mheshimwa rais” akasema Frank na wote wakacheka “ tafadhali msicheke.Huyu ndiye rais wetu mtarajiwa kwa maana hiyo hakuna haja ya kusubiri hadi mapinduzi yafanyike ndipo tuanze kumuita rais.Mambo yanaanza sasa kwani uhakika wa kuchukua serikalini ni mkubwa sana” akasema Frank “ Nadhani nyote mmesikia mheshimiwa David yeye ana uzoefu mkubwa katika serikali na ametupa mwangaza mkubwa sana na muelekeo mkubwa.Bado tunaendelea kuchukua maoni na mitazamo ya kila mmoja wetu hapa.Kabla sijaendelea zaidi naomba na mimi niweke wazi mbele yenu kwamba nitashghulikia suala la jeshi.Nina ushawishi mkubwa kwa makamanda wa vikosi mbalimbali vya jeshi kwa hiyo naomba suala hili niachiwe mimi na nitaliweka sawa.Licha ya nguvu ya ushawishi lakini mkumbuke pia kwamba tuna fedha nyingi sana kwa ajili ya kazi hii.kwa hiyo lazima fedha itumike na panapo fedha hakuna kinachoharibika” akasema Frank na kisha wakaendelea na mjadala ****************** Kengele ya mlango wa chumba cha Elvis ikalia na kumuamsha toka usingizini.Toka walipopata chakula cha mchana alikuwa amelala kutokana uchovu wa safari ndefu.Akajiinua kwa uchovu na kutazama saa yake .Ilipata saa kumi na mbili za jioni.Akainuka akavaa shati na kuelekea mlangoni.Akaufunguamlango na kukutana na muhudumu “ samahani kaka yule mgeni wako uliyesema tumuandalie chumba tayari amewasili” akasema muhudmu “ Doreen ?!! “ Ndiyo kaka.Yupo mapokezi anakusibiri” “ Ok ahsante sana nakuja sasa hivi”akasema Elvis na kuvaa viatu vya wazi vilivyokuwamo mle chumbani akatoka na kuelekea mapokezi.Doreen alikuwa amekaa katika sofa jeusi la pale mapokezi na mara tu alimpomuona Elvis akasimama na kumkumbatia “ Elvis !! akasema Doreen huku akiendelea kumkumbatia Elvis kwa nguvu “ Ahsante sana Doreen kwa kuja.Karibu sana mbeya” “Ahsante sana Elvis .Ninashukuru nimefika salama.Njia nzima nilikuwa na mawazo mengi sana kama uko salama.” “ Niko salama Doreen.Hukupatwa na tatizo lolote njiani? “ Hapana sikupata tatizo lolote .Gari hili bado jipya kabisa” akasema Doreen “ Patricia anaendeleaje? Ulimweleza chochote kuhusiana na safari hii? “ Patricia anaendelea vizuri na sikumweleza chochote kuhusiana na safari hii na wala hajui kama nimesafiri” akasema Doreen “ Ahsante sana Doreen.Kwa sasa naomba ujimwagie maji halafu tupumzike kidogo kisha tutapata chakula cha usiku.Tuna maongezi marefu kidogo baada ya chakula,” akasema Elvis na kumpeleka Doreen katika chumba alichokuwa amemuandalia Ouh jamani ! kwa nini linapokuja suala la Elvis najikuta siwezi kumkatalia kitu chochote ? Nimeendesha gari toka Dar hadi huku bila kujua nini ananiitia”akawaza Doreen baada ya Elvis kutoka mle chumbani.Akavua koti na kulitupa kitandani kisha akavua gauni lake na kubakiwa na nguo ya ndani “ Its cold like hell .Baridi sana huku mbeya.Natamani kama ningepata nafasi ya kulala na Elvis leo..” Akawza Doreen akajifunga taulo na kuingia bafuni akafungua maji ya moto na kuoga “ Kitendo cha patricia kunitaka nizae na mume wake Elvis kimeniweka katika wakati mgumu sana .Kuna hisia za tofauti nimeanza kuzipata kuhusu elvis.Toka nilipolala naye siku ile na kuyashika maungo yake nyeti kila nikimuona mwili wote hunisisimka” akawaza Doreen huku akiendelea kuoga.Picha ya usiku ule akiwa mtupu amelala kitandani kwa Elvis ikamjia kichwani akatabasamu “ Natamani usiku kama ule ujirudie leo hii tena tukiwa huku mbali ambako hakuna mtu wa kumuogopa.” Akaendelea kuwaza Doreen huku akijifuta maji akarejea chumbani na kujilaza kitandani akajifunika blanketi kulikuwa na baridi kali na taratibu kijiusingizi kikamchukua. ************** Akiwa usingizini kwa mbali alisikia kama mlango wa chumba chake unagongwa.Mwanzoni alidhani labda anaota lakini mlango ulipoendelea kugongwa akafumbua macho.Ni kweli kunamtu alikuwa anagonga mlango.Akainuka na kuelekea mlangoni akaufungua na kukutana na sura yenye tabasamu ya Elvis.Kwa muda wa sekunde kadhaa Elvis alibaki anakodolea macho kifua cha Doreen .Kuna kitu kilimvutia pale kifuani.Doreen aligundua kwamba Elvis alikuwa amevutika na sehemu ile ya kifua naye akabaki amesimama na kumuacha Elvis aendee kukisaili kifua chake.Elvis akakohoa kidogo na kusema “ Pole sana na uchovu Doreen na samahani kwa kukuamsha” “ Ahsante sana Elvis.Kuna baridi sana huku na ndiyo maana nikapitiwa na kijiusingizi.Karibu ndani” “ Doreen nimekuja kukutaarifu kwamba ni muda wa kupata chakula cha usiku sasa.” “ Ahsante sana Elvis.Nilikuwa nimejisahau kabisa kuhusu chakula.Karibu ndani Elvis na mimi nijiandae twende “ “ Ahsante sana Doreen .Mimi natangulia hotelini utanikuta kule” “ No Elvis.tafadhali nisubiri tuongozane wote.karibu ingia ndani” “ Ok Doreen niko hapa nje ninakusubiri” “ Ingia ndani Elvis.Are you afraid of me? C’mon I’m not a ghost.Please come in” akasema Doreen “ ahsante Doreen.Badilisha nguo na utanikuta hapa nje” “ Ok Mr shy guy.Just wait for me here .I wont take long” akasema Doreen na kuufunga mlango akamuacha Elvis amesimama pale nje akimsubiri.Baada ya dakika tano akatoka akiwa amevaa nguo nzito za baridi wakaongozana hadi sehemu ya chakula .Hakukuwa na watu wengi zaidi ya raia wachache wa kigeni .Elvis akamuongoza Doreen hadi katika meaza moja iliyokuwa pembeni ambayo msichana mmoja mwenye umbo dogo alikuwa amekaa “ karibu Doreen” akasema Elvis na kumvutia Doreen kiti akaketi.Doreen na Graca wakatazamana .Elvis akatabsamu na kusema “ Doreen samahani sikukutaarifu toka mwanzo lakini katika safari yangu hii nimeambatana na mtu mwingine.Tafdhali kutanana Graca Frank,Ni mtanzania aliyekuwa nchini afrika ya kusini na kwa sasa anaelekea Dar es salaama” akasema Elvis halafu akamgeukia Graca “ Graca kutana na Doreen.Ni mmoja kati ya marafiki zangu wakubwa” Doreen na Graca wakasalimina na kisha wakaendelea kupata mlo wa usiku.Ni Elvis na Doreen pekee waliokuwa wazungungumzaji pale mezani.Graca alikuwa kimya.Pengine ni kwa sababu ya kutokuwa na mazoea nao ya karibu Baada ya kumaliza chakula Elvis akamsindikiza Graca hadi chumbani kwake “ kesho alfajiri na mapema tunaanza safari ya kuelekea Dar es salaam.Doreen amekuja na gari ambalo ndilo tutalitumia.Sikutaka tupande magari makubwa ya abiria kwani sitaki uonekanae. Kwa hiyo nitakuamsha alfajiri na mapema kwa ajiili ya kuanza safari. “ Ahsante sana Elvis kwa msaada wako .Sikujua kama una moyo wa huruma namna hii.Nakuahidi nikifika sehemu salama nitakueleza kila kitu ninachokifahamu” “ Usihofu Graca.Uko salama na utaendelea kuwa salama.Nitakulinda siku zote na hakuna mtu yeyote atakayekudhuru.Kwa sasa endelea kupumzika” akasema Elvis na kugeuka akaanza kuondoka. “ is she yur girlfriend? Akauliza Graca .Elvis ambaye tayari alikwisha ushika mlango akageuka “ Unasemaje Graca? Akauliza “ Doreen.Is she your girlfriend? Akauliza tena Graca “ We’re friends.Good friends” akajibu Elvis “ You look good together.Ok Good night Elvis” akasema Graca “ Good night” akasema Elvis huku akitabasamu akaufunga mlango na moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa Doreen akagonga mlango Doreen akaufungua .Elvis akaingia ndani na kwenda kuketi sofaniKuna baridi sana Elvis.Ninahisi nahitaji kupata mvinyo” akasema Doreen akapiga simu hotelini wamletee mvinyo.Baada ya dakika mbili muhudumu akawasili akiwa na chupa ya mvinyo na glasi mbili.Doreen akamimina mvinyo ule katika glasi na kumpatia Elvis glasi moja. “Ni mara yangu ya kwanza kufika Mbeya.Sikujua kama kuna baridi kiasi hiki”akasema Doreen huku naye akiketi sofani karibu na Elvis “ Mbeya ni mkoa wenye baridi kali sana.Nimewahi kufika mara kadhaa kwa hiyo ninapafahamu vyema na ndiyo maana nikakusisitiza usisahau nguo za baridi” “Ahsante sana kwa kunikumbsha.Bila hivyo sijui ningefanya nini japokuwa hata hivi sasa bado naisikia baridi kali sana.” Akasema Doreen “ Ok tuachane na hayo.Pole sana na uchovu wa safari ndefu” akasema David “Ni safari ndefu sana.Nashukuru nimefika salama na sikupatwa na tatizo lolote njiani” Hongera kwa kuendesha gari kwa umahiri mkubwa,wanawake wengi hawawezi kuendesha gari kwa umbali mrefu namna hii” “Mimi nimekwisha zoea kuendesha gari umbali mrefu.Huwa ninaendesha gari hadi Nairobi hadi Kampala bila matatizo.” Akasema Doreen halafu kimya kikapita “ Patricia aliniambai kwamba umekwenda afrika ya kusini lakini nikastuka uliponipigia na namba za Zambia.Uliamua kurudi kwa kutumia njia ya gari?akauliza Doreen “ Nlilazimika kutumia njia ya gari badala ya ndege.Hii ni kwa sababu ya Graca” “Graca?! Doreen akashangaa “ Graca amefanya nini? “ Kilichonipeleka afrika ya kusini ilkuwa ni kumfuata binti huyu.” “ Kwani Graca ni nani? Kafanya nini? Akauliza Doreen “ Siwezi kukueleza kwa undani sana kuhusu yeye kwa sababu ni mambo ya ndani sana ya kikazi lakini kwa ufupi ni kwamba Graca ana taarifa muhimu sana na maisha yake yako hatarini na ndiyo maana imenilazimu kumuondoa kule afrika ya kusini” “ wanataka kumuua ? ! Doreen akashangaa “ Kwa miaka kadhaa sasa amekuwa akiishi kwa mateso makubwa na kwa taarifa alizonazo lazima nichukue dhamana ya kumlinda.” “ Ouh Elvis pole sana” “ Ahsante sana Doreen.lakini hii ni mojawapo ya kazi zangu.Nimekwisha zoea mambo kama haya” “ hao wanaotaka kumuua wako wapi? Unawafahamu? Akaulizia Doreen “ wako afrika ya kusini na wengine wako hapa nchini na ndiyo maana sikutaka kutumia usafiri wa kawaida wa abiria kwa nia ya kumficha.Toka afrika ya kusini nimepita naye katika njia za uficho ili asionekane.Baada ya kufika hapa nimeona nitafute mtu ambaye ninamuanini wa kunisaidia na nimekuchagua wewe.Ninakuamini sana Doreen and please don’t let me down” Doreen akatabasamu na kusema “ Elvis ahsante sana kwa kuniamini.Naomba kuahidi kwamba katu siko tayari kukuangusha .Sijawahi na sintofanya hivyo kamwe.Chochote utakachokitaka toka kwangu nitakupatia na ndiyo maana niko hapa muda huu kwa sababu ulinitaka nije hapa.Feel free to tell me anything,I mean anything” akasema Doreen na uso wa Elvis ukajenga tabasamu “ nashukuru kwa maneno yako mazito.Nitaendelea kukuamini kwa siku zote za uhai wangu.Kitu kikubwa nilichokuitia hapa ni kwamba Graca anahitaji msaada.kwanza kusafirishwa kwa siri hadi Dar e s salaam na pili kuhifadhiwa sehemu salama.Mtu anayetishia maisha yake ni baba yake mzazi ambaye ni afisa mkubwa jeshini .Kuna mambo ya siri anayoyafahamu Graca kuhusiana na baba yake na tumekubaliana kwamba ili anieleze mambo hayo lazima nihakikishe anakuwa salama.Akisha nieleza nitamfanyia mpango wa kumuhamisha nchi na kumtafutia makazi nchi nyingine akaendelee na maisha yake .Kwa mambo hayo mawili ninahitaji mtu ambaye nina muamini sana” akasema Elvis Doreen akamtazama Elvis usoni.Macho yalionyesha uoga Fulani “ Mbona unaogopa Doreen” akauliza Elvis “ Elvis I’m so scared” akasema Doreen.Elvis akamsogelea akamshika mkono na kumtazama usoni “ Do you trust me Doreen? Akauliza “ Ofcourse I do. I trust you” akasema Doreen. “ Thank you .That the only thing I wanted to hear from you.So don’t be scared.You are more than safe around me” akasema Elvis na kumfanya Doreen atabasamu “ Tell me Elvis.What do yuwant me to do? “ kesho tutarejea dar es salaam.Nataka sehemu ya kumficha Graca,sehemu ambayo hakuna watu wengi wanaingia .Ninataka Graca akae nyumbani kwako kwa muda wakati ninamtafutia makazi mazuri” “ Ahsante sana Elvis kwa kuniamini na kuchagua Graca akae kwangu.Sipingani na mawazo yako lakini ninadhani unahitaji kutafuta sehemu ambayo ni salama zaidi .Pale kwangu ni sehemu salama lakini watu wengi huingia .Mimi ni mtu mwenye mazoea na watu wengi kwa hiyo kuwazuia watu ghafla wasifike nyumbani kwangu kunaweza kuleta udadisi kidogo na wakataka kujua kulikoni.Lakini kuna wazo nimelipata” “ wazo gani? Akauliza Elvis “ Kuna rafiki yangu mmoja ameolewa na mzungu na kwa sasa mzungu huyo anarejea kwao.Kwa kuwa anaondoka na mke wake wameamua wauze kila kitu chao hapa Tanzania .Nyumba yao ni nzuri sana na yenye usalama wa kutosha.Ina uzio mkubwa na ina kila kitu ndani hadi bwawa la kuogelea.Kama tukiona inafaa tuinunue nyumba ile hata kwa kulipa pesa nusu na baadae tutamaliza deni taratibu.Nadhani hii itakuwa ni sehemu nzuri sana kumuhifadhi Graca”akasema Doreen na Elvis akatabasamu “Hilo ni wazo zuri sana na nyumba kama hiy ndiyo ambayo ninaitafuta.Inauzwa shilingi ngapi hiyo nyumba? “ Mimi aliniambia kwamba endapo ningempatia milioni themanini basi angeweza kunipatia nyumba hiyo kwa sababu ni rafiki yangu lakini thamni yake ni zaidi ya milioni mia moja na hamsini.Ni rafiki yangu mkubwa na tunaelewana sana .Ninaweza kuongea naye na bei ikashuka hata zaidi ya hapo na tnaweza hata kumlipa kwa awamu.” “ kama ni hivyo hakuna haja ya kusubiri zaidi .Ongea naye sasa hivi na mwambie kwamba tutampaia shilingi milioni ishirini za kuanzia na zitakazobaki tutamlipa taratibu” akasema Elvis.Doreen akachukua simu yake na kumpigia huyo rafiki yake wakaongea kwa zaidi ya robo saa “ Imekuwa bahati sana kwani mpaka sasa hivi bado hajaiuza na kesho wanaondoka kuelekea Denmark.Amekubali kuchukua kiasi hicho kilichopo cha fedha na kilichobaki tutamlipa kwa kuwa anaondoka kesho asubuhi sana amesema kwamba funguo nitaikuta katika kampuni ya ulinzi ambayo wana mkataba wa kumlindia.Kila kitu amekiacha pale ndani hadi gari. “ wow ! that’s great news”akasema Elvis Naomba unipatie kompyuta yako .Amekupa namba za akaunti yake ya benki? “ Amesema atanitumia muda si mrefu”akasema Doreen huku akilifungua begi lake na kutoa kompyuta yake ndogo na muda huo huo ujumbe mfupi ukaingia katika simu yake “ Tayari amenitumia akaunti yake” akasema Doreen huku akiziandika namba zile na kumpatia Elvis ambaye alianza mara moja zoezi la kuhamisha pesa toka katika akaunti yake na kuzipeleka katika katika akaunti ya rafiki yake Doreen aitwaye Amanda.Alihamisha kiasi cha shilingi million ishirini na baada ya dakika kumi Amanda akapiga simu na kuthibitisha kwamba kiasi kile cha fedha tayari kimeingia katika akaunti yake “ Huu ndio uzuri wa teknolojia.Imerahisisha sana ufanyaji wa biashara.Ingekuwa ni zamani ingenilazimu mpaka kwenda benki na kuchukua kiasi hicho kikubwa cha fedha.Ahsante sana Doreen kwa msaada wako.Umenisaidia kitu kikubwa sana”akasema Elvis.Doreen akatabasamu ,kikapita kimya kifupi Doreen akasema “ Arent you going to involve Patricia in this ? akauliza Doreen.Elvis akainama akafikiri na kusema “ Nitamfahamisha lakini si sasa” “ kwa nini hutaki kumshirikisha katika suala hili? Don’t you trust her? Akauliza Doreen “ I trust her lakini kwa sasa sitaki kumuhusisha katika suala hili sitaki kumuongezea matatizo.Ana mzigo mzito unaomuelemea hivi sasa,sitaki kumbebesha mzigo zaidi.Alionao sasa unamtosha sana” akasema Elvis kwa uchungu “ Nakubaliana nawe Elvis .matatizo aliyonayo Patricia ni makubwa na hahitaji kuongezewa matatizo zaidi” akasema Doreen kimya kikapita “ Unafikiria nini Elvis kuhusiana na suala hili? “ Suala gani Doreen? “ Suala la Patricia” “ Doreen suala la Patricia kukosa mtoto sina namna ya kulitafutia ufumbuzi na hakuna namna ya kufanya ili aweze kupata mtoto.Patricia ni rafiki yako mkubwa na nina imani amekwishakueleza tatizo lake kwamba hawezi kubeba mimba.Kizazi chake kilikwisha ondolewa.I was there when it happened.Hakuna wa kumlaumu kwa kilichotokea kwani bila kufanya vile angepoteza maisha.Ninampenda Patricia na nilimpenda huku nikiyafahamu matatizo yake na nilipomuoa nilikwisha jiandaa kisaikolojia kwamba sintakuwa na mtoto maishani kwa sababu mke wangu hana uwezo wa kunizalia mtoto.Suala hili mimi haliniumizi kichwa hata kidogo .Kinachomsumbua Patricia kwa sasa ni maneno ambayo yameanza kujitokeza toka kwa ndugu zangu wakidai kwamba tumechukua muda mrefu toka tulipooana bila ya kuwa na mtoto.Ndugu zangu wanadai mtoto .Haya ni matatizo ya kawaida na ambayo ninauhakika baada ya suala hili kumalizika nitayaweka sawa.Sintampa nafasi ndugu yeyote kuingilia ndoa yangu.Huu ni upepo tu naamini utapita na mimi na mke wangu tutabaki salama” akasema Elvis “ yah ! hata mimi naomba iwe hivyo.Patricia anateseka sana.” “ usijali suala hili litakwisha tu”akasema Elvis ingawa ilionekana wazi kwamba alikuwa akiumia sana moyoni.Doreen akasema Elvis nafahamu unampenda sana patricia na kwa hilo siwezi kupingana nawe.Pamoja na hayo naomba uwe muwazi kwangu ni kweli hautaki kuwa na mtoto katika maisha yako?Hautaki kuitwa baba katika maisha yako? Hautaki kumpata mrithi wa mali zako? Please be honest with me” Elvis akaninama na kuonekana kuzama katika mawazo.Suala aliloulizwa na Doreen lilionekana kumchanganya sana “ Answer me Elvis” akasema Doreen baada ya ukimya kutawala mle chumbani.Elvis akainuka na kwenda dirishani akafunua pazia na kutazama nje halafu akageuka na kwenda kuchukua glasi yake na mvinyo akanywa kidogo. “ Doreen swali uliloniuliza ni gumu sana na sijui nikujibu nini” " Just be Honest with me” akasema Doreen.Elvis akafikiria tena kidogo na kusema “ Ukweli ni kwamba hakuna mwanandoa ambaye hapendi kuwa na mtoto.Kila mmoja angependa apate mtoto tena hata zaidi ya mmoja.Kuna nyakati huwa najitazama namna ninavyoishi na mke wangu na ninaona furaha yetu ingekuwa maradufu endapo tungepata mtoto.Kwa wazazi wangu mimi ni mtoto wao wa pekee na hawana mtoto mwingine.Kabla hajafariki baba yangu alituachia mali nyingi na mrithi pekee ni mimi.Ningependelea kuwa na mtoto ambaye angerithi mali hizi zote lakini uwezo huo haupo.Mke wangu wa ndoa hana uwezo wa kupata mtoto.Hili si suala dogo hata kidogo ni suala zito lakini ninamshukuru Mungu kwa kunipa nguvu na uwezo wa kulikabili suala hili.Toka awali nilikwisha jitayarisha kisaikolojia kwamba sintakuwa na mtoto ingawa kuna nyakati huwa ninatamani sana mtoto lakini uwezo huo haupo tena:” akasema Elvis .Doreen aliyekuwa kimya akimtazama akainua Glasi yake ya mvinyo akanywa na kusema “ Pole sana Elvis.Ahsante pia kwa kuwa muwazi kwangu.Najua ni suala gumu lakini bado unaweza kulipatia ufumbuzi” “Ufumbuzi gani Doreen? “Patricia anakupenda sana na amekwisha usoma moyo wako na akafahamu kabisa kwamba unatamani kuwa na mtoto na ndiyo maana akakupa ruhusa ya kutafuta mwanamke uzae naye mtoto.Huu si uamuzi mwepesi lakini ameweza kuufanya ili maisha yenu yaweze kuwa na nuru na furaha,” “ I cant do that Doreen,I swear I cant” akasema Elvis “ kama mkeo tayari amekwisha kuruhusu unashindwa nini? Kwa nini uendelee kumtesa mkeo? “ Siwezi kufanya hivyo kwa sasa nafahamu atateseka zaidi pale nitakapozaa nje ya ndoa.Niliapa mbele ya altare kwamba nitampenda Patricia katika shida na raha .Tuko katika wakati wa shida hivyo lazima niishi kiapo change cha kumpenda zaidi hasa wakati wa shida”akasema Elvis “ Patricia hawezi kuteseka kwani tayari amekwisha jiandaa kwa hilo na kizuri zaidi amekwambia kwamba atakutafutia mwanamke anayemuamini na akanichagua mimi.Hata hapo bado haiwezekani? “Doreen nimekwisha kwambia kwamba siwezi kufanya hivyo hata awe nani na hakuna atakayenishawishi nifanye hivyo” Doreen akamtazama kidogo na kuulzia “ Elvis be honest with me.Kinachokufanya ulipinge suala hili kwa nguvu zote ni kwa sababu ya upendo wako kwa Patricia au there is something else? “What ?! akauliza Elvis “ Ina maana hujanisikia? Nimekuuliza kwamba kinachokufanya ulipinge suala hili la kutafuta mtoto nje ya ndoa wakati mkeo amekwisha kupa ruhusa hiyo ni upendo wako kwa Patricia au kuna sababu nyingine? “ Kwa nini unaniuliza hivyo Doreen wakati jibu unalifahamu kwamba nilimpenda Patricia kwa namna alivyo na ndiyo maana siwezi kufanya kitendo kama hicho anachonitaka nifanye.Siwezi kufanya jambo lolote kinyume na kiapo cha kanisani” “ Elvis you are my friend .Please be honest with me” “Be honest with you? yes be honest with me .Is everything ok with you? “Doreen sikuelewi unamaanisha nini kuniuliza hivyo? “ Namaanisha kuhusu uwezo wako wa kumpa mimba mwanamke.Una hakika uko sawa? “ I am ok.Una wasi wasi naweza kuwa na kasoro ndiyo maana ninalipinga wazo la kuzaa nje ya ndoa? Ondoa shaka kuhusu hilo.Hata kama ingekuwa ni kweli basi ingebaki kuwa ni siri yangu na mke wangu lakini kukujibu swali lako ni kwamba mimi sina kasoro ni rijali kama wengine na uwezo wangu siutilii mashaka hata kidogo” akasema Elvis “ Mhhh ! I nina mashaka” akasema Doreen “ Kwa nini unakuwa na mashaka Doreen? Doreen akanywa kidogo kinywaji na kusema “ Nina wasi wasi kwa nini hutaki mtoto wakati mke wako amekwisha kupa ruhusa ya kutafuta mtoto nje ya ndoa. Kama ungekuwa huna kasoro usingekataa” “ Doreen mbona unasisitiza sana kwamba nina matatizo? Sina tatizo lolote .Mimi ni mzima kabisa” “ Can you prove that to me? “ Prove what ? akauliza Elvis “ That you are ok” “ kwa nini nidhihirishe kwako? Wewe hupaswi kufahamu masuala kama hayo na hata kama nikiwa na tatizo ni suala langu la ndani na hapaswi mtu mwingine kufahamu” “ Mhh ! I’m curious” akasema Doreen na kumsogelea Elvis “ Usiogope Elvis.Please come closer” Akasema Doreen “ Unataka kufanya nini Doreen? Akauliza Elvis lakini tayari Doreen alikwisha upeleka mkono wake kunako ikulu na muda ule ule ikulu kukachachamaa “ stop that Doreen.what are you dong?akasema Elvis kwa sauti ya juu.Doreen akatabasamu na kusema “ relax Elvis.Nilitaka tu kuhakikisha mambo yako sawa.Nimeamini uko sawa.” Elvis akamtazama Doreen usoni na kusema Doreen kwa nini unaf…………” kabla hajamalizia sentensi yake Doreen akasema “ Relax Elvis,relax.Hakuna tatizo kila kitu kiko ok” akasema Doreen. Bado Elvis aliendelea kumtazam Doreen usoni kwa macho makali.Hakuamini kama angeweza kufanya kitendo kama kile cha kumshika maeneo nyeti “ Ok Elvis,let us get back to our serious business” akasema Doreen “ Subiri kwanza.Doreen kwa nini umefanya kitendo kile? Akauliza Elvis.Doreen akainua glasi yake akanywa na kusema “ Ok Elvis ,unataka kufahamu ni kwa nini nimefanya vile? Huu hapa ni ukweli.Ukotayati kuufahamu? Akauliza “ Ndiyo.Niambie kwa nini umefanya kitendo kile ? “ Ukweli ni kwamba nilihitaji kuwa na uhakika kama kila kitu kiko vizuri na hauna kasoro yoyote.Ninahitaji ukubali kuzaa na mimi mtoto kwa ajili ya Patricia.Anateseka sana kwa jambo hili.Sielewi ni kwa nini unakuwa mgumu sana kukubaliana na mke wako kuhusu suala hili.Mimi nimekwishakubali kumsaidia Patricia na niko tayari muda wowote kuzaa na wewe lakini kwako limekuwa ni suala gumu .Kwa nini Elvis? Akauliza Doreen Elvis akavuta pumzi ndefu na kusema “ How much she paid you? Elvis namba usinielewe vibaya .Nilikubali kwa moyo mweupe kumsaidia Patricia na wewe pia kumpata mtoto na si kwa sababu ya pesa.I have my own money,I have millions of money na sina shida ya pesa.Nimejitolea tu kumsadia rafiki yangu anayeteseka sana na wala usione ninakulazimisha ukadhani labda nina mapungufu ama ninataka kuwa mke wako wa pili la hasha .Sina lengo hilo bali nia yangu ni kuwasaidia ninyi ,wewe na mkeo kupata mtoto ili ndoa yenu iwe na furaha.Mkeo yuko tayari kwa jambo hilo wewe ndiye unayekwamisha“ akasema Doreen.Chumba kikawa kimya kabisa.Kila mmoja alikuwa akiwaza lake.Elvis akasema I don’t know what to say Doreenm,wewe na Patricia mmeniweka katika wakati mgumu sana”akasema Elvis “ You don’t have to say anything Elvis.Unachotakiwa kufanya ni maamuzi tu.Ingia katika moyo wa Patricia na uangalie ni namna gani anateseka kwa kukosa mtoto.Kwa taarifa yako hakuna kitu kinachomtesa mwanamke kama kukosa mtoto.Think carefully about this” akasema Doreen “ I don’t know Doreen.I real don’t know what t do right now.I’m so confused” akasema Elvis.Doreen akamshika bega na kusema “ Elvis suala ni gumu na linahitaji maamuzi magumu so think like a man and make decision like a man.I’m not forcing you to do it but promise me that you’ll think about this” akasema Doreen Elvis akaniama akafikiri kidogo na kusema “ Ok Doreen.I’ll think about that” akasema Elvis “ Ahsante sana Elvis.Sasa naomba ukapumzike kwani kesho tuna safari ndefu ya kurejea Dar ” akasema Doreen .Elvis akainuka “ Ahsante sana Doreen .Ngoja nikapumzike.Nitakuamsha kesho alfajiri na mapema kwa ajili ya safari” akasema Elvis huku akianza kupiga hatua kuelekea mlangoni.Akaufungua mlango na kabla hajatoka Doreen akamuita “ Elvis !! .Elvis akageuka Sweet dreams” akasema Doreen “ Goodnight Doreen’ akasema Elvis na kuufunga mlango.Taratibu akatembea kueleka katka chumba chake akaingia na kujtupa kitandani “Najua Patricia anaumia sana na suala hili lakini sina namna ya kufanya.Siwezi kuzaa nje ya ndoa hata kama yeye ameridhia nifanye hivyo.Sijui ni kitu gani kimemuingia Patrcia na kumfanya awaze mambo haya na kunitaka nizae na rafiki yake Doreen.Lakini ngoja kwanza niliweke pembeni suala hili nishughulike na suala zito lililoko mbele yangu la Graca.Nitakaa na patricia na kuongea naye kwa kina kuhusiana na suala hili na nitamuelewesha athari zake.Hata mimi sipendi kumuona akiumia lakini huu ni msalaba wetu lazima tuubebe wote” akawaza Elvis na kulala





Saa kumi za alfajri tayari Elvis alikwisha amka na kuanza kujiandaa kwa safari .Akaenda kumgongea mlango Doreen akamuamsha ili ajiandae kwa safari halafu akamfuata Graca akamjulia hali na kumtaka ajiandae kwani saa kumi na moja juu ya alama wangenza safari ya kurejea Dar.Elvis akarejea chumbani kwake na kukaa kitandani.Bado kichwa chake kiliendelea kusongwa na mawazo kutokana na maongezi ya jana na Doreen “ Sitakiwi kuliwaza sana suala hili linaweza kunipotezea mwelekeo mzima wa shughuli yangu ya sasa” akawaza halafu akaitazama saa ya kutani iliyoonyesha ilipata saa kumi na moja kasoro dakika kumi.Akafunga mlango na kuelekea chumbani kwa Doreen “ Tangulia garini ngoja nikamchukue Graca” akasema Elvis halafu akaelekea chumbani kwa Graca akagonga na kuingia ndani.Graca alikuwa amekaa kitandani tayari alikwisha jiandaa “ Pole na baridi ya Mbeya” “ Dah ! Kuna baridi kali sana” akasema Graca na wote wakacheka “ Graca its time to leave” Graca akainuka na kuinua kibegi chake kidogo halafu akamtazama Elvis “ Anything wrong Graca? Akauliza Elvis baada ya kumuona Graca akimuangalia usoni kwa wasiwasi “ Your friend Doreen.Do you trust her? “ with my life” Elvis akajibu “ Good” akajibu Graca halafu wakatoka wakaelekea katika gari la Doreen,Elvis akashika usukani na safari ya kuelekea Dar es salaam ikaanza **************** Ni saa tano za asubuhi katika jiji la Dare s salaam.Kijua ni kikali kama kawaida ya jiji hili.Katika kasri la aliyewahi kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu Daudi sichoma ,gari zaidi ya nane zimeegeshwa katika eneo la maegesho.Utulivu ulikuwa mkubwa sana kulizunguja kasri hili na kama ilivyo kawaida ulinzi pia ulikuwa wa kutosha Ndani ya kasri hili kulikuwa na ukumbi wa mikutano ambamo Daudi Sichoma alikuwa na mkutano na wakuu wa vyama vya siasa vya upinzani kwanza alianza kwa kuwashukuru wote kwa kufika kwao halafu akaeleka katika mada. “ Ndugu zangu nimewaiteni hapa ili http://deusdeditmahunda.blogspot.com/tujadili jambo muhimu sana kwa mustakabali mzima wa nchi yetu na kwa uhai wa vyama vyenu vya upinzani.Nadhani nyote mtakubaliana name kwamba kwa siku za hivi karibuni vyama vya upinzani vimepoteza sana nguvu na taswira yake katika jamii.Chama tawala kimezidi kujiimarisha na kuwa na nguvu sana.Msichangae kwa nini ninajadili nanyi mambo kama haya wakati mimi ni mwanachama wa chama tawala.Naomba niweke wazi kwenu kwama mahusiano yangu na chama changu si mazuri hata kidogo hivi sasa.Nina wapinzani wengi ndani ya chama ambao wanajitahidi usiku na mchana ili wanimalize kisiasa.Mikakati mingi inapangwa juu yangu ili kuweza kunididimiza kisiasa na wamefanikiwa kuniweka nje ya ulingo wa siasa.Nimewavumilia sana na nimefika mwisho.Sintavumilia zaidi .Inanilazimu na mimi nipambane nao na ndiyo maana nimewaiteni hapa leo hii ili kuwapeni mikakati na uwezo wa kukidhoofisha chama tawala.” Akasema David na kukaa kimya akawaangalia wanasiasa wale halafu akaendelea “ Rais wa Marekani amemaliza ziara yake ndefu kuwahi kutokea hapa nchini.Ni ziara ya kihistora na yenye mafanikio kwa serikali zote mbili.Katika ziara hiyo mambo mengi yamefanyika kama vile uzinduzi wa miradi kadhaa mikubwa ya maendelo .Pamoja na yote makubwa yaliyofanyika yenye maslahi makubwa kwa taifa letu kuna mambo makubwa mawili yaliyomleta rais huyu mkubwa wa Marekani” Daudi akanyamaza akanywa maji kidogo nakuendelea “ kwanza kabisa amekuja kutafuta sehemu ambayo jeshi la marekani litajenga kambi yake kubwa kuwahi kuwekwa barani afrika.lengo ni kuendeleza mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi ambavyo vimeonekana kushamiri kila uchao katika eneo hili la afrika mashariki kati na kusini.tayari serikali ya Tanzania imewaahidi kuwapatia eneo hilo ili wejenge kambi kubwa ya kijeshi” Wanasiasa wale wakatazamana usoni.Hawakuwa wakifahamu kuhusu suala hili hivyo lilionekana kuwastua kidogo.Daudi akaendelea “ jambo la pili na kubwa zaidi ni kwamba hivi karibuni Tanzania imegundua kiasi kikubwa cha mafuta kiasi ambacho kinasemekana kinaweza kulingana au kuzidi kiasi chote cha mafuta ya mashariki ya kati.Ugunduzi huo umeifanya Tanzania kutolewa macho na mataifa makubwa na ndiyo maana nimeona katika kipindi hiki toka ilipogundua mafuta kumekuwa na ziara zisizokauka za viongozi mbali mbali wa mataifa makubwa akitembelea nchi yetu.Kutokana na migogoro mingi kulikumbia eneo la mashariki ya kati , bei ya mafuta imepanda mara dufu katika soko la dunia.Kutokana na migogoro hiyo mataifa makubwa yameanza kupunguza utegemezi wa mafuta ya kutoka mashariki ya kati Ugunduzi wa mafuta Tanzania umeleta matumaini mapya kwa mataifa haya makubwa yenye uchumi mkubwa sana .Jambo lililomleta rais wa marekani hapa nchini ni kuitaka serikali ya Tanzania iruhusu serikali ya marekani kuwekeza katika sekta ya mafuta ya gesi na mafuta nchini Tanzania na tayari mikataba imekwisha sainiwa na kwa maana hiyo sekta nzima ya mafuta na gesi imeshikiliwa na wamarekani.Makampuni yetu hayana tena nafasi katika uwekezaji huo mkubwa” akasema David na wakuu wale wa vyama vya siasa wakabaki wanatazamana na minong’ono ikaanza kusikika mle ndani.Wanasiasa wale walionekana kustushwa sana na taarifa ile.David akafurahi moyon kwani plani yake ilianza kufanya kazi.Akakohoa kidogo na kuendelea “ Ndugu zangu nimewaiteni hapa kwa makusudi kabisa kuwaeleza haya yote kwani ni nyie pekee wenye nguvu za kuyazuia yasifanyike.Mtajiuliza mtawezaje kuzuia mambo haya yasifanyike? Ni kweli ni suala gumu kwa sababu tayari serikali imekwisha tiliana mikataba na serikali ya marekani na hakuna namna mtakayoweza kuitengua mikataba hiyo lakini njia pekee hapa ni kutumia umma kuishinikiza serikali .Katika hilo kuna mambo ambayo yanatakiwa yafanyike” akanyamaza kidogo akanywa maji na kuendelea “ kwanza ni kuanzisha kampeni kubwa sana nchi nzima itakayojulikana kama mafuta yetu.Hii itakuwa ni kampeni kubwa ambayo haijawahi kutokea hapa nchini.Itakuwa ni kampeni ya mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya,kata kwa kata,kijiji kwa kijiji,nyumba kwa nyumba na hatimaye mtu kwa mtu.katika kampeni hii wananchi wataelezwa kwa kina serikali ilichokifanya .Nawafahamu ninyi ni mahodari wa kujenga hoja.Nataka mjenge hoja ambazo zitaamsha hasira kwa umma dhidi ya serikali kupinga serikali itengue mikataba yote iliyotiliana sahihi na serikali ya Marekani .kampeni hii itaambatana na maandamano makubwa yasiyo na ukomo .makundi makubwa ya vijana yatachochewa kuandamana na kuweka makambi katika viwanja vya wazi.Maandamano hayo yataambatana na vurugu kama kuchoma matairi,kupiga mawe magari ya serikali kuchoma ofisi na hivyo kuilazimisha serikali kutumia nguvu nyingi katika kuwatawanya makundi ya vijana na katika mapambano hayo jeshi la polisi litalazimika kutumia nguvu kubwa kuwatawanya waandamanaji na hivyo baadhi ya raia watapoteza maisha na hivyo itakuwa ni faida kwetu kwani suala hili litaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa na hapo ndipo jumuia ya kimataifa itakapoingilia katika suala hilo na kuishinikiza serikali ya Tanzania iachane na mipango yake serikali italaumiwa kwa kukiuka haki za binadamu na kwa kiasi kikubwa wananchi hawatakuwa na imani na serikali yao tena na endapo utafanyika uchaguzi ninyi mtakuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda uchaguzi mkuu.Nadhani huu ni mpango mzuri sana.Nyie mnauonaje mpango huu? Akauliza Daudi.wanasiasa wale wakatazamana na nyuso zao zikaonyesha tabasamu.walionekana kuufurahia mpango ule.kwa dakika kama nne hivi walikuwa wakisemezana wao kwa wao “ ndugu zangu nadhani itakuwa vyema kama nikaawacha kwa muda ili mlijadili suala hili kwa muda namna mnavyoweza kulitekeleza.Nitarejea baada ya muda mfupi” akasema Daudi na kutoka nje akawaacha wanasiasa wale wakijadiliana . Akiwa nje ya ukumbi Daud akachukua simu yake kazitafuta namba za simu za Frank akampigia “ hallow David “ akasema Frank “ halow Frank habari yako? Habari za toka jana? “habari nzuri daud.mambo yanakwendaje? “mambo yanakwenda vizuri na nimekupigia kukutaarifu kwamba tayari nimekwisha ianza kazi.Hivi niongeapo tayari niko na wakuu wa vyama vya siasa.Nimeanza nao na hivi sasa nimetoka nje nimewaacha wakijadiliana” “thats great news David.Nilijua tu mpango huu bila ya wewe katu hatuwezi kufanikiwa .Umeonaje mwelekeo wa hao wanasiasa? “ Bila shaka watakubaliana nami.Baada ya muda mfupi nitarejea tena ndani ili kufahamu wameamua nini” akasema David “ Ok David .kazi nzuri sana.Natumai kwa kupitia wewe mpango wetu utafanikiwa “ Ahsante kwa kuniamni na kunishirikisha.Jioni ya leo nitakuwa na kikao na makamu wa rais.Nimekwisha ongea naye na kupanga kukutana naye jioni ya leo.Nina hakika hata naye atakubaliana na mpango huu.Nitakupigia tena simu baada ya kumaliza kikao na hawa wanasiasa” akasema Daudi na kukata simu Mara tu baada ya kumaliza kuongea naFrank simuni David akarejea tena katika chumba cha mikutano alikowaacha wanasiasa wakijadiliana. “ ndugu zangu nadhani mpaka sasa kuna jambo mtakuwa mmekwisha lijadili “ akasema David baada ya kuketi kitini “ Tumejadiliana na tumekubaliana na mawazo yako.Hiyo ndiyo kazi ya vyama vya upinzani,kuidhoofisha serikali iliyoko madarakani.Tuko tayari kwa ajili ya operesheni hiyo” akasema ndugu Makwa Tusangira mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani Tanzania kwa niaba ya wenzake “ pamoja na kukubaliana kuifanya operesheni hii lakini kuna changamoto ya kifedha.Kama ujuavyo vyama vyetu vingi havina vyanzo vya mapato zaidi ya kutegemea ruzuku ya serikali kwa maana hiyo basi uendeshaji wa vyama unakuwa mgumu sana achilia mbali operesheni kubwa kama hii.Pili changamoto nyingine ni ya kiusalama.Nina hakika kwamba mara tu vuguvugu hili litakaposhika kasi na kusambaa mkoani ,serikali lazima itawatafuta waasisi wa vurugu hizo kwa hiyo lazima tutatiwa nguvuni.Hizo ni changamoto kubwa ambazo endapo tutazitafutia ufumbuzi basi operesheni hii itakuwa na mafanikio makubwa” akasema Makwa.David akatabasamu na kusema “ kwanza kabisa niruhusuni niwashukuru kwa kukubali kwenu kuifanya operesheni hii muhimu kwa taifa letu.Changamoto hizo ulizozisema ni changamoto ambazo lazima tuzitafutie ufumbuzi wa haraka.Kuhusu suala la fedha nawaomba msiwe na wasi wasi ninataka mkae na mtengeneze bajeti ya kutosha kufanikisha zoezi hili na mniletee.Pesa ipo ya kutosha msihofu.Nileteeni vile vile mchanganuo namna operesheni itakavyofanyika nchi nzima.Kuhusu suala la usalama kwamba mnaweza kutafutwa na kuwekwa kizuizini msiwe na shaka na hilo pia.Baada tu ya kuuwasha moto na ukasambaa nchi nzima nyie mtaondoka kwa siri nchini na mtapewa hifadhi nchi za nje na operesheni itaendelea kuongozwa na vongozi wa chini.Hakuna atakayegundua kwamaba mmeondoka nchini na mtaendeleza hareakati mkiwa nje ya nchi.jambo lingine ambalo nilisahau kuwaambieni ni kwamba sambamba na harakati hizo ,tutavishawishi pia vyama vya wafanyakazi kuendesha mgomo wa wafanyakazi wa nchi nzima wa umma na wa binafsi kushinikiza serikali iliyopo madarakani kuachia ngazi na hiyo itakuwa ni fursa kwenu kuingia madarakanibaada ya uchaguzi kufanyika kwani tayari mtakuwa juu kisiasa ” akasema Daud Kikao kile kati yake na wakuu wa vyama vya siasa kiliendelea hadi ilipotimu saa kumi na moja za jioni ndipo kilipomalizika.wakuu wale wa vyama vya siasa wote nyuso zao zilikuwa zimetawaliwa na tabasamu zito nahasa baada ya kila mmoja kukabidhiwa bahasha iliyotuna ambayo ndani yake kulikuwa naiasikikubwa cha pesa. Walipeana mikono kupongezana kwa kikao kile chenye manufaa makubwa kwao na kisha wakaagana kwa miadi ya kuonana naye tena baada ya siku nne watakapokuwa tayari wamekaa kikao na kutengeneza bajeti ya operesheni nzima ********************* Saa mbili za usiku Elvis,Doreen na Graca wakawasili jijini Dar e s salaam wakitokea Mbeya.Ilikuwa ni safari ndefu .Elvis ndiye aliyekuwa dereva siku hii akimsaidia Doreen Welcome home Graca” akasema Elvis .Graca akatabasamu.uso wake ukaonyesha furaha ya kurejea tena ndani ya jiji hili halafu akanyong’onyea baada ya kukumbuka mambo yaliyomkuta na kubwa zaidi lililomuogopesha ni kuhusu usalama wake Hatimaye wakawasili nyumbani kwa Doreen.Graca aliyeonekama kuchoka sana alipelekwa chumbani kupumzika halafu Doreen akarejea sebuleni alikomuacha Elvis “ Doreen ahsante sana kwa msaada wako Bila wewe nina hakika kazi yangu ya kumsafirisha Graca ingekuwa ngumu sana” akasema Elvis Doreen akatasamu na kusema “ Hupaswi kunishukuru Elvis.Nimefanya kile ninachopaswa kukifanya na nimefurahi kuwa sehemu ya msaada kwako.” “ Ahsante sana Doreen.Mungu akubariki sana” akajibu elvis na wote wakakaa kimya “ Elvis unakwenda kulala nyumbani kwako usiku huu? Akauliza Doreen.Alvis akanima akafikiri kidogo na kusema “ Natamani kama ningekwenda nyumbani nikaonane na mke wangu Patricia lakini siwezi kufanya hivyo.Natakiwa kumlinda Graca kwa kila namna niwezavyo.Endapo watu wanaomtafuta watagundua kwamba Graca yuko hapa hawatapoteza hata dakika moja watafika na kuwadhuru wote watakaowakuta.Sitaki hilo litokee kwa hiyo nitalala hapa kuwalinda wewe na Graca.Kuhusu sehemu ya kulala usipate shida kabisanitalala hapa hapa sofani.Nimekwisha zoea kukesha macho” akasema Elvis “ Elvis tafadhali usinielewe vibaya kukuuliza vile.Nashukuru kwa kuamua kulala hapa usiku wa leo na kutulinda.Hapa ni nyumbani kwako na siku zote unamuda wowote.Nyumba yangu ni kubwa na ina vyumba vya kutosha vya kulala na endapo ukipenda unaweza hata kulala chumbani kwangu” akasema Doreen na wote wakaangua kicheko “ Usijali Doreen hapa sebuleni panatosha sana” akasema Elvis “ Elvis tutaongea baadae kwa sasa ngoja nikawaandalie chakula cha usiku .Wakati naanda chakula naomba nikupeleka chumbani kwangu ukaoge na upumzike kidogo kuondoa uchovu wa safari” akasema DoreenUhhmmm Doreen kuna jambo nataja kukuomba.Ninaomba umpigie simu Patricia na kumjulia hali ila usimweleze chochote kuhusiana na mimi kuwapo hapa kwako wala safari ya Mbeya.”akasema Elvis “ Sawa Elvis,nitampigia .Twende chumbani ukaoge” akasema Doreen na kumuongoza Elvis hadi chumbani kwake.Kilikuwa ni chumba kikubwa na kizuri “ Chumba chako kizuri sana Doreen.Hongera sana” “ Ahsante Elvis lakini hakiwezi kuzidi kile cha Patricia.” Akasema Doreen na kumfungulia Elvis mlango wa bafu akamuacha akioga na yeye akaelekea jikoni kuandaa chakula cha usiku Baada ya kumaliza kuoga Elvis akarejea sebuleni.Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi na mara akainga Doreen na kumkuta Elvis pale sebuleni “ Elvis ,mbona umetoka chumbani ? unaogopa nini?Unatakiwa upumzike safari ilikuwa ndefu sana”akasema Doreen.Elvis akatabasamu “ Usijali Doreen,hata hapa panatosha sana kupumzika.Vipi umempigia simu Patricia? “Ndiyo nimempigia na anaendelea vizuri na hana tatizo lolote” “ Ahsante sana” akajibu Elvis .Doreen akaendelea kumtazama usoni “ Mbona unanitazama hivyo Doreen? Akauliza Elvis “ uhhmm !! its nothing.Ngoja na mimi nikaoge halafu tutajumuika sote mezani kwa chakula cha usiku”akasemaDoreen nakuelekea chumbani kwake kuoga.Kisha oga wote watatu wakajumuika katika chakula cha usiku na baada ya kumaliza kula wakaelekea sebuleni “ Graca pole sana na safari ndefu “ akaanzisha maongezi “ Ahsante sana Elvis.Pole sana nawe Kuendesha gari umbali ule mrefu si kazi ndogo” “Ahsante ila mimi nimekwisha zoea safari kama hizi” akajibu Elvis “ This is your house? Akauliza Graca “ hapana Graca hapa si nyumbani kwangu.Hapa ni nyumbani kwa Doreen’ “ wewe na Doreen ni wapenzi?akauliza graca “ hapana ,sisi si wapenzi bali ni marafiki wakubwa.Mimi tayari nina mke wangu anaitwa Patricia”akasema Elvis Graca akamtazama Elvis usoni na kusema “kwa hiyo utaniacha hapa na kwenda nyumbani kwako?Are you sure I’m safe here? Elvis akatasabamu kama kawaida yakena kusema “Usihofu Graca Sintaondoka na kukuacha hapa peke yako.Nilikuhakikishia usalama wako kwa hiyo nitaendelea kukulinda.Kuhusu usalama hapa ni sehemu salama sana lakini kesho tutahamia katika sehemu salama zaidi ya hii .Kuna nyumba ambayo nimeinunua maalum kwa ajili yako na ndipo utakapoishi hadi hapo tutakapofanya mpango mwingine kuhusiana na maisha yako kwa hiyo usihofu kitu chochote” Tabasamu kubwa likajengeka usoni mwa binti yule mrembo kwa maneno yaleya Elvis “Ahsante sana Elvis kwa msaada wako mkubwa.katika misha yangu sijawahi kukutana na mtu mwenye moyo wa huruma kama wewe” “ Usijali Graca,ni jukumu langu kukusaidia” akajibu Elvis halafu kukawa kimya “ mkeo anajua kwamba uko hapa?akauliza Graca “ hapana hafahamu” “ kwa nini hujamwambia .Dont you trust her? “ I do trust her with my life lakini kwa sasa siwezi kumweleza chochote kuhusiana na suala lako.Nitamfahamisha muda ukifika”akasema Elvis “ Ok Elvis nadhani kesho tutakuwa na muda mzuri zaidi wa kuongea.Kwa sasa nimechoka sana naomba nikapumzike”akasema Graca akainuka na kuelekea chumbani kupumzika.Baada ya dakika tano Doreen akaingia sebuleni “ Elvis tayari nimekwisha kuandalia chumba cha kulala ukapumzike.Safari ilikuwa ndefu sana “akasema Doreen “Ahsante Doreen lakini nitakaa hapa hapa sebuleni kuhakikisha usalama wenu usihofu kuhusu mimi.Hizi ni kazi zangu na nimekwisha zizoea.tafadhali nenda kalale upumzike” “hapana Elvis huwezi kukaa hapa sebuleni peke yako usiku kucha.Usalama hapa ni mkubwa tu.Nyumba zote za hapa jirani tumeweka walinzi kwa hiyo usalama kuzunguka eneo hili ni mkubwa”akasema Doreen “ Doreen tafadhali usihofu.I’ll be fine.Nenda kapumzike.Kesho tutakuwa na siku ndefu kidogo.Vipi kuhusu kazini kwako? Hakuna tatizo ?akauliza Elvisa hakuna tatizo lolote kazini.Nimekwisha omba ruhusa ya siku kumi”akasema Doreen “ ahsante sana,Sasa nenda kapumzike”akasema Elvis huku akiufungua mlango na kutoka nje akaikagua nyumba yote kuhakikisha iko salama halafu akarejea sebuleni akazima kila kitu kukawa na ukimya . ****************** Kumepambazuka na siku mpya imeanza.Saa kumi na mbili za asubuhi ilimkuta Elvis akiwa macho.Usiku mzima hakuweza kufumba macho akihakikisha Graca na Doreen wanakuwa salama. “habari yako Elvis” Doreen akamsalimu Elvis . “ Ouh Doreen umeamkaje? Akauliza Elvis huku akijinyoosha kwa uchovu “ Pole sana kwa uchovu wa usiku Elvis” “usijali Doreen umeamka salama lakini? “ Niko salama kabisa Elvis” “Nafurahi kusikia hivyo” “ Elvis nadhani ungeenda chumbani upumzike walau kidogo.usiku mzima umekesha hapa ukitulinda” “ Ahsante sana Doreen lakini huu si wakati muafaka wa kupumzika.Dakika moja tu inatosha sana kwa watu wanaomtafuta Graca kuingia na kumfanyia chochote.I cant let that happen”akasemaElvis .Doreen akamtazama kisha akasema “basi twende ukaoge tujiandae na siku ya leo”akasema Doreen akamuongoza Elvis hadi chumbani kwake.wakati Elvis akiendelea kuoga Doreen akaenda kumuamsha Graca Saa mbili za asubuhi wote watatu wakajumuika mezani wakapata kifungua kinywa . “Graca ,tukitoka hapa tunaelekea katika nyumba ambayo utakuwa ukishi hadi hapo tutakapokufanyia utaratibu mwingine wa kwenda nje ya nchi .Uwepo wako hapa nchini unatakiwa uwe ni wa siri kubwa”akasema Elvis wakiwa mezani wakiendea kupata kifungua kinywa “ Ahsante sana Elvis.Lakini nina swali nataka kuuliza” “Uliza usihofu Graca” “katika nyumba hiyo unayonipeleka nitaishi na nani? Nitaishi peke yangu? Elvis na Doreen wakatasamana,halafu Elvis akasema “ hapana hautakuwa peke yako,nitakuwa pamoja nawe.” “Vipi kuhusu mkeo na watoto?akauliza Graca “ Usijali kuhusu hilo,hakutakuwa na tatizo lolote.” Akajibu Elvis Waliendelea kupata kifungua kinywa na walipomaliza wakaingai katika gari la Doreen wakaondoka.Breki ya kwanza ilikuwa katika ofisi za kampuni ya ulinzi ambako Amanda rafikiye Doreen aliacha funguo za nyumba aliyomuuzia Elvis.Doreen akajitambulisha na akakabidhiwa funguo kwani taarifa zake tayari zilikuwepo pale ofisini.Kishapata funguo safari ikaendelea kuelekea katika jumba lile “ wale jamaa wameniuliza kama tutapenda kuingia mkataba wa kuilinda nyumba ile kwani mkataba wao na Amanda umekwisha sitishwa.Sijawapa jibu nimewaambia wasubiri kwanza tujadiliane” “ Good.hakuna haja ya kuwa na ulinzi.Graca nitamlinda mwenyewe” akasema elvis. Hatimaye wakawasili katika jumba lile kubwa na la kupendeza.Jumba lile lilikuwa limezungukwa na ukuta mkubwa wenye rangi yeupe na juu ya ukuta kulikuwa na nyaya kwa ajili ya usalama. “wow ! what a wonderfull place!! ELvis akasema kwa furaha baada ya kuingia ndani ya jumba lile na kuishuhudia mandhari nzuri ya kupendeza.Katika nyumba ile kulikuwa na vyumba vinne vya kulala,sebule ,chumba cha maongezi,maktaba,sehemu ya kufulia,jiko,gereji ya gari na chumba maalum kwa ajili ya ibada.Elvis alifurahi mno kuipata nyumba kama ile.Ingemfaa sana katika kazi zake “Ahsante sana Doreen.Nyumba hii ni nzuri sana na inafaa.Ina kila kitu ninachokihitaji”akasema Elvis. “There is one more thing’ akasema Doree “ whats that? Akauliza Elvis “ Kuna chumba cha chini kwa chini kwa ajili ya usalama.Endapo usalama ukiwa tete basi unangia katika chumba cha chini” Elvis akashindwa kujizuia furaha yake na kujikuta amemkubatia Doreen halafu wakaelekea katika chumba kikubwa cha kulala .katika ukuta wa kile chumba kulikuwa na kifaa Fulani mithili ya mita ya umeme .Doreen akabonyeza namba kadhaa na mara sehemu ya sakafu ikafuguka .Wote wakabaki na mshangao mkubwa.Kulikuwa na ngazi za kushuka chini.Taratibu wakaifuata ngazi ile na kukutana na varanda ambalo mbele yake kulikuwa na mlango ambao nao ulifunguliwa kwa namba ,wakaingia katika chumba kikubwa na kizuri chenye kila kitu “ I lovethis place” akasema Graca “ Doreen unastahli pongezi kubwa .nyumba hii ni sahihi kabisa kwa mimi kuishi.” Akasema Elvis halafu wakarejea sebuleni “ sasa Doreen kuna mambo ambayo nataka uyafanye kwa siku ya leo” “ usijali elvis .I’m at your service” akasema Doreen huku akitabasamu “ Nataka upite madukani umfanyie Graca manunuzi .Mnunulie nguo nzuri ,viatu vipozodi na kila utakachoona kinamfaa.Baada ya hapo ufanye pia manunuzi ya chakula na vinywaji vya kututosha kwa wiki mbili au zaidi.”akasemaElvis akachukua kompyta ya Doreen na kufungua akaunti yake akapunguza shilingi milioni tatu na kuzituma katika akaunti ya Doreen “ Elvis basi ngoja niwahi nikaanze kufanya manunuzi hayo.Nina hakika sintakawia sana.Una mpango wa kutoka baadae? Elvis akafikiri kidogo na kusema “ Kama ikinilazimu kutoka nitatumia gari la Amanda” “ sawa .Amanda aliniambia kwamba gari lake ni zima na halina tatizo lolote”akasema Doreen akachukua vipimo vya Graca na kutoka mle sebuleni.Elvis akamsindikiza hadi garini “ Elvis are you sure you want to live here? Akauliza Doreen “ Itanilazmu kufanya hivyo kwa kipindi hiki ambacho Graca atakuwa hapa.Dhamana yote ya usalama wake nimeibeba mimi kwa hiyo natakiwa nimlinde kwa kila namna kwani ndivyo nilivyomuahidi” “ Vipi kuhusu Patricia? atakuelewa? “ najua itakuwa ngumu kwake kunielewa lakini sina namna nyingine ya kufanya.Graca anazo taarifa nyeti sana kwa hiyo anatakiwa alindwe” akasema Elvis.Doreen akamtazama usoni na kusema “ Una hakika taarifa hizo zina umuhimu mkubwa kiasi cha kukufanya ujitoe namna hii? “ Doreen naomba usinielewe vibaya lakini taarifa alizonazo Graca ni za muhimu sana kwangu na nchi kwa jumla” “Ok Elvis.Tutaonana baadae” akasema Doreen na kuingia garini akaondoka .Elvis akarejea sebuleni alikomuacha Graca “ Nyumba hii ni nzuri sana .nani alikuwa akiishi hapa? Akauliza Graca “Kuna mzungu mmoja ndiye aliyekuwa akiishi hapa na sasa amerejea kwako” “ Ni nyumba nzuri sana.Nimeipenda” akasema Graca “ hii ndiyo sehemu salama ambayo nilikuahidi kwamba utaishi.Hakuna mtu yeyote atakayejua kama uko hapa.Pamoja na usalama uliopo lakini nitafunga pia kamera za ulinzi kila kona ili kuzidisha ulinzi zaidi.” “ Ahsante sana Elvis kwa namna ulivyojitahidi kunisaidia Sijui nitakulipa kitu gani”akasemaGraca “ Usiwaze sana kuhusu kulipa.Nimefanya kile ambacho ninapaswa kukifanya.”akasema Elvis.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Elvis akasema “ Graca nimetimiza ahadi yangu.Nilikuahidi kukutoa pale hospitali afrika kusini na kukupeleka sehemu salama.You are safe now.Now it’s your turn to tell me everything you know about your father ”akasema Elvis Graca akainama akazama mawazoni halafu akainua kichwa na kusema “ Katika familia yetu tulizaliwa watoto wawili tu mimi na kaka yangu Edwin.Wakati bado ninasoma Edwin akajiunga na jeshi na kwa bahati mbaya alifariki katika maozezi ya kijeshi wakati wakipanda mlimaKilimanjaro kwa kuangukiwa na mawe yaliyokuwa yakiporomoka na kuwaponda yeye na wenzake wawili ambao wote walipoteza maisha.Nilibaki mimi peke yangu.Maisha yetu yalikuwa mazuri na hatukuwa na tatizo lolote.Kila nilichokitaka nilikipata” Akanyamaza akameza mate na kuendelea “ Siku moja ulitokea ugomvi kati ya baba na mama.Sikujua chanzo cha ugomvi huo lakini nilisikia mama akimlalamikia baba kwamba aachane na mambo yake anayoyafanya.Sikujua ni mambo gani hayo ambayo mama alimtaka baba kuachana nayo.Nilidhani labda ni mambo yao ya wanandoa,yawezekana labda baba akawa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.Sikuwahi kumuuliza mama sababu ya ugomvi wao.Maisha yaliendela kama kawaida lakini mama alionekana kubadilika sana.Hakuwa katika hali yake ya kawaida niliyomzoea.Niligundua kuna jambo lililokuwa linamsumbua.Nilijaribu sana kumdadisi aniambie ni kitu gani kilichokuwa kinamsumbua lakini hakunieleza chochote.Siku moja baba aliwahi kuondokana kusahau funguo za chumba chake ambacho huingia yeye pekee.Chumba hicho amehifadhi vitu vyake muhimu zikiwemo nyaraka zake nyingi.Mama aliingia katika kile chumba na kuanza kupekua,akatoka na mkoba uliokuwa na kompyuta ndogo ndani yake.Akanipatia mkoba ule na kunitaka niufiche mahala ambako hakuna yeyote anayeweza kuuona.Alinisisitiza sana kwamba nisimuonyeshe mtu yeyote .Niliuchukua mkoba ule na kwenda kuuhifadhi kwa rafiki yangu Salha.Kumbe katika kile chumba cha baba kulikuwa na kamera ndogo ambayo iliweza kuchukua picha za kila anayeingia mle chumbani wakati baba akiwa hayupo na kumtumia baba moja kwa moja katika simu yake kwa hiyo baba aliweza kugundua kwamba mama aliingia mle katika ofisi yake na akachukua kompyuta yake ndogo.” Akasema Graca halafu akanyamaza kidogo na kuendelea Jioni ya siku ile kulitokea tena ugomvi mkubwa sana baba akitaka mama arudishe kompyuta yake ndogo aliyoichukua toka ofisini kwake.Mama alikataa kata kata kwamba hakuchukua kompyuta ile lakini baba akamuonyesha picha zilizochukuliwa na kamera lakini bado mama alikataa kwamba hakuchukua ile kompyuta.Nilitamani nimwambie baba kwamba kompyuta yake ninayo mimi ili kuumaliza ule ugomvi lakini nikaogopa kwa namna alivyokuwa amekasirika.Nilikumbuka pia kwamba mama aliniambia kwa namna yoyote ile nisithubutu kumpa mtu yeyote kompyuta ile hadi hapo atakaponipa maelekezo yake” Graca akanyamaza kidogo halafu akaendelea “ wakiwa chumbani nilimsikia mama akimtaka baba aachane na biashara haramu alizokuwa akifanya.Moja kwa moja akili yangu ikanituma kwamba huenda baba akawa anajishughulisha na biashara ya madawa za kulevya na ndiyo maana akawa na utajiri mkubwa tofauti na kipato chake anacholipwa kama mwanajeshi.Baada ya siku hiyo hakukuwa tena na maelewano baina ya mama na baba kwani kila mmoja alianza kulala chumba tofauti na mwenzake.Niliendelea kumdadisi mama chanzo cha ugomvi wao na biashara haramu ambayo baba anaifanya lakini hakuwa tayari kuniambia bali alinisihi niendelee kuitunza kompyuta ile kwani ndiyo yenye kila kitu kuhusiana na anachokifanya baba.Baada ya wiki tatu alipata safari ya kwenda Morogoro na akiwa njiani alinitumia ujumbe mfupi kwamba atakaporejea atanieleza kila kitu.Hayo yalikuwa ni mawasiliano yake ya mwisho kwani mama hakurejea tena.Alipata ajali na kufariki.Nina uhakika mkubwa kwamba baba alihusika katika ajali ile iliyosababisha kifo cha mama kwani kabla sijapata taarifa za kifo cha mama alinifuata na kunitaka nimueleze mahala ilipo kompyuta aliyonipa mama.Nilikana kutofahamu chochote lakini baba akaninyang’anya simu na kunionyesha meseje niliyotumiwa na mama.Nilijiuliza sana alijuae kama mama alinitumia ujumbe ule? Alinitolea vitisho vingi sana lakini sikuogopa na niliendelea kukana kupewa kompyuta na mama.Jioniya siku ile ndipo nilipopewa taarifa za kifo cha mama.Niliumia sana” akanyamaza kidogo na kufuta machozihalafu akaendelea “ Baada ya kumaliza msiba alinifuata tena na kuendelea kunitisha ili nimpatie ule mkoba lakini bado niliendelea kukana kupewa mkoba wowote na mama.Vitisho vilipozidi ikanibidi kwenda kuichukua kompyuta ile kwa Salha na kuificha kwa mpenzi wangu David.Niliamini kule itakuwa salama.Kabla ya kuipeleka kwa David ilinilazimu kwanza kuiwasha na kuangalia ni kitu gani kilichokuwamo ndani yake na nikastuka sana kwa nilichokigundua” akasema Graca “ Uligundua nini Graca? Akauliza Elvis “ Kupita kompyuta ile niligundua kwamba baba amekuwa akijishughulisha na biashara ya kuuza silaha.Yeye na wenzake wamekuwa wakifanya biashara hii kwa muda mrefu na ndiyo chanzo cha utajiri wake mkubwa.Niligundua kwamba silaha hizo wamekuwa wakiziagiza toka nje ya nchi na kisha huziingiza hapa nchini kama silaha za jeshi la Congo na kisha huzisafirisha kuzipeleka kwa waasi wanaopigana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kujipatia fedha nyingi sana.Hiyo ndiyo biashara ambao mama alikuwa akimkanya baba kuacha kujihusisha nayo.” Graca akanyamaza akainama chini.Elvis akahisi shati lake linaanza kuloa jasho.Ilikuwa ni taarifa yenye kustusha sana.Graca akainua kichwa halafu akasema “ Siku moja usiku baba akanikamata akanifungia katika chumba kimoja akanitesa sana akinitaka nimuonyeshe mahala ilipo kompyuta yake.Alinipiga sana usiku huo lakini sikumweleza chochote.Alipoona nimegoma kumpa jibu akaniacha.Alfajiri na mapema nikawahi kwa David na kumuomba anipe ile kompyuta yake.Kumbe wakati naenda kwa David kuna watu walikuwa wananifuatilia.Nikiwa chumbani kwa David watu wale waligonga mlango kwa nguvu ,David akanipitishia dirishani nikakimbia pamoja na kompyuta ile.Na asubuhi ile ndio ulikuwa mwisho wa mimi kuonana na David kwani alikamatwa na kufunguliwa shtaka la kumbaka mwanafunzi yaani mimi” Graca akainama akafuta machozi na kuendelea “ Nilipotoka pale kwa David nikaelekea moja kwa moja kwa padre kalistus ambaye ndiye paroko wa parokia yetu na ananifahamu vyema.Aliponiona katika hali ile alistuka sana lakini sikumueleza chochote kuhusu kilichonipata ,nilichomuomba kwa wakati ule ni anihifadhie ile kompyuta na asijaribu kuifungua ndani.Aliniahidi kufanya kama nilivyomuomba halafu nikaondoka.Ni hapo ndipo nilipolazimika kujifanya mgonjwa wa akili” Graca akafuta machozi na kuendelea “Nilipelekwa hospitali ya magonjwa ya akili na nikaanza kudungwa sindano wakiamni mimi nina matatizo ya akili.Baada ya wiki moja nikapandishwa ndege na kupelekwa afrika kusini katika hospitali ile ulikonitoa” akasema Graca. “ Pole sana Graca.Simulizi yako imenisikitisha sana sana.Sikutegemea kama baba yako anaweza kuwa na roho mbaya kiasi hicho.Nakupongeza kwa ujasiri wako” “ Ahsante sana Elvis.kwa sasa najiona nimeutua mzigo mzito sana na nimeufikisha sehemu husika.Nilikuwa nikijiuliza sana sehemu ambayo ninaweza kwenda kuripoti kuhusu jambo hili lakini nashukuru Mungu amekuleta wewe .Tafadhali Elvis naomba ulifanyie kazi jambo hili na uhakikishe wahusika wote wanachukuliwa hatua ukianzia na baba yangu.” Akasema Graca “ Graca ninashukuru sana kwa kuniamini na kunieleza mambo haya mazito.” Akasema Elvis “ Unayepaswa kushukuriwa ni wewe kwani bila wewe nisingeweza kuondoka palehospitali” akasema Graca kikapita kimya Elvis akamtazama Graca na kusema “ Graca taarifa hizi ulizonipatia ni taarifa nzito sana na ninakuahidi kuzifanyia kazi kiukamilifu.Maelfu ya raia wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wamekuwa wakiuawa na waasi ambao wanatumia silaha wanazouziwa na Frank na kundi lake.Lazima nihakikishe kwamba wote wanaohusika na mtandao huu wanatiwa hatiani na wanahukumiwa kwa makosa wanayoyafanya” akasema Elvis na kunyamaza kifupi kisha akauliza “ Ulisema kompyuta ile uliipeka kwa padre? “ Ndiyo.Nilimpa Padre kalistus anitunzie” Nitahitaji kuipata kompyuta hiyo ili niweze kukusanya taarifa za kutosha kuhusiana na jambo hili.Kwa maana hiyo itatutalzimu kwenda kuichukua.usiwe na hofu yoyote ukiwa na mimi” akasema Elvis “ Hakuna tatizo Elvis tunaweza tukaenda.” akasema Graca.Elvis akaelekea katika chumba cha gari ambamo kulikuwa na gari aliyoiacha Amanda.Ilikuwa ni gari nzuri. “ Wow ! what a nice car” akasema Elvis huku akitabasamu,akalikagua gari lile na kuhakikisha liko vizuri.Akalitoa nje kisha wakaondoka kuelekea kwa padre Kalistus *****************







Ni saa tatu za asubuhi Brigedia Frank akiwa amesimama sebuleni kwake mkononi akiwa na glasi ya pombe kali kama kawaida yake.Mkono wa kushoto alikuwa na sigara ikitoa moshi. “ Najuta kwa nini Mungu alinipa mtoto kama Graca.Yeye na mama yake wote hawana faida yoyote wangu zaidi ya hasara na karaha.Graca akeshe akimuomba Mungu wake nisimtie mikononi mwangu.Aendelee kujificha hivyo hivyo .Nikimpata safari hii sina hakika kama nitamuacha hai.Na huyu shetani Elvis kama kweli ni yeye ndiye aliyemtorosha mwanagu basi ninaapa nitamuonyesha kazi.Safari hii ameingia sehemu mbaya sana vijana wanasema ameingia choo cha kike na nitamuonyesha mimi ni nani” akawaza Frank na kunywa funda kubwa la mvinyo akavuta na sigara yake akapuliza moshi halafu akachkua simu na kumpigia Pascal “ hallow Frank” akasema Pascal baada ya kupokea simu “ habari yako pascal? “ Habari nzuri kuna habari yoyote mpya? “ David kanipgia simu asubuhi na kunitaarifu kwamba kikao chake na makamu wa rais hakikuweza kufanikiwa kwani makamu wa rais alipatwa na kikao cha dharura kwa hiyo kikao chao kitafanyika leo na kesho jioni kutakuwa na kikao cha pamoja ili kupeana taarifa za maendeleo katika majukumu tuliyokabidhiana.Leo saa saba mchana nitakuwa na kikao na makamanda watano ambao tulianza maongezi yetu jana lakini hatukumaliza kwa hiyo baadae tutaendelea.Taarifa zaidi tutapeana kesho jioni katika kikao.Vipi kuhusu Elvis? Umepata taarifa zake zozote? “ Mpaka sasa hivi sia taarifa zozote za Elvis.Nimejaribu kufanya uchunguzi kwa kupitia watu wangu wa uwanja wa ndege na Julius nyerere na wamenihakikishia kwamba ni kweli Elvis alipanda ndege ya shirika la ndege la afrika kusini na kuondoka nchini lakini hakuna mahali kunakoonyesha kwamba tayari amerejea nchini.Mara tu atakaporejea ama atatumia njia ya ndege basi nitataarifiwa mara moja.Vipi kuhusu Graca kuna taarifa zozote umepokea? “ Hakuna taarifa zozote hadi hivi sasa.Graca hajaonekana na juhudi za kutafuta zinaendelea.Nina hakika Elvis ndiye aliyemtorosha na kumpeleka kusikojulikana kwa sababu anazozijua yeye.Nakuhakikishia Pascal kwamba safari hii huyu kijana amejiingiza mwenyewe katika tanuru la moto.Kitakachomkuta itakuwa ni fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama yake na kuingilia mambo yasiyowahusu” “ Unadhani kuna jambo ameligundua kuhusiana na sisi na ndiyo maana akaenda kuonana na Graca? “ Ninahisi hivyo.Ninahisi kuna kitu atakuwa ameking’aza lakini hana uhakika nacho na ndiyo maana anatafuta uhakika .Hatupaswi kumpa nafasi ya kutuchunguza.Sisi ni mtandao mkubwa na wenye nguvu na hatuwezi kushindwa na mtu mmoja na hasa katika wakati huu ambao tuna mpango mkubwa sana ulioko mbele yetu.Endelea kufanya uchunguzi tujue mahala alipo ili tumzimishe haraka sana” akasema Frank “ usijali Frank.Ninaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala hili na ninakuhakikishia kwamba katu Elvis hawezi kutuumiza vichwa vyeti.Nitakuwa nakutaarifu mara kwa mara kila nitakapopata taarifa za kuonekana kwa kenge huyu” “Ok Pascal .Tuwasiliane baadae” akasema Frank na kukata simu.Akanywa funda moja na mara sura ya Graca ikamjia akauma meno kwa hasira “ Pone pone yako uendelee kujificha huko huko ulikojificha kwa sababu endapo utajitokeza tu nitalifuta jina lako haraka sana katika orodha ya walio hai.Najilaumu sana kuwa na mtoto kama wewe.I hate you !! akasema kwa hasira halafu akaenda ukutani akaitungua picha kubwa ya http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Graca “ Hustahili kuitwa mtoto wangu.Wewe ni shetani mkubwa” akasema kwa hasira halafu akaenda nje na kutupa picha ile katika pipa la takataka “ To me you are dead already !! akasema Frank wakati akiitupa picha ile ya mwanae Mara tu baada ya Frank kukata simu pascal akazitafuta namba za simu za Arafa msichana anayefanya kazi katika ofisi za akina Elvis na kumpigia.Simu ikaita bila kupokelewa,hakukata tamaa akapiga tena na safari hii ikapokelewa “ Hallo Arafa” akasema pascal “ pascal,Elvis hajarudi,nitakufahamisha atakaporejea” akasema sarafa na kukata simu “ Bastard !!!!..” akasema kwa hasira pascal.Kitendo cha Arafa kumkatia simu kilimkera sana Yawezekana akawa na shughuli nyingi siku ya leo na ndiyo maana amenijibu vile kwa dharau”akawaza Pascal ***************** Gari aina ya Toyota harrier liliwasha taa ndogo ya njano ya upande wa kulia ishara ya kukata kona kuingia katika lango kuu la kanisa la mt.Anthony wa padua na kuelekea moja kwa moja katika maegesho.Hakukuwa na magari mengi siku hii mahala hapa.mlango wa gari upande wa dereva ukafunguliwa akashuka Elvis halafu akazunguka upande wa pili na kufungua mlango akashuka Graca.Akasimama kwa sekunde kadhaa akilitazamakanisa lile akatabasamu na kupiga hatua kuelekea katika ofisi ya parokia.Kabla ya kuelekea katika ofisi kuu akaongoza hadi katika ofisi ya katekista akabisha hodi na kuruhusiwa kuingia,akakinyonga kitasa na kujitoma ndani akamuacha Elvis nje akimsubiri.Mara tu alipoingia mle ofisini mzee mmoja mwenye mvi nyingi kichwani akapatwa na mshangao mkubwa “Graca !! akasema huku akiinuka na kumkumbatia Graca “Oh Graca,umerudi !! Mungu mkubwa sana” akasema Yule mzee aliyeonekana kumfahamu vyema Graca “Nimefurahi kukuona tena mzee Abel” Akasema Graca na kuketi kitini Ama kweli Mungu anaweza.Nimekuwa nakukumbuka sana katika maombi yangu ya kila siku na Mungu amesikia kilio chetu na leo umerejea tena .Karibu sana.Vipi hali yako? Akasema mwalimu Abel “nashukuru sana mwalimu Abel kwa sala na maombi yako.Kwa sasa mimi ni mzima na ninaendelea vizuri” akasema Graca “karibu sana Graca” mwalimu Abel akamkaribisha tena Graca.Kikapita kimya kifupi Graca akasema “Mwalimu Abel mimi si mkaji sana nimepita hapa mara moja kukusalimu lakini shida yangu kubwa iliyonileta ni kuonana na padre kalistus.Ninaweza kumpata? Padre kalistus yupo ila yuko katika ibada.Wana mafungo ya wiki mbili hapa parokiani lakini ninaweza kukuitia.Subiri kidogo hapa ofisini nikamuite” akasema Mwalimu Abel huku akiinuka na kabla hajafika mlangoni Graca akamuita “mwalimu Abel kuna jambo lingine nataka kukuomba” “Omba Graca” akasema mwalimu Abel “Ninaomba zaidi yako na padre kalistus,asifahamu mwingine yeyote kama niko hapa.Nina sababu zangu za kuomba hivyo” “Usihofu kuhusu hilo Graca.Hakuna atakaye fahamu chochote .Nisubiri nikamuite padre kalistus” Baada ya dakika kumi hivi mwalimu Abel akarejea “Padre kalistus ameelekeza akukute katika ofisi yake.Twende nikupeleke” akasema mwalimu Abel na kumuongoza Graca katika ofisi ya padre Kalistus na kumuacha pale akimsubri.Zilipita dakika kadhaa na padre akawasili “Graca !! akasema padre na Graca akasimama wakasalimiana “Sikuamini mwalimu Abel aliponieleza kwamba umekuja.Vipi maendeleo yako? Vipi hali yako? Pole na matatizo yaliyokukuta” “Ahsanate sana Padre.Nawashukuru sana kwa kuniombea bila kuchoka na kwa msaada mkubwa wa sala zenu ninaendelea vyema” Pole sana Graca.Nilistushwa mno niliposikia kuhusu matatizo yaliyokupata.Nini hasa kilitokea? Wote hapa hatuelewi ni kitu gani hasa kilikupata kwa sababu kila mtu anaongea analolifahamu” “Padre,mambo yaliyonikuta ni mengi sana na itachukua muda kukueleza yote.Nitatafuta wasaa nitakuja nikueleze kila kitu.Kwa sasa nimepita kuuchukua ule mkoba niliokupa unitunzie.Bado unao? “Ndiyo bado ninao na nimeuhifadhi sehemu salama kama ulivyoomba”akasema Padre kalistus halafu akaenda chumbani kwake na baada ya muda akareje ana ule mkoba aliopewa na Graca. Mkoba wako huu hapa.Uko salama kabisa na haujawahi kufunguliwa” “Ahsante sana baba Padre.Nakuahidi nitakuja tena siku nyingine kukusimulia mkasa wangu” “karibu sana Graca.Muda wowote ukiwa na tatizo lolote usisite kuja nasi tutakusaidia’ “Ahsante sana padre,wewe ni baba yangu wa kiroho na nitakuja kukueleza kila kitu ila kuna jambo moja nataka kukuomba’ “Jambo gani? “Naomba asifahamu mtu yeyote kama nimefika hapa na kama nilikupa mkoba unitunzie” Padre kalistus akamtazama Graca usoni na kuuliza Graca kuna kitu gani kinaendelea? “Nitakuja kukueleza baba padre.Ahsante sana kwa kunitunzia mkoba wangu” akasema Graca na kutaka kuondoka lakini padre akamzuia na kumtaka apige magoti ambariki na baada ya kubarikiwa akainuka wakaagana na kutoka mle ofisini,moja kwa moja akaelekea mahala walipoegesha gari .Elvis aliyekuwamo garini akashuka na kumpokea Graca ule mkoba akamfungulia mlango akaingia wakaondoka. “Elvis huo ndio mkoba wenye kompyuta yenye ushahidi wa kila kitu nilichokueleza.Huo mkoba ni chanzo cha matatizo yangu yote na sababu ya mama yangu kufariki.Tafadhali naomba wote wanaohusika wakamatwe na wachukuliwe hatua kwa uharamia wanaoufanya.Ninakukabidhi kompyuta hiyo nikiwa na imani kwamba imefika katika mikono salama”akasema Graca “Ahsante sana Graca.Nakuahidi hakuna yeyote katika mtandao huu atakayesalimika.Wote watafikishwa mbele ya sheria tukianzia na baba yako Frank” “Ahsante Elvis.Tunaelekea wapi?akauliza Graca “ kwa sasa tunaelekea nyumbani kwangu.Kuna vitu ambavyo nahitaji kuvichukua” akasema Elvis. Safari ikawa ya kimya kimya na baada ya saa moja hivi wakawasili nyumbani kwa Elvis.Akapiga honi geti likafunguliwa na mtumishi wa ndani “kaka Elvis ,karibu sana.Shikamoo” akasalimia “Marahaba Stella,hujambo? ‘Sijambo kaka pole na safari” “Ahsante sana.Vipi likizo yako ilikuaje? Wazee nyumbani hawajambo? “Nyumbani wote wazima wanawasalimu sana” akasema Stella mtumishi wa ndani wa akina Elvis ambaye alikuwa amekwenda nyumbani kwao kwa mapumziko na sasa amerejea “Elizabeth naye hajambo? Akauliza Elvis “Ameondoka asubuhi ya leo kuelekea Iringa” akasema Stella Sawa Stella mimi nilikuwa na safari ya kikazi na nimerejea” akasema Elivs na kuelekea chumbani kwake.Akakitazama chumba chake na kutabasamu “Home sweet home” akasema na kuchukua simu yake iliyokuwa mezani akaiwasha na kuzitafuta namba za Patricia akampigia lakini simu ya Patricia haikuwa ikipatikana Nyuma ya kabati kubwa la nguo kulikuwa na mlango akalisukuma kabati na kuufungua mlango akaingia katika chumba kidogo.Hiki kilikuwa ni chumba maalum ambacho huhifadhi vitu vyake vya siri na huingia yeye na Patricia pekee.Akakusanya vitu alivyoona vinaweza kumsaidia akapakia katika begi kubwa akarejea tena chumbani kwake akachukua baadhi ya vitu vyake akapakia katika begi lingine na kutoka akakutana na Stella “Kaka unasafiri tena? Akauliza Stella na kumpokea Elvis begi moja. “Ndiyo nimepata safari nyingine ya kikazi” akasema Elvis kisha wakaongozana na Stella hadi garini.Stella akastuka kidogo baada ya kumuona Graca ndani ya gari.Hakujua kama Elvis alikuwa na mtu mwingine garini.Elvis akapakia mabegi yake garini na kumgeukia Stella “Dada yako akirudi mwambie nimerudi toka safari lakini nimepata tena safari nyingine ya kiazi” akasema Elvis akageuza gari na kuondoka una nyumba nzuri sana elvis” akasema Graca ‘Thank you” akajibu Elvis halafu akachukua simu yake akajaribu kumpigia tena Patricia lakini bado simu haikuwa ikipatikana,akaamua kuizima kabisa simu Waliwasili makazi mapya na kukuta tayari Doreen amekwisha rejea “Nilipatwa na woga baada ya kurejea na kukuta nyumba tupu.Welcome home.Lunch is ready” akasema Doreen na kuwaongoza akina Elvis hadi chumba cha chakula .Baada ya kupata chakula Elvis akaendelea na kazi ya kufunga kamera za ulinzi na kuziunganisha na kompyuta yake na hivyo kuweza kuona kila pembe ya nyumba ile. ***************** Saa kumi na moja za jioni Patricia akarejea nyumbani.Mara tu baada ya kushuka garini akakutana na sura yenye tabasamu ya Stella ‘Shikamoo dada.Pole na kazi” akasema Stella na kumpokea Patricia mkoba “Marahaba habari za hapa? “Habari nzuri dada.Kaka Elvis amerudi’ “Elvis amerudi? “Ndiyo dada” “Yuko ndani? Akauliza Patricia kwa furaha Hapana amekwisha ondoka.Alikuwa na haraka na hakukaa sana.Aliingia ndani na baada ya muda akatoka na mabegi mawili akasema nikwambie kwamba amekwisha rudi lakini ameondoka tena” “Alikuwa peke yake? “Hapana ,hakuwa peke yake.Alikuwa na msichana mmoja ndani ya gari” Patricia akasimama kwa dakika moja akifikiria halafu akachukua mkoba wake na kuingia chumbani. “Kwa nini Elvis hakunitaarifu kama anarejea leo?Amekwenda wapi tena?siku zote aondokapo kama mimi sipo huwa anaacha ujumbe mezani,mbona leo hajaacha ujumbe wowote ?huyo msichana aliyekuwa naye garini ni nani?” Patricia akajiuliza maswali mfululizo lakini akakosa jibu.Akafungua chumba cha siri cha Elvis na kukuta vifaa vingi havipo. “Huyu Elvis hii kazi yake imeanza kunichosha.Kila mara yuko kazini hana mapumziko maalum.Sipati muda wa kutosha wa kuwa naye,Oooh gosh!Sasa ndo naanza kuuona ubaya wa kazi hii aliyoichagua .Sijui ni kwanini aliamua kuifanya kazi hii. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwa daktari au mhandisi lakini akachagua kuifanya kazi hii ambayo inamnyima maisha mazuri.I’m in hell right now and I need him by my side but he’s away” akawaza patricia halafu akachukua simu na kujaribu kumpigia Elvis lakini simu yake haikuwa ikipatikana. “Where is he now? Huyo mwanamke aliyekuwa ameongozana naye ni nani? Wako wapi muda huu na wanafanya nini? Nashindwa kujizuia kuwa na wivu.ninaelewa Elvis ananipenda na hawezi kabisa kunisaliti lakini kwa hali ilivyo hivi sasa anything can happen” akawaza Patricia halafu akaingia bafuni kuoga.Kisha maliza kuoga akavaa vizuri akajitazama katika kioo na kuvuta pumzi ndefu “I’m so pretty .Mungu amenijalia uzuri wa kipekee lakini kwa sasa uzuri wote huu hauna faida yoyote kwangu.Sina thamani yoyote” akawaza Patricia halafu akachukua mkoba wake akamuaga Stella na kuingia garini akaondoka Mita kama mia mbili toka aliache geti la nyumba yao simu yake ikaita akatupia jicho kutazama mpigaji alikuwa ni mama mkwe wake yaani mama yake elvis.Patricia akaguna na kuitupa simu ile katika kiti cha pembeni na kuiacha ikiendelea kuita “Huyu mama sitaki kupokea simu yake anaweza akaniharibia kabisa siku yangu kwa maneno yake ya kejeli.Toka alipoanza kuongelea masuala ya mtoto,nimejkuta nikimchukia sana.Nina wasi wasi anaweza hata akaivunja ndoa yetu kamasintasimama imara” akawaza Patricia. Baada ya simu yake kutopokelewa na Patricia mama yake Elvis akaamua kupiga simu ya mezani ambayo ilipokelewa na Stella.Mama Elvis akamuuliza Patricia “Dada Patricia hayupo .Ameondoka muda si mrefu sana” akasema Stella “Mume wake naye yupo? akauliza mama Elvis “Kaka Elvis amekwenda safari” “Mhhn ! Mama Elvis akaguna kidogo na kuuliza tena “Patricia amekwambia anaelekea wapi? “Hapana mama hajaniambia anaelekea wapi” “Kwa namna alivyokuwa amevaa wakati anatoka unadhani amekwenda kazini? “Sina hakika kama amekwenda kazini kutokana na mavazi aliyoyavaa.Ninafahamu mavazi yake ambayo hupenda kuvaa akienda kazini.Nina hakika hajaenda kazini” “ Sawa ahsante Stela” akasema mama Elvis na kukata simu Patricia aliendelea na safari yake mara ukaingia ujumbe katika simu yake.Kwa kuwa alikuwa barabarani alishindwa kuusoma ujumbe ule. Aliwasili Silvano hotel mahala panapofanyika sherehe ya kumkaribisha daktari bingwa wa neva za fahamu toka Texas marekani anaitwa Dr Stephen Washington.Daktari huyu bingwa aliombwa na serikali kwa maombi maalum ya serikali ya Tanzania ili kuimarisha kitengo cha neva za fahamu na alitarajiwa kuwepo nchini kwa miaka minne Toka amefika nchini yapata wiki moja sasa amekuwa na ukaribu mkubwa na Patricia ambaye amemsaidia sana kuyafahamu na kuyazoea mazingira mapya ya kazi.Usiku huu uongozi wa hospitali uliamua kufanya sherehe ndogo ya kumkaribisha rasmi Patricia akaegesha gari na kabla hajashuka akachukua simu ili ausome ujumbe ule ulioingia wakati akiwa barabarani.Akausoma ujumbe ule akaegemea kiti huku machozi yakimtoka.Akarudia kuusoma tena ujumbe ule uliotoka kwa mama mkwe wake ambao ulisomeka hivi “ Mumeo akitoka na wewe unatoka.Hivyo ndivyo ulivyofunzwa kwenu? Kaa jitulize nyumbani muache mwanangu akanitafutie mjukuu kwa wale walio tayari kumzalia mtoto” “Patricia alihisi kama kisu kikali kimepenya na kuuchoma moyo wake.Alihisi maumivu makali ya moyo.Aliumizwa mno na maneno yale mazito ya dharau na kashfa.Alishindwa afanye nini akabaki ameegemea kitu akilia “Najuta kwa nini nilikubali kuolewa na Elvis.Nilijua lazima mambo kama haya yatajitokeza tu.Ee Mungu nisaidie nipe nguvu ya kuhimili kipindi hiki kigumu katika maisha yangu.Niko katika majaribu makubwa.Sina jib.….” Patricia akatolewa mawazoni na mtu aliyegonga kioo cha dirisha.Haraka haraka akafuta machozi na kushusha kioo “Samahani mama una tatizo? Akauliza kijana aliyekuwa amevalia sare za ulinzi “Hapana sina tatizo” akajibu Patricia na kupandisha kioo cha gari akachukua mkoba wake na kushuka akaelekea ukumbini huku akihisi kushindwa kutembea kutokana na miguu kuwa mizito.Kabla ya kuingia ukumbini akaenda katika chumba cha wanawake akachukua poda na kujipaka usoni.Hakutaka mtu yeyote agundua kama alikuwa analia.Alijitazama katika kioo na kujiona yuko sawa akaelekea ukumbini.Tayari wengi wa wageni walikwisha wasili akiwepo Dr Stephen Usiku huu Patricia alikuwa mkimya sana na hakuonekana kutaka maongezi na mtu yeyote kitu ambacho si kawaida yake.Pamoja na kumfahamu patricia kwa mud amfupi,Dr Stephen aligundua patricia hakuwa sawa. “Kuna tatizo lolote Dr Patricia? akauliza Dr Steven “Hapana hakuna tatizo” akajibu Patricia na kwa mbali Dr Steven akayaona machozi katika macho ya Patricia Patricia akainuka na kwenda katika chumba cha wanawake.Bado machozi yaliendelea kumtoka.Akajifuta machozi na kurejea ukumbini.Sherehe zikaanza.Dr Steven alijiuliza maswali mengi kuhusiana na tatizo linalomsumbua Patricia Wakati sherehe ikiendelea wageni waliendelea kuburudika kwa vinywaji mbalimbali Patricia alikuwa akinywa mvinyo mkali.Alitaka atulize mawazo.Alitaka ayasahau matatizo yake yote aliyonayo.Hatimaye ukawadia wakati wa kucheza muziki.Dr Steven ambaye naye alikuwa anatumia mvinyo akamshika mkono Patricia na kumuomba wakacheze.Wakati wakicheza muziki wa taratibu Patricia akajikuta akipatwa na hisia za ajabu akahisi kama anacheza na Elvis na mara Dr Steven akagundua Patricia alikuwa analia “Patricia kuna tatizo gani? Nini kinakuliza?akauliza Dr Steven akijaribu kumbembeleza Patricia “Steven tafadhali naomba uniondoe hapa.” Akasema huku akilia.Dr Steven akahisi lazima kuna jambo zito lililomsibu Patricia.Akamshika mkono na kumuongoza nje ya ukumbi akampeleka katika bustani.Bado patricia aliendelea kulia kwa kwikwi “Patricia tafadhali nieleze una tatizo gani? Akauliza Dr Steven “Dr Steven siwezi kuvumilia zaidi ya hapa !! akasema Patricia “Nini kimetokea?Una tatizo gani?Niambie tafadhali mimi ni rafiki yako nitakusaidia” akasema Dr Steven.Patricia akamtaka Dr Steven ampeleke katika gari lake.Steven akamshika mkono akamuongoza Patricia kuelekea katika gari lake akamfungulia mlango akaingia.Patricia akampa Dr Steven funguo za gari. “Nikupeleka nyumbani? Akauliza Dr Steven baada ya kuwasha gari “Tafadhali niondoe eneo hili Steven.Nipeleke kokote.” akasema Patricia. “ Nyumbani kwako? “Hapana sitaki kwenda nyumbani kwangu.Nipeleke sehemu yoyote nikapumzishe kichwa lakini si nyumbani kwangu” akasisitiza Patricia.Dr Steven akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akaondoa gari ******************** Ukimya wa hali ya juu ulitawala katika eneo zima kulizunguka kasri la aliyewahi kuwa waziri mkuu David Sichoma.Licha ya ulinzi anaopewa na serikali lakini David ana walinzi wake maalum aliowakodisha toka nje ya nchi kwa ajili ya kumlinda wakisaidiwa na mbwa maalum wawili wenye mafunzo.Kwa ulinzi ulikuwa mkali sana eneo hili. Saa mbili na dakika ishirini za usiku gari tatu zikawasili katika makazi ya David.Geti kuu likafunguliwa na gari zile zikaruhusiwa kupita na kuelekea sehemu ya kuegesha.Watu saba wakashuka toka ndani ya gari mbili na wote walivaa vifaa vya mawasiliano masikioni .Baada ya kuhakikisha eneo liko salama mmoja wao akaufungua mlango katika gari la kati kati akashuka makamu wa rais mheshmiwa Shafi Abdulkhareem Omar akalakiwa na David.Walisalimiana kwa furaha kubwa kisha David akamuongoza makamu wa rais kuelekea ndani akifuatana na walinzi wake hadi katika sabule kubwa .Makamu wa rais akawaomba wasubiri hapo kwani alikuwa na maongezi ya faragha na David.Wakaingia katika chumba cha pembeni kilichoonekana kama maktaba kilichokuwa na mlango wa kioo lakini maongezi hayakuweza kusikika nje. “karibu sana mheshimiwa Shafi” akasema David “Ahsannte sana David.Nimefurahi sana kukutana nawe tena usiku huu.Maisha yanakwendaje?Naona mambo si mabaya toka uachane na mambo ya siasa mwenzetu unazidi kuwa kijana badala ya kuzeeka” Kauli ile ya makamu wa rais ikamfanya David aangue kicheko kikubwa “Usemayo yanaweza kuwa na ukweli Shafi.Toka nimeachana na siasa hizi za majitaka nimeeleekeza nguvu zote katika kuimarisha afya yangu.Ninakula vizuri na kufanya mazoezi ya kutosha na ndiyo maana unaniona nimenawiri namna hii.Vipi huko serikalini mnaendeleaje? “Huko ni kama kawaida.Siku ikiisha salama unashukuru Mungu lakini kwa kuwa tumechagua wenyewe kuingia katika siasa hatuna budi kukubaliana na kila linalojitokeza” “Vipi kuhusu mahusiano yako na rais yanakwendaje? Yameimarika siku hizi?David akauliza “kwa kweli mpaka leo mimi na mheshimiwa rais bado hatuna mahusiano mazuri kitu ambacho kinaifanya kazi yangu kuwa ngumu sana.Ninafikikiria baada ya kumaliza kipindi changu,ninataka niachane kabisa na siasa niishi kama wewe” “Pole sana mheshimiwa.Mambo kama hayo katika ulingo wa siasa hayakosekani” “Nalifahamu hilo” akajibu makamu wa rais halafu kikapita kimya kifupi na makamu wa rais akasema “David nilikuwa na kikao usiku huu lakini nimekiahirisha hadi kesho asubuhi ili nije kuonana nawe kama ulivyonisisitiza .Naamini una jambo la muhimu sana uliloniitia hapa” akasema makamu wa rais “Kwanza kabisa nakushukuru sana mheshimiwa kwa kuitika wito.Ni heshima ya pekee umenipa na nina hakika kufika kwako hapa leo haujapoteza muda bure”akasema David “Mr Shafi ,nimekuita hapa kwa ajili ya kuongelea suala zito linalohusu maslahi mapana ya nchi yetu na mustakabali mzima wa maisha yetu ya kisiasa” Akanyamaza tena na kumtazama makamu wa rais aliyekuwa kimya akimsikiliza halafu akaendelea “Hivi majuzi tumepokea ugeni mzito wa rais wa marekani.Ni ugeni wa kihistoria sana.Sambamba na lengo la rais huyo kuja kusaidia miradi kadhaa ya kimaendeleo lakini kuna mambo makubwa mawili yaliyomleta.Nina hakika unayafahamu mambo hayo ni mambo gani kwani hata katika maamuzi yake nawe umeshiriki” akasema David na kumstua kidogo Shafi “Ina maana tayari umekwisha fahamu mambo yaliyofanyika katika ujio ule wa rais wa marekani? makamu wa rais akashangaa “Mr Shafi dunia ya sasa inazidi kuwa ndogo kwa hiyo hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika bila kujulikana.Taarifa zote ninazo kuhusiana na mikataba ya mafuta ,gesi na suala la ujenzi wa kambi kubwa ya kijeshi ya jeshi la marekani hapa nchini” “Mambo yote haya umeyapataje? Akauliza Shafi Usishangae Mr Shafi.Mimi ni mtu mwenye vyanzo vingi vya taarifa .Tuachane na hayo.Nimekuita hapa ili tuweze kujadili masuala ya msingi sana yanayohusiana na namna hayo niliyokueleza” akasema David na kutulia kidogo halafu akaendelea “Juzi tulipata ugeni wa watu wawili toka nchi za mashariki ya kati zenye kuzalisha mafuta kwa wingi duniani na ambazo uchumi wake mkubwa unategemea mafuta.Watu hao walitumwa kama wawakilishi wa serikali na makampuni makubwa ya mafuta toka eneo la mashariki ya kati.walitumwa hapa Tanzania kufuatia kikao kilichofanyika baina ya nchi zinazotegemea mafuta kwa uchumi na wakuu wa makampnuni makubwa ya mafuta.Katika kikao hicho walijadili hali ya biashara ya mafuta duniani na tishio la biashara hiyo baada ya makampuni ya marekani kuruhusiwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya mafuta nchini Tanzania.Hofu kubwa iliyonayo mataifa ya mashariki ya kati ambayo uchumi wake mkuu unategemea mafuta kwani kiasi cha mafuta ni kwamba kiasi cha mafuta kilichogunduliwa Tanzania ni kikubwa sana na endapo marekani itakuwa ndiye mwekezaji pekee wa mafuta hayo hapa Tanzania kuna hatari kubwa sana soko la mafuta ya mashariki ya kati kuyumba sana na hivyo kuhatarisha chumi zao.Kwa sasa sera ya marekani ni kupunguza utegemezi wa mafuta ya kuitoka nje hasa mashariki ya kati kwa hiyo uwekezaji watakaoufanya Tanzania utaifanya marekani na washirika wake ambao ni wanunuzi wakubwa wa mafuta hayo wasihitaji tena mafuta kutoka mashariki ya kati na hivyo bei ya mafuta kushuka na chumi za nchi za mashariki ya kati kuyumba.Baada ya majadiliano marefu umefikia uamuzi kwamba jambo hili ni hatari kwa mataifa ya kiarabu.Hii ni vita mpya kati ya marekani na mataifa ya kiarabu yanayozalisha mafuta.kwa mantiki hiyo basi mataifa hayo yameazimia kupambana na marekani kwa kila namna wanayoweza ili kuhakikisha kwamba mpango wao wa kuwekeza katika sekta ya mafuta Tanzania haufanikiwi” akatulia akamtazama makamu wa rais na kuendelea “Wajumbe hao waliotumwa Tanzania wametukabidhi sisi kazi hiyo ya kuhakikisha kwamba jambo hilo halifanikiwa” Kimya kikatawala mle chumbani.Baada ya dakika moja makamu wa rais akauliza . “Nimekusikiliza vizuri David lakini bado sijakuelewa vizuri.Mataifa hayo ya kiarabu yanataka ninyi mfanye nini? Mtawezaje kulifanikisha hilo wanalolitaka? “Kikubwa wanachokitaka ni sisi kuhakkisha kwamba mpango huo wa makampuni makubwa ya mafuta ya marekani kuwekeza Tanzania haufanikiwi na badala yake makampuni ya kiarabu ndiyo yapewe nafasi hiyo ya kuwekeza katika sekta ya mafuta hapa Tanzania na hivyo kuendelea kulitawala soko la mafuta duniani.Kingine wanachokitaka ni kuhakikisha kwamba mpango wa serikali ya marekani kutaka kujenga kituo kikubwa cha kijeshi hapa Tanzania halifanikiwi” Makamu wa rais akainama na kufikiri kwa muda halafu akinua kichwa na kusema ‘Bado umeniacha gizani David.Jambo hili linawezaje kuzuiwa? Tayari mikataba imekwisha sainiwa na hakuna namna ya kuweza kuitengua.Suala hili haliwezekani” akasema Shafi. Linawezekana kabisa Mr Shafi’ akasema David “Inawezekanaje David? “kwa kuiangusha serikali iliyopo madarakani” Kauli ile ilimstua mno makamu wa rais.Akasimama na kumtazama David kwa hasira na kusema “Sikutegemea kama katika dunia hii ya leo bado kuna watu wenye mawazo ya kijinga kama yako David.Siamini macho yangu David !! Ni wewe kweli !! akasema makamu wa rais kwa mshangao mkubwa “Nmeshangaa sana.Sikujua kama unaweza ukawa na mawazo ya kipumbavu namna hii.Nilidhani umeniitia jambo la maana kumbe ni huu ujinga.Ahsante kwa kunipotezea muda wangu” Akasema makamu wa rais na kuinuka akataka kuondoka. “Mr Shafi calm down .tafadhali usiondoke.Naomba uendelee kunisikiliza” Akasema David “Siwezi kukaa hapa na kuusikiliza upuuzi wako huu.Ninakuonya David usijaribu kabisa kufanya hicho unachofikiria kukifanya wewe na wenzako” akasema makamu wa rais “Naomba unisikilize mr Shafi.Nipe dakika tano tu na utaamua nini cha kufanya” akasema David huku akiushika mkono wa makamu wa rais na kumsihi aketi.Shafi akaketi.









Haya niambie hicho unachotaka kuniambia” akasema Shafi kwa ukali. “Hata mimi nilipoingizwa katika mpango huu nilistuka zaidi yako na nilihamaki kama wewe lakini baada ya kutulia na kusikiliza kwa makini nilielewa na nikauona umuhimu wa mpango huu na mwishowe nikaamua kushiriki” akasema David na kumtazama David “Shafi sisi ni wanasiasa na tunafahamiana vyema.Tunafahamu nia zetu na nini tumefuata katika siasa.Kila mwanasiasa lengo lake kubwa ni kupata madaraka ya juu kabisa ya uongozi.Ilikufikia malengo yake kila mwanasiasa anatumia kila mbinu ili aweze kufikia malengo yake” Akatulia na kumtazama Shafi ambaye alionekana kuanza kupunguza hasira na kumsikiliza David “Shafi wewe si mgeni wa mambo machafu yanayofanyika katika ulingo wa siasa.Siasa zetu zimejaa mambo mengi machafu na sina haja ya kuyasema kwani unayafahamu.Mimi nimekuwa waziri mkuu na wewe ni makamu wa rais unafahamu vyema nini ninaongelea” David akatulia akamtazama makamu wa rais na kuendelea “Shafi ninakufahamu vizuri sana.Kwa muda mrefu umekuwa ukiasisi kwa siri harakati za Zanzibar ijiondoe katika serikali ya muungano na iwe dola huru.Nina fahamu wewe ndiye uliye nyuma ya vuguvugu linaloendelea hivi sasa kutaka Zanzibar ijiondoe kutoka katika serikali ya muungano.Ninazo taarifa zote kuhusu ushiriki wako katika suala hili” akasema David “David unathubutuje kunitamkia maneno hayo ya kipuuzi? Mimi ni makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni mtu mwenye dhamana kubwa na kamwe siwezi kwenda kinyume na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania niliyoapaa kuilinda” akasema kwa ukali Shafi “Shafi naomba upunguze jazba ndugu yangu na tuongee vizuri tuelewane.Nadhani mimi unanifahamu vizuri na unafahamu vile vile kwamba haya nikwambiayo ni ukweli mtupu.Hata hivyo tuachane na hayo mambo na tujielekeze katika jambo la msingi” akasema David na kumtazama Shafi ambaye alionekana kuanza kushusha jazba “Shafi nafahamu lengo lako kubwa ni kuitawala Zanzibar na ndiyo maana unafanya harakati za chini chini ili Zanzibar ijitenge.Kwa uhalisia suala la Zanzibar kujitenga na kuwa dola huru ni gumu sana na njia pekee ya kuhakikisha kwamba hilo linawezekana ni kwa kutumia njia ya mapinduzi.Shafi huu ndio ule muda uliokuwa unausubiri wa kutimiza lengo lako la kuiongozaZanzibar huru.Endapo utaungana nasi na tukafanikiwa kuiondoa serikali ya jamhuri ya muungano madarakani mimi ndiye nitakayekuwa rais wa Tanzania na bila kuchelewa tutauvunja muungano na wewe utakuwa rais wa Zanzibar iliyo huru.Sina hakika kama utakuwa tayari kuiachia fursa hii iliyojitokeza itakayokusaidia kutimiza malengo yako.Ni wakati wako wa kuamua kama utapenda kushirikiana nasi” akasema David.Shafi akainama akafikiri kwa muda wa kama dakika moja hivi halafu akatoa pakiti la sigara akawasha moja na kuvuta kisha akasema “Mpango wenyewe mmeupangaje? Nani na nani wanashiriki katika huo mpango wenu? David akatabasamu na kukohoa kidogo akamueleza Shafi namna mpango mzima ulivyoandaliwa na maendeleo yake.Alipomaliza maelezo yale Shafi akajikuta anatabasamu “Sawa David.Nimekuelewa na nimeuelewa mpango mzima.Nitashirikiana nanyi lakini kwa masharti.Baada ya mipango yote kwenda vizuri nitaomba nialikwe katika kikao cha wahusika wote ili na mimi nipate nafasi ya kuzungumza nao” akasema Shafi Mazungumzo yaliendelea hadi saa saba za usiku walipoagana na makamu wa rais akarejea katika makazi yake****************** Saa mbili za usiku baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku Elvis akamuomba Graca aende chumbani kwake kupumzika kwani alionekana kuchoka sana.Sebuleni pale wakabaki Elvis na Doreen wakitazama runinga “Elvis mlienda wapi mchana na Graca? Akauliza Doreen “Kuna mahala Graca alinipeleka” ‘Tayari amekwisha kueleza kile ambacho aliahidi kukueleza? “Ndiyo amekwisha nieleza” “Good” akajibu Doreen na ukimya utawala “Doreen” akaita Elvis na kuuvunja ukimya “Unasemaje Elvis? “Nataka nikushukuru kwa dhati kabisa kwa namna ulivyojitolea kunisaidia.Umenisaidia msaada mkubwa .Ahsante sana” Doreen akatabasamu na kusema “Elvis kama nilivyokuahidi kwamba siku yoyote na muda wowote mimi niko tayari kukusaidia kwa msaada wowote unaouhitaji.Usihofu kuomba chochote toka kwangu” “Ahsante sana Doreen” Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Doreen akasema “Elvis kwa muda gani unategemea kukaa hapa? Swali lile likaonekana gumu kidogo kwa Elvis akafikiri kidogo na kusema “Sifahamu ni kwa muda gani lakini hadi hapo nitakapokamilisha zoezi la kumtafutia Graca makazi ya kudumu nje ya nchi.Kwa hali ilivyo Graca hatakiwi kuishi hapa nchini kabisa.Ninafikiria kumfanyia mpango wa kumpeleka Marekani akaishi kule.Nitaanza kulishughulikia suala lake kuanzia kesho” “Unadhani unafanya vizuri kutomshirikisha Patricia ili ajue ni kitu gani kinachoendelea hivi sasa? “Nafahamu sifanyi vizuri lakini sina namna nyingine ya kufanya.Suala ninaloshughulikia ni zito na hapaswi kufahamu chochote” “Nafahamu hilo Elvis lakini huoni kama utakuwa unauumiza sana moyo wake ? “Nafahamu ataumia na hata mimi ninaumia pia lakini sina namna nyingine ya kufanya.Lazima niishi hapa kwa muda ili kumlinda Graca ambaye amenipa taarifa nzito sana na pili kulishughulikia suala zito kwa mustakabali wa taifa.Leo mchana nilifika hadi nyumbani kwangu nikajaribu kumpigia simu Patricia lakini simu yake haikuwa ikipatikana.Niliacha maagizo kwa mtumishi wetu wa ndani amfahamishe kwamba tayari nimerejea toka Afrika kusini lakini nimekwenda katika kazi nyingine.Tafadhali naomba usimueleze Patricia chochote au hata kumuonyesha mahala nilipo” akasema Elvis.Doreen akatabasamu na kuuliza “Elvis you are so handsome and intelligent.Kwa nini usiachane na kazi hii kwani hufanani nayo kabisa.Kazi hizi zinahitaji mtu uwe na moyo mgumu na mwenye uwezo wa kuua muda wowote .Elvis una moyo wa huruma ,una sura nzuri ya upole na ulipaswa kuwa daktari na si kazi hii.Please think twice about this job.If you cant do it for yourself doit for Patricia.Wewe ndiye mfariji wake mkuu na angependa awe nawe kila wakati lakini kazi hii inakufanya uwe mbali naye hata kwa nyakati zile anazokuhitaji sana” akasema Doreen .Elvis akatabasamu na kusema “Wewe si mtu wa kwanza kuniuliza swali kama hilo.Wengi wananiuliza lakini kazi hii nimeipenda mwenyewe na ninafurahia kuifanya.lakini ni kazi yenye changamotokubwa kwani inanifanya nisimuamini mtu yeyote hata mke wangu na inaniweka mbali na familia na hata mke wangu.Najua anateseka kwa hilo lakini sina namna nyingine” “Sawa nimekuelewa Elvis” Akasema Doreen halafu kikapita kimya kifupi akasema “Elvis leo nitalala hapa.Sitaki kuondoka kuwaacha peke yenu” Usihofu Doreen we’ll be ok.Umefanya kazi kubwa na sasa unapaswa uende ukapumzike” ‘Nitapumzika hapa hapa leo” akasisitiza Doreen.Elvis akamtazama kana kwamba ameshangazwa kwa kitendo kile cha Doreen kuamua kulala pale “Mbona unaniangalia hivyo Elvis? Hutaki nilale hapa? “si hivyo Doreen.Nyumba hii ni kubwa na ina vyumba vya kutosha.Jisikie huru.lakini vipi usalama nyumbani kwako? “Usijali kuhusu nyumbani kwangu.Siku zote ni salama lakini binafsi najihisi ni salama zaidi nikiwa hapa na ninyi.Tukiachana na hayo Elvis kuna jambo nataka nikuombe” “Omba Doreen” Nataka na mimi nije niishi hapa na ninyi.” Elvis akatabasamu na kusema “Are you serious? “Yes I’m serious.Elvis kwa sasa hata mimi najiona siko salama.Tumesafiri safari ndefu toka Mbeya .Vipi kama kuna watu walikuwa wanatufuatilia?Naomba tafadhali uniruhusu nikae hapa pamoja nanyi ili nijihakikishie usalama” akasema Doren.Elvis akamtazama halafu akasema “Uko sahihi.Samahani sana Doreen kwa kukuingiza katika matatizo makubwa.Sin..” Kabla hajamaliza sentensi yake Doreen akamsogelea na kumzika mdomo kwa kidole chake. Shhhhh !!! don’t be sorry.” Akasema Doreen. “I’m going to bed” akasema na kuinuka akaenda katika chumba alichokuwa amekiandaa kwa ajili yake.Elvis naye akainuka akaeleka katika chumba cha maktaba ambacho aliamua kukitumia kama ofisi yake.Akaushika mkoba ule aliopewa na Graca akaufungua na ndani yake kulikuwa na kompyuta ndogo.Akaiweka mezani na kuitazama. “Kazi imeanza” akasema huku akiichomeka kompyuta ile katika umeme na kuiwasha halafu akaanza kufungua faili moja moja kuangalia kilichomo Ilimchukua zaidi ya saa tatu kumaliza kupitia mafaili yote yaliyokuwamo katika kompyuta ile.Uso wake ulikuwa unatoa kijasho chembamba.Akainuka na kuelekea jikoni akachukua chupa ya maji ya kunywa Katika kompyuta ile Elvis alikutana na mambo mengi.Ni kweli kulikuwa na biashara iliyokuwa ikiendelea baina ya baadhi ya maafisa wa jeshi na waasi wa C201 wanaopigana na serikali Kongo.Kwa miaka ya hivi karibuni kundi hili la waasi limeonekana kuwa hatari sana kiasi cha kuilazimisha jumuiya ya kimataifa kutuma kikosi maalum cha wanajeshi wake kwenda kuungana na jeshi la kongo kupambana na waasi hao Kupitia kompyuta ile,Elvis aligundua kwamba kuna mtandao mkubwa unaowahusisha watu wa ndani na nje ya nchi ambao kwa pamoja wamekuwa wakifanya biashara ya silaha na waasi hawa na kuvuna pesa nyingi ikiwemo madini ambayo waasi hubadilishana na silaha Hakukuwa na majina kamili ya wahusika wakuu wa mtandao huu lakini katika kumbu kumbu za barua pepe ambazo Frank alizihifadfhi katika kopmyuta hii zilionyesha alikuwa akifanya mawasilianio na mtu mmoja aliyeitwa Deusdedith m.m.Huyu ndiye aliyeonekana kupewa taarifa za mara kwa mara na Frank.Wakati mwingine ilionekana mtu huyu akitoa maelekezo nini kifanyike.Barua pepe nyingine toka kwa Frank kwenda kwa Deusdedith zilikuwa zikionyesha kiasi cha malipo walichopokea baada ya mauzo ya silaha na mara nyingine kiasi cha madini kilichopatikana kwa kubadilisha na silaha.Viambatanisho vya miamala ya fedha vilionyesha kwamba malipo yalikuwa yakifanyika kupitia benki moja iliyopo Uswisi.Ilionyesha kuna watu waliokuwa wakikifadhili kikundi hiki cha waasi cha C201 toka nje ya Congo Kitu kingine alichokigundua Elvis ni kwamba silaha hizo huja nchini kama silaha za jeshi la Congo na husafirishwa kama vile zinakwenda Congo lakini huishia katika mikono ya waasi. “Watu hawa wana roho za kinyama sana.Hawana ubinadamu hata kidogo.Kitendo cha kuwauzia silaha waasi hawa ni kitendo kisichovumiliwa kwani wamekuwa wakizitumia silaha hizi katika mauaji ya raia wasio na hatia.Miezi miwili iliyopita tumezika wanajeshi wetu watatu waliouawa na waasi hawa kwa silaha hizi hizi zinazouzwa na akina Frank.Kibaya zaidi hata ndani ya jeshi la Congo kuna watu ambao wanahusika na biashara hii.Hili ni jambo zito mno” akawaza Elvis “Graca ni msichana shujaa na anastahili kupongezwa kwa kitendo chake cha ushujaa alichokifanya.Bila yeye katu jambo hili lisingefahamika na ndugu zetu wa Congo wangeendelea kuteseka na kuuawa kila uchao.Mateso yote aliyoyapata hayatakwenda bure.Lazima wale wote wanaohusika na biashara hii haramu wafikishwe mbele ya sheria.Ninaapa sintaulaza mgongo wangu kabla ya wahusika hawa wote kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.” Akawaza huku akiendelea kupitia kumbu kumbu za mawasilianoya Frank Katika barua pepe moja iliyotoka kwa Deusdedith m.m alimwelekeza Frank kuna mtu ambnaye ameona anaweza akafaa katika mpango wao wa kumuua kanali Norman Sulayi ambaye alianza kuonekana kuwa hatari kwao.Alimtumia namba za simu za mtu huyo ambaye alimtaja kama kahaba alyekubuhi aitwaye Victoria mapenzi.Alimtaja kuwa ni kahaba ambaye amekuwa akitumiwa na vigogo na watu matajiri kwani gharama zake ni kubwa na ni mwanamke mzuri sana.Elvis alistushwa na taarifa ile “Kanali normal alikufa katika mazingira tata mno.Mpaka leo sababu ya kifo chake haijajulikana.Sasa nimepata picha halisi inaonekana naye alikuwamo katika mtandao huu na walionekana kutofautiana hivyo wakaona ni vyema kama wakimuua.Na walimuua kwa kumtumia kahab huyu …dah !Mtandao huu unaonekana hatari mno.Huyu Deus ni nani? Akajiuliza Elvis “Lazima nihakikishe watu hawa wanafahamika” akachukua simu yake akaziandika namba za simu za Victoria mapenzi na kupiga.simu ikaita lakini haikupokelewa,akapiga tena na safari hii ikapokelewa “hallow” ikasema sauti nzuri ya mwanamke upande wa pili “Hallow habari yako.Naongea na Vicky? “Ndiyo.Wewe ni nani? “Naitwa Robin.” Elvis akadanganya “Unahitaji nikusaidie nini Robin usiku huu? Kama ni huduma usiku huu wa leo sina nafasi labda kesho” “Vicky sihitaji huduma ya mwili lakini kuna mambo Ambayo nataka nizungumze nawe.Nitakulipa vizuri sana” “Mambo gani hayo? Akauliza Vicky “Siwezi kukwambia simuni hadi tutakapoonana ana kwa ana” “sawa.Tuonane kesho saa tatu kamili katika hoteli yangu inaitwa Angel Vicky hotel.Umesema unaitwa Robin? “Ndiyo.naitwa Robin” “Sawa Robin,ukifika utajitambulisha mapokezi na utaletwa moja kwa moja ofisini kwangu.Nitawapa taarifa zako.Kumbuka ni saa tatu kamili juu ya alama.Ukichelewa zaidi ya hapo sintakuwa na muda na wewe kwani nina watu wengi wa kuonana nao” akasema Vicky na kukata simu “Natumai kupitia kahaba huyu ninaweza kupata kitu cha kunisaidia kumfahamu huyu Deus ni nani.Yeye anachokijali ni fedha kwa hiyo kwa kutumia fedha ninaweza kupata mambo mazuri toka kwake” Akawaza Elvis na kuendelea na kazi yake “Ndiyo maana Frank alikuwa radhi kumuona mwanae akiteseka na alikuwa tayari hata kumtoa uhai wake kwa sababu ya nyaraka hizi muhimu muhimu.” Akawaza Elvis na alipotazama saa yake tayari ilikuwa ni usiku wa manane.Akaizima kompyuta ile na kuelekea chumba cha kulala. ***************** Dr Steven aliendesha gari taratibu huku akijiuliza kitu kilichomsibu Patricia.Toka amefahamiana naye hakuwahi kumuona akiwa katika hali hii.Siku zote Patricia alikuwa mcheshi na mwenye furaha lakini hali aliyokuwa nayo usiku huu ilimtia hofu sana Dr Steven na kumpa hamu ya kutaka kufahamu kile kilichomsibu rafiki yake huyu mkubwa hapa Tanzania ili aone namna ya kumsaidia “Lazima Patricia amepatwa na jambo zito sana .Kwa muda huu mfupi niliofahamiana naye nimegundua ni mwanamke jasiri lakini kitendo cha kumuona akiangusha machozi usiku huu kimenistua sana.Kwa nini mrembo huyu amwage mwachozi?Nini kimemsibu? akawaza Dr.Steven Hakulifahamu vyema jiji la Dar hivyo alikuwa anaendesha taratibu huku akijaribu kuangaza angaza akitafuta hoteli nzuri ambayo angempeleka Patricia kupumzika “Angel Vicky hotel” Dr Steven akalisoma bango kubwa pembeni ya barabara. “Inaonekana ni hoteli nzuri ambayo Patricia anaweza akapumzika ngoja nimpeleke hapa” akawaza Dr Steven akapunguza mwendo wa gari na akaingia katika hoteli ile iliyokuwa na mandhari ya kuvutia mno “Hapa panaweza kukufaa kupumzika usiku wa leo? Dr Steven akamuuliza Patricia wakiwa katika maegesho ya magari “Ndiyo panafaa.Ninachokihitaji mimi ni kuwa mbali na nyumbani tu” akasema Patricia halafu wakashuka na kuelekea hotelini wakapatiwa chumba namba 102 ghorofa ya tano.Baada ya kuingia katika chumba hicho,Patricia akaelekea bafuni,akajitazama katika kioo machozi yakamtoka “Sikutegemea kama siku moja nitaumizwa kiasi hiki.Uko wapi Elvis? Laiti ungekuwepo ungenifariji na mateso haya niyapatayo.Kwa mara ya kwanza leo toka tumeoana ninaiona nyumba yangu chungu na ninalala nje.Maneno yale ya mama yameniumiza mno.I’m deeply hurt and I need someone to comfort me” akawaza Patricia halafu akajifuta machozi na kurejea chumbani akaketi sofani“Ungependa kutumia kinywaji chochote nikuagizie Patricia? Akauliza Dr Steven “naomba mvinyo wowote tafadhali’ akasema Patricia na Dr Steven akapiga simu akaomba waletewe mvinyo “Patricia toka nimefika hapa Tanzania wewe ndiye uliyenipokea na kunisaidia nimeyafahamu na kuyazoea mazingira kwa haraka.Ni furaha yangu kukutana na mtu kama wewe ambaye ni rafiki wa kila mtu ,usiyekaukiwa tabasamu usoni lakini usiku wa leo nimestuka kukuona ukilia.Nimeogopa na nimejiuliza maswali http://deusdeditmahunda.blogspot.com/mengi kulikoni ukawa katika hali hii?Kitu gani kimekusibu?Tafadhali naomba unieleze Patricia nini kimekupata? Una tatizo gani? Niko hapa kukusaidia nieleze tafadhali” akasema Dr Steven Mvinyo ukaletwa Patricia akamimina katika glasi akanywa na kumtazama Dr Steven kisha akasema “Siku ile nilisimama mbele ya Altare ya Mungu na mbele ya mashahidi nikaulizwa kama nitakuwa tayari kusimama imara na kuvumilia katika taabu na shida,furaha na huzuni nikajibu kutoka moyoni kwamba nakubali .Sikujua kama ningekutana na kipindi kigumu katika maisha yangu ya ndoa kama ninachokabiliana nacho sasa” akasema Patricia Nini kimetokea katika ndoa yako Patricia?Umekwaruzana na mumeo? Akauliza Dr Steven “Hapana sijakwaruzana na mume wangu.Elvis ananipenda mno na kamwe hatuwezi kukwaruzana” “Nini basi kimekupata hadi ukawa katika hali hii? Akauliza Dr Steven Patricia akafikiri kidogo na kusema “Mimi na mume wangi mpaka leo hatujabahatika kupata mtoto.Hilo limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa ndugu za mume wangu.Wamekuwa wakinitolea maneno machafu ya kejeli na kuniumiza sana.Nyumba yangu kwa sasa naiona chungu ndiyo maana nimeamua kuja hapa hotelini kupumzika na kutuliza akili yangu” “Pole sana.Kwa nini mpaka leo hamjabahatika kupata mtoto? Akauliza Steven.Patricia akamueleza kila kitu kuhusu historia yake na kwa nini hawezi kupata mtoto.Dr Steven akaguswa sana na histotia ile ya patricia akamsogelea akamkumbatia kumfariji “Pole sana Patricia.Historia yako imenigusa sana hata mimi.Ndugu za mumeo hawapaswi kukutenda hivi.Mnaonaje endapo wewe na mumeo mkawaeleza hali halisi kwamba hamuwezi kupata mtoto? Akauliza Dr Steven “Hilo ni kosa tulilolifanya toka mwanzo kutokuwaeleza ukweli.Laiti kama tungewafahamisha ukweli kusingekuwa na matatizo haya yote” akasema Patricia .Baada ya muda Dr Steven akauliza “Mumeo yuko wapi? Alitakiwa awe nawe katika kipindi kigumu kama hiki” “Yuko safarini kikazi.Ana safiri mara kwa mara .Muda wake wa kukaa nyumbani ni mdogo sana na ndiyo maana umeona leo nimeshindwa kuvumilia kukaa nyumbani mwenyewe nimeamua nije nipumzike mbali na nyumbani.” akasema Patricia na kumtazama Dr Steve “Steven umewahi kuhisi upweke hadi ukajiona kama uko peke yako duniani? “Ndiyo.Nimewahi kupitia kipindi kigumu kama hicho cha upweke mkubwa pale mke wangu Laura alipofariki kwa ajali ya ndege miezi miwili tu baada ya kufunga ndoa.Nilihisi dunia nzima imenitenga .Ilinichukua muda mrefu kidogo kurudia katika hali yangu ya kawaida kwa hiyo ninaelewa hali unayokabiliana nayo kwa sasa” akasema Dr Steve. Ukapita ukimya na baada ya muda akauliza “Patricia unataka nikusaidie nini katika jambo hili linalokuumiza?Niko tayari kukusaidia kitu chochote hata kama ni kwenda kuzungumza na mama mkwe wako niko tayari” akasema Dr Steven “Ahsante sana Steven lakini ninachokihitaji ni kuufanya usiku wangu wa leo kuwa mzuri.Kwa masaa haya machache nataka niyasahau mateso yangu” akasema Patricia na kumkumbatia Dr Steven akambusu.Alionekana kulemewa na kilevi na hakujali alichokuwa anakifanya. “Patricia una hakika unataka kufanya hivi? Akauliza Dr Steven kwa wasi wasi Patricia hakujbu kitu akaendelea kumbusu Steven huku akimfungua vifungo vya shati.Tayari alikwisha dhamiria kufanya kitendo kile na Dr Steven.Mara moja Dr Stene naye mashetani yake yakaamka akaanza kutoa ushirikiano. “Kama kwa kufanya hivi nitakuwa namsaidia kuyapooza machungu yake ya moyo ngoja nimsaidie” akawaza Dr Steven ********************** Saa kumi na mbili za asubuhi ilimkuta Elvis akiwa tayari ameamka.Macho yalikuwa mazito kutokana na kulala kwa muda mchache.Taratibu akajizoa zoa pale kitandani akanywa maji kisha akapiga magoti na kumshukuru Mungu kwa siku mpya na kumuomba amuongoze kumlinda katika kazi ngumu iliyoko mbele yake.Hakusahau pia kumuombea mke wake Patricia ili aweze kuwa salama hasa katika kpindi hiki ambacho atakuwa mbali naye kutokana na kazi nzito inayomkabili.Alipomaliza kufanya maombi yale akachukua simu yake akaiwasha na kumpigia simumke wake Patricia lakini bado simu yake haikuwa ikipatikana.Kichwa chake kikajaa mawazo mengi “Nina hakika atakuwa salama.Yawezekana atakuwa ametingwa na kazi nyingi” akawaza Elvis na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha Graca akabonyeza kengele ya mlangoni,mlango ukafunguliwa.Uso wa Graca ulikuwa na tabasamu kubwa “Elvis karibu.Habari za asubuhi? “Habari nzuri sana Graca.Umeamkaje?Samahani kwa kukuamsha” “Usijali Elvis.Nimekwisha amka kitambo nilikuwa natazama runinga.Umemkaje wewe? “Nimeamka salama.Endelea kupumzika nimepita kukujulia hali na kukutaarifu kwamba baadae nitatoka kuna mahala nina kwenda utabaki hapa na Doreen” “Sawa Elvis.Kwa sasa nina amani kwani tayari mzigo wote nimekwisha utua kwako.” Akasema Graca na kumfanya Elvis atabasamu kisha akaelekea katika chumba alicholala Doreen.Mlango ulikuwa wazi lakini Doreen hakuwemo chumbani.Akaelekea jikoni na kumkuta Doreen akiwa katika harakati za kuandaa kifungua kinywa. “Habari za asubuhi Doreen” Elvis akamsalimu “Nzuro Elvis.Umeamkaje? “Nimeamka salama kabisa” akasema Elvis aliyekuwa akimkodolea macho Doreen ambaye alikuwa amevaa gauni fupi sana na kuyaacha mapaja yake meupe yaonekane.Doreen akageuka na kukuta akitazamwa na Elvis “Mbona unaniangalia namna hiyo Elvis? Akauliza Doreen.Elvis akatabasamu kidogo na kusema “Nategemea kutoka asubuhi hii kuna sehemu ninakwenda.Kuna jambo nataka unisaidie” “Sema chochote Elvis nitakusaidia” akasema Doreen huku akitabasamu ‘Nimejaribu kumpigia simu Patricia asubuhi ya leo lakini bado simu yake haipatikani.Naomba baadae unisaidie kumtafuta na uhakikishe yuko salama na kamwe usimweleze chochote kuhusu kinachoendelea” “sawa Elvis nitafanya hivyo” “Ahsante Doreen” Akasema Elvis na kwenda kujiandaa. “Ilipotimu saa moja na robo tayari alikuwa amejiandaa akapata kifungua kinywa kisha akaondoka. Kabla ya kwenda kuonana na Vick kama walivyokubaliana usiku,Elvis akapita kwanza ofisini kwao ili kutoa taarifa kwa mkurugenzi wake kwamba amekwisha rejea toka safari.Saa mbili na dakika nane akawasili katika jengo la idara yao.Tayari wafanyakazi wengi walikwisha fika na kila mmoja alitaka kusalimiana na Elvis kwani alipendwa na kila mmoja.Alisalimiana nao haraka haraka halafu akaelekea kwa mkurugenzi wake “Karibu sana Elvis.Pole na safari” akasema mzee Meshack Jumbo mkurugenzi wa idara ya ujasusi Tanzania baada ya Elvis kuingia ofisini kwake “Ahsanate sana mzee” akasema Elvis. “Vipi safari yako ilikuwa na mafanikio? Akauliza “Ndiyo mzee Ilikuwa na mafanikio makubwa sana.Kila kitu kimekwenda kama nilivyotarajia” “Good.nadhani sasa ni wakati wa kunieleza nini hasa unachokichunguza” akasema mzee Meshack “mzee nilikuahidi kukueleza kila kitu pindi nitakaporejea lakini naomba kwa sasa unipe nafasi ili nikaonane na mtu mmoja muhimu sana katika jambo hili ambaye nimeahidiana kuonana naye saa tatu kamili asubuhi hii.Mara tu baada ya kuonana naye nitakuja hapa kukueleza ni jambo gani ninalolifuatilia.Kwa ufupi tu ni kwamba ni jambo kubwa na zito” akasema Elvis.Mzee Meshack Jumbo akamtazama kwa makini halafu akasema “Sawa Elvis.Nenda kaonane na huyo mtu na ukioshaonana naye urudi hapa.Nitakusubiri kutaka kulifahamu suala hilo” akasema mkurugenzi “Ahsante mzee” akasema Elvis na kutoka huku akiitazama saa yake.Hakutaka kuchelewa miadi yake na Victoria .Wakati akielekea katika gari lake akasikia mtu akimuita.Akageuka na kukutana na Sofia “Sofia ! akasema Elvis “Elvis kuna kitu nimesahau kukwambia.Kuna mtu mmoja anaitwa Pascal ni mfanyakazi wa idara ya usalama wa taifa amekuwa ananipigia simu kukuulizia na akadai kwamba kuna jambo anataka kukueleza.Nadhani ingekuwa vyema kama ungeonana naye” “Ahsante sana Sofia kwa taarifa hizo.Nitalishughulikia suala hilo” akasema Elvis na kuingia garini “Tayari Pascal amekwisha fahamu kwamba ninahusika kwa namna Fulani kupotea kwa Graca.Mapambano yameanza” akawaza Elvis akiwa garini kuelekea Angel Vicky hotel kuonana na Victoria kahaba anayetajwa kuwa na utajiri mkubwa Saa tatu kasoro dakika kumi,tayari alikuwa analitazama jengo la ghorofa saba ambalo juu yake kulikuwa na maandishi makubwa Angel Vickly hotel.Ni moja kati ya hoteli nzuri jijini Dar es salaam. “Hoteli nzuri sana hii.Ni kweli kazi ya ukahaba ndiyo imemuwezesha Vick kumiliki hoteli kubwa namna hii? Hapana lazima kuna kazi nyingine anaifanya na kazi ya ukahaba atakuwa anaitumia kama mwavuli kuficha kazi zake nyingine zinazompatia fedha nyingi.Kuna ulazima wa kumfanyia uchunguzi







na kumfahamu vyema lakini kwanza ngoja nitafute taarifa za kuhusiana na mtandao wa akina Frank” Akawaza Elvis.Akaegesha gari na kushuka akaelekea moja kwa moja mapokezi ambako alijitambulisha kama Robin na ana miadi ya kuonana na Vicky.Mmoja wa wasichana aliyekuwa mapokezi akainua simu na kupiga sehemu Fulani na baada ya dakika mbili akaja mwanadada mmoja aliyependeza kwa mavazi aliyovaa akamchukua Elvis na kumpeleka katika chumba kimoja kikubwa “Madam amesema umsubiri hapa anakuja sasa hivi” akasema Yule muhudumu na kutoka “Haiwezekani kabisa mtu anayefanya biashara ya ukahaba akamiliki hoteli kama hii.Uchunguzi wa kina unahitajika hapa.Lazima kuna mambo mazito yanayoendelea kuhusu huyo kahaba yanayotakiwa kuchunguz………………” akaondolewa mawazoni baada ya mlango kufunguliwa na mwanamke mmoja mrefu mwembamba mwenye weupe wa kung’aa kuingia.Alivaa suti fupi nyeusi kiasi kwamba sehemu kubwa ya mapaja yake ilikuwa wazi.Alikuwa na nywele ndefu alizozibana kwa nyuma.Uzuri wake ulimstua kidogo Elvis.Hakutegemea kabisa kama Vicky angekuwa mzuri vile. “Hallo Robin.Karibu sana” akasema Vicky kwa sauti laini sana huku uso wake ukipambwa na tabasamu pana.Kati kati ya meno yake meupe kulikuwa na mwanya uliozidi kumpendezesha kimwana huyu hasa anapotabasamu. “Hivi ni kweli huyu ndiye kahaba Victoria? Akawaza Elvis wakati akimpa mkono Vicky ambaye vidole vyake vyote vilichafuka kwa pete za dhahabu. “hallo Vicky” akasema Elvis “karibu sana”akasema Vicky na kuketi katika sofa akitazamana na Elvis “Ahsante sana” akajibu Elvis “You are so handsome.Sina hakika kama tumewahi kuonana.Ulipataje namba zangu? Namba ile huwa naitoa kwa watu wachache sana na wa muhimu tu” akasema Vicky Usijali Vicky nimeipata wapi namna yako lakini fahamu tu wewe ni mtu maarufu sana hapa mjini na kwa kuwa nilikuwa na shida na wewe nilihangaikahadi nikaipata namba yako” akasema Elvis na Vicky akatabasamu “Nikusaidie nini Robin? Akauliza Vicky “Kama nilivyokueleza jana usiku simuni kwamba shida yangu mimi ni tofauti kidogo na huduma unayotoa lakini nitakulipa vizuri sana na wewe utafurahi” akasema Elvis “Nieleze ni shida gani hiyo ili nione namna ninavyoweza kukusaidia.Kitu kingine uko tayari kwa gharama zangu? “Usihofu kuhusu gharama.Ninafahamu unatoza kiwango cha juu cha pesa kwa watu unaowahudumia kwa hiyo nimekwisha jiandaa kwa hilo” akasema Elvis. “Gharama zangu ni kubwa na ndiyo manaa huwa ninahudumia watu maalum tu.Nitakapoisikia shida yako nitajua nikutoze kiasi gani” akasema Vicky huku uso wake ukiendelea kuwa na tabasamu lisilokauka.Elvis akasema “Shida yangu mimi si kubwa.Kuna taarifa naihitaji toka kwako” “taarifa gani Robin? “Unamfahamu mtu mmoja anaitwa Norman? “Norman?!! Vicky akastuka sana na lile tabasamu lake likatoweka “Ndiyo.Alikuwa kanali wa jeshi” Vicky bado alionyesha mstuko mkubwa.Akafikiri kidogo halafu akasema “Sina kumbu kumbu ya kumfahamu mtu yeyote anayeitwa Norman.Mimi huwa nahudumia watu wengi na wengi wao ni watu wenye nyadhifa na wafanya biashara wenye pesa.Sina kumbu kumbu za wateja wangu kwani huwa ninapata wateja wapya karibu kila siku.Nani kakueleza kwamba ninamfahamu mtu huyo? Akauliza Vicky Elvis akamtazama kwa makini na kuuliza “kanali Norman amekwisha fariki dunia na siku aliyofariki dunia ulionekana naye.Unaweza kukumbuka chochote? Sura ya Vicky ikaonyesha kukashirishwa kwa swali lile “Robin mambo gani hayo unayaongea.Tafadhali naomba usinipotezee wakati wangu kwa upuuzi huo unaonieleza.Nina mambo mengi sana ya kufanya na sina muda mchafu.Kama hauna jambo la maana la kunieleza tafadhali inuka uende zako” akasema Vicky kwa ukali “Tafadhali usikasirike Vicky.Sina lengo baya kwa maswali yangu.Ninahitaji tu kumfahamu mtu huyo” akasema Elvis “Unataka kumfahamu ili iweje? Wewe ni polisi? Umetumwa kunipeleleza? Akafoka Vicky Hapana Vicky mimi si polisi wala sina nia yoyote mbaya.Naomba tu unieleze kama unamfahamu mtu huyo na nikulipe pesa zako tumalize biashara yetu.Niambie nikulipe shlingi ngapi kwa ajili ya taarifa hiyo? Akauliza Elvis. “Robin nadhani mimi na wewe hatuna cha kuzungumza tena.Nakuomba utoke uende zako.Mambo unayoyaongea mimi siyaelewi kabisa.Taarifa za namna hiyo ulipaswa kuwauliza polisi na si mimi.Tafadhali naomba uondoke.Sina muda wa kupoteza na wewe!! Akasema kwa ukali huku akimuelekezea Elvis mlango “Unamfahamu Deusdedith? Elvis akauliza Swali lile likazidi kumpandisha hasira Vicky akamtazama Elvis kwa jicho la chuki kana kwamba anataka kumvamia na kumrarua “Naomba uondoke haraka sana kabla sijaita walinzi wangu wakutoe kwa nguvu humu ndani.!! Akasema Vicky na Elvis akainuka “sawa ninaondoka Vicky .Naomba ufikirie nilichokuomba .Nitakupigia simu kujua umefanya maamuzi gani.Kumbuka nitakulipa fedha nyingi kwa taarifa hiyo.More than ten million” akasema Elvis na kutoka nje akimuacha Vicky akiwa amefura kwa hasira “Huyu mtu ni nani? Amezipataje taarifa hizi? Tayari nilikwisha sahau kuhusu Norman lakini yeye amenikumbusha kila kitu.Amejuaje kama nilionekana na Norman siku ile?Inaonekana suala lile tayari limevuja.Inaonekana kuna watu wanaanza kulichunguza suala hili na huyu Robin ni mpelelezi.Ngoja nimpigie simu Frank nimtaarifu.Niliwaonya toka mwanzo wahakikishe siingii katika matatizo na wakaahidi kufanya hiyo lakini mamabo yamebadilika tofauti na tulivyokubaliana.They must do something.Sitaki kuingia katika matatizo kwa sasa” akawaza Vicky huku macho yake yakionyesha woga wa wazi.Akainua simu na kwa haraka akampigia Frank “hallow Frank” akasema Vicky baada ya Frank kupokea simu hallow Vicky.habari za siku? Akauliza Frank “Mi mzima sijui wewe” “Niko salama.Nimeshangaa leo umenipigia simu asubuhi asubuhi namna hii.Kwema huko? Akauliza Frank ‘Frank kuna tatizo limetokea asubuhi hii” “Tatizo gani Vicky? “Ni kuhusiana na lile suala la Norman” “Norman ?!! Frank akashangaa “Ndiyo.Kuna mtu alinipigia simu jana usiku anaitwa Robin akaniomba tuonane leo .Nilidhani ni mteja mpya na alipofika alianza kuniuliza Kama ninamfahamu Norman.Nilistuka sana kwani suala lile tayari nilikwisha lisahau.Nilimkatalia kwamba simfahamu Norman,akaendelea kusisitiza kwamba nilionekana nikiwa na Norman siku ile alipofariki.Nilichanganyikiwa nikapandwa na hasira ikanilazimu kumtimua.Wakati akiondoka akaniuliza tena kama ninamfahamu Deusdedith nikachanganyikiwa zaidi.Frank mliponika kazi mlinihakikishia kwamba katu suala hili haliwezi kujulikana lakini tayari kuna watu wamekwisha hisi kwamba ninahusika na kifo kile cha kanali Norman.Nimechanganyikiwa na sijui nifanye nini.Mtu Yule anaonekana ni mpelelezi na anafahamu mambo mengi kuhusiana na kifo cha Norman .Tafadhali Frank naomba ufanye kila linalowezekana kuhakikisha siingii matatizoni” akasema Vicky akiwa katika hali ya wasi wasi mwingi.Suala lile likaonekana kumstua sana Frank,akavuta pumzi ndefu na kusema “Kijana mwenyewe yukoje? Umewahi kumuona? “Ni mara yangu ya kwanza kumuona .Namna alivyo kwa kweli ninashindwa kumuelezea.Please do something Frank.I don’t want trouble .Ulinihakikishia kwamba hakutakuwa na tatizo loloye sasa matatizo yameanza.Please help me!!! Akasema Vicky Kimya cha sekudne kadhaa kikapita kisha Frank akasema “Ok usiogope Vicky.Ninakuja hapo sasa hivi naomba unisubiri” akasema Frank na kukata simu ***************** Dr Steven ndiye aliyekuwa wa kwanza kustuka toka usingizini.Akatazama saa iliyoonyesha ni saa mbili kasoro dakika kumi za asubuhi.Pembeni yake alilala Patricia ambaye alionekana bado kuwa katika usingizi mzito.Dr Steven akamtazama kwa makini na kutabasamu “Patricia ni mwanamke mrembo sana.Hata akiwa usingizini bado uzuri wake wa asili unaonekana.Analala kama malaika.Anatabasamu hata akiwa usingizini” akawaza Dr Stenven huku akizichezea nywele za Patricia. “Kwa nini mwanamke kama huyu anateseka kiasi hiki?Patricia ana kila sifa nzuri kiasi kwamba namuonea wivu mwanaume aliyemuoa.Inaoenakana mwanaume huyo bado hajaiona thamani ya Patricia na ndiyo maana anadiriki hata kumuacha peke yake kwa wakati huu ambao anamuhitaji sana awe karibu yake.Kama angekuwa ni mke wangu kamwe nisingekubali kumuacha peke yake hasa kwa wakati huu” akawaza Dr Steven huku akitabasamu Wakati Dr Steven akiendelea kumtazama,Patricia akaamka akafikicha macho na kutazama pembeni. Alikuwa mtupu na pembeni yake alikuwepo Dr Steven naye akiwa mtupu.Patricia akahisi aibu kubwa “What have I done?!! akawaza “Unajisiaje Patricia? Akauliza Dr Steven.Patricia hakujibu kitu akazama mawazoni na macho yake yakaonekana kujaa machozi “Nyamaza kulia Patricia.Usiianze siku yako kwa machozi” akasema Dr Steven “Steven ,moyo wangu unauma sana kwa kitendo nilichokifanya.Sikuwahi kufikiria kabisa kwamba siku moja nitaisaliti ndoa yangu.Nimemkosea sana mume wangu kwa kitendo hiki” akasema Patricia Usiumie moyo Patricia na wala usijilaumu.Anayepaswa kulaumiwa ni mumeo ambaye naweza kusema kwa kiasi kikubwa ndiye aliyesababisha ukawa katika hali hii.Amekuacha katika wakati ambao unamuhitaji sana.Yeye ndiye aliyetakiwa kuwa karibu yako katika wakati huu mgumu.Alitakiwa asimame nawe akufariji na akupe moyo wa kupambana na majaribu yote unayokumbana nayo katika maisha yako hivi sasa.Hukuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutafuta liwazo la moyo.Ingekuaje endapo ungekuwa peke yako kwa usiku wa jana? Lolote baya lingeweza kutokea kutokana na hali uliyokuwa nayo” akasema Dr Steven Nakubali jana nilikuwa na hali mbaya sana na nisingeweza kuwa mwenyewe lakinikwa hili nililolifanya nilivuka mipaka.Moyo wangu unaumia sana kwa kitendo hiki nilichokifanya na nitateseka hadi siku naingia kaburini” akasema Patricia “Patricia jambo hili limekwisha tokea na kinachotakiwa hapa ni kuyaruhusu maisha yaendelee.Amka na ujiandae nikupeleka nyumbani ukajiandae kwa ajili ya kuelekea kazini” “Hapana Dr Steven.Leo sintaingia kazini.Siwezi kufanya kazi nikiwa katika hali ya mawazo namna hi.Nahitaji kupumzisha akili yangu.Halafu kuna jambo nataka nikuombe Omba chochote Patricia” “Naomba mtu yeyote asifahamu chochote kuhusiana na hiki tulichokifanya.Hii ibaki siri yetu peke yetu na jambo kama hili lisijirudie tena” “Usihofu Patricia.Hakuna mtu atakayefahamu na wala halitajirudia tena lakini muda wowote ukihitaji mtu wa kukuliwaza au kumweleza kile kinachokusibu mimi nipo nieleze na nitakusaidia” akasema Dr Steven.Patricia akainuka akaenda bafuni kuoga ***************** “Sasa nina uhakika mkubwa kwamba Vicky ana mahusiano na mtandao wa akina Frank na ni wazi anamfahamu mtu huyo anayeitwa Deusdedith kwani ndiye aliyemtumia katika kumuua Kanali Norman.Nimepata sehemu nzuri ya kuanzia.Huyu Vicky atanisaidia kumfahamu Deus.Kwa sasa ngoja niende kwa mkurugenzi ana hamu ya kutaka kujua kile ninachokichunguza” akawaza Elvis huku akielekea eneo la maegesho baada ya kutoka kuonana na Vicky.Wakati akiligeuza gari lake kwa ajili ya kuondoka eneo lile mara akastushwa na kitu alichokiona akabaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa.Katika mlango wa kuingilia pale hotelini watu wawili mwanaume na mwanamke walikuwa wanatoka “Am I dreaming? Thats Patricia my wife !! akasema Elvis kwa sauti ndogo “Hii si ndoto na wala sijafananisha .Kweli yule ni Patricia.Amefuata nni hapa hotelini? halafu mbona hayuko kikazi,mavazi yale aliyoyavaa hupenda kuvaa tunapotoka usiku au kwenda katika sherehe .Alipaswa kuwa kazini muda huu,hapa amefuata nini? Akajiuliza Elvis.Akabaki ameduwaa Patricia na Dr Steven walielekea mahala walikoegesha gari,wakaingia katika gari la Patricia wakaondoka.Dr Steben ndiye aliyekuwa akiendesha gari lile Yule ni Patricia mke wangu nimemshuhudia kwa macho yangu akitoka hotelini akiwa na mwanaume.Ametoka kufanya nini hapa?halafu toka jana simu yake haipatikani.Whats going on? Si kawaida yake kabisa kuzima simu”Akawaza Elvis huku gari la Patricia likivuka geti na kuingia barabara kuu.Bado Elvis alikuwa katika mshangao.Alilitazama gari la Patricia likitokomea akachukua simu na kuzitafuta namba za Patricia akampigia lakini bado simu haikuwa ikipatikana.Akaamua kumpigia simu mtumishi wao wa ndani Stella “kaka shikamoo” akasema Stella Marahaba Stella,habari za hapo nyumbani? “habari nzuri.Pole na kazi” “Ahsante sana Stella.Dada yako yupo hapo nyumbani? ‘Hapana hayupo” “Amekwenda kazini? Stella akababaika kidogo na kushindwa ajibu nini kwani hakujua Patricia alikwenda wapi “Mbona hunijbu Stella?Nimekuuliza dada yako amekwenda kazini? “Hapana sifahamu kaka” “Hufahamu?Hukuwepo wakati anaondoka? Akauliza Elvis kwa ukali kidogo na kumfanya Stella aogope “Kaka naomba niseme ukweli.Dada Patricia aliondoka jana jioni lakini hakuniaga anakwenda wapi na mpaka sasa bado hajarejea” akasema Stella “Ulivyomuona wakati anaondoka alikuwa anaenda kazini? “Hapana kaka,sina hakika kama alikuwa anakwena kazini kwani alivaa gauni la kutokea usiku” Elvis akavuta pumzi ndefu na kuegemea kiti halafu akasema “Ahsnte Stella.Naomba usimweleze kama nimekupigia simu” akasema Elvis na kukata simu.Akazama katika mawazo mengi halafu akampigia simu Doreen “hallow Elvis” akasema Doreen baada ya kupokea simu “ Doreen ,tayari umeondoka hapo nyumbani? Ndiyo Elvis.Nimekwisha ondoka nimemuacha Graca anapumzika.Ninataka nielekee kazini nikaombe likizo ya dharura ya mwezi mmoja.Vipi kuna mahala unataka unitume? “Nakukumbusha tafadhali usisahau kwenda kumuona Patricia” “Hapana Elvis siwezi kusahau.Nikimaliza mizunguko yangu nitakwenda kuonana naye” akasema Doreen “Ahsante Doreen” akasema Elvis na kukata simu akaizima kabisa “Siku yangu imeanza vibaya.Ngoja kwanza nikaonane na mkurugenzi halafu nitajua nini cha kufanya.I’m so confused right now.Patricia hakulala nyumbani jana na leo hii ninamshuhudia akitoka hotelini akiwa ameongozana na mwanaume.Je alilala pale hotelini? Yule mwanaume aliyekuwa naye ni nani? Akajiuliza maswali na kukosa majibu akaondoka ****************** Baada ya kutoka hotelini kwa Vicky,Elvis akaelekea moja kwa moja ofisini kwa mkurugenzi wake Mr Meshack Jumbo.Mara tu baada ya kushuka garini hakutaka maongezi na mtu akaelekea moja kwa moja ofisini kwa mkuu wake “Karibu Elvis” akasema Mr Meshack “Ahsane sana mzee” akajibu Elvis na kuketi.Mkurugenzi akafunika faili alilokuwa analipitia na kumtazama Elvis “Nadhani umekuja kunifahamisha kile ambacho umekuwa unakichunguza” akasema mkurugenzi,Elvis akamueleza kila kitu hadi alipofikia.Kimya kikatawala mle ofisini alipomaliza kutoa maelekezo yake kwa mkurugenzi. “Kuna nyakati niliwahi pata fununu toka kwa mtu mmoja aliyeko ndani ya serikali ya Congo kwamba waasi wanaopambana na serikali yao wana silaha kali ambazo zinapitia Tanzania.Taarifa hiyo ilidai kwamba kuna mtandao wa watu wanaofanya biashara hiyo walioko Tanzania na ndani ya serikali ya Congo DRC.Sikuzipa uzito mkubwa sana taarifa hizo kwa kuwa sikuwa nakiamini sana chanzo hicho cha taarifa lakini kwa hili ulilonieleza leo ninaamini kwamba jambo hili kweli lipo.Hii ni aibu kwetu,aibu kwa nchi yetu ambayo jeshi lake limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inapatikana Congo lakni kuna watu ndani ya serikali wanawauzia silaha waasi.Hili ni suala zito Elvis” akaseam Meshack na kukuna kichwa .Taarifa ile ilimstua sana “Elvis suala hili ni suala zito na lazima tumtaarifu rais haraka ili kwa pamoja tujue nini cha kufanya na tuudhibiti mtandao huu haraka iwezekanavyo” akasema Meshack Jumbo huku akiinua mkono wa simu na kutaka kubonyeza namba,Elvis akamzuia “Mzee usimtaarifu kwanza rais.Hatuwezi kufanya hivyo kwa sasa.Tunachtakiwa kufanya ni kuanza kwa uchunguzi ili tuufahamu kwa kina mtandao huo ndipo tumtaarifu rais.Kuna uwezekano mtandao huu ukawahusisha watu wazito serikalini kwa hiyo tukimtaarifu rais mapema kabla hatujawafahamu inaweza ikavuruga uchunguzi wetu” akasema Elvis.Meshack Jumbo akamtazama Elvis na kusema “Elvis hili ni jambo zito la kitaifa na hatuwezi kuendelea nalo bila kiongozi wa nchi na amiri jeshi mkuu kulifahamu” akasema Meshcak Nakubaliana nawe mzee kwamba jambo hili ni zito sana na kuna ulazima wa kumtaarifu rais lakini kwa sasa sidhani kama ni muda muafaka kwa yeye kulifahamu.Nipe muda zaidi niendelee kufanya uchunguzi wangu na baada ya kupata taarifa zenye uhakika zaidi tutamtaarifu rais” akasema Elvis Meshack Jumbo akafikiri kwa muda halafu akasema “Sawa ninakubaliana na wazo lako lakini hata hivyo inabidi tuunde timu Ambayo utaiongoza kwa ajili ya kulichunguza jambo hili kwa haraka.” “Hapana mzee.Hakuna haja ya kuunda timu.Niache niendelee na uchunguzi wangu na pindi nikiona kuna ulazima wa kuomba nguvu zaidi nitakueleza lakini kwa sasa nataka niendelee na uchunguzi mimi mwenyewe” akasema Elvis. “Are you ssure? “Ndiyo mkurugenzi.Nina hakika ninaweza kulishughulikia suala hili mwenyewe.Uwezo wangu unaufahamu vyema na endapo nitahitaji msaada nitakueleza” akasema Elvis Meshack Jumbo akamtazama Elvis kwa makini na kusema “I trust you Elvis .Sina shaka kabisa kwamba unaweza ukalichunguza suala hili lakini bado nina mashaka makubwa kwa mtu mmoja kuweza kupambana na mtandao mkubwa kama huu ambao wahusika wake bado hawajulikani” akasema Meshack Jumbo kwa wasi wasi “Usiwe na wasi wasi mzee ninaiweza kazi hii” akasema Elvis Baada ya tafakari ya dakika mbili Meshack Jumbo akasema “Sawa Elvis.kwa kuwa ninakuamini nitafanya unavyotaka lakini inabidi tufanye kazi hii bega kwa bega sisi wawili.Siwezi kukuachia kazi hii peke yako,lazima na mimi nishiriki” “Ahsante mkurugenzi kwa kukubali ombi langu.Hata hivyo kuna mambo mawili nataka nikuombe msaada wako.kwanza ni kuchunguza akaunti za benki za Frank ili tujue mwenendo wake wa kifedha .Tufahamu anapokea fedha toka wapi na anatuma kwenda wapi.Hii inaweza kuwa njia moja ya kuufuatilia mtandao huu.Pili ni kufuatilia mawasiliano ya Frank na kujua anawasiliana na akina nani na wanaongea kuhusu nini.Yule mwanamke Victoria ambaye alitumika kumuua kanali Norman naye anatakiwa achunguzwe anakoishi.Kuna kitu anakifahamu.Nataka kufahamu mahala anapoishi ili nimfuate nyumbani kwake.Naomba tuma kijana mmoja amfuatilie na afahamu mahala anapoishi na nipate majibu kabla ya jioni leo” Akasema “Sawa Elvis.Huyu mwanamke anaweza akasaidia sana.Endapo tutampata huyo Deusdedith tunaweza kupata taarifa za muhimu za kutusaidia kuubaini mtandao huu kwani inaonekana ni mtu mwenye sauti ndani ya mtandao” “Kweli kabisa mzee.Halafu kuna jambo lingine ambalo nahitaji msaada wako” “Jambo gani Elvis? “Ni kuhusiana na usalama wa Graca.Kama nlivyokueleza kwamba baba yake Frank anamtafuta kwa udi na uvumba na kwa sasa tayari amekwisha fahamu kwamba nimemtorosha na tayari wanajua nini nitakipata toka kwake kwa hiyo watamtafuta kwa kila uwezo walio nao na wakifanikiwa naamini watamuua.Kutokana na uzito wa suala hili sina hakika kama nitaweza kumlinda Graca muda wote kwa hiyo nataka umsaidie huyu binti ambaye amepitia maisha magumu sana na ya mateso mengi” akasema Elvis “Nakubaliana nawe Elvis.Niachie suala hilo nitalishughulikia.Ametupa taarifa za muhimu sana na lazima tumlinde” akasema meshack. “Ahsante sana Mkurugenzi.Huo utakuwa ni msaada mkubwa sana kwa binti huyu” akasema Elvis Walijadiliana mambo kadhaa kwa saa zaidi ya moja na kisha Elvis akarejea katika makazi yakeya muda.Bado kichwa chake kiliendelea kuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na mkewe Patricia “Is she cheating on me? Akajiuliza swali hili marakwa mara Nimemfahamu Patricia kwa miaka mingi na sina kumbu kumbu kama amewahi kunidanganya au kunificha na ndiyo maana nimepata shida sana kufahamu pale hotelini alikuwa anatafuta nini.I do trust her very much lakini jana haja rejea nyumbani alikuwa wapi? Kwa nini simu yake kaizima?akaendelea kujiuliza “Suala hili limetokea kwa wakati huu ambao ninashughulkia suala lingine zito.Patricia ni zaidi ya maisha yangu.Ninampenda kwa namna ambayo siwezi kuielezea.Patricia ni maisha yangu.Kwa mara ya kwanza ninaanza kuyaonja machungu ya kazi hii.Siku zote nimekuwa mvumilivu sana lakini naona uvumilivu huu unaelekea kunishinda.Nimekuwa nikitumia muda mwingi kwa kazi kuliko ule ninaotumia nikiwa na mke wangu.Endapo nitagundua kwamba Patricia anatoka nje ya ndoa sifahamu nitafanya nini ” akawaza Elvis ********************* Mara tu alipomaliza kuzungumza na Vicky simuni,Frank akampigia simu Pascal na kumpatia taarifa zile zilizomstua sana “Nilijua tu,mambo haya lazima yatatokea kama Elvis amempata Graca.Tayari amefahamu kila kitu na sasa anaanza kutusaka.Frank kazi imeanza” akasema Pascal na kimya kifupi kikapita “Uko wapi Pascal? “Niko hapa Ramona restaurant napata supu” “Nisubiri hapo ninakuja sasa hivi.Nataka tukaonane na Victoria” akasema Frank na kwa haraka akaelekea katika gari akaondoka kumfuata Pascal. Nusu saa baadae tayari alikwisha mpitia Pascal na walikuwa njiani kuelekea hotelini kwa Vicky “Kwa nini huyu Elvis atokee wakati huu wa neema kubwa kwetu na kutaka kuvuruga mipango yetu yote? Anaonekana ni kijana mwenye kihere here sana cha kuchunguza maisha ya watu” akasema kwa hasira Frank “Frank lazima tukubali tuna kazi ya ziada ya kufanya ili kumzuia Elvis asiendelee kutuchimba.Kwa hatua aliyofikia ni wazi tayari atakuwa na taarifa zetu na anachokifanya hivi sasa ni kutuchimba.Tayari Graca atakuwa amemuelekeza kila kitu kuhusiana na biashara tunayoifanya.Ninamfahamu vyema Elvis.Huyu ni nyoka mwenye sumu kali sana na ambaye anatakiwa kupondwa kichwa haraka sana.He’s very dangerous” akasema Pascal na Frank akaupiga usukani kwa hasira. Najilaumu sana kwa uzembe wangu wa kutunza kumbu kumbu hadi Yule mwanamke akazipata na kumpa mwanae Graca.Najlaumu sana kwa nini nilimuoa mwaname mjinga kama Yule ambaye naye kanizalia mtoto mjinga mwenye akili kama zake.Wao ndio chanzo cha haya yote.Nilifanya kosa lingine kubwa kumuacha Graca hai hadi leo.Aombe sana nisimtie mikononi mwangi kwani sintampa tena nafasi hata ya kutamka neno lolote.Nitampata tu hawezi kujificha kamwe” akasema Frank kwa hasira “Vipi kuhusu Vicky? Tayari Elvis amekwisha gundua kwamba ana mahusiano na sisi kwa hiyo tayari amekuwa ni hatari kwetu.Tutamfanyaje? akauliza Pascal “Wewe unafikiria tumfanye nini? Frank naye akauliza “Kwa sasa Vicky ndiye njia pekee ya Elvis kuweza kupata taarifa zetu.Vicky atakuwa katika hatari kubwa.Yawezekana akawa anamfuatilia kwa siri bila yeye kujua.Frank hatupaswi kumpa Elvis nafasi ya kumpata Vicky” akasema Pascal “Unataka tufanye nini Pascal? Unataka tumuue Vicky? Frank akauliza “Hivyo ndivyo tufanyavyo kwa wale wote ambao wanaonekana hatari kwetu” akasema Pascal “No ! we cant do that.We cant kill her.Yeye ndiye atakaye tusaidia kummaliza huyu mdudu anayetufuata kwa nyuma kama fisi,Elvis !! “What are your plans Frank? Pascal akauliza “Just wait and see” akasema Frank Walifika katika hoteli ya Vicky wakaelekea moja kwa moja ilipo ofisi yake .Vicky alikuwa amesimama dirishani huku mkononi akiwa na glasi ya pombe.Alionekana wazi kwamba alikuwa katika mawazo mengi. “Hallo Vicky” akasema Frank “You have to http://deusdeditmahunda.blogspot.com/tell me right now what is going on? You promised me that there will be no trouble.who was that man? Akauliza kwa ukali Vicky bila hata salamu “Please calm down Vicky” akasema Frank akijaribu kumtuliza Vicky aliyeonekana kuwa na hasira nyingi.Frank na Pascal wakaketi vitini halafu Frank akasema Hebu tueleze Vicky,tukio zima namna lilivyokuwa” “Jana usiku” akaanza kueleza Vicky “Nilipigiwa simu na mtu nisiyemfahamu akajitambulisha kwangu anaitwa Robin.Alisema kwamba ana shida na mimi.Nilipanga kuonana naye leo na asubuhi ya leo akafika kama nilivyomtaka afanye.Shida yake kubwa ambayo alikuwa tayari kunipa fedha nyingi ni kutaka kujua kama ninamfahamu mtu aitwaye Norman.Niliposikia jina hilo niliogopa na kustuka mno.Nilikana kumfahamu mtu huyo halafu akaniambia kwamba kama simfahamu mbona nilionekana naye siku ile kabla hajafariki? Niliogopa zaidi aliponikumbusha kuhusu jambo hilo ambalo tayari lilikwisha nitoka akilini.Naamini Yule jamaa atakuwa mpelelezi.Nilikasirikka na kumtaka atoke haraka ofisini kwangu na wakati akitoka akaniuliza kama ninamfahamu Deusdedith.Nilizidi kuogopa nusura nitokwe na haja ndogo.Baada ya kumtishia kumuitia walinzi akaondoa zake.Jambo hili limenichanganya sana kwa sababu Yule jamaa anaonekana kunifahamu sana na kulifahamu suala zima la mauaji ya Norman.Tafadhali naombeni mnisaidie sitaki kuingia katika matatizo” akasema Vicky “Pole sana Vicky kwa mstuko ulioupata .Tunakuahidi mambo yote yatakaa sawa” How can I trust you again Frank?Mara ya kwanza uliniambia hivyo hivyo lakini leo hii tayari nimejulikana” akasema Vicky. Frank akamtazama Vicky usoni halafu akasema “Tayari tumekwisha mfahamu mtu huyo.Jina lake si Robin kama alivyokwambia bali anaitwa Elvis na ni mfanyakazi wa idara ya ujasusi’ “I’m finished !! akanong’ona Vicky “Vicky nadhani niliwahi kukutaarifu kwamba ninaye mtoto mwenye matatizo ya akili anatibiwa afrika kusini.Hivi majuzi huyu Elvis amemfuata mwanangu Afrika kusini na kumtorosha amempeleka mahala kusikojulikana.Kupitia mwanangu huyo ameweza kuyafahamu mambo yangu mengi ambayo niliyahifadhi katika kompyuta ambayo huyo mwannagu aliiba.Pamoja na hayo nakuomba usiogope Vicky kwani nitahakikisha mwanaharamu huyu hafiki kokote.Safari hii amejiingiza yeye mwenyewe katika tanuru la moto na hatatoka salama.Kitu ambacho nataka kifanyike sasa hivi ni kukupeleka mafichoni shambani kwangu wakati tukiendelea kulishughulikia suala hili.Ndani ya kipindi kifupi sana lazima Elvis awe ametoweka katika ardhi ya Tanzania” “Frank niko tayari kwenda mafichoni lakini tafadhali naomba safari hii maneno yako yawe ya kweli na uhakikishe kwamba suala hili linakwisha.Timiza ahadi yako na unitoe katika matatizo” akasema Vicky “Vicky naomba usiwe na hata chembe ya woga kuhusu suala hili.Wewe mwenyewe utashuhudia Elvis akiuawa na amani itatamalki tena” akasema Frank ‘Nitashukuru kuona hilo likitekekelzwa.Yule jamaa ameninyima amani kabisa.Lini utanipeleka mafichoni? “Right now !! akasema Frank na Vicky akastuka ‘Right now?







Ndiyo.Hakuna muda wa kupoteza kwani tayari umekwisha anza kumulikwa na Elvis na hatujui ana mipango gani kwa hiyo lazima tuchukue tahadhari mapema ya kukupeleka sehemu salama kwa sasa” Akasema Frank “Sikutegema kabisa kama siku moja mambo yangeweza kugeuka namna hii” akalalamika Vicky ‘Usiogope Vicky.Suala hili litakwisha lakini kabla ya kwenda huko mafichoni kuna jambo ambalo tunatakiwa kulifanya.Tutakwenda nyumbani kwako na kuondoa kila kitu ambacho kinaweza kumsaidia Elvis au mtu yeyote Yule ambaye anakufuatilia” Akasema Frank bila kupoteza wakati wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Vicky ******************** Alipomaliza mizunguko yake aliyoipanga Doreen akawasili nyumbani kwa akina Elvis kuonana na Patricia.Alikaribishwa sebuleni na Stella mtumishi wa ndani kisha akaenda kumtaarifu Patricia ambaye alielekeza Doreen amfuate chumbani.Doreen alipoingia chumbani akastuka sana kwa hali aliyomkuta nayo Patricia.Macho yalikuwa mekundu na yamevimba “Patricia !! Doreen akastuka sanaDoreen ! Karibu” akasema Patricia kwa sauti ya uchovu huku akiinuka na kukaa kitandani “Patricia what happened? Are you sick? Akauliza Doreen.Patricia akavuta pumzi ndefu na kusema “Doreen siumwi ndugu yangu” ‘Kama huumwi kitu gani kimetokea? Toka jana nimejaribu kukutafuta lakini simu yako haipatikani.Hali yako imeniogopesha sana” Patricia akanyoosha mkono wake na kuchukua simu iliyokuwa pembeni akaiwasha na kuitupa pembeni huku jumbe nyingi zikiingia mfululizo lakini hakutaka kujishughulisha nazo “Patricia hebu nieleze una tatizo gani? Akauliza Doreen “Doreen unanifahamu vizuri mimi ni mwanamke mvumilivu na mwenye ujasiri mkubwa lakini kwa sasa naona ninaelekea kushindwa kuvumilia tena” “Kuna nini kimetokea? Akauliza Doreen.Patricia akainama akafuta machozi na kusema “Doreen nashindwa nianzie wapi kukueleza” “tafadhali nieleze Patricia.Mimi ni rafiki yako nitakusikiliza na nitakusaidia kwa lolote” akasema Doreen huku akimsaidia Patricia kufuta machozi “Doreen nimefanya jambo baya sana ambalo sikutegemea kulifanya katika maisha yangu” akasema Patricia Umefanya nini Patricia? Patricia akamtazama Doreen kwa muda halafu akasema “Nimetembea nje ya ndoa yangu Doreen.Nimemsaliti Elvis” akasema Patricia na kushindwa kujiuzia akaanza kulia tena.Doreen akabaki katika mshangao “Doreen I’m so stupid !! akasema Patricia “Nyamaza kulia Patricia.Tafadhali nieleze ilikuaje hadi ukafanya hivyo?Shetani gani alikuingia hadi ukaamua kufanya hivyo Patricia? Patricia akafuta machozi na kusema “Jana tulikuwa na sherehe ya kumkaribisha Dr Steven Washington anayetokea Marekani.Nilirudi nyumbani kujiandaa kwa sherehe hiyo nikapata taarifa toka kwa Stella kwamba Elvis amerejea na kuondoka tena kwenda katika kazi nyingine.Aliyenitibua zaidi ni Stella ambaye alinieleza kwamba Elvis alikuwa na mwanamke ndani ya gari.Sikufichi Doreen nilijikuta nikiwa na wivu mkali.Nilijiuliza maswali mengi kuhusu mwanamke huyo aliyekuwa na Elvis katika gari ni nani na wanakwenda wapi?Kilichonishangaza zaidi ni Elvis kutonitaarifu moja kwa moja kwamba amerejea.Nilihisi mambo mengi na kudhani yawezekana hakuwa amekwenda Afrika kusini kama alivyoniambia,yawezekana amepata mwanamke mwingine.Baadae niliamua kuyapuuza mawazo haya na kuendelea na safari kwenda katika sherehe.Nikiwa njiani mama mkwe akanipigia simu lakini sikupokea akaamua kuniandikia ujumbe” Patricia akaufungua ujumbe ule aliotumiwa na mama mkwe wake akamuonyesha Doreen ambaye alipousoma sura yake ikabadlika akashikwa na hasira “Huyu mama mkwe wako ni mzima kweli?Anawezaje kukuandikia ujumbe mchafu kama huu? Akasema Doreen kwa hasira “Patricia wewe ni mvumilivu sana.Ningekuwa mimi nisingejali ni mama mkwe ningekwenda kucharuana naye.Huu ni udhalilishaji mkubwa sana.Hii imevuka mipaka!! Akasema Doreen “Doreen hiyo ndiyo hali halisi ilivyo hivi sasa.Ninapitia kipindi kigumu sana na ndiyo maana nilipousoma ujumbe huo nlichanganyikiwa na kushindwa nifanye nini.Nililia sana na kujiuliza aliko Elvis.Yeye ndiye mtu pekee ambaye huwa ananifariji katika nyakati kama zile.I needed him so badly.I needed someone to comfort me.kwa hali niliyokuwa nayo ningeweza hata kufanya kitu kibaya.Sikutaka kurejea nyumbani.Nyumba hii ni nzuri lakini kwa sasa naiona kama gereza la mateso.Ni katika hali hiyo nikajikuta nikilala na Dr Steven ” akasema Patrica na kuinama akaufunika uso kwa viganja vya mikono “I made the biggest mistake in my life” akasema Patricia “Usilie Patricia na wala usijilaumu .Ninakufahamu vizuri sana na ninaamini hukufanya kwa kukusudia.Ulihitaji faraja na mtu pekee ambaye alitakiwa kukufariji ni Elvis lakini hakuwepo.Wa kulaumiwa hapa ni Elvis na si wewe.Kwa wakati kama huu Elvis alipaswa aachane kwanza na kazi zake na kukaa nawe.Wewe ni wa thamani kubwa sana kwake kuliko hata kazi hiyo anayoifanya” akasema Doreen “Doreen nimekwisha ongea kuhusu kazi hiyo hadi nimechoka.Elvis hataki kumsikiliza mtu yeyote kuhusiana na kazi hiyo.Doreen nina matatizo makubwa katika ndoa yangu na mengine siwezi kuyaweka wazi inabaki siri yangu” akasema Patricia “Naelewa unachokisema Patricia lakini haya yote yasingetokea kama isingekuwa kazi hii ya Elvis.kwa nini asiache na kufanya kazi nyingine?Halafu kuhusu mama yake umewahi kumueleza namna anavyokutenda na kukutumia jumbe za kejeli namna hii? Akauliza Doreen.Wakati patricia akijiandaa kujibu mara simu yake ikaita.Akatazama mpigaji na kustuka “mbona umestika ? akauliza Doreen “rais ananipigia” rais ?!! akauliza Doreen “Ndiyo.Nimeshangaa kwani si kawaida yake kunipigia simu na hasa mida hii” akasema Patricia na kuipokea simu ile “baba shikamoo” akasema Patricia kwa adabu “Marahaba Dr Patricia.Hujambo? “Sijambo baba.hajambo mama? “Mama yako hali yake si nzuri na ndiyo maana nimekupigia simu.Nimeambiwa kwamba leo hujafika kumuona.Una tatizo lolote? akauliza rais “Nilipatwa na dharura asubuhi ya leo na kushindwa kuja.Mama amepatwa na tatizo gani? Hali yake imebadilika sana ,nadhani ungekuja kumuangalia wewe mwenyewe kama utakuwa na nafasi muda huu” “Ok nakuja sasa hivi” akasema Patricia “Ahsante sana Dr Patricia na samahani sana kwa usumbufu” akasema rais na kukatasimu. “Mke wa rais hali yake si nzuyri hivyo natakiwa niende ikulu mara moja kumtazma.Doreen tutaongea zaidi kesho.Nitaktafuta” Akasema Patricia wakaagana Doreen akaondoka akimuacha Patricia akijiandaa kwenda ikulu ******************* Saa tisa na dakika kumi alasiri,Doreen akawasili katika makazi ya muda ya Elvis.Graca alikuwa sebuleni akitazama filamu.Wakasalimiana na Doreen akauliza kama tayari Elvis amerejea akaambiwa tayari amerejea na yuko chumbani kwake anapumzika.Doreen akaelekea chumbani kwa Elvis akagonga mlango Toka amerudi Elvis alikuwa amejifungia chumbani kwake akijaribu kuwaza mambo mbalimbali .Kikubwa kilichotawala kichwa chake ni kitendo cha kumuona mke wake paticia akitoka hotelini akiwa na mwanaume mwingine .Akiwa katika tafakari mlango wake ukagongwa akavaa shati na kwenda kuufungua. “Doreen.karibu sana” Akasema Elvis kwa sauti ya uchovu “Umeshindaje Elvis? Akauliza Doreen ‘Nimeshida salama” akasema Elvis na kumkaribisha ndani Doreen ‘habari za huko utokako? Mambo yote yamekwenda vizuri? Elvis akauliza “Ndiyo.Kila kitu kimekwenda vizuri kabisa.Vipi kuhusu wewe mambo yako yamekwenda sawa? “mambo yamekwenda vizuri” akasema Elvis na kimya kifupi kikapita “Umefanikiwa kuonana na patricia? Elvis akauliza Ndiyo nimeonana naye” “Ulimfuata kazini? “Nimemfuata nyumbani.Kazini hakuingia leo” “Is she fine? Elvis akauliza “Some how” akajibu Doreen .Elvis akavuta pumzi ndefu na kuuliza “Where was she last night? Doreen akastuka kwa swali lile “Umeuliza nini Elvis? Akasema Doreen “Nimeuliza Patria amekwambia jana usiku alikuwa wapi? Swali lile likamfanya Doreen atetereke katika kujibu.Alistuka Elvis amefahamuje kuhusiana na suala lile la Patricia kutokulala nyumbani kwake Sielewi kwa nini umeuliza swali kama hilo? Unahisi Patricia halali nyumbani wakati haupo? Don’t you trust her? Akauliza Doreen.Elvis akamtazama kwa makini machoni na kusema “Tell me the truth Doreen.Patricia alikuwa wapi jana usiku? Ninafahamu wewe ni rafiki yake mkubwa na hakuna kitu anachoweza kukuficha” Akasisitiza Elvis “Elvis kwa nini unakuwa na mashaka na mke wako? Mbona Patricia hajanieleza kuhusiana na jambo lolote la yeye kutokuwepo nyumbani jana usiku? Tafadhali muamini mkeo.Anakupenda mno” akasema Doreen.Elvis akainuka akaenda dfirishani akachungulia nje.Doreen akainuka na kumfuata akamshika bega “Elvis kuna nini? Mbona umebadilika hivyo? Elvis akageuka akamtazama Doreen na kusema “Siku ya kwanza kukutana na Patricia nilijua yeye ndiye mwanamke wa maisha yangu.Toka dakika hiyo upendo wangu kwake haujawahi kupungua na unaongezeka siku hadi siku.Kwanguyeye ni kila kitu.Ninampenda zaidi ya ninavyoweza kueleza” akanyamaza kwa muda halafu akasema “Asubuhi ya leo nimemuona mke wangu Patricia akitoka hotelini akiwa ameongozana na mwanaume mmoja ambaye simfahamu.Kwa muonekano aliokuwa nao ilionyesha wazi kwamba hakuwa kazini kwani mavazi aliyoyavaa ni ya kutokea usiku.Nilimpigia simu mfanyakazi wetu pale nyumbani akasema kwamba Patricia aliondoka jana jioni na hakurejea nyumbani.Najiuliza kama hakulala nyumbani alilala wapi? Alilala hotelini? Yule mwanaume aliyekuwa naye ni nani? Je alilala naye? Kama hakulala naye pale hotelini alitoka kufanya nini?Doreen nina wasi wasi kwamba Patricia ananisaliti.Kuna uwezekano mkubwa akawa anatoka nje ya ndoa yetu” akasema Elvis na kuonekana kuumizwa sana na jambo lile.Doreen alikuwa katika wakati mgumu .Alitamani amueleze ukweli Elvis lakini akaogopa Namuonea huruma Elvis.Ameumizwa mno na kitendo cha kumuona Patricia akitokea hotelini akiwa na mwanaume mwingine.Itakuaje nikimweleza ni kweli patricia amemsaliti? Hata hivyo kama tayari amekwisha waona wakitoka hotelini na papo hapo ana u hakika kwamba Patricia hakulala nyumbani ni vigumu kuamini kwamba Patricia hakulala na Yule mwanaume aliyekuwa naye.Ni bora nimweleze ukweli ili kulimaliza suala hili.Endapo atagundua kwamba ninalifahamu jambo hili na nikamficha hataniamini tena.Hii ni nafasi yangu pia ya kujisogeza karibu zaidi na Elvis” akawaza DoreenElvis naomba nikueleze ukweli” Akasema Doreen.Elvis akainua kichwa na kumtazama “Ni kweli Patricia hakulala nyumbani jana na nitakueleza kisa chote kilichotokea kwani amenieleza kila kitu” akasema Doreen na kumueleza Elvis kila kitu kama alivyoambiwa na Patricia bila kuacha hata neno moja.Elvis alipandwa na hasira kali “Kumbe ni ndugu zanu ndio wanaochangia kuivurga ndoa yangu!! Akasema Elvis kwa hasira akachukua simu ya Doreen akaandika namba za mama yake na kupiga. “Hallow” ikasema sauti ya mama yake baada ya kupokea simu Mama shikamoo.Ni mimi Elvis hapa ninaongea” akasema Elvis “Oh ! Elvis kumbe umesharejea toka safari.mambo yako yanakwendaje? Akauliza mama yake “Mama sina muda mrefu wa maongezi.Ninataka kuweka sawa baadhi ya mambo.Tafadhali mama usiingilie ndoa yangu.Kaa mbali na mke wangu na sitaki mtu yeyote awe wewe au ndugu yeyote mwingine kumkoseshaamani mke wangu.Sitaki kusikia mtu yeyote akimuuliza habari za mtoto.Yeyote atakayethubutu kwenda na kumuuliza eti mbona hutuzalii mtoto atakutana na mimi.Leave us alone!!! Akasema Elvis na kukata simu. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza na mama yake kwa ukali namna ile. “Umefanya vizuri Elvis kuwaeleza ukweli.” Akasema Doreen “Doreen uliwahi kunieleza kwamba kazi yangu imenifanya nijiweke mbali na Patricia.Ulikuwa sahihi.Patricia ananipenda sana na hawezi kufanya kitendo kama kile bila sababu.Yote haya yamesababishwa na mimi.Nimekuwa nikitumia muda mwingi sana katika kazi kuliko muda ninaoutumia na mke wangu.Japokuwa imeniumiza kusikia mke wangu ametembea nje ya ndoa lakini lazima nikubali ukweli kwamba chanzo ni mimi.Patricia anahitaji faraja na mtu pekee ambaye nilipaswa kuwa karibu naye kumfariji ni mimi” akasema Elvis na kuzama mawazoni “Doreen I need to be alone for now” akasema na taratibu Doreen akatoka mle chumbani akamuacha Elvis peke yake “Kwa nini maisha yangu yanakuwa hivi? Kwa nini nashindwa kuwa na maisha ya kawaida nifurahi na mke wangu Patricia?kwa nini ndugu zangu wanaingilia ndoa yangu na kutaka kuivuruga? Akajiuliza.Aliwaza mambo mengi sana “Mimi nadhani suluhisho pekee ni kuachana na hii kazi ili niokoe ndoa yangu inayotaka kuzama.Patricia amelazimika kutembea nje ya ndoa na chanzo cha haya yote ni mimi.Sitaki kumuona Patricia akiendelea kuteseka.Amani furaha na upendo lazima virejee tena katika ndoa yangu.Ili haya yote yafanikiwe lazima niachane na hii kazi haraka” akawaza “Nafahamu nina jukumu kubwa mbele yangu la kufumua mtandao mkubwa na hatari wa watu wanaofanya biashara ya kuuza silaha kwa waasi wa Congo lakini kutokana na suala zito linalomkabili Patricia kwa sasa sina budi kuwapa nafasi wengine waendelee na kazi hii niliyoianza.Natakiwa kuwahi kujenga nyumba yangu inayoanza kuweka ufa” Akawaza Elvis na sura ya Graca ikamjia“Lakini kabla ya kuacha kazi hii lazima nihakikishe kwamba huyu binti anakuwa katika sehemu salama.Nilimuahidi hivyo na lazima nitekeleze nilichomuahidi.Siwezi kumuacha hivi hivi.Nitamsisitiza mkurugenzi alishughulikie kwa haraka suala lake ili limalizike mapema na mimi niweze kurejea nyumbani kwangu” akawaza Elvis ***************** Saa kumi na mbili za jioni hali ilikuwa ya utulivu mkubwa ndani ya jumba kubwa la brigedia Frank kwaju lililopo katikati ya shamba lake.Ndani ya jumba hili watu watatu walikuwa wamekaa sebuleni wakiongea.Brigedia Frank alikuwa pamoja na mshirika wake wa karibu pascal pamoja na Victoria ambaye wamempeleka kule shambani kwa ajili ya kumficha “Vicky sisi inabidi tukuache hapa kwa muda.Kuna sehemu tunahitajika usiku huu.Usiwe na hofu yoyote kuhusu usalama wako.Mahali hapa ni salama sana.Hata hivyo nitarejea mimi baadae.Siwezi kukuacha hapa peke yako” akasema Frank huku akitazama saa yake ‘I’m so scared Frank.Sijazoea kukaa sehemu yenye ukimya mkubwa kama hii.No one is moving around. Gosh ! its’s like hell !.tafadhali Frank ukimaliza shughuli zako njoo mara moja sina hakika kama nitaweza kupata usingizi usiku wa leo nikiwa peke yangu ndani ya jumba hili” akasema Vicky “ Usihofu Vicky,mara tu nitakapomaliza mambo yangu nitarejea mara moja.Kila unachokihitaji ndani ya jumba hili utakipata.Jisikie huru” akasema Frank halafu akamfanyia ishara Pascal wakaondoka. “Una hakika utarudi kama ulivyomuahidi Vicky au ulikuwa unamdanganya kumuondoa woga? Akauliza Pascal “Ndiyo nitarejea.Ni dhambi kumuacha malaika kama Yule alale peke yake.Lazima na mimi niufaidi uumbaji wa Mungu usiku wa leo.Japokuwa Vicky ni kahaba lakini si rahisi kumpata.Ana pesa nyingi na mapenzi anafanya kwa starehe ndiyo maana kwa usiku mmoja anatoza hadi milioni tano.Hii ndiyo sababu nimeitisha kikao cha leo kianze mapema ili niwahi kujipumzisha na Vicky mwanamke kahaba mwenye uzuri wa kipekee” akasema Frank huku akitabasamu ‘Vipi kuhusu Elvis? Namna gani tutaweza kumuondoa? Frank akatabasamu na ksuema “Usijali Pascal.Elvis ni mtu mdogo mno.Masaa yake ya kuishi yanahesabika.Sisi ni watu wenye nguvu sana na hatuwezi kukubali kutiwa tumbo joto na mdudu mdogo kama Elvis.Mambo yetu yote yatakwenda kama tunavyotaka na hakuna wa kutuzuia” akasema Frank huku safari ikiendelea Saa moja na nusu za usiku wajumbe wote wanaotakiwa kuhudhuria kikao cha usiku huu tayari wamekwisha wasili na Frank akafungua kikao “Ndugu zangu kwanza kabisa napenda kuwashukuru kwa kufika kwenu katika kikao cha leo.Kama mtakumbuka katika kikao kilichopita tulipeana majukumu kadhaa kwa baadhi yetu ambayo yatatupa uelekeo mzima kuhusiana na mpango wetu.Kikao cha leo ni maalum kabisa kwa ajili ya kupeana taarifa ni wapi tumefikia.Namkaribisha kwanza rais wetu mtarajiwa David ili aweze kutueleza amefikia wapi katika jukumu alilopewa” David akatabasamu baada wajumbe kumpigia makofi “Ahsanteni sana.Nashukuru sana ndugu zangu kwa heshima hii kubwa.Tuzidi kuomba ili mambo yaende kama tunavyotaka” Akasema “Katika kikao kilichopita nilikabidhiwa majukumu mawili.Moja ni kuonana na makamu wa rais na kumshawishi aungane nasi na pili ni kuongea na wanasiasa na kuwashawishi waanzishe maandamano yatakayokuwa na lengo la kupinga kitendo cha makampuni ya Marekani kupewa fursa ya kuwekeza katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini.Mambo haya yote mawili nimeyafanikisha vizuri kama mlivyoniagiza.Kwanza kabisa nilionana na wakuu wa vyama vya upinzani.Kwa bahati nzuri wakuu wote niliowaalika kuonana nao walifika.Niliongea nao kwa kirefu na ninapenda kuwataarifu kwamba wamekubali kufanya niliyowaomba.Wamekubali kuungana na kuanzisha maandamano makubwa yasiyo na ukomo yatakayoambatana na vurugu.Kwa sasa tayari wameanza maandalizi ya kampeni hiyo kubwa ya kitaifa na nimewataka ndani ya siku mbili waniletee mchanganuo wa gharama zote za kampeni hiyo.Ni pesa nyingi itahitajika lakini hatuna namna lazima tutumie pesa.Wanasiasa hawa hawaelewi ni kitu gani kilicho nyuma ya kampeni hiyo.Hawaelewi kama nyuma ya kampeni hiyo kuna mipango ya kuiangusha serikali.Siku yoyote ndani ya wiki hii mtasikia tamko la pamoja la wenyeviti hawa wa vyama vya upinzani nchini la kuzindua rasmi kampeni hiyo” David akanyamaza na wajumbe wakampigia makofi.Akaendelea “Kwa upande wa makamu wa rais nilifanikiwa kuongea naye.Haikuwa kazi nyepesi kumshawishi lakini nilitumia kila aina ya ushawishi na hatimaye nikafanikiwa kumshawishi akakubali.Kwa hiyo napenda kuwatamkia rasmi kwamba makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni mwenzetu katika harakati hizi.Japokuwa kuna masharti aliyatoa lakini yanatekelezeka hivyo msiwe na hofu.Makamu wa rais ni mtu muhimu sana katika mchakato huu.Yeye ndiye atakayetusaidia kutupa taarifa mbali mbali za ndani ya serikali”akasema David na wajumbe wakampigia tena makofi “Jukumu lingine ambalo bado natakiwa kulifanya ni kuwashawishi baadhi ya viongozi wa serikalini na wote ambao wataonekana kuwa na umuhimu katika mchakato huu.Kuna baadhi ya mawaziri ambao nadhani watafaa kuhusishwa.Si mawaziri tu bali kuna watu wengine ambao ni muhimu nao wakashirikishwa pia.Nadhani katika kikao kijacho tayari nitakuwa nimekwisha fanya hiyo kazi na nitakuja na majibu” akasema David na kukaa “Ahsante sana mheshimiwa rais mtarajiwa” akasema Frank “Tunashukuru kwa kazi hiyo kubwa uliyoifanya.Kwa upande wangu mimi nilikabidhiwa jukumu la kuwashawishi makamanda wa vikosi vitakavyoasi.Kazi imekwenda vizuri na tayari nimefanikiwa kuwashawishi makamanda wawili na wamekubali.Makamanda watatu bado kuna mambo hatujakubaliana lakini tunaendelea na maongezi na nina uhakika muda si mrefu tutafikia makubaliano.Kikao kijacho nitakuwa na jibu zuri la kuwapeni” akasema Frank Majadiliano yakaendelea hadi ilipotimu saa tano za usiku wajumbe wakaagana na kuondoka isipokuwa Frank na Pascal waliokuwa na maongezi na David “Frank uliniambia una tatizo.Ni tatizo gani? Akasema David “David kuna tatizo limejitokeza .Kuna mdudu amejitokeza ambaye asipodhibitiwa haraka anaweza kuleta madhara makubwa kwetu” akasema Frank “Mdudu gani huyo? Akauliza David kwa wasi wasi.Frank akamueleza kila kitu kuhusiana na Elvis. “Huyo kijana tutamdhibiti vipi? Ni wazi anaonekana ni hatari sana kwetu”Akauliza David. ‘Ndiyo maana tumekuja kwako kuomba msaada wa kumdhibiti huyu kjana haraka iwezekanavyo” Akasema Frank “Hebu nielezeni ninaweza kusaidia vipi kumuondoa huyo kijana? “Nataka umweleze makamu wa rais.Kitengo anachofanyia kazi Elvis kimehamishiwa katika ofisi yake kwa hiyo yeye ana sauti kubwa na atatoa amri huyo kijana auawe” akasema Frank ‘Endapo makamu wa rais akatoa amri Elvis auawe nyie mmejipangaje? Atauawa vipi? “Ataelekezwa aende mahala akaonane na mtu mwenye taarifa za muhimu sana na huko tutawapanga watu wetu watamshambulia na kuuawa.Kifo chake hakitahojiwa kwa sababu mkurugenzi wake atakuwa anafahamu kila kinachoendelea hivyo atahakikisha hakuna aina yoyote ya uchunguzi utakaofanyika.Mwenye uwezo wa kufanikisha haya ni makamu wa rais pekee” akasema Frank.David akainama na kukuna kichwa chake akafikiri kwa muda na kusema “Sawa Frank.Niachie suala hilo nilishughulikie Nitazungumza na makamu wa rais na nitamueleza kila kitu.Nitakupa jibu asubuhi”akasema David “Ahsante sana David.Suala hili ni la muhimu mno endapo tusipowahi kumdhibti mtu huyu kuna hatari akatuvurugia kila kitu” Usihofu Frank.Nitajitahidi kufanya kila linalowezekana ili tulimalize jambo hili na kusiwe na kizingiti chochote katika mpango wetu” akasema David kisha akaagana na Frank kwa ahadi ya kumpigia simu asubuhi na mapema.Frank na Pascal wakaondoka **************** Mara tu baada ya akina Frank kuondoka David akampigia simu makamu wa rais kupitia namba yake maalum “Halow David” akasema makamu wa rais baada ya kupokea simu “Hallo Mr Shafi.Samahani kwa kukusumbua usiku huu” “Bila samahani David.Nadhani kuna jambo la muhimu unataka kunieleza” “Ndio Mr Shafi.Kuna jambo ambalo limejitokeza na linahitaji utekelezaji wa haraka na ambaye anaweza kulifanya jambo hili likamalizika ni wewe” “Jambo gani hilo David” David akamweleza makamu wa rais kila kitu kuhusiana na Elvis. Makamu wa rais akanyamaza na kufikiri kwa muda kisha akasema “Ok David.Niachie suala hili nilishughulikie kesho asubuhi halafu nitakupigia simu kukufahamisha” akasema makamu wa rais wakagaana na bila kupoteza muda Dr Shafi mkurugenzi wa idara ya ujasusi akamuomba afike nyumbani kwake asubuhi na mapema “Kazi imeanza.Haya ndiyo mambo ambayo sikuwa nayataka” akasema Dr Shafi kwa sauti ndogo na kuelekea chumbani kwake kulala ******************** Kwa muda sasa Elvis alikuwa akiitazama mishale ya saa kubwa iliyokuwa inapishana na kubadilisha majira.Muda ulizidi kuyoyoma na hadi mida hiyo ya saa saba za usiku hakuwa amepata usingizi.Kichwa chake kilijaa mawazo mengi “Endapo ningechagua kufanya kazi nyingine maisha yangu yangekuwa mazuri sana hivi sasa.Hata hivyo bado sijachelewa,baada tu ya Graca kuondoka utakuwa ni mwisho wangu kuifanya kazi hii.Najua si jambo jepesi lakini kwa ajili ya Patricia nitafanya kila linalowezekana” akawaza Elvis Wakati akiendelea kuwaza mara mlango wake ukagongwa akainuka na kwenda kuufungua.Alikua ni Doreen “Doreen hujalala mpaka mida hii? Akauliza Elvis huku macho yake akiwa ameyaelekeza katika kifua cha Doreen ambacho kilibeba matiti yaliyojaa ambayo yalionekaa kwa urahisi kutokana na nguo nyepesi ya kulalia aliyoivaa. Elvis samahani kama nimekusumbua” akasema Doreen “Hujanisumbua Doreen. Una tatizo lolote? Akauliza Elvis “Nimeshindwa kabisa kupata usingizi Elvis.nNaweza kuingia ndani? Akauliza Doreen “Bila wasi wasi.karibu ndani” akasema Elvis na Doreen akaingia ndani.Mwili wote wa Doreen uliweza kuonekana vyema kupitia nguo ile nyepesi aliyoivaa.Elvis akajikuta akisismka mwili mzima akafunga mlango na kwenda kuketi sofani.Doreen naye akainuka mahala alipokuwa amekaa akamfuata Elvis “Elvis najua una mawazo mengi sana yanayokusumbua kichwa chako na kubwa ni hili suala la Patricia ambalo naamini limekuumiza mno.Hata mimi nimeumia vile vile kwaniPatricia ni rafiki yangu kipenzi.Pamoja na hayo naomba usihuzunike sana Elvis.Hayo ni majaribu katika ndoa yenu na yatakwisha” akasema Doreen na kuupeleka mkono wake kifuani kwa Elvis na kuanza kumpapasa.Elvis akamzuia “Unafanya nini Doreen? Kwa sauti laini ya kimahaba Doreen akasema “Please don’t say no Elvis.I want to make you happy.Just for tonight I want you to forget the world.Please Elvis” akasema Doreen “Doreen tafadhali nakuomba inuka uende chumbani kwako ukalale.Siwezi kumsaliti Paticia.Nampenda mno mke wangu na hata wewe unalifahamu hilo” akasema Elvis.Doreen akinuka na kupiga magoti huku akiendelea kumpapasa Elvis mabegani “Nafahamu unampenda na kumheshimu mkeo lakini je yeye anakuheshimu? Amevunja kiapo cha ndoa kwa kutembea na mwanaume mwingine.Japo anasema ni mara moja lakini utamuaminije? Unafahamu ni mara ngapi anafanya hivyo? Akauliza Doreen “Please stop that Doreen.Tafadhali usiendelee kuniumiza kwa suala hili’ “That’s the reason I’m here Elvis.To make you happy and forget what happened.Forget about Patricia just for tonight” akasema Doreen kwa sauti laini huku akiendelea kumpapasa Elvis.Taratibu Elvis akaanza kupandwa na hisia na mwili ukamsisimka.Doreen akaendelea na utundu wake na taratibu akaivua fulana ya Elvis na kukishuhudia kifua kilichojengeka akazidi kupagawa.Elvis alishindwa kujizuia akajikuta ameanza kutoa ushirikiano na kuzidi kumpagawisha Doreen.Baada ya dakika zipatazo kumi wakajikuta wakiogelea katika mahaba mazito.Kwa mara ya kwanza Elvis akavunja kiapo cha ndoa na kumsaliti mkewe ****************** akampiga simu Meshack Jumbo





http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mishale ya saa ilionyesha ni saa tisa za usiku.Bado Patricia hakuwa amepata usingizi.Pembeni ya kitanda chake kulikuwa na chupa ya pombe ambayo amekuwa akinywa tangu aliporejea toka ikulu alikoenda kumtazama mke wa rais.Macho yake mazuri yenye kurembua muda wote leo hii yalikuwa yamemvimba kutokana na kulia sana.Alikuwa katika wakati mgumu mno katika maisha yake Taratibu akainuka na kwenda sofani akafuta machozi na kuinua macho juu “Ee Mungu wangu kwa nini umeniacha peke yangu nateseka namna hii? Kam unayaona mateso ninayopata naomba usiniache.Simama nami ee bwana ili niweze kuyashinda majaribu yote yanayokuja mbele zangu” akaomba halafu akaufunika uso wake kwa viganja vya mikono “Elvis uko wapi ? Nakuhitaji sana katika wakati huu mgumu ninaoupitia.Neno lako moja tu linaweza kuniondolea haya maumivu yote niliyonayo na nikawa na furaha kuliko wanawake wote duniani.I love you Elvis,I love you so much.Please come back !! Akatolewa mawazoni baada ya picha ya Dr Steven kumjia “I cheated on my husband.Kwa namna ninavyompenda mume wangu Elvis sikutegemea kama siku moja ningeweza kumsaliti.Nilikuwa nawaza nini hadi nikavunja kiapo cha uaminifu katika ndoa?Jambo hili litanitesa hadi siku ninaingia kaburini” akawaza Patricia “Upendo wa Elvis kwangu siwezi kuuelezea.Ananipenda kupita kitu choche na siku zote amekuwa akisimama pamoja nami na amekuwa niwe mwanamke mwenye furaha zaidi.Anaifahamu hali yangu na ameikubali.Kwa nini nimekosea mtu kama huyu?Sifahamu nini kitatokea siku akigundua kwamba nimetembea nje ye ndoa” Patricia akazidi kulia “ lakini kwa upande wa pili haya yote yamesabishwa na yeye mwenyewe kuwa mbali nami hasa wakati huu wa matatizo makubwa niliyo nayo ambayo yanasababishwa na ndugu zake” Patricia akainuka na kwenda katika picha kubwa ya Elvis iliyotundikwa ukutani akaitazama. “I’m sorry Elvis.I’m real sorry.Nimekukosea sana na sijui nitafanya nini ili uweze kunisamehe kosa hili” akasema Patricia ambaye alionekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa. “Sikutegemea kama siku moja nitapata wakati mgumu katika maisha yangu kama hivi sasa.Naona kama dunia inaniadhibu kwa makosa niliyoyafanya ya kuitoa ile mimba wakati ule ninasoma” akalia Patricia na kwenda kujitupa kitandani ***************** Saa kumi mbili za Alfajiri ilimkuta mkurugenzi wa idara ya ujasusi Meshack Jumbo nyumbani kwa makamu wa rais Dr Shafi Abdulkareem Omar.Aliwahi sana kufika kutokana na agizo la makamu wa rais aliyemtaka afike nyumbani kwake asubuhi na mapema. Baada ya dakika tano toka mzee Jumbo alipowasili makamu wa rais akatokea wakasalimiana halafu wakaeleka katika chumba Fulani kwa maongezi “Mr Jumbo kwanza nakuomba samahani sana kwa kukusumbua.Sikupaswa kuonana nawe asubuhi kama hii lakini kutokana na unyeti wa suala nililokuitia imenilazimu kufanya hivyo” akaanzisha mazungumzo Dr Shafi. “Usijali mkuu.Hizi ni kazi zetu na muda wote tuko kazini kwa ajili ya kuhakikisha kwamba nchi yetu na watu wake wanakuwa salama” akasema Meshack Jumbo “Nafurahi kusikia hivyo Mr jumbo”Akasema Dr Shafi “Mr Jumbo mimi na wewe tuna historia ndefu.Tumekuwa na ushirikiano mkubwa sana na kutokana na uongozi wako thabiti idara yako imekuwa ikifanya kazi zako kwa mafanikio makubwa.”akasema DrShafi.Meshack Jumbo hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu kwa mbali Mr Jumbo” akasema Dr Shafi halafu akatulia kidogo kisha akasema “Nimekuita hapa kwa jambo moja muhimu sana.Nadhani unaelewa fika kwamba pamoja na idara yako kushughulikia mambo makubwa ya ulinzi na usalama wa nchi yetu kuna baadhi ya mambo ambayo hatutakiwi kuyagusa na hata kama tukiyafahamu inatulazimu tuyaache kwani kuyaingilia kunaweza kuipasua nchi”Akasema Dr Shafi na kunyamaza kidogo halafu akasema “Kuna kijana wako mmoja ameingia mahala kusikomuhusu na endapo hatutachukua hatua za haraka kumdhibiti nchi yeu itatikisika” Ni kijana gani huyo na ameingia mahala gani? “Anaitwa Elvis” Akajibu Dr Shafi “Elvis !! Mzee Jumbo akastuka sana “Ndiyo.Anaiwa Elvis.Mbona umestuka sana Mr Jumbo? “Dr Shafi,imenilazmu kustuka kwa sababu unapomzunguzia Elvis unazungumzia kuhusu vijana wachache sana wazalendo ambao wako tayari hata kuimwaga damu yao kwa ajili ya nchi hii” “Sina shaka na uadilifu na uzalendo wake na tunajivunia kuwa na kijana kama huyu lakini pamoja na yote hayo mazuri aliyoyafanya kwa hivi sasa ni mtu hatari mno kwa taifa letu” Mzee Jumbo akainuka na kumtazama Dr Shafi kwa mshangao “Dr Shafi naomba nikuweke wazi kwamba Elvis ni kijana ninayemuamini pengine kuliko wote katika idara yangu.Unaposema eti ni hatari kwa taifa nashindwa kukuelewa” Dr Shafi akatabasamu kidogo na kusema “Usiwe na jazba Mr Jumbo,naomba ukae tuongee kuhusiana na masuala haya mazito” Mzee Jumbo akakaa halafu Dr Shafi akaendelea ‘Mr Jumbo nadhani unafahamu fika kwamba kuna mambo ya ndani kabisa ya kiserikali ambayo yanafahamika kwa watu wachache tu na hata hao wachache hata kwa kuutoa uhai wao hawawezi wakatoa siri.Sifahamu kwa namna gani lakini huyu kijana Elvis ameweza kufahamu jambo moja kubwa na zito la siri na lengo lake ni kulianika jambo hilo kwa umma.Mara tu jambo hili likifika kwa umma wa watanzania taifa litatikisika.Hakuna anayetaka hilo litokee hasa kwa wakati huu ambao tumeanza kufanya vizuri kiuchumi” akasema Dr Shafi Meshack Jumbo akavua miwani yake na kuiweka mezani,akakumbuka mambo yote aliyoambiwa na Elvis jana kuhusiana na biashara ya silaha “Mheshimiwa makamu wa rais unaweza kuniambia ni jambo gani hilo la hatari aliloligundua Elvis? Nahitaji kulifahamu” akasema Mzee Jumbo “Kwa sasa sintaweza kukueleza ni jambo gani kwani bado uchunguzi unaendelea kuhusiana na amefahamuje jambo hilo lakini naomba uniamini kwamba kwa sasa Elvis ni hatari sana kwa taifa” “Mheshimiwa makamu wa rais ninapata kigugumizi unaponieleza kwamba Elvis ni hatari na kwamba ana jambo analifahamu ambalo ni hatari kwa taifa.wakati mimi kama mkuu wake wa kazi sifahamu chochote kuhusiana na suala hilo naomba unifafanulie tafadhali” akasema Meshack Mr Jumbo utafahamishwa kila kitu mara uchunguzi ukikamilika.Wakati uchunguzi ukiendelea kuna jambo nataka lifanyike haraka sana” Kimya kifupi kikatanda mle chumbani baada ya muda Dr Shafi akasema “I want Elvis dead by today evening” “What ?!! mzee Jumbo akastuka na kusimama “That’s impossible.We cant do that!! Akasema “Mr Jumbo hilo ni agizo umepewa na lazima ulitekeleze kama ulivyoagizwa!! “Mheshimiwa makamu wa rais nafahamu idara ninayoiongoza iko chini yako na wewe unaweza kutoa amri ya kitu chchote kifanyike ndani ya idara yangu na mimikazi yangu ni kutekeleza lakini kwa hili unaloliagiza nataka kupata sababu itakayoniridhisha kwa nini Elvis auae? “Mr Jumbo nimekwisha kueleza kwamba Elvis ni mtu hatari kwa maslahi ya taifa na kwa maana hiyo lazima tumuondoe haraka sana kabla hajasababisha madhara makubwa” Uso wa mr Jumbo uliloa jasho.Hakuamini kama maneno yale yanatoka katika kinywa cha makamu wa rais “Dr Shafi wewe ni mkuu wangu na siku zote nimemkuwa nikitii maagizo yako lakini katika hili utanisamehe.Siko tayari kufanya hivyo unavyonitaka nifanye.Elvis ni kijana ambaye taifa linatakiwa kujivunia kuwa naye na si kufikiria kumuua” Dr Shafi akaonekana kuanza kukasirika,akasema “Mr Jumbo si mara ya kwanza tumewakata kauli baadhi ya vijana wetu ambao wamekuwa na mwelekeo hasi na hatari kwa taifa.Umesahau kuhusu Alfred Chiteka? Vipi kuhusu David Agomwile?Diana katope je?hawa walikuwa ni vijana mahiri na wenye mchango mkubwa kwa taifa lakini kwa sababu waligusa mahala wasipotakiwa ilitulazimu tuwaondoe na hivyo ndivyo tutakavyofanya kwa Elvis.Lazima naye tumuondoe hata kama ana umuhimu mkubwa kwa taifa” akasema Dr ShafiMeshack Jumbo alionyesha kuchanganyikiwa .Akasema “Dr Shafi usinidanganye eti Elvis anatakiwa kuuawa kwa ajili ya maslahi ya nchi.Huo ni uongo wa mchana.Ninakufahamu vyema umekuwa ukitumia idara yangu kulinda maslahi ya vigogo na wakati mwingine kupelekea hata kupoteza maisha ya vijana wazalendo wenye uchungu na nchi yao.Elvis siko tayari kumuangamiza kwa sababu ya maslahi ya wakubwa!! akasema kwa hasira Meshack Jumbo huku akigonga meza.Kitendo kile kikamkasirisha sana Dr Shafi “MrJumbo tafadhali naomba tusilifanye jambo hili kuwa gumu.Mimi ni mkubwa wako kiazi na idara yako iko chini yangu kwa maana hiyo nikisema kitu hakuna wa kukipinga.Kama hutakuwa tayari kutekeleza maagizo yangu basi nitatafuta watu wengine ambao wako tayari kuyatekeleza.Nadhani unaelewa ninamaanisha nini” akasema Dr Shafi “Huu ni mtihani mkubwa kwangu.Elvis amegusa maslahi ya vigogo na sasa maisha yake yako hatarini.Hapana siwezi kuwapa nafasi ya kumuua Elvis.Lazima nimsaidie.I have to do something” akawaza Mr Jumbo kisha akasema “Dr Shafi wewe ni kiongozi wangu na siwezi kupingana na maamuzi yako.Utanisamehe kwa matamshi yangu ni kutokana na namna nilivyostuka kwani Elvis ni mmoja wa vijana ninaowaamini sana.Lakini hata hivyo hainizuii kumuondoa kwa maslahi mapana ya taifa.Niko tayari kufanya hivyo lakini nina ombi moja.Hakikisha damu ya Elvis haipotei bure bali iwe ni kweli kwa maslahi mapana ya nchi vinginevyo damu ya kijana huyu itaendelea kutulilia hadi siku ya mwisho” akasema Meshack Jumbo.Kauli ile ikaonekana kumfurahisha Dr Shafi akatabasamu na kusema “Sasa tunaweza kuzungumza.” Akacheka kidogo kisha akaendelea “Mr Jumbo uongozi ni kitu kigumu sana na wakati mwingine tunalazimika kufanya maamuzi magumu na mojawapo ni hili la kumuondoa Elvis.Ninakuhakikishia kukupa taarifa kuhusu uhatari wa Elvis mara uchunguzi ukikamilika ndani ya kipindi kifupi toka sasa.Pili kuna kijana atakuletea kamzigo Fulani naona ukapokee.Kuna kijihela cha kunywea maji kama milioni mia moja” Mzee Jumbo akatabasmu na kusema “Nimekuelwa vizuri Dr Shafi.Niambie unataka kazi hii tuifanye lini? “Soon as possible.Nataka hadi saa sita za usiku leo Elvis asiwepo katika dunia hii.Mpango wote uko hivi.Utapigiwa simu na mtu asiyejulikana akikueleza kwamba mtu anayetafutwa sana na serikali ya Tanzania akihusishwa na vitendo vya kigaidi Abdullah Abdullah ameonekana katika msitu wa Ngezi .Utamtuma Elvis aende akafanye uchunguzi na huko atakutana na vijana walioandaliwa na watamzimisha.Kila kitu tayari kimeandaliwa na tukio linatakiwa litokee saa nne hadi tano leo asubuhi.Hakuna uchunguzi utakaofanyika kwani itaonekana ni kifo kilichotokana na ajali kazini” akasema Dr Shafi “Dr Shafi nimekuelewa vizuri sana lakini naomba ufahamu kwamba moyo wangu unaumia mno kwa jambo hili lakini sina namna nyingine ya kufanya.Maslahi ya taifa lazima yalindwe” akasema Jumbo Maongezi yaliendelea saa moja na dakika ishirini Mesachk Jumbo akaondoka “Toka nimekuwa kiongozi katika idara hii ya ujasusi hili ni jaribu langu la kwanza kubwa na zito.Elvis kuuawa?? Tena kwa ajili ya kulinda maslahi ya vigogo !!akawaza “Nilijua lazima jambo hili aliloligundua Elvis limletee matatizo makubwa.Biashara ile ya silaha inafanywa na vigogo wakubwa na wamekwisha fahamu kwamba wamegundulika hivyo wanataka kummaliza Elvis ili siri zao zisigundulike” Akawaza Meshack jumbo “Makamu wa rais naye anahusika na mtandao huu ndiyo maana hataki kabisa Elvis aendelee kuuchimba mtandao huu kwani atagundua vitu vingi na wanataka afe na biashara zao ziendelee kama kawaida.Siwezi katu kuruhusu Elvis auliwe.Katika suala hili na mimi lazima niingie katika mapambano.Kwanza kupambana kumlinda Elvis na pili kupambana kuuficha mtandao huu na vile vile kuitokomeza kabisa biashara haramu ya silaha inayofanywa na hawa vigogo wa jeshi wakishirikiana na watu waliomo serikalini” Akawaza Mzee Jumbo ***************** Baada ya dakika tano toka alipoondoka Meshack Jumbo,makamu wa rais Dr Shafi bado alikuwa na mawazo mengi “Elvis Tarimo !! akawaza Dr Shafi “Inaonekana ni kijana mahiri sana katika kazi yake na ndiyo maana hata Meshack alistuka nilipomtajia mpango wa kumuua.Kwa upande Fulani nafsi yangu inanisuta kuidhinisha kijana mahiri kama huyu auliwe lakini kwa upande mwingine ninalazimika kufanya hivyo.Kama tayari amekwisha anza kumchunguza Frank basi kuna uwezekano mkubwa akaweza kuchunguza na kuugundua ule mpango wetu wa kuiangusha serikali.Sitaki hilo litokee kwani ikitoea mpango huu ukajulikana basi tumekwisha.Nitakosa kila kitu na kuozea gerezani. Tunatakiwa kuchukua tahadhari angali bado mapema.Kitu chochote au mtu yeyote ambaye ataonekana kuwa ni kikwazo kwetu lazima tumuondoe haraka sana.Katika suala hili sintakuwa na huruma hata chembe” akawaza Dr Shafi na kumpigia simu David “hallo mheshimiwa Shafi” akasema David baada ya kupokea simu “Habari za asubuhi David? “Habari nzuri Dr Shafi.Nimestuka kidogo na simu hii ya asubuhi asubuhi” “Usistuke David,nimekupigia kukupa taarifa kwamba nimetoka kuongea na Meshack Jumbo mkurugenzi wa iadara ya ujasusiasubuhi hii na kila kitu kimekamilika” “That’s good news” “It’s real good news but it wasn’t easy.Jumbo anamuamini sana Elvis na ilikuwa kazi ngumu kumshawishi akubaliane na mpango wa kumuua.Lakini nashukuru alinielewa na akakubali.Kinachofuata sasa ni kujiandaa kuutekeleza mpango huu” akasema Dr Shafi na maongezi yao hayakuchukua muda mrefu wakaagana ****************** Elvis ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka.Pembeni yake alikuwa amelala Doreen.Elvis akahisi uchungu sana kwa kitendo kile cha kumsaliti mke wake Patricia. “Sijui shetani gani amenishawishi hadi nikakubali kuingia katika mtego wa Doreen na kumsaliti mke wangu ambaye niliapa mbele ya madhabahu kwamba nitampenda kwa moyo wangu wote” Akawaza Elvis na kuinama “I’m so stupid.Very stupid !! akasema Elvis kwa sauti akjilaumu kwa kitendo kile.Doreen aliyekuwa amelala akafumbua macho na kumtazama Elvis huku akirembua macho yake.Asubuhi hii alizidi kuonekana mrembo “You are not stupid Elvis” akasema Doreen huku akiupeleka mkono wake kifuani kwa Elvis. Tafadhali Elvis usijilaumu kwa hiki tulichokifanya.You needed it and Patricia wasn’t here.Hata hivyo you are amazing.Mambo unayaweza.Thank you so much Elvis” akasema Doreen “You are crazy.Hiki tulichokifanya ni kosa kubwa sana” akasema Elvis “Usiseme hivyo Elvis.Huna cha kujutia kwa sababu hata Patricia naye amefanya kama wewe.Unajua ni mara ngapi amekuwa akichepuka?Tafadhali usiwe na mawazo hayo.Just relax.You are with me now.Ulichokikosa kwa Patricia utakipata kwangu na kwa muda huu tutakaokuwa tunaishi hapa just forget about Patricia.Niko hapa na nitakupa kila aina ya raha ya hii dunia.I need you Elvis,I need you so badly in my life” akasema Doreen.Elvis akakunja uso na kutaka kusema kitu lakini simu yake ikaita akaichukua na kutazama mpigaji alikuwa ni Meshack Jumbo akasita kupokea “Mbona hutaki kupokea hiyo simu,inatoka kwa Patricia? Akauliza Doreen baada ya kuona Elvis akisita kuipokea ile simu “Inatoka kwa mkurugenzi.Si kawaida yake kunipigia asubuhi namna hii,nahisi lazima kuna jambo” Akasema Elvis “Pokea usikie anachokuambia”akasema Doreen na Elvis akaipkea ile simu “Shikamoo mzee” Marahaba Elvis.Nahitaji kukuona haraka sana” Elvis akastuka kidogo na kuuliza “Kuna nini mkurugenzi? “Kuna suala linahitaji ufumbuzi wa haraka sana” “Tukutane wapi mzee? Akauliza Elvis “Tukutane pale kwa Salhat” akasema Mkurugenzi “Sawa mzee ninaelekea huko sasa hivi”akasema Elvis “What hapened? Akauliza Doreen baada ya kuona Elvis amebadilika “Mkurugenzi anahitaji kuniona sasa hivi” “Kuna nini? “Hajanieleza kuna nini lakini kwa namna alivyosisitiza inaonekana kuna jambo.I have to go” akasema Elvis na kuinuka akaingia bafuni akaoga haraka haraka na kutoka akavaa na kuchukua funguo za gari akamuaga Doreen na kutoka mbio kuelekea gereji akafungua geti na kuondoka “Jamani Elvis katika kazi zote za hii dunia kwa nini ukaichagua hii? Hufanani kabisa na hii kazi” akasema kwa masikitiko Doreen akimchungulia Elvis dirishani akiondoka. “Lazima kuna jambo kubwa limetokea.Si kawaida ya mkurugenzi kunitaka tuonane haraka tena si ofisini bali kwa Salhat kimada wake.Nini kimetokea? Akajiuliza







Elvis ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka.Pembeni yake alikuwa amelala Doreen.Elvis akahisi uchungu sana kwa kitendo kile cha kumsaliti mke wake Patricia. “Sijui shetani gani amenishawishi hadi nikakubali kuingia katika mtego wa Doreen na kumsaliti mke wangu ambaye niliapa mbele ya madhabahu kwamba nitampenda kwa moyo wangu wote” Akawaza Elvis na kuinama “I’m so stupid.Very stupid !! akasema Elvis kwa sauti akjilaumu kwa kitendo kile.Doreen aliyekuwa amelala akafumbua macho na kumtazama Elvis huku akirembua macho yake.Asubuhi hii alizidi kuonekana mrembo “You are not stupid Elvis” akasema Doreen huku akiupeleka mkono wake kifuani kwa Elvis. “Tafadhali Elvis usijilaumu kwa hiki tulichokifanya.You needed it and Patricia wasn’t here.Hata hivyo you are amazing.Mambo unayaweza.Thank you so much Elvis” akasema Doreen “You are crazy.Hiki tulichokifanya ni kosa kubwa sana” akasema Elvis “Usiseme hivyo Elvis.Huna cha kujutia kwa sababu hata Patricia naye amefanya kama wewe.Unajua ni mara ngapi amekuwa akichepuka?Tafadhali usiwe na mawazo hayo.Just relax.You are with me now.Ulichokikosa kwa Patricia utakipata kwangu na kwa muda huu tutakaokuwa tunaishi hapa just forget about Patricia.Niko hapa na nitakupa kila aina ya raha ya hii dunia.I need you Elvis,I need you so badly in my life” akasema Doreen.Elvis akakunja uso na kutaka kusema kitu lakini simu yake ikaita akaichukua na kutazama mpigaji alikuwa ni MeshackJumbo akasita kupokea “Mbona hutaki kupokea hiyo simu,inatoka kwa Patricia? Akauliza Doreen baada ya kuona Elvis akisita kuipokea ile simu “Inatoka kwa mkurugenzi.Si kawaida yake kunipigia asubuhi namna hii,nahisi lazima kuna jambo” Akasema Elvis Pokea usikie anachokuambia”akasema Doreen na Elvis akaipkea ile simu “Shikamoo mzee” “Marahaba Elvis.Nahitaji kukuona haraka sana” Elvis akastuka kidogo na kuuliza “Kuna nini mkurugenzi? “Kuna suala linahitaji ufumbuzi wa haraka sana” “Tukutane wapi mzee? Akauliza Elvis “Tukutane pale kwa Salhat” akasema Mkurugenzi “Sawa mzee ninaelekea huko sasa hivi”akasema Elvis “What hapened? Akauliza Doreen baada ya kuona Elvis amebadilika Mkurugenzi anahitaji kuniona sasa hivi” “Kuna nini? “Hajanieleza kuna nini lakini kwa namna alivyosisitiza inaonekana kuna jambo.I have to go” akasema Elvis na kuinuka akaingia bafuni akaoga haraka haraka na kutoka akavaa na kuchukua funguo za gari akamuaga Doreen na kutoka mbio kuelekea gereji akafungua geti na kuondoka “Jamani Elvis katika kazi zote za hii dunia kwa nini ukaichagua hii? Hufanani kabisa na hii kazi” akasema kwa masikitiko Doreen akimchungulia Elvis dirishani akiondoka. “Lazima kuna jambo kubwa limetokea.Si kawaida ya mkurugenzi kunitaka tuonane haraka tena si ofisini bali kwa Salhat kimada wake.Nini kimetokea? Akajiuliza ENDELEA SEASON 3 Salhat beauty salon ni saluni yenye jina kubwa jijini Dar inayomilikiwa na Bi Salhat mwanamke mwenye asili ya kiarabu ambaye uzuri wake ni wa kipekee kabisa.Mama huyu alikuwa na mahusiano ya siri ya kimapenzi na Mr MeshackJumbo.Inasemekena kwamba ni MeshackJumbo ndiye aliyesaidia kumtorosha mama huyu toka katikati ya mapigano nchini Syria na kumtafutia kibali cha kuishi nchini Tanzania na kumsaidia kupata uraia wa Tanzania .Jumbo na Salhat wana mtoto mmoja wa kike anaitwa Faizat.Mahusiano haya ni ya siri na anayefahamu siri hii ni Elvis ambaye ndiye aliyetumiwa na MeshackJumbo kuhakikisha kwamba Salhat anafika salama nchini Tanzania na hivyo kumfanya mtu peke anayeyafahamu kwa undani mahusiano ya siri ya Salhat na MeshackJumbo Nje ya jengo ilipo saluni hii kubwa na nzuri kulikuwa na magari kadhaa yameegeshwa ya wateja wakihudumiwa asubuhi kabla ya kwenda makazini.Elvis akashuka garini akaangaza angaza kuhakiki usalama halafu akafungua mlango na kuingia ndani.Wateja hawakuwa wengi asubuhi hii na mara akagonganisha macho na bi Salhat ambaye alitabasamu na kumfuata “Karibu Elvis.Umeadimika sana.Siku hizi unaonekana kwa nadra” “Nimebanwa na kazi Salhat na ndiyo maana sifiki mara kwa mara kuwajulieni hali lakini nitajitahidi kukutembela kila pale nipatapo muda.Vipi maendeleo ya Faizat? “Faizat anaendelea vyema” akasema Salhat halafu akamuuliza Elvis kwa sauti ndogo “Elvis kuna nini kimetokea?Mbona Meshackamekuja hapa jasho linamvuja asubuhi asubuhi? “Mzee Meshacktayari amefika? “Ndiyo amefika kitambo kidogo anakusubiri” “Katumia usafiri gani?Sijaliona gari lake hapo nje” “Hakutumia gari lake amekuja na piki piki.Hata mimi nimeshangaa sana kwani sijawahi kumuona Meshack amepanda piki piki .Kitu gani kinaendelea Elvis? Akauliza Salhat kwa wasi wasi “Hata mimi sifahamu nini kimetokea hadi nitakapoonana naye.Yuko wapi? Bila kupoteza muda Salhat akampeleka Elvis katika chumba alimokuwamo MeshackJumbo Shikamoo mzee” akasema Elvis “Marahaba Elvis.Ahsante sana kwa kufika kwa wakati” akasema Meshackhuku akivua miwani yake na kujifuta machoni halafu akamgeukia Salhat aliyekuwa amesimama akimtazama “Salhat lile gari liko tayari? “Ndiyo liko tayari” Akajibu Salhat. “Elvis twende tuondoke” akasema Meshackna kuinuka.Salhat akawaongoza wakapita mlango wa nyuma wakazikuta gari tatu zimeegeshwa “Tumieni gari hili hapa” akasema Salhat akiwaonyesha gari la kutumia.Elvis akachukua funguo kwa Salhat wakaingia garini na kwa kupitia geti la nyuma wakaondoka “Tunaelekea wapi mzee? Akauliza Elvis “Samawati beach hotel” akajibu MeshackJumbo.Elvis akaendelea kukanyaga mafuta bila kumsemesha chochote.Mara kwa mara MeshackJumbo alikuwa anageuka kutazama nyuma akihakiki kama kuna gari lolote linawafuata “Relax Mr jumbo.No body is following us” akasema Elvis. “Are you sure? “Yes” akajibu Elvis Iliwachukua takribani dakika arobaini kufika Samawati beach hotel, moja ya hoteli tulivu iliyo pembezoni mwa bahari ya Hindi.Walishuka garini na kutafuta sehemu tulivu wakakaa “Pole sana mzee” Elvis akaanzisha maongezi.Ilimlazimu kumpa pole MeshackJumbo kutokana n na hali aliyokuwa nayo. “Ahsante sana Elvis.leo kijasho kimenitoka.Tangu nimeanza kuifanya kazi hii nadhani leo ndiyo siku yangu ngumu zaidi” akasema Meshack “Kuna nini kimetokea mzee?akauliza Elvis.Kabla MeshackJumbo hajajibu ikaletwa supu waliyoagiza,akanywa halafu akasema “Nilipigiwa simu jana usiku na makamu wa rais Dr Shafi akinitaka nifike nyumbani kwake leo alfajiri na mapema.Sikujua ananiitia nini lakini kwa namna alivyonipa msisitizo nilihisi kuna suala zito analonitia” akatulia na kunywa supu kisha akaendelea “Nilifika nyumbani kwake alfajiri kama alivyonitaka tukaingia katika chumba cha maongezi ya siri na tukaanza maongezi.Alianza kunieleza mambo mengi tofauti tofauti na mwisho akanieleza kile alichoniitia.Alisema kwamba kuna mmoja wa vijana wangu ambaye amenusa harufu ya jambo Fulani na ameanza kulifuatilia.Aliweka wazi kwamba mtu huyo ni wewe.Ingawa alikataa kata kata kunieleza ni jambo gani umelinusa na unalifuatilia lakini nilijua lazima litakuwa ni suala la ile biashara ya silaha” akanyamaza akanywa supu na kuendelea “Kama ulivyoniambia awali kwamba yawezekana mtandao wa vigogo wanaojihusisha na biashara hii ya silaha ni mkubwa na siwezi kushangaa kama Dr Shafi naye ni mmoja wao.Katika maelezo yake alisema kwamba jambo unalolifuatilia ni zito na athari zake ni kubwa kitaifa na kimataifa endapo watanzania watalifahamu.Ili kuendelea kulinda maslahi ya vigogo waserikali wanaojishughulisha na biashara hizi haramu Dr Shafi na wenzake wamefanya maamuzi” Meshackakasita na kumtazama Elvis usoni “Wameamua nini mzee? Elvis akaulizaWameamua…” akataka kusema na kusita tena “Nieleze mzee wameamua nini? “wanataja uuawe” Elvis akatoa kicheko kidogo na hakuonyesha kustushwa hata kidogo na taarifa ile.MeshackJumbo akamshangaa “Elvis kulikoni unafurahi kwa taarifa hizi mbaya?Hili si jambo dogo kama unavyolichukulia kimzaha.Ni jambo zito sana.Watu hawa wamekwisha kuona wewe ni hatari na kikwazo kikubwa kwa biashara zao hivyo suluhu pekee hapa ni kukuua.Wamekwisha dhamiria hivyo na watafanya kila wawezavyo kuhakikisha kwamba wanatimiza lengo lao.Hupaswi kuweka mzaha katika jambo nyeti kama hili.Nafahamu unaweza kuliona ni jambo dogo kwa kuwa unao uwezo wa kujilinda lakini hawa jaama ni wanyama sana na wana nguvu.Wanatumia madaraka waliyonayo kufanikisha mipango yao.Huwezi pambana nao ukiwa mwenyewe lazima watakumaliza tu” akasema MeshackJumbo akionekana kukerwa sana na namna Elvis alivyolipokea suala lile “Nimekuelewa mzee na nimecheka kidogo kwa sababu tayari nilikwisha fahamu jambo kama hili lipo na linaweza kutokea muda wowote.Nilikuwa na imani kubwa kwamba katika biashara hii ni kubwa na inahusisha watu wazito na kitendo cha kuingiliwa maslahi yao ni kujichimbiakaburi.Ninafahamu vizuri mambo haya yanavyokwenda mzee na kile nilichokuwa nimekifikiria tayari kimetokea.Tayari tumefahamu kwamba vigogo wakubwa wa serikali nao ni wanufaika au wanashiriki katika biashara hii na ndiyo maana wako tayari kuondoa kizingizi chochote kinachojitokeza mbele yao ili biashara yao isikwame.Hii ni vita kali mzee” akasema Elvis “Elvis nashukuru kama ulilitambua hilo mapema na ukajiandaa.Sasa tuna uhakika mkubwa kwamba mtandao huu unawahusisha watu wakubwa wa serikali na makamu wa rais akiwemo.Hatuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba anahusika lakini kwa hili alilolitamka leo nina uhakika mkubwa kwamba na yeye ni mmoja wao.Elvis naomba ufahamu kwamba ofisi yangu imekuwa ikitumiwa vibaya kwa muda mrefu makamu wa rais ambaye idara ninayoiongoza iko chini yake.Amekuwa akitumia idara yangu mara kadhaa kuficha baadhi ya maovu yanayofanywa na viongozi wetu na kwa kwa kutumia kigezo cha usalama wa nchi tumewatoa kafara baadhi ya vijana mahiri na wazalendo walionusa harufu ya mambo yanayofanywa na wakubwa na kuanza kuyafuatilia.Kila maslahi ya wakubwa yalipoguswa basi hutolewa amri ya kumnyamazisha mtu huyo hata kama ni tegemeo kwa taifa na amri zote hizo hutolewa na makamu wa rais.Ndani ya mwaka huu pekee tayari tumekwisha wapoteza vijana watatu mahiri na sasa wanataka wakuondoe na wewe baada ya kuzinasa siri za mtandao wao.Siko tayari jambo hili liendelee” akasema Meshackna kumalizia supu yake “Elvis wewe ni kijana wangu.Nimekupokea na kukulea katika kazi hii na ninakuchukulia kama mwanangu kwa maana hiyo katu sintakubali jambo kama hili litokee kwako.Nitakulinda kwa kila nguvu niliyonayo” akasema Meshackhuku akigonga meza kwa hasira.Kimya kifupi kikatanda “Makamu wa rais aliponieleza kuhusu suala hili nilikataa na hii siko tayari kufanya hivyo wanavyotaka nifanye.Alijaribu kunishawishi nikakataa ikamlazimu kuanza kutumia vitisho.Aliniambia kama ninakataa itamlazimu kutafuta watu wengine wenye uwezo wanaoweza kufanya kazi hiyo ya kukutoa uhai.Kauli ile ilionyesha wazi kwamba wamedhamiria kukuua hivyo ikanilazimu nikubaliane naye kwamba nitatekeleza ombi lake” akasema MeshackJumbo halafu Elvis akauliza “How am I going to die? “Kwa mujibu wa mipango waliyoipanga ni kwamba itapigwa simu ofisini kwangu na mtu ambaye hafahamiki na atasema kwamba amemuona Yule mtu ambaye tumekuwa tukimsaka kwa muda mrefu akihusishwa na milipuko ya mabomu Arusha ajulikanaye kamahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Abdullah.Mtu huyo atasema kwamba Abdullah anajificha katika msitu wa Ngezi.Baada ya kupokea taarifa hiyo nitakutuma uende huko na tayari wao watakuwa wamewaandaa vijana wao eneo hilo na utakapofika watakushambulia kwa kustukiza na kukuua” Meshackakanyamaza akamtazama Elvis na kusema “I”m so scared Elvis.Sijawahi kuogopa katika maisha yangu kama sasa.Nimechanganyikiwa na sijui nini cha kufanya” akasema MeshackJumbo “Tafadhali usiogope mzee wangu.Najua hili ni jambo zito lakini nashukuru kwa kuwa muwazi kwangu kuhusiana na mpango wao wa kuniua.Mpango huu wa kuniua unaonyesha ni jinsi gani jambo hili tunalolifuatilia lilivyo kubwa .Hakuna ubishi kwamba hata makamu wa rais naye anahusika katika mtandao huu na ndiyo maana ametoa amri niuawe.Tayari wamekwisha anza kuingiwa na hofu na ndiyo maana zinafanyika kila juhudi ili waniondoe nisiwe kikwazo kwa biashara yao kuendelea.Kama makamu wa rais naye anajihusisha na mtandao huu ni wazi kuna mambo mengi makubwa yanayofanywa na huu mtandao zaidi ya biashara ya silaha na ambayo tunapaswa kuyafahamu.Nina uhakika mkubwa kwamba kuna mambo mengi mazito yanayofichwa kwa hiyo tunatakiwa kwanza kuwafahamu wote waliomo katika mtandao huu na pili kufahamu mambo wanayoyafanya na mwisho kuwafichua uovu wao” “Elvis vita hii haitakuwa nyepesi” akasema Meshackkwa wasi wasi “Nalifahamu hilo mzee kwamba vita hii si ndogo kwani tunapigana na watu wenye nguvu na uwezo mkubwa ila hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kupambana.Mtandao huu ni hatari mno lakini kwa namna yoyote itakavyokuwa lazima tupambane nao.Damu nyingi za watu wasio na hatia inamwagika huko Congo kwa sababu ya silaha zinazouzwa na mtandao huu.We have to stop them!! “Elvis narudia tena huu si mtandao wa kufanyia masihara.Ndani yake kuna watu wazito.Kuna makamanda wa jeshi na sasa tumeona hata makamu wa rais naye anashirikiana nao na bado hatujui nani na nani wanahusika .Tayari wamedhamiria kukuua and they’ll do anything to make sure you die.Suluhisho pekee ambalo tunaweza kulifanya kwa sasa ni wewe kupotea.Go far away from here.Nitashughulikia kila kitu ili uweze kutoweka.Usipofanya hivyo hawa jamaa watakuua na mimi sitaki hilo litokee” Akasema Meshack “Mzee Jumbo nakushukuru sana kwa kunijali na kujitolea kunisaidia kwa kiwango kikubwa namna hii.Umekuwa nami toka siku ya kwanza nilipoianza kazi hii lakini naomba kwa mara ya kwanza nitofautiane nawe.Sintakimbia wala kujificha.Wakati umefika wa kupambana na mtandao huu na kuyaanika maovu yao kwa dunia nzima.Sijali nini kitatokea lakini lengo langu ni kufikikisha mwisho biashara hii haramu na uovu huu ukome.Marais wetu wanahangaika kila uchao kutafuta amani ya Congo lakini amani haitapatikana kama hawa watu wanaoendelea kuchochea mapigano ya Congo hawatadhibitiwa.Mzee mtandao huu ni mkubwa na inaonekana una wafadhili wake kutoka nje ya nchi kwa hiyo lazima tupambane nao kwa gharama zozote.Kukimbia si suluhu ya kulimalizia suala hili na wala hakutaweza kuuzuia mtandao huu na mamia ya watu wataendelea kuteketea huko Congo kwa silaha zinazouzwa na akina Frank na genge lake.Mzee lazima tupambane nao” akasema Elvis.Mzee MeshackJumbo akakuna kichwa chake na kusema “Namna gani tutapambana na watu hawa?Ni wazi nguvu yao ni kubwa kuliko sisi.Mtandao huu kama ulivyosema unaonekana umeanzia huko nchi za nje.Tutawezaje kuukata mzizi wake? “Tunaweza mzee.Tunaweza kupambana nao” akasema Elvis “Kivipi? Akauliza mzee Meshack Kwa mimi kufa” Mzee MeshackJumbo akastuka na kumtazama Elvis kana kwamba anatazama kitu cha kutisha “Mbona umestuka hivyo mzee? akauliza Elvis “I don’t understand you Elvis.Suala hili ni zito mno lakini wewe unaingiza mzaha” “Hakuna mzaha mzee.Kama ulivyosema nguvu yetu sisi ni ndogo na hatuwezi kupambana na mtandao huu mkubwa na hata nikisema nikimbie watanitafuta mahala kokote nitakakokimbilia kwani mtandao wao ni mrefu sana.Njia pekee ya kupambana nao ni mimi kufa.They want to kill so I have to die” akasema Elvis MeshackJumbo bado aliendelea kumuangalia Elvis usoni kwa macho ya mshangao “Nashindwa kukuelewa Elvis.Una maana gani unapotamka hayo maneno?Please Elvis these people are very dangerous and they’ll kill you !! akasema Meshack “Mzee nina maana kwamba watu hawa tayari wamekwisha tambua kwamba nimewagundua na jambo hili linawapa joto sana na ndiyo maana suluhisho pekee walilonalo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba wananiua ili biashara zao ziendelee kama kawaida bila matatizo.Baada ya mimi kufa hawatakuwa na wasiwasi tena kuhusu mambo yao kuingiliwa na wataendelea na biashara zao wakiamini kikwazo kikubwa kwao kimeondoka.Kwa hiyo mzee lazima mimi nife.Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuufuatilia na kuufutilia mbali mtandao huu.Najua unastuka ninaposema kwamba lazima nife.Hapa ninamaanisha kwamba nitatengeneza kifo changu ili hata hao jamaa waamini kwamba ni kweli nimekufa.Baada ya kushuhudia jeneza langu limefukiwa kaburini basi lengo lao litakuwa limetimia na wataendelea na shughuli zao huku mimi nikipata nafasi nzuri zaidi ya kupambana nao” akasema Elvis MeshackJumbo akavuta pumzi ndefu na kusema “Hapo sasa nimekuelewa unachokimaanisha.Lakini suala la kutengeneza kifo lina changamoto nyingi na linatakiwa lifanywe kitaalamu mno vinginevyo endapo kutafanyika hata kosa dogo basi unaweza ukapoteza maisha kabisa.Tunapaswa kujipanga sana katika jambo hilo” akasema MeshackJumbo “Ni kweli mzee.Suala hili ni gumu na linachangamoto zake lakini pamoja na ugumu na changamoto zake lakini lazima tulifanye.Hii ndiyo njia pekee ya kutuwezesha kupambana na hawa jamaa.Hili suala linawezekana kufanyika lakini tunahitaji kuwashirkisha pia watu kadhaa.Wa kwanza ni daktari wetu wa idara Dr Philip maguswa.Yeye ni mtaalamu na mzoefu katika mambo haya.Atatupa mawazo mazuri zaidi ya kufanikisha mpango huu.Amepata mafunzo makubwa nchini Ujerumani kwa hiyo ni msaada mkubwa kwetu.Tutawashirikisha pia watu wa chumba cha maiti hospitali kuu ya St Clara.Wale haitakuwa shida kubwa kuwashawishi kwani ni pesa tu itatumika na kila kitu kitakwenda sawa” Akasema Elvis na kuendelea “Mpango wenyewe utakuwa hivi.Utapokea simu toka kwa hao jamaa kama alivyokuelekeza makamu wa rais na utamwagiza katibu wako anitaarifu nifike ofisini haraka sana.Lengo ni kuweka ushirikishwaji kwa watu wengine pia wa pale ofisini.Nikifika ofisini utanielekeza nikafanye uchunguzi kuhusiana na mtu tunayemtafuta anayedaiwa kujificha katika msitu wa Ngezi na wakati unanipa maelekezo hayo wanatakiwa wawepo vijana wengine wawili wa idara yetu.Lengo hapa ni kulifanya jambo hili lisionekane kuwa siri.Katika maelekezo yako utataka niongozane na vijana hao lakini mimi nitapinga na kutaka niachwe niende mwenyewe nikafanye uchunguzi na wewe utakubali kwa sharti kwamba mimi nitangulie halafu wewe na hao vijana mtakuwa nyuma yangu ili kunipa msaada pindi ukihitajika.Mimi nitakwenda huko eneo la tukio na nitafanya kile ninachotakiwa kufanya na baada ya hapo nitawasiliana nawe kukutaarifukwamba kila kitu tayari kisha mtasogea eneo la tukio halafu Dr Philip mtakayekuwa mmeongozana naye atanichukua na kuniingiza katika gari lake kunikimbiza hospitali ya St.Clara ambako kila kitu kitakuwa kimewekwa sawa nao watathibitisha kwamba nimefariki.Baada ya hapo maandalizi ya mazishi yatafanyika.Siku ya mazishi ni watu wachache tu watakaoruhusiwa kuniona katika jeneza wakiwamo viongozi wachache wa juu na makamu wa rais akiwemo ili athibitishe kwamba ni kweli nimekufa.Baada ya mazishi ndipo picha likapoanza.unaonaje kuhusu mpango huu? akasema Elvis MeshackJumbo akakuna kichwa kutokana na maelezo yale ya Elvis.Akafikiri kidogo na kusema “Huu ni mpango mzuri sana na utekelezaji wake unahitaji pia kutumia fedha nyingi.lakini suala la fedha halitakuwa na tatizo kwetu kwani Dr Shafi alisema kuna kiasi kikubwa cha fedha nitapatiwa kwa ajili ya kufanikisha mpango huu wa kukuua.Pesa hizo ndizo tutakazozitumia katika kupamba nao” Akasema Meshack “Pamoja na hayo mzee kuna vitu vya muhimu nitavihitaji” akasema Elvis “Sema unavyohitaji Elvis ili vifanyiwe kazi mara moja” “Kuna mtu namuhitaji katika mpango huu” Unamuhitaji nani? “Namtaka Steven mugo. “Unamtaka Steven Mugo?!! MeshackJumbo akastuka sana “Ndiyo mzee.Namuhitaji Steven Mugo.Yule ni mzoefu katika mambo makubwa kama haya na zaidi ya yote ninamuamini kuliko wote katika idara yetu.Nahitaji mtu wa kushirikiana naye katika jambo hili lakini lazima awe ni mtu jasiri,mwepesi kutekeleza mambo na kufanya maamuzi ya haraka na Steven Mugo ndiye hasa anayefaa MeshackJumbo akavua miwani yake na kuiweka mezani akakuna kichwa “Elvis tafadhali naomba uchague mtu mwingine ambaye unaona anaweza akakufaa kushirikiana naye katika mpango huu na si Steven Mugo.Kuna vijana wengi katika idara yetu wanafanyakazi nzuri sana na mahiri katika kazi.Chagua yeyote na mimi nitakupa ila si Steven Mugo.Yule hatuwezi kumpata kwani unafahamu fika yuko kizuizini kwa usalama wa nchi.Alitoa siri za usalama wa nchi na hili ni kosa kubwa .Tafadhali naomba usahau kuhusu Steven .Tafuta mtu mwingine.Huyu hatutaweza kumpata kabisa” akasema MeshackJumbo.Elvis akakohoa kidogo na kusema “Mzee namuhitaji Steven Mugo pekee.Kuna nguvu kubwa inatumika kushinikiza kwamba Steve alifanya h ivyo anavyotuhumiwa kufanya yaani kuvujisha siri za usalama wan chi lakini ukweli ni kwamba Steven hakufanya hivyo na hahusiki kabisa na uvujishaji wa taarifa zile za siri za kuwakamata na kuwatesa majasusi wa nchi jirani.Nimelifanyia uchunguzi suala hili na nimebaini kwamba Steven hahusiki hata kidogo bali ni mpango uliosukwa na wakubwa Fulani ili kummaliza nguvu.Sababu kuu iliyomfanya aangukie katika tuhuma hizi ni sababu za kipuuzi kabisa na za kibinafsi zaidi lakini kwa kuwa aliingia katika anga za watu wenye nguvu basi wameamua kumuonyesha nguvu zao ila ukweli ni kwamba Steve hana hatia.Tafadhali mzee naomba ufanye kila linalowezekana ili nimpate Steven.Nakuahidi baada ya suala hili kumalizika mimi na yeye tutawasilisha mezani kwako ushahidi usio na shaka wa kuonyesha kwamba Steven hakuhusika na kuvujishwa kwa taarifa za siri” MeshackJumbo akainama na kufikiri kwa muda akashusha pumzi na kusema “Elvis umeniweka katika wakati mgumu sana lakini hata hivyo nitaangalia namna ya kufanya ili aweze kupatikana lakini hakikisha kwamba hatoroki na wala hafanyi jambo lolote litakalomuingiza katika matatizo makubwa.Nimeamua kujitoa mhanga kuubeba mzigo huu kwa kuwa ninakuamini Elvis hivyo usiniangushe tafadhali.Mchunge sana Steven asituingize katika matatizo mengine.Kitendo cha mimi kumtoa tayari kitakuwa kimeniweka matatizoni na sitaki kuongeza matatizo zaidi kwa wakati huu ambao tuko katika matatizo makubwa” akasema Meshack. “Usihofu mzee.Steven ni kijana mzuri na atakuwa na msaada mkubwa kwetu .Naomba sasa umuite DrPhilip ili afike hapa mara moja tumueleze mpango huu na yeye atupe mawazo yake” akasema Elvis na MeshackJumbo akatoa simu akampigia DrPhilip akamtaka afike mara moja pale hotelini *******************





Ilimlazimu Dr Philip kutumia usafiri wa pikipiki ya kukodi kumfikisha Samawati beach hotel kwani mkurugenzi wake MeshackJumbo alimtaka asitumie gari.Alimlipa kijana wa piki piki akaangaza pande zote kuhakiki usalama wake halafu akaingia hotelini akaelekea moja kwa moja mahala alikokuwa MeshackJumbo “Karibu sana Dr Philip.Nashukuru umefika kwa wakati” “Imenilazimu kutumia bodaboda” akajibu Philip “good.Umefanya jambo zuri.Una hakika hakuna aliyekuwa anakufuatilia huko utokako? “Hakuna mzee.Ni salama kabisa” akasema Dr Philip “Mzee uliniambia uko na Elvis,mbona simuoni hapa? Akauliza DrPhilip Kabla MeshackJumbo hajajibu kitu Elvis akatokea,akasalimiana na Dr Philip na maongezi yakaanza “Dr Philip hatuna muda mwingi mahala hapa kutokana na jukumu kubwa lililoko mbele yetu” akasema Meshackakanyamaza kidogo halafu akaendelea “Sina shaka nawe hata kidogo Dr Philip na ndiyo maana nimekuita hapa kukushirikisha jambo kubwa .Nina imani utakuwa ni msaada mkubwa kwetu kwani jambo ninalotakakukushirikisha ni la siri kati yetu sisi tuliopo hapa” akanyamaza tena na kumtazama Philip ambaye alitikisa kichwa kukubaliana na kile alichokisema Mechack Jumbo. “Alfajiri ya leo nimeitwa na makamu wa rais nyumbani kwake.Jambo aliloniitia ni zito na la kustusha.Kuna mtandao wa watu unaofanya biashara haramu na ndani ya mtandao huo wamo vigogo wa serikali na baadhi ya wafanya biashara wakubwa.Elvis amegundua biashara wanazozifanya na baada ya kugundua kwamba wamekwisha fahamika wanataka wamuue Elvis kwani tayari amekuwa kikwazo kwao” Dr Philip akapatwa na mstuko mkubwa.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita. Mzee umenistua sana kwa hiki ulichokisema .Ninaomba unifafanulie kidogo nilifahamu jambo hilikwa kina” akasema DrPhilip “Ni hivi” akasema Elvis “Katika siku za karibuni nimefanikiwa kugundua kuhusiana na mtandao unaofanya biashara ya kuwauzia silaha wasi wanaopambana na serikali ya Congo.Mtandao huo unawahusisha watu waliomo ndani ya serikali hapa Tanzania na ndaniya serikali ya Congo.Silaha hizo huagizwa nje ya nchi na kupita katika bandari yetu halafu huishia mikononi mwa waasi wanaopigana na serikali ya Congo ambao huzinunua kwa pesa nyingi na wakati mwingine kubadilishana na madini.Uchunguzi wa mtandao huu na hii biashara bado unaendelea lakini wakati uchunguzi ukiendelea hawa jamaa wamegundua kwamba wamefahamika na suluhisho pekee walilonalo ni kuniua ili wawe salama.Leo alfajiri mkurugenzi ameitwa na makamu wa rais nyumbani kwake na akapewa maagizo ya kuhakikisha ninauawa siku ya leo” akasema Elvis. “Sijawahi kupata taarifa mbaya na ya kustusha kama hii toka nimeanza kazi.Wanataka kumuua Elvis?!! Akasema kwa mshangao Dr Philip. “Najua umestuka sana Dr Philip lakini naomba nikutoe wasiwasi kamba lengo lao haliwezi katu kufanikiwa.Nilipoanza kulichunguza jambo hili nilitegemea kitu kama hiki kingeweza kutokea kwa hiyo nilikwisha jiandaa kisaikolojia.Hizi ni changamoto tunazokumbana nazo katika hizi kazi zetu” akasema Elvis. “Elvis mimi kwa mara ya kwanza nimekasirishwa mno na hiki kitendo kinachotaka kufanywa na hawa vigogo.Sikutegemea kama watu hawa wanaweza kufikia maamuzi makubwa namna hii ya kutaka kukuua mtu kama wewe.Elvis hawa watu kama dhamira yao ni kutaka kukuua basi hawatalala usingizi hadi wahakikishe mpango wao umetimia.Elvis you have to run.Go far away from here” akasema Dr Philip Elvis akatabasamu kidogo na kusema “Ahsante kwa ushauri DrPhilip na hata mkurugenzi alinieleza hivyo kwamba nikimbie lakini mimi siwezi kukimbia.Lazima nipambane nao.Nimekwisha gundua biashara yao haramu lazima niifikishe mwisho.Nitapambana nao hadi dakika ya mwisho.Kukimbia si suluhu kwani hata huko nitakakokimbilia wanaweza wakanisaka na kunipata wakaniua” “Elvis mtandao huu ni mkubwa na una watu wenye nguvu kubwa.Kama maelekezo ya kukuua yametoka kwa makamu wa rais ni wazi mtandao huu ni mkubwa na unaweza kufanya jambo lolote walitakalo kwa wakati wowote.You have to run brother” akasema Dr Philip “Dr Philip nataka lengo lao litimie” “Lengo gani? Akauliza DrPhilip “Wanataka kuniua basi lazima nife ili wawe na amani na waendelee na biashara zao kama kawaida” akasema Elvis na kuzidi kumchanganya Dr Philip “Nashindwa kukuelewa Elvis.Watu hawa wanataka kukuua na wewe bila wasi wasi unakubali wakuue?Kifo chako kitakuwa na msaada gani kwa watu wasio na hati wanaoendelea kuteseka huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo? Tafadhali lifikirie upya hili suala na usilifanyie mzaha!!akasema Dr Philip “Hakuna mzaha katika hili DrPhilip .Kutokana na umuhimu wake ndiyo maana nimekuita hapa ili kwa pamoja tujadiliane namna nitakavyokufa .Ninataka nitengeneze kifo changu ili watu hawa wanaoniwinda wawe na amani na wendelee na shughuli zao.Nataka wawe na uhakika kwamba sipo tena duniani na hiyo itakuwa ni fursa kwangu ya kuwachuguza vizuri na kuufahamu mtandao wao wote” Dr Philip akatikisa kichwa na kusema “Kidogo sasa ninaanza kukuelewa Elvis unachomaanisha.Tayari nilikwisha taharuki kusikia kwamba unataka kufa” akasema Dr Philip “Ahsante kwa kunielewa Dr Philip.Ni kweli kifo changu kitakuwa cha kutengeneza lakini chenye uhalisia mkubwa.Mpango wenyewe umekaa hivi.Mkurugenzi atapigiwa simu na mtu ambaye atajitambulisha kwamba anatoka katika chombo cha usalama na atampa habari kwamba mtu anayetafutwa sana na serikali kwa kuratibu mashambulio mawili ya mabomu jijini Arusha Abdullah Abdullah ameonekana katika msitu wa Ngezi.Baada ya kuipokea taarifa hiyo mkurugenzi atanituma mimi niende huko Ngezi kufanya uchunguzi wa taarifa hizo ambako tayari kuna watu watakuwa wamewekwa ili wanimalize pindi tu nikitokea” akasema Elvis. “Huo ni mpango walioupanga wao ili wanimalize.Sisi mpango wetu ni huu.Akishapokea simu hiyo toka kwa hao jamaa ,mkurugenzi atanituma katika msitu wa Ngezi.Mkurugenzi akiambatana nawe mtanifuata kwa nyuma.Katika eneo nitakaloelekezwa atakuwepo Steven Mugo yeye ndiye nitakayeshirikiana naye katika operesheni hii.Mimi na Steve tutapambana na hao jamaa watakaokuwa wamewekwa hapo kunimaliza na kisha nitawataarifu wewe na mkurugenzi mtafika pale mara moja na wewe kama daktari wa idara utathibitisha kwamba nimekufa na kisha nitapelekwakatika hospitali ya St Clara ambako watathibitisha pia kwamba nimekufa.Katika hatua hiyo wewe ndiye utakayechukua nafasi kubwa kwani itahusisha sana utaalamu wa hali ya juu na ndiyo maana tumekuita hapa ili kwa pamoja tujadili namna ya kufanya kuufanikisha mpango huu” akasema Elvis. Dr Philip akavuta pumzi ndefu na kusema “Nimeusikia mpango Elvis ni mzuri lakini unahitajika utaalamu mkubwa sana na endapo kutaokea kosa hata dogo tu basi tunaweza tukakupoteza moja kwa moja.Naomba niwatoe wasiwasi kwamba jambo hili linawezekana kabisa kukafanyika na kwa upande wangu ninaweza kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuufanikisha.Kuna dawa inaitwa Mephotexis II ambayo hutumiwa na majasusi.Hii ni dawa ambayo inampoteza mtu fahamu kwa muda mrefu na mtu yeyote akimuona mtu aliyepotezwa fahamu kwa dawa hii atahisi amekufa.Dawa hii ni hatari na endapo ikikosewa hata kidogo ikazidishwa basi hautaamka tena.Baada ya tukio la msituni kumalizika nitakuchoma dawa hiyo na utaonekana kama mfu.Mimi ndiye daktari wa idara nikishathibitisha kwamba umekufa hakuna atakayehoji tena.Mkurugenzi atatoa taarifa rasmikwamba umekufa.Baada ya hapo umechagua hosptali ya St Clara lakini napendekezatusiitumie hospitali ile kwani kuna watu wa dini pale na inaweza kuwa vigumu kuwashawishi wakubali kujiunga nasi katika mpango wetu.Nashauri tutumie hospitali ya Rajesh Memorial hospital.Mmiliki sa hospitali ile Dr Rajesh ni rafiki yangu na nina uhakika lazima watakubaliana nami kirahisi.Tutakupeleka pale nao pia watatoa ripoti yao kuthibitisha kwamba ni kweli umekufa.Baada ya hapo nitakuzindua na kukutibu jeraha utakalokuwa umelipata la risasi kisha utaenda mapumzikoni ukisubiri siku ya mazishi” Dr Philip akanyamaza akamtazama Elvis na mzee Meshackkisha akasemaHakuna yeyote atakayeruhusiwa kukuona katika chumba cha maiti hadi siku ya mazishi ambayo napendekeza yafanyike haraka kesho kutwa.Kitakachofanyika siku ya mazishi ni kwamba katika jeneza utakamowekwa kutafungwa kifaa maalum cha kukusaidia kupumia.Mirija miwili midogo itatoka katika kifaa hicho na kuingia mdomoni mwako.Hii ni kwa ajili ya kuingiza hewa safi mwilini.Hakuna atakayeweza kuiona mirija hii kwani itakuwa imefunikwa na bendeji itakayofungwa kuanzia puani hadi shingoni kwa kisingizio kwamba sehemu hiyo imeharibiwa kwa risasi.Kaburi utakamozikwa litajengwa kitaalamu sana ili kuruhusu hewa kuingia ndani.Kwa kigezo kwamba umeumia vibaya sana kwa risasi mwili wakohautaonyeshwa hadharani isipokuwa kwa watu wachache sana wa karibu wakiwemo viongozi ili upatikane ushahidi kwamba ni kweli umekufa.Shughuli za mazishi itabidi zichelewe kidogo ili hadi tutakapofika makaburini kijua kiwe kinazama.Kwa kuwa muda utakuwa umekwenda shughuli zitafanyika haraka haraka hapo makaburini na watu wataombwa kurejea majumbani na kuwaacha mafundi wakilifunika kaburi.Baada ya watu kuondoka mafundi hao nao wataondolewa kwa kigezo cha kufanya mambo ya kiusalama na hapo ndipo Stevenatakapoingia na gari lenye jeneza lingine na tutalibadilisha jeneza kisha kaburi litafunikwa na picha itaishia hapo” Kimya kikatawala.Baada ya muda Elvis akasema “Una mpango mzuri sana Dr Philip.Ahsante kwa mchanganuo huo mzuri.Binafsi ninakubaliana na mpango huo japo kuna baadhi ya vitu tutaviongeza ili kuuweka mpango huu vizuri zaidi” “hata mimi sikutegemea kama Dr Philip unaweza kuwa mwepesi wa kufikiri namna hii.Nimeupenda mpango huu.Natumai kama ukienda vizuri basi lengo letu litafanikiwa” akasema mzee MeshackJumbo Majadiliano marefu kuhusiana na mpango ule yaliendelea na hatimaye wakatawanyika ili kwenda kuanza maandalizi.Dr Philip akaelekea Rajesh memorial hospital kuonana na Dr Rajesh ,mzee MeshackJumbo na Elvis wakaelekea katika nyumba alikofungwa Steven Mugo. ****************** “Sasa nayakumbuka maneno ya Patricia ambayo amekuwa akiniambia mara kwa mara kwamba katika kazi zote za dunia hii kwa nini niliamua kufanya kazi hii?Ninaipenda sana kazi hii lakini kwa sasa ninaanza kuyaonja machungu yake.Ni kazi iliyojaa hatari kila kukicha.Wanataka kuniua.Nitakufa kama wanavyotaka lakini hawajui kama nitarejea kama mzimu na kuwawinda usiku na mchana.Hawatapata usingizi na mwisho wa yote nitahakikisha mtandao wao wote unasambaratishwa.Sintafumba jicho hadi pale nitakapohakikisha mtu wa mwisho katika mtandao huu ametiwa nguvuni.Siwezi kukimbia na kwenda kujificha mbali wakati ndugu zetu wa Congo wakiangamia kwa silaha zinazouzwa na genge hili la maharamia.Lazima nipambane nao hadi mwisho” akawaza Elvis na kumkumbuka Patricia akahisi kuumia moyoni “Masikini Patricia mke wangu sipati picha atakuwa katika hali gani pindi akipata taarifa za kifo changu.Pamoja na yote yaliyotokea katika ndoa yetu lakini kuna kitu kimoja tu ninachokiamini,Patricia ananipenda mno na atakapopata taarifa za mimi kufariki maisha yake hayatakuwa sawa tena.She”ll never be the same ! nifanye nini sasa? Akajiuliza Elvis wakiwa garini “Jambo hili la kifo changu litawaumiza watu wengi sana hasa mke wangu kipenzi na mama yangu,pia ndugu zangu,lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kutengeneza kifo changu ili niweze kuumaliza mtandao huu hatari.Hata nikiamua nikimbie bado maisha yangu hayatakuwa na amani na nitakimbia hadi lini?Kitu pekee hapa ni kutulia na kupambana.Nisipofanya hivi maisha ya watu wengi yataendelea kupotea .Hawana mwingine wa kuwaokoa zaidi yangu” akawaza Elvis “Nina imani Patricia atanielewa nitakapokuja kumueleza dhumuni la kufanya hivi.Japokuwa itakuwa na ugumu kuelewa lakini nitajitahidi hadi aelewe kwamba nilifanya hivi kwa ajili ya kuwaokoa mamia ya watu wasio na hatia wanaopoteza maisha katika nchi jirani ya Congo” Akaendelea kuwaza Elvis “Najaribu kutengeneza picha namna Patricia atakavyoumia.Sikutegemea kama itatokea siku nitamuumiza Patricia kiasi hiki.Naomba Mungu aniwezeshe nimalize kazi hii salama na baada ya kazi hii sitaki tena kuendelea nayo.Nataka nitulie na mke wangu nimfute machozi na kumrejesha katika hali yake ya kawaida.Nataka kuwa huru niishi maisha yenye furaha na mke wangu Patricia” Elvis akaendelea kuumiza kichwa kwa mawazo.Muda wote toka wametoka Samawati hoteli mzee MeshackJumbo amekuwa kimya na hakuongea lolote.Alionekana kusongwa na mawazo mengi.Elvis aliligundua hilo akageuza shingo na kumtazama mzee Meshackaliyekuwa ameinamisha kichwa “Mzee !! akaita Elvis na kumstua MeshackJumbo toka mawazoni Usiwaze sana mzee haya mni mambo ya kawaida katika kazi zetu” akasema Elvis “Ndiyo Elvis ni mambo ya kawaida lakini nashindwa kujizuia kuwaza kwa sababu jambo tunalokwenda kulifanya ni kubwa na la hatari sana.Endapo tutakosea kidogo tu basi tutapelekea mauti yako jambo ambalo sitaki litokee” Elvis akavuta pumzi ndefu na kusema “Ni kweli mzee.Jambo hili ni la hatari sana na kosa dogo tu basi nitakwenda moja kwa moja lakini kitu kimoja kinachonipa matumaini ni kwamba namuamini sana Dr Philip.Nina imani atasimamia zoezi hili na litakuwa na mfanikio” Hata mimi namuamini sana Dr Philip lakini kuna makosa ya kibinadamu yanaweza yakatokea na kusababisha maafa.Sitaki jambo lolote likutokee Elvis na ndiyo maana nathubutu kusema kwamba mpango huu ni mzuri lakini moyo wangu hauna amani kabisa .Vipi kuhusu mkeo?Utamuacha katika hali gani?Ni vipi endapo atagundua kwamba ulimdanganya kuhusu kifo chako?Ndugu zako je watakuchukuliaje pindi wakikuona ukiwa hai hali walihakikisha kwamba umefariki dunia na wakakuzika kaburini? Elvis haya ni maswali ambayo nimekuwa najiuliza kuhusiana na mpango huu tunaotaka kuufanya.Mimi bado nakushauri Elvis kama inawezekana ukubaliane na mpango wangu wa kuondoka kwenda mbali wewe na mkeo na nitawasaidia kwa kila kitu ili muweze kuyaanza upya maisha yenu huko mbali na uachane kabisa na kazi hizi.Ninakupenda sana kijana wangu na ndiyo maana ninakuomba ufanye hivi” akasema mzee MeshackJumbo “Mzee ondoa hofu.Nilikwisha sema kwamba siwezi kukimbia kabisa na wala kukimbia si suluhu ya matatizo haya.Nitabaki hapa na tutaendelea na mipango yetu kama tulivyoipanga.Nitapambana na hawa watu na kama ikitokea nikafariki basi nitakuwa nimekufa kishujaa kwa kutetea damu zawananchi wanyonge wa Congo wasiendele kuuawa.Kuhusu mke na ndugu zangu ni kweli wataumia na hata mimi ninaumia sana moyoni kila nikivuta picha namna mke wangu Patricia atakavyoumia lakini hakuna namna nyingine ya kufanya kuwasaidia ndugu zetu wa Congo zaidi ya kufa.Ninaamini zoezi hili likikamilika basi nitamuelewesha na atanielewa tu lakini kuna jambo moja nataka nikufahamishe mzee wangu” akasema Elvis “Jambo gani? “Baada ya operesheni hii kumalizika na wote tukawa salama hii itakuwa ndiyo kazi yangu ya mwisho.Nataka kuachana na kazi hii na kuanza maisha mapya” Elvis kazi hii huwezi kuiacha.Ni kama vile ukipakwa mafuta ya kichungaji huwezi kuacha uchungaji utaendelea hadi kifo chako.Kwa hiyo sahau kabisa kuhusu kuacha kazi hii.Tunakutegemea sana na hata taifa bado linakuhitaji hivyo ni mapema sana kuanza kufikiria kuacha kazi hii” akasema mzee Jumbohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mzee msimamo wangu ndio huo kwamba hii ni kazi yangu ya mwisho .Nimefanya maamuzi haya kwa ajili ya mke wangu Patricia ambaye ameteseka kwa muda mrefu kutokana na kazi hii.Nimekosa muda wa kutosha wa kuwa naye.Naomba unielewe mzee wangu” akasema Elvis.mzee Jumbo akafikiri kwa muda na kusema “Sawa tutaangalia lakini sijui kama itawezekana” akasema Jumbo na kumuelekeza Elvis njia ya kupita kuelekea mahala alikofungwa Steven Mugo.Ni watu wachache tu aliokuwa wakifahamu mahala aliko Steven,hata Elvis mwenyewe hakuwa akipafahamu Waliwasili katika nyumba iliyozungushwa ukuta mrefu wenye rangi nyeupe.Kuuzunguka ukuta ule kulipandwa nyasi nzuri za kupendeza .Elvis akasimamisha gari katika geti kubwa jeusi.MeshackJumbo akashuka garini na kwenda katika nguzo moja ya geti ambako kulikuwa na kifaa Fulani mithili ya mita ya umeme wa luku akabonyeza namba kadhaa halafu ukatoka mwanga na kummulika usoni.Baada ya muda geti likaanza kujifungua na toka ndani akaonekana mtu mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi.Meshackakamfanyia ishara Elvis aingize gari ndani.Mzee Jumbo akasalimiana na yule jamaa aliyekuwa ndani Elvis akashuka garini na kuwafuata “Elvis kutana na Meja Adolf kutoka jeshi la polisi .Yeye ndiye anayesimamia ulinzi wa nyumba hii” Akatambulisha Mzee Jumbo kisha akamgeukia Adolf “Meja Adolf kutana na Elvis,yuko katika ofisi yangu” Meja Adolf akatabasamu Oh,kumbe wewe ndiye Elvis.Nimekusikia mara kwa mara lakini sikuwahi kupata bahati ya kukutana nawe ana kwa ana.Karibu sana Elvis” akasema Meja Adolf.Mzee Jumbo akamuomba Elvis waongozane kuelekea ndani “Nadhani ni mara yako ya kwanza kufika hapa Elvis” akasema mzee Meshackwakipiga hatua kuelekea ndani zaidi “Ndiyo mzee ni mara yangu ya kwanza.Sijawahi kufika mahala hapa” “Hapa ni mahala pa siri ambako huwa tunawahifadhi watu mbali mbali kwa mfano rais wa Burundi aliyepinduliwa na kukimbilia Tanzania aliishi hapa ,baadhi ya viongozi wengine wandani na nje pia wamewahi kuishi hapa.Kwa sasa Steven Mugo pekee ndiye anayeishi humu ndani akiwa chini ya uangalizi maalum wakati uchunguzi wa suala lake unaendelea” akasema mzee Jumbo huku akiufungua mlango wa chumba kimojawapo na kuingia katika sebule nzuri.Jumbo akamuomba Elvis amsubiri pale sebuleni halafu akaelekea katika chumba anakolala Steven Mugo akabisha hodi mara tatu na sauti toka ndani ya chumba kile ikamruhusu aingie ndani.Taratibu akakinyonga kitasa na kuingia ndani.Steven Mugo alikuwa amejilaza kitandani huku akivuta sigara.Alipomuona MeshackJumbo akachukua gazeti na kuanza kusoma.Hakutaka kumtazama usoni.Mzee Jumbo akaketi katika sofa lilokuwamo mle chumbani akavuta pumzi ndefu na kusema “Habari yako Steven” Steven hakujibu kitu akaendelea kusoma gazeti lake “ Najua hukutegemea kama ningekuja kukuona muda huu na ninafahamu kwamba hautaki kabisa kuiona sura yangu hapa.Ninafahamu mimi nawe hatutazamani usoni hasa kutokana na jambo lililotokea lakini kilichonileta hapa si kulionelea suala hilo ila kuna mtu nimemleta anahitaji kukuona” Steven Mugo akaliweka chini gazeti lake na kumtazama mzee Jumbo “Mgeni gani? Kwa mara ya kwanza baada ya karibu mwaka mmoja na nusu toka amefungwa katika nyumba hii Steven akamsemesha Jumbo “Ni mtu ambaye hukutegemea kabisa kumuona.Uko tayari kuonana naye? Steven Mugo akafikiri kwa muda na kusema “sawa,mlete nionane naye” MeshackJumbo akatoka kwa haraka na kumfuata Elvis “Steven amekubali kuonana nawe.Nafasi ni yako Elvis ongea naye na tafadhali mshawishi akubali kujiunga nawe” akasema MeshackJumbo.Elvis akainuka na kuingia katika chumba alimo Steven. Kwa sekunde kadhaa Elvis na Steve walikuwa wanatazamana.Kila mmoja alikuwa anamshangaa mwenzake.Steven akainuka pale kitandani alipokuwa amekaa na kumfuata Elvis wakakumbatiana kwa furaha “Elvis ! akasema Steven kwa mshangao “Siamini kama hisia zngu zilikuwa za kweli.Nilijua tu lazima siku moja utakuja.Niliwahi kuota kwamba wewe ndiye utakayekuwa mkombozi wangu na leo ndoto ile niliyoota imetimia na Elvis umetia mguu wako hapa .karibu sana” akasema Steven na kumkaribisha Elvis katika sofa lililokuwamo mle chumbani kisha akaenda sebuleni na kurejea na chupa kubwa ya mvinyo na glasi mbili akamimina mvinyo katika glasi zile na kumpatia moja Elvis “Pole sana Steven” akasema Elvis “Ahsante Elvis.Nashukuru umekuja kuniona na ujio wako huu ninaamini utakuwa na neema kubwa kwangu.Elvis nimekuwa nikiishi katika jumba hili kwa miaka kadhaa sasa na hakuna mtu aliyewahi kuja kunitazama zaidi ya huyu mzee wenu na walinzi wa hapa wanaonilinda.Japo ninapata kila ninachokihitaji lakini ni mateso makubwa kuwamo ndani ya jumba hili” akasema Steven. “Pole Steven.Mambo haya yatakwisha tu usihofu” akasema Elvis Elvis ninateseka bila kosa.Nina hakika unazifahamu tuhuma ninazokabiliana nazo lakini naomba nikuweke wazi kwamba sikufanya hicho ninachotuhumiwa kukifanya.Sina kosa lolote nimefungwa hapa bure.Please Elvis help me brother.Bila wewe kunisaidia nitafia ndani ya jumba hili .Nadhani kuna watu wanataka kuniangamiza bila kosa lolote.Do you believe me Elvis?” akauliza Steven.Uso wake ulionyesha huruma. “I do believe you Steven and I”m here to help you .I”m here to take you out of here” akasema Elvis. Steven akashindwa kujizuia kwa furaha aliyoipata akainuka na kumpa mkono Elvis “Ahsante Elvis kwa kuja kunitoa kifungoni.Nimeteseka mno.Tafadhali naomba usiniache humu ndani leo” akasema Steven kwa furaha Elvis akamueleza Steven kila kitu kuhusiana na kinachoendelea baina yake na mtandao wa akina Frank.Steven akavuta pumzi ndefu na kusema “Dah,hawa watu nina hasira nao sana.Usijali Elvis mimi niko pamoja nawe na nitafanya kila niwezalo ili mpango huu ufanikiwe.Nina hasira sana na hawa viongozi wenye kutumia madaraka yao kukandamiza wanyonge.I swear this time I’m going to show them who I real am” akasema Steven kwa hasira “Ahsante Steven kwa kukubali kujiunga nami.Nina imani kubwa nawe na nina uhakika vita hii tutashinda.Naomba unipe dakika mbili nizungumze na mkurugenzi” akasema Elvis na kutoka akaelekea sebuleni alikokuwapo MeshackJumbo “Vipi mambo yamekwendaje? Akauliza Mzee Jumbo “mambo mazuri mzee.Steven amekubali kushirikiana nami” “Good” akasema mzee Jumbo halafu akamtazama Elvis kwa makini na kusema “Elvis kabla hatujatoka hapa una uhakika na hiki unachotaka kukifanya kuhusu kumtumia Steven katika operesheni hii? Akauliza.Elvis akatabasamu kidogo na kusema “Ndiyo mzee nina uhakika na ninachotaka kukifanya.Ninamfahamu vyema Steven Mugo na ndiyo maana nikamchagua yeye ashirikiane nami.Ondoa hofu mzee kila kitu kitakwenda vizuri” “Nashukuru kusikia hivyo kwani siku zote ninayaamini maneno yako lakini mambo yakienda vinginevyo tutakuwa tumejiingiza katika hatari kubwa sana.Tafadhali naomba usimuache Steven afanye jambo lolote la kijinga na kutuletea matatizo sisi tuliomtoa humu hasa mimi” akasema Mzee Jumbo. “mzee naomba usihofu chochote.Tafadhali niamini” akasema Elvis “Nakuamini Elvis” akasema mzee Jumbo kisha akaongozana na Elvis wakaingia chumbani kwa Steven “Steven mkurugenzi ana jambo anataka kukueleza” akasema Elvis na Steven akamtazama mzee Jumbo kwa jicho la chuki .Mzee Jumbo akakohoa kidogo na kusema “Steve nadhani Elvis amekwisha kuelekeza kila kitu kinachoendelea na kwa nini tumekuja hapa hapa kwa hiyo sitaki kupoteza muda kwa kuyarudia yale uliyokwisha elezwa.Ni kutokana na suala hilo alilokueleza Elvis nimeamuakufanya maamuzi magumu sana ya kukutoa humu ndani.Naomba ufahamu kwamba maamuzi haya niliyoyafanya yataniletea matatizo makubwa lakini kutokana na uzito wa jambo tunalokwenda kulifanya na baada ya kuhakikishiwa na Elvis kwamba wewe ndiye pekee anayekuhitaji katika operesheni hii nimelamika kukutoa humu ndani.Ninachokuomba ni kwamba tafadhali usifanye jambo lingine lolote tofauti na kile atakachokuelekeza Elvis.Vile vile naomba usijaribu wala kufikiria kutoroka kwani kwa………………” “Usihofu mzee” Steven akamkatisha mzee Jumbo “Siwezi kutoroka .Kama ningetaka kutoroka ningekwisha ondoka kitambo sana lakini ninaziheshimu mamlaka zilizoniweka humu ndani na ndiyo maana mpaka leo hii niko humu ndani.Siwezi kutoroka kwa sababu sikuwahi kufanya kosa lolote la kunifanya nikimbie.Nitaendelea kuipigania haki yangu hadi pale nitakapoipata .Kama hakuna kingine cha kuniambia tunaweza kuondoka? Akauliza Steven.Elvis na MeshackJumbo wakatazama “Elvis mnaweza kwenda mimi nitabaki hapa kuna mambo nataka kuyaweka sawa.Usijali kuhusu usafiri nitatumia gari la Meja Adolf.Nenda kajiandae kwani muda wowote toka sasa shughuli itaanza” akasema kwa sauti ya chini mzee Jumbo.Elvis na Steven wakatoka na kuingia katika gari wakaondoka kurejea kwa Salhat alikoliacha gari lake. “Namchukia sana Yule mzee.Kwa zaidi ya mwaka sasa leo hii ameweza kusikia sauti yangu.laiti angekuja peke yake ningeweza hata kumfumua magumi.yeye ni sababu ya mimi kuteseka namna hii.Anafahamu kabisa kwamba sina kosa lolote lakini ameshindwa kunitetea” akasema Steven “Usijali Steven mambo haya yatakwisha tu.Ninakuahidi baada ya mambo haya kumalizika basi tutaanza kulishughulikia suala lako na utasafishwa dhidi ya tuhuma zinazokukabili.Mpaka hapa hesabu tayari suala lako limekwisha” Sijui nikushukuruje Elvis kwa kuja kunisaidia .Bila wewe ningefia katika ile nyumba.Hata hivyo sitaki tena kuendelea na hii kazi.Nafikiria kuanza shughuli nyingine .Nitafungua biashara na nitaishi maisha mazuri tu” akasema Steven “Wazo lako ni sawa na langu.Mimi ninaipenda kazi hii lakini nitaachana nayo kwa ajili ya kuwa karibu na Patricia” “Oh ,anaendeleaje mkeo? Tayari mmekwisha pata mtoto? Akauliza Steven na Elvis akahisi kama kuna kitu kimemgonga kichwani. “ Bado hatujapata mtoto” akajibu “mnasubiri nini Elvis? Unataka ufe bila kuacha ukumbusho duniani? Nyie mliobahatika kuoa mnatakiwa kuwa na watoto kwa sababu hizi kazi zetu hazitabiriki muda wowote unaweza poteza maisha” akasema Steven “Ni kweli hayo uyasemayo na ndiyo maana nimefanya maamuzi kwamba hii ni kazi yangu ya mwisho ili nipate muda mzuri wa kuwa na mke wangu.Yeye ndiye kila kitu kwangu.Nitaacha kila kitu nikipendacho kwa sababu yake” akasema Elvis “Patricia anafaa kujivunia sana kuwa na mwanaume anayempenda kama wewe.Toka nimekufahamu ukiwa na Patricia sijawahi kukuona ukiwa na mwanamke mwingine wa pembeni au hata kusikia sifa zako mbaya.Hata mkeo ni mwanamke mtulivu sana.Mna bahati ninyi kukutana.Uamuzi unaotaka kuuchukua Elvis ni uamuzi sahihi na mimi nitakusaidia tutapambana hadi tuhakikishe kwamba tunawafyeka hawa wote wanaosababisha maisha ya ndugu zetu huko Cogo yanapotea kila uchao huku wao matumbo yao yakishiba kwa mauzo ya silaha wanazowauzia waasi” “Mimi na Patricia tuna historia ndefu na ndiyo maana ninasema niko tayari kuacha kila kitu nikipendacho kwa ajili yake” akasema Elvis na mara akakumbuka mambo alioyoyafanya na Doreen na akakumbuka namna alivyomkuta Patricia akitoka hotelini akiwambaya.Hata mkeo ni mwanamke mtulivu sana.Mna bahati ninyi kukutana.Uamuzi unaotaka kuuchukua Elvis ni uamuzi sahihi na mimi nitakusaidia tutapambana hadi tuhakikishe kwamba tunawafyeka hawa wote wanaosababisha maisha ya ndugu zetu huko Cogo yanapotea kila uchao huku wao matumbo yao yakishiba kwa mauzo ya silaha wanazowauzia waasi” “Mimi na Patricia tuna historia ndefu na ndiyo maana ninasema niko tayari kuacha kila kitu nikipendacho kwa ajili yake” akasema Elvis na mara akakumbuka mambo alioyoyafanya na Doreen na akakumbuka namna alivyomkuta Patricia akitoka hotelini akiwatu na ilikuwa ni bahati mbaya.Sikuwa nimedhamiria kufanya kitu kama kile japokuwa Doreen amekuwa akihitaji sana kufanya mapenzi nami toka alipopewa ruhusa hiyo na Patricia kwa kusudi la kuzaa mtoto na mimi.Sijui nilikuwa nawaza wapi hadi nikajikuta nikinasa katika mtego wa Doreen.Ni vipi kama akija leo na kunieleza kwamba ana mimba yangu?Nitakataaje wakati nimefanya naye mapenzi? ” akawaza Elvis







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog