Simulizi : Peniela (2)
Sehemu Ya Tano (5)
“ Peniela anataka kuongea na wewe”
“ Ouh my God ! mambo yameharibika ! akasema John na kuchukua ile simu
“ hallo peniela”
“ John nahitaji kujua jason umemchukua kwa ajili gani?
“ Peniela samahani sikukutaarifu toka mapema kwamba nitamchukua Jason wa ajili ya mahojiano .Kikubwa nilichotaka lukifahamu kutoka kwake ni kwamba kwa nini alitoa taarifa polisi kwamba Elibariki yuko pale kwako? Mtu kama huyu ni wa kukaa naye mbali sana kwani akifahamu siri yako yoyote ile lazima ataitoa kwa polisi.tafadhali penny naomba usiwe na urafiki na watu kama Jason.Ni watu wabaya sana.Watu wanaokuzunguka ambao unawaita ni watu wako wa karibu si watu wazuri hata kidogo.Nimegundua vile vile Elibariki ana mahusiano na mtu mmoja anaitwa Mathew ambaye nimemfahamu ni mtu hatari sana kwetu.Ninahisi atakuwa anakuchunguza na anamtumia Elibariki kupata taarifa zako.Mwisho wa siku atafahamu kwamba wewe ni Tweam SC41 na akiligundua hilo tutakuwa na kaziya ziada ya kufanya kwa hiyo Peniela nakuomba tafadhali sana angali bado mapema achana kabisa na hawa watu.” Akasema John Mwaulaya
“ Is that all? Umemaliza? Akauliza Peniela
“ Penn…” akasema John lakini Peniela akamkatisha
“ naomba unisikilze vizuri sana John. Kwa miaka hii yote umeyaongoza maisha yangu na kuyapeleka ulivyotaka wewe.Sijawahi kukulalamikia hata siku moja kwa nini umeyafanya maishayangu yakawa hivi.Umeniingiza team SC41 ambako nimekuwa kama chombo cha starehe huku nikiwafaidisha ninyi na hao wamarekani.Nimefanya kila ulichoniamuru hata kiwe cha hatarikiasi gani.Maisha yangu hayako sawa na wanawakewengine,siruhusiwi kuwa na mpenzi wala familia na yote hayo nimeyavumilia na sijawhai kulalamika lakini kwa hili mlilolifanya leo mmevuka mipaka na kuanza kuingilia hadi watu wangu wa muhimu sana.jason na Elibariki ni watu wangu wa muhimu sana ambao hata mnifanye nini siwezi kuachana nao,narudia tena siwezi kuachana nao.Ni watu ambao wamenisaidia hadi leo hii niko huru na mnanitumia katika kazi zenu.Nilipatwa na matatizo na kunusurika kufungwa lakini ninyi nyote mliniacha na kunitenga kama siyo mwenzenu lakini ni Jason na Elibariki ndio waliosimama pamoja nami katika kipindi chote cha matatizo wamepambana na hatimaye nikaachiwa huru.hawa ni watu wangu wa muhimu sana na mkimuumiza mmoja wao mjue mmeniumiza mimi pia.Kwa mara ya kwanza ninahisi kuumizwa sana na maamuzi yako john.I’m deeply hurt.” Akasema Peniela
“ Peniela nimefanya hivi kaa ajili ya usalama wako na wa kwetu pia.Nielewe kwamba watu hawa si wazuri hata kidogo na unatakiwa kuanza kuepukana nao.Kama Jason ameweza kudiriki kwenda polisi na kutoa taarifa za kuonekana kwa Elibariki nyumbani kwako na nyumba yako ikazingirwa na polisi unadhani anaweza kushindwa kutoa taarifa zako akigundua kwamba wewe ni Team SC41? Lazima atakuripoti tu.Peniela ..”
“ John No! sitaki kabisa watu wangu wa karibu waguswena mtu yeyote yule.Nimekwisha kwambia kwamba ukimgusa Elibariki au Jason basi utakuwa umenigusa na mimi pia kwa hiyo ninasema naomba Jason aachiwe haraka sana.”
“ Peniela calm down. Hili ni suala ambao unatakiwa ulifikirie kwa umakini mkubwa.Angalia kwa sasa tuko katika hatua za mwishoni kabsia za kukamilisha operesheni yetu kwa hiyo hatuhitaji tena kikwazo cha aina yoyote ile.Elibariki ambaye unasema kwamba unampenda anashirikiana na Mathew mtu hatari sana,unadhani ni kwa nini Elibariki anatafuta ukaribu na wewe? Ni kwa sababu anatumiwa na Mathew kukuchuguza ”
“ John shitaji maongezi yoyote nawe ninachohitaji ni Jason aachiwe huru .Nataka nisikie toka kwako kitu kimoja tu, Jason anaachiwa huru ama haachiwi? Akaliza Peniela kwa ukali.John Mwaulaya akaonekana kukereka sana na kauli ile ya Peniela
“ Peniela naomba usisahau mtu unayeongea naye ni nani kwako? Akasema John kwa ukali
“ Ni nani kwangu? Ni mtu katili asiye na hata chembe ya huruma,mtu mwenye moyo wa kishetani” akasema Peniela bila kuogopa.John mwaulaya akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Peniela kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimetukanwa na mtu tena si mtu baki bali mtu ambaye nimemlea kama mwanangu kwa miaka mingi.”
“ John sijakutukana nakueleza ukweli,hujawahi kuniudhi kama ulivyoniudhi leo.Kitendo cha kumchukua Jason na kuanza kumtesa bila hata ya kunishirikisha mimi kwanza kimeniumiza sana.Endapo Josh asingesahau simu yake na Jason akaitumia kunipigia basi maisha yake yangekuwa hatarini mko tayari hata kumuua kama hatawapa taarifa mnazotaka.How could you do this to me John? Sitaki maongezi zaidi nataka Jason aachiwe mara moja”
“ Peniela huna mamlaka ya kuniamuru chochote.Mimi ndiye ninayepaswa kukuamuru na ninakuamurukwamba kuanzia sasa sitaki ukaribu wowote na Elibariki.Mahusiano yake nawe yamekufa rasmi kuanzia sasa” akasema John kwa ukali
“ Huwezi kuniamuru niachane na Elibariki John.Yule ni rafiki yangu ni mpenzi wangu na kama ukitaka kumdhuru basi anza na mimi kwanza.”
“ Peniela narudia tena kukuonya naomba unisikie ninachokwambia na usiende kinyume na ninachokuamuru.Wewe ni binti mdogo sana na huwezi kushindana na mimi hata kidogo” akasema John
“ what are you going to do John? Are you going to kill me? Try.Come and kill me.I’ll destroy you John.I swear I will destroy you.!! Akasema Peniela kwa hasira.
“ Peniela this is my last warning.Sintakuvumilia kabisa kwa maneno yako unayonitolea.Usinidharau kwa vile unaniona niko kitandani .Naomba usinilazimishe nikuchukie Peniela.” Akafoka John
“ John naomba usinilazimishe na mimi nipambane na wewe. Mimi ndiye niliyeyashika maisha yako kwa sasa kwa hiyo utafanya kile takachokuamuru John.Natoa dakika thelathini Jason awe ameachiwa ,na kama hutafanya hivyo nitasahau kama wewe umenilea toka nikiwa mdogo na nitakuweka katika kundi la maadui zangu .I will destroy you John.Kumbuka una dakika thelathini za kumuachia Jason .Chaguo ni lako”
“ Peniela unacheza na moto wewe mtoto.Mimi huwa sichezewi namna hiyo na watoto.I’m a devil sasa usitake kuuona ushetani wangu.Nakuonea huruma sana kukuadhibu kwa sababu bado ninakupenda sana.”
“ Ungekuwa unanipenda usingenifanyia mambo kama haya uliyonifanyia.Umeniingiza katika kundi lako na ukayaharibu maisha yangu.Umenivurugia ndoto zangu zote za maisha ,umenifanya nikawa mtumwa wako,nikakufanyia kazi zako kwa kuutumia mwili wangu ,Maisha yangu yamekosa amani,yamekosa furaha,kila siku ninaishi katika hatari kubwa.Nimechoka John .Ninasema nimechoka .I need my freedom back na ninajua hutaweza kuniachia huru kwa sababu mnautegemea mwili wangu katika kufanikisha mipango yenu.” Akasema Peniela
“ Don’t try me Peniela !! akasema John kwa ukali huku akianza kuvuta pumzi kwa shida
“ You have thirty minutes to free Jason .Mkimuachia nataka anipigie simu na aniambie kwamba ameachiwa.baada ya nusu saa bila kupokea simu yake nitajua mmepuuza agizo lagu na mtaona nitakachowafanyia” akasema Peniela na kukata simu.JohnMwaulaya kwa hasira akairusha simu ileukutani ikavunjika .Alianza kuhema kwa taabu sana.Josh akamuita daktari anayemuhudumia na kwa haraka akamuwekea kifaa mdomoni cha kumsaidia kupumua.Hali yake ilibadilika ghafla.
******
“ Sijawahi kukasirika kama nilivyokasirka leo.Kitendo cha kumteka Jason na kwenda kumtesa ni kitendo ambacho kimenikasirisha na kuniumza sana.Jason ni mtu wangu wa karibu na ninamthamini sana.Amenipigania kwa kila namna na hadi leo hii niko huru.Yeye na Elibariki walisimama na mimi wakati ule dunia yote imenitenga.Hawa ni watu wangu ambao niko tayari kuyaweka hatarini maisha yangu kwa ajili yao.Nafahamu kwa sasa mimi na Jason tuna matatizokidogo kutokana na kuwagonganisha na Elibariki lakini hii haijaiondoa thamani yake kwangu.Bado ni mtu muhimu sana kwangu na ndiyo maana alipopata nafasi ya kupiga simu akanipigia mara moja akifahamu kwamba ninaweza kumsaidia.Siwezi kumuacha Jason ateseke.Ninajua lazima watamtesa sana ili awape taarifa na husan taarifa za Mathew kwan ndiye anayeonekana kuogopwa sana na John.”akawaza Peniela akiwa garini akitokea hospitali
“ Nimekuwa mtumwa wa Team Sc41 kwa miaka mingi na sasa nimechoka.Wamenitumia wanavyotaka na sasa wanaanza kuingia hadi kwa watu wangu wa muhimu.Wanataka kunipangia hadi marafiki.Nitaishi vipi bila ya kuwa na marafiki ? Watu wangu wa muhimu watanielewaje? Akajiuliza peniela
“ lazima mambo haya yafike mwisho.Endapo hawatamuachia Jason katika muda niliowapa Iswear lazima nitapambana nao vibaya sana.Nadhani Team SC41 wakati wake umefika.” Akawaza Peniela akasimamisha gari pembeni ya bara bara akachukua simu na kumpigia Mathew
“ hallow Peniela habari yako?akasema Mathew baada ya kupokea simu
“ habari nzuri sana Mathew.Ninaomba unisaidie niongee na Elibariki” akasema peniela
“ kwa sasa siko nyumbani ,nimetoka kidogo nitakaporejea nitampatia simu utawasiliana naye’ akasema Mathew
“ ok Mathew ahsante sana” akajibu Peniela na kukata simu
Hali ya John Mwaulaya ilibadilika sana baada ya kumaliza kuongea na Peniela simuni.Alikuwa akivuta pumzi kwa shida hali iliyomlazimu daktari wake amuwekee kifaa cha kumsaidia kupumua.
“ Martin, is he going to be ok? Akauliza Josh aliyekuwa na wasi wasi mwingi na haliya John
“ I don’t know” akajibu Martin kijana ambaye ana taaluma ya udaktari na ambaye amekuwa akimuhudumia John mwaulaya kwa kindi kirefu
“ Tutafanya nini sasa? Akauliza Josh
“ Subiri kwanza usikate tamaa mapema,baada ya muda atarejea katika hali yake ya kawaida’ akasema Martin.
Pamoja na kuvuta pumzi kwa shida lakini John mwaulaya alionekana kutaka kusema jambo,akamfanyia josh ishara asogee karibu halafu akakitoka kile kifaa cha kumsaidia kupumua
“L.e..le….uhhpphh..” akashindwa kuongea na kukirudisha tena kifaa kile mdomoni.Baada ya sekunde kadhaa akakitoa tena na kujitahidi kuongea
“ Let…hi..him..gooo..!! akasema John huku akinyoosha kidole katika luninga iliyokuwa ikimuonyesha Jason aliyekuwa amelala chini baada ya kipigo kikali alichopewa na Josh baada ya kutumia simu yake kuwasiliana na Peniela
“ Are you sure John ? akauliza Josh kwa mshangao kidogo.John Mwaulaya akamfanyia ishara ya mkono kwamba amuache Jason aende zake.Josh akaonekana kama vile hakubaliani na kitendo kile John akamfanyia ishara amsogelee akatoa kile kifaa cha kumsaidia kupumua akasema
“ Mpigie Pen..nniela..mwambie tum..tu..tumemuachia Jas..’ akasema John kwa taabu,martini akakirudisha kifaa kile mdomoni mwa John
“ Umesikia alichokwambia Josh? Go do it ! John hahitaji kuongea tena mida hii.Go Josh” akasema Martin na Josh akatoka mle chumbani akaelekea katika chumba alimo Jason.Akamtazama alivyokuwa amelala pale chini
“ Una maisha marefu zaidi ya paka kenge wewe.Leo ningekufanyia kitu kibaya sana umshukuru Peniela.bila yeye sijui kama ungetoka humu una meno yote”akawaza Josh huku akimtazama Jason kwa hasira sana. Akamuendea pale chini na kumpiga teke la mgongo.
“ Inuka paka we! Akasema kwa ukali na kumuinua Jason aliyekuwa akivuja damu akamtazama kwa hasira na kusema
“ Una bahati sana .Tunakuachia uondoke lakini ukithubutu kufumbua mdomo wako na ukasema chochote kuhusiana na kilichotokea leo ,nakuhakikishia kwamba haitatuchukua dakika thelathini sisi kufahamu na hautakuwa na sehemu ya kukimbilia kwani tutakusaka katika kila kona na tutakupata.Nikikupata nitakufanyia kitu kibaya sana,nitakuondoa jino moja moja kwa kutumia hili koleo” akasema Josh huku akimuonyesha jason kifaa kile kidogo
“ Nitakukata sikio moja moja na kukumwagia tindikali.Nitakukata kiuongo kimoja kimoja and you will die slowly but in great pain.kwa hiyo jihadhari sana usifanye jambo lolote lile kinyume na maagizo ninayokupa.Tumeelewana? akauliza Josh kwa ukali
“ N..dn..ndiyo..” akajibu Jason huku bado damu ikiendelea kumtoka mdomoni.Josh akamrejeshea vitu vyake vyote halafu akamuamuru ainuke wakatoka mle chumbani wakaelekea nje.
“ Ingia katika gari lako uondoke haraka sana,na tafadhali yafanyie kazi yale niliyokueleza.Ukienda kinyume chake litakapokupata hakuna anayeweza kukusaidia tena.keep your mouth shut” akasema Josh .Jason akaingia katika gari lake na kuliwasha kabla hajaondoka Josh akamwambia asubiri.Akachukua simu yake na kumpigia Peniela
“ hallo Josh,nategemea simu hii itakuwa ni ya kunifahamisha kwamba mmemuacha Jason na hajaumizwa” akasema Peniela mara tu baada ya kupokea simu
“ Peniela ongea na mtu wako huyu hapa” akasema Josh na kumpa Jason simu
“ hallo peniela’ akasema Jason
“ Jason ! are you ok? Akaulizaa peniela.Jason akamtazama Josh aliyekuwa katika dirisha la gari akimuangalia
“ ndiyo peniela.I’m ok.Wameniruhusu niondoke” akasema Jason
“ Wamekutesa? Wamekuumiza ? akauliza Peniela
“ hapana hawajanitesa ,walikuwa wakiuliza tu maswali “
“ Ok good.Naomba usiende nyumbani kwako.Nenda moja kwa moja nyumbani kwangu nisubiri pale mimi niko njiani ninaelekea huko .tafadhali fanya hivyo Jasoni kwa usalama wako” akasema peniela
“ sawa peniela nitafanya hivyo” akajibu Jason na kisha akamrejeshea Josh simu yake.
“ hallo peniela,kuna ktu ambacho ninataka kukueleza”
“ Kitu gani josh?
“ Hali ya John si nzuri toka ulipoongea naye simuni.Anavuta pumzi kwa shida sana”
“ Josh naomba usiniambie habari hizo kwa sasa.Sina chochote cha kufanya kwa sasa “akasema Peniela
“ peniela,John ndiye kongozi wetu na baada ya Osmund kufariki John hana tena msaidizi.Wewe ndiye ambaye tunakutegemea “
“ Josh please ,nina mambo mengi ya kufanya kwa sasa.Naomba uniache kwanza nitakupigia simu baadae.Jitahidini kufanya vile muwezavyo kumsaidia” akasema Peniela na kukata simu.
“ John amekwisha nitoka kabisa akilini na sitaki hata kusikia habari zake.Ninachokifikiria kwa sasa ni namna ya kuwalinda watu wangu wa karibu,Elibariki na Mathew wasidhuriwe na mtu yeyote.Kama ikitokea akapoteza maisha its ok.Amezoea kutoa roho za wenzake na yeye zamu yake imefika.John ni mtu ambaye amenilea toka nikiwa mdogo na amenifikisha hapa nilipo lakini ni mtu mkatili sana na hafai kuonewa huruma.Binafsi ameniharibia maisha yangu na kunipotezea kabisa mwelekeo mzima wa maisha yangu.Amenichefua zaidi baada ya kuanza kuwaandama na watu wangu wa karibu .Kwa sasa kuna kitu kimoja tu ninachokifikiria kukifanya….” Akawaza Peniela
“ Sijui jason atanielewaje kuhusiana na tukio hili .Watu ninaoshirikiana nao wamemteka na kumtesa sana.Hakuna kitu cha kuficha tena hapa kwani kila kitu kiko wazi.Tayari amekwishagundua kwamba ninashirikiana na akina Josh ambao wamemteka na kumtesa .Tayari amekwisha fahamu kwamba nina mahusiano na watu hatari.Taswira yangu kwake imekwishabadilika na sina namna nyingine ya kufanya kumfanya aniamini tena zaidi ya kumweleza ukweli mimi ni nani. Siwezi kuendelea kujificha kwani tayari nimekwisha fahamika.Hii yote imesababishwa na akina John kufanya mambo kwa kukurupuka bila kutumia akili.Nadhani mwisho wa Team SC41 umekaribia sana.”akawaza Peniela na kuongeza mwendo wa gari kuelekea nyumbani kwake kumuwahi Jason
Alifika nyumbanikwake na kulikuta gari la Jason liko nje.Akashuka garini haraka na kwenda kugonga mlango wa gari la Jason ambaye alipomuona Peniela akashusha kioo na kumstua sana Penny baada ya kuona damu nyingi ikimvuja.
“ Ouh my God Jason!..akasema Peniela kwa mshangao akafungua geti haraka haraka wakangiza magari ndani.Jason akashuka huku akichechemea.Peniela akamfuata na kumkumbatia
‘ Oh Jason jamani Pole sana” akasema Peniela Jason hakujibu kitu.Peniela akamshika mkono na kumuongoza hadi chumbani kwake akamvua koti na shati vilivyokuwa vimeloana damu akamshika mkono akamuingiza bafuni.
“ peniela you dont have to do this” akasema Jason
“Jason please let me do this” akasema Peniela huku akiufungua mkanda na kumvua Jason suruali halafu akafungua maji na kumuogesha .Kisha maliza zoezi hilo akachukua kisanduku cha dawa akampaka dawa katika majeraha yote aliyoyapata kutokana na kipgo cha Josh
“ Thank you penny’akasema Jason
“ Please Jason you don’t have to thank me” akasema peniela
“ lazima nikushukuru Peniala.Umeniokoa .Bila wewe watu wale wangenitesa na kuniua.Umeyaokoa maisha yangu” akasema Jason
“ Jason Pole sana kwa kitendo ulichofanyiwa na wale watu.Naomba ufahamu kwamba nimeumizwa sana na kitendo hiki.Hawakutakiwa wakufanyie jambo kama hili ” akasema Peniela huku akimtazama Jason kwa huruma
“ Usijali peniela mimi ndiye niliyefanya ujinga wa kwenda polisi na kutoa taarifa za Elibariki kuonekana nyumbani kwako.Utanisamehe sana kwa jambo hili la kijinga nililolifanya .Niliposikia kwamba Elibariki yuko hapa kwako niliingiwa na wivu mkubwa na niliumia moyoni kwa nini awepo hapa na ndiyo maana nikalazimika kwenda kutoa taarifa polisi kwa lengo la kulipiza kisasi .Peniela naomba unisamehe pia kwa tuko lile nililolifanya siku ile la kusababisha ugomvi mkubwa na Elibariki hapa nyumbani kwako ugomvi uliosababisha nimpige Elibariki na chupa kichwani.Nilishindwa kudhibiti hasira zangu na kufanya kitendo kile cha kijinga ambacho ningeweza hata kusababisha kifo cha Elibariki na ningekuingiza wewe katika matatizo makubwa.Lakni yote haya niliyoyafanya yamesababishwa na pendo wangu mkubwa nilionao kwako.Ninakupenda sana Peniela na ninasika wivu mkubwa kukuona ukiwa na mwanaume mwingine hasa hasa Elibariki”akasema Jason.Peniela akamtazama akamuonea huruma sana.
“ Pole sana Jason.Hukutakiwa kufanya vile ulivyofanya .Hata hivyo nimekwisha kusamehe Jason kwa sababu wewe ni mtu wangu wa karibuna wa muhimu sana.Tumekuwa marafiki kwa muda mrefu na hatujawa kukorofishana.Umesimama na mimi dunia nzima iliponitenga nilipopata matatizo kwa hiyo wewe ni mtu ambaye una nafasi kubwa sana ndani ya moyo wangu .Kuhusiana na kilichotokea leo kuna mambo mengi sana ambayo tunatakiwa kuyaongea na kuyaweka sawa.Kuna masuala ambayo mnatakiwa kuyafahamu lakini kabla ya yote kuna mahala tunatakiwa kwenda.Unafahamu anakoishi Mathew? Akauliza peniela
“ Ndiyo ninapafahamu ” akajibu Jason
“ Ok jiandae tunaelekea huko”akasema Peniela
” Tunaenda kufanya nini huko kwa Mathew? Akauliza Jason
“ Kuna mambo ambayo mnatakiwa kuyafahamu.”akasema Peniela
“ peniela kabla hatujaelekea huko kuna jambo nataka niulize.Watu wale ni akina nani? Unahusiana nao kivipi? Akauliza Jason
“ Usijali kuhusu hilo Jason.Utafahamu kila kitu lakini kwa sasa naomba ujiandae tuelekee kwa Mathew.”akasema Peniela akafungua kabati lake la nguo na kutoa trakisuti nyeusi na kumpatia Jason avae kwani nguo zake zote zilikuwa zimetapakaa damu.Kisha vaa wakatoka wakaingia garini na kuondoka kuelekea kwa Mathew.Mara tu baada ya kuliacha geti Peniela akachukua simu na kumpigia Mathew
“ Hallow Peniela” akasema Mathew
“ Mathew ninaelekea nyumbani kwako,uko wapi?
“ Unakwenda nyumbani kwangu? Mathew akashangaa
“ Unapafahamu nyumbani kwangu? Akauliza Mathew
“Sipafahamu ila niko na Jason ndiye anayenipeleka huko” akasema Peniela
“ Unakwenda kufanya nini?
“ Ninahitaji kuonana nanyi nyote.Kuna mambo ambayo nataka kuongea nanyi” akasema Peniela
“ Penela kwa sasa bado niko katika mizunguko yangu ya kikazi ukifika nisubiri usiondoke,sintakawia sana”akasema Mathew
“ sawa Mathew” akasema Peniela na kukata simu
“ Unamfahamu Mathew? Akauliza Jason
“Ndiyo ninamfahamu yeye na Anitha pia ” akasema Peniela na kumshangaza Jason.Hakujua kama tayari Mathew na peniela wanafahamiana
“ Peniela ni msichana hatari na nimemuogopa sana.Sikuwahi kuhisi hata siku moja kama anaweza kuwa na mahusiano na watu hatari kama wale.lakini watu wale ni akina nani? Shughuli zao nini nini? Ni majambazi? Akajiuliza Jason
“ hapana sina hakika kama wale jamaa ni majambazi.Inaonekana shughuli zao ni zaidi ya ujambazi.wale hawaonekani kama ni majambazi.Ninahisi wanaweza kuwa ni mtandao unaojihusisha na madawa ya kulevya.Ninaweza kuamini hivyo kutokana na jumba lile kubwa walimonipeleka .Lilikuwa ni jumba la kifahari sana ambalo kwa pesa ya ujambazi si rahisi kulijenga .Lazima watakuwa wakijishughulisha na biashara haramu na kama ni hivyo basi hata Peniela naye atakuwa akijihusisha na mtandao huu na ndiyo maana ni binti ambaye anaishi maisha ya hali ya juu sana na akaweza kumiliki yale maduka makubwa mawili ya nguo ambayo hata hivyo yalifilisika alipopata matatizo ya ile kesi ya mauaji.Pamoja na kumalizika kwa kesi yake na kukuta biashara zake zote zimefilisika lakini bado Peniela hajatetereka kiuchumi na anaishi bado maisha ya hali ya juu.Nilitegemea kwamba baada ya kutoka gerezani atakuwa katika hali mbaya kiuchumi na nilikwishajipanga kumsaidia lakini haonekani kabisa kuyumba na maisha yake yanaendelea kama kawaida.Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusiana na suala hili kwamba ni wapi Peniela anakopata pesa za kuendesha maisha yake na leo hi nimepata jibu.Nimeanza kumuogopa sana” akawaza Jason
“ Ninampenda sana Peniela lakini kwa tukio la leo sina hakika kama peniela ni mwanamke anayenifaa.Ukimuona namna alivyo huwezi kumdhania kama anaweza kuwa na mahusiano na watu hatari kama wale.Ninajilaumu hata kwa nini nilifahamiana naye.” Akawaza Jason huku akimtazama Peniela kwa jicho la wizi .
“ Ninaanza kuingiwa na hisia kwamba huenda hata kifo cha edson Peniela akawa anahusika.Suala hili linatakiwa lifanyiwe uchunguzi.Ninakubaliana kabisa na ule usemivusemao kwamba umdhaniaye siye ndiye. Akaendelea kuwaza jason
Safari ilikuwa ya kmya kimya na mara chache waliongea pale Jason alipomuelekeza Peniela njia za kupita hadi walipofika nyumbani kwa Mathew
“ wow ! the house is so big like a palace”akasema Peniela.Mlinzi ambaye hulinda jumba la Mathew tayari alikwisha pewa taarifa za wageni wale akawafungulia geti wakaingia ndani.
“ The house is so beautiful” akasema Peniela akitabasamu na kuufurahia uzuri wa jumba lile la Mathew.Walikaribishwa sebuleni na mlinzi ambaye alipewa maelekezo kwamba awahudumie kwa vinywaji wageni wale.
Sauti za kufungwa kwa milango ya gari zikamstua jaji Eliabriki akafikiri kwamba Mathew na Anitha wamerejea.Akatoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni.Alistuka mno baada ya kukutanisha macho na Peniela .Alitamani kuamini kwamba ile ilikuwa ni ndoto lakini haikuwa ni ndoto bali ni kitu cha kweli alichokuwa akikishuhudia.Peniela alikuwa sebuleni akiwa na jason hasimu mkubwa wa Elibariki.Mara tu alipokutanisha macho na Jason wote wakabaki wakishangaana .
“ Penela my love!..akasema jaji Elibariki .Pemiela akainuka na kwenda kumkumbatia kwa furaha kubwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ouh Elibariki I missed you so much my love” akasema Peniela.Kama ilivyokuwa kwa Elibariki Jason naye alibaki akishangaa kwani hakutegemea kama angekutana na Elibariki pale nyumbani kwa Mathew.
‘ what is he doing here? Akauliza Eliariki kwa ukali huku akimtazma jason kwa hasira
“ peniela whats going on? Why is this bastard here ? Naye Jason akauliza kwa hasira
“ Hey guys..its time now to stop your childish things..You have to stop fighting .What are you fighting for ? akauliza Peniela kwa ukali
“ I hate this bstard so much” akasema Jason
“ I hate you too ..Sikupendi sana Jason” akasema jaji Elibariki huku akitaka kumfuata Jason.Peniela akamzuia
“ Elbariki stop.!!..Do you want to keep on fighting because of me? Ok fine keep on fighting and kill each other” akasema Peniela na kuondoka akaenda kuketi sofani.Jaji Elibariki na jason wakabiki wanatazamana kwa hasira.
“ Nimewaachia uwanja mpigane.Mbona hampigani?akauliza Peniela
“ If I see you near Peniela again I swear in heaven and earth I’m going to kill you” akasema jaji Elibariki na kumfuata peniela pale sofani akakaa pembeni yake.
“ Peniela I’m so sorry .sikutegemea kama ningekutana na huyu kijana hapa.” Akasema jaji Elibariki.Jason akakasirika na kuinuka
“ Elibariki nimekuvumilia sana na sintavumilia tena dharau nyingine yoyote toka kwako.Unadhani ninakuogopa? Akaulizia Jason huku akimsogelea jaji Elibariki.Peniela akamfuata na kumshika mkono
“ Jason naomba ukae na sitaki mtu yeyote aongee zaidi yangu” akasema Peniela kwa ukali.Wote waili Jason na Elibarii wakabaki kimya
“ nawashangaa sana mnapoendelea kupigana kila siku na kutishiana maisha kwa sababu yangu.Mimi ni nani kwenu?Chombo cha kuwastarehesha hadi mfikie hatua ya kutaka kutoana uhai? Akauliza peniela kwa ukali
“ Ninyi nimarafiki na hamna haja ya kugombana.Ni aibu kubwa mkisikika waheshimiwa kama ninyi mnagombana kwa sababu ya mwanamke.” akasema Peniela.
“ Ni huyu ndiye aliyeanza haya yote kwa kuvamia mapenzi ya wat…”akasema jaji Elibariki na akakatishwa na Peniela
“ Elibariki stop.Nimesema sitaki mtu yeyote aongee zaidi yangu” akafoka Peniela
“ Mimi na wewe nani aliyevamia mwenzake.Unajua nimetoka wapi na Peniela? Wewe una mke wako rudi katika ndoa yak……………”akasema Jason lakini akakatishwa na Penny
“ Jason Stoop ! nimesema hiki ni kikaochangu na nyote mnatakiwa make kimya”akasema peniela.akawatazama mashababi wale ambao kila mmoja alikuwa amefura kwa hasira akimtazama mwenzake kwa chuki
“ Ninyi nyote hampaswi kuchukiana wala kugombana.Mnayepaswa kunilaumuna kunichukia ni mimi kwa sababu ndiye niliyekubali kulala nanyi nyote wawili.Hakuna kati yenu aliyefahamu kwamba mwenzake anatembea na mimi hadi siku ile mlipokutana.Kwa maana hiyo basi mnatakiwa mkae na mmalize tofauti zenu.Nimewakutanisha hapa makusudi kabisa ili muweze kumaliza tofauti zenu ninyi wenyewe.Mnatakiwa muongee na muelewane na baada ya hapo kuna jambo kubwa ambalo nataka kuwaambia.kwa sasa nitaondoka na kuwaacha ninyi peke yenu na nitakaporejea nataka muwe mumemaliza tofauti zenu na ndipo tutakapoweza kukaa na kuongea.Siwezi kuongea nanyi sasa hivi wakati ambao kila mmoja wenu amefura hasira kama simba.” Akasema peniela na kuchukua mkoba wake.
“ peniela siwezi kuendelea kukaa hapa.Ninaondoka pia”akasema Jason
“ jason you cant go anywhere.Kaeni hapa na mmalize tofauti zenu ninyi wenyewe.Ninyi ni marafiki na hampaswi kugombana .Be like men ! …akasema peniela na kutoka mle sebuleni akaingia garini na kuondoka.Akiwa garini akachukua simu yake na kumpigia Mathew
“ hallow Mathew ,nimekwisha fika kwako na nimeondoka ila nitarejea baadae kidogo nina maongezi makubwa na Elibariki pamoja na Jason.Kuna mambo ambayo nahitajiku yaweka sawa kati yao’ akasema Peniela
“ sawa Peniela hata sisi tutarejea nyumbani muda si mrefu kwani shughuli yetu tuliyokuja kuifanya tunatarajia kuikamilisha muda si mrefu” akasema Mathew na kukata simu
“ Kuna ulazima wa kufahamu john anaendelaje? Akajiuliza Peniela
“ hakuna haja.sitaki kujua anaendelea vipi.Akili yangu imenituma katika kitu kimoja tu na ambacho ndicho ninakwenda kukifanya.Its time to take down Team SC41.Hakuna aliywahi kufikiria kitu hiki lakini mimi ninakwenda kukifanya.Najua ni hatari lakini sintakata tama I’ll die trying.Nimegundua kwamba bila kufanya hivi sintakuwa huru na sintakuwa na maisha ya kawaida” akawaza Peniela halafu akazitafuta namba za simu za Captain Amos akampigia
“ hallow Peniela” akasema Captain Amos
“ hallow amos.habari yako?
“ habari nzuri peniela ,vipimaendeleo yako?
“Ninaendela vizuri Amos.Nimekupigia kutaka kufahamu kuhusu ule mpango wa kunikutanisha na Dr Kigomba.Maandalizi yanakwendaje? akaulizia Peniela
“ Kila kitu kinakwenda vizuri sana Peniela na jioni ya leo nitakukutanisha naye.Kwa sasa ninaandaa sehemu ya kukutania na nitakutumia ujumbe baadae kukujulisha sehemu ya kukutania.Kitu ambacho ni cha muhmu wakati wa kuonana usionyeshe kama unanifahamu.Utajifanya kwamba ni mara ya kwanza mimi na wewe tunaonana.Kitu kingine ni kwamba jitahidi jambo hili liende kwa haraka kwani muda wowote Dr Joshua anaweza akamkabidhi Dr Kigomba ule mzigo.kwa hiyo lazima tufanye haraka sana kujenga mahusiano ya haraka”
“ usijali Amos.Kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.Huna haja ya kuwa na wasi wasi na mimi” akasema Peniela na kukata simu
*******
Jaji Elbariki na Jason waliendelea kukaa pale sebuleni hakuna aliyetaka kumsemesha mwenzake.Baada ya kama dakika kumi na saba toka Peniela aondoke jaji Elibariki akasema
“ Ok Jason,nimeamua kujisusha .Lets talk like men.” Akasema jaji Elibariki
“ You want to talk? Sina muda wa kuongea nawe Elibariki” akasema Jason
“ Jason lets be like men.Lets talk about this !” akasema jaji Elibariki
“ Ok unataka kuniambia nini? Akauliza Jason
“ Peniela yuko sahihi.Hatuhitaji kugombana.Binafsi sikuwa nikifahamu kama nawewe unampenda Peniela .Nilianza kumpenda peniela wakati wa kusikiliza kesi yake na baada ya kesi kumalizika ndipo nilipooanza kuwa na ukaribu naye na hakuwahi kunieleza chochote kuhusu wewe.Yeye alichoniambia nikwamba hakuwa na mpenzi kwani mpenzi wake alikuwa Edson pekee.Nilimweleza ninavyompenda na alinikubalia tukawa wapenzi.Nilistuka sana siku ile nilipokuona umetokea ghafla mle ndani wakati tukifanya mapenzi.Nilistuka zaidi pia uliponieleza kwamba Peniela ni mpenzi wako.Sote wawili hatukuwa tukifahamu kwamba tulikuwa tunatembea na mwanamke mmoja.Kwa maana hiyo baadaya kuligundua hili ni wakati wetu sasa wa kusameheana na kusahau yaliyopita.Hatuna haja ya kugombana kwani sote tumedanganywa kwa hiyo hata tukigombana hatutapata mshindi.” akasema jaji Elibariki.Maneno yale ya jaji Elibariki na sauti ya upole aliyoitumia kidogo vikamfanya Jason atulize hasira .Akakohoa kurekebisha koo na kusema
“ Nimefahamiana na Peniela kwa muda mrefu kidogo na wakati huo bado alikuwa katika mahusiano na Edson.Baada ya kupatwa na matatizo yake nikasimama pamoja naye kama rafiki.Baada ya kesi kumalizka na akashinda kwa kuwa tayari nilikuwa na hisia za kumpenda mrefu niliamua kuitumia vizuri nafasi hiyo na kumueleza hisia zangu.Peniela akanielewa na akanikubalia kwamba tuwe wapenzi na hakuwahi kunieleza kama ana mahusiano na mtu mwingine yeyote.Siku ilenilipowakuta mkifanya mapenzi na ukatokea ule ugomvi,Peniela alinipigia simuna kunifahamisha kwamba kuna mtu yuko ndani kwake na mtu huyo amekuwa akimsumbua sana kwa muda mrefu akimtaka kimapenzi.Alinambia kwamba niwahi haraka kwa kuwa mtu yule hakuwa na nia njema na alikuwa na wasi wasi kwamba mtu yule angeweza hata kumbaka.Nilifika haraka sana na kukuta kwamba ni wewe ,nilikasirika sana na ndipo ugomzi ule ukatokea.Jana baada ya kutoka katika msiba wa Noah,nilipata taarifa toka kwa Mathew kwamba uko salama na uko kwa Peniela.Nilisikia wivu mkubwa na ndipo nikaenda kutoa taarifa kituo cha polisi na kuwafahamisha kwamba uko pale” akasema Jason na kumstua sana Elibariki
“ It was you? Jaji Elibariki akashangaa
“ yes it was me”akasema Jason
“ ouh my God I cant believe this” akasema jaji Elibarii
“Utanisamehe sana Elibariki kilichonifanya nikafanya jambo lile ni kutawaliwa na wivu na hasira .Sikujua kama kwa kufanya vile nitahatarisha maisha yako”akasema jason.jaji elibariki akakaa kimya kidogo akainama na baada ya sekunde kadhaa akainua kichwa na kusema.
“ katika watu wote ambao ningewadhania sikuwahi kufikiri kama ungeweza kufanya kitu kama kile Jason”
“ Tusameheane Elibariki,nililfanya vile kutokana na hasira na wivu tu.” Akasema Jason
“ Ok tusahau yaliyopita” akasema Elibariki
“ nashukuru sana Elibariki.Ni kweli hatuna sababu ya kupigana kama alivyosema Peniela.Hakuna kati yetu aliyefahamu kama tuna mahusiano na mwanamke mmoja.Wa kulaumiwa hapa ni Peniela” Akasema Jason
“ kweli kabisa Jason.Kuna jambo nimeliona baada ya kuniambia kwamba Peniela alikupigia simu na kukufahamisha kwamba kuna mtu ambaye anataka kumbaka na ukaja ukanikuta mimi.Sikuwahi kutaka kutenda kitendo kama hicho na wala sikuwahi kumlazimisha kimapenzi Peniela.Mimi na yeye tulikubaliana kuwa wapenzi kwa mioyo yetu yote na wala hakukuwa na shinikizo lolote toka kwangu kumtaka anikubali.Kuna picha ninaipata hapa kwamba peniela alitembea na sisi sote wakati akijua kwamba ni marafiki na zaidi ya yote alitaka tukutane uso kwa uso.Ninakumbuka siku ile alitaka tufanye mapenzi sebuleni kumbe lengo lake ni ili utukute pale.” akasema jaji Elibariki
“ Mimi alivyonipiigia simu aliniambia kwamba nikifika nipite moja kwa moja ndani milango iko wazi” akasema Jason
“ Umeona Jason. ! Ni wazi peniela alitaka jambo lile litokee yaani mimi na wewe tukutane,tugongane ,alitaka utukute mimi na yeye tukiwa sebuleni tukifanya mapenzi.Alitaka tugombane,tuchukiane na alifanikiwa lengo lake kwani tuligombana na nusura nipoteze maisha.kwa nini lakini alifanya hivi?kwa nini alitaka mimi na wewe tugombane?akauliza jaji elibariki
“ Elibariki Peniela ni msichana hatari sana,na leo nimelifahamu hilo”
“ Umefahamu kitu gani?akauliza jaji Elibariki
“ Sote hatukuwa sahihi kuhusiana na mtu tuliyekuwa tukimpigania kiasi cha kutishiana kutoana uhai.”
“ kwa nini unasema hivyo Jason? Akauliza Elbariki
“ Peniela hayuko kama vile tunavyomchukulia.Ni mtu hatari sana”akasema Jason
“ Jason bado sijakuelewa.Hebu nifafanulie nifahamu” akasema jaji Elibariki
Jason akamueleza jaji Elibariki kila kitu kilichotokea
“ dah ! ninahisi joto kali.maneno uliyonieleza ni mazito sana.”akasema jaji Elibariki na kusimama akaenda katika friji akachukua maji baridi akanywa na kurejea tena sofani
“Peniela ! Nimemuogopa sana”akasema jaji Elibariki.Akawaza tena kidogo na kusema
“ Ninaweza kukubalina nawe Jason kwamba peniela ana mambo mengi sana tofauti na tunavyomfahamu.Baada ya maelezo hayo kuna kitu nimekikumbuka,wakati nikiwa palekwake kuna nyakati alikuwa akipigiwa simu na hakutaka kupokea mbeleyangu.Alikuwa akitoka na kwenda kuongelea mbali.Hakutaka nisiyasikie maongezi yake.Inaonekana wazi kwamba kuna kitu alikuwa anakificha.”akasema jaji Elibariki
“ Ninavyohisi mimi wale jamaa watakuwa wakijihusisha namadawa ya kulevya kwa sababu jumba lille alikonipeleka Josh si jumba la kawaida.Ni jumba la kifahari sana.kama si madawa ya kulevya basi watu wale watakuwa wakijihusisha na biashara za haramu .Ninahisi vile vile kwamba hata kifo cha Edson,Peniela atakuwa akihusika.” Akasema Jason
“ Hapana.Katika kifo cha Edson Peniela hahusiki kabisa.tayari wahusika wamefahamika” Akasema jaji Elibariki
“ mmekwisha wafahamu? Akauliza Jason kwa mshangao
“ Ndiyo tayari tumekwisha wafahamu lakini bado kuna uchunguzi unaendelea ili kupata taarifa zenye uhakika zaidi “akasema elibariki
“Ni akina nani hao? Akauliza Jason
“ Ni jambo lenye maelezo marefu na ninadhani tusubiri atakapokuja Mathew ndiye atakayekuelezea kila kitu.” Akasema jaji Elibariki
“Sikuwa na taarifa hizo kabisa.Nilidhani kwamba baada ya ugomvi ule kutokea kila kitu kilisimama’akasema Jason
“ hapana Jason.Mambo yaliendelea.Akina Mathew waliendelea kufanya kazi na wamepiga hatua kubwa kuna mambo ambayo yamegundulika na ambayo akina Mathew wanayafanyia kazi.Mathew anaweza kukufafanulia vizuri zaidi kama bado utahitaji kuendelea na operesheni ile tuliyoianza”
“ Niko tayari Elibariki.Niko tayari kuendelea nayo.Nina hamu sana ya kutaka kumfahamu kwa undani peniela ni nani ,na wale jamaa anaoshirikiana nao ni akina nani.”
“ basi kama ni hivyo tumsubiri Peniela jioni atakaporejea kwani ameahidi kuja kuzungumza nasi jambo kubwa,sijui ni jambo gani hilo analotaka tulizungumze” akasema jaji Elibariki.
“ Yawezekana labda anataka kuja kuongelea kilichotokea asubuhi ya leo kwani nilimuuliza kuhusiana na watu wale akaniambia kwamba ataniambia baadae kila kitu .Atanipa ukweli kamili”
“ basi itakuwa vyema tukiendelea kumsubiri.so are we ok now? Akasema jaji Elibariki
“ yes we’re ok.Sisi ni wanaume na hatupaswi kugombana kwa sababu ya mwanamke”
‘ Ahsante sana Jason.nashukuru sana. “ akasema jaji Elibariki,akasimama wakashikana mikono.walimaliza tofauti zao na urafiki ukarejea tena.
Saa tisa za alasiri Mathew na Anitha wakarejea nyumbani baada ya mzunguko mrefu wa siku.Walikuwa wakiifanyia uchunguzi ile taarifa ya kuhusiana na kilichosababisha kifo cha Dr Flora ,iliyotolewa na madaktari bingwa toka hospitali kuu ya taifa.Sebuleni waliwakuta Jaji Elbariki na Jason ambaye uso wake ulikuwa umevimba na una majeraha.Wote wakashangaa
“ Jason nini kimetokea? Umepata ajali? Akauliza Mathew
“ Hapana Mathew si ajali.Nilipata matatizo kidogo nitakusimulia” akasema Jason.
“ Elibariki umeshindaje? Akauliza Anitha
“ Nimeshinda salama kabisa.Poleni na mizunguko” akasema Elibariki
“ Ahsante sana.Tunashukuru tumerejea salama”
“ Mmefanikiwa kupata habari zozote kuhusiana na mke wangu? Akauliza Jaji Elibariki
“ Tulikuwa katika hospitali kuu ya taifa ambako mkeo amelazwa lakini hatukufanikiwa kumuona kwani ulinzi ni mkali sana katika wadi aliyolazwa.Lakini kwa mujibu wa taarifa tulizozipata ni kwamba hali ya mkeo bado si nzuri ingawa ulifanyika upasuaji wa kuondoa risasi mwilini lakini bado hali yake haijawa nzuri na bado anapumua kwa msaada wa mashine .Tuzidi kumuombea kwani kwa sasa anahitaji sana sala zetu” akasema Mathew.Elibariki akainamisha kichwa.Akazama mawazoni.
“ Elibariki najua hiki ni kipindi kigumu sana kwako lakini usijali tuko pamoja.Tutamuombea Flaviana na Mungu atasikia maombi yetu na atamponya.” Akasema Anitha
“ Ahsanteni sana.”akasema Elibariki
“ peniela alikuja hapa? Akauliza Mathew
“ ndiyo alikuja hapa ,mimi ndiye niliyemleta” akasema Jason
“ Alisema kwamba kuna jambo anataka kuja kutuambia ni jambo gani hilo? Aliwadokeza chochote? akauliza Mathew
“ hapana hakutueleza jambo lolote alisema atarejea baadae jioni” akasema Elibariki
“ ok Good.Tumsubiri tuone anataka kutueleza kitu gani.” Akasema Mathew na kuchukua chupa ya maji baridi akanywa alisikia joto sana.
“ Mambo yamekwendaje huko? Akauliza Elibariki
“ Nadhani tuelekee katika chumba cha kazi,kuna mambo ya kujadili “akasema Mathew na wote wakainuka na kuelekea katika chumba cha kazi
“ Jason karibu sana .Kwa muda mrefu tumekukosa katika vikao vyetu na ninadhani Elibariki amekwisha kuelezea kwa undani mahala tulikofikia hadi hivi sasa kuhusiana na ile kazi mliyotupa ya kuchunguza kuhusu mauaji ya Edson,kwa hiyo tunaweza tukaendelea na mambo mengine”akasema Mathew
“Hapana Mathew.Jason bado hajafahamu chochote kinachoendelea kuhusiana na ile kazi tuliyowakabidhi” akasema Elibariki
“ What?! Hafahamu chochote? you guys don’t contact? Akashangaa Mathew
“ Mathew kuna mambo ambayo hatukuwa tumeyaweka wazi kwenu kuhusu mimi na Jason” akasema jaji Elibariki akamtazama Mathew kisha akaendelea
“ kwa sasa hatuna tena sababu ya kulificha jambo hili ni bora tukaliweka wazi kwenu ili mlifahamu”akasema Elibariki akarekebisha koo na kuendelea
“ kwa siku za hivi karibuni mimi na Jason tulikuwa katika mgogoro na hatukuwa na maelewano baina yetu .Kilichotokea ni kwamba…..”akashindwa kuendela na kuwatazama akina Mathew.
“ elibariki tueleze kuna tatizo gani? Akauliza Mathew
“ Kilichokuwa kimetokea ni kwamba sote wawili mimi na Jason tulijikuta tukigongana kwa mwanamke mmoja,Peniela” akasema na kuwatazama akina Mathew huku akiona aibu kidogo
“ Hicho ni kitu cha kawaida kwa wanaume.Nini kikatokea baada ya kugongana? Akauliza Mathew
“ Sote wawili mimi na Jason hatukujua kama kila mmoja ana mahusiano na Peniela.Mimi nilimfuata kwa wakati wangu na Jason naye alimfuata kwa wakati wake.Kilichotokea siku ile tulipogongana ni kwamba Peniela alinipigia simu nikiwa katika msiba wa mama mkwe na kuniambia kwamba ananihitaji sana.Ni usiku ule ambao mlikwenda kufanya uchunguzi wa kilichomuua mama mkwe.Nilipofika kwake akaniomba tufanye mapenzi na kwa kuwa hata mimi nilikuwa na hamu naye sikukataa,tukafanya mapenzi.Kwa kuwa alikuwa na hamu sana na mimi hakutaka hata tuende chumbani akataka tufanyemapenzi sebuleni.Wakati tukifanya mapenzi mara ghafla akaingia Jason na kutukuta tukifanya mapenzi.Uliibuka ugomvi mkubwa kati yetu kila mmoja akimtuhumu mwenzake kumchukulia mwanamke wake.Ugomviule ukapelekea Jason anipige chupa ya kichwa na ndiyo hili jeraha mnaloliona hapa kichwani.Nilipoteza fahamu na niliporejewa na fahamu niliwakuta watu Fulani sebuleni kwa peniela ambao wakaondoka na peniela na wawili kati yao wakanipeleka hospitali.Toka siku ule mimi na Jason hatukuwa katika maelewano na hatukuongea hadi leo hii.”akasema jaji Elibariki na kuwatazama akina Mathew .
“ Imekuwaje leo mkakutana na kumaliza tofauti zenu?akauliza Mathew
“ Kilichotokea leo ni kwamba peniela ametukutanisha mimi na Jason na kututaka tumalize tofauti zetu” akajibu jaji Elibariki
“ peniela again? Huyu huyu aliyewagonganisha na sasa amewakutanisha na kuwataka mpatane? Mathew akashangaa
“Ndiyo.Kuna jambolililompelekea akafanya hivyo”akajibu Jason
“ jambo gani?akauliza Mathew
“ Ilikuwa hivi” akasema jason
“ baada ya ugomvi ule mimina Elibariki hatukuwa tena na mawasiliano yoyote hadi niliposikia kupitia vyombo vya habari kwamba amenusurika katika shambulio na hajulikani yuko wapi.Ni wewe Mathew uliyenifahamisha kwamba Elibariki yuko kwa Peniela.Kwa kuwa bado nilikuwa na ugomvi naye nilikasirika sana na sikutaka kabisa kumuona akiwa na Peniela hivyo wazo lililonijia haraka haraka ni kwenda kutoa taarifa polisi ili Elibariki aondolewe pale kwa Peniela.Sifahamu nini kilitokea lakini leo asubuhi kuna kijana mmoja anaitwa Josh alinifuata nyumbani kwangu akidai kwamba kampuni yao inanihitaji kuwafanyia kazi ya uwakili.Nilikubaliana naye na tukaongozana hadi katika jumba moja kubwa ambalo alidai kwamba mkurugenzi wake ndipo anaishi.Tulipofika pale nikageuziwa kibao nikafungiwa katika chumba na kuanza kuhojiwa maswali kuhusiana na kwa nini nilipeleka taarifa polisi kwamba Elibariki yuko kwa Peniela na maswali mengine wakiniuliza kama ninakufahamu Mathew na walitaka kujua pia unafanya kazi gani n.k .Baadae Josh akanionyesha picha zilizochukuliwa katika kamera iliyofungwa kwa siri nyumbani kwa Peniela.Katika picha ile niliwaona wewe na Anitha mkiwa mmeambatana na Peniela usiku mkiingia ndani.Nikagundua kwamba watu wale walikuwa na mahusiano ya karibu na Peniela.Yule kijana Josh aliondoka ghafla na kuiacha simu mezani nikautumia mwanya huo kumpigia simu peniela na nakumuomba aniokoe kwani niliamini anawafahamu watu wale.Ktendo kile kilimuudhi sana Josh akanishushia kipigo kikali na ndiyo haya majeraha mnayoyaona.Dakika kumi baadae nikaachiwa niende zangu lakini kwa sharti kwamba nisimweleze mtu yeyote kilichotokea na endapo nikienda kuripot kwa vyombo vya usalama basi watafahamu na wataniua.Peniela aliniomba nisiende nyumbani kwangu bali niende nikamsubiri nyumbani kwake.Nilifanya hivyo na kwenda nyumbani kwake nikamsubiri akaja akanitibu haya majeraha na kisha akanitaka nimlete huku akanikutanisha na jaji Elibariki akatutaka tumalize tofauti zetu na kwamba atakaporejea jioni kuna jambo kubwa anataka kutueleza. Kwa hiyo basi tumeongea na tumemaliza tofauti zetu na tunamsubiri atakaporejea ili atueleze alichotaka kutueleza.”akasema Jason
“ Pole sana Jason kwa kilichokupata.Hata hivyo ninafurahi sana kuona mkiwa mmemaliza tofauti zenu .Hivi ndivyo wanaume wanavyomaliza mambo yao.”akasema Mathew kikapita kimya kifupi Elibariki akasema
“ Mathew nadhani Peniela anahitaji kufanyiwa uchunguzi mkubwa kwani anaonekana kuwa na mambo mengi.Anaonekana kuwa na siri kubwa.”
“ Suala la Peniela tutalijadili baadae lakini kwa sasa Jason anahitaji kufahamishwa kilichotokea ili tweze kwenda sawa .Ni kwamba mpaka hivi sasa tumekwisha piga hatua na tayari tumefahamu ni kwa nini Edson aliuawa .” Akasema Mathew na kumsimulia Jason kuhusiana na walichokigundua katika kufuatilia kifo cha Edson.
“ kwa hiyo Jason,hapo ndipo tulipofikia hadi hivi sasa kuhusiana na kifo cha Edson.Kwa hiyo kwa sasa tnaweza kwenda pamoja” Akamalizia Mathew
“ Poleni sana kwa kazi kubwa na ngumu mliyoifanya hadi mkagundua suala hili zito.Sikuwa nikitegemea kabisa kama jambo hili litakuwa namna hii” akasema Jason
“ Ndivyo hivyo lilivyo_Ok tuachane na hayo kwa kuwa sasa wote tunakwenda katika mstari mmoja basi tuendelee na pale tulipokuwa tumeishia.” Akasema Mathew
“ Kuhusu majibu ya zile karatasi bado sijapokea chochote kutoka kwa wale washirika wangu
Wa kule Israel ambao niliwaomba wanisaidie kutafuta kilichoandikwa katika zile karatasi.Nadhani bado hawajapata jibu na pindi wakipata jibu watanifahamisha.Kuhusu ile ripoti ni kwamba taarifa hii haina ukweli wowote.Orodha hii ya madaktari walioorodheshwa hapa si ya kweli na tumefuatilia kila sehemu hadi wizara ya afya na hawana madaktari bingwa wenye majina haya.Kwa maana hiyo basi tayari tumekwisha pata uhakika kwamba taarifa ilehaina ukweli wowote na ni taarifa ya kutunga.Hii ina maana tulikuwa sahihi kwamba dr Flora aliuawa kwa sindano ya sumu kama taarifa yetu ilivyokuwa ikionyesha.Kitendo cha Dr Joshua kuikubali taarifa hii ya uongo na kukataa taarifa ya kweli tuliyompatia kinatufanya tuamini kwamba inaweza kuwa anafahamu ama alishiriki katika kupanga kifo cha mke wake.Ukianza kuangalia namna mlolongo wa mambo yalivyokwenda tunalazimika kuamini kabnisa kwamba haiwezekani mambo yote haya yakafanyika bila ya rais kufahamu. Hatuna ushahidi wa moja kwa moja kumuingiza rais katika mambo haya lakini tunalazimika kuamini kwamba lazima atakuwa anafahamu ama ameshiriki.” Akasema Mathew
“ Guys endapo ikigundulika kwamba rais ameshiriki katika jambo hili nini kitafanyika? Akauliza Jason
“ kama ikigundulika kama rais ameshiriki katika jambo hili ni kitu kimoja tu kitakachofanyika.We’ll take him down.”akasema Mathew
“ Hii si kazi rahisi.Kumuondoa madarakani rais sijambo dogo”akasema Jason
“ Linavyoonekana si jambo dogo lakini ni jambo dogo kama tukiwa na ushahidi wa utosha wa kumtia hatiani.Kuwa rais si kwamba uko juu ya sheria.Ukivunja sheria za nchi lazima ushughulikiwe kama wahalifu wengine.kwa hiyo jamani kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kuhakikisha kwamba tunapata ushahidi wa kutosha kuthibitisha kwamba Dr Joshua anahusika katika jambo hili na hadi hapo tutakuwa na nguvu ya kumuondoa .Ninachowaomba kuanzia sasa ni kujiandaa kwani tunakoelekea si kuzur hata kidogo.Tunakwenda katika shimo la moto na kifo kwa hiyo kila mmoja wetu ajichunge na amchunge mwenzake.Sote tukiwa kitu kimoja na kuifanya kazi hii kwa umoja wetu basi tunaweza kulimaliza suala hili lakini akitokea mwenzetu mmoja akaenda kinyume na sisi basi tutakwama na tutakuwa tumejitengenezea hatari kubwa”akasema Mathew
“ Mathew mimi siogopi kitu na katika suala hili nipo tayari kwa lolote” akasema jaji Elibariki
“ What about you Jason?akauliza Mathew
“ Hata mimi siwezi kupingana na ninyi wenzangu kwani sote lengo letu ni moja tu.Kuhakikisha haki inatendeka.Hata hivyo suala hili ni pana sana na linahitaji watu wengine wa kutusaidia.Sisi peke yetu hatuwezi .” akasema Mathew
“ Unayosema ni ya kweli Jason.Pindi tutakapofanikiwa kuwa na ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Dr Joshua kwa vitendo hivi basi tutatafuta uungwaji mkono lakini kwa sasa tuelekeze nguvu katika kutafuta ushahidi wa kutosha kuweza kumtia hatiani Dr Joshua.” Akasema Mathew
“ Vipi kuhusu peniela? Naye suala lake linakuwaje? Peniela ana mahusiano na wale jamaa ambao kama hisia zangu ni za kweli basi watakuwa wakijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ama biashara nyingine haramu.Tunatakiwa naye pia tumchunguze.”akasema Jason
“ Suala la Peniela ni suala la tofauti kidogo na lenyewe litashughulikiwa kwa namna yake peke yake.Tumuweke pembeni kwa sasa na tushughulike na suala hili kubwa kwanza”akajibu Mathew
“ Ni suala la tofauti? Akauliza Jason kwa mshnagao kidogo
“ Ndiyo Jason.Ninamfahamu Peniela na suala lake liko tofauti kidogo na wala watu hao anaoshirikiana nao si wauza madawa ya kulevya.”akasema Mathew
“ kama si wauzaji wa madawa ya kulevya ni akina nani basi? Akauliza jaji Elibariki
“ kwa kuwa yeye mwenyewe amesema kwamba atakuja jioni ya leo kwa ajili ya kuzungumza nasi basi tumsubiri na atakapofika tutajua anatakakutueleza jambo gani “akasema Mathew
Baada ya maongezi yale jason akaomba atumie gari la Mathew kwenda nyumbani kwake mara moja kwani gari lake aliliacha kwa Peniela.
******
Ni saa kumi na mbili za jioni,Peniela yuko mbele ya meza iliyoshehehi vipodozi vya kila aina akimalizia kuuremba uso wake.Jioni hii alikuwa amependeza kuliko kawaida.Uzuri wake uliongezeka mara dufu.Alivalia gauni jekundu refu lililoenda sambamba na umbo lake jembamba.Yatosha kusema kwamba kama ni kutoa maksi basi peniela usiku huu angezoa maksi zote mia kwa namna alivyokuwa amependeza.Akajitazama tena katika kioo kikubwa akatabasamu
“ I’m so pretty.Ninamshukuru Mungu kwa kunipendelea uzuri huu na ni uzuri huu ambao umekuwa ni kama ua lenye harufu nzuri ambalo huwavutia nyuki kulitembelea na kuling’ang’ania.Pamoja na uzuri huu sina maisha ya kawaida kama wenzangu.Uzuri huu umenifanya niishi maisha mabovu na yasiyokuwa na hata chembe ya furaha ndani yake .Msichana mwenye uzuri kama wangu anatakiwa aishi maisha mazuri akiwa na mume bora na familia yenye furaha .”alipowaza kuhusu suala la familia mara akamkumbuka jaji Elibariki.
“ Sijui Elibariki na Jason watakuwa katika hali gani hivi sasa.Niliwakutanisha makusudi kabisa ili wamalize tofauti zao.Ninataka kuongea nao wakati hawana tofauti na kwa pamoja tunaweza kusaidia katika kuimaliza team SC41.Nimekwisha dhamiria kukimaliza kikundi hiki kwa hiyo siwezi kufanya jambo hili peke yangu ninahitaji waku wa kunisaida , watu ambao ninawaamini nao si wengineni Elibariki na Jason.Nikifanikiwa kuimaliza Team SC41 basi nitakuwa huru na maisha yangu na nitakuwa na jaji Elbariki mwanaume ninayetaka kuanza naye maisha mapya.Ndiye mwanaume ninayempenda.Sijali kama ana mke au hana yeye ndiye mwanaumeambaye ninataka kuishi naye na lazima niwe naye”akawaza peniela halafu akachukua mkoba wake mwekundu na kujitazama tena katika kioo.
“ Kila kitu kimekaa vizuri.its time now to go” akawaza na kutoka akaingia garini akaondoka kuelekea mahala alikoelekezwa na Amos ili akutane na katibu wa rais dr Kigomba.
“ Hii ni kazi yangu ya mwisho ninakwenda kuifanya kwa kutumia mwili wangu na baada ya kuikamilisha basi nitakuwa huru kuishi maisha ya kawaida kama wengine.Baada ya kazi hii hakutakuwa tena na Team SC41” akawaza peniela akiwa garini
“Natamani kufahamu John anaendeleaje lakini nafsi yangu inakataa kabisa.Ili niweze kujiweka huru natakiwa kwanza kumchukia John mwaulaya na ndipo nitakapoweza kupambana naye vizuri na hatimaye kuimaliza Team Sc41.Najua ni kikundi chenye nguvu lakini nitajitahdi kwa kila namna niwezavyo kuweza kukimaliza kikund hiki nandiyo maana ninawahitaji sana Elibariki na Jason katika jambo hili”akawaza Peniela.
“ Sijawahi kukutana na Dr Kigomba ana kwa ana lakini ni namfahamu kwa sura.Hata hivyo hawezi kunitisha kwani nimekwisha kutana na watu wenye nguvu na wakutisha zaidi yake .Kama nimefanikiwa kumtia Dr Joshua mikononi siwezi kushindwa kumuweka Dr Kigomba mfukoni na akajisahau kabisa.Mimi ndio Peniela na usiku wa leo atanifahamu vizuri”akaendelea kuwaza Peniela .
Hoteli Silvano ni moja kati ya hoteli kubwa za kitalii jijini dare s salaam.Ni hoteli ambayo hutumiwa na watalii wenye uwezo mkubwa kifedha kwani inasemekena ndiyo hoteli inayoongoza kwa kuwa na gharama za juu sana hapa nchini.katika hoteli hii ndiko Peniela na Dr Kigomba watakutana.Geti la kuingilia hotelini hapa lilikuwa wazi peniela akaingia na kuelekea katika maegesho akaegeshagari na kuvuta pumzi ndefu kabla ya kushuka.
“ Hii ni kazi ya mwisho ninakwenda kuifanya” akawaza Peniela na kisha akafungua mlango wa gari akashuka na kuelekea moja kwa moja mapokezi.Katika mlango wa kuingilia ndani ya hoteli alisimama kijana mmoja nadhifu aliyevaa suti iliyompendeza sana akamsalimu Peniela kwa adabu na kumkaribisha ndani.Peniela akatabasamu kwa mapokezi yale mazuri na moja kwa moja akaelekea mapokezi ambako alijitambulisha na bila kupoteza muda kijana mmoja akaitwa na kuombwa aongozane na Peniela kumpeleka sehemu anakotakiwa kuelekea.
Hoteli ilikuwa kimya sana na kwambali katika baa ya hotelini hapo kulisikika muziki wa ala uliokuwa ukiwaburudisha wageni.Peniela alipelekwa hadi ghorofa ya tano na kukaribishwa katika chumba kikubwa na kizuri.Hakukuwa na mtu yeyote ndani ya chumba kile alikuwa peke yake.Baada ya dakika kumi mlango ukafunguliwa wakaingia watu wawili peniela akawatambua mara moja.Walikuwa ni Captain Amos na Dr Kigomba.Dr Kigomba alionyesha mshangao mkubwa baada ya kukutana na Peniela .
“ hallow peniela”akasema Captain Amos akimpa mkono Peniela.
“ naitwa Amos mimi ndiye ambaye nimekuwa nikiwasiliana nawe katika simu” akasema Captain Amos
“ Nafurahi sana kukufahamu Amos” akasema peniela
“ Ninaitwa dr Kigomba.Mimi na Amos ni marafiki wakubwa” akasema Dr Kigomba.
“ Nafurahi kukufahamu dr Kigomba .Nadhani ninyi nyote hatujawahi kuonana “ akasema peniela
“ Hapana hatujawahi kuonana na hata mawasiliano yako nilipata taabu sana kuyapata” akasema captain Amos.
“ Ok vizuri.Uliniambia kwamba unashida kubwa na mimi.Ni shida gani hiyo?akauliza Peniela bila kuchelewa.Hakutaka kupoteza muda
“ Peniela nimekuita tukutane hapa lakini si mimi mwenye shida.Huyu mwenzangu ndiye mwenye shida na wewe.kwa maana hiyo basi nitawaacha ninyi peke yenu muweze kuongea na akueleze ana shida gani” akasema Captain Amos na kuinuka akatoka nje akawaacha mle chumbani Dr Kigomba na Peniela.
Kimya kikatawala mle chumbani walimobaki Dr Kigomba na Peniela.Uzuri wa peniela ulimchanganya sana Dr Kigomba na kumfanya ababaike namna ya kumuanza.Hakuwahi kukutana ana kwa ana na peniela na hakufikiri kama anaweza kuwa ni mwanamke mzuri kiasi hiki.
“ Amos alikuwa sahihi Peniela ni binti mwenye uzuri usio wa kawaida.Sikuwahi kukutana naye ana kwa ana na kuushuhudia uzuri wake.Ana uzuri ambao siwezi kuuelezea.Siwezi kukubali kumkosa mrembo huyu,lazima nimpate.Nashukuru Dr Joshua kwa kunipa jukumu la kumchunguza Peniela kwa amenikutanisha na malaika.” Akawaza Dr Kigomba .Peniela naye alikuwa ametulia akiwa na glasi yake ya wine akinywa taratibu akimsubri Dr Kigomba aanzishe maongezi.
“ Nimegundua Kigomba tayari ameanza kuniogopa.Nimeiona sura yake namna anavyohangaika kutaka kunianza.Hii ni dalili nzuri kwangu kwamba kazi yangu itakuwa rahisi sana.Ngoja nimsubiri aanzishe maongezi “ akawaza Peniela akiendelea kunywa wine taratibu sana.Dr Kigomba akakohoa kidogo na kurekebisha tai yake akasema
“ maisha yanakwendaje Peniela?
“ maisha yanakwenda vizuri sana.Kila kitu kinakwenda vizuri na ninamshukuru Mungu”
“ Vizuri sana.kazi zinakwendaje?
“ Kazi nzuri tu.Ninaendelea vizuri.Vipi kwa upande wako kazi zinakwendaje? Unafanya kazi hospitali gani? Akauliza Peniela na kumfanya Dr Kigomba acheke kidogo
“ Peniela mimi si daktari wa kutibu magonjwa bali ni daktari wa ssheria.Kuhusu kazi yangu mimi ni katibu wa rais “
“ Wow ! “ Peniela akajifanya kushangaa sana
“ Kumbe niko na mtu mkubwa hapa bila kuelewa.Katibu wa rais ni mtu mzito.Nimefurahi sana kukutana nawe Dr Kigomba”
“ Hata mimi nimefurahi sana kukutana nawe peniela.” Akasema Dr Kigomba
“ Amos naye anafanya kazi gani?
“ Amos naye pia anafanya kazi ikulu kama daktari wa familia ya rais.”
“ Ouh ! Kumbe leo nina bahati sana ya kukutana na watu wazito .”akasema Peniela huku akiachia tabasamu kubwa.Baada ya kimya kifupi Dr Kigomba ambaye alikwisha anza kumzoea peniela akauliza
“ Peniela unajishughulisha na nini sasa hivi baada ya matatatizo yako kumalizika?
“ Unazungumzia yale matatizo ya kesi ? akauliza peniela
“ Ndiyo.Tena naomba nichukue nafasi hii kukupa pole kwa matatizo yale”
“ Ahsante sana Dr Kigomba nimekwisha poa.Ninamshukuru Mungu kesi ilimalizika salama ,mahakama haikunikuta na hatia na ikaniachia huru.Baada ya kesi kumalizika nimerejea tena katika maisha ya kawaida na nimekutana na changamoto nyingi za kimaisha mfano kabla ya kwenda gerezani nilikuwa na maduka makubwa mawili ya nguo na….” kabla hajaendelea dr Kigomba akaingilia kati
“ Niliyafahamu maduka yako,mke wangu alikuwa anapenda sana kununua nguo toka katika maduka yako”
“ ouh kumbe ulikuwa ukiyafahamu maduka yangu.Kwa hiyo baada ya kesi kumalizika nimekuta maduka yangu yamefilisika ,biashara zangu karibu zote zilikufa kutokana na watu kutokuwa waaminifu kwani wengi waliamini kwamba ningefungwa maisha gerezani au kuhumumiwa kifo.Hivi sasa ninajipanga upya ili niweze kuzifufua tena biashara zangu zote” akasema Peniela
“ Pole sana Peniela.Wanadamu hawana wema hata kidogo.lakini usijali kuhusu hilo.Kwa vile sasa uko huru kila kitu kitarejea kama kilivyokuwa awali na hata zaidi ya awali.watu wa kukusapoti na kukushika mkono tupo na mimi nitakuwa mmoja wao katika kuchangia maendeleo yako.Watu waliofanya kitendo kile cha kukusingizia kesi walifanya kitendo kibaya sana lakini serikali ipo na siku moja watabainika tu”akasema Dr Kigomba
“ Mwanaharamu huyu angejua kama ninamfahamu zaidi ya anavyojifahamu wala asingethubutu kuongea upuuzi wake huu mbele yangu.Natamani hata nimvamie nimng’oe pua yake” akawaza Peniela halafu akauliza
“ Dr Kigomba ulisema kwamba una shida na mimi.Ni shida gani hiyo? Akauliza Peniela kwani hakutaka kuendelea kusimuliana hadithi za maisha
“ Uhhm..ni kweli peniela nilikuwa nahitaji sana kukuona na sikujua ningekupata vipi ndiyo maana nikamuomba Amos anisaidie niweze kukupata kwani yeye anafahamiana na watu wengi na angeweza kupata mawasiliano yako.Nashukuru sana hukupuuza wito wake na umekuja kunisikiliza na inaonyesha ni namna gani ulivyo mstaarabu na mwenye adabu”akasema Dr Kigomba
“ Siku zote sina tabia ya dharau na Amos aliniomba kiustaarabu sana nije nionane nanyi na nikaona ni vyema nikavunja ratiba zangu na kuja kukusikiliza” akasema Peniela.Dr Kigomba akafikiri kidogo na kusema
“ peniela nimekuita hapa kwa jambo moja kubwa.”
“ Ndiyo nakusikia Dr Kigomba” akasema peniela huku akimkazia macho
“ Uuhm… Peniela kilichonifanya nitake kukutana nawe usiku huu hapa ni kwamba nimevutiwa nawe,na ninataka mimi nawe tuwe marafiki.kwa ufupi ninahitaji kuwa na uhusiano na wewe.Umenivutia sana Peniela na nimeshindwa kuvumilia kwa hiyo nimekuita hapa ili kukueleza jambo hilo.Ninakupenda sana Peniela na ninataka uwe mpenzi wangu”akasema Dr Kigomba.Peniela akanywa wine kidogo halafu akamtazama Dr Kigomba na kutabasamu
“ Kigomba I can see you have a wedding ring” akasema Peniela huku akicheka kidogo.Dr Kigomba akatabasamu kidogo na kusema
“ To be honest I have a wife and kids and..”
“ kama una mke na watoto unahangaika nini Dr Kigomba? Akauliza Peniela
“ Unajua katika ndoa huwezi ukapata kila kitu unachokihitaji kwa hiyo kama huwezi kupata kitu unachokihitaji basi unaruhusiwa kutoka kwenda kutafuta nje.Ninahitaji mapenzi motomoto ninahitaji vitu vingi ambavyo mke wangu hawezi kunifanyia.Siwezi kuelezea sana jambo hili lakini naomba tu ufahamu kwamba ninakuhitaji sana Peniela.Nitakupatia kila kitu unachokihitaji katika maisha yako.If you need a house,a car au kitu chochote kile nieleze nitakupatia.” Akasema dr Kigomba
“ Dr Kigomba kwa nini unataka kumfanyia hivyo mke wako? Kwa nini unataka kumsaliti na kuvunja kiapo chenu cha ndoa? Akauliza Peniela
“ Ouh Peniela ,naomba tusijadili kuhusu mambo hayo na tujadili kuhusu mimi na wewe.Peniela ninakuhitaji sana uwe mpenzi wangu na nitakufanyia kila kitu unachokihitaji katika katika maisha yako.”
“ Dr Kigomba nashind………….” Akataka kusema peniela lakini Dr Kigomba akamuwahi
“ Peniela kwani una mchumba? Akauliza Dr Kigomba
“ hapana sina mchumba kwa sasa.Mpenzi wangu niliyekuwa naye alikuwa ni edson na akauawa.baada yake sina tena mchumba” akasema Peniela
“ kama ni hivyo kwa nini basi usinipe nafasi hiyo Peniela ? Nipe nafasi ya kukutunza,kukuenzi na kuyafuta majeraha yote ya nyuma uliyoyapata.Ninastahili kabisa nafasi hiyo Peniela.Tafadhali naomba usininyime nafasi hii ya kukuonyesha upendo ”akasema Dr Kigomba
“ Sina muda mrefu wa kuzungushana na huyu paka shume ambaye hata kutongoza hajui,ngoja nimkubalie tu ili niokoe muda kwani natakiwa kuonana na akina Elibariki usiku huu” akawaza Peniela
“ Dr Kigomba umeniweka katika wakati mgumu sana kiasi kwamba ninashindwa kusema hapana kwa ombi lako.Hata hivyo kwa hali niliyo nayo hivi sasa baada ya kuyamaliza yale matatizo ,ninahitaji sana msaada.Ninahitaji sana mtu ambaye anaweza akanikwamua hapa nilipo na kuniwezesha kusimama tena.kwa kuwa umeonyesha kutaka kunisaidia ili niweze kurejea katika maisha yangu ya kawaida basi mimi sina namna nyingine zaidi ya kuridhia ombi lako.Nitakuwa mpenzi wako na nitakutimizia kile ulichokikosa kwa mkeo lakini naomba unihakikishie kwamba hautaniingiza katika matatizo mengine na mkeo wala familia yako.Sihitaji tena matatizo yoyote yale” akasema Peniela.Dr kigomba akainuka na kumfuata peniela pale sofani alikokuwa amekaa.Alikuwa na furaha ya ajabu,furaha ya ushindi wa kumpata kimwana yule ambaye uzuri wake uliyafanya mapigo ya moyo wake yaende mbio.
“ Peniela ahsante sana kwa kunikubalia ombi langu,Huwezi kujua ni furaha kiasi gani niliyonayo moyoni mwangu kwa kunikubalia kuwa mpenzi wako.Ninajiona ni mwanaume mwenye bahati sana kukupata mwanamke mrembo kama wewe.Nakuahidi kwamba sintakuletea matatizo yoyote yale na badala yake nitafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha bora zaidi kuliko yale ya awali .Nitakufanyia mambo makubwa ambayo hukuwahi kuyafikiria,I’ll make you a queen.Peniela sisiti kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako na usisite kuniambia chochote kile unachokihitaji na nitakufanyia.Ila kuna jambo nataka unihakkishie”
“ Jambo gani Dr Kigomba?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ninataka unihakikishie kwamba ni kweli hauna mahusiano na mwanaume mwingine yeyote yule? Kama unaye naomba uniambie ili nijue kwamba nina ingia katika mahusiano na mtu ambaye ana mahusiano na mwanaume mwingine.Mimi pia ni mume wa mtu na nimekuweka wazi kuhusu suala hili na hata pete ya ndoa hii hapa sijaitoa kwa hiyo naomba na wewe uwe wazi kwangu kama kuna mtu ana mahusiano na wewe hata kama ni mume wa mtu nitaelewa.”akasema Dr Kigomba
“ Dr kigomba kwa nini unasisitiza kutaka kufahamu jambo hilo la mahusiano ? Nimekwisha kwambia kwamba sina mahusiano na mtu yeyote yule.Au huniamini?” Akasema peniela
“peniela usinielwe vibaya kusisitiza kulifahamu jambo hili kwa sababu unajua tunaingia katika mahusiano kwa hiyo lazima tufahamiane vizuri.Nitahitaji kuja nyumbani kwako mara kwa mara kwa hiyo sihitaji kukusabishia matatizo ya aina yoyote ile kama una mpenzi wako nahata mimi sihitaji kujisababishia matatizo yoyote.Kwa hiyo ninataka unithibitishie kwamba ni kweli hauna mchumba na uko peke yako”
“Niko peke yangu.Thats all I can say” akasemaPeniela
“ Nashukuru kwa kunihakikishia hilo” akasema Dr Kigomba huku akiendelea kumuangalia Peniela kwa matamanio.Peniela akaligundua hilo naye akajilegeza .Dr Kigomba akamsogelea karibu zaidi
“ Peniela unataka nikufanyie kitu gani? Akauliza kwa sauti ya taratibu halafu akaupitisha mkono wake shingoni mwa Peniela ambaye hakuonyesha kustuka wala kuuondoa.Kigomba akafurahi sana moyoni kwani alichokuwa akikitaka sasa anakaribia kukipata
“ Tell me Peniela unahitaji kitu gani nikufanyie? Akauliza Dr Kigomba na kuusogeza mdomo wake karibu na mdomo wa Peniela.Taratibu Peniela akauinua mkono wake na kuupeleka maeneo nyeti ya Dr Kigomba na kusababisha mvurugano eneo hilo.
“ I want this.I miss this so much”akasema Peniela kwa sauti laini huku akiishika ikulu na kumfanya Dr Kigomba azidi kuchanganyikiwa.Peniela hakutaka kupoteza muda akaanza manjonjo yake .Dr Kigomba naye hakutaka kubaki nyuma naye akaaka kuonyesha umahiri wake katika sekta hii naye akaanza manjonjo yake.Baada ya dakika kumi hali ikazidi kuwa mbaya Dr Kigomba akamuinua peniela na kumpeleka kitandani na bila kuchelewa mchaka mchaka ukaanza.Ulikuwa ni mtanange mkali kwani kila mmoja akitaka kumuonyesha mwenzake ujuzi wake.Mpaka wanamaliza mzunguko mmoja Dr Kigomba alikuwa hoi akihema kwa kasi.Mchaka mchaka aliokimbizwa na peniela haukuwa mdogo.
“ peniela nimekuvulia kofia.Sijawahi kukutana na mjuzi kama wewe katika haya mambo.Nilikuwa sahihi kukutaka mtu kama wewe kwani ndiye unayenifaa.Umenionyesha vitu adimu ambavyo sijawahi kuonyeshwa.Ahsante sana peniela .Sema chochote ukitakacho nami nitakusikiliza na kukitekeleza” akasema Dr Kigomba huku jasho likiendelea kumtiririka.Peniela akatabasamu
“ Nilijua tu,lazima atachanganyikiwa .Mpaka hapa nadhani kazi yangu imekamilika.Nimeuvaa uhusika vizuri na tayari Kigomba ameingia mfukoni.” Akawaza peniela huku akimuangalia Kigomba na kutabasamu
“ Kigomba hata mimi ninashukuru sana kwa raha ulizonipa .Umenipeleka mbio sana.Ngoma hii unajua kuicheza vizuri.”akasema Peniela
“ peniela I’m serious,niambie chochote unachokitaka nikufanyie ili niwe na uhakika kwamba nitakuwa nawe siku zote.Hata ukisema nimuache mke wangu kwa ajili ya kuwa nawe niko tayari” akasema dr Kigomba.Peniela hakujibu kitu akatabasamu
“ Say something Peniela.Neno lako ni amri kwangu” akasema Kigomba
“ Kigomba ninachokihitaji toka kwako ni hiki ulichonifanyia leo.Hicho ndicho ninachokihitaji zaidi kwani ndicho nilichokikosa zaidi’ akasema peniela na Kigomba akamvuta kwake akamkumbatia na kumbusu.
“ Peniela nitakufanyia mambo makubwa sana.naomba uniamini’ akasema Dr Kigomba
“ Ninakuamini Dr Kigomba.Nisigeweza kuuachia mwili wangu kama sikuamini.”akasema Peniela.
“Ahsante sana peniela kwa kuniamini.Usiku wa leo umekuwa ni wa kipekee sana kwangu.”
“ Hata mimi pia usiku huu umekuwa mzuri na umenikutanisha na mtu mkubwa sana katika nchi hii.Nafurahi kukutana nawe.Nadhani sasa baada ya kufahamiana na kuufungua ukurasa wetu mpya basi niruhusu niondoke na tutapanga tena siku na mahali pa kukutana.”
“ peniela kwa nini tusilale leo hapa hapa hotelini? Bado nina hamu sana na wewe’
“ Hapana Dr Kgomba kwa leo haitawezekana kwa sababu sikuwa nimejiandaa kwa kuja kulala.Nina hakika hata wewe pia hukuwa umejiandaa kama leo hii utakuja kulala hapa kwani hukujua kama ningeweza kukukubalia ombi lako.Go back to your wife.Tutapanga siku nyingine ya kukutana na tutakesha usiku mzima nikikuonyesha vitu ambavyo hujawahi kuviona.Next time nataka tukutane kwangu na utakuwa wangu kwa usiku mzima” akasema peniela
“ Natamani sana siku hiyo ifike haraka peniela”akasema Dr Kigomba
“ Vipi kuhusu kesho unaweza kupata nafasi ?
“ Siwezi kukosa nafasi kwa ajili yako Peniela.Niko tayari kuahirisha kila kitu kwa sababau yako”
‘ basi usijali jiandae kwa usiku wa kesho.I’ll be yours for the whole night” Akasema peniela na kumbusu Dr Kigomba halafu akainuka na kwenda kuvaa nguo zake na kisha akamuaga Dr Kigomba akaondoka.
“ Dr Kigomba amechanganyikiwa kabisa mzee wa watu hadi ananitamkia kwamba yuko tayari kumuacha mkewe kwa ajili yangu.Hivi mimi nina kitu gani ambacho kila mwanaume ninayetembea naye ananing’ang’ania na hataki tena kuachana na mimi? akajiuliza Peniela akiwasha gari lake na kuondoka pale hotelini
“ Yawezekana labda kuna kitu nimebarikiwa nacho kinachowachanganya sana hawa wanaume.Hata hivyo ninashukuru mpango wangu umekwenda vizuri sana kama nilivyokuwa nataka.Dr Joshua ,Dr Kigomba wote katika mifuko yangu kwa hiyo kilichobaki hapa ni kuimaliza kazi yangu.Lakini kabla ya yote natakiwa usiku huu nikaonane na Elibariki na Jason.Ngoja kwanza nimpigie simu Mathew” akawaza Peniela na kuchukua simu akampigia Mathew
“ hallow Peniela,habari yako?
“ habari nzuri Mathew.”
“Peniela uko wapi mbona hutokei? Mathew na Jason wanakusubiri mpaka wamekata tamaa kwamba hutakuja tena” akasema Mathew
“ Niko njiani ninakuja nilikuwa na udhuru kidogo.Are they ok? Akauliza Peniela
“ Una maanisha nini kwa swali hilo Peniela? Akauliza Mathew
“ Nina maanisha hawana matatizo yoyote,je wanaongea ?
“ Hawana tatizo lolote na wanaongea vizuri.Ni marafiki wakubwa hawa “ akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.Niko njiani ninakuja naomba mnisuburi” akasema peniela na kukata simu
“ Ahsnate Mungu kwa Elbariki na jason kupatana.Sasa mipango yangu itakwenda vizuri kama ninavyotaka.Elibariki na Jason ninawahitaji sana katika jambo hili.Halafu kuna kitu nimekuwa nikijiuliza sana bila kupata jibu huyu Mathew ni nani ? Anafanya kazi gani? Kwa nini Elibariki na Jason wanamuheshimu sana ? Nitamuuliza Elibariki anifahamishe kuhusiana Mathew pengine naye anaweza akawa ni mtu wa msaada kwangu katika jambo hili” akawaza Penny
“ natamani sana kujua kama John anaendeleaje lakini kwa namna akivyoniudhi sitaki hata kumsikia.Ngoja kwanza nimalize suala hili la operesheni 26B halafu nitaangalia pengine ninaweza kumsaidia na pengin…………….” Peniela akastuliwa mawazoni na mlio wa simu yake.Alikuwa ni captain amos
“ Halow Amos” akasema Perniela baada ya kupokea simu
“ Peniela good Job.Kigomba amenipigia simu na kunieleza namna alivyochanganyikiwa kwako.Amekiri kwamba hata ile kazi aliyopewa na Dr Joshua ya kukuchunguza haitaki tena yeye anachotaka ni kuwa na wewe tu.Huu ni wakati wetu Peniela wa kuimaliza operesheni 26 B.Endelea kumchanganya Kigomba na nitakuwa nikikufahamisha kila kinachoendelea.” Akasema Captain Amos
“ Usijali Amos.Kigomba tayari nimemuweka mfukoni na ninachosubiri ni kuikamilisha tu operesheni yetu.” akasema Peniela
“ Nitakufahamisha pindi rais atakapomkabidhi Dr Kigomba ule mzigo” akasema Amos na kukata simu.Akaelekea moja kwa moja nyumbani kwake akaoga na kubadili mavazi halafu akaelekea nyumbani kwa Mathew
Captain Amos alipomaliza kuongea na Peniela simuni na kumueleza namna alivyomchanganya Dr Kigomba katika kipindi kifupi,akaiweka simu ile pembeni akachukua simu nyingine akaiwasha kisha akazitafuta namba Fulani na kupiga .Simu ikapokelewa na mwanamama mwenye sauti ya kukwaruza
“ namba yako tafadhali” akasema yule mwanamama
“ VP 8601/W” akasema Captain Amos na bada ya sekunde kama ishirini hivi Yule mwanamama akasema
“ 3600 North.Savana ” akasema yule mwanamama na mara moja Captain Amos akaelea maelekezo yale yalimanisha nini.Akawasha gari na kuendelea na safari yake
“ Jackson atakuwa amenisubiri sana.Sijui kwa nini leo ametaka nikakutane naye pale Savana hoteli.Alinisisitiza sana kwamba lazima leo nionane naye.” akawaza Captain Amos.
Aliwasili Savana Hoteli.Geti la kuingilia hotelini lilikuwa limefungwa mlinzi akafika kumsikiliza,Amos akatoa kijikadi Fulani chenye namba mlinzi yule akaondoka nacho hadi katika kijichumba chake kilichokuwa na kompyuta akakiingiza kikadi kile katika mashine Fulani ndogo halafu akakitoa na kumfungulia Amos geti.Mlango wakuingilia ndani ya hoteli ulikuwa umefungwa ,akakinyonga kitasa na kuingia ndani akaelekea mapokezi ambako alimkuta mwanadada mmoja mrembo.Haikuwa ni mara ya kwanza kwa Captain Amos kufika hapa Savana hoteli kuonana na Jackson kwani ndiye mmiliki wa hoteli hii kubwa na nzuri.Katika hoteli hii kikundi Fulani cha watu hukutana mara kwa mara hasa nyakati za usiku na kujadili mambo yao.Captain Amos naye alikuwa ni mmoja wao.
“ Namba yako tafadhali” akasema yule mwanadada na Amos akamtajia namba yake halafu akaiandika katika kompyuta yake na kuinuka kitini akamuomba Amos aongozane naye.Walielekea katika chumba kimoja ambacho kilikuwa kinafunguliwa kwa kutumia namba na ndani ya chumba kile kulikuwa na ngazi iliyokuwa ikishuka chini wakaifuata ngazi ile na kushuka chini wakakutana na varanda refu na kulifuata na hatimaye wakawasili katika mlango mmoja ambao nao ulikuwa ukifunguliwa kwa namba maalum.Pamoja na kuja hapa mara kadhaa lakini Amos hakuwahi kufika sehemu hii aliyoletwa .Yule mwanadada akabonyeza namba na mlango ukafunguka akamkaribisha Amos aingie ndani.Ndani ya chumba kile kulikuwa na watu sita.Amos akastuka baada ya kuwaona baadhi ya watu ambao hakuwa ametegemea kuwaona pale.Kwa sekunde kadhaa alionekana ni kama vile amepigwa na butwaa akiwashangaa watu wale aliowakuta mle ndani.
“ Karibu sana Amos kwani ni wewe tu ambaye tulikuwa tunakusubiri.” Akasema Jackson Matila
“ Ahsante sana.”akajibu Amos na kuwasalimu watu wale mle ndani kwa heshima kubwa halafu Jackson akaendelea
“ Amos sikukwambia kama kuna watu utakutanana nao leo na ndiyo maana umeonyesha kustuka sana.Tumekuwa tukionana mimi na wewe mara kwa mara lakini leo hii nimeona nikushirikishe katika kikao kimojawapo cha juu kabisa cha umoja wetu na ukutane na vigogo wa nchi hii.Naomba nichukue nafasi hii kufanya utambulisho mfupi.Wa kwanza kabisa ambaye unatakiwa umfahamu usiku huu ni rais wetu mstaafu mzee Deus Mkozumi,natumai unamfahamu lakini hujawahi kukutana naye ana kwa ana.Pia tunaye Profesa Rafael kujilwa,huyu ni waziri mkuu mstafu natumai naye pia unamfahamu.Tunaye pia Benard mkeka,huyu ni mtu mwenye wadhifa mkubwa katika chama,tunaye Generali Adam,tunaye pia Ndikana mluwo.” Akasema Jackson na kuendelea
“ Ndugu zangu huyu ni yule kijana wetu ambaye amekuwa akitufanyia kazi ya kutukusanyia taarifa za kila kinachoendelea ndani ya Ikulu anaitwa Captain Amos.Yeye ni mtu wa karibu sana na rais Dr Joshua na ndiye amekuwa msaada wetu mkubwa katika kupata taarifa nyingi.Karibu taarifa nyingi ninazowapatieni huwa zinatoka kwake.Nimeona leo hii nimualike katika kikao chetu kikubwa kabisa ili muweze kusikia kutoka kwake kuhusiana na hatua kubwa iliyofikiwa katika kuiokoa package E21 isiuzwe. Karibu sana Captain Amos iliuweze kutupa taarifa ya kina kuhusu nini kimefikiwa hadi hivi sasa kuhusiana na package E21” akasema Jackson na kuonyesha heshima mbele ya vigogo wale Amos akasimama.
“ Awali ya yote napenda sana nitoe shukrani za pekee kabisa kwa kunialika na mimi katika kikao hiki kikubwa na kukutana na watu wakubwa kama ninyi ambao sikutegemea kama siku moja ningeweza kukaa nanyi kama tulivyo hivi sasa.Kuhusiana na Package E21 ni kwamba mpaka sasa tunaendelea vizuri.Mipango yote iko safi.Mawasiliano yanaendelea kati ya rais na wanunuzi wanaoitaka package ile na pindi wakifikia makubaliano basi Dr Joshua atamkabidhi Dr Kgomba katibu wake ambaye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi.Team SC41 nao wamepiga hatua tayari katika kuipata package hiyo na tayari wamekwisha mpandikiza mtu wao kwa viongozi wakuu.Wanamtumia msichana mmoja aitwaye Peniela ambaye tayari yuko katika mahusiano ya kimapenzi na Dr Joshua na usiku huu kabla sijaja hapa nimeuunganisha na Dr Kigomba na wameanzisha mahusiano tayari kwa hiyo watu hawa wote wawili tayari amewadhibiti na wote wamekufa wameoza kwake.Dr Kgomba akishakabidhiwa mzigo huo ,team SC41 kwa kumtumia Peniela watauchukua na halafu sisi tutauchukua mzigo huo toka kwao.Tayari kila kitu kimekwisha andaliwa na kinachosubiriwa ni mzigo huo ukabidhiwe kwa Dr Kigomba.” Akasema Amos na wote wakampigia makofi
“ Good.Kazi nzuri imefanyika lakini nina swali moja,” akasema Benard mkeka.
“ Unadhani hawa Team SC41 hawawezi kugundua kwamba pamoja na kuwa ni mtu wao lakini una mpango wa siri wa kuichukua package hiyo toka kwao?
“ Hapana hawawezi kugundua chochote.Isitoshe kwa hivi sasa Team SC41 haina nguvu sana kwani kiongozi wake mkuu John Mwaulaya anaumwa sana kwa hiyo nguvu yake si kama awali japokuwa bado wana nguvu lakini hawawezi kugundua lolote kuhusu mimi.Katika hilo ondoeni shaka kabisa.”akasema Amos
“ Huyu msichana peniela mna mawasiliano mazuri? Unaamini anaweza kuifanya kazi hii kikamilifu na kuipata hiyo package? Akauliza tena Benard Mkeka
“ Ninamuamini sana peniela,Ni msichana mwenye uwezo mkubwa na ndiye anayetegewa na team SC41 katika operesheni hii.Peniela amefanikiwa kumuweka Dr Joshua katika mikono yake na kumpeleka atakavyo na hivi sasa Dr Joshua haambiwi lolote kuhusu Peniela.Usiku huu Peniela amefanikiwa kumnasa tena Dr Kigomba kwa hiyo ni msichana mwenye uwezo mkubwa sana.Isitoshe katika operesheni hii hayuko peke yake,kuna watu nyuma yake kama mimi ambao tunamuelekeza njia za kupita ili kuipata package hiyo.” Akasema Amos
“ Sawa Amos tunakuachia suala hili wewe ulishughulikie na likamilike bila matatizo yoyote.Tunakutegemea sana.Hakikisha Package ile haiondoki nje ya mipaka yetu ” Akasema mzee Deus Mkozumi rais mstaafu wa Tanzania,akamtazama Amos kwa makini na kusema
“ Amos binafsi napenda nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya na nimefurahi sana leo kukutana nawe ana kwa ana.Jackson amekuwa akinipa taarifa zako mara kwa mara kuhusu kazi unazozifanya japokuwa wakati mwingine ni katika mazingira ya hatari kubwa lakini unazifanya kwa umahiri mkubwa na tunazipata taarifa kwa wakati.Tumekuwa tukizifanyia kazi taarifa zako zote na kuhakikisha kwamba nchi inakwenda kadiri tunavyotaka sisi iende na si kwa matakwa ya mtu mmoja mjinga kama Dr Joshua” akasema Deus.Akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Nilipata taarifa za kuhusiana na kitendo cha kikatili alichokifanya Dr Joshua cha kumuua mke wake Dr Flora kwa sababu tu ya kugundua kuhusiana na mpango wa kuiuza package E21. Dr Flora na mke wangu walikuwa marafiki wakubwa na mimi na familia yangu tuliumizwa mno na kifo kile.Nilitaarifiwa kwamba kuna jaji moja wa mahakama kuu ambaye amemuoa mtoto wa dr Joshua ananitwa jaji Elibariki alifanya uchunguzi na kugundua kilichomuua Dr Flora kwamba ni sumu lakini ilipogundulika kwamba tayari ameifahamu siri yakatolewa maelekezo kwamba auawe.Nilipopata taarifa hizo za kutaka kuuawa Elibariki ,nikatoa maelekezo kwamba zifanyike kila jitihada kuhakikisha kwamba jaji huyo anaokolewa na ninashukuru kwamba hilo ulilifanya vyema Amos na kufanikiwa kumuokoa Elibariki.Ninachotaka kufahamu ni maendeleo ya huyu jaji.Anaendelaje? Yuko sehemu salama kwani ni mtu ninayemuhitaji sana” Akauliza mzee Deus na kumshangaza kidogo Captain Amos kwani hakuwahi kufikiria kama maagizo yale ya kumuokoa jaji Elibariki yalitoka kwake.
“ Elibariki yuko sehemu salama .Siku ile alipookolewa aliomba apelekwe kwa Peniela ambako alikaa hadi usiku wa jana alipogundulika na kuondoka kwenda kujificha sehemu nyingine ambako ni salama zaidi kwake” akasema Amos
“ Peniela again? Akauliza Ndikana mluo huku akicheka
“ Elibariki na Peniela wana mahusiano ya siri ya kimapenzi” akasema Amos na kuwafanya watu wote mle ndani waangue kicheko.
“ Huyu Penielani ni msichana wa namna gani? Mbona kila mahala amepashika yeye? Dr Joshua,Dr Kigomba na hata jaji Elibariki ! Akauliza mzee Deus
“ Peniela ni msichana mwenye uzuri wa kipekee kabisa na kama nilivyowaeleza awali kwamba anautumia uzuri wake kumnasa mwanaume yeyote amtakaye.Team SC41 ndiye wanayemtegemea kutafuta taarifa toka kwa watu mbalimbali ” akasema Amos
“ Ok good.Nafurahi kusikia kwamba Elibariki anaendelea vizuri.Anatakiwa alindwe sana hasa kwa wakati huu ambao nina hakika nguvu kubwa inatumika kumtafuta.Siri anayoifahamu Elibariki ni kubwa na inatosha kabisa kumuangamiza Dr Joshua na ndiyo maana anatumia nguvu kubwa kumtafuta. Elibariki ni kijana ambaye nina mpango naye mkubwa sana na ndiyo maana nikataka aokolewe na awe salama na ninaagiza tena kwamba alindwe kwa kila namna ” akasema mzee Deus
“ Amos kwa kukuzidishia uelewa zaidi ni kwamba Dr Joshua ni mtu ambaye mimi nimemlea kisiasa ndani ya chama.Alikuwa ni muadilifu sana na mchapakazi.Nilimuandaa Dr Joshua kwa ajili ya kushika nafasi kubwa nchini kwani alionyesha uwezo wa juu sana wa uongozi katika nyadhifa mbali mbali alizopewa ndani na nje ya chama.Wakati kipindi changu cha uongozi kinakaribia ukingoni mchakato wa kumpata mrithi wangu ukaanza na bila kusita nilimpendekeza Dr Joshua kwani niliamini anaweza kukikalia kiti kile.Nilitaka mrithi wangu awe ni mtu ambaye atakuwa akifuata ushauri wangu kwangu kwani mimi nimehudumu ikulu kwa miaka mingi kabla sijawa rais na baadae nikawa rais.Nilichokitaka kikatimia na Dr Joshua akawa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Baada tu ya kushika madaraka Dr Joshua alibadilika sana na amekuwa akifanya mambo mengi ya ajabu sana .Mwanzoni nilikuwa naye karibu nikimshauri namna ya kuongoza ofisi kubwa kama ile lakini baada ya muda hakutaka tena niwe nikimshauri lolote na nikaamua kukaa pembeni lakini hata hivyo sikutaka kabisa kujiweka pembeni na kumuacha afanye mambo namna anavyotaka yeye na ndiyo maana nikamuagiza Jackson akuingize Amos katika umoja wetu ili tuweze kupata kila taarifa ya kile anachokifanya Dr Joshua.Taarifa ile ya kutaka kuuza package E21 ilinistua sana.Naomba niwaeleze ukweli kwa sababu wakati wa uongozi wangu niliilinda kama mboni ya jicho.Hata mimi nilikumbana na vishawishi vingi vya kutaka kuiuza package ile lakini sikuwa tayari kufanya hivyo.Hapa majuzi nilimpigia simu nikijaribu kumuonya kwamba aachane na mpango wake huo wa kuiuza package ile lakini tulishindwa kuelewana na badala yake alinitolea maneno ya dharau na kashfa kubwa na zaidi sana alifikia hatua ya kutaka hadi kuniua.Alimtaka generali Adam huyu hapa ,kubuni mpango wa kuniua bila kujua kwamba Adam ni mtu wangu mimi na asingeweza kufanya jambo kama hilo.Amenisikitisha sana Dr Joshua na sintomvumilia tena na ninataka kumuonyesha kwamba mimi nina nguvu zaidi yake.Nataka kumuondoa katika madaraka mara tu zoezi la kuiuza package E21 litakaposhindikana. Hapa ndipo Elibariki anapokuja kuingia.Yeye ana ushahidi mzito sana wa kuweza kumtoa Elibariki madarakani na akafungwa miaka mingi na hata ikiwezekana maisha gerezani.Ninataka kumtoa madarakani kwa aibu.” akasema mzee Deus.Watu wote walikaa kimya kabisa wakimsikiliza.
“ Tukiachana na hilo la Dr Jason ,kuna jambo lingine kubwa ambalo ninataka kuwashirikisha nyote.Ni kwamba nimefikiria baada ya kumuondoa Dr Joshua madarakani ,huyu kijana jaji Elibariki ndiye tumsimamishe kugombea nafasi hii kwani anafaa sana.” Akasema Deus Mkozumi na watu wote mle ndani wakawa ni kama wamepigwa na mshangao
“ What ?!! akashangaa Benard Mkeka.Kauli ile ya Deus iliwastua sana wale wajumbe mle ndani ya kile chumba
“ Deus are you serious about this? Akauliza Profesa Raphael Kujilwa.
“ yes I’m serious.Nimepitia kwa umakini wasifu wa Elibariki na nimejiridhisha kwamba anafaa na anaweza.Umri wake unaruhusu kikatiba kugombea nafasi ya urais,nimchapakazi,na elimu ya kutosha kabisa na zaidi ya yote wakati huo uchaguzi utakapofanyika jina lake litakuwa juu sana kwani ndiye atakayefichua kila kitu alichokifanya Dr Joshua kwa umma kwa hiyo nafasi yake ya kushinda uchaguzi ni kubwa sana.”
“ Deus kauli yako imenistua sana japokuwa bado sijafahamu umeona nini hadiukafikiria hivyo laini ninachojiuliza hata kama sisi tutamkubali ndani ya chama je watamkubali ? Sina uhakika kama ndani ya chama anaweza kuwa na nafasi kwani hakuna anayemfahamu.”akasema Ndikana Mluwo
“Kukubalika ama kutokukubalika ndani ya chama si hoja yenye mashiko.Sisi tulipo hapa ndio chama na tunaweza tukafanya chochote .Kitakachofanyika ni kwamba mara tu baada ya kumuondoa Dr Joshua ,Elibariki ataachana na kaziyake ya ujaji na hivyo kuwa huru kuingia katika siasa. Guys mnaweza msikubaliane na mimi kuhusiana na suala hili lakini nawahakikishia kwamba nimekwisha ona mbali sana na Elibariki ni mtu ambaye atatufaa sana.Nina sababu zangu za kusema hivyo.Kwa sasa kipindi cha pili cha uongozi wa Dr Joshua kinaelekea ukingoni na tayari kuna makada wengi wamekwisha anza kujitafutia nafasi hiyo kwa hiyo tunatakiwa kumtafuta mtu ambaye ni wa tofauti sana na ambaye hakuna aliyemtarajia.Mtaona hapa kwamba Elibariki ni mtu sahihi kwa sababu kwanza hana kundi lolote katika chama na pili hana kashfa yoyote,na vile vile kitendo atakachokuwa amekifanya cha kufichua maovu ya Dr Joshua kitamuweka katika nafasi nzuri kuchaguliwa kwani kumg’oa rais madarakani si kitu chepesi.Sifa nyingine Elibariki bado kijana na ana nguvu za kutosha kwa hiyo atapata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa vijana.Ndugu zangu chama kinahitaji mageuzi makubwa na mageuzi haya yataanzia kwa kumuweka madarakani rais kijana kama Elibariki.Najua kila mmoja wenu akilitafakari suala hili kwa makini sana atakiona kile ninachomaanisha.” Akasema Mzee Deus na kikao kikaendelea hadi usiku mwingi na kisha wakatawanyika kwa makubaliano ya kukutana tena siku nyingine kulijadili kwa upana wake suala lile alilolipendekeza mzee Deus.
Peniela aliwasili nyumbani kwa Mathew,mlinzi akampigia sImu Mathew na kumfahamisha kwamba peniela amewasili akamruhusu amfungulie geti aingie ndani.
“ Its hard to do this but I hve to.lazima niwaeleze ukweli akina Elibariki.Bila kufanya hivyo sintaweza kabisa kujitoa katika team SC41 na maisha yangu hayataweza kamwe kubadilika” akawaza Peniela na kushuka garini akaelekea mlangoni akabonyeza kengele .Katika chumba cha kazi kilichokuwa na mitambo na luninga kubwa tatu ukutani,Mathew na Anitha walikuwa walimkagua Peniela kupitia katika kifaa kilichofungwa pale mlangoniili kukagua kama ana silaha amakitu chochote kinachoweza kuwa kinarusha mawasiliano na kuyapeleka sehemu nyingine.
“ She’s clean” akasema Anitha baada ya kuridhika kwamba Peniela hakuwa na silaha walakitu chochote cha kurusha mawasilianokupeleka sehemu nyingine. Mathew akatoka na kwenda mlangoni kumlaki Peniela
“ karibu Peniela” akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew. Samahani kwa kuwasumbua usiku huu” akasema Peniela
“ usijali P eniela ,unakaribishwa muda wote.katika nyumba hii watu hawalali “ akasema Mathew na kumkaribisha Peniela sebuleni walikokuwa wamekaa jaji Elibariki na Jason.Mtu wa kwanza kusalimiana naye alikuwa ni jaji Elibariki ambaye alimfuata na kumbusu halafu akamsalimu na Jason kwa kumpa mkono kisha akaketi kitini
“ Samahani sana kwa kuwaweka hadi mida hii.Nilikuwa na shughuli moja ya muhimu sana iliyonichelewesha ” akasema Peniela
“Usijali Peniela,hata kama ungekuja asubuhi lazima tungekusubiri tu” akasema jaji Elibariki na wote wakacheka.
“ Ok.Mmeshindaje toka muda ule nilipowaacha? Are you ok now? Akauliza Peniela ambaye uso na sauti yake vilionyesha kwamba hakuwa akihitaji mzaha wowote
“ We’re good.Tuko sawa.Tumeongea na tumeyamaliza yale mambo” akasema Jason
“ Good..I’m so happy for that.You are real men” akasema Peniela na mara akatokea Anitha wakasalimiana.
“ Peniela unatumia kinywaji gani? Akauliza Anitha
“ Ahsante sana Anitha,naomba kama una whsky yoyote tafadhali” akasema Peniela Anitha akaenda kumletea mvinyo ,akanywa funda kubwa.Watu wote pale sebuleni walikuwa kimya wakisubiri kusikia Peniela anataka kuwaambia kitu gani
“ Ninashukuru kwamba ninyi nyote mko hapa .Nilikuwa nawahitaji sana nyote muwepo ili tuongee jambo moja muhimu sana” akaanzisha mazungumzo Peniela bila kupoteza wakati
“ Kwanza kabisa ninakushukuru Mathew kwa kunikaribisha hapa kwako .Ninashukuru vile vile kwa kuendelea kuhakikisha usalama wa Elibariki”akanyamaza na kunywa funda moja la mvinyo
“ Nina mambo mengi sana ambayo ningependa kuwaeleza usiku huu lakini kutokana na muda nitawaeleza mambo mawili au matatu makubwa ya muhimu kwa sasa.” Akanyamaza tena akawaangalia akina Mathew kisha akaendelea
“ Nadhani nyote mnafahamu kuhusiana na kesi ya mauaji iliyokuwa ikinikabili.Ninawashukuru sana Jason wakili wangu na jaji Elibariki kwa kunipigania na hatimaye nikawa huru.Baada ya kesi ile kumalizika jaji Elibariki na Jason walitaka kwenda ndani zaidi kulichimba suala lile na kumfahamu muuaji.Leo hii naomba niwaeleze ukweli kwamba sikutaka jambo lile lifanyike kwani tayari nilikuwa nikimfahamu muuaji.”akasema Peniela na wote mle ndani wakastushwa na kauli ile isipokuwa Mathew
“ Ulifahamu aliyemuua Edfson? Akauliza Jason
“ ndiyo nilifahamu mtu aliyemuua Edson na sikutaka kufumbua mdomo wangu kusema .Niliogopa ningeuawa kwani ni mtu mzito na mwenye nguvu” akasema Peniela
“ Who is that? Akauliza Jason.Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Ni mheshimiwa rais”
Kimya kifupi kikapita mle ndani na baada ya sekunde kadhaa akasema
“ Ulijuaje kama rais ndiye aliyemuua Edson? Akauliza jaji Elibariki
“ Nimekuja hapa kuwaelezeni ukweli wa kila kitu kwa hiyo msihofu nitawaeleza kila kitu kilivyo.”akasema na kukaa kimya kidogo akaendelea
“ Kabla sijaingia katika mahusiano ya kimapenzi na Edson ,tayari alikuwa katika mahusiano na mtoto wa rais aitwaye Anna na wakati huo mimi nilikuwa na mahusiano ya siri na mheshimiwa rais” akasema Peniela.Uso wa jaji Elibariki ukabadilika.Hakuwa ametegemea kusikia jambo kama lile.
“ Unasema ulikuwa na mahusiano na nani? Akauliza jaji Elibariki
“ Tafadhali usihamaki Elibariki utafahamu kila kitu hatua kwa hatua.Usikuhuu ni usiku utakaojaa ukwelimtupu wa kila jambo.Nilikuwa katika mahusiano na rais Dr Joshua na mpaka sasa bado niko katika mahusiano naye “
“ Shetan…..” jaji Elibariki alipandwana hasira za ghafla akainuka na kutaka kumfuata Peniela lakini Mathew akawahikumdaka akamzuia
“ Elibariki please calm down.Msikilize kwanza Peniela anataka kutueleza jambo gani.Tafadhali naomba usihamaki “akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.Nafahamu umekasirika kwa sababu unanipenda,lakini naomba utulie na usikie kila kitu ninachotaka kuwaeleza” akasema Peniela
“ Endelea peniela” akasema Mathew
“ Wakati nikiwa katika mahusiano na mheshimiwa rais, siku moja alinialika katika sherehe moja kubwa iliyokuwa ikifanyika ikulu .Katika sherehe hiyo ndipo nilipokutana na Edson na urafiki wetu ukaanzia hapo na baadae tukawa wapenzi.Dr Joshau aligundua kuhusu mahusiano yangu na Edson na alikasirika sana na kupanga mpango ule wa kumuua Edson na mimi nikabebeshwa mzigo ule wa kesi, lengo lake likiwa ni kuniangamiza kabisa.Japo nilimfahamu muuaji lakini sikuthubutu kufumbua mdomo wangu kusema chochote kwa sababu endapo ningethubutu kufanya hivyo basi ningeuawa mara moja ”akasema Peniela na kukaa kimya kidogo huku Elibariki akiendelea kumuangalia kwa macho makali ya hasira
“ Ilitokeaje wewe na rais mkaingia katika mahusiano ya kimapenzi? akauliza Anitha
“ Ni hadithi ndefu kidogo ila nitawaeleza hilo baadae lakini kwa sasa naomba mniruhusu niwaeleze kile nilichokusudia kuwaeleza usiku huu ” akasema Peniela akawaangalia watu wote mle sebuleni na wote walikuwa kimya wakimtazama,akaendelea .
“ baada ya kesi ile iliyokuwa ikinikabili kumalizika na mahakama kuniachia huru,Jaji Elibariki na Jason waliamua kuanzisha uchunguzi ili kulichimba zaidi suala lile na kufahamu nani aliyemuua Edson kwani wote waliamini mimi si muuaji.Niliogopa kwa wao kujiingiza katika suala hili kwani Endapo wangelichimba jambo hili kwa ndani wangeweza kugundua kwamba rais ana mkono wake katika mauaji yale na wangekuwa katika hatari kubwa kwani ninamfahamu vizuri Dr Joshua .Elibariina Jason ni watu wangu wa karibu na wa muhimu sana.Wote wana nafasi kubwa sana ndani ya moyo wangu na katika maisha yangu kwa ujumla kwa hiyo sikuwa tayari kuwaona wakiingia katika matatizo makubwa na kuhatarisha maisha yao.Niliogopa kuwaeleza ukweli wa jambo hilo na kwa hiyo nikatafuta njia ya kuweza kuwavuruga wasiendelee na mpango wao na nikaamua kuwagombanisha.Wenyewe wanafahamu kitu kilichotokea na wakavurugana..Mtanisamehe sana Elibariki na Jason kwa nilichokifanya hadi mkagombana ,lakinisikuwa na njia nyingine ya kuweza kuwazuia msiendelee na mpango ule wa kulichimba kiundani suala la lile la mauaji ya Edson.” Akasema peniela .Elibariki alimuangalia Peniela kwa jicho kali.
“ Sikuwahi kuhisi kama Peniela anaweza kuwa namna hii.Dah ! ama kweli umdhaniaye siye,ndiye.Nilikuwa tayari kufanya kila linalowezekana iliniwe naye lakinikmbenilikuwa najiingiza katika mdomo wa joka kubwa bila kujua.Nilidanganywa na uzir wake wa nje lakini kumbe ndani hana hata chembe ya ubinadamu.Siku ile Jason aliponipiga na chupa kichwani ningeweza hata kupoteza maisha kumbe yote ilisababishwa na Peniela.”akawaza jaji Elibariki akiendela kumuangalia Peniela kwa chuki
“ Ulimuuliza Dr Joshua sababu ya kumuua Edson? Akauliza Mathew
“ Nilimuuliza na akaniambia kwamba alifikia maamuzi yake kutokana na mimi kumsaliti kwa kuanzisha mahusiano na Edson kwa hiyo alitaka wote wakose na mimi nikaozee gerezani na ndiyo maana nikabebeshwa mzigo wa ile kesi kubwa” akasema Peniela.Mathew akamtazama na kusema
“ Alikudanganya”
“ alinidanganya? Peniela akashangaa
“ Ndiyo.dr Joshua alikudanganya kuhusu sabau ya kumuua Edson”
“ Unajuaje kama alinidanganya? Akauliza Peniela
“Tayari tunafahamu kila kitu kuhusiana na kifo cha Edson na ninisababuya yeye kuuawa.”
“ You know? Peniela akazidi kushanga
“ How do you know? Who are you Mathew? Akauliza Peniela
“ Nadhani Elibariki ndiye anayeweza kukueleza kila kitu kuhusiana na mimi.Elibariki please tell Peniela everything’ akasema Mathew.Jaji Elibariki akamtazama Peniela na kusema
“ Kutokana na mambo mengi yasiyo ya kawaida niliyoyaona wakati wa usikilizwaji wa kesi iliyokuwa ikikukabili ,niliazimia kwamba lazima nilifanyie uchunguzi wa kina suala hili na nifahamu ukweli wake.Nilimshirikisha Jason wazo langu na kwa pamoja tukakubaliana kulifanyia uchunguzi suala hili.kwa kuwa sisi wawili hatuna ujuzi wowote wa kufanya mambo haya ya uchunguzi na sikutaka kulichunguza jambo hili kwa kutumia jeshi la polisi nililazimika kutafuta mtu ambaye ana ujuzi na uzoefu wa kutosha wa mambo haya na ndipo nilipomfuata Mathew na kumuomba msaada wake katika jambo hili.Mathew ni mzoefu wa siku nyingi katika kazi hizi,amekwisha fanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa na kwa sasa anafanya kazi zake binafsi” akasema jaji Elibariki na kuendelea
“ Mathew aliwaita wenzake wamsaidie kuifanya kazi hii na mmoja wao ni huyu hapa Anitha na Noah aliyepoteza maisha wakati akiniokoa katika lile shambulio . Kitendo cha Peniela kunivuruga mimi na Jason kwa kutugombanisha hakikuathiri chochote kuhusu mpango wetu wa kulichunguza sualahili ,kwahio Mathew na wenzakewaliendelea na uchunguzi wao.Ni hayo tu ninayoweza kusema kuhusiana na Mathew na kuhusu namna walivyochunguza atakueleza yeye mwenyewe” akasema Elibariki akionekana kuishiwa kabisa maneno ya kusema
“ Peniela nadhani sasa umenifahamu mimi ni nani na kazi yangu ni nini.” Akasema Mathew na Peniela akatingisha kichwa kukubaliana naye,Mathew akaendelea
“ Tumelichungza suala hili na tumegundua kwamba Edson aliuawa kwa amri ya rais lakini kilichopeleka auawe si kwa sababu ya wewe kuingia katika mahusiano naye bali ni kwa sababu nyingine kabisa.Tumegundua kwamba Edson alikuwa akishirikiana na watu Fulani ambao walimtumia katika kuiba nyaraka za siri Ikulu.Nyaraka hizo walipanga waziuze kwa mabilioni ya fedha.Kwa bahati mbaya yeye na watu wote aliokuwa akishirikiana nao wote wamekwisha fariki kwa sababu ya nyaraka hizo na kwa bahati nzuri nyaraka hizo tumezipata na kwa sasa tunazifanyia uchunguzi wa kina kuzifahamu zinahusianana na nini kwani zimeandikwa kwa lugha ya kisayansi na sisi hatuelewi ni kitu gani kilichoandikwamo.Nadhani sasa umeelewa sababu iliyopelekea kifocha Edson.” Akasema Mathew.Peniela alionekana kustushwa sana na taarifa ile.
“ sikuwa nikilifahamu jambohilohilo .Niliaminimanenoaliyoniambia Dr Joshua .Nashukuru kwa kunifahamisha ukweli.’ akasema Peniela.
“ Dr Joshua asingeweza kukueleza ukweli kwa sababu inaonekana nyaraka hizo zina kitu kikubwa sana ndani yake na ndiyo maana wote waliozishika wamepoteza maisha.” akasema Elibariki
Peniela akainama chini akaonekana kujawa na mawazo
“ Ilikuaje hadi ukaanzisha mahusiano na mheshimiwa rais?akauliza Mathew
“ Ni hadithi ndefu kidogo lakini nitawaeleza ukweli wa kila kitu kinachoendelea kwani nina hakika hata ninyi mpaka mmefikia hatua ya kufahamu kuhusiana na jambo hili basi mtakuwa mmekwisha fahamu mambo mengi”akasema Peniela.Akakaa kimyakidogona kuendelea
“ Mimi ni Team SC41.Sina hakika kama mnafahamu au mmekwisha sikia kuhusu Team SC41 “ akasema Peniela na kuzidi kuwachanga Elibariki na Jason ambao hawakuwa wakifahamu chochote kuhusiana na Team SC41.
“ we already know what team SC41 is” akasema Mathew
“ You know? Peniela akashangaa
“ Peniela we don’t know anthything.Kama Mathew anafahamu kuhusu hiyo team unayoisema ni yeye mwenyewe lakini sisi hatufahamu chochote kuhusianana hiyo team ” akasema jaji Elibariki
“ I’m sorry guys ,sikuwahi kuwaeleza chochote kwamba katika uchunguzi wetu tuligundua uwapo wa team SC41 lakini hakukuwa na ulazima wa kuwaeleza kwa sababu kikundi hiki hakikuhusika na kifo cha Edson ”akasema Mathew
“ Ulipaswa kutuweka wazi kuhusu kila kitu Elibariki. Kwa hiyo team SC41 ni akina nani? shughuli zao ni nini? Akauliza Elibariki.
“ Team SC41 ni kikundi cha siri kinachofanya kazi zake kwa siri hapa nchini na katika ukanda wa afrika mashariki.Kikundi hiki kilianzishwa kwa siri na serikali ya marekani kwa ajili ya kulinda maslahi yake katika ukanda huu wa afrika ya mashariki.Kazi kubwa ya kikundi hiki ni kuhakikisha kwamba maslahi ya Marekani yanalindwa na yanakuwa salama.Serikali ya Marekani imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la afrika mashariki kwa hiyo wameweka kikundi hiki makusudi ili kiwe ni kama jicho la kuhakikisha kwamba hakuna hatari yoyote katika uwekezaji wao.Team SC41 imekita mizizi yake ndani ya serikali na wanafahamu kila kinachoendelea ndani ya serikali na endapo kuna mpango wowote wa kuhujumu maslahi ya marekani basi watafahamu mara moja.Mimi ni mmoja wao japokuwa kazi yangu mimi ni tofauti na wengine.Kazi yangu mimi ni kutafuta taarifa Fulani toka kwa mtu.Endapo kuna mtu ambaye team SC41 wanahitaji kitu Fulani toka kwake basi hunitumia mimi.Hujenga mahusiano na mtu huyo na kisha huhakikisha kwamba nimekipata kitu hicho au taarifa hiyo inayotakiwa.” akasema Peniela
“ Kuingia katika mahusiano na Dr Joshua ulikuwa ni mpango wa team yako au ulipenda mwenyewe? Ama kuna kitu ulikuwa unakitafuta? Akauliza jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa mkali sana.
“ Ulikuwa ni mpango wa TeamSC41 wala haikuwa ni kwa mapenzi yangu.Kuna kitu walikuwa wanakihitaji toka kwake na ndiyo maana wakanitumia mimikuanzishamahusiano naye” Akasema Penielahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ni kitu gani mnachokitafuta kwa Dr Joshua? Akauliza Mathew
“ Package E21” akajibu Peniela
“ Package E 21?.Ni kitu gani hicho? Akauliza Mathew
“ Hata mimi sifahamu ni kitu gani na hakuna aliyewahi kunieleza package hiyo ina nini lakini inaonekana ni kitu chenye thamani kubwa kwa sababu Package hiyo inafichwa ikulu na hata hapo ikulu kwenyewe anayefahamu mahala ilipo ni rais peke yake .Dr Joshua anataka kuiuza package hiyo kwa matrilioniya fedha.Dr Flora mke wa rais aligundua kuhusu jambo analotaka kulifanya mume wake na alijitajhidi sana kumsihi mume wake asiiuze package hiyo lakini bila mafanikio na ndipo alipoamua kuwaeleza wanae kile anachotaka kukifanya baba yao na mchana wa siku ambayo alipanga kuonana na wanae jioni ili awaeleze anachokifanya baba yao akafariki dunia.Aliuawa ili asiweze kutoa siri”
“ What ?! Dr Flora aliuawa kwa sababu ya hiyo Package? Akashangaa jaji Elibariki.
“ Ndiyo.Dr Flora aliuawa ili asiweze kutoa siri hiyo.”akasema Peniela.Kila mtu alikuwa kimya pale sebuleni.
“ Una uhakika gani kwamba Dr Flora aliuawa ili asiweze kutoa siri? Akauliza Mathew
“ katika biashara ya package hiyo Dr Joshua anashirikiana na watu wengine wawili.Katibu wake Dr Kigomba na daktari wa familia ya rais anaitwa Captain Amos.Hawa ndio wanaofahamu kila kitu kuhusianana biashara nzima ya package hiyo.Captain Amos naye yuko team SC41 na ndiye anayetupa taarifa zote kuhusiana na kila kinachoendelea ikulu.Captain Amos ndiye aliyemchoma sindano ya sumu Dr Flora kwa amri ya rais.” Akasema Peniela
“Mawazo yangu yalikuwa sawa kabisa kwamba Dr Flora aliuawa.Nilitegemea tu kwamba lazima kifo chake kitakuwa kimesbabishwa na jambo kubwa na kama anavyosema Peniela nikwamba aligundua kuhusiana na hiyo package anayotaka kuiuza Dr Joshua na ndipo alipouawa.Package hiyoni ya nini? Inamahusiano yoyote na hizi nyaraka alizoziiba Edson? Mhh! Mambo haya yanazidi kuwa magumu.” Akawaza Mathew.
Jaji Elibariki alikuwa ameinama amekishika kichwa chake
“ Ouh Mungu wangu ! akasema Elibariki halafu akainua kichwa akasema
“Mathew tulikuwa sahihi kabisa kuhisi kwamba Dr Joshua atakuwa akihusika na kifo cha mkewe na ndiyo maana nguvu kubwa ikatumika kuhakikisha sababu ya kifo cha Dr flora haijulikani.Kumbe tulipompelekea ile taarifa yetu ya uchunguzi iliyobainishakwamba dr Flora aliuawa kwa sumu tulikuwa tunajipalia makaa ”akasema Elibariki na kumstua peniela
“ Mlifahamu kilichomuua Dr Flora? Akauliza Peniela
“Ndiyo tulifahamu kila kitu.”akasema Mathew
“ Badaa ya kifo cha Dr Flora ilitolewa taarifa kwamba mwili wake usifanyiwe uchunguzi wowote kubainisababuya kifo chake na badala yake ikatolewasababu ya jumla kwamba kilichomuua ni shinikizo la damu. Mke wa Elibariki aliingiwa na hofu kuhusu kifocha mama yake namazingira kilivyotokea hivyo akamuomba mume wake amsaidie kuweza kuufahamu ukweli.Elibariki likuja kwangu akaniomba nimsaidie kufanya uchunguzi wa kubaini kilichomuua Dr Florana nusura tungepoteze maisha yetu wakati wa kufanya uchunguzi huo lakini mwishowe tuliubaini ukweli .Tuligundua hadi aina ya sumu iliyomuua Dr Flora .Baada ya hapo Elibariki alimpelekea mheshmwia rais majibu yale ili ayafanyie kazi bila ya kufahamu kwamba ni yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya yale mauaji”akasema Mathew
“I’m impressed with you guys.Namna mnavyofanya kazi zenu mmenifurahisha sana” akasema Peniela
“ Baada ya Dr Joshua kugundua kwamba tayari Elibariki amegundua kilichosababisha kifo cha dr Flora aliamuru auawe na ndipo lilipopangwa lile shambulio ambalo alinusurika kuuawa”akasemaMathew.Jaji Elibariki naye akasema
“ Katika shambulio lile alitokea mwanamke mmoja na kunichukua toka eneo la tukio na akanikabidhi kwako.Mpaka leo sijamfahamu mwanamke yule ni nani na kwa nini aliniokoa.Hakutak……”kabla Elibariihajaendelea Penielaakaingilia kati
“That’s Jessica.Naye ni team SC41.Alipewa maagizo ya kukuokoa na Amos .”akasema Peniela.
“ Dah ! nimechoka kwa kweli.Hawa team SC41 wako kila mahala ,but why they saved me? Akauliza Elibariki.Kabla Peniela hajajibu kitu Mathew akauliza
“ John mwaulaya anaendeleaje?
Swalilile lilimstua mno Peniela.Hakuwa ametegemea kama Mathew anamfahamu John
“ Umesema John mwaulaya? Akauliza peniela
“ Ndiyo.John Mwaulaya.is he ok? Akauliza Mathew
“ Do you know him?
“ yes I know him” akasema Mathew
“ John mwaulaya ni nani? Akauliza jaji elibariki
“ Ni kiongozi wa team SC41”akajibu mathew
“ Unafahamiana na kiongozi wa team SC41? akauliza Elibariki kwa mshangao
“ Ndiyo ninamfahamu.Japokuwa si marafiki lakini mimi na yeye tun historia .Nitawaeleza siku nyingine ninamfahamuje John mwaulaya lakini usiku huu ni usiku wa peniela ,ametueleza mambo makubwa kabisa na kutufunulia mambo mengi mazito.Peniela endelea kutueleza kile ulichokusudia kutueleza” akasema Mathew,Penielaakaendelea
“ baada ya kunusurika katika ajali ile ,Elbariki alikuja nyumbani kwangu kwani aliamini ni sehemu salama.Ni kweli ni sehemu salama na alikuwa salama hadi pale Jason alipokwenda kutoa taarifa polisi kwamba Elibariki yuko kwangu.Taarifa zile zilimfikia Amos naye akamtaarifu kiongozi wangu John mwaulaya aliyeamuru Jason akamatwe na aeleze kwa nini alitoa taarifa zile kwa jeshi la polisi.Alikuwa na wasi wasi kwamba yawezekana Jason akawa anafahamu mambo mengi kuhusu team SC41.Walimteka Jason na kumtesa na ndipo alipopata nafasi ya kunipigia simu na kunifahamisha kwamba ametekwa.Nilichukizwa mno na kitendo kile cha kuwateka na kuwatesa watu wangu wa karibu na hiyo ndiyo sababu niko hapa nikiwaeleza haya yote niliyowaeleza ambayo sikupaswa kuwaelezakitendo kile na hii ndiyo sababu niko hapa kwenu mida hii nikiwaeleza haya yote niliyowaeleza na nikihitaji msaada wenu.” akasema Peniela akaak kimya kidogona kusema tena
“ I need your help guys”
“Our help? Akauliza Mathew
“ yes. Your help.”
“ Unahitaji msaada gani? Akauliza Mathew
“ To take down Team SC41”
Watu wote mle ndani walibaki kimya wakimtazama Peniela.Ni Mathew aliyefungua mdomo wake na kumuuliza
“ You want to take down Team SC41?
“ yes I do” akajibu Peniela
“ Nataka kuimaliza kabisa team Sc41” akasisitiza.Sauti na sura yake vilionyesha wazi kwamba alikuwa amedhamiria kufanya alichokisema.Mathew akamtazama kwa makini sana na kuuliza
“ Kwa nini unataka kuimaliza team SC41?
Peniela bila kusita akajibu
“ Sababu kubwa inayonifanya nitake kuimaliza team SC41 ni ili niwe huru.Ninataka nianze kuishi maisha mapya tofauti na haya ninayoishi sasa .Nataka kuishi maisha ya kawaida kama wenzangu.Baada ya kuingia team SC41 maisha yangu yaliharibika na ndoto zangu zote za maisha kuyeyuka.Mnionavyo hapa sina maisha ya kawadia kama wenzangu,siwezi kuwa na mpenzi,siwezi kuwa na familia na siwezi kufurahi kama wanawake wenzangu.Nimechoshwa na maisha haya,nimechoshwa na kuutumia mwili wangu kama bidhaa kwa faida ya Tweam SC41,ninataka kuachana na aina hii ya maisha na ili niachane nayo lazima nitoke team SC41 na hakuna namna ninayoweza kutoka Team SC41 zaidi ya kukimaliza kabisa kikundi hiki.John Mwaulaya ameniahidi kwamba ataniachia niwe huru lakini sina hakika kama atatimiza lengo lake na kwa hiyo lazima nifanye jitihada za kujiweka huru mimi mwenyewe na kuimaliza Team SC41 ndiyo njia pekee.I need your help guys.Nimewaeleza ukweli huu ambao sijawahi kumweleza mtu mwingine ili mnielewe na mnisaidie .” Akasema Peniela
“ kwani ilikuaje hadi ukajiunga na Team SC41? Akauliza Anitha
“ Ni hadithi ndefu kidogo. Lakini nitawaelezeni kwa ufupi ili na ninyi mpate picha.”akasema Peniela na kunyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Mimi ni yatima.Nilipopata akili nilijikuta katika kituo cha kulelea watoto yatima.Mpaka leo hii sijawahi kupata taarifa zozote za kuhusu wazazi au ndugu zangu.Kitu nilichoambiwa na mama Bernadetha mlezi wangu ni kwamba nilipelekwa pale kituoni na mtu aitwaye John Mwaulaya ambaye ndiye mfadhili wangu amekuwa akinihudumia kwa kila kitu.Nikiwa pale kwa mama Bernadetha niliishi maisha mazuri,nilipata kila kitu nilichohitaji kiasi kwamba nilijiona sawa na watoto wengine wote.John mwaulaya alikuwa akinitumia kila kitu kupitia kwa mama Bernadetha.Nilimshukuru Mungu kwa kunijalia mfadhili kama yule ambaye alikuwa akinipatia kila kitu.” Peniela akanyamaza kidogo akanywa whysky na kuendelea
“ Nilianza masomo katika shule ya kimataifa,na gharama zote zililipwa na John.Nilikuwa ni mmoja wa wanafunzi wenye uwezo mkubwa darasani.Nilisoma vizuri hadi nilipofika darasa la saba.Kwa maisha niliyoishi ilikuwa vigumu kuamini kwamba nilikuwa ni mtoto nisiye na wazazi kwani niliishi maisha kama mtoto wa tajiri mkubwa.Katika miaka hii yote sikuwahi hata siku moja kuonana na mfadhili wangu John ingawa nilitaka sana kumuona walau niweze kumjua ni mtu wa namna gani .Pamoja na maombi hayo ya siku nyingi lakini John Mwaulaya hakuwahi kujitokeza hata siku moja nimuone na sikuelewa ni kwa nini.Nilipomuuliza mama Bernadetha alisema kwamba John ni mtu wa safari nyingi wa hiyo atakapopata nafasi nitaonana naye.Miaka ilikwenda hadi nilipohitimu darasa la saba.Nakumbuka siku ya sherehe ya kumaliza darasa la saba ndiyo siku ambayo nilifanikiwa kuisikia sauti ya John Mwaulaya.Siku hiyo nilichukuliwa na mama Bernadetha na akanipeleka katika jumba moja kubwa la kifahari akanieleza kwamba jumba lile ni langu nimepewa zawadi na John Mwaulaya kwa kumaliza darasa la saba.Jumba lile lilikuwa kubwa ,zuri na la kifahari sana na nilipewa pia wahudumu wa kunihudumia .Usiku wa siku ile John mwaulaya alinipigia simu akajitambulisha,nilifurahi sana kuisikia sauti yake.Niliendelea na masomo ya sekondari na huku akiendelea kunihudumia kwa kila kitu na hadi ninamaliza kidato cha sita bado sikuwa nimebahatika kuonana na John mwaulaya ana kwa ana.Nilipomaliza kidato cha sita na matokeo kutoka mazuri,John alinitaarifu kwamba alikuwa amenitafutia chuo nchini marekani .Nilifurahi sana na nikajiandaa na kuelekea marekani.Nilipofika kule nilipelekwa katika chuo ambacho kinafundisha masomo tofauti kabisa nay ale ambayo nilikwenda kuyasomea.Chuo hicho kinafundisha mambo yanayohusiana na Team SC41.Mwanzoni sikuwa tayari kujifunza kuhusu masuala hayo lakini nilikamatwa na kuingizwa katika chumba Fulani na kufungiwa humo na baada ya kutolewa mle nilijihisi mtu mpya kabisa kwani nilikubaliana na masomo yote yahusuyo Team SC41.Nilijifunza mafunzo yale kwa miaka miwili nikarejea Tanzania na kujiunga rasmi na team SC41 Tanzania.Hata baada ya kujiunga na teamSC41 bado sikuwahi kuonana na John mwaulaya hadi hivi majuzi nilipochukuliwa na kupelekwa mahala anakoishi nikaonana naye kwa mara ya kwanza akiwa anaumwa sana.” Akasema Peniela .
“ kumbe wana hadi chuo cha kujifunzia? Akashangaa Jason ambaye kwa muda wote wa mjadala ule alikuwa kimya
“ Ndiyo wana chuo tena kikubwa tu kinachotoa kozi mbali mbali.Team SC41 imesambaa katika sehemu mbali mbali duniani ambazo nchi ya Marekani imefanya uwekezaji mkubwa na ndiyo maana kuna chuo kabisa cha kujifuniza kuhusu kazi za Team SC41.Kuna mafunzomengi yanatolewa katika chuo hiki yakiwamo mafunzo ya kijeshi ,mafunzo ya kiintelijensia na mengine mengi.” Akasema peniela
“ Katika chumba hicho ulichoingizwa na ukatoka ukiwa na mtazamo mpya ni kitu gani hufanyika hadi kuwabadili watu mtazamo na kuwafanya wakubali kujiunga na Team SC41? Akauliza Anitha
“ hata mimi sielewi huwa nini kinafanyika lakini ukitoka mle unajiona ni mtu mpya kabisa.” Akasema Peniela
“ I know what they do” akasema Mathew
“ do you know? Akauliza jaji Elibariki
“ yes I know.” Akajibu Mathew
“ Kuna teknolojia ambayo huitumia katika hucheza na akili ya mtu na ukishatoka mle ndani basi akili yako tayari inakuwa imejazwa mambo mengi kuhusiana na team SC41 .” akasema Mathew
“ Nakubaliana nawe Mathew kwamba yawezekana ni kweli wakawa wanatumia teknolojia hiyo kwa sababu ukitoka tu ndani ya hicho chumba hata kama ulikuwa mbishi kiasi gani basi utafuata kila wanachokuelekeza na utajikuta unaipenda team SC41.” Akasema peniela
“ Kama wanawafanyia hivyo basi watu hawa ni mashetani kwani wana waharibu watu akili zao kwa faida ya nchi yao.Ninyi mnapata faida gani kama team SC41? Akauliza Anitha
“ faida kubwa ambayoninaweza kuisema tunaipata ni kuishi maisha mazuri kutokana na mishahara mikubwa wanayotulipa.Tunalipwa mamilioni ya fedha kama mishahara ambayo inatuwezesha kuishi maisha ya kifahari lakini mambo mengine yote tunayoyafanya ni kwa maslahi ya marekani.” Akasema Peniela.
“ Serikali yetu inafahamu chochote kuhusiana na kuwepo kwa kikundi hiki hapa nchini? Akauliza Jason
“ Hapana .Serijkali bado hawafahamu chochote kwa sababu kikundi hiki kinafanya shughuli zake kwa siri kubwa ingawa tayari kimekwisha kita mizizi hadi katika serikali kuu “
“ kwa hiyo kazi zao tunaweza kusema ni sawa na ujasusi? Akauliza jaji Elibariki
“ Tunaweza kusema kazi zao zinafanana na hizo ingawa wanachoangalia wao ni maslahi ya marekani pekee.Kama kuna hatari yoyote katika maslahi ya marekani basi tunawataarifu makao makuu.Mfano kama kuna mpango wowote wa kubadili mikataba ya uwekezaji au kuna chokochoko zozote za chini chini kuhusiana na uwekezaji uliofanywa na marekani hapa nchini basi taarifa hizo huzipata mara moja kwa sababu tayari kuna mizizi ndani ya serikali.Hata hivyo naomba mnielewe ndugu zangu kwamba Team SC41 inashughulika na mambo yale yahusuyo maslahi marekani tu.” Akasema Peniela
“ hata hivyo kikundi hiki bado ni hatari kwa usalama wa nchi yetu na tunatakiwa tukiondoe.Lakini tutawezaje kukiondoa ? Tutakapokigusa kikundi hiki tutakuwa tumeyagusa maslahi ya Marekani na kunaweza kukatokea mgogoro kati ya serikali yetu na serikali ya Marekani ” Akasema jaji Elibariki
“ Ndiyo manaa nimekuja hapa ili kupata mawazo yenu” akasema Peniela
“ peniela,we’ll help you take down team SC41 “ akasema Mathew
“ How ?! Elibariki akauliza
“ let me figure out how we can take down team SC41 lakini ninawahakikishia ndugu zangu lazima tutaiondoa .Bila hata Peniela kuleta ombi lake ,binafsi tayari nilikuwa katika mpango wa kuimaliza kabisa team SC41 ” Akasema Mathew
“ Ulikuwa na mpango huo? Akauliza Peniela
“ ndiyo nilikuwa na mpango huo”
“ kwa nini ulitaka kuiondoa team SC41? Akauliza jaji Elibariki
“ Ni hadithi ndefu kama nilivyo waambia awali .Mimi na John mwaulaya tuna historia ambayo ndiyo sababu iliyonifanya nitake kulipiza kisasi kwa kitendo walichonifanyia.” Akasema Mathew
“ What happened? Mna historia gani wewe na John mwaulaya? Akauliza Peniela.Mathew akainama akazama katika mawazo mengi ,wote wakabaki kimya wakimtazama,wakisubiri kusikia atasema nini.Baada ya kama dakika moja Mathew akainua kichwa na kusema
“ John mwaulaya na team yake ndiyo chanzo cha mimi kuishi maisha haya “akasema Mathew na kisha akawasimulia kila kitu kilichotokea hadi familia yake ikateketezwa.Hadithi ile ikamuumiza sana Peniela.
“ John is a monster” akasema Peniela
“ Kumbe ukatili wake hajauanza jana ,na tayari amekwisha umiza watu wengi .Sikutegemea kama angeweza kufanya ukatili mkubwa kiasi hiki. Hapo kabla nilikuwa na hamu sana ya kutaka kumfahamu John mwaulaya lakini kwa sasa sina hata hamu ya kumuona tena.He’s a monster.Ni kwa sababu yake leo hii mimi nimekuwa na maisha haya.Kama isingekuwa yeye leo hii mimi ningekuwa na maisha yangu mazuri tu yenye furaha.Ndani ya Team Sc41 hakuna mtu ambaye anaweza kusema kwamba maisha yake yana furaha.Wote maisha yetu yako hivi hivi na ukikosea kidogo tu basi hawakuachi wanakuua kimya kimya.Ni kikundi cha hatari sana hiki kwa hiyo ndugu zangu nahitaji sana msaada wenu ili kwa pamoja tuweze kukiangamiza kikundi hiki.Mimi niko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kukimaliza kikundi hiki.Ninazifahamu siri nyingi za Team SC41 kwa hiyo basi nitawaeleza kila kitu kuhusiana na kikundi hiki ” akasema Peniela
“ Peniela nimekusikiliza kwa makini maongezi yako,na ninapenda kukupa pole sana kwa mambo yote yaliyokupata.Mwanzoni nilikuwa na hasira na wewe sana kwa mambo ambayo umeyafanya lakini kwa sasa nimekuelewa na niko tayari kuungana nawe katika kuiondoa hiyo team SC41.Pamoja na hayo kuna jambo nataka kuuliza,huyu John mfadhili wako hajawahi hata mara moja kukueleza chochote kuhusiana na asili yako? Akauliza jaji Elibariki
“ Elibariki nashukuru sana kwa kunielewa .Umeuliza kama vile ulikuwa katika akili yangu .Nina maswali mengi ya kumuuliza John mwaulaya na moja wapo ni hilo hapo la kuhusiana na wapi alinitoa hadi akanifikisha katika kituo kile.Nataka kufahamu asili yangu na mwenye kujua haya yote ni John pekee.”akasema Peniela
“ Hata hivyo” akaendelea
“ Siku ya kwanza niliyoonana naye alinipa kikasha Fulani ambacho alisema kwamba nisikifungue hadi pale nitakapokuwa nimeikamilisha operesheni 26B.Aliniambia kwamba kasha hilo haliko kamili kwa hiyo inanibidi nitafute makasha mengine mawili ili liweze kukamiliza na alinielekeza kwa mtu ambaye alisema nimuone na ndiye atakayenipa maelekezo yote kuhusiana na mahala makasha mengine yaliko.John alisema kwamba niyatunze sana makasha hayo kwani ndimo kuna kila kitu kuhusiana na mimi” akasema Peniela
“ Kasha hilo liko wapi? Akauliza Mathew
“ Nimelihifadhi katika sehemu salama”
“ Ok Good.Endelea kulihifadhi na baada ya kukamilisha kila kitu basi mimi binafsi nitakusaidia katika kuutafuta ukweli kuhusiana na asili yako,wazazi wako,na ndugu zako” akasema Mathew
“ Me too.Count me in” akasema jaji Elibariki
“ Nashukuruni sana jamani kwa kujitolea kunisaidia.Jambo hili limekuwa likiniumiza akili yangu kwa miaka mingi .Ninataka sana kufahamu mimi ni nani lakini sijui nianzie wapi.Natamani sana kulifungua kasha lile ili nifahamu kilichomo ndani lakini ninaogopa kwa sababu John alisema kwamba nilifungue kasha lile pale tu ambapo operesheni itakuwa imemalizika.Kwa sasa nimeanza kuwa na matumaini kwamba nitafahamu asili yangu.” Akasema Peniela
“ Peniela usijali.Ninakuhakiisghia kwamba tutakusaidia katika hilo suala na hata katika kuiondoa Team SC41.Lakini kuna jambo ambalo ninaliomba toka kwako kama mbadala wa kukusaidia mambo haya yote mawili”
“ Jambo gani Mathew? Akauliza Peniela
“ Ninaihitaji hiyo package pindi utakapoitwaa toka kwa Dr Kigomba” akasema Mathew.Peniela akashangaa na akabaki akimuangalia Mathew.Watu wote mle sebuleni wakabaki kimya wakisubiri kusikia atatoa jibu gani
“ Team SC41 wameitafuta package hii kwa muda mrefu na kwa sasa ambapo wanakaribia kuipata watakuwa macho sana ili kuhakikisha kwamba inatua katika mikono yao.Hata hivyo nitafanya kila linalowezekana ili package hii iweze kutua katika mikono yetu.Mimi na ninyi tuko timu moja sasa kwa hiyo usijali Mathew nitahakikisha package hiyo unaipata.” Akasema Peniela
“ Ahsante sana Peniela .Ninakuhakikishia kwamba utakuwa salama tutakulinda hadi mwisho wa operesheni hii na tutafanikiwa kuiondoa kabisa Team SC41.Kwa sasa baada ya mjadala mrefu na kufahamu mambo mengi ambayo hatukuwa tumeyafahamu,tuna kazi kubwa tatu mbele yetu.Kazi ya kwanza ni kuitafuta hiyo package na kuhakikisha kwa gharama zozote zile tunaipata.Kazi ya pili baada ya kuipata packge hiyo ni kumuondoa Dr Joshua katika uogozi na kumfikisha katika vyombo vya sheria na kazi ya tatu ambayo lazima tuifanye ni kuiondoa Team SC41 .” akasema Mathew
“ Kitu tunachotakiwa kukifanya kwa nguvukuanzia sasa ni kukusanya ushahidi wa kutosha kuweza kumtia hatiani Dr Joshua.Yule ni mkuu wa nchi kwa hiyo kumshitaki kwa namna yoyote ile tunatakiwa tuwe na ushahidi mzito sana wa kumuhusisha na matukio makubwa ya kijinai.Tukio la kwanza ni katika kifo cha mkewe.Tuna uhakika mpaka hivi sasa kwamba amehusika lakini tunatakiwa tuwe na ushahidi mzito wa kuthibitisha ni kweli alihusika katika kifo cha mke wake.Tukifanikiwa kumpata katika hili basitutawezakumuangushakirahisi sana ” Akasema Mathew
“ Mathew kuna kitu nimekifikiria kinachoweza kuturahisishia kazi ” akasema Anitha
“.Ili kuweza kupata kile tunachokihitaji,tunatakiwa tuwatumie hawa watu wawili wa karibu na Dr Joshua.Kuna huyu Dr Kigomba na Captain Amos.Hawa watatusaidia sana kuweza kukipata kile tunachokitafuta.Mapendekezo yangu ni kwamba kwa kuwa sasa hivi Peniela ameiingia katika mahusiano na Dr Kigomba basi tuitumie vyema fursa hiyo .Kuna teknolojia ambayo tutaitumia na kuiweka katika simu ya Dr Kigomba na sisi tutakuwa tukifuatilia kila atakachokuwa akikiongea Dr Kigomba kupitia simu yake na vile vile kuna jambo lingine tutakalolifanya,tutaweka kifaa kidogo sana katika mkufu ambao Peniela atampatia kama zawadi ili awe akiuvaa kila siku.Kupitia saa hiyo tutaweza kufahamu mahala aliko na tutaweza pia kusikia kila atakachokiongea kwa hiyo itakuwa rahisi kwetu sisi kufahamu mahala aliko na vile vile kifa hiki kitatuwezesha sisi kusikia kila anachokiongea na myuyeyote .Hii itakuwa njia rahisi sana kunasa mawasiliano yake na Dr Joshua au na watu wengine na kwa hiyo hata atakapokuwa amepewa hiyo package basi itakuwa rahisi kwetu sisi kufahamu kila kitu.Jambo hili tutalifanya pia kwa Dr Joshua.Peniela atampatia mkufu ambao tutaweka kifaa kidogo sana ambacho kitatuwezesha sisi kusikia kila atakachokuwa akikiongea a vile vile tutaweza kumfuatilia kwa ukaribu sana.Nadhani hii inaweza kuwa njia rahisisana ya kufanikisha mpango wetu na kupata ushahidi wa k utosha dhidi ya Dr Joshua” akasema Anitha.
“ Ahsante Anitha kwa mawazo hayo mazuri.Natumai tukitumia njia hiyo tunaweza tukafanikiwa kwa wepesi sana.” Akasema Mathew
“ hata mimi nakubaliana na wazo hilo la Anitha” akasema Jaji Elibariki
“ Jason wewe unasemaje? Unaonekana uko kimya sana” akasema Mathew
“ Mimi pia sina kipingamizi na wazo hilo alilolitoa Anitha kwani teknolojia ndiyo njia pekee ya kutuwezesha kupata ushahidi wa uhakika na tunaouhitaji” akasema Jason
“ Ok vizuri.Kwa kuwa wote tunakubaliana na wazo alilolitoa Anitha,turudi sasa kwa muhusika mkuu wa jambo hili.Peniela kwa upande wako unasemaje? akauliza Mathew
“ mimi kwa upande wangu sina tatizo na ninashukuru kwa mawazo hayo mazuri ya Anitha.Mimi nitafanya kama mtakavyonielekeza .Lolote linalowezekana kufanyika kwa ajili ya kuimaliza team SC41 na kuwatia hatiani Dr Joshua na mtandao wake mimi niko tayari kulifanya.” Akasema peniela
“ nashukuru kusikia hivyo Penny”akasema Mathew.
“ Anitha atashughulikia suala hilo na hadi kesho mchana kila kitu kitakuwa tayari.Lini unategemea kuonana na Dr Kigomba?
“ Tumepanga tuonane kesho jioni”
“ Good.Kwa hiyo kesho mpaka hiyo kesho jioni kila kitu kitakuwa tayari na tutamaliza hili suala ” Akasema Mathew.
“ Mathew kuna mtu wa tatu ambaye naye anaweza akawa ni ushahidi mzuri sana wa kuweza kumtia hatiani Dr Joshua.Ni Captain Amos.Huyu ndiye aliyemuua Dr Flora kwa amri ya rais kwa hiyo ni mtumuhimu sana kwetu” akasema Peniela
“ Ni kweli Captain Amos ni muhimu sana katika jambo hili lakini kwa sasa nadhani tumuweke kwanza pembeni kwani yeye ndiye anayekupa maelekezo na taarifa zote kuhusiana na package hiyo.Tukimvuruga sasa tunaweza kuikosa hiyo package.Amos tutashughulikanaye baadae mwisho wa mchezo” akasema Mathew na kukawa kimya
“ Jamani nawaona tayari mmechoka.Umekuwa ni usiku mrefu lakini ulioambatana na mambo mengi makubwa .Nadhani ni wakati sasa wa kwenda kupumzika.Kesho tutaamkia katika mambo mengine mapya na inawezekana siku ya kesho ikawa ni siku ndefu sana.Mambo mengi yanaweza yakatokea kesho”akasema Mathew.
“ Mathew kabla ya kutawanyika nina jambo nataka kuongea na Elibariki na Jason pekee” akasema Peniela.Mathew wna Anitha wakaondoka pale sebuleni wakawaachia nafasi
“ Simulizi ya Peniela imenisismua sana.Sikutegemea kama historia yake iko namna hii. But Mathew do you trust her ? akauliza Anitha wakiwa katika chumba chao cha kazi
“ I do trust her.Peniela ametueleza ukweli halisi na hajaficha hata jambo moja.Ninaamini ana lengo la dhati la kuisambaratisha Team SC41.” Akasema Mathew
“Vizuri kama unamuamini.Lakini kuna kitu bado najiuliza sana,hiyo package itakuwa na nini ndani yake? Inaweza kuwa na uhusiano wowote na zile karatasi tulizozipata ambazo Edson aliziziiba ikulu? Akauliza Aitha
“ Hata mimi ninahisi hivyo,yawezekana zikawa na mahusiano Fulani na hiyo package anayoisema Peniela. Tukipata taarifa za kutoka kwa wale jamaa zangu niliowaomba msaada kuhusiana na nini kimeandikwa katika zile karatasi basi tutaweza kupata japo mwangaza .Nitawapigia simukeshoasubuhi kufahamu kama wamefanikiwa kufahamu kuhusiana na nini kimeandikwa katika karatasi zile“
Baada ya Mathew na Anitha kutoka sebuleni walibaki Peniela ,Elibariki na Jason.Peniela akawatazama usoni kwa zamu na kusema
“ Jamani nimeona nitumie fursa hii kuongea nanyi maneno machache usiku huu kabla ya kwenda kulala.Kwanza kabisa ninashukuru sana kwa kuzimaliza tofauti zenu na kuwa marafiki tena.Moyo wangu umefarijika sana.Mmeonyesha ukomavu mkubwa .” Akasema peniela akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Usiku wa leo nimewaelezeni ukweli wangu na ninafikiri kwa hivi sasa ninyi nyote mmekwishanifahamu mimi ni nani baada ya kuwapa maelezo yale.Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba samahani sana kwa jambo nililowafanyia lakini nililifanya kwa nia njema tu ya kutaka kuwaweka mbalimbali ili uchunguzi wa kifo cha Edson usifanikiwe . Nilifahamu hatari iliyopo katika kulichunguza jambo hili.Pamoja na hayo nwapongeza sana kwa kusimama imara na hatimaye mmeweza kuufahamu ukweli.Hakunakati yenu aliyekuwa akinifahamu kwa undani.Kila nilichowaeleza ni cha kwelikabisa na ninaomba mniamini kwamba nina nia ya dhati ya kutaka kuiondoa team SC41 ili niweze kuwa huru.Katika hili ninawahitaji sana ninyi wawili mniunge mkono.Najua kila mmoja kwa sasa atakuwa bado ana hasira na mimi lakini ninaomba msifanye hivyo kwani nimekwisha waeleza sababu za mimi kufanya vile nilivyofanya.Hata hivyo kuna jambo ninataka niliweke wazi mbele yenu .” akasema peniela na kunyamza kidogo akawatazama wanaume wale waliokuwa kimya wakimsikiliza
“ Jason wewe ni mtu ambaye una nafasi kubwa sana katika maisha yangu.Umekuwa rafiki wa kweli.Umesimama na mimi hata kwa nyakati zile ambazo wengine hawakuweza.Thamani yako kwangu ni kubwa mno na siwezi kuielezea kamwe.Ninafahamu unanipenda kwa moyo wako wote na umenionyesha kwa vitendo ni namna gani unanipenda na hata mimi nakupenda sana .Elibariki nawe hali kadhalika una nafasi kubwa na ya kipekee kabisa katika moyo na maisha yangu.Umenionyesha kunipenda na kunijali.Ninyi nyote wawili ninawapenda sana..Ninaamini nyote pia mnanipenda kupita maelezo .Mimi kama binadamu ninahitaji kuwa na mararafiki,ninahitaji pia kuwa na mpenzi na ndiyo maana ninataka kufanya kila linalowezekana kuiondoa Team SC41 ili niweze kuwa huru kwa hiyo basi kwa kuwa ninyi nyote ninawapenda na ninyi nyote mnanipenda imenilazimu nifanye maamuzi ni yupi hasa ambaye ninataka niwe naye ” akanyamaza kidogo na kusema
“ Nitakuwa na Elibariki.Ninafahamu Elibariki ananipenda sana japokuwa tayari ana mke wake lakini ndiye ambaye moyo wangu umempenda na ndiye mwanaume ninayetaka kuanza naye maisha mapya.Jason ninaomba usinichukie mimi au Elibariki kwa maamuzi haya .Moyo wangu umenituma nifanye hivyo kwa hiyo nina amini kwamba mtaelewana na hakutakuwa na ugomvi tena kati yenu” akasema Peniela
Kimya kikubwa kikatawala mle ndani.Jason na Elibariki wakaangaliana .
“ Jason kuna chochote unachotaka kusema? Akauliza Peniela
“ Hapana.Sina chochote cha kusema.Nimekubaliana na maamuzi yako.Ninakupenda sana lakini ninaamini kwamba haikuwa bahati yangu ,ninaamini iko siku na mimi nitampata Yule ambaye atakuwa ameumbwa kwa ajili yangu.” Akasema Jason halafu akamgeukia Elibariki
“ Elibariki ninafahamu una mke wako wa ndoa lakini Peniela ameamua kukupenda.Umeisikia historia ya maisha yake imejaa mateso matupu.Peniela anahitaji kuanza maisha mapya yaliyojaa furaha na anahitaji mtu ambaye atamshika mkono na kumuondolea kumbu kumbu zote za nyuma,mtu ambaye atampenda na kumjali kwa moyo wake wote.Mtu ambaye atamuingiza katika ulimwengu mpya uliojaa kila aina ya furaha.Amekuchagua wewe japokuwa uko katika ndoa kwa sababu anaamini kwamba wewe ndiye mwenye sifa hizo.Wewe ndiye ambaye utampatia furaha ya maisha yake.Kwa hiyo nakuomba uwe muangalifu sana,nitakuwa nyuma yako kama kivuli na ukithubutu kumtoa chozi Peniela,I swear I’m going to take her away.” Akasema Jason.Jaji Elibariki akatabasamu na kusema
“ Ahsante sana Jason kwanza kwa kukubaliana na maamuzi ya Peniela na pili kwa kunikumbusha jukumu langu kubwa kwa Peniela.Huna haja ya kunifuata nyuma kama kivuli kwa sababu nina hakika hata siku moja Peniela hatatoa chozi.Nitafanya kila ninaloweza kulifanya kuhakikisha kwamba Peniela hatoi chozi.” Akasema jaji Elibariki .Peniela alikuwa akitabasamu
“ Thank you guys..NInashukuru sana.Ninyi ni wanaume wa ukweli mnayamaliza mambo kiume.Nimefurahi sana kuwa na watu kama ninyi katika maisha yangu.’ Akasema Peniela na kisha akainuka na kuwaomba Jason na Elibariki wasimame kisha wote wakakumbatiana.
“ Ahsanteni sana guys sasa ni wakati wa kupumzika kama alivyosema Mathew.Nadhani tutaonana kesho mchana” akasema Peniela
“ Are you sure you want to go? Akauliza Elibariki
“ Yes ! I have to go Elibariki.Tutaonana kesho.Nitandoka na Jason kwani gari lake liko pale kwangu” akasema Peniela.Mathew akaitwa wakamuaga na kuondoka kwa miadi ya kuonana tena kesho yake.
“ Peniela are you sure you did the right choice? Akauliza Jason wakiwa garini baada ya kuondoka nyumbani kwa Mathew
“ What choice? Akauliza Peniela
“ Kuingia katikamahusiano na Elibariki ambaye tayari ana mke wake wa ndoa”
Peniela akacheka kidogo na kusema
“ Nilidhani mambo yale tumekwisha yamaliza Jason “
“ Ndiyo yamekwisha lakini si unajua ninakujali sana na ninataka niwe na uhakika kama unakifahamu kitu unachotaka kukifanya.”
“ Nina uhakika na maamuzi yangu Jason naniko tayari kukabiliana na change moto zote zitakazojitokeza” Akajibu Peniela kwa ufupi
“ Sawa Penny lakini kumbuka siku zote kwamba mimi niko hapa na ninakupenda na nitakuwa tayari kukupokea muda wowote ukinihitaji.Ukihitaji mtu wa kuongea naye,kubadilishana mawazo,mtu wa kulia naye ,usiende mbali niko hapa ninakusubiri.” Akasema Jason
“ Nashukuru sana Jason.Una mchango mkubwa sana kwangu.Siku zote nitakujali na kukuthamini kama rafiki wa kweli” akasema Peniela na kisha safari ikaendelea.
Walifika nyumbani kwa Peniela Jason akachukua gari lake akaondoka na Peniela akaenda chumbani kwake kulala.Kabla ya kulala akaona ni bora ampigie simu Dr Joshua kumjulia hali na kumuonyesha ni namnagani anamjali.Akachukua simu na kupiga lakini simu ikaita bila kupokelewa,akapiga tena simu ikaita bila kupokelewa
“Yawezekana Dr Joshua atakuwa tayari amelala mida hii au atakuwa katika shughuli nyingine.Nitaongea naye hata kesho” akawaza Peniela na kuweka simu mezani akapanda kitandani.Kabla hajajilaza simu ikaanza kuita.
“ Its him” akasema Peniela na kuinuka akaenda akaichukua na kupokea
“ Hallow Dr Joshua akasema peniela
“ Hallow peniela.Hujambo malaika wangu? Umenistua kidogo kwa simu hii ya usiku mwingi.Nimeogopa nikadhani labda una tatizo “ akasema Dr Joshua
“ Usistuke Dr Joshua.Nimekosa kabisa usingizi nimekuwa na mawazo mengi nikikuwaza wewe na ndiyo maana nikaona ni vyema endapo nitakupigia walau nisikie sauti yako”
“ Nashukuru sana Peniela kwa kunikumbuka.Hata mimi nimekukumbuka na nilitamani sana kukupigia simu walau niisikie sauti yako lakini nilishindwa kutokana na kubanwa sana na vikao”
“ Pole sana Dr Joshua” akasema Peniela
“ Ahsante peniela” akajibu Dr Joshua na halafu kikapita kimya kifupi.Baada ya sekudne kadhaa Peniela akauliza
“ Vipi hali ya mwanao Flaviana?
“ Flaviana bado hali yake si nzuri.Nimeshauriana na madaktari na kesho atapelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.Nimeagiza apelekwe nchini afrika ya kusini.Nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha mwanangu anapona” akasema Dr Joshua
“ Pole sana Dr Joshua.Aliyefanya kitendo hiki Elibariki tayari amekamatwa?
“ Hapana bado hajakamatwa lakini tayari jeshi la polisi limekwisha pata fununu za mahala alikojificha kwa hiyo muda wowote nina hakika watamtia nguvuni” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua nafahamu uko katika wakati mgumu sana hivi sasa.Naomba ufahamu kwamba hauko peke yako.Niko pamoja nawe katika wakati huu mgumu.Ninakupenda ”
“ Nashukuru sana Peniela kwa kusimama pamoja nami hasa katika wakati huu mgumu.Ninakupenda sana “
“ Hata mimi nakupenda pia dr Joshua .Samahani sana kwa kukusumbua usiku huu.Nimefurahi nimesikia sauti yako.Sasa waweza kupumzika.” Akasema Peniela
“ Hata mimi nimefarijika sana kuisikia sauti yako Peniela .Ulale salama malaika wangu kesho nitakupigia simu kukutaarifu hali ya Flaviana inavyoendelea” akasema Dr Joshua wakaagana na kukata simu
“Huyu mzee angejua siku zake zinahesabika wala asingethubutu kuniita mimi malaika.Kama angenifahamu alitakiwa kuniita ziraili wake kwani hajui kilichomo moyoni mwangu” akawaza Peniela na kujitupa kitandani akalala.
Ulikuwa ni usiku mgumu sana kwa jaji Elibariki.Kila alipojaribu kufumba macho na kuusaka usingizi,picha ya peniela ilimjia
“ Ama kweli peniela ameniingia katika kila mshipa wa mwili wangu.Sipati usingizi nikimuwaza yeye tu” akawaza jaji Elibariki halafu akainuka na kukaa
“ Mke wangu Flaviana yuko hospitali akiyapigania maisha yake lakini akili yangu yote inamuwaza peniela tu.mwanamke huyu ana kitu gani cha kutupumbaza sisi wanaume kiasi hiki? Kila mwanaume ambaye anatembea naye basi hayuko tayari kuachana naye.Hii ni sababu iliyopelekea hata Jason atake kuniua siku ile kwa kunipiga na chupa kichwani.Peniela amefanikiwa hadi kumteka mkuu wa nchi na sasa ametua kwa katibu wake Dr Kigomba.Uwezo wake mkubwa wa kuweza kumnasa mwanaume yeyote umewafanya Team SC41 wamtumie sana katika shughuli zao nyingi .Sina hakika kama kuna mwanaume timamu ambaye anaweza akamkataa peniela.”akaendelea kuwaza jaji Elibariki na uso wake ukajenga tabasamu baada ya kuyakumbuka maneno aliyoyasema peniela mbele ya Jason
“ Nitakuwa na Elibariki.Ninafahamu Elibariki ananipenda sana japokuwa tayari ana mke wake lakini ndiye ambaye moyo wangu umempenda na ndiye mwanaume ninayetaka kuanza naye maisha mapya “http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Katika wanaume wote amenichagua mimi niwe mpenzi wake.Ninajisikia furaha na fahari kubwa sana kwani hata mimi ninampenda sana peniela kwa moyo wangu wote.Najua nitakutana na changamoto nyingi lakini nitazishinda .kwa ajili yake niko tayari kwa jambo lolote lile” akawaza jaji Elibariki na mara sura ya mke wake Flaviana ikamjia
“ Naomba nisamehewe kwa mawazo haya lakini nina hakika kwa Flaviana nilikosea njia na ndiyo maana ndoa yetu imetawaliwa na migogoro isiyokwisha.Nyumba yetu imekuwa haina furaha hata kidogo.Kwa Peniela hali ni tofauti kabisa.Pamoja na matatizo yote tuliyonayo sasa hivi lakini tukikutana upendo wa dhati unajidhihirisha kati yetu.Ninaamini Peniela ndiye hasa mwanamke wa maisha yangu.Flaviana ni mke wangu lakini amenifanyia mambo mengi mabaya lakini nimekwisha msamehe kwa mambo yote aliyonifanyia ila sina hakika kama bado moyo wangu una mapenzi tena kwake.Namuombea Mungu apone na akishapona na masuala yangu yakamalizika basi sintakuwa na na la ziada zaidi ya kuhitimisha safari yetu ya maisha ya pamoja kama mume na mke ili nianze maisha mapya na Peniela.Nina hakika kwa wakati huo tayari Dr Joshua atakuwa amekwisha fikishwa mbele ya vyombo vya sheria na nina imani Flavian atakuwa akinichukia mno kwa kitendo hicho kwa hiyo hata kama tukiendelea pamoja we’ll never be happy .Ni bora tuachane na kila mmoja akaendelea na maisah yake”akaendelea kuwaza jaji Elibariki akainuka na kuchungulia nje halafu akakaa tena kitandani
“ Peniela ametueleza mambo makubwa na mazito usiku wa leo na nimemuelewa vizuri sana.pamoja na hayo kuna vitu ambavyo nimejiuliza sana kuhusiana maisha yake na sijapata jibu.Peniela ametoka wapi? John alimtoa wapi? Alimuokota au ilikuaje akafika mikononi mwake na kumpeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima? Akajiuliza jaji Elibariki
“ Huyu mtu John mwaulaya atakuwa akifahamu kila kitu kuhusiana na Peniela.Kuna kila ulazima wa kumsaidia peniela kufahamu kuhusiana na asili yake.Ninahisi yawezekana labda team SC41 wakawa wakiiba watoto na kuwakuza ili wawatumie baadae kwa kazi zao kama walivyofanya kwa peniela.Nina wasiwasi yawezekana labda wazazi wa peniela wakawa bado wako hai .Nitawaeleza akina Elibariki asubuhi ili tulishughulikie jambo hili na kuufahamu ukweli kuhusu Peniela.”akawaza jaji Elibariki na kujilaza tena kitandani
******
Kumekucha tena,siku nyingine imeanza.Saa mbili za asubuhi gari moja la kifahari lenye rangi nyeupe likafunguliwa geti na kuingia katika nyumba ya John Mwaulaya.Toka ndani ya gari lile wakashuka vijana wawili waliovaa suti nzuri za gharama kubwa.Moja kwa moja wakaingia ndani na kukutana na Josh wakasalimiana na kwenda kukaa sebuleni.
“ Karibuni sana Jacob na Paul” akasema Josh akiwakaribisha wale vijana
“ Ahsante sana Josh.Vipi kuhusu hali ya mzee? Tunaweza kumuona na kumueleza kuhusiana na suala lile nililokwambia? Akauliza mmojawapo wa vijana wale
“ Jacob,mzee hali yake si nzuri sana kwa sasa na sina hakika kama litakuwa jambo la busara kumueleza mambo hayo kwa sasa.Kitu cha msingi tunachotakiwa kukifanya ni kuwapokea wageni hao na kuwaleta moja kwa moja kuja kumtazama John na kisha waendelee na mambo mengine “ akasema Josh
“ John ndiye kiongozi wetu mkuu na kwa sasa baada ya Osmund kufariki hatuna tena kiongozi mwingine wa kutuongoza.Pamoja na ugonjwa wake lakini John ndiye tunayemtegmea atuongoze.Ugeni huu ni mkubwa na lazima tumueleze” akasema Jacob.Josh akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Hapana Jacob.Kwa hali ya John ilivyo kwa sasa hatutakiwi kumshirikisha katikamasuala yoyote ya kikazi.Mimi ndiye ninayeshinda na John na ninauelewa ukubwa wa ugonjwa wake.Hata hivyo kuna kitu gani ambacho hatukifahamu? Sisi tunaweza kujiongoza wenyewe kwani kila mmoja wetu anafahamu majukumu yake ya kazi…” akasema Josh halafu akawa ni kama mtu aliyekumbuka kitu Fulani na kusema
“ Nina wazo,kwa nini tusimfahamishe Peniela ?
“ peniela? Jacob akaonyesha kama kushangaa
“ Ndiyo .Peniela ni mtu ambaye anaifahamu vizuri sana team SC41.Ni mtu ambaye anaainiwa sana na ndiyo maana akapewa operesheni 26B.Nadhani Peniela ni mtu ambaye anafaa sana kutuongoza kwa wakati huu ambao John mwaulaya hajiwezi.Nina hakika hata John mwenyewe atakubaliana na maamuzi yetu ya kumtaka Peniela atuongoze kwa wakati huu” Akasema Josh na wale wenzake wakakubaliana naye.Bila kupoteza wakati Josh akachukua simu yake na kumpigia Peniela
“ Hallow Josh.habari yako? Akasema Peniela baada ya kupokea simu
“ habari yangu nzuri sana.Ninaendelea vizuri.” Akasema Josh
“ Josh nilitegemea baada ya tukio la jana hutanipigia simu tena.What is it this time? Kuna mtu mwingine umeelekezwa umteke? Akauliza peniela ambaye sauti yake ilionyesha wazi kwamba hakuwa ameifurahia simu ile toka kwa Josh
“ Peniela samahani kwa kukusumbua asubuhi hii na ninaomba tusahau yale yaliyotokea jana.Nimekupigia kukutaarifu kuhusu jambo moja muhimu sana”
“ jambo gani hilo Josh? akauliza Peniela
“ Kuna wageni wanakuja leo kutoka makao makuu marekani.Watu hawa wanakuja kwa ajili ya kazi maalum za kiofisi pamoja na kuja kumuangalia John mwaulaya kuhusiana na afya yake.Kwa sasa baada ya Osmund kufariki hatuna tena kiongozi mwingine ambaye anatuongoza kwani John mwaulaya bado hajiwezi.Kwa sasa hali yake katu si nzuri hata kidogo na kwa hiyo basi hatutaki kumuhusisha na masuala yoyote ya kuhusiana na Team Sc41 kwa maana hiyo tumeona tuwasiliane nawe ili uweze kulishughulikia suala hili la hawa wageni na vile vile uwe kiongozi wetu wa muda” akasema Josh.Ilimchukua Peniela muda kidogo kujibu
“ Wageni hao wako wangapi? Akauliza Peniela
“ wako wageni sita.”
“ Wanakuja saa ngapi? Akauliza Peniela
“ saa tano za asubuhi leo watakuwa wamefika” akasema Josh.Peniela akakaa kimya akafikiri na kusema
“ sawa nitafika hapo nyumbani sasa hivi.Nisubirini” akajibu peniela
“ Ahsante sana.By the way aren’t you going to ask? Akauliza Josh
“ To ask about what?
“ about how he’s doing?
Peniela akafikiri kidogo na kusema
“ How he’s doing?
“ bado hali yake si nzuri sana” akasema Josh
“ Ok .Ninakuja huko sasa hivi” akajibu peniela na kukata simu
“ Peniela amekubali na amesema anakuja muda si mrefu.Msiogope ndugu zangu hatujakosea kumtaarifu peniela.Hata John mwaulaya anamkubali na kumuamini sana peniela “ akasema Josh
“ mambo yameiva.Nadhani watu hawa anaowasema Josh watakuwa wanakuja kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanaondoka na Package.Nakumbuka nilipoongea na Osmund kwa mara ya mwisho alinitaarifu kwamba imekuja taarifa toka makao makuu kwamba operesheni 26B lazima ikamilike ndani ya kipindi kifupi na alinitaka tukutane ili tuweze kupanga mikakati ya namna ya kuikamilisha operesheni hiyo.Sikupata bahati ya kuonana naye akafariki dunia.Ninadhani wageni hawa tu wanaokuja leo lengo lao ni kuja kuhakikisha kwamba operesheni hiyo inakamilika na wanaondoka na package. Natakiwa kuwasoma ni watu wa namna gani na wanafuata nini.”akawaza peniela na kisha akaamka na kuanza kujiandaa kuelekea nyumbani kwa John mwaulaya.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
Sauti ya mtu aliyekuwa akiongea na simu karibu na mlango wa chumba chake ndiyo iliyomstua jaji Elibariki toka usingizini.Akainuka akajinyoosha na kukaa kitandani.Bado macho yake yalikuwa mazito kwani alichelewa sana kupata usingizi kutokana na mawazo mengi.Kitu cha kwanza kilichomjia akilini baada ya kuamka ni kuhusiana na hali ya mke wake Flaviana.
“ sijui mke wangu Flaviana atakuwa katika hali gani huko aliko.Natamani sana kujua maendeleo yake lakini sijui nitapata wapi taarifa .Maisha yangu sasa yamekuwa ya kujificha ndani na siwezi kuiweka sura yangu nje.Ninamchukia sana Dr Joshua yeye ndiye chanzo cha haya mambo yote.Mtu huyu asiye na huruma amemuua mke wake na sasa mwanae yuko mahututi hospitali akipigania maisha yake yote ni kwa sababu yake.Aliwatuma watu kuja kuniua na badala yake mwanae ndiye aliyepatwa na masahibu na mimi nimeangushiwa mzigo huu .Kwa kweli lazima ifanyike kila aina ya jitihada kuhakikisha kwamba Dr Joshua anafikishwa mbele ya mkono wa sheria na anaondolewa madarakani.Hana roho ya huruma hata kidogo.Lazima madhambi yake yote yaanikwe kwa umma ili wamjue rais wao ni mtu wa namna gani” akawaza jaji elibariki halafu akainuka akavaa fulana
“ Ngoja nikaongee na Mathew yeye anaweza akanisaidia kupata taarifa za maendeleo ya Flaviana.” Akawaza jaji Elibariki na kuufungua mlango na mara akakumbuka kitu
“ Nimekumbuka ,Peniela anaweza akajua hali ya mgonjwa inakwendaje kwa kumuuliza Dr Joshua.Ngoja nimwambie Mathew ampigie simu asubuhi hii niongee naye” akawaza jaji Elibariki na kuelekea katika chumba cha kazi ambamo alimkuta Anitha.Wakasalimiana na akamueleza kwamba Mathew bado alikuwa amelala.Moja kwa moja Elibariki akaenda kugonga chumbani kwa Mathew ambaye aliamka na kuufungua mlango
“ karibu sana Elibariki.Habari za toka jana? Akauliza Mathew
“ habari nzuri sana Mathew.Pole na uchovu.”
“ ahsante sana Elibariki karibu ndani “ akasema Mathew na jaji Elibariki akaingia ndani
“ Mathew samahani sana kwa kukuamsha” akaanzisha mazungumzo Elibariki
“ Usijali Eli.Hujanisumbua na tayari nilikwisha amka” akasema Mathew
“ Mathew kuna mambo mawili ambayo yamenileta hapa.Jambo la kwanza ninataka kufahamu hali ya mke wangu inavyoendelea huko hospitali .Ni vigumu kwa mimi kujua kinachoendelea lakini nimegundua kwamba tunaweza kumtumia Peniela ili kufahamu kinachoendelea hospitali.Yeye ana mahusiano na Dr Joshua kwa hiyo anaweza akampigia na kumuuliza hali ya mgonjwa inaendeleaje kwa hiyo ninakuomba umpigie simu Peniela ili tuone kama anaweza akatusaidia katika hilo.Jambo la pili ambalo nimekuwa nikilifikiria usiku kucha ni kuhusiana na Peniela.Nilimsikia vizuri sana jana maelezo yake na kuna mswali nimejiuliza.Ametokea wapi? John alimtoa wapi? Wazazi wake ni akina nani? Inawezekana Team Sc41 wakawa wakiwateka watoto na kisha kuwakuza na kisha baadae wakaja wakawatumia katika shughuli zao kama vile ilivyotokea kwa Peniela.Alichukuliwa na John na kupelekwa katika kituo cha kulelea watoto na kisha akaendelea kumuhudumia kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na kumsomesha katika shule nzuri na za gharama kubwa lengo kubwa likiwa ni kuja kumtumia baadae kwa shughuli zao.Alipelekwa kusoma nchini Marekani na kule akapatiwa mafunzo ya Team SC41.Ninadhani yawezekana wakawepo wengi tu ndani ya Team SC41 walio na historia kama ya Peniela.Tunatakiwa tulichunguze suala hili tufahamu undani wake na tumsaidie Peniela kufahamu asili yake.Yawezekana wazazi wake wakawa bado hai na wakawa bado wanamtafuta mtoto wao aliyepotea.Unaonaje kuhusu suala hili Mathew? Akauliza jaji Elibariki
“ Elibariki wazo lako zuri na ninaweza kukubaliana na wewe kabisa kwamba yawezekana Team SC41 wakawa wakiwachukua watoto na kisha kuwakuza na baadae kuja kuwatumia katika shughuli zao.John Mwaulaya ana majibu kuhusiana na wapi alimtoa Peniela na wapi waliko wazazi wake.Kwa sasa itakuwa vigumu sana kwa John kuweka wazi jambo lolote lile kuhusiana na Peniela kwani kwa kufanya hivyo atakuwa akihatarisha operesheni yao ya kuipata package.Nimefikiria kitu kimoja hatuwezi kumsubiri John Mwaulaya lazima tuanze mapema kumsaidia Peniela kuutafuta ukweli kuhusiana na asili yake.Leo hii hatuna kazi kubwa mchana na nitakachokifanya nitakwenda katika ile nyumba ya kulelea watoto alikokulia Peniela na nitamuhoji mmiliki wa kituo hicho pengine tunaweza tukapata kitu cha kuweza kutusaidia kufahamu Peniela ametokea wapi.” Akasema Mathew
“ Hilo ni wazo zuri sana Mathew .Kuna ulazima mkubwa sana wa kufahamu Peniela ametokea wapi.Peniela ana nia ya dhati ya kuanza upya maisha yake na itapendeza endapo ataanza maisha yake upya huku akifahamu kuhusiana na asili yake” akasema Elibariki.Mathew akachukua simu na kumpigia Peniela
“ Hallow Mathew habari za toka jana? Akasema Peniela baada ya kupokea simu
“ Habari nzuri Peniela.Umeamkaje?
“ Nimeamka salama Mathew.Elibariki hajambo?
“ Mbona Elibariki peke yake? Sisi wengine hutukumbuki? Akauliza Mathew na kumfanya Peniela aangue kicheko
“ Mathew ninyi nyote ni watu wangu msijali.Wote wazima lakini?
“ Sisi sote wazima kabisa .Elibariki naye mzima sana.Huyu hapa ongea naye” akasema Mathew na kumpa Elibariki simu aongee na Peniela
“ Hallow Peniela habari yako?
“ Habari nzuri Elibariki.Umeamka salama?
“ Ndiyo Penny.Nimeamka salama .Vipi wewe umeamka salama?
“ Ndiyo nimeamka salama japokuwa kila nilipofumba macho ni sura yakot u ndiyo iliyokitawala kichwa changu” akasema Peniela halafu kikapita kimya kifupi Elibariki akasema
“ Peniela kuna jambo ninataka unisaidie.Ni kuhusu kupata taarifa za maendeleo ya Flaviana” akasema jaji Elibariki
“ Ouh tena nimekumbuka.Niliongea na Dr Joshua simuni nikamuuliza kuhusu Flaviana akasema kwamba hali yake bado si nzuri hata kidogo na ameshauriana na madaktari kwamba wamkimbize nje ya nchi kwa matibabu zaidi.Halafu kuna kitu kingine aliniambia .Alisema kwamba tayari jeshi la polisi wana fununu kuhusu mahala ulipo kwa hiyo muda wowote wanaweza wakakukamata.Nimeogopa sana kwa taarifa hizi.” Akasema Flaviana na kumstua sana jaji Elibariki ambaye alibaki kimya akiwaza
“ Kuna nini Elibariki mbona umestuka namna hiyo? Akauliza Mathew
“ Peniela anasema kaambiwa na Dr Joshua kwamba tayari jeshi la polisi wana fununu za mahala nilipojificha.I’m so scared Mathew” akasema jaji Elibarki.Mathew akamfanyia ishara ampatie ile simu
“ Hallo Peniela” akasema Mathew
“ Pafadhali naomba msiwe na wasi wasi wowote hata kama polisi wana fununu kwamba Elibariki yuko hapa kwangu lakini hakuna atakayeweza kumuona.Hapa ni sehemu salama kwake na ninarudia tena hakuna anayeweza kumuona wala kumpata.Ndani ya nyumba hii waweza kuishi hata maisha yako yote bila ya mtu mwingine kufahamu kwa hiyo naomba ondoa kabisa wasi wasi kuhusiana na Elibariki.Jambo la pili ninataka kufahamu kuhusu mahala ulikolelewa.Ulituambia kwamba ulilelewa katika kituo cha watoto yatima ni kituo gani hicho ulicholelewa?
“ Kwani kuna nini Mathew? Akauliza Peniela
“ Usiogope Peniela.Naomba unielekeze tafadhali” akasema Mathew na Peniela akamuelekeza
“ Ahsante sana Peniela .Kuhusu lile suala tuliloongea jana la kuhusiana na ile mikufu tutakayoweka vifaa vya kielektroniki itakuwa tayari hadi mchana wa leo.Kila kitu kikiwa tayari Anitha atakufahamisha na atakuletea vifaa hivyo ili kuepusha wewe kuonekana hapa mara kwa mara kwani yawezekana ukawa unafuatiliwa” akasema mathew
“ Sawa Mathew.Halafu kuna jambo nataka nikutaarifu”
“ Jambo gani Peniela?
“ Nimepigiwa simu asubuhi hii kuna watu wanakuja toka makao makuu ya Team Sc41 marekani na ninahisi wanakuja kuhakikisha operesheni inakamilika na kisha waondoke na package.Hivi sasa najiandaa ili nikawapokee uwanja wa ndege” akasema Peniela.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Peniela wachunguze vizuri ni watu wa namna gani na wanadhamiria kufanya nini kisha unitaarifu mara moja” akasema Mathew na kukata simu akamgeukia Elibariki
“ Mambo yanaiva,kuna watu wanakuja toka marekani kuja kusimamia zoezi la uchukuliwaji wa package na kisha kuondoka nayo.Lakini ndani ya hiyo package kuna nini mpaka iwe ni package yenye umuhimu mkubwa kiasi hiki? Akauliza Mathew
“ Lazima kitakuwa ni kitu kikubwa chenye thamani kubwa sana “ akasema Elibariki
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ hallow mheshimiwa “ akasema mzee Augustine baada ya waziri mkuu kupokea simu
“ samahani kwa kukusumbua mheshimiwa waziri mkuu mkuu”
“ Bila samahani Augustine”
“ Mheshimiwa waziri mkuu unakumbuka mchana nilikupigia simu na kukwambia kwamba pengine ningeweza kuja kukuona jioni ya leo?
“ Ndiyo nakumbuka Augustine”
“ Ok mheshimiwa basi nahitaji kuja kukuona usiku huu.Nina jambo kubwa sana ambalo haliwezi kusubiri hadi kesho.” Akasema mzee Augustine
‘ Ok Mr Augustine.Kama unaweza kuja hapa katika makazi yangu nitakusubiri”
“ Ahsante sana mheshimiwa .Ninakuja hapo muda si mrefu.Naomba nikufahamishe vile vile kwamba nitaongozana na vijana watatu.” Akasema mzee Augustine na kukata simu
“Waziri mkuu amekubali kuonana nasi kwa hiyo hatuna muda wa kupoteza hapa.Twendeni nyumbani kwake tukaonane naye.” Akasema mzee Augustine na kuyabeba mafaili yale na kwa haraka wakaingia garini na safari ya kuelekea kwa waziri mkuu ikaanza.
ENDELEA………………..
Saa tatu na nusu za asubuhi Peniela akawasili katika makazi ya John Mwaulaya akapokelewa na Josh.
“ Karbu sana peniela” akasema Josh na kumuongoza Peniela hadi sebuleni ambako kulikuwa na vijana wengine wawili waliovalia nadhifu.
“ Peniela kutana na Jacob na Francis ,hawa wako ofisi kuu na wamekuja kwa ajili ya lile suala nililokueleza.” Akasema Josh.Peniela akasalimiana na wale vijana na kuketi
“ Haya niambieni mlichokuwa mnataka kuniambia”akasema Peniela ambaye alionekana kuwa na haraka “
“ Peniela ni kama vile nilivyokueleza simuni.kwanza ni kuhusiana na mtu wa kutuongoza japo kwa muda mfupi.Alipoanza kuumwa John mwaulaya alimteua Osmund awe kiongozi wetu hadi alipofariki.Kwa sasa hatuna tena mtu wa kutuongoza hasa katika kipindi hiki ambacho John mwaulaya anaumwa na tukjokatika operesheni kubwa .Sisi watatu tumekaa na kuona kwamba tukuchague wewe utuongoze kwa wakati huu ambao hatuna mtu wa kutuongoza.Jambo la pili ni kuhusiana na ugeni unaokuja leo hii.Kuna wageni sita wanakuja leo wakitokea makao makuu nchini marekani.Bado hatufahmu nini kinawaleta watu hawa kwa hiyo tunahitaji mtu wa kuwapokea wageni hawa na kufahamu kilichowaleta.Tunaaminikwambawewe unaweza ukalibeba jukumu hilo Peniela” Akasema Josh.Peniela akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
“Kwa nini ninyi peke yenu mfanye maamuzi kama haya ya kunitaka mimi niwaongoze? Mna hakika wenzenu watakubaliana nanyi? Akauliza Peniela
“ Watu wote wamekuwa wakijiuliza kuhusiana na nani ambaye atatuongoza .Kila mmoja wetu anafahamu majukumu yake lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya bila ya kupewa ruhusa na maelekezo toka kwa kiongozi kwa hiyo sisi kwa niaba ya wenzetu tunakupendekeza wewe ili uwe kiongozi wetu japo kwa muda na nina imani kwamba hata wenzetu wote watakubaliana na mapendekezo yetu.Wewe ni mtu unayeifahamu vyema team Sc41 na unaweza ukatuogoza vizuri.Tunaomba utukubalie ombi letu la kutaka utuongoze” akasema Jacob.
“ kwa kuongezea hapo alipoisha Jacob,hata mzee John mwenyewe ameonyesha kukukubali sana na anakuamini .Nina hakika hata akisikia kwamba tumefanya maaamuzi ya kukuomba utuongoze atakubaliana nasi” akasema Josh.Peniela kama kawaida yake akanyamaza kidogo akawaangalia wale vijana na kisha akasema
“ Ok nitafanya mnavyotaka lakini ni kwa wakati huu tuu wanaokuja hawa wageni.Baada ya wageni kuondoka basi John au makao makuu watawachagulia mtu mwingine wa kuwaongoza.Ok tuachane na hayo ,wageni hao wanaokuja tayari wametafutiwa mahala watakapofikia? Akauliza Peniela
“ Masuala yote alikuwa akiyashughulikia Osmund na hatufahamu kama tayari walikuwa wametafutiwa sehemu ya kufikia au bado”
“ Ok isiwe taabu,kuna hoteli nyingi nzuri hapa jijini. Nadhani Maryrose 72 hotel itawafaa sana. Josh shughulikia suala hilo ili wageni hawa watakapowasili tuwe tayari tumewatafutia sehemu nzuri ya kufikia.Jacob na Francis tunakwenda uwanja wa ndege kuwapokea wageni.” Akasema Peniela na kabla hawajaondoka akaomba Josh ampeleke chumbani kwa John Mwaulaya akamuangalie.
John mwaulaya alipomuona Peniela ameingia mle chumbani kwake alifurahi na kujitahidi kutabasamu.
“ P..Pe.Peniela..” akasema John kwa sauti dhaifu.Peniela akamtazama mzee yule pale kitandani ambaye alikuwa amelala hajiwezi akamuonea huruma sana.Akamsogelea karibu.
“ Pole sana John.” Akasema Peniela
“ Ahsante Penny…Ahsante kwa kuja kuniona” akasema John mwaulaya na kumfanyia ishara peniela asogee karibu zaidi.
“ Peniela najua sina muda mwingi wa kuendelea kuishi.I’m going to die soon.Kama nikifariki kabla operesheni 26B haijakamilika ,tafadhali hakikisha kwamba unafanikiwa kuikamilisha kwani ni operesheni muhimu sana.Ikisha kamilika nenda kaendelee na maisha yako.Kuna mambo mengi ambayo nilitaka nikufanyie kablaya kufa ili niweze kuyatengeneza upya maisha yako niliyoyaharibu lakini kutokana na afya yangu kuzorota sina hakika kama nitaweza tena kuyanfanya kwa hiyo nakusihi hakikisha ukikamilisha operesheni hii unaachana kabisa na team SC41.Go far away from here and live your life.Find yourself a man and start a family” akasema John.Peiela akalengwa na machozi
“ John you are not going to die.Iwill do anything in my power to make sure that you get well” akasema Peniela
“ usisumbuke Peniela.Sina maisha marefu .Tafadhali shughulikia kwanza suala la operesheni 26B na baada ya hapo shughulikia kuyajenga upya maisha yako.Nilikukabidhi kasha moja na kukupa maelekezo nini cha kufanya pindi ukiikamilisha operesheni 26B .Fuata maelekezo yangu niliyokupa’ akasema john mwaulaya.
“ Usiseme hivyo John.Nitafanya kila linalowezekana mpaka nihakikishe umekuwa salama.Utapona John.Nakuhakikishia utapona.Doctors are on the way coming.You’ll be ok John” akasema peniela
“ Peniela najua unanipenda na unaumia kuniona hivi lakini nakuhakikishia kwamba hata ufanye nini sintaweza kupona.Tafadhali usipoteze muda na mimi tena.Nimekwisha ishi vya kutosha hapa duniani na sehemu kubwa ya maisha yangu nimeishi nikiwa ndani ya team SC41 .Nimefanya mambo mengi makubwa,nimetoa uhai wa watu wengi na sasa na mimi ni wakati wangu umefika.I have to face death” akasema John.Peniela akashindwa kujizuia kutoa machozi
“ John..! akasema peniela lakini John akamfanyia ishara asiseme chochote.
“ Peniela ninakiona kifo changu.Sina ujanja wa kuweza kukikwepa.Ninakusi usiendelee tena kuwa ndani ya Team SC41.Mimi nimefanya mambo mengi mabaya ndaniya kikundi hiki.Nilikuwa nikitoa roho za watu bila huruma na sikujua kwamba sikumoja na mimi nitachungulia kifo.Sitaki uishi maisha kama niliyoishi mimi ndani ya Team SC41 na ndiyo maana nakuomba ukiikamilisha operesheni 26B achana kabisa na team SC41 na uende ukaishi mbali uendeshe maisha yako.”akasema John.Peniela akashindwa kuendelea kumuona John katika hali ile akatoka huku akilia.Josh akamfuata.
“ Its ok peniela.Tafadhali usilie.John will be fine” akasema Josh.
“ jana nilikuwa na hasira na John na sikutaka hata kumuona lakini baada ya kumuoa akiwa pale kitandani hajiwezi nimejikuta nikiumia tena” akasema Peniela.halafu akafuta machozi na kuufungua mkoba wake akatoa mkebe wa poda akajipaka usoni .
“ Josh muda unakwenda sana ,shughulikia suala lile la hoteli ya kufikia wale wageni.Suala hili la ugonjwa wa John niachie mimi nitalishughulikia” akasema peniela na kisha akaongozana na akina Jacob wakaingia katika magari yao na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege
“ Nilimchukia sana John kwa kitendo chake cha kumteka Jason na kumtesa lakini baada ya kumuona tena leo hasira zangu zote zimepotea na nimejikuta nikumuhurumia tena.Pamoja na yote mabaya aliyoyafanyia lakini kuna mengimazuri ameyafanya katiamaisha yangu kwa hiyo natakiwa na mimi nionyeshe japo msaada wangu mdogo kwake kama shukurani zangu.Ni kweli ni yeye aliyeyaharibu masha yangu lakini ni yeye ambaye alihakikisha ninalelewa na kukua bila tatizo lolote licha ya kutokuwa na wazazi.Nadhani sintafanya jambo jema kama nikiweka hasira mbele na kumuacha mzee yule ateseke kitandani bila ya msaada.Team SC41 ni kama wamemtelekeza.Nitawasiliana na yule daktari rafiki yake afanye haraka kuja ili aweze kumfanyia upasuaji “ akawaza peniela akiwa garini kuelekea uwanja wa ndege
******
Saa nne za asubuhi,Mathew kwa kufuata maelekezo aliyopewa na peniela,aliwasili katika kituo cha kulelea watoto ambako ndiko Peniela alikolelewa toka akiwa mdogo..
“ Kituo kizuri sana.” Akawaza Mathew na kushuka garini akaeleka getini kulikokuwa na mlinzi aliyemuuliza shida yake.Mathew akaeleza shida yake kwamba ni kuonana na Bi Bernadetha mkuu wa kile kituo.Mlinzi yule akamfahamisha kwamba kwa wakati huo Bernadetha alikuwa mgonjwa na alikuwa amelala ndani na hatakiwi kusumbuliwa.Mathew akasisitiza kwamba ana jambo la muhimu sana lililompeleka pale.Mlinzi yule bado aligoma kabisa kumruhusu Mathew kuingia hadi alipokabidhiwa noyto mbili za elfu kumi kumi .Huku akitabasamu akamuomba Mathew amsubiri pele pale getini akaingia ndani na baada ya kama dakika tano akatoka na kumruhusu Mathew aingie ndani.
Nyumba ya bi Bernadetha ilikuwa pembeni ya bweni la ghorofa la watoto yatima anaowatunza.Alikaribishwa sebuleni na msichana mmoja , akapatiwa kinywaji na baada ya kama dakika kumi hivi Bi Bernadetha akatokea.kwa kumuangalia tu ungetambua kwamba alikuwa anaumwa kwa namna alivyokuwa amedhoofika.likuwa akitembea taratibu na kwa msaada wa fimbo
“ karibu sana kijana “ akasema Bi bernadetha kwa sauti ya chini
“ Ahsante sana bibi.Shikamoo” akasema Mathew
“ marahaba mwanangu”akajibu yule bibi
“ Pole sana bibi unaendeleaje? Akauliza Mathew
“ Hivyo hivyo mwanangu,Mungu ananisaidia.Magonjwa yananiandama.Ninasumbuliwa na kisukari,shinikizo la damu, mara miguu inavimba yaani ni mateso kila kukicha.Huu uzee nao unachangia sana kuumwa umwa.” Akasema bibi Bernadetha.
“ Pole sana bibi Mungu atakusaidia na utapona tu”
“ nashukuru kijana wangu.Nimeambiwa una shida na unahitaji kuniona”
“ ndiyo bibi nimekuja kwako nina shida kidogo na samahani sana kwa kukusumbua.Mimi ninaitwa Mathew na jambo kubwa lililonileta hapa ni kutaka kupata taarifa kuhusu msichana mmoja aliyewahi kulelewa hapa anaitwa Peniela.” Akasema Mathew na mara tu bi Bernadetha alipolisikia jina Peniela akastuka kidogo
“Peniela!..”
“Ndiyo bibi”
“ Ni mwanangu huyu na muda mrefu sijamuona wala hajafika kunijulia hali yule mtoto.Yuko wapi ? Yuko salama? Anaendeleaje na maisha yake? Akauliza bi Bernadetha
“ Peniela ni mzima ila sina hakika kama anafahamu kuhusiana na ugonjwa wako.Nina imani angekwishakuja kukutazama.Mara ya wisho umeonana naye lini? Akaliza Mathew.Bi Bernadetha akakaa kimya kidogo akazama katika kumbu kumu zake na kusema
“ Ni zaidi ya mwaka mmoja uliopita.” Akasema
“ Kuna tatizo lilimpata Peniela na ndiyo maana alishindwa hata kuja kukutazama.” Akasema Mathew
“ Alipatwa na tatizo gani? Akauliza Bi Bernadetha kwa wasi wasi
“ Kuna matatizo yalimpata akawekwa kizuizini lakini kwa sasa matatizo hayo yamekwisha na yuko huru.” Akasema Mathew
“ masikini Peniela ndiyo maana sijamuona akija kunisalimu.Nilishangaa sana kwani haikuwa kawaida yake kupitisha mwezi mmoja bila kuja kunitembelea.Wewe ni nani wake? mume wake? Akauliza Bi Bernadetha na Mathew akacheka kidogo
“Hapana bibi.Mimi si mume wake.Peniela bado hajaolewa”
“ anasubiri nini huyu binti? Nimekuwa nikimsisitiza kwamba aolewe bado mapema ili niweze kuwaona wajukuu zangu lakini sijui kwa nini mpaka leo hii hataki kabisa kuolewa”akasema Bi Bernadetha na kimya kifupi kikapita Mathew akasema
“ Bibi nimekuja hapa kutaka kufahamu kuhusiana na historia ya Peniela.Alifikaje hapa? Ana ndugu zake ? Wewe ni mtu pekee ambaye anamfahamu vizur Peniela na historia yake na ndiyo maana nimekuja kwako kutafuta taarifa hizo.” akasema Mathew.Bi Bernadetha akaonyesha wasi wasi kidogo na kuuliza
“ Kwa niniunataka kufahamu kuhusu historia ya peniela? Kuna tatizo gani limetokea?
Mathew akamtazama yule bibi kwa makini na kuamua kumdanganya
“ Bibi nadhani itakuwa vizuri kama niikuwekawazi ili uweze kunielewa .Mimi ni mchumba wa Peniela na kama ikimpendeza Mungu tunaweza tukafunga ndoa.Kabla hatujafunga ndoa nahitaji kumfahamu mwenzangu vizuri,asili yake ametoka wapi,ndugu zake ni nani n.k.Alinieleza kwamba yeye ni yatima na amekulia hapa na ndiyo maana nimekuja hapa bila ya yeye kufahamu ili noweze kulithibitisha hilo na kumfahamu vizuri mwenzangu ikiwemo na tabia zake kwani wewe ndiye uliyemkuza.” akadanganya Mathew.Bi bernadetha akatabasamu kidogo baada ya kusikia uongo ule wa Mathew
“ Ouh kumbe wewe ndiye mchumba wa Peniela.Ungejitambulisha toka mwanzo baba.Nimefurahi sana kukujua mwanangu.Karibu sana.Mimi ndiye niliyemlea peniela toka akiwa mdogo kabisa.Ninampenda sana peniela kama mtoto wangu wa kumzaa mwenyewe.” Akasema bi bernadetha na kukaa kimya kidogo.Mathew alikuwa makini akimsikiliza bibi yule aliyekuwa akiongea kwa sauti ndogo.Bi Bernadetha akaendelea
“ Peniela aliletwa hapa akiwa mdogo sana na mtu mmoja aitwaye John Mwaulaya.Huu ndiye baba yake mzazi Peniela” akasema Bi Bernadetha na kumstua sana Mathew ingawa hakutaka kuonyesha mstuko ule mbele ya yule bibi
“ John alisema kwamba alimchukua Peniela kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa na tabia za kukesha baa na kufanya ukahaba huku akimuacha mtoto nyumbani akiteseka nahivyo alimua kumchukua na kumleta hapa ili nimlee.Alinitaka nimlee kwa siri bila ya mtu kufahamu.John aliniambia kwamba hataki peniela afahamu kama yeye ni baba yake.Ninamsifu John kwani alijitahidi sana kutoa ushirikiano na misaada mingi katika kumlea peniela.Misaada toka kwa John mwaulaya ilikuwa ikimiminika kila leo na ndiye aliyejenga hilo bweni la ghorofa unaloliona hapo nje.Nilimfahamisha Peniela kwamba vile vitu vyote alivyokuwa akivipata vilitoka kwa mfadhili aliyejitolea kumsaidia .Alitamani sana kumfahamu mfadhili huyo ni nani lakini hadi anamaliza darasa la saba hakuwa ameonana na mfadhili wake ambaye ni baba yake mzazi.” Bernadetha akanyamaza kidogo na baada ya muda akaendelea
“Peniela alipomaliza darasa la saba John alimzawadia jumba kubwa la kifahari na hapo ndipo peniela akahama nyumbani kwangu na kuanza rasmi maisha yake.Pamoja na kuwa na maisha yake lakini bado tuliendela kuwa karibu.Nilikuwa namtembela mara kwa mara kuhakikisha anaendelea vizuri.Alifanikiwa kumaliza kidato cha sita na akafaulu vizuri sana na baadae akanitaarifu kwamba anaelekea marekani kwa masomo ya chuo kikuu.Alipomaliza masomo yake alirejea nchini na tuliendelea kuwasiliana na kutembeleana kama kawaida lakini ghafla akapotea na sikumuona tena na nikadhani labda amekwenda kuendelea na masomo zaidi.Sikupata nafasi ya kutafuta taarifa zake kwani na mimi nilianza kusumbuliwa na magonjwa .Nimestuka sana uliponiambia kwamba alikuwa amefungwa gerezani” akasema Bi Bernadetha
“ Bibi,Peniela sasa yuko huru na mambo yake yamekwisha malizika.”
“ Ouh ahsante sana Mungu kwa kumjalia mtoto Yule amekuwa huru tena.Alifanya kosa gani hadi akawekwa kizuizini? Akauliza Bi Bernadetha
“ Alisingiziwa kesi “ akajibu Mathew kwa ufupi halafu kukawa kimya tena
“ Bibi huyo John aliwahi kukueleza aliko mama yake Peniela ?
“ John hHajawahi kunieleza mahala aliko mama yake Peniela.Alichowahi kunieleza ni kwamba mama yake Peniela alikuwa na tabia mbaya na alikuwa akifanya biashara ya ukahaba na ndiyo maana aliamua kumchukua mtoto na kumleta hapa na hakutaka kabisa Peniela amfahamu mama yake “
“ Kwa nini John alikataa usimweleze Peniela kama yeye ni baba yake?
“ Sifahamu ni kwa nini alifanya vile.Kila nilipomuuliza hakutaka kunipa jibu na alisisitiza nimwele peniela kwamba yeye ni mfadhili wake.Sina hakika kama mpaka sasa Peniela amefaikiwa kuonana na John kwani alikuwa akikwepa mno kuonana naye.” akasema Bi Bernadetha.Mathew akainama akafikiri halafu akasema
“ Bibi nakushukuru sana kwa kunikaribisha na kunipa maelezo mazuri.Nimefurahi sana kwa maelezo uliyonieleza.Nakuahidi nitarejea tena hapa kwako siku si nyingi kujua maendeleo yako na nitamfahamisha peniela kuhusu ugonjwa wako ” Akasema Mathew
“ Ahnte sana kijana wangu lakini kuna jambonataka nikuweke wazi.Nimekueleza jambo hili lakini tafadhali sana naomba usimweleze Peniela kwani ndiyo yalikuwa makubaliano yangu na John na sikuwahi hata mara moja kuyavunja kwa kumueleza Peniela kwa hiyo naomba na wewe usithubutu kumweleza chochote.Iko siku John mwenyewe atamueleza “ akasema Bi Bernadetha
“ Nimekuelewa bibi na sintafanya hivyo.Nitakachofanya nitamueleza tu kwamba nimekuja kukutembelea na kukuta unaumwa na nitamsisitiza kwamba aje akutembelee.” akasema Mathew kisha akamuaga Bi Bernadetha na kuondoka
“ John Mwaulaya ni baba yake Peniela??..akajiuliza Mathew akiwa garini
“ Hapana hainiingii kabisa akilini eti John Mwaulaya awe ni baba yake Peniela halafuakatae mwanae kumfahamu.Hili ni jambolisilowezekana.Kama kweli ni baba yakena hakutaka peniela afhamu na badala yake akatambulishwa kwake kama mfadhili basi kuna kitu alikuwa anakificha na ambacho lazima nikifahamu.Amakweli dunia imekuwa ndogo sana.Hatimaye mimi na John mwaulaya tunakwenda kukutana tena uso kwa uso.This time I’ll be the one making him talk.” Akawaza Mathew
Abiria waliokuja na ndege ya shirika la ndege la Emirates walianza kutoka nje ya uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.Peniela akiwa ameongozana na Jacob na Francis tayari walikuwapo hapo uwanjani wakiwasubiri wageni wao waliofika na ndege hii.Mikononi mwao kila mmoja alikuwa na picha mbili za wageni wanaowasubiri kwani hawakuwahi kukutana nao hata mara moja.Ni Peniela aliyekuwa wa kwanza kumtambua mmoja wa wageni wale waliokuwa wakiwasubiri.Nickson Strawberry alitambulika kwa urahisi kutokana na mtindo wake wa nywele .Alikuwa na nywele ndefu alizozikusanya kwa nyuma na kuzifunga.
“ That’s Nickson “ akasema Peniela na kumuita Nickson akasimama akageuka na kutmazama Peniela, akamfuata.
“ hallow Nickson.karibu sana Tanzania” akasema Peniela
“ Ahsante sana.” Akajibu Nickson
“ Naitwa Peniela na hawa ni wenzagu Jacob na Francis” Peniela akafanya utambulisho mfupi
“ Peniela !.akashangaa Nickson
“ wewe ndiye Peniela?! Akasema Nickson na kumkumbatia Peniela kwa furaha
“ Nimefurahi sana kuonana nawe Peniela” akasema Nickson kisha akawaita wenzake akawatambulisha.Alikuwepo Joe Levernsky mmarekani mweusi ,alikuwepo pia Bill beherds,Stanley Phoenix,Alexander Piscat na Edwin Washington.Kisha salimiana wakaelekea katika maegesho wakaingia katika magari mawili waliyokuja nayo akina Peniela na kuondoka
“ Nilitegemea kumuona Osmund hapa uwanjani.Yuko wapi?akauliza Nickson aliyekuwa amekaa kiti cha mbele pembeni ya Peniela
“ Osmund? Peniela akashangaa
“ Ndiyo” akajibu Nickson
“ Ina manaa hamna taarifa? Peniela naye akashangaa
“ taarifa gani penela?
“ Kuhusiana na Osmund”
“ Hatuna taarifa zozote kuhusiana na osmund.Tulipopanga safari hii yeye ndiye tuliyekuwa tukiwasiliana naye kwani ndiye aliyekuwa akiongoza team SC41 badala ya John lakini kwa siku kama tatu hivi hapatikani simuni hivyo ikatulazimu kwenda nje ya taratibu za team Sc41 na kuwataarifu vijana ofisi kuu dare s salaam kuhusu ujio wetu.Mara nyingi safari kama hizi hufanyika kwa siri.Yuko wapi Osmund? akauliza Nickson
“ Nini kinaendelea katika Team SC41? Kama tukio linaweza likatokea huku Tanzania na ninyi makao makuu msilifahamu basi ni hatari sana.Inaonekana wazi kwamba hakuna mawasiliano kati ya ofisi ya Dar es salaam na ofisi kuu Marekani.Ninaamini Team SC41 Tanzania ina watu wengi ambao wangeweza kuwapa taarifa.Kwa nini washindwe kutuma taarifa za matukio yanayotokea huku ? akauliza Peniela
“ Unayosema Penielani ya kweli kabisa.Toka John mwaulaya alipoanza kuumwa kumekuwa na tatizo katika ofisi ya Dar es salaam.Alimteua Osmund lakini bado hali ilikuwa ile ile.lakini usijali tumekuja kuweka mambo sawa na kila kitu kitakwenda vizuri sana.Kuna taarifa gani ya kuhusiana naOsmund? Akauliza Nckson.Peniela aliyekuwa akiendesha akapunguza mwendo na kusimama katika foleni kisha akasema
“ Osmund amefariki dunia”
“ Osmund amefariki dunia? Lini ?Akashangaa Nickson
“ Ndiyo tena si Osmund pekee bali na Dr Burke ambaye alitumwa kuja kufuatilia hali ya ugonjwa wa John .” akawema Peniela na kumstua sana Nickson ,aliyebaki anamtazama Peniela hadi pale gari zilipoanza kusogea
“ Peniela taarifa hizi ni ngeni kabisa kwetu.Hatukuwa tukifahamu chochote kilichotokea.Hapa ndipo unapokuja ukweli kwamba John mwaulaya alikuwa na nafasi kubwa sana katika team SC41.Kabla hajaumwa mambo kama haya hayakuwepo kabisa.Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi hivi sasa kuhusiana na mauaji hayo? Akauliza Nickson
“ Hapana.hakuna aliyekamtwa hadi hivi sasa “ akajibu Peniela.Nickson akainama akafikiri halafu akainua kichwa na kusema
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Peniela kuna tatizo kubwa Team Sc41 Tanzania.Kuna kitu kinachoendelea hapa kwa sababu haiwezekani watu wawili wote team SC41 wauawe kwa wakati mmoja.Lazima tulifanyie uchunguzi suala hili ili tufahamu ukweli.Ninahisi kuna kitu hakiko sawa ndani ya team SC41 na hii ni hatari sana” akasema Nickson
“ Unahisi Dr Burke na Osmund waliuawa na mtu toka ndani ya team SC41? Akauliza Peniela
“ Sina hakika bado kama ni mtu toka ndani ya team SC41 lakini mazingira ya vifo hivyo yanatia shaka sana kwani inaonekana wazi waliuawa na mtu aliyekuwa na sababu Fulani.Lakini tutafahamu kila kitu baada ya kufanya uchunguzi wa kina.” Akasema Nickson
“ Ninajiuliza endapo tusingekuja,tusingetaarifiwa kuhusu kifo cha Osmund na Dr Burke? Huu ni udhaifu mkubwa sana umeonekana katika Team Sc41.Kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuisuka upya team SC41. Ahsante sana Peniela kwa taarifa hizi.kazi yetu itakuwa kubwa sana tofauti na nilivyokuwa nikitazamia.Team SC41 tanzania inatakiwa isukwe upya ili iwe imara kama ilivyokuwa mwanzo.Tukiachana na hayo vipi hali ya John mwaulaya? Akauliza Nickson
“ hali ya John si nzuri hata kidogo.kwa siku kadhaa hapo kati kati hali yake ilikuwa nzuri na wote tukawa na matumaini kwamba muda si mrefu atapona lakini ghafla hali yake ilibadilika na mpaka leo bado si nzuri.Anahitaji matibabu makubwa,kuna rafiki zake madaktari wanaweza wakaingia muda wowote kwa ajili ya kuja kumfanyia upasuaji” akasema Peniela
“ hakuna haja tena ya hao madaktari.Tumekuja na madaktari bingwa wawili kwa ajili tu ya kuja kuangalia ukubwa wa tatizo la John na kumpatia tiba.John anatakiwa kupatiwa tiba toka kwa madaktari wanaotambuliwa na Team SC41 .Usijali atapona tu” akasema Nickson na safari ikaendelea kimya kimya
“watuhawa wanataka kuisuka upya Team SC41 ili iwe na nguvu kama zamani Wakati nikiwa katika mikakati ya kuisambaratisha.Nimekwisha azimia kulifanya hilo na lazima nihakikishe linafanikiwa.Halafu kuna kitu nimekikumbuka kuhusiana na mauaji ya Dr Burke na Osmund.Nina hakika kabisa John alihusika katika vifo vya Dr Burke na osmund.Hawa jamaa wakifanya uchunguzi wao na kugundua kwamba John alishiriki sijui watafanya nini,nahisi wanaweza hata wakamuua.” Akawaza peniela huku safari ikiendelea.
Josh alimtaarifu kwamba kila kitu kuhusiana na mahala pakufikia wageni wale kilikuwa kimekamilika,Peniela akawapeleka kwanza hotelini kila mmoja akapata chumba chake halafu wakaondoka tena kuelekea nyumbani kwa John Mwaulaya ambako walipokelewa na Josh na moja kwa moja wakapelekwa chumbani kwa John mwaulaya ambaye alifurahi kuonana tena na watu wale baada ya muda mrefu.Kisha salimiana wote wakatoka na kuelekea katika sebule ya John Mwaulaya kwa ajili ya maongezi.Nickson ndiye aliyeongoza kikao kile kifupi
“ Peniela ,Josh,Jacob na Francis,kwa niaba ya wenzangu wote napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa mapokezi yenu mazuri.Sina haja ya kurudia kujitambulisha tena kwani tayari sote mnatufahamu kwa hiyo basi nitakwenda moja kwa moja katika mambo makuu yaliyotuleta hapa.’ Akasema Nickson
“ jambo kubwa la kwanza lililotuleta hapa ni kuhusiana na operesheni 26B.Hii ni operesheni muhimu sana kwetu kwa hiyo tmelazimika kuja na kuifuatilia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kwamba inakwenda kama inavyotakiwa na inakamilika.Tulimpa maelekezo Osmund kwamba ndani ya mwezi huu tunatakiwa tuwe tumeikamilisha operesheni hii na kuipata package hiyo muhimu sana kwa marekani na dunia kwa ujumla.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari ni kwamba mawasiliano kati ya Dr joshua na wanunuzi wa package hiyo yamekwisha anza na muda wowote wanaweza wakafikia makubaliano.Tayari akaunti za benki zimekwisha funguliwa ambako wanunuzi hao wanatakiwa kuweka kiasi kikubwa sana cha fedha na kisha watakabidhiwa mzigo wao.Kwa gharama zozote zile hatutaki jambo hili litokee kwa hiyo lazima tuhakikishe tunaipata hiyo package.kwa hiyo nahitaji kusikia toka kwenu mmefikia wapi hadi hivi sasa? Akauliza Nickson
“ Nadhani peniela anaweza akajibu vizuri zaidi swali lako kwani yeye ndiye kiongozi mkuu katika operesheni 26B” akasema Josh
“ Ni kweli kama alivyosema Josh.Mimi ndiye niliyekabidhiwa jukumu la kuhakikisha kwamba tunaipata pachage hiyo_Operesheni hii ilisimama kwa muda wa kama mwaka mmoja hivi baada ya mimi kuingia matatizoni lakini baada ya matatizo kumalizika operesheni imeendelea tena na ninapenda kukuthibitishia kwamba tumepiga hatua kubwa tayari.Ili kujiweka katika hatua nzuri ya kuipata package hiyo tayari nimejenga uhusiano wa kimapenzi na rais Dr Joshua pamoja na katibu wake .Vilevile tunaye captain Amos.Huyu ni mshirika mkubwa wa rais katika bashara hii na yeye ndiye ambaye ananipa taarifa za kila kinachoendelea kwa hiyo ushirikiano baina yetu ni mkubwa na tunachoshubiri kwa sasa ni siku ambayo package hiyo itatolewa ikulu kisha tuichukue.” Akasema peniela
“ Hongera sana peniela.Umefanya kazi kubwa na nzuri.Sisi tutakuwa nyuma yako kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri.Tutapata wasaa mzuri wa kujadili kwa upana kuhusiana na namna bora tunavyoweza kulikamilisha jambo hili hapo baadae.”akasema Nickson.
“ Nickson kuna jambo nataka kuuliza .Hiyo package ina nini ndani yake? Nimeyatoa mhanga maisha yangu kwa ajili ya kitu ambacho sikifahamu.Nadhani ni wakati mzuri sasa wa mimi kufahamu kitu ambacho nimekuwa nikihangaikia kwa muda huu mrefu ni kitu gani hasa.” Akauliza peniela
“ peniela wewe ni teamSC41 na ukiwa ndani ya kikundi hiki unakuwa ni kama askari mpambanaji,ukiambiwa fanya kitu Fulani basi unakifanya bila kuhoji.Sintaweza kukueleza kwa sasa kwani ni nje ya taratibu za team SC41.Una swali lingine?”akasema Nickson.Peniela akatingisha kichwa ishara kwamba hana tena swakli lingine lakini moyoni alikuwa amekasirika sana
“ Tuendelee.Jambo la pili lililotuleta hapa ni kuhusiana na afya ya John Mwaula.Kama mnavyofahamu ni kwamba John Mwaulaya hawezi kutibiwa katika hospitali za serikali wala haruhusiwi kuonekana nchini marekani kwa hiyo anatakiwa kutibiwa na madaktari walio ndani ya team SC41 pekee na ndiyo maana katika ujio huu tumeambatana na madaktari bingwa wawili wa mambo ya mishipa ya fahamu na kazi iliyowaleta hapa ni kumuhudumia John.”akasema Nickson
“ jambo la tatu ambalo tutalifanya tukiwa hapa ni kuhakikisha Team SC41 inasukwa upya na inarejea kuwa na nguvu kama zamani kabla John hajaanza kuumwa na jambo la mwisho kabisa tutahakikisha mwili wa Dr Burke unarejeshwa nyumbani kwa mazishi.Hayo ndiyo mambo ambayo tuyafanya katika kipindi ambacho tutakuwa hapa Dar es salaam.” Akasema Nickson.Sebule yote ilikuwa kimya.Nickson akaendelea
“ Nadhani mpaka hapo tumeelewana kwa hiyo kinachofuata sasa hivi sote tutaelekea kupata chakula cha mchana na baada ya hapo madaktari watarejea hapa kwa ajili ya kuanza kumfanyia John uchunguzi na wengine tutaelekea katika ofisi kuu ya team SC41 Tanzania tutasalimiana na watu wote pale na shughuli itaanzia hapo.Tukisha pata chakula cha mchana madaktari watarejea hapa ili waendelee kumfanyia uchunguzi John wakati sisi tukiendelea na kazi nyingine.Ninachoomba toka kwenu ni ushirikiano wenu mkubwa kwani bila ninyi hakuna tutakachoweza kukifanikisha.Kipindi hiki kifupi tutafanya kazi usiku na mchana hadi tuhakikishe kwamba tumefanikisha mambo yote.” Akasema Nickson
“ Nickson ninashukuru sana kwa ujio wenu huu ambao utakuwa na faida sana kwetu sote na team SC41.Ninashukuru sana kwa kuwaleta madaktari kwa ajili ya kuangalia afya ya John.Kwa kuwa jioni ya leo tutakuwa pia na kikao kikubwa kujadili kwa upana kuhusu mambo haya yote hususan operesheni 26B basi kwa mchana huu sintaweza kupambatana nanyi kuna jambo la muhimu na kwenda kulishughulikia ambalo linahusiana pia na operesheni yetu.Jacob na Francis watawapeleka katika ofisi kuu na mtakutana na watu wengine wote huko” akasema Peniela.
“ sawa peniela hakuna tatizo.Tutaonana jioni ya leo” akasema Nickson kisha wakaagana na kuondoka na kuwaacha Josh na peniela
“ Kazi imeanza.Wiki hii itakuwa ni wiki ngumu sana kwa Team SC41.Mambo mengi yatafanyika ndani ya wiki hii” akasema Josh,Peniela akamtazama kwa makini na kusema
“ Josh kuna kitu nataka kukuuliza na tafadhali naomba unipe jibu la kweli” akasema Peniela
“ Uliza chochote Peniela nakuahidi nitakueleza ukweli” akasema Josh.Peniela akamtazama na kuuliza
“ nani alimuua Dr Burke na Osmund?
Swali lile likamstua sana Josh.Alibabaika akasindwa ajibu nini
“ Naomba unijibu Josh.Nani alimuua Osmund na Dr Burke? Uko karibu sana na John muda wote na John hakuwa akimtaka kabisa Dr Burke aje na nina hakika ni yeye ndiye aliyetoa amri Dr Burke auawe .Kwa kuwa yeye hawezi kuifanya kazi hiyo lazima alimtuma mtu toka ndani ya team SC41.Niambie nani alifanya mauaji yale? Nina hakika unafahamu.” akasema Peniela.
“ Kwani kuna nini Peniela? Dr Burke na Osmund wamekwisha fariki na suala hili liko mikononi mwa polisi wakilifanyia uchunguzi”
“ Unawaona watu hawa waliokuja? Tayari wamehisi kwamba kuna mtu ndani ya Team SC41 ndiye aliyefanya mauaji yale na wanaanza uchunguzi wao mara moja na nina hakika lazima watampata na wakimjua nadhani unafahamu kitu watakachomfanyia.Josh kama unamfahamu mtu aliyefanya mauaji yale tafadhali nieleze” akasema Peniela.Sura ya Josh ilibadilika na alionekana kuogopa sana..
“ Peniela its me” akasema Josh.Peniela akamuangalia kwa mshangao mkubwa.
“ katika watu wote sikutegemea kama ni wewe ambaye unaweza ukafanya kitendo hiki” akasema peniela
“ Peniela nilifanya kwa kuwa John aliniomba nifanye.Siku zote nimekuwa mtiifu kwa John na hata aliponituma nikaifanye kazi hii sikusita kufanya hivyo.John alidai kwamba Dr Burke alikuwa na lengo la kumuua na tulitakiwa kumuwahi.Kama tusingemuwahi Burke basi angemuua John.Tafadhali Peniela kama kuna lolote unaloweza kunisaidia katika hili naomba unisaidie” akasema Josh.Peniela akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Kwa kuwa ni John ndiye aliyekutuma nitakusaidia,tutatafuta namna ya kuweza kulitatua jambo hili.” Akasema Peniela.
*****
“Lazima leo nionane uso kwa uso na John mwaulaya.Lazima ukweli kuhusiana na Peniela ujulikane leo.Jason anapafahamu nyumbani kwa John kwani ndiko alipelekwa siku aliyotekwa”akawaza Mathew baaad ya kutoka katika kituo cha kulele watoto yatima alikolelewa Peniela.Akachukua simu akampigia Jason.
“ habari za asubuhi Jason” akasema Mathew baada ya Jason kupokea simu
“ habari nzuri sana Mathew.Habari za toka jana? Akauliza Jason
“ habari nzuri Jason.Uko wapi mida hii?
“ kwa sasa niko ofisini kwangu.”
“ Jason nahitaji kuonana nawe.Nielekeze mahala ofisi yako ilipo ili nikufuate hapo” akasema Mathew na Jason akamuelekeza mahala iliko ofisi yake .
“Kwa mara ya kwanza bada ya miaka mingi hatimaye nakwenda kukutana ana kwa ana na John Mwaulaya mtu ambaye aliiteketeza familia yangu.Kwa leo sintamfanya lolote kwani ninakwenda kwa ajili ya suala la Peniela lakini safari nyingine nitamfuata rasmi kwa ajili yangu na ninahisi huo utakuwa ndio mwisho wake.Kwa kumpa salamu tu,leo lazima aeleze ukweli wote kuhusiana na Peniela.Wakati ule John ndiye aliyekuwa na nguvu na kunifanya hadi nikaikimbia nchi yangu lakini safari hii mambo yamebadilika na mimi ndiye mwenye nguvu kuliko yeye.He will talk “ akawaza Mathew na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni rafiki yake wa kutoka nchini Israel ambaye alimtumia zile karatasi zilizoibwa ikulu zilizokuwa zimeandikwa fomula za kisayansi
“ hallow Yash “ akasema Mathew
“ Mathew habari za Dar es salaam?
“ habari za huku nzuri sana .habari za huko?
“ Hata huku kwema tu” akajibu yash
“ Mathew tayari nimeikamilisha ile kazi uliyoniomba nikusaidie.Samahani imechukua muda kidogo lakini ilinilazimu kukutana na wanasayansi wakubwa ili kuweza kutambua kilichoandikwa katika zile karatasi.Nimekutumia kila kitu katika anuani yako ya barua pepe utasoma na kuelewa kila kitu”akasema Yash
“ Ahsante sana yash kwa msaada wako mkubwa.” Akajibu Mathew
“ Mathew karatasi zile umezitoa wapi? Akauliza Yash
“ Kuna jambo nalichunguza kwa sasa na ndani ya uchunguzi huo nikazipata karatasi hizo.Kwa nini umeuliza hivyo Yash?
“ nimeuliza hivyo kwa sababu ya ukubwa wa kitu kilichoandikwa ndani ya zile karatasi.Kama ni kitu hicho kipo kweli basi ni kitu cha hatari kubwa sana lakini kama hakipo basi karatasi hizo ni za kutunza sana kwani ni hatari mno na sijui zimefikaje huko.”
“ unaweza ukanipa japo kwa ufupi ni kitu gani hicho ? Akauliza Mathew
“ Nimekufafanulia kila kitu katika barua pepe niliyokutumia.” Akasema Yash
“ Ahsante sana Yash”
“ Mathew ,nitakupigia tena simu jioni ili tuongee vizuri zaidi” akasema Yash na kukata simu
“ Nini kimeandikwa katika zile karatasi kiasi hata cha kumstua Yash ? Lazima kitakuwa ni kitu kikubwa na kizito na ndiyo maana akina Edson walitaka kuziuza kwa mabilioni ya pesa” Akawaza Mathew akiwa njiani kuelekea ofisini kwa Jason
Aliwasili katika ofisi za Jason wakasalimiana na bila kupoteza wakati Mathew akauliza
“ Jason unaweza kupakumbuka nyumbani kwa John Mwaulaya ulikopelekwa siku ile”
“ Ndiyo ninapakumbuka.” Akajibu Jason
“ Ninaomba unipeleke” akasema Mathew
“unataka kwenda nyumbani kwa John mwaulaya? Jason akashangaa
“ Ndiyo nataka kwenda kuonana na John Mwaulaya.Kuna mambo ambayo anatakiwa kuyaweka wazi kuhusiana na Peniela”
“ mambo gani hayo Mathew? John ni mgonjwa unadhani anaweza akakueleza chochote kwa hali aliyonayo ? akauliza Jason
“ He will talk.Take me there” akasema Mathew.Jason huku akiwa na wasi wasi akavaa koti lake na kutoka wakaingia katika gari la Mathew na kuondoka kuelekea nyumbani kwa John Mwaulaya.Safari ilitawaliwa na maongezi machache sana hadi walipofika katika jumba la John mwaulaya.
“ Hapa ndipo nyumbani kwa John mwaulaya” akasema Jason
“ Wow ! jumba kubwa na la kifahari.Hawa watu ni kweli wanalipwa pesa nyingi sana kama alivyosema peniela.” Akasema Mathew na kisha akasimamisha gari katika geti .
“ Shuka kabonyeze kengele “ akasema Mathew.Jason akashuka na kwenda getini akabonyeza kengele mara tatu halafu akasuburi.Baada ya dakika tano mlango wa geti ukafunguliwa .Aliyeufungua alikuwa ni Josh ambaye alipatwa na mstuko mkubwa alipoonana uso kwa uso na Jason.Kwa sekunde kadhaa walibaki wanatazamana.
“ Jason !!..akasema Josh
“ What brings you here? Akauliza Josh.Jason akafumbua mdomo kutaka kusema kitu lakini akasita baada ya kusikia mlango wa gari unafunguliwa hakujibu kitu akageuka baada ya kusikia mlango wa gari ukifunguliwa,akashuka Mathew.Josh alimtazama vizuri sana na kuikumbuka ile sura.Ni yule mtu aliyeonekana katika kamera za nyumbani kwa Peniela.Akaingiwa na woga
“ hallow “ akasema Mathew
“ Josh .Naitwa Josh “ akasema Josh na kumpa mkono Mathew
“ Josh naitwa Mathew” akasema Mathew
“ Karibuni sana.Niwasidie nini? akauliza Josh
“ Nahitaji kuonana na John Mwaulaya.”
“ John Mwaulaya? Nani kawaambia John anaishi hapa? Akauliza Josh
“ Josh naomba usinipotezee muda wangu.Utatupeleka kwa John mwaulaya au nitumie nguvu? Akasema Mathew huku akipeleka mkono mahala iliko bastora yake.Josh akaogopa akafungua geti Mathew akamwambia Jason aingize gari ndani .Jason akalitambua gari la Peniela lililokuwamo mle ndani.
“ Peniela yuko hapa? Akauliza Jason
“ Ndiyo yupo”akajibu Josh
“ Ok vizuri sana.Tupeleke aliko John” akasema Mathew na Josh akaanza kuwapandisha ghorofani kilipo chumba cha John mwaulaya.Ndani ya chumba cha John alikuwemo Peniela na Dr martin ambaye amekuwa akimuhudumia John mwaulaya kwa muda mrefu.Mlango ukafunguliwa akaingia Josh akiwa amefuatana na Mathew na Jason.Wote mle chumbani wakastuka sana.
“ Mathew ! Jason !..akasema peniela kwa mshangao na kumfanya John Mwaulaya ageuze shingo yake na kutazama mlangoni.
“ mungu wangu ! akasema John mwaulaya kwa sauti ndogo .Naye pia alikuwa ameogopa sana.Mathew akasogea hadi karibu na kitanda cha John Mwaulaya akamtazama kwa macho makali sana.Peniela akaogopa
“ John mwaulaya,hatimaye tumeonana tena uso kwa uso .” akasema Mathew
“ Mathew what are you doing here? Akauliza Peniela
“ peniela nimekuja kuonana na John Mwaulaya.Nimefurahi sana kukukuta na wewe hapa ili usikie kile ambacho ninataka John akieleze mbele yako”
“ Mathew ,John is sick and he cant talk” akasema Peniela kwa wasi wasi.
“ he will talk” akasema Mathew.
“ Mathew !!..what are you doing? Akasema peniela huku akipiga hatua kumuendea Mathew.Jason akamzuia.
“ John mwaulaya,japokuwa imepita mika ming lakini nina hakika sura hii bado unaikumbuka vizuri sana.kama umeisahau nitakuja siku nyingine kukukumbusha lakini kwa leo nimekuja kwa ajili ya jambo moja tu, Peniela.” Akasema Mathew na kumstua kidogo Peniela.John mwaulaya alikuwa anatetemeka.
“ Ulimpeleka Peniela usiku katika kituo cha kulelea watoto yatima na ukadai kwamba umemchukua toka kwa mama yake na ukataka alelewe pale.Ulimwambia mama mwenye kile kituo kwamba peniela ni mwanao lakini hukutaka afahamu kama wewe ni baba yake na badala yake ukajiita mfadhili wake.Umemfanyia Peniela mambo mengi mabaya na kuyaharibu kabisa maisha yake,umemuingiza katika Team SC41 na umezifuta kabisa ndoto za maisha yake na mmekuwa mkimtumia kwa kazi zenu kwa manufaa ya serikali ya marekani.Ninataka mbele ya Peniela uungame ukweli wewe ni baba yake mzazi? Akauliza Mathew kwa ukali.Peniela alipigwa na butwaa asiamini kile alichokisikia .Akamkazia macho John mwaulaya kusikia atatoa jibu gani.
“ John answer me!!..akafoka Mathew
“ Sifahamu chochote juu ya hayo unayoyasema” akasema John kwa sauti ndogo.
“ John nitazame vizuri machoni.Nina uhakika na ninachokisema na sina utani hata kidogo.” Akasema Mathew na kumuinamia John
“ John nitazame vizuri machoni.I’m a monster kwa hiyo naomba usiniudhi.Nataka useme ukweli kwamba wewe ni baba yake mzazi Peniela? Akasema kwa ukali Mathew
“ I don’t know anything” akajibu John kwa sauti ndogo .
“ John this is the last chance ..are you Peniela’s father? Akauliza Mathew kwa ukali.John akajibu kwa kumfanyia ishara kwamba haelewi chochote.Mathew akakasirika na kuchomoa bastora yake.Peniela akaogopa sana
“ Mathew what are yo doing? Akauliza lakini Mathew hakumjali
“ Mathew unataka kufanya nini? Akauliza Peniela kwa wasi wasi
“ I’ll count to three and if you cant answer me I’m going to kill you John ! akasema kwa ukali Mathew
“ Mathew No ! Don’t do that !! akasema Peniela huku akilia
“ Jason hold her” Mathew akamuamuru Jason amshike Peniela ili asimsogelee.
“ Three…..!!!akaanza kuhesabu Mathew huku amemuelekezea John bastora
“ Two ….!!!!
“ Mathew noo!!!!..dont do that !!..akapiga kelele peniela.
“ On………..” Kabla Mathew hajamaliza kutamka John Mwaulaya akasema
“ Ok ok..I’ll tell you..put your gun down” akasema John mwaulaya aliyekuwa akitetemeka
“ ok tell her the truth! akasema kwa ukali Mathew huku akimtazma John kwa macho ya hasira
John akamfanyia ishara peniela asogee karibu na kuanza kumsimulia kilichotokea kuhusiana na wazazi wake.Alisimulia mkasa mzima uliotokea na kupelekea kuwaua wazazi wote wa peniela.Peniela alibubujkwa na machozi mengi.John akamgeukia Mathew
“ Hiyo ndiyo historia ya Peniela.Nilishindwa kabisa namna ya kumueleza nikiogopa kumuumiza na ndiyo maana nilitaka afahamu kuhusu yeye baada ya mimi kufariki dunia.Nilijua lazima atanichukia sana akifahamu kwamba mimi ndiye niliyewaua wazazi wake.Nilimuwekea kila kitu kuhusiana na historia yake katika makasha matatu ikiwamo na picha za wazazi wake.” Akasema John.Peniela alimuangalia kwa hasira huu machozi yakimtoka.
“Leo nilikuja kwa ajili ya Peniela.Safari ijayo nitakuja rasmi kwa ajili yangu.Jiandae “ akasema Mathew na kutoka Peniela akamfuata
“ Mathew thank you so much.Umenisaidia nimefahamu jambo kubwa sana.Sikuwa nikifahamu chochote kuhusiana na wazazi wangu.John amenificha siri hii kwa miaka mingi.I hate that bastard so much.”akasema Peniela
“ Elibariki aliniomba nikusaidie kuufahamu ukweli kuhusiana na asili yako na ninashukuru ukweli umedhihiri.Naomba ukweli huu usivuruge mipango yetu.”
“hakuna kitakachovurugika Mathew.I’m a very strong woman.Kila kitu kitakwenda kama tulivyokipanga.hata hivyo nina swali nataka kukuuliza.”
“ Uliza Peniela”
“ Ulipomuelekezea John bastora na kuanza kuhesabu,ulidhamiria kumpiga risasi kama asingesema chochote ?
Mathew akatabamu kidogo na kusema
“ No ! I just wanted him to talk”
“ ahsante Mathew.Ahsante sana.Tutaonana jioni .Mwambie Elibariki nashukuru sana kwa kunijali.Bila yeye kuwa na mawazo haya nisingeufahamu ukweli kuhusu wazazi wangu“ akasema peniela na kurejea tena ndani akakuta hali ya John mwaulaya imebadilika ghafla.Ikawalazimu wawaite haraka wale madaktari wawili waliokuja toka marekani kwa lengo la kuja kuangalia afya yake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MCHAKATO WA KUIPATA PACKAGE MUHIMU UMESHIKA KASI NA KILA UPANDE UNAJIANDAA KUIPATA NINI KITATOKEA ? FLAVIANA MKE WA JAJI ELIBARIKI BADO YUKO MAHUTUTI HOSPITALI NINI HATIMA YAKE? NINI HATIMA YA JOHN MWAULAYA? KIKUNDI KIDOGO CHA WATU WENYE NGUVU NA USHAWISHI KIKIONGOZWA NA RAIS MSTAAFU KINAPANGA KUMUONDOA MADARAKANI DR JOSHUA NA WANAFIKIRIA KUMPENDEKEZA JAJI ELIBARIKI KUWANIA NAFASI HIYO JE WATAFANIKIWA LENGO LAO ? MWISHO WA SIMULIZI YA PENIELA SEASON 2..TUKUTANE TENA KATIA SEASON 3 HIVI KARIBUNI
MWISHO
0 comments:
Post a Comment