Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

I DIED TO SAVE THE PRESIDENT - 5

 





    Simulizi : I Died To Save The President

    Sehemu Ya Tano (5)



    I DIED TO SAVE MY PRESIDENT







    Najaribu kutafakari dhamira ya wanasiasa hawa kulazimisha mkutano wao ufanyike wakati jeshi la polisi limeupiga marufuku?Endapo mkutano huo utafanyika ni wazi kutazuka vurugu kati ya wafuasi wao na jeshi la polisi na kila mara kunapotokea vurugu kati ya polisi na wafuasi wa vyama vya siasa lazima maisha ya watu kadhaa yapotee kwani hufika mahala ambapo polisi hulazimika kutumia nguvu kubwa zaidi baada ya wafuasi hao kugoma kutii amri." Akawaza Elvis halafu mara jambo likamjia akilini "Kuna wazo linanijia.Yawezekana labda dhana ya wanasiasa hawa ni kulazimisha kufanyika kwa mkutano usio kuwa na kibali wakiamini kabisa kwamba kutatokea vurugu kwani lazima jeshi la polisi liwatawanye wafuasi wao na kitokea vurugukunaweza kutokea vifo na majeruhi na hii inaleta sifa mbaya kwa serikali kwamba inakandamiza demokrasia na kuua raia wake.Sioni kama kuna lengo lingine zaidi ya hilo kwa wanasiasa hawa kulazimisha kufanyika kwa mkutano wao leo licha ya kupigwa marukufu na jeshi la polisi.Ninahisi kwamba hizi ni njama chafu za David na washirika wake za kutaka kuichafua serikali iliyoko madarakani ionekane haifai na utakapofika wakati wa uchaguzi basi agombee urais kwa tiketi ya chama cha upinzani.Kwa David inawezakana lengo lake likawa hilo lakini vipi kuhusu Dr Shafi?Yeye ana ajenda gani?Kwa nini ashirikiane kwa siri na David na hawa wanasiasa?Yawezekana kuna zaidi ya ninavyofikiri.Tutapata jibu baada ya kufanya uchung....." Graca akaingia pale sebuleni akiwa na glasi ya juisi akamuweka Elvis mezani "Elvis my love karibu kinywaji." akasema Graca huku akimsugua sugua Elvis mgongoni "Ahsante sana Graca.Umekuwa ni msaada mkubwa kwetu" akasema Elvis "Usijali Elvis.Nina furahi na mimi kuwa na mchango wangu hata mdogo katika jambo hili" akasema Graca na kumbusu Elvis akaanza kumpapasa kifuani "Graca not now" akasema Elvis "Elvis you have to relax.Umekuwa ukifanya kazi mfululizo toka jana usiku na inakulazimu upumzike.Mwili nao unahitaji mapumziko ili uweze kuhimili mikiki mikiki hii inayoendelea" Graca hatuna muda wa kupumzika kwani watu tunaowatafuta hawapumziki hata kidogo.Kila dakika wako kazini wakihakikisha kwamba hatufanikiwi .Hatuwezi kuwapa nafasi hata ndogo wakafanikiwa kutoroka kwani tayari tumepiga hatua kubwa.Tayari tumefanikiwa kuwafahamu vinara wakubwa wa biashara hii ya silaha na tayari tunafahamu mahala zinakotoka na namna zinavyosafirishwa.Bado tunaendelea kufanya uchunguzi kuubaini mtandao huu wote.Tunahisi bado kuna watu wengine wakubwa ambao hatujawabaini lakini kwa mwendo tunaokwenda nao tutawabaini wote.Mafanikio haya yote yametokana na wewe" "Ni furaha kubwa kusikia kuhusu mafanikio hayo makubwa mliyoyafikia.Ninawaombea muweze kulimaliza salama suala hili.Mimi niko tayari kwa msaada wowote ule muda wowote ule nitakapohitajika kufanya hivyo"akasema Graca "Endelea na shughuli zako ninakwenda kumuangalia Winnie" akasema Elvis na kwenda katika chumba alimo Winnie "Winnie"akaita Elvis na Winnie akafumbua macho.Tayari alikwisha amka.Elvis akamsogelea karibu zaidi "Unajisikiaje sasa hivi? "Nina maumivu makali kichwani na mwili wote unauma.Where am I? akauliza Winnie "Usiogope uko sehemu salama.Tumekutoa katika hatari" akasema Elvis na Winnie akataka kuinuka lakini akauma meno kwa maumivu Elvis akamsogelea na kumsaidia kuinuka akakaa kitandani.Akamtazama Elvis na machozi yakaanza kumtoka "Nyamaza kulia Winnie.Uko sehemu salama"akasema Elvis "I'm sorry...I'm very sorry!! Elvis akakaa kitandani akamshika Winnie mkono "Usilie Winnie.Nieleze tafadhali nini kilitokea?Kwa nini uliondoka? Wale jamaa wamekupataje? akauliza Elvis na Winnie akaendelea kulia "Nieleze tafadhali"akasema Elvis lakini bado Winnie aliendelea kulia.Elvis akatoka akaelekea jikoni na kurejea na bakuli la supu akakaa kitandani na kumnywesha Winnie ambaye alionekana kuwa na njaa.Alihakikisha amekunywa supu yote "Haya nieleze nini kilitokea?Kwa nini ukaamua kuhatarisha maisha yako wakati tulikwishakueleza kwamba huko nje ni hatari kuna watu wanawatafuta?Elvis akauliza "Samahani sana.Dada yangu yuko wapi? "Vicky aliondoka asubuhi na hajarejea tena hadi mida hii.Hakuaga mtu na hatujui mahala aliko" akasema Elvis na Winnie akastuka sana akaweka mikono kichwani "Oh my God Elvis,find my sister.She's in danger!! "In danger?How do you know she's in danger? akauliza Elvis "I'm sorry Elvis kwa hiki nitakachokueleza.Nilijipeleka mwenyewe kwa Frank" "What ?!!! "I'm sorry Elvis I wanted to save my sister"akasema Winnie na kuanza kulia "Relax Winnie .Nieleze kila kitu" Winnie akamueleza Elvis kila kitu alichokifanya.Elvis akavuta pumzi ndefu "Kwa nini ulifanya vile Winnie?kwa nini hukusikia kile tulichokueleza?Huoni kwamba kwa kufanya hivyo umehatarisha maisha yetu na hata dada yako maisha yake umeyaweka hatarini? akauliza Elvis "I'm sorry Elvis.Nilidhani kwa njia ile nitamsaidia dada yangu aweze kuachana na kazi hii.Sikujua kama wale jamaa ni wabaya kiasi kile" "Umefanya kosa kubwa sana Winnie.Nataka kufahamu kitu kimoja,wakati mnazungumza ulinitaja hata mara moja kwa jina? akauliza Elvis na Winnie akaonekana kuogopa kujibu "Nijibu Winnie ni muhimu sana kwangu kujua" Winnie akatikisa kichwa kukubali,Elvis akasimama "I'm sorry Elvis" akasema Winnie "It's ok Winnie dont cry.Nataka nikueleze kwamba ulichokifanya hakikuwa sahihi na umeongeza matatizo badala ya kuyapunguza.Watu wale uliokwenda kuonana nao si watu wazuri hata kidogo.Ni watu makatili na wasio na utu.Sisi na dada yako tuko katika operesheni ya kuwatafuta na kuwafikisha katika sheria kwani wanajihusisha na biashara haramu ya silaha.Wanawauzia silaha waasi wanaoua watu huko mashariki mwa Congo.Tunataka tuufute kabisa mtandao wao.Watu hawa baada ya kufahamu kuwa tumewagundua walitaka kuniua na ikanilazimu kughushi kifo changu na hivi sasa wanaamini kuwa nimekufa.Nimefanya hivi ili niweze kupata nafsi nzuri zaidi ya kuufahamu mtandao wao na kuwafagia wote.Kitendo cha kufahamu kuwa niko hai kitavuruga kila kitu kwani watajificha na nitashindwa kufanikisha uchunguzi wangu" "I'm sorry Elvis..I'm real very sorry" akasema Winnie.Chumba kikawa kimya.Elvis alionekana kuzama mawazoni.Akatafakari halafu akamgeukia Winnie "Unahisi dada yako atakuwa wapi? "Sina hakika lakini yawezekana akawa katika hatari.Tafadhali Elvis nisaidieni kumtafuta dada yangu" akasema huku machozi yakiendelea kumtoka. "Ok.Let me see what we can do to find her.Endelea kupumzika" akasema Elvis na kutoka mle chumbani.Alihisi kuchanganyikiwa Kwa hili alilolifanya Winnie anastahili hata kukatwa kichwa.Kwa nini akafanya vile na kurudisha nyuma kile tulichojitolea maisha yetu kukipigania?Kwa maelezo aliyowapa akina Frank ni wazi hivi sasa watakuwa na mashaka kama kweli nimefariki dunia.Hii itafanya kazi yetu iwe ngumu wakati tumekwisha fika hatua nzuri." akawaza akielekea chumbani kwake "Ngoja niwasubiri akina Steve wareje tujue namna ya kufanya kwani tayari huyu Winnie ameharibu kila kitu.Natamani nikamchape vibao lakini haitasaidia kitu.Kilichopo hapa ni kutafuta namna ya kuendelea na operesheni yetu licha ya huyu limbukeni kuharibu kila kitu" akawaza Elvis na kukaa kitandani akaweka mikono kichwani akazama mawazoni ******************* Frank aliwasili nyumbani kwa Elizabeth.Hali iliyokuwapo mahala hapa ni kama vile hakukuwa na msiba.Watu hawakuwa wengi kama ilivyozoeleka mahala kunapokuwa na msiba.Walikuwepo ndugu wachache na wengine ni wafanyabiashara marafiki wa familia wa hapa nchini na wengine wa kutoka nje ya nchi.Waombolezaji wote walikuwa wamekaa katika bustani kubwa na nzuri na huko kila kitu kilipatikana.Kulikuwa na vyakula na vinywaji vya kila aina.Watu walikuwa wakila na kunywa kama vile hakuna jambo la huzuni linaloendelea . Frank alipofika akapokewa na walinzi na kuelekzwa sehemu ya kuegesha na aliposhuka tu akakutana na mwanadada maalum ambaye kazi yake ilikuwa ni kuwapokea wageni waliokuwa wakifika pale msibani na kuwaelekeza sehemu za kuketi "Poleni sana" akasema Frank baada ya kushuka garini na kupokewa na mwanadada yule aliyekuwa amevalia gauni refu jeusi lililomkaa vyema "Tunashukuru sana mzee" akasema Yule mwanadada ambaye kila alipotabasamu vishimo vilionekana katika mashavu yake.Akamuelekeza sehemu ya kwenda kuketi lakini kabla hajaelekea huko Frank akasema "Ninahitaji kuonana na madam Elizabeth.Yuko sehemu gani? Yule mwanadada akampeleka mahala waliko waombolezaji wengine halafu akaenda kumjulisha Elizabeth kuhusu Frank.Elizabeth akawaomba radhi watu aliokuwa amekaa nao akaongozana na yule mwanadada hadi mahala alikokaa Frank.Elizabeh akamtaka amfuate wakaelekea ndani "Karibu Frank"akasema Elizabeth wakiwa katika chumba cha mazungumzo. "Madam utanisamehe sana kwa kuja mida hii lakini imenilazimu nije kutokana na suala la dharura lililotokea" akasema Frank "Nini kimetokea Frank? "Madam kuna jambo limetokea ambalo naona limevuka mikono yangu na linahitaji nguvu ya ziada kulimaliza." "Nieleze Frank ni jambo lipi?Usiniambie umeharibu tena kwani safari hii sintakusamehe" akasema Elizabeth kwa sauti ya juu kidogo "Jana usiku nilipigiwa simu na binti mmoja akajitambulisha kwamba anaitwa Winnie ni mdogo wake na Vicky" "Bado unaendelea na masuala ya Vicky?Nilikukanya uachane na masuala hayo!!! akasema Elizabeth "Sikuwa naendelea na suala hilo naomba unisikilize madam" "Endelea"akasema Elizabeth "Winnie alinitaka tuonane.Nikamuelekeza sehemu ya kukutana na tulipoonana akanieleza mambo ambayo yalinistua kidogo" "Alikueleza nini?akauliza Elizabeth "Alikuja kuniomba nimsaidie dada yake.Alidai kwamba dada yake hahusiki chochote na kifo cha Pascal.Anasema kwamba kuna watu wawili ambao walimtumia dada yake katika kumuua Pascal.Walifahamu kuwa ana ukaribu na Pascal hivyo wakamtaka amuite pale hotelini na wakatishia kumuua asipofanya hivyo.Vicky akampigia simu Pascal na kumtaka afike pale hotelini na wale jamaa wakamuua" Sura ya Elizabeth ikabadilka kwa maneno yale ya Frank akakunja sura.Frank akaendelea "Winnie anadai kwamba wale jamaa waliwapeleka katika nyumba fulani wakawafungia na Winnie akasikia wale jamaa wakimlazimisha Vicky awapeleke sehemu ambako wanaweza wakanipata na ninahisi lengo lao lilikuwa ni kunimaliza na mimi pia.Walitishia kumuua mdogo wake endapo atakataa na Vicky akashindwa kukataa akakubali kuwapeleka sehemu ambako anaamini wanaweza wakanipata.Usiku huo wakaondoka na kumuacha Winnie hapo katika hiyo nyumba na akafanikiwa kutoroka ndipo aliponitafuta na kunitaka nimsaidie kumuokoa dada yake.Nilimtaka anipeleke katika hiyo nyumba walimokuwa wamefungwa tukaenda huko lakini hatukufanikiwa kukuta mtu.Tukiwa pale nikapata ujumbe katika simu kuwa namba za kufungulia mlango wa ofisi yangu ya siri katika nyumba yangu ya shambani imebadilishwa nikahisi kuna watu wamevamia nikaenda haraka sana na kukuta kweli ofisi yangu imevamiwa na kuvurugwa sana.Sikufanikiwa kuwapata hao jamaa.Nilirejea tena katika ile nyumba lakini hakukuwa na mtu nikalazimika kuwaacha vijana wawili wachunguze nani watakaokuja pale.Niliondoka na Winnie na kumpeleka mafichoni" Frank akanyamaza na kumtazama Elizabeth aliyekuwa amewasha sigara akivuta mfululizo.AkaendeleaAsubuhi ya leo nikapigiwa simu na Vicky akanitaka tuonane.Tulipoonana nikamtaka anieleze wale watu waliomteka ni akina nina wako wapi lakini akakana kutekwa wala kuwafahamu hao jamaa.Nilishangaa kwa kauli zao zinazokinzana ikanilazimu kumchukua Vicky kumpeleka mahala nilikomficha Winnie ili nikaupate ukweli na nilipofika pale nikakuta vijana waliokuwa wanamlinda Winnie wamekufa na Winnie hayupo.Nikiwa hapo nkapigiwa simu na Irene akanitaka nionane naye.Nikaenda kuonana naye na akanieleza kwamba kuna watu wawili walifika nyumbani kwake asubuhi na wakamtisha kwa bastora na kumtaka angozane nao.Walianza kumuhoji kuhusiana na kampuni ya Pendeza na wakaanza kumtesa ikamlazimu kuwaeleza ukweli kwamba kampuni ile ni ya kwangu.Walikuwa na nyaraka tulizotolea mzigo wa mwisho bandarni na wakauliza maswali mengi kuhusiana na mizigo yetu namna tunavyoisafirisha na Irene akawaeleza kila kitu kisha wakamuachia na ndipo aliponipigia simu" Elizabeth akaitupa chini sigara aliyokuwa anaivuta na kuisigina kwa kiatu kisha akamtazama Frank kwa hasira "Frank nimechoka sitaki tena kusikia upuuzi kutoka kwako.Hii ni mara ya mwisho kusikia ukinieleza ujinga unaoendelea kuufanya.Next time I'll shoot you right here!!!..Nina mambo mengi yananikabili kwa sasa hivyo inuka nenda karekebishe makosa yako.Make sure before sunset you find those bastards and kill them.You understand?!! akasema Elizabeth kwa ukali "Madam Elizabeth nimekuja kwako kukueleza na kukuomnba msaada kwa sababu ni suala ambalo limevuka nguvu yangu." "Unashindwaje kuwatafuta hao jamaa?How could you let them enjoy doing what they like?Umekuaje siku hizi Frank?Ukishindwa katika hili hutakuwa unanifaa tena nitatafuta mtu mwingine anayeweza kufanya kazi!! akasema Elizabet na maneno yale yakamkera Frank akasimama "Madama Elizabeth sitaki nikuvnjie heshima lakini nimekuja hapa nina tatizo ambalo linatuhusu sote hivyo nataka unisikilize hadi nitakapomaliza.Jambo hili ninalokueleza ni muhimu sana na endapo utalipuuza we'll all go down so sit there and listen to me" akasemaFrank.Elizabeth akamtazama Frank kwa hasira na kusema "Frank toka lini umeanza kunipa amri?Mapembe hayo yameota http://deusdeditmahunda.blogspot.com/lini?Unafahamu unazungumza na nani?Mimi si kama hao wanawake zenu,mimi ni mtu mwingine tofauti kabisa.Ninaogopwa sana na hata na magenge makubwa ya kimafia.Ninaweza hata sasa nikaamua usitoke tena nje na maisha yako yakaishia humu humu ndani.Dont play with me.Na hii ni nafasi ya mwisho usithubutu tena kuniamuru chochote.Umesikia Frank? akauliza Elizabeth.Frank akapiga magoti na kuomba msamaha "Nisamehe madam Elizabeth sintarudia tena utovu wa nidhamu" akasema Frank "Stand up.Malizia unachotaka kunieleza kisha uondoke.Nina mambo mengi sana ya kufanya.Wakati wangu wa kukutana nawe na kusikiliza upuuzi wako bado haujafika" akasema Elizabeth na Frank akaketi "Nataka unieleze kwa nini hawa jamaa wamekushinda?Hauna nyenzo za kukuwezesha kuwapata? "Madam hukuniacha nimalizie nilichotaka kukueleza.Tuna tatizo madam.Kwa mujibu wa maelezo aliyonipa Winnie ni kwamba moja kati ya watu hao wawili waliokuwa wamewashikilia na ambao ninaamini ndio waliovamia ofisi yangu shambani na ndio waliomteka Irene na kuwaua wale vijana wawili na kumchukua Winnie ni Elvis" "Elvis?!! akauliza Elizabeth kwa mshangao mkubwa "Elvis yupi?Kuna Elvis mwingine ameibuka ukimuacha yule aliyekufa?akaulizaKwa wasifu aliouelezea Winnie,Elvis huyo anafanana sana na Elvis yule aliyekufa.Elvis anafanana na mcheza mpira wa kikapu wa Marekani Stephe curry na hicho ndicho kitu cha kwanza alichokielezea Winnie nilipomuuliza kuhusu huyo Elvis.Kingine ambacho kilinipa tatizo ni pale aliponieleza kwamba mwanangu Graca naye yumo katika hiyo nyumba walimokuwa wamefungwa na hao watu aliowataja kwa majina ya Elvis na Steve.Ukumbuke ni Elvis aliyemtorisha Graca kutoka Afrika kusini kwa hiyo taarifa hiyo ikanipa shida kidogo" "That must be a ghost.That woman isn't telling the truth" akasema Elizabeth "Lakini Winnie hakuonekana kama anadanganya.Nilimtazama machoni na alikuwa anasema kweli"akasema Frank na ukimya ukatanda na Elizabeth akawasha sigara akavuta mikupuo kadhaa,Baada ya dakika mbili akauliza "Are you sure Elvis died? Swali lile likambabaisha kidogo Frank "Answer me Frank" akasema Elizabeth "Elvis alikufa" "Nani alithibitisha? "David alithibitisha hilo na hata mimi na Pascal tulikuwepo msibani na jeneza lenye mwili wa Elvis likaletwa na watu wakatoa heshima zao za mwisho" "You saw him in the coffin? akauliza Elizabeth "I didnt.Waliobahatika kutoa heshima za mwisho ni marafiki na ndugu wachache kwani alikuwa ameumizwa vibaya kwa risasi maeneo ya kichwani hivyo hawakuruusu kila mmoja amuangalie" akasema Frank.Elizabeth akawa kimya kwa muda akatafakari halafu akamgeukia Frank "Ulinieleza kwamba David ndiye aliyeshughulikia mpango mzima wa kumuua Elvis? "Ndiyo madam" akajibu Frank "Nisubiri hapa ninakuja sasa hivi.David tayari yuko hapa" akasema na kutoka akamucha Frank peke yake mle ndani.Baada ya dakika saba Elizabeth akarejea na safari hii akiwa ameongozana na David Sichoma "David nimekuleta hapa ili kwa pamoja tuzungumze suala muhimu sana ambalo limejitokeza na linahitaji kushughulikiwa haraka sana" akasema ElizabethNini kimetokea Madam? akauliza David kwa wasi wasi "Kabla sijakueleza chochote nataka unijibu.Are you sure Elvis died? akauliza Elizabeth na swali lile likamshangaza kidogo David "Yes he died.Why? akauliza David "Are you sure? "Yes I'm sure.Elvis tayari amekufa na kuzikwa.Kuna nini kwani?akauliza David "Ulihakiki kama kweli amekufa? "Frank aliponiomba nimsadie kumuua nilimuomba makamu wa rais anisaidie naye akamkabidhi jukumu hilo mkurugenzi wa idara ya ujasusi Meshack Jumbo na kumtaka ahakikishe Elvis anakufa na ndivyo ilivyokuwa.Elvis akafa na makamu wa rais akajulishwa naye akanijulisha.Nilituma watu wangu kuhakiki kama kweli Elvis amekufa na wakahakiki kweli amekufa na kuzikwa"akasema David "Ahsante David kwa taarifa hiyo na kutuhakikishia kwamba Elvis amekufa lakini kuna taarifa nyingine ambayo amekuja nayo Frank.Elvis ameonekana akiwa hai." "What?!! David akashangaa "That's impossible.Elvis amekwisha kufa na kuzikwa.Anayedai kumuona ameona kivuli chake japo sitaki sana kamini katika mambo hayo.Elvis hataonekana tena" akasema David kwa kujiamini "David pamoja na maelezo hayo uliyoyatoa nataka ufanyike uchunguzi mkubwa kwamba kweli Elvis amekufa?Nataka mtu aliyepewa jukumu la kumuua Elvis apatikane ili tupate uhakika kama kweli Elvis amekufa au vipi" Madam Elizabeth una wasiwasi labda Elvis hakufa? "Ninakuamini sana David lakini siwezi kuzipuuza taarifa za Elvis kuonekana hai.Anza kulishughulikia hilo na mpaka jioni ya leo nataka huyo mkurugenzi wa ujasusi aliyepewa jukumu la kumuua Elvis awe amepatikana na atuthibitishie kwamba kweli Elvis amekufa.Achana na kila unachokifanya nenda kalishughulikie hilo na jioni ya leo nataka majibu" akasema Elizabeth na David akainuka na Elizabeth akamsindikiza nje kisha akarejea ndani "Sasa ni zamu yako.Nataka mpaka jioni ya leo hao watu wawili ambao wanaanza kuonekana kuwa kikwazo kwetu wawe wamepatikana na tuwajue ni akina nani .Mtumie huyo Vicky kupata taarifa muhimu za kuwahusu hao jamaa.Kama mpaka saa kumi na mbili jioni ya leo hautakuwa umefanikiwa kuwapata mimi mwenyewe nitabeba jukumu na nitazungumza na huyo Vicky na asiombe jambo hili lifike huko.Nenda kaanze kazi mara moja na saa kumi na mbili kamili nipigie simu nijulishe umefikia wapi" akasema Elizabeth na Frank akaondoka.Elizabeth akaenda moja kwa moja chumbani kwake akawasha sigara na kuanza kuvuta mfululizo "Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ninahisi uoga kutokana na taarifa za kukinzana kuhusiana na kifo cha Elvis.Ninahisi woga kwa sababu huyu jamaa tayari anafahamu kuhusu biashara ya silaha ambayo Frank anaisimamia na endapo atachimba kwa undani zaidi anaweza akagundua mambo mengine ambayo hatakiwikuyafahamu.Mdogo wake Vicky anadai kwamba Elvis yupo hai na ndiye aliyewateka yeye na dada yake.Vicky yeye anadai kwamba hakuna jambo kama hilo na David naye anathibitisha kuwa Elvis amefariki.Nani kati yao anasema kweli?akawaza na kuvuta mkupuo mkubwa wa sigara "Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akatuthibitshia kuwa Elvis amekufa au vipi naye ni mkurugenzi wa idara ya ujasusi.Kwa mujibu wa David huyu ndiye aliyepewa jukumu la kuhakikisha Elvis anakufa na ndiye aliyemthibitishia makamu wa rais kuwa Elvis amekufa.Huyu lazima apatikane leo hii.Vile vile kuna ulazima wa kumuhoji tena Vicky naa kufahamu kuhusiana na hao watu waliokuwa wamemteka ni akina nani.Jambo lingine ambalo limenistua ni baada ya nyaraka kuibwa ofisini kwa Frank.Watu hawa wakiachiwa watapiga hatua kubwa sana na kuvuruga kila kitu kinachoendelea hivi sasa." akawaza Elizabeth ********************** Kichwa cha David kilijaa mawazo mengi sana baada ya kutoka nyumbani kwa Elizabeth "Kwa nini madam Elizabeth anadhani Elvis hajafariki dunia? Frank kaitoa wapi taarifa hiyo kuwa Elvis yuko hai?Huu si ukweli hata kidogo kwani Elvis tayari amekufa na kuzikwa.Makamu wa rais hawezi kunieleza kitu ambacho hana uhakika nacho.Hata hivyo ngoja nifanye uhakiki kama anavyotaka madam" akawaza David na kuchukua simu akampigia makamuwa rais Dr Shafi "Samahani kwa kukusumbua tena Dr Shafi"akasema David baada ya Dr Shafi kupokea simu "Bila samahani David.karibu" akasema Dr Shafi "Ahsanate sana.Dr Shafi kuna taarifa ambayo nimeipata imenistua kidogo na ndiyo maana nimelazimika kukupigia simu." "Ndiyo David" akasema Dr Shafi "Kuna taarifa za kustusha kidogo zinadai kwamba Elvis ameonekana akiwa hai" "Elvis?!! Dr Shafi akastuka sana "Ndiyo Dr Shafi" "Taarifa hizo zimetoka wapi?Kaonekana wapi na lini? "Kuna mtu ambaye ametoa taarifa hizo kwa mmoja wa washirika wangu kuwa Elvis yuko hai" Thats not true.Elvis amekwisha fariki dunia na hayupo tena duniani.Mimi mwenyewe nilihudhuria mazishi yake na nilikuwa miongoni mwa watu wachache waliofanikia kumuona Elvis akiwa ndani ya jeneza iweje leo aonekane akiwa hai?Hilo haliwezi kutokea David labda huyo aliyetoa taarifa hizo ameona mzimu au mtu aliyefanana na Elvis lakini si Elvis halisi.He's dead"akasema Dr Shafi na David akavuta poumzi ndefu "Dr Shafi utanisamehe kwa hili si kwamba sikuamini lakini unaonaje endapo tutafanya uchunguzi ili kujiridhisha na taarifa hizi kuwa si za kweli?akauliza David "Unataka tufanyaje David?Tufukue kaburi? "Hapana sijamaanisha tufukue kaburi bali tumpate mtu aliyepewa jukumu hilo la kumuua Elvis na atuthibitishie kuwa kweli Elvis amekufa.Mimi na wewe hatuna wasi wasi kuhusu suala hili lakini wenzangu katika umoja wetu wana wasiwasi sana na wanataka uthibitisho kuwa Elvis amekufa.Tukimpata huyu aliyethibitisha kifo cha Elvis atatusaidia kuondoa mkanganyiko huu." "Niliyemkabidhi jukumu la kumuua Elvis ni Meshack Jumbo na ndiye aliyenithibitishia kuwa Elvis amekufa na akanitumia hadi picha za maiti yake.Kwa hiyo unataka tumpate Meshack Jumbo? "Ndiyo Dr Shafi.Tunapaswa kumpata na ili athibitishe kuwa kweli Elvis amekufa" "Hili sasa ni suala lingine.Huyu ni kiongozi mkuu wa idara ya ujasusi na kumpata kwake si kazi nyepesi hata hivyo niachie jambo hili nione namna nitakavyofanya.Nitawatuma vijana kumteka ili isijulikane kuwa ni sisi na kisha atapelekwa mahala pa siri na huko atahojiwa kuhusianana kifo cha Elvis.Kama hatutaupata ukweli basi itatulazimu kufukua kaburi la Elvis na kujiridhisha kama kweli amekufa.Nitawaandaa vijana kuifanya kazi hiyo na pale watakapokuwa tayati nitakujulisha" "Ahsante sana Dr Shafi.Bado ninaendelea kufuatilia hali ya mambo na nitaendelea kukujulisha kila kinachoendelea huku" akasema David na kukata simu Dr Shafi alipomaliza kuzungumza na David simuni akaegemea kiti chake akionekana kuwa na mawazo mengi "Hili jambo limeanza kuchukua sura mpya.Kwa nini wameanza kuhisi kuwa Elvis hajafa?Kaonekana wapi? Sidhani kama suala hili linaweza kuwa limeibuka tu hewani lazima lina msingi wake na halitakiwi kupuuzwa kwani katika dunia ya sasa lolote linawezekana.Atakapopatikana Meshack Jumbo ataeleza ukweli wote" akawaza Dr Shafi ***************** Juliana aliwasili mahala alikopanga kukutana na Steve.Akampigia simu na kumbe tayari Steve alikwisha wasili muda mchache uliopita akamuelekza mahala alipo Juliana akamfuata "Karibu Juliana" akasema Steve ambaye alikuwa ameongozana na Omola "Habari yako dada" akasema Juliana akimsalimu Omola Huyu anaitwa Omola ni mwenzetu anatoka nje ya nchi bado hafahamu kiswahili" akasema Steve "Omola huyu ni Juliana ambaye tumekuja kuonana naye" akasema Steve akianza kutumia lugha ya kiingereza ili Omola aweze kuelewa "Juliana,nafurahi kukufahamu" "Hata mimi nimefurahi kukutana nawe Omola.Karibu sana Tanzania" akasema Juliana "Juliana awali ya yote nikuombe samahani kwa usumbufu huu mkubwa tunaoendelea kukupatia"akasema Steve "Usijali Steve hakuna usumbufu.Muda wowote ule mkihitaji msaada wangu niko tayari kuwasaidia" "Ahsante sana.Kabla hatujakueleza kilichotuleta hapa nataka kufahamu umefikia wapi kuhusiana na ile kazi tuliyokuomba utusaidie? "Baada ya kufika nyumbani nimewasiliana na yule mtu niliyekueleza na akakubali kunisaidia.Kama nilivyokueleza huyu jamaa ni mtu wa karibu sana na mama na anazifahamu siri zake nyingi.Amenieleza kwamba mama anatumia majina mbali mbali katika shughuli zake.Hata yeye mwenyewe halifahamu jina lake halisi kwani mama ana vyeti vya kuzaliwa zaidi ya vitano vyenye majina tofauti na vimetolewa katika nchi tofauti tofauti.Jina Shanon Blank ni moja ya majina yake anayoyatumia katika mambo yake ya biashara nchini marekani.Kila nchi anakowekeza hutumia jina tofauti.Hata pasi za kusafiria anazo zaidi ya kumi za nchi mbali mbali.Hilo ndlio nililofanikiwa kulipata" "Ahsante sana Juliana huo ni msaada mkubwa umetupa.Kama ulivyohisi ni kweli mama yako anajihusisha na mitandao ya kihalifu na ndiyo maana anatumia majina tofauti ili isiwe rahisi kujulikana.Tumewahi kumtafuta kwa jina lake la Elizabeth lakini hatukufanikiwa kwani hakuna rekodi http://deusdeditmahunda.blogspot.com/zozote za jina hilo.Majibu haya yametupa mwanga mkubwa na tutayafanyia kazi"akasema Steve "Tukiachana na hilo kuna lingine ambalo nataka nikujulishe.Baada ya kuachana muda ule tulipokutana,tuligundua kwamba kuna mtu anakufuatilia na ndiyo maana nikawa ninakupa maelekezo.Tulifanikiwa kumpata mtu huyo na akakiri kweli ametumwa na mama yako akufuatilie.Katika simu yake tulimkuta ana picha yako ukiwa na Meshack Jumbo na Patricia.Aliipiga picha hiyo na kumtumia mama yako.Nimeona nikueleze jambo hili ili uwe makini sana kwani tayari mama yako ameanza kukutilia mashaka nyendo zako" "Dah ! nimestuka sana.Sikujua kama mama ameanza kunifuatlia.Nitajitahidi sana kuwa makini kuanzia sasa.Huyo jamaa aliyetumwa kunifuatilia yuko wapi? 'Tulimuacha aende zake lakini alichokipata hatathubutu tena kukufuatilia" "Ahsanteni sana" "Kubwa ambalo tumekuitia hapa tunahitaji tena msaada wako" "Hakuna tatizo nielezeni mnahitaji nini na mimi nitawasaidia" Nadhani sijakueleza lakini mimi na wenzangu tunachunguza mtandao wa watu wanaofanya biashara haramu ya silaha na waasi wanaopigana na serikali ya Congo.Kwa muda mrefu kumekuwa kunaibuka vikundi vya waasi vikipambana na serikali ya Congo na maisha ya watu wengi yamepotea na wengine kukimbia nchi yao na kwenda kuishi nchi za ugenini kama wakimbizi.Watu wanaofanya biashara hii wapo hapa nchini na ni mtandao mrefu unaohusisha watu matajiri na wengine ni viongozi katika serikali ya Tanzania na Congo.Katika uchunguzi wetu tumebaini kwamba Shanon Blank ambaye ni mama yako ndiye kinara katika biashara hii ya silaha" "Jesus Christ!!! akasema Juliana kwa mshangao mkubwa Nilijua mama anajihusisha na mambo haramu lakini sikuwahi kuhisi kama anaweza akajihusisha katika biashara kama hii" akasema Juliana "Shanon Blank..." Steve akaendelea "Anashirikiana na Joe Gregory ambaye ulitueleza ndiye mshirika wake mkuu wa biashara nchini Marekani.Huyu Joe ni tajiri sana anamiliki biashara kadhaa kubwa na ana kiwanda cha kutengeneza bunduki kubwa na ndogo na silaha nyingine.Kwa kutumia kampuni ya McLorien inayomilikiwa na mama yako hutuma silaha ambazo huja kama bidhaa za nguo na viatu na hutumwa katika kampuni ya Pendeza ambayo inamilikiwa na mtu mmoja anaitwa brigedia Frank na huyu ndiye anayefanya harakati zote za kuhakikisha mzigo unafika nchini Congo kwa waasi.Tumefanikiwa kupata mawasiliano kati ya Shanon na mtu mmoja anaitwa Patrice Lwibombe ambaye tunaamini ana mahusiano na waasi kwani katika mawasiliano hayo tuliyoyanasa Shanon anamtaka Patrice kuharakisha malipo ya mzigo walioupokea ambao tunaamini ni silaha,Patrice akamjibu kwamba wamechelewa kufanya makusanyo kutokana na mapambano kuwa makali baina ya vikosi vyao na vile vya serikali vikisaidiwa na vile vya umoja wa Afrika.Huyu ndiye ambaye tunamsaka tumjue ni nani na yuko wapi na vile vile mahusiano yake na waasi" akasema Steve na kunyamaza akamtazama Juliana "Siamini eti kwa sababu ya pesa mama ameamua kujiingiza katika biashara kama hii.Huu ni uuaji kwani silaha wanazowauzia hao waasi ndizo zinatumika kuua watu wasio na hatia" akasema Juliana na kwa mbali macho yake yakaonekana kulengwa machozi "Juliana tunataka kuusafisha mtandao huu na kuimaliza kabisa hii biashara hivyo tunahitaji msaada wako" "Niambie chochote mnachohitaji na mimi nitakifanya.Nimepata hasira sana kwa haya anayoyafanya mama.Ninaona aibu hata kuzaliwa katika familia kama hii.Niambie tafadhali mnataka nifanye nini? "Tunataka kumfahamu Patrice Lwibombe ni nani na yuko wapi. Tutaweza kulifanikisha hilo endapo tutafanikiwa kuipata kompyuta au simu ya mama yako.Nina imani lazima mama yako anawasiliana na Patrice kwa simu au kwa barua pepe hivyo tukiweza kupata kimojawapo kati ya simu yake ya mkononi au kompyuta anayotumia tutaweza kupata mambo mengi yanayohusiana na mtandao huu na hata kuwafahamu wengine ambao hatujawagundua bado.Can you do that for us? akauliza Steve.Juliana akainamisha kichwa kwa muda akatafakari halafu akasema "Chumbani kwa mama si rahisi kuingia lakini siwezi kushindwa nitatafuta namna ya kufanya hadi niweze kufanikiwa kupata kimoja wapo.Mama ana simu zaidi ya tatu ila kompyuta mpakato anazo mbili.Nitajitahidi niweze kupata hivyo vyote ili muweze kuvifanyia uchunguzi" "JItahidi kuipata simu yake anayotumia sasa na ukishaipata unipigie nitakupa maelekezo namna ya kufanya.Tutaingiza programu fulani katika simu hiyo na itaunganishwa katika hii kompyuta yangu na tutakuwa na uwezo wa kusikia mazungumzo yake yo.." Omola akanyamaza baada ya mlio fulani kutokea katika kompyuta yake.Akamtaka Steve asogee karibu "Nimepata tena mazungumzo mengine ya makamu wa rais yaliyorekodiwa kwa muda wa nusu saa iliyopita.Tafadhali sikiliza halafu utanieleza amesema nini" akasema Omola na kuanza kucheza rekodi zile.Yalikuwa ni mazungumzo ya makamu wa rais akizungumza na watu mbali mbali kupitia simu yake .Mara sura ya Steve ikabadilika baada ya kusikia rekodi mbili za mwisho "Kuna nini Steve mbona umestuka? akauliza Omola.Steve akamuelezea kila kitu kuhusiana na mazungumzo yale ya makamu wa rais na David Mpigie simu Elvis mueleze kila kitu ili hatua za haraka zichukuliwe kumuokoa Meshack" akasema Omola "Steve subiri kidogo.Mimi pia nimesikiliza hicho ulichokuwa unakisikiliza na nimestuka kusikia habari za Elvis.Ni Elvis yupi anayezungumziwa?akauliza Juliana.Steve na Omola wakatazamana "Oh my God ! akasema Steve kwa sauti ndogo "Tafadhali nieleze Steve ni Elvis yupi anayezungumziwa?Ni Elvis yupi ambaye alikufa lakini ameonekana akiwa hai? akauliza Juliana "Tumefanya nini?Juliana hakutakiwa kabisa kusikia au kufahamu jambo lolote kuhusiana na Elvis.We've done a huge mistake.Tumejisahau na tukazungumza mambo haya mbele yake wakati tukifahamu kabisa huyu ni mtu wa karibu na Patricia.What am I going to do?akawaza Steve "Steve mbona hunijibu?Hawa ambao wamesikika wakizungumza ni akina nani?Kwa nini wanamzungumzia Elvis?Ni Elvis yupi anazungumzia?Nieleze ukweli tafadhali bila kunificha" akasema Juliana "Steve muda unakwenda na tukiendelea kuchelewa hapa tutasababisha Meshack aingie katika hatari kwani hajui chochote kinachoendelea dhidi yake.Mjibu Juliana swali lake tuondoke" "Nijibu Steve" akasema Juliana "Sawa Juliana sina namna hivyo lazima nikueleze ukweli kwani wewe kwa sasa ni mwenzetu na sioni sababu ya kukuficha kitu.Hawa uliowasikia wakizungumza ni makamu wa rais na waziri mkuu mstaafu David Sichoma.Tumegundua kwamba makamu wa rais ana mahusiano na mtandao wa akina Frank wa kuuza silaha lakini bado tunaendelea kumchunguza na ndiyo kazi anayoifanya Omola.Kuna programu ameitega katika simu ya makamu wa rais ambayo hurekodi mazungumzo yote na kutupa taarifa kila baada ya nusu saa.Kwa upande wa David huyu tumegundua kwamba anashirikiana na wanasiasa wa vyama vya upinzani katika kuandaa mkutano wa hadhara utakaofanyika leo mkutano ambao umepigwa marufuku na jeshi la polisi lakini wao wanadai kwamba mkutano huo utafanyika kama ulivyopangwa.David tumeanza kumchunguza tufahamu nini dhamira yake ya kuungana na wanasiasa ingawa tayari tunazo taarifa kuwa ana mipango ya kuwania urais nadhani katika uchaguzi ujao" "Subiri kidogo Steve,kuna jambo umelifungua kichwani kwangu" akasema Juliana "David waziri mkuu mstaafu ni rafiki wa mama na jana nilimkuta nyumbani mama akanitambulisha kwake.Baada ya kuondoka mama akaniambia kwamba David alikuja pale kwa maongezi na akadai kwamba katika mazungumzo yao David alimwambia anataka kuchukua nafasi ya urais na akamuahidi kwamba endapo akipata urais mimi ataniteua kuwa waziri wa maliasili na utalii" "Kweli?! akauliza Steve "Kweli kabisa Steve.David na mama ni marafiki.Sikuwa nalifahamu hilo hadi jana nilipomkuta nyumbani" "Juliana kama nilivyokueleza awali kwamba mtandao huu wa mama yako unahusisha watu wakubwa.Nina imani urafiki wao si wa bure kuna jambo linaendelea kati yao na kwa kuwa tumeanza kumchunguza David tutafahamu kila kitu anachokifanya" "Naomba sasa kufahamu kuhusu Elvis aliyekuwa anazungumziwa na makamu wa rais na David"akasema Juliana na zikapita sekunde kadhaa Steve akitafakari halafu akasema "Sina ujanja Juliana lazima nikueleze ukweli.Elvis anayezungumziwa hapa ni mume wa Patricia" "What?!!..Are you serious? akauliza Juliana kwa mshangao "Juliana Elvis mume wa Patricia hajafa yuko hai" Juliana akapatwa na mshangao mkubwa akasimama na kumtazama Steve kwa macho makali Steve ninakuheshimu sana lakini naomba usinitanie namna hiyo"akasema Juliana na Steve akamuomba aketi "Elvis aligundua kuwepo kwa biashara ya silaha kupitia kwa Graca mtoto wa Frank.Walipofahamu kuwa tayari wamegundulika wakataka Elvis auawe hivyo wakamtumia makamu wa rais ambaye naye alimuachia jukumu hilo Meshack na hapo ndipo ulipochezwa mchezo wa Elvis kughushi kifo chake na watu wote wakaamini kwamba amekufa.Alifanya hivi ili akina Frank waendelee na biashara zao bila hofu na yeye apate nafasi nzuri ya kuwatafuta na hatimaye kuufutilia mbali mtandao huu.Kwa bahati mbaya tayari wameanza kuwa na wasiwasi kwamba yawezekana Elvis hajafa na hii imetokana na hatua kubwa ambayo imekwisha pigwa katika kuwachunguza hawa jamaa ndani ya kipindi kifupi.Kwa hiyo Juliana huo ndio ukweli halisi,Elvis hajafa na anaendelea na mapambano kuhakikisha kwamba anaufagia mtandao wote wa akina Frank.Hii ni siri kubwa na tunaofahamu ni sisi watu wachache.Nimekwambia wewe kwa sababu ni mwenzetu na umejitoa kupambana pamoja nasi hivyo hatuwezi kukuficha kitu" "Dah ! haya ni maajabu ya Musa.Patricia anafahamu chochote kuhusu jambo hili? "Hapana Patricia hafahamu chochote.Juliana muda unakwenda tutazungumza zaidi tukipata nafasi tunakuomba uyafanyie kazi hayo tuliyokueleza na ukifanikiwa tuwasiliane mara moja.Onyo ninakupa hapaswimtu yeyote kufahamu kuhusu suala ili la Elvis kuwa hai hasa Patricia" akasema Steve wakaagana "Wamefahamuje kama Elvis yuko hai? akauliza Omola "Hata mimi ninashangaa kwa sababu hii ni siri kubwa ambayo tunaoifahamu ni sisi wachache.Sijui wamefahamu vipi.Ngoja nimpigie Elvis nimfahamishe tulichokipata" akasema Steve na kupunguza mwendo wa gari akampigia Elvis simu "Elvis mambo yameharibika" "Kuna nini Steve? Mmeonana na Juliana?akauliza Elvis "Wameanza kuwa na wasi wasi kwamba haujafa" "Tayari ninafahamu jambo hilo" "Unafahamu?Umefahamuje?akau liza Steve "Ni Winnie ndiye aliyewaeleza akina Frank kuwa niko hai.Ninyi mmefahamuje? Tumenasa mazungumzo ya makamu wa rais na David muda mfupi uliopita.David anamueleza makamu wa rais kwamba wafanye uchunguzi kuthibitisha kifo chako kwani umeonekana ukiwa hai na wamekubaliana kwamba wamteke Meshack Jumbo wamuhoji ili aseme ukweli.Elvis tufanye haraka sana kumuokoa mkurugenzi yuko katika hatari kubwa" "Oh my God !! mko wapi sasa hivi? "Tumeachana na Juliana muda si mrefu na tumeanza safari ya kurejea nyumbani"akajibu Steve "Endelea na safari mimi ngoja niwasiliane na mkurugenzi halafu nitakujulisha nini tufanye" akasema Elvis na kukata simu na haraka haraka akampigia Meshack Jumbo.Simu ikaita na kukatika bila kupokelewa.Akapiga tena "C'mon Jumbo pokea simu" akasema Elvis kwa sauti ndogo huku mapigo ya moyo yakimwenda kasi aliingiwa na woga mwingi kuhusu maisha ya Meshack.Mara simu ikapokelewa na Elvis akashusha pumzi "Hallo" ikasema sauti ya Meshack Jumbo "Mzee uko wapi? "Nimetembelewa na wageni wanatoka afrika kusini niko nao hapa Venus hotel ambako tunapata chakula cha mchana" "Mzee nakuomba uondoke hapo haraka sana.Hauko salama" akasema Elvis "Elvis usihofu kuhusu mimi.Hapa kuna usalama wa kutosha na isitoshe tunao walinzi wetu wanaotulinda.Vipi huko mnaendeleaje? "Mzee Jumbo huu si utani nakuomba tafadhali ondoka hapo sasa hivi si salama kwako kwa sasa" "Kwa nini unasema hivyo?akauliza Meshack na mara akaingia ujumbe katika simu yake. "Elvis I'll get back to you" akasema Meshack "Mzee list......" akasema Elvis lakini tayari simu ilikwisha katwa. Meshack akaufungua na kuusoma ujumbe ule "Hotel Yvona room 83...Be there before 2.00 pm.It's important Mbutolwe "Huyu binti ana tatizo gani hadi asisitize nikaonane naye kabla ya muda huo .Kuna taarifa anazo za muhimu?akajiuliza Meshack Yawezekana kuna taarifa za muhimu sana amezipata kwani alikuwa kiongozi wa timu niliyoiunda kuchunguza kifo cha mke wa waziri wa zamani wa ulinzi wa Rwanda aliyeuawa katika hoteli moja hapa Tanzania.Inawezekana kuna taarifa nyeti amezipata na anataka kunishirikisha na ndiyo maana amenitumia ujumbe hu.."Mara simu ya Meshack ikaita alikuwa ni Mbutolwe "Hallo" akasema Meshack "Mzee natumai umeupata ujumbe wangu"akasema Mbutolwe "Nimeupata" "Naomba tekeleza ujumbe unavyotaka" akasema Mbutolwe na kukata simu "Lazima kuna jambo la muhimu sana ananiitia ngoja nikamtazame" akawaza Meshack akirejea ukumbi wa chakula ambako wageni wake walikuwa wanaendelea kupata chakula.Elvis aliendelea kupiga simu mfululizo lakini Meshack hakupokea.Alipoona mkurugenzi hapokei simu yake akampigia Steve "Steve nimempigia simu mkurugenzi kumuonya kuwa yuko katika hatari lakini hanielewi nimeendelea kumpigia simu hapokei tena.Something is wrong we need to hurry" akasema Elvis "Amekueleza yuko wapi? "Yuko Venus hotel,ile iko karibu na Mawingu tower.Steve elekeeni hapo haraka sana mimi nami ninakuja sasa hivi nitawakuta hapo" akasema Elvis na kuingia haraka chumbani kwake na kwa haraka akabadili mwonekano wake kwa kuweka ndevu bandia akavaa kofia na kuchukua silaha zake akaziweka katika mkoba mdogo na kumuaga Graca kisha akatoka na kutembea kwa kasi akielekea katika hoteli moja iliyoko umbali wa kama dakika kumi hivi.Alitembea haraka haraka na kuna wakati alikuwa anakimbia hadi alipofika katika hoteli ile ambako kulikuwa na taksi kadhaa akaingia katika mojawapo ya taksi na kumtaka dereva ampeleke Venus hotel Meshack Jumbo alimaliza kupata chakula na wageni wake akawaomba radhi kuwa amepata dharura ikabidi waagane kwani wageni wale walikuwa na safari ya kuelekea Arusha jioni ya siku ile.Baada ya kuagana nao akaondoka hadi katika gari lake na kumtaka dereva wake ampeleke Yvona hotel. Akiwa garini akakumbuka Elvis alimpigia simu na kumtaka aondoke pale hotelini haraka kwani yuko katika hatari Elvis alikuwa anamaanisha nini aliponitaka niondoke haraka pale hotelini niko katika hatari?Is something going on?akajiuliza halafu akachukua simu na kumpigia Elvis "Mzee uko wapi? "Nimekwisha ondoka pale Venus hotel kwa sasa ninaelekea Yvona hotel Mbutolwe ameniita pale kuna jambo anataka kunieleza.Kuna nini kinaendelea nakumbuka kuna jambo ulinieleza lakini sikukuelewa" "Una hakika umeitwa na Mbutolwe? "Ndiyo.Kuna kazi nilimpa na kuna jambo anataka kunieleza hivyo ninakwenda kuonana naye Yvona hotel nikitoka hapo nitakupigia unielekeze mahala mlikohamia nije niwatembelee na kujua mnaendeleaje"akasema Meshack na Elvis akawa kimya hakusema chochote kwa sekunde kadhaa "Elvis" akaita Meshack "Mbutolwe anafanya nini hapo hotelini?akauliza Elvis "Sijafahamu bado anafanya nini lakini amenitumia ujumbe na kunitaka nikaonane naye hapo.Amenielekeza nimkute chumba namba 83" "Sawa mzee ukitoka hapo unijulishe ili nikuelekeze mahala tunakoishi hivi sasa"akasema Elvis "Kuna jambo ulinieleza uliponipigia simu lakini hukunifafanulia,ni jambo gani hilo?Kuna hatari gani? "Usijali mzee tutazungumza utakapokuja hapa" akasema Elvis na kukata simu "Simuelewi Elvis alikuwa anamaanisha nini aliposema kuwa niko katika hatari ?Mbona hajanifafanulia ni hatari ipi hiyo iliyokuwa inanikabili? akajiuliza Meshack Jumbo Mara tu alipokata simu Elvis akampigia simu Steve "Steve, mzee amekwisha ondoka Venus hotel,anaelekea hotel Yvona anakwenda kuonana na Mbutolwe.Tuelekee huko.Mko wapi hivi sasa? "Tupo barabara ya Umoja na tumefika hapa katika ubalozi wa Urusi" "Good.Ingia bara bara ya Sambaa halafu nisubirini pale karibu na kanisa la Mashahidi wa Yehova.Ninakuja na taksi" akasema Elvis na kumtaka dereva aongeze mwendo Dereva wa ile taksi alikuwa mzoefu sana wa barabara za jiji la Dar hivyo haikuchukua muda mrefu wakawasili mahala Elvis alikopanga



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    awakute akina Steve akamlipa dereva na kushuka na kuliona gari la akina Steve likiwa limeegesha pembeni ya barabara upande wa pili wakimsubiri.Akavuka haraka haraka,tayari akina Steve walimuona na kumfungulia mlango akaingia "We have to hurry" akasema Elvis na Steve akawasha gari wakaingia barabarani "Nimezungumza na mkurugenzi muda mfupi uliopita yuko njiani anaelekea Yvona hotel na ninaamini bado hajafika.Kutokea hapa hadi hotel Yvona si mbali tutamuwahi kabla hajafika huko" akasema Elvis "Umemueleza tulichokigundua? "Nimemueleza lakini anaonekana kutonielewa.Hivi sasa anakwenda Yvona hotel kuonana na Mbutolwe ambaye amemtaka akaonane naye pale.Ninajiuliza kama kuna jambo ambalo anataka kumueleza mkurugenzi kuna njia zetu za kuwasilisha taarifa za siri na si kumuita mkurugenzi sehemu kama zile.Nahisi huu ni mtego umeandaliwa ili kumpata mkurugenzi.Tunatakiwa kumuwahi kabla hajafika na kuhakiki kama huu si mtego umewekwa ili kumkamata.Kuna chochote mmekipata kwa Juliana?" akauliza Elvis "Juliana amefanya uchunguzi kuhusu mama yake na amegundua kwamba anatumia majina tofauti tofauti na ana vyeti vya kuzaliwa zaidi ya vitano" "Huyu mwanamke ni mhalifu mkubwa wa kimataifa" akasema Elvis "Kweli Elvis huyu lazima anajihusisha na masuala ya kiuhalifu na ndiyo maana anatumia majina tofauti tofauti ili asijulikane.Tumempa kazi Juliana ya kuhakikisha anafanikiwa kuipata simu au kompyuta ya mama yake na ameahidi kufanya kila awezalo kupata mojawapo ya vitu hivyo kati ya simu au kompyuta.Tukiachana na hilo la Juliana tumepata pia mazungumzo kati ya makamu wa rais na David " akasema Steve na Omola akacheza ile rekodi ya maongezi ya makamu wa rais na David.Elvis akaisikiliza halafu akairudia tena kwa mara ya pili akashusha pumzi "Dah ! akasema na kufuta jasho usoni "Makamu wa rais alipokea agizo la kuniua kutoka kwa David ambaye kwa mujibu wa maelezo yao kuna watu wanashirikiana naye na ndiyo maana akamweleza makamu wa rais kuwa yeye hana wasiwasi hata kidogo kama nimekufa ila washirika wake.Ni akina nani hao washirika wake ambao wametaka mimi niuawe?akauliza Elvis "Elvis kuna kitu tumekigundua kutoka kwa Juliana.David na Elizabeth wana mashirikiano,ni marafiki wakubwa" akasema Steve "Kama ni hivyo basi jibu tumekwisha lipata.David naye anashirikiana na akina Elizabeth katika biashara ya silaha.Naye pia yumo katika mtandao huu wa akina Frank na ndiyo maana akamuomba makamu wa rais niuawe.Tunatakiwa pia kuchunguza kuhusu mipango yake ya chini chini na makamu wa rais ya kuwatumia wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani katika kusababisha vurugu.Mkutano ambao umepangwa kufanyika leo lazima utakuwa na vurugu kwani hauna kibali cha jeshi la polisi lakini wameendelea kuwasisitiza wafuasi wao kuhudhuria kwa wingi mkutanoni leo.Nini kipo nyuma ya haya wanayoyafanya?akauliza Elvis "Elvis kuna kitu kinanijia kichwani,kama David ana mashirikiano na akina Elizabeth na Frank hudhani labda nao watakuwa nyuma ya mkutano huu wanauandaa?akauliza "Siwezi kulipinga hilo lakini kama wako nyuma ya harakati hizi za kisiasa nini hasa lengo lao?Tuendelee kuwachunguza na tutapata majibu"akasema Elvis "Kuna taarifa zozote kutoka kwa Vicky hadi hivi sasa? akauliza Omola "Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kutoka kwa Vicky.Nimezungumza na mdogo wake ambaye tayari amezinduka na amenieleza mambo yaliyonishangaza sana.Amenieleza kila kitu alichokifanya" akasema Elvis na kunyamaza kimya kwa muda kisha akasema "Winnie hakukamatwa na akina Frank bali alijipeleka yeye mwenyewe" "Yule binti ana wazimu !!! akasema Steve kwa hasira "Amekiri kwamba aliwaeleza akina Frank kila kitu kuhusu sisi na ndiyo chanzo cha Frank kuanza kuwa na wasi wasi kuhusiana na mimi kuwa hai" "Kwa nini akafanya ujinga huo? Ningekuwa karibu ningemchapa makofi kwa ujinga alioufanya"akasema Steve "Anasema kwamba alifanya haya ili kumuokoa dada yake.Hakutaka dada yake afany.........." "Elvis tumefika" akasema Steve na kukata kona akaingia Yvonahotel.Hakukuwa na magari mengi eneo la maegesho. "Kwa mujibu wa mkurugenzi ni kwamba amepanga kuonana na Mbutolwe chumba namba 83.Naamini bado hajawasili.Mimi na Omola tutakwenda kufanya uchunguzi katika chumba hicho ili tuwe na uhakika nini hasa kinacho..." "Elvis" akaita Steve na kumkatisha Elvis "Mkurugenzi tayari amefika.Gari lake lile pale na anashuka" akasema Steve "Oh my God,tumechelewa,lakini hakijaharibika kitu tunakwenda ndani na kumlinda mkurugenzi dhidi ya chochote kitakachotokea.Omola utabaki garini mimi na Steve tunakwenda ndani kumfuata mkurugenzi" akasema Elvis na kuweka sawa silaha zake wakashuka na kutembea kwa tahadhari kubwa kuelekea ndani Meshack jumbo baada ya kushuka garini akaingia ndani ya hoteli na kuelekea mapokezi akauliza chumba 83 kiko ghorofa ya ngapi na kujibiwa kipo ghorofa ya tatu.Akapanda lifti na kuelekea ghorofa ya tatu.Milango ya lifti ikajifungua ilipofika ghorofa ya tatu akashuka na kuanza kukitafuta chumba namba 83. Steve na Elvis hawakupita mapokezi wakapitia upande wa hoteli na kupanda ngazi zinazoelekea vyumbani wakiwa katika tahadhari kubwa.Hawakutaka kutumia lifti ili kuweza kuyasoma mazingira yalivyokuwa. "Mpaka sasa sijaona hatari yoyote"akasema Steve wakipanda ngazi kukitafuta chumba namba 83 Mimi bado ninaamini mkurugenzi hayuko salama hadi pale tutakapohakikisha yuko katika mikono yetu" akasema Elvis wakaendelea kupanda ngazi wakafika ghorofa ya tatu. Meshack Jumbo alipofika chumba namna 83 akagonga mlango na sauti kutokea ndani ikamruhusu kuingia.Ilikuwa ni sauti aliyoifahamu vyema ya Mbutolwe mmoja wa wafanyakazi wa idara yake.Akakinyonga kitasa na kuingia ndani.Alipatwa na mstuko mkubwa ambao hakuutarajia mara nyuma yake wakatokea watu wawili wakiwa na bastora na kumtaka asipige ukelele wowote bali aingie ndani ya chumba kimya kimya.Meshack Jumbo hakuwa na ujanja akaingia ndani ya kile chumba.Mwili ulimtetemeka kwa alichokiona mle ndani Happy mtoto wa mwisho wa Meshack alikuwa amefungwa katika kiti akiwa na sare za shule.Meshack alihisi mwili wote unamtetemeka kwa woga.Nyuma ya Happy walikuwepo watu wawili waliofunika nyuso zao kwa kofia na kuacha macho pekee.Pembeni alikuwepo Mbutolwe. "Daddy help me !!akasema Happy huku akilia.Meshack akapandwa na hasira zilizochanganyika na woga akamgeukia Mbutolwe. "Mbutolwe what's the meaning of this? akauliza kwa ukali na mmoja wa wale jamaa akasogeza kiti na kwa sauti ya ukali Mbutolwe akasema "Sit !! "I cant believe this.Mbutolwe ni wewe kweli unayenifanyia hivi? akauliza Meshack kwa hasira "Mzee Meshack hatutaki kupoteza muda wako na wetu.Uko hapa kwa jambo moja tu.The truth!! "Before anything please let my daughter go !! akasema Meshack "Meshack hapa ulipo huna nafasi ya kutoa amri bali utafanya kila tutakachokuamuru sisi !! akasema Mbutolwe "What truth do you want? "Is Elvis alive or not ? akauliza jamaa mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi "Who are you to ask me that? akauliza Meshack na yule jamaa akamsogelea na kumnasa kofi kali lililompeleka hadi chini akamfuata na kumsindikiza na teke la tumbo halafu akawaamuru wenzake wamuinue na kumuweka kitini.Damu zilikuwa zinamtoka mdomoni Please dont hurt my dady!! akalia Happy.Yule jamaa akamsogelea Meshack na kumshika kidevu akamuinua kichwa "Ninapokuuliza unatakiwa unijibu na si kuniuliza swali.Hapa mimi ndiye mkuu hivyo unapaswa kuniheshimu!! akasema yule jamaa aliyekuwa na macho yaliyojaa ukatili "Nataka utueleze Elvis yuko hai au amekufa?Ni hilo tu ndilo tunalotaka utujibu kisha tutakuachia wewe na binti yako lakini kama utaendelea kuwa kiburi you and your daughter both will die" akasema yule jamaa.Meshack hakujibu kitu. "Muda unakwenda Meshack answer me !! akasema yule jamaa kwa ukali akimtikisa tikisa Meshack na ghafla Meshack akamtemea mate usoni.Yule jamaa akatoa kitambaa akajipangusa halafu akamsogelea Meshack na kumvurumishia makonde mfululizo hadi alipoanguka chini. Steve na Elvis walifika ghorofa ya tatu na kuanza kufuatilia namba za vyumba.Kulikuwa na watu wawili wamesimama nje ya chumba namba 83 na pembeni kidogo kulikuwa na mwanamama akifanya usafi. "Mkurugenzi yuko mle ndani na wale jamaa pale nje wanalinda usalama.Tutakachokifanya tutakapokaribia pale utajifanya umeteleza halafu utamgonga yule mwanamama anayefanya usafi na utaipiga teke ile ndoo yake ya maji lengo ni maji yawarukie wale jamaa wawili waliosimama nje ya mlango na mimi nitamalizana nao ili tuweze kupata nafasi ya kuingia ndani" Elvis akamuelekeza Steve wakati wakitembea katika varanda.Wale jamaa waliokuwa wamesimama katika mlango wa chumba 83 wakawatazama akina Elvis wakija na ghafla Steve akafanya kama alivyoelekezwa na Elvis.Akateleza na kumgonga yule mama aliyekuwa anafanya usafi halafu akaipiga teke ndoo ya maji yakamwagika na kuwarukia wale jamaa waliokuwa mlangoni.Kitendo kile cha kumwagiwa maji machafu kiliwakasirisha mno wale jamaa wakamfuata Steve pale chni kwa wepesi wa aina yake akachomoa bastora na kumuelekezea.Wakati Steve akimdhibiti yule jamaa aliyemfuata pale chini,Elvis naye akamdhibti yule mwingine aliyebaki halafu akamuamuru yule mwanamama aliyekuwa anafanya usafi afungue chumba namba 82,kwa haraka akafungua na wakawaingiza ndani wale jamaaMeshack Jumbo yuko wapi?akauliza Elvis kwa sauti ndogo.Yule jamaa hakumjibu. "Last chance where's Meshack Jumbo? akauliza Elvis "Simfahamu Meshack Jumbo" akasema yule jamaa na ghafla bila kutarajia Steve akaizinga bastora yake iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti na risasi mbili zikatoka kwa haraka zikatua katika kichwa cha yule jamaa akaanguka na roho ikamtoka.Yule mwenzake macho yakamtoka pima "Umeona kilichompata mwenzako?Nawe sasa hivi utakwenda kuzimu,tuonyeshe alipo Meshack haraka sana" akasema Elvis na yule jamaa huku akitetemeka akawaeleza kwamba Meshack alikuwa katika chumba kilichofuata. "Steve get rid of that woman" akasema Elvis na Steve akamshika yule mfanya usafi akamkaba na kumpoteza fahamu. Elvis akamuongoza yule jamaa taratibu wakatoka ndani ya kile chumba wakaenda chumba 83 akamuamuru afungue mlango.Yule jamaa akakinyonga kitasa lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani "Who's that?ikauliza sauti toka ndani "It's me Kendric" akasema yule jamaa "What do you want? ikauliza sauti toka ndani "Open the door.I have something impotant to tell you" akasema yule jamaa na mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja akatokeza kichwa.Kufumba na kufumbua Elvis aliyekuwa nyuma ya Kendric akaruka teke kali akaupiga mlango ukafunguka na kumuangusha yule jamaa aliyekuwa ameufungua.Kama vile wamepeana ishara,Elvis akamvuta pembeni yule jamaa aliyekuwa amemtanguliza mbele halafu Steve akajirusha ndani bastora yake ikiwa mkononi.Alipokuwa anarukia ndani aliwaona namna wale jamaa walivyokuwa wamekaa mle ndani na mara tu alipotua chini kwa kasi ya umeme akaizinga bastora yake na zikatoka risasi mfululizo zilizowapata jamaa waliokuwa wamezifunika nyuso zao kwa kofia wakaanguka chini halafu akakipiga teke kiti alichokuwa amefungwa binti wa Meshack Jumbo kikaanguka chini.Kitendo kile kikawastua wale jamaa wengine na mmoja aliyekuwa karibu na mlango akataka kuchomoka lakini akakutana na Elvis aliyemtandika teke kali la uso akaanguka chini halafu akampiga kichwa kizito Kendrik akaanguka chini na kupoteza fahamu huku damu ikimtoka puani. "Tulieni hivyo hivyo mlivyo" akaamuru Steve lakini ghafla Mbutolwe akaruka teke kali la haraka lililompata Steve na kumpeleka ukutani papo hapo yule jamaa aliyekuwa anamuhoji Meshack akamsogelea na kumtandika teke lingine la mbavuni akaanguka chini akigugumia kwa maumivu.Elvis aliyekuwa nje akabiringika na kuingia ndani akiwa na bastora mbili mkononi na kuachia risasi zilizompata yule kiongozi wao akaanguka chini.Meshack Jumbo akapata nguvu ya ghafla na kuinua kiti na kwa nguvu zote alizokuwa nazo akampiga nacho Mbutolwe kichwani akaanguka chini.Akamfuata pale chini na kuanza kumpiga na kiti kichwani na mchirizi wa damu ukaonekana mahala alipoangukia Mbutolwe.Elvis akamfuata "Imetosha mzee.She's dead" akasema Elvis halafu akamfuata Steve aliyekuwa bado amelala chini "Steve are you ok? akauliza "Mshenzi yule amenipiga teke la mbavu ninahisi maumivu makali sana eneo hili la mbavu" "Pole sana.Dr Philip atakuja kukutazama but right nowhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ we need to go" akasema Elvis na Steve akajitahidi kusimama.Haraka haraka Elvis akawavuta wale watu waliokuwa nje akawaingiza ndani na kuufunga mlango "Ahsanteni sana vijana kwa kuniokoa.Sikutegemea kabisa kama ningeweza kuokolewa.Nilijua maisha yangu na mwanangu yamefika mwisho" akasema Meshack Jumbo Usijali mzee.Tumetimiza lile tulilopaswa kulifanya.Steve wapekue wote uone kama kuna chochote chakuweza kutufaa" akasema Elvis na Steve akaanza kuwapekua "Imeniumiza sana hawa wawili walioficha nyuso zao ni vijana ninaowafahamu na mimi ndio niliowapendekeza kuingia katika kikosi cha walinzi wa makamu wa rais.Kwa nini leo wame nifanyia hivi?Ndio maana wameficha nyuso zao kwa aibu ili nisiwatambue" akasema Meshack Jumbo baada ya kuwavua kofia walizovaa wale jamaa wawili wakificha nyuso zao "Usiwalamu sana mzee.Hawana kosa lolote bali wanatekeleza maagizo waliyopewa"akasema Elvis "Who sent them?Who ever did this to me must pay!! akasema na kumkumbatia mwanae aliyefunguliwa kamba na Steve "Wamekuumiza kokote hawa washenzi? "Hawa ni akina nani baba?akauliza Happy huku akitetemeka kwa mambo aliyoyaona mle ndani "Mzee tunatakiwa kuondoka hapa mara moja" akasema Elvis na Meshack akamshika mkono mwanae wakatoka mle ndani wakaelekea chini. "Mambo yameanza kuharibika.Tayari wameanza kuwa na wasi wasi kama kweli Elvis amekufa.What happened?Kitu gani kimewafanya waanze kuchunguza kama amekufa?Waliofanya hivi lazima ni mtandao wa akina Frank na wenzake na kama ni hivyo basi familia yangu itakuwa katika hatari kubwa.Kama wameweza kumpata Happy na kumtumia ili kunilazimisha niweke wazi kama Elvis amekufa au mzima basi wanaweza wakaifuata familia yangu nyumbani.I'll have to protect my family" akawaza Meshack akiwa garini baada ya kuondoka pale Yvona hotel "Elvis samahani sana kwa kukupuuza.Ulijaribu kunionya kuhusiana na hatari lakini sikuelewa ni hatari gani.Niliamini niko salama na hata nilipopata ujumbe kutoka kwa Mbutolwe sikuwa na hata chembe ya wasi wasi kwani ni mtu ambaye ninamuamini sana.Aliponiita nilijua kuna jambo amelipata anataka kunieleza ndiyo maana nikawaacha wageni nilikuwa nao nikawahi pale Yvona hoteli kumbe ulikuwa ni mtego.Mlifahamuje kama niko katika hatari? akauliza Meshack Jumbo .Elvis akamtaka Omola acheze ile rekodi ya makamu wa rais na David.Meshack akaisikiliza na kushika mdomo kwa mshangao "Mambo haya ni vigumu kuyaamini.David kumbe ndiye anayetoa maelekezo haya kwa makamu wa rais !! akasema Meshack Jumbo kwa mshangao "Ndiyo mzee.David amekuwa anatoa maelekezo kwa Dr Shafi.Tumegundua David ana mashirikiano na Elizabeth na hii inatufanya tuamini kwamba naye pia yumo katika mtandao huu wa kuuza silaha.Bado tunaendelea kumchunguza makamu wa rais ili tujue kama naye ana mahusiano yoyote na mtandao huu wa akina Frank.Tumegundua vile vile kwamba makamu wa rais na David wako nyuma ya mkutano wa vyama vya siasa unaopangwa kufanyika leo licha ya jeshi la polisi kuupiga marufuku" akasema Elvis na kumtaka Omola aicheze ile rekodi ya makamu wa rais na David wakizungumzia kuhusu mkutano.Meshack akaisikiliza kwa makini halafu akasema "Kazi kubwa mmeifanya vijana wangu.Haya ni mambo makubwa sana mliyoyagundua.Hapa lazima kuna jambo kubwa.Viongozi hawa wakubwa kujihusisha na masuala kama haya lazima kuna ajenda kubwa nyuma yake" "Kuna taarifa tumezipata kwamba David ana mipango ya kuwania urais na tunahisi labda anataka kuwania urais kwa tiketi ya upinzani na ndiyo maana ameanza harakati zake chini chini" "Anataka kuwania urais?! Meshack akashangaa Kama ni hivyo basi yeye na Dr Shafi wana lengo moja la kutaka kujiunga na upinzani.Hilo si jambo baya lakini wanatakiwa wafuate taratibu na si kufanya mambo yao kwa siri.Tuachane na mambo hayo ya wanasiasa na tujikite zaidi katika kuutafuta mtandao wa kuuza silaha lakini kabla ya yote Elvis nahitaji kuihamisha familia yangu na kuificha sehemu salama.Watu hawa wanaweza wakaitumia familia yangu kunitafuta hivyo siwezi kuendelea kuiweka familia yangu katika hatari.Nisaidie tafadhali kwa hilo" "Usijali mzee.Familia yako itakuwa salama.Nina mtu ambaye anaweza akaificha familia yako kwa muda huu ambao tunaendelea kupambana." "Ahsante sana Elvis." akasema Meshack ana Elvis akachukua simu yake akampigia Doreen akamueleza kwamba kuna watu atawapeleka pale kwake kwa ajili ya kujificha.Doreen hakuwa na kipingamizi hivyo moja kwa moja wakaelekea nyumbani kwa Meshack Jumbo kuiondoa familia yake. **************** Alipotoka nyumbani kwa Elizabeth Frank alielekea moja kwa moja mahala alikopelekwa Vicky. "Sikutegemea kabisa kama mambo yangeharibika namna hii.Katika wakati ambao mipango yetu imeanza kwenda vizuri ndipo vinapoibuka vikwazo ambavyo hatukuvitarajia kabisa.Lakini haya yote yamesababishwa na Graca.Pone pone yake aendelee kujificha lakini endapo nitafanikiwa kumpata sintakuwa na huruma naye hata kidogo.Tayari amekwisha ingia katika orodha ya maadui zangu na nitamfanya kama ninavyowafanya maadui zangu wengine.Nitamuua kikatili sana.Sioni sababu ya kuwa na mtoto kama yule ambaye hana faida yoyote kwangu.Yeye ndiye aliyeniingiza katika haya matatizo yote.Kama asingejiunga na Elvis na kumpa siri zangu mida hii ningekuwa nimetulia ninakula mvinyo nikijiandaa kuwa waziri wa ulinzi." Frank akahisi mwili unamsisimka alipomkumbuka Elvis,akakunja sura kwa hasira "Huyu ndiye chanzo cha matatizo haya yote.Je ni kweli yuko hai? Winnie hakuonekana kama anasema uongo lakini mtu pekee ambaye alipaswa kutoa ukweli kuhusiana na Elvis kuonekana ni Vicky ambaye yeye ameleta hadithi nyingine kabisa.Nilitegemea kumtesa mdogo wake mbele yake ili kumfanya afunguke lakini naye amechukuliwa na watu wasiojulikana.Je ni nani hawa waliomchukua Winnie?Wamejuaje kama yuko pale?akajiuliza "Lazima ni watu wataalamu sana walioweza kufahamu mahala alipofichwa Winnie na nina hakika Vicky atakuwa anafahamu kila kinachoendelea.Nimepewa hadi saa kumi na mbili kuhakikisha amesema yote.Nitampa mateso makali na ataongea kila kitu" akaendelea kuwaza Frank Aliwasili katika nyumba alimokuwamo Vicky.Obi na vijana wake walikuwa wameimarisha ulinzi "Kila kitu kinakwenda vizuri hapa? akauliza Frank baada ya kushuka garini na kupokewa na Obi Kila kitu kinakwenda vyema mkuu.Wale vijana wetu tayari tumewahifadhi kimya kimya bila familia zao kufahamu chochote kwani wanaweza wakafanya uchunguzi na sisi tukajiweka matatani" "Good.Waelekeze vijana wako waimarishe ulinzi nataka nimtese mwenyewe huyu Vicky na leo ataeleza kila kitu" akasema Frank na kuelekea ndani katika chumba alimowekwa Vicky.Akamtazama kwa hasira halafu akavua koti na kulitupa chini "Vicky naomba unisikilize vizuri.Safari hii nimekuja kikazi hivyo sitaki kupotezewa muda wangu nawe.Nitakuuliza swali moja tu na endapo utashindwa kunijibu basi sintakuwa na huruma nawe hata kidogo" akasema Frank "Frank nimekwisha kueleza kwamba siwezi kuzungumza nawe jambo lolote bila ya kumuona kwanza mdogo wangu Winnie.Bring Winnie here and we'll talk" akasema Vicky "Vicky inaonekana bado hujanifahamu vyema na leo nitakuonyesha upande wangu wa pili ambao bado haujaufahamu vyema.Utanisamehe sana kwa hilo" akasema Frank "Unapoteza muda wako Frank huwezi kupata chchote toka kwangu hadi nimuone mdogo wangu Winnie" akasema Vicky "Tutaona" akasema Vicky na Frank akamuita Obi "Andaa kila kitu niwekee hapo mezani" akasema na Obi akatoka "Vicky sipendi nikuumize naomba kwa mara ya mwisho uniambie wako wapi wale watu waliokuteka? Yuko wapi Elvis? Frank nimechoshwa na hilo swali lako.Mara ngapi nikwambie kwamba siwafahamu hao watu !! akasema Vicky kwa ukali.Obi akarejea akiwa na sanduku la chuma akaliweka mezani na kuanza kutoa vifaa mbali mbali vya kutesea akavitandaza mezani "Mfunge mikono mning'nize katika kamba" akasema Frank na Obi akamshika Vicky mikono akaifunga na kumning'iniza "Good.Muondoe hizo nguo zote"akaamuru Frank.Obi akazivua nguo za Vicky akabaki mtupu.Frank akachukua fimbo yenye mikia sita iliyofungwa vyuma vyenye makali nchani mwake akamsogelea Vicky na kwa kutumia nguvu akamchapa na fmbo ile mgongoni,vile vyuma vyenye makali vikazama katika nyama na Frank akavuta kwa nguvu vikamchana chana Vicky mgongo "Aaaaaggghhhhhhh!!!!!!!! Vicky akapiga ukelele mkubwa.Frank hakujali akamchapa tena na kuongeza maumivu zaidi huku Vicky akiendelea kupiga kelele na damu kumtoka "Where is Elvis?! akauliza Frank "I..I..I dont know...." akajibu Vicky.Frank akamchapa tena kwa nguvu na ile fimbo lakini Vicky hakutamka chochote. "This is not working" akasema Frank akiwa amejawa na hasira baada ya kumuona Vicky ameloa damu mwili mzima lakini hakuwa ametamka chochote.Akaenda mezani akachukukua chupa fulani na kuibonyeza ikatoa maji akammiminia Vicky mwilini akatoa ukelele mkubwa sana kwa maumivu makali aliyoyasikia Tell me where is Elvis?!! akauliza Frank kwa ukali lakini Vicky hakumjibu akaendelea kutoa ukelele wa maumivu.Frank akamwagia tena lakini licha ya maumivu makali aliyoyahisi na kuuona mwili wote unawaka moto hakuthubutu kutamka chochote "Huyu ni mwanamke wa aina gani anayeweza kuvumilia mateso ya namna hii?Hata wanaume hawawezi kuvumilia mateso ya aina hii.Haya maji pekee ya maumivu yanatosha kabisa kumfungua mtu yeyote aliye mgumu kufunguka na akasema kila kitu.Hata hivyo nitaendelea kumtesa na atasema kila kitu" akawaza Frank akachukua kifaa chakukatia vyuma na alipomkaribia akagundua Vicky hakuwa na fahamu "C'mon wake up !! akasema na kumnasa Winnie kofi zito Nataka nikuondoe hizi nyeti zako kwani ndiyo sababu ya wewe kuendelea kuwa hai mpaka sasa.Nilikuwa na mipango ya kukuua lakini ni hizi nyeti zilizonifanya nibadili mawazo baada ya kuonja utamu wake.Nitakuondoa kiungo kimoja kimoja hadi utakaposema kile ninachokitaka" akasema Frank na kumuangalia tena Vicky ni kweli hakuwa na fahamu.Akamuita Obi na kumtaka amfungue amuweke kitandani azinduke.Damu ilikuwa imeacha kutoka kufuatia yale maji ya maumivu makali aliyomwagiwa. "Mkuu taratibu usije ukamuua kwani tunamtegemea sana kupata taarifa muhimu.Akikushinda nipe mimi kazi hiyo na atasema tu" akasema Obi "Nitamalizana naye mimi mwenyewe leo.Lazima atasema kila kitu.Nitampa mateso ya kila aina na atasema tu!! Hakikisha anazinduka haraka"akasema Frank na kutoka mle chumbani. "Mwanamke wa aina gani huyu?Mateso haya yote niliyompa hajathubutu kusema chochote?Mateso haya hata wanaume huwa wanashindwa kuyavumilia lakini bado amefumba mdomo wake.Sikutegemea kama angeshindwa kusema kitu baada ya kumwagiwa yale maji ya maumivu.Amenishangaza mno ujasiri wake.Au anasema kweli?Kama ndiyo nani basi mkweli kati yake na Winnie?Kwa nini Winnie anitafute kunieleza maneno yale ambayo kwa asilimia kubwa ninaamini ni ya kweli halafu anatokea Vicky na kudai kuwa maneno yale hayakuwa ya kweli?I'm confused lakini huyu Vicky leo lazima atanieleza ukweli" akawaza Frank akiwa ananawa mikono akifuta damu iliyomtapakaa mikononi Obi alimfungua Vicky akamlaza kitandani na kumfungua kamba zote akaanza kumpepea ili azinduke "Dah ! Kwa kuwa ni kazi tu ndiyo maana ninamtesa lakini kama si hivyo kamwe nisingeweza kumtesa mwanamke mzuri kama huyu.Ukimtazama akiwa mtupu unaweza pata uchizi wa ghafla na uzuri wa kipekee sana"akawaza Obi akimtazama Vicky kwa matamanio.Taratibu akampapasa Vicky mapajani "Frank amemuumiza sana.Mrembo kama huyu hastahili kuumizwa namna hii" akawaza Obi akiendelea kuyapapasa mapaja ya Vicky ambayo licha ya kwamba yalikuwa yameloa damu lakini bado yaliendelea kuvutia.Ghafla kukatokea jambo ambalo Obi hakuwa amelitegemea kabisa.Vicky aliinuka ghafla na kwa nguvu akamrukia Obi akampiga kichwa kilichomfanya Obi aone nyota akajibamiza ukutani.Vicky akaruka toka kitandani kwa lengo la kumfuata Obi lakini tayari Obi alikwisha jua dhamira ya Vicky akainua chupa iliyokuwa karibu akairusha lakini Vicky akaiona akaikwepa.Obi akajirusha mzima mzima na kumvaa Vicky wote wakaanguka chini kisha akaanza kumshindilia makonde mazito.Mara Vicky kwa kutumia miguu yake akamkaba Obi kabali na kumuangusha chini.Obi akajitahidi kujitoa katika kabali ile lakini Vicky kwa kutuima nguvu zake zote alizobaki nazo akahakikisha Obi hachomoki.Obi akatambua kwamba Vicky alikuwa vizuri na kama angefanya mzaha angeweza kupoteza maisha.Akanyoosha mkono na kuushika mguu wa meza iliyokuwa na vifaa vya kutesa akaivuta na meza ile ikaanguka na vifaa vile kutawanyika chini,akaokota kisu na kutaka kumchoma nacho Vicky lakini kwa jicho kama la tai akauona mkono wa Obi ukiwa na kisu ukimuelekea sehemu za kifuani akauzuia kwa mkono wake wa kushoto halafu kwa kutumia mkono wa kulia akachukua chupa iliyoanguka karibu yake iliyokuwa na kimiminika akampulizia Obi usoni na akasikia akitoa ukelele na akaangusha kile kisu akakiokota na kukizamisha tumboni mwa Obi.Akaitoa miguu yake shingoni kwa Obi halafu kwa hasira akakizamisha kile kisu kwa mara nyingine kifuani kwa Obi mahala ulipo moyo na Obi akaanza kutapa tapa akikata roho.Vicky akajiegemeza ukutani akitweta. "I need to get out of here.!!akawaza na mara akasikia hatua za mtu akainuka na kuchukua kisu alichokitumia kumuulia Obi akaenda kujificha pembeni ya mlango. "Ob.............." akasema mtu aliyeufungua mlango na kwa kasi ya umeme Vicky akaurusha mkono wenye kisu akimlenga usoni yule jamaa ambaye kwa sauti alimtambua ni Frank lakini alikiona kitendo kile na akaupiga mkono ule wenye kisu kikaanguka halafu akamvuta Vicky na kumpa ngumi nzito iliyompeleka chini na ndipo alipoweza kuona kile kilichokuwa kimefanyika mle chumbani.Obi alikuwa amelalia dimbwi la damu hakuwa na uhai tena.Frank akatetemeka kwa hasira Umemuua Obi?!!! akaulizia huku akitoa bastora yake kwa lengo la kumfuata Vicky pale chini alipokua ameanguka na ghafla bila kutegemea Vicky akamkata ngwala na Frank akaanguka mzima mzima kama furushi akagongesha kichwa sakafuni.Vicky akainuka ili aweze kumkabili lakini Frank akaokota kisu na kukirusha kikamchoma Vicky begani na wakati akijaribu kukichomoa Frank akasimama na kumtwisha tena ngumi nyingine iliyompeleka Vicky sakafuni na bila kupoteza muda Frank akamfuata pale chini na kumkalia juu akaanza kumvurumishia makonde mazito. "Who are you ?Leo utanieleza wewe ni nani.Hakuna aliyewahi kupambana na Obi akabaki hai!!! akasema Frank.Vicky akakiona kile kisu alichochomwa begani kikiwakimeanguka karibu naye akakiokota na kukizamisha mbavuni mwa Frank "Aaaghhh!!! Frank akapiga ukelele mkubwa na Vicky akaitumia nafasi hiyo akamsukuma akaanguka.Mwili wa Vicky haukuwa na nguvu,akajizoa zoa ili kumkabili Frank ambaye alikua chini akigugumia kwa maumivu.Mara Frank akaiona bastora yake ikiwa karibu akaiokota na kugeuka huku damu ikimtiririka na kumnyooshea Vicky "Stay where....yo..you...are...." akasema akiwa katika maumivu makali na damu ikiendelea kumtoka mahala alipochomwa kisu "Frank put the gun down"akasema Vicky "I'm going to kill y...." kabla Frank hajamaliza sentensi yake Vicky akaruka na kuupiga teke ule mkono uliokuwa na bastora ikaanguka akaokota kifaa cha kukatia vyuma akakiwasha na bila kupoteza hata sekunde moja akakipitisha katika sikio la kushoto la Frank na kuliondoa.Frank akatoa ukelele mkubwa.Vicky akiwa bado na hasira akakipitisha kifaa kile katika goti na kuukata mguu. "Aaagghhh..!!!! akapiga ukelele wa maumivu. "Wewe hasa ndiye niliyekuwa nakutafuta.Leo nimekupata na ni zamu yako kwenda kuungana na wale ambao wameuawa kwa sababu ya silaha ambazo wewe na mtandao wako mmekuwa mnaziuza kwa waasi.Ni wakati wenu wa kulipa uovu wenu!! akasema Vicky akamtazama Frank kwa hasira halafu akaliondoa tena sikio lingine la Frank kwa kutumia kile kifaa Mtu katili sana wewe na tayari umekwisha ua watu wengi.Unastahili kufa kifo cha maumivu makali mno.Sintakuacha hai" akasema Vicky huku Frank akihangaika pale chini na hakuweza kuzungumza tena lakini sura yake iliyokuwa imeloa damu ilionyesha alikuwa kaika maumivu makali mno. "Unastahili kufanyiwa ukatili huu!!! akasema Vicky akiwa amejawa hasira na kukishika kiganja cha mkono akakikata halafu akachukua ile chupa yenye maji ya kuongeza maumivu akamwagia sehemu zile alizomkata na Frank akajinyonga nyonga kwa maumivu makali aliyoyapata. "Unastahili kuyapata maumivu makali kabla hujafa.Maumivu kama haya ndiyo wanayoyapata ndugu zetu wa huko Congo ambao maisha yao yamekuwa magumu kwa sababu yako wewe na wenzako" akasema huku akimtazama Frank aliyekuwa amelalia dimbwi la damu "Natamani nikukate kiungo kimoja kimoja ili ufe kwa maumivu makali sana lakini hautaweza kuishi tena.Ninakuacha ufe taratibu na hii ni salamu kwa wenzako wote wajiandae tunakuja" akasema Vicky na kuiokota bastora ya Frank "Umenitesa sana bazazi wewe na ulikuwa na lengo la kuniua lakini wewe ndiye utalayetangulia mbele za haki na ukajibu maswali kwa roho za watu zilizotolewa kutokana na silaha mnazouza"akasema Vicky halafu akampekua Frank na kumkuta na simu mbili moja ikiwa ni ile ya kwake "Ouh thanks God" akasema na kuiwasha ilikuwa na chaji kidgo sana na mda wowote ingezima.Akamtazama Frank ambaye alikuwa anatapa tapa pale chini akionekana hatakuwa na muda mrefu wa kuishi "Nguvu zimeniisha na siwezi kuendelea kupambana tena na hawa jamaa kwani inaonekana wako wengine huko nje.I need help.I have to call Winnie" akawaza Vicky halafu akazifafuta namba za Winnie akapiga.Simu ikaita na kupokelewa "Hallow dada " akasema Winnie na Vicky akashusha pumzi "Winnie uko wapi? Are you safe? "Dada niko salama.Niko hapa kwa akina Elvis.They saved my life.Wewe uko wapi dada? akauliza Winnie huku machozi yakimtoka "Oh thak God .Nilikuwa na wasi wasi sana na usalama wako.Winnie uko karibu na akina Elvis? "Hapana wametoka wote niko na Graca pekee.Uko wapi dada?akauliza Winnie "Winnie I'm in trouble and I need help.Nahitaji msaada wa akina Elvis haraka sana" akasema Vicky "Where are you ?Nielekeze nije hapo nikuchukue haraka sana" akasema Winnie "Not you Winnie.I need Elvis and Steve people who can fight" akasema Vicky "Nisubiri kidogo nimuulize Graca kama ana mawasiliano ya akina Elvis" akasema Winnie na kutoka akamfuata Graca akamuuliza kama ana mawasiliano na akina Elvis "You want to run again? akauliza Graca "Graca please its Vicky.She's stuck some where and she needs help.Kama una mawasiliano na akina Elvis nipe nizungumze nao tafadhali" akasema Winnie Oh.Elvis amenipa simu mpya ambayo nitakuwa naitumia katika kuwasiliana nao ngoja nimpigie" akasema Graca na kuchukua simu yake iliyokuwa na namba mbili tu za Steve na Elvis akampigia Elvis "Graca" akasema Elvis baada ya kupokea simu "Elvis kuna jambo limetokea hapa muda si mrefu na linahitaji msaada wenu" "Jambo gani? "Vicky amepiga simu na anahitaji msaada wa haraka sana" "Vicky?Yuko wapi? akauliza Elvis na Graca akampa simu Winnie " Elvis its me Winnie.Vicky amenipigia muda si mrefu katika simu yangu na amenieleza kwamba yuko mahala na anahitaji msaada wenu wa haraka." Sawa Winnie naomba unipe namba zake za simu niwasiliane naye" akasema Elvis na Winnie akampa namba za Vicky na bila kupoteza muda akampigia Vicky "Hallo Vicky,where are you? What happened to you? akauliza Elvis "Elvis listen tome.Simu yangu inakaribia kuisha chaji na sifahamu mahala nilipo hivyo naomba mtumie ile programu ya Omola aliyotumia kumtafuta Winnie kunitafuta na kujua mahala nilipo.I'm in great danger so please help me" akasema Vicky "Sawa Vicky.Stay where you are and we'll be there very soon.Please make sure you are safe" akasema Elvis na kukata simu akamfuata Omola "Omola Vicky amepiga simu na yuko katika hatari anahitaji msaada wetu.Tumia ile programu yako uliyotumia kumtafutia Winnie ili tujue mahala aliko Vicky" akasema Elvis na bila kuchelewa Omola akawasha kompyuta yake na kuanza kuitafuta simu ya Vicky "Nimeipata" akasema na kumuonyesha Elvis mahala alipo Vicky.Elvis akamfuata Meshack Jumbo "Mzee sisi tunahitaji kuondoka.Tumepata taarifa Vicky yuko katika matatizo na anahitaji msaada.Utaongozana na Steve hadi kwa Doreen ili ahakikishe nyote mko salama.Usihofu kuhusu familia yako itakuwa salama.Ninamuamini Doreen" akasema Elvis "Usijali Elvis,ahsante sana kwa kila kitu"akasema Meshack Jumbo halafu Elvis akamfuata Steve "Steve Vicky amepiga simu muda si mrefu yuko katika matatizo na anahitaji msaada.Mimi na Omola tunakwenda huko.Tayari Omola amekwisha pata mahala aliko Vicky.Wewe utaongozana na Meshack Jumbo kuelekea kwa Doreen.Make sure they are all safe.Ukiwafkisha salama utamchukua Meshack Jumbo na kumleta kule kwenye kambi yetu ila familia yake itaendelea kukaa pale kwa Doreen hadi mambo yatakapomalizika" akasema Elvis "Sawa Elvis.Endapo mtahitaji msaada usisite kunijulisha nami nitakuja mara moja" akasema Steve na Elvis akamfuata Doreen "Doreen mimi ninaondoka kuna sehemu ninakwenda mara moja.Tafadhali hakikisha familia hii inakuwa salama.Muda wowote ukihisi hatari nijulishe haraka" akasema Elvis na bila kupoteza muda akaingia garini na Omola wakaondoka kumfuata Vicky









    Dr Makwa Tusangira kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania aliingiia katika chumba cha maongezi alimokuwamo waziri mkuu mstaafu David Sichoma,akajimimnia mvinyo katika glasi akagugumia wote akamtazama David na kusema "David nakuona una wasi wasi sana.Usihofu ndugu yangu jambo hili litafanikiwa .Tumejipanga vizuri na hata sasa nimetoka kuzungumza na wenzangu kila kitu kiko vizuri na ni wakati wa kuondoka kwenda kuanza harakati kwani muda umefika" "Dr Makwa sina wasiwasi nawe hata kidogo ninaamini kila kitu kitakwenda kama tulivyotarajia.Kuna chochote kingine utahitaji kabla hujaondoka? "Kila kitu kiko sawa endapo kuna chochote nitakihitaji kwa dharura nitakujulisha" akasema Dr Makwa huku akiongeza tena mvinyo katika glasi na kunywa funda kubwa "This is it David.Ukombozi unaanza.Wish me lucky" akasema Dr Makwa na kumkumbatia David wakaagana.Dr Makwa akaingia katika gari maalum aliloandaliwa na David huku akisindikizwa na magari mawili ya walinzi aliopewa na David akaondoka katika makazi yale ya waziri mkuu mstaafu na kwenda kuungana na wenzake katika mkutano wa hadhara waliopanga kuufanya katika viwanja vya jamhuri. Toka ilipotimu saa nane za mchana tayari watu walianza kujitokeza katika viwanja vya jamhuri kwa ajili ya kuitikia wito wa viongozi wao kuja kuhudhuria mkutano mkubwa waliouitisha.Polisi walikuwepo eneo la tukio ili kuwazuia watu kukusanyika lakini kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo idadi ya watu ilivyozidi kuongezeka na kuwapa wakati mgumu polisi kuwatawanya.Maelekezo yakatolewa na viongozi wakuu wa jeshi la polisi kwamba wasiwafanye chochote wananchi hao waliokusanyika bali wawasubiri viongozi wao walioitisha mkutano ule bila kibali wawatie nguvuni.Hadi ilipotimu saa kumi tayari viwanja vya jamhuri vilikuwa vimefurika watu.Kulikuwa na shamra shamra nyingi na watu wakiendelea kuimba nyimbo za hamasa wakiwasubiri viongozi wao.Saa kumi na nusu mmoja wa wahasishaji akapanda juu ya gari lililotengezwa mfano wa jukwaa akashika kipaza sauti na kutoa salamu ya hamasa kisha kusema "Ndugu zangu kutokana na ulinzi uliopo hapa viwanjani viongozi wetu hawataweza kufika hapa kwani wanasubiriwa wakamatwe na jeshi la polisi hivyo tumeelekezwa kwamba tuanze maandamano kuelekea katika ofisi zetu za chama na huko tutawakuta viongozi wetu wanatusubiri.Mpo tayari? "Ndiyoooooooooooo!!!!! ikapigwa kelele kubwa "Mpo tayariiiiiiiiiiii...!!!!akauliza tena "Ndiyooooooooooooooo!!! wakajibu wanachama "Ahsanteni sana.Ninawasihi msiogope chochote tunaandamana kwa amani bila kufanya vurugu kuelekea katika makao makuu ya chama.Tanzania ni nchi huru hivyo ni haki yetu kuandamana na kufanya mikutano yetu ya siasa.Ukombozi unaanza leo ndugu zangu.Narudia tena kuwasihi msiogope bali twendeni kwa amani tukiimba hadi katika ofisi za chama tukakutane na vongozi wetu" akasema yule muhamasishaji na kumalizia kwa salamu ya hamasa kubwa na kisha kuyaanzisha maandamano kuelekea katika ofisi za chama chao Yalikuwa ni maandamano makubwa kutokana na uwingi wa watu waliokuwa wamehudhuria katika viwanja vya jamhuri na hivyo ililazimika shughuli mbali mbali kusimama barabarani ili waandamanaji waweze kupita na hii ilisababisha usumbufu mkubwa hasa kwa wasafiri ambao walikuwa wanarejea majumbani kwao jioni hii.Maandamano yalianza kwa amani wakipita barabara ya mzee Juma kisha wakaingia barabara ya Arusha na huku kote walikopita ililazimu magari na shughuli nyingine kusimama kwa muda.Maandamano yalipofika katika maungio ya barabara ya Mbuni na Mbuyuni yakakutana na kikosi cha polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa wamejipanga kuwazuia wafuasi wale wasiendelee na maandamano yao. Jeshi la polisi lilifuata taratibu zake za kuwataka waandamanji wale watawanyike kwani maandamano yale hayakuwa halali lakini waandamanaji waliendelea kuimba huku wakitoa maneno ya kejeli kwa jeshi la polisi na hata wengine kuanza kuwarushia mawe.Licha ya waandamanaji http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kugoma kutawanyika bado jeshi la polisi likaendelea kutumia busara na kuwataka watawanyike kwa amani lakini bado waandamanaji waliendelea kugoma na ndipo polisi walioanza kuwatawanya kwa kutumia gesi za machozi.Waandamanaji walifahamu kinachoweza kutokea hivyo wakawa wamejiandaa kwa chupa za maji kwa ajili ya kunawa usoni na hapo ndipo vurugu kubwa zikaanza.Matairi yakakusanywa na kuchomwa hivyo kulianya eneo hili lenye maduka makubwa makubwa kutanda moshi mzito mweusi.Mapambano kati ya polisi na waandamanaji yakaendelea na ghafla polisi watatu wakaanguka na kufa papo hapo na mara moja wakagundua kwamba polisi wale walikuwa wamepigwa risasi ndipo amri ikatolewa kwamba polisi wajihami kwa risasi za mpira kwani miongoni mwa waandamanaji walikuwepo pia wenye silaha za moto.Polisi wakapiga juu risasi za baridi ili kuwaogpesha waandamanaji lakini hawakuogopa na badala yake polisi wengine wanne wakaanguka na kufa kwa kupigwa risasi na hapo ndipo walipolazimika kuanza kutumia risasi za moto. Katika makao makuu ya chama alikuwapo Dr Makwa na wenzake wakataarifiwa kwamba mambo tayari yameharibika hivyo kwa haraka wakatawanyika kwenda mafichoni kila mmoja alipoajua yeye.Dr Makwa akarejea nyumbani kwa David "Tayari mambo yameanza na nimetaarifiwa mpaka sasa zaidi ya polisi kumi wamekwisha fariki dunia na waandamanaji wengi wanaonekana chini wakiwa wamekufa kufuatia kupigwa risasi na polisi.Kwa sasa ninaanza kuwahamasisha na watu wa mikoani pia wajiandae kwani vugu vugu hili halitaishia tu Dar es salaam bali litasambaa nchi nzima" akasema Dr Makwa "Kazi nzuri sana Dr Makwa.Usihofu kuhusu usalama wako.Hapa uko salama na endelea kufanya kazi zako kwa uhuru ukiwa hapa.Nataka kesho asubuhi mikoa yote ile mikubwa iwake moto.Kote maandamano yaanze" "Usijali David kila kitu kitakwenda vyema kwani tumejipanga vizuri.Kitu cha msingi ni fedha zote tunazozihiaji ziwepo tayari kwani moto huu hautazimika hadi tutakapoingia ikulu" "Kuhusu Fedha usiwe na shaka hata kidogo kwani zipo za kutosha.Ngoja nishughulikie suala hilo" akasema David na kutoka akaelekea chumbani Safari ya kuelekea ikulu imeanza na kwa mbali tayari nimeanza kuinusa harufu ya jengo lile zuri.Siku si nyingi sana toka sasa nitatangazwa rais mpya wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Wale wabaya wangu wote labda waote mabawa wapae watoweke kabisa katika ulimwengu huu kwani hakuna atakayebaki salama.Nitahakikisha wote ninawafyeka.Wale wote walionihujumu kisiasa wakati wao wa kuishi maisha magumu umewadia.Siku zao zinahesabika" akawaza David huku akitabasamu akazitafuta namba za Frank akampigia lakini simu haikupolewa,akapiga tena bado simu haikupokelewa "Nitampigia tena baadae.Ngoja niwasiliane na Dr Shafi nimjulishe kinachoendelea"akawaza David na kumpigia simu Dr Shafi Hallo David..Mambo naona yameanza.Nimepokea simu muda si mrefu rais ananitaka katika kikao cha dharura kufuatia kinachoendelea huko mtaani hivi sasa.Una taarifa zozote? "Ninazo taarifa za kila kinachoendelea huko mtaani.Mambo yameanza vyema na yamekwenda kama vile tulivyokuwa tunataka.Mpaka sasa taarifa tulizonazo ni kwamba polisi zaidi ya kumi wamekwisha uawa na hii imefanyika ili kuwalazimisha polisi watumie nguvu kubwa kuwatawanya waandamanaji .Hili limefanikiwa kwani hadi sasa miili ya watu kadhaa inaonekana ikiwa imezagaa barabarani na tunategemea vurugu hizi kuendelea usiku kucha kwani timu ya uhamasishaji inafanya kazi nzuri na vijana wanaendelea kuhamasiswa wasirudi nyuma bali waendelee kupambana na polisi" "Mwanzo mzuri David.Vipi kuhusu akina Dr Makwana wenzake,wako salama? "Wote wako salama kabisa na kila mmoja yuko mafichoni.DrMakwa ninaye hapa na yuko salama kabisa anaendelea na kazi zake akiwa hapa.Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba kesho vuguvugu hili litaendelea pia hadi mikoani na halitakoma hadi tuhakikishe tunaing'oa serikali madarakani" "David ninaenda kuoanana na rais .Tutaongea zaidi baadae .Kama kuna chochote mtahitaji kutoka kwangu usisite kunijulisha" "Sawa Dr Shafi" "Kingine David nakumbusha kuhusu umakini mkubwa unatakiwa katika jambo hili.Hawa wanasiasa wanatakiwa kuendelea kukaa mafichoni hadi hapo mambo yatakapotulia kwani naamini hivi sasa watakuwa wanasakwa mno na jeshi la polisi.Wakikamatwa na wakahojiwa we'll all go down.Tafadhali hakikisha wote wanakuwa salama.Ikilazimika kuwaficha hata nje ya nchi nieleze nitasaidia kwa hilo" akasema Dr Shafi "Dr Shafi vipi kuhusu yule mkuu wa idara ya ujasusi tayari amekwisha patikana? "Mpaka sasa bado sijapokea taarifa zozote kutoka kwa vijana niliowatuma kazi hiyo lakini naamini bado watakuwa wanaendelea na hilo zoezi na litakapokamilika basi nitakujulisha"akasema Dr Shafi na kukata simu.David akatabasamu na kumpigia tena Frank lakini simu haikupokelewa "Frank ana tatizo gani?Mbona hapokei simu? Huu si wakati wa kukaa mbali na simu hta kidogo,mambo ndio yameanza"akawaza David ***************** Elvis na Omola wakifuata maelekezo ya ile programu ya kompyuta wakafika katika nyumba ambayo waliamini ndimo alimo Vicky "Ni hapa" akasema Omola akihakiki programu yake.Kabla hawajashuka garini wakatokea watu wawili.Elvis akamtaka Omola washuke.Wakafungua milango na kushuka wakawafuata wale jamaa "Hey ! Tuwasaidie nini?akauliza mmoja wao "Samahani kaka,hapa ni kwa bibi Blandina Msakwa? "Blandina?akauliza tena yule jamaa huku akimtazama mwenzake "Ndiyo.Ni hapa au tumepotea nyumba? "Nani kawaelekeza hapa? "Tumeelekezwa na kuwa ni hapa" "Huyo mtu haishi hapa.Nendeni mkaulize huko kwa majirani wengine" akasema yule jamaa "Samahani sana kwa usumbufu.yawezekana aliyetuelekza alikosea"akasema Elvis na kisha yeye na Omola wakageuka kama vile wanaondoka kurejea katika gari lao lakini ghafla wakageka na kutoa bastora wale jamaa wawili wakapatwa na mstuko mkubwa.Mmoja akataka kuchomoa bastora yake lakini Omola alikiona kitendo kile na kuachia risasi kadhaa kutoka katika bastora yake na yule jamaa akaanguka na kutoa mguno.Yule mwenzake aliyebaki sururali yake ya jeans rangi ya bluu ikaloa sehemu za mbele alijisaidia haja ndogo.Mguno ule wa kukta roho alioutoa yule jamaa aliyepigwa risasi ukamstua jamaa mwingine aliyekuwa ndani akafungua mlango mdogo wa geti na kuchungulia.Elvis alimuona na kumvurumishia risasi lakini akawahi kufunga mlango. "Go after him!! akasema Elvis na Omola akamfuata yule jamaa kwa tahadhari kubwa.Akaufungua mlango mdogo wa geti na kuingia ndani akawaona watu wawili wakihangaika kupanda ukuta ili waruke upande wa nyuma.Mmoja wao akageuka na kumuona Omola akamvurumishia risasi lakini Omola akajificha nyuma ya mti halafu kwa sabaha kali akaachia risasi iliyompata mmoja shingoni akaanguka chini na akabaki mmoja.Omola akajitokeza na kumtaka ajisalimishe.Akaitupa chini bastora na kunyoosha mikono.Akamfuata na kuichukua bastora yake akamsachi hakuwa na silaha nyingine. Elvis akamuamuru yule jamaa aliyekuwa naye nje amvute mwenzake aliyepigwa risasi amuingize ndani akafanya hivyo halafu akamuunganisha na yule ambaye alikuwa amedhibitiwa na Omola "Mmeona kilichowatokea wenzenu,kama mnataka kuendelea kuishi jibuni kwa ufasaha kila nitakacho wauliza" akasema Elvis "Ninyi ni akina nani?Mnafanya nini hapa? "Sisi hapa ni walinzi tu.Tumepewa kazi ya kuilinda hii nyumba" "Nani kawapa hii kazi? "Ni Obi" Yuko wapi Obi? akaulzia Elvis "Obi yuko ndani" "Yuko na nani humo ndani?Wako watu wangapi? "Ndani kuna watu watatu,Obi na tajiri na mwanamke mwingine hatumjui" "Tajiri?!akauliza Elvis "Ndiyo.Tajiri mwenye kazi" akasema yule jamaa "Anaitwa nani? "Hatumjui.Sisi tunayemfahamu ni Obi"akasema yule jamaa halafu Elvis akamuinua na kumtaka aelekee mlangoni "Fungua mlango" akaamuru Elvis na yule jamaa akafungua mlango ukafunguka.Sebuleni hakukuwa na mtu yeyote na nyumba ilikuwa kimya.Elvis akampiga yule jamaa pigo moja la kichwani akaanguka na kupoteza fahamu.Elvis akamfanyia ishara Omola ampoteze fahamu yule jamaa mwingine na kufumba na kufumbua Omola akmtadika yule jamaa pigo zito na kumuacha akiwa hana fahamu akatembea kwa tahadhari kumfuata Elvis "Kuna mtu yeyote humu ndani?akauliza "Nyumba iko kimya sana.Twende kwa tahadhari hawa watu wamo humu ndani" akasema Elvis kwa sauti ndogo na kuanza kuzunguka ndani ya nyumba ile na ghafla wakaona mlango wenye mchirizi wa damu.Elvis akamfanyia ishara Omola halafu wakausogelea mlango ule na taratibu Elvis akakinyonga kitasa cha mlango na kuufungua kisha wakajitoma ndani wakakutana na kitu cha kustusha.Damu ilikuwa imesambaa kila mahala na watu wawili walikuwa wamelala katika damu hawakuonekana kuwa na uhai tena.Pembeni ya ukuta alionekana mwanamke mmoja akiwa amelala sakafuni akiwa ameloa damu.Elvis akamfuata na kugundua ni Vicky "Vicky!! akaita Elvis na kujaribu kumtingisha lakini Vicky hakuweza hata kufumbua jicho.Mapigo ya moyo wake yalikuwa chini sana. "Omola haraka sana tumuokoe Vicky hali yake si nzuri hata kidogo" akasema Elvis huku akimuinua Vicky na kutoka naye nje.Omola kabla ya kutoka akawapiga picha wale watu wawli waliokuwa wamelala katika damu ambao hawakuwa na uhai tena "Inaonekana kulikuwa na shughuli nzito humu ndani" akawaza Omola wakati akitoka na kukimbia kumfuata Elvis ambaye aliondoa gari haraka sana.Akachukua simu na kumpigia Dr Philip Dr Philip ninakuomba uache kila unachokifanya sasa uelekee tena katika makazi yetu mapya kuna mtu amejeruhiwa ana hali mbaya sana ninakuja naye sasa hivi" "Sawa Elvis ninafanya hivyo" akasema Dr Philip "Nimechunguza kwa haraka haraka mle ndani kunaonekana kulikuwa na shughuli nzito sana.Ni akina nani wale jamaa wengine waliouawa mle ndani?Inaonekana wameuliwa kikatili sana ila nimepiga picha maiti zao na vile vile nimechukua simu mbili zilizokuwa pemeni ya Vicky"akasema Omola "Kikubwa kwa sasa tujitahidi Vicky awe salama.Atatueleza kila kitu kilichotokea na kwa nini alifika pale" akasema Elvis akiendesha gari kwa kasi Waliwasili katika makazi yao,geti likafunguliwa na kwa haraka Vicky akashushwa na kuingizwa ndani.Tayari Dr Philip alikwisha fika na kwa haraka akaanza kumuhudumia.Winnie alipomuona dada yake akiwa katika hali ile akaangua kilio.Elvis akamtaka anyamaze.Omola akamuonyesha Elvis picha zile alizozipiga katika kile chumba walimomkuta Vicky. "Vicky alifikaje hapa?Inaonekana kulikuwa na mpambano mkali sana hadi akafanikiwa kuwaua hawa jamaa wawili.Watu hawa ni akina nani?Nyuso zao zote zimetapakaa damu kiasi ni vigumu kuwatambua.Ngoja atakapozinduka atatujulisha nini hasa kilijiri na hawa aliowaua ni akina nani" akasema Elvis akachukua simu na kumpigia Steve akamjulisha kuwa tayari wamekwisha mpata Vicky na alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu na Dr Pilip.Steve akamfahamisha Elvis kwamba walikuwa wamewasili nyumbani kwa Doreen na muda wowote yeye na Meshack Jumbo wataanza safari kuelekea katika makazi yao.Elvis akaenda katika chumba ambamo Vicky alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu "Ameumizwa sana,hata hivyo itanilazimu kwenda kuchukua chupa zaidi za damu kwani amepoteza damu nyingi sana.Imekuwa vyema mmewahi kumpata lakini mngechelewa kidogo angepoteza maisha" akasema Dr Philip "Dr Philip fanya kila unaloweza kuhakikisha Vicky anakuwa salama.Kuna mengi tunahitaji kuyafahamu kutoka kwake" akasema Elvis Usijali Elvis nitafanya kila ninaloweza na Vicky atakuwa salama" akasema Dr Philip na kuondoka kwenda kufuata damu ya kumuongezea Vicky. "Elvis ahsante sana kwa kumukoa dada yangu.Japokuwa hali yake si nzuri lakini ninashukuru kwani yuko katika mikono salama.Sina cha kukulipa Elvis na samahani sana kwa yote niliyoyafanya.I was so foolish.I didnt know what I was doing" akasema Winnie huku akilia "Usilie Winnie kitu kikubwa kwa sasa ni kumuombea Vicky aweze kupata nafuu.Wewe pia bado unahitaji mapumziko.Nenda kapumzike nitakujulisha hali ya dada yako inavyoendelea" akasema Elvis By the way Elvis waliofanya hivi mmewafahamu ni akina nani? akauliza Winnie "Bado hatujawafahamu ni akina nani ila mahala tulipomkuta Vicky kulikuwa na mapambano makali na watu wawili wamekufa naamini hao ndio walimteka.Atakapozinduka atatueleza mengi kuhusiana na watu wale na nini kilitokea" "Ahsante Elvis.Mungu akubariki sana.Nakuomba tafadhali hakikisha dada yangu anakuwa salama" akasema Winnie na kwenda chumbani kupumzika.Dr Philip akatoka katika chumba alimokuwamo Vicky na kumjulisha Elvis kwamba anakwenda kuchukua damu pamoja na dawa nyingine kwa ajili ya Vicky.Elvis akaingia katika chumba alimo Vicky ambaye bado hakuwa na fahamu akamtazama kwa muda halafu akasema kwa sauti ndogo "You are so beautifull.Hukutakiwa kufanya kazi kama hizi.Baada ya suala hili kumalizika nitakushauri uachane na hizi kazi na ujishughulishe na biashara zako.Watoto wazuri kama ninyi ni pambo la hii dunia hamustahili hata kidogo kufanyiwa ukatili mkubwa kama huu" akawaza na mara mlango ukagongwa alikuwa ni Omola "Anaendeleaje Vicky? akauliza Omola akiwa ameishika kompyuta yake "kwa mujibu wa daktari anaendelea vyema ila amepoteza damu nyingi na Dr Philip amekwenda kufuata damu zaidi pamoja na dawa" "Vicky ni jasiri na atakuwa salama" akasema Omola Tumuombee awe salama kwani tunahitaji kufahamu kutoka kwake kuhusiana na wale watu tuliowakuta mle chumbani wamekufa ni akina nani" "Elvis kuna jambo nimelipata kuhusiana na makamu wa rais na David" akasema Omola wakatoka mle chumbani wakaenda sebuleni "Nimepata rekodi nyingine ya mazungumzo kati ya makamu wa rais na David ambayo yamefanyika muda si mrefu sana" akasema Omola na kumchezea Elvis mazungumzo yale ya makamu wa rais Dr Shafi na David.Elvis akatoa kitambaa na kujifuta jasho.Alihisi joto "Toka awali nilihisi lazima kuna jambo kubwa lililoko nyuma ya mkutano ule wa siasa na sasa tayari tumeupata ukweli kwamba ajenda kuu ya mkutano ule ambao ndio chanzo cha machafuko yaliyotokea leo ni kuing'oa serikali.Makamu wa rais na David wakishirikiana na wanasiasa wa vyama vya upinzani lengo lao ni kuanzisha machafuko ambayo yataing'oa serikali iliyoko madarakani.Huu ni uhaini.Watu hawa ni mashetani kabisa.Watu wanaangamia katika mapambano kumbe lengo lao ni kupata madaraka.Huu ni ukatili uliopitiliza kabisa!! akasema Elvis kwa hasira "Nadhani wanataka kuiga kile kilichotokea katika baadhi ya nchi ambapo kulitokea maandamani na machafuko ya bila kukoma na serikali zilizokuwa madarakani zikang'oka.Lengo lao ni hilo"akasema Omola "Sawa kabisa Omola kwani katika mazungumzo yao David anamsisitiza Dr Shafi kwamba vijana wanaendelea kuhamasishwa waendeleze vurugu na kesho vurugu hizo zitahamia pia katika mikoa mikubwa.Lengo lao ni vurugu zisambae nchi nzima na serikali itatumia nguvu kubwa kumaliza vurugu na maandamano hayo na lengo la waandaaji wa maandamano na vurugu hizo ni kuilazimisha serikali kutumia nguvu kubwa na kupelekea watu kuuawa hivyo kuifanya jumuiya ya kimataifa kupiga kelele kubwa na wakati mwingine kuingilia kati kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kisingizio cha kukiuka haki za binadamu.Maisha ya watu hasa vijana wadogo yanapotea kutokana na uchu wa madaraka wa watu wachache tu " akasema Elvis "Kwa hiyo tunafanya nini?akauliza Omola Watu hawa ambao wako nyuma ya jambo hili ni hawa hawa ambao tunaamini ndio wanaojihusisha na biashara ya silaha kwa waasi wa Congo.Huu unaonekana ni mtandao mkubwa na uliosambaa sana.Nadhani sasa itatulazimu kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja.Tuumalize mtandao wote wa biashara ya silaha na vile vile tulizime jaribio hili la kutaka kuiondoa serikali madarakani.Tunao ushahidi ambao hauna mashaka kuhusiana na mpango ya hawa jamaa na tayari tunawafahamu ni akina nani hivyo tunachotakiwa kufanya ni kufahamu nani na nani wamo katika mpango huu wa kuiondoa serikali madarakani" "Kwa nini tusiwataarifu vyombo vingine kama jeshi la polisi kuhusiana na hiki tulichokigundua ili tuokoe watu zaidi wasiendelee kuuawa? akauliza Omola "Kitu muhimu ni sisi kuhakikisha tumechunguza kwa kina na kuwafahamu wahusika wote na kisha kuwakamata na kuwakabidhi kwa vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake" akasema Elvis "Elvis nimekumbuka kitu" akasema Omola na kwenda katika chumba chake na baada ya muda akarejea "Nilichukua simu mbili zilizokuwa pembeni ya Vicky katika kile chumba" akasema Omola na kumkabidhi Elvis zile simu.Moja ilikuwa imezima ambayo Elvis akaitambua ni simu ya Vicky.Akaichukua nyingine kubwa nyeupe akaanza kuipekua.Kitu cha kwanza alichokifanya katika simu ile ni kufungua sehemu ya kuhifadhi picha na kustuka baada ya kuziona picha kadhaa za Frank. "Frank!! akasema Elvis kwa sauti ya mshangao na kuendelea kuzitazama picha zile.Katika picha kadhaa Frank alionekana akiwa baa akiwa na Pascal wakipata kinywaji huku wakiwa na wanawake wawili. "Umesema Frank?Omola akauliza "Ndiyo.Kuna picha hapa katika hii simu ambazo zinamuonyesha Frank akiwa na Pascal wakiwa baa wakipata kinywaji.Pia zipo picha nyinginezo zikimonyesha Frank katika sare za kazi" "Je hii ni simu ya Frank? akauliza Omola "Ninahisi hivyo.Ichunguze laini hii ya simu imesajiliwa kwa jina gani?akasema Elvis na Omola akaichukua ile simu ya Frank lakini kabla hajafanya chochote ikaanza kuita na jina la mpigaji lilionyesha ni David. "Kuna mtu anapiga simu hapa anaitwa David" akasema Omola "David?!!.Elvis akauliza "Ndiyo" "Usiipokee hiyo simu ili tuzichunguze namba hizo pia tufahamu ni David yupi anayempigia" akasema Elvis na simu ile ya David ikaita na kukatika bila kupokelewa na baada ya sekunde kadhaa ukaingia ujumbe uliosomeka "Frank naomba uwasiliane nami mara tu uupatapo ujumbe huu,ni muhimu sana" "Tayari tumepata jibu hii ni simu ya Frank.Je Frank ni mmoja wa watu waliouawa mle ndani? akauliza Elvis "Kama ni simu ya Frank basi lazima naye ni mmoja wa watu waliouawa mle ndani.Unamfahamu Frank kwa sura? akauliza Omola "Hapana.lakini kuna njia rahisi ya kufahamu kama mmoja wa watu waliouawa mle ndani ni Frank" akasema Elvis na kwenda kumchukuahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Graca.Akaichukua simu ya Omola akamuonyesha Graca picha alizopiga Omola "Ninaomba kwa makini sana zipitie hizo picha na ujaribu kuona kama utaweza kumtambua mmoja kati ya watu utakaowaona katika hizo picha.Samahani kwa picha hizi zinatisha kidogo" akasema Elvis na Graca akaanza kuzitazama picha zile.Sura za watu wale zilikuwa zimechafuka kwa damu lakini ghafla baada tu ya kuiona picha ya pili Graca akastuka This is my father !! akasema kwa mstuko .Elvis na Omola wakatazamana "Graca itazame tena picha vizuri na uhakikishe kama unachokisema ni cha kweli" akasema Elvis. "Elvis ninamfahamu baba yangu vizuri.Hata kama nikikurupushwa usingizini nitamtambua.Huyu ni baba yangu Frank Kwaju.What happend to him?Where is he?akauliza Graca ambaye macho yake tayari yalianza kuonyesha wasiwasi.Elvis akamshika mkono na kumketisha sofani "Graca you have to be brave.Tulipokwenda kumfuata Vicky mahala alipotuelekeza tumekuta kuna watu wawili katika chumba alimokuwamo.Watu hao ndio hao unaowaona katika picha.Kwa bahati mbaya wote wawili hawana uhai.They're both dead.I'm so sorry Graca" akasema Elvis "Graca pole sana" akasema Omola na macho ya Graca yakajaa machozi.Elvis akamkumbatia na Gaca akikilaza kichwa chake kifuani kwa Elvis huku machozi mengi yakimtoka.Alikuwa analia kwa kwikwi "Tunamsubiri Vicky azinduke ili atueleze nini hasa kilichokuwa kimetokea mahala pale.Yeye ndiye anayefahamu nani waliofanya mauaji yale ya baba yako"akasema Elvis.Graca akainua kichwa akamtazama Elvis "Elvis I need to be alone now" akasema Graca "Kama kuna chochote unakihitaji tafadhali nieleze" "Ahsante Elvis" akasema Graca na kuelekea chumbani huku akilia Anatia huruma sana Graca"akasema Omola "Frank alikuwa ni mkatili sana kwa mwanae.Graca amepitia mateso makali kutoka kwa baba yake.Alimtesa kama si mwanae wa damu lakini siku zote damu ni nzito kuliko maji.Pamoja na ukatili wote aliofanyiwa na baba yake lakini kifo chake kimemuumiza Graca.Hawezi kuonyesha usoni lakini moyoni ameumia sana" akasema Elvis na kumsimulia Omola kila kitu kuhusiana na Graca "Dah ! Kumbe amepitia mambo mengi sana licha ya umri wake.Anatuhitaji sana kwa wakati huu.Tunapaswa tuwe naye karibu " akasema Omola "Tuachane na suala hilo na tujielekeze katika kumtafuta huyu David aliyekuwa anawasiliana na Frank ni nani?akasema Elvis na Omola akazichukua zile namba za David akaziingiza katika kompyuta yake akabofya kidogo na baada ya muda akasema "Namba hizi ni za David Sichoma" "Oh my God ! Elvis akashangaa "Huyu ni waziri mkuu mstaafu ambaye ndiye anayewasiliana na makamu wa rais.Kama David na Frank wanawasiliana hii ina maana kwamba hata David naye yumo katika mtandao wao wa biashara ya silaha.Sasa picha kamili imejileta yenyewe namna mtandao huu ulivyo mkubwa na sasa tunaona kuna mambo mengine wanajishughulisha nayo zaidi ya biashara ya silaha.Wana panga mipango ya uhaini.Wanataka kumuondoa rais aliyeko madarakani.Hili si jambo dogo hata kidogo.Kwa nini lakini wanafanya hivi?Kwa nini wanataka kuiondoa serikali madarakani?Nani kawatuma?akauliza Elvis "Elvis maswali haya ni madogo lakini majibu yake ni mazito sana na tutayapa majibu endapo tutawapata wahusika wakuu wa mtandao huu.Tukiwapata tukawah............."Omola akanyamaza baada ya kengele ya getini kusikika.Elvis akainuka akatoa bastora yake na kueleka getini kwa tahadhari kubwa.Akachungulia na kumuona Steve akalifungua geti wakaingia ndani.Steve alikuwa na Meshack Jumbo "Mambo yamekwenda vizuri huko? akauliza Elvis wakiwa sebuleni "Kila kitu kimekwenda vizuri.Nawashukuruni sana kwa kuniokoa mimi na familia yangu leo hii.Isingekuwa ninyi nadhani mpaka mida hii ningekuwa nimekufa" akasema Meshack Jumbo "Usijali mzee,ni wajibu wetu kufanya vile tulivyofanya" akajibu Elvis "Vicky anaendeleaje?akauliza Steve "Bado hana fahamu lakini Dr Philip ametuhakikishia kwamba anaendelea vyema,hajaumia sana isipokuwa amepoteza damu nyingi" "Nini hasa kilichotokea?Nani waliokuwa wamemshikilia?akauliza Meshack Jumbo.Elvis akawaelezea kila kitu kilivyokuwa na halafu akawaonyesha picha walizofanikiwa kuwapiga wale watu wawili waliokutwa wamefariki ndani ya kile chumba walimomkuta Vicky "Hawa ni akina nani?Mmewatambua? akauliza Steve Tumfanikiwa kumtambua mmoja wao.Ni brigedia Frank Kwaju" Meshack Jumbo na Steve wakatazamana kwa mshangao "Frank?akauliza Meshack Jumbo "Ndiyo.Tulipiga picha miili ile na tukamuonyesha Graca na mara tu alipoziona picha akamtambua baba yake Frank.Kwa hiyo ni wazi sasa Frank Kwaju amefariki dunia" akasema Elvis "dah ! akasema Steve "Nani huyo ambaye amemuondoa huyu jamaa duniani kikatili namna hii?akauliza Meshack Jumbo huku akitazama tena pichaya Frank "Bado hatufahamu ni nani aliyefanya kitendo hiki tunamsubiri Vicky yeye ndiye mwenye kufahamu kila kitu kilichotokea.Akizinduka atatueleza nini kilichotokea ila naamini ni yeye ndiye aliyewaua wale jamaa"akasema Elvis "Nilimtamani sana Frank nikutane naye ana kwa ana" akasema Steve "Aliyekutana naye amefanya kile ambacho ungekifanya pindi ungekutana naye.Hata hivyo kuna jambo lingine pia" akasema Elvis na kuwachezea mazungumzo ya makamu wa rais na David.Meshack Jumbo akabaki mdomo wazi "This is unbeliavable.Elvis una hakika hizi sauti ni za makamu wa rais na David?akauliza Meshack Jumbo akionekana kuwa na wasi wasi mwingi "Usiwe na wasi wasi wowote mzee Jumbo.Unazozisikia ni sauti za makamu wa rais Dr Shafi na waziri mkuu mstaafu David" "Vijana hili sijambo dogo lazima rais afahamishwe kuhusu hili suala ili aweze kuchukua hatua stahiki za haraka sana kuzima mpango huu!! akasema Meshack "Hapana mzee hatutamtaarifu rais mpaka hapo tutakapokuwa na taarifa na ushahidi wa kujitosheleza kuhusiana na hili suala.Tunapaswa tuwafahamu wote wanaopanga njama hizi.Huu ni mtandao mrefu hivyo kabla ya kumjulisha rais ni lazima kwanza tuhakikishe tumewafahamu watu hao ni akina nani,na nani yuko nyuma yao?Siku zote kunapokuwa na mipango kama hii ya mapinduzi lazima kuna watu walio nyuma ya mipango hiyo kwa manufaa yao hivyo hata mpango huu lazima kuna watu walio nyuma yake ambao lazima tuwafahamu" Elvis itachukua muda mrefu kuwafahamu watu hao ni akina nani kwa vile tayari tunawafahamu wahusika wakuu ambao ni makamu wa rais na David basi tumjulishe rais na wakamatwe mara moja na hao watawataja wenzao wanaoshirikiana nao.Suala hili halipaswi kuchukua muda mrefu.We have to do it now!! akasema Meshack Jumbo "Mzee suala hili ni kubwa na zito.Hatuwezi kukurupuka na kumuendea rais bila ya kuwa na ushahidi wa kujitosheleza.Unadhani rais atatuelewa kwa sababu tu ya ushahidi wa sauti za maongezi ya makamu wa rais na David?akauliza Elvis na Meshack akawa kimya "Watu hawa ni viongozi wakubwa wa serikali hivyo tunapowaingiza katika jambo kubwa kama hili lazima tuwe na ushahidi usio na mashaka hata kidogo kwamba wanahusika katika kutaka kuiangusha serikali" akasema Elvis "Elvis tutapoteza muda mwingi kuwachunguza hawa jamaa wakati wao wanaendelea na harakati zao na maisha ya vijana wanaoingizwa barabarani kuandamana yanaendelea kupotea endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuwadhibiti hawa jamaa.Ukiacha hilo usalama wa rais hivi sasa uko mashakani kwani hawa jamaa wanaweza wakamuua hivyo lazima tumlinde rais" "Rais atakuwa salama tutamlinda"akasema Elvis "Una uhakika gani atakuwa salama na utamlinda vipi wakati wewe tayari umekufa na hauwezi kuonekana mtaani?Elvis tafadhali tusilifanye suala hili likawa gumu,mimi maamuzi yangu ni kumjulisha rais.Naomba kusiwe na mabishano yoyote tena kuhusu suala hilo.Endapo litatokea jambo baya na ikagunudlika kwamba nilifahamu kuhusiana na mipango hii ya mapinduzi na nikawa kimya basi lazima na mimi nitachukuliwa hatua.Sitaki jambo hilo linitokee hivyo nitamjulisha rais kuhusu jambo hili kusudi hatua za haraka zichukuliwe"akasema Meshack Jumbo na kutoa simu akaiwasha kwa lengo la kumpigia rais lakini Elvis akamnyang'anya "Mzee ninakuheshimu sana na ninakuomba usikilize na ufuate kile ninachokueleza.Hii ni kazi yetu na ninakuomba utuache tuifanye namna tunavyoona sisi inafaa.Wewe kaa pembeni subiri matokeo kutoka kwetu.Tuko tayari kufanya kazi hii kwa kila uwezo tulio nao na ninakuhakikishia tena kuwa hawa jamaa hawatafanikiwa lengo lao.Naomba uniamini na uiamini timu ninayoiongoza" akasema Elvis "Elvis nielewe kijana wangu, maisha ya rais yako mashakani.Yuko katika hatari kubwa ya kuuawa.Tukifanya masihara rais anaweza akafikwa na jambo baya .Tunao uwezo wa kumuokoa rais dhidi ya njama hizi ovu na lazima tufanye sasa,si kusubiri" akasema Meshack Jumbo "Mzee narudia tena kukuhakikishia kwamba rais atakuwa salama.Watu hao hawatafanikiwa lengo lao na ninakuhakikishia kwamba tu......."Elvis akakatishwa na Mzee Jumbo "Elvis kwa nini hutaki kunielewa?!! akauliza Meshack kwa ukali.Elvis naye akakasirika na kusimama akamtazama Meshack kwa hasira "Mzee nakuonya kwa mara ya mwisho kwamba hii ni kazi yetu.Sisi ndio tuliobaini kuwepo kwa mipango hii ya kuiangusha serikali na sisi ndio tutakaohakikisha kwamba jambo hilo halifanikiwi.This is what I died for.I won't let my death be for nothing.I died to save my president and thats what I'll do!! akasema Elvis kwa ukali "No ! akasema Meshack na kugonga meza kwa hasira "Ninyi nyote bado mko chini yangu na mtafanya kila kitu kutokana na maelekezo yangu.Hakuna atakayekwenda kinyume na mimi!! akasema Meshack kwa sauti kali.Ghafla kukatokea kitu ambacho hakuna aliyekitegemea.Elvis aligeuka haraka kwa kasi na kumtandika Meshack Jumbo ngumi nzito iliyomfanya apepesuke akamfuata na kumtandika kichwa kizito Meshack akaanguka chini.Hakuwa na fahamu "Steve mchukue kamfungie chumbani.Haweze kuwa kikwazo kwetu kufanikisha kazi zetu!! akaamuru Elvis na Steve akamvuta Meshack Jumbo hadi chumbani akamfungia "Elvis wazee kama hawa hawahitaji nguvu kubwa kuwanyamazisha.Tayari wamejichokea unaweza ukampiga kichwa kizito na ukajikuta umemmaliza kabisa.Kwa bahati nzuri mzee huyu ana mazoezi vinginevyo kwa kichwa kile angeweza kupoteza kabisa maisha" akasema Steve huku akicheka "Kaniudhi sana yule mzee na atakaa humo humo hadi pale tutakapokamilisha operesheni yetu.Tuachane na hayo ya mzee tuendelee na kazi yetu..... .." akasema Elvis na kengele ikalia Steve akatoka kwenda kuangalia mgongaji alikuwa ni Dr Philip akiwa amerejea na dawa pamoja na damu kwa ajili ya Vicky.Hakutaka mazungumzo mengi akaelekea moja kwa moja katika chumba alimo Vicky akaendelea kumuhudumia "Tumuache Dr Philip aendelee kumuhudumia Vicky sisi tuendelee na kazi.Steve kuna jambo lingine tumeligundua pia.Waziri mkuu mstaafu David na Frank wanafahamiana na ukitazama simu ya Frank utagundua David amempigia zaidi ya mara nne ila simu haikupokelewa na akaamua kutuma ujumbe kwamba ampigie kuna suala la muhimu.Tayari picha imekuja kuwa hata David naye lazima atakuwa katika mtandao wa akina Frank.Kama David naye yumo katika mtandao wa akina Frank hii inaaashiria kwamba katika suala hili la mipango ya mapinduzi hata hawa akina Frank nao wapo pia.Tuendelee kuchunguza zaidi na tutafahamu mambo mengi na ndiyo maana nimemkatalia mzee Jumbo kwamba tusimjulishe kwanza rais kuhusiana na hili suala hadi hapo tutakapokuwa tumepata ushahidi wa kujitosheleza.Hili si suala la kukurupuka na kumueleza rais.Tumueleze pale tutakapokuwa tayari na ushahidi wa kutosha"akasema Elvis "Ninakubaliana na maamuzi yako ya kumfungia yule mzee chumbani.Kwa maelezo haya yaliyopatikana mchezo unazidi kuwa mtamu.Hawa hawa ambao tulikuwa tunawatafuta kwa uuzaji wa silaha ndio hawa hawa wanaosuka mipango ya kuiangusha serikali.Huko mjini hivi sasa ni heka heka kubwa.Barabara nyingi zimefungwa kufuatia vurugu kubwa zinazoendelea.Watu hawa inabidi tule nao sahani moj............." akasema Steve na kunyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni Juliana "Juliana habari ya muda huu?Vipi maendeleo yako?akauliza Steve "Ninaendelea vyema Steve.Nimekupigia kukujulisha kwamba Patricia hayuko tena hapa nyumbani tayari amehamia ikulu" "Thats good news" akasema Steve "Jambo la pili ni kwamba mpaka sasa sijafanikiwa kuingia chumbani kwa mama.Chumba chake kimefungwa na hakuna anayeruhusiwa kuingia zaidi yake.Ninaomba univumilie na nikipata nafasi baadae nitaingia na kuchukua kompyuta zake" "Sawa Juliana endapo utafanikiwa utanijulisha ila tunaihitaji sana kompyuta hiyo.Jitahidi kila uwezavyo kuipata" akasema Steve na kuagana na Juliana "Anasemje Juliana?akauliza Elvis "Ana taarifa mbili.Kwanza ni Patricia' "Kafanya nini Patricia? akauliza Elvis "Patricia tayari ameondoka pale nyumbani kwao na ameelekea ikulu" "Oh thank you Lord" akasema Elvis "Taarifa ya pili ni kwamba mpaka sasa bado hajafanikiwa kuingia chumbani kwa mama yake hivyo bado hajaipata kompyuta ile tunayoihitaji" akasema Steve.Elvis akafikiri kidogo halafu akasema Frank ana mahusiano na Elizabeth na mpaka sasa ninaamini hajafahamu kama Frank amekufa hivyo tutafanya jambo moja.Kwa kutumia simu ya Frank tutamtumia ujumbe Elizabeth na kumuelekeza afike katika ile nyumba ulimo mwili wa Frank na ataamini kuwa ujumbe huo umetoka kwa Frank hivyo atafika mahala hapo.Lengo ni kumuondoa nyumbani ili Juliana aweze kupata nafasi ya kuingia chumbani kwake na kuichukua kompyuta tunayoitaka" "Huo ni mpango mzuri sana.Akifika pale atakutana na mshangao wa mwaka." akasema Steve "Haitaishia hapo.Tutamtumia pia ujumbe David naye atafika mahala hapo hapo na watakutana.Lengo hapa ni kumuondoa David nyumbani ili tuweze kumpata Dr Makwa Tusangira ambaye amejificha nyumbani kwa David akihofia kukamatwa na polisi.Tukimpata Makwa atatueleza kila kitu na tutaweza kuwafahamu pia watu wengine ambao wanashiriki pia katika mpango huu wa kuipindua serikali" akasema Elvis "Huo nao ni mpango mzuri lakini swali langu ni kwamba ni jambo lipi hasa tunalishughulikia kwa sasa.Kutafuta mtandao wa silaha au kuuzima mpango wa mapinduzi?akauliza Steve "Kutokana na umuhimu wake na uharaka kwa sasa tujikite zaidi katika kulizima jaribio hili la mapinduzi.Katika suala la silaha tayari tumepiga hatua kubwa.Tumewafahamu wahusika wakuu na sasa tunaendelea kumtafuta Patrice Lwibombe na nina uhakika mkubwa kwamba haitachukua muda mrefu kabla ya kumfahamu ni nani na yuko wapi.Kwa ufupi naweza kusema kwamba tunakwenda na mambo yote mawili kwa wakati mmoja kwani watu hao hao wanaohusika na biashara ya silaha ni hao hao wanaoonekana kuhusika pia katika mpango wa mapinduzi" "Sawa Elvis basi tuanze maandalizi ya kazi ya jioni ya leo kwenda kuvamia nyumbani kwa David na kumchukua Dr Makwa Tusangira" akasema Steve kisha wakaendelea na mipango kuhusiana na kazi ya usiku ya kuvamia nyumbani kwa David na kumchukua Dr Makwa Tusangira.









    Elizabeth akiwa na waombolezaji wengine waliokuja kumfariji kufuatia kifo cha mumewe akausoma ujumbe ulioingia katika simu yake.Ulitoka kwa Frank "Naomba tukutane saa moja na nusu mtaa wa Luvigo nyumba No 63.Kuna jambo zito la muhimu sana kuhusiana na mipango yetu nataka tulizungumze.Kuna mtu muhimu sana ambaye tutakutana naye atakayetusaidia sana katika masuala yetu.Hivi sasa niko katika mazungumzo naye" Elizabeth akarejea tena kuusoma ujumbe ule halafu akajibu "Frank siwezi kufika huko mahala unakotaka nije.Naomba wewe na huyo jamaa mfike hapa nyumbani ,nina wageni wamekuja kunifariji siwezi kuwaacha" akautuma ujumbe ule na baada ya sekunde kadhaa ukarejea ujumbe akaufungua na kuusoma "Ni mtu mzito na hataki kuonekana na watu wengi hivyo ametaka tukutane hapo mahala nilipokueleza.Tafadhali jitahidi ufike muda huo bila kukosa" Elizabeth akausoma ujumbe ule na kutafakari halafu akajibu "sawa nitafika ila ninaomba kikao kisichukue muda mrefu ,sitaki wageni wangu wanaokuja kunipa pole waboreke" Baada ya kuutuma ujumbe ule akampigia simu David "Madam Elizabeth.Habari za jioni? "Habari nzuri David.Naamini unalo jibu zuri mpaka sasa.Yule mtu amepatikana?Amekwisha hojiwa kuhusu Elvis? "Mpaka sasa bado sijapata mrejesho wowote kutoka kwa Dr Shafi ambaye nilimpa jukumu hilo la kuhakikisha Meshack Jumbo anapatikana.Nilizungumza naye muda fulani bado hakuwa amepokea taarifa kutoka kwa watu aliowatuma.Nitampigia baadae kidogo kumuuliza alikofikia kwani hivi sasa hapatikani simuni yuko katika kikao na rais" "David nilikuelekeza suala hili lifanyike haraka sana kabla ya jua kutua lakini mpaka sasa hakuna majibu yoyote ya kuridhisha.Hili si suala la kufanyia masihara David.Ni suala muhimu mno.Tunahitaji kujiridhisha kama Elvis kweli amekufa au yuko hai.Hatuwezi kuzipuuza taarifa za kuonekana kwake hai.Endapo ukishindwa kupata taarifa hadi kesho asubuhi basi itatulazimu kubomoa kaburi lake na kujiridhisha kama kweli yumo kaburini au kifo chake kilikuwa ni kiini macho.Elvis ni mtu hatari sana kuwepo hai" akasema Elizabeth "Madam Elizabeth naomba nikuondoe hofu kwamba jambo hilo litafanikiwa na nina uhakika kwamba hadi mida hii tayari watu waliotumwa kumtafuta watakuwa wamekwisha mpata na yuko mahala akisubiri kuhojiwa.Makamu wa rais atakapomaliza kikao na rais atanijulisha kila kitu" "Sawa David.Utanijuliha pindi ukipata taarifa yoyote kutoka kwa makamu wa rais" "Nitakujulisha Madam.Vile vile kuna suala nataka nikujulishe ingawa naamini hadi mida hii tayari utakuwa umekwisha lisikia.Tayari operesheni imeanza na hadi hivi sasa kuna vurugu kubwa inaendelea mtaani.Vijana wanaendelea kupambana na polisi na tunashukuru kwa siku hii ya kwanza mambo yamekwenda vyema.Mpaka sasa kuna idadi kubwa ya vifo na majeruhi.Matukio yote yamerekodiwa na timu iliyopewa jukumu hilo la kurekodi kila kitu na kuanzia kesho matuko yote ya mauaji ya raia yataanza kurushwa katika vyombo vya habari vikubwa duniani na dunia itaanza kupaaza sauti kulaani mauaji hayo na wakati huo huo maandamano na vurugu vitaendelea katika mikoa mingine na itafika mahala ambapo serikali itashindwa kuyadhibiti maandamano na hapo ndipo jeshi litakapoingilia kati na kuchukua nchi" akasema David "Kazi nzuri sana David.Sina wasiwasi kabisa kuhusu suala hili nina imani mahala ulipo hapaharibiki kitu.Utakuwa rais wa Tanzania muda si mrefu sana ila zingatia suala la Elvis"akasema Elizabeth huku akitabasamu "Inshaallah.." akasema David na kukata simu,akajaribu kumpigia makamu wa rais lakini simu yake haikuwa ikipatikana "Bado yuko kwenye kikao" akawaza na mara ukaingia ujumbe uliotoka kwa Frank haraka haraka akaufungua na kuusoma "David nimeshindwa kupokea simu zako niko katika kikoa muhimu na watu fulani muhimu sana ambao watatusaidia mno katika kufanikisha mpango wetu.Ninakuomba tukutane saa moja na nusu mtaa wa Luvigo nyumba namba 63.Kuna mambo mazito ya kujadili na hawa jamaa.Fika bila kukosa" David akatabasamu baada ya kumaliza kusoma ujumbe ule "Ninachompendea Frank ni mtu wa mipango.Naamini atakuwa amepata watu wazito wa kutusaidia katika operesheni yetu" akawaza halafu akarejea katika ofisi yake alipokuwapo Dr makwa. "Vipi maendeleo Dr Makwa? "Mpaka sasa kwa taarifa nilizozipokea kuna watu zaidi ya ishirini wanaripotiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa wengine vibaya sana.Nimetaarifiwa kwamba mapambano bado yanaendelea na polisi wanaendelea kutumia silaha za moto kukabiliana na vijana.Mambo yanakwenda vizuri sana David na tufanikiwa" akasema Dr Makwa. ******************* Saa moja na dakika kumi na moja Elizabeth akiwa na walinzi wake wawili wakaondoka bila kuaga mtu yeyote.Tayari Steven alikwisha mjulisha Juliana mpango waliouanda ili kumuondoa mama yake pale nyumbani hivyo Juliana alikuwa makini akimchunguza mama yake na mara tu alipoondoka akamfuata Editha mtumishi wa nyumba ile ambaye anaaminiwa sana na mama yake "Mama Editha ninaomba funguo ya chumbani kwa mama kuna kitu nakihitaji nimepigiwa simu na watu wa Uingereza sasa hivi na mama ametoka" akasema Juliana na yule mwangalizi wa nyumba ambaye huishi hapa wakati wao wakiwa Uingereza hakuwa na wasi wasi hata chembe akampa funguo ya akiba Juliana akaenda kufungua chumbani kwa mama yake na kuchukua kompyuta mbili ndogo zilizokuwa mezani akatoka na kumrejeshea yule mama funguo kisha akaingia garini na kumpigia simu Steve. "Steve tayari nimezipata zile kompyuta.Tukutane wapi ili nikupatie uzipitiea?Inabidi tufanye haraka haraka kabla mama hajarejea" akasema Juliana na Steve akamuelekeza sehemu ya kukutana "Omola una hakika utaweza kumaliza kwa haraka kuzikagua kompyuta zote mbili kabla Elizabeth hajarejea nyumbani kwake? akauliza Elvis wakiwa garini wakielekea nyumbani kwa David "Sina hakika kama tunaweza kumaliza kukagua kila kitu kwa muda huu mfupi.Nashauri tuogozane na Juliana ili niweze kupata nafasi ya kuendelea kuzikagua tukiwa garini na mara tu mtakapomaliza na mimi nitakuwa nimemaliza" akasema Omola Hilo haliwezekani.Juliana hapaswi kujua kama niko hai.Yule ni mtu wa karibu sana na Patricia" akasema Elvis "Tayari anajua kila kitu" akasema Steve aliyekuwa katika usukani na Elvis akamtazama kwa mshangao "Anajua?!!..Amejuaje?akauliza "Nilimueleza kila kitu" "Oh Steve kwa nini ukafanya hivyo? "Utanisamehe Elvis,nililazimika kumueleza ukweli ila alielewa na hawezi kumueleza kitu Patricia" "Ulifanya kosa kubwa Steve kumueleza Juliana kwamba niko hai" " Nilikuwa na Steve alipomueleza Juliana na hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumueleza na niliyesababisha hadi akajua ni mimi.Unatakiwa unisamehe sana kwani sikujua kama Juliana ni mtu wa karibu sana na mkeo" akasema Omola "Ok tuachane na hilo.Mnashauri tufanye nini?akauliza Elvis "Nashauri tuongozane na Juliana kama alivyoshauri Omola ili wakati tukiwa katika operesheni yetu yeye atabaki garini na atakuwa anatusaidia kufahamu kila kinachoendelea hapo kwa David kwa ile kamera maalum atakayoirusha na wakati huo huo atakuwa anendelea kuzipitia kompyuta za Elizabeth" akasema Steve "Sawa hakuna tatizo" akasema Elvis na safari ikaendelea kuelekea mahala walikopanga kuonana na Juliana Saa moja na dakika arobaini na tatu Elizabeth akawasili mahala alikoelekezwa na kulikuta gari moja nje.Kwa mwangaza mkubwa wa taa iliyokuwapo getini aliweza kumtambua mtu aliyekuwa nje ya lile gari alikuwa ni David. "David ?!! akashangaa "Amefuata nini hapa?akajiuliza.Akafunguliwa mlango akashuka na kumfuata David ambaye alishangaa sana alipomuona Elizabeth pale "Madam Elizabeth !! akasema kwa mshangao "David " akasema Elizabeth "Mbona uko hapa mida hii madam?akauliza akionekana kuwa na wasiwasi "Wewe nawe unatafuta nini hapa? "Nimeitwa na Frank.Alinitaka tukutane hapa.Nimefika na kubonyeza kengele ya getini lakini hakuna aliyekuja kufungua.Najaribu kupiga simu yake haipatikani" akasema David Hata mimi Frank amenitumia ujumbe na kunitaka nikutane naye hapa mida hii kuna mtu muhimu wa kuzungumza naye" akasema Elizabeth Walikaa hapo nje kwa dakika zaidi ya kumi ndipo David aliyekuwa ameongozana na walinzi wawili akamtuma mmoja kujaribu kupanda ukuta na kuchungulia ndani kama kuna dalili zozote za kuwepo watu.Mlinzi yule kwa haraka akisaidiwa na mwenzake akapanda ukutani na kuchungulia ndani akaziona gari mbili "Naona kuna gari mbili ziko humu ndani " akasema yule jamaa "Kama wapo humu ndani kwa nini hawafungui geti?Hawasikii kengele? Au yawezekana kengele ni mbovu" akasema Elizabeth na mmoja wa wale vijana wa David akalisogelea getu na kugundua mlango mdogo wa pembeni ya geti haukuwa umefungwa akausukuma ukafunguka,David akatabasamu "Muda wote huu tumekaa hapa nje hatukukumbuka hata kuangalia kama mlango uko wazi.Nenda ndani wajulishe kuwa mimi na madam tuko hapa nje " akasema David na yule jamaa akaelekea ndani.Baada ya dakika tatu akarejea kwa kasi "What happened? akauliza David "Mzee hakuna dalili za kuwepo mtu humu ndani na kilichonistua nimeona kuna alama za damu sakafuni" David na Elizabeth wakatazamana "Madam let's get out of here.Hapa si sehemu salama.Nahisi kuna hatari" akasema David kwa wasi wasi No.We're not going anywhere! akasema Elizabeth na kuwaita walinzi wake na wale wa David "Tunaingia humu ndani,tunakwenda kuangalia hizo damu zimetoka wapi?Kama kuna hatari yoyote tutakabiliana nayo" akasema Elizabeth na akiwa ameongozana na wale walinzi wakaingia ndani.Kulikuwa kimya sana na hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu ndani.Walipofika katika mlango wa kuingilia sebuleni wakakutana na alama za damu. "Hizi ni alama za kiatu ambacho kimepita juu ya damu" akasema Elizabeth ,mlango wa sebuleni ulikuwa wazi wakaingia ndani.Hakukuwa na mtu http://deusdeditmahunda.blogspot.com/sebuleni na zile alama za kiatu zilizokanyaga damu zikaonekana.Elizabeth akawataka wale walinzi watawanyike vyumbani kukagua damu ile imetoka wapi na kama kuna mtu yeyote ndani ya ile nyumba yeye akabaki sebuleni akiwa na David.Baada ya dakika mbili mmoja wa walinzi akaja na kumtaka Elizabeth aongozane naye.Akampeleka hadi katika chumba kulimokuwa na miili ya watu wawili waliouawa kinyama sana. "Frank!!! Oh my God !!! akasema David kwa mstuko mkubwa.Elizabeth alipigwa na butwaa akahisi baridi ikimpenya mwilini.David alihisi kutetemeka mwili kutokana na woga wa ghafla uliompata "Madam let's get out of here! Who ever did this must be around !! akasema David kwa woga "Quis unquam hoc esse non reddere!! akasema Elizabeth kwa lugha ya kilatini akiwa na maana yeyote aliyefanya vile lazima alipe.Elizabeth akapiga magoti na kumtazama Frank. "Mauaji haya yamefanyika muda mrefu na si hivi karibuni.Aliyefanya mauaji haya alitaka tuje tushuhudie alichokifanya na ndiyo maana akatumia simu ya Frank kututumia jumbe akitutaka tufike hapa akiamini kwamba tukifika hapa tutashuhudia alichokifanya.Alichokitaka amefanikiwa na ujumbe umefika.Tumeona alichokifanya na kinachofuata naye asubiri salamu zangu!!! akasema Elizabeth kwa hasira kisha akamtaka David watoke nje "Nani lakini kafanya ukatili huu? akauliza David kwa sauti yenye kitetemeshi ndani yake "Kwa mazingira yalivyo ndani ya chumba kile, inaonekana kulikuwa na mapambano makubwa lakini amewaua watu wangu kikatili sana.Mtu aliyefanya mauaji yale lazima ni mtu mwenye ujuzi wa hali ya juu na mbinu za kupambana.Sikutegemea kabisa kama Frank angeweza kuuawa namna hii tena kwa wakati huu ambao tunamuhitaji sana!! akasema Elizabeth "Madam hapa nilipo nimechanganyikiwa na sijui nini cha kufanya.Frank alikuwa ni kila kitu katika mipango yetu" akasema David na kuinamisha kichwa chini "Kuna taarifa zozote kutoka kwa makamu wa rais kuhusiana na Meshack Jumbo?akauliza Elizabeth "Hapana sijapokea taarifa zozote kutoka kwake mpaka sasa" "Call him again" akasema Elizabeth.David akachukua simu na kumpigia makamu wa rais Dr Shafi lakini bado simu yake haikuwa ikipatikana Bado simu yake haipatikani"akasema David.Elizabeth akafikiri kidogo kwa muda halafu akasema "Twende tuondoke David tusije tukakutwa hapa na polisi kwani yawezekana huu ukawa mtego ili tukutwe hapa na tukaonekana wauaji "akasema Elizabeth wakaondoka **************** Steve aliyekuwa dereva aliendesha gari hadi mahala walikopanga wakutane na Juliana, akaegesha gari na kumpigia simu Juliana akamjulisha kwamba tayari wamefika na dakika chache baadae Juliana akawasili na kumpigia simu Steve akamtaka amuelekeze mahala walikoegesha gari lao.Juliana akashuka garini akiwa amebeba kompyuta mbili.Steve akashuka akampokea kompyuta zile akamfungulia mlango na kuingia ndani "Hallo Juliana" akasema Omola "Habari Omola." akasema Juliana "Juliana una hakika kwamba hakuna mtu aliyekuwa anakufuatilia? "Naamini hakuna" akasema Juliana "Ok good.Let's go" akasema Steve na kuwasha gari "Tunaelekea wapi?nahitaji kurejea nyumbani haraka kabla mama hajarudi.Huko mlikomtaka aende mna hakika atachukua muda mrefu?akauliza Juliana "Tunahitaji muda kidogo wa kuweza kuzipitia komputa zote na ili kupata muda huo inabidi Omola afanye kazi hii wakati akiwa garini kwani tunamuhitaji pia huko tuendako.Usijali Juliana hatutachukua muda mrefu" akasema Steve "By the way .." akasema Steve "Kuna mtu muhimu sana ambaye hatukuwa tumekutambulisha kwake.Kutana na Elvis" akasema Steve na kunyamaza kidogo halafu akasema "Elvis kutana na Juliana" Elvis aliyekuwa amekaa kiti cha mbele pembeni ya Steve akageuka na kumtazama Juliana "Hallo Juliana" "Hallo .El..Elvis" akasema Juliana kwa sauti yenye kitetemeshi "Juliana ahsante sana kwa kuwa karibu na Patricia" "Usijali Elvis.Patricia ni mtu wangu wa karibu sana.Nimefahamiana naye muda mrefu toka angali mnasoma kule Tanga" akasema Juliana Juliana kuna jambo nataka niliweke sawa.Umefahamu siri hii kubwa ambayo ni watu wachache sana wanaoifahamu hivyo nataka asifahamu mtu mwingine yeyote hasa Patricia.Tumeelewana? akauliza Elvis "Hakuna tatizo Elvis.Your secret is safe with me" akasema Juliana "Good." akasema Elvis na safari ikaendelea "Omola kuna chochote umekipata katika kompyuta hizo?akauliza Elvis baada ya Omola kuanza kuzikagua kompyuta zile alizoleta Juliana "Naendelea kupekua.Nahitaji muda kidogo" akajibu Omola Walifika eneo la Chongwe na kushika njia inayoelekea Chongwe kwa waziri mkuu.Ni eneo lililo kimya sana ambako hukaa matajiri na viongozi.Waliiacha njia inayoelekea nyumbani kwa waziri mkuu mstaafu wakachepuka na kufuata njia iliyokuwa inaelekea karibu na hospitali ya Huruma,wakakunja kulia na kufuata barabara inayoelekea katika soko la samaki halafu wakaingia mtaa wa Uwemba.Kiwanja cha waziri mkuu mtaafu David kilikuwa na ukubwa wa ekari kumi na nane hivyo kiliweza kutokeza hadi katika mtaa huu wa Uwemba.Kiwanja kilikuwa kimezungushiwa ukuta mkubwa na juu ya ukuta huo kukawekwa nyaya maalum za umeme kuongeza ulinzi.Sehemu kubwa ya eneo hili la waziri David lilikuwa ni shamba la matunda mbali mbali.Steve akasimamisha gari pembezoni mwa barabara . "Hapa panafaa sana.Hili ni eneo la nyuma na huku kote kuna shamba la matunda." akasema Steve wakashuka na kufungua boneti ya gari halafu wakaweka alama za pembe tatu mbele na nyuma ya gari ili yeyote atakayewaona ajue gari lile lilikuwa na hitilafu.Omola akatoa kamera ndogo iliyotengenezwa mithili ya ndege akaiweka betri na kuiwasha halafu akaiunganisha na kompyuta yake akairusha kuelekea ndani.Kwa yeyote ambaye angeiona angedhani ni ndege kutokana na muonekano wake.Alikuwa anaiongoza kwa kutumia kompyuta yake na ilikuwa inaleta picha moja kwa moja katika kompyuta.Aliipeleka taratibu ili kusoma hali ya ulinzi ilivyo ndani ya jengo lile.Wakati kamera ikieleka ndani Steve na Elvis walikuwa wanajiandaa kuingia ndani kwa kupitia ukutani.Kila mmoja alikuwa ameweka sikioni kifaa maalum cha kuwawezesha kuwasiliana na Omola ambaye atakuwa akiwaongoza kwa kutumia ile kamera ndege aliyoirusha mle ndani. Walipokuwa tayari wakausogelea ukuta na kwa haraka Elvis akawa wa kwanza kuupanda hadi juu na bila kugusa nyaya zile za umeme akaruka na kutua ndani,Steve naye akafanya hivyo kisha wakaanza kuelekea ndani wakifuata ujia uliokuwepo kati ya mstari mmoja wa matunda na mwingine.Walitembea kwa tahadhari kubwa hadi walipotokeza katika eneo pana la wazi ambalo kati kati yake ndipo lilipokuwepo jumba la David. "Omola ,Omola unanipata?akauliza Elvis "Ninakupata Elvis.." "Vizuri.Tayari tumetokeza katika eneo la wazi na kutokea hapa tunaweza kuiona nyumba.Tuelekeze njia kama tayari umepata picha ya eneo lilivyo" "Kwa picha nilizozipata hakuna watu eneo hilo la nyuma na nimeona kuna walinzi wawili tu wakiwa eneo hilo lakini waliondoka na hawajarejea tena.Upande wa mbele kuna walinzi watatu ambao kwa picha niliyoipata wamekaa nje wanapata chakula.Piteni kwa kutumia mlango wa nyuma uliopo karibu na bwawa la kuogelea" akasema Omola. "Nitatangulia" akasema Elvis na kuchomoka kutoka pale mahala walipokuwa akaanza kuelekea katika mlango wa nyuma uliokuwa karibu na bwawa la kuogelea.Kulikuwa kimya kabisa na hakukuwa na mtu yeyote eneo hili.Akaenda kujificha nyuma ya pipa la maji.Steve naye akafanya kama alivyofanya Elvis Elvis nimewaona tayari.Hakuna hatari yoyote mpaka sasa mnaweza kuendelea" akasema Omola na akina Elvis wakainuka kutoka pale nyuma ya pipa la maji wakaangaza halafu wakatembea kwa tahadhari kuelekea mlangoni.Mara tu walipofika mlangoni akasikika mtu akizungumza na simu akielekea kule kule mlangoni. kwa haraka sana wakajificha nyuma ya sanamu ya Simba iliyokuwepo karibu na mlango. Mlango ukafunguliwa akatoka mwanamke mmoja akizungumza na simu.Hakuwa na hofu yoyote na wala hakujua kama kulikuwa na watu wamejificha hapo karibu.Mwanamke yule aliendelea kuzungumza na simu na akaenda kukaa katika eneo la bembea za watoto .Elvis na Steve wakautumia mwanya huo wakatoka taratibu katika ile sanamu na kuingia ndani wakazima taa halafu wakajibanza pembeni ya mlango.Yule mwanamke alipomaliza kuzungumza na simu akarejea ndani "Loh ! taa imeungua ?akasema baada ya kukuta taa imezimika.Akaufungua mlango na kuingia ndani ghafla akajikuta akikabwa na mkono yenye nguvu na kuzibwa mdomo "Ukitaka kuwa salama usipige kelele yoyote.Nyamaza hivyo hivyo" akasema Steve aliyekuwa amemkaba yule mwanamke. "Tuonyeshe mahala alipo Dr Makwa yule mgeni wa David" akasema Elvis "Naombeni msiniuie jamani nitawaonyesha mahala alipo" akasema yule mwanamke kwa sauti ndogo ya wasi wasi. Kuna watu wangapi humu ndani? "Kuna watu saba humu ndani.Wengine wako sebuleni wakiangalia runinga" akasema yule mwanamama "Haraka tupeleke alipo Dr Makwa" akasema Elvis na yule mwanamama akaanza kuwaongoza kuelekea katika chumba alimokuwamo Dr Makwa. "Chumba chenyewe hiki hapa" akasema yule mwanamama kwa sauti ndogo.Steve aliyekuwa nyuma ya yule mama akamkaba na kumpoteza fahamu akamlaza chini taratibu Elvis akausogelea mlango na kugonga taratibu,mlango ukafunguliwa na jamaa ambaye alikutana na pigo moja kali la uso akaangukia ndani kisha Elvis akajitoma ndani akiwa na bastora yake.Kitendo kile kiliwastua sana wale jamaa waliokuwemo mle ndani.Mmoja wa wao akachomoa bastora haraka kutoka katika koti lake lakini Elvis alikwisha muona na kwa wepesi wa aina yake akaachia risasi zilizomsambaratisha na kumrejesha kwa mola wake.Dr Makwa ambaye naye alikuwemo mle ndani akapatwa na mstuko mkubwa sana akajificha chini ya meza.Elvis akamfuata na kumtaka atoke haraka sana.Huku akitetemeka Dr Makwa akatoka chini ya meza "Vijana wangu tafadhalilini nitawapa kila mnachokihitaji.Nitawapa pesa yoyote ile mnayoitaka,magari na kitu chochote kile" akasema huku akitetemeka "Shut up !! akasema Elvis Yule jamaa aliyepewa pigo akaangukia ndani na kujifanya amepoteza fahamu akatoa bastora yake taratibu lakini Steve aliyekuwa amesimama mlangoni alikiona kitendo alichotaka kukifanya yule jamaa na hakuchelewa akamsambaratisha haraka.Dr Makwa akazidi kutetemeka na Elvis hakumpa nafasi ya kujieleza akampa pigo kali akaanguka chini na kupoteza fahamu "Omola,tayari tumempata Dr Makwa tunaanza kutoka nje.Vipi hali ya usalama huko? akauliza Elvis "Nje ninaona hali nzuri.Hakuna ulinzi wowote huku nyuma.Walikuja watu wawili kuchungulia na kuondoka.Walinzi wote wamejirundika sehemu ya mbele" akasema Omola na Steve akambeba Dr Makwa akamuweka begani wakaanza kutoka mle ndani wakitumia njia ile ile waliyopita.Hawakukutana na mtu yeyote hadi walipokaribia kufika katika mlango wa kutoka nje. "Omola tunatoka nje kuna mtu yeyote umemuona? akauliza Elvis "Hakuna mtu yeyote huku nje"akasema Omola.Elvis akaufungua mlango wa kutokea nje wakaanza kuondoka kwa tahadhari kubwa wakipita njia ile ya kuelekea katika shamba la matunda.Wakafika sehemu ile waliyoitumia kuingilia Elvis akapanda na kukata zile nyaya za umeme halafu wakampandisha Dr Makwa na kumshusha kwa nje wakampakia katika buti ya gari na kuondoka kwa kasi "Kuna chochote umekipata kutoka katika kompyuta hizo? Elvis akamuuliza Omola. "Ninamalizia kupekua" akasema Omola na safari ikaendelea hadi walipoliacha gari la Juliana.Omola akamkabidhi kompyuta zake mbili "Juliana ahsante sana.Tutakujulisha nini tumekipata kutoka katika kompyuta hizi.Kwa sasa jitahidi uweze kuwahi kuzirejesha ulikozitoa na kama utahisi kuna hatari yoyote ile kutoka kwa mama yako tujulishe tafadhali na tutakusaidia" akasema Elvis "Ahsanteni sana Elvis nitaendelea kuwasiliana nanyi na nitawajulisha kama kutakuwa na hatari yoyote" akasema Juliana akaondoka na kuingia katika gari lake.Akina Elvis walihakikisha ameondoka ndipo nao wakaondoka "Kuna kitu umekipata kutoka katika zile kompyuta? akauliza Elvis "Kuna vitu vingi nimevipata kutoka katika komputa zile hasa ile ndogo nyekundu.Nimekuta kuna taarifa mbalimbali za kifedha ambazo ili kuzifahamu vyema tutalazimika kuwa na mtaalamu wa mambo haya ya fedha.Inaonekana hizi ni taarifa za fedha anazotumiwa na wataalamu wake wa mahesabu karibu kila siku.Ni fedha nyingi sana zinazoonekana katika taarifa hizo, pamoja na taarifa hizo kuna kitu kingine nimekigundua.Nimekuta picha ya aina ya silaha wanazoziuza.Ni bunduki za hali ya juu na za kisasa mno.Ukiacha silaha hizo kuna mawasiliano ya barua pepe ya mtu anayetumia jina la Stella Kendrick.Hili ninaamini ni mojawapo ya majina ya Elizabeth anayotumia.Katika mawasiliano hayo Stella anawasiliana na mtu mmoja anayetumia anuani ya mk3001 na nilipodukua zaidi nikafahamu jina la mtu huyo ni Keneth Mwaibuka ambaye alimjulisha kuhusu kukwama kwa makontena kumi na mbili bandarini na Keneth akaahidi kulishughulikia suala hilo kwa haraka.Vile vile akamjulisha kuwa magari manne ambayo yamezuiliwa kwa kigezo cha kodi akamtaka ahakikishe magari hayo yanatolewa haraka bandarini.Inaonyesha huyu jamaa ndiye anayetumika katika kusaidia kutoa mizigo ya silaha na vitu mbalimbali bandarini." akasema Omola "Tutamchunguza na tutamjua ni nani.Huyu naye ni mtu muhimu pia.Kuna kingine ambacho umekigundua? "Nimepata pia mawasiliano kati ya Shanon na Patrice Lwibombe.Mengi wanayozungumzia ni masuala ya kifedha.Bado sijafanikiwa kumpata huyu Patrice ni nani na yuko wapi" Tumeshindwa tena kumpata Patrice ni nani lakini msikate tamaa tutamfahamu tu.Kwa kuwa tayari tumewafahamu wahusika wakuu ni akina nani tusiumize kichwa sana kwani kupitia kwao tutaweza kumfahamu Patrice ni nani.kwa sasa tuelekeze nguvu katika kuyazima mapinduzi haya yanayotaka kufanyika" akasema Elvis Waliwasili katika makazi yao na Graca akawafungulia geti.Elvis akagundua kitu katika sura ya Graca "Graca kuna tatizo lolote? akauliza Elvis "Hali ya Vicky ilibadilika ghafla na ikamlazimu Dr Philip amuondoe hapa na kumpeleka hospitali.Alijaribu kuwapigia simu lakini nyote simu zenu zilikuwa zimezimwa.Mpaka sasa hatujui hali yake ikoje" akasema Graca na ndipo Elvis akakumbuka kweli kwamba alikuwa amezima simu na kuiwasha akampigia simu Dr Philip akitaka kufahamu hali ya Vicky inaendeleaje "Elvis hali ya Vicky ilibadilika ghafla na nikalazimika kumleta hospitali.Nilitaka kuwajulisha lakini simu zenu zote hazikuwa zikipatikana" "Vipi sasa hali yake inaendeleaje? "Elvis ninajitahidi sana kufanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya Vicky but I have to be honnest with you brother,I dont know if she's going to make it.Mimi ni daktari na ninajua ninachokisema" akasema Dr Philip na Elvis akavuta pumzi ndefu. "Dr Philip sijui niseme nini lakini nakuomba ufanye kila kinachowezekana ili kujaribu kuokoa maisha yake.We still need her" akasema Elvis kisha akaingia ndani Nimewasiliana na Dr philip hali ya Vicky si nzuri na hana uhakika kama atapona.She needs our prayers right now" akasema Elvis na wote wakashikana mikono na Graca akaongoza maombi kumuombea Vicky. "Now let's get back to work" akasema Elvis baada ya kumaliza maombi.Dr Makwa akachukuliwa na kuingizwa katika chumba kinachotumika kama stoo akavuliwa shati na kufungwa barabara katika kiti halafu Elvis akachukua kichupa fulani kidogo akakifungua na kumuwekea Dr Makwa puani akapiga chafya mfululizo.Steve akamsogelea na kumnasa vibao viwili na ndipo Dr Makwa akapata fahamu "Please dont kill me!! akasema Dr makwa kwa uoga mwili ukimtetemeka.Elvis akavuta kiti na kuketi karibu yake "Habari yako Dr Makwa.Pole kwa misukosuko inayokukuta na samahani sana kwa kukuchukua kwa njia hii" "Ninyi ni akina nani mnataka nini kwangu? akauliza Dr Makwa "Kuna mambo machache ambayo nahitaki kuyafahamu kutoka kwako.Nataka kwanza uniambie kwa nini uko pale kwa waziri mkuu mstaafu David Sichoma? akauliza Elvis na Dr Makwa akainamsha kichwa.Steve akaenda nyuma yake na kumtandika kofi zito la shingo "Ukiulizwa unajibu haraka hatuna muda wa kupoteza!! akasema Steve kwa ukali. "Tafadhali msinipige jamani nina matatizo ya moyo" "Hautapigwa kama utajibu kila swali tunalokuuliza" akasema Steve Nitawajibu" akasema Dr Makwa "David ni rafiki yangu wa muda mrefu na pale kwake aliniita nikajihifadhi kwa sababu ninatafutwa na jeshi la polisi kwa kuandaa mkutano usiokuwa na kibali na kusababisha vurugu kubwa inayoendelea hadi hivi sasa mtaani" akasema Dr Makwa "Kwa nini ukafanya hivyo Dr Makwa? Kwa nini ukahamasisha kufanywa mkutano usiokuwa na kibali?Kwa nini ukapuuza agizo la jeshi la polisi lililopiga marufuku mkutano huo? "Sisi ni wanasiasa na tumekuwa tunaonewa na kunyanyaswa kwa muda mrefu hivyo tumeona wakati umefika wa kudai haki.Tunalilia haki yetu,tunataka nchi itawaliwe kwa misingi ya haki na si ukandamizaji unaoendelea hivi sasa"akasema Dr Makwa "Hakukuwa na njia nyingine ya kufanya kufikisha ujumbe wenu kwa serikali badala ya kuchochea vurugu? "Tumejaribu sana kufikisha kilio chetu serikalini lakini tumepuuzwa na sasa tumechoka tumeamua kudai haki yetu kwa lazima" akasema Dr Makwa "Sawa nimekuelewa.Nataka sasa utueleze familia yako iko wapi? "Familia yangu? "Ndiyo.Iko wapi? Dr Makwa akawa kimya.Steve aliyekuwa nyuma yake akamnasa tena kofi lingine kali la mgongo "Jamani mtaniua ...." "Jibu swali unaloulizwa.Familia yako iko wapi? "Familia yangu ipo" "Ipo wapi? "Ipo nyumbani" Unaweza kuwapigia simu? Dr Makwa akasita na kukaa kimya "Dr Makwa tafadhali jibu!! akasema Elvis "Familia yangu iko nje ya nchi" "Umeisafirisha familia yako nje ya nchi na kuwahamasisha watoto wa wenzako waingie mtaani kufanya vurugu na kuuawa.Kwa nini ninyi wanasiasa mnakosa ubinadamu?Unajua mpaka sasa ni vijana wangapi tayari wamekwisha poteza maisha kutokana na vurugu ulizoziasisi?akauliza Elvis "Vurugu wamezianzisha jeshi la polisi.Endapo wangeturuhusu kufanya mkutano wetu kwa amani mambo haya yote yasingetokea" "Nani unashirikiana nao katika kuandaa machafuko haya? Mimi na wenzangu hatukupanga machafuko bali tuliungana kwa pamoja ili kuweza kuandaa mkutano ambao tungeutumia katika kufikisha malalamiko yetu kwa serikali." "DrMakwa nimeanza kukuuliza maswali kwa upole na nitapenda kama tukiendelea na maongezi yetu namna hii hadi mwisho.Tafadhali usitulazimishe kutumia nguvu.Sisi si watu wabaya lakini ukitulazimisha tuwe watu wabaya utatamani ungekutana na mtoa roho kuliko sisi" akasema Elvis "Vijana nimewajibu vizuri sana kila mnachoniuliza.Sielewi ni kitu gani hasa mnakitafuta toka kwangu" akasema Dr Makwa.Elvis akamtazama kwa hasira na kusema "David anahusikaje katika machafuko haya yaliyoanza leo? David ?!! Dr Makwa akastuka sana "David hahusiki kwa lolote lile na haya yanayoendelea yule ni rafiki yangu tu" akasema Dr Makwa kwa wasi wasi. "Dr Makwa tumekuleta hapa tunafahamu kila kitu.David ni mmoja wa watu walio nyuma ya haya mliyopanga kuyafanya.Nini hasa lengo lenu?akauliza Elvis na Dr Makwa akawa kimya "Dr Makwa nataka uniambie ni akina nani wengine unashirikiana nao katika mpango huu wa mapinduzi?nafahamu wazo la kutaka kuipindua serikali halikuja hivi hivi lazima kuna watu wako nyuma yenu.Nani aliyewataka muipindue serikali? akauliza Elvis "Lengo letu sisi ni kuondoa serikali madarakani kwa kutumiamaandamano kama ilivyotokea katika baadhi ya nchi watu waliandamana na serikali zilizokuwa madarakani zikaachia ngazi.Hatuna lengo la kufanya mapinduzi kwa kutumia silaha" "Dr Makwa utaniudhi endapo utaendelea kuniambia uongo.Nataka unieleze ukweli mtupu kwani bila hivyo hautaweza kutoka hapa salama na mipango yenu yote itashindikana!! akasema Elvis na kumtaka Steve ailete kompyuta ya Omola .Steve akileta kwa haraka na Elvis akamchezea Dr Makwa mazungumzo yale ya David na makamu wa rais.Rekodi zile zilipomalizika Dr Makwa alikuwa anatiririkwa jasho.Elvis akaiuka na kuvua shati akamtaka Steve alete kisanduku chenye vifaa vya kutesea.Kisanduku kikaletwa na kuwekwa mezani wakati wa mzaha umekwisha sasa tunaanza kazi" akasema Elvis "Hayo uliowasikia ni mazungumzo ya unayedai ni rafiki yako waziri mkuu mstaafu David Sichoma pamoja na makamu wa rais Dr Shafi.Nadhani umekisikia kila walichokiongea.Ni wazi kinachoendelea hivi sasa ni moja ya mipango yenu ya kuiangusha serikali.Nani aliyeko nyuma yenu?Nani anayefadhili mpango huu wa uhaini?akauliza Elvis huku akichukua koleo dogo na kumtaka Steve amvue Dr Makwa suruali yake.Elvis akamvuta korodani na kuiminya kwa kutumia ile koleo na Dr Makwa akapiga ukelele mkubwa kwa maumivu makali aliyoyapata. "Huu ni mwanzo tu.Bado utapata mateso ya kila aina hadi pale utakapoeleza kila kitu kuhusiana na mipango yenu ya uhaini" akasema Elvis "Basi basi...nita...nitawaeleza kila kitu" akasema Dr Makwa akiwa katika maumivu makali "David alinifuata na kunitaka niwakusanye wakuu wote wa vyama vya siasa vya upinzani na akatueleza kwamba anataka atushirikishe katika mpango wa kuiondoa serikali madarakani na akasema kwamba jukumu letu katika mpango huo ni kuandaa vurugu ambazo zitasababisha serikali iliyoko madarakani iachie ngazi.Tukaandaa mkutano huu uliofanyika leo na hata pale ambapo jeshi la polisi liliupiga marufuku sisi tulishinikiza ufanyike kwa lengo la kuanzisha vurugu na jeshi la polisi.Kilichotokea leo na kinachoendelea kutokea ni matokea ya mipango yetu.Sikujua kama hata makamu wa rais yumo pia katika mpango huu.Mambo haya ninayosikia wakiyazungumza hayakuwepo kabisa katika makubaliano yetu" "Dr Makwa hili jambo mlilolipanga ni uhaini na endapo utafikishwa katika vyombo vya sheria adhabu yake ni kifungo cha maisha gerezani.Right now I'm your only help.Nitakusaidia endapo tu utaamua kunieleza ukweli wote wa kuhusiana mipango yenu.Kama utaamua kufunguka na kunieleza kila kitu nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kukusaidia kuepuka adhabu itakayokukabili endapo utafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.Nitakusaidia uweze kuungana tena na familia yako kwani vinginevyo hautaiona tena familia yako uliyoikimbiza nje ya nchi.Dr Makwa wewe ni msomi mkubwa unaongoza chama kikubwa cha siasa chenye wafuasi wengi.Ni mtu mwenye heshima kubwa katika jamii kwa nini ukakubali David akutumie kufanikisha mipango yako?Alikuahidi kitu gani hadi ukakubali kushiriki katika jambo hili?Tafadhali nieleze kila kitu kwani mipango yenu yote tayari imekwisha julikana na haitaweza kufanikiwa.It's over !!" akasema Elvis na Dr Makwa akainamisha kichwa akilia "Dr Makwa okoa muda tafadhali!! akasema Elvis Dr Makwa akamueleza Elvis kila kitu kuhusiana na mipango yao ya mapinduzi.Hakuficha kitu chochote. "Huo ndio ukweli kijana wangu.Naomba unisaidie kama ulivyoahidi kuwa utanisaidia kuninasua katika jambo hili" David anatoa wapi pesa zote hizi za kugharamia jambo hili kubwa?Elvis akauliza "Hajanieleza chochote kuhusu wapi anatoa fedha ila alichonieleza ni kwamba nisiwe na wasi wasi na suala la fedha kwani zipo za kutosha na kiasi chochote ninachokihitaji nimueleze atanipatia." akajibu Dr Makwa halafu akakumbuka kitu "Kuna kitu nimekikumbuka.Baada ya wataalamu wetu kuandaa mchanganuo wa gharama zote za operesheni hii nilimpelekea David akanihakikishia kwamba kila senti tuliyoiorodhesha itapatikana.Kesho yake akanifuata ofisini kwangu kijana mmoja akajitambulisha kwangu anaitwa Pascal Situmwa na akadai kwamba yeye na David ni washirika na akaanza kunihoji kuhusiana na ule mchanganuo na ndipo nilipoanza kujua kwamba David hayuko peke yake katika mpango ule ana wenzake ingawa sikuwahi kuwafahamu zaidi ya huyo Pascal niliyemuona kwa macho" akasema Frank "Pascal is dead now" "Unamfahamu?Nini kilimua?akauliza Dr Makwa "Dr Makwa kama kuna jambo lingine ambalo unadhani linaweza kutusaidia kufahamu nani hasa aliye nyuma ya suala hili tueleze tafadhali" "Vijana nimekwisha waeleza kila kitu.Hakuna nilichokificha.Kama ningekuwa ninafahamu nani aliye nyuma ya jambo hili ningekwisha waeleza.Nawaombeni sana jamani mnisaidie nisijulikane kama nimeshiriki.Ni tamaa tu ya fedha na madaraka viliniponza.Niko chini ya miguu yenu naombeni mnisaidie" akasema Dr Makwa.Elvis akamtazama kwa makini halafu akamtaka Steve amchukue akamfungie katika moja wapo ya vyumba "Elvis do you believe him? akauliza Steve "Yes I do.He's telling the truth. Kwa maelezo haya ya Dr Makwa tuna uhakika kwamba mtandao wa akina Frank ndio hasa uliopanga mpango huu wa mapinduzi kwa kuwatumia hawa wanasiasa.Nani ambaye yuko nyuma ya mpango huu wa kuiondoa serikali madarakani?Lazima kuna mtu ambaye anafadhili mpango huu kwa fedha.Hilo ni swali ambalo tunapaswa kulitafutia majibu usiku huu kabla hakujapambazuka"akasema Elvis "Elvis ulifanya chaguo sahihi kabisa kuamua kufa kwani bila kufanya hivyo haya yote yasingegundulika.Kufa kwako kumeokoa maisha ya watu wengi ikiwemo na rais ambaye naamini hawa jamaa wangemuua.Nini kinafuata baada ya kumpata Dr Makwa na kufahamu kwa undani jambo hil...." Steve akanyamaza baada ya simu ya Elvis kuita .Alikuwa ni Dr Philip.Elvis akaipokea kwa woga "hallo Dr Philip"akasema na Dr Philip akawa kimya kwa sekunde kadhaa "Dr Philip!! akaita Elvis "Elvis,I'm so sorry.She didn't make it.I'm very sorry" akasema Dr Philip .Elvis akanyong'onyea ghafla kwa taarifa zile "Dah ! akasema na kumtazama Steve "She's gone" akasema Elvis na uso wa Steve ukabadilika kwa mstuko alioupata









    "Dr Philip endelea kushughulikia kila kitu kuhusiana na kuuhifadhi mwili wa Vicky kuna suala tunaendelea kulishughulikia na baada ya kukamilika tutaungana nawe hapo hospitali.Mpe pole sana Winnie" akasema Elvis na kukata simu "One soulder down......." akasema Steve "But we have to continue fighting.We must save president.." akasema Elvis na ukimya wa zaidi ya dakika mbili ukapita kila mmoja akitafakari lake kisha Elvis akasema "She's gone too soon .Tulimuhitaji sana Vicky katika wakati huu" akasema na kunyamaza akatazama chini kwa muda kisha akainua kichwa na kusema "Steve kwa heshima ya Vicky lazima tuhakikishe tunalimaliza suala hili usiku wa leo.Tuhakikishe kwamba tunawapata wale wote wanaojihusisha na biashara ya silaha na vile vile kuwapata wale wote waasisi wa machafuko haya yaliyoanza leo yenye lengo la kuiondoa serikali madarakani." akasema Elvis sura yake ikiwa na hasira za hali ya juu "Kuna watu wawili tu ambao tukiwapata wataweza kutoa majibu ya maswali yetu yote ambao ni David na Elizabeth.Hawa wanafahamu kila kitu.David anafahamu nani yuko nyuma ya mpango wa mapinduzi na Elizabeth atatusaidia kufahamu mtandao wote unaojihusiaha na biashara ya silaha"akasema Steve "Kila kitu kinamalizika usiku wa leo!! akasema Elvis "Vipi kuhusu Omola.Tutamwambiaje kuhusu Vicky? Hatutamwambia kitu chochote kwa sasa hadi hapo tutakapokuwa tumemaliza misheni yetu" akasema Elvis kisha wakamfuata Omola aliyekuwa chumbani akijipumzisha "Vipi hali ya Vicky? akauliza Omola "Bado hatujapokea tararifa zozote kutoka kwa Dr Philip.Tunaamini atapona.Omola kuna jambo ambalo tumeamua kulifanya usiku huu.Baada ya kugundua kwamba watu wanaopanga mpango wa kuipindua serikali ni wale wale wanaojihusiaha na biashara ya silaha tumeamua tuwakamate wote na kuwafikisha sehemu husika.Operesheni yetu tunaimaliza usiku wa leo.Watu pekee ambao tunaamini wanaweza wakatupa majibu ya maswali yetu yote ni wawili tu,David na Elizabeth.Tukiwapata hawa tutamaliza kila kitu.Kwa hiyo tunataka kwanza kuwafahamu mahala walipo.Tuliwatumia ujumbe kupitia simu ya Frank ili wakutane sehemu moja na ninaamini wote watakuwa wamekutana mahala hapo na yawezekana hadi muda huu tayari watakuwa wamegundua kwamba Frank amekufa.Kifo cha Frank kitawafanya wabuni mbinu mpya za kuendeleza mipango yao lakini kabla hawajafanya hivyo wanatakiwa wawe katika mikono yetu" akasema Elvis "Itabidi tupate namba za simu anayotumia Elizabeth ili tuweze kumfuatilia na kujua mahala alipo.Namba za David tunazo tayari" akasema Omola na Elvis akamtaka Steve ampigie simu Juliana "Hallo Steve.Nimefika salama na Juliana baada ya kupokea simu ya Steve "Hilo ni jambo jema sana.Juliana nimekupigia kujua kama umefika salama vile vile kukujulisha jambo moja." "Nakusikiliza Steve"akasema Juliana "Tumeamua kumaliza kila kitu usiku wa leo.Tumegundua kwamba mama yako Elizabeth au vyovyote vile anavyoitwa anahusika yeye na mtandao wake katika vurugu za kisiasa zinazoendelea hivi sasa zilizopelekea vifo vya vijana wengi huko mtaani.Lengo lao kuu ni kuipindua serikali iliyoko madarakani.Ukiacha hilo,tumegundua pia kwamba mama yako anajihusisha na biashara ya silaha kwa waasi wa Congo.kwa hiyo basi tumeamua kumtia nguvuni usiku wa leo na tumeona tusifanye hivyo kabla hatujakujulisha wewe kwanza" akanyamaza baada ya kusikia Juliana akivuta pumzi ndefu "Juliana are you ok? "I'm ok Steve.Endelea" "Tunahitaji kufahamu mahala alipo mam a yako hivi sasa hivyo tunaomba utusaidie kutupatia namba yake ya simu anayotumia sasa ili tuweze kumtafuta na kujua mahala alipo na tumtie nguvuni" "Steve hizi ni taarifa njema japo zinastusha lakini tayari nilikwisha jiandaa kwa jambo hili kwa hiyo ninatoa baraka zangu mama akamatwe na ahojiwe kuhusiana na mambo yote haramu ambayo amekuwa akiyafanya yeye na wenzake.Kufikia hatua ya kutaka kuipindua serikali huu ni uhalifu uliovuka mipaka.Wanatakiwawakamatwe haraka sana.Pamoja na hayo yote ambayo mmeyagundua kwake lakini nahitaji sana ahojiwe kuhusiana na vifo vya mdogo wangu na mpenzi wangu.Ninaamini anafahamu sababu ya vifo hivyo na lazima atakuwa anawafahamu wahusika hivyo awataje na wafikishwe mbele ya sheria.Sintajali kama mama yangu akifungwa kifungo hata cha maisha,ninachojali mimi ni haki itendeke" "Ahsante sana Juliana.Tunakuahidi tutafanya kila linalowezekana kuhakisha kuwa anatueleza kila kitu kuhusiana na vifo hivyo.Tukiacha hayo kuna jambo lingine ambalo tunaomba utusaidie kulifahamu.Kuna mtu anaitwa Patrice Lwibombe ambaye ana mahusiano na waasi na bado hatujafahamu yuko wapi.Tunaomba utusaidie tuweze kumfahamu ni nani na yuko wapi? akasema Steve na Juliana akamuahidi kulifanyia kazi suala hilo akampatia namba za simu za mama yake na kukata simu.Steve akampatia namba zile Omola ili aanze kuzifanyia kazi ***************** David na Elizabeth wakiwa garini baada ya kuondoka katika ile nyumba alimouliwa Frank ,simu ya David ikaita mpigaji alikuwa makamu wa rais Dr Shafi.David akaipokea haraka haraka "Hallo Dr Shafi.Nimekutafuta sana siku ya leo bila mafanikio" akasema David "Toka wakati ule tumekuwa na vikao mfululizo na rais na ndiyo maana simu yangu ilikuwa imezimwa.Vipi maendeleo huko? "Huku mambo yanakwenda vyema .Tayari moto umewashwa na unaendelea kusambaa kila sehemu na hadi kufikia kesho baadhi ya mikoa maandamano yataanza na ndani ya muda mfupi nchi nzima itakuwa imesambaa maandamano" "Vizuri sana,nafurahi kusikia hivyo.Katika kikao tulichokaa na rais hakuna jambo lolote ambalo wameligundua hadi sasa.Rais ameelekeza kwamba wale wote walioandaa machafuko haya akina Dr Makwa na wenzake watiwe nguvuni na ameagiza jeshi la polisi kutotumia nguvu kubwa ili kuepuka maafa zaidi kwani hadi jioni hii taarifa za vifo ni watu arobaini na mbili na polisi kumi na watatu.Mnatakiwa kuendelea kushawishi vurugu zaidi na nimerejesha zile kompyuta mahala pake.Mama bado hajarejea"akasema kuwalazimisha polisi watumie nguvu kubwa.Vipi wanajeshi wako tayari?akauliza Dr Shafi "Dr Shafi kabla hatujafika huko nataka kufahamu kuhusiana na Meshack Jumbo.Tayari amepatikana?Ni muhimu sana kwetu kumpata yule mzee" "I'm sorry David.Taarifa nilizozipata mara tu baada ya kutoka katika kikao ni kwamba wale vijana niliowatuma kwenda kumchukua Meshack wamekutwa wameuawa katika hoteli moja.Ninasubiri taarifa rasmi ili tujue wamekufaje na uchunguzi uanze mara moja.Mpaka sasa Meshack Jumbo hajakamatwa na hajulikani alipo" "Oh my God !! akasema David "I'm so sorry David lakini ninakwenda kuunda timu nyingine usiku huu na watamtafuta Meshack usiku kucha hadi apatikane.Hakutapambazuka kesho kabla Meshack Jumbo hajapatikana.Naomba uniamini" akasema Dr Shafi "Ninakuamini Dr Shafi lakini nakusistiza tena kwamba Meshack ni muhimu mno kwetu kwani anazo taarifa za muhimu sana kuhusiana na Elvis.Huyu kijana tuna wasiwasi mkubwa yuko hai bado.Taarfa za kuonekana kwake zinatuumiza vichwa sana na hatuwezi kuzipuuza.Endapo ni kweli huyu jamaa yuko hai basi mipango yetu inaweza kushindikana ndiyo maana ninahitaji kumpata Meshack Jumbo ili kujiridhisha kuwa Elvis yuko hai au amefariki na kuzikwa" "Nitajitahidi David na kwa timu nitakayoiunda ninaamini hadi kufika asubuhi tayari tutakuwa tumempata Meshack na kuufahamu ukweli" "Good.Kuhusu wanajeshi kumetokea tatizo kidogo lakini haliwezi kutuzuia katika mipango yetu.Kuna mtu mmoja anaitwa Brigedia Frank Kwaju ambaye alikuwa anashughulikia kuandaa wanajeshi watakaochukua nchi na tayari kila kitu amekwisha kiweka vizuri ila kwa bahati mbaya jioni hii tumekuta ameuawa.Hili si tatizo sana kwani hata mimi ninaweza kulishughulikia hilo la wanajeshi" "Nani kamuua?Unadhani kifo chake kimesababishwa na hili suala letu? akauliza Dr Shafi kwa wasiwasi "Bado hatufahamu nani kamuua ila tunafanya uchunguzi wa haraka kumbaini muuaji" "David mnapaswa kuwa makini mno.Muuaji huyo anapaswa atafutwe haraka sana na apatikane tujue kwa nini kamuua huyo Frank.Huu si wakati wa kufanya mzaha hata kidogo.Jambo hili likivuja we'll all go down.Tafadhali kuweni makini sana.Mimi nitawasiliana nawe muda wowote nitakapopata jambo ambalo naamini linatufaa"akasema Dr Shafi wakaagana na kukata simu "Bad news" akasema David "Meshack Jumbo bado hajapatikana mpaka mida hii.Ile timu iliyotumwa kwenda kumkamata wote wamekutwa wamekufa" akasema David na Elizabeth akaupiga usukani kwa hasira "Damn it !!! "Kwa nini kila tunachokipanga hakiendi tunavyotaka?Kuna tatizo gani?Lakini haya yote yanatokea kwa sababu ya kukosa umakini.Laiti ningelishughulikia suala hili mwenyewe haya yote yasingejitokeza.It was my mistake and now I have to fix it!! akasema kwa hasira.Safari ikaendelea kimya kimya na baada ya muda Elizabeth akauliza "Meshack Jumbo is well protected.Hatutaweza kumpata kirahisi kama anavyosema huyo makamu wako wa rais.Unafahamu alipozikwa Elvis? "Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba Elvis amezikwa katika makaburi ya Mkwajuni" "Are you sure? "Hivyo ndivyo niliambiwa" akasema David. "You are not sure.Ndiyo maana mambo yanakwenda kombo.Hamjiamini na kila mnachokifanya.Niliwaamini nikijua mtaweza kuhakikisha kila kitu kinakwenda vyema lakini hakuna mlichokifanya,kila kitu kinakwenda hovyo.Nakuonya David kama operesheni hi itashindikana I'll Kill you.Sikutanii katika hili.Tazama mwenzako Frank ameuliwa kikatili kutokana na uzembe wake.Kutokuwa kwake makini kumegharimu maisha yake" akasema Elizabeth kwa hasira na kuchukua simu akampigia Juliana "Juliana uko nyumbani? "Ndiyo mama niko na wageni" "Sawa mimi nimetoka kuna mtu nimekuja kuonana naye nitachelewa kidogo.Uko karibu na Patricia? "Samahani mama sikukujulisha mapema kutokana na kutingwa na wageni,Patricia amekwisha ondoka" "Ameondoka?Amekwenda wapi? "Ameitwa na rais akaishi ikulu.Patricia ni daktari wa mke wa rais hivyo kufuatia kifo cha mume wake rais na mke wake wakaona ni vyema endapo watamchukua na kuishi naye ikulu" "Oh sawa.Kuna jambo nataka unisaidie kama unaweza kulifahamu" "Jambo gani mama? "Unafahamu Elvis mume wa Patricia amezikwa katika makaburi gani? "Elvis amezikwa makaburi ya Mkwajuni.Kwani kuna nini mama? "Kuna mtu nilikuwa nazungumza naye hapa anamfahamu Elvis na hakujua amezikwa wapi.Endelea kukaa na wageni nitakuja muda si mrefu sana" akasema Elizabeth na kukata simu "Tunaelekea makaburi ya Mkwajuni kutafuta ukweli kuhusu Elvis.Tutalifukua kaburi lake ili tujue kama kweli yuko hai au alifariki dunia" "Madam...." David sitaki ushauri wowote kwa sasa nimeamua kuushika usukani na kila kitu kitakwenda kama ninavyotaka mimi.Vijana watakwenda kutafuta zana na tutalifukua kaburi kuubaini ukweli" akasema Elizabeth. Walifika Rosana hotel wakapata chakula wakati walinzi wao wanakwenda kutafuta zana na waliporejea wakaondoka kuelekea makaburi ya Mkwajuni kutafuta ukweli kuhusu Elvis ******************* Wakati Omola akiendelea kuwatafuta David na Elizabeth kwa kutumia programu yake, Elvis na Steve wakaenda kumtazama Meshack Jumbo ambaye alikuwa amezinduka na kujiegemeza ukutani. "Mkurugenzi" akasema Elvis na Meshack Jumbo akamtazama kwa macho makali yaliyojaa hasira "Elvis ni wewe kweli unayenifanyia mimi hivi?akauliza "Samahani sana mzee wangu lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukufungia humu.Mzee tumetafakari mimi na wenzangu na tumeamua kulimaliza suala usiku wa leo na halafu utamtaarifu rais kama ulivyokuwa unahitaji.Kabla hatujafanya hivyo tunapaswa kuwa na ushahidi wa kutosha usio na shaka yoyote kuhusiana na jambo hili na vile vile kuwapata wahusika wakuu wote.Kwa hiyo mzee tunakwenda kuwatafuta David na Elizabeth ambao ndio vinara katika mpango huu wa mapinduzi.Tunaamini kuwa tukiwapata hawa basi mpango wote utakuwa umefika mwisho.Wakati mimi na Steve tukienda kuwatafuta akina David kuna jambo nataka nawe ulifanye" akasema Elvis na kumtazama mzee Jumbo "Unataka nifanye nini? akauliza "Tunaye hapa ndani Dr Makwa Tusangira mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani hapa nchini na ametueleza kila kitu kuhusiana na mpango huu namna walivyoupanga.Nimemuahidi kumsaidia kumuondoa katika kesi hii endapo atakubali kushirikiana nasi.Tayari amekwisha piga simu kwa washirika wake na kuzuia mipango yote isiendelee na sasa kuna kitu nataka akifanye.Nataka awapigie simu wakuu wenzake wa vyama vya siasa ambao hivi sasa wamejificha sehemu mbali mbali na awatake wakutane katika hoteli ambako hukutana kwa ajili ya mikutano yao na wakifika hapo wote watiwe nguvuni" "Unataka niombe msaada wa polisi?akauliza Meshack "Hapana mzee.Hili suala bado halijafika mahala pa kuwajulisha polisi.Baada ya kuhakikisha kwamba tumepata kila tunachokihitaji ndipo tutawajulisha jeshi la polisi na kuwakabidhi watuhumiwa wote kwao ili taratibu nyingine zianze.Utakachofanya utatuma vijana wako ambao watakwenda katika hiyo hoteli na kuwatia nguvuni wanasiasa wote halafu watafungwa mahala pa siri ili tuweze kuwafanyia mahojiano na kuupata ukweli na kukusanya ushahidi zaidi" "Huo ni mpango mzuri.Let's end this" akasema Meshack Jumbu huku akijitahidi kuinuka na Steve akamsaidia Nimechoka sana nadhani muda wa kupumzika umekaribia.Baada ya suala hili kumalizika nitaanza taratibu za kustaafu kwani umri wa kustaafu kwa hiyari umekwishafika" akasema Meshack Jumbo halafu wakatoka mle chumbani wakaeleka katika chumba alimokuwamo Dr Makwa Tusangira "Am I free to go now? akauliza Dr Makwa baada ya akina Elvis kuingia mle ndani "Not yet Dr Makwa.Kuna suala nataka ulifanye.Nataka uwapigie simu wenzako wote mlioandaa maandamano haya ambao hivi sasa wamejificha sehemu mbali mbali na uwatake mkutane katika hoteli ambayo huwa mnakutana kupanga mipango yenu." "Unataka kufanya nini ?akauliza Dr Makwa kwa wasi wasi Are you going to do it or not?akauliza Steve huku akimsogelea na Dr Makwa akaogopa "NItafanya hivyo mnavyotaka ila naombeni mtunze ahadi yenu ya kunisaidia" akasema Dr makwa na kuchukua simu yake akaanza kuwasiliana na wenzake "Mzee wakati Dr Makwa anawasiliana na wenzake tuma timu ya vijana iende hapo hotelini ili kujiweka tayari na muda wowote watakapokuwa wametimia utawapa maelekezo wawatie nguvuni" akasema Elvis na mara simu ya Steve ikaita alikuwa ni Juliana "Hallo Juliana" akasema Steve "Steve kuna kitu kimetokea muda si mrefu sana nimeona nikujulishe.Mama kanipigia simu akaniuliza mahala alikozikwa Elvis nikamuelekeza.Sijui ameuliza hivyo kwa lengo gani hasa" akasema Juliana "Ahsante sana Juliana kwa taarifa hizo ambazo naamini zitatusaidia sana.Vipi kuna kitu chochote umekigundua kuhusu Patrice Lwibombe? "Hapana bado.Nitakujulisha nitakapopata jambo lolote" akasema Juliana "Sawa Juliana na sisi tunaendelea na lile zoezi na likikamilika tutakujulisha" "Steve naomba msitumie nguvu kubwa sana wakati mnamkamata mama" akaomba Juliana "Tutalizingatia hilo" akajibu Steve na kukata simu "Juliana anadai kwamba mama yake amempigia simu na kumuuliza kuhusu mahala alikozikwa Elvis"akasema Steve na mara akatokea Omola na kuwaita wakaelekea sebuleni "Kuna mambo mawili nimeyapata.Kwanza David na Elizabeth wote wako sehemu moja." akasema na kuwaonyesha akina Elvis mahala walikokuwapo akina David "Haya ni maeneo ya Mpeteni na huku ndiko yaliko makaburu ya Mkwajuni ambayo muda si mrefu Elizabeth alikuwa anamuuliza Juliana" akasema Steve "Jambo la pili nimepata tena mazungumzo kati ya makamu wa rais na David" akasema Omola na kuyacheza mazungumzo yale ya makamu wa rais na David. "Ahsante sana Omola kwa msaada wa proigramu hii kwani tumeweza kupata mambo ambayo ingetuchukua muda mrefu kuyafahamu.Kumbe tayari kunawanajeshi wameandaliwa kuchukua nchi.Hawa jamaa wamejipanga na wamedhamiria kweli kuchukua nchi.Kumbe Frank alikuwa ni mtu muhimu sana kwao kwani ndiye aliyefanikiwa kuwashawishi wanajeshi wakubali kufanya uasi na kuchukua nchi.Watu hawa ni wanyama sana na hawapaswi kuonewa huruma.Tuwawahi kabla hawajaendelea na mipango yao zaidi" akasema http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Elvis "Kufuatia mazungumzo hayo ya David na Dr Shafi kuna kitu nimekipata.David na Elizabeth wanataka kwenda katika makaburi ya Mkwajuni ili kujiridhisha kama kweli nimekufa"akasema Elvis "Unadhani wanataka kufukua kaburi?Meshack Jumbo akauliza "Bila shaka lengo lao ni hilo.Tunatakiwa kufanya haraka kuwawahi" akasema Elvis wakaanza kujiandaa haraka haraka.walichukua kila walichoona kingeweza kuwafaa halafu wakaondoka wakimuacha Omola alinde usalama pale nyumbani ****************** Makaburi ya Umoja Mkwajuni ni makaburi mapya kabisa ambayo yalikuwa katika mfumo mpya wa kulipia hivyo kupafanya mahala hapo kuwa sehemu nzuri na ya kuvutiwa kutokana na uangalizi wake mzuri.Eneo la ndani ya makaburi kulipangwa vizuri na bado maboresho yalikuwa yanaendela ili kupafanya mahala pale pavutie zaidi ikiwa ni pamoja na kuweka taa ili hata usiku shughuli za mazishi ziweze kufanyika. David na Elizabeth wakiwa na walinzi wao wakawasili katika makaburi yale na kuelekea moja kwa moja katika geti la walinzi "David stay in the car.Let me finish this" akasema Elizabeth na kushuka garini akawafuata wale walinzi,akawasalimu na wakataka kufahamu shida yake "Samahani ndugu zangu,ninaitwa Sarah ninaishi Dubai.Nilipata taarifa za kifo cha rafiki yangu ikanibidi kufunga safari kutoka Dubai kufika hapa kumbe tayari amekwisha zikwa.Kesho ninasafiri kurejea Dubai alfajiri na mapema hivyo nimekuja hapa ili niweze kupata nafasi walau nilione na kuweka maua katika kaburi lake.Tafadhalini naombeni mnisaidie" akasema Elizabeth kwa sauti ya upole iliyowafanya walinzi wale waamini alichokuwa anakisema Mama kwanza pole sana kwa msiba wa rafiki yako,lakini hapa tuna taratibu zetu zilizowekwa.Ikifika saa moja jioni haruhusiwi mtu yeyote kuonekana ndani ya eneo la makaburi kwani bado hakuna taa.Tungeweza kukuruhusu ukaingia huko lakini wakuu wetu wakikukuta huko sisi hatutakuwa na kazi tena" akasema mmoja wa jamaa aliyeonekana kama ndiye mkubwa wa zamu ile ya ulinzi "Jamani nawaombeni mnisaidie.Sintachukua muda mrefu" akabembeleza Elizabeth " Hapana mama hatutaweza kukusaidia kwa hilo kwani tunalinda ajira zetu.Tafuta wakati mwingine uweze kuja kuliona kaburi la rafiki yako" akasema yule jamaa.Elizabeth akafungua mkoba wake na kutoa bunda la noti akampatia yule mkubwa ambaye alitumbua macho asiamini alichokiona. "Kwani ndugu yako anaitwa nani? akauliza yule jamaa huku akiingia katika ofisi yake na kuzifungia fedha zile katika droo "Anaitwa Elvis" Yule jamaa akafungua kitabu chake kikubwa chenye orodha ya watu wote wanaozikwa hapo akalitafuta jina la Elvis akalipata "Anaitwa Elvis Tarimo.Amezikwa kitalu B.Twende nikupeleke" akasema yule jamaa na kuchukua funguo akamtaka mwenzake aliyekuwa naye aendelee kulinda wakati yeye akimpeleka Elizabeth ndani.Alipofungua tu geti ghafla Elizabeth akatoa bastora yenye kiwambo cha kuzuia sauti na kumtandika risasi mbili akaanguka chini halafu akamgeukia yule mwenzake naye akampiga risasi ya kichwa akaanguka chini kisha akawaita vijana wake wakawabeba wale walinzi na kuwaficha ndani katika maua.Ndani kulikuwa na vibao vya maelekezo,kulikuwa na kibao kinaelekeza kitalu A na kingine kinaonyesha kitalu B wakafuata njia inayoelekea kitalu B wakayakuta makaburi na kisha wakaanza kulitafuta kaburi la Elvis wakalipata.Tayari lilikuwa limejengwa kwa ustadi na kuwekwa urembo na kulifanya livutie sana.Haraka haraka Eizabeth akawaelekeza wale vijana waliokuwa na vifaa waanze kulibomoa lile kaburi. "David muda si mrefu tutaufahamu ukweli" akasema Elizabeth ambaye hakuwa na hata chembe ya wasi wasi tofauti na David ambaye alikuwa mkimya na alionekana mwenye woga mwingi.Haikuwa kazi nyepesi kulitindua zege lile lililotumika kufunika kaburi na baada ya kuona kazi inazidi kuwa ngumu,Elizabeth akaamuru kaburi lichimbwe kwa pembeni . Elvis na Steve waliwasili katika makaburi ya Mkwajuni,wakaegesha gari lao mita kadhaa kutoka eneo lile la makaburi halafu wakatembea kwa miguu kulifuata geti huku wakiendelea kupewa maelekezo na Omola aliyekuwa akiwafuatilia akina David kupitia kompyuta yake.Walifika karibu na geti la kuingilia ndani na wakayakuta magari mawili yameegeshwa nje. "Haya lazima ni magari yao" akasema Elvis kisha akamtaka Steve amkinge, akatembea kwa tumbo kuelekea eneo kulikoegeshwa zile gari mbili.Akazifikia na kuchungulia ndani hakukuwa na mtu yeyote kisha kwa kutumia bastora yake yenye kiwambo cha sauti akayapiga risasi matairi kadhaa yakatoka upepo halafu akarejea kwa Steve "Elvis hapa kuna ulinzi lakini sijaona hata mlinzi mmoja katika sehemu yao" akasema Steve "Hiyo ni ishara kuwa tayari wamekwisha wateka au kuwaua.Twende ndani" akasema Elvis wakatembea kwa tahadhari hadi katika ofisi ya walinzi ambayo ilikuwa tupu na Steve akagundua kitu. "Damu!!.Inaonekana tayari walinzi wamekwisha uawa" akasema Steve wakaingia ndani ya makaburi.Kulikuwa giza lakini Steve alifahamu mahala alikozikwa Elvis akamuongoza wakatembea kwa tahadhari kubwa.Mara kwa mbali wakaona mwangaza wa tochi na vishindo vya watu kuchimba kitu kigumu "We got them.Wanaharibu kaburi wanataka kujua kama nimo kaburini ama vipi" akasema Elvis kwa sauto ndogo.Wakapeana maelekezo namna ya kuwakabili watu wale kisha kila mmoja akapita sehemu yake wakiwa wanatambaa kwa tumbo kuelekea sehemu walipo wale jamaa Kazi ya kulichimba kaburi la Elvis iliendelea kwa kasi huku Elizabeth akiwahimiza wafanye kwa bidii kubwa.Alikuwa amesimama pembeni kidogo akiwa na David huku bastora yake ikiwa mkononi.Sehemu kubwa ya juu ilikwisha ondolewa "Aliyejenga kaburi hili anastahili pongezi" akasema David "Nadhani alifahamu kuwa hakuna mtu ndani yake ndiyo maana akajen....." kabla hajamaliza sentensi yake zikasikika sauti za risasi kutoka katika bastora yenye kiwambo na vijana wanne waliokuwa wakichimba kaburi lile la Elvis wakaanguka chini. "What happened? akauliza David kwa wasi wasi huku yeye na Elizabeth wakichuchumaa chini "Stanley !! akaita Elizabeth lakini mara akajikuta akiguswa na kitu cha baridi sikioni mwake. "Tupa chini silaha yako na uinue mikono yako juu!!! ikamuamuru sauti kali kutoka nyuma yake.Elizabeth alitii amri aliyopewa na kunyoosha mkono wake taratibu kuipeleka chini bastora yake lakini ghafla akageuka na kutaka kumkabili yule jamaa aliyekuwa nyuma yake ambaye ni Elvis lakini Steve alikiona kitendo kile na kuachia risasi tatu zilizotua katika kiganja cha mkono ule wenye bastora akaanguka chini.Elvis akamuwahi na kumkanyaka kichwani huku Steve akiwahi kumdhibiti David Bila kupoteza muda Steve akatoa pingu na kumfunga Elizabeth halafu wakamwagia dawa katika jeraha lile la risasi mkononi mwa Elizabeth ili kuzuia damu kutoka kwa wingi na kisha wakamchoma sindano ya usingizi na hazikuputa sekunde kadhaa akalala.Steve akamuweka begani Elvis akamuongoza David wakaondoka "Jamani msiniue..msiniue jamani..Mimi ni waziri mkuu mstaafu..Ninazo fedha nying............" "Shut up!! akafoka Elvis Wakatoka nje ya eneo la makaburi na Steve akaenda kulileta gari lao wakawapakia Elizabeth na David wakaondoka "Tumewapata kirahisi sana tofauti na nilivyokuwa nimetegemea." akasema Steve "Hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho.Baada ya muda mrefu wa kuishi kama wako peponi sasa ni muda wao wa kuishi kama wako motoni hasa huyu mwanamke leo atajuta kuzaliwa binadamu!! akasema Elvis huku akiuma meno kwa hasira 'Tafadhali vijana wangu naombeni msiniue.Nitawapa kila kitu mkitakacho.Niambieni mnataka nini vijana wangu,kama fedha ninazo nyingi sana na nitawapa kiasi chochote mkitakacho" akasema David aliyekuwa amefungwa mikono kwa nyuma.Steve aliyekuwa amekaa naye nyuma akamnasa kibao kizito "Hii ni picha tu ya kitu unachokwenda kukutana nacho huko uendako" akasema Steve Walifika katika makazi yao wakamshusha Elizabeth aliyekuwa katika buti.Dr philip akaitwa haraka sana ili kuja kumuhudumia kabla hawajamfanyia mahojiano.David akatupwa katika chumba cha stoo "Mzee tumefanikiwa kuwapata wote wawili,David na Elizabeth.Vipi huku mmefanikisha lile zoezi? akauliza Elvis "Zoezi limefanikiwa na wote wamekamatwa na nimewaelekeza vijana wakawafunge katika ile nyunba alimokuwa amefungwa Steve kisha tutawafanyia mahojiano.Hongereni sana vijana wangu kwa kazi hii kubwa na ngumu.Kupitia watu hawa wawili tutaweza kupata taarifa zote.Tafadhalini vijana fanyeni kila muwezalo kuhakikisha kwamba mnapata taarifa kutoka kwao." Usijali mzee tutapata taarifa zote." "Vizuri.Vipi kuhusu suala la kumtaarifu rais?akauliza Meshack Jumbo "Bado kuna kitu tunapaswa kukifahamu.Ni nani aliye nyuma ya mpango huu wa mapinduzi?Naamini hawa jamaa hawakuwa peke yao lazima kuna watu wako nyuma yao.Tukiwapata hao basi tutamjulisha rais.Kwa sasa tujielekeze katika kupata taarifa kwa kina zaidi" akasema Elvis halafu wakaenda katika chumba alimo Dr Makwa "Hallo Dr Maka" akasema Elvis "Nimemaliza kazi yenu.Mnanisaidiaje kuniondoa katika sakata hili? akauliza Dr Makwa.Elvis akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akatoa kicheko kidogo cha dharau You are so stupid Dr makwa.After all you've done do you think we're going to let you go?Mpaka sasa idadi ya watu waliokufa kutokana na vurugu ulizoziasisi haijulikani,unataka tukuache uondoke?Familia yako inafurahia hivi sasa wakila na kunywa kwa raha zao huko nje ya nchi wakati familia za wengine hivi sasa kuna vilio baada ya watoto wao kupoteza maisha kufuatia vurugu ulizozianzisha kwa tamaa zako za fedha na madaraka.You want me to let you go!!..akasema Elvis huku akimtazama Dr Makwa kwa hasira "Uliniahidi hivyo kwamba nikikueleza ukweli utanisaidia kuniondoa katika hili sakata.Tafadhali nakuom......" Hakumaliza sentensi yake Elvis akamnasa kibao kizito kilichompeleka chini.Steve akamuinua na kumtandika kichwa kilichomfanya apepesuke na kujigonga ukutani akaanguka chini.Akachukua panga lililokuwa karibu lakini Elvis akamzuia "Hatutakiwi kumuua.Huyu bado tunamuhitaji sana.Ni shahidi muhimu sana.Mfunge kabisa asije akajiua" akasema Elvis halafu akampigia simu Juliana kwa kutumia simu ya Steve "Hallo Juliana ni mimi Elvis hapa ninaongea.Tafadhali usitamke jina langu kama uko na watu karibu" "Nimekuelewa.Vipi maendeleo ya lile zoezi mmelifanikisha? akauliza "Zoezi tumelifanikisha lakini mama yako ameumizwa kidogo mkononi ila anaendelea vyema.Daktari anakuja kumtibu jeraha kisha tutaanza kumuhoji" akasema Elvis "Hongereni sana Elvis.Tafadhali hakikisheni mumemuhoji na kupata taarifa zote mnazozihitaji na vile vile msisahau kuhusiana na kupata taarifa ya vile vifo" "Tutafanya hivyo Juliana.Umepata chochote kuhusiana na Patrice Lwibombe? "Hapana bado sijafanikiwa.Nilikuwa na wageni ndiyo maana nikakosa hata muda wa kufanya upekuzi" akasema Juliana "Juliana nina ombi moja kwako.Kwa kuwa mama yako tayari tunaye huku tunataka kufanya upekuzi chumbani kwake ili tuone kama tutaweza kupata kitu cha kutusaidia katika uchunguzi wetu" "Hakuna tatizo kabisa kuhusu hilo.Mnakuja wote? "Hapana anakuja Steve peke yake mimi nitabaki hapa" akasema Elvis "Sawa ninamsubiri hapa" "Vipi kuhusu Patricia?Una taarifa zozote kuhusiana na maendeleo yake? Amenipigia simu muda si mrefu sana anadai anaendelea vyema.Usihofu nitakuwa naye karibu sana" "Ahsante sana"akajibu Elvis na kukata simu Elvis akamuelekeza Steve aende kwa Juliana na kufanya upekuzi chumbani kwa Elizabeth .Dr Philip alifika na kuanza kumuhudumia Elizabeth ambaye bado hakuwa na fahamu.Baada ya kulitibu jeraha lile Elvis akamuita Omola wakaenda sebuleni na kumtaka Dr Philip amueleze ukweli kuhusiana na Vicky.Omola alilia machozi mengi sana kufuatia kifo kile cha rafiki yake mkubwa Vicky.Elvis akamtaka aende chumbani akapumzike "Sasa ni muda wa kazi" akasema Elvis akaelekea katika chumba alimofungwa David akamtoa na kumpeleka sebuleni.Meshack Jumbo na Dr Philip nao pia walikuwepo.Alikuwa ameloa jasho mwili mzima. "Hallo mheshimiwa David.Usiwe na hofu.Hapa tumekuleta na tutazungumza kama marafiki.Take a deep breath" akasema Elvis na David akavuta pumzi ndefu "Again take a deep breath ! "Good.Relax now.You need something to drink?Whisky ,wine,water or coffee? akauliza Elvis "W..wa..ter.." akasema huku sauti yake ikikwama.Elvis akamletea glasi la maji akamfungua pingu akanywa "Sintakufunga tena pingu nataka tuzungumze kwa amani.Kabla ya yote naomba nifanye utambulisho.Huyu pembeni yangu anaitwa Dr Philip ni daktari kutoka idara ya ujasusi,yule mzee pale ni mkurugenzi wa idara ya ujasusi anaitwa Meshack Jumbo naamini mnafahamiana kwani alihudumu pia hata katika wakati ukiwa waziri mkuu.Mimi naitwa Elvis Tarimo." akasema Elvis na David akatamani ageuke upepo apotee.Alitumbua macho na miguu yake ikaonekana ikitetemeka "Pale makaburini mlikuwa mnataka kuthibitisha kama nimekufa,I'm not dead !! "No ! No !..I can't believe this !! You are a ghost ! a ghost !! akapiga ukelele wa woga.Elvis akatabasamu na kumimina mvinyo katika glasi akanywa "Nadhani sasa umethibitisha kwamba mimi ni halisi na si mzimu kwani mzimu hauna tumbo na wala haunywi mvinyo" Bwana ndiye mchungaji wangu..." akasema David na Elvis akamkatisha "Huo ulikuwa utangulizi sasa ni wakati wa mazungumzo.Nitakuuliza maswali na ninaomba unijibu kila kitu na endapo utashindwa kuonyesha ushirikiano basi huu utakuwa ni mwisho wako.Hauta liona tena jua la kesho asubuhi.Hauta muona tena mpenzi wako Samira"akasema Elvis na kumstua sana David alipotaja jina la Samira "David wewe ni waziri mkuu mstaafu,umehudumu katika jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi na kabla ya hapo umeshika nyadhifa kadhaa katika serikali,ni mtu mwenye heshima kubwa katika jamii na hata sasa baada ya kustaafu siasa bado umeendelea kuheshimika sana ndani na nje ya nchi.Kitu gani hasa kimekushawishi utake kurejea katika siasa?tuanzie hapo tafadhali"akasema Elvis "Mimi..." akasema David na sauti ikakwama akakohoa kidogo kurekebisha koo halafu akaendelea "Mimi nimekwisha staafu siasa na sijihusishi tena na mambo hayo" akajibu David "Tunafahamu umestaafu siasa lakini kwa siku za hivi karibuni umerejea tena katika siasa kwa mlango wa nyuma na umekuja na mikakati mizito ya kuhakikisha unakuwa rais wa Tanzania.Swali langu nini au nani kakushawishi urejee tena katika siasa tena safari hii ukitaka kushika nafasi kubwa zaidi ya uongozi pasi na kufuata taratibu? Swali lile likambabaisha David. Jibu David nani kakushawishi urejee tena katika siasa wakati umekwisha staafu? "Si kweli kwamba ninataka kuwania urais.Mambo hayo nimekwisha achana nayo" akasema David "David inuka twende! akasema Elvis na kumshika mkono David akampeleka katika chumba alimo Dr Makwa. "Unamfahamu huyu? akauliza Elvis.David alipatwa na mstuko mkubwa na ghafla sehemu ya mbele ya suruali yake ikaloa alikuwa amejisaidia haja ndogo.Hakutegemea kabisa kumkuta Dr Makwa mle chumbani "Unamfahamu huyu? akauliza Elvis "Uhhm..uhhmm..." David akajiuma uma na kushindwa kutoa jibu.Elvis akamnasa kibao kikali kilichompeleka chini kwani miguu yake haikuwa na nguvu. "Unamfahamu huyu? "Ndiyo" akajibu David kisha Elvis akamrejesha sebuleni "Dr Makwa tumemchukua nyumbani kwako na tayari ametueleza kila kitu kuhusiana na mipango yenu yote.Mpaka dakika hii maandamano na mipango yote ya vurugu imesitishwa na aliyefanya hivyo ni muandaaji mkuu wa maandamano ambaye ni Dr Makwa.Mpaka dakika hii wenyeviti wote wa vyama vya siasa ambao wameshiriki katika kuhamasisha vurugu za leo wamekwisha kamatwa na wanakwenda kuhojiwa kuhusiana na mipango yenu ya kuiangusha serikali.Its over David.Kila kitu kimekwisha.Tamaa zako zote zimekutokea puani." akasema Elvis "I'm sorry." akasema David huku akiweweseka kama mwendawazimu "David hili nikosa la uhaini na unafahamu adhabu ya kosa kama hili.Awali ilikuwa ni kifo lakini kwa sasa ni adhabu ya maisha gerezani.Usiku huu nitakukabidhi kwa vyombo husika ili taratibu za kuwafungulia mashitaka wewe na wenzako zianze mara moja kwani tayari tunao ushahidi wa kutosha wa mipango yenu miovu.Tunafahamu kila kitu unachokipanga wewe na wenzako akiwamo makamu wa rais Dr Shafi." David akazidi kuchaganyikiwa alipopewa habari za Dr Shafi "Tunafahamu kuwa wewe ndiye uliyempa maelekezo Dr Shafi kwamba mimi niuawe,wewe ndiye uliyemuelekeza Dr Shafi,mzee Meshack Jumbo auawe pia.Tunazo rekodi za mazungumzo yako yote ya simu na Dr Shafi na muda si mrefu makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atatiwa mbaroni kwa tuhuma za uhaini.It's over David but I can help you if you choose to cooperate with me.Ninaweza kukusadia David kuondokana na adhabu inayoweza kukukabili endapo utafikishwa mbele ya vyombo vya sheria" "Please help me!! akasema David huku ameloa jasho kama vile amemwagiwa ndoo ya maji "What do you want? Kitu chochote nitakupa tafadhali naomba unisaidie"akasema David "Nataka kufahamu jambo moja tu.Nani walio nyuma ya mpango huu?Nani wanafadhili mapinduzi haya? akauliza Elvis Nitakuwa na uhakika gani kwamba utatimiza ahadi yako ya kuniondoa katika jambo hili?akauliza David "Right now I'm your only hope so you either choose to tell me what I want or to end your life in prison" akasema Elvis "Ok ok nitakueleza" "I real dont know them ila nilialikwa katika kikao na Frank na huko ndiko nilikowakuta watu fulani wawili wenye asili ya kiarabu na wakajieleza kwamba wao ni wawakilishi wametumwa na mataifa makubwa ambayo chumi zake zinategemea mafuta"David akawaeleza akina Elvis kila kitu kilicotokea katika kikao kile cha kwanza ambapo mipango ya mapinduzi ilianza kuandaliwa Baada ya mkutano huo ndipo kila kitu kikaanza"akaendelea "Nilimfuata makamu wa ais Dr Shafi na kumshawishi akubali kujiunga nasi ili hapo tutakapokuwa tumeichukua nchi yeye aweze kuwa rais wa Zanzibar.Vile vile nikawashawishi viongozi wa vyama vya siasa kuanzisha maandamano na vurugu na wakati huo huo baadhi ya wanajeshi walikuwa wanaandaliwa ili kuweza kuchukua nchi pale vurugu zitakapokuwa zimezidi."David akaeleza mipango yao yote waliyokuwa wameipanga "David maelezo yako marefu lakini bado swali langu hujalijibu.Ni nani hawa ambao walileta mpango huu kwenu? "Nilichowaeleza ni kitu cha kweli kabsa.Watu hao siwafahamu undani wao" akasema David David this is the last chance to save yourself.Tell me the truth" akasema Elvis "Elvis huu ni ukweli mtupu" "David ninataka sana kukusaidia lakini kwa kuwa umeshindwa kunieleza ukweli nitalazimika kukuunganisha na wenzako na gazeti la kesho asubuhi litapambwa na picha zenu wewe na makamu wa rais mkiwa katika mikono ya polisi mkituhumiwa kwa uhaini.Inuka haraka !! akaamuru Elvis na David akasimama "Elvis tafadhali usinipeleke huko.Nisaidie tafadhali.Meshack Jumbo I'm so sorry.Nisamehe mzee wangu !! akasema David.Elvis akamtaka amfuate "Elvis kuna kitu nimekikumbuka" "Sema haraka" "Watu wale siwafahamu kiundani lakini huyu mwanamke Elizabeth mliyenikamata naye anawafahamu na ndiye aliyewaelekeza kwa Frank." akasema David na Elvis akamtaka aketi na amueleze kwa kituo kuhusiana na Elizabeth kujihusiaha na mpango ule wa mapinduzi "Elizabeth alinipiga simu na kunitaka nikamuone akanieleza kwamba amekuja kwenye mazishi ya mumewe Deusdedith.Elizabeth akanieleza kwamba watu wale yeye ndiye aliyewatuma.Alisema kwamba kabla ya kuja huku watu wale walimfuata kwanza yeye na wenzake wakawaeleza kuhusu mpango wao wa kuipindua serikali na ndipo alipomuelekeza Frank aanze kuandaa timu itakayoandaa mapinduzi.Elizabeth ndiye anayewafahamu watu hao ni akina nani,mkimuhoji yeye atawaeleza kila kitu" Ok good.Umekuwa rafiki mkubwa wa Elizabeth.Tueleze anajishughulisha na mambo gani? "Elizabeth ni mfanya biashara mkubwa.Anazo biashara katika nchi mbali mbali duniani" "Nafahamu ni mfanya biashara lakini nafahamu kuna ambo anajihusisha nayo tofauti na biashara .Ni mambo gani hayo?Nieleze tafadhali.Ukweli wako ndiyo msaada wako" David akainamisha kichwa akafikiri kwa muda kisha akasema "Elizabeth anajihusisha na magenge ya kimafia.Mumewe Deusdedith alikuwa kiongozi wa genge mojawapo na baada ya kufariki Elizabeth ameshika uongozi.Fedha zake nyingi anazipatia katika biashara zake hizi.Ana mtandao mkubwa katika nchi mbali mbali.Mkimuhoji atawaeleza ukweli." "Unamfahamu Patrice Lwibombe? "Patrice Lwibombe?akauliza David "Ndiyo .Unamfahamu? "Lwibombe ni mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa kikundi kimoja cha waasi wa Congo ambaye amefungwa kifungo cha maisha nchini Congo.Baada ya baba yake kufungwa Patrice ameendeleza mapambano dhidi ya serikali ya Congo" "Anaishi wapi Patrice? "Kwa taarifa nilizonazo Patrice anaishi nchini Ubelgiji" "Ahsante sana kwa taarifa hizo David sasa nenda kapumzike na tutaendelea nawe baadae" akasema Elvis na kumpeleka David chumbani.









    Philip ni muda wa kumuhoji Elizabeth.Naamini hadi sasa atakuwa amekwisha zinduka"akasema Elvis kisha wakaongozana wakaelekea katika chumba alimokuwamo Elizabeth.Mara tu mlango ulipofunguliwa Elizabeth akafumbua macho kutazama aliyeingia mle ndani.Dr Philip akampima halafu akamgeukia Elvis "Anaendelea vyema hana tatizo lolote unaweza ukaendelea kumuhoji" "Ahsante sana Dr Philip" akasema Elvis na kuvuta kiti akamsogelea Elizabeth.Meshack Jumbo yeye akakaa juu ya meza iliyokuwa karibu na mlango "Hallo Elizabeth!! akasema Elvis "Who are you?!! "My name is Elvis Tarimo" "I knew it !! This bastard isn't dead !! akasema kwa sauti ndogo iliyojaa hasira "Aaagghhhhh !! akasema Elizabeth kwa hasira na kutaka kuinuka lakini mikono yake ilikuwa imefungwa vyema na pingu zanye mnyororo. "Relax Elizabeth.Nimekuleta hapa kwa ajili ya mazungumzo muhimu.Tumekuwa tunakuchunguza na tayari tunafahamu mambo mengi kuhusu wewe" akasema Elvis na kumtazama Elizabeth aliyekuwa ameukunja uso wake kwa hasira "You'll soon pay for this you bastard !! akasema Elizabeth "Nchi yetu leo imeshuhudia machafuko yaliyosababishwa na wanasiasa waliopuuza amri ya jeshi la polisi ya kutokufanya mkutano wa siasa na hadi hivi sasa tuongeavyo kuna mapigano yanaendela kati ya polisi na wafuasi wa vyama vya siasa wanaoendelea kufanya vurugu katika mitaa mbali mbali ya jiji.Vurugu hizi zimepangwa pia kusambaa hadi mikoani na lengo kuu la vurugu hizi ni kuiondoa serikali iliyoko madarakani.Tayari tumegundua mipango yote iliyopangwa na tumegundua kwamba wewe ni kiongozi wa mpango huu wa mapinduzi hayo yaliyopangwa kufanyika.Sitaki kuzungumza sana kwani tayari wenzako wote wamekwisha kiri kila kitu mlichopanga kukifanya na tayari kila kitu kimesitishwa.Hakuna tena vurugu na wala mpango ule wa mapinduzi haupo tena.Wahusika wote wakuu wa mapinduzi haya wamekwisha kamatwa na wako nguvuni hivi sasa.It's over Elizabeth"akasema Elvis Aaaaggghh !! I swear you'll pay !!!akasema Elizabeth kwa hasira "Tunao tayari wanasiasa wote walioshiriki kuandaa vurugu hizo na vile vile tunaye David ambaye amekiri kila kitu.Hata hivyo nina maswali machache kwako.Nani aliye nyuma ya mpango huu wa mapinduzi?akauliza Elvis "Siwezi kuhojiwa na paka kama wewe" akasema Elizabeth kwa hasira "David amenieleza kwamba kuna watu wawili waliodai kutumwa na nchi ambazo chumi zake zinategemea mafuta kwamba ndiyo waasisi wa mpango huu wa mapinduzi je ni akina nani hao?Nani aliye nyuma yao?Elvis akauliza tena na Elizabeth akakaa kimya "Nijibu Elizabeth" akasema Elvis "Siwezi kupoteza muda kuzungumza na kinyago kama wewe.You want to kill me? Kill me now but I wont tell you anything ! akasema Elizabeth.Elvis akachukua mashine ya kutobolea na kumsogelea Elizabeth. "Nitakutoboa jicho la kulia na kama utaendelea na kiburi nitatoboa jicho la kushoto na utabaki kipofu kwa maisha yako yote yaliyobaki.Na kama bado utaendeleza kiburi cha kutotaka kusema chochote nitakukata vidole vyote vya mikono na vya miguu.Sintakuua bali nitakupa mateso makali na nitakuharibu kila mahala.Hautatazamika tena.Nitakukata ulimi hautaweza kuzungumza tena.Hautaweza kufanya chochote.Utaishi maisha ya shida na taabu nyingi na utaomba ufe lakini hautakufa.Now answer me !! akasema Elvis kwa ukali na kuiwasha mashine ile ya kutobolea akaisogeza karibu na jicho la Elizabeth.Mara mlango ukagongwa kwa nguvu,Meshack aliyekuwa karibu akaufungua wakaingia Steve na Juliana "Elvis don't do it!! akasema Steve na Elvis akasitisha kile alichotaka kukifanya "Steve kuna nini?Elvis akauliza Elizabeth alistuka mno alipomuona mwanae Juliana "Julie?! akauliza kwa mshangao asiyaamini macho yake "You sold me to thiese people?Umeamua kushirikiana na hawa wapumbavu?Hawa si watu wazuri they are monsters.!! "I'm sorry mother.Hawa si waongo bali ni watu walioyatoa maisha yao kwa ajili ya kuipigania nchi yao ambayo inabomolewa na watu kama wewe na wenzako.Sikutegemea kabisa kama mama unaweza kuwa na roho ya kinyama namna hii.You are a monster !! akasema Juliana huku akilia "Juliana nini kimetokea?Elvis akauliza "Elvis let them talk!! akasema Steve wakasogea pembeni na kumpa Juliana nafasi ya kumkaribia mama yake "Juliana wamekudanganyanini hawa jamaa kiasi cha kunifanyia hivi mama yako ambaye nimekuzaa na kukulea kwa mapenzi makubwa?.akauliza Elizabeth Juliana akaufungua mkoba wake na kutoa komputa yenye umbo dogo akaiwasha na kisha akamsogelea mama yake .Elizabeth alipomuona Juliana na kompyuta ile akatetemeka midomo "Uliificha kompyuta hii mbali sana ili asiione mtu yeyote na kumbe ndani yake kuna uchafu wote unaoufanya.Hii ni ripoti ya daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa baba na kubaini licha ya baba kusemekana alikufa katika ajali ya ndege lakini alikutwa na risasi tatu mwilini na akathibitisha kwamba kuna uwezekano baba aliuawa kabla ya ajali ya ndege kutokea.Ukamuandikia barua pepe mtu mmoja anaitwa Jimmy na kumtaka alishughulikie suala lile haraka ili uchunguzi usifanyike.Tell me mother why you killed my father? He loved you with all his heart but why you killed him?!! akauliza Juliana huku akilia "Explain to me mother why ?? akauliza tena Juliana huku akimtingisha mama yake "Waambie hao mashetani wenzako watoke nje" akasema Elizabeth na Juliana akawaomba akina Elvis watoke mle chumbani ili azungumze na mama yake.Elvis akamtaka Juliana watoke kwanza nje wazungumze. "Juliana nini unataka kukifanya? akauliza Elvis "Nataka mama anieleze kila kitu.Tumefanikiwa kuupata ushahidi wa kuthibitisha kwamba baba aliuawa na mama anahusika katika kifo hicho.Elvis I want her to confess everything to me" "Good.Follow me" akasema Elvis na kuongozana na Juliana hadi chumbani kwake akampa kamera ndogo ya siri. "Vaa hii kamera ifiche kifuani na kila utakachokizungumza na mama yako tutakirekodi ili uwe ni ushahidi.Sisi tutakuwa tunaangalia kila kitu mtakachokizungumza.Tafadhali fanya kila uwezalo kuhakikisha mama yako anaungama kila kitu na awataje wenzake wote anaoshirikiana nao katika biashara zake haramu hasa ya silaha.Mdanganye kwamba nao uwezo wa kumsaidia kumuondoa mikononi mwetu endapo atakueleza kila kitu" akasema Elvis na Juliana akaivaa ile kamera ndogo kifuani mahala ambako mama yake asingeweza kuiona halafu akarejea katika chumba alimo mama yake akaufunga mlango . "It's me and you now.Nieleze kila kitu kwa nini umemuua baba? Alifanya kosa gani hadi ukamuua?akauliza Juliana "Hata nikikueleza haitakusaidia kitu wewe bado mtoto mdogo Juliana .Hebu waambie hao jamaa wanifungue ili tukaendelee na maisha yetu.Kuna mambo mengi yananisubiri yakiwamo mazishi ya baba yako.Tafadhali washawishi waniache haraka sana kabla mambo makubwa hayajawakuta" "Mama naomba nikuweke wazi kwamba ninashirikiana na hawa jamaa na mimi ndiye niliyewaomba wakufanyie uchunguzi baada ya kutoridhishwa na mwenendo wako.Nilifahamu kuna mambo unayafanya kwa siri lakini sikufahamu ni mambo gani na ndiyo maana nikawaomba hawa jamaa wanisaidie kukuchunguza.Mama kwa sasa hatima ya maisha yako yote iko mikononi mwangu.Ni mimi ambaye ninaweza kukusaidia ukatoka hapa au nikawaelekeza hawa jamaa wakukabidhi katika vombo vya dola ambako utafunguliwa mashitaka na kufungwa maisha kwani tuhuma zinazokukabili ni nyingi.NItaweza kukusaidia endapo utanieleza ukweli wote bila kunificha" Elizabeth akamtazama Juliana kwa muda na kuuliza "Kitu gani hasa unachohitaji kukifahamu? "Nataka kufahamu mambo gani unashughulika nayo kwa siri ?Nieleze kila kitu ambacho hukuwahi kunieleza.UKifanya hivyo nitawashawishi hawa jamaa waweze kukuachia huru kwani ni mimi ndiye niliyewapa kazi hii.Chaguo ni lako mama" akasema Juliana "Siamini kama nimesalitiwa na mwanangu wa kumzaa mwenyewe.Juliana nimekulea kwa mapenzi makubwa leo unanifanyia hivi? "Mama muda unakwenda.Kama hutataka kunieleza ukweli nitawaacha hawa jamaa waendelee na taratibu zao na utaishia gerezani.Mama huna ujanja tena.hakuna atakayeweza kukusaidia zaidi yangu" akasema Juliana.Elizabeth akamtazama Juliana na machozi yakamtoka halafu akasema "Kama hivyo ndivyo utakavyo nitakuleza kila kitu" akasema Elizabeth "Good.Anza na kifo cha baba" akasema Juliana "Waambie hao wanaharamu waje wanifungue mikono yangu" "Hapana mama utakaa hivyo hivyo hadi hapo nitakaporidhika mimi" "Fine" akasema Elizabeth na kunyamaza kimya kidogo halafu akasema "Ni kweli ninahusika katika kifo cha yako.I killed him" akasema Elizabet na Juliana machozi yakaanza kumporomoka "Why mother !! Why you killed him? "Kuna mambo mengi ambayo huyafahamu kuhusu baba yako.He was a monster!! Alikuwa mkatili sana na ndiye aliyenifanya nikawa hivi nilivyo leo.Nilipoolewa naye alianza kunifundisha mambo mengi aliyokuwa anayafanya ikiwamo kushirikiana na vikundi mbali mbali vya kimafia" "Oh my God !!akasema Juliana kwa masikitiko "Ndiyo.baba yako alimuua kiongozi wa kikundi chao na yeye akawa kiongozi.Siwezi kukueleza kila kitu lakini itoshe tu kufahamu kwamba mimi na baba yako tunajihusisha katika mitandao ya kimafia na baba yako ndiye aliyekuwa kiongozi"akanyamaza akamtazama Juliana halafu akaendelea "Hivi karibuni huyu jamaa Elvis aliweza kugundua jambo fulani na kuanza kumfuatilia baba yako na ndipo nilipolazimika kumuua kwani bila kufanya vile lingekuwa ni anguko letu kubwa.Ajali ile ya ndege iliyomuua baba yako ilikuwa ya kupangwa lakini Deus aliuawa kwa risasi."Elizabeth akanyamza baada ya Juliana kuongeza kilio "Umetaka nikueleza ukweli?Huo ndio ukweli wenyewe uliouhitaji" akasema Elizabeth halafu akaendelea "I killed your father to protect you.Huwezi kuelewa lakini mambo yatakapoanza kuharibika ndipo utakaponielewa ninamaanisha nini" "Niambie kuhusu Godson na Joseph.Ulihusika katika vifo vyao?Wiki moja kabla ya kifo chake Godson alinionya nisijihusishe kabisa na miradi ya familia na hakunieleza kwa nini akafariki dunia kinyama.Ulihusika katika kifo chake? "I'm sorry Julie.Mauaji yale yalikuwa kwa ajili ya kulipiza kisasi.Kuna watu ambao nilitofautiana nao katika biashara na wakamuua Godson kulipiza kisasi lakini watu hao wote wamekwisha lipa uovu wao hawako tena duniani,wamekufa wote.Kuhusu Joseph naye vile vile mauaji yale yaliilenga familia yetu.Kuna watu waliokuwa wanatudai kiasi kikubwa cha fedha na walimuua Joseph ikiwa kama salamu kwamba endapo hatutawalipa pesa zao basi wangekuua wewe.Watu hao pia tayari tumekwisha washughulikia wote.Hakuna atakayecheza na familia yangu akabaki salama" akasema Elizabeth na Juliana akazidisha kilio.Elvis akaufungua mlango na kuingia mle chumbani baada ya kusikia Juliana akilia. "Elvis please give me more minutes" akasema Juliana huku akilia "Tuachane na hayo,umejiingiza pia katika mipango ya uhaini kwa kutaka kuiangusha serikali ukishirikiana na akina David.Mama una tatizo gani?Kwa nini ukajiingiza katika mambo makubwa na ya hatari kama haya?Hukuwaza kama nini kitatokea endapo mipango yenu ingeharibika? "You are still a child and you know nothing !Bado unaona mambo kwa jicho la kitoto.Mpango huu ulikuwa mkubwa sana na endapo ungefanikiwa tungekuwa katika daraja la juu mno Juliana.Sikukurupuka katika kujingiza kwenye mpango huu.Ni bahati mbaya imetokea wewe na hao wenzako uliochagua kushirikiana nao mmeharibu mpango wetu.Umeniudhi mno Juliana kwa jambo hili ambalo hata wewe mwenyewe lingekufaidisha kwani endapo David angekuwa rais ungekuwa waziri wa utalii na tungepata faida nyingi sana.Nilianza kukuingiza katika ramani ya mafanikio lakini umechagua wewe mwenyewe kuishi katika umasikini" "Nani aliye nyuma yenu mama?Nani anawafadhili?Nani anayetaka nchi yetu iingie katika machafuko?Nani anataka kuvuruga amani na mshikamano uliopo nchini? "Hata nikikueleza hutaelewa chochote" "Nieleze tafadhali nitakuelewa" "Huu ni mpango ulioandaliwa maalum kwa ajili ya maslahi ya nchi na endapo ungefanikiwa nchi ingefaidika sana kupitia rasilimali yake ya mafuta ambayo kwa sasa imeuzwa kwa wamarekani.Kitendo alichokifanya rais wenu cha kuwakabidhi sekta ya mafuta wawekezaji wa kutoka Marekani kinatishia chumi za mataifa ambayo yanategemea biashara ya mafuta.Hicho ndicho chanzo cha haya yote yaliyotaka kutokea" "Umesema nchi zinazozalisha mafuta.Ni nchi ipi hasa? "Huu ni muunganiko wa nchi kadhaa ambazo chumi zake zinategemea mafuta na lengo likiwa ni kuwaondoa wawekezaji wa kimarekani katika sekta ya mafuta ya Tanzania ili waweze kulinda chumi zao" "The last thing !! akasema Juliana "Nataka kufahamu kuhusiana na biashara yako ya silaha.Who is Patrice Lwibombe and how to get him? akauliza Juliana "kwa hilo siwezi kukueleza chochote.Hiyo ni siri yangu hadi naingia kaburini" "Mama hii si siri tena.Tayari tunafahamu mambo mengi kuhusiana na biashara yako.Nieleze tafadhali nani na nani wanahusika?Mnaifanyaje biashara yenu?Nijibu ili nikusaidie.Watu hawa ni http://deusdeditmahunda.blogspot.com/wakatili sana na mateso yao ni makali mno.Sitaki niwape nafasi wakutese wakuharibu haribu,nijibu tafadhali ili nikusaidie nikuondoe katika mikono yao" "I'm not scared Juliana!! akasema Elizabeth "Last chance mother !! akasema Juliana "Tell them to go to hell!! akasema Elizabeth Nimekupa nafasi umeshindwa kuitumia hivyo ninawaruhusu hawa jamaa waendelee na taratibu zao" akasema Juliana na kugeuka akaanza kupiga hatua kuelekea mlangoni "Juliana wait" akasema Elizabeth "Uliniahidi kunisaidia kunitoa hapa.Nini unataka kukifanya? "Mama nieleze kila ninachokitaka na nitakusaidia utoke hapa salama" akasema Juliana "Fine." akasema Elizabeth na kumueleza Juliana kila kitu kuhusiana na biashara ile ya silaha namna wanavyoifanya pamoja na wote wanaohusika. "Nimekueleza kila kitu ni wakati wako wa kutimiza ahadi yako.Waambie hao mashetani waniache niende zangu" akasema ElizabetJuliana akatoka na kuwakuta akina mathew wakiwa nje ya kile chumba wakimsubiri wakiwa na kompyuta ya Omola wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea mle chumbani kati ya Juliana na mama yake. "Do you believe she's telling the truth? Steve akauliza "Yes I do believe her" akasema Juliana "Ahsante sana Juliana kwa kutusaidia tumeweza kupata maelezo haya ya kina kutoka kwa mama yako ambayo yatatusaidia kuumaliza kabisa mtandao huu wote.Pole sana Juliana kwa yote yaliyokupata nadhani sasa unaweza ukaturuhusu tuendelee na taratibu zetu.Tunao tayari ushahidi mkubwa kuhusiana na mambo yote mawili mpango wa mapinduzi na biashara ya silaha hivyo tunataka kuanza mchakato wa kuwakabidhi watuhumiwa kwa jeshi la polisi ili wamalizie uchunguzi na kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria.Watu wengine wote wanaohusika watatafutwa na kupatikana hata Patrice atasakwa na kupatikana.Kazi kubwa imekwisha fanyika na ni wakati wa kukabidhi kijiti kwa taasisi nyingine" akasema Elvis "Elvis huyu ni mama yangu aliyenibeba tumboni kwa miezi tisa akanizaa na kunilea lakini kwa haya aliyoyafanya sintaweza kuwa na msaada wowote kwake.Anastahili kufikishwa mbele ya sheria.Anastahili adhabu kali.Inaniuma sana kumuona mama yangu maisha yake yakiisha namna hii lakini sina namna ya kumsaidia lazima alipe maovu aliyoyafanya.Nitaendelea kuwalilia Godson na Jose kwa miaka yote watu wangu niliowapenda ambao wamekufa kwa sababu yake yeye na baba.Natamani baba angekuwepo ili naye ajumuishwe katika kesi hii .Hata hivyo huko aliko ataipata hukumu ya haki kwa yale yote aliyoyafanya hapa duniani.Nini kinafuata baada ya hapa? akauliza "Kinachofuata kwa sasa ni kumtaarifu rais kila kitu kabla ya kuwakabidhi watuhumiwa kwa jeshi la polisi.Au unasemaje mzee Meshack? "Hiyo ndiyo hatua inayofuata lazima rais afahamu kila kitu kwani ni yeye atakayetoa amri ya kukamatwa kwa makamu wa rais.Elvis hili jambo mlilolifanya ni kubwa na historia itawakumbuka.Mmeiokoa nchi kutumbukia katika machafuko,mmeokoa maisha ya raia wasio na hatia waliokuwa wanauawa nchini Congo kwa silaha zinazouzwa na akina Frank na kikubwa zaidi mmeokoa pia maisha ya rais kwani kutokana na mipango iliyokuwepo tayari maisha yake yalikuwa hatarini.Mmefanya kitu kikubwa sana Elvis na wenzako.Japo tumepoteza mwenzetu lakini mafanikio yaliyopatikana ni makubwa sana" akasema Meshack Jumbo. "Call him " akasema Elvis na Meshack Jumbo akampigia simu rais "Mr Jumbo,habari za usiku huu mzee wangu.Tumekutafuta sana mchana bila mafanikio,uko wapi?Mbona hukuwa unapatikana? "Mheshimiwa rais mimi ni mzima na nimekupigia ninahitaji kuonana nawe.Nina mambo makubwa nahitaji kukueleza sasa hivi" akasema Meshack "Mzee Jumbo muda wowote unakaribishwa.Ninakusubiri hapa ikulu,njoo mara moja nina mazungumzo nawe pia"akasema rais na kukata simu "Ni wakati sasa wa kwenda kuonana na rais,mko tayari?akauliza Meshack "Mimi sintakwenda huko nitabaki hapa kuwalinda hawa watuhumiwa wetu na isitoshe Patricia yuko hapo ikulu na sitaki kuonana naye.Nendeni na mumueleze rais kila kitu.Msiache hata neno moja."akasema Elvis "Usijali Elvis tutakuwakilisha kwa rais na tutamueleza kila kitu bila kuacha hata neno moja kama ulivyoelekeza" akasema Meshack Jumbo.Elvis akaenda kumchukua Omola na kumtaka aongozane na akina Steve kuelekea ikulu kuonana na rais. Baada ya Meshack Jumbo akiwa amefuatana na Steve,Juliana na Omola kuondoka kuelekea ikulu kuonana na rais,Elvis akachukua sahani ya chakula na kumfuata Graca chumbani akaufungua mlango na tayari Graca alikuwa amepitiwa na usingizi.Akamsogelea na kumuamsha "Oh Elvis."akasema Graca na kukaa kitandani "Tafadhali kula chakula Graca unahitaji nguvu" "Thank you Elvis but I'm not hungry" "Graca usiwe na hofu tena.It's over.Tumeimaliza kazi.Tayari wahusika wakuu wote wa ule mtandao wa baba yako tumewatia mikononi na wengine wataendelea kutafutwa.Tumempata tayari kinara wa biashara hiyo na yuko humu ndani.Hivi tuongeavyo mzee Jumbo na akina Steve wamekwenda kuonana na rais kumueleza kila kitu kilichotokea na baada ya hapo tutawakabidhi polisi waendelee na taratibu nyingine.Wakati wa hofu na mashaka umekwisha ni wakati wa kufurahi na kuanza maisha mapya" "Oh Elvis" akasema Graca kwa furaha na kumkumbatia Elvis akambusu "Kumalizika kwa sakata hili ni kiashiria kwamba tunakwenda kuyaanza maisha yetu mbali na hapa.Au unarejea kwa mkeo Patricia?akauliza Graca "I dont know yet" akajibu Elvis "Elvis wewe ndiye furaha yangu,wewe ni ndugu yangu,wewe ni kila kitu changu kwa sasa,nakuomba usiniache.Nakuhitaji sana Elvis katika maisha yangu.Maisha yangu hayatakuwa na furaha tena endapo sintakuwa nawe.Najua bado unampenda mkeo lakini naomba unipende na mimi pia.Nitakupa kila ukitakacho.Nitakuwa muaminifu na mtiifu kwako" "Graca,I dont know what to say ila kula kwanza chakula halafu tutazungumza masuala haya baada ya mambo kutulia" akasema Elvis na kumlisha Graca chakula "Tutafuatilia tujue taratibu za mazishi ya baba yako na kisha ushiriki kwani wewe ndiye mtoto pekee na unatakiwa ushiriki mazishi" "Elvis nitashiriki mazishi lakini sihitaji kitu chochote kutoka katika mali za baba.Mali zote zimetokana na pesa iliyoloa damu.Nataka kuanza maisha yangu mwenyewe na hata kama ni utajiri basi nipate utajiri wa halali na si utajiri kama wa baba.Vipi kuhusu Vicky anazikwa lini? Bado hatuna taarifa rasmi ila baada ya ndugu kukaa na kupanga Winnie atatujulisha" akasema Elvis.Walizungumza mambo mengi na ilipofika saa tisa na dakika ishirini kengele ya getini ikagongwa Elvis akaenda kuchungulia akamuona Steve lakini hakuwa peke yake.Alikuwa amefuatana na gari tatu.Akafungua mlango Steve na wale alioongozana nao wakaingia ndani "Elvis hawa ni walinzi wa rais ambao amewatuma kuja kuwachukua Elizabeth na David na kuwapeleka kuwahifadhi sehemu salama wakati wakisubiri hatua zaidi.Tumemueleza rais kila kitu na amesema kwamba anahitaji kuonana nawe usiku huu" akasema Steve.Elvis hakuweza kukataa wito wa rais akamchukua Graca wakaondoka kuelekea Ikulu. "Elvis Tarimo" akasema rais kwa furaha baada ya Elvis kuwasili ikulu. "Mheshimiwa rais" akasema Elvis kwa adabu na rais akawaomba waketi. "Elvis sijui nianzie wapi.Nimeelezwa na mzee Jumbo na wenzako hawa kila kitu kilichotokea na mwili wangu ulinitetemeka kwa woga kwa niliyoyaskia.Haikutosha nikapewa pia vielelezo kadhaa kuthibitisha kila kilichotokea.Elvis sipati neno zuri la kukushukuru zaidi ya ahsante sana.Wewe na wenzako mmefanya kazi kubwa na ya kizalendo mmeilinda nchi na mmenilinda hata mimi ambaye nilikuwa katika hatari kubwa.You died to save me and your country.Thank you so much Elvis.Kama usingekuwa wewe na wenzako nchi hii ingeingia katika machafuko makubwa" akasema rais akiongea kwa hisia kubwa sana Mheshimiwa rais ni wajibu wetu kufanya haya tuliyoyafanya na tumetanguliza uzalendo na utaifa mbele na hatimaye tukafanikiwa kupata ushindi huu dhidi ya hawa maharamia" akasema Elvis Walizungumza mambo mengi na kwa upana zaidi hadi ilipofika saa kumi na moja za alfajiri ndpo walipoagana na wakati rais akiwasindikiza akaomba kuzungumza pembeni na Elvis "Elvis sikutaka kuzungumza nawe jambo hili mbele ya wenzako.Nini mipango yako baada ya haya mambo kukamilika? "Mheshimiwa rais ,mke wangu Patricia,ndugu zangu ,rafiki zangu na hata mama yangu wote wanafahamu na kuamini kuwa nimekwisha fariki hivyo sitaki kuzua taharuki miongoni mwao.Nahitaji kupotea na kwenda kuishi mbali na hapa labda kwa baadae ninaweza kurejea na kuwaeleza kilichotokea.Nataka waendelee kuamini kwamba tayari nimekwisha fariki" "Nadhani hilo ni wazo zuri kwani umezikwa siku si nyingi na ukijitokeza kwa sasa utawapa wakati mgumu sana na hasa mkeo Patricia na wanaweza wasikupokee wakiamini ni mzimu.Vile vile ukijitokeza itakulazimu kueleza sababu ya kwa nini ulighushi kifo chako jambo ambalo litakufanya ujulikane kazi yako na kukuweka katika hatari zaidi kwani watu hawa bado wana mtandao mrefu.Wewe na wenzako hamtakiwi kujulikana kabisa hivyo nakubaliana nawe uende ukaishi mbali na hapa.Rais wa Marekani ni rafiki yangu mkubwa sana na nitakuombea hifadhi uishi huko na utapewa uraia waMarekani kwa jina jipya na hautatambulika tena kama Elvis Tarimo.Utatafutiwa kazi nzuri ya kufanya au chochote kile utakachoamua kukifanya kama kilimo au biashara ili uweze kuendesha maisha yako.Elvis nakuahidi nitamtunza sana Patricia na kumpati akila kitu ambacho kitamfanya awe na maisha mazuri na hatapata taabu yoyote ile" "Ahsante sana mheshimiwa rais lakini nitaomba ninapoondoka niondoke pia na Graca kwani hana ndugu tena hapa na nilimuahidi kumsaidia kuyaanza upya maisha yake" "Elvis usiwe na wasi wasi.Chochote unachokihitaji utakipata.Nyote mlioyatoa maisha yenu kwa ajili ya jambo hili mnastahili kuthaminiwa .Kuhusu Steve ninafikiria kumteua kuwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa baada ya Meshack Jumbo kustaafu.Unashauri nini? Anaweza kufaa?akauliza rais "Steve ni mchapakazi mzuri,mzalendo wa kweli kwa nchi yake,haogopi chochote na yuko tayari hata kuyaweka hatarini maisha yake akiwa kazini.Ana mchango mkubwa sana katika operesheni hii.Amefanya kazi kwa muda mrefu na ameiva barabara.Nadhani ni wakati sasa wa idara hii ya ujasusi kuwa na kiongozi kijana mwenye mawazo mapya kuliko kila wakati kuwa na viongozi wazee" akasema Elvis na wote wakageuka wakamtazama Meshack Jumbo na kutoa kicheko kidogo halafu wakaagana na rais akarejea ndani na mzee Jumbo akamfuata Elvis akamtaka wazungumze kidogo ninafikiria kumteua kuwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa baada ya Meshack Jumbo kustaafu.Unashauri nini? Anaweza kufaa?akauliza rais "Steve ni mchapakazi mzuri,mzalendo wa kweli kwa nchi yake,haogopi chochote na yuko tayari hata kuyaweka hatarini maisha yake akiwa kazini.Ana mchango mkubwa sana katika operesheni hii.Amefanya kazi kwa muda mrefu na ameiva barabara.Nadhani ni wakati sasa wa idara hii ya ujasusi kuwa na kiongozi kijana mwenye mawazo mapya kuliko kila wakati kuwa na viongozi wazee" akasema Elvis na wote wakageuka wakamtazama Meshack Jumbo na kutoa kicheko kidogo halafu wakaagana na rais akarejea ndani na mzee Jumbo akamfuata Elvis akamtaka wazungumze kidogo Elvis mimi bado nina kikao na rais kwani amewaita wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama asubuhi hii tukutane na tulijadili suala hili na kutokana na uzito wake yawezekana tusiweze kuonana mara kwa mara lakini naomba nikushukuru kwa mara nyingine tena kwa yote uliyoyafanya.Umeniokoa mimi na familia yangu.Nitaendelea kukuombea daima ili uweze kuwa na maisha mazuri huko uendako ila nina ombi moja kwako" "Nakusikiliza mzee wangu" akasema Elvis "Naamini wewe na Patricia mmefikia mwisho na uwezekano wa kurudiana ni mdogo sana hivyo nakushauri ukaanze maisha mapya mbali na hapa.Achana na kazi hizi na uanze maisha mengine lakini utakapoondoka usimuache Graca.Ni binti mzuri,ana kila sifa nzuri,ana heshima adabu na anakufaa.Mpe nafasi.Kayatengenezeni upya maisha yenu na ninakuhakikishia Elvis mtakuwa ni wenye furaha kubwa katika maisha yenu.Haitakuwa rahisi kwako kuishi bila Patricia lakini hiyo ni sadaka ambayo itakubidi uitoe kwa taifa lako.Patricia ni mwanamke mrembo atabahatika kupata mwanaume mwingine watapendana na isitoshe sisi sote tupo na tutaendelea kumuangalia na kuhakikisha hakuna kitu atakachopungukiwa" akasema Meshack Jumbo "Mzee Jumbo,hilo ni suala ambalo nilikuwa ninazungumza na rais muda mfupi uliopita na nimeamua kwenda kuishi mbali na hapa na sintaondoka mwenyewe bali nitaongozana na Graca.Sitaki kumpa wakati mgumu Patricia.Itanilazimu nikubali kumuacha aendelee na maisha yake kwani tayari nimekwisha msababishia jeraha kubwa moyoni mwake ambalo litachukua muda kupona.Nimeupokea ushauri wako na nitauzingatia" Tayari kulianza kupambazuka na maongezi hayakuchukua muda mrefu Elvis na wenzake wakaondoka wakimuacha Meshack Jumbo ikulu.Walirejea katika nyumba ile ya Vicky wakakusanya kila kilicho chao wakaondoka kurejea katika makazi yao ya awali.mara tu walipofika katika makazi yao Elvis akawa na maongezi na wenzake "Ndugu zangu mimi si mzungumzaji sana na sioni neno zuri la kuwashukuru.Kutoka katika sakafu ya moyo wangu naomba niseme ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu mkubwa katika suala hili.Tusingeweza kufanikiwa kama si kwa kila mmoja wenu kujitoa mhanga.Haikuwa kazi nyepesi lakini kwa uchache wetu tumeweza kuifanikisha na tumeweza kumuokoa rais na nchi iko salama.Tumempoteza mwenzetu Vicky lakini amekufa kishujaa na historia itamkumbuka kwamba aliwahi kufanya jambo jema kwa nchi yake.Kila mara tusisahau kumuombea ili Mungu amrehemu huko aliko.Ukiacha msiba huo wa Vicky,wenzetu Juliana na Graca nao pia wamefiwa na wazazi wao na hii yote ni misiba yetu,tuungane pamoja hadi mwisho.Jambo la mwisho kabla hatujakwenda kupumzika ni kwamba baada ya kuimaliza operesheni hii nimefikiria sana na nimeona haitakuwa vyema kama nitajitokeza kwa Patricia kwa wakati huu.Nitazua mkanganyiko mkubwa sana katika jamii.Nimeamua kuondoka kwenda kuishi mbali.Nitakwenda kuishi Marekani na nitaondoka na Graca ili naye akaanze maisha mapya kama nilivyomuahidi." akanyamaza na kuwatazama wenzake halafu akaendelea "Steve utashughulikia kulijenga upya kaburi langu lililoharibiwa ili siri hii iendelee kubaki humo kwa siku zote.Ninaamini hakuna kati yetu ambaye atathubutu kuitoa siri hii ya mimi kuwa hai kwa mtu yeyote wa karibu na hasa Patricia.Nimemsababishia jeraha kubwa la moyo na sitaki aendelee kuumia zaidi endapo nitajitokeza.Narudia tena kuwashukuruni ndugu zangu kwa yale mliyoyafanya na sasa tukapumzike"akasema Elvis MIAKA MIWILI BAADAE Imekwishapita miaka miwili toka Elvis na wenzake wafanikiwe kulizima jaribio la mapinduzi na vile vile kuusambaratisha mtandao uliokuwa ukifanya biashara ya silaha na waasi wanaopigana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Mara tu baada ya kuusambaratisha mtandao huu ikiwa ni pamoja na kuwakamata viongozi wao Elizabeth na Patrice Lwibombe, kikundi cha waasi kilichoisumbua serikali ya Congo kwa miaka mingi na kuua watu wengi wasio na hatia kilisambaratishwa na amani ikarejea mashariki mwa Congo. Kwa Tanzania,watu wote walioshiriki katika mpango wa mapinduzi walikwisha kamatwa na kushtakiwa kwa uhaini na baada ya kesi kuunguruma kwa muda wa mwaka mmoja hatimaye Elizabeth,makamu wa rais Dr Shafi,David sichoma na wengine wote waliojihusisha katika njama zile za kuiangusha serikali wakakutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.Mtandao wote uliojihusisha katika biashara haramu ya silaha ulikamatwa na wahusika wote wakatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alitimiza ahadi yake kwa kumteua Steve kuwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa baada ya mzee Meshack Jumbo kustaafu.Steve tayari amekwisha funga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Samira na wamejaliwa mtoto mmoja Snura.Winnie mdogo wake Vicky alihitimu shahada yake na kujikita katika kuendeleza miradi iliyoachwa na dada yake.Juliana aliuza sehemu kubwa ya mali walizokuwa nazo na kuanzisha kampuni yake kubwa ya mavazi pamoja na kufungua biashara nyingine.Hakutaka kuendelea kujihusisha kwa namna yoyote na biashara za mama yake.Licha ya maendeleo yake mazuri katika kampuni yake iliyojulikana kwa haraka sana alikuwa katika penzi zito na Dr Philip na walikuwa na mipango ya kufunga ndoa.Doreen rafiki mkubwa wa Patricia na ambaye alimsaidia sana Elvis alihamia nchini Norway waliko wazazi wake hakutaka tena kuishi Tanzania baada ya Elvis kuondoka na kumuacha kwani alikuwa na mategemeo makubwa ya kuanza naye maisha mapya. LOS ANGELES - MAREKANI Ni saa mbili za usiku kwa saa za Marekani,Elvis alikuwa sebuleni na mpenzi wake Graca huku mtoto wao Devotha akicheza katika zuria zito,walikuwa wanazipitia picha walizotumiwa na Steve za harusi ya Patricia na Dr washington iliyofungwa katika kanisa la mtakatifu Zakaria na baadae kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika hoteli ya Samawati beach. "Ilikuwa ni sherehe kubwa na iliyofana sana" akasema Graca "Ninamuona Patricia akiwa na uso uliojaa tabasamu.She's happy.I'm so happy to see her like this.Naamini tayari amekwisha nisahau na ameamua kuendelea na maisha yake.Kwa hatua hii ninaweka nukta katika kitabu chetu na kukifunga kabisa.Mungu atanisamehe sana kwa yote niliyomtendea Patricia" "Elvis usijilaumu sana.Haikuwa dhamira yako kumuacha Patricia lakini ilikulazimu kufanya vile.What you did,saved president and the country you love." akasema Graca "Uko sahihi Graca.Kwa hili nililolifanya nimeokoa maisha ya watu ambao wangeangamia bila hatia kwa silaha zilizouzwa na mtandao wa akina Frank.Kwa sababu ya maamuzi yale,mashariki mwa Congo hivi sasa kuko salama.Kile kikundi cha waasi kilichokuwa kinapambana na serikali ya Congo kwa miaka mingi hakipo tena.Ni kwa sababu ya maamuzi haya niliyoyafanya,nchi yangu imetulia na inapiga hatua kwa kasi kubwa sana.Kama tusingefanikiwa kuzima jaribio lile la mapinduzi hivi sasa nchi yetu ingeendelea kunyonywa na kuzidi kudidimia katika umasikini.Kingine ni kwamba nilimuokoa rais ambaye waTanzania wanampenda na ambaye anafanya mambo makubwa sana hivi sasa na kuufanya uchumi wa Tanzania upae kwa kasi ya kushangaza.Uko sahihi sipaswi kujilaumu sana japo kuna nyakati ninaumia kwani sintaweza kuwa karibu tena na wale watu wangu wa karibu na sintaweza kurejea tena Tanzania" "Elvis,samahani kwa hili nitakalokuuliza" "Bila samahani uliza Graca" "Patricia tayari amefunga ndoa na umekiri kwamba kitabu chako na yeye umekifunga rasmi,vipi kuhusu sisi? Elvis akatabasamu na kusema "Kitabu kimoja kikifungwa kinafunguliwa kitabu kingine.Nimekifunga kitabu changu na Patricia na sasa nafungua kitabu cha Elvis na Graca" akasema Elvis na kumtazama Graca kwa sekunde kadhaa halafu akauliza "Will you merry me Graca? Graca akamkumbatia Elvis na kumporomoshea mabusu mazito mazito. "Yes.!! Yes!!..Nimesubiri kauli hii kwa muda mrefu.Nakupenda sana Elvis na ninakuahidi nitakuwa mke mwaminifu kwako.NItakupa furaha katika maisha yako yote" akasema Graca . "Ahsante Graca.Nakupenda pia"akajibu Elvis na mipango ya ndoa yao ikaanza usiku ule ule bila kuchelewa .

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    TAMATI

0 comments:

Post a Comment

Blog