Simulizi : Milioni Thelathini
Sehemu Ya Pili (2)
“Haraka ya nini, Salma? Kwani nimeanza kuzeeka?” badala ya kujibu, Chris naye alimtupia swali.
“Hapana, hujazeeka,” Salma alijibu. Kisha akaongeza, “Lakini we' mwenyewe si unaona jinsi dunia ilivyoharibika siku hizi? Ukimwi nje, nje! Ni vizuri mtu ukaoa na kutulia na mkeo.”
Chris aliachia tabasamu la mbali huku akimtazama Salma usoni, akijaribu kutafakari kama hayo aliyoyasema yalimtoka kwa dhati au ilikuwa ni aina fulani ya mzaha. Macho yao yakagongana.
Salma naye akatabasamu, kisha akacheka.
“Wewe umeolewa?” hatimaye Chris alimuuliza.
“Bado,” Salma alijibu akiyaepuka macho ya Chris.
“Kwa nini?”
“Basi tu.”
“Basi tu?” Chris alimbana. “Una maana hauna mpango wa kuolewa?”
“Sio hivyo.”
“Ila?”
“Sijampata nimpendaye, na sijampata anipendaye,” Salma alijibu huku akilikuza tabasamu lake na kumtazama Chris kwa namna ya kutamka mengi zaidi ya hayo aliyokwishayatamka.
Chris aliguna. Kisha akasema, “Basi kumbe hatutofautiani. Lakini mambo hayafanywi kwa papara. Naamini ipo siku kila mmoja wetu atampata wake. Yote ni mipango ya Mungu.”
Ghafla kimya kikatanda. Macho ya Salma yakahamia kwenye mfuko wa nailoni uliokuwa mapajani mwa Chris. “Vipi, nd'o umeleta mzigo nijichagulie?” hatimaye alimuuliza.
“Yeah.”
Salma aliutwaa mfuko na kuchungulia ndani yake kisha akauweka juu ya stuli. “Nahitaji umakini katika kuchagua,” alisema huku akinyanyuka. Akavuta hatua akielekea chumbani kisha ghafla akasita, akageuka na kumtupia swali Chris. “Unatumia kinywaji gani?”
“Chochote kilichopo.”
“Chochote?” Salma alimuuliza huku akimtazama kimasikhara.
“Nikikupa bia utakunywa?”
“Nitajaribu.”
“Gongo?”
Chris alicheka. “Kwa mwanamke kama wewe, sidhani kama itakuwa rahisi kuyaweka maisha yako hatarini kwa kuhifadhi kinywaji hicho ndani mwako,” alisema.
“Kipi cha ajabu? Watu wanahifadhi ngozi za binadamu ndani, itakuwa gongo?”
Kwa mara nyingine Chris alicheka. “Sawa, umeshinda mama. Kwa hiyo unataka kunipa kinywaji gani, bia au gongo?”
“Humu ndani kuna bia, maji, soda na juisi.”
“Ok, kile utakachokunywa wewe ndicho nitakachokunywa mimi.”
Salma alimtazama kidogo kisha akanyanyuka. Akavuta hatua akilifuata jokofu. Akachanganya miguu mtoto wa kike, uchokozi wake wa kutingisha makalio ukizidishwa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipolifungua jokofu alitoa makopo manne ya bia kisha akageuka na kumuuliza Chris, “Utachanganya na toti mbili, tatu za kinywaji kikali?”
Chris aliguna kisha akatabasamu kwa mbali. Kisha naye akauliza,
“Salma, unataka kunizimisha?”
“Aah, wapi. Nakuuliza hivyo kwa kuwa hizi ni Tusker, na wanaume wengi hudai kuwa Tusker ni bia za wanawake.”
“Ok, una kinywaji gani kingine?”
“Kuna whisky; Canadian Club Classic.”
Hakikuwa kinywaji kigeni sana kwa Chris. Aliwahi kuinywa whisky hiyo siku moja alipokwenda Beachcomber Hotel katika mipango tyake ya pesa. “Nipe toti tatu tu.”
“Poa.”
Dakika chache baadaye vinywaji vilikuwa mbele yao. Na baada ya kushusha mafunda kadhaa vinywani mwao, Salma alivitoa vitenge vilivyokuwa ndani ya mfuko. Akaviangalia kwa makini kisha akasema, “Vyote ni vizuri. Nashindwa kusema kipi kinafaa zaidi ya kingine.”
Chris alitwaa glasi kwa mara nyingine na kuipeleka kinywani. Akameza funda zito la kinywaji chake. Akakunja uso kidogo na kumtazama Salma. Macho yao yakagongana. Salma akatabasamu na kuyaepusha macho yake kwa namna ya kuona haya.
“Lakini kwa leo sikuja rasmi kwa biashara,” Chris alisema. “Hiyo ni zawadi yako tu.”
“Zawadi?” Salma alimtazama kwa mshangao.
“Ndiyo, ni zawadi tu, bibie,” Chris alisisitiza huku akimtazama Salma kwa macho yaliyoongea jambo jingine, nje ya biashara iliyowakutanisha, macho ya yaliyosihi jambo fulani kwa msisitizo wa aina yake. Yalikuwa ni macho yaliyomvutia Salma. Akatamani kuwe na tamko jingine la wazi kufuatia macho hayo yalivyomtazama. Kwa kiasi kikubwa mwili ulimsisimka.
Akashusha pumzi ndefu na kunywa mafunda mawili, matatu huku akiyaepuka macho ya Chris. Hatimaye akapiga moyo konde na kuifukuza aibu iliyokuwa ikimsumbua.
“Ya kweli hayo?” hatimaye alimuuliza Chris huku akimtazama tena.
“Sikutanii, Salma. Nimetamka hayo kutoka moyoni.”
Salma hakujibu kwa maneno. Aliipitisha mikono shingoni kwa Chris, akajisogeza, nyuso zao zikakaribiana, Salma akambusu kwenye shavu la kulia, kisha la kushoto.
Na kama vile haitoshi, akaupenyeza ulimi wake kinywani mwa Chris, tendo ambalo halikukumbana na pingamizi lolote. Wakatulia kwa takriban dakika nzima katika hali hiyo kisha wakatengana.
Wakatazamana kwa namna ya kipekee, macho yao yakizungumza mengi yaliyo mioyoni mwao. Moyoni mwa Salma aliona kuwa huo ni mwanzo mzuri kwake. Nafsi yake iliridhika.
“Nashukuru sana,” hatimaye Salma alisema kwa sauti yenye kijimkwaruzo cha mbali, macho yake yaliyolegea yakimtazama Chris sawia. Akaongeza, “ Sijui...sijui nikushukuru vipi ili unielewe. Naamini kauli haitoshi.”
Chris alitabasamu kidogo kisha akanywa tena ule mchanganyiko wake wa bia na pombe kali. Safari hii aligugumia. Bia ya pili ikafunguliwa. Hawakuishia hapo, hatimaye walijikuta kila mmoja akiwa amekunywa bia nne.
Sasa Salma alichangamka zaidi. Akasimama na kuifuata televisheni. Akatwaa mkanda mmoja wa video na kuupachika kwenye deki. Ulikuwa ni mkanda wenye nyimbo zenye miondoko ya taarabu.
Akaiwasha. Kioo cha televisheni kikaanza kutoa picha ya waimbaji wa kike na wa kiume wa kundi moja la taarabu wakiimba. Mdundo safi wa ala za wimbo huo ukasikika.
“....WEWE NI WANGU...WEWE NI WANGU ...CHUKUA CHOCHOTE KWANGU...CHANGU NI CHAKO...CHUKU...CHUKU...CHUKUA...TUMIA UTAKAVYO...NAKUPA VYOTE...”
Hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno yaliyoimbwa katika kibwagizo cha wimbo huo. Muziki ulipokolea, wanawake wawili, watatu wakaanza kucheza, wakinengua viuno kwa umahiri wa aina yake. Macho ya Salma na Chris yakatekwa na unenguaji ule. Salma alionekana kukunwa vilivyo na unenguaji wa wanamuziki hao.
Hakuvumilia, alisimama na kuanza kucheza, akifuatisha aina ya uchezaji wa wanamuziki wale walioonekana kwenye mkanda wa video. Akacheza, akacheza, aibu zikiwa zimemwacha umbali wa maelfu ya kilometa, machoni mwake na akilini mwake.
**********
SALMA alikuwa mnywaji mzuri wa bia. Lakini unywaji wake haukuwa kama huu wa jioni hii. Alikuwa msiri. Akizingatia kuwa hawara yake, Abdulrahman Sadick alikuwa ni mtu wa 'swala tano' hakupenda aibaini tabia yake hiyo ya unywaji bia. Hivyo alikuwa makini. Kama Abdulrahman amelala kwake Salma leo, basi kesho yake, piga, ua, lazima alale Magomeni Mapipa ambako ndiko alikokuwa na nyumba yake na familia yake.
Huo ndio ulikuwa utaratibu wa Abdulrahman, utaratibu ambao baada ya kutekelezwa zaidi ya mara tano, Salma alijenga imani kuwa ni tabia iliyokwishageuka sheria. Na kwa kuwa pia Salma alishabaini kuwa Abdulrahman hulaani sana anasa, hususan dansi, taarabu na pombe, hakutaka kuweka bayana kwa Abdulrahman juu ya tabia na mapenzi yake kwa bia.
Ni Abdulrahman aliyemnunulia nyumba hiyo. Ni Abdulrahman huyohuyo aliyemjazia samani za kisasa ndani ya nyumba hiyo, na, ni Abdulrahman huyohuyo aliyemnunulia hilo gari, Toyota Land Cruiser GX pamoja na kumfungulia akaunti benki, akaunti yenye pesa kiasi cha 5,000,000/=.
Ni mwanamume gani ambaye angekuwa radhi kutekeleza hayo kwa kigezo cha uhusiano wa mapenzi? Haikumjia akilini kuwa hayo yanaweza kufanywa hata na wanaume watatu kati ya kumi wenye mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao wa kike au hata wake zao. Aliyoyafanya Abdulrahman dhidi yake, yalimfanya amheshimu kwa kiasi kikubwa.
Ndiyo, alimheshimu, lakini heshima hiyo haikuwa pingamizi zito la kumfanya aache kunywa walao bia moja hata mbili katika siku atakazolazimika kulala peke yake katika nyumba hiyo ya kifahari. Ataupataje usingizi kama atalala peke yake bila ya kunywa bia au kuliwazwa na Abdulrahman kwa maneno au kustareheshwa kwa vitendo?
Ni katika kuepuka taabu ya kuusaka usingizi usiku, ndipo alipoamua kuendelea na tabia yake ya kunywa bia pale ilipotokea akabaki peke yake, tabia aliyokuwa nayo kabla Abdulrahman hajamwona, akammezea mate na kumtamkia aliyopenda kumtamkia. Jioni hii, Abdulrahman hakuwepo, na si kwamba ilikuwa ni kwa jioni hiyo tu, bali kwa wiki nzima au zaidi ijayo.
Siku mbili zilizopita, Abdulrahman alimuaga kuwa alikuwa na safari ya Muscat ambako angechukua wiki tatu na kurejea. Ilikuwa ni safari, kama safari nyingine za nje alizokwenda. Kuna wakati alikwenda Misri, kuna siku alikwenda Dubai na kuna siku ambazo alikwenda Syria.
Kwa nini asiifurahishe nafsi yake kwa muda huo alio peke yake? Kwa nini asiutumie uhuru huo alionao?
Ni kwa nafasi aliyokuwanayo, ndiyo maana sasa alikuwa kishakunywa funda kadhaa za kopo la tano la bia. Na ni kwa uhuru huo alioupata ndio ikawa sababu ya kumfanya asijali kusimama na kuanza kucheza, akinengua na kunengua kiasi cha kumfanya Chris aisahau kwa muda bia yake, akabaki akimkodolea macho
Salma alikuwa mtundu na mahiri katika fani ya uchezaji muziki, hususan muziki wa kimwambao. Alijituma vilivyo katika kuucheza wimbo huo wa taarabu, akinyoosha vidole vya mikono kwa staili ya aina yake, macho kayalegeza kama mgonjwa wa malaria aliyedungwa sindano ya Quinine. Kwa ujumla alionekana kukolezwa na midundo ya wimbo huo.
Chris alimtazama kwa makini, akishindwa kuamini kama kiuno kile kilikuwa na mfupa. Akajenga imani kuwa yeyote aliyebahatika kupenya katikati ya miguu ile ya Salma, basi alipata kile alichokihitaji katika kuiridhisha nafsi yake, kile ambacho hata yeye alihisi moyo ukimshinikiza akiombe.
Wakati Salma akiendelea kucheza kwa umahiri mkubwa, alibaini kuwa Chris alimtazama, zaidi ya utazamaji wa kawaida. Alionyesha bayana kuwa kuna kitu alichohitaji, zaidi ya kuvutiwa na uchezaji wake. Na ni hilo alilolihitaji Salma!
Sasa hakutaka kumchelewesha mwanamume wa watu. Akamfuata pale sofani na kumuuliza, “Vipi, Chris wewe siyo mpenzi wa rusha-roho?”
Chris aliachia tabasamu hafifu kisha, badala ya kujibu, naye akauliza, “Kwa nini unaniuliza ivo?”
Huku akiendelea kucheza, japo sasa alipunguza manjonjo, Salma akasema, “Ungekuwa mpenzi wa rusha-roho ungekuja kunipa tafu.” Alipoona Chris anasitasita, akaongeza, “Njoo basi tucheze walao huu wimbo mmoja.”
Bado Chris alionyesha kusitasita. Salma akamfuata na kumshika mkono. Akamvuta taratibu. Chris akatii. Akanyanyuka na kujimwaga katikati ya sebule akimkaabili Salma. Salma akaipitisha mikono shingoni kwa Chris na kumsogeza karibu yake. Wakawa wakicheza huku Salma akiendelea kunengua taratibu.
“Shika hapa,” Salma aliipeleka mikono ya Chris kiunoni kwake.
Mwili ukamsisimka Chris. Shetani akampanda kichwani pale alipokipapasa kiuno cha Salma na wakati mwingine kutomasa robota lililotulia chini ya kiuno hicho.
Wakati huo Salma naye akawa akimpapasa mgongoni kwa namna ya kipekee iliyomtia wazimu Chris. Mgusano wa miili yao ukawa kichocheo kingine kilichozua msisimko usioelezeka kirahisi. Chris akawa akihema kwa shida. Mara Salma akamsukuma taratibu kurudi nyuma. Mwanamume akarudishwa hadi wakalifikia sofa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chris akajikuta akiliangukia sofa chali, Salma akamwangukia kifuani na kuendelea kunengua taratibu na kiufundi zaidi, akiufuata mdundo wa wimbo ule wa taarabu. Mwili wake teketeke ukawa unabinuka na kubonyea hapa na pale juu ya Chris kama mawimbi baharini huku miguu kaitanua na mikono kaikita kushoto na kulia mwa Chris.
Mara Salma akaupenyeza ulimi kinywani mwa Chris huku vidole vyake laini vikizamishwa masikioni. Chris akajiona yu katika wakati mgumu zaidi. Alihisi akipaa hewani kwa namna ya ajabu, ambayo ni vigumu kuielezea. Mwili ulimsisimka kwa kiwango kisichokadirika.
Akiwa ni mwanamume kamili, aliyekamilika katika idara zote maungoni, Chris alishabaini kuwa Salma kishavuka mpaka, na kwamba alihitaji huduma, zaidi ya hapo walipofikia. Dakika chache baadaye walikuwa katika hatua nyingine, wakiziridhisha nafsi zao kwa mateso yaburudishayo.
**********
“CHRIS umenibaka,” Salma alitamka kwa sauti iliyodhoofu, kijimkwaruzo cha mbali kikijitokeza katika sauti hiyo. Wakati huo alikuwa akimtazama Chris kwa macho ambayo ni kama vile yalikuwa yakitamka “kazi yako inaridhisha...”
“Hapana, ni wewe uliyenibaka.”
Salma alicheka. “U'shasikia lini mwanamke akimbaka mwanamume?” hatimaye aliuliza huku akijitoa sofani na kuanza kujifunga tena ile kanga yake ambayo katika kipindi kifupi kilichopita ilisahaulika zuliani.
“Hilo sijalisikia,” Chris alisema. “Lakini ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke naye ana uwezo mkubwa wa kubaka.”
“Kwa vipi?”
“Atatumia hila za kike bila nguvu kuhusishwa,” Chris alifafanua. “Mwanamume atachanganywa kwa vituko vya ajabu kiasi cha kujikuta akilitenda lile ambalo hakutarajia kulitenda. Na kwa mwanamke wa aina yako, mwenye sura inayovutia na umbo linalotamanisha, ni rahisi sana kuivuruga akili ya mwanamume mwenye msimamo mkali.”
Salma alimtazama kidogo Chris kisha akamuuliza, “Kwa hiyo umechukia?”
“Hapana, sijachukia. Nimefurahi, na kwa ujumla umenifurahisha sana.”
“Asante,” Salma alinong'ona huku akimbusu shavuni, akambusu mdomoni na kumbusu kitovuni.
Wakati huo mkono mmoja ulikuwa katikati ya miguu ya Chris, ukipapasa na kutomasa kwa namna ya kipekee. Akamtazama tena Chris usoni sawia. Macho yao yalipokutana, Salma akahisi vitu fulani visivyoelezeka vikimtambaa mwilini. Akatamani kulirudia zoezi lililohitimishwa muda mfupi uliopita.
Hata hivyo alijitahidi kuuhimili mhemko huo uliomwingia. Akajitoa sofani hapo kivivuvivu. Akajifunga kanga vizuri kisha akaondoka kwa mwendo wake wa kujitupatupa. Mara ghafla aligeuka na kumtazama Chris kwa macho 'yaliyochoka.' Kisha akamwambia, “Mpenzi, subiri nikaoge. Au twende tukaoge.”
Siyo kwamba Chris alikuwa ni mgeni wa wanawake. La. Tangu alipoamua kutema masomo na kufanikiwa kupata pesa katika yale matukio matatu ya awali, tayari alishadiriki kuchukua wanawake wasiopungua kumi na watano, na hao wakiwa ni wanawake ambao machoni mwa wanaume wengi walichukuliwa kuwa ni wa daraja la kwanza.
Huyu Salma naye, machoni na akilini mwa Chris alikuwa ni mwanamke wa daraja la kwanza. Sifa hiyo ilitokana na sura yake, umbo lake na utundu wake pale alipomruhusu kupenya katikati ya miguu yake. Lakini sifa hiyo haikuweza kumfanya Chris abweteke na kukubali kila aambiwacho na mrembo huyo.
Papohapo alipinga, “Hapana. We’ kaoge tu. Mi' nitaoga baadaye.”
“Unaogopa?” Salma alimuuliza huku akimkazia macho. “Unaogopa nini? Unaogopa nini wakati nilishakwambia kuwa sina mtu? Una wasiwasi wa kufumaniwa?” tabasamu la mbali likachanua usoni pake.
“Siyo kwamba naogopa kufumaniwa. Naiamini kauli yako kuwa huna mwanamume. Lakini us'jali. Ni mapema mno kufikia hatua hiyo unayotaka.”
******
WIKI mbili baada ya siku hiyo uhusiano wao ulikuwa umekomaa, uhusiano ambao kwa Salma ulikuwa wa dhati wakati kwa Chris ulikuwa ni wa kuiridhisha tu nafsi kwa starehe za chumbani. Hakuwa mjinga, akili yake ilifanya kazi kwa usahihi, na alihakikisha anafanya kila jambo kwa utaratibu mzuri, utaratibu alioamini kuwa hautamtia mashaka yoyote Salma.
Mara mbili, tatu walikuwa wametoka pamoja jioni na kwenda kwenye baa maarufu kunywa bia. Asubuhi hii, ikiwa ni miongoni mwa siku ambazo Chris alilala usiku kucha hapo kwa Salma, Chris alimuuliza, “Leo itakuwaje?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ki-vipi?”
“Si unajua leo ni wikiendi? Itakuwa shwari kama tungepata lunch eneo tofauti na tulikokuzoea.”
Salma alifikiri kidogo kisha akamuuliza, “Kama wapi unapopaona panafaa?”
Chris naye alionyesha kufikiri, kisha akajibu, “Twende Kinondoni.”
“Kinondoni?!”
“Yeah, Kinondoni, pale Kingo House. Unapafahamu?”
Salma alitikisa kichwa akionyesha ishara ya kukataa, kisha akatupa swali: “Ni sehemu iliyotulia?”
“Sana tu. Hata msosi wao ni wa ukweli.”
“Ni Kinondoni ipi?”
“Jirani na soko la Juhudi, maarufu kama soko la Ma-TX.”
“Pale jirani na makaburi ya mwembejini?”
“Hapohapo.”
“Ni jengo la ghorofa moja, zamani kulikuwa kunapigwa muziki wa dansi kila mwisho wa wiki?” Salma aliongeza.
“Ndiyo, kumbe unapafahamu.”
Ukimya ukatawala. Kila mmoja alionekana kuzama mawazoni.
“Kwa hiyo?” Chris akauvunja ukimya huo.
“Shwari tu.”
Chris akashusha pumzi ndefu kisha akasema, “Nitakuwa nyumbani hadi saa sita mchana. Kisha nitatangulia. Kwa mimi ninayeishi Kinondoni Shamba, nitafika pale baada ya dakika tano au kumi tu kwa kutembea. Nikishafika nitakupigia simu. Sawa?”
“Ok.”
**********
SIGARA mkono wa kushoto, gazeti mkono wa kulia, Chaka alikuwa mbali kimawazo. Alikuwa ndani ya ukumbi wa baa, Zanzibar Hotel, Mtaa wa Zanaki katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Aliitazama saa yake na kuguna. Ilitimu saa 4.15 asubuhi. Akashangaa kwa nini Chris hajampigia simu hadi muda huo ilhali siku iliyopita walikubaliana kuwa hadi saa 4.00 wawe wameshawasiliana.
Kelele za wateja waliojazana ukumbini humo, pamoja na macho ya makahaba wa kike na mashoga hazikuwa kero za kumfanya ashindwe kutafakari mambo yake. Yeye alizama kwenye kinywaji chake kilichokuwa mezani, sigara ikiendelea kuteketea, fikra zikiwa juu ya Chris.
Mara katikati ya mawazo yake akasikia simu yake ikiita. Akaitoa mfukoni na kuitazama kwenye kioo. Jina la CHRIS lilikuwa likitawala. Akaminya kitufe cha kupokelea na kuitega sikioni. “Sema,” ndivyo alivyoanza.
“Uko wapi?” upande wa pili ulihoji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“City centre. Wewe?”
“Muda huu niko home.”
“Home? Yaani Kinondoni au...”
“Nd'o maana'ake.”
“Kwa hiyo inakuwaje?”
“Siki'za,” Chris alitamka kwa msisitizo. “Kati ya saa sita, saa saba na kuendelea tutakuwa pale Kingo House tukipata lunch. Unapafahamu?”
Chaka alicheka. “Swali gani hilo Chris? Yaani mtu ka' mimi nisipajue Kingo House?”
“Basi uje pale ukakione kifaa chenyewe,” Chris alisema.
“Nije katika mida hiyo ya kati ya saa sita na kuendelea, sio?”
“Yeah. Yeye anaweza kufika kuanzia sita na nusu.”
“Poa,” Chaka alisema na kukata simu.
Mfumo wa maisha ya Chaka haukutofautiana sana na ule wa Chris. Yeye aliikimbia shule wakati akiwa katika muhula wa pili wa darasa la sita huko Mkuranga mkoani Pwani.
Akalivaa jiji la Dar es Salaam na kuamua kuishi na mjomba wake katika kitongoji cha Buguruni. Miaka miwili baadaye, utun
utundu wa kujifunza fani hii na ile ulimfikisha eneo la Gerezani, Kariakoo ambako alikuwa msaidizi wa fundi makenika mmoja aliyeishi hukohuko Buguruni.
Wepesi wa kudaka mafunzo ya umakenika ulimfanya ajue kuendesha gari kwa kipindi kifupi cha miezi mitatu tu ya awali katika eneo hilo. Mwaka mmoja baadaye alikuwa fundi mzuri na dereva jasiri.
Ndipo alipoamua kuangaza macho mbele. Akajiingiza katika mfumo mpya wa kupata pesa kwa njia aliyoamini kuwa ni fupi na yenye mafanikio bora. Ni katika mfumo huo mpya wa maisha ndipo alipokutana na kufahamiana na Chris. Wakashirikiana katika lile tukio la kumpora gari dereva teksi kule Bunju. Akaanza kukomaa katika kazi hiyo.
Kwa siku hii, alitarajia kufanya kazi nyingine, kazi ambayo Chris alimwahidi malipo ya shilingi milioni 5. Hivyo, hadi alipokata simu, dalili njema za mafanikio zilikuwa mbele yake.
“Lete bia nyingine,” kwa sauti ya kujiamini alimwagiza mhudumu aliyepita mbele yake.
******
ENEO la vinywaji na maakuli pale Kingo House lilikuwa tulivu Jumamosi hii. Hakukuwa na wateja waliozidi ishirini, na robo tatu yao walikuwa wakila chakula huku waliosalia wakiwa na chupa za vinywaji mbalimbali mbele yao. Gari jeusi aina ya Toyota Land Cruiser GX liliingia katika eneo hilo saa 6: 40.
Dakika chache baadaye, Salma, akiwa amevaa T-shirt nyeupe, suruali nyeusi ya jeans, miwani mieusi usoni na kofia pana kichwani aliteremka na kuangaza macho huku na kule katika ukumbi huo maridadi. Hatimaye alianza kuvuta hatua fupi akiifuata meza iliyokuwa pembezoni mwa eneo hilo.
“Samahani kwa kuchelewa,” alimwambia Chris ambaye ndiye mtu pekee aliyekuwa hapo mezani.
“Us'jali, bado hakijaharibika kitu,” Chris alisema.
Salma alivuta kiti na kuketi. Kisha akauliza, “Vipi, we u'shakula?”
“Bado. Tulikubaliana kuwa tutapata lunch pamoja, vipi tena niwe mroho na mlafi?”
Salma aliangaza macho huku na kule katika mandhari ya eneo hilo. Kisha akauliza, “Kuna chakula gani hapa?”
Chris alimsogezea kijikaratasi chenye orodha ya vyakula. Wakati Salma akiendelea kusoma, mara mhudumu akawafikia. “Karibuni. Niwasaidie?” aliwauliza.
“Ugali, samaki,” Chris aliagiza.
"Dona au sembe?" mhudumu alihitaji ufafanuzi.
"Dona."
"Na samaki gani?"
"Kwani mna samaki gani?"
"Wa baharini na mugebuka ya Kigoma na sato wa Mwanza."
"Fanya mugebuka wa kushiba."
“Mimi niletee Ndizi- Bukoba kwa kuku,” Salma alisema.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda mfupi baadaye walikuwa wakivishambulia vyakula walivyoagiza. Lakini Chris hakufika mbali, mara akakunja uso na kuisogeza pembeni sahani ya chakula.
“Vipi tena?” Salma alihoji huku akimtazama Chris kwa mshangao.
“Kuna kitu nimesahau.”
“N'nini?”
“Pesa za watu,” Chris alijibu huku akikunja uso. “Kuna mtu atakuja hapa kuchukua pesa zake. Tatizo ni kwamba sijaenda benki kuzichukua.”
“Yaani hilo nd'o limekufanya uache kula? Au kuna jingine?”
“Hakuna jingine. Ni hilo tu. Tatizo, mtu mwenyewe yule hana maana. Anatukuza ahadi za kizungu. Akija hapa na nikampa hadithi nyingine, hatanielewa. Ataanza kulalama ovyo.”
“Kwa hiyo suala hilo ni muhimu zaidi ya chakula?”
“Inaweza kuwa hivyo,” Chris alijibu huku akinyanyuka kitini. Akamtazama Salma na kumwambia,“Niazime gari niwahi CRDB mara moja.”
“Kumbe unajua kuendesha?!”
“Mbona siku nyingi tu.”
“Leseni unayo?”
“Kwa hapa sina. Iko nyumbani.”
“Trafiki wakikubamba?”
Chris alicheka. “Tanzania kuna trafiki?” alimuuliza huku akionyesha kutobabaika. Akaongeza, “Usihofu. Sikuanza leo kuendesha gari. Isitoshe ni'shawahi kumaliza mwaka mzima bila ya leseni hai, na barabarani natanua bila matatizo yoyote.”
Salma alitoa ufunguo na kumpatia. “Utachukua muda gani?”
“Haifiki hata nusu saa. Si unajua leo ni wikiendi, hakuna foleni barabarani, hasa hii njia ya wakubwa.”
“Ni CRDB ya branch gani?” Salma alimuuliza.
“Ni pale Azikiwe Branch.”
“Azikiwe Branch pale Posta Mpya?”
“Yeah.”
“Ok.”
Wakati Chris akilifuata lile Land Cruiser la Salma, alitupa macho katika pembe moja na kuiona sura ya mtu aliyemtarajia. Mtu huyo alikuwa kaketi huku chupa ya bia ikiwa mbele yake, sigara mkononi. Chris akaingia ndani ya gari na kuondoka.
Hakuwa akielekea CRDB. Safari yake ilikuwa ni ya Kimara, hivyo
alikanyaga kibati cha mwendo hadi kwenye geti la nyumba ya Aloyce Tarimo. Geti likafunguliwa, gari likapenya ndani. Huko akaonana na mwenyeji wake na kumwambia, “Hiki ndicho kifaa chenyewe. Unakionaje?”
Aloyce Tarimo alitikisa kichwa akionyesha ishara ya kukubali. Akawa akilitazama gari hilo kwa makini. Akalizungukia kila upande akilikagua kisha akaingia ndani na kupiga swichi. Injini ikaitika bila ya wasiwasi.
Akalizungusha humo ndani ya yadi kisha akalirejesha pale alipomwacha Chris. Akateremka . “Kwa hiyo nd'o inakuwaje?” alimuuliza huku akimkazia macho.
“Nakusikiliza wewe.”
“Bado umesimamia palepale?”
“Nd'o maana'ake.”
“Thelathini ni nyingi sana, Chris. Punguza kidogo.”
“Haipungui, Tarimo,” Chris alijibu.
“Hata kidogo?”
“Hata senti moja! Vipi Tarimo, mbona unaanza kurudi kwenye mjadala huku tu'shazungumza tukayamaliza? Hivi unaweza kun'ambia bei halali ya Land Cruiser ikiwa dukani? Huoni kama hii tunakupa bure tu?”
Aloyce Tarimo alishusha pumzi ndefu kisha akasema, “Ok, us'jali. Kwa hiyo itakuwa lini?”
“Ukae mkao wa kula, mwanangu,” Chris alisema kwa majigambo, macho makavu, akimtazama sawia Aloyce Tarimo. “Uwe tayari-tayari, ikiwezekana hata leo tunakuja kamili.”
“Unaweza kuja leo?” Aloyce Tarimo alimuuliza huku akimtazama kwa namna ya kutomwamini.
“Kwa nini isiwezekane? Cha muhimu ni uaminifu, baasi! We' nipe uhakika kama uko fiti, mida-mida mwanangu, tucheze vya kuchezeka.”
“Mimi tena?” Aloyce Tarimo alijigamba. Sauti yake ilijaa kebehi na uso wake ukionyesha ni jinsi gani anavyojiona kuwa yuko katika daraja la juu, yu miongoni mwa matajiri ishirini wanaoongoza duniani.
“Nakujua. Kwa hiyo?”
“Ukiweza njoo leo. Ukishindwa leo, siku yoyote utakayopanga kuja unipigie simu kwanza, saa sita kabla ya kuja.”
“Poa,” Chris alitamka kwa kujiamini, tabasamu likichanua usoni pake.
Akatwaa funguo kutoka mkononi mwa Aloyce Tarimo kisha akaingia garini na kuondoka.
**********
ALOYCE Tarimo alikuwa miongoni mwa wakazi wenye umaarufu katika kitongoji cha Kimara Baruti jijini Dar es Salaam. Karakana zake mbili kubwa za magari, baa tatu zilizohusisha pia ulaji wa nyama ya nguruwe maarufu kwa majina ya 'kitimoto' na 'mbuzi katoliki' na malori matatu makubwa ya mizigo yaliyokuwa yakifanya safari za ndani na nje ya nchi vilikuwa ni vigezo vya kutosha kumfanya hata mgeni wa eneo hilo amchukulie kuwa ni miongoni mwa watu waliopiga vita umaskini, na wakavishinda vita hivyo kwa kishindo.
Ni mtu mmoja tu, kati ya mamia ya wakazi wa eneo hilo aliyeijua siri ya mafanikio ya Aloyce Tarimo. Ni Antony Sabba.
Antony na Aloyce walikutana kiajabu-ajabu jijini Dar es Salaam, urafiki baina yao ukazaliwa, ukakua na hata ukakomaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo Aloyce Tarimo alikuwa ni mfanyabiashara mdogo aliyejishughulisha na uuzaji wa bidhaa ndogondogo Mtaa wa Msimbazi. Wiki sita baada ya kuianza biashara hiyo ya saa, vijiredio vidogo na vikorokoro vingine hatimaye asubuhi moja akajikuta akiwa na mwenzake ambaye alikuwa na biashara ya taulo, soksi na leso.
Ni lafudhi zao zilizowaunganisha. Kila mmoja alipokuwa akizungumza, mwingine alisemea moyoni, “Huyu ni Mchaga.” hatimaye Aloyce Tarimo akaamua kukata mzizi wa fitina. Siku moja akamuuliza,“Kwani wewe umetokea wapi, aisee?”
“Rombo,” Antony Sabba alijibu na kuongeza: “Na wewe?”
“Hata mimi natoka Rombo.”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment