Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MWANAHARAMU - 1

 








IMEANDIKWA NA : HAKIKA JONATHAN



*********************************************************************************



Simulizi : Mwanaharamu

Sehemu Ya Kwanza (1)



“Shikamoo madamu …”,



“Marahaba, hamjambo? “,



“,Hatujamboo …”,



“Haya kaeni ,tuanze kipindi cha siku ya leo…”,



Ilikuwa ni sauti nzuri yenye kuvutia, sauti ya mwalimu wa kike aliyefumdisha kidato cha sita katika shule ya sekondari St Peter, shule yenye mchanganyiko wa jinsia zote mbili, yaani wavulana na wasichana. Kama kawaida, mwalimu huyu aliyefundisha somo la Kiswahili aliingia dalasani mapema sana kwa ajili ya kutimiza wajibu wake kama mwalimu …



Wanafunzi wa kidato cha sita, katika mchepuo huu wa HKL takribani wote walikuwa na jinsia ya kike, isipokuwa wavulana wachache tu ambao hawakupenda kusoma masomo ya sayansi wakidai walitaka kuwa waandishi wa habari, sababu kuu iliyowafanya wao kusoma mchepuo huu …



BAADA YA ROBO SAA;



“Shikamoo mwalimu, “



“Mwalimu, nakusalimia “,



Sauti iliyorembwa na kuwaacha midomo wazi wanafunzi ilisikika, wengi walicheka sana baada ya kusikia sauti hii isipokuwa Joanitha, msichana ambaye alijikuta akidondosha chozi. Kwani alichukizwa na mabadiliko ya ghafla ya mtu aliyekuwa akimpenda sana, japo hakuwahi kufungua mdomo wake na kumtamkia jambo hilo.



“Hivi wewe Jackson, unanini? nini kimekukuta?. Sasa hivi ndio unafika shuleni, isitoshe unakuja umejiremba kama mtoto wa kike, bado umeenda mbali zaidi unabadilisha mpaka sauti na mwendo wako wa kutembea. Haraka sana nikukute ofisini, potea mbele yangu …”,



Mwalimu huyu wa kike aliyejulikana kwa jina la madamu Jesca, alitikisa kichwa chake kuashiria kumsitikia kijana Jackson. Kwani tabia zake zilibadilika ghafla, na kuwa gumzo shuleni hapo miezi michache iliyopita. Japo aliitwa na kushauriwa kuhusiana na mwenendo wake huu ambao uliacha sintofamu katika vichwa vya walio wengi, lakini Jackson ndio kwanza alizidi kubadilika kadri siku zilivyozidi kwenda. Sauti alianza kuiremba kila alipozungumza, poda na lipstick ziliipamba sura yake, kitendo ambacho kilisababisha walimu wote wa St Peter kumkalisha chini kijana huyu na kumshauri, kinyume na matarajio yao. Jackson hakubadilika! kadri miezi na siku zilivyokatika, ndivyo tabia mbaya ya Jackson ilizidi kuota mapembe …



“Huyoooo, dume jike hiloo “,



Wanafunzi wenzake hawakusita kumzomea Jackson, kwani aliondoka kwa mwendo wa maringo kuelekea ofisini, sehemu ambayo alielekezwa na mwalimu wake wa kiswahili. Madamu Jesca alishindwa kabisa kuendelea kufumdisha, akiwa na hasira alichukua vitabu vyake na chaki zake kisha kurudi ofisini …



“Fyuuuuu, yenu yanawashinda. Kazi kufuatilia ya watu …”,



Akiwa anatembea kwa maringo, aliwalaani wanafunzi wenzake huku akielekea katika majengo ya uongozi wa shule.Sauti ambayo haikusikika hata kidogo, kwani ilimezwa na kelele za wanafunzi ambao walikuwa wanamzomea …



Japo wanafunzi wa mchepuo huu wa HKL walimzomea kwa fujo Jackson, huku wengine wakiruka mpaka juu ya meza zao. Lakini msichana mrembo Joanitha alijilaza katika meza yake, akihuzunika kwa siri sana ili asiweze kugundurika na mtu yoyote …



Alijiona kama mwanamke asie na bahati katika maisha yake, tangu akiwa mtoto aliahidi kujitunza mpaka atakapo pata mwanaume aliridhika naye, alifurahi sana alipojiunga kidato cha tano katika shule ya St Peter. Kitendo cha kuwepo shuleni hapa kwa miezi kadhaa, moyo wake uliangukia kwa kijana handsome huku akiwa na weusi wa asiri uliomfanya kuvutia. Joanitha aliapa kumtamkia ukweli Jackson siku atakapohitimu kidato cha sita, huku akifuatilia nyendo za Jackson ili amfahamu kwa undani zaidi …



Hapo ndipo alijikuta akianza kumuhofia Jackson, kwani siku zote alikuwa na marafiki wengi wa kike kuliko wa kiume. Hakupenda kushiriki michezo ya kiume shuleni kama mpira wa miguu, bali alipendelea kucheza mpira wa pete na wasichana wa kike. Jambo ambalo lilimuuma Jonitha kwani alikuwa na wivu ,japo hakuwahi kutamka neno nakupenda mbele ya Jackson.



“Mimi nilisema, huyu ni punga! mnabisha, oneni sasa, hata sauti yake ameanza kuiremba “,



“Kweli kabisa, Jackson anatuaibisha wanaume. Hafai kusoma na sisi, lazima afukuzwe …”,



Wavulana wachache waliokuwa wanasoma mchepuo mmoja na Jacksoni walifoka, walionekana kuchukizwa na tabia ya mwenzao. Huku wakiahidi kuhakikisha Jacksoni anafukuzwa shuleni. Maneno ambayo yalipenya katika masikio ya Joanitha, na kumuumiza mtima wake kwani hakuwa tayali kuwa mbali na Jackson, isitoshe hakuwa tayali kumuona kipenzi chake anakosa masomo.…



Joanitha hakuona sababu ya kuendelea kubaki shuleni, alichukua kibegi chake kisha kutokomea huku kelele nyingi zikimsindikiza na kuzidi kumchanganya.



“Huyooo, anapenda dume jike wakati wanaume rijali tupoo, “



“Hiloooo “,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Aibu zimemzidi, anondoka! nyoo”,



Wanafunzi wa kike na wa kiume, wote walimsindikiza Joanitha kwa kumzomea. Huku rafiki yake Doreen akitoka nje na yeye kumfuata rafiki yake ili amfariji, alimtambua vizuri sana rafiki yake. Siku zote alihitaji msaada wa mawazo pale alipochukizwa na kukerwa …



“Joanitha, “



“Joanitha, simama please “,



“Nimesema niache, sina bahati mimi sijui nimemkosea nini Mungu “,



“Hapana usiseme ivyo, chako ni cha kwako tu kama Mungu kakupangia .”,



“Hapana,nimejitunza sana,nimemtumikia Mungu wangu kama inavyotakiwa.Kwa nini ananifanyia hivi,kwanini anataka kuniondolea furaha yangu”,



“,Hapana Joanitha,unakufuru Mungu.Unachotakiwa kufanya ni kukaa chini ma kuangalia unamsaidiaje Jacksoni,naamini ukifanikiwa kumkomboa utaudhibitishia ulimwengu kuwa wewe ni shujaa na una mapenzi ya dhati kwa Jackson,tofauti na watu wanaomtenga bila kumsaidia …”,



Doreen alijitahidi kumtuliza rafiki yake kipenzi, hawakuwa marafiki tu bali walikuwa kama ndugu kwani kila jambo walifanya kwa pamoja na kushirikiana.Walienda nyumbani au shuleni pamoja, walishauriana kwa kila jambo na kutunziana siri mbalimbali.

“Sawa, nimekuelewa. Ngoja nikapumzike. Siwezi kuendelea kusoma “,



“Huniachi peke yangu, twende wote. Robert na wenzake watanisimanga sana juu yako …”,.



“Yeye naye, nimeshasema simtaki!! mimi kumpenda Jacksoni yeye inamuuma nini? “,



“Haya bana shoga angu, tuondoke “,



Hatimaye Doreen na Joanitha walitokomea eneo la shule, huku wakielekea mahali ambapo Joanitha alikuwa amepaki gari lake. Gari ambalo alizawadiwa na baba yake siku alipofaulu vizuri kidato cha nne kwa kufaulu vizuri sana. Hakutaka kuchukua masomo ya sayansi na kuwa daktari kama baba yake, bali alitaka kuwa mwandishi wa habari japo baba yake hakupendezwa na fani hiyo …



………………………………



“Wewe Jacksoni, tumeshakuonya kuhusu tabia hizi. Kwanini hausikiii? “,



“Mimi sio Jacksoni, naitwa Aunt Jacky, kuanzia leo mnitambue kwa jina hilo …”,



“Unasemaje we mtoto?, walimu mmesikia upuuzi wa mwanafunzi wenu …”,



“Tumesikia mkuu, afukuzwe huyu anatuharibia wanafunzi wetu. “



“Hapana, wazazi zake waitwe kwanza “,



“Sasa, ondoka hapa na urudi baada ya wiki mbili ukiwa na wazazi wako. Pitia kwa sekretari uchukue barua yako …”



Kikao cha ghafla, kikao cha uongozi wa shule ya sekondari St Peter. Kilikutana ghafla kumuhoji mwanafunzi wao Jacksoni. Walijikuta wakishindwa kuelewana na kuamua kumrudisha nyumbani, huku akipatiwa wiki mbili aweze kuja na wazazi wake shuleni. Bila hofu yoyote, na bila kuwaogopa walezi wake. Jacksoni akiwa amejibatiza jina la Aunt Jacky, alitokomea mbele ya macho ya walezi wake huku akitembea kwa maringo. Mwendo wa kike ambao uliwaacha midomo wazi walimu wote wa St Peter, huku wakitikisa vichwa vyao kwani waliamini Jacksoni tayali alikuwa amepotea na wasingeweza kumbadilisha tena …



Barabara ilikuwa na msongamano wa magari mengi sana, mvua ilinyesha kwa muda mfupi tu na kuleta kero nyingi kwa watumiaji wa barabara hii kuu ya jiji la Gano. Bila kujali mvua hii, Joanitha alikamatilia uskani wa gari lake dogo aina ya Alteza. Huku pembeni yake akiwa ameketi rafiki yake kipenzi aliyeitwa Doreeni..



Kichwa chake kilijaa mawazo tele, huku ubongo ukifikili mambo makubwa zaidi ya uwezo wake. Hakumuwaza mtu mwingine kichwani kwake zaidi ya Jacksoni, mvulana pekee aliyetokea kumpenda sana japo hakuwahi kumwambia licha ya wanafunzi wake dalasani kuzitambua hisia zake dhidi ya Jacksoni. Mvulana ambaye tabia yake ilibadilika kila kukicha, na kutokea kuwa gumzo kila kona aliyokatiza. Watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Facebook na Instagram walimfahamu sana Jacksoni, kwani alijipiga picha nyingi huku akiwa na mapozi ya kike. Mapozi ambayo yalimfanya ajulikane zaidi,kwani alikuwa kinyume na maadili ya Kiafrika.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Shitii! foleni haisogei, tuache gari mahali hapa halafu tutembee. “



“Yani na mvua yote hii tutembee wakati gari lipo, sikuelewi Joanitha. “



“Basi tutachukua bodaboda ili tuwahi kufika nyumbani, “



“Bodaboda tena! situtapata ajari buree, na mvua hii wamevuta mibangi bangi yao, situtavunjwa miguu. Joanitha unawahi wapi? “,



Doreen hakumuelewa kabisa rafiki yake, tangu watoke shuleni na kuanza kurudi nyumbani. Joanitha alikuwa na mawazo kuliko siku zote, kitendo ambacho kiliashiria kuwa jambo ambalo lilitokea asubuhi shuleni kwao kuhusu Jacksoni. Kilikuwa ndio chanzo kikuu cha mawazo mengi kwa rafiki yake huku akiongea vitu ambavyo vilimchanganya na kumshangaza sana Doreeni. Kwani siku zote rafiki yake hakuwahi kupanda bodaboda, wala kutembea kwa miguu na isitoshe wakati wa mvua.



“Nataka niwahi, nianze kutafuta namna ya kumsaidia Jacksoni. “,



“Waooh, hapo utakuwa mwanamke shujaa! nakuunga mkono kwa asilimia zotee. Tuvumilie foleni, tukifika kwenu kila kitu kitakuwa sawa. “



Tabasamu zuri liliipamba sura ya Doreeni, alifurahishwa na maneno aliyoyaongea rafiki yake. Kwani siku zote aliamini tatizo sio kulikimbia bali kulikabili, japo ilikuwa ni ngumu sana tena kumsaidia mtu kama Jacksoni ambaye jamii ilikuwa imeanza kumtenga. Bila shaka hata Joanitha alikuwa katika hatari hiyo, pale ambao angeonekana karibu na Jacksoni.Mvulana maarufu aliyejulikana kwa jina la Aunty Jacky, kutokana na tabia zake za kike alizokuwa nazo.



…………………………………



Robert alifurahi sana, kitendo cha wanafunzi wote kumuunga mkono kumpinga mwanafunzi mwenzao Jacksoni zilianza kuzaa matunda. Aliamini Jacksoni atakapofukuzwa shule, basi itakuwa rahisi yeye kumpata Joanitha. Msichana ambaye alitokea kumpenda sana, japo alitukanwa na kudharirishwa kila alipomtamkia neno nakupenda, msichana huyu wa kitusi na mtoto wa daktari bingwa katika hospitali ya rufaa ya jiji la Gano.



“Lazima nimpate! Kwa gharama yoyote ile, niko tayali kuua ili tu nipate nafasi katika moyo wake. “



“Humuwezi mtoto wa kitajiri yule, nauli tu ya daladala tunakosa. Mzee wako amejipiga piga amepata ada ya kukusomesha shule za wenye nazo, soma ndugu yangu……”,



“Acha kunizingua boya wewe, maisha yangu hayakuhusu. Pita hiviii ……”,



“Kwanza imekuaje leo unatembea njia moja na sisi, oya! wadau tubadili njia, huyu dogo snichi kinazi! kama vipi tupite zetu road nyingine …”,



Robert na kundi lake wakiwa wanatembea kwa miguu kurudi nyumbani, hakusita kupiga stori mbili tatu na rafiki zake, kwani shughuli za shule zilisitishwa ghafla kutokana na utovu mkubwa wa nidhamu uliyo oneshwa na Jacksoni. Kwani tabia zake ziliichafua shule, jambo ambalo mkuu wa shule hakuwa tayali kulikubali. Alisitisha masomo kwa siku hiyo, akidai walimu walikuwa na kikao. Kikao ambacho kiliketi kwa kengo kuu la kumuhoji mwanafunzi wao, Jacksoni Mtei.



Mtoto wa mfanyabiashara wa kimataifa, jijini Gao. Mfanyabiashara aliyetambulika kwa jina la Mtei kutokana na bidhaa ya sabuni ya kuogea iliyonunuliwa na kupendwa na watu wengi barani Afrika.



“Apite hiviii! tena iwe mwanzo na mwisho kunifatilia, bila hivyo korodani zako nitazibana na praizi na kukuchoma na bisibisi tumboni “,.



Robert aliyeonekana kuwa muhuni kupitiliza, moja ya tabia ambayo ilimfanya amkose Joanitha. Alimuonya mmoja kati ya rafiki zake aliyejaribu kumshauri bila mafanikio. Jambo ambalo lilimpelekea atengwe, kwani Robert na wenzake waliokuwa wakimsapoti walibadili njia na kupita njia nyingine kabisa tofauti na rafiki yao aliyewapinga kila siku kutokana na tabia zao mbovu.



Baadhi ya walimu, pamoja na wanafunzi wenye tabia nzuri walijalibu kushauri kijana huyu asitishe urafiki na kundi la Robert lakini alikataa. Siku zote kijana huyu aliamini kutatua tatizo sio kulikimbia, bali ni kulikabili jambo ambalo lilimtia moyo kijana huyu aliyejulikana kwa jina la Kendrick.



“Sawa, ipo siku mtabadilika na kuyakubali maneno yangu “,



“Toka huko mlokole weyee, kawahubirie wenzako makanisani huko “,



Sura pana yenye macho mekundu, macho ambayo yalionesha matumizi ya bangi kwa kijana huyu.kijana ambaye alikuwa rafiki wa kufa na kuzikana wa Robert, alimfokea Kendrick huku wakitokomea machoni mwa uso wa Kendrick na kupita njia nyingine …



…………………………………



Gari zuri aina ya prado liliingia katika jengo kubwa la kifahari, jengo ambalo lilimilikiwa na mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la Mtei. Jacksoni akiwa ameketi kiti cha nyuma, dereva wake alilisogeza gari eneo la parking ya magari huku akimtazama Jacksoni kwa macho ya huba. Siku zote alimpenda sana Jacksoni kwani alimuhonga pesa nyingi sana, kutokana na mwili wake mzuri wa kimazoezi aliokuwa nao. Mwili ambao ulimtamanisha sana Jacksoni na kufanya kila njia aweze kulihonja penzi la dereva huyu. Mwanzoni dereva alikataa katu katu huku akidai dini yake haikumruhusu kufanya dhambi hiyo na isitoshe alimuheshimu sana bosi wake mzee Mtei na angelitambua jambo hilo bila shaka angempiga na bastora yake.



Siku zote pesa sabuni ya roho, kijana Jacksoni alimuwekea kiasi cha shilingi milioni moja mkononi. Huku akimuahidi zawadi kibao, jambo ambalo lilipelekea dereva huyu kukubali na kuanzisha mapenzi ya siri na Jacksoni.



“Mbona shuleni umetoka mapema? Kwanini unawaza sana “,



Dereva wake na Jacksoni huku akitoka nje ya gari alimuuliza swali Jacksoni, kwani tangu watoke shuleni mpaka wanafika nyumbani alikuwa kimya tofauti na siku zote.



“Siko sawa, nikitulia nitakwambia”,



Bila shaka dereva huyu hakukosea, Jacksoni alikuwa na mawazo mengi kupita kiasi. Jambo la kwanza ni kuhusu wazazi wake kuhitajika shuleni, jambo lingine ambalo lilimuuma kupita kiasi ni baada ya kugundua mwanaume aliyekuwa anampenda alikuwa anamfatilia msichana aliyeitwa Joanitha, msichana ambaye walisoma nae kidato kimoja.



“Robert why unanifanyia hivi, kwanini?. Lazima nikwambie ukweli kuwa nakupenda na lazima niudhibitishie ulimwengu kuhusu jambo hilo …”,



Jacksoni alishuka kwenye gari huku akisoma ujumbe wa meseji uliotoka kwa rafiki yake wa kike, ujumbe ambao ulimfahamisha kuhusiana na Robert kumpenda Joanitha, huku akiapa kuhakikisha anampata hata kwa kutoa uhai wa mtu. Jacksoni alijuta kuwa kimya siku zote, kwani hakuwahi kuwasilisha hisia zake kwa Robert hata siku moja. Jambo ambalo limepelekea Robert kupenda kwingine, tena kwa msichana mrembo wa kitajiri aliyeitwa Joanitha.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nitatumia pesa bwanaa, Robert mtoto wa mjini. Anapenda sana starehe, lazima nimpate, mimi ndio Aunt Jacky origino na sio fotokopi. “



Jacksoni alijigamba huku akiingia ndani kwa maringo, na kuzidi kumpagawisha dereva wake aliyebaki nyuma akimtazama.



“Ama kweli wengine wanazaa watoto, lakini wengine ni watoto haramu. Tena Mwanaharamu haswaaa “,



Dereva wa Jacksoni alizungumza kwa ukimya maneno ya hasira, kwani alichukizwa na tabia za Jacksoni japo pesa ilimuingiza katika dhambi bila kupenda na kujikuta akishawishika na kukubali ombi la Jacksoni miezi michache iliyopita.



…………………………………



Kwa takribani saa nzima,Joanitha na Doreen waliwasili nyumbani. Joanitha alifika katika chumba chake, haraka sana alipekua vitu vyake chumbani kwake. Kitendo ambacho kilipelekea Doreeni amshangae, kwani hakutambua anatafuta nini. Kwa mwezi sasa Doreeni aliishi kwa rafiki yake Joanitha, kwani waliomba ruhusu kwa wazazi wao wawe pamoja na kushirikiana kwenye masomo, kwani mtihani wa taifa wa kidato cha sita ulikuwa umekalibia.



“Natafuta kitabu cha baiolojia “,



“Mmh, kweli mapenzi ni kichaa. Sasa wewe unasoma sayansi? “,



“Hapana, lakini ninavyo vya sekondari, tena kidato cha tatu lazima wazungumzie matatizo ya watu kama Jacksoni “,



“Hapana, mimi nakushauri twende kwa madaktari na watalaamu wa Saikolojia. Bila shaka tutajifunza mengi kuhusu Jacksoni “,



“Hilo nalo neno, ndio maana nakupenda bestie “,



Nyuso za tabasamu zilionekana kwa mara nyingine. Joanitha alipokea uahauri kutoka kwa rafiki yake, ushauri ambao aliamini ungefanikisha malengo yake na kumkomboa Robert kutoka katika janga hili ambalo liliyabadilisha maisha yake kila kukicha.



………………………………………………………………………………



Wazazi wake Jacksoni hawakufahamu kitu chochote kuhusu tabia za mwanao huyo wa kiume, waliamini alikuwa ni mwanaume rijali kama wanaume wengine. Muda wote walikuwa bize na biashara zao, waliondoka asubuhi na mapema kisha walirudi usiku wa manane. Safari za nje ya nchi hazikukatika, jambo ambalo lilipelekea Jacksoni kukosa malezi bora ya baba na mama …



“Kwahiyo utafanya nini, na bosi hayupo? “,



“Nitamsubili mpaka atakapo rudi kutoka Dubai. Kuhusu swala la shule lisikusumbue kabisa, kwanza nimechoka kusoma. “,



Dereva alimuuliza swali Jacksoni baada ya kuingia ndani na kumkuta akiwa ameketi kwenye sofa, katika sebule kubwa iliyokuwa imejaa samani za kutosha na kumvutia mtu yoyote aliyekanyaga ndani ya nyumba hii kubwa ya kifahari ya bwana Mtei …



Hakuwa na sababu ya kuendelea kumuuliza maswali Jacksoni aliyekuwa bize akichezea simu yake aina ya Iphone six. Kwani majibu aliyopatiwa yalionesha ni kiasi gani hakupenda kusoma, dereva yule alitoka nje ili kuendelea na mambo yake …



Kumbe Jacksoni alikuwa bize kuchati na Robert, baada ya kutumiwa namba yake na rafiki yake kisha kumpatia pesa za kutosha kwa kazi hii ndogo ya kutafuta namba ya Robert. Alifanya kila njia ilimradi ampate mvulana huyu, mvulana ambaye alimpenda Joanitha kupita maelezo huku tabia zake za kihuni zikimfanya akose hadhi ya kuwa na Joanitha. Jambo ambalo halikuwa kweli hata kidogo, kwani tabia za kike alizokuwa nazo Jacksoni zilikuwa mbaya zaidi kuliko tabia za Robert, lakini Joanitha alimpenda Jacksoni kama alivyo huku akifanya jitihada za kumkomboa.



“Haloo! nakuomba uchukue bodaboda, akulete katika hoteli ya Kilimanjaro green view, chumba namba sita. Pesa hiyo iliyoingia kwenye simu yako ni ya kwako …”,



Jacksoni akiitumia sauti yake ipasavyo, aliiremba na kumvutia mwanaume yoyote yule. Baada ya kumtumia Jacksoni kiasi cha shilingi milioni mbili, alimpigia ili kumjulisha mahali atakapo mkuta. Kwani tayali alikuwa ameshalipia chumba na kila kitu …



Baada ya kumaliza kutoa maelekezo, alikata simu yake huku akinyanyuka kutoka katika sofa alizokuwa amekalia. Mwanzoni alikuwa bize na simu, hivyo basi hakuisikia sauti ya dereva wake alipokuwa anamuaga jambo ambalo lilipelekea aanze kumtafuta.



“Derevaaa! Jonsonii, Jonsoniii …”,



“Naam, niko nje naosha gari, “



“Ok sawa! malizia, ngoja nijiandae, nataka unipeleke sehemu, kuhusu pesa usjali …”,



“Sawa bosi “,



Jacksoni alirudi chumbani kwake kujiandaa, huku akimpatia maelekezo dereva wake baada ya kumkuta nje akiifanyia usafi gari. Jacksoni alimuwaza tu Robert muda wotee, aliona ndio muda sahihi wa yeye kuonja penzi la kijana huyu aliyempenda kwa muda mrefu sana bila kumwambia. Hakuona sababu ya kuendelea kukaa kimya na kuutesa moyo wake …



…………………………………



Robert alifika katika mtaa ambao alikuwa anaishi, aliagana na rafiki zake huku kila mmoja akielekea nyumbani kwao.Kichwani alipanga mipango namna ya kumpata Joanitha. Mtoto wa kike aliyekuwa mrembo dalasani kupita wasichana wote, jambo ambalo lilimfanya kushika kichwa muda wote akitafakali …



“Mambo my …”,



“Freshii ,nani mwenzangu? “,



“Joanitha …?”,



“Nani? umesema nani vile? Joanitha naye mfahamu mimi …”



“Ndio Joanitha …”,



Robert akiwa amesimama nje ya geti la nyumba yao, ghafla meseji iliingia. Bila shaka mtu huyu hakumfahamu kwani namba ilikuwa ngeni kwenye simu yake, alichokifanya ni kumuuliza jina mtu aliyemtumia meseji. Hakuamini macho yake, kwani mtu huyu alimjibu na kumwambia alikuwa ni Joanitha. Hajakaa vizuri, muamala uliingia katika simu yake, hakuamini alichokisoma kwani zaidi ya milioni moja ilikuwa imetumwa na mtu aliyejitambulisha kama Joanitha



Kutokana na ujanja wake wa mjini, pengine alizani yuko kwenye mtego kutokana na mikasa mingi ya kihuni waliosababisha kila siku hasa kupigana na watu walio wachokoza. Ilibidi apige ili kujidhihirisha kama kweli aliyemtumia pesa alikuwa Joanitha au laa! ,lakini simu yake ikapokelewa na sauti nzuri ya kike ikimfahamisha hakuwa na salio kwenye simu yake…



Alichanganyikiwa,alijiona mjinga kukaa bila salio wakati alikuwa mwanaume.Wakati anaendelea kujuta,simu yake ilianza kuita.Bila kuchelewa aliipokea,kwani aliyemtumia pesa na kujitambulisha kama Joanitha alikuwa amempigia.



“Sawa! dakika sifuri natia timu, si unanijua? “,



Alimjibu mtu aliyempigia simu baada ya kusikia sauti nzuri ya kike iliyofanana sana na sauti ya Joanitha ,bila kupoteza muda Robert alibonyeza kitufe cha kengele katika ukuta wa geti lao. Ili awahi kuonana na mtu ambaye siku zote alimpenda sana, bila kutambua kuwa aliyempigia na kumtumia pesa hakuwa Joanitha bali Jacksoni. Mvulana ambaye alikuwa na tabia za kike shuleni kwao, na kupelekea kuwa gumzo kila kona ya shule yao. Jacksoni alitumia Jina la Joanitha ili iwe rahisi kumshawishi Robert kukubali ombi lake la kukutana naye katika hoteli ya Kilimanjaro green view, hoteli kubwa ya kitalii iliyopatikana katika jiji la Gano.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kusema ukweli Jacksoni alifanikiwa plani yake, kwani Robert aliingia ndani kwao kwa fujo na shangwe nyingi, huku akitazama muamala wa pesa aliokuwa ametumiwa. Aliwaza kukutana na Joanitha na wala sio kitu kingine …



…………………………………



Wingi wa watu wenye magonjwa mbalimbali walisheheni katika hospitali ya jiji la Gano, huku madaktari mbalimbali pamoja na manesi wakiwa bize kuwahudumia na kuokoa maisha ya watu. Joanitha na Doreeni walifika katika hosptali hii, huku wakiwa makini wasiweze kuonwa na baba yake Joanitha, kwani alifanya kazi katika hospitali hii kama daktari mkuu …



“Welcome! umekuja kuonana na baba yako, “



“Hapana,tena naomba usimweleze kuhusu uwepo wetu mahali hapa…,tunahitaji kuonana na daktari wa saikolojia…”,



“Sawa mwanangu ,haina shida!nyosha korido hii,kisha kunja kulia.Chumba cha kwanza kilichoandikwa “Saikolojia” ingia,utahudumiwa…”,



“Sawa mama asante,”



Joanitha alikutana uso kwa uso na nesi aliyemfahamu,kwani mara nyingi alifika katika hospitali hii kuonana na baba yake na wala sio kutibiwa.Lakini siku ya leo ilikuwa tofauti,hakutaka kuonana na baba yake aliyejulikana kwa jina la dokta Benny,bali alitaka kuonana na daktari aliyehusika na maswala ya saikolojia ikiwemo ushauri nasaha.Hakuishia hapo,bali Joanitha alimsisitiza nesi yule mwenye umri sawa na mama yake kutomweleza chochote baba yake dokta Benny kuhusu uwepo wao hospitalini hapo.



…………………………………



BAADA YA ROBO SAA:

Ukimya ulikuwa umetawala sana katika chumba hiki cha daktari bingwa wa saikolojia,huku sauti za watu watatu pekee zikisikika na

Kutawala chumba hiki.



“Hakuna ukweli wowote kuhusu kuzaliwa na vichocheo vingi vya kike kuliko vya kiume,kati ya asilimia mia moja,asilimia moja pekee ndio wanazaliwa na vichocheo vingi vya kike kuliko vya kiume.Huku asilimia tisini na tisa wakijiingiza katika mapenzi ya jinsia moja kwa kuiga,ushawishi kutoka kwa wenzao,utandawazi pamoja na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wao”



“Kwahiyo daktari unatusaidiaje?,maana rafiki yetu huyu wa kiume anazidi kuharibika siku hadi siku…”,



“Hamna namna nyingine ya kumsaidia zaidi ya kuja naye mahali hapa tumtibu kisaikolojia zaidi,halafu inatakiwa muwe karibu naye mkimushauri taratibu na sio kumtenga…”,



“Sawa daktari,tutajitajidi…”,



“Sawa wanangu karibuni tena…”,



Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Joanitha, Doreeni pamoja na daktari. Mazungumzo ambayo yalionekana kuanza muda mrefu kidogo. Joanitha pamoja na Doreeni walinyanyuka katika viti vyao ili waweze kuondoka, huku kichwani wakiwa wamepata mwanzo wa kuanzia kumsaidia Jacksoni japo ilikuwa ni vigumu kuwa naye karibu. Kwani jamii ingewatenga kutokana na tabia zake hizi za kike, japo Joanitha hakulizingatia sana jambo hilo, aliwaza namna ya kumuokoa mtu amupendaye na wala sio kitu kingine.



…………………………………



“Jonsonii! tuondokee! pesa hii itakutosha kutanua tukifika huko, naomba unisubili mpaka nitakapo maliza kilicho nipeleka “,



” ,Sawa bosi, nimekuelewa “,



Dereva alipokea bunda la pesa lililojaa noti za elfu kumi kumi, huku akimshangaa na kumtamani Jacksoni kwa jinsi alivyopendeza. Japo alikuwa wa kiume, lakini alikuwa na sauti nyororo huku makalio yake makubwa yakimfanya azidi kuvutia zaidi hasa kwa wanaume rijali ambao hawakuona haya kutembea na watu wenye tabia kama za Jacksoni…



Bila kuchelewa aliliondoa gari kwa kasi, huku geti ambalo lilikuwa likiongozwa kwa rimoti likijifunga na kudumisha ulinzi katika jumba la bwana Mtei. Kwa mwendo huu, ndani ya dakika chache tu, wangewasili katika hoteli ya Kilimanjaro green view. Jambo ambalo linge mfurahisha Jacksoni, kwani alitaka kufika chumbani kabla ya Robert hajafika ili kukamilisha mipango yake na kumnasa Robert kirahisi.



Gari aina ya prado ilitembea kwa mwendo wa kasi sana, wakati mwingine bila kujali hata alama za barabarani. Jacksoni alitaka afike katika hoteli ya Kilimanjaro green view mapema sana kabla ya Robert, jambo ambalo lilimfanya amuhimize dereva wake Jonsoni kukanyaga mafuta kadri ya uwezo wake wa uendeshaji.



“Kanyaga mafuta! usiwaogopee trafikiii bwana weee! tutawapa hela ya chai, usjali kabisa nakuaminia …”,



“Sawa bosi! ndani ya dakika kumi tutafika, japo inatakiwa niwe makini tusisababishe ajali …!”,



“Sawa kipenzi!,kuwa makini …”,



Jacksoni akiwa ameketi kiti cha mbele, pembeni ya dereva wake. Alizungumza na Jonsoni huku akiwa anaiweka sura yake katika mvuto zaidi, huku akijitazama kwenye kioo. Yani alikuwa amependeza kupita kiasi, jambo ambalo lingemfanya binadamu yoyote kutomtambua kama alikuwa wa kike au wa kiume kama angemtazama haraka haraka. Kichwani alimfikilia Robert tu na wala sio kitu kingine, hali hii ilipelekea safari ionekane kuwa ndefu kumbe sivyo. Fikra zake na hamu ya kumshuhudia ampendae ndiyo iliyomuendesha na kumfanya aione safari ndefuuu ………



DAKIKA TANO BAADAE;



“Daah, siamini kama tumefika! “,



“Tumefika, amini hivyo bosi wangu …”,



“Ngoja nilisogeze gari parking …”,



“Sawa, sijui wamefuata maelekezo niliyo wapatia! …”,



“Maelekezo gani bosii? “,



“Hamna hayakuhusu usjali,halafu nitakukuta hapa nje. Kaa kwenye vile viti kunywa, kula na kamwe usithubutu kuondoka kabla sijamaliza shughuli zangu. “,



“,Sawa bosi! “,



Prado nyeusi iliyokuwa na vioo tinted, vioo ambavyo havikuruhusu mtu yoyote kumuona mtu aliyeko ndani ya gari. Ilisogea taratibu eneo lililokuwa limesheheni magari mengi ya kifahari, bila shaka sehemu hii ilikuwa ni ya kupaki magari. Ndani ya gari mazungumzo kati ya Jacksoni na dereva wake aliyeitwa Jonsoni yaliendelea, huku Jonsoni akipatiwa maelekezo ili asije haribu kazi yake na kumwaga unga wake!



“Welcome Kilimanjaro green view hoteli, nina amini huduma zetu mtazifurahia …”,



“Ok asante! “,



Jacksoni akiwa amevaa wigi, hakuna aliyemtambua kirahisi kama alikuwa mwanaume. Sauti nzuri ya kike,sauti ya msichana mrembo aliyekuwa amevalia sare ya uhudumu wa hoteli hii bila shaka alikuwa kitengo cha mapokezi ya wateja. Alimsalimia Jacksoni aliposhuka ndani ya gari huku akiwa hajamtambua kama alikuwa ni wa kiume au wa kike, Jacksoni alimjibu neno Asante! kuashiria kukubali mapokezi yake, jambo ambalo lilimfanya muhudumu kuamini kama mtu aliyempokea alikuwa wa kike kutokana na sauti yake.



Jacksoni kwa mwendo wa maringo alitembea kuingia ndani ya jengo la hoteli hii ya kifahari, jengo ambalo lilikuwa na ghorofa takribani kumi kuelekea juu. Macho ya matamanio kutoka kwa wanaume wengi yalishindwa kujizuia, na kujikuta wakimtumbulia macho kijana Jacksoni. Japo alikuwa ni wa

wa kiume, alishindwa kutambulika na isitoshe alipendeza zaidi kupita wasichana wengi waliokuwepo mahali pale.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Heloo! samahani, nilifanya bukingi ya chumba katika webusaiti yenu mtandaoni, sijui ninaweza pata chumba changuu ?…”,



“Ooooh, wewe ndio aunty Jacky? umelipia mtandaoni chumba namba sita! “,



“Yap! ndio mimi, nazani kila kitu kiko sawa. “,



“Ndiyo, kiko sawa! na funguo zako hizi hapa “,



Muhudumu wa mapokezi, sehemu ya kulipia vyumba. Tofauti kabisa na muhudumu wa mwanzo aliyempokea Jacksoni, alimkabidhi funguo zake Jacksoni huku akionekana kushangazwa na muonekano wa Jacksoni. Matiti hakua nayo, lakini alikuwa na makalio makubwa kama ya wanawake. Isitoshe sauti ndio kabisaa, sauti ya Jacksoni ilikuwa nyororo na nzuri sana kitendo ambacho kilipelekea muhudumu yule kuamini kwamba Jacksoni hakuwa mwanaume kamili bali punga tena mzoefu.



“Sawa kaka! pandisha ghorofa ya pili hapo, utakiona chumba chako …!!”,



“Samahani dada! mimi ni mwanamke kama wanawake wengine na siyo kaka kama ulivyosema, chunga kauli yako! “,



“Basi nisamehe buree, ulimi hauna mfupa! “,



Muhudumu alijishusha ili asifukuzwe kibarua chake, hakuona sababu ya kurumbana na Jacksoni na kukera wateja wa hoteli yao. Japokuwa hakuwa na makosa, ilibidi atengue kauli yake iliyopingwa vikali na Jacksoni ili asiharibu kazi yake. Kwa upande wa Jonsoni, dereva wake Jacksoni. Aliketi nje ya hoteli, sehemu nzuri iliyokuwa imeandaliwa spesho kwa ajili ya watu wanao punga upepo. Jonsoni alichafua meza na vinywaji vya kila aina, jambo ambalo lilipelekea kutazamwa kwa matamanio na baadhi ya wanawake waliokuwepo jirani naye.



…………………………………



Jacksoni alifika ndani ya chumba namba sita, chumba kikubwa na kizuri. Chumba hiki kilionekana kuwa cha gharama kubwa, kwani kilikuwa na uchafu wa kila aina mpaka vinywaji vya bei kali. Jacksoni alichukua chumba hiki makusudi, kwani alifahamu Robert ni kiasi gani alipenda starehe hasa ulevi wa pombe kupindukia.



“Leo amepatikana! lazima nionje utamu wake, nakupenda sana Robert! “,



Jacksoni alizungumza peke yake, huku akifunga vioo vya chumba chake. Hakuishia kufunga vioo pekee, bali alishusha mpaka pazia za chumba hiki. Alifanya makusudi, kwani alitambua ni kiasi gani Robert atashangaa na kupaniki kama akiingia na kumtambua Jacksoni, kama mwanga utaachwa kiasi kile. Giza kubwa lilitanda ndani ya chumba namba sita, baada ya vioo vyote kufungwa pamoja na pazia zake. Kisha Jacksoni ali alivua nguo zake na kubaki na nguo za ndani, kisha alijilaza kitandani. Kilichobakia ni kumsubili kipenzi wake aweze kufika, ili aweze kuupatia furaha moyo wake.



Aliona Robert alikuwa amechelewa, ilibidi achukue simu yake kuwasiliana naye huku akiwa amejilaza kitandani.

…………………………………



Robert aliingia ndani kwao huku akishangilia, jambo ambalo lilimshangaza mfanyakazi wao wa nyumbani. Hakuona sababu ya kumsalimia kwani walikuwa na rika sawa, na kupitiliza moja kwa moja katika chumba chake. Haraka haraka alibadilisha nguo zake za shule, na kuvaa nguo zake alizozitumia katika pati mbalimbali. Madaftali alitupa kule!, viatu kule! bila hata kuoga, akaanza kujiandaa kwa kutoka tena!



“Tisheti na jeans, chini travota! lazima mtoto akubali …”,



Robert aliongea peke yake kama mwendawazimu, huku akiendelea kujiandaa kwa ajili ya kuonana na Joanitha. Bila kutambua kuwa aliyempigia simu na kutaka wakutane Kilimanjaro green view hoteli hakuwa Joanitha bali Jacksoni, mvulana aliyetambulika kwa jina la aunty Jacky kutokana na tabia zake za kike ambazo ziliwachukiza watu wengi hasa wanaume, kwani zilidharilisha uanaume wao!



Kwa takribani dakika ishirini, Robert alikuwa amekamilika! alipendeza zaidi ya siku zote alizokuwa akienda kujirusha na rafiki zake klabu. Siku hii alinukia marashi mazuri ambayo hakuwahi kuyatumia tangu ayanunue, kutokana na kukosa mahali sahihi pa kuyatumia. Lakini leo hii aliona ndiyo wakati wake kutumika, siku ambayo alikuwa anaenda kuonana na kipenzi cha moyo wake Joanitha pengine hata kuonja penzi lake kabisaa.



“Unaenda wapi! rudi ule kwanza! “,.



“Hapana, nitakula nikirudi baadae “,



Dada wa kazi alilalamika, kwani Robert alitoka ndani kwa spidi ya hali ya juu na kuonekana kama alikuwa akiwahi mahali fulani.Kitendo ambacho dada wa kazi hakupendezwa nacho, kwani mtoto wa bosi wake aliondoka bila kula jambo ambalo lingesababisha afokewe kama tu mama na baba yake wangerudi na kugundua mwanao hakuweza kula.



“Sawa, wakirudi utajuana nao wewe mwenyewe mimi simoo! “,



“Watajijua bwana, na ualimu wao wanataka waniendeshe kama vile mimi mwanafunzi wao.Mimi mtoto wao bwanaa !…”,



Akiwa anatokomea na kutoka getini, alimjibu dada wa kazi huku akiwakejeli wazazi wake. Kwani wote wawili walikuwa walimu wa shule za msingi, baba yake alikuwa mwalimu mkuu na mama yake alikuwa mwalimu wa kawaida. Wazazi wake katika maisha yao yote walibahatika kupata mtoto mmoja tu ambaye ni Robert, ndio maana alideka sana na kufanya kila kitu alichokitaka bila kukalipiwa na wazazi wake.



“Mpenzi umefika wapi? njoo nakusubili! “,



“Umeshafika hotelini Joanitha wangu? “,



“Ndio nimefika, wahi nakusubili! niko chumba namba sita. “,



“Sawa niko njiani, “



Ghafla meseji ziliingia katika simu ya Robert, na kujikuta akitamani hata kupaa kama ndege ili afike hotelini mapema, kwani tayali Joanitha alikuwa ameshafika hotelini kama alivyoambiwa kupitia meseji.



“Bodaboda! bodaboda! “,



“Nikusaidie nini kaka! wapi unaenda? “,



“Fasta nipeleke Kilimanjaro green view hoteli, shilingi ngapi? “,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Buku tu mkuu! “,



“Basi nitakupa mwekundu! Cha muhimu fanya fasta tufike dakika sifuri tu …”,



“Poa utakubali kaka! “,



Dereva wa bodaboda aliondoa pikipiki kama mwendawazimu, kwani pesa aliyoahidiwa ilikuwa nzuri tena pesa ya kufanyia kazi kwa siku nzima na wakati mwingine kukosekana kabisa. Lakini leo hii aliahidiwa kulipwa kwa safari moja tu, jambo ambalo lilimfurahisha na kumfanya aongeze mwendo ili amridhishe na kumfurahisha mteja wake.



…………………………………





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog