Simulizi : Mwanaharamu
Sehemu Ya Pili (2)
Joanitha na Doreeni walikuwa ndani ya gari huku wakiwa wamechoka sana. Tangu watoke asubuhi shuleni mpaka muda huu, walikuwa bado hawajapumzika, na sasa walikuwa njiani wanatoka hospitalini kumuona daktari wa saikolojia. Vichwa vyao vilijaa mambo mengi sana huku kila mmoja akifikili namna ya kufanya ili kufanikiwa kumuokoa Jacksoni kutoka katika tabia yake hii ya upunga.
“Ngoja tupite Kilimanjaro green view tupunge upepo! nimechoka sana na nina njaa kali balaa …”,
“Kama mimi tu, twende tukale na kunywa angalau tupumzishe akili na vichwa vyetu…”,
Kwakuwa njia kuu ya kutokea katika hospitali kuu ya jiji la Gano ilipakana karibu na hoteli ya Kilimanjaro green view.Joanitha akiwa amekamatilia uskani, taratibu alikata kona kutoka barabara kuu ya kutokea hospitalini na kufuata njia ya kuelekea katika hoteli hii ya kitalii kwenda kujipatia chakula na kupumzisha akili zao kwani walichoka sana kutokana na pilikapilika za hapa na pale katika siku hii …
……………
Hali ya utulivu ilikuwa imetawala katika hoteli ya Kilimanjaro green view, huku kila mmoja aliyefika mahali pale akijaribu kuitumia pesa yaka ipasavyo!! watoto wa mjini walijitupa na kuogelea ndani ya bwawa la kuogelea lililokuwa nje ya hoteli, na kuchangamsha watu ambao walikuwa wakiburudika na vinywaji mbalimbali huku mziki wa taratibu ukipigwa na kuzidi kuwapagawisha wateja wote wa hoteli ya Kilimanjaro green view.
Gari dogo aina ya Alteza lilikata kona kuelekea eneo la kuegesha magari, na kusababisha watu wote waliokua nje ya hoteli kugeuka na kulitazama. Sio kwamba walilishangaa kwa uzuri wake lahasha, bali lilikuja kwa mwendo wa kasi sana mwanzoni kabla ya kupunguza mwendo huo kwa breki kalii iliyosababisha gari kuserereka.
“Aaaaa! bwanaaaee unazingua! mwendo gani huo unaokera wenzako, au gari ndo umelinunua leo nini? “,
Jamaa mmoja aliropoka baada ya kukerwa na breki ya gari ambayo Joanitha na Doreeni walikuwemo ndani yake. Kwani alisitisha shughuli zake za kulisakata rumba na kubaki akimtazama mchawi wake kwa hasira za hali ya juu. Lakini hakuna mtu yoyote aliyejali kelele zake hasa Joanitha, kwani alilisogeza gari lake mara hii kwa mwendo wa taratibu tofauti na awali. Huku akiwa amechoka kupita kiasi! na isitoshe tangu asubuhi hajatia chochote kinywani mwake …
“We mseng * wewe! kwanini unatusumbua watu na starehe zetu? au unalingia kisura chako, nitakipas…u …”,
Mwanaume yule ambaye alionekana kulewa chakalii, huku pombe alizokunywa zikimzidi uwezo. Aliyumba taratibu kuelekea eneo ambalo Joanitha na Doreeni walikuwa wamepaki gari lao. Mdomo wake ulitema matusi ya kila aina kutokana na hasira alizokuwa nazo, mara baada ya kukutana uso kwa uso na Joanitha alipofungua tu mlango wa gari lake. Joanitha alimanusura apigwe na konde zito kichwani mwake, kama siyo walinzi shupavu wa hoteli hii kumdhibiti mlevi huyu basi sura yote ya Joanitha ingechakazwa.
“Niacheni nimuonyeshe! hawezi kunivurugia starehe yangu hata siku moja! mimi ndiyo Gusa unate bwanaa weee! kanigusa mwenyewe, muacheni anase mtegoni …”,
Walinzi wa hoteli hii hawakuwa na haja ya kumpiga mteja wao huyu aliyeonekana kuzidiwa na pombe kupita kiasi. Bali walimtoa nje ,mbali kabisa na eneo la hoteli ili asiendelee kuwasumbua wateja wengine.
Joanitha akiwa mwenye mawazo mengi hata hakumjali mlevi huyu, bali aliongozana na rafiki yake kipenzi Doreeni kuelekea katika viti vizuri vya hoteli hii ili kuketi na kuhudumiwa. Ghafla Doreeni alishangaa kuliona gari la Jacksoni mahali palee, wakati akiwa katika hali ya kuangaza huku na kule katika kona zote za Kilimanjaro hoteli .
“Joanitha! Joanitha …!gari la Jacksoni lile paleee, bila shaka yuko mahali hapa. “,
“Acha utani wako, mimi nimechoka ujue! “,
“,Kwelii sikudanganyii. Angalia mkono wako wa kushoto, yani rangi na namba za gari ni zilezile …”,
“Khaaa! huyu ni Jacksoni. Lazima yuko hapa! twende tukaketi kwenye viti vilee, halafu tupeleleze mpaka tufahamu yuko wapi na anafanya nini? kama amekuja kustarehe tu, basi tuungane naye …”,
“Haswaa! ndiyo wakati mzuri wa kuwa karibu naye, tuondoke …”,
Joanitha na Doreeni walizungumza kwa sekunde kadhaa, kisha taratibu walielekea kuketi. Muda huu wote, midume kadhaa ilikuwa ikiwamezea mate. Lakini hawakujali hilo, kama pesa walikuwa nazo za kutosha. Bali walikuwa makini kuangaza huku na kule ili kujaribu bahati yao ya kuonana na Jacksoni maarufu kama aunt Jacky. Jina ambalo alilipenda zaidi pale alipoitwa jina hilo, tofauti kabisa na jina lake halisi la Jacksoni …
“Karibuni hotelini kwetu, tuwasaidie nini? “,
“Piza na juisii! pesa yako hii hapa, maana muda wowote tunaondoka “,
“Hapana, chakula chenu kimeshalipiwa na yule mkaka. Kasema niwapatie chochote mnacho hitaji …”,
Muhudumu alikataa pesa ambayo alikabidhiwa, wakati alipokuja kuchukua oda ya chakula kutoka kwa wateja wake. Hali hii ilisababisha Doreeni na Joanitha kugeuka ili kumtazama mtu ambaye ilidaiwa alilipia kila kitu kwa ajili yao, jambo ambalo lilisababisha wapigwe na butwaa kwani walimtambua vizuri sana mtu aliye walipiaa …
“Mhh si Jonsoni huyo dereva wa Jacksoni!, halafu inaonekana amelewa sanaa na hajitambui, twende tukaketi naye naamini tutafahamu mambo mengi.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
…………………………………
“Buku kumi yako hii hapa mkuu! asante sana! “,
“Poa broo! pamoja sana …”,
Bodaboda ilifika na kupaki umbali wa mita kadhaa kutoka eneo la hoteli. Huku Robert akiwa na haraka kupita kiasi. Kwani muda mrefu ulikuwa umepita tangu awasiliane na Jacksoni huku akiamini aliyewasiliana naye ni Joanitha kumbe sivyo. Hakuwa na muda wa kupoteza! alilipa pesa ya bodaboda, kisha kuingia hotelini kukutana na mtu ambaye alimpenda kupita kiasi. Kwa mwendo wa haraka macho yake yalikutana uso kwa uso na gari dogo aina ya Alteza ambalo lilikuwa limepaki mwanzoni kabisa wa magari mengine, bila shaka halikuwa na muda mrefu mahali pale.
“Daaah! demu ni mwenyewe nilizani utanii! kudadekii! halafu ameshafika …”,
Robert alizungumza peke yake baada ya kulishuhudia gari la Joanitha, gari ambalo alilifahamu vizuri sana. Kitendo ambacho kilipelekea asiangaze sehemu yoyote nje ya hoteli, jambo ambalo lilimfanya ajutie baadae. Macho yake yote yalikuwa bize kutazama mlango wa hoteli hii kubwa ya kitalii, na kwenda kuingia bila kutambua kuwa Joanitha halisi alimuacha njee!
“Naitwa Robert! naenda kuonana na mgeni wangu chumba namba sita! “,
“Tayali ameshafika! nenda ghorofa ya pili. Bila shaka utamkuta …”,
“Shukrani, “,
Kwa ustaarabu wa hali ya juu, Robert alijieleza baada ya kufika mapokezi. Tofauti kabisa na ustaarabu mzuri alioutumia, kwani muhudumu wa mapokezi alimshangaa sana huku akimpatia maelekezo namna ya kukutana na mgeni wake. Muhudumu yule aliamini Robert alijihusisha na mapenzi ya jinsia moja ndiyo maana alikuwa akienda kuonana na Jacksoni, lakini hakuhoji jambo lolote zaidi ya kutimiza wajibu wake.
Kwa upande wa Robert alifikili alionewa wivu kwa kumiliki mtoto mkali kama Joanitha, mtu ambaye hakuendana na hadhi yake hata kidogo ndio maana muhudumu alimshangaa sana.
“Watu wengine bwaanaa! wivu tu! na mwaka huu mtanikoma …”,
Bila kutambua chochote kile, Robert aliongea kwa sauti ya chini huku akipandisha ghorofani kwenda kuonana na asali wa moyo wake. Alimlaani vikali muhudumu wa hoteli hii, bila kutambua kuwa jambo usilo lijua ni kama usiku wa giza.
…………………………………
Jonsoni aliendelea kutanua, kunywa na kula huku baadhi ya wanawake waliomuona mwenye pesa nyingi wakitafuta namna ya kujipendekeza kwake ili wampige hela.
Hawakutambua pia hata Jonsoni alikuwa akiwatamani kadri pombe zilivyo mkolea, lakini alipojaribu kunyoosha mkono wake ili awaite warembo hawa kwa kutumia ishara. Ghafla alisikia breki kali ya gari na kumfanya asitishe lengo lake huku akigeuza shingo lake kulitazama gari hili ambalo liliwakwaza watu wengi na kuvuruga starehe za watu kutokana na breki zake za fujoo …
Alipogeuza shingo lake kulitazama gari hili, alishangaa kuona gari ambalo halikuwa geni machoni pake. Lakini kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu zake mahali alipowahi kuliona gari hii, jitihada zake ziligonga mwamba kutokana na kulewa kupita kiasi. Jambo ambalo lilisababisha abaki akiwa amepigwa na butwaa kulitazamaa …
“Waaoh Mungu anaumba bwanaa wee! ona vyomboo hivyo …”,
Kwa sauti ya kilevi Jonsoni alizungumza, huku akiwashangaa wasichana warembo walioshuka kwenye gari hii ambayo ilipaki hotelini kwa fujo. Hakusita kuwasifia, japo sura zao hazikuwa ngeni machoni pake, na kubaki akiwasindikiza na macho yake mpaka mahali walipoketi.
Ndipo alipoamua kufanya jambo la haraka kuwapata, kwani uzuri wao uliwazidi mabinti ambao alitaka kuwaita mwanzoni.Alimuita muhudumu na kulipia kila kitu kwa ajili yao, ili tu aweze kuwapata na kuburudika nao pamoja …
Muhudumu yule alipokea pesa kisha kuelekea katika meza ya Joanitha na Doreeni kwenda kuwahudumia. Hakuhitaji malipo ya aina yoyote kwani tayali alikuwa ameshalipwa, jambo ambalo liliwashangaza sana wasichana hawa ambao walikuwa wazuri sana kwa sura, japo Joanitha alikuwa mzuri sana kumpita rafiki yake Doreeni. Hawakusita kuhoji ili wamtambue mwanaume aliyewalipia chakula na vinywaji, jambo ambalo liliwafanya washangae zaidi kwa mtu aliyewalipia walimtambua vizuri sana ……
“Muhudumu umesikia? tuletee chakula kwa mwanaume yule aliyetulipia, tunaenda kukaa kwake …”,
“Sawa, nimewaelewa msijali “,
Wakiwa na malengo yao kichwani, baada ya kukubaliana kwenda kuketi meza moja na Jonsoni ili wamuhoji mawili matatu. Walimpatia maelekezo muhudumu, kisha walinyenyuka kumfuata Jonsoni bila hata kuangaza pembe zote za hoteli. Kichwani waliwaza namna ya kumuhoji Jonsoni aliyekuwa amelewa chakalii, bila kutambua kuwa Robert alifika hoteli hapa na kisha kuingia ndani kabisa ya hoteli wakati walipokuwa bize kujadiliana kuhusu Jonsoni.
Lakini Jonsoni yeye alikuwa akitabasamu tu baada ya kuona wasichana hawa warembo wakija mahali ambapo alikuwa ameketi, na kujiona mjanja sana pengine kuliko wanaume wote duniani. Daah! fahamu zilianza kumrudia taratibu Jonsoni, kadri Joanitha na Doreeni walivyokua wakimsogelea ndivyo alivyojikuta akianza kuwatambua.
………………………………
Jacksoni akiwa amejilaza kitandani huku giza likiwa limesheheni ndani ya chumba, alizuia simu yake isitoe mwanga uliokua ukiangaza chumbani mara baada ya kusikia vishindo vya miguu uelekeo wa chumba chake. Kisha haraka sana alijongea taratibu kuusogelea mlango wa chumba chake na kujibanza karibu kabisa na mlango …
“Hodiii! “,
“Sukuma! kuko wazi “,
Sauti nzuri ilimjibu Robert alipogonga mlango wa chumba, sauti ambayo ilimchanganya na kumfanya aingie kwa pupa kwani pepo la ngono lilimtawala na kuamini sauti aliyoisikia ilikuwa ya Joanitha kumbe sivyo!
Mikono laini ilimpokea Robert na kumkumbatia, mara tu alipoufungua mlango na kuingia chumbani. Kutokana na uzoefu katika maswala ya mapenzi, hakushangazwa na taa ambayo ilikuwa imezimwa .Bali alionyesha ushirikiano kwa kumkumbatia Jacksoni huku akibonyeza bonyeza makalio yake makubwa. Hakuwa na hofu yoyote kuhusu mtu aliyemkumbatia ,bali aliamini alikuwa ni Joanitha kwa asilimia mia moja kutokana na mikono yake laini huku wigi la Jacksoni likiificha sura yake isionekane vizuri na isitoshe kulikuwa na giza.
Mambo yalikuwa vuta nikuvute katika chumba cha hoteli ya Kilimanjaro green view, Robert alimshika Jacksoni huku na Jackson akamshika kule. Kila mmoja alimtamani mwenzake kutokana na hisia kali za kimapenzi alizokuwa nazo, kwani Jacksoni alimpenda sana kijana huyu na siku zote alitamani kuipata nafasi kama hii ambayo alikuwa ameipata, kilichobakia ni kuitumia ipasavyo. Kwa upande wa Jacksoni alimpenda msichana mrembo darasani kwake aliyeitwa Joanitha, lakini jitihada za kumpata ziligonga mwamba kila alipomtemea sumu msichana huyu. Hivyo basi, hakuamini alipoipata fursa ya kukutana na Joanitha hotelini, bila kutambua kuwa aliyemuita hotelini sio Joanitha bali Jacksoni …
Kama unavyojua mwanaume rijali alivyo, anaweka ngono mbele na sio kitu kingine. Ndivyo ilivyotokea kwa Robert kwani hakuendelea kuhoji mara tu alipoingia ndani ya chumba kisha kupokelewa kwa mahaba mazito kutoka kwa Jacksoni, kilichobakia ni kutoa ushirikiano wa juu kwa mwenzie.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Oshiiii bebi, you kill me! ,nakupenda sana Robert wangu, nakupendaa! “,
Jacksoni alianza kuongea lugha zingine, huku akichanganya kiswahili na kimombo. Sehemu alizoguswa zilizidi kumpagawisha, kwani alibonyezwa makalio yake kwa ufundi wa hali ya juu na mtu ambaye siku zote aliota kuwa wake Kichwa cha Robert kilizidi kulewa sifa baada ya kusikia sifa nzuri alizopewa na mtu ambaye alifikiri ni Joanitha kumbe zivyo, jambo ambalo lilimfanya azidi kuwa mbunifu ili amlainishe mapema sana na kulila tunda lake..
Taratibu alisogeza mikono yake kupapasa mwili wa Jacksoni, huku wote wakiwa katika hali ya kukumbatiana. Kwa mwendo wa kinyume nyume walitembea polepole na kutupana kitandani.
“Kwichiiii! …Kwichiiiii! “,
Mlio wa kitanda uliwapokea kwa shangwe, kwani kwa muda mrefu uwanja ulikosa wachezaji kutokana na bei kali ya chumba hiki. Hisia za wachezaji zilikua zinazidi kuongezeka, huku ushirikiano wao ukiwa mkubwa kadri muda ulivyokwenda.
“Joanitha! Joanithaa! …”,
Sauti ya mshangao ilitoka mdomoni mwa Robert,mara baada ya kupeleka mikono yake katika matiti ya mtu aliyefikiri ni Joanitha na kuambulia embe dodo changa kabisa tofauti na matiti makubwa sana na mazuri ambayo Joanitha halisi alikuwa nayo. Kutokana na hisia za Jacksoni kufika mbali zaidi! sauti ya mshangao ya Robert haikueleweka na Jacksoni bali alizidi kujiachia ili kumpatia nafasi kipenzi chake azidi kumuhudumia.
Japo kijana Robert hakujibiwa baada ya kumuita Joanitha, aliendelea kujituma ili asimkwaze mpenzi wake. Wote kwa pamoja wakiwa juu ya kitanda, huku machale yakianza kumcheza kijana Robert kuwa pengine msichana aliyekuwa naye uwanjani hakua Joanitha halisi bali malaya tu wa mtaani aliyekuwa na nyege za kufa mtu. Lakini je malaya gani alikuwa na pesa nyingi za kuchezea kiasi hicho? ilihali alijiuza hata kwa buku ili apate pesa za kujikimu?, maswali ambayo hakuwa na majibu yake.
“Oyaaa! weee! nani mbona sikuelewi ,puuu!puuu!…?”,
“Joanitha…aa…aa,”
“Hapana Joanitha gani hana chuchu! Joanitha gani anandevu, Joanitha gani anavaa wigi? “,
Hatimaye mwizi alikamatika, huku Robert akilaani baada ya kupeleka mdomo wake katika kinywa cha Jacksoni na kubadilishana mate kwa sekunde kadhaa. Uvumilivu ulimshinda na kujikuta akitema mate sakafuni, kwani bila kutegemea mikono yake iliyokuwa ikitalii katika maeneo yote ya mwili wa Jacksoni. Ilitua katika kidevu ambacho kilisheviwa vizuri sana, huku vipere kadhaa vikiwa vimeota kumlaani mtu huyu kwa kitendo chake cha kuzinyoa ndevu ambazo hazikuwa na hatia. Palepale Robert hisia za mapenzi zikamtoweka, na kujikuta akiligundua wigi ambalo mtu aliyekuwa akifikiri ni Joanitha alikuwa amelivaa jambo ambalo ni kinyume na tabia za Joanitha. Kwani tangu amfuatilie maisha yake, katika jitihada za kulisaka penzi lake. Hakuwahi kumuona akiwa amevaa wigi, ilihali alikuwa na nywele nzuri ambazo zilisukwa kila kukicha tena mitindo ya kisasa!
“Heee! kumbe ni wewe mseng * ? .Daaah!, kwa mara ya kwanza nimekua falaaa, tena zaidi ya mafalaa !,haiwezekani unitie mikosi kiasi hichi? “,
Dume la mbegu, lilijitazama huku likijiona kama lilichafuliwa na uchafu wa hali ya juu. Akiwa mwenye hasira, alijipangusa kama ishara ya kujisafisha kwa vitu alivyofanya na Jacksoni, mara baada ya kuusogelea ukuta kuziwasha taa ili apate kutatua maswali yake ambayo yalimsumbua kichwani. Taa haikuwa na roho mbaya, iliangaza mpaka chini ya uvungu jambo ambalo lilisababisha Jacksoni aumbuke. Ndipo alipokumbuka majibu ya dharau ambazo alionyeshwa na muhudumu wa mapokezi wa hoteli hii, mara tu alipokitaja chumba ambacho mgeni wake alifikia.
“Nisamehe Robert! nakupenda! nitakupa kila kitu unachokitaka ili tu uwe wanguu. “,
“Hebu toka uko! nitakuua buree, nashangaa Joanitha anakupenda ilihali watu kama sisi tupo …”,
Katika hali ya majibizano hotelini, Robert alijikuta akimtaja Joanitha wakati akimfokea Jacksoni na kusitisha hatua zake alizokuwa akizipiga kutoka chumbani, ili akamsimulie Joanitha kila kitu na kujipatia sifa. Lakini swali, je ataaminika kwa yale atakayomsimulia Joanitha?.Jambo ambalo lilimfanya asimame ili kutafuta vithibitisho kwa jambo alilotaka kwenda kulifanya.
“Waao! usiniache, nitakupa chochote kile unachotaka. Naomba unipe nafasi katika
moyo wako …”,
Jacksoni maarufu kama aunt Jacky alitabasamu, mara baada ya kuliona tabasamu feki katika uso wa Robert na isitoshe alisitisha lengo lake la kutaka kutoweka hotelini. Bila kutambua kuwa Robert alikuwa na malengo yake mengine yaliyo mfanya kunyongonyea, na kuanza kujishusha ghafla mbele yake.
“Unanipenda? “,
“Ndiyo nakupenda? “,
“Utanipatia chochote na kunifanyia chochote ninachotaka! “,
“Ndiyo nitafanya! “,
“Haya kaoge, mimi nikiwa nakunywa bia zangu mbili tatu. Ukitoka kuoga, kisha kunywa na wewe tufurahi pamoja …”,
“Kwanini lakini, mimi niko safii! usinifanyie hivyo bebi pliziiii? “,
“Hunipendi eee! ngoja niondoke zangu. “,
“,Hapana usiondoke, ninaenda! “,
Jacksoni alitabasamu huku macho yake akiyalegeza kupita kiasi, moyoni aliamini alipata kile alichokuwa anakitaka bila kutambua kuwa alikuwa mtegoni. Haraka sana alikimbia kwa mwendo wa kike kuelekea bafuni, ili aoge fasta na kuja kuinjoi na mpenzi wake ambaye alionesha tabasamu feki kwa punga huyu …
“Kudadeki! tayali saa kumi, hapa ninafanya mishe fasta na kurudi nyumbani fastaaa ………”,
Bila kupoteza muda! Robert alianza misheni yake kwa kuchukua chupa mbili za konyagi kali, na kuanza kuelekea chooni kwa mwendo wa kunyata huku akiangalia saa ya ukutani. Kazi yake ilikuwa rahisi sana kutokana na choo kujitenga na bafu ndani ya chumba hiki, hivyo basi alimwaga pombe hizi chooni mithili ya mtu ambaye alikuwa anajisaidia choo ndogo. Jambo ambalo lilisababisha Jacksoni kutohisi jambo lolote baya zaidi ya kuendelea kujimwagia maji kwa fujo ili awahi kula raha na Robert.
“Hapa tayali! kama staa wa muvi la kipelelezi, mimi ndio bingwa wa mipango ya kuua majambazi hahaaa! “,
Cheko la kinafkii lilisikika kwa chini sana, kutokana na sauti ya chini iliyozungumzwa na Robert ambaye alijiona mshindi. Taratibu alianza kufungua mlango wa choo ,na kurejea tena kwenye friji iliyokuepo ndani ya chumba kile cha kifahari.
“Hapa sasa namuua kimya kimya! Joanitha hatampenda tena! Upendo wake wote kwa punga huyu lazima ahamishie kwangu. “
Pombe nyingine aina ya konyagi, ilichanganywa na maji katika grasi tofauti tofauti takribani tatu. Huku yeye akibaki mikononi mwake na grasi moja tu ya maji ambayo hakuichanganywa na kilevi chochote kile …
Hakusita kutoa maneno ya kejeli, kwani plani zake zilielekea kukamilika. Bila kupoteza muda aliketi eneo la chakula ndani ya chumba kile kile, huku chupa zile mbili za konyagi alizozimwaga chooni zikiwa mezani. Mkononi mwake alishika grasi yake ya maji na kunywa taratibu ,huku grasi zingine tatu zikiwa zimeandaliwa upande mwingine wa meza kulipokuwa na kiti …
“Bebiiiii! nimemaliza, heee!umemaliza konyagi zote hizi mara hii?”,
“Ndiyoo…o…o,njoo tuburudike mpenzi wangu.Tukimaliza tupeane raha…a…a…”,
Kwa sauti ya kilevi,Robert alijilazimisha kutamka maneno ya mapenzi baada ya Jacksoni kutoka bafuni akiwa na mwonekano mpya, kwani alijiweka vizuri zaidi tofauti na mwanzoni ili kumfurahisha Robert.Jacksoni moja kwa moja alifika na kuketi kisha kuparamia grasi zake ambazo aliamini ziliandaliwa kwa ajili yake,huku moyoni akiamini Robert alikuwa amelewa chakali kumbe sivyo…
…………………………………
Nje ya hoteli ya Kilimanjaro green view,Joanitha na Doreeni walibadili meza na kwenda kuketi na mtu aliyewalipia chakula bila wasiwasi wowote isitoshe walimtambua vizuri.Moyoni walikuwa na lengo mojaa kuu,kumpeleleza mtu huyu aliyekuwa amelewa kupita kiasi ili watambue mawili matatu kutoka kwake…
“Karibuni waremboo,kumbe ni nyinyi nilizani wengineee…”,
“Ndiyo ni sisi!!,
“Mwanafunzi mwenzenu yuko hotelini na mgeni wake wanakula rahaa,naamini ni mwanaume wakee!”,
“Hee!mwenzetu yupi?Jacksoni ama?”,
“,Ndiyooo,Jacksoni, yuko na mwanaume bila shaka wanakula rahaa tu. Karibuni na nyie tule raha …”,
“,Sikubali! sikubali! mpaka nitambue upuuzi anao ufanya? na nimtambue mwanaume huyo anaye mdanganya Jacksoni wangu! “,
Bila kutambua kuwa dereva wake Jacksoni alikuwa anaweka kibarua chake hatarini, aliropoka kila kitu kutokana na pombe kumzidia. Jambo ambalo lilimfanya Joanitha ashindwe kuvumilia, na kukimbia kuelekea ndani ya hoteli huku Doreeni akiwa nyuma yake kumfuata.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shughuli mbalimbali za kiofisi zilifika ukingoni katika hospitali kuu ya jiji la Gano, hali ambayo ilipelekea baadhi ya huduma kusimama kwani tayali wafanyakazi mbalimbali walianza kufungusha dokomenti zao za kazi ili kurejea katika majumba yao …
Ndivyo ilivyotokea kwa daktari mkuu wa hospitali hii, aliyejulikana kwa jina maarufu la dokta Benny. Hakuwa zamu usiku ,hivyo basi hakuona sababu ya kuendelea kubaki hospitalini wakati muda wa kazi ulikuwa umepita.
“Kazi ngumu! uchovu mpaka naona uvivu kuendesha gari, lakini no way! kuliko kuwa na dereva akaniharibia mwanangu bora niendelee kukamata uskani ……nampenda sana mwanangu “,
“Hahaaahaa, inaonekana umechoka sana mkuu mpaka unaongea peke yako. Bila shaka unamlinda sana mwanao asipotee, ndiyo maana kila siku yuko karibu na wewe muda wotee.…”,
“Ohoo! dokta Ashrafu kumbe umenisikia! ndiyo nampenda mwanangu, ndiyo maana ananitembelea kila siku kazini kwangu, ili ajue namna tunavyohangaika kutafuta pesa apate chochote cha kuweka kinywani ……”,
“Kwakweli, ndiyo maana hata leo kaja kukutembelea. Mtoto wako anakupenda sana na anaonekana anaheshima japo kichwani anaonekana mwenye mawazo mengi! “,
“Mmmh mbona leo hajafika au umemfananisha? “,
“Hapana sijamfananisha, namfahamu vizuri mtoto wako. Kafika hapa akiwa ameongozana na rafiki yake, lakini kichwani alionekana kuwa na mawazo mengi nilipojaribu kuisoma saikolojia yake, kwakuwa nilikuwa bize sikuweza hata kusalimiana naye na isitoshe niliamini alifika ofisini kwako kuonana na wewe. “,
“Duuu! leo alikuwa shuleni, kama hujamfananisha basi atakuwa ni yeye. Ok nitamuuliza isije ikawa anamuwaza mama yake isije ikawa shidaa nyingine …”,
“Ok bosi! jioni njema, see you tomorrow “,
“Ok …,take care brother …”,
Dokta Benny akiwa pembeni ya gari lake aina ya BMW, aliagana na rafiki yake kipenzi waliyefanya naye kazi katika kitengo kimoja cha upasuaji hospitalini .Hakuona ukweli wowote wa maneno ambayo aliweza kufahamishwa na rafiki yake huyo, kwani siku hiyo ilikuwa ni siku ya masomo jambo ambalo ilikuwa vigumu kwa mwanae kufika hospitalini kwake na isitoshe asiingie hata ofisini kwake kumsalimia. Bila kupoteza hata chembe ya sekunde, aliingia ndani ya gari lake tayali kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwake kupumzika.
…………………………………
Mzee Mtei na mke wake wakiwa nchini Dubai, katika harakati mbalimbali za kibiashara. Ujumbe wa barua pepe unaingia katika simu zao huku wakiwa hawatambui mtu aliyewatumia ujumbe huo, japo alijitambulisha chini kabisa ya ujumbe huo …
“Sina shida ya pesa, lakini msipokuwa makini mtoto wenu atalichafua jina lenu na kampuni yenu itashuka kibiashara.Kwani maadui zenu watatumia tabia zake kuwachafua. Tumieni pesa zenu kumuokoa mtoto wenu kwani hali yake ni mbaya kwa sasa…naitwa KENDRICK “,
Ni ujumbe ambao uliandikwa huku ukiwa umeambatanishwa na picha nyingi zisizo na maadili zilizokuwa zimepigwa na mtoto wao kisha kurushwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram. Jambo ambalo lilizua mtafaruku baina ya mzee Mtei na mke wake …
“Hee! aunt Jacky! my son are you serious? Is this how we are preparing you to be among the richest young people in Africa? (Hee! aunt Jacky! mtoto wangu uko siliasi? Hivi ndivyo tunakuandaa kuwa mmoja kati ya matajiri vijana Afrika? …”,
“Don’t blame my son! haya yote wewe ndiyo umesababisha, nilikwambia usimpeleke kusoma America. Ona sasa?
“Paaaaaa! “,
“Yaniii unanipiga? unanipiga kwa kumtetea mwanangu? ok, thanks lakini tambua wewe ni sababu ya mwanangu kuharibika …”,
“,Paaaaah! …”,
Kibao kingine kilisikika na kusababisha mama yake Jacksoni kuweweseka, huku akitaka kudondoka chini lakini walinzi shupavu wa mzee Mtei waliwahi kumdaka.Mzee Mtei alikuwa na hasira zilizosababisha mpaka mikono yake kutetemeka, siku zote alimpenda mwanae na kumpatia kila kitu alichohitaji ili afanye vizuri katika masomo yake na isitoshe alikuwa ni mtoto wake pekee aliyebahatika kumpata tangu wafunge ndoa na mke wake miaka arobaini iliyopita.
“Mpuuzi kweli wewe, nilimpeleka America kusoma na sio kujifunza ushoga. Ukiendelea kuongea ujinga wako nitakuua …,mpaka sasa amesha nichafua mbele ya wafanyabiashara na taifa langu kwa ujumla …!,”
Mzee Mtei alimuonya mke wake ambaye alikuwa anaugulia maumivu makali, mikono yake yote miwili iliyashika mashavu yake ambayo yalichapwa kofi na mikono bapa ya mzee Mtei katika pande zote mbili.
“Paul, hakikisha unaandaa tiketi nne za ndege ya leo usiku. Chukua fly Emirates daraja la VIP, leo usiku lazima turudi Gano …”,
“Poa bosi! nimekuelewa “,
“Siyo umenielewa! yani sasa hivi ondoka kafanye jambo hilo, shughuli zote za biashara nchini Dubai zisitishwe kwa muda mpaka tutakaporudi tenaa…”,
Pande la baba, mlinzi mkuu kati ya wawili waliomlinda mzee Mtei na mke wake. Mlinzi shupavu aliyejulikana kwa jina la Paul Agustino alipotea machoni kwa mzee Mtei haraka sana kwa ajili ya kwenda kutekeleza majukumu aliyopewa. Mzee Mtei aliwaza namna ya kurudi nchini Gano haraka sana kabla mambo hayajaharibika zaidi.
…………………………………
Doreeni alikimbia huku akimsihi rafiki yake asitishe lengo lake alilokuwa anataka kwenda kulifanya ndani ya hoteli, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Jonsoni. Doreeni aliamini hatari kubwa ingetokea kama angemshuhudia Jacksoni akiwa na mpenzi mwingine tena wa jinsia yake, bora angemkuta na mwanamke na sio mwanaume.
“Joanitha! plizi usiende, plizi nakuomba “,
“Hapana! siwezi kuendelea kuwa mjinga …lazima nimshuhudie huyu mpuuzi anayemdanganya Jacksoni. “,
“Sikiliza nikwambie! Huko utasababisha vurugu, pengine hata kesi ya jinai ambayo utamuweka mzee wako sehemu mbaya. Wakisema wewe ni mwizi? wakisema umewaletea vurugu? je unaudhibitisho Jacksoni ni mpenzi wako? je akikukana? utajibu nini rafiki yangu mbona unataka kunisababiashia matatizo”,
Maneno mazito ya Doreeni yalimgusa Joanitha, na kupenya vizuri katika ubongo wake. Kiasi kwamba alijikuta anasimama ghafla bila kutegemea na kuanza kulia kama mtoto mdogo. Alimlaumu Mungu pengine hata kwa kuwahi kumchukua mama yake mzazi ambaye aliamini ametangulia mbele za haki, japo hakuwa na uhakika wowote kwani kila alipomuuliza baba yake kuhusu mama hakuna jibu lolote alilopatiwa zaidi ya kuahidiwa kuambiwa ukweli siku moja …
“Kwanini mimi kwanini lakini, Mungu nimekukosea nini? Kanisani nakuimbia? sadaka nakutolea, mbona unanifanyia hivi ……” ,
Maswali ya Joanitha ambayo yaliambatana na machozi ya uchungu yalisikika, jambo ambalo liliwafanya hata wateja wengine wenye huruma kudondosha chozi kwani maneno mazito ambayo Joanitha aliyazungumza yaliumiza kupita kiasi.
“Usilie! tukae hapa hapa tushuhudie mtu ambaye atatoka na Jacksoni, halafu tutajua tunafanya nini sawa dada yangu. Usilie unanikwaza ……”,
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Atanitambua mpuuzi huyu, ngoja atoke. Haiwezekani kila siku mimi ni wa kulia tu …”,
Joanitha alizungumza kwa sauti ya chini na ya upole tofauti na awali, huku rafiki yake kipenzi akimfuta machozi yake kwa kutumia kitambaa, machozi ambayo yalilowesha mpaka brauzi ya Joanitha.Bila kutambua hali halisi ambayo ilikuwa inaendelea ndani ya chumba cha hoteli, na kuleta hali ya sintofahamu kama wakibahatika kumshuhudia mubaya wao …
…………………………………
Robert aliendelea kutimiza malengo yake kwa kumlewesha pombe Jacksoni, huku Jacksoni akiamini hata Robert alikuwa anakunywa pombe kumbe sivyo na isitoshe alikuwa hajalewa hata kidogo.
“Kunywa! Kunywaa, leo ni furaha tu mimi na wewe …”,
“Asanteeee mpenzi, nilisubili siku kama ya leo kwa muda mrefu, hatimaye uko na mimi laazizi ” ,
Jacksoni akiwa amelewa chakalii aliropoka kwa hisia kali kwa Robert, huku kijana muhuni sana tena mtoto wa uswazi akianza kuichomoa simu yake mfukoni ili ajiandae kukamilisha kazi yake. Alihitaji picha mbaya zaidi za kumdhalilisha Jacksoni, ili Joanitha asitamani tena kumpenda mvulana huyu mwenye tabia za kike kimapenzi bali ahamishie mapenzi yake kwa Robert.
Kichwa cha mzee Mtei kilijawa na mawazo lukuki, huku akiwa hatambui ni kiasi gani atawaadhibu wale wote ambao wamechangia mtoto wake kuharibika. Aliamini kulikuwa na mtu kamlaghai mtoto wake, pengine mwenye pesa nyingi kumshinda yeye na ndiyo maana akakubali kujiingiza katika mapenzi ya jinsia moja …
“Yaani mpaka unafikia hatua ya kujiita aunt Jacky? wewe ni Jacksoni mwanangu, the future big boss ama mwingine?. Hapa kuna kitu siyo bure, hapa kuna roho za watu lazima zipotee ……” ,
funda la sigara lilivutwa, huku moshi mwingi ukijibu mashambulizi kwa kutorokea kupitia matundu mawili puani kwa mzee Mtei. Alijiuliza maswali mwenyewe na kujijibu mwenyewe, huku akiitazama akaunti ya mtandao wa instagram. Akaunti ambayo mwanae alijisajili kwa jina la ajabu, huku akiwa amepiga picha nyingi za kujidharilisha na kudharilisha mpaka wazazi wake. Kwani zilipokelewa tofauti na jamii, huku wakimuhusisha mzee wake kusapoti tabia za mwanae kwani hakumuonya hata siku moja bila kutambua kuwa mzee Mtei hakufahamu kitu chochote kilichokuwa kinaendelea kutokana na kubanwa na majukumu mengi …
“Huyu mpiga picha na yeye lazima afe, hawezi kumpiga picha mtoto wangu na kumdharilisha kiasi hiki. …”,
.
Mzee Mtei aliendelea kuzitazama picha chafu za mwanae, huku akiahidi kumfanyia kitendo kibaya mtu ambaye alimpiga picha mwanae tena picha za kumdharilisha. Aliona muda hauendi, ili giza liingie aweze kusafiri kurudi Gano japo hata swala la tiketi lilikuwa bado halijaletewa majibu na mtu ambaye alitumwa kulishughulikia.
………………… ………………
“Bebii simama, nataka nikupige picha sawa ee! Jiachie unavyotaka, mapozi mazuri ya kunipagawisha ikiwezekana hata nguo toa tu ……………”,,
“Sawa mpenzi, chochote unachotaka mimi nakufanyia. “,
Robert aliamini alichokuwa anataka kufanya kilikuwa ni sahihi kabisa, bila kutambua hatari kubwa iliyokuwa mbele yake pengine hata kuuawa na mzee Mtei kama angelitambua ukatili huo ambao mwanae alikuwa anafanyiwa. Jacksoni kutokana na kuzidiwa na pombe, kila jambo ambalo alikuwa analifanya aliliona sahihi. Haraka sana alianza kujikunja mapozi ya kila aina, huku Robert akiwa ameiseti simu yake vizuri na kufotoa mapicha …
Zoezi liliendelea kwa takribani dakika kumi tu, huku Robert akiwa amekusanya picha nyingi za kutosha,picha ambazo aliamini zingesaidia kwa asilimia kubwa kumpata Joanitha kumbe sivyo!Robert alikuwa anajichimbia kaburi lake mwenyewe …
“Kunywa mpenzi kunywa! nakupenda sana …”,
Siku zote muhuni hana huruma, Robert alianza kumuhimiza Jacksoni kunywa pombe ili azime. Jambo ambalo lilifanikiwa, kwani aunt Jacky aliendelea kufakamia balimi za kutosha na kujikuta akijitupa kitandani mara baada ya pombe kukata mawasiliano ndani ya kichwa chake. Kwa furaha kubwa, kijana Robert alimfunika vizuri Robert kwa kutumia shuka, huku akiangalia saa ya ukutani ambayo ilionyesha tayali yalikuwa ni majira ya saa moja jioni ……
“Kudadeki! dingi lazima aninyofoe koromeo, mambo yameshaharibika. Japo Joanitha sijampata, huyu mseng* alinizidi ujanja lakini lazima Joanitha awe wangu kupitia picha hizi “,
Robert alitoka ndani ya chumba kama ndege, huku akiwa hafamu ni kiasi gani baba yake atapaniki kama atamkuta akiwa ameshafika nyumbani. Lakini hakujutia sana kwa kudanganywa na Jacksoni, kwani alikuwa ameingiza kiasi kadhaa cha pesa na isitoshe kapata picha muhimu ambazo aliamini zitamsaidia kwenye upelelezi wake. Kwa spidi alizotoka nazo alisahau hata kufunga mlango wa chumba, na kubaki wazi kama vile lango la hoteli ya mama ntilie.
…………………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa takribani nusu saa, dokta Benny aliwasili katika jengo lake la kifahari. Hali ya wasiwasi ilimkumba, kwani jumba lake lilikuwa na watu wawili tu waliosalia. Dada wa kazi pamoja na mlinzi wa getini …
“Gari la Joan liko wapi. Inamaana Joan na Doreeni bado hawajafika? pengine dokta Ashrafu aliyoniambia yana ukweli ndani yake. Ngojaa!! “,
Siku zote dokta Benny aliipenda kumwita mwanae kwa kifupi, kwani jina lake lilionekana kupendeza zaidi kama likitamkwa kwa kifupi kuliko kirefu. Haraka sana aliingia ndani ya jumba lake ili kudhibitisha mawazo na fikra zake.
“Neyma! Neymaa!
“Abeeeeh baba! “,
“Wenzako wako wapi? “,
” ,Leo wametoka shule asubuhi sana, walifika hapa na kukaa kwa takribani nusu saa hivi kisha waliondoka. Lakini wanaonekana hawana furaha kama siku zotee …”,
“Au kuna mmoja wao ana mimba? ina maana dokta Ashrafu aliyoniambia yana ukweli kwa asilimia mia moja. Kwanini waje hospitalini kwa siri bila mimi kugundua? kama hawana mimba basi kuna mmoja wao ni mgonjwa na hawataki mimi nifahamu …lazima nifahamu ukweli “,
“Baba kwani vipi? kuna tatizo lolote …”,
“Hapana! hakuna tatizo usjali, nenda kaendelee na majukumu yako. Niandalie chakula kisha nikaoge …”,
“,Sawa baba! “,
Dokta Benny japo alibadilika ghafla, lakini hakutaka binti yake wa kazi agundue jambo lolote lile. Alimpatia maelekezo, kisha alichukua simu yake na kuanza kuzitafuta namba za mtoto wake wa kike aliyeitwa Joanitha. Hakuona sababu ya kuendelea kukaa kimya, pengine kulikuwa na tatizo kubwa zaidi ambalo lilimkumba mwanae. Hivyo alitaka kumpigia simu afahamu mahali alipokuwa, wakati giza tayali lilikuwa limeingia.
…………………………………
Joanitha na Doreeni waliendelea kusimama katika lango la hoteli, huku baadhi ya watu wakiwanyoshea vidole na kuwashangaa kwani hawakuwaelewa kabisa..Mara mmoja alie,mwingine amfute machozi mwenzake.Mara wajadiriane jambo fulani,huku wakiangaza kila kona ya hoteli jambo ambalo lilianza kuwatia mashaka hata baadhi ya walinzi wa hoteli hii…
“Dady is calling……”,
Kioo cha simu ya Joanitha kilisomeka kwa lugha ya kizungu,kuashiria baba yake kumpigia simu jambo ambalo lilimfanya ashituke kupita kiasi.Aliamini baba yake atakuwa na wasiwasi kupita kiasi,kwani tangu azaliwe hakuwahi kuchelewa nyumbani kiasi hiki.
“Doreeni!baba ananipigia?”,
“Amekupigia?heee!leo tumekwisha”,
“Sasa nimwambie tuko wapi…,kwani saa ngapi?”,
“Sasa hivi ni saa mbili kasoro,hebu tuondokee!pokea mwambie tunakuja……”,
Joanitha na Doreeni walianza kukimbia kuelekea mahali ambapo gari lao lilikuwepo,huku Joanitha akiipokea simu ya baba yake.Baadhi ya watu ambao walizifuatilia nyendo zao tangu mwanzo walipokanyaga hotelini,waliwaona kama vituko tena vichaa haswaa.Kwani hawakuwaelewa kwa vituko na vimbwanga walivyokuwa wanavionyesha…
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Dady aim driving! tuko njiani tunakuja… “,
“,Ok!take care…”,
Dokta Benny alimsihi mwanae kuwa makini,kwani alijidhihirisha alikuwa yuko salama japo alidanganywa.Kwa upande wa Joanitha na Doreeni walijipakia katika gari lao dogo,na kuliondoa kwa mwendo ule ule wa kasi kama waliokuja nao.
…………………………………
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment