Simulizi : Mwanaharamu
Sehemu Ya Tatu (3)
BAADA YA DAKIKA TANO;
Mara baada ya Joanitha na Doreeni kutoweka kama upepo eneo la hoteli. Kwa takribani baada ya dakika tano kupita, Robert alitoka ndani ya hoteli huku akikimbia, jambo ambalo lilimshangaza mpaka muhudumu wa mapokezi. Kwani Robert hakupita ofisini kusaini kama alikuwa anatoka nje, na alimaliza kuonana na mgeni wake au angerudi ndani kwa mara nyingine. Jambo ambalo lilimfanya muhudumu kupiga simu katika chumba cha Jacksoni, huku simu ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kuzidi kumtia wasiwasi muhudumu …
Hali ya wasiwasi ili muandama muhudumu wa mapokezi katika hoteli ya Kilimanjaro green view, baada ya kupiga simu ya Jacksoni kwa masaa kadhaa bila kupokelewa. Hakuona sababu ya kuendelea kukaa kimya bali alitoa taarifa kwa walinzi wa hoteli kuelekea chumba namba sita kwenda kuangalia usalama wa mteja wao…
Walinzi walipanda ghorofani haraka sana, kutokana na kuwa na wasiwasi baada ya kusimuliwa mkasa mzima na muhudumu. Kitendo cha Robert kutoka chumbani akikimbia, huku simu ya mteja wao ikiwa haipokelewi kiliashiria hali ya hatari kwa mteja wao ambaye ni Jacksoni Mtei kwani Robert alifika hotelini kama mgeni tu na wala sio mteja rasmi …
“Vipi kulikoni! kimetokea nini ,sijui nitamueleza nini bosi kama kuna mauaji yamefanyika …”,
“Hapana! hakuna jambo baya ambalo limetokea. Inaonekana watu hawa wanafahamiana, japo tumekuta mlango ukiwa wazi na mteja akiwa amelala fofofo …”,
“Hajaibiwa kwelii, na kwanini atoke anakimbia? “,
“Kwanza tumemkuta akiwa amelala, na mezani kulikuwa na chupa nyingi za pombe. Jambo ambalo linaonesha ametumia kilevi kupita kiasi, lakini majibu mazuri tutapata kesho asubuhi akiamka …”,
“,Sawa Asanteni …”,
Muhudumu aliwashukuru walinzi wa hoteli ambao walienda kuchunguza usalama wa Jacksoni, na kumuhakikishia kuwa mteja alikuwa ni mzima japo alipitiwa na usingizi mzito ndiyo maana hakupokea simu yake. Walinzi hawakua na majibu ya maswali yote ya mfanyakazi mwenzao, na kumuhakikishia kupata ukweli zaidi siku inayofuata Jacksoni atakapo pata fahamu …
…………………………………
Hatimaye tiketi za ndege zilifika mikononi mwa mzee Mtei, alitakiwa kujiandaa haraka sana yeye na familia yake kwa safari ya kurudi Gano. Shughuli zote za kibiashara zilisitishwa kwa lengo moja tu, kurudi Gano na kutatua tatizo ambalo lilimkumba Jacksoni …
“Bosi! tiketi zimekamilika, tunapaswa kuondoka saa tatu na nusu usiku huu …”,
“Ok! mama Jacksoni, jiandae …,sina wasiwasi na nyinyi vijana wangu. Paul na Mwenzako hakikisheni usalama wetu na mtu yoyote hapaswi kufahamu kama tunasafiri, je wakati wa kukata tiketi umezingatia hilo …”,
“Ndiyo bosi, tiketi zote zimeandikwa jina langu na sijazungumza na mtu yoyote kuhusu jambo hili. Kwahiyo swala la usalama tuachie sisi …”,
Mzee Mtei kama mfanyabiashara mkubwa, alikuwa na maadui wengi kila kona katika mataifa mbalimbali hasa China, Dubai na nchini kwake Gano. Siku zote aliishi na kwa machale, ndiyo maana alitaka kurudi haraka sana Gano afahamu kila kitu kuhusu mwanae Jacksoni. Isije ikawa ni mchezo amechezewa ili kumchafua kibiashara, jambo ambalo hakuwa tayali kukubaliana nalo.
“Sawa kamanda wangu! I appreciate you …”,
Siku zote mzee Mtei aliwapenda na kuwa amini vijana wake hasa Paul Agustino, kwani hawakumuangusha katika kazi. Alihakikisha anawalipa mshahara mnono, ili wasije wakamgeuka na kuanza kumuibia kimya kimya kwani tayali walitambua siri zake nyingi za kutengeneza pesa jambo ambalo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Vijana wake walimpenda na kumuheshimu kama Mungu mtu, huku mara kadhaa wakihatarisha maisha yao ili kuyaokoa maisha ya bosi wao wa kichaga maarufu kama mzee Mtei.
“Lakini baba Jacksoni! unaona ni sahihi kurudi nyumbani bila kumtarifu hata mtoto wetu Jacksoni …?”,
“Ndiyo! ni sahihi sana, kwanza ni salama kwetu, pili hatutasumbuliwa na mapaparazi uwanja wa ndege na tatu ni moja ya njia ya kujua ukweli kuhusu tabia chafu ya mtoto wetu …”,
” ,Sawa baba! Rodgers bring my hand bag …!,”
“,Ok mama! Nakuletea …”,
Mama yake Jacksoni tangu apigwe makofi na mume wake alitambua ni kiasi gani alikuwa amekasirika, ilibidi akubaliane naye kwa kila jambo ili kuepusha shari zaidi. Hakuona sababu ya kujiandaa zaidi kwani alikuwa anarudi nyumbani, tena safari ya masaa sita ndani ya ndege. Alimuagiza mmoja kati ya walinzi wake aliyeitwa Rodgers mkoba wake wa mkononi tayali kwa ajili ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dubai ili kukwea pipa kurudi Gano.
Kwa sekunde chache tu mkoba wake ulikuwa mikononi mwake, huku Rodgers akiwapatia miwani yao ya kuwalinda. Miwani ambayo iliwasaidia kutambua siraha katika mikusanyiko ya watu, kwani ilionyesha mpaka kile kilichofichwa ndani ya mavazi ya watu mbalimbali. Jambo ambalo liliwatahadharisha kuwa makini naye, kama wangegundua siraha yoyote.
“Haina msaada kwa sasa! nitaivaa bdae …”,
“Mama Jacksoni siku zote ninakusihi uache kupuuzia mambo, shauri yako!.Vijana wangu tuondokeni, nina amini kila kitu kiko sawa “,
“,Ndiyo bosi, tunaweza kuondoka …”,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kundi la watu wa nne lilianza kutoka chumbani, ili kuelekea katika lifti ambayo ingewashusha kutoka ghorofa ya ishirini, mahali ambapo chumba chao kilikuepo ili kuwasafirisha mpaka chini kabisa ghorofa ya kwanza. Mzee Mtei na walinzi wake walikuwa wamevaa miwani ya bei kali machoni mwao, huku mama Jacksoni akipuuzia jambo lile kwani aliona kama haikua wakati sahihi wa kuivaa. Alisahau ule msemo wa wahenga usemao, utajiri ni mzigo na kuhatarisha maisha yake …
Mama yake Jacksoni alimuwaza mwanae tu, siku zote alimpenda sana na alichangia kwa kiasi kikubwa katika malezi mabovu ya mwanae. Siku zote hakumuonya alipomuona akijichanganya watoto wa kike badala ya wanaume, hakutaka kumkwaza mwanae bila kutambua kuwa alikuwa anamuharibu. Hakuwahi kumkataza asifanye shughuli za ndani kama kupika, kuosha vyombo na kudeki. Kwani aliamini alikuwa sahihi kabisa alipodai anamsaidia kazi housegirl kumbe ulikuwa ndiyo mwanzo wa Jacksoni kuharibika. Mambo yaliharibika pale Jacksoni alipoenda America kusoma masomo ya sekondari, huko ndiko alipovurugwa saikolojia yake kama mwanaume kiasi kwamba aliaminishwa mwanaume ana uwezo wa kuzaa kama mwanamke kama tu akifanyiwa upasuaji maarumu. Hakuweza kulipinga jambo hilo, kwani aliwashuhudia baadhi ya wanaume wakiwa tayali wameshabadili maumbo yao waliyozaliwa nayo, huku wakipandikizwa maumbile ya kike, matiti pamoja na sifa zingine zilizowafanya waonekane kama wanawake haswaaa!. Loo! America kubaya asikwambie mtu.Kuna kila uchafu ambao hufikirii binadamu mwenye akili timamu, aliyeumbwa na Mungu anaweza kuufanya…
…………………………………
Doreeni na Joanitha walitumia takribani nusu saa, kutoka hotelini mpaka nyumbani kwao. Njia nzima walifikiria ni namna gani wanaweza kumwelezea mr Benny, baba yake Joanitha aweze kuwaelewa kwani haikuwa kawaida yao tena kama watoto wa kike waliolelewa katika maadili ya Kiafrika. Haipendezi hata siku moja, mzazi kufika nyumbani kabla ya mtoto …
Tofauti kabisa na fikra zao, dokta Benny hakuwauliza jambo lolote lile. Bali aliketi sebuleni akifatilia taarifa ya habari, huku akiwa bize kusoma kitabu kilichohusika na mambo ya saikolojia …
Walimsalimia kisha kuelekea moja kwa moja kwenye meza ambayo ilikuwa na chakula chao, kutokana na njaa waliyokuwa nayo. Kwani hotelini hawakuweza kula chakula walichoagiza na kulipiwa na Jonsoni, kutokana na kutoweka katika meza ya Jonsoni mara tu walipoketi na kupokea taarifa mbaya kuhusiana na Jacksoni. Taarifa ambayo ilimshitua Joanitha, na kutoweka pasi kujua alipokua anaelekea, na Doreeni kumfuata kama nzi amfuatapo kikojozi.
Dokta Benny alikuwa bize kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kuangalia taarifa ya habari, kusoma kitabu halisi cha saikolojia na kusoma saikolojia ya Doreeni pamoja na Joanitha. Sura zao zilionesha siri nzito ikiwa imejificha katika vichwa vyao, huku ubongo wao ukifanya mambo makubwa kupita mawazo yao …
“Joanitha na Doreeni kuna tatizo linawasumbua! msipo nieleza nikawasaidia, nina amini mtapata matatizo makubwa ……”,
“Hapana baba tuko sawa, “
“,Baba usjali!!!! tuko sawa. Hatuwezi kukuficha kitu …”,
Nidanganyeni, lakini tambueni nimekula chumvi nyingi kuliko nyinyi. Mimi ni daktari, hivyo basi mpaka sasa nimetibu wagonjwa wengi zaidi ya elfu moja. Nina uzoefu mkubwa kuhusu magonjwa ya binadamu na saikolojia yake, huwezi kufika na kula chakula bila hata kunawa halafu uniambie wewe ni mzima? ,isitoshe mmeingia ndani na viatu, wakati haijawahi kutokea. Siku zote tunavua viatu mlangoni, tukiwa tunaingia ndani …
“Haaaa! “,
Doreeni na Joanitha waliguna, huku wakijishangaa.Walitazama mikono yao, kweli walikula bila kunawa. Hawakuishia tu kutazama mikono yao, bali walijishangaa kwa kuingia ndani na viatu na kujikuta wakiona aibu. Aliyoyasema dokta Benny, baba yake Joanitha ni ukweli mtupuu! bila kuwa na chembe hata ya uongo ndani yake …
Robert aliwasili nyumbani kwao, tabasamu liliipamba sura yake kwani siku hiyo wazazi wake walichelewa kufika nyumbani tofauti na siku zote. Kichwani aliwaza jambo moja tu, kumchafua Jacksoni ili Joanitha amdharau. Moja kwa moja alielekea bafuni kuoga, jambo ambalo lilikamilika ndani ya dakika tano tu. Kutokana na shauku kubwa aliyokuwa nayo, kutaka kumchafua Jacksoni, kijana aliyependwa na Joanitha japo alikuwa na kasoro kubwa katika mwili wake. Huku akiwatukana matusi ya nguoni wanaume rijali kama Robert pale walipojaribu kumtongoza.
“Kanikomesha! na mimi namkomesha! huwezi nitia mkosi kiasi hiki, ety unanipenda …mwanaume kabisa wewe nakupeleka wapii! ………”,
Robert aliongea huku akifakamia chakula, kutokana na njaa kali aliyokuwa nayo. Mkononi alionekana kuchezea simu yake ya kupangusa maarufu kama smatifoni. Kila alipotaka kuziposti mtandaoni, roho yake ilisita. Hakutambua ni kwanini roho yake ilimkatalia kufanya jambo hilo, na kujikuta akiamua kuziposti picha alizompiga Jacksoni katika grupu moja la Whatsap. Grupu ambalo halikuzingatia maadili hata kidogo, jambo ambalo lilimvutia Robert kujiunga nalo …
Masikini Robert aliingia kwenye matatizo makubwa bila kutambua, laiti kama angelitambua hatari kubwa iliyoko mbele yake bora angeahirisha lengo lake la kumchafua Jacksoni. Picha zilisambaa kwa kasi ya ajabu katika mitandao ya kijamii, huku chanzo akiwa ni Robert. Kwani picha mara baada ya kupostiwa na Robert katika grupu la Whatsap, watu walifowadi picha za Jacksoni katika magrupu mengine na kujikuta zikisambaa zaidi na zaidi. Wengine walizihifadhi picha hizo katika simu zao, huku vyombo mbalimbali vya habari hasa magazeti ya udaku wakifurahia jambo hilo kwani wangeingiza pesa nyingi sana kupita picha za Jacksoni, mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Gano …
…………………………………
Joanitha kweli alikuwa hana furaha, baba yake alitambua mwanae hakuwa na furaha lakini Joanitha alikataa katu katu kumweleza baba yake ukweli kuhusu chanzo cha matatizo yake. Dokta Benny hakutaka kuwa na haraka, alitambua kumlazimisha mwanae amweleze ukweli ingekua vigumu hivyo ilibidi akae kimya na kutafuta njia nyingine ili atambue ukweli na kumsaidia mwanae…
“Joanitha usilie! mbona unalia, unaenda wapi? malizia kula kwanzaa …”,
Joanitha alianza kulia ghafla, hakuona sababu ya yeye kulia sebureni. Kwani baba yake angelitambua chanzo cha yeye kuangua kilio ghafla mithili ya mtu aliyefiwa,jambo hilo lilitokea pale tu baba yake alipomaliza kuzungumza naye. Tangu atoke hotelini alikuwa hajaifungua simu yake, jambo ambalo lilimfanya aifungue kwa pupa kwani tayali alikuwa amefika nyumbani. Heee! nguvu zilimuishia, hakuamini alichokiona. Picha za ajabu ziliingia katika simu yake, picha ambazo mtu aliyempenda alipigwa akiwa katika mapozi ya ajabu tena ya kike …
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe ni “Mwanaharamu “!! ,shetanii kabisaaa “,
Msichana mrembo Joanitha alifoka, huku akikimbia kuelekea chumbani kwake. Kama kawaida ya Doreeni siku zote alikuwa bega kwa bega na rafiki yake, alimfuata ili kujua chanzo cha rafiki yake kuangua kilio ghafla kiasi kile mara tu alipoifungua simu yake …
“Wewe ni “Mwanaharamu ” huwezi kujidharilisha kiasi hiki, ulimwengu utanichukuliaje mimi. Sifai kuwa na wewe, sifai! nakupenda sana lakini nimenyosha mikono juu, eee! Mungu nimekukosea nini?”,
Joanitha aliropoka maneno yaliyomfanya hata baba yake kushituka,kwani hakuwahi kutambua kama mwanae ameanza kujihusisha na mapenzi na isitoshe alikuwa bado kidato cha sita.Dokta Benny alipojaribu kutafakari maneno ambayo mwanae alikuwa akizungumza chumbani kwake huku akilia,aliamini kwa asilimia kubwa mwanae alikuwa amesalitiwa.Jambo ambalo lilimfanya amkumbuke mke wake,mama yake Joanitha kwani pesa ndizo zilimfanya asalitiwe na kutengana na mke wake…
“Itakuwa ana mimba?halafu aliyempatia mimba kamkataa,lakini mbona sijawahi kuona dalili zozote za ujauzito kwa Joan?”,
Baba yake Joanitha,maarufu kama dokta Benny aliendelea kujihoji maswali yasiyokuwa na majibu,katika siku zote ambazo zilikuwa mbaya ni siku hii.Siku ambayo aliifananisha kabisa,na siku ambayo alitengana na mke wake kipenzi mama Joanitha.Dokta Benny alizima tv,na kufunika kitabu chake alichokuwa anasoma kisha alielekea chumbani kwake.Moyo wake ulimuuma,na kimkosesha furaha kwani hakuwa tayali kuendelea kusikia kilio cha mwanae…
“Baba umesahau simu…”,
“Niletee chumbani……,hapana hebu niletee hapa…”,
Kweli alichanganyikiwa,tangu lini akamruhusu binti wa kazi kuingia chumbani kwake,ilihali hata nguo zake pamoja na usafi wote wa chumbani Joanitha ndiyo alifanya.Huku nguo za ndani akizifua mwenyewe,ili kuitunza heshima yake kama baba wa familia.Haraka sana alitengua kauli yake,huku akisimama aweze kuletewa simu yake baada ya kuisahau kwenye sofa.Kwa mwendo wa unyonge alielekea chumbani kwake baada ya kupatiwa simu yake,huku sauti za kilio za Joanitha zikipenya katika masikio yake na kumuumiza kupita kiasi…
…………………………………
Doreeni aliingia chumbani na kumkuta rafiki yake akiwa amejilaza akilia,simu yake ikiwa imetelekezwa pembeni yake.Kila alipojaribu kumnyamanzisha Joanitha,jitihada ziligonga mwamba huku akionyeshwa ishara kwa kutumia kidole aweze kuchukua simu.Hakuona sababu ya kuchukua simu,wakati rafiki yake anaendelea kulia.Aliipuzia simu ,na kumtuliza rafiki yake kwanza…
“Niache nilie nipunguze hasira zangu.Mwanaume gani anapendwa lakini hathamini hisia za mtu,chukua simu uone upuuzi alioufanya kama unaweza kuvumilia kama ni wewe!!”,
Hapo ndipo Doreeni alielewa ishara zote alizokuwa anaelekezwa ili achukue simu ya Joanitha,haraka sana aliipalamia na kujikuta akijuta kuichukua.Kwani alimanusura aitupe chini,kutokana na kushuhudia uchafu usiokuwa wa kawaida…
Mkono wake wa kushoto uliufumba mdomo wake,huku macho yakimtoka kama panya aliyebanwa na mlango.Baada ya kukutana uso kwa uso na picha ya Jacksoni akiwa amevaa bikini,huku akiwa ameyabinua makalio yake mithili ya dadapoa aliyekuwa akitangaza biashara yake…
Picha zilikuwa nyingi tena zenye kukera,huku namba iliyomtumia picha Joanitha ikiwa ngeni kabisa.Doreeni alianza kupekua simu ya Joanitha huku na kule,meseji nyingi ziliingia kutoka kwa watu tofauti tofauti wakimfahamisha kuhusu Jacksoni kwani picha zake zilikuwa gumzo katika nchi yote ya Gano.Doreeni alipojaribu kufungua mitandao ya kijamii hali ilikuwa ni ile ile na kujikuta akiizima simu bila kupenda…
“Sisi tunakushauri kila siku,mfute Jacksoni katika kichwa chako.Yule hana tofauti na wewe,kwani hana tofauti na mwanamke kwa sasa lakini unaona kama hatukupendi.Shauri
yakoo…”,
Ilikuwa ni meseji ambayo Doreeni aliisoma katika simu ya Joanitha,na kuamua kuzima simu bila kupenda.Hakuona sababu ya kumnyamanzisha tena rafiki yake kwani alikuwa na machungu makubwa,alimuacha alie mpaka pale hasira zake zitakapo pungua na moyo wake kusuzika…
…………………………………
Chumbani kwa baba yake Joanitha hakukukalika, mzee wa watu mara asimame, akae ,mara atembee tembee chumbani. Mara alale tena, yote hayo ni kutokana na mawazo mengi ambayo yalimsumbua kuhusu mwanae …
“Kesho nitaitisha kikao cha ghafla baina ya madaktari wangu. Kutunza siri za mgonjwa ni wajibu wetu, lakini mara nyingine tunapaswa kutoa siri hizo ili kuokoa maisha ya watu wengi zaidii. Aliyemuhudumia mwanangu leo, inatakiwa anieleze nini kinamsumbua mwanangu, hakuna njia nyingine zaidi ya hii …”,
Dokta Benny akiwa anatembea tembea chumbani kwake, alipata jambo la muhimu katika fikra zake ambalo aliamini lingemsaidia kujua ukweli na kutambua namna ya kumsaidia mtoto wake wa kipekee aliyejulikana kwa jina la Joanitha
Nusu saa ilikuwa imepita tangu mzee Mtei na familia yake kuiacha ardhi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, ndege kubwa aina ya Boeing 777 inyomilikwa na shirika la ndege la Uingereza maarufu kama fly Emirates ilikuwa imepakia abiria wengi zaidi ya mia mbili. Huku wengi wakiwa ni wafanyabiashara wakubwa wa kizungu na kiarabu, huku wachache sana wakiwa na ngozi nyeusi ya Kiafrika. Miongoni mwa abiria wachache wa Kiafrika waliokuwa ndani ya ndege hii ni familia ya Mtei, mfanyabiashara maarufu nchini Gano anayemiliki kiwanda na kampuni inayotengeneza sabuni maarufu ya kuogea barani Afrika inayojulikana kama Mtei soap.
“Tutafika saa kumi au saa kumi na mbili! nina hasira sana na wanaotaka kunichafua, lazima damu imwagike kwa wale wote ambao wamehusika na jambo hili …”,
Mzee Mtei alizungumza, huku mke wake akimsikiliza bila kumpatia jibu lolote. Tangu apigwe makofi, hakuona sababu ya kuchangia jambo lolote lile kwani angeonekana kumtetea Jacksoni jambo ambalo lingemkasirisha mume wake. Mzee Mtei alipoona hajibiwi alijishtukia, hakuona sababu ya kuendelea kuongea bali alichukua “headphones ” kubwa na kuzipachika katika masikio yake, kisha alianza kusikilizia mziki mzito wa tv ndogo iliyokuwa mbele ya kiti chake. Huku usingizi ukimnyemelea taratibu, macho yake yalifumba na kufumbua jambo ambalo liliashiria usingizi kutaka kumzidi nguvu …
…………………………………
Jonsoni alizidiwa na pombe, na kujikuta akilala palepale mezani. Kutokana na hoteli hii kuwa kubwa na kujaa watu muda wote, hakuna aliyemjali bali wateja waliendelea kula raha kama kawaida. Wanaume waliopata wanawake palepale hotelini, waliingia nao ndani katika vyumba vya wageni kukidhi haja zao. Hakuna yoyote yule aliyemjali mwenzake, kila mtu aliburudika na kujirusha kadri alivyoweza …
Mziki ulipigwa! watu waliogelea katika bwawa, dadapoa walijiuza na biashara haramu za madawa ya kulevya zilifanyika ndani ya hoteli hii kubwa na ya kifahari.Sio biashara ya madawa ya kulevya pekee iliyofanyika,bali hata michezo mingine haramu kama Kamali ilifanyika ndani ya hoteli hii…
Lakini ndani ya sekunde chache tu,majira kama ya saa tano usiku.Hali ya hewa ilibadilika katika maeneo yote ya hoteli,jambo ambalo lilisababisha baadhi ya shughuli kukwama.Waandishi wa habari wa magazeti pendwa pamoja na vyombo vya habari visivyo vya kiserikali walivamia hoteli na kwenda moja kwa moja katika ofisi za mapokezi…
Ni muda wa saa moja sasa ulikuwa umepita ,tangu muhudumu wa hoteli hii pamoja na walinzi wake kupata jibu la maswali ambayo walijiuliza kuhusu Robert.Walitambua yeye ndiye alimpiga picha Jacksoni na kuichafua sifa ya hoteli yao,kwa kumlewesha pombe Jacksoni bila yeye kujitambua jambo ambalo ilikuwa ni sahihi kabisa…
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naitwa Mwasaki,natokea Gano yetu Tv.Unazungumziaje picha chafu ambazo mtoto wa kigogo maarufu hapa Gano kupigwa picha,picha ambazo inasemekana kapigiwa katika hoteli yenu kwani nembo za hoteli yenu zinaonekana katika chumba alichopigiwa picha…”,
“Sisi kama hoteli hatujapendezwa nalo,na lazima tutamshitaki muhusika.Ukiangalia vizuri picha hizo,kapigwa akiwa katika hali ya ulevi na inaonekana mpiga picha alifanya hivyo kwa faida yake binafsi.Pengine kuichafua hoteli yetu au kumchafua kijana…”,
“Je,picha alizopiga ni sahihi kwa maadili ya nchi yetu ya Gano? …”,
“,Siwezi kukujibu kwa sasa! swali lako ni zaidi ya uwezo wangu …”,
“,Umesema unaitwa nani? “,
“,Naitwa Jacline, muhudumu wa Kilimanjaro green view …”,
“Asante sana! naitwa Mwasaki,kutoka Gano yetu Tv …”,
” ,Shukrani …”,
Jitihada za kumpata meneja wa hoteli zilingonga mwamba, kwani alifichwa makusudi baada ya kupatiwa taarifa nzima kuhusu hali halisi ilivyotokea. Waliona bora wasitishe kabisa kuliongelea swala hili katika vyombo vya habari, kwani wangezidi kuichafua hoteli yao na kuifanya ikose wateja kabisa …
“Hapa inatakiwa kijana huyu aondolewe mahali hapa, mapema sana kabla hapajakucha! nina amini asubuhi tutatembelewa na waandishi wengi wa habari, pengine hata askari polisi kutoka katika vyombo vya dola …”,
“Hapana bosi! nashauri turipoti polisi kabla ya yote bila hivyo tutaonekana tumechangia jambo hilo kutokea …”,
” ,Kweli tufanye hivyo! hata sisi tunamsapoti Jacline …”,
Kikao kifupi cha faragha,kiliendelea mara baada ya waandishi wa habari kutoweka. Meneja ilibidi azungumze na wafanyakazi wake ili wapate ufumbuzi haraka sana, kwani tayali hoteli yao ilikuwa imeshachafuliwa. Haraka sana maamuzi yalifikiwa, bila kupoteza muda jeshi la polisi lilipatiwa taarifa ili kufika hotelini na kudumisha ulinzi. Waliamini kwa asilimia mia moja Jacksoni lazima angeshambuliwa na raia wenye hasira kali hasa wanaume, kwa kuwadharilisha na kupotosha maadili ya watoto wao na jamii kwa ujumla bila kujali alikuwa ni mtoto wa kigogo au laaa! …
…………………………………
Robert alifurahi sana usiku huu, tangu amalize kula na kuelekea chumbani kwake kujipumzisha alitabasamu na kucheka muda wote. Jambo ambalo liliwashangaza hata wazazi wake pale waliporudi nyumbani. Waliitambua furaha ya mtoto wao isiyokuwa ya kawaida, na kujikuta wakijiuliza maswali mengi bila majibu …
“Una nini wewe? au unakichaa! “,.
“Hapana mama! ni furahaa tu hahahaa.Mimi ni mshindiii …”,
“Umeshinda nini? “,
“,Mama hata nikikueleza huwezi nielewa, ni ushindi wa kipuuzi tu, nenda kapumzike uwahi kazini kesho ……”,
Robert alikuwa sahihi kabisa, ushindi alioupata ulikuwa ni wa kipuuzi na asingemshirikisha mtu mwenye akili timamu akampatia sapoti. Mama yake alitoka katika mlango wa chumba cha mwanae huku akiwa na sintofahamu katika kichwa chake, alihisi pengine mwanae alikumbwa na malaria kali kumbe sivyo. Robert alifurahi sana baada ya kufanikiwa kumchafua Jacksoni, bila kutambua kuwa muda wowote maisha yake yalikuwa hatarini. Bora akamatwe na polisi kwa makosa aliyo yafanya kuliko mzee Mtei, baba yake Jacksoni. Kwani mzee Mtei lazima angehakikisha anakitenganisha kichwa chake na kiwiliwili, ndipo moyo wake ungeridhika …
…………………………………
Jacksoni sasa alikuwa maarufu katika nchi yote ya Gano, asiye kuwa anamfahamu sasa aliweza kumfahamu kupitia picha ambazo zilisambazwa na Robert. Kila mmoja alizipokea picha hizi kwa hisia tofauti, huku wengi wakiamini alifanya kwa makusudi hasa baadhi ya walimu wa chache wa shule aliyokuwa anasoma na kuapa kumfukuza shule pale tu atakapo ripoti na mzazi wake …
“Ameidharilisha shule yangu vya kutosha! sasa ameenda mbali zaidi na kuichafua shule yetu kimataifa zaidi, siwezi kukubali! siwezi, Jacksoni wewe sio mwanafunzi wangu tena …”,
Mwalimu mkuu alikwazwa na kitendo kile ambacho kilifanywa na Jacksoni, akiwa kitandani amejilaza. Usingizi ulitoweka kabisa mara baada ya kupokea picha chafu za Jacksoni huku waandishi mbalimbali wa habari wakimsumbua kupitia simu yake ili aweze kuzungumza mawili matatu kuhusu picha hizo ambazo zilisemekana ni za mmoja kati ya wanafunzi wake …
…………………………………
“Mimi nilisema, afukuzwee! kwakua baba yake ana pesa na ni mtu maarufu mkamtetea. Ona sasa, naamini haya yote yasingetokea kama tungekua tumeshamfukuza …”,
Mwalimu mwingine aliyejulikana kwa jina la mr Nyoshanyosha, jina maarufu ambalo alibatizwa na wanafunzi wake katika shule ya st Peter. Siku zote alisimamia maadili, na kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mstari ulionyooka. Lakini hali ilikua tofauti alipotaka Jacksoni afukuzwe, kwani walimu wenzake hasa mkuu wa shule walimpinga na kudai asifukuzwe kabla wazazi wake hawajaitwa shuleni. Jambo ambalo halikuwa na ukweli hata kidogo, kwani siyo wanafunzi wote wenye makosa makubwa walifukuzwa baada ya kuonywa mbele ya wazazi wao bila mafanikio, ilitokea tu kwa Jacksoni kwakua wazazi wake walikuwa na pesa kama ujuavyo mwenye pesa sio mwenzako!
Mwalimu huyu wa nidhamu alichezea simu yake, huku akiwa hana usingizi kabisaa. Alijuta kwa adhabu ya wiki mbili ambayo walimpatia Jacksoni, kisha arudi shuleni akiwa na mzazi wake. Jambo ambalo lilisababisha Jacksoni aendelee na tabia yake mbaya, pengine aliona kama uongozi wa shule ulimuogopa na usingeweza kumfukuza hata afanye jambo baya kiasi gani …
…………………………………
Gano;
SAA 11;00 A; M
Uwanja wa ndege wa jiji la Gano, ulifurika waandishi wa habari baada ya kupokea tetesi za mzee Mtei kuwasili na ndege ya asubuhi kutoka Dubai. Hawakutaka wapitwe na habari hata moja, kila mmoja alikuwa bize kuangaza huku na kule maeneo ya wageni kuitafuta sura ya mfanyabiashara huyu maarufu …
Hatimaye uvumilivu wao ulizaa matunda, kwa mbali mzee Mtei akiwa sambamba na mke wake walijongea kutoka nje ya uwanja huku wakionekana kuwa na haraka kupita kiasi. Nyuma yao walikuwa na walinzi shupavu ambao hawakuwa tayali kuruhusu hata nzi kupita, ili kumsumbua bosi wao …
“Bosi! naripoti kutoka Sauti yetu tv, unatwambia nini kuhusu yaliyotokea usiku uliopita? “,
“Siwezi kusema chochote kwa sasa! naomba mniache …”,
“Bosi! au umefurahishwa na kitendo cha mwanao kupiga picha za nusu utupu, katika mavazi ya kike ……?”,
“Nimesema sifahamu chochote, hebu niachenii …!”,
Mzee Mtei alikwapua kifaa kimoja cha kurekodia na kukitupa chini, jambo ambalo lilipelekea waandishi wengine wa habari kuogopa kumsogelea bosi huyu wa kichaga. Walitambua ni kiasi gani alikuwa na hasira, jambo ambalo lilipokelewa na watu wengi katika fikra tofauti tofauti. Mzee Mtei aliyoyazungumza ni sahihi kabisa, kwani hakutambua chochote kile ambacho kilitokea usiku uliopita. Jambo ambalo lilimfanya awe na maswali mengi kichwani …
“Bosi! Jonsonii hajafika, lakini tulimfahamisha kuwa tunawasili asubuhi, aje na gari kutupokea ……”,
“What? ina maana Jonsoni mpaka sasa hajafika? kuna nini kimetokea hapa katikati mbona sielewi ……”,
“Sifahamu bosi …”,
“Tuchukue taksi haraka sana, nimechoshwa na mipicha ambayo tunapigwa bila mpangilio. Lazima kuna sababu ambayo imesababisha Jonsoni asifike kutupokea, na pia kuna sababu iliyo wajaza waandishi wa habari mahali hapa …”,
Mama yake Jacksoni aliongea huku picha za kila aina zikimiminika, kila hatua waliyokuwa wanapiga waliweza kupigwa picha na mapaparazi japo walikataa katu katu kufanya mahojiano ya aina yoyote ile. Kwa sekunde tu walifika eneo la magari madogo ya abiria, kisha kujipakia bila kupenda ili tu kukwepa picha ambazo walipigwa bila mpangilio …
Askari walifika asubuhi na mapema, siku iliyofuata baada ya tukio kutokea katika hoteli ya Kilimanjaro green view. Wateja wengi walikuwa wameshatokomea kwani shughuli mbalimbali zilisitishwa, huku wengi wao wakiogopa kuhojiwa na waandishi wa habari pamoja na polisi ambao walionekana kuzagaa kila kona ya hoteli …
“Samahani kaka sijui unaitwa nani? “
“Ninakuuliza, unaitwa nani na umefika hapa muda gani? “,
Jonsoni alikurupuka kutoka usingizini, huku mwili wake ukiwa na uchovu usio wa kawaida. Kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu, ubongo wake uligoma kuleta kumbukumbu sahihi kichwani mwake na kubaki akimtazama askari aliyeonekana kumuuliza maswali bila kumpatia muda wa kutosha kufikiria majibu ya kumpatia …
“Kwanza nini kimetokea? mbona polisi wako mahali hapa, pamoja na waandishi wa habari? “,
“Yani mimi nakuuliza swali na wewe unaniuliza badala ya kunijibu. Uko sawa kweli?”,
Jonsoni hakukumbuka jambo lolote lile kwa wakati huu, kutokana na pombe alizokunywa usiku uliopita. Jambo ambalo lilipelekea askari aliyekuwa anamuuliza maswali mawili matatu kuachana naye, kwani alimdharau Jonsoni kwa majibu yake aliyompatia na kumuona kama mtu asiyekuwa na msaada wowote kwake …
Kitendo kile kilipelekea Jonsoni kuendelea kujitafakari, huku akiwa hatambui ilikuwaje mpaka yeye akafika hotelini pale. Pombe sio chai! hakukumbuka chochote kile, jambo ambalo lilipelekea achukue simu yake pengine angepata mawili matatu ya kumsaidia …
“Fika uwanja wa ndege asubuhi na mapema, chukua gari yoyote na sio prado ya Jacksoni …”,
Meseji iliyotumwa kutoka nje ya nchi, iliingia katika simu ya Jonsoni. Jambo ambalo lilipelekea aisome meseji mara mbili mbili, bila kutambua nini afanye. Hofu ya kufukuzwa kazi ilimtawala, hasa akimtafakari mzee Mtei asivyopenda upuuzi katika kazi hata siku moja …
“Usiondoke kabla sijamaliza shughuli zangu ” ,
Akiwa amepigwa na butwaa kama mwendawazimu! maneno ambayo Jacksoni alimtamkia usiku uliopita aliyakumbuka, na kujirudia rudia katika kichwa chake, na kumbukumbu yake yote kurudi kwa mara nyingine tenaa …
“Bora bosi anikute nyumbani, itakua rahisi kumdanganya. Kuliko kutonikuta nyumbani,hakuna muda wa kupoteza zaidi ya kuondoka mahali hapa !…” ,
Jonsoni alinyanyuka katika meza aliyokuwa ameketi na kulala usiku kucha, kisha alikimbia moja kwa moja kuelekea maeneo ya mapokezi bila kujali baadhi ya askari ambao walionekana kuzunguka ovyo hotelini …
“Katika hali isiyokuwa ya kawaida,mmiliki wa kampuni maarufu ya Mtei soap Limited. Amevunja kifaa cha mwandishi wa habari, mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Gano .Bosi huyo alionekana kukataa kuhojiwa, na kujikuta akiwa mkali kwa yoyote yule aliyetaka kufahamu kuhusu tuhuma zinazomkabili mwanae nikiripoti………” ,
Dereva wa Jacksoni hakuona sababu ya kuendelea kutazama runinga iliyokuwa ndani ya hoteli, kwani ilizidi kumpatia machungu. Haraka sana alianza kujieleza alipofika mapokezi, ili afahamu bosi wake alikuwa wapi!
“Naitwa Jonsoni! dereva wa Jacksoni, nahitaji kuonana na Jacksoni kisha niondoke naye mahali hapa …”,
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jonsoni alitoa kitambulisho chenye picha yake, kitambulisho ambacho kilikuwa na maelezo yake yote ikiwemo saini ya mzee Mtei. Mara tu alipomaliza sentesi yake kujitambulisha, tayali kundi kubwa la askari na waandishi wa habari walimzunguka ili kufahamu kitu ambacho kilitokea …
“Kwa sasa huwezi kuondoka naye! kwa sababu za kiusalama, naomba uwe mpole ndugu yangu ……”,
Jibu ambalo Jonsoni alipatiwa lilizidi kumuweka katika wakati mgumu, kwani hakutambua chanzo cha yeye kukataliwa kuonana na Jacksoni. Ilibidi ashike kichwa chake tu bila kuamua jambo lolote lile,kwani hakufamu nini afanye kwa wakati ule na isitoshe mzee Mtei alikuwa amewasili kutoka Dubai……
…………………………………
Jacksoni alikurupuka kutoka usingizini,na kujikuta akiwa katika mavazi ambayo hata yeye aliyashangaa.Chupa za pombe zilitapakaa kila kona ya chumba huku harufu kali ya pombe ikipenya katika matundu mawili ya pua yake…
“Hapa kuna mchezo umechezeka sio buree! “,
Alizungumza huku akivaa nguo zake haraka haraka ili kupotea eneo lile,kichwani alijilaumu kwa kutumia kilevi kupindukia huku akiikumbuka sura ya Robert mara mbili mbili kichwani mwake.Mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi sana,huku akiamini kuna jambo la aibu ambalo alifanya na Robert bila kujitambua kutokana na kutumia pombe kupita kiasi…
“,Robert yuko wapi!kwanini aondoke bila kunipatia taarifa,au ameniibia?” ,
Mtoto wa watu alijiuliza maswali mengi kichwani,maswali ambayo yalikosa majibu kabisa.Hakutambua kama Robert aliondoka usiku uliopita mara tu yeye alipopitiwa na usingizi,na sio asubuhi kama alivyo fikiria.Ndani ya sekunde chache tu alikuwa amekamilika, mkoba wake ulikuwa katika mkono wake wa kushoto huku kichwani akiwa amevalia wigi lake zuri la bei kali. …
Kwa mwendo wa maringo,huku akiwa na haraka alitoka ndani ya chumba chake ili kutoweka eneo lile kwani machale yalimcheza na kutojiamini hata kidogo…
“Mumy is calling……” ,
ghafla simu yake ilianza kuita,na kujikuta akichanganyikiwa.Hakuamini kama aliyekuwa anampigia simu alikuwa ni mama yake mzazi,kwani siku zote waliwasiliana kwa kutumia mitandao ya kijamii hasaa Whatsap na Skype akiwa nje ya nchi na sio simu ya kawaida. Simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, kisha ilikata yenyewe …
“Au mama yuko Gano?, kwanini afike bila kunipatia taarifa.?,mbona sielewii? ” ,
Mkono wake ulitetemeka huku kijasho chembamba kikimtoka. Hofu aliyokuwa nayo haikuwa ya kawaida, kwani haikuwa kawaida kupigiwa simu na mama yake katika mazingira ya kutatanisha kiasi kile …
Alizima simu yake mara tu ilipokata, kisha akaidumbukiza katika mkoba wake. Kilichobakia ni kushuka haraka ghorofa ya pili ili arudi nyumbani haraka iwezekanavyo, japo hakutambua Jonsoni alikuwa mahali gani kwa wakati kama huu na isitoshe funguo za gari alikuwa nazo yeye …
…………………………………
Taksi ambayo ilimpakiza mzee Mtei na familia yake iliondoka uwanja wa ndege na kasi ya ajabu, ili kukwepa mapaparazi ambao walikuwa na uchu wa kupata taarifa yoyote ile iloyokuwa gumzo mtaani ili kujitengenezea pesa ndefu…
Mzee Mtei aliitambua hali hii,na kuamini kulikuwa na sababu kuu iliyosababisha jambo hili kutokea na wala sio tu taarifa za mwanzoni alizozipokea kutoka nchini Gano akiwa bado Dubai…
“Dereva tupeleke mtaa wa Hewasafi,pesa hii hapa!” ,
“Mbona pesa nyingi sana hizi bosi wangu,?”,
“,Kuhusu pesa hizo usjali,nitakwambia sababu ya kukupatia pesa nyingi kiasi hicho.Endesha gari kwanza unifikishe nyumbani na familia yangu…”,
Dereva hakuendelea kuhoji,bali alendelea kukanyaga mafuta kuutafuta mtaa ambao uliishi watu wenye pesa na maarufu katika jiji hili kuu la nchi ya Gano.Mtaa huu ulipatiwa jina hili la Hewasafi,kwani mtu yoyote alikaribishwa kwa harufu nzuri ya chakula tena cha matawi ya juu.Pale tu alipokanyaga mguu wake mahali hapa,kama sio harufu ya kuku aliyekuwa akikaangwa basi harufu ambayo ingesikika ni ya pilau yenye madikodiko kedekede…
“Baba Jacksoni!mbona sielewi,nini kimetokea?”,
“Usjali mke wangu,ndiyo maana nimempatia pesa ya kutosha dereva huyu.Naamini atatueleza kila kitu tutakapofika nyumbani,”
Dereva alitabasamu huku akifurahi kwa uvumilivu aliokuwa nao,kwani mwanzoni alitaka kumropokea mzee Mtei pale tu alipoingia ndani ya gari lake akiwa na familia yake huku wakijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu.Alimfahamu vizuri sana,lakini moyo wake ulikuwa mzito kila wakati alipotaka kuufungua mdomo wake kuwaeleza wateja wake kuhusu habari ya mjini kwa sasa jambo ambalo lilizaa matunda kwani alikabidhiwa pesa nyingi takribani milioni moja ili tu aweze kuufungua mdomo wake na kusema kila kitu alichokifahamu bila kuficha hata chembe ya ukweli…
………………………………
Hali ya wasiwasi ilitawala katika nyumba ya mzee Timotheo, pamoja na nyumba jirani. Polisi walivamia nyumba hii asubuhi na mapema, kisha kuwaamsha kwa fujo wanafamilia ambao walilala fofofo bila hili wala lile …
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Niacheni! sio mimi, sijafanya hivyo! niacheniiii …”,
“Paaaah! twendee ukaisaidie polisi, utajieleza mahakamani na sio mahali hapa …”,
Kofi zito lilitua katika shavu la Robert na kujikuta akiwa mpole bila kupenda, wazazi wake hawakua na cha kufanya zaidi ya kumuonea huruma kijana wao. Tuhuma alizokuwa nazo ni kubwaa, jambo ambalo lilipelekea apelekwe msobemsobe bila kupatiwa hata muda wa kujistiri. Kwani alitoka na boksa pale alipogongewa mlango wake, na kupelekwa kituoni kama alivyo …
“Kafanya nini mwanangu! Msinipigie mwanangu tafadhali ……”,
“,Kafanya nini si tunauliza?, ni haki yetu kujua. Halafu siyo haki kumpiga mtuhumiwa kabla ya hukumu yake, nitawashtaki nyie vijanaa kuweni makini …!”,
Mzee Timotheo aliwachimba mkwala askari ambao walionekana kumbeba mwanae, huku wakimchapa makofi kuituliza jazba yake. Hakuna aliyemsikiliza, bali askari wale walimpakia Robert kwenye defender ya polisi na kutokomea naye huku wananchi wengi na majirani wakiwa hawatambui sababu kuu ya Robert kukamatwa …
“Fikeniii poliisii, mtatambua makosa ya kijana wenu …”,
Askari mmoja aliyekuwa akining’inia juu ya mabomba ya defender ya polisi, alizungumza huku vumbi kubwa likitimka kutokana na mwendo mkali ambao polisi waliomtia nguvuni Robert waliondoka nao. Jambo ambalo lilipelekea mzee Timotheo na mkewe kupiga chafya nyingi mfululizo, huku wakipatiwa ushirikiano na majirani wambeya ambao hawakutaka kupitwa na hatua hata moja kuhusu Robert kukamatwa. Chafya ambazo majirani hawa walipiga zilikuwa kali kupita kiasi, kwani wengine walikuwa karibu kabisa na gari la polisi kabla ya kuondoka …
…………………………………
Dokta Benny aliamka asubuhi na mapema kuelekea kazini, huku mtoto wake wa kike pamoja na rafiki yake wakiwa bado hawaja amka. Kama daktari mkuu, hakupaswa kuchelewa kazini bali alipaswa kuwahi ili kuonesha mfano wa kwa wadaktari wadogo wadogo ambao aliwaongoza …
Kama kawaida yake alipenda sana kujisomea, hasa magazeti ili kutambua taarifa mbalimbali ambazo zilijili katika siku hii mpya. Taratibu alijipenyeza katika foleni ndefu, kwani wananchi wengi walielekea katika shughuli zao jambo ambalo lilipelekea vyombo vingi vya usafiri kujaa abiria na kuweka msururu mrefu barabarani. Dokta Benny aliipaki gari yake ya kifahari pembeni kabisa ya barabara, kisha alishuka kwenye gari kuelekea eneo la wafanyabiashara wa magazeti ili kununua nakala zake ili aweze kujisomea …
“Mtei azaa Mwanaharamu ,Mtei avunja kifaa cha Mwanahabari uwanja wa ndege. Kumbe aunt Jacky ni mtoto wa bilionea Mtei, kwa mara ya kwanza mtei apanda taksi uwanja wa ndege, mtoto wa mtei amchafua baba yake kwa kujipiga picha za utupu ……”,
Bila kutegemea dokta Benny alikutana uso kwa uso na vichwa cha habari katika magazeti ya Udaku, sio kwamba alipendezwa na magazeti ya aina hii lahasha. Mtu aliyetajwa kwenye gazeti alimfamu vizuri sana, ndiye mtu ambaye aliyabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa na kuamua kuishi peke yake. Kwani dokta Benny hakuwaamini wanawake tena, na wala hakuwa tayali kusikia chochote kile kuhusu mapenzi ndiyo maana alikosa amani pale tu alipohisi mwanae ameanza kujihusisha na mapenzi akiwa bado
msichana mdogo …
“Chukua bosi! ni jero tu, kuhusu mtoto wa bilionea Mtei kuliwa tigo ndiyo habari ya mjini kwa sasa …” ,
Kwa lugha ya kihuni, muuza magazeti alichomoa nakala ya magazeti ambayo yalionekana kumshangaza dokta Benny kisha kumpatia. Bila shida yoyote! dokta Benny alichukua magazeti yale, huku akichukua na magazeti kadhaa ya siasa kisha alitoa pesa na kuondoka eneo lile …
“Bosi chenji yakoo! “,
Muuza magazeti alishangazwa na elfu kumi aliyopatiwa, huku mteja wake akitokomea bila kusubili chenji yake. Kutokana na ishara aliyopewa na mteja wake, hakuwa na haja ya kuendelea kuuliza bali alifurahi kupata zali hili la mentali asubuhi na mapema kiasi hiki. Macho yake yalisindikiza gari la bei kali ambalo mteja wake aliondoka nalo, mpaka pale lilipopotea katika macho yake …
“Daaah ukipata wateja watano kama hawa kila siku, lazima utoke kimaisha. Leo hata nisipo uza gazeti lingine freshii tu, nimeshapata hela ya kula siku tatu mfululizo …”,
Muuza magazeti alitabasamu na kuzungumza mwenyewe, huku wafanyabiashara wenzake wakimshangaa na kumuonea wivu. Kwani walishuhudia kila kitu ambacho kilitokea, huku mwenzao akilamba mwekundu asubuhi na mapema jua likiwa bado hata halijachomoza.
…………………………………
Jacksoni alifika eneo la mapokezi kama aliyechanganyikiwa, huku akishangazwa na waandishi wa habari pamoja na askari ambao walionekana kumuhoji Jonsoni. Ghafla kundi lile kubwa lilisitisha kumzingira Jonsoni, na kumfuata muhusika mkuu ambaye ni Jacksoni. Kwa mara hii vurugu zilikuwa kubwa kutoka kwa waandishi wa habari, jambo ambalo lilipelekea polisi kuwazuia waandishi wa habari kutimiza majukumu yao kwani pengine wangemdhuru Jacksoni kwani kila mmoja alitaka kumuhoji ili apate taarifa bora na ya kuvutia zaidi ya mwenzake.
“Kuna nini! Jonsoni tuondoke mahali hapa sio salama …”,
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jacksoni alitoweka haraka sana, huku Jonsoni akimfuata. Kichwani aliamini kulikuwa na tatizo ambalo limetokea, pengine kuna mtu alivujisha siri za yeye kuwa na mwanaume hotelini japo hakuwahi kufika katika hoteli hii na isitoshe wafanyakazi wengi wa hoteli hii walikuwa hawamfahamu kama ndiye mtoto wa Mtei, mtoto wa kipekee kabisa …
Polisi walifanya kazi ya ziada kuwalinda dhidi ya vurugu za waandishi wa habari, huku wakishirikiana na walinzi wa hoteli ya Kilimanjaro green view ……
Bila kupoteza hata sekunde, Jonsoni aliingia kwenye gari na kuiwasha .Huku Jacksoni akijipakia kwa kupitia mlango wa upande wa pili. Picha za kutosha zilipigwa, huku gari likiwashwa na kuondolewa eneo la tukio kwa kasi ya ajabu. Alimanusura baadhi ya waandishi wa habari wagongwe, kwani walilizunguka gari hili aina ya prado bila kuogopa usalama wao na isitoshe walikuwa wanazuiwa na polisi bila mafanikio …
…………………………………
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment