Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MWANAHARAMU - 4

 












Simulizi : Mwanaharamu

Sehemu Ya Nne (4)







Gari aina ya BMW liliendeshwa kwa taratibu sana, jambo ambalo liliwakera baadhi ya madereva ambao walikuwa na haraka zao. Kitendo cha dokta Benny kuwa bize kusoma magazeti, magazeti ambayo yalimshangaza sana kwa ujumbe wake. Yalisababisha ajisahau kama alikuwa barabarani anaendesha gari …



“Achaa dharau mseng* wewe! hicho kigari chako hata mimi ninaweza kubeti nikaotea na kukinunua. Hebu endesha, acha kusoma magazeti kabla hatujakigongaa …”,



Sauti ya hasira ilipenya katika masikio ya dokta Benny, kwani kioo cha upande wake wa kulia kilikua wazi. Hakua na haja ya kumlaumu konda wa daladala aliyemtukana, bali alitelekeza magazeti yake na kuliondoa gari lake kwa kasi ya ajabu ili tu kumridhisha aliyekuwa akimtupia maneno machafu. Ujumbe ambao ulijirudia rudia katika magazeti aliyoyasoma ulizidi kuzunguka katika kichwa chake, na kumfanya aendelee kukanyaga mafuta ili afike kazini haraka iwezekanavyo na kutafuta ukweli kuhusu yale aliyoyasoma …



………………………………



“Unaweza kuniambia nini kinachoendelea hapa nchini na kinacho nihusu mimi au familia yangu? ……”,



“Ninakuuliza? nini kinaendelea ?”,



Mzee Mtei aliwasili nje ya geti lake, huku utulivu wa hali ya juu ukiwa umetawala. Dereva taksi alikuwa bize kulishangaa jumba la bilionea huyu, huku akikiri kuna watu walikuwa na mapesa na sio pesa ndogo ndogo za kununua madafu, kitendo ambacho kiliepelea kutoelewa maswali aliyoulizwa na kujikuta akikurupushwa aliposhikwa begani na kuulizwa swali kwa mara nyingine tena …



“Jana usiku kuna picha za utupu za mwanao zilisambaa, akiwa amepigwa picha hizo katika hoteli ya Kilimanjaro green view. Lakini inaonekana alipigwa bila kujitambua, kwani pembeni kulionekana chupa kadhaa za bia zikiwa tupuu. Sifahamu zaidi ya hicho bosi naomba kuondoka …”,



Taarifa waliyopatiwa iliwakata maini, mzee Mtei ,mke wake pamoja na walinzi wake. Nguvu ziliwaishia na kujikuta wakibaki wamesimama tu, walishindwa waelekee ndani au waketi chini. Huku dereva taksi aliyawaleta akitokomea mbele ya macho yao …

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Baada ya Jonsoni kuliondoa gari eneo la hoteli ya Kilimanjaro green view, njia nzima alitafakari namna ya kumwelezea bosi wake mpaka amuelewe. Wasiwasi ambao alikuwa nao haukuwa wa kawaida, huku akijitahidi kulikanyaga mafuta gari ili ajalibu bahati yake, pengine angewahi kufika nyumbani kabla ya mzee Mtei. Kwa upande wa Jacksoni hali ilikuwa ni tofauti, kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi pengine zaidi ya Jonsoni huku akifikiria chanzo cha waandishi wa habari pamoja na askari kuwepo maeneo yale ya hoteli bila kupata majibu sahihi …



Hakuona sababu ya kuendelea kuwaza na kuwazua peke yake, wakati Jonsoni alikuwepo eneo la tukio. Aliamua kumshirikisha, pengine angepata majibu ya maswali yake …



“Jonsoni! Jonsoni! mbona unawaza kiasi hicho? uko sawa kweli? ……”,



“Siwezi kuwa sawa wakati niko hatarini kufukuzwa kazi? “,



“Nani akufukuze kazi na kwa makosa gani? hebu punguza basi mawazo, mimi siwezi kukufukuza kazi kwani hujanikosea jambo lolote lile …”,



“Hapana Jacksoni, sio wewe wa kunifukuza kazi bali wazazi wako. Baba yako na mama yako wamefika kutoka Dubai na sijui kwanini wamerudi ghafla kiasi hiki? ” ,



“Unasemaa? “,



“Ndiyo, mzee Mtei amerudi na isitoshe nilitumiwa meseji tangu jana nikawapokee, kutokana na kutumia pombe kupita kiasi nimejikuta nafungua simu yangu muda mfupi tu uliopitaa ……”,



“Mungu wangu weee! ndiyo maana mama kanipigia, nimekwishaa! “,



“Kakupigia! “,



“Ndiyo kanipigia, simu imeita mpaka basi huku mimi nikiwa sijielewi kabisa. Hapa kuna kitu sio bureee ……” ,



Ujumbe mzito ambao Jacksoni aliupokea kutoka kwa Jonsoni, ulizidi kukivuruga kichwa chake huku akiamini kwa asilimia mia moja kuna jambo zito ambalo lilimleta baba yake ghafla bila kutoa taarifa. Alibaki tu amejilaza kwenye kiti cha gari, huku akitamani gari liluke ili wafike nyumbani haraka iwezekanavyo kabla ya mzee Mtei kufika …



…………………………………



Baada ya kupigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa, kutokana na kupokea ujumbe mzito uliowachanganya. Mzee Mtei alikisogelea kitufe cha kengele kilichokua ukutani na kukibonyeza. Alikibonyeza kwa fujo kutokana na hasira alizokuwa nazo, ndani ya muda mfupi tu hatua za miguu zilisikika kuashiria ujio wa mtu getini …



“Shikamoo baba! karibuni …”,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Marahaba. Jacksoni yuko wapiii? ninashida naye mara moja, tena haraka sana …” ,



“Jacksoni aliondoka na Jonsoni tangu jana mchana, mpaka sasa hawajarudi. Polisi wamefika nyumbani kumuulizia, nimekosa majibu ya kuwapatia. Sijui kafanya nini na sijui wameelekea wapi? ” ,



Dada wa kazi alilifungua geti la kufunguliwa kwa limoti, na kujikuta akiyakutanisha macho yake uso kwa uso na mzee Mtei. Hakuishia kukutanisha macho na mzee Mtei pekee, bali alimpokea mkoba mama Jacksoni na kujibu maswali ambayo aliulizwa mfululizo na mzee Mtei ambaye alionekana kuwa na hasira kupita kiasi.



“Mama Jacksoni unaona matatizo ya mwanao, tumezaa mwanaharamu na sio mtoto. Mtoto anafikia hatua ya kulala nje, hili jumba lote nani alale? “,



“Nimesikia baba Jacksoni, yameshatokea. Haina haja ya kulaumiana, nyumbani tayali tumefika tunachotakiwa kufanya ni kutafuta namna ya kumsaidia …”,



“Wee Rechoo!”,

“Abee baba ”

“Hebu kuja hapa “,



Dada wa kazi alisitisha safari yake ya kupeleka mizigo ndani, kisha alirudi kusikiliza jambo ambalo aliitiwa na bosi wake. Huku wakijadiliana mambo ambayo hayakumuhusu kutokana na udogo wake na nafasi aliyonayo katika familia, ilibidi awapishe na kuelekea ndani kabla ya kuitwa tena akiwa hata hajafika mbali …



“Unaizungumziaje tabia ya Jacksoni tangu niondoke miezi mitatu iliyopita ……”,



“Baba ninawaheshimu na sijawahi waongopea hata siku moja, siku zote nilitimiza majukumu yangu japo wakati mwingine nadharauliwa kutokana na umri wangu kuwa mdogo. Kiufupi Jacksoni amebadilika, sasa hivi hana tofauti na mimi na wakati mwingine nikianika nguo zangu nisipokuwa makini anazichukua na kuzivaa yeye ……!”,



“Unasemaje Recho? “,



” Ndiyo mama! Jacksoni anawanaume, Jacksoni anafikia kumuita Jonsoni mpenzi lakini nikijaribu kuzungumza nakaripiwa na kutukanwa. Najua hamuwezi kuniamini, lakini ukweli mtaupata kupitia Cctv Kamera ……”,



Siku zote mzee Mtei alikuwa na busara na hekima, ndiyo maana alipendwa sana na wafanyakazi wake. Kwa maelezo tu aliyopatiwa, alijipapasa mfukoni mwake kisha kumpatia noti kadhaa za elfu kumi kumi binti yake wa kazi aliyeitwa Recho. Jambo ambalo lilimfurahisha na kuapa kuzidi kuwa mwema mbele ya bosi wake …



“Paul na mwenzako! tumerudi Gano sababu ya kijana wangu, shughuli za kibiashara zimegoma kwa muda usiojulikana. Sasa nawapa siku hii ya leo, pumzikeni huku mkifanya upelelezi mdogo hapa nyumbani, chunguzeni kamera zote, ninaamini mtafahamu mambo mengi. Kesho vukeni mipaka, mkawatafute wale wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine kunichafua…”,



“,Sawa bosi! “,



Mzee Mtei hakua na haja ya kuzungumza sana. Aliwapatia maelekezo vijana wake, kisha alielekea ndani kupumzika yeye pamoja na mke wake. Usiku kucha hawakulala vizuri kutokana na safari, hivyo basi ulikuwa ni wakati sahihi wa wao kupumzisha miili na akili zao ambazo ziliwaza muda wotee kuhusu kijana wao…



…………………………………



Joanitha aliamka akiwa na mtazamo mpya, hakutaka kusikia chochote kile kuhusu Jacksoni. Aliapa kutopenda tena, kwani mwanaume aliyempenda alikuwa ni Jacksoni na ndiyo huyo ambaye alitaka kuwa kama mwanamke. Doreeni hakupingana na fikra za rafiki yake, japo hakuamini kama kweli Jacksoni alifutwa katika kichwa cha Joanitha kwani swala la mapenzi kwa mtu sio la kufuta haraka tu kama wino kwenye karatasi.Inahitaji muda mrefu, tena kwa msaada wa madaktari wa saikolojia ili uwe katika hali nzuri zaidi …



Siku hiyo alijishughulisha na shughuli mbalimbali za usafi nyumbani, ili kujisahaulisha machungu. Hawakuona umuhimu wa kwenda shuleni kwa siku hii, ilibidi wapumzike ili kukiweka kichwa chake katika hali nzuri zaidi kimawazo. Doreeni hakutaka kwenda peke yake shuleni, alibaki nyumbani ili kubadilishana mawazo na rafiki yake,asiweze kukumbuka machungu ya kile ambacho kimetokea …



…………………………………



Dokta Benny aliwasili hospitalini, kabla hata ya muda wa kazi kuanza. Aliitisha kikao kifupi, kwa lengo moja tu kumsaidia mwanae katika matatizo ya kimapenzi ambayo yalikuwa yanamsumbua…



“Madaktari wenzangu nimewaita! mwanangu ana tatizo la saikolojia, ubongo wake unawaza kupita kiasi ili kufanya mambo makubwa yasiyo wezekana. Je ni nani aliyeonana na mwanangu siku iliyopita? bila yeye mwanangu hawezi kupona, kwani hali imekua mbaya zaidi …” ,



“Ok dokta Imaculata tuonane! wengine mnaweza kuendelea na shughuli zenu. “,



Dokta Benny aliwaruhusu madaktari wengine kuondoka, huku akibaki na daktari wa saikolojia aliyejulikana kwa jina la Imaculata. Yeye ndiye alinyoosha mkono, kuashiria kuhusika na matibabu ya Joanitha na rafiki yake Doreeni siku iliyopita …



Bila kupoteza muda walianza mazungumzo yao, mazungumzo ambayo yalikifungua kichwa cha dokta Benny na kupata majibu ya maswali ambayo alikuwa akijiuliza bila kupata majibu ……



“Mwanao na rafiki yake, walikuja jana mahali hapa wakitaka kumsaidia rafiki yao ambaye ni gay (shoga). Wanadai mvulana huyo wanasoma naye na ni rafiki yao kipenzi …niliwambia wajitahidi kumleta mahali hapa ili tumsaidie kisaikolojia zaidi …”,



“Mungu wangu! bila shaka ni Jacksoni ,maana Jacksoni ndiye anasoma na mwanangu”,



“,Jacksoni ndiyo nani?, “



“Huyu hapa kwenye gazeti! ni mtoto wa mama Joanitha, mtoto huyu walizaa na mzee Mtei mara tu baada ya kuachana na mimi …”,



“Jacksoni huyu ambaye taarifa zake zimeenea usiku kucha? ni mtoto wa mkeo? “,



“Ndiyo! lakini tunza siri hii, nimekwambia tu kwa vile umenifamisha kuhusu mwanangu. Hakuna mtu ambaye anaifahamu siri hii, nikiisikia sehemu yoyote nitatambua chanzo ni wewe! wengi wanafahamu mama yake Joanitha ameshafariki …”,



“Natambua hilo, hata mimi niliamini amefariki. Kuhusu siri hii usjali, pia usisite kunijuliasha kuhusu hali ya mwanao …”,



“Ok! kazi njema …”,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Dokta Imaculata, mama mwenye umri wa makamo. Bila shaka alikula chumvi nyingi, alitoka katika chumba cha mkutano walichokuwa wamebaki wawili tu, ili kwenda kuendelea na majukumu mbalimbali ya kikazi. Kichwani alijiuliza maswali mengi kuhusu siri aliyoambiwa, huku akiahidi kuitunza kama alivyoaminiwa na kuambiwa.



………………………………………………………………………………………………



Robert kwa mara ya kwanza aliingia rumande, japo alikulia uswazi na kushiriki vitendo kadhaa vya kihuni lakini alikuwa hajawahi kuingia mahabusu. Siku zote alisikia tu kwa watu kuwa gerezani dirisha ni dogo na liko usawa wa bati, mara oooh! gerezani wananyea ndoo na kuna kunguni za kumwagaa. Leo hii kila kitu alikishuhudia kwa macho yake mwenyewe …



“Hebuu kaa humo mpuuzi wewe, mpaka siku shitaka lako au dhamana yako itakaposikilizwa …”,



Robert akiwa ndani ya boksa tu, alisukumwa ndani ya chumba ambacho kilijaa mahabusu wengi. Alijikuta akipokea kipigo cha kutosha na kuanza kulia kama mtoto mdogo, kwani alijikuta anakanyaga mahabusu kadhaa kutokana na kutokuwepo mahali pa kukanyaga …



“Kwanza amekuja uchi, hajui kama ni muda mrefu hatujaonana na wake zetu! leo lazima aolewe, hawezi kutukanyaga wakubwa zake …”,



Maneno ya kejeli yalipenya katika masikio ya Robert, huku hasira zikimpanda katika kichwa chake. Aliapa kutoana roho na yoyote yule atakaye jaribu kumgusa na kumfanya kama mke wake. Bora afe kuliko kushuhudia akitendewa unyama na ukatili, huku akiwa na akili timamu kabisa …



“Mimi siyo Jacksoni, ama zangu ama zake kwa yoyote yule atakaye nigusa …”,



Mtoto wa uswazi Robert alizungumza peke yake moyoni mwake, huku akilia kwa maumivu makali mara tu alipowekwa mahabusu na kujikuta akikanyaga wenzake kitendo kilichopelekea apokee kipigo kikali. Kwani mwanga ulikuwa hafifu sana, huku harufu kali ya mikojo ikipenya katika mapua yake. Bila shaka watu hawa walijisaidia haja kubwa na ndogo, humu humu ndani ya chumba hiki.



“Toa kelele zako! hapa sio msibani, unatuvurugia starehe zetu ebooo! “,



Jamaa mwingine alifoka, na kumchapa kibao Robert. Alimanusura watwangane kama sio onyo kutoka kwa askari polisi aliyechungulia na kuchimba mkwala akiwasihi wanyamanze. Jambo ambalo liliwafanya waachiane mikono huku kila mmoja akirudi mahali pake na kujikunyata, japo hawakuridhika na onyo kali walilopewa kama tu wakidhubutu kutwangana makonde wakiwa mahabusu na kuahidi kutiana adabu wakati mwingine…



…………………………………



Walinzi wa bwana Mtei walichunguza Cctv kamera zote ndani ya nyumba, na kujikuta wakipandwa na hasira dhidi ya Jonsoni. Sio tu peke yao waliopandwa na hasira hata bosi wao mzee Mtei pamoja na mkewe, kwani walishuhudia jinsi Jonsoni alivyofanya mapenzi ndani ya gari mara kadhaa na Jacksoni. kwani waliogopa kufanyia uchafu huo chumbani ili kuzikwepa kamera ambazo zilitapakaa kila kona ndani ya nyumba.



“Paaaa! “,Kompyuta kubwa ilipasuliwa na mzee Mtei, kompyuta ambayo iliunganishwa na kamera zote katika jumba hili la kifahari la bwana mtei. Kwani alishindwa kuvumilia pale tu walipojaribu kukuza tukio moja ambalo lilifanyika ndani ya gari na kupelekea gari kutikisika hali ambayo haikuwa ya kawaida. Hawakuwa na haja ya kuendelea kuhoji, kwani wote tayali walikuwa ni watu wazima kilichobakia ni kuchukua maamuzi sahihi dhidi ya Jonsoni …



“piiiiii! piiiii! …”,



Honi ya gari ilisikika, na kuwashitua mzee Mtei pamoja na vijana wake. Kwa upande wa mama Jacksoni mapigo ya moyo wake yalienda kasi sana, huku akiwa haamini kama kweli mwanae aliingiliwa kinyume na maumbile tena na mfanyakazi wake ambaye alimuajiri mwenyewe …



Wote kwa pamoja walitoka nje, huku dada wa kazi akielekea kulifungua geti kuliruhusu gari ambalo lilipiga honi liweze kuingia. Bila shaka yoyote gari lilikuwa la Jacksoni, kutokana na mlio wake wa honi uliosikika …



“Kamateni mbwa huyu, kisha nendeni mkamfungie stoo mpaka pale atakaponijibu maswali yangu bila hivyo namuua …”,



Kabla hata gari halijapaki vizuri, Paul na Rodgers walilizunguka huku wakimchomoa kupitia dirishani Jonsoni akiwa bado hata hajazima gari. Kwa upande wa Jacksoni alishindwa afanye nini, na kujikuta akitoka ndani ya gari bila hata kujifanyia tathmini juu ya mwonekano wake…



“Haaaa! mwanangu leo hii unavaa wigiii, unajipaka lipshine? unajipodoa, na isitoshe unavaa viatu vya kisigino kama mama yako! …”,



Mshituko ambao alikuwa nao mama yake Jacksoni haukuwa wa kawaida, dunia aliiona kama inazunguka huku taratibu macho yake yakifumba na kuanza kudondoka chini .Kwani muonekano ambao alikuwa nao mwanae haukuwa wa kawaida kama alivyomzoea…



“Mamaaaaa! “,



“Paaaaa! “,



“Wewe ndiyo chanzo cha yote mwanaharamu wewe! sina hakika kama wewe ni mwanangu niliye kuzaa, sina hakika kama umezaliwa na mke wangu au alikuokota na kuniongopeaa …”,



Bila kutegemea, Jacksoni alikutana uso kwa uso na kofi zito na kujikuta akidondokea kulee pale tu alipojaribu kumkimbilia mama yake mara tu alipondondoka chini kutokana na mshituko na isitoshe alikuwa na matatizo ya presha ambayo yalimsumbua kwa muda mrefu …



Jacksoni alilia kwa kwikwi, huku akiwa haamini maneno ambayo baba yake alimtamkia. Siku zote wazazi wake walimtetea na kuwa upande wake, lakini kwa upuuzi huu hakuna binadamu yoyote ambaye alikuwa tayali kumuunga mkono …



“Kamataa na mwanaharamu huyu! peleka stoo hakikisha anafungwa asiweze hata kujikuna …”,



“Babaaa! usinifanyie hivyoo …”,



“Mimi siyo baba yako, mwanzo na mwisho! nisisikie tena unaniita hivyoo …”,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwa sauti ya kike, Jacksoni alipojaribu kumshawishi baba yake ili atengue kauli yake. Jitihada ziligonga mwamba na kuambulia onyo kali ambalo lilipelekea kujuta kwa maumbile yake aliyokuwa nayo. Saikolojia yake ilikuwa imeshabadilika na kuamini kuwa alizaliwa hivyo, kumbe haikuwa kwelii …



…………………………………



Mzee Mtei alikuwa na wagonjwa wawili katika nyumba yake, mke wake aliyepoteza fahamu pamoja na mwanae ambaye alibadilika ghafla na kuwa na tabia za kike. Haraka haraka alichomoa simu yake na kumpigia daktari wake wa kihindi ili afike nyumbani haraka sana kutoa msaada …



“Haloo! naongea na dokta Ranjibhai …”,



“Ndiyo bosi. Bila shaka ni Mtei,isn’t it? “,



“It is…,! wahi nyumbani kwangu unipatie msaada “,



Simu ilikata, huku vijana wake wakiwa bize kumpepea mke wake mara baada ya kukamilisha zoezi la kumfunga Jacksoni ndani ya stoo. Sehemu moja kabisa na Jonsoni.Ilibidi aungane nao kuendelea kumpatia huduma ya kwanza mke wake, wakiwa wanavuta subila kumsubili daktari wake aliyefanya kazi katika hospitali ya wahindi maarufu kama Agakhan …



…………………………………



Dokta Benny kazi zake ziligoma kabisa ndani ya siku hii, mawazo yake yote yalikuwa bize kutafakari uhusiano wa utata kati ya mwanae pamoja na ndugu yake Jacksoni ambaye ni mtoto wa mzee Mtei .Aliamini kabisa Joanitha na Jacksoni walikuwa ni marafiki wa kawaida tu, jambo ambalo lilipelekea awaze na kuwazua namna ya kumweleza kuwa yule aliyetaka kumsaidia sio tu rafiki yake bali ni kaka yake tena tumbo moja kabisa japo baba tofauti. Hakutambua ni kiasi gani mwanae ataumia,lakini ili asiumie zaidi na kujenga uhusiano mzuri kati ya watoto hawa. Alitakiwa kufanya juu chini kuhakikisha Jacksoni anarudi katika hali ya kawaida, japo mke wake mama yake Joanitha alimsariti kwa umaskini wake na kuamua kwenda kuolewa na bilionea Mtei kabla dokta Benny akiwa bado hajahitimu mafunzo yake ya udaktari shahada ya kwanza…



“Siwezi kuolewa na wewe! nakuachia mwanao, na marufuku kumweleza ukweli kwamba mimi ni mwanae! mwambie mama yake kafariki, ili atambue kuwa sikupendi na siko tayali kuishi maisha ya kimaskini. Kuzaa na wewe ni bahati mbaya tu, tena kwa tamaa za ujana! “,



Baba yake Joanitha maarufu kama dokta Benny, alidondosha chozi mara tu alipoyakumbuka maneno ya mwisho ambayo mke wake alimtamkia siku ya mwisho alipoondoka na kwenda kuolewa na bilionea Mtei. Maneno ambayo yalimchoma kama mkuki, kwani alimkana mpaka mtoto wake wa kumzaaa ambaye ni Joanitha …



“Ama kweli wahenga walisema, malipo ni hapa hapa duniani. Alimkana mtoto wake leo hii amekuwa mkubwa tena binti anayejitambua, na kuzaa na bilionea aliyemkimbilia mtoto ambaye amewaaibisha na kuwachafua nchini na kimataifa! Ok wacha niache kujaji, mimi sio Mungu naomba anisamehe lakini penye ukweli hatuna budi kusema! “,



Bila kusahau magazeti yake yaliyokuwa juu ya meza katika ofisi yake, aliyachukua kisha kutoweka kurudi nyumbani kwani shughuli za kiofisi ziligoma kabisa. Asije akaua watu, kwani udaktari ni kazi ngumu tena inayohitaji umakini na taaluma ya hali ya juu hasa kitengo chake cha upasuaji.



Familia ya mzee Timotheo ilikosa furaha. Tangu wafunge ndoa miaka mingi iliyopita walibahatika kupata mtoto mmoja tu, mtoto ambaye walitegemea kuwa mrithi wa mali zao kadhaa ambazo zilimtia kibuli Robert na kujiona kama vile alikuwa tayali amewini maisha. Nyumba mbili walizokuwa nazo, pamoja na piki piki moja tu ya baba yake aina ya Yahamaha ndiyo iliyomtia kibuli Robert japo zilikuwa mali chache tena ambazo angechekwa sana kama angezitaja mbele za watu.Robert ambaye ndiyo furaha yao pekee ndani ya nyumba alikamatwa na polisi tena akisindikizwa na kipigo kikali, kipigo ambacho kiliwaumiza wazazi wake kwani hawakutambua makosa ambayo kijana wao aliyafanya …



“Robert kafanya nini? amempa mimba mtoto wa watu au kapigana na watoto wa wakubwa? “,



“Sijui mume wangu, twende kituoni tutafahamu huko huko! “,



“Eti Angela? kaka yako kafanya nini? “,



“Sifahamu bosi! alitoka hapa nyumbani jana asubuhi baada ya kurejea kutoka shuleni, bila hata kunisemesha alijiandaa na kutokomea kwenye misele yake, bila shaka alienda kwa rafiki zake na ndipo aliporudi jioni muda mfupi tu kabla ya nyie kufika! “,



“Ahaaaaa! basi huko ndipo alipogusa visivyoguswa! mama Robert tuondokee, tutajua huko huko kituoni. “,



Wakiwa wamepanda kwenye pikipiki yao, walipokea maelekezo machache kutoka kwa binti wao wa kazi. Huku wakiwa katika mavazi nadhifu kabisa, mzee Timotheo alikuwa amevaa suti nyeusi yenye heshima haswaa kama mwalimu mkuu lakini kwa upande wa mama yake Robert alikuwa amepigilia kanga nzuri kwenye mwili wake na kumpatia heshima zote alizostahili. Safari ya kuelekea kituo cha polisi ilianza rasmi, kwani ndiyo mahali pekee pa kutambua makosa ambayo mtoto wao aliyafanya ili waweze kumrudisha mikononi mwao …



…………………………………



Mama yake Jacksoni baada ya kupepewa na kupata hewa ya kutosha, fahamu zake zilirudi katika hali ya kawaida huku daktari wa familia akiwa bado hajafika. Kwa msaada wa Paul, mlinzi hatari sana wa mzee Mtei. Mama yake Robert alipatiwa msaada wa kutembea kupelekwa sebuleni kujipumzisha.Angalau mzee Mtei alitabasamu na kuwa na amani alipomuona mpenzi wake, mwanamke aliyetumia pesa nyingi sana kumpata akiyafumbua macho kwa mara nyingine tena. Jambo ambalo lilibakia kichwani kwake ni kwenda kumuonya Jonsoni na kumpatia adhabu aliyostahili kwa kulala na mwanae kinyume na maumbile yake …



“Haloo bosi! kijana aliyemchafua mwanao katika hoteli yetu tayali amekamatwa na yuko mikononi mwa polisi, tunaomba radhi kwa jambo lolote lile ambalo limetokea. Naitwa Hans meneja wa ………”,



Mzee Mtei akiwa anaelekea katika stoo ambayo Jacksoni na Jonsoni walifungwa kwa kamba ngumu za katani, huku wakiwa wameketi kwenye viti. Ghafla simu yake iliita, huku namba ikiwa ngeni kabisa katika macho yake mawili ambayo Mungu alimjalia. Haraka sana aliipokea kwani aliheshimu simu kuliko kitu chochote kile, kwani simu nyingi alizopigiwa mara kwa mara zilihusiana na maswala ya kibiashara na hakuwa tayali kupoteza wateja kwa kuwacheleweshea mizigo yao kama tu angekosa mawasiliano nao kwa wakati.



“Heee! mpuuzi huyu nitamuadhibu mwenyewe na siyo polisi! “,



Kabla hata sentesi ya mtu aliyempigia simu mzee Mtei haijamalizika, mzee Mtei alikata simu huku akiongea maneno ya kejeli kwa hasira. Alifurahi kwa muhusika mkuu wa tukio kukamtwa, lakini hakufurahishwa na kitendo cha polisi kuendelea kumshikilia mikononi mwao. Alitaka amuadhibu yeye mwenyewe na siyo polisi!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ni muda mrefu umepita tangu atoe roho ya mtu, mara ya mwisho aliua ili kujitengenezea mazingira ya kumpata mke wake mrembo ambaye ni mama yake Jacksoni. Lakini kila alipojaribu kutumia nguvu za kawaida kumpata mke wake ilishindikana, kwani mke wake ambaye ni mama Jacksoni hakumpenda kwa dhati mzee Mtei japo alitoka katika familia ya kimaskini na isitoshe mchumba wake maarufu aliyejulikana kama Bensoni alikuwa ni mwanafunzi wa chuo tena asiye na lolote lile. Ndipo mzee Mtei alipoamua kumwaga mabilioni katika familia ya mama yake Jacksoni, hakuishia hapo mwanamke huyu mrembo alipatiwa cheo kama bosi mkuu wa mzee Mtei katika kampuni yake ya kimataifa inayohusika na maswala ya uzalishaji wa sabuni za kuogea. Hapo ndipo moyo wake ukageuka na kuhamisha mapenzi yake yote kwa bilionea huyu, hakujali kama alizaa na Bensoni lahasha! alichojali ni maisha mazuri ya kimalikia, wala sio ufukara ambao amekua nao na kumfanya adharaulike licha ya uzuri ambao Mungu alimbariki. Wazazi wake wote walikuwa upande wa mzee Mtei kwani waliondolewa katika umaskini, na isitoshe walimshawishi mwanao afunge ndoa kabisa na mzee Mtei na bila kipingamizi chochote mama yake Jacksoni alikubali. Bensoni hakusita kulipigania penzi lake, alizunguka huku na kule bila mafanikio huku ndugu zake wakiuawa kikatili pale tu walipojaribu kulitetea penzi la kijana wao na msomi pekee katika ukoo wao …



“Upumzike kwa amani Mama na baba, kuanzia leo nitasoma kwa bidii na kumtunza Mwanangu huyu asiye na hatia. Nitahakikisha nakuwa daktari bingwa wa upasuaji na saikolojia ili taifa na dunia wanitambue, kuanzia leo mwanangu ataitwa Joanitha kama kumbukumbu ya mama yangu, “



Ni maneno ambayo Bensoni au dokta Benny aliyazungumza mbele ya makaburi mawili ya wazazi wake, mara baada ya kupigwa risasi nyingi na kufa kikatili bila msaada wowote pale tu walipofungua midomo yao kutetea haki za penzi la mtoto wao ambaye alinyanganywa mchumba na bilionea Mtei.Huo ndio ukawa mwanzo wa mafanikio ya Bensoni, alifuta kila kitu katika kichwa chake kuhusu mapenzi! huku mapenzi yake yote akihamishia kwa mwanae Joanitha aliyempatia jina la bibi yake, mama yake Bensoni au dokta Benny. Dokta Benny alizihamishia nguvu zote kwenye kusoma kwani msaada wake uliobakia ulikuwa ni elimu, na kujinyakulia shahada kedekede katika kitengo cha afya,huo ndiyo ukawa mwanzo wa utajiri wake…



…………………………………



“Weee mpuuzi! picha hizi za kipuuzi na kunichafua umezipiga lini, nani kakupiga? na tabia hizi za mapenzi ya jinsia moja umezianza lini? “,



“Hapaanaa baba, mimi ni mwanamke kama wanawake wengine? “,



“What? ni wewe kweliii? acha kunitusi nitaumwaga ubongo wako sasa hivi …”,



“Ndiyo baba! tena usithubutu kuyaingilia maisha yangu, Jonsoni nampenda usimfanye kitu chochote. Tena nakuomba popote pale utakaposikia jina Robert, naomba usimguse! “,



“Paaaaaaaaa! “,



“Jonsoniiii usifeee Jonsonii, nakupendaa! Dady you have killed my Jonsoni, I hate you dady, nakuchukiaa baba “,



“Mimi siyo baba yako tenaa!! ………Huyu mpuuzi maskini, ninaemulisha ndiyo amekuharibu. Nimemuua ili ujue ni kiasi gani sipendi kudharilishwaaa … ,Paul njoo utoe huu mzoga mahali hapa! kisha nendeni mkamtoroshe na kumteka huyo Robert aliyeshiriki kuniharibia mwanangu.! “,



Bila hata kutoa ukelele wowote ule, kichwa cha Jonsoni kilisambaratishwa kwa bastora pale tu Jacksoni alipojaribu kumtetea, bila kutambua kuwa alitumia njia mbaya kumtetea na kujikuta amemuangamiza kabisa. Alionesha msimamo wake, kwani aliamini alikuwa sahihi kwa yale aliyokuwa akiyafanya na kutaka hisia zake kuheshimiwa bila kujali kuwa alikuwa kinyume na maadili ya nchi yake. Jacksoni bila kutambua kuwa tayali alikuwa amechafuliwa, tena kwa kupigwa picha mbaya na mtu aliyempenda sana, alijikuta akimtahadharisha baba yake asithubutu kumdhuru kijana huyu aliyeitwa Robert pale tu atakapilisikia jina lake likitajwa na kujikuta akiharibu mambo zaidi na zaidi. Kwani ni muda mfupi tu ulikuwa umepita mzee Mtei alifahamishwa kuhusu kukamatwa kwa Robert, haraka haraka alitambua kuwa mtoto wake pamoja na kijana huyu aliyetambulika kwa jina la Robert walikuwa na mahusiano na ndiyo maana kijana huyu aliitumia nafasi hii kumpiga picha Jacksoni …



“Babaa usifanye hivyo! nitajiua, Robert akifa na mimi niue tu.Nampendaa”,



“Kama kufa ufe tu,kwani sioni umuhimu wako kwa sasa!”,



“Mbona binadamu hamna huruma,mimi sikujiumba bali Mungu ndiye aliniumba…,bora ningebaki Americaa na si kuja huku nchi ambayo haiheshimu haki za binadamu……”,



“Unasemaje we mjingaa?Americaa ulienda kusoma? au kujifunza kuwa mwanaharamu,nimepoteza pesa nyingi kukusomesha lakini pesa zangu zimeenda buree.Nina apa mbele yako,mimi ni mchaga na nimeaga uchagani!pesa zangu haziendi buree,lazima damu itazidi kumwagika……,Paul!nendaa kaniletee mpuuzi mwenzake,Rodgers tokeni hapa nikitoa amli sitaki uzembeee”,



“Sawa bosi……!”,



Mzee Mtei mara hii alikuwa mkali tena zaidi ya pilipili,alimuona mtoto wake kama shetani kwani alibadilika na kuwa tofauti kabisa na jinsi walivyomzoea.Hakutambua kuwa Jacksoni alibadilika siku nyingi tu,na tabia yake ilizidi kukua kwa kasi kutokana na kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wake.Siku zote wazazi wake walikuwa bize kwenye biashara zao,na kukosa hata sekunde tu ya kuzungumza na kijana wao kuhusu maadili …



…………………………………

Baada ya kutoka ofisini kwake, dokta Benny alikwenda moja kwa moja katika ofisi ya daktari wake msaidizi kwa lengo moja tu kumuachia majukumu ya kikazi. Hakuishia kuwa daktari mwenzie tu bali walikuwa ni marafiki walio shibana na isitoshe walifanya kazi katika kitengo kimoja cha upasuaji japo dokta Benny hakuishia tu kuhusika na upasuaji bali alikuwa na ujuzi mkubwa katika masuala ya saikolojia …



“Dokta Ashrafu kazi zimegoma, nina mawazo kibao kuhusu mwanangu ……”,



“Kuna nini bosi? vipi bado swala lile la jana kuhusu Joanitha linakuchanganya? “,



“Ndiyo, tena sasa hivi limefikia mbali na isitoshe hapa katikati kuna siri nzito niliificha …ngoja niende nyumbani nikapumzike harafu nitakufahamisha kila kitu mambo yakiwa sawa ……!”,



“Sawa bosi, kuhusu kazi usjali hakiharibiki kitu …”,



“Poa, kazi njemaa “,



Taratibu dokta Benny alitoka katika ofisi ya rafiki yake, kisha kuitafuta njia kuelekea sehemu ambapo kulikuwa na maegesho ya magari, maalumu kwa ajili ya wafanyakazi na wagonjwa wa hospitali hii kubwa ya kiserikali katika jiji la Gano …



Dokta Benny alitoweka eneo la hospitalini akiwa mwenye mawazo mengi sana, safari hii ilikua ni ya kurudi nyumbani kwake ili kujipumzisha na kuhakikisha anazungumza na binti yake Joanitha ili ajue ni namna gani ataweza kumsaidia. Japo alikuwa anatambua kila kitu, kwani dokta Imaculata alikuwa tayali ameshamueleza kila kitu kuhusu jambo ambalo pengine lilikuwa chanzo cha matatizo ya binti yake …



Tofauti na wakati akiwa hana mawazo, alitumia muda mrefu akiwa barabarani huku akikoswa na ajari mara kadhaa. Kuna wakati alimanusura amgonge mwendesha baiskeli, kutokana na fikra zake kuwa mbali lakini Mungu si Athumani dokta Benny aliwahi kufunga breki za gari na kuiepuka ajari hii …



Kumbukumbu za kila aina zilimsumbua ndani ya kichwa chake, na kumfanya akumbuke machungu ambayo alikuwa ameshayasahau. Maumivu yalirudi upya, huku nafsi ikimpinga kwa kile ambacho alikuwa anataka kukifanyaa …



“Lazima nimwambie ukweli Joanitha! nimechoka kuulizwa kuhusu mama yake, nimechoka!, tayali amekua! ni wakati wake kufahamu ukwelii ……”,



Baada ya kutumia muda wa kama lisaa limoja akiwa barabarani, ghafla alifunga breki mbele ya jengo lake la kifahari huku akizungumza peke yake kama mwenda wazimu …



Kitendo cha Jacksoni, punga maarufu jijini Gano kuandikwa katika magazeti na vyombo vingine vya habari kama mtoto wa mzee Mtei, na isitoshe alisoma na Joanitha shule moja kilimchanganya sana akili yake kwani moja kwa moja alitambua kuwa Joanitha na Jacksoni ni ndugu tena wa mama mmoja. Huku akiwa hafahamu ni kiasi gani mtoto wake atalichukulia jambo hilo pale tu atakapomweleza ukweli…



“Piii, pii! piiiiiiiiii ………”,



“Lakini kama ni mtoto wake, kwanini Jacksoni na Joanitha wana umri sawa? isije ikawa nahisi vibaya tu, pengine mzee Mtei alimzaa kijana huyu kabla hata hajafunga ndoa na mama Joanitha …anyway! nitafahamu mbele kwa mbele! “,



Daktari huyu mwenye pesa nyingi kwa sasa, mmoja kati ya matajiri wakubwa jijini Gano aliendelea kupiga honi huku akili yake ikizidi kufikilia na kujiuliza maswali mengi. Muda huo huo, geti kubwa lilifunguliwa kuliruhusu gali la kifahari la dokta Benny kuingia ndani kwa ajili ya maegesho…



“Heeee! hawajaenda shulee! jana wametoka mapema, leo hawajaenda kabisa mmmh hii hali sio ya kuendelea kuifumbia macho. Nisipokuwa makini, mwanangu ataharibikaaa ……!”,



Macho ya dokta Benny yalikutana uso kwa uso na macho ya binti yake Joanitha, kwani Joanitha ndiye aliyefungua geti hili. Hapo ndipo alipojaribu kuitazama saa yake ya mkononi, na kujikuta akizidi kuwa na wasiwasi mkubwa kwani alihisi Joanitha na Doreeni hawakwenda shule na isitoshe ilikua ndiyo saa saba mchana …



“Joanithaa! “,



“Abee baba, shikamoo? “,



“Marahaba, mbona mapema hivii?mwenzio Doreeni yuko wapii?”,



“Yuko ndani anafanya usafi.”,



“,Sawa,nakuomba kidogo nikute sebuleniii…”,



Wasiwasi ulimtawala Joanitha,siku zote hakupenda kumkwaza baba yake kwa kupuuzia masomo.Kichwa chake kilianza kutafuta majibu ya maswali atakayoulizwa haraka iwezekanavyo,huku swali la kwanini hawajaenda shule likiwa namba moja…



Kwa unyonge alimfuata baba yake aliyekua anaingia ndani mara tu alipomaliza kulipaki gari lake,baada ya kulifunga geti huku masikio yake yakisikiliza kwa makini kauli ambayo baba yake alikuwa anaizungumza.



………………………………

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Dokta wa kihindi alieyejulikana kwa jina Ranjibhai, alifika katika jengo la mzee Mtei. Hakutambua kama kuna mauaji yoyote ambayo yalikuwa tayali yameshafanyika, mazungumzo na bosi wake mzee Mtei yalianza huku wakiwa sebuleni mahali ambapo mama yake Jacksoni alikuwa amepumzika. Mzee Mtei alitoka stoo baada ya dokta Ranjibhai kuwasili, stoo ambayo alifanya mauaji ya Jonsoni huku mwanae Jacksoni akiwa amefungwa kwa kamba ngumu na isitoshe alishuhudia ukatili ambao Jonsoni alitendewa bila huruma.



“Mama Jacksoni hana tatizo lolote, sema presha yake ilipanda kutokana na mshituko. Inatakiwa apate muda wa kutosha kuipumzisha akili yake, na asipewe haraka taarifa za kumshitua ……”,



“,Sawa, vipi kuhusu tatizo la mwanangu Jacksoni …!”,



“,Mtoto wenu tatizo lake ni dogo sanaa, lakini sina uwezo wa kumtibu …”,



“,Tatizo lake litakuaje dogo halafu ushindwe kumtibu! mbona unachukulia mambo kirahisi rahisi hivyo ndugu yangu ……”,



“Ndiyo! haumwi, bali tu saikolojia yake imeaminishwa misimamo na fikra tofauti, pengine kwa kuiga au kushawishiwa na watu. “,



“Tatizoo unaongea sana, mimi au wewe hakuna mwanasiasa kati yetu! ,wewe nambie! mwanangu anapona au haponi? na matibabu yake nayapata wapi, hapa kwetu Gano ?India, Marekani au mwezini. Kokote mimi naenda, sina mtoto mwingine zaidi ya Jacksoni ……”,



Japo mzee Mtei alionekana kumkalipia mtoto wake Jacksoni, huku akimtisha kifo na pengine kumkana. Lakini ukweli ulibaki palepale, mzee Mtei hakua na mtoto mwingine zaidi ya Jacksoni ,hakuwa na budi kupambana mpaka hatua ya mwisho kuhakikisha mwanae anapona na kuwa mwanaume kamili …



“Hapa Gano kuna daktari bingwa wa upasuaji na saikolojia, ana elimu ya juu sana kunizidi hata mimi.Kutokana na elimu yake na uwezo mkubwa, serikali imemuajiri katika kitengo cha upasuaji katika hospitali ya jiji, kwahiyo hata ukitaka kuonana naye itabidi umuombe amtibu mwanao na sio kumpelekesha pelekesha tu.Kwa elimu yake aliyonayo haupaswi kumpelekesha, jishushe amuokoe mwanao bila hivyo Jacksoni tutampoteza kabisaa ……”,



“,Sawa dokta, nimekuelewa! hata sasa hivi twende, kwanza anaitwa nani?? “,



“,Tumesoma naye India, katika chuo kikuu cha Delhi. Ndiye Muafrika pekee kufuzu masomo ya Phd kwa kiwango cha juu kabisa katika chuo hiki tangu kianzishwe, anaitwa Bensoni Mapunda, yeye anapenda kujiita dokta Benny ……”,



“,Umesema anaitwa nani?? “,



Mzee Mtei na mke wake, walijikuta wakikumbwa na mshangao mara tu lilipotajwa jina la Bensoni Mapunda. Wote kwa pamoja walimfahamu vizuri mtu huyu, huku mara ya mwisho kukutana naye alikuwa mwaka wa pili akisomea shahada ya miaka mitano katika chuo kikuu cha Afya nchini Gano. Hakuna aliyeamini kama kijana huyu mdogo angefikia kiwango hiki, na kujikuta akiona aibu kwani moyo wake ulimsuta kwa mabaya aliyomtendea. Mzee Mtei aliwaua ndugu zake Bensoni Mapunda, wazazi wake na isitoshe akamnyanganya mpaka mke. Huku mama yake Jacksoni akikumbuka maamuzi yake ya kikatili aliyoyafanya na kumkataa Bensoni kwa umaskini wake mpaka kumkana mtoto waliyezaa naye pamojaa …



“Kamweee! hawezi kunisamehe, hata kama ni mimi nisingeweza. “,



“,Bosi kwani vipi?, “



“,Dokta, unayemsemea ni huyu huyu Bensoni Mapunda muha wa kule Kigoma……”,



“,Ndiyo ,ni huyo huyo mama yangu …”,



“,Tumekwishaa! ubaya wetu tuliofanya leo tumeumbuka, kweli dunia huzunguka. Usimdharau mtu yoyote aliyeumbwa na Mungu hata siku mojaa ……”,



Kabla hata mama yake Jacksoni hajamalizia kutoa maelezo mafupi kuhusu Bensoni aliyemfahamu, dokta Ranjibhai alimkatisha kauli yake kwani tayali alimtambua mtu aliyetaka kumsema. Kwani ndiye huyo huyo ambaye aliamini angewasaidia, huku wao wakijuta kwa yale waliyomfanyia huku ndoto za Jacksoni kupona zikitoweka katika vichwa vyao. Kwani adui yao ndiye msaada pekee kwao, lakini hawakutambua kama kweli adui yao angekubali kuwasaidia au laa! kwani tayali alipoteza ndugu na wazazi chanzo kikiwa ni nguvu ya pesa ya bwana Mtei …



Paul na Rodgers walikerwa sana na kitendo cha mtoto wa bosi wao kuzarilishwa, sifa mbaya ambazo zilimchafua kibiashara mpaka bosi wao mzee Mtei. Mmoja kati ya watuhumiwa ambaye ni Jonsoni, tayali alikuwa ameshauawa kikatili kwa kupigwa na risasi kichwani mwake. Huku mwili wake ukiwa umepakiwa kwenye kiroba kabla ya kwenda kutupwa nje ya mji …



“Hapa giza likiingia tutaingia kirahisi. Kimya kimya tutawabamiza askari wawili na kuvaa mavazi yao. Hapo dogo tuna mchukua kirahisi ……”,



“Hapo umenena, sasa hivi wanoko kibaoo! “,



“,Vipi umesahau pafyumu!! “,



“,Weeee!thubutu,hata siku moja siwezi kusahau siraha yangu muhimu tena kwenye misheni hatari kamaa hii.Kuiba mateka tena kituo cha polisi siyo rahisi rahisi kwa utawala huu,ukizubaa kitanzi kinahusu!”,



” ,Hahahaaaahaa”,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Makamanda wawili wa kutegemewa na mzee Mtei,walikuwa wameketi umbali wa mita kadhaa kutoka eneo la kituo cha polisi.Hawakusita kupiga stori mbili tatu huku wakionyesha meno yao kwa sauti ya juu ili kujiongezea siku za kuishi.Mada kuu waliyokuwa wakijadiriana mezani ni namna ya kuvamia kituo cha polisi na kuhakikisha wanaondoka na Robert,huku Rodgers akijiamini kwa siraha ya kupulizia,dawa kali ya usingizi ambayo ilimfanya mtu aliyeivuta kusinzia ndani ya takribani sekunde mbili mpaka tatu pale tu itakapoingia katika mfumo wake wa fahamu.Dawa ambayo wao waliifahamu kwa jina la pafyumu kutokana na kumvutia mnusaji tena na tena pale tu alipoinusa kwa mara ya kwanza na kujikuta akiambulia usingizi wa pono tena kukoroma haswaa!.Kwa upande wa askari polisi wao hawakujali shughuli zozote za wapita njia ambazo ziliendelea nje,wao waliendelea kutimiza majukumu yao kama kawaida bila kutambua kuwa kulikuwa na maadui walikuwa wanawanyemelea nje ya jengo lao…







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog