Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MWANAHARAMU - 5

  











    Simulizi : Mwanaharamu

    Sehemu Ya Tano (5)





    NDANI YA KITUO KIKUU CHA POLISI(GANO)

    Pilikapilika ndani ya kituo kikuu cha polisi hazikuisha,huyu alifanya hivi,yule akafanya vile.Hakuna ambaye alionekana kukaa bila kazi yoyote,isipokuwa maafisa wa polisi wenye vyeo vikubwa ndiyo walionekana kuzunguka kwenye viti vyao na kusubilia kuweka saini kwenye mafaili ya kesi mbalimbali…



    “Haloo mkuu!

    habari yako samahani,nimekuja kufuatilia kesi ya mwanangu……”,



    “,Baba tusaidie!mwanangu ameletwa hapa asubuhi,tumekuja kufuatilia kesi yake.Kafanya nini?”,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Timotheo pamoja na mke wake,walifika kituo cha polisi ili waweze kufahamu kuhusu kesi ya mtoto wao Robert.Bila kutegemea walikutana na dharau ya hali ya juu,kwani afisa huyu mwenye cheo cha “sergent” alizunguka tu kwenye kiti chake,huku akipuliza taratibu sigara yake ya kizungu maarufu kama Kiko.Kwa muda mrefu walikuwa hawajatambua chanzo cha dharau hizi ambazo walikuwa wanaonyeshwa,na kujikuta wakitambua kila kitu.Kwani afisa huyu alivua kofia yake na kuinyosha mbele yao mithili ya chombo cha sadaka,kwa kuwa walikuwa na shida na walitaka kumtoa mtoto wao kipenzi kwenye mateso.Baba yake Robert alijipapasa na kuchomoa elfu kumi,kisha aliiweka ndani ya kofia ile.Mama yake Robert hakuwa nyuma,hata yeye alitaka mwanae atoke mahabusu haraka iwezekanavyo.Alichomeka mkono wake katikati ya chuchu zake na kuibuka na noti mbili za elfu kumi kumi,kisha aliziweka ndani ya kofia ya afisa yule……



    “Haya eleza shida zenu! niwasaidie nini? “,



    Baada ya kupata kile alichokitaka, askari huyu alikaa vizuri ili kuzungumza na wazazi wa Robert. Mazungumzo yalianza haraka sana ,huku askari huyu akionesha uchangamfu na utayali wa hali ya juu kutoa msaada kwani tayali alipewa pesa ya vocha. Dunia haina haki, labda kwa wenye pesa tu! pata shida utaukumbuka msemo wangu ……



    “Mtoto wetu anaitwa Robert, amekamatwa nyumbani asubuhi tena na kipigo juuu?tunataka kujua amefanya nini?” ,



    “,Mtoto wenu ana kesi nzito! kampiga picha za utupu na kumchafua mtoto wa Mtei, “,



    “,Unasema? amemchafua mtoto wa Mtei …?”,



    “,Ndiyo, tena wanasema kamuingilia kinyume na maumbile japo wanasoma shule mojaaa ……”,



    “Mungu wangu! hata huyu Robert kwanini agombane na watoto wa wakubwa, si anatafuta kifo huyu, mama yake nitabaki na nani wakati ndiyo huyo huyo mtoto mmoja……”,



    Wazazi wa Robert alimanusura waanguke chini kwa presha walipolisikia jina la Mtei, japo watoto wao walisoma shule moja. Sio kwamba mzee Timotheo alikuwa na pesa nyingi kumsomesha Robert katika shule ya kitajiri, lahasha bali hawakuwa na watoto wengi. Walikuwa na uwezo wa kumtimizia alichokitaka kwani alikuwa ni mmoja tu tena wa kiume …



    “Msihuzunike sanaa! atatokaa, nitalisimamia mimi lakini naomba mnifikilieee …………”,



    “,Sawa mkuu! pesa utapata lakini timiza kwanza kazi yetu ……”,



    Baba yake Robert alimpatia mawasiliano kwa maandishi, kisha walinyanyuka wote kwa pamoja akiwa na mke wake tayali kwa ajili ya kurudi nyumbani. Kwani walikatazwa kuonana na mtoto wao mpaka pale atakapoachiwa huru au kupatiwa dhamana kutokana na kesi yake kuwa ngumu …



    …………………………………



    Baba yake Joanitha alifika na kuketi sebuleni, huku mtoto wake Joanitha akiketi na yeye sebuleni. Dokta Benny aliona ndiyo wakati pekee wa yeye kuzungumza na binti yake na ikiwezekana kumweleza kila kitu kuhusu siri ambayo aliificha muda mrefu, lakini kwa upande wa Joanitha alikuwa na wasiwasi sana kwani alifikiri baba yake alikasirishwa na kitendo cha wao kutokwenda shule kirahisi rahisi namna hii na isitoshe walikalibia kufanya mitihani ya taifa ya kidato cha sita …



    “Usiondoke! njoo ukae hapa ……”,



    “,Sawa baba, shikamoo! “,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ” ,Marahaba Doreeni hujambo? “,



    “,Sijambo! “,



    “,ok! Usiondoke, hata wewe mazungumzo yanakuhusu kama mwanafamilia, umesikia mwanangu. Kuwa huru hapa ni kama kwenu sawaa eee! “,



    “,Sawa baba! “,



    Doreeni akiwa sebuleni anafuta vumbi kwenye sofa alitaka kuwaachia uhuru Joanitha na baba yake wazungumze, na kujikuta hata yeye akikaribishwa kushiriki mazungumzo hayo. Huku wakiwa hawafahamu nini hasa dokta Benny alitaka kuzungumza, na kubaki wakijiuliza maswali mengi bila majibu yoyote …



    “,Joanitha! “,



    “,Abeee baba! “,



    “,Jacksoni ni nani kwako? “,



    Mapigo ya moyo ya Joanitha yalianza kupiga kwa kasi, kwani hakuamini alichokisikia na kubaki akimtazama tu baba yake kwani hakuwa na jibu la haraka haraka kumpatia na isitoshe hakulitegemea swali kama hilo. Siyo tu Joanitha ambaye alishangazwa na swali ambalo aliulizwa bali hata Doreeni hakuamini kile alichokisikia,



    “Nijibu, wala usiogope! kuwa huru, nipo kwa ajili ya kukusaidia binti yangu. Unapokosa furaha hata mimi nakosa furaha …”,



    “,Tunaasoma…a naye…e …”



    “,Ndiyo nafahamu, lakini kuna zaidi ya kusoma naye ……”,



    Hapo ndipo Joanitha alishindwa kuendelea kujibu, kwani majibu yalionesha baba yake alitambua kila kitu kumuhusu yeye na kubaki kusubili baba yake angesema nini …



    …………………………………



    “Kwahiyo dokta Ranjibhai unatushauri nini! maana msaada wetu kumponya mtoto wetu ni Bensoni na ndiyo hivyo sisi tumesha mkosea, je unatusaidiaje? “,



    Mzee Mtei alikuwa mpole,mwanzoni hakutambua pesa wakati mwingine hazina maana kama kuishi vizuri na watu. Kwani tayali alikuwa anaelekea kuumbuka, kwani aliamini itakua vigumu kwa asilimia mia moja kusamehewa na mtu huyu kwa makosa makubwa aliyo mtendea. Je vipi kuhusu Jacksoni?



    “Fanyeni kila njia, muonane naye na kuombana msamaha. Amesaidia wengi na hana shida yoyote, namfahamu vizuri mtu huyu na sikutambua kama mnafahamiana na kama mliwahi kukosana …!”,



    Hapo ndipo ukisikia, yenye mwanzo hayakosi mwisho. Leo hii mwisho wa ubaya na kutumia pesa kama kivuli cha kutenda maovu ulikua umefika, sio mzee Mtei wala mke wake. Wato walishika tama kama yatima, huku wakijutia kwa dhambi nyingi walizozifanya hasa kwa dokta Benny miaka mingi iliyopita …





    Dokta Ranjibhani hakuwa na sababu ya kuendelea kubakia katika nyumba ya bosi wake ,kwani tayali mama yake Jacksoni alikuwa ameshafanyiwa vipimo na kupatiwa dawa kadhaa za kumsaidia. Kwa upande wa Jacksoni, dokta Ranjibhai alimshauri mzee Mtei namna ya kumsaidia, ilibaki juu yao kujishusha mbele ya dokta Benny na kumuomba msamaha au kupuuzia ushauri wake …



    “Tatizo lolote likitokea, msisite kunijulisha. Mimi naondoka … ,bado nina majukumu mengine hospitalini na isitoshe giza limeshaanza kuingia …”,



    Bila hata kusubili jibu lake, pengine aweze kusindikizwa kama alivyozoea. Dokta Ranjibhai aliondoka kutokana na kutingwa na majukumu mengine na isitoshe tayali alikuwa ameshatoa msaada wa kutosha. Aliondoka huku mzee Mtei na mke wake wakiwa wameshika tamaa tu, na kukosa maamuzi ya kuchukua ili kumsaidia kijana wao Jacksoni…



    “Mimi nitajishusha, lakini!akijifanya kunijia juu sitaendelea kumnyenyekea,nitaachana naye!”,



    “,Lakiniii baba Jacks……”,



    “,Lakini nini?,hata kama tulimkosea anapaswa kutusaidia yeye kama daktari,hivyo basi! tutamuomba msamaha,akikataaa basii!pesa ipoo,tutasafiri hata mwezini kufuata matibabu ya Jacksoni……”,



    Jeuri ya pesa ilizidi kumtafuna mzee Mtei,aliamini pesa ndiyo kila kitu na hakuona sababu ya kujishusha kama tu akijaribu kufanya hivyo na asiweze kupatiwa kile alichohitaji……



    “,Sawa,ngoja tumpigiee,aje nyumbani!namba ndiyoo hii,………”,



    Mama yake Jacksoni ni muda mrefu alikuwa hajaonana na Bensoni,japo muda mwingine alijutia kwa yale alihoyafanya lakini alikosa nafasi hata ya kumuomba msamaha mwanaume huyu.Aliamini mwanae aliyemuacha ni mdogo tayali alikuwa mtu mzima,hivyo aliona ndiyo nafasi pekee ya yeye kuiona damu yake kwa mara nyingine.Kama ujuavyo damu ni nzito kuliko maji…



    Akiwa anaichunguza namba kwa makini ,namba aliyopatiwa na dokta Ranjibhai.Alizungumza na mume wake bila kujibiwa,huku nafsi mbili zikipingana katika nafsi yake.Moja ikimtaka apige simu,huku nyingine ikisita kwani alitakiwa kujipanga kabla ya kuongea na adui yake tena aliyemfanyia dhambi kubwa.Hakutambua kuwa Bensoni ni yule yule na hakubadirika chochote kile, zaidi ya kuwa na maisha mazuri kwa sasa tofauti na zamani. Lakini kuhusu hekima na upoleee ndo kabisaa, tena kwa sasa sifa zake hizi ziliongezeka na kuwa maradufu …



    …………………………………



    Dokta Benny aliketi kwa utulivu kwenye sofa, akiwa amekunja vizuri magazeti yake mkononi huku Joanitha na Doreeni wakiwa hawatambui chochote kile kuhusu magazeti haya, pengine yalikuwa yanahusu siasa kama sikuzote baba yake alivyozoea kujisomea taarifa mbalimbali kumbe sivyo!



    “Kwanza nitangulize samahani! japo sizani kama nimekukosea! “,



    “,Samahani kwa lipi?, mbona sikuelewi baba! “,



    “Utanielewa tu Joanitha!. Pili, naomba nikufahamishe kuwa mama yako yupo hai tena anaishi hapahapa Gano? “,



    “,Unasemaje? “,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “,Ndiyo! hebu tuliza jazbaa, kaa, tulia nikweleze ukweli. Naamini umekua mkubwa siwezi kuendelea kukuficha. “,



    “,Mama yako aliolewa na bilionea miaka mingi iliyopita, huku mimi nikiwa mwaka wa pili chuoni. Hakutaka kuvumilia umaskini wetu, isitoshe wazazi wake ambao ni bibi yako na babu yako walipatiwa pesa nyingi na kuwa mamilionea na kujikuta wakinichukia. Hawakutaka kunisikia tenaa, bali walihimiza mama yako aolewe na mwanaume aliyewapatia mapesa mengii ambaye ni bilionea Mtei ……!”,



    “Mtei! baba yake Jacksonii?? “,



    “,Ndiyo baba yake Jacksoni ,ndiyo maana mwanzoni nilikuuliza Jacksoni ni nani kwako! mwanzoni nilizani labda umepewa mimba, lakini Jacksoni hawezi fanya hivyoo! naamini siyo rijali kabisa……”,



    “,Baba! huyu huyu Jacksoni tunayesoma naye, baba yake mzazi ndiyo kamuoa mama yake Joanitha? “,



    “,Ndiyo Doreeni, mnachotakiwa kuniambia ni ukweliii tu! ili nijue namsaidiaje mwanangu, maana hawezi kumsaidia Jacksoni kirahisi hivyo jambo ambalo linapelekea afikilie kupita kiasi kuzidi uwezo wa ubongo wake! “,



    Baba yake Joanitha, dokta Benny. Alizungumza huku binti yake machozi yakianza kumchuruzika mashavuni mwake, kwani dhambi ambayo baba yake alifanyiwa na kusalitiwa ilimchoma kupita kiasi. Siku zote baba yake alihangaika kumlea na kumsomesha, bila msaada na malezi ya mama wakati mama yake alikuwa karibu kabisa japo alifikiri pengine alishafariki kumbe sivyo ……



    “,Mama mbona unanifanyia hivi! I hate you mama! nakuchukiaa ……”,



    “Usimchukie mama yako, nimekwambia siri hii ili kumsaidia Jacksoni na pia kukusaidia wewe umfahamu mama yako …!sasa nambie usinifiche, Jacksoni ni nani yako? “,



    “,Baba nampenda sana Jacksoni lakini sijawahi kumwambia, lakini nilipogundua matatizo yake. Kuonesha upendo wangu, roho ikanishawishi nianze jitihada za kumsaidia lakini tunasoma naye darasa moja! pengine hata hatusalimiani, kwani hatuna mazoea yoyote yale! na mara nyingi ananikwepa, kwani alishatambua nampenda, wakati yeye anaamini mimi na yeye ni sawa. Wote ni wasichanaa! pliz dady! nakuomba tumsaidie Jacksoni, kwa sasa hawezi kuwa mwanaume wangu tena lakini tayali ni ndugu yangu. Mama yake ni mama yanguu …”,



    “,Hongera kwa ujasili binti yangu !Hayo ndiyo maneno ambayo nilitaka kuyasikia, jikazee usiliee ……”,



    “,Najua baba! but inaumaaa, mama yangu hawezi kunitelekeza kiasi hiki! na isitoshe akaachana na wewe, inaonesha ni kiasi gani ana tamaa! naumiaa ……”,



    “,Ndiiiii ……!!……ndiiii, ndiiii…!”,



    Ghafla mlio wa simu ulisikika, kipindi dokta Benny akiyakunja kunja magazeti yake na kuyaweka kwenye kapu la taka sebuleni. Kwani tayali alifahamu kila kitu kuhusu Jacksoni, hivyo basi! hakuwa na sababu ya kumuonesha binti yake magazeti yale, kwani angezidi kumchoma kutokana na taarifa mbaya zilizoandikwa kumuhusu Jacksoni. Bila kupoteza muda alipokea simu yake, na kuisogeza katika sikio lake la kushoto …



    “Haloo! Habarii! nani mwenzangu? ” ,



    “,Mke wake Mtei, mama yake Jacksoni! na isitoshe ni mama yake mwanao, kabla ya yote natanguliza samahani. Ni miaka mingi imepita, sijaweza kukutana na wewe, naomba kukutana na wewe tuzungumze! ” ,



    ” ,Heeeeee! namba yangu umeipata wapi? na nikutane na wewe tuzungumze nini? unataka kuniua?, mume wako anataka kuniua? sina muda huo, “



    ” ,Hapana! usiseme hivyoo, tunamatatizo makubwa sana na msaada ni wewe,mimi na mume wangu tunataka kuonana na wewe ili tuzungumze. Njoo nyumbani, ikiwezekana na mtoto tuliyezaa wote …”,



    Mama yake Jacksoni alikata simu huku akiwa anaanza kulia, kwani majibu aliyopatiwa na dokta Benny yalimchoma na kumuumiza kupita kiasi. Alijuta kwa mambo aliyoyafanya miaka mingi iliyopita, lakini hakua na jinsi tayali ilikuwa imeshatokea. Mume wake mzee Mtei, alimsogelea na kumkumbatia ili kumfariji kwani wote kwa pamoja walisikia majibu ambayo dokta Benny aliyazungumza …



    “,Sizani kama atakujaa! Jacksoni haponi tenaa! “,



    “,Tumuombee Mungu, anaweza kubadilisha msimamo wake na kutii ombi letu ……”,



    ” ,Hawezi !hawezi kujaaa, bado anakinyongo kwani maneno yake yanazungumza. Lakini yotee ni wewe chanzo, leo hii sijui mwanangu anaumri gani kisa tu tamaa! “,



    “,Aaaah! unafika mbalii, utanikwazaaa! punguza jazba mke wangu, yote haya ni mapenzii. Nisamehee imeshatokea! “,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mzee Mtei na mke wake waliendelea kuzungumza, huku mama yake Jacksoni akilia na kutoa machozi kama mtoto mdogo. Hawakuwa na sababu ya kuendelea kulaumiana zaidi ya kumwachia Mungu …



    …………………………………



    Baada ya simu kukatwa, dokta Benny alijilaumu kwa hasira na maneno aliyo yazungumza. Kwani hakutaka Joanitha atambue kwamba alimchukia mama yake, ili iwe rahisi yeye kumshawishi ampende mama yake kwani pengine hakustahili kutengwa na mtoto kwani hakumzaa peke yake. Wote walikuwa na haki ya kufaidi matunda ya mtoto wao …



    “,Baba! giza limeingia,kwa sasa haiwezekani. Lakini kesho nenda ukawasikilize, ninamini kuna jambo la muhimu wamekuitia …”,



    “,Haina jinsi! Mungu ndiye anapaswa kuhukumu, basi tu hasira zilinikumba! kesho asubuhi tutaendaa wote, na vifaa vya matibabu kabisa ya Jacksonii……” ,



    “,Nitafurahi sanaa! lakini kwani kuna vipimo vya kumfanyia Jacksoni? “,



    “,Ndiyo, tenaa sanaa! inapaswa apimwe virusi vya ukimwi ,kwani kajihusisha na mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo ni hatari sanaa …” ,



    Joanitha alitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na baba yake, huku akijifuta machozi yake kwani tayali moyo wake ulikuwa na amani …



    ……………………………………………………………………………………



    Giza tayali lilikuwa limeshaingia, kama ambavyo lilikuwa linasubiliwa kwa hamu na Paul pamoja na Rodgers. Kwa muda wote ambao walikuwa eneo la polisi, eneo ambalo lilipakana na maduka na vibanda vya mama ntilie.Vijiwe hivi Viliwawezesha kukamilisha upelelezi wao na mipango yote kama walivyohitaji …



    “Pita huku na mimi nizungukie kwa kulee …,yoyote yule utakaye kutana naye ni halali yako …”,



    Kama ujuavyo mjini, hakuna anayekufuatilia. Kila mmoja anajali maisha yake, jambo ambalo linarahisisha maisha ya mjini kwa ujumla. Jambo hili la kuishi bila kufuatiliana, lilichangia kwa kiasi kikubwa Paul na Rodgers kuikamilisha misheni yao. Kwani tangu mchana walipofika eneo la mama ntilie, hakuna aliyewauliza hata jina lao. Mpaka mama ntilie alipofungasha mizigo yake mida ya jioni, bila kutambua hata majina yao. Alipuuzia kila alipowashuhudia vijana hawa kuwa bize kukichunguza kituo cha polisi kilichokua jirani, na kujutia kwa kupuuzia yale aliyo yaona kwani siku iliyofuata mambo ya ajabu yalitendeka katika kituo hiki cha polisi na kulichafua taifa kwa ujumlaa …



    Baada ya giza kuwa nene, Rodgers na mwenzie walinyanyuka kwenye banda la mama ntilie walipokuwa wameweka kambi kisha kugawana majukumu tayali kwa ajili ya kuianza misheni yao …



    Kwa mwendo wa serekasi waliruka ukuta na kutumbukia ndani, kama bahati tu askari nje ya kituo walikuwa wawili tu.Taratibu walinyata,huku wakiwasogelea askari hawa ambao walikuwa wameshika siraha zao kizembee …



    “Aaaa…aa…ah …” ,



    Askari hawa walijalibu kupiga kelele lakini ilishindikana, na kujikuta wakipoteza uhai bila kutegemea. Kwani walipigwa roba za nguvu, tena ghaflaa bila kujiandaa na kufa kifo cha kikatili bila huruma. Kwani Rodgers na Paul hawakuwa na masihara katika kazi hata siku moja …



    “Boy! badilisha nguo fastaa, tuna dakika tano tu kuikamilisha misheni yetu “,



    “,Poa bosii !wapulizie pafyumu tuzamee ndanii …”,



    Rodgers alikifinya kipafyumu chake, usawa ambao upepo ulielekea na kuingia ndani kabisa ya kituo. Dawa ya usingizi, ambayo ilikua ndani ya kichupa cha kupuliza mithili ya pafyumu.Ilipulizwa na upepo na kusafiri kwa kasi ya ajabu kuingia ndani ya jengo …



    “,Hee! Kwishaa ujanjaa wao, “



    Paul na Rodgers walichungulia ndani ya kituo cha polisi na kushuhudia askari wote wakiwa wamesinzia ghafla tu tena kwa mapozi tofauti. Walitabasamu kwa furaha kwani waliamini dawa yao ya usingizi ilikuwa imefanya kazi yake ipasavyo …



    Haraka sana walielekea ndani ya kituo huku wakijiamini kupita kiasi, bila kutambua kuwa walikuwa mtegoni kushambuliwa …



    …………………………………



    Robert akiwa mahabusu machale yalimcheza, na kumfanya awe makini zaidi. Kwani hakuwahi kudanganywa na machale yake hata siku moja !siku zote machale yake yaliashiria hatari tu na wala sio kitu kingine …



    Hali hii ilipelekea ajisogeze karibu na nondo za mlango wa mahabusu, ili ashuhudie ni kitu gani hasa kilichomkosesha raha .Huku wafungwa wenzake wakimtukana na kumpatia matusi ya kila aina …



    “,Mtoto wa mama! amekumbuka nyumbani, wakati ndiyo kwanza mahabusu siku ya kwanza!! Gerezani utaishi kwelii wewe !”,



    “,Nenda huko mseng* wewe! Sasa hivi unanidharau kakini kesho utanikumbuka …”,



    Robert aliendelea kushika nondo za mahabusu, huku akiwa bize kuangalia nje ya jengo la polisi. Kwani akiwa gerezani hasa karibu na mlango, alikuwa na uwezo wa kushuhudia chochote kile kilichoendelea nje kama wapita njia hasa wakati wa mchana …



    Mara tu baada ya kumaliza kumjibu mfungwa mwenzake aliyemkejeli, ghafla alishuhudia walinzi wawili wakinyakuliwa na kisha kuvutwa gizani. Hakuamini alichokiona, lakini katika hali ya kuwa makini kuangaza nje atambue kama watu hao walikuwa wema au laa! alibahatika kushuhudia vivuli kadhaa, vikipuliza kitu bila shaka ilikuwa sumu jambo ambalo lilimfanya afumbe pua zake kujilinda na sumu hii iliyopulizwa na watu wasiojulikana …



    ,kama ambavyo hisia zake zilivyohisi! askari mmoja mmoja kituoni alianza kudondoka chini taratibu, huku harufu nzuri ikienea kituoni. Kila aliyevuta harufu hii, alijikuta akindoka chini hali ambayo ilimfanya Robert kuchukua maamuzi ya haraka na kuzidi kuziba mapua yake ili kujilinda na sumu ile…



    “,Mungu wangu!bado unanipenda…”,



    Robert alizungumza,kwani askari mmoja aliyehusika kuwalinda huku muda wote akihakikisha usalama wa mahabusu.Alijikuta akidondoka karibu na mlango,mahali alipokua Robert.Haraka sana alipenyeza mkono wake na kuzichomoa funguo za selo.Hakuishia kuchomoa funguo tu,bali alilifungua kabisa na kutokomea huku mahabusu wengine wakiwa tayali wamelala fofofo…



    Kijana huyu wa uswazi,mtoto wa mjini alisita kukimbia moja kwa moja nje ya kituo.Ilibidi ajibanze kwenye mlango wa kuingilia kituoni ili azisome hisia za maadui zake.Kwani angeenda kichwa kichwa alikuwa anauawa badala ya kujisaidia…



    …………………………………



    Rodgers na Paul wakiwa wamevaa mavazi ya kuzuia sumu hii mapuani,waliingia kituoni bila kutambua kuwa mtuhumiwa wao ambaye ni Robert alikuwa amejificha nyuma ya mlango.Kwa upande wa Robert mapigo yake ya moyo yalienda kasi sana,kwani maadui walikuwa na miili mikubwa hivyo basi ilikuwa ngumu kupambana nao.Isitoshe walionekana kumtafuta Robert ili waondoke naye.Hakuwa na njia nyingine ya kujiokoa,zaidi ya kutimua mbio ili kujikomboaa…



    “,Paaaaah!paaaah…!”,



    “,Aaaaah!Naaakufa…a…aa”,



    Mlio wa bastora ulisikika,kwani risasi mbili zilifyatuliwa na kutoa uhai wa Robert.Pale tu alipojaribu kukimbia,kwakuwa walimpania kwa muda mrefu na isitoshe hawakuwa tayali kulaumiwa.Waligeuka kwa kasi ya ajabu mara tu waliposikia vishindo vya miguu,na kumpiga risasi mbili Robert.Moja tumboni nyingine kifuani.Kutokana na kupigwa na risasi sehemu mbayaa,ndani ya sekunde tu Robert aliiaga dunia na ndiyo ukawa mwisho wake…



    …………………………………



    ASUBUHI SIKU ILIYOFUATA ;

    Mzee Mtei alifurahishwa na taarifa aliyoipokea kutoka kwa vijana wake, na moyo wake ukawa na amani kwani watuhumiwa wakuu waliohusika kuchamfua mwanae walikuwa tayali wamepokea hukumu yao!



    “Kilichobakia ni kumtibu Mwanangu! nendeni mumlete sebuleni lakini asifunguliwe kamba, muacheni hivyoo hivyoo …!”,



    “,Sawa bosi! !,”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vijana wa kazi wa mzee Mtei, walielekea stoo. Rodgers alimchukua Jacksoni na kumpeleka sebuleni, akiwa amefungwa kamba. Huku Robert akiuchukua mzoga wa Jonsoni ambao ulipakiwa kwenye kiroba, kisha aliupeleka kwenye buti la gari tayali kwa ajili ya kwenda kutupa maiti yake …



    Haya yote yalifanyika, mara baada ya kupokea taarifa kuwa, familia ya dokta Benny ilikuwa njiani kuja kwa mzee Mtei kwa ajili ya mazungumzo pamoja na matibabu ya Jacksoni…



    …………………………………



    Hakuna ambaye alikuwa hapafahamu kwa mzee Mtei katika jiji hili la gano, kwa mwendo takribani wa nusu saa njiani. Gari zuri aina ya BMW lilipaki nje ya geti, na kupiga honi kadhaa ili liweze kufunguliwa …



    Mlinzi aliyekua amevalia sare kama za polisi, alilifungua geti ambalo lilifunguliwa kwa limoti. Na kumruhusu dokta Benny kuliingiza gari lake ndani ya jumba hili la kifahari. Kweli aliamini pesa ndiyo kila kitu, kwani jumba hili lilikuwa na ukuta mrefu pamoja na mifumo mingi ya ulinzi jambo ambalo ilikuwa ni vigumu kwa mwizi kupenya na kutaka kuiba …



    Kwakuwa alikuwa na majukumu mengi, alilipaki gari lake ili akamilishe kazi mapema na kuendelea na mambo mengine. Huku Joanitha na Doreeni wakifungua milango ya gari ili kutoka …

    …………………………………

    DAKIKA KUMI BAADAE :

    “Huyu ndiyo mtoto wetu anaitwa Joanitha, huyu ni rafiki yake! ” ,



    “,Joanitha, mimi ni mzee Mtei na huyu ni mke wangu ambaye pia ni mama yako mzazi. Bila shaka umeshaelezwa kila kitu, sina budi kurudia. Tunaomba tusameheane kwa yote yaliyotokea ……”,



    “,Joanitha ni dada yangu,? “,



    “,Ndiyo Jacksoni, ni stori ndefu lakini ngoja utibiwe mambo yatakua sawa .”,



    “,Mwananguu, “



    “,Mamamaa ” ,



    “,Nisamehe Joanithaa, nisamehee mwananguu ……” ,



    “,Nimekusamehee mama …”,



    Kila mmoja aliguswa na tukio hili la familia hizi mbili kuweka pembeni tofauti zao, wengi walitokwa na machozi ya furaha. Huku dokta Benny akiwa bize kuchukua vipimo vya damu vya Jacksoni palepale sebulenii, waliiamini afya yake ndiyo maana walifanya vipimo bila uficho.Kwa upande wa Jacksoni alikuwa kimya tu, huku akiona kama maigizo yakifanyika nyumbani kwao bila kufahamu jambo lolote lile…



    …………………………………

    BAADA YA SAA MOJA;

    “,HIV positive? heee! Jacksoni ameathirikaa! “,



    “,Nini au umekosea kupimaa? “,



    “,Haya ni majibu ya pili, yote yametoa the same results …”,



    “,Mwananguu Jacksoniii, umefanyaa niniiii. Mwananguuu umefanyaa nini …”,



    Furaha zilitoweka ghafla,dokta Benny alifanya vipimo mara mbili mbili na majibu yalitoka ni yaleyale.Katika vipimo ya Jacksoni,hatua ya kwanza kumtibu matatizo yake.Uvumilivu ulimshinda na kujikuta akiropoka,na kushindwa kutunza siri ya mgonjwa wake kama moja ya kiapo cha daktari…



    “Puuuuu!”,



    “,Babaaaaa!”,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Jacksoni alimkimbilia baba yake aliyeanguka ghafla kutokana na mshituko kuhusu afya ya mwanae,japo hakuwa na matatizo yoyote yale kwani mama yake ndiye alisumbuliwa na matatizo ya presha lakini Mungu si Athumani presha haikupanda kama awali.Jacksoni alijaribu kuyafumbua macho ya baba yake wapiii,alipojaribu kumpiga piga aamke wapii.Tayali roho yake iliaga mwilii…



    “,Unatangaziwa kutoka televisheni ya taifa ya Gano,mtuhumiwa wa kumdharilisha mtoto wa bilionea Mtei anayejulikana kwa jina la Robert.Ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi katika kituo cha polisi,huku wauaji wakiwa hawajajulikana nikiripo……” ,



    “,bab…a…aa, umemu…u”,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla Jacksoni hajamalizia sentesi yake ya kumlaumu baba yake ambaye tayali alikuwa ameshafariki,sauti yake iligoma kutokana na mshituko wa taarifa ya habari iliyotangazwa katika tv yao ambayo ilikuwa imewashwa muda wotee.Jacksoni alidondoka katika kifua cha baba yake na kufa palepale,kwani kipenzi cha moyo wake Robert aliuawa tena kikatili na muhusika mkuu akiwa mzee Mtei……



    “,Kumbe Robert ndiye alihusikaa?”,Joanitha alizungumza na kujishika tama huku akishuhudia vifo vya ghafla mbele ya macho yake,tangu azaliwe.Tofauti na dokta Benny ambaye alikuwa ameshazoea, ilibidi afanye kazi ya ziada kumnyamanzisha mama yake Jacksoni na Joanitha, mke wake mzee Mtei aliyepoteza watu wawili kwa mpigo …



    ……MWISHO WA UBAYA NI UBAYA …

0 comments:

Post a Comment

Blog