Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

NITAKUPATA TU - 1

 






IMEANDIKWA NA : IBRAHIM MASIMBA



*********************************************************************************



Simulizi :Nitakupata Tu

Sehemu Ya Kwanza (1)



*********

Alihisi ilikuwa sauti ya mwanamke, sauti ambayo mwanzo alidhani haikuwa ya mwanamke kutoka na usiku ule kuwa vigumu. Lakini sauti ile bado ilikuwa ikisikika katika ngoma za masikio yake. Sauti ya mwanamke akilia na kuomba msaada, sauti ikipiga kelele za hali ya juu kuonyesha kwanba kunakitendo kiovu kinatendeka. Bado hakuijali sauti ile, alichukulia kwamba labda atakuwa ni malaya amekula pesa za watu sasa analazimishwa kulipa. Bado akapuuza akitembea kuelekea nyumbani kwake. Licha ya kupuuza lakini safari hii, sauti ikasikika tena kwa karibu. Sauti ambayo ilipita masikioni na kwenda kuweka kituo ndani ya kina cha moyo wake. Sauti nayo ikazidi kuhanikiza, lakini safari hii kwa aina ambayo ili msisimua. Aina ambayo ilifanya kengele za hatari kugonga kichwani. Binti anayefukuzwa kulitaja jina lake usiku ule kulimpa mashaka makubwa. Kwa mara ya kwanza mkono wake ukashuka mpaka alipoihifadhi bastola yake. Kitendo cha kuitwa jina katika mazingira yale kulimpa hisia kuwa kulikuwa na namna, namna ambayo ilitengenezwa kwa aina fulani ya kutaka kitu kutoka kwake. Wamejuaje niko hapa? Walijuaje nitapita njia hii tena katika muda huu? Yalikuwa maswali yaliokisumbua kichwa chake, yalikuwa maswali yaliomfanya aziamini hisia zake, hisia ambazo hazikuwahi kumuangusha. Sasa akatembea kwa umakini mkono ukiwa juu ya Bastola. Hakujali tena kelele za mwanadada yule. Licha ya kutokuwa na ulahai wowote katika sauti yake, lakini hakutaka kuliamini hilo, akaendelea kutembea.. lakini hakufika popote akausikia mlio wa bastola, mlio ambao uliambatana na yowe, yowe kutoka kwa mwanadada yule. Kwa mara ya kwanza akageuka nyuma, akageuka kukiangalia kilichotokea nyuma.. naam akamuona mwanadada amelala chini tena barabarani. Hakuonekana kama alikuwa hai. Mbele kidogo ya ulipoangukia mwili wa binti yule, aliwaona wanaume wawili waliovalia makoti meusi wamesimama. Walikuwa wanaume hasa kwa kuwaangalia. Hakutaka kuupoteza muda, hakutaka kuupoteza muda kuwepo eneo lile. Akatokomea akiwaacha wanaume wale wamesimama wakimuangalia. Alitembea akijiuliza maswali mengi sana. Kama lengo lilikuwa ni yeye kwa nini wamemuua yule msichana? Walitaka nishuhudie kitu gani na kwa madhumuni yapi? Haiwezekani watoke huko kisha waje wamuulie mtu mbele yangu harafu mimi wasinifanye kitu, kuna zaidi ya hili. Alijisemea peke yake akiufungua mlango wa nyumba yake, akaingia ndani moja kwa moja akaenda kujibweteka kwenye kiti. Sauti ya mwanamke yule bado ilikuwa ikijirudia kichwani mwake, bado aliisikia bado masikioni mwake. Akajaribu kuivuta kumbukumbu ya sauti ile kuona kama angeugundua ulahai katika sauti ya mwanamke yule, lakini hakukuwa na kitu chochote kilichoashiria kwamba mwanamke yule alikuwa akimrahai. Ilikuwa sauti iliokatika ukweli, haikuwa na hata shaka ndani yake. Lakini sasa kwa nini mazingira yake yalikuwa ya kutilia mashaka? Hilo likamfanya ainuke na kuelekea bafuni ambapo alijimwagia maji kisha akarudi chumbani kwake. Akachagua mavazi ya kimichezo akavaa na baada ya hapo akachukua bastola yake na kutoka pale kuelekea kule alipoangukia yule mwanamke. Muda wote aliutamani ukweli wa jambo lile. Haikuwahi kutokea mtu kuuawa mbele ya macho yake. Hii ilikuwa mara ya kwanza na ilimtia mashaka sana. Alitaka kwenda kumuona marehemu, alitaka kumuona kwa kuwa aliamini angekipata kile ambacho kingemsaidia katika kumfahamu marehemu. Akaurusisha mlango kisha akalifunga geti kwa ndani kisha yeye akauparamia ukuta na kuangukia upande wa nje. Hii ndio ilikuwa njia yake awapo katika shughuli ambayo alihisi ilikuwa na hatari mbele yake. Alipotua akachepuka na kutafuta njia mbadala tofauti na ile alioipita mwanzo. Alitembea usiku sambamba na vivuli vya miti, hata alipotokea sehemu ile bado palikuwa kimya na hata mwili wa mwanamke yule bado ulikuwepo ukionyesha kutokuwa na uhai. Macho yake yaliozoea giza yalikuwa yakizunguka maeneo yote, bado hakuiona dalili ya uwepo wa mtu katika eneo lile. Hakuiona dalili ya kufuatiliwa wala kuwekewa mtego. Mkono wake ulikuwa juu ya bastola akipiga hatua kuufuata mwili uliolala chini bila uhai. Damu ilikuwa imeunda dimbwi kubwa. Akaufikia mwili ule na kuanza kuuangalia kwa makini.



Kwa kuwa hakutaka kuupoteza ushahidi, alichokifanya ni kutoa gloves na kuzivaa mikononi. Akaushika mwili wa binti yule na kuugeuza. Cha kwanza kukiona ni matundu matatu ya Risasi kifuani. Lakini kilichomchanganya katika matundu yale ni jinsi matundu yale yalivyo. Mpigaji alionekana kusimama kwa mbele na sio nyuma kama alivyokuwa akidhani. Hilo likampa picha, picha ya kuwa yeye ndie alikuwa mlengwa. Alikuwa mlengwa kutokana na ukweli kwamba marehemu alionekana hakuwa akikimbia. Bali alikuwa ameshikwa na alikuwa akilazimishwa kukifanya kitu. Alikuwa akilazimishwa kumuita yeye. Hapo akapata picha nzima kuwa alikuwa akihitajika yeye na sio huyu msichana. Alichokifanya nikuupekua ule mwili, hapo akakutana na vitamburisho vitatu, pamoja na kadi moja kubwa ambayo hii iliikuta kwenye Mkoba, pamoja na Simu yake ya mkononi. Akavichukua vyote na kuvisunda mifukoni. Baada ya hapo akapata wasaa wa kuiangalia sura ya mwanadada huyu. Hapo akakutana na sura nzuri na yakuvutia.



"Watu wanaroho ngumu, ya nini kumuua mtoto mzuri kama huyu? Alinong'ona huku akiinuka tayari kwa kurudi kwake.



***********



Chumba chote kilikuwa kimya, kila mmoja alikuwa ametulia akitizama mbele kuliko na Tv kubwa. Walikuwa wakiangalia taarifa ya habari kutoka shirika la utangazaji nchini. Kila mmoja alikuwa akitarajia kutangazwa kwa habari fulani ambazo zingewafurahisha. Kila mmoja ndani ya chumba kile alikuwa akiisubiri taarifa hiyo kwa hamu. Alikuwa akisubiri kile ambacho kingewafanya wao wawe katika kiwango cha juu katika biashara zao. Lakini ilikuwa kinyume wa kile walichokitarajia. Taarifa ambayo walikuwa wakiisubiri kwa hamu haikuja kama vile walivyotarajia. Bali vijana wao wanne walikuwa wamekamatwa wakiwa na mzigo wa madawa ya kulevya. Walikamatwa na maafisa wa usalama uwanjani hapo. Kila mmoja akapagawa, kila mmoja akahisi labda yupo ndotoni. Mzigo wao wenye thamani ya bilioni ishirini na mbili za kitanzania ulikuwa umekamatwa. Wakawaona vijana wao wakisukumwa kuelekea katika chumba maalum kwa ajili ya mahojiano zaidi. Chumba kikazizima kwa taharuki. Mmoja akaiendea simu yake na kupiga namba fulani. Muda mfupi simu ya upande wa pili ilikuwa ikiita. Iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata aliporudia bado hali ilikuwa pale pale.. hilo likawafanya watu wale watizamane.



"Haiwezekani!! Mmoja akanguruma.



"Kuna mchezo, huyu mwingine aliongea huku akishindwa kuuhimili presha.



"Jimmy hawezi kutufanyia hivi!!!" Mwingine akaongeza.



Lakini bado haikuondoa ukweli kwamba Mzigo wao ulikuwa umekamatwa na kulikuwa na uwezekano hata wao wenyewe wakatajwa. Bado simu haikupokelewa, bado iliendelea kuita kwa muda mrefu. Wajumbe wote wakazidi kushangazwa na hali ile. Lakini kabla hawajakaa sawa wakaisikia simu ikiita. Safari hii ilikuwa ikipigwa.



"Jimmy!!" Aliita.



"Jackson!!" Naye akaita..



"Atafutwe Teddy Harryson!!" Aliongea Jimmy kisha bila kusubiri maelezo yoyote akakata simu. Wajumbe wote wakaangaliana, hakuna alieamini maneno ya Jimmy. Kila mmoja alikuwa akiwaza mzigo wao uliokamatwa. Kitendo cha kuambiwa wamtafute Teddy Harryson bila kupewa maelezo yoyote kuliwakera baadhi ya wajumbe. Lakini wakiwa bado kwenye Mshangao wa kutokumuelewa Jimmy, simu ikatoa mliokuonyesha kuna ujumbe umeingia.



"Mpigie Teddy Mwambie akailete Roho ya Binti mmoja ambaye alikuwa chanzo cha kukamatwa kwa mzigo wetu. Nataka nikikupigia simu kwa mara nyingine unipe taarifa ya Roho Ya huyo Binti kuwasili hapo." Ulisomeka Ujumbe Ule.



ITAENDELEA

[18:28, 18/02/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU



SEHEMU YA 002



Mwandishi Ibrahim Masimba

*******



Ilihitajika Roho ya Binti aliesababisha kukamatwa kwa mzigo wao. Mzigo ambao ulikuwa wa mamilioni ya shilingi. Ilikuwa ni lazima wampigie simu Teddy kwa kuifanya kazi ya kuileta roho ya mwanamke huyo. Ilikuwa ni amri kutoka Kwa Jimmy, amri ambayo ilitakuwa kutekelezwa katika usiku ule. Hilo likafanyika na Roho ya mwanamke alietakiwa ikaletwa sehemu husika. Licha ya kumuua mwanamke yule lakini bado hawakuridhika kwa hilo kutokana na kutokuupata mzigo wao. Wajumbe wote waliokuwepo ndani ya Chumba, wakaufanya mkutano wa kujadili kipi cha kuufanya ili kuupata mzigo wao. Ni ndani ya mkutano huo likapitishwa Jina la Masimba. Alitakiwa kutafutwa kwa lazima, alitakiwa kutafutwa ndani ya muda ule. Kutafutwa kwa kazi maalum. Kazi ya kujua nani alikuwa nyuma ya ukamatwaji wa Mzigo wao wa madawa. Hawakuamini kuwa mwanamke yule pekee anaweza kuwa chanzo cha kupotea kwa mzigo wao. Walitambua kuna mchezo mchafu, mchezo ambao ulikuwa ukichezwa nyuma ya pazia. Muda mfupi kijana mmoja alitoa simu yake na kutafuta namba, alipoipata akabonyeza batani ya kijani, muda wa sekunde tano simu ikaanza kuita.



"Dogo!" Ilisikika sauti upande wa pili.



"Yeah Mkuu!!" Alijibu kijana Yule.



"Kuna nyekundu au kijani?" Lilikuwa swali kutoka kwa masimba. Alitambua simu nyingi za usiku kutoka kwa kijana huyo hazikuwa za usalama hata kidogo.



"Nyekundu Mkuu, kuna kitu tunahitaji ukifanyie kitu, lakini hatuwezi kuongea kwenye simu. Tukutane coco beach muda huu kama muda upo." Akajibu dogo.



"Nitakuwa hapo muda mfupi, mtanikuta pale kwenye mishkaki." Akajibu Masimba huku akikata simu. Hakutaka kupoteza muda, alichofanya ni kumuamsha Mpenzi wake, akamuaga kuwa anakwenda coco beach na asingechelewa kurudi. Akaruhusiwa huku akiombwa kutozidisha masaa mawili. Alitoka nyumbani kwake kinondoni manyanya, akaelekea kituo cha pikipiki, hapo akamueleza dereva wapi anaelekea. Muda mfupi alikuwa juu ya pikipiki akielekea coco beach kuitikia wito. Kuambia kuwa kuna nyekundu ni dalili ya kuwepo kwa kazi ya umwagaji damu. Alikuwa ni mtu wa kutumainiwa katika mipango mbalimbali. Alishapewa kazi nyingi na zote alizifanya katika weledi wa hali ya juu. Siku zote aliishi kutokana na kufanyakazi ambazo ni tofauti na kazi yake ya halali. Licha ya kuwa afisa usalama wa Taifa tena wa kutegemewa, lakini upande mwingine alikuwa akishiriki mipango mingi ya hatari. Baada ya Dakika tano walikuwa wamewasili eneo la coco beach. Akashuka kwenye pikipiki, akaingiza mkono mfukoni akatoa noti ya Elfu tano akampa dereva, kisha bila kusubiri chenji akapiga hatua kuelekea pale alipowaambia wakutane. Alitembea kama mtu wa kawaida, suruali ya Jeans, tshirt nyeupe na raba nyeupe miguuni zilimfanya abadirike na kuonekana kama kijana. Akaendelea kutembea macho yake yakitembea huku na huko. Mbele kidogo akaiona gari ambayo aliifahamu. Ilikuwa gari inayotumiwa na watu wake. Hii ilimaanisha kuwa wao walishafika kabla yake. Akaendelea kutembea akiipita gari ile kama hakuiona, alipoipita akainama na kuzuga kama anafunga viatu. Lakini muda huo huo macho yake yakitembezwa kwa ustadi mkubwa. Ni hapo alipokiona kitu ambacho kwanza kilimshangaza na pili kilimtia hofu. Wakati ameinama akifunga viatu, alimuona mtu kama Mpenzi wake. Alimuona mwanamke kama Teddy akitembea kwa kificho ndani ya fukwe za coco. Hilo lilimshangaza, halikuishia kwenye kumshangaza tu, bali lilimpa hisia tofauti. Hakuwa amemfananisha Na haitatokea amfananishe Teddy. Lakini amefuata nini hapa? Mbona kama alikuwa akinifuatilia? Yalikuwa maswali, maswali ambayo alihitaji kupata majibu katika wakati ule.



Akaendelea bila kugeuka nyuma, hakutaka kufanya hivyo kuogopa kumshtua Teddy. Hatua kama tano kabla hajawafikia watu wake, masimba akaitoa Ishara kwa watu ambao walikuwa wamekaa mbele yake. Ishara ambayo ilijibiwa haraka na watu wale, kilichofuatia ni kuingia ndani ya gari na muda ule gari likaondoshwa pale coco na kurudi katikati ya mji. Ulikuwa mchezo ambao hakuna ambaye aliuelewa mapema. Wote walijua kwamba lazima wangezungumza palepale ufukweni. Lakini haikuwa hivyo, kila mmoja alishangazwa na mabadiliko ya Masimba.



"Nipeni kazi nishukie hapa." Ilikuwa sauti kutoka kwa masimba. Wajumbe wote wakashangazwa na haraka ile. Mmoja akataka kuhoji lakini alipoangaliana na macho ya Masimba akafumba mdomo na hakukumbuka tena kutaka kuuliza.



"Tuokoeni muda, aliongea tena masimba, safari hii akitaka kuufungua mlango.. lakini akashikwa bega na kijana yule. "Nadhani umeisikia taarifa habari ya jana kuhusu kukamatwa kwa mzigo wa madawa ya kulevya? Akauliza huku akimuangalia masimba usoni.



"Yeah nimeona na nilikuwepo eneo hilo." Akajibu akiangalia nyuma.



"Basi ule mzigo ni wa kwetu na tunahisi kuna mmoja wetu atakuwa ameivujisha taarifa za kukamatwa kwa mzigo wetu kwa faida zake." Alieleza kijana yule kwa kirefu kisha akaongeza "Tuna mashaka na Jimmy Lambert, tuna mashaka kwa kuwa anaonyesha kutokuwa na uchungu na mabilioni yetu yaliopotea.





"Umesema mnamuhisi kuwa amewageuka? Akauliza masimba.



"Ndio, tunahisi kwa kuwa hana uchungu na Bilioni ishirini na mbili. Safari alijibu mtu mwingine tofauti na kijana. Masimba akakaa kimya kwanza akionekana kuwaza kitu. Alipokuja kuinua kichwa chake akatingisha kichwa kuonyesha kubaliana na kazi ile. "Tambueni hii kazi ni ngumu na ya hatari sana, ninakwenda kuifanya kwa kuwa pesa iliopotea ni nyingi. Lakini pia naenda kinyume na kazi yangu. Hivyo basi naomba nitakapoanza kuifanya kazi hii sitaki kusikia chochote kikizungumzwa. Pia pesa yangu nusu niingizieni kwenye account yangu.. kisha tukutane Mbagala rangi tatu baada ya sikutano nitakuwa na chochote cha kuwaeleza!!" Akaongea masimba akishuka ndani ya gari tayari kwa kuelekea kwake. Ule wasiwasi wa kumuona mkewe pale coco beach ndio kwanza ukaanza baada kushuka kwenye gari. Kila alipojaribu kutafuta sababu ya mkewe kumfuatilia nyuma nyuma hakuipata. Hakuwahi kumuhisi mkewe tofauti lakini kwa kitendo cha leo akahisi kuna kitu mpenzi wake amekihisi ama labda wivu ndio unamsumbua.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

*******

Aliingia nyumbani akiwa hana wasiwasi, baada ya kuingia akaongoza chumbani ambapo alimkuta mkewe akiwa amelala. Akamuangalia kwa muda mrefu bila kufanya lolote. Alimuangalia mpenzi wake huyu kwa muda mrefu bila kufanya kitu chochote. Hakutaka kwenda pale kitandani, kuna kitu alitaka kukifanya kwa wakati ule.alivikumbuka vitamburisho na mkoba wa yule dada alieuawa usiku wa jana. Akatembea mpaka sehemu yake ya siri ambayo ndio huhifadhi mambo yake mengi. Akavichomoa vitu alivyovichukua kwa marehemu yule, akatoka nje kabisa na kuanza kuvitizama. Jina lake mwanamke yule lilisomeka kama Asteria Paul. Alikuwa mfanyakazi wa Uwanja wa ndege. Akahisi kitu kama kengele zikigonga kichwani mwake. Alihisi kuna kitu kipo nyuma ya mauaji yale. Akarudisha vitambulisho na kuiwasha simu ya binti yule. Baada ya muda akaenda kwenye majina ya watu waliompigia.. Hakuamini Macho yake Pale alipokutana na namba ya Mpenzi wake ikiwa ndio namba ya mwisho kumpigia marehemu..





Namba ya Mwisho kumpigia marehemu ilikuwa namba ya Mpenzi wake. Hilo likamsisimua mwili wake, ile hisia kwamba mpenzi wake ndiye aliemuona kule coco beach sasa ilikuwa imeupata ushahidi wake. Lakini bado kichwa chake kilikuwa kizito kupindukia kuamini kwamba Teddy ni Mhusika katika tukio la kuuawa kwa mwanamke yule. Hilo halikumpa mashaka zaidi lakini alijiuliza ni vipi ameweza kufanya hilo wakati alikuwa naye ndani kwa kipindi chote. Ni katika kuyawaza hayo ndipo akaikumbuka siku iliopita pale alipoagwa na Teddy kuwa anakwenda kwao na hatarudi kwa siku hiyo. Kulikumbuka hilo kulizidi kuusisimua Mwili wake. Alitanbua kuna kila dalili za mpenzi wake kuhusika na kifo cha mwanamke yule. Lakini alijiuliza sababu za kumuua mwanamke mbele yake kulikuwa na maana gani kwake? Walikuwa wakimpa ujumbe gani kwake. Hapo akaipata hamu ya kuendelea kuichunguza simu ya marehemu Asteria. Jina la pili kukutana nalo ni la Mtu ambaye aliambiwa amchunguze. Lilikuwa jina la Jimmy Lambert. Alikuwa mmoja kati ya watu waliowasiliana na Asteria Muda Mfupi kabla ya kifo chake. Kila alichokuwa akikiona kilikuwa kama ndoto asioiamini. Kwa nini jina la Teddy kisha Jimmy? Teddy yupo wapi katika hili? Ana husika vipi katika kifo cha mwanamke huyu? Yalikuwa maswali mazito sana, maswali ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati ule. Hakuwa na jibu kwa wakati ule lakini ilikuwa lazima kulitafuta jibu kabla hakujapambazuka. Aliinuka na kuvirudisha vitu vyake sehemu yake, alipohakikisha kila kitu kipo sawa akaanza kutembea kuelekea nje ya nyumba yake. Hakupata hamu ya kulala kwa wakati ule. Uhusiano wa kifo cha mwanamke yule na urafiki wa Jimmy na Teddy kilikuwa kitu kilichomtia shaka na kuvuruga kichwa chake. Safari hii hakutaka kutumia usafiri wa kukodi, aliamua kutumia gari yake mwenyewe. Alikuwa amekata shauri ya kuelekea magomeni Mikumi nyumbani kwa rafiki wa mpenzi wake. Alitambua huko anaweza akaupata Ukweli kuhusu mauaji ya Binti yule na Uhusiano uliokuwepo kati ya Jimmy na Teddy. Kwa kuwa barabara haikuwa na magari, hapakuwa na ugumu wowote. Aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida huku akiwa makini kuangalia kama alikuwa akifuatiliwa. Lakini hapakuwa na kitu chochote kilichomtia wasiwasi. Baada ya muda alikuwa akiegesha gari umbali mfupi kutoka iliponyumba ananyoishi Rafiki wa mpenzi wake. Ilikuwa nyumba kubwa ya vyumba sita, sebule, choo sambamba na jiko. Hakuwa akiishi na mtu kutoka na mumewe kutokuwepo hapa nchini. Masimba alishuka na kuufunga mlango wa gari kisha akaongoza kuelekea getini kwa nyumba ile. Giza lilikuwa limechukua sehemu kubwa huku ukimya nao ukitawala kuonyesha kwamba watu wengi walikuwa wameshalala. Alitembea taratibu huku akiwa makini na kila kitu, alipolifikia geti akataka kuligonga lakini akagundua kuwa lilikuwa wazi. Hilo likamstaabisha, tokea amfahamu mwanamke huyu hakuwahi kumuona ama kukuta geti hili likiwa wazi. Kitendo cha leo kilimstaabisha sana. Akakata shauri aingie pasipokuligonga geti. Akalisukuma taratibu na kuzama ndani. Hapo pia akashangazwa kwa ukimya ambao aliukuta ndani. Taa zote zilikuwa zikiwaka, mlango wazi lakini hakukuwa na sauti yoyote kuashiria kama kulikuwa na mtu ama lah. Hilo likampa machale, akajivuta zaidi kuufuata mlango.. akaukuta ni kweli ulikuwa uko wazi. Akaingia na kusogea ndani, bado alipokewa na ukimya. Ukimya ambao hakuwahi kukutana nao katika jumba lile. Ukimya uliomfanya aichomoe bastola yake na kuishikilia mkononi. Akatembea kwa makini huku macho yake yakicheza pande zote. Bado hakuiona dalili ya kuwepo kwa mtu. Akaendelea kutembea huku umakini ukiongezeka. Akatokea sebuleni, kutokea sebuleni tu akahisi mwili ukisisimka.. sebule ilikuwa ilikuwa imevurugwa na vitu kutupwa huku na huko..



Akaikamata bastola yake vizuri kisha akaanza kusogea mbele zaidi na zaidi. Hatua saba mbele akaiona michirizi ya damu. Umakini ukaongezeka zaidi na Zaidi. Akatembea mdomo wa bastola ukitangulia. Alikuwa akitembea kuifuata michirizi ile ya damu. Alikuwa amejiweka tayari kwa kila kitu. Akaendelea kuifuatilia michirizi ile nyuma nyuma, mbele kidogo Akaiona ikiwa imeishia mlangoni mwa chumba fulani mle ndani. Hapo akasimama kwanza, baada ya hapo akausukuma mlango kisha kujitoma ndani. Hapo akajikuta akitizamana na Mwili wa Rafiki Wa Teddy Ukiwa umelala chini huku damu zikionekana kutuama. Akatembea mpaka pale ulipo mwili wa dada yule. Hakuonekana kuwa na uhai, hakuonekana kama alikuwa hai. Masimba akautazama mwili wa mwanadada yule kwa muda wa kama sekunde tano bila kufanya lolote. Kichwa chake kilikuwa kimevurugika, asteria, na sasa alikuwa ameuawa mwanamke huyu. Kipi kipo nyuma katika mauaji haya? Bado alitaka kujua kiundani zaidi, wakati akiwa bado ameduwaa asijue nini anatakiwa kufanya, akaisikia miguu ya watu ikitembea kisha minong'ono ikafuatia. Akatulia tuli huku mdomo wa bastola akiuelekeza mlangoni. Bado hatua za miguu na minong'ono ikaendelea kusikika, Sasa zilikuwa sasa hatua zile zilikuwa zikiukaribia mlango ule, punde akakiona kitasa kikitikiswa, wakati huo huo mlango ukasukumwa.. hakusubiri chochote kitokee, hakusubiri chochote kivuruge plani yake, mlio mdogo mfano wa chafya ukasikika, bastola ikakohoa mara mbili.. Hapakuwa na kelele. Ilikuwa miguno tu, miguno ilioambatana na kutambarajika kwa watu. Masimba akaurudia umakini wake, akatembea mpaka pale ilipolala ile miili ya watu wale wawili, akainama na kuigeuza miili. Zilikuwa sura ngeni machoni, hakuwahi kuwaona popote watu hawa. Alichokifanya nikuwapekua watu wale nakuchukua kila alichokiona kinafaa, kisha akatoweka eneo lile kwa kupitia mlango wa nyuma wa nyumba Ile.



Aliondoka kwa kupitia mlango wa nyumba ile. Kichwa chake kilishavurugwa kama sio kuvurugikiwa. Hakuamini kama tukio la kuuawa kwa mwanamke yule lingeyavumbua mambo makubwa kama yale tena kwa muda mfupi. Lakini ni nani waliomuua Rafiki huyu wa Teddy? Kwa nini wamuue? Au waliniona nikiondoka nyumbani wakaamua kunifuatilia? Kama walinifuatilia kwa nyuma ni vipi damu ilikuwa imeganda kuonyesha mauaji yalifanyika muda mrefu kidogo? Maswali hayo yakampa hamu ya kumchunguza mkewe, sio mkewe tu bali hata na Jimmy. Kwani aliondoka nyumbani akiwa peke yake, hakuona kitu chochote kilichompa wasiwasi kama alikuwa akifuatiliwa, sasa ilikuwaje kufika tu nyumbani kwa mtu aliekuwa akimuhitaji amkute ameuawa? Hilo likampa kile ambacho hakuwahi kukiwaza, tukio la coco beach lilibeba tukio zima la kuuawa kwa mwanamke huyu. Akatambua kuwa alitakiwa kuwa makini, alitambua kama atakwenda ndivyo sivyo basi anaweza asiimalize kazi hii. Alijua kama mkewe ni mshirika wa Jimmy na kama ni kweli ni yule aliemuona coco beach, basi alijua kuwa lazima atakuwa akitembea na macho ya watu kila mahali. Akairudia gari yake kwa kutokea uelekeo tofauti, baada ya kuikuta gari yake akawasha kitufe fulani cha kucheki usalama, aliporidhika muda mfupi alikuwa barabarani akielekea nyumbani kwake huku akiubeba utulivu wa Hali ya Juu. Hakutaka kumpa mashaka mpenzi wake, alitaka kumchunguza chini kwa chini. Muda mfupi alikuwa akiingiza gari ndani ya geti la nyumba yake. Akashuka na kurudi getini tena, baada ya kulifunga akaongoza kuingia ndani. Ile anaufungua mlango akapokewa na macho ya Teddy yakimtizama katika namna ya kuvutia. Yalikuwa macho malegevu, macho yanayohitaji kitu fulani. Masimba alilijua hilo, lakini hakutaka litendeke. Akapiga hatua mbili tatu mpaka aliposimama mwandani wake. Akamkumbatia kwa upendo wa hali ya juu. Walibaki wamesimama katika kumbatio lile, kumbatio ambalo lilidumu kwa muda wa dakika mbili. Kila mmoja akiliwaza lake. Punde walikuwa wakiachiana lakini huku wakiwa wanatizama.. kila mmoja alikuwa akimuangalia mwenzake kwa upendo. Lakini upendo ambao haukubeba maana nzima ya kutizamana kwao. Kwa mbali Masimba alikigundua kile ambacho kilifichika katika mtizamano ule. Kulikuwa na wasiwasi Machoni kwa mpenzi wake. Hakusubiri zaidi kumuangalia, aliushika mkono wake na kuelekea naye chumbani, hapo wakapokewa na kitanda, kitanda ambacho leo hili kilichelewa kuupumzisha mwili wa Masimba. Akaendelea kupiga hatua kuelekea pale kitandani. Alipofika alimlaza teddy kisha naye akayatoa mavazi yake kisha kujilaza kando ya Teddy. Wakauvuta usingizi kwa muda, usingizi ambao haukua rahisi kwa masimba. Sauti ya mwanamke alieuawa usiku wa juzi bado iliendelea kusikika masikioni mwake, bado hakujua kwa nini ilikuwa vile, bado hakujua wauaji walikuwa na lengo gani. Akapanga siku inayofuata kuelekea nyumbani kwa marehemu. Alitaka kwenda kupeleleza na kujua nini ambacho kipo nyuma. Alitaka kuujua ukweli juu ya kifo cha Asteria, alitaka kujua kuna uhusiano gani na Jimmy. Akaivuta shuka usoni, kisha kuutafuta usingizi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



*******



"Lazima Tumuue." Ilisikika sauti kutoka ndani ya chumba fulani. "Hawezi kucheza na sisi, hata hao waliomtuma tutawamaliza kabla ya jua la kesho kutwa." Aliendelea kuunguruma mwanaume yule. Alikuwa mwanaume wa makamo, mweusi na mwenyekitambi ambacho kilimfanya aonekane kama mkurugenzi au waziri katika wizara fulani. Ukimuondoa mwanaume huyo pembeni alikaa Jimmy na kushoto kwake alikaa mwanaume mwingine ambaye muda wote alikuwa kimya. Kilikuwa kikao ambacho hakikuwa rasmi. Kikaa ambacho kiliitishwa na watu watatu baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa vijana wao wawili. Hilo liliwapa mashaka makubwa sana, mashaka ambayo hapo mwanzo hawakuwa nayo. Ukweli waliujua na walimjua muuaji. Licha ya kumjua muuaji lakini hawakuwaza kama lingefika huko. Hawakujua kama Masimba angeanza kwa kuwatia Hasara, hawakujua kama wangewapoteza watu wao ambao walikuwa ni msaada mkubwa kwao, kwa mara ya kwanza wakajikuta wakikijutia kitendo cha kumuua Asteria Mbele ya Masimba. Walijua kitendo hicho ndicho kilichosababisha yote ambayo yalitokea usiku wa jana. Kila mmoja akatulia akihitaji kuipa utulivu akili yake ili kupata majibu sahihi juu ya kudili na mtu huyu ambaye ameonekana kuwa kikwazo kwao. Hakuna ambaye aliinua mdomo ama kuufumbua kuzungumza na mtu mwingine. Walinyamaza kumsubiri mtu ambaye ndie mtu wa mipango, walikuwa wakimsubiri Teddy Kupata majibu ya kipi ambacho kilitokea na kipi ambacho kifanyike. Kila mmoja NITAKUPATA TU



SEHEMU YA 003



********



Namba ya Mwisho kumpigia marehemu ilikuwa namba ya Mpenzi wake. Hilo likamsisimua mwili wake, ile hisia kwamba mpenzi wake ndiye aliemuona kule coco beach sasa ilikuwa imeupata ushahidi wake. Lakini bado kichwa chake kilikuwa kizito kupindukia kuamini kwamba Teddy ni Mhusika katika tukio la kuuawa kwa mwanamke yule. Hilo halikumpa mashaka zaidi lakini alijiuliza ni vipi ameweza kufanya hilo wakati alikuwa naye ndani kwa kipindi chote. Ni katika kuyawaza hayo ndipo akaikumbuka siku iliopita pale alipoagwa na Teddy kuwa anakwenda kwao na hatarudi kwa siku hiyo. Kulikumbuka hilo kulizidi kuusisimua Mwili wake. Alitanbua kuna kila dalili za mpenzi wake kuhusika na kifo cha mwanamke yule. Lakini alijiuliza sababu za kumuua mwanamke mbele yake kulikuwa na maana gani kwake? Walikuwa wakimpa ujumbe gani kwake. Hapo akaipata hamu ya kuendelea kuichunguza simu ya marehemu Asteria. Jina la pili kukutana nalo ni la Mtu ambaye aliambiwa amchunguze. Lilikuwa jina la Jimmy Lambert. Alikuwa mmoja kati ya watu waliowasiliana na Asteria Muda Mfupi kabla ya kifo chake. Kila alichokuwa akikiona kilikuwa kama ndoto asioiamini. Kwa nini jina la Teddy kisha Jimmy? Teddy yupo wapi katika hili? Ana husika vipi katika kifo cha mwanamke huyu? Yalikuwa maswali mazito sana, maswali ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati ule. Hakuwa na jibu kwa wakati ule lakini ilikuwa lazima kulitafuta jibu kabla hakujapambazuka. Aliinuka na kuvirudisha vitu vyake sehemu yake, alipohakikisha kila kitu kipo sawa akaanza kutembea kuelekea nje ya nyumba yake. Hakupata hamu ya kulala kwa wakati ule. Uhusiano wa kifo cha mwanamke yule na urafiki wa Jimmy na Teddy kilikuwa kitu kilichomtia shaka na kuvuruga kichwa chake. Safari hii hakutaka kutumia usafiri wa kukodi, aliamua kutumia gari yake mwenyewe. Alikuwa amekata shauri ya kuelekea magomeni Mikumi nyumbani kwa rafiki wa mpenzi wake. Alitambua huko anaweza akaupata Ukweli kuhusu mauaji ya Binti yule na Uhusiano uliokuwepo kati ya Jimmy na Teddy. Kwa kuwa barabara haikuwa na magari, hapakuwa na ugumu wowote. Aliendesha gari kwa mwendo wa kawaida huku akiwa makini kuangalia kama alikuwa akifuatiliwa. Lakini hapakuwa na kitu chochote kilichomtia wasiwasi. Baada ya muda alikuwa akiegesha gari umbali mfupi kutoka iliponyumba ananyoishi Rafiki wa mpenzi wake. Ilikuwa nyumba kubwa ya vyumba sita, sebule, choo sambamba na jiko. Hakuwa akiishi na mtu kutoka na mumewe kutokuwepo hapa nchini. Masimba alishuka na kuufunga mlango wa gari kisha akaongoza kuelekea getini kwa nyumba ile. Giza lilikuwa limechukua sehemu kubwa huku ukimya nao ukitawala kuonyesha kwamba watu wengi walikuwa wameshalala. Alitembea taratibu huku akiwa makini na kila kitu, alipolifikia geti akataka kuligonga lakini akagundua kuwa lilikuwa wazi. Hilo likamstaabisha, tokea amfahamu mwanamke huyu hakuwahi kumuona ama kukuta geti hili likiwa wazi. Kitendo cha leo kilimstaabisha sana. Akakata shauri aingie pasipokuligonga geti. Akalisukuma taratibu na kuzama ndani. Hapo pia akashangazwa kwa ukimya ambao aliukuta ndani. Taa zote zilikuwa zikiwaka, mlango wazi lakini hakukuwa na sauti yoyote kuashiria kama kulikuwa na mtu ama lah. Hilo likampa machale, akajivuta zaidi kuufuata mlango.. akaukuta ni kweli ulikuwa uko wazi. Akaingia na kusogea ndani, bado alipokewa na ukimya. Ukimya ambao hakuwahi kukutana nao katika jumba lile. Ukimya uliomfanya aichomoe bastola yake na kuishikilia mkononi. Akatembea kwa makini huku macho yake yakicheza pande zote. Bado hakuiona dalili ya kuwepo kwa mtu. Akaendelea kutembea huku umakini ukiongezeka. Akatokea sebuleni, kutokea sebuleni tu akahisi mwili ukisisimka.. sebule ilikuwa ilikuwa imevurugwa na vitu kutupwa huku na huko..



Akaikamata bastola yake vizuri kisha akaanza kusogea mbele zaidi na zaidi. Hatua saba mbele akaiona michirizi ya damu. Umakini ukaongezeka zaidi na Zaidi. Akatembea mdomo wa bastola ukitangulia. Alikuwa akitembea kuifuata michirizi ile ya damu. Alikuwa amejiweka tayari kwa kila kitu. Akaendelea kuifuatilia michirizi ile nyuma nyuma, mbele kidogo Akaiona ikiwa imeishia mlangoni mwa chumba fulani mle ndani. Hapo akasimama kwanza, baada ya hapo akausukuma mlango kisha kujitoma ndani. Hapo akajikuta akitizamana na Mwili wa Rafiki Wa Teddy Ukiwa umelala chini huku damu zikionekana kutuama. Akatembea mpaka pale ulipo mwili wa dada yule. Hakuonekana kuwa na uhai, hakuonekana kama alikuwa hai. Masimba akautazama mwili wa mwanadada yule kwa muda wa kama sekunde tano bila kufanya lolote. Kichwa chake kilikuwa kimevurugika, asteria, na sasa alikuwa ameuawa mwanamke huyu. Kipi kipo nyuma katika mauaji haya? Bado alitaka kujua kiundani zaidi, wakati akiwa bado ameduwaa asijue nini anatakiwa kufanya, akaisikia miguu ya watu ikitembea kisha minong'ono ikafuatia. Akatulia tuli huku mdomo wa bastola akiuelekeza mlangoni. Bado hatua za miguu na minong'ono ikaendelea kusikika, Sasa zilikuwa sasa hatua zile zilikuwa zikiukaribia mlango ule, punde akakiona kitasa kikitikiswa, wakati huo huo mlango ukasukumwa.. hakusubiri chochote kitokee, hakusubiri chochote kivuruge plani yake, mlio mdogo mfano wa chafya ukasikika, bastola ikakohoa mara mbili.. Hapakuwa na kelele. Ilikuwa miguno tu, miguno ilioambatana na kutambarajika kwa watu. Masimba akaurudia umakini wake, akatembea mpaka pale ilipolala ile miili ya watu wale wawili, akainama na kuigeuza miili. Zilikuwa sura ngeni machoni, hakuwahi kuwaona popote watu hawa. Alichokifanya nikuwapekua watu wale nakuchukua kila alichokiona kinafaa, kisha akatoweka eneo lile kwa kupitia mlango wa nyuma wa nyumba Ile. alikuwa akiitizama saa yake. Muda ulikuwa muda ulikuwa ukienda bila kumuona Teddy, kila mmoja akashangazwa na kitu kile, kila mmoja lishangazwa na kuchelewa kufika kwa Teddy, mmoja akaona aipige namba yake japo kumuuliza. Lakini kinyume chake namba haikuwa inapatikana. Hilo likawashangaza wote, liliwashangaza kwa kuwa taarifa alikuwa nayo na aliahidi kufika hapo katika muda husika. Lakini muda huu alikuwa hapatikani kabisa. Kila mmoja akasonya, akasonya huku akitukana matusi ya nguoni.



*****

Wakati akisubiriwa kule na watu wake, teddy alionekana akiingia katika maeneo ya nyumba ya rafiki yake. Ni ile nyumba ya rafiki yake alieuawa jana.aliukuta umati wa watu umezunguka eneo lote huku polisi wakiwa wamezungusha utepe kuonyesha kuwa hapakutakiwa mtu kupita hapo. Alipenya katikati ya watu mpaka karibu kabisa na waliposimama askari wa usalama. Akawasogelea kisha kuongea nao mawili matatu, wakaonekana askari wale wakimruhusu kupita kuingia ndani ya nyumba ya Rafiki yake. Alitembea bila kuonyesha wasiwasi wowote mpaka sebuleni ambapo aliwakuta wataalam wa picha wakiendelea kupiga picha mbali mbali, pia walikuwepo wanausalama kadhaa wakitizama hiki na kile, akawapita na kuelekea kule ambapo ilielekea michirizi ya damu. Akatembea akiangalia hiki na kile. Hatua tano akamuona mtu ameinama akiichunguza miili ya watu wawili ambao walikuwa wamelala katikati ya damu. Alimtambua mtu huyo na alimjua. Alikuwa mpenzi wake. Alikuwa masimba akiitizama miili ya wanaume wawili aliowauaa Jana. Akataka kusimama lakini alijikuta akiendelea kutembea baada ya masimba kugeuka na macho yao kukutana.



Alitaka kusimama asiendelee na safari yakuelekea pale alipochuchumaa Masimba. Kitendo cha kumkuta mpenzi wake kulimpa picha mbili tofauti. Picha ambazo hazikuonyesha kumfurahisha yeye. Hata masimba alipogeuka na macho yao kukutana, bado alitembea na bado alikuwa akimuangalia kwa mashaka. Hata masimba alikitambua kitendo kile, lakini hakutaka kumshtua, hakutaka kumuonyesha kama anajua kitu. Baada ya Teddy kusogea pale, kwa mara ya pili masimba akainua uso na macho yake kumtizama Teddy. Alimuangalia kwa muda kisha kurudisha macho yake kwenye mwili wa Marehemu, alimuona jinsi alivyolala uso wake ukiwa umekunjamana kutokana na maumivu ambayo aliyapata wakati anauawa. Kila alipokuwa akimuangalia marehemu ndipo hasira juu ya mpenzi wake ziliongezeka. Alitambua kuuawa kwa mwanamke huyu ilikuwa ni kuzibwa mdomo juu ya kitu fulani ambacho hata yeye alihisi kuwa labda utakuwa ule mzigo. Kwa mara nyingine akajiapiza kuyafikia makazi ya Jimmy Lambert. Matundu mawili ya risasi kifuani na mawili shingoni ikikuwa ni kithibisho kuwa marehemu huyu hakutakiwa kuachwa hai. Baada ya kuridhika na kile alichokifanya pale akainuka, akaongea mawili matatu na mpenzi wake, alipomuacha hapo akaongea na wana usalama kisha akaondoka maeneo yale kuelekea nyumbani kwa Marehemu Esteria. Kwa kuwa hapakuwa mbali na eneo ambalo alikuwepo, masimba hakuona tatizo kutembea kwa miguu.. alitembea huku sura ya wasiwasi ilionyesha mpenzi wake ikijirudia. Hakuwa na wasiwasi pale alipotembea hapa na kutokea pale. Hakuwa na mashaka kuwa anafuatiliwa kwa kuwa walikuwepo vijana ambao walikuwa wakimfuatilia kwa nyuma kuangalia nani ambaye alikuwa nyuma yake. Bado alitambua mkewe alikuwa nyuma ya matukio haya, alijua Teddy alikuwa katika hili. Hilo lilimpa matumaini ya kugundua kuhusu mzigo uliokamatwa, na hata kuugundua ukweli mwingine ambao umefichwa kwa njia moja ama nyingine. Akaifikia nyumba ya marehemu Asteria. Askari walikuwa wengi wakilinda eneo lote. Kila mmoja alikuwa makini kwa kila hatua. Masimba akawafikia na kuongea nao mawili matatu, punde alikuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya nyumba ile iliojaa waombolezaji. Kila mtu alionekana ni mwenye uchungu sana. Kila mmoja alikuwa akilia kwa uchungu wa hali ya juu. Hilo likampa Masimba wakati mgumu. Wakati wakupata maelezo kutoka kwa ndugu wa marehemu Asteria. Alitembea macho yakitizama kila sura ya mtu aliekuwepo pale, siku zote alitambua kuwapo katika tukio lile na umati wa watu kiasi kile, ni njia moja wapo ya kuweza kumtambua ama kumshuku kwa macho, vile tu hisia zake zitakavyo. Kila sura ilionyesha majonzi, kila mmoja alionyesha kuumizwa na kifo cha Asteria. Hilo likamfanya masimba aikumbuke sauti ya msichana yule wakati alipokuwa akimuita. Hapo akahisi kitu kikimkaba kwenye koo. Kwa nini hakusimama kumsaidia binti huyu anayeonyesha kupendwa na watu? Alipewa kazi ya kuchunguza mzigo uliokamatwa, mzigo ambao haijulikani kama ni wote ambao umekamatwa. Lakini sasa alikuwa amebeba uchunguzi wa vifo vya watu wengine wawili. Vifo ambavyo vinaonyesha kuwepo na uhusiano wa kupotea kwa mzigo ambao alipewa kazi ya kuuchunguza. Alitembea kwa utulivu mpaka sehemu moja ambayo walikaa wakina mama wengi wakionyesha kumshika mama mmoja ambaye alionekana hajiwezi kwa kilio. Baada ya kufika hapo akaongea na dada mmoja ambaye alifanana sawia na marehemu Asteria.



"Wamemuua mdogo wangu, wamemuaa kwa sababu ya uaminifu wake kazini!" Alianza kuongea dada yule huku akiangua kilio.



"Najua una uchungu, najua unaumia, lakini hatuna lakufanya kwa kuwa limeshatokea. Naomba ufute machozi kwa kuwa niko hapa kwa kazi yakutaka kujua nani wapi nyuma ya kifo hiki. Futa machozi. Kisha nataka unijibu maswali kwa uchache. Aliongea masimba huku sasa akitoa kijitabu kidogo.



"Tunaweza kuanza mazungumzo.. nataka kujua kila kitu unachokijua wewe kuhusu marehemu.' Akaongea masimba huku akijiandaa.

Dada wa Asteria alimuangalia Masimba, kisha kwa sauti ya upole akaanza kumueleza.



"Asteria ni Mdogo wangu na mimi ndio msiri wake. Hakuwa akinificha chochote katika maisha yake. Wiki mbili zilizopita alinipigia simu akiniambia kwamba kuna kitu anataka kunieleza, lakini kitu chenyewe ni Cha hatari na hatuwezi kuzungumza kwenye simu. Baada ya kuniambia hivyo nilimshauri aje nyumbani anieleze kisha tuangalie hatua za kuchukua. Kweli Asteria alikuja siku ya pili yake usiku, tena akiwa katika mavazi ya ajabuajabu ambayo yalifunika mpaka uso wake. Ki ukweli aina ile ya mavazi na uingiaji wake ndani, ulinifanya nihisi kuwa kweli mdogo wangu alikuwa katika hatari. Basi sikutaka kumhoji kuhusu yale mavazi na hata uingiaji wake, nilimtaka aniambie tatizo lake. Ndipo hapo aliponieleza kuwa kuna watu matajiri wanataka wasaidiwe kuingiza madawa ya kulevya yenye thamani ya mamilioni ya shilingi. Lakini sasa wanataka wawasaidie kuingizwa na kama yakifanikiwa Basi kila mmoja katika kitengo chao angepewa shilingi milioni mia tano. Na wenzake wotw wamekubali na anayesubiriwa ni yeye. Baada ya maelezo hayo nikamwambia wewe unaamua nini? Akasema yeye hayupo tayari, na aliongeza kuwa alitaka kukutana na mpelelezi aitwaye masimba amueleze hicho kitu kwa kuwa kulikuwa na mtu wake wa karibu anashirikiana na mtu anayeitwa Jimmy pamoja na viongozi wa serikali. Siku ambayo aliondoka hapa kumfuata Huyo mpelelezi, mdogo wangu hakurudi Tena akiwa hai. Amerudi akiwa marehemu." Alimaliza kuongea yule dada wa marehemu huku akiangua tena kilio.



Mishipa ya hasira na uchungu ilikuwa usoni kwa masimba. Kumbe marehemu alikuwa akimtafuta yeye, kumbe marehemu alikufa akitaka kuikabidhi siri mikononi mwake. Kwa nini hakusimama kumsikiliza. Masimba akatulia akifikiria kwa uchungu. TEDDY mpenzi wake alikuwa akihusika katika kifo cha Asteria. Akainuka akitaka kuondoka lakini akashikwa bega. Alipoinua kichwa alikutana na sura ya mama mzaZi Wa Asterina, akimuangalia kwa macho makali, macho ambayo hayakuonyesha woga. Wakaangaliana tena na tena.. Mama akataka kuongea kitu lakini sauti haikutoka.



*********



Walikaa kwa muda mrefu wakiisubiri simu kutoka kwa Teddy. Lakini bado simu yake haikuwa ikipatikana. Kila mmoja alikuwa akichanganywa na Ukimya ule. Lakini wakati wakiendelea kusubiri wakauona mlango ukifunguliwa. Teddy alikuwa akiingia akionekana hana tabasamu lake. Kila mmoja akabaki ameduwaa akimuangalia mwanadada huyu usoni.



"Kuna watu wawili wanatakiwa kufa". Akaongea Tedy kisha ukimya na hamaniko kutoka kwa watu wale likionekana. Kila mmoja alikuwa amekanganywa na maneno ya Teddy. Huna ambaye aliinua kinywa chake kuongea chochote. Mshangao bado uliwazubaisha. Wakiwa bado katika hilo teddy akaingeza.



"Hili Suala lipo mikononi mwa Idara ya Usalama wa Taifa. Vijana wanafanyakazi kubwa sana kutokana na vifo hivi. Masimba amelishikia bango hili suala na muda sio mrefu tunaweza kuumbuka." Teddy akaeleza mienendo yote ya masimba, mazungumzo yake na ndugu wa asteria. Na kuhusu watu wao waliouawa usiku wa kuamkia leo na kutoweka kwa Simu zao. "Sasa ni lazima mama wa Asteria na dada yake wauawe katika njia yoyote. Tukiwaachia hapa kisha wakakutana tena Na masimba kamwe hatutaweza kupona. Ni lazima wafe na ikibidi Hata Masimba Naye atawafuata...





Lazima tuwaondoe duniani, na ikibidi hata masimba atawafuata huko huko kuzimu. Hili suala bado gumu sana. Kukutana kwa masimba na wenzetu kule coco beach, kutoweka simu ya Marehemu Asteria pamoja na simu za vijana wetu, ni moja kati ya vitu hatari sana. Ninachoamini mimi Dada wa marehemu Asteria kuna kitu atakuwa anakijua kuhusu kifo cha mdogo wake, nilazima asteria alimpa siri kuhusu sisi. Kwa hiyo ilikujiweka katika mazingira sahihi nilazima tuwaondoe hawa watu. Nina amini hata masimba kuna kitu amekigundua kwangu, nadhani hata pale coco beach aliniona ndio maana hawakukaa sana. Sasa ni wajibu wetu kufanya kile ambacho kitatuweka salama zaidi. Kwani hata watu wa Idara ya Usalama Wa Taifa wamecharuka katika hili, nahawa ndio wanaompa nguvu huyu mwanaume, kwahiyo kwangu mimi nimemaliza na hii ndio mipango yangu." Aliongea Teddy kwa kirefu huku akiwaangalia wanaume wale wa tatu kwa zamu.



Kila mmoja alionekana yupo mbali kimawazo, kila mmoja alionekana akitafakari kuhusu jambo hili. Ukimya ukachukua nafasi katika eneo la chumba chote. Ni kweli hakikuwa kitu kidogo, lakini licha ua ukubwa wa kitu hiki hauwezi kuzuia mapambano. Mapambano sababu ya kupigania mamilioni yao ya Shilingi. Walikuwa tayari kumuua mtu yoyote kwa sababu ya pesa. Kila mmoja alikuwa akiutafakari ujumbe ulioletwa pale. Walihitajika kuawa watu wawili, na ikibidi watu watatu. Watu ambao watawafanya wao waishi kwa usalama zaidi. Watu ambao watakifanya kitendawili cha mzigo wao kubaki katika usiri nzito. Lakini watamuuaje masimba? Nani atainua bastola na kulenga kichwa ama kifua cha masimba? Hayo yalikuwa maswali ambayo yalikuwa yakipita vichwani mwao. Bado ukimya ulitawala na bado hapakuwa ni mtu wa kuzungumza. Kama Idara ya usalama imecharuka nini hatima yao katika hili. Walijua hapakuwa panahitajika nguvu, wakajua kutumia nguvu nikutafuta kushindwa katika hili pambano. Kila mmoja alitaka kuwa huru katika hilo. Kama simu za vijana wale zimetoweka, na simu zenyewe zilikuwa na mawasiliano walioyafanya na vijana hawa, nini ambacho kingewaponyesha.. hapo ndio walipouona Umuhimu wa kumuondoa Masimba kwanza kabla ya dada na mama wa Asteria. Kwa mara ya kwanza Jimmy aliamua kusimama kuzungumza kuhusu hilo. Kila mmoja alikuwa akimtizama akisubiria kusikia kile alichotaka kukizungumza.



******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya kumaliza kuongea na mama wa Asteria sambamba na dada yake, masimba akaona ni muda wa kuelekea nyumbani kwake huku akifikiria ni kipi ambacho atakifanya kuhusu mpenzi wake. Hakutaka kukurupuka katika hilo lakini kule kuambiwa na dada wa asteria kuhusu ukaribu wake na mmoja ya watu wenye mzigo huo, kulizidi kuitoa picha kuwa bado Teddy ni mhusika katika matukio yote ya mauaji. Ukianzia kuikuta mamba yake kuwa namba ya mwisho kuwasiliana na marehemu Asteria, kumuona coco beach usiku ule, kuonyesha wasiwasi alipomkuta akikagua miili ya watu wale mawili ni matukio ambayo yalimuaminisha na kuzifanya hisia zake kuwa sahihi. Licha ya kutembea pasipo na tahadhali, lakini bado alitanbua kuwa alikuwa na vijana wake wakimuangalia kila hatua. Alitambua umuhimu wa vijana wake. Wakati anataka kutokea kituo cha magomeni Hospital, akavutiwa na kitu fulani ambacho alikiona upande wa pili wa barabara. Licha ya kitu hicho pia hata simu yake ilipokea ujumbe kutoka kwa vijana wake. "Kuna vichwa viwili Vimeunda Urafiki nawe" ulisomeka ujumbe huo. Haikuwa kazi ngumu kuijua maana halisi ya ujumbe ule. Hata macho yake yalipoangaza katika maeneo yale ni kweli yakakutana watu wawili ambao walikuwa katikati ya umati wa watu ambao walikuwa wakisubiri usafiri wa kuelekea makwao. Ingawa watu hawa walijichanganya na abiria, lakini bado muonekano wao ulikuwa ni wakipekee, bado hawakuonekana kutulia hasa machoni mwao. Kila wakati walikuwa wakimwangalia Masimba kwa namna fulani ya kipekee. Aina ambayo haiwezi kufichika machoni kwa watu wenye fani ya ujasusi. Watu wale wawili, wakike na kiume bado walisimama wakionekana wakisubiri kitu, hata pale magari yaliposimama bado hawakupanda, bado hawakuonyesha kama walihitaji kupanda. Masimba akatabasamu kisha kupiga hatua akielekea pale waliposimama. Alitembea sawa na watu wengine waliokuwa wakiivuka barabara. Hata walipofika kituoni, gari ya kwanza kusimama masimba akapanda akiwaacha watu hawa wakihamanika. Lakini bahati nzuri konda aliwaona na kumuomba dereva asimame. Ni wakati watu wale wakipanda ndipo masimba alipoisikia miluzi na mayowe kutoka nje, watu waliokuwa wakishangilia kitu walichokiona. Akaruhusu macho yake yaelekee huko. Hapo hata yeye akashikwa na butwaa la muda, butwaa huku macho yakivutika kwa kile kinachopita nje.



Alikuwa akitembea kama twiga nyikani, alikuwa akitembea kama anaiogopa ardhi. Miguu ilitua kwenye ardhi kanakwamba haitaki. Alitembea akijitupa huku na huko. Kivazi chake kifupi kilikuwa kikiwavuta na kuwakata shingo wanaume kwa wanawake. Hata alipokuja kuingia kwenye daladala bado masimba alikuwa akimtizama, bado alikuwa akimuangalia twiga huyu, twiga alietoroka mbugani na kuja mitaani. Binti alikuwa haonyeshi kujali, haonyeshi aibu na kingine hakuonyesha kwamba labda angemuonea yoyote aibu. Ndio kwanza alikuwa akijipinda na Kujigeuza. Alikuwa akijishika hapa na kujiachia hapa. Hata pale alipokuwa akimtizama alihisi alikuwa akitizamana na Heaven Sent, ama alikuwa akiitizama picha yake. Alikuwa mzuri, alikuwa ameumbwa na alikuwa akivutia hata kutizamwa. Ni hapo binti yule alipotupa macho yake usoni kwa Masimba. Hata masimba alipomtupia jicho na hata macho yao kukutana, Kuna kitu kilionekana machoni kwa mwanamke yule. Kitu ambacho hakikuwa kigeni wala kipya machoni kwa Masimba.



Wakatizamana tena na tena. Masimba hakuwa mjinga katika kile ambacho kilikuwa kikitokea pale. Muda wote alimuangalia yule msichana akikitafuta kile ambacho kilifichwa upande wa pili. Alikitafuta kile ambacho kingempa picha huyu alikuwa nani. Macho pekee ya mwanadada yule hayakuweza kumpa jibu la kwamba huyu alikuwa nani. Jicho legevu kama mtu alieupoteza usingizi kwa muda mrefu halikuweza kumpa majibu alioyataka. Kwa jicho la mwanamke huyu hata jasusi ama mpelelezi wa kiwango cha aina yoyote asingeweza kuligundua hilo. Akakumbuka kuwa kulikuwa na watu wengine, watu ambao walikuwa wakimuandama kila hatua. Aliwatambua na kuwajua, alihitaji kuutafuta ukweli kutoka kwa hawa na yule mwanamke alievaa mavazi ya kutamanisha. Alitaka kujua kama kunakujuana, kutambuana na hata kufahamiana. Alitaka kuifanyakazi kwa kutumia akili zake. Macho yake yakatembea taratibu yakizibwa na gazeti. Muda wote alihitaji kupata ujumbe kutoka kwa wenzake wakimjulisha kuhusu huyu mwanamke. Lakini hilo halikuwezekana kwa wakati ule, si kuwezekana kwa kuwa hawawezi, la hasha! Hata vijana hawakuwa wamemjua huyu mwanamke. Akatulia na kutulia tena, punde konda akatangaza kituo kinachofuata. Akili yake ikachemka kwa haraka, kilikuwa kipimo sahihi cha kugundua kama yule mwanamke ni abiria ama alikuwa mmoja kati yao. Akainuka naye akijiandaa kushuka.. macho yake muda wote yalikuwa machoni kwa watu ambao waliambatana naye, kuambatana kwa maana ya kumfuatilia. Bado alikikosa kile ambacho alikuwa akikitafuta. Bado hakufanikiwa kugundua kama walikuwa wakifahamiana ama lah. Akatembea akisogea mlangoni. Alikuwa makini kwa kila hatua, mikono yake ilikuwa tayari kuifanya kazi kama ingebidi. Daladala ikasimama kituo cha kinondoni mkwajuni. Masimba akashuka akiwa pamoja na abiria wawili watatu. Baada ya kushuka hakutaka kuangalia nyuma. Alitembea akiingia hapq na kutokea pale. Safari yake Hiyo ikaishia Eneo la kinondoni studio. Licha ya kutambua kuwa alikuwa akifuatiliwa tokea pale magomeni, cha kushangaza hakuwaona tena watu wale. Alitumia mbinu zake zote lakini bado hakufanikiwa kugundua chochote. Akatembea sasa akiivuka barabara fulani katika mitaa ile ya kinondoni, wakati anakikaribia kituo fulani cha teksi, mara akaisikia sauti ya mtu ikimuita, sauti ambayo ilikuwa ngeni kwake. Akaipuuza kama hakuwa amesikia. Lakini kwa mara nyingine sauti ile ilikuwa ikimuita tena. Sasa alionekana mtu yule akimuita tena huku akimfuata kule alipokuwa akielekea. Ilikuwa sauti ya mwanamke, sauti ya mtu ambaye hakuwahi kumuona achilia mbali kuisikia sauti ile. Akajipa kazi ya kugeuka, ni kweli akageuka.. macho yake yakamuona mtu, mtu yule yule ambaye alipanda pale kwenye daladala, mtu yule yule ambaye alimuacha ndani ya daladala. Lakini sasa alikuwa akimuita tena kwa jina lake, jina ambalo halitumii sana. Hakuuficha mshangao, hakuuficha kwa mtu kama yeye kugundua. Amenijulia wapi? Kwa nini anifuate mpaka huku? Nini anakitaka kwangu? Alijiuliza maswali mengi huku akisimama kumsubiri mwanamke yule.



Mwanamke yule akatembea kwa mwendo ule ule wa kuogopa kuikanyaga ardhi. Bado masimba alikuwa akipata kukitafuta kile ambacho alikikosa kule alipotoka. Bado mwanamke yule hakuonyesha uhatari na vilevile hakuonyesha kama alikuwa ni mtu wa misukosuko. Wakakutana na kwa mara ya kwanza wakishikana mikono. Wakasalimiana wakiangaliana. Masimba alimuangalia machoni kwa muda mrefu akikitaka kile ambacho alikihisi. Lakini bado huyu hakuonyesha kama ni mmoja kati ya hao. Bado jicho lake legevu lilitengeneza urembo wa kumvutia mwanaume yoyote lijali. Akataka kusema kitu, lakini kabla hajafanya hivyo akausikia mlio wa simu yake. Akaichomoa kutoka mfukoni na kukutana na kiboksi cha Ujumbe mfupi wa maneno, kuonyesha kuna ujumbe umetumwa. Kidole kikashuka na kuruhusu ujumbe ule kufunguka.



"Ni mmoja wao kuwa makini." Ulisomeka ujumbe ule. Ujumbe uliomfanya atabasamu na kucheka. Kwa mara ya kwanza alikuwa amekutana na mtu ambaye amefanikiwa kuyarahai macho yake. "Ni Mmoja Kati yao" neno lile likajirudia kichwani. Akahamisha macho kwa mwanamke huyu. Bado akakutana na jicho legevu, jicho ambalo liliuficha uhalisia wa kikazi.



"Nadhani hatutaweza kuongea kwa sasa. Chukua mawasiliano yangu nitafute saa mbili usiku. Bila shaka unanifahamu sana hivyo na mimi nataka nikufahamu." Aliongea Masimba huku akitoa business card yake na kumkabidhi mwanamke yule, huku akiondoka katika eneo hilo.



*********



Alishuka na kuingia nyumbani kwake. Akili yake ilikuwa imevurugwa kutokana na mambo kuonekana kuharibika mapema sana. Kitendo cha kuingia kwa masimba katika sakata hili, hakikuwa kitu kizuri kwake na kwa wengine. Hakutakiwa masimba kuijua hii mipango. Lakini kuuawa kwa Asteria wakati akitaka kuonana na masimba kumeharibu kila kitu. Kifo cha Asteria ndicho kikichomuibua masimba. Kutoweka kwa simu ya marehemu na mazungumzo yale, alihisi masimba atakuwa amegundua kuwa yeye ni mshirika wa Mpango ule. Teddy alijikuta kichwa chake kikiwa kizito. Teddy alijikuta katika wakati ambao hakuwahi kuwa nao. Akaelekea chumbani kwao, akaongoza mpaka sehemu anapoweka bastola yake. Akafungua na kuichukua kisha kuishika mkononi. Aliitizama huku akiwaza. Alikuwa tayari kumuua Masimba iwapo atagundua kama anaijua siri yao. Alikuwa tayari kumuua mpenzi wake kwa sababu ya pesa. Akasimama akiiangalia bastola. Hapo akakumbuka penzi lao lilipoanzia. Alikumbuka mengi.. moyo ukakosa ujasiri. Muda ule ule akahisi mikono ikimshika kiunoni kisha sauti nzito ikasikika. "Usiogope Mpenzi Nakupenda Sana... ilikuwa sauti ya Masimba. Teddy hakutegemea, hata alipogeuka na macho yao kukutana.. Hakuweza tena kumuangalia MASIMBA..





Usiogope nakupenda sana mpenzi. Ilikuwa sauti ya masimba, sauti ambayo ilitokea nyuma yake.hakuwa amejiandaa na hilo, hakuwa amelitegemea lile la masimba kuwepo pale ndani. Hili likamnyong'onyeza. Akatamani kuongea kitu lakini maneno hayakutoka. Hakujua muda ambao masimba alifika nyumbani, hakutegemea uwepo wake hapo, na hata pale alipokumbuka kitendo alichokifanya, alichoka kwa kuwa alitambua kuwa masimba alikuwa amekishuhudia kitendo kile. Akaiona akili yake ikishindwa kumsaidia katika kulitatua hili ambalo lilikuwa mwisho wake. Hata pale mikono ya masimba ilipokuwa akipapasa kiuno chake, bado Teddy hakuweza kumjibu. Bado bastola yake ilikuwa mkononi, bado hasira zilionekana usoni, na hata dhamira ya mauaji ilijengeka kupitia macho yake. Hakuweza tena kumuangalia masimba, hakuweza tena kuuinua uso wake kumtizama. Alitazama pembeni na alikuwa ameinamia chini. Mwili ulikuwa unatetemeka, alijikuta kwenye wakati mgumu kupambana na moyo wake. Moyo uliojaa mapenZi juu ya masimba, moyo ambao haukuwahi kumpenda mwingine zaidi ya huyu mwanaume. Mwanaume ambaye alichukua asilimia mia moja katika moyo wake? Ni vipi ataweza kuitumia bastola kumlenga huyu mwanaume? Ni vipi angeweza kukiruhusu kidole chake kutekenya kitufe kuruhusu risasi imuue Masimba? Ni vipi pale atakapoiona Risasi ikimtupa masimba chini huku damu zikisambaa? Hapo akauona ugumu, ugumu wa kufanya kile ambacho alitaka kukifanya, lakini vilevile aliyafikiria mabilioni ya shilingi. Kwa mara nyingine akakiona kichwa chake kikitaka kupasuka. Lakini mpapaso wa mikono ya masimba ukamfanya teddy aachie mguno. Mpapaso ambao ulipanda mpaka kwenye kifua chake kilichobeba viazi vidogo. Mikono hiyo ikatulia hapo kwa muda ikitomasa na kuchezea kwa ustadi mkubwa. Hilo likaanza kumlegeza teddy, likamuacha teddy akisinzia na kulegea. Masimba akamgeuza na kufanya wote watazamane. Watazamane katika namna ya kuhitajiana. Jicho lilikuwa usingizini na hata midomo ikawa tayari kupokea zawadi. Wakatizamana zaidi, muda huu nguo zilikuwa zikitupwa chini baada ya kuvuliwa. Bastola ilianguka pasipo hata teddy kugundua. Alikuwa akihema kama mwizi, alikuwa akihema kama ametoka kukimbia mbio ndefu. Hakuwa teddy yule aliekuwa ameapa kumpoteza masimba. Hakuwa teddy yule mwenye uwezo wa kunyoosha mkono kumuua masimba. Huyu alikuwa kondoo, kondoo anayetii mamlaka ya bwana. Akasogezwa kitandani, hata yeye mwenyewe akasogea, akakalishwa kitandani, hata mwenyewe akakaa, na hata kulala, akalala huku macho yake yakiwa yamefumbwa na kufumbika. Midomo bado ilihitaji kupokea kitu, kitu ambacho kingeianzisha safari nyingine. Ilikuwa hivyo.



*****

Alishtuliwa na mlio wa simu yake, akaupeleka mkono pembeni yake ambapo alikuwa amelala masimba. Lakini akashangaa kutokuwepo kwake. Bado simu yake iliita, lakini aliendelea kuipuuza. Sasa alikuwa akiinuka kutoka pale kitandani na kuelekea kule sebuleni. Akalifunua pazia akidhani atakutana na masimba hapo, lakini hapakuwa na mtu. Hilo likamshangaza tena na tena. Haikuwa kawaida ya masimba kumuacha kitandani. Wakati akiendelea kuumizwa na hilo bado simu chumbani iliendelea kuita. Safari hii mpigaji alikuwa akipiga kwa mara ya tatu. Akakata shauri kurudi chumbani kwenda kuipokea simu hiyo. Akazivuta hatua zake taratibu akiwa mtupu kama alivyozaliwa.akasogea na kuingia chumbani huku mawazo yakiwa ni wapi alipoelekea masimba. Akaifikia simu na kuichukua, macho yakatua juu ya kioo.. akakutana na jina la mtu alieufanya moyo wake upige kwa haraka. Jimmy Lambert ndiye aliekuwa akiipiga simu. Akakipeleka kidole chake na kupokea simu.



"Jimmy." Aliita tedy kwa sauti ndogo yenye kuonyesha uchovu.



"Vipi umelala au?" Lilikuwa swali kutoka kwa Jimmy.



"Yeah! Nilikuwa nimelala, kuna lolote? Alijibu kisha kuuliza.



"Naomba Uje Tegeta muda mfupi ujao, kuna mtu nataka mkutane, mfahamiane na mtambuane. Tumeona tukutafutie mtu wa kusaidiana naye." Alijibu Jimmy kisha akakata simu bila kusubiri jibu kutoka kwa Teddy. Hilo la kutafutwa kwa mtu likaupa mashaka moyo wake. Ni kweli pesa alizitaka na kuzihitaji. Ni kweli anampenda masimba kuliko maelezo. Lakini hata kama atamuua masimba, wapo wanaume wengine ambao watamuoa. Kinachotakiwa ni kupanga njia ipi sahihi ya kumuua. Kwa mara nyingine roho yake, akili yake ilikuwa tayari tena kumuua masimba. Alikuwa amedhamilia na alikuwa ameamua kumpoteza. Alichokifanya ni kujiandaa kwa safari ya kuelekea huko tegeta huku akiwa na nguvu na maamuzi sahihi.



Wakati yeye akitoka na kulifunga geti, masimba alikuwa nyumba ya tatu kutoka pale. Alikuwa amesimama hapo kwa muda mrefu akitizama kila kitu ambacho kiliendelea pale. Muda mfupi akamuona mpenzi wake akilifunga geti na baada ya hapo akamuona akiondoka pale kwa kutembea kwa miguu. Bado alitulia akiendelea kuangalia kila kitu ambacho kilikuwa kikitendeka pale. Bado mpenzi wake aliendelea kutembea akielekea kituo cha daladala. Hilo pia lilimpa nafasi ya kumfuatilia pasipokuonekana. Simu ilikuwa sikioni akiwasiliana na vijana wake, alikuwa akiwaeleza kila kitu cha kufanya. Aliwaaachia wao kazi ya kumfuatilia Teddy. Alichokuwa akipokea ni maelezo ya nini kinaendelea katika hilo.



******

Teddy alitembea mpaka kituo cha daladala, alipofika hapo akatulia akiangaza macho yake huku na huko. Alikuwa ametulia kwa muda akitizama kila mienendo ya watu. Alikuwa na hisia za kufuatiliwa, lakini kila alipopitisha macho yake sehemu zote, hakuweza kumuona mtu ambaye labda angepata mashaka naye. Baada ya kuhakikisha hilo, akaingia kwenye daladala na muda mfupi gari likaondoka likielekea Tegeta. Ilikuwa safari ambayo kwake ilikuwa muhimu sana. Walikuwa na mzigo wa mamilioni ya shilingi lakini bado haikuwezekana kuuza kutokana na matukio haya yanayoendelea kutokea hakuwa tayari kuiacha pesa ile kwa sababu ya mwanaume. Moyoni alijisemea kwamba labda angekuwa mama yake ndipo angefanya hivyo. Wakati akiwaza hakujua kwamba kuna watu walikuwa siti ya nyuma yake wakimtizama. Walikuwa vijana wawili wadogo kiumri, vijana ambao kwa kuwaona ungedhani labda ni wanafunzi wa sekondary. Lakini haikuwa hivyo, hawa walikuwa vijana kutoka kitengo nyeti katika nchi hii. Walikuwa wakiendelea kuzungumza hili na lile, huku mara moja moja wakimtupia jicho mwanadada huyu. Kilikuwa kitu kizuri sana kumfuatilia mtu ambaye hajui kuwa anafuatiliwa. Gari ilipofika tegeta kwa ndevu vijana wale wakasimama tayari kwa kushuka. Hata teddy naye alikuwa akishuka hapo. Alitangulia yeye kushuka, kisha wakafuatia wao kushuka. Baada yakushuka vijana wale wakangoza kuelekea barabara fulani. Hata teddy alikuwa nyuma yao akifuata barabara ile. Hakujua kuwa waliombele yake hawakuwa mabishoo kama alivyodhania, bali walikuwa makachero wakifuatilia kila hatua yake na kila kitu anachokifanya.



Hakujua kuwa alikuwa njia moja na wanausalama. Hakujua kuwa vijana waliombele yake walikuwa wanausalama, tena wakimfuatilia yeye. Bado aliongoza akitembea kwa umakini, akichungulia na kuangalia kila sehemu kwa chati. Alikuwa tayari kumuua mwanaume anayempenda kwa sababu ya pesa. Licha ya kuwa tayari lakini hakuujua mwisho wa mambo yale utakuwa nini. Kingine kilichomtatiza ni mtu ambaye ameambiwa kuwa ameongezwa katika kazi ile ya kumfuta masimba katika uso huu wa dunia. Kilikuwa kitu kigumu mwanzo lakini kila alipokumbuka kifo cha Asteria na Rafiku yake, alijikuta akinong'ona mwenyewe. Muda nfupi baadae alikuwa akiingia ndani ya Bar moja maeneo yale ya tegeta. Baada ya kuingia, akaongoza mpaka moja kwa moja katika vyumba vya eneo lile. Akauendea mlango wa chumba ambacho huwa wanakutaniana. Akaugonga mlango katika namna ambayo ilitambulika ama kuzoeleka miongoni mwao. Mlango ukafunguliwa kisha akaruhusiwa kupita. Alipoingia mlango ukafungwa tena. Macho yake yakatembea usoni kwa kila mmoja, shauku yake ilikuwa ni kumuona mtu ambaye aliambiwa atakuwa nao katika sakata lile. Kila mmoja ndani ya chumba kile alikuwa kimya, ukimya ambao uliyaruhusu macho yao kutizamana. Sura ya mwanamke mrembo ndio sura pekee ngeni ambayo ilimpa majibu kuwa huyu alikuwa ndie mtu alieletewa ili kusaidiana naye. Akasogea macho yake yakilazimisha kutizamana na mwanamke huyu. Alikuwa akifanya hivyo kutaka kujua kama huyu mwanamke atakuwa mmoja kati ya watu wa aina yake. Ni kweli walitizamana, ni kweli waliangaliana na kuangaliana tena na tena. Lakini hakufanikiwa kukiona kile alichokuwa akikitafuta. Macho ya mwanamke huyu hayakumuonyesha kile alichokuwa anakitafuta. Hayakumjulisha kama yeye alikuwa nani. Bado yalikuwa macho ya kulegea, macho ya kusinzia na kibaya zaidi hayakumuonyesha chochote kile. Hilo likaonyesha kumpa mashaka. Akatafuta mahala puzuri na kukaa. Bado macho yake hayakuacha kuonyesha mashaka. Bado hakumuamini mwanamke yule. Ndio alikuwa mrembo, ndio alikuwa mzuri na alivutia katika kutizamwa na hata kuwekwa ndani na wanaume. Lakini licha ya uzuri huo bado hakukiona kile ambacho kingempa picha, picha kwamba anaweza kuzimudu kashkash zote za wanausalama. Akauvuta muda huku akimtizama Jimmy na wengine waliokuwepo pale ndani. Alitaka kusikia kutoka kwake, alitaka kusikia kwamba huyu ni nani, na ni vipi atamudu kupambana na masimba. Jimmy ni kama aliyasoma mawazo ya Jenipher. Akasimama kutoka pale alipokaa kisha kupiga hatua kusogea mpaka pale alipokaa Jenipher. Akamuangalia kwa muda kisha akanena.



"Nimekuletea Shetani yule akusaidie kumuondoa masimba katika uso wa dunia hii.." yalikuwa maneno yaliozunguka kichwani kwa teddy. Hakuuamini ushetani wa mwanadada yule. Alimuona ni kama wadada wa mjini na asingeweza chochote.



"Jimmy unadhani ataiweza hii kazi? Tambua tunachokifanya ni kazi ya kifo. Na hii kazi tunaifanya kwa siri sana. Pia tambua watu tunaopambana nao hawana masihara. Una uhakika yule mrembo ni shetani kweli?" Aliongea Jenipher akionyesha kuwa na mashaka.



Tabasamu likachanua usoni kwa Jimmy, kisha likafuatiwa na kicheko, kicheko ambacho kilitumika kama jibu kwa maswali ya Teddy. Wote wakasimama kwa pamoja kisha kushikana mikono. Mkataba ukaingiwa na makubaliano kufikiwa. Kilichobaki ilikuwa kazi ya kumuondoa Masimba, kisha wabia wenzao, harafu kugawana mzigo wao.



********



Wakati Vijana Wake wakiwa tegeta, masimba ndio kwanza alikuwa akiiisimamisha gari mtaa wa pili kutoka nyumba anayoishi Jimmy. Baada ya kushuka akaufunga mlango. Baada ya kuufunga mlango akaangaza huku na huko, aliporidhika akatembea bila wasiwasi kuelekea ilipo nyumba ya Jimmy. Hakuwa na wasiwasi juu ya kuingia katika jumba hilo kwani vijana wake walikuwa wakimpa taarifa za kile kilichokuwa kikiendelea kule tegeta. Alijua ndani ya muda huo alikuwa na uwezo wa kuingia na kutoka pasipo wasiwasi wowote. Alitembea kama mwananchi wa kawaida akiangalia hiki na kangalia kile. Mtaa wote ulikuwa kimya, hapakuwa na watu ambao wangemsumbua ama kumtilia mashaka. Mzigo umekamatwa na kutangazwa katika vyombo vya habari. Lakini cha ajabu mzigo huu unaonyesha kutokukamatwa, unaonyesha kuna mchezo nyuma ya sakata hilo. Nani yupo nyuma ya jambo hili? Ndio kitu peke ambacho alijiuliza masimba pasipo kupata majibu. Akaendelea kutembea huku mazingira yakimpa uhuru wa kufanya kitu. Sasa alikuwa akiangaliana na jumba la Jimmy Lambert. Lilikuwa jumba la kifahari, likiwa limezungushiwa Uzio, uzio ambao ulikuwa mrefu kiasi chake. Ukiondoa hilo pia jumba hilo lilizungushiwa nyaya maalum za umeme ambazo zilisaisia kuongeza usalama wa jumba lile. Pia licha ya hivyo vitu, lakini pia hapakuwa na walinzi. Mlinzi alikuwa mmoja ambaye alikaa kwenye geti la mbele. Baada ya kuliangalia vyakutosha sasa aliamua kuingia ndani. Huyu aliamulia kuingia katika Geti la mbele. Akasogea akitembea kawaida sana. Mlinzi wa kampuni binafsi alikuwa mlangoni mkononi akiwa ameshikilia bunduki aina ya gobole. Masimba akasogea zaidi na zaidi mpaka karibu kabisa na mlinzi yule. Kabla hajazungumza naye chochote, Masimba akachomoa simu kisha kumpa mlinzi yule. Mlinzi akasita kwanza kuipokea. Akamwangalia mtu huyo usoni, mtu ambaye alikuwa akimpa simu pasipokuongea naye chochote. Macho yake yakakutana na tabasamu, tabasamu ambalo liliitoa hofu ya mlinzi yule.



"Ongea Na Jimmy Lambert ana maagizo anataka kukupa." Akaingea Masimba pasipo masihara. Mlinzi yule akalifanya kosa la kupiga hatua kumsogelea Masimba. Hakufanikiwa kusogea tena kwani pigo moja la karate likatua Shingoni. Mlinzi akatambarajika chini. Akamvuta na kumuweka kando ya maua ya jumba lile. Alipohakikisha hawezi kuonwa na watu, alilisukuma geti na kujitoma ndani. Alitembea kwa tahadhari kubwa mpaka uani mwa jumba lile. Akasimama hapo akiangalia zilipo camera za usalama za jumba la Jimmy. Baada ya kuhakikisha hamna chochote kile, akachomoa funguo zake malaya kisha kuichomeka sehemu, punde mlango ulikuwa ukifunguka na kumruhusu Masimba Kuingia. Baada ya kuhakikisha ameingia, masimba akaichomoa bastola yake na kuanza kuingia kila sehemu akipekua. Kwa kuwa alikuwa akipewa taarifa na vijana wake juu ya uwepo wa jimmy na washirika wake, hakuwa na wasiwasi katika kupekua. Alifungua vyuma karibia vyote kwa kutumia funguo malaya na kuvipekua. Hakuweza kupata kitu chochote. Wakati anaingia kwenye chumba anacholala jimmy, ndipo hapo alipouona mlango mdogo, mlango ambao alizani labda ni wachoo ama bafu.. lakini alipoutingisha ulikuwa mgumu na haukuwa unafunguka kwa Funguo Malaya.





Mlango ulikuwa mgumu na haukuweza kufunguka hata kwa funguo malaya. Hilo likamfanya masimba atulie kwanza. Alitulia akiwaza ni kipi cha kufanya ili kuufungua mlango. Akawaza na kuwazua huku akijaribu mara kwa mara kuufungua mlango. Lakini bado mlango ulikuwa mgumu kufunguka. Akaachana na kimlango hicho kisha kuiendea droo ya kitanda. Hapo pia akatumia funguo malaya kufungua, safari hii alifanikiwa. Baada ya kuifungua droo ile, akayatupa macho yake kwa chati ndani yake. Cha kwanza kukiona zilikuwa funguo kama tano, funguo ambazo mara moja alitambua kuwa ni zile ambazo huwenda zinatumika kuufungua mlango ule. Akazitwaa kisha kurudi pale mlangoni. Zoezi la kufungua likaanza tena. Safari hii haikumchukua muda, kimlango kile kikafunguka.. macho yake yakapokewa na mabegi matano, mabegi ambayo aliyatambua kuwa ndio ule mzigo ambao ulitangazwa kukamatwa uwanja wa ndege. Kichwa chake kikachemka kwa haraka sana, alitakiwa kuondoka na mabegi yale katika muda ule. Alitaka kuliacha hili suala katika kutuhumiana wenyewe kwa wenyewe. Lakini kuna kitu kimoja kilikuwa kikimtatiza.. mzigo huu usingeweza kutoka pale airport kwa nguvu ya Jimmy pekee. Jimmy hakuwa na uwezo wa kuishawishi Idara ya Usalama pasipo kuwepo kwa msaada wa mtu mwingine hapa. Mtu huyo ni nani? Lilikuwa swali pekee lililosumbua kichwani mwake. Alitambua lazima kuna uwepo wa mtu tena mkubwa sana katika sakata lile. Kwa mara ya kwanza majukumu yakaendelea kuongezeka. Sasa alikuwa akimuhitaji huyu mtu wa tatu. Lakini pia alitambua ahadi ya kupigiwa simu na mwanamke yule mrembo. Baada ya kufikiria kwa muda mrefu pasipokupata majibu sahihi, akaona huu ulikuwa wakati wa kuondoka pale ndani, lakini akajiapiza kwamba ni lazima atoke pale akiwa na mzigo ule. Akavuta begi la kwanza kisha la pili, alipotaka kuvuta begi la tatu, masikio yake yakainasa michakato ya miguu ya mtu, ikionyesha kusogea pale mlangoni. Masimba akainuka haraka na kujisogeza pembeni kidogo ya mlango. Punde akauona mlango ukifunguliwa kisha mdomo wa bastola ukatangulia Mbele, bado akaendelea kutulia, hata mtu yule alipoingia bado hakujitoa pale. Alitaka kumfahamu huyu alikuwa nani.akamsubiri mtu yule aurudishie mlango ndipo amkabili. Hilo likafanyika, muda mfupi mtu yule alikuwa akitizamana na mdomo wa bastola huku macho yasio na mzaha yakimtizama. Mtu yule hakulitegemea hilo, akajikuta akiupoteza umakini, sasa alikuwa akitetemeka. Hakuonekana kama ni mjuzi katika misukosuko, bali huyu alionekana kuwa mgeni katika medani hii ya mapambano. Masimba akaendelea kumtizama huku bastola yake ikiwa imelengwa kwenye paji la uso la mwanaume yule. Mara tukio la ajabu likatokea, tukio ambalo lilimfanya masimba aamini kuwa huyu mtu alikuwa mbwa koko. Mkojo ulikuwa ukimtoka na kulowanisha mavazi yake. Hilo lilimfanya masimba apange kumtumia katika kuyaondoa mabegi katika chumba kile. Punde alikuwa akiishusha bastola na kuanza kumtizama mateka wake. Hakuongea naye chochote zaidi ya kumpa Ishara ya kufanya kile ambacho alitaka kukifanya. Muda mfupi walikuwa wakitoka nje huku wameongozana, mateka yule akiwa na mabegi mawili makubwa, hata masimba naye ilikuwa hivyo. Bastola ilikuwa mkononi akimuongoza mtu yule njia za kupita. Wakafanikiwa kutoka getini pasipo na ugumu wowote kwani bado mlinzi yule hakuwa amerudiwa na fahamu. Alimuongoza mateka wake mpaka mahali alipoiacha gari yake. Wakapakia mabegi yao na muda mfupi walikuwa wakiondoka hapo kwa pamoja huku bado bastola ikizigusa mbavu zake.



******

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ilikuwa yapata majira ya saa nne usiku wakati Teddy akiwa njiani kuelekea kimara nyumbani kwa dada wa Asteria tayari kwa kwenda kuifanyakazi. Wakati anayavuka mataa ya ubungo, simu yake ya kiganjani ikawa inaita. Akasonya huku akiitoa simu yake kutoka mfukoni. Jina la Jimmy likasomeka kwenye kioo cha simu yake. Haraka akapokea na kuipeleka simu sikioni.



"Rudi mikocheni Haraka." Baada ya maneno hayo simu ikakatwa, rudi mikocheni haraka kisha simu kukatwa ni kitu ambacho kilimchanganya akili yake. Atumwe akawaue ndugu wa Asteria, wakati bado hajakamilisha hilo aambiwe arudi mikocheni tena! Ulikuwa ujumbe ulioonyesha hapakuwa na usalama. Akaavunja sheria za barabarani kwa kugeuza gari sehemu ambayo haikuruhusiwa. Watu waliokuwa pembeni mwa barabara sambamba na askari wa usalama barabarani walikishuhudia kitendo kile kwa karibu sana. Hata walipomsogelea kutaka kumsimamisha, Teddy akawapelekea gari kwa kasi sana, askari wakaruka na kuangukia pembeni. Teddy akakanyaga mafuta gari ikawa inatembea kwa mwendo wa hatari. Kila mmoja alikuwa akiiangalia gari kwa mshangao. Wengine waliahangilia na hata kupiga miluzi, lakini wachache walilaani huku wakitukana matusi mazito. Teddy hakusikia ndio kwanza alikuwa akiipita Changanyikeni na sasa alikuwa akiitafuta mwenge. Kila mmoja aliekuwa akiitizama gari ile ilivyokuwa ikiendeshwa, alifumba macho akiogopa kutizama. Wakati anafika maeneo ya Mwenge mataa, mbele yake akakiona kile ambacho kilimfanya aupunguze mwendo. Mbele yake kurukuwa na diffender tano za palisi na Askari wasiopungua Ishirini, kila mmoja akiwa na Sub Machine Gun akiwa ameilekeza kule lilipo gari la TEddy. Amri ikatolewa akitakiwa kushuka akiwa amenyoosha mikono juuu.. Teddy akatii huku bastola akiiacha ndani ya gari. Aliposhuka chini tu huku akiwa amenyoosha mikono askari wengi walimtambua kuwa alikuwa ni mwenzao, lakini licha ya kumtambua huko hawakuacha kumuuliza hili na lile. Baada ya kama dakika tano walimuachia na kumtaka kuwa muangalifu.



********



Alisimamisha gari nje ya jumba la Jimmy, akashuka na kuingia ndani. Hapo akapokelewa na mwili ambao haukuonekana kama una Uhai. Mbele yake alisimama Jimmy sambamba na washirika wao kila mmoja akionekana kuchanganyikiwa. Tedy bado hakuwa amekielewa kile kilichokuwa kikiendelea humo ndani. Hata pale alipoambiwa aingie chumbani hakuwa bado anatambua kile ambacho kimetokea. Alipoingia chumbani kisha kutupa macho yake pale kwenye hazina yao, Teddy akaporomoka chini akiwa ameishiwa nguvu. Mzigo wao wao wa Mamilioni ya Shilingi ulikuwa umetoweka. Mzigo uliomfanya awe tayari kumuua Mpenzi wake haukuwepo tena. Mzigo uliomfanya amuue Asteria haukuwepo tena. Umeenda wapi? Nani amewazunguka? Masimba? Hapana!! Juma Kitumbe? Inawezekana!!! Yalikuwa mawazo yaliopishana kichwani mwake. Alipoinua kichwa kuwatizama Wenzake, alijikuta Akitizamana na Midomo Miwili Ya Bastola.



Alikuwa akitizamana na midomo miwili ya bastola. Washikaji wakiwa katika umakini wa hali ya juu. Teddy hakuamini kile alichokuwa akikitizama. Akataka kujaribu kumuuliza Jimmy kinachoendelea, lakini sauti haikutoka, akabaki akiitizama midomo ya bastola ambayo ilikuwa umbali mfupi kutoka usawa wa paji la uso wake. Akili yake ikaganda, ikashindwa kufanya kazi kwa wakati, mzigo umepotea, harafu tena anashikiwa bastola! Hilo likamchanganya kama sio kumshangaza. Akakitamani kitendo kile kiwe ndoto, lakini bado haikuwa hivyo. Mzigo haukuwepo na kibaya zaidi alikuwa akitizamana na midomo ya bastola. Akainamisha kichwa chini akijaribu kukiamini kile kinachoendea pale. Kwa mara nyingine akainua kichwa kutizama tena, lakini safari hii hakukiona kile ambacho alikiona mwanzo. Hakuwa akitizamana tena na midomo ya bastola, hapakuwepo na watu wawili waliokuwa wameshika bastola. Walipotea na kutokuonekana kabisa. Mbele ya macho yake alisimama Jimmy pekee. Hata Jimmy hakuwa yule wa tabasamu. Huyu alionekana kuchanganyikiwa na hata kukata tamaa. Uso ulikunjamana kwa hasira, sasa alikuwa akimtizama Teddy kwa macho yake makali. Uso wake ulikuwa ukiongea kifo, macho yake yalikuwa yakiitangaza shali. Kila alipokuwa akimuangalia Teddy mishipa ya hasira ilikuwa ikizidi kuharibu taswira yake. Alikuwa akihitaji kuongea na Teddy. Alitambua teddy hakuwa mhusika wa kilichotokea, alimjua tena na pia aliufahamu uaminifu na hata msimamo wake. Asingeweza kukifanya kile. Hilo likampa ugumu kuongea, kitendo cha watu wao kumnyooshea Bastola kilimpa wakati mgumu sana. Alimjua fika katika medani ya mapambano, alimjua fika katika medani ya mapigano, huyu alikuwa ni zaidi ya Jean Claude Van Damme na hata zaidi ya Don Yen na Hata Jet lee. Kitendo cha kumnyooshea bastola ni kumkosea sana. Hilo likamfanya Jimmy awe mnyenyekevu mbele ya mwanadada huyu. Lakini kile alichokitegemea hakikuwa hivyo.uso wa teddy haukuwa katika masihara tena, alimuangalia Jimmy kwa macho yenye maswali lukuki. Akatamani kuongea neno moja lakini hakuipata nafasi hiyo. Teddy alisimama na kupiga hatua bila hata kumuangalia Jimmy. Alitembea akitoka katika jumba lile akiwa ni mwenye hasira sana. Aliuhisi mchezo mzima kuchezwa na watu wake hao ili kumzunguka. Hilo hakuwa tayari kuliona likitokea. Alikuwa tayari kumuua yoyote katika hilo. Alishakubali kumuua masimba sababu ya mzigo ule, sasa kwa nini hawa wanataka kunizunguka?

Lilikuwa swali ambalo lilikivuruga na kukichanganya kichwa cha teddy. Bado Jimmy hakuweza kuongea kitu. Bado jmmy alikuwa akimkodolea macho. Teddy akakiinua kichwa chake kwa mara ya pili kisha kumuangalia tena jimmy. Macho yake yalikuwa yakiongea kitu kingine kabisa. Hakuwa teddy yule mrembo na mwenye tabasamu, huyu alikuwa teddy tofauti kabisa. Bado hakuyaondoa macho yake usoni kwa Jimmy. "Huu ndio Wema wangu? Haya ndio malipo ya kuwasaidia mzigo wenu? Umenisahau mimi ni nani? Umesahau kuwa ninauwezo wa kuwaua kwa muda mfupi tu? Sasa naomba uniambie ukweli, nataka kuujua mzigo uko wapi na nani ameuondoa hapa. Usipokuwa mkweli maiti yako itakutwa humu ndani. Aliongea teddy akimuangalia jimmy pasipo kupepesa macho bastola ikiwa mkononi. Jimmy alijikuta midomo ikimkauka, akajikuta mate yakishindwa kupita kooni. Alimtizama teddy machoni kwa muda mrefu akitamani kuongea kitu. Hakupata neno la kuongea, alijikuta akianza kutetemeka. Jimmy leo alikuwa akimuogopa teddy.



Akaona kukaa kimya kutasababisha makubwa. Kwa sauti ya uoga akaanza kuelezea kila kitu tokea waliporudi na kuikuta maiti ya mlinzi, akaeleza walivyoingia ndani wakishuhudia mzigo wao ukiwa haupo. Hakuficha chochote kile. Baada ya Jimmy kumaliza kuongea teddy hakuongea kitu. Alipiga hatua mpaka nje pale ulipolazwa mwili wa mlinzi yule. Akaufunua na kuuangalia kwa makini. Cha kwanza kukiona ni jeraha shingoni kwa marehemu yule.



"Masimba!" Lilikuwa neno pekee kutoka kwa teddy. Hili likamfanya jimmy aliekuwa amesimama nyuma kidogo ya teddy asogee na kuonyesha kushangazwa. "Masimba aliingia hapa na ndiye aliefanya hiki kitu. Na kama kweli ni yeye alieuchukua mzigo, itabidi uwasiliane na mwamvita muda huu, ili watakapo kutana ajue anatakiwa kufanya nini." Aliongea teddy akitoka pale akionyesha ni mwenye mawazo.



*********

Ulikuwa usiku wa saa mbili na nusu pale simu ya Masimba ilipotoa sauti kuonyesha kulikuwa na ujumbe mfupi wa maneno. "Upo wapi Masimba? Uliuliza ujumbe ule. Masimba akatulia kwanza kujipa muda wa kufikiria.



"Nipo nyumbani!" Alijibu nakutulia tena.



'Bila shaka utakuwa upo tayari kwa sasa kukutana na mimi?" Ujumbe mwingine ukaonyesha kuuliza.



"Yeah! Naomba tukutane Ngamia Pub kigamboni, nadhani panafaa kwa aina ya maongezi yetu.". Alituma ujumbe huo ambao ulipokewa kwa ukimya wa muda mrefu. Kwa mtu aina ya Masimba aliutambua ukimya ule. Aliutambua kwa maana moja. Mwanamke yule alikuwa akifanya mawasiliano na watu wengine, watu ambao alitambua lazima watakuwa wameshaanza kuelekea sehemu ya mkutano wao. Hakuwa na shaka kwa kuwa Charty John alikuwepo sehemu ya tukio akimuangalia kila aingiaye na kutoka. Hakuwa na shaka kuhusu hilo.



Muda mfupi alikuwa akiingia maliwatoni, akajimwagia maji, kisha kutoka na kuyaendea mavazi yake. Baada ya kuvaa na kujiangalia akachukua bastola zake mbili revolver colt na dernng up automatically na kuziweka sehemu yake. Baada ya kumaliza hapo akaweka vitu vyake sawa pale ndani. Muda mfupi alikuwa akiliacha jumba lake akielekea sehemu ya tukio akiwa katika tabasamu la aina yake. Siku zote alipenda kucheza na watu wa aina yake, alipenda kucheza na watu walioupenda mchezo ule. Alitaka kumalizana na hawa kisha kurudi kwa teddy. Alitaka kumfanya kuwa wa mwisho.



*****



Sehemu kubwa ya eneo hili la mjimwema lilikuwa limechangamka watu wakionyesha kuifurahia siku hii. Muziki ilikuwa ukisikika, muziki ambao ulikuwa ukiwa burudisha vijana kwa wazee. Sehemu yote ilikuwa katika hali ya kupendeza na hata kuvutia. Charty alikuwa pembeni kabisa macho yake yakiwa busy kutizama kila tukio linaloendelea hapo. Muda mfupi akaiona gari aina ya Toyata ikisimama eneo la maegesho. Macho yake yakavutiwa na watu walioshuka kwenye gari ile. Hayakuvutiwa kwa uzuri wa mavazi yao ama sura zao, bali alivutiwa kwa kuwa ndio wale aliowaona mchana wakimfuatilia masimba. Hilo likamuweka kwenye utayari. Muda mfupi akamuona mwanamke yule akiingia pale, alikuwa katika mavazi ya aina yake. Sketi fupi ilioishia juu ya magoti kwa juu kabisa. Sketi ya kubana na kusababisha mistari ya chupi aliovaa kuonekana kwa uwazi zaidi. Wateja wote wakageuka kutizama kule alipokuwa akitokea mwanamke yule. Miluzi ikasikika na shangwe kutamalaki. Wakati mwanamke yule akiendelea kuwahenyesha wanaume na kuzivunja shingo zao, masimba ndio kwanza alikuwa akiwasili eneo la tukio, bastola mbili zikiwa kiunoni, akitembea kuelekea pale pale.



Wakati masimba akishuka eneo la Ngamia Pub, macho yake yalikuwa yakiangaza huku na kule kuangalia nani na nini walikuwa wakimtiza. Kila aliemuona alikuwa kwenye mambo yake, hakuna ambaye alikuwa akimtizama. Hilo halikumfanya ajiamini kabisa, bado akatembea akiangalia huku na huko. Hata pale macho yake yalipomuona mwanamke mrembo alieketi pembeni, bado masimba hakuvutika kumtizama. Macho yake yalikuwa yakitizama upande mwingine kabisa. Hakutazama huko kwa makusudi, bali alikuwa akimtizama mtu ambaye alikuwa akimfananisha. Alifanana kabisa na mpenzi wake, alifanana kabisa na teddy. Akahitaji kufanya kitu ambacho kingemuaminisha kwamba mtu yule alikuwa mpenzi wake. Kengele ya tahadhali ikagonga kichwani pale alipowaona watu watatu wengine wakimtizama. Tabasamu mubashara likachomoka usoni kwake, halikuwa tabasamu la kufurahi wala kuwavutia wasichana waliojazana pembeni. Hili lilikuwa tabasamu la kukubali kile ambacho alikiwaza. Kile ambacho alijua lazima kitendwe na yule mwanamke. Alitambua baada ya kuwasiliana na kumwambia sehemu ambayo wangekutana, ni lazima naye angeisambaza taarifa ile. Hilo aliliamini na hapa alikuwa akilithibitisha. Vichwa vitano vilivyokaa sehemu tofauti vilikuwa vikimtizama yeye. Vikimuangalia na hata kumshuti basi wangefanya hivyo. Akaendelea kusogea akimuangalia yule mtu anayefanana na mpenzi wake. Ni kweli alikuwa teddy, ni kweli alikuwa yeye! Kwa nini yeye? Kwa nini hapa muda huu? Yupo kwenye hili? Hilo likamshangaza tena na tena. Lakini kwakuwa alikuwa na watu wake eneo lile, alijua kila kitu kingewekwa wazi, ingawa hakupewa taarifa ya uwepo wa Teddy, hilo halikumsumbua kwa kuwa alimjua teddy. Aliutambua uwezo wake wakijasusi, alitambua uwezo wake wakujibadilisha. Hilo halikumfanya Awalaumu vijana wake.



Akaifikia meza ambayo ilikaa mwanamke yule. Hakusubiri kukaribishwa, bali alivuta kiti na kukaa.



"Bila shaka sikatazwi kukaa hapa!" Aliongea huku akimtupia mwanamke yule jicho. Bado akakutana na jicho lile lile la ulaghai, jicho ambalo bado liliendelea kumdanganya Masimba. Jicho la usingizi, jicho la kuvutia na hata kubadilisha mtazamo wa watoto wakiume.



Kabla hajajibu, akaliachia tabasamu, tabasamu ambalo liliendelea kuufanya uso wake ung'are na uzuri kuongezeka.



"Sio hapa tu, hata nyumbani, tena chumbani kabisa ungekaribishwa." Akajibu mwanamke yule akiendelea kutabasamu.



"Kumbe hata chumbani nakaribishwa, kwanini tumekuja hapa? Akauliza masimba huku macho yake yakiendelea kutembea usoni kwa mwanamke huyu. Kuna kitu alikuwa akikitafuta, lakini usoni kwa mwanamke huyu bado hapakuonekana kile ambacho alikuwa akikitafuta. Sura ya mwanamke huyu ilipambwa na uzuri wa haja, uzuri wa kuvutia na kuwavutia wengi.



"Nimekuita hapa ili tufahamiane, pia kuna mawili matatu nahitaji tuongee!" Baada ya maneno hayo, mwanamke yule akaonekana kuwa tofauti, safari hii hapakuwa na tabasamu wala mbwembwe. Uso wake ulikuwa uso wa kazi. Hilo likamfanya Masimba naye abadilike. Lakini ubadilikaji wake haukuwa ubadilikaji ule. Huu ulikuwa ubadilikaji wa kuiteka akili ya mwanamke yule. Wakatizamana kwa muda kila mmoja akitafuta kilichopo ndani ya mwenzake.



"Naitwa Mwamvita Rajabu, ni ndugu wa binti alieuawa juzi usiku. Nimekuja hapa jijini leo asubuhi kufuatilia kile ambacho kimesababisha kifo cha ndugu yangu." Aliongea mwanamke yule huku akiendelea kuivaa sura ya Huzuni. Licha ya sura hiyo lakini kwa Masimba bado sura ile haikuwa katika huzuni hiyo, bali ilikuwa katika huzuni ya kulazimishwa.



'"Wewe ni Polisi, afisa usalama ama? Na kwa nini umeniona mimi pekee ndiye wakuongea nawe? Sasa aliuliza masimba safari hii ikiwa makini kumuangalia mwanamke yule usoni. Bado sura yake iliendelea kuwa na huzuni, lakini kitu kingine mwanamke yule alikuwa kimya akionyesha kupatwa na huzuni zaidi. Kwa jasusi aina ya masimba hakuwa mgeni wa mbinu zile, hakuwa mgeni kwa kuwa alijua mwanamke yule hakuwa na jibu kwa wakati ule. Ukimya wake haukusababishwa na huzuni bali swali aliloulizwa halikuwa na majibu. Safari hii mwanamke yule akainua uso wake na kumwangalia masimba. Hata macho yao yalipokutana, safari hii Masimba alikiona kile ambacho alikuwa akikitafuta. Macho yao yalikuwa yakielezana kwamba wote ni watu katika fani moja. Wote walikuwa majasusi wa kiwango cha hali ya juu.



"Nadhani umenitambua sasa, nadhani ulichokuwa unakitafuta umekiona." Akaongea mwanamke yule akiendelea kumuangalia masimba.



Tabasamu likachanua usoni, tabasamu ambalo lilifuatiwa na kicheko. Hakikuwa kicheko cha furaha, hiki kilikuwa kicheko cha ushindi. Ni rahisi kumuua adui unayemjua kuliko usiemjua. Kitendo cha mwanamke huyu kuongea kile alichokuwa anakitafuta kikampa kuamini kwamba hata huyu ni mmoja wao.



"Yeah! Nimekiona na nimepata majibu. Lakini bado hujaniambia wewe ni nani? Na umeniita hapa kutaka nikujue ama kuniambia ulichoniitia? Safari hii masimba aliongea kwa ukali huku macho yako ya kibadilika.



"Hupaswi kujua masimba, hupaswi kunijua. Lakini nakuomba uachane na hili ulilolianzisha. Hutafika popote masimba." Safari hii aliongea akichezesha midomo.



"Bahati mbaya aliekuelekeza kwangu amekosea. Kamwambia mimi huwa sitishwi na wala siogopagi. Sitaacha na sitarajii kuacha, lakini nadhani leo kuna kitu umesikia. Basi ile ni kazi yangu mimi." Alijibu masimba kwa kejeli. Alishajua adui zake washakuwa waoga, wameshaanza kumhofia. MASIMBA akasimama na kuanza kuondoka eneo lile. Alimuacha mwanamke yule akijisonya, akitamani kumlipua.. lakini haikuwa amri kwa siku hiyo.

[16:28, 13/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU



SEHEMU YA 013



Akamuangalia masimba alipokuwa akiondoka katika eneo lile, akatamani kuichomoa bastola yake ili ikiwezekana airuhusu risasi, lakini hakutaka kufanya hivyo kwa kuamini kuwa masimba hawezi kuwa pale peke yake. Akashuhudia akitembea na kupotelea katika upeo wake. Kuondoka kwa masimba kukampa nguvu ya kuamini kuwa masimba hakuwa mtu wa kutishwa. Aliamini hilo baada ya maneno yake. Akatamani kusimama kuwapa ishara watu wake ambao walikuwa katika maeneo tofauti. Lakini bado alisita akiamini kuna macho yapo mahali yakimtizama kwa kila alichokuwa akikitenda. Akajipa uvumilivu huku akishusha kinywaji kinywani. Masimba baada ya kuachana na mwanamke yule alitembea akitoka eneo la pub ile. Macho yake bado yalikuwa yakiangaza kuhakikisha kama kwelu mwanamke aliyekaa pembeni kabisa mwa Pub ile alikuwa Mpenzi wake. Lakini safari hii macho yake hayakumuona Teddy, hayakumuona mwanamke ambaye alidhani ni Mpenzi wake, bali yalimuona mtu mwingine, tena mwanamke harafu alikuwa amevaa mavazi kama yale yale aliokuwa amevaa Teddy. Hilo likampa tafsiri kwamba ulikuwa mchezo, ulikuwa mchezo ambao ulichezwa kwa kipindi kile. Ni kweli mwanzo alimuona Teddy, nikweli alikuwa na uhakika huo, lakini cha ajabu safari hii alikuwa akimuona mwanamke mwingine, mwenye sura nyingine, lakini alievaa mavazi yanayofanana na yale aliovaa Mpenzi wake. Lakini huyu hakuwa teddy! Mshangao kilikuwa kitu cha kwanza kutokea usoni kwake. Akaona ni wakati wakuondoka hapo kwa kuwa alikuwa akihitaji kwenda kuongea na Mama wa Marehemu Asteria, sambamba na dada yake. Akatoka akaelekea sehemu ambayo aliipaki gari yake. Alitembea macho yake yakiangalia kila kitu, hatua kadhaa kabla ya kufika kwenye maegesho ya magari akakiona kivuli, kivuli kuonyesha uwepo wa mtu karibu na alipoipaki gari yake. Kengele za hatari zikagonga kichwani kwake, hakujua kwa nini lakini alijikuta akiushusha mkono wake pale alipohifadhi bastola yake. Hakutaka kukiamini kile alichokiona. Akaendelea kutembea akikiangalia kile kivuli.. lakini kabla hajagundua chochote akausikia mlipuko mkubwa, mlipuko ambao ulisababisha hata yeye kutupwa pembeni kabisa na kuanguka mfano wa furushi. Gari yake na magari mengine yalikuwa yakiwaka moto kuonyesha kuwa alitegewa bomu kwenye gari yake. Eneo lote la mjimwema likawa katika taharuki, watu walikuwa wakikimbia huku na huko kila mmoja akipigania kuiokoa nafsi yake. Sehemu yote ikageuka vilio, iligeuka somalia kwa muda mfupi. Pale alipoangukia masimba ndio kwanza alikuwa akirudiwa na akili zake, alikuwa akifumbua macho huku akijaribu kuvuta kumbukumbu. Kumbukumbu ambayo haikuwezekana kurudi kutokana na mkanganyiko na vilio vya watu. Akatambaa na tumbo mpaka pembeni kidogo. Muda mfupi alikuwa akisimama huku akishuhudia gari yake ikiteketea, gari ambayo alipewa kama zawadi na mwanamke mmoja hivi baada ya kumfanyia kazi yake ipaswavyo.



Bado hakuamini kama amesalimika... akaituliza akili yake, alitaka kuirudisha kumbukumbu kabla ya mlipuko ule. Kivuli cha mtu kilikuwa kitu pekee alichokiona. Kivuli ambacho hakufanikiwa kumuona mhusika halisi wa kivuli kile. Kwa mara ya kwanza akashukuru. Ilikuwa ni lazima aondoke pale, ilikuwa ni lazima apotee hapo, akaipima nguvu katika mwili wake. Alipoiona inatosha akaanza kupiga hatua huku hisia kuwa teddy alikuwa mmoja kati ya wapangaji washambulie lile. Akatembea akijichanganya na watu waliokuwa wakipita katika eneo hilo wakikimbia. Naye alikuwa akikimbia sambamba nao, ni wakati akikimbia ndipo alipomuona tena Teddy akitokea upande ule ambao alikiona kivuli kabla ya mlipuko.. Hata yeye alikuwa akikimbia, hata yeye alionyesha kufadhaika, Alionyesha kutafuta kitu, hakuwa teddy yule kiburi, hakuwa teddy yule gaidi na mwenye usiri. Huyu alikuwa teddy aliechanganyikiwa. Hili likamvutia Masimba kulitizima. Lakini wakati hilo halijafika popote akaishuhudia gari ikisimama pale alipokuwa amesimama teddy. Gari iliposimama milango ikafunguliwa, teddy akaingia kisha gari kuwashwa. Kilikuwa kitendo kilichofanyika kwa sekunde mbili, kitendo ambacho kilimfanya masimba aduwae. Kitendo ambacho kilimpa picha na kumuaminisha kuwa teddy hakuwa Teddy yule walioanzana akiwa ndio kwanya yupo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi. Hakuwa Teddy Yule wa Ifakara, hakuwa Teddy yule mwenye kutangaza mapenzi ya kweli. Huyu sio teddy yule anayetoka Idara ya usalama wa Taifa, hakuwa teddy yule alietoka urusi katika mafunzo ya juu ya Ujasusi. Huyu alikuwa Teddy Muuaji, teddy msaliti. "NITAKUPATA TU" Ndio kauli pekee aliotamka wakati gari ile ikimpita kwa mwendo wa kasi.



*********



Palikuwa na ukimya wa ajabu, ukimya ambao kwa mbali ulikuwa ukiondolewa na mbwa waliokuwa wakibweka. Alikuwa hapo kwa minajili ya kuongea na dada wa marehemu Asteria. Alitembea kama kama kawaida akielekea mlangoni mwa nyumba ile. Muda wote macho yake yaliozoea giza yalikuwa yakiangaza huku na huko. Akaufikia mlango, akasimama kwa muda kisha akaanza kuangalia eneo lote, alipoona hakuna mtu wa kumtilia mashaka, akaugonda mlango kwa mara ya kwanza, hakujibiwa, kwa mara ya pili hapakuwa na majibu tena.. alipogonga kwa mara ya tatu, akasikia nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni, wakati akiusubiri mlango ufunguliwe akashangaa kumuona mtoto mdogo akilia kwa ndani. Hilo hakulitarajia, mkono wake ukashuka na kuichomoa bastola.. kabla hajaingia mlango ukafunguliwa kisha sura ya mtoto mdogo wa miaka kumi alietapakaa damu mwili mzima akatokea. Masimba hakutaka kuuliza, akamuweka mtoto pembeni kisha kuingia ndani, sebuleni akapokelewa na damu iliosambaa kila sehemu, huku miili ya watu wawili ikiwa imelala ikionyesha haina uhai. Masimba akaisogelea miili iliokuwa imelala katikati ya damu. Godfrey Maboba akiwa na mkewe Irene Charles walikuwa wamelala katikati ya dimbwi la damu wakiwa maiti. Walikuwa wamepigwa risasi vifuani mwao. Masimba akainama kwa uangalifu, akawaangalia marehemu. Bado walikuwa wa moto kuonyesha hawakuawa muda mfupi uliopita. Wakati ameinama hapi akakisikia kitu mfano wa chafya, kitu ambacho kilitokea dirishani. Aliujua mlio ule, aliujua haukuwa mlio mwingine bali wa bastola. Masimba akawahi kuchupa huku akisahau uwepo wa mtoto wa marehemu. Wakati anatua nyuma ya kiti pale sebuleni, akajikuta akitua sambamba na mwili wa Mtoto Yule ukiwa hauna Uhai....

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Alikuwa akiitizama maiti ya mtoto yule. Mwili wake ulikuwa na matundu mawili ya risasi maeneo ya kifuani. Alikuwa amelala huku damu zikishuka taratibu ba kuanza kuilowesha sakafu. Masimba akaduwaa kwa muda wa sekunde tano akishindwa kuamini kile anakitizama. Mtoto asiye na hatia alikuwa ameuawa kifo kibaya, kifo ambacho hakupaswa kuuawa hivyo. Hakuwahi kulia na hakuwa mtu wa kulia katika maisha yake, lakini mwili wa mtoto huyu ulimliza na kumuumiza. Macho yake yalikuwa yamemtazama yeye kana kwamba yalikuwa yakimuuliza. Yakimuuliza ni lipi kosa lake ambalo amelitenda mpakq kuuawa, alikuwa akimuukiza kwa nini alimuachia mpaka risasi zile zikapenya? Masimba chozi likadondoka, kiganja cha mkono kikayafunika macho ya mtoto yule. Ndio kwanza akakumbuka kuwa alikuwa mbele ya maiti watatu, mbele ya maiti ya Godfrey Maboba mkewe pamoja na mtoto wao. Mikoni ikawa inamtetemeka huku hasira juu ya watu wale zikipanda. Ni wakati akiendelea kuangalia hapo akashuhudia mlango ukipigwa teke kisha watu zaidi ya kumi wenye silaha nzito wakaingia. Walikuwa ni askari wa kikosi maalum (special forces) askari ambao walikuwa na mafunzo ya kupambana na watu wa aina yoyote. Bunduki zao zilikuwa mbele zikimtizama Masimba. Hawakuonekana kuwa na utani, hawakuonekana kuwa ni wenye masihara. Walionekana walikuwa tayari kufanya chochote. Amri ikatolewa ya kumtaka masimba kutupa silaha yake chini. Hilo masimba akalitii, alilitii huku akili yake akifanyakazi ya zaida. Alijua kikosi hiki kimekuja hapa kwa sababu ya kumuangamiza. Ulikuwa ni mpango ambao umepangwa makusudi kwa sababu ya kumkwamisha. Mpango ambao ulitengenezwa mahususi na mtu mzito katika serikali. Special forces hawawezi kuja sehemu kirahisi, special forces hawawezi kutumwa kwenda kumkamata mtu mmoja. Hata kama mtu mwenyewe ni yeye, special forces hutumika katika sehemu ngumu ambazo sio za kawaida. Sasa nani ambaye ametoa orders ya wao kuja hapa katika jumba hili? Kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, alitambua kuwa lazima ameuziwa kesi ya mauaji. Akaitupa bastola yake chini. Kiongozi wa kikosi kile ambaye alikuwa na cheo cha Luteni Kanali akasogea pale aliposimama masimba. Bado bunduki zilimtizama yeye, bado bunduki zilikuwa zikicheza na mikono yake na hata uelekeo wa macho yake. Kiongozi wa kikosi kile maalum akasogea. Akasogea tena na tena, sasa alikuwa akitizama uso kwa macho na masimba. Punde mkono wa kiongozi yule ukazama mfukoni na kuibuka na pingu. "Wanataka wanifunge pingu? Lilikuwa swali la kwanza kujiuliza. Lakini kabla hajakaa sawa akakisikia kitu kizito kikitua kisogoni. Akaliona giza likiingia machoni mwake, akataka kujizuia asianguke, lakini haikuwa hivyo, muda mfupi alikuwa yupo chini. Hakujua tena kilichoendelea.



*******



Alihisi maumivu makali kichwani hasa upande wa kisogoni. Maumivu makali sana ambayo yalikifanya kichwa chake kionekane kizito. Akataka kuuasogeza mkono wake aguse sehemu ile, lakini alijikuta akishindwa, hakushindwa kwa kuwa mikono haikuwa na nguvu, bali alishindwa kwa kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa pingu. Hilo likamfanya atulie kwanza kuiruhusu akili yake ifanye kazi. Akavuta kumbukumbu ya nini ambacho kimetokea kabla ya kufikishwa pale. Akajaribu kwa muda lakini hakuweza kwa wakati ule. Hakutaka kushindwa katika hilo, akaendelea kukumbuka, punde taswira ya picha ya mtoto mwenye matundu mawili ya risasi ukiwa umelala sakafuni, ikamjia usoni. Taswira ambayo ilimkumbusha mengi sana. Kifo cha Asteria, kifo cha mwamvua, kifo cha dada wa asteria, mumewe pamoja na mwanawe. Maiti za watu wote watano zilikuwa zikipita kichwani mwake. "TEDDY nitakupata tu. Risasi yangu kutoka kwenye bastola yangu lazima ikifumue kichwa chako. Aliwaza huku sauti ya marehemu Asteria Ikiendelea kujirudia. Hapo akakumbuka pale alipowaona Askari wa kikosi maalum wakiingia. Akakumbuka wakati akitizamana na yule Luteni Kanali. Kufikia hapi akakumbuka kila kitu. Akatambua kwa nini yuko pale. Kwa mara ya kwanza akafumbua macho, cha kwanza kukiona baada ya kufumbua ni uzuri wa chumba alichomo. Kilikuwa chumba kizuri sana, chumba chenye upana wa kutosha. Kilikuwa na dirisha kubwa la kioo, dirisha ambalo halikuwa linaonyesha nje. Akageuza shingo akiendelea kukichunguza chumba kile. Macho yake yakanasa kitu mfano wa flash kikiwa kimewekwa juu ya Dirisha. Hakikuwa kitu kigeni kwa mpelelezi kama yeye. Alitambua kuwa zilikuwa camera ambayo ilikuwa ikichukua picha kutoka mle chumbani na kurusha sehemu fulani katika jengo lile. Bado akaendelea kuangalia tena na tena kujua jengo aliyomo liko sehemu gani. Haikuchukua muda kugundua kuwa alikuwa katika chumba cha siri ndani Ya Makao Makuu Ya idara ya usalama wa taifa yaliyopo Kijitonyama. Kwa nini ameletwa hapa? Ina maana hata hawa wenzake wanaamini kwamba amefanya mauaji? Hilo likamchanganya, hilo likamfanya atamani kuonana na kiongozi wake. Lakini hata kama angeonana naye angemwambia nini wakati kazi hii alikuwa akiifanya kwa siri bila kuihusisha Idara? Hapo akauona ugumu, hapo akaiona hatari ya kushtakiwa na kupewa kesi ya mauaji. Akatulia akifikiria nini akifanye.



Dakika kumi baadae akauona mlango ukifunguliwa, kisha watu watatu wakaingia. Hawakuwa wageni kwake. Bali uingiaji wa watu hawa ulizidi kumtia hofu na kumtisha zaidi. Sekunde mbili alikuwa akiangalia na Mkurugenzi Wa idara ya usalama wa Taifa Kanali Godliving Kimaro pamoja na maafisa wawili wa ngazi za juu wa Polisi.



"Masimba Muuaji umezinduka? Lilikuwa swali kutoka kwa mzee yule ambaye hakuonyesha kutokuwa na utani. Masimba bado alikuwa ametulia, bado alikuwa akihisi yupo katika ndoto. Alishakuwa masimba muuaji, alishakuwa msaliti. Kama bosi wake mkuu naye anaamini ni Muuaji, nani ambaye atamuamini? Wakati akiwaza hilo sauti ya mkurugenzi Ikamzindua kutoka huko.



"Licha ya taifa kupoteza pesa nyingi kukusomesha katika mataifa mbalimbali, lakini leo umeamua kuisaliti nchi yako, umeamua kuisaliti nchi kwa sababu ya kuwatetea wauza madawa ya kulevya. Unaua watu kwa sababu ya kuahidiwa fedha? Umeitia aibu System nzima, umeitia aibu Idara hii. Mtu ambaye unategemewa kama wewe leo unafanya huu upuzi? Kuanzia leo idara inakufukuza kazi na utakabiliwa na kesu ya mauaji na pia utaishi katika kizuizi mpaka ukweli wa hili utakapo kuwa mwingine."



Yalikuwa maneno ambayo yaliusisimua mwili wa masimba, sio mwili tu bali hata moyo na roho yake. Alitambua jimmy Lambert na washirika wake walikuwa wamemuwahi. Walikuwa wamemuwahi na kummaliza kabisa. Macho yake ya kazi yakamtizama mzee kimaro usoni. Sasa walikuwa wakiangaliana kwa muda. Macho yao pekee ndio yalikuwa yakiongea. Masimba akamlazimisha mzee aendelee kumtizama. Wakatizamana tena na tena. Kisha Bila kuongea kitu mzee kimaro akabonyeza kitufe fulani mle ndani, sehemu nne zikafunguka kisha wakaonekana watu wanne wakiingia.



TUKUTANE KESHO

[11:51, 21/03/2017] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU



SEHEMU YA 015



Walikuwa watu watatu, watu ambao hawakuonekana kuwa na masihara yoyote. Bado masimba hakuwa akiamini. Akili yake haikuwa ikikubaliana na kile kinachoendelea pale. Hakuamini kama idara aliyoifanyia kazi inaweza kuja kudanganyika kwa urahisi kiasi kile. Walikuwa wakimjua vizuri katika majukumu mazito yote aliyowahi kushiriki, alinusurika mara tatu katika matukio ya hatari. Lakini leo hii alikuwa amewekwa kizuizini. Tena akipewa kesi ya kuhusika na mauaji ya Godfrey Maboba na familia yake. Idara kubwa yenye wajuzi wa hali ya juu katika masuala ya ujasusi leo ilikuwa ikidanganywa na watu. Watu ambao wanaiharibu jamii ya Tanzania kwa kuuza madawa ya kulevya. Yalikuwa mawazo na fikra zilizozidi kuipandisha hasira. Akaziangalia pingu ambazo ziliifunga mikono yake. Alizitazama kwa muda bila kuongea kitu. Kwa mara nyingine akainua kichwa chake na kumuangalia Mkurugenzi Mr Godliving Kimaro. Aliyagandisha macho yake usoni na kutaka kuongea kitu. Lakini machozi yake yakashuka mashavuni pasipo kutarajia.. hilo halikutarajiwa na wote waliokuwepo pale, kwa mara ya kwanza toka amjue Masimba ndio alikuwa akilishuhudia chozi lake. Ndio alikuwa akimuona Masimba akilia. Bado macho yake yalikuwa usoni kwa Chief. Lakini haukupita muda mrefu watu wale wakamuinua juu na kuanza kumkokota kutoka ndani ya chumba kile. Bado macho yake yalikuwa kwa Chief, aliendelea kumuangalia mpaka alipotelewa kabisa ndani ya Chumba kile. Safari yao ikaishia kwenye gari moja ambayo ilikuwa imepaki nje. Kufika pale mlango ukafunguliwa kisha ishara ya kimtaka aingie ikifuatia. Bastola zilikuwa zikimtizama huku wanaume waliovalia suti nyeupe wakiwa makini naye. Hakubisha na hakutaka kufanya rabsha yoyote. Akatii na kuingia ndani ya gari. Aliwekwa katikati huku bado midomo ya bastola ilimtizama. Watu waliomuweka hawakujishughulisha naye, hawakuwa wakiongea chochote. Walikuwa watu wa kazi, watu ambao kukuondoa kwao ni suala la kawaida. Hawakuwa wao tu, ndani kulikuwa na watu wengine wanne ambao nao walikuwa ni mfano wa hawa watatu. Hapo bado akauona ugumu wa kulianzisha. Hakutaka kufanya mapema kiasi kwa kuogopa kuharibu mipango yake. Akaendelea kutulia, punde akamuona mmoja akiishika mikono yake, ufunguo ukapita, punde pingu zikajiachia. "Usione tunakufungua ukajaribu kuleta ujanja. Ukifanya hivyo risasi itakuwa halali kichwani kwako." Alinguruma mmoja kati ya watu wale. Masimba hakuwa amemsikia, mawazo yake hayakuwa pale, alikuwa akimuwaza Teddy, alikuwa akimuwaza mwanamke huyu, mwanamke ambaye alitokea kuchukua sehemu kubwa katika maisha yake. Alimpenda Teddy, alimuamuni na kumheshimu. Hakuwahi kuwaza kama itakuwepo siku teddy angekuwa mnyama. Hakuwahi kuwaza kama angeweza kuja kumgeuka. Hakuwa na mashaka juu ya kukamatwa kwake, alitambua kinachofanywa ni kushurutishwa ili ataje wapi alipoyapeleka madawa ambayo ameyachukua kwa Jimmy. Bado aliendelea kukaa kimya huku gari ikiendelea kutembea. Alikuwa tayari kumuua mtu yoyote. Bado sauti ya Asteria ilikuwa ikijirudia kichwani mwake. Asteria binti mzuri, binti ambaye amekufa akiuomba msaada kutoka kwake, hata pale alipoukimbuka mwili wa mtoto yule alihisi kuwa na deni kubwa. Alitaka kumtafuta mwamvita, alitamani kuonana naye kwa vyovyote. Lakini kwa muda ule haikuwezekana tena. Lakini alitamani na aliipenda staili ya mwanamke yule. Punde akasikia kitu kama mfano wa geti likifunguliwa. Sekunde kumi baadae gari ilikuwa ikisimama. Milango ikafunguliwa kisha Masimba akatakiwa ashuke. Akatii huku midomo ya bastola na mitutu kutoka kwa walinzi wa Jumba lile ikimsindikiza.



***********



Alikuwa amelala kitandani akiitizama picha ambayo walipiga na masimba mwanzoni mwa mahusiano yao. Ilikuwa picha ambayo ilimkumbushe mengi sana katika maisha yake. Ilikuwa siku ya kwanza kukutana kwao, ilikuwa siku ambayo Teddy alikuwa amepata pass maalum. Akaitizama picha ile kwa muda mrefu sana. Alikuwa akiuvuta muda kumsubiri masimba. Bado moyo wake ulikuwa ukipambana na mapenzi, bado moyo wake haukutaka umuache masimba. Ni kweli aliitaka pesa, ni kweli aliipenda pesa, lakini pesa hii haiwezi kusababisha akamuacha masimba. Akaiweka ile picha pembeni na kuchukua nyingine. Hii ni picha ambayo ndio ilikuwa na kumbukumbu mbaya na nzuri kwake. Ilikuwa picha iliopigwa nchini Urusi wakiwa sambamba na wapelelezi wa shirika la kijasusu la Nchi hiyo, FSB zamani likijulikana kama KGB. ni picha ambayo walikuwa katika oparesheni moja katika mji moja katika nchi ya Syria. Ni misheni hiyo ambayo kama sio umakini na uwezo wa masimba basi angerudi jina. Lilikuwa tukio baya kukumbukwa lakini ni Masimba huyu huyu aliejitolea kuhatarisha maisha yake sababu yake. Kumbukumbu ya tukio nzima ilikuwa ikijirudia. Ni wakati akiliwaza hilo ndio mawazo yake yalipopitea baada ya kuusikia mchakato wa viatu vya mtu. Akajiinua kitandani mkononi akiwa ameikamita bastola yake. Akatembea akihisi labda alikuwa masimba, lakini utofauti wa siku ile ndio ulimpa wasiwasi wa kuhisi labda mtu huyu hakuwa masimba. Siku zote alitambua masimba hakuwa akiingia kwa kupitia mlangoni. Akaendelea kutembea akielekea kwa nje. Hakupitia mlango wa kawaida bali aliamua kutumia mlango wa siri ambao huwa unatokea moja kwa moja mpaka nje. Macho yake yalikuwa yakipita na kuingia hapa na kutokea pale. Muda wote masikio yake yalikuwa yamesimama mithiri ya sungura akitaka kunasa hiki na kile. Dakika mbili alikuwa nje ya nyumba yao akiangaza huku na huko. Palikuwa na giza sambamba na miti ambayo iliizunguka nyumba yote na kutengeneza kivuli. Akatulia kwanza akiangaza macho yake huku na kule. Punde akamuona mtu akichupa kutoka kwenye mmoja kati ya miti ile na kutumbukia kwa ndani. Mwili ukamsisimka. Japokuwa palikuwa na giza lakini mtu yule hakuwa Masimba kutokana na umbo lake. Akaipa muda akili yake kuwaza na kulitafuta jibu. Alikuwa nani katika nyumba yao na alikuwa akitaka nini? Hakuweza kupata jibu kwa wakati ule, lakini kwa mbali alianza kuhisi kuwa wenzake walikuwa wakimgeuka. Ingawa hayakuwa mawazo ya asilimia mia, lakini hakuna mtu mwingine ambaye angeweza kufika pale. Akaendelea kutulia akitizama zaidi na zaidi, kwa mara nyingine akamuona mtu wa pili naye akichupa na kutua ndani. Huyu wa pili alimsisimua zaidi kutokana na muonekano wake. Alikuwa ni mwanamke, tena mwanamke mwenye ujuzi.



Teddy hakutaka kusubiri, sekunde ile ile akarudi ndani kwa kupitia mlango ule ule wa siri. Muda wote alikuwa akijiuliza juu ya watu hawa. Akatokea kwa ndani kisha kutulia.. aliangaza macho kwa muda punde akakiona kama kivuli kimepita hatua hamsini kutoka pale alipotulia, sekunde ile ile akakiona kivuli cha pili pili kikipita. Muda ule ule akawaona watu walewale wawili wakichupa kutoka nje ya nyumba yao. Teddy akaduwaa. Kuduwaa kwake sio kuduwaa bure lakini alitambua watu hawa walitumwa na Jimmy kumchunguza yeye ama wametumwa na Idara ya Usalama wa Taifa kunfuatilia. Wazo la idara ya usalama hakuwa na mashaka nalo, lakini kuhusu Jimmy alikuwa na Uhakika nalo kwa kuwa ni siku hii mchana ambayo walimtishia kwa bastola, na sasa walituma watu ambao hakujua ni kina nani na wamekuja pale kwa sababu gani.





Hisia za kwamba watu wale walitumwa na idara ya usalama wa taifa zilikuwa ndogo sana ukilinganisha na hisia kuhusu Jimmy. Ulikuwa mchana tu walipomtisha kwa bastola, lakini muda huu alikuwa akiwashuhudia watu wakiuruka uzio wa nyumba yao, watu ambao waliuonyesha kile ambacho kilimthibitishia kuwa watu waliomtembelea walikuwa na uwezo mkubwa sana, kutokana na namna ya utokaji wao. Hilo likampa wasiwasi, wasiwasi ambao hakuwa nao hapo mwanzo. Kwa nini watu hawa wamekuja hapa? Wametumwa na nani na kwa sababu ipi? Hilo likampa utimamu wa akili, utimamu wa kutokurupuka. Alitaka kuujua ukweli kuhusu watu hawa ambao bado walikiumiza kichwa chake. Kwa mara ya kwanza aliutamani uwepo wa Masimba. Kwa mara ya kwanza alimkumbuka masimba, hakuogopa kuhusu kujua kwake, muda ule alimhitaji kama msaada na mtu wa pekee katika hili. Lakini masimba hakuwepo na hakujua wapi alipo mpaka muda huo. Hata hilo lilimchanganya pia, kwa nini mpaka muda ule masimba hajarudi? Ama amekufa katika tukio la kulipuliwa kwa gari yao? Hilo likamfanya teddy aamue kurudi sehemu ya tukio. Alitaka kumsaka masimba ajue wapi alipo. Hilo likamrudisha mpaka ndani, macho yake yakiangaza huku na kuangalia kule, alitaka kujua kama watu wale wamefanya chochote. Ni kweli alikiona kile ambacho alikiwaza. Watu wale walikuwa wamepekua sebuleni mpaka chumbani kwa utaalam wa hali ya juu, kitu ambacho kwa macho ya mtu wa kawaida hawezi kugundua. Aliangalia kwa muda na kuchunguza kila kitu chake. Alipogundua kipo salama, alibadili mavazi yake, akachukua bastola zake mbili na kuzichomeka sehemu tofauti ndani ya mavazi yake. Akaurudisha mlango, safari ya kuelekea Mjimwema ikaanza. Alikuwa ameshakijenga kisasi na chuki juu ya Jimmy na washirika wake. Alijiapiza endapo kweli Jimmy yupo nyuma ya matukio haya, basi atahakikisha anampoteza.



******

Alishuka sehemu ya tukio na kupokelewa na askari waliovaa magwanda sambamba na utepe wa kuonyesha kwamba sehemu haikuwa salama. Akatembea mpaka pale akisalimiana na baadhi ya askari, lakini alipotaka kuingia ndani ya eneo lililozungushiwa utepe akazuiwa na makachero wa polisi waliovalia mavazi ya kiraia. Teddy hakuongea wala kujitambulisha kwa chochote, bali alimuangalia kachero yule kama sekunde mbili, kachero yule hakumuangalia tena teddy. Alitoa ruhusa kwa teddy kupita. Alipoingia akajikuta akitizamana na miili ya watu watatu ambayo ililazwa chini kuonyesha kuwa haikuwa na uhai. Akatembea akiiona hofu moyoni mwake, hofu kuwa masimba alikuwa ameuawa, hofu ya kumpoteza mpenzi wake na hofu ya kutishwa na watu. Ingawa hakuwahi kuogopa, lakini hili lilimtia hofu. Mikono yake iliokuwa akitetemeka sasa taratibu ilikuwa ikishuka tayari kwa kufunua shuka. Hatimaye akaikamata kisha kuifunua, moyo wake ukachanua kwa tabasamu, tabasamu mwanana baada ya kugundua kati ya miili ile mitatu, hapakuwa na mwili wa masimba. Akairudisha shuka, akainuka akitoka nje ya utepe wa polisi. Macho kadhaa yalikuwa yakimtizama katika aina ya maswali. Hilo halikumfanya aogope, bado alitembea macho yake yakitizama kila sura za makachero waliokuwwpo pale kwa chati. Alitaka kujua nani ambaye alikuwa akimtizama kwa hila. Tokea alipowaona watu wale kule nyumbani kwake, hakutaka kuamini kama hakuwa akitembea na macho ya watu ama kutembea sambamba na watu. Aliamini kuwa kama watu wamediriki kuingia ndani ya nyumba yake, kisha kuifanyia upekuzi katika muda usiozidi dakika moja, hakuamini kama wanaweza kumuacha atembee peke yake. Lazima watakuwepo watu ama mtu ambaye anaifanya shighuli ya kumfuatilia. Lakini macho yote aliotizamana nayo bado hayakuonyesha hila. Yalikuwa macho ya kawaida japokuwa palikuwa na giza.



********



Jumba lilikuwa na walinzi wenye silaha nzito, wote walikuwa katika suti nyeusi kuonyesha kuwa walikuwa watamu katika medani ya kimapigano. Wote walikuwa wameizunguka gari huku midomo ya silaha zao zikielekezwa ilipo simama ile gari. Hata mlango ulipofunguliwa watu wale hakuongea chochote zaidi ya kumpa ishara masimba ashuke. Masimba akatii huku bado midomo ya bastola sambamba na bunduki za walinzi zikimtizama. Alitembea akiwa amewekwa kati. Kila hatua yake na uchezaji wa mikono yake, ulikuwa ukiangaliwa kwa ukaribu. Kila mguu wake ulipokuwa ukipiga hatua na kutua chini, macho ya Walinzi wale nayo yalikwenda sambamba. Wakaufikia mlango mmoja mkubwa wa vioo. Kufika hapo tu mlango ukajifungua na wote wakaingia ndani wakiwaacha walinzi nje. Kutoka hapo wakaongoza mpaka ndani ya lifti ambayo iliwapaleka mpaka ghorofa ya saba. Wakashuka na kupokewa na watu wengine, hawa ndio waliomchukua masimba huku wale waliokuja naye wakirudi na ile lifti. Bado akili ya masimba ilikuwa haipo katika utimamu wake. Alitambua sehemu alipo, aliitambua kwa kuwa hata yeye alikuwa jasusi. Lakini kitendo cha kuletwa ndani ya jengo hilo akichanganya na maneno ya Chief, alitambua kuwa lazima kuna jambo kubwa nyuma ya pazia. Akajiambia asubiri, alikuwa akiamini subira tu ndio ingeweza kumfanya ajue kile kinachoendelea. Watu hawa waliomuongoza kwa mara ya pili, walikuwa zaidi ya watu, hawa hawakuwa hata na tabasamu. Kila mmoja alikuwa akiatizama kila kinachotokea. Macho yao yalikuwa yakizunguka kama kinyongo. Yalimtizama na kumchunguza, yalimuangalia kwa kina. Hata pale macho yao yalipokuwa yakitizamana, kila mmoja alimtambua mwenzake.



Wakaufikia mlango mwingine, mlango huu haukufanana na kote walikopita, mlango huu haukuonekana kama ulikuwa mlango, lakini kule kukanyaga sehemu ya nje kuukaribia, kukaonekana kitu mfano wa shimo. Masimba akasita kuingia, akataka Kurudu nyuma. Hakufanikiwa hilo, kitu kizito kikatua tena kichwani. Akakiona kiza mbele yake. Akajaribu kupambana na giza lile, lakini akashindwa. Akaruhusu Macho Yake Kuingia giza. NI KWELI YAKAINGIA GIZA. HAKUJUA KILICHOENDELEA.





Alipambana akikataa giza kuuchukua mwanga wa mboni za macho yake, lakini haikusaidia kitu. Akakubali giza liyafunike macho yake. Na kweli ndivyo ilivyokuwa.



Alikuja kushtuka baada ya masaa mawili na kujikuta katika chumba kidogo. Chumba ambacho hakikuwa na kitanda isipokuwa maji tu. Tena maji ya baridi kupindukia. Mwanzo wakati anapatwa na fahamu alidhani labda alikuwa pembezoni mwa bahari ya hindi kutokana na maji yale. Akafumbua macho zaidi na zaidi, akayaona mazingira yale. Akahisi kukata tamaaa. Aliyajua matumizi ya chumba kile. Hakuna mtu ambaye aliwahi kutoka akiwa hai kati ya wote walioingizwa. Akainua kichwa chake na kuangalia juu, akakumbuka mengi aliowahi kulifanyia taifa lake, akakumbuka aliponusurika vifo mara kadhaa kwa sababu ya usalama wa taifa lake. Lakini yote yamesahaurika, lakini yote yalisahaulika kwa sababu ya watu wachache. Hata yeye alipelekwa ndani ya chumba kile ambacho hutambulika kama kuzimu. Alitakiwa naye afe, alitakiwa naye asirudi akiwa hai. Bado maji yaliendelea kumtesa na kumsulubu. Akainua macho na kutizama mwisho kabisa wa chumba kile. Aliamua kujaribu bahati yake, hakutaka kamwe kufa kikondoo, hakuamini kama angeshindwa kutoka pale. Aliamini atatoka tena atatoka akiwa salama. Akauvaa ujasiri na kuutoa uoga na ukataji tamaaa. Akainuka kutoka pale chini, akasimama kwa muda akiendelea kutupa macho yake kila pembe ya chumba kile. Akaunyoosha mwili wake kuupima kama una nguvu, aliporidhika akaanza sasa kutembea ndani ya kichumba kile. Kwa kuwa maji yalikuwa yamejaa mpaka kiunoni, hakuwa akiona chini alipokuwa akitembea. Alipokuwa akipiga hatua nyingine akajikuta akijikwaa kwenye kitu mfano wa mwili wa binadamu. Hilo likamfanya asite kuendelea kutembea, alikuwa amesimama akijishauri kitu. Alishaamua kufanya chochote, akili yake ikahitaji kufanyakazi mara mia zaidi ya kawaida yake. Hakutaka kushughulika na kitu mfano wa mwili wa binadamu aliyoukwaa. Alihitaji kufanya kitu kikubwa cha kumuondoa pale ndani. Akajaribu tena kutembea lakini safari bado alikikanyaga kile kitu mfano wa mwili wa binadamu. Kitu kama hisia kikamjia kichwani, hisia ya kwamba mtu huyu anaweza kumsaidia. Kwa kuwa siku zote aliziheshimu hisia zake, Masimba akainama na kuanza kutafuta chini ya maji. Kweli mikono yake ikagusa mwili wa binadamu. Baada ya kuugusa, akahakikisha mikono yake inaukamata ule mwili na kuanza kuusimamisha. Alipambana kwa muda na alipofanikiwa kuusimamisha akashangaa kumuona mtu anayemjua. Mwili wa mtu yule ulikuwa ni wa mmoja kati ya vijana ambao walikuwa wakimsaidia katika kazi yake.



Hilo hakulitegemea, kengele za hatari zikakigonga kichwa chake. Mmoja kati ya vijana waliokuwa wakimsaidia kazi kuuawa, alijua ilikuwa ni mbinu ya watu waliomfikisha pale. Alitambua vijana wote aliokuwa anasaidiana nao watauawa iwapo kama yeye ataendelea kuwepo pale mahabusu ya kuZimu. Akaendelea kuutizama wili wa kijana yule, hasira zikaonekana usoni. Kuuawa kwa maafisa usalama wa taifa kwa sababu ya manufaa ya watu wachache kulimpa sana hasira. Aliitambua hizi zilikuwa hila za Jimmy Lambert na maafisa waandamizi wa serikali. Alijua wote hawa walikuwa wakishinikizwa kusema wapi ulipo mzigo wa madawa ya kulevya aliouchukua nyumbani kwa Jimmy. Hilo likamfanya aihisi hatari hata kwa teddy, alihisi hata yeye ipo hatari atageukwa na kitakachofuatia ni yeye kupotezwa kama walivyofanya kwake. Kwa mara ya kwanza alitamani amuone teddy amwambie, kwa mara ya kwanza alitaka kumwambia teddy hatari iliombele yake. Alitaka kumwambia ukweli wa mambo. Lakini angetokaje wakati yupo kuzimu, alitokaje wakati muda mfupi ujao atakuwa maiti. Masimba akasonya huku akikifanya kitu ambacho hakuwa amekiwaza. Mikono yake ilizama kwenye mavazi ya marehemu yule. Akahisi kukigusa kitu katika mavazi ya marehemu yule. Akaongeza kasi ya mikono punde akakitoa kitu kile ambacho kilikuwa mfano wa golori. Tabasamu likachanua usoni mwake. Kilikuwa kitu maalum cha kufungulia sehemu zisizowezekana. Kitu ambacho hutumiwa sana na mashirika makubwa ya Kijasusi Hasa CIA na M15 pamoja na M16 ya Uingereza. Akakitizama kwa muda, harafu akakiwasha na kuanza kukizungusha kwa mikono yake akikielekeza kila upande. Sekunde kumi hazi kufika, maji yote yakapotea kisha chini kwa pembeni pakaachia. Mlango mkubwa ukaonekana mbele yake. Hakutaka kusubiri kwa kuwa alitambua huwa kuna muda maalumu. Sekunde ya kumi na mbili alikuwa nje ya chumba kile akitembea kuifuata korido ambayo ilikuwa akielekea kama Chini ya ardhi. Hakuwa na bastola, hakuwa na silaha ya aina yoyote, lakini alikuwa tayari kwa lolote. Jengo lillikuwa kimya kanakwamba hapakuwa na mtu ndani yake. Macho yalikuwa yakiangalia kila kona ya Jengo. Muda mfupi alikuwa ameibukia sehemu ambayo haikuwa kimya. Sauti za watu zilikuwa zikisikika kwa umbali mfupi kutoka mahala aliposimama. Wakati akifikiria nini afanye akavisikia vishindo vya mtu akisogea mahala pale. Akajiandaa kumkabili kwa mikono yake. Punde akamuona mtu akipita, alikuwa mwanamke. Alionekana na mlinzi wa Jengo lile. Alikuwa na Bunduki aina ya Oxcelf SG mkono. Alikuwa akitembea akiangalia huku na huko. Masimba akaona ulikuwa muda sahihi wa kufanya kitu. Alichokifanya ni kumtokea yule msichana kwa nyuma na kumpigia mluzi. Msichana yule akageuka akidhani aliitwa na mwenzake. Lakini alijikuta akikutana na flying kicks kutoka kwa masimba. Kwa kuwa hakutarajia kitendo kile, mwanamke yule akajikuta akishindwa kuzuia mapigo yale, na kuruhusu mateke yale kumtupa chini kama furushi.





Yalikuwa mateke mazito kwake, mateke ambayo yalipigwa katika aina ya kushtukiza. Alianguka kama furushi la mahindi. Hakuweza kuinuka. Alikuwa ametulia akionyesha kupotewa na fahamu. Masimba hakusubiri, alimfuata pale chini kisha kumpekua. Vitendo vyote hivyo vilitendeka katika muda mfupi tu. Alichukua bastola ambayo aliikuta kwenye mavazi ya binti yule, akaondoka akimuacha amelala sambamba na bunduki yake. Kwa kuwa alikuwa analitambua jengo lile, na kwa vile alishawahi kupita katika majengo yanamna ile. Haikuwa kazi ngumu kuzikwepq camera za usalama ndani ya jengo lile. Safari hii aliubadilisha mwelekeo, aliubadilisha mwelekeo sababu hakutaka kuua ama kukutana na wanausalama wasiolijua tatizo. Alitaka kuondoka bila kumwaga damu ya mtu isipokuwa pale itakapobidi kufanya hivyo. Akachepuka hapa na kutokea pale, mpaka alipofika karibu na lango la kutokea baharini ndipo aliposikia king'ora cha hatari. Hapo akahisi kwamba alikuwa hatarini. Akaondoka akiongeza kasi kuwahi kutoka ndani ya jengo. Hakutaka kukamatwa tena, hakutaka kurudi tena mikononi mwa watu wa usalama wa taifa. Alitaka kwenda kuwafikishia ujumbe wale waliomsingizia. Wale waliomuwekea mtego na kusababisha yeye kukamatwa..



******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Muda ulikuwa unakwenda lakini bado hakumuona Masimba, alikuwa amezoea kutokumuona masimba akiwa nje ya nyumba, lakini hili la leo lilimshangaza na kumtia wasiwasi. Matukio ya muda mfupi uliopita, kisha kutokufika kwa masimba mpaka muda ule, ni kitu ambacho kilimpa wasiwasi. Akaendelea kuivuta subira huku muda wote macho yake yakiitizama saa iliokuwa ukutani. Muda uliendelea kusogea, hakumuona Masimba, hakuiona ishara kwamba masimba atarudi. Hilo likaufanya usingizi wake upae, hakuiona sababu ya kulala. Kwa mara ya kwanza alikuwa akimuhitaji Masimba kuliko siku yoyote nyingine. Angelalaje wakati masimba hakurudi. Angelalaje wakati amegeukwa na watu aliowaamini? Akainuka kutoka kitandani kwa mara nyingine. Hakuuona usalama wa kuendelea kuwepo pale. Akayapitia mavazi yake sambamba na bastola zake mbili. Akazivuta hatua kuliacha jumba lao. Wakati anamaliza kufunga mlango wa nje akausikia mngurumo wa magari, magari zaidi ya moja, michuno ya matairi ndio kitu pekee kilichomfanya Teddy ahisi uhatari. Uhatari ambao alianza kuuona pale watu waliovalia suti nyeusi wakipaa angani na kutua ndani katika namna inayovutia, namna ambayo ingekuwa burudani kama ungekuwa ukiitizama. Teddy hakuwa mgeni na kikundi hiki, kikundi maalum cha kulinda viongozi wa taifa hili. Kuwaona wakitua pale katika aina ile, lilikuwa jibu kuwa Masimba ameshageukwa, masimba ameshaharibu. Kutua kwa watu wale kukafuatiwa na kitendo ambacho kilimuacha Teddy akiwaangalia. Walipotua kwa ndani kila mmoja alikuwa akichupa katika namna yake na kwa upande wake, hata walipomkaribia Teddy hawakuonyesha kutaka utani. Midomo ya bastola ilielekezwa kwake, macho ya watu yakimtizama katika aina ya kumuuliza maswali. Ni katika maswali hayo kupitia macho yao Teddy alipohisi kitu. Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida. Masimba hakufika, watu kuivamia nyumba yao, gari yao kulipuliwa na sasa kuvamiwa na kikosi maalum cha kumlinda Rais ni suala zito sana. Aliiona siku ile haikuwa nzuri kwako, haikuwa nzuri kwa kilichotokea. Macho yalikuwa yakimuangalia yeye kwa aina ya maswali. Naye akajibu kwa aina ya sijui kwa kutumia macho. Hawakutaka kumsikiliza, wawili wakapita huku wangine wakiendelea kumuweka kati. Hazi kupita sekunde hata ishirini walikwisha toka wakiwa na baadhi vitu mikononi mwao. Hawakuongea tena na mwanamke yule zaidi ya kumpita na kuondoka wakimuacha amesumama. Muda huo huo akayasikia magari yakiondolewa kwa kasi. Bado Teddy alikuwa ameduwaa, bado teddy alikuwa akisafiri mbali kimawazo. Kupotea kwa madawa ya kulevya, kushikiwa bastola na washirika wenzake haikuwa picha nzuri kwake. Alijua kutakuwa na msukumo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Lakini bado hakulipata jawabu, nani amelazimisha hili? Masimba atakuwa wapi muda huu? Kwa nini Kikosi maalum cha kumlinda Rais kiwe kwenye hili suala la kumtafuta masimba? Hayo na maswali mengine mengi ndio yaliomchanganya teddy.



Hakuona sababu ya kuendelea kubaki pale. Aliondoka usiku ule ule akiamua kwenda nyumbani kwa Jimmy Lambert. Aliamua kwenda huko kwa kuwa alitaka kuujua ukweli kuhusu hiki kinachoendelea kutokea. Pia alitaka kujua ni nani ambao walikuja nyumbani kwake. Ilikuwa safari ambayo alihisi ingekuwa ya Hatari. Wakati akiwa juu ya usafiri akielekea nyumbani kwa Jimmy, akamuona mtu, hakumtilia manani pale alipomuona mara ya kwanza, lakini akajikuta akimuangalia yule mtu ambaye sasa alikuwa akitembea kama mlevi. Macho yake yakavutika kumuangalia mtu yule tena na tena. "Masimba!? Yalikuwa maneno pekee kutoka kinywani kwake. Kilichofuata ni kuufungua mlango ili kushuka,lakini ya kufanya hivyo akaliona gari, gari ambalo hapo mwanzo aliliona karibu na nyumbani kwake. Hapo akagundua alikuwa akifuatiliwa. Mawazo yakumfuatilia yule mtu mlevi yakaisha. Alimtambua kuwa mtu yule ni Masimba. Alimtambua kwa urahisi kwa kuwa alimjua masimba.

******



Aliendesha gari mpaka maeneo ya Ambience club, akaipaki gari na kushuka kisha kuongoza moja kwa moja mpaka ndani ya ukumbi. Akatafuta sehemu nzuri ya kukaa. Katika kuangaza kwake akaiona meza moja ikiwa tupu. Akasogea hapo, akavuta kiti nakukaa. Baada ya kukaa hapo, mhudumu akasogea na kumuuliza kinywaji gani ambacho angetaka kutumia. Teddy akamjibu na baada ya hapo akaendelea kutulia akiwaza na kuwazua kile alichokiona kule njiani. Masimba akiyumba njiani, masimba akitembea katika aina hii ya ulevi? Kuna nini kimemtokea Masimba? Kuna nini kimetokea nyuma ya hiki anachokifanya masimba? Ina maana kuna hili tu ama kuna kingine nyuma? Mawazo yake hayo yakakatizwa na mtu aliyemuona akiingia. Huyu alihisi kumuona mahala, wakati akiendelea kuangalia hilo akamuona mtu mwingine akiingia. Huyu alikuwa amejibadilisha sana. Licha kujibadilisha huko lakini alimjua licha ya kujibadilisha kwake. HUYU ALIKUWA MASIMBA



Licha ya kujibadilisha sana, licha ya kuonekana kama mtu mwingine, lakini kwa teddy haikuwa hivyo. Alimjua Masimba, alimjua kama alivyokuwa akiujua mwili wake. Akayahamisha macho yake sasa akimtizama mtu yule aliyeingia. Mtu ambaye aliwahi kumuona sehemu, mtu ambaye uingiaji wake ulikuwa wa kinamna fulani. Bado mtu yule alikuwa amesimama akiangaza kama mtu mwenye kutafuta kitu. Hilo lilimpa uhakika kuwa kijana yule alikuwa akimtafuta yeye, lakini hili la kufika pale kwa masimba nalo hilo kiasi fulani likakipa kichwa wakati mgumu wa kufikiria. Muda mfupi alikuwa akitembea kama mlevi akiyumba, lakini muda huu hakuwa yule wa kuyumba. Na alifika pale akiwa mwingine. Jibu lake lilikuwa moja tu, jibu lake lilikuwa ni kwamba, masimba alimuona wakati anaondoka na ile gari, masimba alikuwa karibu na nyumbani na inawezekana masimba alishuhudia kila kitu kilichotokea. Hilo likausisimua mwili wake, alijikuta tabasamu matata likichanua usoni mwake. Lakini licha ya tabasamu hilo, macho yake hayakuganduka kumuangalia kijana yule. Alikuwa akimtizama kwa uhuru kutokana na uwepo wa kiza sehemu alipokaa. Kijana yule baada ya kuangaza huku na huko bila kuona kitu, akatoka ndani ya ukumbi akionyesha kuelekea sehemu za nje. Bado Teddy alijipa subira. Alitaka kuhakikisha kama kuna watu wengine ama. Licha ya kuvuta subira kwa dakika mbili, hakumuona mtu yeyote akitoka kumfuata kijana aliyetoka. Hilo likamfanya atake kusimama kuelekea huko, lakini kabla ya kufanya hivyo alitaka kumuangalia masimba kama alikuwepo ama lah! Akafanya hivyo, lakini hakumuona masimba, akaangaza tena na tena lakini bado hakumuona Masimba Akainuka naye akielekea nje ya ukumbi wa club. Alitembea akidance kufuata midundo ya muziki uliokuwa ukiporomoshwa. Alipotokea nje, macho yake yakapokewa na makelele ya watu wakionekana kupagawa. Hilo likamvutia, akaamua kuelekea kule zinapotokea kelele. Muda wote mikono yake ilikuwa tayari kwa chochote ambacho kingetokea. Akafanikiwa kujipenyeza katikati ya umati na kusogea mpaka mbele kabisa. Mwili wake ukamsisimka baada ya kuuona mwili wa mtu ukiwa umelala kifudifudi huku sehemu ya mgongoni kukiwa na mpini wa kisu kuonyesha mtu yule alikuwa amechomwa. Akasogea zaidi na zaidi mpaka karibu kabisa. Alikuwa yule yule kijana aliyetoka ndani muda sio mrefu akiwa amelala katikati ya dimbwi la damu. Hilo likamshangaza, katika yote aliyoyategemea hakuwaza kama mtu yule angeuawa kwa aina ile. Swali likabaki kwake ni nani aliyemuua kijana huyu? Swali hilo likamfanya arudi tena ndani ya Club, kurudi kumuangalia masimba kama yupo ama lah. Alitaka kwenda kumuangalia masimba. Kitendo cha masimba kuingia na kijana yule, kisha muda mchache mtu huyu auawe katika namna hii! Hapo akajua kuna kitu. Teddy akahisi akili yake ikishindwa kufanyqkazi. Mambo yaliomtokea siku hii ya leo yalikivuruga kichwa chake, alitakiwa kutulia kwanza, alitakiwa kuituliza akili yake kwanza. Alitambua anapitia katika wakati mgumu na wahatari sana. Akaingia tena ukumbini safari hii akiwa makini tofauti na mwanzo. Macho yake yalimtizama kila mtu, yakamdadisi na kumchunguza. Muziki bado ulikuwa ukiporomoshwa, watu walikuwa wakiserebuka pasipokujua chochote kilichotokea nje. Akajimwaga katikati akinengua kwa staili hatari sana. Alikuwa akisakata katika staili ambayo ilisababisha macho kadhaa ya watu wamtizame na wamuangalie. Wanaume wa kwale walianza kukitamani kiuno cha teddy. Kule kukata kiuno na kwenda mpaka chini kiliwafanya watu wa wehuke. Sasa vitu havikalika.



Hilo halikuwastaabisha hao tu, hata masimba aliyekuwa amebana pembeni alikuwa akimtizama mama watoto wake akikizunguusha kiuno. Hata pale alipokuwa akienda mpaka chini bado macho yake hayakuamini. Ni kweli ni mume mtarajiwa wa teddy, nikweli anaishi na Teddy lakini hakuwahi kufikiria kama ni mtamu kiasi hiki katika kudance, hakufikiria kama ule utamu wa kitandani una utamu mwingine. Hakumwangalia teddy tu, macho yake yaliangaza kila upande akiutizama usalama wa mwanamke huyu. Alitizama kama ataona hila zozote lakini hakuziona.



*********



"Haiwezekani, nasema tena haiwezekani!!!" Ilikuwa sauti ya jimmy lambert ikinguruma katika chumba kimoja chenye watu wasiopungua watano. Alikuwa amechukia kupita kiasi. Mishipa ilikuwa imemtoka usoni huku mikono yake ikiwa imekunjwa. Alikuwa akitoka upande huu wa chumba kwenda upande ule. Alikuwa amechanganyikiwa vya kutosha. Taarifa kuwa Masimba ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa Idara ya Usalama wa Taifa ilimchanganya sana. Hakuitegemea hiyo taarifa, alichokitegemea kilikuwa ni kupatikana kwa mzigo wao ambao uliibiwa na Masimba. Lakini hazikuwa taarifa hizo, hazikuwa taarifa nzuri kwake.



"Mtu anatoroka chini ya usalama wa taifa? Mtu anatoroka pasipokuua? Mtu ambaye anaishi na mamilioni ya pesa yetu. Kwa nini asingeuawa tu? Aliendelea kufoka huku akiendelea kuzunguka mle chumbani. Wajumbe wengine walikuwa kimya wakumuangalia. Hakuna ambaye aliinua kinywa chake kumjibu kitu chochote. Kila mmoja alikaa kimya akifikiria jinsi ya kujinasua katika hili.



"Tumemkosa Masimba, na mpaka sasa hajulikani aliko, pia nina mashaka teddy amegundua kitu kutoka kwetu. Ameonekana Ambience club akicheza na akionekana ni mwenye furaha sana. Yaani sisi tunaumiza vichwa huku, mwenzetu anafurahi huk.... alikatizwa na mlio wa simu yake ikiitakuonyesha kwamba alikuwa akipigiwa. Aliichomoa mfukoni kabla ya kupokea akaangalia jina la mpigaji. SILENT KILLER lilisomeka Jina juu ya kioo cha simu yake. Jimmy akasita kuipokea simu. Hakujua kwa nini lakini alihisi haikuwa simu ya usalama. Macho yake yaliwaka mithili ya paka, pia alikuwa akiwatizama wajumbe wenzake mmoja baada ya mwingine. Hata wao walimtizama sura zao zikiacha maswali, sura zao zikiachwa na mshangao. Hata simu ilipokatwa na mpigaji kurudia tena ndipo Jimmy akakurupuka na kuipokea. Hakuongea kitu kingine zaidi ya kuitoa simu sikioni na kuwageukia washirika wenzake. Huku midomo ikimtetemeka kwa hasira akajiondoa pale na kusogea kisha kujibweteka Juu ya kitu.



"Saidi Mbega ameuawa muda huu katika mazingira ya kutatanisha, nje ya Ambience Club. Vijana wetu waliweka mtego wa kumnasa Teddy lakini kabla hawalifanya hilo, wakapewa taarifa za kifo cha mwenzao. Aliongea Jimmy akionyesha kuchoka kimwili, kiakili mpaka kimawazo.



Ilikuwa taarifa iliyopokelewa kwa mshtuko na wajumbe wale. Walitambua kuwa wanatakiwa kufanya kazi usiku na mchana kufanikisha kujua pale alipo masimba.



********



Sauti za mbwa zilikuwa pekee zikiosikika usiku ule, hapakuwa na sauti ya binadamu katika eneo lote. Ukimya ulikuwa umechukua sehemu kubwa ya sehemu yote ya mikocheni. Hilo halikumsumbua sana Teddy, alikuwa hapo kwa kazi moja, kazi ya kuonana na Jimmy. Kuongea na Jimmy sambamba na kujibiwa maswali yake. Ukimya wa eneo na giza la usiku vilimsaidia teddy kuifikia nyumba ya Jimmy pasipo kizuizi chochote. Hata alipozunguka kwa kupita kwenye vivuli vya miti bado hapakuwa na kizuizi. Bado hakupata ugumu wowote. Hilo likamfanya apate mashaka. Mashaka ambayo yalimfanya ajiulize swali. Wako wapi walinzi wa Jimmy? Kabla hajapata majibu Akahisi kitu cha baridi kikimgusa kisogoni. TULIA HIVYO HIVYO...



Kitu cha Baridi kikagusa kichwani, kisha sauti nzito ikafuatia.. TULIA HIVYO HIVYO. Teddy akatulia kama alivyoamliwa. Akili yake ilitakiwa kufanyakazi zaidi ya uwezo wake. Alitakiwa kufanyakitu ambacho kingemtoa sehemu ile. Akatii na kutulia zaidi na zaidi. Hakutaka kuwa kondoo kufuata kila anachoambiwa. Mikono ilikuwa juu kuonyesha kutii amri. Sauti ikaamrisha tena, safari hii sauti ikimwambia atembee kuelekea kule ilipo nyumba ya Jimmy Lambert bila kugeuka nyuma. Ni kweli teddy hakugeuka, ni kweli teddy aliongoza kuelekea alipoambiwa. Muda wote alitembea akicheza na kivuli cha mtu wa nyuma yake, mtu ambaye alimshikia bastola. Hatua ya kwanza mpaka ya tano zilipotea pasipokufanya kitu, sio kama hakupenda, sio kwanba hakutaka kufanya, alitaka na alitanani sana, lakini bado umbali ulikuwa tatizo, wakati wakiianza hatua ya sita, teddy akakisikia kishindo na ukelele kutoka nyuma yake. Akakumbuka kutakiwa kutokugeuka, hakugeuka.. lakini hatua moja nyingine akagundua kutokukiona kivuli cha mtu ambaye alikuwa nyuma yake. Hilo likamfanya ageuke sasa.. akageuka.. Cha kwanza kukiona ni mwili wa mtu uliolala kuonyesha kuwa haukuwa na uhai. Hilo halikumshangaza sana, alijua Masimba alikuwa nyuma akimlinda. Hilo likampa uhueni na moyo wa kusonga mbele. Alikuwa ameamua Kumuona Jimmy Lambart. Hakuwa na hofu lakini hakutaka kujiamini tena. Muda wote alitembea akiwa makini kwa kila hatua. Alitaka kuzijua mbivu na mbichi. Hakuhofia na wala hakuogopa. Muda mfupi alikuwa nyuma ya uzio wa Jumba la Jimmy. Kwa kuwa alilijua lile jengo kwa undani zaidi, akaamua kuingia kwa kuruka uzio. Muda mfupi alikuwa akitua ndani bila kutoa kishindo. Kutoka hapo akachapuka mpaka pembeni mwa mlango wa kuingilia ndani kabisa. Hapo akatulia kwa muda kusikiliza kama kuna mtu yoyote, lakini bado ukimya ulimpa majibu kuwa hapakuwa na mtu. Akaunyoosha mkono wake mpaka sehemu ya chini ya mlango. Akagusa sehemu na bila kuchelewa mlango ukajifungua. Baada ya mlango kufunguka, akaichomoa bastola yake na kuingia ndani kwa tahadhali kubwa. Mdomo wa bastola ulikuwa umetangulia mbele tayari kwa kufanya kazi. Bado hapakuwa na sauti za kitu chochote ambacho kingemtambulisha uwepo wa watu ndani ya jumba lile. Kimya kilichukua nafasi yake, kimya kilichofanya Teddy aendelee kusogea na kusogea. Akavipita vyumba viwili pasipokusikia chochote kile. Hilo likamfanya aamini kuwa Jimmy hakuwepo hapo ndani. Alimtambua jimmy awapo nyumbani huwa mtu wa kupendelea muziki. Ukimya huo ulimaanisha kwamba hapakuwa na mtu ndani ya jengo hilo. Akaendelea kusonga mbelembele. Mdomo wa bastola ukiendelea kutangulia mbele. Akaukuta ukumbi ambao mara nyingi waliutumia kwa mikutano. Hapo bado macho yake hayakukiona kitu. Bado hakufanikiwa kumuona yoyote. Bado ukimya uliichukua sehemu kubwa. Bado akaivuta subira, bado aliitaka subira tayari kumsubiri, lakini hilo likapotea baada ya kuusikia mngurumo wa gari kutoka nje, kisha kuishia hapo hapo pasipokuendelea. Akaamini kuwa Huyo alikuwa Jimmy, hata sauti ya geti kufunguliwa ilipopenya masikioni mwake, alitambua kuna mtu alikuwa akiingia. Mawazo kuwa Jimmy ndiye yalikuwa asilimia themanini. Akajivuta mpaka karibu na mlango wa kungilia ndani kwa upande wa mbele ya nyumba. Hapo akatulia akiisubiri hatma ya mtu huyo.



Haukupita muda akakiona kitasa kikitingishwa kisha mlango kufunguliwa. Watu watatu wakaingia bila wasiwasi. Lakini Jimmy hakuwa mmoja mmoja wao. Hawa walikuwa wengine, hawa walikuwa wageni kwake. Kwa kuwaangalia walikuwa wageni kabisa. Akaendelea kuwatizama vijana wale. Aliwaangalia katika utulivu mkubwa. Kutokuwepo kwa Jimmy kulimshangaza sana. Haikuwahi kutokea Jimmy kuwatanguliza watu nyumbani kwake bila yeye mwenyewe kuwepo. Aliwatizama watu wale walivyojibweteka pale sebuleni, moyoni akacheka. Alitabasamu na hata kufurahi. Alikuwa na uwezo wa kuwamaliza kwa risasi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, lakini hakutaka kufanya hivyo. Alihitaji subira, ni subira ambayo ingemkutanisha na Jimmy. Ni kweli, katika muda ule ule akamuona Jimmy akiingia sambamba na mwanamke. Aliwatizama walivyokuwa wakitembea. Alikuwa na uwezo wa kuwapiga risasi kwa urahisi, lakini hakupenda kufanyq hivyo. Wakati Jimmy na mwanamke yule wakitembea kuelekea sebuleni. Jambo jingine la kuustajabisha kama sio kushangaza likatokea. Nyuma ya Jimmy na mwanamke yule, akamuona masimba naye akitokea. Akitokea akitembea kikawaida kana kwamba alikuwa akiingia nyumbani kwake. Hili nalo likimfurahisha, hili nalo likamfanya sasa asitishe kufanya chochote aendelee kumshangaa Masimba. Ilikuwa pichq nzuri iliovutia kuitazama. Hata pale jimmy alipokuwa akijibweteka ndipo nadhani alimuona masimba. Mshtuko alioupata Jimmy baada ya kumuona masimba ndani ya nyumba yake, iliwafanya vijana wake waipeleke mikono yao mifukoni mwao tayari kwa kutoa bastola.



Hakuna aliyeujua wepesi wa masimba, hakuna aliyejua ni muda gani masimba alitumia, lakini wote wakajikuta wakimtizama mwenzao ambaye alikuwa akigalagala chini baada ya kulimwa shaba ya kifua. Hakuna aliyeamini, Jimmy ndio hakuamini kabisa. Macho yake yalimtoka mishipa ya usoni ikaonekana. Midomo miwili ya bastola ilikuwa ikimtizama. Masimba hakuonyesha utani, macho yake yalikuwa yakiwaka na kuwaka. Jimmy akatamani kuongea lakini sauti haikutoka. Mate yalimkauka na maneno hayakutoka kabisa. Alikuwa akimsikia masimba lakini hakuwahi kuonana naye. Leo alikuwa akimuangalia, huku pia midomo miwili ikimtizama.



"Jimmy nadhani kiburi chako cha kuwa karibu na viongozi imekupa mamlaka ya kujipa utawala katika nchi hii. Unaonekana una nguvu kuliko Rais, Makamu wake na Waziri mkuu. Imekupa mamlaka ya kuua watu wasio na hatia kwa sababu ya kufanikisha biashara yako haramu. Asteria anakosa gani hadi kumuua? Uchungu wa taifa lake ndio kisa cha kumuua. Dada wa Asteria na mumewe Godfrey Maboba sambamba na mtoto wao, ni kosa lipi wamefanya? Sasa leo nimekuja na mimi. Nimechoka kutumiwa watu wa Idara ya Usalama wa taifa. Nimechoka kupambana na watu wengine kwa ajili yako. Sasa nataka uniambie ukweli kabla sijaruhus......... kabla hajamalizia maneno yake mlango ukasukumwa kwa nguvu, wakaingia watu watatu na kuanza kuvurumisha risasi pale alipokaa Masimba.. Lakini hazikumkuta, bali zilipita na kutua kwa kichana mwingine, yowe la Uchungu likamtoka. Watu wale wakaendelea kushambulia bila tahadhali. Hawakujua Teddy alikuwepo pale, hawakujua kwamba alikuwa nyuma yao tena na Bastola mbili katika mikono yake, huku vidole vikiwa kwenye trigger tayari kwa Kuruhusu Risasi





Hawakujua kwamba nyuma yao alikuwepo teddy, tena akiwa na bastola mbili mikononi, vidole viwili vikiwa tayari kwenye trigger kuruhusu risasi. Alikuwa akizihesabu sekunde, hakutaka kufanya kwa haraka sana kukifanya kile alichotaka kukifanya. Sekunde ya kwanza ilipita wakati kidole bado kikiwa kwenye kitufe cha kuruhusu risasi. Hata sekunde ya pili ikapita patupu pasipo kitendo chochote. Lakini sekunde ya tatu haikupita na kwenda bure, bastola ikakohoa mara tatu mfululizo, risasi zikatua na kupenya pale zilipoagizwa, watu watatu walikuwa chini wakivuja damu katika kuonyesha hawakuwa hai. Kilikuwa kitendo mujarabu machoni kwa Teddy, kitendi kilicho mfanya atabasamu. Aliipenda damu, alipenda kuiona ikitoka mwilini kwa mtu na aliihusudu zaidi pale yeye awapo chanzo cha kutoka kwa hiyo damu. Hakutoka pale kwa haraka, bado aliendelea kutizama pale alipoangukia Jimmy. Bado alitaka kuitumbukiza Risasi katika kichwa cha mtu huyu. Licha ya kuangalia sana lakini hakuonekana, hakumuona Jimmy na kibaya zaidi hakumuona Masimba na hatq mmoja kati ya wale watatu walioingia. Sebule ilikuwa kimya, ukimya wa kuonyesha hapakuwa na mtu. Hilo likamfanya auvute muda, hilo likayafanya macho yake yawe makini kwa kila kitu. Bastola mbili bado zilitangulia mbele. Lakini ukimya nao bado uliendelea kutamalaki. Sasa alikuwa ameamua kujitokeza, kujitokeza kuangalia zaidi na zaidi, ikiwezekana aondoke kabisa. Lakini wazo hilo likapingwa na hisia zake, bado hapakuwa na usalama wa yeye kujitokeza. Akaangaza macho yake pembeni kama ataona chochote cha kumsaidia, akakiona kisadolini kidogo ambacho kilionekana kama kimejaa maji. Akainama na kukichukua, baada ya hapo akajaribu kukitupa upande mwingine kama angeweza kugundua chochote, lakini haikuwa hivyo... Bado ukimya uliendelea kuwepo. Hilo likampa uhakika kwamba hapakuwa na watu eneo lile. Akaipiga hatua ya kwanza na ya pili, alipotaka kupiga hatua ya tatu akasikia yowe likitokea nyuma yake. Yowee lililofuatana na mgugumio wa maumivu kutoka kwa mtu. Hakutaka kugeuka kuangalia, kugeuka kwake nyuma kungesaidia kupigwa Risasi iwapo angekuwepo mtu wa kufanya hivyo. Alichokifany yeye ni kuchupa na kuangukia pembeni. Akatulia akiangaza huku na huko. Bado ukimya ulichukua nafasi yake. Hapakuonekana kama kuna tukio kutokana na ukimya. Hapakuonyesha kuwepo kwa mtu. Nani amelifanya tukio lililopita muda mfupi? Masimba! Ndiye mtu pekee wa kulifanya hili, lakini amekalia wapi? Mbona Jimmy haonekani, nani amepigwa risasi nyuma yangu? Amepigwa na Masimba au na mtu gani? Kabla hajalipata jibu bastola ikagota tena kwa mara ya pili kisogoni. Tofauti ya huyu na yule wa mwanzo, huyu hakuongea kitu. Aliendelea kuikandamiza bastola kisogoni. Kabla hajakaa sawa, akashikwa na kugeuzwa kwa nyuma.



Hapo akajikuta akitizamana uso kwa uso na Masimba, Bastola yake ilikuwa bado kichwani kwa teddy. Macho yake yalikuwa yamebadilika kupindukia. Sura yake haikuonyesha utani, sura yake haikuwa na masihara. Teddy akatulia akimuangalia masimba, alitulia akihofu na kuwa na mashaka na mabadiliko yale. Macho ya Masimba hayakuonyesha ule utani. Macho ya masimba yalimaanisha kitu kingine. Akakiona kidole cha Masimba kikishuka kwenye kitufe cha kuruhusu risasi. Akauona uso wa Masimba ukiendelea kubadilika. Hakuonyesha masihara, hakuonyeshq utani, macho yake yalisomeka kifo na sura yake aliongelea mauti. Teddy bado alitulia, bado alikuwa akiiomba toba. Alitulia kuruhusu chochote, haikuwa hivyo wala vile, bali ilikuwa hivi. Bastola ilishushwa kisha bila kuambiwa chochote akamuona masimba akiondoka. Akiondoka huku akiachwa yeye akiwa amesimama. Hakubaki hapo, alikuwa nyuma akimfuata Masimba. Alikuwa nyuma akimfuata mpenzi wake. Hakuwa na wazo tena la kukumbuka uwepo wa Jimmy.



*********

Chumba kilikuwa kimya, kila mmoja alikuwa kimya akimtizama mwenzake kwa utofauti. Wakati teddy akimtizama masimba kwa staili ya nisamehe, masimba alikuwa akimtizama kwa staili ya nautaka ukweli. Uso wake haukuwa na tabasamu, mishipa ya hasira bado ilichukua sehemu kubwa usoni. Sura ya Asteria, Godfrey Maboba sambamba na familia yake, bado zilikuwa usoni mwake. Kumuangalia teddy kulifuatana na kumbukumbu ya mtoto aliyelala mbele ya macho yake akiwa na matundu mawili ya Risasi. Mtoto ambaye hakuwa na hatia, mtoto ambaye hakujua chochote kile aliuawa kwa risasi. Chanzo kikiwa teddy. Ni teddy huyu huyu aliyetaka kumuua kule kigamboni. Kufikia hapo akaanza kutembea kusogea pale aliposimama teddy. Teddy bado hakusogea wala hakurudi nyuma. Alisimama pale pale akimuangalia masimba usoni.



"Kwa nini Umemuua Asteria na familia yake?" Lilikuwa swali, swali ambalo halikutarajiwa na teddy. Sio kutarajiwa kwa kuwa alidhani masimba anajua. Lilikuwa swali ambalo lilimshtua na kumgutusha kupita kiasi. Ni kweli alipewa amri ya kumuua Asteria, lakini hakumuua yeye kwa kuwa alimfahamu Asteria tokea wapo wote Ifakara. Alimfahamu asteria kwa undani zaidi, na hata familia yake aliijua. Ingawa alipokea kweli amri lakini asingeweza kumuua asteria na hata dada yake. "Sikumuua Asteria wala familia ya dada yake. Ni kweli amri ya kuua nilipewa, lakini kabla sijatekeleza hilo wakatumwa watu wengine wakaua ili nionekane mimi ndio nimefanya. Kuhusu familia ya dada yake sikuhusika na chochote kwa kuwa tukio lililotokea mjimwema Kigamboni lilinichanganya baada ya kugundua kuwa gari yetu ndio imelipuliwa na wewe ukiwemo ndani yake. Hilo likanifanya nirudi tena kigamboni kuangalia uwezekano wa kuuona mwili wako lakini sikuuona. Hapo nikatambua kuwa hukuwepo ndipo niliporudi nyumbani kukusubiri. Teddy alimueleza Masimba kila kitu kilichotokea, hata kuvamiwa na walinzi binafsi wa taasisi nyeti. Hakuacha kuongelea usaliti na kukubali kuwa alikuwa tayari kusaliti.



"Nani Yupo nyuma ya mpango wenu wa kutorosha madawa kutoka kwenye mikono ya usalama? Aliuliza Masimva.



"Jimmy Lambert!" Akajibu Teddy



"Ukimtoa Jimmy?



"Yupo mtu mwingine mkubwa sana, lakini mtu huyo anajulikana na watu wawili tu." Akajibu teddy.



"Nani na nani wanamjua?



"Jimmy na suresh. Akajibu teddy

Lilikuwa jibu ambalo halikutegemewa na masimba. Akamuangalia teddy zaidi na zaidi, akihitaji ahakikishiwe kama jibu hilo lina ukweli. Bado teddy alimjibu pasipo na wasiwasi. Alimhakikishia kwamba Suresh alikuwa mmoja kati ya watu wanaomfahamu mmoja ya vigogo waliokuwa nyuma ya mpango huo. Akamuangalia Tena, kisha kwa sauti tofauti akamuuliza. "Unajua kuwa nilikamatwa na kupelekwa makao makuu kabla sijahamishiwa katika nyumba moja ya siri inayomilikiwa na usalama wa TAIFA?



"Mwanzo sikujua, lakini nilipowaona walinzi wale nikajua hili suala limepelekwa mamlaka nyingine. Nilijua utakuwa umeharibu ama njama za kukushurutisha uonyesha ulipo mzigo wa madawa zinaendelea." Akajibu Teddy.



"Upo tayari kuwa na mimi au bado unaitaka pesa?

AKAULIZA MASIMBA HUKU AKIMUANGALIA TEDDY USONI.





"Tokea niliposhikiwa bastola na walinzi wa Jimmy, nilishaamua kuachana nao. Nilishaamua kuondoka katika kile tulichokuwa tunakifanya. Nipo upande wako tokea pale ulipokoswakoswa kulipuliwa. Nilifadhaika sana kwa kushindwa kugundua kile kilichotendwa. Ulikuwa mpango wao na hawakupenda kunishirikisha. Kule kuuona ule mlipuko nikauona moyo wangu ukiingia simanzi. Nipo na wewe na nitakuwa na wewe mpaka mwisho wa hili. Lakini nina hofu, wanaweza kuniua Masimba." Aliongea Teddy akimuangalia Masimba. "Lakini nina hofu" lilikuwa neno lililojirudia kichwani mwake. Teddy alikuwa ana hofu, teddy alikuwa akiogopa, akiogopa kitu gani? Lilikuwa swali pekee kichwani kwa masimba. Hakuwahi kumsikia popote teddy akiwa na hofu ya kitu chochote. Aliipenda damu na kuyapenda mapigano. Hakuogopa kifo bali alikuwa akipenda sana kuua. Lakini kwa nini leo ana hofu? Hofi ya nini? Hofu ya kuuawa ama? Hilo likamfanya masimba amgeukie Teddy na kumuangalia. Macho yake peker yalijenga maswali lukuki kwenda kwa teddy. "Umeanza lini kuogopa teddy, umeanza lini kuwa muoga? Hukuogopa Tulipokuwa Syria, uje uogope hapa, tena kwa watu wasio na chochote kile. Unaweza kunieleza kile unachoogopa?. Teddy alimuangalia masimba kwa muda, alimuangalia kana kwamba ndio alikuwa akimuona leo. Kweli aliyapenda mapambano, hakuiogopa damu na hakukiogopa kifo. Lakini leo alikuwa akikiogopa kifo na kuiogopa damu. Alijishangaa na kutokujiamini. Teddy leo alikuwa akikiogopa kifo? Lilikuwa jambo pekee lililokisumbua kichwa chake. "Masimba ingawa unawaona watu hawa si lolote lakini ni hatari hasa kwa watu ambao wapo nyuma ya mzigo uliouchukua. Mtu huyo alie nyuma, ndiye mtu pekee ninaye muogopa. Anaweza kuamua chochote kwetu na tukapotea. Unadhani ni mtu gani mwenye uwezo wa kuruhusu mzigo kama ule uchukuliwe kirahisi? Unadhani na afisa gani mwenye uwezo huo? Aliye nyuma ya tukio hili mi mtu mkubwa. Tunaweza kupotea endapo hatutakuwa makini. aliongea teddy akiendelea kumuangalia masimba. Hata masimba alinyamaza kwanza akimuangalia Teddy. Alizidi kushangazwa na uoga wa mwanamke huyu. Uoga ambao hakuwahi kuuonyesha huko mwanzo. "Teddy tulipokuwa Syria tulikuwa tukipambana na watu gani? Tulipitia mangapi Teddy? Ni mara ngapi tumenusurika kifo? Mbona huwa muoga kama leo hii? Hiki unachonionyesha leo ni tofauti? Tuachane na uoga nataka kumjua huyu mtu. Nataka kumfahamu usiku wa leo ama kesho. Nataka nimfahamu kwa njia yoyote. Suresh ndio atakaye niambia. Lakini hata wewe naamini unamjua mtu huyo. Inaonyesha kuna kiapo umekula cha kutokutoa siri nio maana unaogopa. Lakini kama wewe unashindwa kuniambia mimi kwa kuhofia kuuawa, basi mimi nitauawa kwa kumtafuta na kumjua huyu mtu." Aliongea masimba huku akionyesha kutokuwa na masihara. Teddy akachwa katika tafakuli zito, ni kweli aliogopa na kuhofia. Ni kweli alimuogopa mtu huyu, lakini atakuwa tayari kumuona masimba akiuawa kwa sababu ya woga wake? Yupo tayari kukisaliti kiapo kwa ajili ya uoga wake? Hapana! Hapana! Alijikuta akitamka maneno hayo kwa sauti kubwa, sauti iliomtoa kwenye uoga na kumpa ujasiri. Muda mfupi alikuwa akibembea kwenye kifua cha Masimba. Alikuwa tayari kupambana bila kuhofia. Na moyo wake ulimtuma kufanya hivyo pasipokuogopa.



*******

Moshi mzito ulikuwa angani ukipita na kupenya kwenye matundu ya watu mbalimbali kabla ya kutoka ndani ya chumba kile. Chupa tatu za Jack Daniels zilikuwa mezani zikitekezwa kama sio kuteketea. Watu wanne walikuwa wameizunguka meza hiyo wakiendelea kuburudika tani yao. Mwanaume alikuwa mmoja lakini wanawake walikuwa watatu. Kila mmoja alikuwa ana uhuru wa kuushika mwili wa mwanaume yule pasipo na masharti yoyote. Mwanaume naye alikuwa akifurahishwa na vitendo vyote. Akicheka na kuongea hili, punde akamuona mtu mmoja akingia chumbani hapo pasipo na taarifa. Mtu huyu alikuwa akionekana akivuja jasho sambamba na mavazi yake kuchafuka kwa damu. Hilo likamfanya kinywaji kilichopo mdomoni kumpalia. Akaruhusu mshangao machoni mwake, mshangao ambao haukudumu hasa pale mtu yulr alipoanza kuvuta hatua kusogea pale alipo. Bado macho hayakuweza kuupoteza kabisa mshangao ule. Hata pale mtu yule alipoifikia meza yake ndipo alipogundua kama kuna watu ambao hawakupaswa kuwepo pale. Akawapa ishara wanawake wale watoke. Hata wao hawakuchelewa. Baada ya kutoka kwa wanawake wale, sasa alikuwa akimtizama mtu huyu. Hakuwa mwingine bali alikuwa Jimmy

Alikuwa Jimmy akionyesha kulowa damu.



Jimmy alikuwa na hofu kubwa Moyoni, machoni na hata uso wake uliongea hofu. Alikuwa akitetemeka kanakwamba ametoka kunyeshewa mvua, alitetemeka kanakwamba ndani ya chumba kulikuwa na baridi kama ya Arusha na Hata mbeya. Hilo lilikuwa geni kwa Suresh, hilo lilikuwa geni machoni mwa kijana huyu mwenye asili ya India. Jimmy amelowa damu na tena alikuwa akitetemeka!! Jimmy leo alikuwa na hofu? Jimmy leo alikuwa akiogopa? Hilo likawa gumu kwa mhindi yule kulikubali. Bado mhindi yule alimuangalia Jimmy Kwa wasiwasi. Akainua glass na kupiga mafunda matatu kisha kuirudisha pale pale. Alimjua Jimmy kindani, alimjua jimmy kimipango na hata kimapigano, jimmy hakuwahi kumuogopa mtu, hakuwa kutetemeshwa na mtu, leo hii Jimmy alikuja akitetemeka tena huku amelowa Damu. Nani amelifanya hili? Teddy? Hapana! Teddy hawezi kufanya kitu kama hiki. Bado hakutaka kuamini kile alichokuwa akikiwaza. Maswali yake mengi sana yalikosa majibu kwa kuwa mtu mwenyewe wa kumjibu alikuwa kimya. Alikuwa kimya kama bubu ama zuzu. Hilo likamfanya Mhindi yule kusimama. Akapiga hatua huku akiyumba huku na huko kumfuata Jimmy. Sasa alimkaribia kwa karibu sana. Akamuangalia kwa umakini wa hali ya juu. Akashangaa kumuona Jimmy akiwa hana hata kovu, akiwa hana hata jeraha la kucha. Hilo likaendelea kumshangaza. Hilo likaendelea kumuweka njia panda. Akataka kuinua mdomo kuongea kitu, lakini hakufanikiwa kufanya hivyo kwani muda ule ule Teddy alikuwa akiingia pale katika mwendo wa twiga nyikani. Alikuwa akitembea na kunesa huku na kule, macho yake yakiangalia hapa na kucheki kule. Ulikuwa mshangao wa mhindi yule uliomshtua Jimmy na kumfanya naye ageuke kuangalia kule mlangoni.



Ndio aligeuka, na akakiona kilichopo nyuma yake midomo ikamkauka jimmy. Hofu ikaongezeka maradufu. Akataka kurudi nyuma lakini akajikuta miguu ikiwa mizito. Miguu haikuweza kusogea popote. Yule mhindi mkono ulishashuka tayari kwa kuichomoa bastola yake. Lakini jicho alilotazamwa na Teddy,. Likaufanya mkono wake uondoke hapo haraka. Teddy akaendelea kutembea zaidi na zaidi, alikuwa makini kwa kila hatua aipigayo. Masikio yalikuwa yakinasa kila mchakato hata kama ulikuwa wa sisiminzi. Akasimama hatua mbili kutoka waliposimama Jimmy na Suresh. Macho yake yalikuwa yakimtizama mmoja mmoja pasipo kuongea chochote kitu. Bado Mhindi yule akashangazwa na hali ile, bado Mhindi yule hakuamini kama Teddy anaweza kufanya kile anachokifanya pale.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Nimekuja kuuliza mgao wangu kutoka kwenye ule mzigo." Aliongea teddy akizidi kuwatizama. Licha ya hilo swali lakini hapakuwa na aliemjibu. Wote walikuwa kimya.



"Naondoka siku nitakayokuja tena naomba niukute mgao wangu, kinyume na hapo nitaondoka na Roho zenu." Baada ya kuongea maneno hayo teddy akageuka akiondoka kwa mwendo ule ule. Mpaka unapotelea mlangoni, si Jimmy wala Suresh aliyeongea kitu. Wote walikuwa kimya. Jeuri ya Teddy ilipitiliza. Uso wa Jimmy sasa Ulibadilika kabisa. Mishipa ya Hasira ilionekana waziwazi.



"TEDDY LAZIMA UFE, LAZIMA TUKUONDOE HAPA DUNIANI." akanong'ona Jimmy Kwa Sauti ya Chini.



"Yeah, lazima afe lazima tumuue. Kinyago tulichokitengeneza wenyewe hakiwezi kututisha. Sasa ameitangaza vita na hatafika popote tutamzima.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog