Simulizi :Nitakupata Tu
Sehemu Ya Tatu (3)
Ni asubuhi tulivu na yenye mawingu ya hapa na pale. Masimba alikuwa ametulia mahali akiitizama barabara na watu wake. Alikuwa hapo baada ya kuhaha usiku mzima akimtafuta Teddy pasipokumuona. Alikuwa hapo akiituliza akili yake akiwaza wapi ambapo teddy alikuwa amekwenda. Alijaribu kuwasiliana na Dee plus kumuuliza kama alikuwa na fununu kuhusu teddy na hata mtoto, lakini jibu alilopewa halikumridhisha. Kwamba teddy hakuonekana tokea mchana wa jana. Hilo likampa shaka kuhusu mwanawe france. Hakujua wapi teddy alikuwa amempeleka. Hilo likaendelea kumuumiza kichwa. Alichokifanya ni kuondoka pale na kuingia mtaani kunusa kama atapata chochote. Cha kwanza alichoamua ni kuelekea kijitonyama kuonana na Chief. Aliamua kufanya hivyo ili kujua alipo mwanawe na kuhusu kuweka angalizo katika watu kujua kuhusu mwanawe. Kuhusu france aliamua kumsaka kimya kimya. Aliwasili kijitonyama pale na kulakiwa kwa mshangao na baadhi ya wanausalama waliomtizama. Kila mmoja alikuwa na taarifa ya kuuawa kwa mama yake mzazi. Kwa nini yuko hapa? Yalikuwa maswali bila majibu. Salaam na pile zikachukua sehemu yake. Akawajibu kwa kichwa kisha kuingia ndani. Baada ya hapo akaongoza mpaka ofisini kwa Chief. Hapo akakutana na pole nyingine kutoka kwa sekretari wa Chief.
"Pole Masimba! !!...
"Nitapoa pale waliomuua mama yangu nitakapo tumbukuza risasi zangu kwenye vichwa vyao." alijibu masimba alimuacha Dada yule akishangaa.
"Mzee yupo ama katoka? Akauliza masimba. Kabla yule dada hajajibu mlango wa ofisi ya Chief Ukafunguliwa. Akatoka Mwamvita na Jimmy. Macho yao yakakutana na macho ya Masimba. MSHTUKO alioupata Mwamvita Ulishuhudiwa na kila mmoja pale. Chief ndiye aliyepigwa zaidi na butwaa. Macho ya Masimba yalikuwa yakimtizama Mwamvita. Alitamani kumuua mbele ya watu. Alitamani kumtafuna mbichi. Mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa hasira. Hilo Chief alilishuhudia hakuwahi kumuona kijana wake akiwa vile. Alihisi lolote litatokea, ni kweli mkono wa masimba ulikuwa ukishuka mahali alipohifadhi bastola yake. Tukio la kuuawa kwa mama yake likajirudia tena na tena kichwani kwake. Lakini chief alimuwahi na kumshika mkono akimtaka waingie ndani ya ofisi.
Chief hakukitegemea kile kilichotokea pale. Mshtuko wa mwamvita na mikono ya masimba kutetemeka kisha kushuka chini ilikuchomoa bastola, vilikuwa vitu vilivyomchanga. Yeye ni jasusi mwandamizi. Kilichotokea pale alihisi uwepo wa kitu kikubwa nyuma yao. Akamuangalia Masimba kwa makini sana. Alimuangalia akimsoma uso wake. Alichokutana nacho kikaitengeneza hofu, hofu ambayo hakujua ilipotoka. Ni vipi amuogope na kumjengea hofu kijana wake. Hilo likampa ujasiri wa kutaka kumuuliza Masimba. Wakati akitaka kuuliza, masimba akainua uso wake na kumtizama Chief. "machozi" ya machozi yalikuwa machoni kwa masimba yakishuka taratibu mashavuni. Chief akaendelea kupigwa butwaa. Masimba alikuwa akilia? Masimba anadondosha machozi? Ni kutokana na kifo cha mama yake au nikule kukutana kwao na Mwamvita? Kabla ya kupata majibu ya maswali yake. Masimba akainuka na kutoka ofisini huku nyuma akiubamiza mlango wa ofisi ya chifu kwa nguvu. Hata hili likikuwa Jipya kabisa kwake. Akauona uhasama kati ya Masimba na Mwamvita. Hilo likamfanya ahisi kuwa mwamvita na masimba wanajuana ama mwamvita anahusika na kifo cha mama wa Masimba. Akatamani kuuliza, alitamani kupata majibu kutoka kwa watu hawa wawili. Lakini sana sana kutoka kwa masimba ambaye alikuwa ni kijana wake. Hata yeye alianza kuhisi kitu kwenye kukutana kwake na Mwamvita kabla hawajawa wapenzi. Alijua ulikuwa mkutanishano wa kimipango. Ulikuwa ni mpango uliosukwa. Wazo hilo likamfanya atamani kuchukua simu yake ili kumpigia Mwamvita, lakini kabla hajafanya hivyo mlango ukafunguliwa.. akamuona Masimba akirudi mle ndani. Akamuangalia mkuu wake kwa muda kisha kwa sauti yenye Hasira akanena. "Ningejua Jana ningewaua pale mbezi. Nilikuwa na uwezo wa kuwaua wote kwa Risasi, lakini nilighairisha kutokana na uwepo wako. Watu waliotoka humu ndani ni wahusika katika mauaji ya waziri mkuu. Na hata mama yangu ameuawa kwa sababu ya hili suala. Wameuchukua uhai wa mama yangu kwa sababu ya hili suala. Nakamilisha ushahidi ili nimlete Jimmy hapa. Cha ajabu hata idara yetu inamtafuta lakini leo unamleta. Sasa sikia leo nakuletea kichwa cha Mpenzi wako mwamvita. Nitamuua kwa mkono wangu. Yeye ndiye aliyemshuti mama yangu mbele ya macho yangu. Nitamuuua. Hili nakwambia wewe na ukimwambia na kusababisha apotee nitakuua wewe. Nitakuua Chief Kama nilivyomuua Waziri mkuu kutoka na ujinga aliokuea akiufanya. Nimekwambia ili ujue kuwa sishindwi chochote." Aliongea masimba huku akilia. Aliondoka ndani ya ofisi akiwamuacha Chief katika mshangao. Mdomo uko wazi mshangao ukitawala usoni kwake. Kwamba Masimba ndio kamuua waziri, kwamba waziri alikuwa akifanya upuuzi, ni kweli ndio amefanya. Kwamba Mwamvita ndiye amemuua mama wa masimba mbele ya masimba? Lina ukweli kiasi gani hili? Jimmy anahusika na kifo cha waziri? Kwamba Masimba Jana Aliingia nyumbani kwa mwamvita? Yamekuwaje Haya? Masimba amechanganyikiwa? Yalikuwa maswali lukuki kichwani mwake. Katika maswali hayo kile cha mwisho ndicho kilichomtisha. Aliwalea vijana wake lakini kuna kipindi walimtia hofu.
Akainua simu na kupiga sehemu tatu tofauti. Baada ya hapo akatulia. Hazikupita dakika tano mlango ukafunguliwa. Aliyeingia ndani alikuwa mwanamke. Tena mwanamke ambaye hakuwahi kumjua. Huyu alikuwa amevalia buibui liliuficha mpaka uso wake. Mkonono alionyesha kushika kitu mfano wa CD. Chief akamuangalia mtu huyu kwa muda bila kuongea na mgeni wake. Mgeni huyu aliyemvamia ofisini kwake pasipo na taarifa. "Chukua hii cd.. kuna vingi vitakusaidia ikiwa ni pamoja na kumjua aliyemuua waziri mkuu." Aliongea mwanadada yule akiunyoosha mkono wake kumpa chief ile CD. Chief akamuangalia yule mwanamke kabla ya kuipokea CD na kuiweka kwenye Droo. Alikuwa katika kipindi kigumu sana. Imekuaje mtu huyu amepata ruhusa ya kuingia humu bila kuzuiwa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Wakati mwanamke yule mwenye baibui akiingia ofisini kwa mkurugenzi, masimba alikuwa amekaa ndani ya jengo lile Akitizama mlango wa ofisi ya Chief. Uingiaji wa mwanamke yule ulimtia wasiwasi kutokana vazi lake. Mwanzo alidhani labda ni kachero wa hapo, lakini alipotoka mara hii mawazo akayaondoa baada ya kuuona wasiwasi machoni kwa mgeni huyu wa Chief. Akamuacha amtangulie kwa mbele kisha yeye kufuata nyuma. Mtu yule alikuwa akitembea akigeuka kila wakati hofu yake akiona kama anatafutwa. Masimba bado alikuwa akimuangalia kwa umbali wa hatua kama Hamsini. Wakati mtu yule akiuendea mlango wa mwisho kabla hajalifikia geti, masimba alishapita kwa njia nyingine na kutokea sehemu tofauti kabisa na Eneo lile. Akatulia katikati ya watu wakiongea huku macho yake akitizima pale pale kwenye mlango. Alikuwa amemlia mashaka mwanamke yule. Alitambua alikuwa ametoka mahala na alikuja pale ofisini kwa Chief kuleta kitu fulani. Mashaka hayo yalitokana na mwanamke yule kuonekana ni mwenye wasiwasi wakati wa kuingia na hata kutoka. Muda mfupi akamuona yule mwanadada akitoka pake nje, akaanga angaza huku na huko. Baada ya muda akaonekana ikisimamisha tax kisha kuondoka eneo lile. Masimba akaendelea kutulia. Alijua na kuhisi kuwa mwanamke yule hakuwa peke yake. Alijua lazima kuna watu mahali fulani wakitimzama na kumfuatilia kwa kila kitu anachofanya. Aliendele kutulia akiangalia hilo. Ni kweli alichokuwa akikiwaza kwani baada ya dakika mbili kupita tokea mwanamama yule aondoke, akawaona watu watatu wakiondoka kutokana katika sehemu fulani na kuongoza wakitembea kama watu ambao hawakuwa wakijuana. Aliwaangalia watu wale akiwa bado amekaa hap0. Alikuwa amehisi uwepo wa mtu ama watu wengine eneo hilo. Ni kweli kama mwanzo wanaume wawili wengine wakasimama na kuanza kuondoka lakini hawa wakienda uelekeo tofauti na watu waliowatangulia. Hilo sasa likampa uhakika kwamba kina Jimmy ni wengi, licha ya wingi huo lakini aliamini Siku ilikuwa siku ya mwisho yaMwamvita kuivuta hewa ya mwenyezi Mungu. Alipohakikisha hapakuwa na watu wengine wakuwatilia shaka, masimba aliinuka na kusogea barabarani nia ikiwa ni kuisubiria tax iliyoondoka na yule mwanamke. Alisubiri kwa dakika kumi nzima lakini hakuiona ile tax ikirudi. Hilo likampa wasiwasi kuwa huwenda dereva yule ameshauawa mpaka wakati huo. Wakati akiliwaza hilo akaiona ile tax ikitokea kwa mbali. Kwa kuwa alikuwa amekalili namba za gari haikuwa shida. Alisimama barabarani na kupunga mkono. Baada ya hapo tax ikasimama. Masimba akaisogelea na kuufungua mlango wa nyuma. "Nipeleke ulipompeleka yule mwanamke. " aliongea masimba bila kuongeza neno lolote. Dereva akitii akawasha gari na safari ikaanza. Kila mmoja alikuwa kimya, dereva akiwaza pesa masimba alikuwa akiwaza kuhusu mwanamke aliyeingia na kutoka Ofisini kwa Chief. Kitu kwamba Chief amepelekewa kitu na kupewa shinikizo ni kitu pekee ambacho kiligonga kichwa chake. Hakuwahi kumuona wala kumjua mwanamke yule. Hilo likampa uhakika kuwa Jimmy alikuwa ameongeza watu wakumsaidia. Wakati wamefika Sinza kumekucha Masimba akamuona mwanamke akitembea pembezoni mwa barabara. Huyu alivaa suruali ya Jeans na Tishirt yake nyeupe. Chini alikuwa amevalia raba nyeupe sambamba na miwani ya juu ilionekana kwa watu wengine lakini kwa Masimba ikionekana ni miwani maalum inayovaliwa na majasusi. Licha ya mwanamke huyu kujibadilisha kimavazi lakini hakuweza kumpoteza masimba. Alikuwa ni mwanamke aliyetoka ofisini kwa chief muda mfupi uliopita. Akamwambia dereva yule wa Tax aisimamishe gari pembeni mwa kituo fulani cha tax. Dereva akatii kwa kusimamisha gari. Masimba akalipa kisha kushuka bila kuongea kitu. Muda wote macho yake yalikuwa kule kwa yule mwanamke. Alitembea kwa umakini akikwepa kuonekana. Safari ya mwanamke yule ikaishia kwenye saloon moja ya kike pale pale kumekucha. Masimba akatulia pembeni umbali wa hatua mia akiangalia kule kwenye saloon ile ya kike. Akasubiri kwa dakika kumi nzima lakini hakumuona mwanamke yule akitoka. Hilo likampa wasiwasi mkubwa sana, muda mfupi alikuwa akimuita kijana mmoja ambaye alikuwa anapiga Debe pale kituoni.
"Mambo vipi mzee!!? Akasalimu masimba baada ya kumuita mpiga debe.
"Fresh mkuu, nipe dili mwana." Akajibu mpiga debe yule.
"Kuna kitu nataka nikuulize lakini kabla sijakuuliza kamata hii."alisema masimba huku akumkabizi kijana yule noti ya Elfu kumi. Kijana yule akaipokea huku akimuangalia Masimba usoni.
"Duh respect mwana niulize tu nitakujibu kama nitakuwa najua chochote. Aliongea yule mpiga debe akionyesha kutabasamu kwa noti ile.
"Nahitaji kuhusu ile saloon pale. Akaongeza masimba huku akimuonyeshea kidole kuelekea ilipo saloon.
"Wewe ni Njagu au ni mwana usalama?" Akauliza yule teja huku akionyesha hofu kwa mbali. Hilo likamvutia Masimba. Akakiona kitu cha kufanya.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana mimi sio njagu wala Usalama wa Taifa. Mimi ni mtu wa kawaida. Nimekuja hapa na dada mmoja muda mfupi uliopita. Ameingia pale ndani lakini mpaka sasa simuoni akitoka." Alijieleza masimba akimtoa hofu. "Ooh wewe ndio umekuja na Dada V...? Aaah kwani hujui kinachoendelea mle ndani? Pale ni saloon kwa nje lakini palepale kuna mlango wa kutokea nyuma anbapo hapo kuna vigogo wengi wa serikali. Akajibu teja.
"Wanafanya nini Hao Vigogo? Au kuna danguro? Akauliza Masimba akijifanya hajui chochote kinachoendelea.
"Wewe kweli mgen.... akakatisha maongezi baada ya kumuona mwanamke mmoja akitoka. Hilo likamvutia Masimba kutizama kule. Macho yake yakavutiwa na mwanamke aliyetoka mle ndani. Hakuvutiwa kimapenzi bali alivutiwa kwa kuwa alikuwa ni mwanamke yule yule aliyeingia muda mfupi uliopita. Alionekana akuangaza huku na huko kama ni mwenyekutafutq kitu, punde akarudi tena ndani. Haikupita hata dakika, akawaona vijana wengine watatu tena wa kiume wakitoka. Hawa walionekana ni kama wale wakongo wanaokaa kwenye masaloon hapa mjini. Lakini muonekano wao haukufanana na watu hao. Masimba akaiona hatari ya kuendelea kuwa pale. Akamuomba Yule mpiga debe amuelekeze anapoishi ili aweze kurudi usiku kuongea naye chochote. Mpiga debe yule alimtajia Masimba mtaa na sehemu anayoishi. Baada ya hapo akatoa Noti mbili za elfu kumi kumi na kumpa huku akimuachia onyo la kutokumwambia yoyote kile walichoongea. Baada ya hapo Masimba akaondoka pale kurudi anapoishi kwa maandalizi ya kurudi usiku kwa maswali zaidi pia na kazi zaidi.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakutaka kugundulika mapema kwamba alikuwa katika viunga vile. Kutazama kwa mwanamke yule kulimpa mashaka kwamba kuna kitu atakuwa anakitafuta. Akamuaga teja yule na kuondoka katika eneo lile la Sinza. Safari hii akaamua kuelekea nyumbani ili aanze kwanza kumtafuta Teddy na kujua wapi alipo mwanawe France. Muda wote alikuwa akiikumbuka sura ya mama yake. Alijua mama yake angeamka siku yoyote na kuwa hai tena. Hakujua kuwa mama hakuamka na kamwe hataamka. Kwa mara ya kwanza tokea asubuhi akamkumbuka Dee plus. Alitaka kujua wapi alipofikia kuhusu wapi teddy alipo. Lakini hakutaka kufanya pale pale, alitaka kusubiri afike nyumbani kwanza ndipo angemtafuta. Alifika nyumbani kinondoni kigiza kikiwa ndio kwanza kinaimeza nuru ya mchana na kuukaribisha usiku huu tulivu kwa wengine. Nyumba yake ilikuwa kimya kuonyesha kutokutembelewa na mtu, achilia mbali kuishi watu. Aliiongoza mpaka getini bila wasiwasi, akajaribu kulisukuma geti la kuingilia, akashangaa likufunguka "mtego" lilikuwa neno la kwanza kutamkwa katika kinywa chake. Akafungua geti taratibu na kuingia ndani. Hapo akakutana na mwanga hafifu kutokana na kumezwa na kugiza kile cha saa moja usiku. Bado ukimya ulitawala na bado kengele za hatari ziliendelea kukigonga kichwa chake. Akatembea safari hiii bastola ikiwa mkononi. Alitembea taratibu akiufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba. Akili yake ilikuwa ikimwambia kuna hatari. Mawazo yake yalikuwa yakimwambia kuhusu hatari. Hakutaka kupuuza katika hilo. Umakini ukaongezeka zaidi na zaidi. Alipoufikia mlango akajaribu kuufungua. Cha ajabu mlango ulifunguka kuonyesha kuwa haukuwa umefungwa. Akaingiza kichwa na kuchungulia ndani. Hapo akapokewa na giza tototo ambalo halikumsaidia kuona chochote. Akaufungua mlango zaidi akaingia mwili wote. Akatembea mpaka kwenye swichi na kuwasha taa zote mle ndani. Baada ya kuwashataa akajikuta akidhangaa baada ya kuona matone ya damu sakafuni. Hilo lilikuwa jambo ambalo hakulitegemea. Akaendelea kuangalia kwa umakini huku Bastola mkononi. Alitembea kufuata matone yale ya damu. Bastola ilikuwa ikitangulia. Kila alipokuwa akigeuka hata bastola iliangalia huko. Matone ya damu bado yaliendelea. Moyo wake ulikuwa ukidunda akihisi labda mwanawe France alikuwa ameuliwa na Teddy. Akahisi jasho likimvuja pale alipoyaona matone yale yakiishia nje ya mlango wa chumba chake. Hapo akasimama na kuivuta pumzi. Punde akausukuma mlango na kuangukia ndani. Macho yake yakatua Juu ya mwili wa mtu. Ukelele wa Hofu na uchungu ukamtoka. Dee plus alikuwa amelala kifudi fudi sakafuni, mwili wake ukiwa hautananiki kwa kuchakazwa na risasi. Akahisi bastola ikimponyoka na kudondoka chini. Hakuamini macho yake. Akausogelea mwili wa Dee Plus na kupiga magoti mbele yake. Mikono yake ikatamani kuushika mwili ule lakini mikono haikumruhusu. Alikuwa akitetemeka kwa hasira. Alikuwa akitetemeka kwa hofu ya kuuawa hata kwa wanawe. Alimtegemea Dee plus katika vita hii. Alimtegemea Dee plus katika kumsaidia hili. Leo alikuwa amepiga magoti mbele ya mwili wake. Ni jana tu walikuwa wakimzika mama yake, lakini leo na yeye alikuwa marehemu tena akiwa ameuliwa kinyama.
Masimba akautizama mwili wa Dee plus zaidi na zaidi. Wakati akiutizama mwili wa Dee, akakiona kitu mfano wa picha pembeni kwa mwili wa Dee. Huku mikono ikimtetemeka akanyoosha na kuichukua ile picha. Kuitizama tu, akahisi machozi yakimdondoka. Ilikuwa picha yake akiwa pamoja na watoto wake na mama yake pamoja na Tedy. Kilichomchanganya ni kukuta katika picha ile kuna sura za watu wawili zimepigiwa alama ya X. Sura ya kwanza ilikuwa ya mama yake mzazi. Picha ya pili ilikuwa ya mwanawe France. Ina maana France wamemuua? Lilikuwa swali lililomuasha masimba. Lilimuamsha kutoka kwenye kulia mpaka kwenye umasimba wake. Masimba yule ambaye hajawahi kukiogopa kifo. Akaitizama ile picha kwa muda, kisha achovya kidole chake kwenye Damu ya Dee plus na kuchora alama ya X kwenye picha ya Teddy. "Nitakuua Teddy, Nitakuua kabla ya jua la kesho." Alitamka masimba huku akiinuka akiutizama mwili wa Dee plus. Hakuwa akiamini mpaka muda ule. Mama kisha Dee plus harafu mwanawe France ndani ya siku mbili. Akaona huu ni wakati wakuacha kuutafuta ushahidi wa waziri mkuu katika uhusika wake katika biashara ya madawa ya kulevya. Alitaka kudili na uandaaji wa tiketi kwa sababu ya kuwasafirisha watu watano. Alikuwa ni lazima aandae tiketi hizo katika muda unaotakiwa. Ni lazima Mwamvita aondoke, ni lazima Jimmy apotee, Teddy lazima afutike katika uso huu wa Dunia. SURESH NA BEN nao wanatakiwa kwenye safari hiyo. Sasa hakutaka kwenda kwa yule teja, aliamua kumtafuta Mwamvita. Hawezi kumuacha aendelee kuivuta hewa wakati mama yake alikuwa amelala kaburini. Atamuachaje Teddy wakati alishaufumba mdomo wa france na Dee plus? Hakuwa tayari kuutafuta ushahidi. Alitaka kuua kwanza kisha ndio afanye alichotakiwa kufanya. Akaona amuarifu chief juu ya kifo cha Dee Plus. Akafanya hivyo katika muda ule, kisha akaongeza na kusisitiza kuhusu kile alichomwambia kuhusu Mwamvita. Chief akaitikia kanakwamba yeye ndiye alikuwa mfanyakazi wa chini. Akiitikia huku akihisi kuvurugwa kwa kile alichokisikia. Akauona umuhimu wa kuwaweka walinzi kadhaa katika chumba alichokazwa Mtoto wa Masimba. Sasa hakuwa akiwaamini hata watu wa chini yake. Alijikuta kila kitu akitaka kukifanya yeye. Hakutaka hili suala lifike popote. Aliamua kuuufumba mdomo wake huku akifuata angalizo alilopewa na Masimba la kutomwambia Mwamvita chochote. Sasa alikuwa amekaa kimya na kushika tama.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Moyo wake haukuwa tayari kuwaacha watu hawa wakiwa hai. Alijaribu kumtafuta Mwamvita kila sehemu lakini hakufanikiwa kumuona popote pale. Hapo akaamua kumshirikisha Chief katika hili. Alitambua lazima kutakuwa na mawasiliano kati yao. Safari hii hakutaka kumpigia simu, alitaka kumfuata nyumbani kwake kwa kuwa alitaka kupata taarifa kwa kina. Akaondoka kule mafichoni kwake na kuelekea mpaka masaki. Kufika hapo akaambiwa Chief hayupo ameelekea ikulu kuitikia wito. Hilo likamfanya atulie kwa muda akitafakari nini cha kufanya. Alihitaji kujua alipo mwamvita na Hata Teddy. Lakini mpaka muda huo hapakuwa na fununu ya wapi walipo watu hawa. Hapo ndipo alipoona umuhimu wa kumfuata yule Teja kule Tandale kwa mtogole mtaa maarufu uitwao Yemen. Alihisi kama kwenda huko kunaweza kumpa taarifa ama kunusa chochote kinachohusiana na Mwamvita na Hata Teddy. Alipenya chochoro hii na Chochoro ile. Punde alikuwa amefika katika eneo hilo ambalo kwa hapa Dar es salaam liliogopeka sana Hasa kutokana na kuwa na wapiga kabali wenye uzoefu mkubwa kuliko sehemu yoyote hapa Tanzania. Akapita kwenye chochoro nyingine mpaka kuibukia kwenye nyumba ambayo alikuwa akiishi Teja yule. Ilikuwa nyumba nzuri ambayo kama ungewahi kuiona usingeamini Teja yule alikuwa akiishi katika nyumba ile. Ukimya ulikuwa umetawala huku kukionyesha kuwa Watu walikuwa wamelala mle ndani. Akaugonga mlango mara ya kwanza kisha mara ya pili. Akaisikia sauti kutoka ndani ikiuliza.
"Nani huyo?
Hakujibu bado alikuwa akuugonga mlango. Punde akasikia nyayo za mtu zikisogea mlangoni. Harafu komeo likasikika likifunguliwa kwa ndani. Sura ya mwanaume wa makamo ikatokea.
"Shikamoo mzee wangu!! Alisalimia Masimba.
"Marahaba, karibu ndani. Aliitikia mzee na kukaribisha. "Nilikuwa namuuliza Vickita Visenti kama yupo. Alisaili Masimba akimuangalia yule mzee usoni.
"Huyu kijana leo naona ameuliziwa sana. Muda sio mrefu walikuja mwanaume na mwanamke kumuuliziA, Sasa nakuona na wewe!!!. Nenda kule mwisho upande wa kulia ndio chumba chake kulipo." Alitoa maelezo yule mzee huku akimuonyesha masimba kwa kidole. Masimba akaingia ndani na kuongoza mpaka kule alipoelekezwa. Kufika mlangoni akasimama na kuchungulia ndani kupitia tundu la ufunguo. Jicho lake likatua kwenye mwili wa Yule teja akionyesha kulala. Baada ya kuona hivyo akaushika mlango na kuufunguq taratibu na kuingia. Kuingia kulikofuatana na Kutupa maji pale Kitandani. "MICHIRIZI YA DAMU" Ndicho kitu peker kilichoonekana pembeni mwa Vickita.
Mwili wa tejayule ulikuwa umelala kanakwamba alikuwa kwenye usingizi wakawaida, ukimuangalia juu juu unaweza kudhani alikuwa usingizini lakini michirizi YA damu pembeni mwa ule Mwili ndio kitu kilichomwambia masimba kuwa mtu yule alikuwa ameshasafirishwa kwenda kuzimu. akaufungua mlango akaingia ndani nakuurudisha mlango akabaki ndani akiutizama Mwili wa kijana yule. kisu kidogo kikiwa kifuani kwa kijana huyu. kwa mara nyingine alikuwa amewahiwa na watu wale. watu ambao walianza kumtia hofu nakujua kuwa alikuwa akionekana kila mahala alipokuwa akipita . akasogea mpaka kitandani alipo mwili wa kijana yule. wakati akitembea taratibu ndani ya chumba, macho yakagota kwenye pazia la dirisha. hapo akauona uwazi ambao aliutilia mashaka. uwazi uliokuwepo ulikuwa na uwezo wa kupitisha mdomo wa bastola . akasimama kwanza akikitizama hicho. baada ya kutizama sana akageuza macho kuuangalia tena mwili wa kijana. hapo akakiona kitu kilichofanya kengele za hatari kugonga kichwani Kwake. usawa wa kusimamia mtu endapo atataka kuuchunguza mwili ndio usawa ambao uliachwa uwazi. masimba hakuwa mjinga kiasi hicho. aliujua mtego, aliujua kwa kuwa kama angesogea mbele zaidi basi risasi kutoka kwa mtu ambaye alihisi kuwepo kwake kwa nje ya chumba kile. alichokifanya nI kurudi nyuma nakuizima taa kisha kuondoka taratibu bila kupiga kelele. akatokea sebuleni na kuondoka kwa kutokea mlango wa mbele. hiyo ilikuwa mbinu ya kijasusi, siku zote unapoingia sehemu ukakuta kuna tukio la kutisha kisha ukaiona hila fulani ndani yake, unachotakiwa kufanya ni kutoka hapo kwa kutokea mlango ulioingilia kwanI kwa mazingira ya kifo kilichotokea watu wanaweza kukutengenezea "mlango" wa kifo kwa kutumia kifo kilekile kilichotokea. aliujua akipita mlango wa uani unaweza kuwa mtego kwake kwa kuwekewa mazingira ya kupigwa Risasi. Alitembea taratibu safari hii akiamua kuwatafuta Teddy Harry na mwamvita kwa sabab ya kuwaondoa hapa chinI ya jua. bado tukio la kupigwa risasi kwa mama yake na kuuawa kwa Dee Plus lilikuwa likikisumbua kichwa chake. alitembea usiku ule akihitaji kuelekea mbezi beach anapoishi mwamvita alitambua kuwa Angeweza kumpata kwa wakati ule. alikuwa MakinI kwa kila hatua, alikuwa akitembea na damu ya watu nane mikono mwake. Alihitaji kuilipa damu iliyomwagwa kwa mikono yake. alikuwa pekee Katika HilI. Alitakiwa kulimaliza pasipokuimwaga damu ya mtu mwingine. Hakutaka kumshirikisha mtu katika hili. Hakumuamini mtu kabisa. Kwa alichotendewa na Teddy hakutaka kumuamini tena mtu. Alumpenda teddy, akamthamini kutoka ndani ya moyo wake. Lakini Teddy hakuliona hilo. Akafanya usaliti na kuja kumuua mama yake mzazi. Akaona haitoshi akawajeruhi watoto ambao hawakuwa wakijua chochote kilichokuwa kikiendelea. Alitaka kuutumia usiku ule kuichukua roho ya mwamvita. Hii ilikuwa mission ngumu kwake, mission ambayo haikuwa na msaidizi. Hakutaka kumtafuta msaadizi kutoka idara nyeti ya usalama. Mama yake alikuws amelala na hata Dee plus hakuwa macho tena. Mara hii alikuwa akipita pale Lugalo military Base usiku ule. Alikuwa akiiangalia kambi ile. Kambi iliyompokea kwa mara ya kwanza wakati alipotoka kwenye mafunzo ya awali. Kambi ambayo ilimpa ujasiri na nguvu ambazo ziliwafanya wakuu wake wamhamishie Idara ya usalama wa Taifa. Aliitizama kambi ile kwa makini sana. Akamkumbuka major general Hayati Imran Hussein kombe, ambaye alikuja kuwa mkurugenzi wa Idara ya usalama wa Taifa. Ndio huyu aliyekuja kuuawa na polisi walipomhisi kuwa alikuwa mwizi wa magari. Licha ya kujitambulisha kwake lakini polisi wale walimpiga risasi mbele ya mkewe. Mkewe pekee ndiye aliyepona baada ya kutoroka kupitia kwenye mashamba ya mahindi. Hata pale wauaji walipohukumiwa kifungo cha kunyongwa lakini walikuja kuachiwa huru pasipo maelezo yoyote. Kuliwaza hilo likamtoa machozi.. Punde alikuwa akiipita lugalo na kukipandisha kilima cha kuifikia Mbezi. Baada ya kufika tangi bovu, akamuomba Dereva yule amshushe hapo. Dereva akaegesha pembeni kisha kumruhusu masimba kushuka. Baada ya kushuka alimuacha yule dereva aondoke, kisha naye akaondoka pale akitembea kwa miguu.
Ulikuwa usiku wa malipo na usiku wa kupeleka tiketi na hata usafiri. Mbezi yote ilikuwa kimya sauti za pekee zikisikika. Hapakuwa na sauti ya mkazi ama mpita njia yoyote yule isipokuwa magari machache tu yaliokuwa yakipita barabarani.. alitembea na kivuli cha miti wakati mwingine akikwepa taa za magari mpaka alipoifikia Africana. Kufika hapo akaangalia huku na huko lakini leo hapakuwa na watu, kwani hata ile bar ambayo jana aliikuta wazi. Leo ilikuwa imefungwa na hapakuwa na kitu chochote. Wakati akiendelea kuchunguza hiki na kile, mara akauona mwanga wa taa za gari zikusogea maeneo yale. Akajibanza kwenye jumba fulani bovu, hapo akaliona gari ya kifahari ikipita. Aliitizama kwa sekunde kazaa akaondoka pale akiifuata nyuma nyuma. Alikuwa akihama hapa na kuhama pale. Alikuwa akitembea kama mcheza sinema. Mpaka gari ile inasimama Nje ya geti la jumba analoishi Mwamvita, masimba naye alikuwa umbali wa hatua tatu tu. Mlango ukafunguliwa akashuka mwamvita akiwa sambamba na watu wawili. Kati ya hao mmoja tu ndiye aliyemtambua. Alikuwa yule mwanamke alikuja ofisini kwa chief mchana ule na ndiye aliyehusika na kifo cha yule teja. Wote wakaingia ndani pasipokuacha mtu yeyote nje. Ulikuwa muda wa sekunde mbili zilizotumiwa na Masimba kuifunua buti ya gari na kujitupa ndani yake. Akatulia kama Dakika mbili akawasikia watu wakirudi wakiongea.
"Huyu Teddy itabidi itafutwe popote na kuuawa. Hawezi kujiondoa katika mpango huu. Ni lazima mzigo tuupate na lazima Masimba na Teddy tuwasafirishe kuzimu. Nimejisikia raha sana kumuua Dee kwa mkono wangu. Ndio maana hata mama wa masimba alipoleta ujinga sikumkopesa. Teddy atafutwe popote sambamba na yule mtoto." Alijitapa mwamvita bila kujua maneno yake yalikuwa yakimchoma Masimba. Alitamani kufungya buti na kutoka. Lakini kitendo cha kusikia teddy haonekani, kilimpa faraja ya kutambua kuwa France alikuwa hai.
"Teddy tutampata nyie msijali. Tunachotakiwa kufanya ni kuendelea kumlaghai Chief aweze kuitisha Mkutano na Wana Habari ili aionyeshe ile video inayomuonyesha Masimba akimuua waziri. Tukilifanikidha hilo tutakuwa tayari." Akaongea mwanamke mwingine huku wakiingia kwenye gari na muda mfupi akaliona gari likitembea. Hakujua wapi walipokuwa wakielekea. Na pia hakuwa akiyasikia tena mazungumzo ya watu wale. Muda wote alikuwa akifikiria jinsi ya kulimaliza hili. Ilikuwa ni lazima azuie chief kuitisha mkutano na waandishi wa habari na pia alitakiwa kuizuia hiyo video ama aipate na iwe mikononi mwake. Alikuwa lazima afanye hivyo huku akiamini kuwa angemsaka Teddy hata pale atakapo wamaliza hawa. Gari ilitembea kwa dakika kama Ishirini na tano ama thelathini. Ghafla akasikia likipunguza mwendo na kupiga honi kadhaaa. Mara lango likafunguliwa akahisi gari ikiingizwa ndani. Punde gari ilikuwa ikisimama. Akaisikia milango ikifunguliwa kisha akasikia hatua za watu zikitembea kuelekea ndani. Baada ya ukimya fulani kutawala, akafunua buti na kuchungulia kwa nje. Hapo akauona uwazi wa kuweza kutoka. Sekunde ya pili alikuwa akiangukia pembeni na kuchupa tena mpaka sehemu fulani ambayo ilikuwa na mbaombao. Akatulia hapo kwa muda akitazama kila kitu kinachoendelea mle ndani. Alikaa hapo kwa muda wa kama dakika tano akawaona watu walewale wakitoka. Wanne kati yao wakajipakia ndani ya gari lakini Mwamvita hakufanya Hivyo. Baada ya maongezi Mawili matatu gari ile ikaondoka huku mwamvita yeye akirudi ndani. Baada ya mwamvita kuingia Masimba naye aliianza kutambaa kwenye ukuta mpaka penbeni mwa jumba lile. Kufika hapo akaliona dirisha Moja la kioo likiwa wazi. Akasogea mpaka hapo na alipolifikia akachungulia kwa ndani. Macho yake yakakutana na mwamvita akiwa hana hata nguo maungoni mwake. Alikuwa akielekea bafuni kuoga. Baada ya Mwamvita kutoka mle chumbani Masimba akasogeza kioo na kujitumbukiza ndani tayari kumsubiri mwamvita. Akachepuka mpaka kando ya mlango na kutulia hapo. Akatulia hapo kwa Dakika Tano. Punde akasikia nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni. Punde akamuona mwamvita akiingia akiwa mtupu vile vile.
Punde akamuona Mwamvita Akiingia tena akiwa mtupu. Alikuwa kama alivyozaliwa. Hilo halikumfanya masimba ashtuke. Bado alitulia huku bastola yake aina ya Revolver colt 48 ikiwa mkononi. Akamuacha mwamvita aingie kwanza. Na alipohakikisha ameingia Masimba akaufunga mlango kwa ndani. Mwamvita hakukitegemea kitendo hicho. Kwani baada ya kuusikia mlango ukifungwa akageuka akiwa mtupu vile vile. Akakutana na Mdomo wa bastola ukimtizama. Alikuwa akiangalia na masimba. Alikuwa akiangaliana na mtu ambaye alijua na kuhisi labda alikuwa Tanga kwenye mzima. Masimba hakuongea wala hakuwa anafanya chovhote. Bado alimuangalia Mwamvita kwa utulivu huku macho yake yakicheza pande zote. Kidole kikashuka taratibu kwenye kitufe cha kufyatulia Risasi. Rukia alikuwa akitokwa jasho jingi, alikuwa akikiogopa kifo. Akatamani kuongea kitu lakini akashindwa. Punde risasi ya kwanza akafyatuka na kutua kwenye kifua cha mwamvita. Risasi ya pili ikatua kichwani na kukifumua kichwa cha Mwamvita. Risasi ya tatu na nne zilitua kwenye matiti yake yote. Kila ilipokuwa akiifyatua risasi alikuwa akikumbuka kifo cha mama yake. Alikuwa akipiga risasi kwa Hasira, mwili mzima wa mwamvita ulikuwa umetapakaa damu. "Wasalimie kuzimu.. waambie bado naendelea kuwakusanya wote tayari kwa kuwapeleka huko." Aliongea Masimba huku akiuangalia mwili wa mwamvita. Baada ya kuhakikisha mwamvita amekwishakukata roho akauacha mwili pale pale kitandani kisha yeye akatoka Nje kupitia pale pale Dirishani. Safari hii aliamua kurudi Sinza kumekucha tayari kukijua kile ambacho kinaendelea ndani ya Saloon ile kilichosababisha mpaka Teja yule kuuawa. Alifanikiwa kutoka pasipokuonekana. Akaanza kuutafuta usafiri katika eneo lile ambalo bado hakujua ni wapi. Alitembea usiku usiku pasipokupata usafiri mpaka karibu na kijimji fulani Hivi. Hapo akafanikiwa kuiona pikipiki ambayo ilikuwa akipita. Alichokifanya ni kuisimamisha kisha kuwambia Dereva wapi anapoelekea. "Duh Bro mbona Huku ni Mbali sana na Sinza!! Alishangaa Dereva yule huku akianza kuonyesha wasiwasi Juu ya Masimba. Ndio kwanza masimba alikuwa akishtuka kwamba kumbe hakuwa ndani ya Jiji. "Kwani hapa ni wapi ndugu Yangu? Hatimaye Masimba akauliza huku akitabasamy ilikumtoa hofu kijana yule. "Hapa ni Bagamoyo brother, kwani unatokea wapi? Akajibu kijana yule kisha kuuliza tena.
Ikabidi masimba adanganye ili kupata usafiri wa kumrudisha jijini Dar es salaam. Hakutaka kuchelewa kwa kuwa bado kazi ilikuwa ngumu. Bado alikuwa na mission ngumu sana katika usiku. Usiku wa malipo ya damu ya watu wasio na hatia. Alitamani sana kuwamaliza wote kwa usiku ule ili aanze kumtafuta Yule Malaya Teddy. Alitaka kumuua mwisho kabisa. Hapo ndipo alipoona umuhimu wa kumdanganya kijana huyu. Uongo ambao ulimlainisha kijana na kukubali kumbeba Masimba kumpeleka Jiji Dar es salaam. Pikipiki ikaendeshwa usiku kwa usiku kwa mwendo wa kutisha na kuogopesha. Ilikuwa ni lazima aimalize mission katika muda wa masaa mawili yaliobaki, kwani saa yake ya mkononi ilikuwa ikimwambia ilikuwa saa saba na nusu usiku. Wakati wanaikaribia Bunju wakaiona gari ikija kwa mbele yao. Dereva akaupunguza mwendo kwa kuogopa kukamatwa. Masimba alimsisitiza aendelee kuendesha na Asiogope. Dereva akatii na kuanza kuendesha. Mbele kidogo kuikaribie ile gari wakapigwa mkono. Masimba akamwambia kijana yule asimame na Asiogope chochote. Kijana yule akasimamisha pikipiki na kutulia. Punde wakawaona watu watano wenye makoti makubwa wakisogea. Mkono wa Masimba Ukashuka taratibu alipoihifadhi bastola. Lakini watu wale waliposogea sans akagundua kwamba ni Askari. Akautoa mkono kisha akashuka. Polisi nao Wakawasogelea mpaka pale.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Naomba Leseni yako ya udereva." Polisi mmoja akaamuru. Dereva yule hakuwa na leseni ya udereva. Baada ya Masimba kuona dereva wake ana hangaika. Akasogea karibu na kumuita askari mmoja pembeni. Askari yule akasogea kwa umakini sana huku SMG ikiwa mkononi. Kumfikia masimba tu akapewa kitanbulisho kimoja kati ya vingi alivyonavyo masimba. Baada ya kukipokea na kukiangalia, askari yule akakamaa kwa Saluti. Kitambulisho kikarudishwa kwa mwenyewe kisha wakaruhusiwa waendelee na Safari yao. Askari wote walikuwa wakintizama Masimba kwa mshangao. Hawakuwahi kumuona Zaidi ya kumsikia. Hawakuwahi kumuona Zaidi Ya kuona na kusoma sifa zake. Wakaendelea kumuangalia mpaka anatokomea. Hawakuwa wameamini na licha ya kutokuamini macho yao lakini walifarijika sana kumuoba mtu huyu.
*********
Kama ilivyo kwa maeneo mengi ya Jiji la dar es salaam kutokukosa watu hata iwe usiku wa maneno, ndio hali ambayo aliikuta Masimba Baada ya kufika hapo. Bado madada poa walikuwa kwenye biashara za kuuza miili yao. Mateja wengi bado walikuwa barabarani wakipiga debe na hata usafiri wa kukupeleka popote bado ulikuwa ni wakumwaga. Alishuka kumekucha na kumlipa dereva wa pikipiki pesa yake. Basda ya hapo akamwambia anaweza kurudi na asiwe na wasiwasi. Baada ya kuachana na dereva yule, masimba akatembea kama mtu wa kawaida mpaka nyuma ya Jengo ambalo kwa mbele ndio kulikuwa na Ile flemu yenye saloon. Cha ajabu lilikuwa jengo kubwa sana. Jengo ambalo lilikuwa na vyumba vingi sana. Na kingine kilichokuwa kikimshangaza ni miguno ya watu wanaofanya mapenzi kila pale alipokuwa anasogea. Hilo likampa shaka na kuamini labda jumba hili lilikuwa na danguro ama ni gesti bubu. Akaendelea kutembea na ukuta wa jengo lile mpaka alipofika mbeli kidogo ndio akauona mlango wa kuingilia. Kuuona mlangoni huo kuliendana na kuwaona walinzi watatu waliokuwa wakizunguka hapo, mikononi wakiwa na Bunduki kubwa. Kuwaona walinzi wale kukampa picha halisi kuwa sehemu ile haikuwa gesti wala danguro bali kulikuwa kukifanyika Biashara nyingine zaidi, tena biashara kubwa na ya hatari. Akaongeza umakini safari hii akiamua kupambana kwa Mikono. Akatafuta njia nzuri ya kuwakabili walinzi wale. Akaendelea kuwatizama kama atawaona walinzi wengine, lakini aligundua walikuwa walewale watatu. Muda huu alikuwa amehama pale na kuhamia huku. Alitaka kuwazunguka na kuwatokea kwa nyuma. Aliwaangalia kwa hatua zao na ukaaji wao. Akahamisha macho kwa kila mmoja aliyekuwa pale. Wote walikuwa wamesimama sehemu moja wakiongea. Alikuwa na uwezo wa kuwachapa Risasi wote lakini hilo akaliacha baada ya kuyaona mazingira. Akatembea na giza mpaka karibu kabisa na walinzi wale. Sekunde hii alikuwa akisogea kwa karibu zaidi. Ulikuwa ni muda wa kuwaonyesha kwa nini Aliaminiwa na Taifa. Akawatokea pale pale kwa kushtukiza. Yaani sekunde hii walikuwa wenyewe wakiongea, lakini sekunde ya pili walijikuta wakiwa wanne. Alikuwa ameongezeka mtu mmoja katikati yao. Mtu ambaye aliwashangaza na hata kuwafanya wababaike. Haiwezekani muda huu waongee watatu, harafu sekunde ile ile aongezeke wa nne. Mikono yao ikataka kushuka kwenye tufe la kuachia Risasi. Ni wakati huo kila mmoja alikuwa akiugulia maumivu. Yalikuwa mapigo yaliompigwa katika namna ambayo hakuna ambaye aliiona. Kila mmoja alikuwa ikigugumia kwa maumivu huku akishika kwenye korodani. Hakutaka kuwapa nafasi ya kujiuliza. Lakini wakati akijiandaa mmoja akarusha teke lakini likapita hewani baada ya kukwepwa kwa ustadi. Akarusha tena ngumi tano mfululizo lakini zilipita hewani. Safari hii akakutana na teke la Taya. Akajikuta mlinzi yule akiisalimia sakafu. Wakati huo walinzi wengine walikuwa wamekaa sawa. Yakafuata mapigano yaliochukua dakika mbili tu. Walinzi wote walikuwa chini wakiwa hawana uhai.
Akawaacha chini wakiwa wamelaliana. Sasa akawa anaingia ndani ya jengo lile kwa kupitia mlango wa ule ule. Bado miguno ya mapenzi ilikuwa ikisikika. Bado malalamiko ya mahaba yalikuwa yakitamalaki katika ngoma za masikio yake. Hapo akahamisha mawazo yake kwa Teddy, alimkumbuka Teddy kwa mengi. Alikuwa msichana wa kipare lakini alikuwa akiyajua mapenzi kama mzaramo ama mngoni. Alikuwa akijua kuutumia mwili wake mwembamba kwa utulivu na ufundi mkubwa. Ukimuona akiwa kwenye uwanja wa fundi seremala ungehisi labda alitokea Tanga yalikozaliwa mapenzi. Akapita akiyalazimisha masikio yake yatii kile ambacho alikwenda kukitenda. Akalifungua geti taratibu na kuchungulia kwa ndani, hapo akakutana na giza totoro. Akalifungua zaidi na zaidi kisha kujipenyeza ndani. Bado utulivu haukuwepo, bado miguno iliendelea. Akatembea sambamba na ukuta mpaka karibu kabisa na kibanda ambacho kilionyesha kilikuwa ni cha walinzi. Akatulia hapo akaangalia kila kona kwa chati. Kwa kuwa alikuwa amezoea giza, kwa kuwa macho yake yalizoea hali hiyo. Akafanikiwa kuwaona watu waanne katika sehemu tofauti. Licha ya uwepo wa watu wale, lakini hawakuonyesha kama walimuona Masimba. Hilo likamfanya masimba asonge mpaka karibu na mlango wa kuingilia ndani. Kufika hapo akaisikia minong'ono ikitokea ndani. Masimba akachomoa bastola kisha kuiweka Tayari. Bado minong'ono iliebdelea tena na tena. Punde akahisi ukimya lakini ukimya huo haukudumu sana, kwani Ndani ya Sekunde kumi miguno ikaanza kusikika kutoka ndani...
Ukimya ukachukua nafasi maeneo yale. Hakuwa akisikia tena ile minong'ono. Akausogelea mlango katika aina fulani ya ukimya. Hata alipoufikia mlango bado hapakuwa na kizuizi chochote. Masimba akajaribu kutizama huku na huko, lakini bado hapakuwa na kizuizi. Bado hapakuwa na mtu. Mkono wake ukashika kitasa na kukizungusha, mlango ukamtii kama mfano wa mbwa anapomtii chatu. Bastola ilikuwa imetangulia Mbele tayari kumuondoa mtu yoyote. Akaufungua zaidi kisha kuingia. Alipoingia ndani alipokewa na ukimya tena. Kuingia kwake tu hata ile miguno ikapotea. Akaikamata bastola zaidi na zaidi. Kidole bado kilisubiri kuifanya kazi yake. Kazi ya kutoa tiketi na hata usafiri. Usafiri wa kuwapeleka watu kuzimu. Alitaka wakapumzike sambamba na mama yake na hata Dee. Alitaka wakajibu mashtaka yake mbele ya Asteria na Familia yake. Kuingia hapo akapokewa na harufu ya mipira ya kiume. Harufu ya condom ilikuwa imetawala katika nyumba ile. Akaongeza hatua mbele kuwatafuta wasafiri. Akaipita sebule bila kukutana na kizuizi chochote. Aliposogea mbele akasikia vishindo vya mtu vikionyesha mtu kusogea kule alipo. Punde akamuona mwanamume akitokea katika giza lile. Giza ambalo alishindwa kutambua kwa nini limeachwa kutawala pale ndani. Mwanaume yule akatembea na kupita karibu na Masimba bila kumuona. Masimba akamuacha apite, alivyopita akamtokea kwa nyuma na kumkata karate ya Shingo. Mtu yule akaanguka kama mzigo. Baada ya kuhakikisha mtu yule hayupo hai, akamsachi mifukoni. Akamkuta na Bastola mbili sambamba na vitamburisho kadhas. Vyote akavichukua na kuvisunda mifukoni. Baada ya kumaliza vyote akamshika na kumuweka pembeni. Akasogea pale na kuanzs kutembea kuingia ndani alipotokea yule mtu. Wakati anaukaribia mlango akasikia watu wakiongea kwa ndani. Katika mazungumzo yao akahisi walikuwa watatu kutokana na mchanganyiko wa Sauti zao.
"Mbona Fred harudi? Richie hembu muangalie inawezekana amezima. Aliisikia sauti ikitokea ndani. Masimba akajua kuna mtu anakuja. Hivyo akajibanza pembeni. Mara akauona mlango ukifunguliwa kisha mtu tena akatokea. Masimba akamuacha asogee mpaka usawa wake. Hata alipoufika usawa ule akajikuta akiguswa na kitu cha barifi. Kisha sauti nzito ya mwanaume ikanguruma. "Tulia kama Ulivyo, ukifanya chochote sitasita kukusafirisha kuzimu." " mtu yule hakutarajia lile, akahamanika na kutaka kupiga kelele. Masimba akamuwahi kwa pigo moja ya kidogoni, mtu yule akaanguka kama furushi. Masimba akamuwahi na kumshindilia ngumi kama tano. Mtu yule akatepeta kama mlenda. Alimpekuwa mifukoni. Huyu hakuwa na Silaha yoyote zaidi ya paketi tano za condom. Akamuacha sasa alikuwa akizama ndani kuwakabili watu ambao walikuwa ndani. Aliusukuma mlango taratibu na kuchungulia kwa ndani. Watu wawili walikuwa wamepakatana miguuni. Kilichomshangaza huku ndani taa hafifu zilikuwa zikiwaka. Nuru hiyo ndio iliyofanya macho yake kutua kwa watu wale wawili. Mwanaume na mwanamke. Akaufungua mlango tena na kupiga mluzi. Yule mwanaume aliyekuwa amempakata mwanamke akamuomva mwanamke asimame kisha yeye kusogea pale mlangoni huku akiuliza.
"Richie kuna nini? Aliuliza mtu yule huku akiufungua mlango pasipo na tahadgari. Akajikuta akikutana na mapigo matatu ya kung fu. Mtu yule akapepesuka na kwenda kumuangukia mwanamke yule. Masimba hakuitoa nafasi hiyo kwa mtu yule kuinuka. Akawawahi wote pale chini huku mdomo wa Bastola ukiwatizana sawa sawia. Wote walikuwa wakitweta kwa hofu. Kila mmoja alikuwa ameyatoa macho yake akimtizama Masimba. Hofu ilikuwa ikionekana machoni mwao. Hofu ambayo haikufanana na uonekanaji wa watu hawa. "Nimekuja na tiketi zenu za kuzimu, nimekuja na usafiri wa kuwapeleka huko. Lakini mkinijibu maswali yangu naweza kufikiria kuwaacha." Aliongea masimba Akiwatizama watu wale pasipo kuonyesha utani. "Usituue tutakujibu maswali yako." Aliongea mwanamke yule akitetemeka.
"Jimmy na suresh wako wapi? Akauliza masimva.
"Mimi sijui unauliza nini. Alijibu yule mwanaume akimuangalia masimba usoni. "Narudia tena wako wapi Jimmy na Suresh? Aliukiza tena safarii hii akiuinua mkono ulioshika bastola. "Unataka nikujibu mara ngapi? Nimesema sijui.. akajibu tena yule mwanaume. Muda ule ule mlipuko mdogo ukatokea, bastola ya nasimba ilikuwa imekohoa. Risasi ikatua kwenye paja lake la kushoto. Akapiga yoweee kubwa sana. "Utasema hutasema? Akauliza masimba huku bado bastola yake ameielekeza kwa mtu yule aliyekuwa akigumia kwa maumivu. Wakati mtu yule akiharibu kujibu mlango ukasukumwa kwa nguvu huku risasi kama mvua zikimiminwa mle ndani. Masimba akajivingirisha chini kisha kuchupa na kuangukia pembeni. Risasi zikapita muda ule ule akasikia yowee kutoka pale alipowaacha wale majambazi. Baada ya muda wa dakika tano. Risasi zikakoma ukimya ukatawala Eneo lote. Masimba Bado alikuwa amejificha pale akiwaangalia wale watu. Hata wao walionekana wakitafuta kitu. Hapo akajua walikuwa wakimtafuta yeye. Hakutaka kuwachelewesha, bastola yake ikakohoa tena mfululizo. Watu wanne walikuwa wakianguka mithili ya magunia. Walikuwa tayari kwenye safari ya kuzimu. Baada ya kuhakikisha amewamaliza wote akainuka na kusogea pale. Hapo akagundua hata yule mateka wake wakiume alikuwa ameuawa. Lakini kilichomshangaza ni kutokumuona mwanamke yule. Wakati akiendelea kutafuta akasikia kilio kutoka chini ya kiti kikubwa . Punde akamuona msichana yule akiinuka huku akitetemeka. Bastola ya masimba tayari ilikuwa ikimtizama. Lakini alipomuangalia vizuri usoni.. Akajisemea malaika huyu hapaswi kufa. "Nifuate tuondoke hapa kabla polisi hawajaja." Aliongea Masimba Huku akimvuta yule msicgana waondoke mle ndani.
******
Walikuwa wawili tu ndani ya chumba cha hoteli ile. Bastola ilikuwa bado mkononi kwa masimba akuendelea kumuangalia mwanadada yule aliyekuwa akitetemeka kwa hofu.
"Unaitwa nani? Akauliza masimba akiendelea kumtizama.
"Nani.!!!? Mimi au... aliuliza Binti huku akitetemeka.
"Kwani hapa tuko wangapi?" Akauliza Masimba akimuangalia tena.
"Tupo wawili." Akajibu tena Hofu ikionekana machoni.
"Basi tambua nakuuliza wewe.. naomba unijibu kabla sijabadili maamuzi." Aliongea Masimba.
"Naitwa SALHA ....." akajibu msichana yule. "Umefikaje pale kwenye ile nyumba na nani amekufikisha? Aliuliza Masimba akiendelea kumuangalia. "Nimeletwa pale na Jimmy. Wakati ananileta aliniambia kuwa amenitafutia kazi, lakini nilipofika aliniweka pale kama Msimamizi wa Biashara yao. Alijibu yule msichana. "JE ni Biashara gani inafanywa pale? Na kwa nini ulipogundua kazi ulioambiwa haipo, wewe ukaendelea kukaa? Binti yule akamuanglia Masimba kisha kwa sauti yake ya upole akajibu. "Naogopa kukwambia wataniua..... Maana nishatishiwa kupigwa bastola. Baada ya kumuuliza kwa nini ana muogopa mtu mmoja aitwaye masimba.". " kwahiyo una muogopa Jimmy lakini huniogopi mimi? Tambua mimi ni israil nikiamua ufe haufikishi sekunde moja. Naomba nijibu maswali yangu kabla sijakupa tiketi yako." Alinguruma Masimba akimuangalia binti yule. Salha akainua uso na kumwangalia masimba kisha kwa Sauti dhaifu akasema ....
Binti akainua uso kisha kwa sauti dhaifu akasema. "Biashara inayofanyika pale ni uingizaji na usambazaji wa madawa ya kulevya hapa nchini. Kuna viongozi wengi wa serikali, wabunge na mawaziri ni watu wenye hisa kwenye biashara hiyo. Na wafanyakazi wote tuliambiwa kwamba nilazima tufumbe midomo yetu la sivyo tutauawa. Wenzangu wengi wameshauawa kutokana na kuivujisha siri hii. Nadhani hata nami nipo njiani kuwafuata. Kama usiponiua wewe basi wataniua wao." Alijibu msichana yule hofu ikionekana kwenye macho yake. Masimba akamuangalia kwa nukta kisha akamuuliza tena.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unaweza kunitajia majina ya mawaziri watatu unaowajua? Swali hilo lilionekana kuwa gumu kwake. Akamuangalia Masimba kisha akaonekana kufikiria kwa muda. Harafu akashtuka kutoka huko na kutingisha kichwa kabla ya kusema. "Hapana siwezi kufanya hivyo, nitauawa.". Hilo likaonyesha kumkwaza masimba. Akamuangalia kwa muda huku mdomo wa bastola ukimlenga msichana yule. "Naomba unijibu maswali yangu, la sivyo nitakusafirisha kuzimu sekunde hii hii. Kama hujui mimi ndiye Masimba ninayeogopewa na mabosi zako. Nina uwezo wa kukufanya chochote. Sitaki unilazimishe kufanya hili." Aliongea huku akiendelea kumiangalia mwanamke yule. Akausoma mshtuko kutoka usoni kwa mwanamke yule. Mshtuko uliotokea baada ya kulitaja jina lake. Sasa akaiona hofu ikiyeyuka katika uso wa mwanamke yule. Tabasamu hafifu likaupamba uso wake. Lakini ghafla akaliona tabasamu likiyeyuka na kupotea ghafla kama mshumaa kwenye upepo mkali. Sura ikagubikwa na hofu tena. Ni hofu hiyo iliyompumbaza masimba. Ni hofu hiyo hiyo iliojenga maswali lukuki kichwani kwa masimba. Tabasamu katika sekunde tatu, lakini tabasamu likapotea katika sekunde ya nne na ya tano. Hofu ikamuingia tena mwanamke huyu. Kwa nini hofu? Kwa nini aogope? Anaogopa Jina langu ama anawahofia watu wake? Yalikuwa maswali, maswali ambayo hayakufanikiwa kupata Jibu katika wakati ule ule. Kwani ni muda ule aliokuwa akiongea na Salha akauona mlango ukitingishwa kisha kukasikika mlango kugongwa. MASIMBA NA SALHA wakatizamana, waliangaliana katika namna ya kuulizana "Huyo ni nani" hakukuwa na mwenye jibu. Lakini hapo hapo akamuona Salha ikisimama na kuufuata mlango. Hata hilo likamshangaza na kumburudisha machoni na hata Moyoni. Hakuburudika kwa utamu wa mtikisiko wa Nyuma wa Binti huyu, hakuburudika kwa kulitamani hilo, bali aliutamani uamuzi wake na kujiamini kwake. Huyu alikuwa kama Teddy Harry Wake. Huyu alikuwa Teddy yule wa kipindi kile. Teddy aliyekuwa haogopi risasi na hata kifo. Hilo likamkumbusha Syria. Kwenye mission ngumu ambayo haikuwahi kutokea. Salha alikuwa ni mfano huo. Licha ya hilo lakini bado alikuwa makini na kila hatua ya binti huyu. Hatua ya mwanamke ambaye alionyesha kuwa na vitu vingi. Hofu ikapotea usoni, hofu ikapotea katika muda huu huu. Alikuwa mfano wa kinyonga, alibadilika kila wakati. Kila hatua yake ilikwenda sambamba na mdomo wa bastola wa Masimba. Hakumuacha ageuke akiwa pekee. Ni pale alipoufikia mlango ndipo likatokea la kutokea. Mlango ukasukumwa wakaingia wanaume katika aina ya kuburudisha na kusisimua. Kila mmoja aliingia akiruka hapa na kutua pale. Ilitia raha na hata kuburudisha pia. Lakini wakati akiliangalia hilo hata yeye alikuwa ameshahama pale na kuangukia pembeni. Ni wakati akitua hapo chini akimuona mwanamke yule akifanya kitu ambacho kilimfanya ashangae. Binti alikuwa akionyesha burudani. Alikuwa akihama hapa katika kuwakabili watu wale. Alikuwa akipiga mateke ngumi na hata vichwa. Alikuwa akichanganya kung fu kareti na hata martial combat. Ilikuwa burudani kumtizama na ilikuwa burudani kumuangalia. Haikupita hata dakika mbili tayari wanaume wale walikuwa wamelaliana wakiwa hawana uhai. Hilo likikuwa jingine kwake. Licha ya uzuri wake, licha ya urembo na muonekano wake lakinikumbe alikuwa ni Hatari. Binti yule akaufunga mlango tena na kurudi pale alipokuwa Masimba amesimama. "Nipo tayari kukujibu maswali yako. Nipo tayari kukujibu chochote kile utakacho." Aliongea Salha akimuangalia Masimba. Masimba naye akamtizama. Wakatizamana na kutizamana. Kulikuwa na sumaku machoni kwa mwanamke huyu wa kichaga. Macho yalikuwa yakiongea vitu vingi sana. "Nadhani lipo swali langu hukunijibu." Akakumbusha, Kisha akaongeza, "nataka kujua majina ya mawaziri na hao wabunge. Pia nataka kufagamu walipo Jimmy na Suresh." Salha akamuangalia Masimba kisha kwa sauti ambayo haikuwa na Hofu Akajibu.
"Mawaziri ni Haji Mvula waziri wa maliasili na utalii. Waziri Utajiju Nyuma wa mambo ya Nje na mwingine Alikuwa Waziri mkuu ambaye amemuua wewe juzi. Wabunge ni Hagare Maro wa jimbo la tarime. Selestine pascal wa ukerewe na bibi Grace Bwahama wa kigamboni. Akajibu Salha.
"Jimmy na Suresh wako wapi?" Akauliza tena Masimba. "Jimmy na Ben Wamemfuatilia Teddy kwani inasemekana ametoroka hapa jijini akiwa na mtoto wako waliemchukua baada ya kumuua mama yako mzazi. Inasemekana Teddy aliomba likizo ya ghafla kazini na alipokubaliwa jana alionekana akitoka Airport na tokea hapo hakuonekana tena mpaka muda huu. Baada ya kufuatilia huku na huko waligundua Teddy alikuwa ameelekea Arusha akiwa na mwanao tayari kwa kuihama Nchi. Wakapiga simu kwa watu wetu kule kuwapa taarifa na kuwataka wafuatilie hilo lakini majibu yaliokuja ni kwanba Teddy hakuonekana Airport wala kwenye barabara yoyote. Ndipo jimmy na Ben walipoamua kwenda arusha kuongeza nguvu."
Teddy ametoroka na mtoto na inasemekana wameelekea Arusha. Lakini tulipowasiliana na watu wetu kule hawakumuona Teddy popote pale licha ya kupekuwa viwanja vyote vya ndege sambamba na kuangaliwa kwa umakini kwa kila gari ambayo ilikuwa ikiingia arusha na kutoka. Hivyo basi Jimmy na Ben wameelekea huko kumtafuta Teddy ili wamuue ili wamchukue mtoto wako iwe chamba cha kukufanya wewe urudishe mzigo uliouchukua." Aliongea salha akimtizama masimba kwa umakini. Alitaka kugundua nini ambacho angekishuhudia machoni kwake. Lakini hakukutana na chochote kile, hakukiona alichokuwa anakitafuta. Licha ya masimba kutokushtuka kwa taarifa ile, lakini moyoni na kichwani hakuwa katika usawa. Hakuwa katika utimamu wa kiakili na hata kimwili. Alimuwaza france, alimuwaza mwanaye aliempenda sana. Hakutaka kukubali mwanawe kupotezwa. Alinhitaji mwanawe akiwa hai. Alimuhitaji france akiwa kwenye tabasamu lake alilolizoea. Lakini alipofikiria kuhusu Teddy kutoroka bado mwanamke huyu aliiyumbisha akili yake. Bado mwanamke huyu hakueleweka upi msimamo wake. Alifanya mauaji na usaliti wote sababu ya Kundi lao. Hata kuuawa kwa mama yake, Teddy alikuwa nyuma ya kifo cha mama yake. Lakini leo hii tena Teddy alikuwa akisakwa na Jimmy, teddy leo alikuwa ametoroka tena akiwa kwepa Jimmy na Kundi lake. Kwa nini amekimbia? Kipi kimemfanya akimbie Tena akiwa na france. Akaiona Hatari mbele yake endapo atamuacha Jimmy amfikie Teddy. Alitambua ungekuwa nwisho wake sambamba na mwanawe france. Hapo akaamua kufanya kitu. Akarudisha macho kwa Salha. Wakaangaliana kwa mara nyingine. Kila mmoja akisoma kilicho ndani ya macho ya Mwingine. Kila mmoja alijua yupo na nani. Licha ya salha kudanganya kuwa ni mfanyakazi wa kawaida haikuwa hivyo. Huyu alikuwa Jasusi. Alisomeka na Masimba alilitambua hilo. "Naelekea Arusha kumrudisha Teddy na France, nina kisasi na teddy na nitapenda kumuua kwa mikono yangu. Naomba tuondoke hapa nikakuache sehemu salama. Lakini kukuacha huko itabidi ufumbe na usiufumbue Mdomo wako. Ukifanya hivyo nilichomfanya mwamvita Muda mfupi uliopita ndio nitakachokifanya kwako." Alinguruma masimba huku akianza kutembea kuelekea Nje. Licha ya Masimba kutembea kuelekea nje, lakini Salha bado alikuwa amekaa. Alionyesha kupigwa na bumbuwazi. Maneno yaliyotamkwa na Masimba yalimuingia sawasawa. Kwamba mwamvita amekufa? Kwamba mwanamke yule katili ameuawa? Kilikuwa kitu kigumu kukiamini. Alijikuta akiwa kondoo mbele ya Masimba. Alimfuata kwa nyuma akihitaji kukijua kile alichokisia. Hata alipomkaribia Masimba bado aliilazimisha miguu yake kutembea. Akamuangalia Tena masimba. Lakini kabla hajaongea chochote simu yake ikaonyesha uhai. Kuna mtu alikuwa akimpigia. Akaitoa simu na Kuitizama. Jimmy,neno pekee lililosomeka Juu ya kioo. Akasita kisha kumuangalia Tena Masimba. Kuangaliwa kule akatambua kulikuwa kuna kitu. "Jimmy anapiga.!! Ilikuwa sauti iliyomvuta Masimba karibu na Salha. "Pokea, harafu muulize yuko wapi na wamefikia wapi." Ilikuwa amri kutoka kwa Masimba, amri ambayo ilitekelezwa muda ule ule.
********
Alikuwa juu ya kaburi la mama yake Masimba akilia kwa uchungu katika usiku ule. Moyo wake ulikuwa umepondekapondeka. Alikuwa akijuta na hata kulia kwa sauti. Hakuna baya ambalo alifanyiwa na huyu mama. Siku zote alimpenda kuliko hata mwanawe Masimba. Alikuwa akisuluhisha migogoro yao kwa upendo mkubwa. "Nisamehe mama yangu, bila ujinga wangu leo hii nisingekupoteza. Tamaa ya pesa imenifanya niusahau utu wako. Imenifanya nisahau mapenzi yangu kwako. Nikafanya kitu ambacho sasa nakiwaza. Mama nipo hapa nikishindwa kujua wapi nitakwenda. Masimba ananisaka aniue mama. Masimba anitafuta anilete huko, sina uwezo na ujasiri wa kusimama mbele yake kumuomba msamaha. Sina ujasiri hata wa kumuangalia Machoni. Mama nakisubiri kifo changu hapa hapa Juu ya kaburi lako. Nataka Risasi ya Masimba Inilipue nikiwa hapa. Nitamwambiaje mama na hata baba yangu? Vicky atanielewaje katika hili niliofanya? Ataniacha? Vipi mwanangu patra? Hapana Nastahili kufa." Yalikuwa maneno aliyotamka Teddy akiwa juu ya kaburi. Alikuwa Tanga badala ya Arusha. Alitambua asingeweza kufika arusha bila kutiwa nguvuni. Kitu alichoona ni kushinda juu ya kaburi ya mama yake Masimba. Alishinda hapo huku france akimuacha nyumbani kwao kibugumo Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
*****
Alishuka Handeni Usiku wa Saa sita kwa Usafiri wa kukodi. Baada ya kushuka hapo akaongoza Moja kwa moja mpaka nyumbani kwao ambapo bado watu walikuwa wanalala Matanga. Aliwakuta wengi wa watu wakiwa wamelala huku wachache tu ndio waliokuwa wakiota moto. Aliwasalimia wachache waliokuwepo na kuanza kuongea nao. Kufika hapo akakutana na vilio kutoka nyumbani kwa mzee First wazo,. Hapo akagundua kuwa tayari taarifa za kifo cha Dee Plus zilikuwa zimefika hapo kijijini. Wakaongea mpaka asubuhi kulipokucha. Watu wakajiandaa kwa sababu ya kwenda kuchimba kaburi la kumhifadhi Dee plus. Wakiwa bado wanajiandaa wakalisikia yowe kutoka kwa mmoja wa watoto ambaye alipita karibu na makaburi. Watu waliokuwepo msibani wakageuka na kutizama huko. Wengine walishaanza kukimbia kuelekea kule wengine wakibeba silaha tayari kwa lolote. Masimba ndio aliyekuwa wa kwanza kufika pale makaburini. Macho yake yakatembea katika sekunde ile ile. Macho yake yakatua juu ya kaburi la mama yake. Akamuona mtu akiwa amelala juu akionyesha kudhoofika mwili. Hakushangazwa na kule kudhoofika, bali alishangazwa na mtu aliyejuu ya kaburi. Teddy alikuwa juu ya kaburi la mama yake. Kaburi la mwanamke ambaye alihusika katika kumuondoa duniani. Alikuwa amelala na alikuwa akionyesha kuchoka sana. Wakati huo watu wengine nao walikuwa wameshafika. Kila mmoja alikuwa akikiangalia kile kinachoendelea pale. Mwanamke wanayemjua alikuwa akilia, akilia juu ya kaburi la mama wa masimba. Kaka yake Masimba aitwaye Samwebondo ndiye aliyepiga hatua kuelekea pale kaburini. Dada zake masimba naye wakaungana naye kuelekea pale. Sekunde hii walikuwa wakimbeba Teddy akiendelea kulia. Licha ya ndugu wote kufanya hivyo lakini kwa Masimba haikuwa hivyo. Bado alisimama akimuangalia Teddy Hasira zikimchemka. Alitamani kuchomoa bastola yake na kumlipua. Alitamani kumuendea pale na kufanya lolote. Lakini hakuweza hilo, kwa kuwa macho ya watu yakaanza kumtizama na minong'ono kuanza taratibu. Watu walianza kuhoji katika hili. Walianza kuhoji ulipo utu wa masimba. Wakamlaumu tena na tena. Masimba hakuwasikiliza. Akaondoka pale akiwaza na kuwazua. Alitaka kumuua Teddy, hakutaka alione Juaa la kesho, lakini angemuuaje wakati tayari teddy alikuwa mikono mwa ndugu zake tena akiwa mwenyewe pasipo mtoto wake? Kwa nini hakuelekea arusha na kuamua kuja huku? Inamaana tokea majuzi alikuwa pale juu ya kaburi. Alijiuliza huku akijilazimisha kutembea kurudi nyumbani. Hapo akakutana na kitu kingine. Dada zake walikuwa wamembadili nguo na sasa walikuwa wakimpeleka bafuni kwa minajili ya kumuogesha. Hapo akatamani kuwaambia ukweli. Alitamani kupaza sauti lakini hakuweza. Hawakuweza kwa kuwa dada zake walimpenda na Hawakujua kama alikuwa nyuma ya kifo cha mama yao. LAITI WANGEJUAA!!@@@??? SIDHANI KAMA KUNGEKUWA NA HATA MMOJA ANGEMGUSA.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawakujua chochote kuhusu kuhusika kwa teddy katika kifo cha mama yao. Walimpenda Teddy kama wifi yao. Hawakujali hali ambayo alikuwa nayo Masimba. Masimba bado alikuwa amejiinamia mahali akifikiria. Hakuonyesha kujali katika kile ambacho kilikuwa kikiendelea. Alimpoteza Dee plus kwa sababu ya Teddy, kama sio Teddy kumsaliti leo hii mama yake mzazi asingekufa. Lakini usaliti wa teddy umesababisha madhara makubwa sana kwake. Leo hii teddy alikuwa mbele yake katika nyumba ya mwanamke yule yule aliyemuua? Alikuwa amepokewa kama malkia. Mwanamke aliyemuua mama yake alikuwa akifurahiwa na ndugu zake wote. Sasa alikuwa akienda kuogeshwa kama mwali ama mtu maalum. Moyo ukampasuka hasira zikiendelea kupanda. Muda huu alikuwa akijipapasa bastola yake. Ni jana tu aliachana na Dee katika aina ya kazi yao. Ikimpa Dee kazi ya kumtafuta Teddy.. lakini leo hii Dee alikuwa marehemu. Alikuwa amepigwa risasi zisizo na Idadi. Akatamani ainuke ili aondoke zake arudi dar es salaam, lakini angeondoka vipi bila kumzika Rafikiki yake? Kuliwaza hilo kulimfanya Masimba Atulie. Punde akawaona ndugu zake wakimfuata pale alipo wakiwa wameongozana na Teddy. Wamemshika huku na huko. Hilo hakulitegemea na Hata kuliwaza. Hilo hakuliamini na hakutaka iwe. Lakini ulishakuwa. Teddy alikuwa mbele ya miguu yake akiwa amepiga magoti akilia. Alikuwa katika kuuomba msamaha kwa kile kilichotokea. Ingawa asingeweza kurudisha uhai wa mama lakini bado aliliona kosa lake. Akaanguka miguu kwa Masimba akilia na kulia. Masimba bado alikuwa kimya akimtizama. Akimtizama teddy huku fundo kubwa likiwa kooni. Ni teddy huyu huyu aliyemuondoa Asteria, Mwamvua na Hata familia ya Asteria. Ni teddy aliyemleta Mwamvita kwao mpaka kumuua mama yake. Ni Teddy aliyewapiga watoto katika mapigo ambayo haya stahili. Teddy leo alikuwa miguuni mwake akagalagala. Teddy leo alikuwa akihitaji kusamehewa. Ni msamaha gani angeweza kutoa? Je akiutoa huu msamaha roho za watu waliouawa kwa kushiriki kwake zitarudi? Yalikuwa maswali yaliohitaji Majibu, yalikuwa maswali yaliohitaji ufumbuzi kwa wakati ule ule. Ni ufumbuzi gani angeupata pale kwa wakati ule? Hakujua!! Na kamwe asingejua. Alipoinua uso kutizama mbele yake, akakutana na macho ya ndugu zake yakimtizama katika namna ya kuumuuliza. "Hana mbwani hano, mbona hachikuelewa" (kuna nini hapa mbona hatuelewi).. Kila mmoja alikuwa akihitaji Majibu kutoka kwake. Angejibu nini wakati akijibu kutatokea jingine tena kubwa.
"Welewe chigambile ichindeni, mwanangwa kumtenda zeze? Aliuliza mjomba wake aitwae kilango almaarufu kwa Jina la kabanza. Akimaanisha kutaka kujua ukweli nini ambacho amemtenda Mtoto wa watu. Masimba hakuweza kujibu. Bado alikuwa akikumbuka tukio la mwamvita. Mwili wa Mama yake ulipotupwa juu baada kupigwa risasi. Mama anauma na mama anaumiza. Akainama tena kisha kumuangalia mjomba wake. Machozi yakashuka mpaka mashavuni. Masimba alikuwa akilia mbele ya ndugu zake. Wote walikuwa kimya wakiwatizama wapenzi hawa. Hawakuijua siri ambayo ilikuwa mioyoni mwao. Bado alikuwa akilia machozi. Punde mikono yake ilishuka na kushika mabega ya Teddy. Teddy akaacha kulia na kuinua uso kisha kumtizama Masimba. Macho yao yaliojaa machozi yakiangaliana kwa zaidi ya dakika mbili. "Mapenzi" ndio kitu kilichoonekana machoni mwao. Ndio kitu kilichozungumzwa katika macho yao. Punde walikuwa wakikumbatiana kwa nguvu kila mmoja akilia. Teddy ndiye aliyeonekana akilia na kujutia zaidi. Ndugu wakaungana nao katika kilio, kilio ambacho mara hii kikageuka na kuwa msiba. Wote walikuwa wakimkumbuka mama yao.
******
Walikuwa wawili tu chumbani wakitizamana. Safari hapakuonekana mapenzi machoni kwa huyu kijana wa kiume. Uso wake ulikuwa umekunjamana kwa hasira. Alikuwa akimtizama mpenzi wake kwa hasira. Bastola ilikuwa mkononi akimuangalia Teddy. "Kabla ya yote nahitaji kujua alipo mwanangu France. Aliongea Masimba huku macho yake yakimuangalia Teddy. "Yupo Nyumbani Toangoma. Nilimuacha kwa kuwa nilikuwa na maamuzi magumu."alijibu Teddy huku akimuangalia masimba zaidi na Zaidi. "Mpigie Vicky niongee na France, ole wako unidanganye nitakuua kwa mikono Yangu..." teddy hakujibu, alichokifanya nikuchukua Simu ya Masimba na kuingiza namba ya Vicky, kisha akaipeleka sikioni. Muda mfupi simu ilikuwa ikiita. "Hellow Mume mambo?" Alisikika sauti ya upande wa pili kutoka kwa Vicky ambaye ni mdogo wa Teddy. "Safi mke, naomba Kuongea na Mwanao mkubwa.." aliongea Masimba. "Yupi patra au nani? Akauliza Vicky huku akionyesha kushangaa. MASIMBA NA TEDDY wakatizamana. Haikuwa kawaida kwa vicky kutokumjua Mtoto mkubwa.
"Hapana sio Cleopatra, nataka kuzungumza na France." Alijibu masimba. Ukimya wa ghafla ukatokea upande wa pili. Mshangao na kengele za hatari zikagonga vichwani mwao. Ukimya wa ghafla wa Vicky uliwashangaza.
"Vicky bado upo hewani bado?." Akauliza Masimba. "Ndio nipo hewani mume. Lakini nimeshangaa kwa simu yako kumhitaji France. Wakati kuna mtu amekuja hapa akadai mmemtuma amchukue France awaletee? Aliongea Vicky huku naye akianza kuhisi hali kutokuwa sawa. Kengele ya Hatari ikalia. Pale pale Teddy akaichukua simu kisha kwa sauti ya kupagawa akasema. "Ni nani amekuja hapo nyumbani? Niambie Vicky!!" Huku vicky akionyesha kuchanganyikiwa akamjibu "alikuja rafiki yako yule wa kike akaniambia umemtuma mtoto..." jibu hilo likakifanya kichwa cha Teddy kufanyakazi kwa Haraka. "Mwamvita utanikoma nikikukamata." Aliongea teddy bila kujua kuwa mwamvita hakuwa hai. Alishasafirishwa kuzimu. "Mwamvita hawezi kufufuka kwenda kumchukua France. Huyu Atakuwa Salha. Mwamvita nilishaamuua na kilichokuwa kikifuata ni kifo chako." Alijibu Masimba akimuacha teddy kwenye mshangao. "Salha umemjuaje salha?" Akauliza teddy sasa akimuangalia Usoni kwa makini. "Hatuna muda wa kujibizana na kuukizana. Naamini unazijua njia zote wanazopitia watu hawa. Nimekupa hii kama nafasi ya Mwisho. Ukingengeuka na nikahisi chochote nitakuua Teddy. Naomba Ubaki hapa nyumbani. Sitaki uwaambie chochote. Nasikitika kuondoka nikiacha mazishi ya Dee plus. Lakini hakuna namna ngoja niwahi. Tutaonana Dar es salaam." Aliongea masimba huku akisimama na kuanza kupiga hatua. Teddy akamuwahi na kumkumbatia. Punde ndimi zikagusana. Nahitaji tuongozane masimba. Nahitaji kupambana kufidia damu yote nilioshiriki kuimwaga. Nitakupeleka kila ngome ninayoijua na tutafanya kile ambacho unakitaka." Akaongea Teddy huku akimuangalia Masimba. Hata masimba akamtizama. Safari ya Dar es salaam ikaanza huku masimba akiwa makini sana juu ya Teddy.
*******
Kilikuwa kikao kidogo kilichokuwa kikifanyika nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kilikuwa kikao kidogo kilichowakutanisha washirika wote wa biashara ya kulevya hapa nchini. Viongozi wa serikali, wabunge na maafisa na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali ya kigeni. Ni kati ya watu waliokusanyika katika kikao hiki. Kila mmoja alikuwa kimya akitega sikio kusikia lolote kutoka kwa mwanamkakati wa kuingiza biashara hiyo bwana Jimmy Lambert. Kila mmoja alikuwa akimuangalia mwenyekiti wengi wakishangazwa na ule uonekanaji wake katika siku ya leo. Jimmy alikuwa mpole sana. Alikuwa amejiinamia akiitizama picha ya mwamvita. Picha ya mpiganaji wake alieuawa usiku uliopita. Akainua uso wake na kuwatizama wajumbe wenzake....
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jimmy akainua macho yake na kuwatizama wajumbe wote. Akakuta hata wao walikuwa wakimtizama kwa umakini wa hali ya juu. Akarudisha tena macho yake chini na kuitizama picha ya Mwamvita. "Ndugu zangu nimewaita hapa si kwakupongezana kama tulivyozoea. Nafahamu kuwa wote mnafahamu kinachoendelea tokea kufariki kwa Mlinzi wetu mkuu ambaye alikuwa ndio kiongozi wa Serikali Bungeni. Ndugu zangu tokea kufariki kwake tumekuwa tukiishi katika tafakuri na sintofahamu kubwa. Tumekuwa tukishambuliwa na kupelelezwa. Watu wetu wanazidi kuuawa huku ngome zetu nazo zikivamiwa na kuharibiwa. Ndugu wajumbe wakati hayo yote yakiendelea sikuwa nimewahi kuwaita hapa. Tulikuwa kimya tukiiuangalia upepo unapovuma na wapi unapoelekea. Lakini kilichotokea Jana katika ngome yetu ya kumekucha na tukio la kuuawa kwa Mlinzi wetu na muuaji mkuu wa Kitengo chetu. Ni wazi kuwa sasa mambo yameanza kwenda mlama. Mtu mmoja tu anatusumbua anavyotaka! Kwa nini Masimba atambe na kutufanya sisi kama watoto wakike. Kwa nini tunamuacha atambe kama yeye ndiye Mwanaume? Na habari ambazo tunazo mikononi Mwetu ni Kwamba Masimba ameelekea Arusha kumfuata Teddy baada ya kuambiwa kwamba Teddy anataka kuvuka mpaka kuelekea nchini Kenya. Vijana wetu wapo makini lakini cha kushangaza mtu huyu bado hakuonekana popote pale. Hoteli na Nyumba zote za kulala wageni tumepenyeza Watu wetu, kwenye viwanja vya ndege pia tumefanya hivyo na hata katika Njia zile za panya vijana wapo huko. Lakini kama ninavyosema bado Masimba na Hata Teddy hawakuonekana popote. Hilo limetufanya tuamini kuwa watu hawa wapo hapa hapa Dsm ama wapo Arusha na inaonekana wametuzidi ujanja. Ndugu zangu Hii vita ni kubwa vita ambayo itatulazimu sasa tuwe na watu wenye uzoefu mkubwa. Itatulazimu sasa kuitumia tena Idara ya Usalama wa Taifa kwa mara nyingine ili kupambana na Masimba." Wakati akiendelea kueleza mjumbe mmoja akainua mkono kuonyesha kuwa kuna jambo alitaka kulizungumza. Jimmy lambert akamruhusu aongee. "Ndugu mwenyekiti nimekusikiliza kwa makini sana kwenye mazungumzo yako. Lakini nilikuwa na mawili matatu ya kukueleza. Bila shaka unatambua sisi ni wabunge wa bunge la jamhuri. Inawezekana sisi tukawa tunajua mengi kuliko nyie. Tetesi ambazo nimezipata kutoka kwa rafiki yangu ambaye anafanya kazi pale Ikulu ni kwamba. Tayari muuaji wa Waziri mkuu amejulikana lakini kizuizi cha kutangazwa Jina lake kunatoka kwa Mkurugenzi Wa Idara ya Usalama Wa Taifa ambaye alimwambia Rais kuwa asifanye maamuzi yoyote kwa kuwa kuna jambo kubwa lipo nyuma ya mauaji hayo. Hivi ninavyo kwambia ndugu mwenyekiti muuaji ndio amepewa Jukumu la kuleta hilo jambo kubwa lililosababisha kifo cha Waziri na hivi sasa masimba anaripoti Ikulu na Sio kwa DG. Kingine ni kuhusu Masimba na Teddy kusemekana kuwa wameelekea Arusha. Lakini ukweli ni kwamba Masimba na Teddy wapo Tanga. Wapo pamoja na wamerudisha umoja na mapenzi yao. Waambie Vijana waelekee Tanga watoke huko Arusha." Aliongea mjumbe yule akionekana kujiamini. Maneno yale yakaufanya Ujumbe wote kuwa kumya kwa muda. Ukumbi uliingia ubaridi kila mmoja akiwaza lake. Kila mmoja aliuhisi ugumu katika hilo. Rais tayari anamjua muuaji, lakini DG wa Tiss amezuia kutajwa ama kuchukuliwa Hatua kwa Muuaji kwa kile kunachosemekana kuna Jambo kubwa limejificha Nyuma ya Kifo cha Waziri mkuu. Harafu mtu anayetuhumiwa kufanya mauaji ndiye ambaye amepewa Kazi ya kukichunguza kilichopo nyuma ya kifo hicho. Kama suala ni hivyo ni nani atapona katika hili? Kama mtu amemuua Waziri mkuu anayetembea na walinzi maalum wenye mafunzo yote, je atashindwa kuwaua wao? Hilo ndilo lililowatia Hofu na kuupa ukimya Ukumbi wote. Waliijua hatari kama wataliacha hili liendelee. Kwa mara nyingine Jimmy akainua uso na kuwatizama wenzake. Akakutana na Hofu machoni mwao. Yeah! Ilikuwa hofu kubwa sana tena sana. Hata yeye moyoni aliiona hofu moyoni mwake. Alitabasamu mdomoni lakini moyoni alikuwa na hofu. Baada ya kufikiria sana akachukua Simu na kuongea Maneno kadhaa kisha kuirudisha mahala pake. Akawaangalia tena wajumbe akatabasamu. Lilikuwa tabasamu lililopokewa kwa staili tofauti na wajumbe. Hawakujua kile ambacho Mwenyekiti alikujua.
*****
Mume wangu hii ni vita kubwa, vita yangu ambayo inanihusu mimi. Hivi ni vita nilioianzisha, vita ambayo nitaimaliza mimi hata kama nitakufa. Damu ya mama italipwa na mikono yangu. Sitaki uniache kwenye hii mission. Najua mengi sana tena sana. Ni wakati wa kuikusanya nguvu ambayo niliidhoofisha kwa muda mrefu sana." Aliongea teddy akiwa mtupu kama alivyozaliwa pembeni akiwa amelala Masimba. Walikuwa wakitizamana baada ya kuimaliza safari yao ya kupashana miili joto. Teddy alikuwa ameupandisha mguu kwa Masimba akimtizama machoni. Ni muda mrefu ulikuwa umepita pasipo hilo kufanyika. "Tukimaliza hii kazi nahitaji tupate mtoto mwingine wa kike. Si unamuona Amanda jinsi alivyo." Aliongea Teddy huku akisogea zaidi. "Usijali hata mimi natamani tungekuwa na mtoto wa kike. Lakini tumalize hii kazi. Tukishamaliza tutaondoka hapa Tanzania." Iliongea masimba akiichukua Chuchu ya Teddy na Kuitia mdomoni. Kilichofuata hapo ilikuwa ni shuhuli iliyomuacha teddy akigumia kwa Raha.
Ilikuwa ni siku nyingine yenye pilika nyingi, siku ambayo Masimba aliamua kuianza kazi Rasmi ya kuutafuta Uovu wa Waziri mkuu. Leo hii akiwa kwenye Suti kali na kuvutia alikuwa ameamua kutembelea Ofisi ya Waziri mkuu. Alitaka kwenda hapo kwa sababu ya kuianza kazi yake. Kabla ya kwenda hapo aliwasiliana kwanza na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama. Taarifa ikatumwa ikulu kueleza safari ya Masimba. Punde majibu yalikuja kwamba ameruhusiwa. Masimba akachukua Gari kutoka mafichoni wanapoishi na Safari ya kuelekea ofisi ya Waziri mkuu ikaanza. Kufika maeneo ya Tabata akakumbuka kuwa alimuacha Salha katika nyumba fulani. Akakata shauri kwenda hapo kumuangalia kwa kuwa aliamini Salha hakuwa amemteka France bali alikuwa amemchukua ki usalama zaidi. Alijua kama Salha angekuwa amemteka France basi mpaka sasa angeshapokea Amri ya kufanya chochote. Gari ikabadili mwelekeo sasa ilikuwa akielekea tabata Matumbi. Muda mfupi gari ilikuwa ikisimamishwa kwenye maegesho fulani ya magari. Masimba akashuka na kutembea kwa miguu mpaka aliposimama mlinzi wa parking ile. Baada ya maneno manne matatu, masimba akaingiza mkono mfukoni na kutoa noti ya elfu kumi na kumpa mlinzi. Sasa akaiacha Parking ile akitembea kuelekea eneo fulani la siri. Wakati anakaribia eneo hilo kuna kitu akakikanyaga, punde ardhi ikafunguka masimba akaingia kisha ardhi kujifunga tena. Kufika ndani akapokelewa na ngazi ambazo zitamshusha moja kwa mmoja mpaka mlangoni mwa nyumba fulani kule chini. Akaufungua mlango na kupokelewa na sebule pana ambayo ilikuwa kimya na tulivu. Baada ya kuingia hapo cha kwanza kukutana nacho ni picha ambayo aliipiga akiwa na Dee plus. Akaitizama kwa uchungu sana. Baada ya kuingalia kwa muda akaiweka na kuufuata mlango unaofuata. Akaufungua na kutokea kwenye sebule nyingine. Hapa akajikuta akitabasamu baada ya kumuona France amelala pembeni mwa Salha. Masimba akawatizama wote kwa kuvutiwa. Akasogea mpaka alipolala France na kumbusu Shavuni. Machozi yalikuwa yakimtoka taratibu. Hakutaka kuwaamsha alijua salha alifanya hivyo kwa kuhakikisha usalama wa mwanawe. Kwa mara ya kwanza alianza kumuamini Salha. Akaufungua mlango na kutoka tena kwa kupitia pale pale. Muda mfupi baadae alikuwa barabarani akielekea ofisini Kwa Waziri Mkuu.
*******
Wakati masimba akielekea nyumbani Kwa waziri mkuu, Teddy alikuwa Barabarani Akielekea nyumbani kwa Mbunge Wa Tarime Maro Hagare. Alitaka kuwaondoa wajumbe wote ambao walikuwa wakihusika katika biashara ile. Bastola zake zilikuwa zimehifadhiwa sehemu tayari kwa kufanya kile kikubwa. Aliwajua na aliwatambua kwa undani zaidi. Hakutishwa na ulinzi wa majumba yao. Alikuwa ameichukua kazi ya mtoa roho. Alikuwa ameibeba Tiketi ya mbunge yule ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa na mshirika mkubwa wa Biashara ile Haramu. Alifika nyumbani kwa mheshimiwa majira ya saa nne asubuhi. Aliuchagua muda huo kwa kuwa alijua kwa muda huo mbunge huyo alikuwa amelala kutokana na kutokuwepo kwa familia yake. Alipofika nyumbani hapo akaookewa na mlinzi kwa bashasha kwa kuwa walikuwa wakifahamiana. Baada Teddy Kuingia ndani akaona hakuna sababu ya kumuacha hai mlinzi Huyu. Siku zote katika kazi hizi hawakutakiwa kuacha Ushahidi Nyuma. sekunde hii Bastola ilikuwa mkononi na wakati huo huo mlio mithiri ya Chafya ukasikika. Mlinzi akaanguka chini huku akiwa amekishikilia sehemu ya kifua chake.
Mlinzi akaanguka chini huku akiwa ameushikilia upande wa kushoto wa kifua chake. Muda mfupi aliungana na mwamvita kwa safari ya kuzimu. Kwa kuwa bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia mlio. (Silence )mlio ule haukusikika hata umbali wa hatua kumi. Teddy akaongoza kuelekea ndani ya Jumba lile. Alipoufikia mlango akausukuma, lakini akagundua ulikuwa umefungwa. Akajaribu tena bado ulionyesha kuwa ulikuwa umefungwa. Teddy akaingiza mkono mfukoni na kuchomoa funguo malaya. Akautia kwenye tundu la kitasa, taratibu mlango ukamtii. Akauvuta mguu wake na kuingia ndani taratibu. Punde alikuwa kwenye sebule pana iliyopambwa na vitu kibao. Akaangaza huku na huko lakini bado hakumuona mtu yoyote. Hilo likamuaminisha kuwa hapakuwa na mtu yoyote. Akapiga hatua na kuivuka sebule. Sasa alikuwa akielekea kwenye vyumba vya Jengo lile. Kupita chumba cha kwanza na chumba cha pili, masikio yake yakanasa sauti ya kumwagika kwa maji, maji kutoka kwenye mabafu. Akaubadili uelekeo ule, sasa alikuwa akielekea kule bafuni. Mdomo wa bastola ulikuwa mbele tayari kwa kutoa usafiri kwa mtu yoyote ambaye atakuwa kiherehere. Akavuka na kuufikia mlango wa bafuni. Mlango haukuwa umerudishwa. Ulikuwa waziwazi kabisa. Mdomo wa bastola uliotangulia ndio uliomgutusha mbunge yule na kutaka kukurupuka. Lakini alipoiona sura ya mtu aliyeikamata Bastola akatulia akimuangalia vile vile akiwa mtupu. Teddy naye hakuiona aibu ya kuiangalia ile Manati. Alimtizama huku bastola ikiendelea kuwa mbele. Teddy akaivuta hatua mpaka hatua mbili kutoka pale aliposimama Mbunge Yule. Akaunyoosha mkono mpaka kilipo kitu ya mbunge yule. Bastola ikagusa kwenye shina la mnazi. Mbunge yule hakuwa na kauli tena ya kuongea. Aongee nini wakati alikuwa akikitizama kifo. Kifo ambacho kilikuja kwa njia ya ghafla. Kidole kikavuta trigger na muda ule ule mlipuko mdogo ukasikika. Bastola ilikuwa amefanyakazi ya kuvitenganisha viungo vyote vya uzazi. Teddy akasonya huku akigeuka. Alikuwa tayari ametoa tiketi na hata usafiri wenyewe. Mbunge yule alikuwa njiani akielekea kuzimu muda ule. Teddy akarudi mpaka sehemu ya maktaba katika jumba lile. Hapo akaonekana akiangalia hiki na kuacha kile. Alipekuwa hili na kuliacha. Muda mfupi baadae akaonekana akichukua nyaraka fulani kabla ya kuondoka mle ndani na kurudi tena nyumbani. Mkononi alikuwa amebeba nyaraka zinazoonyesha kuwa ni muhimu. Alitembea kwa machale akiwa amejibadilisha. Huyu hakuwa Teddy yule. Huyu alikuwa teddy yule yule wa Syria na Teddy yule wa Russia. Alirudi katika uteddy wake. Alirudi katika fani aliyoipenda kuliko zote. Fani ambayo hapo mwanzo wazazi wake wakikosa kumuunga mkono kutokana na kumtaka Arudi Shule. Lakini teddy alilikataa hilo kwa kuwa alilipenda Jeshi. Alikwenda hivyo hivyo pasipo sapoti ya wazazi wake. MAMA yake alihitaji mtoto asome, na mtoto alilihitaji Jeshi. Alianza pale Ruvu kabla ya kuhamia kule Ifakara. Leo hii alikuwa amerudi akiwa Teddy. Teddy yule aliyeipenda damu na teddy yule ambaye kuua kwake kilikuwa kitu cha kawaida. Siku zote hakuiogopa Damu na Aliipenda Sana.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa aliamua kurudi rasmi kumsaidia mpenzi wake. Aliamua kuutafuta ushahidi kwa njia ya kuua. Aliua kwanza baadae ndio anautafuta ushahidi. Kwake ilikuwa Risasi kwanza kusha kuhoji baadae. Kanuni ambayo hata Jeshi la polisi huwa wanatumia sana. Kukukamata kwanza, kisha kuhoji baadae. Hata Teddy alikuwa na maamuzi hayo. Alitaka kuua kwanza kisha maswali baadae. Alitaka kumuonyesha masimba kuwa hayupo kwenye mkumbo kama mwanzo. Alitaka kumuonyesha kuwa anajua kona zote na mienendo yote ya watu anaopambana nao. Hakuna kinjia wala kichochoro ambacho hakukijua katika biashara ile. Baada kummaliza mbunge yule na kuchukua ushahidi ambao alidhani utamsaidia. Teddy aliondoka pale akiwaza kurudi nyumbani, lakini mawazo yake ya kurudi huko aliyakatisha baada ya kumuwaza mkurugenzi mmoja wa shirika moja la kigeni ambaye alikuwa ni Mshirika katika biashara hiyo. Huyu alikuwa mtu wa kwanza kumrubuni na kumuingiza katika ushirika wa biashara hiyo kwa mara ya kwanza. Aliona afuate huyu katika kazi yake ya kuwaondosha. Ingawa kulikuwa na ugumu lakini Teddy hakuogopa hilo.
*****
Alishuka Ofisi ya waziri mkuu na kupokewa na maafisa usalama wa Ikulu ambao hawakuongea naye sana zaidi ya kumruhusu aingie katika ofisi ile. Kwa kuwa alitoa maagizo ya kuwakuta watu watatu mle ndani, ni kweli aliwakuta watu wale ambao alikuwa ni mkuu wa Idara ya Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu Binafsi wa Waziri. Sambamba na Waziri mwenye zamana wa wizara ile. Baada ya kuachana na wana usalama masimba aliingia ofisini na kitendo bila kuchelewa akamuita mkurugenzi wa Mawasiliano. Alikuwa mwanamama wa makamo, mwanamama anayekadiliwa kuwa na Umri wa Miaka 55. Alikuwa mwanamke mwembamba mwenye mvi kidogo kichwani. Huyu aliitwa Nina Mndeme. Alikuwa ni Mwanamke aliyehudumu katika Ofisi hiyo kwa takribani Miaka kumi na Tano. Alikuwa ni mwanamke wa kipare, mcheshi na mwenye bashasha kubwa. Aliingia katika chumba kile na kukutana na kijana huyu ambayr kwa kumtizama tu, akajua walikuwa ni vijana wa Mzee Godliving Kimaro.
"Shikamoo Mama!!" Alisalimia masimba akimuangalia mwanamama yule.
"Marahaba, hujambo baba..? Aliitikia kisha kuuliza. "Sijambo Mama.. nimekuja hapa kuhojiana na wewe katika mambo fulani fulani ambayo yanahusiana na kifo cha mzee hapa ofisi." Aliongea Masimba na kumkazia macho yule mama akihisi labda angekutana na Mshangao wowote, lakini haikuwa hivyo. Mwanamama yule alikuwa akimuangalia Masimba huku tabasamu likichanua mdomoni. Tabasamu ambalo halikuonyesha chochote kile. Yaani halikuwa na Kebehi. "Nipo tayari kutoa ushirikiano kwako ikiwa kila kitu kitakuwa ndani ya mamlaka yangu." Alijibu mama yule. Masimba akamuangalia tena kwa mara nyingine. "Mama huyu unayeongea naye hapa ni kama rais, nina baraka zote mpaka kuwa hapa. Nataka unijibu kila kitu hata kama hakipo kwenye mamlaka yako. Kwa kuwa hata mimi nina mamlaka ya kukupeleka kuzimu endapo utanificha chochote." Akaongea Masimba, safari hii akiuondoa ule ucheshi wake na kuivaa sura ya kazi. Licha ya kubadilika huko na hata kauli yake. Bado mwanamke yule aliendelea kutabasamu pasipo kuwa na wasiwasi. "Nataka kujua mawasiliano ya Hayati. Simu alizokuwa akipigiwa, alizopiga, ujumbe mfupi wa maneno na hata barua pepe. Pia nataka kujua mawasiliano yake binafsi sambamba na Simu yake ambayo inasemekana ilipouawa haikuwepo. Aliongea Masimba huku akimuangalia mwanamama yule. Bado tabasamu lilitamalaki usoni mwake. Hata kabla hajajibu chochote, mwanamama yule akainuka kitini na kuelekea kwenye meza kubwa ambayo ndani yake kulikuwa na makablasha mengi. Akavuta moja na kurudi mpaka pale kitini na kumkabidhi Masimba. "Mawasiliano yote aliyokuwa akiyafanya marehemu utayakuta humo. Lakini kuhusu simu yake hapo ndipo kidogo pana utata. Kwani baaada ya kutangazwa kifo chake tu, wakaja watu fulani ambao walikuwa marafiki wa mheshimiwa na kuiomba wakisema kuwa ilikuwa ikihitajika ofisini kwa chief." Alijibu Mama yule huku akimuangalia masimba safari akiwa sio mtu wa tabasamu. Kengele ya hatari Ikalia kichwani kwake. Hapakuwa na watu waliotumwa na mkurugenzi wa idara kuichukua simu hiyo. Hapa lazima kuna unamna. Hapa lazima kuna siri kubwa imetaka kufichwa." Unaweza kuwakumbuka watu waliokuja kuchukua hiyo simu?" Akauliza Masimba safari hii akionekana ni mwenye mawazo. Yule mama hakukurupuka Kujibu.. alifikiria kwa muda, mara akainuka tena na kuelekea sehemu tofauti. Safari hii akimuita Masimba waingie wote kwenye chumba fulani ndani ya Ofisi ile. Masimba akainuka huku mkono wake mwepesi ukicheZa karibu na sehemu Muhimu alipoihifadhi bastola yake. Akavuta hatua kisha kuingia ndani. Hapo akapokewa na mitambo mingi sana. Hapo akagundua alikuwa chumba cha kuongozea camera za Usalama mle ndani. Akasogea karibu na mama yule ambaye alikuwa akihangaika kufungua kitu fulani. Punde chumba kizima kikawa katika mwanga fulani baada ya screen kadhaa kuwaka. Baada ya mama yule kuwasha, akabonyeza sehemu Fulani, watu wawili wakaonekana wakiingia ndani ya Ofisi ya waziri mkuu. Masimba akamuomba yule mama awavute kwa karibu. Mama akafanya hivyo.. Punde Sura za watu wale zikasogea na kusogea. Macho ya Masimba Hayakuweza kuamini kile alichokuwa akikiona. Mbele ya kioo kulikuwa na sura za watu wawili anaowafahamu sana.
*******
Zilikuwa sura za watu ambao aliwafahamu kabisa. Walikuwa watu kutoka kikosi maalum cha kuwalinda viongozi. Hawa huendeshwa ama kuagizwa na Rais, makamu, waziri mkuu sambamba na mkurugezi wa idara ya ujasusi. Hawa wawili walikuwa vijana wale ambao walimkanata na kumpeleka kule kuzimu. Lakini leo hii wameingia ofisi ya waziri mkuu na kuichukua simu ambayo ingeweza kumsaidia yeye kwenye kazi yake. Hilo hakuwa amelitegemea kwa kuwa hapo mwanzo alidhani Simu ipo mikononi mwa Wana usalama. Akaziangalia zile sura kwa muda kisha akageuka tena kumuangalia yule Mama. Akili yake haikuwa pale kabisa. Bado aliuona utata katika kuupata ushahidi wa kuuthitishia ulimwengu kuhusu ubaya wa waziri. "Kuna kingine Mama unachojua ukiondoa hivi vichache.? aliuliza Masimba. Mama yule hakumjibu kwa maneno bali akaondoka pale na kuingia katika kichumba kingine. Akatoka na mfano wa bahasha na kumkabidhi masimba. "unachokitafuta kuhusu waziri vyote viko humo ndani. Humo ndio utamjua waziri. Nimekupa hiyo bahasha nikiwa najua nina hatarisha maisha yangu. Lakini siogopi, hata nikifa leo najua nimekufa sababu ya Nchi yangu." Aliongea mama yule huku tabasamu lake likiyeyuka Usoni. Sasa alikuwa katika Uso wa Hofu. Hofu juu ya kifo, hofu juu ya kutoa siri ambayo hakutakiwa kuijua ama kuitoa. Masimba akamuangalia mwanamke huyu kwa muda mrefu. Alimuona ni kama malaika aliyetumwa kwake. "Mama naitwa Masimba, nadhani ushawahi kunisoma mahala ama kunisikia sehemu nikitajwa. Kama nikiwa hai hakuna ambaye atakugusa." Aliongea masimba akimpiga piga yule mama mgongoni. Mama aliganda kwa mshangao, mshangao wa kutokuamini maneno kutoka kwa kijana yule. Masimba ni Huyu? Anawezekana vipi kuwa huyu? Mbona hafanani na sifa anazopewa? Hapana huyu sio masimba. Huyu ni muongo..!! Yalikuwa maswali yalitiririka kichwani kwake. Hakuamini kuwa mtu yule ni masimba. Ni hapo akataka kurudisha macho kumuangalia tena Usoni. Lakini akaendelea kupigwa na butwaa baada ya kujikuta yuko peke yake. Masimba hakuwepo lakini kilichomshangaza Zaidi milango Ilikuwa bado imefungwa. Atakuwa amepitia wapi? Alijiuliza mama yule akiangaza huku na kule. Bado hakumuona Masimba. Bado hakumuona kijana huyu aliyekuwa akizisikia sifa zake. Akatoka ofisini mle haraka hadi pale alipowaacha wenzake. Akawakuta wamejiinamia wakionyesha kuanza kuchoka . "Amepita hapa, lilikuwa swali la kwanza Bi Nina baada ya kutokea pale. "Nani? Wenzake wote wakamuuliza wakimtizama kwa mshangao. "Yule kijana niliyekuwa naye ndani." Akajibu Huku akipepesa macho yake huku na kule. "Hatuja muona mtu hapa." Nao wakajibu wakitizamana.
*****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati kule ofisi ya waziri mkuu wakimtafuta masimba, yeye ndio kwanza alikuwa anavuka Hotel ya kilimanjaro akielekea posta. Alikuwa akitembea kwa miguu kwa umakini wa hali ya juu. Aliijua sasa vita ndio ilikuwa imeiva. Alitambua wakati huo alikuwa akisakwa na kutafutwa. Lakini hilo halikumtisha wala kumuogopesha. Alijua kucheza na watu hawa, na ukitaka kucheza nao ni lazima uwe muwazi na usiwaogope. Hilo ndilo lililomfanya atembea mpaka ilipo benki ya taifa ya biashara. Wakati anaukaribia mlango akawasikia polisi wawili wakiongea kwa sauti ya chini kuhusu tukio la kuuawa kwa mbunge. Ingawa walikuwa wakiongea kwa sauti ya chini lakini kwenye masikio ya Masimba ilikuwa ni sauti kubwa. Moyoni akajua tayari teddy ameshaianza kazi. Akatawapita huku akitabasamu akiuendea mlango wa kuingia ndani ya Jengo lile lenye Benki. Baada ya masimba kuingia, haikupita dakika gari moja alionekana ikipaki pembezoni mwa Benki ile. Kisha wakashuka wasichana wawili na mvulana mmoja sambamba na mtoto wa kiume mwenye umri wa Miaka Saba. Baada ya kushuka kwa wanawake wale, wakaangaza kidogo kisha akaonekana yule mwenye mtoto wa kiume akiuendea mlango Huku wale wawili wakionyesha kumsubiri. Msichana yule aliingia ndani kisha kuchukua karatasi ya kujaza tayari kwa kutoa pesa. Lakini wakati akijazajaza ile karatasi alionekana akigeuka huku na huko katika aina fulani ambayo kama umtu wa kawaida usingeweza kugundua.
Baada ya masimba kuondoka pale Ofisi ya waziri mkuu, alijua kabisa kuwa lazima alikuwa akifuatiliwa na watu mahali fulani. Hakuwa na wazo la kuingia pale Benki, lakini ilikuhakikisha hisia zake kama ni za kweli ndipo alipoamua kuingia hapo benki. Na hata alipoingia alipanda mpaka ghorofa ya tatu sehemu ambayo ilikuwa na chumba cha kuongozea Camera za usalama ndani ya Jengo lile. Akajitambulisha kisha kuomba kuangalia gari zinazoingia sambamba na watu. Wataalam wakamkaribisha. Ni hapo alipoishuhudia gari ile ikiegeshwa kisha kushuka kw watu watatu sambamba na mtoto mdogo wa kiume. Mwanzo walitaka kumpoteza kutokana na kutowatilia mashaka. Lakini kuingia ndani ya benki kwa mmoja kati ya watu wale walioingia sambamba na mtoto mdogo, kuliyafanya maamuzi yake kubadilika ghafla. Uangaliaji na ugeukaji wa mwanamke yule ilikuwa ni majibu tosha kwamba aliyeingia pale licha ya kuwa na mtoto mdogo, alikuwa mmoja kati yao. Alikuwa mtu wa fani kama yake. Yaani alikuwa ni Shushushu. Akavutiwa na hilo. Macho yake yakaendelea kumtizama mwanadada huyu katika namna ya mshangao. Jimmy alikuwa na watu wangapi nyuma ya biashara hii? Swali hilo likamfanya amkumbuke mwandani wake Teddy. Akamtafuta katika namba yake ya kifucho. Licha ya simu kusikika kuita lakini haikupokewa. Akapiga tena na tena lakini hali ilikuwa ni vile vile. Hakuhisi chochote kile katika hilo. Bali aliamini Teddy alikuwa sehemu akifanya kitu. Akageuza macho kwa tetere huyu, tetere aliyekuja na kifaranga chake. Akaiona hamu na kiu, kiu ambayo ilihitaji glass ama kikombe cha maji katika wakati huu. Huyu alikuwa masimba na alikuwa jasusi. Bado alipendezwa na ule utizamaji na hata uangaliaji wa watu wale. Sasa akaamua kuinuka akiondoka katika chumba kile. Akashuka ngazi mpaka chini kabisa sehemu ya wateja. Hapo akajifanya kuongea na watu wawili wa tatu. Akaiendea karatasi kisha kuijaza na kuelekea kwenye foleni. Sasa alikuwa amesimama nyuma ya msichana yule mrembo. Walitenganishwa kwa umbali wa nusu Hatua tu. Walikuwa wakipumuliana na kila mmoja kuisikia pumzi ya mwenzake. Hilo likaileta Raha katika roho ya masimba. Raha ambayo ilikuja pale yule mtoto mdogo alipokuja na kumkumbatia miguu. Hilo akalipenda. Mikono yake ikashuka na kumuinua mtoto na kumbeba kwa mikono yake. Sasa walikuwa wakicheza na kutaniana katoto kale. Katoto ambako kalitokea kumzoea kabakwamba kalishawahi kumuona mahala fulani. Hapo ndipo alipomuona mwanadada yule akitamani kugeuka. Alitaka kumuangalia masimba, wakati mwingine mikono yake ilikuwa akienda uelekeo ambao masimba alikuwa akiu0na. Zamu ikatembea hatimaye ikafika zamu ya msichana yule. Akasogea kwa mwendo wake wa madawa. Alijikaza asionekane kama anatetemeka, lakini hilo aliliona machoni mwake. Baada ya binti kuhudumiwa na kumaliza shida yake ndipo alipogeuka ili kumchukua mtoto. Wakakutanisha macho yao, wakaangaliana na kuangaliana. Wakajuana na kutambuana. "Nenda kwa mama. Mwambie mama tutaonana siku nyingine. Nitamtafuta kwa muda wangu." Aliongea masimba akimshusha mtoto ili kumruhusu aende kwa mama yake.
*******
Kama lilivyoeneo lote la Oystebay mchana huwa kimya sana. Hata leo hii lilikuwa kimya sana kutokana na wakazi wengi wanaoishi eneo hilo kuwa makazini ama wengine kuwa ndani ya majumba yao. Teddy alikuwa mtu pekee ambaye alionekana akitembea katika barabara moja yenye utulivu. Alionekana kutulia sana katika utembeaji wake. Macho yake madogo hayakuacha kutizama kila upande katika namna impendezayo mtu yoyote yule. Hakuuonyesha wasiwasi na wala hakuonyesha kwamba alikuwa akikifuata kitu. Alitulia na kutulia. Alikuwa njiani kupeleka tiketi ya kifo kwa mkurugenzi fulani wa Shirika la kigeni. Muda wote alikuwa akitabasamu. Na hata pale alipolifikia geti la jumba analoishi mkurugenzi yule akalakiwa na mlinzi wake. Na kwakuwa walikuwa wakifahamiana, waliongea maneno mawili matatu, kisha akalisukuma geti na kuingia ndani. Mlinzi hakujua nini ambacho kinaendelea. Akamfuata Teddy kwa Nyuma. Lakini hatua yake ya tatu akahisi kitu kikipenya kifuani. Ulikuwa kama ubaridi fulani hivi. Lakini punde akaelemewa na kuupiga mweleka. Damu zilikuwa zikishuka kifuani. Teddy hakugeuka nyuma, alikuwa akitembea kuingia ndani ya jumba. Nyuma akiiacha maiti ya mlinzi yule ikiwa imelala pasipokuwepo na Uhai. Baada ya kuufikia mlango wa kuingilia ndani ya Jumba lile, akaibonyeza kengele ya mlangoni. Zilipita sekunde kumi bila mlango kufunguliwa. Akausukuma mlango kujaribu kama uko wazi. Naam! Mlango ulikuwa wazi na mbaya zaidi alipokelewa na dimbwi la damu iliyotapakaa pale sebuleni. Vitu vilikuwa vimetupwa ovyo kuonyesha kwamba kulikuwa na vurugu zilizofanyika. Teddy akaingia sasa akiwa tayari kwa chochote. Akaufunga mlango kwa ndani sasa akiitizama ile damu. Bado ilikuwa mbichi kabisa kuonyesha aliyefanya tukio hilo amelifanya katika muda ule. Lakini mpaka muda ule hakujua nani ambaye aliuawa katika damu ile iliyosambaa. Teddy akaongeza umakini zaidi na zaidi. Hatua kumi mbele juu ya ngazi akaukuta mwili wa mzungu yule ukiwa umelala kifudifudi huku KISU KIKUBWA KIKIWA KIMESIMAMA KATIKATI YA MGONGO.
TEDDY AKAPATWA NA BUMBUWAZI. Nani huyu amefanya hivi? Ni swali pekee alilojiuliza ambalo hakupata JIBU KWA MUDA ULE.
Teddy akasimama akiwa ameduwaa akiutizama mwili wa mwanaume yule wa kizungu uliolala katikati ya dimbwi la damu. Nani amemuua mwanaume huyu? Nani anawaua watu hawa? Anawaua kwa sababu gani? Je wanaficha ushahidi? Yalikuwa maswali tata kichwani kwa teddy. Bado bastola ilikuwa mkononi akiinyoosha kuelekea kule ulipo lala mwili. Sasa akaamua kusogea akiwa makini kwa kila hatua. Akauruka mwili ule kisha kuingia ndani kabisa ya chumba cha mwanaume yule. Kuingia huko macho yake yakainasa vurugu, vurugu iliyofanywa kabla ya mwanaume yule kuuawa. Kila kitu kilikuwa chini ama kimevunjika ama kusambaa. Damu ilianzia ndani kabla ya sebuleni. Muonekano wa mtu yule aliyeuawa ilionyesha kuwa aliuawa akiwa kule sebuleni. Lakini kuvurugika kwa vitu sambamba na matone ya damu yalikivuruga kichwa cha teddy. Ilionyesha waliouawa walikuwa wawili. Ilionyesha aliyeuawa chumbani alikuwa mwingine. Ni hapo alipoipata hamu, hamu ya kumtafuta ama kumuona mtu mwingine aliyeuawa. Lakini angemtafutia wapi ikiwa hapakuwa na sehemu nyingine ya kutokea? Hapo ndipo alipoifanya akili yake kufanya kazi. Akatambua lazima kuna sehemu kuna mlango wa kupitia. Mlango ambao ndio uliotumiwa na watu kumficha huyu marehemu wa pili. Umakini ukaongezeka. Teddy akaangalia kila upande kama angeweza kugundua chochote. Lakini haikuwa rahisi. Haikuwa rahisi kwa kuwa hakuuona mlango wala alama yoyote iliomuonyesha kama kuna sehemu ya kupitia. Bado hakuamini alitaka kuhakikisha ukweli, mawazo yake yalimwambia ipo sehemu. Ni hapo wakati akiwaza hilo alipouona ufa ukutani. Lakini kilichomgutusha, huu haukuwa ufa wa kuonyesha dalili ya kubomoka kwa ukuta. Bali huu ulikuwa ufa wenye kunyooka kuonyesha kwamba ulitengenezwa maalum. Teddy akasogea huku umakini ukiwa katika kiwango cha juu. Alipoufikia ule ufa akafanya kama anaugusa ukuta, punde akashangaa ukuta ukijifungua. Akatupa macho ndani kwa chati, damu tena ilionekana mle ndani. Sasa akaamua kuingia kabisa kwenye chumba kile cha siri akiifuatilia ile damu. Damu iliyotapakaa katika chumba kile cha siri. Kuingia kwake ndani kukafuatiwa na tukio la kujifunga kwa ule ukuta. Punde akajikuta akitizamana na wanaume wanne walioshiba kama wacheza mieleka. Ni katika kasi ile ile teddy akataka kunyoosha bastola afyatue risasi. Lakini hakuwahi kulifanya hivyo. Kwani kwa wepesi wa unyoya, akajikuta akipokea mateke matatu mfululizo kutoka kwa mmoja kati ya wale wanaume wanne. bastola yake ilikuwa pembeni sasa alikuwa amesimama akiwa mikono mitupu. Wanaume wale wakamtizama kwa dhihaki. Wakamtizama wakimdharau. Muda mfupi wakaanza kumfuata wote kwa pamoja. Teddy akawa anarudi nyuma. Ni kipindi akigota ukutani ndipo alipouona ukuta ukifunguka tena. Akamuona mwanamume akiingia katika namna itiayo burudani Moyoni na Hata machoni. Mwanaume aliyeingia mfano wa kivuli. Teddy akataka kwenda kumkumbatia, lakini hakuweza kufanya hivyo. Hakuweza kwa kuwa uingiaji ule ulimpa kihoro. Kwanza hakuamini kama mtu huyu anaweza kuwa pale. Akamuangalia alivyokuwa akitembea, akahisi labda alikuwa akumtizama Joram kiango, akahisi huyu labda ni willy gamba.
Hata wanaume wale wanne walikuwa wameduwaa wakimwangalia kijana huyu aliyekuwa akiingia. Sio kwamba hawakumjua, sio kwamba hawakumuona, bali hawakutarajia hilo. Hawakutarajia ujaji wa mwanaume yule. Yule ambaye waliambiwa yupo tanga kwenye msiba wa mama yake. Lakini leo hii alikuwa mbele yao akitembea kama dume. Dume ambalo halikuonyesha hofu. Hata wao wakalishangaa na kuduwaa. Hawakumuangalia Teddy tena, wakamuache Teddy akinata na kuzunguka. Masimba akampita Teddy kisha kwenda kusimama mbele ya wanaume wale. Haikuchua hata sekunde katika tendo lile lililotendeka. Tendo lililowaacha wanaume wawili kati ya wanne wakianguka chini. Kila mmoja alikuwa akitoka damu kooni. Kisu kilikuwa kimepita kwenye shingo zao. Hili liliwashtua wanaume wawili waliobaki. Wakaamua Kujaribu bahati yao. Mmoja akatupa teke ambalo lilimpata Masimba na kusababisha bastola yake kuanguka. akabaki mikono mitupu. Ngumi zikapigwa katika aina fulani inayovutia. Licha ya kuwa na miili mikubwa lakini wanaume wale walikuwa wakiziweza ngumi. Yalikuwa mapambano yaliyodumu kwa Dakika Sita. Mapigano ambayo yalimfanya teddy ajisikie Hamu. Sio hamu ya tendo bali ilikuwa hamu ya kupambana. Lakini alipokuja kutizama Chini akaiona miili ya wanaume wale ikiwa sakafuni wakivuja damu. Baada ya kuwamaliza wale, masimba akamshika teddy na kumuongoza. "Hatutakiwi kuwa hapa, kuna mtu anatembea na sisi. Kuna mtu anaufuta ushahidi. Lazima tumjue." Aliongea masimba huku wakitokea mlango wa nyuma wa jengo lile kuelekea Nje. Wakatoka nje kabisa ya jumba lile. Ilikuwa safari ya kumtafuta mtu anayewazidi kwa kuwaua wale watu muhimu. Ni lazima wafanye hivyo. Safari hii ikaishia mpaka katika ile nyumba ya siri. Humo ndani wakapokewa na France sambamba na Salha. Hilo likaonyesha kumshtua Teddy. Hakutegemea kukutana na lile. Hakutegemea kumuona Salha sambamba na france pale ndani. Hapo akahisi kitu kikiupenya Moyo wake na kujikuta akitamani kuongea kitu. Sio kwamba alimuogopa Salha bali kitendo cha kumkuta pale akiwa na france ambaye alikuwa mikononi mwake ilimfedhehesha sana. Masimba aliligundua hilo mapema. Masimba aliugundua wivu katika uso wa teddy. Wivu sambamba na kutokuamini ni moja ya vitu vilivyomchanganya. Akamsogelea Teddy na kumkumbatia, "usihofu mama huyu ni mmoja kati yetu.. alichokifanya kumchukua France ilikuwa ni usalama wa mtoto sambamba na Familia. Watu hawa wangegundua hili tungempoteza Vicky sambamba na familia nzima.." aliongea Masimba. Teddy akanyamaza kwa muda, kisha akasogea na kumkumbatia france.
*******
Ulikuwa usiku wa manane pale Masimba alipokuwa mezani akikagua nyaraka alizopewa na yule mama wa ofisi ya waziri mkuu. Alikuwa akipekua moja baada ya nyingine. Akaisoma kwa makini na kupitia kila neno. Mawasiliano ya waziri mkuu na baadhi ya watu. Nyaraka muhimu za uingizaji na usambazaji wa biashara ya madawa ya kulevya. Biashara ya pembe za ndofu ni kitu ambacho kilikuwa kikifanywa na Ofisi ya waziri mkuu. Mikakati na mipango ya biashara hiyo ilisukwa kwa ustadi na watu wazito ndani ya serikali. Tembo, twiga na hata meno ya tembo vilisafirishwa kwenda china na watu wanaonekana kama Watalii. Kila mstari aliokuwa akiusoma alijikuta mwili ukimsisimka kutokana ya kile kilichomo ndani ya nyaraka zile. Waziri mkuu alikuwa ametengeneza genge la uharifu kwa kutumia cheo chake. Lasilimali za Nchi zilikuwa zikisafirishwa kila uchwao kwa kupitia mipakani na hata kwenye viwanja vya ndege. Hakikuwa kitu cha kawaida. Akainuka pale na kurudi chumbani. Moja kwa moja akaiendea simu yake, alipoichukua akatafuta namba ya chief. Sekunde mbili simu ilikuwa hewani. "Kuna tatizo kijana?" Aliongea chief kwa sauti ya usingizini. "Nipo kazini mkuu na unaitambua hii kazi. Nakuja muda mfupi hapo nataka unipeleke Ikulu." Akajibu masimba. "Ikulu muda huu? Hujui kuwa kuna sheria na taratibu zake za kuingia. Unadhani usalama wa ikulu wataturuhusu? Alijibu chief kwa aina ya swali. "Wewe ni nani hapa nchini? Mimi ni nani hapa nchini? Ongea na rais muda huu kuwa tunakwenda hapo." Alipomaliza kuongea hayo akakata simu bila kusubiri jibu la Mkurugenzi. Kisha akageuka kitandani kumuangalia Teddy Harry aliyekuwa amejiegemeza kitandani. Akakutana na macho ya teddy yakimtizama. Haya kuwa macho ya kawaida. Yalikuwa macho yanayohitaji kukijua kitu. Teddy alihitaji kuambiwa kitu. Masimba akamtizama sana.. punde walikuwa wamekumbatiana. "Naenda Ikulu mpenzi..Kuna kitu ambacho siwezi kubaki nacho hapa. Naomba uwe mlinzi wangu kwa nyuma yangu. Nataka umuangalie yule ambaye anatembea nasi. Hakikisha huonekani na wana usalama wengine." Aliongea huku akimuachia teddy na kuifuata bastola yake. Akatoka mle ndani akifuatana na Teddy tayari kwa safari ya kupeleka nyaraka Ikulu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ILikuwa safari ya kuelekea ikulu. Safari ambayo ilikuwa ni mwanzo wa kuupeleka ushahidi ambao utaweza kumshawishi rais wa nchi katika kuamini sababu za kuuawa Waziri mkuu. Alitoka na Teddy lakini muda fulani teddy akarudi kwa kupitia njia nyingine tayari kwa kuwa mtu wa nyuma ya Masimba. Huyu alikuwa ndiye mlinzi na mchunguzaji mkuu wa Masimba. Akarudi ndani kisha kutulia tuli. Masikio yake aliyatega huku na huko katika kuusikia mchakato hata wa sisiminzi. Akatulia kwa muda fulani bila kusikia chochote. Akainuka taratibu na kuurudisha mlango na kuelekea mbele zaidi. Wakati akiukaribia mlango akausikia mlango kama unafunguliwa Taratibu. Akachepuka pembeni na kutulia huku macho yakitizama mlangoni. Taratibu akakiona kivuli cha mtu kikitokea pale mlangoni. Mavazi aliyovaa sambamba na kiza kile hapakuwa na tofauti ya mfanano. Akakaza macho yake na kutizama kwa umakini Zaidi. Akamuona mtu akipita taratibu na kuuendea mlango. Kabla hajaufungua akaangaza huku na huko. Teddy bado alikuwa akimuangalia kwa ukaribu sana. Licha ya ukaribu huo lakini bado hakuwa amemgundua kwamba alikuwa ndani. Baada ya mtu yule kuangalia huku na huko akaufungua mlango kwa utaalamu ambao ulimfanya Teddy ahisi mtu huyu alikuwa ni jasusi kupindukia. Baada ya kuufungua mlango mtu yule akatoka tena safari hii akinyata mfano wa paka. Punde alikuwa akitokea juu ya ardhi. Baada ya kutokea hapo akatulia pembeni kuangalia kama alikuwa akifuatwa. Haikuwa hivyo, haikuwa hivyo kwa kuwa hapakuwa na mtu aliyekuwa akimfuatilia. Akainuka na kuianza safari. Wakati yeye akiondoka katika namna ile, pembeni kidogo alisimama Teddy akimuangalia mtu yule. Mtu ambaye mpaka kufikia pale hakuwa amemjua wala kumgundua kuwa alikuwa nani. Alipoondoka alipokuwa amejibanza, Teddy naye akafuatia nyuma kwa umakini. Ilikuwa ni lazima Teddy awe makini kwa kuwa alijua alikuwa akimfuatilia mtu ambaye ni mjuzi wa mambo yao. Alihakikisha mtu yule hampotei kwenye upeo wa macho yake. Alihakikisha mtu yule hampotei kabisa. Bastola mkononi akazidi kumfuatilia kwa umakini. Mtu yule alipofika karibu na barabara ya mandela. Akasimama kisha kitendo bila kuchelewa akaiona gari mmoja ikija kwa kasi na kusimama karibu kabisa na miguu ya mtu yule. Baada ya gari kusimama milango ikafunguliwa kwa kasi. Ni hapo alipokuwa akipanda ndani ya gari ndipo Teddy alipogundua mtu yule alikuwa nani. Ni wakati mtu yule anaupeleka mguu wake juu ili apande, kofia iliyomficha sura yake ikaanguka. Alikuwa Salha, alikuwa yule yule salha waliokuwa wakiishi naye. Salha aliyekuwa akiishi na France. Leo alikuwa akipakiwa kwenye gari fulani. Alikuwa akienda wapi? Kufanya nini? Na wale ni wakina nani? Yalikuwa maswali mfululizo kuchwani kwa Teddy. Maswali ambayo hayakupata majibu kwa wakati ule. Akabaki kuwa mtazamaji katika tukio lile, akiangalia namna atakavyoondoka hapo. Kwa wakati ule hakuwa na uwezo wa kujitokeza kwa kuwa sehemu yenyewe haikumruhusu. Punde akaiona gari ikiondoka kwa kasi akielekea buguruni. Hapo akakumbuka kumjulusha masimba juu ya kilichotokea. "Nimeona kikundi cha nyuki kimepita hapa na kuondoka na nyuki jike tunayeshi naye." Aliongea Teddy kwa Lugha ya Mafumbo. Lugha ambayo ilitumika sana katika masuala ya kijasusi. "Nimeona, nimewaona. Hapa tunapoongea nami nipo nyuma ya nyuki hawa pasipo wenyewe kujua. Cha kufanya naomba urudi mzingani ukamuondoe Nyuki mdogo." Alijibu masimba kwa lugha ile. Lugha ambayo waliifahamu wachache katika medani ile ya Kijasusi." Baada ya maongezi hayo na Masimba, Teddy akatii na kurudi nyumbani kama alivyoambiwa.
********
Gari aliyopanda SALHA sasa ilikuwa ikiiacha barabara ya maendela na kuchukua barabara ya uhuru. Safari ilikuwa ikiendelea huku gari hii ikionekana ikielekea kariakoo. Baada ya kuipita rozana na malapa, sasa ilikuwa ikielekea eneo la Ilala boma. Baada ya kufika Bungoni gari ikaingia kushoto na kuchukua barabara ya Kawawa. Sasa gari ilikuwa akielekea magomeni katika mwendo wa kasi sana. Bado masimba alikuwa nyuma akilifukuzia. Muda wote alikuwa ndani gari chakavu mali ya halmashauri ya Jiji la Dar es salam. Lililokuwa likitumika kama kubebea takataka Usiku. Bado alikuwa kwenye umakini mkubwa. Baada ya gari ile kufika maeneo ya kigogo roundabout akashuhudia ikiegeshwa pembeni, kisha watu watatu wakashuka. Baada ya watu wale kushuka na kuingia kwenye nyumba moja, akaishuhudia ile gari ikiondoka pasipo Salha kushuka. Hilo likampa utata kidogo, utata ambao hakujua wapi angeweza kuanza. Alihitaji sana kuwapata wale vijana. Alihitaji sana kujua wapi anapoelekea Salha. Alitakiwa akili yake iamue kufanya kitu kimoja, kitu ambacho kingempa muda wa kuwahi masaki. Akaona ni wakati wa kumfuata Salha. Shida yake alitaka kujua ni wapi Salha anaelekea. Uondokaji wake pale nyumbani haukuwa wa hatari. Kwa nini kutokumbeba france kisha kutembea umbali mrefu kutoka pale mafichoni kuifuata gari barabarani, Masimba Alijua salha hakutaka watu hawa wapajue pale mafichoni. Lakini vijana hawa ni kina nani? Nani yupo ndani ya gari Na Salha? Yalikuwa maswali mazito sana. Maswali ambayo yanahitaji majibu katika muda ule kabla hapajapambazuka. Jina la Falycious Benee lilikuwa la kwanza kumjia kuchwani mwake. Huyu alikuwa ni mwanaidara ambaye alikuwa akiifanya kazi kwa siri akiishi uswahilini. Muda wote alionekana kama mswahili lakini haikuwa hivyo. Kila alipokuwa akipita alikuwa kazini. Alikuwa akichukua hiki na kile. Akaichomoa simu yake na kuandika ujumbe mfupi ambao akautuma kwenye namba ya falycious. "Nyumba 0679 roundabouts nataka majibu yake ifikapo saa moja."... baada ya kuutuma ujumbe ule sasa akaamua kushuka kwenye gari lile chakavu na kukiendea kijiwe fulani cha pikipiki. Akamuita dereva mmoja pembeni na kuongea naye mawili matatu. Kitambulisho chake kikafuata sambamba na shilingi laki moja. Dereva akakubali kutoa pikipiki yake kumuachia Masimba. Kilikuwa kitendo kilichotendeka kwa dakika moja. Dakika ya pili Masimba alikuwa barabarani akiufuatilia ile gari. Pikipiki ilikuwa ikitembea katika utulivu wa hali ya juu. Bastola mbili bado zilimpa nguvu masimba ya kufuatilia. Hata wakati anafika kwenye makutano ya barabara ya morogoro, bado gari aliyopanda salha ilikuwa mbele ikitembea taratibu ikielekea maeneo ya magomeni. Masimba akaendelea kuwa makini kwa kila hatua. Wakaipita magomeni na sasa walikuwa wakielekea manzese. Hata walipoupita manzese bado gari ilizidi kusonga. Kufika shekilango ikaingia barabara hiyo na kwenda kuegesha gari nje ya maegesho ya Hotel ya Rombo View. Masimba akawapita na kuendelea kusonga mbele. Mbele kidogo akaisimamisha pikipiki kwenye bar fulani. Akamuita mlinzi na kumpa elfu kumi kisha kumuomba amlindie pikipiki. Baaada ya hapo akatembea kwa miguu kurudi nyuma kuuelekea Rombo view.
Baada ya kufika hapo akasimama kwa muda akiangaza, punde akamuona mlinzi akisogea na kutaka kumuuliza. Kitambulisho mkononi kwa Masimba kikamuacha mlinzi yule akirudi nyuma kwa woga. Baada ya mlinzi yule kusogea, masimba akaongoza moja kwa moja mpaka ndani ya Hotel. Hapo ndani akamkuta mtu wa mapokezi akimaliza kuandika vitu fulani. Akasogea mpaka pale.. "habari za saa hizi dada? : akasalimia masimba.
"Nzuri kakA! Nikusaidie nini? Akauliza mwanadada yule. "Nahitaji kujua watu waliongia sasa hivi wameelekea Chumba namba ngapi." Akajibu masimba taratibu akimuangalia yule mpangaji.
"Kaka hapa hatuna utaratibu huo wa kutoa siri za wateja." Alijibu yule msichana. Wakati wote macho ya masimba yalikuwa yakitizama kwa chati katika daftari lile. Macho yake yakatua kwenye jina la mtu anayejiita marlon. Chumba namba 045 A .. akajifanya anamuaga yule Dada na kushuka chini. Kabla hajatokea kwa Nje akageuka tena na kugeuza kurudi kule juu. Kufika pale mapokezi hakumuona yule Dada zaidi ya Matone ya damu na Mburuziko wa Mwili wa Binadamu. Bastola mkononi hatua kuelekea ulipo mburuziko zikafuata. Hatua kumi mbele ndani ya bafu zile akamkuta mhudumu amelala katikati ya Dimbwi la damu. Huku kisu kikiwa tumboni...
Mwili wa mhudumu aliyemuacha sekunde dakika moja iliyopita, alimkuta akiwa mfu amelala katikati ya dimbwi la damu huku kisu kubwa imesimama katikati ya tumbo. Utumbo ulikuwa nje ukining'inia kwa pembeni. Bado mwili ulikuwa wa moto na damu ilikuwa ndio kwanza inatembea. Kengele za hatari zikagonga kichwani kwa masimba. Aliujua uhatari wa kupambana na mtu wa aina hii. Mtu aliyetumia sekunde kufanya mauaji ya aina hii. Hilo pekee lilimpa ujumbe kuwa ndani ya hoteli ile kulikuwa na mtu hatari sana. Mtu ambaye hatakiwi kuachwa. Akarudi nyuma na kuuacha mwili wa mhudumu yule ukiwa bado umelala katikati ya damu. Akairuhusu miguu yake itembee katika namna ya utayari , mikono ilikuwa tayari hata pale alipokuwa akipanda ngazi. Akanyoosha kuelekea pale kwenye chumba alichokisoma kwenye daftari la wateja. Chumba alichohisi kuwa atakuwa ameingia Salha na mwanaume Yule aitwaye marlon. Masikio yakinasa huku pua zikiinusa harufu ya damu. Harufu ambayo bado ilikuwa ikisumbua katika matundu ya puA zake. Hatua ishirini mbele akauona mlango wa chumba kile. Mlango ambao hakuonyesha kufungwa bali kuegeshwa tu. Akaongeza umakini mkono wake ukiwa umenyooshwa kwa mbele kuilekeza bastola pale. Hata alipoangalia chini matone ya damu kutoka ndani ya chumba kile yalimrejesha katika utambuzi yakinifu katika medani ile. Sasa alikuwa ameuweka mwili katika aina yoyote ya mapambano. Akageuka na kuelekea pale. Masikio yakinasa kushoto, kulia na hata kisogoni kusikia chochote kitu. Bado damu ilikuwa ikitembea taratibu. Mlango uko wazi na kisha damu. Kuna nini? Ama ni mtego? Lilikuwa swali lisiliteguliwa kwa wakati ule. Mguu wake wa kushoto ukausukuma mlango huku bastola imetangulia. Baada ya mlango kumpa nafasi ya kuangalia ndani, akatupa macho kwa haraka.. hakukiona kitu zaidi ya damu.. Hilo likamfanya aingie ndani kabisa.. Kuingia ndani akajikuta akitizama na kitu ambacho hakukitegemea, tukio ambalo lilimfanya ahisi kwanba anaitizama picha za video zisizopendeza machoni mwake. Alihisi kile anachokitizama hakikuwa kitu cha kweli. Ni punde alikuwa akimtizama akiingia akiwa hai. Lakini sasa alikuwa akimtizama akiwa maiti. Akimtizama akiwa amechinjwa shingo na kutenganishwa. Hakuwa anamtizama mtu mwingine, hakuwa akimtizama mnyama ama picha za video. Bali alikuwa akimtizama Salha akiwa uchi wa mnyama huku kichwa na kiwiliwili vikiwa vimetenganishwa. Hakukiamini kitu hicho, hakuamini kama Salha ameuawa katika namna ile. Akarudi nyuma na kuiacha ile hoteli akiwa amechanganyikiwa. Akiwa amefura kwa Hasira. Aliamua kuwarudia vijana wale kule kigogo. Akatembea katika namna ya kuonyesha kutokuwa makini. Hakupita hatua hata nne akaisikia sauti ikitokea nyuma yake.. sauti ya mwanaume asiye na utani.. mwanaume shupavu. "Tupa Bastola yako chini na usigeuke." Masimba akatii akijiona mpumbavu. Akauona mwisho wake, akajua kwanza safari hii hawezi kupona. Akaituma bastola chini kisha kuinyanyua mikono juu. Akakisikia kidole cha mtu wa nyuma yake kikiitoa risasi katika chemba cha usalama. Sasa alikuwa akilipuliwa. Lakini kabla ya hilo akahisi umajimaji ukimmwagikia katika mavazi yake. Maji maji ambayo yalimfanya ageuke kuangalia nyuma. Hapo akakutana na tukio jingine la kushangaza. Maiti ya mtu ilikuwa nyuma yake, maiti ya mtu ikiwa haitazamiki kwa Risasi. Kichwa kikiwa kimefumuliwa. Yalikuwa matukio yaliyotokea katika kipindi kifupi sana. Ndani ya sekunde thelathini. Nani amemuokoa katika hili? Nani amemuua huyu mtu..? Akiwa anajiuliza akamuona mtu akitokea, mtu ambaye aliiduwaza akili yake kwa sekunde tano. Teddy Harry alikuwa akitokea taratibu akitembea kuelekea pale aliposimama yeye. Teddy mwanamke wa maisha yake. Teddy mzuri na hata teddy mtamu. Mkononi alikuwa ameishikilia bastola ya kirusi Special colt 38. Alikuwa akitembea kwa madaha yote. Alikuwa akinataka katika mwendo wake wa twiga.
Alifanana na Nuru wa Joram kiango, akifanana na Yule Veronica wa Willy gamba. Alikuwa mfano wa Regina wa Sudi. Alinata na kunata. Alipofika aliposimama Masimba teddy akajitupa kifuani huku akimgonga Masimba Mgongoni. "Kuwa makini Baba ningekupoteza mpenzi wangu. Aliongea teddy akiendelea kujilaza kifuani kwa masimba. Kwa mara ya kwanza masimba akaamini Teddy alikuwa amebadilika. Teddy alikuwa amerudi katika uaminifu wale. "Nimeamini mpenzi, nimekuamini kutoka moyoni. Huu niwakati wa kuondoka." Aliongea masimba wakitoka Ndani ya Hotel. Walitoka kama kawaida pasipokutiliwa shaka. Wakatoweka katika namna ambayo hakukuwa na mtu aliyewaona au kuwatilia shaka
*******
Wakati Masimba akielekea masaki nyumbani kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi, teddy alikuwa akielekea kigogo baada ya kupewa maelezo na Masimba kuhusu kushuka kwa vijana wale ambao anahisi watakuwa na maelezo kuhusu aliyemuua Salha. Alisaidiwa na giza usiku ule kutembea bila kuonekana mpaka kigogo. Akapokelewa na sauti za mbwa waliokuwa wakibweka. Teddy akatulia gizani kwa muda akiichunguza nyumba aliyoambiwa. Ilikuwa nyumba nzuri pekee katika Nyumba zote zilizolizunguka eneo lile. Licha ya uzuri huo lakini pia ilizungushiwa miti ya michongoma ambayo iliifanya nyumba hiyo ionekane kama kichaka. Upande wa nyuma wa nyumba ile kulikuwa na migomba mingi ambayo ndani yake palionekana uwepo wa kinjia kilichopita katikati ya migomba. Teddy akahama pale nakuzunguka upande mwingine wa Jengo lile. Akakutana hata upande ulijengwa na kupandwa migomba kama Upande aliopita. Akaangaza macho huku na huko alipoona kuna utulivu wa kutosha Teddy alijibunua na kuchupa kisha kutua ndani katika sekunde ile ile. Utuaji wake ulikuwa mfano wa paka anayenyatia panya. Baada ya kutua hapo akapokewa na giza nene na totoro. Taa zisizo na mwanga ndizo zilizokuwa zikiwaka ndani ya Nyumba ile. Wimbo wa Shania Twain still the one ndio pekee uliosikika ukihanikiza katika nyumba ile. Wimbo ulioonyesha uburudishaji wa miili ya mtu kutoka mahala fulani. Akaachana na hilo sasa akawa anatafuta nafasi ya kuingilia ndani ya nyumba ile. Hakutaka kufanya haraka kutokana na kutokiamini sehemu ile. Aliogopa na kuogopa kugutukiwa mapema. Aliamini kwa mazingira yale hapakosi mtu anayetizama usalama. Kutoka pale alipo akaokota kupo ambalo lilikuwa pembeni yake na kulitupa upande mwingine tofauti na alipo, nia ikiwa ni kujua kama kuna mtu au lah.
Hazikupita hata dakika akamuona mtu akitokea katikati ya migomba. Mtu huyu alikuwa amevaa mavazi meusi ambayo yalifanana kabisa na giza la sehemu ile. Mtu yule mkononi alikuwa amekamatia bunduki aina ya Sub Machine Gun. Akazunguka akiutizama kila upande. Teddy akaanza kutambaa mfano wa nyoka kuelekea pale aliposimama yule mlinzi. Alikuwa mfano wa kiza na mfano wa kivuli cha migomba. Hata alimfikia karibu mlinzi yule hakumuona. Teddy akafyatuka mfano wa mshale na kumtia kabari na kuanguka naye chini. Kufika chini akamshika shingo na kuivunja. Yule mtu akakata roho pale pale. Baada ya kummaliza akamburuza mpaka katikati ya Migomba. Akamuacha hapo yeye akaanza kusonga kuelekea ndani ya Nyumba ile. Alitembea kwa umakini wa hali ya juu. Alitembea kwa umakini mpaka pembozini mwa nyumba. Hapo akatulia kusikiliza sauti. Bado sauti ya wimbo wa shania ilikuwa ikipenya masikioni mwake. Akaongeza hatua nyingine mpaka mlangoni. Akausukuma kidogo, akauona mlango ukifunguka. Akagundua haukuwa umefungwa.. Akausukuma tena kidogo, akajikuta yupo ndani ya korido moja ndefu. Akasogea haraka ili kuipita ile korido. Akiwa anakaribia kuimaliza, mlango wa mbele yake Ukafunguliwa...
Wakati anaimaliza korido mlango wa mbele yake ukafunguliwa, akamuona mwanaume akitokea, kilikuwa kitendo cha sekunde Teddy kumuondoa mtu yule kwa kumpiga Risasi ya kichwa. Baada ya mtu yule kukata roho Teddy akampekua mifukoni. Humo akakuta mtu yule akiwa hana kitu cha maana. Baada ya hapo teddy akaongoza na kuingia ndani ya chumba alichotoka yule mwanaume. Baada ya kuingia akapokewa na manukato sambamba na mtiririko wa maji kutokea bafuni. Akaufunga mlango kwa ndani huku Bastola mkononi. Akapiga hatua akielekea kule maji yanaposikika kumwagika. Wakati anataka kuufikia mlango wa bafuni akasikia mchakato kama wa kitasa cha mlango ukifunguliwa. Akageuka kuangalia nyuma.. ni kweli ilikuwa hivyo.. kitasa kilikuwa kikitingishwa kuonyesha kulikuwa na mtu kwa nje. Teddy akarudi na kufanya kama anaufungua mlango.. kitendo bila kuchelewa akamuona mwanaume akiingia mkononi akiwa na bastola akionyesha kuwa na wasiwasi sana. Kwa kuwa hakujua kama ndani kuna mtu, ilikuwa ni Rahisi sana Teddy kufanya kile alichotarijia. Pigo Moja la kareti lilitosha kumpeleka chini mtu yule. Hata baada ya kuanguka chini Teddy alimfuata na kumnyonga shingo. Baada ya hapo akamburuza mpaka mwisho mwa chumba kile na kumfunika. Baada ya hapo akakaa hapo chumbani kumsubiri mtu aliyekuwa akioga bafuni. Huyu alihisi ni mwanamke, alijua huyu ndiye atakayesema nani aliondoka na marehemu Salha. Baada ya kukaa kwa dakika kama tano hivi, akausikia mchakato wa miguu ya mtu akitembea taratibu kuja pale sebuleni. Punde akamuona mwanadada mwenye asili ya kisomali akiingia pale chumbani akiwa amejifunga Taulo lililoishia juu ya magoti na kuyafanya mapaja yake yawe wazi. Alikuwa mzuri na mrembo sana.. alikuwa mrefu mithili ya Twiga. Aliingia akitembea katika aina ya mwendo wa kinyongo. Ukiachana na hilo mwanamke huyu hakushtuka pale alipomuona Teddy pale Chumbani. Hakushtuka kwa mwili na hata macho. Macho yake hayakuionyesha hofu, hofu ya kuhofia na hata kuogopa. Tabasamu la kifedhuli liliipamba sura yake. Tabasamu lakinyama lilitawala katika uso wake. Akapita na kwenda kukaa sehemu fulani. Akimuangalia teddy katika macho fulani yenye maswali. Maswali ambayo hayakuwa na majibu. Alijiukiza kutembelewa na Mwanamke mwenzie. Mwanamke ambaye amejikaribisha chumbani kwake pasipo taarifa. Mwanamke huyu ni nani? Ameingiaje hapa chunbani kwangu? Amewapitaje walinzi hadi kuingia humu? Alijiuliza mwanamke yule huku sasa akiyaruhusu macho yake yamtizame Teddy. Ya mtizame mwanamke huyu ambaye hakuwa na mashaka. Wakatizamana!! Naam! Walitizamana na kutizamani. Nuru ya utambuzi ikang'ara mithili ya mbalamwezi isiyo na kizuizi cha mawingu. Nuru iliyomulika mpaka katika undani wa viumbe hawa. Walijuana na kutambuana katika aina moja na aina nyingine zote. Mwanamke yule akatambua kuwa amekuwa ametembelewa na Teddy Harry, mwanamke ambaye hakuonyesha masihara. Mwanamke ambaye alikuwa akizisikia sifa zake duniani kote. Leo alikuwa naye ndani ya chumba chake. Mwanzo wakati anaingia hakuwa anamuogopa. Lakini hapa sasa alikuwa na hofu. Hofu juu ya kifo. Kufika hapo ndipo alipoangaza pembeni kuangalia msaada. Mwili wa mlinzi ulikuwa umetambalajika sakafuni ukiwa hauna uhai. Hilo likaonyesha kumshangaza mwanamke yule. Ni katika mshangao huo akainuka kwa kasi ya ajabu akielekea pale alipokaa Teddy. Alikuwa akipiga mapigo mfululizo. Yote yalikuwa yakipita patupu. Yote yalipita hewani na wakati huo huo akaisikia ngumi nzito ikitua usoni. Ilikuwa ngumi iliyomtupa chini mithili ya fulushi la mihogo. Hakuchelewa kuchupa akipiga mapigo mengine, safari hii alibadili mapigo.. alikuwa akichanganya Kung Fu na Hata Karate. Hakujua Teddy ni waaina gani.
Ni ndani ya sekunde ile ile akajikuta yupo chini baada ya kupigwa mapigo mawili yaliomungia sahihi mwilini. Alipotaka kuinuka akakutana na mdomo wa bastola ukimtizama. "Tulia kama ulivyo.. Usipende kucheza na watu kama sisi." Aliongea teddy huku akimtaka asimame. Kweli mwanamke yule akatii, akasimama akiwa anavuja damu. Lakini akiwa amesimama akimuangalia Teddy, tukio la ajabu likatokea.. ni tukio ambalo lilimfanya Teddy achupe na kudondokea pembeni. Risasi mbili zilizokusudiwa zimmalize Teddy, zilitua kifuani kwa mwanamke yule wa kisomali na kumtupa hewani kabla ya kutua chini akiwa marehemu. Teddy hakukitegemea kabisa kitendo kile. Hata alipoinuka kumfuata mwanamke yule, tayari alikuwa maiti. BADO GIZA LIKAENDELEA.
*********
Alisimamisha pikipiki nje ya geti la jumba la mkurugenzi wa usalama wa taifa. Masimba akashuka na kutembea kuelekea ndani ya jengo hilo. Wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na nusu usiku. Akapokelewa na walinzi wa Jumba lile. Akakaguliwa kama destuli na kuruhusiwa kuingia ndani. Alitembea akipanda ngazi mpaka juu kabisa sehemu ya mikutano. Wakati anaikaribia sehemu hiyo akashangazwa na kuwaona walinzi binafsi wa rais. Wakati mshangao wake ukiendelea, akashangazwa zaidi Baada ya kumuona Rais akitokea mbele yake akiwa sambamba na makamu wa Rais. Hilo hakuwa amelitegemea kwake. Kuwakuta viongozi wa nchi pale ilimpa kufahamu kuwa Ushahidi wake ulikuwa ukihitajika sana. Masimba akasogea mpaka karibu na waliposimama Viongozi wale wa nchi. Akawapa mkono na kusalimiana nao kwa muda. Baadaa ya hapo akafungua vifungo vya kote lake na kuchomoa bahasha ambayo aliikabidhi mikononi kwa rais, kisha hata bila kusubiri chochote akapiga hatua kuondoka pale akiwaacha wakimtizama katika namna ya kumshangaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipotoka pale safari yake haikuwa ya kurudi nyumbani, bali iliunganisha kuelekea nyumbani kwa Suresh. Ilikuwa zamu yake ya kusafirishwa
Ilikuwa ni lazima asafirishwe kupelekwa kuzimu katika usiku ule ule. Bado pikipiki aliyoichukua kwa dereva yule ilikuwa ikimsaidia kutoka hapa kuelekea pengine. Muda wote alikuwa akiitizama saa yake ya mkononi. Ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro. Ndani ya jiji la dar es salaam ndio watu walikuwa wakiamka kujiandaa kwenda makazini. Alitaka kuutumia muda huo kukamilisha kile alichokipanga. Kile ambacho alitaka kifanyike katika muda ule. Alitaka kuipenyeza Risasi kichwani kwa suresh kabla ya Jua la Asubuhi kuchomoza. Pikipiki ikatembea barabarani ikiteleza. Sasa alikuwa akiipita mbagala kuelekea nje ya Jiji la Dar es salaam. Muda wote alikuwa akipishana na watu waliokuwa wakienda makazini. Bado muda haukuwa tatizo kwake kuwahi nyumbani kwa Suresh. Muda mfupi baadae pikipiki ilikuwa ikisimama kwenye kichochoro kimoja pembezoni mwa ukuta mkubwa uliozunguka jumba analoishi Suresh. Kwa kuwa ni nyumba ambayo aliifahamu. Hapakuwa na ugumu Masimba kuruka na kuangukia ndani. Baada ya kutua tu alijibingilisha mpaka pembeni. Wakati anatambaa kuelekea sehemu nyingine, akajikwaa kwenye bati na kuanguka chini. Wakati ametulia hapo akaliona jibwa likimjia kwa kasi.. huku likibweka. Wakati hajiweka tayari mbwa lile likamrukia na kumvaa. Haikuwa kazi ndogo.. Masimba akaanza kubingirishana na yule mbwa pale chini. Alitakiwa kupambana hasa kwani alijua endapo angechelewa basi walinzi wangetokea na kufanya mapambano yawe magumu. Bado alimgalagaza mbwa yule na alipofanikiwa kumuweka chini ili amtie shaba.. Akahisi kitu kizito kikitua kichwani kwake. Akamuachia mbwa na kwenda chini huku giza likiibeba nuru ya macho yake.
Masimba hakujua tena kile kilichoendelea. Akaruhusu giza kuifuta Nuru ya macho yake. Akatulia na kutulia.
*****
Teddy alishangaa muda kakatika bila Masimba kufika nyumbani. Kwani walipoachana usiku ule alimwambia kuwa angerudi katika muda wa usiku ule. Lakini mpaka saa mbili ile hakuwa amemuona Masimba pale nyumbani. Hilo likampa shaka na wasiwasi mkubwa, alihisi masimba alikuwa kwenye hatari ama atakuwa ameshakufa. Kwa kuwa wakati wanaachana alimeambia anaelekea nyumbani kwa Chief.. Teddy Hakuona sababu ya kuendelea kukaa pale ndani. Alitaka kwenda kumtafuta Masimba, alitaka kuinasa habari kuhusu wapi alipo mwanaume wake. Akaondoka mle ndani akipanga kuelekea masaki. Masaki sehemu ambayo ilikuwa ya mwisho Masimba kusema kwamba anaelekea huko. Hakutaka kumuacha France, aliamua kumchukua na kuelekea naye huko. Japo ilikuwa ni hatari lakini asingemuacha mtoto katika jumba lile akiwa peke yake. Alijiandaa na kumuandaa France, muda mfupi baadae walikuwa Njiani akielekea Masaki. Kujua taarifa ya mtu sahihi kwake. Alifika masaki asubuhi ile na kupokelewa na Walinzi wa Chief. Akawasalimia na kuwaambia adhma yake ya kuonana na Chief. Simu ikapigwa moja kwa moja na majibu yalipokuja yakamkuta Teddy tayari yupo ndani akizikwea ngazi. Alihitaji kufahamu wapi alipoelekea Masimba baada ya kuondoka hapo. Alizimaliza ngazi na kutokea katika chumba maalum cha Chief. Aliingia akiwa katika sura yake nzuri lakini isiyokuwa na tabasamu. Macho yake yakakutana na macho ya Chief ambayo yalionyesha kuwa hayakupata mapumziko kwa muda mrefu. "Karibu Sana Mama..." aliongea Chief kwa sauti yake tulivu. "Ahsante Baba Yangu, nimekaribia lakini sikuja kukaa mzee.. nimekuja kukuulizia kuhusu muwendaji wako mkuu hajarudi jana." Aliongea Teddy macho yake yakimuangalia chief usoni kutafuta kitu machoni kwake. Alitaka kuumsoma Chief katika aina na mtindo aujuaye yeye. Lakini akakutana na macho ya chief yasio na hofu. Macho ya chief yaliyo yakawaida kabisa kuonyesha hakuwa na mashaka. "Teddy umepoteza uwezo wako uliokuwa nao mwanzo.. Teddy wa mwanzo anapotokewa na hali hiyo alianza kwanza kuutafuta ukweli.. Teddy yule hakuwa akifunga safari kuja ofisini ama hapa nyumbani. Aliitenda kazi ya kumtafuta kwa mikono yake mwenyewe. Umeingia wapi muwindaji wangu? aliongea Chief kwa sauti yenye umakini wa hali ya juu. Teddy akainua uso na kumtizama mzee kwa mara ya pili. Maneno ya chief yalikuwa na ukweli ndani yake. Hakuwahi kuja ofisini wala nyumbani kwa Chief. Aliutafuta ukweli mwenyewe. Hilo likamfanya ainuke na kumuaga chief. Alitaka kwenda kumtafuta Masimba na kumrudisha akiwa hai ama mfu. Alitambua Masimba atakuwa sehemu ametekwa ama kuuawa. Wakati anakaribia kutoka mlango wa mwisho wa jumba la mkurugenzi akaisikia Sauti ya Chief ikimuita. "Teddy Rudi ndani mara moja!!" Ilikuwa sauti ya Chief, mara hii ikionyesha haipo kwenye ukawaida. Teddy akageuka na kurudi ndani. Akitembea Huku macho yake yakipepesa huku na huko. Tofauti ya Chief ya safari hii ilimuonyesha kuwa chief ameipata habari mbaya. Alipomkaribia Chief, chief akanyoosha mkono na kumpa kikaratasi fulani. "Muwindaji wangu amefungiwa sehemu fulani pembezoni mwa Jiji.. Chukua hiyo namba, nenda kwa watu wa Mamlaka ya Mawasiliano Wakwambie hiyo namba imetuma ujumbe kutoka wapi. Nenda Ofisini waambie wakusaidie kupata taarifa ya namba hiyo." Aliongea Chief huku akigeuka kurudi ndani. Teddy hakusubiri, kile alichokuwa akikifikiria ndicho ambacho kimetokea. Akaliacha jengo la chief. Akatembea mpaka alipoiacha Gari yake. Akaufungua mlango wa gari na kujipakia. Safari yao ikaanza kuelekea kijitonyama.. njiani mawazo yaliendelea kumzonga juu ya kutekwa kwa masimba. Nani atakuwa amemteka? Je wamempeleka wapi? Aliyawaza yote huku akimuangalia France aliyekuwa amekaa pembeni. Akakumbuka kwamba alipewa namba na hakuifungua kuiangalia. Akaichukua karatasi ile na kukifungua. Punde alikuwa akiitizama namba ya mtu anayemfahamu. Mtu ambaye alimtambua na kumjua kiundani Zaidi. Alikuwa akiitizama namba ya suresh. Kengele ya tahadhali ikagonga kichwani.
Alitambua Jimmy na washirika wake ndio wako nyuma ya kutoweka kwa masimba. Hapo ndipo alipoipata hamu ya kuweka laini yake ya zamani. Aliwaza kufanya hivyo kwa kuwa aliamini angetumiwa ujumbe kutakiwa kufanya kitu kwa sababu ya kuachia Huru kwa Mpenzi wake. Akaegesha gari pembeni na kuitoa simu yake kisha kuipachika laini husika. Baada ya kuiweka na kukaa sawa.. Muda ule ule akaiona simu yake ikiita, alipoangalia Jina la mpigaji moyo ulimpiga paa baada ya kuona namba ya Chief. Haraka haraka akaipokea.. "hallow baba!!" Aliita Teddy.
"Umefika ofisini tayari? Aliuliza Chief akionyesha wasiwasi kwa sauti yake.
"Hapana, lakini nishamtambua na kuwatambua wote." Akajibu.
"Umewatambua na kuwajua? Ni kina nani? Wamenitumia ujumbe nikutafute nikwambie uupeleke mzigo wao ili tumchukue Masimba." Aliongea chief.
"Hawapelekewi chochote na Masimba atarudi akiwa hai na Salama. Niachie mzee hii ni vita yangu mimi. Masimba aliingia katika Hili kimakosa. Naomba ukae kimya na usijibu chochote." Aliongea Teddy na kukata simu. Sasa alikuwa akiingia kazini rasmi, alikuwa akiingia katika kazi nzito na ya Hatari. Aliujua ugumu na alitambua hatari yake. Hapo ndipo alipoamua kumpeleka France nyumbani kwa Chief. Alitaka kuwa huru katika kuifanya kazi yake. Alitaka kuwaonyesha kuwa hakuwahi kutishwa na akaogopa. Wakati akiwaza Hayo simu yake Ikaita. Kutizama namba ya mpigaji ilikuwa ni namba ile ile ya Suresh. Akaipokea na kuipeleka Sikioni. "Tunauhitaji Mzigo wetu, la sivyo utaiokota maiti ya mpenzi wako." Aliisikia sauti ya upande wa Pili ikiinguruma. Ilikuwa sauti tofauti na ya Suresh.. hii ilikuwa ngeni masikioni kwake. "Sileti chochote, hampati Chochote, na Masimba nitakuja kumchukua mimi mwenyewe." Alijibu Teddy.
Ukimya wa Ajabu ukatokea, kisha kicheko kikafuata. "Teddy wewe ni mdogo sana.. huwezi kupambana na sisi. Nakuonya usithubutu kufanya lolote utampoteza Masimba na hata wewe mwenyewe utapotea." Bado mtu wa upande wa pili alisikika akinguruma.
"Sijawahi kutishwa kisha nikaogopa. Nakipenda kifo na naipenda Damu pia. Nimeshatoka sehemu hatarishi kuliko. Sasa naomba nikwambie.. sitafanya chochote kile mnachohitaji, lakini ninachokisema ni kwamba Masimba atatoka na mzigo hautatoka. Mwambie Jimmy na Suresh sijawahi kushindwa kile ninachokiamua. Vita ndio imeanza." Aliongea Teddy kisha akakata simu. Aliuona uoga wa adui zake. Aliuona uoga wa kina Jimmy. Hili lilionyesha ni jinsi gani watu hawa walivyo waoga.
******
Alihisi kama yupo kwenye kina cha maji kilichommeza kiwiliwili chote. Kichwa chake pekee ndicho ambacho kilibaki. Hewa nzito na harufu mbaya ni vitu pekee vilivyomfanya aanze kufumbua macho yake taratibu na kutizama. Giza, ndio kitu cha kwanza kukutana nacho pale alipoyafumbua macho yake. Alijaribu kuangaza huku na kule kama ataona kitu chochote, lakini hakukiona chochote kile. Bado giza lilitanda kila kona. Akatulia kwa muda kuipa utulivu akili yake, alitaka kuipa muda wa kufikiria hatimaye kufanya maamuzi sahihi. Chumba alichofungiwa kilimpa majibu ya wapi alipo. Akaendelea kuwaza na kuwazua, akainuka pale chini na kukaa kitako. Akaitizama mikono yake ambayo haikufungwa na chochote kisha akacheka. Ni kosa kubwa kumuacha Jasusi mfano wake katika Uhuru wa aina yake. Kumuacha huru katika namna ile ilikuwa ni kumpa nafasi ya kufanya akitakacho. Aliamini angetoka katika muda wowote na katika namna yoyote. Punde akasikia nyayo za watu zaidi ya mmoja zikisogea kuelekea pale ndani. Masimba akarudi chini katika kuzuga kuwa bado hakurudiwa na fahamu. Kwa aina fulani ya kutizama akawaona watu wawili wakiingia ndani huku watatu waliokamatia bunduki nzito wakibaki mkononi wakiitizama kila hatua huku wakiwa tayari kwa chochote. Akaendelea kutulia wakati watu wale walipombeba na kuanza kutoka naye ndani ya chumba kile kinachoonekana kama kuzimu. Alitulia akiangalia kwa umakini, alilichunguza Jengo lile ili akianzisha Rabsha iwe ni rahisi kutoka.
Bado watu wale waliendelea kusonga mbele ndani ya jengo hilo. Wakaufikia mlango mmoja uliotengenezwa kwa chuma. Mmoja akabonyeza kitufe kimoja mara lango likafunguka. Macho ya masimba yakakutana na chumba ambacho ndani yake damu nzito na mabaki ya Binadamu vilisambaa kila kona. AKAJUA SASA ALIKUWA AKIINGIZWA KWENYE CHUMBA CHA MATESO. AKAUANDAA MWILI WAKE TAYARI KWA KUKABILIANA NA MATESO HAYO
Chumba kilitapakaa damu sambamba na mabaki ya binadamu. Muonekano wa chumba kile ni mfano wa kuzimu. Harufu ya uozo na hewa nzito ilikuwa mara mia na chumba alichotolewa. Wakamuingiza katika namna ya kutaka kumfunga kwenye kiti. Wakati wao wakilitaka hilo masimba macho yake yalikuwa kwa wale watu watatu waliokuwa wameshikilia bunduki. Alikuwa makini kwa kila hatua ya watu wale. Alihitaji kuliona kosa lao ili autumie muda ule kujiokoa. Macho yalikuwa makini zaidi ya majasusi wa CIA katika mission ya kumsaka Osam Bin Laden. Kila walipopiga hatua hata yeye macho yake yakavutika katika namna ya upigwaji wa hatua. Aliupenda na kuuhusudu utembeaji wa aina ile. Utembeaji uliokuwa ukisadifu utaalam na ujuaji katika tulivu, sikivu na elevu. Walionyesha kwamba ni watu wa aina gani, walionyesha hakuwa wa kawaida na pia walikuwa sio watu wa mchezo. Hilo halikuwa tishio kwa masimba, halikuwa tishio machoni kwa mwanaume huyu. Hakuogopa kwa kuwa hawakuwa maridadi katika kulitafuta na kulimudu lolote. Hakuogopa risasi na hata mapigano ya mikono.. alishapitia katika mission mbalimbali akiwa na nchi washirika. Akatulia chini wakati wanaume wale wawili wakitaka kumfunga kwenye kiti. Alizuga kulegea kama maiti, alionekana kama Mfu. Hawakuonyesha kujali katika hilo. Wakajiweka huru huku watu wale wenye silaha wakiweka silaha zao Chini. Hilo lilikuwa kosa kubwa katika hii kazi ya kijasusi. Lilikuwa kosa kubwa katika sheria na mikakati yakimapambano. Hukupaswa kuiacha nafasi ya namna ile, hawakupaswa kumpa uhuru katika hilo. Kitendo cha wao kuweka silaha zao chini tu, kikafuatiwa na kufyatuka kwa Masimba katika namna ya mshale na kuachia mapigo ambayo yaliwapata sahihi wanaume hawa wawili. Kwa kuwa yalikuwa mapigo makali wanaume wale walupepesuka na kuwaangukia wenzao waliokuwa wakishangaa, wote wakaenda chini. Hapo ndipo Masimba alipocharuka na kupambana kiume. Yalikuwa mapambano magumu kwake, yalikuwa mapambano ya kufa na kupona. Mapambano yaliodumu kwa dakika takribani Kumi. Damu ilikuwa imetapakaa.. wanaume watano walikuwa chini wakiwa wametulia. Hawakuwa wakipumua tena. Hata masimba alikuwa ametapakaa damu mwilini. Nguo zake zilikuwa zimechanika mpaka magotini.
Akainama na kuikota bunduki moja na kuishika mkononi. Akatoka akitembea huku mdomo wa bunduki ukiwa umetangulia mbele. Hakuogopa katika namna ile. Hakuogopa katika kutembea. Lakini kila alipokuwa akitembea alihisi ukimya ukiongezeka ndani ya Jengo lile. Akatembea kwa umakini akiendelea kuangalia huku na huko. Cha ajabu kila alipotembea ndani ya Jengo lile hakufanikiwa kuona mtu yoyote mwingone Zaidi ya Ukimya tu. Alitembea na kutoka ndani ya Jengo lile. Kutoka kwake nje akapokelewa na pori kubwa. Jengo lile lilikuwa katikati ya pori kubwa sana. Hapakuonekana Njia zaidi ya Nyasi ndefu tu. Hilo likamfanya ageuke nyuma kutizama ndani alipotoka. Bado akashangazwa na hilo. Hapakuonyesha uwepo wa watu, wala kuishi kwa watu eneo hilo. Hata ile njia ya kupita hakuijua wala kuiona. Jengo lote lilizungukwa na Nyasi Ndefu. Akaamua kurudi ndani tena kuitafuta simu yake ili awasiliane na Teddy. Alijua Teddy ni lazima anaijua sehemu hii alipo. akarudi mpaka chumba kile cha mwanzo lakuni hakuona chochote. Hata alipokwenda chumba cha pili hakuiona Simu yake isipokuwa simu za watu wale. Akainama na kuichukua Moja, akaiandika namba ya teddy mpya.. lakini Haikupatikana. Alipopiga ile ya zamani Tabasamu likaurudia uso wake baada ya kuona inaita.
"Hallow Dady.." Teddy akaita kwa jina ambalo lingeweza kumjulisha kama aliyepiga ni Masimba au lah.
"Yeah D..aliitika Masimba.
"Uko salama? Uko wapi? Na hii namba ni ipi? Aliuliza Teddy akionyesha kuwa na wasiwasi. "Nilipo sipajua Teddy. Nimekupigia kwa kuwa wewe ulikuwa unawajua hawa. Nipo katikati ya pori fulani lakini sijajua ni wapi. Hii simu nimeichukua kutoka kwa hawa maiti hapa. Tafadhali njoo haraka. Akaongea Masimba.
"Nakuja nishapajua, usiondoke wala kupiga hatua kuitafuta njia mpaka nifike.. Hiyo sehemu sio salama na imetegwa mabomu chini ya Ardhi." Aliongea Teddy .. masimba hakujibu, alichokifanya ni Kukata Simu na Kutulia ili kumsubiri Teddy.
Wakati akiendelea kumsubiri Teddy, akausikia mngurumo kama wa gari. Mngurumo ambao haukuchukua muda mrefu ukapotea katika ngoma za masikio yake. Akatulia akishangaa na kusikilizia. Punde akasikia michakato ya miguu ya mtu ikinjogea ndani ya jumba lile. Bunduki bado ilikuwa mkononi akijibanza akiangalia kule kule zinaposikika hatua. Hazikupita sekunde tano akamuona mtu mmoja akitembea kuingia pale ndani. Mkononi alikuwa amekamatia Bastola. Akamuangalia Vizuri mwanamke huyu. Kuigundua siri yake kukampa tabasamu la kukata na shoka. Alikuwa ni yule mwanamke waliyekutana pale Benki. Mwendo wake aliyoonyesha kutokuja kitu kinachoendelea pale. Hata alipobakiza hatua tano kufika usawa ule ambao masimba alijibanza, ndipo alipoihisi Tofauti. Akataka kugeuka Nyuma kutizama huko. Lakini kabla hajalifanya hilo MDOMO WA BUNDUKI UKATUA SHINGONI. USIJARIBU KUJITINGISHA..... NI SAUTI ILIYOSIKIKA NYUMA YAKE.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mdomo wa bastola ulikuwa shingoni katika namna ya kushindwa hata kuigeuza shingo yake. Binti yule akahamanika na kujikuta akiupoteza umakini na hata uwezo. Punde mlango wa upande mwingine ukafunguliwa. Mwanamke mrefu mwembamba alikuwa akiingia kwa ule mwendo wake wa twiga. Alikuwa akitembea kanakwamba alikuwa akiigopa ardhi. Mkononi alikamatia Bastola yake. Alikuwa Teddy Harry akiingia ndani ya jengo lile.. akasogea taratibu kwa namna ambayo alikuwa tayari kwa chochote. Macho yake yakatua kwenye mwili wa Masimba, mwili ambao ulionekana kutapakaa Damu. Nguo zilizochanika na hata damu kuvilia. Teddy hakumjali msiçhana yule ambaye alikuwa akitizamana na mtutu wa Bunduki iliyoshikiliwa sawa sawia na Masimba. Teddy akasogea tena na tena. Alipofika pale waliposimama akakifanya kitu ambacho hata Masimba hakukitegemea. Kitu ambacho kiliuonyesha ukatili wa hali ya juu. Bastola yake ilifanya kazi ya kukifumua kichwa cha mwanamke yule. Risasi tano zilikuwa zimekigawanyisha kichwa na kuufanya ubongo uliochanganyika na damu kuruka juu na kusambaa chumba kizima. Hakulijali hilo, hakujali teddy akasogea na kujitupa kifuani kwa masimba. Alijilaza huku akilia kwa sauti ndogo. Hali aliyonayo Masimba ni hali ambayo hakuwahi kumuona. Moyo wake uliumia sana kumkuta kwenye hali ile. Moyo wake ulihuzunika sana. "Teddy sio muda wa kulia mama, nilazima tuondoke hapa kwa muda huu. Nilazima tuondoke hapa kwa kuwa kazi bado ni ngumu. Nataka kichwa cha suresh katika usiku wa leo. Nataka wote wanaohusika wapewe usafiri." Aliongea masimba huku akimtoa teddy kifuani. Punde walikuwa wakiondoka katika Jengo lile akiongozwa na Teddy. Walipita katika njia ambazo hakuzielewa. Hakuwahi kuwaza kama katika nchii kulikuwa na vitu vya aina ile. Walipita katika njia ambazo kama asingekuwa Teddy basi angebaki Jina. Mabomu yakutegwa yalikuwa yamepandwa chini ya ardhi. Alitembea akifuata hatua za teddy hakutaka kwenda tofauti kabisa. Kila sehemu ambayo teddy alipita alikuwa akimuonyesha kila kitu ambacho kilikuwepo katika eneo lile. Moyoni masimba alikuwa akifarijika kwa kile alichokuwa akikitizama. Alihitaji kuijua njia kwa kuwa alitaka kurudi akiwa peke yake. Hivyo ilimlazimu kukalili njia ile... wakati wanakaribia kuumaliza ule msitu, teddy akamsimamisha kwanza. Wakasimama hapo kwa muda teddy akionekana ni mwenye kufikiria kitu. Alikaa kimya kwa muda wa dakika mbili, baada ya hapo akamwambia Masimba waondoke katika njia mbili tofauti. Teddy alihitaji kila mmoja apite katika njia yake. Masimba hakutaka kulipinga hilo. Akatembea akimuacha Teddy akimuangalia. Akimuangalia katika namna ambayo hakuilewa. Masimba akatembea akiruhusu miguu yake kutembea kwa tahadhari. Hakugeuka nyuma kumuangalia teddy, aliamini teddy alibaki nyuma kama mlinzi wake. Alitembea kwa umbali mrefu kidogo bila kumuona Teddy. Hata alipotokea sehemu Teddy alipiacha gari bado teddy hakuonekana. Hilo likampa shaka masimba, shaka ya kuhisi kitu kutoka kwa teddy. Akauvuta Muda akisubiri kufika kwa Teddy. Lakini wakati akifikiria hilo akakisikia kishindo, kishindo kilichofuatiwa na Milipuko na moto mkubwa kusambaa angani. Hilo halikutegemewa na Masimba, hilo halikutegemewa kwa kuwa alihitaji kulifanya yeye. Kwa nini Teddy? Yalikuwa mawazo yaliyokuwa yakipingana kichwani mwake. Moto ukaendelea kuwaka huku vishindo vya mabomu vikisikika. Licha ya hilo bado hakumuona teddy, bado teddy wake hakuwa ametokea. Bado Teddy hakuwa amefika. Hilo likampa mashaka makubwa. Mashaka ambayo yalimfanya ahitaji kurudi Tena kule alikomuacha teddy. Ni wakati huo akiutizama moto akashtuliwa na sauti ya mtu ikitokea nyuma yake. Hii ilikuwa sauti ya Teddy. Akageuka akionyesha kutokuamini. Macho yake yakakutana na tabasamu kutoka kwa teddy. "Tuondoke Mume wangu." Aliongea Teddy akiufungua mlango ili Masimba aingie.
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment