Search This Blog

Saturday 5 November 2022

NITAKUPATA TU - 2

 








Simulizi :Nitakupata Tu

Sehemu Ya Pili (2)





******

Muziki ulikuwa ukisikika kwa mbali ukitokea ndani ya nyumba moja kubwa maeneo ya mbezi beach. Taa nyekundu zilikuwa zikiwaka kuonyesha kuwa ulikuwa usiku thabiti, usiku wa mahaba na usiku wa mapenzi. Mwanamke alikuwa katika vazi jepesi la kulalia ambalo hili lilimuonyesha mpaka nguo yake ya ndani aliovaa. Mkononi alikuwa na glass ya mvinyo mwekundu huku pembeni yake kukiwa na bastola. Muda wote alikuwa akiitizama saa ya ukutani kanakwamba ndio kwanza alikuwa akiitizama. Kila baada ya sekunde alikuwa akiitizama saa yake ya ukutani. Akaonyesha kukerwa na kitu, muda mfupi alinyanyuka na kuliendea pazia la dirishani. Alipolifikia akalifunua kisha akaanza kutupa macho yake nje akiangalia uzuri wa jiji la dar es salaam. Alisimama hapo kwa muda wa dakika kama mbili akitizama nje. Alionekana akimsubiri mtu, mtu ambaye alikuwa mpenzi wake ama hawara. Lakini bado muda ulizidi kwenda bila kumuona huyo mtu. Akiwa ameanza kukata tamaa akaliona gari nyeusi ikisogea taratibu ikielekea uelekeo wa kwake. Moyo wake ukachanua kwa tabasamu safi. Bado aliuvuta muda akiitizama gari ile ikiendelea kusogea. Punde mkono wake wa kulia ukapanda mpaka juu ya titi lake lake la kushoto. Akaishika chuchu na kuanza kuichezea polepole. Mara akaisikia honi ikitokea kwa nje. Akashuka taratibu kwa mwendo wake wa mapozi. Mtoto wa kipare alitembea kama analazimishwa. Alikuwa mwamvita Rajabu. Alikuwa hapo kwa minajili ya kuuburudisha mwili wake. Akaufungua mlango akaelekea huko kulifungua geti. Ni wakati akilifungua geti akashangazwa na kitu ambacho alikiona. "DAMU" Ndio neno pekee kumtoka mdomoni kwake. Kwenye mlango wa gari la mtu wake ilionekana damu ikichuruzika. Damu ikitoka ndani ya gari na kudondokea sakafuni. Hakulitegemea wala kulitarajia. Hilo likamfanya aduwae kwa sekunde kadhaaa akishindwa kufanya maamuzi. Hakuliwaza hilo, mwili wake uliwaza mapenzi, moyo wake ulihitaji kuburudishwa, lakini mbona damu tena? Hilo likamuondoa katika mawazo. Punde bastola yake ilikuwa mkononi akijivuta kuelekea garini. Macho yakizunguka mfano wa bundi alizidi kusogea. Akaufikia mlango kisha kuushika. Kwa kasi ya umeme akaufungua mlango...

"Mamaaaa" kwa mara ya kwanza Mwamvita akapiga yowe huku mwili wake ukimtetemeka. Mbele ya macho yake alikuwa akiiutizama mwili wa mpenzi wake ukiwa ukiwa umelalia usukani wa gari huku kichwa kikiwa hakitamaniki kutokana na kufumiliwa kwa Risasi. Akashikwa na woga, akaogopa na kutaka kurudi nyuma. Lakini akajipa utulivu, kukimbia haikuwa suluhu ya hiki kinachotokea. Alitakiwa kulijua tatizo, alitakiwa kujua nani ambaye amefanya mauaji haya. Akaendelea kuuangalia mwili wa mpenzi wake, damu ilikuwa ikiendelea kuvuja. Akaizunguka gari akiutafuta kila upande. Hakumuona mtu, ingawa hakumuona lakini akakiona kitu ambacho kilimpa hisia tofauti. Hii ilikuwa magazine ya risasi. Kwa nini magazine? Na kwa nini iko hapa? Ina maana hakuuawa hapa? Kama hakuuawa hapa, nani alikuja na hii gari hapa? Haya yalikuwa maswali, maswali ambayo bado hakupata jibu. Wakati akiendelea kujiuliza, mara akaiona gari nyingine ikija na uelekeo ule. Uelekeo wa nyumbani kwake. Akarudi na kujitupa uvunguni mwa gari. Ujaji wa gari ili ulimshtua sana. Akatulia pale uvunguni akiangaza macho kuelekea kule mbele. Bastola ilikuwa mkononi mdomo ukiitizama gari ile. Kidole kilikuwa tayari kwa kuiruhusu risasi akaamua kuivuta subira. Gari ile ikaendelea kusogea na kusogea. Hakuendelea tena baada ya kufika hatua sita, gari ikasimama kisha taa kuzimwa. Ukimya wa ajabu ukatokea. Hakushuka MTU kutoka kwenye gari na hapakuwa na dalili yoyote ya kushuka kwa MTU. Hata yeye akatulia akitaka kukiona kile kitakachotokea. Baada ya ukimya wa dakika mbili akauona mlango wa gari ukifunguliwa. Punde akashuka MTU ambaye alimtambua. MTU ambaye alimjua. Licha ya kumtambua lakini hakujitokeza. Bado hakuamini MTU na bado hakutaka kumuamini. MTU aliyeshuka alikuwa Jimmy . Hata pale alipoanza kusogea pale kwenye gari bado Mwamvita hakujitokeza. Bado alivumilia kuuona mwisho. Jimmy alikuwa amesogea na sasa alikuwa ameikaribia gari, macho yake yakakiona kitu mfano wa maji yakichuruzika kutoka ndani ya gari. Hakuwa mgeni wa maji Yale, na hakuwa mwepesi wakuamini kwamba yalikuwa maji. "Damu" ndio neno lililogonga kichwani. Wakati huo huo mkono wake ukashuka kiunoni na kuchomoa bastola yake. Akaendelea kusogea kwa hatua za mashaka. Akaufikia mlango ambao ulikuwa wazi. Macho yake yakatua juu ya mwili wa binadamu uliofumuliwa kichwa kwa risasi, akahisi baridi ikimuingia, baridi ya woga na fadhaa. Aliogopa na kuogopa. Hakuwahi kukiona kifo cha aina ile. Ni hapo alipokumbuka kuwa Mwamvita alikuwa ndani ama naye atakuwa ameshauawa. Akaliendea geti na kujaribu kulisukuma. Geti likamtii. Akaingia ndani sasa akiwa ameuvaa ujasiri. Hakuwa muoga tena. Akaanza kuzikwea ngazi kuingia ndani kabisa ya jengo. "Jimmy nipo huku." Ilikuwa sauti iliomfanya Jimmy ageuke kwa kasi ya umeme huku bastola mkononi. Hata alipomuona Aliyemuita hakuishusha bastola. Alikuwa akimuangalia Mwamvita kwa mashaka. Mashaka yakutokumuamini kwa kile alichokiona nje. Hakuwahi kuona Unyama wa aina ile. Kwa Mara ya kwanza akauona Umuhimu wa kuongeza watu. Hakuwahi kufikiria hilo.



*********

Alikuwa akiishi kama mwizi kama sio kibaka. Muda wote alikuwa akibadilika kama kinyonga. Mtaani alikuwa akitafutwa na wana usalama wa kila aina. Kila hoteli ilipandikizwa watu maalum wa kuchunguza kila aingiaye na atokae. Anayekuja kula na hata wale waliokuwa na mambo yao binafsi. Kila mmoja alikuwa akiangaliwa kwa umakini sana. Wana usalama walikuwa wakimtafuta masimba kila kona ya mtaa na hata mji. Wakati huku Dar yakiendelea hivi, Masimba alikuwa nje kidogo ya jiji LA dar es salaam. Hakuwa huko kwa sababu ya kuogopa purukushani za maafisa usalama wanao msaka. Bali alikuwa nyumbani kwa Mama wa Marehemu Asteria kupata kile ambacho alitaka kupewa kabla ya kifo cha mwanawe na hata mwanawe wa pili. Alitelemka kwenye daladala kama abiria wa kawaida. Kichwani alijifunika kwa kofia aina ya cowboy. Chini alivaa suruali sambamba na raba ambazo zilisababisha aonekane kama kijana mtanashati pale kijijini. Baada ya kushuka hapo akaingia sehemu yenye huduma ya vyakula. Akatafuta sehemu nzuri na kutulia kisha kuagiza chakula. Baada ya chakula kuletwa, akaanza kula taratibu huku macho yake yakiangaza huku na huko kuona kama alikuwa akifuatiliwa ama lah!





Macho yake yalikuwa yakimtizama kila atokae na hata aingiae. Muda wote alikuwa akimshuku kila mtu ambaye angeingia na kusimama pasipo kufanya kitu. Alijua kinachoendelea Jijini ni kutafutwa kwake katika namna ya kipekee. Alitambua kujiokoa kutoka kuzimu ni kitu ambacho mkurugenzi na majasusi wote wasingekubali. Hakuna mtu alieingizwa ndani ya chumba kile na kutoka akiwa hai. Lakini kwake yeye aliweza na kuthubutu. Hilo ndio lingekuwa chanzo cha kutafutwa kwake. Na sio kutafutwa tu bali kupotezwa kabisa katika uso wa dunia hii. Maelezo kutoka kwa Teddy juu ya kinachoendelea kilimsisimua sana mwili wake. Watu wenye suti sambamba na waliovalia mavazi ya kawaida walikuwa wakipishana kumtafuta katikati ya jiji. Hata wale wa kike waliokuwa wakitembeza mboga za majano walikuwa wakimtafuta yeye. Nyumba yao haikukosa kuangaliwa kila wakati, wasichana wachafu wenye mabeseni yenye mboga za majani walipita kila wakati. Yote hiyo ilikuwa ni kutafutwa kwake. Hakuihofu taarifa hiyo kutoka kwa teddy, hakuiogopa kwa kuwa alikuwa ameizoea purukushani, alishazoea mapigano na hata kusumbuana na wana usalama. Aliutazama ujumbe ule kutoka kwa teddy kwa makini, aliporidhika akairudisha simu mahala pake. Akaendelea kula huku sasa akiiwaza kazi iliyo mbele yake. Kazi ambayo mwanzo haikuwa ngumu, kazi ambayo aliichukulia kama kazi ya kawaida. Lakini sasa ilikuwa ngumu baada ya kuingilia na Idara ya usalama wa taifa. Kitendo cha mkurugenzi kumkalipia kilionyesha ni kiasi gani mkurugenzi amekubali kudanganywa. Hakuamini na hakutaka kuamini kama Jasusi mwandamizi kama yeye anaweza kudanganywa kwa hila kisha kukubali. Hata alipowaza nani alipanga kile kilivhotokea hakuweza kugundua. Kuuawa kwa Godfrey Maboba na familia yake, kisha kukutwa na kikosi maalum cha kupambana na ujangili wa kutisha, ni mpango ambap ulipangwa na kutengenezwa na watu wanaomfahamu. Nani alimuona wakati anakwenda nyumbani kwa dada wa Marehemu Asteria. Hilo likampa picha kuwa mtu anayeogopewa na Teddy inawezekana ndio mpangaji wa haya matukio. Ndio huyu aliyemshawishi hata DG wa TISS akubali kukitenda kile ambacho hakuwaza kama kitatendwa na Mtu mwenye mafunzo yote kama yeye. Ni nani huyu anayeogopewa? Ni nani huyu mwenye nguvu kuliko Idara ya Usalama wa taifa? Ina maana hata kile kitengo chenye watu watano kimeshindwa kumgundua huyu mtu? Nina huyu? Yalikuwa maswali yaliyomtia hamu, hamu ya kumuona na kumjua huyo mtu. Alitaka kuonana naye uso kwa uso ama kumtafuta na kuhojiana naye kupitia mawasiliano. Hakuwahi kumuogopa mtu na hakuwahi kuogopa kabisa. Aliyawaza hayo akiendelea kula taratibu. Mara moja moja hakuacha kuangalia nje. Baada ya kumaliza kula sasa alikuwa tayari kwenda kwa mama wa marehemu Asteria. Akainuka kama kawaida huku macho yake yakimuongoza kwa kila hatua. Akakiacha kimgahawa kile na kuchepuka mpaka upande wa pili wa barabara. Ingawa alikuwa mgeni katika maeneo yale ya mkuranga, lakini alikuwa na maelezo yote ya kumfikisha nyumbani kwa mama Asteria. Alitembea kama mtu wa kawaida, wakati akiikaribia nyumba ile akamuona mtu akitoka ndani. Mtu ambaye alimshangaza na kumsisimua, mtu ambaye hakuamini kama angemuona pale. Alikuwa Teddy akitoka ndani ya Nyumba ya Mama wa Marehemu Asteria. Hilo likamstaajabisha, likamshangaza na kumduwaza. Teddy amefikaje huku, teddy amekuja kufanya nini huku? Yupo na nani? Wakati akijiuliza hilo, akamuona mtu mwingine ambaye alizifanya kengele za hatari kulia kichwani mwake. Huyu alikuwa Mwamvita, huyu alikuwa yule mwanamke aliyehusika na mlipuko kule kigamboni. Kwa Mara ya pili teddy alikuwa ameasi. Teddy alikuwa ameamua kurufi kundini kwake. Alikuwa ameikubali pesa na sio taifa lake. Kumbe wakati anatoa taarifa kuhusu wanausalama kuiweka chini ya uangalizi alikuwa akiipumbaza akili yake. Kumbe alikuwa yupo katika mipango ya kufika huku. Akauona usalama wa Mama Asteria kuwa mdogo.



Hakuweza kukurupuka, bado aliwatizama hasa akimuangalia Teddy. Alimuangalia kwa muda wote huku mishipa ya hasira ikajitokeza. Akawaona wakishuka ma kujipakia ndani ya gari kisha kuondolewa kwa kasi. Bado masimba aliduwaa, akili yake ilimtuma kuwahi pale, lakini bado kuna kitu alikihofu. Wakati bado anashindwa kitu cha kuamua, akamuona mama wa Asteria akitoka akiwa sambamba na kitoto kingine kidogo cha kike. Masimba akajitokeza sasa akielekea pale. Hatua ya kwanza kupiga akahisi kitu, kitu ambacho hakukijua. Hatua ya pili akahisi kitu kingine ambacho hata hiki hakukijua. Hatua ya tatu akagundua kuwa alikuwa akitizamwa na mtu kutoka sehemu fulani. Akaendelea kutembea akiziamini hisia zake, hisia ambazo hazikuwahi kumdanganya. Sasa akaikaribia nyumba ile, zilikuwa ni hatua tano kutoka ilipo nyumba. Kengele za hatari zikagonga tena. Safari zikiambana na uhatari wenyewe. Mama alikuwa akitabasamu, alikuwa akimuangalia masimba. Mkono alikuwa ameshikilia simu kubwa, simu ambayo kwa macho ya Masimba haikuwa simu, haikuwa simu ya aina yoyote bali ilikuwa rimoti, akili za masimba zikafanya kazi kwa haraka sana.. akaanza kukimbia huku akimuomba mama yule aitupe ile rimoti. Kabla hajamfikia akashuhudia mama yule akibonyeza kitu. Kilikuwa kitendo cha sekunde tatu Masimba kuruka hewani na kutua pembeni kabisa ya barabara. Mlipuko mkubwa ukasikika. Moto mkubwa ulikuwa angani huku jumba la mama wa Asteria likiwaka moto. Kilikuwa kishindo kilichotingisha mji wote wa mkuranga. Masimba alikuwa akikimbia kwenye moto kwenda kumuokoa yule mama. Hakuujali moto, hakujali kelele za watu ambao walikuwa wakipiga kelele. Alikimbia na kuingia katikati ya moto. Baada ya kuingia akaanza kutafuta. Alitafuta kwa shida kutokana na hewa nzito. Wakati anataka kukata tamaa akasikia sauti ya mtu akilia. Akaangalia hapo kwa tabu, akamuona Mama wa Asteria akiungua huku akimngika mjuu wake asiungue. Haikuwa picha nzuri kuitizama. Alisogea haraka na kumshika yule bibi. Akataka kumuinua lakini yule mama akamzui. Hata macho yake yalikuwa yakionyesha kukata tamaa.



"Naku....faaa mwa mwa.. nangu.. nao..mba muokoe huyu ni..nia.che mimi nife." Aliongea mama kwa uchungu huku machozi yakimtoka. Masimba hakuchelewa akamuangalia mama kwa sekunde. Akamuachia mkono huku akilia kwa uchungu. Akamchukua mtoto na kuanza kutoka naye. Hakutoka kupitia alipoingilia bali alitokea kwa upande wa nyuma. Mtoto alikuwa begani. Akafanikiwa kuuvunja mlango wa nyuma. Akatoka sambamba na mtoto yule. Akakimbia naye mpaka sehemu ambayo kulikuwa na watu wengi akasimama kisha kuomba maji. Hayakuwa maji ya kunywa, mwili wa mtoto ulikuwa na moto. Akamuweka mtoto chini ili apewe huduma ya kwanza. Lakini kumuweka tu chini akagundua mtoto alikuwa ameshakufa. Ameshakufa sambamba na bibi yake. Masimba hakuamini, hakuamini kama yule mtoto amefariki. Akaendelea kumtingisha kwa nguvu huku akilia. Lakini halikuubadilisha ukweli. Mtoto yule alikuwa ameshakufa. Masimba akamuangalia kanakwamba haamini kama yule mtoto amekufa. Teddy alikuwa amemrudisha tena kwenye maumivu. Akasimama huku watu wakimshangaa. Akarudi kwenye utimama wake. Ilikuwa ni lazima arudi kwenye utimamu wake. Kila kitu kilikuwa kigumu kwake. Alikuwa teddy pekee aliyeijua safari yake ya kwenda mkuranga. Ni yeye aliyejua kwamba anakwenda kuonana na mama wa Asteria. Kwahiyo hapa alijua teddy ndiye amehusika na kitendo kile cha kinyama

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Teddy pekee ndiye aliyekuwa akiifahamu safari yake. Safari ya kwenda kuongea na Mama wa Asteria. Lakini ni Teddy huyu huyu ambaye alimuona akiwa sambamba na mwamvita. Teddy ambaye alimueleza kuwa hakuwa tena kule. Teddy ambaye alimuamini na kuamini maneno yake. Lakini leo hii teddy alikuwa ameamua kuimaliza familia ya Asteria. Mama yake alikuwa akiendelea kuteketea na moto, huku mtoto mdogo wa kike akiwa amelala mbele yake akiwa hana uhai tena. Hilo likamuuma sana? Licha ya kuumia lakini hakutakiwa kuwa pale. Ulikuwa muda wa kuondoka na kupotea kabisa. Hakujali macho yaliokuwa yakimtizama, hakujali vilio na ving'ora vya polisi.. aliondoka akiwa amechanganyikiwa, aliondoka akiwa na Hasira na teddy, alitamani kupiga Risasi katika kichwa chake. Alianza na Asteria akafuatia Mwamvua, kisha dada yake na familia yake akiwemo Mumewe, Mr Godfrey Maboba. Sasa ameamua kuwamaliza wote. Kuna siri gani hapa nyuma? Ina maana ni mzigo tu wa madawa ndio sababu ya vifo vyote vile? Hapo akahisi kitu kingine, alihisu kuna kitu kingine nyuma ya mauaji haya. Alihisi hivyo na aliamini hivyo. Akaamua sasa kumfungia kazi Teddy, alitaka kwenda kumuonyesha kuwa yeye ni mtu mwingine katika medani ile. Kama mzigo wa madawa ameshauchukua kipi kinampa hofu teddy? Kwa nini aendelee kuua? Hakuweza kujibu hilo swali bali akasonya na kutukana tusi zito. Baada ya kutembea sana akajikuta akitokea sehemu yenye kituo cha daladala, bila kujali macho ya watu, akajipakia ndani ya costa moja na safari ya kurudu dar ikaanza. Muda wote wa safari alikuwa amekiinamisha kichwa chake kwenye siti akiliwaza tukio lililotokea punde. Sauti ya mama wa Asteria ilikuwa ikijirudia kila wakati. Tukio zima liliendelea kumtesa. Akatamani afike Dar akamuone Teddy. Alikuwa tayari ameapa kwenda kuitumbukiza Risasi Kichwani kwa Teddy. Ni wakati akiliwaza hilo akausikia Ujumbe ukiingia kwenye simu yake. Akataka kupuuza, alitaka kutoitazama simu, lakini akaisikia sauti ikimwambia "wewe ni mpelelezi unayetafutwa usipuuze kitu."!!! Akaitii sauti ile. Muda mfupi vidole vyake vilikuwa na kazi ya kuifungua Meseji.



"Uko salama, nasikia kuna nyumba imelipuliwa huko!!!? Ulisomeka Ujumbe ulionekana kutumwa na Teddy. Hilo pia hakuliacha lipite hivi hivi. Teddy alikuwa akimchezea akili yake, teddy alikuwa akimuona mjinga. Lakini kingine kilichomfurahisha ni kule kugundua kuwa teddy hakuwa amemuona wakati akitoka ndani. Hilo likampa uhuweni wa kumfikia pasipo rabsha yoyote. Teddy alikuwa ameingiwa na tamaa, ni yeye na mwamvita waliotoka ndani ya nyumba ya mama wa Asteria. Lakini muda huu anamtumia Ujumbe kuhusu kilichotokea, alikuwa akiipima akili ya masimba. Hakuona sababu ya kumjibu, akaitizama simu kwa muda kisha kuirudisha mfukoni. Alimchukia teddy na bado alitamani kufika Dar es salaam akutane nae.



*******

Alishuka maeneo ya mbagala saa moja na nusu usiku. Baada ya kushuka hapo akaona ilikuwa muhimu kumpigia teddy kutaka kujua wapi alipo. Akatafuta sehemu yenye utulivu akaipiga simu ya teddy, lakini cha ajabu haikuwa hewani. Akajaribu tena na Tena lakini bado hali ikawa ni hivyo. Simu ya teddy haikuwa ikipatikana. Akakiona kitu ambacho alikihisi hapo mwanzo. Teddy alikuwa amemchezea akili yake, inawezekana alimuona kule ndio maana akamtumia ule ujumbe. Sasa kutokupatikana kwa teddy kilikuwa ni kitu kingine cha kushangaza. Akaona haukuwa muda wa kuendelea kubaki mbagala. Ilikuwa ni lazima arudi kinondoni kwa usiku ule. Lakini kabla hajaamua kurudi lazima awasiliane na rafiki zake ambao wapo katika nafasi nyeti nchini. Wa kwanza kumpigia alikuwa Dee Plus, huyu alikuwa mmoja kati ya vijana wake. Aliongea naye mawili matatu. Baada ya hapo akarudi tena kituo cha daladala. Hapo akachukua usafiri wa kuelekea huko.



********

"Masimba anaelekea mkuranga kwa mama wa Asteria. Hakikisheni anazuia au mama anafutwa katika uso huu wa Dunia." Ilikuwa sauti ya teddy akiongea na mwamvita. Simu hiyo alipiga baada ya kikao kizito kati yake na washirika wenzake kufanyika na kufanikiwa kumrudisha teddy kundini. Ni simu hiyo ambayo iliwalazimu teddy na mwamvita kuelekea mkuranga. Ni simu hiyo iliyotumika kumtumia ujumbe masimba kwamba alikuwa akisakwa na wanausalama. Ujumbe ule kwenda kwa masimba ulitumwa na teddy wakati huo wakiwa mkuranga. Aliutuma mahususi ili kumfanya masimba achelewe kurudi Jijini, ili watu wao waendelee na utafutaji wa mzigo wao ambao uliibiwa. Licha ya watu waliotumwa kuipekua nyumba ya masimba nje ndani na ndani nje. Hawakuweza kupata chochote. Hawakuweza kuupata mzigo wao, mzigo ambao ndio chanzo cha mauaji na uasi uliofanywa na Teddy. Lakini kingine ambacho kiliwashangaza Jimmy na washirika wake, nikule kuambiwa hata masimba hawakumuona kule mkuranga. Ni taarifa hiyo ambayo bado ili wachanganya na kuwafanya kila mmoja awaze lake.. ndipo hapo amri ilipotoka kwamba wategeshe bomu ndani ya nyumba ya mama wa Asteria na kabla ya hapo walipewa amri ya kumsubiri masimba hapo. Muda ulivyokuwa ukisonga na kutokuonekana kwa masimba ndipo maamuzi ya kilichotokea mkuranga yakafanyika. Hawamuona masimba wakati akisogea pale, hawakumuona kwa kuwa walikuwa katika uharaka wa kuondoka. Na hicho ndicho walichokosea.



**********



Simu ya teddy bado haikupatikana licha ya kuipiga mara kwa mara. Bado hakikuwa kitu cha kawaida kwake, teddy amtumie meseji lakini ndani ya muda huu alikuwa hapatikani. Haikuwa kawaida kwake, haikuwa kawaida kwa kuwa alimfahamu teddy. Wakati akiwaza hilo akausikia mlio wa simu yake kuonyesha kwamba alikuwa akipigiwa. Ikaichomoa simu, akatupa macho Juu ya kioo, akakutana na namba mpya. Akaitizama ile simu kwa muda bila kuipokea mpaka ilipokatika. Hakuwa na utaratibu wa kupokea namba ngeni katika kazi yake hii ya hatari. Baada ya ile simu kuita na kukata bila kuipokea, akapata hisia za kuingalia namba ile vizuri, alitaka kumjua mmiliki na alitaka kujua inapigwa kutoka wapi. Muda mfupi alikuwa akiongea na simu Nyingine hewani. Baada ya kukata akatulia akisubiri kupata maelekezo kutoka kwa mtu wake. Haikupita muda muda mrefu simu yake ikaita tena. Alikuwa ni yule mtu wake. Akaipokea na kuongea kwa dakika kama moja hivi kabla ya kuikata simu. Mwili wake ulisisimkwa na kushikwa na ubaridi. Namba mpya iliompigia ilipigwa kutokea katikati ya jiji la dar es salaam maeneo ya posta. Ilikuwa taarifa aliyoitegemea kqbisa. Alijua simu hiyo ilitoka kwenye moja ya majengo yanayomilikiwa na Idara ya Usalama Wa Nchi. Hilo likamfanya aamue kuelekea huko, alitaka kwenda kumjua mwenye namba ile. Hakuwa na sababu ya kuogopa wakati alikuwa akisakwa. Baada ya daladala aliopanda kufika maeneo ya uhasibu alishuka, kisha akachukua usafiri wa pikipiki mpaka maeneo ya posta. Alishuka na kulipa ujira kisha kuongoza kuelekea pale ambapo alipakusudia. Alitembea kwa uangalifu mpaka maeneo ya bandarini nje ya kituo cha mabasi yaendayo kasi. Kulikuwa na umbali mfupi sana kutoka kwenye jengo binafsi linalotumiwa na usalama wa taifa. Jengo ambao lilikuwa likitizamana na Makao makuu ya Mamlaka ya mapato Tanzania. Vilevile ulikuwa umbali mfupi na kilipo kituo kikuu cha polisi Dar es salaam (Central police) baada ya kusimama hapo kwa muda akiangalia hili na lile, akaichomoa simu yake, kisha akaitafuta ile namba harafu akaipiga akiwa mkononi pasipo kuipeleka sikioni. Baada ya kuita tu, akaikata kisha akaondoka pale kwa haraka mpaka pale kituo cha posta ya Zamani. Akatulia pale huku macho yake yakitizama kule alipotoka. Haikupita hata sekunde thelathini, akawaona watu wanne ambao hawakuonyesha kama wako pamoja wakipishana huku na huko. Hakuwa mgeni na majasusi, aliwajua na kuwatambua hata kama wamejibadilisha kwa kiasi gani.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Aliwajua wanausalama na kuwatambua. Hata wangekuwa umbali gani haikuwa shida kwake kuwafahamu. Akaendelea kuwaangalia huku akiondoka pole pole kutoka eneo lile. Utimamu wa akili bado ulimpa uhuru na uwezo wa kutenda kile ambacho alipaswa kufanya kwa wakati ule. Alijua uwezo wa wanausalama wa Tanzania. Aliutambua weledi wao. Kwahiyo alitakiwa kuwa makini kwa kila hatua. Bado alikuwa akiwaona watu wakiongezeka katika eneo husika kutokana na kumulikwa na taa za magari. Kuna ambao walikuwa wakiyumba kama walevi, wengine walikuwa wamevaa mavazi chakavu wakionekana kuokota vitu chini. Hicho ndio kitu ambacho alikitaka masimba. Alitaka kuhakikisha ni kweli alikuwa akitafutwa? Kuipiga simu akiwa pale alitambua angegundua chochote kama ni kweli namba ile ilitumiwa na watu wa usalama. Hilo likafanikiwa, hata wale walevi na omba omba waliokuwa pale ilikuwa ni mbinu ya wanausalama. Akaendelea kutizama kila kilichokuwa kikiendelea. Purukushani ilikuwa kubwa sana, purukushani ya watu na hata magari yaliokuwa yakipita huku na kule. Wana usalama wengi walikuwa wakipanda kwenye mabasi ya mwendokasi, wengine walikuwa madirishani wakichungulia kwa ndani. Ni hapo alipoiona gari aina nissan patrol ikitembezwa taratibu. Haikuwa gari ngeni machoni mwake, ilikuwa gari anayoifahamu vizuri tu. Ilikuwa gari ambayo ilitumiwa mara nyingi na watu tofauti wa idara. Hii ilikuwa gari iliyotumiwa mara nyingi na kitengo kimoja ambacho kipo ndani ya Idara. Kitengo ambacho hujulikana kama black mambaz. Macho yake yakazidi kuitizama gari ile. Wakati ikielekea katikati ya jiji, masimba naye alisimamisha pikipiki, akamuomba aifiatilie gari iliyombele yao kwa siri. Dereva yule hakubisha, taratibu akaanza kuifuatilia gari ile ambayo sasa ilikuwa ikielekea maeneo ya posta mpya. Muda wote masimba alikuwa akiitizama ile gari. Alitaka kujua ni wapi inapoelekea. Akamwambia dereva aache magari manne yatangulie mbele yao ili kutokuwagutusha watu waliokwenye gari. Dereva wa pikipiki akatiii. Akaendesha huku akiwa makini na kila kitu. Punde wakaiona gari ikiingia barabata ya Allhasan Mwinyi. Magari ya mbele yao nayo yakaelekea huko. Wakaendelea kuifuatilia ile gari. Baadaa ya kupita daraja la salenda ile gari ikaacha barabara Ally Hassan Mwinyi ikaingia barabara ya kinondoni. Hapo dereva akageuka kumuangalia masimba. Masimba akampa ishara ya kuendelea kuifuatilia kwa nyuma. Baada ya kuifuatilia kwa muda wakaiona gari ile ikisimama maeneo ya kinondoni Manyanyq. Masimba akamwambia dereva yule aipite ile gari pasipo kuonyesha wasiwasi wowote. Baada ya kuipita ile gari na kutembea mbele kidogo. Masimba akamwambia asimame hapa, akachomoa noti tatu za Elfu kumi na kumkabidhi yule dereva. Baada ya kumkabidhi aliondoka taratibu kurudi nyuma pale ilipoegesha gari waliokuwa wakiifiatilia. Alitembea kwa umakini mkubwa mpaka jirani kabisa na iliposimama ile gari. Akaangaza macho yake kwa umakini kule gizani. Punde akawaona watu wawili ambao wakikuwa wamesimama kwa kumpa mgongo. Walikuwa wamevaa mabaibui kuficha sura zao, lakini maumbo yao hayakumfanya masimba kupotea. Mbele yake alikuwa akiwatizama Teddy Sambamba na Mwamvita wakiwa wamempa Mgongo. Hapo akaongeza umakini, sasa alikuwa akiwaangalia kwa karibu zaidi. Bado walionekana wakiongea kitu, bado walionekana kulikuwa na mazungumzo yakifanyika. Punde akaiona gari ya kifahari ikisogea taratibu katika eneo lile. Ilikuwa gari ya bei mbaya, gari ambayo thamani yake iliweza kuhudumu kwenye wizara kama tatu za hapa nyumbani. Wakati akiendelea kuiangalia ile gari ikisogea, macho yake yakavutiwa na watu wawili wengine waliongezeka pale. Kitendo bila kuchelewa akawaona watu wale wakimuongoza teddy kuelekea kwenye ile gari ambayo bado ilikuwa ikitembea. Akaliangalia tena lile tukio la teddy kupelekwa kwenye gari. Haukuwa ukokotwaji wa kawaida,haukuwa ukokotwaji wa hiari bali ulikuwa ukokotwaji wa lazima. Kwani kuna wakati teddy alikuwa akigoma lakini alikuwa akilazimishwa kwa mtutu wa bunduki. Kilikuwa kitendo kilichofanyika kwa muda wa nusu dakika na hata alipoifikia gari na mlango kufunguliwa akashuhudia pigo la kitako cha bastola likitua kisogoni kwa Teddy. Hilo likaufanya mwili wake kuingiwa na ganzi, damu kusimama kwa muda huku mwili wake ukitetemeka. "Naam mapenzi yalichukua sehemu yake. Aliumia sana katika kile ambacho kilitendwa kwa Teddy. Licha ya yote aliotendewa na teddy bado alimpenda. Bado alimuhitaji katika kina cha moyo wake. Akaendelea kushangaa na kuduwaa. Teddy alikuwa akiadhibiwa, teddy alikuwa akipelekwa sehemu ambayo si salama kwake. Alitambua kama angemuacha bila kufanya kitu basi asingemuona teddy akiwa hai tena. Hakulikubali hilo na hakuwa tayari. Ilikuwa lazima afanye jambo, jambo la kumuokoa teddy. Lakini hawa waliomchukua ni nani? Na wanampeleka wapi? Haukuwa muda wa kutafuta majibu wala kujiuliza maswali. Muda mfupi alikuwa kwenye tax wakiwa nyuma ya gari iliyombeba teddy, wakiifuatilia kwa nyuma. Muda wote alimhimiza dereva kuongeza kasi na kuhakikisha gari ya mbele haiwapotei. Hilo likafanywa kwa umakini, bado katikati yao waliyaacha magari matatu kama kanuni nyingi za kipelelezi zilivyo. Mpaka wanafika magomeni usalama na gari kuonyesha ishara ya kuingia barabara ya morogoro hata wao wakafanya hivyo. Kufika mbele kidogo eneo la magomeni usalama, wakaiona gari wanayoifuata Ikiingia maeneo ya ukumbi maarufu kwa burudani ya muziki wa mwambao uitwao Travertine Hotel. Baada ya gari ilikukatisha na kuingia kabisa masimba alishuka kwa haraka ni baada ya kulipa ujira wa Dereva, akaongoza kama mtu wa kawaida kuelekea hotelini hapo. Bastola zilikuwa kila upande ndani ya mavazi yake. Hatua tano mbele akakutana na madada poa wanaofanya biashara ya kuuza mili yao katika eneo hilo. Akamuita mmoja na kusimama naye pembeni kama wafanyavyo wanunuzi. Lakini yeye hakumuita hapo kwa sababu ya kutaka huduma, bali alitaka kuutumia kama moja ya kuzuga ili ajue ni wapi twddy anapelekwa. Akasimama na yule binti tena ni baada ya kumpa yule chqngudoa elfu kumi. Macho yake yalikuwa yakitizama kule iliposimama ile gari. Akaushuhudia mlango ukifunguliwa. Kwa kuwa palikuwa karibu sana, alikuwa akishudia kila kitu ambacho kilikuwa kikitendeka.



Baada ya mlango wa gari kufunguliwa wakashuka watu watatu tofauti na wale wa mwanzo. Kati yao mmoja wao alikuwa amebeba kitu kama furushi begani. Baada ya watu wale kushuka wakaongoza moja kwa moja kwenda ndani upande wa hotel. Bado masimba alitulia akichunguza kila kitu. Baada ya watu wale kuingia ndani, huku nyuma mlango wa kati ukafunguliwa tena. Mara hii akashuka mtu mzima ambaye sura yake ilifunikwa kwa kofia ya pama. Baada yq mtu yule kushuka akaonekana akiongozwa na walinzi ambao kwa kuwaangalia tu.. walikuwa ni walinzi wale wa kulinda viongozi wa Kitaifa. Lakini hapa walionekana wakimlinda huyu mtu aliyeshuka kwenye gari. Haikuwa sawa kwa presidential protect unit kuwa katika eneo hili tena kwa mtu ambaye hahusiki na serikali. Hilo likampa wasiwasi wa kutaka kujua zaidi. Teddy kupelekwa ndani, kisha mtu huyu kushuka naye kuelekea huko kilikuwa kitendo kilichomshtua. Hatua ya kwanza aliipiga akimuacha yule changudoa akishangaa. Hatua ya pili, changudoa hakukubali naye akawa anafuata kwa nyuma. Hatua ya tatu alishamfikia masimba na sasa walikuwa wakitembea sambamba wakizipanda ngazi wakiwa kama wa penzi. Kwa kuwa kulikuwa na giza hakuna aliyeweza kumgundua. Baada ya kumaliza ngazi na kutokea mapokezi akashangazwa na watu waliotapakaa. Watu ambao sura zao zilikuwa zikiongea lugha moja. WOTE WALIKUWA MAIFISA USALAMA WA TAIFA.



Watu waliokuwa wakiongea lugha moja, watu ambao kwa kuwaangalia wangekujulisha wao ni kina nani. Masimba bado akilimshikilia changudoa wake. Mwili na mikono vikiwa kwenye utayari. Hata yeye macho yake yalikuwa yakiwatizama. Sasa alikuwa akienda mapokezi na changudoa wake. Changudoa aliemuokota nje na kumfanya kama chambo cha kumuingiza hapo hotelini. Kufika mapokezi hakuongea chochote zaidi ya kuchomoa bulungutu la pesa na kuliweka juu ya meza ya mapokezi. Mhudumu alitmhamaki kutokana na wingi wa pesa zilizowekwa mezani. Hata changudoa naye alikuwa katika hamaniko, hamaniko lililozaa sononeko la moyoni. Alikuwa akiitafuta pesa kwa kuuza utu wake, lakini leo hii amakutana na mtu anayeitumia pesa kwa fujo. Wote wakabaki wameduwaa wakiisubiria kauli ya masimba. Kauli kuhusu matumizi ya pesa ile. "Nataka kujua watu waliobeba mzigo wamekwenda chumba namba ngapi. " ilikuwa sauti iliopenya masikioni mwa watu hawa wawili, mhudumu na changudoa. Hawakujibu wala kupata jibu kwa wakati ule. Huyu ni nani? Na kwa nini anataka kujua? Yalikuwa maswali ambayo hayakupata majibu kwa wakati ule. "Fanya hivyo uchukue pesa kama hutaki hii hapa itakuwa zawadi yak0." Alinong'ona safari hii sura yake ikiwa haina masihara. Wasichana wote waliduwaa. Hawakuduwaa kwa kutokujua cha kufanya, bali waliduwaa baada ya kuuona mdomo wa bastola ukichungulia. Binti akatii bila kuonyesha wasiwasi. Akainuka na kuwapa ishara wafuatane. Ishara ambayo haikuonekana popote. Bado changudoa alikuwa mkono wake wa kushoto. Walitembea kwa hatua za umakini huku macho yake yakitambazwa kila sehemu kwa utulivu. Wakawapita wanausalama na kuanza kuipanda ngazi kuelekea juu. Hatua tano baada ya kutokea kwenye korido wakauona mlango wa mbele ukifunguliwa. Watu wawili aliowafahamu walikuwa wakitoka hapo. Alikuwa Jimmy sambamba na mtu mwingine mwenye asili ya kihindi. Masimba akainama kisha kuonekana akimbusu changudoa yule.alifanya kitendo kile mpaka pale walipopishana na watu wale ndio wakaacha. Hapa akaukuta uhuru, hapakuwa na wanausalama na hapakuwa na mtu mwingine. Ishara ikafuata kutoka kwa mhudumu yule. Ishara ya kuwaonyesha kwamba hapa ndio sehemu yenyewe. Akaimpa ishara ya mwanamke yule kuugonga mlango. Muda wote yeye alikuwa ameikamata bastola akitizama nyuma. Mhudumu akaugonga mlango kwa mara ya kwanza, kukapita kimya, mara ya pili bado hapakuwa na mtu wa kujibu. Wakati mhudumu yule akigeuka amuulize masimba cha kufanya,. Mlango ukafunguliwa kisha mtu kuchungilia. Kilikuwa kitendo cha nusu dakika kufanywa na Masimba. Kwani wakati dakika inatimia masimba Alikuwa ndani huku mtu yule aliyechungulia akivuja damu. Macho yake yalishatambaa kila upande mle chumbani na kukinasa kitu kilichompandisha Hasira. Teddy alikuwa juu ya kitanda akiwa na nguo ya ndani tu, huku fahamu zikiwa bado zimempotea. Hakushughulika sana na teddy. Bastola yake ilikuwa ikimuangalia mtu yule. Hata alipomuangalia mtu yule na macho yao kuonana hakuamini. Hakuamuni mtu aliyekuwa akitizamana naye. Hakuamini kumuona mtu huyu akiwa chumbani na Teddy. Alikuwa kiongozi mzito wa serikali. Kiongozi wa ngazi za juu kabisa katika nchi husika. Mtu mwenye jina kubwa katika jamii na katika nyanja za kimataifa. Alimuangalia kisha kumuangalia teddy pale kitandani. Haukupita muda sauti ya chafya ikasikika ndani ya chumba kile. Damu ikaruka na kusambaa chumba kizima. Yule changudoa hakutegemea kuliona lile tukio kufanywa na mtu huyu aliyemchukulia kama mteja. Akataka kupiga kelele lakini alipouona mdomo wa bastola unamtizama, akanyamaza akibaki anatetemeka. Macho yake yalikuwa yakiutizama mwili wa kiongozi wa nchi ukiwa umalala katikati ya dimbwi la damu. Masimba akaufunga mlango kwa ndani kisha kumvuta mwanamke yule.



"Sikiliza naomba unisikilize kwa makini. Ukileta ukaidi kilichompata huyo mtu hapo hata wewe kitakupata. Nataka tuondoke humu ndani tukiwa na huyu dada kwa kupitia mlango wa dharura wa hoteli hii. Sasa chukua hii bastola, mimi nitambeba huyu mwanamke, wewe utakuja nyuma yangu ukinilinda. Yoyote ambaye atajitokeza piga risasi. Umenielewa?



Changudoa yule akajibu kwa kutingisha kichwa. Akachukua mavazi ya Teddy na kumvisha. Muda mfupi walikuwa Nje ya chumba kile wakielekea nyuma ya hoteli kwenye mlango wa dharura. Kilikuwa kitendo kilichotendeka kwa muda mfupi sana. Kitendo ambacho hakikuchukua hata dakika mbili. Wakatembea kwa uhuru bila kukutana na chochote. Mpaka wanatokea nje hawakuonekana na mtu yoyote. Baada ya kufika nje wakaivuka barabara kama wanaelekea magomeni mapima. Hatua kadhaa mbele wakaiona tax mbele yao, wakaisimamisha, kisha kumuomba jamaa awapeleke kimara mwisho. Dereva akawasha gari na safari ya kimara kuanza. Baada ya kutembea mpaka magomeni mwembe chai, masimba akachomoa burungutu la pesa na kumpa yule changudoa.



"Shuka hapa nitakutafuta, lakini nakuomba ufumbe mdomo wako." Akanong'ona masimba huku akimpa kile kitita. Binti akakipokea huku akionyesha wasiwasi. Hiyo haikuwa dalili nzuri kwa masimba. Baada ya kushuka na kuondoka masimba akamuomba dereva ashuke amfuatie msichana yule kwani kuna kitu ambacho alisahau kumwambia. Dereva hakuwa na hiyana, akaipaki gari pembeni mwa barabara. Masimba akashuka na kuanza kumfuatilia mwanamke yule bila mwenyewe kujua kama anafuatiliwa. Ilimchukua masimba dakika tano kuifahamu nyumba ambayo anaishi msichana yule. Baada ya kuigundua nyumba ile akarudi kwenye gari.



*******



Siku zote kazi ya kijasusi huwaga hazitakiwi kuacha ushahidi nyuma. Kifo cha kiongozi yule wa nchi alijua kitaibua mambo mengi sana. Alijua msako utakuwa mkali na hoteli nzima lazima ipekuliwe. Alitambua wahudumu na hata baadhi ya wapangaji watatiwa kashkash kutokana na hilo. Ni katika kashkash hizo nipo watakapo mpata mhudumu ambaye alikuwa zamu katika siku hiyo. Alitambua akipatikana mwanamke yule basi na hata yule changudoa angepatikana. Hapo kila kitu kingewekwa wazi na angejulikana kwamba ni yeye aliyetengeneza mauaji hayo. Baada ya kuwaza sana akaona hakuna njia nyingine zaidi ya kuwafuta watu hawa wawili kwenye ulimwengu. Ilikuwa ni lazima mhudumu auawe na ilikuwa bora zaidi kwa changudoa yule kuondolewa uhai ili kuufuta ushahidi. Hilo hakutaka kulifanya yeye, hili aliamua kumpa rafiki yake. Akachomoa simu yake na kubonyeza namba kadhaaa. Akaipeleka simu sikioni. Baada ya muda simu ikapokelewa.



"Don." Ilisikika sauti kutoka upande wa pili.



"Dee plus kuna watu wawili nahitaji uwasafirishe kuzimu usiku huu kabla ya jua la asubuhi." Alinong'ona Masimba.



"Nipe ramani, nina hamu sana ya kupambana." Alijibu Dee plus.



Muda mfupi alikuwa akipewa maelezo yote ya kufuata kufanikisha safari za watu hao.



"Nimekuelewa Don, nimeshachukua tiketi zao nawapelekea muda sio mrefu." Akajibu De plus. Masimba akakata simu kisha kugeuka na kumtizama teddy pale kitandani. Alikuwa akimpenda sana teddy. Akajisogeza na kujilaza pembeni yake.



******

Ilikuwa yapata saa kumi na mbili za asubuhi, wananchi wengi wakiwa bado vitandani.. Kila mmoja alishtushwa na wimbo wa Taifa kupigwa asubuhi ile. Hakikuwa kitu kiliozoeleka kwa watu. Punde ikasikika sauti ya kiongozi wa nchi akitangaza kitu ambacho kilimshtua kila mtu.



"Ndugu wanachi, nasikitika kutangaza kifo cha Waziri wenu mkuu kilichotokea usiku wa jana. Nawaomba wote muwe kwenye utulivu katika kipindi hiki kigumu. Mambo mengine mtaendelea kupewa kadili muda utakavyo kwenda."... ilikuwa taarifa iliomsha watu, watu wakaanza kukaa vikundi vikundi wakiongea hili na lile. Kila mmoja akionyesha kuguswa na kifo cha kiongozi huyu wa nchi. Wakati watu wakiendelea kuhuzunika, upande mwingine, wanausalama walikuwa wakihaha kila sehemu kutafuta chochote cha kuwasaidia lakini haikuwa hivyo. Hawakupata chochote. Ni wakati huo walipopqta taarifa kuwa kuna changudoa mmoja alionekana akiwa na mwanaume ambaye anahisiwa kufanya mauaji hayo.



******

Kunachangudoa mmoja ambaye inasemekana alionekana akiwa na mwanaume ambaye begani alimbeba mtu, walichukua tax lakini walipofika magomeni mwembechai mwanamke yule alishuka na haukupita muda na huyo mwanaume naye akatelemka akimuaga mtoa taarifa kuwa kuna maagizo amesahau kumpa yule mwanamke. Alikwenda huko kwa muda wa dakika tano, kisha kurejea na kuomba apelekwe kimara. Yalikuwa maelezo kutoka kwa dereva wa tax aliyekodiwa usiku wa jana hotelini pale. Kikundi cha wanausalama kikatumwa huko na kingine kimara,wengine wakabaki pale hotelini wakihangaika na camera za usalama sambamba na mhudumu ambaye alikuwa zamu siku ya mauaji. Barabara zikafungwa kwa muda huku magari yakipekuliwa na madereva kutiwa kashkash. Mhudum Hakuwepo hotelini ama hakuonekana kabisa. Wanausalama walipekua hata chini ya mazuria. Kila kitu kilikuwa kikitiliwa shaka. Wengine ambao walielekea chumba cha kuongozea camera, nao wakapigwa na butwaa. Hapakuwa na chochote katika camera zile. Hapakuonekana mtu wala kikundi cha watu. Hapakuonekana mtu wa kutilia mashaka katika hilo. Bado wataalam wakahangaika huku na huko lakini hapakuonekana chochote. Hata wakati Waziri Mkuu akiingia haikuonekana kwenye camera. Hilo likawafanya wachoke. Kitu kwamba mpango huo ulipangwa mapema kama ya ujio wa mheshimiwa waziri likatawala akilini mwa wanausalama. "Nani amelifanya hili? Nani ameingia na kutekeleza mauaji haya ya waziri mkuu? Je kuna kisasi hapa? Kipi kilimtoa waziri nyumbani kwake mpaka kuja hapa? Ni mtu gani alimbeba mtu? Na ni nani aliyebebwa? Yalikuwa maswali yaliovisumbua vichwa vya wanausalama. Maswali ambayo hayakuwa rahisi kujibiwa kwa wakati ule. Wakatamani hata kumhoji marehemu mwenyewe awaambie. Walitamani waziri ainuke na kukitegua kitendawili kile. Lakini kilikuwa kitu kigumu kama kulazimisha jua kuwaka usiku na mbalamwezi kuangaza mchana. Vichwa vyao vilichoka na kuchokeana. Wakatafakari sana huku wakitamani zingekuwa zama zile, zama za kina Joram Kiango na Willy Gamba. Wasingesubiri waambiwe katika hili bali wangeamua wenyewe. Wasingesubiri muuaji apotee bali wangemtafuta na kumrudisha ama kumsafirisha. Zilikuwa Nuru na Tunu pekee katika nchi ya Tanzania. Nuru iliyong'ara kama Madini ya TANZANITE. Lakini hapakuwepo na Willy Gamba wala Joram Kiango, alikuwepo mtu mmoja aitwaye Masimba, alikuwepo mtu huyu ambaye uwezo wake ulijulikana katika mipaka na mataifa yote. Lakini wana usalama wengine hawakujua kilichopo nyuma. Ni hapo walipokuwa wakiliwaza hilo, wakapewa taarifa kuonekana kwa matone ya damu katika chumba fulani. Wote wakaelekea huko. Hata walipofika hapo ni kweli waliyaona matone ya damu. Damu ilikuwa imeganda kuonyesha haikuwa ya muda ule. Hatua kumi mbele ndani ya pipa ndani ya chunba kile wakauona mwili wa mwanamke ukiwa hauna uhai. Kila mmoja kengele ya hatari ikagonga kichwani. Hawakuamini kama hata huyo changudoa alikuwa salama. Kwa mara ya kwanza wakakili kuwa walikutqna na mtu anayeijua kazi yake. Mtu aliyewajua na kuwatambua.



*****

Baada ya Dee plus kupokea maelezo kutoka kwa masimba, alichokifanya ni kuondoka usiku ule akiamua kuanzia pale hotelini. Alitambua kazi ya kumpata changudoa yule ilikuwa rahisi kuliko kwenda kuharibu camera za usalama. Hakutaka kuchukua gari yake kwa kuhofia kujulikana. Bali alichofanya ni kuchukua usafiri wa pikipiki ambao ulimpeleka mpaka magomeni. Akashuka kama mtu wa kawaida, kisha akaongoza mpaka hotelini. Alipanda ngazi kama mteja, lakini wakati anatokea mapokezi akapokelewa na mhudumu anayeonekana ni mwenye wasiwasi. Uso wake ulikuwa ukiongea hofu tu. Alionyesha woga wawaziwazi. Dee plus akatabasamu ili kuitoa hofu kwa mwanamke yule. Lakini hilo halikufanikiwa, mwanadada yule alikuwa na hofu. Kuna wakati alijaribu kuongea vitu lakini hayakusika masikioni kwa dee plus.



"Habari yako mrembo? Dee plus aliamua kujizungumzisha ili kujaribu kumvuta mwanamke yule. Lakini bado salamu haikujibiwa.



"Kaka naomba nikwambie kitu lakini sio hapa." Akaropoka mwanamke yule akionyesha kupagawa. Dee plus akatingisha kichwa, kwa mara ya kwanza alikubaliana na masimba suala la kutaka kuwasafirisha watu hawa. Kwa muonekano wa huyu mhudumu asingeweza kuufumba mdomo wake kama angekutana na wanausalama. Hakuchelewa kumvuta mpaka sehemu aliyotakiwa. Binti naye bila kujua ameletewa tiketi ya kifo, akaufumbua mdomo na kutaka kuongea... hakupewa hiyo nafasi, tayari basi lilimfika tayari kwa kumchukua. Risasi mbili kutoka kwenye bastola yenye kuzuia mlio zilipenya upande wa kushoto wa kifua chake. Hakuweza kupiga ukelele wowote. Alitupwa umbali wa hatua tatu akaanguka chini. Alikuwa maiti tayari. Baada ya kuhakikisha mwanamke yule hatafumbua mdomo tena, akamuinua na kumtupia ndani ya pipa. Sasa alikuwa akihamia kwenye chumba cha camera za usalama katika hoteli ile. Aliwapita wana usalama akiwa amevaa kitamburisho kama mfanyakazi wa hoteli ile. Akaingia pasipokuonyesha wasiwasi. Muda wa dakika kumi akatoka ndani akiwa ameshaimaliza kazi na sasa ilikuwa safari ya kuelekea nyumbani kwa changudoa yule. Akawapita wanq usalama kwa mara ya pili bila kushtukiwa na yoyote yule.



*******



Ni nyumba yenye watu wengi, nyumba ambayo asubuhi hii iliwakuta watu wakiwa kwenye vikundi vidogo vidogo wakijadili na kuongea kuhusu kifo cha waziri mkuu wa nchi. Kila mmoja alikuwa akiongea kile ambacho ana uhakika nacho. Huku wengine wakiongelee kuuawa kwa waziri kunatokana na mwanamke, wengine walikuwa wakilihusisha hili suala na mtifuano wa kisiasa unaoendelea nchini. Watu kutekwa na watu wasiofahamika ni kitu ambacho kiliufanya mjadala juu ya kifo cha kiongozi mkuu wa nchi upambe moto. Wakati wakijadiliana hilo, wakashtushwa na gari jeusi likisimama mbele ya uwanja wa nyuma ile. Kabla hawajakaa vizuri, wakashtushwa na kuwaona watu wanne wakishuka. Ushukaji wa watu wale ulikuwa ukitia fora na kuogopesha miongoni mwa watu wachache waliokuwepo pale. Kila mmoja akaliacha alilokuwa anaongea, macho yao sasa yalikuwa kwa watu ambao tayari walishaufikia mlango wa nyumba ile. Hakuna aliyeinua mdomo kuongea chochote. Sura za watu hawa hazikuwa sura za kawaida. Punde mmiliki wa nyumba ile akafika naye akionekana ni mwenye wasiwasi. Macho ya watu waliokuwa wakimtizama yalimfanya atetemeke. Hakuna aliyeongea chochote zaidi kutoa kitu mfano wa picha na kumuonyesha. Mama yule akaipokea na kuitizama. Bila kuongea chochote akawaongoza watu wale kuingia ndani. Hatua mbili tatu akawaonyesha kwa kidole chumba anachoishi msichana yule. Sekunde moja wanausalama walikuwa mlangoni mwa chumba kile. Kila mmoja bastola ilikuwa ikitizama ndani. Ukagongwa kidogo, lakini cha kushangaza mlango ukafunguka kuonyesha haukuwa umefungwa.

Wanausalama wakaangaliana huku kengele za tahadhari zikigonga kichwani. Mmoja akaukamata mlango na kuufungua taratibu. Wote macho yao yakatizama ndani... wakaushuhudia mwili wa mwanamke ukiwa mtupu umelala kitandani pembeni kidogo kukiwa na dimbwi kubwa la damu. Wote wakaangaliana. Simu za upepo zikatembea kona zote za nchi. Sasa kila kitu kilikuwa kigumu. Wanausalama wakaingia na kuuanza kuuchunguza. Risasi mbili za kifua upande wa kushoto zilitosha kuuchukua uhai wa mwanamke huyu. Licha kupekuwa kila sehemu, lakini wanausalama wale hawakufanikiwa kugundua ama kupata chochote. Wakatoka nje na kumuita tena mama mwenye nyumba, safari hii wakamuomba awaitie wapangaji waliokuwepo hapo usiku uliopita.



Mama yule akawaita wote, kisha akawatambulisha kwa wana usalama. Kila mmoja akanyamaza kimyq huku wengine presha ikianza kupanda.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sisi ni wanausalama tumekuja hapa kufuatilia kuhusu mauaji yaliyotokea usiku wa jana." Alijitambulisha mmoja huku akionyesha kitambulisho chake. Wapangaji wote wakatizamana. Wakatizamana huku sura zao zikishindwa kuuficha mshangao. Mshangao ambao hata wana usalama wenyewe waliligundua hilo. Haiwezekani kifo cha mtu mkubwa nchini uchungizi uje ufanyike pale. Kama kawaida ya wanawake wa magomeni walivyo na midomo mirefu, hawakuchelewa kuuliza hilo.



"Sasa kipi mmetuitia hapa? Ina maana mauaji ya waziri yamefanywa na mtu wa nyumba? Alihoji mama chausiku huku akiwaangalia wana usalama kwa zamu.



Hawakumuangalia yeye bali walitoa ishara wapangaji wa sogee. Wakafanya hivyo, mmoja ya wana usalama akaufungua mlango na kuwataka wote waangalie ndani. Kila mmoja akafanya hivyo.





Wapangaji na mwenye nyumba wote wakatupa macho yao chumbani kwa msichana yule. Hakuna aliyeshindwa kunyamaza, kila mmoja akalitaja jina la mungu kwa imani yake. Wapo waliopiga mayowe na wapo walionung'unika moyoni. Mama mwenye nyumba akabaki ameduwaa kana kwamba alikuwa haamini kile alichokiona. Dimbwi la damu pembeni ya mpangaji wake lilimfanya ahisi presha kupanda. Wanausalama wakaufunga mlango na kuwageukia wapangaji tayari kwa kuwahoji.



"Nani ambaye alikuwepo jana wakati marehemu akirudi? Lilikuwa swali la kwanza kuulizwa. Wapangaji wote wakaacha kulia, wakanyamaza na kuanza kuwaangalia. Mara mmoja wa kike akajitokeza mbele.



"Wewe ndiye ulimuona akirudi? Akaulizwa tena.



"Hapana! Bali tulikuwa wote pale travertine hotel, mpaka pale alipotokea mkaka mmoja na kumchukua." Akajibu yule msichana huku akiendelea kulia. Jibu lake hilo likawafanya wapelelezi wale waangaliane.



"Yukoje huyo mtu? Na alikuja kama nani? Swali jingine akarushiwa.



"Ni kijana mmoja hivi mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, ukimuangalia kwa woga unaweza kudhani ni mcheza sinema wa Hollywood. Na pale alikuja kama mteja na kumchukua mwenzetu." Akajibu yule dada. Jibu la kwanza likawafanya watizamane kwanza. "Ana mwili wa mazoezi, ukimtizama kwa woga unaweza kudhani ni mcheza sinema wa Hollywood. " yalikuwa maneno yaliyojirudia vichwani mwa wana usalama wale. Jina Masimba lilijengeka ndani ya akili zao.



"Baada ya hapo ikawaje baada ya kuondoka na huyo mtu? Lilikuwa swali jingine. "Baada ya hapo sikumuona tena mpaka sasa mlipokuja nyie ndio nagundua kumbe Rose ameuawa." Akajibu msichana yule na kuangua kilio. Wanausalama wakaangaliana tena. Wakiwa bado hawajaamua kuendelea na maswali, wakamuona msichana mwingine akisogea mbele na kusimama.



"Mimi nilimuona wakati anaingia, na muda mfupi baada ya kuingia alikuja mwanaume na kumuulizia. Kwa kuwa mara nyingi sana anafuatagwa sana, nikamuonyesha huyo kijana chumba chake. Baada kumuonyesha sikumuona huyo mwanaume alipotoka na muda huu ndio mmenishtua kuniambia Rose amekufa." Akaeleza mwanamke yule. "Je mtu aliyekuja mara hii anafanana na huyo aliyetajwa na mwenzako? Wakauluza wana usalama. "Hapana hawafanani kabisa, huyu hakuwa yule aliyeshuka kule hotelini. Licha ya huyu naye kuwa na mwili wa mazoezi, pia alikuwa mweupe na mwenye kovu kwenye jicho la kushoto." Akajibu mdada yule.

"Dee plus" lilikuwa jina lililopita vichwani mwao. Sasa walikuwa wamepata picha, aliyeshuka kule hotelini yalikofanyika mauaji alikuwa masimba. Aliyekuja kufanya mauaji ya changudoa aliyenunuliwa na Masimba alikuwa Dee plus. Hapa imekuaje? Kwa nini mtu aingie ndani na masimba kisha aje auawe na Dee plus? Ina maana huyu Changudoa alikuwa na Masimba wakati akitekeleza mauaji ya waziri mkuu? Kwa hiyo baada yachangudoa huyu kushuhudia kifo cha waziri mkuu kilichofanywa na Masimba, wakaona nao wampoteze ili kupoteza ushahidi? Kipi kipo nyuma ya mauaji haya? Kwa nini waziri alikuwa akimshawishi DG wa TISS wampoteze masimba? Yalikuwa maswali mazito ambayo yangepaswa kujibiwa na wahusika wenyewe. Wakati wakijiuliza hayo ikaingia simu kutoka kwa wenzao ambao walikuwa hoteli. Ni simu hiyo ambayo ilizidi kuwachanganya. Camera za usalama hazikuonyesha chochote katika hoteli hiyo. Hata waziri mkuu akiingia hazikuonyesha chochote. Kubwa zaidi ni kwamba mhudumu aliyekuwa zamu usiku hapo hotelini ameuawa kwa kupigwa Risasi mbili kifuani tena kwa staili kama aliyouawa huyu changudoa. Wakaangaliana tena na tena. Kazi ilikuwa ngumu kupindukia.



******

Kwanza alihisi kama alikuwa ndotoni akiota kitu ambacho kamwe kisingeweza kutokea. Akajaribu kujitingisha kuona kama alikuwa kweli anaota. Hapana haikuwa hivyo, haikuwa hivyo kwa kuwa bado alikuwa akikisikia kilekile alichokisikia hapo mwanzo. Ilikuwa sauti ya mtangazaji wa Televsheni akitangaza kifo cha mtu anayemfahamu kwa ukaribu zaidi. Sekunde hii alikuwa akifumbua macho yake na kushangaa akipokewa na nuru safi yenye kuangaza mfano wa Jua la asubuhi. Alikuwa hana nguo hata moja mwilini huku akiwa amefunikwa kwa shuka safi na zito. Hilo hakulitilia mashaka, bado alitaka kuliona kwa macho kile alichokuwa akikisikia. Maumivu ya kisogoni bado hakutaka kuyaulizia maswali. Alitaka kuona na kusikia, alitaka kujua kama ni kweli kile alichokisia. Kwa taratibu akageuza macho yake na kutizama kule ilipo tv. Macho yake yakapokewa na wana Usalama wakionyesja kuhaha. Polisi walikuwa wametanda kila sehemu wakipekua na kuwahoji watu wote. Maandishi yaliyopita chini ndio yaliyompa kiwewe. Ni kweli ama naota? Waziri ameuawa vipi? Ni nani amemuua huyu? Yalikuwa maswali ambayo yalimfanya akae kitako na kushika tama. Akauona muda ule ni wakujua alikuaje mpaka akafika pale. Kumbukumbu yake ikaanza kurudi taratibu, kwanza alikuwa mkuranga kummaliza mama wa asteria. Wakarudi mpaka katikati ya mji katika moja ya majengo ya siri ya usalama wa taifa. Hapo wakajaribu kumpigia masimba ili kumjua alipo kwa kutumia mitambo yao. Simu ya Masimba haikupokelewa.. lakini ndani ya nusu saa masimba akapiga tena akiwa jirani na hapo. Akakumbuka walipoondoka mpaka kinondoni akiwa sambamba na mwamvita. Punde tukio zima likajirudia. Hasa kuwekewa bunduki kisha kupigwa kwa kitako cha bastola kisogoni. Machozi taritibu ya kaanza kushuka. Alijitolea kwa kila kitu kwa sababu ya kikundi chao. Akamsaliti masimba kwa sababu yao. Alifanya kila kitu kwa sababu ya faida yao, lakini leo walikuwa wakimsaliti na kutaka kumuua. Hilo likamuuma sana. Bado macho yake hayakubanduka kwenye Tv. "Nani amemuua waziri na kuniokoa mimi? Ina maana masimba ndio amefanya hay..... Kabla hajamaliza kujiuliza maswali mlango wa chumba alichopo ukafunguliwa. Akageuka na kutizama huko. Macho yake yakakutana na macho ya masimba aliyekuwa akiingia. Teddy hakuuficha mshangao machoni mwake sambamba na hofu usoni mwake. Macho yake yakashindwa kumiangalia kwa muda mrefu. Maswali na aibu ya usaliti vikauvaa uso wake. Ni masimba huyu huyu aliyemuokoa mara ya kwanza katika mazingira ya kifo. Ni masimba huyu tena amemuokoa kwa mara ya pili tena kwa kumuua mtu ambaye yeye alimuogopa sana. Hakuwa na shaka kwamba masimba ndiye aliyemuua waziri mkuu. Lakini swali alimuuaje mtu ambaye alikuwa na VIP PROTECTION kwa kila anapotembea na kuwa mahala popote? Je baada ya kuzimia kutokana na kupigwa alipelekwa wapi? Na kwa nini walimgeuka wakati alishaamua kurudi kwao? Hapo ndipo alipoukaza uso wake na kumuangalia masimba usoni, akitegemea kukutana na mikunjo ya hasira. Haikuwa hivyo, tabasamu lilitanda usoni kwa masimba. Macho yake yalikuwa yakimuangalia Teddy katika utulivu. Teddy akashindwa kuvumilia, sekunde hii alikuwa amesimama akipiga hatua kumfuata Masimba. Alikuwa akitembea kwa kuyumba. Bado tabasamu lilitanda usoni kwa masimba. Tabasamu ambalo lilitoweka ghafla baada ya teddy kusimama mbele yake. Tukio la kulipuka nyumba ya mama wa asteria na kusababisha kifo chake na mjukuu lilijirudia. Bastola ilikuwa mkononi mdomo wake ukimtizama teddy. Hapakuwepo utani kabisa machoni kwa masimba. Teddy akashtuka kisha baridi ikauvaa mwili wake. Kidole cha masimba kikashuka mpaka kwenye trigger. Sasa alikuwa akikivuta kitufe tayari kwa kumlipua teddy. NIWAKATI HUO HUO MLIPUKO MDOGO UKASIKIKA HUMO NDANI.



Chumba kizima kilikuwa kimya, kila mmoja akiwa amejiinamia chini akiwaza na kuwazua.hakuna aliyeamini taarifa kwamba waziri amekufa. Tena amekufa kwa kupigwa risasi. Ameuawa vipi? Na nani? Teddy? Ama ni nani? Yalikuwa maswali tata, yalikuwa maswali ambayo yalikosa majibu. Wao ndio walikuwa na waziri, wao ndio waliokwenda na waziri kule magomeni. Wakamuacha na teddy pale hotelini kwa pendekezo lake. Alitaka kumuonja teddy autambue utamu wake, alipanga atakapofanikisha hilo basi atamuua Teddy kwa mikono yake. Lakini kinyume chake waziri ameuawa yeye huku akiachwa peke yake. Hakuna mlinzi aliyemshuhudia teddy au muuaji akitoka chumbani kwa waziri. Hicho kilikuwa kitendawili, kitendawili ambacho hakikupata mtenguaji. Hakuna ambaye haujui ulinzi wa viongozi wa nchi. Hakuna asiyejua wanausalama wanavyokuwa makini katika kazi yao. Lakini Usiku wa Jana walinzi hao hawakutenda kilichozoeleka. Hapo wakauona mwisho wao, mwisho wa maovu yote waliokuea wakitenda. Waliishi kifahari na kufanya kila kitu wakilindwa na mtu ambaye Leo hii alikuwa hayati. Wakiliwaza hilo punde wakauona mlango ukisukumwa kisha sura ya mwanadada akijipenyeza hapo ndani. Alikuwa mwamvita akitembea akionyesha kuchoka. Hata yeye sasa alikuwa akiona muda unakwenda ndivyo sivyo. Yalikuwa mmoja kati ya watu waliotumwa kwenda kunusa kilichopo nyumba ya kifo cha mfadhili wao. Mkononi alikuwa amekamatia kitu mfano wa karatasi. Baada ya kusogea mpaka karibu na watu wale akabwaga kitu alichokishika mkononi. Watu wale wakasogea kila mmoja akielekeza Hicho lake pale mezani. Macho yao yakajikuta yakiangalia picha mbaya. Wasichana wawili tofauti walikuwa wameuawa katika staili mbili tofauti. Wakati mmoja akionyesha kulala katikati ya dimbwi la damu, huyu wa pili alionekana amewekwa ndani ya pila, lakini kitu kilichowasisimua zaidi, ni pale kugundua kila marehemu alikuwa na matundu ya risasi upande wa kushoto wa kifua. Hilo likawafanya kwanza wawe kimya wakimtizama Mwamvita Usoni. Bado hawakuijua sababu ya kuwaletea zile picha. Lakini baada ya kuangaliana kwa mda huku macho ya mwamvita yakiongea, wakarudisha macho pale chini. Jimmy akaziangalia sura za marehemu wale kwa sekunde tano tu, akawakumbuka. Aliwakumbuka wote kwa pamoja. Mmoja alikuwa mhudumu wa hoteli yalikofanyika mauaji, na mwingine alikuwa ni changudoa, Naye alikuwa akifanyia biashara pale pale travertine magomeni. Hapo akaunganisha picha na kupata jibu kwa nini picha zilikuwa pale.



"Wamesafirishwa kama kufumbwa midomo. Hawa ndio wangetupa majibu juu ya kilichotokea. Ni wakati wa kufanyakazi bila kumtegemea mtu. Tukae tukijua kuwa hata sisi tutachunguzwa. Tutaanza kufuatiliwa na tutanuswa kila tutakapo pita. Jimmy nadhani wewe utahojiwa, nadhani utafuatiliwa kuliko sisi. Unatakiwa makini zaidi. Kama teddy yupo salama mpaka mud huu ni lazima atataka kulipiza kwa kilichotokea. Naadhani mapambano yameanza sasa." Aliongea mwamvita huku akiendelea kutizama zile picha. Wrote mle ndani wakaafiki. Ilikuwa lazima wamsake Teddy.



****

Ofisi za idara ya usalama wa taifa zilikuwa katika hekaheka kubwa. Vijana walikuwa mtaani wakinusa na kutafuta chochote. Shinikizo kutoka kwa rais ndio kitu kilichokuwa kikiivuruga akili ya mkurugenzi wa usalama wa Taifa Mr Godliving Kimaro. Muda wote alikuwa akipakipigiwa simuakiulizwa hili na lile. Hasa akiulizwa wapi amefikia katika suala hili. Kichwa chake kilikuwa kimevurugika, hakuwa akijua wapi pa kuanzia na hata kumalizia. Taarifa za kwamba mhudumu wa Zamu katika hoteli alimouawa WazirWaziri naye ameuawa katika aina ya kuufumba mdomo asiongee chochote. Changudoa aliyesemekana kwamba ameonekana akiwa na mwanaume anayetuhumiwa kufanya unyama huo naye ameuawa. Tena wote wakiuawa katika staili moja kwakupigwa risasi kifuani. "Alikuwa kijana aliyejengeka kimazoezi mwenye muonekano kama mcheza sinema. Begani alimbeba msichana aliyeonekana kupoteza fahamu" alikuwa akiirudia taarifa aliyotumiwa na vijana wake. Taarifa ambayo bado haikumfumbua na kumtoa gizani katika sakati hili. Kilikuwa ni lazima ajue na atambue nani alionekana na waziri kabla ya kifo chake. Hakuchelewa katika hilo, muda mfupi baadae simu yake ilikuwa sikioni akiipiga namba Fulani.

[4/12, 16:11] ibrahim: Simu ilikuwa sikioni akiongea na namba Fulani. Alikuwa akitoa maelekezo ya nini kifanyike katika muda ule. Wana usalama hawakuwa wametulia, kila sehemu walijaa. Mpaka inafika jioni bado hapakuwa na chochote cha maana kilichofanyika. Kila mmoja alikuwa akihisi na kuongea hiki. Ni katika hao mmoja peke take ndiye alikaribia kufahamu ukweli. Suala kwamba aliyeua alikuwa Masimba hilo hakuwa na shaka nalo, lakini angemuaminisha vipi mkurugenzi? Akaona huu ulikuwa wakati wakuliondoa suala hili katika kutuhumiwa kina jimmy na kulihamishia mikononi kwa Masimba. Alitambua kama likiachwa kisha lijekugundulika kwamba waziri alikuwa nyuma ya biashara haramu hata wao wasingepona. Akainuka na kuuendea mlango wa chumba chake. Akaufungua mlango na kutoka nje. Alihitaji kwenda kumuona mkurugenzi wa usalama. Huyu alikuwa mmoja kati ya wale waliompa kazi masimba

[4/12, 17:48] ?+255 717 808 444?: Alikuwa ni yule aliyempa masimba kazi ya kufuatilia mzigo wao. Kazi ambayo ndio iliyomfanya masimba kuingia katika matatizo haya , matatizo yakuweka rehani maisha yake kwa kunusurika kulipuliwa pale alipotegewa Bomu kwenye gari. Lakini Leo alikuwa ameamua kuukandamiza msumali wa moto katika kidonda kibichi. Gari yake ya kifahari ikatembea kwa mwendo wa taratibu katika barabara za hili jiji. Mawazo ilikuwa ni kujivua katika hili ambalo kama lingefanikiwa basi wangekuwa sehemu nyingine. Lakini kwa kuwa halikufanikiwa basi aliamua kulitenda hili taratibu na akiwa peke yake. Hakupenda kuwaambia wala kuwashilikisha wenzake. Gari ikaenda kuegeshwa kwenye maegesho ya magari katikati ya jiji la dar es salaam. Akatembea kwa miguu akielekea katikati ya jengo moja ambalo hutumiwa sana na Idara ya usalama wa Taifa. Muda wote aliokuwa akitembea hakuacha kuangalia nyuma, alikuwa akihofu kuwa alikuwa akifuatiliwa. Hata alipogeuka hakumuona yeyote, wala kuona macho yanayomtazama kwa hila. Akaufikia mlango wa jengo hilo , vijana waliokuwa pembeni wakamuangalia sekunde kadhaa kisha wakaonyesha kumuacha aendelee na safari yake. Hawakumuacha tu kwa kumuacha Bali ilikuwa amri kutoka ndani. Akaufungua mlango kisha kuuruhusu mwili wake uingie.. Miguu ikitembea kuelekea ndani kabisa. Macho machache yalimtizama na mengine mengi kumpuuza. Aliamua kufanya hivyo, aliamua kuusema ukweli ili ijulikane nani amehusika kuisafirisha roho ya Waziri.



*****



Mdomo wa bastola ulikuwa ukimtizame Teddy. Sura ya mtu asiye na masihara ilikuwa mbele yake. Alimjua masimba kwa mda mrefu, lakini hakuwahi kumuona akiwa katika hali hii. Hasira, chuki, na neno kifo ndio kitu pekee kilichosomeka kwenye USO wa mtu huyu. Macho yake yakashuhudia vidole vikishuka taratibu katika kitufe cha kufyatulia risasi. Teddy akatamani kuongea kitu. Mdomo haukufumbuka na wala maneno hayakutoka. Akabaki kumuangalia masimba katika sina ya upole na kutia huruma. Alikuwa ni mwenye majuto. Hakuweza kuvuta hata sekunde alishuhudia Risasi Ikipita pembeni kidogo ya kichwa chake na kwenda kuchimba ukutani. Teddy Hakuamini Macho yake, Akaporomoka chinu akiuomba msamaha, lakini Masimba hakuwepo pale. Alishaondoka mbele yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

alihitaji kuongea chochote na masimba, alihitaji kuuomba msamaha katika matendo yote aliyoyatenda. lakini masimba hakuwepo, hakumuona mbele ya macho yake. kwa mara nyingine akajaribu kuirudisha kumbukumbu, kumbukumbu ambayo hakuwa nayo. amefikaje mikononi kwa masimba? wakati alikuwa sambamba na mwamvita na wanausalama wengine? nini kilinitokea? hapo akauruhusu mkono wake kushika nyuma ya kisogo. jeraha dogo ndio kitu kilichoirudisha kumbukumbu. naam alikumbuka kile kilichofanywa juu yake pale waliposimama pale kinondoni. hapo tukio zima likajirudia. akasimama na kuyaendea mavazi yake ambayo yalikuwa pembeni kidogo mwa kitanda. akayavaa. akafunua mtoto wa kitanda, macho yake yakatua kwenye bastola yake sambamba na vitu vyake vingine. akavichukua na kuvisunda mifukoni. dakika zilizofuata alikuwa akishuka ngazi akiicha nyumba ile huku kichwa kikiwa kizito. hakujua kile kilichosababisha wenzake wamgeuke. aliua na kumsaliti masimba lakini bado hakuonekana kufanya lolote kwa wenzake. kwa wakati huu hakuwa muoga tena. aliamua kupambana nakundi lake. kama mzigo wa madawa alikuwa na uhakika kuwa anao masimba, sasa kipi ambacho kina mfanya asisaidiane na masimba? .alimaliza kushuka ngazi na kuufikia mlango wa kutokea nje, akaufungua taratibu na kutupia macho yake kwa nje, alishangaa kukutana na vichaka, vichaka ambavyo viliizunguka nyumba nzima. katikati kulikuwa na kijinjia chembamba ambacho kilitumika kama njia kwa watu wanaoishi hapo. Hilo likamshangaza kwanza. hakuwa anapajua pale, hakuwa anaijua sehemu ile. akajipa moyo na kutoka katika nyumba ile akikifuata kile kinjia chembamba. alitembea katikati huku macho yake yakizunguka huku na huko, mazingira hayakuwa rafiki sana ki usalama kwake. sehemu ile haikuonyesha kuwa makazi ya watu na hapakuwa dalili ya uwepo wa watu. alitembea kwa muda wa dakika kumi bila kukutana na mtu. hilo likaendelea kumtisha na kumtia hofu. lakini ni ndani ya muda ule akausikia ngurumo wa pikipiki.

[4/14, 14:01] ibrahim: Ni katika muda ule ule akausikia mngurumo wa pikipiki katika maeneo ya jirani na pale alipokuwa akiendelea kutembea. Mngurumo ule ukaendelea kusogea, sasa alikuwa akiusikia ukisogea karibu kabisa na yeye. Muda mfupi teddy alikuwa amehama pale njiani na kujitupa pembezoni mwa barabara. Sasa alikuwa nyuma ya kichaka akitizama kule barabarani. Haikupita hata dakika akaiona pikipiki aina ya Honda ikitokea. Juu yake alikaa MTU ambaye alimfahamu. Juu yake alikaa mwana usalama dee plus. Alikuwa akiiendesha pikipiki kanakwanba hapa kuwa na hatari kwake. Teddy akamuangalia sana dee plus mpaka alipopotea machoni. Masimba, kisha dee plus! Kuna nini hapa? Ina maaana Dee yupo na Masimba katika suala hili? Yalikuwa maswali ambayo hayakuwa na majibu.

*****

Walichoka vichwa vyao, hawakuwa wameupata usingizi tokea walipopata taarifa ya kifo cha waziri mkuu. Walikuwa wakikesha wakinusa hiki na kile. Mkanganyiko uliojitokeza katika kifo cha waziri mkuu. Kitendo cha watu ambao wangeweza kuwapa mwanga katika mkasa huu kuuawa kulizidi kuwapa ugumu katika kumjua muuaji kwa kuwa mpaka sasa walikuwa wakimhisi Masimba kutokana na wajihi wa muuaji waliopewa na dereva tax. Simu zilikuwa zikimiminika kutoka kwa wana usalama mbalimbali

[4/14, 18:39] ibrahim: Wana usalama walikua wakiripoti kutoka kila sehemu. Licha ya hivyo hakuna ripoti yoyote ambayo iliwasaidia kumpata muuaji ama kusaidia japo kupatikana kwa mwanga katika hili. Walihangaika zaidi ya kuhangaika. Walipekuwa kila sehemu lakini bado hawakupata chochote cha kuwasaidia. Sasa kila mmoja alikuwa amechoka na kuchoka, kila mmoja alitamani kusema ameshindwa, kila mmoja alitamani japo kupata dakika tatu za usingizi. Lakini haikuwa hivyo. Simu za chief zilikuwa zikiwasumbua sana. Kila wakati alihitaji kujua walipoishia katika hili. Ni wakati kila mmoja ameinama chini akifikiria hilo, simu ya mmoja kati yao ikaupata uhai. Simu ilikuwa ikiita. Mwana usalama yule akaichukua simu kisha kuitizama. Aliikuta namba mpya, aliikuta namba ambayo haikuwa imehifadhiwa. Kabla hajaipokea akatoa ishara ya kuiunganisha simu ile. Baada ya hapo akaipokea.. " Magomeni Makuti nyumba namba 089 kuna MTU atawafaa katika tukio hili." Baada ya kauli hiyo simu ikakatwa na simu kuzimwa kabisa. Wote wakatizamana... Hawakutaka kuchelewa, simu zikapigwa sehemu mbalimbali, wapelelezi waliokaribu na sehemu lilipotokea tukio wakaanza kusogea sehemu walioambiwa. Hata wale waliokuwa katika ofisi za muda nao walitoka wakielekea huko. Kila mmoja alikuwa akiifikiria ile simu. Simu iliyopigwa na MTU asiefahamika. Dakika kumi na tano baadae walikuwa karibu kabisa na nyumba husika. Macho yao yakiwanusa askari kanzu kibao waliosimama kama wahuni ama watu wenye mambo yao. Makachero wale wakashuka kisha wawili wakaongoza kuelekea kwenye ile nyumba. Wakati wanaukaribia mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba ile, wakawaona wasichana wawili wamesimama wakionyesha kuongea kitu. Maafisa wale wakasogea mpaka karibu yao. Kabla hawajatoa salamu, wakamsikia msichana mmoja kati ya wale waliosimama akimuaga mwenzake. Hawakujishuhulisha naye, macho yao yote yalikuwa katika mazingira yanayoizunguka nyumba ile. Kila sehemu ilijaa watu wao.. Wakamfikia mwana Dada yule kisha kumsabahi. Baada ya salamu wakamueleza kile ambacho walikifuata pale. Kubwa likiwa ni kuwa wanamgeni wao katika nyumba ile.

Binti akakitigisha kichwa chake huku akiwatizama vijana waliosimama mbele yake. " Nyie ndio wageni wa Khadija? hatimaye akauliza binti .

"Ndiyo, sisi ndiye haswa wageni." Baada ya kuangaliana kwa nukta hatimaye wakajibu. Binti hakuongea tena, aliwakaribisha na kuwaongoza kuelekea chumba cha huyo Khadija. Wana usalama walikuwa makini kwa kila hatua. Mazingira ya jumba lile , yalikuwa yakitia mashaka. Kufika mbele kidogo binti akaonyesha kidole akiwaonyesha makachero wale chumba cha huyo Khadija. Wana usalama wakamtaka wangozane ili awe mgongaji. Binti hakubisha, hatua tano mbele wote walikuwa wamesimama mlangoni mwa chumba cha Khadija. Binti waliyemkuta akaanza kuugonga mlango, licha ya kuugonga kwa muda mrefu, lakini hapakuwa na uitikiaji kutoka ndani. Kengele za hatari zikagonga vichwani mwa makachero wale. Mikono ikashuka na kuingia mifukoni mwao, wakampa ishara binti. Ishara ya kujaribu kuufungua mlango.. Binti akashika kitasa na kukinyonga. Mlango ukafunguka, wakati huo huo macho ya wana usalama yakatua ndani "Damu" ni neno lililogonga vichwa vyao.. Hatua iliyofuata wote walikuwa wamesimama mbele ya maiti ya mwanamke, Kisu kikubwa kikionekana kuzama tumboni.. WAKATIZAMANA





Kisu kilizamishwa katikati ya tumbo la mwanadada yule. Wana usalama wakatizamana na kutizamana. Mtu wa tatu mwenyekufahamu juu ya kilichotokea alikuwa ameuawa kinyama. Nani amelifanya na hili? Nani amemjua huyu mwanamke? Walikuwa kwenye bumbuwazi la takribani sekunde kumi. Kila mmoja alikuwa amesafiri kimawazo, kila mmoja alikuwa akiwaza kile walich0kutana nach0. Maiti ya msichana huyu ilikuwa imetulia kitandani. Binti aliyewasindikiza hapo naye alikuwa katika fadhaha. Hakuwa akiamini kile alichokuwa akikitizama mbele ya macho yake. Ni dakika tano zimepita tokea alipokuja yule mwanamke, mwanamke mwenye shangwe na bashasha, mwanamke aliyemchangamkia kana kwamba wanafahamiana. Ni mwanamke huyu aliyemuulizia marehemu, ni mwanamke huyu aliyeingia chunbani kwa marehemu na kutoka. Kutoka katika muda ule ule, hakukawia tokea kuingia na hata kutoka. "Ni yeye, ni yeye aliyemuua!! Hii ilikuwa sauti iliyotamkwa na kupenya katika ngoma za masikio ya makachero waliokuwa wamepigwa butwaa. Macho yakamuangalia dada huyu kisha swali likafuatia. Swali ambalo liliulizwa na makachero wote. "Nani?...

"Mwanamke!!. Akajibu huku akiendelea kufuta machozi. "Mwanamke gani? Wakauliza tena wanausalama. "Mliyenikuta naye hapo nje. Ni yeye aliyemuulizia marehemu na ni yeye aliyetoka humu chumbani. Harafu pia hata marehemu aliyoonyesha kutokumfahamu huyu mwanamke." Alijibu mwanamke yule.



Wanausalama wakamuangalia wakimkazia macho. Bado walikuwa katika kiza kizito. Sekunde mbili baadae simu zikasambaa kila kona. Mwanamke mwembamba mrefu afuatiliwe na kukamatwa. Kwa kuwa nyumba ile ilikuwa imezungukwa na wana usalama, haikuwa vigumu kumkunbuka mwanamama huyu. Kwani wakati akitoka kwenye ile nyumba walimuona. Licha ya kumuona lakini walikuwa wameshachelewa, kwani wakati taarifa inakuja tayari mwanamke yule alikuwa amekwisha tokomea. Licha ya wana usalama kuhangaika na kuwasiliana kwa muda ule, hapakupatikana taarifa yoyote ya kuwasaidia. Wote wakarudisha macho yao tena kwa binti yule. Walihitaji kupata mawili matatu kutoka kwa mwanadada yule juu ya mwanamke aliyemhisi kufanya mauaji hayo.



"Sisi ni maafisa wa polisi, tuko hapa kumfuatilia marehemu baada ya kuambiwa ana habari fulani." Vitambulisho vyao vilikuwa mbele kumuaminisha mwanamke yule. Baada ya kuviangalia kwa muda, mwanamke yule akawarudishia huku akionekana akitetemeka kwa mbali. "Tunahitaji kujua kuhusu marehemu. Alikuwa nani? Alifanya kazi wapi? Na kipi kingine unafahamu ambacho kinaweza kuwa ndio chanzo cha kifo chake. Yalikuwa maswali ambayo yalimfanya mwanadada yule kuangalia juu kama ni mwenye kufikiria kitu, kisha kwa sauti ya kukata tamaa akanena.



"Binti alikuwa ni changudoa, hiyo ndio kazi ambayo ilimuweka hapa mjini. Akajibu binti huku macho yake yakiusgangaa mshangao kutoka kwenye sura za makachero hawa.



"Enhe ukiacha uchangudoa kipi kingine ambacho alikifanya? Lilikuwa swali la pili.



"Hakuwa na kazi nyingine zaidi ya hiyo." Akajibu.



"Biashara hiyo alikuwa akiifanyia wapi?



"Travertine hapo usalama." Akajibu. Kwa mara nyingine wana usalama wakatizamana. Wakaki wakitizamana makachero wale, yule mwanamke akaongeza. "Kingine ambacho nahisi kimesababisha huyu binti kuuawa ni kushuhudia watu wa mwisho kuingia na waziri pale hotelini sambamba na rafiki yake kushudia mauaji ya Waziri mkuu. Wote walikubaliana leo hii wakaongee na vyombo vya usalama. "Wana usalama wakaangaliana tena. Watu wawili waliomuhimu na msaada mkubwa walikuwa wamesafirishwa kuzimu. Wamesafirishwa ili kuzibwa midomo. Hawakutakiwa kufumbua mdomo kuliongea hili popote na hilo lilikuwa limefanikiwa.



******



Alihitaji kujiondoa katika hili ambalo limetokea. Kucharuka kwa wana usalama kulizua hofu na mashaka miongoni mwao. Waliiona njia ya kujitoa katika hili ni kumchoma masimba kwenye vyombo vya usalama. Walitaka kushindilia msumari wakiamini Masimba bado alikuwa akitafutwa na vyombo vya usalama. Walilijua hilo kwa kuwa hata wao walikuwa washirika wa waziri mkuu. Hata wao walikuwa wakilijua shinikizo ambalo alikuwa akipewa mkurugenzi wa Idara ya ujasusi kuhusu kutafutwa kwa masimba. Wakata kulitumia hilo kump0teza masimba. Hawakujali kuwa wao ndi0 walikuwa chanzo, chanzo cha kile kinachoendelea. Leo hii walikuwa wamepanga kwenda kuonana na mkurugenzi wa idara ya ujasusi nyumbani kwake. Wali0na hii ni kama njia bora na sahihi kwao katika kujisafisha na hilo. Muda wao wa kukutana ilipangwa kufanyika usiku wa siku hiyo, ilikuwa ni lazima wamuone kwa njia yoyote.



Ilikuwa usiku wa saa tano, ukimya ulikuwa umetawala katika viunga vy0te vya oysterbey. Hapaku0nekana mtu y0y0te zaidi ya gari moja moja ambazo zilikuwa zikipita kuelekea sehemu mbalimbali huku nyingi zikiwa ni za wakazi wa eneo hilo. Pembeni kidogo mwa barabara ile alisimama mtu mmoja macho yake yakitizama nyumba fulani ambayo ilikuwa mbele yake. Mtu huyu alikuwa hapo baada ya kupenyezewa taarifa kuwa wapo watu ambao walipanga kwenda kulitangazia taifa kwamba yeye alikuwa ndiye muuaji aliyeitoa Roho ya waziri. Ilikuwa taarifa alioipuuza baada ya kuipata, lakini baada ya kuchunguza kwa makini majibu alioyapata yalikuwa ni yale yale. "Unataka upewe hii kesi. Unachotakiwa ni kuwawahi watu hao" ulisomeka ujumbe ambao alitumiwa na wake usiku wa siku ile. Hapo ndipo alipoamua kutos tiketi kwa watu hawa, watu ambao wao ndi0 chanzo cha haya yanayoendelea kufanyika.



Macho yake bad0 yalitizama nyumbani pale, hapakuonekana uwepo wa watu, hapaku0nyesha kama kuna mtu ndani yake. Wakati akiliwaza hilo akaziona taa za magari zikimulika mbele ya nyumba ile. Punde akaisikia honi ya gari. Moyoni akafurahi kwa kuamini mwenyeji wake alikuwa amerejea na ulikuwa muda wa kuipeleka tiketi yake. Akauvuta muda akisubiri geti lifunguliwe mtu wake aingie ndani. Muda wote mkono wake ulikuwa juu ya bast0la yake. Hazikupita dakika mbili gari ilikuwa imeshaegeshwa ndani. Mwanaume akaondoka pale pembezoni mwa barabara na kuanza kusogea taratibu kuelekea ndani ya nyumba ile. Giza la usiku lilimfanya ahisi ni mwanga katika macho yake. Alilipenda giza kama alivyokuwa akiipenda bastola yake, haikuwa bastola tu bali hata mwandani wake. Mwandani ambaye alimfanya ajihisi yu peponi kamasio paradise. Akaifikia nyumba ile kwa karibu san. Ilikuwa nyumba iliyozungushiwa ukuta mrefu sana mithili ya jumba la ikulu. Juu ya ukuta ule kulipitishwa nysta za umeme na kuufanya uzio ku0nekana ni hatari. Akaangalia kwa dakika kama mbili, baada ya hapo akaamua kuingilia kwenye lango la mbele kule ambapo alikuwepo mlinzi. Akatembea kama mpita njia mpaka alipotokea lango la mbele. Macho yake yapaka yalikuwa yakiangalia huku na huko.. muda kidogo akamuona mlinzi akizunguka zunguka.. Hapo akaamua naye kujitokeza na kuanza kutembea akielekea pale.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Muda mfupi baadae alikuwa akitizamana na mlinzi wa jumba lile. Masimba akas0gea kama mpita njia mwenye kutaka kuuliza kitu. Mlinzi naye hakushtuka katika hilo, akasogea kumsikiliza zaidi mtu huyu ambaye alimjia kama mhitaji. Hatua ya kwanza na yapili zilikwenda bila kutokea chochote, hatua mbili kabla hajamfikia mtu yule kikatokea kitu cha kustaajabisha kwake na hata kwa masimba, taa zote za jumba lile zilikuwa zimezimwa katika namna ya kushangaza. Hilo likamvuta masimba, likamvuta likimtoa pale alipokuwa na kumsogeza upande tofauti. Ni muda huo huo alipoisikia sauti ya mlinzi yule ikilalama katika aina ya maumivu. Lilikuwa lalamiko ambalo halikudumu hata kwa theruthi ya sekunde. Ukimya ukarudi tena katika utawala wake. Ukimya wa kutisha na kuogopesha. Masimba bado akaivuta dakika nyingine ya pili ili kuangalia kile kinachotokea. Kelele ya mlinzi ilimaanisha kuwa alipigwa shaba. Hilo halikubishwa katika kichwa na akili ya masimba. Hakujua huyu alikuwa nani katika wakati huu, wakati ambao alijipanga mwenyewe na hakuwa amemwambia mtu yoyote kuja kwake hapa. Haukuwa muda sahihi wa kujiuliza maswali, ulikuwa muda wa kukijua kile kilichotokea. Hilo likamfanya masimba airuhusu miguu yake kutembea, mkononi aliikamatia bastola yake, sasa akaamua kwenda ueleke0 tofauti, aliamua kurudi kule alipotoka. Akaufikia ukuta wa jumba lile, akautizama kwa makini safari hii akitaka kufanya kitu. Hakujua kile kilichotokea ndani na hata kile kilichompata mlinzi. Muda huu alikuwa juu ya mti mmoja kati ya mingi iliozungushiwa kwenye jumba lile. Aliupanda na alipofika usawa wa uzio ule akajitoa pale juu ya mti na kutua chini bila kutoa kishindo. Baada ya kutua, akachepuka na kubana pembeni. Bado ukimya wa kuogofya ulichukua sehemu kubwa. Akajitoa pale alipokuwa amebana na kusogea kuelekea mlango wa nyuma. Kila hatua yake moja ilikuwa ikienda sambamba na macho yake. Akaufikia mlango na kutulia hapo. Bado hakusikia chochote kutoka ndani. Hamu ya kujua kilichotokea ikaongezeka, hamu haikumithilika. Hilo likamfanya akinyonge kitasa ku0na kama mlango ungefunguka. Ni kweli mlango ulikuwa wazi, ni kweli mlango haukuleta kizuizi "ameingilia hapa" lilikuwa neno lililogonga kichwani kwake. Akausukuma mlango taratibu na kuruhusu macho yake kutangulia kutizama ndani. Lakini hakufanikiwa kukiona kitu kutokana na giza. Akaufungua zaidi kisha kuingia kabisa. Hatua tatu mbele alihisi kukanyaga kitu mfano wa maji. Hilo likamfanya kutaka kuinama kuangalia. Pua zake zikainasa harufu ya damu. Damu mbichi iliokuwa ikichuruzika kutoka mahala fulani katika mwili wa binadamu. Damu ikamsisimka. Akahisi kuwahiwa na mtu katika hili. Lakini alikuwa nani? Lilikuwa swali ambalo halikupata majibu. Na hakutaka kupata jibu kwa wakati ule. Akahama pale na kuendelea kusogea mbele, hakupiga hata hatua tatu akajikuta akijikwaa kwenye kitu mfano wa mwili wa binadamu. Akaongeza umakini na kuugusa mwili ule. Akajikuta akionyesha mshangao baada ya kugundua mwili uliolala chini ulikuwa mwili wa mtoto mdogo ukiwa hauna uhai. Alitegemea kuona mengi lakini hilo hakulitegemea. Mtoto kuuawa kwa risasi!!!ni nani huyu? Lilikuwa swali lisilo na majibu. Ina maana mzigo uliyopotea ndio chanzo cha hays yansyotokea? Bado alikuumiza kichwa chake kwa maswali.



Wakati anapewa kazi ya kufuatilia mzigo uliopotea hakujua kama kazi ingemfikisha huku. Hakujua kama yangetokea haya. Hamu yake ya kuwajua wauaji wa Asteria ndiyo sababu ya leo hii Masimba kutafutwa. Akaucha pale chini mwili wa yule mtoto asie na hatia. Akasogea zaidi na zaidi, kutokea tu sebuleni akashtuka baada ya taa zote kuwashwa. Hazikuwashwa patupu bali zikafuatiwa na mngurumo wa gari kutoka nje. "Wamekimbia" alinong'ona masimba huku sasa akishuhudia kile kilichotendeka. Watu watano walikuwa chini wamelaliana juu ya dimbwi la damu huku risasi zikionekana kuiharibu miili yao. Hilo likamshangaza Masimba, sio kushangazwa na nauaji yale bali watu waliouawa. Kwa mara ya kwanza akauhusudu uwezo wa mtu huyu, uwezo wa muuaji huyu. Watatu kati ya watu watano waliouwa pale walikuwa ni watu wake, watu ambao alitaka kuwapa tiketi zao. Lakini alishangaa kuwakuta wote wakiwa wamesafirishwa tayari tena na mtu ambaye hakuwa akimjua. Hili likampa shaka na hata wasiwasi kwamba inawezekana kuna watu au mtu anatembea naye katika hili.



********



Vifo vya wasichana watatu ambao ndio pekee waliokuwa wakiwajua wauaji kiliitikisa sana idara ya ujasusi. Sasa wapelelezi walikuwa wakikesha katika vyumba vya watu hudika wakizani kwamba wanaweza kupata chochote cha kuwasaidia. Licha ya kujaribu kupekuwa katika makazi yote ya marehemu hawakufanikiwa kupata chochote cha kuwasaidia. Mtu pekee aliyekuwa amebaki katika hilo alikuwa ni yule dereva tax. Huyu alikuwa amefichwa katika jengo moja linalomilikiwa na wana usalama. Leo waliamua kurudi tena baada ya mambo kuendelea kuwa magumu. Licha ya kuhojiana naye sana lakini waliamini kwamba wanaweza kupata chochote kwa mara nyingine. Hawakutaka kupuuza hilo. Muda mfupi baadae walikuwa ndani ya chumba wakihojiana na mtu huyu. Wana usalama wakaendelea hili na lile. Wakimtaka akumbuke zaidi kile ambacho alikiona kabla ya kukodiwa na watu hao ambao bado walikuwa wakisakwa na wana usalama mpaka muda ule

. Dereva wa tax akakaa kimya kwa muda akiwaza hili na kuwazua. Kwa mara ya kwanza alianza kukijutia kitendo cha kutoa siri ambayo akuwa nayo. Usumbufu wa maswali na hata vitisho ilikuwa kawaida kwa wanausalama wengi duniani hasa pale wanapohitaji kitu. Vitisho ilikuwa sehemu moja na mbinu ya mwisho kuitumia pale wanapokutana na ugumu katika mbinu zao nyingine. Dereva bado alikuwa kimya akijaribu kukumbuka kilichotokea kabla ya kuwapata watu wale watatu usiku ule. Haikupita dakika hata tatu tayari alikuwa ameshakumbuka kitu. Gari ya kifahari ikiingia, kisha walinzi watano wakashuka kabla ya mtu fulani kushuka. Mtu yule hakuwa ameshuka peke yake bali alikuwa sambamba na watu wengine watatu. Wawili walikuwa watu weusi na mmoja alikuwa raia mwenye asili ya Asia. Yeah walikuwa watu hao. Baada ya kukumbuka hilo akainua macho na kuwatizama tena wana usalama, kisha kwa sauti ya chini akasema. "Yeah nimekumbuka. Wakati mheshimiwa akishuka, alishuka sambsmba na watu wengine watatu. Wawili walikuwa weusi na mmoja alikuwa na Asili ya Kiasia. Hao walikuwa tofauti na walinzi ambao walishuka kabla." Wana usalama wakaangaliana kisha mmoja akanena..



"SURESH SIGH na JIMMY LAMBERT LAZIMA WATAFUTWE KUANZIA SASA. HAWA NI WATU AMBAO WATA...... kabla hajamaliza kauli yake, simu yake ya mkononi ikaiiita.. Kutupa macho juu ya kioo cha simu akakutana na Jina Chief. Hakupokea kwa muda ule.





******

CHIEF ndio jina lililosomeka juu ya kioo cha simu yake. Hakuipokea kwa wakati ule. Macho yake yaliwatizama wenzake kisha kuitizama tena simu. Sio kwamba alikuwa akiogopa kuipokea simu bali hakuwa na la kumwambia mkuu wake. Akaiacha simu iendelee kuita mpaka ilipokata. Baada ya simu kukatika, kachero yule akauandika ujumbe kwa lugha ya mafumbo na kuutuma kwa Chief. Baada ya kumaliza hilo akamgeukia dereva wa tax. "Utaendelea kuishi hapa kwa Usalama wako mpaka pale hili jambo litakapokwisha." Baada ya kusema hilo makachero wale wakatoka mle ndani tayari kwa safari ya kwenda kuwatafuta Jimmy na Suresh.



*****



Ilikuwa yapata majira ya saa tatu na nusu usiku pale teddy aliposhuka kwenye bajaj pembezoni mwa ufukwe maarufu jijini dar es salaam, ufukwe wa coco beach. Baada ya kushuka hapo akaongoza taratibu mpaka sehemu mmoja iliyojitenga pekee akakaa na kutulia. Hakuwa hapo kwa sababu ya burudani bali alikuwa pale kwa minajili ya kuipa akili yake utulivu. Mambo yaliokuwa yakiendelea yalizidi kumchanganya na kuifanya akili yake ishindwe kufanya maamuzi. Ni mara tatu amenusurika kufa kwa kupigwa risasi, mara ya nne amenusurika kufa baada ya kugeukwa na wenzake kisha kumpoteza fahamu. Mpaka muda ule hakuwa akijua ni vipi ameokolewa katika kisanga kile. Hakujua ni vipi masimba amemtoa katika kifo ambacho kilipangwa kufanywa juu yake. Ni masimba huyu huyu alijitolea kila kitu na uwezo wake kuhakikisha yeye anarudi kwenye uhai. Hakumuacha pale alipowekwa matatani. Hata pale aliposhiriki kuua familia ya Asteria, bado masimba alimpa nafasi ya kubadilika. Licha ya hayo yote bado moyo wake ulikuwa katika mtihani mzito. Aliihitaji pesa na aliuhitaji mzigo wa madawa ya kulevya alionao Masimba. Aliutaka kwa njia yoyote. Hakuhitaji mzigo ule uingie mikononi mwa serikali. Aliutaka na aliuhitaji. Licha ya kuuhitaji huko, lakini hakujua angeweza kuutoaje mikononi mwa mwanaume yule. Hilo ndio lililomfanya afike usiku ule katika fukwe zile za coco beach kujaribu kuwaza hili na lile ili kupata majibu. Kichwa chake alikiinamisha chini huku mikono yake ikiuchezea mchanga. Mawazo yalikuwa yakipishana kichwani. Kuna kipindi katika akili yake alikuwa anawaza na kujilaumu kwa nini akutane na Masimba. Pesa zikaiteka akili yake, pesa zilimfanya aisahau nafasi ya masimba moyoni mwake. Aliihitaji pesa na aliuhitaji mzigo kwa gharama yoyote. Kwa mara ya kwanza akalikumbuka jina la mtu, mtu ambaye angeweza kupanga naye na kupata majibu. Lakini hakujua angewezaje kumpata huyu mtu. Kwani ulipita muda mrefu sana pasipokuonana. Akaichomoa simu yake mfukoni na kubonyeza namba fulani. Baadae simu upande wa pili ikasikika ikiita. Sekunde tatu baadae sauti nzito ikasikika upande wa pili. " Beni Bomphe naonge."



"Teddy killer hapa naongea, nakuhitaji kwenye fukwe za coco beach muda huu kama upo hapa Mjini." Akaingea teddy kisha kukata simu bila kusubiri jibu kutoka upande wa pili. Uso wake ulikuwa kwenye tabasamu matata sana, sasa uhakika wa kuupata mzigo alikuwa nao. Akaendelea kuwaza na kuwazua, baada ya dakika kumi na tano akamuona mtu akitembea taratibu katika fukwe zile. Kijana mweupe mwenye mwili uliojengeka kimazoezi alikuwa akiangaza huku na huko kama mwenye kutafuta mtu. Teddy akainuka na kumsogelea kijana yule. Muda mfupi baadae walikuwa wamesimama wakitizamana. "Habari za masiku Beni?" Akasabahi teddy.



"Nzuri mkuu, naona nchi imetingishwa." Akajibu beni huku akiongeza na maneno kadhaa. "Yeah! Ukiwa mshenzi lazima upate malipo ya kishenzi. Akajibu teddy huku uso wake ukionyesha kujua kila kitu.



"Usiniambie unamjua alietenda hili? Akaongeza ben huku akishindwa kuuficha mshangao.



"Yeah! Namjua! Alijibu kwa kifupi kisha akamuomba Ben waongee kile ambacho amemuitia.



Kwa shingo upande ben akakubali na kufuatana na teddy mpaka sehemu waliokuwa wamekaa mwanzo. "Nipe dili mama nitoweke hapa, watu kama sisi hatuonekani ovyo." Ben akatamka akimuangalia teddy. Teddy akamueleza ben kila kitu huku akificha vichache sana. Ni maelezo ambayo yalichukua dakika kama sita hivi. Baada ya maelezo yote kutoka kwa teddy, beni akatulia huku akimuangalia Ted usoni. Baadhi ya maneno kutoka kwa teddy hayakumuingia akilini. Aliujua uhusiano wao na masimba tokea ndio kwanza wanajiunga na idara ya ujasusi. Lakini haya ambayo yanatoka kinywani kwa teddy yalimuacha na kigugumizi. "Lazima tumuondoe masimba? Hata ikibidi hata familia yake tuitumie katika kuupata huu mzigo? Ni baadhi ya kauli ambazo zilimuacha Ben akiwaza.



"Kwahiyo unataka masimba asafirishwe? Hatimaye akauliza tena.



"Yeah nahitaji kuupata mzigo, kwahiyo ni lazima tumsafirishe. Pakitokea ugumu familia yake itahusika katika kutupa huu mzigo. Sina huruma wala mapenzi katika hili." Akajibu teddy huku kila kitu kikionyesha kuwa hakuwa akitania. Hilo pia halikutegemewa na ben. Lakini kwa kuwa aliitaka pesa Aliamua kukubaliana na teddy kuifanya kazi ile ambayo ilikuwa hatari. Alimjua masimba na aliujua ugumu wake. Kitendo tu cha kusikia kile alichokifanya kwa waziri mkuu ilimthibitishia ni kiasi gani ameingia kwenye vita nzito. Akamuangalia teddy kwa sekunde kadhaa kisha kwa sauti ya kujiamini akasema. "Nitaifanya hii kazi kwa moyo wangu wote. Ikiwa nitamuua masimba ama familia yake, basi damu yao itakuwa juu yako. Ikiwa ataniwahi mimi basi nadhani damu yangu pia itakuwa juu yako." Baada ya kuongea hilo akainuka na kuanza kuondoka huku hofu ikiwa imeutanda moyo wake. Hakupenda kupambana na mtu kama masimba, sio kwa kuogopa lakini alikuwa akimheshimu kama mtu aliyemfanikishia naye kufika pale.



*******



Alikuwa mfano wa simba aliyejeruhiwa, hakutaka kuwapa nafasi maafisa usalama kumtambua kama yeye ndiye aliyehusika na mauaji ya Waziri mkuu. Hilo likimlazimu masimba kutokulala kabisa kabisa akiwasaka Suresh, Jimmy na Mwamvita. Walikuwa watu pekee waliokuwa wakilifahamu hili. Alitaka kumalizana nao kwanza kabla ya kuangalia nini anatakiwa kukifanya. Usiku huu alikuwa maeneo ya sinza afrika sana akitizama kama anaweza kuwaona wabaya wake. Alikuwa ametulia akiendelea kunywa taratibu bia yake. Macho yake yalikuwa yakimtizama kila mmoja ambaye alikuwa akiingia ndani ya bar ile. Muda mwingi alitumia kuitazama saa yake. Muda ulikuwa ukisonga bila kumuona mtu wala kupata chochote kutoka kwa Dee plus. Kazi aliyompa ya kumfuatilia teddy bado haikuzaa matunda. Bado hakumuamini tena teddy. Aliutambua utamani wa teddy na hata mabadiliko yake. Licha ya kumtoa mkononi mwa kifo bado alijua ama kuhisi teddy anaweza kubadilika tena. Hilo likamfanya Masimba mpe dee plus kazi hiyo, kazi ya kuijua mienendo ya teddy. Hilo likampa ugumu wa kuamini kama hakuna chochote. Akauvuta muda akisubiri chochote. Punde mlio wa sms kwenye simu yake ukamgutusha kutoka mawazoni. Mkono ukazama mfukoni na kuibuka na simu. Sekunde moja iliitosha kuufungua ujumbe ule na kuusoma. "Wadudu wawili wamekaa ufukweni wakidonoa chini." Ulisomeka ujumbe. Ilikuwa lugha aliyoielewa, lugha ambayo ilimpa hamu ya kuwajua hao wadudu wawili na kile wanacho kidonoa.



"Ustawi" alijibu kwa neno hilo huku akiirudisha simu mfukoni. Lakini hazikupita hata dakika moja simu yake ikaita. Akaitoa tena mfukoni na kuangalia namba ya mpigaji. "CHIEF" ndio jina lililosomeka. Roho ikapaaa na damu kumsisika. Akapeleka kidole kwenye kitufe cha kijani kisha kuipeleka simu sikioni.



"Nakuhitaji nyumbani muda huu." Baada neno hilo simu ikakatwa. Masimba akaduwaa.hakuamini kupigiwa simu na mkuu wake wa kazi hasa ukiangalia jinsi alivyokuwa akisakwa. Niende? Lilikuwa swali pekee alilojiuliza. Lakini kabla hajapata jibu la swali lake akamuona Dee plus akiingia. Akampa ishara ya kumtaka asogee.. Dee Plus akasogea kisha bila kuongea kitu mfano wa picha na kumkabidhi Masimba



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Akapewa kitu mfano wa picha, akaikunjua kutoka kwenye kitu kama gazeti na kuitupia macho. Akakutana na picha ya Mpenzi wake akiwa sambamba na mtu ambaye alimfahamu sana. Mtu ambaye alimkuza katika fani hadi kufikia hapo. Aliitizama picha kwa muda kisha akairudisha mikononi kwa Dee plus. "Hakikisha hawakupotei au hakikisha unakijua kile ambacho wamekizungumzia." Aliongea masimba akiunyoosha mkono. Dee plus aliichukua ile picha na kuondoka akimuacha masimba akiendelea kuburudika. Bado alihitaji kujua kile ambacho teddy na ben walikuzungumza pale ufukweni. Dee plus akaondoka safari hii akielekea katikati ya mji. Alitaka kuanza na ben kwanza. Kwa kuwa alikuwa na hisia kuhusu kikao cha pale ufukweni mwa bahari. Bastola mbili zilikuwa sehemu tofauti mwilini. Alimjua teddy na pia ben, licha ya kuwajua huko lakini hakuhofia kwa kuwa hata yeye alikuwa mmoja kati yao.



Picha ya teddy na ben wakiwa ufukweni mwa bahari ni kitu ambacho kilimjengea maswali masimba katika kichwa chake. Muonekano wa watu hawa katika picha aliyoitazama muda mfupi uliopita hapakuonekana ishara ya mapenzi juu yao. Ukaaji na jinsi walivyokuwa wakitizamana ilionyesha uwepo wa kitu nyeti kilichokuwa kikijadiliwa na watu hawa wawili. Hisia kwamba teddy anapanga mipango ovu juu yake ilikuwa akikigonga kichwa chake. Haikuwahi kutokea teddy na ben kuwa na ukaribu huu.. hilo likampa mashaka na wasiwasi. Hisia kwamba teddy bado hajabadilika bado ziliendelea kumsumbua. Akatamani kumfuata na kwenda kumuuliza kwa kuwa bado alimpenda sana. Hata alipokumbuka usaliti aliotendewa na watu wake, akahisi labda alimtafuta ben kwa ajili ya kumpa kazi ya kuwafutilia mbali jimmy na washirika wake. Vifo vya watu sita katika nyumba fulani ni ishara kuwa yupo mtu anayetembea naye kila sehemu. Kwa mara ya kwanza akawaza kuitumbukiza risasi kichwani kwa mwanamke huyu. Ni dhahiri kuwa mapenzi kwake tayari yalishakwisha. Akaendekea kuuvuta muda tena na tena. Wakati wa kuianza hii kazi hakuwaza kama angefika huku. Hakuwaza kama yangetokea haya. Kwa mara ya kwanza akakumbuka wito wa DG wa idara ya Ujasusi. Wito ambao kidogo ulionyesha kumtatiza katika kuukubali. Sekunde hii alikuwa amekaa akiwaza, sekunde ya pili alikuwa akiukaribia mlango wa kutokea tayari kwa safari ya kuelekea kwa Chief. Alitembea kwa miguu mpaka maeneo ya bamaga, hapo akachukua tax tayari kwa safari ya kuelekea masaki nyumbani kwa mkurugenzi. Muda wote alikuwa kimya wakati tax akisonga kuelekea masaki. Mara moja moja alikuwa akiangalia kwenye vioo vya pembeni kuona kama anafuatiliwa, lakini haikuwa hivyo. Hapakuwa na gari wala usafiri wa aina yoyote. Wakati tax inafika kwenye mataa ya Morocco, akaiona gari nyeupe kupitia kioo cha pembeni akiwafuatilia. Ingawa gari ile ilikuwa katikati ya magari mawili, lakini hilo halikumfanya asigundue kuwa inamfuatilia yeye kwa kuwa, wakati anatoka pale afrika sana, -hii gari aliipita ikiwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara. Hakuongea kitu wala kuonyesha mabadiliko yoyote, dereva naye akaendelea kuendesha pasipokugundua kitu. Wakavuka mataa sasa wakielekea maeneo ya oysterbey. Alipoiangalia ile gari, akaiona nayo ikiendelea kusogea tena ikiwa katikati ya yale magari matatu . Hapo kengele za hatari zikaendelea kugonga kichwani mwake. Hisia kwamba yale magari matatu yalikuwa katika safari moja ikamjia. Kwa mara ya kwanza akajipapasa sehemu alipoihifadhi bastola yake. Baada ya kuhakikisha ipo akatabasu huku akimuomba dereva aelekee ulipo ubalozi wa ufaransa. Dereva akatii na kuuongeza mwendo, huku nyuma magari yale nayo yakaongeza.



Muda mfupi dereva akasimamisha gari pembeni mwa barabara. Masimba na dereva wote wakashuka, masimba akatia mkono wake mfukoni na kutoq noti mbili za elfu kumi kumi na kumpa yule dereva. Wakati dereva akijipapasa kutafuta chenji ya kumrudishia masimba. Muda ule ule gari zile zikawapita kwa mwendo ule ule, lakini kufika mbele kidogo zikaacha barabara inayokwenda posta, mbili zikaingia kushoto kwenye barabara inayokwenda Masaki nyingine moja ikapita kama inaelekea daraja la salenda. Kila kitu kilichokuwa kikitendeka pale kilimsisimua na kumfurahisha masimba. Kila kitu kilichokuwa kikitendeka ulikuwa ni mpango uliosukwa na DG wa Tiss. Alizijua gari na vile vile alizitambua mbinu husika. Hakuogopa tena.. dakika ile ile akaliacha eneo lile akiwa juu ya usafiri wa pikipiki.



*******



Ukimya ulikuwa umechukua nafasi yake kama kawaida katika eneo lote la masaki. Walinzi wa idara zote walikuwa wakizunguka kila kona kuwalinda viongozi wote. Makachero walikuwa kila sehemu wakinusa hiki na kufanya kile. Masimba alishuka umbali wa hatua hamsini kutoka yalipo makazi ya chief. Akatembea taratibu macho yake ya kitizama kila sehemu. Maafisa usalama na jeshi maalum la usalama wa taifa walikuwa wamezagaa kila upande wakiangalia usalama. Masimba akatembea kanakwamba hakuwa akiwaona walinzi na hata maafisa wengine. Akalikaribia geti, hapo akasimamishwa huku mitutu ya bunduki ikielekezwa kwake. Mtu mmoja alieonekana kama mkuu wa ulinzi akamsogelea masimba kwa ukaribu. Alipomfikia na kugundua alikuwa nani alimpa heshima kisha kumuongoza kuelekea ndani tayari kwa kukutana na Chief. Geti likafunguliwa masimba akaongozwa mpaka ndani pembeni kukiwa na watu maalum kutoka kikosi cha walinzi wa viongozi yaani VIP PROTECTION UNIT. Kufika ndani akaongozwa mpaka ndani ya jumba. Kuingia tu akukatana na macho ya chief mr godliving kimaro akimtizama. Hayakuwa macho ya kutisha machoni mwake, yalikuwa macho ya kawaida na macho ambayo hayakuwa na chochote. Wakaangaliana tena na tena, kila mmoja akimtizama mwenzake. "Shikamoo Mzee." Hatimaye masimba asabahi. Chief akaitika kwa kichwa kisha akampa ishara ya kukaa katika moja ya viti pale ndani. Masimba akakaa pasipo kubisha. Macho yake yalikuwa yakimuangalia Chief. Hata chief naye akawa ana muangalia usoni. "Bila shaka nadhani unajua kuhusu hiki kilichotokea hapa nchini. Mambo yamekuwa magumu sana, mashinikizo kutoka mamlaka za juu yamezidi. Mkuu wa nchi anataka kupata taarifa kuhusu hiki kifo. Lakini bado wenzako wameshindwa kupata chanzo cha kilicho nyuma ya hili tukio. Wote ambao tulidhani wangeweza kutufumbua katika hili nao huuawa katika mazingira ambayo nadhani ni kutaka kuuficha ukweli. Nimekuita hapa kukupa hii kazi, kushindwa kwa idara zetu za ujasusi ni aibu kwa nchi na kwa dunia. Mheshimiwa rais ametishia kuwaomba CIA NA MOSSAD katika kumgundua muuaji huyu ama chanzo mauaji hayo. Fanya ufanyavyo na kwa njia zako zote ili tufahamu hili. Unaruhusiwa kutumia chochote katika hili."aliongea chief akionekana kukerwa na hiki ambacho kinaendelea kutokea. "Masimba hakutaka kuongea kwa muda ule. Kichwa chake kilikuwa kikiifikiria kazi hii aliyopewa. Kazi ya kumtafuta muuaji wa waziri mkuu, muuaji ambaye alikuwa ni yeye mwenyewe. Akatamani kumjibu kwamba mimi ndiye muuaji, lakini akauacha huo mpango. Angejichunguzaje wakati muuaji alikuwa yeye? Hapo akauona umuhimu wa kuwawahi Jimmy, suresh na mwamvita. Alitambua watu hawa ndio watakuwa mashahidi juu ya maovu ya Hayati. "Unadhani mtuhumiwa wa mauaji aliyenusurika kufa kwa amri yako anaweza kuifanya kazi nzito kama hiyo tena akitumwa na watu wale wale wali0mtuhumu? Akauliza masimba masimba. . Safari hii akibadilika.



"Najua kwa nini nimekuita hapa, hayo mengine achana nayo, nimeunusa ukweli ndio maana kama mkuu wa idara nikakuita." Akajibu Chief.



"Sawa nitafanya naomba muda wa wiki mbili nitarudi hapa nikiwa na ushahidi ama mtuhumiwa mwenyewe. Ninachoomba ni ruhusa kutoka mamlaka za juu kuipekua nyumba zote zinazomilikiwa na marehemu." Lilikuwa ombi ambalo lilimduwaza chief. Hakulitegemea hilo. Akakaa kimya kama sekunde ishirini kisha kwa sauti yake akasema. "Sawa nitazingatia ombi lako." Baaada ya jibu hilo la chief, masimba akainuka na kutoka tayari kwa kuondoka huku akicheka kimoyomoyo.





ILIPOISHIA.. alikuwa akicheka kimoyomoyo. Akicheka baada ya kupewa kazi ya kumtafuta muuaji, huku muuaji akiwa ni yeye mwenyewe. Je nini kitaendelea? Shuka nayo.



******



Alitembea sasa akitaka kufanya haraka katiks kulimaliza hili. Suresh, Jimmy na Mwamvita kisha teddy sambamba na Beni Bomphe wote lazima waondoke katika uso wa dunia. Sasa alikuwa huru kuifanyakazi yake. Sasa alikuwa huru kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya kwa kificho. Mbinu ya kuwasafirisha wasichana wale watatu kilikuwa kitu sawa kabisa. Hii ili saidia kulificha hili suala mpaka sasa. Idara ya ujasusi kushindwa kupata fununu za nani muuaji lilikuwa jambo muhimu sana katika kazi yake. Rais akitaka kuyaomba mashirika ya kijasusi kuja kusaidia katika sakati hili, hilo pia lilimpa tabasamu, tabasamu la pongezi kwa kuwa ameifanya kazi hii katika weledi mkubwa. Kufanikiwa kuizidi maarifa idara ya kijasusi Tanzania halikuwa jambo dogo. Kwani hakuna ambaye hawajui hawa watu. Akaliacha eneo la masaki katika namna ya kufurahi. Kwa mara ya kwanza akaona kuna umuhimu wa kurudi nyumbani kwake. Nyumba ambayo aliisusa katika kipindi chote alichokuwa akitafutwa. Leo alitaka akauangalie mzigo wake, mzigo ambao ndio unasababisha teddy kuufanya usaliti. Muda wote alitembea akiomba Mungu aipate ruhusa ya kupekua nyumba zote ambazo zilimilikiwa na waziri mkuu. Kuipata ruhusa hiyo itamfanya kukamilisha kazi aliyopewa katika wakati ule alioomba kupewa.



******



Baada ya kutoka pale coco beach, teddy alienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake kinondoni. Aliikuta nyumba ikiwa kwenye mabadiliko makubwa. Ilionyesha wana usalama walipiga kambi hapo na kuipekuwa nyumba yao nje ndani. Kila kitu kilikuwa katika mpangili0 wake ule ule lakini vikionyesha kupekuliwa katika umakini wa hali ya juu. Teddy akasimama hapo kwa muda akitizama hiki na kile. Akili yake ilikuwa akiufikiria mzigo uliopotea. Licha ya kujua umechukuliwa na Masimba lakini hakuwahi kujua ni wapi ambapo masimba aliuficha mzigo ule wa mamilioni ya shilingi. Tamaa ya pesa ikamuingia, akaona ulikuwa ni wakati wa kuutafuta ule mzigo. Alikuwa na uhakika wa kuwepo mle ndani ama kule ambako alipelekwa wakati alipopoteza fahamu. Akairuhusu miguu yake kuingia kila chumba na kila sehemu za siri ambazo huwa wanatumia kuhifadhi vitu vyao. Tamaa ya pesa ilikuwa imeshamuingia mtoto huyu wa kipare. Hakuwaza tena mapenzi wala pesa, hakuwaza mipango yao ya baadae alichokiwaza ni ule mzigo. Mzigo ambao ulimfanya au na yeye kunusurika kuuawa mara kadhaa. Alipekuwa na kutafuta kila sehemu lakini hakupata kitu, hakupata mzigo wala kitu chochote. Akarudi chumbani akionyesha kuwaza hili na lile. Mishipa ya hasira bado haikuondoka usoni mwake. Chuki dhidi ya masimba ikaongezeka zaidi na zaidi. Alitamani kuiruhusu risasi kukipasua kichwa chake pale ambapo angefanikiwa kumuona. Baada ya kuwaza sana akaona ajimwagie maji kwanza ili akitoka aelekee kule alipoamkia akaendelee kuutafuta mzigo. Yote hayo aliyawaza akiwa anajua masimba bado ni anarafutwa. Hakujua kile kilichotokea muda mfupi uliopita. Akayatoa mavazi yake na kubaki kama alivyozaliwa. Akapiga hatua mpaka bafuni. Akafungulia maji na kuyaacha yamwagikie mwilini. Wakati maji ya kizidi kumpa uhueni kumbukumbu juu ya kilichotokea usiku wa jana ikaanza kujirudia. Mauaji ya mama wa Asteria kwa kutega bomu kwenye nyumba yake, ulikuwa mpango ambao ulipangwa afe pamoja na Masimba. Ni yeye aliyetoa taarifa kwa Jimmy kuhusu safari ya masimba nyumbani kwa mama wa Asteria. Kilichotokea mpaka masimba kupona hakukijua. Alipowaza tukio la kusalitiwa na wenzake kisha kupigwa kichwani na kupoteza fahamu, alihisi moyo ukizizima. Masimba alimuokoa na kumtoa mikononi mwa kifo. Lakini leo alitaka kumuua masimba kwa sababu ya pesa. Hilo likaonyesha kumtuliza kwa muda lakini bado mawazo yake yalikuwa kwenye pesa. Akayaondoa mawazo yale kwa kuichukua sabuni na kuanza kujipaka mwilini. Ni wakati akilifanya hilo akausikia mlango ukifunguliwa kisha nyayo za mtu zikasikika kuingia pale ndani. Akayafunga maji kisha kutulia mle mle bafuni. Miguu bado iliendelea kutembea pale chumbani. Akaangalia pembeni kidogo sehemu ya kuwekea vifaa vyake, lakini hakuiona bastola yake, alikuwa ameisahau pale chumbani sambamba na mavazi yake. Akaendelea kutulia huku bado mtu yule akionekana kuhangaika hapo chumbani. Akatamani kutoka mle bafuni lakini hakuweza kwa kuwa kulikuwa na ugumu, pia alikuwa uchi na bastola yake ilikuwa chumbani. WakAti akifikiria nini cha kufanya, mtu yule akasikika akitoka mle chumbani kisha kupotelea. Teddy akaufungua mlango na kuchungulia kwa nje, macho yake yakamuona mtu akimalizikia kwenye kiza. Kwa kuwa alikuwa uchi huku akiwa bado na povu la sabuni, teddy alitoka mpaka ndani na kuingia chumbani. Cha kwanza kukiangalia ilikuwa bastola yake. Akaiona ikiwa pale pale alipoiacha. Akaangalia na vitu vingine. kitu alikikuta kikiwa kipo pale pale. Yule ni nani? Na alikuja hapa kufanya nini? Yalikuwa maswali ambayo hayakuwa na majibu.



******



Wana usalama walikuwa mtaani wakiendelea kuwafuatilia Jimmy na Suresh. Kila sehemu walikuwepo na hata kwenye makazi yake ya siri yalikuwa yakichunguzwa kwa umakini wa hali ya juu. Muda wote walioanza kumchunguza bado hapakuwa na chochote walichokipata kutoka kwenye uchunguzi wao. Mawasiliano yao yalikuwa yameingiliwa na kufuatiliwa kwa kila hatua. Hakukuwa na mawasiliano ya kutia shaka. Licha ya hilo wanausalama bado walikuwa wakiendelea kufuatilia. Katika kufuatilia huko wakagundua kuwa Jimmy huwasiliana na namba karibu tano kwa kila siku. Namba hizo huwa haipiti dakika mbili mpaka tano pasipokuwasiliana. Hilo likawatia shaka wana usalama wale. Kwani hata walipoifuatilia mawasiliano ya Suresh walikutana na namba zile zile na mawasiliano yale yale na muda ni ule ule kama yale ambayo hufanyika kwa Jimmy. Wote wakahisi uwepo wa mawasiliano yasiofaa kati ya watu wale... leo hii vijana wawili walikuwa wamekaa maeneo buguruni kwa mnyamani wakibishana sambamba na vijana kuhusu sakata linaloendelea hapa nchini kuhusu kutekwa kwa watu na kupotea kwa mwanaharakati na mkosoaji mkuu wa serikali ya Tanzania Ben John Saatisa. Wakati wengine wakiilaumu serikali hasa Idara ya Ujasusi, wengine walikuwa wakikihoji chama chake kwa kukaa kimya muda wote mpaka pale mitandao ya kijamii kuibua suala hilo. Licha ya ubishi huo, lakini walikuwa hapo kwa kazi maalum. Kazi aliowaleta hapo ilitokana na kugundua kuwa mmoja kati ya watu wanaowasiliana na Jimmy pamoja na Suresh alikuwa akiishia katika viunga hivyo vya buguruni. Walibishana hapo lakini macho na mawazo yao yalikuws mbele ya jumba fulani kubwa. Hapo ndipo anapoishi mtu wao waliokuwa wakimfuatilia. Wakati mabishano yakiendelea, wakaiona ikiingia taratibu katika eneo la jumba hilo. Punde lango likafunguliwa na ile gari kupita ndani moja kwa moja. Vijana wale hawakuonyesha chochote bado waliendelea kubishana. Ikiwa hazikupita hata sekunde kumi tokea kuingia kwa hari hilo. Wakamuona mwanadada mrefu na mrembo sana akichungulia kutoka ndani kisha kuufunga mlango. Haukupita muda tena wakamuona muokota makopo akipita akielekea pale kwenye lango la jumba lile. Macho yao yakahamia kwa muokota makopo yule. Muokota makopo ambaye aliwashangaza na kuwaduwaza. Hakuwa muokota makopo kama anavyoonekama.. bali huyu alikuwa mtu kama wao.. Yaani hata yeye alikuwa ni kachero, lakini hawakujua kwa nini yuko pale na imekuaje Akajibadili na kuwa muokota makopo.



Alikuwa muokota makopo, muokota makopo ambaye hakuonekana kufanana na kazi hiyo. Bado wakaendelea kumtizama. Hata wakati analifikia geti na kuligonga bado walikuwa wametulia wakimtizama. Suruali iliyochanika, kofia chakavu na fulana ya hovyo haikuwafanya wapelelezi hawa waamini kile walichotakiwa kuaminishwa. Kuaminishwa kuwa huyu alikuwa mchafu tena muokota makopo. Kila mmoja akaendelea kumtizama safari hii kwa umakini. Wakataka kuaminishwa kuwa hakuwa mtu kama wao, lakini hilo halikutokea kwao kuamini. Kuamini kuwa yule ni mwenda wazimu. Walijua na kutambua kuwa yule alikuwa mwenzao. Geti likafunguliwa na mwanadada yule yule aliyelifunga mwanzo, hakuna aliyetegemea kutokea kwa kilichotokea. Kwani muda mfupi walikuwa wakimuangalia yule mtu kama muuza machupa. Hata wakati akiliendea geti walilijua hilo. Lakini kitendo cha geti kufunguliwa na kushuhudia ule upigaji wa muokota makopo yule, wakabaki wameduwaa. Mwanadada aliyefungua geti alikuwa chini nje kidogo ya geti akiwa hana fahamu. Mtu yule muokota makopo akageuka na kuwapa ishara ya kumchukua mwanamke yule. Hapo ndipo walipomtambua na kumjua muokota makopo. Huyu alikuwa Dee plus, huyu alikuwa kijana wao. Baada ya kuitoa ile ishara Dee plus akalifungua geti taaratibu na kuzama ndani. Macho yake yakakumbana na giza, giza ambalo ilikuwa ishara kuwa jumba lile halikuwa linaishi watu wa kawaida. Kingine kilichomstaajabisha ulikuwa ni ukimya. Ukimya ambao hapo mwanzo haukuwepo. Bastola ilikuwa mkononi wakati akiuendea mlango wa jumba lile kwa kupitia chini ya magari ambayo yalikuwa pale ndani. Bado ukimya uliendelea kutanda na kumfanya Dee plus a0ngeze umakini. Alipoufingia mlango kwa upande wa nyuma akasimama kwanza kusikiliza kama atasikia kitu chochote. Lakini bado hakuisikia sauti ya tv wala sauti ya redio. Jumba lilikuwa kimya kabisaa. Akaendelea kusonga mbele. Baada ya kutembea hatua kadhaa, akaukuta mlango ukiwa wazi, hapo akasita kwanza. Akasimama upenuni mwa jumba lile. Mbele yake akiutizama mlango ambao ulikuwa wazi. Licha ya kusubiri kwa muda wa dakika moja, lakini hakuweza kumuona mtu yoyote akitoka ama kuingia. Hapo akaamua kusogea mbele zaidi kuufuata mlango. Alipoufikia akatembeza macho yake ndani kwa sekunde moja akitegemea kuona chochote lakini hakuliona hilo. Sasa akaamua kuingia ndani kabisa. Bado ukimya na giza viliendelea kuwepo hata ndani. Bastola mkononi, macho yakitembea huku na huko akafanikiwa kuingia mpaka sitting room. Bado ukimya haukuondoka hapa. Akatulia hapo akiangalia kama mtu wake atakuwepo hapo, lakini bado hakumuona mwenyeji wake. Sebule haikuonyesha dalili ya uwepo wa watu hapo. Hilo pia likamshangaza kama sio kumduwaza.



Akainuka akipanga kuitafuta switch ili awashe taa aangalie. Wakati anafika karibu na swichi akaisikia sauti ya mtu akigugumia kwa maumivu. Akaacha kwanza alichotaka kukifanya alatulia ilikusikiliza kwa makini. Bado sauti dhaifu ya mtu aliye0nyesha yupo kwenye hatua za mwisho aliendelea kuisikia safari hii kwa karibu. Dee plus asogea mdomo wa bastola ukiwa mbele. Mbele kidogo akakanyaga kitu mfano wa maji. Kabla hajajua ni kitu gani, harufu ya damu ikasikika puani. Akatambua kuwa ilikuwa damu tena inawezekana ni damu ya mtu yule anayegumia kwa maumivu. Hapo akaliacha hilo la damu na kuanza kumsaka majeruhi. Kengele za tahadhari zikilia kichwani kwake. Haikuwa sawa na hapukuwa na usalama tena. Alishawahiwa na mtu. Kitendo cha kuukuta mlango uko wazi kisha kulikuta hili la dimbwi la damu ilikuwa ishara kuwa tayari kuna mtu amemuwahi katika hili. Hii ilikuwa ile ile staili ya fumbana midomo. Hata huyu naye alikuwa amezibwa mdomo kutotakiwa kuongea chochote. Nani atakuwa amelifanya hili wakati hii ilikuwa ni siri ya idara ya ujasusi? Nani anavujisha hili kutoka ndani ya idara ya usalama wa Taifa? Tuna wanaotusaliti? Tuna wanaovujisha hili? Nani amejua nani atakuja huku ndani? Yalikuwa mawazo yaliyomsogeza mpaka chini ya sakafu alipolala mtu yule. Bado alikuwa akiugulia maumivu. Akainama kumuangalia mtu huyu kama anaweza kupata lolote, lakini haikuwa hivyo, mtu yule akampa ishara ya kuwasha taa.. Dee plus akainuka huku bado bastola iko usawa wa mtu huyu. Akarudi nyuma na kuiwasha taa.. sebule yote ikawa nyeupe. Hapo akashtuka baada ya kukutana na watu watatu wakimtizama. Teddy, Ben na Mwamvita. Wote walikuwa wakitabasamu huku teddy akipiga makofi. Dee plus hakushtuka na hukuwajali, bado macho yake yalikuwa yakiutizama mwili wa mtu yule aliyelala katikati ya dimbwi la damu. Akili yake ikafanya kazi kwa haraka. Akageuka kuwaangalia watu wale watatu, hakuamini macho yake pale alipokutana na midomo mitatu ya bastola ikimtizama huku sakafuni kukiwa na miili ya wale vijana wawili ikiwa haina uhai. Hakuacha kuuonyesha mshangao wake. Watu watatu ambao alikuwa akiwatizama hawakuuonyesha utani wala masihara. Hata pale walipokuwa wakimsogelea hakujua nini cha kufanya. Ilikuwa miujiza tu kutoka mikononi mwa viumbe hawa watatu. Viumbe ambao hawakuwahi kuwa na roho kibinadamu. Akasimama akimuangalia zaidi teddy. Kwa mara ya kwanza alikuwa akiushuhudia unyama wa teddy. Hakuonyesha kama hata yeye ni kachero. Hapa aliubeba unyama unyama. Wote wakamfikia katika muda ule ule. Midomo ya bastola zao iliugusa mwili wa Dee plus. Wakimtizama katika kila aina ya vitendo na ishara. Nadhani hawakuwa wakimjua vizuri dee plus, nadhani hawakuwa wakimjua kwa kuwa hawakuweza kusimama kwa muda ule. Mapigo fulani ya kijapani yalisababisha bastola zao kuanguka chini pasipo wao kutaraji. Sasa walikuwa wakitizamana, wakiangaliana na hata kusogeleana. Dee plus alikuwa akiwatizama jinsi walivyokuwa wanakuja. Ni wakati hilo likifanyika mlango ukafunguliwa kwa kasi huku risasi zikivurumishwa ndani ya sebule. Hakuna aliyesimama hapo bali kila mmoja akachupa kwa upande wake. Moshi wa baruti pekee ndio uliyesikika ndani ya chumba kile. Dee plus alikuwa amebana nyuma ya meza kubwa macho yake yakitizama kila upande. Ukimya ulikuwa umechukua nafasi kubwa ndani ya jumba. Hakuna hata mmoja ambaye alikuwa akipumua. Pale alipojibanza Dee plus nyuma yake kulikuwa na mlango mdogo ambao mwanzo hakuwa ameuona. Hata mtu ambaye alikuwa akimimina risasi naye alikuwa amejibanza kimya. Sebule bado ilikuwa giza kutokana na risasi zilizokuwa zikivurumishwa kuipasua taa. Dee akaufungua mlango taraatibu na kuingia ndani ya Chumba kile kisha kuufunga tena. Wakati akitaka kugeuka nyuma aondoke, akamuona mtu mle ndani. Huyu alikuwa mwanadada. Alikuwa akitetemeka huku akiwa hana hata vazi maungoni mwake. Alikuwa akitetemeka sana na licha ya kutetemeka huko pia alikuwa akivuja damu maeneo mbali mbali ya Mwili wake. DEE PLUS AKATULIA AKIMTIZAMA HUKU MDOMO WA BASTOLA UKIMLENGA MWANAMKE YULE. Hakutaka kumuamini kwa asilimia zote. Hata katika kazi zao za kijasusi hakutakiwa kumuamini mtu yoyote. Kitendo cha teddy kutaka kumuua ni kuonyesha ni jinsi gani binadamu hawaaminiki. Akaichukua khanga ambayo ilikuwa juu ya meza akamtupia na kumtaka watoke mle ndani. Kwa kuwa mwanamke yule alikuwa mwenyeji wa jumba lile akamuongoza Dee plus kutoka katika jumba lile wakiacha milindimo ya risasi ikiendelea.



*******



Alihitaji kuupata ujumbe kutoka kwa Dee plus kutoka sehemu fulani aliyomtuma. Lakini muda ulikuwa umekwenda sana na bado hakuwa amepata ujumbe huo pia Dee plus hakuwa amefika. Hilo likampa wasiwasi kidogo. Akaamua kumpigia, lakini simu yake ilikuwa ikiita tu pasipokupokelewa. Hata hilo hakulitegemea. Akili yake ikamwambia dee plus alikuwa msambweni. Wakati akitaka kuinuka tayari kwa safari ya kumfuatilia.. mlango ukafunguliwa akaingia dee plus, hakuwa mwenyewe bali alikuwa na mwanamke aliyeonyesha kulowa damu. Hapo akagundua kuwa mawazo yake kwamba Dee alikuwa msambweni yalikuwa sahihi. Akawaangalia wote kwa pamoja, lakini kabla hajazungumza chochote simu ya Masimba ikaita. Akaichomoa simu mfukoni na kuangalia Jina la mpigaji. Alikuta simu inatoka kwa mama yake mzazi. Machale yakamcheza.. akahisi hatari kwa mzazi wake sambamba na wanawe France na Yaseer. "Hallow Mamaaa!!!!! Akaita masimba..



"Tunahitaji mzigo wetu!! La sivyo utakuta maiti za wanao na mama yako mzazi." Haikuwa sauti ya mama yake, bali ilikuwa sauti ya mtu mwingine ambaye hakuweza kumgundua.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwa muda masimba akapigwa na bumbuwazi, butwaa la kutokuamini alichokisikia. Simu ilishakatwa na haikuwa ikipatikana tena. Mama yake na watoto wake Yaseer na France walikuwa chini ya himaya ya watu asio wajua. Hasira zikaendelea kuchemka ndani kwa ndani. Aliwapenda sana wanawe na hata mama yake. Hakupenda waguswe na kubughuziwa na mtu yoyote. Lakini leo kuna watu ambao wamekwenda kuugusa moyo wake na roho yake. Walikwenda kumtingisha na kumtia hofu. Walikwenda kuonyesha kuutaka mzigo kwa njia nyingine. Ni nani hawa wanacheza na watoto wangu? Ni nani hawa wanacheza na mama yangu? Yalikuwa mawazo yaliyomuondoa pale ndani. Alitaka kuondoka katika muda ule kuelekea kwao Handeni. Alitaka kuwahi kukabiliana na watu hawa. Mzigo ni wa nini kwangu? Watu wangu wanathamani kuliko hata huu mzigo. Wakati anaukaribia mlango wa kutokea akaisikia sauti ya Dee plus ikimuita. Hapo ndipo alipogutuka na kugundua kuwa Dee plus alikuwa pale ndani tena akiwa na mwanamke aliyeliwana damu. Akageuka na kumtizama Dee plus, macho yao yakaongea kwa sekunde mbili, sekunde ya tatu masimba alikuwa akiufungua mlango akiondoka pale kwa safari ya Tanga. Safari ya kuupeleka mzigo sababu ya kuwaokoa watu wake. Alitembea hasira ikichemka, alitembea kana kwamba ni kichaa. Bastola mbili zikiwa mwilini katika sehemu tofauti. Alikuwa ameingiq vitani rasmi, alikuwa ameingia kwenye mapambano. Teddy, mwamvita, suresh na jimmy ilikuwa ni lazima wafe. Ilikuwa ni lazima waondoke. Muda mfupi alikuwa sehemu moja katika nyumba yake ya Siri maeneo ya kijitonyama. Alikuwa ndani ya chumba akiuchukua ule mzigo tayari kwa kuupeleka sehemu husika. Alikuwa tayari kufanya kila kitu kwa sababu ya watoto na mama yake. Baada ya kuweka kila kitu katika hali nzuri, safari ya kuelekea Handeni ikaanza. Alikuwa katika kiwango kikubwa cha hasira, alimtoa teddy moyoni na hata rohoni. Alikuwa tayari kumuua kwa mikono yake mwenyewe. Alikuwa tayari kuufumua ubongo wa mwanamke huyu mpuuzi. Alitambua ni yeye ambaye alikuwa nyuma ya hili suala la kushikiliwa mateka kwa wazazi wake. Hakutaka kumwambia mtu yoyote zaidi ya Dee plus. Hata Chief hakutaka kumwambia kwa kuwa anaweza kuongea na wasaidizi wake wakaivujisha. Alitaka kupambana mwenyewe, alitaka hili suala liishe mikononi mwake. Suala la kifo cha waziri mkuu akaliweka pembeni kwanza. Mawazo yalikuwa kwa watoto wake na bibi yao. Wakati akipita kwenye daraja la wami akaliona gari likimpita kwa kasi sana. Mwendo wa gari lile ulimshangaza sana lakini kwa kuwa halikumhudu akaamua kuachana na mawazo kuhusu hilo. Akaendelea kuendesha gari kwa mwendo wa wastani. Wakati anafika mkata ili aingie kwenye barabara iendayo Handeni, mlio wa sms ukaingia kwenye simu yake. Akaitoa simu mfukoni, akakutana na Jina la My love juu ya kioo cha simu. Sms kutoka kwa Teddy hiyo ilimshtua. Akaufungua ujumbe ule huku moyo wake ukiwa na wasiwasi mkubwa. "Najua ushajua mpaka sasa mimi ni nani. Naomba upeleke mzigo ukiwa pekee yako, ujanja wowote utakaoufanya utakuja kuokota maiti za hawa vifaranga vyako." Ulisomeka ujumbe ule. Akaurudia kuusoma tena na tena. Hakutaka kuamini kama ulikuwa ukitoka kwa teddy mwanamke aliyekuwa akiimba mapenzi kila siku. Mwanamke aliyekuwa akimwambia Nakupenda kila siku. Akaurudia tena na Tena ulitumwa kweli na Teddy. "Nitakupata tu na Nitakuua kwa mkono wangu." Akajisemea mwenyewe huku akiirudisha simu mfukoni. Teddy alikuwa ameonyesha yeye ni nani katika hili. Aliamua kujiweka wazi. Akaipita mazingara na kuitafuta SUA. Gari ikatembea na kutembea katika mwendo wa kawaida.



******



Mji wa Vibaoni ulikuwa umepoa kwa ukimya, wakazi karibia wote walikuwa wamelala huku mbwa tu wakisikika wakibweka. Alitembea kwa miguu baada ya kuiacha gari sehemu ya mbali kidogo. Alitembea usiku ule akiwa na mavazi maalum ya kutembelea usiku. Kutoka kijiji cha kwambwembwele alipoiacha gari, akapitia barabara iendayo arusha eneo maarufu liitwalo kwa kadenge. Akatembea usiku ule pasipokukutana na kitu chochote mpaka alipotokea maeneo ya Shule ya Msingi mlimani (zamani alijulikana kama vibaoni) baada ya kufika hapo akatulia kwanza akiangalia nyumba yao. Macho yake yakawaona watu wawili ambao walikuwa wamesimama Nje ya nyumba yao. Aliendelea kuangalia mara akauona mwanga wa taa za gari ukisogea taratibu. Masimba akaendelea kidogo akitizama kwa makini. Akamuona mtu mwingine akitokea nyuma ya nyumba ya mzee Mauya. Baba mzazi wa Rukia Mauya. Baada ya kutoka mtu yule akaonekana akiisogelea gari ambayo ilikuwa tayari imesimama karibu na nyumba yao. Akaondoka pale na kupitia nyuma nyuma mpaka pembeni mwa uwanja wa shule ya msingi. Wakati huo watu wale bado walikuwa wamesimama huku mmoja wao akiongea na simu. Punde akauona mlango wa gari ile ukifunguliwa, wakashuka watu wawili ambao aliwatambua kwa haraka. Alikuwa mwamvita na Ben. Hata alipoiangalia gari ile vizuri aliitambua kuwa ni ile gari iliyompita kule wami. Baada ya watu wale kushuka akawaona wakiingia ndani ya nyumba yao kisha wakatoka wakiwa wanawasukuma watoto wake na mama yake. Wakati hilo likifanyika mlango mwingine wa gari ile ukafunguliwa. Safari hii alishuka teddy mkononi akiwa ameshikilia bastola. Kwa kuwa watoto na hata mama wa masimba walikuwa wakimjua,wakamkimbilia na kutaka kumkunbatia. Haikuwa hivyo, haikuwa hivyo kwa kuwa Teddy hakulitaka hilo. Akashudia wanawe wakipaa angani baada kupokea mapigo kutoka kwa teddy. Hakuvumilia hilo, muda huo huo alikuwa amechupa hewani na kuwadaka watoto wake kabla ya kufika chini. Akatua nao chini katikati ya watu wale huku mdomo wa bastola ukiwa kichwani kwa Teddy. Kilikuwa kitendo ambacho hakikutarajiwa na watu wale, kitendo ambacho kiliwaacha kwenye hamaniko. Wakati hilo likiendelea mama yake masimba akachoropoka na kutaka kukimbilia pale alipokuwa mwanawe. Hakumfikia wala kusogea.. Bastola ya Mwamvita Ikakohoa na wakati ule ule Masimba akamshuhudia mama yake akipaa juu na kuanguka chini. Damu zilikuwa zikivuja kifuani. Masimba hakuamini hilo, hakuamini kama chini pale amelala mama yake. Akakurupuka kukimbilia ulipolala mwili wa mama yake mzazi. Wakati huo huo wanakujiji nao walikuwa wakiinuka kutokana na kuusikia mlio wa bunduki. Baada ya kuona watu wameanza kuamka majumbani mwao, wakambeba mtoto mmoja na kuingia naye kwenye gari kisha kui0ndosha gari kwa mwendo wa kasi wakimuacha masimba akilia juu ya mwili wa mama yake.



Alikuwa haamini kama mama yake ndiyo yule aliyekuwa amelala pale chini damu ikivuja kama maji. "Mnala inuka chilonge. Usekunasa mnala wezi ukuluwo na walonge na yuhi? Inuka mnala." ( inuka mama tuongee, usiniache mama, wajukuu zako wataongea na nani? Inuka mama) alilalamika masimba huku akimtingisha mama yake. Lakini haikusaidia kitu, mama yake hakuwa na kauli tena. Alikuwa katika hatua za mwisho za uhai wake. Pale pale akashuhudia mama yake akikata kauli na kugeuza shingo. Muda mfupi akaacha kupumua. Mama yake alikuwa amekufa mikononi mwake. Mama yake alikuwa amekufa kwa ajili yake. Mwamvita alikuwa amemuua mama yake. Akashindwa kuongea kwa muda. Mama yake alikuwa amenyamaza kimya. Akainuka na kusimama pembeni akiuangalia mwili wa mama yake. Lakini alipoangalia pembeni hata mwanawe Yaseer alikuwa ameanguka akitokwa na damu puani, mdomoni na masikioni. Alikuwa amepoteza fahamu. Muda ule ule difenda ya polisi yenye askari kumi wenye silaha nzito ikawasili. Wakashuka na kuanza kupiga picha za tukio lile. Muda ule ule gari aina ya wagonjwa ikafika na kumchukua yaseer. Kila kitu kilitokea kwenye kipindi kifupi sana. Muda ambao ulibadilisha maisha ya masimba. Hakujua kama mwanawe atapona kutokana na pigo la Tedd na pia hata france naye hakujua kama atakuwa salama. Watu walikuwa wengi wameuzunguka mwili wa mama wa masimba. Mama ambaye alikuwa ni maarufu sana pale vibaoni na Handeni yote kwa ujumla. Vilio vikatawala huku watoto wa kike wa marehemu wa kipoteza fahamu kwa taarifa hiyo. Muda wote Masimba hakuwa akiongea taswira ya mwamvita akimshuti mama yake ilikuwa ikijirudia. Matundu matano ya risasi kifuani yaliuondoa uhai wa mama yake. Akaitamani iwe ndoto, aliitamani iwe kama hadithi ya kusadikika. Lakini mwamvita aliutoa uhai wa mama yake. Mbele ya macho yake ulilala mwili wa mwanamke mwenye thamani kuliko mwanamke yoyote duniani. Akainuka akipiga hatua kwa mara nyingine akielekea ulipolala mwili wa mama yake. Hakuufikia kama mwanzo, kizunguzungu kikali kikamfanya aanguke chini, macho yakaingiwa na Giza na hakuona kilichoendelea.



******



Alijifungia chumbani akilia kwa uchungu. Pembeni aliuweka mzinga wa pombe kali. Macho yake yalikuwa yamevimba kwa kilio na majuto. Mbele kidogo kwenye kitanda kidogo alikuwa amelala france mtoto wa masimba akitibiwa na Daktari binafsi. Taswira yake ikalikumbuka tukio la mwamvita kuruhusu risasi kumuua mama wa masimba. Akakumbuka kumuona mama yule akiinguka. Chozi likashuka na kushuka Zaidi. "Hukustahili Kufa mama yangu. Umenitendea mema sana tokea nilipokujua . Nisamehe mama yangu ni samehe kwa ujinga wangu. Aliongea Teddy akilia. Kichwani akavuta taswira ni hali gani alionayo masimba kwa muda ule. Akainuka na kutoka nje ya kile chumba. Safari yake ikaishia chumba kingine mle ndani. Akaichomoa bastola yake na kuinyanyua juu mdomo wa bastola ukagusa kichwani mwake. Teddy alitaka kujiua. Hakuweza kulivumilia lile. Kidole kikashuka mpaka kwenye kitufe cha kufyatulia risasi.





Kid0le kikashuka mpaka kwenye kitufe cha kufyatulia risasi. Akaivuta pumzi kwa muda. Akili yake ilikuwa ikikinzana na moyo wake. Moyo ulihitaji atende kile, lakini akili ikakataa kutii matakwa ya moyo. Bado akatulia kidole kikiwa kwenye kitufe. Alikuwa ametulia akiusikilizia uamuzi wa vitu viwili. Uamuzi wa kukatisha maisha yake ama kufuata kingine. Ni katika kuwaza huko akapata maamuzi mapya. Maamuzi ambayo yalimfanya aishushe bastola yake. Akatulia akiufikiria uamuzi mpya alioupata. Akili yake ilimwambia aondoke hapa Tanzania aende nchi yoyote akatafute sehemu ya kuishi akiwa sambamba na France. Huo ulikuwa uamuzi wake, maamuzi ambayo hakutaka kumshirikisha mtu. Akatoka ndani ya chumba kile na kurudi kule alipomuacha Daktari akimtibia France. Akaufungua mlango na kuingia macho yake yakakutana na macho ya france yakimtizama kwa wasiwasi. Teddy akatabasamu tayari kwa kuuondoa wasiwasi ule. Akapiga hatua mpaka pale alipokuwa amelala. Akapiga magoti na kuushika mkono wake. Akayapeleka macho yake usoni kwa france. Akahisi kama alikuwa akitizamana na Masimba kutokana na kufanana kwao. France alikuwa ni Masimba mtupu. Alimuangalia sana mwisho wake akashindwa kuyazuia machozi yake yasishuke. Bado mwili wa mama yake masimba ulipopaa angani baada ya kupigwa risasi na Rukia ulikuwa ukijirudia. Roho ikamuuma na kumuuma. Ule ushujaa wote ukapotea kabisa. Sasa alikuwa ameivaa hofu na kuuvaa woga. Alikuwa aki0gopa kukutana na masimba. Hapo ndipo alipozidi kuona umuhimu wa kuondoka hapa nchini. "Nakupenda sana mwanangu Frances. Wewe ndio pekee furaha yangu pekee iliyobaki. Najua baba yako atanitafuta na hata kuniua. Lakini kabla hajaniua nataka nikwambie kuwa Nakupenda mwanangu na ninataka tuondoke hapa tukaishi Ulaya. Nia yangu nikukufanya uishi kwa furaha." Baada ya kuongea hayo akainuka na kuondoka pale nyumbani. Alitaka kuipanga mipango kimya kimya pasipo ku0ngea na mtu yoyote. Hata kupokea simu ya Mwamvita hakuwa akifanya hivyo ndio maana leo hii hakuwa katika makazi yake yanayojulikana.



****



Bado hakuwa na fahamu na hakuwa akijua kile kilichokuwa kinaendelea. Handeni ikazizima kwa majonzi na vilio. Kila mmoja aliyesikia kifo cha mama huyu alisikitika sana. Watu wakaendelea kumiminika kutoka maeneo mbalimbali. Muda mfupi nyumbani ulijaa umati wa watu. Kila mmoja alikuwa akisikitika na kulaani kile kilichotokea. Vijana wenye uchungu wakataka kuleta fujo kwa kuwalaumu polisi. Lakini hawakujua, hawakujua kuwa Polisi hawakuwa na kosa lolote. Masimba bado hakuwa na fahamu, ndio kwanza madrip ya maji yalikuwa yakimiminika kwenye mishipa. Habari zikasambaa kama moto wa kifuu. Idara ya ujasusi ikaipata taarifa hiyo. Ilikuwa taarifa iliyowashtua wengi. Katika wote hao Dee plus pekee ndiye aliyeumia sana. Alimjua mama wa Masimba kwa kuwa waliishi jirani kabisa nyumba zao zipakana kwa hatua tano tu. Hakutaka kuliamini hilo katu. Akaona kulikuwa na umuhimu wa kumpigia masimba. Licha ya kupiga sana na simu kuita, lakini simu haikupokelewa. Dee plus akaamua kuipanga safari katika muda ule kuelekea Handeni. Hakutaka kuchelewa.. muda mfupi baadaye alikuwa barabarani akielekea handeni. Asingeweza kubaki Dar wakati Vibaoni imepatwa na msiba. Aliitembeza gari kwa mwendo wa kutisha, trafiki walio jaribu kumsimamisha njiani walikutana na kitanbulisho. Wakamuacha aendelee kwenye safari yake. Saa tano na nusu asubuhi alikuwa akiingia katika viunga vya vibaoni. Alipokelewa na umati wa watu sambamba na vilio. Aliufungua mlango na kushuka. Hakuongea na mtu zaidi ya kuongoza mpaka nyumbani kwa kina masimba. Alipokuwa akikaribia macho yake yakakiona kitu ambacho kilitafanya machozi ya mdondoke. Chini ya ardhi ya nyumba ya Wanamchiwa mbele kidogo ya uwanja wa nyumba, damu nyingi ilikuwa imetuwama chini. Akasogea mbele huku miguu ikimtetemeka. Akaiangalia ile damu kwa muda wa dakika mbili bila kuongea kitu. Baada ya kuangalia akageuka na kurudi ndani ya gari. Akaliwasha gari na kuliondoa gari kuelekea hospital ya Wilaya ya Handeni. Moyo ulikuwa ukibubujikwa na damu, hakuwahi kufikiria kama Teddy angekuwa mnyama kiasi kile. Moyoni mwake hata yeye akaapa kumuondoa katika uso wa dunia hii. Teddy lazima uilipe hii damu ya mama. Lazima uilipe kwa gharama yote. Muda mfupi alikuwa kwenye maegesho ya magari hospital pale. Alishuka na kukutana na makachero wengine ambao walitoka Dar es salaam. Akawasalimia, kisha akawapita na kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti. Wakati anausukuma mlango kuingia ndani.. macho yake yakatua juu ya mwili wa mama wa masimba. Matundu matano ya risasi yalikuwa yamekiharibu kifua. Dee plus akashikwa na butwaa.. miguu ikawa mizito kupiga hatua. Akasimama akiutizama mwili wa mwanamke yule asiye na hatia. Punde mlango ukafunguliwa akahisi kilio cha kwikwi kikitokea kwa nyuma yake. Akageuka taratibu kumtizama huyu anayelia. Macho yake yakamuona masimba akiwa ameshikiliwa huku na huko. Alikuwa akitia huruma sana.. machozi yalikuwa yakishuka kama maji. Akamuangalia huku akisogea. Kufika karibu yake akasimama mbele yake. "Don.!!! Aliita Dee..



"Teddy amenilazimisha nimuue. Teddy amekitafuta kifo ambacho nilikuwa tayari kukighairisha. Wameniulia mama yangu na kuwaumiza wanangu. Yaseer yupo mahututi amesafirishwa leo na makao, lakini france wameondoka naye na sijui hali yake." Aliongea masimba akiendelea kulia akitembea kuelekea pale ulipo mwili wa mama yake



******



Ulikuwa muda wa mazishi ya mama yake. Alikuwa amesimama pembeni akilia wakati masheikh walipokuwa wakiuombea mwili wa mama yake. Dada zake na kaka zake hawakuwa na hali, kila mmoja alikuwa akigalagala kwa vilio. Wajukuu na ndugu wengine hawakukamatika. Kwa masimba alikuwa bado haamini. Haamini kama ndio mwisho wa mama yake. Taswira ya mwamvita akimshuti mama yake iliendelea kujirudia kichwani kwake. Bado alikuwa akikunbuka risasi zili zilivyomtupa chini mama yake. "Mwamvita nitakuua kwa mikono yangu." Akanong'ona taratibu. Swala ya kuuswalia mwili wa marehemu ikaendelea kama kawaida na mwisho watu wakaubeba mwili ma marehemu kuupeleka katika nyumba yake ya milele. Umati uliohudhuria ulimshangaza kila mmoja hasa wale majasusi waliokuja kumpa msaada masimba. Kila alipokuwa akitembea taswira ya mwamvita haikuondoka usoni mwake. Mazishi yakafanyika na watu wote wakarudi nyumbani. Lakini cha ajabu alipotafutwa masimba hakuonekana. Hata kaka yake samwebondo alipotumwa akamtizame makaburini hakumuona. Na hakuwa masimba pekee bali hata Dee plus hakuwepo. Hilo likawashangaza wana ndugu wote simu yake haikupatikana na hata sehemu zote alizotafutwa hakuonekana. Kila mmoja akaongea anachokijua ili mradi tu. Masimba hakuonekana hata usiku ulipoingia.



******



Upepo ulikuwa ukivuma mithiri ya milipuko. Ndio kwanza Masimba alikuwa akiingia katika jiji la dar es salaam. Safari hii aliamua kuendesha gari mpaka Bunju nje kidogo ya jiji la dar es salaam. Kuelekea huko kulitokana na kuogopa kundulika mapema na watu wanaomtafuta. Kingine kilichomsogeza Huko ni ukaribu wa sehemu anapoishi mwamvita. Aliendesha gari mpaka bunju A nyumbani kwa Neema Mtobwa. Aliipaki gari umbali mfupi kutoka nyumba alioishi neema. Akatembea kwa miguu mpaka usawa wa jumba analoishi Neema. Hakutaka kupitia mlangoni, alichupa na kudondokea kwa ndani. Hapo akatembea tena na kuufungua mlango wa nyuma. Mlango ukamtiii!! Hapo akaingia ndani bila wasiwasi. Akatembea mpaka sebuleni. Hapi akakutana na Neema mtobwa akiwa amejilaza kwenye kiti. Akamsogelea na kumtingisha. Neema akafumbua macho yake, akajikuta akitizamana na masimba. Akainuka na kumkumbatia kwa nguvu. "Pole sana Masimba. Nimesikia kutoka ndani kilichotokea. Lakini kwa nini uko hapa wakati ndio kwanza mama amezikwa leo!!!!@ aliongea neema aki0nyesha kushangaa.



"Neema, mama yangu ameuawa na hatarudi tena. Nitabaki vipi handeni wakati waliomuua mama yangu wanafurahi? Nimekuja kuwapeleka kuzimu wakaungane na Mama Yangu.""....





Neema alimuangalia masimba kwa muda bila kuongea kitu. Alikuwa akikiangalia kile ambacho kipo ndani yake. Maumivu, majonzi na hata machozi ni kitu ambacho alikisoma ndani ya macho ya Masimba. Kingine alichokiona ni hasira na utayari wa kufanya chochote. Hakuwa na lakuongea. Maneno yalimuishia mdomoni. Akashuhudia masimba akitoweka machoni mwake mithili ya mzimu. Akitembea akionyesha hakutaka mashauriano na mtu. Alikuwa katika safari ya kumfuata Mwamvita nyumbani kwake mbezi beach. Moyo wake ulijaa uchungu, alikuwa akitembea huku akibubujikwa na machozi. Alikuwa akilia hasa pale alipouona mwili wa mama yake ukifukiwa. Akajua hatamuona tena. Akajua hata muona mwanamke huyu aliyemjali sana. Bastola zake bado zilikuwa mahali tulivu. Akatembea mpaka kituo cha daladala. Akajivuta machozi kisha akatulia akisubiria daladala. Muda mfupi akaiona daladala ikija huku konda akipiganikiza vituo. Ilipodimama alikuwa wa kwanza kupanda. Baada ya kupanda akatulia kwenye siti akitizama nje kupitia dirishani. Kwa kuwa ulikuwa usiku , barabara haikuwa na foleni. Wakajikuta wakitumia dakika saba kufika mbezi Africana. Baada ya gari kusimama, masimba akashuka taratibu na kuanza kutembea taratibu kuelekea nyumba anayoishi Mwamvita. Alitembea kama mtu wakawaida na mwenye shughuli zake akipishana na watu na hata polisi wa Doria. Bado hakuwajali na bado hakuwatizama. Akaingia uchochoro fulani na kwenda kutokea mtaa wa pili sehemu ambayo alikuta panabar. Baada ya kutokea hapo kwenye bar, akasogea hapo na kutafuta kiti. Kwa kuwa ilikuwa sehemu kimya sana licha ya kuwa na bar, lakini pia aliiona kuwa ilikuwa sehemu nzuri yakutulia kuuvuta muda akiwasubiri watu wapungue aweze kuingia kwa Mwamvita kwa Urahisi. Baada ya kuvuta kiti akamuita mhudumu na kumuomba ampelekee mzinga wa Whisky. Mhudumu akafanya hivyo na muda mfupi baadae Masimba alikuwa akimimina kinywaji mdomoni huku macho yake yakicheza kila kona. Kwa kuwa sehemu aliyokaa ilikuwa na giza aliweza kuwaona wote waliokuwa wakiingia. Alitulia akiendelea kunywa taratibu mpaka saa saba kasoro usiku ndipo alipoondoka hapo akiifuata barabara inayoelekea nyumbani kwa Mwamvita. Alitembea kwa kufuata giza mpaka nyumba ya pili kutoka nyumba anayoishi Mwamvita. Akasimama hapo akiitizama vizuri nyumba anayoishi mwamvita. Nyumba yote ilikuwa giza kasoro taa moja tu ya chumba ndio ilionyesha kuwaka tu. Hilo alilitegemea kwa kuwa alijua baada ya tukio lile lazima mwamvita angejidhatiti. Akaondoka hapo sasa akipiga hatua kuelekea kule. Akauvuka uzia wa nyumba ile, akajikuta sasa akitazamana na nyumba ya mbaya wake.



Akatulia hapo kwa muda bila hata kufanya chochote. Alikuwa akifikiria ni nini afanye ili kuingia mle ndani. Kuwaka kwa taa moja katika jumba lile haikumfanya masimba ategeke. Siku zote aliamini kuwa chumba kilichowashwa taa hakikuwa na watu. Watu walikuwa katika chumba kingine kabisa. Hilo akaliamini na ndio lililomfanya asimame. Aliamini mwamvita alikuwa sehemu ndani ya nyumba na sio katika chumba kile kinachowaka Taa. Hilo likamfanya umakini uongezeke. Safari hii bastola aliishikiria mkononi. Akasogea mpaka kwenye ukuta wa Jengo lile. Akauangia ukuta ule kama atauweza. Baada ya kujiridhisha sasa alikuwa akiuparamia ukuta mfano wa nyani, muda mfupi akaangukiwa ndani pasipokutoa sauti. Baada ya kuanguka pale alijiinua haraka mpaka upande mwingine. Wakati akitembea alijikuta akijikwaa kwenye ndoo za bati. Ukelele ukatokea. Hilo likamuongoza masimba mpaka chini ya mti. Akajibanza hapo kuona kama kelele zile zingemleta mtu pale. Ni kweli hakuwa mbali na mawazo yake. Punde akawaona watu watatu wenye silaha wakitokea pande tofauti. Kila mmoja alikuwa akitokea upande wake. Katika kitu ambacho hakukitarajia ni kuwaona walinzi hao. Kwa mara ya kwanza Hili likamshangaza. Mwamvita kulindwa na watu wenye silaha nzito. Hata alipowaangalia watu hawa kwa uzuri aliwatambua kwa karibu. Kuwatambua huko kulampa picha ya kinachoendelea. Walinzi waliokuwepo pale walikuwa walinzi wanaomlinda Chief. Hilo lilimaanisha chief alikuwa hapo ndani. Hilo likamuongezea umakini. Wazo kuwa Chief alikuwa upande huu lilikigonga kichwa chake. Lakini akalitupilia mbali baada ya kuwaona watu wawili wakiufungua mlango na kuchungulia Alikuwa Chief akiwa sambamba na Mwamvita. Chief alikuwa kwenye Bajama huku Mwamvita akiwa kwenye mtandio mwepesi uliofungwa kihasarahasara. Bado macho ya masimba hayakutulia. Yalicheza na walinzi wote na hata wakati mwingine yakiwaangalia chief na mwamvita. Mpango wa kumuua mwamvita ulikuwa umekuwa mgumu kutokana na uwepo wa Chief. Akaaona haukuwa muda muafaka kwa siku ile. Hakutaka kumfanya chief aelewe kinachoendelea. Aliamua kuighairisha hukumu ya mwamvita akiipanga kufanyika siku inayofuata. Baada ya walinzi wale kuangalia na kutokuona kitu, wakaturudi kila mmoja katika nafasi yake. Ni muda huo masimba alipochupa na kutua nje kisha kutokomea gizani.



*****



Alimbeba France mikononi akiondoka katika nyumba ile ya siri. Ulikuwa usiku wa saa saba Teddy alipoamua kuondoka katika Jiji la dar es salaam akielekea arusha kabla ya kuvuka mpaka na mkuingia kenya. Alitembea usiku ule kuogopa kugundulika mpaka alipofika maeneo ya barabarani. Akasimamisha pikipiki na kujipakia kisha safari ya kibamba. Alitaka kwenda kulala chalinze iwe rahisi kuondoka pasipokujulikana. Hakujali kazini kwani aliomba likizo ya miezi miwili akisingizia kwenda kukaa matanga kwenye msiba wa mama mzazi wa mpenzi wake. Baada ya dakika kumi na tano alikuwa kibamba. Akashuka na kumlipa dereva wa pikipiki kabla ya kusogea mbele kidogo sehemu ambayo ilipaki gari aina ya Noah. Baada ya kuifikia ile gari mlango ukafunguliwa. Akampakia France kisha yeye na baada ya hapo gari ikang'oa na kuianza safari. Safari ya kuuhama mji kwa muda. Alijua hasira za masimba zingeisha mwilini mwake. Moyo wake ulikuwa ukivuja kwa maumivu. Machozi yalikuwa bado yakishuka. Hakujua mwisho kama ingekuwa vile. Tamaa ya pesa imeondoa utu wake. Sasa alikuwa akiukimbia mji alioupenda. Akimuacha mpenzi kwasababu ya tamaa. Hakutegemea hilo kabisa kichwani kwake.



*********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog