Search This Blog

Saturday 5 November 2022

NITAKUPATA TU - 4

 







    Simulizi :Nitakupata Tu

    Sehemu Ya Nne (4)







    "Mambo yamesha kuwa mabaya, tayari majina yetu yametua ikulu na ushahidi wote upo mikononi kwa masimba. Abanwe mpaka aongee ukweli tusimuache katika hili." Ilikuwa sauti ya Mbunge wa jimbo la Kigamboni Bibi Grace Bwahama akiongea na wajumbe katika kikao kile kilichoitishwa baada ya kukamatwa kwa Mpelelezi Hatari. "Masimba Bado yupo mikononi mwetu, tutajua nini chakumfanya. Tunachotakiwa kukifanya hivi sasa ni kumtafuta kwanza teddy ili tumfutilie mbali. Hili la majina kufika Ikulu lisikupe shaka tutalishughulikia kwa uhakika na litakwisha. Chakufanya ni kuongea na Mr Jacob John Okoth Atuongezee nguvu katika suala hili. Teddy ameonyesha jeuri kubwa kwa kuwa anatufahamu. Nilazima tutumie huku kutufahamu kwake kumuulia mbali. Tunajua ni lazima aanze kutuwinda katika namna yoyote. Nilazima tumuwahi kabla hatujafanya Rabsha yoyote. Naomba tutulie, nitaongea na Mr Okoth nadhani leo hii vijana wake wata... kabla hajamaliza kauli yake simu yake ikapata uhai. Alipotizama juu ya kioo akakutana na namba maalum wanazo wasiliana wao kwa wao.. Kabla hajaipokea akawatizama wenzake kwanza. Haikuwa kawaida kupigiwa kwa namba ile. Huku moyo ukimdunda na mikono kutetemeka akaipokea simu. "Jimmy Lambert naongea." Akaongea Jimmy huku mapigo ya moyo yakimuenda Kasi. "Bosi Secret Base inawaka moto.. makombora yanalipuka kwa sasa." Ilisikika sauti ya upande wa pili. "Ooh my God!! Nini kimetokea? Na ilikuwaje? Akauliza Jimmy Mshangao ukiupamba Uso wake. "Sijui lakini nahisi mtu wetu ametuzidi ujanja na ameamua kufanya alichokifanya." Alijibu mtu wa upande wa pili. "Wewe unaongelia kutoka wapi kwa sasa?" akauliza Jimmy.



    "Nipo mafichoni karibu na Eneo la tukio. Alijibu mtu yule. Mara mlipuko mkubwa ukasikika. Hata jimmy aliusikia kwa kuwa bado simu ilikuwa hewani. Hapo akaamini ni kweli Kambi yao ya Siri ilikuwa ikilipuka. Akaikata simu huku akiigonga meza. "Teddy nitakuua kwa mikono Yangu. Nitakuua mimi mwenyewe." Alifoka jimmy akiendelea kupiga ngumi kwenye meza. Kilikuwa kitu kilichowashangaza wadau wenzake. Kila mmoja alikuwa akimuangalia Jimmy Alivyokuwa akihamanika huku na huko. Kwa nini Teddy? Teddy ana nini? Yalikuwa maswali yaliohitaji majibu kutoka kwa Jimmy. Jimmy ambaye alikuwa akitetemeka. "Secret Base Inateketea kwa Milipuko. Teddy na Masimba wameamua kututia vidole vya machoni. Wameamua kututia Hasira. Ni kosa kubwa tumefanya kuwaamini vijana wale mbele ya mtu kama Masimba. Vijana watakuwa wamefanya kosa. Tena kosa kubwa ndio maana masimba anatuadhibu." Aliongea Jimmy safari hii akiinuka kabisa. Chumba kizima kikatawaliwa na ukimya. Ukimya uliozua maswali vichwani kwa watu hawa. Kila mmoja akiwaza kile alichokiamini. Lakini kwa upande wa jimmy, masimba alikuwepo kwa mbali, alikuwa kwa mbali kwa kuwa masimba hakuijua ile kambi. Hakujua kama Chini yametegwa mabomu. Ni teddy tu ndiye aliujua ukweli. Alijua kila kitu kuhusu kambi ile. Ni teddy aliyefanya tukio hili. Ni Teddy alieamua kuwatia hasira. Jimmy alikuwa akiapa huku akibubujikwa machozi. Hakuamini alichokisikia. Sasa akaamua kutoka ukumbini pasipo kuongea na mtu. Alichanganyikiwa na hata kuvurugwa. Alipotoka nje kabisa alipajipakia ndani ya gari, akawasha na kuliondoa kuelekea sehemu ya Tukio.



    ********



    Baada ya kutoka kule kwenye kambi ya Siri. Masimba na Teddy wakarudi mpaka nyumbani kwao. Walipoingia tu ndani teddy akamuendea masimba kisha kumkumbatia. "Pole sana Mume wangu, mimi ndiye niliyesababisha wewe uumie. Kama sio tamaa yangu haya yote yasingetokea. Ona ulivyoumia kwa ajili ya ujinga Wangu. Nisamehe Mpenzi wangu. Nimeamua kusimama na na wewe. Nimeamua kuwa sambamba na wewe. Nisamehe sana." Aliongea teddy huku akimuangalia masimba usoni katika jicho la aina yake. Jicho legevu lenye kushawishi. "Najua yote, lakini hupaswi kujilaumu kwa sasa. Kama sio wewe na kama sio kifo cha Asteria P Paulo nadhani mpaka leo Nchi yetu ingekuwa katika hatari kubwa sana. Bila wewe nisingeijua biashara hii uliyokuwa ikimhusisha mpaka kiongozi mkuu wa nchi. Teddy mimi kukusamehe sio kwamba nimejilazimisha. Niliamini na kukuamini. Nilijua hiii ni vita yetu mimi na wewe. Nilijua ni hii ni vita ya kuwakomboa vijana wengi wanaoendelea kuharibiwa na madawa ya kulevya. Tusingeligundua hili ama asingeuawa Asteria Basi Taifa lingeendelea kuwa katika kipindi hatari zaidi. SIO WAKATI WA KUJILAUMU MAMA, HUU NI WAKATI WA BASTOLA ZETU KUIFANYA KAZI ILIYOBAKI



    "Sio wakati wa kuomba msamaha, ni wakati wa kuziacha Bastola zetu zifanyekazi. Niwakati wakulipigania taifa. Niwakati wakuliokoa taifa kutoka kwa watu ambao nia yao ilikuwa kuharibu Taifa Zima. Tunejitolea kufa na kupona ili kulizima hili. Unatakiwa kusimama Imara huku bastola tukiiacha Ikifanya kazi yake." Aliongea masimba huku akimuangalia Teddy machoni. Akimuangalia katika namna ya kumjaza nguvu. Muda wote walijua wapo katika vita ya kutetea na kuwapigania Vijana wanaoendelea kuharibiwa kwa madawa ya kulevya. Alikuwa tayari kufa kwa sababu ya Hilo. Wakaangaliana na kuangaliana, midomo ikakutana na menginr kuendelea. Mengine yakuiburudisha miili yao na kuipa nguvu. Kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake.. hamu ya kuweza kuifanya dunia iwahurumie. Hapakuwa na kizuizi hata pale walipoangukia kitandani. Hawakuwa na kizuizi hata pale kitanda kilivyowapokea na kuwapa hifadhi. Burudani ikatendeka katika namna ya ufundi mujarabu. Ufundi ambao ulimuacha teddy akiichanisha miguu zaidi na Zaidi. Akiutoa uhuru katika namna ya kumsusumia mtendaji. Ulikuwa mchezo mzuri sana, ulikuwa mchezo wa kuvutia na kupendeza. Mchezo ambao mwisho wake uliwaacha wote wakitazama kwa muda kila mmoja akiwa pembeni kwa mwenzake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******



    Upepo ulivuma taratibu katika pwani ya bahari ya hindi eneo la kigamboni. Ulikuwa upepo uliovuma katika aina fulani ya kuuongeza uhai katika namna ipendezayo. Pembeni kabisa mwa fukwe maarufu itwayo Mikadi, watu wawili walikuwa wamekaa pembezoni kabisa mwa ufukwe ule huku macho yao yakitizama mlango wa kuingilia katika fukwe hizo. Walionekana ni wenye kusubiri kitu ama kuchunguza kitu. Nyuso zao zisizo hata na tabasamu zilikuwa zikizunguka huku na kule kuonyesha umakini. Hawakutaka kupitwa ama kuachwa na kitu chochote. Mmoja akiwa amevaa kaptura fupi na tishite ya kumbana sambamba na viatu vyepesi chini. Huyu wa pili alikuwa mrefu mweusi, alivaa suruali ya kitambaa, shati la rangi nyekundu, sambamba na Viatu vyeusi. Huyu hakuonekana kama ni Raia wa Tanzania. Watu hawa wawili hawakuwa hapo kwa bahati mbaya. Walikuwa hapo kwa sababu ya kuianza kazi yao. Kazi iliyowatoa nchi kenya na kuwaleta hapa Tanzania. Kazi ya kufuata nyendo za watu watatu ambao walikuwa hatari sana. Leo walikuwa hapa mikadi wakiwa na picha ya Vicky mkononi. Vicky mdogo wa Teddy. Fununu za watu na uchunguzi wao wa awali waligundua kuwa Vicky alipenda sana kutembelea Hapo kila mwisho wa wiki. Hivyo ilikuwa Rahisi kuianza kazi yao mapema ili kumlazimisha teddy afanye kile wanachotaka hasa pale watakapo kuwa wamemteka Vicky. Macho yao yakaendelea yakiangalia kila mtu aliyekuwa akiingia hapo.

    Wakati wao wakilifanya hilo la kumsubiria Vicky, kushoto kwao umbali wa hatua ishirini alikaa msichana mmoja mrembo sana akionekana kuchezea simu huku mara moja moja akiwatupia macho wanaume wale wawili. Mkononi alikuwa na camera ndogo ya kirusi yenye ukubwa mfano wa kibiriti. Ilikuwa camera maalum ya kuchukua matukio makubwa katika muda mfupi na kwa siri sana. Safari ya msichana huyu kuja hapa kwenye fukwe hizi ilianza tokea usiku wa Jana pale alipowaona watu hawa wakishuka uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Uonekanaji wa watu hawa walipokuwa wakishuka sambamba na wengine watano ndio sababu iliyofanya yeye kuamua kuingia kazini sambamba na wenzake ambao nao walijigawa katika kuwafuatilia watu hawa huku wakiripoti moja kwa moja Makao makuu ya Idara Ya ujasusi. Kila kitu kilifanywa kwa usiri mkubwa sana tokea pale Masimba alipowasilisha Ushahidi baadhi wa kumhusisha hayati waziri mkuu na biashara haram ya madawa sambamba na nyara za serikali. Majasusi wengi walikuwa wakiwafuatilia Jimmy sambamba na washirika wengine. Kila alipokuwa akikanyaga Jimmy, watoto wa makumbusho nao walikuwa wapo nyuma wakinusa na kutafuta wapi kapita. Ulikuwa upepelezi wa kiwango cha hali ya juu. Hata pale Jimmy alipokwenda kuwapokea vijana hawa katika uwanja wa ndege, mbwa wa kunusa harufu yoyote iliyojificha walikuwa nyuma yake wakimtizama. Ingawa vijana wale walishuka tofauti pale uwanjani, lakini haikuwa ngumu majasusi hawa kuwagundua. Hotel walizofikia zikawekwa wahudumu wazuri wakike ambao walikuwa ni undercover. Mienendo yao ikachunguzwa kila walipotoka na hata kurudi. Wana usalama wakike na kiume walikuwa wakipishana kama wafanyakazi wa hotel husika.



    Hata leo hii walipotoka na kuja pale kwenye ufukwe , nyuma hawakujua kuwa wapo wa na usalama wakiwafuatilia kwa siri kubwa. Wakiwa wao wamekaa wakichunguza wanaoingia na wanaotoka, watu watatu waliokaa sehemu tofauti macho yao yalikuwa yakiwatizama wao kufuata kile ambacho wao wanakitenda. Macho ya wana usalama wengine yalikuwa yakifuata uelekeo wa macho ya watu wale, huku yule wakike akichukua picha za video na kutuma makao makuu. Wakiwa bado katika hilo wakamuona mtu akiiingia katika namna ya kuvutia. Alikuwa mwanamke mrefu mwembamba, alionekana mfano wa msichana wa kinyarwanda kwa mwendo wake na hata umbile lake. Aliingia akiwa amewashikilia watoto watatu, watoto ambao kwa muonekano walikuwa ni wachangamfu sana. Huyu alikuwa vicky mdogo wa Teddy. Alikuwa sambamba na Abby, Queen na Amanda. Alikuwa akiingia hapo kukutana na mtu ambaye alimpigia simu usiku wa jana na kumuomba wakutane hapo kwa mazungumzo. Vicky alitembea huku akipepesa macho yake huku na huko. Simu ilikuwa sikioni akiipiga namba ya mtu husika ambaye alimwambia yupo hapo mikadi. Watoto nao walikuwa wakimtizama kwa namna fulani ya kusubiri kuambiwa twendeni huku. Wakati wote huo macho ya wanausalama hayakucheza mbali na hapo. Ni wakati wakilitizama hilo wakamuona Vicky akipaaa juu na kuanguka chini. Kilikuw kitendo kilichotendeka ndani ya sekunde tano. Watoto wakapiga mayowe.. wana usalama wakagundua kuchelewa kwao, huyu akatoka hapa na yule kutoka pale.. kila mmoja akiwakimbilia watoto waliokuwa wakilia Juu ya mwili wa vicky ambao ulitapakaa Damu. Ilikuwa taharuki kubwa katika fukwe zile. Macho ya wanausalama wengine yalizama kwenye kutizama mtu ambaye angeonyesha utofauti katika eneo. Wakati watu wakiendelea kukimbia hovyo, watu hawa wawili nao waliinuka na kuanza kuelekea sehemu ya tukio. Huyu msichana naye akainuka kuelekea huko akihakikisha hagunduliki kwa mtu yoyote. Alikuwa akitembea huku macho yake yakitembea huku na huko. Hatua kumi katika mbio hizo akamuona mtu akijiunga katika msafara ule wa watu wawili. Watu ambao yeye alikuwa nyuma yao akiwatizama. Mtu huyu watatu ni mtu ambaye ilimbidi apunguze mwendo kumuangalia vizuri. Mshangao ukatamalaki usoni. Pale alipomgundua mtu huyu. Alikuwa Amemuona Masimba akijiunga na watu hawa. Ni wakati akilishangaa hilo, akaliona Jingine, jingine ambalo lilimuacha mdomo wazi.



    Alikuwa Masimba katikati ya watu wale. Watu ambao walikuwa wakiwachunguza na kuwafuatilia. Wakati akilifikiria hilo akaliona jingine likitokea katika uharaka ambao hakuutarajia na kuutegemea. Watu waliokuwa wameongozana na masimba wakikimbia kwa pamoja sekunde mbili nyuma, sekunde hii walikuwa wakianguka chini katika namna ya kushangaza. Matundu mawili kwenye miili ya watu wawili ilitosha kubwambia na kumjulisha mwanadada yule kuwa hapakuwa na uhai katika miili iliyotambalajika pale chini. Miili ya hawa watu wawili waliokuwa katika uchunguzi. Hata pale Masimba alipogeuka na kumwangalia mwanamke yule kisha kutabasamu, mwanadada yule ndio kwanza alikuwa akigundua kuwa masimba alikuwa amewagundua hila zao katika kuwafuatilia watu hawa. Akaruhusu macho yake yamtizama masimba alivyokuwa akitembea katika aina imvutiayo, Akahisi labda Alikuwa akimtizama Willy Gamba. Akaliacha hilo lipite katika aina ya kuuburudisha moyo na hata moyo wake. Alikiwa akimtizama masimba kanakwamba alikuwa akilitizama tunda tamu kutoka juu ya mti mbichi. Hakujua ni saa ngapi alifika sehemu ya tukio. Mbele ya macho yake mwili wa mtoto mzuri ulikuwa umelala chini ya mchanga damu zikichuruzika. Amanda, Abby na Queen walikuwa wakilia pasipo mpangilio. Masimba alikuwa chini ya mwili wa Vicky wakati wanausalama wengine walikuwa wamemkinga kwa kumuweka katikati. Macho yao yakitizama Huku na Huko. Vicky hakuwa akipumua tena, alikuwa ametulia Juu Ya mchanga akiwa tayari ni Marehemu. Hilo lilionekana kama ndoto kichwani kwa Masimba. Ndoto ambayo asingependa kuiota katika maisha yake. Ni vipi atamwambia Teddy kuhusu hili? Huo ulikuwa mtihani mkubwa sana. Akainuka pale chini safari akiwaendea watoto wale waliokuwa wakilia. Alipowafikia aliwakumbatia kwa pamoja kabla ya kuondoka nao huku akilindwa na Wana usalama sambamba na wanajeshi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kitengo cha mizinga ambao kambi yao ilipakana na ufukwe ule. Aliongozwa mpaka kwenye gari ambayo ilikuja na wanausalama wale. Akawapandisha watoto kisha naye kujipakia. Kabla ya kuondoka akamvuta mwana usalama mmoja na kuongea naye kitu. Baada ya hapo akawasha gari na kuondoka akipishana na Gari zaidi ya tano za polisi zikielekea Sehemu ya tukio. Aliendesha gari huku kichwa chake kimevurugika. Kitendo cha vicky kupigwa Risasi huku yeye yupo hapo hapo kilikuwa kitu cha aibu sana. Ni jana tu usiku alipoipata taarifa ya Vicky kupigiwa simu. Ni yeye aliyemruhusu Vicky akutane na watu hao waliompigia simu licha ya hapo mwanzo kukataa, licha ya Teddy kuukataa huo mpango , lakini Masimba alimhakikishia usalama wa Vicky kuwa kitakachotokea Atakibeba yeye. Leo hii hapa Vicky alikuwa amelala akiwa hana uhai. Atamwambia nini Teddy? Lilikuwa swali lililomkoroga na kumvuruga. Alitambua kosa lake kubwa ni kushindwa kumlinda Vicky mpaka kupelekea kuuawa. Ingawa hakujua wapi alipofeli, lakini moyoni alijikuta akimsifu muuaji aliyeifyatua Risasi na kumuua vicky. Alimsifu kwa vitu vitatu, vitu ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kuvitambua. Cha kwanza ni Usiri wa mtu huyu aliyemuua Vicky. Usiri wakuingia mahala pasipokuonekana. Kitu cha pili ni ufyatuaji wake wa Risasi katika kadamnasi ile. Ufyatuaji wa aina ile hufanywa na watu wataalam katika taaluma ile. Kuiruhusu risasi kumfikia mlengwa akiwa amezungukwa na umati wa watu ilionyesha mtu huyu alivyo hatari.



    Kitu cha tatu niuondokaji wa mtu huyu eneo lile baada ya kufanya mauaji. Hakumuona akiondoka katika eneo lile la fukwe. Hakumuona akisimama na hata kukimbia katikati ya umati. Hilo kwa Kwake lilikuwa suala jingine, suala ambalo lilimpa uhakika kuwa kazi ile ilikuwa ngumu sana na ilifanywa na mtu mwenye utaalam wa hali ya juu. Kumuua mtu katikati ya umati kisha kuondoka katika namna ya kutokuonekana ni wazi kuwa muuaji alikuwa Jasusi wa kutupwa. Akayatoa mawazo yake huko sasa alikuwa akiwafikiria watu wale wawili ambao aliwaua. Hawa ndio watu pekee ambao aliwahisi kuwa ndio waliompigia simu Vicky.. hakutambua kuhusu uwepo wa mtu wa tatu licha ya kuwahi kwake mapema kufika sehemu ya ahadi. Damu ya vicky ilikuwa mikononi mwake, damu ya vicky ni damu ambayo ilitakiwa kulipwa kwa mikono yake. Hali ilishakuwa katika kuhitaji umakini sana. Alipofikiria taarifa hii itakapomfikia Teddy, kipi kitafuata, hakujua lakini aliuona mwisho wake katika mahusiano yao. Teddy alimpenda Sana Vicky, alimpenda kupita uwezo. Nini ambacho kitatokea Masimba atakapompa taarifa? Haikuwa Rahisi sana kuipokea hiyo. Akapiga moyo konde na kuelekea huko.



    ******



    Alikuwa amejilaza kitandani akiisubiri kwa hamu taarifa ya kukutana kwa vicky na watu hao waliompigia simu. Muda wote alikuwa amejilaza akimuwaza mdogo wake, lakini kitu kimoja ambacho kilianza kumshangaza tokea asubuhi ni kuhusu moyo wake kupiga kila pale alipolitaja au kukumbuka ahadi ya vicky na watu hao. Alijua vicky hakuwa na ujuzi wowote katika kupambana na hata kutumia Silaha. Alijua ni rahisi sana watu kumuondoa kama wataamua. Hata pale alipomkataza kukacha wito huo, alijua mdogo wake hawezi kuwakwepa watu hao. Aliendelea kusubiri huku wasiwasi ukizidi. Hata mlango ulivyofunguliwa kisha mtu kuingia, Teddy hakuinuka bali aliinua macho na kutizama. Akajikuta akiangaliana na tukio ambalo lilimpa baridi. Alikuwa akiwatizama wadogo zake wote watatu wakiwa wanamuangalia Huku wakilia. Macho yake yakatua kwenye mavazi waliovaa. "Damu" ndio kitu alichokiona. Punde alikuwa amechupa pale kitandani akaelekea waliposimama Wadogo zake. "Sweet Yuko wapi Vicky? Aliuliza Teddy akimtingisha mdogo wake kwa nguvu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Samahani Mpenzi, Ujinga wangu umesababisha kumpoteza Vicky. Vicky hatupo naye tena." Ilikuwa sauti kutoka mlangoni. Sauti ambayo haikusikika vizuri masikioni kwa Teddy.



    "Una Semaje Masimba? Unasemaje wewe? Namtaka vicky wangu akiwa Hai hapa. Sitakusikiliza kwa chochote." Aliongea Teddy safari hiii akiinuka kumfuata Masimba. Bastola yake mkononi akimuendea kwa shari. Machozi yalikuwa yakishuka mashavuni. "Namhitaji mdogo wangu akiwa hai.. la sivyo nitakuua au kuviua vifaranga wako wale wawili." Aliongea Teddy akionyesha kutokuwa na utani kabisa. Alikuwa akimaaanisha kile alichokuwa akisema. Masimba bado alitulia akimuangalia Kwa umakini. Sio kwamba hakuumizwa na kifo cha Vicky, sio kwamba hakuwa na maumivu juu ya kilichotokea. Alikuwa na maumivu sana moyoni. Lakini maneno ya Teddy kuwa atawaua watoto wake hakuwa amelitegemea kabisa. Awaue wanawe France na Yaseer? Kilikuwa kitu ambacho hakukitegemea. "Unataka kuwaua wanangu kwa sababu ya kilichotokea? Wanangu wanahusika nini katika hili? Niue mimi mwenyewe ili ufurahi.. waache watoto wangu. Aliongea masimba huku akiushika mkono wa Teddy ulioshika bastola na kuinua Juu usawa wa kichwa chake. "Naomba Uniue mimi, Yaseer na France naomba uniachie. Mbona wewe ulisababisha kuuawa kwaa mama lakini sikutaka kulipa kisasi? Mbona mwanangu Yasser mpaka leo yupo hospitalini kwa sababu yake, lakini sikulipa kisasi kwa hao? UNADHANI SIKUUMIA



    Wewe Mbona umesababisha kifo cha mama yangu, uliona nikienda kulipa kisasi? Mwanangu Yasser mpaka leo yupo hospitalini sababu yako, uliniona nikienda kuwagusa Amanda na Abby? Au kuna siku umeniona nimemgusa sweet na hata patra? Unadhani mimi siumii? Unadhani sijaumia kumfukia mama kwa upuuzi wako? Ningetaka kukuua mpaka sasa ungekuwa marehemu. Lakini kwa kuwa umeona kitu kilichofanyika ni makusudi, ruhusu risasi yako iniondoe Hapa Duniani. Mtu badala utulie tuangalie tunapambana vipi na watu hawa wewe unapayuka payuka tu. Piga hiyo risasi yako sasa. Aliongea Masimba huku akiutingisha mkono wa Teddy. Teddy akaganda kama sanamu huku mdomo wa bastola ukiwa kwenye paji la uso wa Masimba. Punde akaishusha bastola kisha kuwafuata wadogo zake na kutoka nao ndani ya Nyumba huku akimuacha Masimba akiwa ametulia akimuangalia. Kichwa chake bado hakikutulia kutokana na kifo cha Vicky. Hakuna kitu kilichomkosesha amani katika kazi yake hii kama kuzudiwa akili na watu. Alipenda siku zote kuibuka mshindi katika kila kitu anachokianzisha. Lakini leo hii alikuwa amezidiwa ujanja na mtu mmoja. Ujanja na mtu ambaye hakujua alikuwa ni nani. Aliondoka pale aliposimama na kuelekea kitandani kwake. Uso wake ulionyesha kuchoka sambamba na mwili wake. Hakupenda kilichotokea kimtoe kwenye njia ya kuimaliza hii kazi. Hakupenda kilichotokea kiharibu mipango yake. Ni kweli vicky amekufa lakini kufa kwake hakutufanyi sisi tukakata tamaaa. Hilo likamuamsha hapo kitandani mpaka bafuni. Maji yakamiminika mwilini kisha sabuni kupita juu. Alipotoka hapo akaingia chumbani na kuchagua mavazi fulani. Punde alikuwa akitoka akiwa mtu mwingine. Mawazo yake aliamua kurudi sehemu ya tukio. Alitaka kurudi Ufukwe wa Bahari ya Hindi sehemu alipouawa Vicky. Alitaka kurudi kwa mara hii akiwa kwenye utimamu. Utimamu wa akili sambamba na mwili. Lakini aliamua kupita hoteli zote ambazo aliambiwa kuwa walifikia wageni hawa ambao wawili kati yao ndio wale waliouawa Jana. Alitaka kwenda kuuliza kama kuna chochote kimenuswa hasa baada ya tukio la jana pale ufukweni. Alifika hotelini na kupokelewa na 'wahudumu' kwa bashasha na ukaribu. Akachagua sehemu ya pembeni kabisa mwa hoteli ile. Akakaa hapi na kuagiza Chakula. Mhudumu mrembo aliyevalia kinadhifu akatokea mbele yake akiwa na sahani ya chakula na matunda mkononi. Kufika kwenye meza ya masimba akainama na kukitua kile chakula pale mezani. Baada ya kukitua hapo akaondoka katika namna ya kuvutia. Baada ya mhudumu yule kuweka chakula pale na kuondoka, masimba akaiinua kidogo sahani ya chakula, akakutana na bahasha ndogo ya kaki. Akaiangalia kwa umakini kidogo, baadae akafanya kama kupuuzi na kuendelea na chakula. Baada yakumaliza kula akatoka ndani ya hoteli na kutembea kwa mguu kuelekea sehemu yenye kijiwe cha tax. Muda wote alikuwa akitembea huku macho yake yakizunguka huku na huko. Alichokifanya na kuamua kukutembea ili kuw ni mbinu moja wapo ya kutaka kujua kama anafuatia ama lah.



    Mpaka anafika kwenye kituo cha tax hakuona mtu yoyote aliyekuwa akimfuatilia hata kumtilia mashaka. Akaingia kwenye tax kisha kuamuru dereva ampeleeke kigamboni.



    Kitendo cha dereva kutajiwa jina la sehemu husika anayotakiwa kwenda hakuficha mshangao wake. Akatamani kuuliza, lakini kabla yakuuliza akaamua kumtizama abiria wake huyu anayetaka kupelekwa huko ufukweni. Macho ya mtu huyu yalimfanya Dereva anyamaze. Hakutaka tena kuuliza. Akakanyaga mafuta na muda mfupi walikuwa wakivuka pantoni wakielekea Ufukwe wa mikadi. Muda wote huko hakutaka kuifungua bahasha aliyopewa. Alitaka kwanza kufika eneo la tukio ndipo hapo angepata muda wa kuifungua bahasha.



    ******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ufukwe ulimlaki katika utulivu wa hali ya juu wakati huo ikikaribia kufika saa moja za usiku. Ukimya wa ajabu ulimpokea aliposhuka kwenye tax na kuongoza ndani. Utepe wa rangi ya manjano sambamba na Askari wenye silaha nzito walimpokea katika namna ya kumuangalia. Mwili wa Vicky haukuwepo tena kuonyesha kuwa ulikuwa umepelekwa chumba cha kuhifadhia maiti. Aliongoza na kuwapita askari wale kisha kuongoza sehemu ile ambayo alikuwa amekaa mchana ule kabla ya kifo cha vicky. Alitulia pale akiangaza macho huku na huko. Kanakwamba angeweza kumuona muuaji. Mawazo yake yakaishia kwenye bahasha ndogo ambayo alipewa na wanausalama pale hotelini. Akaichukua kutoka kwenye koti lake na kuishika mkononi. Wakati akitaka kuanza kuifungua akaisikia michakato ya miguu kama ya mtu. Sekunde moja mkono wake ulikuwa juu ya bastola yake tayari kwa kufanya lolote. Lakini alijikuta akitizamana na mwana usalama yule aliyemuacha pale ufukweni wakati wa tukio. "Kuwa makini kijana unapoingia anga hizi katika namna hiyo." Aliongea Masimba huku akimpa ishara ya kijana yule kukaaa.



    "Sorry mkuu imenibidi nitumie njia hii kukwepa macho ya watu. Watu tunaopambana ni hatari sana. Kama tumeweza kuambulia patupu mchana na kumpoteza msichana yule, basi tutambue watu ni Hatari zaidi." Aliongea kijana yule akikaa chini. "Nikweli usemayo, maana kwa Jinsi muuaji alivyotuacha katika umati ule. Nilazima tuwe makini. Vipi una kitu chochote umekinasa baada ya mimi kuondoka? Akauliza Masimba. "Yeah kuna kitu nimekipata mkuu. Baada ya taharuki ile na ule mkanyagano wa watu kuna kitu ambacho nilikiona wakati wewe ukiondoka." Akajibu mtu yule. "Kitu Gani? Aliuliza Masimba. "Mwanamke mwenye mtoto mdogo." Akajibu kijana yule.



    "Mwanamke mwenye mtoto? Akauliza Masimba kwa Utulivu. "Yeah mwenye mtoto mdogo, alikuwa mtu wa mwisho kutoka humu ufukweni baada ya taharuki. Utokaji wake na hata uangaliaji wake, haukua wa kawaida. Nilipolishtukia hilo nikaamia kumfuatilia kwa siri bila mwenyewe kugundua. Lakini wakati tunafika pale feri, mwanamke yule alinipotea katika mazingira ya kutatanisha. Na sikumuona tena licha ya kuwasiliana na wenzetu." Alijibu kijana yule. "Mwanamke mwenye mtoto mdogo? Lilikuwa swali lililojengeka kichwani kwa masimba. Taswira ya mwanamke mwenye mtoto aliyemuona kwenye jengo la benki ya taifa ya biashara ilimjia usoni kwake. Lakini mwanamke yule mbona aliuawa? Hilo pia likamchanganya. Huyu mtoto alikuwa nani? Na kwa nini anatembea na watu hawa? Hawa wanawake ni wakina nani? Kama yule aliuawa huyu wa leo ni nani?. Yalikuwa maswali yaliokiumiza kichwa cha masimba. Akauona ni muda wa kuifungua ile bahasha. Akaifungua kisha kukitoa kitu kilichokuwa ndani yake. Ikajikuta akitizamana na picha, picha ya mwanamke akiwa na mtoto mdogo wa kiume. Chini kulikuwa na maandishi madogo "Mwananyamala A". Baada ya kusoma maandishi yale akaunyoosha mkono wake kumpa kijana yule aitizame ile picha. "Mtu wetu ndio huyu, huyu ndiye nilimuona hapa ufukweni muda mfupi uliopita." Aliongea yule kijana akiirudisha picha ile mikononi kwa Masimba. "Tuondoke hapa twende mwananyamala, nataka nikapate maelezo kutoka kwa mwanamke huyu." Aliongea masima akiinuka tayari kwa kuianza safari kuelekea mwananyamala.



    ******



    Kama ilivyo wilaya ya kinondoni ifikapo usiku, ndicho walichokutana nacho masimba na kijana yule waliposhuka pale mwananyamala. Madada poa walikuwa wengi wakiwaiita na kuwaonyesha biashara yao ya kuuza sukari guru. Kila mmoja alikuwa akipandisha nguo yake na kuwaonyesha kile kitu. Masimba na kijana yule hawakuonyesha kulishangaa hilo. Wakaingia kwenye uchochoro fulani uliowapeleka mpaka uwanja wa ccm mwinjuma. Wakapita pembeni mwa kituo kidogo cha polisi. Walipoingia katika uchochoro mwingine wakajikuta wakitizamana na Nyumba husika.



    Walikuwa wakitizamana na nyumba husika. Nyumba ya mwanamke anayesadikika kuwa ndio aliyemuua Vicky katika fukwe za mikadi. Ilikuwa nyumba nzuri ambayo ilizungushiwa ukuta wenye urefu wa kawaida. Mbele kulikuwa na geti moja kubwa sambamba na mtu mmoja ambaye alikaa nje akiwa na gongo mkononi kuonyesha kuwa alikuwa mlinzi wa mahala pale. Masimba akamuonyesha ishara yule mpelelezi mwenzie azunguke upande wa nyuma wa nyumba ile. Huku yeye akiamua kupitia getini kuongea na mlinzi yule. Aliondoka pale akitembea katika mwendo wa taratibu. Mwendo ambao ulimuonyesha kama ni mpita njia wa kawaida. Alipofika karibu kabisa ya mlinzi yule akainua mkono kama ishara ya kumtaka kusogea. Mlinzi yule akiwa na rungu mkononi akasogea mpaka pale alipokuwa amesimama Masimba. Lakini wakati akisubiria kusikia chochote kutoka kwa mtu huyu aliyemuita, akashtukia mdomo wa bastola ukiigusa shingo yake. Mlinzi yule akashtuka nusura ya kuanguka. "Naomba unifungulie geti niingie ndani, ukileta ubishi tu naufumua Ubongo wako." Aliongea masimba huku akiukandamiza Mdomo wa bastola shingoni kwa Mlinzi yule. Huku mlinzi yule akitetemeka alitembea taratibu kuelekea getini. Baada ya kufika hapo akainama na kulifungua geti kisha kutangulia ndani. Bado mdomo wa bastola ulikua nyuma yake ukimsindikiza. Macho ya masimba yakapokewa na kiza fulani kuonyesha kuwa mwenye nyumba hakuwa mtu wa kuwasha taa katika nyumba hiyo. Kitendo cha kuingia sambamba na mlinzi kikafuatiwa na pigo la kitako cha bastola kutua kisogoni. Mlinzi yule akaanguka chini taratibu na kupoteza fahamu. Akaondoka hapo akinyata mpaka mlango wa kuingilia ndani. Wakati akitaka kuugusa mlango wa kuingilia ndani, akausikia mngurumo wa gari ukitokea kwa nje kuonyesha kwamba kuna gari ilikuwa imesimama. Akajivuta haraka mpaka nyuma ya geti kisha taratibu akaanza kulifungua geti mpaka usawa unaotakiwa. Punde akaiona gari ikiingia ndani. Ni gari ambayo aliikumbuka kuiona mahali fulani. Akaitizama gari ikitembea mpaka nyuma ya jengo sehemu ambayo ilikuwa na sehemu maalum ya kuegesha magari. Akauona mlango ukifunguliwa kisha mwanadada yule akishuka. Alikuwa yule yule wa kwenye picha aliyopewa, na alikuwa yule yule aliyemuona pale benki siku ile. Baada ya mwanadada yule kushuka akaonekana akiangalia kitu fulani ambacho wao hawakuwa wamekiona wala kukifahamu. Baada ya hapo akaufuata mlango, lakini kabla hajaufikia mlango, mwanamke yule akazimisha mkono mfukoni na kuchomoa bastola kisha kuishikilia mkononi. Macho yake aliyaelekeza getini akitizama kila kitu, geti lilifungwa na mlinzi hakuonekana pale. Mwanadada yule akasogea huku bastola ikiwa mkononi.



    Lengo lake ilikuwa kwenda mpaka nje bila kujua kwamba sehemu anayoelekea ndipo sehemu ambayo alisimama MASIMBA. Akaendelea kutembea zaidi na zaidi, akaendelea kutembea akiupita mti ambao ulikuwa umepandwa ndani ya nyumba ile. Kuupita mti akalifikia geti na kutaka kulifungua. Mchakato wa vishindo vya mtu nyuma vikamfanya ageuke mithiri ya mshale. Lakini alikuwa amechelewa, kwani wakati anageuka akakutana na pigo moja lililomlegeza. Pigo lililotua kwenye mishipa ya fahamu. Binti akaanguka chini mithili ya furushi. Masimba akainama ili kumuinua yule mwanamke tayari kwa kuondoka naye. Lakini hakuwahi kufanya hivyo, hakuwahi kwa kuwa muda ule ule akawaona watu wakiingia mithili ya Ninja. Walikuwa wakishuka na ukuta mfano wa Paka. Tayari Masimba alishahama pale nakuuzunguka mti kisha kukaa nyuma yake. Macho yake yalikuwa yakiwaangalia watu hawa walioingia mfano wa Ninja. Aliuangalia utembeaji wao na hata pishana yao. Alikuwa na uwezo wa kutumia risasi lakini hakutaka hilo kutokana na kutaka kuwajua watu hawa. Kila utembeaji wao na namna ya kujipanga kwao akatambua kuwa hawa hawakuwa watu wa kawaida, hawakuwa watu wa nchi hii. Hawa walikuwa wengine kutoka nchi nyingine. Watu hawa wakamjengea maswali, maswali ambayo yalimuweka katika kutokufahamu namna Jimmy na watu wake walivyoota mizizi katika nchi hii ya Tanzania. Bado hakutaka kuiruhusu bastola yake kufanyakazi. Alitaka kuwaangalia watu hawa lakini vile vile alihofia mwanamke yule aliyepoteza fahamu kurudiwa na fahamu.



    Wakati hilo likiendelea mara akaiona taa ya sebuleni ikiwashwa, kitendo hicho kikaonyesha kutokutarajiwa na hata hawa watu waliofika hapo. Kwani kuwashwa kwa taa kukawafanya hata wao washangae huku kila mmoja akichupa na kuangukia pembeni katika namna ambayo ulionekana ujuaji wao katika medani hiyo. Ukimya wa ajabu ukatamalaki katikati yao. Kila mmoja alikuwa ametulia katika sehemu yake. Punde taa zikazimwa kwa mara nyingine. Kisha milio ya risasi ikafuatia



    Taa zikazimwa na wakati ule ule risasi zikaanza kuvulumishwa kama njugu. Watu wale walikuwa wakichupa katika aina itiayo raha machoni. Raha ya kuwaangalia na hata kupambana nao. Masimba hakuliona hilo kama ni la kawaida. Bado alikuwa ametulia akimuangakia mwanamke yule aliyemuua Vicky. Hakutaka aondoke na kupotea katika macho yake. Hakutaka aondoke kabla hajatapika ukweli wote. Hilo likamfanya awaangalie watu hawa katika umakini wa hali ya Juu, Umakini wa hatua zao na hata mienendo. Bado risasi zilikuwa zikivurumishwa. Safari hii mpigaji huyo wa risasi alikuwa amebadili uelekeo. Sasa alikuwa akipiga kuelekea pale walipojibanza watu hawa mfano wa ninja. Ni hapo Masimba alipohitaji kufanya kitu, alijua kijana mwenzie ndiye ambaye anaifanya hiyo shughuli. Ukauona ulikuwa muda wake, muda wake kumsaidia. Akajiondoa pale mfano wa kivuli. Akitembea na giza kuelekea upande ule walipo watu wale. Bastola mkononi macho yakiangalia huku na huko. Alikuwa akifuata usawa wa kule zinapotoka Risasi. Kule ambako alihisi kuwepo kwa kijana yule. Wakati anakaribia kwenye mti mmoja nyuma kabisa ya nyumba ile, akamuona mru akiwa amejibanza pembeni kidogo mwa ukuta wa nyumba ile. Mkono wenye bastola ukanyooka kuelekea huko. Punde mlipuko mdogo ukasikika masikioni kwake mwenyewe, mlio ulioambatana na mtu kupiga yowe la uchungu kisha kutulia katika muda huo huo. Masimba akazidi kusonga, bado risasi zilisikika masikioni mwake. Sasa alikuwa amefika pale alipoangukia mtu yule. Risasi ilikuwa imefumua kichwa chake, imekifumua katika aina nayotia Raha. Wakati bado anauangalia mwili wa mtu huyu aliyekuwa amekufa. Akauona mlango wa nyumba kubwa unaotokea nyuma ukifunguliwa. Kufunguliwa kwa mlango wa nyuma ya nyumba kubwa kukafuatana na ukomo wa milio ya Risasi. Hilo likamfanya hata yeye atulie na kutizama nani atatoka ndani katika muda ule. Hazikupita hata sekunde tano akamuona mtu akitoka kisha kuuparamia ukuta na kuangukia upande wa pili. Wakati akilishangaa hilo akamuona mtu wa pili akitokea pia hata yeye alifanya kama alivyofanya mtu huyu aliyetangulia. Lakini kilichomsisimua kwa huyu mtu wa pili ni kule kumjua kwake, alikuwa ni yule msichana. Msichana ambaye muda mfupi uliopita alikuwa amepiteza fahamu.. Hakutaka kuliacha hilo lipite, hakutaka kuliacha liende pasipo kwenda nalo. Wakati akijitayarisha kupiga hatua kusonga pale, akamuona mtu watatu akitoka, mtu ambaye aliruka katika namna fulani ambayo ilikuwa tofauti na hawa. Huyu alikuwa ni yule mpelelezi mwenzake. Hata yeye alichupa lakini wakati huo huo akiupiga mluzi wa ishara ya hatari. Haukuwa mluzi usiofahamika, ulikuwa mlio uliokuwa ukitoa ishara ya kuwa na hatari sehemu husika. Sekunde hii alikuwa amesimama na hata sekunde ya tatu akikuwa akitua Nje lakini ndani ya Sekunde ya Tano Mlipuko mkubwa Ukatamalaki eneo lote. Nyumba ile ilikuwa akiteketea kwa moto. Akasimama mahali kuitizama nyumba ilivyokuwa ikiteketea. Aliitizama kwa Ghadhabu kubwa. Hatimaye alikuwa ameshindwa kumtia nguvuni muuaji Wa Vicky. Hili lilimuuliza sana. Akaondoka Eneo la tukio akiapa kuufanya usiku ule, kuwa usiku wa kufa na kupona. Ulikuwa ni wakati wa kupambana na Jimmy. Watu aliowaona wajiingia pale hawakua watu wa kawaida. Aliiona hatari na ugumu wa kazi hii endapo ataendelea kumuacha Jimmy akipumua. Ilikuwa ni Lazima amsafirishe ili kuizima hii mipango yake. Mipango ya kuchukua watu kutoka sehemu fulani kuwaleta sehemu fulani kwa minajili ya kujilinda asifikiwe. Hilo lilimfanya aipate hamu ya kwenda kuongea na Teddy. Hamu ya kwenda kumtoa kwenye ukataji tamaa na kumjaza nguvu za kupambana. Nguvu za kulipa kisasi kutokana na kifo cha Mdogo wake. Aliondoka Mwananyamala usiku ule akielekea Toangoma kigamboni nyumbani kwa marehemu vicky.



    ******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Alikuwa amejiinamia machozi yakishuka taratibu machoni. Hakua akiamini kile alichokuwa akikitizama. Mbele ya macho yake ulikuwepo mwili wa mdogo wake ukiwa umelala bila uhai. Aliutizama mwili wa Vicky akishindwa kupambana na maumivu ndani ya moyo wake. Maumivu makali ambayo yaliileta Hasira moyoni mwake juu ya Masimba. Alijikuta akimchukia masimba katika aina ambayo haikuweza kumithilika. Ni kweli alimwambia kuhusu mdogo wake kutokuwa mzoefu katika kile anachotaka kukifanya. Alimtahadharisha masimba kuhusu uhatari wa watu hawa katika kumpeleka vicky. Lakini ubishi wa masimba ukamfanya afanye kile ambacho alikiamini. Ni hilo lililosababisha kumpoteza Vicky. Kumpoteza mdogo wake kipenzi. Mdogo wake aliyekuwa akimpenda sana. Aliinua uso wake kuuangalia tena mwili wa vicky. Machozi yaliendelea kushuka zaidi na zaidi. Mdogo wake alikuwa ametuli sehemu ya mochwari akiwa kama amelala. Alikuwa kama amefumba macho. Vicky alikuwa hapumui tena. Hakujali uwingi wa maiti kule mochwari, alitaka kulala mle ndani na mdogo wake. Alitaka kukaa na mwili wa vicky. "Masimba nimekufanya nini mpaka unifanyie haya? Nimekufanya nini mpaka uniondolee kipenzi changu? Masimba Roho inaniuma na kuniuma. Sitajali wewe ni nani, sitajali ulikuwa nani kwangu nitakuua Masimba, kama sio wewe nitawaua wanao na hata ndugu zako. Damu ya mdogo wangu haiwezi kwenda bure. Masimba nitakuua tu." Aliongea Teddy huki akiendelea kuushika mwili wa Vicky. Wakati akilifanya hivyo akauona mlango wa Mochwari ukifunguliwa kisha akamuona Masimba akiingia taratibu akiwa amechafuka mavazi yake kuonyesha kwamba alitoka kwenye pata shika. Alitembea taratibu mpaka ulipo mwili wa Vicky. Aliutizama kwa Muda kisha kwa sauti ya huzuni akanena. "Vicky najua damu yako ipo mikononi mwangu, najua damu yako inaweza kunigharimu damu za watu wengine kwa ujinga wangu. Lakini nauapia moyo wangu na hata mwili wako. Sitalala wala kula mpaka nimpate muuaji. Sitapumzika popote pale mpaka siku nitakapo waua watu hawa. Pumzika Vicky wangu, siku ya mazishi yako hautazikwa peke yako. Nadhani unaweza kuzukwa sambamba na wanangu. Sambamba na damu yangu." Alipomaliza kusema hayo akamuangalia Teddy usoni. "Teddy najua una hasira na mimi. Najua hata wanangu umepanga kuwaua. Nakupa Ruhusa, nenda kawaue wote harafu tuone kama ukiwaua Vicky atarudi. Kwa heri ya kuonana nitarudi tu pale nitakapo waua Jimmy na vibaraka wake." Baada ya maneno hayo masimba akatoka mle ndani na kutokomea mtaani akimuacha teddy akiangua kilio. Aliondoka akiamua kwenda kumtafuta mwanamke yule. Hakutaka kupumzika mpaka pale atakapompata mwanamke yule aliyeitoa Roho ya Vicky. Safari yake katika usiku huu ilikuwa safari ya kufa na kupona. Ilikuwa safari ya usiku kucha ya kukesha katika mapambano. Usiku wa damu na hata kifo. Aliamua kuibeba kazi hiyo peke yake, aliamua kuifanya kwa kuwa yeye ndiye aliyeianza. Usiku huu aliamua kuanzia kigamboni katika mtaa mmoja uitwao tungi. Ulikuwa mtaa ambao aliishi Mbunge wa kigamboni Bibi Grace Bwahama sambamba na familia yake. Aliamua kuanzia hapo kwanza akiamini ni lazima angemkuta hapo. Alikodi pikipiki ambayo ilimpeleka mpaka mjimwema. Kutoka hapo akachukua tax ambayo ilimpeleka mpaka mtaa maarufu uitwao magengeni. Baada ya kufika hapo akachepuka mpaka kwenye bar maarufu iitwayo kwa chacha. Kufika hapo akaungia ndani ya bar kwa kupitia mlango wa nyuma. Wakati anaingia eneo hilo akamuona kijana mmoja akipita mbele yake. Akamuita na kumvuta pembeni.



    "Mambo vipi dogo?. Akasabahi masimba.



    "Safi kaka, nikusaidie nini?. Akajibu na kuuliza.



    "Nyumba anayoishi mbunge wetu unaijua?. Akauliza tena.



    "Yeah naijua sana mkuu, tena mwenyewe yupo hapa hapa ndani." Akajibu kijana yule akinyoosha kidole kumuonyesha Masimba kule ambapo alikaa mbunge yule. Masimba akainua macho kucheki, ni kweli alimuona bibi grace akiwa na vijana sambamba na kina dada wakionyesha kufurahia kitu.



    "Chukua hii mwanangu utapata hata supu." Aliongea masimba akimkabidhi kijana yule noti mbili za elfu kumi kumi. Kijana yule huku akionyesha kutokuamini, akapokea pesa ile huku akimuangalia Masimba usoni.



    "Ahsante sana kaka, Mungu akupe wepesi na upate zaidi ya hii. Umenifaa sana." Aliongea kijana yule kwa unyenyekevu. "Usijali, lakini nisingependa haya niliokuuliza useme popote." Alionya Masimba. "Usijali kaka sitaongea popote." Baaada ya Kujibu hilo wakaachana kila mmoja akienda na njia yake. Masimba akatafut meza nzuri ambayo ingemuwezesha kuiona meza aliokaa mbunge wa kigamboni. Alikuwa akihitaji kufanya shambulizi akiwa pale pale mezani alipokaaa. Baaada ya kuipata meza iliyotupu akaichoma Bastola yake ambayo ilikuawa ndani ya gazeti na kuiweka juu ya meza. Macho yake yakawa yanautafuta upenyo wa kuipata nafasi kumlipua mbunge yule. Alitaka kumuondoa akiwa pale pale katikati ya watu.



    Bastola ilikuwa juu ya meza tayari kumuondoa mbunge wa kigamboni. Hakutaka kutumia muda mwingi kumfikia. Alichokitaka ni kumuua na kumuondoa katika uso wa hii dunia. Aliendelea kuutafuta usawa wa kuifanya kazi yake. Wakati huo wote mhudumu bado hakuwa amefika kuulizia oda. Hiyo ilikuwa ni bahati kwake. Muda mfupi alikuwa ameupata usawa, usawa wa kuweza kuiruhusu risasi kuingia mwilini kwa mbunge yule. Akaupeleka mkono wake ndani ya Gazeti. Mkono ukaishika bastola na kidole kikashuka chini ya kitufe cha kufyatulia Risasi. Sekunde ya pili risasi ilikuwa imeshatoka ikielekea ilipotumwa. Punde kichwa cha mbunge yule kikafumuka huku mwenyewe akitupwa nyuma na kwenda kujibamiza ukutani. Hakuweza kuinua mguu tena. Alikuwa tayari ameshakufa. Purukushani na mayowe ya watu yakamuondoa masimba pale alipokuwa amekaa na kujichanganya na watu waliokuwa wakikimbia hovyo huku wakipiga kelele. Alitoka mtaa wa magengeni akitembea mpaka Kituo maarufu kiitwacho Tungi stendi. Kufika hapo akaongoza mpaka alipotokea barabara iendayo kisiwani. Hapo akasimama akiangalia watu walivyokuwa wakimiminika kuelekea kule alipolifanya tukio la kumuua Mbunge wa Kigamboni. Hakutaka kusubiri wala kushangaa watu waliokuwa wakikimbizana. Alisimamisha Bajaji ambayo ilimpeleka mpaka feri, hapo akavuka mpaka upande wa pili. Hapo akachukua bodaboda ambayo ilimpeleka mpaka masaki. Nia yake ilikuwa ni kwenda kuwaangalia watoto wake. Ingawa Aliamini Teddy asingeweza kufanya kile kitu, lakini alitaka kuhakikisha watoto wanabaki kwenye usalama. Alishuka kwenye pikipiki na kuanza kutembea kwa miguu akielekea nyumbani Kwa Chief. Moyo wake ulikuwa umechafuka sana. Moyo wake ulikuwa umegeuka mithili ya mnyama. Alitamani angempata mwanMke yule. Alitamani kumpata aliyemuua vicky ili aongee naye mawili matatu. Risasi tano aliziweka kwa sababu ya kuuondoa uhai wa Mwanamke huyo. Hakuamini wala kukubali kushindwa, siku zote aliamini hakuzaliwa kwa sababu ya kushindwa. Aliamini kushinda siku zote. Kifo cha Asteria P Paulo sambamba na familia yake. Kifo cha mama yake sambamba na Dee Plus hata kama alimuua Mwamvita lakini aliamini bado alikuwa akidaiwa Damu. Damu ya watu waliouawa pasipo na hatia. Ni wapi angemuona Jimmy ili wahojiane kwa risasi? Ni wapi angemuona Suresh ili ampe tiketi yake? Hilo ndilo pekee ambalo alikuwa akilihitaji kwa aina na njia yoyote.



    ******



    Vilio vilikuwa vimetawala eneo lote la nyumba ile katika mitaa maarufu ya Toangoma. Nyimbo za kusifu na kuabudu zilikuwa zikisikika sehemu yote na kuwafanya waombolezaji nao kufuatia. Mama wa marehemu aitwaye Nina mndeme alikuwa ameshikwa huku na huku wakati wakuuga mwili wa mtoto wake. Hakuwa na nguvu ya kutembea.. Teddy alikuwa pembeni akiwa amesimama akibubujikwa na machozi. Hakuwa akiamini kama ndio kweli alikuwa akimuaga mdogo wake. Alilitizama tukio lile kama mtu anayeangalia kitu asichokiamini. Akasogea kuelekea lilipo jeneza la mwili wa mdogo wake. Akamuangalia Vicky aliyekuwa ametulia. Vicky aliyekuwa hapumui tena.

    [20/05 3:44 PM] Ibrahim Masimba: Machozi yakashuka mfano wa maji. Mfano wa maji yaliokuwa yakitiririka kutoka kwenye chem chem. Akakishika kichwa cha mdogo wake na kukiangalia katika muda ule. Hakuwa akiamini kama ndio alikuwa akimuaga vicky. Akalibusu paji lake la Uso. Punde akamuona mtoto wa marehemu aitwaye Cleapatra akitembea akisogea pale. Alikuwa mtoto mdogo ambaye bad0 alimhitaji mama yake. Lakini ukaidi na ubishi wa Masimba ukasababisha Vicky aondoke na kumuacha Patra. Teddy akaongeza kilio pale mtoto yule alipolisogelea sanduku huku akilia. Hakuna ambaye hakulia, hakuna ambaye hakuguswa na kitendo kile. Hata masimba alikuwa akiliA, Hata Masimba alikuwa akitokwa na machozi. Alikuwa akimuangalia mtoto wa vicky kwa uchungu, alikuwa akimuangalia kwa hasira. Kama asingekuwa yeye mtoto yule asingekuwa akilia pale. Ujinga wa kutokujiandaa ama kuhisi hatari kumemfanya ampoteze vicky. Hilo likamuuma na kumuuma. Hata alipokumbuka kuwa alimkosa muuaji wa vicky alijiona kweli alikuwa mjinga. Mtu kama yeye hakupaswa kufanya ujinga kiasi kile. Hakupaswa kuufanya ujinga wa namna ile. Bado alimuangalia mtoto yule alivyokuwa akilia. Ni hapo alipokuwa akimuangalia Cleopatra ndipo alipokutanisha macho na Teddy. Wakatizamana katika aina fulani ya mashaka. Licha Teddy kumti zama masimba katika macho ya shari na kisasi, masimba yeye hakukionyesha hicho kabisa. Bado macho yake yalitengeneza neno mapenzi. Bado macho yake yalionyesha kuhitaji hili na lile. Bado macho yake yalionyesha kuumizwa na kilichokuwa kikiendelea. Macho yake yaliokuwa yakidondosha machozi ndiyo yaliyo mvuta teddy aliyekuwa bado akimtizama. "Masimba analia" lilikuwa neno la kwanza kukigonga kichwa chake, akaongeza udadisi katika kumuangalia huko. Ni kweli masimba aliumia na kuumizwa, ni kweli Masimba alionyesha kuteswa na kitu moyoni. Teddy akaiona hatia katika moyo wake, licha ya matendo yake lakini hakupenda kumuona mwanaume huyu akilia. Akasogea sambamba na patra kuelekea pale aliposimama Masimba. Lakini wakati bado akitembea kumfuata, akashuhudia masimba akiondoka eneo lile na kutokomea katikati ya waombelezaji. Ni wakati alipokuwa akiliangalia hilo akaipata taarifa ya kuuawa kwa mbunge wa kigamboni Bibie Grace Bwahama . Ni taarifa hii na uondokaji wa Masimba vilivyompa majibu kuwa mtaani na sehemu nyingine haziko salama. Mkono wa Masimba ulikuwa umeanza kutoa tiketi moja moja kwa kila mtu. Kwa mara ya kwanza moyo wake ukashikwa na ile hali ya mapenzi. Alikuwa akimpenda Masimba. Licha ya kashfa zote na Tuhuma anazorushiwa, lakini bado alimpenda Masimba. Ni kweli hata masimba alikuwa akimpenda yeye. Hata sms alizokuwa akitumiwa zilimuumiza na alijaribu kuchukua maamuzi ya kuachana naye. Lakini bado Teddy alikuwa moyoni mwake. Lakini Mbona Masimba Ana0ndoka katika mazishi ya Vicky? Lilikuwa swali ambalo halikupata majibu kwa wakati ule. Majibu Juu ya kuondoka kwake. Alitamani wabembelezane, alitamani waambiane na kunong'onezana. Lakini haikuwezekana kwa kuwa Masimba Hakuwepo pale. Akamuangalia patra kisha akatabasamu. Tabasamu la uchungu na la kuumiza.



    ***********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hakuvumilia kumuangalia mtoto wa marehemu akilia, hakuvumilia kumuona teddy akilia kwa kosa alilosababisha. Damu ya Vicky ilikuwa mikononi mwake. Alihitaji kuilipa damu ya Vicky. Alihitaji kumuua mwanamke aliyemuua Vivky. Ni mawazo hayo yaliompa uamuzi wa kuelekea ofisini kwa mkurugenzi wa ujasusi kwa mara nyingine. Ila kabla ya safari hiyo aliamua kurudi tena katika Hoteli fulani ambayo walikuwepo watu wawili waliotiliwa shaka. Wanausalama wa kike walikuwa hapo wakibadilishana Zamu. Hata wale waliojifanya wauza mihogo ya kuchoma sambamba na Mahindi walikuwa nje ya hoteli wakihakikisha wanaigundua mienendo ya watu hawa waliokuja kama wageni. Safari hii hakutaka kupitia lango la mbele, bali alipitia Mlango wa nyuma ambao pia ulikuwa ukitizamwa na Wana Usalama kwa kila kinachoendelea hapo. Aliwapita wana usalama waliozagaa na kuuendea mlango, ukaufungua na kuingia ndani kisha kuufunga tena. Alifanya hivyo pasipokusalimia kwa watu aliowakuta hapo. Alipoingia ndani akajikuta akitokeza sehemu ya Jikoni. Hapo pia palikuwa na wanausalama kadhaa. Akawapita akitoka hapa na kuingia ndani kabisa ya Hotel. Alipoingia tu mbele kidogo akawaona watu wawili waliokaa lakini kwa kumpa mgongo. Kilichomvutia sio kukaa kwao katika eneo lile, ila ni kule kumuona Yule mtoto ambaye humuona akiwa na yule mama akiwa mmoja wao. Huku umakini ukiongezeka masimba akawapita na kusogea mbele zaidi pasipo kuonekana. Alipohakikisha watu hawa hawakumuona, alivuta kiti kilichokuwa pembeni akakaa hapo. Baada ya kukaa hapo haukupita Muda wanausalama wengine watatu wakaingia. Lakini uingiaji wao haukuwa ule uliozoeleka. Hawa waliingia kama wasafisha vyumba na watandikaji vitanda. Watu hawa wakipoingia mmoja akamfuata masimba na kuongea naye mawili matatu. Baada ya sekunde mbili wakaondoka na Masimba, hata waliporudi muda mfupi. Walirudi wakiwa tofauti. MASIMBA hakuwepo.



    Ilikuwa ni mbinu iliyotumika ili kuwezesha masimba kuingia ndani kufanya uchunguzi wao. Kujifanya wafanya usafi ulikuwa ni mkakati uliosukwa ili kufanya kile ambacho walihitaji kukifanya. Masimba alikuwa ametulia sehemu macho yake yakiutizama Mlango katika Udadisi Wa Hali ya Juu. Alikuwa hapo akimsubiri mwanamke huyu ambaye aliamini ndiye huyu mwenye chumba hiki. Ndani ya Muda wa Sekunde kama Ishirini akauona Mlango ukifunguliwa, akaiona sura ya mwanamke ikichungulia. Ilikuwa sura ya mwanamke yule yule aliyemuua vicky. Masimba akaendelea kumtizama binti huyu. Hata pale alipoufungua mlango na kuingia kabisa kisha kuufunga tena mlango safari hii akiufunga kwa ndani, Masimba hakuinuka wala hakumfuata. Lakini binti alipoanza kuvua mavazi yake ndipo Hapo Masimba Alichokishuhudia kile ambacho hakuwa amekifikiria. Mtu huyu aliyeamini kuwa Alikuwa mwanamke Haikuwa hivyo. Huyu alikuwa mwanaume tena mwanaume aliyejengeka kimazoezi

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa mwanaume tena mwanaume mwenye mwili uliyojengeka kimazoezi. Hilo hakuwa amelitaraji. Mwanaume? Kumbe huyu hakuwa mwanamke. Hilo likampa mshangao, mshangao ambao ulizidi hasa pale mwanaume yule alipomaliza kuvua mavazi yake. Dakika moja iliyopita alikuwa akionekana kama mwanamke mrembo machoni kwa Masimba, hata pale mikadi beach alimuona kama malaika fulani. Macho yake yalikuwa yakimvutia kila mwanaume amtazamae. Licha ya hivyo kumbe hakuwa mwanamke kama alivyoonekana. Hilo likaongeza hamu ya kumjua huyu alikuwa nani, kwa nini alimuua Vicky? Hilo likamtoa pale alipokuwa amejificha kuelekea pale aliposimama mwanaume yule akijinasibu kama wa fanyavyo wasichana wengine. Bastola mkononi hatua za kunyata mfano wa paka. Bado mwanaume yule hakuwa amemuona, bado mwanaume yule hakuusikia mchakato wa viatu wala hatua. "Niliacha kukuua Mikadi Baada ya kumshuti yule mwansmke nia yangu ikiwa ni kukujua wewe ni nani. Umetoka wapi na umetumwa na nani? Kubwa Zaidi ni uzuri wako na muonekano wako ulinifanya nisite kuchukua maamuzi ili mradi nikukute sehemu niujue uzuri wako kiundani. Lakini kilichonishangaza ni kukuona hapa tena ukiwa umwanaume. Sasa nataka unijibu mwenyewe kwa kinywa chako. Ukileta ujuaji nitakusafirisha ukaungane na Vicky, Yule msichana uliyemuua pasipo na hatia. Sasa nijibu wewe ni nani? Umetoka wapi? Na unayafanya haya kwa kutumwa na nani? Aliongea masimba huku bastola yake ikiwa usawa wa kichwa cha mwanaume yule. Kitendo cha kuisikia sauti ile kutoka nyuma yake kilimshtua na kujikuta akiupoteza umakini katika hili. Kitendo cha kugunduliwa kwamba hakuwa mwanamke bali mwanaume hata hicho pia hakutegemea. Siku zote aliishi kama mwanamke na hata jamii ilitambua hivyo. Aliilinda siri ya muonekano wake kwa gharama kubwa sana. Alimuua kila mtu aliyemgundua na kuiigundua siri yake. Alisafiri katika nchi mbalimbali kufanya kazi za ndani kama mwanamke, kote huko aliua matajiri wake pasipo kugundulika. Lakini leo hii siri yake ilikuwa nje na pia alikuwa akitakiwa kueleza kile anachokifanya. Huyu ni nani? Ni swali lililopita kichwani kwake kwa kasi sana. Kumbe niligundulika wakati nikiua? Kumbe alikuwa na uwezo wa kunishuti na kunifuta hapa Duniani? Huyu ni nani? Yalikuwa mawazo yaliyopishana kichwani. Mawazo ambayo yalimchanganya na kuufanya ujasiri wake kuyeyuka. "Nasubiri majibu yako.." ni sauti kutoka kwa masimba iliyomshtua mwanaume huyu.



    "Niambie kwanza wewe ni nani? Nami nitakujibu kila kitu unachohitaji kutoka kwangu." Akajibu yule mwanaume kwa sauti tulivu na kawaida sana. "Hupaswi kuuliza maswali, unachotakiwa ni wewe unijibu maswali yangu." Alisema masimba huku akimuangalia kwa umakini. "Sikiliza ni kwambie, huna sababu ya kukataa kunijibu.. nataka nikujue wewe ni nani kwanza na kwa nini unaniuliza maswali ya namna hiyo." Alizidi kuongea mtu yule akionyesha kutokujali. Akionyesha dharau za waziwazi. Hakujua huyu mtu alikuwa nani, hakujua anaongea na mtu ambaye mzaha kwake haukuwepo kabisa. Punde kidole kikafanya yake, risasi moja ikapenya kwenye paja la mtu huyu... Yowee la maumivu likamtoka. Alikuwa akianza kulalama hovyo. "Nitakuua kwa risasi moja moja ukiendelea kuniletea jeuri. Haya jibu maswali yangu." Aliongea Masimba Huku bastola bado ameielekeza kichwani kwa mtu huyu ambaye aliakuwa akilalama kwa maumivu. "Mimi sijui unachokisema.. wewe niue tu." Alijibu mtu yule akiendelea kuugulia maumivu.



    "Kumbe unaniletea utani eeeh? Basi sina muda wa kupoteza." Aliongea masimba wakati huo huo akiachia Risasi tatu mfululizo ambazo zilimtupa mtu yule na kwenda kujibamiza ukutani. Alisogea na kumkuta tayari ni marehemu. Baada ya kujua tayari mtu huyu amekufa, akaanza kupekua sehemu tofauti ndani ya chumba kile. Upekuzi ambao ulimsaidia kupata Passports tatu zenye majina Tofauti. Bastola mbili pamoja na vitambulisho vitatu. Kati ya hizo bastola moja ilikuwa imetengenezwa urusi, huku nyingine ikitengenezwa Jamhuri ya Watu wa Czech. Zamani ikijulikana kama Czechslovakia. Pasipoti zilikuwa na majina ya watu watatu Tofauti. Moja ilikuwa na Jina la Veronica Senka ikionyesha ni Raia Wa Uganda. Nyingine ilikuwa na Jina la Janeth Omondi ambayo ilionekana kutolewa Kenya na passpoti ya tatu ilikuwa na Jina la Nusra Kassi akionekana kuwa ni Raia wa nchini kenya maeneo ya mombasa.



    Hata vitamburisho vilikuwa na majina ambayo yalikuwa kwenye passipoti tena yakimuonyesha mtu huyu alikuwa ni mfanyakazi wa mamlaka ya bandari nchini kenya, uganda pamoja na Hapa Tanzania. Passpoti zake zilikuwa zimegongwa mihuri kutoka nchi kadhaa za kiafrika na hata ulaya. Baada ya kuridhika na vitu alivyopata akaamua kutoka hapo kwa kupitia Dirishani tayati kwa safari ya kuelekea Bandarini kuulizia jina la mtu huyu. Kichwani alitambua kuwa Jimmy alikuwa ameweka mizizi katika sehemu zote nyeti za nchi hii. Ilikuwa ni lazima kuing'oa mizizi ilikumuondoa katika Uso huu wa Dunia. Haikuwa kazi rahisi kuifanya lakini aliamini akianza kudili na mtu mmoja moja ni lazima atamuangusha Jimmy.



    ********



    Aliingia bandarini na kulakiwa na msichana mmoja mweupe, mrefu na mwenye sura ya kuvutia. Macho yake makubwa na pua za kinyarwanda ni kitu pekee ambacho kilimfanya Masimba amuangalie mwanamke yule mara mbili mbili. Akavuta hatua mpaka pale kisha kwa sauti yake ya tatu akasabahi. "Habari yako Mrembo"?



    "Salama tu kaka angu, karibu sana na sema shida yako nikusaidie. Aliongea msichana yule kwa sauti ambayo iliuburudisha moyo wa masimba.



    "Naitwa John Raphael, natokea Hazina, nilikuwa nahitaji kumuona Mr Faudhi Facha Mkurugenzi muajiri wa Bandari. Alijibu Masimba huku akimuonyesha kitambulisho chake kinachoonyesha kweli ni mfanyakazi Wa hazina.

    "Una miadi naye? Aliuliza binti yule.



    "Sina miadi lakini ukimwambia kuna mtu anatoka hazina anataka kukuona atanielewa." Alijibu Masimba Huku macho yake yaliyozoea kugundua visivyogundulika ikitalii hapa mpaka kule.



    "Nenda chumba cha Tano ghorofa ya tatu, hapo utakutana na sekretari wake atakusaidia." Alisema mwanamke huyu akimgandishia masimba macho usoni. "Nashukuru nikirudi nitakupitia nikakupe japo soda." Akaongea Masimba akimuacha mwanamke yule akielekea ghorofa ya tatu kwa mkurugenzi Muajiri. Alitembea kwa makini huku macho yake yakipita kwenye macho ya watu kugundua kama kuna macho yanamtizama kwa ghiliba. Lakini hapakuwa na hicho kitu. Kila mmoja alikuwa akiendelea na kazi kama kawaida. Alizipanda ngazi mpaka ghorofa ya tatu, akaongoza mpaka mlangoni mwa chumba husika. Akaugonga mlango kabla haujafunguliwa na binti mmoja mnene na mfupi mweusi. Kuingia na macho yao kutizamana na mwanamke huyu, akiona kitu machoni kwake. Macho ya Dada huyu yalikuwa yakizungumza hofu na wasiwasi. Kwa nini? Lilikuwa swali lililofuatiwa na Salamu.



    "Karibu John.." alisema dada yule huku bado mshangao ukiwa usoni. "Ahsante bibie, bila shaka Taarifa yangu mnayo." Aliongea masimba akimuangalia zaidi mwanadada huyu. "Tumepigiwa simu kutoka mapokezi ndio maana umeona nimekuita Jina lako." Alijibu msichana yule.



    "Ni utaratibu wa siku hizi au umeanza kwangu? Akauliza tena safari hii akihamisha macho usoni kwa mwanamke huyu na kuutizama mlango wa chumba cha mkurugenzi.



    "Hapa sio kwako tu, hata wengine pia ni hivyo." Akajibu mwanamke yule. Lakini kwa masimba aliuona uongo wa Jibu hili. "Naweza kumuona mzeee? Akauliza Masimba.



    "Yeah!, ingia anakusubiri." Alijibu msichana yule. Masimba hakuongea kitu zaidi ya kuongoza ndani kuelekea chumba cha mkurugenzi. Akaugonga mlango.. "pita kijana." Ilikuwa sauti kutoka ndani ya chumba. Masimba akausukuma mlango akaingia. Baada ya kuingia ndani akajikuta akitizama na Ofisi nadhifu iliyopangiliwa vizuri. Kaa hapo bwana masimba. Naona leo nina bahati ya kutembelewa na mtu kama wewe. Kufanya kazi hazina Sio kutu cha kawaida." Aliongee mzee yule akionyesha bashasha usoni. Kwa mtu kama masimba haikuwa bashasha, kwa mtu kama Masimba sauti ile haikuwa ikimaanishe kile ilichokusudia. Sauti ile ilikuwa na kitu ndani yake. Kitu kama dharau na hatakejeli. Hakujali hilo, akavuta kiti na kukaa. "Nashukuru sana mzee wangu, nami nimefarijika kukutana na mtu kama wewe. Naamini kuna mengi ambayo nitajifunza kwako." Naye akaongea Huku akimuangalia mzee yule usoni. Hofu na wasiwasi ni vitu viwili ambavyo vilikuwa ndani ya macho ya mzee huyu. "Okay, nakusikiliza kijana Wangu.." aliongea mzee yule akikaaa sawa.



    "Nashukuru, kuna kitu ambacho nimekutana nacho leo hii huko nitokako, nikaamini nikija hapa kwako naweza kupata majibu ya maswali yangu." Aliongea masimba kwa upole huku akimtizama mzee yule. "Endelea Kijana...."

    "Mzee kabla sijaendelea popote, naomba kumjua mtu huyu. Aliongea masimba akutoa moja ya kitambulisho kati ya vile vitatu na kumpa mzee.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee yule akakipokea na kuanza kukitizama.. Mshtuko usio wa kawaida ukaonekana machoni mwake. Akainua kichwa kumuangalia Masimba. Akakutana na sura tofauti.. hii haikuwa sura iliyoingia hapa muda mfupi uliopita. Hii ilikuwa sura ya kazi. Sura inayomaanisha kile kinachotakiwa kumaanishwa





    Haikuwa sura ile ya mwanzo, hii ilikuwa sura nyingine kabisa. Macho yalikuwa yakimtizama mzee yule pasipo kupepesa kuangalia kando. "Bila shaka unamfahamu huyo mtu, na pia unafahamu kazi zake. Nahitaji kumjua na kujua ni lini alianza kufanyakazi hapa." Akaongeza Masimba. "Mr John nadhani hayo maswali sipaswi kuulizwa na wewe. Muajiri wangu ndiye mwenye mamlaka hiyo pale aonapo kitu hakiendi sawa. Pia hata wanausalama ndiyo wanaweza kufanya hivyo lakini sio mtu wa hazina." Alijibu mzee huku hofu ikiwa imetawala ndani yake. "Mimi ndiye nimekuja badala ya bodi ya mamlaka ya bandari, pia nimekuja kama special Agent.. so nahitaji kupata majibu kuhusu mtu huyo mm0ja mwenye majina matatu tofauti." Alinguruma Masimba huku uso wake ukizidi kuuondoa Uhalisia. "Kijana ya nini tusumbuane, kwanza unaniuliza wewe kama nani? Akabwata yule mzee huku akionyesha kughafilika. "Kama John Raphael kutoka hazina, lakini pia unaongea na Mto roho ambaye ukiendelea kuupoteza muda wangu kesho hutaiona." Aliongea Masimba sasa akilazimisha macho yake yatizamane na macho ya mkurugenzi. "Huyo mtu mimi simfahamu na hata hapa hatuna Jina kama hilo." Akajibu mzee Majibu ambayo kwa kumuangalia tu, alihisi kuwa amedanganywa. "Humjui huyu mtu? Unashindwa kumjua mtu uliyemuajiri mwenyewe? Nikisema unamjua na kumtambua utasema nadanganya? Nikisema nawe ni kibaraka wa Jimmy Na Suresh kama alivyo huyu mtu wako utakataa? Je upo tayari risasi yangu ipenye kichwani kwako kwa sababu ya kuuficha ukweli wa mtu asiyekuhusu? Sasa naomba unijibu kwa umakini, usijaribu kunificha. Nikibadilika nitakupoteza kwa dakika tu." Aliongea Masimba huku akimtizama kwa macho makali. Mshtuko na mfadhaiko vilikuwa dhahri machoni na hata usoni. Mikono ikamtetemeka huku jasho likichuruzika Taratibu licha ya kuwepo kwa mashine za kuleta baridi. Kitendo cha kutajiwa watu hawa wawili kilimvunja nguvu na kumfanya asiwe na la kuongea. Akabaki akimtizama Masimba huku akionekana kutetemeka zaidi. Ni wakati Masimba akilitizama hilo akamuona mzee yule akibadilisha macho na muda ule ule kitu mfano wa damu kikaonekana kifuani kwake. Masimba hakuwa mjinga kiasi hicho asijue kilichotokea. Risasi iliyopitia Dirishani ilikuwa imepenya kwenye kifua cha mkurugenzi. Alikuwa amezibwa mdomo, alikuwa ameondolewa uhai asije kuutapika ukweli wote. Ilikuwa ni njia moja wapo inayotumiwa sana na majasusi kuficha siri husika. Akainua macho kutizama pale ilipotokea Risasi.. akakutana na nafasi ndogo kwenye pazia. Nafasi ambayo alihisi ndio imetumika kumuua Mkurugenzi huyu. Licha ya nafasi hiyo, pia usawa na ukaribu wa alipokaa yeye ilikuwa ni rahisi sana kupigwa yeye Risasi kabla ya mkurugenzi. Kwa nini ameachwa yeye akauliwa mkurugenzi? Lilikuwa swali lililoamsha mashaka. Mtu aliyemuua mkurugenzi alikuwa ni mtu anayemfahamu ama mtu ambaye alipewa oda ya kumuua mkurugenzi na kumuacha yeye. Kilikuwa kitu kigumu kukiamini katika uuaji ule. "Teddy" ndio jina pekee lililopenya kichwani na kuuvuruga ubongo wake. Lakini hilo alilioinga baada ya kutambua Teddy hawezi kuwa pale kutokana na msiba wa Vicky. Ilikuwa ni ngumu Teddy kuiacha maiti ya Vicky kisha aje afanye hivi. Lakini ni nani? Swali hilo alijiuliza wakati ameshaufikia mlango na kutokea ofisi ya sekretari. Kuufungua mlango tu, macho yake yakatua juu ya mwili wa Mwanadada yule ukiwa umelalia juu meza damu ikivuja taratibu na kuilowanisha Sakafu. Naye alikuwa ameuawa katija aina na namna ile ile. Namna ya kufumbwa mdomo asiweze kubweka. Masimba akaiona Hatari, hatari yakuendelea kuwepo ndani ya ofisi zile. Mkurugenzi, kisha sekretari, ilikuwa picha mbaya kwake. Ilikuwa ni lazima aondoke hapo. Aondoke kwa kupitia uelekeo mwingine, alijua alikuwa akitizamwa mahala fulani. Licha ya kutizamwa huko, lakini bado alimhitaji kumuona mwanadada yule wa mapokezi. Mambo kutokea kwa kasi namna hii ni wazi kuwa taarifa ilikuwa imesambaa. Imesambaaa kupitia kwa mtu, mtu ambaye amemuona kwa mara ya kwanza. Nani ameniona kuisambaza Taarifa hii katika muda mfupi huu? Jibu lilikuwa moja tu, veronica Senka Alikuwa msambaza taarifa , ilikuwa ni lazima apatikane kwa njia yoyote ile. Akaondoka akipitia sehemu tofauti na alikoingilia. Wakati akitoka Nje ya jengo, akauona msululu wa magari ya polisi wakikosi maalum ukiingia pale. Kilikuwa kikosi cha kupambana na uharifu wa aina yoyote. Kuuona msafara huo na alipounganisha na matukio ya kuuawa watu wawili katika muda mfupi.. alipata Jibu kuwa ni yeye aliyekuwa akitafutwa, ni yeye aliyetumiwa kikosi kile, ni yeye anayetafutiwa sababu ili wanaomuamini Wasimuamini. Hilo likamfanya azidi kuwa makini katika uondokaji. Uondokaji machoni mwa watu ambao walikuwa hapo.



    ********

    Kwanza alishikwa na kitu kama ganzi, pili akashindwa hata kuongea na kipi akifanye. Butwaa hili lilimfanya mtu huyu aingie pasipo yeye kufanya maamuzi. Uso wake ukatagayari pale macho yake yalipogongana na macho ya mtu huyu aliyeingia kwenye ofisi zao katika mchana huu. Tabasamu mdomoni na uchangamfu wa kuzuga ukauchukua uso wake. Hata kijana huyu alipomsogeleo, bado tabasamu tamu halikuondoka usoni kwake. Hata alipojitambulisha kuwa anaitwa John Raphael, hakuonyesha kushangaa kwa kuwa alishamjua mtu huyu. Hakukuwa na mtu ambaye hakumjua Masimba. Lakini alipohitaji kuonana na mkurugenzi Muajiri, kengele za tahadhali zikalia kichwani kwa binti huyu.. hata pale masimba wakati akielekea kwa mkurugenzi hakuwa na maamuzi yoyote. Hakujua angeamua nini kwa wakati ule. Mpaka anaanza kuzipanda ngazi, bado hakujua nini afanye. Alimuona Masimba kama mtu ambaye anasingiziwa, mtu ambaye hafanani na kile kisemwacho juu yake. Wakati akiyawaza Hayo simu yake ikapata uhai. Simu yake ilikuwa ikiita. Namba ya mpigaji ndio iliomfanya akurupeke. "Jimmy" ndio neno ambalo lilisomeka Juu ya kiio cha simu yake. "Boss wangu.!! Alipokea Veronica.



    "Yeah mtoto mzuri uko wapi leo?"aliuliza Jimmy.. "nipo kazini ila tumetembelewa leo." Akajibu Veronica. "Mmetembelewa na nani? Rais au nani?. Akauliza Jimmy safari hii kwa sauti tulivu. "Masimba yupo hapa, ametutembelea na sasa anaelekea kuonana na mkurugenzi muajiri. Nadhani kunatatizo boss maana alivyoingia sio kawaida." Aliongea Veronica. Hata aliposubiri jibu kwa Jimmy hakulipata kwa muda ule. Alipoita tena akagundua simu ilikuwa imekatwa. Baada ya Jimmy kupewa taarifa ya masimba kufika bandarini na kuhitaji kuonana na mkurugenzi ili mshtua sana. Kwa jinsi alivyomjua Masimba, alijua hapakuwa na usalama. Akapiga simu hotelini kwa vijana wake, jibu alilopewa lilimfanya atetemeke. Mmoja wa vijana wake shupavu maarufu kwa Jina la Jike dume alikuwa ameuawa. Akahisi mambo kutokuwa sawa, haraka akapiga simu kwa Ben kisha kumpa maelekezo ya nini cha kufanya. Ndicho ambacho kilitumika kuwaondoa watu walea katika ofisi ile.



    ******



    Alifika msibani kwa mara ya pili tena, aliwakuta watu wapo katika makaburi tayari kwa muhifadhi vicky. Alisogea taratibu akikwepesha macho yake kumuangalia Teddy aliyekuwa ameshikiliwa huku na huko akilia kwa uchungu. Sala ya kumuombea marehemu ikachukua nafasi yake. Baada ya sala mwili wa Vicky ukaanza kushushwa kaburini kuhitimisha safari yake ya mwisho hapa duniani. Ulikuwa wakati mgumu sana. Mama Vicky hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea. Wakati wote huo masimba alikuwa makini akiangalia macho na sura za waliohudhuria mazishi. Hakutaka kuamini kwamba usalama ulikuwepo. Muda wote hakutulua akigeuka huku na kule. Akigeuka katika ya kupendeza. Uvaaji na hata muonekano wake haukuwa kama ule aliotoka nao ofisi za bandari. Hapa alikuwa ni Masimba mwingine. Kila hatua na kila ishara ya waombolezaji ilichunguzwa na kutiliwa mashaka. Vijana walioongezwa kuudumisha ulinzi na kunusa chini kwa chini nao walikuwa makini sana. Hata kama mtu alikuwa akijikuna basi aliangaliwa mara tatu tatu. Aliangaliwa na hata kufuatiliwa. Alichunguzwa kwa ukaribu zaidi na hata kupewa kashkash ambazo hazikuonekana machoni kwa waombolezaji. Macho yao yalikuwa katika sura ya mwanamke fulani ambaye alikuwa ametokea hapo na katika muda huo. Macho ya wanausalama yakamkaribisha katika aina ya tunakushuku. Tunakutuhumu na tutakujua. Akaangalia kila hatua na kila macho yake yalipokuwa yakigeuka kwa kutembea huku na kule. Huyu alikuwa yule mwanamke aliyekuwa pale ofisi za bandari. Huyu alikuwa yule aliyeisambaza taarifa za kufika hapo kwa masimba, taarifa iliyosababisha kuuawa kwa mkurugenzi. Lakini sasa alikuwa hapa makaburini, amekuja kama na nini na amefuata kipi? Hilo ndilo lililojengeka kichwani kwa masimba, hilo ndilo lililojengeka kuwa kuna namna. Mpaka mtu huyu kufika hapa makaburini ni wazi kuwa alikuwa akintafuta yeye. Alikuwa akijua kabisa binti huyu alikuwa hapo kwa kazi maalum. Kazi ya kumpeleleza yeye. Hilo likamvutia kwa kuwa alikuwa anamtaka na kumhitaji. Mazishi yakafika tamati na watu wakaanza kurudi majumbani kwao. Vijana wa usalama walikuwa wakitembea pembeni mwa familia ile kwa karibu sana kuonyesha kuwa walinusa chochote kitu. Masimba bado macho yake yalikuwa kwa Veronica. Bado macho yake yalitaka kujua kile ambacho msichana huyu amekifuata. Kile ambacho angekihisi machoni na hata kupitia mienendo yake. Kumkuta ofisi za bandari, mauaji ya mkurugenzi na sekretari wake, kisha kuja kwenye mazishi ya Vicky ni mambo ambayo yalimuacha katika maswali ambayo hayakupata majibu. Alihisi hata taarifa ya kufika kwake pale Bandari yeye ndiye aliyeisambaza na kisha kutumwa watu wa kuua.



    Watu waliendelea kurudi nyumbani kwa wafiwa bila kujua chochote. Bila kutambua kuwa palikuwa na mchezo wa aina yake. Macho kwa mwanamke yule hayakuganduka. Aliitizama miguu yake na kuutizama mwendo wake. Mwende ambao ulimuonyesha kuwa mwanamke yule hakuwa peke yake. Mwili wake ulikuwa ukitoa ishara fulani katika kujulisha watu kitu fulani. Wakati mwili wake ukitembea katika namna ya kutoa taarifa. Macho yake yalikuwa yakitembea kwa aina fulani ya kinyonga ili kuwapoteza waliokuwepo na wale ambao alijua wako mahali na wanamuangalia yeye. Hakujua hilo na pia hakulitambua hilo. Hakutambua kuwa kuna macho mawili ambayo hayajawahi kushindwa kugundua kitu. Macho ambayo hung'aza mpaka ndani. Kila uelekeo wa macho yake hata masimba aliangalia huko. Kila alipokuwa akiuchezesha mguu hata macho ya Masimba yalikuwa yakitizama. Hatua zisizopungua kumi mbele mkono Wa Veronica ukawa unashushwa taratibu kuelekea mahala fulani katika vazi lake.. Hata mkono wa Masimba nao ukafanya hivyo, na Hakuwa masimba pekee, bali Hata wanausalama Wengine mikono ilikuwa Mfukoni tayari kwa tukio la aina yoyote.



    Hata macho ya wana usalama wengine yalikuwa yakimtizama. Mikono mifukoni tayari kwa kufanya chochote. Bado vero alikuwa akitembea katika aina ile ile ya kuwachanganya wanausalama. Alikuwa akionyesha kitu ambacho wana usalama hawakukijua wala kukigundua. Lakini wakati akifanya yote hayo hakujua kama alikuwa akiangaliwa na mtu mwingine ambaye yeye hakumjua na hata kule kugundua kama yeye ndio yule. Hakuwa peke yake katika kutokujua na hata kugunduahuko. Hata watu ambao walikuwa pembeni kidogo hawakumuona mzee huyu ambaye alikuwa akifuatilia kila kitu. Licha veronica kutembea huko akiutupa mkono huku na huko macho yake yakipelekwa sehemu fulani, haikuyasumbua macho ya mwanaume huyu aliyekuwa amesimama pembeni. Wakati wanausalama wakiyumbishwa na uelekeo wa macho yake, hukunyuma bado mtu yule aliuangalia upande ule, upande ambao haukuwa ukitizamwa katika namna fulani ivutiayo. Upande ambao haukutizamwa na veronica. Mtu huyu akajikuta akivutiwa na mwanadada huyu katika kule kutembea, kutenda na hata kudanganya. Hii ilimfanya aamini kuwa huyu ni jasusi wa hali ya Juu. Jasusi mwenye uzoefu wa kutisha. Wakati akiyapa burudani macho yake akamuona Teddy akigeuza kichwa huku na huko. Hata mkono wa teddy ulikuwa umeshuka katika namna ambayo ni ngumu kugundulika kwa macho ya kawaida. Hata naye alikuwa amekinusa kitu, hata huyu alikuwa amegundua uwepo wa hatari mahala hapo. Masimba kubadilika, wana usalama kuhaha huku na huko ni kitu ambacho kilimvutia Teddy. Lakini mpaka watu wanafika nyumbani kwa mama wa marehemu hapakuwa na kilichotokea. Kila mtu alikuwa akihangaika huku na huko. Teddy akahitaji kuongea na masimba katika namna yoyote. Macho yake yakaifanyakazi ya kumuita mwanaume yule. Alihitaji kufahamu nini ambacho kinaendelea. Nini ambacho kinafanyika. Lakini akiwa bado ana mtizama akamuona Masimba akiongea na simu, kilichofuata ni kuondoka katika eneo lile akumuacha Teddy akishangaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *****

    Ulikuwa ukumbi tulivu wenye ustarabu wa hali ya juu tofauti na kumbi nyingi za burudani hapa mjini Dar es salaam. Ulikuwa ukumbia uliopo kando kando mwa bahari ya Hindi maeneo ya Kawe. Watu walikuwa wengi wakiburudika kwa vinywaji na hata kucheza muziki. Wengi waliokuwepo ukumbini hapo walikuwa ni askari wa jeshi la wananchi kutokana na ukumbi huo kuwa karibu na kambi ya jeshi ya Lugalo. (LUGALO MILITARY BASE). Pembeni kabisa mwa ukumbi ule alionekana mtu mzima wamakamo akiwa amekaa kwenye kiti akionyesha kuendelea na kinywaji huku wakati mwingine akionyesha kutingisha kichwa kufuatia mziki uliokuwa ukiporomoshwa hapo. Muda wote huo hakuacha kuutizama mlango wa mbele na hata ile milango ya siri ambayo waliitumia wao kama wao. Huyu alikuwa mzee Godliving Kimaro Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Alikuwa hapo kwa miadi ya kukutana na mzee mwingine ambaye alkuwa mmoja kati ya wale watu watano wanaosemekana ndio wanaoiendesha nchi hii na kumpangia mkuu wa nchi nini cha kufanya. Huyu alikuwa ni mtu mkubwa katika Jeshi la wananchi akiwa na Cheo cha meja jenerali.Yalikuwa maongezi ya siri kuitishwa katika eneo hilo licha ya uwazi huo. Siku zote wao waliamini mazungumzo ya Siri hufanyika hadharani ili kuondoa mashaka na kutokutiliwa wasiwasi. Hawakutaka kukutana kwenye maofisi ama mahotel makubwa kuhofia kumulikwa na watu. Hivyo waliiona sehemu ile kuwa ni zuri na yenye usalama. Askari kadhaa waliomuona mzee huyu akiingia hapa walimtupia macho bila kuhisi chochote kwa kuwa ilikuwa kawaida kwa mtu huyu kuingia hapa kila siku. Meje Jenerali Louis Chomboko alitembea taratibu kwa mwendo wake wa kikakamavu mpaka sehemu ambayo amekaa Chief. Alipomkuta alimsalimia katika nidhamu zote za kijeshi, na baada ya hapo wakakaa. "Ndio bwana kimaro naona safari hii unapata muda sana wa kupumua. Nimesikia unavijana wako wamekufanya utulie kabisa licha ya hili tukio la kuuawa kwa Waziri Mkuu.," alianza meja jenerali Chomboko huku akimtizama Chief kwa makini. Chief hakuongea kwa haraka, alichokifanya nikukaa kwa muda akifikiria kisha kwa sauti ya upole akanena.



    "Ni kweli unayosema bwana Chomboko, lakini ni vijana hao ambao wanaufanya ofisi yangu niione chungu.".... " Uione chungu wakati kuna ushahidi Ikulu? Aliongea Mej-jenerali huku akimtizama Chief kwa mshangao. Mshangao ambao haukuwa na kikomo. "Najua hilo, lakini kuna jingine limetokea leo. Siamini kama hujalisikia. Hilo ndio limenfanya mkuu anipigie simu kuniuliza kulikoni. Aliongea Chief huku akiipeleka Glass ya p0mbe kinywani.



    "Lipi hilo? La kuuawa kwa Mkurugenzi muajiri wa Bandari na sekretari wake? Sasa Mr Chomboko akauliza huku umakini ukiongezeka.



    "Yeah ni hicho kitu.. Rais amenipigia na kuniuliza inakuwaje kijana wako anaua watu hovyo.. Anachotaka yeye hawa watu ambao ushahidi upo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Hivyo ameagiza niongee na Kijana wangu ili aachane na hili suala. Aviachie vyombo vya usalama viifanyekazi yake." Alijibu Chief huku uso wake ukionyesha kukata tamaa. Ukimya wa Ajabu ukapita kati yao. Kila mmoja alikuwa akitafakari kitu chake. "Anaposema awaachie wana usalama wafanye kazi yao, kwani Masimba ni mtu gani? Ina maana yeye hatoki ndani ya usalama? Ni nani angejua mabaya ya huyu bwana kama sio masimba kuyaibua? Hapaswi kufanya hivi.. Idara za usalama lazima zifanyekazi zao kwa uhuru. Sioni Tatizo la masimba hapo. Na kukwambia ukweli ni kwamba Masimba hakuuwa yeye, bali watu wale waliuliwa na watu wengine ili kufumbwa mdomo wasiropoke. Masimba alishagundua baada ya kumuua mkora mmoja pale hotelini, aligundua kuwa mtu yule alikuwa mmoja kati yao na alikuwa akipitisha vitu vingi na kuajiri watu ambao hawafahamiki. Sasa sidhani kama Rais anajua haya mambo." Aliongea meja jenerali Chomboko kwa kirefu akionyesha kufahamu kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea. Maelezo ya Mr Chomboko yalionyesha kumburudisha sana Chief, sasa alikuwa akianza kutabasamu kwa mbali. Kutabasamu hasa baada ya kujua kumbe watu hawa nao wanafahamu kile kinachoendelea. "Kumbe ndiyo hivyo? Sasa mbona hamuongei naye kumueleza hili? Hii hii kazi anayoifanya Masimva ni Ngumu.. ni kazi ambayo inalibeba Taifa. Amepoteza mama kwa sababu ya nchi yake. Aaachwe asafishe hiki alichokianza. Ndio maana nimekuja kuongea nawe ili umwambie hili. Kijana aachwe afanyekazi asichanganywe." Akasema Chief huku akionyesha kuchoshwa na kauli ya mkuu wa nchi. "Haina Sababu ya kuchoka, ujumbe nitaupeleka baada ya kutoka hapa tu. Na ninaamini ataelewa na kijana ataendelea kuifanya kazi hii." Aliongea Meja Gen. Chomboko. Wote wakatabasamu na kucheka kwa pamoja.



    *****



    Alitakiwa aiache kazi ya kuwafuatilia kina Jimmy, alitakiwa kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama viifanye kazi hiyo. Kichwa chake alikiinamisha chini akifikiria watu waliouawa kwa sababu ya kazi ambayo leo alikuwa akiambiwa aiache. Asteria, Mwamvua, Dada wa Asteria, mumewe na hata mtoto wao. Dee plus na Vicky kisha mama yake Mzazi. Nani anaweza kurudisha roho hizi? Nani anaweza kuwarudisha watu hawa? Je nani ataurudisha utimamu wa mateja waliotopea kwenye matumizi? Yalikuwa maswali yaliyokisumbua kuchwa chake. Alichokifanya ni kuinuka na kuendea mlango ili kutoka nje akaanze kazi ya kumfuatilia mwanadada Veronica. Wakati akiufungua mlango ili atokea, akakutana uso kwa uso na Teddy aliyekuwa amesimama hapo mlangoni. Wakatizamana kwa muda wa sekunde tano. Kutizamana kuliko mfanya Masimba Arudi chumbani akifuatiwa na Teddy. Mlango ukafungwa wakisimama na kutizamana. "Nimekuja kuongea na wewe, nataka nimjue aliyemuua mdogo wangu Vicky." Aliongea Teddy Taratibu Akimuangalia Masimba Usoni. "Hayupo tena hapa Duniani. Naona Roho yake inakaribia kufika mbinguni. Nimeshamuua." Alijibu masimba akimtizama Teddy. Hata Teddy naye akamtizama. Wakatizamana na kutizamana. "Rais Ametoa amri kuwa niachane na kazi hii ya upelelezi juu ya haya yote yanayoendelea. Ameniambia niviachie vyombo ya usalama." Aliongea Masimba safari akijibweteka Chini. Teddy hakujibu kwa haraka. Bali alimuangalia kwa muda kisha kwa sauti ya Uchungu akanena. "Kama anaweza kurudisha roho za walipotea katika mapambano haya tutaacha. Kama hawezi basi mpaka nihakikishe Risasi zangu zinapasua kichwa cha Jimmy. Watu wameharibu vijana harafu waachwe. Hata sisi ni wana usalama siwezi kutii wala kukubali. Nitaacha kwa mdomo lakini nitafanya kwa vitendo." Aliongea Teddy akionyesha kutokuwa na masihara. Masimba alimuangalia kwa muda kisha kwa sauti ile ile ya kuonyesha kuwa hakuna masihara akanena. "Ningeomba hii kazi uniachie mwenyewe, sitaki kukupoteza Teddy.. nataka nikutengeneze uwe mwanamke wa maisha yangu." .. Teddy akamuangalia Masimba kwa Muda. Alimtizama kanakwamba alikuwa hamfahamu. "Masimba hii ni kazi yangu sio yako. Ulipoifanya panatosha. Leo nitaanza kukuletea Kichwa cha Ben, sitaki mdogo wangu asindikizwe na muuaji wake nataka aende na watu wengine wengi tu."



    Yalikuwa maneno ya Teddy akionyesha hakuwa na masihara katika hilo. Suala la kuanbiwa wao waachane na suala lile lilikuwa ni tusi kubwa kwao. Ni siku ile tu amemzika mdogo wake kutokana na suala hilo. Kumwambia aliache lilikuwa ni tusi kubwa, tusi ambalo kamwe wasingelivumilia. "Ni kweli hatuhitaji kuingiliwa katika hili, hatuhitaji kufundishwa nini cha kufanya. Nimemuomba Chief akaonane na Mzee Louis Chomboko wazungumze ili iwe rahisi kwetu kuifanya hii kazi. Pia nataka wewe uende bandarini ukaonane na yule binti wa leo pale makaburini. Yeye ni mfanyakazi wa pale na siku ambayo waliuawa watu wawili yeye ndiye niliemkuta mapokezi. Tukimfuatilia huyu tunaweza kupata mengi kuhusu Jimmy na Suresh. Mimi nitakwenda pale kwenye mazishi ya mbunge wa kigamboni siku ya kesho. Naweza nikanusa na kupata mawili matatu. Lakini pia umakini unatakiwa kuna vijana wenzetu wanakesha wakinusa hili ili kuijua mizizi ya watu hawa. Na ili kulimaliza hili nilazima tujue kila kitu kinachohusiana na hii biashara ya madawa sambamba na Nyara za serikali. Narudia tena hawa watu ni hatari, kwa jinsi walivyojibadilisha na kumuua Vicky kisha kuondoka pasipo kujulikana ni wazi watu hawa ni hatari sana. Kuwa makini na sihitaji kukupoteza tena." Aliongea Masimba akimuangalia Teddy usoni. "Nimekuelewa Masimba, nimejeruhiwa na kifo cha Vicky, nataka nikuonyeshe kuwa serikali haikukosea kunipeleka Urusi na hata Cuba katika mafunzo ya juu ya ujasusi. Nisamehe kwa kauli zangu za pale mwanzo. Hasira zilinizidi.. naomba unisamehe mpenzi." Aliongea Teddy huku akisigea na kumkumbatia masimba.



    ******



    Pilika pilika zilikuwa nyingi katikati ya jiji la Dar es salaam kwa asubuhi hii, watu wenye haraka walikuwa wakihaha wakishika hiki na kushika kile. Walikuwa wakitoka hapa na kutoka pale. Vibaka na wezi wa mifukoni nao hawakukosekana hapo katika kuitafuta riziki yao. Ndani ya jengo moja lililopo mtaa wa mkwepu pale posta mpya. Watu sita walikuwa wameizunguka meza tokea asubuhi hiyo mpaka muda huo pasipikupata muafaka. Kila mmoja alikuwa akipingana na huyu kwa hoja ambazo ukizisikiliza zinaweza kukuvutia na kukufanya ukisikilize kile ambacho kinazungumzwa. Watu sita hao ambao walikuwa wamiliki na waanzilishi wa mtandao wa kuuza na kununua madawa ya nchini Tanzania, walikutana asubuhi hiyo kuzungumzia kile kinachoendelea katika mapambano yao dhidi ya wana usalama. Kitendo cha kuuawa watu wao wawili siku ya jana katika ofisi za bandari lilikuwa ni pengo la tatu kupata katika kundi hili ambalo lilitaka kuifanya Tanzania kuwa katika Himaya na Utawala wao. Tukio la kuuawa kwa Waziri mkuu, kulipuliwa kwa kambi yao ya Siri na kuuawa kwa mkurugenzi Muajiri wa mamlaka ya Bandari ni matukio ambayo yaliwafedhesha na kuwaumiza sana. Kwani waziri mkuu alikuwa ndiye mhimili mkubwa katika masuala yote ya usalama na upitishwaji wa mizigo yao popote pale katika mipaka ya nchi hii. Tukio la kulipuliwa kwa Secret Base ambayo ndio ilikuwa kambi ya kuhifadhia mizigo yao nalo lilikuwa tukio baya ambalo liliwatingisha kwa namna moja ama nyingine. Mzigo ulioteketea kwa moto katika kambi hiyo ya siri ulikuwa ni mara tatu ya mzigo ambao ulitoroshwa airport kabla ya kuibiwa na Masimba. Tukio la tatu ni la kuuawa kwa mkurugenzi muajiri .. hili pia ni tukio ambalo liliwashtua sana. Watu wao wengi katika kazi yao waliajiriwa hapo kwa nguvu ya mkurugenzi huyu. Mizigo yao mingi ya magendo ilikuwa ikipitishwa hapo kutokana na nguvu ya mtu huyu. Vijana wengi wenye mbinu zote waliingia nchini na kupandikizwa hapo kama wafanyakazi kutokanana nguvu za mtu huyu aliyeuawa. Hilo ndilo lililowafanya leo hii wawepo katika Jengo hili wakikutana hapo katika kulitafutia muafaka suala hili. Suala la mtu huyu aitwaye masimba sambamba na mwandani wake aitwaye Teddy. Watu wawili hao ndio watu ambao walikuwa wakiwakosesha Raha. Hawakuwa wakila na kulala usingizi sababu ya watu hawa wawili. Hawa wamekuwa ni mwiba mchungu kwao, mwiba ambao ulikuwa ukiwachoma huku ukiwaacha na Alama kama sio Vidonda. "Tumeshindwa Kumdhibiti Huyu Masimba na mwandani wake? Tuna vijana wangapi wenye ujuzi katika medani lakini mbona hawaonyeshi kile tunachokitambua.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Licha ya kumkamata masimba kwa mara mbili nzima lakini tumeshindwa kufanya maamuzu. Mamuzi ya kumuua. Hili ndio kosa ambalo tumlifanya. Tukio la vijana wetu kumuua Mkurugenzi mchana wa jana pia ilikuwa ni mbinu ya kuificha siri iliyofichika hapo. Lakini ukiondoa hilo ni kwamba pale pataandamwa. Wana usalama watapageuza Njia ya kupita. Njia ya kufika kila wakati ili kuutafuta ukweli. Ukweli wa kile kilichofichwa kwa risasi ya vijana wetu. Kumbukeni Bandarini na Airport ni sehemu ambayo kuna watu wetu wengi. Kujulikana kwa hili la Bandarini ni kutaka kujulikana kwa haya mengine. Ni wajibu wetu kuwaambia vijana wetu ni wajibu wao kuwa makini katika kuwafuatilia hawa watu. Hatuwezi kushindwa na mtoto huyu ambaye tulimlea wenyewe." Aliongea mjumbe mmoja uso wake ukionyesha kukosa raha kabisa.



    "Ni kweli ulichokisema mwenyekiti. Hapa nilazima Bandarini na Airport wana usalama watapafanya ndio kwao. Kitendo cha mtu huyu kuuawa mbele ya masimba ndicho kitakachoamsha hisia za Masimba kuwa bandarini hapana usalama. Vijana wetu wamelikosea hili. Wamefanya haraka sana.

    [05-25, 13:53] Masimba Wa Teddy: Alisema mjumbe mwingine ambaye wazo lake liliungwa mkono na wajumbe wengine. "Ni kweli tunahitaji kulifanya hili lisijirudie Tena. Nilazima wenzetu waliopo pale bandarini na hata pale Airport ni lazima tuwaondoe kwa kificho. Tukumbuke wote hapa tunadhamana na vyeo vya juu katika Serikali ya Nchi hii. Kumbukeni tukiliacha hili liendelee vitanzi vitakuwa halali yetu. Mimi naomba tufanye kazi moja ya kuwauwa watu hawa. Tuwaue watu wa bandarini Airport na hata wenzetu wa pale uhamiaji. Mauaji haya yafanywe na vijana wetu wakiongozwa Jimmy. Hili suala ni zito na ili kujiepusha ni lazima tuendelee kuwafumba watu midomo yao kabla huyu masimba na Teddy hawajawafikiq. Pia kuna suala ambalo nililisahau. Ni kwamba majira ya Saa nne usiku kuna kikao kilifanyika katika ufukwe wa Kawe. Kikao hicho kilikuwa cha watu wawili tu. Watu hao si wengine bali walikuwa ni Meje Generali Louis Chomboko sambamba na Mr Godliving Kimato Director General wa Tanzania Intelligence and Security Services (TISS). aliyenipa habari hizo hakuniambia kikao hicho cha watu wawili kilikuwa kikizungumzia masuala yapi. Sasa ni wajibu wetu kumpata Major General Chomboko ili tupate kujua kile ambacho kimezungumzwa." Aliongeza mjumbe wa tatu ambaye suala lake liliwafanya wajumbe wote sita wakae kimya kwa muda wakitafakari hilo. Wengi walimjua na kumtambua mzee Chomboko kutokana na wadhifa wake aliowahi kuushika akiwa Jeshi la wananchi wa Tanzania. Lakini pia walijua bado alikuwa afisa Usalama mwandamizi sambamba na ushauri wa kiulinzi na kiusalama anaoutoa ama kuwajibika kuutoa katika Serikali na hata vyombo vya kiusalama. Licha ya kujua hilo lakini hawakujua hili la kuwa kwake katika kitendo kile cha watu watano ambacho kilijulikana kama Finally system in the decisions. (Kitengo cha Mwisho katika Maamuzi). Hawakujua kuwa Meja jenerali Chomboko hakuwa mtu wa kufuatiliwa kwa urahisi kutokana na kutembea kwake na watu maalum ambao huwezi kuwaona katika namna yoyote. Watu ambao walikuwa mfano wa giza hata katika mwanga wa Jua la mchana. Watu ambao walikuwa hatari katika aina yoyote ya Mapigano ya mikono, silaha na hata mateke. "Hili lako limekuja katika Muda ule Muafaka. Muda ambao tunatakiwa tumlazimishe General chomboko aifanye kazi yetu. Lakini kabla hatujamuendea ni lazima tutekeleza mara moja katika kuwaondoa watu hawa katika maeneo tulioambiana hapa. Kwa kumalizia Naomba vijana waambiwe mara moja wawe macho na wawe tayari kwa Mapambano." Aliongea mwenyekiti wa mkutano ule, kisha kuufunga wakiahidiana kukutana jioni hiyo katika Jengo hilo hilo.



    ******

    Macho yake yalikuwa yameelekezwa kwenye lango la ofisi za bandari akitizama kila mtu atokaye na aingiaye. Ushungi na baibui vilimfanya Teddy aonekane kama mwanamke wa kiislam anayefuata misingi yote ya Dini yake. Macho yake yalikuwa kule kumuangalia Veronica Senka. Msichana ambaye alianza kazi ya kumfuatilia tokea pale alipokabidhiwa na masimba. Alifika hapo mapema sana akitaka awe wa kwanza kuingia katika eneo hilo la bandari. Hata alipofanikiwa kuingia na kukaa kwa muda mrefu hakuwa amemuona mwanamke huyo. Alivumilia kwa muda mpaka pale alipomuona mwanamke yule akishuka kutoka kwenye gari moja ya kifahari aina ya Ranger Rover. Akatulia hapo akimwangalia mwanadada yule alivyokuwa akitembea. Mwendo wa mwanadada huyu haukuwa mwendo kama wa wanawake wengine. Mwendo wake ulisadifu ufedhuli. Ulisadifu roho mbaya na hata ukatili. Kwa mara ya kwanza akashangaa bandari kuajili mtu wa aina hiyo. Mtu ambaye muonekano wake pekee ulionyesha kule ambacho kimefichika ndani yake. Hilo likamfanya ahisi uwepo wa kitu kisichoeleweka hapo bandarini. Akatuliza macho yake kumuangalia kiumbe huyu. Wakati kiumbe huyu akiukaribia mlango wa ofisi ile, vijana wawili wakatokea kwa mbele yake kisha kumpa kitu kama kikaratasi. Baada ya kupewa kikaratasi hicho wale vijana wakapita wakimuacha mwanamke yule akiingia ndani ya ofisi. Hilo akaamua kuliacha. Punde akainuka tayari kwa kuanza na vijana wawili walioonekana wakimpa Vero kikaratasi. Aliondoka pale akihakikisha hatiliwi Shaka na Macho ya watu waliojazana Hapo. Macho ya upekuzi na hata udakuzi. Akafanikiwa kutoka nje ya eneo la bandari sambamba na vijana wale. Baada ya kutoka hapo akawaona wale vijana wakijipakia kwenye Ranger Rover ambayo muda mfupi ilitoka kumshusha Vero. Baada ya vijana wale kuingia ndani ya Gari, Teddy akazuga kama anavuka barabara, mbele kidogo akaifika gari aliyokuja nayo. Bila hata dereva kuambiwa wapi pa kwenda, gari iliwashwa na kuanza kuifuatilia gari ile. Hilo kwa Teddy lilikuwa sio jambo la kawaida, jambo ambalo hakulitarajia, hakuwa amemuacha dereva kwenye hii gari, hakuwa amemuacha mtu mwingine ndani ya gari hii. Kwa nini hakuingia upande wa Dereva akaingia upande wa Abiria? Amekosea na kupanda gari isiyo ya kwake ama ilikuwaje Hapa? Wakati akijiuliza maswali hayo akakisikia chuma kikigota kwenye kichwa chake. Kisha sauti tulivu ya kike ikitamalaki katika ngoma za masikio yake. "Tulia Teddy,. Uliona umjanja sana kufuatilia mambo yasiokuhusu. Sasa naamini leo ni Mwisho wako. Nakuapia hutaliona Jua la Kesho." Kufikia hapo Teddy akagundua kuwa alikuwa ameingia katika mikono ya kina Jimmy. Lakini kukumbuka kuwa Masimba alikuwa Eneo hilo kulimpa nguvu na kuamini hata kutekwa kwake Masimba alishuhudia na kuliona hilo. Teddy akatulia tuli kama alivyoambiwa.





    Teddy akatulia kama alivyoambiwa. Akaiacha gari iendelee kutembea huku akiamini uwepo wa macho ya masimba kung'amua kilichotokea hapo. Bado mdomo wa bastola haukuondoka kisogoni, bado mdomo wa bastola haukushushwa. Bado uliachwa pale pale, kikubwa zaidi ni ukimya ndani ya gari. Hakuna aliyeinua mdomo kuongea chochote. Kwa Teddy hilo lilikuwa tukio ambalo hakulitaraji, tukio ambalo hakujua kama lingetokea mahala hapo na kwa staili hiyo. Kwa mara ya kwanza aliusifu uwezo wa kiuchungizi wa watu hawa. Alijulikana mapema licha ya kujibadili. Alitambukiwa mapema tokea akiingia hapo na pia alichukuliwa kirahisi mfano wa kuku wa mdondo. Gari ikaendelea kutembea pasipokujua wapi anaelekea. Muda wote alijitahidi kuangalia nje, lakini kila alipokuwa akilitenda hilo mdomo wa bastola ulizigandamizwa kichwani. Wakati anaendelea kuliwaza hilo wakashtuliwa na kishindo kikubwa kilichotokea, kishindo ambacho kilisababisha gari yao kuyumba na kwenda kuyavaa magari mengine yaliokuwa yameegeshwa pembeni mwa barabara. Kitebdo hicho kikasababisha Dereva kutupwa nje kwa kupitia kwenye kioo.. huku mwanamke aliyekuwa amemuweka Teddy bastola akichupa na kuangukia kwa Nje.. hilo lilikuwa ni jambo ambalo Teddy aliliona mapema hasa kutokana na kuiona gari ambayo ilikuwa nyuma yao kwa tofauti ya magari matatu. Kwahiyo iliposikia kile kishindo alijua nini ambacho anatakiwa kufanya. Ni muda huo akiliwaza hilo akamuona mwanamke aliyekuwa nyuma yake akichupa na kuangukia nje.. Hata yeye akalifanya hilo. Muda mfupi alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakikimbizana huku na huko wakipiga kelele. Licha ya kukimbia huko lakini macho yake yalikuwa yakimtafuta mwanamke yule aliyetoka ndani ya gari na kukimbia. Aliendelea kukimbia akiangalia kila upande. Licha ya kuangalia huko hakumuona msichana yule akata kusimama ili arudi kule alipotoka. Lakini hilo alililipinga, hapakuwa na sababu ya kurudi pale. Lakini akaona kusimama pembeni kutizama mienendo ya watu katika tukio lile kilikuwa ni kitu muhimu. Alisimana pembeni mwa jengo moja la Ghorofa. Macho yake yalikuwa yakitizama mkimbizano wa watu. Mkimbizano ambao alihitaji sana kukiona kitu ndani yake. Macho yake hayakutulia kutizama huku na kule. Punde akaiona ile gari aina ya ranger rover iliomshusha veronica kule bandarini ikisogea taratibu. Macho yake yakaongeza umakini kuitizama. Gari ile ikapita eneo la tukio na kuongoza kama inakwenda posta mpya. Teddy akaona ulikuwa muda wa kufanya hivyo. Muda mfupi alikuwa ndani ya Tax akiifuatilia ile gari kwa nyuma. Muda wote alikuwa akimsisitizia dereva kutokuipoteza ile Ranger Rover machoni mwake. Dereva alikuwa akitii kila alichokuwa akielekezwa ama kuambiwa na teddy. Gari ikaendelea kuhama barabara kutoka hapa na kwenda kule. Walipofika kwenye mnara wa Askari posta mpya, gari ile ikachukua barabara iendayo kivukoni. Lakini mbele kidogo wakaiona ikisimama mbele ya New Africa Hotel. Dereva tax naye akaisimamisha pembeni mwa kituo cha tax palepale hotelini. Mlango wa Ranger Rover ukafunguliwa, watu wawili wakashuka na kuingia ndani. Hawa hawakuwa watu anaowafahamu, wote walikuwa wageni machoni mwake. Wakati akiwashangaa watu wale mara akaiona bajaji ikisimama mbele kidogo na sehemu iliposimama gari. Akashuka Veronica akionyesha ni mwenye wasiwasi. Baada ya Vero kushuka alisimama Nje kidogo na kuzungumza mawili na watu ambao walikuwa ndani ya ranger rover, kisha akaongoza na kuingia ndani. Teddy bado alikuwa Ndani akishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Muda wote alikuwa akichunguza kila upande kama angefanikiwa kuona mtu yeyote anayewafuatilia. Lakini hakuona chochote. Akaingizs mkono mfukoni na kutoka na noti mbili za elfu tano tano na kumlipa dereva. Baada ya hapo akaufungua mlango wa tax na kushuka atembea kuelekea njia tofauti. Kufuka mbele kidogo akasimama sehemu ambayo huuzwa vitabu. Baada ya kupekua hiki na kile Teddy akatoa pesa na kuchukua kitabu kiitwacho MIKATABA YA KISHETANI kilichoandikwa na Hayati Ben Mtobwa. Baada ya kukinunua akakitia ndani ya baibui na kuridi tena kule hotelini. Muda wote macho yake yalitembea na sura ya kila mtu. Alihitaji kujua hakuna jicho lolote linalomtizama kwa uchu. Alihitaji kufahamu kama alikuwa akifuatiliwa ama la!. Hilo akaligundua katika namna ya kipekee. Mbele ya jengo fulani upande wa pili mwa barabara akakiona kitoto. Kitoto kidogo kikicheza kanakwamba mama yake alikuwepo karibu. Macho yake yakavutiwa na yule mtoto, sio kuvutiwa kwa upendo. La hasha!! Bali muonekano na jinsi mtoto yule alivyokuwa akizungusha macho kanakwamba kuna kitu ambacho anakiangalia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Macho ya mtoto yule yalikuwa yakizunguka katika aina ambayo kama ungekuwa mtu wa kawaida usingeweza kugundua wala kung'amua chochote. Kila wakati macho yake yalitizama huku na hata kuangalia upande wapili wa barabara. Hilo kwa teddy halikuwa jambo la kawaida. Alihisi mtoto huyu hakuwa mtu wa kawaida. "Aliyemuua Vicky ni mwanaume aliyejibadili na kuwa na muonekano wa kike. Pia hupenda kutembea na kitoto cha kiume." Hatimaye Teddy Alikuwa amekumbuka maneno ambayo aliambiwa na masimba usiku uliopita. Moja kwa moja akatambua kuwa mtoto mwenyewe alikuwa huyu. Je alikuwa na nani? Lilikuwa swali ambalo lilipita kichwani kwake. Alihisi uwepo wa mtu mahala akimwangalia yule mtoto. Wakati analiwaza hilo akamuona mtu akitokea kule kule alipotokea yeye wakati anakuja na tax. Huyu alikuwa masimba akitembea kwa mwendo wa kawaida, hata pale walipokutanisha macho yao hapakuwa na chochote zaidi ya macho yao kusema "huyu ndio mtoto mwenyewe". Kisha kila mmoja akiendelea na Hamsini zake. Wakati masimba akitembea akielekea ndani ya new afrika hotel, Teddy alikuwa akiivuka barabara akielekea kule ambapo anacheza yule mtoto. Alitembea kama mtu mwingine mwenye haraka zake. Hatua ya kwanza mpaka ya tano ikapita pasipo kutokea kwa rabsha. Hatua ya Sita haikupita hivi hivi.

    [05-26, 18:26] Ibrahim Masimba: MHatua ya sita haikupita hivi, haikupita kwa kuwa tayari kitu kikasikika na pia kuonekana. Mlio wa risasi, naam mli0 ambao ulitoa burudani ya kuogofya katika macho na hata masikio. Wakati Teddy akichupa huku na kule katika aina fulani hivi. Mtoto aliyekuwa akicheza mbele yake tayari alikuwa amepaaa na tayari alikuwa ameanguka chini damu zikivuja kifuani. Lilikuwa tukio lililofanyika ndani ya dakika moja. Mtoto alikuwa akicheza muda mfupi akionyesha kufurahi, mtoto huyu muda huu roho yake ilikuwa ikipaa ikirudi kwa muumba wake. Hata wakati Teddy akichupa na kutua sehemu nyingine hakufikiria kama mtoto yule angekuwa maiti katika muda huo. Ni hilo lililomfanya atupe macho yake katika ghorofa zote. Ni muda huo katika jengo la Hoteli ya New Afrika akakiona kioo kikirudishwa kuonyesha muuaji alikuwa hapo. Lakini hakuinuka katika muda huo. Bado aliuona ni kama mtego. Hakuna muuaji mwenye kuweza kufanya kile ambacho kimefanywa muda mfupi. Mauaji kutokea kisha dirisha kufungwa katika muda huo huo.. akapuuza na kutulia pasipo kufanya chochote. Akaendelea kutulia akitafuta namna ya kuondoka Eneo la tukio pasipo kuonekana. Alitaka kuondoka kwa kuwa alijua ameonekana na pia alihisi mtoto yule kauawa kutokana na kule kuonekana kwake akimfuata. Muda mfupi baadae alikuwa akiondoka hapo akielekea upande wa pili wa kituo cha daladala posta. Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilionyesha kuuvuruga akili yake. Kujulikana kwa urahisi machoni kwa watu wanaowapeleleza ni ishara mbaya katika masuala yote ya kijasusi. Kuuawa kwa mtoto yule mbele ya macho yake ni kitu ambacho kiasi fulani kilimpa hofu na kumtetemesha. Ina maana muuaji angeamua angemuondoa yeye katika namna fulani aipendayo. Hapakuwa na ugumu wa kuuawa ikiwa mtu aliyembele yake ameuawa. Kufikia hapo akaona ndio muda muafaka wakumtafuta Masimba ili aongee.. ili afahamu kama yeye ndiye aliyetumbukiza Risasi kifuani kwa mtoto. Alitaka kufahamu yule mtoto alikuwa nani na amefikaje katika himaya ya watu hawa. Ikabidi asogee pembeni mwa jengo la Benjamin Mkapa. Akaichomoa simu yake tayari kumpigia Masimba. Lakini kabla hajafanya hivyo Ujumbe mfupi ukaingia katika simu yake. "Unaandamwa Kuwa makini ". Ulikuwa ujumbe kutoka kwa namba ngeni, namba ambayo hakumjua mmiliki. Hakutaka kujiuliza zaidi ya kuondoka hapo akiingia katika mkusanyiko wa watu na kupenya kwenye Magari. Alipofika mbele kidogo akatulia pembeni mwa Jengo la Posta ili kuangalia kama alichoambiwa ni kweli. Haikupita hata dakika akawaona watu wawili ambao ni wale walioshuka kwenye Ranger Rover pale New Afrika Hoteli. Walikuwa wakihaha kutafuta huku na huko. TEDDY akatamani kucheka Jinsi watu wale walivyokuwa wakihangaika na kuhaha huku na Huko. Aliendelea kuwaaangalia watu wale kwa muda mpaka pale walipoondoka hata yeye akaamua kuondoka.



    *****



    Giza totoro liliupamba mtaa huu na kusababisha kutokuonekana kwa mtu yoyote isipokuwa sauti pekee za mbwa ndizo zilizosikika. Masimba alikuwa amesimama sehemu katikati ya giza macho yake yakiwa barabarani kuiangalia gari ya Suresh. Yalikuwa makazi mapya ya Suresh tokea kutokea kwa tukio la kuuawa kwa Waziri mkuu. Hata kule Mbagala hakuwa akiishi. Ilimchukua Masimba siku tano katika uchunguzi wake kugundua sehemu ya Makazi ya Suresh. Usiku huu aliamua uwe usiku wa kumuondoa Suresh katika Ulimwengu huu. Alisubiri kwa muda wa dakika tano, ndipo alipovuta hatua kusogea katika Jengo analoishi Suresh. Alitaka Suresh amkute katika himaya yake, amkute akiwa ndani akimsubiri kama sio kumngojea. Alitembea katika kiza kile akitembea sambamba na vivuli vya miti, alipokaribia karibu na uzio uliozungushiwa nyumba ile, akaisikia minong'ono huku Harufu ya Bangi ikipita katika matundu ya pua yake. Vijana walikuwa wakiuvuta mmea. Hilo likampa imani kuwa walinzi hawa hawawezi kuwa katika kiwango cha kupambana naye. Akavuta tena hatua kwa umakini. Bastola ilikuwa kiunoni lakini hakupenda kuitumia. Akaendea kunyata mpaka umbali wa hatua kumi kutoka pale walipo. Akasimama akafikiria kipi cha kufanya ili kuingia ndani ya jengo pasipo kuleta Rabsha. Hapo ndipo alipoamua kuuparamia mti kwa umakini mkubwa na alipofikia usawa wa uzio ule alijitupa na kutua ndani kwa wepesi kama Bua.







    Akatua chini mfano wa ubua. Akatoka hapo akitembea na tumbo mpaka nyuma ya kibanda ambacho kimejengwa kwa ndani. Akatulia hapo kwa muda akitizama kama atamuona mtu yoyote yule. Mtu ambaye atatokea ama yule ambaye atahisi uwepo wake. Hapakuwa na mtu na hapakuwa na dalili yoyote ya uwepo wa mtu. Akasogea tena na tena akiitafuta njia ya kuingilia kwa ndani. Wakati anakaribia kuufikia mlango, akausikia mngurumo wa gari ukitokea kwa nje, kisha akalisikia lango likifunguliwa kisha ule mngurumo wa gari ukaendelea kusikika. Sekunde mbili baadae akahisi gari ikisimama. Hapo akatambua kuwa Suresh ndiye aliyekuwa ameingia hapo. Akaufuata mlango na kukinyonga kitasa. Mlango ukafunguka, akaingia ndani kwa mwendo wa Taratibu, mwendo ambao haukusikika hata kwa mtu ambaye yuko mbele kwa umbali wa hatua mbili. Wakati akiifikia sehemu fulani ndani ya jumba hilo akaisikia sauti yenye lafudhi ya kihindi kutokea nje. Hapo akajua kuwa huyo lazima atakuwa ni suresh. Akaendelea kusubiri, ndani ya sekunde akauhisi mlango ukifunguliwa kisha kusikia hatua za mtu zikitembea. Kwa kuwa kulikuwa na giza Masimba Hakujua mtu huyu alikuwa nani. Akaendelea kutulia akimngojea apite. Manukato mazuri puani na hatua za taratibu zilitosha kumfahamisha masimba na kumueleza kuwa mtu huyu alikuwa ni mwanamke. Mtu huyu alikuwa ni mwanadada. Wakati akiliona hilo mwanamke yule alikuwa amefika usawa wa pale mahali aliposimama. Masimba akamuacha apite kwanza kisha akaanza kumfuatilia nyuma nyuma. Bado hatua zake zilikuwa zile Zile ambazo hazikusikika. Lakini kwa nini jumba lote hili limejengwa huku na lipo giZa? Ni swali alilojiuliza wakati mwanamke yule akiufungua mlango wa chumba kilicho mbele yao. Kabla mlango haujajifunga masimba akawahi na kujitumbukiza. Hata hapa walipoingia bado kiza kiliwapokea, licha ya ukimya huo lakini pia sehemu hii iliuonekana kama stoo ama chumba kinachotumiwa kwa shughuli ambayo haikutakiwa kuonekana. Mabox sambamba na mifuko mikubwa ambayo ilionekana kujazwa vitu ilikuwa imehifadhiwa vizuri sana. Macho yake bado yalikuwa yakimtizama mtu yule. Kumtizama mwanamke yule. Kumtizama katika utimamu wa kiakili na kimwili. Mikono yake ilikuwa tayari kuichomoa bastola na kumuulia mbali, lakini hakutaka kufanya hivyo kwa kuwa alitaka kujua kule aliko suresh na wapi anapoelekea mwanamke huyu. Wakaipita ile sehemu na kutokea sehemu nyingine. Bado giza liliendelea kutawala katika jengo hilo. Mbele kidogo akauona ukuta, ukuta ambao ulikuwa ukionyesha ulikuw mwisho wa ile safari yao. Mwisho kwa kuwa haapa kuonyesha kama mbele kuna mlango uliokuwa ukiendelea. Lakini uelekeo wa mwanamke huyu ulionyesha uwepo wa kitu fulani. Akaona ulikuwa muda wa kumuwahi. Muda wa kumzuia kusogea ama kusonga mbele. Ilikuwa sekunde tu iliyotosha kuufanya mdomo wa bastola kumtekenya mwanamke yule ubavuni. "Tulia dada na usijaribu kufanya chochote.. " aliongea masimba huku mdomo wa bastola akizidi kuugandamiza.



    "Wewe nani kwani? Na utanataka nini? Umeingiaje humu ndani?." Aliuliza mwanamke maswali mfululizo akionyesha kutetemeka. "Sio shughuli yako kujua nimeingiaje, ilaunapaswa kujua kile ninachokitaka. Sasa ninachokitaka ni roho ya Suresh. Na nataka unisaidie kumpata. Ukikaidi hata wewe roho yako nitaiweka katika orodha ya roho zile ambazo zimepangwa kupelekwa kuzimu. Naomba uongoze ulipokuwa unakwenda bila kufungua mdomo wako, la sivyo hutaliona Jua la kesho." Alinguruma masimba huku akiendelea kuugandamiza mdomo wa bastola mgongoni kwa binti. "Kaka mbona unanionea? Mbona suresh simfahamu na sijui unachoongea.!!.." aliongea binti akionyesha kutokujua kitu. "Binti usinilazimishe nikuue. Usinilazimishe niufumbe mdomo wako kwa risasi. Unafanya ninachotaka hufanyi? Alisema Masimba huku akimuangalia msichana. "Fanya kwa kuwa unaongea kitu nisicho... uwiiii nakufa... " hakuimaliza kauli yake, risasi kutoka kwenye bastola ya masimba yenye kiwambo cha kuzuia mlio ikapenya kwenye paja lake la mguu wa kushoto. Binti akalalama kwa maumivu. Hakujua kama Masimba alikiwa hatanii. "Naona sasa umekipata kile ambacho ulikuwa ukikihitaji. Naomba ufanye kama nilivyokwambia, nataka unionyesha alipo Suresh kabla sijakumaliza." Alisema Masimba huku sasa akimuonyesha Ishara ya kumtaka abonyeze kitufe kimoja kati ya vitatu vilivyopo ukutani. Msichana huyu akigugumia kwa maumivu akabonyeza kitufe, punde ukuta ukajifungua na kuacha uwazi kama mlango. Masimba akamtaka aongoze kuingia ndani. Binti hakuwa mbishi tena. Akaongoza ndani huku akigugumia kwa maumivu. Muda wote bastola ilikuwa mkononi tena mgongoni kwa mwanamke huyu. Walipopita kwenye ule uwazi binti akabonyeza vitufe kwa ndani sehemu ikajifunga tena wote wakajikuta ndani ya chumba kizuri na kilichopambwa sana. Kilionekana kuwa ni chumba cha kulala.



    "Msubiri suresh atakuja hapa muda mfupi.." aliongea yule msichana huku akimuangalia Masimba Usoni. Macho yake yakurembua yalikuwa usoni kwa masimba. Ingawa macho yalikuwa usoni kwa Masimba, lakini mkono wake ulikuwa ukishuka taratibu sehemu ambapo palihifadhiwa bastola. Lakini hakujua kuwa macho ya masimba yalishamuona zamani, yalishamuona wakati mkono ukielekea sehemu hiyo. Mkono wa mwanamke yule haukufika hapo, haukufika sehemu husika. Risasi mbili zilitosha kuumaliza uhai wa binti huyu. Akajilaza taratibu kitandani akiwa maiti. Baada ya kugundua ameshakufa akamuweka vizuri na kumfunika na shuka, kisha yeye akatulia pembeni ili kumsubiri suresh akiwa katika giza lile lile. Aliona ulikuwa ni mpango bora na kurahisisha kazi kuanza na watu hawa ambao walikuwa kama matawi katika biashara hii.

    [05-28, 13:44] Ibrahim Masimba: Ulikuwa ni mpango mzuri kuanza na watu hawa. Ulikuwa mpango mzuri wa kulimaliza hili suala katika aina kama hii. Jimmy na Suresh ndio chanzo cha kuharibika kwa watoto wengi. Vijana wengi walitopea katika utumiaji wa madawa ya kulevya kutokana na hawa watu wawili wakishirikiana na viongozi wa serikali. Ni aibu kuwaacha wakiendelea kuishi wakati huku mtaani vijana wengi walikuwa wameharibika na kuharibikiwa. Alioona hukumu sahihi ya Watu hawa ni Risasi, risasi ya kichwa ndio hukumu sahihi kwa watu hawa. Leo hii alikuwa chumbani kwa suresh akimsubiri huku pembeni yake kukiwa na maiti ya mwanamke ambaye alionyesha kuwa ni kimada wa Suresh. Alikuwa ametulia vilevile na giza bastola yake ya Kirusi Revolver colt 48 ilikuwa mkononi ikisubiri kuitoa roho ya suresh na kuisafirisha. Alitaka kuipeleka kuzimu, alitaka kuipeleka ikakutane na watu wote waliouawa na waliokufa kutokana na Matumizi ya Madawa ya Kulevya. Akaivuta subira katika aina ya kutokukata tamaa. Punde ukuta ule ukajifungua kisha akaonekana mwanaume wa kihindi akiingia taratibu. Baada ya kuingia mtu huyu akabonyeza vitufe mlangoni na ukuta ule kujifunga tena. Baada ya kufanya hivyo akatembea kwa madaha mpaka iliposwichi ya kuwashia Taa katika Chumba kile. Akaupeleka mkono na kuwasha.. nusura azimie kwa mshtuko baada ya kumuona Masimba akiwa ametulia pembeni huku Bastola yake ikiwa anamtizama yeye. "Karibu sana Mr Suresh.. Pia nisamehe kwa kukuingilia kwa Njia hii. Sikuwa na budi isipokuwa kufanya hivi." Aliongea Masimba akitizamana na Suresh katika aina fulani iliyompendeza machoni kwake. Masimba akainuka na kusimama Bastola Ikiwa mkononi bado. "Suresh leo nimeamua kuja mwenyewe kukuuliza machache ambayo nadhani utanijibu pasipo kuleta purukushani." Aliongea Masimba sasa akisogea karibu kabisa na Suresh. Suresh bado hakuinua mdomo wala macho kutizama. Alikuwa muoga kupindukia, alikuwa akitetemeka na hata midomo kukutana. "Suresh sasa naomba kaa pale ujibu maswali yangu. Naomba ujibu nitakavyo usije ukaniacha nikakupoteza kama huyo malaya wako." Bado aliongea Masimba huku akimuonyesha Suresh sehemu sahihi ya kukaa. Suresh bila kubisha akaongoza mfano wa kondoo. Akajibweteka chini akionyesha kuwaza kitu. Kitu ambacho hakujua ni vipi angeweza kukipata. Mwili wa mwanamke uliolala ukiwa hauna uhai ulimtisha na kumtia Hofu. Sasa alikuwa akikiangalia kifo mbele ya macho yake. Kifo ambacho alipenda kukitenda kwa watu wengine. Leo Ilikuwa zamu yake, leo ilikuwa zamu ya kifo chake. Akainua macho kumtizama masimba na hata kuuangalia unbali sahihi. Umbali kutoka alipo masimba na hata kutaka kujaribu kumvamia. Bado macho ya Masimba yalimuangalia kwa umakini na upole. Bado macho ya Masimba yalikuwa yametulia usoni kwake. Hakupepesa na hata kuangalia sehemu Tofauti. Alimtizama akikisoma kilicho katika akili yake. "Mbona ananitizama hivi? Mbona haonyeshi kuogopa? Yalikuwa maswali yaliogonga kichwani kwa Suresh. Akaamua kutulia na kuitafuta mbinu nyingine. "Suresh nahitaji kujua ukimuondoa Hayati waziri mkuu, ni nani mwingine yupo nyuma ya biashara hii mnayoifanya? Akauliza masimba kwa sauti tulivu. Suresh akakaa kimya kana kwamba hakuwa amelisikia swali hilo. "Suresh naongea na wewe, nani yupo nyuma ya hii biashara? Akauliza tena Masimba. Lakini bado Suresh hakutaka kujibu. Bado suresh alikuwa kimya. "Suresh usitake nitumie nguvu katika hili utajuta.." alilisisitiza Masimba. "Sijui unachozungumzia Ndio maana sina majibu ya maswali yako. Pia huwezi kuvamia nyumba za watu na kuua watu hovyo. Hata kama wewe ni mpelelezi hatuendi hivyo." Akajibu Suresh kwa sauti yenye kejeli ndani yake. "Suresh naomba unijibu maswali yangu. Narudia tena sitaki kutumia nguvu.. tambua ukinilazimisha na nikatumia utaumia." Narudia mara ya mwisho, ni nani yupo nyuma ya Biashara Yenu ukimtoa Waziri mkuu.? Akarudia tena.



    "Sijui unachozungumzia na sielewi unachosema. Kama unaona una hofu na mimi nipeleke kwenye vyombo vya dora." Akajibu Suresh kwa kejeli tena.



    "Sawa nimekuelewa. Lakini nikwambie kuwa sitakupeleka kwenye chombo chochote cha dora, bali nitakusafirisha kukupeleka Kuzimu. Sasa pokea hiyo kwanza." Aliongea Masimba huku bastola ikikohoa na risasi kwenda kupenya kwenye mkono wa kushoto... "haapana haapaana utanionea bure mimi sijui chochote." Aliongea Suresh huku akihamanika. Muda ule ule akakurupuka na kutaka kwenda kumvaa Masimba. Hakuujua Wepesi wa Masimba. Hakuujua wepesi wa mtu huyu. Kwani muda ule ule akajikuta akipokelewa na mateke matatu mfululizo. Mateke yaliyomrudisha chini na kumuacha akitweta. "Inuka upambane, wewe si mwanaume? Inuka tena nikumalizie." Aliongea masimba huku akimuangalia Suresh aliyekuwa akitweta pale chini. "Sasa naomba unijibu kabla sijakipasua kichwa chako kwa risasi. Huwa nawachukia sana watu wa aina yako. Mmeniharibu mamilioni ya vijana kwa uroho wenu wa pesa. Sasa niambie nani yupo nyuma yenu." Alifoka masimba. "Unajisumbua na kupoteza muda wako. Niue tu maana hutapata chochote kutoka kwangu." Aliongea Suresh huku akionyesha hana masihara. Haikupita sekunde Suresh alionekana kuilaza Shingo Yake pembeni huku mapovu meupe ya kimtoka mdomoni. Kilikuwa kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa. Suresh alikuwa amejiua kwa kumeza vidonge fulani ambavyo hutumiwa Sana na majasusi wengi duniani kuepusha kutoa siri hasa pale unapobanwa. Suresh aliamua kuifuata njia hiyo. Alikuwa amekufa bila kutoa siri ama kitu chochote ambacho kingeweza kumsaidia masimba.



    Hakuwa akipumua na hakua hai tena. Alikuwa amekufa akimuacha masimba kwenye giza totoro. Giza la kujua kile ambacho alitaka kukijua kutoka kwake. Kile ambacho kingemsaidia kumjua yule aliyenyuma ya hawa vijana. Hakuamini kama wakina Jimmy wangeweza kuwa wao kama wao. Alihisi uwepo wa watu wengine, alihisi uwepo wawatu wengi katika biashara hii. Hapo ndipo alipoamua kuipekua nyumba ya Suresh. Alianzia kuipekuwa kwa kuangalia kila sehemu. Kila alipoangalia hakuweza kufanikiwa kitu. Licha ya kujitahidi lakini hakupata kitu chochote cha kumsaidia. Baada ya kuuona ugumu huo akaona huu ulikuwa muda wa kufanya kile ambacho kingewapa hasara watu hawa. Alitoka mle chumbani na kutembea mpaka nje sehemu ambayo yaliegeshwa magari. Kufika hapo bado giza lilikuwa totoro. Bado hakumuona mtu yoyote. Jambo hilo lilimfanya agundue kuwa walinzi wa jumba hili walikuwa Nje wa Kilinda. Alichokifanya ni kuelekea kwenye gari moja kati ya zile, akafungua tanki la mafuta kisha kuyaachia yote ya mwagike ardhini. Baada ya kuhakikisha mafuta yamelowesha ardhi na sehemu za magari mengine yalioegeshwa hapo. Masimba akapiga hatua kama kumi kisha kutoa kibiri maalum mfukoni. Akakiwasha na kukitupia katikati ya magari yale. Mlipuko mkubwa ukasikika, moto mkubwa ukawaka.. wakati huo masimba alikuwa ameshachupa akiondoka taratibu sehemu ya tukio akiliacha Jengo lile likiteketea pamoja na vitu vingine vyote vilivyopo ndani. Alikuwa akitabasamu, akitabasamu akifurahishwa na kilichotokea. Muda wote aliyapenda mapambano, alipenda kupambana na hakuogopa hilo. Akaendelea kutembea katika giza akipishana na magari ya zimamoto yakielekea huko.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******

    Alijiinamia akifikiria kile ambacho

    [05-30, 14:51] Ibrahim Masimba: Alikuwa ameinama chini akifikiria kile ambacho anatakiwa kukifanya. Kitendo cha kutekwa bandarini kabla ya kuokolewa kilimpa mawazo sana. Alijua kuwa alikuwa akitembea na watu kila sehemu. Alijua kuwa alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba. Hilo likampa tafakuli thabiti katika kulitenda lile ambalo alipaswa kulitenda. Lile ambalo lingemuweka Huru na kumfanya afurahie mapenzi yake na mumewe kipenzi Masimba. Lakini kwa sasa hawakuipata nafasi hata ya kuburudisha miili yao na nafsi zao. Hawakuupata muda wa kumtafuta mtoto wa pili. Watawezaje kufanya hivyo ikiwa wote wanatafutwa? Watawezaje kufanya hivyo wakati kuna macho kila mahali yakimtizama? Hawakuwa na Njia ya kufanya isipokuwa kuwa kabili watu hawa. Ni lazima Jimmy na Suresh wauawe. Hilo akalipitisha. Ni wakati akiliwaza hilo akaisikia sauti ya mtangazaji wa Tv akitangaza habari. Akitangaza habari ambayo iliushtua moyo wake na kuisisimua Damu mwilini mwake. "Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Suresh Patel Sigh sambamba na mwanamke asiyetambulika. Wameuawa kwa kupigwa risasi kisha nyumba yao kuchomwa moto. Habari kamili itawajia baadae." Ilikuwa habari ile ambayo ilimuacha Teddy kwenye mawazo. Ilimuacha teddy katika tabasamu. Masimba alikuwa ameshaifanya kazi yake. Hilo likampa tumaini jipya. Naye sasa aliamua kumtafuta Jimmy. Aliamua kumtafuta kwa ajili ya kulipa kisasi. Kisasi cha kuuawa kwa mdogo wake.



    Ingawa jimmy hakuwa muuajii katika suala la Vicky. Lakini alijua bila Jimmy kila kitu kisingetokea. Akajiinua pale alipokaa na kuiendea droo. Akaifungua na kutoa bastola zake mbili. Baada ya hapo akazipachika mwilini katika sehemu tofauti ambazo haziwezi kufikiwa kirahisi na macho au mikono ya watu. Akatoka mle chumbani sasa akiamua kurudi pale bandarini lengo likiwa ni kumtafuta Veronica Senka. Mwanamke mjuzi na mwenye kujibadilisha kutokana na mazingira. Alitembea taratibu mpaka kituo cha daladala Cha Ubalozi lengo likiwa ni kuangalia kama alikuwa akifuatiliwa ama la. Lakini mpaka anafika hapo na kuvuka upande wa pili kisha kupanda basi hakuweza kumtilia mashaka mtu yeyote anayemfuatilia ama anayemtizama kwa Hila.. kila mmoja alikuwa busy na Shughuli zake. Baada ya gari aliyopanda kufika maeneo ya daraja la salenda, akausikia ujumbe ukiingia kwenye simu yako. Akaitoa simu kwa haraka na kuufungua ujumbe kisha kuusoma. "Shuka kwenye gari uliyopanda. Nenda Magomeni kagera nyumba namba O912 kuna mtu anatakiwa kuondolewa hapa Duniani." Ulisomeka ujumbe huo kutoka kwa Masimba. Ile kujua tu kuwa Masimba yupi katika macho yake kila aendapo kulimburudisha sana. Alitambua sasa alikuwa ameingia kazini Rasmi. Dakika hii alikuwa chini akitembea baada ya kushuka kwenye basi. Akatembea mpaka pembezoni mwa barabara sehemu ambayo kulikuwa na kijiwe cha bodaboda. Teddy akaidandiq moja kisha kumuomba Dereva aendeshe kuelekea magomeni kagera. Sehemu ambayo aliagizwa kwenda kumpa mtu tiketi ya kuzimu. Muda wote damu yake ilikuwa ikimsisimka. Aliupenda mchezo wa kuua kuliko mchezo wowote. Alishuka magomeni mwembechai na kuanza kutembea kwa mguu akielekea kagera. Muda wote macho yake yalihama hapa na kwenda kule yakitizama kile kile ambacho ilikitizama kule mwanzo. Hakuiona hila yoyote kutoka kwa watu aliokuwa akipishana naye. Kila mmoja alikuwa tofauti na kawaida sana. Muda huu alikuwa akiifikia kagera. Akaingia kwenye mitaa miwili mitatu, mtaa wa tano alijikuta akitizamana na Nyumba husika. Nyumba anayotakiwa kuipeleka tiketi ya mtu anayetakiwa kusafirishwa kwenda kuzimu. Mkono wa Teddy ulishika tiketi ya kifo cha mtu huyu asiyemjua. Ilikuwa nyumba ndogo ya wastani ya vyumba visivyopungua vitano kwa kuitizama. Licha ya hivyo pia ilikuwa imejengwa mfano wa gorofa kwa kupandishwa nyumba nyingine kwa juu. Uzio wake haukuwa mrefu wala mfupi sana. Ulikuwa uzio wa wastani na mbele ya Jengo hilo kukiwa na geti kubwa Jekundu. Nyaya za umeme zilikuwa zimepita kuonyesha nyumba hiyo ilikuwa ikilindwa na mitambo maalum. Akaitizama kwa makini mpaka aliporidhika akaamua kupiga hatua kuelekea hapo. Kwa wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na moja jioni. Bado watu walikuwa wengi na kwa magomeni unaweza kudhani labda kumekucha.

    [05-30, 14:51] Ibrahim Masimba: Kwa kuwa macho ya watu yalikuwa mengi, Teddy akaamua kutembea tararibu akielekea hapo. Bastola zake zilikuwa mahala pale tulivu mahala ambapo hapakufikiwa na macho ya mtu yoyote. Mazingira ya nyumba hii yalianza kumpa mashaka pale tu alipokaribia geti la nyumba ile. Ni kitu cha ajabu sana kuambiwa ukaue mtu kisha uikute nyumba hiyo ikiwa haina ulinzi. Hilo lilimpa hisia fulani, hisia ambazo zilikuja kuamsha kengele za hatari hasa baada ya kuibonyeza kengele. Licha ya kubonyeza mara nyingi zaidi, lakini hapakuwa na majibu kutoka kwa mtu wa ndani. Akaamua kujaribu kulifungua geti. Kitendo cha kulisukuma geti, akaliona likifunguka lenyewe taratibu. Teddy akitizama kwa chati ndani. Lakini hakuweza kumuona mtu. Hakuweza kumuona mtu yeyote ama kitu ambacho kingemthibitishia uwepo wa mtu mahala hapo. Hilo likazidi kumfanya aongeze umakini. Mguu wa kulia ulikuwa Ndani huku wa kushoto ukifuatia. Sekunde nne baadae alikuwa akiingia ndani mwili mzima. Alikuwa akitizamana na uwanja usiokuwa na mtu isipokuwa magari ya kufahari yaliyoegeshwa hapo. Ukimya pia kilikuwa kitu kingine kilichoitawala nyumba hiyo. Teddy akatembea taratibu safari hii bastola yake ikiwa mkononi huku mdomo ukiwa umetangulia mbele. Akaupita uwanja kwa usalama pasipo chochote, akauendea mlango akaugusa.. Hata mlango pia ukafunguka. Kufunguka kuonyesha kuwa haukuwa umefungwa. Hilo likamuongezea umakini. Akaufungua mlango taratibu kisha kujipenyeza ndani. Hapo akaikuta sebule tupu, licha ya utupu huo lakini bado Tv ilikuwa ikifanyakazi kuonyesha kuwa palikuwa na mtu muda mfupi uliopita. Hilo pia halikuwa la kupuuzwa. Wakati akilishangaa hili la Tv, akakiona kipisi cha sigara kikiwa bado kinamoto kuonyesha kuwa mvutaji alikuwa hap0 muda mfupi uli0pita. Hilo pia hakulitaka lipite. Alitambua hapo palikuwa na mtu, alitambua hapo ndani kuna mtu. Lakini mtu huyu atakuwa amejificha mahala fulani. Akaiacha sebule katika namna hii, katika namna ya masikio ya sungura, masikio ya kunasa hiki. Akakifuata chumba ambacho kilikuwa hatua kama kumi kutoka sebuleni. Kukifikia chumba hicho alishangazwa na alichokiona. Licha ya chumba kuwa wazi lakini pia vitu vilionyesha kutupwa tupwa hovyo. Akaingia taratibu macho yake yakizunguka huku na huko mithili ya Bundi. Kila kitu ndani ya chumba kile kilikuwa kimetupwa huku na huko kuonyesha kuwa palikuwa pakitafutwa kitu muda mfupi uliopita. Mikono yake ikashika hiki huku macho yakitizama kile. Hakuona chochote cha maana. Akakiacha chumba kile huku mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele. Akaendelea kutembea na kutembea. Hata pale alipotokea kwenye chumba cha pili hali ilikuwa ni ile ile. Alikuta mlango wazi na pia hata vitu vilikuwa vimetupwa Hovyo. Hakutaka kuingia, akapita hapo na kwenda kutokea kwenye sebule nyingine. Mbele ya sebule hii akakutana na kitu kingine kilichomsisimua. Alikutana na matone ya damu. Ukutani na hata sakafuni. Licha ya matone hayo hapakuonekana uwepo wa mwili wa mtu yeyote. Sebule ilikuwa tupu kabisa. Kufika hapo Teddy alikuwa amejua kile kilichotendeka. Alikuwa amewahiwa muda mfupi uliopita. Amewahiwa na watu ambao hakuwatambua. Wakati hilo likimuweka gizani, akayaona matone ya damu yakitokea Juu ya Silling board. Ilikuwa damu ikivuja kutoka Juu kuonyesha kuwa kuna mtu majeruhi yupo huko. Kwa umakini wa Hali ya Juu akaikanyaga meza kisha ufungua mfuniko ambao ulitengeneza sehemu maalum ya kuingilia. Wakati akihisi labda atakutana na giza totoro. Hali ilikuwa tofauti. Kulikuwa na mwanga kama mchana. Akatanguliza kichwa na kuchungulia. Akashangaa baada ya kuuona ukumbi mkubwa kama wa mikutano. Lakini katikati ya Ukumbi huo alilala mtu akiwa katikati ya dimbwi la Damu.



    HATARIIIIIIII



    Wakati akidhani macho yake yatakutana na giza, hali ilikuwa tofauti, macho yake yakakutana na mwanga. Na haukuwa mwanga tu bali kulikuwa na ukumbi mkubwa tu. Ni katika ukumbi huo katikati ulilala mwili wa mtu, tena katikati ya dimbwi la damu. Akajivuta kwa juu na kuingia moja kwa moja kupitia sehemu ile. Baada ya kuingia akakiona kingine, kingine ambacho hakukidhania hapo mwanzo. Licha ya mlango mdogo wa kwenye silling board lakini juu ukishaingia kulikuwa na nafasi kubwa ambayo mtu unaweza kutembea pasipo na wasiwasi. Mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele, kidole kikiwa tayati kuifyatua Risasi. Akatembea kuufuata mwili wa mtu yule, mwili ambao ulilala katikati ya dimbwi. Macho yake yalitizama kwa umakini, masikio yake yaliinasa mivumo yote na sauti ya kitu chochote. Muda mfupi alikuwa pembeni ya mwili wa mtu yule. Mwili ambao sasa aliugundua kuwa ulikuwa wa mwanaume tena. Mwanaume wa makamo mwenye umri wa miaka inayofikia miaka hamsini. Kisu kilikuwa tumboni huku damu ikivuja kama maji. Akamgeuza ili kuutizama mwili wa mwanaume yule. Muda wote mikono ilikuwa tayari kwa chochote. Sura ya mwanaume yule baada ya kumgeuza haikuwa ngeni machoni mwake. Haikuwa ngeni kwake na hata jamii pia. Alikuwa Baba Askofu Ibrahim Lexandre Rengima. Askofu wa kanisa katoriki Jiji dar es salaam. Alikuwa yeye aliyekuwa amelala katikati ya dimbwi la damu. Kisu kikiwa kimesimama tumboni. Akili yake ikasimama kwa muda, ikasimama kutokana na kulikuta hili ambalo hakulitegemea. Baba Askofu Rengima kuuawa. Pili jingine ni Masimba kumtuma kuja kumuua mtu katika Nyumba hiyo. Nyumba ambayo inaonekana ilikuwa ni ya Askofu, askofu anayeheshimika sana hapa nchini na hata Nchi za Jirani. Kwa nini Masimba amtume hapa? Je alimtuma akijua mhusika ni Baba Askofu? Nani amemuua Askofu ikiwa yeye ndiye alitakiwa kufanya hivyo? Yalikuwa maswali ambayo hayakuwa na majibu. Licha ya kutokuwa na Majibu lakini alitambua Masimba pekee ndiye mwenye majibu ya maswali haya. Akaona aichomoe simu yake Aongee na masimba. Wakati akiipeleka simu sikioni, akaisikia sauti ikimuita, sauti dhaifu na sauti iliyokatika hatua za Mwisho. Haikuwa sauti ya mtu mwingine, bali ilikuwa sauti ya Baba Askofu. Teddy akaikata simu haraka kisha kumuinamia Askofu. Akagusa mapigo ya moyo wake. Kwa mbali akausikia moyo ukidunda. Wakati akitaka kujua nini cha kufanya akaisikia sauti ya Askofu ikimwambia. "Chu..chu.chukua ba..hasha pale me..mezani umpelekee ma..masimba. harafu ne..neenda nyumba ...naa namba 123 shekilaaang.... kabla hajamalizia kauli yake. Akashuhudia askofu akinyooka na kutulia. Alikuwa tayari amekata Roho. Teddy akainuka na kuelekea mezani. Meza ambayo aliambiwa kuna bahasha. Bahasha ambayo ilitakiwa kumfikia Masimba kwa wakati ule. Masimba huyu huyu aliyemtuma aje hapa kuitoa roho ya mtu. Hilo lilimshangaza na kumchanganya. Licha ya kuchanganyikiwa huko, lakini alitakiwa kuichukua bahasha kisha kuelekea Shekilango nyumba namba 123. Akaangalia mezani kwa juu hakuona chochote. Lakini alipotizama kwa makini akauona mchoro ukielekeza mahali fulani. Ulikuwa mchoro uliofichwa kwa macho ya kawaida. Mchoro ambao hauwezi kuonekana kwa macho ya watu wengine. Hapo akatambua Askofu alikuwa ni Zaidi ya Askofu. Michoro yake ilisadifu kile kilichopo ndani yake. Kile kilichopo katika ubongo na utaalamu. Kifupi kwa michoro ile alitambua Askofu alikuwa ni Jasusi. Je alikuwa jasusi wa upande upi? Teddy hakulisubiri Jibu. Tayari sekunde hii alishaibeba bahasha na alikuwa akishuka kuelekea Nje. Wakati anakaribia sehemu ile maalum ya kupitia simu yake ikapata uhai. Akaitoa kwa haraka. Kutizama mpigaji alikuwa Masimba.



    Akaipokea kwa Haraka. "Usipitie ulipoingilia, pita nyuma ya nyumba kuna mlango wa Siri. Hakikisha unatoka salama." Aliongea masimba na muda ule ule simu ikakatwa. Teddy akashangazwa na hili. Hili la masimba kujua kile ambacho yeye anafanya. Kwa mara ya kwanza tokea wawe wapenzi akakili kuwa hakukosea kuwa na mwanaume huyu. Lakini hili la kujua kile anachokifanya ndani pekee ndicho kilichomsymbua. Kilichomtesa na hata kumshangaza. Akafuata maelezo yote. Muda mfupi alikuwa barabarani akielekea Shekilango. Bado kizungumkuti cha askofu alikuwa nani kilimtatiza. Kutoka magomeni Kagera mpaka Shekilango hapakuwa mbali sana. Hivyo kwa usafiri wa bodaboda alitumia dakika nne tu kufika hapo. Akashuka pembeni mwa ukumbi maarufu kwa Disco Uitwao Sunsiro. Baada ya kushushwa hapo na kumlipa dereva wa pikipiki. Teddy akachepuka mpaka pembezoni mwa Pub fulani iliyokuwa pembeni mwa barabara. Baada ya kukaa na kuagiza kinywaji, teddy akaanza kunywa taratibu huku akitizama kule ilipo barabara ya kuelekea sehemu husika aliyoambiwa na Askofu. Macho yake yalikuwa yakinasa na kufuatilia kila sura ya mtu amba gari iliyokuwa ikitokea kule. Wakati akiendelea kutizama kama ataona chochote, akashangazwa na kuiona gari moja yenye nembo ya Ikulu ikitoka maeneo hayo hayo ya Legho ikielekea barabara iendayo kule. Gari ya ikulu? Ndio swali lililogonga kichwa Cha teddy. Kengele ya Tahadhali ikaendelea kugonga kichwa chake. Gari ya ikulu maeneo haya inafuata nini? Ama kuna kitu ikulu inakijua? Ni maswali yaliyopita kichwani kwake. Akataka kuwasiliana na masimba. Lakini kabla ya kufanya hivyo akamuona mtu ambaye aliufanya moyo wake Upige. Macho yake Yalimuona Veronica Senka, Veronica yule yule aliyemuona kule bandarini. Lakini huyu hakuwa anaelekea kule, bali alikuwa akitoka kule ilipoelekea gari yenye nembo ya Ikulu. Akayaacha macho yake yamuangalie mwanadada huyu. Alikuwa akitembea pasipokuwa na wasiwasi. Hilo pia likamsisimua. Kujiamini kwa veronica kilikuwa kitu kilichomvutia sana Teddy. Aliwataka watu wa aina hii na kuwahusudu. Hilo likamfanya aendelee kumtizama. Kumtizama kulikoishilia kwenye gari moja iliyopaki pembezoni mwa barabara. Hapo akamuona Vero akipanda kisha gari kuwashwa na kuondokewa taratibu. Bado Teddy hakutubutu kuinuka. Bado aliamini uwepo wa watu katika eneo hilo. Watu wanaotizama nani ataifuatilia gari ile. Akaendelea kukausha na kujikausha. Dakika mbili kupita baada ya Vero kuondoka, akaiona ile gari yenye nembo za ikulu ikirudi. Hata ilipopita macho yake yakawanasa watu wanne waliokaa sehemu tofauti tofauti wakiinuka na kila Mmoja kuelekea kwake. Hilo likamfanya atabasamu. Atabasamu kwa kuwa aliutambua uwepo wa watu hawa. Akauvuta muda tena na tena. Aliuvuta muda katika namna ya kuangalia mazingira. Kuangalia endapo kulikuwa na mtu mwingine. Lakini hapakuwepo na dalili hiyo. Kabla hajainuka kuelekea huko akaona amtaarifu Masimba kuhusu kile alichoshuhudia. Kile alichokiona kwa macho yake. Gari yenye nembo ya Ikulu na kumuona veronica. Akautuma ujumbe katika lugha ya mafumbo, lugha ambayo haikuwa rahisi kusomwa na askari ama mtu yeyote. Hata baadhi ya watu wa Idara ya ujasusi hawakuweza kuielewa lugha hiyo. Akavuta muda ili kuyapata majibu, alivuta muda kupata majibu kutoka kwa masimba. Lakini Muda ukasonga pasipo masimba kujibu ujumbe wake. Hilo likamjulisha kuwa inawezekana Masimba hayupo sehemu Husika. Ama alikuwa msambweni. Hilo likamuinua Teddy kutoka sehemu aliyokaa. Sasa alikuwa akielekea kule alipoagizwa na baba Askofu. Akatembea kwa umakini kwa mwendo wa pole pole. Umbo lake la kike kike likamfanya aonekane kama mpita njia. Kwa kuwa hakuwahi kufika maeneo hayo, ilimbidi aanze kuitafuta nyumba husika. Alizunguka mitaa mitatu, mtaa wa nne akafanikiwa kuiona nyumba husika. Hii ilikuwa nyumba ikiyojengwa mfano kama wa nyumba ya baba Askofu.



    Lakini tofauti ilikuwa ni uwezekwaji. Wakati ya baba Askofu ikiezekwa kwa Vigae. Hii ilikuwa imeezekwa kwa bati. Lakini ujengajwi ulikuwa wa aina moja. Hilo halikutegemewa na Teddy. Alipiga hatua kuifuata nyumba hii akiwa makini kabisa. Kuiona gari yenye nembo ya ikulu kisha Veronica. Kukampa picha kuwa lolote linaweza kutokea katika Eneo hili. Hakujua kwanini lakini kitendo alichokiona muda mfupi uliopita aliamini kuna kitu kizito sana. Akalifikia geti la nyumba ile. Akafanya kama alikofanya kule kwa Askofu. Lakini hata hapa hali ilikuwa kama ile, hali ikuwa ukimya pia hapakuonekana uwepo wa watu ndani ya nyumba hiyo. Akaligusa geti kwa mara nyingine. Geti lilikuwa wazi kama lilivyokuwa wazi kule kwa askofu. Akalifungua na kuingia ndani pasipo ukelele wowote. Magari manne ya kufahari yaliyoegeshwa ndani uzia wa nyumba ile yalimjulisha kuwa huyu mtu alikuwa ni mwenye uwezo. Akatembea safari hii bastola yake ikiwa tayari mkononi. Nyumba hii ilimpa wasiwasi kutokana na ilivyokuwa katika ukimya. Hata alipoufikia mlango bado hapakuwa na chochote kile. Akausukuma mlango kidogo, akauona mlango ukijifungua. Macho yake yakatembea ndani katika uharaka wa aina yake. Safari hii sebule haikuwa kama kule kwa askofu. Sebule hii ilikuwa hovyo hovyo kabisa kuonyesha hapakuwa na kitu cha Heri. Kila kitu kilikuwa kikizungumzia ushari na unyama. Damu sambamba na Jicho moja la mtu ni vitu vilivyokuwa chini ya sakafu ya sebule. Akaitizama hali ile kwa umakini mkubwa sana. Punde simu yake ikaupata uhai tena. Akaitoa huku bado umakini ukiwa ndani yake. "Ondoka sehemu hiyo upesi." Ulisomeka ujumbe huo. Ujumbe kutoka kwa Masimba. Teddy akaganda kwa muda, akaganda katika namna ya kushangaaa. Kabla hajajua kipi cha kufanya Akalisikia geti likifunguliwa. Kufungukiwa kwa aina fulani ya kutia hamasa. Alipichungulia akawaona watu kama sita wenye silaha

    [05-31, 13:37] Ibrahim Masimba: Walikuwa watu sita waliokamatia Bunduki kubwa. Walikuwa wakiingia hapo ndani mfano wa watu wanaokwenda vitani. Teddy akatulia akiwatizama walivyokuwa wakitenbea. Akajiondoa pale taratibu na kusogea mbele kidogo sehemu ambayo palikuwa na kujichumba. Akajibanza hapo bastola yake ikiwa tayari mkononi. Punde akausikia mlango wa sebuleni ukitiwa teke kisha watu wakasikika wakiingia kanakwamba walikuwa katika uwanja wa vita. Bado Teddy akaendelea kutulia akuwasoma watu hawa. Watu ambao walionyesha kuwa kimya baada ya kuingia hapo. Hata yeye hakuwa katika hali hiyo. Kifo cha Askofu, Bahasha aliopewa ikiwa ni pamoja na kuagizwa ni vitu ambavyo hakutaka kuondoka hapo bila kuondoka akiwa na majibu kamili. Hakuogopa kifo kwa kuwa alitamani kuuawa na alipenda kuua. Akasubiri kwa hamu kubwa, kidole chake kilikuwa tayari kuruhusu risasi. Licha ya kutulia kwa muda huo, bado sebule ilikuwa kimya na bado hapakusikika vishindo wala minong'ono. UKIMYA ULITAWALA KANAKWAMBA HAPAKUINGIA WATU





    Walikuwa watu sita wenye silaha nzito. Watu ambao waliingia pale katika namna ambayo hata Teddy mwenyewe alijiuliza. Ukimya ulitawala kanakwamba hapakuwa na watu walioingia hapo sebuleni. Mkononi alikamatia bastola yake aina ya semi automatic pistol huku sehemu fulani ndani ya mavazi yake kukiwa na Sig-sauer p20 nayo ikiwa imetulia ikisubiri kuifanyakazi hiyo. Ukimya, kwa nini ukimya wakati watu wameingia hapa muda mfupi uliopita? Tena watu sita wenye silaha nzito? Huu ukimya ni wa nini? Wameenda wapi watu hawa? Ni maswali aliyojiuliza Teddy huku mikono yake ikiwa tayari. Sekunde, dakika na sasa ilikuwa inafika dakika ya tatu, babo ukimya, bado hapakusikika chochote kutoka sebuleni. Hata nyayo hazikusikika. Sehemu ilikuwa kimya, ukimya ambao ulimaanisha hakuna kitu chochote. Teddy hakutaka kuamini hilo. Bado aliuamini muda, bado aliitambua Subira kama kitu muhimu sana kwenye eneo kama hilo. Semi Automatic pistol Bado haikuondoka mkononi. Bado kidole hakikutoka sehemu ya kufyatulia Risasi. Macho yake yakaanza kulizoea giza lilikilokuwa limeanza kutanda kwenye nyumba ile. Kuanza kuingia kwa giza kukampa uwezo wa kuona kilichokuwa kikiendelea. Kwani ni wakati giza likiingia akahisi kuisikia michakato ya hatua za watu. Michakato ya miguu ikitembea katika aina ya kunyata. Akajiweka tayari, akajiweka akikabiliana na watu waliokuwa wakisogea. Punde akakiona kivuli mtu, mtu ambaye mavazi yake yalifanana kabisa na giza lililopo mle ndani. Mdomo wa bastola ukainuka na kutizama kule kilipo kivuli. Muda mfupi alikuwa akimuona mtu akipita akiwa kimya kabisa. Hakusubiri ainue mguu wa pili. Semi automatic pistol ikakohoa. Ikatoa cheche na kumwaga njugu. Ulikuwa mlio mfano wa chafya ama kuvunjwa kijiti. Risasi ilikuwa imepenya kooni kwa mtu yule. Hakuweza kuongea wala kupiga kelele. Akaporomoka chini akiwa amelishika koo lake. Teddy katulia Tena na kuhama Upande mwingine, akasimama pembeni mwa mlango. Macho yake yalikuwa mbele, macho yake yalikuwa yakitizama mlangoni. Lakini safari hii ukimya ulirejea Tena. Hapakusikika chochote tena. Hata zile hatua za watu zikakoma na nyumba nzima ikawa kimya. Ni wakati huo akiwa ametulia akausikia mngurumo wa gari nje nyumba hiyo. Mngurumo ambao uliishia getini kuonyesha kuwa gari ilikuwa imesimama nje ya geti la nyumba hiyo. Mara akalisikia geti likifunguliwa kisha mngurumo wa gari ukasikika tena. Safari hii gari hii ilikuwa ikiingia ndani ya uzio wa nyumba hii. Teddy akajiuliza huyu ni nani?kabla hajapata jibu. Akausikia mlango wa ndani ukifunguliwa. Kisha michakato ya miguu ya watu ikasikika kusogea. Bado Semi Automatic ilikuwa mkononi akisubiri kutoa hukumu nyingine. Miguu hii sasa ilikuwa ikiukaribia mlango wa chumba alichokuwa ametulia. Miguu ikasikika tena safari hii ikiwa katika usawa wa chumba kile. Lakini cha ajabu hakumuona mtu, hakumuona akipita na hata kivuli chake hakukiona. Huyu ni nani? Mbona kama mzimu? Lilikuwa swali ambalo halikudumu sana akauhisi ukelele wa sauti ya mtu ukitokea mbele kidogo ya pale alipojibanza. Hakuliacha hilo limpite, hakuliacha liondoke na hata kwenda hivi hivi. Akajitoa taratibu, alitaka kwenda kuona na hata kumuangalia huyu mtu. Alitaka kushuhudia na kuona huyu mtu alikuwa nani na kwanini ameingia pasipokuwa na wasiwasi. Bastola mkononi huku macho yakipambana na Giza ndani ya nyumba ile, Teddy alinyata kwa umakini mkubwa mpaka nje ya chumba kile. Licha ya kunyata na kutokea hapo, lakini hakuona chochote zaidi ya ukimya kwa mara nyingine. Hata yule mtu aliyekuwa akipiga ukelele hakusikika tena. Nyumba ikarudi kwenye kimya tena. Hilo halikumbabaisha jasusi huyu wa kike. Bado aliyatembeza macho yake, macho yaliyozoea giza. Hazikupita sekunde tano, akaisikia kelele tena ikitokea juu. Hii ilikuwa sauti ya mtu wa makamo. Mtu ambaye alionyesha kuwa na umri mkubwa. Safari hii sauti ya mtu huyu ilikuwa ikitoka kwa maumivu ya kipigo ama kubanwa na kitu. Alikuwa akilia kama mtoto huku akisema hajui kitu huku akiwataka wauaji wakamuone Baba Askofu Ibrahim Lexandre Rengima. Kutajwa kwa jina la baba Askofu katika mateso ya mtu huyu anayelia kukamfumbua tena kutoka kwenye giza. Alitambua mtu huyo anayepiga kelele ndiye mtu aliyetumwa kuja kumuona na kumuokoa. Lakini kama ni hivyo kwa nini Masimba alimtuma kwenda nyumbani kwa Askofu kumuondoa mtu? Mtu mwenyewe ni nani na kama ni Baba Askofu kwa nini nimemkuta akiwa amejeruhiwa? Ina maaba kulikuwa na mtu mwingine zaidi ya Askofu na mtu huyu anayepiga kelele? Yalikuwa maswali mfululizo, maswali yaliyopita kichwani kwa Teddy. Maswali ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati ule wakati sauti ya mteswaji ikizidi kutamalaki.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Akauona upuuzi kuendelea kujiuliza, upuuzi ambao ungemfanya akose kile ambacho alitakiwa kukipata. Akaliacha eneo hilo sasa akielekea sehemu hiyo. Kila alipozidi kusogea ndipo hapo sauti zilipozidi kutanda katika masikio. Akiwa amebakisha hatua kazaa kufika sehemu husika, akawa anakisikia kile ambacho kilikuwa kikitamkwa kutoka ndani. Kikitamkwa na Mteswaji kujibu maswali ya Mtesaji. "Tunaitaka bahasha uliopewa na baba Askofu. La sivyo nitakuua sasa hivi." Aliisikia sauti hiyo ambayo ilipenya mpaka ndani ya moyo wake. Sauti ambayo aliijua. Ilikuwa sauti Ya Ben. Sauti ya mtu katili kuwahi kumuona.



    "Sina bahasha yoyote, kama mnaniua niueni tu." Ilisikika sauti hii. Sauti ya mtu aliyetayari kufa sababu ya bahasha ambayo ilikuwa mikononi kwake. Akauona ulikuwa muda wa kufanya kitu, muda wa kufanya kile ambacho kingemuokoa mtu huyu. Ulikuwa wakati wa kumuua Ben. Akatoka hapo sasa akikifuata kile chumba. Lakini kabla ya hapo alitaka kuitafuta swichi ya kuwashia taa. Alitaka kuitumia mbinu hiyo kujua watu hawa wako wapi. Akaendelea kupapasa huku na huko kutafuta anachokitafuta. Baada ya kutafuta sana akaiona swichi hiyo. Huku bastola ikiwa tayari akaifyatua Swichi. Nyumba yote ikawa nyeupe. Watu wanne waliojificha pale ukumbini wakashtushwa na kuduwaa kwa sekunde. Ni wakati wa mduao huo, semi automatic ikakohoa na kumwaga risasi. Watu watatu waliku wamepaa angani kwa Risasi na hata walipokuja kufika chini walikuwa marehemu. Hilo halikutegemewa na watu waliokuwepo hapo ndani. Milio ya risasi ikalindima kutoka kwa wakora hawa waliokuwa wakifyatua risasi hovyo bila kujua hatari mbele yao. Teddy bado alikuwa ametulia, bado alikuwa akiwatizama wakora wale walivyokuwa wamehamanika. Alitamani hata kucheka, alitamani hata kuwaita. Lakini muda huo akamuona mtu akitokea katika aina iburudishayo moyoni na hata machoni. Mtu huyu alikuwa akiyupa kwa wepesi wa karatasi, wepesi wa sisiminzi na hata wepesi wa ubua. Alitoka hapa akienda pale katika namna ambayo ilivutia sana. Alikuwa masimba huku mikono yake yote ikiwa na bastola. Mkono wa kushoto alikuwa na Bastola aina ya PPQ (polizei pistole quick defense) iliyotengenezwa Nchini Italy na mkono wa kulia alikamatia bastola aina ya Springfield XD ambayo hii ilitengenezwa katika nchi ya Marekani. Alitia raha kumtizama na hata kumuangalia, Teddy akapandwa na Mzuka, mzuka wa Kushambulia. Wakati mara ya kwanza alikuwa atumia Bastola moja, Safari hii akaichomoa bastola yake nyingine. Bastola iliyotengenezwa nchini Brazil. Wakati kulia kulia alikuwa na semi automatic, kushoto alikuwa na SIg -sauer p320. Masimba alikuwa akishambulia kutoka mbele, teddy naye alikuwa akimlinda masimba kwa mbele. Ilikuwa burudani katika aini yenye kutoa raha. Kila risasi ilipelekwa sehemu husika, kila ilipotumwa, risasi ilikwenda hapo. Hakufika wala kuchukua Dakika. Zilikuwa sekunde thelathini tu. Kila mkora alikuwa yupo chini akivuja damu.. alikuwa marehemu huku matundu ya Risasi yakionekana Kifuani. Wakatizamana katika macho ya upendo, macho ya kujali na hata kuaminiana. Macho yao yalikuwa yakiongea mapenzi. Hawakujali walikuwa sehemu gani, midomo yao ikakutana katika namna fulani uburishayo nafsi. Lakini hawakufika katika lengo lao, lengo la kuburudika zaidi. Kwani macho ya masimba yakamuona mtu. Mtu ambaye alikuwa ameuinua mdomo wa bunduki yake aina ya combart shotgun akiwa lenga wao. Akiwa lenga pale waliposimama. Hakuwahi kufanya alichotaka kukifanya. Alifanya kile ambacho akukitarajia. Risasi mbili zikatoka mahali apo.. moja ikatua begani kwa Ben na nyingine katikati ya paji la uso. Ben ajayumba na Bunduki yake mkononi na kwenda kujimwaga chini. Alijibwaga tayari akiwa maiti. Wakati huo ndio kwanza Teddy alikuwa akigeuka. Akigeuka kuangalia kile ambacho kilitendwa na kufanywa. Ben alikuwa chini kichwa kikiwa kama chapati. Risasi ilikuwa imefumua kichwa cha ben. Teddy hakulitegemea na hata kuliwaza. Aliporudisha macho Usoni kwa Masimba akakutana na tabasamu. Tabasamu lililomfanya Teddy ajilaze kifuani kwake. Kifua ambacho kilikuwa maalum kwa sababu yake. Ikawa hiyo.





    Ilikuwa hivyo na ikawa hivyo. Ndimi zao zikakutana huku chini ya sakafu damu ikichuruzika. Harufu ya damu ilikuwa imetawala eneo hilo, harufu ambayo waliipenda na hata kuwavutia. Hawakuogopa damu wala hawakuziogopa maiti. Bado walikumbatiana wakiburudika na kuburudika. Lakini haikuchukua muda wakaachiana. Walikumbuka kuwa wapo kazini. Wapo katika kazi hii ya kifo. Kazi ambayo ilikuwa ikitembea na vifo vyao mikononi. Naam! Huu ulikuwa muda wa kumfuata mtu huyu, muda wa kumfuata mtu yule ambaye muda mfupi uliopitwa alikuwa akishurutishwa aujue na kuusema ukweli. Nilazima wajue kwa nini Askofu alimtaka Teddy afike pale. Ilikuwa ni lazima wamjue na kutambua hilo. Kila mmoja akapiga hatua kuelekea chumba kile, chumba ambacho sauti ya mtu ulikuwa akisikika. Kuingia hapo wakapokelewa na Dimbwi la damu. Juu yake alikuwa amelala mtu, alilala mtu ambaye kwa kumuangalia tu, ungejua huyu atakuwa ni marehemu. Hatua za umakini zikafuatia, hatua za kuelekea ulipolala mwili. Wakaufikia mwili wa mtu yule ambaye alikuwa uchi wa mnyama. Wakatizamana tena huku kila mmoja akiwa makini. Huku kila mmoja akiwa tayari kwa kuifyatua Risasi. Wakaugeuza mwili wa mtu huyu waweze kuufahamu. Wakafanikiwa kuugeuza, kila mmoja macho yakamtoka baada ya kuiona sura ya huyu Marehemu. Hakuna aliyekiamini kile alichokuwa akikiangalia. Macho yao yalikuwa yakitizama sura ya Sheikh mkuu wa mkoa. Hata huyu kisu kikubwa kilikuwa kimesimama tumboni. Kila mmoja akainua macho. Wakaangaliana kwa muda. Baba Askofu, na sasa alikuwa ameuawa Sheikh Mkuu Wa Mkoa. Kuna nini hapa? Ni swali ambalo lilipenya kichwani kwa Teddy. Swali ambalo lilimfanya amuangalie Masimba kwa Mara nyingine. Akimuangalia akihitaji kupata majibu. Majibu ya kile ambacho kimejificha nyuma ya Vifo vya watu hawa. Alitaka kujua kwa nini aliagizwa na Masimba kwenda kumuondoa mtu nyumbani pale kwa Baba Askofu. Hata Masimba akamuangalia kwa Umakini. "Haya ndiyo malipo ya Tamaa. Kilichofanyika kwa watu hawa ni kuzibwa midomo yao ili wasikutane nasi." Aliongea Masimba akiwa bado anamuangalia yule marehemu. Jibu la masimba lilionekana kumshangaza Teddy. Lilimshangaza kwa kuwa hakuwahi kuwaona watu hawa katika biashara kipindi yupo huku. Sasa hii tamaa anayosema Masimba ni Ipi? Lilikuwa swali lililofanya amtizame tena Masimba. "Najua hujawahi kuwaona watu hawa ndio maana unashangaa, lakini Mengi utayaona kwenye Hiyo bahasha uliopewa. Tunatakiwa kuondoka hapa. Huu mchezo nadhani kuna mtu ndani ya Ikulu anaucheza. Lazima tuwe makini na lazima Tuondoke hapa. Aliongea Masimba huku akiuvuta mkono wa Teddy ili kuondoka hapo. Teddy akafuata kama kondoo. Akili yake ilikuwa imesimama kwa muda kutokana na maneno haya kutoka kwa Masimba, maneno kwamba watu hawa ni wa moja katika biashara hii. Kwamba watu hawa nao walikuwa kundi moja na Jimmy na hata Waziri? Kwamba Baba Askofu alikuwa Mmoja wa wana kikundi? Kwamba Sheikh Mkuu wa mkoa alikuwa ni mmoja katika hili? Akaitamani ndoto. Ndoto ya kumtoa katika hili. Aliiona Dunia Jinsi ilivyokuwa ikiwapoteza watu. Akiwaaangamiza katika Matendo mabaya. Kwa mara nyingine akataka kumuuliza Masimba. Kumuuliza kuhusu ukweli huu. Kuhusu hili linalotokea. Lakini macho ya Masimba yakauziba mdomo wake. Macho ya Masimba yalikuwa yakimzindua kutoka katika hili. Kutoka katika lindi la mawazo alionayo. Alitakiwa katika utimamu wa kimwili na hata kiakili. Alitakiwa katika umakini wake wa siku zote. " Alitakiwa kurudi kuwa Teddy kama Teddy. Ilikuwa hivyo na akawa hivyo.



    ********

    Walikuwa wawili ndani ya chumba kimoja, walikuwa wamejiinamia kila mmoja akiwaza kile ambacho kiliutawala ubongo wake kwa wakati huo. Wakati Teddy akiwaza mkanganyiko na mambo yanavyozidi kumshangaza. Masimba alikuwa akiwaza kile kilichopo ndani ya Ile Bahasha. Bahasha ambayo Teddy alipewa na Askofu Ibrahim Lexandre Rengima. Ingawa hakuwa ameifungua kwa kipindi kile lakini aliuhisi usiri mzito kuwepo ndani ya bahasha hili. Kama sheikh mkuu wa mkoa na Baba askofu walikuwa washiriki katika biashara ile, alihisi kuwepo kwa watu wengine wazito kupindukia. Kuiona Gari yenye nembo ya Ikulu sehemu zote mbeli, kisha kuwakuta wahusika wameuawa hii ilitoa picha kuwa hata ndani ya Ikulu kuna watu ambao wapo nyuma ya Biashara hii. Kitendo cha Idara ya Ujasusi kubadilika na kutotaka kuwaunga mkono katika hili ilimaanisha kwamba kuna kitu kizito ambacho hatakiweza Peke yake. Alitambua wanaweza kuuawa muda wowote na kushindwa kuimaliza kazi hii. Kama ikulu inatumika katika hili hii ilionyesha kuwa ilikuwa Hatari kubwa sana kwa upande wao. Hilo likamfanya amkumbuke rafiki yake, Rafiki ambaye walikuwa wote katika purukushani za kuchunguza kifo cha mke wa Rais. Mkasa ambao hautakaa usahaurike maishani kwake hasa baada ya kuigundua njama ya kutaka kumpindua Rais alieko madarakani kwa Wakati. Alikuwa amemkumbuka mwanaharamu, alikuwa amemkumbuka Nemisis The Bastard. Mwanausalama mwenzake Raia Wa Africa ya Kusini. Alimkumbuka katika aina fulani ya kuuhitaji msaada zaidi. Msaada wa kiuchunguzi na hata kuwasafirisha watu kuzimu. Hilo akalipitisha kichwani kwake. Lakini kabla hajamwambia alitaka kukijua kile ambacho kilikuwemo ndani ya Bahasha kutoka kwa baba Askofu. Kwa mara ya kwanza Masimba akainua uso wake, macho yake yakamtizama mwandani wake aliyekuwa pembeni yake akionekana kusafiri umbali mrefu kimawazo. Hakuwa hapo na hakuonekana kuwepo Hapo. Teddy alikuwa amesafiri umbali mrefu kimawazo. Akamsogelea na kumkumbatia kwa mapenzi yote. Kwa upendo wote na hata mahaba yote. Taratibu macho yao yakatizamana. Yakaangaliana na kuangsliana. Macho ya Teddy yaliijenga hofu, macho ya Teddy yalionyesha kuhofu kitu. Hilo lilikuwa jipya moyoni kwa masimba na Hata machoni. Teddy alikuwa akiogopa na Teddy alikuwa akihofia. Teddy alikuwa katika hofu, mduao na hata Bumbuwazi. Teddy anaogopa? Teddy ana hofu? Ameianza lini hii? Akajiswali mwenyewe pasipo majibu ya aina yoyote. "Teddy umeanza kuogopa? Umeanza lini kuwa muoga?. Aliuliza Masimba huku akimuangalia kwa umakini. Teddy hakujibu bali aliinua macho zaidi na kumuangalia masimba. Midomo yake ilikuwa ikicheza kutaka kuongea kitu lakini haikuwa hivyo. Hakuongea wala hakufumbua mdomo. Hata hili lilimshangaza Masimba, hata hili hakulitegemea. Teddy kushindwa kuongea? Hapana hawezi kuwa Teddy. Alijisemea mwenyewe huku akimtizama Zaidi. "Dady Nahisi Ikulu inahusika katika mapambano haya. Nahisi kuna kitu ikulu ama watu wanaoishi ikulu wapo nyuma ya hii biashara. Na kama ni kweli huioni hatari mbele yetu? Nadhani umeiona gari yenye nembo ya ikulu ikielekea pale nyumbani kwa Sheikh mkuu, na pia nadhani umewaona wana usalama ambao walikuwepo eneo lile tena kwa siri kubwa sana. Hii inaonyesha nini kwetu?" Aliongea Teddy huku akishindwa kuificha hofu. Hofu ambayo ilichukua nafasi kubwa usoni. "Ni kweli nimeona kila kitu, na hata hii gari yenye nembo ya Ikulu ulipishana nayo kidogo tu pale nyumbani kwa Baba Askofu. Hii inaonyesha watu hawa waliouawa ilitakiwa kuwa hivyo kabla hawajaingia mikononi mwetu. Kwahiyo kilichopo sasa hivi ni kutafuta na kujua ni nani ambaye alikuja na ile gari. Na tukishalifahamy hilo tutamtafuta mhusika." Aliongea masimba huku akikilaza kichwa cha Teddy kifuani. "Kwa nini Ulinituma nikamuue Baba Askofu?. Akauliza Teddy kwa mara nyingine huku akiuvaa uso wa kazi. "Nilikutuma kwa kuwa Alikuwa mmoja kati ya wahusika wakuu katika Biashara hii." Akajibu Masimba kwa Utulivu. "Ulijuaje hilo?" Akauliza tena. Ni swali hilo lililoubadirisha uso wa masimba. Sasa alikuwa akimtizama Teddy kwa macho ya sio na utani. Swali lake lilikuwa la kitoto kwa mtu mwenye uzoefu wa kiusalama kama yeye. "Swali gani la kitoto hilo unaloniuliza? Kwa hiyo mimi naweza kubuni tu kuwa mtu fulani anafanya biashara hii? Unajua kwa nini amekupa hiyo bahasha na kukwambia uilete kwangu?" Aliongea masimba kwa kufoka huku akimuangalia teddy. "Sio kwamba ni swali la kitoto, nimeuliza kwa kuwa kuwa kuwa kwangu kule sikuwahi kuwaona hata siku moja katika mikutano yetu." Akajibu Teddy kwa upole huku akikichezea kifua cha Masimba. "Naomba bahasha hiyo tuifungue, lakini tambua hii vita sasa tunapigana Na taasisi ya Urais. Kama gari za Ikulu zinatumika katika haya huku tunakoelekea ni kubaya. Usiikubali hofu ichukue sehemu kubwa katika Maisha yako. Hii ni vita ambayo inaweza kutupoteza na kutufuta katika Dunia hii. Licha ya kutufuta kwenye uso huu, lakini pia hatutokuwa na chochote cha kutukumbuka. Unatakiwa uitoe hofu na kuitokomeza. Ujuzi tulio nao utusaidie kutufikisha katika mwisho wa hii safari." Aliongea masimba kwa kirefu. Maneno yake yakamuingia Teddy na kumsisimua. Ulikuwa wakati wa kupambana, ulikuwa wakati wa kutumia ujuzi wao wote kuhakikisha hili linafika mwisho. Kwa nini awe na Hofu? Kwa nini aogope? Tokea lini yeye akaogopa Risasi? Tokea lini yeye akakiogopa kifo? Akazidi kujilaza kifuani kwa Masimba. "Nipo tayari Kupambana Dady? Nipo tayari kufanya kila kitu kwa sababu yako na sababu ya nchi yangu." Aliongea Teddy katika namna ambayo ilimsisimua. Muda wote huo hakuwa ameitoa Bahasha, hakuwa ameitoa kwa kuwa hakuambiwa afanye hivi. Akapeleka mkono mahali ambapo aliihifadhi Bahasha. Akaitoa na kumkabidhi masimba. Wakati masimba akitaka kuifungua Bahasha, simu yake ya Mkononi ikaita. Akatulia kwanza akimuangalia teddy machoni. Teddy naye akamkazia macho huku wivu ukionekana Shahiri machoni mwake. Alikuwa akihisi labda mpigaji ni Mwanamke. Masimba akaitoa Simu Mfukoni kwake, kabla ya kuipokea akatizama jina la mpigaji.. Major General Chomboko. Haraka akaipokea simu. "Utahitajiwa Ikulu Muda huu, lakini Make sure kabla hujaondoka hapo ulipo unaweka vizuri hiyo Bahasha. Ikipotea Hiyo basi Hata wewe Hutakuwa na Njia ya Kujinasua." Aliongea Major General Chomboko. Kisha pasipo kusubiri chochote. SIMU IKAKATWA.



    MASIMBA AKAMTIZAMA TEDDY NA HATA TEDDY AKAMTIZAMA MASIMBA.



    BADO KAZI YAO ILIKUWA NGUMU



    "Nahitajika Ikulu Teddy. Lakini nimeambiwa nihakikishe bahasha na itunza na kuiweka vizuri. Kwani tukiipoteza nami nitafutwa kwenye uso huu wa dunia." Aliongea masimba baada ya kukatwa kwa Simu. "Nani amekupigia na kwa nini iwe hivyo?" Akauliza Teddy. "Teddy naomba ushtue ubongo wako ufanye kazi kama ulivyokuwa unafanya kule Syria. Maswali unayouliza hayapaswi kuulizwa na Afisa usalama wa kiwango cha Juu kama wewe. Kifupi ni kwamba nahitajiwa ikulu, lakini naamini hakutakuwa na usalama. Simu niliopigiwa na Meja jenerali Louis Chomboko ni simu inayonifanya niamini kuwa maisha yetu yapo hatarini hasa mimi hapa." Alijibu Masimba akionyesha kuipoteza furaha na hata tabasamu. "Dady unaniweka kwenye wakati mgumu, umeuweka moyo wangu katika sintofahamu. Tafadhali tuliache hili suala. Sitaki kukupoteza Masimba wangu. Aliongea Teddy kwa sauti ya Hisia. Alikuwa akimuangalia mpenzi wake usoni. Akashindwa kulizuia chozi lake lishuke mashavuni. Teddy alikuwa akilia, tena alikuwa na hofu ya kumpoteza masimba. Lakini hilo halikumfanya masimba abatilishe uamuzi wa Kwenda Ikulu. "Teddy siwezi kuliacha hili hata kama litanigharimy maisha yangu. Nipo tayari kufa kwa sababu ya nchi hii. Kama Rais ataona nastahili kufa basi nipo tayari. Nimempoteza mama na Dee Plus. Tumempoteza Vicky juzi tu hapa. Kuna roho za watu wengi wamekufa kutokana na hili. Nani anaweza kuirudisha roho ya Mama yangu Mzazi? Nani atairudisha Roho ya Vicky au Dee plus? Nipo tayari kufa. Kama wataweza kuwarudisha vijana walionyongwa na kuharibiwa na madawa?. Sikiliza Teddy naondoka nakuachia bshasha hii, hii bahasha ndio uzima na uhai wangu. Ukipoteza hiyo Bahasha utakuwa umenipoteza mimi. Itunze kama unavyotunza mapenzi yetu. Najua nikiondoka hapa kuna watu watakuja hapa. Kuna watu watakufuatilia ili kuichukua hiyo bahasha. Naomba upigane kama ulivyopigana tulipokuwa urusi na hata Syria. Pigana kwa Ajili yangu na Pigana sababu ya Nchi hii. Hata kama wataniua, naomba uje uwaambie wanangu mkasa huu. Acha niende mpenzi." Aliongea masimba na kumkumbatia Teddy kwa nguvu. Naye alishindwa kuvumila. Chozi la uchungu lilikuwa likishuka. Hakumsubiri Teddy atamke lolote. Akamuacha Teddy akiangua kilio chumbani wakati yeye alikuwa akiufungua mlango tayari kwa safari. Akili yake ilikuwa imevurugika katika kiwango kikubwa sana. Alihisi viongozi wa nchi yake hawakumpenda na hata kuthamini kile ambacho amekifanya. Leo hii alikuwa amegeukwa na Idara zote za usalama isipokuwa watu wachache tu ndani ya Idara hizo. Akatembea taratibu akielekea nje kabisa. Wakati akitembea akahisi uwepo wa mtu nyuma yake. Mtu ambaye alikuwa akilia. Akageuka taratibu, akageuka kumuangalia mtu huyo anayelia. Alipogeuka macho yake yakamuona Teddy akitembea Huku akilia. Akasimama kwa kupigwa na Butwaa. Akimuangalia Teddy alipokuwa akitembea. Hata walipokutana wote wakakumbatiana. "Teddy wewe ni shujaa, usiuruhusu udhaifu huu uondoe ule moyo wa kijasusi ulionao. Moyo wa kupambana katika aina yoyote. Siendi kufa nitarudi mama." Aliendelea kuongea masimba akimbembeleza Teddy. Hatimaye Teddy akatulia na kumuangalia tena masimba. Macho yake ambayo hayakuuonyesha utani tena. "Nenda Dady, naamini hawana uwezo wa kufanya chochote. Nakuamini na nina aamini kuhusu hili. Vita hii ni kubwa, vita hii ni vita dhibi ya utawala usiofuata Sheria." Aliongea Teddy akirudi katika uteddy wake ule ule. Tabasamu la uchungu likajitokeza Usoni. Masimba hakusubiri Tena, hakusubiri hilo liendelee. Akajitoa kwenye mwili wa Teddy na kuanza kuipiga hatua kuufuata mlango wa kutokea. Mwanga wa jua umlikaribisha Masimba katika aina ya kuburudika kabisa. Macho yake yalikuwa kwenye miwani maalum ya kiusalama huku hatua zake moja moja zikiikanyaga Ardhi kana kwamba alikuwa akiiogopa. Mwendo wake pekee usingeweza kukuvuta na kuhisi labda huyu alikuwa fulani. Bali kama ungemuona kwa wakati huo ungejua huyu lazima ni chekibobu fulani hivi mtoto wa mjini. Lakini licha ya mwendo huo bado macho yake yalikuwa yakitizama kwa hila pembezoni mwa barabara na maeneo yote yanayoizunguka Hoteli aliyomuacha Teddy. Sura nyingi alizoziona hapo hazikumpa mashaka kwa kuwa hazikuwa sura za kazi. Hata macho ya watu aliowaona pale hayakumtia wasiwasi kabisa kwa kuwa hayakuonyesha kama yalikuwa yakimtizama kwa hila. Akaongeza mwendo tena mara hii akibadili muelekeo ili kuona kama anafuatiliwa. Lakini haikuwa hivyo. Alikuwa peke yake katika njia hiyo. Hata moyo wake ukapata faraja baada ya kujua kuwa Teddy hatakuwa matatizoni. Lakini wakati anaumaliza mtaa fulani kabla ya kutokea barabara kuu, akapitwa na Magari mawili, magari ambayo yalimfanya asite kwanza kutembea. Akasimama pembezoni mwa barabara akiyatizama Magari yale mpaka yalipokwenda kusimama umbali mfupi kutoka pale Hotelini alipo Teddy. Hilo likamfanya ajipapase mifukoni kuitafuta simu yake. Lakini licha ya kujipapasa huko hakuiona. Akakumbuka kuwa simu yake aliiacha kitandani katika chumba kile alichomuacha Teddy. Hapo akaona kuna ulazima wa kurudi. Kwa kuwa gari zilisimama kwa upande wa mbele, Masimba akaona apitie mlango wa nyuma.



    ******

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Teddy alikuwa amejiinamia kitandani akiitafakari kazi iliyombele yao. Kazi ambayo ilikuwa hatari na ngumu sana. Kazi ambayo ingeweza kuwapoteza na kuwafuta katika ulimwengu huu. Akainua uso wake juu kutizama darini. Akaiweka mikono yake pamoja kisha kupiga alama ya Msalaba. Kwa mara nyingine alikuwa amemkumbuka Mwokozi wake. Baada ya kufanya Ishara hiyo akainuka na kuiendea ile bahasha, akaichukua na kuishika mikononi mwake. Aliitizama ile bahasha kwa muda mrefu pasipo kufanya kitu chochote. Wakati akielekea kitandani ili kufungua ili kuangalia kilichopo ndani. Akausikia mlango wa chumba alichomo ukigongwa. Akasita kwanza kufungua, mlango ukagongwa mara ya pili, Teddy akatulia. Wakati huo huo wazo la kwamba watu hawa sio wakawaida likamjia kichwani. Alichofanya ni kuikunja ile bahasha na kuitumbukiza ndani ya nguo yake ya Ndani. Baada ya kumaliza kufanya hivyo, akaufuata mlango kisha kufungua. Mdomo wa bastola ndio kitu cha kwanza kukutana nacho. Kitu cha pili akasukumwa kurudishwa ndani. Watu watano wenye miili ya kutisha wakaingia ndani. Ni watu ambao Jenipher aliwatambua, ni watu ambao aliwajua na anawajua. Wote wakatizamana kwa muda bila kuongea kitu. Hawa kuzungumza kwa mdomo bali macho yao yalionyesha kule ambacho walikihitaji, kukitaka na hata kukichukua. "Tunaomba mzigo ambao mlipewa na Baba Askofu." Ilikuwa sauti ya mmoja kati ya watu wale akionyesha kutokuwa na masihara.



    "Mzigo gani unausemea? Na mnamsemea Askofu yupi? Akajibu Teddy naye akionyesha kutokujua chochote. "Teddy hatukuja hapa kupoteza muda, bila shaka unatambua ukipewa oda unatakiwa kufanya sio kuuliza." Bado aliongea yule mtu huku akimuangalia Teddy usoni. "Oda ninayo tekeleza ni oda kutoka kwa Waziri mkuu, Raisi, Makamu na DG pekee. Nyie ni nani na mnatoa oda kama nani? Aliuliza Teddy huku akijiandaa na chochote ambacho kingeweza kutokea. "Teddy usitulazimishe kufanya kitu ambacho utakijutia.". Alionya mtu yule. "Dereck Usijifanye hujui kanuni za kiusalama. Nijibu hapa umetumwa na nani kati ya watu hao niliokutajia? Kwa nini uzungukezunguke tu. Pia nashanga.... kabla hajamalizia kauli yake. Ngumi nzito ikatua tumboni na kumfanya apepesuke huku maumivu makali yakisikika. "Tumekwambia usitulazimishe tukuumize tukashindwa kuangaliana. Tunachotaka ni bahasha tu." Alizidi kuunguruma mtu huyu.



    "Fanyeni mnachotaka kufanya, sina bahasha wala simjui huyo Askofu. Mnashindwa vipi kujibu maswali yangu?. Aliongea Teddy kwa kufoka. "Carlos fanya kazi yako. " baada ya dereck kusema hivyo, Kijana huyo akamsogelea teddy kisha kumkamata. Wakaifunga mikono yake kwenye kitanda. Baada ya hapo wakaanza kumtandika ngumi mfululizo. Zilikuwa ngumi zilizompa maumivu makali sana. Alijaribu kuvumilia kwa muda mrefu sana. Lakini baadae alisalimu amri. "Subiri ni ni.. nitasema." Aliongea Teddy huku damu zikimvuja. "Carlos muache kwanza atueleze..." aliongea derick huku akimuangalia Teddy kwa macho makali. Wakati wakisubiri Teddy aseme, wakausikia mngurumo wa kitu. Mngurumo ambao kila mmoja aligeuka bastola mkononi kuangalia kule unapotokea mngurumo. Macho yao yakakutana na simu, simu ambayo ilikuwa ikiita. Hata Teddy hakuwa ameiona simu ya masimba. Kitendo cha kugundua Masimba ameisahau simu yake kulimpa nguvu kuwa masimba atarudi hapo. Akauvuta muda na kuuvuta tena.



    ******



    Baada ya kugundua simu yake ameisahau pia kuyaona magari ya kisimama na watu wa aina fulani wakishuka, masimba akapanga kurudi. Lakini safari hii hakurudi kwa njia aliyotokea. Bali alikuwa amerudi kwa Njia tofauti ya kuingilia Nyuma ya Hoteli Hiyo. Alitembea akihakikisha haingii kwenye macho ya watu hawa. Akafanikiwa kufika nyuma ya hoteli hiyo.. akapenya uani na kufanikiwa kuingia ndani ya hotel pasipokuonekana. Kwa kuwa alikuwa amehesabu namba ya chumba chake wakati anaingia na hata kutoka. Ilikuwa ni rahisi kujua chumba chake kilikuwa sehemu gani. Akafikiri kidogo akaona nilazima apitie juu ya silling board ili kuepusha kuonekana. Chumba cha kwanza akakutana na miguno, hapo akajua watu walikuwa kstika shughuli yao. Chumba cha pili kilikuwa kimya. Akachungulia kwenye Tundu la Ufunguo, akakuta kwa ndani hapakuwa na mtu. Akachomoa Funguo zake malaya na kuitumbukiza kwenye tundu la kitasa. Sekunde iliyofuata masimba alikuwa ndani ya chumba kilichoonyesha kutandikwa vizuri. Akaaangalia juu akaiona sehemu maalum ya kupita. Akachukua kiti na kukiweka juu ya kitanda. Kisha akakanyaga na kupata urahisi wa kuutoa ule mfuniko. Baada ya hapo akajivuta kwa juu. Akafanikiwa kuingia pasipo wasiwasi. Baada ya kuhakikisha ameingia akaurudishia mfuniko, kisha kuanza kusota na tumbo kuelekea kwenye chumba alichomuacha Teddy. Ulikuwa ni mbuluziko mithiri ya nyoka, mbuluziko ambao haukutoa kishindo wala sauti. Akafanikiwa kufika usawa wa chumba chake. Kilio cha Teddy ndicho kilichomshtua, kilichomwambia kuwa Teddy alikuwa matatani. Masimba hakuchelewa.. Tayari Bastola mkononi na sekunde hii alikuwa akielekea pale ulipomfuniko wa kutokea.



    Alikuwa akitambaa akiuendea mfuniko tayari kwa kutoka nje. Kelele za Teddy bado zilikuwa zikipenya masikioni na hata moyoni. Chuki na hasira zikapanda kwa pamoja. Hata alipoufikia mfuniko na kuufungua, hakuna hata mmoja ambaye alimuona. Hata alipotua katikati ya watu hawa. Kila mmoja akainekana kuduwaa. Kila mmoja hakulitegemea na hata kutarajia. Masimba akauwahi mlango na kuufunga kwa ndani. Kisha akageuka na kumtizama Teddy wake pale kitandani alipofungwa mikono yake kwa nyuma. Macho yake yakapokewa na damu iliyokuwa ikivuja kutoka kwenye mwili wa huyu malaika wake. Damu iliyokuwa ikishuka kutoka kwenye kinywa cha huyu mrembo. Kinywa cha mwanamke wa maisha yake. Kinywa cha mpenzi wake. Baada ya hilo akageuza macho kwa watu hawa ambao Bunduki bado zilikuwa mikononi. Bado hawakuweza kuzitumia. Bado hawakuruhusu mikono yao kufanya hivyo. Waliganda mfano wa barafu, waliganda mfano wa masanamu. Carlos hakuwa Carlos na Hata Derick alikuwa kimya. Kimya kama hakuwa yule. Aligwaya na pia alikuwa ameelemewa na mduwaa. Hakuuona umuhimu wa bunduki zaidi ya kumuangalia Masimba. Macho yake yakakutana na macho ya Masimba yaliokuwa yakiwaka. "Carlos mfungue huyo mwanamke hapo. Kisha hayo maswali mliokuwa mnahitaji huyu ajibu, mtaniuliza mimi na nitawajibu mimi." Aliongea masimba kwa sauti ya utulivu. Bado macho yake yalikuwa kwa Kipenzi Chake. Carlos akasogea kitandani na kufanya kama kile alichotakiwa kukitenda. Akaifungua kamba mikononi kwa Teddy. Baada ya kufunguliwa kamba kikatokea ambacho hakuna aliyekitarajia. Hata masimba hakutegemea kitu kile kutokea pale tena kutendwa na Teddy. Lakini wasichokitegemea ndicho kilitendeka. Carlos alikuwa chini kichwa kikiwa kimepasuka. Risasi kutoka kwenye Semi Automatic pistol zilitosha kukipasua kichwa cha Carlos. Derick akapagawa huku wengine wakichachawa. Sasa mdomo wa Semi automatic ulikuwa ukikitizama kichwa cha Derick, kichwa ambacho hakikuimaliza hata Sekunde moja. Tayari ubongo na damu ulikuwa hewani ukisambaratika na kutapakaa ndani ya chumba kile. Harufu ya Damu na Mauti ikasikika kwenye pua za watu wake. Huyu hakuwa Teddy wa muda mfupi uliopita, huyu hakuwa Teddy wa kipindi chote. Alikuwa teddy mtamu na mwenye kuvutia katika medani hiyo. Alikuwa mtamu na mwenye kuleta hamu. Bado bastola mkononi na Bado macho yakiwatizama watu hawa waliobaki. Watu hawa walioshtushwa na kilichotokea. Hapakuwa na utani wala masihara. Hapakuwa na utani katika macho na hata uso. Macho yalikuwa yakieleza kifo. Ni wakati wakiendelea kushangaa wakauona mlango ukisukumwa. Licha ya kusukumwa haukufunguka. Haukufunguka kwa kuwa Masimba aliufunga kwa ndani. Bado hawakujali kusukumwa kwa mlang0, lakini haikuchukua hata nusu dakika. Kitasa kilikuwa kikishambuliwa kwa Risasi kisha mlango kusukumwa huku watu wengine watatu wenye silaha mikononi wakiingia. Hawakujua kilichokuwa ndani, hawakujua kile ambacho kimewapata wenzao. Wakaingia wakiamini wanaweza. Waliingia wakiamini wanauwezo wa kupambana. Lakini kitendo cha kuingia ndani ya chumba kile. Wakapokewa na Risasi kutoka kwenye Bastola iliyoshikilia na Teddy aliyekuwa Akivuja Damu. Wote wakaanguka chini wakirusha miguu huku na huko. Teddy alikuwa kama amechanganyikiwa, teddy alikuwa kama mwenda wazimu. Chumba kilitapakaa damu huku harufu ya kifo akitamalaki chumba chote. Maiti za watu nane zilikuwa chini. Watu ambao walikuwa wana Usalama waliotumwa Bahasha. Bahasha ambayo ilikuwa na vitu vingi ndani yake. "Jifute damu hiyo tuondoke upesi, hii sehemu sio salama." Aliongea Masimba huku akichukua kitambaa ili kumsaidia Teddy kuifuta damu. Wakati anakichukua kitambaa simu yake ikaita tena. Macho yake yakaenda moja kwa moja kwenye kioo cha Simu. "Chief" ndio maneno yaliyosomeka Juu ya kioo. Masimba hakuipokea kwa muda ule. Akaiacha iendelee kuita mpaka ilipokata yenyewe. Alikuwa na maana yake kutokuipokea Simu ya Chief. Alitaka kujua kama watu hawa wametumwa na Idara au la. Kutokupokea simu kungemuwezesha Chief kujua kile ambacho kimetokea. Baada ya simu kukata, haikupita Hata Dakika moja, simu ya mmoja kati ya maiti zilizotambarajika Chini ikaita. Teddy na Masimba wakaangaliana. Kabla hajasema chochote Masimba akaichukua simu kutoka Mfukoni kwa maiti yule. "General Chomboko" ndio Jina lililosomeka juu ya kioo cha simu ile. "Mmh" masimba aliguna, aliguna kwa mshangao mkubwa. Kuliona Jina la Jenerali Chomboko kwenye simu ya mkora yule kulimshangaza. Kulimshangaza kwa kuwa ni huyu huyu mzee aliyepiga simu muda mfupi na kumwambia kuhusu kuitwa kwake Ikulu. Lakini muda huu jina lake lilikuwa likionekana Juu ya simu ya watu waliotumwa kuja kuichukua Bahasha. Akanyamaza na kutulia, hakuongea zaidi ya kuushika mkono wa Teddy na kuanzA kupiga hatua wakitoka ndani ya Hotel.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *******



    Simu yake ya mezani ilikuwa ikiita katika usiku huo. Ilikuwa sio kawaida kupigiwa simu usiku mwingi kama ilivyoleo. Alijiinua Taaratibu na kuunyoosha mkono wake mpaka iliposimu. Akaisogeza karibu kisha moja kwa moja akaipeleka sikioni. "Hellow General Chomboko.!! Ilikuwa ni sauti kutoka upande wa pili. Sauti ambayo ilikuwa ikitoka kwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. "Kimaro mbona usiku, kuna tatizo?" Aliuliza General Chomboko bila hata kusalimia. "Chomboko Hutakiwi kuruhusu uzee uchukue uwezo wako wa kiugunduzi. Chomboko yule wa kipindi kile asingeniuliza hili bali kutaka ufumbuzi." Akajibu Mr kimaro.



    "Nimezeeka kwa sasa, nimewaachia nyie ambao bado mnadai. Tuyaache hayo, mpaka kunipigia simu usiku huu nahisi kuna jambo ambalo halikajakaa sawa." Akajibu jenerali Chomboko. Chief akatulia kwa Muda. Ukimya ukachukua mahala pake. "Kuna Bahasha imepotea mikononi mwa Askofu Ibrahim Lexandre Rengima. Bahasha hiyo inasemekana ipo mikononi mwa Masimba na Mwandani wake. Inasemekana Bahasha hiyo ina mambo mengi ya Siri na ya Hatari sana kwa Nchi. Sasa Mheshimiwa Rais Ameagiza kesho Masimba aitwe Ikulu apeleke bahasha hiyo walioichukua mikononi mwa Baba Askofu Rengima. Sasa nimekupigia kukuomba ushauri katika suala hili. Nimejaribu kuongea na Teddy lakini majibu aliyonipa ndio yaliyonifanya niinue mkonga wa simu nikupigie." Akaeleza Chief kwa kirefu. Jenerali chomboko akatulia kwa muda huku akitafakari maelezo hayo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya ujasusi. Baada ya kutafakari sana, akauliza. "Teddy amekujibu nini?"....



    "Teddy amesema kama tuna uwezo wa kurudisha Roho ya Mdogo wake, roho ya Dee plus na Roho ya mama mzazi wa masimba, wataisalimisha Bahasha Hiyo. Lakini kama hatuna uwezo huo, basi hawataisalimisha Bahasha hiyo." Akajibu Chief.



    "Kwa nini Mheshimiwa Rais Anaitaka Hiyo Bahasha? Akauliza generali Chomboko.



    "Hata mimi bado sijajua kile kinachosababisha yeye kuihitaji hiyo bahasha na ni vipi ameijua kwamba ipo kwa askafu. Na kingine kinachonishangaza ni kuonekana kwa gari yenye Nembo ya Ikulu, ikitoka sehemu zote ambazo waliuawa Viongozi wa dini ambao wote wana Uhusiano na Hiyo Bahasha. Hapa ndipo ambapo pana nishangaza na kunipa wasiwasi." Akajibu Chief. Jibu la chief likaibua ukimya mwingine kutoka kwa General Chomboko. Kichwa chake kilikuwa kikifikiria mengi katika hili linaloendelea. Hili suala kukingiwa kifua na mheshimiwa Rais ni kuonyesha uhalisia kuwa kuna kitu anakijua na hata kukifahamu. Ameijuaje bahasha iliyochukuliwa nyumbani kwa Askofu. Ni nani aliyekwenda huko na gari ambayo ilikuwa na Nembo ya ikulu? Hayo yalikuwa maswali machache kati ya mengi aliokuwa nayo. Ilishaanza kuiona hatari, alishaanza kuuona msuguano katika idara. Idara ya usalama wa nchi. Lakini haya yote ni kwa sababu gani na zipi? Baada ya kujiuliza Maswali hayo yasio na majibu, akakumbuka kuwa bado Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Yupo Kwenye laini. "Mr Kimaro vijana wako wapo nyuma ya suala hili. Ikiwa wewe mkuu wao hujui gari ile ilikwenda kufanya nini huko, ina maana kuna vitu vinafanyika pasipo wewe kushirikishwa. Sasa swali la kujiuliza Je Hili lililoibuka kwa sasa lina baraka ya kiti cha rais?" Akamaliza jenerali kwa kuuliza swali. "Nahisi lina baraka ndio maana anaihitaji hiyo bahasha. Unachotakiwa kufanya naomba umuarifu masimba kuhusu hili na pia hakikisha hiyo bahasha haifiki mikononi kwa rais wala Haipotei. Hiyo bahasha kuwepo kwake ndio uhai wa vijana hawa. Ikipotea ama kufika mikononi kwa Rais, basi tutakuwa tumepoteza watu sahihi." Aliongea Chomboko akionyesha kukijua kitu fulani. "Sawa nimekuelewa na nimekupata. Nakupongeza mwenzangu kwa kupata mwanga katika hili." Alijibu Jenerali. "Nadhani Asubuhi nitaongea na Masimba mimi mwenye ili kumpa Tahadhali katika hili." Akajibu kisha simu zikakatwa.



    *****

    Alimshika Teddy mkono na kuongozana naye kutoka katika viunga vya hoteli ile. Muda wote wakati wakitembea walikuwa wakihakikisha hawaingii mikononi kwa macho ya maadui zao.kichwani kwa masimba kulipishana mambo mengi sana. Vitu ambayo vilizidi kuisumbua akili ba hata kukivuruga kichwa chake. Kwa nini anahitajika Ikulu? Kwa nini Rais anaitaka Bahasha walioichukua kwa Baba askofu? Kwanza Rais amejuaje kuhusu hili? Kwa nini General chomboko awapigie simu watu hawa, wakati jana na hata Leo alinitahadhalisha? Ina maana hii vita iliyoanza kama utani leo hii imekuwa kubwa mpaka kumgusa Rais? Ni maswali hayo yaliomfanya amgeukie teddy. Akamwangalia kwa macho yake yenye kutia moyo. Kisha kwa Sauti ya utulivu akasema. "Teddy mke wangu, wakati huu lilipofikia hili ni wakati hatari kuliko huko tulipotoka. Naanza kuhisi kitukutoka ndani ya Taasisi kubwa hapa nchini. Naanza kuhisi kuwa tumegusa maslahi ya wahisani katika biashara hii. Niwakati wetu wa kusimama katika kupambana na hili. Meja jenerali chomboko ana kitu anachokijua kuhusu hili kinachoendelea. Teddy Nakupenda na sitaki kukupoteza katika hili. Wakati huu mimi nikielekea Ikulu, nakuomba wewe uwe ndani ya gari binafsi ukielekea Tanga kupanga mikakati ukiwa na hiyo bahasha. Bahasha ambayo imeonyesha kuleta sintofahamu kwa Nchi yangu. Natambua ni kiasi gani Chief Anasumbuliwa kwa sababu yetu. Nakuomba nenda Tanga ukajifiche huko hata kama huku wataniua utajua wapi pakuanzia." Alioongea masimba kwa mara ya kwnza machozi yakichungulia machoni. Hata Teddy alikuwa akilia sana. "Hapana Dady, siwezi kukuacha katika hili, siwezi kukuacha katika mapambano haya. Ufe mbele yangu au Nife mbele Yako." Aliongea Teddy akimaanisha kile anachokisema. "Fanya nilichokwambia Teddy, bahasha tulionayo hatupaswi kuwa nayo mikononi mwetu. Ondoka hapa jijini Upesi." Baada ya kuongea hilo akisubiri Teddy ajibu simu yake ikaita. Kuitizama namba ya mpangaji akagundua ilikuwa ni Namba ya Ikulu. Akamuonyesha Teddy kisha akaipoke.. "Tuna kusubiri wewe." Ilikuwa ni sauti iliyotoka upande wa pili, kisha simu ikakatwa. Masimba akaduwaa kwa muda akimuangalia Teddy. 'Kwaheri Teddy... fanya nilichokwambia." Akaaga masimba huku akiondoka akimuacha Teddy AMEDUWAA

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alibaki ameduwaa akimtizama Masimba akiondoka katika upeo wa macho yake. Akamtizama kana kwamba asingemuona tena. Kana kwamba asingemuona kwa miaka yote. Akatamani kumuita, akatamani japo amfuate, akatamani hata kuongea naye. Lakini kila kitu kilikuwa kigumu. Kilikuwa kigumu kwa kuwa masimba alikuwa akipotelea katika upeo wa macho yake. Akatambua kuwa alikuwa amemaliza dakika moja pale kitu ambacho kingekuwa ni Hatari kwake endapo angetokea mtu au watu wakumfuatilia. Muda mfupi baadae alikuwa ndani ya bajaj akielekea katikati ya jiji. Ulikuwa uamuzi ambao aliuchukua kutoka moyoni mwake. Hakupenda kumuacha nasimba. Moyo wake ulikuwa mzito kuliko chochote. Masimba kwake alikuwa anathamani kuliko bahasha ambayo alikuwa ameishika mkononi. Bahasha ambayo ilikuwa na maslahi kwa nchi. Hakujua ama alisahau kipaumbele cha usalama wa Taifa ni kuwa mzalendo kwa nchi yake. Kutoka moyoni kwake alimuona Masimba ni Bora kuliko nchi yake. Alitaka kuuona mwisho wa Masimba. Akaipa utulivu akili yake. Akaipa muda wa kutafakari kile ambacho alitaka kukifanya. Hakujua Bahasha ilikuwa na mambo gani mambo yake. Wakati bahaj akifika kwenye mataa ya faya, moyo wake ukamlipuka baada ya kuyaona magari mawili nyuma ya bajaj. Yalikuwa magari ambayo aliyatambua. Magari ambayo moja kwa moja alijua yalikuwa yakimfuatilia yeye. Wakati akilishangaa Hilo, akashtuka baada ya kumuona mtu akiingia kwenye bajaj na kutulia. Mtu huyu hakumzungumzisha Teddy bali aliingea na Dereva Akimtaka Ageuze bajaj na kuirudisha atokapo. Bado Teddy aliduwazwa na hilo, bado Teddy hakupata wasaa wa kuliuliza hilo. Akili yake ilikuwa imehama mbali na parefu sana. Akili yake haikuwa kwa mtu yule bali akili yake ilimuwaza sana Masimba. Alihisi hata muona Tena Masimba, alihisi hataweza kumpata tena mtu. Kuingiliwa na mtu ndani ya bajaji na kumtaka dereva wa Bajaj ageuze alikotoka, hilo hakulijali kutokana na uingiaji wa mtu huyu. Uingiaji ambao haukuonyesha labsha na hata chochote kile. Uingiaji wa mtu huyu ulijaa urafiki na haukuwa katika kile kinachoitwa kazi. Aliingia kanakwamba alipewa ama kupewa Lifti. Hakuonyesha bsstola wala silaha youote. Licha ya kufanya hivyo lakini sura ya mtu huyu iliongea naye vitu vingi sana. Kwanza haikuwa na tabasamu, pia sura hii haikuonyesha kama iliwahi kutabasamu. Dereva akataka kuhoji lakini jicho lililomtizama kutoka kwa mgeni wao huyu lilimfanya aigeuze Bajaj kama alivyoambiwa na mtu huyu. Muda wote huo bado Teddy hakuzinduka katika bumbuwazi. Bado alikuwa mbali sana. Sauti kutoka kwa mgeni Huyu ndio iliyomzindua na kumrudisha katika uhai. Uhai wa kutambua huyu ni nani na alikuwa nani. Alitambua alikuwa hapo kwa sababu ipi. "Teddy kwa nini unakuwa mkaidi kutii unachoambiwa? Upo tayari kumpoteza Masimba?. Mtu huyu akazidi kumuuliza, akamuuliza akimuacha akiyatafakari maneno yake. Maneno yaliyoanza kuirudisha Akili yake. akatambua hawa walikuwa watu waliotumwa na Chief ama Meja jenerali Chomboko. Akatambua kuwa ni kweli bahasha hii ilibeba maisha yao. Hakutakiwa kubaki hapa mjini. Alitakiwa aondoke. Lakini ataondokaje ikiwa hajui kile kinachoendelea juu ya Masimba? Ni swali ambalo halikupata majibu. Halikupata majibu kwa kuwa Tayari alipewa Ishara ya kushuka. Ishara ya macho pasipo sauti. Ishara ambayo aliitii kwa kushuka. Aliposhuka tu akashangaa kuiona gari moja aina ya Toyota Land cruiser ikisimama miguuni na wakati huo huo mlango ukafunguliwa na yeye kuingizwa ndani ya gari. Ni kitu kilichofanyika ndani ya dakika moja tu. Dakika ambayo iliacha mshangao kwa dereva yule wa bajaj. Hakuwaona watu walivyoshuka na hata walipompotea kwenye upeo wa macho yake. Wakati amepigwa na butwaa asijue hili. Akamuona mtu mwingine tena mwanamke mrembo. Mwanamke huyu hakuongea chochote isipokuwa kuunyoosha mkono wake ulioshika noti mbili za elfu kumikumi. Akionyesha kuikabidhi mikononi mwa kijana huyu. Hata pale alipoipokea bado mwanamke yule hakusimama. Bali alipotea katika aina ile ile. Aina ya penzi kupotea kipindi cha uchumba. Hakumuona na hapakuwa na mtu. Wote walipotea. Akatabasamu, tabasamu la kukata tamaaa, kisha muda ule ule akaiondoa bajaj kuelekea kijiweni kwake.



    ******







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog