Simulizi :Nitakupata Tu
Sehemu Ya Tano (5)
Muonekano wa ikulu ulimlaki masimba kwa hali ambayo ilikuwa tofauti sana. Watu maalum walikuwa pembeni wakifanya shughuli zao. Shughuli ambazo zilikuwa ni geresha. Hilo aliligundua baada ya kushuka wizara ya Elimu na kuanza kutembea Taratibu kuelekea Geti kubwa la kuingilia ikulu. Watu waliokuwa wakionyesha kufanya Shughuli sasa walikuwa wakimuangalia masimba kila alipokuwa akipiga hatua. Alikuwa akitembea kwa umakini akiufikiria wito wa kuitwa na Rais wa nchi. Moyo wake ulikuwa tayari kwa kitu chochote ambacho kingemtokea. Alijua hata kama akifa atakuwa ameipigania Tanzania kwa kiwango cha hali ya juu. Akalifikia geti na kukaribishwa na Wana Usalama wa Ikulu. Akaongozwa kuelekea sehemu husika akiwa sambamba na wana Usalama wasiopungua sita. Walitembea naye kila hatua ya mguu wake, wakaangalia wote upande pale ilipotokea masimba kufanya hivyo. Mbele ya lango la kuingilia ndani Akapokewa na wakuu wa Idara waandamizi. Alipokewa na watu ambao kwa kuwaona tu alijua kile ambacho kingeenda kutokea ndani. CDF Sambamba Na IGP Wote walikuwepo nje ya lango kumpokea Masimba. Muda wote walikuwa wakimtizama kijana wao, wakimtizama katika sura za bashasha. Muda wote alikuwa akichungwa na kutizamwa katika namna ambayo hata mwenyewe aliitilia shaka. Akasalimia kwa Utii na Heshima. Baada ya hapo akaongozwa moja kwa moja mpaka sehemu ambayo alitakiwa kufika. Sehemu ambayo ulitakiwa kufanyika huo mkutano. Kila alipokatiza ndani ya majengo ya Ikulu Ulinzi ulikuwa wa kutisha. Aliongozwa mpaka ndani ya chumba maalum. Chumba ambacho hakikuwa na mtu yoyote. Hapa Masimba akaambiwa akae ili apewe maelekezo mengine. Wakati anasubiri kile alichoambiwa Asubiri akawaona watu wawili wakiingia hapa chumbani. Watu hawa haikuwa ngumu kuwagundua. Hiki kilikuwa kikosi maalum cha kumlinda Rais. Wote waliingia, kisha kusimama mlangoni. Hawakumuangalia Tena Masimba. Wote walikuwa wakitizama Nje walikotoka. Haukupita Muda mrefu Rais naye akaingia pale akiwa sambamba na Mpambe wake sambamba na Walinzi wengine. Baada ya Rais kuingia Masimba Akasimama kwa Heshima zote. Rais akasogea akielekea alipokaa Masimba. Akaunyoosha mkono kumsalimia mwana usalama huyu ambaye hakuonyesha wasiwasi wowote. Wakati rais akitabasamu na kucheka. Usoni kwa masimba hapakuwa na Tabasamu. Alikuwa akimuangalia Rais kwa macho yasiotizama pembeni. Katika macho ambayo yalitaka kusoma kile ambacho kilikuwa ndani ya Rais Wa Nchi. Baada Ya salaam Masimba akapewa Ishara Ya Kukaa. Baada ya wote kukaaa mlango ukafungwa na walinzi wote kutakiwa kutoka Nje. Ndani akabaki mheshimiwa Rais na Masimba Wakitizamana.
*******
Kitendo cha Rais wa nchi kuitaka bahasha yenye Siri kubwa ya nchi kuliwashangaza wakuu wa Idara zote za Usalama Wa Nchi. Simu Zilitembea katika usiku ule kwa Lugha ambayo haikuwa Rahisi kueleweka machoni kwa Watu. Mawasiliano kati ya CDF, IGP, Chief na Hata Major General Chomboko yalimalizika Saa moja Asubuhi wote wakiwa na Azimio Moja. Azimio la kumtaka Masimba kutokuiwasilisha bahasha ile mikononi Mwa Rais. Baada ya kufikia muafaka wa kile kilichozungumzwa, ndipo walipotumwa Watu binafsi kumfuatilia Masimba na Teddy ili kuhakikisha Bahasha haingii mikononi mwa Rais. Hata pale Teddy alipochukua bajaj watu hawa walikuwa nyuma yake wakihakikisha hafiki kule anapotaka kwenda. Amri iliyotolewa ilikuwa ni lazima Teddy Aondoke ndani ya jiji hili. Nilazima apotee na asionekane. Ilitakiwa hivyo kwa kuwa Kuna kila dalili ya Masimba Kushurutishwa kutoa Bahasha kwa Njia Yoyote ile
Alikuwa akitizamana na kiongozi mkuu wa nchi. Alikuwa akitizamana naye katika namna ya kumsoma. Katika namna ya kumuangalia kwa umakini. Alikuwa tayari kufanya chochote pasipo kuhofia kitu. Rais alikuwa akimuangalia Masimba pasipo kupepesa jicho lake pembeni. Alikuwa na nia ya kumtia hofu, alikuwa na shida ya kumfanya masimba amuigope. Lakini hakumjua huyu masimba alikuwa nani, hakujua masimba alikuwa mtu wa kutokuogopa kitu. Muda ukazidi kuyoyoma huku wakitizamana. Bado Rais hakufumbua kinywa chake kuongea kile alichotaka kukiongea. Hata masimba naye aliiweka heshima mbele, nidhamu ya uzalendo na hata heshima ya kikazi. Akazidi kukaa kimya akisubiri kuambiwa kile alichoitiwa. "Nauomba ule mzigo mliouchukua nyumbani kwa Askofu Rengima. Nitakupa kiasi chochote cha pesa uitakayo." Kwa mara ya kwanza kiongozi wa nchi alizungumza. Maneno yake yakamfanya Masimba ainue macho yake na kumtizama Rais. Alimuangalia kwa umakini huku akilazimisha Rais amuangalie na kumsoma kupitia Macho yake. "Sikuwahi kufika nyumbani kwa Askofu na wala sijawahi kuonana naye, na kwahivyo hakuna mzigo niliopewa na Mtu huyo Mheshimiwa Rais." Akajibu Masimba akiendelea kumtizama Rais usoni mwake. Jibu lake likaonyesha kumfanya rais kuukunja uso wake. Licha ya muda mfupi kuukunjua lakini tayari masimba alikuwa amehisi kitu. Kitu ambacho alipanga kutoondoka ikulu mpaka akijue. "Masimba Mwanangu hii ni fursa ya kutengeneza maisha yako. Hili suala unaloendelea nalo halitafika popote. Bora upewe pesa yako uishi vizuri na familia yako. Na uachane na hili. Nakueleza haya kwa kuwa Nakupenda na Tanzania Haitaki kukupoteza. Hembu fikiria hilo kwanza. Aliongea mheshimiwa safari hii akiongea kwa upole sana. Jibu hilo lilionyesha kumkera Masimba, jibu hilo lilimfanya Masimba amtizame kwanza Rais. "Unajua hili suala limepoteza watu wangapi? Unajua hili suala limeharibu maisha ya vijana wangapi? Leo hii unapata wapi nguvu ya kulisema hili? Mama yangu amelala Kaburini kwa sababu ya suala hili, leo unaniambia hilo? Kama unaweza kuwarudisha wote waliokufa kwa suala hili nitakubaliana na wewe. Otherwise risasi yangu itamuua kila mmoja hata kama ni wewe." Akajibu Masimba akiendelea kumuangalia Rais pasipo hofu yoyote. Macho yake yalikuwa yakisomeka vingine Kabisa. Jibu la Masimba likaonyesha kumtingisha Rais, kitendo cha kusema atamuua hata yeye kilikuwa kitu kibaya sana kwake. Akamuangalia Masimba kwa muda mrefu sana bila kuongea chochote. "Unadhani ni kitu Rahisi hicho unachokisema? Unadhani nikiamua unaweza kutoka hapa? Akauliza Rais naye akionyesha kuhamanika. "Kama nimeweza kutoka Ikulu ya Rais Vladimir Putin Wa Russia basi hapa hakuna ambacho kitanisumbua. Na ungekuwa na uwezo wa kunifuta basi usingeniita hapa. Umeniita hapa kwa kuwa unajua na kutambua kuwa mimi ni nani. Kwa ajili ya Tanzania Nipo Tayari Uniue ama kunipoteza." Alijibu Masimba akimaanisha kile ambacho anakitoa moyoni. "Usijidanganye Masimba kumbuka Nchi ndio imekusomesha mpaka kufika hapo ulipo. Kumbuka Gharama ya kukusomesha wewe ingeweza kutengeneza maisha kwa watu wengine. Tambua hilo kijana. Pia kukuita hapa sikukuogopa bali tunakupenda. Tukikutaka Hutusumbui kabisa." Akajibu Rais.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwahiyo kama Umenisomesha ndio unitumie katika kuwaua wa Tanzania wenzangu? Ndio unitumie kufanikisha Madhambi yako? Ndio unitumie kukubali nje yangu iharibiwe? Nimeapa kuwa mzalendo kwa Tanzania. Ukiona Hii kazi ndio inakufanya uniambie hayo basi kuanzia leo Mimi sio Mwana Usalama katika nchi hii. Aliongea Masimba huku akichomoa kitambulisho chake na kukiweka juu ya meza. Ni muda ule ule mlango ukafunguliwa na wana usalama. Kila mmoja alikuwa Tayari kwa chochote. Lakini tofauti na walivyotegemea, wakakutana na Tabasamu la Masimba. Tabasamu lililokificha kitu moyoni mwake. Muda ule ule akainuka, aliamua kuinuka kuelekea nje ya chumba kile akikiacha kitambulisho juu ya meza. Kilikuwa kitendo ambacho hakikutegemewa na Rais. Bado alikuwa katika mzubao wa kutoamini. Kutoamini kule kunakofanywa na kijana huyu. Akatamani aamuru akamatwe lakini moyo wake uliijenga hofu. Hofu ambayo hata yeye hakuijua. Akamsindikiza Masimba kwa macho, akamsindikiza alivyokuwa akitembea. "Ni mtoto sana huyu hawezi kunishinda." Alijisemea akikiangalia kile kitambulisho. Kitanburisho ambacho kiliachwa Juu ya meza. Maafisa wa ikulu sambamba na wakuu wa idara zote za usalama waliokuwa wamekaa sehemu ya siri wakilitizama tukio lile kila mmoja alitoka baada ya kumuona masimba akitoka huku kitambulisho chake akikiacha mikononi mwa kiongozi wa Nchi.
[06-08, 14:36] Ibrahim Masimba: Alitoka akiwa ni mwenye Hasira. Aliamua kuiacha kazi aliyoipenda. Kazi aliyoitendea haki tokea mwanzo kabisa wa maisha yake. Hakuuona umuhimu wa kuendelea kuwa katika Idara hiyo. Idara inayosahau misingi ya kuanzishwa kwake. Idara ambayo imekuwa ikishiriki siasa za nchi hii. Mama yake, dee plus, vicky na watu wengine ni Roho ambazo zimeondolewa kwa sababu ya hili linaloendelea. Kwa nini Rais ameamua kulikingia kifua hili suala. Ni nani ambaye yupo nyuma mpaka kusababisha msimamo huu dhaifu kwa kiongozi huyu wa nchi. Akaamua Rasmi kuiacha kazi yake. Kazi hii ambayo ilikuwa ni hatari katika maisha yake. Akairuhusu miguu yake itembee katika namna ya kuliwahi lolote lile. Hakujali taharuki aliyoiacha huko ndani. Hakuwa tena mwana usalama, hakuwa tena Yule Masimba Tegemezi katika nchi hii na Idara ambayo aliitumikia na kunusurika kuuawa katika mission mbalimbali alizotumwa kuipigania nchi. Akalifikia geti kubwa la kutokae nje. Alikuwa akitembea kana kwamba hakuna chochote ambacho kimetokea. Hata macho ya watu waliokuwa wakimtizama kwa hila, hakujali na hata kuwafuatilia. Akatembea na kutembea akikipita Chuo cha Usimamizi wa Fedha Ifm. Hatua kumi mbele alikuwa akifika makao makuu ya Jeshi la magereza. Akili yake bado haikuwa imetulia. Akili yake bado ilikuwa akifikiria Sauti na kauli za rais wa Nchi. Kuna wakati alikuwa akijisonya na hata kuongea peke yake. Aliipenda Tanzania kwa Moyo wake Wote. Kuiwaza Tanzania kukafanya akili yake imkumbuke Teddy wake. Teddy ambaye alimuacha katika Gesti waliolala usiku uliopita. Teddy ambaye alimuacha hapo kituuoni akiduwaa na kushangaa. Hapo akauona Ulazima wa kumtafuta. Ulazima wa kumuona mtu huyu, mtu ambaye alikuwa ni Muhimu kwake. Wakati akifikiria kuichomoa simu yake ili amtafute Teddy, macho yake yakamuona mtu ambaye uliyafanya mapigo yake ya Moyo kwenda kasi. Umbali wa hatua hamsini kutoka alipo akamuona Jimmy. Jimmy Lambert yule ambaye alikuwa akimtafuta kwa Udi na Uvumba. Hicho nikitu ambacho kilimshangaza, kilimshangaza kwa hiki ambacho alikuwa akikiona mbele yake. Jimmy aliyekuwa amemtafuta kwa muda mrefu bila kumuona, leo alikuwa hatua hamsini mbele yake. Akatabasamu akicheka kimoyo moyo. Kisha akajiuliza. Inakuwaje Jimmy ajitokeze Muda mfupi baada ya yeye kuiacha kazi Hii? Hilo likamfanya acheke kwa mara ya pili. Akaiona vita ambayo imeanza kupiganwa na taasisi kubwa nchini. Alitambua kutokea kwa Jimmy mbele yake ulikuwa ni mpango uliosukwa. Ulikuwa ni mtego ambao alitegewa ili umnase. Hilo aliligundua mapema. Hivyo akaamua kumpita Jimmy pasipokumuangalia. Pasipokuonyesha kama amemuona. Akatembea mbele zaidi mpaka lilipo jengo la Freemason. Akatulia hapo kwa muda akitizama viatu kutoka kwa wachuuzi waliokuwa wakiuza. Hakuwa na Shida ya viatu, lakini alikuwa hapo kwa kuwa alitaka kujua kama Alikuwa akifuatiliwa au la!. Wakati ameinama hapo akawaona wadada watatu nao wakisogea hapo. Hawa walikuwa wadada warembo kuwahi kutokea machoni Mwake. Walikuwa wazuri hasa. Kila mmoja alikuwa na mkoba mkononi kuonyesha kuwa Alikuwa Nwanafunzi katika chuo cha Usimamizi wa fedha, ama mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania. Utembeaji wa wasichana hawa ukampa hamu ya kusimama vizuri, akageuka na kutizama nyuma. Cha kushangaza akapokewa na matabasamu Kutoka kwa watoto hawa. Kengele za Hatari zikalia kichwani mwake. Ni kengele hizo zilizomuamsha na kumuweka kwenye majibu kuwa Alikuwa anaandamwa tokea alipoondoka pale Ikulu. Alijua kuwa alikuwa anatafutiwa sababu ya kufutwa hapa Duniani. Akajiapiza kuwa mtulivu katika kipindi hiki. Utulivu ambao haukutakiwa kufanya chochote kile. Akawangalia Wasichana wale kwa muda mfupi kisha akaamua kuondoka Zake.
******
Kwani Masimba ni nani? Kwani Masimba anafaida gani kwangu? Kwani nikiipeleka hii Bahasha kwa mheshimiwa Rais na nikapewa kile Rais alichoniahidi atanionea wapi? Yalikuwa maswali kutoka kwa Teddy akijiuliza mwenyewe baada ya kuachwa katika nyumba moja ya Siri. Roho ya usaliti na tamaa ya pesa vilishamuingia. Sasa alikuwa akitamani tena kumsaliti, alikuwa akiitamani sana Pesa. Taarifa aliyopewa muda mfupi kuwa Masimba amekataa kutaja kiasi chochote cha pesa anachotaka kilimsikitisha sana. Aliitamani pesa na kuipenda sana. Pesa kwake ilikuwa na thamani kuliko penzi na hata utu wa Masimba. Hakujua masimba alikuwa akihangaika kwa sababu ya Tanzania. Hakujua Masimba aliwapoteza Ndugu zake sababu ya Kazi hii. Kwa mara ya kwanza akatamani sana kutoka ndani ya jengo lile la siri. Kwa kuwa bahasha alikuwa nayo ndani ya nguo zake akaona kuondoka hapo ndio ingekuwa njia Bora. Kile kilio na kiapo cha muda mfupi kilianza kuyeyuka taratibu. Hapakuwa na kiapo wala kilio tena. Tamaa ya pesa tayari ilimchukua Teddy. Muda mfupi alikuwa akiinuka pale akiyatoa mavazi yake na moja kwa Moja akielekea bafuni. Alikuwa kwenye mkakati wa kuianza safari ya kuondoka katika Jumba hilo. Muda mfupi baadae akatoka chumbani akiwa kama Alivyozaliwa. Akauendea mlango kisha kubonyeza kengele ya hapo mlangoni. Punde mlinzi wa Jumba lile akafika na kuufungua Mlango. Macho yakamtoka baada kukutana na tukio la Teddy kuwa uchi kama Alivyozaliwa. Mlinzi akaupoteza umakini huku akilishangaa umbo la mtoto huyu. Teddy alikuwa akikipenda kitu hicho sana, akaanza kupiga Hatua kumfuata mlinzi yule aliyekuwa ameduwaa. Hatua ya kwanza, hatua ya pili na hata ya tatu, zikamkuta mlinzi yule akiwa chini akivuja Damu. Baada ya kuhakikisha mlinzi amepoteza uhai, teddy akamvuta kwa ndani, kisha kumpapasa na kuchukua vitu mbalimbali. Baada ya Hapo akayaendea mavazi yake, akavaaa kisha akaondoka Hapo Ndani Bastola Ikiwa Mkononi. Wakati anaukaribia mlango walioingilia,akauona Mlango ukifunguliwa kisha mwanaume wa makamu Akaingia hapo. Macho yake yalipotua Usoni kwa Teddy akagundua Teddy alikuwa Amesaliti na kutaka kutoroka na bahasha ile. Meja Jenerali Louis Chomboko akaupeleka mkono wake sehemu alipoihifadhi Bastola yake. Lakini mkono wake Haukufika popote. Risasi Mbili zikatua kifuani kwake na kumtupa chini. Teddy alikuwa ameamua kuasi tena. Baada ya Mzee Chomboko kupigwa Risasi na kuanguka chini, Teddy akatoka mle ndani na kuanza kusimamisha magari. Wakati Teddy akisimamisha Magari tayari kwa kuondoka, Masimba ndio alikuwa Akifika hapo tayari kwa kuonana na Meja Jenerali Chomboko.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Teddy akisubiri gari ili kuondoka eneo lile, ndio Muda Huo ambao Masimba alikuwa akishuka hapo akiwa katika mawazo sana. Alitembea taratibu akihakikisha hakuna macho ya mtu ama watu yanayomuangalia. Muda wote alikuwa makini kwa Kila Hatua. Wakati anaukaribia mlango wa nyumba ile akauhisi mwili wake ukisisimka. Kitendo hicho kilitokea vbaada ya kuuona mlango wa nyumba ile ukiwa wazi. Haikuwa kawaida kwa mlango wa nyumba kama hizo kuwa wazi, haikuwa kawaida kwa kuwa ni sehemu ambayo haikupaswa kuachwa wazi. Akajikuta akijipapasa mfukoni mahala ambapo aliihifadhi bastola yake. Alipoigusa akaachia tabasamu mwanana. Akaipiga hatua nyingine huku miguu na mikono ikiwa tayari kwa lolote. Akaufikia mlango kisha kuingia moja kwa moja ndani. Kengele za hatari zikalia baada ya kukutana na michirizi ya Damu. Michirizi ambayo iliachwa kutokana na muonekano wa kitu kilichojiburuza. Roho yake ikampaa huku bastola ikiwa mkononi mwake. Miguu ilikuwa ikimtetema kila pale alipohisi kuwa Mtu aliyeiacha damu hapo ni Teddy. Hakuwa Tayari Teddy afe, hakuwa Tayari Teddy auawe. Hakuwa tayati kumpoteza Teddy kutokana na kuwa alimpenda. Alimpenda zaidi ya anavyowaza na Hata kufikiria. Akaufuata mburuziko ule. Hatua tatu mbele akakiokota kitu, kitu kilichomfanya akubali kuwa mtu aliyepigwa Risasi alikuwa Teddy. Chini aliiona bahasha. Bahasha ambayo ilikuwa na Siri kubwa. Akaikota huku mikono ikitetemeka. Moyo ukazidi kumpasuka baada ya kuiona bahasha imefunguliwa huku kile kilichodhaniwa kuwa siri hakikuwepo. Akahisi Dunia ikizunguka. Ni vipi kama Teddy ameuawa na kilichopo ndani ya Bahasha kupitea? Ataishi kweli katika amani wakati kilichopo ndani ya bahasha ndio kilikuwa kitu cha kumuweka kwenye usalama? Akaitupa bahasha na kuzidi kuufuatilia ule mburuziko. Mbele kidogo akamuona mtu ambaye hakuamini kama alikuwa Yeye, Meja Jenerali chomboko alikuwa amelala katikati ya Dimbwi la Damu. Damu ambayo ilikuwa ikitembea sakafuni kuonyesha mauaji haya hayakutendeka muda mrefu. Hilo likamfanya Masimba azidi kuchanganyikiwa. Muda mfupi baadae alikuwa pembeni mwa mwili wa Meje Jenerali Chomboko. Masikio yake yakausikia mkoromo na sauti dhaifu kutoka kwa Mzee huyu. Hii ilimaanisha kuwa hakuwa amekufa, alikuwa katika hatua za mwisho kufa. Akamuinamia na kujaribu kuongea naye.. lakini haikuwezekana, haikuwezekana kwa kuwa mzee hakuwa akiongea chochote. Hakuweza kuongea kwa kuwa hakuwa na muda mrefu wa kuishi. Hakuonyesha kama ni mwenye kupona. Punde akauona mkono wa Mzee Chomboko ukinyooka huku kidole chake kukichofya katikati ya Damu kisha kuandika pale sakafuni. "Teddy ameasi. " yalikuwa maneno makali yalioukata Moyo wa Masimba. Akajikuta akitetemeka huku Hasira juu ya Teddy ikizidi kuchukua nafasi. Akiwa katika Hilo akamuona Mzee chomboko akinyoosha miguu, kisha kutulia. Alikuwa amekufa, alikuwa amekufa katika kifo cha kumpigania yeye. Teddy alikuwa amesababisha kupotea tena kwa mtu muhimu katika Maisha Yake. General chomboko alikuwa ni mtu muhimu kwake akimlinda katika hatari, hatari ambayo ingeshampoteza. Leo hii alikuwa amelala katikati ya dimbwi la damu tena akiwa maiti. Tena akiuawa na Mkono wa Teddy. Teddy aliyekuwa akilia muda mfupi uliopita. Teddy aliyenusurika kuuawa mara kadhaa. Teddy aliyesema alikuwa akimpenda, aliyekuwa akimhitaji na kulia kwa Ajili yake. Lakini leo hii amemuuua Mzee chomboko na kutoroka na bahasha ambayo ndiyo ilikuwa zamana ya Maisha yake. "TEDDY NITAKUPATA TU NA NITAKUUA KWA MIKONO YANGU." Baada ya kutamka hilo akainuka na kutoka katika jengo hilo la Siri. Maandishi ya jenerali chomboko yalikuwa yakijirudia Kichwani "TEDDY AMEASI". Alihisi akili yake haifanyi kazi kwa muda ule. Hakuiona furaha tena. Wakati hilo likiendea kumsumbua kichwani, simu yake ya mkononi ikatoa mlio. Ilikuwa ikiita. Akaichomoa na kukutana na Jina la Chief. Mkurugenzi Wa Idara ya Ujasusi alikuwa akimpigia.
Akaipokea haraka na kuipeleka sikioni. "Naomba wahamishe watoto wangu kutoka hapo walipo. General Chomboko No more. Teddy Ameasi na Bahasha ametoroka nayo." Aliongea masimba kwa Haraka bila kusubiri maelezo. "Nililifahamu hilo mapema, nilimfahamu yule mtoto ni mwenye tamaa. Vijana wangu wamemuona katikati ya Mji. Nadhani anataka kwenda kuonana na Rais. Cha kufanya wewe sasa hivi unatakiwa kushughulikiwa. Kwahiyo unachotakiwa ni kuwa makini na usijionyeshe. Vijana wangu wapo sambamba naye na nataka wamzuie kabla hajaingia lango la Ikulu. Nimehuzunika sana kumpoteza Chomboko. Teddy Hastahili kuachwa Hai. Ukishindwa wewe nitaifanya mimi hiyo kazi." Aliongea Chief kisha kukata simu. Masimba akaganda kwa muda, Teddy ameonekana katikati Ya Mji. Anaonyesha kuwa anaelekea Ikulu. Ni maelezo hayo yaliompa masimba muelekeo sahihi kwa kipindi hicho. Damu ya Asteria P Paulo Damu ya Dee Plus damu ya Mama yake na Sasa Damu ya Mzee chomboko ilikuwa mikononi mwake. Ulikuwa ni muda wa kuilipa Damu Hiyo. Ulikuwa muda wa kuwawahi kabla ya kumuwahi. Ulikuwa muda wa kuelekea Posta, ulikuwa muda wa kutembea kila anapokanya Teddy. Ilikuwa ni lazima ampate. Ilikuwa nilazima Amuue.
******
Alikuwa akitembea bila kujua alikuwa akitembea na watu. Hakujua kuwa vijana wasiopungua wanne walikuwa wakitembea naye kwa kila hatua. Walitakiwa kuhakikisha haiingii katika viunga vya ikulu. Hiyo ndio ilikuwa amri kutoka kwa Chief. Teddy hakujua kuwa wauza urembo wawili, muuza pweza kwenye sinia na hata muuza vitambaa walikuwa vijana ambao walikuwa wakimfuatilia yeye. Aliwachukulia kama wamachinga bila kujua kuwa yupo kwenye tageti. Alitembea Kwa mwendo wa kawaida mpaka eneo la Feri. Akatafuta sehemu nzuri na kutulia kandokando ya bahari. Alikuwa akitizama maji huku mawazo yakimzonga. Kile alichokifanya alijua sio kizuri lakini moyo wake ulikuwa tayari kwa lolote. Kwa kuwa alitambua Kitu alichokichukua Kwenye Bahasha ndio dhamana ya Uhai wa masimba. Alijua Masimba Angeuawa muda wowote kitu ambacho kitasababisha yeye kupata pesa zote. Hilo likamfanya asahau mapenzi na ubinadamu wote. Alikuwa tayari Masimba afe ili mradi yeye achukue mamilioni ya shilingi. Muda wote vijana waliokuwa wakimfuatilia bado hawakumpa nafasi. Lakini wakati wakiendelea na hilo wakamuona Teddy akisimama akitembea taratibu kuelekea soko la samaki feri. Hata wao bado walikuwa nyuma katika namna hiyo hiyo. Wakimuangalia kwa umakini. Teddy akaingia ndani ya Soko la samaki, lakini wakatia akiingia hapo akageuka kwa chati kutizama nyuma. Tabasamu la kugundua kitu fulani likatamalaki. Aligundua kuwa alikuwa akifuatiliwa kwa nyuma na vijana wa usalama wa Taifa. Hapo akaongeza umakini akiitafuta njia ya kuwatoroka watu hawa. Kitendo cha kuwaona watu hawa wakimfuatilia, kulitoa majibu kuwa tayari ameshagundulika kile alichokitenda. Kilichokuwa kikimpa nguvu ni kule kujua kuwa Masimba alikuwa Ikulu na isingeweza kutoka huko. Na mpaka kuja kutoka kwake, yeye tayari alikuwa yupo mbali na hatakuwa hapa nchini. Kwa mara ya kwanza akamkumbuka Jimmy, ilikuwa ni lazima ukutane na Jimmy. Ilikuwa ni lazima aongee na Jimmy ili kufanikisha adhma yake. Alijua kabisa akichelewa na akaingia mikononi kwa masimba basi angeuawa hata kwa kukatwakatwa. Hakuwa tayari kwa hilo. Ilikuwa ni Lazima amtafute Jimmy. Au ilikuwa lazima Atafute njia ya kuonana na Rais Wa Nchi. Alikuwa tayari kuitoa karatasi ile aliyoichukua kwenye bahasha. Ilikuwa tayari kuitoa ili apate pesa za kumuondoa hapa nchini.
**********
[06-09, 16:04] Ibrahim Masimba: Alishuka posta mpya akiwa kwenye utofauti wa sura, mavazi na hata utembeaji. Alikuwa ni kama babu kizee mwenye kutembelea mkongoja. Mvi zilipangana kichwani kuonyesha kuwa mzee huyu alikuwa amekula chumvi nyingi. Baada ya kushuka hapo akasogea pembeni sehemu ambayo hukaa watu. Naye akakaaa hapo. Baada ya kukaa, akatoa kitabu chake na kuanza kusoma taratibu huku macho yake yakizunguka kwa hila yakiitizama sura ya kila apitaye na hata wale ambao walikuwa wakipanda magari. Alikuwa masimba akiwa hapo kwa sababu maalum. Alikuwa hapo akimtafuta Teddy katika Utofauti kama huo. Aliamua kuingia kazini kwa staili hiyo akiamini anaweza kuuepuka mkono wa wana usalama. Pia alitambua angeweza kumpata Teddy kwa urahisi. Muda wote macho yake hayakutulia sehemu moja. Alikichunguza hiki na kukiangalia kile. Hata waliokuwa kwenye bajaj alikuwa akiwatizama katika namn ambayo hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kuligundua Hilo. Muda ukasonga bila kumuona mtu. Kagiza kakaanza kuiingia akiwa bado yupo hapo. Alikuwa ametulia safari hii akionyesha akipuliza kiko. Moshi ulikuwa ukipaa hewani taratibu na kuileta burudani kwenye nafsi yake. Wakati akilifurahia hilo simu yake ikaingia Sms.. "Kuku wako imeshindwa kuingia kwenye banda. Wanao wamemtafuta lakini hawamuoni." Ulikuwa ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya mafumbo. Ujumbe ambao ulipokelewa kwa mwili wake kusisimka. Teddy alikuwa amewapotea vijana waliokuwa wakimfuatilia. Ilikuwa taarifa iliyousisimua sana mwili wake. Taarifa ambayo ilimfanya ahisi Teddy alikuwa ameshagundua hilo la kufuatiliwa. Akasimama hapo akitaka kuelekea upande wa pili wa barabara. Wakati ikitaka kulifanya hilo, akamuona mwanamke aliyevaa nguo chakavu huku juu akiwa amebeba kapu lililoonyesha kuwa lilikuwa na samaki. Licha ya uchakavu wa mavazi, licha ya ubebaji wa Kapu lile, licha ya kuonekana kama muuza Samaki, bado hakuweza kumpotea Masimba, bado hakuweza kumpoteza masimba. Alimtambua na alimjua. Lakini kwa nini yuko hivi? Lilikuwa swali ambalo halikujibiwa, lilikuwa swali ambalo halikupata muda wa kuulizwa. Misuguano ya tairi za gari zikaleta mayowe kwa watu waliokuwa karibu na kituo cha daladala posta mpya. Gari aina ya Coaster iliyokuwa ikifanya safari yake kati ya Mbezi na Posta ilikuwa nyang'anyang'a baada ya kugongwa na gari kubwa iliyokuwa akipita kwa mwendo wa kasi. Hilo likaifanya shingo ya Masimba kugeuka, kugeuka kutizama kwenye ajali hiyo. Hata pale alipokuja kugeuza shingo na kukumbuka kuwa alikuwa amemuona Mwanamke Anayemfahamu.. Hakuweza Kumuona Tena, licha ya kutokumuona lakini pia hata lile kapu alilokuwa amelibeba kichwani, lilikuwa limeachwa pale pale chini Watu Wakilishangaa. Hakuamini
Alimuona mwanamke anayemfahamu akiwa kwenye mavazi chakavu, licha ya mavazi hayo lakini pia kichwani alikuwa amebeba kapu chakavu ambalo ndani yake lilionekana kuwa na samaki. Lakini baada ya Ajali hii, ajali ambayo ilionekana kupangwa. Hakumuona tena Veronica Senka. Hakumuona Vero zaidi ya kapu la samaki ambalo lilikuwa chini huku samaki wakitawanyika. Hilo likampa mzubao wa kama sekunde tatu, mzubao ambao uliondoka pale tu aliposikia ving'ora vya magari ya hospitali pamoja na magari ya polisi. Akarudi mpaka pale alipokuwa amekaa; akakaa na kujirudisha kwenye muonekano wa kizee. Muonekano ambao ulimfanya aipate heshima. Alikaa hapo mawazo yake yakiwa kwa Teddy, alikaa hapo mawazo yake yakimuwaza mwanamke huyu. Licha ya wazo hilo lakini hakuacha kujiuliza kuhusu Veronica. Veronica mwenye kapu la samaki. Veronica ambaye aliliacha kapu lake la samaki. Veronica aliyepotea katika aina fulani ya kimaajabu. Kwa nini Baada ya Ajali naye akapotea? Kwa nini baada ya Ajali apotee? Ama ajali ilikuwa ni ya kupangwa? Kama imepangwa nani ambaye ameipanga na kwa nini? Hayo pekee ni maswali yaliomsogeza mpaka sehemu yenye mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiwasaidia majeruhi. Nia ilikuwa ni kuwatizama majeruhi hawa na hata madereva wa Gari iliyoligonga hili gari la Abiria. Lakini cha ajabu madereva wa ile gari kubwa hawakuwepo ndani ya gari na hapakuwepo na dalili ya uwepo wao eneo hilo. Nyundo kubwa ya Hatari ikagonga kichwani kwake. Gari igongwe pasipo na sababu kisha madereva wapotee? Mara moja akatambua ajali ile ilipangwa na sababu ya kupangwa kwake ni kutaka kuwapoteza watu kutoka machoni kwa watu. Hata Vero alimshangaa kwa sababu ya Kuzingatia kile kinachoendelea kwenye Ajali. Wakati akiliwaza hilo akaupata ujumbe tena kutoka kwa chief. Ujumbe ulioandikwa wa Lugha ile ile ya Mafumbo. "Ndege anaruka kuelekea Kinondoni akiwa sambamba na tetere katika urafiki wa mashaka. Bado tunampeleka kwenye banda." Ulisomeka ujumbe huo. Ujumbe uliokuwa ukimjulisha kuwa Teddy alikuwa sambamba na Veronica. Hilo likamuondoa hapo mpaka kwenye kituo cha Tax Nje ya Jengo la Benjamin Mkapa. Muda mfupi baadae alikuwa barabara akielekea kinondoni kumchukua Teddy. Alijua Teddy hakuwa na uwezo wa kufika Ikulu. Alijua Teddy hakuwa na nguvu hiyo tena. Alitambua alichokitafuta Teddy ni nguvu ya kumuwezesha kuingia mikononi kwa Ikulu. Muda wote alikuwa Akuwasiliana na Chifu akimwambia kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kati ya Wana usalama waliokuwa wakimfuatilia Teddy na Veronica. Tax iliendelea kukata mbuga, dereva ikipenya hapa na kupenya pale. Wakati wanaiacha barabara ya Morogoro kuifuata barabara inayoelekea kinondoni mkwajuni, wakapitwa na magari mawili yakiwa kwenye mwendo wa kasi sana. Kwa kuwa Masimba hakuwa na mawazo mengine zaidi ya kumuwaza teddy hakuyafuatilia Magari yale. Bado alikuwa akimhimiza Dereva aendelee kuendesha gari. Mbele kidogo baada ya kukipita kituo cha Kanisani, wakakutana na foleni. Ilikuwa foleni iliyowashangaza yeye na Dereva wa Tax. Kwa kuwa wakati huo wa Usiku hapakuonyesha uwepo wa magari mengi katika barabara hiyo. Muda ukawa unayoyoma bila foleni kusogea. Masimba akajipapasa na kutoa Elfu kumi kisha kumuomba Yule dereva ili yeye ashukie hapo. Dereva hakuwa na hiana. Masimba akashuka akiwa na mkongoja wake mkononi. Baada ya kutembea kama hatua Tano, akavutiwa na umati wa watu uliokusanyika umbali mfupi kutoka pale alipo. Kingine kilichomvutia ni uwepo wa Askari wa Kikosi maalum sambamba na Askari Kanzu waliotapakaa Eneo lote. Masimba akajikongoja na kusogea kwa karibu Sana. Hatua kadhaaa mbele macho yake yakatua kwenye miili ya watu watatu ikiwa imelazwa chini ikiwa haina uhai. Kuwatizama kwake kwa mara moja kulitosha kumfanya agundue kuwa waliouawa walikuwa ni Wana Usalama waliokuwa wakimfuatilia Teddy. Hilo likamfanya aondoke pale kwa haraka sana. Alitaka kutafuta sehemu tulivu ili aweze kuwasiliana na Chief.
*******
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chief hakuwa akipatikana kuonyesha simu yake ilikuwa imezimwa. Hilo nalo pia lilianza kukivuruga kichwa cha Masimba. Ni muda mfupi uliopita alikuwa akiwasiliana na Chifu akimueleza kule ambapo walikuwa wakielekea Teddy na Veronica. Lakini muda huu alikuwa hapatikani Huku Vijana wake wameuawa kinyama. Hakikuwa kitu cha kawaida kwake kutokea kwa hilo. Hakikuwa kitu cha kawaida kwa hilo lililotokea. Akailazimisha akili yake iamini. Akaitaka akili yake iamini kuwa chifu alikuwa katika hatari ama shinikizo kutoka mamlaka iliyomteua. Akauona Muda wa Mapambano umewadia, muda wakujitokeza katika vitendo. Aliamua kurudi kazini kuirudisha heshima ya mtu. Muda mfupi baadae alikuwa Juu ya pikipiki akielekea katikati ya Mji. Alikuwa akielekea mahala fulani kwa sababu ya kitu fulani. Alihitaji kwenda kupumzika hata kwa dakika tano. Ni katika safari hiyo alipomkumbuka Mwanaharamu. Alihitaji kumuita katika hili. Alitambua angekuwa msaada mkubwa sana. Lakini kabla hajamuita Huyu, alitaka kwanza kujua pale ambapo Alihifadhiwa mkurugenzi Wa Idara ya Usalama Wa Taifa. Alifika maeneo yale ya Posta ya Zamani. Akachepuka mpaka maeneo ya kanisa la St Joseph. Hapo akazunguka mpaka nyuma ya Jengo la Kanisa hilo. Hapo nyuma palionekana kibanda kidogo ambacho kilionekana kama ni Chumba kinachotumiwa kwa Shughuli za kanisani. Baada ya kusimama na kuugonga mlango kwa Ishara inayotakiwa. Mlango wa kijumba kile ukafunguliwa kisha masimba akapewa Ishara ya kuingia. Baada ya Masimba Kuingia ndani mlango ukafungwa. Ingawa kwa Nje Kilionekana kama kijumba kidogo lakini kwa ndani ilikuwa ni Jumba kubwa. Mbele yake Alikuwa amesimama mtu mwenye umri usiopungua miaka 60. Alikuwa ni mwanaume mwenye asili ya Bara la Ulaya. Licha ya kuwa mzee lakini bado mwili wake ulionekana kuwa na nguvu sana. "Karibu kijana wangu, na pole kutokana na Hii sintofahamu ambayo unae ndelea kupambana nayo." Aliongea mzee yule wa kizungu kwa kiswahili kizuri sana huku akimpa masimba kikombe cha chai. "Nashukuru Mr Raymond Peterson. " alijibu Masimba kwa Kifupi kisha akapiga Fundo la chai kisha kutulia. Hata mzee Raymond Naye Alikuwa ametulia akimtizama Kijana huyu Jinsi alivyochakaa. "Kijana Mambo yalipofikia ni pagumu. Unatakiwa utumie Ujuzi wako wote usiingie mikononi mwa Mamlaka za Juu. Kuna fununu nimeipata kutoka kwa vijana wangu kuwa kuna uwezekano wa wewe kubebeshwa Tuhuma kwa Kifo Cha Mr Chomboko. Na hapa tunapoongea Tayari Mkurugenzi Amepelekwa kusikojulikana. Na hivi Punde Teddy Atawasili Ikulu kupeleka kile ambacho kitakufanya wewe uwe maiti." Alitoa maelezo mzee yule huku akimuangalia Masimba machoni. Macho yake hayakuonyesha kudanganya, macho yake yalikuwa yakikimaanisha kile ambacho alikuwa akikisema. Chief alikuwa amefichwa mahali fulani huku Teddy akibakisha dakika chache kuwasili ikulu ilikuuwasilisha mzigo kwa Rais. "Sitakubali hili litokee kamwe, nimeshapoteza roho za ndugu zangu. Siwezi kuruhusu kilichotoka kwenye bahasha kimfikie Rais. Nipo tayari kufa. " aliongea masimba huku akitembea ndani ya Sebule hii. Mzee Raymond akamuangalia kijana huyu kwa muda mrefu sana. Akajikuta akiukumbuka mkasa uliomfanya atoroke katika jiji la milan nchin Italy na kuja kuishi Tanzania kama Msimamizi wa masuala ya Kanisa Katoliki Katika Africa ya Mashariki. Alikumbuka kipindi kile akiwa muumini wa kundi la kiharifu Lililoitingisha Italy Katika miaka ya themanini mpaka Tisini. Kundi ambalo lilifahamika kama Mafia. Aliikumbuka Asubuhi moja akiwa katikati ya jiji la milan kwa shughuli za kila siku za kundi hilo la kinyang'anyi. Akiwa katikati ya jiji hilo ndipo hapo ilipotoka oda ya yeye kutakiwa kumuua waziri mkuu wa Nchi hiyo.. Simone Masimiliano Kutoka na Waziri huyo kutenda matendo ambayo yalikuwa kinyume Na maelekezo ya Kanisa Katoliki. Ni tukio hilo lililosababisha yeye kutoroshwa katika usiku huo huo mpaka Jijini Washington Dc kabla hajapanda ndege ya Kumleta katika Nchi Hii aliyopo leo. Muda wote aliheshimiwa na viongozi wa nchi kutoka na busura na ushawishi alionao kwa Wananchi.
"Hutakiwi kuwa na Haraka Masimba. Ukifanya Haraka Hutaweza kulitenda Hili. Hili suala limeshafika sehemu ambayo utulivu unahitajika. Vijana wangu bado wanaangalia uwezekano wa kumzuia Teddy akiwa Hai. Na kama itashindikana Kumkamata Akiwa Hai basi wamlipue Ili asipeleke madhara katika Taifa hili. Kitu kilichomo kwenye ile bahasha ni hatari kwa maisha ya masikini wote. Wenye pesa ndio watakao weza kupona. Ama wale wasio na tamaaa ya kutumia vitu hivyo ndio watapona. La sivyo kila siku tutawachukua kwenda kuwatibu Watu ambao tunawaharibu Wenyewe kwa kutengeneza sumu." Yalikuwa maelezo yalimpa masimba mwanga. Mwanga ambao ulimfanya aanze kuhisi kile ambacho alikihisi hapo mwanzo. Lakini kitu hiki no kitu gani mpaka rais aubadili msimamo wake?
[06-10, 16:52] Ibrahim Masimba: Hiki ni kitu gani ambacho Hakitakiwi kufika kwa Rais? Hapo akageuka kwa mara nyingine kutizama aliposimama mzee Peterson. Akamtizama Kwa macho yake mawili, macho yaliokuwa yakiongea kitu. Kitu ambacho hata mzee Raymond alitanbua umuhimu wake. Ndio maana akaamua kuwatumia Vijana wake katika kulifuatilia hilo suala. "Mr Raymond ningependa kujua alipo Chifu, pia nataka kujua hiki ambacho kilikuwa ndani ya bahasha ile. Kina husiana nini na Biashara hii Ya Madawa ya Kulevya na ni kwa vipi Kiongozi wa Nchi analikingia kifua hili suala? Aliuliza Masimba Huku akiendelea kumuangalia Mzee yule. Mzee Raymond naye akamuangalia kwa muda kisha kwa sauti yake ya upole akamuuliza. "Ina maana unapambana Bila kujua kinachokuweka kwenye Hatari? Akauliza.
"Wakati napambana nilidhani napambana na wauza madawa ya kulevya. Na wakati napigana nilijua napambana kwa kutetea Taifa langu." Akajibu Masimba.
"Unadhani inawezekana Waziri mkuu kutenda kitu bila Rais kujua?" Akauliza tena mzee Raymond. "Unataka kujaribu kusema nini hapa? Ina maana Rais alikuwa akiigiza katika maagizo yske huku akujua yeye ni mmoja wao? Akauliza Masimba huku sasa akimuangalia Vizuri mzee Raymond. "Unadhani nani ambaye alikuwa akiwaua watu fulani katika pitapita zenu? Unadhani nani alikuwa akiwafumba midomo yao? Akauliza Mzee Raymond. Ukimya wa muda ukapita kisha akaendelea. "Sikiliza Masimba, kila kilichokuwa kikifanyika yalikuwa ni maigizo. Rais wenu alikuwa analijua hili. Hata kifo cha waziri mkuu kilipotokea Ulitakiwa wewe uuawe. Na Mtu wa kukuua alipangwa awe Teddy kwa kuwa Teddy alikuwa mmoja kati ya Watiifu wanaomtii mkuu. Kuacha kukuua haikuwa Amri yake, bali aliambiwa akuache ili Waupate mzigo wao wa Bilioni mia mbili ishirini na mbili ambao uliuchukua Nyumbani kwa Jimmy. Kwa Taarifa yako Teddy licha ya kuwa Jasusi wa Idara pia Ni Special Agent wa CIA Ambao wapo Nyuma ya Hiki kitu. Kitu kinachokuweka Hatarini ni betri maalum ya kuundia kemikali fulani zenye sumu ambazo huchanganywa katika madawa na kusababisha madawa kuwa na bei na gharama kubwa. CIA, NSA NA HATA FB ndio wanaosapoti hili. Kwahiyo Hatari ya kukupoteza Ipo. Ndio maana niliamua kumtuma Veronica Awe kama Ngao yako. Yule Sio mmoja kati yao, Yule yupo upande wako. Anakulinda kwa kila hatua. Hata pale posta ulipojibadilisha Ulijulikana. Na ile ajali iliyotokea pale Ilikuwa ni kukulinda na kukuokoa. Bastola ilikuwa Tayari kukumaliza kutoka kwa mtu ambaye aliyekuwa mle ndani ya Daladala. Vero ndiye aliyeifanya kazi ile. Kama sio vero ungeshageuka Maiti."
"Kama Sio Veronica ningeshakuwa maiti? Veronica huyu aliyemteka Teddy Nje tu ya kibanda hiki? Mbona kama naona unaongekea kitu kigumu sana Mzee?.. Akauliza Masimba haku akionyesha kutokukubaliana na Maneno ya Mzee Raymond. Veronica amuokoe yeye? Teddy awe pandikizi la CIA? Imekuwaje Veronica akapewa jukumu la kumlinda yeye wakati huo huo inasemekana yupo na Teddy mahala fulani? Bado hakutaka kuamini na hata akili yake haikutaka kuamini kile ambacho alitaka kuamini. Bado alijiona katika kizungumkuti katika Suala hilo. Ni katika kuwaza hilo akawakumbuka wanawe. Akamkumbuka Yaser na France. Mara ya mwisho alikumbuka kutoa maagizo kwa watoto wake kuondokewa sehemu ambayo walihafadhiwa hapo mwanzo. Lakini Muda huu alikuwa akipata taarifa kuwa Chief Amepelekwa mafichoni. Je wako wapi watoto wake? Swali hilo likamfanya ainue macho kumtizama mzee Raymond tena. Alihitaji kujua kila kitu ambacho hakuwa akikijua. "Mzee naomba kujua kila kitu ambacho sikuwa na kijua kuhusu ofisi hii kujua haya yote. Pia wanangu walihifadhiwa eneo fulani na hata mara ya mwisho kuwasiliana na Chifu nilimwambia kuhusu hilo. Nitahiraji kujua pale walipo kwa sasa." Aliongea Masimba akimuangalia mzee huyu. "Mr Masimba najua wewe ni mpelelezi wa kiwango cha juu sana kuwahi kumuona. Lakini kiwango chako kinashushwa na mapenzi uliyonayo kwa mwanamke huyu. Mwanamke huyu ndiye amekushusha kutoka pale ulipokuwa kipindi kile ulipokuwa Russia na Hata Syria. Ofisi ilikusifu sana pale ulipoanza kuhisi ushirika wa Teddy katika masuala haya ya usaliti. Mara nyingi ulikuwa ukiapa kumuua lakini hukufanya hivyo. Na hata pale bastola yake ilipomuua mama yako na Baadae kumuua Dee Plus wewe ulijua muuaji alikuwa Mwamvita. Lakini kiuhalisia Aliyemuua Mama yako Alikuwa ni Teddy. Pale alipowashambulia wanao na mama kutaka kwenda kumvaa , ndipo hapo alipofyatua risasi ambazo zilimmaliza mama yako. Ukitaka kugundua hilo kumbuka umbali ambao alikuwepo nwamvita na ugumu wake katika kuifyatua risasi. Teddy ndiye aliyefanya hayo. Hata kifo cha Dee plus yeye ndiye aliyemuua ingawa baadae alikuja kwenu kukuomba msamaha lakini ilikuwa Geresha tu. Nia kubwa na Amri ambayo ilitoka Makao makuu ya CIA ni kuuliwa kwako wewe. Na hilo lilitakiwa kutekelezwa na Jimmy ambaye ni Mmoja wa kati ya Majasusi wa NSA (national security Agency). Lakini Jimmy akawa anasita kutoka na Amri ya Kiongozi wa Nchi kuwa kukuua wewe mapema kutatibua Hali ya usalama nchini. Hivyo wakawa wanakuacha ili uendelee kumuamini Teddy na Mwisho wa Siku Wakuue. Ushiriki wa Waziri Mkuu na Kiongozi wa Nchi katika suala hili ulianza pale Nchi Yenu ilipotaka kuingia mkataba na Nchi Ya Urusi. Rais alikataa kutokana na kuwajua warusi walivyo katika masuala ya Kiusalama. Na baada ya Marekani kuligundua hilo ndio wao wakaingia kwa gia ya msaada na kuisaidia Tanzania Kijeshi, ki uchumi na Hata Katika Masuala mengine.
Kuhusu Ofisi hii kuyajua hayo, kumbuka Ofisi Hii inafanya kazi kwa karibu na Viongozi wakuu wa Ulinzi na Usalama. Mtu wa kwanza kuniomba Msaada wa kutafuta mtu wa kukulinda alikuwa ni Meja Jenerali chomboko. Yeye ndiye wa kwanza kunieleza hili suala katika usiri mkubwa tulipokuta Geneva Uswis Katika mkutano wa Kiroho baada ya Papa Francis Kudhuru katika Nchi hiyo. Hapo ndipo Meja jenerali aliponieleza hili na kuniambia upo katika Hatari ya kuuawa kwa Amri ya Cia na Kiongozi wa nchi. Ni hapo nilipomtafuta Veronica ambaye kipindi Hicho alikuwa ni Mwanakikundi wa Kundi letu la Mafia." Yapo mengi sana lakini kwa Uchache ni Hayo. Kifo cha Jenerali Chomboko Unataka kupewa wewe ili iwe rahisi kukupoteza. Kitendo cha wewe kutoka Ikulu na Kukutana na Jimmy nyuma ya Benki Kuu ya Tanzania, ilikuwa ni Mmoja ya Mkakati wa kukuua baada ya kuamua kuachana na Kazi yako. Hivyo tambua unawindwa, Tambua huna kinga tena ya kukuzuia wewe kuuawa. Itabidi ujilinde na uitumie bastola na Usiruhusu alichonacho Teddy Kifike kule anapotaka kukifikisha."alimaliza kuongea Mzee raymond Huku akimuacha masimba katika kizingiti Chenye giza. Giza totoro ambalo halikuutoa hata theruthi ya Mwanga. Teddy ndiye aliyemuua mama yake, Teddy ndiye aliyemuua Dee plus. Kumbukumbu yake ikarudi nyuma tena. Siku ya kuuawa kwa mama yake. Watoto wake walipotaka kwenda kumkumbatia Teddy huku wakimuita Mama Yao. Shambulio lake kwao na kukurupuka kwa Mama yake. Kufika hapo akafumba macho, ni kweli Risasi Haikutoka kwenye Bastola ya Mwamvita. Teddy Ndiye aliyeifyatua risasi kweli. Kuligundua hilo kulimfanya Masimba Asimame akitweta. "NITAKUPATA TU TEDDY NA NITAKUUA." Aliongea huku akiruhusu machozi kutoka. Mambo mengi aliyoelezwa na Mzee huyu vilimuonyesha ni Jinsi gani Marais wa nchi za Kiafrika wanavyokuwa vibaraka wa nchi za magharibi. Rais kusaini mikataba ya kinyonyaji na hata kukubali wananchi wake kudhurika ni kitu ambacho hakikubariki. "Naingia kazini Rasmi, naingia katika vita hii nikiwa sio masimba wa Idara ya Usalama wa Taifa. Bali masimba mzalendo na mpenda nchi yake. Najua naweza kupoteza Maisha yangu lakini lazima nilifanye hili katika Usiku Huu. Lazima nilizuie hili. Najua watoto wangu wako hapa lakini Waambie nitarudi nikiwa Hai na kama nitakufa, waambie nimekufa kwa Ajili ya Damu ya bibi yao na pili Taifa langu la Tanzania." Baada ya kuongea hayo Masimba akatoweka pale ndani akimuacha mzee Raymond Akitingisha kichwa. Alitingisha kichwa kwa kumuonea huruma na alitingisha kichwa kwa kuwa alitamani kumrudisha Masimba katika utimamu wake. Lakini ni wakati huo akiliwaza hilo akamuona Masimba Akirudi tena hapo ndani. "Nipe uelekeo wapi alipo Veronica kwa sasa. Hii ni kazi yangu nitaibeba mwenyewe."aliongea masimba macho yake yakionyesha kuzamilia alichookiongea. "Wapo maeneo ya Msasani karibu na Ubalozi wa Marekani. Taarifa nilioipata muda huu ni kwamba kuna vijana wa usalama wameuawa walipokuwa wanajaribu kumfuatilia Teddy. Lakini bado hajapotea kwenye macho ya Veronica. Ingawa Teddy hayupo peke yake.". Akajibu Mr Raymond. Masimba akatoweka Tena.
******
"Haiwezekani kuna mtu atakuwa amelivujisha hili. Nina uhakika Masimba hakuwa amemuona Isabella Ndani ya Daladala. Ile ajali inaonyesha kuna watu wanatembea na sisi." Alifoka Teddy akiwa pembeni ya kiti ndani ya gani aina ya Toyota Rav 4. "Hata mimi nimeweza kuhisi hilo. Kwani wakati tunamfuatilia hatukumuona mtu yoyote. Sasa Najiuliza Nani ambaye ameitengeneza Ajali ile iliyomuua Isabella?"" Akajibu dada mmoja ambaye alikuwa mmoja kati ya wale watatu ambao walikuwepo pale alipokuwa Masimba Akichagua viatu. "Basi nishapata majibu, kuna watu wanatufuatilia. Jaribu kumpigia simu Jimmy mueleze Hili. Pia mwambie anaowatuma wawe ni watu wanaomjua Masimba. Nahisi yupo nyuma ya Suala hili na pia nahisi ile ajali imemshtua." Aliongea Teddy safari hii akiwa makini kuangalia kupitia kioo cha pembeni. Roho yake ilikuwa imeshageuka huku mapenzi juu ya Masimba ya kiyeyuka mithiri ya barafu juani. Alikuwa akiiangalia pesa kana kwamba hakuwahi kuishika. Muda wote alikuwa akiitizama betri ndogo ambayo alikuwa nayo katika sehemu fulani ya siri. Muda wote alikuwa akiwasubiri Wenzake kwa Ajili ya kuianza safari kuelekea Ikulu. Safari ambayo ilikuwa ni ya mwisho kwake kuwepo hapa nchini. Alitaka kupotea na kutoonekana tena. Ili kutotaka kufuatiliwa alikuwa ametamani kumuua masimba kisha watoto harafu yeye kupotea. Alijua mpaka muda ule masimba alikuwa Ameshajua Huyu ni Mtu wa aina gani. Ni wakati akiliwaza hilo akamuona mtu mmoja akitembea pembezoni mwa barabara. Kwa kumuangalia mtu huyu angemfananisha kabisa na Lundo la Vijana Walioharibika kutokana na Matumizi ya madawa ya kulevya. Lakini huyu hakuwa mmoja kati yao, alimtambua na kumjua kuwa alikuwa kijana wao. Alikuwa mmoja ya makachero wa siri waliojipenyeza na kuishi maisha ya pamoja na Raia wa Tanzania. Alikijua Kiswahili na alikizungumza kuliko hata Mtanzania mwenyewe. Kijana yule aliyekuja na kidumu kidogo cha Maji sambamba na kitambaa mkononi. Alitembea mpaka pembezoni mwa kioo Cha Gari. Akainama kama anafuta vioo vya gari ile. Baada ya muda Teddy akaonekana kutoa pesa na kumpa kijana yule kisha kuondoka. Baada ya kijana yule kuondoka gari ikachepuka kushoto na kushika barabara Kuelekea msasani huku akiamini kuwa walikuwa salama.
*******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuondoka pale nyuma ya kanisa kwa Mr Raymond. Masimba aliamua kuingia kazini akiamini kuwa Teddy alikuwa ni Adui namba moja kwake. Alitambua hili baada ya kufumbuliwa juu ya aliemuua mama yake na hata ndugu yake kipenzi dee plus. Alitaka kumuua Teddy kwanza kabla ya kwenda kwenye mamlaka za Juu. Safari yake Ya kwanza iliishia mpaka kinondoni Manyanya katika nyumba ambayo alikuwa akiishi. Aliingia kwa Usiri mkubwa mpaka ndani ya Nyumba. Akaongoza mpaka sehemu fulani alipokuwa akihifadhi Vitu vyake kwa Siri. Baada ya Kuingia Hapo macho yake yalitua ukutani kwenye hazina yake ya Silaha. Macho yake yakatua Juu ya bastola mbili Ruger Sr na Armalite Ar 24. Akazichukua na kuziweka Sehemu husika. Akachukua na magazine kadhaa za Risasi pia akaweka sehemu Husika. Baada ya kumaliza hilo akaamua kutoka hapo kuelekea msasani. Muda wote huo bado hakuwa amefanya mawasiliano na Veronica. Aliondoka hapo kwa kupita njia zake za kificho. Dakika sita baadae alikuwa maeneo ya Namanga. Muda wote macho yake yalikuwa yakitembea nje kuangalia kama angeweza kumuona mtu yoyote. Aliiendesha gari taratibu akihakikisha hapitwi na kitu chochote kile. Wakati akikipita kituo Cha Mbuyuni, akaliona gari limesimamishwa pembeni mwa barabara. Mwanamke na mwanaume walikuwa wameliegemea gari wakifanya uasherati wao. Mara ya kwanza alipoliona alitaka kupuuza. Lakini alipotizama ukaaji na vitendo vya watu wale, akaiona Namna, namna ambayo ilimwambia wale walikuwa watu wake. Watu ambao wako upande fulani ama upande wake yeye. Wakati analifikiria Hilo akayaona magari mawili mengone yakipita kwa kasi. Magari hayo yakafuatiwa na gari nyingine ambayo hii haikuwa katika mwendo wa kasi. Masimba akaisimamisha gari aliyokuwa akiendesha kisha akainama kuchungulia kwenye matairi lengo likiwa ni kuangalia kile kinachoendelea pale. Bado watu wale wawili walikuwa pale wakidendeka pasipokuwepo kwa wasiwasi. Haikupita muda akawaona watu wale wakiingia kwenye gari yao na muda ule ule gari ikaondoshwa kuelekea mahala ambapo ni tofauti na kule zilikoelekea zile gari tatu. Masimba bado alikuwa ametulia. Alihisi kuwepo kwa mchezo wa hatari
Akauhisi Mchezo, mchezo wa Hatari ambao unachezwa hapo. Ni wakati akilifikiria hilo likatokea Jingine. Likatokea hili ambalo hakulitegemea. Gari aliyokuja kwa mwendo wa kasi akidhani ni ya watu baki, haikuwa Hivyo, haikuwa hivyo kwa kuwa muda ule ule vioo vya magari yale vilishushwa kisha risasi zikaanza kuvulumishwa kuelekea pale pale alipokuwa amesimama Masimba. Hakuwa mzito katika kuling'amua hilo. Muda mfupi baadae masimba alikuwa angani akizikwepa Risasi. Alikuwa katika namna ambayo ilikuwa ikitia burudani Hata kwa watu wenyewe waliokuwa wakimshambulia Masimba. Alikuwa akiruka Hapa na kuruka pale. Alikuwa akiingia hapa na kutokea pale katika Ustadi wa kipekee. Katika ustadi ambao uliyonyesha kwamba hakuwa mtu wa utani. Alipokuja kutua alijikuta akiwa nyuma ya kichaka kilichopo pembezoni mwa Barabarani. Bastola ilikuwa mkononi tayari kwa kufanya kile kilichombele yake. Lakini Eneo lote lilikuwa kimya kanakwamba hapakuwa pametokea kitu chochote katika eneo hilo. Bado alikuwa ametulia akitizama. Taratibu akaanza kuburuzika kwa tumbo akiondoka hapo akielekea Sehemu Nyingine. Alitembea kwa tumbo mpaka alipofikia sehemu ambayo kulikuwa na Ukuta kwa Upande mmoja. Kufikia hapo akatulia Tena safari hii akiamua kutizama kule alipotoka. Ukimya. Ukimya ndio kitu ambacho kilitawala katika Eneo lote. Eneo ambalo muda mfupi Uliopita lilikuwa katika sekeseke la milindimo ya Risasi. Hilo halikumpa Masimba tumaini la kuinuka. Alichokifanya ni kuendelea kutizama alipotoka. Macho yake yalikuwa yakihitaji kulifanya giza, ligeuke kuwa mchana wa mwanga. Ni wakati huo alipouona umeme Ukizimwa maeneo yote na Kulifanya giza kutamalaki. Masimba akajua kinachotaka kufanywa. Sekunde hii alikuwa yupo chini akitizama Alipotoka, lakini sekunde aliyofuata Alikuwa ameparamia ukuta na kuangukia Upande wa Pili. Bado hapa kuonesha kuwepo kwa watu, bado giza lilitawala kila upande kuonyesha kuwa hapakuwepo na uwezekano wa kukosekana kwa wakora. Hazikupita Dakika mbili tokea kuzimwa kwa umeme, milio ya Risasi Ikatawala. Milio ambayo ilimuacha Masimba katika sintofahamu ya nini na nani wanapambana. Suala kuwa Veronica Alikuwa Yeye Halikuwa katika kichwa Chake, hakuliwaza kwa kuwa alijua Vero Asingeweza kukubali kumuacha Teddy. Sasa Huyu ni nani? Hilo ndilo ambalo aliliwaza. Bado milio ilikuwa Ikisikika kwa Ukaribu. Masimba akauona kuwa ulikuwa muda wa kusaidia mapambano. Swali lililokisumbua kichwa chake Je ni nani ambao walikuwa wakipambana. Je hata kama atapambana, je atajua wanaomsaidia wako upande Gani? Kuwaza huko kukamfanya Atulie. "Masimba sogea huku, ilikuwa ni sauti iliyomuita katikati ya milindimo ya Risasi. Tena hii ilikuwa sauti ya kike. Sauti ya mtu aliyemfahamu. Hii ilikuwa sauti Ya Veronica. Sauti ambayo ilimzindua na kujua kule anapotakiwa kukifanya. Hakuelekea upande ulipotokea sauti ya Vero, bali alielekea upande Tofauti. Upande ambao ulikuwa Tofauti. Akainuka na kuanza kutembea Taratibu kabisa. Akafanikiwa kukifikiwa kiwambaza cha nyumba ambayo ilikuwa mwishoni kabisa mwa Ukuta ule. Kufikia hapo Masikio yake yakanasa mchakato, mchakato wa miguu ya watu zaidi ya mmoja. Akatega Masikio yake zaidi ya Zaidi. Bado michakato ya miguu akaisikia ikizidi kusogea. Akauinua mkono wake wenye Bastola tayari kwa kuachia Risasi. Alikuwa makini kwa kuwa alijua anapambana na Oda kutoka mamlaka za Juu. Alitakiwa kuwa makini zaidi na Zaidi. Wakati akiwa hapo akawaona watu wawili wenye sub machine Gun Mikononi wakitokea kwa mbele yake. Inavyoonekana watu wale hawakuwa wamemuona Masimba. Masimba akawasubiri wasogee kwa kuwa hakutaka kuitumia Bunduki Kuua Watu wale, alitaka kuitumia mikono yake pekee. Akawasubiri waendelee kusogea. Hatua mbili kabla ya kumfikia Masimba akajitokeza mbele yao. Kwa kuwa hawakuwa wamejiandaa na kitu hicho, watu wale wakashikwa na Mfadhaiko ambao uliwapotezea sekunde kadhaa za kushangaa. Ni muda huo ambao aliutumia masimba kuwapa mapigo yaliyowaacha watu hawa wakianguka chini. Hakusubiri wainuke, hajusubiri wafanye chochote. Mlio mdogo mfano wa chafya ya binadamu kutoka kwenye bastola yake ilitosha kuruhusu Risasi zilizowapata watu wale na kuwaulia mbali.
Baada ya kuhakikisha watu wale wamekufa, hakutaka kuchelewa. Aliondoka hapo kwa kuuparamia ukuta kisha kuangukia Nje Tena. Baada ya kutua chini akatembea taratibu huku akikutana na miili ya Askari ikiwa chini ikivuja Damu. Akatambua hii ilikuwa kazi ya Veronica. Ilikuwa kazi ambayo ilionyesha ujuzi na Utaalam wa Veronica. Ilimuonyesha ni kiasi gani Veronica alikuwa Hatari. Akatembea na kutokea barabarani. Alipotokea tu barabarani, gari moja ikaja kusimama mbele yake. Kabla hajakaa sawa mlango ukafunguliwa na Kutakiwa kuingia ndani ya gari. Masimba akasita kwanza, lakini Baada ya kumuona Veronica Yupo ndani ya Gari, naye akaingia. "Teddy Yuko wapi? Lilikuwa swali la kwanza baada ya Masimba kutulia. "Amepewa hifadhi Kwenye Ubalozi wa Marekani. Nadhani kuna mpango unataka kufanyika kumuwezesha kumfikisha Ikulu." Akajibu Veronica Huku Akimuangalia Masimba. "Mbona uko hapa, nani atamuona atakapotolewa. Ukizingatia kuna Handaki limechimbwa Chini kwa Chini Mpaka Baharini?" Akauliza Masimba akionyesha Umakini wa Hali ya Juu. Kila kitu kipo kwenye utaratibu. Hataweza kuondoka hapo pasipo sisi kujua." Akajibu Veronica Akionyesha kutokuwa na wasiwasi kabisa. Lilikuwa jibu ambalo lilimfanya Masimba ageuke na kumtizama Veronica. Macho yake yenye maswali yalikuwa yakimuangalia mwanamke huyu katika aina fulani ambayo hata Veronica mwenyewe Aliitambua. "Unamjua Teddy Vizuri? Unakijua kile kichwa? Nipe majibu ya kuniridhisha. Usiongee Juu juu Veronica." Alisema huku akiendelea kumuangalia. Vero hakujibu bali alichomoa kidude fulani ambacho kilikuwa na ukubwa kama wa Simu. Akakiwasha na kumpa Masimba akiangalie Kwa Umakini. Macho ya masimba yalikuwa yakiliangalia jengo la Ubalozi Wa Marekani kupitia Kile kitu mfano wa Simu. Alikuwa akiangalia pande zote mpaka ndani ya Ubalozi. Kilikuwa kitu kilichomfanya Masimba amtizame Tena Veronica. Moyoni kwake alikubali kwamba ni kweli mtu huyu alikuwa ni Hatari. "Aiseee!! Nimeamini hiki unachokitenda. Hakika Ulijiandaa vya kutosha kutokana na Hali hii." Aliongea Masimba akikirudisha kile kidude mikononi kwa Veronica. "Una mpanga gani kwa Muda huu ambao tunamtega mtu wetu? Akauliza Veronica akimuuliza Masimba. "Usiku huu nataka niutumie kujua pale alipo Mkurugenzi Wa Idara ya Ujasusi. Nikitoka hapo nataka nikamalizane na Jimmy Lambert kabla ya kummaliza huyu Teddy." Akajibu huku akitizama kwa nje. "Unaijua Sehemu iitwayo Buzuruga ndani ya Jiji la Mwanza? Akauliza Veronica. "Napafahamu sana, nilishafika mara nyingi kila nilipokuwa na kwenda kuwahifadhi watu hapo." Akajibu Masimba. "Basi Chief inasemekana Yupo huko, na Ameshushwa Jioni Hii Kwa Usafiri wa Helkopta." Akajibu Veronica. Wakati akiongea na Masimba, kile kitu mfano wa Simu kikatoa Mlio. Veronica akakitoa haraka kisha kukiwasha. Macho yao yakawaona watu zaidi ya Sita wakiingia Mle ndani. Muonekano wa watu wale haukufichika machoni kwao. Walikuwa wana Usalama tena Wale Walinzi Binafsi Wa Rais. "Kazi imeanza, naona Rais ametuma Walinzi binafsi kwenda kumchukua Teddy." Akasema veronica Huku akimuonyesha masimba. "Tunatakiwa kufanya Jambo. Walinzi hawa ni wale wenye nafunzo ya Hali ya Juu. Na hawawezi kwenda sehemu bila uwepo wa Rais mwenyewe. Ninachoamini Rais yupo hapo na atakuwa katika Mazungumzo na Teddy. Hembu tusogee kuelekea maeneo hayo." Aliongea Masimba huku akiwaaangalia Vizuri Walinzi wale.
*******
Ulikuwa Ujio wa Siri kufanywa na Rais wa Nchi katika Ubalozi wa marekani. Ziara hiyo siri ilifanyika pasipo kujulikana popote. Na pia imefanywa baada ya mazungumzo ya Rais Wa marekani na Rais Wa nchi hii. Mkakati uliokuwepo ilikuwa ni lazima Biashara iendelee ili waendelee kupata pesa bila kujali Athari ambazo zilikuwa zinawapata Wananchi. Msaada wa mamilioni ya shilingi anayopewa sambamba na mikopo ilisababisha kiongozi wa nchi akubali kila mpango unapangwa na serikali ya marekani. Ni usiku huo baada ya mazungumzo na Rais Wa Marekani. Ndipo Rais alipoamua kuifanya Ziara ya Kuja hapo ubalozini kwa kutumia Njia maalum ambayo ilipita chini ya Ardhi nia ni kuja kuonana na Teddy. Sio rais wala wasaidizi wake waliotambua kuwa teddy alikuwa ni wakala maalum wa CIA. Hakuna aliyejua kuwa Teddy alikuwa ni special Agent wa CIA. Walimchukulia Teddy kama mwenzao. Walichukulia kile anachokifanya kinatokana na kile ambacho ameahidi Rais. Hawakujua katika pesa ambayo rais ameahidi itarudi katika mikono ya Serikali ya Marekani. Ulinzi ulitisha kila upande. Chumba alichokuwa amewekwa Teddy kilikuwa kikilindwa na mitambo maalum ambayo ilikuwa na uwezo wa kutokuruhusu Makombora ya Aina yoyote kuingia na hata kulipua. Rais alitembea akiongozwa na Makomandoo maalum ambao ndio waliokuwa Walinzi Binafsi wa Ubalozi. Sambamba na walinzi Binafsi wa Rais. Kila mmoja alikuwa ni mwenye Tabasamu. Kila mmoja sura yake ilikuwa ikionyesha furaha. Mavazi ambayo alivaa Rais Kwa siku Hiyo yaliupoteza muonekano wake. Hakuweza kugundulika kuwa ni yeye. Hata ule mtambo maalum Haukuweza Kumtambua Rais, ingawa Masimba alijua kuwa kuwepo kwa kikosi kile hata Rais hakuwa Mbali. Ilikuwa ni lazima wa hakikishe kwa njia yoyote ile Wanazuia Kitu hicho kutua mikononi mwa kiongozi. Ilikuwa ni lazima wauvamie Ubalozi wa Marekani na Kuufanya mashambulizi. Lakini swali lilikuwa Je Watafanikiwa? Hilo likabaki kuwa swali lililomtoa Masimba ndani ya gari. Alihitaji kufika Ndani Ya Ofisi Za Ubalozi na alihitaji kumzuia Teddy na pia alihitaji kuipata betri maalum yenye kuzalisha kemikali ambazo hutengenezwa kwa kuongezwa kwenye Madawa na kuyafanya madawa kuwa na Thamani kubwa. Ilikuwa ni lazima azuie hilo katika Aina yoyote na kwa Njia Yoyote. Hata kama alikuwa ni kufa yeye Hakujali hilo.
Ilikuwa ni lazima waingie ndani ya Jengo la ubalozi wa Marekani. Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo ili kumzuia Teddy. Ilikuwa ni kazi ngumu sana kuingia katika Jengo hilo. Jengo lenye mitambo mbalimbali ya kuzuia watu na hata mabomu kupenya. Hilo likawa zito kulitenda, licha ya kuonekana kuwa zito, lakini ilikuwa ni lazima kuwakabili watu wote na kuzuia kilichokuwa kikitaka kutendeka. Ilikuwa ni lazima watende kwa sababu ya wananchi wa Tanzania. Ilikuwa ni Lazima walitende kwa sababu ya kuwaokoa Vijana wengi. Wakaivuka barabara wakiwa sambamba na Veronica. Walikuwa wakielekea kule kule kwenye Jengo. Akili na mawazo ya kila mmoja yalikuwa kule. Bastola zilikuwa zimekaa mahali salama tayari kwa kazi. Wakaipita salama Barabara na kuufikia upande wa pili. Walitembea kana kwamba hawakuwa wakienda sehemu hiyo kwa pamoja. Masimba alikuwa mbele huku veronica akisogea kwa nyuma. Alikuwa akimlinda Masimba. Alikuwa akimwangalia Masimba, kila hatua aliyokuwa Akipiga Masimba alihakikisha hata yeye jicho lake lilitua hapo. Ilikuwa kazi ngumu na ya hatari. Walikuwa Tayari kuua hata wao kufa. Nia ilikuwa ni kuizuia Betri maalum isiingie mikononi mwa Kiongozi wa Nchi. Ilikuwa nilazima Wamzuie Teddy. Baada ya kitembea Chini kwa chini wakatokea sehemu yenye Kichaka. Hapo Masimba akasimama akimsubiri Vero. Hata vero alipofika Masimba Alimvuta Pembeni kisha kuanza kumwambia kile walichopaswa kufanywa. "Veronica hii ni nafasi ya mwisho ambayo inaweza kuamua Uhai wa Maisha Yetu. Hii ni nafasi ya kuutangaza Ushujaa wa Nchi yetu. Lakini vile vile inaweza kuwa ni nafasi ya mwisho kuivuta hewa Hii kama hatutakuwa Makini. Tambua unakwenda kupambana Sababu ya Tanzania. Unaenda kupigana sababu ya wananchi wote waliokata tamaa kutokana na viongozi kusaini mikataba ya kinyonyaji. Tunakwenda kupigana kuzuia kuendelea kuharibika kwa vijana kutoka na Biashara Inayoendelea. Na Mwisho nakwenda kupambana kwa sababu ya Roho ya Asteria, familia Yake, Dee plus, vicky, Mzee Chomboko na Mwisho ni Roho Ya Mama Yangu Mzazi. Twende tukaikomboe nchi kutoka mikononi mwa wachache." Aliongea Masimba Huku wakikumbatiana na Veronica. Muda mfupi walikuwa njiani wakielekea katika uwanja wa Vita. Damu zilikuwa zimechemka. Aliujua Ugumu ambao wangekutana nao. Alitambua ugumu walionao katika kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.
Masimba na Veronica walitembea kwa uangalizi mkubwa. Muda wote bastola zilikuwa mkononi kumlenga mtu yoyote. Wakafanikiwa kuukaribia ubalozi huo ambao muda huo bado Palikuwa peupe kutokana na Taa zilizokuwa zikiwaka. Taa hizo zilisababisha ugumu wa Masimba na Veronica kupita hapo. Wakiwa wametulia wakiangalia Jinsi ya kuingia. Wakashtushwa baada ya umeme kuzimwa karibia eneo lote la Jiji la Dar es salaam. Jiji lote lilikuwa Giza katika namna ambayo hawakuitegemea. Hawakutegemea kwa kuwa waliuhisi kama ni mtego. Mtego wa kuwatega wao. Kwa nini umeme uzimwe wakati wao wakiwa kwenye eneo la tukio? Kwa nini usizimwe kabla ya hapo. Wote wakatulia kwa sekunde kadhaa wakiliangalia hilo. Ni muda huo Veronica alipomuangalia Masimba kisha kumwambia kitu. Kitu ambacho kilitamkwa kwa sauti ndogo ambayo haikuweza kupenya na kufika hata umbali wa hatua mbili. Lilikuwa neno ambalo likiwafanya kila mmoja ainuke na kuitafuta Njia. Jengo la ubalozi wa marekani lilijengwa katika uthabiti wa hali ya Juu.. Huku Mitanbo ya Ulinzi ikilizunguka eneo lote. Hali hii ilikuja baada ya milipuko ya Mabomu katika Majengo ya Balozi Zao mwaka 1998 hapa Dar es salaam na Nairobi nchini Kenya. Tokea milipuko hiyo serikali ya marekani aliamua kujenga Majengo ya Kisasa ambayo hayakuwa rahisi kuingilika na hata kushambuliwa. Wakati masimba akielekea kaskazini Veronica alikuwa akielekea Magharibi. Kila mmoja akatembea huku akizidi kuwa makini kutokana na hali ya sintofahamu iliyotokea Hapo. Upande Wa Veronica Akafanikiwa kuufikia ukuta uliozungushiwa katika Jengo hilo. Akauangalia Ukuta ule kwa muda mrefu akiangalia namna ya kuingia Humo ndani. Akiwa bado ametulia Huku Giza likimsaidia kutoonekana, akasikia Vishindo vikitokea Nyuma yake. Haukupita Muda Akawaona askari wawili wenye silaha nzito wakisogea sehemu alipokuwa amejificha. Akatulia tuli katika ya giza. Kwa kuwa alikuwa katika mavazi meusi ilikuwa ni vigumu sana watu kumuona kutokana na kuendana kwake na giza. Askari wale wakazidi kusogea wakionyesha kuwa hawakushtuka na wala hawakumuona. Akawasubiri wasogee Zaidi.. safari ikiirudisha Bastola mahala pake. Alihitaji kupambana kwa mikono. Alitaka kupambana katika aina hii ya Ugumu katika Hilo. Akaivuta subira na kuanza kuhesabu hatua ya kwanza, hatua ya pili na hata ya tatu. Hatua ya nne na tano ikamkuta Veronica akiwa hewani kwa mapigo kadhaa. Mapigo ambayo hayakusaidia kwa Askari wale kujitetea. Baada ya kuwaua, Veronica alimvua Askari mmoja mavazi yake, kisha kuyatia Mwilini. Alifanana kabisa na walinzi wa Ubalozi. Akachukua Bunduki ya mlinzi mmoja sasa akiiweka begani. Akaanza kutenbea huku akikumbuka maelezo aliowahi kupewa na Mkuu wake wa Genge la Mafia. Maneno ambayo yaliendelea kuishi moyoni na hata kichwani. Maneno hayo yalimsaidia na kumtoa katika Hatari nyingi sana wakati wa mission katika Nchi ya marekani. "Kila palipo na Ubalozi wowote wa Marekani. Katika nchi yoyote Duniani, kazima kuwe na Ulinzi unaoonekana na Ulinzi Usio onekana. Ulinzi Unaoonekana ni Ule Wa walinzi na mitambo mingine yakiusalama. Na Ule ambao hauonekani ni wa milipuko ambayo hupandikizwa chini ya Ardhi. Kwa hiyo unapotembea katika Sehemu Hiyo ni Lazima Uwe muangalifu na uwe Makini katika kile unachokifanya. Yalikuwa Baadhi ya Maneno kutoka kwa mkuu wake. Akatembea akiyafuatilia maelezo hayo. Bunduki ilikuwa mkononi akitembea mfano wa walinzi wenyewe. Hatua zisizo pungua Kumi mbele akawaona walinzi wengine watatu wenye bunduki na Sare mfano wake.. alichokifanya ni kuchomoa Bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia mli0. (Silence ). Ilikuwa ni lazima aitumie bastola hiyo katika namna ya kuirahisisha kazi yake. Ilikuwa ni ngumu kwa Sehemu Alipokuitumia mikono yake na Hata bunduki yake. Ndicho alichokifanya. Muda Mfupi Baadae Risasi zikatoka na kuelekea zilipotumwa. Hazikuweza kukosea njia katika namna yoyote ile. Kila risasi ilipita na kuingia Sehemu husika. Sehemu ambayo ilitumwa ama kuagizwa kufika hapo. Walinzi watatu walikuwa wakipaa angani katika namna Iliyotia Burudani kutoka kwa mtumaji mwenyewe. Hata Veronica alipofika eneo ambalo waliangukia Askari wale Hakuhangaika katika Kuwaangalia. Aliwapita Safari hii akiiingia ndani Ya Geti. Akiingia kama mlinzi wa Eneo husika. Akapita kana kwamba alikuwa akipita katika mlango wa chooni na hata nyumbani kwake. Hakuwa na mashaka, hakuwa na wasiwasi na hata hofu haikusomeka usoni na Hata machoni Mwake. Aliingia kama sehemu aliyoizoea na hata kuijua.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Veronica akilifanya hilo kwa upande wake. Upande Wa masimba hakuwa amekutana na ugumu huo. Upande wake hapakuwa na Labsha na hata kasheshe. Alipita hapa na pale kama kawaida. Ukuta Mrefu uliozunguka Jengo lile Haukuwa Tatizo kwake. Alijua angeweza kuingia. Mawazo yake yalikuwa ni Kumteka Teddy na kuondoka naye. Hakuhofia kile ambacho kingetokea. Muda mfupi alikuwa akitizamana na geti dogo na La Siri. Ni muda huo akilitizama hilo geti, akaliona geti likifunguliwa, kisha muda ule akawaona watu wakichungulia. Akabana kwenye giza. Punde akawaona makachero wa CIA ambao walikuwa wakihudumu hapo Wakitoka. Kisha wakafuata Walinzi Maalum Wa kiongozi wa Nchi. Mtu aliyefuatia alikuwa Teddy akiwa katikati ya Makomandoo kadhaa wa Marekani na Watanzania. Teddy alikuwa katika Ulinzi mzito kama kiongozi Wa Taifa la Marekani. Walinzi wenye Silaha Nzito walikuwa wakimuongoza na kumkinga. Licha ya kuonekana kwa Walinzi Maalum Wa Rais, lakini kiongozi huyo hakuwepo. Hakuwepo na hakuonekana kabisa hapo. Akili ya masimba ikafanyakazi kwa Haraka. Alijua Teddy alikuwa akiwapeleka Watu hawa Mahala ambapo alikuhifadhi kitu hiki. Wakati akiendelea kukiangalia hiki akamuona mtu mwingine akiwa kwenye mavazi yanayofanana na Walinzi. Naye alikuwa nyuma akifuatia. Mtu huyu wa mwisho kutoka akaufanya uso wake Uchanue kwa Tabasamu. Tabasamu malidhawa.. kwa Mara ya kwanza akaukubali uwezo wa Veronica. Kwa Mara ya kwanza akamuona Veronica kuwa ni Jasusi wa kutupwa. Kile kitendo cha kumuona katika Msafara ule wa majasusi wale wa CIA ni moja ya sifa kubwa Ambayo makachero wengi hawana. Lakini walikuwa wakielekea wapi na Teddy? Lilikuwa swali ambalo alijua angelipata Wapi na saa Ngapi. Akatulia akiendelea kuusoma Mchezo.
Teddy alikuwa kwenye ulinzi wa hali ya juu. Ulinzi ambao uliongozwa na makomandoo sambamba na majasusi wa CIA. Lakini licha ya hilo, kilichomburudisha Zaidi ni Kule kumuona Veronica. Veronica aliyekuwa naye muda mfupi uliopita. Alikuwa katika msafara ule tena akiwa katika sare na mavazi maalum wanayovaa walinzi Wa Jengo hili la ubalozi wa Marekani. Amefikaje ndani na kuwa mmoja kati yao? Ni swali lililomsisimua Masinba, sio kumsisimua kwa woga ama burudani. Bali mwili ulimsisimka kwa utembeaji ule wa Majasusi wale. Walikuwa wakitembea kanakwamba wapo katika Ardhi ya Marekani. Licha ya kuinyonya nchi yenye rasilimali nyingi sana, pia waliimfanya Nchi hii kama shamba la kuchuma mali na kutokomea nazo. Akauvuta Muda naye akitaka kujua kule wanapoelekea. Hata walipompita pale ambapo alikuwa amejificha, bado Masimba alitulia akiwatizama. Alikuwa na Uwezo wa Kumtwanga Teddy Risasi, lakini Hakutaka iwe hivyo. Alitaka kumuonyesha Teddy kuwa anauwezo kuliko hata yeye. Alitaka kumuonyesha kuwa alikuwa akiifuatilia na kuipigania Tanzania. Akaruhusu Teddy na walinzi wake wampite. Akatembea nao kwa nyuma kila pale walipotembea. Alitaka kuwatizama ni wapi walipokuwa wakielekea. Alitaka kujua ni wapi Teddy ameuhifadhi betri ile. Majasusi wakimarekani wakazidi kutembea wakiingia Ndani Zaidi. Bado Veronica alikuwa nyuma na Hata Masimba hakuwa mbali na watu hawa. Tanzania yake ilikuwa katika moyo wake. Hakutaka kujua wapi alipokuwa rais. Alichotaka kufanya ni kukipata kile ambacho kilisababisha Teddy kuwa msaliti. Muda mfupi watu wale wakatokea katika barabara fulani ya vumbi. Hapo walikutana na msululu wa magari yapatayo matano. Yalikiwa magari yasio na namba. Yalionekana kuwa magari mapya. Baada ya Teddy na majasusi wale kuyafikia magari yale, milango ikafunguliwa katika aina fulani ya Uharaka. Teddy akatakiwa kuingia ndani ya Gari. Wakati Huku wakilifanya hilo kwa Teddy, tayari bastola ya Masimba ilikuwa mkononi. Tayari alikuwa tayari kulizuia hilo. Muda mfupi baadae alikuwa ameiruhusu Bastola kutoa Risasi. Risasi ambayo ilikwenda kutua katikati ya kifua kwa jasusi mmoja wa kimarekani. Akapiga yowe kubwa huku akitupwa angani mithiri ya furushi. Ilikuwa risasi iliyopenya katika kifua cha Jasusi yule. Risasi ikamtupa angani huku yowee kubwa likifuatia. Majasusi wengi wa kimarekano wakacharuka. Kila mmoja alikuwa akichupa na kuangukia mahala pengine. Kilikuwa kitendo kilichofanywa katika muda mfupi ambao ulimacha Teddy akiwa amesimama tena akiwa katika mzubao. Kulikuwa na uwezekano wa kumshuti. Lakini muda mfupi Komandoo mmoja wa kimarekani akampitia kwa kumbo mpaka chini. Kila kitu kilichokuwa kikitokea Masimba alikuwa pembeni akitizama. Kutokumuona Vero katika viunga vile, hakukumpa shaka. Hakukumpa shaka kwa kuwa alijua na kutambua kinachotokea. Hata yeye alikuwa akihama hapa akienda kusimama sehemu nyingine. Sehemu ambayo ilikuwa na giza totoro tofauti na kule alipotoka. Ukimya ulikuwa umechukua sehemu kubwa sana. Hapakuonekana uwepo wa watu. Hapakuonekana ni sehemu ambayo ilikuwa na Rabsha. Masimba akatulia akiendelea kutizama mbele. Kutizama kama angemuona Veronica. Komandoo yule aliyemkumba Teddy hakuinuka katika wakati ule. Alijua nini ambacho kinaendelea Hapo. Alijua watu wale walikuwa wakipotea katika namna fulani. Ni wakati huo akikiangalia hicho, ndipo hapo akakiona kile ambacho alitaka kukiona hapo mwanzo. Veronica Tayari alianza kugawa tiketi katika aina ile ile ambayo ilitakiwa. Miili ya watu kadhaa ilikuwa imetambarajika chini kuonyesha kuwa Vero alikuwa akiua watu taratibu. Ulikuwa uuaji ambao ulimfanya Masimba aamini kuwa huyu alikuwa Mafia kweli. Hilo likampa nguvu ya kuinuka na kuanza kusonga kuelekea kule kule. Kuelekea pale walipolala watu wale walioonyesha hawakuwa na Uhai. Hatua ya kwanza ikamuacha ikiivuka barabara, hatua ya pili alishaivuka barabara. Hatua ya tatu alijikuta akiisalimia Ardhi baada ya kujikuta akiisalimia Ardhi. Wakati akitaka kujitayarisha kuinuka akakutana na kitu kizito ambacho kilitua kisogoni na kumfanya Arudi chini. Giza likaanza kuyagubika macho yake. Akataka kujaribu kupambana na Giza. Hakuweza, hakuweza kwa kuwa alihisi kitu kingine kikitua kichwani. Hakupata nguvu na Uwezo Tena wa kufumbua macho yake. Alijikuta akizidiwa na giza. Akatulia kana kwamba Alikuwa Maiti.
********
Moscow Russia.
Mkurugenzi wa Shirika la Kijasusi la Urusi (KGB) Bwana Vandelov Pashovic. Alikuwa Ofisini kwake akiwa ametulia akiangalia hiki na kile upenuni mwa Ofisi ile ambayo ilikuwa katikati mwa jiji la Moscow. Alikuwa akiangalia hiki akiwaza kuhusu taarifa aliyoipata muda mfupi uliyopita kutoka africa, kuwa Kuwa shirika la Kijasusi la Marekani lilikuwa limeiuzia Nchini Ya Tanzania Mtambo maalum wa kutengeneza Kemikali hatari zinazotumika kuchanganywa na madawa ya kulevya. Mara ya kwanza baada ya kupewa taarifa hiyo alitaka kuipuuza. Lakini badala ya kuifuatilia hiyo taarifa na kuupata ukweli kuhusu hilo. Akajikuta akihitaji kulichunguza Hilo suala. Alihitaji kuujua huo Mtambo, alihitaji kuuondoa huo mtambo mikononi mwa Serikali ya Tanzania. Baada ya kutafakari kwa Kina akaona awasiliane na Vijana wake ambao walikuwa Nchini Rwanda kwa . maalum ya Umoja wa Mataifa. Aliwataka Vijana Hao waingie katika nchi ya Tanzania ili kuchunguza taarifa hizo na wampe Majibu katika Masaa sabini na mbili. Ni kweli vijana hao watatu wakaingia Nchini Tanzania kama Watafiti wa Masuala Ya Ufaidikaji wa Rasilimali kwa Watanzia Wenyewe. Walipoingia katika nchi ya Tanzania Cha kwanza Walichokifanya ni kuonana na Mtu Mmoja Aitwaye Mr Raymond ambaye alikuwa ni Mshirika wa karibu wa Genge la Mafia Katika nchi ya Italy. Ni mtu huyu ambaye aliletwa na Kanisa katoriki kama msimamizi mkuu wa madhehebu hayo katika Afrika. Msukumo wa kuonana na Mtu huyu, ulitokana na Taarifa ambayo waliipata baada tu ya kuingia Chini Tanzania kuwa kuna mzee mmoja anaweza kuwasaidia katika Hilo. Ni usiku huo ambao Vijana wale walifika pale, ndio usiku ambao Walikutana na Veronica. Kukutana kwao hapo ni baada ya Veronica kuitwa na Mr Raymond kukifuatilia kile kile ambacho vijana hawa watatu walitaka kuijua Taarifa yake. Baada ya vijana hawa tatu kufika katika makazi ya Mzee Huyu ambaye alipachikwa cheo cha Usimamizi wa makanisa ukanda wote wa Africa ya Mashariki. Ndipo walipokutana na Veronica Senka Ambaye naye alitumwa na Genge la mafia kuufuatilia mtambo huo ambao kwa upande wa Kundi la Mafia waliihitaji betri pekee ambayo ndio husukuma Mtambo huo. Baada ya vijana wale kufika na kufanya mazungumzo ya kina na Mzee Raymond kisha kugundua kuwa wapo katika kufuatilia kitu kimoja. Wakatuma Taarifa hiyo kwenye Ofisi za KGB Jijini Moscow. Baada ya Taarifa Hiyo kutua mezani kwa mkurugenzi wa KGB. Mazungumzo ya kina yajafanyika kwa pande mbili. Upande wa Mafia pamoja na Shirika la Kijasusi la Urusi. Baada ya mazungumzo ambayo yalichukua Takribani siku sita makubaliano yalifikiwa kwa Shirika la kijasusi la Urusi kukubaliana na Kundi la Mafia kuangalia Namna ya Kuipata hiyo betri kisha watajua nini cha kufanya. Baada ya makubaliano Hayo Kufikiwa. Veronica ndipo alipopewa Jukumu la kuipata Hiyo Betri Kutoka mikononi mwa Serikali ya Tanzania. Jukumu ambalo alitakiwa kulifanya akiwa na Special Agent's wa KGB. Kazi ya kufuatilia ikaanza kwa Watu hawa kuanza kujiingiza ndani ya Serikali. Ni katika ukaribu huo wakaweza kuunda ukaribu na Serikali hasa kwa Waziri. Ni katika ukaribu huo ndipo walipoambiwa Betri Hiyo ipo mikononi kwa watu wawili ambao waliheshimika katika jamii yote ya Kitanzania. Wakati hilo likiendelea likatokea Suala la kupotea Kwa mzigo wa Mamilioni ya Shilingi. Mzigo ambao ulichukuliwa katika mazingira ambayo special Agent's wa KGB pamoja na Veronica walikuwa nyuma ya Hilo. Nikatika hilo kuliko ibua mzozo kati ya Washirika wa mzigo huo. Ni mzozo huo uliomuibua Masimba, ni mzozo huo ambao ulichukua maisha ya Asteria P Paulo ambaye alikuwa akiujua ukweli. Wakati Special Agent's walipomuua Asteria Walikuwa wakipata maagizo kutoka kwa Teddy na Hata Veronica. Kwahiyo Veronica na Teddy ni watu ambao wanafahamiana lakini pia ni watu ambao walikuwa wakiwakilisha mashirika tofauti. Wakati Teddy akiwa ni Afisa Usalama wa Shirika la kijasusi la Tanzania (Tiss) pia alikuwa ni Special Agent wa Shirika la kijasusi la Marekani CIA (Central Intelligence Agency ). Pia Veronica Alikuwa ni Special Agent wa Mafia, na Vile vile alikuwa akiwakilisha shirika la Kijasusi la Urusi (KGB) (KOMITET GOSUDARSTVENNOE BEZOPASNOSTI) AMBALO kwa kiingereza lilijulikana kama (committee for state Security, foreign intelligence and Domestic security Agency of the Soviet Union ). Licha ya kufahamiana Huko na kuifanya kazi kwa pamoja. Teddy na Veronica Kila mmoja alikuwa akitumiwa na Mtu ambaye yupo nyuma. Wakati Teddy akitumiwa na Viongozi Wakuu wa Nchi. Veronica yeye alikuwa akitumiwa na Mzee Raymond wa Kundi la Mafia. Waliifanya kazi ya kufuatilia Mtambo Hasa Wakiitaka Betri ya ule mtambo. Wakati wao wakiendelea ndipo hapo Masimba alipoibuka na kuanza kulifuatilia hilo suala. Kitendo cha masimba kuanza kulifuatilia lile suala kukaleta Ugumu katika kufanikisha uzalishaji wa Kemikali hizo kitendo ambacho kilisababisha rais Amruhusu Teddy kumuua Masimba. Wakati mpango wa kumuua Masimba ukiendelea kusukwa kwa umakini ndipo ulipotokea Mzigo wa Madawa kupotea nyumbani kwa Jimmy. Kabla suala la Mzigo halijapoa ndipo yalipotokea Mauaji Ya Waziri. Mauaji Ambayo yalifanyika baada ya Waziri mkuu kumteka teddy, kisha kutaka kwenda kumuingilia kimwili. Mauaji ya waziri mkuu ndiyo yalimfanya Rais Aamue kuitoa Betri ile Kisha Kuikabidhi kwa Watu Wawili ambao walikuwa Maarufu Sana Katika Jamii kutokana na Ucha Mungu Wao. Betri ilikuwa mikono mwa Askofu Ibrahim Lexandre Rengima sambamba na Sheikh mkuu Wa Mkoa Dk Ramadhani Chilemba. Hili suala alilifanya Rais Kwa Siri akimshirikisha meja Jenerali Chomboko. Licha ya kulifanya hili kwa Siri, lakini Veronica na Teddy waliinusa fununu ya hilo. Na siku ambayo alipewa maagizo na Masimba kwenda kumuua Askofu na kukuta ameshauawa. Alitambua veronica ndiye aliyeyafanya mauaji yale. Licha ya kumuwahi Baba askofu lakini hawakuipata bahasha kwa kuwa Baba Askofu Hakuwa tayari kuitoa kwa kuwa alitaka imfikie Masimba. Kwahiyo Veronica na Teddy walikuwa ni watu wawili wanaofanya kazi pamoja lakini kila mmoja akiwakilisha upande Mwingine. Baada Ya Veronica kugundua masimba anauwezekano wa kuipata Ile betri ndipo hapo likipoundwa Tukio fake ili kumuaminisha masimba kuwa Veronica Alikuwa mtu sahihi Kwake. Ndio maana aliipata hamu ya kwenda pale Kanisani kuonana na mzee Raymond Bila kujua kuwa watu hawa hawakuwa upande wake.
*********
Alifumbua macho taaratibu kama mtu aliyekuwa akitoka kwenye usingizi. Maumivu nyuma ya kichwa chake yalimkumbusha kitu kilichotokea Mpaka yeye kufika Hapo Ndani. Akataka kuupeleka mkono wake kisogoni, lakini alipojaribu kufanya hivyo akajikuta hawezi kwa kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa pingu. Akaendelea kuangaza huku na huko kama angeweza kuona kitu. Lakini Giza totoro ndani ya Chumba kile, halikumpa uwezo macho yake kuona Chochote. Akatulia akimuwaza Veronica. Alitambua kama Veronica ameliona tukio la kutekwa kwake, basi atafanya lolote kumuokoa. Hakujua kwamba hata Veronica Hakuwa Rafiki kwake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa sehemu ngeni machoni mwake, licha ya ugeni huo lakini vile vile Giza lilikuwa limechukua sehemu yake, macho yake hayakuweza kukiona chochote kilichopo hata hatua tatu kutoka pale alipolazwa. Mikononi alikuwa na pingu kuonyesha kuwa alikuwa mikononi mwa watu wa usalama. Maumivu kichogoni yakairudisha kumbukumbu yake, kumbukumbu ambayo ilimrudisha mpaka viunga vya ubalozi wa Marekani. Kumbukumbu iliyomkumbusha mapigo mawili aliyoyapata wakati alipokuwa akiiruka miili ya marehemu. Hisia kuwa ulikuwa mtego juu yake zikampitia kichwani. Miili ya watu kutambarajika chini, kisha muda ule ule kushambuliwa. Haikuwezekana katika hilo. Haikuwezekana katika kuliamini kichwani mwake. Licha ya kuamini huko, lakini alipomkumbuka Veronica tabasamu likatamalaki, tabasamu ambalo liliishia usoni kwake. Tabasamu ambalo halikufika kwa mwingine Zaidi Yake. Hakujua kuwa Veronica Ni Special Agent wa Mafia na KGB, hakujua kuwa Veronica Alikuwa Naye akiihitaji Ile betri. Hakujua kuwa Veronica na Teddy walikuwa wakufahamiana. Walikuwa katika mission moja lakini kwa malengo tofauti. Aliamini Vero alikuwa ameshuhudia kutekwa kwake. Alitambua muda wowote angefika Hapo. Akauvuta muda huku akijaribu kuifanya mikono yake kutoka Nyuma na kurudi kwa mbele. Lakini kabla hajafika popote akausikia mlango ukifunguliwa kisha kuisikia miguu ya mtu ikitembea Taratibu kuelekea pale alipokuwa Amelala. Hisia kuwa mtu huyu alikuwa sio mwema kwake ikamjia kichwani. Muda mfupi kidogo akajibingilisha na kuihama ile Sehemu. Ni sekunde mbili ya kufanya hivyo akapishana na mvua ya Risasi zikichimba Mahala ambapo alikuwepo. Baada ya Risasi kuvurumishwa kwa muda kisha kuachwa, taa za chumba kile zikawashwa. Sehemu yote ikawa nyeupe kutokana na Mwanga. Mbele ya macho yake Alikuwa amesimama Teddy akionyesha kushangazwa. Licha ya Risasi alizopiga lakini sehemu haikuwa na Mtu. Risasi za Semi Automatic zilikwenda patupu zikiichimba Sakafu. Teddy akashikwa na mshangao, mshangao ambao ulimpa masimba mwanya wa kusimama na kwenda kumkumbuka. Wote wakaanguka chini huku bastola ikiruhusu risasi ambazo hazikuleta madhara. Sasa ilikuwa ni purukushani. Teddy alikuwa Chini huku masimba akuwa juu akimkandamiza kwa mikono yake miwili. Teddy alikuwa akifurukuta. Teddy hakuwa na uwezo wa kugeuka. Lakini wakati hilo likiendelea Masimba alijikuta kitu chenye ncha kali mfano wa sindano kikiingia shingoni. Haukupita muda mrefu masimba akayaona macho yake yakiingia giza. Muda ule ule akawa kimya. Teddy aliinuka kutoka pale chini alipokuwa amebanwa akiwa ameishika shingo yake huku akikohoa. Bila kujali Masimba alikuwa katika hali gani, Teddy akaanza kumtandika masimba kwa Mateke huku akitukana na matusi ya nguoni. Baada ya kumtandika vya kutosha Teddy alimuacha Masimba akivuja damu kisha yeye kuondoka. Watu wawili walioonekana kuwa walinzi walimuangalia Masimba kwa Muda Mrefu bila kuongea kitu. Masimba alikuwa amelala kama mzoga akionyesha kama hakuwa na Uhai. Mateso yote hayo kwa sababu ya kuitetea nchi yake. Ilikuwa akiitetea Tanzania na watu wake.
Alikuwa amelala chini mfano wa mfu. Hawakujali hilo wala Teddy hakuiona huruma kutoka moyoni mwake. Alisahau mapenzi yao, akasahau wema wa masimba. Akasahau ahadi zote.. na hata mwisho kuutoa upendo ndani ya moyo wake. Hakuwa Teddy yule wa kipindi kile. Huyu alikuwa mnyama. Huyu alikuwa tayari kumpoteza masimba kwa mkono wake. Huyu alikuwa tayari kumuua. Tayari betri ilikuwa mikononi mwake. Tayari alishafanya mawasiliano na Makao makuu ya CIA kuwaeleza kila kitu. Kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea kwenye mission hii. Hakuwa na mapenzi tena na Masimba. Hakuwa na mapenzi tena katika moyo wake. Alitii miko ya ujasusi, alitii kanuni za kikachero. Teddy hakuwa na ile huruma Tena. Teddy alikuwa akiusadifu utaalam wake. Masimba akaburuzwa na kuwekwa ndani kabisa. Damu bado ilikuwa ikishuka taratibu kutoka mdomoni, puani na hata sehemu nyingine za mwili. Wakamuacha hapo kamzoga ulioachwa ufe. Mlango ukafungwa na taa zikazimwa Tena na watu wote kuondoka mle ndani. Masimba bado alikuwa chini akiwa hanafahamu. Wadudu wakali wakaanza kumshambulia kutoka pale chini. Hakujua chochote kwa kuwa alikuwa amepoteza fahamu. Akaendelea kushambuliwa kwa usiku ule. Hata kulipokucha mwili wake ulikuwa umefimba, mwili wake ulikuwa hautamaniki kwa kuutizama. Hakuwa akiangalika na hata kutamanika. Alikuwa sio masimba yule aliyekuwa akipambana, hakuwa masimba yule aliyekuwa akiwadhibiti watu takribani Ishirini. Huyu alikuwa mfu ambaye alibakiza muda mfupi tu kuivuta Pumzi ya Dunia hii. Aliachwa afe taratibu, aliachwa apotee katika chunba kile. Hapakuwa na Msaada tena.
******
"Hapana Haiwezekani, nasema haiwezekani. Siwezi kumuacha Masimba afe, siwezi kuliacha hili litendeke. Masimba hastahili kufa, masimba hastahili." Aliongea Veronica akiwa amekaa chumbani kwake. Alikuwa amejikunyata akifikiria hali ambayo alikuwa nayo Masimba. Ilikuwa ni lazima afanyekazi kumuondoa pale ndani ya chumba alichofungiwa. Kwa mara ya kwanza alikuwa akikiuka miiiko ya mafia. Alikuwa akikiuka miiko ya kijasusi. Aliamua kuutoa Moyo wake kwa sababu ya Masimba. Muda mfupi uliopita alimuona Masimba akiwa katika hali ambayo ilimhuzunisha. Kwa muda mfupi ambao alikuwa amekaa na Masimba alitokea kumpenda sana. Alitokea kumheshimu na kuipenda kazi yake. Alikuwa mzalendo na Alikuwa mpiganaji wa Kweli. Veronica akajiinua pale kitandani. Akaelekea mpaka kwenye droo. Alipofika aliifungua kisha kuchomoa bastola yake na kuipachika kiunoni. Baada ya hapo akatoka moja kwa moja mpaka Nje ya hoteli anayoishi. Kufika hapo akasimama kwa muda kabla ya kuchukua usafiri wa tax kuelekea bagamoyo kwenye moja kati ya kambi za Siri za Idara ya Usalama Wa Taifa. Sehemu ambayo ndipo alipohifadhiwa masimba. Hakujutia kile ambacho kingetokea baada ya hapo. Alichowaza ni kumtoa Masimba katika Eneo lile. Hakujali adhabu atakayo pewa atakapo Gundulika. Alikuwa tayari katika mapambano yoyote ambayo yangemlazimu. Ulikuwa usiku hivyo barabara iliruhusu. Tax ilikuwa ikitembea katika mwendo wa kasi sana. Muda mfupi walikuwa wakiingia bagamoyo. Kufika bagamoyo Veronica akashuka kisha kulipa, harafu akachepuka kuingia kwenye uchochoro ambao ulimuongoza moja kwa mmoja mpaka kwenye jengo fulani ambalo kwa Nje yake ilionekana ni kama kampuni Fulani. Kwa kuwa alijulikana hakupata tabu ya kuingia ama kuulizwa maswali. Alichokifanya ni kuingia moja kwa moja mpaka ndani kabisa. Jengo lilikuwa kimya kuonyesha kuwa hapakuwepo na walinzi wengi. Alitembea akikutana na baadhi ya wana usalama, lakini kwa kuwa alikuwa akifika hapo, Veronica aliachiwa apite. Muda mfupi alikuwa kwenye chumba ambacho alihifadhiwa Masimba. Bado alimkuta Masimba akiwa bado yupo kwenye hali mbaya. Bado alikuwa amelala pale pale damu zionekana kuganda. Veronica alimuangalia masimba kwa Muda, alimuangalia kwa kipindi kirefu sana. Kwa mara ya kwanza Chozi lake likashuka na kudondoka chini. Alikuwa akilia kwa mara ya kwanza. Akamuinamia na kumgusa kifuani. Akagundua alikuwa akihema kwa nguvu, aligundua Masimba bado Alikuwa Hai. Alichokifanya ni kusogea pembeni na kuiziba na kitambaa camera ya Usalama. Baada ya kuhakikisha kuwa kila kitu kipo tayari, Veronica akachuchumaa kujitutuma kwa nguvu zake zote. Akafanikiwa kuumbeba Masimba na kuanza kutoka naye kwenye chumba kile. Kwa kuwa aliifahamu ile kambi vizuri, hakupata tabu katika kutoka huku akiwa na masimba begani. Baada ya kufanikiwa kutoka hapo salama. Aliingia ndani ya Msitu ulioizunguka kambi ile. Alitembea akiwa na Masimba begani bila wasiwasi. Alihitaji kufika kwenye kijiji chochote kile ili kuutafuta Usafiri ndani ya Usiku ule tayari kwa kuondoka na Masimba kuelekea Sehemu yoyote ile ambayo itakuwa mbali na Bagamoyo na Hata Dar es salaam. Alitembea usiku ule wa giza bila kukutana na kitu chochote. Ingawa alikuwa amechoka lakini hakutaka kupumzika. Baada ya kutembea kwa muda wa masaa mawili, hatimaye akatokea kwenye kijiji kimoja ambacho hakikuwa na nyumba nyingi. Baada ya kutokea kijijini hapo, akapata matumaini ya kuupata usafiri wa kuwaondoa Sehemu hiyo. Alisimama kwa Muda wa saa kama moja hivi akiusubiria usafiri. Lakini bado hapakutokea usafiri aina yoyote. Akaendelea kuvuta muda, mara wakausikia mngurumo wa Gari Ukitokea umbali fulani kuonyesha kuna Gari ambayo ilikuwa akija maeneo yale. Veronica Akamuinua Masimba na kusimama katikati ya Barabara huku Masimba Akiwa Begani. Punde akauona mwanga wa taa za gari ukitokea kwa mbele yake. Ilikuogopa kuwatisha watu kwenye gari, akaichomeka Bastola yake kiunoni. Akaanza kuupunga mkono hewani. Gari ikaendelea kuja kwa mwendo wa kawaida. Gari ilipofika karibu na aliposimama Veronica, Ikasimama.
"Naomba Msaada mpenzi Wangu anaumwa." Aliongea Veronica Huku akisogea Dirishani.
"Mnaenda Wapi kwani? Kwa nini usimpeleke Bagamoyo Mjini? Aliuliza Dereva huku akiufungua mlango na Kushuka. Kitendo cha Dereva Huyu kushuka kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu na Veronica. Muda ule ule mdomo wa bastola ulikuwa Shingoni kwa Dereva yule. "Naomba tusaidiane kumpandisha Huyu mgonjwa wangu Garini. Nitakupa kiasi fulani cha pesa. Ila ukileta ujanja maiti yako itaokotwa Hapa kesho." Alinguruma Veronica huku akiendelea kuugandamiza mdomo wa Bastola shingoni kwa dereva. "Taratibu dada na bastola hiyo. Nipo tayari kukupeleka popote." Alijibu dereva huku akimshika Masimba Vizuri. Veronica Hakujibu, alichokifanya nikusaidiana na Dereva yule, punde walikuwa Njiani wakielekea Chalinze, kupitia msata. Ndani ya gari hapakuwa na mtu wa kuongea na mwenzake. Veronica Alikuwa kimya akiifikiria hali ya Masimba, wakati Dereva alikuwa akifikiria Bastola Aliyoshikiwa na Mwanamke huyu. Baada ya ukimya wa kipindi kirefu, dereva akashindwa kuvumilia.
Akaona Amuulize Veronica. "Dada kwani Mgonjwa Anatatizo gan?.
"Haikuhusu, unachotakiwa Endesha gari nisijefumua kichwa chako kwa Risasi.," akajibu Vero akionyesha hakutaka Mashauriano wala hakuhitaji kuulizwa Maswali. Lakini kwa upande wa Dereva hakukoma kuuliza maswali. Aliendelea kuuliza maswali huku akiuondoa woga machoni mwake. "Dada Hali ya mgonjwa ni mbaya, kumbuka hapa tupo wawili na gari yenyewe haitembei kwa mwendo wa Haraka. Tunachotakiwa ni kuutafuta msaada. Msaada wa kumsaidia huyu mgonjwa. Hayo mambo ya Amri achana nayo." Alisema yule dereva huku akimuangalia Veronika. Veronica akabaki kimya akifikiri cha kufanya. Kichwa chake kilikuwa na vitu viwili. Kimoja ni kutaka kumuamini Dereva na Chapili ilikuwa ni kutokumuamini. Baada ya kufikiria sana akaona amuamini. Akaona ni kweli kile kilichosemwa na Dereva. "Nahitaji msaada, mpenzi wangu amechomwa sindano ya sumu. Mpaka kufika Chalinze naweza kumpoteza. Naomba unisaidie. Ila nakuonya Ukiufungua Mdomo tu.. Nitakuua kwa mikono yangu." Aliongea Veronica Akionyesha Hatanii. "Sawa nitazingatia Dada yangu."alijibu Dereva Huku akihama barabara ya rami na kuingia ya Vumbi. Gari ikatembea usiku ule mpaka katikati ya Pori. Giza lilikuwa limetanda kila upande. Veronica tayari Bastola ilikuwa mkononi. "Tumshushe Mgonjwa tutembee nae." Akaongea dereva huku akimshusha Masimba toka ndani ya gari, kisha kumuweka Begani. Safari ya kutembea kuelekea katikati zaidi ya msitu ikianza. Walitembea kwa muda wa dakika kumi. Mbele yao wakakiona kijumba cha bati. Kilikuwa kijumba ambacho kilijengwa katikati Ya msitu. Baada ya Dereva kukifikia kibanda akamshusha Masimba na kumuweka chini. Wakati akijiandaa Kuugonga Mlango, Akasikia sauti ikitoka nyuma yao. Tulia Hivyo hivyo na Utupe Bastola yako Chini. Veronica Akatiiiiiiii
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tulieni Hivyo hivyo, kisha wewe tupa silaha yako chini." Ilikuwa sauti kutoka nyuma yao. Sauti ambayo haikuonyesha utani ndani yake. Veronica Akatii kwa kuitupa Bastola Chini. Akatulia tuli huku akiamini kuwa inaweza kuwa amesalitiwa na huyu Dereva. Wakati akiwaza hilo akakatishwa na sauti ya mtu huyu. "Nyie ni nani? Na kwa nini mko hapa?. Veronica akabaki kimya huku akimuangalia dereva ambaye alimtia tumaini kwa kuwa hakuonyesha kujali. "Ni mimi Charles, nimemleta huyu dada ana mgonjwa ambaye hali yake sio nzuri." Alijibu dereva huku akionyoosha kidole kama ishara ya kumuonyesha. Huku akiwa amekamatia Sub Machine Gun Mtu yule aliyekuwa akionekana kama mtu mzima. Kitendo cha kuiona ile bunduki kulimpa Veronica hisia. Hisia kuhusu mtu huyu ambaye alijibadilisha ili aonekane Mganga. Mganga gani amejengeka kimazoezi kwa aina Hii? Mganga gani ameweza kuikamata SMS kwa Staili hii? Yalikuwa maswali ambayo hayakuwa na majibu. Maswali magumu. Kwa mara nyingine sauti ya mwanaume huyu ikatamalaki katika ngoma za Masikio yao. "Muingizeni Ndani mtu huyu, fanyeni haraka." Veronica na dereva wakasaidiana kumuingiza Masimba ndani akiwa bado na Hali ile. Baada ya Masimba kuingizwa ndani. Taa za kijumba kile zikawashwa. Baada ya Taa kuwashwa, dereva na Veronica wakaangaliana. Kuangaliana kulikotokea baada ya mtu yule kumuita Jina Masimba. Veronica ndiye aliyeshikwa na mshangao kuliko hata dereva. Kile alichokuwa akikiwaza mwanzo, kitu ambacho alikuwa na uhakika nacho kuhusu mtu huyu. Alihisi alikuwa usalama , alihisi alikuwa ni mtu ambaye aliwahi kuwa sehemu fulani. "Masimba, masimba, unatatizo gani? " aliita mtu yule huku akimtingisha masimba. Lakini bado masimba hakuweza kuitika. Alikuwa ametulia kama Maiti.. Veronica bado alikuwa kwenye bumbuwazi. Bado alikuwa kwenye mshangao. Hata mwanaume yule alipoingia kwenye kichumba kidogo, bado Veronica alikuwa katika mshangao. Maswali lukuki yalikuwa yakikipita kichwani kwake. Bado alitaka kumfahamu huyu mtu, akalazimisha macho yake yamuangalie mwanaume huyu ambaye mara hii alikuwa ametoka akiwa na kiboksi mkononi. Hata huyu mwanaume naye akamtizama, akamtizama kwa aina ya kutaka Veronica ajue kuwa yeye alikuwa nani. Wakaangaliana tena na Tena. Veronica alikuwa akikitizama kile alichokuwa anataka kukijua. Alikuwa anamuangalia Mtu ambaye alikuwa ni mmoja kati yao. Macho yao yakatizamana tena na tena huku yakiongea. Mwanaume yule alimruhusu Veronica kusoma kila kilichopo ndani yake. Ni muda huo ambao Veronica akimtizama mtu huyu, akakiona kingine mkononi kwa Mtu yule. Kitu ambacho kilimthibitishia kile ambacho alihitaji kukijua. Mtu yule alikuwa ameishika sindano na kichupa chenye dawa ambayo ilitumika kutolea sumu kwa mtu yoyote ambaye angehisiwa kuchomwa sindano ya Sumu. Hakubisha kuwa huyu mtu alikuwa jasusi. Licha ya kuwa Jasusi, lakini bado hakujua alikuwa nani na alimtambuaje ama kumjua Masimba.
Baada ya kuishika ile sindano, mtu huyu akasogea mpaka pale alipolala masimba na kupiga magoti. Akaichoma sindano kwenye mfuniko wa kichupa na Kuivuta. Baada ya dawa kujaa kwenye bomba akautafuta mshipa mmoja mwilini na kuchoma ile sindano. Baada ya Kuchoma na kuiruhusu dawa kuingia mwilini mtu yule akainuka na Kuingia chumbani. Safari hii akatoka na kitu mfano wa kalamu, lakini ndani yake kukiwa na dawa ya Majimaji. Baada ya kufika hapo tena akautanua Mdomo wa Masimba kisha kuimimina Dawa kinywani. Baada ya kufanya Hivyo.. akamfunika vizuri kisha kukaa pembeni Yake. Macho yake yalikuwa yakimtizama masimba tu kwa muda wote. Yalikuwa yakimuangalia kanakwamba hakuwa akikiamini alichokuwa akikiona. Macho yake yalionyesha kitu ambacho kilimvuta Veronica. Macho ya mtu huyu yalikuwa yakiongea na mwili wa masimba. Hakuwa akiongea kwa mdomo lakini macho yake yalikuwa yakikizungumza kitu fulani. Baada ya Dakika kumi kupita huku ukangaliana kule kukiichukua sehemu yote ya kijumba na kuuleta Ukimya. Masimba akaanza kukohoa mfululizo. Tabasamu usoni kwa veronica halikukauka. Nguvu na imani kuwa masimba alikuwa salama ikarudi kichwani mwake. Lakini aliporudisha macho kwa mtu huyu bado alikutana na hali ile ile, bado mtu yule alikuwa akimuangalia masimba huku macho yake yakizungumza. Yakizungumza kile ambacho kila Veronica alipotaka kukisoma hakufanikiwa. Masimba akaendelea kukohoa mfululizo, damu ikishuka Kutoka mdomoni, damu ikiruka kila pale alipokuwa akikohoa. Kwa mara ya pili mtu huyu aliinua uso na kumuangalia Veronica, kisha dereva aliyemleta Veronica. "Mnaweza kuondoka sasa mkamuacha mgonjwa hapa. Veronica hutakiwi kulala hapa usiku huu. Hutakiwi kwa kuwa ulichokifanya unaweza kupewa Adhabu ya kifo. Unajua adhabu za Kundi la Mafia lilivyo." Yalikuwa maneno yaliompumbaza veronica, maneno yaliomshtua na hata kumtia baridi. Hakutegemea kujulikana mapema hivi. Hakutegemea mtu huyu angeweza kumjua hivi. Huyu ni nani? Lilikuwa Swali lililohitaji majibu kutoka Kwa Mtu Huyu. Lilikuwa swali ambalo majibu angeweza kuyapata kumtoka kwa mtu huyu. Mtu ambaye alionyesha kumjua kuliko mwenyewe anavyojijua. Veronica akabaki ameduwaa akimuangalia mtu huyu. Alikuwa akimuangalia katika namna ambayo Ilimfanya mtu yule atambue kuwa kuna kitu kinahitajika. "Hii kazi ni ngumu Veronica. Nilitambua Masimba alikuwa akipambana pasipo kumjua Teddy na Pasipokukujua wewe. Lakini hayo yote tutayaongea baada ya kuupata muda. Unatakiwa kuondoka hapa usijekulifanya suala hili kuwa kubwa." Aliongea yule mtu huku safari hii akihamisha macho yake kumuangalia Dereca. "Charles naomba umpeleke huyu dada mpaka dar es salaam. Pitia barabara zile zile ambazo tulikuwa tumepita." Alitoa maagizo mtu huyu huku akisimama na kuingia tena Chumbani akiwaacha Veronica na Charles wakiendelea kuangaliana. "Tuondoke Hapa Veronica. Aliongea Dereva yule akisimama tayari kwa kuondoka. Veronica naye akafanya hivyo.
******
"Nahitaji kumjua yule mtu." Aliongea Veronica akimwambia Charles walipokuwa Njiani kurudi Jiji dar es salaam. "Unadhani mimi namjua?" Akauliza Charles Huku akiwa kwenye usukani. "Nafikiri unamjua ama kama Humjui, basi utakuwa na ufahamu kidogo juu ya mtu yule." Akajibu Veronica. Charles hakuongea chochote akanyamaza kwanza akionyesha kufikiria kitu. "Simfahamu Zaidi ya hapo. Ila kuna wakati niliwahi kuhisi kuwa labda mtu yule alikuwa Usalama Wa Taifa ama mtu ambaye aliwahi kuwa katika Shughuli inayofanana na kitu kama hicho." Akajibu Charles. "Kitu gani kilichokifanya uhisi kuwa labda alikuwa mtu Wa Idara nyeti? Akaendelea kuuliza Veronica. "Kuna wakati nilikuwa nikikutana na watu fulani ambao ukiwaangalia unaweza kudhani ni Makamandoo wale tunaowaona kwenye TV. Kuna wakati nilikuwa nikikuta mpaka Raia Wa Kigeni." Akajibu Charles, majibu ambayo yalianza kumfanya Veronica Aanze kuhisi kuwa alikuwa sahihi kuwaza. " wewe ulijuana naye vipi? Akauliza Tena Veronica.
"Tulikutana kwenye bar moja maeneo ya bagamoyo mjini. Yeye alikuwa pembeni akiwa amekaa sambamba na Binti mmoja mwembamba hivi. Nilikuwa hapo nikipata moja moto moja baridi. Sasa wakati tuko hapo wakatokea wababe fulani wakataka kumchukua mwanamke yule ki nguvu. Ndipo hapo nilipomuona akifanya kile ambacho hufanywa na watu tunaowaona kwenye Video. Jamaa alikuwa akipiga Ngumi na Mateke kama Jean Claud Van Damme. Alikuwa akiruka hewani na samasoti kama Jet Li. Hapo ndipo kila mtu pale akashangaa. Kwanza muonekano wake ulionyesha kuwa alikuwa Mtu mzima. Lakini kile alichokuwa akikifanya pale utadhani alikuwa kijana. Basi baada ya Valangati ile kuisha wale watu wakatupotea katika mazingira fulani ambayo hakuna mmoja kati yetu kwenye ile Bar Alitegemea. Waliondoka mfano wa kuyeyuka. Ni katika kuondoka hapo ndipo nilipookota pochi yake ambayo alionyesha kuidondosha wakati wa purukushani. Pochi Hiyo ndiyo iliouleta ukaribu na mtu Huyu. Ukaribu ambao ulinikutanisha na watu wengi wa Ajabu. Pia kuna siku niliiokota Hii picha katika eneo lile." Aliongea Charles Akimkabidhi Veronica picha ndogo. Vero akaichukua kisha kwa kutumia Mwanga Wa Simu Akaiangalia. "The Bastard.....??? Ilikuwa sauti kutoka kwa Veronica Huku mshangao ukigubika uso wake. Macho yake yalikuwa yakiitizama Sura ya Mwanaharamu, macho yake yalikuwa yakiitizama Picha ya Nemisis. Macho yake yalikuwa yakimtizama mpelelezi Mashuhuli Afrika. "Kuna kitu ndani yake na kuna namna kwa mtu yule kuwepo pale msituni. Nataka kumfahamu kwa nini yuko pale na Kwa nini picha ya mtu huyu imekutwa pale." Aliongea Veronica Akionyesha kushangaa.
"Una mfahamu huyo mtu?" Lilikuwa swali kutoka kwa Charles. "Yeah namfahamu zaidi. Sasa nimepata picha na kujua ni kwanini mtu huyu ananijua kiasi hiki na kwa nini anamjua Masimba. Nitamjua tu Ni Nani." Akajibu Veronica huku akiiendelea kuitizama picha ile.
******
Mji wa bagamoyo na vitongoji vyake ulikuwa katika hekaheka kubwa kutoka katika vyombo vya dora. Askari wenye makwanda na waliovaa kiraia walikuwa wakizunguka katika Mji wote wa bagamoyo wakiwa na picha ya Masimba mikononi mwao. Idara ya usalama wa Taifa ilikuwa imesambaza wapelelezi wengi katika kila kona kunusa huku na huko. Taarifa ya kutoroshwa kwa Masimba iliitingisha Serikali sambamba na Idara zake. Mikutano mitatu ya Siri ilikuwa imekwishafanyika katika sehemu tatu tofauti. Kikao cha kwanza kilifanyika Katika Ubalozi wa Marekani, Cha pili kilifanyika Kwenye nyumba za Siri za Serikali. Wakati cha tatu kilifanyika Ikulu. Vikao vyote hivyo havikufikia muafaka baada ya washirika kuhisi kuwa kuna usaliti umefanyika mpaka kufanikisha kutoroka kwa Masimba. Kila sehemu ilikuwa ikipekuliwa na kila nyumba ilikuwa ikiangaliwa kwa namna ya pekee. Askari walikuwa wakihaha huku kila wakati wakipokea maelezo kutoka kwa wakubwa zao. Mpaka inafikia saa kumi za Jioni hapakuwa na fununu ya wapi pale alipo masimba. Camera za usalama ndani ya kambi ya Siri ya Usalama wa Taifa zilionekana kutokuchukua picha ya aina yoyote. Kingine ambacho kiliongeza ugumu walinzi ambao walikuwa zamu usiku huo kila mmoja alikutwa akiwa amekufa kwenye Chumba chake. Kila mmoja alikuwa amechinjwa shingo. Hilo likavifanya vikao kuendelea kuitishwa ikulu. Kwa mujibu wa taarifa ambazo ikulu na Idara ya Usalama ilikuwa nayo ni kwamba. Masimba Hakuwa na Uwezo wa kutembea wala kusimama. Pia walikuwa na Taarifa kuwa sindano aliyochomwa asingeweza kuchukua wiki atakuwa Ameshapoteza Maisha. Sasa kama Taarifa Imekuja kwamba Masimba Ametoroshwa, Kwa nini Walinzi Waliokuwa zamu wameuawa sehemu zao walipokuwa wanaishi? Ina maana hawakuuawa usiku, bali waliuawa asubuhi. Kama ni Asubuhi ni nani ambaye ameua? Inaonyesha huyu muuaji alirudi kuja kuufuta Ushahidi baada ya usiku kumtorosha masimba. Kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, aliyefanya mauaji haya ni mtu anayefahamika. Ni mtu ambaye analifahamu suala hili. Yalikuwa mawazo ya wajumbe wote waliokuwepo katika kikao kile. Kikao ambacho kiliirudisha Taharuki miongoni mwao. Taharuki ambayo haikutakiwa kupewa nafasi kwa wakati huo. Simu zikapigwa sehemu mbalumbali za Nchi. Majasusi Wa Idara ya usalama wa Taifa walikuwa wakihaha kila kona. Wakati Ndani Ya Nchi ya Tanzania Msako ukiendelea. Teddy alikuwa ndani ya Jiji la Nairobi Akiwa na majasusi wa CIA sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Walikuwa katika kikao kizito kilichokuwa kikijadili kuhusu uwezekano wa kuendeleza Biashara na Nchi ya Tanzania. Pia alikuwa hapo kupokea Zawadi ambayo ilitolewa na Rais Wa Marekani kama Pongezi ya Kufanikisha kwake kuipata betri. Ni wakati wakijadili hilo, Teddy akapokea Taarifa kutoka kwa Marafiki zake. Ni taarifa hiyo ambayo ilimfanya asimame haraka. Usimamaji wake Ulimshangaza kila mmoja pale ndani. Hata macho ya wajumbe wale yalipomtizama Teddy, wakayaona Mabadiliko makubwa. Alikuwa amebadilika kama sio kuchanganyikiwa. Midomo yake ilikuwa ikicheza akitaka kuongea kitu. Lakini hakuweza kufanya hilo. Hakuweza kuongea Tena. Punde akautwaa mkoba wake na Kutoka Nje ya kikao pasipo kuongea chochote. Ilikuwa ni lazima Arudi Dar es Salaam kwa wakati huo. Alitaka kwenda kuhakikisha kile alichoambiwa. "Ni nani aliyemtorosha masimba na kuwaua Walinzi? Lilikuwa Swali lililomkuta Teddy Akiwa Ndani ya Tax akielekea uwanja wa Ndege wa Jomo kenyatta TAYARI KWA KURUDI TANZANIA.
Alichanganyikiwa kwa taarifa aliyopewa. Taarifa iliyomlazimu kurudi Tanzania. Masimba alikuwa ametoroshwa, masimba alikuwa ameondoshwa kwenye kambi ya usalama wa taifa. Kilikuwa kitu kigumu kukiamini. Kichwa chake kilikaribia kupasuka kwa mawazo. Aliujua ugumu wa kazi endapo itakuwa ni kweli masimba ametoroka. Kwa mbali Teddy alikuwa akiipata hofu, hofu ya kifo na hofu ya kuuawa na Masimba. Alitambua safari hii hata weza kuachwa akiwa hai. Tax ikatembea kwa mwendo wa kawaida pasipo kufanya haraka. Hata walipofika Uwanja wa Ndege wa Jommo Kenyatta Tayari alikuwa amechelewa. Moja kwa moja ikabidi afanye mawasiliano na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani. Baada ya mawasiliano hayo muda mfupi baadae akawaona watu wawili wakisogea kuelekea pale iliposimamia Tax. Watu wale wakajitambulisha kisha kumwambia kuwa walikuwa pale kwa maagizo ya Waziri wa Marekani. Teddy akaeleza kile alichokuwa akikihitaji kwa muda ule. Akaambiwa awafuate Watu wale kwa nyuma. Safari yao iliishia mpaka kwenye kampuni Moja binafsi. Akaambiwa asubiri kidogo. Muda wote Teddy alihitaji kuondoka hapo. Alitaka kwenda kuhakikisha mwenyewe. Taarifa hii ilikuwa imemchanganya kabisa. Kwenye account yake ya benki tayari pesa yake ilikuwa imeingizwa kama Ahsante yake. Ilikuwa pesa nyingi sana pesa ambayo kama angeamua kuondoka Hapa nchini na kwenda kuishi popote Duniani Angeliweza hilo. Lakini alitambua hata kama angeenda wapi basi nilazima Angetafutwa na Masimba popote pale. Alitambua kwa kile alichokifanya angesakwa popote pale. Alichotaka kukifuata ni kwenda kulihakiki hilo. Alijua kuwa lazima kuna mtu ambaye ameshiriki katika kumtorosha Masimba. Taarifa kuwa camera za Usalama hazikupata tukio lolote hilo lilimfanya aamini kuna Mtu ndani Ya Idara lazima atakuwa Amekengeuka. Muda mfupi baadae mlango ukafunguliwa kisha akaongozwa na watu wale kutoka Nje sasa wakielekea ndani kabisa ya Uwanja Wa Ndege. Baada ya kuingia kabisa akaongozwa mpaka kwenye ndege moja ambayo aliambiwa ndio hiyo ambayo itamsaidia kutoka hapa kuelekea Nchini Tanzania.
*******
Alishuka uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere majira ya saa mbili na nusu. Kukanyaga Ardhi ya Uwanja tu macho yake yakapokewa na macho ya watu ambao aliwatambua. Hawa walikuwa (I.0) intelligence officers. Hawa walikuwa watu ambao ni nadra sana kuwatanbua kutokana na unyeti wa kazi zao. Hawa watu huwa ni marufuku kujitambulisha popote na kamwe huwezi kuwakuta wamebeba silaha yoyote. Intelligence Officers silaha yao namba moja ni Akili yake tu. Taarifa zao huwa zinakusanywa kupitia Informers Volunteers (watoa taarifa wa kujitolea) ama bribed informers (watoa taarifa wa kununuliwa kwa pesa) Hata Coerced informers (watoa taarifa wa kulazimishwa kwa nguvu ama vitisho). Teddy aliwaangalia mara moja tu kisha kuongoza moja kwa moja kutoka ndani ya kiwanja hicho. Hakushangazwa na Usalama waliojazana kiwanjani, alitambua wote walikuwa wakimtafuta masimba. Baada ya kutoka Nje ya uwanja alichukua Tax ambayo ilimpeleka moja kwa moja Bagamoyo Usiku ule ule. Kichwa chake hakikuamini Kama Masimba alikuwa Nje ya Tanzania, Hakuamini kuwa masimba anaweza kutoroshwa kupitia uwanja wa Ndege. Alitambua masimba alikuwa ndani Tanzania. Na alitambua atakuwa Dar es Salaam ama atakuwa kule kule bagamoyo. Alitaka kuutumia Usiku ule kunusa taarifa zote ili kujua pale alipo Masimba. Tax ilitembea kwa mwendo wa kasi huku ukimya ukichukua Nafasi yake. Hakuna ambaye aliongea wala kuzungumza. Tax ikatambaa na kutambaa mpaka saa mbili na Nusu walikuwa tegeta. Kila tax ilipokuwa ikizidi kutembea, ndivyo Moyo wa Teddy ulipokuwa ukizidi kukosa Amani. Hakuwa akijiamini Tena. Hakuwa akijiamini kutokana na woga. Licha ya woga huo lakini ilikuwa ni lazima Afike na ilikuwa Lazima Atambue kule ambapo amepelekwa Masimba na Nani ambaye amefanyakazi hiyo.
******
Wakati Teddy akielekea bagamoyo kutafuta chanzo cha kutoroshwa kwa Masimba. Veronica Alikuwa ndani ya Nyumba ya Siri akiwa ametulia akifikiria kile ambacho ameamua kukifanya. Kilikuwa kitu cha hatari sana kuwasaliti watu kama Mafia. Siku zote unapokuwa katika kundi hili hutakiwi kutoka ama kusaliti kwa Njia yoyote. Alijua hukumu ambayo angeipata kama angegundulika na genge la mafia kuwa amesaliti. Moyo wake ulikuwa umemsukuma kumsaidia Masimba. Alikuwa tayari kwa chochote ambacho kingetokea huko mbeleni. Alikuwa tayari kupambana hata na viongozi wake lakini hakuwa Tayari kumuona Masimba akiuawa. Aliamini anauwezo wa kumsaidia na aliamini anauwezo wa kuipata betri Ambayo tayari iliingia mikononi kwa mwa Serikali. Muda wote alikuwa akitamani kumuona Masimba akitembea. Mawazo hayo yakamfanya Veronica Asimame na kutoka ndani ya hoteli ile. Hakujua alielekee wapi katika usiku ule, lakini mawazo yake yalimtaka kufanya hovyo. Akaufunga mlango na kuanza kutembea Taratibu kuelekea upande wa ukumbi wa kulia Chakula. Alitembea taratibu macho yake yakiangalia Huku na kule. Akai ngia ukumbini akitembea taratibu. Sura yake nzuri ikiwa katika tabasamu matata sana. Macho yake mazuri yalikuwa yakimtizama kila mmoja kanakwamba alikuwa akiwatega ili wamtizame. Hatua zake zilikuwa kawaida huku macho yake yakivuta kila sura ya mtu aliyekaa Hapo. Macho yake hayakushindwa kuwagundua wana usalama watatu ambao walikaa katika utatu tofauti. Kila mmoja alikuwa sehemu yake akipata kile ambacho aliagiza. Hakuwajali wala kuwatizama. Akawapita akiendelea kuitafuta sehemu Nzuri ya Kukaa. Muda wote machale hayakuondoka kichwani. Licha ya wapelelezi wengi wa Tanzania kutawaliwa na Usiri, lakini wengi hugundulika kwa sababu ya staili zao. Akawapita akiongoza kama mtu anayeelekea Msalani. Haikuwa msalani kama wengi walivyotegemea. Kwani baada ya kufika msalani akachepuka kidogo na kuuparamia ukuta na kuangukia upande wa pili. Alimkumbuka Masimba na Alitaka kurudi Bagamoyo Usiku ule ule. Aliiona hamu kubwa ya kutaka kukaa na Masimba. Alichapua mpaka upande wa pili wa Barabara. Wakati anaumaliza ukingo wa barabara hiyo, simu yake ikaingia Ujumbe. Kwa haraka Huku akitembea akaufungua kisha kuusoma. "Teddy yupo Bagamoyo Ameshuka Muda huu. Nenda kaichukue Betri. Ukishaipata itumbukize Risasi kichwani Kwa Masimba. Tiketi yako utaikuta Inakusubiri Hapa." Ulisomeka Ujumbe ule uliotumwa kwa Veronica ukitoka kwa Mr Raymond. Veronica akauangalia tena Ule ujumbe alijikuta akitabasamu. Tabasamu la kejeli. Tabasamu ambalo liliishia Usoni tu. Aliuona ugumu kwake kuitumbukiza Risasi kichwani Kwa Masimba. Alikuwa tayari kumuua Teddy, lakini Hakuwa Tayari kumuua Masimba. Akauangalia ujumbe ule pasipokuongea kitu. Kitu kilichomtisha ni watoto wa Masimba kuwa Mikononi kwa Mzee Raymond. Na alitambua hilo litaleta ugumu pale masimba atakapo upata nafua na kuamua kurudi kazini. Kichwa chake kikaanza kuwaza kitu cha kufanya. Kama alikuwa anautaka usalama wake nilazima awaondoe watoto wale mikononi kwa Mzee Raymond. Ni lazima Yasser na France waondoke. Mawazo yake hayo yalinfanya aache safari ya kwenda Bagamoyo. Akaamua kuelekea Nyuma ya Kanisa la St Joseph kuwapata watoto wa Masimba. Hakuchelewa katika hilo. Muda mfupi alikuwa akishuka Maeneo ya Posta ya Zamani. Akachepuka kidogo na kuuzunguka upande wa nyuma. Wakati anaanza kupiga hatua kuelekea hapo, akaiona gari moja akitoka pale. Ilikuwa gari aina ya Nissan patrol. Veronica akijabanza pembeni kwanza ili Gari ile ipite. Baada ya Gari ile kupita, veronica akajitokeza akaanza kutembea akielekea ndani. Kengele za tahadhali zikaanza kugonga baada ya kuufikia mlango wa kijumba na kuukuta upo wazi. Sijui ni kitu gani alichohisi, lakini Muda ule ule bastola ilikuwa mkononi. Akaingia taratibu huku macho yake yakitizama kila upande. Ukumbi ulikuwa kimya kuonyesha kuwa hapakuwa na mtu hapo ndani. Hapo umakini Ukaongezeka Maradufu. Sasa alikuwa akiupita ukumbi ule katika namna ya kufutia na kutia Raha. Ni muda mfupi tu ameonyesha kutumiwa ujumbe na Mr Raymond. Lakini cha Ajabu hata dakika mbili bado anakutana na hili la kutokuwepo kwa Mr Raymond. Kufika hapo akakumbuka kuwa France Na Yasser waliishi hapo ndani baada ya kutoroshwa Kutoka kwenye Jengo la Siri walilokuwa Wakiishi. Kuwakumbuka watoto hao kukamfanya auvuke ukumbi ule akielekea kule walipokuwa wakiwekwa watoto wale. Kabla hajakifikia Chumba walichokuwa wakiishi watoto wale, akayaona matone ya damu chini. Hayakuwa matone kama matone, bali yalikuwa madimbwi madogo madogo ya Damu. Damu ambayo bado ilikuwa mbichi kabisa. Akajiongeza na kusogea zaidi na Zaidi. Kidole tayari kilikuwa kwenye Trigger. Kidole kilikuwa tayari kuiruhusu Risasi. Veronica Akatembea zaidi sasa na Kuufikia mlango wa chumba Husika. Akaufungua mlango wa chumba ambacho waliishi watoto wa Masimba. Alipougusa tu mlango ukafunguka kuonyesha kuwa haukuwa umefungwa. Mlango ulikuwa wazi hata France na Yasser hawakuwepo. Lakini kilichomshangaza humu ndani ya chumba hapakuwa na Vurugu ama damu. Akatoka na kuurudisha mlango. Akaondoka Eneo lile..
Akili yake haikuwa imetulia kabisa, kutokuwepo kwa Mzee Raymond sambamba na Watoto wa Masimba ni kitu ambacho kilimchanganya sana. Aliijua hii ingekuwa vita ya Mafia na FSB dhidi ya CIA na Serikali Ya Tanzania. Kama ni kweli Mr Raymond Ameuawa, basi Kitakachotokea hapa nchini ni kitu ambacho kingeondoka na watu wengi. Sasa alikuwa Njiani Akielekea Bagamoyo. Alikuwa Njiani kumfuata Teddy katika Usiku huu. Usiku ambao alipata taarifa kuwa Teddy Alikuwa huko. Naye akaamua kwenda huko ili wakakutane tena.
*******
Kwanza alihisi labda alikuwa katika usingizi, kitu cha pili akahisi labda alikuwa nje katika sehemu ambayo alikuwa ametupwa. Alijaribu kufumbua macho taratibu, lakini hakuweza hilo kutokana na uzito wa macho kutokutaka kufumbuka. Akatulia akisikiliza kwa makini kana angetambua mahala ambapo alikuwepo. Bado hakusikia sauti wala vishindo vya binadamu. Bado kulikuwa na ukimya ulisadifu kuwa hakuwepo katika sehemu yenye mkusanyiko wa watu. Bali alikuwa katika Sehemu ya peke yake. Sehemu ambayo hapakuwepo na kiumbe chochote. Akatulia akiendelea kuipa Akili yake utulivu. Utulivu wa kukumbuka kile ambacho kilimfikisha hapo. Wakati akiivuta hiyo kumbukumbu hiyo. Akasikia Vishindo vya mtu vikisogea mpaka mahala alipokuwa amelazwa. Mtu huyu akaanza kumshika kuanzia kichwani mpaka Maeneo ya Kifuani. Hii haikuwa mikono ya Mwanamke bali mwanaume. Mikono iliyomikakamavu. Mikono Ambayo ilikuwa migumu kupindukia. Bado akatulia na Kitulia. Bado akatulia Huku akitamani Kufumbua macho lakini Bila mafanikio. Punde akakisikia kitu kama sindano kikiingia kweny mshipa wake. Punde akauhisi Usingizi mzito. Usingizi ambao haukuchukua Muda kumfanya Asikumbuke tena alichokuwa akikikumbuka. Akatulia akiuruhusu usingizi kuichukua NAFASI.
Usingizi ukaichukua nafasi na kumfanya asisikie kingine tena. Masimba akarudi kwenye usingizi mzito, usingizi ambao ulikuwa ndio tiba kwake.
*****
Giza lilimpokea Teddy ndani ya bagamoyo, hakutaka kuchelewa kuelekea kule alikopanga kuelekea. Ilikuwa ni lazima afike sehemu hiyo katika usiku ule ule. Wana usalama waliosambaa sambamba na Askari Kanzu (CID) hakumshtua wala kumfanya aache kile alichotaka kukifanya. Mkoba begani kwa mwendo wa Twiga akaliacha eneo aliloshukia, sasa alikuwa akiitafuta na hata kuifuata Njia iliyo sahihi ya kumpeleka Huko. Kiunoni alikuwa na bastola sambamba na sehemu nyingine tatu za siri. Moyo wake ulikuwa katika vita nzito ya kumtafuta Mtekaji na hata mtekwaji. Hakutaka kusikia Masimba yupo hai. Alitaka kusikia kifo chake. Hii ilikuwa ni vita ya kuipigania Roho yake. Vita ambayo aliianzisha yeye na pia ataimaliza yeye. Muda huu tayari alikuwa amefika katika maeneo ya kambi ile ya Siri ya mafunzo kwa Majasusi wa Usalama wa Taifa. Akapokewa na macho ya watu wanaomjua na wasiomjua. Hakuongea na yeyote zaidi ya kupita na kuingia Ndani Zaidi. Alitembea ndani ya kambi ile mawazo yakimpeleka moja kwa moja katika namna ya kutoroshwa kwa Masimba ndani ya kambi hiyo. Camera na mitambo mingine ya usalama ilikuwa kila mahali huku mingine ikiwa katika Usiri mkubwa. Ni nani aliyemtorosha Masimba? Ni swali ambalo alijiuliza wakati Akiufungua mlango wa chimba alichokuwa amewekwa Masimba kabla ya kutoroshwa. Ugumu wa chumba hiki kwa muonekano asingeweza kutoroshwa na mtu asiyeijua Idara. Aliyemtorosha Masimba alikuwa ni jasusi mwandamizi na mtu wa ndani sana. Haiwezekani mitambo na Camera za usalama zisinase chochote. Kuna sehemu itakuwa imechezewa tu. Lakini atakuwa nani aliyemtoa humu ndani? Lilikuwa swali ambalo lilimfanya atoke hapo ndani. Sasa alikuwa akielekea chumba kinachoongoza mitambo na camera zote. Aliufungua mlango na kuingia ndani. Macho yake yakaenda moja kwa moja kwa vijana watatu waliokuwa wakihangaika huku na huko kuliangalia hilo tatizo. Teddy akawaangalia kwa muda mrefu huku macho yake yakitizama Huku na kule. Aliyazungusha macho yake kila kuta ya chumba kile. Shida yake ilikuwa ni kugundua kile ambacho alitaka kugundua. Hakuona chochote katika kutizama huko. Akaamua kusogea mpaka pale walipokaa Vijana wale. Hakutoa salama bali alichofanya ni kuwauliza. "Nini kinaendelea Hapa?. Vijana wale wakamuangalia kwa muda pasipo kumjibu kitu. Akili zao zilikuwa zimechoka kwa kazi hii. Hakuna aliyetayari kumjibu. Wakamuangalia Kwa Muda Wa dakika moja bila kuongea wala kujibu walichoulizwa. "Hii ni Order kutoka Ikulu mnahitaji kunijibu sio kukaa kimya." Akaendelea kunguruma Teddy. Lakini bado watu hawa waliendelea kumtizama Usoni. Bado watu hawa hawakumjibu. Mmoja akampa ishara ya kusogea pale kwenye mitambo. Teddy akasogea mpaka sehemu Husika. Mmoja kati ya wale vijana akarudisha nyuma mfumo wa matukio ya Jana kuanzia mapema. Teddy akaanza kutizama kwa umakini Zaidi matukio yote ya Awali. Matukio ambayo yalichukuliwa na mifumo ya Kiusalama mle ndani. Licha ya kuangalia kwa Muda Mrefu na kwa Umakini mkubwa bado hakufanikiwa kuona chochote. Harafu Cha ajabu camera hazikuzimwa wala kuchokonolewa popote. Anaonekana aliyeingia alikuwa Jasusi Zaidi Yao, pia alikuwa fundi mkubwa katika masuala yote nyeti. Mtu achukuliwe Ndani ya kambi ya siri ya Idara ya usalama. Harafu hapo hapo mitambo ya usalama isimuone? Lilikuwa ni swali lililomchosha na kumpa wasiwasi. "Huyu ni Zaidi ya Jasusi, huyu ni zaidi yetu. Nimefanya kazi hii kwa miaka kumi na tano lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili. Inawezekana Mossad ndio wamekuja kumchukua Kiongozi." Aliongea kijana mmoja Huku akizunguka ndani ya chumba kile. Kila mmoja alikuwa ameshindwa kugundua chochote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Teddy akatoka hapo muda huu akielekea kwenye vyumba ambavyo walikuwa wakiishi walinzi waliouawa usiku huo. Akiwa amechanganyikiwa huku kichwa chake kikishindwa kufanya kazi vizuri, akalifikia eneo lile. Wakati anataka kuingia ndani ya moja kati ya vyumba hivyo, akaona alama ya kiatu kwenye mchanga. Hakuchanganywa na ile alama tu ya kiatu, kilichomchanganya ni kile alichokiona katikati ya soli zile za kiatu. Hakutaka kuamini kama wana usalama walishindwa kugundua hilo. Katikati ya soli za kiatu kile kulionekana alama zenye ncha mfano wa kisu. Ilikuwa imechimba Ardhini. Moja kwa moja akatambua nini ambacho kilifanyika kwa walinzi. Hawakuchinjwa kwa mkono bali kwa kisu maalum kilichotengenezwa katika viatu maalum Hapo akachuchumaa na kuangalia kwa umakini zaidi. Ni kile kile alichokuwa akikiona. Akawaita vijana watatu wengine waliokuwa karibu. Baada ya kuwaita na kuwaonyesha. Akaongea nao mambo kadhaa wa kadhaa, akaondoka katika viunga vile akielekea sehemu nyingine Kabisa.
*******
Aliuhisi mwanga wa jua ukimmulika Usoni. Taratibu akafumbua macho yake ili kuweza kuliona jua. Macho yakapokewa na Nuru ya mwanga wa Juu la Asubuhi. Jua ambalo lilimpa Joto. Joto ambayo haikuwa kama zile joto nyingine. Kufanikiwa kufumbua macho na kupokelewa na mwanga wa Jua. Kulimpa uwezo zaidi wa kuzungusha macho yake taratibu. Macho yake yakatua kwenye udongo ambao ulionekana kukandikia kijumba hicho. Paa la bati likikuwa karibu kabisa kuonyesha kuwa alikuwa sehemu ya kijijini. Sauti za ndege na wanyama ndizo zilizomuaminisha kuwa alikuwa shamba, alikuwa kijijini ama alikuwa shamba. Akainua macho yake zaidi na zaidi huku akiigeuza Shingo yake. Macho yake yakatua kwenye Bastola. Bastola ambayo ilikuwa Pembeni Mwa Kitanda alicholala. Bastola aina ya MM9. Hilo likamfanya ainuke zaidi huku akiiangalia kwa umakini. Kushtuka kutoka usingizini, kisha kuikuta bastola pembeni take ni kitu ambacho hakikutegemea. Licha ya kutokukitegemea lakini ni kitendo ambacho kilimrudisha kwenye kumbukumbu ya kilichotojea. Akalikumbuka Tukio kuanzia ubalozi wa Marekani na hata kwenda kuwekwanda ndani ya chumba ambacho baadae alikuja Teddy kwa dhamira ya kumuua. Kumbukumbu yake iliishia pale alipochomwa kitu mfano wa Sindano na kupoteza fahamu. Kama ni Hivyo ni kwa nini sasa ameshtuka na kujikuta amelazwa hapa huku pembeni kukiwa na Bastola. Je yupo wapi hapa? Kwa nini ameamka na kujikuta huku? Nani amemuokoa kutoka mikononi kwa Teddy na serikali? Hayo yalikuwa maswali tata. Bado hakuwa na kumbukumbu kama kuna mtu anaitwa Veronica. Mtu ambaye aliamua kuwasaliti wenzake kwa Ajili yake. Mtu ambaye ameisaliti mafia kwa sababu yake. Bado kumbukumbu ya kile kilichofanywa na Teddy kilikuwa kikimuumiza. Teddy huyu ambaye muda wote alihubiri mapenzi. Mapenzi Dhidi ya Masimba. Lakini leo amekuwa Teddy Huyu, teddy ambaye simu yake kwa sasa Inashinda na mwanaume. Mwanaume ambaye hapo mwanzo alisema hamhusu. Jimmy Lambert. Akajitizama na kuitizama bastola tena. Wakati akiliwaza Hilo akamuona Mtu akiingia akitembelea Mkongoja Akionekana kama Babu. Licha ya Masimba kurudiwa na kumbukumbu katika muda ule, bado kumbukumbu zake hazikupotea. Macho yake yalipotua Usoni kwa Babu huyu. Tabasamu na mshangaa pamoja Vikatamalaki. Alikuwa akitizamana na mtu ambaye alimfahamu. Mtu ambaye hapo awali hakujua kama atakuwa yupo katika eneo. Mtu ambaye alimjua. Lakini amefikaje Hapa? Na kwa nini yupo katika mabadiliko haya? Amenipata wapi ama kuniokota wapi? Yalikuwa Maswali, yalikuwa maswali ambayo hakuyapatia Majibu. Wakati akishangazwa na uingiaji wa Huyu Mtu, safari hii akaingia mtu mwingine. Huyu ndiye aliyeufanya Moyo wake uchanue kwa tabasamu. Uchanue kwa furaha na hata uzizime kwa Mapenzi kama sio hisia za Mapenzi. Alikuwa akitizamana na Veronica. Alikuwa akimuangalia mwanamke huyu ambaye ameonyesha kumpigania katika hatari. Furaha iliyoikuwa ikizizima moyoni mwake ilisababisha Ainuke pale Alipolala huku akumita Veronica. Akimuita Veronica kwa sauti ya Kutokuamini. Haikuchukua sekunde moja wakajikuta wamekumbatiana. Veronica alikuwa amelala kwenye kifua cha mwanaume huyu. Walikuwa wakiangaliana kwa macho ya kuitana na hata kuvutana. Macho ya ulegevu na hata macho ya mapenzi. Nyuso zao zikasogeleana huku Kila mmoja akitabasamu. Sekunde hii ya tatu walikuwa wakinyonyana ndimi zao. Ikawa hivyo na hivyo zaidi ya hivyo. Bado babu huyu aliyesimama na mkongojo pembeni alikuwa akiwaangalia. Aliuona Upendo na Hata mapenzi katika nyuso za watu hawa.. "sio wakati wa mapenzi, sio wakati wa kulia katika hili. Mnatakiwa kusimama ili kulimaliza hili. Tayari betri ipo mikononi mwa Rais wa Tanzania. Tayari betri inaendaa kuuwasha mtambo wa kutengenezea Kemikali za kuwaharibu Vijana Taifa hili. Ni wakati wetu kujaribu kulizuia hili." Aliongea Veronica Akijiondoa Mwili kwa masimba. Kujiondoa akimuacha masimba akishangazwa na Taarifa hiyo. Taarifa ya betri kurudi mikononi mwa Serikali. "TEDDY NITAKUPATA TU. NA NITAKUUA KWA MIKONO YANGU." Aliongea masimba sasa akimfuata yule Babu. "The Bastard hutakiwi kujificha katika uzee. Njoo katika Ujana tuifanye hii kazi." Bado masimba alizungumza huku akitembea. Wote wakatabasamu kwa pamoja kisha wakakumbatiana. Utatu Mtakatifu Ukazaliwa. Utatu ambao ulikuwa tayari kwa kulipigania Taifa la Tanzania. Taifa ambalo limekuwa shamba la kuchumwa mali kwa muda mrefu.
******
Walikuwa Watatu katika chumba hiki cha hoteli katika jiji la Dar es salaam. Alikuwa veronica, Masimba sambamba na Mwanaharamu. Masimba na Veronica walikuwa wakimtizama huyu Mwanaharamu usoni kwake. Mipango juu ya kuipata hii betri ilikuwa ikipangwa katika aina ambayo isingekuwa rahisi kugundulika. Lakini kabla ya mkakati wa kuipata Betri, ulifikiwa muafaka wa kuwapata watoto wa Masimba sambamba na Mzee Raymond ambaye anaonekana kulijua sana hili suala. Kazi hii ya hatari ilipangwa kufanya kwa siku hii. Kwa sababu ya hali ya Masimba kutokutengeamaa, Veronica na Mwanaharamu ndiyo ambao waliipanga kuifanyakazi hii. Veronica hakuonyesha woga, woga wakulisaliti kundi kubwa na hatari sana Duniani. Kundi ambalo liliweka Mizizi duniani kote. Kundi la Mafia. Moyo wake ulikuwa tayari kuingia katika uhatari. Aliamua kuasi katika kundi ambalo miko yake unaposaliti ni kifo. Kifo cha kinyama ama kutekwa na kufungiwa sehemu maalum ambayo hutumika kama Jela. Veronica hakuiona hiyo Hatari, aliamua kwa moyo wake kuingia rasmi katika kazi hii. Ilikuwa kazi Ya kifo, kazi ambayo ni lazima wajitoe kafara. Walikuwa tayari kwa kazi hiyo, walikuwa tayari kupambana katika mapambano ya aina yoyote.
*******
Ulikuwa usiku tulivu, usiku ambao ulimkuta mtu huyu katika eneo ambalo mara nyingi sana hupatikani watu fulani fulani. Alitulia hapo kwa utulivu wa Hali ya Juu. Mkononi alikuwa na kikombe kidogo cha Kahawa sambamba na kashata. Alikuwa akipiga fumbo taratibu huku macho yake yakitizama kila mtu ambaye alikuwa akipita karibu na kijiwe hicho. Hakuwa hapo kwa makusudi bali alikuwa hapo kwa kazi maalum. Aliambiwa mtoto wa kwanza wa Rais wa Nchi alikuwa akifikaga hapo kupata kahawa akiwa na marafiki na hata Walinzi wake. Alitulia hapo kanakwamba hakuwa na sababu ya msingi ya kufanya. Punde gari aina ya Land cruiser V8 ikaonekana ikitokea kwa mbali kwa mwendo wa Taratibu ikisogea maeneo yale. Mtu huyu aliyekuwa akimimina kahawa mdomoni akaendelea kufanya hivyo kanakwamba hakuliona tukio la gari hiyo kusogea. Baada ya Gari kusogea Zaidi na Zaidi kisha kuegeshwa. Mlango ukafunguliwa kisha mtoto wa Rais akashuka akiwa sambamba na Walinzi wake pamoja na Marafiki. Baada ya mtoto wa Rais kushuka sambamba na Watu wake. Wakasogea mpaka sehemu fulani ambayo ilionekana kupangwa kwa Ajili Yake. Kabla ya kupelekewa kahawa uchunguzi Ukafanywa kisha ndipo mtoto huyu wa Rais akaruhusiwa. Muda wote mtu huyu alikuwa akitizama kwa hila bila kujulikana. Alikuwa akiwaangalia na walinzi wengine ambao walikuwa wamesimama Barabarani wakionekana kutofuatilia kile kilichokuwa kikiendelea hapo. Mtu huyu hakuwa hapa kwa bahati mbaya, alikuwa hapa kwa kazi moja. Kazi ambayo waliona ndio sahihi kwa wakati huo. Ilikuwa ni Lazima Wampate Mtoto wa Rais Ili kulazimisha waipate betri Hiyo. Aliendelea kunywa kahawa taratibu. Hata mtoto wa Rais alipoingia ndani ya gari, Bado mtu huyu aliendelea kunywa. Hakuwa na Haraka Yakuinuka kwa kuwa Alijua kuna macho yapo sehemu yatizama ENEO HILO.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuwa na Haraka ya kuinuka kwa kuwa alijua kuna mtu yupo sehemu akimtizama. Hata wale watu wawili ambao walikuwa wamesimama umbali mfupi kutoka kilipokijiwe cha kahawa bado hawakuondoka. Walionyesha bado walikuwa na maongezi marefu. Hata Mtu yule naye akakakaa na kuwatizama. Haukupita muda mmoja kati ya watu waliokuwa wakifanya mazungumzo akaaga na kuondoka akiivuka barabara kuelekea maeneo ya Posta mpya. Yule mmoja naye Alikuwa amerudi nyuma akiongoza kama alikuwa akielekea chuo cha Elimu ya Biashara. Mtu huyu alikuwa akiwatizama huku akicheka kimoyomoyo. Aliitambua kasumba ya Wana usalama wengi. Aliitambua staili yao na pia aliitambua aina yao ya maigizo. Kilichokuwa kikifanywa na watu wawili waliokuwa wakizungumza ndicho kitu kilichotoa mwanya kwa Wana usalama wengine kuondoka na mtoto wa Rais. Baada ya kuhakikisha hakuna mtu mwingine wa kumtilia mashaka. Alilipa pesa ya kahawa kisha akainuka na kuiendea Gari yake aliyekuwa ameipaki pembezoni kidogo mwa barabara. Akaingia ndani ya gari, safari ya kuelekea alikopaswa ikaanza. Wakati gari ikiendelea kutembea taratibu, bastard akafungua sehemu fulani ndani ya gari na kutoa kitu mfano wa Saa. Baada ya kukitoa kitu Hicho akaingiza maneno kadhaa. Katika sekunde ile ile kitu kile kikawaka. Akasubiri Kidogo Kisha Akaingiza namba za Gari Iliyoondoka na Mtoto wa Rais. Akaendelea kusubiri huku Gari ikiendelea kutembea. Dakika Tano mbele Kitu kile mfano wa Saa Kikaonyesha Neno Oysterbay block no 451. Bastard akatabasamu na wakati huo huo akakizima kitu kile mfano wa saa. Kwa mara nyingine alikuwa ameingia kwenye mission ya Hatari. Mission ambayo Ina mkutanisha mara nyingine na Wana usalama. Wana usalama wa Tanzania. Kichwa chake hakikusahau mission ya kwanza ambayo ilimlazimu Kusafiri mpaka Nchini Canada. Alikuwa sambamba na MOA, JENIPHER Sambamba Na Neema. Ilikuwa mission ngumu sana kupambana na mashirika makubwa ya Kijasusi Duniani. Ni mkasa ambao ukiwapa Sifa kubwa, Sifa ambayo ilishawishi mpaka mataifa makubwa ya kijasusi kuamba kufanya kazi na watu hao. Mkasa ambao Uligundua Siri kubwa Iliyojificha Nyuma ya Mauaji ya Mke Wa Rais. Leo hii alikuwa amekutana tena na Masimba. Lakini safari hii sio masimba pekee yake, bali alikutana na Veronica. Vero Mwanamke Kutoka Nchini Italy. Veronica Ambaye alikuwa ni mwanachama Mwandamizi wa Kundi la Mafia. Gari akazidi kushika kasi, alihitaji kwenda kumchukua Mtoto wa Rais kwa sababu ya kymshinikiza Baba yake Aitoe ile betri. Alijua ilikuwa kazi ngumu, lakini ilikuwa Lazima Aifanye. Ilikuwa lazima atengeneze hilo. Akalivuka daraja la Salenda. Mbele kidogo akaingia kulia kam anaelekea Masaki. Kufika Mbele kidogo akaingia kushoto na kuingia katika Eneo hilo. Akaongoza mpaka sehemu maalum ya kuegeshea magari. Baada ya kuegesha gari, akashuka akaifunga milango vizuri kisha kusogea mpaka alipomlizi wa Sehemu hiyo. Baada ya kumfikia mlinzi alichomoa noti ya Elfu kumi akamkabidhi mkononi akimuacha mlinzi yule akifurahi. Baada ya kumalizana na Mlinzi, Bastard akatembea kwa kawaida kuliacha eneo hilo. Akatokea kwenye Chochoro moja Ambayo ilimuongoza kuelekea lilipo jengo ambalo aliishi mtoto wa Rais. Hakuogopa chochote kile.
Alikuwa tayari kwa kila ambacho kiko mbele yake. Akaupita uchochoro ule pasipo kutokea rabsha yoyote. Mbele kidogo akauvuka Uzio wa Kiwanda fulani. Baada ya kuuvuka Uzio Huo akajikuta akitizamana na jengo ambalo alikuwa akiishi mtoto wa Rais. Akatulia kwanza akilitizama Jengo lile Kwa Umakini Mkubwa. Macho yake yalikuwa yakitizama na kuhesabu askari ambao walikuwa hapo. Askari wa nne wenye Bunduki walikuwa Geti la mbele sambamba na wana usalama wengine watatu. Upande wa nyuma wa Jengo hili pia walisimama Askari watatu na wengine ambao walivaa kiraia. Akaamua kuhama Eneo hilo na kuizunguka lile Jengo. Muda wote alikuwa akiwatizama walinzi ambao walikuwa mbele yake. Hawa walikuwa wawili tu, huku mmoja akionyesha kuwa Amelala. Akaona hapa ndipo sehemu sahihi ya kuingia ndani Alitaka kuingilia hapo katika namna yoyote ile. Alitambua sehemu ile ndiyo ingeweza kumfanya aingie ndani bila wasiwasi. Akahama Upande ule na kukivuka kibarabara fulani. Baada ya kuvuka hapo. Sasa alikuwa amewakaribia Walinzi hawa wawili. Akatembea Akinyata taratibu, alikuwa akitembea mfano wa chui. Kwa mwendo wa silika akachupa na kutua katikati ya walinzi hawa. Kilikuwa kitendo cha sekunde tu kutendeka. Mlinzi mmoja alikuwa chini akiwa ameshika koromeo. Wakati mlinzi huyu wa pili akikurupuka kutoka usingizini. Akakutana na Ngumi moja ya Shingo iliyompeleka Chini. Wakati mlinzi huyu akihangaika kuinuka, bastard akamuwahi pale chini na kumnyonga Shingo. Baada ya Kummaliza Huyu akageuka kumuendea huyu mwingine. Lakini akakuta Tayari Alikuwa Amekufa. Hapo akaongoza kuelekea kwenye Nyumba hii. Haukupita Muda alikuwa ameshauparamia ukuta na kuingia Ndani. Kitendo cha kutua tu, akaichomoa Bastola Yake. Akaanza kutambaa taratibu kuelekea ndani kabisa ya nyumba. Alitembea akifuata vivuli vya miti. Kufika mbele kidogo akasimama kwenye shina la mti baada ya kusikia sauti za watu kwa mbali. Akatega sikio zaidi na zaidi. Akagundua sauti zilikuwa zikitokea ndani kidogo ya Jengo lile. Akatulia hapo zaidi na zaidi. Punde mlango ukafunguliwa kisha uso wa binti mrembo ukaonekana kuchomoza katika tabasamu tamu. Hakuwa binti pekee bali alikuwa na Mtoto wa Rais. Kila moja alikuaa amevaa pajama wakionyesha kuutafuta ubaridi. Ubaridi ambao hakuujua ni wa nini mpaka pale binti yule aliyekuwa na mtoto wa Rais alipolitoa vazi lile pekee Mwilini. Pale alipobakia kama alivyozaliwa. Alipokewa na Chuchu safi na za kuvutia kama za Mtoto Swahiba. Chuchu ambazo zilifaa kwa kunyonya kulamba na hata kumalizia kwa Shida nyingine. Alikuwa mweupe chuchu zikisimama mithili ya michongoma. Huyu alikuwa ni zaidi ya Shunie na Hata Heaven Sent. Huyu alikuwa Akivutia na kutia hamasa mfano wa Black woman Wa Jf. Alivutia na kutia hamu. Uwanja wake wakuchezea ulikuwa na Majani Madogomadogo ambayo yaliupendezesha na kuufanya upendeze. Ni umbo lililoutatanisha Ubongo wa Mwanaharamu. Umbo ambalo lilisababisha mtafaruku kichwani kwa binadamu huyu aliyelaaniwa. Akatamani aitumie bastola kumuondoa mtoto wa Rais ili akichukue kiumbe hiki. Kiumbe ambacho hakikufanana na Nuru na Hata Mwadi. Huyu alifanana kabisa na Tete. Tete ambaye alikuwa akimilikiwa na Jasusi liitwalo muteba. ( R.I.P Elvis Musiba) akatamani kuitupa bastola yake ilikuwavamia watu hawa aondoke na Binti Huyu. Hata pale binti alipojilaza kwenye kitanda maalum pale nje kisha kuiachanisha miguu yake huku na Huko bado Mwanaharamu alilitizama tukio hili. Hata pale mtoto wa Rais aliposogea na kukaaa karibu ya malaika yule. Bado Mwanaharamu akatulia kanakwamba hakuwa anakiangalia kitendo hiki. Macho yake yakajakubadilika baada ya mkono wa Binti Yule usio na Adabu ulipoingia ndani ya Vazi la Mtoto wa Rais. Mkono ambao ulitulia kwa muda ukitafuta kitu ambacho ulipoteza. Mkono huo ndio uliomkumbusha kuwa alikuwa hapo kwa mission maalum. Yupo hapo kwa Ajili ya kumchukua Huyu mtu. Dakika hii alikuwa ameinuka akielekea pale walipokuwa watu hawa wakifanya ufirauni. Binti mdomo wake ulikuwa ukipanda na kushuka maeneo fulani, wakati mtoto wa Rais alikuwa amesinzia akisikilizia kitu ambacho hakikujulikana. Kutokana na kilichokuwa kikitendeka pale, watu hawa hawakumuona Mwanaharamu alipokuwa Akisogea hapo. Mwanaharamu akatembea na muda mfupi alikuwa Amesimama hatua mbili kutoka Walipo watu hawa. Mdomo wa bastola kumgusa mwanamke huyu ndicho kilichowashtua wote. Mwanamke kuinua Macho yake na kukutana na Mdomo Wa Bastola, akajikuta akipiga yowee. Ni yowee lililoifanya Bastola Ya mwanaharamu Ikohoe. Risasi zikiingia kifuani Kwa Binti Huyu na kumtupa umbali wa hatua kumi na tano. Risasi Nyingine Zikikifumua kichwa Cha Mtoto wa Rais. Hapakuwa na Jinsi zaidi ya alichokifanya. Mipango yake Ilikuwa imevurugwa na Mwanadada huyu. Hakutaka kuupoteza muda. Akataka kuondoka na kutoweka eneo hili. Lakini hakuwahi kufanya hivyo. Akashuhudia wana usalama katika namna iliyovutia. Kuvutia kwa mapambano. Muda huo huo akasikia Risasi zikivurumishwa kuelekea kwake. Hakuchelewa wala kusubiri chochote kitokee. Alikuwa amechupa tayari na wakati huo huo akiachia risasi mfululizo kuelekea walipo walinzi. Risasi Zilivurumishwa bila kukoma. Walinzi hawa hawakutaka kumpa nafasi Mwanaharamu. Mwanaharamu akatambua hapo ilikuwa ni Lazima Aondoke hapo kabla ya wana usalama wengine kufika. Akainyanyua Bastola yake na kuilenga taa. Muda mfupi baadae Sehemu yote ilikuwa Giza. Hapo ndipo alipoinuka taratibu na kutambaa mpaka usawa wa ukuta. Akajivuta Taratibu na kufanikiwa kuanguka upande wa pili. Baada ya kutua salama, akatembea taratibu na giza mpaka fukwe za coco. Kutoka hapo akajichanganya na watu ambao walikuwepo hapo. Kabla ya kurudi kwenye maegesho ya Magari na kuichukua gari yake, nakuondoka taratibu katika eneo hilo. Wakati akijua ameshamaliza kile alichokitenda. Akawaona watu watano Wenye Silaha wakiwa mbele yake. Baada ya kuwafikia mmoja akampa Ishara ya kumtaka asimamishe gari. Mwanaharamu Akatiii!! Akaisimamisha Gari na kuizima kabisa. Akatulia tuli kuwasubiri watu hawa ambao sasa walikuwa wakimsogelea.
Akatulia kuwasubiri watu hawa. Kitambulisho maalum tayari kilikuwa mkononi kuwaonyesha watu hawa. Kitambulisho ambacho kingemuonyesha yeye alikuwa nani katika nchi hii. Watu wale wakasogea huku bunduki zao zikiwa tayari kwa chochote. Mmoja akasogea kwa Tahadhali mpaka dirishani mwa gari ya Mwanaharamu. Kabla Hajagonga kioo Cha Mlango wa gari, kioo kikashushwa.
"Habari yako Ndugu?. Sauti ya Mtu huyu aliyeonekana ndiye mkuu katika kundi hili akauliza. "Salama tu, habari yako!" Alijibu kisha kuuliza. "Tunaomba ushuke tuweze kupekua gari yako." Bila kujibiwa salamu yake amri ikatoka. Wakati bado akifikiria kile cha kujibu. Akashuhudia watu wale waliopembeni wakisogea. Hakutaka kuchelewa wala kuupoteza muda. Kitambulisho kikaonyeshwa. Mkuu yule akakitizama Mara mbili mara tatu. Akakirudisha huku akiomba msamaha kwa kilichotokea. Kitambulisho chake kilichomtambulisha Kama Jasusi Wa CIA kilitosha kuwaaminisha wana usalama hawa kuwa mtu huyu hakuwa mmoja kati ya waliofanya kilichotokea. Bila kujibu akapandisha kioo na kuliondoa gari kwa mwendo wa Taratibu. Tayari mipango yake ilikuwa imefeli lakini kwa kilichotokea alihisi ilikuwa njia bora ya kuwafanya watu hawa waanze kuweweseka. Ingawa nia yake ilikuwa ni kumteka mtoto wa Rais ili kumshurutisha Baba yake aitoe Betri maalum. Lakini hata hili lililotokea halikuwa baya. Halikuwa baya kwa kuwa alijua mapambano ndiyo yatakuwa magumu. Alipenda sana kupambana Kwenye uhatari. Alipenda sana kupambana kwenye ugumu. Na mwisho alipenda sana kuonyesha kuwa yeye alikuwa nani katika medani hii ya kimapambano. Gari ikatembea akipanga muda huu kwenda kuanza kufuatilia Wapi walipopelekwa watoto wa Masimba. Hakutaka kupumzika mpaka pale atakapopata taarifa ya kumuwezesha kufahamu walipo watoto. Alitembea usiku ule akipishana na Askari wa vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na Usalama. Moyoni kwake aliumia sana Baada ya kuwaza kuwa wanajeshi na polisi wetu walikuwa wamejiingiza katika Siasa. Taaluma yao na Sheria zao kama vyombo vya ulinzi walisahau kabisa. Sasa hivi hata Askari walikuwa ni wanasiasa. Aliendelea kuendesha gari huku akiendelea kuumizwa na hilo.
********
Alijiinamia peke yake ndani ya chumba kile cha hoteli. Alikuwa amejiinamia Akiwaza na kuwazua kila kitu alichopoteza kwa kuipigania nchi yake. Alikumbuka watu waliopotezwa na suala hili. Alimkumbuka Marehemu Asteria. Msichana ambaye aliuawa mwanzo tu mwa mkasa huu. Akamkumbuka Dee plus na mama yake mzazi. Akawakumbuka vijana ambao walikuwa wakiteseka katika hilo, vijana ambao waliendelea kuteswa na kuumizwa kwa matumizi ya madawa. Akamkumbuka Teddy kwa mara nyingine. Tukio la kumiminiwa Risasi na teddy likajirudia taratibu. Ni wazi kuwa teddy alikuwa amezamilia kumuua. Ni kweli teddy alikuwa Tayari kumuua. Kama sio kuondoka Eneo husika basi risasi zisizopungua tano zingeuchakaza mwili wake. Kufikia hapo akatulia Zaidi akifikiria. Ilikuwa lazima apambane na ilikuwa tayari aondoke usiku ule kwenda kuianza kazi. Haikuwa sahihi kwake kuendelea kukaa hapo ndani wakati tayari Betri ipo mikononi mwa Rais. Akainuka na kusimama katikati ya chumba. Lakini kitendo cha kusimama akajikuta akipatwa na kizunguzungu. Kizunguzungu ambacho kilimlazimu arudi pale kitandani. Ilikuwa wazi kuwa hawezi kupambana na hawezi kwenda mstari wa mbele. Akarudi kitandani huku akiruhusu chozi lake kushuka. Alikuwa akilia taratibu. Alikuwa akiipigania nchi yake, alikuwa akiwasaidia wananchi wasio na uwezo. Lakini kitendo cha rais kumgeuka kilimtesa na kumsumbua kichwani. Safari hii akawaza kitu ambacho hapo mwanzo hakuwahi kuwaza. Aliwaza kumuua Rais, alipanga kumuua rais sambamba na teddy. Huo ndio uamuzi ambao alioupitisha. Ni Lazima risasi itumbukie kwenye uso wa Rais. Alikuwa tayari kwa hilo. Alikuwa tayari muda wowote. Alimchukia Teddy na pia alimchukia Rais. Hakuona kama Ni kiongozi ambaye angeweza kuliongoza Taifa hili. Akajikuta hali ile ya kupoteza nguvu ikiwa tatizo kwake. Tatizo lakutokukifanya kwa wakati ule ambacho alikipanga kukifanya. Ilimuumiza sana hali ile. Kila alipokuwa akiitizama picha ya rais ambayo iliwekwa ndani ya kile chumba ndipo hapo hasira zilivyozidi kupanda. Alitamani kuinuka muda ule ule kumfuata mtu . Kitendo cha kushirikiana na majasusi wa CIA na serikali ya marekani kuwaharibu wananchi kilikuwa kitendo ambacho alikichukia. Kitendo ambacho kilitokea kumuona kiongozi huyu wa nchi kuwa hapaswi kuishi pamoja na Teddy na hata Jimmy. Wakati akiliwaza hilo pale chumbani mara akashtushwa na Taarifa kutoka kwenye TV pale chumbani. Taarifa iliyokuja kama Habari mpasuko (Breaking news) kwamba Mtoto wa Rais alikuwa ameuawa kwa kupigwa Risasi kichwani akiwa na Mpenzi wake. Habari ikaongeza kuwa muuaji aliufanya unyama huo wakati walinzi wa mtoto huyo wa Rais wakiwa ndani. Kwa Taarifa Zaidi endelea Kufuatilia HANDENI TV kukujuza kila kitakachoendelea Hakuamini macho yake na hata masikio yake. Ingawa kifo hakifurahiwi lakini kwa mara ya kwanza Masimba akatabasamu. Akatabasamu akitingisha kichwa. Akajua hii ilikuwa kazi ya mwanaharamu, alijua hii ilikuwa kazi ya mwanaharamu huyu aliyelaaniwa. Akauona ushindi kwa mbali ukijisogeza. Kumuua mtoto wa Rais ulikuwa ujumbe tosha kwa Serikali na Vibaraka wake. Hakuna Ujumbe mzuri na mtamu katika vita ya Akili kama Ujumbe wa Damu. Sasa Rais alikuwa ametumiwa Ujumbe wa kumwambia Bado mapambano yanaendelea. Akajilaza kitandani Taratibu Akiwa katika tabasamu mwanana. Alitamani apone ili amkabili Teddy, alitaka kumuua Teddy kwa Mikono yake mwenyewe. Mkono uliomuua Waziri mkuu ndio Mkono ambao utamuua Teddy. Ilikuwa ni lazima Teddy Afe. Ni lazima betri ipatikane kuwaokoa vijana wanaoendelea kupotea. Kuliwaza hilo kwa muda likamfanya aukumbuke mzigo wa madawa wa mamilioni ya Shilingi aliyoyachukua Mikononi kwa watu hawa. Ilikuwa ni lazima akauone na Kuupata. Lakini hakutaka kuwa na Haraka Zaidi ya kuivuta subira. Ni kweli alitulia ili kuivuta subira.
*****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Paja zake nzuri zilikuwa wazi zikionekana pasipo na kificho. Alikuwa ametulia pembezoni mwa ukumbi wa msasani club akipata vinywaji huku kivazi chake kifupi kikiyavuta macho ya wanaume wakwale. Macho ambayo hayakuondoka katika paja za mwanamke huyu ambaye hakujali kutizamwa. Kunawakati alikuwa akiiachia miguu yake makusudi na kusababisha hata nguo yake ya ndani kuonekana. Aliumbwa akaumbika, alipewa na kulidhika na hata kupendelewa na kukubali. Alikuwa na macho mazuri na yakuvutia katika Usiku. Midomo na Dimpoz zake unaweza kumfaninisha na mwanadada mwenye umbo tamu Kama Tumosa. Miguu yake ilipendeza na kuvutia. Bado macho ya Wanaume Wa Kwale yalikuwa Yakipita Juu ya paja zile. Wanaume ambao walikuwa wakipagana vikumbo kwa macho kumtizama mwanadada yule. Hakuwa mwingine huyu kiumbe, bali alikuwa Veronica Senka. Alikuwa hapo kwa sababu ya kumhitaji Jimmy Lambert. Alikuwa hapo akitaka kuipeleka tiketi kwa mtu huyu. Mtu huyu ambaye mkono wake ulikuwa na watu hawa. Mtu huyu ambaye aliubadilisha ubongo wa Mtoto Wa Kipare. Mwanaume huyu ambaye alikuwa jasusi wa kutupwa akitumika kama wakala wa Siri wa CIA. Alikuwa hapo akiamini mtu huyu hawezi kukosa kufika hapo. Akaendelea kujiachia akionyesha kutokujali. Kila wakati alikuwa akitizama saa yake. Wakati hilo likiendelea, punde akaonekana mhudumu wa Mahala pale Akisogea pale alipokaa. Veronica Akafanya kama hakumuona, akaendelea kumimina kinywaji kinywani. Mhudumu yule alipofika akauonyoosha mkono na kumkabidhi Veronica kikaratasi kidogo. Bila kuongea kitu Veronica akakipokea kisha kukikunjua pale pale. "Nakuomba Hapa ndani." Ni maandishi yaliyoandikwa yaliyomfanya atabasamu. "Ananiomba Niingie ndani? Lilikuwa swali ambalo hakutaka kulijibu. Akainuka na Bia zake mbili mkononi Taratibu Akasogea sehemu ambayo alitakiwa. Baada ya kufika kwenye meza hiyo ambayo alikuta imekaliwa na kijana mmoja mmoja hivi, Veronica Naye akakaa hapo muda huu akionyesha kuyumba. "Karibu Mrembo wangu karibu sana." Alitamka kijana yule akimpa mkono Veronica. Veronica Akaupokea mkono, kisha kwa sauti ya kilevi akanena. "Ahsante Sana Kijana mzuri wa Sura. Inaonekana hata kitandani uko vizuri." Maneno hayo yalimfanya kijana huyu atabasamu, tabasamu la kuvutia ama kufurahishwa na maneno yale.
"Hapana mrembo, miye kitandani nipo sifuri kabisa."akajibu tena huku akiushika mkono wa Veronica. "Mh!! Wifi ndiye anaujua ukweli." Akajibu Veronica huku kwa mara nyingine akitupia jicho kwenye Saa yake. "Naitwa ADK, ni mfanyabiashara wa Mahindi na maharage. Naishi mikocheni." Akajitambulisha Kijana Yule. "Naitwa Rehema, naishi Mwananyamala kisiwani. Akajibu Veronica Huku mara hii akiruhusu macho yake ya kurembua yamtizame Kijana huyu. Ni kweli macho yao yakaangaliana. Tofauti na kijana huyu kusema kuwa anafanya biashara, veronica aligundua kitu kingine kabisa machoni mwa kijana huyu. Alikutana na macho ya Ulaghai, macho yanayotambulisha kitu kingine kabisa. Macho yanayomwambia kuwa Mtu huyu ni Mmoja wa watu wale ambao hawakutakiwa kujulikana. Yaani alikuwa jasusi wa kutupwa. Kingine ambacho Veronica kilimvutia kwa huyu kijana ni kule kuyapeleka macho yake sehemu fulani katika namna ambayo Kama ungekuwa Mtu Wa Kawaida basi usingegundua kitu. Ni Sehemu Hiyo ambayo ilimpasa hata yeye kutizama huko. Kutizama katika namna ambayo mtu huyu hakuwez kung'amua Chochote kile. Ni hapo alipomuona Yule ambaye alimhitaji. Alimuona Jimmy Akiwa ametulia pembeni kabisa mwa ukumbi Ule. Taratibuuu Akatabasamu. Tabasamu ambalo halikugundulika machoni kwa kijana huyu aliyejipachika ufanya biashara. "Sawa bibie Rehema, naweza kusema leo nina Bahati kubwa sana kukutana na wewe." Baada ya kuongea hilo akapiga fundo moja la bia kisha kuitua glasi pale mezani, kisha akaendelea. "Licha ya kuwa na bahati hiyo, lakini naona bahati hii ni ya bosi wangu." Alipomaliza kuongea Hilo akamuangalia Veronica usoni. Kwa kujua kuwa mtego wake ulikuwa unakwenda kunasa. Veronica alikuwa amelilegeza jicho na hata miguu. Akatuliza macho yake machoni kwa kijana yule. Akamuona kijana alivyokuwa akihangaishwa. Hakujua kuwa alikuwa Akiongea na mtu hatari, hakujua kuwa alikuwa akiongea na Mtoa Roho. Vero akaruhusu macho ya kijana huyu yaendelee kukiona kile alichokikusudia. Hilo ndilo lililompa kile ambacho alikuwa akikihitaji. Punde akamuona Kijana yule akiinuka huku mambo yakiwa sio mambo.
Zijapita kama dakika mbili pasipo mtu huyu kurudi. Wakati akilishangaa hilo. Akamuona yule yule mhudumu wa kwanza akisogea pale mezani kwake. "Unatakiwa Uingie Upande Wa Nyumba ya Kulala Wageni. Nifuate." Aliongea mhudymu yule huku akigeuka kuelekea kule ndani. Veronica hakuchelewa. Muda huu alikuwa amesimama akimfuata Mwanadada yule kwa nyuma. Macho yake yalikuwa yakizunguka huku na huko kuona kama alikuwa akisindikizwa. Ni kweli alikuwa akisindikizwa, akisindikizwa na macho ya wanaume wa kwale. Katika macho hayo kulikuwa na macho mengine ambayo hayakumuangalia kama macho ya wengine. Haya yalikuwa macho maalum. Macho ambayo Yalitaka kitu tofauti zaidi ya mapenzi. Veronica hakujali. Akaongoza ndani akitembea kwa Mwendo wake Wa pozi.
********
Alisimamisha gari kwenye maegesho ya Magari Nje ya ukumbi wa Msasani. Akashuka na kuufunga mlango kisha kuongoza kuelekea pembezoni mwa ukumbi. Wakati akikaribia sehemu husika. Akamuona Veronica akiwa amejiachia. Hapo akagundua Veronica alikuwa kwenye mtego. Alikuwa kwenye mawindo. Mwanaharamu akamkwepa kwa kupitia upande mwingine. Hakutaka waonane na Veronica. Alitaka kufuatilia ama kukiona kile alichokiona veronica. Wakati akiendelea kutulia upande tofauti na Veronica. Macho yake yakamuona Jimmy akiwa sambamba na mtu mmoja pamoja na mhudumu. Hazikupita hata sekunde thelathini akamuona Mhudumu yule akisogea sehemu aliyokuwa amekaa Veronica. Mwanaharamu bado aliendelea kutulia hapo. Hata pale alipomuona Veronica akiingia kwa ndani. Hata yeye akafanya hivyo. Hata pale alipokuwa akiongea na yule kijana, bado mwanaharamu aliendelea kumuangalia tu. Wakati kijana yule alipoinuka na kumuacha Veronica pale. Hata Mwanaharamu naye akasimama. Wakati kijana yule anampita Jimmy na kumpa ishara fulani. Mwanaharamu Alishuhudia kila kitu. Akatambua kuwa Hapakuwa na Usalama upqnde Wa veronica. Ilikuwa ni lazima afanye kitu. Ni kweli alikifanya. Punde tu alikuwa akitembea sambamba na kijana yule aliyekuwa akiongea na Vero.
punde alikuwa akitembea sambamba na kijana hiyu. Kijana ambaye hakujua mtu aliye hapo nyuma yake alikuwa nani. Ni muda huo huo wakati hawa wakitembea sambamba wakiingia ndani, ni wakati huo ambao Veronica Alikuwa akiinuka naye akaongoza kuelekea ndani alikoambiwa aelekee. Bastola zake mbili zilikuwa sehemu fulani katika mwili ule. Alikuwa akitembea akionyesha kutokuwa na wasiwasi. Kuonyesha kutokuwa na kitu chochote cha kuhofia. Veronica alitembea kanakwamba alikuwa ndani ya sebule ya nyumba yake. Hakuogopa wala hakuwa na mashaka, achilia mbali hofu. Hakuiona hofu, hakuuona Woga. Alikuwa tayari kwa chochote kile. Aliivuta miguu yake akizihesabu hatua zake, macho yake yalikuwa mbele yasimpotee yule kijana aliyeambiwa amfuatilie. Alihakikisha hafanyi makosa kwenye hili. Ni wakati akiangalia akamuona mtu akijiunga kwenye msafara wa kijana yule. Akitembea nyuma kidogo ya kijana yule. Hilo likampa fikra katika kichwa chake, mstari wa uhatari ukapita kichwani na tabasamu likashuka usoni. Naam! Alikuwa akiangaliana na Mwanaharamu, Mwanaharamu ambaye waliachana mahali akimuaga kuwa anakwenda kumfuatilia mtoto wa Rais. Lakini dakika hii alikuwa akimuona hapa tena akiwa sambamba na Mshenga wake. Mshenga ambaye alitumwa kama kiunganishi na mtu huyu ambaye walimhitaji na kuihitaji Roho yake. Hilo likamshangaza Akiamini kuwa Binadamu huyu aliyelaaniwa Anaweza kuharibu mipango yake. Lakini haikuwa Hivyo, punde akamuona Kijana yule akiingia kwenye chumba kimoja kati ya vitatu vilivyosehemu moja. Lakini mwanaharamu akapita akikifuata chumba kingine. Alama ya dole gumba katika kificho likauzindua Utimamu Wa Veronica. Sasa Alitambua kuwa Walikuwa katika kazi Moja. Ni hatua tano kutoka chumba alichoingia kijana yule pua zake zikainasa Harufu ya Manukato. Kabla hajajua nini kinafuata akauona Mkono wa mtu ukikishika kiuno chake. Mtu huyu hakuishia kukishika kiuno tu, bali mkono ukashuka kidogo na kuligusa paja kabla ya mkono kuanza kupanda juu kuliko kosa Adabu. Veronica Hakuonyesha Kujali. Ndiyo kwanza alikuwa amejilegeza huku akijitahidi mkono ule usifike kule ambapo alihifadhi Bastola yake. Mtu huyu akamlazimisha watembee wakielekea katika chumba kile. Mlango ulikuwa wazi na alitakiwa aingie Ndani. Veronica Hakusita. Alimhitaji Jimmy na Aliihitaji Roho ya Jimmy. Akamtii kama Ngamia anavyotii pale anapotakiwa kuchinjwa. Hata pale mkono wa Jimmy ulipokuwa Unagusa urembo ule wa Kiafrika uliopangiliwa kiunoni. Bado Veronica Hakuleta fujo na Hata kutulia. Wakaingia ndani kisha mlango ukasindikwa na kufungwa kwa Ndani. Veronica Akajikuta Akitupwa Kitandani na kwenda kuangua Chali. Miguu yake haikutaka tena kuzuia kile ambacho Jimmy alikitaka. Alihitaji kumlegeza Jimmy Hatimaye kumuua. Punde akamuona Jimmy Akiuvua mkanda wa Suruali yake. Punde akaiona Suruali ya Jimmy ikifika Magotini. Veronica Bado Alijigeuza Huku na Kule. Bado alikuwa akiichanua Miguu yake kumtega Jimmy. Jimmy akavutika kwa paja lile la Veronica. Macho yakamtoka na tamaa kumuingia. Veronica alikuwa akimsoma kwa Umakini Mkubwa. Hakutaka kufanya kosa lolote. Alitambua kosa lolote ambalo angelifanya lingemghalimu Maisha Yake. Alihitaji kumuua Jimmy katika Namna Impendezayo. Aina ambayo aliipenda yeye. Bado alikuwa amejilegeza akimsubiri Jimmy apande kitandani. Jimmy Naye akasogea na kujilaza kwa pembeni.
Lakini katika namna ambayo hakuitariji. Akauona Mkono wa Jimmy Ukiwa na kitu cha moto. Jimmy alikuwa na Bastola mkononi. Bastola ambayo tayari mdomo wake uligusa mbavu za Veronica. Hilo likaonyesha kumgutusha Veronica. Akili alitaka kuanzisha labsha. Lakini hilo akalipinga, alihitaji utulivu. Alihitaji kuutumia mwili wake kumpumbaza Jimmy. Akatulia Tuli akimuangalia Jimmy kwa macho yake malegevu. Macho ambayo yalikuwa na uwezo wakumlevya wa Aina Fulani. Macho haya yalifuatiwa na mkono wa Vero kuushika mkono wa Jimmy na kuupeleka katikati mwa Mlima usambara.. mkono wa Jimmy ukatulia hapo katika namna ya kucheza na mlima huo. Mlima ambao ulipendezeshwa na kizibo kile cha Asali kilichofiti. Veronica Alitaka kuhakikisha Jimmy anakamatika kiurahisi. Akaulazimisha mkono ule uendelee kutalii mahala hapo. Ukigusa hiki na kugusa kile. Punde mkono ule wa Jimmy ukaanza Kukishusha kizibo kile Cha Asali. Bastola bado ilikuwa imenyooshwa kwa Veronica ambaye bado alikuwa katika uigizaji mkuu. Uigizaji wa Kupendezwa na kilichotendeka. Ndani ya Dakika moja Tayari nguo ile ilishafika Miguuni. Sasa Jimmy alikuwa akipanda kifuani Huku Bastola Ikiwa kwenye paji la Uso la Veronica. Jimmy hakuonyesha tabasamu licha ya kuonyesha tamaa. Wakati akiishusha bukta yake Tayari kwa kitendo kinachofuata, mlango ukagongwa. Jimmy Akageuza Shingo.... Hilo lilikuwa kosa kubwa, kosa ambalo hakutakiwa kulifanya katika maeneo yale. Kitendo cha kugeuka kilimpa nafasi Veronica Kuachia mateke matatu ya haraka Ambayo yalimtupa Jimmy Huku na Bastola yake kule. VERONICA akachupa na kutua Chini. Mkononi Alikuwa amekamatia Bastola Akitembea Taratibu pale alipoangukia Jimmy ambaye kwa wakati huo alikuwa Akijizoazoa. "Jimmy Lambert NSA special Agent.. Kutana na Veronica Senka Mafia Special Agent. Aliongea Veronica Akitembea taratibu ndani ya Chumba kile. "Uroho wenu na tamaa zenu ndio zimewafanya mkubali kuwaharibu vijana wengi wa Tanzania. Tamaa Yenu ya kumiliki utajiri mkubwa ndio umewafanya hata watu waliopewa Madaraka makubwa ya kuongoza nchi. Kufanya mambo ya ajabu yasio na Ubinadamu. Mtambo ambao uliletwa hapa nchini na serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wenu sambamba na Nyie Vibaraka. Umeharibu Mamia na maelfu ya Vijana hapa nchini. Sasa nimekuja hapa kuichukua Roho Yako. MASIMBA ndiye amenituma kujakuichukua Roho yako. Aliongea Veronica Huku Bastola ikiwa imetangulia mbele. Hakuwa na masihara na wala hakuonyesha chochote usoni. Uso wake ulibeba matamshi yake. Uso wake ulibeba kile ambacho alikuwa akikinena. Jimmy Aliyekuwa Amesimama akitweta hakuwa na namna. Alikuwa akikiona kifo machoni mwake. Alikuwa akikiona usoni na hata machoni kwake. Mdomo wa bastola ulikuwa ukimtizama yeye. Bastola ambayo ilikamatwa vizuri mikononi kwa Mtu huyu. Wakati Veronica Akiendelea kumuangalia Jimmy, Taratibu Akamuona Mwanaharamu Akiingia taratibu. Aliingia katika aina ambayo ilimshangaza na kumuogopesha Jimmy. Bila kutegemea Jimmy akajikuta akiropoka pale macho yake yalipotizamana na Macho ya Mwanaharamu. "Bastard!!!!???. Licha ya kuita lakini hakujibiwa. Hakujibiwa kwa Mdomo bali kwa Risasi Ya jicho. Risasi ambayo ilikifumua kisogo cha Jimmy. Hilo halikutarajiwa Na Veronica. Hakulitaraji Kabisa. Alishawahi kuwaona Mafia wakiua lakini Hiki alichokuwa Akikiona kwa Bastard kilikuwa kitu ambacho kilimsisimua. Hakutaka kumuacha Mwanaharamu Amuadhibu Jimmy. Naye alihitaji kuipenyeza Risasi Kichwani Kwa Jimmy kwa Ajili ya Masimba. Muda huu Risasi Mfululizo zilikuwa zikiingia Kwenye Mwili Wa Jimmy Lambert. Na huo Ndio Ukawa mwisho Wa Jimmy. "Okota Nguo yako tuondoke Haraka." Mwanaharamu Akamwambia Veronica Huku akicheka. Kwa aibu za Kike Veronica akaiokota nguo yake kisha bila mwanaharamu kutarajia, Veronica Akavaa pale pale mbele ya macho ya Mwanaharamu.
*******
Mipaka yote ilikuwa imefungwa, viwanja vya ndege havikuruhusu ndege kuruka. Anga ilikuwa imezibitiwa Huku ndege za jeshi la wana Anga zikionekana kuzunguka Anga lote. Vizuizi viliwekwa kila mahala katika barabara. Mabasi na magari makubwa ya mizigo hayakuachwa hivi hivi. Kila gari lilikuwa likipekuliwa na kukaguliwa. Watu walikuwa wakiangaliwa zaidi ya mara tano na Hata sita. Mtu mmoja alitizamwa na hata kuangaliwa na macho laki moja. Kila jicho lilimtizama na kumsoma. Kila Jicho halikumuacha katika aina yoyote ile. Walitizamwa na kuangaliwa sana. Askari walisambazwa kila mahali. Taarifa ya kifo cha mtoto wa Rais ilikuaa imesambaa kama Upepo. Amri ya kuzuia magari na ndege kutokusafiri ikatolewa katika uharaka unaotakiwa. Nyumba za kulala wageni safari hii hazikuachwa kabisa. Hata zile bubu zilikuwa zikivamiwa na kupekuliwa. Mitaa Yote ya Tungi Ilikuwa haiangaliki kutokana na uwingi wa wana usalama. Tokea kifo cha mtoto wa Rais kilipotokea usiku ule, tayari vijana kadhaa walishakamatwa kila upande wa Tanzania. Wana usalama walikuwa wakihaha kila upande nia ikiwa ni kumpata Muuaji ambao wao walijua ni Masimba. Licha ya kuwakamata vijana Hao lakini Tageti yao haikuwa hivyo. Kila saa Simu za Siri zilikuwa zikipigwa kila upande wa upekuaji ule. Msisitizo wa masimba kuuawa ulikuwa ukitolewa katika kila simu ambayo ilikuwa ikipigwa. Neno apigwe risasi kabla ya mahojiano ndiyo amri iliyotawala katika kila wale wote walioshiriki upekuzi Ule. Magazeti nayo hayakuwa Nyuma katika Kuripoti tukio lile. Kila gazeti lilikuwa na kichwa cha habari kilichosheheni habari zilizochambuliwa. "MTOTO WA RAIS AUAWA AKIWA NA HAWARA." Kilikuwa kichwa cha Habari chw Gazeti la HANDENI LEO. Chini kukawa na maandishi madogo yasemayo. "Inasemekana mpelelezi mashuhuli Tanzania ndiye aliyefanya Mauaji Hayo". "MTOTO WA RAIS AUAWA KINYAMA. ALIKUWA NA HAWARA." hili lilikuwa Gazeti La Mwananchi. "WHAT GOES AROUND COMES AROUND" hili lilikuwa Gazeti la JAMII FORUMS LEO. hili ndio gazeti pekee lililogusa na kuchambua habari yote kwa kina. Mwandishi alionyesha kulijua Hili kwa undani. Akaingia Ndani Akiuandika mgogoro kati ya mtu anayetuhumiwa. Aliuandika mgogoro tokea pale ulipopotea mzigo wa madawa. Kuuawa kwa Asteria Sambamba na watu wengine. Kuuawa kwa Dee Plus, sambamba na Salha Lema. Alidadavua hata kifo cha mama wa masimba huku akiongeza na kunusurika kuuawa kwa masimba mara kadhaa. Tena wakitumiwa Watu wanne. Akiwemo mpenzi wa Masimba Aitwaye Teddy. Gazeti hili lilimfunua kila mtu ambaye alihusika. Mwisho likamaliza kwa Kusema. "Kuruhusu masimba kufa ni sawa na kuruhusu vijana wote wa Taifa Hili kuangamia. Tusiruhusu hilo litokee." Lilimaliza gazeti hili huku mwandishi akionekana ni mwenyekujua Mengi ambayo yanaendelea katika sakata la mauaji ya mtoto wa Rais. Ni habari ambayo iliwapendeza wasomi wengi Wasomi wengi waliisoma ile Habari kwa Utulivu Mkubwa. Kila mmoja akausoma mstari kwa mstari. Wanasiasa nao wakaichukua Habari ile wakijiapiza kuipeleka Bungeni ili kwenda kujadiliwa kwa Maslahi mapana ya Nchi. Maswali mengi yalijengeka vichwani mwao kuhusu kilichoandikwa. Kwa nini Huyu Mpelelezi aliyekuwa akililetea Sifa Taifa letu leo anataka kuuawa. Ni hili lililowafanya wabunge kumhitaji Masimba kwa Udi na Uvumba. Walihitaji kumuona, walihitaji kufanya Mahojiano. Hawakujua kuwa Masimba kwa wakati huo alikuwa Amelikamata Gazeti La JAMII FORUMS LEO. Alikuwa akiipitia Habari ile kwa Umakini. Akiusoma Mstari kwa Mstari. Akisoma kwa vituo na kuweka Alama kwa sehemu ambayo alihisi hakuwa ameelewa. Alimsoma Mwandishi Yule katika Namna ya kutaka kumjua. Kichwani kwake Alitambua aliyeandika Hakuwa Mwandishi Wa Habari Wa Kawaida. Hakuwa Mwandishi Wa Habari Za Uchunguzi Kama Marehemu Josephat Isango. Huyu alikuwa ni Jasusi tena Jasusi Wa kupindukia. Jasusi ambaye alionyesha Kulijua Hili Suala kwa Undani Zaidi. Akaitizama Tena na tena Habari ile. Akiuangalia Uandishi ili kumtambua aliyefanya kazi hiyo. Ni kitu kilichomchukua dakika kumi kumgundua Mwandishi wa Habari hii. "CHIEF" ndio neno pekee alilotamka huku akitabasamu. Chief ndiye aliyekuwa ameifanya kazi ile. Chief ndiye mwandishi Wa Habari Hii Mfano wa Makala. Akatabasamu na kutabasamu. Kitendo cha kugundua kuwa Mzee Godliving Kimaro Yup0 Hai kulimpa furaha sambamba na Tabasamu. Alitambua kwa maandishi yale na mapambano yanayoendelea. Basi Muda sio Mrefu vita hii itafika Mwisho. Baada ya kuisoma ile habari, taratibu Akainuka kutoka pale kitandani na kusimama. Akajionyoosha kidogo mwili wake. Akauona Uzima wa Mwili wake. Muda huu alikuwa ameamua kuupasha mwili Wake. Aliamua kuunyoosha Mwili wake kwa Mazoezi Makali. Alikuwa amerudi kwenye utimamu wa Mwili na Akili. Katika Utimamu wa kimapambano. Baada ya kupasha mwili wake akaelekea Bafuni Kujimwagia Maji. Taratibu akawa anayaacha Maji ya mwagike Huku akimuwaza Teddy. Alikuwa Tayari kumuua kwa Mikono yake. Tukio la kummiminia Risasi Mfululizo ndani ya chumba alichokuwa Amefungiwa. Kulimpa Jibu Kuwa Teddy Hapaswi Kuishi.. Teddy Hapaswi kuachwa Hai. Na Sio Teddy tu, Hata kichwa Cha Mkuu Wa Nchi ni lazima Kiondoke. Ni lazima aelekee kule walikoelekea Masikini wote waliokufa kwa njaa Sababu ya Mikataba Mibovu sambamba na Waathirika Wote wa Kemikali iliyonyunyiziwa kwenye Madawa. Baada ya Kumaliza Kuoga, akatoka Bafuni. Akajifuta Maji. Baada ya Hapo Akavaa Mavazi Yake kisha akaanza kutoka ndani ya Chumba. Wakati Akiukaribia Mlango.. Akausikia Ukigongwa. MASIMBA AKATULIA HUKU MKONO UKISHUKA PALE ALIPO HIFADHI BASTOLA YAKE.
Wakati akiukaribia Mlango, akausikia ukigongwa. Akatulia huku mkono wake ukishuka mahala alipohifadhi Bastola. Bado mgongaji alikuwa akiendelea kugonga zaidi na zaidi. Bado hakuitika na bado hakusogea. Mgongaji naye akaongeza ugongaji katika Namna ambayo ilianza kuamsha kengele za Hatari Kwenye Kichwa Cha Masimba. Akautoa mkono pekee pasipo na Bastola,kisha akausogelea Mlango na kutaka kuufungua. Lengo lake halikukamilika.. ni muda ule ule mlango ulipopigwa kikumbo watu wanne wenye bastola wakiingia ndani. Hawakuujua wepesi wa mtu huyu, hawakuujua Wepesi wa Masimba. Kilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua tayari bastola ilikuwa mkononi na wakati Huo huo Bastola akiruhusu kutoa cheche. Watu wanne Walikuwa Chini Wamelaliana. Meneja wa Hoteli aliyefuatana na watu hawa alipoona Kilichokuwa kikifanywa. Akataka kukimbia, kukimbia ajiokoe na Hata kukimbia Kwenda kuitoa Taarifa. Hakujua kitendo Hicho kingempa Tiketi na Nauli yake. Ni kweli Hakufika Hatua mbili kutokana na uzito wa Mwili wake. Risasi zikakifumua kisogo na kuuruhusu Ubongo kuruka na kuichafua Korido yote. Kwa kuwa Bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti.. Tukio lile halikufika popote kwenye Masikio ya Watu. Masimba akaondoka hapo kama mtu wa kawaida. Alirudi mpaka mapokezi na kuukabidhi Ufunguo. Akaondoka Taratibu Akitabasamu na kutamani kucheka. Wana Usalama waliokuwepo nje hawakumuona kwa kuwa kutoka kwake ndani ya hoteli kukafuatiwa na kitendo cha kusimama kwa gari miguuni mwake. Kioo kikashushwa huku sura ya binadamu aliyelaaniwa ikitamalaki. Masimba hakuuliza. Akajipakia Kwa Haraka na Muda ule ule gari ikaondoshwa kwa mwendo wa kawaida. "Vipi Kiongozi umepona? Akauliza Mwanaharamu huku akiendelea kuendesha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nimekufa ndio maana Unaniona Hapa. " akajibu Masimba na kusababisha wote waangue kicheko. "Yuko Wapi Veronica? Aliuliza Masimba huku akijitahidi kutizama kwa Dirishani kuangalia kama Wanafuatiliwa. "Anafuatilia Sehemu waliopelekwa watoto sambamba na Mzee Raymond. Kuna fununu kuwa CHIEF yupo mahala salama sambamba na watoto." Akajibu Mwanaharamu.
"Kwahiyo Chief, Mzee Raymond na Watoto wapo sehemu moja?" Akauliza Masimba akionyesha uso wake kubadilika. "Tunahisi hivyo, isitoshe leo nimemsoma Chief kwenye Gazeti la JAMIIFORUMS LEO." Akajibu mwanaharamu akiendelea kutabasamu. "Hata mimi nimemsoma na kumuelewa. Naomba nipeleke Tabata. Kuna sehemu lazima nifike kwa wakati huu. Pia Itabidi ukitoka kunipeleka huku nakuomba nenda kwenye mazishi ya Meja Jenerali Luois Chomboko. Unaweza kunusa ama kupata cha kutusaidia. " akajibu Masimba.
"Ahsante Mkuu nimekuelewa. Ila ningekushauri upumzike Mpaka kesho ndipo uianze hii kazi." Akajibu Mwanaharamu na kutoa Ushauri.
"Bastard umenisahau leo?" Akauliza Masimba akimtizama usoni.
"Hakuna Jasusi yoyote asiyekufahamu wewe. Kila mmoja anakujua kwa sifa kedekede. Najua kilichokichwani kwako ni Kumuondoa Teddy. Nakuruhusu kulifanya hilo. Lakini nasikitika kusema kuwa Veronica Amekusaidia kumuondoa mmoja. Jimmy Yupo Safarini kuelekea kuzimu." Aliongea Bastard katika Mzaha Ambao ulipokelewa na Masimba katika namna ya kutabasamu. Ni kweli alikuwa ameshangazwa na Veronica. Kitendo cha kumuua Jimmy Hakukitarajia kabisa. Masimba akageuza macho tena kumtizama Mwanaharamu. Lakini akamkuta mwanaharamu akikitizama kitu, kitu ambacho kilimfanya atizame kule. Masimba naye akapeleka macho sehemu hiyo. Gari moja aina ya Noah Ilikuwa ikitembea Taratibu sambamba na wao. Ilikuwa ikionyesha kuwa wanafuatiliwa kwa nyuma. Hilo halikumpa Hofu Masimba na hata Mashaka katika uso Wa Mwanaharamu. Muda wote binadamu huyu aliyelaaniwa alikuwa akitabasamu kuonyesha kufurahishwa na kile alichokuwa akikitizama. Walipofika maeneo ya Ubungo mataa wakaacha barabara ya Mandela, wakaingia Barabara ya Morogoro. Walipoiangalia ile Toyota Noah Bado ilikuwa nyuma ikiwafuatilia kwa mbali. Kufika Maeneo Ya kimara Bucha. MASIMBA AKAMWAMBIA MWANAHARAMU achepuke kwenye barabara kubwa, aingie Barabara ya Vumbi. Bastard akafanya hivyo.. Wakati wakiingia Hapo kwa mbele yao kukawa kuna gari kubwa lililobeba Kontena lilikuwa likitaka kupita. Bastard akaliwahi kabla halijaingia barabarani. Wakapita huku nyuma wakilianya gari ile Ikiziba barabara na Kusababisha Noah Ile Kushindwa kupita. "Simamisha Gari hapo Gereji." Aliongea Masimba. Mwanaharamu Akaingia Upande Wa Kushoto Wenye Gereji na kuisimamisha gari.
Wakati mwanaharamu Akiiweka gari Vizuri Masimba alikuwa tayari yupo Chini akitembea taratibu kurudi kule nyuma. Bastard hakujiuliza Mara mbili. Hata yeye Alijua nini ambacho Masimba alihitaji kwenda kufanya. Hakuchelewa kushuka. Muda huu alikuwa sambamba na Masimba lakini kila mmoja akionyesha kutokumfahamu mwenzake. Walitembea sawa lakini pasipo kuongeleshana wala kuonyesha kuwa walikuwa wakijuana.
Macho ya Masimba yalikuwa yakitizama pembeni kiasi, huku macho ya mwanaharamu yakiwatizama mafundi gereji waliokuwa hapo wakihangaika na kutengeneza magari. Wakati mwanaharamu akibadili uelekeo kuelekea pembeni kidogo mwa barabara waliotokea. Akaiona Ile Noah kwa mbali ikiwa imesimama pembezoni mwa barabara huku mtu mmoja akiwa ameinama akitizama kitu. Wakati huyu wa Pili alisimama akionyesha kuongea na yule aliyeinama. Wakati mwanaharamu Akiendelea kuwaangalia watu wale waliokuja na Noah. Mara akamuona Masimba akitokea Nyuma ya Ile Noah. Hilo kwanza halikutegemewa na Mwanaharamu. Akasimama kwanza kutizama kile ambacho kingeendelea Hapo. Alimuangalia masimba alipokuwa akitembea. Akipiga hatua kuelekea mahala hapo. Mahala ambapo walisimama hawa watu Wawili. Akasogea kana kwamba alikwisha zoeana na Watu hawa. Hata alipowafikia na kusalimiana nao, bado watu hawa walikuwa wakimtizama, walikuwa wakimwangalia katika namna ya mshtuko na Fadhaa. Wakati hawajajiandaa katika hilo, Wakamuona mtu wa pili akisogea hapo. Huyu alikuwa Mwanaharamu. Huyu alikuwa mtu mwingine kichaa kuliko wengine.
********
[06-27, 19:40] Ibrahim Masimba: Alikuwa mwanaharamu aliyelaaniwa. Huyu alikuja kama mtazamaji mahala hapa. Sio utizamaji wa macho tu. Ni utizamaji wa kutumia mdomo sahihi wa Bastola. Kuwaacha watu hawa ulikuwa ni mwiko kwao. Safari hii watu hawa walikuwa wakitizamana na watu hawa wengine. Sura ya masimba na sura ya Bastard hazikuwa sura ngeni kwao. Hazikuwa sura wasizozijua. Licha ya kuwajua huko lakini haikuondoa Sheria kufuata mkondo Wake. Bastola kutoka sehemu fulani ya Mwili wa Mwanaharamu, ulikuwa imeshikwa sambamba na koti kuwafanya watu wasishuhudie kilichokuwa kikiendelea. Lakini pia hawakuujua wepesi kutoka kwa watu hawa. Ni muda huo ikaonekana bastola ya mwanaharamu ikipaa angani baada ya kupigwa teke la mkono na mmoja kati ya watu hawa wawili. Hilo halikuonyesha kumchuuza Mwanaharamu. Bado alitulia na kuyadhibiti mapigo kazaa kutoka kwa mtu huyu. Wakati hili likiendelea tayari yule mmoja alikuwa chali akivuja damu sakafuni baada ya kupigwa Dhoruba kadhaa na Masimba. Ulikuwa ni mchezo uliochezwa kwa Dakika moja na nusu. Mchezo ambao hapakuwa na mpita njia yeyote aliyeng'amua kilichokuwa kikiendelea. Baada ya Tukio hilo wakaondoka hapo na kurudi ndani ya gari.
*****
Giza halikumpa ruhusa ya kukiona kile kilicho mbele ama kinachokuja mahala hapo. Alikuwa ndani ya Endeo ambalo alihisi hapo ndipo alipo Mzee Raymond sambamba na watoto wa Masimba. Ulikuwa msitu mzito na wenye wanyama wakali sana. Mingurumo yao Mikali ingeweza kumuogopesha mtu yoyote. Lakini kwa Veronica ulikuwa ni kama Wimbo Masikio. Tena wimbo mtamu ulioimbwa na Celine Dion ama Shania Twain. Hakuogopa hilo na hakuogopa kilichokuwa kikitoka hapo msituni. Alichohitaji ilikuwa ni kurudi Na watu hao. Alihitaji kurudi na wote ambao angewakuta huko. Mkononi alikuwa amekamatia Bastola macho yake yakijaribu kupambana na Giza. Giza ambalo halikuhitaji kumpa hata ule mwanga. Akainuka hapo akielekea huko, akitembea katika namna fulani hivi ya kuogopa kutoa kishindo. Akatembea akikifuata kinjia kimoja kati ya vinjia vingi ndani ya msitu huo. Mzee Raymond alikuwa ni mtu muhimu sana katika ili. Ilikuwa ni lazima ampate. Ilikuwa ni lazima Amrudishe pale alipokuwa akiishi. Ilikuwa ni lazima afanye hivyo kabla ya Kundi la Mafia Kutuma watu wengine ambao kama Wangekuja. Basi wangeanza kumuua Yeye kabla ya kumtafuta Mzee Raymond.
Hakutaka kuchelewa kumtafuta mzee Raymond kwa kuuhofia usalama wake. Kanuni ya kundi la mafia zilikuwa ngumu sana kitu ambacho alikiogopa sana. Ilikuwa ni lazima Aifanye Hiyo kazi. Ilikuwa ni lazima ampate Mzee Raymond. Kuchelewa kulifanya hilo na kusababisha kutumwa kwa wengine ni wazi kuwa hatakuwa na maisha marefu. Akatembea usiku ule katika giza. Njia moja ndiyo aliyoiamini kuwa ingemfikisha mahala alipotaka kufika. Nguo zake nyeusi Zilimfanya afanane na giza. Hakuweza kuonekana kwa Urahisi. Alitembea huku bastola ikiwa mkononi, alitembea kidole kikiwa tayari tayari kwa kutuhusu Risasi. Muda wote alikuwa akiliwaza hili, muda wote alikuwa akiwaza mwanzo wa mission. Hakutambua kama kungekuwa na ugumu ule. Wakati anakuja hakujua kuwa angekutana na kizingiti hiki. Hakujua kuwa hapakuwa na utani. Kwa mara hii alikuwa akiuona ugumu katika hili. Aliihitaji betri kuliko hata masimba. Alimhitaji Mzee Raymond Kuliko Hata Yasser na France. Alitamani kuipata betri ili aweze kutoweka katika Dunia hii. Alitambua ukaribu aliyoujenga kwa Masimba hautasababisha Chochote kile. Alijua mpaka sasa Masimba alikuwa akimuamini. Alitaka kuitumia nafasi Hiyo kuipata Betri ambayo Tayari ilikuwa mikononi mwa Rais. Mtu pekee ambaye aliona anaweza kuifanya kazi yake ya Kuipata Betri kuwa ngumu ni Mwanaharamu. Ni Binadamu Yule aliyelaaniwa. Binadamu ambaye ana matendo ya Hatari. Huyu Pekee ndiye ambaye angemletea Tabu. Huyu pekee ndiye alijua atamtatiza katika hili. Ilikuwa lazima Mtu Huyu afe. Lazima mtu huyu aondolewe Hapa chini Ya Jua. Ni lazima Bastard aondoke kabisa. Alipomfikiria Zaidi Akaiona Hofu moyoni. Moyo wake Ulikuwa Ukimdunda Sana. Akaona Ulikuwa ni wakati wa kuuhitaji Msaada. MSAADA kutoka FSB na Hata Mafia. Ilikuwa nilazima apate watu wa kumuondoa Mwanaharamu. Akatembea huku sasa akianza kuuona mwanga kwa mbali. Mwanga ambao ulionyeshakuwa palikuwa na makazi ya Binadamu. Makazi ambayo yalikuwa ni Maalum. Bado akaendelea kusogea na kusogea. Wakati akikikaribia kichaka fulani akaisikia sauti, sauti ambayo ilimwambia kuwa sehemu hiyo palikuwa na watu. Wakati akiendelea kunyata kusogea hapo, akaisikia Harufu ya Moshi. Moshi kutoka kwenye sigara ngumu. Ulikuwa ni moshi wa bangi. Moshi ambao ulikuwa ukipulizwa na watu. Akauona wakati wa mapambano ukiwa umefika. Wakati wa safari ya kuipata Betri. Akatembea kwa hatua za Panya, hatuA za kuiogopa Ardhi. Muda mfupi alikuwa akimuona mtu mmoja akiwa pembeni akiipuliza. Mtu huyu alikuwa ameuegemea mtu akiendelea kuipata ladha. Hilo likamfanya Asite kwanza. Ni muda huu tu ambao alikuwa akizisikia sauti za Watu Wawili. Lakini muda huu alikuwa akimuona mmoja. Akimuona peke yake. Wakati akiendelea kuwaangalia watu hawa ambao kwa wakati huu akagundua kuwa walibeba bunduki. Akamuona mtu wa pili akiongezeka. Huyu alikuwa akitokea kichakani kuonyesha kuwa alikwenda kufanya kitu. Baada ya mtu wa Pili kurudi, Veronica Akaanza kuipiga hatua za Taratibu kuelekea pale.
Akafanikiwa kufika karibu kabisa na watu hawa. Kuwafikia kulikofuatana na Mluzi kutoka kwa Veronica. Mluzi ambao ulizifanya shingo za watu hawa kugeuka. Ulikuwa ni kama mchezo wa Kuigiza. Mchezo ambao haukutarajia. Risasi mbili zikapita katika vichwa vya watu hawa. Hakuna hata mmoja ambaye aliomba maji. Wote wakatambarajika chini wakiwa maiti. Baada ya kuwamaliza watu hawa wawili, Veronica akawapekuwa haraka haraka.. mifukoni hakuona chochote kile cha maana Zaidi Ya Misokoto ya Bangi. Alichokifanya ni kuiokota Bundiki moja na kuipachika begani. Hapo akaendelea kutembea safari hii akiwa makini zaidi. Alikuwa akitizama kila upande, alikuwa akitizama kwa umakini. Baada ya kutembea kwa muda wa dakika kama Kumi, akakiona kizuizi mbele yake. Walinzi wasiopungua kumi wenye Silaha nzito walikuwa wakizunguka huku na huko wakionyesha kuwa makini. Kuliona hilo kukamfanya atulie kwanza Ilikuona ni Jinsi gani ataweza kupambana na watu wale. Aliwaangalia walivyokaa, akawaangalia walivyokuwa wakizunguka na kuziba kila mahali. Hapo akauona Ugumu Wa kuingia ndani ya eneo lile kwa Urahisi. Ilikuwa ni lazima apambane, ilikuwa ni lazima Aingie hapo kuwaokoa watu hawa hasa Mzee Raymond. Akauona ulikuwa wakati wa kubadilisha njia, na pili ilikuwa ni lazima aingie ndani kwa njia yoyote. Muda huu alikuwa akiirudisha bastola mahala pake huku akiikamatia SMG Mikononi safari ya kuingia msituni Ikiendelea.
*******
Wakati Veronica akiwa katika eneo lile la msitu nje kidogo ya Jiji la DSM. Masimba ndio kwanza alikuwa anashuka pembezoni mwa nyumba moja ambayo ameambiwa kuna mtu anataarifa za kumpa. Baada ya kushuka tu, akachapuka akiuendea mtaa wa pili amba0 ndipo ilipo nyumba aliyoambiwa kuna mtu anaweza kumsaidia. Simu alizowapigia marafiki zake ambao bado walikuwa ndani ya Idara ndiyo iliomfikisha hapo. Alihitaji kulimaliza hili mapema. Alihitaji kulimaliza ili aweze kuianza safari ya kumtafuta Teddy. Muda wote alihitaji kumuweka mtu Huyu katika mikono yake. Alihitaji kumuua Teddy kwa ubaya alioutenda kwake. Hakukuwa na huruma Hata chembechembe za upendo. Akaufikia mtaa ule. Kufika hapo akaanza kutembea kwa hatua za Tahadhali. Taarifa aliyopewa ni kwamba hii ilikuwa nyumba ya Mhariri na mmiliki wa Gazeti la Jamii Forums Leo. Bwana MAX MERO. Mhariri ambaye Gazeti lake ndio lililoripoti kwa Kina kuhusu kile ambacho kinaendelea Hapa Nchini. Akaendelea kutembea akiubadilisha uelekeo wake. Safari hii aliamua kuizunguka nyuma ili kuweza kuingia kwa nyuma. Alitambua kutokana na habari iliyoandikwa kwenye Gazeti lake, lazima Atakuwa akiangalia na Macho fulani kutoka mahali fulani. Wakati akiukaribia uchochoro ambao ulikuwa ukitenganisha Nyumba ya Bwana MERO na nyumba ya mtu mwingine. Akakisikia kishindo kikitokea mbele yake. Akasita kutembea kwanza ili kuangalia Nini ambacho kimesababisha kishindo. Kusimama hapo kukafanikisha kuwaona watu wakiruka na kutua kwa ndani. Akawaangalia watu wale kwa umakini mkubwa. Hawa walikuwa watu kutoka Sehemu nyeti. Akaiona Hatari kwa Bwana MERO. Akasogea taratibu mpaka usawa wa ukuta wa Nyumba. Kufika Hapo akatulia kwanza akiitafuta namna ya kufanikisha kuingia pasipo kuonekana. Ilikuwa lazima awahi kuhofia hatari itakayomkuta Mhariri Huyo. Sekunde hii alikuwa akiliwaza hili, lakini sekunde iliyofuata Alikuwa ameuruka ukuta na kutua ndani bila kutoa mchakato wa Chochote kile. Ukimya ulikuwa umetawala eneo lote. Ukimya kanakwamba hapakuwa na mtu sehemu ile. Hilo halikumshangaza kutokana na watu aliyo waona wakiingia muda ule Ukimya ndani ya nyumba ni kitu ambacho hakukiwaza. Watu walikuwa wameingia muda huu , sasa mbona Nyumba yote ipo kimya? Lilikuwa swali ambalo hakutaka kulijibu kwa maneno. Hakutaka kukisumbua kichwa chake. Alihitaji kwenda kujipa majibu kwa Vitendo. Akatembea huku bastola yake ikiwa imetangulia mbele. Akakivuka kijumba ambacho kilionekana kama kilikuwa cha mbwa. Akipopiga hatua mbili mbele akakutana na kitu kilichomshtua. Mbwa watatu walikuwa wamelala chini huku kila mmoja akivuja Damu. Hapo akatambua kuwa Mhariri na Mmiliki wa Gazeti Alikuwa katika Hatari. Akawaangalia mbwa wale kwa muda wa sekunde kama tano hivi. Sekunde ya Sita alikuwa ameufikia mlango wa kuingilia nyumba kubwa. Akaupeleka mkono ili kukinyonga kitasa, lakini Sauti ya Mwanamke kutoka ndani akionyesha kupiga kelele, ndiyo iliyomzuia Kushika kitasa. Akaurudisha mkono safari hii akifikiria kipi cha kufanya. Alitakiwa kuitafuta njia ya kuwasaidia watu hawa. Akiwa bado yupo hapo akiwaza nini afanye, akausikia mlio wa bastola. Mlio ambao ulijirudia kama mara tano. Hilo halikumfanya Masimba Ashangae. Muda mfupi alikuwa yupo ndani akiangaliana na sebule iliyotapakaa damu sambamba na miili ya binadamu. Lakini katika watu hawa hakuwepo Mhariri wala familia yake. Bali waliouawa walikuwa hawa hawa watu aliowaona wakiingia. Na kingine ni kutokuiona familia na hata mtu huyu aliyefanya hiki kilichofanywa hapa sebuleni. Hapakuwa na mtu, hata mwanamke aliyekuwa akipiga mayowe hakuwepo. Hilo likausisimua mwili wake. Hilo likamfanya atabasamu. Alijua kuna mtu ndiye amemuwahi kuifanya kazi hiyo. Lakini atakuwa nani Huyu? Hilo lilikuwa swali ambalo lilimkuta akiwa nje ya jumba lile. Akatembea usiku kurudi alipotoka huku akikikosa kile ambacho alitakiwa kwenda kukifuata sehemu ile. Alitamani kumjua na kumtambua akiyewapukutisha watu wale na kuondoka na Mhariri sambamba na familia yake. Hapakuwa na mtu yeyote yule ambaye alitambua ama kujua kama yeye atakuwa hapo. Kufanywa kwa tukio lile katika muda mfupi kama ule ni dalili kuwa alikuwa akimulikwa na kutizamwa na kufuatiliwa kila kona. Haikuwa dalili nzuri katika namna ile ya Kijasusi. Japo haikuwa nzuri lakini kwa nini mtu aliyefanya hivi akaondoka pasipo kumsubiri? Lilikuwa swali jingine ambalo hakutaka kutafuta majibu kwa wakati huo. Kwa kuwa ulikuwa muda wa mapambano, alitambua majibu angeyapata kila pale muda utakapokuwa ukisonga.
********
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa lazima apitie njia nyingine, ilikuwa ni lazima atafute Njia mbadala ya kufika ndani ya majengo yale pasipokupitia Getini. Akaianza safari ya msituni. Safari ya kufa na kupona. SMG ilikuwa imetangulia mbele tayari kwa kumuondoa mtu yoyote yule. Akafanikiwa kuipata Njia fulani ambayo alianza kuifuata kwa umakini. Akaipiga hatua ya kwanza na ya pili. Hatua ya Tatu akauhisi mchakato. Mchakato wa Majani. Kabla hajajua ni kitu gani akausikia Tena mvumo. Mvumo ambao kwa safarii aliutambua na kutambua kuwa haukuwa wa kawaida. Wakati anataka kugeuka ili kuondoka katika namna ya kuukwepa ule mvumo. Alijikuta akitandikwa mateke manne mfululizo ambayo yalimtupa mpaka Chini mithili ya Mzigo. Akasimama Haraka ili kumkabili mtu huyu. Akajikuta Akitizamana na Teddy Akiwa amesimama mbele yake akimtizama kwa macho ya Dharau. KARIBU KUZIMU.. AKATAMKA TEDDY AKIINUA BUNDUKI KUMLENGA VERONICA.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment