Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

PENIELA (STORY YA KIJASUSI) - 2

 






Simulizi : Peniela (Story Ya Kijasusi)

Sehemu Ya Pili (2)




Vipi uko tayari?

“ Kareem I’m sorry.Leo sintaweza kwenda ,nimepatwa na dharura.Samahani sana kwa usumbufu.Labda siku nyingine” akasema Penny na kumstua Kareem

“ What ?!!!..

“ I’m so sorry Kareemkwa leo sintaweza kwenda”

“ How could you do this Penny? What am I going to tell him? Akauliza Kareem

“ Tell him that I don’t have time today” akasema Penny na kumgeukia Jason

“ Jason can we go?



Jason akainuka na kumfuata wakatoka nje akamfungulia Penny mlango wa gari akaingia halafu wakaondoka na kumuacha Kareem akiwa amesimama mlangoni hajui afanye nni

“ Sorry Peny”

“ Sorry for what?!!..akauliza Peny

“ Nimekuvurugia ratiba zako.Kama ulikuwa na miadi na mtu ungenitaarifu mapema ili tuahirishe kazi yetu”

“ Usijali Jason.Kuna mtu nilikuwa nahitahi kuonana naye jioni ya leo lakini haikuwa na umuhimu mkubwa.

“ Your boyfriend? Akauliza Jason

“ I don’t have a boy friend Jason” akasema Penny na kumfanya Jason atabasamu



Waliwasili Moniz 5 star hotel,wakashuka garini wakapanda lifti hadi ghorofa ya tano wakashuka na kuanza kutembea katika varanda refu huku wakisoma namba za vyumba.Walisimama katika mlango wa chumba namba 204.Jason akabonyeza kengele ya mlangoni na baada ya dakika moja mlango ukafunguliwa na jaji Elibariki akajitokeza.Wakaingia ndani

“ Hallow Penny. habari yako? Akasema jaji Elibariki

“ habari nzuri Jaji Elibariki.Pole na majukumu”

“ Ahsante sana Penny.Vipi unaendeleaje na maisha mapya?

“ Ninaendela vizuri sana jaji.Mwanzo unakuwa mgumu lakini baada ya muda nitazoea na kurudia hali yangu ya kawaida.” Akasema Penny.Jason akapiga simu hotelini na bila kuchelewa muhudumu akafika akiwa na toroli lenye vinywaji akaviweka mezani.



Jason akaomba awaache Jaji Elibariki na Penny yeye kaenda kuendelea na majukumu mengine

“ Penny ni mara ya kwanza mimi na wewe kukutana,lakini utakuwa mi mwanzo wetu pia kufahamiana rasmi” akaanzisha mazungumzo Jaji Elibariki baada ya Jason kuondoka na kuwaacha wao wawili pekee mle chumbani

“ Ni kweli mheshimiwa Jaji,Sikuwa nakufahamu hapo kabla na nilikufahamu tu pale ulipoanza kuisikiliza kesi iliyokuwa inanikabili.Nafurahi sana kukutana nawe ana kwa ana.Nilistuka Jason aliponiambia kwamba unahitaji kuniona,lakini kwa upande mwingine nikafurahi kwa sababu hata mimi nilikuwa na wazo la kukutafuta na kukushukuru kwa kuniachia huru.” Akasema Penny Jaji Elibariki akatabasamu

“ Penny si mimi niliyekuachia huru bali ni Mahakama baada ya kujiridhisha kwamba hukutenda kosa. Na hiyo inatokea si kwako tu bali kwa wote wanaofikishwa mahakamani na kukutwa hawana makosa,mahakama huwaachia huru.” Akasema jaji kikapita kimya cha sekunde kadhaa

“ Penny nadhani Jason amekwisha kueleza kwa ufupi kuhusiana na kilichotufanya tukutane leo hii.” Akasema Elibariki

“ ndiyo,alinieleza kwa ufupi” akajibu Penny

“ Nimeifuatilia kesi hii toka ilipoanza na nikagundua kwamba kuna nguvu kubwa iliyotumika ili kuhakikisha kwamba unapatikana na hatia na hatimaye kufungwa.



Nimejiuliza sana ni kwa nini nguvu kubwa itumike namna hii ikiwa ni pamoja na kuwasilisha kila aina ya ushahidi ambao kama Jaji usipokuwa makini unaweza kabisa kumtia mtu hatiani. Kutokana na mwenendo mzima wa kesi namna ulivyokuwa,nime

shawishika kuamini kwamba kuna kitu kipo nyma ya kesi hii.Kuna kundi la watu ambao walifahamu kabisa kwamba hukutenda lile kosa lakini walisimama imara kuhakikisha kwamba unabambikiwa kesi ile na kukutwa na hatia na hatimaye kuhukumiwa kwa mauaji.Ninachojiuliza,je watu hawa ni akina nani? Kwa nini walitaka ufungwe? Nani alimuua Jason? Akasema jaji Elibariki na kunywa mvinyo kidogo halafu akaendelea

“ Kutokana na maswali hayo ambayo nimekuwa nikijiuliza bila ya kupata majibu,ninalazimika kuamini kwamba pamoja na kukuacha huru lakini bado usalama wako uko mashakani.Watu hawa bado wako nyuma yako na watakuandama usiku na mchana bila kulala hadi wahakikishe kwamba lengo lao limetimia.



Kwa hiyo basi nimekuita hapa kukutaarifu kwamba mimi na wakili wako Jason tumeamua kufanya uchunguzi kisiri siri na kumjua muuaji wa Edson.Ni hiyo tu ndiyo itakuwa salama yako na sisi sote pia.Unaweza ukaona kwamba hali ni shwari lakini naomba nikuhakikishie kwamba hali yetu kiusalama si nzuri hata kidogo.Ninachokiomba toka kwako ni ushirikiano wako ili kwa pamoja tuweze kumtafuta na kumpata muuaji na kumfikisha mbele ya mkono wa sheria.Tukimpata muuaji tutajua sababu ya wewe kubambikiwa kesi ya mauaji.



Tutauweka ukweli wazi ili jina lako lisafishwe katika jamii”

Penny akanywa kinywaji kidogo na kusema

“ Jaji Elibariki,kama nilivyomwambia Jason kwamba nakubaliana na wazo hilo la kufanya uchunguzi wa kumbaini mtu aliyefanya mauaji yale.Niko tayari kutoa ushirikiano wangu wa kila namna ili tuweze kumbaini mtu huyo” akasema penny

“ Nashukuru sana Penny kwa hilo.” Akasema jaji Elibariki na kunywa funda moja la mvinyo

“ Kabla ya kuanza kwa uchunguzi au kuamua nini tufanye,ningependa kwanza kufahamu machache kutoka kwako kuhusiana nanamna tukio lile lilivyotokea na wewe ukajikuta ukitiwa hatiani.Samahani lakini kwa kukukumbusha mambo ambayo unajitahidi kuyasahau.” Akasema jaji Elibariki



Penny akafumba macho na kufikiri kwa muda halafu akasema

“ Ilikuwa ni siku ya Jumamosi,mimi na edson tulipanga tutoke kwa chakula cha jioni.Sikujua anataka kunipeleka sehemu gani kwani alisema angenifanyia surprise.Vile vile alisema kwamba kuna jambo analotaka kunieleza usiku huo” Penny akanyamaza akanywa mvinyo kidogo na kuendelea

“ Alitaka kunipitia nyumbani kwangu lakini nikakataa na kumwambia nitampitia yeye nyumbani kwake na siku hiyo tutatumia gari langu jipya.Saa moja na nusu niliwasili nyumbani kwake na kubonyeza kengele ya getini ambayo iliita kwa dakika kadhaa bila majibu.Nikajaribu kufungua eti na kukuta liko wazi.



Mlango wa kuingilia sebuleni ulikuwa umefungwa kwa funguo nikahisi labda Eddy atakuwa ametoka na kwenda maeneo ya karibu.Nilikuwa na funguo aliyonipa yeye mwenyewe nikafungua na kuingia ndani.Nilikaa sebuleni kwa takribani dakika kumi bila kutokea nikaamua kumpigia simu ambayo iliita bila kupokelewa.Nili

patwa na wasi wasi ikanibidi kupanda ghorofani katika chumba chake cha kulala.Nilipoingia tu ndani nikakutana na picha ambayo sintakuja kuisahau katika maisha yangu.”



Akanyamaza kidogo na kunywa mvinyo halafu akaendelea

“ Nilimkuta Edson akiwa amelala kitandani,huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu.Kifuani pake kulikuwa na bastora .Nilipatwa na taharuki nikaenda kuishika bastora ile nikaiweka pembeni na kuanza kumuangalia Eddy kama bado mzima.Nilichanganyikiwa na kutaka kutoka ili nikatafute msaada.Wakati nashuka ngazi nikikimbia kwenda kutafuta msaada nikakutana na watu wanne waliodai kwamba wamesikia mlio wa risasi.Nilishindwa kuongea .Wakanikamata na kudai kwamba nimemuua Eddy.Nilipelekwa polisi na kufunguliwa mashitaka na kilichoendelea baada ya hapo unakifahamu hadi pale uliponiachia huru..”akasema Penny na mara simu yake ikaita..



“ Samahani nilisahau kuizima simu” akasema Penny na kuitoa simu ile akatazama mpigaji na mara sura ikambadilika.Hakuipokea simu ile akaikata na kuizima kabisa.Jaji Elibariki akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Pole sana Penny kwa yote yaliyotokea.Lakini kuna jambo moja nataka kulifahamu.Unahisi ni kitu gani Edson alitaka kukueleza?

Penny akafikiri na kusema

“ Hapana sifahamu alitaka kunieleza nini lakini alisema kwamba ana jambo la muhimu la kuniambia usiku huo”

“ Kwa muda gani ulikuwa naye katika uhusiano?

“ Ni zaidi ya mwaka mmoja.Tulianza kwa siri lakini baada ya yeye kuachana na mpenzi wake Anna,tukaamua kuweka wazi mahusiano yetu”

“Hapo kabla uliwahi kuwa na mpenzi ambaye mliachana?

“Hapana ,sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi hapo kabla.Edson alikuwa ni mwanaume wangu wa kwanza”

“ Uliwahi kupokea vitisho vyovyote toka kwa mpenzi wa zamani wa Edson au mtu mwingine yeyote?

“ Maneno na vitisho haviwezi kukosekana.Tulikuwa tunatumiana jumbe mbali mbali za kutishana,kutuk

anana na hata kupigiana simu za vitisho”

“ Unadhani Anna anaweza akawa na mkono wake katika kifo cha Edson?

Penny akafikiri kidogo na kusema

“ Hapana ,sidhani kama anaweza kuwa amehusika na kifo kile “

“ kwa nini?

“Kwa sababu alimpenda sana Edson “

“Hufikiri kwamba Anna aliumizwa sana baada ya kuachwa na Edson na hivyo akaamua kumuua ili kulipiza kisasi?

“ Sidhanikama Anna anaweza akafanya hivyo kwa namna alivyompenda Edson.” Akajibu Penny na kimya kidogo kikapita

“ Kama si Anna ,unahisi nani anaweza akawa ni muuaji?



Akauliza Jaji Elibariki.Penny akainama akafikiri kwa muda na kusema

“ Hapana mheshimiwa sifahamu kabisa nani anaweza kuwa muuaji”

Kimya kifupi kikapita halafu jaji Elibariki akasema

“ Penny kuna jambo lolote ambalo hukuwahi kumueleza mtu yeyote Yule ambalo ungependa kuniambia na linaloweza kutusaidia katika uchunguzi wetu?

Swali lile likamfanya Penny anyamaze kwa muda wa zaidi ya dakika mbili halafu akasema

“ Hapana mheshimiwa,mambo yote nimekwisha yasema.



Hakuna ambalo sijalisema”

Waliendelea kuongea mambo mengi na muda ulipofika Jason akarejea na kumchukua Penny akamrejesha kwake.Akiwa njiani kurejea nyumbani kwake ,Jaji Elibariki akampigia simu

“ Halo jaji” akasema Jason

“ Jason,umemfikisha penny salama?

“ Ndiyo nimemfikisha salama.Niko njiani kuelekea nyumbani “

“ Ok Jason.Nimezungumza mambo mengi na Penny lakini kuna jambo moja nimeligundua toka kwake”

“ jambo gani Jaji?

“ Kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Edson lakini hayuko tayari kuliweka wazi”

“Are you sure? Akauliza Jason

“ yah ! I’m sure.



Kuna kitu anakifahamu lakini hayuko wazi kukisema.”

“ sasa tutafanya nini?

“ Tutaendela na uchunguzi wetu kimya kmya bila ya kumshirikisha Penny.” Akasema Jaji Elibariki

Jason akafikiri na kusema

“ Ok Jaji.Tutaonana kesho na tutajadili kwa kirefu” akasema Jason na kukata simu





Baada ya Jason kuondoka,Penny akaenda chumbani kwake akajitupa kitandani.Alionekana kuwa uso wenye tabasamu

“ Ni mara ya kwanza nimetoka out baada ya mwaka mzima.Wow it was wonderfull. Elibariki is real a gentleman. Nimefurahi sana kukaa meza moja naye.Nii mtu ambaye ndiye aliyenifanya niwe huru.Bila yeye kwa sasa ningekuwa gerezani maisha yangu yote au nikisubiri kunyongwa.Sintaweza kumsahahu katika maisha yangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Hata hivyo he’s so cute.Ni jaji kijana na mwenye moyo wa huruma” akawaza Penny huku akitabasamu lakini mara akabadilika na kuonekana kuwa na mawazo

“ Jason na Jaji Elibariki wanataka kujiingiza katika jambo la hatari kubwa.Suala la kifo cha Edson si suala rahisi kama wanavyolichukulia.Ni jambo zito na la hatari .Mjadala wake ulikwisha fungwa na hakuna tena uchunguzi wowote utakaofanyika tena.Natamani kuwaambia wasiendelee na kitu wanachotaka kukifanya lakini nashindwa.Ninachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba hawafanikiwi katika usala hili na hivyo kukata tamaa na kuacha kabisa kuchimba undani wa kifo cha Edson.Hii itakuwa ni kwa ajili ya usalama wao wenyewe” Akawaza Penny na kustuliwa na mlio wa simu.



Akatazama mpigaji akakutana na namba ambazo hazikuwa na jina mara moja akawa amemtambua mpigaji. Akavuta pumzi ndefu halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea

“ Hallow “ akasema kwa sauti ya uchovu.Sekunde kadhaa zikapita halafu sauti ya upande wa pili ikasema



“ Hallow Penny.How are you?

“ I’m fine.How are you? Akajibu Penny

Kimya kifupi ikapita tena na mtu Yule akauliza

“ Penny kwa nini umenifanyia dharau kubwa kama leo? Lini utaufungua moyo wako kwangu? Lini utakuwa tayari kukaa na kunisikiliza? Ikauliza sauti ile nzito iliyoongea kwa upole.Penny akashindwa kujibu

“ Kwa nini umeshindwa kuja kuonana nami kama tulivyokuwa tumepanga? Akauliza mtu Yule.Penny akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Mr President can we stop this?



“ Stop what ?

“ Mr President we can go on like this.Its time to end things now” akasema Penny

“ Penny ni hapo tu unaponiudhi “

“ Dr Joshu …” akataka kusema kitu Penny lakini Dr Joshua akamzuia

“ Don’t say anything Penny.You know exactly how much I love you and I’ll never stop loving you” akasema Dr Joshua kwa sauti yenye ukali kidogo.

“ Acha kunidanganya Dr Joshua !! “ Penny naye akasema kwa sauti yenye ukali kidogo ndani yake



“ Sikudanganyi Penny na sijawahi kukudanganya kwamba ninakupenda kwa moyo wangu wote.”

“ Liar !!..” akasema Penny

“ Kama unayoyasema yana ukweli usingekubali kuona nikitaka kuangamia.Unsingethubutu kuniona nikiozea gerezani na kunusurika kufungwa maisha wakati ukijua kabisa kwamba sikutenda lile kosa.Sikumuua Edson .Pamoja na kufahamu hilo lakini bado hukufanya lolote kunisaidia na badala yake ukakubali nibambikiwe kesi ile ili nikafungwe.You don’t love me at all” akasema Penny kwa hasira

“ Penny I love you.



real do.Najua hutaamini lakini fahamu kwamba niliumia kukuona ukiwa gerezani lakini nilishindwa namna ya kukusaidia kwa sababu kwa wakati ule bado ulikuwa umenikasirisha mno na nilitamani hata ufungwe gerezani ili nisikuone tena katika maisha yangu yote.Kitendo cha kuanzisha mahusiano na Yule kijana Edson kiliniumiza sana na ndiyo maana yakatokea yale yaliyotokea lengo likiwa ni kukufunza adabu kidogo ili uwe na heshima kwa watu wazima na wenye nguvu.” Akasema Dr Joshua .Penny akafuta machozi.Dr Joshua akaendelea



“ Penny naomba nikuweke wazi kwamba moyo wangu uliumia mno na kuvunjika pale ulipoingia katika mahusiano na yule kijana Edson na ukanisaliti na kwa sababu yako akamuacha hadi mwanangu Anna.Pamoja na yote yaliyotokea bado ninashindwa kukutoa moyoni mwangu.Bado nakuhitaji Penny katika maisha yangu.Ni wewe tu ambaye unaweza kunipa furaha ninayoihitaji.Tafadhali Penny naomba tuyasahau yote yaliyopita na tuufungue ukurasa mpya.”



Penny akafikiri kidogo na kusema

“ so you killed him !..” akasema Penny huku machozi yakimdondoka mashavuni

“.Yes I did.You are mine Penny,and mine alone.yeyote ambaye atataka kuchukua nafasi yangu kwako sintasita kumfanya kama nilivyomfanya Edson na ukumbuke kwamba siku ukifungua mdomo wako ndiyo utakuwa mwisho wako kwa hiyo basi …….” Dr Joshua akakatishwa na Penny ambaye machozi yalikuwa yanamtoka



“ You are a devil..!!” akasema Penny kwa ukali

“ Penny naomba unielewe kwamba nina kupenda na nitafanya kila linalowezekana ili mimi na wewe tuwe pamoja.My wife is sick and will die soon.Hawezi kunipatia kile ninachohitaji na ninachokipata toka kwako.She’ll die soon and you’ll be the first lady so please open your heart for me….” Akasema Dr Joshua



“ Dr Joshua,naomba hii iwe ni mara ya mwisho kunipigia simu.Wewe ni rais wa nchi na una mke wako wa ndoa kwa hiyo naomba uachane kabisa na mimi.Tafadhali angalia masuala makubwa ya nchi na mke wako mgonjwa.She needs you” akasema Penny

“ Penny kwa nini hutaki kunielewa? Nimekwisha kwambia kwamba hakuna kitu zaidi ya kifo kitakachoweza kunitenganisha na wewe.Nimekuchagua wewe tu na nitafanya kila niwezalo na nitatumia nguvu zote nilizonazo mpaka niwe nawe tena.Najua unanichukia sana kwa sasa lakini tutayamiliza mambo haya na tutakuwa wamoja tena. No woman will say no to me” akasema Dr Joshua.



Penny akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Let us have a deal Dr Joshua”

“ A deal !!..

“Yes a deal. I’ll keep my mouth shut.I’ll never tell anybody that its you who killed Edson and I’ll die with my secret if you’ll let me go”

“ hahaha Penny unanifurahisha sana.I’ll never let you go and you’ll keep your mouth shut because I did that for us,me and you.So we don’t have a deal.I know down deep in your heart that you do love me.”

“ I don’t love you Joshua and I’ll never love you”

“ Who do you love? Wakili wako Jason?



Au jaji Elibariki? Penny akastuka baada ya kutajiwa jina la Elibariki

“ So you are following me ?!! akauliza Penny

“ Penny ninafahamu kila hatua unayoipiga.Ninafahamu jioni hii umekataa mwaliko wangu na ukaenda kuonana na Jaji Elibariki.Be careful.Jaji Elibariki amemuoa mwanangu lakini sintosita kumuadhibu pale atakapoamua kuvuka mipaka na kumsaliti mwanangu kama Edson alivyomsaliti mwanangu Anna.”

Penny akahisi kuishiwa nguvu akashindwa aseme nini.

“ Penny nitakuwa na safari ya kwenda Arusha wiki ijayo kwa hiyo jiandae nawe utakwenda Arusha.Kareem atashughulikia kila kitu kuhusu safari hiyo.Kwa heri Penny” akasema Dr Joshua na kukata simu.Penny alihisi jasho likimchuruzika .



“ I’m back to a living hell.!..Nayachukia sana maisha haya lakini sina namna tena tayari nimenaswa.Endap

o nitaenda kinyume na huyu mzee kuna uwezekano yakanifika makubwa .Nimeponea chupu chupu kesi ya mauaji na safari hii lazima niwe makini sana kwa kila ninachokifanya.” akawaza Penny huku kijasho kikimchuruzika na mara simu yake ikaita,akatazama mpigani na kubonyeza kitufe cha kupokelea



“ Hallow” akasema

“ Penny don’t say No to Mr president.Fanya kila atakachokuamuru ufanye.We’re so close” ikasema sauti ile na kukata simu.Penny akahisi kuchanganyikiwa.





Penny alikaa kitandani akazama katika tafakari nzito.Simu mbili toka kwa watu wawili tofauti alioongea nao muda mfupi uliopita zilimchanganya sana.

“Sijui nini itakuwa hatima ya maisha yangu.Sijui nitaendelea na maisha haya hadi lini? Nimechoka sasa na maisha haya na ninahitaji kuwa huru na mimi niishi maisha ya kawaida.Nimepewa amri ya kuendeleza mahusiano na Dr Joshua japokuwa moyo wangu hautaki kabisa.Kamuua Edson kijana ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote.



I was deeply in love with him.Kama haitoshi nikaangushiwa kesi ile kubwa ya mauaji ambayo nusura inipeleke maisha gerezani.Yote hii ni kwa sababu ya wivu wa Dr Joshua.He’s a powerfull man and he can do anything.Sikuwa nataka kuwa na mahusiano naye ya namna yoyote ile baada ya kuachiwa huru lakini najikuta nikilazimishwa kukubali kuendeleza mahusiano naye ili kuikamilisha kazi .



I hate that bastard.” Akawaza Penny huku akijifuta jasho

“ Lakini kwa sasa ngoja niwe mpole na niendelee kumkubalia kwa kila anachotaka lakini iko siku moja atalia na kuomboleza. Kitendo alichokifanya cha kumuua Edson kimeniumiza mno na iko siku atalipia uovu huu.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuhakikisha kwamba Jason na Jaji Elibariki wanaachana na kutafuta muuaji wa Edson.



Wanajiweka katika hatari kubwa sana bila wao wenyewe kujua.Hawa ni watu wangu wa muhimu sana na sintokubali kuona kwa namna yoyote ile mmoja wao yakimpata kama yaliyompata Edson.” Akawaza Penny na kuinuka akaelekea bafuni kuoga kwani jasho jingi lilikuwa linamtiririka

“ kuna nyakati huwa siamini kama ni kweli nimeweza kufanikiwa kumchanganya mkuu wa nchi,mtu anayeheshimika ndani na nje ya nchi, kwa kumpa penzi la kiwango cha juu .Mzee Yule amechanganyikiwa kiasi cha kumuombea mke wake anayesumbuliwa na saratani afariki mapema ili aweze kuwa na uhuru na mimi anioe na anifanye first lady.Hahaha laiti angejua angeyafuta kabisa mawazo yake.Ngoja nivumilie na kujifanya mjinga na kumsikiliza kila atakachokisema kwa sababu kimebaki kipindi kifupi sana kukamilisha kazi yangu” akawaza Penny akiendelea kuoga.



********

Saa mbili za asubuhi Jaji Elibariki aliondoka nyumbani kwake na kuelekea ofisini .Si kawaida yake kuondoka mapema hivi lakini kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na mke wake Flaviana ilimlazimu kuwahi kuondoka.

“ Siku ya pili sasa mimi na Flaviana hatuongei.Nimechoshwa na maisha haya ya mikwaruzano kila siku.Flaviana ni mwanamke ambaye anataka kuwa na sauti ndani ya nyumba na maamuzi yake yawe ndiyo ya mwisho.Yote hii ni kwa sababu yeye ni mtoto wa rais.



Siko tayari kuendelea kuvumilia dharau zake.Siko tayari kuendelea kuishi maisha yasiyokuwa na furaha hata kidogo eti kwa sababu ya kiapo cha ndoa. “Akawaza jaji Elibariki na mara sura ya Penny ikamjia

“ Sura ya Penny toka niliponana naye jana hainitoki kichwani.Ninamuwaza kila dakika.Yawezekana ni kutokana na uzuri wake.Ni mtoto mzuri mno.Ameumbwa akaumbika.



Ana uzuri wa kipekee mno ambao sijui nimfananishe na nani.Jana nilipomuona namna alivyokuwa amependeza niliogopa na kudhani labda ni malaika.Hakuwa Penny Yule ambaye nilizoea kumuona mahakamani ” akawaza Jaji Elibariki wakati akikata kona kuingia Lavenda Restaurant kupata kifungua kinywa kwani aliondoka nyumbani bila kupata mlo wa asubuhi.



“ Katika maongezi yangu na penny jana usiku sijaweza kugundua chochote cha kuweza kunipa mwanga kuhusu wapi nitaanzia uchunguzi wangu.Nilivyomsoma penny ni kama vile hataki tena kujihusisha na masuala yoyote yanayohusiana na kifo cha Edson.Nadhani anajitahidi kujisahaulisha yaliyopita lakini pamoja na hayo kuna kitu nimekiona katika macho yake ambacho kinanifanya niamni kwamba kuna kitu anakifahamu lakini hayuko wazi kukisema. Siwezi kumlazimisha kusema kila kitu anachokifahamu .Kama kuna kitu hataki kuniambia basi nitakifahamu kwa njia nyingine.Ninaapa nitalichimba suala hili hadi mzizi wa mwisho.Nataka nimdhihirishie rais na familia yake kwamba ninapofanya maamuzi huwa sikurupuki tu.



Lazima nimpate muuaji ” akawaza jaji Elibariki halafu akampigia simu Jason na kumfahamisha kwamba wakutane mahala walikokutana jana asubuhi

Kisha maliza kupata kifungua kinywa,akaondoka na kuelekea moja kwa moja katika sehemu waliyopanga wakutane na Jason.

Dakika kumi na mbili toka awasili mahala walikopanga kukutana,Jason akawasili.Wakasalimiana na bila kupoteza wakati wakaanza kujadili kile kilichowakutanisha pale



“ Vipi kuhusu jana,mambo yalikwendaje? Akauliza Jason.

“ Jana mambo yalikwenda vizuri ingawa si vizuri sana lakini si mbaya kwa kuanzia.Niliongea mambo mengi na Peniela na alikubali kushiriiana nasi ili kumbaini nani muuaji wa Edson.Alinieleza kwa ufupi tu namna mahusiano yake na Edson yalivyokuwa na hadi siku mauaji yalipotokea.Hakuna kitu kipya katika maelezo yake.Maneno aliyoniambia jana ndiyo yale yale ambayo aliyasema mahakamani.Lakini hata hivyo kuna kitu nilikigundua baada ya kuongea naye.Kuna kitu anakifahamu lakini hayuko tayari kukisema.Hiyo nayo inazidi kunipa mshawasha wa kutaka kufahamu kwa undani zaidi kuhusiana na jambo hili.” Akasema Jaji Elibariki.Jason akafikiri kidogo na kusema



“ Penny ni rafiki yangu na nimekuwa nikiisimamia kesi yake kwa muda wa mwaka mzima na ninakubaliana nawe kwamba Penny ni msiri sana.Ana ambo mengi ambayo hajawahi kuyaweka wazi na huwa hataki kabisa kuyaongelea.Kwanza ni kuhusiana na familia yake.Kwa muda wa mwaka mzima sijawahi kuiona familia yake au ndugu yake yeyote Yule .Najiuliza mara kwa mara ndugu zake wako wapi? Sijapata nafasi ya kumuuliza kuhusu suala hilo na wala hajawahi kunieleza chochote.Nakubaliana nawe kabisa kwamba kuna mambo ambayo penny anayafahamu lakini hayuko tayari kuyaweka wazi.”



“ Kama ni hivyo basi” akasema jaji Elibariki

“ itatubidi tufanye mambo mawili.Kwanza inatubidi tumfahamu huyu Edson alikuwa mtu wa namna gani.Tuyafahamu maisha yake alikuwa akiishi vipi,marafiki aliokuwa akiambatana nao,tutachunguza pia nyumbani kwake na mwisho tutafuatilia mawasiliano yake na watu mbali mbali ambao alikuwa akiwasiliana nao na hasa wale aliowasiliana nao siku tatu kabla ya kifo chake vile vile tutaipitia tena taarifa ya uchunguzi toka jeshi la polisi .Tunatakiwa tufahamu kila kitu kuhusiana na Edson.” Akasema Jaji Elibariki akanyamaza kidogo halafu akaendelea.



“ Jambo la pili ambalo tunatakiwa tulifanye ni kumchunguza Penny” akanyamaza na kumtazama Jason

“ Lazima tumfahamu Penny lakini ni baada ya kumfahamu Edson” akasema Jaji Elibariki.

Waliendelea na majadiliano na baadae wakaondoka kila mmoja akaelekea ofisini kwake .



Baada ya kuachana na Jaji Elibariki,Jason aliamua kuelekea nyumbani kwa Peniela.Hakuwa ameongea naye toka asubuhi hivyo akaamua kwenda kuonana naye kabla hajaendelea na mambo mengine .

“ Ninakubaliana na Jaji Elibariki kwamba Penny ni mwanamke msiri sana.Ninaamini hakumuua Edson lakini nina imani kuna mambo ambayo anayafahamu kuhusiana na kifo cha Edson lakini hayuko tayari kuyaweka wazi.Anyway tutachunguza na tutapata jibu” akawaza Jason akiwa njiani kuelekea kwa Penny



Ilimchukua dakika thelathini kuwasili katika makazi ya Penny.Katika geti la kuingilia ndani kulikuwa na makufuli makubwa manne kuashiria kwamba hakukuwa na mtu ndani.Jason akatoa simu yake na kumpigia lakini hata simu yake haikuwa ikipatikana.Jason akaingiwa na wasi wasi mkubwa.





Dakika zilizidi kuyoyoma na Jason bado aliendelea kusimama nje ya nyumba ya Penny ,asijue la kufanya.Alikuwa na wasi wasi mwingi pengine Penny amepatwa na matatizo lakini kilichompa moyo ni yale makufuli yaliyokuwa getini ambayo yaliashiria kwamba hakukuwa na mtu yeyote ndani

“ Penny kaenda wapi? Na kwa nini amezima simu yake? Akajiuliza

“ Nina wasi wasi asijekuwa amepatwa na matatizo kwani hali ya usalama wake bado si nzuri hata kidogo.Kuna haja ya kuimarisha ulinzi hapa nyumbani kwake hadi hapo hali ya usalama itakapokuwa shwari.Nitaongea naye na kama atakuwa tayari nitamkodishia walinzi toka katika kampuni binafsi ya ulinzi ili wailinde nyumba yake na kila sshemu aendako.” Akawaza Jason akiwa nje ya gari lake



“ Lakini kwa nini niwe na wasi wasi kuhusu maisha ya Penny kiasi hiki? Na kwa nini niko hapa mida hii? Sikuwa na ratiba ya kufika hapa siku ya leo lakini tazama mahala nilipo sasa hivi,nipo nje ya geti la Penny.What am I doing here? Akajiuliza Jason

“Kuna kitu kimoja tu kilichonileta hapa.Kumuona Penny.Lakini kumuona Penny kwa makusudi yapi? Hapo ndipo ninapokosa jibu.Sina sababu yoyote ya msingi iliyonileta hapa.Mahusiano yangu na Penny ni katika masuala ya kisheria tu nasi vinginevyo kwa hiyo sipaswi kuwa na hofu yoyote kuhusu yeye wala kuyafuatilia maisha yake wala kuja hapa kwake mara kwa mara na kwa muda ninaotaka.Kazi yangu ilikuwa kumsimamia kesi na baada ya kesi kuisha natakiwa nimuache aendelee na maisha yake kama kawaida.Siku akiwa na tatizo atanitafuta” akawaza Jason halafu akaingia garini na kuondoka



“ Lakini moyo wangu unakataa kabisa kukaa mbali na Penny.Nimekuwa naye katika kipindi chote alichopata matatizo makubwa na tayari tumejenga ukaribu mkubwa kati yetu kwa hiyo si rahisi kuachana naye” akawaza Jason huku akiongeza mwendo wa gari na kulipita gari la mbele yake

“ Kuna kitu kimoja ambacho nimekuwa nakihisi kwa muda mrefu sasa lakini nimekuwa nikikwepa kuwa wazi.I’m falling in love with Penny.Kwa muda wmrefu nimekuwa na hisia hizi lakini nimekuwa nikijizuia ili kumaliza kwanza masuala ya kesi iliyokuwa ikimkabili.Kwa sasa baada ya kesi kumalizka na Penny yuko huru,sina sababu ya kuendelea kuzificha hisia zangu kwake.Siwezi tena kuendelea kujizuia.” Akawaza Jason na mara sura ya penny ikamjia kichwani akatabasamu



“ Penny ni msichanamwenye uzuri wa kipekee kabisa ambaye sioni wa kumfananisha naye.Mimi na yeye tunaendana karibu katika kila kitu na ana kila sifa ninayoihitaji kwa mwanamke wa maisha yangu.Lakini kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kinanila akili yangu toka jana.Nikiwa pale kwake jana alikuja Yule kijana nadhifu kuja kumchukua ili kumpeleka mahala. Ni wazi alikuwa na miadi na mtu Fulani tena inaonekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa kifedha.Je mtu huyo ni nani na wana mahusiano gani? Akajiuliza Jason na kuvuta pumzi ndefu



“ Nitamfuatilia mtu huyo hadi nimfahamu ni nani na ana mahusiano gani na penny.Nasikia wivu mkubwa kila nikiwaza kwamba yawezekana pengine mtu huyo na penny wakawa na mahusiano ya kimapenzi.Natak

a penny nimmiliki mimi peke yangu” akawaza Jason.Moja kwa moja alielekea ofisini kwake na kitu cha kwanza baada ya kuingia ofisini alitoa simu yake na kujaribu kupiga namba za simu ya Penny lakini hazikuwa zikipatikana “ Penny yulo wapi leo?Amepatwa na nini?Nitaendelea kumtafuta hadi nimpate.Sintolala usingizi leo hadi nitakapoongea naye simuni na kujua kama yuko salama.” Akawaza Jason na kuendelea na kazi zake.



**********



Ni saa tano za asubuhi,jiji la Arusha likiwa na ubaridi uliotokana na mvua za manyunyu zilizoendelea kunyesha,lakini sughuli za kujitafutia kipato ziliendelea kama kawaida.Katika hoteli ya kifahari ya Kobe Village ,Peniela msichana mwenye uzuri wa kipekee alikuwa ghorofani akilitazama jiji hili lililobarikiwa uzuri wa kipekee kabisa,likionekana kwa uzuri kutokea hotelini pale

“ geneva of Africa” akawaza Penny huku akitabasamu.

“ Nimerejea tena katika maisha yangu niliyoyazoea.Haya ndiyo maisha niliyokuwa nikiishi na ninayotaka kuendelea kuishi.To live like a queen.Nina hakika baada ya kumaliza shughuli yangu nitaishi maisha kama haya au hata zaidi ya haya.” Akawaza na mara dada mmoja mwenye kuvalia nadhifu kabisa akamfuata na kumsalimia

“ Madam,wewe ndiye Penny?



Akauliza Yule dada mwenye sauti ya upole baada ya kusalimiana

“ Ndiye mimi” akajibu penny

“ Ok.Naitwa Zulfa,ninafanya kazi katika dula la mavazi na urembo hapa jijini Arusha liitwalo Samia Fashion.”

“ Ouh Samia Fashion,ninawafahamu sana hawa.Wana maduka yao makubwa hata jijini Dare s salaama na Nairobi.Ulikuwa unasemaje Zulfa?”

“Nimeelekezwa na bosi wangu nije nikuchukue nikupeleke dukani kwetu kwa ajili ya kufanya manunuzi ya nguo na vitu vingine.Amesema uchukue chochote kile unachohitaji” akasema Zulfa.



Huku akitabasamu Penny akaingia chumbani kwake akajiweka tayari halafu wakaondoka

“ Hii ni kazi ya kareem kwani alinikataza kubeba mzigo wowote na kuniahidi kwamba nitanunua kila kitu huku Arusha” akawaza Penny akiwa garini kuelekea Samia fashion Hakuna aliyekuwa akifahamu kwamba penny yuko jijini Arusha.Kareem mlinzi wa rais ambaye anamuamini mno na ambaye huwa anamtuma katika mambo yake mengi ya siri,ndiye aliyemsafirisha Penny toka Dar hadi Arusha baada ya kupewa maelekezo na rais. Saa tisa za usiku alimpigia simu penny na kumtaka ajiandae kwa safari ya kuelekea Arusha.Hakuwa na kipingamizi kwani alikwishapewa maelekezo ya kukubali chochote atakachoambiwa na rais.



Saa kumi na moja juu ya alama lilifika gari na kumchukua kumpeleka uwanja wa ndege akapanda ndege maalum ya kukodi kuelekea Arusha ambako alikwisha andaliwa chumba katika hoteli ya kifahari ya Kobe village. Katika duka la Samia FashionPenny alifanya manunuzi makubwa na kurejea hotelini kwake



“ Dr Joshua safari hii amepania hasa kuusuuza moyo wangu na ndiyo maana ananifanyia mambo haya makubwa kiasi najihisi kama malkia.Atapata anachokitaka lakini na mimi nitakipata ninachokitaka na baada ya hapo mimi na yeye mkataba utavunjwa na nitaishi maisha ya hali ya juu kuzidi haya.” Akawaza Peny akiendelea kujaribisha mavazi aliyonunua.

“ safari hi sintofanya tena kosa nikipata tu nafasi namaliza kila kitu.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumpa Dr Joshua penzi la kiwango cha juu ambalo hajawahoi kupewa na mwanamke yeyote chini ya jua .Ninafahamu udhaifu wake ulipo na hapo ndipo nitatumia kumshikia na kumfanya asifurukute na baadaya hapo yeye mwenyewe ataniachia njia na nitafanya ninachokitaka” akawaza.



***********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Jaji Elibariki akiwa ofisini kwake akapigiwa simu na katibu muhtasi wake na kumfahamisha kwamba kuna mgeni wake ambaye ni Anna mtoto wa rais.jaji Elibariki akatoa ruhusa aruhusiwe kuingia ofisini i.

“Shikamoo shemeji” akasema Anna ambaye uso wake ulionyesha dhahiri kwamba alikuwa na hasira

“ marahaba Anna.Hujambo? “ Sijambo “ akajibu kwa ufupi na kuvuta kiti akaketi “ Nimekuja kusikiliza ulichoniitia” akasema Anna kwa sauti ya juu kidogo

“ Anna nashukuru kwa kufika kwako.Nilikuwa na hofu pengine hutafika” akasema Jaji Elibariki “ Go straight to the point ,sina muda mwingi wa kukaa hapa” akasema anna kwa sauti iliyoonyesha dharau kidogo

“ Anna nimekuita hapa ili tuongelee kuhusiana na jambo liilotokea siku mbili zilizopita kuhusiana na kesi iliyomalizika iliyomuhusisha Penny.” Mara tu alipotamka jina la Penny ,Anna akabadilika usoni

“ Please !..



I don’t want to hear anything about penny” akasema anna kwa ukali.

“ Tafadhali naomba tuliza jazba Anna ili tuongee kwa undani kuhusu suala hili”

“Tuongee kuhusu nini tena ?Tayari umekwisha toa hukumu na muuaji umemuachia huru sasa unataka tuongee nini zaidi?

“ tafadhali naomba unisikilize Anna kile nilichokita hapa ” akasema Jaji Elibariki



“ Nitakusikiliza kama una lingine la kuniambia lakini si suala la hukumu uliyotoa ukamuachia muuaji.Hujui ni namna gani nilivyompenda Edson.Kitendo cha kumuachia huru muuaji aliyemuua mtu niliyempenda wakati kuna kila aina ya ushahidi kuthibitisha kwamba penny alimuua Edson kimenifanya nikutoe thamani kabisa na sina hakika kama unafaa kuwa mmoja wa wanafamilia yetu.Tulikutegemea utende haki lakini umepindisha haki ukampendelea Yule kahaba…..”



Akasema Anna na kumpandisha hasira Jaji Elibariki ambaye alisimama na kumnyooshea Anna kidole kwa hasira

“ Anna naomba iwe ni mara yako ya kwanza na ya mwisho kunionyeshea dharau namna hii.Nimekuita hapa kwa lengo zuri tu ili tuongee na tusaidiane kumpata muuaji wa Edson lakini wewe hutaki kunisikiliza na badala yake unanifanyia dharau.Nimechoka kuwavumilia wewe na familia yenu yote kwa dharau mnazonifanyia.Mimi ni jaji wa mahakama kuu na sifanyi maamuzi kwa shinikizo la mtu yeyote awe ni rais au nani.Ninatenda haki kwa kila mtu.Naomba vile vile iwe ni mwanzo na mwisho kumuita Penny kahaba.Mara nyingine ukithubutu kuja na kutoa matusi katika ofisi hii nitasahau kama baba yako ni rais wa nchi na nitakuharibu sura yako.Toka haraka ofisini kwangu !! ” akasema kwa hasira jaji Elibariki.



Aliku wa amekasirishwa mno na maneno aliyoyatamka Anna

“ Sawa ninaondoka lakini ukae ukijua kwamba huna muda mrefu katika kiti hicho ambacho umepewa tu kwa hisani ya baba yangu” akasema Anna huku akiondoka.Maneno yale yakazidi kumkasirisha sana jaji Elibariki.Alitamani amrukie na kumuadhibu vikali lakini akajitahdii kujizuia na kumuacha aondoke.



“ Dah ! Sijawahi kukutana nafamilia yenye dharau kama hii.Nilimuita kwa nia njema tu ya kuja kuongea masuala ya msingi ili tushirikiane kumbaini muuaji wa Robin lakini nimeambulia matusi na dharau.Sijawahi kudharauliwa kiasi hiki katika kazi yangu na sintokubali kamwe kuendelea kudharauliwa hasa na familia hii.” Akawaza jaji Elibariki huku amefura kwa hasira.Akachukua simu yake na kuzitafuta namba fulani akapiga “ Hallo Mathew” akasema Jaji Elibariki



“ hallo jaji.habari za siku? Leo umenikumbuka ndugu yangu lazima utakuwa na tatizo.”

“ Ni kweli nina shida ndugu yangu nahitaji kukuona” akasema Elibariki

“ Unataka tuonane saa ngapi?

“ sasa hivi.Uko wapi?

“ Niko nyumbani kwangu”

“ Ok njoo utanikuta lakini tafadhali naomba uje peke yako.Sitaki uwe umeambatana na mlinzi yeyote”

‘ Nitakuja mimi mwenyewe.dereva wangu ana matatizo ya kifamilia na nimempa likizo ya muda” akasema Elibariki

“ Good” akajibu Mathew na kukata simu.jaji Elibariki akainuka akavaa koti lake na kutoka “ It’s time for action now” akasema jaji Elibariki huku akiingia garini.

“Mbivu na mbichi lazimazijulikane katika kipindi kifupi” akasema kwa sauti ndogo



Jaji Elibariki waliwasili katika jumba moja kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa.Alipiga honi mara tatu na toka katika mlango mdogo wa geti akatokeza mlinzi akiwa na mbwa mkubwa akamfuata Elibariki katika gari

“ habari yako mkuu” Akasema Yule mlinzi aliyevalia sare za ulinzi za kampuni binafsi ya ulinzi

“ Habari nzuri.Nina miadi na ndugu Mathew” akasema jaji Elibariki

“ Wewe ndiye Elibariki? Akauliza Mlinzi

“Ndiye mimi”

“ Ok.taarifa zako ninazo” akasema Yule mlinzi huku akiingia ndani na kufungua geti.Jaji elibariki akaingia .



Mbwa watatu wakubwa wakalizingira gari lile na kuanza kubweka kwa nguvu.jaji Elibariki akaogopa kushuka ndani ya gari kwa namna mbwa wale walivyokuwa wakubwa.Mlinzi akafika mara moja na kuwatuliza akawapeleka katika nyumba yao.Elibariki akashuka na kuongozwa na mlinzi hadi ndani.Akakaribishwa sebuleni.Ilikuwa ni sebule kubwa yenye vitu vingi vya thamani.Baada ya dakika kama nne hivi Mathew akatokea.Ni mtu mmoja mfupi mwenye mwiliwa wastani.



“ Mheshimiwa jaji.habari za siku ndugu yangu?

“ habari nzuri Mathew.Maisha yanakwendaje?

“ maisha yanakwenda vizuri.Mungu ananiwezesha.Vipi wewe mambo yako yanakwendaje?

“ Mambo yangu yanakwenda vizuri lakinisi vizuri sana.”

‘Nini tatizo Elibariki? Mpaka uje kwangu lazima ni tatizo kubwa.Niambie nini tatizo? Niko tayari kukusaidia.Wewe ni rafiki yangu mkubwa.Hukuniacha wakati nina matatizo .” akasema Mathew huku akiwasha sigara yake na kuvuta

“ Mathew,kuna kijana mmoja anaitwa Edson alikuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano ikulu,aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake.Baada ya mauaji hayo mpenzi wake alituhumiwa kwamba ndiye muuaji na kufunguliwa mashtaka.



Kesi imeendeshwa kwa muda wa mwaka mzima na wiki hii nimetoa hukumu na kumuachia huru Yule msichana.Hakuwa na kosa lolote.Hakumuua Edson lakini nguvu kubwa ilitumika kushinikiza mahakama imkute na hatia na hatimaye afungwe maisha gerezani.Shinikizo kubwa lilitoka ndani ya familia ya rais kwani kijana huyo Edson aliwahi kuwa na mahusiano na binti wa rais kabla ya kuachana naye na kuingia katika mahusiano na Penny. Kwa hivi sasa hali si shwari ndani ya ndoa yangu.Mke wangu na ndugu zake wananichukia sana kwa maamuzi niliyoyafanya ya kumuachia huru Penny .Wao wanaamini kwamba penny ndiye aliyemuua Edson.Nimekuwa nikidharauliwa mno na watu hawa kutokana tu na kutenda haki. Baada y kutafakari sana nimeamua kufanya jambo moja la muhimu.



Kumtafuta mtu aliyemuua Edson ili kwanza kuudhihirishia umma wa watanzania kwamba sikukurupuka katika kufanya maamuzi yale na pili kumlinda Penny.Watu ambao walitaka akutwe na hatia na hatimaye apewe adhabu hawatamuacha hivi hivi.Lazima watamuandama na kuhakikisha wanamuondoa kwa namna nyingine.Mathew nimekuja kwako sina msaada mwingine,sina mtu mwingine ambaye anaweza akanisaidia katika jambo hili “ akasema jaji Elibariki.Mathew akainuka na kuelekea katika kabati kubwa akalifungua na kuchukua chupa kubwa ya mvinyo akamimina katika glasi mbili na moja akampatia Elibariki.Akagugumia pombe yote iliyoko katika glasi halafu akavuta mikupuo miwii ya sigara na kupuliza moshi mwingi hewani kisha akasema



“ This is a serious issue than I thought” akasema Mathew kwa sauti ndogo.

“ Si suala dogo hili Mathew na ndiyo maana nimekuja kwako ili unisaidia.Wewe umebobea katika masuala haya ya uchunguzi,umekwisha fanaya kazi katikaidara ya ujasusi ya taifa na una uzoefu mkubwa wa masuala kama haya.Naomba unisaidie kumbaini nani muuaji wa Edson na kwa nini alimuua.Tukifanikiwa katika hilo kila kitu kitakuwa shwari kabisa” akasema Elibariki.Mathew akainama akafikiri tena na kusema

“This girl ..Pe.. Jina lake nani ? Limenitoka kidogo” akasema Mathew

“ Anaitwa penny”

“ Good.This girl Penny who is she to you? Swali lile likamchanganya kidogo jaji Elibariki akafikiri na kusema

“ She’s just an Innocent girl.



Ni mtuhumiwa ambaye hakuwa na kosa na ndiyo maana nikamuachia huru”

“ Eli haujajibu swali langu.Ninafahamu alikuwa mtuhumiwa na hakuwa na kosa .Ninachotaka kufahamu ni mahusiano yako na msichana huyu.Ni ndugu yako,rafiki yako au mpenziwako.Usiogope kuwa muwazi kwangu.” Akasema Mathew

“ Hatukuwahi kufahamiana hapo kabla hadi nilipoanza kuisikiliza kesi yake.Hatukuwahi kuwa na urafiki lakini kwa sasa naweza kusema kwamba tumekuwa marafiki.”

“ Urafiki wa namna gani? Wa mtu na mpenzi wake au urafiki wa kawaida? Akauliza Mathew

“ Ni urafikiwa kawaida tu .” Mathew akavuta sigara na kupuliza moshi halafu akasema

“ Eli nakufahamu vyema,usingeweza kupoteza wakati wako kulishughulikia suala hili kama msichana huyu hana maana yoyote kwako.Please be honnest with me.



I want to help you” “ Ok Mathew,umetaka niwe muwazi na ninakuwa muwazi.Ni kweli msichana huyu ametokea kunivutia sana na tayari nimeanza kuwa na hisia za kimapenzi kwake na ndiyo maana ninajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kumlinda”

“ Sawa Eli,ahsante kwa kuwa muwazi.Nitakusaidia.” akasema Mathew halafu akavuta mikupuo miwili ya sigara na kuizima akatoa nyingine katika pakiti akaiwasha.



“ Kwanza naomba ufahamu kwamba hili si suala rahisi kama unavyolichukulia. Ni suala zito na la hatari kubwa.Lakini nakuhakikishia kwamba tutamtafuta muuaji wa huyo kijana kokote alipo na nitahakikisha ninampata.Sikuwa nikitaka kufanya kazi yoyote ya hapa nchini lakini nitaifanya kazi hii kwa sababu yako” akasema Mathew huku akivuta sigara na kupuliza moshi mwingi hewani

“Mathew ninashukuru sana kukubali kunisaidia katika suala hili.Hata hivyo siko peke yangu katika suala hili.Nina mwenzangu aitwaye Jason ambaye ni wakili wa Penny.Ndiye aliyemsimamia Penny katika kesi hii.”

“ Sawa nimekuelewa Elibariki.Mimi niko tayari kufanya kazi hiyo kwa kutumia uwezo wangu wote.



Naomba unipe muda kidogo wa kutafakari namna nitakavyoweza kuifanya kazi hii.Naomba nionane nanyi kesho asubuhi ili niwape mchakato mzima namna nitakavyoifanya hii kazi. Akasema Mathew halafu wakaendelea na maongezi mawili matatu Jaji Elibariki akaondoka



*********



Saa moja na nusu za jioni,jiji ni Arusha bado mvua za manyunyu zinaendelea.Katika hoteli ya kifahari ya Kobe Village Peniela yuko chumban kwake amejilaza..Pembeni ya kitanda chake kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa na chupa kubwa ya mvinyo akiendelea kunywa tarataibu huku akifurahia muziki katika runinga.Kengele ya mlangoni ikalia kuashiria kwamba kulikuwa na mtu.Akainuka na kwenda kufungua mlango akakutana na muhudumu aliyevaa suti nzuri nyeusi akiwa na kifurushi mkononi

“ madam kuna mzigo wako umeletwa”akasema Yule muhudumu huku akimpa Penny karatasi ya kusaini kwamba amepokea mzigo.Akasaini karatasi ile na kujifungia chumbani akakifungua kile kifurushi kilichofungwa vizuri.

“ Lazima mzigo huu utakuwa umetoka kwa Kareem” akawaza Penny wakati akikifungua.Ndani ya boksi lile kulikuwa na simu nzuri sana ya gharama kubwa



“ Wow ! what a nice phone” akasema Penny huku akitabasamu.Toka ndani ya lile boksi kulikuwa na kikaratasi kidogo kilichomuelekeza penny aiwashe simu ile.Akaiwasha na kuichunguza ndani,hakukuwa na namba yoyote ya simu iliyoandikwamo.Wakati akitafakari ikapigwa simu akaipokea.Aliitambua sauti ya mpigaji,alikuwa ni Kareem.

“ Hallo Penny” akasema kareem

“ Hi Kareem.”



“ Habari za Arusha?akauliza kareem

“ habari nzuri ila kuna baridi sana huku.?

“ Ok.Usizime hii simu.Mzee atazungumza nawe baada ya dakika chache.” Akasema Kareem na kukata simu.Baada ya dakika kama nne hivi simu ikaita tena kwa namba nyingine tofauti na zile za mwanzo,akabonyeza kitufe cha kupokelea



“ Hallo Penny” ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Penny aliitambua ilikuwa ni ya mheshimiwa rais Dr Joshua.

“ Hallo Dr Joshua. Habari yako ? akasema Penny kwa sauti laini “ Habari yangu nzuri.habari za Arusha?

“ huku Arusha kwema kabisa .Habari za Dare s salaam?

“ Huku ni kawaida tu” akasema Dr Joshua

“ Penny mimi ninakuja huo kesho kutwa jioni kwa ajili ya mkutano wa marais wa afrika mashariki utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia jumatatu ijayo.Katika siku hizo zote tatu nitakuwa nikionana nawe baada ya kumaliza shughuli zangu.



Nina mambo mengi sana ambayo nataka kuzungumza nawe na zadi ya yote ukumbuke ni mwaka mzima umepita sasa na sitapata ile raha ya aina yake toka kwako.Nataka unipe raha ,nifurahi “

“ Usijali Dr Joshua.Utapata kila unachokihitaji.Nimefurahishwa sana na namna unavyonijali na kunitunza.Nimeamini kwamba ni kweli umedhamiria kuufungua ukurasa mpya kati yetu.” Akasema Penny na kumfanya Dr Joshua acheke kidogo.



“ Ni furaha yangu kama umeridhika na huduma unayoipata Penny.Wewe ni malaika wangu tumia kitu chochote ukitakacho bila kujali gharama.Omba chochote ukitakacho nitakutimizia’ akasema Dr Joshua

“ Ahsante Dr Joshua.Mambo mengi tutaongea ukishakuja huku”

“ Ok Penny .Endelea kupumzika ,tutakuwa wote kesho kutwa.Nimefurahi kuongea na wewe” akasema Dr Joshua na kukata simu. Baada ya Dr Joshua kukata simu ikaingia tena simu nyingine toka kwa kareem

“ Halloo kareem” akasema Penny

“ Penny kuna jambo nimeona nikukumbushe.Simu hiyo ni maalum tu kwa ajili ya kuwasiliana na rais na mimi pekee.Usije ukathubutu kumpigia mtu mwingine yeyote.Isitoshe ukumbuke tulivyokubaliana hakuna kumpigia simu mtu yeyote Yule na kumweleza kwamba uko Arusha.Umenielewa penny?

“ Ndiyo kareem nimekuelewa” akasema Penny na kareem akakata simu

“ mambo yangu yote yanakwenda vizuri sana.Kila kitu kimekaa katika mstari na kinachofuatia sasa ni kuicheza karata yangu ya mwisho.Sitaki kufanya makosa safari hii.Hiki ndicho kipindi cha lala salama” akawaza Penny.



**********



Jaji Elibariki alirejea nyumbani kwake saa tatu za usiku na kumkuta mke wake Flaviana amekaa sebuleni akitazama filamu.Hakumsalimu akapita moja kwa moja hadi chumbani kwake akabadili nguo na kuingia bafuni akaoga halafu akajitupa kitandanina kuanza kusoma kitabu cha hadithi .Baada ya dakika kama ishirini hivi mke wake akaingia mle chumbani na kusimama pembeni ya kitanda.Alionekana wazi alikuwa na hasira

“ Eli ni tabia gani hiyo umeianza ya kuingia ndani bila hata salamu? Akauliza Flaviana.Jaji Elibariki akajifanya kama vile hajasikia akaendelea kujisomea kitabu chake cha hadithi



“Nakuuliza Eli ni tabia gani hiyo ya kuingia ndani bila hata ya kutoa salamu? Nini kinakupa kiburi siku hizi? Au ni hao wanawake unaowakingia kifua ndio wanaokupa kiburi siku hizi? akauliza kwa dharau Flaviana.Taratibu bila kuongea chochote Jaji Elibariki akainuka na kumfuata mkewe na kumzaba kibao kikali kinachomfanya apepesuke na kuangukia kitandani

“ Na iwe ni mwisho kunidharau nakunitolea maneno ya kashfa.Nimechoshoshwa na dharau zako .Nilikwisha kuonya kuhusiana na tabia hii ya dharau hukutaka kunisikia.”akasema kwa hasira Elibariki huku penny akiendelea kulia kwa nguvu.Ni mara ya kwanza toka wameoana Jaji Elibariki kumpiga kofi mke wake.



“ Ahsante Elibariki..ahsante sana..Wewe si mtu wa kunipiga mimi !...” akalia kwa uchungu Flaviana.

“ Toka nimezaliwa hata baba yangu hajawahi kunipiga kofi sembuse wewe ng’ombe ! ..Kauli ile ikampandisha hasira Elibariki na kuanza kumshushia mke wake kipigo kikali kilichomfanya apige ukelele mkubwa .Jaji Elibariki hakujali kelele zile akaendelea kumpa kipigo mkewe.Hadi anamuachia Flaviana alikuwa anavuja damu.



“ Siku nyingine usithubutu kabisa kunidharau paka wewe ..! akasema jaji Elibariki huku akitweta kwa hasira Huku akilia,Flaviana akaingia bafuni na kujifuta damu zilizotoka katika majeraha yaliyotokana na kipigo kikali

“ Eli umenipiga hadi kunitoa damu.Sasa nitakuonyesha mimi na wewe nani mwenye nguvu.I swear in heaven and earth lazima nikuonyeshe kazi na hautanisahau mpaka unaingia kaburini”akasema kwa hasira flaviana na kutoka kwa kasi akaingia katika gari lake na kuondoka kwa kasi

“ Nimechoshwa na dharau za familia hii.Yote hii ni kwa sababu baba yao ni rais .Hapana hawawezi kunitisha hata kidogo,hakuna aliye juu ya sheria.” Akasema jaji Elibariki kwa hasira.





Jaji Elibariki alikaa kitandani na kuanza kutafakari maisha yaketoka alipokutanana Flaviana ,wakapendana,wakwa wachumbanabaadae wakafungandoa.Aliyatafakari maisha yake ya ndoa toka walipooana hadi leo hii

“ Sina hakika kama tuliingia katika ndoa tukiwa tumejiandaa vya kutosha.Sina hakika kama tulikuwa na mapenzi ya kweli au zilikuwa ni tama tu za ujana.Toka tumeyaanza maisha yandoa hakuna amanindani mwetu.It’s been a living hell to me.Tukiwa nje tunaonekana ni watu wenye mapenzi mazito lakini hajuna ajuaye siri yetu ya ndani.Maisha yetu yamejaa mifarakano,dharauna ugomvi.Nimechoshwa na maisha haya.Nimechoka kuwadanganya watu kwamba tunapendana kwa dhati wakati si kweli.Nadhani ni wakati muafaka sasa wa kufanya maamuzi na kila mmoja wetu akatafute furaha ya maisha yake.Siwezi kuendelea na maisha kama haya” akawaza halafu akaenda katika kabati dogo lililokuwa mle chumbani akalifunguana kutoa chupa ya mvinyo akajimiminia katika glasi akanywa na mara sura a Peny ikamjia kichwani “ Penny !!..akasema kwa sauti ndogo huku akitabaamu

“ Mwanamke kama Penny anafaa sana kuwa mke.Aba uzuri wa kipekee ambao sioniwa kumfaanisha naye na ana adabu na hata ukiongea naye utabaini wazi kwamba ni mwanamke mqwnye heshima kubwa/Jaji Elibarikiakaendelea kuwaza na mara akastuliwa namlio wa simu.Akaichukuana kutazmaa mpigaji ,alikuwa ni baba mkwe wake Dr Joshua,rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

“ Kazi imeanza” akasema kimoyo moyo na kubonyeza kitufe cha kupokelea simu

“ Hallo mzee shikamoo”

“ Marahaba mheshimiwa jaji,habari za kwenu?

“ Habari nzuri tu mzee,sijui ninyi huko”

“ Sisi wazima.Eli uko wapi?

“ Niko nyumbani mzee”

“ Ok vizuri.Nakuomba hapa ikulu sasa hivi nina maongezi nawe” akasema Dr Joshua na kukata simu

“ Flaviana amekwenda kunishitaki kwa baba yake akidhani labda nitamuogopa.Sintomuogopa mtu yeyote hata kama ni rais wan chi.Kuanzia sasa yeyote atakayenidharau kwa namna yeyote ile nitapambananaye” akawaza huku akivaa koti na kutoka kueleka ikulu kuonana na baba mkwe wake. Ilimchukua dakika zaidi ya hamsini kuwasili katikamakazi ya rais.Baada ya kama dakika kumi na tatu toka awasili ,Dr Joshua akajitokeza sebuleni.Jaji Elibariki akasimama wakasalimiana “ Mheshimiwa jaji ,hebu nieleze nini kimetokea huko kwenu na kusababisha umpige mwenzako na kumuumiza kiasi kile? Akaanzisha mazungumzo Dr Joshua.Elibariki akavuta pumzi ndefu na kisha akamsimulia rais kila kitu kilichotokea na kusababisha apandwe na hasira na kumpiga mkewe.

“ Nimekuelewa Elibariki ,lakini pamoja na yote aliyoyafanya mwenzako ulitakiwa ujizuie, hukupaswa kufikia hatua ya kumpiga mwenzako namna ile.Migongano ndani ya nyumba ni kitu cha kawaida na suluhisho lake ni kukaa mkaongea mkayamaliza na si kurushiana makonde.Wewe kama kichwa cha nyumba unahitajika uwe na busara ya hali ya juu “ akasema Dr Joshua

“ Nakuelewa mzee,lakini nilifikia maamuzi ya kumpiga kidogo mke wangu kutokana na dharau alizoniletea.Kama nilivyokueleza mzee ni muda mrefu sasa amekuwa akinidharau sana na leo hii uvumilivu ulinishinda nikaona bora nimuonye kidogo” akasema Elibariki “ Siku nyingine endapo atakuletea dharau na kiburi,wasiliana nami moja kwa moja kabla ya kuchukua maamuzi ya kumpiga.Sipendi sana kuona mwanangu yeyote akilia machozi na hasa ya kupigwa na mwanaume” akasema Dr Joshua

“Lakini mzee, Flaviana ni mke wangu na mambo yetu yanndani tunayamaliza wenyewe.Haitapendeza kila siku niwe nakupigia simu na kukwambia kwamba mwanao amenidharau.Naomba mzee utuachie mambo yetu ya ndani tuyamalize sisi wenyewe.” Akasema Elibariki

“Kuyamaliza kwa staili hii ya kutoana damu? No !.. Sitaki kabisa mwanangu aguswe tena na kutolewa damu.Usinione ninaongea nawe hapa lakini nimechukizwa mno na kitendo ulichokifanya leo cha kumpiga mwanangu.Naomba kisijirudie tena.Marufuku kumfanya mwanangu sehemu ya mazoezi” akasema Dr Joshua kwa sauti ya juu yenye amri ndani yake .Jaji Elibariki akakereka sana kwa maneno yale ya baba mkwe wake

“ Lakini mzee………….” Akataka kusema jambo ,akazuiwa na Dr Joshua

“ Hakuna cha lakini…..Nimesema sitaki mwanangu aguswe and that’s fnal.Sitaki tena mjadala.Hata akikukosea vipi sitaki umpige.Nieleze mimi mwenyewe nitaongea naye” akasema kwa ukali Dr Joshua “ lakini mzee huyu ni mke wangu na amekuwa akinifanyia mambo mengi ya dharau ambayo siwezi hata kukueleza.Unapoongea maneno kama hayo unampa nguvu ya kufanya anachokitaka kwangu kwa kuwa anajua baba yake anamtetea” akalalamika Elibariki.Dr Joshau akasimama na kumsogelea “ I’m her father and I’m warning you….” Akasema Dr Joshua.maneno yale yakamkera sana Elibariki naye akasimama. “ Yes 1 you are her father but I’m her husband !!.... akasema Elibariki kwa sauti ya juu kidogo.

“ Elibariki,tafadhali chunga sana maneno unayoongea mbele yangu.Wewe bado hauna uwezo wa kusimama na kubishana na mimi.Ukumbuke kwamba ni mimi ndiye niliye kutoa huko maporini na kukupandisha hadi hapa ulipo.kwa hiyo kuwa makini sana siku nyingine unapoongea na mimi.Nina uwezo wa kukufanya chochote kile” akafoka dr Joshua.Elibariki akamtazama kwa macho makali na kusema

“ Naomba unisikilze mzee.Nimechoshwa na wewe na wanao kila mara kunisimanga kutokana na cheo hiki.Naomba mfahamu wewe na wanao kwamba cheo hiki hukunipa wewe bali nimepewa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania na nimepewa kwa sababu ninafaa na nina vigezo vyote vya kuwepo hapa nilipo.Kwa maana hiyo naomba muache kuanzia sasa kunisakama kuhusiana na cheo hiki.Kitu kingine mnachotakiwa kukifahamu ni kwamba ofisi hii si mali ya familia,kwa hiyo si wewe wala wanao mnaoweza mkanishinikiza nifanye kazi yangu kwa matakwa yenu.Ninaifanya kazi yangu kwa mujibu wa sheria za nchi na si kwa kumfurahisha mtu Fulani..”akasema kwa ukali na kutoka kwa hasira akimuacha Dr Joshua akishangaa.

“ Nimemueleza ukweli wake,akichukia shauri lake,nimechoshwa na dharau zao” akawaza Elibariki huku akiingia katika gari lake na kuondoka

“ Kichwa changu kimevurugwa kabisa na Yule mzee.I need someone to talk to.I need some comfort” akawaza na mara sura ya penny ikamjia

“ penny !!... I need to talk to her.pengine kichwa changu kinaweza kutulia” akapunguza mwendo wa gari akatoa simu na kuzitafuta namba za Penny ,akapiga lakini haikuwa ikipatikana.

*********

Asubuhi na mapema jaji Elibariki aliamka na kufanya mazoezi ya viungo halafu akajianda na kuondoka.Flaviana hakurejea nyumbani usiku toka alipoondoka

“ Nadhani huu utakuwa ni mwanzo wa maisha mapya.Sina hakika kama kuna suluhu yoyote itapatikana tena baina yangu na Flaviana.Ni wakati sasa wa kuanza kuitafuta upya furaha ya moyo wangu ambayo nilitegemea kuipata kwa Flaviana lakini kumbe nilikuwa najidanganya.Nimeambulia karaha badala ya raha.Toka nilipomuoa hadi hivi leo hata mtoto amekataa kunizalia kwa kisingizo cha kutokuwa tayari.Hapana imetosha sasa.Maisha haya lazima yafikie mwisho.Kwa sasa ngoja kwanza nielekeze nguvu kumtafuta muuaji wa Edsoni ili Penny aweze kuwa salama” Mara tu alipomkumbuka Penny,akatabasamu na kutoa simu yake akazitafuta namba za Penny akapiga lakini bado simu yake haikuwa ikipatikana.

“ Ameamua kuizima simu yake,inawezekana hataki usumbufu toka kwa watu.Ametoka katika matatizo makubwa na anahitaji muda wa kukaa mwenyewe atafakari maisha yake bila usumbufu toka kwa watu” akawaza Jaji Elibariki Moja kwa moja alielekea Mandarini Hotel mahala ambako hupenda sana kwenda kupata kifungua kinywa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Watu wengi wananishangaa ni kwa nini mtu kama mimi,Jaji wa Mahakam kuu ninakuja kupata kifungua kinywa hotelini? Hawajui Kero nilizonazo katika ndoa yangu.lakini soon mambo yote haya yatakwisha and I’ll be happy again.” Akawaza wakati akiendelea kupata kifungua kinywa. Toka Mandarin hotel,akaelekea ofisini kwake ambako hakukaa sana akatoka akaelekea mahala alikopanga akutane na Mathew.



Dakika kumi baada ya kuwasili Malaika Lounge mahala walikopanga wakutane na Mathew,Jason akawasili, wakasalimiana akavuta kiti na kuketi

“ Jason” akaanzisha mazungumzo Jaji Elibariki

“ kama nilivyokueleza simuni ,nimefikiria sana kuhusiana na jambo tunalotaka kulifanya na kuona ugumu wake .Sisi tumebobea katika masuala ya sheria na hatuna taaluma yoyote ya kufanya uchunguzi.Ni kwa sababu hii nimelazimika kumtafuta Mathew Kwanga” akanyamaza kidogo ,akamtazama Jason na kuendelea.

“ Mathew Kwanga aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa na aliacha kazi hiyo baada ya familia yake yote kuteketezwa kwa moto.Kwa hivi sasa yeye ni mtu anayekodishwa na mataifa kazi za siri za kiuchunguzi .Ni mtu aliyebobea mno katika kazi hizi .Nina imani atatufanyia kazi nzuri “ akasema Jaji Elibariki

“Umefanya jambo la msingi sana mheshimiwa jaji.Hata mimi nilikuwa nafikiria kukushauri tufanye kitu kama hicho.Sisi peke yetu hatuwezi kulifanikisha jambo hili .Tunahitaji msaada wa mtu mwenye uzoefu wa kutosha na mambo haya.Natumai Mathew ni chaguo sahihi na atakuwa na msaada mkubwa sana kwetu” akasema Jason

“ Exactly !...Thats my point..Mathew ni mtu ambaye tumefahamiana kwa muda refu na sina shaka yoyote na uwezo wake.Ni mtu mwenye uwezo wa hali ya juu sana.By the way how’s Peniela? Akauliza Jaji Elibariki.Jason akaguna kidogo na kusema

“ Siku ya pili sasa hapatikani simuni”

“ May be she needs sometime alone. Unajua ametoka katika matatizo makubwa kwa hiyo yawezekana akahitaji kuituliza akili yake bila bughudha za watu.Let’s give her sometime” akasema Jaji Elibariki na mara Mathew akatokea.Alikuwa ni kijana nadhifu aliyevaa suti nzuri iliyompendeza

“ Hallo gentlemen…” akasema Mathew huku akipeana mikono na akina Jason

“ Mathew kutana na Jason,wakili maarufu sana hapa Tanzania.” Bila kuchelewa Jaji Elibariki akaanza kutoa utambulisho

“ Jason kutana na Mathew Kwanga.Ni rafiki yangu wa siku nyingi na mtu aliyebobea katika masuala ya kiuchunguzi”

Jason na Mathew wakashikana mikono kwa kujuana

“ Mtanisamehe sana ndugu zangu kwa kuchelewa .Nilipatwa na dharura ya ghafla” akasema Mathew

“ Usijali Mathew.Hakuna kilichoharibika.Nadhani umelifanyia kazi lile suala letu” akasema Jason

“ Ndiyo mheshimiwa Jaji.Nimejaribu kutafakari kwa kina kuhusiana na kazi mliyonipa na namna nitakavyoweza kuifanya.Naomba niwaweke wazi kwamba kazi hii si ndogo kama mnavyoifikiria. Edson alikuwa mfanyakazi katika kitengo cha habari Ikulu,huyu si mtu mdogo kama watu wanavyoweza kudhani.Ninashawishika kuamini kwamba lazima aliuawa kwa sababu maalum.Kazi yetu ni kuitafuta sababu hiyo iliyopelekea yeye kuuawa pamoja na watu waliomuua na kesi kumuangukia Peniela.Kazi hii si nyepesi lakini nawaahidi kwamba hakuna yeyote ambaye alikuwa na mkono wake katika mauaji hayo atabaki salama.Nitawatafuta katika kila pembe ya nchi hii na dunia mpaka nihakikishe nimewatia mikononi wale wote waliofanya kitendo hicho cha kinyama na mzigo wote wakamuangushia Penny.” akanyamaza kidogo na kuendelea

“ Kabla hatujaendelea mbele zaidi naomba tukubaliane kwanza kitu kimoja.kazi hii ni ya gharama kubwa.Kabla sijaingiza mguu wangu katika uwanja wa mapambano nahitaji kufahamu kama mtakuwa tayari kwa gharama za shughuli hii japokuwa haitakuwa kubwa kwani ninaifanya tu kwa ajili ya ninyi ndugu zangu lakini sikuwa nataka kufanya kazi yoyote hapa nyumbani.” Akasema Mathew.Jason na Jaji Elibariki wakatazamana na Jason akasema

“ Tuko tayari Mathew.Usihofu kuhusu gharama”

“ Ok Good.Sasa tunaweza kuendelea” akasema Mathew.

“ Katika kazi hii pia nitashirikiana na watu wawili.Wa kwanza ni Anitha Monera na wa pili ni Noah Ikuso.” Akasema Mathew huku akiwapa akina Jason mafaili ya watu hao wayapitie

“ Anitha Monera ana miaka ishirini na tisa.Ni mtanzania anayeishi nchini Marekani.Huyu ninamuita ni mchawi wa kompyuta. Anaichezea kompyuta kwa kiasi cha kushangaza .Nimekuwa nikimtumia sana katika kila kazi ninayoipata na siwafichi ndugu zangu huyu amekuwa ni msaada mkubwa kwangu na ndiye amenifanya nifanikiwe katika kila kazi ninayopata” akanyamaza kidogo na kuendelea

“ Noah ikuso naye ni mtanzania pia.Ana umri wa miaka thelathini na tatu .Aliwahi kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa .Ni kijana mahiri na hodari katika kazi.Ninao wengi ambao ninaweza kufanya nao kazi hii lakini nimewachagua hawa wawili ambao naamini wanatosha sana kuikamilisha hii kazi kwa umahiri na haraka” akasema Mathew.Jason na jaji Elibariki waliendelea kupitia mafaili ya vijana wale halafu Jason akasema

“ Kwa upande wangu sina kipingamizi chochote.Kama unawaamini vijana hawa kwamba wanaweza kazi basi unaweza kuwatumia”

“ Yah ! ninawaamini sana.Ni mahodari na hawana mchezo katika kazi.” Akasema Mathew,kikapita kimya kifupi akauliza

“ Kuna kitu kimoja bado hamjaniweka wazi.Nina hakika nitawapata watu hawa waliofanya kitendo hiki,lakini je wakipatikana nini kitafuata? Wanashughulikiwa vipi? Au mtawakabidhi katika mikono ya dola?

“ Lengo letu sisi ni kuwafichua na kuwakabidhi katika mikono ya dola.Kitu kikubwa kinachonisukuma mimi na mwenzangu tuwe tayari kugharamia jambo hili ni kuudhihirishai umma wa watanzania kwamba sikufanya maamuzi ya kukurupuka kumuachia huru Peniela.Nataka watu wawe na imani na mahakama kwamba ndicho chombo pekee chenye kutenda haki bila kujali mtu.Hatuna lengo la kulipiza kisasi,bali tukimbaini muuaji tutamfikisha katika mikono husika na sheria itachukua mkondo wake na sisi tutabaki salama.” Akasema Jaji Elibariki

“ Ok sasa nimekuelewa mheshimiwa jaji.usijali watapatikana tu.Kitu kingine ninachohitaji ni kumpata Peniela ili niweze kuongea naye mawili matatu kwani yeye ndiye aliyekutwa eneo la tukio.Nataka niyafahamu mazingira ya tukio namna yalivyokuwa.” akasema Mathew

“ Peniela leo ni siku ya pili simu yake haipatikani na sijui yuko wapi.” Akasema Jason

“ Are you sure she’s ok? Akauliza Mathew

“ Sina hakika sana kwa sababu jana nilikwenda nyumbani kwake lakini getini kulikuwa na makufuli na ilionyesha wazi kwamba hakukuwa na mtu ndani”

“ Ok Vizuri.Wakati tukimsubiri nitaanza uchunguzi wangu kwa Edson.Ninataka mnielekeze mahala alipokuwa akiishi na baada ya hapo mtaendelea na kazi zenu kama kawaida na mimi nitaendelea na kazi yangu,popote nitakapokwama na kuhitaji msaada wenu nitawaambia” akasema Mathew.Wakaendelea na kikao chao na kupeana maelekezo kadhaa halafu Jason na Mathew wakaeleekea mahala alipokuwa akiishi Edson.

“ Umeshawahi kuonana na huyo kijana Edson? Akauliza Mathew wakiwa garni

“ Hapana sijawahi kuonana naye hata mara moja”

“ Umewahi kuingia ndani mwake?

“ Ndiyo nimeingia mara moja tu wakati kesi ikiendelea.Kuna wakati iliilazimu mahakama ihamie hapa kuthibitisha madai ya upande wa mashtaka.”

“ Ok Good.” Akasema Mathew na safari ikaendelea.

Jason akaegesha gari nje ya nyumba aliyokuwa akiishi Edson

“ Ni hapa” akasema.Mathew akaitazama nyumba ile halafu akashuka na kumuomba Jason amsubiri garini.Akaelekea getini akabonyeza kengele ya getini na baada ya dakika moja mlango mdogo wa getini ukafunguliwa akatoka kijana mmoja .

“ Habari yako ndugu”

“ Habari yangu nzuri.Karibu sana.Nikusaidie nini? Akauliza Yule kijana

“ Samahani ndugu yangu.Nimemkuta Edson? Akauliza Mathew

“ Edson?!.. yule kijana akashangaa

“ Ndiyo Edson.”

“ Yawezekana umekosea nyumba.Hakuna Edson anayeishi humu ndani”

“ Yawezekana nimekosea .Ninaishi nje ya nchi na mara ya mwisho nilipokuja huku Tanzania Edson alinileta hapa mahala alipokuwa anaishi na ndiyo maana nimekuja moja kwa moja hapa.Yawezekana nimepotea nyumba lakini kumbukumbu zangu zinaniambia ni hapa hapa.” Akasema Mathew

“ Anafanya kazi wapi huyo Edson? Pengine naweza kukusaidia kumtafuta “ akasema Yule kijana

“ Edson anafanya kazi ikulu” akajibu Mathew

Yule kijana akamtazama Mathew kwa mshangao kidogo na kuuliza

“ Mara ya mwisho mliwasiliana lini ?

“ Nina zaidi ya mwaka sasa sijawasiliana naye”

“ Dah ! pole sana kaka.Kama unamuongelea huyo kijana aliyekuwa akifanya kazi ikulu ni kweli alikuwa akiishi hapa lakini inasemekena aliuawa na ndiyo maana wazazi wake wakaamua kuiuza nyumba hii”

Mathew akaonyesha mstuko mkubwa.

“ Dah sikuwa na taarifa hizo.Ahsante sana kwa taarifa hizo ndugu yangu.Nitakwenda kuwapa pole wazazi wake” akasema Mathew na kurejea garini.

“ Wazazi wa Edson wamekwisha iuza nyumba hii .Kwa maana hiyo vitu vyote vya Edson viliondolewa hapa na nina hakika vilipelekwa nyumbani kwa wazazi wake.Nahitaji kukagua vitu vyake.Nahitaji kuikagua simu aliyokuwa akiitumia na kompyuta yake kama bado vipo.“ akasema Mathew

“ Kama ni hivyo itatulazimu kwenda nyumbani kwa wazazi wake na kuonana nao na kuwaomba kupitia vitu hivyo” akasema Jason

“ Hiyo ndiyo hatua inayofuata.Unafahamu mahala wanakoishi wazazi wake?” Akasema Mathew.

“ Ndiyo ninapafahamu.Baba yake ni mtu maarufu sana hapa mjini..” akasema Jason..

“ Ok.Kama tukionana na wazazi wa Edson tukaongea nao tunaweza kupata japo sehemu ya kuanzia.” Akasema Mathew.





Jason na Mathew wakawasili katika makazi ya wazazi wa Edson.Lilikuwa ni jumba kubwa la kifahari lililozungukwa na ukuta mkubwa.

“ Wow ! inaonekana wazazi wake ni watu wenye kujiweza sana kiuchumi” akasema Mathew

“ Ndiyo.Wanamiliki biashara kadhaa kubwa kubwa hapa mjini.Ni watu wenye kujiweza sana” akasema Jason huku wakishuka na kuelekea katika geti.Mathew akabonyeza kengele ya getini na mlinzi aliyekuwa amevaa sare za kampuni binafsi ya ulinzi akafungua mlango mdogo wa geti

“ Habari zenu jamani” akawasabahi

“ Habari zetu nzuri.Habari za hapa?

“ Za hapa nzuri.Niwasaidie nini? Akauliza Yule mlinzi

“ Tuna hitaji kuonana na mzee Robinson Kobe”

“ Mzee si rahisi kumpata mida hii.Yuko katika shughuli zake.”

“ Vipi kuhusu mama? Yeye tunaweza kumpata? Akauliza Mathew

“ Hata mama naye ametoka “

“ Unaweza kutuelekeza mahala tunakoweza kumpata mama au mzee?

“ naweza kuwaelekeza ofisi ya mama ilipo lakini mzee ni mtu mwenye mizunguko mingi sana na kumpata si rahisi hata kidogo” akasema mlinzi na kuwaelekeza katika ofisi ya Bi Hellen Kobe mama wa Edson.Bila kupoteza muda Mathew na Jason wakaingia garini na kuelekea Kobe Shopping mall ambao ndiko iliko ofisi ya Bi Hellen.

Waliwasili Kobe’s shopping mall wakaegesha gari na kushuka wakaingia ndani ya jengo.Watu walikuwa wengi sana wakifanya manunuzi ndani ya jengo hili lililokuwa na biashara nyingi ndani yake

Kwa kutumia Lifti wakapanda hadi ghorofa ya tano iliko ofisi ya Bi Hellen Kobe mama wa Edson

“ Sina hakika kama Bi Hellen atakubali kuongea nasi endapo ataniona” akasema Jason

“ Kwa nini? Akauliza Mathew

“ Ananifahamu .Tumekuwa tukionana mahakamani wakati wa kesi na ananifahamu mimi ndiye wakili niliyemtetea mtuhumiwa wanayeamini kwamba ndiye alimuua mtoto wao.Lazima atakuwa na hasira nami” akasema Jason

“ Usijali Jason.Ataongea tu” akasema Mathew kwa kujiamini

Kabla ya kuingia katika ofisi ya Bi Hellen Kobe iliwalazimu waonane kwanza na katibu muhtasi wake ambaye aliwasiliana naye na kuwaruhusu waingie wakaonane naye.Wakati wakiingia ndani ya ofisi Bi Hellen,alikuwa anaongea na simu na mara tu alipokutanisha macho na Jason,mkono wa simu ukamponyoka na kuanguka mezani.Alistuka sana.

“ Ouh my gosh ! This is unbelievable !!..akasema Bi Hellen

“ You again….!!..Umeamua kunifuata hadi huku..!! akafoka Bi Hellen

Jason na Mathew hawakusema kitu wakaingia mle ofisini na kusimama mbele ya meza.

“ Shikamoo mama” akasema Mathew.Bi Hellen hakujibu kitu akainua mkono wa simu na kumpigia katibu muhtasi wake

“ Irene naomba tafadhali watoe watu hawa ofisini kwangu haraka sana.” Akasema kwa ukali Bi Hellen.Mathew akamnong’oneza kitu Jason ,akatoka mle ofisini.Bado Bi Hellen aliendelea kumuangalia Mathew kwa jicho kali hata baada ya Jason kutoka.Katibu muhtasi wa Bi Hellen akaingia mle ndani kwa ajili ya kumtoa Mathew ,huku akitabasamu Mathew akamwambia

“ Its ok Irene.Nina maongezi kidogo na mama ya muhimu sana.Naomba dakika tatu halafu nitatoka.We’re not here for trouble” Irene akamtazama Bi Hellen ambaye alimtazama Mathew usoni kwa sekunde kadhaa halafu akamfanyia ishara aketi kitini.

“ mama naomba nikusalimu tena shikamoo” akasema Mathew baada ya kuketi

“ Marahaba kijana.Una shida gani manake Yule mwenzako tayari amekwisha niharibia siku yangu.Simpendi na sitaki hata kumtia machoni”

“ Mama utanisamehe kwa kuongozana naye lakini ilinilazimu kufanya hivyo kwa sababu jambo lililonileta hapa hata yeye linamhusu vile vile” akasema Mathew

“ Ni jambo gani hilo lililowaleta? Akauliza Bi Hellen

“ Ni kuhusiana na mwanao Edson”

Bi Hellen akastuka kidogo

“ Edson?!

“ Ndiyo mama”

“ Unataka kunieleza nini kuhusu Edson?

“ Mama ,mimi naitwa Mathew ni mtu ninayefanya kazi za kiuchunguzi na kwa sasa ninafanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanao Edson” akasema Mathew

Bi Hellen akavuta pumzi ndefu ,akaweka kalamu yake mezani na kusema

“ Sikuelewi una maanisha nini unaposema unafanya uchunguzi wa kifo cha mwanangu.Tayari uchunguzi ulikwisha fanyika na muuaji akapatikana,akapandishwa kizimbani lakini kwa sababu wanazozijua wao mahakama ikamuachia huru,sasa unanishangaza unaposema kwamba unafanya uchunguzi wa kifo cha Edson” akasema Bi Hellen

“ Mama ,ninatamani sana tuongee jambo hili kwa upana wake lakini hapa si mahala pake.Naomba kama utakuwa tayari tuonane jioni ya leo nyumbani kwako ukiwa wewe na mzee na tutaongea kwa kina kuhusiana na jambo hili” akasema Mathew

“Mathew naona unanipotezea muda wangu wa kufanya kazi.Hakuna haja ya kufanya uchunguzi tena wakati kila kitu kiko wazi na muuaji alikwisha patikana lakini akaachiwa huru.Sisi tumekwisha muachia Mungu”

Mathew akamtazama Bi Hellen kwa makini na kusema

“ Mama ,mtu mnayeamini kwamba ndiye aliyemuua mwanenu siye.Peniela hakumuua Edson” akasema Mathew huku akiinuka.

“ Saa moja jioni ya leo nitakuja kuzungumza nanyi.Hakikisha mzee naye yupo ili tuzungumze sote kwa pamoja” akasema Mathew na kuondoka.Moja kwa moja akaelekea mahala walikoegesha gari ambako alimkuta Jason akimsubiri garini

“ Nilifahamu toka mwanzo Yule mama asingekubali kuongea nasi pindi akiniona.She hates me” akasema Jason

“ Usijali Jason.Jukumu letu ni kuwahakikishia kwa vitendo kwamba Penny hakumuua kijana wao.Si rahisi kukuamini kwa sasa lakini itafika wakati ambao wataamini tu. Jason nipeleke nyumbani kwa Penny” akasema Mathew.

“ Nyumbani kwa penny? Jason akashangaa kidogo

“ Yah ! nataka kwenda nyumbani kwa Penny”

“ Penny hayupo nyumbani kwake na hakuna anayeelewa yuko wapi”

“ Usijali Jason.Take me there” akasema Mathew huku akiendelea kuipekua kompyuta yake ndogo.

Baada ya Mathew kutoka mle ofisini ,Bi Hellen alimuita katibu muhtasi wake na kumuomba ampatie dawa zake kwani tayari alianza kujisikia vibaya.Maneno aliyoambiwa na Mathew yalimchanganya sana.

“ Yule kijana ni nani? Akawaza

“ Nani kamtuma afanye uchunguzi huo wakati uchunguzi wa awali ulikwisha fanyika na muuaji akapatikana? Kwa nini aliongozana na Yule wakili aliyemtetea muuaji wa mwanangu? Akawazza Bi Hellen akiwa amekiegemeza kichwa chake kitini.Hakujisikia tena kutaka kufanya kazi yoyote

“ No! hakuna mtu mwingine aliyemuua mwanangu zaidi ya Yule kahaba Peniela.Yeye ndiye aliyekutwa eneo la tukio na kuna kila ushahidi unaoonyesha kwamba ndiye aliyermuua Edson.Simuelewi huyu kijana anaposema kwamba anataka kufanya uachunguzi wakati uchunguzi ulikwisha fanyika na Mahakama ikamuachia mtuhumiwa” akaendelea kuwaza Bi Hellen na kuhisi mwili wake kuanza kutokwa na jasho jingi,akamuita dereva wake na kumuomba amrejeshe nyumbani

“ Yule kijana Mathew amenichanganya sana.Nashindwa nimuamini ama vipi.Amekitonesha kidonda changu kinachojaribu kupona” akawaza Bi Hellen akiwa garini kurejea nyumbani

*********



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog