Search This Blog

Saturday 5 November 2022

PENIELA (STORY YA KIJASUSI) - 3

 






Simulizi : Peniela (Story Ya Kijasusi)

Sehemu Ya Tatu (3)




Jason na Mathew waliwasili nyumbani kwa Peniela.

“ Nisubiri humu humu garini” akasema Mathew huku akivaa glovu na kushuka akaenda getini,akatoa kidude Fulani toka katika koti lake na kulifungua kufuli lililofungiwa mlango mdogo wa geti akaufungua na kuingia ndani.

“ Huyu Mathew anaenda kufanya nini nyumbani kwa Penny wakati mwenyewe hayupo? Itakuaje iwapo Penny atagundua kwamba tumeingia ndani mwake wakati hayupo? Nina hakika akigundua hilo hataniamini tena na kuna hatari hata ukaribu mimi na yeye utapungua. I cant let that happen kwa sababu nina mipango mikubwa kuhusu Penny. Sijapendezwa na namna anavyoifanya kazi yake huyu jamaa” akawaza Jason akiwa garini

Ukuta ulioizunguka nyumba ya Peniela uliwekwa vipande vidogo vidogo vya chupa kwa juu.Mathew akapanda juu ya pipa tupu na kuweka kidude Fulani kati kati ya chupa zile akashuka na kuelekea katika majani mazuri yaliyooteshwa mbele ya nyumba ile ,akaufungua mkoba wake na kutoa kitu fulani mfano wa kipepeo akakibonyeza na kukirusha katikati ya majani yale.Yeyote ambaye angekiona angejua moja kwa moja yule ni kipepeo halisi. Kisha maliza kuviweka vitu vile akatoka akafunga geti na kurejea garini.

“ We can go now” akasema Mathew.Jason akavuta pumzi ndefu na kuliondoa gari maeneo yale.

*********

Katika jengo moja pembeni kidogo ya jiji la Dare s salaam,watu nane wameizunguka meza kubwa ya duara.Ni saa ya pili sasa wako katika kikao kizito.Mtu mmoja mwembamba mrefu ambaye uso wake ulikuwa umekunjana kwa hasira alikuwa akiongea kwa sauti kubwa

“Narudia kusema kwamba sitauvumilia tena uzembe kama huu mlioufanya.Haiwezekani siku ya pili leo msijue mahala aliko Penny.Amekwenda wapi? Mmempoteza vipi katika mitambo yenu wakati mlipaswa kumfuatilia saa ishirini na nne ? Naomba nirudie tena kuwaweka wazi kwamba Peniela ndiye dira yetu. Bila yeye hakuna kitu kinachoweza kufanyika.Operesheni 26B haiwezi kufanikiwa bila yeye.Kwa mwaka mzima ambao alikuwa gerezani akituhumiwa kila kitu kilisimama,na kwa sasa wakati amerejea na kila kitu kimeanza kwenda upya mnafanya tena uzembe.Ninaapa kwa mbingu na nchi kwamba sintouvuilia uzembe wa aina yoyote ile kuanzia sasa.Peniela anatakiwa afuatiliwe kwa saa ishirini na nne. Hamtakiwi kumuacha hata dakika moja.Nawaweka wazi kwamba endapo operesheni 26B itashindwa kufanikiwa kwa sababu ya uzembe tu wa watu basi tujihesabu sisi sote ni marehemu.I want to live,I don’t want to die so I cant lost my soul because of one stupid.If you mess again you’ll die first” akasema kwa ukali Yule jamaa.Watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza na walionekana kuingiwa na woga mwingi.Kijana mmoja aliyevalia suti nyeusi na shati jekundu akakohoa kidogo na kusema

“Captain,tulijitahidi kumfuatilia Penny kwa karibu lakini kifaa ambacho huwa anatumia kwa ajili ya mawasiliano nasi kilizimwa usiku wa manane.Tulipokwenda asubuhi nyumbani kwake kufanya uchunguzi tulikutana na makufuli,Penny hakuwepo.Toka amemaliza kesi iliyokuwa ikimkabili Penny anaonekana hataki tena kushirikiana nasi.Hatoi ushirikiano wa aina yoyote.Sina hakika kama yuko tayari kuendelea na operesheni hii” akasema Yule kijana na kumfanya Captain agonge meza kwa hasira

“ Kwa nini mlienda asubuhi?? Ilitakiwa muda ule ule ambao mmeona tukio lile la kukatika kwa mawasiliano mngenitaarifu mara moja ili nijue nini cha kufanya.Uzembe wenu unatugharimu sisi sote.Narudia tena kwamba hili ni onyo la mwisho.Kuhusu Penny kutotoa ushirikiano hilo niachieni mimi.Atake asitake lazima afanye tunavyotaka sisi na si vinginevyo.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea

“ Leo usiku nina kikao na wakuu cha kujadili kuhusu operesheni 26B ambayo inatakiwa kuzinduliwa rasmi upya.Kabla sijaelekea kikaoni usiku wa leo nahitaji kupata taarifa kwamba tayari mmekwisha fahamu mahala alipo Penny.Kuanzia sasa nendeni tena katika vifaa vyenu,fungueni kompyuta zenu,nendeni katika satellite na mjue wapi aliko Penny.Mna kila kitu kinachotakiwa kwa hiyo ifanyeni kazi na kabla ya saa mbili usiku wa leo nataka ripoti.” Akasema kwa ukali Captain na kutoka mle katika chumba cha mikutano akaingia ofisini kwake akajifungia.Alihisi kichwa kizito kwa mawazo.





Saa moja kasoro dakika nane za jioni,Mathew alisimamisha gari nje ya nyumba ya Bwana na Bi Robinson Kobe wazazi wa Edson.Jioni hii alikuwa ameambatana pia na wakili Jason.Geti lilifunguliwa wakaingia ndani

“ Mathew una hakika watakubali kuongea nasi wakiniona nimeongozana nawe? Akauliza Jason kwa wasi wasi

“ Usijali Jason.Wataongea nasi tu” akasema Mathew huku akibonyeza kengele ya mlango wa sebuleni ambao ulifunguliwa na mwanadada mmoja mwembamba mrefu.Aliwakaribisha sebuleni na kuwahudumiwa vinywaji na baada ya dakika kama tatu hivi wazazi wa Edson wakatokea.Bi Hellen alikuwa anatembea kwa uchovu na ilionekana wazi kwamba hali yake haikuwa nzuri.Hii ilitokana na mstuko alioupata mchana baada ya kuongea na Mathew na kumkumbusha kuhusiana na kifo cha mwanae Edson .Jason na Mathew wakasimama na kuwasalimu wazee wale kwa heshima .Bado Bi Hellen aliendelea kumuangalia Jason kwa macho makali sana .Ilionyesha wazi kwamba hakupendezwa na uwepo wake pale

“ Karibuni vijana” akasema mzee Robinson Kobe

“Nimeambiwa kwamba mna jambo mnataka kuzungumza nasi”

“ Ndiyo mzee.Tulionana na mama mchana na tukaomba tukutane na kuonana nanyi.Tuna jambo tunataka kuzungumza nanyi wazee wetu” akasema Mathew

“ Ni kuhusu nini? Akauliza mzee Robinson

“ Ni kuhusu mwanetu Edson”

“ Kuna jambo gani kumuhusu Edson? Kesi yake imekwisha malizika na mtuhumiwa akaachiwa huru.Huyo mwenzako anafahamu kila kitu kwani yeye ndiye aliyekuwa akimtetea mtuhumiwa” akasema mzee Robinson

“ Nalifahamu hilo mzee” akasema Mathew na kunyamaza kidogo kisha akaendelea

“ Wazee wangu naomba kwanza nijitambulishe kwenu kwa sababu huyu mwenzangu tayari mnamfahamu.Mimi naitwa Mathew Kwanga.Kazi yangu ni mchunguzi wa kimataifa.Ninapokea na kufanya kazi mbali mbali za kiuchunguzi toka sehemu mbali mbali duniani” akanyamaza kidogo na kuendelea

“ Nilifuatwa na ndugu zangu hawa wawili.Jason na mwingine ambaye tulitakiwa kuwa naye hapa lakini amepata udhuru .Yeye ni Jaji Elibariki ambaye alikuwa akiisikiliza kesi ya mauaji ya Edson.” Akasema Mathew.Wazazi wa Edson wakatazamana baada ya jina la Jaji Elibariki kutajwa

“ Ndugu zangu hawa “ akaendelea Mathew

“ Waliniomba niwasaidie kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo chenye utata cha kijana wenu Edson na kumfahamu nani muuaji”

Kabla hajaendelea mzee Robinson akaingilia kati

“ Kijana Uchunguzi ulikwisha fanyika na mtuhumiwa akapatikana japokuwa mahakama kwa sababu wanazozijua wao wakamuachia huru. Sioni haja ya kufanya tena uchunguzi kwa sababu jambo hili sisi tumekwisha muachia Mungu kwani yeye pekee ndiye mwenye kutenda haki.Duniani hapa hakuna haki” akasema mzee Robinson akionekana kukata tamaa

Jason aliyekuwa kimya toka wamefika akakohoa kidogo na kusema

“ Mzee naomba na mimi niongee kidogo” akasema huku akitazamana na mzee Robinson.Akaendelea

“ Naomba niwafahamishe wazee wangu kwamba Peniela siye muuaji wa Edson?

Kauli ile ilimfanya mzee Robinson amtazame kwa jicho kali na kusema

“ Kijana ,nafahamu kwamba wewe ni mwanasheria mahiri kabisa na umeifanya kazi yako vyema ya kuishawishi mahakama ikakubali kumuachia huru mteja wako.Najua hata siku moja hutakubali kwamba mteja wako alimuua mwanetu.Yote hii ni kwa sababu anakulipa pesa nyingi.Pesa inaweza kufanya jambo lolote hata kupindisha sheria na wenye hatia wakaachiwa huru.Ndiyo maana hapo awali nilisema kwamba haki inapatikana mbinguni tu.Huku duniani hakuna haki.” Akasema mzee Robnson

“Hapana mzee.Si hivyo unavyofikiri.Sheria na Mahakama vimewekwa ili kutoa haki.Mahakama haiko kwa ajili ya kupindisha sheria na kulipendelea kundi fulani la watu kwa sababu ya pesa zao au nafasi zao.Peniela aliachiwa huru baada ya mahakama kuridhika kwamba hakuwa na hatia.Hakutenda kosa.Hakumuua Edson.Baada ya kesi kumalizika na Peniela kuachiwa huru ,Jaji Elibariki ambaye ndiye aliyetoa hukumu ile alinifuata na kunieleza nia yake ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kifo cha Edson.Aliamua kufanya hivyo kutokana na sintofahamu nyingi alizozigundua katika mwenendo mzima wa kesi ile.” Jason akanyamaza kidogo na kusema

“ Kumekuwa na maneno mengi na hisia tofauti kuhusiana na hukumu ile kwa hiyo tunataka tufanye uchunguzi wa kina tuufahamu ukweli.Tumfahamu muuaji wa edson na kumfikisha sehemu husika apate adhabu stahili.Kwa kuwa sisi ni wanasheria na hatuna taaluma ya kiuchunguzi tumeamua kutumia gharama zetu kumkodisha huyu ndugu yetu Mathew aweze kuifanya kazi hiyo.Yeye amebobea katika masuala haya ya kiuchunguzi,amekwisha fanya kazi katika idara mbali mbali nyeti za kiusalama hapa nchini kabla ya kuamua kufanya kazi zake binafsi.Kabla ya kuanza kufanya uchunguzi wake Mathew ameona ni bora aje azungumze nanyi mambo kadhaa. “ akasema Jason.Kimya kikatawala pale sebuleni.Mzee Robinson aliinama akatafakari huku akikuna kichwa chake.Baada ya dakika mbili akainua kichwa na kusema

“Natamani niamini maneno uliyoniambia kijana wangu lakini nafsi yangu inakataa kabisa. Sidhani kama kuna kitu cha kunishawishi niamnini kwamba Penny siye aliyemua mwanangu” akasema mzee Robinson

“ Mzee wangu sina kitu cha kukushawishi kwa sasa lakini naomba unipe muda kidogo tu na nitakuwa na cha kukukushawishi uamini hivyo.Ninachohitaji toka kwenu sasa ni ushirikiano tu” akasema Mathew.Mzee Robinson akainama akafikiri na kusema

“ Unahitaji nini toka kwetu?

“ Mzee,mimi ni mzoefu katika masuala haya .Nimekwisha fanya chunguzi mbali mbali za vifo vyenye utata kama hiki cha mwanao.Mara nyingi kinapotokea kifo kama hiki kunakuwa na sababu Fulani nyuma yake.Sitaki kuongea sana lakini ninachotaka kukisema ni kwamba tutaifahamu sababu hiyo na kwa nini Edson aliuawa.Sahauni uchunguzi uliopita na tushirikiane katika uchunguzi huu tunaotaka kuufanya. Kitu cha kwanza ninachotaka kukifahamu toka kwenu japo kwa ufupi tu ni kuhusiana na mwanenu Edson alikuwa ni mtu wa namna gani?

Mzee Robinson akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Edson alikuwa ni mtoto pekee wa kiume kati ya watoto wanne tulionao.Kimakuzi Edson tumemlea katika maadili mazuri.Alikuwa ni kijana mtaratibu sana na asiye na makuu.Alipohitimu shahada yake ya mawasiliano nchini marekani alirudi nchini na akapata kazi katika kampuni moja ya simu na baadae akapata kazi ikulu katika kitengo cha mawasiliano ambako alifanya kazi hadi mauti yalipomkuta.Kitabia Edson hakuwa na tabia ambayo naweza kusema kwamba ni mbaya,hakuwa mnywaji wa pombe ,wala mtumiaji wa kilevi chochote kile.Muda mwingi aliutumia kwa kusoma na kufanya kazi zake.Alipoanza kazi ikulu alianzisha mahusiano na kimapenzi na Anna binti wa rais.Urafiki wao ulianza toka wakiwa wadogo kwa sababu familia zetu mbili ni familia rafiki kwa muda mrefu sana.Baada ya kuingia katika mahusiano na Anna,tuliamua kumpatia moja ya nyumba zetu aishi ili aweze kuwa huru.Edson na Anna walipendana sana na sote tulikuwa na matarajio makubwa kwamba siku moja familia zetu mbili zingeweza kuunganishwa na hawa vijana lakini ghafla tukasikia kwamba wamefarakana na tayari Edson alikuwa katika mahusiano na msichana mwingine aitwaye Peniela.Hatukutaka kuingilia mambo yake ya kimahusiano tukamuacha aendelee na Peniela hadi pale mauti yalipomkuta.Kwa ufupi hivyo ndivyo ninavyoweza kumuelezea mwanangu Edson japokuwa kuna mambo mengi sana ambayo naweza kuyaeleza. Kuhusiana naye” akasema mzee Robinson

“ I see….He was a nice guy..” akasema Mathew

“ Yah ! ..” akajibu mzee Robinson

“ Siku chache kabla ya kifo chake ulifanikiwa kuonana naye? Alikuwa katika hali gani? Kuna kitu chochote ambacho hakikuwa cha kawaida kwa namna ulivyomuona? Akauliza Mathew.Mzee Robinson akafikiri kidogo na kusema

“ Nilionana naye wiki mbili kabla ya kifo chake.Alikuja ofisini kwangu tukaongea kidogo akaondoka.Alikuwa katika hali ya kawaida kabisa.Ninachokumbuka ni siku tatu kabla ya kifo chake alimpigia simu mama yake usiku na kuongea naye.Alikuwa anamsalimu tu.Hakuwa na kawaida ya kupiga simu usiku lakini hakusema kama ana tatizo lolote ” akasema mzee Robinson

“ Nilifika katika nyumba aliyokuwa akiishi Edson nikaambiwa kwamba umeiuza” akasema Mathew

“ Ndiyo niliamua kuiuza ile nyumba. Sikutaka kuendelea kuimiliki ile nyumba baada ya mwanangu kuuliwa ndani yake” akasema mzee Robinson

“ Vifaa vyake mmevihifadhi wapi? Akauliza Mathew

“ Tuna nyumba ndogo iko huko nyuma ndiko tumevihifadhi”

“ Nitahitaji kuvipitia baadhi ya vitu vyake kama vitabu vya kumbu kumbu ili tuonne kama kuna kumbu kumbu yoyote isiyo ya kawaida ambayo anaweza kuwa aliiweka vitabuni ,vile vile kompyuta yake pamoja na simu” akasema Mathew

“ Edson alikuwa na vitabu vingi sana kwani alikuwa msomaji mzuri.Nadhani tunaweza kuchukua siku kadhaa kuvipitia vyote kuchambua kimoja kimoja.Kuhusu kompyuta zake ni kwamba hazikuwahi kuonekana na hatujui ni nani aliyezichukua.Simu yake pia haikuwahi kuonekana.Hatuelewi ni kwa nini vitu hivi vilitoweka katika mazingira yenye utata mkubwa. Akasema mzee Robinson

“ Baba Eddy..! akaita Bi Hellen

“ Kuna kitu nimekikumbuka.Katika mojawapo ya chungu cha maua kilichokuwa chumbani kwake siku tunahamisha vyombo vyake ilianguka laini ya simu ambayo nimeihifadhi ndani.Nadhani inaweza ikawa ni ile laini ya simu ambayo aliitumia aliponipigia simu mara ya mwisho kwa sababu hakutumia namba zake ninazozifahamu.” akasema Bi Hellen

“ Ok,nitaomba unipatie laini hiyo ya simu ili tuifanyie uchunguzi.Inaweza ikawa na jambo la muhimu kwetu” akasema Mathew na Bi Hellen akainuka akaelekea chumbani kuchukua laini ile ya simu

“ Bado sijapata jibu ni kwa nini muuaji aliondoka na kompyuta na simu wakati Edson alikuwa na kiasi cha shilingi milioni ishirini ndani.” Akasema mzee Robinson

“ Shida yao haikuwa pesa.Kuna kitu walichokuwa wakikitafuta ambacho ni zaidi ya pesa” akasema Mathew

“ Kwa mbali hata mimi ninaanza kupata picha kwamba mauaji ya kijana wangu ni tofauti kabisa na tunavyofikiri.Yawezekana kuna mtu au kitundi cha watu waliofanya mauaji yale na si Yule msichana aliyekuwa akituhumiwa” akasema mzee Robinson.Mathew na Jason wakatazamana.

“ Ahsante sana mzee kwa kuliona hilo.Jukumu letu sasa ni kubaini mtu huyo au kikundi cha watu waliotekeleza mauaji hayo “ akasema Mathew .Bi Helen akarejea na kumpatia ile laini ya simu aliyoikuta katika vifaa vya Edson

“ Wazee wangu nashukuru kwa kutusikiliza .Mimi na wenzangu tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba tunaufahamu ukweli.Nitakuwa nikiwapa taarifa za mara kwa mara kuhusiana na uchunguzi wetu unavyoendelea .Ninachoomba suala hili liwe ni la siri na asifahamu mtu mwingine yeyote kwamba kuna uchunguzi unaendelea .” akasema Mathew

“ Msijali vijana wangu,muda wowote mnakaribishwa.Hapa ni nyumbani kwenu na milango iko wazi muda wote.Chochote mnachokihitaji msisite kutueleza tuwasaidie.” Akasema mzee Robinson

“ Tunashukuru sana wazee wetu.Sisi tutajitahidi kwa kila tuwezavyo kuhakikisha tumelichimba suala hili hadi katika mzizi wake na tuufahamu ukweli.Endapo kuna chochote kile mnaachoona kinaweza kutusaidia katika uchunguzi wetu msisite kututaarifu” akasema Mathew. Wakaagana na kuondoka.

“ Tayari kuna mwanga umeanza kuonekana,” akasema Mathew

“ kuna sababu iliyowafanya watu watu waliofanya mauaji ya Edson waondoke na kompyuta zake na simu.Kuna kitu gani walikuwa wanakificha? Kwa kuwa Edson alikuwa katika masuala ya mawasiliano inawezekana kuna jambo alikuwa analifahamu ambalo hakupaswa kulifahamu na kusababaisha kifo chake.Tutajua tu ni jambo gani hilo” akasema Mathew.Jason akaitika kwa kichwa alikuwa kimya sana .Mawazo yake yote yalikuwa kwa Peniela.Alijiuliza maswali mengi mahala aliko na kwa nini ameizima siku yake

“ Baba Eddy !.. akaita Bi Hellen baada ya Mathew na Jason kuondoka

“ Niliwadharau wale vijana lakini wamenifumbua macho na kwa sasa hata mimi nimeanza kuamini kwamba kuna watu walimuua mwanangu kwa sababu maalum ingawa itanichukua muda mrefu kuamini kwamba Yule msichana Peniela hakuhusika na kifo cha Edson” akasema bi Hellen.Mzee Robinson akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Peniela hakumuua Edson” akageuka na kujifunika shuka akalala mke wake akabaki akimshangaa

*********

Jason alimfikisha Mathew nyumbani kwake na kisha akaendelea na safari ya kuelekea kwake.Mathew akaingia ndani mwake na kitu cha kwanza alichokifanya ni kuelekea katika chumba chake kikubwa kilichokuwa na runinga kubwa nane zilizotundikwa ukutani.Akaziwasha runinga zote na zikaanza kuonyesha picha zikaanza kuonekana.

“ wow ! my birds are working” akasema na kukaa kitini akaanza kufuatilia picha zile zilizokuwa zikionekana katika runinga.Runinga namba sita ilikuwa ikionyesha makazi ya Peniela.Vifaa vile mithili ya vipepeo Mathew alivyoviweka katika nyumba ya Peniela mchana vilikuwa ni kamera ambazo zilikuwa zikionyesha kila kilichokuwa kikiendelea katika makazi yale.Alizipeleka mbele picha zile na hakukuonekana mtu yeyote akiingia katika makazi yale hadi ilipotimu saa mbili na dakika ishirini na mbili.Geti dogo lilifunguliwa na watu wawili wakaingia kwa kunyata huku wakiwa na bastora mikononi.

“ Who are these people? Akajiuliza Mathew huku akiisogelea karibu runinga yake.





Watu wale wawili walikuwa makini sana wakiangaza huku na huko halafu wakaweka kitu Fulani kidogo katika mlango wa kuingilia sebuleni kwa Penny.

“ Wanaweka nini pale? Akajiuliza Mathew na kuikuza picha ili aone kitu kile kilichokuwa kimewekwa pale mlangoni.

“ Kamera !..” akasema kwa sauti ndogo

“ Wameweka kamera .Kwa nini wameweka kamera mlangoni? These people looks so professional” akawaza Mathew.

Baada ya kuweka kamera ile mlangoni kwa Peniela,kwa kutumia vifaa maalum wakafungua mlango wakaingia ndani.Mathew hakuweza kuona kilichokuwa kinaendelea ndani kwa sababu hakuwa ametega kamera yoyote ndani ya nyumba ya Penny.Baada ya kama dakika kumi hivi watu wale wakatoka na kuondoka na kuzidi kumchanganya Mathew

“ Watu wale ni akina nani? Wamefuata nini kwa Peniela? Akaendelea kujiuliza Mathew.Akarudisha tena picha nyuma na kuwatazama vizuri watu wale

“ Watu hawa ni akina nani ? kwa nini wameweka kamera mlangoni kwa Penny.Mle ndani waliingia kufanya nini? Akawaza huku akiendelea kuwatazama wale wale jamaa katika runinga.

“ Hapa kuna jambo ambalo si la kawaida.Watu hawa wamekuja wakiwa na bastora mkononi na tena wanaonekana ni watu makini na wazoefu.Mhh! suala hili si dogo kama ninavyolifikiri.Tayari nimepata sehemu ya pili ya kufanyia uchuguzi .Natakiwa kuwafahamu watu hawa ni akaina nani, na nini lengo la kuja kwa Peniela wakati mwenyewe hayupo.” Akawaza Mathew na kuprint zile picha za wale jamaa.

“Bado sipati jibu watu wale ni akina nani na kwa nini wameweka kamera nyumbani kwa Penny.Nadhani lengo lao ni kufuatilia kila kinachoendela pale. Inaonekana kuna watu ambao wanafuatilia nyendo za Penny na walifahamu fika kwamba kwa muda huu hayupo nyumbani ndiyo maana wakaingia na kufanya walichotaka kukifanya.Watu hawa lazima niwafahamu na nini lengo lao kwa Penny.Ninaanza kuwa na wasi wasi sana kuhusiana na maisha ya Penny.Inaonekana yuko katika hatari kubwa.Kuna watu wanaomfuatilia ambao sijui lengo lao ni nini .Penny yuko wapi? Kwa mujibu wa Jason ni kwamba siku ya pili leo Penny hajulikani yuko wapi .Kesho nitaanzia kazi kwa Penny.Lazima nifahamu yuko wapi ” Akawaza Mathew na kuondolewa katika mawazo na simu iliyoita.Zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake

“ Hallow ! akasema

“ Hallow kaka,kuna mtu anahitaji kuongea nawe.” Ikasema sauti ya upande wa pili.Baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti tamu ambayo aliitambua mara moja

“ Hallo Mathew” ikasema sauti ile

“ Anitha ! akasema Mathew

“ Niko hapa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere”

“ Ouh gosh ! Kwa nini hukuniambia utaingia muda gani ili nije nikupokee?

“ Hapana sikutaka kukusumbua Mathew.Hapa ni nyumbani.Nisubiri hapo hapo nyumbani nitachukua taksi” akasema Anitha na kukata simuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ The hacker is here…” akasema Mathew kwa sauti ndogo huku akitabasamu.

“ Bado Noah.yeye aliniambia anakuja kesho.Kazi imeiva” akawaza Mathew huku akiendelea kuziangalia picha mbali mbali zilizokuwa zinapita katika runinga zilizokuwamo mle ndani.

**********

Penny alijiangalia katika kioo kikubwa ,kugeuka nyuma akajitazama na kutabasamu

“ Siku zote huwa sina wasi wasi na uzuri wangu” akasema Penny kwa sauti ndogo huku akiikoleza rangi ya mdomo.Akachukua kichupa kidogo cha uturi na kudondoshea matone machache shingoni.

“ Leo lazima Dr Joshua atapagawa na mimi.Ni muda mrefu sana hajakutana nami.Nitampa vitu adimu ambavyo vitampagawisha na kumchanganya .Huu ni wakati wa kutumia kila aina ya ujuzi nilionao ili niweze kuimaliza kazi” akawaza Penny huku akichukua mkoba wake mdogo na kufungua mlango.Nje ya mlango wake alisimama kijana mmoja aliyevalia nadhifu.

“ Uko tayari? Akauliza Yule kijana

“ Ndiyo niko tayari.Tunaweza kwenda” akasema penny na kuongozana na Yule kijana mpaka katika gari moja la kifahari akafunguliwa mlango na kuingia kisha wakaondoka.

“ Najua Jason na Jaji Eklibariki watakuwa wamenitafuta sana baada ya kutoniona kwa siku ya pili leo.Natamani niwataarifu kwamba niko salama lakini naogopa kwani Kareem alinionya nisimpigie simu mtu yeyote na kumfahamisha kwamba niko Arusha.” Akawaza Penny akiwa garini

“ Sijui wamefikia wapi ule mpango wao wa kumtafuta muuaji wa Edson.Nikirudi nitawashauri waachane na jambo hili kwani lina mkanganyiko mkubwa na ni hatari kwa usalama wao.Sitaki yeyote kati yao apatwe na tatizo lolote.Hawa ni watu wangu wa muhimu sana bila wao hivi sasa ningekuwa ninakula maharage ya jela. ” Akaendelea kuwaza na mara picha ya Jason ikamjia kichwani .

Saa tatu na dakika arobaini wakawasili Meru view hotel,moja kati ya hoteli kubwa sana afrika mashariki na kati.Ni katika hoteli hii ndipo alipofikia rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania Dr Joshua tayari kabisa kwa ajili ya kuongoza kikao cha wakuu wa nchi za afrika msahariki kinachotarajiwa kufanyika jijini Arusha kwa muda wa siku tatu.Ulinzi ulikuwa mkali sana kuizuguka hoteli hii na kila gari lililoingia hapa ililazimika kukaguliwa na askari.Gari alilopanda Penny halikukaguliwa likapita moja kwa moja hadi katika maegesho ya viongozi wakuu mlango ukafunguliwa na Penny akashuka.

“ Wow ! what a beautiful place” akawaza Penny huku akitabasamu akiifurahia mandhari ile ya kupendeza ya hoteli ile kubwa.Yule kijana ambaye hakuwa muongeaji alimuongoza Penny hadi katika mlango wa nyuma wakaingia ndani ya hoteli na kwa kutumia lifti wakapanda hadi ghorofa ya sita wakashuka na kulifuata varanda refu.Hakukuwa na mtu anayeranda randa katika ghorofa hii zaidi ya walinzi wa rais ambao walikuwa makini na kila aliyeonekana eneo hili. Hakuna kati yao aliyethubutu kumuuliza chochote Penny kwani alikuwa ameongozana na mmoja wa walinzi wa rais.Moja kwa moja akampeleka Penny hadi katika chumba cha rais akagonga mlango ukafunguliwa na Kareem mlinzi wa rais.

“ Penny karibu ndani” akasema Kareem huku akimshika mkono na kumuelekeza aketi sofani.Kilikuwa ni chumba kikubwa na kizuri mno.Kwa muda wa sekunde kadhaa Kareem aliendelea kuchezea simu yake halafu akainua kichwa na kusema

“ Unatumia kinywaji gani Penny?

“ Nipatie mvinyo tafadhali” akasema Penny.Kareem akamletea chupa ya mvinyo na kumuwekea mezani

“ Mheshimiwa rais bado yuko katika kikao.Utaendelea kumsubiri” akasema Kareem na kuendelea kuchezea simu yake kubwa

“ How’ve u been Kareem? Maisha yako yanakwendaje? Akaamua kuanzisha maongezi Penny baada ya kuona Kareem amekuwa kimya sana na ilionyesha hakutaka maongezi

“ I’m ok Penny.I’m doing fine.Samahani kama umeboreka lakini niko kazini.Tuna marais karibu watano watahudhuria mkutano mkubwa wa marais wa afrika mashariki kuanzia kesho kwa hiyo yatubidi tuwe macho sana katika ulinzi ndiyo maana unaniona nimekuwa kimya sana nafuatili akila kinachoendelea hapa hotelini”

“ Usijali Kareem.Ninaelewa” akasema Penny na kuelekeza macho yake runingani akitazama muziki

“ Kareem ! akaita Penny baada ya muda

“ Unasemaje Penny? Akauliza Kareem

“ Nitakuwepo hapa Arusha kwa muda gani?

“ As long as present wants” akajibu Kareem, kwa ufupi

“ No Kareem.I need to go back to Dar as soon as possible.” Akasema Penny

Kareem hakumsemesha kitu akaendelea na kazi zake

Saa sita na dakina nane mlango wa chumba cha rais ukafunguliwa na Dr Joshua rais wa jamhuri ya muungano akaingia

“ Where is she? Akamuuliza Kareem ambaye alimfanyia ishara kwamba tayari yuko chumbani

“ Thank you Kareem.Thank you so much.From now I need a privacy.No calls no any disturbance” akasema Dr Joshua

“ Ok Mr President” akajibu Kareem kwa adabu.Dr Joshua akakinyonga kitasa cha mlango na kuingia chumbani kwake.Ilimlazimu avue miwani yake ili ajiridhishe kwamba alichokuwa akikiona kitandani binadamu wa kawaida na si malaika .Kiumbe kilichokuwa kimejilaza katika kitanda kilichotandikwa mashuka mazuri meupe kilikuwa na uzuri usio wa kawaida.

“ Penny ! akaita

“ Dr Joshua ! akasema Penny kwa sauti ndogo.Dr Joshua akafunga mlango na kumuendea Penny akamkumbatia kwa nguvu

“ Welcome back my angel” akasema Dr Joshua .Penny hakutaka kupoteza muda akammwagia mzee Yule mabusu mfululizo na kumchanganya. Dr Joshua akajikuta akianza kuhema kwa nguvu.Taratibu akatoa ulimi na kuuingiza kinywani kwa Dr Joshua ambaye alianza kutoa miguno.Penny akamvua koti taratibu huku akiendelea kumfanyia manjonjo yaliyozidi kumpagawisha Dr Joshua. Taratibu akalegeza tai na kuitoa halafu akaanza kufungua vifungo vya shati .Alikichezea kifua cha mzee yule kwa ufundi mkubwa halafu akaufungua mkanda wa suruali yake ikaanguka chini akabakiwa na nguo ya ndani,Penny akaivuta taratibu nguo ile ya ndani akaishusha hadi magotini halafu akapiga magoti na kuanza kufanya utundu maeneo ya ikulu.Dr Joshua hakuwa akijiweza tena.Penny akamsukuma akangukia kitandani halafu akafungua zipu ya gauni lake likaanguka chini.Dr Joshua mate yakamtoka alipoushuhudia mwili mwororo wa kimalaika wa msichana aliyesimama mbele yake.Taratibu akaivua nguo yake ya ndani na kupanda kitandani na kuendeleza utundu.Dr Joshua alibaki akilalama kwa raha alizokuwa akipewa.Baada ya dakika kumi na tano tayari walikuwa wakiogelea katika ulimwengu wenye raha isiyoelezeka.

*******

“ Ouh Peniela..nakosa neno la kusema kwa raha ulizonipa.I missed you .I missed this….” Akasema Dr Joshua akiwa hoi baada ya kumaliza mzunguko mmoja.Penny akajiinua na kumsogelea akambusu na kukilaza kichwa chake kifuani

“ I missed you too Dr Joshua..Umri umekwenda lakini bado una nguvu kama kijana wa miaka kumi na nane.You make me so happy” akasema Penny

“ Muda wote uliokaa gerezani ukikabiliwa na kesi nilikosa raha na amani.Kwa sasa najiona kijana tena.You are amazing my angel” akasema Dr Joshua huku akizichezea nywele za Penny

“ Don’t lie to me Dr Joshua.Kama ningekuwa na umuhimu kwako usingekubali kuniona nikiteseka gerezani mwaka mzima kwa kosa ambalo sikulitenda na zaidi ya yote ulishinikiza nifungwe kifungo kirefu gerezani.You didn’t stand by my side.Pamoja na mateso yote na hata kunusurika kwenda maisha gerezani lakini sikufumbua mdomo wangu na kuongea lolote kuhusiana na kifo cha Edson.Ninajua wewe ndiye uliyeamuru watu wako wamuue Edson kwa sababu unazozijua mwenyewe lakini kwa kuwa ninakupenda Dr Joshua mpaka leo hii hakuna mtu anayefahamu chochote” akasema Penny na machozi yakamtoka alipomkumbuka Edson.Dr Joshua akamfuta machozi na kusema

“ Tafadhali usilie Penny.Usilie malaika wangu.Kuna mambo mengi ambayo yametokea kitu cha kwanza ninachokihitaji toka kwako ni msamaha wako.Ni kweli nilikuacha ukaingia katika matatizo makubwa na sikusimama pamoja nawe.Penny please forgive me my angel.We have so many to talk” akasema Dr Joshua.Penny akainua kichwa akamtazama na kusema

“ Nimekwisha kusamehe Dr Joshua na ndiyo maana niko hapa.Umesema tuna mambo mengi ya kuongea hata mimi nina mengi ya kuuliza lakini kwanza nataka unieleze kwa nini Edson aliuawa? Akauliza Penny.Dr Joshua akachukua kitambaa na kujifuta jasho,akainuka na kwenda mezani akajimiminia mvinyo na kupiga funda kubwa.



“ Kwa nini unataka kufahamu Penny? Akauliza Dr Joshua

“ Edson was my friend and my lover so I need to know why you ordered him killed” akasema Penny

“ He was your lover ! akasema Dr Joshua kwa sauti ya juu.Penny hakujibu kitu akakaa kimya

“ You cheated on me !

“ I loved him..He was such a gentleman” akasema Penny na Dr Joshua akakaa kimya akazunguka chumbani halafu akasema

“ Unataka kuufahamu ukweli?

“ Ndiyo nahitaji kuufahamu ukweli “ akasema Penny.Dr Joshua akamsogelea akamshika mkono na kusema

“ Ni wivu ndio ulionifanya nitoe maamuzi yale.Ninakupenda mno Peniela na nilipogundua kwamba unanisaliti kwa kutembea na Yule kijana nilikasirika sana.Penny wewe ni wangu peke yangu na sitaki unichanganye na mtu yeyote hususani hawa vijana wadogo.Kijana Yule hakuwa na kitu chochote cha kukupatia .Nilikuahidi kukupa kila fahari ya dunia hii lakini bado ukanisaliti.Penny I’m a powerful man in the country so I can do anything when I’m angry.Nakupa uhuru nieleze kitu chochote na kila unachokitaka nitakupatia lakini ubaki kuwa wangu peke yangu na usije ukanichanganya na mtu mwingine.” Akasema Dr Joshua

Penny akafuta machozi na kumtazama Dr Joshua kwa macho makali

“ Hukutakiwa kufanya vile.Hutakiwi kuwa na wivu na mimi,wewe ni mtu mwenye familia yako.You cant control me.You cant give me all that I want.You cant be there all the time when I need you.I’m a human Dr Joshua and I have needs” akasema penny kwa sauti ya juu

“ Penny mara ngapi nikwambie kwamba wewe ni kila kitu kwangu? Unataka niende katika luninga na kuutangazia ulimwengu kwamba ninakupenda? Niko tayari kufanya hivyo kama hiyo itakufanya uufungue moyo wako na kuniruhusu niingie ndani.Nipe nafasi ya kukuonyesha ni namna gani ninakupenda Penny.Forget that I’m married and I have a family.Not all marriages are real.Some are in papers. Kama ukinipa nafasi ndani ya moyo wako ,nitakuweka katika nafasi ya juu kuliko wanawake wote wa nchi hii.You’ll be the first lady.So why cant we skip the past and talk about our bright future? Akasema Dr Joshua Penny akamuangalia na kusema

“ Najaribu kukubaliana nawe lakini bado moyo wangu na maswali mengi ambayo yanahitaji majibu sahihi Dr Joshua.”

“ Just one question Penny.One question only” akasema Dr Joshua

“ Kwa nini kesi ile ya mauaji ya Edson iliniangukia mimi na ukakubali kuniona nikinusurika kuangamia wakati ukijua kabisa kwamba sikutenda kosa? Kwa nini hukufanya lolote kunisaidia kama kweli unanipenda?

“ Hayo ni maswali mawili Penny.Nitajibu swali moja tu” akasema Dr Joshua ,akanywa funda moja la mvinyo na kusema

“ I was angry” akasema na kunyamaza

“ I was angry for what you did to me and I wanted to destroy you.Nilitaka ufutike kabisa katika dunia hii,nilidhani kwamba ile ilikuwa ni njia muafaka ya kuweza kukusahau,but I was wrong.Penny naomba uelewe kwamba tayari umeniingia katika kila mshipa wa mwili wangu na siwezi kukutoa tena.Ninaomba utambue kwamba nilipata wakati mgumu sana kwa maamuzi yale na hilo ndilo jambo ambalo nitaendelea kulijutia hadi siku ninaingia kaburini.Tafadhali naomba utafute ndani ya moyo wako unisamehe na tuendelee na mapenzi yetu kama zamani.Nilifanya kosa kutaka kukupoteza mara ya kwanza safari hii sitaki tena kurudia kosa .Please lets not talk about the past .Lets not ruin our lovely night.Lets open new chapter in our book.” Akasema Dr Joshua kwa sauti ya kubembeleza,akamvuta Penny na kumkumbatia akambusu

“ Nimekwisha kusamehe Dr Joshua kwa sababu ninakupenda na ndiyo maana niko hapa ila tafadhali nakuomba usifanye tena jambo kama lile.Kama kuna tatizo kati yetu tafadhali naomba uniadhibu mimi na si watu wengine wasiokuwa na hatia.Please don’t hurt people that I love”

“ Siwezi kufanya hivyo tena kama utanihakikishia kwamba hautakuwa na mahusiano na mtu mwingine zaidi yangu. Niambie chochote kile nitakupatia Penny.I have power ,money and everything to make you live like a queen”

‘ Dr Joshua I’m still young and you are getting old.You have a family,you have a wife on bed,you have huge responsibilities and you cant be there all the time that I need you……………..” Penny hakumaliza sentensi yake Dr Joshua akamkatisha

“ I’ll be there ! Anytime you need me just call me and I’ll be there.Kwako sintakuwa na neno la hapana.Niambie chochote unachokitaka nitakutimizia” akasema Dr Joshua na kumfanya Penny atabasamu

“ This is the moment I’ve been waiting .Tayari ameingia mwenyewe katika nyavu na kilichobaki sasa ni kumvua tu.Ni wakati wangu sasa kumaliza kazi yangu” akawaza Penny

“ Dr Joshua kabla ya yote kuna jambo ambalo nataka nikuombe”akasema penny

“ Omba chochote Peniela.Kila kitu katika nchi hii kipo chini yangu” akasema Dr Joshua

“ Ninao watu wangu wawili ambao ni zaidi ya marafiki.Niko nao karibu sana watu hawa.Naomba kwa namna yoyote ile watu hawa wasije wakadhurika.Wana mchango mkubwa sana katika maisha yangu.Can you give me your word that you wont hurt them?” akasema Penny.Dr Joshua akatabasamu na kusema

“ I give you my word Penny.Who are they?

“ Wakili wangu Jason pamoja na Jaji Elibariki”

Dr Joshua akastuka kidogo baada ya kusikia jina la jaji Elibariki likitajwa

“ Usihofu Penny.Jaji Elibariki ni mwanangu.Amemuoa binti yangu. Ni kijana makini na mchapakazi na ndiyo maana nikamchagua kuwa jaji wa mahakama kuu.Nafahamu wewe na yeye ni marafiki na baada tu ya kumalizika kwa kesi mlikutana kwa chakula cha usiku.Nadhani ulikwenda kumshukuru kwa kukuachia huru” akasema Dr Joshua huku akicheka

“ Kwa hiyo umeweka watu wa kunifuatilia maisha yangu? Akauliza Penny

“ Ni kwa sababu ya usalama wako Penny.

“ Tafadhali naomba uwaondoe watu wako wasiendelee kunichunguza.I can defend myself.Siku nikigundua kwamba bado watu wako wanaendelea kunfuatilia it’ll be the end of us”

“ Ok Penny nitawaondoa kama ndivyo unavyotaka lakini ukumbuke kwamba wewe ni mke mtarajiwa wa rais kwa hiyo unahitaji ulinzi.Sema kingine unachokitaka” Penny akatabasamu na kusema

“ Kwa sasa kingine ninachokihitaji ni hiki” akasema na kulivuta taulo alilojifunga Dr Joshua na kumsukuma kitandani halafu akaanza tena kumfanyia utundu na baada ya dakika kadhaa wakaingia tena katika mzunguko mwingine.Ulikuwa ni usiku wa aina yake kwa Dr Joshua.

***********

Kengele ya mlangoni ililia kuashiria kwamba kuna mtu mlangoni.Mathew akainuka na kwenda kuufungua.

“ Anitha the devil ..!! akasema kwa furaha Mathew baada ya kuufungua mlango na kukutana na Anitha

“ Welcome my dear.Welcome home” akasema Mathew huku akikumbatiana na Anitha

“ Thank you so much Mathew.” Akasema Anitha

“ Ungenitaarifu muda ambao utatua ili nije nikupokee “ akasema Mathew

“ Usijali Mathew,hapa ni nyumbani na hauna haja ya kupoteza muda wa kufanya mambo mengine kwa kuja kunipokea.Npe habari kazi inaendeleaje? Akauliza huku akifungua friji na kutoa chupa ya mvinyo akajimiminia katika glasi.

“ Hautaki hata kupumzika Anitha? Pumzika kwanza halafu mambo ya kazi yatafuata baadae” akasema Mathew na kumfanya Anitha acheke kidogo

“ Mathew you know me,I work like a devil. Nimekuja kikazi kwa hiyo tufanye kazi na mambo mengine yatafuata baadae” akasema Anitha.Mathew akatasamu na kusema

“ Kazi tayari imeanza na mpaka sasa hakuna hatua kubwa iliyopigwa japo kuna mwangaza kidogo tayari nimeupata” akasema Mathew.Anitha akageuza kichwa na kumtazama Mathew akasema

“ Nilipata kazi ya pesa nyingi nchini Brazil ambayo nilitakiwa nikaifanye wiki hii lakini nimelazimika kuweka pembeni kwanza ile kazi na kuja kuimaliza kwanza kazi uliyoniitia. Nipe taarifa za kina kuhusiana na kazi hii” akasema Anitha huku akiifungua mizigo yake na kutoa zana zake za kazi

“ Ahsante sana Anitha kwa kuahirisha mambo yako mengine na kuja kuungana nami.Hata mimi pia nimelazimika ksimamisha baadhi ya shughuli zangu kwa ajili ya shughuli hii. Si kazi yenye malipo makubwa lakini ni muhimu sana kwa rafiki zangu” akasema Mathew

“ Kuna kijana mmoja aitwaye Edson,ambaye alikuwa mfanyakzi wa kitengo cha mawasiliano ikulu,aliuawa na watu wasiofahamika na kesi hiyo kumuangukia msichana mmoja aitwaye Peniela . Jaji Elibariki ambaye alikuwa akiisikiliza kesi ile aligundua kwamba msichana Yule aliyekuwa akituhumiwa hakutenda kosa hivyo akalazimika kumuachia huru.Baada ya kesi kumalizika alishawishika kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kesi ile kutokana na sintofahamu kadhaa alizozigundua wakati wa usikilizwaji wa kesi.Aliungana na wakili Jason aliyekuwa anamtetea mtuhumiwa na kwa pamoja wakaamua kunipa kazi hii kutokana na kwamba wao hawana taaluma ya uchunguzi.Kwa hiyo naomba ufahamu kwamba tunaifanya kazi hii kuitafuta haki na vile vile kuwasaidia rafiki zetu” akasema Mathew

“ Kesi hii inafanana na ile ya Justine Abangiza wa Rwanda” akasema Anitha huku akiunganisha vifaa vyake

“ Yah ! zinashabihiana sana ingawa hii ya Edson ina utofauti kidogo” akasema Mathew

“ Nimeongea na wazazi wake jioni ya leo .Nilitaka tu kufahamu mtoto wao alikuwa ni mtu wa namna gani.Kabla ya hapo mchana wa leo nilikwenda nyumbani kwa Peniela,msichana aliyetuhumiwa kumuua Edson, na kutega kamera mbili ,niliporudi nimekutana na picha hizi” akasema Mathew na kumuonyesha Anitha zile picha za wale watu walionaswa katika kamera nyumbani kwa Penny

“ They look so professional “ akasema Anitha

“ Yah ! Wanaonekana wazoefu sana .Ninachojiuliza ni kwa nini wametega kamera mlangoni kwa Penny?

“ Jibu ni jepesi Mathew,Wanataka kuangalia kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny.Cha kujiuliza ni kwa nini wanataka kutazama kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny?Kwa nini Peniela anachunguzwa? Au watu hawa yawezekana wakawa ni walinzi binafsi wa Peniela? Akauliza Anitha

“ Sina hakika kama watu wale ni walinzi wa Peniela kutokana na namna walivyoingia.Wanaonekana wazi kufahamu kwamba muda ule Peniela hakuwepo nyumbami ndiyo maana waliingia kwa kunyata na kuweka ile kamera nadhani kwa lengo la kutaka kufahamu mienendo ya Penny.Tunachotakiwa kufahamu watu hawa ni akina nani na nini lengo lao la kumchunguza Penny.Tayari tuna sehemu nzuri sana ya kuanzia uchunguzi wetu.Sehemu nyingine ya kufanyia uchunguzi ni katika laini ya simu ya Edson. Wauaji waliondoka na simu na pamoja na kompyuta zake zote.Inaonekana wazi kwamba kuna kitu kilichokuwa kinafichwa na ndiyo maana wauaji wale hawakuwa na shida na pesa na wakaondoka na vitu hivyo tu.Wakati wa kuhamisha vifaa vyake,ilipatikana laini ya simu ikiwa imefichwa katika chungu cha maua.Sielewi ni kwa nini aliificha laini hii ya simu lakini nina imani hakutaka ionekane kwa sababu maalum.Inaweza ikawa na msaada kwetu.Tunatakiwa tuichunguze laini hii pia” akasema Mathew.Anitha hakujibu kitu aliendelea na kazi yake ya kuunganisha mitambo yake. Nusu saa baadae alimaliza kuunganisha mitambo yake akaiwasha na kujaribu

“ Everything is in position.We can start our job now” akasema Anitha



“ Kazi ya kwanza ambayo tunaweza kuifanya usiku wa leo ni kuichunguza laini hii ya simu ili tufahamu Edson alikuwa akiwasiliana na akina nani kwa siri.Tukiwafahamu watu ambao aliwasiliana nao kwa siri kuna jambo tunaweza tukalipata toka kwao.Nina hakika lazima kuna sababu iliyomfanya Edson akaificha laini hii isionekane na mtu yeyote” akasema Mathew na kumpa Anitha ile laini ya simu akaipachika katika kifaa fulani kidogo mithili ya mkebe na kuanza kuibonyeza kompyuta yake.Baada ya sekunde kadhaa Anitha akaguna

“ Vipi mbona unaguna Anitha? akauliza Mathewhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Laini hii ya simu imewekewa uzio.” Akasema Anitha

“ Una maana gani unaposema uzio?

“ Nina maana kwamba mtumiaji aliiwekea program maalum ambayo inaiwezesha laini hii ya simu kutumika katika simu yake tu .Inaonekana huyu jamaa alikuwa ana ufahamu mkubwa sana wa kompyuta”

“ Unaweza kuiondoa hiyo program? Akauliza Mathew

“ Ndiyo.Ninaweza kuiondoa.Hivi ni vitu vidogo sana kwangu” akasema Anitha huku akiendelea kucheza na kompyuta yake.Baada ya dakika saba akaegemea kiti na kuvuta pumzi ndefu

“ Tayari”

“ Congraturations” akasema Mathew lakini mara Anitha akaguna tena

“ This is strange !..Anitha akashangaa

“ Nini Anitha?

“ Inaonekana Edson alitumia laini hii ya simu kuwasiliana na watu wawili pekee.”

“ watu wawili ?! Mathew naye akashangaa

“ Ndiyo.Ameitumia kwa watu wawili tu”

“ Unaweza ukatafuta ni akina nani hao?

Anitha akaendelea kubonyeza kompyuta yake na baada ya dakika nne akasema

“ Kwa mujibu wa taarifa toka kampuni ya simu ya Tanphone namba hizo ni za Hellen Francis Kobe na nyingine ni ya Brigita samini.Inaonyesha Edson na Brigita wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara na hata siku moja kabla ya kifo chake Edson aliongea na Brigita kupitia laini hii.” Akasema Anitha

“ Hellen francis Kobe ni mama yake mzazi Edson na alinieleza kwamba kuna siku mwanae alimpigia simu kwa kutumia namba ngeni nadhani ni hii.Huyu Brigita simfahamu ni nani.Inawezekana alikuwa ni mtu muhimu sana kwa Edson na ndiyo maana akawa akitumia laini ya pekee kuwasiliana naye.” Akasema Mathew na kuziandika namba zile za Brigita katika simu yake akajaribu kupiga lakini hazikuwa zikipatikana.

“ Inawezekana mawasiliano ya watu hawa wawili yalikuwa ni ya siri mno.Inawezekana hata huyu Brigita hii akawa na laini ya ya siri ambayo huitumia kuwasiliana na Edson” akasema Mathew na kuzitafuta namba za simu za mzee Robinson Kobe na kumpigia

“ Hallo Mathew” akasema mzee Roinson baada ya kupokea simu

“ Samahani mzee wangu kwa kukupigia simu mida hii” akasema Mathew

“ Bila samahani Mathew.Kuna kitu chochote ninachoweza kukusaidia?

“ Ndiyo mzee.Ninataka kujua kama unamfahamu mtu anayeitwa Brigita Samini”

Kimya cha sekunde kadhaa kikapita halafu mzee Robinson akasema

“ Ninamfahamu Brigita.Edson aliwahi kunitambulisha kwake kwamba ni marafiki wakubwa.Brigita anafanya kazi katika hoteli ya kitalii ya Potina palace.”

“ Ok ahsante sana mzee” akasema Mathew na kukata simu

“ Brigita na Edson ni marafiki wakubwa kwa mujibu wa mzee Robinson.” Mathew akamwambia Anitha

“ Kama walikuwa na urafiki mkubwa kwa nini basi wawasiliane kwa siri? Akauliza Anitha

“ Hicho ndicho tunachotakiwa kukifahamu. Haiingii akilini kama watu ni marafiki wakubwa halafu wawasiliane kwa siri.Lazima kuna sababu iliyowafanya wawe na mawasiliano ya siri ” akasema Mathew na kuchukua kitabu chenye namba za simu za makampuni mbali mbali akaitafuta Potina palace hoteli anayofanya kazi Brigita.Akaipata na kuchukua namba zao za simu akapiga.

“ Karibu Potina palace nikusaidie nini? Ikasema sauti nzuri ya mwanadada baada ya kupokea simu

“ Namtafuta dada mmoja anaitwa Bigita Samini ni mfanyakazi wa hapo hotelini kwenu” akasema Mathew

“ Wewe ni ndugu yake?

“ Hapana mimi ni rafiki yake “

“ Samahani ndugu yangu Brigita hatunaye tena hapa hotelini.Alikwisha fariki dunia.”

“ Amefariki dunia?

“ Ndiyo alifariki dunia “

“ Alifariki lini na nini kilimuua?

“ Alilipukiwa na gesi na kufariki yeye na familia yake yote yapata mwaka sasa” akasema Yule dada na kumtajia Mathew tarehe ambayo Brigita alifariki dunia.Mathew akashukuru na kukata simu.

“ Vipi wanasemaje? Akauliza Anitha

“ Mambo yanazidi kuibuka.Brigita alifariki dunia wiki moja tu baada ya Edson kufariki dunia.Alilipukiwa na gesi na wakafariki yeye na familia yake yote ” akasema Mathew na kimya kikapita

“ Walikuwa wakiwasiliana kwa siri na hata vifo vyao vimetokea kwa kufuatana.Mathew kuna kitu hapa si bure.Kama walikuwa ni marafiki kuna jambo lazima watakuwa wakilifahamu kwa pamoja au wakilificha na ndiyo maana hata mawasiliano yao yalikuwa ya siri kubwa na hawakutaka mtu mwingine yeyote Yule afahamu kama walikuwa wakiwasiliana.Siri hiyo waliyokuwa wakiificha ndiyo iliyowagharimu maisha yao.” Akasema Anitha

“ Anitha inatosha kwa leo.Tupumzike na kesho tuanze kazi rasmi.Tutaanza kazi kwa kutafuta taarifa za Brigita Samini .Anaonekana ni mtu muhimu sana katika suala hili” akasema Mathew.Anitha akamtazama na kutabasamu halafu akazima kompyuta zake

“ Uko sahihi Mathew.Leo imekuwa ni siku ndefu sana.Tupumzike ili kesho tuanze kazi “ akasema Anitha



Kumekucha Dar es salaam,saa tatu za asubuhi Iliwakuta Mathew na Anitha nje ya hoteli ya kitalii ya Potina Palace.Waliegesha gari na kushuka wakaingia hotelini na moja kwa moja wakaelekea mapokezi ambako walimkuta mwanadada mmoja mrembo wakajitambulisha kama rafiki wa Brigita Samini aliyekuwa akifanya kazi pale hotelini.Yule mwanadada wa mapokezi akashangaa kidogo na kuuliza

“ Hamkuwa na mawasiliano naye au ndugu zake?

“ Sisi tunaishi Marekani na kwa muda msrefu kidogo hatukuwa tumewasiliana naye.Mara ya mwisho tulipowasiliana naye alituelekeza kwamba anafanya kazi hapa.” Akasema Mathew

“ Poleni sana ndugu zangu.Brigita hatuko naye tena,alifariki dunia yapata mwaka mmoja sasa umepita” akasema yule dada ambaye kitambulisho cha kazi alichokivaa kilionyesha anaita Stella manana .Mathew na Anitha wakaonyesha mstuko ili kumfanya Yule dada asiwe na wasi wasi wowote kuhusu wao.

“ Nini ilikuwa sababu ya kifo chake? Akauliza Anitha

“ Mtungi wa gesi ulilipuka na kusababisha nyumba yao iteketee kwa moto.Hakuna hata mtu mmoja aliyetoka hai.Ilikuwa ni ajali mbaya sana.Brigita alikuwa ni meneja wetu na mtu mwenye roho nzuri sana na kila mtu hapa alimpenda “

Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Mathew akauliza

“ Kuna mtu yeyote ambaye alikuwa ni mtu wake wa karibu sana ili aweze kutuelekeza kwa ndugu zake tukawape pole? Akauliza Mathew

“ Brigita alikuwa na marafiki wengi na kila mtu alikuwa ni rafiki yake lakini kuna mmoja ambaye alikuwa ni rafiki yake mkubwa anaitwa Subira.Kwa sasa hayupo hapa hotelini anasomea shahada ya hoteli pale Ikandala University.Kama mnahitaji taarifa za kina kuhusiana na Brigita mtafuteni huyo Subira kwani ni yeye anayewafahamu hadi ndugu zake “ akasema Yule dada na kuwapatia namba za simu za Subira wakaagana Mathew na Anitha wakarejea katika gari lao.

“Mpigie simu Subira tufahamu yuko wapi” akasema Mathew.Anitha akaziandika zile namba katika simu yake na kupiga.Simu ikaita na kukatika,akapiga tena ikaita lakini haikupokelewa

“ Simu yake inaita tu lakini haipokelewi” akasema Anitha

“ Jaribu tena kumpigia.Isipopokelewa tutamfuata pale pale chuoni kwao” akasema Mathew ,Anitha akapiga tena na safari hi ikapokelewa

“ Hallow !..Ikasema sauti ya mwanadada upande wa pili

“ Hallow naongea na nani? Akasema Anitha

“ Unaongea na Subira Abdul.Wewe ni nani mwenzangu?

“ Ninaitwa Anitha”

“ Nikusaidie nini Anitha? Akauliza Subira ambaye alikuwa na sauti ya upole

“ Subira ninahitaji kukuona.Nina maongezi nawe kidogo” akasema Anitha

“ Una maongezi na mimi? Subira akashangaa

“ Ndiyo Subira.Nahitaji sana kukuona”

“ Ni maongezi kuhusu nini? Halafu mbona sikufahamu?

“ Usihofu Subira.Hata mimi sikufahamu nimepewa namba zako za simu pale Potina Palace ulipokuwa ukifanyakazi kabla ya kuanza kusoma.”

“ Ok Unataka tuongee jambo gani?

“ Mimi ni rafiki wa siku nyingi wa Brigita Samini ambaye nimeelezwa kwamba wewe ulikuwa na ukaribu naye mkubwa .Ninaishi Marekani kwa sasa na nimekuja kwa mapumziko mafupi.Nimeenda kumtembelea Brigita mahala nilikomuacha akifanya kazi kipindi cha kama mwaka mmoja uliopita nikaambiwa kwamba alifariki dunia katika ajali ya moto.Nimestuka sana .Ninataka kufahamu mengi kuhusiana na kifo hicho na hata kuwafahamu ndugu zake ili nikatoe pole.Nimeelekezwa kwako kwamba unaweza ukanisaidia kwa hilo Subira” akasema Anitha

“ Kwa sasa uko wapi? Subira akauliza

“ Kwa sasa ninaondoka hapa Potina Palace.wewe uko wapi?

“ Mimi niko chuoni hapa Ikandala University.Ninamalizia kipindi cha mwisho .Unaweza ukaja kunisubiri hapa chuoni nimalize kipindi?

“ Usijali Subira ninakuja” akasema Anitha na kukata simu

“ Yuko chuoni anamalizia kipindi,anasema tumfuate tukamsubiri” Anitha akamwambia Mathew

Wakiwa njiani, kuelekea chuoni,Mathew akawasiliana na Jason kutaka kujua kama Penny amekwisha rejea lakini mpaka muda huo Jason hakuwa na taarifa zozote za kumuhusu Penny

“ Penny atakuwa amekwenda wapi? Mpaka leo hajaonekana na hajulikani yuko wapi” akasema Mathew

“ Unahisi anaweza kuwa amepatwa na tatizo? Akauliza Anitha

“ Sina hakika sana lakini hata kama hajapatwa na tatizo bado hayuko salama.Bado nawafikiria watu wale walioingia ndani ya nyumba yake jana na kuweka kamera za siri ni akina nani na wana lengo gani kwa Penny.Nashawishika kutaka kumfahamu vizuri zaidi Penny.” Akasema Mathew

“ Have you met her? Akauliza Anitha huku akiendelea kucheza na kompyuta yake

“ No I haven’t” akajibu Mathew

Waliendelea na safari hadi walipofika Ikandala University,Anitha akamtumia Ujumbe Subira kumfahamisha kwamba tayari wamekwisha fika wako nje wanamsubiri.Baada ya dakika ishirini Subira akatoka.Hakuwa akimfahamu Anitha hivyo ikamlazimu kumpigia simu ,Anitha akamuelekeza mahala walipo akawafuata

“ Habari yako Subira” akasema Anitha.Subira alionyesha hofu kidogo alipogundua kwamba Anitha hakuwa peke yake bali alikuwa na Mathew

“ Habari yangu nzuri.habari zenu?

“ Habari zetu nzuri.Pole na masomo”

“ Ahsante” akajibu Subira

“ Subira huyu hapa ni mwenzangu anaitwa Mathew kwa hiyo naomba usiwe na hofu.” Anitha akafanya utambulisho kwani alimuona Subira akiingiwa na uoga.

“ Subira hatutaki kuchukua muda wako mwingi kwani najua una shughuli nyingi za kufanya.Tunaweza kupata sehemu hapa karibu tukakaa na kuongea japo kwa dakika chache? Akauliza Anitha

“ Kuna hoteli pale karibu tunaweza kwenda kukaa tukaongea” akajibu Subira halafu wakaongozana kuelekea katika hoteli iliyokuwa kandoni mwa chuo.

“ Subira kama tulivyoongea simuni,mimi ni rafiki wa siku nyingi wa Brigita.Kwa sasa ninaishi Marekani na nimerudi nchini kwa mapumziko mafupi.Ni muda umepita sijawasiliana naye na mara ya mwisho kuwasiliana naye alinielekeza mahala anapofanyia kazi nikamwambia kwamba nikija Tanzania nitamtembelea.Nimefika kumtembelea mahala alikonielekeza anafanya kazi nikakutana na taarifa hizi za kustusha za kifo chake.Nimeumia sana.Hebu nieleze japo kwa undani kidogo nini kilitokea na kusababisha kifo chake? Akauliza Anitha.

Subira akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Brigita alikuwa ni rafiki yangu mkubwa na tulikuwa tunaelewana mno.Usiku wa siku alipofariki tulipanga twende taarabu mashauzi Classic lakini baadae alibadili maamuzi na kuniambia kwamba hangekwenda tena Mashauzi kwani alipigiwa simu na babu kwamba wanatakiwa waonane jioni ya siku ile.Safari yetu ikawa imeishia hapo,hatukutoka tena hadi nilipopata taarifa za kifo chake asubuhi.Kwa kweli hata mimi niliumia mno na hadi leo hi bado ninaendelea kuumia.Nilimpenda sana Brigita.Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa inasemekana kwamba mtungi wa gesi ulilipuka na kusababisha maafa yale” akasema Subira

“ Pole sana Subira” akasema Anitha

“ Nimekwisha poa” akajibu subira

“ Umesema kwamba mlipanga muende mashauzi Classic lakini mkaahirisha aliposema kwamba alipigiwa simu akaonane na babu.Huyu babu ni nani?

Subira akatabasamu kidogo na kusema

“ Brigita alikuwa na mahusiano na mzee mmoja hivi ambaye ndiye aliyemjengea nyumba,akamnunulia gari na ndiye aliyekuwa akimuhudumia kwa kila kitu.Mzee Matiku alifariki dunia wiki mbili tu baada ya Brigita kufariki kwa kujipiga risasi ya kichwa.Inasemekana kifo cha Brigita kilimuumiza sana na ndiyo maana akaamua kujimaliza kwa risasi. ”

“ Dah ! akasema Anitha

“ Nakumbuka Brigita aliwahi kuwa na mahusiano na kijana mmoja hivi anaitwa Edson.Aliwahi kunitumia picha wakiwa naye.Gosh he was very handsome,je waliachana hadi akaamua kuingia katika mahusiano na huyo mzee? Akauliza Anitha

“ Edson ninamfahamu lakini naye alikwisha fariki dunia.Aliuliwa na mpenzi wake.Ninachokifahamu mimi,Brigita na Edson walikuwa wanakutana kwa siri.Hakuwa akimpenda mzee Matiku na alikuwa naye kwa ajili ya pesa zake tu lakini moyo wake ulikuwa kwa Edson.Mzee Matiku alikuwa na wivu uliopitiliza na aliwahi kumwambia Brigita kwamba siku akimkuta na mwanaume mwingine basi huo ungekuwa ni mwisho wake.Brigita alimuogopa sana mzee Yule hivyo akawa akiwasiliana na Edson kwa siri.Mzee Edson alikuwa akimfuatilia sana hadi alimuwekea kifaa maalum katika simu yake cha kuchunguza watu aliokuwa akiwasiliana nao.Hakutaka kabisa amuone na mwanaume yeyote zaidi yake.Brigita alianza kuchoshwa na mahusiano yake na Yule mzee na kila siku alikuwa akiniambia kwamba siku moja lazima atakuja kumkimbia .Aliniambia kwamba kuna biashara wanataka kuifanya na Edson na endapo ikifanikiwa basi watapata pesa nyingi na kisha atamkimbia mzee yule na kuhama kabisa nchi.Hakuwahi kuniambia ni biashara gani walitegemea kuifanya na Edson.Siku moja aliniambia kwamba kuna kitu amekichukua toka kwa mzee Matiku ambacho endapo angegundua basi kingemletea shida sana.Hakuniambia ni kitu gani hadi alipofariki.” Akasema Subira

“ Huyo mzee Matiku alikuwa anafanya kazi gani? Alikuwa na familia?

“ Mzee Matiku ni mfanyabiashara,ndiye mwenye ile hoteli niliyokuwa nikifanya kazi na ndiyo maana Brigita alikuwa na kazi nzuri sana pale.Watu wanasema kwamba ni mwanajeshi mstaafu.Wanasema kwamba aliwahi kuwa mlinzi wa rais miaka ya nyuma sana.Kwa upande wa familia mzee Matiku hakuwa na familia” akasema Subira.

“ Subira nashukuru sana kwa kunipa mwanga kuhusiana na kifo cha rafiki yangu Brigita.Kwa sasa kuna mahala ninatakiwa kwenda ila nitakutafuta mwishoni mwa wiki tukae tuongee na unieleze mambo mengi kuhusiana na Brigita na pia unitambulishe kwa ndugu zake unaowafahamu ili niweze kuwapa pole.Ahsante sana kwa muda wako na tutaonana tena” akasema Anitha huku akifungua pochi yake na kumpatia Subira kiasi cha dola hamsini za Marekani halafu wakasimama na kuondoka

“mambo mapya yanazidi kuibuka kila siku.Kwa sasa tuna mtu mwingine ameongezeka katika uchunguzi wetu,babu Matiku.” Akasema Mathew wakiwa garini wakiondoka maeneo ya chuo

“ Brigita alikuwa na mahusiano na mzee Matiku na wakati huo huo akawa na mahusiano ya siri na Edson.Walikuwa wakiwasiliana kwa siri ili mzee Yule asigundue na ndiyo maana laini ile ya simu ya Edson iliwekewa uzio ili mtu mwingine asiweze kugundua walichokuwa wakikiongea.Kwa mujibu wa Subira siku chache kabla ya kifo chake Brigita alimweleza kwamba kuna kitu alikichukua toka kwa mzee Matiku je ni kitu gani hicho? Ni biashara gani aliyokuwa akiifanya na Edson ambayo ingewapatia pesa nyingi kiasi cha kumfanya Brigita afikirie hatan kukimbia na kuhama nchi? Akauliza Mathew

“ Majibu ya maswali haya yanakuwa magumu kupatikana kwa sababu wahusika wote ambao wangeweza kutupatia majibu wamekwisha fariki.Tumerudi katika sifuri .Lakini kuna muunganiko wa kifo cha Edson,Brigita na mzee Matiku.Sababu ya vifo vyao ni moja.Ninahisi hicho kitu Brigita alichokichukua toka kwa mzee Matiku alimshirikisha pia Edson na inawezekana ndiyo iliyosababisha vifo vyao.Je ni kitu gani hicho? Ni biashara gani walitaka kuifanya? Mzee matiku ni nani? Nadhani ili tupate mwangaza tunatakiwa tumfahamu pia huyu mzee ni nani ,vyanzo vyake vya mapato n.k.Yawezekana akawa ni mtu aliyekuwa akijishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya..” akasema Mathew lakini akastuliwa na Anitha

“Mathew…!!” Anitha akaita

“ Kamera kipepeo nyumbani kwa Penny imetoa mlio.Kuna watu wanaingia nyumbani kwa Penny” akasema Anitha.Mathew akasogeza gari pembeni na kusimama akawatazama watu wale waliokuwa wakiinga kwa Penny kupitia kompyuta ya Anitha

“ Ni sura zile zile za jana.Who are these people? Wanatafuta nini kwa penny?

“ We need to find out” akasema Mathew huku akiwashuhudia watu wale wakiufungua mlango wa Penny na kuingia ndani

“ Twende nyumbani kwa Penny.Leo lazima tuwafahamu” akasema Mathew na kuwasha gari wakaelekea nyumbani kwa Penny



“ Wanafungua mlango wa sebuleni ,wanaingia ndani” akasema Anitha aliyekuwa akiwatazama wale jamaa kupitia kompyuta iliyounganishwa na kamera zilizoko nyumbani kwa Peniela

“ Kwa bahati mbaya hakuna kamera yoyote niliyoweka ndani ya nyumba ya Penny kwa hiyo hatuwezi kujua wanakwenda kutafuta kitu gani mle ndani lakini leo lazima tupate majibu watu hawa ni akina nani na wanatafuta nini kwa Penny” akasema Mathew ambaye alikuwa makini sana katika usukani

Waliwasili katika mtaa anaoishi Penny wakasimamisha gari nyumba ya tatu toka nyumba ya Penny.

“ We’re here.Nyumba ya Penny ni ile yenye bati jekundu.Ngoja tuendelee kuwasubiri wale jamaa watoke” Mathew akamuonyesha Anitha nyumba ya Penny

“ Wow ! Nyumba nzuri sana.Anafanya kazi gani Penny? Akauliza Anitha

“ Penny ni mfanya biashara.Ana maduka makubwa ya urembo na mavazi” akajibu Mathew

Waliendelea kukaa ndani ya gari wakiikodolea macho kompyuta na mara mlango wa mbele wa nyumba ya Penny ukafunguliwahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“ Wanatoka” akasema Anitha

“ Ok Get ready” akasema Mathew huku akiwasha gari

Wale jamaa walitoka wakafunga geti na kuingia katika gari lao wakaondoka.Mathew na Anitha wakawafuata

Toka nyumbani kwa Penny ,walielekea hadi katika duka moja la kuuza vyakula mmoja wao akashuka na kuingia ndani ya duka lile na baada ya muda mfupi akatoka akiwa na mfuko mkononi ,wakaendelea na safari yao bila kujua kama walikuwa wakifuatiliwa na akina Mathew

Saa sita na dakika nane wakawasili Miseko hospital,moja kati ya hospitali kubwa nchini.

“ Wamefuata nini hapa hospitali? Akauliza Mathew

“ Lazima kuna kitu wamekifuata hapa.Tuendelee kuwafuatilia.Ninaingia katika mfumo wa kompyuta wa hapa hospitali ili niweze kuwafuatilia kupitia kamera za ulinzi zilizoko hapa hospitali “ akasema Anitha

Wale jamaa wakashuka garini na kuangaza huku na huko halafu wakaanza kutembea kwa kasi kuelekea kusini mwa hospitali kuliko na wodi za kulipia na zile wa watu maarufu

“ Wanaonekana kuelekea sehemu ziliko wodi za watu maarufu.Anitha wewe utabaki ndani ya gari mimi nitawafuatilia nione wanakwenda kufanya nini kule katika wodi.Endelea kuwafuatilia kupitia kamera “ akasema Mathew huku akiweka sikioni kifaa cha mawasiliano kati yake na Anitha.Akakijaribu na kuona kinafanya kazi ,akashuka garini

“ I’m in now.I can access every thing.Ninawaona wale jamaa kwa kupitia kamera 4g ambayo imeelekezwa kusini” Anitha akamtaarifu Mathew aliyekuwa akitembea kwa kasi kuwafuata wale jamaa ambao hawakuwa na wazo kwamba wanafuatiliwa

“ Good Job Anitha,keep an eye on them” akasema Mathew. Ukubwa wa hospitali hii ulichangia kuwepo kwa idadi kubwa ya watu.Karibu magonjwa yote yalikuwa yakitibiwa hapa hivyo hospitali hii ilikuwa ikipokea mamia ya wagonjwa kila siku toka katika sehemu mbali mbali za nchi na hata nchi za jirani

“ Mathew nimebadilisha kamera na sasa natumia kamera 6 C” Anitha akamtaarifu Mathew

“ Ok Anitha.Endelea kuwafuatilia.Hata mimi bado sijawapoteza.Niko nao sambamba” akasema Mathew

Wale jamaa walinyooka na kuingia katika jengo lililokuwa na kibao VIP Private 2.

“ Wanaingia VIP Private 2” Mathew akamwambia Anitha

“ Ok nimekwisha waona.Itabidi ufanye haraka ili usiwapoteze kwa sababu mle ndani ninaiona kamera moja tu inayofanya kazi .Kamera nyingine zote inaonekana hazifanyi kazi.” akasema Anitha.Mathew akaongeza mwendo na kuacha umbali mfupi baina yake na wale jamaa.Watu wale hawakutaka kutumia lifti ,wakapanda ngazi kwa miguu hadi ghorofa ya nne ambayo ilionekana kuwa kimya sana.Wale jamaa wakasimama nje ya mlango mmoja wakagonga na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa wakaingia ndani. Mathew aliyekuwa akitembea kwa uangalifu mkubwa ili wale jamaa wasije wakastuka kwamba anawafuatilia akatazama pande zote hakuona mtu,akaukaribia mlango ule na kusoma namba zilizobandikwa juu.

“ Anitha wameingia chumba namba PV2 – 78.Angalia katika orodha ya wagonjwa tufahamu ni nani aliyelazwa katika chumba hiki” akasema Mathew.Baada ya kama dakika moja Anitha akasema

“Katika chumba hicho amelazwa mgonjwa mmoja anaitwa John Mwaulaya Albert,anasumbuliwa na tatizo la kupoteza fahamu mara kwa mara”

Mathew akastuka sana aliposikia jina lile la John Mwaulaya Albert

“ Anitha umesema John Mwaulaya Albert? akauliza Mathew

“ Ndiyo.Do you know him? Akauliza Anitha.Mathew hakujibu kitu .Alionekana wazi kupatwa na mstuko

“ Mathew say something.Do you know him? Akauliza tena Anitha

“ Subiri kidogo Anitha” akasema Mathew halafu akaukaribia ule mlango na kujaribu kutega sikio ili asikie kinachoongelewa ndani lakini hakusikia chochote.Alionekana kuchanganyikiwa ghafla

********

Gari mbili nyeusi ziliwasili katika eneo la kuegeshea magari katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro .Watu wanne waliovalia suti nyeusi wakashuka wawili toka katika kila gari.Mlango wa kati wa gari lililotangulia ukafunguliwa na mwanadada mmoja mwenye uzuri wa kimalaika akashuka.Alikuwa amevalia koti kubwa la kujikinga na baridi.Toka katika gari la pili,mabegi matatu yakashushwa na kuanza kukokotwa kuelekea ndani ya uwanja wa ndege kulikokuwa na ndege maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya mwanadada huyu mwenye uzuri usio na kifani.Baada ya hatua kama tano hivi ,simu ya mmoja wa wale vijana ikaita akaipokea na kisha akampatia Yule mwanadada waliyekuwa wameongozna naye

“ Madam Penny mheshimiwa rais anataka kuongea nawe.” Akasema Yule jamaa .Penny akaichukua ile simu na kuiweka sikioni

“ hallo” akaita

“ Hallo my angel.Tayari umeshafika uwanja wa ndege? I’ve missed you already” akasema Dr Joshua rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania

“ I’ve missed you too Dr Joshua,hivi sasa ndio tumewasili uwanjani tunaelekea ndegeni”

“ Penny ,hakuna sababu ya msingi iliyonifanya nikupigie simu .I just…I ..Just want to talk to you,to hear your voice and tell you how much I do miss you.Peniela thank you so much for everything.” Akasema Dr Joshua

Peny akatabasamu na kusema

“ Thank you too Dr Joshua for everything.You know how to treat a woman.You made me so happy.” Akasema Penny

“ Nafurahi kusikia hivyo Penny lakini bado sijakufanyia kitu chochote kikubwa cha kuweza kunishukuru.Thi

s is just the beginning Penny.I’ll make you a Tanzanian queen.From now you are going to live like a queen” akasema Dr Joshua

“ Ahsante sana Dr Joshua.” Akasema Penny

“ Ok Penny.Najua nikiwa Dar es salaam nafasi yangu ya kuonana nawe itakuwa ndogo sana kutokana na kazi lakini nitajitahidi kadiri inavyowezekana kuonana nawe mara kwa mara ndiyo maana nimekuhamishia katika nyumba ambayo itakuwa rahisi kwangu mimi kufika mara kwa mara.Nisikucheleweshe Penny tutaongea mengi tutakapoonana Dar es salaam Jioni ya leo nitakuwa mgeni wako na kukupa habari njema ” akasema Dr Joshua

“ Ouh Dr Joshua ,you are so sweet.See you later” akasema Penny na kukata simu

“ Nimemchanganya sana huyu mzee kiasi kwamba hafikirii kitu chochote kingine zaidi yangu.Hahaha…the old man is deadly in love with me..Now that I can control him the way I want ,its time to finish my job.Kuna nyakati namuonea huruma sana huyu mzee kwa namna alivyokufa akaoza kwangu na kuwa tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yangu,lakini sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya kufanya kile ninachotakiwa kukifanya.” Akawaza Penny akiongozwa na walinzi wale wa rais kuelekea katika ndege maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kumrejesha Dar es salaam.Aliingia ndani ya ndege na kukaa,akafumba macho na kukumbuka mambo yote yaliyotokea jijini Arusha

“ Dr Joshua amejitahidi kufanya kila alichoweza ili kunifanya niwe na furaha. Nilivaa uhusika vizuri sana na kumfanya aamini kwamba nimefurahi na ninampenda.Yule mzee ananipenda sana na yuko tayari kufanya kitu chochote kunifanya niwe na furaha.Amenipatia jumba jipya pembeni ya bahari ili iwe rahisi kwake kufika katika muda wowote anaoutaka.Pamoja na yote haya anayoyafanya kwangu lakini si mtu wa saizi yangu.I don’t love him at all na toka ndani ya moyo wangu nina kisasi naye kikubwa sana kwa kumuua Edson kijana niliyempenda kwa moyo wangu wote.Ngoja niendelee kuuvaa uhusika hadi hapo mambo yangu yatakapotimia ndipo atakapogundua kwamba mimi si malaika kama anavyodhani” Akawaza Penny akiwa angani akielekea Dare s salaam

********

Baada tu ya kumaliza kuongea na Penny simuni,Dr Joshua akiwa amejifungia chumbani kwake akazitafuta namba Fulani katika simu yake na kutaka kubonyeza kitufe cha kupigia lakini akasita.Akaenda dirishani akatazama nje na kuzama katika mawazi kwa muda wa dakika kadhaa halafu akasema kwa sauti ndogo

“ let me do it”

Akabonyeza kitufe cha kupigia na kuiweka simu sikioni.Baada ya muda smu ikapokelewa

“ Captain Amos” akasema Dr Joshua

“ Hallo mheshimiwa “ akasema Captain Amos

“ Mgonja anaendeleaje?

“ Hali yake iko hivyo hivyo.Bado si nzuri .”

“ Ok Captain.Do it” akasema Dr Joshua.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita Captain Amos akasema

“ Are you sure Mr President?

“ yes I’m sure.Do it. And Captain Amos,Thank you so much for this” akasema Dr Joshua na kukata simu.

Captain Amos aliyekuwa ni daktari wa familia ya rais akaegemea ukuta akawaza kwa dakika kadhaa halafu akachukua mkoba wake na kuelekea katika chumba cha mke wa rais,akagonga mlango ukafunguliwa na msaidizi wa mke wa rais

“ Muda wa matibabu sasa” akasema Captain amos na Yule msaidizi wa mke wa rais akatoka.

Captain Amos akachukua kichupa kidogo chenye dawa toka katika mkoba wake akainyonya dawa ile katika bomba la sindano na kumchoma mke wa rais

“ I’m sorry for this madam first lady” akasema Captain Amos na kutoka mle chumbani

********

Kwa muda wa dakika tatu Mathew aliendelea kusimama nje ya mlango wa kile chumba walichoingia wale jamaa.Alitamani ajue kilichokuwa kinaendelea mle ndani

“ Mathew talk to me” Anitha akasema

“ Anitha una hakika umesoma vizuri jina la mtu aliyemo ndani ya chumba hiki? Akauliza Mathew

“Chumba PV 2 – 78 amelazwa mgonjwa anayeitwa John Mwaulaya Albert.Kwani vipi Mathew.Unamfaha

mu mtu huyo?

Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Yah ! Ninamfahamu.Kama ni kweli aliyemo ndani ya chumba hiki ni John Mwaulaya basi mambo si rahisi kama tunavyofikiri” akasema Mathew kwa sauti ndogo huku akiwa makini akiangalia kila upande kuhakikisha usalama wake kwani alikwisha anza kuhisi hatari eneo lile

“ Mathew who is this guy John Mwaulaya ? Akauliza Anitha

“ Anitha tutaongea baadae.Eneo hili si salama hata kidogo.Please stay in the car and don’t get out” akasema Mathew

“ Mathew whats going on? Akauliza Anitha.Mathew hakujibu kitu .Kuna watu wawili walikuwa wakija kwa kasi.



Mathew alihisi wale jamaa wanamfuata ikamlazimu kuingia katika choo kilichokuwa chumba cha tatu kutoka kile chumba.Wale jamaa wawili waliouwa wakija kwa kasi wakaingia nao katika kile chumba alicholazwa John Mwaulaya.

“ Lazima nipate uhakika kama ni kweli mtu aliyelazwa mle ndani ni John Mwaulaya.Kama kweli ni yeye basi tutakuwa tumeingia katika hatari kubwa.” Akawaza Mathew akiwa amejificha chooni huku macho yake akiwa ameyaelekeza katika kile chumba cha John akitaka kufahamu kila kilichokuwa kikiendelea.

“ Mathew !.akaita Anitha

“ Hallow Anitha” akasema Mathew kwa kunong’ona

“ Say something.Whats going on over there? Akauliza Anitha

“ Anitha endelea kukaa ndani ya gari,bado ninaendelea kuwafuatilia hawa jamaa” akasema Mathew

“ Mathew mbona hutaki kunieleza nini kinachoendelea huko juu?

“ Anitha,nitakueleza lakini si sasa.” Akasema Mathew

Baada ya dakika kama thelathini hivi ,mlango wa kile chumba ukafunguliwa na jamaa wanne wakatoka wakiwa wameongozana na daktari mmoja wa kizungu

“ Anitha,wametoka watu wanne ndani ya kile chumba wameongozana na daktari mmoja wa kizungu.Nadhani wanashuka chini” Mathew akamtaarifu Anitha

“ Ok nitawaona katika kamera watakapofika chini” akasema Anitha

“ Tunamuhitaji Yule daktari wa kizungu.” Akaelekeza Mathew

“ Nimekusoma Mathew” akajibu Anitha

Mathew akatoka mle chooni alimokuwa amejibanza na kutembea kwa kasi akishuka chini kuwawahi wale jamaa.

“ Mathew tayari nimewaona wale jamaa katika kamera.Wako wanne na daktari mmoja wa kizungu.Wale jamaa wameagana na Yule dakatari ambaye kwa sasa anaongea na daktari mwenzake.Namuona Yule daktari ana kitambulisho katika koti lake .Ngoja nimvute karibu nifahamu jina lake” akasema Anitha

“ Ok Anitha.Achana na wale jamaa.Elekeza macho kwa daktari.Mimi niko ghorofa ya pili ninashuka ” akasema Mathew

Baada ya sekunde kadhaa Anitha akasema

“ I’ve got him !”

“ Anaitwa Michael Rodriguerz “

“ Good Job Anitha “ akajibu Mathew tayari akiwa ghorofa ya kwanza

Bado Dr Michael aliendelea kuongea na daktari mwenzake.Mathew akawapita halafu akaenda kusimama nje katika maua

“ Anitha niko hapa nje nikimsubiri atoke” akasema Mathew

“ Mathew , Dr James anatoka nje ya jengo anaelekea upande wa mashariki nadhani ndiko iliko ofisi yake” akasema Anitha

“ Ok Anitha nimekwisha muona,ninamfuatilia” akasema Mathew na kuanza kutembea taratibu akimfuata Dr Michael

“ Mathew nimetafuta kwa haraka haraka taarifa za Dr Michael ni kwamba ana umri wa miaka 53,ni mzaliwa wa Mexico,amesoma nchini Marekani ,Mexico na Urusi.Ni baba wa watoto watatu,Peter,Michael jr na Celine .Mke wake anaitwa Michelle Donalds mzaliwa wa Texas marekani.Dr Michael ni daktari bingwa wa mishipa ya fahamu” akasema Anitha

“ Thank you Anitha.Dr Michael sasa anaingia katika jengo lenye ofisi.Sintoweza tena kuingia mle ndani kwa sababu kuna kibao hapa kinachoonyesha kwamba huruhusiwi kuingia ndani kama si muhusika.Endele

a kumfuatilia kupitia kamera” akasema Mathew na kuanza kurudi mahala walikoegesha gari

“ John Mwaulaya !..” akawaza Mathew na mwili wote ukamsisimka

“ Bado siamini kama kweli ni yeye ndiye aliyelazwa ndani ya chumba kile hadi nitakapomtia machoni ndipo nitaamini” akawaza Mathew huku akitembea kwa kasi .Mara Anitha akaumuita

“ Mathew ,Dr Joshua ametoka,anaelekea katika eneo la kuegesha magari ya madaktari,anaingia katika gari lenye namba BV36P44.Umefika wapi ? akauliza Anitha

“ Tayari nimekwisha fika Anitha” akasema Mathew wakati akilikaribia gari lao.Alitembea kwa haraka akaufungua mlango na kuingia ndani

“ Ameelekea wapi? Akauliza Mathew huku akiwasha gari

“ Ameelekea geti la Mashariki”

“ Ok twende tuondoke tutamuwahi hapo bara bara kuu.” Akasema Mathew na kuwasha gari wakaondoka

Walisimama kwa dakika tatu kusubiri nafasi ya kuingia barabara kuu na mara Anitha akaliona gari la Dr Michael akamuonyesha Mathew

“ Ok.Nimemuona” akasema Mathew na kuingia barabarani akiacha magari matatu kati yao na Dr Michael

“ Hatupaswi kumpoteza.Tunamuhitaji sana” akasema Mathew

“ Mathew whats going on? Who is John mwaulaya? Nimejaribu kutafuta taarifa zake lakini hakuna mahala nimeweza kupata.Who is he? Akauliza Anitha

“ Tutaongea baadae Anitha lakini kwa sasa tuelekeze macho yetu kwa Dr Michael tusije tukampoteza.” akasema Mathew

“ Mathew tunaifanya kazi hii pamoja,na ili tufanikiwe tafadhali naomba uwe muwazi kwangu katika kila jambo ili tusaidiane mawazo nini cha kufanya” akasema Anitha

“ Usihofu Anitha.Kuna mambo mengi sana ambayo unahitaji kuyafahamu lakini kwa sasa tuyaweke pembeni na tuhakikishe hatumpotezi Michael” akasema Mathew.Anitha hakuuliza kitu tena wakaendelea na safari yao ya kumfuatilia Dr Michael.

Baada ya kutoka hospitali,Dr Michael alikwenda moja kwa moja Tanganyika Internationa school akaegesha gari na baada ya dakika kama tatu hivi ,mwanadada mmoja akatokea akiwa amemshika mkono mtoto mdogo .Dr Michael akamkumbatia Yule mtoto na kuwafungulia mlango wakaingia garini halafu wakaondoka.

“ Yule mtoto anaitwa Michael jr.Ni mtoto wa pili wa Dr Michael na Yule mwanadada aliyeongozana nao nadhani ni mtumishi wao” akasema Anitha

Waliendelea kumfuatilia Dr Michael bila ya yeye kufahamu kama anafuatiliwa.Toka pale shuleni Dr Michael hakupita sehemu nyingine ,alielekea moja kwa moja nyumbani kwake.Alipofika kwake alipiga honi akafunguliwa geti na kuingia ndani kisha geti likafungwa

“ Whats next ? akauliza Anitha

“ Najaribu kutafakari nini cha kufanya” akasema Mathew na mara mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na Yule mwanadada aliyekuwa ameongozana na Dr Michael toka shuleni akatoka.

“ Yule dada anatoka.Amebeba mkoba wake inaonekana kama vile anaondoka” akasema Anitha

“ Go get her.We can use her .Tunahtaji kumpata Yule mtoto wa Dr Michael na itakuwa rahisi kama tukimtumia yeye” akasema Mathew.Anitha akashuka garini na kutembea kwa haraka akamfuata Yule dada ambaye alikuwa akitembea taratibu huku akiongea na simu.Mara tu alipomaliza kuongea na simu Anitha akamsalimu

“ Habari yako dada”

“ Habari yangu nzuri.Habari yako? Akasema Yule dada ambaye alikuwa na sauti laini ya upole

“ Naitwa Anitha,mwenzangu unaitwa nani? Akasema Anitha hukuakitabasamu

“ Naitwa Lydie Masawe” akasema

“ Nafurahi kukufahmu Lydie.Unaelekea wapi hivi sasa?

“ Naelekea nyumbani lakini nitapita kwanza saluni kurekebisha nywele na kucha”

“ Sawa Lydie,nadhani ni mara ya kwanza mimi na wewe kuonana”

“ Ndiyo ni mara ya kwanza dada Anitha.Sina kumbu kumbu kama tumewahi kuonana” akasema Lydie

“ Ok Lydie.Kama hutajali nina maongezi nawe kidogo kuhusu kazi.Sijui unaweza kuwa na nafasi sasa hivi? Au kama unaelekea uko saluni,nina usafiri wangu tunaweza tukaongozana na tukapata wasaa wa kuzungumza” akasema Anitha.Lydie hakuwa na wasi wasi wakaelekea mahala akina Mathew walikoegesha gari

“ Lydie huyu ni dereva angu anaitwa Mathew” Anitha akafanya utambulisho mfupi baada ya kuingia garini

“ Mathew tupeleke Zulphat beauty salon” akaelekeza Anitha.

Ndani ya gari walikuwa wakiongea mambo mbali mbali yahusuyo urembo kwa ujumla hadi walipowasili Zulphat beauty salon moja kati ya saluni kubwa za akina mama jijini Dar.Lydie alitengenezwa kwa gharama za Anitha kwani saluni hii ni moja kati ya saluni zenye gharama kubwa.Baada ya hapo wakaelekea Ibona hotel kwa ajili ya maongezi

“ Lydie nimekuleta hapa ili tuweze kuongea kwa utulivu na nafasi” akasema Anitha wakiwa katika bustani tulivu

“ Nakusikilza dada Anitha”

“ Lydie umeolewa? Akauliza Anitha ili kutaka kumfahamu vizuri

“ Hapana bado ila nina mtoto mmoja”

“ Hongera.Mwanao yuko wapi? Akauliza Anitha

“ Yuko kwa babu yake huko Moshi”

“ Kwa nini usimchukue ukaishi naye?

“ Natamani sana kufanya hivyo lakini hali ngumu ya maisha inanilazimu nimuache kwa babu zake”

“ Sawa nimekuelewa Lydie.Sasa dada yangu bila kupoteza wakati nimekufuata nina kazi moja ambayo nahitaji unifanyie.Endapo utakubali basi unaweza ukapata pesa ambayo itakusaidia sana katika kuondokana na maisha haya duni na ukaanzisha biashara zako mwenyewe na hutafanya tena kazi kwa mtu na utakuwa na uwezo wa kuishi na mwanao na kumpatia elimu bora ” akasema Anitha

“ Nitashukuru sana dada Anitha kama utanipatia kazi ambayo itaniwezesha niweze kupata mtaji wa kujiajiri mwenyewe.Niambie ni kazi gani unataka nikufanyie? Una mtoto wa kulea?”

“ Hapana sina mtoto bado Lydie lakini kuna kazi nyingine ndogo tu tena ya masaa machache.Kwanza nieleze pale kwa Dr Michael unafanya kazi gani?

“ Kazi yangu ni kumlea Michael Jr.Asubuhi kumuandaa na kumpeleka shule ambako huwa nikishinda huko hadi saa nane mchana.Dereva huja kutuchukua na kuturudisha nyumbani.Saa tisa kamili ndiyo mwisho wangu wa kazi na hurejea nyumbani” akasema Lydie

“ Ok Lydie sasa ni hivi,kuna taarifa muhimu sana tunayoihitaji toka kwa Dr Michael na ambayo hawezi kutupatia hivi hivi,kwa hiyo tunahitaji kutumia njia mbadala kuipata taarifa hiyo.Nahitaji kumtumia mtoto wake Michael kumtisha kidogo ili aweze kunipatia taarifa hiyo” akasema Anitha na kumtazama Lydie

“ Wewe ni polisi? Akauliza Lydie kwa wasi wasi

“ Hapana,mimi si polisi lakini kazi zangu zinafanana kidogo na za polisi.” akajibu Anitha

“ Kwa hiyo unataka kumtumiaje Michael Jr?

“ Nitamtumia kama chambo ili niweze kuipata taarifa ninayoitaka toka kwa Dr Michael.Najua anampenda sana mwanae hivyo akisikia kwamba mtoto wake yuko mikononi mwangu lazima atatoa taarifa hiyo ninayoitaka” akasema Aitha.Lydie akaonekana kuogopa sana

“ Dada Anitha naona siwezi kuifanya hiyo kazi.Ni kazi ya hatari sana na inaweza kunisababishia matatizo.Hilo ni kosa kubwa na endapo nikishikwa na polisi nitaweza hata kufungwa kwa kosa la utekaji na mwanangu akabaki akiteseka.Utanisamehe dada yangu sintoweza”

Anitha akatabasamu kidogo na kusema

“ Usiogope Lydie.Suala hili haliwezi kwenda polisi kwa sababu mimi ninafanya kazi kwa niaba ya polisi kwa hiyo hata kama likifika kwao wananifahamu kwamba niko kazini na lengo langu si kumuumiza mtoto huyo wala Dr Michael,bali ni kupata taarifa hiyo muhimu sana kwa usalama wa taifa.”

“ Pamoja na hayo dada Anitha bado naona sintoweza.Sijawahi kufanya kazi kama hiyo hata mara moja,zaidi ya yote familia ile wananipenda na kunihudumia vizuri ,siwezi kuwafanyia kitendo kama hicho” akasema Lydie.Anitha akamtazama kwa sekunde kadhaa na kumuuliza

“ Lydie unatoka katika mkoa wa Kilimanjaro,si ndiyo?

“ Ndiyo”

“ Ninawafahamu watu wa Kilimanjaro hususani wanawake ni watafutaji wazuri wa pesa.Ni wapambanaji wa kweli katika kutafuta maisha.Wanaitafuta pesa bila kuchoka na hawaogopi changamoto zilizoko mbele yao na hiyo ndiyo siri ya wao kufanikiwa sana.Tunawaona wengi hapa Dar es salaama namna walivyofanikiwa ,namna walivyochangamka kuitafuta pesa,hawakuja hapa mjini kutazama maghorofa au kuza sura zao nzuri,bali wamekuja kutafuta pesa.Ninakupa fursa ya kujikwamua kiuchumi naomba usiipuuze.Please Lydie wake up.This is your chance.Vaa uhusika wa mwanamke wa kichaga asiye ogopa changamoto na ukubali kuifanya kazi hii ndogo lakini yenye maslahi manono.Niambie unahitaji kiasi gani nikupatie? Akauliza Anitha.Lydie akainama akafikiri

“ Ok ngoja nikutajie .Mimi nitakupa Tsh Milioni saba ili uweze kunifanyia kazi hiyo” akasema Anitha na mara Lydie akainua kichwa

“ Kiasi hicho kiko tayari?

“ Ndiyo kipo tayari.Uko tayari kuifanya kazi hii?

“ Kama mtanilipa kiasi hicho cha pesa mimi niko tayari lakini kwa sharti moja tu kwamba mnipatie kwanza kabla sijawafanyia kazi hiyo kwa sababu ninaweza nikahatarisha usalama wangu halafu msinilipe chochote nikawa nimeharibu kazi yangu na maisha yangu”

“ Usihofu kuhusu pesa hata sasa hivi unaweza ukapewa mradi tu ukubali kuifanya hiyo kazi” akasema Anitha

“ Mimi niko tayari kuifanya.Si umesema suala hili haliwezi kufika polisi?

“ Ndiyo haliwezi kufika polisi”

“ Ok nielekeze unataka nifanye nini?

“ Asubuhi utampeleka Michael Jr shule kama kawaida.Saa tano za asubuhi tutakuja na gari na utawaambia waalimu kwamba umepigiwa simu uwahi kurejea nyumbani.Utatukabidhi mtoto na tutakukabidhi mzigo wako na utapotea na huo utakuwa ni mwisho wako kufanya kazi pale kwa Dr Michael.Sisi tutakaa na Yule mtoto kwa masaa machache na Dr Michael atakapotupatia taarifa yetu basi tutampatia mtoto wake.Nakuhakikishia tena kwamba hatuna lengo la kumdhuru mtoto wala mtu yeyote” akasema Anitha.Wakakubaliana na Lydie halafu wakaagana

“ Amekubali japo haikuwa rahisi kumshawishi.Imenilazimu kumtajia dau kubwa ndipo akakubali.Tutamlipa Tsh Milioni saba.” Akasema Anitha baada ya kuachana na Lydie na yeye kurejea garini alikomuacha Mathew

“ Good.Una hakika hawezi kutusumbua au kutuletea matatizo? Akauliza Mathew

“ She wont.She needs money.” Akajibu Anitha

“ Ok Good.Noah amenipigia simu tayari amekwisha wasili.Timu imekamilika” akasema Mathew

“ Wow that’s great.So whats next?

“ Kwa sasa tunatakiwa kuwasiliana na Elibariki ili tumfahamishe kuhusiana na pesa hii ili watupatie au kama hawana basi tutatumia za kwangu na wataturejeshea.Hatuwezi kukwama kwa sababu ya pesa” akasema Mathew

*********

Eugenia Conrad,msaidizi wa Dr Flora Johakim mke wa rais,alitoka mbio ndani ya chumba cha Dr Flora huku akipiga kelele. Walinzi walimkamata na kumuuliza kulikoni kupiga kelele zile

“ Mama Flora !!....Mama Flor……………!!!” hakumaliza sentensi yake akaanguka na kupoteza fahamu.Koplo Winifrida mlinzi wa Dr Flora akakimbia hadi chumbani kuangalia kuna nini,na ghafla akahisi miguu inamuisha nguvu.Dr Flora Johakim mke wa rais alikuwa amelala kitandani huku damu zikimtoka mdomoni na puani.Akajikaza na kukisogelea kitanda na kuita

“ Dr Flora.!!,Dr Flora !!....

Dr Flora hakutikisa hata ukope.Haraka haraka Winifrida akakimbilia katika simu akampigia Captain Amos daktari wa familia ya rais ambaye alifika mara moja na vipimo akampima na kuamuru liitwe gari la wagonjwa haraka.Gari la wagonjwa likafika Dr Flora akapakiwa na kukimbizwa katika hospitali ya jeshi.Pale akapimwa na kukutwa tayari amekwisha fariki.Baada ya kuthibitishwa kwamba amefariki dunia Captain Amos akampigia simu Dr Joshua

“ Hallow Captain” akasema Dr Joshua

“ Mr President its done.She’s dead”

“ Thank you Captain Amos.Niko njiani narejea Dar es salaam” akasema Dr Joshua na kukata simu.Captain Amos alibaki amesimama ameegemea mti.Alikuwa na mawazo mengi sana.

“ I’ve killed the first lady…Please forgive me lord” akawaza Captain Amos





Ndege aliyopanda Peniela akitokea jijini Arusha ilitua katika uwanja wa ndege wa kiataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam .Pale uwanjani kulikuwa na gari mbili zimeandaliwa kwa ajili yake .Moja ikiwa ni kwa ajili ya yeye kupanda na nyingine ilikuwa na walinzi wanne wa kumlinda.Baada ya kuingia katika gari akaomba apelekwe moja kwa moja katika nyumba ambayo Dr Joshua alimtaka ahamie mara tu atakaporejea Dar es salaam.

“ Nimerejea Dar es salama kama malkia.Naya penda maisha haya lakini ni kwa muda mfupi tu.” Akawaza penny akiwa garini.Uso wake haukukaukiwa na tabasamu .

Waliwasili katika jumba ambalo Dr Joshua alikuwa amempatia.Lilikuwa ni jumba kubwa zuri la kifahari la ghorofa tatu lililokuwa kandoni mwa bahari ya Hindi.Toka lilipojengwa halikuwahi kukaliwa na mtu yeyote.Alifunguliwa mlango na kuingia ndani,ambako kulikuwa na uzuri wa kipekee.Kulikuwa na samani za kupendeza za hali ya juu za gharama kubwa bila kusahau nakshi mbali mbali za kuvutia mno.Alishindwa kuizuia furaha yake pale alipoingia katika chumba cha kulala.

“ Wow ! This is amazing” akasema kwa furaha.Kilikuwa n i chumba kikubwa na kizuri mno chenye kila kitu cha thamani ambacho angehitaji kiwepo chumbani.Alienda katika dirisha kubwa na kuishuhudia madhari ya kupendeza ya bahari ya Hindi

“ This place is like paradise” akasema

“ Nimeipenda sana hii nyumba ni nzuri mno.Ina kila kitu ninachokihitaji” akasema Penny huku ajkishuka na kwenda kuangalia muonekano wa n je.Nje ya jumba lile la kifahari kulikuwa na viwanja vya michezo mbali mbalikama kikapu ,tenisi na wavu.Kulikuwa pia bwawa la kuogelea na bustani nzuri yenye maua na miti ya kupendeza.Lilikuwa ni jumba la kifahari mno.

“ Nimelipenda mno jumba hili na ninatamani kama ningeishi hapa lakini sintoweza.Nlimkubalia Dr Joshua kule Arusha lakini ni vigumu sana kwa mimi kukaa hapa.Sina mpango wa kuwa na mahusiano ya muda mrefu na yeye.Baada tu ya kazi yangu kumalizika mimi na yeye hatutakuwa na mahusiano tena.Uhusiano wetu utakuwa umefikia mwisho.” Akawaza Penny akiwa njiani kueleka nyumbani kwake

“ Natamani nifahamu jaji Elibariki na Jason wamefikia wapi kuhusiana na mpango wao wa kufanya uchunguzi juu ya kifo cha Edson.Sitaki waendelee na mpango wao ule kwa sababu ni hatari kubwa kwao.Sitaki wapate madhara yoyote yale kwani ni watu wangu wa karibu na wana umuhimu mkubwa katika maisha yangu. Kwa maana hiyo basi itanilazimu kutafuta namna nitakayoweza kuwafanya wasiendelee na mpango wao ule.Lazima niuvuruge ili kuwasaidia “ akawaza

Aliwasili nyumbani kwake akafunguliwa geti na kuingia ndani .Akaagana na wale walinzi wakaondoka.

“ Home sweet home”akasema kwa furaha alipoingia tena katika sebule yake

“Ninaipenda mno nyumba yangu na katu siko tayari kwenda kuishi sehemu nyingine”akawaza huku akipiga hatua kuelekea chumbani kwake.

Mara tu alipoingia chumbani kwake alipatwa na mstuko wa ghafla.Aligundua vitu havikuwa sawa.

“ Someone was here.Kuna mtu aliingia humu ndani ” akasema kwa hasira na woga

“ Vitu vyangu haviko sawa kama nilivyoviacha.Kuna mtu alikuja kupekua nyumba yangu.Atakuwa nani huyu ? Kitu gani walikuwa wanatafuta? Akawaza Penny akiwa amekasirika kupita kiasi na mara akakumbuka kitu,akaiwasha kompyuta yake na kupitia anuani yake ya barua pepe akaziona picha za mtu aliyefungua kasiki lililokuwa ukutani.Kasiki lle lilikuwa na kamera ya siri ambayo huchkua picha ya kila anayelifungua na kuirusha moja kwa moja katika anuani ya parua pepe ya Peniela.

“ Bastard !! akasema Penny kwa hasira baada ya kuiona picha ya jamaa mmoja aliyevaa glovu nyeusi mikononi akiwa ameshika heleni zake alizokuwa amezihifadhi katika kasiki

“ It’s them !!..”akasema na kuvuta pumzi ndefu

“ Kitu gani awlikuwa wakikitafuta humu ndani?.Watu hawa sasa wameanza kunichosha.Nilipatwa na matatizo na kunusurika kuingia gerezani lakini hawakunisaidia lolote.They are monsters.” Akawaza na kukaa kitandani

“Najilaumu sana kuingia katika kazi hii.Kwa sasa siwezi tena kujiengua.They have me in their hands.They control me” akainama na kudondosha chozi

“ kama ingekuwa ni kwa ridhaa yangu basi nisingekubali kujiunga nao .Nimekasirishwa mno na kitendo chao cha kuingia ndani mwangu na kupekua bila ruhusa yangu.Huu ni ukosefu wa adabu na ustaarabu.Ninafanya kazi zao vizuri lakini bado hawataki kuniacha walau niwe na maisha ya kawaida.Nilitegemea baada ya kumaliza mwaka mzima nikiwa gerezani nikiendelea na kesi yangu wasingesumbuka nami tena lakini walipofahamu nimeshinda kesi mara moja wakaendelea kuniandama na kunitaka niendelee na kazi yao .I’m tired with this life.I’m tired with them.Baada ya kazi hii kumalizika sitaki tena kufanya kazi yoyote tena.Chochote kitakachotokea na kitokee tu lakini nimechoka sasa.I need to live a normal life.I need my freedom back.” Akawaza Penny na mara akastuliwa na mlio wa simu ya mezani.Katika meza ya simu kulikuwa na simu tatu na iliyokuwa ikiita ilikuwa ni simu ya rangi nyeusi.

“ Its them ! akasema kwa hasira nakuichukua simu ile akabonyeza kitufe cha kupokelea

“ hallow “ akasema kwa sauti ya juu yenye kuonyesha wazi alikuwa amekasirika

‘ hallow Peniela” Ikasema sauti ya upande wa pili.Penny akastuka kidogo kwani haikuwa ile sauti aliyoizoea

“ Welcome back Peniela” akasema tena Yule jamaa upande wa pili

“ Who are you ? and where is he? Akauliza Penny

“ Relax penny.From now on you’ll be talking to me.My Code is 00P688.Muda wowote ukiwa na shida yoyote kubwa na unahitaji ufumbuzi au msaada wa haraka nitafute kwa kutumia code hiyo na utasaidiwa haraka sana.By the way where were you? Akauliza Yule jamaa ambaye alikuwa akiongea kwa taratibu sana

“ Kwa nini nyumba yangu imepekuliwa ? Don’t you trust me? Akauliza Penny kwa ukali

“ I’m sorry penny ,lakini ulipotea ghafla na hatukujua uko wapi kwa hiyo ni jukumu letu kuhakikisha kwamba uko salama na ndiyo maana tukaingia ili kufahamu kama umepatwa na tatizo lolote.Ni jukumu letu kuhakiki usalama wako Penny”

“ Naomba iwe ni mwanzo na mwisho kuingia ndani mwangu wakati sipo na wala sitaki kufuatiliwa na mtu yeyote Yule.Ninafanya kazi zangu vizuri kama mnavyotaka kwa hiyo naomba msivue mipaka.” Akasema Penny kwa ukali

“ Ok nimekuelewa Penny lakini siku nyingine kama una safari au unahitaji faragha, nitaarifu nifahamu li tujue kwamba uko salama.Vipi kuhusu mahusiano yako na mheshimwa rais yakoje toka umemaliza kesi?Mmeonana tayari? Akauliza Yule jamaa ambaye hakutaka kujitambulisha jina

“ Mahusiano ni mazuri,tunaendelea vizuri.Tayari nimekwisha mrudisha katika mstari na sasa ninaweza kuendelea kuimalizia kazi yangu.”

“ Ok vizuri penny.Jitahidi kwenda kwa kasi kidogo kwa sababu muda uliopangwa kwa operesheni hii unakaribia kumalizika na tusipofanya haraka kilakitu kitavurugika.” Akasema Yule jamaa

“ Hii si kazi rahisi kama mnavyodhani na haiwezi kwenda kwa haraka kama mnavyotaka.Inahitaji kutumia akili sana ili kuikamilisha kwa hiyo naombeni msiniharakishe.Niacheni niifanye kazi hii kadiri ninavyoona inawezekana.Pale ikulu si kama uwanja wa disko.Ile ni sehemu ngumu mno kuingilika kwa hiyo kuweni na subira” akasema penny

“ Nakuelewa penny lakini operesheni hii imechukua muda mrefu sana tofauti na tulivyokuwa tumeipanga.Na hii ilisababishwa na wewe kusahau kazi yako na kujiingiza katika masuala ya kimahusiano hadi kupelekea ukakutwa na yale matatizo.Jitahidi operesheni hii i malizike haraka kwani bado kuna kazi nyingi zinakusubiri” akasema Yule jamaa na kumstua Penny

“bado kuna kazi nyingine? I’m sorry guyz,nikisha kamilisha kazi hii nahitaji mapumziko.I need a break .I need back my normal life” akasema penny

“ Hahahaa..!! Penny we don’t have normal life and we don’t have time to rest.We workd day and night to make sure the nation is safe and people live their normal life.That means we’ve sacrificed our life for the people of this nation.Without us they cant sleep,so forget about break !.Nahitaji kuuona mpango kazi wako kabla ya saa mbili usiku leo ili nione kama unaenda katika njia sahihi.” Akasema Yule jamaa

“ Ok nitakutumia mpango kazi lakini ni baada ya siku mbili.Kuna mambo ambayo lazima niyaweke sawa kwanza.” Akasema penny

“ hakuna siku mbili Peny.Nahitaji leo kablaya saa mbili usiku uwe umenitumia.! Akasema kwa sauti ya juu Yule jamaa

“ tafadhali naomba usiniamrishe namna hiyo.You don’t know what I’m going through right now.You all depend on me to complete this mission so you’ll have to listen to me.Nimesema nitakutumia baada ya siku mbili and that’s final” akasema Penny

“ Ok Peny ,One more thing ,usiache kuvaa heleni yako hata siku moja.Ile ndiyo njia peke e ya mawasiliano kati yetu na wewe.” Akasema Yule jamaa na kukata simu.Penny alikuwa akitweta kwa hasira.Yule jamaa alikuwa amemchefua sana.

“ Who is this guy? Yule wa zamani amekwenda wapi? Akajiuliza.

“ Sifahamu nimepata wapi ujasiri wa kubishana na mtu huyu.These people controls me all over.when will I be free? When I will live a normal life? ..akawaza Penny

Akiwa amejilaza kitandani mwingi wa mawazo simu anayoitumia kuwasiliana na rais ikaita

“ Huyu mzee atapata uchizi mwaka huu.Kila wakati anataka kuongea na mimi” akawaza Penny halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea

“” Hallow Dr Joshua”akasema

“ Hallo Penny.Umeshafika?

“ Ndiyo nimekwisha fika Dr Joshua na kwa sasa niko kitandani nimepumzika”

“ Ok pole na safari.Ulikwenda kuiona nyumba?

“ Ndiyo,nilikwenda kuiona.Ni nyumba nzuri mno.”

“Umeionaje inakufaa? kama haikufai niambie nikupatie nyingine.Ninazo nyumba nyingi tu hapa jijini”

‘ Dr Joshua nyumba ile ni nzuri mno na ni nyumba ya ndoto zangu.Ina kila kitu ninachokihitaji na kukipena katika nyumba”

“ nafurahi kusikia hivyo Penny.Nifahamishe una hamia lini?”

“ Dr Joshua I’m sorry.Sintoweza kuhamia katika ile nyumba”

“ kwa nini penny? Mbona tulikwisha kubaliana uhamie pale ili iwe rahisi kwa mimi kufika muda wowote ninaoutaka?

“ Nimebadili mawazo Dr Joshua.Baada ya kuiona nyumba ile nimegundua kwamba siwezi kuishi pale.Its too big for me. I need normal and simple house” akasema Penny

“ Penny my angel wewe ni mwanamke ninayekupenda kuliko ninavyoweza kukueleza.Nina mipango mikubwa sana juu yako.Nataja uishi maisha kama ya malikia.I am the president of United republic of Tanzania and I can give you anything you want.Nataka upate kila starehe ya dunia hii.Tafadhali naomba ukubali kuuishi katika ile nyumba Penny” akasema Dr Joshua

“ Dr Joshua nadhani unafahamu toka tumefahamiana sijawahi kukutamkia neno hapana.Nimekuwa mtu wa kusema ndiyo kwa kila jambo unaloniambia lakini leo naomba niseme hapana.Sintoweza kuishi katika ile nyumba.Nitaendelea kuishi hapa katika nyumba yangu hii ndogo”

“ Ok Penny kama unapenda kuendelea kuishi hapo niruhusu basi niifanyie ukarabati mkubwa ili iwe na mandhari ya mke wa rais.Please don’t say No Peniela”

Peniela akatabasamu na kusema

“ Siwezi sema ndiyo kwa haraka Dr Joshua .Let me think about it” akasema penny

“ Ok Ahsante Penny.Halafu kuna jambo nataka nikutaarifu”

“ jambo gani Dr Joshua?

“ My wife is dead”

Kimya cha sekunde kadhaa kikapita,Penny akauliza

“ When did this happen?

“ Amefariki mchana huu.Hivi sasa niko katika maanadalizi ya kurejea Dar es salaam.”

“ So sorry for your loss Dr Joshua.”

“ Thank you so much the next first lady.Nitakupigia simu baadae .I have to go ,ndege iko tayari”akasema Dr Joshua na kukata simu.

“ Dr Flora is dead ?! This is weird! Amekufa kwa ugonjwa gani? Nilimuona siku ya hukumu ya kesi yangu alikuwa mzima wa afya akiwa ameongozana na wanae,iweje afariki ghafla namna hii? Akajiuliza penny

“ Lakini mbona Dr Joshua haonyesi kuguswa na kifo cha mkewe? Anaongea nami kama vile hakuna kilichotokea na hapo hapo anafanya utani kwa kuniita the next first lady.Si mara moja amekuwa akinitamkia kauli hii ya kwamba mimi ni mke wa rais mtarajiwa.Alijua kwamba mkewe atafariki muda si mrefu ? .Ninapatwa na mashaka kuhusianana kifo hiki cha Dr Flora”akawaza Penny halafu akachukua simu na kumpigia simu Jason akamfahamisha kwamba tayari amekwisha rejea.



*******************

Jaji Elibariki alikuwa akijiandaa kutoka ofisini kwake ili akakutane na akina Mathew waliokuwa wamemtaka aonanenao kuhusiana na ile fedha wanayoihitaji, mara simu ikaita.Akaitazama na kukuta ni mkewe Flaviana ndiye alipiga

“ Flaviana leo kaamua kunipigia simu !..Kashangaa

“ Yawezekana hasira zake zimekwisha ? Akajiuliza

“ kwa dharau alizonionyeshea sina hamu naye tena.”akawaza jaji Elibariki huku akivaa koti lake na kuiacha simu ikiita na kukatika bila kuipokea..Ikaanza kuita tena na kumlazimu aipokee

“hallow” akasema

“ hallow” ikasikika sauti ya Flaviana lakini ilionyesha kana kwamba analia

“ Flaviana why are you calling? akauliza jaji Elibariki huku sura yake ikiwa imekunja ndita kuonyesha kwamba hakupendezwa na simu ile ya mkewe.Flaviana hakujibu kitu akaendelea kulia

“ Flaviana kinachokuliza kitu gani? Kama huwezi kunieleza kilichokufanya ukanipigia simu I’m going to hang up now.I have so many things to do” akasema Jaji Elibariki

“ My mother is dead” akasema Flaviana

“ What ?!!!..jaji Elibariki akastuka

“ My mother…Is dead”akasema tena Flaviana

Jaji Elibariki akapatwa na mstuko mkubwa. Kwa sekunde kadhaa akabaki kimya halafu akauliza

“ Amefariki saa ngapi?

“ Mchana huu”

“ Uko wapi sasa hivi? Akauliza Jaji Elibariki

“ kwa sasa niko hapa katika hospitali kuu ya jeshi” akasema Flaviana

“ Ok ninakuja hapo sasa hivi” akasema jaji Elibariki huku akifuta kijasho kilichoanza kumchuruzika.Taarifa ile ya kifo cha Dr Flora ilimstua sana.

“ Nini kimemuua Dr Flora ghafla namna hii? Nafahamu alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu lakini hali yake haikuwa mbaya na jana usiku nilimsikia akizungumza na mwanae.” Jaji Elibariki alikuwa amekaa mezani akiwaza .Akachukua simu na kumpigia simu Jason akampa habari zile na kumtaka aende akaonane na akina Mathew ili alijadili suala lile la pesa wanazozihitaji,yeye akapanda gari na kuelekea hospitali kuu ya jeshi .http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Aliwasili katika hospitali kuu ya jeshi na kukuta magari mengi yameegeshwa.Ulinzi ulikuwa mkali sana na watu haakuruhusiwa kuingia ndani bila sababu maalum.Alijitambulisha getini kama jaji wa Mahakama kuu na mume wa Flaviana mtoto wa Rais,akaruhusiwa kupita.Aliegesha gari na akashuka na kuangaza huku na huku akijaribu kumtafuta mkewe mara akamuona Genevive binamu yao akina Flaviana.Wakasalimiana na kumuuliza mahala aliko Flaviana.

“ Sina hakika kama unaweza kuonana naye muda huu.Amepumzishwa katika chumba alikuwa amepoteza fahamu baada ya kuonyeshwa mwili wa mama yake”

“ Nipeleke mahaal alipo.I need to see her” akasema Jaji Elibariki.Genevive akamuongoza hadi katika chumba ambacho Flaviana alikuwa amepumzishwa.Nje ya mlangow a chumba kile alikuwepo muuguzi aliyekuwa akizuia mtu yeyote asiingie mle chumbani kama si daktari.Jaji Elibariki akajitambulisha kama mume wa Flaviana na kuruhusiwa kupita.Flaviana alikuwa amelala kitandani na alipomuona mumewe akaangua kilio.Jaji Elibariki akamfuata pale kitandani akamkumbatia na kumfariji

“ Pole sana Flaviana.” Akasema.

“ Eli,mama yangu amekwenda.” Akasema Flaviana huku akilia

“ Tafadhali usilie Flaviana.Its gonna be ok.I’m right here” akasema jaji Elibariki huku akimfuta mke wake machozi .

“ Nini kimesababisha kifo cha mama? Akauliza jaji Elibariki

“ Mpaka sasa hivi hatufahamu chochote kuhusiana na nini kimemuua.Madkatari bado hawajasema chochote lakini daktari wa familia Captain Amos anasema ni shinikizo la damu.Eli,inaniuma sana kumpoteza mama yangu.Jana usiku nimeongea naye akanipigia simu na kuniambia kwamba leo anahitaji kuonana nasi mimi na Anna kuna jambo la maana mno anataka kutueleza lakini kabla ya kuonana naye amefariki dunia ghafla.Inauma sana Eli.Ninaumia mno”

“ Pole sana Flaviana” akasema Jaji Elibariki na kuendelea kumbembeleza mkewe.

“ Jambo gani alilotaka kuwaambia?

“ Sifahamu Eli,sijui alitaka kutuambia nini lakini alisisitiza mno.Inaonekana alikuwa na jambo kubwa la kutueleza.” Akasema Flaviana na kuendelea kulia

“ Kifo cha ghafla cha Dr Flora hata mimi kinanipa mashaka mno.Alitaka kuwaeleza nini wanae? Kwa nini afariki ghafla kabla hajakutana na wanae? Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na kifo hiki” akawaza Jaji Elibariki





Mathew na Anitha walirejea nyumbani na kukutana na Noah aliyekuwa amewasili kitambo akiwasubiri.

“ Welcome home Noah” akasema Mathew

“ Nimekwisha karibia kaka.Poleni na kazi”

“ Ahsante sana “ wakajibu Mathew na Anitha

“ Mtanisamehe kwa kuchelewa.Kuna kazi ambayo nimelazimika kuiacha ili kuja kuungana nanyi katika kazi hii.Mmefikia wapi mpaka hivi sasa? Mmekwishaianza kazi? Akauliza Noah

“ Usihofu Noah wala haujachelewa sana.Mpaka sasa hatujapiga hatua kubwa sana lakini kidogo kuna mwanga Fulani ingawa kadiri tunavyozidi kulichimba suala hili tunagundua kwamba suala hili haliko kama tulivyolitazamia.Suala hili ni zaidi ya mauaji ya Edson.Tunatakiwa tuzidi kulichimba zaidi lakini naomba niwaweke wazi ndugu zangu kwamba kadiri tunavyolichimba suala hili ndivyo tutakavyozidi kukutana na mambo mazito na ya hatari.Please guyz, no matter how danger we’ll be facing,don’t ever give up.Lets fight till the end.Sitaki kuwaficha ndugu zangu kazi hii ni ya hatari kuliko zote tulizowahi kuzifanya kwa hiyo naomba kabla hatujaenda mbali sana kila mmoja atafakari na afanye maamuzi .” Akasema Mathew

Dakika moja ikapita ya ukimya,kila mmoja alikuwa akitafakari.Anitha ndiye aliyekuwa wa kwanza kuuvunja ukimya

“ Mathew,wewe umekuwa ni mshirika wangu,tumekuwa kama mapacha,nimefanya nawe kazi nyingi na za hatari lakini mara zote tunapokuwa pamoja hakuna kazi imewahi kutushinda.Nikiwa pamoja nawe,sina wasi wasi hata kidogo na jambo lolote lile.Uliponieleza kwamba kuna kazi ambayo tunatakiwa tuifanye sikujiuliza mara mbili,niliachana na kazi ambayo nilikuwa nimeitwa nikaifanye nchini Brazili ,kazi yenye pesa nyingi sana ,nikaja kuungana nawe.Kwa moyo mmoja natamka kwamba niko tayari kwa lolote.I’m in”

“ Ahsante sana Anitha.Vipi kuhusu wewe Noah? Akauliza Mathew

“ Me also.I’m in” akasema Noah

“ Ok good.We’re team now.Naomba nisiwaogopeshe lakini tambueni tu kwamba tunakwenda kukutana na mambo mazito na tunatakiwa tusimame imara tusitetereke.This is war and we as soldiers we have to fight”

“ Mathew kama tulivyokueleza ni kwamba tuko tayari kwa mapambano.Siku zote hatuogopi kitu .Nielezeni mmefikia wapi mpaka sasa hivi? Akasema Noah

“ Tumeanza kwanza kumchunguza Edson alikuwa ni mtu wa namna gani.Tumegundua kwamba Edson alikuwa na mahusiano na dada mmoja aliyeitwa Brigita ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa siri.Tumeipata laini ya simu ambayo Edson alikuwa akiitumia kuwasiliana na Brigita . Tumegundua kwamba Brigita alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na mzee mmoja aliyeitwa mzee Matiku.Mzee huyu ndiye mmiliki wa hoteli aliyokuwa akifanyia kazi Brigita na ndiye aliyemuwezesha kwa kila kitu.Alimjengea nyumba,akamnunulia gari na kila kitu.Kwa mujibu wa Subira ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana na Brigita alisema kwamba Brigita alikuwa na mpango wa kumtoroka mzee huyo kwani hakuwa na mapenzi naye bali alimpendea pesa zake.Brigita alimweleza Subira kwamba alikuwa akitegemea kupata pesa nyingi kutoka katika biashara aliyoifanya na Edson ambayo hakuwahi kumueleza ni biashara gani ,pesa ambayo ingemuwezesha hata kwenda kuishi nje ya nchi.Hapa ninahisi walikuwa na mategemeo ya kupata pesa nyingi sana kutoka katika hiyo biashara.Subira alitueleza kwamba kuna siku Brigita alikuwa na wasi wasi sana na akamwambia kwamba kuna kitu amekichukua kwa mzee Matiku na ana wasi wasi endapo akigundua anaweza akamletea shida.Hakumueleza Subira ni kitu gani hicho na baada ya siku kadhaa akafariki dunia katika ajali ya moto.Inasemekana kwamba mtungi wa gesi ulilipuka na kusababisha nyumba ya Brigita kuteketea na kuwateketeza watu wote waliokuwamo ndani yake.Hii ilitokea wiki mbili tu baada ya Edson kuuawa.Wiki kadhaa baada ya Brigita kufariki dunia mzee Matiku naye alijiua kwa kujipiga risasi ya kichwa.Hadithi ya Edson,Brigita na Matiku ikaishia hapo kwa sababu hatufahamu ni biashara gani ambayo Edson na Brigita walikuwa wanaifanya na ambayo kupitia kwayo walitegemea kupata pesa nyingi . Hatuelewi pia ni kitu gani ambacho Brigita alikichukua kwa mzee Matiku .Picha tunayoipata hapa ni kwamba kuna kitu kilichokuwa kikiendelea baina ya watu hawa watatu.Watu hawa walikuwa na mahusiano na wote wamekufa tena vifo vya utata na ambavyo havikupishana katika kutokea sana.Alianza Edson akauawa kwa risasi,akaja Brigita akafa kwa moto,na mwisho akamalizia mzee Matiku ambaye alijipiga risasi. Lazima hapa kuna sababu iliyopelekea vifo vya hawa watu watatu.Tunatakiwa tuchunguze sababu hiyo ni ipi.” Akasema Mathew akanyamaza kidogo na kuendelea

“ Huo ulikuwa ni upande mmoja tulioanza kuuchunguza.Upande mwingine ni msichana ambaye aliangushiwa tuhuma za mauaji ya Edson aitwaye Peniela .Huyu alikuwa na mahusiano ya wazi ya kimapenzi na Edson .Pamoja na kila aina ya ushahidi kutolewa mahakamani ukimuhusisha Penny na kumuua mpenzi wake ,bado jaji wa mahakama kuu aliyekuwa akiisikilza kesi ile Jaji Elibariki hakuridhika kwamba Penny alitenda kosa na akaamua kumuachia huru.Baada ya kumuachia huru ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa suala hili ili kuufahamu ukweli.Aliungana na Jason wakili aliyekuwa akimtetea Penny mahakamani na kwa pamoja wakaamua kunipa kazi hiyo mimi kwa kuwa wao hawana taaluma yoyote ya kufanya uchunguzi.Bado sijakutana na Peniela na kuongea naye kwa sababu toka nimeanza kazi hii hajaonekana na hajulikani yuko wapi lakini atakapoonekana ni lazima tutamuhoji na kufahamu vitu kadhaa .Nilipata wazo la kutaka kumchunguza Penny hivyo nikaenda nyumbani kwake nikatega butterfly camera na jioni niliporudi nikaona kitu cha kushangaza kidogo.Watu wawili waliingia ndani mwa Penny na kutega camera katika mlango wa kuingilia sebuleni.Sifahamu ni kwa madhumuni gani walitega kamera ile lakini kwa picha ya haraka haraka ilionyesha wazi kwamba walikuwa wakitaka kufuatilia nyendo za Penny.Iwapo wangekuwa ni watu wenye nia njema basi wasingeingia wakati mwenyewe hayupo. Hiyo ilikuwa ni jana.Leo asubuhi tulipomaliza kuongea na Subira watu wengine wawili walinaswa na kamera yetu wakiingia nyumbani kwa Penny.Hatufahamu walikuwa wakihitaji nini ndani mwa Penny lakini baada ya kutoka tuliwafuatilia wale jamaa wakatufikisha Miseko hospitali.Tuliwafuatilia kila sehemu waliyokwenda na kila walichokuwa wakikifanya na tukagundua kwamba walikwenda kumuona mtu aliyelazwa katika chumba PV 2 – 78 .Anitha aliingia katika mfumo wa kompyuta wa hospitali ile na kugundua kwamba aliyekuwa amelazwa katika chumba kile ni John Mwaulaya Albert.” Mathew akanyamaza akafikiri kidogo na kuendelea

“ Baadae tulimfuatilia pia daktari ambaye alikuwa na wale jamaa ndani ya chumba cha John Mwaulaya ,daktari huyu anaitwa Michael Rodriguerz .Tumegundua kwamba ana mtoto wake mmoja anaitwa Michael Jr anasoma katika shule ya kimataifa ya Tanganyika na kila siku huwa anaongozana na mfanyakazi wake aitwaye Lydie masawe kwenda na kurudi shuleni.Tayari tumekwisha ongea na Lydie na amekubali kufanya kazi yetu kwa malipo ya Tsh million saba.Kesho tutamteka mtoto wa Dr Michael na yeye ndiye atakayetupa taarifa zote kuhusiana na mgonjwa Yule aliyelazwa ndani ya kile chumba.Ninataka tupate uhakika kama kweli mgonjwa huyo ni John Mwaulaya ninayemfahamu.Kama ni mwenyewe,we’ll be dealing with something big…” kengele ya mlangoni ikalia.Akasitisha alichotaka kukisema akainuka na kwenda kuufungua akakutana na mlinzi ambaye alimweleza kwamba kuna mtu getini anaitwa .Mathew akamfuata Jason getini na kumkaribisha ndani

“ Hallow Jason,Karibu sana” Mathew akamkaribisha Jason ndani

“ Ahsante sana Mathew” akajibu Jason kisha wakaelekea ndani

“ Jason kutana na Anitha na Noah wale watu niliowataarifu kwamba nitashirikiana nao katika operesheni hii.” Mathew akafanya utambulisho mfupi.Jason akasalimiana na akina Anitha halafu akaketi

“ Nilimtegemea Jaji Elibariki jioni hii” akasema Mathew

“ Ndiyo.Ni Jaji Elibariki aliyetakiwa kufika hapa jioni hii lakini amepatwa na matatizo kidogo na hivyo kunilazimu mimi kusitisha shughuli zangu na kuja badala yake”

“Amepatwa na matatizo gani? akauliza Mathew

“ Mama mkwe wake amefariki dunia.Mke wa rais Dr Flora amefariki dunia leo alasiri”

“ Mke wa rais amefariki?!..Mathew akashangaa

“ Ndiyo amefariki”

“ Nini kimesababisha kifo chake?

“ Hakuna taarifa rasmi mpaka sasa hivi kwani madaktari wanaendelea na uchunguzi wao kubaini kilichomuua lakini kwa mujibu wa daktari wa familia ya rais anadai kilichomuua ni shinikizo la damu”

“ Dah ! mpe pole sana Jaji Elibariki” akasema Mathew halafu kikapita kimya kifupi

“ Mathew Jaji Elibariki alinielekeza kwamba kuna mzigo unatakiwa”

“ Ndiyo Jason.Tumekwisha ianza rasmi kazi na kuna taarifa Fulani ya muhimu ambayo tunaihitaji.Mtu ambaye atatusaidia ili tuipate taarifa hiyo anahitaji kiasi hicho cha pesa nilichomtaarifu Jaji Elibariki” akasema Mathew.

“ Mmefikia wapi mpaka hivi sasa? Kuna mwangaza wowote? Akauliza Jason

“ Kwa sasa ni mapema mno kusema chochote lakini kazi inakwenda vizuri na baada ya siku kadhaa tutakuwa na cha kusema kuhusiana na uchunguzi wetu lakini kwa sasa hatuwezi sema chochote.Tuachieni kwanza tuendelee kuchunguza.Timu hii unayoiona hapa huwa hishindwi na kitu chochote.Tutalichimba suala hili hadi mzizi wake na mtakipata kile mnachokihitaji” akasema Mathew

“ Ahsante sana Mathew.Basi kama ni hivyo mimi sintakuwa mkaaji sana,nimewapitishia mzigo mliokuwa mkiuhitaji.” Akasema Jason na kufungua begi lake akatoa pesa na kumpatia Mathew

“ Milioni nane hizo.” Akasema

“ Ahsante sana Jason.” Akasema Mathew.Jason ambaye alionekana kuwa na haraka akainuka ishara ya kutaka kuondoka

“ By the way,umepata taarifa zozote za Peniela? Akauliza Mathew

“ Ndiyo.Penny amenipigia simu alasiri ya leo,tayari amekwisha rejea.”

“ Alikwambia alikwenda wapi?

“ Hapana hajanieleza chochote bado”

“ Ok Good.Anafahamu chochote kuhusiana na uchunguzi unaoendelea?

“ Tulimdokeza awali kwamba tunataka kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha Edson lakini kuhusu kuwakabidhi ninyi jukumu hilo bado hana taarifa zozote”

“ That’s great.Msimueleze chochote kwa sasa.Hatakiwi kufahamu chochote kuhusiana na uchunguzi unaoendelea hivi sasa.Tumuache kwanza apumzike ametoka katika matatizo makubwa” Akasema Mathew na kuagana na Jason

“ Kwa nini Jason alichagua kuwa mwanasheria? Akauliza Anitha baada ya Mathew kurudi akitoka kumsindikiza Jason

“ Kwani kuna ubaya gani akiwa mwanasheria? Akauliza Noah

“ He’s too handsome to be a lawyer” akasema Anitha

“ Kijana mzuri kama Yule alitakiwa awe rubani au meneja kama wa benki au kazi yoyote nyingine kubwa kubwa .” akasema Anitha

“ Hiyo ndiyo kazi ambayo yeye anaipenda na kwa taarifa yako Jason ni wakili mahiri sana hapa nchini ambaye hajawahi kushindwa na kesi.Alipenda kuwa wakili na anaifanya kazi yake kwa moyo mmoja” akasema Mathew

“ Pamoja na hayo bado sikubaliani na yeye kufanya kazi hii ya uwakili.Haimfai hata kidogo.Hapendezi kuwa wakili”

“ Kwani mawakili wakoje hadi Jason asipendeze akiwa wakili?

“ They have ugly faces because they are always angry” akasema Anitha na wote mle ndani wakaangua kicheko kikubwa.

“ Ok guyz lets get back to business.Kuna jambo ambalo toka mchana nimekuwa nikimuuliza Mathew na akaniahidi kunieleza tutakapo pata wasaa.Nataka kufahamu John Mwaulaya Albert ni nani? Akauliza Anitha.Mathew hakujibu akaenda katika friji akachukua vipande vya barafu akaweka katika glasi halafu akamimina mvinyo ndani yake akanywa.



********************




ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog