Search This Blog

Saturday 5 November 2022

SAUTI YAKE MASIKIONI MWANGU - 3

 








Simulizi : Sauti Yake Masikioni Mwangu

Sehemu Ya Tatu (3)





Basi alichokifanya ni kwenda kule kule uwanjani akiamini atamkuta Jisu na amrudishie mzigo wake. Lakini mambo yalikuwa tofauti, siku aliyokwenda hakumkuta Jisu ingawa katika angalia angalia yake alimuona Meja; alikumbuka kwamba jamaa huyo na yule muuza bangi walikuwa pamoja.

Akamfuata, akamsalimu.

“Poa dogo. Nambie.” Akajibu Meja.

“Braza kuna Ishu hapa. Tunaweza kusogea kwa pale tuongee?”

“Aina noma.” Meja akainuka. Wakasogea kwa pembeni.

“Enhee, sema dogo.”

“Braza unakumbuka siku zile polisi walivyokuja hapa?” Akauliza Mkuki.

“Lini? Unasemea hii juzi? Maana hapa polisi ni kama nyumbani kwao mdogo wangu.”

“Ndiyo, juzi kulivyokuwa na mechi ya Mafisi na Wakali wa Danta.”

“Ndio. Nakumbuka. Imekuweje?”

“Wakati mnakimbia yule braza mwingine, yule mweusi hivi mwenye ndevu za timbalendi, alidondosha mfuko wake. Mimi niliukota.”

Meja akashituka. “Ule mfuko wa bangi!?” Akauliza.

“Ndiyo.”

“Uko wapi?”

“Nyumbani.”

“Uko vile vile, hujaugusa?”

“Ndiyo.”

“Kudadadeki! Tunaweza kwenda kuuchukua sasa hivi?”

“Sawa tu.”

“Twenzetu. Halafu nitakupeleka kwa mwenyewe. Lazima akutie vitu mdogo wangu, lazima upate ganji. Unajua ule mzigo ndo ulikuwa kila kitu kwa jamaa, biashara yake yote iko pale. Tangu upotee amekuwa mgonjwa, hata hapa graundini hatokei. Twenzetu.” Akaeleza Meja kisha akamchukua Mkuki wakaanza safari.

“Oyaa. Wapi hiyo?” Wenzake wakamauuliza.

“Nakuja wanangu. Dogo anamchongo hapa, ngoja nikausimamie.” Akawajkbu na wakatokomea huko yeye na Mkuki.

Walifika nyumbani kwa kina Mkuki, Meja akasuburi nje, Mkuki akaingia ndani na punde akatoka akiwa na ule mfuko. Meja akauchukua kwanza, akaufungua kuthaminisha kisha aliporidhika wakaondoka.

Safari yao ilifika tamati alipokuwa akiishi Jisu, yeye alikuwa amepanga chumba kimoja maeneo ya huko huko Tandale.

“Hapa ndo gheto kwa jamaa.” Akasema Meja huku akibisha hodi.

“Nani?” Jisu aliuliza kutokea ndani, sauti yake ilisikika ya kama mgonjwa.

“Meja hapa.”

“Poa. Tulia, nakuja.” Akajibu Jisu, kisha sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.

“Vipi?” Akauliza Jisu akiwa amesimama katikati ya mlango wa chumba chake.

“Umemuona huyu dogo? Ni ninja mmoja hatari sana. Tuingie ndani nikupe mchongo mzima.” Akasema Meja.

Basi Jisu akaingia ndani, Meja akaufata kisha Mkuki akawa wa mwisho.

“Rudishia mlango dogo.” Jisu akamwambia Mkuki, naye akafanya hivyo.

“Kaa chini dogo ninja. Hapo.” akasema Meja kumuelekeza Mkuki, naye akafanya hivyo. Akatulia kwenye kiti karibu na alipokuwa ameketi Meja.

Chumba cha Jisu kilikuwa ni gheto kweli kweli, kulikuwamo na kitanda kidogo cha futi tatu kwa sita chenye godoro lililolegea mithili ya ulimi wa mbwa, maboksi makubwa matatu ambayo alikuwa akiyatumia kama kabati kuhifadhia nguo na makorokoro mengine. Kulikuwepo ma meza ndogo pia pamoja na kiti cha kutosha watu watatu ambacho Meja na Mkuki walikalia.

“Sasa Jisu, huyu dogo ana mchongo. Hivi unaitwa nani dogo.” Akaanzisha mazungumzo Meja.

“Mimi? Naitwa Mkuki.”

“Umesikia kwanza hilo jina? Dogo ni mkuki kweli. Anachoma kinomanoma,” akapamba Meja, alikuwa ni mtu wa maneno mengi kweli kweli kwa kipindi kile.

Akaendelea.

“Sasa umeona huu mfuko? Una bangi zako uzoangusha juzi. Kumbe dogo alichumpa, akaziokota, akayoyoma nazo. Kwahiyo leo kaja kukucheki graundini hajakukuta.”

Kitendo cha Meja kueleza kwamba bangi zimeokotwa kilimfanya Jisu ashindwe kujizuia kufurahi, alijikuta akicheka kwa furaha mno kiasi kwamba hata Mkuki akagundua kuwa jamaa huyo alikuwa na meno meusi kutokana na uvutaji wa sigara wa kiasi kikubwa.

“Ziko vizuri?” Akauliza Jisu huku akicheka.

“Yaani kama zilivyokuwa. Dogo kanambia hajazigusa. Au siyo dogo?”

“Ndiyo.”

“Umesikia. Ndo maana namuita huyu dogo Ninja. Dogo mpe mzigo wake.” Akasema Meja, hapo Mkuki akajisogeza kidogo karibu na Jisu, akanyoosha mkono kumkabidhi ule mfuko.

Jisu akaupokea, akaufungua na kutazama; mara akaachia tabasamu zito.

“Dogo we ni Ninja. Nimeamini.” Akasema Jisu na kuongeza na swali. “Unaishi wapi?”

“Bondeni kule.” Akajibu Mkuki.

“Anakaa karibu na kwa kina Supa.” Meja akatoa ufafanuzi zaidi.

“Basi poa mdogo wangu. Kwa hiki ulichokifanya lazima nikutoe. Sema hapa sina kitu. Baadae nitakutafuta basi ili tugawane umaskini.” Akasema Jisu akimaanisha lazima ampe zawadi Mkuki kwa kile alichokifanya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Hivyo ndivyo Mkuki alivyofahamiana na Meja kabla ya kwenda kukutana naye China, na tangu siku ile walikuwa ni maswahiba wakufa na kuzikana. Mkuki akawa ni mmoja wao sasa, akajifunza yote yaliyomfanya afanane na kina Meja. Alianza kunywa pombe, kuvuta sigara na hata bangi pia. Aliongozana nao kila mahali na sasa Meja na Jisu ndiyo ikawa ‘kampani’ yake ingawa walikuwa wamemzidi sana umri.

***********************************

Akiwa bado pale pale kwenge mgahawa Meja alikuja akiwa amebadilisha nguo, amevaa nguo zake binafsi.

“Sasa. Twenzetu.” Akamwambia Mkuki.

“Ushamaliza kazi?”

“Hapana. Nimeomba ruhusa tu. Ningesema nikae hadi muda wa kutoka ungenisubiri sana.” Akafafanua Meja kisha safari ya kuelekea nyumbani kwake ikaanza.

Walikwenda kwa miguu tu, hapakuwa mbali sana kutoka ofisini kwa Meja kiasi kwamba labda wangehitaji usafiri; ilikuwa ni kama mwendo wa nusu saa kwa waendaeo kwa miguu.

Njiani walipiga soga na kuulizana mambo mbalimbali hasa kuhusu jinsi ambavyo walifika China.

“We uliponaje?” Aliuliza Meja.

“Yaani kaka hata sielewi. Nadhani ni Mungu tu ameamua kuniacha hai. Yaani ulivyotokea ule mlipuko sikuelewa kilichoendelea. Nikaja kushtukia naamka kwenye sehemu ambayo hata siiijui, ni Thaiwan huko, kuna mzee aliniokota ufukweni ndo nikaishi kwake muda wote....” akaeleza Mkuki, hapa akisimulia maisha yake yote ya kwa mzee Wong lakini akijitahidi kufupisha baadhi ya mambo.

“Ndo nikadandaia boti, ndo imenileta hapa China.” Akamaliza kusimulia Mkuki. “Wewe ilikuwaje?” Akaamuuliza Meja.

“Mimi ile ngoma ilivyolipuka tu nikaangukia baharini, nikajitahidi kuogelea kama dakika kumi fulani, nikaja kupewa msaada na Wachina fulani hivi walikuwa na boti. Kuja China wakataka kunipelekea ubalozini, nikawapiga chenga, nikaingia zangu mtaani, nikaanzisha harakati zangu, mambo ndo kama hivi unavyoniona.” Akasema Meja.

Pengine stori zao walizielewa wenyewe lakini ukweli ni kwamba Meja na Mkuki walifika hapa walipo leo baada ya kuzamia meli ili wakatafute maisha bora nchi za Ulaya-- kwa kipindi hicho, miaka ya 1990 kurudi nyuma, kuzamia ughabibuni kwa kutumia meli za mizigo ulikuwa ni mchezo kabambe kwa vijana.

Walifanikiwa kukaa kwa siku tatu tu ndani ya meli hiyo iliyokuwa ikieleka nchini Ireland na siku ya nne wakakamatwa na walinzi wa meli. Walinzi wa meli hiyo walikuwa na adhabu moja kubwa kwa ajili ya wazamiaji wanaowakamata. Huwachukua na kuwafungua kwenye msalaba wa chuma walioutengeneza maalum kwa ajili ya kazi hiyo kisha hushindana kuwapiga risasi za kichwa huku wakiwekeana dau; mchezo huu waliuuita “Headshot betting”, yaani ‘kamali ya kulenga kichwa’

Matumaini ya kina Mkuki kuishi Ulaya yalianza kupotea tangu walivyotiwa mbaroni; wote walifahamu huo ndio utakuwa mwisho wa uhai wao, na baada ya kuuliwa watatupwa baharini na kuwa chakula cha samaki.

Basi wakwanza kupandishwa pale msalabani alikuwa ni Jisu, alichukuliwa na askari wawili huku mwenyewe akijitahidi kuwa mpole, alijua kwamba hakukuwa na muawana katika hilo, kifo kilikuwa ni jambo la lazima kwa pale walipofikia.

Wakampandisha, wakamfunga mikono na miguu ili asichimoke, basi akawa ananing’ia pale msalabani kama Yesu wa kwenye filamu.

Askari mmoja akachukua bastola ndogo waliyokuwa wakiitumia, akasogea mbele ya wote, kwenye eneo ambalo mtu anayelenga anatakiwa kusimama. Akanyanyua bastola kumuelekezea Jisu pale juu huku lengo lake likiwa ni kumpiga risasi ya kichwa ili akombe dau waliloliweka askari wote wanaoshiriki mchezo huo.

“Paaa.” Mara Mlio wa risasi ukasikika, hapo Mkuki, Meja na wote walishuhudia damu zikiruka kutoka kichwani mwa Jisu; basi Askari wakaanza kushangilia kana kwamba kile kinachotendeka kilikiwa ni cha kufurahisha mno.

Risasi ile ilimpata Jisu kichwani kama ilivyotakikana, na si kumpata tu bali ilitwaa kabisa uhai wake—Alikufa na kuacha ndoto  zote za kutafuta  maisha ughaibuni zikining’inia pale juu, msalabani.

Mkuki na Meja walizidi kuchanganyikiwa? Walilia kama watoto wadogo huku wakiwasihi na kuwaomba wale askari waachie ingawa hakuna hata mmoja aliyewajali, wote akili zao zikikuwa kwenye pesa za kamali ile ya kishenzi waliyokuwa wakiicheza.

Baada ya mshindi wa kwanza kupata kitita chake cha pesa dau jingine likachangwa, kisha baada ya hapo askari watatu wakaenda kumfungua Jisu pale msalabani na mwili wake ukatupwa baharini papo hapo ili awe chakula cha samaki. Kisha wakaja walipo Mkuki na Meja, na sasa ikawa ni zamu ya Mkuki.

Wakamchukua, wakamvuta kuelekea msalabani. Yeye hakuwa mtulivu kama alivyokuwa Jisu, aliwasumbua kwa kukukuruka huku na huko lakini walimmudu kwa sababu walikuwa ni watu watatu, wakakamavu na walimpiga pia.

Wakamfikisha msalabani akiwa hoi kwa kipigo cha muda mfupi tu. Wakampandisha msalabani na kumning’iniza kama ilivyokuwa kwa Jisu. Alikiona kifo, aliisikia sauti ya umauti, akanusa harufu ya kaburi na mguso wa kunyofolewa roho pia aliupata. Alijuta kufahamiana na kina Meja, alijuta kuwa mmoja wao kwenye safari ya kwenda kutafuta maisha bora ughaibuni. Alijutia kila kitu.

Basi baada ya kutundikwa askari mmoja akachukua ile bastola yao, akasogea pale ambapo anayelenga husimama, akanyanyua bastola yake kumlenga Mkuki; mwenyewe Mkuki alifumba macho ili asione chochote kitakachoendelea, alizungumza na Mungu wake pia na kumuomba msamaha wa kila jambo baya alilowahi kulifanya ili atakapofika huko Akhera apokelewe kwa ukarimu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ghafla mlio wa risasi ulisikika, hata Mkuki mwenyewe aliusikia, akajua kwamba hiyo ni risasi aliyotumiwa kwa ajili ya kutolewa uhai wake. Lakini ajabu ni kwamba zilipita sekunde tano akiwa hai—hapo akagundua kwamba mlengeji alimkosa.

Akafungua macho Mkuki, lakini alichokiona kilimstaajabisha mno. Alimuona yule askari aliyekuwa akimlenga amelala chini akitokwa damu huku ile bastola yake ikiwa pembeni.







Ghafla milio ya risasi nyingi zaidi ikaanza kurindima, hapo sasa wale walinzi walionekana kukimbia huku na huko kama wendawazimu.

Meli ilikuwa imevamiwa na kundi kubwa na maarufu la maharamia watekaji meli ambao walikuwa wakijijta “New generations Pirates” ; yaani “Maharamia wa Kizazi Kipya”. Kundi hilo lilikuwa na Makao Makuu yake nchini Somalia, lilikuwa limesheheni vijana wengi wa kiafrika waliopata mafunzo ya kijeshi na uharamia.

Wenyewe huteka meli kwa oda maalum kutoka mataifa makubwa yenye mvutano hasa wa kibaishara; kwa mfano Taifa la China linaweza kuwatuma wakateke meli ya Marekani lakini haya hufanyika kwa usiri mkubwa, wanaofahamu huwa ni viongozi wa juu wa kundi.

Siku hiyo walipata oda ya utekaji meli hiyo kutoka kwa nchi ya Korea Kaskazini, na lengo kuu ilikuwa ni kutwaa madini ya Uranium ambayo hutumika kutengenezea mabomu ya Nyukilia, na inasemekana kwamba, mzigo huo ulikuwa ni wa taifa la Marekani bali waliwatumia Ireland kama daganganya toto ya mataifa mengine kwa sababu kwa kipindi hiko dunia ndiyo ilikuwa mbioni kuzisimamisha imara juhudi za kupiga vita utengenezaji wa  mabomu ya nyukilia ambapo kimsingi taifa la Marekani  ndiyo lilikuwa kinara la kuhakikisha hilo linafanikiwa.

Basi mapambano yalikuwa ni makubwa mno, meli ikageuka kuwa uwanja wa vita.  Walinzi wa meli walishambuliwa mno, na walishindwa kabisa kuwazuia maharamia hao kwa sababu walikuwa wengi sana. Ilikuwa ni vita ya dakika kumi tu na tayari meli ilikuwa chini ya maharamia hao, na sasa wakawa wanaongoza kuelekea Korea Kaskazini badala Ireland.

Baada ya hali ya utulivu kuchukua nafasi ndipo sasa Mkuki na Meja walipewa msaada na wale maharamia huku wakiamrishwa kuwa miongoni mwao. Ilibidi wakubaliane nao tu kwa sababu walichokuwa wanakihitaji kwa muda ule ilikuwa ni uhai.

*******************************

Taarifa ya kutekwa kwa meli ya Ireland iliifikia serikali ya Marekani. Haraka kilifanyika kikao cha dharura cha viongozi wa juu wa serikali hiyo na wakayajadili madhara makubwa ya endapo madini yale yatawafikiwa mahasimu wao Korea Kaskazini.

Tamati waliamua kwamba ni lazima meli ile isambaratishwe mapema kabla mzigo haujafikishwa Korea na hivyo ndivyo ambavyo ilifanyika.  Serikali ya Marekani, kupitia jeshi lake waliachia kombora la masafa marefu lililokwenda kubutua meli yote hiyo, na kwa kipindi hicho meli ilikuwa karibu kabisa na Thaiwan ambapo Mkuki aliishi na mzee Wong na Mei Lee.

Basi meli yote ilisambaratishwa na bomu lile, mahariamia karibu wote waliuawa na kuishia baharini lakini Mungu aliamua kufanya miujiza yake kwa Mkuki na Meja.

Mkuki yeye alipoteza fahamu mara baada ya bomu kuisambaratisha meli, lakini maji ya bahari yakamchukua hadi kwenye fukwe za Thaiwan ambapo mzee Wong alimuokota na kumsaidia kumpa matibabu.

Meja yeye aliogela kwa muda mefu kidogo hadi alipata msaada kutoka kwa Wachina waliokuwa karibu na meli ile, na hivyo ndivyo walivyookoka.

*************************************

Walifika kwenye jengo alilokuwa akiishi Meja, jengo la ghorofa saba na yeye Meja alikuwa akiishi ghorofa ya nne. Lifti ya jengo hilo ilikuwa imeharibika, hivyo walipanda juu kwa kutumua ngazi tu.

Dakika chache wakafika mbele ya mlango wa nyumba yake, Meja akatoa funguo mfukoni, akafungua mlango wakaingia.

“Karibu.” Akasema Meja kumwambia Mkuki ambaye mara baada ya kuingia alijikuta akishindwa hata kuketi chini kwa kushangaa.

Meja alikuwa akiishi mahala pazuri mno, kiasi kwamba Mkuki aliona kama Mungu alikosea sana kwa kutokumuumba yeye kuwa Meja. Aliingiwa na wivu usioelezeka, alitamani kila kitu kilochokuwa mle ndani hata akajilaumu mwenyewe kwanini alikawia kuja China na kuendelea kuishi kule Thaiwan vijijini.

Nyumba ya Meja ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko na stoo ndogo. Hapo sebuleni palivutia mno, ‘fanicha’ za gharama na za kisasa zilikuwepo, vifaa vya umeme kama vile televisheni kubwa na ya kisasa, redio, kiyoyozi na kadhalika, vyote vilikuwemo hapo. Hakika Mkuki alishindwa kulizuia bumbuwazi lake.

“Keti basi.” Meja akamwambia.

“Dah! Meja hongera sana. Una maisha mazuri mno.”

“Kawaida tu Mkuki. Kaa chini basi.” Akasema Meja.

Mkuki akakaa chini huku bado akiwa katika hali ile ile ya bumbuwazi, wivu na tamaa.

“Nakuletea juisi.” Akauliza Meja.

“Sawa. Sawa tu Meja.” Akasema.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Meja akaenda jikoni, huko ndipo lilipokuwa friji. Punde akarejea akiwa na glasi kubwa yenye juisi, akamkabidhi Mkuki naye akaketi.

“Najua hujala. Lakini inabidi tumsubiri mke wangu aje kukupikia.” Akasema Meja.

Mkuki akatabasamu kidogo.  “Ndo Nilitaka nikuuliize. Ulinambia una mke na mtoto lakini siwaoni.” Akasema.

“Ndo hivyo. Watarudi. Tuna duka la kuuza maua mbele mbele huko. Kwahiyo mke wangu ndo anauza.”

“Duka lenu wenyewe!?”

“Ndiyo.”

Mkuki akaguna huku akitingisha kichwa kama anayejilaumu. “Kaka shikamoo. Nimekukubali. Saluti kwako.”

“Asante.”

“Wanarudi saa ngapi?”

“Jioni. Nadhani baada ya masaaa mawili watakuwa hapa.” Akaeleza Meja.

Baada ya pale stori zikashika hatamu huku Meja akimuhahidi Mkuki kwamba atamtafutia kazi ili naye ajikimu kimaisha na ikiwezekana kuanzisha maisha yake kama yeye.

Saa moja na nusu baadae mke wa Meja alirudi nyumbani. Alifungua mlango bila kubisha hodi, mtoto wao akatangulia kuingia, na alipomuona baba yake tu alimkimbilka na kukumbatia. Akamsalimu kwa Kichina; hiyo ndiyo lugha waliyokuwa wakiitumia katika mazungumzo ya kila siku.

Mke akaingia pia, akasimama mlangoni kwanza akimtazama Mkuki, hakutarajia kukuta mgeni nyumbani.

Alikuwa ni mwanamke wa Kiafrika, mnene mwenye umbo la kibantu, mweusi haswa na mrefu, hakuwa na sura ya kuvutia sana lakini alitazamika na kutambulika kuwa ni mwanamke; yeye alikuwa ni mtu kutoka Ghana, na kwa majina alikuwa akiitwa Onyuletwa Ojuku.

“Karibu.” Akasema Onyuletwa kumwambia Mkuki kwa Kichina.

“Asante.” Akajibu Mkuki.

Yule mwanamke akapita moja kwa moja hadi jikoni, akaweka mzigo aliyokuwa ameibeba kisha akarudi sebuleni, akaketi karibu na mume wake.

“Salama!?” Mume akamuuliza.

“Safi tu.” Mke akajibu.

“Sawa. Sasa tuna mgeni hapa. Huyu bwana anaitwa Mkuki, ni rafiki yangu sana, na ni miongoni mwa wale wenzangu niliokwambia tulikuwa pamoja kwenye meli, kwahiyo tulikuwa tunaishi pamoja Tanzania.”

“Sawa. Karibu shemeji.”

“Asante sana.”

“Mkuki. Huyu ndo mke wangu, ndo sababu ya mimi kuja china, ningebaki Tanzania ningekutana naye wapi?” Akatambukisha kwa mtindo wa masihara Meja na wote wakacheka. Kisha mtoto naye akaambiwa amuite Mkuki Baba mdogo na baada ya hapo Meja akamuomba mke wake apike chakula kitamu kwa ajili ya mgeni.

**********************************

Kitu kimoja kuhusu Mkuki hakikuwekwa wazi kwa mke wa Meja, hawakumueleza kwamba Mkuki hataondoka, ataendelea kukaa nao kwa muda fulani.

Meja alificha suala hilo kwa sababu alijua madhara yake. Yeye na mke walikuwa na makubaliano hawatakuwa na familia ya kuzidi watu watatu, yaani wao pamoja na mtoto wao mmoja.

Ilipofika jioni Onyuletwa alimuita mumewe chumbani na kuhoji kulikoni, mbona mgeni hana dalili za kuondoka.

**********************************

Kitu kimoja kuhusu Mkuki hakikuwekwa wazi kwa mke wa Meja, hawakumueleza kwamba Mkuki hataondoka, ataendelea kukaa nao kwa muda fulani.

Meja alificha suala hilo kwa sababu alijua madhara yake. Yeye na mke walikuwa na makubaliano hawatakuwa na familia ya kuzidi watu watatu, yaani wao pamoja na mtoto wao mmoja.

Ilipofika jioni Onyuletwa alimuita mumewe chumbani na kuhoji kulikoni, mbona mgeni hana dalili za kuondoka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nilisahau tu kukwambia. Mkuki hana sehemu ya kuishi? Kwahiyo tutakaa naye kwa siku kadhaa wakati mimi nikiwa namtafutia kazi, akiwa vizuri ataondoka.” Alimueleza.

“Hapana. Hiyo nimekataa Meja. Hatuna uwezo wa kumudu familia kubwa namna hiyo, na tulishakubaliana.”

“Najua lakini hatuna namna. Kwahiyo inabidi tumsaidie tu.”

“Hatuwezi Meja. Fanya uwezavyo aondoke kesho.”

“Mke wangu hatuwezi kufanya hivyo. Mkuki amenisaidia sana. Pengine bila yeye nisingekuwa saa, aliniokoa kwenye kifo.” Akasema Meja; hapa akimdanganya mke wake ili kumshawishi kumsadia Mkuki.

“Hiyo siyo sababu Meja. Rafiki siyo Mungu hata akuokoe na kifo. Mimi na wewe tukikubaliana kuhusu kubana matumizi ya pesa, sasa leo anakuja mtu tena bila taarifa eti tuishi nae, ina maana tuongeze matumizi?  Hapana Meja. Mwambie tu aende. Hatuwezi kuwa na maendeleo tunayoyatafuta kwa mtindo huo.”

“Nimekwambia ni kwa muda mfupi. Tatizo nini? Kwahiyo unataka nimfukuze rafiki yangu? Ndugu yangu?.”

“Najua unatumia uanaume wako kwenda kinyume na makubaliano lakini ufahamu kwamba hilo halitusaidii Meja, linatudidimiza.”

“Kwahiyo?”

“Anakaa kwa muda gani?”

“Wiki mbili mpaka tatu. Hatozidisha hapo.”

“Sawa. Lakini naomba zisipite, utanichukia Meja.”

“Usijali mke wangu.” Akasema Meja na wakayamaliza namna hiyo yeye na mke na tangu hapo Mkuki akaishi pale rasmi.

*****************************

Wiki moja baadae Mkuki akapata kibarua pale pale alipokuwa akifanya Meja; alikuwa ni mbeba maboksi ya vyakula kama vile samaki kutoka na mazagazaga mengineyo kutoka sokoni.

Mambo yalikwenda vizuri, maendeleo yalionekana, kwani kabla hata hajatia mkokoni mshahara wake wa wiki ya kwanza alikuwa ameshaanza kuonja marupurupu ya kazi hiyo aliyoyapata kwa njia za ujanja ujanja kama vile kuuza baadhi ya vyakula anavyobeba na kadhalika.







Mpango nambari moja ulikuwa ni kupata pesa ya kumuwezesha kuhama pale kwa Meja, akaishi peke yake ili awe huru zaidi kujipangia mambo.

Wiki mbili zilifika akiwa bado kwa Meja, na siku hiyo ya kumi na nne ilikuwa ni siku ambayo iliyafanya maisha yake kuwa na taswira nyingine mpya kabisa tofauti na mipango yake.

Siku hiyo muda wa kumaliza kazi ulifika, alijimwagia maji na kujiandaa kurejea nyumbani. Meja alipumzika siku hiyo, kwahiyo safari ya nyumbani ilimuhusu peke yake tofauti na siku nyingine ambazo huongozana wakati wa kuja na kuondoka.

Lakini kabla hata hajaondoka mfanyakazi mwenzake alimfata na kumpa ujumbe wa kwamba kuna mtu anamuita—mgeni wake.

“Ni nani?”

“Sijui. Yupo nje hapo.”

“Yukoje? Ni mwanamke au mwanaume?”

“Unaonaje ungeenda kumuona ili hayo maswali unayoniuliza yasiwe na umuhimu tena?” Akasema mleta taarifa.

Basi Mkuki akiwa tayari kwa ajili ya kuondoka akaendea mbele kwenye mlango wa wateja kuingia mgahawani. Hakuona mtu hata alipotoka, alitazama huku na huko, na kote kulikiwa kweupe. Akasogea kwa mbele kidogo, eneo lililokuwa na maegesho ya magari kwa ajili ya wateja wa mgahawa lakini pia hakuona mtu.

“Mkuki.” Mara alisikia sauti ya kike ikiita kutoka nyuma yake, sauti anayoifahamu tena si kidogo, sauti anayopenda kusikia, sauti yenye kuyapendeza masikio yake, sauti yenye nguvu ya kuponya, yenye uwezo wa kuligeuza donda kuwa kovu, na kuvo kufutika kabisa,  yenye kujaza kilogramu za furaha ndani ya nafsi, sauti yenye kuubembeleza moyo na kuituliza roho, ikatuliwa mwanana.

Akageuka Mkuki, na hapo macho yake yakatua kwa mwanamke anayenfahamu pia, tena anayemfahu mno, kupita maelezo. Alikuwa amesimama umbali mfupi kutoka pale alipo alipo.

“Mei Lee!?” Mkuki akaita kana mwamba haamini alichokuwa anakiona.

Mei Lee hakudiriki kumjibu, badala yake alijichoropoa mbio kutoka pale alipo kulekea kwa mkuki, alipomfikia akajirusha na kumkumbatia kwa kujing’ang’aniza mno huku akitoa kilio cha kugugumia, kilio cha kike.

Mkuki naye hakutaka kumuachia, alimkumbatia vile vile huku akimbembeleza hadi sasa wakawa ni kama maigizo kwa baadhi ya wateja waliokuwa wakiingia na kutoka mgahawani.

Dada alilia si kisogo, tena kilio kikavu, kilio kitupu, wala hakutoa sauti kuzungumza neno hata moja.

Basi baada ya kumbato refu Mkuki akamtaka Mei Lee watoke eneo lile, akamchukua hadi kwenye mgahawa mdogo uliopo karibu na mgahawa anaofanyia kazi Mkuki, alimpeleka huko kwa ajili kuzungumza. Waliagiza kahawa, kinywaji muhimu na cha gharama nchini China, na baada ya kuhudumiwa uwanja ukawa wao sasa.

Mkuki alikuwa ametingwa na kizungumkuti, hakujua aanze kuuliza swali lipi kati ya, Kwanini uko hapa? Umefikaje hapa? Au umejuaje niko hapa?; yote yalikuwa ni maswali ambayo yangemsaidia kukata kiu yake ya kufahamu kinachodendelea.

Pia, kabla ya kuendelea Mkuki alimuomba Mei Lee aachie wazi uso wake kwa sababu kwa upande wake hakukuwa na umuhimu wa kuufunika kwa nywele namna ile.





“Kwanini uko hapa?” Aliamua kuanza na swali hilo, lakini hakuuliza kwa sauti ya kibabe kana kwamba alikuwa akimlaumu kuwa pale, bali alizungumza naye taratibu na kwa upendo kama afanyavyo siku zote.

Badala ya kujibu Mei Lee alianza kulia kilio kizito cha kugugumia kiasi kwamba Mkuki akapata kibarua cha kumbembeleza; binti aliacha kulia alipoamua mwenyewe dakika chache baadae.

“Niambie Mei Lee. Kwanini uko hapa?” Akauliza tena Mkuki.

“Ulitukimbia?” Akauliza kwa upole Mei Lee badala ya kujibu swali.

“Hapana…” akajibu Mkuki, kisha akafikiria kidogo jinsi ambavyo angeyapanga maneno na kumuelezea Mei kilicchotokea japo kwa ufupi. “Sikuwakimbia, na wala si mpango wangu kuwa hapa China. Yote ni kwa sababu ya matatizo makubwa yaliyonikuta kule kisiwani.” Akaeleza.

“Na Maufeng?” akauliza tena Mei Lee. Mkuki akatulia kidogo, akamtazama usoni Mei Lee, na macho yao yalipogongana mtoto wa kiume akatazama chini kwa unyonge kana kwamba alikuwa na hatia juu ya kile alichoulizwa.

“Sielewe ni nini kimempata, nilishangaa tu niko nyumbani, askari wanakuja, wananikamata, wanasema nimemuua.” Akaelezea Mkuki.

“Hukumuua?”

“Hapana. Siwezi kufaunya hivyo Mei Lee. Maufeng alikuwa ni rafiki yangu muhimu na hata wewe unajua.”

“Sawa. Na ulipanga kurudi lini nyumbani?”

“Mipango ikikaa sawa. Lakini kwa sababu nimekuona tunaweza tukarudi hata sasa hivi” alizungumza Mkuki, ingawa hilo la  kurejea halikuwa likitoka moyoni, alilisema kwa sababu ilipenda kuona Mei Lee akifurahi, na alijua hilo litamfurahisha.

“Turudi? Tutaishi wapi?” akauliza Mei Lee, hapa sauti yake ikisika kama yenye mirindimo ya kilio kwa ndani.

“Nyumbani, kwa mzee Wong, au wewe unatakaje?” akauliza Mkuki huku sasa akimatazama Mei Lee usoni kwa macho makavu. Mei Lee  naye alimtazama bila aibu, ikawa ni macho dhidi ya macho, na ndani ya sekunde chache tu macho ya Mei Lee yakaanza kutiririsha mifereji ya machozi.

“Mei Lee, nyamaza. Mimi si nipo hapa mbele yako, unalia nini sasa?”

“Baba amekufa Mkuki, wamemuua.” Yakamtoka Mei Lee.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Papo hapo Mkuki alibadilika ghafla, aliganda mithili ya mtu aliyetumbukizwa ndani ya jokofu lenye baridi kali sana, hakutaka kukataa kile alichokisikia lakini haikuwa rahisi kukikubali. Ilikuwa ni kama taarifa yenye uchuro, haikumpendeza kabisa.

Mei Lee alilia, ni kama yeye ndiye ambaye alipewa taarifa ile mbaya. Ilibidi Mkuki acheze nafasi yake ya kiume, alinyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kwenda kumbembeleza msichana, yaani ni kama walikuwa kwenye maombolezo.

Mei Lee akatulia kidogo, lakini bado kwikwi za kilio zilisikika. Hali ilipokuwa shwari kwa kiasi fulani Mkuki alimtaka binti amuelezee ilivyokuwa.

“Walikuwa wanakutafuta wewe. Wakamkamata ili awaonyeshe ulipo.”

“Mimi!? Nani aliyekuwa akinitafuta? Kwanini?”

“Familia ya kina Maufeng. Wanasema uliimua ndugu yao, walitaka kukua pia” akaeleza Mei Lee.

Mkuki akahisi ganzi mwili mzima kwa taarifa ile, hakutarajia kutokea jambo la aina hiyo hata kidogo. Alijiona ni mkosefu aliyepitiliza, kumsababishia kifo mtu asiye na hatia ambaye awali alimuonya juu ya safari yake ya kwenda kisiwani Jiaju kutafuta pesa nyingi. Alihisi ametenda dhambi kubwa mno, dhambi isiyostahili toba, dhambi yenye kukumbukwa. Alitamani dunia ifikie mwisho kwa sababu alijihisi ni mwenye gundu lisilotakata hata kwa kuoga makombe, kila alichokigusa kilinuka harufu ya uozo, harufu mbaya mno. Au kama si dunia kufika tamati basi alitamani muda urejee nyuma, ajikute nyumbani kwao Tandale na atafute kibarua kingine cha kufanya na si kujichanganya na kujidanganya kwenda kusaka maisha bora ughaibuni kiasi cha kuwasababishia wengine matatizo makubwa namna hii.

Mzee Wong aliuliwa na ndugu wa Maufeng ambao baada ya mtoto wao kuuwawa kule kisiwani taarifa ziliwafikia kwamba ameuawa na Mkuki, lakini Mkuki huyohuyo alitoroka gerezani na kutokomea kusikojulikana. Hivyo familia ikivamia nyumbani kwa mzee Wong wakimtaka awaonyeshe wapi alipokimbilia Mkuki. Kwa kuwa mzee Wong hakuwa akifahamu lolote kuhusu Mkuki, wale watu walimchukulia kama anaficha hivyo wakamuua yeye na walitaka kumuua na Mei Lee ila yeye alifamikiwa kuwatoroka na kukimbia.

Mei Lee akafanya alichokijua, akapanda boti iendeayo China kutoka Thaiwan na kufika hapo Hong Kong ambapo alikutana Mkuki; haya yote aliyasimulia Mei Lee.

“Umejuaje kama niko hapa?”

“Nilikuwa nakuona hapa kila siku kwa siku tatu sasa.”

“Kwanini huku nishitua.”

“Nilikuwa naogopa.” Akaeleaza Mei Lee.

“Kwahiyo ulikuwa unalala wapi siku zote hizo?”

“Nje.” Akasema Mei

Basi wakaongea mengi hata wakajisahau, giza likaingia na kuwakuta bado wako palepale na hapo sasa mkuki ndipo akakumbuka kama kuna suala la akurudi nyumbani. Akamtaka Mei Lee waondoke, huku akimuomba aendelee kuacha wazi uso wake kama ambavyo alimtaka afanye mara baada ya kukutana.

Waliondoka pamoja hadi nyumbani kwa Meja; alipokuwa akiishi Mkuki. Eneo lilikuwa kimya mno kwa sababu ulikuwa ni muda wa usiku ambao watu wengi walikuwa ndani mwao.

Walipandisha moja kwa moja hadi ghorofani, huku Mkuki alijipanga kweli kweli jinsi ya atakavyomtambulisha Mei Lee na kueleza kwamba itabidi alale naye pale.

Walifika mlangoni, Mkuki akabisha hodi, wakiwa hapo waliona taa zimewashwa ndani, kisha punde kidogo mlango ukafunguliwa, alikuwa ni Meja aliyefungua—akaonana na Mkuki.

“Vipi? Mbona mpaka saa hizi?” Akauliza kwa kiswahili Meja huku sura yake ikionekana yenye chukizo; hakuwa amefurahishwa na jambo lile.

“Kuna ishu ya dharura ilijitokeza.” Akajibu Mkuki; hapo mgeni wake akiwa bado hajaonwa na Meja.

“Poa. Ingia” akasema Meja akitangulia ndani.

Mkuki akamtolea ishara Mei Lee ya kwamba amfuate kisha akaingia ndani; Mei Lee pia akaingia, hapo sasa ndipo Meja alipomuona.

Sura ya Mei Lee iliulipua moyo wa Meja, alishituka sana na laiti kama angemuona bintu huyo bila kuwepo kwa rafiki yake Mkuki basi huenda angetoka mbio huku akipiga mayowe ya uomba msaada wa kwamba amekutana na zimwi lenye kuitisha.



“Nani huyu?” Akauliza Meja kwa Kiswahili.





“Nani huyu?” Akauliza Meja kwa Kiswahili.

Mkuki hakujibu mara moja, alitengeneza kimya cha sekunde tano, “Ni stori ndefu Meja. Nadhani kesho tutaongea vizuri.” Akasema.

Meja akamtazama, taswira ya hasira iliuchafua uso wake lakini hakutaka kuzibadilsiha hasira hizo kuwa maneno; alijua pengine angezungumza maneno mabaya yasiyofaa kumwambia rafiki yake huyo kipenzi.

“Ina maana atalala hapa?” Akauliza Meja.

“Ndiyo. Lakini ni....”

“Basi. Usiendelee. Usiku mwema. Usisahau kuzima taa.” Akasema Meja kisha akaelekea chumbani kwake akimuacha Mkuki na Mei Lee pale sebuleni. Aliondoka kwa hasira mno.

“Twende.” Mkuki akamwambia Mei Lee huku akitangulia kwenye kordo ya vyumba vya kulala, alipofika kwenye swichi akazima taa, halafu akafungua mlango wa chumba chake wakaingia ndani. Akawasha taa ya chumbani.

“Karibu.” Akamwambia mgeni wake huku akimuoneshea ishara ya kwamba aketi kitandani; Mei Lee akafanya hivyo na Mkuki mwenyewe akaketi kitandani pia pembeni kidogo ya pale alipokuwa Mei Lee.

Chumba kikawa kimya kwa zaidi ya sekunde theleathini, hakuna aliyethubutu kumsemesha mwenzake wala kujikohoza, wote walikuwa kama mabubu; kama watu ambao ndiyo mara ya kwanza wanakutana.

“Una usingizi sio?” Mkuki akavunja ukimya kwa swali. Mei Lee akaitikia ndiyo kwa kutingisha kichwa tu.

“Basi utalala hapa.” Akasema Mkuki akimaanisha atala kitandani.

“Na wewe?” Mei Lee akauliza.

Mkuki akamtazama kidogo kabala ya kumjibu. “Popote.”Akasema huku akitabasamu.

“Hapa pia?” Akauliza Mei Lee akimaanisha kwamba na Mkuki pia atalala kitandani.

“Ndiyo.” Akajibu kwa kujiamini Mkuki na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Walilala kitanda kimoja lakini kwa mtindo wa mzungu wa nne. Tena walilala kwa utilivu bila yeyote kati yao kufanya ghadhabu ya aina yoyote kwa mwenzie, walilala kama kaka na dada wa kuzaliwa tumbo moja tu.

*********************************

Asubuhi waliamshwa na hodi za fujo zilizokuwa zikigongwa mlangoni mwa chumba chao, Mkuki akaamka, akatazama nje kupitia dirishani akagundua kumekucha, kisha akateremka kitandani, akaenda mbiombio mlangoni kufungua mlango.

Hapo akamuona mke wa Meja akiwa amefura kweli kweli....

“Yuko wapi huyo malaya wako? Naomba mtoke nyumbani kwangu sasa hivi.” Akabatwa mke wa Meja tena kwa kichina kiasi kwamba hata Mei Lee alisikia na kuelewa.

Mkuki akabaki ameduwaa pale mlangoni asijue cha kufanya, kwamba amjibu au afuate ile amri aliyopewa ya kuondoka.

“Naongea na wewe hunielewi? Nyumbani kwangu sio gesti, hii ni nyumba ya kuishi, ufuska mkafanyie huko mbele.” Akawaka. Alikuwa ni mwanamke kutoka Ghana, na kwa taarifa tu ni kwamba wanawake wengi kutoka Afrika Magharibi ni wazuri kwenye kuchonga mdomo.

Mkuki akaamua kumtolea uvivu.

“Usinipelekeshe. Na nina uwezo wa kutoondoka nikitaka.” Akasema.

“Unasemaje? Hunijui eeh? Ngoja sasa.” akasema yule mwanamke kisha akamsukumia pembeni Mkuki ili aingie ndani kwenda kumtoa kimabavu Mei Lee.

Basi papo hapo Mkuki akashituka, kumbe haikuwa kweli, ilikuwa ni ndoto ambayo pengine ilizaliwa na mawazo yake mwenyewe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mei Lee alikuwa bado amelala, yeye Mkuki akaamka, akasogea dirishani, akakunja pazia na kugundua  kuwa tayari kumekucha. Akiwa bado pale dirishani alisikia hodi, akashituka kidogo kwa sababu kila kitu kilikwenda kama ndotoni.

Hodi ikaendelea.

Mkuki akaenda mlangoni kufungua. Akamuona Meja, ndiye aliyekuwa akibisha hodi.

“Uko poa?” Meja akamuuliza kwa kiswahili.

“Ndiyo. Za kuamka.”

“Safi tu. Shemeji vipi?”

Mkuki akajichekesha kidogo. “Sio shemeji yako bhana.”

“Kumbe?”

“Ni dada yangu tu.”

Meja akacheka. “Una dada mchina? Poa. Njoo tuzungumze.” Akamwambia.

Mkuki akatoka, akafunga mlango akamfuta Meja aliyekuwa anaelekea sebuleni, walipofika wakaketi kwenye viti.

“Nataka tuongee moja kwa moja bila konakona Mkuki. Ni hivi, ulichokifanya jana sijakilewa kabisa.”

“Kipi?”

“Kuhusu mgeni wako. Umerudi usiku halafu na mtu, we unaionaje hiyo braza.”

“Haijatulia.”

“Umeona eeh! Sasa mke wangu bado hajajua kama kuna mgeni, na ameshaenda dukani, kwahiyo jitahidi kutofanya hivi tena.” Alisema Meja. Yeye alifikiria kwamba Mei Lee ni mpenzi wa Mkuki, hivyo atakuwa amekuja tu na asubuhi hiyo ataondoka.

Mkuki aligundua ule mkanganyiko aliousababisha, sasa akawa anapanga jinsi atakavyofikisha taarifa kwa Meja kwamba Mei Lee hana pakulala, hivyo lengo la kuja nae pale ni waishi pamoja.

“Sasa mimi natangulia. Utanikuta kazini.” Akasema Meja, kisha akasimama tayari kwa safari lakini kabla hajapiga hata hatua moja akauliza. “Na ile usoni mwake ni nini? Aliunguaga na moto?”

“Hapana. Ndo aivyozaliwa.” Akajibu Mkuki na kuongeza. “Lakini Meja kuna jambo naomba tuzungumze.”

“Kwahiyo nikae?”

“Ndiyo.”Akasema Mkuki, Meja akakaa palepale alipoinuka.

“Utanisamehe kama nitakukwaza kaka, lakini ukweli ni kwamba nahitaji msaada wako katika hili kama ambavyo umesaidia mahala pa kulala, mahala pakuishi.” Akasema Mkuki na kuendelea. “Unakumbuka nilvyokusimulia kuhusu nilivyosaidiwa na mzee mmoja na binti yake kule Thaiwan?”

“Ndio.” Meja akajibu.

“Basi yule binti ni huyu.”

“Kuna kitu sijaelewa.” Akasema Meja na kuendelea. “Unakumbuka ulichonisimulia kuhusu safari yako kutoka Thaiwan hadi hapa?”

“Ndiyo nakumbuka.”

“Ulinambia umetoroka, na hawajui uko wapi. Sasa amejuaje uko hapa? yaani mmekutana vipi yaani?”

“Iko hivi Meja; baada ya mimi kutoroka huyu msichana na baba yake wakavamiwa na ile familia ya yule jamaa niliyekwenda naye kisiwani.....” akasema Mkuki na hapo akasimulia kila kilichotokea kama ambavyo alisimuliwa na Mei Lee.

“... kwahiyo alitorokea huku. Yaani ni kama Mungu ameamua kutukutanisha tena.” Akamalizia kuelezea Mkuki.

“Naomba niseme kitu nilichokielewa kabla hujamaliza.” Akasema Meja.

“Sawa.”

“Unamaanisha huyu binti pia hana sehemu ya kukaa. Unataka tuishi naye hapa, sio?”

Mkuki akatulia kidogo, jibu la swali lile lilikuwa gumu zaidi ya chuma. “Ndiyo. Lakini ni kwa muda tu. Nikihama nitaondoka naye.”

“Kudadeki! Hiyo haiwezekani broo. Tena naomba usinielewe vibaya, usije ukafikiria kwamba mimi sitaki kukusaidia lakini ukweli ni kwamba msaada unaouhitaji kwa wakati huu ni mgumu sana. Mimi siwezi.”

“Naelewa Meja lakini unajua wewe ndiye ndugu yangu hapa China, sina mwingine wa kunisaidia.”

“Naelewa kila kitu Mkuki, nimeamua tu kukwambia ukweli. Unajua hata wewe kuwa hapa ni kutokana na ubishi wangu tu, mke wangu alikuwa hataki kabisa kwa sababu tulishakubaliana kwamba familia yetu ni mwisho watu watatu tu, mgeni akija siku tatu anaondoka. Maisha ya China ni magumu sana Mkuki, kila kitu kinahitaji pesa. Na si mimi si mke wangu sote tuko ugenini, sote tumekuja kutafuta maisha kisha tutarejea nyumbani, sasa kama tutaishi tukiwasaidia wengine ni lini tutatimiza lengo lililotuleta China. Nielewe. Wewe ni mshikaji wangu, ni mdogo wangu, sitaki kukupangia kuhusu maisha yako, namaanisha sitaki kukushawishi eti labda umtelekeze huyo demu, ila kama unataka kumsaidia tafuta njia nyingine lakini kwa hapa nyumbani hapana.” Akasema Meja.

“Sawa. Nimekuelewa.” Akaitikia kwa unyonge Mkuki.

Basi Meja akasimama, akaongoza hadi mlangoni, akafungua mlango lakini kabla hajatoka akamgekia Mkuki. “Nisamehe dogo kama nitakuwa nimekukosea.” akasema kisha akatoka na kufunga mlango.

Mkuki alibaki ameduwaa asijue la kufanya, hakuwa na pesa ya kusema labda akampangie Mei Lee chumba hotelini na wala hakuwa na ujasiri wa kuweza kumtelekeza msichana huyo. Alihisi yeye ndiyo chanzo cha matatizo yote, hivyo alikuwa na jukumu la kumuangalia Mei Lee kwa jicho la karibu.

Hapo ndipo Mkuki alipotamani ardhi ipasuke, litokezee shimo kubwa mno, atumbukie humo kisha ardhi ijifunge ili watakaobaki watamfute miaka nenda rudi na wasimpate. Alijihisi amebeba mzigo mkubwa sana, yaani kama konokono mwenye gramu 9 aliyetishwa jumba la kobe lenye kilo 12, ni msigo mzito hakika.

Alihisi na kizunguzungu, alihisi kutoelewa na zaidi alijuta kwanini alidiriki kuikimbia ardhi ya nyumbani alipozaliwa mama yake yake  kwa sababu za kipuuzi. Hakika alichanganyikiwa na kuna muda alitamani hata kunywa sumu, afe, akapumzike.

“Uko sawa.” Mara akasikia sauti ya Mei Lee ikimuuliza hivyo kutokea nyuma ya pale alipoketi.

Akageuka, akamuona amesimama.

“Aah! Umeamka?” Akauliza Mkuki badala ya kujibu swali aliloulizwa.

“Ndiyo.”

“Basi jiandae tuondoke.”

“Tunaenda wapi?" Akaukiza Mei Lee. Mkuki akaonekana kutulia kidogo akitafakari jibu la swali lile kwa sababu ukweli ni kwamba hakuwa akijua wapi atakwenda naye baada ya pale.

“Aaah. Jiandae tu twende.” Akajibu kwa kifupi tu Mkuki.

Mei Lee akamtazama kwa sekunde kadhaa na kuna kitu akagundua, akamsogelea na kuketi pembeni yake, akamshika mkono na kuuminyaminya kana kwamba hawakuwa kaka na dada; walikuwa ni wapenzi.

“Wamekataa mimi kuishi hapa?” Akauliza taratibu Mei Lee.

Mkuki akashituka kidogo, hakutarajia swali lile kwa sababu aliamini wakati anazungumza na Meja, Mei Lee alikuwa amelala, lakini pia hata kama alikuwa macho, asingeelewa chochote kwa sababu walizungumza kwa kiswahili.

“Hapana. Hapana. Hawajakataa.” Akasema.

“Najua wamekataa. Sikia. Mimi nitarudi kuishi nilipokuwa naishi awali, wewe endelea kuishi hapa. Sitaki kuwa tatizo katika maisha yako Mkuki.” Akasema Mei Lee. Yalikuwa ni maneno machache lakini makali kama miiba, yakapenya na kuingia ndani mwa Mkuki, yakasambaa kila kwenye mshipa wa damu na kwenye neva zote, yakausugua na moyo wake kama msasa na hapo akashindwa kujizuia kutokwa chozi mtoto wa kiume.

Mei Lee naye alikuwa ni nani hata asiambukizike huzuni ile, naye akaanza kulia pia. Vilio vya kimya kimya vikatawala ndani pale, ni mifereji ya machozi machoni ndiyo iliyozungumza tu—hakika walilia sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sasa Mkuki akaamua kuchukua jukumu la kiume, akaanza kunyamaza, kisha akamsogeza Mei Lee na kumkumbatia, na kumlaza kifuani mwake huku akimpigapiga mgongoni taratibu.

Lakini ghafla mlango ulifunguliwa, akaingia Mke wa Meja na akawakuta Mkuki na Mei Lee katika hali ile ile. Ubongo wake ulipokea alichokiona ndani ya nusu sekunde tu, na papo hapo ukampa jibu kwamba Mkuki aliingiza mwanamke ndani baada ya kuachwa mwenyewe nyumbani.

“Mungu wangu!” Akang'aka, papo hapo Mkuki na Mei Lee wakaachiana na kumtazama.

****************************





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog