Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

AFANDE ANAHUSIKA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : RAMAAH MZAHAM



    *********************************************************************************



    Simulizi : Afande Anahusika

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ni story ya kiupelelezi inayomuhusu Afande Kalindimya ambae anahamishwa

    kutoka mkoa mmoja nje ya Dar na kuletwa Jijini Dar es Salaam.

    Anaingia kwa kasi na kutishia usalama wa wahalifu,

    Kasi yake inawafanya hata majambazi yaanze kugwaya na kuamua sasa kumchafua

    maksudi ili kumuharibia CV yake na kumvunja moyo, ili ikiwezekana aonekane hafai

    na kutolewa pale alipo ama kufukuzwa kabisa.

    Kazi ilikuwa ni ngumu sana, kila tukio lililotokea, Afande Kalindimya alipambana nalo hasa,

    ikafikia hatua kwenye vikao vya Parade, minong’ono ikasikika bila kujulikana ni nani anaesema,

    bali sauti zilisikika zikisema



    ‘AFANDE ANAHUSIKA!’



    Je ni afande yupi anaehusika? Kwanini iwe ni minong’ono?

    Hebu twende pamoja mdau ili kumjua huyo afande anaehusika.



    Sio ajabu kuingia ofisini na kuketi, baada ya sekunde chache simu kuita, lakini aghalabu mno kuingia ofisini na kukuta simu ikiita, hiyo ndio hali iliyomtokea Inspekta Kalindimya wa makao makuu ya Polisi kitengo cha Upelelezi.

    Alifungua mlango na kukutana na simu hiyo iliyokuwa ikiita, ilimshangaza, maana ilionekana kama ni simu ambayo ilikuwa ikisubiria yeye aingie ndani ndio ianze kuita, akaitazama na kujiuliza kulikoni hali ile? Mbona inamtia shaka?

    Moja kwa moja bila kuketi hata kwenye kiti chake, alielekea moja kwa moja kwenye mkono wa simu na kuunyanyua, mezani palikuwa na karatasi nae akatoa kalamu mfukoni, huwa ni kawaida sana simu za pale ofisini kutaka kuandikwa mara kwa mara, ni mara chache sana kukutana na simu ambazo hazina maelezo ama maelekezo.

    Baada ya kuweka sawa karatasi yake, akauweka sikioni bila kuongea chochote kile. Mtu wa upande wa pili alikuwa ni kama anaemuona vile Inspekta Kalindimya, hakumsalimia bali alimpa maelezo tu.

    “Afisa Mpelelezi, nina hakika ninaongea na Inspekta Kalindimya, hivyo basi, nenda mtaa wa Mikumi, eneo la Magomeni, Nyumba namba 14, Block DD, kaokoe maisha ya mrembo aitwae Mwanahamis, anaetarajia kuuawa muda mfupi toka sasa, namaanisha muda huu huu, fanya haraka nenda sasa hivi, ukichelewa kidogo ameuawa binti huyo” aliongea kwa harakaharaka na kukata simu bila hata ya kutoa nafasi kwa Inspector kuhoji.

    Inspector Kalindimya akabaki ameshika mkonga wa simu mkononi pasina kuwa na maamuzi ya haraka, tayari maeneo aliyotajiwa alikuwa ameyaandika kwenye karatasi aliyokuwa nayo, lakini kichwani alikuwa akijiuliza, je ni kweli kuna tukio? Isije kuwa ni katika michezo tu ya raia ambao hutumia vibaya namba za simu za sehemu za usalama ili tu kuwasumbua.

    Lakini kichwani akaamua ni heri tu atoke aende, hata kama amedanganywa huenda kuna chochote kitu ataokota hukohuko kuliko kukaa ofisini kusubiri matukio yamfuate. Akatoka nje hadi kwenye gari yake na kuingia ili kuanza safari ya kuelekea Magomeni Mikumi kwenye nyumba aliyo elekezwa.

    Alikuwa akitokea barabara ya Kawawa, amefika maeneo ya mataa ya Kinondoni Studio, simu yake ya mkononi ikaita, namba iliyotumika ilikuwa ni simu ya mezani, lakini kutokana na utambuzi alionao, aliweza kuijua kuwa ile namba si namba ya ndani ya nyumba, bali ni ya kwenye Call box.

    Roho ikamshituka, akahisi kuna jambo, basi akaipokea na kuichomeka kwenye spika za ndani za gari yake na kuongea na mpigaji hali ya kuwa akiwa na umakini wake barabarani vilevile. Mtu aliepiga simu hii, sauti yake ilifanana sana na mtu aliepiga simu awali, lakini safari hii aliongea kwa utaratibu na kuanza kwa kutupa lawama nyingi kwa Inspector Kalindimya

    “Inspector Kalindimya, kama leo nitaamua kukuburuza mahakamani kwa kosa la uzembe lililosababisha kifo cha raia mwema, mlipa kodi asie na hatia, nitakua nimekosea?” sauti yake ilikuwa ni ya upole sana.

    “Sidhani kuwa wakati huu umepiga simu kuniambia jambo hilo la kunilaumu,”

    “Ok! Wewe ndio utakuwa mshukiwa wa kwanza wa kifo hiki cha Mwanahamisi ambacho kimetokea kwa uzembe wako,” simu ikakatwa tena kama awali bila kuhoji lolote Inspector.

    Inspector alishtuka na kuongeza mwendo wa kasi ya gari lake ili kuwahi kufika eneo lile ambalo ameambiwa kuwa mauaji, hii simu ya pili ikamchanganya zaidi, alitamani kupaa ili awahi kufika eneo husika, lakini ikawa haiwezekani, maana gari si ndege.

    Kilichomsaidia ni kuwa muda ule hakukuwa na Jam kubwa sana barabara ya Kawawa, hivyo aliweza kutembea kwa kasi kubwa zaidi ili aweze kufika haraka eneo hilo aliloambiwa, alipofika Magomeni kanisani, akakata kona kushoto kuingia Morogoro Road, kama anaelekea eneo la Jangwani hadi eneo la Mikumi.

    Kufika kituoni pale ndio akasimamisha gari na kutoa ile karatasi yake ya maelekezo aliyo andika wakati akiongea na mtu aliempa jina la Raia mwema. Aliiangalia na kuiweka kichwani ramani ile kisha akashuka nje na kusogelea nyumba mbili tatu. Namba alizoziona ni zingine, lakini hizo namba ndio zikampa taswira ni wapi ilipo hiyo nyumba anayoitafuta.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutokana na muonekano wa namba za nyumba zile zilivyokuwa, akajua kabisa nyumba anayoitafuta itakuwa upande wa barabara ya Kawawa. Hivyo akarudi na kuingia garini mwake, akaingia tena barabara ya Morogoro na kwenda mbele kugeuza ili kurudi kwenye mataa na hatimae akarudi Kawawa akiwa kama anaelekea mzunguko wa Kigogo.

    Mbele kidogo akakatisha kona na kuendesha gari taratibu huku akisoma namba za nyumba, akaweza kuiona nyumba anayoitafuta, hivyo akaenda mbele zaidi na kupaki mbele kidogo, akashuka na kuangalia usalama wa eneo lile na kulock gari yake.

    Taratibu kwa mwendo wa kiuenyeji, akaeleka kwenye ile nyumba aliyo elekezwa, alipoifikia aliona ni nyumba ambayo inaonekana ipo shwari kabisa, kwani nje palikuwa na kina dada kadhaa wamekaa wakisukana huku wakiongea kwa mabishano.

    Hali ile ikampa matumaini kuwa huenda ndio kile alichokuwa akihofu cha kusumbuliwa na raia ndio kilichomtokea nae kwa sasa, lakini akadhamiria tu kuingia ili aweze kumuona Mwanahamisi na ikiwezekana aongee nae, huenda kuna chochote akaambulia, wazo hili aliliamini zaidi.

    Kwa sura ya tabasamu pana, akawasogelea na kuwasalimia, walikuwa ni waungwana, waliitika na kumkaribisha huku wote wakionesha shauku ya kutaka kujua kilichomfikisha pale, nae kama mtu aliejua vile, hapo sasa ndio akamuulizia Mwanahamis, wakamwambia Mwanahamis ameingia ndani kwake muda uleule, kama vipi aende tu ndani mwake atamkuta.

    Akawauliza ni wapi kilipo chumba chake? Wakamuelekeza, akawashukuru na kuelekea huko kilipo hicho chumba, kwa mwendo wa taratibu na minyato, tena ya hatua ndogo ndogo huku mkono wake ukiwa umeigusa bastola yake aina ya Revolver 12, akausogelea mlango wa Mwanahamis ambao sasa tayari alikuwa ameujua kutokana na maelekezo aliyokuwa amepewa mwanzo hapo nje.

    Mabinti waliobaki nje wakaanza kuongea kwa ishara na sauti ndogo huku wakitabasamu na kugonga mikono yao kama ishara ya kuelewa kitu Fulani hivi, lakini Inspekta yeye hakuwepo kabisa pale, tayari alikuwa ametokomea ndani.

    Bahati mzuri mlango wa chumba cha Mwanahamis ulikuwa nusu wazi, akagonga zaidi ya mara tatu na kuwa ni kimya, akapata hofu kuwa huenda ni kweli kuna tukio limetokea, kwa tahadhari kubwa, akitumia mguu wake wa kushoto huku mkono wa kulia ukiwa umeshika bastola yake, akausukuma taratibu, na kuingia ndani.

    Baada ya kuingia ndani akakutana na maiti ya msichana mrembo kweli akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani, chini kidogo ya titi la kushoto, mahala ulipo moyo, hivyo kifupi alichomwa kisu cha moyo.

    Akairuka maiti ya mrembo huyo na kukikagua chumba vizuri kama kuna chochote, lakini hakuweza kuona kitu chochote ambacho aliona kina athari kwake wala kuona cha kumsaidia, akarudisha bunduki yake sehemu ya nyuma ya kiuno na kuisogelea tena maiti sasa.

    Awamu hii aliisogelea kwa ajili ya uchunguzi wa awali, pasina kuigusa maiti, akaikagua na kuiangalia kwa umakini, kuna kitu aliweza kukiona, kisu kilichochomwa kwenye mwili wa mrembo huyo kilikuwa ni kisu chenye mpini wa Plastic wenye rangi ya Pink.





    “Inspector Kalindimya, kama leo nitaamua kukuburuza mahakamani kwa kosa la uzembe lililosababisha kifo cha raia mwema, mlipa kodi asie na hatia, nitakua nimekosea?” sauti yake ilikuwa ni ya upole sana.



    Sauti ambayo ilimfanya Inspekta Kalindimya aulize kwa sauti ya kawaida sana isio hata na chembe ya hofu;



    “Sidhani kuwa wakati huu umepiga simu kuniambia jambo hilo la kunilaumu,”

    Endelea;



    “Ok! Wewe ndio utakuwa mshukiwa wa kwanza wa kifo hiki cha Mwanahamisi ambacho kimetokea kwa uzembe wako,” simu ikakatwa tena kama awali bila kuhoji lolote Inspector.



    Inspector alishtuka na kuongeza mwendo wa kasi ya gari lake ili kuwahi kufika eneo lile ambalo ameambiwa kuwa mauaji, hii simu ya pili ikamchanganya zaidi, alitamani kupaa ili awahi kufika eneo husika, lakini ikawa haiwezekani, maana gari si ndege.



    Kilichomsaidia ni kuwa muda ule hakukuwa na Jam kubwa sana barabara ya Kawawa, hivyo aliweza kutembea kwa kasi kubwa zaidi ili aweze kufika haraka eneo hilo aliloambiwa, alipofika Magomeni kanisani, akakata kona kushoto kuingia Morogoro Road, kama anaelekea eneo la Jangwani hadi eneo la Mikumi.



    Kufika kituoni pale ndio akasimamisha gari na kutoa ile karatasi yake ya maelekezo aliyo andika wakati akiongea na mtu aliempa jina la Raia mwema.



    Aliiangalia na kuiweka kichwani ramani ile kisha akashuka nje na kusogelea nyumba mbili tatu. Namba alizoziona ni zingine, lakini hizo namba ndio zikampa taswira ni wapi ilipo hiyo nyumba anayoitafuta.



    Kutokana na muonekano wa namba za nyumba zile zilivyokuwa, akajua kabisa nyumba anayoitafuta itakuwa upande wa barabara ya Kawawa.



    Hivyo akarudi na kuingia garini mwake, akaingia tena barabara ya Morogoro na kwenda mbele kugeuza ili kurudi kwenye mataa na hatimae akarudi Kawawa akiwa kama anaelekea mzunguko wa Kigogo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbele kidogo akakatisha kona na kuendesha gari taratibu huku akisoma namba za nyumba, akaweza kuiona nyumba anayoitafuta, hivyo akaenda mbele zaidi na kupaki mbele kidogo, akashuka na kuangalia usalama wa eneo lile na kulock gari yake.



    Taratibu kwa mwendo wa kiuenyeji, akaeleka kwenye ile nyumba aliyo elekezwa, alipoifikia aliona ni nyumba ambayo inaonekana ipo shwari kabisa, kwani nje palikuwa na kina dada kadhaa wamekaa wakisukana huku wakiongea kwa mabishano.



    Hali ile ikampa matumaini kuwa huenda ndio kile alichokuwa akihofu cha kusumbuliwa na raia ndio kilichomtokea nae kwa sasa, lakini akadhamiria tu kuingia ili aweze kumuona Mwanahamisi na ikiwezekana aongee nae, huenda kuna chochote akaambulia, wazo hili aliliamini zaidi.



    Kwa sura ya tabasamu pana, akawasogelea na kuwasalimia, walikuwa ni waungwana, waliitika na kumkaribisha huku wote wakionesha shauku ya kutaka kujua kilichomfikisha pale, nae kama mtu aliejua vile, hapo sasa ndio akamuulizia Mwanahamis, wakamwambia Mwanahamis ameingia ndani kwake muda uleule, kama vipi aende tu ndani mwake atamkuta.



    Akawauliza ni wapi kilipo chumba chake? Wakamuelekeza, akawashukuru na kuelekea huko kilipo hicho chumba, kwa mwendo wa taratibu na minyato, tena ya hatua ndogo ndogo huku mkono wake ukiwa umeigusa bastola yake aina ya Revolver 12, kuhakikisha kama ipo.



    Akausogelea mlango wa Mwanahamis ambao sasa tayari alikuwa ameujua kutokana na maelekezo aliyokuwa amepewa mwanzo hapo nje.



    Mabinti waliobaki nje wakaanza kuongea kwa ishara na sauti ndogo huku wakitabasamu na kugonga mikono yao kama ishara ya kuelewa kitu Fulani hivi, lakini Inspekta yeye hakuwepo kabisa pale, tayari alikuwa ametokomea ndani.



    Bahati mzuri mlango wa chumba cha Mwanahamis ulikuwa nusu wazi, akagonga zaidi ya mara tatu na kuwa ni kimya, akapata hofu kuwa huenda ni kweli kuna tukio limetokea, kwa tahadhari kubwa, akitumia mguu wake wa kushoto huku mkono wa kulia ukiwa umeshika bastola yake, akausukuma taratibu, na kuingia ndani.



    Baada ya kuingia ndani akakutana na maiti ya msichana mrembo kweli akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani, chini kidogo ya titi la kushoto, mahala ulipo moyo, hivyo kifupi alichomwa kisu cha moyo.



    Akairuka maiti ya mrembo huyo na kukikagua chumba vizuri kama kuna chochote, lakini hakuweza kuona kitu chochote ambacho aliona kina athari kwake wala kuona cha kumsaidia, akarudisha bunduki yake sehemu ya nyuma ya kiuno na kuisogelea tena maiti sasa.



    Awamu hii aliisogelea kwa ajili ya uchunguzi wa awali, pasina kuigusa maiti, akaikagua na kuiangalia kwa umakini, kuna kitu aliweza kukiona, kisu kilichochomwa kwenye mwili wa mrembo huyo kilikuwa ni kisu chenye mpini wa Plastic wenye rangi ya Pink.



    Lakini pia kilikuwa kina maandishi kwenye mpini huo, maandishi yalikuwa ni meupe, akainama ili aweze kuyasoma vizuri zaidi, hayakuwa maandishi, bali zilikuwa ni namba, akaziangalia na kuzisoma namba zile kwa sauti 426474 na kusimama akiwa hajielewi.



    Inspector akatoka nje hadi walipo wale wanawake na kuwaomba msamaha huku akiwataka wamfuate ndani haraka iwezekanavyo, wote wakanyanyuka kwa papara na kumfuata alipo, wakamkuta amesimama kwenye uwa wa nyumba ile katikati.



    Kwa mara nyingine akawaomba wamuoneshe kilipo chumba cha Mwanahamis, karibu watu wote walimuonesha chumba kilekile alichoingia yeye, akatikisa kichwa na kuwaambia wote waingie ndani huku yeye akiwa ametangulia kuingia.



    Baada ya kuingia mle ndani, walichokiona… Wanawake wale wakaangusha kilio.





    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Inspector Kalindimya akawanyamazisha na kuwauliza kama wanamjua Yule aliekufa pale, mmoja kati ya wale kinadada akasema huyo ndio Mwanahamis mwenyewe ambae yeye aliowakuta nje na kuwaulizia.



    Akamteua mmoja amuite Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, alifuatwa na kuja pale muda uleule akiwa na shauku ya kutaka kujua wito ule wa ghafla kama ni salama ama lah, japo aliemfuata alionesha kabisa kuwa hakuna kheri huko atokapo!



    Inspector akaji tambulisha kwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa na kwa wale wengine pia ambao walikuwa hawajamtambua japo walikuwa wamehisi tu kuwa huyo ni askari, kisha akamwambia dhumuni la kumuita pale, pia akamueleza ni vipi alipata taarifa ya kifo kile na kisha akaanza kuwahoji wale aliowakuta.



    Mtu wa kwanza kumuhoji ni Mwenyekiti mwenyewe wa Serikali kama anamjua marehemu, Mwenyekiti alikiri na kutoa historia fupi huku akionesha kumsifu marehemu kwa tabia njema, Inspekta aliporidhia akamshukuru.



    Kisha akafuatia Yule ambae yeye alijitambulisha kwamba alikuwa akisukwa na marehemu, alikuwa ni mama wa makamo kiasi, akasema kuwa walikuwa wamekaa akimsuka kama ambavyo yeye aliowakuta wameketi, lakini simu ya Mwanahamis ikaita wakati akiendelea kumsuka.



    Akaongea na kusema ngoja niangalie ndani basi, wote kila mmoja alikuwa na yake, maana story ilikuwa imepamba moto, hakuna alieshughulishwa na simu ya mtu, maada tu ndio ilikuwa na nafasi.



    “Je alimuaga mtu yeyote?” alihoji Inspekta Kalindimya…



    “Kwa kuwa ni mimi ndio aliekuwa akinisuka, kama unavyoona nywele zangu zilipofikia, akaniomba dakika 5 tu aingie ndani na kusema hachelewi,”



    “Ulimuuliza anaenda wapi?” aliuliza afisa mpelelezi.



    “Hapana, si mimi tu, kati yetu hakuna yeyote aliemuuliza wakati huwa si kawaida yetu, hupenda kuulizana kila wakati mwenzetu anapotoka, labda kwa kuwa tulimuona akiingia ndani na tulijua kama anataka kutoka ni lazima yeye mwenyewe tu angetuaga sisi hata kabla hatujamuuliza.” Alijitetea mama huyo aliekuwa akisukwa.

    “We mtu anakusuka, halafu anakuomba muda wako yeye aende sehemu, hukuhofu yeye kuchelewa japo alisema hachelewi?” aliendelea kuhoji afande mpelelezi.



    “Sikuwa na hofu yoyote maana mimi leo Sikuwa na safari yoyote, nipo nyumbani tu na hata yeye niliamini hivyo, kuwa haendi mbali maana alionesha dalili ya kuingia ndani huku,”



    “Ok! Sawa unaweza kuendelea…” huku akiandika Inspector akamruhusu aendelee kuongea.



    “Dakika kama 5 hivi nawe ndio unafika, hapo sasa ndio picha ikaja kuwa ni wewe ndio ulikuwa ukiongea nae kwenye simu, na kama ulikuwa makini uliona ulipofika watu wote wakawa ni wakarimu sana kwako, waliamini wewe una ukaribu na Mwana, Masikini Mwanahamisi wangu,” mtu mzima akaanza kulia tena. Inspector akamtuliza na kumwambia wamalizie kwanza mahojiano.



    “Tulishtuka pale uliporudi mara ya pili na kutuambia tukufuate haraka na tulipofika ukatuuliza tena kilipo chumba cha Mwanahamisi wakati sisi tayari tulikuonesha awali, hapo ndio tukapata shaka sote,” alimaliza mwanamke Yule na kumtazama Inspector kama ana swali lingine kwake.



    Inspector Kalindimya alitulia kidogo na kuwatazama wengine kisha akamrudia tena mama Yule na kumuuliza;



    “Ok! Unataka kuniambia kuwa pale alipokuwa akikusuka Mwanahamis, alinyanyuka kwa ajili ya simu tu? Na si kitu kingine?” lilikua ni swali jepesi kabisa.



    “Ndio Inspector,” nae akalijibu kiwepesi vilevile pasina kujua mpelelezi anawaza nini.



    “Hakuna mtu yeyote aliepita pale wakati nyinyi mkiwa hapo?”

    “Hapana,” hili swali sasa walijibu kwa pamoja, maana alivyouliza alikuwa akiwatazama kwa zamu



    “Je huku ndani hakukuwa na mtu amabe alikuwa yupo huku? Yaani kama si chumba hiki chake, bali chumba kingine ama hapo uwani?”



    “Hapana afande, mara nyingi sana sisi sote huja humu ndani kwa Mwanahamis asubuhi mara tu tuamkapo kwani yeye alikuwa ni mtu wetu sana na hivyo hata leo kabla ya kuwa hapo nje, sote uliotukuta hapo nje, tulikuwa humu ndani,” alijibu dada mwingine swali lile.



    “Ni kipi mlichokuwa mkifanya humu ndani?”

    “Tulikuwa tukisikiliza taarabu na kisha tukanywa chai ndio hapo baadae tukamua tutoke nje afande,”



    “Ni nini kiliwafanya mtoke nje wote kwa pamoja?” aliendelea kuandika maelezo yao.



    “Tulikubaliana tuhamie nje kutokana na joto kuwa limezidi humu ndani kama unavyoona udogo wa nafasi yenyewe hapa chumbani,”



    “Baada ya kuingia huku ndani yeye na kuwaacha nyie nje. Nini kilitokea?”

    “Hakuna chochote kilichoendelea hadi wewe ulipofika pale na kutusalimia na hadi sasa kilichojiri ni hiki…”



    “Sawa, ni nani mmiliki wa nyumba hii?” swali hili lilimlenga Mwenyekiti wa Serikal za mitaa, akasema kuwa mwenye nyumba hayupo Jijini Dar es Salaam, anaishi mkoani Simiyu, ila pale ana mwakilishi wake tu ambae nae ni mpangaji aliedumu zaidi mle ndani.



    “Ni huyu hapa dada, tumezoea kumuita Mamaa Kubwa” huku akimuonesha kwa kidole, afande akamtazama mwanamke huyo bonge la mtu ambae kwa wakati huu alikuwa akilia, huku wakiwa kwa sasa wametoka nje ya chumba na kuiacha maiti ikifunikwa shuka na Mwenyekiti wa Mtaa.



    Afande akamwambia

    “Mamaa Kubwa, Naomba nikutambue kama mama mwenye nyumba, kwani hatuwezi kumuhusisha mwenye nyumba moja kwa moja kwa sasa, kwani bado ni mapema sana, nadhani umenielewa?” Alimuuliza huku akimtazama, nae akatikisa kichwa kukubali na Inspekta akamsemesha tena



    “Kuna maswali kadhaa nitalazimika kupata majibu toka kwako, hivyo futa machozi na unipe ushirikiano wa kutosha ili tuweze kumjua muuaji wa shoga yako na kumtia nguvuni haraka iwezekanavyo,”



    Akaitikia huku akijifuta machozi kwa kanga yake na kumtazama afande ambae bado kalamu ilikuwa mkononi mwake.



    “Kuna mlango tofauti na huu ambao mimi nilipita wakati nikiingia humu ndani?”

    “Hakuna baba yangu, huku uwani njia tofauti na ile uliyopita wewe, haipo nyingine zaidi ya haya mabanda yaliyozunguka ambayo ni ya wapangaji wengine,”



    “Hebu naomba tusogee na unioneshe,” wakasogea kule yalipo mabanda ambayo yamepangwa vema kama ni chumba na sebule kila banda moja.



    Yalikuwa mawili na kila moja likiwa limejitosheleza kila kitu wakati lile la MwanaHamis likiwa ndio dogo, kwani lenyewe lilikuwa ni la chumba kimoja tu bila chochote, halikuwa na sebule, bafu wala jiko.







    “Umeniambia mabanda haya ni ya wapangaji wengine, wapo wapi hao wapangaji wako?” hapa alihoji lakini hakuwa akiandika.



    “Hili banda la kwanza ambalo ni chumba na sebule, kwa sasa hakina mtu, mwenyewe alihama tangu wiki iliyopita na hadi sasa bado dalali hajatuletea aina ya mtu tunaemtaka,” alimaliza kuongea huku akigeuka upande mwingine palipo na banda jingine.



    “Banda hilo linamilikiwa na mwanadada mmoja ambae ni mwandishi wa habari za uchunguzi, kwa sasa anatakriban mwezi mmoja na nusu hajaonekana hapa akiwa amehamishiwa nje ya Dar kikazi,”



    Maelezo ya Mamaa Kubwa yalijitosheleza na kumfanya Inspector amgeukie Mwenyekiti aliekuwa amesimama kushoto kwake na kusemahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Mwenyekiti na mama hapo, naomba tuzunguke kukagua mandhari ya nyumba,” huku akichora vitu Fulani kama ramani hivi kwenye daftari lake dogo la mkononi, wakaanza kuzunguka huku na kule. Waliizunguka nyumba nzima.



    Baada ya kumaliza kuizunguka nyumba Inspector akatoa simu na kuwasiliana na wenzake waliopo kituoni ili kupata msaada wa usafiri kwa ajili ya kuiondoa maiti pale nyumbani ili kuipeleka hospitali kwa ajili ya maandalizi zaidi ya kiuchunguzi.



    Alirudi chumbani na kukagua kila sehemu ajue ni wapi ambapo huenda muuaji alipitia, maana akili yake ilimgomea kabisa kusema kuwa Mwanahamisi amejiua



    “Angejiua asinge andika namba hizi, bila shaka ameuawa, ndio maana hata simu nikapigiwa, lakini je muuaji amepita wapi hadi kumuua huyu mtu?”



    Chumba kizima alikikagua, aliangalia dari wala halijatobolewa, akatoka nje na kuangalia juu ya bati, lakini pia hali ilikuwa ni shwari tu.



    Kila eneo alilofikiria yeye alilikuta likiwa ni salama kabisa, alishindwa kabisa kung’amua ni wapi mtu huyu alipitia iwapo hakupita kwenye mlango ule? Na baada ya yale mauaji ni wapi muuaji amepita kutoka nje?



    “Ama yawezekana akawa bado yupo humu ndani? Lakini mbona amenipigia simu na kunipa maelezo haya? Ni nani alienipigia simu? Ina maana ndio muuaji? Aliumiza sana kichwa Inspector Kalindimya na hakufanikiwa kupata jibu hadi gari ya Polisi kutoka kituo cha Oysteybay ikawa imewasili ikiwa na askari kadhaa walio kikazi zaidi.



    Walipowasili walianza ukaguzi wa awali wa marehemu huku Inspector akiamuru simu ya marehemu itafutwe na apewe pindi ikionekana, lakini jitihada zote zilishindikana, ilionekana kama simu ile imechukuliwa, maana mle ndani haikuonekana.



    Maiti ilichukuliwa na askari kwa ajili ya kuipeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi juu ya chanzo cha kifo kile, huku ikiacha simanzi kwa majirani ambao tayari walianza kumiminika pale ndani.



    Inspector akiwa bado hajaridhika kabisa na kile alichokiona kwenye nyumba ile, akamoumba namba ya simu Mwenyekiti na kisha akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa taratibu huku akifikiria ni kwanini mpigaji wa simu alimwambia kuwa anahusika na kifo kile



    “Na ukizingatia kuwa baada tu ya mauaji mimi nimekuwa ni mtu wa kwanza kuingia mle chumbani sehemu ambapo maiti nimeikuta, ama muuaji ana mpango wa kuniuzia kesi? Halafu kwanini alinijulisha mapema kabla ya tukio na kisha akapiga tena kunilaumu baada tu ya tukio ? Kuna nini hapa kati?”



    Alikosa majibu na kuichukua tena karatasi ya ramani aliyochora na kuitazama upya akiwa kwenye mwendo wa taratibu.



    Bado hakuweza kugundua ni wapi huyo mtu anaweza kuwa alipita, ndani ya nafsi yake aliweza kusikitika mno na kuikunja karatasi yake ya ramani akiwa anakaribia kituo cha Polisi. Aliingia ndani ofisini mwake na kujipweteka juu ya kiti chake kiuvivu kabisa, hakuwa sawa tena.



    Akilini alipanga kurudi tena huko ili kujiridisha pindi atakapo maliza shughuli zingine za pale ofisini. Lakini akiwa anaiweka ramani ile ndani ya file alilofungua juu ya kesi ile ya mauaji, kuna msukumo Fulani ukamvaa, kuna kitu alikihisi.



    Alijiuliza, akabidhi lile jalada kwa mkuu wa upelelezi wa mkoa ili lipangiwe mpelelezi kwanza au aende sehemu ile ambayo kuna wazo jipya amelipata? Akaona ni heri tu aende huko kwanza ili akikabidhi jalada liwe na mwanzo mzuri kwa yeyote atakae kabidhiwa.



    Moja kwa moja hadi garini nje ya ofisi na kuelekea kulekule alipotoka, yaani nyumbani kwa Marehemu MwanaHamisi, safari hii hakuteremka kabisa wala hakusimama, bali alipita tu kama mpita njia na kuzunguka eneo lile.



    Akiwa analiangalia kwa umakini mkubwa hasa alipofika upande wa pili wa jengo lile alilokuwa akiishi MwanaHamis, kwa usawa uleule wa ile nyumba palikuwa na jingo la ghorofa kadhaa.



    Alipaki pembeni na kutoa simu yake kisha akampigia simu mwenyekiti wa Mtaa na kumtaka afike pale alipo yeye, akamuelekeza na kumwambia afanye haraka ili waweze kufanya kile kilichosababisha amuite.



    Mwenyekiti alifika nae alishuka na kuelekea kwenye jumba hilo hadi ndani, alijitambulisha na kutoa kitambulisho chake, baada ya kujitambulisha akawaambia anataka kwenda usawa wa vyumba ambavyo madirisha yake yanatizama upande wa pili wa barabara ile.



    Ilikuwa ni nyumba inayo milikiwa na Watanzania wenye asili ya Kiasia, walitoa ushirikiano wa kutosha, wakamuonesha kila sehemu ambayo alihitaji. Huku akichora ramani husika akaendelea tu kutazama usawa wa nyumba aliyoishi marehemu.









    Hakuna ambacho aliweza kukigundua, kutokana na mandhari ya jingo lile isingewezeana kwa mtu kutoka Ghorofani na kwenda upande wa pili, maana ilikuwa imezibwa kabisa, sehemu zilizokuwa zimeachwa wazi zisingeweza kufanya mtu apitishe angalau mguu tu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado akili yake haikuweza kutambua ni vipi muuaji aliingia chumbani kwa Mwana, akashuka toka kwenye ghorofa ile na kuzama garini kwake kisha akaondoka kimyakimya akiwa na mawazo kedekede.



    Hivyo ndivyo alivyoimaliza siku ile ya kwanza…

    **********



    Siku ya pili ilikuwa ni siku ya mazishi ya MwanaHamis baada ya shughuli zote za uchunguzi wa mwili wa marehemu kukamilika, mazishi yakiwa yamepangwa kufanyika saa saba adhuhuri kwenye makaburi ya Mwananyamala hapo hapo Jijini Dar es Salaam.



    Watu walifika kwa wingi hasa mara tu maiti iliporudishwa kutoka hospitali kwenye uchunguzi, Mwana alikuwa ni mtu wa watu hasa, hivyo hata habari ya kifo chake ili washtua wengi ambao bado walikuwa hawajaamini.



    Wengi walifika pale wakidhani kuwa wanaweza kujua ni vipi Mwana aliuawa, nani alimuua na kwa njia gani kilitokea kifo hicho bila kujua kwamba hilo tukio huchukua muda mrefu sana hadi kumpata muuaji huku uchunguzi ukigharimu muda, pesa na hata maisha ya wengine.



    Inspector Kalindimya alikuwepo pale msibani sambamba na maaskari wenzie kadhaa waliokuwa pale kufuatilia kama kuna lllote ambalo wanaweza kulipata likawasaidia kwenye uchunguzi wao.



    Pembeni ya Inspekta Kalindimya, alikuwepo Inspekta Jitu, moja kati ya wasaidizi wakubwa wa mpelelzi aliekuwepo pale na kuhamishwa ili kupisha ujio wa Inspekta Kalindimya.



    Walikuwa makini sana kufuatilia kila hatua iliyokuwa ikiendelea wakiwa na umakini mkubwa na wa hali ya juu, hawakupenda hata tukio dogo liwapite pale walipo, hivyo waligawana maeneo ya kufuatilia wakati taratibu za mazishi zikiendelea.



    Mazishi ya waislamu, kwa kiasi kikubwa huwa ni tofauti na mazishi ya kikristo, maana waislam wanawake wao hawachanganyiki na wanaume japo msibani, na hata hapo ilikuwa hivyo, upande wa wanaume walikuwepo askari wawili wengine tofauti na Mainspekta hao.



    Mmoja kati ya askari wale alikuwa akifuatilia tu kujua kama kuna mtu anawafuatilia wale mainspekta na hususan Inspekta Kalindimya. Wakati huyo askari mwingine nae alikuwa na kazi yake maalum aliyokuwa amepangiwa.



    Kwa upande wa wanawake kule, Inspekta Kalindimya alikuwa amemuweka askari mmoja ndani kabisa ya chumba cha ndugu wa marehemu kufuatilia ili kujua ukaribu wa watu watakaokuja na huenda wakapata dodoso, alimtaarifu iwapo atamuwekea shaka mtu yeyote, basi asisite kumjulisha kwa njia yeyote.



    Makubaliano yale yalimpa imani kubwa mno Inspekta akiamini kuwa amejipanga barabara, leo alijua kama itatokea kufuatiliwa ama kufuatilia juu ya mazishi ya Mewanahamis, basi huyo mfuatiliaji hatochomoka.



    Saa 7 kasoro, kama kawaida waliwasili masheikh kwa ajili ya kuendesha ibada malum ya mazishi, wakati wao wakiendelea kusoma hitma ile, Inspekta akasikia simu yake ikiita. Ilimshitua sana, hakutegemea kabisa simu yake kuita muda ule japo haikuwa na mipaka ya kuita.



    Alichokifanya ni kuitoa na kuangalia ni nani aliempigia, akaona kuna namba ya mezani, ikiwa ni ngeni kwake kabisa. Kabla ya kupokea alihisi kitu, akatazama kila upande, akianza mbele yake na kugeuka hadi nyuma akitazama kwa tahadhari kubwa na jicho pembe. bila kujua ani nini anaangalia pande hizo.



    Pale mtu yeyote angemuuliza unaangalia nini hakika angesema hajui ni kipi anacho tazama. Alitaka kupokea,lakini akaona hatokuwa sahihi kupokea eneo lile ambalo bado kunaawatu wanafanya ibada ya kumsomea marehemu, kwa kulinda heshima, akanyanyuka na kusogea pembeni.



    Hata Yule askari aliempanga kumfuatilia kwa ukaribu alimuona kwa mbali sana akiwa kama mtu ambae hana habari hata kidogo, kumbe nae alikuwa makini kuliko alivyojua yeye, lakini hakujali.



    Akapokea sasa kwa sauti ya taratibu, maana tayari alihisi kitu, alikuwa ameshisi ni mtu yuleyule aliekuwa akimpigia awali, ndio huyo amepiga tena… na kweli hicho ndicho kilichotokea, sauti ilkuwa ni ileile, sasa ilikuwa ikimpa pole ya kushughulishwa na msiba wa Mwana.



    Hakujibu lolote Inspekta, alikuwa yupo kimya tu hadi sauti ile ya kiume nzito safari hii tofauti na awamu zilizopita, ikamwambia



    “Inspekta baada ya kukupa pole napenda kukwambia nakuonea huruma sana, maana nahisi utakuwa kwenye wakati mgumu mno kwa sasa,” ilisema sauti ile kwa kejeli, nae Inspekta akaijibu kwa dharau



    “Sema shida yako, nitakata simu,” alisema kutishia tu, kwani nae alitamani mno kujua ni kipi kipya jamaa amekuja nacho.



    “Ha ha haa! Unaonekana dogo una jeuri sana, lakini usiogope mimi nitakufundisha kazi…”



    “Sawa, lakini tambua mimi kazi niliisha fundishwa huko CCP Moshi, na ndio maana sasa unaniona nipo kwenye ajira katika kupambana na wapumbavu na wajinga wajinga kama wewe.



    Sasa kama huna cha kusema, ni heri ukampigia simu mkeo na kumtongoza upya, sawa?” aliongea maneno makali katika hali ya kawaida tu ili kumtia jazba Yule mtu aseme shida yake, maana moja kati ya masomo aliyopitia akiwa Chuo Cha Polisi Moshi.





    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Moja ya mbinu ya kumlazimisha mtu kusema jambo, walifundishwa ni kumtia mtu jazba wakati ambao anatoka kwenye hali ya kawaida, basi ni lazima ataropoka tu chochote lakini ni cha kweli.



    Hiyo ndio iliyotokea, alipomwambia vile, jamaa akamwambia



    “Inspekta tambua mara zote ninapokupigia simu mimi ujue nina habari njema kwangu na mbaya kwako,” akanyamaza kidogo kisha akaendelea



    “…Inspekta hili ni game, kila siku kwenye game lazima mmoja ashinde, mimi daima huwa ni mshindi kwa sababu ndio ninae andaa hii game, ingekuwa ni bao, ningesema najua wapi pa kukufungia,



    Lakini hii ni ‘Game of death’ huu ni mchezo wa kifo, kumbuka kuwa ni mimi ndio nimeuandaa, sasa basi wewe kwa kuwa umekuja kasi, nataka nikupumzishe kidogo nje ya ofisi ya Serikali, iwapo hutakubali kuachana na kesi hii.



    Si umesikia Askari mwenzako mmoja aliuawa siku chache zilizopita? Basi ni kwa kimbelembele chake, achana kabisa na kazi hii, namaanisha kazi ya Upelelezi, we upo vizuri kwenye biashara, rudi uraiani acha watu wafanye kazi zao, sawa Inspekta?”



    “Ha ha haa! Nilijua naongea na mwanaume mwenzangu, kumbe naongea na kibinti Fulani hivi kijoga joga? Sawa mrembo, nimekuelewa, nitafikiria ombi lako, maana sisi jeshini tumepewa option ambazo siwezi kumuambia mwanamke ambae sina hakika ya kuwa nae kwa muda Fulani…”



    Maneno ya shombo aliyoyatoa Inspekta alijua dhahiri yatamkera mtu wa upande wa pili, lakini wala haikuwa hivyo, bali jamaa akajibu kwa kujiamini kabisa



    “Hilo unaloiga wewe ndio lilipelekea kifo cha kizembe kabisa cha Inspekta mwenzio, nawe unapita mulemule, sasa Napata picha ya kweli kwamba nyote mmefundishwa mbinu ileile, sasa ole wako…” Inspekta akamkatisha



    “Ndio hapo utakubali kuwa Serikali ni hatari, tambua kila kitu kuhusu wewe kipo mikononi mwangu sasa, na muda si mrefu nitakutia nguvuni,” aliongea kumtia hofu, na kwa sasa alifanikiwa, kwani jamaa akasema kwa kujitetea kwa haraka



    “Unajidanganya Inspekta, na ili kukuonesha kuwa mimi nipo vizuri zaidi kuliko wewe, muda huu kuna tukio nafanya, na baada ya hao watu kunywa chai ambayo nimeigharamia mimi, yaani wakati jeneza la Marehemuu Mwana likitoka, andaa tena mazishi ya Mwana,”



    “We ni mwendawazimu, naona hofu ya kutiwa mikononi tayari imeisha kuvaa,”



    “Nisikilize Inspekta Kalindimya, mimi huwa sina utani kwenye kazi ninazopanga kufanya, hivi sasa ni saa saba na dakika moja, pishana na hilo jeneza la Mwana, si unaliona linatoka?” aliuliza mtu wa upande wa pili, kisha akaendelea



    “Wakati lenyewe likitolewa nje, wewe nenda chumbani kwa Mwana, huko ndio kuna kila kitu, kwa heri, msalimie afande Jitu, naona anajiuliza tu unaongea na nani muda wote huu, ha ha haa!” alicheka kwa sauti iliokuwa kubwa na kumghasi hata Inspekta Kalindimya.



    Kabla hajaongea lolote, Simu ikakatwa na kuanza kuwatazama watu waliopo pale kwa umakini wa hali ya juu mno, alikuwa akiangalia kama kuna mtu yeyote anaemtazama, lakini aliona kila mtu akiwa busy na kilichompeleka pale.



    Sasa kweli tayari jeneza lilikuwa linaonekana kutolewa kupitia mlango mkubwa wa nje kutoka ndani, akaamua kuliwekea maanani lile lililosemwa na mpiga simu, akamtaka Inspekta Jitu amsubiri garini ili yeye aende ndani mara moja.



    Kichwani alijipa moyo kuwa huenda huyo aliepiga simu ni mtu wa karibu na familia ya Marehemu, na yawezekana aliona maiti imeachwa nje ya jeneza na kuogopa kusema mbele yao, sasa amemtumia yeye kama mjumbe ili salamu zifike.



    Kwanza akasogea hadi lilipo jeneza la Marehemu na kulikagua kwa macho, je maiti ipo mle ama lah! Alipoona maiti ipo kutokana na mfungo wa mkeka kama wanavyofanya waislamu, mfungo wa pipi.



    Akasogea pembeni na kumuita mmoja wa wana ndugu aliekuwa yupo karibu sana na kumuomba amuhakikishie.



    Kwanza alijitambulisha yeye ni nani na kumba wasogee pembeni na kisha akamueleza juu ya jambo hilo, jamaa baada ya kuridhishwa na utambulisho huo, ndio nae akasema kwamba ana hakika maiti ipo ndani ya jeneza, kwani hata nae ameshiriki kuiweka mle ndani ya jeneza.



    Akamshukuru na kuachana nae.



    Moja kwa moja akaelekea ndani hadi chumbani kwa marehemu Mwana, hapo akiwa na simu mkononi akiandika sms kumuuliza askari wa kike aliepo ndani vipi mazingira ya mle ndani yalivyo? Aliandika sms fupi tu lakini wenyewe walielewana.



    Akarudisha simu mfukoni huku akiwaomba kina mama njia ya kupita, maana walikuwa ni wengi sana hadi kiasi ambacho aliamini hata sasa mpiga simu anamsumbua tu juu ya kumwambia aende huko chumbani kwa marehemu.



    Alifika hadi kwenye mlango wa chumba cha marehemu na kukuta umefungwa, lakini haukufungwa na kitasa, bali ilikuwa umeshindikwa tu. Akanyonga kitasa na kuingia ndani tena kwa tahadhari. Alichokiona ndani alishtuka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Alisimama na kuangalia kwa mshangao mkuu huku akionesha kabisa kushtushwa na tukio hilo.



    Alikuwa na haki ya kushtuka, maana aliona maiti ya msichana mrembo kweli kweli ikiwa juu ya sofa ya watu wawili, ambao kwa mtizamo wa haraka haraka ilionekana kabisa maiti ile haina muda mrefu tangu kutokea kwa kifo kile.













    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog