Search This Blog

Friday 28 October 2022

KISASI - 2

 









    Simulizi : Kisasi

    Sehemu Ya Pili (2)







    ***PAMELA***



    “Hapana Nancy hawezi kufanya hivyo, hana sababu ya kufanya hivyo” nilitokwa na machozi kila nilipokuwa nikimtetea, nilimpenda sana Nancy japo nilimpenda sana Patrick kuliko mtu yeyote.

    “Nancy ni nani” aliuliza Patrick huku akinitazama kwa jicho kali, sikuwa na la kumjibu kwakuwa ilitakiwa nitumie mda mrefu kumuelezea kuhusu Nancy ili anielewa na awe tayari kuyapokea yale nitakayomwambia.

    “Nancy ndiye aliyetenda hili na si mtu mwingine Pamela” alidakia Felly kabla sijamjibu Patrick swali lake, nilikuwa nikimtazama Felly na hapo alifungua tena ile laptop yake na kuendelea kuelezea;

    “Nilikuambia mapema kuwa kama mpigaji alikuwa ni mtu mwenye uzoefu wa kushika bastola basi asingiweza kumkosa Patrick kwa ile kona aliyokaa (huku akielekeza kwenye projekta), na kama angemkosa au kucheza mkono kidogo basi ingemchubua mkono wake wa kushoto, lakini haikuwa hivyo badala yake ilipita futi 6 toka alipokuwa Patrick, kwa maneno mengine mtu huyo mkono wake ulicheza kutokana na ule mtikisiko wa risasi ilipokuwa inatoka. Sasa kama ulicheza na kama alikuwa sio mzoefu basi inamaana mkono ulishtuka, na kama ulishtuka basi ni wazi kuwa lazima atakuwa ameufunga mkono kwa sasa” alivuta pumzi na kufungua tena sehemu nyingine kisha aliendelea.

    “hii hapa ni picha iliyopatikana kwenye kamera za zahanati ya Hilton, mita mia saba hamsini kutoka hapa, ilikuwa ni picha iliyonaswa lisaa limoja baada ya tukiohilo kutokea, itazame kwa makini huyu ni Nancy, alikwenda siku hiyo akiwa ameushikilia mkono, na alifungwa bandeji mkononi, sasa ukiangalia alifungwa mkono wa kushoto hii inamaana kuwa Nancy anatumia mkono wa kushoto, baada ya mimi kufatilia juu ya faili la Nancy katika zahanati hiyo nilikuta limeandikwa kuwa alianguka kwenye ngazi. Kwenye siku ya tukio Nancy hakwenda kazini, alikuwa nyumbani siku nzima kwakuwa siku hiyo haikuwa siku ya kazi, hii inamaana kuwa kama Nancy alikuwa hayupo kazini basi angekuwa ameanguka kwenye ngazi za nyumbani kwake, lakini pia nyumbani kwake yeye hakuna ngazi fupi wala ndefu hivyo ni ngumu sana kwa yeye kuwa ameanguka kwenye ngazi” aliongea Felicity na mimi nilikosa namna ya kumtetea tena Nancy, ilikuwa wazi kuwa yeye ndiye aliyehusika.

    “Kwahiyo unataka tuliweke vipi hili jambo, uchunguzi wote nimeufanya kwa siri bila kushirikisha ofisi hivyo nasubiri uniambie nini cha kufanya” Felicity aliniweka katika wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi.

    “Naomba tuongee nje Felly” nilijivuta pale na kufungwa taulo langu vizuri kisha nilitoka nje na Felly nae alitoka.

    “Tushughulike na hili swala nje ya ofisi yako, unajua dhahiri kujaribu kuua ni kosa kubwa sana, nipe muda niongee na Nancy juu ya hili, sitakuwa tayari kumuona Nancy akienda jela Felly” niliongea na Felly huku machozi yakinitoka. Nilifahamu kuwa nilimuumiza sana Nancy kwa kumwambia kuwa nisingeweza tena kuwa na yeye kwakuwa nilimpenda sana Patrick, mimi na Nancy tulipendana sana na naelewa kuwa alifanya vile kwakuwa hakuwa tayari kunipoteza. Nancy alikuwa mtu mzuri sana na mpaka kufikia kufanya vile inaonyesha kiasi gani alishindwa kuvumilia maumivu ya nilichomwambia, hivyo huo ulikuwa muda wangu wa kumfanya aachane na anachotaka kukifanya.

    ****

    Kazi kubwa niliyokuwa nayo ilikuwa kumueleza Patrick ukweli wa kila jambo, nilimkwepa sana lakini kila mara aliponitazama usoni niliona kabisa deni nililokuwa nalo kwake na sasa niliona ipo haja ya kumuambia ukweli.

    “Patrick nadhani sasa ni wakati muafaka wa kukueleza kila kitu kuhusu mimi na pia kuhusu Nancy” nilimwambia huku nikitazama chini kwa aibu.

    “Am listening”(nakusikiliza) alinijibu na kukaa sawa akinitazama, nilianza kumueleza historia yangu yote ya kipindi cha nyuma toka udogo wangu ila nilipofika kwenye kuelezea kuhusu mimi na Nancy nilisita kwanza nilijiuliza Patrick atanichukuliaje.

    “Nancy ni nani na kwanini atake kuniua” aliniuliza huku akiwa amenishika mikono yangu kama ishara ya upole.

    “Baada ya hayo yote kunitokea, niliwachukia sana wanaume, sikuwa na hisia na wanaume. Mbali na dokta Anderson kujitahidi kunisihi nisahau kila kitu lakini haikuwa rahisi, hivyo nikiwa kazini kama daktari kipindi cha mwanzoni, alikuja mgonjwa aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa na damu mfululizo, nilitakiwa kumfanyia uchunguzi lakini nilikuja kugundua kuna dawa alikuwa akimeza ndizo zilimletea tatizo hilo, hivyo nikalazimika kumpangia kliniki ili kumpa ushauri nasaha na kumfanya aachane na zile dawa, nikiwa kwenye kliniki siku moja yule mgonjwa alikuja na tulikuwa tumejifungia ofisini kwangu akawa amelala kitandani kavua nguo zote ili nimfanyie uchunguzi, alinishika mkono wangu na kuupeleka kwenye uke wake akawa kama ananisugulia, nilipata msisimko wa ajabu na siku hiyo ndipo niligundua kuwa nilikuwa na hisia na mwanamke mwenzangu, sikuipenda ile tabia lakini taratibu nilizoea na hati maye nilimfanya yule Mgonjwa kuwa mpenzi wangu, na ndiye huyu Nancy, nilimpenda sana na nlijitoa kwake, nikilala kwake na yeye akilala kwangu na kufanya mambo yote kama wapenzi, malengo yetu ya yalikuwa motomoto na wote tulijaliana katika kila hali, siku zote Nancy alikuwa akinipenda na kuvutiwa na mwili wangu, vivyo hivyo na mimi nilimpenda sana na nilivutiwa na kili kilichokuwa katika mwili wake” nilivuta pumzi kidogo na kumtazama Patrick aliyekuwa ametoa macho kama vile anaota;

    “hali ilikuja kuwa tofauti wewe ulipoletwa pale hospitali, haswa pale Mary alipokuacha na kuondoka zake, nilikuwa nikikuhudumia kwa karibu sana na sikuwa na mtu mwingine wa kumwangalia kwa ukaribu bali wewe tu, nilianza kukupenda taratibu na hisia zangu juu ya Nancy zilianza kupotea na nilianza kumkwepa, nilikuwa nataka kuanza maisha mapya hasa kwakuwa kupitia wewe niliona Tumaini jipya tena hapo hisia juu ya wanawake wenzangu zilikatika kwakuwa haikuwa utamaduni wangu, nilifahamu kuwa nilichokifanya kilikuwa ni kosa hata mbele za mungu lakini sikuwa nikifikiria sawia, hivyo nilitaka kulibadilisha hilo kwa kuanza tena upya kila kile nilichokuwa nikikiamini, hivyo siku moja asubuhi nilimuita Nancy nyumbani kwangu na hapo nilikuwa na nia ya kumueleza kubadilisha kwangu mawazo juu ya hisia zangu kwake”



    ******

    Ilikuwa majira ya saa nne asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kazini, jana yake nilikuwa nimempigia simu Nancy kuwa ningetaka kuongea nae na hapo ilikuwa ni wiki mbili toka mara ya mwisho nilipoonana nae. Wakati niko chumbani nikipaka mafuta mlango ulifunguliwa na Nancy aliingia moja kwa moja bila ya kupiga hodi, alianza kunishikashika na kunibusu kila sehemu huku mikono yake akiipitisha kwenye sehemu zangu za siri, sikuwa na hamu ya kufanya alichotaka lakini kwakuwa nilikuwa ninatafuta njia rahisi ya kumuambia ili anielewa nilijilazimisha na kuanza kumshikashika na yeye, tulianza kufanya tulichokuwa tukikifanya na baada ya kumaliza tulikwenda kuoga na baada ya hapo, Nancy alichukua nguo yangu ya ndani na kuanza kunivalisha, ndipo nilipomshika mkono nakumuomba tuongee.

    “Kuna kitu nataka kukuambia Nancy” nilimvuta na kumkalisha chini wakati huo wote tukiwa watupu, alipandisha miguu yake kitandani na kuweka kichwa chake kwenye mapaja yangu na kunitazama.

    “Nancy kwenye maisha kuna muda kila mtu hufanya mambo fulani kwasababu, kila mtu hujikuta katika mkondo mbovu kwasababu tu alitaka mwenyewe au maisha yalimchagulia namna ya kuishi, lakini hayo yote huwa ni matokeo ya bahati mbaya ambayo kuna muda kwa uzembe wetu au kwa kuyaamini yale tusiyoyasimamia tunajikuta tukiyatenda yasiyo mema, nimegundua nilipojikwaa Nancy na ninataka nirudi nyuma nianze upya, sifurahishwi tena na mahusiano tuliyonayo kwani huu sio utamaduni wa mwanamke, hisia zangu kwako zimeyeyuka mfano wa theluji ichemshwayo, nakupenda lakini sitaki tena tuendelee hivi” alinyanyuka baada ya kusikia maneno yale na kuamua kukaa huku akilia.

    “haiwezekani mpenzi, siku zote tumekuwa pamoja leo hii unataka uniache kwa kusingizia huna hisia na mimi? Niambie ni nini unataka nikufanyie, unataka nini mpenzi wangu na mimi nitafanya, niambie tafadhali” Nancy aliongea huku akilia kama mtoto, nilimuonea huruma sana lakini huo ulikuwa msimamo wangu na nilikuwa tayari kuusimamia mda wowote.

    “sitaki chochote Nancy, umekuwa mtu mzuri sana kwangu na umenionyesha mapenzi ya kweli na mimi nashukuru sana kwa hilo lakini kwasasa yupo ambaye inanibidi niwe naye” nilimueleza kwakujikaza lakini huo ndio ulikuwa ukweli wangu.

    “ni nani huyo” aliuliza.

    “ni Patrick, yule mgonjwa ninayemuhudumia pale hospitali.

    “yani unaniacha kisa yule mfu? Nini kimekupata Pamela,,eehh, unahitajika kupumzisha akili mpenzi, yani yule mtu amekaa miaka na miaka hajaamika, mtu anayetegemea kufa muda wowote ndo akuchanganye kisi hicho kweli?” kabla hajamaliza kuongea tayari alikuwa ameshanichefua kumuita Patrick mfu.

    “ishia hapohapo Nancy, vaa nguo zako ondoka sitaki kukuona, nampenda sana huyo unayemuita mfu, hivyo nakuomba wewe uondoke hapa” nilimsukuma na kuchukua nguo zangu kisha nilikwenda kuvalia nguo sebuleni.

    “Pamela naomba unisamehe sikuwa na maana ya kukuudhi mpenzi wangu, naomba unielewe” alinifata huku akinishika na kujaribu kunituliza.

    “Nimekuelewa Nancy ila mimi na wewe basi, sitaki tena usagaji, siko tayari tena na nina uhakika kama wazazi wangu wangekuwa hai wangeniua kwa hili, nampenda Patrick huo ndio ukweli mpya ambao inabidi mimi na wewe tuwe nao kichwani na tujue kuwa mambo yameishia hapo” nilimuambia hivyo na kuondoka pale sebuleni nikamuacha akilia, nilichukua vitu vyangu na nilipofika pale sebuleni nilisimama na kumtazama.

    “Nancy hakuna jinsi inabidi ukubaliane na hilo nililokuambia kwakuwa hakuna suluhu zaidi ya wewe kukubali, tafadhali nyanyuka tuondoke nataka nifunge nyumba yangu. Hapo ndo ilikuwa mwisho wa mapenzi yangu na Nancy.

    *****

    Yalikuwa matarajio yangu kuwa Patrick angekuwa mkali na pengine angeweza hata kutaka kuondoka na kuniacha lakini hali ilikuwa tofauti kabisa, baada ya kumueleza ukweli wa kila jambo Patrick alinivuta na kunikumbatia.

    “usijali kila mtu anahistoria mbaya katika maisha yake, lakini ikitokea ukajua unapokosea na kuamua kujirudi na kujirekebisha basi hiyo ni faraja ndani ya moyo wa kila mmoja aliyechukizwa na tabia yako ya awali, hivyo usiwe na hofu, nenda kanisani katubu zambi zako na mungu atakusaidia, ila ipo haja ya kuongea taratibu na Nancy, na mimi ndiye nitakwenda kuongea nae” nilishtuka kwakuwa sikutegemea awe mpole kiasi kile lakini kilichonichaosha ni pale aliposema kuwa anataka kuongea na Nancy.

    **SIKU MBILI MBELE**

    Jioni tukiwa tumetoka matembezini Felicity alinipigia simu na kunitaarifu kuwa alikuwa ameshakamilisha uchunguzi kuhusu ajali aliyoipata Patrick miaka zaidi ya sita iliyopita, hivyo aliniambia twende mimi na Patrick nyumbani kwake kwakuwa ndiko kuna vifaa anavyoweza kutumia kutuelezea.

    Tuliondoka hadi kwa Felicity na tulipofika kwake alitukaribisha kisha tukakaa kwa muda kidogo wakati yeye akiwa ndani na baadaye alituchukua na kutupeleka kwenye chumba fulani kama darasa dogo kisha aliwasha kompyuta kubwa iliyokuwa ukutani na kama kawaida yake alianza kuelezea.

    “nilianza kufanya uchunguzi juu ya ile ajali kwa kufatilia wale trafiki waliokuwa wakifatilia ile kesi, sikuile wakati ile ajali inatokea inaonekana njiani kulikuwa na ile gari iliyosababisha ajali kwa zaidi ya masaa mawili ikifanya doria njia ile, mazingira ya ajali yanaonyesha kuwa ile ilikuwa ajali ya kupangwa, swali ni je nani alipanga ajali hiyo? Na majibu ni kwamba, toka Patrick aje







    **SIKU MBILI MBELE**

    Jioni tukiwa tumetoka matembezini Felicity alinipigia simu na kunitaarifu kuwa alikuwa ameshakamilisha uchunguzi kuhusu ajali aliyoipata Patrick miaka zaidi ya sita iliyopita, hivyo aliniambia twende mimi na Patrick nyumbani kwake kwakuwa ndiko kuna vifaa anavyoweza kutumia kutuelezea.

    Tuliondoka hadi kwa Felicity na tulipofika kwake alitukaribisha kisha tukakaa kwa muda kidogo wakati yeye akiwa ndani na baadaye alituchukua na kutupeleka kwenye chumba fulani kama darasa dogo kisha aliwasha kompyuta kubwa iliyokuwa ukutani na kama kawaida yake alianza kuelezea.

    “nilianza kufanya uchunguzi juu ya ile ajali kwa kufatilia wale trafiki waliokuwa wakifatilia ile kesi, sikuile wakati ile ajali inatokea inaonekana njiani kulikuwa na ile gari iliyosababisha ajali kwa zaidi ya masaa mawili ikifanya doria njia ile, mazingira ya ajali yanaonyesha kuwa ile ilikuwa ajali ya kupangwa, swali ni je nani alipanga ajali hiyo? Na majibu ni kwamba, toka Patrick aje huku kulikuwa na mawasiliano yakifanyika kwenye mgahawa wa Roshan uliopo chini ya hoteli aliyofikia, mawasiliano hayo yalikuwa yakifanywa kati
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ya mtu anayeitwa George mwenye namba yenye code namba +255 ambayo ni ya nchini Tanzania na Mary ambaye ndiye mkeo uliyekuwa naye. Mawasiliano hayo ambayo tumefanikiwa kuyapata yalikuwa yakifanyika kila siku kati ya saa 9:45 na 10:34 usiku. Mawasiliano hayo yalikuwa ya aina nyingi, kuna siku walifanya mawasiliano ya simu na kuna kipindi waliwasiliana kupitia barua pepe. Maongezi hayakuwa wazi kwakuwa walikuwa wakiongea katika lugha ambayo waliijua wao wenyewe, lakini tulichofanikiwa kukijua ni kwamba mawasiliano haya kila mara yalitaja kampuni iitwayo PATRIMARY, na pia kuna barua pepe moja ilikuwa ikiuliza aina ya jina jipya ambalo lingefaa kuwa mbadala wa lile la mwanzo, na katika majibu ya Mary pamoja na mambo mengi anamtaarifu George kuwa jina mbadala ni GEOMARY. Baada ya siku tatu toka wafanye mawasiliano hayo, George alituma ujumbe kwenye simu ya Mary akimtaarifu kuwa tayari ameshafanikiwa kubadilisha na akamwambia sasa anaweza kuingia kwenye tovuti ya www.geomary.co.tz kuangalia kama mambo yote yalikuwa sawa, tulichogundua ni kwamba wakati huu walikuwa wakiandaa tovuti kwaajili ya kazi waliyokuwa waifanye baadaye. Siku ya tukio la ajali magazeti ya nchini Tanzania yaliripoti juu ya ajali ile na waliambiwa kuwa hali ilikuwa mbaya sana, lakini baada ya Mary kuondoka huku na alipofika Tanzania aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelezea kuwa mumewe alifariki na kupotelea baharini wakati wakiwa wanamuhamisha kutoka Fiji kwenda Suva ambapo ndege yao ilipata ajali na kuangukia baharini ila yeye Mary alipona. Waandishi walilipwa ili kuandika habari hiyo na baada ya wiki mtu anayeitwa wakili Mrutu aliwasilisha maombi mahakamani akiiomba mahakama ipokee wosia wa marehemu yaani Patrick alioandika na kuuweka kwa huyo mwanasheria juu ya nani amiliki mali za marehemu. Wosia uliwataja watu wawili tu ambao ni Mary na George, na baada ya mahakama kupokea waliamuru wahusika wapewe mali zile. Majina ya kampuni na mali nyingine yalibadilishwa, na cha kushangaza miezi 9 mbele Mary alijifungua, upelelezi unaonyesha George alifunga ndoa na Mary miezi michache baadaye, hii inamaana kuwa mimba hii Mary aliipata siku alivyokuwa ameshuka Tanzania.”

    “unasemaje? Mimba?” nilimuona Patrick akishtuka kwa kuhamaki.

    *****



    Simulizi ilikuwa imeushika moyo wangu kiasi fulani, mara ghafla nikiwa bado nasikiliza, niliona giza nene na kimya cha hali ya juu kilitanda, sauti niliyokuwa nikiisikia ilikuwa ni ya magari tu yaliyokuwa yakisikika kwa mbali sana huko barabarani.

    “aaaahhh hii nchi hii” nilijisemea moyoni na kubaki nikitafakari mwenyewe juu ya yale niliyoyasikia, nilishangaa sana juu ya alichokifanya Mary lakini bado nilikuwa na maswali mengi sana ambayo sikuwa na majibu nayo.

    “huooooooo” niliropoka kama mwehu vile nilioona taa zinawaka tena, haraka niliwasha kile kiredio na kuchomeka headphones ili nilisikilize, nilipoweka masikioni nilikuta

    Patrick akisimulia.





    ***PATRICK***



    Nilikuwa nimelowa kwa hofu na kutokuamini ukweli wa mambo yaliyokuwa yanatokea hapo, haikuwa rahisi kuamini kuwa msichana niliyempenda kwa maisha yangu yote leo hii alikuwa ndiye adui wangu, pengine ni ndoto, hilo lilikuwa ni jambo pekee nililowaza ambalo halikuwa kweli, vitu vilikuwa vinatokea na ukweli ulikuwa umejulikana. Swali kubwa nililojiuliza ni kwanini basi Mary afanye hivyo wakati tayari alikuwa ni tajiri pia na mwenye pesa nyingi.

    “Patrick” nilishtuka toka katika msongo wa mawazo na kukurupuka.

    “Naam” ilikuwa sauti ya Felly.

    “Usiwaze sana kila kitu kitajulika na kila mtu aliyeshiriki kukufanyia chochote atafahamika, nitakusaidia kwenye kila hatua, lakini nakuomba sana usiende nchini kwenu hivi karibuni mpaka mipango yote iwe imefahamika, tutahakikisha unaondoka hapa ukiwa unajua kila kitu” aliongea Felly huku akinitazama.

    “ asante sana Felly, mungu atakulipa” nilimwambia na yeye alinisogelea na kunikumbatia.

    **WIKI TATU MBELE**

    “Majina yako kamili ni nani” aliuliza yule dada mwenye asili ya Asia.

    “Patrick Mfangavo” nilimjibu huku nikimtazama kwa makini.

    “unatatizo lolote kaka, naona kama hauko sawa?” aliniuliza kama vile aliisoma akili yangu.

    “Hapana niko sawa” nilimjibu huku nikitabasamu kama njia ya kumuonyesha kuwa tuko pamoja.

    “Unakumbuka nimekuuliza maswali mangapi?” aliniuliza huku akinitazama usoni bila chembe ya aibu. Niliwaza kwa muda na kujibu japo sikuwa na uhakika wa jibu.

    “matano” nilimjibu na hapo alitizama chini kisha alipoinua macho alinisemesha tena.

    “Kaka naweza kujitolea muda wangu kukusaidia wakati mwingine kama leo hujisikii vizuri, hizi fomu ni za uhamiaji, zinahitajika kujazwa kila kitu kwa usahihi ila kwa hali uliyokuwa nayo hatutaweza kuelewana sana hapa” alinisemesha kwa upole sana lakini nilisisitiza kuwa nilikuwa sawa.

    “Nimekuuliza maswali nane na umejibu yote ila maswali matatu umekosea, moja ni nchi uliyozaliwa, mbili ni muda wako uliokaa Fiji na tatu ni kama umeoa au la” aliniambia na mimi niligundua kuwa ni kweli kabisa kuwa nimekosea. Sikuongea chochote nilinyanyuka na kuondoka.

    Nilimpigia simu Pamela kuwa nitachelewa siku hiyo kwakuwa nilitaka kuwa mwenyewe, nilipofika nje niliingia kwenye gari na kisha nilianza kuendesha kuelekea nisipopajua, sikuwa na leseni lakini nilipewa ruhusa ya kuendesha huku wakinitengenezea leseni nyingine. Umbali wa kilomita kumi nilikuta sehemu kuna uwanja wa mpira na watu walikuwa wakitizama mpira pale, ilikuwa ni majira ya saa 12 jioni na mimi nikaamua kuungana na wale watu kutazama mpira ule mpaka saa moja jioni nilipogeuza na kwenda kwenye hoteli maarufu iliyoko juu ya mlima wa Penvisk, nilinunua pombe chupa kubwa na kuinywa kisha nilipanda juu kabisa ya hoteli hiyo ambapo ulikuwa ukisimama unaona Fiji yote. Mandhari yakuvutia ya eneo lile ilinifanya nikumbuke sana hotel ya Ngurdoto iliyopo nchini Tanzania, katika kipindi cha mwanzo kabisa cha mapenzi yangu na Mary tulienda katika hii hoteli kutembea na tulikaa kwa muda wa siku nne kabla ya kurejea jijini, ni siku hii ambapo Mary alinieleza mipango yake mingi ya kimaisha, lakini moja ya mpango wake mkubwa ulikuwa ni kufunga ndoa na mimi, hii ilinitoa mchozi sana nilipoikumbuka. Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa Mary kuniacha peke yangu tena bila kujua ninini sababu ya kufanya hivyo. Nilisimama pale na kulia sana.

    “maisha hayanyooki siku zote, unatakiwa uwe imara mda wote kukabiliana na kila linalotokea pale litakapotokea” ilikuwa sauti ya msichana, ilinishtua nikaangalia pembeni yangu alikuwa amesimama msichana mwenye umbo dogo aliyekuwa naye akitizama kule nilikokuwa nikiangalia mimi, hakugeuka kuniangalia kama nilikuwa namuangalia.

    “Wewe ni nani?” nilimuuliza kabla ya yeye kugeuza kichwa na kunitazama.

    “Naitwa Khajat Kapur” alinitajia jina lake na kunipa mkono huku akitabasamu, nilipomtazama vizuri alikuwa yule afisa uhamiaji aliyekuwa akinihudumia muda wa mchana.

    “Umekuja kufanya nini hapa”nilimuuliza huku nikiendelea kutazama mbele na yeye akiwa ameegemea chuma nililokuwa nimeweka mikono.

    “Nimekuja kutembea tu, hii ni sehemu ambayo watu wengi wajisikiao upweke huja na kukaa” aliongea hayo na kimya kidogo kilitanda kisha alianza kuongea tena.

    “Kwanini unataka nafasi ya kufanya kazi Fiji” alianza kuongea tena.

    “kwani ni vibaya” nilimuuliza kwa mshtuko.

    “sio vibaya nimeuliza tu” alinitazama kisha alitoka pale na kutembea mpaka mbele kulikokuwa na kiti kisha aliketi na kuniita.

    “Nataka kukupa kazi” aliniambia huku akinitazama usoni.

    “Sihitaji kazi” nilimjibu huku nikiwa naketi kwenye kiti.

    “vizuri ila uwe na uhakika kuwa hauhitaji kazi” aliniambia na kunyanyuka ili aondoke ila nilimkamata mkono na kumsukuma mpaka ukutani kisha nilimkaba huku nikimlazimisha aniambie anataka nini kwangu.

    “utaniumiza, tafadhali niachie” aliongea sauti ya kinyonge kisha nilimuachia.

    “Patrick unahitajika kubadilika kabisa, hii ni Fiji, huwezi kufanya kazi na watu wa huku kama utakuwa huna namna ya kujua kuishi nao. Punguza hasira na upunguze mawazo, kila kitu kitakuwa sawa.

    “wewe ni nani?” nilimuuliza tena.

    “mimi ni rafiki yake na Felly, yule dada aliyekuleta ofisini kwangu mchana wa leo” alinijibu na hapo nguvu ziliniishia kwakuwa nilihisi sikuwa nimemtendea haki kuwa mkali kwake.

    “samahani” nilimuambia huku nikinyanyuka na kurudi kule nilikokuwa nimesimama mwanzoni, nilisimama pale bado machozi yakinitoka na sikujua kwanini, alikuja taratibu na kunifata pale kisha alisimama pembeni yangu kisha alinitazama na kunishika bega.

    “kuna mwisho wa kila jambo Patrick” aliniambia na kunipa bahasha kisha aliondoka. Niliitazama ile bahasha lakini sikuwa nafahamu nini kilichopo ndani, nilitoka mpaka kwenye taa na kufungua, nilichokikuta ilikuwa ni furaha yangu kubwa. Nilishuka mpaka kwenye lift nikaingia ndani lakini nilipofika pale chini sikumuona. Nilirudi kwenye gari yangu na kuingia ndani kisha nilitazama zile karatasi vizuri, zilikuwa ni ruhusa ya mimi kufanya kazi kama nilivyokuwa nimeomba, niliwasha gari na kuendesha kwa haraka sana na baada ya muda fulani nilikuwa nimefika nyumbani.

    “Ulikuwa wapi Patrick, umenifanya nikae na wasiwasi muda wote” aliongea Pamela ambaye nilikuwa nimemkuta pale nje akiwa amekaa.

    “lakini sinilikuambia kuwa nitachelewa kurudi” nilimuambua huku nimemshika mashavu yake na kumbusu, kisha nilimkumbatia na kukumbuka kipindi nikiwa na Mary.

    “Twende ndani Pamela” nilinyanyua ile glas yake ya mvinyo na kuondoka nayo ndani.

    “Tukaoge” aliniambia huku akitabasamu na mimi nilivua nguo na kwenda kuoga nae.

    **MWEZI MMOJA MBELE**

    Tayari nilishaanza kufanya kazi kwenye kampuni ya ANDERSON CONSULTANCY baada ya kufanikiwa kuifungua anuani yangu ya barua pepe na kuchukua vyeti vyangu nilivyokuwa nimewahi kumtumia mtu, nilifanya kazi kama afisa maendeleo na mshauri wa mambo ya ujasiriamali.

    *******

    “Halooo,,Haloooo, Halooo, mbona huongei,,haloo” sikuweza kuongea nilijikuta machozi yakinitoka, nilikata simu na kuanza kulia nikiwa pale ofisini, ilikuwa ni sauti yake kabisa, ile namba ilikuwa ni ya ofisi yao niliitoa kwenye ile tovuti aliyoitamka wakati akiwasiliana na yule jamaa.

    “Hey Mbona unalia Patrick” nilishtushwa na sauti hiyo na alikuwa ni Felly.

    “hamna niko sawa” nilimuambia huku nikifuta machozi.

    “hauko sawa Patrick, umepiga simu kwa Mary si ndio” aliniuliza na sikuwa na namna ya kumdanganya bali kukaa tu kimya. Alinichukua pale na kuniomba akaninunulie chakula cha mchana na mimi nilikubali tukaondoka pale na kuelekea kwenye mgahawa uliokuwa karibu na pale kazini.

    “Patrick kuna mtu anaitwa Drew Barrymore aliwahi kusema, ‘nafikiri furaha ndiyo humfanya mtu kuwa mzuri, watu wenye furaha ni wazuri, Patrick maisha ni leo, kesho ni majaaliwa. Unatakiwa ufanya maamuzi ya kukufanya uwe na furaha sasa hivi, unatakiwa uanze upya na ukubali kuwa mambo yametokea na sasa uangalie mbele zaidi. Utalia kila siku na utajikuta upo palepale katika maisha yako. Fanya uamuzi sasa na uwe na furaha Patrick” yalikuwa maneno ya msingi na ya kunifariji yaliyotoka kinywani mwa Felly, sikuwa na la kusema zaidi ya kulia.

    “Uko sahihi Felly nitafanya hivyo” nilimjibu na kukumbuka kitu fulani.

    “Naomba unielekeze nyumbani kwa Nancy” nilimuomba huku nikishika mikono yake miwili kwa maana kuwa sikutaka anikatalie.

    “sawa, anuani yake ni MDSK 234 Pentagone street, nakuomba uwe makini, kama aliweza kukuvizia akajaribu kukuua hatashindwa kukufyatulia risasi” niliitikia na kumshukuru.





    **JIONI YAKE**

    Baada ya saa za kazi niliondoka mpaka kule nilipoelekezwa na baada ya kufika pale kwa Nancy niligonga mlango na hapo niliruhusiwa na mfanyakazi wake kisha niliingia na nilipofika sebuleni nilikutana nae uso kwa uso.

    “habari yako Nancy” nilimsalimia lakini hakujibu badala yake alianza kutetemeka lakini baada ya mabishano ya muda mrefu sana nilifanikiwa kumtuliza na tulikaa chini tukaongea.

    “Nancy najua jinsi unavyompenda sana Pamela, nafahamu sana mahusiano yenu na Pamela amenieleza kila kitu lakini tafadhali nakuomba sana, heshimu maamuzi yake na pia mimi sina uadui na wewe, mimi sijakufanya chochote, huna sababu ya kuniwinda kama njiwa, nina mengi sana yanayonisibu na roho ya subira kwasasa sina ndio maana nakuomba uache kuniwinda, umenikosa na risasi, leo pengine ningekuwa marehemu lakini nashukuru kuwa niko hai, hivyo kaa mbali na mimi, nakuonya tu kwakuwa mimi sio mtu mzuri sana kwa sasa” baada ya kumuambia maneno hayo nili nyanyuka na kutoka nje kisha niliondoka kurudi, nikiwa njiani kwa zaidi ya kilomita moja niliona kuna gari ilikuwa ikinifatilia, nilikatiza na kupaki sehemu kisha nayo ilikuja na kupaki, nilipotazama ndani ya ile gari alikuwa ni Pamela alinipa ishara ya kwamba nimfate na hapo niliingia tena kwenye gari na kumfata nyuma mpaka tulipofika nyumbani. Tuliingia ndani na tulipofika tu hakukuwa na maongezi Pamela alinishika na kuanza kunibusu huku na kule alifanya hivyo na baada ya kumaliza alinipa makaratasi aliyokuwa ameshikilia mkononi, niliyachukua na kuyasoma kwa makini nikahisi kuchanganyikiwa,

    “hii ni nini Pamela” nilimuuliza huku nikimtazama.

    “nina mimba ya wiki tatu Patrick” aliniambia huku akirukaruka. Ilikuwa furaha kwake ila kwangu ilikuwa ni tofauti, sikuzijua hisia zangu kwake, sikujua ni nini nilitaka kutoka kwake.

    “Patrick najua kabisa akili yako haijatulia najua pengine hukulitegemea hili, ila usijali nitalea mimba na mtoto pia, usijali mana naona umekosa raha” furaha yake iliisha ghafla na kuniambia hayo huku akiondoka na machozi yakimtoka. Lilikuwa ni jambo la kunishtua nililokosa maamuzi nalo, ilitokea haraka sana na sikulitegemea hasa kwa wakati kama ule.

    Nilimfata Pamela ili niweze kuongea naye lakini hakuwa tayari kuongea, alikuwa ameshakasirika na mlango wa chumbani ulifungwa.

    Nilirudi mpaka sebuleni na kuamua kukaa pale mpaka usingizi uliponipitia.

    *****

    Kesho yake asubuhi Pamela alitoka chumbani na kunipita nikiwa pale sebuleni lakini nilimzuia na kumuomba niongee nae.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Patrick umeniudhi sana” aliniambia hukua akilia.

    “najua Pamela, nafahamu kuwa natakiwa kusimama kama mwanaume, lakini pia unatakiwa ujue kuwa kwasasa siko sawa kabisa, akili yangu haijatulia na nina mengi ninayoyafikiria, lakini nitakuwa bega kwa bega kuhakikisha kuwa tunalea mtoto huyo, nisamehe sana kwa nilichofanya” nilimuomba msamaha kwa unyenyekevu na yeye alisogea na kunikumbatia.

    “basi Patrick nenda kaoge kisha tuongozane” niltoka pale na kwenda kujiandaa na baada ya muda mfupi nilikuwa tayari na kurudi mpaka sebuleni nikamkuta Pamela na Felly.

    “mambo Patrick” Felly alinisalimia huku akitabasamu, alikuwa amevaa sare zake za kazi zilizomfanya aonekane mzuri na mwenye kupendeza japo ile bastola aliyokua ameiweka kiunoni ilimfanya aogopeke, mwili wake mzuri uliokuwa umeenda hewani kama wasichana wa Kinyarwanda ulimfanya aonekane mkakamavu na asiyeweza kuzoeleka, alikuwa amebana nywele zake na kuvaa kofia iliyoruhusu nywele zake kutokeza vizuri na kuupamba uso wake.

    “safi umependeza” nilimjibu na kushindwa kujizuia kumsalimia.

    “asante, mimi nimekuja kuna kitu nataka kuwafahamisha kuhusu uchunguzi ninaoendelea nao kuhusu Mary” alituambia na wote tulikaa kimya ili kumsikiliza.

    “okey tunakusikiliza” nilikuwa wakwaza kudakia.

    “ tuanzie pale tulipoishia” alianza kuwasha kompyuta yake na kisha alianza kuelezea.

    “Kipindi Mary alipotoka na kwenda Tanzania na kufanikiwa yeye na George kubadilisha jina la kampuni na baadaye walifunga ndoa kabla ya Mary kugundulika kuwa anamimba, taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti kipindi kile zilikuwa nyingi sana lakini kati ya hizo ni taarifa juu ya maisha ya Mary baada ya kufika nchini Tanzania, kuna muandishi mmoja wa gazeti la kingereza alimuhoji Mary juu ya maisha baada ya kufiwa na mumewe, inaonekana dhahiri kuwa Mary alieleza kuwa mumewe amedariki. Sehemu ya mahojiano hayo inasomeka hivi;

    Mwandishi: Maisha yako bila mumeo unayaonaje.

    Mary: (analia) ni magumu sana, mimi na mume wangu tulikuwa zaidi ya marafiki, tulikuwa ni wapenzi na mapatna katika biashara zetu, yeye ndiye aliyekuwa kioo katika maisha yangu na yeye ndiye alikuwa kila kitu, lakini kuna muda lazima mambo yatokee ili mipango mingine ifanyike.

    Mwandishi: je ni juhudi gani ulizifanya baada ya ndege ile kudondoka baharini iliyokuwa imembeba mumeo ambaye muda mrefu nyuma tulielezwa kuwa alipata ajali akiwa huko.

    Mary: nikishirikiana na mamlaka za kule nilifanya utaratibu wa kumtafuta lakini walisema kwa hali ya baharini si rahisi kumuona.

    Mwisho wa kunukuu,,sasa angalia mahojiano mengine aliyofanya na kituo kimoja cha radio, aliulizwa hivi;

    Mtangazaji: Unawezaje kuendesha biashara zako mwenyewe kwa sasa.

    Mary: ni ngumu sana bila mume wangu , lakini kuna muda lazima mambo yatokee ili mipango mingine ifanyike. Lakini mume wangu alikuwa mtu wa kuchukua tahadhari siku zote, hivyo aliacha utaratibu wa namna mambo yatakavyokuwa iwapo atakuwa amefariki.

    Mtangazaji: ni kwanini umeamua kuolewa mapema hivi tena na mtu wa karibu kabisa wa mumeo?

    Mary: Yalikuwa maelekezo ya marehemu mume wangu kuwa niolewe na mwanaume ambaye niliyeolewa naye sasa” Felly alimaliza kuelezea hayo na mimi nilianza kujisikia kizunguzungu lakini sikuweza kufanya chochote zaidi ya kumsikiliza.

    “hapa kuna kauli inajirudia mara kwa mara kwenye karibu mahojiano matano aliyowahi kufanyiwa maneno hayo ni ‘lakini kuna muda lazima mambo yatokee ili mipango mingine ifanyike’, haya maneno amekuwa akilitumia mara kwa mara. Pia kuna mahojiano ambayo huyo George amehojiwa na yalikuwa hivi;

    Mwandishi: marehemu alikuwa mtu wako wa karibu sana, vipi uendeshaji wa miradi yake bila yeye na ukiwa kama mume mpya sasa wa mke wa marehemu unajisikiaje kwamba marehemu alipenda wewe uwe mume wa mke wake iwapo siku moja itatokea amefariki.

    George: ni pigo kubwa sana lakini najitahidi sana kufanya yote aliyoelekeza kwenye maandiko machache aliyoyaacha, na mimi kuwa mume wa mke wa marehemu naona ni njia ya kumuenzi ndugu yangu.

    Sasa kwa nilivyopitia kila kitu kuhusu mahojiano haya yote na kila aina ya ushahidi uliojitokeza nilikuja kugundua kuwa mlipofunga ndoa kisha mkaja huku ndipo hili jina la George lilipoibuka, huyu mtu alienda kuomba mahakamani kubadilisha jina lake na baada ya muda fulani jina lilikuwa limebadilishwa, na muda wa dakika tano atakuwa akiongea na kipindi cha business times kinachorushwa na SECURE TV ya nchini Tanzania kupitia satellite yeye akiwa kama mmoja wa wamiliki wa makampuni makubwa ya kibiashara” hofu ilinitanda kutokana na yale aliyoyaongea Felly lakini haraka nilishika rimot na kuanza kupekua mpaka nilipoipata ile stesheni kisha mahojiano yalianza kuonekana, nilipotumbua macho mtangazaji alimtangaza mkurugenzi wa kampuni ya GEOMARY, niliisogelea kwa karibu sana TV na ndipo nilipogundua kuwa alikuwa ni MARK..

    “Ohh hii haiwezekani” nilinyong’onyea huku nikijisemea na hapo Felly alianza kuongea tena.

    “inawezekana na imeshawezekana,,Mdogo wako Mark alikuwa ndiye George aliyeshiriki kwenye kila hatua, alibadilisha jina ili kuficha kila kilichotokea, mpango huu unaonekana ni wa muda mrefu sana lakini bado sijajua madhumuni ni nini na nini maana ya maneno aliyoyasema Mary”





    “Kitu pekee kidogo na cha thamani unachoweza kufanya katika maisha yako ni kutafuta nini unachokitumainia, na kikubwa unachoweza kufanya ni kuishi ndani ya matumaini hayo. Sio tu kuyakubali kwa mbali ila kuyaishi kwa undani wake. Matumaini yanaweza kuwa nguvu kubwa yenye msukumo. Inawezekana kabisa kusiwe na miujiza ndani yake, ila ujuapo unachotumainia sana na ukakikumbatia kama mwanga ndani yako basi unaweza kutenda jambo na kuyafanya mambo yatokee kama miujiza…yafanye matumaini yako yaishi..JUKUMU MOJA WAPO LA BINADAMU NI KUFIKIRI KWA NIABA YAKE MWENYEWE” HII NI SEHEMU YA SABA.





    **PATRICK**



    Nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa lakini kitu pekee kilichonipa ahueni ni matumaini. Nilikuwa bado nina matumaini ya kuishi na kupata vitu vyangu kwa gharama ya damu ya mtu au kwa gharama yeyote ile. Niliendelea kuangalia kile kipindi jinsi ambayo Mark alijitutumua kuelezea juu ya kampuni hiyo ambayo yeye ni mkurugenzi. Sikujua ilikuwaje mpaka ikatokea hayo yaliyotokea.

    Nilichokuwa nakumbuka ni kwamba mimi na Mark tulikubaliana sawia kabisa kuwa hakuwa na mahusiano na Mary na kwamba Mary hakuwa anampenda. Nilikuwa sijui kama walikuwa na mpango mwingine wowote juu yangu. Haikuwa rahisi hata kuamini kuwa mambo yalikuwa yakitokea sasa,

    “Kampuni yangu imepiga hatua kwasasa na mimi pamoja na mke wangu tunategemea baada ya yeye kujifungua hivi karibuni tutaanza kufungua matawi mapya huko Kenya na Burundi pamoja na kuboresha matawi yetu hapa nchini. Hii itakuwa ni hatua kubwa kwetu lakini pia kwa huduma zetu kama kampuni ya GEOMARY, lakini hatua kubwa sana kwangu pia katika kuyafanya mambo yatokee. Kubadilisha taswira na muonekanao wa yaliyofichika juu ya mafanikio ndiyo nguzo na shabaha ya maisha yangu sikuzote katika kuleta kwa ukaribu yale niliyopanga kwa muda mrefu”. Hayo yalikuwa maneno ya Mark pale alipokuwa akielezea juu ya mipango ya kampuni yake.

    “hapohapo, embu angalia hapo inarekodi bado” alidakia Felly aliyekuwa akirekodi yale mazungumzo pale kwenye TV na Pamela alimwambia ndiyo ilikuwa inarekodi. Tuliendelea kuangalia kile kipindi na sasa Mark aliambiwa aseme chochote anachotaka kuifahamisha dunia. Alisema hivi.

    “Katika kufanikiwa lazima vijana wajipange vyema, kila mtu ananafasi ya kuwa vile atakavyo, haijalishi njia atumiayo ilimradi upo ukweli wa kila jambo basi mafanikio huja tu pale unapoamua kufanya mambo magumu kuwa mepesi, unapoamua kulitazama jua kwa ukali wake na kufumbua macho pale usiku unapokujia, kufanya yasiyotarajiwa na kuwa na roho yenye uwezo wa kujaribu jambo jipya siku zote. Usiogope lawama kama unataka kufanikiwa, hayo ndiyo yaliyoniwezesha kufika nilipo. Vyombo vya habari ni muhimu sana.” Alimaliza na hapo walishikana na mtangazaji,,,mahojiano haya yalifanyika kwa lugha ya kingereza, baada ya yale mahojiano kuisha Felly alikwenda kwenye kile kifaa cha kurekodi na kuichezesha tena kisha alishika rimoti na kutuambia tusikilize kwa makini upya.

    “sikiliza alichokisema hapa ‘Hii itakuwa ni hatua kubwa kwetu’, anamaanisha nini hapa? Ukisikiliza kwa masikio na mtazamo wa kawaida utaona kama vile ni maneno ya kawaida ila hii ni ishara ya jambo fulani, kati ya Mary na Mark kuna mmoja atakuwa si mtu wa kawaida” aliongea Felly huku akijaribu kurudia yale maneno tena.

    “Ni hatua kubwa kwa maana ya kwamba, biashara yao inakuwa na mtaji pia unakuwa” nilijaribu kutoa yale niliyoyafikiria lakini hata hivyo Felly hakuyasikiliza badala yake aliichezesha tena yale maneno na kuniambia nitazame vidole vya Mark na midomo yake alivyokuwa akitamka maneno yake,,alikuwa akisugua vidole na midomo yake ilionekana kama vile ilikuwa ikieleza kwa kutetemeka kwa mbali pale alipoikuza ile picha.

    “hii inamaana Mark hana uhakika na maana halisi ya maneno anayoyasema, kuna kitu anamaanisha, kama ingekuwa anamaana hiyo ambayo Patrick umeisema basi asingesema tena mbeleni kuwa ‘lakini hatua kubwa sana kwangu pia katika kuyafanya mambo yatokee’, hapa anamaana kuwa kuna mipango miwili, tazama mshipa wa damu wa kichwa wa upande wa kulia alipokuwa akitamka maneno hayo, utagundua ulikuwa umetokeza sana kuliko alipokuwa akitamka akiwa anasema ni hatua kubwa kwao, hii inamaana maneno ya pili aliyatoa kwa hisia za hasira” aliongezea Felly huku akiendelea kuichambua ile video, alikuwa makini kweli na mimi sikuwa na la kuongea.

    “Sikiliza tena hapa anasema ‘haijalishi njia atumiayo ilimradi upo ukweli wa kila jambo basi mafanikio huja tu pale unapoamua kufanya mambo magumu kuwa mepesi’hapa inamaana anahalalisha njia aliyoitumia kuwa tajiri, hili jambo walipanga muda ila inaonekana Mark anampango wake mwingine zaidi ya huo wa pamoja, kwenye sentensi hii ameongea mambo yasiyo na uhusiano ila ni katika kufikisha ujumbe, anasema anasema ‘ilimradi upo ukweli wa kila jambo’ alaf anasema bas mafanikio huja tu pale,,,,anaendelea, ukweli ni upi hapo anaousema je kuna uhusiano gani kati ya hayo aliyoyasema?” nilikuwa nimeshachoka mwili na roho mpaka dakika hii, mambo kwangu yalikuwa ni kawaida ila kwa aliyokuwa akiniambia yalikuwa mambo mazito na ya kuchosha. Nilijaribu kurudisha akili yangu nyuma japo kujua ni wapi Mary au Mark aliwahi kufanya jambo la kunitia wasiwasi lakini sikuona.

    “sikiliza hapa alivyosema tena ‘unapoamua kulitazama jua kwa ukali wake na kufumbua macho pale usiku unapokujia’ alikuwa anamaana si rahisi kulitazama jua au kufumba macho usiku wakati unatembea,,hii ni ishara kuwa unatakiwa kufanya yale usiyoweza yanayoweza kukuletea matatizo,,anakoleza kauli hii anaposema ‘Usiogope lawama kama unataka kufanikiwa, hayo ndiyo yaliyoniwezesha kufika nilipo’, ukiunganisha maneno yake yote hayo na neno la mwisho kuwa vyombo vya habari ni muhimu utajua kuwa anamaanisha, alifanya dhuluma kwakuwa hakuogopa, na alitumia vyombo vya habari kurekebisha ukweli wa jambo husika” alimaliza kuongea na kisha alikaa akinisikiliza kama nilikuwa nina lolote la kusema.

    “Nahitaji kurudi Tanzania” niliwaambia kwa kauli iliyojaa mchosho.

    “Patrick, huendi popote mpaka niwe na uhakika na usalama wako” aliongea Pamela kwa sauti iliyojaa kujiamini na kuondoka pale sebuleni kuelekea chumbani.

    “Patrick bado tupo nusu ya safari, tunatakiwa kujua mambo mengi sana kabla ya wewe kupanga chochote, kila siku unaona kabisa kunaibuka jipya, uchunguzi wa jambo hautakiwi kutolewa uamuzi mpaka pale ambapo kila kitu kitakuwa kimesemwa, kila kitu kitakapokuwa wazi ndipo hapo tutakapojaribu kutafuta mbinu utakazozitumia ili uweze kufanikisha kurudisha kila kitu chako, Mark na Mary ni matajiri wakubwa kwasasa waliojizatiti na wenye kukubalika, hivyo huwezi kwenda kichwakichwa tu na mambo yakawa sawa, nina utaalamu na haya mambo nipe nafasi nikusaidie.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    **MWEZI MOJA MBELE**



    Mimba ya Pamela ilishaanza kujitokeza kwa mbali na sasa nilianza kuwa namsaidia baadhi ya vitu ikiwa ndio ushauri wa daktari.

    Jioni ya siku ya jumatano nikiwa niko nyumbani Pamela alikuja na kunieleza kuwa amepata dharura inabidi asafiri kwenda India kwaajili ya kusoma kozi ya mwezi mmoja ambayo angekuja kuifanyia kazi pale. Ilikuwa ni taarifa ya ghafla na ilibidi nikubaliane naye tu sikuwa na jinsi wala namna ya kuzuia yale yasitokee, nisingeweza kuondoka naye kwakuwa bado nilihitajika kazini na hakukuwa na mtu yoyote wa kufanya kazi zangu.



    *****



    Jioni ya siku hiyo nikiwa na dokta Anderson tulimsindikiza Pamela uwanja wa ndege na alipanda ndege na kuondoka, tulipotoka pale mimi pamoja na mzee Anderson na mkewe tulikwenda kwenye mgahawa mmoja na kupata msosi wa jioni;

    “Patrick lazima sasa ujifunze kuanza upya mambo yako, lazima ukubali kuwa mambo yametokea na usonge mbele zaidi, hiyo ndio njia pekee ya kukusaidia wewe kuwa mpya tena kifikra” aliniambia mama Anderson huku akionyesha kuhuzunishwa sana na namna nilivyokuwa na mawazo.

    “ni kweli mama ila ni ngumu sana kusahau”

    “najua ni ngumu lakini kila lenye ugumu lina suluhisho ndani yake”

    “mama kipindi naanza maisha nilikuwa nimejiwekea misingi ya kuishi na namna ya kuishi, nilikuwa najua nguzo za kuishi na wapi nitapita, nilishatimiza robotatu ya ndoto zangu nilipokutana na Mary, na nilimuamini sana lakini haya yanayotokea sasa hivi yote naona kama ndoto”

    “Maisha ni mazuri sana ukipata wa kukupenda, mimi nilianza mapenzi na Sara miaka 30 iliyopita, moja kati ya wanawake ambao sikuwahi kuwaamini kabisa alikuwa Sara na hilo alikuwa analijua, alikuwa ni mchezaji wa kasino, alikuwa ni mwanamke ambaye kila mtu anamshika na kumfanya chochote, nilimpenda siku ya kwanza nilipokwenda kasino, kipindi hicho nilikuwa daktari kwenye hospitali moja Australia, nilimchukua na kumueleza nia yangu yakuwa naye, haikuwa rahisi sana kumpata lakini baada ya kumfata sana na kumuonyesha nia yangu ya dhati ya kutaka kumtoa kwenye ile hali yake alikubali, niliishi naye kwa mashaka makubwa sana, nilikuwa sifichi pesa zangu bali nilikuwa nikiziweka sehemu anapojua ili nijue kama atachukua au la, lakini kwa mwaka mzima hajawahi kufanya chochote zaidi ya kwamba alikuwa mlevi wa kupindukia, nilijua namna ya kumbadilisha, nikampeleka chuo akasoma na alipata shahada yake ya kwanza ya udaktari, nikamuweka karibu sana na mimi, baada ya mwaka toka amalize masomo tukafunga ndoa na akajifungua mtoto wetu wa kike. Maisha yakianza japo bado nilikuwa simuamini sana, lakini muda ulivyokwenda nilianza kumuamini na kiukweli nilikuwa nimejifunza kabisa kuwa mwanamke anaweza kuwa anafanya kazi yoyote ila kazi yake au vile alivyo haitakuwa utambulisho sahihi wa namna ambavyo atakuwa mwema au mkaidi kwa mumewe. Kipindi cha nyuma nilikuwa mchumba tuliyekuwa tunaimba kwaya kanisa moja huko SUVA, alikuwa ni msichana bikra na aliniambia nimsubiri nisiwe na haraka, tulijuana toka utoto wetu na wazazi walijua vizuri mahusiano yetu, lakini yule binti alikufa kwa kutoa mimba ambayo haikuwa yangu, nilipoteza matumain kabisa lakini nilikuja kugundua kuwa kazi kubwa moja wapo niliyonayo ilikuwa ni kufikiri kwa niaba ya furaha yangu, nilifanya hivyo na nikamuamini tena Sara na sasa ni mke wangu kwa miaka mingi sana. Nakuambia haya nikiwa na maana kwamba sasa hivi unanafasi ya kuyatengeneza upya maisha yako bila kuingia tena kwenye matatizo, umempata Pamela, msichana ambaye nimemlea na nina mfahamu kama mtu makini na asiye na tama, Pamela anaweza kukuonyesha mwanzo mpya kama hutaangalia tena kuhusu yaliyotokea” aliongea hayo na mimi nilitingisha kichwa kuonyesha kuwa nakubaliana naye japo haikuwa kweli, sikuwa tayari kuwa na roho nyepesi namna hiyo ya kuacha mambo yatokee kama hivyo, nilikaa na kuwa sikiliza kwa muda mrefu ila wao hawakujua kuwa sikuwa pale kabisa, akili yangu ilikuwa inapiga mahesabu makubwa kwa jambo kubwa ambalo nilikuwa natafuta mwanzo wangu tu.

    Akili na mawazo yangu yalikuwa yakimuwaza Mary,sikujua adhabu gani nimpe itakayoendana na kile alichokifanya,mda mwingine niliona kama Mary hakuwa na kosa maana yeye ni binadamu,ni kati ya wasichana warembo ambao walipanga kuwa na maendeleo na maisha yao toka utotoni,kuishi na mimi katika hali ambayo nilikuwa nayo kungempa usumbufu mkubwa pengine na aibu mbele ya wasichana wenzake,lakini upande mwingine wa moyo wangu uliniambia Mary hakunipenda kweli toka awali na kama alinipenda asingeniacha ugenini alaf aje kutangaza kuwa nimekufa,,kitu cha mwisho duniani ambacho nilitaka kuamini ni kuwa Mary alikuwa hanipendi toka awali,niliamini kabisa alikuwa akinipenda lakini hali yangu haikumruhusu yeye kuwa na mimi,kuamini huko kulikatishwa na kumbukumbu ya ahadi tuliyowekeana pale kanisani kuwa tutapendana katika shida na raha. Lakini kikubwa ni kwanini alikimbilia kubadili jina la kampuni yangu na kwanini basi alikuwa haraka sana ya kutaka kuzaa na Mark.

    “Patrick vumilia tengeneza kwanza maisha” aliniambia mama Anderson mda mfupi kabla ya wao kuondoka na kuniacha pale nikinywa ule mvinyo niliokuwa nimeuagiza, kwenye mida ya saa 4 usiku nikiwa pale, nilishtuka baada ya mtu kuja na kunifumba macho, niliishika ile mikono nikagundua ilikuwa ni ya mwanamke, lakini sikujua ni nani mpaka aliponiachia.

    “Mambo Patrick” alinisalimu huku akinitazama kwa makini usoni.

    “Safi tu habari yako” na mimi nilizidi kumkodolea macho.

    “Salama, kwanini unapenda kukaa peke yako Patrick” aliniuliza huku akisogeza kiti karibu yangu.

    “Hapana sikuwa mwenyewe, nilikuwa na watu hapa ila wameondoka muda sio mrefu sana, lakini pia ni kweli napenda kukaa mwenyewe hiyo inanifanya nipate muda mwingi sana wa kujifunza” alikuwa akinitazama huku akichezesha nyusi zake.

    “muhudumuu” alimuita muhudumu na alipokuja alimuagiza pombe kali.

    “Khajat kwanini unapenda kunywa pombe na dini yako hairuhusu” nilimuuliza huku nikimtazama, na yeye kwa tabasamu zito alisogea karibu tena na mimi.

    “Dini yetu hairuhusu mambo mengi sana, hata aina za mavazi wengi tunayovaa hayaruhusiwi, kufanya mapenzi kabla ya ndoa pia hairuhusiwi, haturuhusiwi kusuka rasta, kutengeneza nyuso zetu kwa vitu bandia, kuna mengi sana ambayo ukiyafanya haina tofauti sana na kufanya mengine” alinijibu na wakati huo ile chupa ya MCdowell ilikuwa imeshafika aliifungua huku akinitazama na kuweka kisha alikunywa pafu mbili kubwa na kunitazama huku akitabasamu.

    “sasa kama unajua mengi yanakatazwa kwanini unafanya?” niliendelea kumuuliza lakini hakuwa anajibu moja kwa moja.

    “aah ni kama wewe tu unavyofanya mapenzi na Pamela wakati hamjafunga ndoa na unajua ni dhambi” alinijibu kiufupi kisha wote tulicheka, alinimiminia kisha tuligonga glasi na kuendelea kunywa.

    “Ujue wengi hawajui ukweli wangu, mimi nimechukua jina la mama yangu, ila kiukweli mimi ni mpagani, sina dini wala sina imani yoyote, nilichukua jina hili ili nizidi kumchukia mama yangu, namchukia sana ndo mana naishi maisha haya unayoniona, niko kama mwanaume, ninaishi maisha ya uhuru usio na mipaka, nafanya kazi kwa bidii na mimi ni mbinafsi kuliko binadamu yoyote,,hahaa ila usiniulize kwanini namchukia mama yangu kwakuwa sitakujibu” nilikuwa nashangaa tu kusikia hayo, nilianza kugundua taratibu kuwa kila binadamu anahadithi yake ya maisha yake ya kusikitisha na pengine ya kukatisha tamaa ila tunatofautiana namna ya kuzikabili huzuni zetu, kila mmoja aliwahi kupitia jambo gumu lililomkatisha tamaa lakini wengi waliteseka na kukubali matokeo ya jambo hilo na baadaye walisonga mbele.

    Tulikaaa pale tukanywa na kupiga hadithi mpaka saa nane usiku kisha nilirejea nyumbani.

    “ngriii,,,,ngriii” nilikuwa bado nimelala na niliposhtuliwa na ule mlio wa simu niligundua kuwa kulikuwa kumekucha.

    “Haloo” niliitikia kwa ile sauti iliyojaa usingizi.

    “ndio, habari yako”

    “nzuri za kwako Pamela”

    “salama, yani Patrick nikiondoka ndo unalala mpaka muda wa kazini huu mpenzi, sasa utakunywa chai muda gani mpenzi” ilikuwa sauti ya Pamela ikiendelea kunisemesha na hapo nilinyanyuka na kwenda bafuni kuweka mswaki dawa.

    “kazini wataniandalia,,leo nimepitiliza usingizi mama, nilichelewa kulala jana” nilimweleza na kushtuka kuwa natengeneza swali lingine la wapi nilikuwepo mpaka nikashindwa kulala mapema.

    “ulienda kunywa pombe tena Patrick” nilikaa kimya baada ya swali hilo.

    “yeah, kidogo tu” nilimjibu huku nikiweka mswaki mdomoni.

    “unatakiwa upunguze Patrick” aliniambia hivyo na baada ya mazungumzo kidogo tuliagana na mimi niliamua kuelekea bafuni.





    **MWEZI MMOJA NA WIKI MOJA MBELE**



    Siku za kurudi Pamela zilikuwa zimefika lakini hakuwa amerudi kwakuwa alisema wameongezewa muda kidogo ili kumalizia baadhi ya vipindi. Siku zote kila jioni nilikuwa nikienda kwa Felly ilimkupata chakula cha jioni na kuoiga story nyingine nia ikiwa nikumfanya aweze kuharakisha sana uchunguzi juu ya swala langu.

    Jioni ya siku hiyo nilipotoka kazini Felly alinipita na kuniambia twende nyumbani kwake, tulienda na tulipofika alibadilisha nguo na kuingia jikoni na mimi nilienda kumsaidia, tulipika vizuri na chakula kilipokuwa tayari Felly alikwenda kuoga na mimi nilikuwa pale sebuleni nikimsubiri.

    Katika hali isiyokuwa ya kawaida Felly alikuja akiwa na taulo tu, iliyokuwa fupi kabisa na kuruhusu mabaja yake yote mpaka juu kuonekana, inawezekana kwa utamaduni wa kule ilikuwa ni sawa ila haikuwa sawa kwangu na yeye alifanya vile makusudi, alikuja mpaka mbele ya tv na kuinamba akirekebisha kebo hali iliyoacha kila kitu chake nje.

    “Felly unafanya nini?” nilimuuliza huku nikijizuia kumuangalia lakini haikuwa rahisikuacha kumuangalia, alikuwa amejazia mapaja yake yasiyokuwa na mikunjo kutokana na mazoezi aliyokuwa akiyafanya mara kwa mara, alikuwa na mapaja mazuri japo hayakuyafikia yale ya Pamela. Alikuwa ni mzuri sana ndani ya lile taulo na urefu wake ulimfanya azidi kuonekana mrembo kama vile twiga.

    “nimefanyaje kwani Patrick” aliniuliza huku akinyanyuka na kunifata pale kwenye kochi.

    “huoni..uuu…uu…livyo vaa” nilishikwa na kigugumizi hasa alipokuwa amenisogelea na kuachia lile taulo.

    “Hey, Felly acha bhana, si sawa hivi” nilimkatazama na wakati huo alishafika na kufungua shati langu kisha kupenyeza mikono yake na kuanza kucheza na kila alichokikuta.

    “Felly tafadhali acha” nilizidi kumsihi lakini alikuwa amedhamiria na hivyo alikuwa amebibana katika namna ambavyo nisingeweza kufanya chochote, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya yeye kupenyeza mikono ndani ya suruali yangu na mimi nilijikuta nimeshakutanisha mdomo wangu na wake na kuanza kupeleka mrejesho kwa matendo yake.

    “Felly” wote tulishtuka na kutazama mlangoni, aibu ilinipata na kila kitu nilihisi kimepooza.

    “Patrick, kweli ndo unachonifanyia?” alikuwa ni Pamela.

    “Ahh Pamela” sikuwa na la kusema hasa kwakuwa alikuwa sikuwa na cha kujitetea.

    “Felly kweli jamani” aliongea huku akilia lakini Felly hakuonekana kujali sana.

    Pamela aliondoka pale na kwa jazba na kuwasha gari lake kisha alitimka na kuondoka.

    “Felly tumefanya nini sasa” nilimuuliza Felly ambaye bado alikuwa uchi akiwa amelala pale kwenye kochi.

    “hahaa, usijali Patrick kila kitu kitakuwa sawa” aliongea hayo na mimi nilimrushia lile taulo lake ili ajifunike.

    “Kula Patrick kisha nenda kamfate Pamela” aliniambia huku akicheka, nilikuwa nimechanganyikiwa na nilikasirika sana kwa kilichotokea, sikutaka kabisa maisha yangu yote ya sasa kumuona Pamela akiwa na majonzi.

    Sikuweza tena kula nitoka nje na kuondoka mpaka kule nikamkuta Pamela akilia.

    “Pamela samahani nipe mda nijieleze” nilijaribu kumbembeleza lakini hakusikia kitu chochote.

    “sitaki uongee chochote, wewe niliyekuhudumia kwa miaka yote katika hali ngumu leo unanifanyia hivi? Patrick! Aliongea huku akilia, nilimbembeleza lakini haikuzaa matunda.

    “chukua kila kitu chako humu ndani na uondoke, nimekuambia ondoka kabla akili yangu haijabadilika, ni bora ningekuwa na Nancy kuliko wewe, nilikuona ni mwanaume pekee kumbe wewe ni wale wale” aliongea hayo na kwenda ndani akachukua mabegi yangu na kunitupia pale sebuleni.

    “Nimekuambia toka” nilikuwa sina jinsi zaidi ya kuinamba niokote mabegi yangu lakini nilikutana na mguu ukiokanyaga lile begi nisilinyanyue.

    “Pamela huna haja ya kumfukuza Patrick” Felly alimwambia Pamela na hapo niliona kama yeye ndiye alikuja kuharibu kabisa.

    “Felly na wewe ondoka kwangu” niliona jicho la hasira likimtoka Pamela na hapo sikuelewa nini kilikuwa kitokee.

    “Pamela, mchumba wangu hakufa vitani kama ilivyosemekana, alikufa kwa kulipiwa na bomu nililomuwekea mimi ndani ya begi lake lililokuwa na vitu vingine wakati akiondoka kwenda Iraq, siku hiyo wakati anaondoka nilitegesha bomu hilo kwa masaa ambayo yangemkuta akiwa Iraq, hii ni kwakuwa nilimpenda sana, na hiyo ndiyo sababu pia sina mwanaume hadi leo, nilimpenda na nitampenda daima. Nilimuhangaikia maisha yake yote,nilimtoa kwenye kuvuta unga mpaka nikamsomesha na kumtafutia nafasi jeshini ila alikosea kitu kimoja tu, HAKUJUA MIMI NI WA AINA GANI, alikufa na mimi ndiye nilimuua na nilimuua kwakuwa ALIFANYA MAPENZI NA WEWE, nyumba yangu ina kamera nyingi kila sehemu na siku ya tukio mlilewa na mlifanya mapenzi chumbani kwangu na juu ya kitanda changu, nafahamu kuwa hukuwa unampenda ila alikunywesha pombe na wewe ukawa tayari kufanya mapenzi na yeye, sababu ya kukuacha wewe ni kwakuwa ulirubuniwa tu na hukuwa na nia, lakini nilitaka ujifunze, na ndio maana uliponitumia ujumbe kuwa ulikuwa umeshafika uwanja wa ndege nilikuambia ukifika kwako uje kwangu haraka. Patrick amerubuniwa na mimi lakini nia yangu ilikuwa ni kukufundisha kuwa kuna muda kila mtu huumia kwa tendo analofanyiwa na mtu anayemtegemea, siku hiyo uliacha nguo yako ya ndani asubuhi baada ya kuamka ukiwa chumbani kwangu, hii hapa chukua”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “UKOSEFU WA FIKRA HURU NDIO UZAAO UTUMWA WA MAWAZO NA MATAZAMIO HAFIFU,,KIJANA MWENYE FIKRA MPAUKO HUWA NA MAWAZO MGANDO NA MITAZAMO MDEBWEDO, HUFIKIRI KWA LUGHA FULANI NA KUTENDA KWA UTAMADUNI WENYE KILEMA CHA UTASHI...HUWAZA KWA KWENDA MBELE YAKE NA KUTENDA KWA YALIYONYUMA YAKE,,,UKUBWA WA UBOVU WAKE NI MKONDO HASI WA AYAAMINIYO..HUFIKIRI KWA FIKRA TATA ZA WENGINE NA KUPAMBANUA KWA MAWAZO MTAMBUKA YA WASIOJIKUBALI,,MUHIMU KWAKE NI JIONI KILA IANZAPO ASUBUHI.AHUENI YA MAISHA YAKE NI MKONO UNYOOSHWAO ILI KUMBEBA NA SIO KUMUONYESHA NJIA”…..HII NI SEHEMU YA NANE.



    **PATRICK**

    Pamoja na Felly kujitokeza pale na kueleza nia yake ya kufanya hivyo bado hiyo haikuwa sababu ya mimi kusamehewa. Pamela alikuwa mkali sana na hakutaka kunisamehe hata kwa asilimia moja.

    “Ondoka nyumbani kwangu Patrick, ondoka sitaki kukuona hapa” aliongea Pamela huku akilia na kwikwi zikimbana.

    “Sikufanya chochote Pamela, naomba nielewe” nilimsihi huku nikimpigia magoti lakini hakutaka kunielewa. Felly alikuwa bado yuko pale akimtazama Pamela alichokuwa anakifanya.

    “Ulivyotoka na mchumba wangu ulifikiria nini Pamela mbona unashindwa kuelewa hili ambalo Patrick hakufanya?” Felly alijaribu kujielezea lakini hiyo haikusaidia kitu. Haikuwa rahisi kabisa kwa Pamela kuelewa.

    “Felly hili halikuhusu, kaa mbali na mimi. Kama ilitokea kipindi hicho ni kwakuwa mchumba wako alikuwa ameninywesha pombe. Sikufurahia hata mimi na ndio maana namchukia hadi leo. Kama ulikuwa unajaribu kulipa kisasi sina shaka na hilo na wala sina shaka na wewe. Ulitakiwa uniulize kwanza ilikuwaje. Mchumba wako alinibaka kwa tafsiri nyepesi na sio kwamba nilimvulia nguo. Hivyo kama na wewe umembaka Patrick basi ondoka naye kabisa mimi simuhitaji tena hata kwa sekunde moja” yalikuwa maneno ya Pamela kwenda kwa Felly. Sikuelewa vizuri kilichokuwa kikiendelea pale lakini pia sikutaka kuwa sababu ya mnyukano ule wa maneno.

    “Sikiliza nikuambie rafiki yangu mpenzi Pamela. Siku uliyofanya mapenzi na mchumba nilikuwa nimeenda kwenye operesheni ya kijeshi nchini Korea, siku ile ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa na nilirudi nikiwa na furaha sana kwakuwa nilijua nitakuja kuutumia muda wangu na yeye siku hiyo baada ya kuwa nje ya nyumbani kwa zaidi ya miezi miwili. Nilimkosa sana kwa kipindi chote hicho. Lakini nilipofika nyumbani siku ile hakuwa sawa, alikuwa hata hakumbuki kama siku hiyo ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa, hilo halikuwa ni shida sana kwangu. Lakini shida ilikuja kuanza nilipohitaji kufanya nae mapenzi siku ile, hakuwa kwenye hali ya kufanya mapenzi kabisa kwakuwa alikuwa amechoka na alionekana kutokuwa na hamu ya kufanya hivyo hiyo ilinifanya nifanye uchunguzi ni kwanini imekuwa hivi, nilimfahamu sana mchumba wangu kwahiyo anapokuwa hayuko katika hali fulani huwa najua kuna kitu katikati yetu. Nilimuuliza kwanini amechoka sana lakini alinijibu bila kunitazama usoni, hii ilimaanisha kuwa kuna kitu hakuwa anakisema. Hivyo kwakuwa yeye hakuwa anaijua vizuri nyumba yangu ilikuwa rahisi sana mimi kuujua ukweli kama alikuwa anadanganya. Nilikwenda kwenye kamera za pale ndani na kutazama yaliyotokea kwa kipindi hicho, nilikuta matukio ya wiki mbili nzima ambayo mliitumia wewe na mchumba wangu. Mlifanya mapenzi siku ya kwanza ambapo mlikunywa pombe mkalewa na hamkujielewa wote, mkalala kwenye kitanda changu na mkafanya yenu. Alikuja kukuomba msamaha kwa kilichotokea siku mbili mbele na wewe ukamwambia haina shida. Mkaendelea kuwa mnakuja na kushinda kwangu, hiyo haikuwa shida sana kwangu, shida ilikuja pale ambapo mlifanya mapenzi tena usiku wa kuamkia siku ambayo nilikuwa nikirudi nyumbani, usiku wa kuamkia siku yangu ya kuzaliwa. Mlikuwa kwangu na mlikuwa mnakunywa kama kawaida yenu, lakini wakati wewe ukinywa mchumba wangu alikuwa akicheza kujifanya kuwa amelewa lakini kumbe hakuwa amelewa bali alitaka tu ulewe afanye mapenzi na wewe. Na alifanikiwa. Kilichonifanya nimchukie yeye na sio wewe ni kwakuwa baada ya kosa la kwanza ulimwambia hujapenda na si sawa kwakuwa mimi ni rafiki yako. Na pia siku ya tukio la mwisho ulimwambia kuwa hata kama mkilewa vipi kila mtu aiangalie akili yake. Hii haikuwa mara yake ya kwanza na ndio mana niliamua kumfanya asiwepo tena duniani. Hivyo si kwamba ulibakwa, hapana, ili ubakwe lazima uwe hujapata nafasi ya kuepuka kubakwa. Ila wewe ulifanya mapenzi naye kwakuwa ulikuwa na nafasi ya kuepuka kwa kutokunywa naye pombe tena. Hujabakwa ila ulishawishiwa” aliongea Felly huku akizunguka pale sebuleni.

    “Hivyo umeamua kulipa kisasi?” Pamela aliuliza.

    “Sijui kama ni kisasi lakini nilitaka kupata nafasi ya kutoa lililo moyoni mwangu kwa muda mrefu sasa, nilitaka uumie japo kwa dakika mbili tu kama mimi nilivyoumia kwa miaka sasa, ni kisasi kidogo sana hicho kisichokuwa na uhalisia ndani yake. Patrick ni mwanaume ambaye sio tu anakupenda ila si mwepesi sana kukusahau. Nilifanya makusudi na kwakulazimisha kwakuwa nilijua upo karibu na kwangu, hivyo nimefurahi kwamba umeumia kiasi na sasa tunaweza kuanza upya. Ila jua sijafanya chochote na Patrick” alimaliza kuyasema hayo na kuondoka zake. Pamela alikaa chini na kulia sana na nilipomfata kuongea naye hakutaka nimguse.

    “Patrick msimamo wangu bado ni mmoja, ondoka, sikuamini wewe wala Felly. Ondoka kabisa kwakuwa umeniumiza sana”. Sikuwa na namna zaidi ya kuingia ndani na kukusanya kila kilichokuwa changu, nilibeba nguo zangu na kila kitu kisha nilimfata pale sebuleni nikambusu na kuondoka mpaka Villa Hotel ambapo nilipanga chumba.

    *****

    Maisha bila Pamela hayakuwa rahisi kabisa, kwani sikuweza kuonana naye wala kupata taarifa yeyote juu ya mimba yake ambayo kwasasa ilibaki muda mchache sana ajifungue. Nilikuwa nikienda kazini lakini mara nyingi sana nilikuwa nikiwaza juu ya hatima ya maisha yangu.

    ****

    “Hallo” ulikuwa ujumbe wa simu toka kwa Khajat.

    “nambie” nilimjibu kwa neno hilo.

    “Safi, sijakuona muda mrefu sana, kuna tatizo lolote?” aliniuliza lakini sikuwa na kikubwa sana cha kumjibu.

    “Hapana hakuna tatizo” nilimjibu na yeye alinitumia tena ujumbe wa mwisho.

    “Tukutane Cambria jioni hii, upande wa kasino” alimaliza kwa ujumbe huo na mimi nilikubaliana naye.

    ****

    Jioni ya siku hiyo nilikwenda Cambria kukutana na Khajat. Nilfika mpaka sehemu aliyonielekeza lakini sikumkumkuta hivyo ikanibidi nikae tu nikimsubiri. Nilinunua kinywaji na kuamua kuketi sehemu ya peke yangu nikitafakari yaliyokuwa yakitokea kwenye maisha yangu. Niliwaza sana juu ya hatima ya mtoto wangu ambaye atazaliwa hivi karibuni lakini sikupata jibu.

    “Hey, acha kuwaza Patrick maisha ni leo na jana iliyopita, hatuijui kesho yetu hivyo mbali na kuiwaza kesho inayotuumiza inatubidi tuiishi kwa furaha leo iwapo faraja” aliongea Khajat baada ya kufika. Khajati alikuwa ni msichana mwenye umbo dogo lakini mrembo sana, nilikuwa kila nikimuona namfananisha na msichana Kalinda Sharma aliyeingiza kama mpelelezi binafsi kwenye filamu ya THE GOOD WIFE aliyekuwa rafiki wa karibu wa Alicia Florick mkewe na Peter Florick. Khajat alikuwa ni mchangamfu sana lakini aliyetumia ucheshi wake kuficha udhaifu wake wa kimapenzi, hakutaka kupenda wala kuingia kwenye mapenzi kwakuwa tu na yeye hakuwapenda sana wanaume ila alijitahidi kumfanya kila mwanaume rafiki yake mkubwa wanayeheshimiana ili kuzuia hisia za mapenzi kuingia ndani ya moyo wa yeyote kati yao.

    “mh! Asante sana Khajat, huwa siku zote wewe ni mtu wa matumaini” nilimueleza hayo baada ya yeye kumaliza.

    “karibu tena, vipi mchumba wako anaendeleaje” aliniuliza huku akibugia ile pombe kali iliyokuwa kwenye glasi yake.

    “aaahh,” nilivuta pumzi nikakosa cha kusema lakini kabla sijanyanyua tena mdomo na kuongea Khajat alikuwa ameshaanza kuongea tena.

    “Usijali nafahamu kila kitu. Patrick usijione huna bahati, maisha yana mengi ambayo ni msamiati kwenye fikra zetu. Majibu sahihi kwa msamiati ambao huujui ni kubahatisha jibu la swali ambalo hujalisikia. Hivyo unachotakiwa kufanya ni kuiambia imani yako itawale utashi wako”. Sikuyaelewa maneno yake lakini nilikuwa nikijiuliza juu ya busara yake.

    “huwa unatoa wapi maneno hayo Khajat”. Nilimuuliza huku nikimtizama usoni.

    “Nimepitia mengi sana Patrick, mengi sana mazito. Tuondoke” alininyanyua pale na kunishika mkono kisha tulielekea kwenye chumba kimoja ndani ya ile kasino kisha nilimshuhudia akivua nguo zote na kupaki na nguo ya ndani tu

    “Unafanya nini Khajat” nilimuuliza huku macho yakinitoka kama panya aliebanwa na mlango.

    “Nataka nikuonyeshe kitu fulani kwenye mwili wangu” aligeuka na kunipa mgongo, alikuwa na alama za mikwaruzo mikubwa kwenye mwili wake kama vile alichomwa na kitu au kuchapwa sana na waya tena mfululizo.

    “ni nini hicho Khajat” nilimuuliza na kumsogelea kisha nilizishika zile alama ili nijue ni nini kile lakini sikuweza kupata jibu la haraka.

    “Huu ni unyama niliofanyiwa miaka mingi iliyopita, hii ni sababu ya mimi kumchukia mama yangu mzazi” Alivaa nguo zake na kuniambia turudi tulikokuwa. Nilikuwa nimepigwa na butwaa na shauku ya kutakaka kujua tatizo ni nini.

    “Utajua kila kitu siku moja Patrick, nilitaka kukuonyesha tu kuwa kuna watu wanamatatizo mengi sana lakini hawawezi kuyaonysha au kuwa na huzuni maishani mwao. Nimeishi miaka mingi na hata dada yangu hajui kilichonitokea baada ya yeye kutoroka nyumbani akiwa na miaka mitano, alikimbia haya yaliyonikuta mimi. Lakini leo hii nataka unisindikize sehemu nikakufundishe kitu, hivyo malizia kwanza hicho kinywaji alafu tuondoke” alimaliza kuongea na kunyanyuka kisha na mimi nilimalizia kile kinywaji na kunyanyuka kuondoka naye, tulipofika nje aliingia kwenye gari yake na mimi niliingia kisha aliliondoa gari kwa kasi sana.

    Kilomita 15 mbele alilipaki gari pembeni na kunigeukia.

    “Patrick umefanyiwa ubaya si ndio” aliniuliza kwa macho makali.

    “Ndio, Mary amenifanyia ubaya sana” nilimjibu huku na mimi nikimtizama.

    “Unataka kumfanya nini? Aliniuliza huku akinitazama.

    “Sijui hata ninachotaka kufanya” nilimjibu kiunyonge kwakuwa ni kweli sikujua cha kufanya japo nilijua nataka kulipa kisasi.

    “Wakati shemeji yangu amemsaliti dada yangu, nilimuuliza dada yangu swali hilo na alinipa jibu kama lako, lakini nilimuambia kama anataka kulipa kisasi basi ni lazima kwanza achimbe makaburi mawili, moja lake na lingine la shemeji yangu. Katika kulipiza kisasi unaweza kukuta adui yako ananguvu kuliko wewe hivyo lazima ujitolee, ama yeye aingie kwenye kaburi lake au wewe uingie. Unapolipa kisasi hutakiwi kuwa na chakupoteza. Mara unapoanza mbio za kulipa kisasi basi jua kabisa hakuna kusimamal. Hutakiwi kumuogopa adui yako bali kuiamini na kuiabudu hasira yako. Sababu ya kwanini mimi sina dini ni kwakuwa sikutaka kubanwa na amri yoyote ile nitakapokuwa tayari kulipa kisasi. Kuwa na moyo wa uvumilivu na ujasiri wa nafsi nikufundishe maisha” aliongea hivyo huku machozi yakimchuruzika na kuwasha gari, alikanyaga mafuta kwa kasi sana na kuondoka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Njia nzima alikuwa akinieleza mambo ambayo sikuyaelewa sana kwakuwa nilikuwa nawaza juu yake kuwa yeye ni mtu wa aina gani, mshale kwenye sehemu ya kuonysha mwendo kasi ulikuwa unasoma 240 kwa maana kuwa zilikuwa zimebaki 20 tu kumaliza mwendo wote wa gari. Ilikuwa ni kasi ya ajabu sana na machozi yalikuwa yakimtoka sana.

    “Niliisubiri siku hii kwa muda mrefu sana wa maisha yangu, nilipoteza furaha yangu kwa muda mrefu na kuishi nikiwa na furaha ya kughushi kwa siku zote za maisha yangu, kwakuwa mtu mmoja tu aliamua mimi niishi hivyo”. Aliongea huku akilia.

    “kuna nini kwani Khajat?” nilimuuliza tena huku nikimsihi apunguze spidi ya gari.

    “Umeona zile alama mgongoni mwangu, yule aliyenifanyia leo hii nataka na yeye apate uchungu wa kile nilichopata mimi. Sitaki kumuona tena katika maisha yangu. Nimevumilia lakini sina namna ya kutafuta Amani yangu zaidi ya kumfanya asiishi”. Aliongea huku akizidisha spidi.

    “Sasa kwanini umenichukua mimi” nilimuuliza huku nikimgeukia. Roho yangu iliingia woga kiasi na hasa ukizingatia sikuwa na ujuzi na mambo ya kijasusi kama yale.

    “Nakufundisha jinsi ya kuishi na maadui zako, kwenye maisha usiogope kutafuta furaha yako kwa damu ya yule anayeikatisha, tofauti ya mimi na wewe ni kwamba wewe una dini na mimi sina, ila naamini wewe una mungu ambaye ndiye aliyeniumba mimi lakini kwenye kisasi huwa namuomba mungu anisaidie niwaone adui zangu wakitaabika kama mimi” aliongea hayo na hapo alisimamisha gari kwa ghafla.

    “Patrick utakuwa mtu wa kudhulumiwa kwa siku zote za maisha yako. Kuwa mwanaume. Huwezi kulipa kisasi kama huna roho ngumu. Hakuna haja ya kumchekea mtu aliyetaka kukudhuru. Maana halisi ya kulipa kisasi ni kumfundisha adui yako njia bora aliyotakiwa kwenda” aliongezea tena maneno hayo lakini bado nilikuwa na uoga ndani yangu.

    “Lakini kuua ni dhambi” nilimueleza lakini bado hakuelewa akawasha gari na tukaendelea tena na safari.

    “Hakuna anayeweza kuiua roho, dini yako ndivyo isemavyo. Anayeua roho ni yeye tu aliyeiumba. Ninachofanya mimi ni kuua mwili, iwe dhambi au thawabu hilo silijui kwakuwa sifahamu chochote kuhusu maisha ya kusadikika, siishi kwa kusadiki, naishi kwa uhalisia wa kile nikionacho. Historia ya maisha yangu ni uhalisia tosha wa roho mbaya za watu wanaoishi dunia hii, na ili yasimtokee mwingine basi kila mbegu ileteyo madhara na itafukiwa”

    Tulifika eno la msituni na hapo tulishuka kisha aliniongoza njia kwenda kwenye shimbo lenye urefu wa futi sita lililokuwa limechimbwa pale msituni kisha aliniambia nisubiri pale na nilipomuangalia niliona akitoa kitu kwenye buti la gari yake. Kwakuwa ilikuwa ni usiku sikuona vizuri lakini alipofika pale ndio niligundua alikuwa ni mtu aliyefungwa mikono yote.

    “Ni nini unafanya Khajat” nilimuuliza na hakuniambia kitu zaidi ya kunipa jicho kali lililonifanya nikae kimya. Alimfungua kitambaa yule mama aliyeonekana kuwa na asili ya kihindi au kiarabu kisha alimuegemesha kwenye mti na kuanza kumuangalia huku machozi yakimtoka. Yule mama alikuwa amechakaa kwa majeraha mwili mzima yaliyoonyesha kuwa alikuwa amepigwa na kufungwa bandeji.

    “Mama siku uliyotenda kosa kubwa sana kwenye maisha yako, ni siku uliyoacha kuitoa mimba niliyokuwepo mimi. Umekuwa muda mwingi sana ukiniambia kuwa ulinizaa kwa makosa, umenitesa kama mimi si mtoto wako, umenidumbukiza chooni nikaokolewa, ukaona haitoshi ukanifanya mfungwa katika umri mdogo na kunipiga sana kama sikuwa mwanao. Hiyo haikutosha, ukanipeleka mahabusu kwakosa ambalo silijui, nikabakwa mpaka kizazi kikatoka. Nilipotoka ukaona haitoshi wakati nataka kutoroka kwako ukanikamata na kuanza kunitesa tena, yote haya ni kwasababu ulimchukia sana baba ambaye naye ulimuua. Umenitesa sana lakini sikujua kwanini. Mara zote nilikosa pa kwenda kushitaki maana kila sehemu nilijulikana kama mtoto mtukutu, leo hii nataka uniambie sababu ya kunitesa tena nikiwa kwenye umri mdogo vile”. Nilishangaa kwa yale aliyokuwa akiongea Khajat.

    “Wewe sio mwanangu. Wewe ni mtoto wa mwanamke mmoja aitwaye Khajat, alikuwa ni mwanamke katili sana. Alitembea na mume wangu ambaye ndiye yule uliyedhani kuwa ni baba yako. Baada ya kumuambia kuhusu swala la yeye kutembea na mume wangu hakunielewa, aliendelea kupoteza Amani ya nyumba yangu. Taratibu mume wangu akawa hanisikii tena, akaamua kuhama na nyumba. Mimi na mume wangu tulitoka mbali sana, toka kipindi cha shule hadi tulipofikia kuoana. Lakini mama yako alikuwa haelewi, alimfanya mume wangu awe dhaifu na hakuona huruma yoyote. Kuna muda nilimfata mume wangu nyumbani kwa mama yako lakini niliishia kupigwa kama mbwa. Hakunionea huruma kama mwanamke mwenzake, hiyo haikutosha kabisa alikuja na kuchukua kila kitu changu. Akaondoka nacho wakaniacha nikiwa sina chochote. Wakanisingizia kuwafanyia fujo na mahakama ikanihukumu kwenda jela mwaka mmoja. Nilipotoka nilikwenda kwao kumuomba mume wangu tuanze maisha mapya lakini haikuwa hivyo, alinipiga sana siku hiyo kwa shinikizo la mama yako. Nakumbuka mama yako alinipiga na kiti tumboni. Niliumwa na tumbo kwa muda mrefu sana, niliishi kwa maumivu makali na hapo ndipo mama yako aliponichukua niishi nao pale kwakuwa walihofia ningekufa. Mama yako alikuwa ni nesi, hivyo alikataa nisipelekwe hospitali na kwakuwa mume wangu hakuwa na usemi kwake alikubali, sikuwa naweza kutembea hivyo sikuweza kwenda popote. Siku moja mama yako alikuja na daktari ambaye ni kaka yake na akamwambia anitoe kizazi kwakuwa nilikuwa naumwa sana. Walifanya hivyo na hapo hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakati huo mama yako alikuwa na ujauzito wa miezi nane. Baadaye ulipozaliwa na mimi nilikuwa nimepata nafuu. Niliamua kumuua mama yako kwa sumu na kabla hajafa nilimueleza wazi kuwa huko atakapokuwa atashuhudia mwanae akiyapitia magumu niliyoyapitia mimi. Hiyo ilikua ahadi yangu na ndiyo maana niliamua kukutesa nikiamini kuwa huko aliko anaona. Nilimuua mume wangu pia kama njia ya kumaliza hisia zangu” yule mama alihadithia mkasa ulionifanya nione mwili wangu ukitetemeka.

    “Kaburi la mama yangu liko wapi” aliuliza Khajat kwa sauti kavu.

    “Lipo Bombay huko India” alijibu hivyo na hapo Khajat alimuuliza eneo lilipo na yeye alitaja. Alikuwa akiomba msamaha na kumuambia Khajat amsamehe lakini haikusaidia, Khajati aliondoka na kwenda kwenye gari na aliporudi alirudi na mtungi mdogo sana wa gesi wenye kidude cha kupachika puani na mdomoni. Kisha alimvalisha na kuifunga vizuri ile gesi, kisha alinigeukia na kunitazama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nilikuambia unapoanza mbio za kisasi hakuna kusimama, wala kurudi nyuma, hata ikitokea silaha ya kulipia kisasi imedondoka we songa mbele utapata namna nyingine. Ukirudi nyuma au kuyumbishwa na historia uchwara utajikuta umesahau njia ya malipizi” aliniambia huku akiwa amenikazia macho na kumgeukia tena yule mama.

    “Ubaya wa kisasi ni kwamba, mzunguko wake huwa mrefu sana, ungeamua kuishi na mimi vizuri bila kunidhuru ungekuwa salama leo, nisingelipiza na mimi. Lazima kuwe na mtu wa kumaliza kisasi kwa kukubali kukaa bila kulipa kisasi ili kisiendelee, lakini mtu huyo hawezi kuwa mimi. HIYO GESI KIDOGO ITAKAPOISHA NADHANI ITAMAANISHA MWISHO WAKO PIA. Kwaheri” alimsukumia kwenye lile shimbo na kuanza kufukia mpka lilipofunga kabisa na hapo alienda kuleta gari na kupita juu ya lile shimo mara nyingi zaidi mpaka alipohakikisha kuwa udongo umekuwa mgumu.

    “Ingia kwenye gari tuondoke Patrick”







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog