Simulizi : Afande Anahusika
Sehemu Ya Tatu (3)
“Mkuu picha hii ya juzi ipo tofauti na ile ya jana ambayo pia ni tofauti na mandhari ya sasa,” Inspekta alipokea Kamera na kuiangalia picha iliopo, baada ya kuiona tu, akatazama juu kwenye dari la nyumba ile, akaiona tofauti.
Ilikuwa ni tofauti ndogo sana, ambayo ni mpelelezi pekee anaweza kuigundua ama mwenye chumba mwenyewe. Sehemu ya mlango wadari ilikuwa ipo wazi kwa ufinyu mdogo mno.
Wakasogea pale pale chini na kuangalia kwa umakini zaidi, hapo ndio wakahakiki kuwa pale palivyo, hawakupa acha vile siku ya kwanza baada ya mauaji ya MwanaHamis, hapo ndio wakagundua kitu.
“Ni kweli Marsha, juzi picha zinatuonesha palikuwa pamefunikwa vizuri sana hapa kwenye mlango wa dari, iweje leo uwe wazi kidogo? Nahisi hapa kuna uhusiano wa matukio haya ya mauaji yaliyotokea ndani ya chumba hiki” wakatafakari na kumuita tena mama Kubwa.
Walichofanya sasa ni kumuonesha dari na kumuuliza tu kuwa juu ya dari ya nyumba ile kuna vitu huwa wanahifadhi? Akashangaa kwanza kwa kuoneshwa uwazi ule mdogo uliopo na kusema hakuna kitu chochote kinachowekwa darini.
Wakamuuliza tena kuna mtu aliingia baada ya wao kuacha chumba kimefungwa siku ile ya kwanza? Akakana na kusema kuwa hakuna mtu yeyote alie ingia mle ndani zaidi ya MwanaKheri.
Inspekta akamwambia mama mwenye nyumba amletee tochi kama ipo, mama Kubwa akasema anayo, akaifuata na kurudi nayo, wakati huo Inspekta tayari alikuwa amepanda juu na kufunua sehemu ile ya mlango wa dari.
Kwa tahadhari kubwa akaingiza kichwa chae ili kutazama sehemu ya ndani ya dari, alipotazaama baada ya kupewa tochi, hakuweza kuona chochote, akaingia zaidi, alichoweza kuona ni alama ya kujivuta tu na kuweka mistari kuonesha kuwa kulikuwa na mtu kule juu hivi karibuni.
Akashuka na kumtaarifu Marsha kile alichokiona na tangu hapo kukawa hakuna jipya tena, wakamuaga Mama Kubwa na kutoka wakimuahidi mama Kubwa kuwa atawaona tu sana hapo na ikiwa kuna jambo lolote, basi asisite kuwajulisha
“Namba yetu si unayo?” aliuliza Marsha huku akimtazama Mama Kubwa.
“Ndio ninayo ya Inspekta na Joy anayo nyingine ya Yule askari mwingine,” wakatoka na box tupu la majani ya chai na mfuko mtupu wa Sukari hadi garini kwao ili kuondoka.
Wakiwa nje ya gari Inspekta alimrushia funguo Afande Marsh na kushika kitasa cha mlango akisubiri Marsha aingie garini na kumfungulia ili waondoke pale kurejea kazini.
Marsha akashika Sterling na kuondoa gari ile kwa mwendo wa taratibu mno huku akionekana kama amesongwa na mawazo, kushoto kwake alikuwepo Inspekta Kalindimya ambae nae alikuwa kimya kabisa, hivyo kufanya safari kuwa ni ya Kimyakimya pasina yeyote kuongea.
Kimya kilitawala hadi pale Inspekta alipokikata kwa kumuuliza Marsha anayaonaje matukio yale ya mauaji yanayo Endelea? Marsha akaonekana ni kama mtu alietwishwa mzigo mzito asio weza kuubeba.
Lakini akanyanyua ulimi na kuseam inaonesha muuaji alikuwa amejipanga sawa sawa.
“Ni kweli Marsha, kinacho nichanganya kingine ni kuwa vipi ile Cealing board jana hatukuiona?”
“Mkuu umeona jinsi ilivyokuwa imewekwa? Kwa muda ule tulivyokuwa na haraka vile, isingewezekana kuona jambo hilo,” aliongea huku akipangua gear za gari na kunyamaza.
“Inavyo onesha muuaji alijificha juu kwenye Sailing board, lakini sasa aliingiaje?”
“Muuaji atakuwa alilala huko juu na kumuua MwanaKheri, lakini bado jibu halijapatikana, aliingiaje kumuua MwanaHamis?kabla hilo swali halikujibiwa, inspekta akaongezea
“Kingine ambacho naweza kukitazama hapa kwa haraka ni juu ya mauaji, hadi sasa walio uawa ni watu wawili, tena ni marafiki, majina ya wahanga wote wawili yakiwa yana anziwa na Mwana, japo mbele ni tofauti,”
“Na ukitazama kwa umakini utagundua tofauti ya vifo vyao ni masaa kadhaa wala si siku, tena ndani ya chumba kimoja, utata mtupu!” aliongezea Marsha.
“Hapo sasa!Na ajabu zaidi anaaacha ujumbe kwenye visu vya aina moja, Sijui ni kipi amemaanisha hapo?” walikuwa wakijiuliza maswali mengi huku wakiwa hawana majibu hata chembe.
“Inspekta kwa kweli maswali ni mengi sana…”
“Na sisi ndio tunaopaswa kuyatafutia majibu,” aliongea Unspekta na kuufunga rasmi mjadala huo na kimya kikarudi kutawala tena.
Kimya kifupi tu kikakatishwa tena na sauti ya Marsha alieuliza kuwa safari yao inaishia kituoni amam kuna sehemu nyingine? Inspekta akamwambia ampeleke tu nyumbani kwake akapumzishe kichwa maana anahisi tayari ameisha choka japo muda wa kazi haujaisha.
Inspekta baada ya kufika kwake akamwambia Marsha aende tu na gari ila afanye kila linalowezekana wakutane ofisini saa kumi na moja jioni kuna mahali wanapaswa kwenda muda huo.
“Sasa boss wewe utakuwa huna usafiri, unaonaje mimi nikipitia hapa ili kukuchukua?”
“Pia si wazo baya, utafanya vizuri,” akafungua mlango na kutoka kuelekea ndani ya nyumba yake.
Lengo la kurudi nyumbani muda ule lilikuwa ni kujipumzisha kutokana na kuchoka kwa akili yake, lakini mara tu alipoingia ndani, hakujipumzisha kama alivyotamani, bali alipoketi kwenye sofa la watu wawili ambalo aliona ni muafaka kwa yeye kupumzika, akakumbuka kitu.
Alikumbuka ile karatasi ya namba ya simu aliyochukua kwenye kabati la marehemu mwana na kuanza kuiangalia huku akiwa makiinanamba zile. Hakuwa anajua ni kipi anachokitafuta, bali alihisi kuna kitu atakijua kupitia namba zile.
Kwa kuwa hakujua ni kipi akitafutacho pale, akatoa simu yake ya mkononi na kuangalia namba zile za simu zilizompigia ili kumpa taarifa ya vifo vya kina Mwana wote wawili.
Aliziandika pembeni kwenye karatasi ileile ya namba zile za simu alizochukua kwa Mwana na kisha akapiga ofisini kwao na kumtaka mtu wa idara ya mawasiliano (Operator) amueleze namba zile za simu ya mezani ni za wapi.
Alimtajia na upande wa pili ukamwambia utamjulisha baada ya dakika chache, akakata simu na kuendelea na kazi nyingine ndogondogo, uchofu hauku wepo tena, alitamani tu kuendelea kuieleleza ile kesi, aliamini kabisa kuwa muuaji ni mtu ambae haitowapa shida kumkamata.
Operator wa jeshi la Polisi alifanya kazi ile ya kuzitafuta nmba zile ili kuzibaini zilikuwa ni za wapi, haikuchukua muda akampigia boss wake na kumueleza kwamba namba zile zote zilizotumika kumpigia simu zipo Wilaya ya Kinondoni, hizo Call box zake nazo zote mbili, yaani namba zote zilizotumika kumpigia simu yeye Inspekta, nazo zipo Mwananyamala ila ni sehemu tofauti
“Namba iliotumika kukupigia juzi, ipo Mwana nyamala A, na hiyo nyingine haipo mbali, bali ipo Mwana Nyamala Hospitali, utaona kuwa zipo karibi karibu mno, haifiki hata mita mia tatu,” alielezea Operator na kunyamaza.
“Ahsante sana kwa kazi nzuri,” Inspekta alijibu na kukata simu na kuanza tena uchunguzi mpya, maana sasa alibaini kitu kipya.
Alibaini sasa kuwa katika yale matukio yote mawili, muuaji sio mtu mmoja, alitambua kuna watu zaidi ya mmoja ambao wanfanya mauaji yale, ama niseme anaeua na anaepiga simu ni watu wawili tofauti kabisa.
Simu yake ya mkononi ambayo sasa alikuwa ameiweka mezani, akainyanyua na kumpigia simu Jitu kumuuliza alipo. Jitu akamwambia bado hajarejea kutoka huko alipokuwa, akakata simu Inspekta na kumpigia simu Marsha na kumwambia kuwa kitu anataka kuongea nae, aende kwake muda ule.
Marsha akamwambia kuwa amefika ofisini na kumkuta mkuu ambae alimuita na sasa anaelekea huko, hivyo ampe kama nusu saa hivi atakuwa amefika huko kwake, wakakubaliana hivyo na kila mmoja akaendelea na hamsini zake.
Inspekta akaketi vizuri mezani kwake na kuchukua karatasi mpya kabisa, alitaka sasa kucheza na namba zile ambazo zilikuwa zikiachwa kwenye mikono ya visu vya wauaji.
Aliisumbua sana akili yake kwa kujaribu na kufananisha na namba za simu zile alizozichukua kwa Mwana, lakini wapi. Akajaribu kuzijumlisha zile za kwanza na zaz pili kwa kudhani atapata kitu Fulani, lakini bado.
Mara ya tatu akajaribu kuzitoa namba zile zenyewe kwa zenyewe, lakini hakuambulia kitu, kila alichojaribu hakufanikiwa akaona anaichosha akili, aipumzishe kwanza.
Hapo ndio akasikia sauti ya hodi kwenye mlango wake, alipotazama saa akajua huyo atakuwa ni Marsha amefika, alisogea mlangoni na kumfungulia aingie ndani, Marsha alitii na kutoa saluti kwa mkuu wake kisha wakaelekea sofani kuketi.
“Marsha kuna kitu hapa tayari nimekijua, ndio maana nimekuita ili tujue tunafanyeje,” alianza Inspekta kuongea
“Ni kitu gani hicho boss?”
“Nimegundua hapa kwamba Muuaji wa Mwana heri na mtu alienipigia simu ni mtu mwingine, yaani ni watu tofauti kabisa,”
“Kivipi Boss?” akauliza huku akijiweka vizuri kwenye sofa, Inspekta akachukua moja kati ya karatasi yenye maelezo na ramani aliyochora toka Mwananyamala hadi Magomeni, akampa Marsha huku akimueleweshahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwenye ile simu ya kwanza, yaani ya kifo cha Mwanahamis, yenyewe wala hainisumbui kichwa, kuna tofauti ya zaidi ya dakika thelethini tangu kupokea kwangu simu na kutokea mauaji…” akameza mate na kuendela
“Lakini hii simu ya pili, ukiangalia umbali wa Mwananyamala Hospitali hadi Magomeni Mikumi, ndipo hapo ninapopata mashaka, maana ni umbali mrefu mno na kuna tofautiya dakika mbili tu toka nilipo pigiwa simu na tukio lenyewe la mauaji, ndio maana anapata shaka kuwa muuaji wa hili tukio la pili, sio Yule aliepiga simu,” alimaliza Inspekta kuongea na kumsikiliza Marsha nae ana maoni gani, kama alijua akadakia
“Yeah! Ni kweli, haiwezekani kabisa hata kwa dakika 5, achana na hizo mbili ulizosema, ndani ya dakika 3 mtu awe ametoka Mwananyamala Hospitali aje Magomeni Mikumi na kufanya mauaji kisha apotee,” akatikisa kichwa kukataa.
“Tena mpigaji wa simu aliekuwa akipiga si umesema ni mwanaume Inspekta?”
“Ndio Marsha, mara zote amenipigia mwanaume,” alijibu na kumtazama Marsha.
“Kumbuka ile kauli ya Salma kule kwao, huenda ikawa sahihi kabisa hisia zako,”
“Kwamba alimuona marehemu akiwa ameongozana na mtu alievaa hijabu?” alihoji Inspekta kama vile hajiamini hivi, Marsha akaitika kwa kichwa kukubali, lakini Inspekta akakanusha
“Hapana Marsha, hicho wala sio kigezo cha kukikamatia, yawezekana tu akawa ni mwanaume alievaa mavazi ya kike ilimradi tu kukamilisha lengo lake,”
“Dah! Eeh hapa kwazi kweli kweli,” ukimya ukatawala kidogo hadi Inspekta aliekuwa akiangalia ile diary ya upelelezi ule alipoifunga na kumtazama Marsha kisha akamuuliza
“Vipi kwa Mkuu kulikuwa na kheri ama kuna tatizo linguine?”
“Hapana alikuwa anasema kuhusu kesi hii ni kwa nini kesi leo inaingia siku ya nne nae hajui lolote? Nikamueleza tu kuwa hakukuwa na nafasi hata chembe ya kuweza kuonana nae na kuliongelea jambo hili pamoja nae,”
“Sawa kabisa, ni jibu zuri, kwa hiyo amesemaje?”
“Amedai kesho asubuhi kabla hatujatoka kwenda popote tuwasiliane nae, yeye atawahi kufika hivyo tukutane nae tukiwa pamoja mimi nawe,”
“Sasa inategemea, anaweza kuchelewa kufika nasi tumeanza kuelekea kwenye mafanikio, yaani kumsubiri mtu ambae anataka kujua juu ya mauaji ambayo yote yapo kwenye file? Mimi nimepanga kesho tutaanzia sehemu moja hivi ili kwenda kasi na muda wetu,”
“Kwa hiyo unataka kuniambia haitawezekana tena kesho kuonana na Mkuu?” aliuliza Marsh akitaka kupata kauli ya Inspekta.
“No! sijasema hivyo bali nimeweka kama utangulizi, ikitokea tu kuwa tumepata dokezo ama fununu, iwapo itatokea habari yoyote kama emergency, italazimika sisi tuachane na mkuu twende kwanza huko, maana tupo pazuri sasa kwenye upelelezi wetu,”
“Nimekuelewa, lakini nakushauri unapaswa kuonana na Mkuu, kwani inavyoonesha ni kama ana kitu Fulani hivi juu ya kesi hii, mtafute,”
“Kweli Marsha? Kwanini asikwambie wewe ambae umeonana nae ana anajua kuwa mimi nawe sote ndio tunaofuatilia kesi hii?”
“Ni kweli mkuu huenda ni jambo ambalo sijapaswa kulijua,”
“Na kama hujapaswa kulijua basi ujue halihusu kesi hii, maana kama linahusu kesi hii ni lazima utalijua tu, lakini nitamtafuta baadae ama kesho,” alisema huku akikusanya makaratasi yake na kutaweka kwenye diry yake na kumshindikiza Marsha ambae tayari alikuwa akiaga ili kuondoka.
“Lakini Marsha, mazishi ya Mwanakheri si ndio leo hii?” alikumbuka Inspekta na Marsha akakanusha kuwa maiti yenyewe wana ndugu watapewa leo jioni hii, hivyo mazishi wamewashauri yafanyike siku ifuatayo muda wowote.
“Sawa, ushauri mzuri, sasa hakikisha kuwa hakuna chochote kitakacho tokea huko msibani, wapange vijana wa kutosha, kila tukio pale liwe lina mtu anaelifuatilia kwa ukaribu, vyumbani weka watu wetu kama kawaida, unanielewa afande?” Inspekta alitoa maagizo na kumfungulia mlangoa Marsha kisha akaendelea kumtazama.
“Ndio mkuu, maagizo yako yatatekelezwa kama ulivyo sema,” kisha aktoka na kwenda zake akimuacha mkuu wake akijifungia ndani mwake.
**********
Siku ya pili asubuhi na mapema Inspekta aliwasili kituoni na kumchukua Marsha ili kukutana na Mkuu waUpelelezi wa mkoa ambae alitaka kujua ni kwanini hadi wakati ule kesi ile ya mauaji ilikuwa haijamfikia yeye rasmi mezani kwake kwa ajili ya utambuzi na kupangiwa majukumu ya nani aiendeshe?
Inspekta alijitetea kuwa majukumu ya kesi ile ndio sababu ya kufanya ichelewe kumfikia, lakini akamueleza tukio zima na hadi walipofikia sasa na nini mipango yao ya baadae iwapo wao ndio watakaopewa jukumu la kuiendesha kesi hiyo ama kumpa yeyote atake chagukliwa kuendesha kesi ile.
“Sawa basi kama ni hivyo, maana nimeshangaa kuona ukimya ukitawala huku mauaji yakiendelea, hivyo wewe na Marsha mtaendelea na kesi hiyo, wakati ile ya utoroshaji wa Sukari, nayo si ilikuwa chini yako pia?” aliuliza mkuu huku akinyoosha kidole juu kama anaekumbushia kitu Fulani.
“Ndio Mkuu, ile nilikuwa nae pia, Sikuwa peke yangu,” alijibu Inspekta Kalindimya.
“Sawa, sasa hiyo kuanzia sasa ataisimamia jitu, nawatakieni kazi njema,” alimtakia kazi njema na kumpa mkono kisha Inspekta akatoka na kumpitia Marsha aliekuwa amevaa juba maalum kwa ajili ya kwenda kuhudhuria mazishi ya Marehemu MwanaHeri.
Safari hii gari iliendeshwa na Inspekta mwenyewe, hadi maeneo ya Sinza nyumbani kwa kina MwanaHeri ambae ndio marehemu, walikuta watu ni wengi mno huku wengi wakionesha kama wamefuata kujua tu ni kipi kilicho sababisha kifo chake.
Mazishi yalifanyika kwa amani na utulivu mkubwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kwa kiasi cha juu mno lakini hadi wanamaliza kuzika, hakuna baya lolote lililotokea wala dalili yauwepo wa jambo hilo nao haukuwepo.
Walipotoka makaburini wakarejea ofisini moja kwa moja ikiwa ni mchana wa jua kali, hakuna aliekuwa na wazo lolote muda ule zaidi ya kuhitaji kufika ofisini na kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa askari waliokuwepo kule eneo la msiba.
Nao hawakuwa na jipya, siku hiyo amani ilitawala kila sehemu na hatimae wakaimaliza siku hiyo.
**********
Zilipita siku tatu pasina habari yoyote huku wao wapelelezi wakiendelea na kazi yao ya kufuatilia muuaji Yule ni nani.
Jioni moja wakati Inspekta akiwa maeneo ya Sinza nje ya nyumba ya kina MwanaHeri, alikuwa akitoka ndani y nyumba hiyo, alikwenda pale kupata namba ya Mpenzi wa Mwana.
Alifanikiwa kuipata namba hiyo na kuondoka kuliekea gari lake ambalo alikuwa amelipaki upande wa pili wa barabara, kuna mtu akampita kasi sana akiwa na pikipiki aina ya Boxer, lakini mwendo wake ulimtisha kidogo Inspekta, kwani alionekana kama ni mtu ambae alikuwa akimsubiri yeye tu atoke.
Kwa kuwa tayari alikuwa amemuona kwa mbali, alimkwepa lakini alishindwa kumzuia kuendelea na safari yaake, nae akaingia garini na kuondoka eneo lile haraka, tayari aliona lile eneo si salama kwake.
Moja kwa moja akaelekea kituoni na kuketi peke yake ofisini mwake. Akili yake ili mtuma kumpigia simu Mpenzi wake MwanaHeri ambae aliambiwa kwa kipindi chote cha msiba hakuonekana kule nyumbani japo alionekana kwenye mazishi ya MwanaHamisi.
Hapo ndio alipoona kama kuna tatizo, inakuwaje kwenye mazishi ya rafiki wa Mpenzi wake awepo na kwenye mazishi ya Mpenzi wake asiwepo? Akapata shaka na kutamani kumuhoji ili kujiridhisha, huenda alikuwa na tatizo ama alipata shock iliymsababishia ashindwe kufika msibani.
Mwenyewe akajiuliza tu kichwani, kweli alishindwa kufika msibani, lakini hata baada ya kuzika kwanini asifike? Akatoa diary yake aliyo andika namba ile ya simu na kumpigia kwa simu yake ya mkononi.
Simu iliita sana na haikupokelewa, akapiga tena lakini ikawa ni hivyohivyo. Mara ya tatu sasa ikapokelewa na kwa sauti ya kiume aliepigiwa akaipokea na kusema Hello!
Inspekta Kalindimya akajitambulisha na kuomba kuongea na mtu aitwae Loren, aliepokea simu akasema kuwa Loren hayupo ametoka siku ya tatu leo hajaonekana nyumbani na simu aliiacha nyumbani.
Kengele ya tahadhari ikalia kichwani kwa Inspekta Kalindimya, akamuuliza aliepokea simu yeye ni nani? Jamaa akamjibu kuwa yeye ni kaka wa Loren.
“Mmeliripoti tukio hilo kituo cha Polisi?”
“Ndio, na hata nilipoiona simu hii na wewe ulivyojitambulisha ni askari, nikajua huenda tukapata habari aidha ni nzuri ama mbaya, lakini tu nikajua una habari mpya,” aliongea kijana Yule wa upande wa pili akiwa na hofu.
Inspekta akaligundua hilo na kumwambia kwamba ni kweli kuna habari mpya, anapaswa afike kituo cha Polisi Oyster bay kabla ya saa 10 jioni kwa ajili ya kupokea habari hizo ambazo zitakuwa ni nyeti kwake.
“Afande ninaweza kuja hata sasa?” aliuliza akiwa na shauku ya kutaka kujua ni habari gani alizonazo afande, Inspekta akamwambia aende tu wala asihofu, yeye atamsubiri kituoni.
Muda huo ilikuwa ni saa 6, ilipotimu saa 7 mchana, tayari huyo kijana akawa amewasili hapo kituoni na kumuulizia Inspekta, akapelekwa alipo na kuanza nae maongezi.
Kwanza alitaka kujua jina la huyo kaka wa Loren, kijana akajitambulisha kwa jina la Chidy, kisha akamuuliza habari mbali mbali juu ya Loren na kazi yake. Chidy akamwambia kuwa ndugu yake ni mfanya biashara na husafiri mara kwa mara kufuata biashara zake mikoa mbalimbali na hasa huenda kwenye mikoa ile ambayo ipo pembezoni na nchi yetu.
Alikua akiandika tu Inspekta kisha akamuuliza juu ya kutoweka kwa Loren na Chidy akasema hajuibali tangu siku ya juzi hawajamuona na walipoingia chumbani wakaikuta simu yake ikiita na hadi leo hajatokea tena.
“Loren ana familia?”
“Hapana, hakuwa na familia bali ana Mpenzi,”
“Una mjua Mpenzi wake?”
“Ndio ninamjua kwa picha iliopo kwenye simu yake kwani sijawahi kumuona ana kwa ana,”
“Nahitaji kumuona,” Inspekta alimwambia Chidy huku akimtazama usoni, Chidy akazama mfukoni na kutoa simu ya mkononi na kumuonesha picha ya Mpenzi wa Chidy ambayo ilikuwa ipo kwenye display.
Ilikuwa ni picha ya MwanaHeri, inspekta akamuuliza kama anamjua jina lake Yule mrembo. Chidy akasema kwamba hamjui jina lake ila alizoea kumuona ndugu yake akimuita baby.
Hapo sasa ndio akamuuliza kama ana taarifa juu ya kifo cha mtu huyo. Chidy alishtuka sana na kuonesha mshangao tokana na taarifa hiyo na kumwambia Inspekta kuwa haji maana Chidy ndio mtu ambae angemwambia lakini kwa sasa ndio hayupo sasa.
“Kuna mtu yeyote alipiga simu wakati wewe ukiwa nayo?”
“Ni wengi sana na wote walikuwa wakimtafuta dogo na niliwajibu kwamba haonekani kwa sasa, wengi walisikitika na wamekuwa wakipiga simu mara kwa mara kutaka kujua kama ameonekana,”
Waliendelea kuongea kidogo na kumtaka Chidy aiache simu pale kwa ajili ya uchunguzi zaidi na wakati wowote wakimuhitaji na yeye watamuita. Akafanya hivyo na kuiacha simu pale, akaacha namba yake na kusaini makaratasi ya kuthibitisha kuwa ameacha baadhi ya vitu hapo.
Inspekta alianza kuipekua simu ya Chidi ili kuangalia kama atapata chochote, kwanza alianza na namba za simu zilizoingia kwenye simu ile, alizichukua za wiki moja kabla ya tukio la vifo vile na hadi simu ile.
Nyingi namba zilikuwa ni zilezile, lakini chache zilikuwa zimepiga mara moja moja, lakini zote alizi hifadhi kwenye karatasi nyingine huku akiandika hadi muda wa kupiga na kama iliongelewa muda mrefu aliandika pembeni pia.
Kisha alienda kwa namba zilizopiga na kufanya hivyo pia, akahamia kwenye sms na kuanza kuzisoma, alikuta sms nyingi zilikuwa ni za kawaida tu, mwisho akaingia whatsApp, huko ndio hakukuta chochote cha maana. Alipoona kidogo kwenye kumfaa ni kwenye namba za simu tu.
Mwenyewe akajisemea kuwa Loren anaonekana hakuwa ni mtu wa kuchat sana, hivyo hakuwa na lolote la kumuongoza huko, alkamaliza na kuiweka simu ila kwenye mfuko wa juu wa koti lake na kunyanyuka.
Wakati kitoka nje ya jingo la ofisi simu yake ya mkononi ikaita na sasa tena ilitumika Call box, akapokea na kuweka sikioni, hakukuwa na salamu bali alikanywa tu kuwa aachane na ile kesi asijifanye ana kimbelembele, itampotezea kazi kabisa ama hata maisha yake iwapo atazidi kufuatilia.
Alisonya na kumwambia mpigaji amebakiza masaa tu kumfikia hapo alipo, mpigaji akacheka na kumwambia hayo masaa anayosema yeye, basi ni masaa ya kukaa Inspekta ndani ya selo yao
“Mlijenga selo kwa ajili ya wahalifu, sasa leo hiyo selo itakuhusu na wewe kutokana na kuwa na kimbelembele,”
“Ok! Umemaliza? Maana najua ulipo ninasubiri muda tu ufike nije kukukamata kama kuku,” Inspekta alisha jua kuwa Yule muuaji tayari aliingiwa na woga kwa sababu amabzo yeyey mwenyewe anazijua.
“Mimi nawe tutakutana jioni kwenye game yetu kama utakuwa nje ya selo, kwa heri.” Kisha akakata simu na kumuacha Inspekta akisonya na kubadili muelekeo, kutoka kuelekea nje, sasa akaelekea kwa mkuu wake wa upelelezi wa kituo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimkuta akiwa anaongea na saimu, lakini akamkaribisha na kumuonesha kiti huku akiendelea kuongea na simu ile. Alipomaliza akamuuliza kulikoni. Akamwambia tu kuwa anahisi muda wa kumtia nguvuni muuaji umekaribia sana, anahitaji msaada zaidi wakati wowote.
Mkuu wake akamwambia kwamba yeye wakati wowote atakapokuwa na shida ya msaada asisiste kuomba.akatoka na kuahidi kuwasiliana na mkuu wakati huo utakapowadia.
Moja kwa moja akaelekea kwenye ofisi ya Marsha na kumkuta akishughulika na namba za wale maiti, nae alikuwa akiaribu kuziangalia akama atapata ufunuo wowote, lakini wapi.
Hadi anafika mkuuwa ke wa kazi, bado Marsha wala hakuwa hata na habari, alikuwa busy kweli. Alipomsemesha akawa ni kama amemshitua vile na kumtazama.
“Naona ulikuwa mbali sana, lakini pamoja na hayo Yule mjinga amepiga simu tena akijaribu kunitishia na kunitaka kuachana nakazi hii, nimehisi tayari tumemshika pabaya, sasa sijajua ni wapi,”
“Umeona mkuu?Hii itakuwa tayari tumeisha ingia kwenye njia zake na amehisi tumemsogelea, sasa nini cha kufanya?” aliuliza Marsha huku akimtazama usoni.
“Tunatakiwa kwenda kwenye zile call box tukafanye mambo yetu na kuzifanyia uchunguzi wa kutosha, maana zote anazitumia huyo hayawani ni za Mwananyamala,”
“Ooh! Kwa hiyo inabidi tuwasiliane na IT Master wetu?”
“Yap! Kazi hiyo nitaifanya mimi kwanza wewe fanya kazi hii…” alisema huku akizama mfukoni na kutoa simu ile ya Loren na kumpa huku akimpana namba za simu alizochukua toka kwenye kabati la Mwana
“Jaribu kuangalia chochote ambacho kitatufanya tupige hatua moja mbele, hapa lazima tuokote kitu muhimu, hivi vifo viwili vina uhusiano mkubwa na kutoweka kwa mtu huyu,” Marsha akapokea vitu hivyo huku Inspekta akitoka kwenda ofisi ya IT kuongea na master.
Akiwa anaongea na IT Master, akafuatwa na Marsha na kuambiwa anahitajika haraka sana kwenye ofisi ya mkuu wa upelezi mkoa, yaani kwenye ofisi ya RCO, akamuaga IT Master akimtaka aandae vitu vya kufunga sehemu za Call box zaidi ya nne, kisha akatoka huku akimwambia Marsha kuwa akimaliza ama kuambulia chochote awasiliane nae, hapo ndio akaanza safari akiwa na hofu kidogo.
Haikuwa ni kawaida kwa mkuu wake kumuita akiwa mbali na tena kwa wito wa kupitia mtu wa kati, mara zote huwa anampigia mwenyewe ama msaidizi wake ila sasa ndio ilitokea.
Safari yake ilielekea makao makuu ya Polisi yaliyopo katikati ya Jiji jirani ana kituo cha Reli ya kati. Alimkuta RCO ambae alikuwa ameketi na baadhi ya makamanda wa Polisi wa maemneo tofauti akiwepo na Yule wa kituo chake cha kazi.
Alishangaa kukuta mkutano ule usio rasmi, akawatazama na kuwasalimia kisha akaketi pasina hata kuambiwa kwenye kiti kimoja ambacho kilionesha kama ni kiti ambacho kilikuwa ni maalum kwa ajili yake.
Baada ya kuketi RCO akamuuliza ni vipi kuhusu kesi wanayoisimamia imefikia hatua gani? Akawaeleza na kujibu kuwa ipo pazuri na hadi sasa wamefikia hatua nzuri.
Lakini RCO akamwambia inaonekana kama wanasuasua kwenye kesi ile hasa kwenye kumkamata muhusika, Inspekta alijitetea kuwa hapo walipo na wenzie wanajituma sana kiasi ambacho wanakosa hata muda wa kupumzika.
Akaulizwa kama haoni kuna usaliti baina ya wao wenyewe kwa wenyewe? Akasema hakuna kitu kama hicho, RPC ambae nae alikuwepo mle akamwambia kwamba inasemekana kuwa yeye anahusika.
“Inspekta akashangaa kidogo na kuuliza mimi nahusika? Akajibiwa ndio kuwa yeye ametajwa kuhusika na hapohapo akaitwa Jitu ambae alikuwa maeneo hayohayo na kuulizwa juu ya mawasiliano baina ya Inspekta Kalindimya na muuaji.
Akaeleza kila kitu pasina kuongeza kitu, kisha RCO akatoa bahasha kubwa kutoka kwenye droo na kutoa karatasi moja yenye ukubwa wa A4 ndani yake na kumuita askari mmoja aliekuwa amesimama pembeni, bahasha kwa juu ilikuwa imeandikwa ‘AFANDE ANAHUSIKA’ akamwambia ampe Inspekta.
Inspekta Kalindimya alipokea na kuisoma karatasi ile kwa pupa na alipomaliza, akamtazama RPC na kukuta akimtazama yeye, akamuuliza kama amekiona kilichoandikwa mle. Alijibu ndio na kuulizwa ni kipi.
“Ni juu ya tuhuma ya kumdhulumu mfanya bashara wa kuuza visu,” akatulia kidogo, lakini RCO akawa kimya tu akimtazama, hatimae yeye mwenyewe akaendelea
“…lakini mkuu mimi sikusiki na tuhuma hii wala sijawahi kununua visu mtaani…” akakatishwa
“Lakini si umeisoma vizuri hiyo barua? Si umeona hadi namba yake ya simu na hadi mahala ulipomwambia aviweke, sasa unakataa vipi hapo?” RPC alimuuliza.
“Mkuu hapa mimi sielewi chochote juu ya hivyo visu na hata huyu mtu alietajwa hapa mimi simjui pia,”
“Unanithibitishia kwamba hata kwako mahala hapa tulipotajiwa hivyo visu hatutavikuta iwapo tutakwenda nyumbani kwako?”
“Ndio mkuu, hizi zitakuwa ni mbinu chafu tu za watu wasiopenda kazi adhimu inayofanywa na jeshi letu la Polisi,” RPC na RCO wakatazamana na kisha RCO akamwambia kuwa wataongozana pamoja nae ili kwenda kujiridhisha.
Wakanyanyuka huku RCO akimuahidi RPCkuwa watawasiliana baadae. Wakatoka wakiwa ni kundi la askari ambao walikuwa kwenye gari mbili hadi nyumbani kwa Inspekta Kalindimya, huku aakijiamini kabisa akafungua mlango wake wa barabarani na kuwakaribisha.
Kwenye meza yake ya chakula pale pale walipo waliweza kuiona, juu ya meza hiyo palikuwa na kisu cha aina ileile ambacho kimekuwa kikitumika kwenye mauaji ya kina Mwana, hiki sasa kilionekana kama kinatumika mara kwa mara.
Alipokiona tu mwenyewe akasema Shit, na kutamani kukificha, wakasogea wote kwa pamoja na kukitazama, Inspekta akatikisa kichwa tu akiwa kauma mdomo wa chini.
RCO akamtazama na kama vile alitaka kumsemesha, akauchuna na kisha akawageukia vijana wake na kuwaambia waangalie tena sehemu nyingine, akamgeukia Inspekta sasa akamwambia
“Inspekta, vipi kuhusu hivi visu? Aliekuletea anasema vipo 8 na hapa naona kuna kimoja, ukifanya kujumlisha na vile viwili vilivyotumika ina maana ni vitatu, sasa hivyo vitano vipo wapi?”
“Mkuu, yaani hiki kisu mimi ndio ninakiona humu ndani mwangu kwa mara ya kwanza, sijawahi kukiweka humu, najua utaniuliza tunaishi wangapi, lakini kiukweli ni hivyo,” akiwa anatoa maelezo kwa boss wake, akaja askari mmmoja na kukakamaa mbele ya afande mkuu na kumwambia kuw wameviona visu vingine.
“Vipo wapi sasa? Mbona hujavileta?” aliuliza RCO kwa shauku kubwa.
“Mkuu vimefungiwa kwenye kabati ya vyombo sehemu ya chini yenye kioo, hivyo tumeviona kupitia hicho kioo,”
“Hapo ndio mahala alipotaja kuwa alitumwa kuviweka na Inspekta, hebu twendeni akatufungulie…” Mkuu akaanza kuondoka huku akiamwambia Inspekta atangulie hadi ilipo kabati yake ya vyombo.
Inspekta akiwa kama mtu ambae hajiamini vile, akatangulia hadi ilipo kabati yake ya vyombo huko jikoni, alipofika na kuinama hata nae aliweza kuviona visu hivyo ambavyo vilikuwa kama vile vimefichwa.
Akamtazama mkuu wake wa kazi na akakutanisha nae macho, akamwambia afungue.
“Mkuu wakati natoka niliacha funguo hapa, huwa sifungi humu jikoni wala milango ya kabati,”
“Sikuelewi Inspekta, hebu nieleweshe vizuri, mimi shida yangu ni kutoa hivyo visu humo kabatini, sasa funguo ipo wapi?”
“Mkuu, kabla sijatoka hapa palikuwa wazi, na funguo niliacha ikining’inia hapa kwenye mlango wake,”
“Ok! Ulimuacha nani humu ndani?” lilikuwa ni swali la msingi sana lakini halikuwa na maana, kwa sababu Inspekta anaishi peke yake.
Alijaribu kutoa maelekezo ya kutosha lakini hakueleweka, hata nae alijua kuwa hawezi kueleweka, hivyo akaamua awe mpole kwanza wakati akitafuta njia muafaka ya kufanya.
Mkuu akaamuru askari mmoja avunje kioo na kutoa vile visu. Kweli walitoa visu vitano, vinne vikiwa havina alama yoyote ila kimoja kikiwa na namba zingine tofauti na zile za awali.
Inspekta alichoka ghafla, alitamani kufanya kitu ambacho hata hakijui ni kitu gani, ila alitamani kufanya jambo. RCO alivikagua visu vile na kuviweka kwenye mfuko waliokuja nao, kisha akawaambia askari wake watoke nje na kuanzia muda ule wamuweke mwenzao chini ya ulinzi.
Aliwekwa chini ya ulinzi kama alivyoamrishwa na kisha ukachukuliwa ushahidi na kuondoka kuelekea kituoni huku askari wawili wakiwa wameachwa pale kwa ajili ya kuweka mazingira ya usalama.
Akiwa ndani ya gari sasa ndio akili yake ikaanza kuchaji, alihisi sasa ile kauli ya Yule muuaji ni ya kweli, lakini akajiuliza ni vipi aliingia kwenye nyumba ile na hali funguo zote aliondoka nazo mwenyewe?
“Ina maana huyu mtu ananifuatilia kwa kiasi kikubwa mno, ameamua sasa kuondoka hadi na funguo za mlango wa kabati yangu?Kuna nini hapa kati?Na kwanini aondoke nayo? Si angeiacha pale pale? Nahisi kuna kitu tena juu ya hii funguo, si bure,” mawazo mawazo yalikuwa ni mengi, hivyo hadi wanafika ofisi ya RCO yeye hana hata habari.
Aliamriwa ataeremke na kuongozana moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya RCO na kuingia ndani ili kufanya mahojiano mafupi. Akiwa hapo akapigiwa simu Marsha kwamba anahitajika huko haraka, aende akiwa na jalada la kesi za mauaji hayo anayofanyia upelelezi sambamba na Inspekta Kalindimya.
Akajibu sana na akawasha gari ya Polisi na kwenda huko mkoani, aliwasili pale na kuwakuta wakuu wake wa kazi wakiwa wameketi wanajadiliana, yeye alikuwa yupo nyuma ya wakati lakini wakampa maelezo kidogo ambayo dhahiri aliyapinga.
“Mkuu zaidi ya mara moja Inspekta amekuwa akipigiwa simu na kuambiwa juu ya suala la kuachana na kesi hii, nahisi ni mbaya wetu tu huyu anatumia vibaya udhaifu wetu ili kutusambaza,” Marsha alitetea huku akiwa na imani kauli yake itaweza kuwashawishi na kuweka mambo sawa.
RCO alikaa kwa sekunde kadhaa akifikiri juu ya kauli ile na baada ya dkika takriban tatu hivi, akasemahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nilikuwa nimedhamiria kukuweka ndani kipindi chote cha ufuatiliaji, lakini kutokana na kauli ya Marsha, nitakusimmisha tu kazi kwa muda usiojulikana na hivyo tangu sasa mkabidhi makabrasha yote Marsha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zingine,”
“Sawa mkuu!” alijibu huku akisimama na kukauka kwa saluti.
“Utakuwa unaripoti hapa kwangu kila siku saa moja na nusu asubuhi hadi pale nitakapothibitisha ukweli ni upi, sawa Inspekta?”
“Ndio mkuu.”
“Hutatumia gari binafsi tena muda wa kazi, tangu sasa gari ya ofisi itakufuata kukuleta huku na ndio itakayo kurudisha nyumbani baada ya kazi, nafikiri unanielewa?”
“Ndio mkuu ninakuelewa,” Kisha wakatoka na Marsha ambae kichwani alihisi ni uonevu mkubwa amefanyiwa boss wake, lakini hakuwa na cha kufanya, maan ahuyu alie nae ni boss kwake, na aliefanya huo ambao yeye anauona kama ni uonevu, ni boss wao wote.
Kimya kimya wakaelekea hadi kwenye gari ya Inspekta na kuingia, humo ndani ya gari ndio Marsha akampa pole mkuu wake wa akazi ambae alitabasamu na kusema vitu kama vile ni vya kawaida sana makazini
“Jiandae tu nawe kukutana navyo, mafisadi na wazandiki ni watu ambao hatari sana, wakati mafisadi wanashika nchi, wazandiki wao huishika Serikali, basi inakuwa shida kubwa mno,”
“Ni kweli boss, sasa Sijui nifanyeje na kazi hii halafu peke yangu? Alisema Marsha kwa huzuni, kwani tayari aliisha ingiwa na hofu moyoni.
“Pambana tu binti, mbona unaweza? Jiamini tu, utakuza sana CV yako iwapo utalifanikisha hili jambo,” Marsha aliendelea kulalamika
“Bila ya msaada? Peke yangu mimi siwezi, ujue mkuu hii ni kesi kubwa sana kwangu? Yaani inafikia hatua kwamba hata Sijui ni wapi pa kuanzia,”
“Usijali, nafikiri hawatokuacha peke yako, lazima utapewa mtu wa kuendana nae,” Inspekta alizidi kumpa moyo, Marsha nae akaomba kuwa wakati wowote akihitaji msaada wake, basi asisite kumsaidia,
“Sasa Marsha itategemea na msaada upi unataka, ule ulio ndani ya uwezo wangu na kama pia sintoingilia kazi zisizonihusu nitakusaidia, si unajua kuwa suala hilo halinihusu tena? Maana name sasa ni mtuhumiwa,” alijitetea Inspekta na kumfanya afande Marsha atikise kichwa kukubali.
Tayari walifika ofisini kwao na kuingia ndani, huko ndani Inspekta akaliomba file kwa Marsha na kukopi baaadhi ya vitu alivyo hitaji na kumrejeshea pamoja na kumpa diary ambazo alizitumia kuandika maelezo muhimu.
Alipomaliza akaitazama ofisi yake kwa umakini kama mtu ambae anaiaga vile, kisha akachukua alichoona anahitaji, akatoka nje na kuwaaga wenzie akimuacha Marsha kiwa na majonzi.
Safari yake ikaelekea moja kwa moja nyumbani kwake na kuwakuta wale askari waliopangwa kulinda pale kwake wakiwa wanaendelea na jukumu lao. Walimfungulia geti na akaingia ndani, wakati akishuka garini wakakauka kwa saluti kisha yeye akaelekea ndani kwake ili kufanya uchunguzi zaidi juu ya nyumba yake, maana tukio lile la mtu kuingia ndani mwake, bado lilikuwa likimtafuna.
Alijitupia kwanza sofani na kutoa simu yake iliyokuwa kwenye mfuko wa ndani wa koti lake, ilikuwa ipo kwenye silent tangu alivyoiweka wakati akiwa kwenye kikao, sasa alipoitazama akakuta kuna missed call moja tu, namba alihisi kuijua ijua hivi.
Akatoa na kupiga namba hiyo, ilipokelewa na aliepokea safari hii hakuwa mtu mwingine, bali alikuwa ni mtu yuleyule ambae amekuwa akiwasiliana nae mara kwa mara kupitia Call box.
Alipopokea tu cha kwanza akaanza kurekodi maongezi yake na huyo jamaa, alidhamiria sasa kurekodi kila simu ambayo ataona inastahili kuwa ni kumbukumbu kwake.
Jamaa akaanza kwa kumpa pole nyingi na kumwambia anajua kila kitu kilichomtokea lakini ile inatokana na ubishi wake. Afande alimsikiliza tu. Mwisho akamuuliza ina maana alipiga simu kumueleza jambo hilo tu au amna jingine jipya?
Jamaa akamjibu kuwa ipo sababu nyingine ambayo ataijua iwapo atakuwa makini na kumsikiliza hadi mwisho.
"Tegemea kitu kipya leo hii ama kesho, maana mimi nilitaka wewe leo ulale ndani ili nikupunguzie kazi, lakini unaonesha kuwa unakubalika sana kwa huyo Mkuu wako wa kazi sasa basi nabadili mbinu, kesho tutaona nani atakaeshinda game yetu,"
"We huna lolote, malizia tu siku zako za kuwepo uraiani kabla sijakufikia na kukutupua ndani,"
Inspekta bado tu hutaki kunielewa? Game yetu Inaendelea na haitaki hasira, pia kumbuka ni mimi ndio mwenye funguo yako ya kabati... Sidhani kama umejisahaulisha," Inspekta alikumbuka sana lakini aliona haina umuhimu tena, bali akacheka na kusema kiufedhuli akitaka kumkasirisha mtu wa upande wa pili
"Haina kazi tena hiyo, nimeisha haribu kabati, sasa imebakikama scraper tu, ambayo wakati wowote tangu sasa nitaitupa kwenye dampo. vipi kuna kingine?" aliuliza Inspekta kwa kuamini kuwa amemtweza nguvu, lakini kumbe wala haikuwa hivyo, bali jamaa nae akacheka na kusema
"huenda funguo hauihitaji tena, lakini tambua kuwa mimi sio mpumbavu kwa kiasi hicho unachodhani. Na katika kukudhihirishia hilo, nenda chumbani kwako juu ya kabati, kwaheri," simu ikakatwa kimyakimya.
Afande akashusha pumzi na kujiuliza aende ama lah! Akaamua aewnde tu akaangalie kwani hakuna athari yoyote ambayo ataipata iwapo atakwenda kuangalia hapo kabatini.
Akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake moja kwa moja na alipofika kwenye ile kabati hakuona kitu chochote kipya, basi akasonya na kuacha kuangalia kisha akaondoka kurejea kule sitting room kuendelea kujipanga zaidi.
Akiwa ameketi pale Sitting room kama mtu vile aliekumbushwa kitu muhimu, akakurupuka tena.
Moja kwa moja tena hadi kwenye kabati yake ya nguo kule chumbani, safari alichukua na stuli ili aweze kuona vizuri. aliweza sasa kukiona kila kitu kilichokuwepo juu ya kabati ile ya nguo.
ni kitu kimoja tu alichokua akitaka kukiangania lakini alipokiangalia hicho kitu, hakukiona, akashtuka sana, hakutegemea kabisa kutokewa na kitu hicho.
Alichukua simu yake ya mkononi na kupiga tena namba ile. Namba ilikuwa haipatikani, akarudia tena kwa kuhisi labda ni Mtandao lakini wapi… jibu likawa ni lilelile, akaitupia simu kitandani na kujishika kichwa kwa mikono miwili.
“Ukisikia kuwa mateka ndio huku sasa, mtu unaweza kutumika bila kupenda, Mungu wangu.., ninajiokoaje juu ya kikombe hiki?” aliwaza peke yake huku akizunguka chumbani kwake kule na huku.
Akili ilifikia ukomo wa kuwaza, alitamani kumpata huyo mtu aliekuwa akiwasiliana nae lakini hakuwa hewani, akapata wazo la kumpigia Marsha, ambae alimwambia atafika jioni pale nyumbani kwake.
“Si utakuwepo mkuu ama una ratiba ya kutoka?”
“Marsha sipaswi kutoka hapa, nipo kifungoni, natakiwa tu nije nikupe dondoo muhimu zimenifikia nikiwa ndani,”
“Sawa boss, jioni nitafika.” Inspekta akakata simu na kisha akaanza kukagua tena upya chumba chake na kisha akakagua nyumba nzima, lakini hakukuwa na tofauti zaidi ya hiyo aliyoiona juu ya kabati.
Wakati yeye akiwa nafanya uchunguzi kwenye nyumba yake, upande wa pili, Marsha alikuwa sasa nae ameanza kupata hofu juu ya mkuu wake wa kazi, inakuwaje sasa yupo nje ya ofisi na bado anasema anaendelea kupata dondoo?
“Kiukweli Inspekta anapaswa kuchunguzwa, name nimeanza kupata hofu nae.” Alijisemea mwenyewe huku akikusanya makabrasha yake akitoka kwenda kuanza upelelezi wake kama alivyojipanga mwenyewe.
Pasina kujua lolote, Inspekta alianza kazi ya kupeleleza juu ya zile namba, na hasa ile iliompigia, alichukua namba za simu alizochukua kwa marehemu Mwana na zile alizopewa Sinza na kuanza kuzilinganisha.
Aligundua kuwa namba aliyopewa Sinza, ndio namba ambayo imempigia muda mchache uliopita,
“Ahaa! Ina maana ni Loren ndio alieingia humu ndani kwangu? Na kipi kilichosababisha atumie namba yake kuwasiliana name? Huenda kuna kitu hapa kati?” aliwaza sana huku akiwa ameweka mikono yake mdomoni
“Angalau sasa naweza kujua kuwa Loren yupo hai na ndio namuhusisha na matokeo yote haya ya mauaji, lakini Loren yupo vipi?” hapo sasa kaanza kujiuliza ni kipi afanye.
Likamuijia wazo…
Wazo ambalo aliliona ni sahihi sana, wazo hilo lilikuwa ni kumsubiri Marsha afike jioni nyumbani kwake ili wakae na kulijadili jambo hilo bila kujua kichwani kwa Marsha kuna nini.
Aliendelea kuandika hints zake kwenye diary yake na ilipotimu saa tisa mchana, akatoka kwenda kununua chakula, alipenda aje kula nyumbani kwake, hivyo alikwenda hotelini na baada ya muda akarejea na kukaa Mess.
Wakati akianza tu kula, simu yake ikaita tena, akachukua headphones zake na kuzivaa, kisha akapokea na kuanza kurekodi mazungumzo yake. Mtu alikuwa ni yuleyule tena, sasa safari hii alikuja kivingine.
“Inspekta pole sana kwa kuwa kwenye kifungo huru, hahahaaa! Leo nilikuwepo ofisini kwako na kukuulizia nikaambiwa umeenda nyumbani, lakini kwa kuwa name ni mfukunyuku zaidi ya wewe, nikaweza kusikia kuwa umepumzishwa, hongera sana bhana, wanakupenda mno! Maana pigo la leo ambalo lilikuwa linafuata lilikuwa baya zaidi, pumzika kwa amani!”
“Ujue sasa ndio nipo kwenye wakati mzuri zaidi wa kukutia mikononi, nakuahidi kabla jua hili halijachomoza utakuwa kwenye mikono yangu.” Alisema Inspekta kwa ghadhabu, kwani alihisi kuna mtu ndani ya jeshi anawasaliti.
“Huu ni mchezo tu Inspekta, umepangwa na kupangika, wewe wala usikasirike, japo nikiamua ninaweza kukutoa machozi mbele ya mkuu wako wa kazi, lakini any way. Leo nilikuja kukutembelea na kukuletea ule mzigo wako, kwa kuwa sikukukuta, nimelazimika kuondoka, maagizo zaidi anayo afande Marsha, kwaheri kwa sasa!” jamaa akakata simu kama kawaida yake.
Inspekta alihisi kuchanganyikiwa sasa, aliona kabisa kama ni mchezo anachezewa huu sasa ulikuwa ni wa kijasusi,
“Ina maana ni nani anampa taarifa zangu? Amefika kituoni na kuongea na Marsha, amempa maagizo gani tena?” maswali akayakosea majibu akaamua kukaa na kumsubiri Marsha kwa hatua zaidi, hamu ya kula ikakata.
Saa moja usiku, afande Marsha ndio akafika na kuingia mle ndani, akamsalimia boss wake na kisha akaketi kwa maongezi ya awali. Lakini hata nae alionekana ana jambo, lakini tu akawa mpole kwanza.
Inspekta akamueleza juu ya kile ambacho amekipata kutoka kwenye mazungumzo yale na mpigaji
Hivyo Marsha nimegundua kuwa mtu alie ingia humu ndani alikuwa niLoren a ndio huyo ambae amekuwa akinipigia simu mimi mara kwa mara,”
“Unamjua Loren?”
“Hapana na kibaya hata picha yake nayo sijawahi kuiona,”
“Kwa hiyo Inspekta wewe unashauri nini juu ya jambo hili?”
“Mimi ninakushauri jambo la kwanza, nenda kwa kina Loren utafute picha yake na ujue kuna lipi linaendelea, kisha kwa nguvu zote ukisaidiwa na mitandao, uweze kumsoma ni kutoka wapi wapi anapiga simu kwangu, na mwisho unijulishe name ili niweze kuendelea na kazi yangu nikiwa nje ya ofisi,” alimaliza Inspekta na Marsha akatikisa kichwa kukubaliana nae, kisha akazama mfukoni na kutoa funguo mbili na kumkabidhi Inspekta.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati akimpa funguo zile alikuwa makini mnokumtazama kwa jicho la mbali mno, maana aliona kama Inspekta ameshtuka kidogo, akazipokea na kumuuliza amezitoa wapi?
Marsha nae akamuuliza amezitambua? Inspekta akasema ameitambua moja tu ile ndogo ambayo ni ya kabati ile waliovunja kioo ilikutoa visu na ile nyingine haitambui.
Lakini baada ya Inspekta kuiangalia kwa uzuri ndio akagundua kwamba ni funguo ya mlango wake mkuu, ilikuwa imefanana sana kiasi ambacho kama zingechanganywa basi mtu mwingine asingeweza kuzitofautisha, akamtazama Marsha na kumuuliza tena amezitoa wapi.
Marsha akameza mate na kuegamia kwenye kiti chake kisha akamwambia kuwa mtu aliempa funguo zile ndio alimletea ofisini na wanafahamiana sana nae, na maagizo hayo yeye ndio alimpa kwamba aziache pale kwangu na bahati mbaya mimi sikuwepo.
“Hivyo wakati mimi ninafika hapo ndio nikakutana nae akiondoka na funguo hizo akiwa ameziacha Kaunta, ila aliniambia kwamba hayo ni maagizo yako na ulimwambia afanye hivyo,” Inspekta aliishiwa pozi na kusema
“Hili ni game na linaendelea kweli kama nilivyo ambiwa, jina lake je ulimuuliza ni nani?”
“Ndio yeye ni Chidi jina lake na anaishi Sinza,”
“Marsha, hilo jina la Chidy wewe ina maana hulikumbuki?”
“Nalikumbuka sana si ndio jina la ndugu yake na Loren?”
“Ndio, sasa imekuwaje awe na funguo zangu? Ina maana ameonana na Loren na kumpa funguo za nyumba yangu?”
“Kwani wewe ulimpa Loren funguo za nyumba yako?”
“Hapana mimi sijampa, lakini ndio kama nilivyo kwambia hapo awali kuwa katika uchunguzi wangu wa awali, inaonesha kwamba Loren anahusika na hili,”
“Inspekta kwa hili hata mimi sasa naona unanichaganya, aliekuuzia visu alitaja hadi vilipo, na vikapatikana pakiwa funguo haipo na leo inakuja funguo ya kabati sambamba na ile ya mlango mkuu, tena inaletwa na mtu ambae ndugu yake haonekani, mbona mimi sikuelewi hapo?” alionesha dhahiri sasa Marsha kuchanganywa na yale Matukio.
Inspekta hata nae sasa alishangaa kuona hata Marsha nae hamuamini juuya jambo hilo?
Alianza nae kufa moyo taratibu, kwani hata mtu aliemuamini kuwa takuwa upande wake nae sasa anaonesha kuanza kuwa na hofu nae.
Wakiwa kwenye maongezi hayo, ghafla simu ya Afande Marsha ikaita, akaipokea na kusikiliza upande wa pili. Aliepiga alimuuliza kamayupo kazini ama nyumbani, akajibu kuwa nyumbani kwa Inspekta Kalindimya,
“Kuna nini huko hadi muda huu upo huko?”
“No kuna habari ambazo alikuja kunipa, na ndio nilikuwa hapa bado sijaondoka,” wakaendelea kuongea kisha akasema
“Sawa afande,” kisha akamgeukia Inspekta Kalindimya baada ya kukata simu na kumwambia,
“Inspekta, RCO amenipigia simu na kuniambia kuwa unahitajika kituo cha Polisi sasa hivi, kaonane na RPC ofisini kwake lakini tuende pamoja,”
“Kuna nini?” aliuliza kwa mashaka, kichwani akihisi kuwa huenda anaenda kurejeshwa kazini, akasimama na kujiandaa kisha akatoka na kumpitia Marsha aliekuwa nje akimsubiri garini.
Wakati wakitoka akashangaa Inspekta kwa kuwakuta askari wengine tofauti na wale aliowaona mchana, akajiuliza ni vipi mabadiliko yamefanyika ghafla vile? Akamuuliza mmoja wao pale vipi wameenda wapi waliokuwepo?
“Wamepangiwa kazi nyingine na sisi ndio tumekuja kushika nafasi zao,” akawaaga na kuwaambia wawe makini kisha akaelekea kwenye gari.
Wakaondoka na kuelekea moja kwa moja kituoni na kumkuta Marsha akiwa tayari amewasha gari na kuelekea moja kwa moja kituoni na kuingia ofisini kwa RPC ambae pia alimkuta akiwa peke yake.
Alimkaribisha akiwa ameketi kwenye kiti chake cha kuzunguka na kumuuliza alipotoka kazini pale alielekea wapi. Akajibu kuwa alipotoka pale alieklekea nyumbani kwake moja kwa moja na hakupita popote.
Marsha akaingia na kuketi jirani na Inspekta ambae alikuwa amemuuliza swali lingine Inspekta kwamba alipofika kwake alitoka saa ngapi? Jibu likawa kuwa hakutoka kwani alikuwa na kazi nyingi za ndani mwake ikiwepo la usafi.
Inspekta akamtazama Marsha na kumwambia
Afande Marsha, ninazidi kupata mashaka na Inspekta Kalindimya, hapa anasema akuwa leo hajatoka kwake tangu alipokwenda, lakini kuna sehemu ameonekana akifanya mauaji asi tukapigiwa simu muda uleule, sasa nashindwa kuelewa hapa!” alishtuka mno Inspekta na kuuliza kwa mshtuko
“Mimi?” Hakuna aliemjibu swali lake bali wakamtazama kama kwamba wanamuelewa sana kwa mchezo anaoucheza, kisha RCO akamwambia
“Inspekta wakati nchi inakuaminina kukupa kazi ya kulinda usalama wa wananchi, haikuwa na lengo la wewe ndio uwe mtu wa kwanza kupoteza maisha yao, lakii kwa kuwa unakuwa unajaribu kupambana na jeshi ambalo unalitumikia, leo napenda ufahamu kuwa jeshi ni la nchi nzima, jeshi csio la mtu mmoja kusema kuwa kwa kuwa ni lake basi afanye anachotaka, hivyo nitakuweka ndani hadi uchunguzi utakapo kamilika,”
“Sasa Mkuu mimi kosa langu nini?”
“Ina maana kipi hujasikia hapo? Si nimekwambia kuwa umehusika na mauaji leo mchana? Nawe unakataa hujahusika, basi acha tuchunguze kisha tutapata ukweli na ndio utakao amua kipi kifanyike,”
“Sawa Mkuu, lakini mimi si…” kabla hajamaliza kauli yake RPC akasema
“Umenisikitisha sana kuniambia kuwa hujatoka wakati tayari askari nilio waweka kwako wanakiri kuwa ulitoka. Maana tayari wapo hapa niliwaita ili kuwahoji, wamekiri kuwa ulitoka, wewe unakataa kuwa hujatoka, sasa hapo ni kipi mimi nishike?”
Bado Inspekta hakukumbuka kutoka hadi pale alipokumbuka kuwa alitoka na kwenda kuchukua chakula
“Mwanzo ulikataa na sasa unakubali, unanijengea taswira gani? Nalazimika kukuchunguza sana. Maana muda huo uliotoka mle ndani kwako na ndio muda ambao mauaji yaliyotokea jirani na kwako,”
“Afande ni nani alieuwawa?”
“Ni Yule mtu ambae ulimpa funguo za nyumba yako na pia alikuuzia visu lakini pia ili kupoteza ushahidi ukamteka na ili kutusumbua zaidi, ukachukua simu yake na kuiingiza kama chanzo cha upelelezi wa kifo cha Mwana,” alitulia RPC na kuendelea
“Ni kweli umefanikiwa kutusumbua kwa muda huu mchache, lakini kila mtu alishangaa sana wakati Loren, kijana ulie muua alipokuwa akipiga simu na kusema AFANDE ANAHUSIKA, ndio maana nikakusimamisha, lakini kumbe ndio nimekupa nafasi ya kupoteza ushahidi.” Marsha alikuwa akiandika.
Marsha kuna chochote alichokuambia Inspekta?”
“Ndio mkuu, Inspekta alinieleza kuwa na wasiwasi wa kuwa Loren anahusika na mauaji ya Mwana, hivyo alikuwa akiniambia nikitoka pale nifanye mpango wa kuitafuta angalau picha yake…” akamueleza yote aliyosema, kisha RPC akatikisa kichwa na kusema
“Inspekta, unaweza kunieleza ni kwanini umeshiriki kwenye mauaji ya Raia halali wa Tanzania na wasio na hatia?”
“Mkuu, nashangaa tu hapa, maana kwanza mimi sijaua mtu yeyote, pili Loren mimi simjui hata kwa sura na tatu, muda wote mimi nimekuwepo nyumbani ila huo muda tu wa kununua chakua tu pekee,” alijitetea Inspekta huku akiamini kabisa kuwa hawezi kueleweka, kama ambavyo yeye huwa hawaelewi wale anao wahoji.
“Utanishawishi vipi Inspekta hadi nishindwe kuamini kuwa kinacho semwa si kweli?” alihoji RPC akiwa mikono kaweka kifuani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni kwa vile mimi siwezi kufanya hivyo, bali hizi ni mbinu chafu toka kwa watu ambao wamekuwa wakichukizwa na kazi nifanyayo na kuwaumbua,” alijitetea Inspekta na Mkuu akamwambia amthibitishie kile asemacho.
Akatoa simu yake ya mkononi na kuweka sehemu ya maogezi aliyorekodi na kumsikilizisha Mkuu wake wa kazi ambae alimuuliza Inspekta
“Kama ingekuwa wewe ndio Mimi hapa, yaani unaniletea ushahidi kama huo, wewe binafsi ungekubali?”
“Hapana mkuu ila kwa sasa huu ndio ushahidi wangu wa awali,”
“Sasa basi ajabu kitu kingine Inspekta kinachozidi kukutia shakani, ni juu ya kuuawa mtu huyo bila kukutwa kisu kifuani japo ameuawa kwa kisu, ningeweza kukuelewa tu iwapo huyu nae angekutwa na kisu mpfano wa vile aambavyo tumevikuta kwako, ningeweza kushawishika, ila kwa sasa…” alitikisa kichwa kukataa kabisa kumuelewa.
Inspekta sasa alikubali matokeo, akasimama kwa unyonge, RPC akapiga simu sehemu na kuja askari mmoja na kumwambia ampeleke korokororni. Hii ni sehemu maalum wanaposhkiliwa askari waliofanya makosa,
Wakati akitoka Marsha alikuwa amebaki amesimama akimtazama boss wake akipelekwa msambweni, hakuwa na jinsi ya kumuokoa, maana hakujua kama anachotuhumiwa ni kweli ama anasingiziwa.
Alipopotelea mbele huko, Marsha akamuomba Mkuu wake waongee kidogo, alimjulisha kuwa hata nae hana imani na Inspekta Kalindimya, lakini pia bado anaamini Inspekta huenda anasingiziwa.
“Kwa hiyo unasemaje?Unafikiri hastahili kufanyiwa hivi tunavyo mfanyia?”
“Hapana, nafikiri ni lazima achunguzwe, na ili achunguzwe vizuri ninafikiri tumuachie simu yake huku ikiwa ipo kwenye mikono yetu, iwapo tunaweza kuwasiliana na Mtandao anaotumia, kuna baadhi ya mambo wayazuie kutumika kwenye simu hiyo bali yapitie kwetu moja kwa moja, unasemaje mkuu?”
“Fafanua vizuri, bado sijakuelewa,” RPC alimwambia Marsha, ambae nae akamfafanulia mkuu wake wa kazi.
“Sasa kwa swala hilo mbona wala haihitaji Mtandao anaoutumia? Ni suala la kuongea na wataalamu wetu wa teknolojia na Sayansi wanaliweka tu sawa, name nimeipenda hiyo, ni wazo zuri,” alikubali RPC na kumtaka ampe karatasi ili amuandikie barua ya uthibitisho toka kwake kwenda kwa watu wa idara ya Mawasiliano.
Baada ya utaratibu wote kukamilika, alitoka Maarsha na kuelekea hadi kwenye ofisi ya RCO ambapo watu wa kitengo hicho walikuwepo, akawapa ile kazi na kuambiwa akae kama nusu saa hivi kisha awasiliane nao.
Walichukua aina ya simu kwa kutafuta IMEI namba kisha wakafanya vitu vyao, baada ya muda wakamuita Marsha na kumwambia kuwa mambo tayarii mazuri.
“Ok! Kwa hiyo mmefanya kama nilivyotaka mimi ama?”
“Ndio afande, wewe si umetaka simu zote anazopiga na kupokea zipite ofisini?”
Naam, lakini pia upande wa Email na Short Msg na Text zote nazo zipite ofisini, ila picha yoyote isiweze kutoka bali aweze kupokea,”
“Yote hayo ndio yaliyofanyika mkuu kama ulivyotaka,”
“Ahsanteni sana, na kwa herini,” wakati akitaka kutoka wakamuwahi na kumtaka asaini kwenye karatasi zao kwa ajili ya kumbukumbu zao za kiofisi, kisha akatoka kuekea tena ofisini ikiwa ni saa tatu usiku.
Akiwa njiani akaghairi na kuelekea nyumbani kwake, kwani alitaka kwenda kituoni kumpa simu Inspekta, lakini akaamua kwamba atampa hata siku ijayo tu kwani si yupo sehemu salama.
Alirejea kwake na kujitayarisha kwa kulala, lakini usiu wakati akiwa anapitia njozi zake akashtushwa na mlio wa simu, alipotazama simu ile akakuta namba ambayo kwake ilikuwa ni ngeni, alitegemea ataona jina kwenye namba hiyo, lakini haikuwa hivyo.
Alipokea na kutengeneza koo, ila hakusema kitu, mtu wa upande wa pili akasema kumwambia kuwa leo anafurahi kwa kuweza kumsumbua kidogo kisha a akauliza
“Mbona Inspekta sijakuona kwenye maiti ya Loren? Hilo maana lilikuwa ni kama pigo lako kuu, lakini usijali, kwa kuwa leo uliamua kujipumzisha na kuniletea kale kachangudoa, rorho yangu sasa imekuwa kwatu, ungekuja ningekufanyia kitu kibaya sana, ilikuwa nikuandalie pigo lingine takatifu kesho kama utazidi kuwa ni jeuri, nakupa masaa tu uniambie kama unaachana na mimi kabisa ama lah…” akanyamaza kimya tu Marsha, maana simu ile haikuwa yake, aliepiga akauliza
“Ni ujeuri tu ama ni usingizi?Lakini usigope, kwa maelekezo zaidi tutawasiliana kesho, hahahaaa!” sauti ikakata bila kusubiri jibu.
Sasa ndio Marsha akajua ni kwa nini Inspekta alisema hahusiki, nae sasa aliamini kabisa kwamba Inspekta Kalindimya hahusiki, baada ya kupokea simu ile ambayo ni ya huyo Inspekta.
“Yaani mimi ananiita changudoa? Na ni kipi ambacho walipanga kumfanyia Inspekta? Sasa kwanza Inspekta aliwafanya nini hawa watu hadi wamtafute kiasi hicho?” alijiuliza maswali mengi sana na kukosa majibu.
Akajilazimisha tu kulala akiazimia kesho kwenda kuongea na RPC na ikiwezekana pia na RPC ili Inspekta aachwe huru na aendelee kufuatilia jambo hilo. Akavuta shuka na kulala.
Aliamka mapema na kujiandaa kwenda kazini akiwa na azma ya kuongea juu ya alichokisikia.
Moja kwa moja alianzia korokoroni na kumkuta Inspekta akiwa amekaa akitazama nje, chumba alichokuwa amewekwa ni chumb ambacho kilikuwa kipo ghorofani na aliweza kutazama nje bila kuleta madhara yoyte kwake wala kwa wengine.
Ni eneo ambalo asingeweza kudhuru mtu wala kujidhuru mwenyewe, hiyo ndio korokoro ambapo waliwekwa askari wenye vyeo kupisha uchunguzi, sasa ndio Marsha alikuwa nje ya chumba hicho na kumuita Inspekta kwa sauti ya upole akiwa mlangoni.
Inspekta akamsogelea akiwa anaonekana kama ni mtu ambae hajalala, nbalia alimsalimia na kumwambia kwamba anaomba msamaha jana alisahau kumpa simu yake
“Usijali, lakini pamoja na yote haya Marsha, sielewi chochote kuhusu kifo cha Loren, hebu nieleze…” Masha akamkata kauli
“Inspekta hata name najua kuwa wewe hujui lolote, ni usiku mmoja tu umenifanya nitambue hilo,” Inspekta akashangaa
“Kivipi Marsha?”
“Inspekta, chukua kwanza simu yako, acha nikafanye mpango nikutoe mengine tutaongea zaidi ofisini,” akasema huku akimpa smu hiyo kupitia kwenye mlango wa chuma uliowatenganisha kwa kati, mmoja akiwa ndani na mwingine akiwa nje
“Sawa, mimi nipo humu,” nae akapokea ile simu na Marsha akaondoka kwa ahadi ya kurejea baadae.
Akatoka tena na sasa akaingia kwenye ofisiya RPC na kukuta bado hajawasili, akarejea ofisini kwake hadi aliposikia wakijibu maswali kadhaa ambayo kila wakati anapofika pale huwahoji askari waliopo zamu.
Akasubiri hadi alipohisi kwa muda ule atakuwa ameisha ingia ofisini mwake, nae akanyanyuka na kuelekea huko. Alikuta na kuongea nae akimpa maelezo juu ya kilichojiri tangu walivyo achana siku iliyopita.
“Sasa simu hiyo ndio imekufanya uamini kuwa Inspekta hahusiki?”
“Yap Boss, ni moja ya sababu,”
“Haitoshi hiyo, huoni kama labda huenda tayari alikuwa amempanga mtu ampigie simu muda huo?”
“Sasa Mkuu huyo amewasiliana nae saa ngapi hadi kumwambia hivyo? Maana tangu nimefika kwake hajaongea na simu yake hadi tunafika hapa na kukukabidhi simu wewe, hakuwa amejua ambacho kitakacho tokea, sasa huyo mtu amempanga saa ngapi? Hapana mkuu ni kama alivyosema mwenyewe kuwa hii ni sawa na usaliti kwa wasiopenda kazi anayoifanya,”
“Kwa hiyo wewe una ushauri gani sasa?” RPC alimuuliza huku akitazama saa kama vile ni mtu ambae anasubiri muda ufike ama anacheleweshwa na kitu Fulani.
“Mkuu ninashauri Inspekta aachiwe huru na aendelee na kazi hii kama awali, maana inaonekana hata muuaji anaweweseka pindi Inspekta anapoonekana sehemu,”
“Sawa, hebu mlete hapa niongee nae,”
“Marsha akatoka karibu akimbie na kumfuata Inspekta na kurejea nae baada ya dakika chache, wakati wakija wakakutana njiani na RPC akiwa anatoka
“Aah, Inspekta kwanza pole sana, lakini nenda nyumbani kwanza kapumzike, mimi nina dharula mbaya ambayo imelazimika nitoke sasa hivi, nafikiri tutawasiliana, sasa Inspekta?” aliuliza huku akimpa mkono
“Sawa mkuu,”
“Baadae tutawasiliana,” hata kabla Inspekta hajajibu, yeye akawa anashuka ngazi kwa kasi na kutokomea moja kwa moja nje kwenye gari yake na kuwaacha Inspekta Kalindimya na Marsha wakiwa wamesimama wanatazamana, Marsha akauliza
“Sasa Mkuu nipe ratiba yako,”
“Ratiba yangu kwa sasa ni moja kwa moja kwa moja kwa kina Loren, wewe ulifika jana?”
“Ndio nilikwenda mara tu baada ya kusikia hii taarifa ya kifo chake,”
“Nani alitoa taarifa ya kifo hicho?”
“Kwao wenyewe ambao walikuwa wakimtafuta nasasa walimkuta kwenye ghorofa moja lililokuwa likiendelea kujengwa huko maeneo ya Kijitonyama,”
“Vipi ujumbe wowote ulipatikana kwenye maiti?”
“Hapana wala haukukutwa ujumbe wowote, ila kupitia uchunguzi wa awali inaonekana aina ya kisu kilichotumika ni tofauti na vile vya awali, kiasi nahisi muuaji huyu nitofauti na Yule alie waua kina Mwana,”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwanini unasema hivyo?”
“Kwanza hakuacha ujumbe na hiyo si kawaida yake na pili hakutoa taarifa juu ya mauaji yake, wewe unaonaje? Ama yawezekana amekuja kivingine?”
“Kwani Marsha wakati unakuja kwangu tayari tukio lilikuwa limeisha tokea?”
“Ndio, muda ule mimi nimekuja kwako ile ni mara ya pili, mara ya kwanza nilikuja na kuwachukua askari waliokuwa pale getini na kuondoka nao na kuwaacha hao waliopo kisha nikawaleta huku ili kuwahoji nao wakakiri kuwa ulitoka kama ambavyo ulisikia,”
“Dah! Kwa hiyo muda niliotoka mimi na ndio muda alio uawa Loren?”
“Yaani bila tofauti ya hata dakika kadhaa,”
“Mh! Kazi ipo, huyu muuaji ni jasusi, na tukimuendea kasi huyu tutajikamata wenyewe, sasa la msingi hapa ni meme nawe kwenda hospitali kwenye maiti ya Loren kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alipendekeza Inspekta na Marsha akasema ni kweli hawajaendea hata hivyo kuchukua majibu ya utafiti wa chanzo cha kifo cha Loren.
“Lakini Inspekta wewe ni heri tu ukapumzike, nahisi utakuwa haupo vizuri kabisa, niachie mimi niende kisha ukiwa vizuri utanijuza ulipo nitakuja kama ni nyumbani ama uytakuwa umekuja kazini,” alipendekeza Marsha naInspekta akakataa
“Hapana kabisa, nichoke kwa kazi gani name nilikuwa nimeka tu muda wote huo, hapa suala la msingi ni moja kwanza, je muuaji amekujua nawe ama hajakujua?”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment