Simulizi : Anga La Washenzi (2)
Sehemu Ya Nne (4)
“Umeona kitu?” aliuliza mwanaume mmoja rangi maji ya kunde. Hawa walikuwa ni wafuasi wa bwana Sheng. Kwa idadi wanaume watano wakiwa wamekuja hapa kumkomboa mkuu wao.
“Hamna kitu,” mwenzake akamjibu.
Basi wakasonga tena wakiwa wananyata. Wakasonga na kusonga, na baada ya dakika kama sita, wakawa wamefika kwenye mlango wa chumba ambacho amehifadhiwa bwana Sheng.
Na kwa muda wote huo hawakuwa wamemwona mtu yeyote yule. Kitu pekee walichokiona ilikuwa ni gari aina ya cadillac nyeusi ikiwa imeegeshwa kwa nje ya kiwanda hiki.
Basi wakafungua mlango, haukuwa umebanwa na komeo wala loki, wakazama ndani na kumwona Sheng akiwa amejilaza chini hajielewi. Ni pumzi tu ndiyo huashiria kuwa yu hai.
Wakambeba na kuanza kujongea kwenda nje. Wanaume wawili walifanya hivyo, na wengine watatu wakiwa wanawalinda wenzao wakitazama huku na huko kwa tahadhari kubwa. Mikono yao iliyobebelea bunduki ikienda kushoto na kulia, juu na chini.
Wakafanikiwa kutoka nje pasipo mushkeli. Wakasonga zaidi kulifuata gari lao, ila ajabu hawakulikuta. Pale walipoliacha hakukuwa na alama yoyote ile ya gari.
Na hata lile cadillac nyeusi waliyoiona wakati wanakuja, nayo haikuwapo. Wakatazamana kwa bumbuwazi.
Wakatazama huku na kule, hakukuwa na kitu mbali na kiwanda kilichochoka na kufubaa. Mazingira yalikuwa kimya mno. Majani na matawi ya miti yaliyumbishwa na upepo, kisha yakatulia.
***Ndani ya dakika moja na sekunde mbili, watu wale watano waliokuwa wamembebelea Sheng kumwokoa, wakawa wamedondoka chini isijulikane nini kiliwaangusha.
Alah! Baada ya muda kidogo vichwa vyao vikaanza kuvuja damu kulowanisha nyasi na mchanga. Na kumbe vilikuwa vimetobolewa na ncha za risasi!
Risasi hizi zilikuwa zimetokea wapi? … kwa umbali wa kilomita moja na hatua kadhaa, kule juu kabisa ya chumba kimojawapo kilichopo ndani ya kiwanda, ndipo risasi zilipotoka.
Na basi hazikupiga kelele hata kidogo maana midomo ya bunduki ilikuwa imemezwa na viwamba vya kumezea sauti.
Watu hao watano, the intelectual instinct, wakatoka wakiwa wanatembea mwendo wa kubarizi fukweni mwa bahari, wakawaendea watu hao wavamizi, ambao kwa sasa wamekuwa miili tu, wakamnyanyua bwana Sheng na kurudi naye ndani.
“How did they know we are here?” akauliza mwanaume mmoja wa kizungu. Nadhani kwa sasa ni vema tukawatambua kwa majina ili iwe vema, huyu aliyeuliza aitwa Denmark, wenzake wanne ni, Sweden, Ireland, Scotland na Wales.
“We have to know that,” akasema Scotland kisha akamtazama bwana Sheng aliyekuwa amelala hajiielewi. “And we have to before it’s too late.”
“There must be a thing here,” akadakia Denmark. Naye pia akimtazama bwana Sheng. Macho yao wote yalikuwa ya kijanjajanja sana. Na sura zao za watu wa mafikirio ya mbele. “I think we have to take him home,” akashauri bwana Denmark.
Basi wakamtoa bwana Sheng na kumweka kwenye gari yao mpaka eneo wanapokaa. Huko wakamfanyia bwana Sheng ‘scanning’ ya mwili na kubaini ana chip ndani yake. Wakaitoa na Denmark akadhamiria kuiharibu.
“No, don’t do that,” akasema Scotland. Alikuwa ni mwanaume mwenye mwili mpana kuzidi wote. “We need that chip.”
“Yah!” akadakia Wales na kuongezea, “It’ll help us getting the rest of them.”
***
Saa nane mchana ….
Beep … beep … beep … beep
Sauti kwa mbali ilisikika masikioni mwake. Alihisi mwili wake mzito. Alijaribu kufurukuta ila alishindwa. Alihisi viungo vyake vya mwili huenda vimepooza.
Ila hakuchoka kujaribu kupambana kutoka katika wimbi hili la giza. Alihangaika na hatimaye, kama mtu aliyetoka kunusurika kuzama kwenye maji ya kina kirefu, akakurupuka akivuta hewa mafundo makubwa makubwa.
Akatazama kushoto na kulia. Tumbo likamvuta kwa maumivu makali ambayo alishindwa kupambana nayo, akajikuta anarudisha kichwa chake upesi kwenye mto akigugumia maumivu.
Tumboni alikuwa ana bandeji iliyohifadhi jeraha lake la risasi. Pia kwenye mguu wake wa kushoto alikuwa na jeraha la risasi iliyomparasa. Kichwa kilikuwa kinamuuma na fikira zikiwa nzito kuvutika.
Akashusha pumzi ndefu. Akaperuzi chumba alichomo, akagundua ni hospitali tena ya kisasa. Akajiuliza amefikaje hapo, kuna mtu aliyemleta? Hakukumbuka hata tone. Akatazama tena kushoto na kulia.
Kidogo baada ya kutulia akakumbuka namna alivyoingia matatizoni. Mara ya mwisho kuwa na fahamu alivamiwa na kupokonywa kila alichokuwa nacho. Kulitambua hilo kukamfanya azame zaidi mawazoni. Ilikuwa ni kama vile amechokoza fikra.
Akawaza tukio zima na namna ilivyokuwa. Ina maana yule afisa wa serikali alimzunguka? Alijiuliza. Mara mlango ukafunguliwa akaingia nesi, mwanadada mchanga wa kichina. Uso wake ulikuwa mfupi wenye miwani ndogo ya kumsaidia kuona.
Alipomwona mgonjwa wake, akatabasamu na kumuuliza hali yake. Lee, ambaye ndiye mgonjwa, akamwambia anaendelea vizuri. Ila naye akarusha swali juu ya nani aliyemleta hapo maana kuwapo hospitali kama ile, yenye hadhi, haileti mantiki kuletwa na wasamaria.
Nesi akatabasamu, akiwa ameweka mikono yake kwenye mifuko ya koti, akamwambia Lee kuwa ni wasamaria ndiyo walimleta. Na kwasababu ya kitambulisho chake ndiyo maana wakamleta mahali hapo.
Baada ya kujibu hivyo, akamuaga na kumtaka apumzike. Atakuja kumwona tena baadae. Basi akaendaze.
Lee akabaki akiwaza kuhusu hicho kitambulisho ambacho nesi alikiongelea. Akakumbuka ni cha ‘member’ wa familia ya Wu. Alikiweka kitambulisho hicho nyuma ya mfuko wake wa suruali baada ya kusisitiziwa afanye hivyo kabla hajatoka makao makuu.
Akiwa bado fikirani, ghafla anasikia sauti ya kelele na mara inakoma na kuwa kimya kama awali! Anapata shaka. Punde kidogo, anaona kivuli cha mtu mlangoni. Kwa maana mlango ulikuwa umegawanywa nusu ya chini ‘material’ ya mbao na ile nusu ya juu, kioo cha kufifia.
Kivuli hicho kilikuwa ni cha mwanaume mwenye mwili mpana, na kichwa chake alikuwa amekihifadhi na kofia ya wale wapanda farasi.
Mlango ukafunguka …
**
Saa tatu usiku …
Sauti ya mtu akiteta kwenye simu akitumia lugha ya kichina ilisikika toka dirishani. Sauti hiyo ilidumu kwa dakika tatu tu alafu simu ikakata. Baada ya muda mfupi wakaja wanaume watano ndani ya hiyo nyumba, na maongezi yakafanyika.
Bado sauti zao zilikuwa zinatoka dirishani. Na kwasababu dirisha lilikuwa mbali kidogo na sebule, hawakusikika vema nini wanateta. Baada ya kama robo saa, wale wanaume wakatoka na kwenda zao. Nyumba hii ikadumu mwangani kwa dakika kumi, kisha ikawa gizani.
**
Saa nne usiku …
“It’s time,” Wales alimtonya Denmark aliyekuwa ameketi sebuleni. Mwanaume huyo wa kizungu akanyanyuka na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha mwisho. Hata sasa kwakuwa ni usiku wa kulala wote walikuwa wamevalia nguo nyepesi na si suti zao kama ilivyo ada.
Kwenye chumba hicho cha mwisho, ndani alikuwapo Sheng akiwa amewekwa kitini. Alionekana mdhaifu asiye na nguvu. Macho yake yalikuwa yanarembua na hata mdomo wake alikuwa anapata shida kuufumba.
“Hey …” Denmark akaita akimpigapiga Sheng vikofi vya shavu. Kisha akaketi kwenye kiti mbele ya Sheng, nyuma yake Wales na Scotland wakiwa wamesimama.
“Don’t worry it is going to be easy and fast. I won’t last long,” alisema Denmark akimtazama Sheng ndani ya macho yake madhaifu.
“So tell me who are you?” Denmark akauliza.
“My name is Sheng Ping. The East African zonal manager of Wu clan and family from Hongkong, China,” Sheng akajibu vema, hata Denmark akatabasamu na kuwatazama wenzake., “I think we’ve got it.”
Kila alilouliza, Sheng akawa mwepesi wa ndimi basi akafunguka anavyotakiwa. Watu wale walipopata kila walichokitaka katika ‘tape’, Denmark akanyanyuka na kukoki bunduki yake.
“It’s time to die, pal.” akainyooshea mdomo wake kwenye paji la uso la mwanaume huyo, ila kabla hajaifyatua, Scotland akamgusa bega lake na kumwambia, “We still need him.”
“Are you sure?” Denmark akauliza. Kidole chake kilikuwa tufeni.
“Yes, I am sure, we do,” Scotland akajibu. Basi Denmark akashusha silaha yake na kuichomeka kiunoni.
***
Saa nne asubuhi …
“Ndiyo hapa!” akasema mwanaume mmoja mwenye sura mbovu. Alikuwa ni dereva wa gari hili, Murrano rangi ya fedha. Ndani yake kulikuwa na wanaume watano waliobebelea silaha. Na hapa walipokuwa wamesimamisha gari ilikuwa mbele ya nyumba fulani, ghorofa, ambayo haijamaliziwa.
Basi wanaume wale wakashuka wote, na hao wakazama ndani ya jengo hilo. Ndani ya muda mfupi wakatoka wakiwa wamembeba Sheng.
Walimkuta akiwa amelala chini hajiwezi. Wakamsweka ndani ya gari na kutimka pasipo kupoteza muda.
Basi Scotland akatokea mbali kidogo na nyumba hiyo akiwa anatazama gari likiyoyoma, na simu yake ipo sikioni, akasema, “It is on the right track.” kisha akakata simu na kuidumbukiza mfukoni.
Baada ya dakika moja tangu mlango ulipogongwa, ukafunguliwa na kichwa cha mchina kutokeza nje. Kutazamana, akaona Sheng akiwa kabebelewa na wanaume aliowaagiza basi akawapokea na Sheng akaingizwa ndani na kisha maongezi machache yakachukua nafasi.
“Hatukukuta mtu yeyote, isipokuwa mwili wake tu,” yule dereva mwenye sura mbovu aliteta.
“Hatujajua wamemfanyia nini, na hatujajua ni wakina nani kwa lengo gani.”
Basi yule mchina akaguna akimtazama Sheng kwa macho makini. Akatulia kidogo na kusema mawazo yake.
“Kwa asilimia zote watakuwa ni watu wa yule mzungu ambaye Sheng alimuua. Ila kwanini hawakummaliza kwa muda wote huo? Ni nini walikuwa wanafanya naye?” Hata yeye akapatwa na maswali.
Basi isiwe na haja kwa muda huo, ilikuwa ni lazimu bwana Sheng apewe huduma haraka asije fia kwenye ‘mikono salama’. Daktari wa mule mule ndani akaitwa na kumfanyia ‘diagnosis’, baada ya hapo akamtundikia dripu na kutaka kufanya maongezi machache na yule bwana wa kichina.
Daktari huyu alikuwa ni mwanaume mzee mwenye kiwaraza kichwani. Sura ya upole na macho ya hekima za utu uzima. Alivalia koti jeupe ambalo lilionekana kumvaa kutokana na ufupi wake.
Akasafisha koo na kusema, “Bwana huyu ametiliwa sumu.” Aliongea kwa uhakika, ila sauti yake ikiwa chini. “Afya yake ni dhalili hivyo anahitaji uangalizi wa juu mno.” aliposema hayo akakohoa kidogo na kuvuta hewa ndefu kwa pua, kisha, “Namhitaji kule eneo langu la kazi kwa uangalizi zaidi.”
Sasa ameshasema daktari, yule bwana wa kichina akawa hana kipingamizi. Kikubwa akaongozana na daktari mpaka huko ambapo Sheng alipelekwa, akaingizwa ndani ya chumba maalum, ndani ya jengo litumikalo kama sehemu ya kutoa huduma za matibabu ndani ya eneo hilo.
Humo ndani kulikuwa kuna mazingira tulivu, na hata wahudumu wa kutosha, wa China na hata wa hapa nchini.
“Inatosha, yupo mikono salama, waweza kwenda,” alisema Daktari akimtazama bwana yule wa kichina. Naye pasipo kubisha akaendaze. Ila akiwa na maswali kichwani.
Sasa ufisadi wake ulikuwa hatiani. Endapo Sheng akisimama kwa miguu yake ni wazi hatabakizwa na pumzi. Hata akajikuta tumbo likimuuma na kichwa pia.
Baadae, kwenye majira ya saa mbili usiku, akatoka ndani, akiwa amejipaki ndani ya gari nyeusi aina ya discovery, akaelekea zake viwanja akiwa ameongozana na vijana wake watatu wa kazi.
Alilenga kupumzisha kichwa chake kwa mawazo, lakini pia alikuwa na mawazo fulani ambayo alitaka kuwashirikisha hawa vijana wake watatu ambao alikuwa amependezwa nao.
***
Saa sita kuelekea saa saba usiku …
Kuna sauti kubwa ya muziki hapa. Watu wengine wapo ndani ya kiwanja wakijibetua na kunengua kwa mujibu wa midundo ya muziki huo. Wengine walikuwa wamekaa kwenye makochi, na wengine wakiwa wameshikana, wanatomasana ama wamesimama tu wakiongea kana kwamba wanasikiana dhidi ya muziki huu mkubwa.
Mwanga ulikuwa hafifu, ila hewa ya kutosha. Kote palikuwa pametawaliwa na kiza, ila vijitaa vidogodogo vyekundu, vya njano, vya kijani na vya kila rangi vikipitapita huku na huko.
Mahali hapa palikuwa ni klabu ya usiku.
Wakiwa wamekaa kaunta, kila mmoja ana kinywaji chake, na hapo tayari wameshakunywa kadha wa kadha, yule bwana wa kichina, aidha kwa kuona sasa ni muda muafaka wa kuteta, akasema,
“Mmetosheka?”
Wale mabwana alioongozana nao wasiseme kitu, wakatabasamu. Ishara ya kwamba bado ni muda mchanga. Basi yule bwana wa kichina akawaambia wanywe mpaka waseme wenyewe basi.
Lakini wakiendelea huku kunywa, akaendea adhma yake.
“Nataka muwe watu wakubwa sana. Nafikiria kuwapa nafasi nyeti sana pale kitengoni. Mwaonaje?” japo muziki ulikuwa mkubwa, sauti yake nyembamba ya kichina ilipasua na kusikika vema. Wale mabwana wakatabasamu.
Ni wazi pande la nofu la nyama liliwekwa mezani mwa mabwana fisi.
“Aaah safi tu!” akasema bwana mmoja. “Tupo tayari kabisa, au mwasemaje?”
“Yah! Sisi hatuna shida kabisa!” wenzake wakamuunga mkono na tena huku usoni wakijawa na matabasamu ya kiroho, na hata kujichekesha pasipo na msingi.
“You know, nimetazama nikaona mnanifaa sana,” akasema bwana yule wa kichina. “kati ya watu wote nikaona ninyi ndiyo watu wa kutenda kazi na mimi … mna nguvu, na intelligent …” bwana huyu wa kichina akaweka kituo kwa kunywa kwanza fundo moja la kinywaji chake, kisha akaendelea wakati hadhira wake wakimsikiza kwa umakini.
“Ila sasa kuna tatizo moja, moja tu, moja!”
“Lipi hilo?” akauliza mmoja wa mabwana wale. Basi yule bwana wa kichina akanyamaza kwanza, kama mtu anayefikiria, kisha akauliza,
“How far can you go to get this?”
“Uncountable miles,” akasema bwana mmoja. Huyu alikuwa karibu zaidi na bwana huyu wa kichina. Na maneno yake haya yakamfurahisha bwana huyo, akatabasamu, “That’s nice. If then, I have a work for you to do.”
Basi akawaeleza kazi hiyo na alipomaliza kuwaeleza, wakapeana mikono ya kukubaliana. Ila bwana mmoja, yule aliyekaa mbali na bwana huyu wa kichina, akawa na shaka. Akauliza,
“Vipi kuhusu wengine?”
“Wengine!” mwenzake aliye jirani akatahamaki. “Hapa duniani ulizaliwa na nani? Jiangalie wewe ndugu yangu, acha ufala!”
Kuliunga hilo mkono, wengine wakacheka na kisha wakaendelea kunywa na kunywa. Baadae kwenye majira ya saa nane kasoro, bwana yule wa kichina akaona inatosha, basi akawataka waondoke. Ila akaona ni vema kama akipata mwanamke mmoja wa kwenda kumpunguza uzito kwa usiku huo.
Akamwamgiza mmoja wa wale jamaa aliokuja nao amtafutie mwanamke mzuri wa kwenda naye. Pasipo hiyana mwanaume huyo akafanya kazi na ndani ya muda mfupi akarejea na mwanamke mzuri kabisa, mweupe mwenye figa ya kuzembesha.
Na mwanamke huyu, kama bahati au nuksi, alikuwa ni Glady.
Bwana yule wa kichina akapendezwa naye hakika, wakaondoka naye kwenda kujipaki garini warudi makaoni.
**
Mazingira haya hayakuwa mageni. Ni kama vile aliwahi kufika huku, kumbukumbu zake zilimweleza bayana. Alijitahidi kutazama barabara na mazingira, akajikuta anapata picha fulani.
Na kweli hakuwa amekosea kabisa. Macho yake hayakuwa yanamdanganya, hili eneo si geni kwake. Na alipotuliza kichwa vema sasa akakumbuka. Mahali huku alishawahi kumleta yule mwanaume wa kichina aitwaye Lee.
Glady akaminyua mdomo wake. Hapa kidogo akamkumbuka mwanaume yule wa kichina, Lee. Na basi akajikuta anachukua simu yake na kupekua kama jina lake lipo kwenye simu. Akaliona.
Akataka kutext, akasita. Litakuwa jambo la kipumbavu akifanya hivyo. Basi akatulia kwanza akiwaza ujinga fulani kichwani mwake. Punde sauti ya honi ikamtoa fikirani. Walikuwa wameshafika getini. Geti likafunguliwa, wakazama ndani.
Ndimo humu humu! Akaendelea kuhakikisha. Ndimo humu humu alipomleta Lee. Macho yake ya wizi yakawa yanaangaza sana, huku na kule mpaka gari kusimama na kuongozana na wanaume wale kwenda kwenye makazi ya yule mchina.
Yeye akaamriwa aingie ndani, na yule bwana wa kichina akabaki na wale mabwana wengine pale mlangoni. Akateta nao kwa sauti isiyosikika vema, na kisha wakafunga mjadala kwa mchina yule akisema, “Msiniangushe!” wanaume hao wakaondoka zao, bwana yule wa kichina akazama ndani.
Akavua nguo na kwenda kuoga akimwacha Glady peke yake.
Glady akatazama huku na kule. Kimini chake akakivuta akibadilisha pozi la kukunja nne. Punde akanyanyuka na kuchungulia dirishani. Akaangaza nje akijaribu kufikiria ni upande upi yalipo makazi ya Lee. Muda kidogo, akasikia mlango wa bafu ukifunguliwa, basi akarejea kitini.
“Kaoge,” yule mchina akamwambia Glady. Glady akanyanyuka na kwenda bafuni. Akaoga akiwaza kuhusu Lee. Kabla hajatoka, akasikia sauti ya yule mchina huko chumbani. Alikuwa anaongea na simu.
“Hakikisha anakufa kabisa, sawa?”
Glady akashtuka. Akapatwa na maulizo kichwani. Sasa akapata picha juu ya nini yule bwana wa kichina alikuwa anaongea na wale wajamaa. Akaguna. Akapiga moyo konde na kutoka bafuni. Akaketi kitandani.
Bado bwana yule wa kichina alikuwa anaongea na simu.
***
Alikuwa anatoa maelekezo na huku akisisitiza kuwa mlengwa lazima amalizwe kwa namna ya siri isije zua utata. Basi baada ya muda, akanyamaza na kisha kumgeukia bibie Glady. Ila macho yake yalieleza namna gani alivyokuwa yupo nje ya ‘mood’.
“Umekwishaoga?”
“Ndio, kama unavyoniona,” akajibu Glady ila naye akiwa na sura ya woga na maulizo.
“Kuna shida yoyote?”
“Mmh mmh hamna.”
“Mbona unaonekana haupo comfortable?”
“Wala, niko ok tu.”
Kukawa kimya kidogo. Bwana yule wa kichina akatazama chini kisha akashusha pumzi ndefu puani na kuuliza,
“Haujaja na nguo nyingine mbali na zile?” huku akitazama nguo za Glady zilizopo kwenye kiti.
“Hapana, sijaja na zingine. Kwani vipi?”
“Nothing. Nilidhani umekuja na zile nguo za kusisimua, zile zaaa … you know? Anyway, usijali. Nipe muda kidogo. Sawa?”
“Kwani tulikubaliana nilale huku?”
“Kulala itakuwa shilingi ngapi?”
“Utaongezea mara mbili ya ile tuliyokubaliana.”
“Haina shida.”
Bwana yule wa kichina akakwapua simu yake na kusimama, “Ningojee hapa.”
Akaenda zake sebuleni. Glady akatulia pale kitandani kwa muda kidogo kisha akasimama na kwenda mlangoni kutega sikio. Kulikuwa kimya. Ila baada ya muda kidogo akasikia sauti ikianza kuteta na simu.
Kuna wazo likamjia kichwani. Haraka akaendea simu yake na kutafuta jina la Lee. Akajaribu kubipu. Alipoona haiiti, akazama upande wa ujumbe, ila akatoka tena na kwenda kwenye mtandao wa whatsapp, huko akamsaka Lee na kumtumia ujumbe.
**
“Kuna ulinzi, ila tutafanikisha,” alisema bwana mmoja mshirika na yule bwana wetu wa kichina. Aliposema hayo akaweka simu mfukoni kisha akatazama kando, kulikuwa na jamaa yake mwingine. Walikuwa wameazimia kufanya kazi hii watu wawili tu kuepusha msongamano ambao ungelipeleka kushtukiwa.
Akampatia ishara ya kichwa, na huyo mwenzake, kwa haraka, akaenda nyuma ya jengo. Jengo hili ni lile ambalo amelazwa bwana Sheng kwa matibabu zaidi. Na halipo pweke, bali limezingirwa na walinzi kadhaa.
Basi huyu bwana baada ya kutia simu yake mfukoni, akaanza kujongea, punde akamfikia mlinzi na kusalimiana naye, akaumulizia hali ya mgonjwa.
“Anaendelea vema,” akajibu mlinzi, na kisha kama mtu asiye na habari au shaka, akatazama zake kando kuendelea na kazhi yake.
“Naweza kumwona?” bwana yule akanena. Mlinzi akamtazama kwa kukunja ndita.
“Saa hii?”
“Kwani kuna shida?”
“Huoni kama kuna shida? Mgonjwa anatazamwaje saa hii. Daktari amesema anahitaji ma …” upesi akadakwa shingo, kak! Akavunjwa. Akadondoka chini kama mzigo.
Basi bwana yule haraka akasonga ndani asionekane na mlinzi mwingine yeyote. Akadaka korido na kusonga kwa hatua kadhaa kubwa kabla hajakutana na nesi.
“Nikusaidie nini, mlinzi?”
Alikuwa ni nesi wa kichina. Mfupi na mdogo kwa umbo. Sura yake ilikuwa thabiti na macho yenye mkazo. Basi bwana huyu akatabasamu na kusema, “Samahani, ni usiku mkubwa. Nimekuja kumtazama mkuu, kuna machache ya kusema naye.”
“Siwezi nikakuruhusu kwa sasa. Njoo kesho asubuhi.”
“It’s urgent, please. In fact nimeagizwa na mkuu. Hatonielewa kama nikimwambia sijafanikiwa.”
Nesi akashusha pumzi na kuminya lips zake nyembamba. “Ok, ni muda mfupi nakupa.”
Hakujua amempatia kibali muuaji. Bwana yule akatabasamu na kwenda zake upesi akakamilishe kazi. Ila bahati isiwe kwake, hakuwa anajua wapi alipolazwa mlengwa wake. Hivyo ikamlazimu kupoteza kama dakika mbili kabla hajawa mbele ya mtu anayetakiwa kumuua.
Kabla hajafanya hilo, simu yake ikanguruma mfukoni. Akaitoa na kutazama, alikuwa ni mtu aliyemuagiza akafanye tukio. Akapokea na kumwambia kwa kunong’oneza, “I am in, wait.” kisha akakata simu.
Sasa ikawa imebakia kumaliza tu kazi, bwana Sheng akawe historia ya kale inayotisha.
Alikuwa amelala kitandani hajielewi hata linaloendelea. Dripu ilikuwa ipo kwa juu ikidondosha matone, na usoni alikuwa ana ‘nyago’ ya kumpatia hewa ya oksijeni. Mwili wake wote ulikuwa umefunikwa n shuka isipokuwa shemu yake ya kichwa na mikono tu.
Kando kando yake kulikulikuwa na vifaa kadhaa vinavyobeba uhai wake kwa ncha ya kidole. Na pia kulikuwa na kifaa kioo kionyesha maendelea ya mapigo yake ya moyo. Ama kwa hakika yalikuwa hafifu.
Bwana yule akaweka mikono yake shingoni mwa Sheng. Hajaminya, mara akasikia kipyenga cha ‘hafla, Prrrrriiiiiii!!!! prrrrrrrriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Prrrrriiiiiiiiiii! Akatoa macho. Huko nje akasikia vishindo vya watu vikitesa ardhi!
Kwa muda kidogo akawa ametekwa na buwazo. Akimbie? Au amalize kazi yake? Alihisi kutetemeka. Kama angeendelea kumnyonga bwana Sheng, wazi ingelimchukua muda kidogo na yeye huo muda hakuwa nao. Basi afanye nini cha haraka kunusuru roho yake na huku atimize wajibu?
Akanyofoa waya za mashine zimsaidiazo mgonjwa, kisha upesi akatoka nje akikimbia. Kufika nje, akakutana na watu taribani kumi kwa idadi ya haraka. Wote wakiwa wamemnyooshea bunduki, akaamriwa anyanyue kwapa. Akatii.
Kule ndani nesi akawahi chumba cha mgonjwa. Huko akakuta ‘alarm’ zalia kwa fujo na mgonjwa akiishilia uhai. Haraka akarejesha mashine katika hali ya kawaida, na akaokoa maisha ya mkuu wake kwa ncha ya sindano. Mashine ya mapigo ya moyo ikaanza kusoma upya. Akatip! … akatip! … akatip! … akatip!
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mgonjwa akihema kwanguvu ndani ya kinyago.
***
Ngo! Ngo! Ngo! Bwana wa kichina alisikia hodi hiyo, ila akasita kwanza. Macho yalikuwa yamemtoka. Jasho jembamba lilikuwa lamchuruza. Na moyo wake ulikuwa unakita kwanguvu kubisha hodi mbavu.
Hodi ikarudiwa tena. Na hakuwa na namna ya ziada sasa zaidi ya kwenda kuiitikia. Akiwa na kibukta chake, na mwili unamtetemia, akajonga na kutengua kitasa. Nje akawaona wanaume wawili anaowatambua wakiwa wamepigishwa magoti, na wanaume wengine takribani kumi wakiwa wamewasimamia na bunduki.
“Walitaka kumuua mkuu Sheng!” shtaka likatolewa kwa sauti kuu. “Wamevamia hospitali na kuua walinzi wanne katika jaribio hilo!”
“Inawezekanaje jambo kama hilo?” akashangaa bwana huyu wa kichina, kisha akawatazama walengwa na kuwauliza kwa sauti ya ukali kidogo,
“Ni kweli yanayozungumzwa?”
Wale watu wawili wakamtazama. Na kwa soni, akaepusha macho yake kutazama kando.
“Mkuu, wanastahili kuuawa mara moja!” akasema mmoja wa wale mabwana waliowaleta wale mateka. Akaungwa mkono na wenzake wote. Ndio! Wanastahili kuuawa. Na hiyo ndiyo ilikuwa sheria. Hamna anayebakiziwa uhai akidiriki kufanya jaribio la kummaliza mkuu. Na adhabu yake yafanyika mbele ya umati.
Hata bwana huyu hakuweza kulikataa hili kwani litazua mjadala mkubwa na hata kumweka rehani. Basi akakbidhiwa bunduki kutimiza agizo. Bunduki ilikuwa na risasi kumi na nane.
Wakati hayo yote yanaendelea, Glady alikuwa anashuhudia kwa kupitia dirisha. Mambo haya yalikuwa yanamtisha mno. Ametoa macho na kinywa chake kipo wazi.
Risasi zikavuma mara mbili! Wale watu wakadondoka wafu. Wakabebwa na kwenda kuzika kana kwamba mizoga, na huku nyuma wakimwacha bwana yule wa kichina majuto na maumivu makubwa sana kifuani.
Aliingia ndani akamtaka Glady aondoke zake upesi. Na baada ya punde akakutana na jamaa wake mmoja mpangoni aliyebaki. Akiwa amekabwa na donge la uchungu kooni, akasema, “Mpango wetu ulikuwa wa kipumbavu na wenye papara. Sasa tumeshawapoteza wawili.”
Yule bwana akamuuliza, “Una mpango mwingine?”
“Pengine ninao,” akasema bwana huyu wa kichina. “Na sasa nitaufanikisha mwenyesha jua likiwa linawaka.”
Basi hawakuongea sana, jamaa yule akaendaze. Watakutana baadae.
***
Saa tatu asubuhi …
“Do we need to hold on more?” aliuliza Wales akimtazama Denmark. Wote walikuwa wameketi sebuleni, vichwani wa earphones zilizokuwa zinawaletea taarifa toka kwenye kifaa maalum kidogo walichomfungia Sheng. Na mpaka sasa kifaa hicho kiilikuwa kimeshawatanabahisha makazi aliyopo Sheng na hata sauti ya yale yanayozungumwa ndani ya duara la robo kilomita toka kila pande ya dunia ya mahali alipo Sheng. Tena kwa usikivu mzuri.
“No,” akajibu Denmark. “Perhaps we should wait a bit. It seems the are more and more to discover.”
Saa nane mchana.
Japo ilikuwa ni katikati ya siku, yaani mchana, jua halikuwa linaonekana na hali ya hewa ilikuwa ya abridi kana kwamba kuna mvua yaja muda si mrefu. Upepo ulikuwa unapuliza na angani hakukuwa kweupe ama kweusi sana, wastani.
Muda huu, ndani ya jengo ambalo ndilo makao makuu ya familia ya Wu kulikuwa ni kutulivu haswa. Si kwamba watu hawakuwa wanapita, lah! Watu walikuwa huku na kule, wanakatiza kutoka kushoto na kwenda kulia wakiwa wamevalia mavazi yao ya majoho rangi ya karoti,
Hata zaidi wakiteta, lakini kwa ukimya kiasi kwamba ni ngumu kujua kama hapa pana watu kama umefumba macho.
Katika utulivu huu, mara mtu mmoja anakuja kwa kasi akikimbia. Anasimama malangoni na kufungua, kisha anazama ndani upesi. Anaenda moja kwa moja kuonana na ‘master’ na kumweleza kuwa kuna jambo nje anapaswa kwenda kuliona.
Basi pasi na ajizi, master, tumtambue kwa jina hilo, anatoka akiongozana na kijana huyo mpaka nje. Huko wakitembea umbali mfupi, wanakutana na vijana wengine watatu wakiwa wamembelea mwanaume asiyejiweza.
Ni Lee. Master anamtambua. Kabla hajauliza nini kilichotokea, vijana wale wanasema wamemkuta akiwa njiani, amejilaza, hajiwezi. Mgongoni ana matundu mawili ya risasi na mwili wake umejawa majeraha.
Lee anapelekwa kwenye chumba fulani kidogo chenye uhaba wa mwanga, analazwa chini na kisha vijana wale wanaondoka wakimwacha master peke yake. Anawasha mishumaa, na kisha anaanza kuandaa madawa.
Anatwanga hiki. Anamiminia kile. Anachuma hiki. Anaweka pale. Anachanganya hili na lile na mara anapata uji mzito wa rangi ya kahawia. Anampakaa Lee shingoni, kisha anachukua pini kali ndefu, anamchanja na kutoa risasi mwilini.
Kwenye majeraha anatia majani fulani aliyoyaponda na kuyachanganya na unga alioutoa kwenye kibakuli fulani cha udongo juu ya shelfu. Baada ya hapo, anawasha moto kwenye vijiti viwili vyembamba na kisha anaviwacha ndani vikiwa vinafuka moshi mzito.
Anarejea mahali pake pa kazi na anaketi akitafakari kilichomsibu kijana yule, yaani Lee. Akatengeneza mawazo mengi sana kichwani ila akaona ni bora avute subira, alimradi amerejea salama, atapata tu kujua kilichotokea kwa kupitia kinywa cha mlengwa.
***
Saa kumi jioni, Hongkong …
Mlango wa kioo unafunguliwa na anazama ndani jibaba jeusi la miraba minne. Jibaba hili ndilo lile lililopewa kazi ya kumtafuta na kummaliza bwana Lee tangu kipindi kile alichoingia anga za wenyewe.
Anaketi kitini, kiti kinabonyea kidogo. Anasafisha koo lake na kumtazama mwanamke mrembo wa kizungu aliyekuwa mbele yake akitafuna ‘bubblegum’ kwa pozi za kike. Macho ya mwanamke huyu, ndani ya miwani kubwa nyeupe, yalimwangazia huyu mgeni na kumuuliza kwa sauti ya chini ila sikivu,
“Cany I help you, Rob?”
“Surely, you can. You know why I am here.”
Mwanamke huyu akapuliza puto na kulipasua, kiisha akaendelea kutafuna na sasa macho yake yakiangazia tarakilishi yake ya mezani.
“I don’t see any appointment here. Are you sure you’re supposed to be here at this time?”
“Yikes!” jibaba likalaumu. “Please can you do something? You know it gat to be serious issue for me to be here, ayt?”
Mwanamke yule akanyanyua simu yake na kupiga. Akaleza kuna mgeni papo. Basi alipoweka simu mezani akamtazama mgeni wake na kumpatia ishara ya kichwa. Jibaba akanyanyuka na kwenda zake ndani kukutana na bosi.
Bosi huyu alikuwa amevalia suruali ya kitambaa rangi ya bluu na kiatu cheusi safi. Hakuonekana kwa juu na hivyo basi tutamtambua kwa sauti yake nzito kwa sasa.
“I am done,” akasema yule jibaba.
“Sure?” bosi akauliza kwa sauti yake ya kukoroma.
“Sure. Now the document is within our hands and the man is down.”
“Perfect. One step at a time.”
“So what’s next?”
“Future is so exciting, Rob. Full of bloodshed. But now I can confidently declare the death of Wu family. Confidently. It’s just a matter of time.”
Rob akacheka.
“Let me see what I can do today,” akasema bosi na mara Rob akanyanyuka na kwenda zake.
***
Saa kumi na mbili jioni, nchini, kambi ya wachina.
Bwana yule wa kichina alirejeshea mlango wa maabara na kutengenezea suti yake vema. Akapiga hatua kubwa na dhahiri mgongoni akiwa amewekelea kitu fulani ambacho hakutaka kionekane.
Punde akawa ameshafika kwenye makazi yake na baada ya dakika kama kumi hivi, akatoka na kuelekea kule hospitali ya kambi kwenda kukutana na Sheng. Ulinzi ulikuwa umeimarishwa maradufu tofauti na hapo awali. Idadi ya walinzi ilikuwa imeongezeka, takribani kama watu kumi wakiongezwa lindoni.
Akakutana na daktari na kupewa ripoti ya maendeleo ya mgonjwa. Na baadae akapewa ruhusa ya kwenda kumwona mgonjwa. Fursa adhimu aliyokuwa anaitaka. Daktari alimsindikiza ila hakukaa ndani, akamwacha mgeni mwenyewe na mgonjwa.
Bado Sheng alikuwa kwenye hali ya kutojielewa. Ni mashine tu ndizo ambazo zilikuwa zimeshikilia uhai wake. Macho yake hayakuwa yamefumba vema, na alikuwa anahema kwanguvu.
Bwana yule wa kichina akatulia humo kwa kama dakika tano hivi kisha akachomoa sindano ndogo ndani ya mfuniko yenye kimiminika rangi ya manjano. Akatazama usalama. Akasogelea dripu, na kisha akadungia sindano ile ndani ya mfuko na kutikisa fuko hilo la dripu mpaka pale ambapo hali ya kimiminika ilirejea kwenye mazingiira yake ya awali.
Alafu akamwita daktari na kumwambia amemaliza haja yake.
“Anatia matumaini. Amenishika mkono japo hajasema jambo,” alisema bwana yule wa kichina akitabasamu. Hakukaa sana akaenda zake.
Usije dhani bwana huyu ni mjinga kujiweka rehani kiasi cha ‘kifala’. alikuwa anajua anachokifanya na anakijua fika.
Alipofika nyumbani, muda si mrefu akaja yule jamaa wake mmoja aliyebaki, akamweleza, “Nimeshakamilisha kazi. Sasa itachukua juma moja kwa Sheng kufa. Kuanzia sasa atakuwa anakufa taratibu taratibu.”
Yule jamaa mwingine akatabasamu na basi akampatia mwenzake mkono wa pongezi.
**
Saa tatu usiku …
“They have poisoned him,” alisema Scotland. Tayari wanaume hawa wa kizungu wakawa wameshalijua hilo kwa kupitia kifaa chao ambacho wamekipandikiza kwenye mwili wa Sheng.
Katika namna ya kitaalamu, baada ya mabadiliko kadhaa kutokea mwilini mwa mhusika, kifaa hicho kilitoa taarifa kwa waliokiweka.
“But why they did this?” akauliza Wales. “Why do they want to kill their master?”
“There’s something behind here,” akasema Denmark akikuna kidevu. Kwa sekunde kama mbili hivi wakatazamana. Ila punde wakasikia kitu nje. Wakapata shaka.
Walipokuja kutoka, wakagundua kulikuwa kuna mtu ndani ya eneo lao. Kwenye perving, kulikuwa kuna nyayo mbichi za viatu.
Wakatoka hata kutazama nje ya uzio wao wapate kutambua kama kuna yeyote, ila hawakufanikiwa abadani. Walichoambulia ilikuwa ni alama za matairi ya gari kuashiria kwamba mtu huyo alikuja papo na usafiri.
Wakabaki kwenye buwazo na shaka kiasi chake. Mtu huyo atakuwa amesikia kitu gani toka kwao? Ametumwa na nani na amepafahamuje hapo kwenye makazi yao?
Hata waliporudi na kuketi sebuleni wakaendelea kujiuliza. Walikuwa wanaamini wamefanya kila kitu kistadi kiasi cha kutokubakiza kivuli, sasa hii ishara ya mtu kutembelea eneo lao haikuwa njema kabisa.
Sasa ikawalazimu wawe makini sana. Na kwa kuhakikisha hilo, wakaona ni vema wakifunga kamera zao ndogo maeneo mbalimbali ya jengo hilo ili basi iwe rahisi kupata taarifa za uvamizi kabla matokeo hasi hayajachukua nafasi.
Zoezi hilo likafanyika upesi, na kila kitu kikawa kwenye mstari wakiamini kuwa mvamizi yule atarejea tu. Na punde atakapofanya hivyo basi hilo litakuwa kosa lake la mwisho kulifanya kabla hajaenda jehanam.
Ila hawakuwa wanajua. Hata wakati wanafanya ‘installation’ hiyo ya kamera, mtu yule ambaye walimkosa alikuwa anawatazama na hivyo basi akiwa anajua si muda wa yeye kufanya tena jaribio la kuzama mule.
Si kwamba mtu huyu alikuwa karibu, lah! Alikuwa ndani ya gari, kilomita kadhaa tu mbali na ile nyumba ya walengwa. Na macho yake yalikuwa yanasaidiwa na hadubini kalii yenye uwezo wa kupambana na kiza kupekua eneo analolitaka.
Alipotosheka na alichokipata, akaweka hadubini chini na kutabasamu. Na kumbe alikuwa ni Jona. Lakini alipajuaje hapa? Si muujiza. Jona na wenzake walikuwa ni watu wa kwanza kutambua utekwaji wa bwana Sheng na hata makazi ambayo alihifadhiwa kwa kutumia chip ndani ya mwili wa mchina huyo.
Na hivyo basi, watekaji hawa pasipo kujua lolote lile, wakafanya kosa la kumpeleka mateka wao nyumbani ili wamhoji na hatimaye kumtia kifaa chao kitakachowasaidia kuwapatia data.
Kiupofu wakarahisisha kazi ya wakina Jona. Sasa jicho la tai lilikuwa linawamulika kwa karibu zaidi.
“Sasa?” akauliza Miranda. “Kuna haja ya kufanya mambo?”
“Hapana,” akajibu Jona akitikisa kichwa. “Hivi Miranda hujajua kuwa hapa kuna faulo ya mchezo inachezwa? Bado tunatakiwa kuwa watazamaji kwa sasa. Muda utakapofika wa kuvaa jezi basi tutalitenda.”
“Ila kule upande wa Sheng bado wapo kimya,” sauti ya Marwa ilivuma. Kumbe alikuwa kwenye viti vya nyuma vya gari. “Unadhani na wao watakuwa wanapanga kitu?”
‘Sidhani,” akajibu Jona kisha kubinua lips zake. “Kama yule jamaa alivyosema, kuna something behind hapa. Kule kwa kina Sheng kuna jambo linafichwa, ila naamini muda si mrefu mambo yatakuwa bayana. Kama si hivyo, basi wale wazungu wasingekawia kuchukua hatua.”
Basi gari likawashwa, wakatimka. Ila si kwamba jicho la tai lilikuwa linawaacha walengwa wake wapweke, hapana. Kuna namna hapa kamilifu.
***
Saa kumi na moja asubuhi …
Kwa mbali alianza sasa kupata ufahamu. Masikio yake yalisikia sauti ya ndege wakilia huku na kule kumjuza kuwa asubuhi imewasili. Ni kweli mwili wake ulikuwa umechoshwa na purukushani za kuinusuru roho yake, ila bado alikuwa ana nia ya kurudi tena ulimwenguni kujua yanayoendelea.
Akafungua macho japo yalikuwa mazito. Akatazama kushoto na kulia na kisha akajitahidi kunyanyuka akipambana na maumivu aliyokuwa anayasikia. Alipoketi kitako, sasa akasikia vema. Huko nje sauti za watu walio kwenye mafunzo zilikuwa zinavuma. Kiwanja cha kufanyia mazoezi hakikuwa mbali sana na pale alipokuwapo. Lakini hata hivyo sauti hizi zimeanza kuvuma muda si mrefu kwani angelizisikia mapema kabla ya zile za ndege masikioni.
Akapambana kusimama. Akaweza. Ilikuwa ni ajabu mno, na kama ungelimwona jana basi ungelisema mtu huyu, kama kweli angelinusurika uhai, basi ingemchukua miezi kama mitatu au minne au mitano kusimama tena.
Hakika dawa za ‘master’ zilikuwa kali na zenye kufanya kazi mapema mno. Akajivuta kudaka shuka na kujisitiri, kisha akajikokota mpaka nje. Bado hakuwa na mwendo sawia, ila angalau husogea. Na kwa kasi ile ya dawa, basi hata juma lilikuwa kubwa kwake kutengemaa.
Taratibu akajivuta mpaka eneo alipokuwa master, akiwa anafanya meditation kama ada yake kila asubuhi ya mapema, na kusimama hapo pasipo kusema jambo. Alingoja master amalize. Ila ajabu, kama dakika mbili kukatiza, master bado akiwa amefumba macho na hata amempatia mgongo bwana Lee, akamwita kwa jina.
Akamuuliza, ina maana umepona kiasi hicho? Kisha akatabasamu na kugeuka kumtazama. Ni baridi na ametoka na shuka, tena mtu mgonjwa. Akamwelekeza waende mahali penye joto zaidi, wakapate pia na kifungua kinywa.
Baada ya muda kidogo wakawa wapo ndani ya chumba kidogo chenye zulia na mito chini, wakaketi. Punde fupi akaja mwanadada aliyebebelea trey ya kioo na vikombe viwili vya kahawa. Akawapatia.
Walipoanza maongezi Lee akaeleza staajabu yake kuwa pale maana alidhani amekwisha kufa kwenye mikono ya wadhalimu. Vita ilikuwa kali na walikuwa wamedhamiria haswa kumtoa roho.
Basi master wake akamwambia ni kama bahati. Na kama yuko sahihi, basi wadhalimu wale waliolenga kumuua, walishindwa kutimiza hilo kwa uhakiki zaidi baada ya yeye kuzama ndani ya himaya ya Wu, hivyo walivyotupa hizo risasi zao, wakaona inatosha wakajiendea.
Ila zaidi ya hapo, Lee akaeleza mkasa mzima ulivyokuwa. Namna alivyosalitiwa na yule afisa na hatimaye kukwapuliwa nyaraka zote hata zile ambazo alitakuwa kuja nazo.
Master akamtoa shaka kwa kumwambia watajua namna ya kumalizana na afisa huyo. Kwakuwa amepona dhidi ya kifo, basi ni huyo afisa ndiye ambaye ataonja kifo. Na kwa kuanzia muda huo, akamtawaza kuwa kamanda mkubwa wa kamandi ya makao makuu.
Akampa majukumu ya kuongoza kikosi chote kilichopo hapo makaoni, cha watu takribani alfu ishirini. Na hivyo akamtaka baadae nyakati za jioni wakalifanye jambo hilo kuwa rasmi kwa kuliweka bayana kwa kila mtu anayetakiwa kulifahamu.
Basi baada ya kuteta hayo kidogo, wakanyamaza na kupambana na baridi iliyopo kwa kunywa kahawa zao vikombeni. Zikapita kama dakika tatu, Lee akauliza swali, umepata chochote kile toka kule Afrika?
Master akatulia kwanza kidogo kabla hajajibu. Alishusha pumzi ndefu puani alafu akasema kwa maneno machache, hali si shwari. Lee alipotaka kujua zaidi, akamweleza kuwa kuna taarifa walizipata za kutekwa kwa Sheng na watu wasiojulikana. Ila kwa sasa mambo yapo vema kwani ameshapatikana, japo si mzima kiafya.
Lee akapata shaka hapa. Wakina nani hao waliomteka bwana Sheng? Alipoeleza shaka lake, Master akamtoa hofu kwa kumweleza kuwa anaamini Sheng atalimaliza jambo hilo kwani kama lingekuwa kubwa basi angeshalieleza huku makaoni.
Basi kikao kikawa kimezizimia hapo.
Baadae majira ya mchana, Lee akiwa peke yake anakula chakula, jambo lile la Sheng likamjia tena kichwani. Aliona kuna haja ya kuhofia sana kuhusu kile kitu. Ni mtu gani ambaye alikuwa ana uwezo wa kumteka Lee? Je ni wakina Jona? Ama watu wa bwana Brown Curtis?
Akiwa hapo anakula, akaja mtumishi mmoja kumwona. Msichana mchanga wa kichina aliyekuwa amebana vema nywele zake, mwili wake ameusitiri kwenye nguo za kitamaduni.
Msichana huyo alikuwa amebebelea nguo za Lee alizotoka nazo shurbani. Kabla hajaziweka chini akamuuliza Lee kama nguo atazihitaji tena ama akazichome. Lee akafikiri kidogo, akamruhusu msichana huyo akazichome.
Ila mwanamke huyo kabla hajatokomea, Lee akakumbuka jambo. Akamwita mwanamke huyo na kumwambia atazame mfukoni mwa nguo hizo kama kuna simu yake. Alikuwa anabahatisha tu, na kama angeliambiwa hamna,a singeshangaa.
Ajabu, msichana yule baada ya kufanya msako mdogo, akahisi kitu kigumu mfukoni. Alipozamisha mkono na kuchomoa, akatoka na simu. Akamkabidhi Lee na kisha akaenda na zile nguo akachome.
Lee, akiwa haamini, akaipekua simu yake. Na baada ya muda kidogo, kwakuwa alikuwa na hamu kujua zaidi mambo yaliyotokea kule Afrika, aka-‘switch’ laini yake ya kimatumizi kule mtandao wa whatsapp.
Muda kidogo, akapokea jumbe kadhaa. Ikiwemo zile za Glady!
***
Saa saba na nusu mchana, Shanghai, China. Kwenye ghorofa ya ishirini ya nne …
Kulikuwa kuna kikao cha watu wasiozidi watano. Watu hao wote wote walikuwa wamevalia suti nyeusi, na sura zao zikiwa kapuni. Miguu yao ilikuwa imetambaliwa na soksi nyeusi pia na chini wakimalizia na viatu barabara vya ngozi!
Ndani ya eneo hili kulikuwa tulivu, na kiyoyozi chapuliza kwa mbali.
“It is now or never,” sauti nzito ilisema. Na sauti hii kama wewe ni mtu wa kumbukumbu basi ilikuwa ndiyo ile ambayo ilikuwa inateta na Rob jana yake tu baada ya kupewa taarifa ya zoezi la kummaliza Lee.
Bwana huyo alikuwa hapa kikaoni na wenzake. Na mjadala hapa ukiwa ni kumaliza kabisa familia ya Wu kwenye uso wa dunia ili basi kuruhusu wabepari kufanya kazi yao vema na kuondoa kabisa tishio la China kushikilia uchumi wa dunia na kuiendea kombo Amerika.
“This is the time for us to finish the game,” alisema bwana yule mwenye sauti nzito. Wenzake wakaunga mkono hoja. Na hivyo basi wakakubaliana wanaume wale waliopo Afrika, the intellectual instinct, waanze kutekeleza kazi ya kufutia mbali mamlaka ya China ukanda wa Afrika ya mashariki na kati.
Sasa mambo yalikuwa yameanza kupamba moto na vita rasmi ilikuwa imetangazwa, ambapo mataifa makubwa ya kibepari yameazimia kumwangusha tembo huyu mkubwa wa mlengo wa pili kabla hajazidi kutapanya na kuharibu shamba lao.
Kwa namna Uchina ilivyokuwa inakuja juu, si kitu cha kuwaza kuwa hofu kuu inatokota kwenye mioyo ya mabepari. Hii ni alama ya kushindwa. Alama ya kuzidiwa maarifa. Kitu ambacho kamwe hawako radhi kukiafiki.
Basi kikao baada ya muda kikafungwa na mabwana wale wakatawanyika. Ila bwana mmoja, si yule bosi wa Rob, alipokuwa kwenye gari aliongea na simu yake kwa muda mfupi akitoa maagizo. Anataka kambi ya wachina imalizwe haraka iwezekanavyo.
Bwana huyu alikuwa anatimiza tu kile walichokubaliana. Na hao aliokuwa anaongea nao hawakuwa wengine bali the intellectual instinct, kundi haramu la mauaji na mienendo ya kimafia, sasa likiwa limeshaweka makazi yake nchini.
**
Baada ya siku mbili … Dar, Uwanja wa ndege.
Ni majira ya mchana. Lee akiwa anakokota kibegi chake kidogo anaongea na simu akiwa ameweka sura ya kazi. Macho yake yamezibwa na miwani ya jua, na mtindo wake wa nywele ameubadili kidogo. Alikuwa amezilaza, na kwa wingi wake zikawa zinakaribia kugota mabegani mwake.
Punde alipotoka ndani uwanja wa ndege, yaani kuikuta barabara, akatia simu yake mfukoni na kuangaza kushoto kwake. Akaliona gari fulani likiwa laja. Range rover sport nyeusi. Ikasimama mbele yake, akakwea.
Gari likatimka kwa mwendo wa wastani uliokuwa unachanganyia kwenda kasi.
“Vipi, mmemwambia yeyote yule?” akauliza Lee.
“Hapana, hakuna anayejua,” akajibu jamaa aliyekaa kando na dereva.
“Safi sana,” Lee akapongeza na kuuliza, “Sheng anaendeleaje?”
“Yuko kama jana tu. Sioni kama kuna mabadiliko,” akaendelea kujibu yule jamaa aliyeketi karibu na dereva. Wakati akiteta akikunja kunja shingo yake kutazama nyuma alipokuwa ameketi Lee.
“Mpaka sasa hamjajua nani anayehusika na utekwaji wake?”
“Hatujajua. Wala sababu za wale wenzetu kujaribu kumuua.”
Lee akanyamaza. Kitu pekee alichokuwa amewaambia hawa watu ni ujio wake na ufanywe kuwa siri. Hakuna la ziada. Hivyo watu hawa hawajui kama Lee alinasa habari zozote toka kwa dada poa Glady.
“Si huko naelekea, tushike barabara ya kushoto,” Lee alielekeza.
“Kwani hatuendi makaoni?” dereva akauliza.
“Tunaenda,” Lee akajibu, “ila baada ya kutoka kwanza huku.”
**
Ngo! Ngo! Ngo! Ngo!
Glady alifunua shuka akaangaza kwa jicho moja. Bado alikuwa yu kitandani majira haya ya mchana na si ajabu kwani amelala asubuhi ya saa nne. Chumbani alikuwa na mwenzake ambaye alikuwa amelala vibaya kiasi cha kuacha maungo yake wazi.
Mwanamke huyo alikuwa ananuka pombe na hata miguuni bado alikuwa ana viatu vyake vya visigino virefu. Na hapo kitandani kulikuwa na chupa tupu ya Vodka.
“We Esther! Esther!” Glady aliita akimsukumasukuma mwenzake. “Wewe si nilikuambia ukalale kwako? Nani kakuruhusu ulale hapa?” Glady aliuliza. Ila alikuwa anaongea na mfu. Huyo Esther alikuwa hasikii hata tone. Mdomo wake unukao kileo, ulikuwa wazi akikoroma kama amekabwa.
“Wewe!” Glady akaendelea kusumbuka na Esther. “Si naongea na wewe Esther!”
Hodi ikagongwa tena. Sasa akili ya Glady ikakumbuka kuwa ameamka kwasababu ya hodi na si Esther. Akasonya. Kichwa kilikuwa kinamgonga kwa mbali na mwili wake ulikuwa umejawa na uchomvu. Alivuta shuka kwanguvu kumpokonya Esther kisha akajifunika na kwenda mlangoni.
Baada ya kuondoa loki zake duni, akakutana uso kwa uso na Lee.
“Kumbe ni wewe?”
“Ndio ni mimi?” Lee akajibu akiegemea ukuta. Alikuwa ameegesha gari lake mbali kidogo na hapa alikuwa mwenyewe.
“Mbona saa hii jua kali?” Glady akauliza na kisha akapiga mhayo.
“Nina maongezi kidogo na wewe,” Lee akajinasibu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Glady akatikisa kichwa chake akifinyanga lips zake.
“Mchina, nimechoka. Kwanza kama unadhani utanipeleka kule kwenu, sahau kabisa. Kwa niliyoyaona siku ile, yanatosha kabisa!”
“Ndiyo maana nipo hapa,” Lee akateta.
“Ina maana wewe huyajui au?”
“Pengine wewe unayajua zaidi … Sikia, Glady, serious, sina muda sana wa kukaa hapa. Tunaweza tukaongea tafadhali? Sidhani kama itachukua muda mrefu.”
“Ulikuwa wapi siku ile nakutumia message? Hukusikia mlio wa risasi?”
“Sikuwapo hapa, nilikuwa China.”
“Oooh!” Glady akakuna kichwa chake kwa kidole kimoja alafu akapiga tena mhayo. ‘Nimechoka, nataka kupumzika.”
Lee akazamisha mkono wake mfukoni na kutoka na ‘wekundu’ kama sita hivi, akamwonyeshea Glady. Glady akatabasamu.
---
“Alinichukua, ila hakufanya chochote na mimi. Alikuwa bize sana kuongea na simu kupanga mikakati ya mauaji. Ila bahati si yake, wale watu aliowatuma walirejeshwa na akawaua kwa mkono wake mwenyewe,” alieleza Glady akiwa ameketi kwenye ngazi. Lee naye akiwa pembeni yake.
“Ulisikia sababu ya yeye kufanya hivyo?” Lee akauliza. Glady akapandisha mabega yake juu na kusema, “Hapana. Ila nilichosikia ni kwamba usiku ule ungekuwa mkubwa sana kwao. Na hata mimi alin’chukua ili akafurahie siku yake hiyo japo haikuishia kuwa nzuri nadhani.”
“Ahsante,” Lee akasema akisimama. “Nitakuhitaji tena karibuni. Namba yako si ile ile?”
“Umenimiss eenh?” Glady akauliza akimkonyeza Lee.
“Ni kwa kazi. Si kama ufikiriavyo,” Lee akamweleza na kisha akaenda zake.
***
Majira ya saa mbili usiku …
Kulikuwa na ukimya eneo hili. Kwa mbali, kwa mbali sana, maongezi yalikuwa yanasikika kwenye makazi ya bwana yule wa kichina aliyefanya hila ya kummaliza bwana Sheng.
Maongezi haya yalichukua muda mfupi, kama vile dakika mbili tu, na muda mwingi kulikuwa ni kimya. Yaani ukimya ulitawala dakika tano za maongezi haya ambayo kwa jumla na zile mbili zilikuwa saba za makutano.
Baada ya dakika hizo, sauti kubwa ya risasi ikavuma … na tena … na tena! Tatu kwa ujumla. Baada ya hapo, wanaume wawili wakatoka ndani ya makazi hayo wakiwa wamebebelea mwili wa bwana yule wa kichina na kwenda kuufukia, Lee akishuhudia.
Baada ya hilo tukio, akaenda zake hospitali kumwona Sheng aliyekuwa amelala kitandani kwa masiku sasa. Bado hakuwa na nguvu. Na mashine ya oksijeni ilikuwa iimefunika mdomo na pua yake.
Kwa mbali mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo ilikuwa inafanya kazi, ikilia.
Lee akamsogelea Sheng na kumtazama kwa huruma. Ndani ya kifua chake akijiuliza ni nini kilijiri. Alikuwa anatamani sana kujua. Kichwani alikuwa ana maswali kadha wa kadha.
Akiwa amekaa hapo, mara Sheng akafungua jicho lake la kushoto kwa mbali. Akanyanyua vidole vyake kupapasa mkono wa Lee. Lee akashtuka kwa faraja kuona hilo. Akadaka mkono wa Sheng na kumtazama usoni akikodoa.
Kuna kitu Sheng alikuwa anataka kuongea. Uso wake ulionekana kuhangaika akitaka kusema jambo.. Basi Lee akamwondoa mask yake ya kumvutisha hewa, na kisha akasogeza sikio lake kwenye mdomo wa Sheng uliokuwa unamamata kwa mbali ukiwa umeegemia kushoto.
Sheng, akiwa anakoroma na akisikika kwa mbali sana, akamwambia Lee maneno kadhaa ya kichina. Na baada ya kusema hivyo, akakaa kimya. Lee akawahi kumrejeshea kinyago chake cha kuhemea. Ila hakufungua tena jicho wala kuchezesha tena vidole vyake wala kiungo chochote.
Lee akapata shaka, akamwita Daktari haraka. Naye alipokuja, akaenda kungoja nje. Kwa takribani kama nusu saa, daktari na nesi wakawa wapo ndani, vitu vikiingizwa na kutolewa. Baada ya hapo, daktari akiwa amenyong’onya akamwita Lee ofisini.
“Hali inakuwa mbaya kila uchwao. Ilikuwa ni ajabu sumu inaendelea kumtafuna mwili pasipo kujali juhudi zote hizo tulizofanya.” Daktari akatengeneneza miwani yake na kutazama baadhi ya karatasi ndani ya faili, kisha akasema kwa sauti ya chini;
“Tumekawia. Na hili linaelekea kugharimu maisha yake. Tumegundua ndani ya dripu kulikuwa na sumu. Hatujui imefikaje, na mbaya zaidi majibu yake yameshaanza kuonekana mwilini. Amepooza upande wake wote wa kulia. Matumaini yake ya kupona ni hafifu hafifu mno.”
Akiwa hapo, bado taarifa hizi zikiwa ngumu kuzimeza, mara akasikia king’ora cha hatari kikilia kwanguvu! Punde akaja mwanaume mmoja hapo akiwa amebebelea silaha mkononi. Akasema, “Tumevamiwa!”
Lee akamtazama daktari na kumwambia, “Ningoje hapa, nakuja.” kisha akaenda zake na yule jamaa aliyekuja kuleta taarifa. Wakaelekea mpaka huko inaposemekana kuna mashambulizi. Lakini hawakukuta kitu chochote. Zaidi kulikuwa kweli kuna miili ya watu waliokufa ikiwa imezagaa huku na kule.
Jambo hili likamshangaza sana Lee. Walipata kusikia sauti za milio ya bunduki na hata kilio na magugumizi ya watu wakililia uhai lakini kila walipokwenda kutazama, hawakukuta mtu huko zaidi ya maiti.
Lee akatahamaki. Basi akapata wazo. Haraka akaenda control room apate kutazama kinachoendelea kwa kutumia rekodi ya kamera za cctv ambazo zimetundikwa ndani ya jengo hilo maeneo mbalimbali. Lakini alipofika huko, napo akakuta maiti za watu wanaohusika na kitengo hicho. Wote, sita kwa ujumla, walikuwa wameshindiliwa risasi kadhaa wakiwa chini wanamwaga damu. Alipotazama televiisheni, hakuona kitu. Zote zilikuwa na rangi ya bluu kuonyesha kwamba hakuna kinachodakwa na kurushwa kwa muda huo.
Ina maana wavamizi walikuwa tayari wameshaharibu mifumo yote ya kamera! Bado akiwa hapo, mara umeme ukakatika ghafla na eneo lote likabakia totoro gizani. Hapo sasa mambo yakawa magumu kupita kawaida.
Watu wakaendelea kuuawa na maadui wakiwa wanafanya namna ya kutoonekana kwa wepesi. Kwa takribani nusu saa, watu wengi mno wakawa wameuawa. Lee hakuwa na msaada wowote ule, zaidi ya kila mahala kushuhusia maiti na maiti na maiti.
Hapa akapata walakini mkubwa. Haraka akakimbia kwenda kule hospitali kumkuta Sheng.
**
Sauti ya mtu akigugumia ilisikika, na mara ikanyamaza kimya. Upande wa kushoto, akadondoka mtu akiwa anamimina damu kifuani mwake baada ya kukitwa na kisu kirefu chenye ncha nyembamba ndefu.
Hapo muuaji akaonekana akiwa mwanaume aliyevalia mavazi meusi ya kubana kana kwamba wale watu wazamao ndani ya maji. Muuaji huyo hakuwa amebakiza sehemu yoyote ya mwili wake wazi. Nguo yake hiyo ilikuwa imefunika mpaka kinywa na pua, macho yakiwa yamemezwa na miwani iliyobana kuta za uso.
Miwani hiyo ilikuwa inamwezesha kuona vema katika giza hili. Kwenye nyonga zake, alikuwa amebebelea mkanda mwembamba ulioning’iniza bunduki mbili ndogo. Na mikononi alikuwa ana visu viwili vinzvyochuruza damu.
Upesi, baada ya mtu yule aliyekitwa na kisu kudondoka chini, akatokea mtu mwingine mlinzi wa jengo. Alipomwona mvamizi, hakujiuliza mara mbili akarusha risasi kama tano kwa mfululizo. Lakini ajabu hakufanikiwa kumpata mlengwa wake kabisa.
Bwana yule mvamizi alichumpa na kujibiduabidua hewani, na mara kufumba na kufumbua akawa haonekani. Kuja kutahamaki, yule mlinzi akiwa anatazama huku na huko, mara akasikia kishindo cha mtu nyuma yake. Akatazama upesi kwa woga. Na katika haraka ya ajabu, kabla hajabinya kitufe cha risasi, akachomekwa kisu cha shingo.
Akiwa anapapatika na kifo, akabinya kitufe cha risasi kwanguvu, risasi zikamiminika kama mvua, lakini zote zikaenda kombo maana mvamizi alikuwa ameshaelekezea mdomo wa risasi pembeni. Basi bwana yule mlinzi alipoishiwa nguvu, akadondoka chini na kujifia.
Mvamizi akaweka kidole chake sikioni na kuuliza,
“What’s your position?” Sauti ikamjibu kwa mbali isisikike vema isipokuwa kwake mwenyewe. Basi akaongezea kwa kusema. “The building is under control. Seize the man and let’s finish the business.”
Akatoa kidole chake kwa sikio na kupotelea gizani.
**
Kulikuwa ni kimya sasa kupita kiasi. Hata watu hawakuwa wanaonekana wakikatiza huku wala kule tofauti na ilivyozoeleka siku zote.
Hata hapa hospitali palikuwa kimya. Ila hali hiyo haikudumu kwa muda mrefu, wanaume watano wakajiri wakitoa upande wa kushoto wa jengo. Wote walikuwa wamevalia sare, nguo nyeusi zinazobana miili na usoni wakiwa na miwani zilizobana na kushikilia vema nyuso zao.
Wakazama ndani ya hospitali, wakinyookea chumba alichokuwa amelazwa Sheng. Kufungua mlango kutazama, hakukuwa na mtu! Kitanda kilikuwa tupu. Mashine, mipira na waya, zilikuwa pembeni.
“Shit!” akalaani Denmark. Alitambulika kwa sauti yake. Sheng hakuwa ndani!
Basi akamgeukia mwenzake na kusema, “Scot, go look where he is.”
Haraka aliyepewa agizo hilo, Scotland, akatoka ndani na kwenda kule walipokuwa wamepaki gari lao, nje ya Jengo upande wa kulia, kama kilomita moja na nusu hivi. Alienda huko kwa kukimbia. Na hawakutaka kwenda wote kwa maana Denmark alikuwa anaamini Sheng atakuwa amefichwa ama amejificha ndani ya jengo.
Hivyo ni swala la kupewa taarifa na kuifanyia kazi tu.
Baada ya punde, Scotland akatoa taarifa, “He is out of the building!”
Hakuongezea ttaarifa nyingine, akasikia kiganja cha mtu kikimgusa begani. Kutazama, alikuwa ni Lee.
“I’ve got a little problem here,” Scotland akasema akiwa amebinyia kidole chake sikioni. “Let me deal with it, be in touch.” akamalizia taarifa na kisha akaufunga mlango kumkabili Lee.
“Who are you?” Lee akauliza.
“Your destroyer,” Scotland akajibu. “Your breath taker,” akaongezea.
“Who sent you here? Are you are the one who kidnapped Sheng?” Lee akauliza tena. Bwana Scotland akasikika akiguguma kwa kicheko, kisha akasema, “Hell yeah!” na kuongezea, “I don’t think if you have to know who sent us here ‘coz you are going to die in anyway. What help will it give?”
Aliposema hayo, Scotland akachomoa visu vyake nyuma ya kiuno.
“Where’s Sheng?” akauliza.
“You have to go through me to get him,” Lee akajibu kwa kujiamini.
“Ok, if that’s what you want,” akasema bwana Scotland na vita ikaanza. Lee hakuwa na silaha yoyote mkononi mwake. Aliamini kwenye uwezo wake kumlinda na hata kummaliza adui.
Na kwakuwa hakuwa anafahamu uwezo wa adui yake, akaona ni vema ampatia nafasi ya kumuanza. Kwa wakati huo akiwa anaamini adui wake huyo hatakuwa mtu mwepesi kutokana na matukio waliyoyafanya ndani ya jengo.
Hakuwa amekosea. Scotland alikuwa mwepesi mno na zaidi akiwa mwenye nguvu. Lee alijitahidi kukwepa lakini bado akajikuta akipokea ngumi kadhaa na mateke yaliyomrudisha nyuma.
Akaona endapo naye asiposhambulia basi muda si mrefu atajikuta yu hoi na kuwa chakula cha adui. Akaanza naye kujikakamua.
Akatupa ngumi, ikayeya, akatupa tena nyingine nayo ikadakwa, kabla hajaviringitwa, akaruka juu na kuchoropoa mkono wake kisha akajifyatua mateke. Nayo yakapanguliwa.
Scotland akatuma mikono yake yenye visu, Lee akajitahidi kuizuia, lakini Scotland akamzidi ujanja na kumchanja mkono wake wa kuume. Kisha haraka akaviringita miguu ya Lee na kumwangusha chini. Lee akapiga kiwiko mkono wa kushoto wa Scotland, kisu kikaangukia kando, sasa akabaki na kisu kimoja cha mkono wa kuume.
Akawa analazimisha kumtoboa Lee kifuani, Lee naye akikazana kuzuia mkono huo kwa mikono yake yote miwili. Ila ni dhahiri alikuwa anaelekea kushindwa. Ncha ya kisu ilikuwa inasogea taratibu, na ilibakiza kama robo sentimeta kugusa paji la uso la Lee.
Ilibidi afanye jambo la sivyo alikuwa anakufa. Basi akatumia akili yake. Kwakuwa nguvu kubwa Scotland alikuwa ameiweka kisuni, Lee akaachilia mikono yake upesi na kukunja shingo yake haraka. Kisu kikatoboa chini. Na sasa kwakuwa mikono ya Lee ilikuwa huru kwa muda huo mfupi, akagonga shingo ya Scotland maeneo ya pembeni chini kidogo mwa taya, Scotland akalegea.
Lee akachojoa miguu yake na kumkita mwanaume huyo kwenye kende, na kabla hajalalama kwa maumivu, akawa ameshasomba kisu na kumkita nacho shingoni. Akamsukumia pembeni bwana huyo na kuhema kwanguvu. Kazi haikuwa nyepesi hata kidogo!
Alimpofunua usowe na kumtazama hakuwa mtu anayemfahamu.
Akiwa amemaliza kazi hiyo pevu, akampoka bwana huyo funguo wa gari atumie usafiri wao kuyeya na Sheng. Akazama ndani na kutekenya gari, akaweka ‘gear’, kabla hakanyaga mafuta, akasikia kitu kisogoni.
“shut the the car off,” akaamriwa.
Basi akatii amri. Akazima gari na kuweka mikono yake juu. Kukawa kimya kidogo. Alipotazama sight mirror, kioo kikaacho juu ya kichwa cha dereva, akaona sura nyeusi na si ya kizungu kama ambavyo alikuwa anawaza. Na kama haitoshi, sura ile aliyoiona haikuwa ngeni machoni pake.
“Sheng yupo wapi?” sauti ikauliza. Basi Lee akasita kidogo kusema. “Nimekuuliza Sheng yupo wapi?” Swali likarudiwa. Lee akajifikiri kidogo, kisha akasema, “Yupo upande wa kaskazini wa mahalii tulipo.”
“Tumwendee,” akaamriwa. Basi akatia moto kwenye gari na kutimka kwenda huko ambapo Lee alipasemea. Lakini kichwani mwa mchina huyu hakukuwa salama. Alikuwa anawaza mambo ya hatari. Alikuwa anawaza namna ya kujinasua hapa ahepe zake salama.
“Kamwe usije ukafikiri ujinga,” mwanaume yule aliyemwonyeshea bunduki akamtahadharisha. “Punde tu utakapofanya ujinga wako, basi nitatoboa kichwa chako na kukuacha mfu uliwe na mbwa koko!”
Basi hapa Lee akasitisha kwanza mipango yake. Akawaza huyu mtu ni wa namna gani na kivipi aliwaza alchokuwa anakiwazia yeye kichwani. Katika fikra hizo ndipo sasa fahamu zikamjia, kumbe mwanaume yule alikuwa ni Jona.
Ndio! Akili yake ikawa inazoza yenyewe. Ni Jona huyu. Ina maana naye amekuja na wale wazungu au amekuja kwa mambo yake binafsi? Lakini amejuaje haya? Akajikuta akipata mawazo maradufu.
Lakini zaidi akajikuta pia ana sababu ya kuhofia mara mbili. Kwake Jona hakuwa mtu wa masikhara hata kidogo. Kabla ya songombingo lolote lile, alikuwa ni mwanaume waliyemtafuta na kuhangaika kummaliza pasipo mafanikio.
Gari likasimama.
“Yupo pale!” Lee akasema akionyeshea kwa kichwa.
“Shuka, kamlete!” Akaamriwa. Naye pasipo ajizi akashuka na kutembea hatua tano kwendea kizani. Alipotazama kwa macho yake ya wizi, akaona mdomo wa bunduki ukimuelekea. Hakuwa anaweza kutoroka. Aidha akifanya hivyo aenende akiwa majeruh kama atafanikiwa kunusuru roho yake.
Ni kweli. Mwanga wa mbalamwezi haukuwa unamdanganya. Alichokiona kiliikuwa ni sahihi kabisa.
Basi akamnyanyua bwana Sheng aliyekuwa amelala chini, pengine katika hali ya kutojitambua. Akauweka mkono wa Sheng begani mwake na kisha akaanza kujongea kuuendea usafiri.
Ila akilini mwake bado akiwaza. Bado akifafanua. Na macho yake yakiwa yanaangazaangaza kule dirishan ambapo mdomo wa bunduki ulikuwa umetokeza nje tayari kwa ajili ya shambulio.
Akawaza kumtelekeza Sheng. Amweke mbele kama ngao yake kisha yeye akapotea zake salama. Ila akaona si kheri. Hata kama angelifanikiwa kutoka hapo, nini kingelifuata? Si kwamba kazi na juhudi zake zote zitakuwa za kutwangia maji kinuni?
Aliweza kuyawaza haya yote kwasababu ya mwendo wa taratibu aliokuwa anakokotana na mgonjwa Sheng. Mgonjwa huyo alikuwa mzito, na tena hivi hajiwezi, basi uzito ndiyo huwa maradufu. Ilimpasa Lee kutumia nguvu nyingi sana kusonga.
Basi akiwa bado hajafika mlangoni mwa usafiri, mara ghafla akasikia jambo la kumshtua. Ilikuwa ni kama sauti ya kishindo na kaupepo pia. Akatazama upande wake wa kaskazini kwa mashaka. Huko akaona mtu mmoja kwa mbali kama kweli macho yake yalikuwa yanaona sawia.
Mtu huyo alikuwa mweusi kwanzia kichwa mpaka miguu na mkono wake wa kuume ulikuwa umebebelea bunduki yenye mdomo mrefu. Yalikuwa ni mang’amun’amu ya giza? Akajiuliza. Hapana! … Hapana! Sauti ikateta kichwani mwake. Na kwa kumwondoa shaka, mara taa za gari alilomwacha Jona akiwa ndani likawasha ‘full light’, akamwona mtu huyo vema.
Ni kweli alikuwa ni mtu. Ni kweli mkononi alikuwa amebebelea bunduki. Na ni kweli alikuwa amevalia mavazi meusi kuanza juu mpaka chini. Mavazi haya yalikuwa ndiyo yaleyale ambayo alikuwa ameyavaa yule bwana wa kizungu aliyetoka kumuua muda muda si mrefu.
“Panda upesi!” Jona akafoka. Na haikuchukua punde, risasi zikaanza kumwagwa haswa kushambulia gari! Ni kheri Jona alikuwa amefungua mlango wa gari na basi risasi zilizokuwa zinamwelekea Lee na Sheng zikagotea mlangoni. Takriban risasi nane!
Lee alipojitupia humo, pamoja na Sheng, gari likakanyagwa mafuta na kuchomoka kwa kasi mno! Hata mlango ukafungwa wakiwa mwendoni. Gari, kwa pupa na kwa kasi, likamfuata bwana yule aliyekuwa anawashambulia kwa nia ya kumsomba.
Kabla halijafanikiwa, bwana huyo akatoweka. Ilikuwa ni upesi mno kiasi cha kuweza dhani pengine ameyeyuka, ila la hasha! Bwana huyu alikuwa amekwenda hewani mithili ya paka mweusi wa misitu ya Amazonia.
Na kama vile ngedere, akatua kwenye paa la gari liendalo kasi, na akalikamata kwa nguvu mno. Wakati nguo yake ikiwa imeshaji - tune na kuwa yenye mabakamabaka yenye matobo madogomadogo yaliyovimba. Na mikononi kucha zilikuwa zimetokama kana kwamba chui.
Hivyo basi haikujalisha gari lilipelekwaje, hovyo kiasi gani, bwana huyo akawa bado yu paani. Jona akayumbisha gari kwanguvu, akaendesha kwa mwendokasi wa hali zote, bado hakufanikiwa kumng’oa njemba huyo paani!
Na kutulia kidogo, njemba huyo akaanza kumwaga risasi akitoboa paa. Shukrani gari lilikuwa na paa gumu. Waliolitengeneza walilenga liwe hivyo, na si tu kwenye paa, hata huko pande zingine, gari lilikuwa gumu kumeza risasi.
Na punde bwana huyo alipokuwa akishambulia paa kwa risasi, Jona akatambua kuwa adui huyo kwa huo muda atakuwa ameshikilia paa kwa mkono moja, mwingine akiutumia kuushambulia, hivyo akaongeza kuyumbisha usafiri huo kwa pupa na kumnyima nafasi ya kufanikisha zoezi lake.
Akafanikiwa kwa hilo. Na pale adui alipopata upenyo wa kushambulia tena, Jona akafanya mahesabu ya upesi kichwani. Ni hivi, wakati anamwona adui yule akiwa amebebelea bunduki wakati ule alipomulika full light, adui huyo alikuwa amebebelea bunduki mkono wake wa kuume.
Kwahiyo basi adui huyo hutumia mkono huo, wa kuume, kushambulia. Na kwa maana hiyo mkono wa kushoto ndiyo hudaka paa. Na kwa makadirio yake basi, itakuwa vigumu sana kwa adui huyo kuangukia upande wa kulia, kwani atakuwa kajaza balansi upande huo. Hivyo … hivyo upande wa kumwangushia ulikuwa ni huu huu wa kushoto alipoekea mkono.
Basi akamwacha adu afyatua risasi. Akazihesabu, moja … mbili … tatu … nne! Akabinya breki ya ghafla na kuliemazia gari upande wa kushoto kwa kukata kona ya ghafla mno! Mpango ukaitika. Adui alikawia kudaka paa kwa mkono wake wa kuume, na hivyo akawa sasa ananing’inia na mkono wake wa kushoto, upande wa kushoto wa gari.
Bado akawa ngangari. Akanyooshea mdomo wa bundki ndani ya gari. Lakini kabla ajafyatua, Jona akatupa teke lake kutengua mlango wa gari, mlango ukatenguka na kumsomba adui huyo na kumwaga chini! Akabiringita mara tano kabla hajatulia tuli akiskizia maumivu makali. Na huku akitazama gari likiyoyoma.
“****!!” akalaani akipiga kofi ardhini kisha akaweka kidole chake sikioni na kusema, “I’ve lost them!”
**
Gari lilisimama na pasipo kupoteza muda, Jona akachumpa nje na kumwamuru Lee ashuke pamoja na Sheng. Wakatii amri. Lee akiwa anajikokota, akamtua Sheng na kisha wakafuata amri ya Jona ya kumfuata aelekeapo.
Baada ya hatua kadhaa. Wakakuta gari lingine, range rover sport nyeupe. Ndani alikuwapo Miranda, Marwa na Kinoo. Wakapanda humo na kuhepa wakiwa wamelitelekeza gari lili la maadui lililowaleta mpaka hapo.
Zikapita kama dakika nane, na mara gari lingine likafika hapo likiwa na wanaume wanne. Wale ‘the intellectual instinct’. walishuka na kulitazama gari lao, hakuna mtu. Wakanyofoa mfumo wa GPS na kifaa fulani kilichokuwa kinafuatilia ‘chip’ aliyopandikiziwa Sheng mwilini.
Basi wakarejea ndani ya gari lililowaleta na kutimka. Wakaendelea kufuatilia mahali alipo Sheng kwa kutumia chip ile. Na baada ya kama robo saa, wakawa wamefika mahali ambapo ilionyeshwa kwenye ramani kuwa ‘chip’ ipo hapo.
Basi wakashuka na kusogelea hilo eneo. Ajabu wakakuta kuna kikopo kidogo cheupe chenye mfuniko mwekundu. Mmoja akakiokota na kuifunua. Ndani akakuta ‘chip’ yao na karatasi nyeupe yenye ujumbe uliosomeka,
“Welcome to the sky of the damned.” Kumaanisha karibu kwenye anga la washenzi.
Wakaghafirika sana kukumbwa na kadhia hiyo. Aibu iliyoje hiyo? Waliona wamevulia nguo mbele ya umati. Waliona wamedhalilishwa haswa. Wanashindwaje na watu duni kama hawa? Na tena kwa wakati huo wakiwa wamempoteza mpambanaji mmoja vitani?
Basi wakarejea ndani ya gari lao na wasiende popote bali wakae na kujadili cha kufanya kwa maana sasa hawakuwa na namna mbadala, chip ilikuwa imetolewa mwilini mwa Sheng na hata lile gari lao, ambalo kama lingechukuliwa basi wangelifuatilia, nalo limetelekezwa.
Lakini japo walikuwa ndani ya gari kujadili nini kifuate, ajabu wakajikuta ukimya umewatawala. Vinywa vilikuwa vizito na pengine vichwa navyo viligoma kufikiri kwa muda. Wakakaa hapo kwa muda wa kama dakika kumi hivi, kukiwa kimya. Kitu pekee kilichojuza kuwa kuna watu ni sauti za pumzi.
“Let’s go home,” akapendekeza Wales. “It’s not safe out here.”
Basi gari likawashwa, wakatimka. Wakatembea barabarani kwa mwendo wa kama nusu saa, na wakiwa wamekwama kwenye mataa, kwa nyuma, dereva akaona gari la polisi. Akalitazama kwa umakini kwa kupitia side mirror, punde wakaruhusiwa kwenda. Wakaenda.
Na lile gari la polisi huku nyuma likawa linawafuata. Gari hili lilikuwa la modeli kama zile za corola, lakini lenyewe ubavuni lilikuwa lina rangi nyeusi na maandishi makubwa meupe, POLISI, na kwenye paa kulikuwa na taa ziang’azo, nyekundu na bluu.
Hapa bwana Denmark, dereva, akapata shaka juu ya gari hilo. Akafikiri kuliweka gari lao kando wapate kuteta na polisi ila akaona chaguzi hilo halitakuwa jema. Mazingra hayakuwa mazuri kwa wao kufanya tukio eneo hilo endapo wakikosana na hao wanausalama, basi akaendelea kutembea, na kwa tahadhari akaongeza mwendokasi wa gari.
Alipofika mahali alipoona ni ‘salama’ kwao, basi akaegesha gari kando na kungoja. Punde nalo gari la polisi likafika na kuegesha pembeni pia. Akashuka mwanaume mmoja aliyebebelea bunduki mkononi, na kidogo akashuka mwingine. Huyu yeye alikuwa amevalia sare za polisi.
Yule mwenye nguo za kiraia, akaamuru,
“Shuka chini na weka mikono juu!”
Akisema hayo alikuwa amejiweka mbali kidogo na usafiri huo. Na mikono yake imekaa tenge kujihami. Basi kidogo, Denmark akashuka. Ajabu tayari mwili wake ulikuwa umevalia suti nyeusi na si zile nguo ambazo walifanya nazo tukio.
“Is there any problem, officer?” akauliza.
“Yes, there is!” akajibu yule polisi aliyevalia nguo za kiraia. Bila shaka alikuwa ni mpelelezi.
“Raise up your hands!” akaamuru. Bwana Denmark akatii amri.
“Are you alone in that car?”
“Uuuuhm, no! I am with friends.”
“Tell them to get out! Hands up!”
Denmark akawatazama wenzake na kuwapa ishara ya kichwa. Wote walikuwa wamesikia amri ile, basi wakatoka wakiwa wameweka mikono juu. Na wote walikuwa tayari wamevalia suti zao kama yule mwenzao, Denmark.
“Who are you? And where are you coming from?” Afisa polisi akauliza. Denmark akawatazama wenzake kisha akapaza sauti, “We are just tourists. We are from beach.”
“Beach at this time? … may I see your documents?”
“Aahm, sure you may, but they are not here with us. They are where we live in, would you mind taking you there to see?”
Yule afisa akatazamana na mwenzake kwa macho ya mashaka. Alafu akaurudisha uso wake kwa wale wazungu, akawaamuru wageukie na kushika gari kwa ajili ya ‘search’, wakatii. Basi wale polisi wakajongea na kuanza kuwapekua wakipapasapapasa mifuko na maungo yao.
Walipomaliza, wakawakata wanaume hao wasonge kando na gari nalo lipekuliwe. Wakatii. Polisi wakaangaza ndani ya gari na kurusha macho huku na kule. Hakuna walichopata.
“We are sorry. You can just move on with your journey,” akasema bwana polisi akimpatia mkono Denmark.
“Never mind, it’s just normal,” Denmark akasema kwa tabasamu. Yule polisi na mwenzake wakajongea kufuata gari lao, na hawa wakina Denmark wakazama garini waende.
“ … sio wenyewe, sio wenyewe over …” polisi yule mkaguzi akateta na radio call. Lakini hapa ndipo akagundua kuna kitu hakipo sawa. Mkono wake wa kuume uliobebelea radio call ulikuwa na damu! Kutazama vema, ni kweli na si macho yake.
Hapa moja kwa moja akajua damu hiyo alikuwa ameitoa mkononi mwa Denmark. Basi akashuka upesi, lakini kabla hajasema jambo, gari la wakina Denmark likawa limeng’oa nanga na kujiendea. Akarudi garini na kuanza kulifuatilia.
Kwa ishara wakataka gari hilo likae kando. Lakini kwa sasa wakawa wamenoa, gari halikukaa tena kando na badala yake vita ikaibuka!
“Ndio wenyewe! Ndio wenyewe, over! …” polisi aliteta na radio call yake. Macho yakiwa yamemtoka pima kutazama gari walikimbizalo. “… plate number T 457 AAA, New Bagamoyo road! … T 457 AAA New Bagamoyo road, Over!”
Alipomalizia kusema maneno yake hayo akastaajabu kuona gari lile walikimbizalo, likikata kona ya ghafla, likasimama na kurudi nyuma upande wa kushoto. Pap! Wakatazamana na wale polisi. Kilichofuata hapo ikawa ni simulizi ya kusisimua. Risasi zilitupwa haswa, tena ndani ya muda mfupi tu, ila wale polisi hakuna aliyetoka na uhai wake hata mmoja! Wote wakamiminwa damu na kuachwa na matobo matobo kana kwamba karatasi. Kisha wazungu wakapotea!
Na walipofika huko mbele, wakavamia na kukwapua gari lingine kwa usalama. Sasa wakaondoka pasipo mushkeli mpaka kwenye makazi yao.
***
Saa tano usiku …
Ni nje ya nyumba lakini ndani ya uzio. Hapa Lee alikuwa amepigishwa magoti na Sheng akiwa amelazwa chini. Mbele yao kuna watu watatu nao ni Jona, Miranda, Marwa na Kinoo. Mkononi mwa Jona kuna bunduki ndogo na mdomoni mwa bunduki hiyo kuna kiwamba cha kumezea sauti. Na bunduki hiyo tayari ilikuwa ‘imekokiwa’ kwa ajili ya tukio.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapa nje ni baridi. Kuna manyunyu ya mvua. Na kwa namna anga lilivyokuwa limefungamana kwa uweusi, kulionyesha kuna dalili ya mvua kubwa kushuka muda wowote ule.
“Mbio za sakafuni huishia ukingoni,” akasema Jona akimtazama Lee. “Kiko wapi sasa? Leo upo mbele yangu ukiwa huna msaada, na huyo punda wako akiwa amejilaza kama mwana kuku aliyenyeshewa na mvua. Kuna lolote la kusema kabla ya risasi zangu mbili kung’oa uhai wenu usio na maana kwangu?”
Lee akatazama kwanza chini, na kisha akamtazama Sheng ambaye hakuwa na uhakika kama kweli yu hai au lah, kisha akasema, “Mbele ya macho yenu naweza nikaonekana si wa maana kwa sasa kama ukitazama hapa na si mbele. Lakini …” akamtazama Jona machoni. “Lijalo ni kubwa kuliko hili unalolimaliza. Linatisha, na limedhamiria kuuteka ulimwengu mzima.
Kama wataka kweli kulimaliza, kuyamaliza yote for the good of this country na ulimwengu kwa ujumla, basi unanihitaji.”
“Ni kitu gani hicho unachokiongelea?” Jona akauliza.
“Umeona kile kilichokuwa kule,” akasema Lee. “Umewaona wale waliotuvamia na kwa namna walivyofanya kuteketeza kambi nzima ndani ya muda usiozidi lisaa limoja. Kama haitoshi, watu hao si tu kwamba watatumaliza sisi na kwenda zao, la! Bali wataanzisha ngome yao hapa.
Na kwa kupitia ngome hiyo basi watateka kanda hii like never before. Mtashuhudia mauaji makubwa na hata vita kuzuka ili wapate vile vilivyomo ndani ya nchi hii kabla ya kuikausha kuwa jangwa.
Sidhani kama unawafahamu vema watu hawa zaidi ya kuwaonea hapa. Wameanza huko Uchina, na sasa wamefikia hapa. Wataufikia ulimwengu mzima na kuuweka kiganjani. Kisha watamgeuza kila mtu kikaragosi kabla ya kuwa maiti. Amini nakwambia.”
Jona akatulia kidogo kisha akauliza, “Kwahiyo wewe utawamaliza watu hao?”
“Siwezi kufanya hilo hata kidogo. Mimi ni kama chawa tu ndani ya msitu huo mkubwa. Ila ninachoweza kukifanya ni kuwatambua, na hata kuonyeshea wapi wanapatikana. Pengine mkiwa mmedhamiria, mkapate kuwamaliza kabla maji hayajawafika shingoni.”
Kabla Jona hajatia neno, Lee akasema akiwa anatazama chini, “Pengine sisi twaelekea kuisha, lakini lijalo linatuhofisha hata sisi.” Akanyanyua uso wake na kuendelea kuteta, “Nakupa maisha yangu kwa hii ahadi. Niruhusu nikusaidie kuwamaliza watu hawa, na punde tutakapokamilisha hilo, utanipatia bunduki hiyo mwenyewe, nami nitajimaliza.”
Jona, akiwa amefinyanga macho yake, akamtazama Sheng. “Siwezi kumwacha huyu hai. Hana sababu yoyote ya mimi kumbakizia pumzi.”
Akamnyooshea bunduki, lakini Miranda akaishika bunduki hiyo na kusema, “Ngoja kwanza …”
***
“Pengine kabla ya kumuua, tuntamhitaji,” akavuma mwanamke huyo. Watu wote wakamtazama lakini Jona ndiye akamuuliza, “Tutamhitaji kwa kitu gani na ilhali yupo huyu mwingine?”
Miranda akamnong’oneza Jona sikioni, na basi mwanaume huyo akaridhia kumbakiziauhai bwana Sheng, ambaye bado kiuhalisi hakuwa anaonekana kama mwenye matarijio ya kupona. Hata hapa wakati watu wanajadili juu ya uhai wake, yeye hakuwa anafahamu lolote lile.
Tendo pekee la uhai alilokuwa analifanya ni kuhema tu.
Basi Lee na Sheng wakakusanywa na kuingizwa ndani, Lee akahifadhiwa kwenye chumba cha peke yake, kwakuwa bado hakuwa anaaminika. Na Sheng akawekwa pia kwenye chumba chake. Bado usimamizi ukionyeshwa kwa kufungiwa mlango.
Sasa hapo vikawa vimebaki vyumba viwili tu ambavyo viliwapa mawazo wenyeji juu ya namna gani watalala kwa sasa.
Asubuhi ya saa tatu …
“Kinoo, inabidi uende town kuchukua double decker,”alisema Miranda. “Lakini pitia kwanza kwa Kilonzo, chukua pesa hapo. Usijali, ntamtaarifu akupatie.”
Kinoo akapokea maagizo hayo na kwenda zake. Angalau hivyo ndivyo namna walivyokuwa wanaendesha familia yao. Kwakuwa mirija yote ilikuwa imezibwa na hakukuwa na yeyote miongoni mwao ajihusishaye na shughuli rasmi, Miranda alikuwa akichakarika kufufua na kuendeleza vibiashara vyake vya hapa na pale.
Jambo hili lilikuwa linamkwaza sana Jona. Alitamani kusaidia lakini Miranda hakutaka kabisa hilo maana Jona bado hakuwa amesahaulika kwenye taswira za watu, tena kama muuaji wa kamanda wa polisi, na lile tukio lake la kutoroshwa toka kituoni.
Ilikuwa ni hatari kwake kwenda huko nje na kuzurura. Lakini mbali na yote hayo, bado Jona aliona anapaswa kuwa na cha kufanya kumsaidia mzigo wote ulioangukia kwenye mabega ya mwanamke huyu, japo kitu chenyewe hakuwa anakifahamu. Hakuwa anajua ajihusishe na nini awe salama na atoe mchango.
“Hey,” Miranda aliita kumng’oa Jona mawazoni. “Are you ok?”
“Yes, I am,” Jona akajibu akimtazama Miranda kwa tabasamu ambalo halikuwa laendana na macho yake.
“Sure?” Mirand akauliza.
“Yeah! No problem,” Jona akasema akitikisa kichwa. Walikuwa wenyewe sebuleni maana Kinoo aliongozana na Marwa kwenda huko kwa mtu ajulikanaye kama Kilonzo.
“You think about Sheng? … listen, its going to be alright. We need him at this time. Unahitaji antidote kumbuka. Na zaidi we can use him kama frontline wetu kukamilisha kazi. Don’t you think about that?”
Wakati Miranda anasema hivyo, alishika mikono ya Jona na kuiminyaminya. Alikuwa anamtazama Jona kwa macho yanayoongea, kwa macho yanayomaanisha akitamkacho.
“Naelewa,” Jona akajibu. “You don’t have to repeat that, Miranda. Thanks. I appreciate kila unachokifanya for me. Unajitolea sana. Nina deni kubwa sana kwako.”
“No no no. Hauna deni lolote kwangu. Jona, mpaka sasa tupo hapa ni kwasababu yako wewe. Umetupa tumaini na kitu cha kukipigania. Umetufanya tuwe tayari kufa lakini kwa heshima tukiacha historia kuwa tulipambania upande ulio mwema. We thank you for that.”
Basi wakakaa hapo na kuteta kwa kama nusu saa. Kinoo akapiga simu akiwa eneo la kununua kitanda, akamweleza Miranda kuwa kwa pesa waliyoipata kwa Kilonzo, basi aina ya kitanda wanachoweza kukipata si kile alichokuwa anatamania.
Hapo ikawa hamna namna, Miranda akamwambia achukue kilichopo, atajua nini cha kufanya. Alipokata simu, akamwambia Jona, “Inabidi niende.”
Akanyanyuka na kwenda chumbani. Baada ya muda kidogo, akatoka akiwa ameshajiandaa. Amevalia gauni lake matata likabalo kiuno na viatu vyake vya visigino virefu. Mkononi amebebelea pochi ndogo.
“Natoka kidogo. Nitarejea muda si mrefu sana.”
Jona akaitikia kwa kichwa, Miranda akaenda zake akimsindikiza kwa macho.
**
Saa tano asubuhi …
“Miranda, Miranda, ulikuwa wapi siku zote hizo? … ulinikimbia si ndio?”
“Hapana, mpenzi. Sikukumbia. Kwanini nifanye hivyo?” Miranda alijitetea kidhaifu akimtazama Boka usoni. Boka alikuwa ofisini kwake, ameketi kwenye kiti chake kikubwa akizunguka zunguka huku na kule. Amejaa.
“Hivi unajua hata kesi iliendaje, iliishaje?” Boka akamuuliza Miranda.
“Hapana, sijui. Lakini Boka, hatuna haja ya kuongelea yaliyopita tena mpenzi. Yashapita, right? Let’s focus kwa yajayo. Here I am.”
Boka akatabasamu. Akagongagonga kalamu yake mezani mulipojaa mafaili kadha kwa kadha na kusema, “Baba yako mzungu alikutorosha nchini?”
Miranda akatazama chini kwa sekunde tano pasipo kusema jambo. Aliporejesha uso wake juu, macho yalikuwa mekundu na punde yakaanza kumwaga chozi.
“Amefariki,” akasema kwa sauti ya chini. Boka akashikwa na huruma. Akakunja ndita zake kumtazama Miranda kwa pole.
“Amefariki lini na mbona hukunambia, Miranda?”
Basi hapo Miranda akapata upenyo wa kupenyesha ulaghai wake. Akamwambia Boka kuwa hata ukimya wake ulisababishwa na msiba huo. Ilimpasa aende Uingereza kinyume na masharti aliyopewa. Na hata aliporejea hakuwa sawa kabisa. Imemchukua muda kurejea halini.
“Pole sana, mpenzi. Sikuwa nafahamu yote hayo,” Boka alijinasibu. “Ila usijali. Mambo yako sawa sasa. Baada ya yule Kamanda aliyepita kufariki, huyu wa sasa ni rafiki yangu sana. Na hata ndiye yeye aliyefanya jitihada mimi kuwa huru. Kwahiyo hakuna tena haja ya kuhofia.”
Baada ya maongezi haya machache, Boka akafunga ofisi kwa muda na kutoka na Miranda kwenda mahali patakapowa- ‘refresh’. mahali tulivu watakapoweza kuongea kwa uhuru. Huko wakaongea sana, na mwishowe Boka akampatia Miranda pesa taslimu.
“Bado nia yangu ya kukuoa ipo palepale. Tafadhali utakapojihsi poa, tuonane.”
Miranda akaenda zake.
***
Saa kumi jioni …
“We are still looking for …” simu ikakata. “Shit!” Denmark akalalama. Akaweka simu chini na kuwatazama wenzake. “Boss is so mad!” akasema kwa ufupi kisha kukawa kimya kwa sekunde kadhaa. Ni wazi walikuwa katika hali ngumu. Lazima wampate na kummaliza Sheng ili kazi yao isemekane kumalizika.
Denmark akamtazama Wales na kumuuliza, “Anything?”
Wales alikuwa ni mtu ahusikaye na mitandao na mambo ya teknolojia. Ndiye yeye hata aliyehusika na kumpandikiza Sheng chip ndani ya mwili wake. Na kwa kutwa nzima, alikuwa bado anahangaika na tarakilishi yake kuona kama anaweza kupata namna ya kumpata Sheng.
“No,” akasema akitikisa kichwa. “Not yet. I think we should wait more.”
“No, Wales!” akafoka Denmark. “We have no time to waste more. We have limited days here, remember! You have to do something.”
“I do!” Wales akajibu. “I do it everytime. When I tell you to wait just wait because I am on to something. Can’t you see? I don’t just sit and do nothing.”
Basi maongezi haya y kutupiana mipira, yakaendelea mpaka pale majira ya saa moja usiku, ambapo Wales alikuja kutoa taarifa kuwa kuna jambo amelipata kwa kutumia ‘satellite’. Wenzake wote wakajongea na kumskiza.
“I think I’ve found him,” akasema kwa kujiamini.
“Sure?” Ireland akauliza akitoa macho.
“Yes, sure.”
Lakini kabla hajasema jambo hilo, simu ya Denmark ikaita. Kupokea akaambiwa sentensi moja,
“Kill the president before the next night.”
Na kisha simu ikakata. Kabla hajawaambia wenzake jambo, akapiga simu na kuuliza, “What about the chinese man?”
“Kill both of them. The president has already signed many Chinese huge contracts that we cant allow any of them to operate. It is very dangerous. So kill him.”
Simu ikakata tena. Denmark akafikisha taarifa hizo kwa wenzake. Bado wakiwa katika joto hilo, wakasikia sauti ya honi getini.
***
Basi kwa tahadhari kabla hawajakwenda huko getini, wakatazama taarifa za kamera kadhaa walizokuwa wamezipachika kwenye makazi yao. Na walipotazama wakapata kujua kuwa wageni waliopo getini ni polisi.
Wamekuja kufanyaje hapo? Ina maana walijua makazi yao? Hawakuwa na muda mrefu wakujipanga. Denmark akatoka ndani akiwa hajabebelea silaha yoyote. Wenzake wakabaki ndani kwa miadi ya kutazama kinachoendelea na kuchukua hatua pale watakapoona panastahili.
Geti likafunguliwa.
“You are under arrest!” akafoka polisi mmoja akimnyooshea Denmark bunduki. Akamwamuru mwanaume huyo aweke mikono yake kichwani na aongoze kwenda ndani kuwatoa wenzake.
Jumla ya polisi walikuwa sita. Wanne wamevalia sare zao na wawili wakiwa ndani ya mavazi ya kiraia. Basi wakaongozana na Denmark na kuzama naye mpaka ndani. Lakini kabla hawajafanya ukaguzi wao, Denmark akataka kwanza kujua nini kinaendelea kama moja ya haki ya mtuhumiwa.
“You are the suspect of murder of two policemen,” polisi mmoja akaeleza.
“Me?” Denmark akatahamaki. “Ok, may I contact my lawyer, please?”
“After issue us your all valid documents of being here and bring us all of your mates here,” polisi akatoa sharti. Denmark akamtazama pasipo kusema jambo, kisha akaomba ruhusa ya kwenda ndani kuleta vitu vinavyohitajika.
Hapo akakabidhiwa polisi wawili wa kumsindikiza. Sebuleni wakabakia polisi wawili, na kule nje wakiwa wawili wengine. Baada ya muda, Denmark akarudi akiwa amebebelea nyaraka zake, ila wenzake hawakuwapo hapo.
“Where are your mates?” akauliza polisi.
“They are out,” akajibu Denmark. Basi polisi huyo amuulizaye maswali, akawaamuru polisi wale waliomsindikiza bwana Denmark kwa mara ya kwanza, wafanye upekuzi wa nyumba nzima. Agizo likaanza kutekelezeka.
Wakazama vyumbani na kupekuapekuwa huku na kule. Chini na juu. Mikononi mwao wakiwa wamebebelea silaha za moto.
Baada ya muda mdogo, polisi mmoja aliyekuwa anafanya upekuzi akagundua jambo lililomshtua. Alipotazama dirishani kule nje, aliona miili miwili ikiwa imelala chini. Akatahamaki.
Kutazama vema akagundua miili hiyo ilikuwa ni ya wenzao wawili ambao walikuwa wamekaa nje. Akahisi kusisimka. Vinyweleo vikasimama na macho yakamtoka. Wameuawa!
Basi kugeuka aende kutoa taarifa, akakutana uso kwa uso na Ireland. Kabla hajavuta pumzi, akawa ameshambuliwa na kulazwa chini mfu. Ireland akakwapua silaha yake.
Yule polisi mwingine wa pili, akiwa huko chumba kingine, akiwa hana hili wala lile, hajui liendealo. Akaendelea kupekua na kupekua. Kuja kutahamaki amezibwa mdomo. Akafurukuta. Mara akakitwa na kitu kichwani, akadondoka kama mzigo.
Sasa polisi wanne wakawa wapo chini. Walibakia polisi wawili tu ambao wapo sebuleni.
Kwakuwa muda ulikuwa umeenda na wale walioagizwa hawakurejesha taarifa, basi yule polisi, ambaye alionekana ni mkubwa kuliko wenzake kwa cheo, akamtazama polisi aliyekuwa naye hapo sebuleni na kumpatia ishara ya kichwa kuelekea chumbani.
Yule mwenzake pasipo kusita akaenda huko asijue aenda kujitoa uhai. Alipopotelea huko, akapotelea kweli. Sasa Denmark akabaki na yule mmoja pale sebuleni. Muda ukaenda. Akaanza kutabasamu.
Polisi yule akatia shaka. Na muda si mrefu akapewa sababu ya kuhofia zaidi baada ya washirika wote wa Denmark kutoka chumbani, yaani Ireland, Sweden na Wales.
“Would you mind putting your gun down, officer?” akasema Denmark. Polisi akagoma kutii hilo agizo. Akiwa aliyeshikwa na woga, akasonga nyuma mpaka dirishani. Akafungua dirisha na kuchungulia upesi. Akaona wenzake wakiwa chini. Wamekufa!
Mikono yake ikaanza kutetemeka. Na mate yakawa magumu kumezeka. Alikuwa hana ujanja tena, alikuwa hana cha kufanya. Risasi zake kadhaa ndani ya bunduki zisingeweza kumwokoa dhidi ya wadhalimu wale.
***
Usiku wa saa mbili …
“Wameondoka,” alisema Marwa akimtazama Jona. Mwanaume huyo alikuwa ametoka kutazamia kwenye tarakilishi yake kufuatia vifaa walivyoviweka kule kwa wale wazungu.
“Na wale polisi je?” Jona akauliza.
“Sijajua nini kimewakumba,” akasema Marwa. “Gari lao halijatoka. Limebakia ndani.”
Ndani ya nusu saa, Jona na Kinoo wakawa wamefika kwenye eneo husika. Jona akamwambia Kinoo atulie nje kusoma ramani, yeye atazama ndani. Basi akaingia na kupembua. Akakuta maiti za wale polisi, nje, sebuleni na vyumbani. Akapiga picha za maiti hizo na kisha akamtumia Marwa kwa kupitia mtandao, alafu akamtumia ujumbe kumuuliza,
“Watakuwa wameenda wapi?”
Akiwa anangoja majibu, akatoka ndani ya nyumba hiyo na kwendaze mbali pamoja na Kinoo. Muda kidogo ujumbe ukaingia toka kwa Marwa, “Wapo karibu na sisi!”
“Karibu na wakina nani?” Jona akauliza. Punde ujumbe ukaingia toka kwa Marwa ukisema, “Naona kama wanajongea kuja kwenye makazi yetu!”
“Serious, Marwa?”
“Yes. I think they are coming!”
Yote aliyokuwa anayaongea Marwa hayakuwa ya kutilia shaka kwani gari walitumialo wazungu wale lilikuwa limepachikwa kifaa tambuzi cha GPS hivyo wakijua mwenendo wake. Zoezi la upachikaji wa kifaa hicho lilifanywa na Jona kipindi kile almanusura kukamatwa.
Sasa hapa kwenye kioo cha tarakilishi ya Marwa, ‘GPS tracker’ ilikuwa inaonyesha gari hilo likisonga kuja walipo. Na kasi yake ilikuwa kubwa ajabu!
“Kinoo, we have to go! Haraka!” Jona akabwatuka kisha upesi wakaanza kukimbia kufuata chombo chao cha usafiri. Walipokwea, wakatimka upesi, Jona akikamata usukani.
Alikimbiza gari kwa kasi mno. Macho yake yalituama barabarani, mikono yake ilikamatia usukani kwanguvu na miguu yake ikikanyagia mafuta na breki kwa zamu.
“Call Miranda!” Jona akamwagiza Kinoo. Kinoo akafanya hilo jambo upesi. Simu ikaita mara moja na mara ikapokelewa, ikawekwa ‘loudspeaker’.
“Miranda!” Jona akaita. “Ondokeni hapo nyumbani upesi!”
“Hatuwezi!” Miranda akajibu. “Hatuwezi kuondoka kwa sasa, it’s too late! Wameshawasili. Yatupasa kupambana nao.”
“Hamuwezi kupambana mkiwa wawili, hamtaweza kuwamudu. Just escape!” Jona akazidi kusisitiza akitamani gari igeuke kuwa ndege ya kivita.
“No, Jona. Hatuna namna! Huwezi jua huko nje ni hatari kuliko humu ndani. Vipi kama wata ….” simu ikakata.
“Miranda! Miranda!” Jona akaita. “Piga tena!” akamwamuru Kinoo. Simu ikaita tena, haikupokelewa. Walipopiga kwa mara nyingine, ikawa haipatikani. Jona akazidi kuchanganyikiwa. Aliamini Miranda na Marwa wasingeweza kuwazuia watu wale, tena wanne na waliokubuhu kwenye sekta ya mauaji.
Kwake ikawa mtihani mkubwa. Na hata akajuta kwanini alitoka kwenda kule kwenye makazi ya wale wazungu. Ubaya zaidi ni kwamba hakuweza kutoa taarifa hizo polisi. Katika vita hii walikuwa wenyewe tu.
***
“Let’s spread!” akasema Denmark, kisha akamalizia, “Show them no mercy!”
Basi wanaume watatu, Ireland, Wales na Sweden wakagawanyika kuizingira nyumba ya wakina Miranda. Wakati huo wakiwa tayari wameshajivika nguo zao za kazi.
Punde kidogo, umeme ukakatika katika nyumba hiyo na kuwa kiza totoro isijulikane mlango na dirisha lipo wapi. Hapa sasa wale ‘the intellectual instinct’ wakawa wanaona kana kwamba mchana mkavu wa saa nane.
Hakuna huruma. Hakuna mtu yeyote kutoka na uhai.
Basi ndani ya dakika kadhaa, watu hao wakawa wamezama ndani ya nyumba kwa kuvunja milango. Wakafanya msako wao, na ndani ya muda mfupi wakawa wamegundua kuwa wamezamia mtegoni.
Ndio, mtegoni! Ndani hakukuwa na mtu isipokuwa Sheng aliyekuwa amelazwa kitandani. Swala hili likawashtua. Lakini wakiwa werevu wa kutosha, wakang’amua na kujinasua. Wakitumia teknolojia kubwa ya miwani waliyoivaa, wakatambua kuwa kuna nyayo za miguu mahali kadha wa kadha.
Na kama wakina Miranda wakiwa watu waliolitambua hilo jambo, wakajitokeza bayana, yeye pamoja na Lee huku Marwa akiwa ameendelea kufichama.
“Oh! Now you are here!” akasema Denmark, nyuma yake wakiwa wamesimama wenzake kwa ukakamavu. Mandhari yalikuwa ya giza, ila kwakuwa hapa walikuwa nje, basi angalau waliweza kuonana, haswa Miranda na mwenziwe, Lee, ambao hawakuwa wakitumia miwani ya kuonea.
Mbali na giza hilo, kulikuwa kimya.
“We could have killed Sheng already and left, but I wanted to see you, the people who outwitted us,” aliendelea kusema Denmark kwa dharau. Akamtazama Miranda na kisha akahamishia macho yake kwa Lee. Hapo akaganda kwa muda kana kwamba mtu amjuaye ama anamfananisha.
“The Chinese man,,” akasema na kisha kuguna kama mtu aliyekabwa na kicheko. “I think I know you, don’t I?”
Lee hakusema kitu. Kwa namna alivyokuwa anamtazama kulisema nini kipo kifuani mwake. Alikuwa ana pande la chuki. Mikono yake ilikuwa imekunja ngumi kwanguvu. Na pumzi yake ilikuwa inaenda juu na chini kwa kasi.
Denmark akanyoosha mikono juu akisema, “You don’t know who we are, lads! You don’t know anything about us, right?” akatabasamu. “Maybe you are braver more than we could imagine, stronger and bolder … but … but don’t ever mess with us.” Denmark akasema akitikisa kichwa chake na kidole akikipeleka kushoto na kulia. “Don’t ever ever do that. We are not of the same ground.”
“Neither do we,” akadakia Miranda kwa ujasiri. Basi Denmark akamsogelea na kumuuliza, “What do you say?”
“You heard me,” Miranda akamjibu akimtazama usoni. Denmark akatabasamu. Kisha akawatazama wenzake na kupiga makofi. “Wow! What’s so special about you sweet lady?”
“More than you can ever imagine,” akajibu Miranda. “More than you can ever handle.”
“Sure?” akauliza Denmark.
Kabla Miranda hajajibu, Lee akamshika bega mwanamke huyo kama ishara ya kumtaka anyamaze. Miranda hakujali, akajibu, “Totally sure.”
“Miranda,” Lee akaita. “Hatuna haja ya kufanya hili. Mwache mwanakharamu apite. Tuko outnumbered!”
“Kama kufa acha tufe,” akasema Miranda. “Tunakufa mara moja tu, Lee. Siwezi kuwa mdhaifu kiasi cha kudhihakiwa kiasi hiki.”
Lee akashindwa kumtuliza mwanamke huyo. Kwa macho yake akashuhudia wale washirika wa Denmark wakisogea nyuma kidogo kutoa uwanja, na Denmark akasema akimwambia Miranda, “Show me what you have.”
Miranda akamtazama Lee na kumpatia ishara ya kichwa kuwa ampatie nafasi. Lee akasita. Akauliza kwa kunong’ona, “Are you sure?” Miranda akajibu kwa kupandisha kichwa chake, basi Lee akasonga nyuma kwa hatua mbili tu na kisha akasimama akitazama kwa umakini.
Miranda akajiweka tenge, Denmark akamtazama. Mwanamke huyo akatanua miguu yake kutafuta balansi na kisha akakunja ngumi. Denmark akaguna kwa kebehi kisha akamwonyeshea Miranda ishara ya kumkaribisha.
Miranda akaanza kutupa ngumi zake nyepesi za kasi. Denmark akazihepa kama mchezo, ilan kwa makusudi akatengea uso wake ngumi moja iliyomkita upande wa shavu lake la kulia na kumgeuzia uso kando.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Not bad,” akasema. “Any more than that?”
Miranda akakwazika na kauli hiyo. Sasa akafunguka kwa umahiri wake wote, akazirusha ngumi na kujifyatua mateke kama mitego ya porini. Hamaki akamkita Denmark mateke mawili ya kifua na almanusura kumwangusha chini.
Hapa sasa Denmark akatambua mwanamke apambanaye naye hakuwa wa kumpuuzia wala kumdharau. Si bure alikuwa anajiiamini. Sasa akakunja ngumi na kutanua mapaja yake kujisimika ardhini. Akamkaribisha tena Miranda.
Miranda akaja tena akionyesha umahiri wake. Na sasa akidhamiria kumwangusha mwanaume huyu kumkata ngebe. Ila hakujua … Hakujua anatakiwa kuwa mwangalifu mno kuliko anavyodhani.
Sasa akarusha ngumi zake za upesi. Pengine akimweka ‘busy’adui yake huyu ili ampatie shambulio kubwa la hatari litakalomlaza hoi. Lakini hakuwa anafahamu kuwa akiwaza hivyo, naye adui alikuwa akiwaza kingine. Sasa Denmark hakutaka kukwepa ngumi yoyote ya Miranda, na badala yake akaanza kumdhoofisha mwanamke huyo.
Kila Miranda alipotupa ngumi yake, kwa kasi ya umeme, Denmark akatengua ngumi hiyo kwa ngumi yake nzito. Miranda aliporusha ngumi kama sita na tendo hilo toka kwa Denmark likirudia, akaanza kuchoka. Mikono ikamuuma.
Basi kujikomboa, akaanza kutumia miguu yake. Akarusha mateke mfululizo na kwa mkupuo. Napo mchezo ukawa uleule. Denmark alimuumiiza miguu yake wa kupangua kila shambulizi na ngumi zake nzito za upesi. Sasa Miranda akawa amechoka, na hapo bado Denmark hajaanza kumshambulia!
Mwanaume huyo asiwe na huruma, baada ya kutambua kuwa Miranda alikuwa hoi, na sasa anahisi maumivu maungoni mwake, akaanza kutupa mashambulizi. Ngumi zake zilikuwa nyepesi ila nzito maradufu. Hata Miranda alipojitahidi kuzizuia baadhi, bado aliyumba kwa kushindwa kustahimili.
Alipojiweka bayana, akala ngumi mbili, moja ya kifua na nyingine ya tumbo, akacheua damu. Akadondokea chini na kunguruma kwa nguvu kwa maumivu makali. Denmark akatikisa kichwa chake.
“C’mon lady. We are about to start!”
Miranda akatema mate yenye damu pembeni. Akataka kusimama, viungo vilikuwa vinamuuma. Lee akammwekea mkono wake begani kumtuliza kisha akasema kwa sauti ya chini,
“Let me …”
Kisha mwanaume huyo akamtazama Denmark na kujipanga kwa ajili ya pambano. Denmark akatikisa kichwa chake kwa masikitiko. Akampatia ishara mwanaume huyo kumkaribisha. Lee akakataa. Akairudisha ishara hiyo kwa Denmark. Alitaka mwanaume huyo awe wa kwanza kushambulia.
Basi Denmark hakuona tabu. Akaanza kurusha ngumi, viwiko na kila kiungo chake cha mwili kupambani. Mapigo yake yalikuwa ya kasi na mazito. Ilimlazimu Lee awe ‘intensive focused’. Macho na akili yake iwe nyepesi kwenye kufanya maamuzi yenye tija.
Walidumu kwa kama dakika tatu pasipo yeyote kufanikiwa kufikisha shambulizi lake kwa mwenzake. Lakini kwa muda wote huo Lee alikuwa anafanya kazi ya ziada kwani alikuwa anazingatia sana na kujilazimu kufanya maamuzi mepesi mno.
Alikuwa anatumia akili yake kwa kiasi kikubwa huenda tofauti na adui yake, hivyo ilifikia mahali akawa kama mtu aliyechoka kuendana na kasi kama hapo awali. Hapa Denmark akampatia ngumi tatu na kumwangusha chini!
Akang’ata meno kwa hasira. Akanyanyuka upesi na kujiweka tenge kwa ajili ya pambano sasa akiona ni vema kushambulia kuliko kushambuliwa. Njia nzuri ya kujilinda ni kwa kushambulia kwa kasi.
Akaweka nguvu zake zote kwenye mikono yake. Akajitutumua kwa muda. Denmark akawa matatizoni, ila bado akafanikiwa kuyeya na kukwepa, akienda kushoto na kulia, chini na juu … kushoto, kushoto .. kulia, chini! Kando na kando, kushoto, chini!
Alipokaa wazi, Denmark akatumia fursa hiyo kumtwika teke zito na kummwaga chini! Denmark akacheka kidogo na kudhihaki, “that woman his better than you!”
Lee akapandwa na hasira lakini kheri kabla hajafanya lolote, akatambua hilo ni kosa. Kutwaliwa na hasira ukiwa kwenye uwanja wa mapambano hudumaza utumiaji wa akili. Huchochea utumiaji wa nguvu kwa fujo na basi hatimaye kuangamia.
Basi kwanini asitumie njia hii? Akaona kuna haja ya kufanya jambo kumkwaza bwana Denmark. Kuna sababu ya kumpandikiza mwanaume huyo hasira ili amtoe ‘mchezoni’.
“Yes, she is better than me. But at least I look like a man, not like you sweet pie. You are more beautiful than her!” Lee akasema kwa dhihaka akitabasamu kwa mbali akinyanyuka taratibu.
Denmark akabinua mdomo. “I am going to shut that piece of shit forever!” akafoka akimjongea Lee. Akamrushia ngumi nyingi sana kwa hasira. Lee akajificha kukwepa ngumi hizo. Sasa shida kwake ikiwa nguvu kubwa ya Denmark. Mashambulizi yake yalikuwa ya kilo haswa!
Ila sasa hakuwa akitumia akili tena kama hapo mwanzo. Fundo la hasira lilikuwa limemkaba na alitaka kumkomoa mpambani wake ndani ya muda mfupi! Alitaka kumtia adabu.
Huu sasa ndiyo ukawa mwanya kwa Lee. Mwanya wa kutumia akili yake zaidi ya adui yake. Alijua fika unapokuwa na hasira, mazingatio ya kujilinda hupungua, mtu huzingatia zaidi kushambulia. Basi akatafuta mwanya wa kushambulia dhidi ya ‘mvua’ alizokuwa anatumiwa.
Na alipoupata mwanya huyo, akatuma ngumi tatu za haraka, zikamlaza Denmark chini! Wenzake wakamsogelea haraka kumjulia hali.
“Let go of me!” Denmark akawaka akiwasukumia wenzake kando, Alipatwa na hasira maradufu. Uso wake ulikuwa mwekundu. Aling’ata meno yake kwanguvu, akasimama na kumtazama Lee akihema kana kwamba mbogo.
Lee akamkaribisha tena kwa kumuita kwa ishara na kusema,
“Camon my lady.”
Holala! Denmark akanguruma kama simba. Akiwa amekunja uso wake, macho ameyafuma kwa ndita, mdomo ameubinua kama upinde wa mshale, akamsogelea Lee kwa kasi akitengeneza vishindo kana kwamba tembo. Alikuwa amefura haswa. Hakuna alichokuwa anakitaka zaidi ya kummaliza Lee.
Hakika zile dharau zake hakuweza kuzistahimili. Alikuwa amemvua nguo. Alikuwa amemdhalilisha mbele ya wenzake, tena awaongozao.
Basi akatupa ngumi zake kwa fujo. Kwanguvu. Haraka!! Lee akapata kibarua kikubwa cha kujikomboa. Ilikuwa ni kazi kubwa sana kwake kujikiinga dhidi ya mashambulizi haya. Hata kama hakuwa amekubwa, bado mikono yake ilipata maumivu kwani Denmark alikuwa na nguvu mno.
Pale Lee alipokuwa anaona anazidiwa kwa maumivu, basi akawa anasonga nyuma ama kuyeya ‘mazima’ kukwepa kombeo anazotupiwa. Alidumu kwa kama dakika tano, anashambuliwa tu. Anashambuliwa tu! Alishangazwa ni pumzi ya namna gani aliyokuwa nayo Denmark.
Hakuonekana kuchoka wala kupunguza kasi. Kama vile alivyoanza ndivyo alivyokuwa anaenenda. Hakuonekana mtu wa kuchoka muda mfupi ujao, hivyo basi kama Lee hatopata upenyo wa kushambulia, basi muda si mrefu atashindwa tena kujilinda. Atazidiwa. Na huo ndiyo utakuwa mwisho wake.
Akainjika mkono wake wa kuume kukinga ngumi ya Denmark, akainjika na wa kushoto, akarudi nyuma. Akainjika mguu wake kumzuia Denmark kurusha teke. Akainjika tena mkono wake kuume kukinga shambulizi. Akainamisha kichwa, akakipeleka kulia, akakirudisha kushoto kukwepa ngumi.
Alafu akasonga tena kando!
Denmark, kama mtu aliyetambua kuwa Lee anaanza kuzidiwa, akamsongea upesi na kuendelea kumtupia mambo mazito mazito. Mateke, viwiko, ngumi, na hata magoti. Na kweli taratibu mbinu yake ikaanza kuzaa matunda. Sasa Lee akawa akikwepa hii na ile, ijayo inamkomba.
Bahati si kwake, alipochelewa kidogo tu kujikinga, akakumbana na ngumi ya haja ya bwana Denmark iliyofukua taya zake na kumnyanyua juu kama unyoya! Na kabla hajagusa chini, Denmark akapanua mguu wake wa kulia kwenda juu, kisha akamsigina tumbo na kumgotesha sakafuni. Lee akapiga kelele kali!
Aaaaaaggh!! akajikunja kugugumia maumivu makali ya tumbo. Akakunja sura yake akisaga meno.
“Get up bitch!” Denmark akafoka akikodoa macho. Kinywa kilitema mate kana kwamba manyunyu ya mvua ya masika.
“I said get uupp!!”
Akamfuata Lee kwa upesi. Akamzaba mateke mawili ya tumbo. Miranda akashindwa kuvumilia kumwona Lee anashambuliwa kiasi kile. Akapaza sauti, “Stoop!” akisonga kumfuata Denmark, ila kabla hajafika, akastaajabu teke likimsomba kichwa, akajikuta hewani, sekunde, akadondokea chini kama mkungu!
Akapiga yowe la maumivu.
Basi hapa akawa kana kwamba amemtonesha Lee kidonda. Mwanaume huyo akanyanyuka akisema, “Is that the best you have?”
Denmark akaguna kwa kebehi. Akapiga hatua mbili kumfuata Lee. Akatupa mashambulizi yake kama ilivyo ada. Ila kwa sasa Lee hakupumbazia kama muda ule. Ndani ya dakika moja akawa ametambua cha kufanya.
Denmark akazama kosani. Lahaula! Lee akamkandika ngumi tatu za haraka mno. Akiwa anaugulia, Lee akapanda kwa hewa. Baba, akafyatuka teke lililoadhibu taya za Denmark. Na kama haitoshi likafuatia teke lingine. Denmark, na uzito wake, akanyanyuka juu kabla ya kumwagikia chini.
Yote hayo yalitokea ndani ya sekunde tatu tu! Sekunde tatu tu!
Denmark akachumpa kwa mikono yake na kusimama. Hasira zimemjaa pomoni. Akaja kwa kasi kumfuata Lee. Naye Lee hakumngoja kwa sasa. Akajikuta chini ndani ya muda mfupi, akafyagia miguu ya Lee kwa miondoko ya mdudu nge! Na kwa namna miguu yake ilivyokuwa inazunguka kama feni baridi, Denmark akajikuta akiadhibiwa vilivyo.
Sasa akalazwa chini na kutulia. Alikuwa amezidiwa.
“Hey, are you fine?” Sweden akamuuliza Denmark.
“Do I look like that?” Denmark akafoka na kuamuru, “Kill him!”
Basi wale wanaume watatu, Ireland, Sweden na Wales wakapoke agizo hilo la kushambulia. Ila kabla hawajafanya hilo, mara wakasikia gari huko nje. Wakatazamana. Punde si punde geti likafunguliwa na wanaume wawili wakazama ndani!
“We have to go!” akapaza Denmark. Basi mara Ireland akachomoa cha kuchomoa kwenye nyonga yake na kukibamiza chini. Muda si mrefu moshi ukatanda. Watu wakapotelea! Moshi ulipokoma, hawakuonekana wapi wameelekea.
***
“Inabidi tuwe makini sana. Uzembe kama huo unaweza kutugharimu maisha!” alifoka Jona. Walikuwa wote wamekaa sebuleni isipokuwa Sheng aliyekuwa amelala ndani. Ni tulivu haswa. Na hata umeme uliokuwa umekatika, sasa ulirejea.
“Nitahakikisha halitokei tena kosa kama hilo,” akajitetea Marwa. “Sijui nilipitiwaje? Tulikuja kutahamaki wakiwa karibu haswa. Hata kukimbia hatukuweza.”
Kukawa kimya kidogo. Jona akamtazama Lee aliyekuwa anatazama chini. Uso wake ulikuwa umejaa majeraha na hata mwili wake ulikuwa na maumivu ya hapa na pale. Alikuwa ametulia tuli kana kwamba maji mtungini.
“Ahsante sana, Lee,” akasema Jona. “Sitasahau ulichokifanya siku ya leo, unastahili pongezi.”
Lee akatikisa kichwa chake pasipo kusema jambo. Kisha akaendelea tena kutulia.
“Sasa nini kinafuata? Inabidi tuwe na mipango ya kuwamaliza hawa watu kabla hawajaleta madhara.”
Hapo Lee akateta jambo. “Tafadhali,” Kila mtu akamtazama na kumpa masikio.
“Inabidi tuwe makini sana. Watu wale si wepesi kama pengine tudhaniavyo. Tuhakikishe mipango hiyo inakuwa ya akili zaidi kuliko nguvu. Endapo tukisema twende battle na wao, tutapoteza, na haswa sasa hivi wakiwa wameshindwa kuonyesha umwamba wao kwa mara ya kwanza.
Lazima watajipanga zaidi ya mara hii.”
“Lakini,” akasema Jona. “Wamejuaje makazi yetu?”
Akauliza akimtazama Marwa. Marwa akamtazama Lee na kusema, “Nadhani Lee anaweza kutupatia majibu.”
“Mimi?” Lee akatahamaki. “Nitapata wapi majibu hayo?”
“Lee,” Marwa akaita. “Ulikuwa wapi wakati Sheng alipokuwa ametekwa?”
“China,” Lee akajibu.
“Huko nini kikatokea?”
“Mambo mengi tu yalitokea. Siwezi kusimulia yote.”
“Lipi lililokuwa kubwa?”
Lee akafikiri kidogo na kisha akasema, “Nilitawazwa kuwa kiongozi.”
“Na hiyo ndiyo sababu,” Marwa akateta. Lakini bado kila mtu akwa kwenye bumbuwazi. Hawakuwa wameelewa jambo.
“Unamaanisha nini kusema hayo?” Lee akauliza. Uso wake ulihakisi namna ambavyo alikuwa kwenye mkanganyiko.
“Utakuwa una chip mwilini mwako. Kama ile aliyokuwa nayo Sheng. Ujio wenu hapa ndiyo ambao umetuweka sisi bayana. Tumekaa hapa kwa muda, na kama wanaume wale wangekuwa wana namna ya kututambua, basi wangeshalifanya hilo tangu pale Jona aliponusurika kukamatwa nao.
Na kwa upande wa Sheng, chip tulishatoa, sasa nini kinabakia hapo kama kielelezo isipokuwa Lee?”
Basi kuthibitisha hilo, Lee akakaguliwa mwili, na kweli ikagundulikana ana chip mwilini mwake. Akajaribu sana kukumbuka nini kilitokea na ni muda gani aliwekewa chip hiyo. Akili yake ikamweleza kuwa itakuwa muda alivyokuwa yu hoi anaumwa!
Lakini kwanini ilifanyika kwa siri hivyo? Mbona hakushirikishwa? Na je kwa Sheng ilikuwa vivyo hivyo? Maswali haya hakuwa na majibu nayo.
“Sasa tunafanyeje?” akauliza Miranda. “Tuiharibu hiyo chip?”
“Alafu?” Jona akauliza.
“Ili wasiweze kututrace!”
“Hapana,” akasema Jona. “Kwakuwa watu wale itakuwa ngumu kuwatambua mahali walipo endapo wakiacha kutumia ule usafiri, hii chip itakuwa nyenzo nzuri ya kutambua na kuwacontrol.”
“How na ipo mikononi mwetu?” Kinoo akauliza.
“Kama walitumia chip hii kuwaongoza mpaka kuja hapa, basi wataitafuta tena. Tena sasa kwa kulipiza kisasi. Hivyo itakuwa rahisi kuwazamisha mtegoni kwa kuitumia.”
Wazo hilo likaonekana kuwa na hekima ndani yake.
“Na punde tutakapowatia mikononi, basi tutapata getaway nzuri sana ya kuwamaliza pamoja na genge lao!”
***
Saa nne asubuhi …
Sauti ya Denmark akifoka ilisikika chumbani. Baada ya muda mfupi, mlango ukafunguliwa akatoka akiwa na sura nyekundu. Mkononi alikuwa amebebelea simu.
Akaelekea sebuleni na kuketi. Wenzake pia walikuwa huko. Na alipofika, wote wakamtazama kana kwamba wanatarajia jambo kutoka kwake. Ila kukawa kimya kwa muda. Denmark alikuwa amefura. Na kutua fundo lake kifuani akaendea maji ya kunywa na kujijaza mafundo manne makubwa makubwa.
Kisha akahema.
“We have to kill him today. So get prepared.” akasema Denmark. Na asiwe mtu wa kungoja maoni, akaenda zake kurudi chumbani. Wenzake wakabaki wakitazamana.
Ni wazi hali ilionekana si shwari.
***
Majira ya saa kumi na mbili jioni …
“Jona!” Marwa akaja chumbani akiita. Uso wake ulikuwa umepaliwa na hofu. Jona alishtuka toka kitandani na kumtazama. “Vipi?”
“Kuna jambo unatakiwa kuona. Upesi!” Marwa akasisitiza na kisha wakaongozana mpaka sebuleni. Jona akakalia kiti na kutazama tarakilishi. Lakini kabla hajaona kitu, Marwa akasema:
“Wapo karibu na Ikulu. Nadhani ….”
“Watakuwa wameenda kumuua Raisi?” Jona akakatiza kwa tahamaki.
Saa moja na robo usiku, Ikulu.
Walinzi lukuki walikuwa wamesimama kwa nje na hata kutembea ndani. Wengi wao walikuwa wamevalia kaunda suti na kuna baadhi wamevalia sare za jeshi. Watu hao walikuwa na silaha mikononi, japo si wote. Na wale waliovalia kaunda suti walikuwa wana vifaa vya mawasiliano vimepachikwa masikioni.
Mbali na walinzi hao kulikuwa na kamera za ulinzi hapa na pale. Kulionekana kunalindwa haswa. Sidhani kama kunahaja ya kueleza sana namna mahali akaapo Raisi panavyolindwa.
Kulikuwa kumetulia haswa. Na pengine unaweza kusema kuwa mahali hapa ndipo salama kuliko mahali pengine popote nchini. Huenda ikawa kweli, lakini pia yaweza kuwa sio sahihi. Kuna muda yule asiyelindwa ndiye yupo salama zaidi kuliko yule alindwaye. Masikini hulala milango wazi na wakati wale walio juu wakilindwa na binadamu na teknolojia za hali ya juu!
Basi, huwezi amini katika rundo hili la walinzi, watu huthubutu kuja kupavamia. Tena wakiwa wanne tu! Ilikuwa ni ajabu na kweli. Na watu hao wasiwe wajinga kubeba hatari kama hiyo, walikuwa wamejikamilisha ipasavyo.
Masaa kabla ya tukio hili walikuwa wameshatumiwa taarifa zote wanazotakiwa kuzijua kuhusu eneo hili kwa kukusanya taarifa toka kwenye mfumo wa satelaiti. Pili, watu kadhaa washawahi kuja kutembelea eneo hili la Ikulu, si kila mtu ni mwema.
Hukusanya taarifa kidogo kidogo, pengine zinaweza zikawa kidogo, lakini nini hutokea pale kidogo na kidogo huungana? Na tatu, watu hawa kabla hawajavamia hapa, waliitumia vema pwani ipakanayo na jengo vamiwa kutimiza haja zao.
Lakini mbali na yote hayo, kuna kosa moja tu walikuwa wamelifanya. Lipi hilo?
Taratibu taratibu walinzi wakawa wanapunguzwa. Wanadondoshwa chini na kufichwa. Ni kama vile mchezo wa kuigiza uonavyo kwenye televisheni. Wavamizi hawa walikuwa wanafanya mambo yao kwa ustadi wa hali ya juu na pasipo kupoteza muda kwa aina yoyote ile.
Kila kitu kwenye mahesabu. Hata hatua wapigazo. Walitakiwa kuwa humo eneoni pasipo kuzidi dakika arobaini na tano! Na katika hizo, nusu saa pasipo kufahamika kama wapo humo.
Walifanikiwa sana kutimiza hilo. Mpaka dakika ya kumi na mbili hakuna aliyekuwa anafahamu kama nyumba ya Raisi ipo chini ya uvamizi. Na pale ilipogundulikana ikawa hivi …
Mwanaume mmoja, afisa usalama, mweusi mwenye mwili mrefu kakamavu, alisikia sauti za ajabu za wanyama waliomo ndani ya eneo. Akapata hamu kutazama kama moja ya jukumu lake. Aliposonga, akafanikiwa kuona mguu wa mtu ukiwa chini.
Basi haraka akapaza sauti yake kwenye kifaa kutoa taarifa ya tahadhari. Alipofanya hivyo hakungoja majibu, akasonga kuufuata ule mguu, akagundua kuna mwili wa mwenzake umelala hapo pasi na fahamu!
Alikuwa tayari amesachomoa bunduki yake. Akakimbia ila hakufika mbali akakutana na mvamizi aliyevalia barakoa. Mvamizi huyo hakuwa na kitu mkononi isipokuwa glovu zake nyeusi. Macho yake alikuwa ameyafunika na miwani yenye mshikio wa mpira na mgongoni ana begi.
“Weka mikono juu!” afisa akamwamuru kisha akateta na kifaa chake cha mawasiliano, “Nimemkamata mmoja wao! … nimemkamata mmoja wao!”
Alipomalizia kauli hiyo, akastaajabu kukitwa na kitu kichwani. Akadondoka hoi hajiwezi hata ukucha. Lakini je vipi kuhusu taarifa yake aliyoitoa kwa wenzake?
Habari mbaya ni kuwa, hakuna taarifa yoyote ile iliyokuwa inaenda wala kufika kwa yeyote yule! Kabla ya wavamizi hawa kufanya kazi yao, walishahakisha hilo jambo la mawasiliano ya walinzi linapatiwa ufumbuzi. Walipachika vifaa vinne vyeusi, ukubwa wa tofali la kuchoma, kwenye pande nne za dunia zizungukazo Ikulu.
Wakazipanga vema kwa kuzificha alafu wakaziwasha wakiwa tayari wameingia eneoni. Vifaa hivyo vilikuwa vinazalisha nishati kali sana mithili ya ‘radioactive’ ambayo ilikuwa na uwezo wa kupumbazisha ama kuchelewesha jitahada za mwasiliano ndani ya eneo husika.
Na kutokana na kuzalisha nishati hiyo kali, haikuweza kudumu kwa muda mrefu. Hukaa kwa nusu saa tu kabla ya kuzima na kufanya mawasiliano kurudi kwenye hali yake ya awali baada ya dakika tano.
Basi dakika zikaendelea kuyoyoma na kuyoyoma. Na sasa zikiwa zimebakia dakika mbili tu kwa vile vifaa vya mawasiliano kuzima lakini bado haja ya tukio ikiwa bado haijamalizika.
“We have a few minutes!” alitoa tahadhari mmoja wao. Walikuwa wameshashika korido wakielekea chumba walichoamini watamkuta mlengwa wao.
Mara ghafla mbele wakatokea wanaume wawili walinzi, afisa wa usalama. Katika hali hiyo hiyo ya ghafla, mmoja wa wavamizi akachojoa visu vitatu nyuma ya mgongo wake na akavitupa kwa utaalamu wa hali ya juu, vikawakita wale walinzi na kuwadondosha chini.
Haraka wakajongea chumba wakihisicho ndicho chenyewe, kufungua hawakukuta mtu!
Ti ti ti ti ti ti! ‘Alarm’ ikalia kutaarifu vifaa vya kuminya taarifa vimezima! Hivyo basi wakawa na dakika tano tu za kutoka na kutokomea hapo kabla ujumbe wa uvamizi haujawafikia wahusika, aidha kwa mfumo sauti au mfumo picha wa kamera za CCTV.
“We have to go!” mmoja akasisitizia.
“No! We aren’t going anywhere till we finish this!” sauti nyingine ikasema ikiwa na mamlaka ndani yake. Ilikuwa ni sauti ya Denmark.
“He is not here!” sauti nyingine ikatahadharisha. “Just let’s go!”
“He must be here,” Denmark akafoka. “Its whether we get him or we die in here! Let’s search!”
Kiongozi alishasema, hakukuwa na kupinga. Agizo likabebwa na utekelezaji ukaanza mara moja. Wanaume hao wakaanza kupekua huku na kule.
Na hilo ndilo lilikuwa kosa lao kubwa, hawakuwa wanajua haswa Raisi yupo wapi. Taarifa ya kuwa yupo Dar es salaam haikutosha kudhihirisha kuwa atakuwa Ikulu.
Dakika tano zikapita. Mawasiliano yakaanza kurejea. Maafisa wa usalama waliomo ndani ya jengo wakaanza kupata taarifa kadha wa kadha. Japo zilikuja kwa kasi, walitambua kuwa hali si shwari. Na wale wanaohusika na kuendesha mitambo ya CCTV wakaanza kuona taswira mbalimbali viooni.
Sasa taarifa rasmi ikawa wazi kuwa ngome ipo chini ya uvamizi!
Katikati ya taharuki hiyo, king’ora kikasikika kikilia. King’ora hicho kilifika kwenye sikio la kila mtu aliyekuwapo mule ndani ya jengo. Na hali isiwe tenge, king’ora hicho ndiyo kikazidi kuwatia watu vimuhemuhe kupita kiasi kwani kilimaanisha Raisi alikuwa anarejea jengoni.
Kwenye jengo ambalo lilikuwa na wavamizi!
Basi taarifa zikazuka, na Afisa aliyekuwa anahusika na Ulinzi jumla wa Ikulu, bwana Kulanga Hassan, akawapasha wale maafisa wanaokuja na Raisi ya kuwa wasitishe zoezi lao haraka mno na Raisi apewe ulinzi maradufu maana wapo chini ya uvamizi.
Na wakati wao wakifanya maamuzi hayo, wale mabwana wavamizi, wakaona sasa hiyo ndiyo ilikuwa nafasi adhimu ya wao kumaliza kazi. Ilikuwa ni lazima Raisi auawe! Sasa wameshapata uhakika kuwa yupo ndani ya eneo la karibu.
“Mwingize Raisi ndani … narudia, mwingize Raisi ndani. Huko nje si salama. Fanya hivyo haraka iwezekanavyo!” amri ilisikika kwenye masikio ya maafisa waliomo msafarani.
Na punde baada yake, afisa aliyeitoa amri hiyo akavunjwa shingo na wavamizi baada ya kazi yake kuisha. Basi mara punde, gari limbebealo Raisi likiwa limeongozana na magari mengine, likazama ndani.
“Niliwaambia msimwingize ndani!” bwana Kulanga akafoka. “Ndani tumevamiwa, narudia ndani tumevamiwa!”
Ilikuwa ‘too late’ wanasema wazungu. Raisi alikuwa ameshazama eneoni. Kitendo tu cha bwana Kulanga kumaliza kuongea, umeme ukakatika! Eneo lote likawa giza kana kwamba ni chini ya handaki.
Hapa sasa wale wavamizi wakawa mithili ya majini!
Basi katika hali hiyo ya giza na purukushani, maafisa usalama wakawa wanawasiliana na jitihada zao kubwa zikiwa ni kwenye kurejesha kwanza umeme ndani ya eneo. Nuru ilikuwa muhimu sana kwa wakati kama huo.
Lakini papo hapo wawe pia wanawasiliana kwa ajili ya kumdhibiti adui. Ila shida inakuja wapi? Utamdhibitije mtu usiyemwona? Mtu usiyejua yupo wapi?
Kurunzi kubwa zikawashwa na kumulika huku na kule, ila Ikulu ina eneo kubwa, bado haikutosha kutoa kile kinachohitajika haswa. Kwahiyo basi kwasababu hapa mlengwa mkubwa alikuwa ni Raisi, basi afisa wa usalama wakamzingira kumhakikishia usalama.
Wakati huo wengine wakiwa wanachakarika, aidha kwa kumtafuta adui ama kutafuta mwanga, wao wakawa wanahakikisha mkuu huyo wa nchi yupo kwenye mazingira swalama kabisa.
Ukapita muda kidogo. Bado purukushani zilikuwa zinaendelea, zavuma, hapa na pale. Katikati ya purukushaniyo, mara sauti ikasikika kwenye vitega sauti vya maafisa wa usalama ikionya,
“Hakuna kupokea amri kutoka kwa mwingine yoyote isipokuwa kwa mkuu peke yake …. Narudia amri, maagizo hutoka kwa Kulanga pekee … Kulanga pekee!”
Sauti hiyo ikakata. Zikapita kama dakika nne, mara sauti ya Kulanga ikavuma, “Mwingizeni Raisi kwenye chumba cha dharura. Haraka, chumba cha dharura!”
Basi baada ya amri hiyo, maafisa usalama nane wakiwa wanamziba Raisi wakaongozana naye mpaka chumba cha tatu ndani ya jengo Ikulu ambapo walimfungia Raisi humo na wakabaki maafisa watatu ndani yake, na watano kwa nje.
“Raisi yupo ndani? Raisi yupo ndani?” sauti ikauliza kwenye vitega sauti.
“Ndio, mkuu. Raisi yupo ndani. Narudia tena, Raisi yupo ndani.”
“Vizuri!”
Sauti ikakata na kisha kuwa kimya kwa wale maafisa waliokuwa beneti na Raisi, na hata wale ambao wamekaa nje mlangoni.
Lakini huko upande wa pili, mambo hayakuwa mambo. Watu walikuwa wanauawa kwa bunduki zenye viwamba vya kumezea sauti. Damu zilikuwa zinamwagwa kana kwamba jinamizi lenye nguvu pagani limeshuka kwenye uso wa dunia. Maiti zilikuwa mahali kadha wa kadha na ubaya ni kwamba hakuna mtu aliyekuwa anafahamu wauaji wapo upande upi wa dunia!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walikuwa si watu wa kutuama. Walitumia paa, walitumia silaha ndogo ndogo zisizo na madhara ya sauti. Walitumia maarifa na ujuzi wao kwa hali iliyotukuka kabisa. Ilikuwa inashangaza kwa namna ambavyo watu wachache walivyokuwa wanasumbua wale walio wengi.
Mpaka ‘backup’ iliyoombwa kuja kutoa msaada iwasili, basi uharibifu mkubwa utakuwa umetokea hapa.
“Afisa afisa …. afisa afisa…” bwana mmoja alibweka. “Taa zimezimwa zote, imebaki moja tu! Zimezimwa zote imebaki moja tu!” Taarifa ikatolewa na kusambazwa. Kurunzi zote zilikuwa zimezimwa kwa kupasuliwa na watu ambao hawakuwa wanaonekana.
Sasa ilikuwa imebaki kurunzi moja tu iliyo kubwa! Zingine zilikuwa zimegeuzwa kuwa ‘skrepa’ kwa kutobolewa na vifaa vidogo vya vyuma vyenye ncha kali mduara.
Hakuna aliyewaona watu waliotupa vifaa hivyo. Na kwa namna hiyohiyo ndivyo ambavyo watu walikuwa wanauawa. Wengi wao walikuwa wanakutwa wakiwa wametobolewa vifua, shingo au vichwa vyao kwa vifaa vyenye sumu kali iliyokausha miili ya wahusika kwa haraka mno.
“Afisa … Afisa!” sauti ikaita. “Afisa Kulanga amekutwa ameuawa na kupoa … narudia, amekutwa akiwa ameuawa na kupoa!”
Habari hizi zikazidi kuwachanganya maafisa. Lakini zaidi kuwatia hofu!
Mara ya mwisho Kulanga anaonekana ilikuwa ni ndani ya chumba cha kuangazia taswira za CCTV. Huko alikuwa na wataalamu wanne wakiwa wana ‘monitor’ mipango ya kuhakikisha jengo zima linakuwa linaangazwa.
Lakini muda mfupi kabla ya Kulanga kuuawa, kamera zilianza kupoteza mwelekeo. Zilianza kugomagoma na aidha hata kurudia picha. Na kabla tatizo halijafanyiwa kazi, mara kamera zikakaa vema. Kumbe ulikuwa ni mchezo wa mapumbazo.
Ulikuwa ni mchezo wa ulaghai! Na kweli mtegwaji akazama anapotakiwa kuzama.
Ni hivi, wakati video hizo zasumbua, ‘attention’ za watu zilihama. Macho na masikio yao yalikuwa yanaangazia kwenye video na namna ya kukabili tatizo. Kumbe basi mlango unafunguliwa! Hawakujua mlango ulifunguliwaje, kwa kutumia nini, ila wanakuja kutahamaki kuna mtu mlangoni.
Hawajafanya jambo, wakaona vitu vipo hewani, navyo hawakuwa wanajua ni vitu gani, ila wakaja kuvijua baada ya kutua kwenye miili yao. Vilikuwa ni vyuma vyenye ncha na sumu! Japo vyuma hivyo vilitupwa vingi, havikumgusa Kulanga isipokuwa tu kuuchanja mkono wake wa kuume uliobebelea silaha, hivyo akadondosha silaha yake na kuwa mtupu!
Hapo wenzake wote wakiwa tayari wamehamia ulimwengu wa wafu. Walikuwa tayari wamehudumiwa na zile silaha ipasavyo.
“Now we are going to do it by my rules if you want to live, officer,” sauti ya mvamizi ikaruruma. Bwana Kualnga kabla hajataka kuleta ubishi, akatazama mkono wake uliochanjwa. Ulishaanza kubadili rangi kuwa wa zambarau!
***
Afisa usalama wakatazamana. Habari ya kuwa Afisa Kulanga amekutwa mfu iliwatibua akili. Hapa wakapata shaka, mmoja akagonga mlango na kuuliza kama waliomo ndani wako salama. Hawakupata majibu!
Wakagonga zaidi na zaidi, bado kulikuwa kimya. Na kwasababu basi ya kuimarisha usalama, wale maafisa waliokuwemo ndani walikuwa wameufunga vema mlango. Kumbuka hiki kilikuwa ni chumba cha dharura endapo hatari itajiri ndani ya Ikulu hivyo kilikuwa kimesanifiwa katika namna ya ulinzi.
Mlango ulikuwa mzito na makufuli yake yalikuwa kana kwamba vile visanduku vihifadhivyo vitu vya thamani. Si ya kuvunja kwa wepesi hata kidogo.
Basi mabwana hawa, ambao tayari wameshahisi mambo hayako sawa, wakaanza kuhangaikia mlango, na huku wakitoa taarifa juu ya hali waliyomo ili wapate msaada.
***
Ilikuwa ni muda mfupi sasa tangu waone kazi huenda ikawa imekamilika. Basi wakawasiliana na kupanga kutoka ndani ya eneo la Ikulu haraka iwezekanavyo.
Kila mmoja akiwa kwenye ‘angle’ yake wakachoropoka na kukutania upande wa mashariki ya Ikulu. Muda huo sasa vikawa vinaingia vikosi vingine vya wanajeshi na hata maafisa wengine wa usalama.
Wavamizi walipoukaribia ukuta, wakaanza kuchumpa kujikuta nje dhidi ya ukuta mkubwa wa Ikulu walioufanya watakavyo. Wakiwa wamebakia wawili ndani ya eneo la Ikulu, wakaonekana!
Wanajeshi watatu waliokuwa wamebebelea bunduki mikononi, wakawaonyeshea silaha na kuanza kuwafyatulia risasi. Risasi zikaruka kama kumi hivi, na miongonizo zikafanikiwa kumwangusha mmoja wa wavamizi wakati mmoja akifanikiwa kuchumpia nje.
Ila naye alikuwa amejeruhiwa! Alikuwa anakimbia akivuja damu.
Wakaliendea gari lao na kujipaki upesi. Kuwasha gari, halikuwaka! Wakawasha na kuwasha. Bado hakukuwa na amfanikio. Ilikuwa ni hatari mno kubakia hapo kwa usalama wao. Eneo hilo lilikuwa limechafukwa. Lilikuwa ni eneo ambalo lipo ‘busy’ kuliko eneo lolote lile nchini kwa muda huo.
“What’s wrong!” akauliza Denmark, sauti yake ilimtambulisha. Alikuwa anauliza kana kwamba kuna mtu anayejua kinachoendelea hapo ukizingatia yeye ndiye alikuwa dereva.
Alijitahidi sana kuwasha gari pasipo mafanikio. Walipoona wanapoteza tu muda hapo, wakashuka. Kabla hawajaenda popote, wakawa wamezingirwa na watu watatu waliovalia barakoa na kubebelea silaha za moto. Wakapewa na amri ya kunyoosha mikono juu upesi!
Lakini hapahapa, tena ikiwa ni kama sekunde kadhaa tu toka wavamizi wawekwe chini ya ulinzi, vikasikika vishindo vya watu! Mara, “Wale pale!”
Risasi zikaanza kutupwa kwa fujo kuwalenga wavamizi pamoja na wale waliowaweka wavamizi chini ya ulinzi!
Basi hapa ndiyo ikawa salama ya wavamizi. Kushambuliwa kwa pamoja na wale waliokuwa wamewaweka chini ya ulinzi kuliwafanya wote watafute upenyo wa kuokoa maisha yao. Kwahiyo basi wakajikuta wakitawanyika huku na kule.
Wakajikuta wote wakiwa watuhumiwa na wahanga wa risasi zilizokuwa zinamwagwa kama njugu, baada ya kama dakika tano mvamizi mmoja akawa yupo chini kwa kushindiliwa risasi, yule aliyekuwa amejeruhiwa wakati wanafanya jitihada za kuuvuka ukuta wa Ikulu. Wengine wawili wakawa wapo mbioni kutafuta usafiri mwingine wa ziada kuwatoa eneo la hatari.
Na wakati huo wakipambana kwa kurudisha majibu ya risasi walizokuwa wanarushiwa na wale wanajeshi waokozi.
Vita ilikuwa si ndogo. Wanajeshi waokozi walikuwa wengi na hivyo basi mashambulizi yao kuwa makubwa. Kwa muda wote huu wa mashambulizi, eneo lililo karibu la Ikulu lilikuwa limesimama kwa muda. Taharuki ilikuwa imetawala, hofu, vilio na watu kupatwa maruhani!
Eneo hili liligeuzwa kuwa uwanja wa vita ndani ya muda mfupi. Kwa watu wa nchi hii ikawa jambo la kushtusha sana, na habari hizi zikasambaa na kupamba moto huko kwenye mitandao ya jamii na kutengeneza hamu kubwa ya watu kutaka kujua kinachoendelea.
Basi wale wavamizi, wawili waliokuwa wamebaki hai, wakakimbilia baharini na kupoka boti ndogo ya mvuvi. Wakamteka mwenye nayo na kumweka chini ya ulinzi kisha wakawasha mashine na kutimka kuyakata mawimbi.
Muda mfupi kabla hawajatokomea kuacha ‘war zone’, boti zingine mbili, kubwa kuliko ya wavamizi, zikajiri zikiwa zinawafukuza kwa kasi. Mwendo wa boti hizo ulikuwa mkubwa sana, zilikuwa za kisasa na za kivita. Haikuhitaji ufahamu mkubwa kutambua kuwa zilikuwa za jeshi la wana maji.
Mbali na kuwafukuza wavamizi, walikuwa wakiwatupia risasi za moto kuwanyima nafasi ya kupanga mashambulizi ama kutimiza adhma ya kutoroka japokuwa risasi nyingi zilizama majini kuliko kudhuru.
Ndani ya boti hizo kulikuwa kuna kama wanajeshi kumi na mbili, sita kwenye kila mojawapo! Kulikuwa kuna madereva na watu waliobaki wakifanya kazi za ushambulizi. Macho na akili zao zilikuwa zinafanya kazi, huenda, kwa hatua yao ya juu kabisa. Lengo hapa lilikuwa ni kuhakikisha wavamizi hawafanikiwi kuponyoka mkono wa dola.
Basi wakazidi kuwafukuzia na kuwafukuzia. Na kwakuwa boti zao zilikuwa za kisasa zaidi, zilikata mawimbi na kupambana na nguvu ya bahari inavyotakiwa hivyo wakazidi kuwasogelea walengwa wao. Zaidi … zaidi … na zaidi!
Mara …
“Acha kufyatua! Acha kufyatua!” amri ilisikika toka kwa mkubwa wa kikosi, wakiwa sasa wameshaisogelea kwa ukaribu mno boti ya wavamizi.
Ajabu ni kwamba, boti hiyo ya wavamizi ilikuwa bado yayoyoma, mashine yafanya kazi, ila ndani ni kama vile kulikuwa na mtu ambaye hakuwa anatikisika, mtu kama sanamu!
Basi wanajeshi walipogundua hilo wakapatwa na kiwewe. Walipoangaza vema, wakagundua mtu huyo alikuwa amekufa. Na hata hakuwa mvamizi bali mvuvi tu. Hapa wakajita, japo walifanya jitihada, bado wavamizi walikuwa wametoroka!
“Huenda tukawa tumewaua!” Hoja hii kidogo ikaleta mashiko, lakini ikawapunguziia machungu wanajeshi wale dhidi ya kuonekana wamefanya kazi ya kutwanga maji kinuni.
Ila kwa kamanda wa kikosi bado hakuwa ameridhia na hili.
“Tafuteni miili hiyo mpaka pale itakapopatikana. Kinyume na hapo, tutakuwa tumefanya kazi ya kukimbiza pepo.”
Basi wakaanza kurandaranda huku na kule huku na kule kutafuta ushahidi wa miili kuthibitisha kuwa wamefanikiwa kuwamaliza wavamizi. Hawakuambulia chochote kwa masaa mawili.
“Wametoroka,” akasema kamanda wa kikosi. “Hata boti lao halina viashiria vyovyote mbali na huyu mvuvi waliyemuua!”
Habari hizi zikawa za simanzi. Punde, mwanajeshi mmoja akamwita kamanda na kumwambia kuna jambo wanahitaji alitupie macho. Basi kamanda akaitikia wito na kwenda mpaka kwenye kachumba kadogo ka boti hii ya kisasa ambayo nchi ilipatiwa kama msaada toka nchi zilizokwisha endelea. Kwenye kachumba hako kulikuwa kuna mifumo na mashine ya kusaidia mawasiliano. Kilikuwa ndiyo sehemu kitovu ya kupokea na kutuma mawasiliano ndani na hata nje ya boti ikiwa na uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake hata maeneo ya mbali na yenye ufinyu wa mtandao.
Humo kulikuwa na watu wawili, mmoja wao alimwelekezea kamanda kwenye ‘screen’ ya ukubwa wa wastani iliyokuwa imepachikwa ukutani akamwambia,
“Wakati kurunzi inamulika mara ya kwanza, inaonyesha kulikuwa na watu. Unaweza ukawaona kwa mbali …”
Hapa kamanda akafinya macho yake kutazama.
“Lakini baada ya boti kukwepa kurunzi kwa muda wa dakika moja tu, hawakuonekana tena!” mwanajeshi alitoa maelezo kamanda akitazama kwa umakini.
“Ebu rudisha hiyo video nyuma,” kamanda akaagiza. Video iliporejeshwa, akaitazama kwa ukaribu zaidi. Hapa akagundua jambo. Si kwamba wavamizi walikuwa wamepotea baada ya kurunzi la boti yao kwenda kombo, bali watu wao walitoroka mapema zaidi.
Walikuwa wamechezewa akili. Na muda wote ule wakidhani wanawakimbiza wavamizi, walikuwa tayari wamejitosa kwenye maji wakiacha nyavu na vifaa vya mvuvi pamoja pia na mwili wake katika namna kuwalaghai kuwa bado wapo botini.
Hapa kamanda akajiona mjinga sana. Ni kwa namna gani walikuwa wamefanywa kuwa watoto tena karibia na mbele ya macho yao. Lakini pia akawaza, watu hao, yaani wavamizi, watakuwa wameelekea pande ipi ya dunia, nchi kavu ama bado wapo majini?
Taarifa ikasambaa kwa vikosi vingine maeneo mbalimbali kufanya doria ya kuhakikisha wavamizi hao hawatoki salama kwenye pwani yote hii ya Afrika ya Mashariki.
Basi punde kidogo baada ya kufanya hivyo, boti ikatikisika kwanguvu kana kwamba imekumbwa na wimbi kali! Kufumba na kufumbua, ‘alarm’ kali ya hatari ikaanza kulia!
Duuiiiil! Duuiiil! Duuuiiil! Duuuiil! Duiiiil!
Haraka wahusika wakatazama kwenye ‘boat operation system’ kung’amua nini tatizo. Ajabu machoni mwao, wakaona boti yazama! Kando kidogo ya mashine ya kukatia maji kulikuwa na tundu kubwa ambalo laingiza maji ndani kwa fujo haswaa!
Hawajakaa vema, wakasikia milio ya risasi. Kutazama yatokea wapi, wakagundua ni kutoka kwenye boti mwenza. Risasi zilikuwa zinarushwa kwa fujo haswa. Zinapasua vioo na kutoboatoboa boti kuwa chujio.
Risasi hizi zikawanyima kabisaa wanajeshi hawa fursa ya kuikomboa boti yao inayozama kwa kuwafanyia wazingatie zaidi uhai wao dhidi ya ncha za risasi zilizokuwa zinarindima.
Mpaka zinakoma, boti ilikuwa imeshazama nusu na robo. Sehemu yote ya nyuma ilikuwa ndani ya maji. Boti yabinuka juu! Boti ile mwenza ikatokomea kama kishada.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment