Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

UHASAMA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : RAMADHANI K KAONEKA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Uhasama

    Sehemu Ya Kwanza (1)









    Ni kawaida kila ifikapo saa kumi jioni, Goda ni lazima aende katika shule anayosoma mtoto wa bosi wake Mzee Mheshimiwa Anaeitwa Hemedy kwenda kumchukua kutoka shule kumpeleka nyumbani hapo. Sio kwamba hakukuwa na gari la shule, bali Mzee Mheshimiwa alipenda mwanae huyo wa pekee apelekwe na kurudushwa na gari lake binafsi.



    Goda alikuwa ndani ya gari akielekea katika shule anayosoma mtoto wa bosi wake huku akitingisha kichwa chake kufuatisha mdundo wa muziki uliokuwa unapigwa katika radio ya hiyo gari. Alifika katika shule hiyo ya English Medium ikiwa bado kama dakika thelathini ili wanafunzi watoke, Alibadilisha Muziki uliokuwa unakita katika spika za gari na kuweka muziki mwengine ilikuzidi kupata mori wa kusubiri muda wa kutoka wanafunzi wa shule hiyo.



    Iliskika kengele iliyo kuwa inapigwa ndani ya shule hiyo kuashiria kuwa muda wa kutoka wanafunzi umefika,Goda aliangaza macho yake kuangalia getini ili aweze kumuona mtoto wa bosi wake atakapotoka, Baada kama dakika tano kupita alianza kuwaona wanafunzi wakitoka ndani ya shule hiyo, alizidi kuangaza macho yake getini lakini hakuweza kumuona mtoto wa bosi wake mwanzo alidhani huenda ikawa bado yupo ndani ya shule lakini kadri muda unavyozid kwenda ndivyo wanafunzi walivyozidi kupungua, wengiwao walipanda katika gari la shule na wengine walipanda katika magari yao binafsi.



    Hemedy Hakuwa na kawaida kuchelewa kutoka ndani ya shule hiyo ila siku hiyo alichelewa mpaka akampa wasiwasi Goda, Kuna wazo likamjia kwamba huenda ikawa amepanda katika gari la shule ila wazo hilo hakulipa nafasi sana kwasababu alishawahi kupanda gari ya shule kutokana na marafiki zake wote hupanda gari ya shule, alipo rudishwa nyumbani kwao na gari ya shule Mzee Mheshimiwa alimfokea kwa hasira kwa kitendo hicho cha kupanda gari ya shule, huku akimuacha Goda anamsubiria shule bila mafanikio yoyote, yeye alitaka mwanae apelekwe na kurudishwa na gari lake na sio gari la shule, kesho yake alikwenda mpaka shule na kuonana na mwalimu mlezi wa wanafunzi na kumuambia kuwa yeye mwanae hataki apande gari ya shule, Kuanzia siku hiyo Hemedy alipooneka amependa gari ya shule basi alishushwa na kupelekwa kwenye gari iliokuja kumchukua.



    Goda alizidi kuwa na wasiwasi baada ya kuona magari yote yameshaondoka halafu bado hajamuona Hemedy akitoka, akapata wazo kwamba ashuke kwenye gari ili aingie ndani ya shule akaulize kunanini mpaka Hemedy asimuone akitoka nje ya shule. Akashika kitasa cha mlango wa gari na mkono wa kulia ili ashuke chini ila ghalfla akahisi ubaridi katika mkono wake wa kushoto uliokuwa bado umeshikilia usukani, Ubaridi huo ulioanzia kwenye mkono wake ukasafiri mpaka kwenye ubongo wake akijaribu kuutasfiri ni wa nini ila ubongo wake ukakataa kabisa kuutasfiri ubaridi huo ni wa nini.



    Ikabidi ageuze shingo yake kwa kasi ya umeme na ndipo alipo pigwa na butwaa, hakuelewa Hemedy ameingia vipi ndani ya gari hadi yeye asimsikie licha ya hivyo pia hakuelewa Hemedy amepitia kwenye malango upi ikiwa yeye macho yake yote yalikuwa kwenye geti la shule na hukuweza kumuona akitoka kwenye geti la shule.



    "We mtoto umeingiaje humu kwenye gari? Na mbona sijakuona ukitoka kwenye geti la shule na wanafunzi wenzako?" Goda alimuliza kwa mshangao uliochanganyikana na hofu ndani yake, alipotupa macho yake kwenye mkono wake wa kushoto aliuona mkono wa Hemedy ukiwa upo juu ya mkono wake, ndipo hapo alipopata picha kuwa ule ubaridi alio uhisi ulikuwa umetoka kwenye mkon wa Hemedy.



    "Hahahaahah kumbe anko muoga hivyo? Mimi sinimeingia muda mrefu na kukuona wewe unashangaa huko nje, ulikuwa unaangalia nini huko hadi mimi naingia hujaniona?Alisema Hemedy huku akiwa anacheka.



    "Kwanza kabla ya yote umepitia wapi mbona sijakuona ukitoka na getini? Aliongea Goda huku akimuangalia mtoto huyo kwa macho ya kuuliza.



    "Aaaah!! Acha zako bwana anko kwahiyo hukuniona pale getini wakati natoka?

    "Sikiliza wewe mtoto usinifanye mimi mtoto mwenzako embu niambie umepitia wapi maana mimi nimeangalia vizuri kwa macho yangu sijakuona ukitoka na getini"



    "Hahahahah Subiri nikuambie mimi wakati na nataka kutoka nje nilikuona unaangaza macho yako pale getini, nikaona nikufanyie suprise, nikarudi hadi kwenye vyoo ambavyo vipo huko nyuma ya shule, nikaangalia huku na huku sikuona mtu nikaupanda ukuta wa fensi ya shule hadi juu kwa kutumia matofali yaliyo kuwa pembeni kwa ajali ya kujengea vyoo, nilipofika juu kabisa nikaruka hadi nje ya fensi ndo nikazunguka hadi huku barabarani nikaja hadi hapa kwenye gari nikafungua mlango wewe bado unashangaa tu huko nje, nikakaa nakuangalia tu hadi ulipo taka kufungua mlango ndo nikashtua kidogo tu umeshtuukaa" Alimaliza kumuhadithia huku akicheka.



    Goda alibaki ametumbua macho yake kumuangalia mtoto huyo ambae umri wake ni mdogo wa miaka kumi na mbili tu, hakuamini kwamba mtoto kama huyo alielelewa katika maisha ha raha na starehe anaweza akafanya mambo kama hayo, alimuangalia akiwa bado haamini, macho yake yakaganda kwenye mkono wa kulia wa Hemedy uliokuwa na mchubuko uliotoa damu kwa mbali.



    "Nahapo kwenye mkono umefanya nini? Alimuuliza huku akimuonyeshea na kidole chake sehemu iliokuwa na mchubuko.



    Hapo ndipo Hemedy alipo angalia mkono wake na kukuta kweli ulikuwa unatoka damu kwa mbali, alipo acha kuangalia mkono wake akamuangalia Goda kwa macho ya ‘nitafanya' nini maana alielewa mama yake akimuona katika hali hiyo lazima atamuhoji na kupelekea kufokewa na yeye hakupenda hayo yote yatokee.



    "We mtoto sininakuuliza wewe mbona hunijibu unanitumbulia tu mimacho yako"Goda alimuuliza huku akiwa bado anamuangalia machoni.



    "Itakuwa nipale nilipo paramia ukuta" Hemedy alijibu kwa unyonge na uwoga uliochanganyikana ndani yake.



    "Kwani hauna kitambara hapo ujifute hiyo damu?



    Hapo Hemedy akatoa tabasamu la furaha, akachukua kitambara chake ambacho anakiweka mfuko wa nyuma, akajifuta damu yote ila mchubuko haukuweza kuondoka, Baada ya kumaliza kujifuta damu akamuangalia Goda usoni, Goda akamuonyeshea tabasamu tu na kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kawaida.



    "Ila siku nyengine usirudie tena upumbavu wako, wewe unadhani kama ingekuwa umeoneka na mwalimu unaruka ukuta siungeadhibiwa na taarifa zinge fika kwa baba yako nae pia angekuadhibu??



    "Nimekuelewa anko naomba unisamehe sirudii tena naomba halafu usimwambie baba"Alisema Hemedy huku akimuangalia Goda kwa macho ya huruma, Goda akaachia tabasamu na kumnyooshea dole gumba.



    Goda aliendesha gari huku akipiga stori na mtoto huyu wa bosi wake ambae yeye alimchukulia kama mdogo wake tu.



    Baada ya kufika nje ya geti la nyumba yao, Goda alipiga honi mara mbili ndipo geti likafunguliwa na mlinzi aliekuwa kwa ndani.



    Aliendesha gari hadi kwenye paking ya humo ndani na kuliweka gari katika sehemu husika, Alianza kushuka Goda na kuafuatia Hemedy wote wakaelekea ndani ya nyumba hiyo ya kifahari ilio ya gorofa moja.



    Wakaingia hadi sebleni na kumkuta Mwanamke wa makamo amekaa kwenye sofa moja wapo yaliyojazana hapo sebleni. Hemedy baada ya kumuona mwanamke huyo alitupa begi lake la shule chini na kuanzakumkimbila mwanamke huyo ambae hadi muda huo alikuwa ameachia tabasamu usoni kwake. Hemedy alienda na kumkumbatia mwanamke huyo ambae na yeye alitanua mikono ya kumpokea Hemedy.



    "Good evening my mom"



    "Mwanangu nimeshakuambia mimi mama yako sijasoma, sijui kingereza sasa mbona unaniabisha mama ako?Mwanamke huyo alimwambia Hemedy huku akitabasamu.



    "Hahahah Mama nawe sasa kwanini hujasoma? Hemedy aliuliza.



    "Nyie mliopata bahati ya kusoma someni tu kipindi hichi sio sawa na kile cha zamani, ilikuwa mtoto wakike akifika darasa la saba tu haendelei tena na shule eti kwavile atakuja kuolewa na kuwa mama wa nyumbani, basi ikawa tunaishia darasa la saba tu ila mimi nilikuwa nina akili sana sema ndo hivyo tu sikubahatika kuendelea na shule, yani zile akili potofu sijui walizitolea wapi wale wazee wa zamani?



    Baada ya kusalimiana na Mama yake, Hemedy alinyoosha hadi kwenye ngazi na kuzipanda kuelekea juu katika vyumba vya juu ya nyumaba hiyo ya gorofa, huko ndo kilipo chumba chake chakulala, huku nyuma akifuatiwa na Goda akija na begi la Hemedy alilolitupa mlangoni.



    “Hivi anko na wewe pia haukusoma eee? "



    “Kwanini umeniuliza hivyo anko?"



    “Mama sikasema kuwa nyie watu wa zamani hamkusoma?"



    “Hahahahah Anko wewe unamatatizo sana, Mama sikasema wanawake ndo walikuwa hawasomeshwi, halfu mimi sio mtu wa zamani"



    “Kwani wewe unamiaka mingapi anko?"



    “Mimi nina miaka ishirini na nne tu, embu acha kuongea sana vua ngua za shule twende kula, au wewe husikii njaa?" Hemedy alibadilisha nguo za shule na kuingia chooni kwenda na kuoga. Alivyotoka chooni alivalia track suti na jezi ya mpira, baada ya kumaliza kuvaa aliongozana na Goda kuelekea sebleni na kwaajili ya kwenda kula.



    Ilikuwa ni kawaida kwamba Goda alishajizoesha kutokula mpaka hemedy atakapo rudi shule ili ale pamoja na Hemedy. Wakati wanashuka kwenye ngazi kuelekea sebleni, Hemedy alisimama na Kumuangalia Goda kwa uso wa wasiwasi.



    “Vipi mbona umesimama halafu unaniangalia hivyo?"



    “Anko nakuomba usimwambie mama kama nimeruka ukuta shule" aliongea kwa unyonge akiwa bado macho yake ameyagandisha usoni kwa Goda. Hemedi aliogopa sana kufokea na mama yake ndo maana hadi sasa ana wasiwasi kitendo chake alichokifanya shule cha kuruka ukuta kinaweza kujulikana na wazazi wake. Goda alimtolea tu tabasamu na kumshika mkono kwenda nae sebleni.



    *******************************

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ohhhh my only boy how ar..... "



    “Aaa aaa!!! Dady kuanzia leo mimi sitaki kuongea tena kuongea kigereza hapa nyumbani"



    “Kwanini my boy?"



    “Mama hajui kingereza na mimi sitaki tena kuongea kingereza, kwanini hujampeleka kwenda kusoma au wewe hutaki mama akiongea kingereza?"



    “Hapana my son mama yako alikataa mwenyewe kwenda kusoma kingereza sasa na mimi sikutaka kumlazimisha, hata umulize mwenyewe atakuambia".



    Mazungumzo hayo yalifanywa na mtoto na baba yake, Majira hayo ya saa moja jioni ndio muda ambao Mzee Mheshimiwa ana rudi nyumbani kwake akitokea kazini. Mzee Mheshiwa alikuwa ni katika matajiri waliopo katika mji huo wa Tanga, anamiliki showroom ya magari na Sheli za mafuta zilizopo ndani ya mji huo wa Tanga. Mzee Mheshimiwa alipandisha ngazi hadi chumbani alipo ingia mke wake wake.



    “Za kazi mume wangu?"



    “Safi tu",Alijibu Mzee Mheshimiwa na Kuuliza“sijui za hapa nyumbani"



    “Hapa nyumbani tunamshukuru mungu ni wazima".



    Familia ya Mzee Mheshimiwa ilikuwa ni familia yenye furaha kila siku na walimuomba mungu furaha iyendelee kila siku, Mzee Mheshimiwa alifanya kila awezalo ilamradi familia yake iwe na furaha, Halkadhalka pia Mama Hemedy alifanya kila awezalo ili familia yake iwe na furaha.



    Kwakila mwenye mafanikio hakosi maadui na huwezi kuishi na furaha siku zote kwasababu kuna watu hawataipenda furaha uliyo nayo watahakikisha wafanye kila wawezalo ilimradi tu usiwe na furaha.



    Mzee Mheshimiwa alijiona ni mwenye furaha siku zote kila anapoangalia familia yake na mali zake. Hakujua kuwa kuna watu wanao angalia mafanikio yake kwa jicho la tatu, hawakupenda kumuona akiwa na mafanikio kiasi hicho, na walipanga kumfanyia UHASAMA yeye na familia yake na mali zake alizokuwa nazo.



    *****************************



    Majira ya usiku ya siku hiyo hiyo, upande wa pili kulikuwa na kikao kizito kilicho usisha watu watatu wenye mpango wa kumuondosha duniana Mzee Mheshimiwa na familia yake na kuchukua kila kilicho chake ili wajinufaishe wao, watu hawa ndiyo waliopanga kumfanyia UHASAMA Mzee Mheshimiwa.



    “Kama tulivyo panga kuwa tutamvamia usiku akiwa yupo na familia yake ilituweze kumsainisha mali zote halafu baada ya hapo tunaua yeye na na familia yake, au sivyo Mata"



    “Ni thawa kama itakuwa ndo hivyo ilimradi mpango wetu uwende thawa bathi hakuna shaka, ila thatha itabidi Mrutu wewe uthiende eneo la tukio kwathababu yule ni kaka yako anawedha akakujua" Mata hawezi kuongea vizuru kwasababu alikuwa na “Kilimi" kwenye “S" anaweka “Th" akitaka kusema “Sasa" basi atasema “Thatha na kadhalika pia kwenye “Z" anaweka Dh.



    “Hahahaha Mata bwana sasa hatakama akinijua atafanya nini wakati tutamuua hapo hapo?"Aliongea Mrutu kumshangaa Mata kwa maneno aliyo ya sema. Mrutu ni mdogo wake na Mzee Mheshimiwa, Wamezaliwa na Baba mmoja ila Mama mbalimbali.



    “Hatakama ila inabidi wewe uthionekane kwathababu yule ni ndugu yako unawedha ukaleta huruma halafu katika kadhi kama hii hakutakiwi mtu mwenye huruma, Ila wewe itabidi ubaki tu ndani ya gari ututhubirie, thithi tuna ingia ndani tunaua halafu tunatoka tunaondoka dhetu, au wewe unathemaje Moto?"



    “Yeah inabidi iwe hivyo"



    “Poa kama ndo mnavyotaka, sasa kwahiyo hii kazi tutaifanya wenyewe watatu?"



    “Nyie mthijali mimi kuna vijana nawajua ni watu wa kadhi kadhi, nitawaita watuthaidie hii kadhi"



    “Hao vijana wapo wangapi?"



    “Tuta chukua vijana wawili tu wanatosha, halafu nina waamini kwathababu nishawahi kufanya nao kadhi nyingi tu"



    “Sawa wewe inabidi uwasiliane nao sasa hivi uwapange kwamba kazi inaendaje na malipo yao ni shilingi ngapi, ili kazi ikishakwisha tusisumbuane". Moto alihitimisha kikao hicho kifupi kilichokuwa na mpango wa kufanya uhasama kwa Mzee Mheshimiwa.



    Baada ya kumaliza kikao hicho, waliondoka na kuhaidiana kuwa wakutane siku inayofuata ili waifanye kazi waliyoipanga.



    * * * *



    Siku iliyofuata. Nyumbani kwa Mzee Mheshimiwa 3:22 Usiku.

    Akiwa yupo na familia yake wakiwa wapo mezani wanapata chakula cha usiku. Mzee Mheshimiwa alikuwa ni binadamu kama binadamu wengine, hakuweza kujua kuwa siku hiyo kwake yeye na familia yake inaweza kuwa ni siku mbaya. Wahenga hawakukosea walipo sema “Usilo lijua ni sawa na usiku wa giza".



    Mzee Mheshimiwa hakujua kuwa usiku huu kwake unaweza kuwa ni wa giza, na sio yeye tu hata watu aliokuwa nao katika nyumba yake pia hakuweza kujua kuwa usiku wa siku hii unaweza kuwa ni wa giza.



    “Hivi baba wewe unasoma ili baadae ujekuwa nani katika huu ulimwengu?" Mzee Mheshimiwa alimuuliza mwanae Hemedy wakiwa wamemaliza kula chakula na wamekaa sebuleni. Ilikuwa ni kawaida yao kwamba wakimaliza kula chakula cha usiku wanakaa sebuleni kabla ya kwenda kulala na kuongea mawili matatu au kuangalia televisheni iliokuwepo hapo sebleni.



    “Mimi nataka kuwa mwanasheria" alijibu Hemedy.



    “Kwanini unataka kuwa mwanasheria?"



    “Nataka kutetea haki kwa wale wanaodhulumiwa mali zao na kwa wale wanao kwenda jela bila hatia kwa kusingiziwa kesi am........." Ghalfa macho yao wote waliyaelekeza mlangoni baada ya kusikia kishindo cha mlango ukiwa umefunguliwa kwa nguvu. Wakiwa bado wamepigwa na butwaa, waliingia wanaume wanne wawili wakiwa na bunduki mikononi na kuwaelekezea wao.





    “Hapo hapo mlipo, hakuna mtu yoyote kujigutha wala kufanya chochote kile tofauti na maelekedho yangu, nyote mnatakiwa kufuata kile ninachothema" Mata aliwatisha huku akiwa amewaelekezea bunduki. Mzee Mheshimiwa alikuwa katika hofu kuu kuliko wote waliokuwepo hapo japokuwa na wao pia walikuwa na hofu, hawakuzitambua sura hizo zilizo ingia humo ndani, sura zote zilikuwa ni ngeni kwenye macho yao.



    “Nyote pigeni magoti chini" Mzee Mheshimiwa hakuelewa watu hao wanataka kitu gani kwake, maana yeye akifikiria hakuwahi kuwa na UHASAMA na mtu yoyote yule katika ulimwengu huu, alichofikiria yeye kuwa huenda watu hao wanataka pesa na sio kitu kingine, akaamua kuyajaribu mawazo yake kwa kuwauliza wanachokitaka kuwa ndio hicho alicho fikiria yeye.



    “Mnataka nini jamani? Au kama mnataka pesa subirini nikazichukue zipo ndani nije niwape mtuach....."



    “Nyamadha wewe, nani aliekupa ruhutha ya kuongea? Thithi hatutaki petha tu, tunataka na nyaraka dhote dha mali dhako ulidhokuwa nadho ndipo tukuachie na familia yako". Licha ya kuwa Mzee Mheshimiwa anaipenda familia yake, pia alikuwa anazipenda maliza zake, hakutaka masihara linapokuja swala la pesa. Hata hivyo alilinganisha kati ya familia yake na mali zake,kipi bora kwa wakati huo, akafikiria akitoa mali zake zote jinsi atakavyokuwa fukara wa kutupwa akitanga tanga yeye na familia yake, atakavyoomba msaada kwa matajiri wenzake, mwanzo watamsaidia ila mwisho watamchoka, ndipo hapo sasa atakapo tamani kujiua, wazo la kutoa mali zake akaliweka kando kwanza.



    Akafikiria kifo kinafanana vipi? Ila akashindwa kupata jibu kwasababu hakuwahi kufa, hata hivyo pia akijifanya mbishi kuwa hataki kutoa mali zake ili kuokoa uhai wake na familia yake, watamuua na kuzichukua vilevile mali zake japokuwa sio zote, yote hayo yalipita ndani ya kichwa chake kwa haraka sana akitafuata uchambuzi kipi afanye kipi aache, akaona ni bora awape wanachokitaka kwasababu hata hivyo mali zinatafutwa.



    Akiwa bado anawaza, alishtushwa na sauti ya bunduki iliyopigwa kwenye bega la Goda, Goda aligugumia kwa maumivu kwa risasi iliyo ingia kwenye bega lake la kushoto.



    “Huyu tumemuonjesha tu, ukiendelea kutupotezea muda basi ujue tutafumua kichwa cha mke wako". Aliongea Moto huku akiwa na gadhabu, hapo ndipo Mzee Mheshimiwa alipo jua kuwa hakukuwa na utani kwenye suala hilo, aliinuka taratibu na kuongoza njia kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake akifuatiwa na Mata huku akiwa amemuelekezea bunduki kichwani, Mzee Mheshimiwa hakuwa na ujanja mwengine zaidi ya kufuata maelekezo anayopewa, sio kwamba hakuwa na bastola yake, alikuwa nayo ila kwa wakati huo hakuwa na ujanja wa kuichukua kwasababu alikuwa ameelekezewa bunduki kichwani mwake.



    Alipelekwa hadi chumbani kwake na kuuendea mokoba wake wenye nyaraka zote za mali zake, aliuchukua na kurudi nao hadi sebleni huku akiongozwa na Mata aliemuelekezea bunduki kichwani, alimuangalia mke wake jinsi anavyolia, alimuangalia mtoto wake jinsi atakavyo kwenda kuteseka kwa njaa, alifikiria mtoto wake atavyoenda kuacha shule kutokana kukosa pesa ya kumlipia ada, alifikiria jinsi mtoto wake atakavyo poteza malengo yake ya kuwa mwanasheria kama mwenyewe alivyopenda kujakuwa mwanasheria na kuwatetea wanyonge wanaodhulumiwa mali zao kama yeye anavyoenda kudhulumiwa muda si mrefu na watu hao yeye aliodhani kuwa ni majambazi, yote hayo yalipita ndani ya kichwa chake.



    Hakuwa na jinsi nyengine ya kufanya zaidi ya kufuata kile alichoambiwa, akapiga saini kuwa mali zote alizokuwa nazo kwa wakati huo sio zake na amekubali kuzitoa yeye mwenyewe, aliandika barua na kuweka saini huku akiiangalia familia yake kwa masikitiko sana, alitamani iwe ni ndoto halafu baada ya muda mfupi ainuke akute hakuja tokea kitu kama hicho, ila haikuweza kuwa ni ndoto bali ni tukio linalotokea “Live" huku yeye na familia yake wakishuhudia.



    Alipo maliza kuweka saini kila sehemu ya mali zake, aliwapa nyaraka zote, Mata alizipokea na kuanza kuzisoma moja baada ya nyengine, aliachia tabasamu la ushindi na kuwapa ishara wenzake kuwa kazi walioifanya imekamilika, Goda kipindi chote hicho yeye haikujulikana kuwa amekufa au bado ni mzima kwasababu alikuwa yupo chini amelala kimya bila kujitingisha.



    Mata aliyoonekana kuwa ndio kiongozi wao, alitoa ishara amabayo Mzee Mheshimiwa na watu wake hawakuiyelewa, walishtuka tu kuona wafanyakazi wao mmoja baada mwengine akianguka sakafuni na kutulia tuli, hapo ndipo Mzee Mheshimiwa alipoona kuwa mambo yamebadilika, haikuwa kama vile walivyo ahidiwa kuwa wakishatoa mali zote basi wataachiwa waende, kuja kushtuka alimuona mke wake na yeye akienda chini na kutulia tuli kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wake.



    Haikuwa picha nzuri kushuhudiwa na mtoto wake ambae hadi sasa anamiaka Kumi na mbili tu tangu aanze kuiyona hii dunia iliyojaa makatili kama hao ambao kwao kuua ni jambo dogo sana, kuua mtu kwao ni kama kuua mbu ndani ya chandarua, hadi sasa walibakia wawili tu ambao ni wazima yeye na mwanae mpendwa Hemedy, wakati yote yanatokea alikuwa amezibwa mdomo asiweze kupiga kelele, alishuhudia Anko wake akipigwa risasi ya bega na kuenda chini, alishuhudia wafanyakazi wao walivyopigwa risasi za vifua na kwenda chini mbaya zaidi alishuhudia mama yake mzazi akipigwa risasi ya shingo naye pia akiungana na wenzake akaenda chini, akajua baada ya hao kwenda chini basi ni zamu yao yeye na baba yake, alikuwa na umri mdogo hakuwa na ubavu wa kushindana nahao majitu aliyo ya fananisha na izrael mtoa roho za watu, ikiwa baba yake ameshindwa kushindana nao, vipi yeye mtoto mdogo ataweza kushindana na mijitu hiyo? Hakua na namna nyengine zaid ya kusubiri kifo chake.



    Bila kutarajia aliinuka ghalfa na kumfuata mke wake alie kuwa chini kwa wakati huo ameshikilia shingo yake akishindana na malaika mtoa roho almaarufu kama izrael, kabla hajamfikia mke wake, alihisi kama kuna ubaridi katika mbavu zake, alijaribu kuutafsiri ubaridi huo ni wa nini ila akshindwa kupata jibu sahihi, ila ghafla ubardi huo ukabadilika na kuwa umoto wenye maumivu ndani yake, akiwa bado hisia zake hazijampa jibu kuwa ni kitu gani hicho chenye ubaridi na umoto wenye maumivu, akaona asibitishe kwa macho yake mwenyewe kwa vile hisia zake hazija mpa jibu sashihi.



    Akayapeleka macho yake kwenye sehemu yenye ubaridi na umoto wenye maumivu, na kukuta damu zinatoka kwa wingi kwenye mbavu zake, hapo akajua kwamba hiyo ni risasi imepenya kwenye mabavu zake. Kabla hajakaa sawa alipigwa tena risasi ya kichwa na kufumuliwa ubongo wake, na yeye akawa ameungana na wenzake chini sakafuni, wakiwa tayari kwa maandalizi ya kupelekwa makaburini kwenye nyumba zao za milele. Walikuwa ni wafu tayari.



    “Mshtue MRUTU aweke gari sawa tuondoke kabla nzi hawaja kuja". Hayo ndo maneno ya mwisho kuyasikia kabla hajazimia, hakuna kitendo kilichomchanganya akili kama kuona Mama yake ameuliwa mbele yake na Baba yake pia ameuliwa mbele yake tena kwa kifo kibaya cha kupigwa risasi mbili moja ya mbavu, nyengine ya kichwa iliyo sababisha sakafu ichafuliwe na ubongo, akajikuta na yeye kimyakimya anapoteza fahamu bila kutarajia.



    “Tumemalidha twendeni thatha"



    “Na huyu mtoto tunamfanya nini?" aliuliza mmoja wapo katika hawa vijana wawili waliokodiwa.



    “Huyu kashakufa kwa mshtuko kwahiyo haina haja tena ya kummalizia, twenzetuni tusipoteze muda” Moto aliongea na kuwafanya wenzake waanze kutoka mmoja mmoja, hawakusahau mkoba uliokuwa na nyaraka za mali, walitoka nao pia.



    * * * *



    Baada ya nusu saa Hemedy aliinuka kutoka katika ulimwemu mwengine wa kupoteza fahamu, alishangaa kuona Baba, Mama na Wafanyakazi wengine wamelala sakafuni, kitu kilicho mchanganya zaidi baada ya kuona damu sakafuni, alijiuliza imekuaje tena watu wamelala na damu imesambaa sakafuni? Ndipo hapo tukio lililotokea nusu saa kabla lilipo jirudia kichwani mwake, aliinuka kwa haraka sana hadi walipo lala wazazi wake, alilia huku akijaribu kuwaamsha bila mafanikio yoyote, walikuwa wameshakufa alilijua hilo ila hakutaka kukubaliana nalo moja kwa moja, aliendelea kuwaamsha akidhani huenda ikawa kilio chake wanaweza kukisikia ila haikuwa kama alivyotaka iwe, ilikuwa ni kweli usiopingika kuwa wazazi wake wameshaonja umauti kama ilivyosemwa katika vitabu vya dini. “Kila nafsi itaonja umauti"



    Goda alihisi maumivu kwenye bega lake, ila hakuweza kujua maumivu hayo yametokana na nini, akajaribu kurudisha kumbukumbu zake nyuma ili aweze kukumbuka ni kitu gani kinachofanya bega lake liume maumivu ambayo hakuwahi kuyahisi kabla, ni kweli alijaribu kuunganisha tukio lililotokea muda si mrefu kabla hajapoteza fahamu iliyosababishwa na maumivu na kutokwa na damu nyingi kwenye bega, alikumbuka kuwa alikuwa wamekaa sebleni baada ya kumaliza kula, wakawa wanapiga stori, kabla stori hazija isha wakaingia wanaume wanne wakiwa wameshika bunduki, wakimlazimisha Bosi wake atoe nyaraka zote alizokuwa nazo, mwisho kabisa akashtuka amepigwa risasi ya bega, baada ya hapo hakuelewa ni nini kilicho endelea, akapoteza fahamu.



    Alifumbua macho yake taratibu baada ya kusikia sauti ya kilio, sauti hiyo aliijua kuwa ni ya Hemedy mtoto wa bosi wake, akajaribu kujiinua taratibu akiwa bado na maumivu yasio ya kawaida akiyahisi katika bega lake, alikaa kitako na kushuhudia mabosi zake na wafanyakazi wenzake wakiwa wamelala sakafuni, alielewa moja kwa moja kuwa hakukuwa na mzima hata mmoja kutokana na damu zilizotapakaa katika miili yao, akajivuta taratibu kutokana na maumivu aliyokuwa akiyahisi kwenye bega, na kamfanya atambae kama mtoto mdogo.



    Akaanzia kwa wafanyakazi wenzake kuskiiliza mapigo ya mioyo yao na kukuta wote walikuwa wameshakufa, akatupa macho yake kwa mabosi zake, picha aliyoiyona ilimuogopesha hata yeye baada ya kuona ubongo wa Bosi wake Mzee Mheshimiwa ukiwa upo nje, akajivuta tena hadi kwa mabosi zake, hakuwa na haja ya kuhakikisha kuwa wameshakufa kutokana na risasi walizopigwa, zilipigwa katika maeneo ambayo hata angewahi daktari wa aina gani asingeweza kuokoa maisha yao, Mama Hemedy alipigwa risasi ya shingo na Mzee Mheshimiwa alifumuliwa ubongo wake, walikuwa wameshakufa zamani.



    Alichofanya ni kumfuata Hemedy aliekuwa amezing'ang'ania maiti za wazazi wake akiwaamsha bila mafanikio yoyote, alilia kwa uchungu sana kilio ambacho hakuwahi kulia tangu azaliwe, Goda alimfuata na kumuondoa karibu na maiti za wazazi wake na kumpeleka pembeni huku akijaribu kumtuliza, Hemedy alikuwa na uchungu mkubwa sana, alilia kwa kuwapoteza wazazi wake wote wawili kwa wakati mmoja, ali huzunika, ali sikitika, kufumba na kufumbua tayari ameshakuwa yatima.



    Goda maumivu bado yaliendelea kumtesa akafikiria afanye nini kwa wakati huo, ndipo alipo kumbuka kuwa nyumba hiyo ya kifahari ilikuwa na camara za CCTV za kurikodia matukio yote yanayofanywa katika hiyo nyumba, aliinuka kwa taabu sana na kusimama, akajaribu kutembea hadi kwenye ngazi na kupanda kuelekea juu, alipanda kwa taabu sana huku akijisaidia na mkono wake mwengine, alienda hadi katika chumba cha kuongozea kamera na kuanza kuangalia matukio ya siku hiyo, alilipata tukio lililofanyika muda si mrefu, alichukua flash na kuichomeka kwenye kompyuta na kuanza kulinyonya tukio lote, tokea lilipoanza wakiwa wameka sebleni hadi walipoingia watu wasio wafahamu wakidhani ni majambazi hadi walipoondoka, alipomaliza akaichomoa flash na kutoka kwa tabu sana ikiwa hali yake ndo inazidi kuwa mbaya kutokana na risasi iliyozama ndani kabisa kwenye bega lake.

    Alishuka nayo hadi chini na kumkuta Hemedy bado anawalilia wazazi wake, alipomfikia akamshika bega, Hemedy aligeuza shingo yake na kumuangalia Goda, Macho ya Hemedy yalikuwa mekundu kwa kulia.



    “Hemedy shika hii flash ndiyo ina video yote ya mauaji ya wazazi wako, ishike vizuri na usiipoteze, halafu hakikisha unakuwa nayo wewe mwenyewe” Goda aliongea kwa tabu sana huku akimkabizi Hemedy Flash yenye tukio zima la mauwaji ya wazazi wake. Hemedy akaipokea hiyo flash na kuendelea kulia, Goda alimfuata na kum'bembeleza. Ila Hali yake ilizidi kuwa mbaya sana, baada ya kuanza kuona nyota nyota kwenye macho yake.



    “He..medy ondo...ka ha..pa sio sa...lama kwa..ko, na ukumbuke hi..yo fla..sh ndiyo ina tuki...o lote, haya o..ndoka hapa sio sa...la..ma kwa...." Goda hakuweza kuimalizia sentensi yake na yeye akaungana na wenzake walio lala sakafuni. Akawa amekufa.



    Hemedy alilia sana baada ya mtu aliebakia hai na yeye kupoteza maisha, hakua na jinsi nyengine, akanyanyuka na kuiangalia familia yake iliyokuwa imelala sakafuni bila uhai wowote, flash aliyopewa na Goda alipo ambiwa kuwa ndo inatukio zima la mauaji ya wazazi wake, aliitia katika mfuko wake wa suruali na kutoka nje, huko napo alishuhudia miili ya walinzi wao ikiwa nayo imelala chini, moja kwa moja akajua na wao wamekufa.



    Alifungua geti kwa wasiwasi na kutoka hadi nje ya nyumba yao, hakuelewa aende wapi usiku huo, hakuwahi kulala nje ya nyumba yao hata mara moja, na hiyo ilikuwa ndo mara yake ya kwanza kulala nje ya nyumba yao, aliiangalia kwa masikitiko makubwa, alielewa kuwa yeye hadi muda huo tayari ameshakuwa yatima, alielewa kuwa na yeye muda si mwingi ataenda kuwa chokoraa, alijua na yeye kuanzia hapo ni mtoto wa mtaani, hakuwa na namna ya kufanya aliendelea na safari yake asiyoijua mwisho wake ni wapi.



    Akaikata mitaa asijue anapoelekea ni wapi, hadi kwenye kibaraza cha nyumba ambayo haikumaliziwa na kukaa hapo kwa muda mrefu.



    *****************************



    “Baba lucas hivi huo mlio ni wa nini"



    “Sijajua bado ni wa nini ilaa... tuachane nao bwana kwanza mimi nina usingizi acha nilale” Maongezi hayo yalikuwa yanafanyika nyumba ya jirani kabisa na nyumba ya Mzee Mheshimiwa, mlio walio usikia watu hao wa nyumba ya jirani, ulikiwa ni mlio wa kwanza kabisa alipopigwa Goda risasi ya bega baada ya Mzee Mheshimiwa kugoma kutoa nyaraka zake.



    “Mhhhh!!!! Mbona umejirudia tena? Mama lucas alizidi kupatwa na hofu maana ilikuwa sio kawaida, Kabla hawajakaa sawa waliendelea kuiskia kama mara tano tena imelia kwa kufuatana, hapo sasa Baba lucas ndipo alipoelewa kuwa hiyo ni milio ya risasi, akainuka na kuiyendea bastola yake iliokuwemo kwenye droo, akachungulia dirishani ila hakuweza kuona kitu kutokana na ukuta wa fensi ya nyumba yake, akatoka hadi sebleni, hakuelewa afanye nini kwa wakati huo, mara ghafla akamuona mke wake akitoka na simu iliyokuwa ina ita.



    “Nani anayepiga simu usiku huu?” Baba lucas aliuliza.



    “Ni Mzee John” Baba lucas akaichukua simu yake ambayo bado ilikuwa inaita, akaipokea baada ya kugundua kuwa anaepiga simu ni jirani yao.



    “Vipi John mbona wapiga simu usiku kuna nini?"



    “Kwani wewe hukuisikia hiyo milio ya risasi hapo kwa Mheshimiwa?"



    “Nimeisikia, kumbe inatoka hapo kwa Mzee Mheshimiwa?"



    “Ndio tena naona kulikuwa kuna gari hapo nje kwake, kuna watu wametoka kwenye nyumba yake na wamepanda kwenye hilo gari na kuondoka, ila mimi ninahisi ni majambazi hao"



    “Sasa itabidi tupige simu polisi au wewe unasemaje"



    “Eeeeee itabidi iwe hivyo"



    “Sasa nani atakae piga simu, mimi au wewe?"



    “Piga tu wewe" walihitimisha maongezi hayo yaliyo fanyika katika simu, Baada ya kukata simu Baba lucas akawapigia simu polisi na kuwaambia kila kitu, akaambiwa aelekeze mtaa wa tukio lilipo fanyika, akawaelekeza vizuri na kuambiwa kuwa polisi watafika muda si mrefu.



    Baada ya kama dakika kumi na tano wakasikia mlio wa gari nje kwenye nyumba ya Mzee Mheshimiwa, walianza kutoka kwa uoga na kwa uwangalifu mkubwa, maana hawakuwa na uhakika kwamba mlio wa gari waliousikia ni wa polisi au ndo wavamizi wamerudi.

    Walichungulia kwenye uzio wa nyumba yao na kuona ni kweli gari ya polisi ndio imepaki nje ya nyumba ya Mzee Mheshimiwa, Baba lucas na mkewe walitoka hadi nje na kumkuta John na majirani wengine wameshatoka, wote waliongozana hadi ndani ya nyumba hiyo, kwa picha waliyoiona wenye mioyo mepesi walilia na wengine hawakutaka tena kuangalia, maana ubongo wa Mzee Mheshimiwa ulikuwa nje.



    “Jamani tunaombeni nafasi, embu tokeni nje tufanye kazi yetu"

    Kwakuwa polisi wamekuja na wanafanya kazi yao kama wenyewe walivyosema, hawakuwa na budi zaidi ya kwenda kusubiri nje, polisi walipiga picha maiti zote na kupiga simu hospitali kwajili ya kuomba gari la wagonjwa ili kuja kubeba maiti zilizopo eneo la tukio. Maiti zilitolewa moja baada ya nyengine na kupelekwa katika gari la wagojwa lililopaki nje ya nyumba ya marehemu Mheshimiwa, maiti ziliingizwa zote kwenye gari la wagonjwa.



    “Hivi waungwana ni nani aliye piga simu polisi?" askari mmoja anaeitwa Koplo Taure aliwauliza majirani waliokuwa bado wamesimama nje ya nyumba.



    “Ni mimi hapa Afande" Baba lucas alijibu na kujipenyeza kwenye kundi la watu, akafika hadi kwa Koplo Taure.



    “Hembu njoo maramoja tuongee" Baba lucas hakuwa na pingamizi, walienda hadi pembeni kidogo na kuanza kuongea.



    “Unaweza ukaniambia ilikuaje kuaje?"Koplo Taure aliuliza.



    “Mimi nilikuwa nimepumzika nyumbani kwang.........."Baba lucas alielezea tukio zima kama alivyo ambiwa na Mzee John lilivyokuwa.



    “Unaweza Ukaniambia Mzee Mheshimiwa alikuwa anaishi na nani?"



    “Alikuwa anaishi yeye, Mke wake na Mtoto wao mmoja na wafanya kazi wa tano, watatu walikuwa wa kiume na wawili walikuwa wa kike"



    “Huyo mtoto wao anaumri gani?"



    “Mtoto wao ni mdogo tu nahisi ana miaka kati ya kumi hadi kumi na mbili hivi"



    “Sasa mbona sisi hatukuona mtoto yoyote mule ndani, Na tumeangalia nyumba nzima?"



    “Mmmmh! Kwa hapo sasa sijajua, au labda itakuwa wameondoka nae"



    “Wakina nani?"



    “Si hao wavamizi, itakuwa wameondoka na huyo mtoto".



    “Haya asante kwa ushirikiano, acha sisi tuende kituoni, tutaendelea na uchunguzi wa kina"



    “Kwahiyo afande hakuna hata mmoja aliekuwa hai?"



    “Wote wamekufa, hakuna mzima hata mmoja"



    Koplo Taure akaridhika na maelezo hayo mafupi, wakapeana mikono na kumruhusu Baba lucas kuondoka, Maaskari baada ya kufanya uchunguzi wao waliifunga nyumba kwa usalama zaidi na kuondoka zao.



    *************************************



    “Mwiziiii mwiziiii mwiziii"



    Zilikuwa ni kelele za raia wenye hasira kali, wakimkimbiza mwizi majira hayo ya usiku, walikuwa wamechoshwa na vibaka hao wanao sumbua mtaa wao. Kijana mdogo aliekuwa anakimbia kama Usain Bolt ilikuokoa roho yake zidi ya raia wenye hasira kali, alionekana kukata tamaa, maana kila anapo kunja kona ndipo raia wanapozidi kutoka majumbani mwao, na hivyo ilikuwa ni usiku basi kelele ndo zilizidi kupaa na kuwaamsha watu wengine, hakuelewa atafanya nini ilikuiyokoa nafsi yake, alitubu dhambi zake kimya kimya huku akikimbia na kumuahidi mungu kuwa kama atapona kwenye hilo zahma basi atamrudia mungu wake, pamoja na kuwaza yote hayo bado hakuacha kukimbia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hemedy aliziskia hizo kelele za mwizi akiwa bado amekaa kwenye kibaraza cha nyumba hiyo iliyokuwa bado haijamaliziwa, alikuwa na wasiwasi hakuwahi kulala nje hata siku moja, akafikiria afanye nini usiku huo wenye mashaka kwake, ila hakuwa na cha kufanya, alisimama na kuangaza huku na huko, ghafla akamuona mtu akija mbio ule upande aliokuwepo yeye, hakujua akimbie au abaki, kiufupi hakuwa na chaguo sahihi, katika hali ya kuogopesha yule mtu alikuja hadi pale alipo huku akiwa ana hema.



    “Vipi wewe hujaskia kelele za mwizi" yule mtu alimuuliza, Hemedy alizidi kupatwa na hofu, wasiwasi, mashaka na uoga vyote vilimjia kwa pamoja, akabaki ameganda asijue afanye nini, akatingisha kichwa kukubali kuwa ameiskia kelele hiyo ya mwizi.



    “Basi kimbia maana hao watu wakija huku watakuua watadhani wewe ndo mwizi, sasa mimi nakushauri kimbia" Maskini Hemedy hakuelewa kuwa anataka kuingizwa katika matatizo mengine ikiwa yale ya mwanzo ameyakwepa, na kwavile alikuwa ni mtoto wa kishua mambo ya uswazi hakuyajua vizuri, bila kujifikiria bila kujiuliza akaanza kukimbia sehemu asiyoijua, yule kijana baada kuona mpango wake umekamilika, akaingia kwenye ile nyumba ambayo haikumaliziwa ambapo mwanzo alikuwa Amekaa Hemedy, aliingia ndani yake na kutulia tuli.



    Baada ya muda si mrefu alishuhudia kundi la watu wenye silaha kali wakipita mbio mbio kuelekea upande ambao Hemedy ameelekea, walipoisha wote akatabasamu na kujibanza humo humo ndani.



    Hemedy alikimbia mpaka akachoka, akaanza kusikia kelele za mwizi zikizidi kumkaribia, hakuelewa atafanya nini, hakuelewa atajinusuru vipi na hilo zahma ambalo sio lake, hakuelewa asimame au aendelee kukimbia, akaona ni bora aendelee tu kukimbia, kwavile hakuijua mitaa hiyo vizuri akajikuta anaingia katika uchochoro ambao mbele yake kulikuwa na kundi la watu wanakuja mbio kwa hasira wakiwa wameshika silaha kali, Hemedy alisimama na kuanza kugeuza, alikimbia lakini watu hao bado walikuwa nyuma yake, kwavile siku ya kufa nyani miti yote inateleza, Hemedy na yeye alikuwa ni nyani na miti yote ili mteleza, uhai wake siku hiyo aliuona ukimtupa mkono.



    Mbele yake kulikuwa kuna kundi jengine lina kuja wakiwa wameshika silaha kali, Hemedy hakuelewa afanye nini baada ya kuzungukwa na watu hao wenye hasira kali na waizi waliokuwa wanawasumbua kila siku, Bila kuuliza watu walianza kumpiga mawe bila kujali umri wake, walimpiga bila kujua kuwa huyo wanaempa adhabu hiyo, haikuwa ikimuhusu na wala haiku mstaili, walimpiga vibaya sana, huku wakishangilia wakidai kuwa watawakomesha waizi hao mmoja baada ya mwingine hadi waizi wote waishe.



    “Nipisheni, nipisheni”



    Zilikuwa ni kelele za raia mmoja, alie jifanya kuwa na hasira kali kuliko wenzake wote waliokuwepo, pengine hata kumzidi huyo aliye ibiwa, akiwa ameshika kidumu cha mafuta ya petrol, akija nacho kwa gadhabu mbio mbio huku akiwapangua watu, bila ya kufikiria kuwa huyo anayetaka kumfanyia hivyo alikuwa ni binadamu kama yeye, ila kwa vile yeye alitaka sifa kuwa yeye ndio alie leta mafuta ya petrol, akaona afanye kile kitakacho mpa sifa, akafika hadi mbele na kuanza kummiminia mafuta Hemedy waliedhani kuwa ndo yule mwizi walietoka nae mbali.

    Hemedy hali yake ilikuwa ni mbaya sana hakuweza hata kutoa sauti, alikuwa amekata tamaa ya kuishi katika huu ulimwengu, alikuwa anasubiri kifo chake akaungane na wazazi wake huko walipo.

    Kijana mwenye hasira kali kuliko wote, alipo maliza kummiminia mafuta Hemedy, akatoa kibiriti na kukiwasha akiwa yupo tayari kumuunguza Hemedy.







    Polisi baada ya kuhakikisha nyumba ya marehemu Mzee Mheshimiwa, wameiacha katika usalama, maana huo ulikuwa ni usiku halafu nyumba ilikuwa haina mtu, ndo maana wakafunga na kufuli lao na kuanza safari baada ya gari la hospitali lililobeba maiti za wenye nyumba hiyo kuondoka, nao wao wakaanza safari ya kurudi kituoni.



    Wakati wakiwa wapo barabarani, waliskia kelele za watu, ila hawakuelewa kelele hizo ni za nini na zinatokea wapi.



    “Afande Taure unazisikia kelele hizo" askari mmoja aliuliza.



    “Ndio nazisikia ila bado sijajua ni za nini na sijajua pia zinatokea kwa wapi? Embu simamisha gari hapo mbele" Koplo Taure alijibu na kutoa amri ya gari kusimamishwa, dereva akaegesha gari na kutulia, maaskari wote wakawa wapo kimya wakiziskilizia hizo kelele.



    “Afande mbona kama ni huko mbele ndo zinapotoka hizo kelele?" Askari aliuliza.



    “Ndio ni huko mbele, hembu endesha gari haraka tuziwahi hizo kelele, huenda ikawa ndo hao majambazi wamekamatwa" Afande Taure alitoa amri na gari ikaendeshwa kufuata kelele zinapotokea. Kwa mbali waliona kundi la watu wakiwa kama wanapiga kitu hivi, ikabidi dereva awahishe gari haraka sana ili kuwahi.



    “Oyaaaa pira hilo, wazee wanakujaa"



    Kijana mmoja aliekuwepo katika kundi la watu waliokuwa wanampiga Hemedy wakidhani ni mwizi, alitoa kauli hiyo ambayo sio watu wote waliiskia, wengine walikuwa bado wanashangilia wakitaka mwizi achomwe moto, kwa wale ambao walisikia, waligeuka nyuma na kuangalia kuwa walichoambiwa kuwa ni chaukweli, ndipo hapo macho yao yalipotua kwenye gari la polisi lililokuwa linakuja kwa kasi huku likimulika taa zote za mbele.



    Bila kusubiri hadi lifike mmoja mmoja aliaanza kushika njia yake kwa kasi ya umeme, akijaribu kuokoa nafsi yake zidi ya hao polisi waliokuwa wanakuja kwa kasi, kwa wale ambao hawakuskia onyo walilopewa na mwenzao kuwa polisi wanakuja, walishangaa baada ya kuona wenzao wakitimka mbio mbio kila mmoja akielekea njia yake, walijiuliza kuna nini mbona watu wanakimbia? Ndipo hapo walipo shuhudia gari la polisi likiwa karibu kabisa na eneo walilopo, na wao bila kujifikiria mara mbili, walitupa mawe waliokuwa wameyashika kwaajili ya kumuadhibu mwizi, na kila mmoja kuanza kushika njia yake.



    Hakuna ambae alitaka ashikwe na polisi hao, hakuna ambae alitaka akalale kituoni, maana waliujua ule msemo wa kuwa “Polisi kuingia ni bure, kutoka na hela" hakuna hata mmoja alietaka kuingia bure halafu atoke na hela ndo maana kila mmoja akajaribu kuokoa nafsi yake. Kijana mwenye hasira kali kuliko wote, alietaka sifa ya kuwa yeye ndo ameleta mafuta ya petrol kwaajili ya kumgeuza majivu mwizi, na yeye pia aliliona gari la polisi likija kwa kasi, hakutaka kushikwa pekeake, japo kuwa alipenda sifa, ila mbele ya polisi hakupenda asifiwe, akatupa kibiriti, akatupa kidumu kilichokuwa hakina kitu kwa wakati huo baada ya mafuta yote kuenea katika mwili wa Hemedy aliekuwa amelala chini hajiwezi kwa kipigo alichopokea kutoka kwa raia wenye hasira, akashika njia na kupotea gizani. Akatoweka na yeye.



    Maaskari walishuka haraka haraka na kuweka ulinzi eneo hilo, Koplo Taure alishuka na yeye kutoka katika viti vya mbele vya gari hilo, akaenda hadi ulipo mwili wa hemedy na kuchuchumaa, alipokelewa na harufu ga mafuta ya petrol yaliyokuwa kwenye mwili wa Hemedy, alimuwekea kidole chake kwenye pua za Hemedy na kugundua kuwa bado alikuwa ni mzima.



    “Beka hembu njoeni tumchukue huyu naona bado ni mzima"



    Maaskari bila kuuliza walienda hadi ulipo mwili wa hemedy na kum'beba hadi kwenye gari.



    “Dah halafu ni mtoto mdogo kabisa huyu, anatakiwa mda huu awe amelele nyumbani kwao" askari mmoja aliongea.



    “Hii miji toto ya mtaani yaliyotelekezwa na wazazi wao ndo wanakuja kuwa machokoraa na mwisho yanakuwa mavibaka, yanatusumbua sana, lina bahati halijiwezi ila ningelipiga hadi kulivunja miguu lisitembee tena hasilani" askari anayefahamika kwa jina la Mkwaju, aliongea maneno hayo bila kujua huyo anaemdhania ni kibaka ndo huyo mtoto wa Mzee Mheshimiwa, waliedhani kuwa ametekwa na majambazi waliovamia nyumbani kwao.



    Kwakuwa hali yake ni mbaya sana baada ya kupokea kipigo cha mwizi kutoka kwa raia wenye hasira kali, waliamua wampeleke moja kwa moja hadi hospitali ili akapate matibabu. Walipofika hospitali, walimshusha na kupokewa na manesi wa hospitali hiyo na kumpeleka chumba maalumu na kuanza kumpatia matibabu.



    Maaskari baada ya kuona kila kitu kimeenda sawa waliaga na kuahidi kesho yake watarudi kuja kujua hali ya muhalifu wao, hawakuwa na sehemu nyengine ya kuenda, kwavile pia muda ulikuwa umeenda sana na kulikuwa kunakaribia kukucha, wakaongoza gari hadi kituoni ili waendelee na mambo mengine.



    *****************************

    Siku iliyofuata. Kituo cha Polisi Mabawa.



    “Afande Jesca, nimekuita hapa nataka unipetaarifa kuhusiana na tukio lililotokea jana usiku" Mkubwa wa kituo, anaejukikana kwa jina la Inspekta Ganjo, aliongea maneno hayo akiwa ndani ya ofisi yake mbele yake akiwa amesimama askari wa kike.



    “Mkuu, hapo labda nikuitie Koplo Taure maana yeye jana ndie aliongoza msafara huo"



    “Ok niitie mara moja" afande jesca alitoka na kwenda hadi kwenye ofisi ya Koplo Taure, alipofika alipiga hodi, ila hakujibiwa akaamua anyonge kitasa na kuzama ndani, ila hakumuona Koplo Taure, alitoka hadi nje kabisa ambapo aliwakuta maaskari wengine wamekaa, akawauliza mahali alipo Koplo Taure na kuambiwa kuwa ametoka kidogo kwenda kununua vitafunwa vya chai, haikupita muda mwingi, Koplo alirudi huko alipoenda huku mkononi akiwa ameshika mfuko mweusi wa nailoni.



    “Wewe ulikuwa wapi?Mkuu anakuita huko ofisini kwake" Afande Jesca alimuambia hivyo baada ya kufika karibu yao.



    “Nilikuwa nimeenda kununua vitafunio(huku akiangalia mfuko mweusi alioubeba) Kuna nini kwani?"



    “We nenda utajua huko huko" afande jesca aliongea huku akiondoka kuelekea eneo lake la kazi baada ya kufikisha taarifa..



    Koplo Taure baada ya kupewa taarifa hiyo alienda hadi kwenye ofisi yake na kuweka mfuko wake wenye vitafunio alivyotoka kununua mda si mrefu, aliuweka juu ya meza yake na kutoka kuelekea kwenye ofisi ya Mkuu wake, alipiga hodi na kuambiwa kuwa aingie, baada ya kuingia, alipiga salut na kusubiri ambiwe alichoitiwa.



    “Jana wewe ndio uliongoza msafara wa kwenda kufuatilia tukio la ujambazi?"



    “Ndio Mkuu"



    “Sawa, tukio hilo limetokea wapi?"



    “Tukio limetokea mtaa wa Donge kwenye nyumba namba 169 na had......."



    “Whaat?" Inspekta Ganjo aling'aka kwa mshtuko na kumfanya Koplo Taure kurudi nyuma kidogo, maana Inspekta aliipigiza mikono yake kwenye meza na kuinuka katika kiti alichokaa mwanzo.



    “Ume..ume....umesema mtaa wa Donge nyumba namba ngapi?



    “169 Mkuu, walisema anaitwa Mzee nani siju...."



    “Mzee Mheshimiwa?" Mzee Mheshimiwa na Mkubwa wa kituo walikuwa ni marafiki tokea wakiwa wanasoma sekondari, ila walipo maliza sekondari kila mmoja akachaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano kwa shule tofauti, hata hivyo urafiki wao uliendelea mpaka kila mmoja alipopata kazi, Mzee Mheshimiwa aliajiriwa katika bandari ya Tanga, alifanya kazi hapo kwa miaka kadhaa, akaacha na kujiajiri mwenyewe, ndipo hapo alipoanzisha sheli zake za mafuta akaona pia haitoshi akafungua showroom ya magari.

    Na kwa upande wa Inspekta Ganjo yeye alipomaliza elimu yake moja kwa moja akaenda kuomba kazi ya upolisi, kutokana aliipenda kutoka moyoni, basi alifanikiwa kuipata, kutokana na utendaji wake wa kazi akapandishwa cheo mpaka kuwa Inspekta.



    “Ndio Mkuu"



    “Enhee hembu nipe taarifa imekuaje kuaje"



    “Mkuu kwa maelezo tuliyopewa kwa......." alimuelezea yote aliyoambiwa na Baba lucas na aliyoyaona mwenyewe.



    “Kwahayo maelezo uliyoyatoa, unahisi huyo mtoto atakuwa ametekwa na hao majambazi au wewe unahisi nini?" Mkubwa wa kituo aliuliza.



    “Kwa hapo bado sijajua Mkuu”



    “Sawa fuatilia hiyo kesi kwa kina"



    “Ndio Mkuu" alisimama na kuanza kupiga hatua ili atoke, ila kuna kitu alikumbuka, akamgeukia Mkubwa wake.



    “Mkuu, halafu wakati jana usiku tunarudi kituoni, tuliona mtu akipigwa barabarani, kwa haraka haraka sisi tulijua ni mwizi, kwasababu walikuwa wanataka kumchoma moto"



    “Huyo mtu yupo wapi?"



    “Tumempeleka hospitali, na nilikuwa leo nataka niende nikamfuatilie nijue anaendeleaje"



    “Sawa unaweza kwenda, ila huyo mwizi utamleta hapa kituoni halafu ndio tutajua tunafanya nini"



    “Ndio Mkuu" afande Taure alitoka ofisini kwa Mkuu wake na kuelekea katika ofisi yake kuendelea na shuhuli nyengine.



    *************************************



    “Hahahahahah Dah thiku tegemea kama kadhi itakuwa rahithi namna ile, hembu tusherekeeni kwandha" Mata aliongea kwa furaha baada ya kukamilisha kazi yao walioifanya jana.



    “Hata mimi sikutegemea kama itakuwa ni rahisi vile. Vipi mbona Mrutu wewe hauna furaha? Au bado unamuwaza yule marehemu Mzee mheshimiwa? Moto aliongea.



    “Hapana sio hivyo" Mrutu alijibu huku akiwa ana wasiwasi wa waziwazi.



    “Thatha kama thio hivyo ni nini? Acha dhako bwana tufurahie petha ambadho hatuja dhitolea jasho thithi tunaita petha dha wajinga, furahia bwana" Mata aliongea.



    “Mimi simuwazi Mzee Mheshimiwa, kwanza undugu mwenyewe tumekutana kwa baba kila mtu ana mama yake, sasa mimi nimuwaze wa nini?"



    “Sasa kinachokufanya uwe na mawazo hivyo ni kipi? Ujue mimi nilikuwa nakuona tu tangia muda una mawazo siju unawaza kitu gani?"



    “Nyie hamjui tu, ndo maana mnasema hivyo, ile nyumba ina CCTV Camera, kwahiyo lile tukio lote ambalo mmelifanya mjue limerikodiwa" wote wa wili macho yaliwatoka, wao walidhani wameshapoteza ushahidi kwa kuua familia nzima, kumbe bado wanakimbembe chengine, hawakujua watafanya nini, vijasho vyembaba vilianza kuwatoka, walikuwa na wasiwasi pengine hata kumshinda Mrutu aliewapa tarifa hiyo.

    Wakabaki wanaangaliana, wasijue wafanye kitu gani, vinywaji vyote vilivyokuwa mezani kwa ajili ya kujipongeza kazi hiyo waliyo ifanya walivisahau kwa muda huo.



    “Thatha kwanini hukutumbia tokea mwandho?" Mata alikuwa ni katili sawa, ila mbele ya polisi alikuwa ni muoga sana, halafu pia aliogopa jina lake kuchafuka, maana yeye baada ya miaka kadhaa alipanga kuja kugombania Ubunge.



    “Mataa, huu sio muda wa kulaumiana tena, inabidi tukae tupange tunafanya nini, maana hata ukilaumu haitosaidia kitu"



    “Ndo hivyo sasa inabidi tujue tunafanya nini kabla mambo hayaja haribika"Mrutu aliongea.



    “Nimepata wazo" Moto aliongea na kuwaangalia wenzake na kuwaona kuwa kila mmoja ameweka utayari wa kumskiliza. “Kwani ile nyumba si haikai mtu sasa hivi"



    “Ndio hakuna mtu anaekaa" Mrutu alijibu.



    “Safi, itabidi mimi niende, nikaingie hadi kwenye ile nyumba, niingie hadi kwenye chumba cha kuongozea kamera, halafu nifute Data zote, au nyie mnasemaje? Moto alieleza na kuuliza swali.



    “Thatha Moto unauhakika gani? Je kama polithi wameshachukua hizo Data?" Mata alionyesha wasiwasi wake.



    “Hapana haiwezi kuwa hivyo kwasababu kile chumba ni cha siri sana, yani kama sio mtu wapale huwezi kujua, kwanza mlango wenyewe wa kuingilia humo kwenye hicho chumba upo kama ukuta,kwahiyo kwa mtu ambae sio wa pale hawawezi kujua" Mrutu aliwaambia.



    “Thatha wewe vitu vyote hivyo umevijuaje"?



    “Wakati anaijenga ile nyumba mimi ndie nilimpa ushauri kuwa aweke kamera za ulinzi namna hiyo"



    “Thatha tunafanyaje"



    “Itabidi Mrutu unielekeze kila kitu kwasababu wewe si ndio unaejua, ili mimi nikienda nisipate tabu"



    “Poa usijali"



    “Kwahiyo hiyo kadhi utaifanya thaa ngapi?"



    “Nitaifanya kesho usiku"



    “Hahahahaha tusherekeeni bathi, maana tushapata jibu la jambo lililo tuchanganya"



    Waligongesha glas na kuendelea kufurahia mali za dhuluma.



    ***********************************



    Koplo Taure alienda katika hospitali aliyolazwa Hemedy ili kujua hali yake, aliofika aliambiwa na daktari aliewapokea jana kuwa hali yake sio nzuri sana ila matumaini ya kupona yapo, akatoa msisitizo kuwa mgonjwa huyo anahitajika akatoe maelezo kituoni kwa kile kichomkuta jana yake, na kumsisitizia zaidi kuwa amuwekee uangalia asije akafanya kitendo chochote hususani ni kutoroka hospitali hapo, alihakikishiwa atakuwa katika uangalifu mzuri na daktari huyo, akaaga na kuondoka zake kuelekea kituoni.



    Mazishi ya Mzee Mheshimiwa na mke wake yalifanyika kijijini kwao Gombero, Inspekta Ganjo alihudhuria pia mazishi hayo, alikuwa akilia kiume baada ya rafiki yake kipenzi kuingizwa katika kaburi makazi yake ya milele, baada ya kumaliza kufukia kaburi, taratibu nyengine zikafuata kama kumsomea marehemu dua, baada ya hapo kila mtu alianza kuondoka mmoja mmoja, Inspekta Ganjo baada ya watu kuondoka, alichuchumaa kwenye kaburi la rafiki yake kipenzi, na kumuombea mungu amlaze mahali pema peponi, alihuzunika, alisikitika ila ikawa ndio tayari imeshatokea hakua na budi na yeye aliondoka makaburini hapo. Mzee Mheshimiwa akawa amebaki mwenyewe katika kaburi lake, alizikwa pembeni ya mke wake.



    Baada ya mazishi kuisha, Inspekta Ganjo alirudi mjini kuendelea na shuhuli zake, ila picha ya rafiki yake bado haikumtoka kwenye ubongo wake, hakuamini kuwa ndio anatoka kumuhifadhi rafiki yake katika nyumba yake ya milele, hakua na jinsi akajaribu kusahau na kuendelea na mambo mengine.



    ********************************



    “Ndio Mkuu"



    “Nataka kujua hii kesi ya marehemu Mheshimiwa imefikia wapi"



    “Mkuu hii kesi bado ngumu, hadi sasa sijajua nianzie wapi"



    “Unasemaje Afande? Yani hujajua uanzie wapi? Sasa wewe ni askari wa vipi halafu tena hunaata aibu eti unasema sijui nianzie wapi? Hivi unajua kusema hivyo ni kosa, tena kosa kubwa sana inastaili kupata hata adhabu, ok sitokupa adhabu sasa hivi, ninakupa siku ya leo tu, kesho nataka uniletee taarifa umefikia wapi katika uchunguzi wako, unaweza kwenda".



    Koplo Taure hakujua afanye, ni kweli kesi hii kwake ilikuwa ni ngumu kutokana na uwezo wake, ila hakutakiwa kusema vile mbele ya Mkuu wake, ila yeye hakusema vile kwania mbaya, amesema vile akidhani atapewa njia ya kuanzia, ila matokeo yake amepewa siku moja ya kupata chanzo cha kifo cha Mzee Mheshimiwa na familia yake.



    Hakuwa na jinsi alipiga salut na kuanza kuondoka mdogo mdogo, ila kabla hajafungua malango, akasikia anaitwa na mkuu wake, akageuza shingo kitaratibu na kumuangalia Mkuu wake.



    “Nenda kaanzie nyumbani kwake leo usiku" alipewa muongoza na kuambiwa aende.



    ********************************



    Majira ya usiku, Moto alifika hadi katika nyumba ya marehemu Mheshimiwa, lengo lake lilikuwa ni kuingia katika nyumba hiyo na kuingi katika chumba cha kuongozea kamera ili afute data zote za tukio walilo lifanya,alifika hadi pembezoni mwa nyumba hiyo na kukutana na ukimya wa hali ya juu kutokana na eneo hilo kuwa na nyumba zenye mageti, pia ukimya hiyo huo umesababishwa na kuwa mtaa huo unakaaa watu wakishua.



    Aliangalia mazingira na kuona kupo vizuri, akaliendea geti na kujaribu kulifungua na kukuta limefungwa na kufuli, hakutaka kukata tamaa aliuangalia ukuta wa hiyo nyumba na kuona ni mrefu sana akajua hawezi kuupanda, akazunguka nyuma ya nyumba hiyo, bahati ikawa kwake, aliona mti mrefu wa muarubaini, akaupanda hadi juu, hapo aliweza kupaona ndani vizuri tu,



    Akafikiria atafanyaje ili aweze kuingia ndani, akatoa tabasamu baada ya kuona tawi moja limeingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo, akaparamia tawi hilo na kujaribu kuingia ndani ya uzio wa nyumba hiyo, akaruka chini kwenye bustani, hakuwa na ujasiri wa kujihakikishia usalama wake moja kwa moja, alitembea kwa tahadhari akielekea mlango wa mbele wa nyumba hiyo, alipofika akajaribu kunyonga kitasa, bahati ikawa kwake mlango ulikuwa upo wazi, akazama ndani kwa uangalifu akifuata maelekezo aliyopewa na Mrutu, akapanda ngazi na kwenda hadi juu, alipofika kwenye kordo alianza kuhesabu vyumba, chumba chapili ndio chenyewe alichoelekezwa, akanyonga kitasa, bahati ikawa kwake tena, mlango ukafunguka akazama ndani, aliwasha shwichi ya taa na mwanga ukajaa chumba kizima.



    Kama alivyoelekezwa akaenda hadi kwenye kabati, pembeni yake kuna droo akaifungua na kukutana na makaratasi mengi, akayatoa yote na kukutana na shwichi kama ya mwanzo aliyoiminya na kuwasha taa ya humo kwenye chumba, na hiyo pia aliiminya, ghafla ukuta uliokuwepo pembeni ya kabati ukajifungua taratibu, bila kujiuliza akazama ndani, taa zimewaka kwenye chumba hicho, akaona kuna kompyuta moja, akaiyendea na kuanza kupekua mafaili, akitafuta faili la tarehe 13, akatoa tabasamu baada ya kulipata, akalifungua ndani, macho yalimtoka baada ya kukutana na mandishi yaliyosomeka “empty folder”. Ikimaanisha faili hilo halina kitu, Hakukata tamaa alipekuwa mafaili yote ila hakuona video anayo itafuta.



    Alichanganyikiwa akajua tayari video imeshachukuliwa, hakua na jinsi nyengine ya kufanya, akafunga kama alivyokuta na kuanza kutoka chumbani humo.



    Koplo Taure alikuwa yupo ndani ya gari lake akielekea nyumbani kwa marehemu Mheshimiwa, aliendesha kwa kasi kwasababu alichelewa sana. Alipo fika akashuka kwenye gari na kuliendea geti, kwakuwa wao ndo walifunga geti hilo kwaajili ya usalama wa mali za nyumba hiyo, kwahiyo funguo alikuwa anazo, akafungua geti na kuzama ndani, akachomoa bastola yake kwajili ya usalama wake, kwa fikra zake alijua hakuwezikuwa na mtu humo ndani, ila alitoa bastola kwajili ya kujihami na chochote kitakacho tokea mbele yake, aliufikia mlango na kushika kitasa akitaka kuufungua ili kuingia ndani.



    Moto pia aliufikia malango mkubwa ili aweze kutoka nje aende zake baada ya kukosa alichokifuata.....





    Koplo Taure baada ya kunyonga kitasa, mlango ukafunguka, akatulia kama sekunde kumi, alifanya hivyo ili kujihakikishia kama kunachochote kibaya aweze kujihami, alipoona pako kimya, akafungua mlango kabisa na kuingia ndani, alitumia tochi ya simu yake ili kupata mwanga utakao muwezesha kuiyona swichi ya taa ya hapo sebleni, akafanikiwa kuiyona swichi, akawasha taa na kuangaza macho yake hapo sebleni kama ataweza kupata chochote kitakachomsaidia katika upelelezi wake.



    Akatafuta sebleni hapo hadi akachoka ila hakuweza kupata chochote, akaamua kupanda ngazi hadi vyumba vya juu, ili akaangalie kama ataweza kupata chochote kitakacho msaidia katika upelelezi wake.



    Dakika tano nyuma kabla Koplo Taure kuingia ndani ya sebule ya nyumba hiyo.



    Moto wakati anashika kitasa, iliatoke nje akashangaa kuona kitasa kinazungushwa, akaachia haraka na kuruka pembeni hadi kwenye pazia la dirisha lililokuwepo hapo karibu na mlango, akajificha nyuma ya pazia, zoezi hilo alilifanya kwa sekunde zisizo zidi nne, baada ya kama sekunde tano, akaona mtu akiingia humo ndani, taa ikawashwa, hapo ndipo mapigo ya moyo wake yalipoanza kudunda baada ya kuona mtu alieingia ameshika bastola na yeye hakuwa hata na kisu cha kujihami, akajuta kwanini sehemu kama hiyo hakuja na bastola yake.



    Akaona kama kuna kitu anakitafuta tafuta hapo sebuleni, baada ya muda akamuona akipanda ngazi na kuelekea juu ya nyumba hiyo. Hapo hapo bila kuchelewa, akatoka nyuma ya pazia alipo jificha na kufungua mlango, akatoka nje na kwenda kuangalia getini na kukuta geti halijafungwa akatokomea zake.



    Koplo taure alifika hadi vyumba vya juu, akaingia chumba kimoja baada ya chengine akitafuta kitu kitachomsaidia katika upelelezi wake, ila hakuambulia chochote, hapo sasa ndipo alipoona hiyo kesi aliyopewa imekuwa ngumu kwake, kwavile hakupata chochote kitachomsaidia katika upelelezi wake, akaamua aondoke tu, hakujua atamjibu nini Mkuu wake endapo atamuuliza amefikia wapi, kwa mara ya kwanza akakilani cheo chake alichokuwa nacho, akatamani na yeye angekuwa anacheo kikubwa, huenda na yeye angekuwa anaamrisha tu, ila haikuwa hivyo. Atakuaje na cheo kikubwa wakati kazi zenyewe hazifanyi kwa akili? Akabaki na cheo chake cha Ukoplo.



    Moto alipotoka katika nyumba ya Mzee Mheshimiwa, alimpigia simu Mata na kumuliza yupo wapi kwa wakati huo, akaambiwa kuwa yupo nyumbani kwake, akampigia simu Mrutu kuwa wakutane nyumbani kwa Mata ili awaambie alichokikuta nyumbani kwa mzee mheshimiwa.



    ********************************



    “Kwahiyo hukulikuta faili la ile tarehe" Mrutu aliuliza kwa hamaki baada ya kupewa taarifa ya alichokikuta Moto kwenye nyumba ya marehemu Mheshimiwa.



    “Faili nimelikuta, ila video hakuna"



    “Dah thijui thatha itakuaje, unajua tunawedhaa kujulika mapema hata kabla hatuja faidi mali". Mata alionyesha wasiwasi wake.



    “Hivi mrutu, unaweza kuhisi ni nani aliyeichukua ile video?" Moto aliuliza.



    “Au labda itakuwa ni huyo mtu uliyemuona akiingia nyumbani kwa Marehemu Mheshimiwa". Mata aliongea.



    “Mataa, nikuambie mara ngapi, kwamba kile chumba ni cha siri hakijulikani na watu ambao hawa husiki? Au labda itakuwa ni Goda nini? Mrutu aliongea na kuuliza ila katika hao aliowauliza hakuna hata mmoja anaemjua Goda ni nani.



    “Huyo Goda ni nani?"



    “Goda, alikuwa ni mfanyakazi wake anaemuendesha na gari, kwani nyie wakati mnaingia hamkumuona mvulana mkubwa mkubwa hivi?"



    “Ndio tulimuona na yeye ndo wakwanza kumpiga risasi, nilimpiga risasi ya bega" Moto alijibu.



    “Itakuwa ni yeye tu hakuna mwengine, kwani nyie mulihakikisha amekufa kabisa? Mrutu aliuliza.



    “Hapana, sisi tulivyomuona ameanguka chini katulia, sisi tukajua tayari tumeshamuua" Moto alijibu, kipindi chote hicho Mata alikuwa yupo kimya, anawasiwasi baada ya video ya tukio walilolifanya kutoonekana. Alikuwa anawasiwasi kweli si mchezo.



    “Ayaa!! Sasa nyie mmeambiwa na nani kuwa risasi ya bega inaweza ikamuua mtu hapo hapo? Itakuwa alizimia tu, baada yakuinuka akaenda kuichukua tu"



    “Lakini mbona taarifa tulizo zipata zinasema wote wamekufa, ila mtoto wao tu ndo hajaonekana?"



    “We taarifa umezipata wapi"



    “Haaa!! Kwani nyie hamjaangalia taarifa ya habari? Yule ni mtu mkubwa hapa Tanga lazima watangaze tu kifo chake, sasa nyie mnanishangaza mkisema eti hamjapata taarifa"



    “Kumbe pia hamkumuua na yule mtoto wake?" Mrutu aliuliza kwa mshangao.



    “Hatukumuua kwa risasi, ila alikufa kwa mshtuko baada ya kumuona Baba yake tumemfumua ubongo" Moto alijibu.



    “Sasa nyie mbona mnafanya mambo kama vile hii kazi mmeiyanza jana? Mlikuwa na uhakika gani kama alikufa? Haya mbona hajaonekana?". Mrutu alianza kupaniki na kuongea kwa hasira.



    “Mrutu embu pungudha jadhba, hayo ni makotha tu madogo madogo yanawedha kujitokedha katika kadhi yoyote, kwani wewe unahithi nini hadi hapo?" Mata aliyekuwa kimya mda wote aliongea baada ya kuona Mrutu ameanza kupaniki.



    “Mimi kwa mawazo yangu ninavyo hisi, itakuwa Goda na Hemedy walizimia tu, kwahiyo baada ya muda, waliamka na ninavyojua risasi ikipigwa sehemu ambayo ni ngumu sumu kufika kwa haraka hadi kwenye ubongo kama nyie mlivyofanya kumpiga risasi ya bega, ninahisi itakuwa Goda alipata nguvu kidogo na kwenda hadi chumba cha kuongozea kamera, na kuinyonya video yote kwenye flash, ili apate kama ushahidi, ila kama inasemekana yeye alikufa, basi itakuwa flash hiyo alimkabidhi Hemedy kabla yeye hajakufa. Hivyo ndo ninavyo hisi".



    “Wewe si umesema kuwa hiko chumba cha kuongozea kamera hakijulikani na watu wasio husika, Sasa huyo Goda ataingiaje ikiwa yeye hausiki? Moto aliuliza.



    “Goda alikuwa ndie mafanya kazi wake mkubwa, yani tangu Mzee Mheshimiwa anahamia alikuwa yupo nae, huenda ikawa na yeye anakijua hiko chumba"



    “Hapo Mrutu umeongea, huenda ikawa ni kweli kabitha, Thatha tunafanyaje kumpata huyu mtoto?". Mata aliyaunga mkono mawazo ya Mrutu.



    “Hapo inabidi tumtafute tu, na tukimpata tunamuua halafu kama anayo hiyo flash tunaichukua na kuichoma moto tu" Moto alitoa wazo hilo.



    “Je tukimpata halafu ikawa hana hiyo flash, tunafanyaje? Maana hapo mimi nimehisi tu ila sina uhakika" Mrutu aliuliza.



    “Tuna muua tu, halafu baada ya hapo tutajua tufanye nini" Moto aliongea.



    “Kama ni hivyo sawa, tunaanzia wapi kumtafuta?" Mrutu aliuliza.



    “Popote pale, mji wa kwetu huu, tutamsaka hadi tumpate" Moto alijibu.



    “Je kama ameipeleka hiyo flash polisi? Mrutu aliuliza tena.



    “Polisi hawezi kwenda, kwanza mtoto mwenyewe mdogo, hatokuwa na mawazo hayo".

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maongezi yao waliya hitimisha hapo na kila mmoja akainuka na kwenda nyumbani kwake, baada ya kupata muafaka kuwa wamtafute Hemedy kila kona ya jiji na wakimpata waichukue flash ya video, waliodhani atakuwa anayo yeye baada ya kuichukua wamuue, ili wazidi kupoteza ushahidi. Wakamuacha Mata hapo, maana hapo palikuwa ni nyumbani kwake, nawao wakaenda makwao.



    ************************************



    Siku iliyofuta. Kituo cha polisi Mabawa.



    “Kwahiyo unataka kuniambia hukuona chochote kitakacho kuwezesha, kuanza upelelezi wako?"



    “Ndio Mkuu"



    “Sawa hii kesi wewe ishakushinda, vipi kuhusu huyo muhalifu aliekuwepo hospitali, umeenda kumuangalia?"



    “Hapana Mkuu, nilipanga nikitoka ndio niende nikamuangalie"



    “Sawa, unaweza kwenda, ila kumbuka kazi ya polisi sio ya kilelemama kama wewe unavyofanya, usione watu wana vyeo vikubwa, ukadhani wamevipata kwa kufanya kazi kitoto kama unavyo fanya kazi wewe, nimekupa kazi ndogo tu ya kufuatilia kesi ya mtu wa kawaida ila umeishindwa, je kama ungepewa kesi ya kufuatilia kifo cha mbunge? Si ndo unge omba uache kazi kabisa, siku nyengine inabidi utumie akili kufanya kazi, unaweza kwenda".



    Koplo Taure alipiga salut na kutoka nje ya ofisi ya Mkuu wake na kwenda hadi katika ofisi yake, alipofika alikaa kwenye kiti na kuanza kuwaza, aliona kama vile ameonelewa kupewa kazi kama hiyo ambayo kwake yeye aliiyona ni ngumu maana hakuwa na pakuanzia kwenye kuichunguza hiyo kesi.



    ******************************



    “Ndio dokta, unaweza ukaniambia hali ya mgonjwa wangu inaendeleaje?"



    “Amm!!! Mgonjwa wako hali yake sasa hivi, kidogo inaridhisha, jana usiku alizinduka akawa anapiga kelele tu, anaongea vitu vya ajabu ajabu, mara aseme wanakuja kuniua, mara aseme msimuue Mama yangu, mara aseme Msimuue Baba yangu, yani ni vitu ambavyo havieleweki, kwani huyo mtoto ana nini Afande?"



    “Dokta kama nilivyokuambia kuwa huyu mtoto sisi tumemkuta akipigwa na kundi la watu, kwahiyo bado hatujajua ana nini? Hapa tunamsubiria apone ndipo tukamuhoji kituoni".



    “Sawa nimekuelewa, tunaweza kwenda kumuona".



    Waliinuka wote na kuelekea hadi katika chumba alicholazwa Hemedy nakumkuta Hemedy akiwa bado amelala, kutokana na sindano za usingizi walizomchoma kipindi ambacho anasumbua, maana ilikuwa kila akiamka anasumbua kwa kupiga kelele, akidai wanataka kumuua kwahiyo anataka kuondoka zake.



    “Sasa dokta, ni lini ataruhusiwa kutoka hapa hospitali"



    “Kesho, Tutaangalia kama kesho hali yake itakuwa iko vizuri tutamruhusu"



    “Sawa hakuna shida, Kesho mimi nitakuja"

    Baada ya kuagana na daktari anaemtibu muhalifu wake, akaondoka na kulekea katika mizunguko yake anayoijua yeye.



    ****************************



    “Thatha tunafanyaje, maana nyaraka dhote tunadho, kilicho baki thithi ni kujimilikisha Mali dhote"



    “Itabidi tutumie mbinu ambayo itatufanya tusijulikane" Mrutu aliongea.



    “Thatha mbinu hiyo ni ipi? Embu tuambie mawadho yako Bwana Mrutu"



    “Mnajua tunatakiwa tufanyeje?" Mrutu aliongea na kuwaangalia wenzake, akawaona wote wapo makini kumsikiliza yeye. Akaendelea. “ Mata utajifanya kama vile ndie mmiliki wa mali za mzee Mheshimiwa, ila ulimuchia awe mkurugenzi au msimamizi tufanye, wewe ukiwa umeenda nje ya nchi kwajili ya mambo mengine, na kama Mahakama ikitaka ushahidi, basi tuta waonyesha karatasi aliyoiyandika mara ya mwisho kabla ya kifo chake, kwani ile karatasi si aliandika kuwa malizote sio zake na akaweka hadi na saini yake?" Mrutu alitoa maelezo hayo mafupi na kuwauliza swali.



    “Ndio alipiga hadi saini" wakajibu wote kwa pamoja.



    “Safi, sasa kwa vile watu walikuwa wanajua mimi ni ndugu yake, siku tutakayoenda mahakamani, nitasema kuwa ni kweli, Marehemu Mheshimiwa mali zote zile hazikuwa zake kama watu wengi wanavyodhani, ndio hapo sasa wakitaka ushahidi ndipo mtakapo itoa ile karatasi, tena itabidi ipigwe kopi, halisi muwe nayo nyie na ile kopi nitakuwa nayo mimi, baada ya hapo tunaiyonyesha mahakama, bila shaka mahakama watakubali tu, kwasababu ushahidi upo na pia saini ni ya mwenyewe ipo".

    Kicheko cha furaha kilizuka ghafla baada ya ya Mrutu kuhitimisha mbinu watakayo itumia kuzichukua mali za marehemu Mzee Mheshimiwa kiulaini.



    “Aitheee nimefurahi thaaaana, dah thiamini kama ungetoa mpango kama huo, hapo thatha ndio ninakubali kwamba familia yenu inaakili thana" Mata aliongea huku akiwa na furaha ya waziwazi.



    “Sawa, tuachaneni na hayo kwanza, vipi kuhusu ile nyumba ya Mzee Mheshimiwa? Maana imefungwa na polisi kwajili ya usalama na funguo wanazo wao" Moto aliongea.



    “Kuhusu ile nyumba, hakuna tatizo kwasababu mimi ni ndugu yake, nitaenda polisi na kuichukua funguo, si umesema kituo kinachoisimamia hii kesi ni hapo kituo cha polisi mabawa?" Mrutu alimuuliza Moto, maana Moto yeye ndo aliyeiyona taarifa ya habari kuhusu kifo cha Mzee Mheshimiwa na maelezo yote yaliyotolewa aliyaskia pia.



    “Ndio"



    “Basi hakuna shaka, mimi nitaenda kesho, kuchukua funguo"Mrutu aliongea.



    “Na vipi kuhusu kumtafuta huyu mtoto?"



    “Mtoto atapatikana tu".



    Baada ya kuhitimisha kikao hicho, kila mmoja akaenda kwake, kwaajili ya kuitafuta kesho yake. Wakaenda kulala.



    *******************************



    Majira ya asubuhi, Koplo Taure alienda hadi hospitalini, akamuulizia dokta anaemuhudumia Hemedy, kwavile ameshazoeleka ma manesi wa hapo, tangu sikuile alipo mleta Hemedy akiwa hajiwezi, manesi walimuambia kuwa dokta yupo afisini kwake, akaongoza njia hadi ofisini kwa dokta, alifungua mlango akamkuta.



    “Karibu Afande"



    “Nishakaribia, dokta mgonjwa anaendeleaje?"



    “Tumshukuru mungu, maana hali yake leo inaridhisha, unaweza pia ukaondoka nae, twende ukamuone"

    Waliongozana hadi katika chumba alicholazwa hemedy, na kumkuta akiwa yupo macho. Hemedy siku hiyo hakuleta taabu kama siku zote alizokuwepo hapo hospitali anavyofanya, Koplo Taure aliruhusiwa kuondoka nae. Moja kwa moja akaenda nae hadi kituo cha polisi, walipo fika Koplo Taure, kwakuwa ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu asubuhi, Inspekta Ganjo hakuwa bado hajafika kituoni hapo, ikabidi amuache hemedy Mapokezi, ili ahojiwe na Afande jesca.



    Wakati huo huo nae Mrutu alikuwa anaenda hapo hapo kituo cha polisi kwenda kuchukua funguo za nyumba ya kaka yake marehemu Mzee Mheshimiwa, alikuwa anaenda hapo hapo mapokezi alipokuwa Hemedy akihojiwa.





    Hemedy baada ya kuchukuliwa maelezo mafupi na Afande jesca, alichukuliwa na kupelekwa hadi selo, akafungiwa humo.

    Mrutu alipo fika kituoni, kabla hajafika mapokezi akakutana na Koplo Taure.



    “Afande Taure, Vipi?"



    “Poa, niambie Mrutu"



    “Fresh tu kaka"



    “Pole na msiba bwana, sikuwahi kuhudhuria msibani,maana nilikuwa nina kesi niliyopewa niifuatilie, sasa ile ndio imenifanya nisifike msibani"



    “Usijali Afande nishapoa, vipi lakini uko poa kabisa?"



    “Namshukuru Mungu, niko poa kabisa, sijui wewe?"



    “Hata mimi nashukuru Mungu, Tumeshamzika kaka yangu, ila ndio hivyo si unajua kila nafsi itaonja umauti, kwahiyo hakuna budi kumuombea huko alipo, mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi kaka yangu" Mrutu alikuwa akiekti mbele ya Afande Taure, alijifanya anahuzuni nyingi kuondokewa na kaka yake, ila kwa vile usilo lijua ni sawa na usiku wa giza, Koplo Taure akamfariji.



    “Usijali Mrutu, hiyo yote ni mipango ya mungu, leo kwake kesho kwetu, kila mmoja atakufa, kwahiyo usihuzunike sana"



    “Asante Afande"



    “Umekuja kuifuatilia kesi ya kaka yako? Au kuna mengine umefuata?"



    “Ndio, ila pia nimefuata funguo za nyumba ya marehemu"



    “Dah, kichwa kina mambo mengi, funguo zipo ila zipo kwa Mkuu labda tumsubirie kidog...... Basi huyo apo anakuja" Koplo Taure na Mrutu walikuwa wanajuana sana, kujuana kwao kulianzia siku Mzee Mheshimiwa, alipokuja hapo kituoni katika enzi za uhai wake, kuja kufuatilia kesi yake ya madai ya kudhulumiwa kiwanja chake kilichokuwa huko Mwang'ombe, alikuja na Mrutu, Mzee Mheshimiwa aliingia hadi ndani ila Mrutu alibaki nnje, ndipo hapo alipo juana na huyu Afande Taure, baada ya kuanza kupiga stori kujuana.



    Inspekta Ganjo alipofika karibu yao, walimsalimia kutokana wote amewazidi umri, baada ya hapo wakaambiwa wamfuate ofisini kwake, wote watatu waliongozana hadi ilipo ofisi ya Inspekta Ganjo, waliingia ndani baada ya mlango kufunguliwa, walipewa ruhusa ya kukaa baada ya Inspekata Ganjo kukaa, na wao walikaa.



    “Enhee, namiskiliza"



    “Mkuu, huyu ni ndugu yake na marehemu Mzee Mheshimiwa, amekuja hapa kuifuatilia kesi ya kaka yake halafu pia anataka funguo za ile nyumba"



    “Sawa, kwani wewe umeshamuambia chochote?"



    “Hapana Mkuu"



    “Ok, bwana nani vile" Inspekta Ganjo aliongea huku akimuangalia Mrutu usoni, Mrutu alianza kuwa na wasiwasi, hakujua hicho chochote alichotakiwa kuambiwa ni kitu gani, akadhani siri yao imegundulika, hiyo ikampelekea kuanza kutetemeka, akijua amejileta mwenyewe kwenye mdomo wa mamba.



    “Mrutu" alijibu kiuwoga.



    “Ok, bwana Mrutu, kesi ya kaka yako bado uchunguzi unaendelea, na tutajitahidi kuwasaka popote walipo hao majambazi waliyo fanya hivi, na nina kuhakikishia tutawapata tu kwahiyo usijali kwa hilo.

    Inspekta Ganjo hakujua akiongea hivyo ndio anazidi kumpa wasiwasi Mrutu, ambae alikuwa anahusika na tukio la kuondoa roho za familia ya kaka yake.



    “Vipi mbona unatetemeka hivyo?" Koplo Taure alimuuliza Mrutu.



    “Muache atetemeke tu, huo ni uchungu wa kuondokewa na Kaka yake na familia nzima, hata kama ingekuwa ni mimi pia ningekuwa katika hali hii, ila usijali Mr Mrutu tutawapata tu wauwaji.



    Mrutu alikuwa anatetemeka kweli baada ya mkuu wa kituo kusisitiza kuwa wata watafuta waliyo fanya mauji, ila alizidi kutetemeka baada ya Koplo Taure kumuuliza swali kuwa mbona anatetemeka, hakujua angemjibu nini, ila alimshukuru kimoyo moyo, Inspekta Ganjo baada ya kumjibia.



    “Dah, nyie acheni tu, kufiwa na kaka ambae ndie nilikuwa namtegemea kwa kila kitu, inauma sana, yan......" Hakuweza kumalizia sentensi yake, akaangua kilio cha kuigiza mbele ya hao maaskari ili kuzidi kuwapoteza, ni kweli alifanikiwa kuwapoteza maana walianza kumbembeleza, baada ya dakika kadhaa waliwafanikiwa kumyamazisha Mrutu aliekuwa analia kilio cha kuigiza.



    “Pole Mr Mtu, funguo hizi hapa" Insepekta Ganjo alimpa funguo Mrutu, baada ya kuzi pokea akaaga, akaondoka zake.



    “Mkuu, halafu na yule muhalifu aliekuwepo hospitali, leo ndio ameruhusiwa kutoka"



    “Yupo wapi?"



    “Yupo selo"



    “Umesha muhoji?"



    “Hapana Mkuu, ila amechukuliwa maelezo mafupi na Afande jesca"



    “Ok, nenda ukamuhoji sasa hivi"



    “Sawa Mkuu" Koplo Taure, aliinuka katika kiti achokaa, akapiga salut na kutoka hadi nje ya ofisi ya Mkuu wa kituo.



    *****************************



    Mrutu, baada ya kutoka kituo cha polisi, alielekea hadi katika nyumba ya marehemu kaka yake, alipofika akafungua geti na kuzama ndani, alifika hadi katika mlango mkubwa wa kuingilia humo ndani ya nyumba, aliufungua na kuingia ndani, alipoiyangalia seble hiyo, akakumbuka vitu vingi, akakumbuka kuwa ni yeye ndo alimshauri kaka yake, anunue kiwanja hicho kichokuwa maeneo hayo ya Donge, akakumbuka kuwa yeye ndo aliemshauri kaka yake, ajenge nyumba ya dizaini hiyo, akakumbuka alivyoambiwa aishi hapo baada ya nyumba kukumilika, akakumbuka walivyokuwa wakiisha kwa furaha, amani na upendo, akakumbuka alivyopewa uhuru na kaka yake wa kufanya chochote kile ndani na nje ya nyumba hiyo, akakumbuka alivyojengewa nyumba yake maeneo ya Mikanjuni, akakumbuka alivyopewa mtaji na kaka yake huyo aliechangia kumfanyia UHASAMA, akakumbuka mtaji aliyopewa na kaka yake ulivyo mpatia maendeleo hadi ikawa na yeye anajitegemea.



    Alivyokumba wema wote aliofanyiwa na kaka yake, nafsi yake ilimsuta, ili mdhihaki, akaiyonea aibu nafsi yake, akawalaumu waliomshawishi kumfanyia UHASAMA kaka yake, ila yote kwa yote akailaumu nafsi yake, hatakama alipewa mtaji na kaka yake na kumfanya na yeye ajitegemee, ila hiyo haikuweza kumfanya aombe kitu kwa Mzee Mheshimiwa halafu anyimwe, Mzee Mheshimiwa alimpenda kama mdogo wake, japokuwa walizaliwa na baba mmoja ila mama tofauti, ila Mzee Mheshimiwa alimchukulia kama mdogo wake wa kuzaliwa nae tumbo moja.



    Bila kutarajia machozi yalianza kumtoka, safari hii alikuwa analia kweli, alikuwa haigizi kama alivyofanya kituoni mbele ya Inspekta na Koplo Taure, alilia sana, alijuta, alijilaumu, aliilaumu nafsi yake kwa tamaa zilizo muingia, alitamani siku zirudi nyuma ili arekebishe alipokosea, ila haikuwezekana, alitamani iwe ni ndoto ya kusisimua halafu baada ya mda mfupi azinduke kutoka usingizi, akute mambo yote yalikuwa ni njozi tu, ila haikuwa hivyo.



    Baada ya kulia sana na kujuta sana, alifuta machozi na kujipa moyo kuwa yaliyotokea yameshatokea, hakuwa na uwezo wa kuyabadilisha, hata hivyo, alipo waza kuwa muda si mrefu na yeye ataenda kuwa tajiri kwa mali za kaka yake watakazo kwenda kugawana, tabasamu la huzuni likamjia usoni mwake.



    “Nisijipe mawazo sana, hata hivyo ilipangwa afe ili mimi ni nufaike na mali zake, nadhani hata yeye huko alipo atakuwa na furaha akiona mali zake naziendeleza mimi"

    Alijifariji kwa mawazo yake potofu, baada ya yote alifunga mlango na kutoka hadi nje, alipofika hadi nje, alitabasamu baada ya kuona magari matano yamepaki sehemu maaulumu ya kwenye hiyo nyumba. “Itabidi nichukue gari moja, nifanye la kutembelea" aliwaza na kuendelea na safari yake hadi kwenye geti, akalifungua, akatoka nje, akafunga geti vizuri na kuondoka zake.



    Safari yake iliishia nyumbani kwa Mata, alipo fika akamkuta na Moto pia yupo, akawaelezea kila kitu alichokifanya kwa siku hiyo, kuhusu mpango wao, akaelezea alivyoenda hadi kituo cha polisi, akaelezea hadi alipo lia machozi ya kuigiza mbele ya askari, ila hakuelezea alipo lia machozi ya kweli nyumbani kwa marehemu kaka yake, hilo akalinyamazia, hakutaka kuoneka mnafki. Akanyamaza.



    “Hahahhahaha yani wewe unafaa kabitha kuwa muigidhaji, umelia hadi mbele ya athkari, kwa hapo nakupa hongera"Mata aliongea.



    “Ilikuwa ni lazima iwe vile ili niwazuge"



    “Kwahiyo funguo unayo hapo?"Moto aliuliza.



    “Ndio wamenipa"



    “Umehakikisha ndio hiyo yenyewe? Thi unajua tena kwamba polithi hawaaminiki"



    “Walivyo nipa nimeenda hadi kwenye ile nyumba kuhakikisha, ndio yenyewe"

    Wakati wanaongea Moto alikuwa yupo kimya, alioneka kama kuna kitu ana waza, ikabidi wamuulize.



    “Vipi Moto mbona unaonekana unamawazo, kuna nini?" Mrutu aliuliza.



    “Kuna kitu nimekumbuka"



    “Kitu gani hicho? Ndo utuambie thatha"



    “Ni kuhusu yule mtu niliemuona nyumbani kwa marehemu Mzee Mheshimiwa, wakati naenda kufuata ile video"



    “Thatha ndo ana nini" Mata aliuliza kwa wasiwasi.



    “Mimi nahisi itakuwa ni Polisi, maana ile siku niliyo enda, nilijaribu kufungua geti ila nikakuta limefungwa na kufuli, ikamilazimu niruke ukuta, ila baada ya kuingia yule mtu, mimi nilipo pata upenyo wakutoka, nikaenda getini na kukuta geti lipo wazi, hicho ndo kilichonifanya nihisi yule atakuwa ni polisi, maana polisi wao ndo walilifunga lile geti kwa kufuli lao".



    “Sasa kinachokufanya uwe na mawazo ni nini? Wakati funguo tunazo sisi"Mrutu aliuliza.



    “Hapana sio hvyo, mimi nilikuwa naumiza kichwa kuwa, ni nani yule mtu, ila tayari nishapata jibu, ila mimi nashauri tusitumie tena lile kufuli"



    “Kwa hilo usijali"



    Walihitimisha maongezi yao, na baada ya hapo Mrutu alitoka na kumuacha Moto akiwa bado yupo nyumbani kwa Mata, yeye aliondoka na kwenda katika shuhuli zake.



    *********************************



    Koplo Taure, alienda hadi mapokezi na kuchukua funguo za selo aliyomo Hemedy, alipofungua alimtoa hemedy akampeleka hadi katika ofisi yake, kwajili ya kumuhoji maswali.



    “Dogo, naomba uniambie ukweli, ukweli wako ndo utakufanya utoke hapa polisi, umenielewa?"



    “Ndio Afande" Hemedy japokuwa alikuwa na umri mdogo, ila aliijua polisi, alijua kuna kuhojiwa, alijuwa pia kuna kupigwa kama hutoenda sawa nao, na yeye kwavile alikuwa hataki kupigwa, akapanga kujibu yote atakayo ulizwa.



    “Jina lako ni nani"



    “Hemedy"



    “Huna baba" Koplo Taure alimuuliza kwa hasira za kuigiza ili kumtisha.



    “Mheshimiwa, Afande"



    “Nakuuliza kwa mara ya mwisho, sitorudia tena, Jina lako ni nani"



    “Hemedy Mheshimiwa"



    Koplo Taure baada ya kusikia jina hilo, alishtuka, ila hakutaka kuunyosha mshtuko wake mbele ya Hemedy.



    “Dogo, unajua mimi sipo katika utani, na kama nilivyo kuambia mwanzo ukweli wako ndo utakuokoa, Jina lako halisi ni nani? Nimekupa nafasi ya upendeleo kukuuliza kwa mara nyengine, ila mimi sina kawaida ya kuuliza swali moja zaidi ya mara mbili, kwahiyo naomba uniambie ukweli"



    “Afande, jina langu halisi ni hilo, na wala sijakudanaganya, kweli afande"



    Koplo Taure alichanganyikiwa, hakuelewa amuulize swali gani, kutokana na jina la baba wa huyo mtoto kumchanganya, Mzee Mheshimiwa alimjua vizuri, ila hakuijua familia yake, mawazo mengine yalimtuma kuwa huenda ikawa mtoto huyu aliopo mbele yake ni mtoto wa marehemu Mzee Mheshimiwa aliesemekana ametekwa na majambazi yaliyo vamia nyumbani kwao, ila hakutaka kulipitisha wazo hilo, akadhani majina huenda ikawa yame fanana tu.



    “Ok, nisubiri hapa nakuja sasa hivi"

    Hemedy alishikwa na wasiwasi, akajua Koplo Taure amekasirika na hapo ameenda kuchukua vifaa vya mateso, ila hakuwa na jinsi ikabidi atulie aone mwisho wake.



    Koplo Taure baada ya kutoka katika ofisi yake aliyomuacha Hemedy, akaelekea moja kwa moja hadi katika ofisi ya Inspekta Ganjo, alipofika alipiga salut na kutulia.



    “Enheee niambie"



    “Mkuu, yule mtuhumiwa ameongea kitu ambacho kimenishangaza sana"



    “Kitu gani? Embu nieleze"



    “Amesema kuwa yeye ni mtoto wa Mheshimiwa"



    “Sasa tangu lini, Mzee Mheshimiwa akawa na mtoto mkubwa, mtoto wake ni mdogo bwana, itakuwa umefananisha majina tu"



    “Hapana Mkuu, hata huyo pia ni Mtoto mdogo"



    “Unasemaje? Embu twende nikamuone"

    Waliotoka hadi nje ya ofisi, na kwenda kwenye ofisi ya Koplo Taure, walipofika wakanyonga kitasa na kufungua mlango, mlango ulipofunguka wote walipigwa na butwaa, hawakuamini macho yao kwa walichokiona hapo.







    Hali ya Hemedy ili badilika ghafla, kifua chake bado kiliendea kumsumbua, bado kilikuwa na itilafu kutokana na kipigo alichopokea kutoka raia wenye hasira kali wakidhani ni mwizi, Koplo Taure na Insepekta Ganjo, walipoingia walimkuta akikohoa sana hadi machozi yalimtoka, Inspekata Ganjo, alimsogelea na kumuinua kichwa ili amuangalie usoni, ndipo hapo alipo pigwa na butwaa jengine, alikuwa ni Hemedy mtoto wa rafiki yake, majeraha yaliyokuwepo usoni mwake, hayakuweza kumfanya asimtambue “Ndio yeye huyu" Inspekta Ganjo alisema hivyo, bila kuhoji chengine, alimbeba Hemedy hadi nje, alimpakia kwenye gari ya polisi, na kumuambia Koplo Taure aendeshe gari kuelekea Hospitali.



    Hospotali ya Tumaini..

    “Hali ya mgonjwa wenu sio mbaya sana, ila tatizo lipo kwenye kifua chake"



    “Sawa dokta, itachukua muda gani hadi kupona?"Insepekta Ganjo aliuliza.



    “Hapa hadi kupona kabisa, itachukua kama wiki moja, ila maombi yana hitajika, si unajua sisi tunaweza tukasema hali yake sio mbaya sana, ila pia mungu akamchukua hivyo hivyo, kwahiyo hapo kinacho hitajika sana ni maombi"



    “Hadi hiyo wiki atakapo pona kabisa, itagharimu shilingi ngapi"Inspekta Ganjo aliuliza.



    “Hadi hiyo siku atakapo ruhusiwa, ndio tutajua imegharimu shilingi ngapi"



    “Sawa dokta, ila naomba awe katika uwaangalizi mzuri, maana ni mwanangu huyu"



    “Usijali kuhusu hilo, hata kama ingekuwa sio mwanao, sisi tungempa huduma bora, kwasababu sisi tupo kwajili ya wagonjwa, kwahiyo usiwe na shaka"



    “Asante dokta, ila naomba nikaongee nae mara moja nimtoe wasiwasi"



    “Hakuna shaka, unaweza ukaenda"



    Baada ya kutoka katika ofisi ya dokta, walienda katika chumba alicholazwa Hemedy, Inspekta Ganjo aliamua kumpeleka katika hospitali binafsi ili apate matibabu kwa uwangalifu zaidi.



    “Baba naomba unisaidie, wataniua na mimi" Hemedy baada ya kumuona Inspekta Ganjo aliongea hivyo na kuanza kulia, alimuita baba kwasababu ndivyo alivyo zoea tangu kipindi cha marehemu baba yake Mzee Mheshimiwa.



    “Usijali mwanangu, hawatokudhuru tena, mimi nipo pamoja na wewe"Inspekta Ganjo alimuondoa wasiwasi huku akiwa amekaa kitandani akimshika shika kichwa chake, ili kumfariji.



    “Sawa, lakini usiondoke naomba tubaki wote"



    “Usijali mimi nitakuja, kwa sasa hivi wewe utabaki na daktari atakulinda pia, hawato kuua, umesikia mwanangu? Sito chelewa, itakuwa kila muda naja kukuangalia, kwa hiyo wewe usiwe na hofu"



    “Sawa"



    “Subiri niwaagizie wakuletee chai, ule basi maana hizo dawa unazotumia unatakiwa ule sana, ili upone haraka"



    “Sawa"



    Baada ya kuongea na Hemedy na kumtoa hofu, Inspekta Ganjo alienda hadi kwa daktari na kumuomba nesi mmoja atakae kuwa anamletea chakula mgonjwa wake, maana yeye anakazi nyingi kwahiyo hatoweza kila muda kumletea chakula, Dokta akamuita Nesi mmoja kwajili ya kuongea na Inspekta.



    “Maria, embu msikililize huyu mzee" dokta alimuambia nesi wake kwa jina la Maria, na yeye akamgeukia, Inspekta Ganjo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Samahani mama, nilikuwa nataka nikuachie maagizo kwamba mwanangu uwe unampelekea chakula wewe, maana mimi sina muda wa kuja kila saa hapa hospitali kwajili ya kuleta chakula, kwahiyo nilikuwa nataka nikuachie hela kidogo kwajili ya kufanya hiyo kazi"



    “Hakuna tatizo, wewe nionyeshe mgonjwa wako, mimi nitampa huduma hiyo" baada ya maongezi hayo Inspekta Ganjo alipeana mkono na Daktari, akaongozana na nesi hadi katika chumba alichokuwepo Hemedy, Inspekta Ganjo alimuonyesha nesi na kumuachia shilingi kadhaa, kwajili ya chakula cha Hemedy.



    Baada ya kutoka ndani ya hospitali, akanyoosha hadi katika gari la polisi walilokuja nalo, akamuamuru Koplo Taure, aendeshe gari kuelekea kituoni. Baada ya kufika walishuka wote na Inspekta Ganjo alimuambia Koplo Taure amfuate ofisini kwake.



    “Unajua kwamba yule mtoto ndio mtoto wa marehemu Mzee Muheshimiwa" Inspekta Ganjo haikujulikana ameuliza au ameongea, ikamfanya hadi Koplo Taure asijue ajibu ama aendelee kuskiliza, akakaa kimya.



    “Kwani wewe ulivyo muhoji, alikuambia kitu gani?"



    “Sikumuuliza chochote zaidi ya jina lake, alipo nitajia ndio nikashtuka nikaona nije kukuita wewe umsibitishe kama ndie, maana mimi simjui"



    “Sawa, basi jua kwamba yule ndio mtoto wa marehemu Mheshimiwa, aliesemekana kuwa ametekwa na majambazi walio vamia nyumbani kwao"



    “Ndio mkuu"



    “Itabidi tumpe taarifa baba yake mdogo, kuwa mwanae ameonekana au wewe una semaje?"



    “Itabidi iwe hivyo"



    “Sasa tutampataje?"



    “Anapo fanya kazi napajua, alishawahi kunipeleka"



    “Sawa, basi itabidi umfuate na kumpa taarifa hizi, maana itakuwa sio vizuri, mwanae yupo hospitali, halafu yeye hajui"



    “Ndio Mkuu"



    “Mfuate sasa hivi"



    Baada ya maongezi hayo, Koplo Taure aliinuka katika kiti alichokaa na kupiga salut na kutoka hadi nje, alipanda gari ya polisi na kwenda moja kwa moja hadi katika Duka la spea za magari, alilomiliki Mrutu, mdogo wake marehemu Mheshimiwa, alipofika alipaki gari pembeni, alishuka na kuenda hadi ndani ya duka hilo.



    “Za saa hizi broo?" Koplo Taure Alimsalimia kijana aliemkuta hapo dukani.



    “Salama Afande" kijana aliekuwa hapo dukani alijibu, alimuita afande baada ya kumuona ameshuka katika gari ya polisi.



    “Ok, nilikuwa namuulizia Mrutu, sijui nimemkuta?"



    “Bosi bado hajafika, na leo sijui pia kama atakuja"



    “Kwanini unasema hivyo?"



    “Nasema hivyo, kwasababu jana pia hakuja"



    “Basi sawa, acha mimi niende ila akija mwambie Afande Taure amekuja kumtembelea"



    “Sawa"



    “Au nipe namba zake za simu, ili nimtafute kwenye simu"



    “Sawa" Alimtajia namba zake, baada ya hapo Koplo Taure akashukuru na kuingia kwenye gari aliyokuja nalo, alipo ingia kwenye gari akajaribu kuzipiga hizo namba alizopewa, na kuambiwa kuwa mteja anaempigia hapatikani kwa sasa labda ajaribu tena baadae, hakuwa na chakufanya akaamua kuondoka zake.



    Alipofika kituoni, akaenda hadi kwa Inspekta Ganjo na kumueleza kila kitu na kuambiwa kuwa ajaribu tena kumpigia baadaye, baada ya hapo akatoka na kwenda hadi katika ofisi yake kuendelea na kazi nyengine.



    ********************************



    Mrutu siku hiyo simu yake ilikuwa imekufa berti, tangia asubuhi alikuwa yupo mjini akiingia katika maduka ya simu kutafuta betri jengine, alizunguka sana ila akafanikiwa kupata betri katika duka lililokuwepo katika uwanja mkubwa wa mpira wa Tanga, Mkwakani, linalo itwa G7, alivyopata betri, hakuta kwenda sehemu yoyote zaidi ya nyumbani kwake, alipofika akaliweka kwenye simu na kuiweka chaji, hakua na chengine cha kufanya, akaamua alale tu.



    Majira ya jioni aliposhtuka kutoka usingizini, akaenda kuangalia simu yake na kukuta imejaa chaji, akaichomoa chaji na kuiwasha, kitu cha kwanza kukutana nacho ilikuwa ni meseji zilizotumwa na kijana wake wa kazi anaeliangalia duka lake la spea za magari.



    Moyo wake ukashtuka baada ya kuisoma meseji hiyo, alianza kupatwa na wasiwasi usio wa kawaida, “Bosi kuna polisi amekuja kukuulizia hapa dukani leo asubuhi". Meseji hiyo ilimfanya aanze kuloa jasho mgongoni mwake, hakujua polisi huyo ni nani na alikuwa anataka nini.



    Akaachana na meseji hiyo na kuifungua nyengine, “ila amesema yeye ni rafiki yako, anaitwa Afande Teure sijui Taure, ila kitu kama hicho" baada ya kusoma meseji hiyo ya pili kutoka kwa kijana wake wa kazi, akashusha punzi ndefu baada ya kugundua kuwa alieenda kumuulizia alikuwa ni Koplo Taure, hapo hapo akampigia simu kijana wake wa kazi, ili kupata maelezo zaidi.



    “Hallo Bosi" sauti iliyotoka katika spika za simu iliskika.



    “Niambie kolo"



    “Shwari tu bosi"



    “Sawa, enhee embu niambie, leo amekuja askari kuniulizi hapo dukani?" Mrutu aliuliza swali la kipumbavu, kwasababu meseji aliziona na zilitoka kwa huyo huyo anaemuliza.



    “Ndio bosi, alikuja kukuulizia leo asubuhi"



    “Wewe ukamuambiaje?"



    “Mimi nikamubia kuwa haupo"



    “Haja acha maagizo yoyote?



    “Hapana hajaacha maagizo yoyote, zaidi tu aliniambia kuwa alikuja kukutembelea"



    “Ila kazi leo zimeendaje?"



    “Kazi kama kawaida"



    “Basi poa baadaye"



    “Sawa, ila bosi kwani kuna nini, mbona polisi asubuhi asubuhi?"



    “We kolo ni mpumbavu nini, kwani alivyokuja alikuambiaje?"



    “Aliniambia kuwa wewe ni rafiki yake na amekuja kukutembelea"



    “Sasa kinachokufanya ulize maswali mengi ni nini?"



    “Samahani bosi"



    Baada ya maongezi hayo Mrutu alikata simu, na kutuliza presha yake aliyokuwa nayo, akaenda kuoga ili kutoa uchovu aliokuwa nao, alipo rudi, akaikuta simu yake ina miskoli mbili, kabla hajajua ni nani aliye piga simu, simu yake ikanza kuita tena, alipoiyangalia akaona ni namba ngeni, akaipokea.



    “Halow" sauti nzito iliskika kwenye spika za simu.



    “Yes, halow" Mrutu nae akajibu.



    “Samahani, naongea na Mrutu hapo?"



    “Ndio, nani mwenzangu?"



    “Ni mimi Afande Taure"



    “Ooooh, kumbe ni wewe? Naskia leo umekuja dukani kwangu kuja kuniulizia, ulikuwa unataka nini?

    Mrutu aliuliza maswali mfululizo, Koplo Taure hakujua aanze kujibu lipi.



    “Ndio ni mimi bwana, nimekuja leo asubuhi dukani kwako nikaambiwa haupo, nilikuwa nataka nikupe taarifa"

    Moyo wa Mrtu ulipiga Paaaa!!!! Baada ya kuskia neno taarifa, hakujiamini, hakujua taarifa hiyo ni ya nini, akasubiri aambiwe.



    “Taarifa yenyewe ni......." Koplo Taure akamuelezea kila kitu kuhusu kuonekana kwa Hemedy.



    “Asante Afande kesho mimi nitaenda hapo hospitali kwenda kumuona"



    “Hakuna shaka"



    Baada ya kukata simu, mapigo ya moyo wa Mrutu yalikuwa yakienda kasi, akafikiria kuua tu, alijua kuwa Hemedy akipona, atahojiwa ilikuaje na yeye atasema kila kitu na kama kweli Flash ya video ya tukio la mauwaji ya wazazi wake anayo, basi hiyo itakuwa ndio ushahidi, kupelekea kukamatwa kwa wenzake, na wenzake watakapo kamatwa, wataadhibiwa ili wataje wenzao wengine na watamtaja tu na yeye, na hapo ndipo maisha yake yatakopo kwenda kumalizikia gereza la maweni, hakutaka iwe hivyo



    Akapanga kesho akifika hospitali, amuulie huko huko, akafikiria atamuua kwa njia gani, “nikifika pale namkaba hadi anakufa, mmmh!!! Ila mbona kama njia hiyo ni hatari? Nishapata wazo, itabidi afe kwa sumu, eeee njia hii ndo nzuri, itabidi nimtilie sumu kwenye chai nitakayo mpelekea asubuhi, hapo sawa".



    Alijiwazia mwenyewe njia ya kumuondoka Hemedy duniani kabla mambo hayaja haribika, alipopata wazo hilo la kutumia sumu atakayo iweka kwenye chai, endapo Hemedy atainywa basi itaondoka na uhai wake, aka lala na hilo wazo.



    Majira ya Asubuhi yalimkuta Mrutu akielekea hospitali aliyolazwa Hemedy ili akatekeleze azma yake aliyo ipanga ya kumuondoa Hemedy duniani. Alipofika akaelekea moja kwa moja hadi katika chumba alicho lazwa Hemedy, kwakuwa alishaelekezwa chumba na Koplo Taure, kwahiyo haikumpa shida. Alipofika Hemedy alianza kuangusha chozi, baada ya kumuona baba yake mdogo amekuja, alilia sana kuwa wazazi wake wameuliwa na majambazi, ikabidi Mrutu amnyamazishe, na baada ya muda Hemedy alinyamaza, bila kuchelewa, akampa chai yenye sumu ili anywe afe ili apoteze ushahidi.



    Hemedy bila kujua alianza na andazi akalitia mdomoni, baada ya hapo akachukua kikombe cha chai ili anywe........







    “Za saa hizi kaka"



    “Nzuri tu"



    “Samahani, nilikuwa namuomba huyu mgonjwa anywe hizi dawa, baada ya hapo ndio atakunywa chai"



    “Hakuna tatizo, ila si ungemuacha kwanza amalizie kunywa hiyo chai, halafu ndio atakunywa dawa?"



    “Hapana kaka yangu, yani hapa pia amechelewa sana, alitakiwa azinywe mapema sana"



    “Ok, hakuna tatizo"



    “Hemedy, vipi hali yako lakini?"



    “Nashukuru mungu, ila bado kifua kina maumivu kwa mbali"



    “Usijali mdogo wangu, utapona, haya kunywa dawa"



    “Asante nesi, huyo hapo unaemuona ni baba yangu mdogo"



    “Ohooo!!! Karibu, mimi ni nesi ninaemuangalia kwa kila kitu mwanao"



    “Asante nesi, asante sana"



    Hiyo ndo ilikuwa pona ya Hemedy baada ya nesi anae muuguza kutokea na kumtaka asinywe chai kwanza hadi anywe dawa, Mrutu hakuweka sumu kwenye maandazi aliyo ya nunua, ila sumu aliweka kwenye chai, kama Hemedy angeinywa chai iliyoletwa na baba yake mdogo, sidhani kama angeweza kupona. Mrutu alijilaumu kwanini hakuweka sumu na kwenye maandazi, ila hakujilaumu sana, akajua tayari ameshampata kwahiyo hakuwa na wasiwasi nae.



    Baada ya kupewa dawa na nesi, alizinywa na kusukumizia na maji. Baada ya kunywa dawa, nesi akamtaka sasa ndio anywe chai, ila kwa bahati mbaya ikawa chai iliyoletwa na Mrutu, ikawa imepoa, hawakuwa budi zaidi ya kuimwaga kwenye sinki la kunawia mikono lililopo humo humo chumbani.



    “Usijali, subiri nikamletee nyengine"



    Nesi baada ya kuongea hivyo alitoka hadi nje ya chumba alicholazwa Hemedy, kwenda kuchukua chai nyengine, baada ya muda alikuja na chupa na kikombe chengine cha chai.



    “Subiri nikuwekee chai unywe maana hizo dawa ulizokunywa zinahitaji ule sana ili ziweze kufanya kazi"



    “Sasa nesi si umuwekee tu humu humu kwenye hichi kikombe kilichokuwa na chai mwanzo, huoni kama hivyo itakuwa unachafua vikombe, wakati hiki cha mwanzo kipo?"



    “Usijali kaka yangu, hii kazi nimepewa na baba yake nimfanyie, kwahiyo kwangu sio shida"



    “Baba yake yupi aliekupa hiyo kazi?"



    “Sii huyu aliemleta hapa hospitali"



    “Basi hakuna shida"



    Baada ya mpango wake wa kutaka kumuondo duniani Hemedy kufeli, hakuwa na njia nyengine ya kufanya kwa hapo, akapanga kutumia njia nyengine, ikiwa hii ya kumpa sumu imeshindikana.



    Baada ya kumuona Hemedy, akamuaga na kumuahidi kurudi tena baadaye, akaondoka hospitali hapo na kuelekea kwake, kutafuta njia nyengine ya kumuondoa Hemedy duniani, kabla siri yao haija gundulika.



    Majira hayo hayo ya asubuhi, Inspekta Ganjo na yeye alienda hadi hospitalini kwajili ya kumuona Hemedy.



    “Shikamoo baba" Hemedy alimsalimia Inpekta Ganjo baada ya kumuona akiingia ndani ya chumba alicholazwa.



    “Marhaba mwanangu, hujambo?"



    “Sijambo"



    “Vipi hali yako inaendeleaje?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Nashukuru mungu, maumivu kidogo yamepungua ila kifua bado kinasumbua"



    “Usijali mwanangu, utapona kwa uwezo wa mungu"



    “Amina, halfu leo bamdogo kaja"



    Baada ya salamu walianza kupiga stori za muda mfupi na baada ya hapo, Inspekta Ganjo akamuaga Hemedy akaondoka chumbani humo, alipofika kwenye kordo alikutana na nesi anae muhudumia Hemedy na kumkabidhi kiasi chengine cha hela ili hemedy atakapo taka chochote ampatie, baada ya hapo aliondoka kuelekea kituoni.



    *****************************



    Mrutu baada ya kufika kwake, alifikiria njia nyengine ya kumuua Hemedy ila alikosa, akaona ni bora kuwashirikisha wenzake watafute njia ya kufanya ilikumuondoa Hemedy duniani haraka sana.



    Akachukua simu yake na kuwapigia wenzake ilikuwauliza mahali walipo, akawaambia kuwa wakutane nyumbani kwa Mata ili wapange namna ya kumuua Hemedy, Na yeye akajiandaa na kuianza safari hadi katika nyumba ya Mata, walipo pafanya sehemu yao ya kufanyia mikutano yao.



    “Kwahiyo yuko chini ya uwangalidhi wa polithi?"Mata aliuliza kwa hofu, hakika mtu huyu alikuwa anaogopa polisi kuliko kitu chochote..



    “Ndio"Mrutu alijbu.



    “Thatha itakuaje jamani, mbona kama vile kadhi hii inaenda ndivyo thivyo?"



    “Una uhakika kwamba hajawaambia chochote polisi?" Moto aliuliza.



    “Uhakika ninao"



    “Thatha wewe umehakikisha vipi?"



    “Mimi uhakika ninao, bado haja toa maelezo polisi, kwasababu najua tu polisi wangeniambia"



    “Thatha kwanini hajatoa maeledho hadi leo?"



    “Maelezo hawezi kutoa, kwasababu bado ni mgonjwa"



    “Ana nini kwani? Maana thithi thiku ile hatuja mgutha kabitha?"



    “Kwa maelezo waliyonipa kwamba, walimkuta akipagwa na kundi la watu wakidhani ni mwizi, kwahiyo hiyo ndio ilimpelekea hadi hali yake kuwa ni mbaya"



    “Dah, vipi huja muuliza kwamba flash yenye video kama anayo yeye?"



    “Hapana sikumuuliza"



    “Kwanini sasa huja fanya hivyo? Inatakiwa tupate uhakika kwamba flash yenye video anayo au hana?"



    “Sasa je kama hana? Maana mimi siku ile nilihisi tu ila sikuwa na uhakika"



    “Hata kama hana hiyo flash, inabidi afe tu"



    “Thawa, inabidi tupange mpango wa kumuulia kule kule hothpital, kabla hali yake haijaimarika"



    “Nime liona hilo ndio maana nimekuja hapa, tupange jinsi ya kumuua kule kule hospitali"



    “Mimi naona tumpe daktari petha, ili amchome thindano yenye thumu, halafu akiulidhwa atheme hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya, ikapelekea hadi kifo chake, au nyie mna themaje?" Mata alitoa wazo lake na kusubiria majibu kutoka kwa wenzake.



    “Hapana, hapo Mata mimi sikuungi mkono, hiyo njia yako ni hatari mno"



    “Kwanini?" Mata aliuliza



    “Je kama ikigundulika kwamba amechomwa sindano ya sumu, si huyo daktari atatafutwa, akipatikana si atatuja, sasa itakuwa ndio tume fanya nini?" Mrutu alionyesha wasiwasi wake.



    “Thatha wewe hii njia yangu umeikataa, je ile yako ya kumpelekea chai yenye thumu halafu angekufa, wewe thi ndo ungeshikiliwa, maana wewe ndio wakwandha kumpa kitu ale, bathi moja kwa moja ungekamatwa tu"



    “Dah! Hata hivyo pia namshukuru mungu haijatokea, maana sijui ingekueje?"



    “Thatha tufanye nini?"



    “Mimi nitaenda hospitali kumuua" Moto aliongea, wote wakamtizama yeye kwa mshangao.



    “Enhe tuambie utaendaje? ukumbuke yule mtoto anaijua sura yako vizuri, maana sikuile wakati mnavamia pale kwao hamkuvaa hata maksi ili kuziba nyuso zenu"



    “Hadi nimesema hivyo basi ujue nimesha fikiria yote hayo"



    “Haya tuambie hiyo njia yako uliyoipata" Mata alisema.



    “Ni hivi........" Moto aliwaelezea Mpango mzima atakao enda kuufanya, aliwaelezea mwanzo hadi mwisho.



    Wote wakajikuta wanacheka kwa furaha, na kumsifia Moto kuwa anaakili sana.



    “Dah! Yani katika thiku uliyoongea na nikakuelewa bathi jua ni leo, yani leo umeongea kitu ambacho kime nifanya nikuone unaakili thana kuliko hata aliegundua petha, dah! umenifurahisha thana"



    “Moto sio siri hata mimi huo mpango wako nimeukubali na ninauunga mkono kwa asilimia zote"



    “Ndo hivyo sasa"



    “Thatha utaifanya lini hiyo kadhi na thaa ngapi, maana nina wahka wa kujua itafikia wapi, dah! thio thiri huyu mtoto ananichanganya thana"



    “Yani nyie msijali, cha msingi ni kuomba mungu mpango utiki tu, si mna jua hata mchawi anapoenda kuwanga sehemu na yeye anamuomba mungu asikamatwe"



    “Itabidi ikitiki hii ishu, tufuatilie zile mali ili tuzichukue haraka iwezekanavyo"



    “Hata mimi niliwadha hivyo hivyo, maana nishachoka kutembelea kile ki Verostha, nataka na mimi nitembelee V8, nataka na mimi nionekane mtu mbele ya watu"



    “Yani nyie msijali, chamsingi nikuomba mpango ufanikiwe tu, mbona yote hayo yatatokea"



    “Sasa jamani acha mimi niwaache, nielekee dukani, maana tokea juzi sijaenda kabisa" Mrutu aliwaaga wenzake.



    “Itabidi tuondoke wote" Moto aliongea.



    “Thatha kwahiyo mimi ndio mnaniacha peke yangu?"Mata aliuliza.



    “Wewe ulikuwa wataka uwende wapi wakati hapa ndio kwako"



    “Hapana mimi thija themea kuondoka, ila nichothemea mimi kwamba mna ondoka nyote thi bora Moto angebaki tupige wote thtori"



    “Tunge baki ila mimi nataka nikauanze leo ule mpango"



    “Anhaa! Kama ndio hivyo thawa"



    Mrutu na Moto waliondoka nyumbani kwa Mata, walipanda kwenye gari alilokuja nalo Mrutu, Mrutu aliamua kuchukua gari moja kama alivyosema, wakaondoka na kuelekea moja kwa moja hadi dukani kwa Mrutu. Baada ya kukaa sana dukani hapo Moto alitaka kuondoka ili kwenda kuanza mpango walio upanga.



    “Sasa Mrutu acha mimi nikuache ili niufatilie ule mpango"



    “Usijali kwa hilo wewe nenda tu"



    “Basi poa acha mimi niwahi"

    Baada ya kuagana na Mrutu, Moto aliondoka zake kwenda kuanza huo mpango.



    Majira hayo hayo ya mchana, Inspekta Ganjo alifunga safari hadi hospitali, kwenda kumjulia hali Hemedy, baada ya kupata muda kidogo, alipofika aliingia hadi katika chumba alicholazwa Hemedy nakumkuta akiwa anakula chakula alicholetewa na nesi.



    “Nakuona mwanangu unakula tu, hata unikaribishi"



    “Nikukaribishe vipi wakati mimi ni mgonjwa natakiwa nile sana ili dawa zifanye kazi, au unadhani mimi nataka kukaa hapa hospitali kila siku, mimi nishachoka harufu za madawa"



    “Nikumshukuru mungu maana hali yako sasa hivi sio mbaya sana, tofauti na mwanzo, hata uchangamfu wako naona pia umerudi tena, naona leo unaongea kama kawaida yako, ila sasa utundu wako usiulete hadi kwenye dawa, unatakiwa dawa uzimnywe, usilete ujanja ujanja kabisa, au wewe hutaki kutoka hapa hospitali?



    “Mmh!!!! Mimi nataka kuondoka hata sasa hivi, au kwanini baba usiwaambie nikamalizie dawa nyumbani?"



    “Hapana inabidi ukae hapa hapa hadi utakapo ruhusiwa, unataka kuondoka leo je ukifika nyumbani ukizidiwa itakuaje?"



    “Ila mimi nishachoka kuchomwa sindano kila muda, yani sasa hivi hata kukaa viziri pia siwezi kwajili ya kuchomwa masindano tu"



    “Hahahahah, Usijali utatoka tu hospotali, na hayo masindano yataisha pia"



    “Sawa nimekuelewa, ila mama yangu na baba yangu tayari wameshazikwa?"



    “Tayari tumeshawazika, chamsimgi sasa hivi ni kuwaombe kwa mungu tu, awaepushe na adhabu zake"



    Hemedy baada ya kuambiwa hivyo, aliacha kula chakula na kuanza kulia aliwakumbuka wazazi wake, ili bidi Inspekta Ganjo, aanze kum'bembeleza, ilichukua kama dakika kumi na tano ndipo Hemedy akanyamaza, Inspekta Ganjo hakuwa na muda wa kuendelea kubaki hospitali, akamuaga Hemedy na kuondoka zake.



    ******************************



    Majira ya usiku mishale ya saa Nne, alionekana mwanaume alievalia mavazi ya kidaktari, alikuwa amebeba kisahani kilicho kuwa na bomba la sindano na na kichupa cha dawa, aliingia kwenye chumba alicholazwa Hemed, alipoingia alifunga mlango vizuri na kumsogelea Hemedy hadi karibu yake huku akitabasamu, alipomfikia karibu kabisa, alishusha suruali aliyoivaa Hemedy, upande wa kalio lake la kushoto na kufanya kalio la Hemedy lionekane vizuri.



    Alichomoa bomba la sindano na kulikita katika kichupa cha dawa, akainyonya dawa kidogo na kulichomoa bamba kwenye kichupa, baada ya hapo alilipeleka bomba la sindano hadi kwenye kalio la la kushoto la Hemedy, na kulichoma, alihakikisha dawa yote imeingia ndani ya ngozi ya hemedy, akalichomoa na kutabasamu tena, “Nime maliza kazi" Alisema hivyo na kuondoka zake......







    Mtu yule alifungua mlango akatoka nje ya chumba alicholazwa Hemedy, kwenye kordo alikutana na nesi anae muuguza Hemedy.



    “Dokta Imamu, tayari ushamchoma sindano mgonjwa wangu?"



    “Kazi nimeshamaliza, kwahiyo hapa kilichobaki mimi nikuondoka zangu tu maana ninausingizi mwingi sana"



    “Asante dokta Imamu, maana nilikuwa ninakazi nyingi sana hadi nikahofia kupitisha muda wa kumchoma sindano"



    “Usijali, kawaida tu"



    “Vipi, amelala au yupo macho"



    “Nimemuacha huko ndani, yupo macho"



    “Dah! Asante sana dokta kwa kunisaidia, acha basi mimi nikamuangalie mara moja, haja kusumbua lakini?"



    “Hapana, haja nisumbua kabisa, inavyoelekea haogopi sindano kabisa?"



    “Hahaha humju vizuri tu yule mtoto, nimsumbufu kweli yani"



    “Sasa mbona kwangu hajaleta usumbufu?"



    “Nahisi labda itakuwa amekuogopa ila mimi ananisumbua sana"



    “Hahahah Ila anavyoonekana ni mtundu sana"



    “Weee!!! Yani acha tu, halafu anaongea sana, sikumdhania kama atakuwa anaongea vile, yani kila muda natamani nikae nae tu"



    “Haya bwana, angalia asije akakufanya ukawasahau wagonjwa wengine"



    “haiwezi kutokea, mimi nakua nae muda ambao sina kazi"



    “Acha mimi niende maana ninausingizi mwingi sana"



    “Poa we nenda, acha mimi nimfuate"

    Baada ya kuagana na Dokta Imamu, alienda hadi katika chumba alichokuwemo Hemedy, nakumkuta amelala kifudi fudi.



    “Hemedy huo ndio ulalaji gani?" Nesi Maria alimuuliza huku akicheka.



    “Dada maria we acha tu, ili lijamaa lilokuja linaroho mbaya kumshida Iddi Amini"



    “Hahahahah, kwanini?" Nesi maria alimuuliza huku akiwa bado anacheka.



    “Yani linakuja huku liki tabasamu, lilipoanza kunichoma sindano, likaondoa tabasamu, aisee limenichoma sindano ya tako lakini nimeisikia hadi kwenye moyo"



    Hadi hapo Nesi Maria hakuweza kukizui kicheko chake, akacheka kwa sauti ya juu hadi sauti yake ikasambaa chumba kizima.



    “Yani siku nyengine akija kunichoma yeye sindano, nitakataa labda nianze kumchoma mimi kwanza ili ajue maumivu yake, mwenyewe nishakuzoea wewe ukija kunichoma unanimbia nyimbo hadi ukinichoma sindano si isikii kabisa"



    “Kwenda zako huko, itabidi asaivi nimpe yeye ndo akuchome maana mimi unanisumbua, ila unanifurahisha sana we mtoto, yani ukiondoka sijui itakuaje, maana nishakuzoea na vituko vyako"



    “Kwani wewe unapenda niendelee kubaki?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Ndio, ila sasa ndio hivyo haitowezekana, maana inabidi uondoke tu"



    “Mimi sitaki kubaki hapa hospitali, maana naliogopa lile lijamaa linaweza siku nyengine likanichoma sindano hadi nika paralaizi, halafu lilivyokuwa na sifa, lilivyomaliza kunichoma sindano, likasema eti nimemaliza kazi, likaondoka huku likitabasamu, yani hujui tu ila hapa nahisi kama vile sina matako, mi sitaki linichome tena sindano"



    “Usijali hatokuchoma tena"



    Nesi maria alikuwa anacheka tu muda wote kwa vituko vya Hemedy, alimfurahia huyo mtoto, alitokea kumpenda ghafla, alitamani kila muda awe nae wanapiga stori kama hivyo, ila muda mwingi alikuwa yupo na wagonjwa, ni muda mchache sana ndio alikuwa yupo frii, na aliutumia kuwa na Hemedy.



    * * * *



    Siku iliyo fuata. Mwafrika Phamarcy 5:03 asubuhi.



    “Za saa hizi dada yangu?" Moto alimsalimia dada aliemkuta mapokezi kwenye duka hilo kubwa la dawa na vifaa vya hospitalini.



    “Salamu tu, nikusaidie nini?"



    “Kuna vifaa navihitaji"



    “Ok, unaweza ukavitaja"



    “Nilikuwa nataka, mavazi ya kidaktari na bomba la sindano na kichupa cha dawa kilichokuwa kitupu"



    Dada wa mapokezi alimuangalia Moto kwa wasiwasi, hakuelewa mtu huyo anavitaka vitu hivyo ili akavifanyie nini, haikuwahi kutokea hata siku moja mtu wa kawaida kuja kununua vifaa vya hospitali, alishazoea kuona madaktari wa hospitali mbali mbali, kuja kununua vifaa vya hospitali, tena sio kimoja kimoja kama anavyotaka huyu mteja wake mpya, ila kwa vile wao wanataka hela, hakutaka kumuhoji, alichofanya yeye ni kuingia ndani, baada muda alirudi na vitu alivyo vitaka mteja wake.



    “Hivi hapa kaka"



    “Asanate, vyote hivi ni bei gani?"



    Moto alipoambia bei, akalipa na kuondoka zake, kuelekea nyumbani kwa Mata, alipofika akamkuta Mata amekaa sebleni anaangalia tivi.



    “Huwezi amini vitu vyote nimevipata, tena kwa urahisi, yani sikutegemea kabisa"



    “Embu nivione" Mata aliomba avione vifaa vya hospitali alivyo kuja navyo Moto, baada ya kuviona, waliamua wampigie simu Mrutu ili waje kupanga mpango utakavyoenda, baada kama nusu saa Mrutu alikuja hadi hapo nyumbani kwa Mata.



    “Kwahiyo sasa inakuaje" Mrutu na yeye aliongea baada ya kuviona hivyo vifaa.



    “Kama tulivyo panga, kuwa mimi nitajifanya mgonjwa wa tumbo, yani tumbo linaniuma sana, halafu wewe Mata utanipeleka hospitali hiyo hiyo aliyolazwa Hemedy, hata kama wasipoona ugonjwa unaonisumbua, Mata utawalazimisha wanipe kitanda ili waendelee kuiyangalia hali yangu, wakishanipa kitanda, itakuwa mpango wetu umeanza kutiki.



    Halafu hivi vifaa itabidi tuvitie ndani ya begi dogo, ambalo kwa juu nitaweka nguo zangu za kawaida, ikifika usiku, nitabadilisha nguo na kuvaa nguo za kidaktari, baada ya hapo, mimi nitaingia hadi katika chumba alicholazwa yule mtoto, baada ya kuingia humo, nitamchoma sindano yenye sumu hadi nihakikishe ame kufa, halafu kama kutakuwa na uwezekano wa kutoka usiku huo huo basi mimi nitaondoka zangu ila kama hakutokuwa na uwezekana huo, itabidi ni lale halafu asubuhi naondoka zangu.



    “Mbona katika maelezo yako umefanya kila kitu kuwezekana? Mrutu aliuliza.



    “Kivipi yani Sijakuelewa"



    “Umesema kuwa utajifanya unaumwa na tumbo, halafu wasipoona ugonjwa, itabidi Mata awalazimishe wakupe kitanda, je kama wasipo kupa kitandana? Unajua mimi jana huu mpango sikuuelewa vizuri, embu leo nieleweshe"Mrutu aliuliza.



    “Mrutu hakuna kigumu mbele ya hela, kwahiyo kama wakikataa tutawapa hela, mi naamni watakubali tu"



    “Sawa,hapo nimekuelewa, je hizo nguo utazibadilisha wapi? Maana unesema utabadilisha nguo ila hukusema utabadilisha wapi, embu nieleweshe na hapo"



    “Kwani vyoo si vipo? Nitabadilisha hata chooni"



    “Sawa, hapo pia nimekuelewa, umesema utamchoma sindano yenye sumu, je kama ukimkuta yupo macho? Huoni kama hiyo itakuwa ni hatari maana sura yako itakuwa anaikumbuka? Basi tufanye hatoikukumbuka sura yako, je utamshawishi vipi hadi akubali kuchomwa sindano nyengine, maana sindano ya dawa muda huo atakuwa tayari ameshachomwa na daktari" embu nieleweshe na hapo"



    “Itabidi nitumie nguvu tu kama atakataa kuchomwa sindano, yule ni mtoto hawezi kunizidi nguvu"



    “Sawa kama ndio hivyo mimi namitakia safari njema"



    “Embu jaribu hidho nguo tukuone"Mata aliongea.

    Moto bila hiyana akazivaa nguo za kidaktari alizo nunua kwajili ya kazi, hakika hakuweza kutofautishwa na daktari, kama akitokea mtu asiye mjua Moto, bila shaka atasema ni daktari mzoefu, kumbe elimu yake ni ya form four tu, hakuwa na taaluma ya udaktari wa aina yoyote.



    “Dah! Yani hapo kama vile daktari anaemtibu raithi, kuthema ukweli hayo mavadhi yame kupendedha" Mata alisifia.



    “Yani nikishapata hizi hela, itabidi nikasomee udaktari, halafu mata wewe si una miwani yako ile kama ya macho?"



    “Ndio ipo, tena thubiri nikailete" baada ya kuongea hivyo Mata alienda hadi chumbani kwake baada ya muda alirudi akiwa na miwani inayofanana na ya mgonjwa wa macho, akampatia Moto akaivaa, alikuwa na haki hata ya kujiita Profesa, kwajinsi alivyotoka, hakutofautishwa na daktari.



    “Thatha hapo umekamilika, embu tufanye haraka twendhetu huko hothpitali"



    Baada ya muda walijianda na kuianza safari ya kuelekea hospitali waka kamilishe mpango wao walio upanga, baada ya muda walikuwa nje ya hospitali aliyolazwa Hemedy.



    Kama ingekuwa Moto anaigiza katika Bongo Muvi, basi angejinyakulia umaarufu mkubwa sana, maana alikuwa ana ekti kama vile kweli, kwa mtu ambae hakuujua mpango wao, basi angemuonea huruma sana, alishika tumbo lake huku akilia, machozi yalimtoka katika macho yake.

    Manesi walimuwahi na kumuweka juu ya kitanda, na kuanza kumpeleka katika chumba cha matibabu, walipofika kwanza walimchukua vipimo, baada ya muda daktari alimuita Mata hadi katika ofisi yake ili aende kumpa majibu ya ndugu yake.



    “Mgonjwa wako tumempima na kugundua kuwa hana tatizo lolote"



    “Thatha dokta itakuaje athiwe na tatizo wakati mtu anaumwa vile, hata wewe mwenyewe pia umeona"



    “Ni kweli hata mimi pia nimemuona, ila vipimo vinaonyesha hana tatizo"



    “Thatha dokta itakuaje?"



    “Hapa inabidi tumpe dawa zitakazo tuliza maumivu, mimi nahisi itakuwa ni tumbo la kawaida tu na muda wowote linaweza likaacha"



    “Kwahiyo dokta unatakawa kumpa dawa tu hivi hivi?"



    “Sasa ulikuwa unatakaje labda?"



    “Mimi nilikuwa nataka mumpe kitanda hadi kesho muangalie hali yake kama itatulia bathi hakuna tatizo mutamruhuthu"



    “Sawa kama ndio unavyotaka, tutampa kitanda"



    “Bathi nashkuru daktari kwa mthaada wako"



    “Hakuna shaka"



    “Ninawedha kuenda kumuona mara moja?"



    “Unaweza kwenda"



    Baada ya kuagana na daktari, alitoka katika ofisi ya daktari na kuelekea katika chumba alicholazwa Moto.



    “Mpango umekamilika, thatha hapa kadhi imebaki kwako tu"



    “Usijali, imekuaje huko kwa daktari?"



    “Daktari hana lolote, nimempiga kithwahili kakubali ulale hadi kesho"



    “Basi haina shaka mimi hii kazi nitaifanya usiku"



    “Bathi acha nikuache"



    “Poa"



    Baada ya kuaga, Moto alilala kwenye kitanda cha hospitali ili kusubiria usiku afanye kazi iliyomleta hapo hospotali.



    *******************************

    4:30 Usiku. Hospitali ya Tumaini.



    Moto aliinuka katika kitanda cha hospitali hiyo, na kwenda chooni na begi lake dogo, alipofika alibadilisha nguo na kuvaa nguo za kidaktari, akachomoa bomba la sindano na kichupa cha dawa chenye sumu, akavitia mfukoni na kwenda hadi katika chumba alicholazwa Hemedy.



    Alipofika akafungua mlango na kuzama ndani, bahati ikawa kwake, alimkuta hemedy amelala, akamuendea hadi karibu na kuchomoa sindano iliyokuwa katika mfuko wa koti la kidaktari na kutoa kichupa chenye sumu, bila kuchelewa akakita bomba la sindano kwenye kichupa chenye sumu, alivyochomoa bomba la sindano ilikuwa imejaa sumu iliyokuwa kwenye kichupa, akaushika mkono wa Hemedy ili achome sindano yenye sumu katika bega la Hemedy, bila kuchelewa akaipeleka sindano hadi kwenye bega la Hemedy na kuanza kuchoma......







    Kabla hajamchoma sindano, alisikia mlango ukifunguliwa, akaghairisha mpango wake, sindano akaitia haraka kwenye mfuko wa koti la kidaktari.



    “Vipi dokta?" Nesi Maria aliuliza, yeye ndio alieingia humo chumbani.



    “Sa...safi tu"Moto alijbu kwa kutetemeka, akajua tayari mpango wake umegundulika, akasubiri matokeo.



    “Vipi kwani, mbona umeingia chumba hichi, kuna nini?" Nesi Maria hakuweza kumuhisi vibaya, kutokana na kipindi hicho kulikuwa na Madokta wa fildi, kwahiyo akadhani na yeye pia ni mmoja wapo.



    “Samahani, nimekosea chumba"



    “Kwani wewe ulikuwa unaenda kwenye chumba namba ngapi?"



    “Sijui ni Tisa ile, sina uhakika"Akataja chumba alichokuwa yeye.



    “Kama ni chumba namba tisa,basi fuata mkono wa kushoto kutoka hapo nje, utanyoosha hadi kwenye kona utaingia mkono wa kulia, basi kuanzia hapo angalia juu ya milango utaziona namba zimeandikwa kila mlango, wewe zisome hizo namba hiko chumba utakiona"



    “Asantea dokta acha mimi niende"



    “Poa"



    Baada ya kutoka hadi nje alianza kwenda hadi katika chumba alicholazwa yeye, ila kabla hajafika, akaingia kwanza chooni na kubadilisha nguo, akavaa nguo zake za mwanzo na zile za kidaktari akazitia kwenye begi aliloliacha hapo hapo chooni.



    “Kumbe ulikuwa bado hujalala?" Nesi Maria, alimuuliza Hemedy baada Moto kuondoka.



    “Nilikuwa nimelala, ila maongezi yenu ndio yamenishtua"



    “Kwa maongezi gani yale mpaka yakakufanya ushtuke usingizini"



    “Mimi nikilala silali kama nimekufa, yani hata hatua za sisimizi pia zinaweza zika nishtua"



    “Hahahahah, wewe mtoto usinichekeshe, haya sisimizi ana kishindo gani chakufanya ushutke usingizini?"



    “We si hujui tu, ila mimi masikio yangu mazima, halafu pia nina hisia kali sana"



    “Muongo"



    “Huamini?"



    “Ndio siamini"



    “Haya subiri nifumbe macho, halafu nianze kukuelezea ulivyo"



    “Haya fumba macho"

    Hemedy akafumba macho.



    “Kwanza kabisa, upo mbele yangu, halafu umevaa nguo za kidaktari, halafu hapo ulipo unatabasamu,nime kosea?"



    “Hahahhah, mtoto mpumbavu kweli, embu fumbua mimacho yako uko"



    “Nime kosea?"



    “Toka uko, vyote ulivyo vielezea si umeviona, huna hisia wala nini"



    “Kwahiyo hutaki?"



    “Sitaki ndio, tena huyo upumbavu wako nenda kawafanyie watoto wenzako" Nesi Maria aliongea huku anacheka.



    “Haya kama hutaki, mi sikulazimishi"



    “Sitaki ndio"



    “Hivi yule uliokuwa unaongea nae ni nani?"



    “Yule ni daktari wa fildi"



    “Anhaaa! Mimi nilidhani ni yule daktari alienichoma sindano jana"



    “Kwani kama angekuwa ndie ungefanya nini?"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kama ingekuwa ndie halafu kaja kunichoma sindano mimi nisenge kubali"



    “Sasa usingekubali vipi, wakati itakuwa amekuja kukupa dawa, au wewe hutaki kupona?"



    “Hatakama lakini sio kiivyo, ni bora nisipone"



    “Haya bwana, acha nikuache upumzike"



    “Sawa kazi njema"



    ****************************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog