Sehemu Ya Tatu (3)
. Ilikuwa ni nyumba ya mzee mganga wa jadi aliyejulikana kama babu mwana Malunde,alikuwa ni mganga kiboko,. Ndani ya nyumba Zilisikika nyimbo za kinyamwezi zilizo kuwa zikiimbwa na Mwana Malunde,. wakati nje palikuwa hapana mtu mwingine zaidi ya Raymond aliyekuwa akinyatia taratibu kuingia ndani mkononi akiwa kakamatilia kisu kikubwa,. Taratibu Raymond alinyatia na kujitoma ndani kwa kasi,.alimvaa mzee Mwanamalunde na kumkaba koo kwa nguvu zake zote huku akiachia ngumi nzito za mbavu Mwanamalunde mzee wa watu akatepeta,kulia alishindwa kuzungumza pia alishindwa pumzi zilikuwa zimebana kwa zile ngumi za mbavu,. “Leo ni zamu yako kuondoka na kichwa chako mshenzi mkubwa wewe” alisema Raymond kwa hasira huku akiweka kisu chake vizuri mkononi,. “Ko-sa—la—ngu nini?” aliuliza Mwanamalunde kwa sauti yenye kugumia maumivu ndani kwa ndani., Badala ya kujibu Raymond aliachia konde zito lilipasua mdomo wa Mwanamalunde na hata kuzidi kupunguza idadi ya meno mdomoni mwa mzee yule,. Mzee aliachia kilio kikali cha maumivu hapohapo Raymond alimkamata na kupitisha kisu kwa nguvu katika shingo ya Mwanamalunde,.ilikuwa ni kama kama vile anachinja mbuzi wa iddi,. Damu ziliruka hovyo, mzee macho yalimtoka pima, ulimi nao ukiwa toka zaidi nje,.mh! ilikuwa hatari,. Raymond alichinja kabisa kichwa cha Mwanamarunde kisha kile kichwa akakitia katika mfuko wa Rambo akiacha kiwiliwili kikiwa kimelala kihasara hasara katikati ya vibuyu na hirizi pale chini,.kwa mala nyingine Raymond alijisijika raha moyoni mwake, aliona anajitendea haki kabisa,. Baada ya kupachika vema kichwa kile katika mfuko wa Rambo sasa alitoka nje ili apotee mazingira yale, wakati huo tayari giza lilikuwa limefunika kabisa sura ya nchi,. Lakini ghafla!!. Sauti kali ilisikia hatua chache kutoka nyuma yake,. “Hapo hapo ulipo nyoosha mikono yako juu na usifurukute wala kukohoa,. nitamwaga ubongo wako!.,upo chini ya ulinzi,. Raymond Fambo muuwaji!!,. leo kwisha habari yako” ilikuwa ni sauti kali` yenye amri ya vitisho ikitokea hatua tano nyuma ya Raymond punde baada ya kuuwa mkononi akiwa na mfuko wa Rambo aliobeba kichwa cha mtu,. Raymond Fambo tumbo lilimchemka,akili yake ilizunguka,.aliona habari yake 'kushnei' na kiama chake kimefika,. kibaya zaidi mtu yule alimjua hata mpaka jina lake, “Ray nimesema nyoosha mikono yoko juu ukiwa huna chochote mkononi sitanii nitafumua kichwa chako sasa hivi kwa risasi” alisema tena yule mtu kwa sauti kali yenye mikwaruzo,. Raymond alinywea kama maji ya mtungini, alitupa chini mfuko wake wa Rambo uliokuwa na kichwa cha mtu,.! Bado akili yake ilikuwa ikishindana na moyo wake kunyoa ama kusuka,.sauti mbili tofauti zilipenya katika kichwa chake,.moja ilimwambia anyooshe mikono juu na ajisalimishe ili kuepukana na kifo cha risasi,.sauti ya pili ilimwambia asikubali kujisalimisha kwa yule mtu aliye nyuma yake mwenye bunduki badala yake ni bora kufa kuliko kukamatwa na kupelekwa mbele ya mkono wa sheria ambapo huko hukumu yake haitakuwa nyingine tofauti na kifo,. “Tafadhali Ray usinilazimishe kufanya maamuzi ya kukusafirisha kuzimu sasa hivi,. fanya ninavyo kulekeza upesi” yule mtu alizidi kumpa wakati mgumu Raymond,. “Just going on guy...,I don fear any thing” Ray alijibu kwa kimombo akiwa ni mwenye kutokuwa na shaka tena,. “heee!. unajifanya majinuni sasa nahesabu hadi tatu usipo tii amri haki ya mama nitakuonyesha jinsi niivyo jeuli” alisema yule mtu huku akikoki bunduki yake na kumlenga vema Raymond,. Hapo Raymond akageuka taratibu kumtizama yule mtu aliye mvamia kwa mara ya kwanza tangu harakati zake za mauaji zianze,.hakuogopa kifo kwa kujiamini kabisa aligeuka na kutizamana uso kwa uso na mtu yule,. Balaa!! Alikuwa ni koplo Frances Kidogori kutoka kituo cha kati cha stesheni,. Alikuwa ni askari mwenye umri kati ya miaka arobaini na mitano ama sita,. alikondeana mno pengine labda kwa mshahara kiduchu aliolipwa huku majukumu yakiwa chungu nzima,.ni mzee waliyekuwa wakifahamina vizuri kutokana na ushabiki wa kandanda kule katika majumba ya sinema ambako Ray na koplo Kidogori walijuana kutokana na ushabiki wa timu za aina tofauti za kule wingereza Ray akiwa mshabiki mzuri wa riverpool huku koplo Kidogori akiwa mshabiki nambari moja wa Man u,. ubishi wa hoja na uchambuzi yakinifu ndio ulio fanya watu wale kuwa marafiki wapinzani kila inapo fika wakati wa mechi,.sasa siku hii walikutana katika ukinzani mwingine hatari,. “Haki ya mama nakulipuaa!” alisema koplo kidogori kwa wahka mikono yake ikiwa ina mtetemeka! Sijui kwanini,. “Lipua” alijibu Ray kwa sauti yenye kisirani,. “heee! Ibirisi wewe unadhani nashindwa!!. Naweza kufanya hivyo sekunde yoyote,. Huwezi kufanya mauwaji ya kikatili kiasi hiki halafu utegemee nitakuacha, eti kisa tu wewe ni mtu ninae kufahamu!,. haiwezekani hata tone…!, yanii umechukua rikizo kwa ajili ya kufanya udhalimu huu!!,kwanini lakini Ray kwanini??,.” Alisema koplo Kidogori kwa sauti yake nzito isiyo endana na mwili wake, “Ndio nishafanya sasa,. amua unalo taka” Ray alijibu huku akimtizama koplohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kidogori kwa jicho la dharau,. “Paaaaaaaaaaaa!!.” Risasi alitoka katika bunduki ya afande kidogori na kumpata barabala Raymond mwana wa Fambo,. Fambo alitoa sauti kali ya maumivu na kuanguka chini huku damu nyingi zikiruka,.. Hali ilikuwa tete!. “Kwisha habari yako mwanaharamu mkubwa wewe,.nisha kueleza kama wewe kiburi mimi jeuri” alijigamba koplo Kidogori huku akisogea mahala alipo angukia Raymond huku damu zikimvuja kwa wingi ktk mwili na kumwagika ardhini,. Raymond aligumia maumivu makali ya risasi ya mguu wa kushoto aliyotandikwa na koplo Kidogori,. Koplo kidogori baada ya kuona hasimu wake hajiwezi alitoa simu yake ya upepo katika mfuko wake wa suruali tayari kwa kutoa taarifa kwa askari polisi wenzake walio kuwa wametanda kona zote za mji wa tabora kufanya doria,… Ghafla!!!.sauti ya kishindo ikasikika “Puuuuu”ilikuwa ni sauti pigo,. pigo zito na la ghafla alilokutana nalo koplo kidogori,. Alianguka chini huku akigumia maumivu makali katika kichwa chake,. Haruna hakumpa nafasi ya kujihami kwa kutumia kofia ile ile ngumu ya pikipiki aliyo itumia kumpigia, aliinyanyua tena kwa nguvu na kumwezeka nayo katika paji lake la uso,.koplo kidogori aliona nyota,.hakuweza tena kunyanyuka,lakini Richard hakuishia hapo aliendelea kuponda ponda kwa nguvu kichwa cha koplo Kidogori,.damu ziliruka na kutapakaa katika kofia ile ngumu ya pikipiki,.habari ya koplo kidogori ikabaki kuwa innalillahii,. Baada ya kumsafirisha koplo kidogori kwa sir god Richard alimgeukia Ray aliye kuwa akigumia maumivu ya risasi ya mguu pale chini,. “Amka kaka, hapafai tena hapa, amka jikaze twende” alisema haruna Huku akimshika bega na kumnyanyua juu,. “aiseeee! Si..we..zi ku..simama Haruna, siwezi ndugu,hebu nifunge kwanza kitambaa katika jeraha damu inavuja kwa kasi huyu mshenzi{akamtukania mama yake} kanipasua vibaya” alisema Ray huku mishipa ya kichwa ikiwa imemkakamaa., upesi Richard alichana ukingo wa shati lake na kisha kumfunga katika tundu lililokuwa likimwaga damu kwa kasi,. “haya jikaze twende” alisema haruna na kumnyanyua kwa nguvu,.Ray aliachia miguno ya maumivu makali akiwa kisha simama, hata mfuko wa Rambo wenye kichwa cha mwana Malunde haukukumbukwa tena,. taratibu walijikongoja kuingia gizani kuitafuta pikipiki yao.,*******************
Siku hii ya juma tatu ilikuwa ni siku yenye kimuhemuhe katika mji wa tabora mauwaji yaliyo tokea ndio ilikuwa habari ya mjini, wapi ungepita usikute watu wanazungumzia matukio mawili ya mauwaji moja likiwa la askari polisi na lapili likiwa ni lile la mganga maarufu wa kienyeji mjini tabora, Mwana Malunde?. Saa moja na nusu Kilanga na Babra walitoka katika ofisi ya R.P.C mkoa wa tabora wakiwa wamekabidhiwa file la mauwaji ya vikongwe pamoja na taarifa nyingine zote zenye kuhusu kesi ile, Walingia katika tenga la polisi wakiongozana na askari wanne kwa maana ya wao wawili dereva wa tenga la polisi, na C.I.D mwingine ambaye awali alikuwa akifuatilia ile kesi kabla ya kuwekwa kando. Walielekea katika vitongoji vya Isevya walikoishi watu masikini, Ilikuwa ni nyumbani kwa mwana Malunde ambako maiti zote mbili zilikutwa, Moja ikiwa imetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku nyingine ikiwa imebondeka vibaya katika kichwa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment