Search This Blog

Friday 28 October 2022

ASKARI JELA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : HASSAN O MAMBOSASA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Askari Jela

    Sehemu Ya Kwanza (1)







    GEREZA LA NYUMBA YA GIZA

    KATIKATI YA MILIMA IRINGA



    Fujo ndani ya gereza hili zilikuwa zimeshamiri katika upande ambao ulikuwa na sehemu za kufulia nguo, makelele ya wafungwa wa kiume waliokuwa wakishinikiza kupigwa kwa mtu ndiyo yalikuwa yakisikika yakipaa kwa nguvu . Kulikuwa na kundi kubwa sana la wafungwa waliokuwa wamezunguka duara katika eneo la jirani na sehemu mojawapo ya kufulia nguo ndani ya gereza hilo, kulikuwa na mapigano makali sana yaliyokuwa yamezuka ndani ya sehemu ya kufulia nguo ambayo ilipelekea hao watu wakawa wamezunguka kuweza kutazama.

    Mfungwa gani ambaye alikuwa hapendi kuona Askari akipigwa ndani ya gereza hili, walikuwa wakipigwa sana na maaskari hao waliokuwa wameshindikana. Ndani ya gereza hilo ambalo halina hata muongo mmoja tangu lianzishwe, lilikuwa likisifika kwa kuwekwa watu watukutu sana ambao walikuwa wameshindikana na wauaji wakubwa. Hata Askari wenyewe wengi wao walikuwa ni watu walioshindikana kuwekwa kwenye magereza mbalimbali kutokana na ukatili wao waliokuwa wakiufanya. Walitokea kuwa ni watu wenye kuchukiwa sana ndani ya gereza hilo kutokana na huo ukatili wao waliokuwa wakiufanya humo ndani, wafungwa wajeuri baadhi walikuwa wakiwahofia sana na kutokana na kipigo kizito walichokuwa wakiwapa.

    Ndiyo maana hata kupigwa kwa huyo Askari mmojawapo wa magereza aliyekuwa yupo humo ndani ya chumba chenye kufuliwa nguo, walibaki wakishangilia sana. Walikuwa wakiona ni burudisho Askari huyo akipewa kipigo na Mfungwa mwenzao, muda huo Askari wa magereza ambaye alikuwa yupo katikati alikuwa ameshindwa kabisa kuweza kujihami. Alipojairbu kutoa rungu ambalo alikuwa akilitumia mfungwa mmojawapo alimpokonya rungu, aligeuzwa gunia la mazoezi baada ya hapo kutokana na kushindwa hata kujihami. Mfungwa huyo ambaye alikuwa akimfanya gunia la mazoezi naye alijua kumpiga, alikuwa akitumia ujuzi wake wote katika kurusha ngumi ambazo zilikuwa zikimuonesha ni jinsi gani alivyokuwa fundi katika mapigano. Kila alipotumia mbinu mpya kabisa katika kumshmbulia huyo Askari ndiyo wafungwa wenzake ambao walikuwa ni wahalifu wazito, walivyozidi kusngilia kwa ufundi aliokuwa akiuonesha. Askari aliyekuwa akipigwa naye alikuwa amelowa damu uso mzima kwa jinsi alivyochakazwa, alipewa pigo moja la mwisho ambalo lilimtupa chini na ikawa ndiyo mwisho wake na hakusimama tena.

    Mfungwa ambaye alikuwa akitoa kipigo kwa Askari alikuwa ni mwenye sura ya kutisha, aliyejichora michoro mbalimbali mwilini mwake na alikuwa ni mwenye mwili mkubwa sana. Alipoona kaanguka chini aliamua kumfuata ili amalize kabisa mchezo, alikuwa akionekana kabisa kuua halikuwa jambo kubwa sana kwake. Alipomkaribia Askari huyo taa za humo ndani zote zilizimika kwa ghafla, kutokana na gereza hili kujengwa katikati kwenye shimo la mlima. Mwangaza wa kawaida haukuwa ukifika kwenye maeneo yote, hivyo mwangaza wa sehemu za ndani ya gereza ulikuwa ukitolewa na taa maalum zilizokuwa zikiwaka masaa ishirini na nne. Kuzimika kwa taa hizo ni giza linalofuata, kuzimika kwa taa hizo kuliambatana na ukimya wa ghafla sana uliowaingia wafungwa wa eneo hilo.

    "Ohoo! Afande Nkongo" Baadhi ya wafungwa waliropoka
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haikupita hata dakika mbili kulianza kusikika milio ya kupigwa watu eneo hilo, sauti za watu waliokuwa wakilalamika kuumia pamoja na kuachia miguno ya maumivu. Ndiyo zilitawala ndani ya eneo hilo la kufulia nguo. Sauti za kupigwa watu humo zilidumu kwa muda mrefu, taa zilipokuja kuwaka asilimia kubwa ya wafungwa ndani ya gereza hilo walikuwa wana manundu na wengine walikuwa wamepasuka katika sehemu mbalimbli za miili yao Wote walikuwa wakigaragara chini na kiumbe pekee aliyekuwa amesimama alikuwa ni Askari mmoja ambaye hapo awali hakuwepo kwenye tukio hilo. Alikuwa ni Askari ambaye ameenda hewani haswa, mwenye mwili wa kimazoezi, alikuwa ni mweusi na alikuwa na nyota tatu kwenye bega lake. Alikuwa amesimama huku rungu likiwa lipo kwenye mkononi, macho yake makali ambayo yalikuwa yameficha kabisa uzuri wa kiume aliokuwa nao kwenye uso wake ndiyo yalikuwa yakiangaza kwenye eneo ambalo wafungwa wote walikuwa wakigaragara kwa maumivu.

    Hakika ndiye yeye aliyeshusha dhahama hiyo kwa wafungwa wote waliokuwa wakishangilia, muda huohuo kikosi cha maaskari mbalimbali waliokuwa wameshika virungu kiliingia hapo eneo la kufulia nguo ndani ya gereza hilo. Kiongozi wa kikosi hicho alitoa saluti kwa Askari huyo ambaye alikuwa, baada ya hapo walimchukua Askari mwenzao ambaye alikuwa amejeruhiwa na kuondoka naye mahala hapo. Waliwaondoa wafungwa hao waliokuwa wakiugulia kipigo huku Yule Askari akiwa ameweka mikono nyuma akiangalia hadi pale wafungwa wote waliporudishwa vyumbani mwao

    Walimuacha Askari huyo akiwa amesimama pekee akiwa ameweka kirungu alichotolea adhabu nyuma, alikuwa akiyatazama mazingira ya eneo hilo kama vile alikuwayaona kwa awali. Macho yake yaliyojaa ukali hadi yakawa mekundu, hayakuwa yakiisha kabisa kuyatazama mazingira ya hapo.

    ****

    Upande wa pili ndaniya gereza hilihili upande wa vyumba vya maofisa wanawake kulikuwa na mjadala mzito sana uliokuwa ukiendelea, maaskari wanawake waliokuwa na urembo lakini waliosheheni kila aina ya balaa. Walikuwa wamekaa kwenye ofisi hiyo wakiwa wanajadili waliyokuwa wanayajua wao, yalikuwa yakiwahusu wao tu ndani ya ofisi hiyo ndiyo maana wakakusanyika kwa pamoja wakijadilia. Ulikuwa ni muda ambao hawakuwepo kwenye eneo husika kutokana na wafungwa wa kike wengi kuwepo ndani ya vyumba vyao, porojo za kusogeza muda ndiyo zilikuwa zikijadiliwa hapo

    "Jamani mimi kuna kitu nimekiweka ila uzalendo uanishinda" Aliongea mmoja wao

    "Wacha wee Teddy hebu tuambie" Alidakia mwingine

    "Kusema ukweli ASP James nimechizika kwake" Teddy aliongea

    "Wee! Teddy hilo utabaki nalo mwenyewe moyoni bibi" Mwingine kabisa alidakia

    "Kwanini Jamila au hana moyo yule" Teddy aliuliza

    "Mtu mwenyewe yule hata kuongea na mtu tabu utaanzia wapi kumfuata senia kama yule" Jamila aliongea

    "Potelea pote siwezi kukaa kimya kwenye maisha yenyewe haya kutoka hutoki humu" Teddy aliongea

    "Sasa hata kama hivyo utaanzia wapi?" Yule wa kwanza alidakia

    "Rose usinikatishe tamaa shosti" Teddy aliongea

    "Si kama nakukatisha tamaa sote tunamjua yule hadi wewe mwenyewe" Rose aliongea

    Muda huohuo kengere ya dharura ikalia ndani ya gereza hilo, taa ya kengele hiyo ambayo ilikuwa imeunganishwa humo kwenye ofisi yao ilwajulisha kabisa kuwa dharura hiyo ilkuwa imetokea kwenye gereza la wanawake ndani humo. Ilikuwa ni kawaida sana ndani ya gereza hilo na ilikuwa haipiti siku mbili bila kutokea fujo ndani ya gereza hilo kutokana na wafungwa watukutu waliokuwa wakiwekwa humo ndani, iliposikika kengele hiyo kila mmoja alinyanyua kirungu chake. Wote kwa pamoja ambapo walikuwa wamevaa gwanda za mfumo wa suruali walikimbilia kwenye gereza la wanawake. Lilikuwa ni gereza ambalo lipo chini kabisa ya ofisi yao, iliwabidi washuke kwa haraka sana na kiukakamavu kuelekea huko. Walipokaribia eneo la magereza ya wanawake walisikia sauti ya fujo kubwa sana, hiyo iliwafanya wote kwa pamoja waufungue mlango wa mbele wa kuingia kwenye sehemu ambazo zilikuwa na vyumba vingi vyenye wafungwa. Teknolojia ya umeme ya ndani ya gereza hilo haikuwawia vigumu kuufungua mlango huo, walipoufungua tu baadhi ya wafungwa wa kike ambao walikuwa wakiwatambua balaa lao walitawanyika na waliingia vyumbani mwao. Wachache wajeuri waliendelea kusalia huku wakishangilia kama hawajawaona maskari hao.

    Maafande hawa wa kike wenye balaa tofauti na muonekano wao ulivyo, walianza kuwasogelea wale wafungwa wajeuri waliokuwa wapo wamezunguka duara huku wakiwa wanashangilia. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kupiga virungu bila kuangalia mahali popote, wale waliokuwa wakijifanya wabishi na wakajaribu kuwakabili walijikuta wakichezea kipigo cha haja kutoka kwa maaskari hao ambao walikuwa ni wajuzi pia pia kwenye masuala ya mapigano. Muda mchache baadaye fujo yote ilikuwa imetulia na hakukuwa na yeyote ambaye alikuwa akileta ukaidi. Wale ambao walikuwa wakisababisha mkusanyo huo uwepo, walipewa kipigo cha haja. Kupigana kwao walipaona hapana maana kabisa kutokana na kipigo hicho wallichokuwa wamepewa, wote waliingia gerezani wakiwa na manundu kwenye miili yao kutokana na kipigo hicho walichokuwa wamepatiwa kwa kuleta mkusanyiko usio na maana na kupelekea fujo.

    ****

    Upande wa gereza la wanaume chumba kimojawapo cha wafungwa kulikuwa na wafungwa wawili waliokuwa wamepasuka vichwani, wengi walikuwa na manundu kwenye sehemu mbalimbaliza miili yao. Mmoja tu ndiyo hakuwa na nundu wala alama ya kuumia baada ya kuwa alikuwa amebakia humo ndani katika muda ambao wenzake walikuwa wakishangilia kupigwa na Askari, huyo alikuwa ni mtu wa makamo ambaye alikuwa na mwili mwembamba sana pamoja na kimo kirefu. Alikuwa aakiwangalia sana nwekzaek waliokuwa wameumia humo ndani na alikuwa akisikitika sana, alipowaona wengi wao wakijikanda manundu yao alikuwa akiwaonea huruma sana kwa kitu ambacho walikuwa wamekifuata kikiwapa hali hiyo.

    "Aisee Nkongo hafai kabisa yule" Mfungwa mmoja ambaye alikuwa na nundu jirani kabisa na utosi aliongea.

    "Tatizo mlienda kule hakukuwa na haja ya kwenda mngemuachia jamaa balaa lake mwenyewe" Mtu huyo ambaye alikuwa akiwasikitia alisema.

    "Kamishna Wilfred ungejua tulivyokuwa tunawachukia hawa majama wacha tushngilie" Aliongea

    "Ndoni mimi nilikuwa polisi hao nawatambua fika ndiyo maana nikatulia hapa, najua wote humu tumeingia sababu ya uhalifu lakini angalieni na maaskari wa kuwagomea. Si Segerea ile humu wapo walioshindikana watupu" Kamishna Wilfred aliongea

    "Kamishna ingekuwa wewe unaona yule anayekuonea anapigwa ungefanyaje?" Aliulizwa

    "Ningefurahi lakini haina maana kama kufurahi huko nipayuke nafikiri Nkongo nyinyi hamumjui kabisa yaani" Aliwaambia

    "Tena yule jamaa muache asiingie kwenye anga zangu atajuta kabisa" Aliongea mwingine aliyekuwa amepasuliwa.

    "Aisee Godi yule siyo Askari wa kawaida hana hata maelewano mazuri na rafiki zake ana jambo lipo moyoni mwake na nalijua tangu nipo kazini. Usicheze naye kabisa" Kamishna Wifred aliwaonya

    "Ngojea tu jamaa nitamtaimu yule" Godi alipania

    "Kama unaona ni sawa kumpiga basi ungempiga alipowapiga kundi zima akiwa peke yake, si kiumbe yule nitakuja kuwaambia habari yake"

    "Kamishna mbona unamsifia sana jamaa huyo tupe habari yake" Ndoni aliongea akiwa amekaa mkao wa kusikilizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Muda hautoshi kwa leo majamaa watazima taa soon tu na kupita kuzingua, tufanye kesho kama baada ya kutoka kibaruani"

    "Poa" Waliitikia na kisha wote wakabadili mada na kuongea mambo mengine.

    ***

    Afande Nkongo muda huo alikuwa yupo kwenye eneo la chini kabisa ya gereza hilo, ni ndani ya eneo ambalo lina mawe mengi sana ambapo kulikuwa na sehemu iliyokuwa imevunjwa kuingia ndani ilikuwa haijamaliziwa. Mbele yake kulikuwa kuna Mfungwa yule ambaye alikuwa akimpa kipigo Afande mwenzake, alikuwa akivunja mawe kwa nyundo kubwa kuelekea ndani ambapo alikuwa akitengeneza njia ya kuweza kuwekwa reli mpya kabisa. Ndani ya gereza hilo Mzabuni aliyekuwa na jukumu la kuwalisha alikuwa akiingiza chakula kupitia njia hiyo ya reli, vyakula vilikuwa vikingizwa kwa Viberenge. Hivyo hiyo ilikuwa ni sehemu mojawapo ambayo ilikuwa ikitazamiwa kuja kuwekwa reli mpya, kufanya kosa la kumpiga Afande ndiyo lilifanya apewe kazi ya kupasua miamba ya ndani ya milima hiyo ili iweze kupatikana uwazi utaokuwa ukitumika kupitishia chakula na mahitaji mengine muhimu.

    Mkanda ambao ulikuwa umekunjwa kisawasawa ulikuwa umeshikiliwa mkononi na Afande Nkongo, alikuwa ni mwenye cheo kikubwa ndani ya gerza hilo lakini sehemu kazi kama hizo juu ya wafungwa watukutu kabisa alikuwa akizichukua yeye. Ndiyo maana hata huyo aliyediriki kumpiga Askari alimpa yeye adhabu hiyo na alikuwa akisimamia mwenyewe. Kicheo ni mrakibu msaidizi wa jeshi la magereza(ASP), uwepo wake ndani ya gereza hilo kulitokana na ukorofi ambao aliokuwa nao kama walivyo maaskari wenzake.

    Muda huo alikuwa akimtazama yule Mfungwa ambaye alikuwa akipasua mawe kwa nguvu , hakuwa akipepesa macho kabisa na macho yote yalikuwa yapo kwa mfungwa huyo ambaye alikuwa mkosefu. Haikufika hata muda mrefu tangu ampe adhabu hiyo alichoka, ukubwa na ugumu wa miamba ulimfanya asimame kwa ghafla ashindwe kuendelea na kazi. Hapo alitoa ushawishi kabisa kwa Afande Nkongo, akiwa anajishika kiuno kwa kuchoka alisikia mkanda mgumu wa kijeshi ukitua kwenye mgongo wake. Alipoushikilia mgongo mkanda huo ulihamia kwenye kiunoni, akiwa anaugulia maumivu hayo ndiyo alivyozidi kuongezewa maumivu mapya kabisa kutoka kwa. Alipoendelea kujishika katika sehemu ambazo alikuwa akipigwa ndiyo kipigo kilizidi kabisa na akajikuta akishika nyundo mwenyewe na kuendelea kupasua mawe.

    Pumziko la kipigo ndiyo lilifuata baada ya kuishika nyundo na kuendelea kupasua mawe, alikuwa akisikia maumivu sana lakini mbele ya Afande huyu asiyejua hiko hakuwa na huruma naye hata kidogo. Aliendelea kupasua kwa nguvu na hata nguvu zilizpomuishia alijikuta akapigwa mikanda pamoja na virungu ili asimame aendelee kupasua mawe, haikuwa na kupumzika kabisa mbele ya Askari huyu ambaye hakuwa ni mwenye huruma kabisa likija suala la adhabu.

    "Leo utatoka hapa ukipasua tobo la urefu wa mita 100, hutakiona kitanda mpaka ufikie hapo" Afande Nkongo aliongea kwa hasira kama ilivyo kawaida yake akiudhiwa.

    "Afande nimechoka" Alilalamika

    "Kukuonea huruma ni kujipelekea matatizo, nasema pasua mawe hayo. Nilishasema siwapendi watu kama nyinyi sasa ukiendelea kunisemesha ni kichapo"

    Hakuwa na ujanja tena zaidi ya kuendelea kupasua mwamba huo kupatikane nafasi ya umbali huo aliokuwa akitakiwa aupasue, ugumu wa miamba ya mlimani ilikuwa ikimuweka kwenye wakati mgumu sana. Alipofikiri kipigo alichokuwa akipatiwa kila akisitisha kazi ilimbidi tu aendelee. Sura ya msimamizi wa zoezi hilo haikuwa yenye kuwa na huruma naye, ilikuwa imezidi kuchukia sana tofauti na ilivyokuwa hapo awali jambo ambalo lilimfanya asilelemae hata kidogo. Jasho lilikuwa likimtoka si kidogo hadi hata mikono ikawa inateleza, hii ilisababisha aangushe nyundo mara kwa mara. Alikimbilia kuiokota kuhofia kuongezewa dhahama isiyo na lazima, aliendelea kupasua miamba hiyo kwa nyundo kuelekea ndani. Nusu saa ilipita na hakukuwa na dalili yeoyte hata ya kuonewa huruma, mtuhumiwa huyu wa ugaidi na mauaji kama walivyo wengine hakuwa na mtetezi wake. Alikuwa yupo ndani ya shimo lenye urefu, mtetezi wake ndiyo huyo alikuwa akiiteketeza ngazi yake ya kumfanya kuokoka ndani ya shimo.







    Afande huyu alikuwa akitulia kimya tu akimuangalia Mfungwa wake, mlio wa kupasuliwa kwa mawe ndiyo kama ulikuwa ni burudani yake. Ulipokatika huo mlio basi kilichokuwa kikifuata ilikuwa ni kipigo, hakutaka kabisa mlio huo ukatike katikati ya kazi hiyo. Macho yaliyokuwa ni mekundu ambayo yalionekana dhahiri kutokana na kuwepo kwa mwangaza humo ndani ya mlima, yalikuwa yakitua sehemu moja tu katika eneo ambalo alikuwepo yule Mfungwa aliyeleta kadhia kwa Askari mwenzake, Yalikuwa ni kama yalikuwa yamegandishwa, mboni haikusogea pembeni juu wala chini. Zilikuwa zipo usawa ule ambao alikuwa yupo huyo mbishi ambaye hadi muda huo alikuwa ni mwenye kujuta kutokana na ubishi wake. Afande Nkongo alikuwa akiutazama kwa umakini sana mgongo wa mfungwa huyo,ilikuwa ni kama alikuwa akiburudishwa sana kwa kuangalia jinsi ambavyo ulikuwa uking'ara kwa jasho.

    Kugongana kwa chuma kigumu na mawe ya milima hiyo, kulitoa makelele lakini hakukumfanya aache kukaa kwenye eneo hilo kumsimamia huyo Mbishi. Muda huo mwenye kufanya adhabu hiyo alikuwa hajafika hata mita kumi ya kutoboa kuingia ndani kati ya mita mia moja alizokuwa amepatiwa, muda ulikuwa ukiyoyoma kama kipande cha mpira kilichokuwa kimetiwa kwenye moto. Bado alikuwa hajafika asilimia moja ya eneo ambalo alikuwa amepatiwa kama adhabu, misuli yake imara ya kimazoezi ilituna kwa jinsi alivyokuwa akilazimisha uchovu uliokuwa umeanza kumuingia. Ujengekaji wa mwili wake kimazoezi ulionekana barabara kwa jinsi ambavyo alikuwa ameshikilia nyundo hiyo kwa nguvu nyingi sana akigonga miamba, kuhema napo kulikuwa naye mithili ya bolti na gurudumu la chombo cha moto.

    Alijuta kuingia kwenye mikono ya mtu huyu ambaye alimuona ni Malik ndani ya dunia hii, aliona ukatili wake haukuwa na tofauti kabisa na Malik yule ambaye aliwahi kumsikia kwenye vitabu vya dini akilinda lango la Jahannamu. Kutokuwa na usikivu juu ya hali ya mtu, ni sifa tosha kabisa iliyomfanya amfananishe huyo na Mlinzi wa moto mkali kuliko wote, ingawa Malik huyu kwenye roho yake alikuwa akisikia tofauti na yule ambaye alimsoma kiimani ambaye hakuwa akisikia hata kidogo. Sifa za huyo afande ambazo alikuwa akizisikia kila siku zikiwakumbwa wengine, aliweza kukabiliana nazo kwa mara ya kwanza. Alikiri kabisa alikuwa ameingia kwenye anga ambayo haikuwa ikimfaa kabisa.

    Ilipotimu nusu saa akashindwa kujizuia kwani uchovu ulikuwa umezidi kiwango, hatimaye alianguka chini akawa sura ikiwa juu huku macho yake yakiangalia sehemu ya juu ya eneo hilo. Kuanguka huko kulifuatia na hatua nzito za Afande Nkongo, Mfungwa huyo akiwa kwenye uchovu alifunga macho kwa mara moja na alipofungua alikutana na kivuli kikiwa kimekinga taa hiyo aliyokuwa akiitazama. Akiwa bado hajakielewa hicho kivuli alisikia kitu kigumu sana kikitua kwenye bega lake na kisha kikafuata kifuani, hakutaka kujiuliza mara mbili kitu hicho kilikuwa ni nini. Alitambua kabisa huo ulikuwa mkanda mgumu wa kijeshi, alibiringisha kutokana na maumivu aliyokuwa ameyapata. Aliuweka mgongo juu na hapo ni kama alikuwa amemuwekea Afande Nkongo sehemu ya kupiga, mkanda huo ulitua kwenye mgongo wake. Maumivu zaidi aliyapata na hata akafumba macho kwa nguvu, kufumba macho namna hiyo bado hakukushwishi aweze kuonewa huruma na Afande huyu asiye na huruma. Aliendelea kupokea kipigo kizito na muda huo akiwa amechanganyiwa na virungu, kipigo hiko kilidumu hata fahamu zilipomtoka kiliendelea vilevile.

    Usitishwaji wa kipigo hicho ulikuja kutokea baada ya kusikika ukelele mkubwa, huo ulikuwa ukitokea katika upande ambao kulikuwa na njia ya kurudi gerezani. Sauti hiyo kubwa ilikuwa ikifahamika vyema na Afande Nkongo,ilikuwa ni sauti ya nguvu ambayo ilikuwa ikimkataza asiendelee kufanya hivyo alivyokuwa akifanya. Naye alisitisha mara moja na kisha akasimama kuangalia nyuma, alikutana na sura ya Mtu mzima wa makamo mwenye mwili mkakamavu akiwa amesimama. Alipomuona huyo mtu alisimama kisha akatoa heshima, alibaki akiwa amesimama huku akimtazama Mkatazaji wake ambayo alikuwa yupo mita kadhaa kutoka hapo alipo.

    "nini unafanya kijana wangu?" Aliulizwa hakujibu

    "Keshapoteza fahamu huyo, kama ni hatia aliyokuwa ameifanya ungecha" Sauti ya kumlaumu ilirudi tena kumuambia lakini hakushughulika kutia neno.

    Yule Mzee ambaye alikuwa akimtambua vilivyo afande huyo aliyewakuwa amempa heshima, hakushughulika kumuuliza juu ya kimya chake. Alichoamua ni kutoa simu ya upepo ya kisha akatoa amri wa vijana wengine, dakika takribani mbili baadaye waliingia vijana wengine ambao walikuwa na sare za kiaskari na walienda kumnyanyua Mfungwa huyo na kisha wakamtoa eneo hilo na kumuacha akiwa Mkuu wao yupo pamoja na Afande Nkongo. Aliamua kumsogelea Askari huyo wa chini yake ambaye hakuwa akiishiwa hasira, alipomfikia alimkuta akiwa na macho yaaleyale ya kihasira akiwa anamtazama. Hasira hizo hazikuwa zenye kumtisha hata ukali wa sura alionao mmiliki wake, alimshika bega lake la kuume na kisha akamtazama kwa sura ya upole.

    "Najua una machungu sana kijana wangu, ila ukumbuke waliokufafanya uwe katika hali hii si hawapo. Chuki usihamishekwa wengine" Alimuambia

    "Ni ngumu sana kuisahau hii, kila nikiona mwenye nguo kama zangu akiwa anafanya kitu kisichostahiki au hawa watuhumiwa wakifanya haya" Aliongea kwa uchungu

    “Lakini si hao waliokufanya uwe katika hali hii kijana wangu, usichukie maelfu kwa kosa la wachache"

    "Siwezi nawachukia wote hawa"

    "Hiyo siyo sahihi kijana wangu, hebu tutoke tuelekeee kule Bwaloni"

    Wote kwa pamoja waliifuata njia ndefu ambayo iliwapeleka hadi eneo lenye mlango wa chuma, mlango huo ulifunguliwa na Askari wa cheo cha chini na kisho wote wakapita. Walifuata njia nyingine iliyokuwa ikielekea eneo lenye ngazi ambazo walipanda, walitembea wakizipita kona nyingi sana ndani ya gereza hilo. Hatimaye walifika kwenye eneo la juu ya gereza hilo ambako anga lilikuwa likionekana, wote walienda hadi ndani ya Bwalo la chakula la maaskari waliokuwa na vyeo vikubwa ndani ya gereza. Walitafuta mahali pa kuketi kwenye eneo lenye viti vilivyopangwa kimpangilio, muda huo humo ndani kulikuwa na watu wengine kabisa waliokuwa wakiangalia mpira na kushangilia kwa nguvu sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Afande Nkongo naye alipoona kulikuwa na mechi ya kukata na shoka alijikuta akielekeza macho yake huko hulipo Luninga, taratibu ule uso wa kujaa chuki ukapungua na akawa na sura ya kawaida na hapo alianza kuongea na Mkuu wake huyo akiwa hana hasira yeyote ile. Hakika kulikuwa na mechi ya timu mojawapo ambayo alikuwa akiipenda, wote waliangalia huku wakiongea mambo mbalimbali. Haikufika hata muda mrefu timu yake ambayo alikuwa akiipenda iliweka mpira wavuni, alishindwa kujizuia na akajikuta akishangailia kwa furaha sana hadi Maaskari wengiena ambao hawakuwahi kuliona kabisa tabasamu lake wakamtazama. Waliona ilikuwa ni maajabu kwa ASP huyo kutoa kicheko cha kushangilia kwa nguvu.

    Wengi walikuwa wakidhani kuwa alikuwa hana kiungo ambacho kingemfanya acheke kwenye mwili wake ndiyo maana alikuwa ni mwingi wa kununa, kucheka huko kuliwafanya waamini kuwa walikuwa wakiwaza tofauti kabisa na alivyo. Uzuri wake sura yke ulionekana ndani ya siku hiyo ikiwa ni siku ya kwanza kabisa kuangalia mpira akiwa na maofisa wenzake tofauti na kuangalia mpira ndani ya nyummba yake katika gereza hilo. Wengi wao walikuwa ni wenye kumtazama kwa kuibia sana akiwa ni mwenye furaha, hakika alipendeza sura akiwa katika hali hiyo ambayo hakuwa akipenda kujiweka siku zote.

    "Unajua unapendeza sana ukiwa ni mwenye kutabasamu hivyo" Mkuu wake alimuambia huku akitabasamu na yeye,

    Hakujibu chochote alipoambiwa maneno hayo yeye alijikuta akitabasamu, hilo halikumzuia Mkuu wake kuache kuendelea kumsemesha kwani alikuwa ni mtu pekee ambaye alikuwa akipikika naye chungu kimoja naye ndani ya gereza hilo.

    "Unajua sababu ya kukuleta huku, umekuwa ni mwingi wa mawazo hadi unasahau siku muhimu kama ya leo" Alimuambia kisha akatoa kadi akampatia

    Afande Nkongo aliifungua kadi hiyo kwa utulivu wa hali ya juu, alikutana na kadi iliyopambwa vizuri ikiwa na ujumbe wa kumtakia furaha ya siku ya kuzaliwa. Alibakia akishangaa kwani alikuwa hajui kabisa kuwa ilikuwa ni siku muhimu ya kuzaliwa kwake. Mambo mengi yaliyokuwa yamemtinga yalimfanya hata ashindwe kutambua kuhusu hilo, wingi wa mawazo ndani ya ubngo wake nao ulikuwa ni sababu nyingine kabisa ambayo ilimfanya ashindwe kutambua siku yake muhimu sana.

    "Happy birthday, hongera kwa kutimiza miaka 35" Alipongezwa akiwa bado yu ndani ya Mshangao.

    Muda huo huo luninga ikazimwa kwa ghafla na maofisa wote waliokuwa wapo ndani humo, waligeuka nyuma na wakamtazama yeye na kisha wakaanza kupiga makofi huku wakimuimbia kumtakia furaha ya siku ya kuzaliwa. Afande Nkongo alijikuta akiingiwa na tabasamu alipotazama maafisa wenzake wachache waliokuwa wamevaa mavazi ya kiraia wote kwa pamoja wakimuimbia, maofisa hao nao walisogea hadi karibu yake huku wakiendelea kuvigombanisha viganja vyoa na kupelekea kutokea kwa sauti hizo zilizokuwa zikiendana na wimbo huo waliokuwa wakiuimba. Si wanaume wala wanawake miongoni mwa maofisa hao waliokuwa wamevaa vyenye kupendezesha, wote walisogea hadi karibu yake na kila mmoja akiwa na zawadi yake mkononi. Ilionekana wazi lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa limeandaliwa muda mrefu na yeye hakuwa amelitambua, muandaji wa jambo hilo alikuwa ameliandaa vya kutosha hadi kufikia hatua ya Afande Nkongo kutabasamu akiwa na wenzake. Hakika alikuwa ameviondoa vile vyenye kuukera moyo wake, ndiyo maana alikuwa na tabasamu namna hiyo.

    Alikumbatiana na wengi waliokuwa wakihitaji kufanyiwa hivyo, haswa watoto wa kike ambao walikuwa wakihitaji hilo jambo. Hilo halikuwa neno kabisa kwa Afande Nkongo yeye aliona ilikuwa ni jambo la kawaida tu kukumbatiana nao, muda mfupi baadaye alikuwa na zawadi nyingi sana kwenye eneo ambalo alikuwa amekaa. Hilo lilimpa faraja sana na akajikuta akifurahia nao, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa yeye kujishngaa sana kwa jinsi alivyobadilika na hata kutabasamu akiwa yupo na hao watu.

    “Napenda niwahukuruni sana, sina cha kuwalipa" Aliongea baada ya kupokea zawadi na kisha alimtazama Mkuu wake wa Kazi akamwambia, "Baba sina cha kukulipa"

    Furaha ilikuwa imefana ndani ya jengo hilo la Bwalo hadi pale alipoaga kwenda kumtazama mwenzake aliyekuwa hospitsli, aliondoka akiwa amekabidhi zawadi kwa mkuu wake. Aliahidi kurejea tena kuzifuata. Hilo lilikubaliwa na wote waliokuwa humo ndani, alipotoa mguu humo ndani kilichofuata ilikuwa ni mjadala kuhusu yeye.

    "Mkuu leo Afande ana nini namuona siyo kawaida yake, nilijua atachukia" Afisa mmoja aliongea.

    "Cha muhimu niliwaambiwa ukitaka uwe na urafiki naye, la si hivyo hutaongea naye na ukilazimisha ni ugomvi" Mkuu aliongea

    "Kwanini aliulizwa?" Aliulizwa

    "Hilo suala ni gumu kuwaeleza hivi sasa, usije ukaenda kuongea naye kirafiki ukiwa umevaa sare za kazi hamtaelewana labda uwe kikazi" Alieleza

    "Ila unatutisha mkuu"

    "Eleweni hilo, kila mtu ana kipindi alichopitia kwenye maisha yake ndiyo kama Nkongo" Alieleza

    "Ni kijana mzuri mwenye umbo zuri ila ukaaji wake wa kuwa namna ile kila muda kununa kunanishangaza kwa kweli"

    "Huyu ni mtu mmoja mnapaswa mumuelewe jamani"

    "Sawa mkuu"

    ****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda huo Afande Nkongo alikuwa yupo ndani ya chumba kimojwapo cha wodi,ni hospitali maalum ya jeshi la Magereza iliyokuwa imejengwa ndani ya Gereza la Nyumba ya Giza. Alikuwa akitazamana na kitanda cha Askari mwenzake aliyekuwa yupo chini kicheo, alikuwa ni mwenye majeraha mengi sana kwenye mwili wake na kupelekea hata sura yake isitambulike vyema. Afande Nkongo alipouona huo uso wake mwenzake alijikuta akiingiwa na huruma na zile hasira dhidi ya yule Mfungwa zikamjia. Alitamani muda ururdi nyuma ili aweze kumuongezea adhabu Mfungwa yule ambaye alikuwa amesababisha maafa hayo. Hilo halikuwezekana kabisa kwani huyo Mfungwa pia hakuwa ni mwenye fahamu hadi inafikia mida hiyo, yote ni kutokana na kipigo ambacho alikuwa amempatia kutokana na kushindwa kuendelea na kazi. Alibaki hapo akimtazama mwenzake pasipo kukupesa jicho, alikaa kwenye hali hiyo kwa muda mrefu sana hadi pale aliposikia sauti ya mtu akiguna nyuma yake.

    Hapo aligeuka nyuma na kukutana na Afande Teddy akiwa ni yu mrembo kuliko alivyokuwa akionekana, huyu alikuwa ni yule Askari ambaye alikuwa akiwaambi wenzake juu ya kumuhusudu Afande mmojawapo wa humo ndani. Afande Nkongo alipokutana na Afande huyo wa kike alipokea heshima yake kutokana na kuwa mkubwa kicheo kwake, alitikisa kichwa kuikubali heshima hiyo na kisha alirudisha macho kwa mwenzao aliyeo kitadani.

    "Mkuu anaendeleaje?" Aliulizwa

    "Hali ndiyo hiyo kama unavyoiona" Alijibu

    "oooh! God hawa wafungwa dawa yao ni kuwavunja na miguu tu hii too much"

    "Hii atailipia huyo Bazazi, subiri azinduke apate nguvu lile eneo kwa ajili ya reli mpya atalibomoa yeye lote hadi njia ipatikane" Afande Nkongo alipoongea maneno hivyo alisogea hadi jirani na kitanda.

    Alikishika kiganja cha Mgonjwa kwa sekunde kadhaa kisha aligeuka na kuondoka humo ndani akimuacha Afande Teddy akiwa pekee yake. Macho ya Afande Teddy yote yalikuwa yapo kwake kipindi alipokuwa akitoka humo ndani, hadi anapotea kwenye upeo wa macho yake ndiyo alipokumbuka kugeuza macho na kumtazama Mgonjwa. Haukupita muda mrefu tangu atoke Afende Nkongo, aliingia Askari mwngine wa kike ambaye alikuwa si haba kama alivyo huyo aliyekuwa yupo hapo ndani. Huyu hakuwa mwingine ila alikuwa ni Afande Rose mmojawapo wa maafande wa kike aliokuwa nao ofisini.

    "Naona shosti leo ulikuwa naye humu" Aliambiwa

    "Yaani imekuwa maajabu kabisa" Alisema

    "Kivipi tena?"

    "Yaani leo kaongea na uso wake chuki sijauona"

    "Bahati yako bibi huenda kalainika"

    "Mh! Usinitie moyo tu nikaenda kuingia pabaya, ujue nilikuwa najikaza tu hapa ila namuogopa sana"

    "Mh! Haya tuachane na hayo shosti, vipi Kamugo anaendeleaje?"

    "Yaani hali ndiyo kama unavyoiona hapa, hii Minguruwe tunayoichunga ni tabu tupu"

    "Yaani hawa wa kuwavunja miguu kabisa, nasikia huko huyo jamaa kampa kibano hadi kanyamaza kwenye kitanda hadi sasa"

    "Ni bora tu yaani wametukusanya sisi wakorofi tuje kuchunga hawa manguruwe vichaa, ikileta ujinga ni dawa hiyo tu"

    "Ndiyo kazi hii shosti"

    Muda huo walibaki kimya na wakawa wanamtazama Afande Kamugo, walisikitika sana kumuona akiwa kwenye hali hiyo ingawa wao wenyeji walikuwa ni wenye roho ambazo siyo za kawaida.





    Hawakukaa sana kwani muda muda ambao walikuwa wakihitajika kupumzika, ulikuwa ndiyo muda ili waweze kujiandaa na siku mpya. Ulikuwa ni muda wao wasio na zamu kutokana na kupangiwa zamu ya asubuhi Usiku huo walihitajika kupumzika kama ilivyo kwa wanadamu wengine ili waweze kujiandaa kukabiliana na siku mpya. Waliondoka humo wodini bada ya kumuona Askari mwenzao aliyekuwa yu mahututi, hasira zao kwa wafungwa zilikuwa ni kubwa sana pindi walipokuwa wakitoka humo ndani. Walikuwa wakitamani hata wafungwa waliokuwa wamemfanyia hivyo mwenzao wangekuwa wanatoka upande wa kike,ili waweze kuwapa kipigo kizito.

    ALFAJIRI ILIYOFUATA

    Majira ya alfajiri mlio wa kengele ya kuamsha wafungwa ilisikika ikilia kwa fujo, wafungwa walikuwa tayari wameshaanza kuamka na kutoka kwenye vyumba vyao. Walikuwa wakitoka kwa haraka sana kuhofia kipigo kutoka wa maafande ikiwa watachelewa kutoka vyumbani. Maasakari nao hawakuwa nyuma kabisa katika kupita kwenye vyumba mbalimbali vya gereza hilo kuhakikisha habaki mtu humo ndani. Muda mfupi baadaye wafungwa wa kiume makundi kwa makundi walikuwa wapo kwenye ngazi zilizokuwa zikishuka chini wakiwa na vifaa mbalimbali vya kazi, walikuwa wakishuka kwa haraka sana kutokana na kupelekeshwa na maafande ambao walikuwa wapo nyuma yao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walifika hadi eneo ambalo lilikuwa na njia kama ya kupitisha reli ambayo ilikuwa ni tofauti na ile ambayo alikuwa akipewa adhabu yule Mfungwa aliyempiga Askari. Walipofika eneo hilo ambalo kulikuwa na upana wa kutosha waligawanywa makundi, kila kundi lilikuwa na Askari wake ambaye alikuwa akilichunga. Rokoo ilianza kupita kwenye kila kundi hadi pale maaskari walipohakikisha kuwa wapo idadi kamili. Baada ya hapo kila mmoja alishika kifaa chake cha kazi na kazi ikaanza, ilikuwa ni kupasua mawe kutengeneza njia ya kupitisha reli ziingiazo ndani ya jengo hilo kuleta huduma mbalimbali. Wengine walikuwa wakifanya kazi ya kuzoa vipande vya miamba vilivyopasuliwa na kuvipeleka eneo jingine, kila mmoja alikuwa na jukumu lake katika kazi hiyo ngumu ambayo walikuwa wakiifanya humo ndani.

    ****

    Muda huo Afande Nkongo ndiyo alikuwa akitoka kwenye ofisi yake, alikuwa amevaa gwanda la kikazi kama kawaida yake huku mkononi akiwa na rungu ambalo lilikuwa la muhimu kwake. Aliingia moja kwa moja kwenye njia ile ambayo aliipita siku iliyopita, alishuka ngazi hadi kwenye ambalo alikuwa amempa adhabu yule Mfungwa. Alikuwa anayo taarifa ya kuzinduka kwake na muda huo alikuwa akiendelea na adhabu yake, hapo alimkuta akiwa amesimamiwa na maaskari wawili ambao walikuwa wapo chini yake na pembeni kukiwa na Mkuu wake wa kazi ambaye alikuwa amevaa sare za ofisini za kijani.

    Maaskari hao walipomuona waliendelea na kazi ya kusimsmia eneo hilo, Afande Nkongo alitoa saluti kwa mkuu wake na kisha akasogea jirani kabisa na eneo ambalo Mfungwa huyo alikuwa akipasua mawe kufikia umbali ule aliokuwa amemwambia aufikie. Kitendo cha kuiona ile nguo ambayo ni sare ya wafungwa wekundu ulianza kujengeka kwenye macho yake, mishipa midogomidogo ilianza kujitokeza kwenye macho yake. Mkono wake uliokuwa umeshika rungu ulikakamaa sana kuashiria alikuwa na hasira sana, alipofika hapo aliwatazama maasakari wa chini yake waliokuwa wakimsimamia kwa macho ya kihasira sana hadi wenyewe wakaingiwa na hofu.

    "Kaendeleeni na kazi zingine huyu niachieni" Aliwaambia huku akiwatazama kwa macho yake makali.

    "ASP" Mkuu wake wa kazi alimuita

    "Afande" Aliitika na kisha akaageuka nyuma kuelekea alipoitwa, alipofika alisogea kando na Mkuu wake huyo kuteta jambo.

    "Mwanangu wachie hao waendelee naye, wewe kaendelee na kazi za kiofisi"

    "Lakini Baba"

    "Hakuna na lakini naomba fanya hivyo kama unaniheshimu, usiwe na hasira na hawa siyo waliokukosea"

    "Sawa"

    "Pitia ofisi zote za junior wako uhakikishe kama wanafanya kazi kiutiifu"

    Alitoa saluti alipopokea jukumu hilo na kisha alipanda ngazi akiwa ameamua kumridhisha Mkuu wake wa kazi, alipitia kwenye ofisi moja moja ndani ya gereza hilo akianzia kwa wanaume na hatimaye alifika kwenye ofisi za Maaskari wanwake waliokuwa wapo ndani ya gereza hilo. Kitendo cha kufungua mlango wa ofisi hiyo aliwakuta maaskari hao wakike wakiwa wanaongea, wote walipomuona walikakamaa na mkubwa kuliko wao aliyekuwa yupo huo ndani alitoa saluti kwake.

    "Hamna kazi ya kufanya siyo?" Aliwauliza wote walikaa kimya

    "Si nawauliza nyinyi hapo, yaani mnageuza sehemu ya kupigia domo hii ofisi. Haya kila mmoja afanye kazi yake iliyomuweka humu ndani" Alipomaliza kutoa mmri hiyo alitoka nje ya chumba hicho cha ofisi.

    Moja kwa moja alielekea kwenye ofisi zingine ndani ya gereza hilo akiwa anakagua kazi zinavyoendelea, alizimaliza ofisi zote akiwa anawaonya wale wote waliokuwa wakifanya uzembe na hatimaye alishuka hadi eneo ambalo kulikuwa na wafungwa wengi waliokuwa wakifanya kazi. Huko alikuta kazi zikiwa zinaendelea vizuri katika kila upande ndani ya gereza hilo, aliridhishwa na maaskari wale waliokuwa wakisimamia wafungwa kufanya kazi mbalimbali ndani ya gereza hilo. Alipomaliza kupita na kukagua alianza kuridi kupita ofisi moja moja kupanda juu kurudi ndani ya ofisi yake, ilikuwa ni kawaida yake akimaliza kukagua kuanza kupita kuhakiki kwa mara ya pili. Ukaguzi wa aina hii alikuwa akiulenga sana kwenye ofisi za maaskari wa juu kidogo ambapo walikuwa na kawaida ya kuendelea kutegea pindi anapoondoka, baada ya ukaguzi huo wa mara ya pili alirudi tena ndani ya ofisi yake.

    Kuifikia ofisi yake ilikuwa ikimlazimu kupita kwenye vyumba tofauti vya ofisi vya gereza hilo, eneo ambalo lilikuwa linaanza vyumba hivyo kulikuwa na picha mbili ambazo kila akiingia ndani ya ofisi hiyo lazima mojawapo aitazame sana. Picha ya kwanza ilikuwa ni picha ya Mheshimiwa Rais Zuber Ameir na picha ya pili ilikuwa ni picha ya Mkuu wa jeshi la magereza nchini, Kamishna Jenerali. Macho yake yalikuwa yakitua kwenye picha hiyo ya pili kuliko hata picha ya Amiri jeshi mkuu ndani ya nchi hii. Alipochoka kuitazama picha hiyo macho yake huwa mekundu na jambo hilo maaskari waliokuwa wapo chini yake walikuwa wameshaanza kumzoea ingawa hawakujua ilikuwa ikitokana na kitu gani. Aliingia ofisini kwake akavuta kiti na kisha akakaa kuendelea na kazi muhimu, umakini wote ulikuwa kwenye kazi kutokana na utulivu ambao ulikuwa upo ndani ya ofisi hiyo.

    ****

    Muda ambao Afande Nkongo alikuwa akitoka kwenye upande ambao walikuwa wakisimamiwa wafungwa, wale ambao walikuwa wakikaa gereza moja na Kamishna Wilfred walitoa macho kumtazama na kisha wakageuza macho kumtazama mwenzao huyo aliyekuwa ameahidi kuwasimulia juu ya Afande huyo. Wale waliokuwa wamepigwa siku iliyopita walimtazama kwa macho yenye chuki sana, hawakuwa na lolote la kumfanya kutokana na mamlaka ambayo alikuwa nayo ndani ya gereza hilo. Walitokea kumchukia sana lakini chuki yao ilikuwa ni sawa na kazi bure tu, hawakuwa na lolote la kuzituliza chuki zao. Wakisema wajaribu kumpiga hawakuwa na uwezo wa kupigana naye, walikuwa wakijua sana jinsi alivyo hatari kwenye mapigano ya mikono mitupu na hata ya kushika silaha.

    "Kamishna mtu wako huyo" Mfungwa mmoja alimwambia.

    "Inaonekana hamumpendi sana nyinyi majamaa" Aliwambia huku akiendelea kupasua mawe kwa nyundo kubwa sana.

    "Ulisema utatuammbia kuhusu yeye kumbuka Kamishna" Mmoja alimkumbusha

    "Msihofu jamani nitawaambia kila kitu kuhusu yeye subirini wa chai ufike"

    "Hamna noma jamaa"

    Waliedelea na kazi yao ngumu ndani ya gereza hadi ulipofika muda wa chai, kengele maalum ililia na wote wakaweka vifaa chini wakaelekea kwenye eneo la kupata kifungua kinywa. Wafungwa mbalimbali walikuwa wamepanga mistari kueleka kwenye eneo la kuchukua kifungua kinywa chao, mistari ilikuwa ikisogea taratobu sana kutokana na ugawaji wa chakula hicho kutokuwa wa kasi. Ulifika muda wa kupata chakula kwa wale wafungwa waliokuwa wapo pamoja na Kamishna na Wilfred. Baada ya hapo wote walielekea kwenye eneo ambalo walikuwa wamelitenga kwa ajili ya kunywa chai, wote kwa pamoja walikuwa na wahka wa kusikia juu ya Afande ambaye alikuwa ni mkatili kuliko wote ndani ya gereza hilo. Walipoketi tu kila mmoja akiwa na chakula chake walipeleka macho yote kwa Kamishna Wilfred ambaye alikuwa ameshikilia mkate na kikombe cha bati chanye chai.

    "Kamishna tunakusikilia sasa" Aliongea mfungwa mmoja na kumfanya Kamishna Wilfred aweke kikombo chini.

    Akianza kuuweka mkate wake ili upite kwenye mashine za usagaji mdomoni alisimulia, "Japo miaka imesogea sana lakini ndani ya siku hii sitasahau kabisa, ilikuwa ni siku ambayo nilikuwa nimemaliza kidato cha sita. Siku ambayo nilikuwa nimekaa nyumbani kwa muda wa majuma kadhaa, siku hiii ilikuwa ni siku chache tu tangu nifanye maandaalizi ya kujiangaa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa. Siku hiyo nilitoka vizuri nyumbani hadi kituo cha mabasi Ubungo na kisha nilipanda basi la Tanga, kituo cha kushuka ilikuwa ni Kabuku wilayani Handeni. Niliposhuka hapo nilikutana na wanafunzi wengi waliohitimu kidato cha sita wakiwa wanasubiria wapate muongozo. Wote tulikuwa hatujui kambi tuliyokuwa tumepangiwa ilikuwa ipo wapi ndiyo maana tulikaa hapo kwani huko Kambini tayari walikuwa wamepata taarifa ya ujio wetu hivyo ilikuwa ni lazima wafike. Haikuchukua mida tuliona gari la rangi ya kijani kibichi likifika hapo, lilikuwa ni Gari kubwa sana na mara nyingi hutumiwa kubeba mizigo ndani ya kambi za jeshi. Gari hilo lilipofika tu hapo na kusimama mlango wa upande wa mbele ulifunguliwa, alishuka Mwanajeshi aliyekuwa amevaa fulana ya kijani maarufu kama 'greenvest' na kombati la kijeshi. Kichwani alikuwa ameva kofia nyekundu ambayo ilikuwa ikumuonesha kabisa alikuwa ni MP. Huyo alitupa ishara ya kupanda ndani ya gari hilo na wote tukafanya hivyo hatukutaka kabisa kusubiri kutokana na wingi wetu eneo hilo. Nilifanikiwa kupata nafasi ndani ya gari hilo ambapo tulikuwa tumebanana sana. Hapo safari ya kuondoka kwenye eneo hilo kuingia ndani ya kambi ndiyo ilianza, safari ilikuwa ni ndefu sana na njia ilikuwa ni isiyo na lami. Mashimo madogo pamoja na kukutana na miwaruzo mbalimbali kwenye barabara hiyo ya udongo mwekundu uliokauka ndiyo ilifuata. Ilituchukua mwendo wa takribani dakika kumi na tano kufika kwenye eneo la mwanzo la kambini kutokana na barabara hiyo ilivyo. Hapo tulishuka kila mmoja akiwa na mizigo yake aliyokuwa amekuja nayo, mwanzoni mwa eneo la kambi hiyo tulikutana na kibanda ambacho kilikuwa na foleni tofauti za wanafunzi waliokuwa wakiandikishwa kuingia ndani ya kambi hiyo, niliposhuka kwakweli nilichanganyikiwa kabisa na sikujua ni wapi nilipotakiwa kwenda. Ilinibidi nisogee jirani na wanafunzi wenzangu na kisha niulize utaratibu wa hapo, nilisogea hadi kwenye eneo ambalo kulikuwa na mstari mrefu sana na mtu wa mwisho alikuwa ni kijana aliyekuwa amepanda hewani akiwa mwili uliokuwa ukitangaza mazoezi aliyokuwa akiyfanya.

    "Oyaa niaje" Nilimsabahi

    "Safi tu kaka, ishu vipi?" Alinijibuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Safi aisee hivi hapa utaratibu vipi maana sielewi?"

    "Kaka unavyoona hapa ni foleni kulingana na mkoa ambao shule uliyotoka ipo, we wa mkoa gani?"

    "Dar kaka sijui foleni yke ni ipi?"

    "Yaani kaka kama uliotea vile foleni ndiyo hii ya watu wa Dar"

    "Doh! Bora maana mistari mingi nilikuwa nawaza kuzunguka"

    "Umefika kituo chako, naitwa James sijui mwenzangu nani?" Alijitambulisha huku akinipatia mkono

    "Wifred"

    Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kujuana na James kijana ambaye alikuwa na historia nzito katika kipindi cha nyuma cha maisha yake aliyopitia. Tulifanikiwa kumaliza kujiandikisha na kisha tulizisalimisha simu zetu kama sheria ya jeshi linavyotaka. Baada ya hapo wote tuliyokuwa tumemaliza kujiandikisha tuliingia ndani tukiwa tumeongozana na Afande ambaye alikuwa yupo nje katika eneo tulilokuwa tukijiandikisha. Tulipelekwa hadi eneo ambalo lilikuwa na jengo moja kubwa sana. Jengo hilo lilipofunguliwa tulikutana magodoro mapya ambapo kila mmoja wetu alichngua alipendalo. Baada ya hapo kila mmoja alipewa shuka yake mpya kabisa yenye rangi ya bluu, muda huo wote nilikuwa pamoja na James na tulikuwa tukiongea mambo mbalimbali katika kila muda wote. Tulipomaliza hapo tulirudishwa juu tulipokuwa tumetoka na tulienda kuwekwa kwenye eneo ambalo lilikuwa na uwanja mkubwa sana. Hapo tuliitwa majina tena na kisha tuliingizwa ndani na kupelekwa kwenye eneo ambnalo lilikuwa na vyumba vya kulala ambavyo badaye tulikuja kuvitambua kwa jina la anga. Bado James nilikuwa nipo naye karibu katika kipindi chote cha muda tukiwa tumetokea kuwa marafiki wakubwa sana. Nilikuja kulitambua jina lake la ukoo ambalo ni jina la watu wa watu wa kaskazini magharibi, ni James Nkongo ambaye ndiye huyu Anfande Nkongo ambaye mnachukia nyinyi".

    "Dah! Kumbe mmetoka naye mbali namna hiyo ila wewe uliingia jeshi la polisi na yeye kaja huku Magereza ilikuwa vipi?" Alulizwa

    "Kuweni na subira sasa huko kote nakuja kuwaleza"

    "Mzee tunasubiri kwa hamu sana si unaona muda mwenyewe wakunywa chai na kupumzika ni mdogo sana" Aliambiwa

    "Kipindi chote ambacho nilikuwa nikifahamiana naye nilikuwa nikimuona ni mtu mwenye furaha sana, mwenye kutabasamu kila muda hata sura yake yenye mvuto ilianza kuonekana kwa wasichana tuliokuwa tupo nao mafunzoni na hata maafande wa kike wale waliokuwa wakiishi kambini maarufu kama 'service girls'. Pamoja na kunyolewa upara na kukaa kwenye eneo ambalo halikuwa na matunzi mazuri, bado alionekana ni mwenye mvuto sana kwa wasichana. Hili lilimfanya awe karibu sana na wasichna ndani ya kambi hiyo na hata hao maafande katika muda ambao tulikuwa tukikutana wote sehemu ya kula chakula, hili jambo pia lilinifanya na mimi niwe karibu na wasichna hao kwani alikuwa yupo nami katika kila kipindi cha muda. Alikuwa ni mcheshi sana katika kila muda ambao tulikuwa tukikaa naye, hili lilifanya hata kuruti wenzetu tuliokuwa tupo nao Kombania moja kuwa na maelewano nao mazuri sana. Hakuna ambaye alikuja kufikiria huyu pamoja na ucheshi wake mkubwa aliokuwa nao alikuwa na historia nzito ambayo ilikuwa imejificha kwenye maisha yake. Masihara mengi aliyokuwa nayo kumbe alikuwa ni mtu ambaye alikuwa jambo ambalo alikuwa ameliweka moyoni mwake, jambo ambalo lilikuwa ni lenye kusikitisha sana ingawa hakuna aliyekuwa akiwaza kama alikuwa hivyo. Muda wa awali wiki sita za mafunzo magumu ziliposiha kuanza kufanya kazi za kawaida, ndipo nilipokuja kujua kuwa huyu alikuwa na zaidi ya jambo katika maosha. Nakumbuka kabisa ndani ya siku ambayo nilikuja kujua kuhusu hili ilikuwa ni katika muda ambao tulikuwa tukienda shamba, muda huo tulikuwa tumeshamaliza mafunzo ya ulengaji shbaha na hata yale ya ushikaji silaha kwenye gwaride.





    ______________TIRIRIKA NAYO

    Jane ndiyo chanzo cha mimi kujua mengi kuhusu Nkongo nikiwa tupo ndani ya kambi hiyo, binti huyu alikuwa akitoka Kombania tofauti kabisa na sisi tuliyopo. Muda wa kula alikuwa haachi kuja kukaa na sisi kwenye kombania yetu ili apate kuongea na Nkongo, kiukweli alikuwa akimuhusudu sana lakini hakuweza kumwambia. Wala Mhusika hakuwa amewaza kabisa kumpenda huyo binti. Ucheshi mwingi aliokuwa nao ndiyo chanzo cha kumuweka kuwa karibu naye katika kipindi chote ambacho alikuwa akija hapo, hakika alitokea kupendezwa sana na rafiki yangu huyu ambaye alikuwa akificha kitu kigumu sana ambacho hata mimi hakuthubutu kuwahi kunieleza kuhusu hicho kitu hapo awali. Nakumbuka vizuri siku moja majira ya usiku muda ambao maafande walikuwa wameitwa kwenye kikao cha dharura na Kamanda kikosi wa Kambi hiyo, ilikuwa ni majira ya jioni ambapo tulichelewa sana kutoka ndani ya Bwalo la kulia chakula. Siku hiyo Jane aliongea sana na Nkongo tofauti na siku nyingine nyingi, kutokana na kumuhusudu sana aliamua kujisifia sana kuhusu mamlaka ya wazazi wao. Hapo ndipo binti huyu alipojichanganya na kutaja kuwa alikuwa ni mtoto wa Mrakibu mwandamizi wa magereza, jambo hilo lilifanya Nkongo amtazame kwa mshangao sana kama alikuwa amepokea taarifa ya kushtusha. Binti huyo kuendelea kumuonesha kuwa alikuwa akitoka familia inayojiweza ndipo alipotaja jina la Mzazi wake, liliposikiwa vyema kwenye masikio ya rafiki yangu kipenzi. Macho yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu ghafla, mishipa ya damu midogo sana ikaonekana kwenye macho ikiwa imewekwa rangi nyekundu. Ilikuwa ni mara ya kwanza kumshuhudia akiwa kwenye hali hiyo mimi na hata waliokuwa wapo eneo hilo, wote tuliingiwa na mshangao. Yeye hakujali mshangao wetu zaidi ya kunyanyuka na kuondoka akiwa haongei neno lolote, hata maafande wa kike ambao hawakuwa wakihusika kwenye kikao waliokuwa wakiongea na sisi waliiingiwa na mshangao mkubwa sana. Alipoondoka wote waligeuza macho na kunitazama mimi, macho yalionesha ni jinsi gani walikuwa wakihitji kujua kile kilichomuondoa eneo hilo. Sikuwa na jibu la kuwapa kwakuwa sikuwa najua chochote kinachoendelea, nilishindwa hata niwaambie nini kuhusu huyo rafiki yangu kipenzi ambao wote walikuwa wakiamini kabisa kuwa mimi nilikuwa nikijua chanzo cha kilichomtoa eneo hilo.

    "Wil rafkki yako ana nini yule?" Afande mmoja wa kike aliniuliza

    "Mwenzangu leo James nimemuogopa kabisa sikuwahi kumuona akiwa vile" Ndawili mmoja aliongea, hili ni jina ambalo wasichana huitwa huko jeshini.

    "Jamani mshangao uliowakumba nyinyi ndiyo ninao mimi sijui chochote jamani kuhusu James" Niliwaambia

    "Si rafiki yako yule" Niliambiwa

    "Hata kama jamani kuwa rafiki haimaanishi unajua ya moyoni mwa mtu, ngoja nikamcheki huko" Niliwaeleza kisha nikanyanyuka na kutoka Bwaloni nikiwaacha wakiwa na mshangao kila mmoja.

    Nilienda kumtafuta Nkongo kwenye eneo ambalo tunakaa Kombania yetu, sikumuona na wala sikujua alikuwa yupo wapi. Nilihangaika sana katika kumtafuta na hatimaye nilimkuta akiwa yupo kwenye eneo lenye michungwa akiwa amekaa chini amejiinamia, niliposogea karibu na kukaa naye ndipo nilipobaini alikuwa akilia. Sikuwahi kumuona akiwa analia tangu nijuane naye. Hata huzuni pia sikuwahi kuiona kwenye uso wake, hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kumuona akiwa yupo kwenye huzuni kubwa.

    "Mzee vipi mbona unalia?" Nilimuuliza kwa upole.

    "Wil yule Jane sitaki hata kumuona kwenye maisha yangu, nilikuwa najiuliza nimemuona kila nikimuona kumbe kafanana na Ibilisi" Aliongea kwa hasira

    "Mbona sikuelewi mtu wangu kuna kitu gani kingine ulichonificha?" Nilimuuliza

    "Huwa sipendi kuelezea suala hili kabisa, we niache tu"

    "James inamaana tumeanza kufichana siyo poa mtu wangu"

    "Ok, ngoja nikueleze"

    Siku hiyo ndiyo nilijua sababu ya Nkongo kuondoka akiwa amebadalika ghafla na pia ndiyo siku ambayo nilijua alichokificha, jambo hilo nililolijua ndiyo chanzo cha yeye kuwa hivi alivyo hadi hii leo. Ooooh! Alarm imelia turudini kwenye kazi nitawaeleza baadaye muda umeisha" Kamishna Wilfred alikatisha kuelezea baada ya kusikika kengele maalum ya kuisha kwa muda wa kupata kifungua kinywa na hata kupumzika, alikuwa amebakisha kipande kidogo cha mkate ambacho alikimalizia kwa haraka.

    Aliongozana na wenzake kutoka mahala hapo kwenda kwenye eneo lao la kazi, nyuma yao walikuwa wakifuatwa na maafande kama ilivyo kawaida ambao walikuwa wakihakikisha wanafika eneo la kazi na kutimiza jukumu lao.

    ****

    Kipindi ambacho muda wa kupumzika ulikuwa ukikaribia kuisha ndiyo muda ambao Teddy aliingia kwenye bwalo la chakula la maofisa wakubwa ndani ya gereza hilo, aliangaza macho ndani ya bwalo hilo na kisha akayatuliza macho kwa Afande Nkongo ambaye alikuwa akimalizia kifungua kinywa chake akiwa amekaa peke yake kwenye meza. Alijipa ujasiri na kujongea hadi kwenye meza hiyo ambapo alisimama mbele yake, alitoa heshima kwa mkubwa wake huyo na kisha alivuta kiti akaketi. Ndani ya siku hii aliamua kabisa kujitoa mhanga kuliko kukaa na jambo ndani ya moyo wake, ndiyo maana alifika hapo pasipo kuhofia jambo olote.

    "Samahani Afande" Aliomba radhi na kupelekea Afande Nkongo anyanyue uso na kumtazama, Teddy alikutana na jicho kali kabisa ambalo lilitazama sare yake na kisha likatua usoni.

    "Ndiyo" Hatimaye sauti ya mkubwa wake huyo ilitoka.

    "Afande nilikuwa na mazungumzo muhimu sana wewe kama hutojali"

    "Ya kikazi au nje ya kazi?"

    "Nje ya kazi"

    "Sasa hivi ni muda wa nini?"

    "Wa kazi"

    "Sasa maongezi ya nje ya kazi yatahusika vipi muda huu wa kazi, ndani ya wakati ambao muda huu wa kupumzika unaisha"

    "Najua Mkuu ila.."

    "Hakuna cha ila rudi Bwalo lenu si muda wake hayo maongezi yako unayoyahitaji" Ilipotoka kauli hiyo Teddy alibaki akiwa ameumia sana, alishindwa kunyanyuka hata kwenye kiti ingawa alikuwa amepewa amri ya kuinuka hapo kwenye kiti.

    "Unapinga amri ya mkuu wako siyo, nimesema rudi Bwaloni kwenu kabla sijakugeuzia kibao" Ilipotoka kauli nyingine kwa mara ya pili, mwenyewe alisimama akaondoka humo ndani akiwa ameumia sana kwa maneno aliyokuwa ameambiwa.

    Afande Nkongo hakuonesha kabisa ni mwenye kujali hilo yeye aliiona ni sawasawa kutokana na binti huyo kuwa na kitu ambacho alikuwa akikichukia sana, kitu hicho ndiyo alikuwa amekuja nacho huyo binti bila ya kujijua yeye mwenyewe. Gwanda ndiyo kitu ambacho kilifanya akose kabisa hata dakika ya kuongea na mkuu wake huyo, aliondoka akiwana maumivu akiona ameonewa pasipo kujua kilichokuwa kimefanya hayo.

    ****

    Teddy alirudi hadi ndani ya ofisi ambapo walikuwa wapo wenzake waliokuwa ametoka Bwaloni mapema, alikuwa akitokwa na machozi na alipoingia na kukaa kwenye kiti. Alikumbuka kuchukua kitambaa chake na kufuta machozi hayo kisha akaegemea mgongo wa kiti na kutazama juu, alibaki akiwa ameelekeza macho yake juu kuitazama taa yenye mwanga mkali iliyopo ofisni humo. Alikuja kuacha kuitupia macho taa hiyo baada ya kusikia sauti ya mwenzake ikimuita.

    "Teddy" Jamila alimuita na kupelekea ageuza macho na kumtazama.

    "Una nini shosti?" Aliulizwahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yaani hata sijui kwanini Afande James ananitesa namna hii" Alipotoa kauli hiyo chozi lilianza kumtoka tena tena, ule ukatili pamoja na jeuri aliyokuwa nayo kwa wafungwa hapo haukionekana kabisa.

    "Imekuwaje kwani?" Alitupiwa swali kwa mara nyingine, aliamua kuwaleza juu ya kilichotokea.

    "Shosti sasa usilie jamani tulia utamfuata baada ya kutoka ofisini" Alishariwa na rafiki mwingine, muda huo huo kengele ya kuisha muda wa mapumzika ndiyo ililia. Ulikuwa ni muda ule ambao Kamishna Wilfred alikuwa amekatisha kuwasimulia wenzake juu ya kilichotokea katika mingi iliyopita.

    ****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog