IMEANDIKWA NA : FRANK MUSHI
*********************************************************************************
Simulizi : Kisasi
Sehemu Ya Kwanza (1)
“Nayajua mengi kwakuwa nimempa kila mtu nafasi ya kuwa mwalimu wangu,,kila mtu hunifunza kwa yale atakayo,,naheshimu kauli na mawazo ya wote kwa uzito sawa, LAKINI UELEWA NI JUU YANGU”…
**MTANGAZAJI**
“Leo katika kipindi chetu, tutaendelea kusikiliza mahojiano kati ya Patrick na mwandishi wa habari waliowahi kuyafanya kipindi cha nyuma kabla ya leo, tulia kwenye redio yako na kila kitu kitakujia hapohapo ulipo, hatutakuwa na matangazo mengi kutokana na uzito wa simulizi hii ya kusisimua” ilikuwa ni sauti ya mtangazaji wa kituo cha redio cha SPEAK LOUD FM kilichokuwa kikirusha kipindi cha STORY za Iam Frank, saa yangu ya mkononi ilinionyesha kuwa ilikuwa saa nne usiku na pombe zilikuwa zimeivuruga akili yangu, lakini nilikwenda mpaka kwenye jokofu na kuchukua Redbul kisha niliinywa haraka haraka na kurudi ili niweze kusikiliza bila kupata chembe ya usingizi…ile kanda yenye ile simulizi ilichezeshwa na sauti ya msimuliaji ilianza kusikika.
**PATRICK ANASIMULIA**
".........ulifikiri nitanyamaza sio,sikutaka kufanya yote haya ila you forced my hand(uliulazimisha mkono wangu).."ndo sauti ya mwisho niliyoisikia katika masikio yangu ikifuatiwa na maumivu ya kitu chenye ncha kilichoingizwa kwenye mshipa wa damu kichwani mwangu,niligundua ni sindano baada ya kuhisi kama dawa ikisukumwa kuingia ndani ya mshipa ule, hali ya kulewa na usingizi vilianza kunisonga lakini kwa mbali niliweza kuona kama vile Mary alikuwa amezimia, nikajitahidi kutoa sauti lakini sikuweza kabisa, wale watu sikuwaona vizuri lakini walikuwa ni zaidi ya wawili kwakuwa nilizisikia sauti zao kwa mbali wakishauriana, sikuifahamu hata sauti moja, gari letu lilikuwa limeharibika vibaya na ile ajali, sikumbuki ilikuwaje mpaka tukagongana na ile gari ila nilishtuka tu na kukuta tayari ajali imetokea na wale waliokuwa kwenye ile gari ndio walioshuka na kuja kunichoma ile sindano. Maumivu makali yaliutesa moyo wangu haswa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu lakini nikashindwa,,,sikukumbuka kitu chochote, niliishi maisha ya tabu sana katika siku za ukubwa wangu, kila kitu kwenye maisha yangu kilikuwa kipya kabisa, sikumfahamu yeyote katika eneo lile. Sikukumbuka nilipokuwa wala nilifikaje,sikufahamu chochote kuhusu ulimwengu,kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu,sikutamani kufa kwasababu sikujua nini maana ya kuishi na nini faida ya kufa kwa wakati huo,,kwa kweli yalikuwa maisha ambayo sikuwahi kufikiri kama ningeishi. Miaka sita mbeleni nilikuja kutoka nje na ndipo nilipoona bango kubwa nje ya jengo hilo nililokuwemo bango hilo lilisomeka Dr. ANDERSON MENTAL CLINIC,ilikuwa pia anuani chini yake iliyonijulisha kuwa nilikuwa SUVA huko FIJI, mandhari niliyokuwepo niliipenda sana ila sikukumbuka chochote juu ya eneo hilo,niliichukia sana hali niliyokuwa nayo wakati ule,hakuna aliyekuwa akionekana kunijali,kila mtu alikuwa ‘busy’ na kazi yake. Nilijihisi pengine nilikuwa kichaa, iweje kila mtu asinijali au kuniuliza chochote pale nilipokuwa. Hayo yalikuwa maisha yangu kipindi cha mwanzoni mwa uzima wangu wagu wa mara ya pili, niliona watu ambao nilihisi ni tofauti sana na mimi,,,,,nilisogea mpaka mbele kwenye bustani kubwa na kutazama mbele mita 200 nikagundua pale ni karibu kabisa na ufukwe wa bahari.
****
"hallo,,!"niliskia sauti ikiniita wakati nipo pale kwenye bustani nikageuka,alikuwa ni msichana mwenye asili kama yangu lakini sikuwa namfahamu,,alinisogelea karibu nakuanza kunisemesha,nilielewa lugha aliyokuwa akiiongea, niliwahi kuwa nikiiongea sehemu fulani lakini sikukumbuka ni wapi.
“Patrick namshukuru sana mungu uko hai, nashukuru umerudisha fahamu zako” aliongea huku akionekana kweli kuwa alikuwa akilifurahia hilo. Sikumjua huyu dada wala sikufahamu yeye amenijuaje.
“utapona kabisa na utakumbuka kila kitu, tunafanya tuwezavyo kuhakikisha kuwa unarudisha fahamu zako” alizidi kusisitiza huku akifuta machozi.
“wewe ni nani” nilimuuliza huku nikimtazama usoni, hakika sura yake sikuijua kabisa, hata kama sikuwa na fahamu lakini sura yake ni kweli sikuwahi kuiona hata kidogo.
“Naitwa Pamela, ndiye daktari ninayemsaidia dokta Anderson katika matibabu yako, ni mimi ambaye ndiye nakuwa na wewe muda wote kuangalia afya yako, wewe ni sababu ya mimi kuendelea kuwa hapa” aliongea huku akionekana kuangalia pembeni kana kwamba alikuwa akifuta machozi.
“kwanini unalia” nilimuuliza huku nikimgeuza ili aniangalie.
“silii, ni furaha tu kwakuwa umeamka leo” kichwa changu kilikuwa kimejaa maswali mengi sana, lakini sikujua namna ya kuyauliza, kila kitu pale kilikuwa ni michoro kwangu isiyoashiria chochote, nilikuwa nimevurugwa akili na kila kitu kabisa, sikumfahamu yule Pamela na wala sikujua yeye ni nani, sikujua anaposema nimeamka je nililala toka lini, na kwanini kuamka kwangu kuwe ni furaha kwake, kwanini alie kwa mimi kuamka, kwanini alionyesha furaha na kusema nitapona, yeye alikuwa nani kwangu, mimi nilikuwa na thamani gani kwake, hiyo yote ilikuwa ni jakamoyo ndani ya moyo wangu, nilikuwa kama teja lililokuwa likihudhuria kliniki ya ukichaa.
“Pamela, mimi sielewi chochote” nilimuuliza huku nikilia baada ya kujitahidi sana kukumbuka lakini ikashindikana. Hakunijibu chochote badala yake alinishika mkono na kuondoka na mimi mpaka ndani ya ile hospitali. Tulipofika pale aliingia ndani na kutoka na daktari mmoja mzungu aliyekuja pale na kuanza kuongea na mimi kisha Pamela alikuwa akinitafsiria.
“Hellow Patrick am doctor Anderson”(habari Patrick, naitwa dokta Anderson). Alinisalimu na kunipa mkono, na mimi nilimpa mkono.
“We want to discharge you, but you will be under the care of doctor Pamela, you will stay at her place until we are sure that you can stand on your own”(tunataka tukuruhusu lakini utakuwa chini ya uangalizi wa dokta Pamela, utakaa nyumbani kwake hadi tutakapokuwa na uhakika kuwa kuwa unaweza kujitegemea) sauti ya Pamela ilisikika ikitafsiri maneno ya dokta Anderson.
“Pamela don’t bother to interpret, I do understand the language” (Pamela usihangaike kutafsiri, naielewa hiyo lugha), nilimuambia hayo Pamela na yeye alinyamaza kimya.
***
Niliruhusiwa kutoka pale hospitali na sasa tuliingia kwenye gari ya dokta Pamela kuelekea kwake, hapakuwa mbali sana na pale hospitali, muda wa dakika kumi tulikuwa tumeshafika.
“karibu sana Patrick, hapa ni nyumbani kwangu, ndiko ninapoishi, na ndipo ambapo na wewe utaishi” alinikaribisha huku akitabasamu na kuruhusu vishimo vidogo kwenye mashavu yake vionekane, nilikaribia na kuketi huku nikitazama kila kona ya ile nyumba. Ilikuwa ni nyumba ndogo lakini ilikuwa ni nzuri na ilikuwa na mazingira mazuri yaliyovutia.
“Unaishi na nani hapa” nilimuuliza swali wakati alipokuwa akienda kuchukua kinywaji kwenye jokofu.
“naishi mwenyewe, lakini kwasasa nitakuwa nikiishi na Patrick” aliongea hayo na kucheka. Sikumbuki kama niliwahi kucheka toka pale hospitali. Kwa muda mfupi niliokuwa na Pamela nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mtu mwenye kupenda sana kucheka, alikuwa ni mtu mcheshi na anayependa utani muda mwingi. Nilianza maisha haya ya kuishi kwa Pamela na muda mwingi dokta Anderson alikuwa akija pale nyumbani kuniangalia. Pamela na dokta Anderson walikuwa kama ndugu vile ingawaje Pamela alikuwa na asili tofauti kidogo.
****
Asubuhi tulivu ya desemba 1999 ilinikuta nikiwa Suva huko Fiji, ilikuwa ni miezi mitatu sasa toka nitoke hospitali lakini mpaka wakati huo bado sikujua chochote, mbali na kumuuliza Pamela maswali mengi lakini hakuwa tayari kabisa kunieleza chochote, siku zote historia ya maisha yangu na sababu za kwanini sina kumbukumbu yeye hakuziona za maana.
“Patrick leo tunatoka” nilimsikia Pamela akinipa taarifa hiyo asubuhi wakati alipokuja kugonga chumba changu.
“tunaenda wapi” nilimuuliza huku nijiachanisha na shuka zito nililokuwa nimejifunika.
“tunaenda Albert Park, amka ujiandae tunaondoka muda sio mrefu” niliamka na kuanza kujiandaa.
***
Safari ya kuelekea Albert Park ilianza, tulikwenda mpaka Tanoa plaza tukipitia Amy Roas na hapo tulisimama, kisha Pamela aliniambia tushuke tuingie ndani ya lile jengo. Tuliingia mpaka ndani ya jengo lile na kwenda upande wakulia mpaka juu kabisa ambapo tuliweza kuona mandhari yote ya Fiji na kwambali alinionyesha nchi ya Australia. Nikiwa pale juu nilisikia kama sauti yamsichana ikiniita na nilipogeuka nyuma sikuona mtu.
“ni nini Patrick” aliniuliza Pamela lakini sikuwa na la kumjibu, nilipokuwa nimegeuka sikumuona mtu yoyote lakini kwa uhakika kabisa niliona kama kivuli cha msichana niliyehisi kumfahamu, najua hata ningesema Pamela asingenielewa.
“hamna kitu, sijui ni nini nimeona” nilimueleza hayo na yeye alinifata na kunishika kichwa akiniambia kuwa amenileta pale kwasababu japo hakunieleza ni sababu gani hiyo. Alitnitoa pale na kunipeleka ndani zaidi kwenye chumba fulani na hapo nilianza kuhisi mapigo ya moyo yakinienda mbio.
“Pamela kuna nini hapa” nilimuuliza Pamela lakini hakuniambia kitu badala yake alinifunga kitambaa usoni na kuniambia niketi, niliketi huku nikiwa na wasiwasi juu ya kilichokuwa kikitokea pale. Giza lilikuwa limetanda kwenye macho yangu na hofu ilinifika. Nilianza kuona picha ya msichana kwa mbali na sikujua ni nani. Alikuwa msichana mrembo mweupe ambaye nilikuwa naye sehemu kama ufukweni mwa bahari, yule msichana alikuwa akifurahi na mimi nilikuwa nikimkumbatia kama vile tulikuwa wapenzi,,niliogopa sana kwakuwa haikuwa kawaida, alinifungua tena kile kitambaa na kuniuliza nimeona nini lakini sikuwa na la kumjibu.
“mimi ni nani Pamela?” nilimuuliza huku nikiwa kama natetemeka, alinitazama machoni huku akionekana kuzuia machozi.
“ukitaka kujua wewe ni nani lazima uwe makini na kile kikujiacho kwenye fikra zako” aliniambia nakuninyanyua kisha tulienda mpaka kwenye chumba kilichokuwa kulekule ndani kisha alivua nguo zake mbele yangu na kuvaa taulo na kuelekea bafuni, akiwa bafuni nilisikia akiniita lakini kwa uwoga nilivua nguo zangu na kuvaa taulo kisha nikamfata bafuni, nilipoingia alinikumbatia na kuanza kunipiga mabusu mwili mzima, mihemko ya mwili wangu ilikuwa karibu kabisa na hisia zangu hivyo nilianza kulipiza mashambulizi, kila nilipokuwa nikimshika kuna picha ya mwanamke ilikuwa ikinijia, tulitoana bafuni na kuja mpaka kitandania kisha kazi ilianza pale, Pamela alikuwa mtundu sana kitandani lakini kila alipojitahidi kunifanyia mambo flani taswira ya mwanamke mwingine ilikuwa ikinijia, tuliendelea kusumbuana na kuchokozana hisia zetu na mwishowe tulikutanisha maungo yetu ya uzazi, nilipokuwa katikati ya mchezo wakati Pamela akiwa juu kuongoza jahazi niliona sura ya yule msichana tena na kushtuka ana hapo Pamela alizidisha kasi, nilikuwa kama mtoto mdogo vile jinsi ambavyo nilikuwa nikilia na ile sura ya yule mwanamke ilikuwa ikinijia bado.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mary,,,Mary” nilijikuta nikitamka lile jina na hapo Pamela aliacha na kunishika kichwa,,kisha alikuwa akiniangalia kwa makini.
“kafanyaje” aliniuliza kama vile hakuelewa ninachomaanisha, nilinyamaza kwakuwa sikujua namna ya kuendelea kuelezea, hapo Pamela alianza tena kuushika mwili wangu na kuendelea na shughulia yake mpaka nilipokumbuka baadhi ya vitu.
“Mary ni nani Pamela” nilimuuliza kisha alinyanyuka vilevile akiwa uchi na kuondoka kuelekea bafuni, alipokuwa akiondoka nilimtizama na ile picha ilinijia tena. Nilijivuta pale kitandani na kwenda kumfata kule bafuni, alifungua lile bomba la mvua na kunivuta kisha alinikumbatia huku maji yakitumwagikia. Nilikuwa nimetumbua macho na yeye hakuwa anaongea zaidi ya kufungwa macho akiyaruhusu maji yazilowanishe nywele zake laini.
*****
USIKU WA SIKU HIYO.
Tulikuwa tumelala nyumbani kwa Pamela na siku hiyo ilikuwa mara ya kwanza mimi na Pamela kufanya yote yaliyotokea mchana huo.
“Mary ni nani” lilikuwa swali la kwanza kumuuliza Pamela usiku ule. Alikuwa amenilalia kifuani lakini nilipomuuliza alinyanyuka na kuketi.
“Mary ni msichana uliyekuja naye Fiji miaka zaidi ya sita sasa, ni mke wako na alikaa hapa akikuuguza kwa zaidi ya miezi sita ila baadaye aliamua kuondoka baada ya kumwambia kuwa si rahisi wewe kurudisha fahamu tena, aliondoka na hatukujua ni wapi alikwenda, tumejaribu sana kutafuta kumbukumbu zako lakini hatukupata” alinieleza hiku akijikaza ili asilie.
“kwanini sikuwa na fahamu” nilimuuliza.
“ulichomwa sindano ya dicomenzol, inayotumiwa kuchoma wanyama wakali ili kuwafanya watulie, walikuchoma wakazidisha kipimo na hii ilikuwa ni baada ya wewe kupata ajali ambayo hata hivyo tunahisi ilikuwa ni ya kukusudiwa, yani kuna mtu aliitengeneza ili itokee ndo wakuchome sindano ile ambayo ilimaliza kila kitu kichwani mwako”
“Mary Robert”nilikumbuka.
“Unaweza kuwa si wa kwanza kwake, wala wa mwisho kwake, Aliwahi kupenda kabla na anaweza kupenda tena. Lakini kama anakupenda wewe, unajali nini tena? Yeye si mkamilifu, na wewe pia si mkamilifu, na wote wawili hamuwezi kuwa wakamilifu pamoja, lakini kama anaweza kukufanya ucheke, anakunfanya ufikiri mara mbili na anakiri kuwa yeye ni binadamu a anatenda makosa basi mshikilie yeye na mpe kwa kadiri uwezavyo. Anaweza kuwa hakufikirii kila sekunde katika siku, lakini atakupa sehemu ya utu na mwili wake anayojua utaivunja YANI MOYO WAKE. Usimbadilishe, usimchambue, usitegemee makubwa zaidi ya yale awezayo kukupa au yale anayomudu. Tabasamu pale akufurahishapo, muambie pale anapokukasirisha, ana ummis pale anapokuwa hayupo. HAPO UTAKUWA NA FURAHA YA MAPENZI NA WASIWASI WA MAPENZI UTAONDOKA” HII NI SEHEMU YA PILI.
Ile CD yenye ile simulizi iliendelea kusikika redioni na usingizi ulikatika kabisa, nilikuwa najiuliza huyu Mary ndiyo nani na kafanya nini. Baada ya matangazo machache yule mtangazaji wa redio alirudi hewani na kusema kuwa sasa wataweka sehemu ya pili ambayo ni mahojiano kati ya Pamela na Mtangazaji. Nilijiweka tayari kusikiliza na kwenye ile CD ilisikika sauti ya mtangazaji ikimwambia Pamela aeleze kila kitu alichotaka kukisimulia pale.
**PAMELA**
Patrick alikuwa ameanza kurudisha fahamu kitu ambacho nilikuwa nikikiota siku nyingi, ingawaje kitaaluma nilikuwa daktari tena mtaalamu wa magonjwa ya akili na ubongo na taaluma yangu hainiruhusu kukata tamaa ya kumuhudumia mgonjwa ambaye bado anapumua vizuri ila kwa Patrick ilikuwa tofauti, kuna muda nilikuwa nakata tamaa kabisa, alipotelekezwa pale hospitali niliamua kujibebesha mzigo mzima wa jukumu la kusimamia matibabu yake japo nilipata msaada mkubwa sana toka kwa dokta Anderson na mkewe Sara.
Historia ya maisha yangu kipindi cha nyuma ilinifanya kuwa mtu mkatili sana lakini sikuwa hivyo kwa Patrick. Yeye ndiye aliyeanza kunionyesha tumaini jipya lililopotea siku nyingi na kunifanya nianze kuwa mtu wa tofauti kabisa katika maisha yangu.
Nilizaliwa na kuwa yatima miaka mingi sana iliyopita, nilikulia kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha masista na huko tulifundishwa tabia njema na namna ya kuishi na kila mtu, nilipofika kidato cha nne nilianza kujihusisha na mapenzi, sikuwa na akili vizuri, nikajiingiza kwenye mapenzi na kijana Alex ambaye na yeye alikuwa ni yatima pia ila mara nyingi tulikuwa tukionana pale walipokuwa wanakuja kusali kanisani. Nilimpenda sana Alex na niliamini kuwa alikuwa akinipenda pia, nikiwa kidato cha tano nilipata ujauzito na sikujua cha kufanya, nilifukuzwa pale kituoni na baada ya kukataa kusema nani alinipa ujauzito, http://deusdeditmahunda.blogspot.com/nisingeweza kabisa kumtaja Alex kwakuwa ningekuwa nimemuharibia mipango yake ya kimaisha. Nilikuwa tayari kuubeba ule mzigo wa mimba kwakuwa nilimtakia mema hasa nikitegemea kabisa kuwa angekuja kuwa baba wa yule mtoto, hivyo ile mimba ilibaki kuwa ya kwangu na wala Alex hakutaka kusikia, siku moja nilikwenda kama kawaida pale ambapo huwa tunakutana na nikamweleza kuhusu ujauzito ule na aliukana kabisa akasema hajawahi kuwa na mahusiano na mimi, nilimweleza kuwa nia yangu si kumwambia yoyote kuwa yeye ndiye aliyenibebesha ujauzito ila nia yangu ni kumtaka tu ajue kuwa kuna kiumbe chake tumboni mwangu, alikuwa mkali sana na kuniona kama nilikuwa Malaya, siku hiyo alinipiga sana na kunisababishia maumivu makali, niliondoka na kurudi kwenye magofu ya nyumba za watu nilikokuwa nikilala na mchana nilikuwa nikila mabaki ya vyakula vya wahindi. Kila mtu aliniona kama mimi ni Malaya lakini sikujilaumu kwakuwa nilitambua athari za nilichokuwa nafanya na Alex ila niliamua kufanya kwakuwa nampenda.
Siku tatu mbele nilianza kupata maumivu makali sana ya tumbo na baadaye nilianza kutokwa na damu mabongemabonge, sikuwa na wakumlilia zaidi ya kumuomba mungu anisaidie, nilitokwa na damu siku mbili mfululizo huku maumivu ya tumbo yakizidi, sikuwa na dawa ya kumeza kwakuwa sikujua ni dawa gani nimeze na hata fedha ya kununulia dawa sikujua ningeipata wapi, nilikaa nikitafuna majani ya alovera na baada ya kutokwa damu kwa muda wa siku mbili tumbo lilitulia na sikujua madhara ya kile kilichonitokea yatakuwa wapi ila nilichofahamu ni kuwa mimba imetoka.
Katika mihangaiko yangu jijini nilikutana na msichana wa umri kama wangu kwakipindi hicho na yeye aliniambia anakwake hivyo tukakae nae na atanifundisha biashara, nilimkubalia kwakuwa sikuwa na machaguo ya kutosha na hapo alinipeleka kwake, palikuwa na chumba kimoja tu lakini kilichojaa vitu mbalimbali vya thamani, nilikaa pale siku moja lakini nilikuwa nimeshagundua kuwa alikuwa akijiuza,kuna muda mwanaume alikuja pale na walianza kushikana mbele yangu, nilinyanyuka na kutaka kutoka lakini yule dada alinikataza na kuniambia kuwa ile ndiyo biashara na natakiwa nijifunze, nilijizuia sana na kutaka kuondoka lakini bado maisha yale niliyokuwa nikiishi yalikuwa ni hatari sana. Hivyo nilikubaliana na yule dada na tulianza biashara hiyo, nilifanya kwa shingo upande lakini kazi ilikuja kunishinda pale wateja waliokuwa wakija pale walipotaka kufanya mapenzi na mimi kinyume na maumbile, nilikataa katakata na hapo yule msichana alinifukuza kwake, niliondoka na kwenda kwenye kile kituo kuomba wanisaidie lakini walinikataa, hivyo ikabidi niingie mtaani tena, nilikutana na mzee mmoja akaniahidi atanipatia kazi nyumbani kwake na mimi nilikubaliana naye na hapo nilipata kazi ya ndani kwa huyo mzee, baada ya mwezi mmoja tu wa kazi vioja vilianza baada ya watoto wake wa kiume kuanza kunitaka, nilikataa mara nyingi lakini kuna siku wakati yule baba amesafiri tukabaki na wanae watatu wa kiume tu, siku hiyo nilitoka bafuni na kuingia chumbani kwangu, nilipovua kanga na kuanza kujifuta maji nilishtuka kuona wale vijana ndani ya chumba changu, nikajifunika na ile kanga lakini walininyang’anya na wawili walinishika kwa nguvu kisha waliniingilia kwa zamu, niliumia sana kwakuwa walitumia nguvu nyingi sana lakini nilipanga kuja kumuambia baba yao japo waliniambia wangenifanyia kitu kibaya kama ningesema kwa baba yao. Mzee wao aliporudi nilimueleza ukweli lakini hakunielewa zaidi ya kunifokea kuwa nimeleta umalaya wangu ndani ya nyumba yake, niliamua kunyamaza kimya na kuendelea na kazi zangu, ile nyumba hakukuwa na mwanamke kwakuwa mke wa huyo mzee alikuwa nje ya nchi kwa masomo na hata watoto wake walikuwa ni watu ambao hawakuwa wakukaa nyumbani sana.
Wiki tatu baada ya kubakwa na wale watoto, niliamka asubuhi na kujikuta chumbani kwa yule mzee, nilikuwa nimechoka na nilishangaa nilifikaje lakini akili yangu ilikumbuka kuwa jana usiku yule mzee alileta juice na kunipa ili ninywe, nikagundua kuwa aliniwekea kilevi kwenye ile juice na kunibeba hadi chumbani kwake. Kilichoniliza sio yeye kuniingilia kimwili bila ridhaa yangu ila ni yeye kuniingilia kinyume na maumbile, nililia sana lakini hakuonekana kujali;
“sio sawa ulivyonifanyia” nilimuambia huku nikilia lakini hakunisikiliza.
“binti wewe kazi yako hapa nyumbani ndiyo hiyo, yani wewe mimi nikulipe elfu 15 kwa mwezi na nikulishe na ulale kwangu kwa kazi ya kupika, kudeki, kufua nguo za watu wote humu ndani na kufanya usafi mwingine tu?,,ni sawa hivyo kweli? Fedha yote hiyo kwa kazi ndogo tu ya kufanya usafi” aliniambia huku akicheka.
“utajisikiaje kama binti yako ndo angefanyiwa hivyo” nilimuuliza huku nikimtazama.
“mwanangu hawezi kuwa beki tatu, tena nyamaza kabisa usianze kunihubiria hapa, kafungashe mizigo yako uondoke maana utatuwekea sumu huku ndani, fungasha nikitoka hapa uwe nje ya hii nyumba, chukua fedha zako hizo” alinisukuma na kunipa shilingi elfu 30, nililia sana lakini sikuwa na mahali pa kwenda, nilikwenda polisi kuripoti lakini chakushangaza mwanamke mwenzangu aliyekuwa pale ambaye ni polisi alikuwa wakwanza kunifukuza na kuniita mimi Malaya, aliyeonyesha nia ya kunisaidia alikuwa kijana mwingine askari lakini tulishindwana baada ya yeye kunitaka kimapenzi kama rushwa. Niliamua kumuachia mungu kila kitu lakini nilimchukia kila mwanaume duniani na nilipanga kutokuja kuolewa wala kubeba ujauzito kwakuwa kama ingetokea ningezaa mtoto wa kiume nisingempenda kabisa.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ukimwi duniani ambapo shirika la misaada la marekani lilikuwa likifanya kampeni ya kupima kwa hiari, nilikwenda kupima ili nijue afya yangu na hapo ndipo nilikutana na dokta Anderson, nilimueleza kila kitu kuhusu maisha yangu wakati alipokuwa akinipima, na alisema kuwa angenisaidia kurudi shule na mpaka pale ambapo ningetaka kwenda kitaaluma. Nilirudia kidato cha nne kwa msaada wa fedha za mzee Anderson na mkewe Sara, walikuwa nje ya nchi lakini walikuwa wakinitumia fedha vizuri na kwa wakati, nilianza kuona matumaini ya maisha tena na baada ya kumaliza kidato cha nne nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano kilakala sekondari kwa mchepuo wa PCB (fizikia, kemia na baiolojia), kidato cha sita nilifanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza na hapo ndipo dokta Anderson aliponichukua na kunipeleka kusoma nchini Australia kama daktari na baadaye shahada yangu ya pili nilisomea mambo ya magonjwa ya akili, nilifanya kazi na dokta Anderson miaka yangu yote mpaka nilipoomba uraia wa huko na kujivua uraia wa Tanzania, sikuwa na hisia na wanaume kabisa na mwaka mmoja kabla ya kumfahamu Patrick nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke mwenzangu, nilikuwa msagaji lakini yote haya ni kwakuwa hisia zangu zilihama na kwenda kwa wanawake wenzangu.
Yaliyomtokea Patrick yalinikumbusha sana yaliyotokea Tanzania na hiyo ilikuwa sababu ya mimi kujitolea kumsaidia. Kwa ufupi Patrick alirudisha hisia zangu juu ya wanaume, mwanaume pekee niliyekuwa nikimuona kama mungu wangu ni mzee Anderson lakini wengine wote hata madaktari wenzangu niliofanya nao kazi walinijua kuwa sikuwa nawapenda hata kidogo, wengi walijua kuwa mimi ni msagaji na walichukia tabia yangu hiyo lakini kwangu ilikuwa ni faraja na nilijisikia vizuri sana kuwa kwenye mapenzi na mwanamke mwenzangu, nilimpenda sana na yeye alinipenda na alinipa kila nitakacho na wala sikuhitaji mwanaume. Lakini uwepo wa Patrick pale hospitali ulinibadilisha taratibu na hata Nancy ambaye ndiye alikuwa mpenzi wangu alianza kulalamika kuwa nimemsahau, nilimueleza ukweli kuwa kwasasa sitaweza tena kuwa naye kwakuwa nahisi nampenda mtu mwingine. Alilia lakini nilipomueleza kiundani alinielewa. Kwa miaka sita yote Patrick akiwa kitandania kama mfu nilikuwa naye pembeni, kuna muda nililala pembeni naye usiku kucha, kuna wakati nilikuwa siendi kwangu baada ya kazi na badala yake nilikuwa nikikaa pale chumbani kusubiri mda atakaofungua macho, nilitaka japo kuisikia sauti yake, sura yake nzuri na ya kitoto ilinifanya nimpende, nilimuonea huruma kwa alichotendewa lakini pia niliona nina nafasi ya kumsaidia, miaka sita na mwezi mmoja ulipotimia siku hiyo ilikuwa asubuhi nikaona manesi wakikimbizana huku na huko na dokta Anderson alikuwa akikimbia kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Patrick, sikujua kilichoendelea ila nilijikuta nikianza kulia kwakuwa nilidhani Patrick amefariki kwasababu jana yake usiku hali yake haikuwa nzuri, sikuweza kwenda kule kwakuwa nilikuwa naingia kwenye chumba cha upasuaji hivyo nilijikaza na kuingia na jopo la madaktari wengine, tulifanya upasuaji kwa masaa manne mfululizo, baada ya kutoka nilikutana na dokta Anderson aliyekuwa anaonekana akitabasamu;
“Ameamka na yuko salama kabisa” aliniambia huku akinifata na kunikumbatia, niliona kabisa machozi yakinitoka.
“Natumaini furaha yako itazidi Pamela na kazi kubwa kwasasa ni kuhakikisha Patrick anakuwa salama na hali yake inarudi kama mwanzo, naamini hiyo ndiyo kazi kubwa uliyokuwa nayo kwasasa binti yangu” alinieleza hayo na mimi nilipata faraja sana, dokta Anderson aliielewa furaha yangu na siku zote alinichukulia kama Semphroza ambaye ni binti yake aishiye marekani na mumewe. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kabla ya Patrick kuamka.
*******
“Mary Robert” nilisikia Patrick akitaja jina la yule mwanamke aliyemtelekeza, nililia kwa furaha japo nilijua lengo langu la kuwa na Patrick lingekuwa gumu sana kama angekuwa bado anampenda Mary. Nilifanikiwa kukaa na Mary na kuongea naye miezi michache kabla ya yeye kuondoka, alikuwa anaonekana kama msichana wa kisasa zaidi, alikuwa ni mtu wa kuongea na simu kila saa, mtu ambaye ni msiri sana na mtu anayekwenda na mda, hakuwa muongeaji sana wala hakutaka kukaa na mtu mda mrefu, sikuweza kujua kama anampenda kweli Patrick au la japo baada ya yeye kuondoka ndiyo nilikuja kujua kuwa hakuwa mvumilivu.
“Unamkumbukaje Mary Robert” nilimuuliza Patrick ambaye alionekana akiwa ameduwaa huku machozi yakimtiririka.
“sikumbuki, simkumbuki Mary, sielewi kitu” alizidi kulia huku akitazama mbele kama alikuwa akiona kitu, nilimshika na kumkumbatia huku na mimi machozi yakinitoka, ilionekana kama anajitahidi sana kukumbuka lakini haikumsaidia hiyo.
“Tafadhali kama unajua chochote kuhusu Mary nieleze, yeye ni nani, anafanya nini kwenye maisha yangu” aliniuliza huku akilia.
Nilimuacha pale na kwenda kufungua kabati kisha nilitoa boksi lenye barua na pesa ambayo Mary aliiacha kwenye mfuko pale hospitali kabla hajaondoka bila kuaga, sikuwahi kuisoma ile barua kwa miaka yote hiyo, wala sikuwahi hata siku moja kutumia zile pesa. Nilifungua lile boksi na kutoa ile barua na yale mabunda ya pesa nikayaweka pale kitandani kisha nilimkabidhi ile barua na yeye akaifungua, niliona machozi yakimtoka kila alipokuwa akisoma mstari mmoja wa ile barua, sikuwa najua ni nini kimeandikwa kule ndani mpaka nilipoichukua ile barua na kuanza kuisoma. Nilitokwa na machozi na kumgeukia Patrick.
“Pamela ni nini kinaendelea mbona sielewi kila kitu” aliniuliza huku machozi yakiwa yameufumba uso wake, nilimuonea huruma kwakuwa nilielewa maumivu ayapatayo kwa hilo limtokealo. Ile barua ilisomeka hivi;
mpendwa mume wangu,
Nakuandikia ujumbe huu kwa uchungu na masikitiko makubwa. Najua huwezi kupona tena katika maisha yako kwani daktari amenieleza kuwa uwezekano wa wewe kurudisha kumbukumbu zako ni mdogo sana,,nilipenda kuwa na wewe Patrick na unalijua hilo lakini sikuwahi kufikiri kuwa nitakuja kuishi na wewe katika hali hiyo uliyokuwa nayo,,honeymoon ndo chanzo cha yote, huwezi kunikumbuka hata mimi najua,,nilikupenda sana Patrick, lakini nina malengo mengi ya kuyatimiza kabla ya kuingia kaburin hivyo sina budi kukuacha na kwenda kuendeleza maisha huko nyumbani,,nisamehe, sina jinsi ya kufanya zaidi ya kwenda kuwaambia nyumbani kuwa tulipata ajali kwenye boti na ulipotelea baharini,,nimeacha kiasi cha fedha cha kutosha naamini kitakusogeza,, ikiwa hutafanikiwa kuisoma barua hii na ikitokea kuwa umepoteza maisha basi jua kuwa ninakazi kubwa ya KUMALIZIA MENGI NILIYOANZISHA NAKUPENDA,nakupenda sana ila siwezi kuendelea kuishi na wewe hapa maana itakuwa napoteza muda.
MAISHA MEMA Patrick.
Mimi Mary
Ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
Ilikuwa inaelekea saa 5 ya usiku, ile simulizi ilikuwa imenishika sana na sikutamani wamalize, niliendelea kusikiliza mahojiano yale kwa makini sana na yule msichana Pamela alikuwa anaendelea kusimulia.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**PAMELA**
Niliendelea kumtazama Patrick huku nimeshikilia ile barua, alikuwa akifikiria mbali sana na sikujua nimuanzeje kwakuwa alikuwa kwenye wakati mgumu sana.
“Patrick” nilimuita huku nikimshika bega. Alinigeukia na kunitazama huku machozi yakimtoka.
“Usilie Patrick nipo hapa kwaajili yako” nilimsogelea na kumkumbatia, haikuwa rahisi kuvumilia kumuona mtu umpendaye akilia mbele yako kwa maumivu ambayo wewe usingeyavumilia kama ungehitajika kuyakabili.
“Kwanini Mary amenifanyia hivi, sikustahili kufanyiwa hivi” aliongea hayo huku akiendelea kutoa machozi. Alikuwa tayari amesharudisha fahamu na sasa alielewa kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Hii ilinipa faraja sana kwakuwa siku zote nilitamani akumbuke kila kitu tena ili na mimi niwe na furaha, nilimtazama usoni na kuona jinsi gani alikuwa akimpenda Mary na alikuwa anaumia moyoni kwa kilichotokea.
*SIKU TATU MBELE*
“Patrick una mpango gani kwahiyo maana leo ni siku ya pili huongei chochote” nilimuuliza baada ya kuchoka kumuona kila mara akikaa peke yake na kutaka kuwa peke yake, ile hali iliniumiza sana sikuelewa wala kujua nimsaidie vipi, lakini utatuzi pekee niliokuwa nao kwa wakati huo ni kumpenda kwa dhati na kumfanya amsahau Mary japo nilijua fika kuwa kumsahau mtu uliyempenda kwa dhati ni sawa na kujaribu kumkumbuka mtu ambaye hujawahi kukutana naye.
“sijui mpango nilionao Pamela, sijui ni nini nafikiria wala namna ya kufanya chochote” aliongea hayo huku akitazama mbele kabisa ya ufukwe wa bahari.
“Ulijuana wapi na Mary?” ndilo swali nililomuuliza wakati akiendelea kutafakari, alinishika mkono na kuondoka na mimi kuelekea ufukweni na tulipofika alianza kunisimulia historia yake na Mary.
“Nilimjua Mary miaka miwili kabla ya kufunga nae ndoa. Tulikuwa tukiishi naye mtaa mmoja na sikumjua kwa kipindi cha udogo wake bali kipindi cha ukubwa wake. Alizaliwa pale mtaani kwetu kule Tanzania, mimi sikuzaliwa pale, nilizaliwa sehemu nyingine lakini kwakuwa wazazi wangu walikuwa wameachana toka utoto mwangu nililazimika kuja kuishi na baba na mama mwingine ambaye alikuwa na mtoto mmoja aitwaye Mark, kwaiyo katika familia hii tulikuwa wawili tu, mimi na mdogo wangu Mark, katika muda wote tuliokaa pale, nyumba ya kina Mary ilikuwa ikikaliwa na mfanyakazi tu, nilielezwa kuwa mwenye nyumba ile anaishi marekani na anafanya kazi huko, ana mtoto mmoja wa kike na mkewe nalishafariki siku nyingi nyuma. Miaka mingi baadaye walirudi yule mzee na mwanae Mary, alikuwa ni msichana mrembo sana, mrefu wa wastani, mwenye kila aina ya sifa, alikuwa ni mtoto wa kisukuma aliyechanganyika na mnyakyusa, mchanganyiko huo ulizalisha kitu kinachoonekana. Nilipomuona sikushtuka sana kwakuwa sikuwa na mawazo naye. Mara nyingi nilimsikia Mark akimsifu na walikuwa wakiongea mara kwa mara kwenye simu, ni wakati huo ndipo nilikuwa nimeshahama nyumbani na kuanzisha kampuni yangu ya harusi na mapambo, iliyoitwa PATRICK WEDDING AND DECORATION COMPANY LTD, ilikuwa ni kampuni kubwa kuliko zote Tanzania kwenye mambo ya upangaji wa harusi na upambaji. Kampuni hii ilikuwa inachukua tenda kamili za harusi, yaani mtu kama anaharusi au sherehe yoyote anakuja na kutoa fedha yote kwaajili ya sherehe na sisi tulikuwa tunatafuta ukumbi, tunahusika na kuandaa mavazi yao, sare na kadi za waalikwa, muziki na mshereheshaji,tulikuwa tunachukua video kwenye hayo maharusi na kutoa usafiri, pia baada ya kumaliza mkataba wa kusimamia harusi hizo ilikuwa mteja akitaka kwenda mapumizikoni basi tunaingia naye mkataba wa kumfanyia utaratibu wa kwenda na kuhakikisha usalama wake mpaka atakaporudi. Hii ilikuwa ni kampuni kubwa sana iliyoajiri watu zaidi ya hamsini wenye fani mbalimbali, ni kampuni ya ndoto yangu. Nilipokuwa katika shughuli zangu za kikazi nilikuja kukutana na Mary siku alipokuja ofisini kwangu kwaajili ya kuomba kuonana na mimi ili afanye mahojiano juu ya mafanikio yangu na maisha ya mapenzi, hapo ndipo niligundua kuwa Mary alikuwa akimiliki kampuni iliyokuwa ikichapisha jarida la EXLENT MEN lilikokuwa likitoka kila mwezi na kuelezea juu ya wanaume wenye mafanikio walio chini ya umri wa miaka 35. Alikuwa ni msichana mcheshi sana, mjanja na ambaye alijitolea maisha yake kujiimarisha na kuwa mfano wa kuigwa, alikuwa mmoja kati ya wanawake wachache ambao hawakuwa maarufu lakini walikuwa machachari na wachapakazi tena akiwa na umri wa miaka 25 tu.
****
“karibu sana Mary” ilikuwa ni siku aliyokuja rasmi kwaajili ya yale mahojiano, alikuja na timu ya wafanyakazi wake ambao ni wapiga picha na waandishi wengine, ni mara chache saba meneja akaja kuhoji mtu badala ya waandishi waajiriwa ila kwangu mimi alikuja kunihoji yeye mwenyewe, hivyo niliwakaribisha hadi sehemu maalumu iliyokuwa imeandaliwa kwajili ya mahojiano hayo.
“Asante sana ndugu Patrick, najua mimi na wewe tunajuana ila leo nimekuja kikazi zaidi,,hahaa” aliongea huku akicheka na wakati huo wale wengine walikuwa wakifunga kamera zao na muda sio mrefu mahojiano yalianza;
“kwanza nilitaka kujua juu ya mafanikio yako bwana Patrick” aliniuliza swali huku akitabasamu, hapo ndiyo nilianza kugundua hisia zangu kwa Mary, japo alionekana kabisa kuwa alikuwa si msichana mwepesi sana kukubali hisia za mwanaume kuingilia maamuzi ya fikra zake.
“mh,,baada ya kumaliza chuo kikuu ambapo nilisoma mambo ya ujasiriamali, ndiyo niliandika mradi huu wa kuanzisha kampuni, sasa zilikuwa zikihitajika milioni 150 ilikuanzisha mradi lakini niliweza kufanikisha kupata milioni tano tu toka kwa mzee wangu, hivyo nililazimika kuingia benki kuomba mkopo wa milioni 30 kwa kutumia kiwanja nilichopewa na mzee, baada ya kupata mkopo nikaanza mradi wa kuku elf 3 ambao ndio ulionipa mtaji wa kuanzisha hii kampuni” wakati nikimueleza hayo yeye alikuwa makini sana kunitazama usoni, niliona upendo toka kwenye sura yake pale nilipomtazama.
“uuum,,unakipato cha shilingi ngapi kwa project zako zote” aliniuliza huku akicheka.
“napata wastani wa milioni 40 kwa mwezi baada ya kutoa matumizi yote” nilimjibu na kumtazama tena machoni na yeye aliona aibu na kutazama pembeni.
“kwanini hujaoa” aliniuliza huku akitabasamu.
“mmh, nadhani muda bado kidogo, lakini pia wakumuoa bado sijampata, wengi wanatamani mali nilizonazo lakini mimi nahitaji mtu wa kumpenda Patrick na si mali za Patrick” mahojiano kwa siku hiyo yaliendelea kwa muda kidogo na baada ya pale tulipata chakula cha mchana na wafanyakazi wake aliokuja nao pamoja na baadhi ya wafanyakazi wangu. Tulibadilishana namba za simu za mkononi na hapo tulianzisha urafiki wetu. Nilimuajiri Mark kama muhasibu kwenye kampuni yangu na nilikuwa nikimlipa mshahara mara tano zaidi ya wafanyakazi wengine waliokuwa na vyeo vinavyoendana na yeye, yote ni kumfanya yeye kama ndugu yangu awe na maisha bora, ingawaje mimi na Mark hatukuwa karibu sana au kuwa tunakaa na kuzungumza kuhusu mapenzi, bali mda mwingi tukikaa tulikuwa tukiongelea kazi na maisha tu.
**MIEZI MIWILI BAADA YA MAHOJIANO**
Ikawa ni miezi miwili toka Mary aje kunihoji, wakati huo nilikuwa nimeshuka uwanja wa ndege nikitokea Afrika ya Kusini kwenye biashara zangu, nikashtuka kumkuta Mary pale uwanja wa ndege akinisubiri, kilichonishangaza ni kwamba toka baada ya mahojiano nilikuwa nimeongea naye kwenye simu mara mbili tu na sikuwahi kumwambia naenda nje wala kumuambia narudi Dar hivi karibuni.
“umekuja kufanya nini Mary” nilimuuliza pale alipokuja na kunikumbatia.
“Nimekuja kukupokea” aliongea huku akicheka kama kawaida yake.
“Nani kakuambia juu ya safari yangu” nilimuuliza wakati tukitembea kuelekea nje, hakunijibu haraka ila alipokea mizigo yangu na kuingiza kwenye gari yake kisha alinifungulia mlango na kuniambia niingie.
“vijana wangu wale pale wamekuja kutuchukua” nilimuambia huku nikiwa nimesimama namtazama jinsi alivyokuwa akicheka.
“mwambie sekretari wako aende akapande kule na huyo kijana wako mwingine, mimi leo nitakuwa dereva wako na napenda twende kwangu kwanza then nitakupeleka kwako” nilimtizama na kutabasamu, sikuwa na la kusema zaidi ya kumkubalia name niliingia kwenye gari yake tayari kwa kuondoka. Nilipofika kwake hakukuwa na mtu zaidi ya mlinzi wake, ilikuwa ni nyumba ndogo ila yenye bustani kubwa na iliyonakshiwa vizuri sana kwa rangi za kuvutia, alikuwa na magari mawili ya kifahari yaliyopendezesha muonekano wa ile nyumba. Tuliingia mpaka ndani na kisha aliniacha pale sebuleni huku nikishangaa jinsi alivyokuwa amepapamba pale ndani, alirudi na kuniambia kuwa bafu liko tayari kama nataka kwenda kuoga.
“hahaa sio busara kuoga nyumba ya mtoto wa kike” nilimueleza huku nikicheka kama yeye alivyokuwa akicheka wakati akinieleza hayo.
“mimi kwako ni zaidi ya mtoto wa kike, tafadhali nifate nikuonyeshe bafu lilipo na nguo zipo za wewe kubadilisha nilinunua kwaajili yako” aliongea hayo na hakunipa muda wa kuongea chochote, alinitazama huku akitabasamu na kuelekea kwenye korido na mimi nilimfata, aliingia chumbani na kunionyesha bafu la chumba chake na nguo zilikuwa zipo pale kisha alifunga mlango na kurudi sebuleni, nilijiuliza sana nini nia ya Mary kufanya vile.
“Happy birthday Patrick” niliisikia ile sauti baada ya kutoka bafuni na kwenda kwenye meza ya chakula aliyokuwa ameandaa, kiukweli sikuwa na habari kuwa siku hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa, lakini swali lilikuwa ni je Mary alijulia wapi siku yangu ya kuzaliwa na alifanya vile kwa nia gani.
“umejuaje siku hii Mary” nilimuuliza baada ya kumaliza kuzima ile mishumaa.
“Nakupenda Patrick, ndiyo maana nafatilia kila linalokuhusu, natamani sana uwe mume wangu, naamini wewe utanijali na kunipenda kwakuwa nimeona upendo kwenye macho yako” aliongea hayo huku akimaanisha, niliyaamini maneno yake kwakuwa aliyaongea kwa sauti ya ujazo wenye kumaanisha.
“Mary unauhakika na unalolisema hapa? Nakupenda pia na nina hisia na wewe toka siku ulipokuja kunihoji pale ofisini kwangu, lakini nayajua mapenzi vizuri, si kitu cha kukikurupukia sana kama tunavyoweza kukurupukia mambo mengine” nilimuuliza jambo ambalo nilikuwa na uhakika nalo kuwa jibu lake lilikuwa chanya.
“nina jiweza Patrick kiuwezo na kimaisha ninachofata kwako ni penzi tu” aliongea huku akinishogelea na kunishika midomo yangu. Siku ile ilikuwa ndiyo siku ya kwanza ya mapenzi yangu na Mary, nilimvisha pete ya uchumba kama miezi mitatu baadaye na yeye ndiye alikuwa maisha yangu tena, alikuwa faraja yangu na kiongozi wa hisia zangu.
Baaya miezi sita toka nimvishe pete Mary nilisikia kuwa Mary alikuwa na mahusiano na Mark, nilishtuka lakini kwakuwa nilikuwa nina kazi nyingi za kufanya sikutaka kufatilia kwanza lile jambo. Mary nayeye hakuwepo nchini hivyo sikuwa na namna ya kumuuliza kwa ukaribu, nilisubiri hadi siku aliporudi ndipo nilipomuuliza;
“haikuwa hata ni mahusiano, ni utoto tu, mimi na Mark tulisoma shule moja ya msingi na tuliishi kipindi kirefu sana kwa ukaribu na hata sekondari tulisoma nae, yeye ndiye aliyenitoa bikra lakini ilikuwa ni katika hali ya utoto, nilipofika kidato cha tatu mama yangu alifariki na nililazimika kwenda kuishi na baba nchini marekani, niliporudi nilikuwa na mawasiliano na Mark lakini sikuwa nampenda tena” alinieleza hayo na mengine mengi lakini nikaona busara ni kumfata Mark na kumuuliza.
****
Niliondoka jioni ya siku ya jumatano na kwenda nyumbani kwa Mark, haikuwa kawaida kwa mimi kumtembelea sana nyumbani kwake mara kwa mara.
“karibu bro, leo naona umepotea njia” alinikaribisha huku akinitania, Mark alikuwa ni ndugu yangu wa damu, tulizaliwa mama tofauti lakini baba yetu alikuwa mmoja lakini yeye alikuwa na tabia ya tofauti na mimi, mimi nilikuwa muwazi sana, nikikasirishwa huwa nasema ila yeye hata umkasirishe sio rahisi sana kusema au kukuonyesha.
“hapana leo nimekuja kukucheki isijekuwa ushaoa na watoto unao huku ndani lakini husemi,,hahaa” nilimtania na kuingia ndani kisha nilikwenda kwenye jokofu na kujichukulia kinywaji.
“Vipi tena bro, ni kuhusu wazee au ni nini” aliniuliza huku akiwa amesimama.
“Hapana ni kitu kingine, embu keti chini” nilimuambia na yeye aliketi.
“Mark nakaribia kuoa, umri unaenda na nina kila kitu, nafikiri sasa ni muda wa mimi kuoa na kuanzisha familia mapema kabla sijaishiwa nguvu za kutafuta pesa” nilimuambia hayo na kuvuta pumzi, sikujua niliielezee vipi lile swala.
“Ni wazo zuri bro, na naamini Mary atakuwa mke bora kwako” aliongea kwa sauti ya upole iliyojaa unyonge.
“natumaini hivyo lakini kuna swala linanitatiza kidogo” nilimuambia hayo huku nikimtazama usoni.
“ni nini tena bro?” aliniuliza huku akionekana kuhofia kitu fulani.
“Ni kuhusu mahusiano yako na Mary” nilimueleza hayo na kumfanya abadilishe mkao, alionekana hakuwa tayari san kuanza kuliongelea hilo lakini sikuelewa sababu ni nini.
“Bro, mimi na Mary tulikuwa wapenzi, na nadhani kwasasa hakuna linaloendela baina yetu mimi na yeye, kwahiyo wewe endelea tu” alinijibu kwa kifupi sana na alionekana alikuwa amebadilika kabisa, sikujua ilikuwaje mpaka akawa vile lakini niliyachukua maneno yake kama Baraka zake kwangu, hivyo baada ya kumsoma Mary kwa muda mrefu sasa tuliamua kuunganisha kampuni zetu na kuwa kampuni moja, tulikuwa tukishughulika na utoaji wa majarida na mambo ya harusi kwa pamoja, kampuni mpya iliitwa PATRIMARY GENERAL ENTERPRISES LTD, na Mary alikuwa Meneja Masoko na Muhariri mtendaji wa Jarida, Mark alikuwa ni Muhasibu na Mkurugenzi mtendaji, mimi nilibaki kuwa Meneja mkuu, wafanyakazi wote walibaki kama walivyokuwa na wengine tuliwapandisha cheo. Baadaye nilifunga ndo takatifu na Mary na baadaye tulikuja mapunziko huku FIJI, yote yaliyotokea yalitokea tukiwa huku Fiji”. Alielezea Patrick huku akibubujikwa na machozi.
“bado unampenda Mary” nilimuuliza huku machozi yakinitoka, sikutaka aseme kuwa anampenda kwakuwa tayari mimi nilikuwa nampenda yeye.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nampenda sana, sikuwahi kuacha kumpenda” maneno hayo yaliuchoma sana moyo wangu, nilinyanyuka pale na kuondoka kurudi nyumbani, Patrick alibaki pale ufukweni, nilifika mbele kidogo nikasikia mlio mkubwa wa bunduki, nilishtuka na machozi yangu yalikauka, nilipotazama nyuma niliona kwa mbali Patrick akianguka.
“Ulemavu wa fikra mgando tulizonazo juu ya maisha na juu yetu wenyewe huzaa mawazo mpauko yasiyoakisi umuhimu na umaana wa utu wetu na malengo yetu, kuna muda tunafikiri kuwa watu wa aina fulani ndio wawezao kufanya mambo ya maana na yenye maendeleo kwa wao wenyewe, na sisi kujiweka nyuma kwa miakisio ya ubovu wa uteuzi wa fikra sahihi dhidi ya fikra mtambuka. Tunawaza zaidi kuliko kufikiri juu ya hatima ya uzio wa upeo wetu na malengo yetu. Akili zetu hutuongoza katika mwambao wa kukata tamaa na kutojikubali. Tunahangaikiwa kuona kuliko kutazama na kuyafanya ya mwisho kuwa ya kwanza. Sisi ni zao la umakini hafifu wenye kichefuchefu cha kutambua tunapotaka kwenda na njia tupitayo. Ukungu wa fikra potofu huyasonga mawazo machachu tuliyonayo juu ya yale tuyaamaniyo kwenye maisha ya wengine. MABADILIKO NI WEWE,,WEWE NI SERIKALI YA AKILI YAKO.” HII NI SEHEMU YA NNE.”
Ni saa sita na nusu usiku bado sauti ya yule dada ilikuwa ikisikika ikihadithia,,mawazo yalikijaa kichwa changu kwakuwa sikujua majibu ya maswali mengi niliyokuwa nayo, kibaya zaidi ni kuhusu huyu Patrick, mkojo ulikuwa umenibana na sikutaka kutoka nje kwakuwa nilihisi kukosa baadhi ya sehemu, hivyo niliibana miguu yangu vizuri ili kuuzuia, muda kidogo nilisikia mtangazaji akisema kuwa ni mda wa matangazo hapo ndiyo nilikurupuka na kwenda chooni, niliporeje Pamela alikuwa anaendelea kusimulia ule mkasa.
***PAMELA***
Ule mlio wa bunduki uliuumiza sana moyo wangu hasa nilipoona Patrick akidondoka, nilisikia tena mlio mwingine na hapo nikatazama huku na kule kuangalia ni nini kimetokea, nilikimbia bila kujali kuwa na mimi ningeweza kupigwa na risasi, nilipofika pale Parick alikuwa chini, nikapiga haraka simu pale hospitali na ndani ya dakika tatu gari ilikuwa imefika tukampakia na kumpeleka hospitali. Hakuwa na jeraha lolote.
*****
“Ni mshtuko tu na inabidi tumchome sindano ya usingizi apate masaa mengi ya kupumzika, utamuhudumia wewe kwa ukaribu zaidi” alikuwa ni dokta Anderson akinieleza hayo baada ya kutoka kwenye kile chumba Patrick alichokuwa amewekwa. Sikujibu chochote bali nilitoka na kwenda kuchukua mabomba ya sindano nikamchoma kwa haraka sana na kuondoka kuelekea nyumbani kwangu, nilichukua bastola yangu na kwenda mpaka kule ufukweni, nilizunguka kote na pembeni ya vile vichaka lakini sikuona mtu yeyote, nilisogea mpaka pale mbele karibu na Patrick alipokuwa ameanguka na nilipotazama wenye mti niliona ile risasi ikiwa imepenya kwenye ule mti, nilichukua kichuma kidogo nikahangaika mpaka nikaichomoa ile risasi.
“ngriiiii,,,ngriiii” ulikuwa mlio wasimu ukiita ndani ya simu yangu.
“Habari yako Pamela” aliongea yule mtu baada ya kupokea simu.
“Nzuri Felicity habari ya kwako mpenzi” tulisalimiana lakini sikuwa na maneno mengi sana ya kusema.
“upo kwako? Nataka kuja hapo nina shida” nilimuliza huku nikionekana mwenye haraka.
“ndio njoo,,kuna tatizo gani?” aliniuliza lakini kabla hata sijamjibu nilikuwa nimeshakata simu na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani, niliwasha gari na kuelekea kwa Felicity ambapo ni mwendo wa dakika kumi na tano toka kwangu, nilikuwa na mawazo sana na nilikuwa nimeshachoka kwa kufikiri ni nani anataka kumuua Patrick na kwanini, nilihisi kama pengine Patrick alikuwa kwenye matatizo makubwa na sasa alitakiwa kuuwawa ila sikujua nani muhusika na kwanini afe.
***
“karibu Pamela” Felly alinikaribisha na hapo niliingia mpaka ndani kwake, alienda kunichukulia juice kitu ambacho niliona kama ni kupoteza muda ila sikuweza kumwambia aache kakuwa hakuniambia kama anaenda kuleta juice.
“karibu Pamela” alinikabidhi ile juice huku akinitazama usoni.
“kunanini Pamela?” aliniuliza.
“unakumbuka nilikuambia nina boyfriend sasa hivi ila nikakuelezea kuhusu ile ajali yake na kila kitu?” nilimuuliza kwanza.
“Ndio nakumbuka” aliitika huku macho yakiwa yamemtoka, nilijua kuwa aliwaza moyoni pengine Patrick amefariki hivyo sikumuacha akae na mafikirio hayo kichwani mwake hata kwa sekunde moja kwakuwa sikutaka yeyote awaze hayo.
“Leo kama lisaa limoja lililopita amekoswa na risasi kule ufukweni na amepoteza fahamu, sijui ni nani kafanya hivyo lakini naamini wewe unaweza kunisaidia kufanya hivyo” nilimtazama kwa makini huku kijasho chembamba kikinitoka.
“umefanikiwa kuipata hiyo risasi” aliniuliza.
“ndiyo ninayo hapa” niliitoa ile risasi na kumkabidhi.
“sawa nipe muda nitakujibu kesho nitakachokuwa nimekigundua” nilinyanyuka nikamkumbatia na kuondoka.
Felicity alikuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi toka nikisoma shahada ya kwanza tulisoma chuo kimoja, na nilipokwenda kusoma shahada ya pili naye pia tulisoma nae lakini yeye alisoma mambo ya uchunguzi wa kisayansi wa makosa ya jinai(criminal and forensic investigation), baada ya kumaliza shahada ya pili aliajiriwa kwenye maabara ya mkemia mkuu na baadaye alikwenda kitengo cha polisi wa upelelezi, hivyo ni mtu ambaye ni mtaalamu sana wa kufanya uchunguzi wa mambo hayo, nilikuwa na shahuku sana ya kutaka kujua.
KESHO YAKE.
“pipii,,,pipiiii” zilikuwa honi za gari, nilikurupuka toka usingizini na kuchukua shati la Patrick lililokuwa limetundikwa ukutani kisha nikalivaa na kuchingulia dirishani. Niliona gari kule nje nikagundua alikuwa ni Felly, hata sikuhangaika kufungwa shati nikatoka vilevile nikiwa nimelivaa huku nikiwa na chupi tu, nilisogea pale getini na kufungua geti kisha aliingia.
“hey unakuwa kichaa au ni nini” aliniuliza huku akicheka. Alikuwa amependeza, Felly alikuwa ni mzuri ila sikuzote alikuwa akijiweka katika namna ambayo wanaumea wengi waliogopa kumfata, alikuwa ni mrefu na mara zote alikuwa akivaa nguo zake za upelelezi na kuweka bastola yake kiunoni, alikuwa ni msichana lakini ningeweza kumfananisha na nikita au Angelina Jolie kwenye Salt, au Nina Myer kwenye 24 au Anny Walker kwenye Covert affairs, alikuwa ni mtu wa mazoezi na mwalimu wa karate katika chuo cha polisi pia, hayo yaliwafanya wanaume wengi sana wamuogope, japo mwanaume mmoja tu alifanikiwa kuuteka moyo wake lakini alifariki akiwa vitani nchini Iraq kwahiyo mar azote amekuwa akishindwa kutafuta mtu mwingine kwakuwa anashindwa kumsahau yule aliyekuwa nae.
“Felly acha tu mpenzi, nakosa usingizi sasa yani nimepata usingizi asubuhi hii” nilimwambia huku nikitangulia ndani.
“mimi sikai nataka unipeleke hapo ulipoitoa hii risasi” aliniambia huku ameshikilia kiuno na kuyatazama makalio yangu.
“Hey stop that, have you become a Lesb?”(hey acha, umekuwa msagaji) nilimwambia huku nikivuta shati langu na kuingia ndani.
“hahaa you are”(wewe ndiye msagaji) alicheka na mimi niliingia ndani nikavaa suruali na kutoka nje kisha tuliteremka kuelekea ufukweni. Nikamuonyesha ile sehemu.
“sasa kama risasi imekuja hapa inamaana imepita mkono wa kulia wa Patrick kwa futi sita toka alipokuwepo, na itakuwa imetoka mita miamoja mbele yake kwenye kale kamsitu pale, sasa hii inamaana kama angekuwa anataka kumuua Patrick basi risasi isingepita mbali hivyo, na isingepigwa mara ya pili na isionekane kujia upande huu. Lakini pia kama alipanga kumuua Patrick basi huyo mtu atakuwa sio muuaji anayejua kuua na atakuwa ni mwanamke, kwakuwa risasi inapotoka inatoka na mtetemo hivyo kama mkono sio imara basi lazima iyumbe na isifike pale inapotakiwa kufika, hivyo muhalifu wetu hapa kama alikuwa hana shida ya kuua atakuwa ni mwanaume au mwanamke ila kama alidhamiria kumduru Patrick atakuwa ni mwanamke ambaye ni laini na muoga.” Alimaliza kuniambia Felicity na kunishika mkono kisha tuliondoka na kurudi nyumbani. Akili yangu ilijua wazi kabisa hapa itakuwa ni Mary, nilikuwa siwezi hata kuongea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“unahisi anaweza kuwa ni nani” aliniuliza Felly
“sihisi chochote, au pengine atakuwa ni Mary yule mpenzi wake aliyemtelekeza huku” nilimuambia hayo huku nikiwa ninahasira kweli.
“inawezekanaje wakati alishaondoka” Felly aliniuliza na hata hivyo sikuwa nina uhakika na nilichokiongea lakini hiyo ilikuwa ni fikirio langu ka kwanza.
“Sielewi Felly ila fanya uwezavyo umgundue huyo mtu aliyefanya hivyo, hata kama hakuwa na nia ya kumdhuru Patrick lakini nataka kumjua”. Tuliachana yeye akaelekea kazini na mimi nilijiandaa kuondoka kwenda kazini. Nilipofika nilimkuta Patrick amesharudi katika hali ya kawaida na sasa alikuwa nje ya hospitali.
“vipi unajisikiaje Patrick” nilimuuliza kwa shauku nikitaka kusikia tu sauti yake.
“niko salama, nimekumis” ooh aliongea maneno yaliyonipa sana faraja aisee, Patrick alikuwa si mtu hata wa kucheka kwa dakika moja toka arudishe fahamu alikuwa ni mtu wa kukaa kimya tu na kutabasamu kwa mbali.
“oooh Patrick nimekumis pia mpenzi wangu” nilimshika kichwa kwa mikono yangu miwili na kupeleka ulimi wangu mdomoni mwake bila hata ya uwoga.
“inabidi nimtafute mtu aliyenyuma ya haya yote Pamela hivyo nitahitaji kurudi Tanzania” kauli hii ilinivuruga akili na moyo kwakuwa sasa hii haikuwa tena nzuri kwangu. Nilimuachia pale na kunyanyuka nikizunguka huku na kule kama chizi huku machozi yakinitoka, ilikuwa ni ngumu kwangu kwakuwa sikuwa na namna ya kumuachia Patrick asiondoke.
“Pamela, najua hii ni ngumu kwako, natambua hisia zako kwangu lakini nakosa Amani kuishi bila kujua sababu iliyopelekea mimi kukaa kitandani, nataka kujua kila kitu ili nafsi yangu utulie, nataka kufahamu hatma ya mali zangu zote nilizozisumbukia” Alinikumbatia kwa nyuma akapitisha mikono yake kiunoni mwangu na kuikutanisha kwa mbele.
“ni mapema mno Patrick, mimi ni daktari wako, bado ugonjwa wako haujaisha kabisa” nilimuambia huku nilimtoa mikono yake na kumgeukia kisha nilimshika mashavu yake na kumwambia katika sauti ya upole ambayo hata hivyo haikumshawishi.
“nitakuwa salama usijali” aliniambia hivyo na kuondoka pale kisha alisogea mbele kidogo na kugeuka akinitazama.
“Pamela, kukaa hivi bila kazi wala chochote ni shida kwangu, mimi sina cha kufanya hapa, ni bora niende kujua nini kimetokea” aliniambia huku akionekana kujizuia asitoe machozi.
“nimehangaika sana katika maisha yangu Pamela, nimehangaika kufika nilipokuwa nimefika, nilikesha usiku na mchana nikihangaika kila nchi kutafuta maisha, haiwezekani vikapotea tu kirahisi hivi” aliongea huku machozi yakimtoka.
“Patrick naelewa hayo ila yupo mtu atatusaidia kujua hayo tukiwa hapa, na utajua kila kitu na wakati huo utakuwa ukifanya kazi hapa nchini nimeshaongea na dokta Anderson na amesema anaanza kukutafutia kwanza kibali cha kukaa hapa na cha kufanya kazi, kisha tutaanza kufatilia upate kazi hapa” nilimuambia huku nikijitahidi kuongea kwa sauti ambayo angeweza kuielewa vizuri na kumshawishi.
“nitakaa huku hadi lini?” aliuliza
“sijui hadi lini lakini ni hadi upone kabisa na sumu iwe imeondoka mwilini, Patrick nakuhitaji, siko tayari kukupoteza, huwezi kwenda Tanzania kama hujui kila kitu kuhusu safari yako, huwezi kwenda Tanzania ukiwa na milioni 15 tu na ukategemea utafanya kila kitu, hapana ni lazima uwe umejipanga na uwe unajua utaanzia wapi na utaishia wapi, bado hatujajua nani alikufanyia hivyo na kwaiyo unaweza ukaenda nso ukaisha kabisa, nina rafiki yangu anaweza akasaidia” nilimuambia na kumuona akiwa kimya nikajua dhahiri ameshanielewa.
“nataka kuonana na huyo rafiki yako kwanza nimuambie vitu vya kunisaidia kufatilia” aliniambia huku akinitazama kwa jicho kali usoni.
“usijali ila kwasasa anafatilia ni nani alikufyatulia risasi pale ufukweni” nilimueleza huku nikimshika mkono kuelekea kule hospitalini, alikuwa na mawazo sana, nilimpeleka mpaka hospitalini kwangu na kumchukulia dawa kisha alikunywa na hapo nilisaini na kuondoka naye mpaka nyumbani, aliingia kuoga na mimi nianza kumuandalia chakula, alipomaliza alikaa sebuleni huku akionekana kuwa na hasira sana, nilipomaliza kula mimi nilikwenda kuoga na nilipotoka nilikuja mpaka sebuleni nikiwa na kitaulo kifupi ila nilishtuka kumkuta mtu pale.
“hee, umekuja saa ngapi wewe” nilishtuka na kujifunika na pazia.
“hahaa,,nimefika mda sio mrefu na ninaondoka muda sio mrefu, hivyo njoo hapa tuelezane kwanza kisha utafanya kazi zako nyingine” nilitoka na kile kijitaulo mpaka pale sebuleni.
“Patrick usiniangalie” nilimtania huku nikicheka, nilikwenda mpaka pale akanivuta na kunipakata.
“Patrick huyu anaitwa Felicity, ni rafiki yangu, Felicity huyu ni mpenzi wangu anaitwa Patrick, najua hamjawahi kukutana ila kipindi yuko hospitali Felicity aliwahi kuja mara kadhaa kukuangalia” niliwatambulisha kila mmoja kwa mwenzio.
“nashukuru sana kukufahamu Felicity” walishikana mkono na kama kawaida ya Felly huwa hapendagi kupoteza muda.
“Nimefanya uchunguzi na nimeichunguza ile risasi, sasa nataka nikuonyesheni kitu hapa” aliwasha ‘projector’ aliyokuwa ameiweka pale mezani kisha akawasha na laptop yake na kuanza kuelezea.
“Risasi ile uliyoiokota pale inaitwa 2.34 mm rimfire, inatengenezwa uswis na ina milimita 2.3, bastola yake ina 6.1 milimita ni rimedrife, imesajiliwa kwa namba 23kyt45, mwaka jana, ilipigwa kwenye kona ya nyuzi 75 toka upande wa kulia wa alipokuwa Patrick, hii inaonyesha kuwa kama mpigaji alikuwa ni mzoefu wa kutumia bastola basi angeweza kumlenga kama mkono usingecheza. Lakini kwakuwa ulicheza na kupiga futi sita kushoto kwa Patrick inamaana alikuwa amelegeza mkono hivyo mtu kama huyu atakuwa ameshtuka kiwiko cha mkono wake, pia niliende pale eneo la tukio jana baada ya kuachana na wewe pale,,nilikuta kuna miguu ya viatu visivyo na soli na inaonekana aliyepiga aliegemea mti na nywele zake zilibaki kwenye zilishika kwenye magome ya miti na hivyo kuacha nywele kidogo pale ambazo nilichukua na kwenda kuangalia DNA, hivyo baada ya uchunguzi wote nimegundua kuwa aliyefyatua risasi ni NANCY ROVELT”
“WHAAAAT”
“Hakuna haja ya kukata tamaa na kujiona kuwa huna thamani katika mapenzi yako kwakuwa tu kila mahusiano uanzishayo hayawi na mwisho mzuri au ulioutarajia, maisha ya mapenzi ni maisha dhalimu muda mwingine. Unaweza kukutana na mtu sahihi katika muda usio sahihi, na unaweza kukutana na aliyesahihi katika muda usio sahihi. Unachotakiwa kufanya si kukata tamaa bali kuwa makini na muda na unaokutana nao. Kila mtu anapacha wake hapa duniani, inapotokea umekutana na pacha wa mtu, ndipo shida na matatizo huanzia hapo. ATAKUJA MTU KATIKA MAISHA YAKO ATAKAYEKUFANYA UGUNDUE KWANINI HUKUDUMU NA ULIOACHANA NAO” HII NI SEHEMU YA TANO.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Msisimko wa simulizi ile uliufanya uso wangu upauke kama kipande cha muogo wa kiangazi, niligundua kuwa baridi lilikuwa likipenya kwenye lile dirisha dogo la chumba changu na kunifanya nikakamae, lakini hiyo haikunifanya nichoke kusikiliza, tayari yule msichana Felicity ambaye ni mpelelezi alikuwa ameshagundua kuwa Nancy ndiye aliyefyatua ile risasi, moyoni nikajiuliza kwanini Nancy afanye hivyo, lakini sikuwa na jibu. Nilifunga lile dirisha vizuri na kuchomeka makaratasi ili lisifunguke tena na kupitisha baridi kisha nikachukua ‘headphones’ zangu na kuchomeka kwenye redio kisha nikaweka masikioni ili nipate kusikia kwa ukaribu zaidi. Na sasa Pamela alikuwa na kibarua kizito cha kueleza Nancy ni nani. Ikawa hivi;
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment