Search This Blog

Thursday 27 October 2022

AFANDE ANAHUSIKA - 2

 







    Simulizi : Afande Anahusika

    Sehemu Ya Pili (2)





    Inspekta Kalindimya akahisi kuchanganyikiwa, mtu anafanya mauaji mbele ya watu wengi kiasi kile? Mtu huyu ni nani? Amefanikiwa vipi kumuua huyu mtu hapa kwenye kadamnasi? Alijiuliza maswali ya papo kwa hapo na kukosa jibu.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Akatoa simu na kumuita Afande Jitu haraka ndani, afande ni kama alikuwa nje ya chumba, dakika moja tu mbele akawa yupo nae sambamba chumbani na alipoiona tu ile maiti….



    Bila kujua lolote akajikuta amesema ‘Shit’ na kujipiga kofi pajani akiwa ameuma mdomo wa chini na hali kakunja ndita.



    Hata Jitu nae alionekana kuchanganyikiwa, lakini hapo kabla alikuwa na hamu mno ya kutaka kujua mkuu wake wa kazi alikuwa kiongea na nani kwenye simu…

    Lakini hakukuwa tena na muda wa kuhoji juu ya jambo hilo.



    Afande jitu alirudi garini na kuchukua Gloves pair mbili ili kuja kuanza kufanya uchunguzi wa awali kwanza wakati wakiomba usafiri wa kuja kuuchukua mwili wa Marehemu.



    Kawa kawaida, kulikuwa na kisu cha rangi ya Pink kwenye mpini na sasa namba iliyowekwa ilisomeka 6352 huku ndani ya chumba pakiwa hakuna mtu yeyote, walikagua chumba kila sehemu hadi chini ya sofa, lakini wapi, hakaukuwa hata na mdudu.



    Sehemu moja waliisahau, ilikuwa ni kwenye kabati ya nguo, nayo walipokumbuka na kuifungua..,



    Hawakukuta chochote zaidi ya nguo zilizo pangwa vizuri ndani ya kabati, wakaishiwa pozi na kushusha pumzi kwa pamoja kwa mara nyingine tena, wakiwa hawajui ni wapi pa kuanzia.



    Inspekta akatoa simu na kumuita Afande wa kike aliekuwa nyumba kubwa chumba ambacho maiti imeondokea kwenda malaloni, hakukawia akawa amefika, nae alishtushwa na kile alichokiona.



    Inspekta akamwambia amfuate mama mwenye nyumba, anaitwa mama Kubwaa na kumwambia nahitajika chumbani kwa Mwana.



    Mama Kubwaa alichukua dakika takriban mbili, kwani kulikuwa na mtu mmoja alikuwa amekuja kumpa pole, kwa kuwa alikuwa ni mwanaume alishindwa kumkatisha maongezi yake, hata afande Yule wa kike alimkuta nae japo hakumtazama kwa umakini, maana si hilo lililompeleka pale.



    Mama mwenye nyumba akamaliza maongezi nae huyo kijana wa kiume ambae alitoa kiasi cha pesa na kuondoka akimuacha huru sasa Mama mwenye nyumba kuelekea chumbani kwa marehemu, alipoitwa na askari.



    Akafika huku akiwa na imani kuwa itakuwa kuna jambo lolote jipya ambalo huenda jeshi la Polisi limefanikiwa kulipata kwa sasa tangu jana na hivyo anaenda kujulishwa ama wanataka msaada wake kwanza.



    Alipoingia ndani tu, japo mwili wa Marehemu pale sofani ulikuwa umefunikwa, lakini ilijionesha tu ufunikaji ule, haukuwa salama, akajishika kichwa kwa mikono miwili na kusema Mwana kwa sauti ya juu na kuanza kulia.



    Inspekta Kalindimya na Jitu wakatazamana usoni, wakajiuliza Mwana tena? Askari wa kike akamuuliza Mwana yupo wapi? Mama kubwaa akajibu huku akilia kwa kunyoosha kidole kwenye mwili wa Marehemu.



    “Bi mkubwa, mwili wa mwana tayari tumeisha utoa hapa nyumbani na muda huu utakuwa maeneo ya makaburini,” aliongea Inspekta huku Jitu akitikisa kichwa kumuunga mkono. Mama Kubwa nae akaendelea kushikilia palepale



    “Hapana bwana afande, huyu ni Mwana…” sasa hawakuwa na budi ila tu kukubaliana nae, maana yeye huenda anamjua vizuri zaidi kuliko wao

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sawa mama, hapa tuna maswali machache kuhusu Marehemu, tunaomba utusaidie kuyapatia majibu tafadhali,” aliongea Inspekta huku Jitu akiwa tayari na kalamu na karatasi ili kurekodi maongezi yao, mama Kubwa nae akatikisa kichwa kukubali kutoa ushirikiano huku akiitazama maiti ya Yule binti anae onekana alikuwa ni mrembo hasa.



    “Huyu alieuawa unamfahamu?” hivyo ndivyo maswali lukuki yalivyo anza.

    “Ndio ninamfahamu baba,”



    “Jina lake nani?”

    “Anaitwa Mwana,” Alipojibu mama Kubwa, Inspekta Kalindimya akamuuliza kama hilo ndio jina lake halisi. Mama kubwa akaitika kwa kichwa akifuta machozi.



    “Mwana nani? Maana kama ujuavyo haya majina ya kina Mwana, ni kifupi tu, hapo inaweza kuwa ni Mwana Hamisi, MwanaLisa na mfano huo, huyu sasa aliitwa Mwana nani?” aliomba ufafanuzi Jitu.



    “Mmh kwa kweli sina ufahamu wa hilo, kwani hata hili jina la Mwana hatukuwahi kulisikia toka kwake moja kwa moja, bali kutokana na kuitana kwao wa jina wajina, ndio maana tukajua kuwa Yule nae jina lake ni Mwana, ila hakuna yeyote ajuae ni Mwana gani!” alieleza mama Kubwa kwa kirefu.



    “Jina la baba yake?” aliuliza ili kupata maelezo kamili ya marehemu.

    “Kwa kweli hilo silijui, maana hata siku moja sijawahi kumuuliza na sikuona hata huo umuhimu,”



    “Unamfahamu marehemu Mwana huyu kivipi?”

    “Ni rafiki mkubwa wa marehemu Mwana, na ndio alikuwa ni shoga yake kipenzi, kiasi ambacho haikuwahi kupita siku hata moja bila wao kuwasiliana ama kuwa pamoja,”



    “Alikua akiishi wapi Marehemu?”

    “Nasikia tu ya kwamba alikuwa akiisi Manzese Tiptop, ila sifahamu ni nyumba gani,”



    “Ok! Yeye amefika lini hapa?”

    “Ni mara tu baada ya taarifa ya msiba wa Mwana iliposambaa,”



    “Nani alimjulisha juu ya msiba huo?” alihoji Inspekta Jitu, Kalindimya alikuwa yu kimya tu akisikiliza kwa umakini mahojiano.









    “Kwa kweli sifahamu, lakini kuna wengi wamesikia tu kwa watu tofauti hasa ukizingatia MwanaHamis alikuwa ni mtu wa watu,” alijibu tena mama Kubwa.



    “Una maanishaa tangu alivyolala hapa jana hakuondoka tena kwenda popote? Ama alikuwa akitoka toka?”



    “Ndio bwana afande, tangu alivyokuja jana jioni, hajatoka kwenda popote zaid ya kuhama vyumba tu lakini ni humu humu ndani, hadi mauti yamemfika.” Alijibu hivyo mama mwenye nyumba.



    Inspekta alijikuta ameuliza maswali yote na mama alijibu bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, lakini walipofika kwenye swala la muuaji walikwama.



    Muda gani kuyo muuaji aliingia ndani na kufanya mauaji yale na hali watu walikuwa wengi wa kutosha. Hapa sasa alikuwa akijiuliza Inspekta…



    “Ina maana Yule mwenda wazimu amenieleza kweli ama? Mbona kama ananichanganya vile?” akili yake ilikumbuka simu aliyopigiwa na na yule mtu alie mpa jina la raia mwema, lakini alikuwa ni mwanaume, na kawaida wanaume kuingia kwa wanawake ni shughuli pevu.



    Sasa akapata pa kuanzia, akajituliza na kutengeneza koo kisha akamtazama mama Kubwa na kumuuliza



    “Kuna mwanaume gani aliingia ndani ya chumba cha marehemu wakati shughuli za msiba zikiendelea?”



    “Mwanangu siwezi kufahamu, maana tangu jana baada tu wewe na timu yako kuondoka, sisi tukakifunga chumba hihi na funguo ya chumba tukampatia Mwana, huyu marehemu ambae usiku wote wa jana hakukifungua,”



    “Sasa imekuwaje mimi nimekikuta chumba kikiwa wazi?”



    “Afisa kumbuka nimekwambia funguo anayo yeye na ndie umekuta maiti yake pia humuhumu ndani,” Inspekta aliposikia majibu yale, yalimtosheleza kumjibu kuwa mama Kubwa hana jibu la swali hilo.



    Sasa ndio akaenda kwenye point yake moja kwa moja



    “Unakumbuka kuonana na mwanaume yeyote tangu jana baada ya msiba hadi leo hii kabla ya mazishi ya Mwana?” aliuliza swali lile huku akimtazama kwa makini zaidi, hapa ndio aliamini kuwa kuna mwanga ambao utampeleka kwenye mafanikio.



    “Hapana baba yangu, zaidi ya wanaokuja kunipa pole, sidhani kama kuna yeyote,”



    “Hao waliokupa pole je? Unawafahamu kwa sura ama walikuwa ni wapya machoni mwako?”



    “Mmmmh, Karibu wote ni walewale wa hapa mtaani, yaani ni watu tunojuana nao afande,” jibu lile kidogo lilimpa faraja Inspekta na kuona sasa angalau anaweza kufikiria kumpata muuaji kwa urahisi kiasi Fulani, nguvu ikaongezeka na kuendelea kuhoji;



    “Kati ya hao watu, kuna mmoja wapo ni mtu tunae muhitaji sana, nawe pekee ndio unaemjua, sasa tutalazimika kuondoka hapa ili twende kituoni kwa mahojiano zaidi,” alisema inspekta huku akiwatazama wenzie ambao walitikisa kichwa kukubaliana nae huku akimpa wakati mgumu Mama Kubwa



    “Afande, lakini mbona mi sina kosa lolote? Nimefanya nini hadi unipeleke Polisi?” alisema huku akiangusjha kilio.



    “Hapana mama Kubwa, wewe huendi kuwekwa ndani, bali ninakwenda nawe kwa ajili ya mahojiano tu na baada ya kumaliza mahojiano utarudi nyumbani kwako, hivyo wala usiwe na shaka,” alimtoa hofu lakini bado hakuamini kauli ile, akasema kwa kukata tamaa,



    “Ndio huwa mnasema hivyo hivyo, sawa bhana, basi niende na Joyce ili kama mkiniweka ndani aje kutoa taarifa nyumbani,” kauli ile ilitaka kumchekesha Inspekta Kalindimya, lakini akajizuia na kumwambia



    “Hata wakienda na Joyce, hawezi kufika sehemu ambayo wewe utaenda kufanya mahojiano, nakuhakikishia utarudi ukiwa salama tu, nataka tutoke hapa kutokana na unyeti wa jambo lenyewe, we wala usiogope, tambua kule ni kituo cha usalama wa Raia na mali zao.”



    Alimkata maini na Mama kubwa alipoambiwa asimame alikuwa amepoteza matumaini na sasa alihisi huu ndio mwisho wake wa kukaa uraiani, chozi lilikuwa likimtoka bila kificho.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati wakiongea hayo, tayari gari ya Polisi ilikuwa imefika na askari wakiwa na Camera na Stretcher, wakawatoa waliomo ndani huku Yule askari wa kike wakimtaka kuongozana na mama Kubwa hadi ndani ya gari la Inspekta Kalindimya.



    Mama Kubwa alitoka huku akilia, watu tayari walikuwa ni wengi pale uani, wengi walimuonea huruma, hasa jinsi alivyotoka akiwa na huzuni usoni, alipowaona watu ni wengi pale nje, sasa akaangua kilio kabisa na askari akamfungulia mlango aingie ndani ya gari.



    Waliomo ndani waliendelea na kazi zao kama walivyojipanga na baada ya kumaliza tu, wakatoka wakiwa na mwili wa marehemu hadi ndani ya pick up ya jeshi la Polisi na kuondoka.



    Inspekta Kalindimya sambamba na Jitu wakatoka nao pia, Jitu akiwa ni wa mwisho kutoka, akiwa mlangoni, alichomoa funguo ya kitasa iliyokuwa mlangoni kwa ndani na kufunga mlango ule kwa nje huku akiwa na nia ya kuondoka na funguo hiyo.



    Hivyo alimuita dada mmoja ambae alionekana kama ni mwenyeji na kumuuliza jina lake, akamwambia anitwa Joy, alilikumbuka jina hilo na kumuuliza



    “Nafikiri wewe si mgeni ndani ya nyumba hii?”

    “Ndio, mimi ninaishi na mama Kubwa,” alijibu Joy akiwa naonekana kuwa na wasiwasi.



    “Sawa, nimefunga chumba hiki na nimeondoka na funguo, tutarudi, kuweni makini, tukio lolote mkiliona lipo tofauti kidogo, naomba unijulishe kwa kutumia namba ambayo nitakupa, sawa Joy?” alisema huku akizama mfukoni na kutoa kalamu na diary ndogo ambayo alichana karatasi kiasi na kumuandikia namba.







    “Hivyo wakati wowote, ukimuona mtu ambae unamtilia shaka ama ni mgeni kwenye macho yako na humuamini, nijulishe haraka iwezekanavyo, name nitafika muda huo huo, daima sitakuwa mbali na eneo hili, sawa Joy?” alipokea Joy huku sasa akiwa na amani kuwa yeye hachukuliwi kwenda kituoni.



    Jitu alikuwa na funguo ile mkononi bado, sasa ndio akaiweka mfukoni mwake na kutika kuelekea nje na lakini mlangoni Inspekta Kalindimya alikutana na Mwenyekiti wa Serikali za mtaa na kumwambia anaondoka na Mama Kubwa kwa mahojiano nae ofisini ila atarudi baada ya muda watakapomaliza mahojiano yao.



    “Vipi kuna haja ya kuongozana nae?” aliuliza Mwenyekiti.

    “Eer… Ni sawa tu lakini itakulazimu kutafuta usafiri wa binafsi kama hutajali, maana sisi tumeenea kwenye gari tulilokuja nalo,” alimjibu huku nae akitazama saa.



    Mwenyekiti akasema atakuwa akija kwa nyuma yao kwani yeye ana usafiri wake binafsi ambao atautumia kufika huko, wakaagana na wale maaskari wakaingia kwenye gari lao na kutokomea kituo cha Polisi.



    Nyuma wakiwa wamewaacha raia wakiwa na mshangao kwenye vikundi vikundi kadhaa wakijadili juu ya matukio mfululizo yaliyotokea nyumba ile.

    **********



    Safari iliishia kituo cha Oysterbay, hapo ndipo ambapo waliketi na kuanza mahojiano yao. Inspekta alimkaribisha mama Kubwa ambae alikuwa akionesha wasiwasi mkubwa mno kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kituo cha Polisi.



    “Karibu mama Kubwa, jisikie huru kabisa, kwani hapa sio mahakamani, hapa ni kituo cha Polisi, maana ya kituo cha Polisi ni sehemu ya usalama kwa Raia na mali zao, hivyo amini upo sehemu salama kabisa, sawa raia mwema?” Inspekta alijaribu kumtoa hofu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa.



    Maana ile hofu iliyokuwa ikionekana usoni, ilionekana sasa kupungua kiasi Fulani na kuitika kwa kutikisa kichwa ishara ya kukubali. Jitu alikuwa pembeni kama kawaida na kalamu na diary ndogo, akiwa tayari kuandika maelezo atakayotoa kutokana na maswali atakayoulizwa na Inspekta.



    Inspekta Kalindimya akamuuliza swali la kwanza kwa kumwambia kwamba anawakumbuka watu walioingia na kumpa pole? Jibu lake likawa ni lile lile, akaulizwa tena je anaweza kuwataja majina wanaume walioingia mle ndani kwake?



    Aliwataja wanaume wasiopungua watatu, alipoambiwa ataje makazi yao akataja yote,



    “Una ukaribu nao gani watu hawa?” akasema

    “Wote ni jirani zangu hawa,”



    “Vizuri sana, tunaweza kwenda na kuwaona majumbani mwao?” aliuliza afande Yule wa kike akiwa kuna kitu amedhamiria.



    “Hata sasa naweza kuwapeleka kwa mmoja mmoja, kwani wote nawajua wanapoishi,” walimaliza mazungumzo yao huku inspekta Kalindimya akimwambia Afande Yule wa kike ambae alimuita kwa jina la Marsha, aongozane nae sambamba na Jitu kwa hatua zaidi.



    “Mkimaliza mahojiano nao watu hao aliowataja mumuache kwake huyu mama na kama kawaida, yeyote mtakaemtilia shaka tu, mleteni stoo kwa maelezo zaidi,”



    Alimaliza maelekezo yake na kuwaaga akiahidi kuonana nao siku ifuatayo, alitaka siku hii arudi kwake muda ule akapumzike huku akifikiria juu ya mauaji ya wanawake wale.



    Waliondoka na kueleka huko walipoagizwa, walifanya mahojiano na wote lakini hawakufanikiwa kuambulia chochote na mwisho wa siku wakaona ni kama kupoteza muda tu.



    Wakamuacha mama kubwa na kuamua kurejea kazini kwao ili kuendelea na utaratibu mwingine hasa ukizingatia tayari usiku ulikuwa umeisha ingia.

    **********



    Safari ya Inspekta iliishia kwake na kujitupia sofani aiwa amechoka kabisa, siku mbili za kazi ile nzito aliona ni kama siku milioni kwake. Akaanza kufikiria juu ya muuaji Yule ni nani, lakini bado hakuwa na jibu, akamua ajipumzishe ili kujipanga kwa ajili ya siku ifuatayo.



    Asubuhi ya siku iliyofuata akawahi ofisini kuliko kawaida, lengo alitaka kujua ni nini siku iliyopita walikipata huko walipokwenda Jitu na afande Marsha. Aliwasili na kuwakuta wao tayari, Jitu akiwa amesimama na Marsha akiwa anaandika ripoti ile ya siku iliyopita.



    Walimsalimia alipoingia kama zilivyo amri zakijeshi na kisha kumueleza habari nzima ya mahojiano ya siku ile iliopita, alichoka kabisa walipomueleza kuwa hawajaambulia chochote toka kwa watu wale.



    “Mlimuuliza kuhusu mtu ambae aligharamia chai kwenye shughuli?” swali la Inspekta liliwafanya Jitu na Marsha watazamane na kukana kuwa hawajamuuliza.



    “Hapo sasa nanyi ndipo mlipofeli, hilo swali mnaweza kuliona ni la kipuuzi sana, ila ni swali moja la msingi sana, hebu mmoja wenu anifuate twende huko kwa ajili ya hatua zifuatazo,” aliamuru Inspekta na Jitu na Marsha wakatazamana tena, wote wakawa tayari kwa kwenda, Jitu akamwambia Marsha



    “Nendeni nyie, acha mimi niendelee na ile kesi nyingine ya wale majambazi wa Pori la Msanga,” Marsha kwa kuwa alikuwa akiitambua kesi hiyo, akakubali na kubeba diary ndogo huku akijihakiki kuwa yupo tayari na kutoka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Kama mtahitaji funguo ya chumba cha Marehemu Mwana, nimeiweka ndani ya file na kuifunga kwa gundi, ila kwa kuwa mnaenda huko unaweza tu kuibeba, inaweza kuhitajika huko,” ulikuwa ni ushauri mzuri mno ambao Marsha aliuchukua ulivyo na kuirudia funguo.







    Alipotoka Marsha akawakuta Jitu na Inspekta wakiwa kwenye maongezi, Jitu akiwa nje ya gari ya Inspekta akiwa ameinamia usawa wa kioo, na inspekta akiwa ndani ya gari akimsikiliza kwa makini.



    Baadaya Marsha kuingia garini, wakaagana Jitu na Inspekta kwa ahadi ya kuonana wakati ujao hapohapo ofisini.



    Safari ilishia nyumbani kwa mama Kubwa, hapo waliingia na kumkuta mama kubwa akiwa na mtoto mmoja hivi pamoja na Joyce, waliwaomba wawapishe na kisha Inspekta pasina kupoteza muda akamwambia mama kubwa kuwa mtu wanaemuhitaji hadi sasa hawajamjua na bado akasisitiza kwamba ni yeye pekee ndio anamjua na ndio naweza kuwasaidia.



    “Baba yangu wee, mimi simjui muuaji, mbona tayari ningekuwa nimekwambia?” aliomboleza mama Kubwa kwa kudhani anaweza kugeuziwa kibao. Inspekta akaamua kumchanganya kidogo.



    “Najua humjui muuaji kama ambavyo mimi simjui, lakini muuaji amekutaja wewe kuwa unamjua,” na kweli kauli ile ilimtikisa kabisa hadi Inspekta akaiona



    “Kasema mimi ninamjua? Jamanii Sijui ananitakia nini mimi wallahi…” mama Kubwa akaangusha kilio.



    “Mama Kubwa kilio hakina msaada wowote kwako wala kwetu kwa kipindi hiki, jambo la msingi ni kutusaidia tu sisi tumpate muuaji na amani irudi tena kwako kama awali, jana tuliomba utuoneshe watu wa kiume waliokuja kukupa pole na rambirambi, lakini tuliemtaka utuoneshe ulituficha, ni kwanini?”



    “Hapana afande, mimi nilionesha watu wote na hadi makwao tulienda, kwanini niwafiche lakini?”



    “Ok! Kuna mtu mmoja alikupa pesa juzi usiku kwa ajili ya kununua baaadhi ya vitu vya maandalizi ya mazishi, ni kweli ama lah?” aliuliza huku akiwa maemkazia jicho.



    “Inspekta wote hao niliokutajieni walinipa pesa kwani wanajua kuwa Mwana hakuwa na pesa na mimi pia Sikuwa na pesa ya kuweza kusimamia mazishi bila ya msaada,”



    “Una hakika ni hao tu uliotuonesha ndio waliokupa msaada wa pesa?” alihoji Inspekta baada ya kuanza kukata tamaa kutokana na kauli ya Mama Kubwa kuwa ni ya ukweli.



    Kutokana na uzoefu wa kazi yake, aliweza kumjua mtu kwa kile asemacho, kuwa ni kweli ama lah! Sasa kwa mama Kubwa aligundua kuwa hakuwa akidanganya.



    “Ni kweli, ila kuna mtu mmoja alikuja na sukari, akanipa sukari mfuko ule pale,” aliongea kisha akawaonesha mfuko wa sukari uliokuwa na uzito wa kilo 25 ambao kwa sasa ulipungua na kuwa ni wenye kilo kadhaa kwa sasa.



    Baada ya kutazama huko, macho ya Inspekta na ya Marsha yalikutana na wakahisi kuna kengele ya hatari imelia vichwani mwao, walihisi kitu na sasa waliona ni wakati muafaka kukiachia.



    “Huyo ndio mtu tuliekuwa tukimuhitaji, yupo wapi na kwanini hukutwambia mapema? Unaficha muuaji?” yalikuwa ni maswali mfululizo ambayo yalitoka kwenye kinywa cha afande Marsha.



    “Hapana afande, ni vile nyie mliniuliza alienipa rambirambi ya pesa, huyu alikuja alileta tu hiyo sukari na majani ya chai, tena usiku uleule wa kifo cha MwanaHamis, hakunipa hata senti tano nyekundu mimi,” walimuelewa na kuendelea kumuhoji



    “Huyo mtu unamjua?”

    “Hapana simjui bali alijitambulisha kama ni Mpenzi wa zamani wa Mwana,”

    “Alikuwaje? Yaani kama utamuona unaweza kumjua?”

    “Yap! Naweza kumjua kwani tayari amekuja mara mbili hapa ndani, ukiacha siku hiyo ya kuleta sukari na majani, lakini pia alikuja jana hapa wakati ule huyu dada amekuja kuniita,” aliongea mama Kubwa huku akimnyooshea kidole Marsha.



    Inspekta Kalindimya akamuangalia Marsha ambae alionekana kupatwa na mshituko wa mbali ambao ni Inspekta pekee alieuona, Marsha akatikisa kichwa na kusema



    “Ah! Ni kweli nilikukuta na mtu umesimama nae, nilimuona kwa mgongoni mwake tu, na wakati mimi nafika, yeye alikuwa akiondoka, naweza kumkumbuka kwa umbo tu maana sura sikuiona,” alisema Marsha kama vile ni mtu anaejuta hivi.



    Inspekta alikuwa ameanza kupata matumaini ya kumjua mtu huyo, lakini kwa jibu lile la Marsha aliona kama bado tu wapo gizani, akamgeukia mama Kubwa na kumuuliza



    “Ukimuona mara nyingine utamjua, lakini je anapokaa unapajua?”

    “Hapana wala sipajui, maana ndio ilikuwa ni mara ya kwanza kuonana nae siku hiyo, sikuwahi kumuona kabla,”



    “Dah! Huyu muuaji amejipanga sana, anafuta nyayo zake kila alipopita, lakini hivi karibuni tutajua tu, hebu tuuone huo mfuko wa sukari aliouleta,” alisema Inspekta na kusogea pale ulipo.



    Alipoukaribia tu aliweza kuziona namba zile walizozikuta kwenye mpini wa kisu kilicho muua marehemu Mwana, akapata uhakika kabisa kuwa alieuleta mfuko ule ndio muuaji halisi wa Mwana.



    Alitoa diary yake ndogo na kulinganisha namba zile, kisha akamuita Marsha aje kuhakiki na hata nae akathibitisha sasa kwamba kuna uhusiano mkubwa matukio hayo mawili, wakarejea alipo mama Kubwa na kumuuliza kama ana hayo majani ya chai aliyoletewa.



    “Ndio inspekta, alileta box kubwa sana kiasi isingewezekana kulitumia mara moja na kumaliza, ndani kuna pakti nyingi ambazo hata bado hazijatumika, zipo hapa, kama utalihitaji nitakuletea tu,” alisema Mama Kubwa huku akiwa tayari kunyanyuka kulifuata, alisubiri ruksa tu toka kwa Inspekta.



    “Hebu fanya hivyo, lilete nilione,” alimjibu huku akijiweka vizuri kwenye sofa lake kusubiri hilo box liletwe.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mama kubwa akawa tayari kunyanyuka kwenda nje kufuata box hilo, lakini akakumbuka na kumuita Joy ambae alifika punde tu wito ulipomfikia na mama kubwa akamwambia aende Store akalete box la majani ya chai.

    “Nilete paketi moja tu ama box zima?” joy aliuliza akiwa tayari amepiga hatua

    “Lete box lote tu na paketi zake bila kulitoa chochote ndani, yaani lilete kama lilivyo sasa,” alitoa maelekezo Inspekta.

    Joy akaitika sawa na kuondoka akimuacha mam akirudi kuketi chini alipokuwa ameketi awali wakimsubiri na kwa kuwa stoo yenyewe ilikuwa ni jirani tu na pale walipokuwa wameketi wao, alichukua dakika chache tu na kurudi na box hilo.

    Alilifikisha na kumkabidhi Inspekta mbae aliweza kuliona kwa mbali tu likiwa limeandikwa kwa nje kuwa ni dozen moja ya paketi za majani ya chai. Akalipokea na kuanza kulikagua kwa kuligeuza geuza huku na kule, kila upande.

    Muda wote huu Marsha alikuwa akifuatilia kila hatua ya mkuu wake anayoifanya, akiwa naelekea kwenye kuridhika kuwa kile alichodhania kuwa kipo pale, hakipo, sasa akakiona kwenye kipande cha karatasi kilichokuwa kikining’ing’inia huku kingine kikiwa kipo palepale kimeshika.

    Alivyo viunganisha tu, akapata kile ambacho alidhania kukiona pale, alipokiona tu akauma mdomo wake wa chini na kutikisa kichwa kama vile ameelewa kitu Fulani, kisha akampa box lile Marsha na bila kumwambia lolote nae akaanza kutazama eneo lile ambalo alimuona mkuu wake wa kazi akiliangalia.

    Akatazama na kisha akasogeza diary na kuandika tena namba zile, lakini Inspkta akamuuliza kama namba zile amezitambua? Akajibu ndio namba hizo amezijua na amezihakiki kama zina tofauti yoyote.

    “Sasa tunalazimika kuondoka na box hili lakini pia mfuko ule…” aliongea akimtazama Marsha kisha akageuza shingo kumwambia Mama Kubwa

    “…tunaweza kuupata mfuko huo wenye sukari?” kwa haraka bila hata kuhoji, Mama Kubwa akakubali, Inspekta akamwambia abadili na kutoa sukari iliomo mle ndani ili wao waondoke na mfuko mtupu.

    Joy aliekuwa yupo pale bado amesimama, akausogelea na kuusogeza kati na kisha akachukua kindoo kidogo na kumimina sukari ile na kisha akakunja mfuko huo na kumkabidhi afande Marsha ambae aliupokea na kuuweka chini.

    “Bado hilo box, nalo tunalihitaji kwa ajili ya shughuli zetu,” Joy akageuka na kulichukua na kutoka nalo kuelekea tena Stoo huku Inspekta akiwa anaaga kwa mama Kubwa kuwa wataendelea tu sana kufika pale, hivyo yeye asiwachoke.

    “Sawa baba, nitafurahi tu siku moja mkimtia nguvuni huyo muuaji, maana amani imetoweka na tunaishi kwenye mazingira ya wasiwasi mtupu,”

    “Msiogope kabisa, kwa sasa mpo salama kabisa, jeshi lenu linawalinda na chochote kitakacho kuwa kinaendelea hapa sisi tutajua hata kabla ya nyinyi wenyewe kujua, hivyo kuweni na amani tu mama Kubwa,” alimjibu huku tayari Joy akiwa amefika na kusimama nyuma ya Marsha ambae alionekana kuwa tayari kupokea box lile.

    Kama mtu aliekumbuka kitu hivi ama kumkumbuka Joy, akamuuliza

    “nakumbuka muda mchache kabla ya kutoka mwili wa marehemu MwanaHarusi wewe tulikuwa pamoja na ukaondoka na marehemu MwanaHeri, je nimekosea?”

    “Upo sahihi kabisa,” jibu lile lilimfanya Inspekta Kalindimya awaangalie kwa zamu Marsha na Joy, bila kujiuliza mara mbili akawaambia warudi kukaa ili waongee kidogo huku yeye akiwa ni mtu wa kwanza kuketi kwenye sofa lililokuwa jirani lakini likiwa ni tofauti na lile alilokaa awali.

    Baada ya yeye tu kuketi, wengine nao wakafuatia huku Marsha akiwa ni wa mwisho kuketi na aliketi jirani na alipo mama Kubwa.

    “Marsha ilikuwaje hapo? Mbona kama vile sijalielewa swali lako, unasema huyu Joy wakati mlipokuwa chumbani yeye akatoka na marehemu MwanaHeri kabla ya kukutwa na mauti, hebu fafanua kidogo ili nielewe,” aliuliza Inspekta akimtazama Marsha.

    “Yap! Ni kwa kuwa nae tunae hapahapa anaweza kutupa majibu,” kisha nae akamtazama Joy na kumuuliza

    “Nilikuona ukitoka na marehemu, hapo nikiwa namuona tu kama ni mtu tu ndani ya nyumba ile, Sikuwa nikimfahamu, wewe pia nilikuona ukishughulika mara kwa mara kitu ambacho kilinifanya niamini kwamba wewe ni muhusika ndani ya nyumba ile, lakini baadae ulikuja na kumuita Marehemu na bila kipingamizi yeye akanyanyuka kutoka chumbani na mkaelekea nje, je mlienda wapi?”

    “Tulipotoka chumbani mle tulikwenda moja kwa moja hadi nje ambapo nilienda kumuhoji marehemu kwani nilikuwa nimepata ujumbe wake kuwa alikuwa akinitafuta, ndio nikawa nimemuita ili kumsikiliza kwani mle ndani katu tusingeweza kuelewana,”

    “Alikuwa kweli akikuita ama ilikuwa ni habari ambayo si ya kweli?” alihoji Inspekta

    “Ni kweli alikuwa ana shida name,”

    “Shida gani?”

    “Mwana alikuwa amenunua simu mpya, ambayo bado hakuwa anajua kuitumia hivyo mara nyingi mimi nilikuwa nikimsaidia kumuonesha pale alipokwama, hata mara hiyo niliamini aliniita kwa ajili hiyo,” alisema Joy akikumbuka tukio hilo

    “Je ni kweli alikuita kwa ajili hiyo?”





    “Ndio, aliniita kwa sababu hiyo hiyo, lakini Sikuwa na muda wa kutosha kufanya kile alichotaka, kwani muda ulikuwa hauruhusu,”

    “Ni kipi alichokuwa akikihitaji ambacho ulikuwa huwezi kukifanya muda huo?”

    “Kulikuwa na namba ya simu alitaka kuihifadhi kwenye simu yake, alitaka kuisave yaani lakini akawa hawezi, ndio akanifuata mimi kwa ajili ya jambo hilo,”

    “Kwani ilikuwa ni lazima sana kui save kwa muda huo wa kuelekea kwenye muda wa kutoka kwenda kuzika?”

    “Nilimuuliza swali hilo akaniambia kuwa kuna mtu amemuandikia namba hiyo na ipo kwenye screen anahofu ataifuta na wakati ni namba muhimu,”

    “ok! Nini kikafuatia baada ya hapo?”

    “Nikaona kwa kuwa mimi muda hauruhusu, yaani siwezi kumsaidia, basi acha nimtafutie mtu ambae anaweza kumsaidia juu ya jambo hilo, ndio nikamkumbuka Salma mara tu nilipomuona akiwa ameketi na wasichana wenzie jirani na pale tulipokuwa tumesimama mimi na marehemu, nikamuita.” hali ikazidi kuwa tete kwsa Inspekta na afande Marsha, wakatamani kumjua na huyo Salma sasa, Marsha akauliza

    “Salma huyo ni nani?”

    “Ni binti yangu afande,” mama kubwa akajibu haraka haraka akiwa hajiamin9i kabisa, mapigo ya moyo yalionekana kwenda kasi kuliko kipimo chake cha kawaida, Inspekta akomba aitwe pale haraka kama yupo.

    Kwa mara nyingine Joy akatoka na kurudi akiwa ameongozana na binti wa kiasi cha miaka kama 16 hivi, alifika na kuwasalimia kisha akaketi jirani na mama yake, ambapo afande alijitambulisha na kumtambulisha mwenzie, kisha mahojiano nae yakaendelea.

    “Salma unamfahamu marehemu MwanaHeri?”

    “Ndio ninamfahamu,”

    “Unamfahamu kivipi?’

    “Ni rafiki kipenzi wa mpangaji wetu.”

    “Una taarifa juu ya kifo chake?”

    “Ndio ninazo,”

    “Sawa sawa, sasa unajua kuwa wewe ndio mtu wa mwisho kuonekana na marehemu?” lilikuwa ni swali gumu na zito kwa Salma, wote wakamtazama, nae akamtazama mama yake na kumkuta akimtazama yeye pia.

    Inspekta alitaka kujua tu kitu Fulani juu ya jambo hilo, alipoliona akarudi kwenye mahojiano.

    “Unakumbuka mara ya mwisho marehemu alipoonekana nawe, kabla alikuwa na nani?” salma tayari alikuwa maeathirika kwa swali lililopita, akajibu kwa kumuonesha kwa kidole Joy huku akiuma uma sehemu ya pindo la khanga yake.

    “wewe ulikuwa na nani wakati Joy na Mwana wapo pembeni?”

    “Nilikuwa na wanafunzi wenzangu ambao walikuja msibani kunipa pole,”

    “Baada ya kuwaona Mwana na Joy ni kipi kilifuatia?”

    “Dada Joy aliniita na kuniambia nimsaidie kusave namba kwenye simu yake iliyokuwa ipo chumbani kwa marehemu da MwanaHamisi,”

    “Ikawaje?” shauku ikawarejea tena.

    “Da Joy akaondoka na mimi na Dada Mwana tukaenda hadi chumbani kwa marehemu dada Mwana na kuingia ndani ambapo alitoa simu kabatini na kunipa,”

    “Kwa hiyo wewe ukai save hiyo namba?” aliuliza Inspekta na Marsha akaendelea tu kuandika.

    “Ndio nikaisave namba hiyo na kumrejeshea simu yake,”

    “Wakati huo yeye alikuwa wapi na anafanya nini?”

    “Yeye alikuwa kabatini akitafuta kitu Fulani hivi maana alikuwa akichakura chakura kwenye nguo,”

    “Alikwambia ni nini alikuwa akitafuta?” aliuliza Marsha na Salma alitikisa kichwa tu kukataa,

    “Baada ya hapo ikawaje?”Marsha akahoji tena.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi nae tukatoka tukiwa tumeongozana, mimi nikiwa mbele na yeye akiwa nyuma, lakini hatukuachana sana, hadi tulipofika nje akafunga mlango na sasa alikuwa na simu yake mkononi,”

    “Unaweza kuikumbuka hiyo namba ambayo uliisave?” aliuliza Inspekta Kalindimya.

    “Hapana kwa kweli, ila nakumbuka tu jina la Mtandao ila namba yenyewe siikumbuki,”

    “Hiyo namba wakati uki save ulisave kutoka kwenye namba zilizopigiwa ama kwenye missed calls ama kutoka kwenye namba alizopiga?”

    “Hapana, ile namba ilikuwa ipo kwenye screen, ilikuwa haijapiga wala kupigiwa, ni namba inaonesha iliandikwa tu na kuachwa ili mtu asave,” kengele ya hatari ikalia kichwani kwa Inspekta sasa akajidhihirishia kuwa mtu anae fanya mauaji yale si mtu wa taratibu, umakini mkubwa mno unatakiwa.

    “Mh… tunakusikiliza Endelea,” Marsha akamtaka aendelee tu na habari ile nyeti kwao.

    “Mi nilirejea kwa wenzangu na kuketi kama awali, Mwana nae alikuwa amepiga kama hatua tatu mbele hivi akielekea chumba cha wageni wa marehemu na wenyeji ambao ni kina mama, akatokea dada mmoja ambae alikuwa akilia pia, akamkumbatia Mwana na kumpa pole,” akatulia kumeza mate, kisha akendelea

    “Wakati huo hapo nje tulikuta jeneza la marehemu dada Mwana likianza kutoka uwani kwenda barabarani kwa ajili ya kuondoka kwenda makaburini, Mwana akaanza kulia kwa uchungu sana akiwa pembeni ya jeneza, akatokea dada mwingine mmoja hivi, tofauti na Yule wa awali, huyu alikuwa ni mweupe tena ni mrefu na mwembamba kiasi akamnong’oneza sikioni na kisha akamshika mkono, sote tulijua hawa wanajuana tu na hakuna alie shughulishwa nao,” alisema Salma kwa kujiamini kabisa.









    “Wakaelekea wapi?” akauliza Inspekta kwa shauku, watu wote wakiwa wamemtolea macho Salma, hakuna yeyote mle ndani aliekuwa akijua juu ya jambo hilo.

    “Wakarudi kwenye mlango wa marehemu da MwanaHamisi, na da Mwana huyu aliefariki jana akatoa tena funguo na kufungua mlango, wakaingia mle ndani na tangu hapo sikujua tena kilicho Endelea hadi wewe ulipokuja na kuingia mle ndani,”

    “Alitoka saa ngapi huyo dada alie ingia na marehemu Mwana?” Inspekta Kalindimya aliendelea tu kuhoji huku akiwa makini na majibu ya Salma.

    “Noo! Sikuwa makini kabisa kumtazama tangu wakati ameingia hivyo sikujua kabisa niwakati gani alitoka, kwani tulikuwa busy na kutazama jeneza la marehemu likitoka mle ndani kuelekea makaburini,” alijibu binti kwa uhakika kabisa, afande Marsha na Inspekta Kalindimya wakatazamana kujiuliza nani aulize swali lifuatalo, Marsha akaelewa, akamuuliza Salma

    “Alikuwa amevaaje huyo mdada unaemzungumzia hapa?”

    “Alivaa Hijab nyeusi na miwani kubwa pia nyeusi, na kila muda alikuwa ameweka kitambaa chake usoni kama mtu anaefuta machozi vile na hata mara moja hakukitoa kitambaa hicho usawa wa pua na mdomo,” alizidi kufafanua Salma.

    “Ukimuona huyo mdada unaweza kumjua?”

    “Hapana nina hakika siwezi kumjua, maana sura alikuwa akiifunika sana kwa kitambaa usawa wa pua na mdomo na wakati mwingine akiwa anainama chini mara kwa mara,”

    “Je kwa hilo umbo ulilotutajia, kama tutamleta hapa unaweza kumtambua?”

    “Yeah!Kwa umbo hata usiku wa manane naweza tu kumjua ila kwa sura hata nisilidanganye jeshi letu, siwezi kabisa kumtambua.” Alimaliza Salma kujibu na Marsha aliekuwa akiandika mahojiano hayo akamtazama mkuu wake wa kazi.

    “Salma nashukuru mno kwa msaada mkubwa uliotupatia, huenda ukatupatia mwelekeo huko mbele japo kwa sasa bado unatuacha njia panda, ila tu wakati wowote tukikuhitaji, naomba utoe ushirikiano, sawa Salma?” aliuliza Inspekta na Salma akakubali bila kipingamizi.

    Akamgeukia mama Kubwa na kumuuliza

    “Mama Kubwa huyu aliekufa jana jioni nae jina laek ni Mwana, ama nimekosea?”

    “Wala hujakosea, huyu pia ni Mwana, tumejua kuwa anaitwa MwanaKheri,” alijibu mama Kubwa huku akijiweka vizuri, alijua sasa mahojiano yamehamia kwake.

    “Jana hadi usiku tunapo achana nawe, jina hilo la mbele ulikuwa hulijui, leo saa hizi ni asubuhi unasema mmelijua, umelijuaje?” aliuliza Marsha huku akifunua tena diary yake kuandika anayo yasikia pale.

    “Kama unavyojua tena misibani, mengi yanasemwa, hata jina hilo limesemwa semwa tu hadi yakanifikia kuwa jina lake halisi ni hilo,” mama Kubwa aliingiwa na hofu kutokana na kujichanganya na kuchanganywa na maswali ya wale maafisa upelelezi.

    “Ok! Kwa hiyo ni jina ambalo halina uhakika?”

    “Niseme tu hivyo kwa kuwa hatukumsikia mwenyewe, ila ninaamini itakuwa ni jina lake hilo,”

    “Ok! Na Yule mwana aliefariki awali ambae alikuwa ni mpangaji humu ndani, alikuwa akiitwa Mwana nani?” aliuliza Marsha Mauki.

    “MwanaHamisi, MwanaHamisi Rehani,” sasa aliamua kuwa awe anajibu kifupi ili tu asijichanganye.

    Wakatikisa vichwa kuoneshwa kuridhika na majibu yale na kujilaza kwenye sofa na kuangalia juu, akashtuka na kunyanyua shingo ghafla na kumuuliza Marsha Mauki

    “Funguo ya chumba cha Marehemu umekuja nayo?”

    “Ndio mkuu, ninayo hapa,” alijibu huku akinyanyuka na kuitoa kwenye Jeanz yake ya kike aliyovaa huku akimkabidhi mkuu wake.

    “Twende chumbani kwa Marehemu,” wakaongozana huku wakiwa na shauku, Marsha alitaka kujua kuna nini Boss wake amekipata pale ghafla vile na Inspekta nae alitaka kuhakikisha kile kilicho kuja ghafla kicwani.

    Walifungua na kuingia wao wawili tu chumbani, Mama Kubwa alibaki nje, kitu cha kwanza alichokifanya Inspekta ni kwenda moja kwa moja kwenye kabati ya marehemu Mwana na kupangua taratibu vilivyomo, kimoja kimoja.

    Alipofikia hatiua Fulani hivi akamuagiza Marsha aende kwenye gari yake akalete Kamera ili kuna kitu akihakiki mle ndani.

    Marsha akachukua dakika tatu tu kuwa tayari amerudi ndani akiwa na kamera mkononi, akamwambia kuopitia hizo picha zilizopo kwenye Kamera, ahakiki kama kuna mabadiliko yoyote mle chumbani toka walipo ondoka siku ya kwanza.

    “Usishughulishwe na kabati lakini, maana tayari hii nimeisha ivuruga, angalia tu tofauti ya juzi na jana, ama kama ina sumbua tukasafishe kwanza,” aliongea huku akiendelea kufanya kazi yake.

    Kila katratasi aliyoiona mle ndani aliipitia na kuifunua, aliyoiona ina manifaa kwenye kazi yake aliiweka na zile alizoona hazifai aliachana nazo. Marsha akasema ataendelea kuangalia taratibu akivuta subira wakati yeye akifanya kazi yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuna karatasi moja Inspekta akaiona, ilikuwa na namba nyingi za simu, alijaribu kuangalia namba zile, zote zilikuwa na majina ya watu wenye namba hizo, aliona hiyo itamfaa, akaichukua na kuiweka kwenye mfuko wa koti lake.

    Lakini wakati akiiweka, akamsikia Marsha akishtuka kwa mshangao na kumuita

    “Inspekta…” huku akimsogelea mkuu wake, kamera ikiwa mkononi, Inspekta akageuka kumtazama, wakati huo tayari Marsha alikuwa pembeni ya ubavu wake, akampa Kamera na kumwambia…









    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog