Simulizi : Askari Jela
Sehemu Ya Tatu (3)
Majira ya moja jioni James alikuwa yu sebuleni akiangalia luninga, mama yake alikuwa yupo jikoni na kaka yake alikuwa yupo chumbani. Mlango wa kuingia sebuleni kwao uligongwa mara mbili jambo ambalo lilimpeleka kuinuka kwenye kochi na kwenda kuufungua, akili yake ya utoto aliyokuwa nayo hakuwa ameuliza huyo aliyokuwa akigonga mlango huo alikuwa ni nani. Wala hakushughulika kujiuliza huyo aliyekuwa akigonga mlango huo alikuwa ameingiaje ndani hapo bila kufunguliwa lango la magari ambalo mara nyingi sana huwa linafungwa majira yote na hufunguliwa baada ya kugongwa. Akili yake yote ilikuwa imemtuma kuwa huyo aliyekuwa amegonga mlango huo alikuwa ni Baba yake kipenzi ambaye hakuwa amerejea nyumbani ,alitekenya kitasa kwa kutumia ufunguo uliokuwa upo kati yake na hatimaye kitasa hicho kikatii amri. Aliponyonga kitasa na kukifungua kilichofuata hapo ilikuwa ni kuandikwa kwa historia mpaya katika maisha yake, ulikuwa ni mwanzo wa ukurasa wa maisha ambao ulikuwa ni zaidi ya jeraha kwake.
Ugeni uliotangulia baada ya yeye kufungua mlango ilikuwa ni gesi nzito, ugeni ulivamia macho yake na kumpa muwasho wa ajabu sana ambao hakuustahimilia alipiga kelele kutokana na maumivu aliyoyapata huku akitaja jina la mama yake. Kilichofuata hapo ilikuwa ni kutoona kilichopo mbele yake, akiwa kwenye hali hiyo ya kupiga kelele alipokea msukumo wa nguvu sana ambao ulimrudisha ndani ya nyumba. Mama yake na kaka yake walipotoka tu kilichofuata ilikuwa ni kila mmoja kuoneshewa bastola na mtu ambaye alikuwa na silaha, mtu huyo ambaye hawakumtambua na wala hawakuwahi kuiona sura yake aliwaamuru wakae kimya na kisha walale chini. Haikupita hata dakika tangu walazwe chini aliingia mtu mwingine ambaye alikuwa amevaa suti nadhifu sana kama wa awali, mtu huyu alifunga mlango na kisha akabaki akitabsamu sana.
"Salam kwako mke wa SSP" Aliongea mtu huyo wa pili kuingia ambaye alikuwa na upara pamoja na ndevu nyingi kidevuni.
Salamu yake haikujibiwa na alioneshewa sura zilizojaa woga kama vile ndiyo lilikuwa jibu la salamu hiyo, hilo halimkufanya huyu mtu awazingatie na badala yake aliachia tabasamu pamoja na mwenzake ambaye alikuwa amewawekea silaha. Huyu alikuwa na nywele nyingi sana huku kidevuni mwake hana ndevu tofauti alivyo mwenzake, naye alirudisha tabasamu alilopewa na Madevu kisha akawatazama mateka wake walikuwa wamejaa hofu sana.
"Mdomo mzito sana kujibu salamu Bibi wa SSP lakini iliyotuleta hapa si salamu yako utakijua tu" Madevu aliongea kwa mara nyingine kisha akaenda mahali ilipo sebule ya chakula, alirudi akiwa na kiti ambacho alikiweka jirani kabisa na eneo ambalo James alikuwa ameangukia baada ya kuingiliwa na hewa asiyoijua kwenye macho yake. Akiwa na tabasamu lilelile alimnyanyua mtoto huyu ambaye alikuwa amejigonga vya kutosha baada ya kusukumwa, amlishika kwa namna isiyopendeza kabisa na kisha akamuwekea mkono jirani na uso wake. Aliupitisha mkono mara mbili kwenye uso wake James, macho hayakupepepsa kuashiria alikuwa haoni.
"Hongera sana jamaa ile gesi imefanya kazi sasa hawezi kumtambua yeyote yule kati yetu" Aliongea na kisha alimsukuma kwa nguvu hadi akajigonga kwenye kabati la vyombo akaanguka chini, yowe ya uchungu lilimtoka mama yake lakini aliwahiwa na kidole cha shahada kilichowekwa mkono kumuashiria akae kimya.
Wakiwa wapo ndani ya nyumba hiyo mngurumo wa gari ulisikika na hatimaye ukavumia kwenye lango la kuingia ndani ya nyumba hiyo, wote walitambua mhusika aliyekuwa akiiingia eneo hilo hakuwa mwingine ila ni SSP Nkongo. Milio ya honi hapo getini ilisikika ambayo haikuwatia hofu watu wale waliokuwa wapo humo ndani, sekunde kadhaa lango kuu lilisikika likifunguliwa kisha gari hiyo iliingia hadi ndani. Wete humo ndani walisikiliza sauti hadi pale gari hiyo ilipoenda kuegesha na kuzimwa, milio ya viatu ya watu wengi si tu mmoja alisikika ikisogea kwenye eneo la barazani kwenye mlango. Haukupita muda mrefu mlango ulifunguliwa na, aliingia SSP Nkongo akiwa amefuatana na mtu ambaye alikuwa amevaa nguo za kifungwa akiwa amemuwekea bastola kisogoni. Alipoingia tu alifuatana na mwingine ambaye alikuwa amevaa nguo za kifungwa akiwa amesokota rasta, yeye naye alitulizwa chini kama ilivyo familia yake. Wavamiaji wale waliokuwa wapo humo ndani walitazama wote mlangoni, hiyo ilikuwa ni ishara kuwa walikuwa hawajatimia idadi yao kuna mwingine alikuwa akiingia.
****
Umbali kutoka kule shamba alipokuwa amejenga ile nyumba hadi katikati ya mji, ulikuwa ni mkubwa ambao ungemgharimu kupoteza dakika nyingi njiani. SSP Nkongo aliamua kuongeza mwendo wa gari na hatimaye alikuwa amefika katikati ya jiji, dhumuni kubwa ilikuwa ni kwenda kituo cha kati kwenda kuchukua maaskari wa jeshi la polisi ili aongozane nao kwenda kumtia nguvuni ASP Lutonja. Alipokuwa yupo kwenye foleni katikati ya jiji ndiyo akakumbuka alikuwa amesahau kitu muhimu sana, silaha yake aliyokuwa akiitumia ndiyo alikumbuka alikuwa ameisahau. Aliamini kabisa angeongozana na maasakri hao kwenda kumkamata lakini isingewezakana kuwa mikono mitupu, silaha ilikuwa ina umuhimu wake. Mtuhumiwa akiwazidi nguvu maaskari basi silaha hiyo ingewaku na wajibu, hakutka kujiaminia kisa alikuwa ameongozana na Maaskari.
Hakika aliona amefanya uzembe mkubwa sana kuisahau silaha pindi alipoingia nyumbani kwake alipotoka kazini, alifikia hatua ya kujitukana mwenyewe alipokuwa yupo humo garini kwenye foleni. Yale mazoea ambayo sasa amekuwa tabia kila ifikapo nyumbani ni kutoa silaha yake ndani ya gari na kuihamishia ndani, sasa yalikuwa yamemgharimu ndani ya siku hiyo muhimu. Alikuwa amezoea kutotoka tena aingiapo ndani ya nyuumba yake na sasa mazoea hayo yalikuwa yakimgharimu yeye mwenyewe, hakuwa na jinsi zaidi ya kugeuza gari kuiwahi silaha yake a bila ya kujua alikuwa akienda kulikabili balaa jingine kabisa lililokuwa likimgoja ndani kwake.
Kutokana na uwepo wa foleni katika barabara za jijini aliweza kufika nyumbani kwake majira ya Saa moja ikiwa inaelekea saa mbili, huu ulikuwa ni muda ambao nyumbani kwake tayari kulikuwa kumevamiwa na yeye alikuwa hajui kuhusu hilo. Alipofika kwenye lango kuu la kuingilia nyumbani kwake kutokana na wahka aliokuwa nao, alipiga honi kwa fujo. Haikupita muda lango hilo lilifunguliwa huku mfunguaji akiwa hamuoni na wala hakujali kuhusu kumuona yeye alisogeza gari hadi kwenye maegesho na alishuka akiwa ni mwenye haraka. Kitendo cha kukanyaga mguu kwenye ardhi ya maegesho ya nyumbani kwake, kuliambatana na kukutana mdomo wa bastola.
"Geuka nyuma na utulie hivyohivyo" Aliamriwa na mtu ambaye alikuwa amevaa sare za wafungwa, hakutaka kubisha aligeuka kama alivyo na kisha alikuja mtu mwingine ambaye alimpekua halafu akaamriwa aingie ndaani.
Ndipo alipoingia ndani akakutana na familia yake ikiwa imewekwa chini, naye aliongezewa hapo chini na kuwekewa silaha. Muda huohuo vilisikika viatu vya mtu akikanyaga kwenye sakafu ya barazani kuashiria kuwa alikuwa akiingia ndani ya nyumba hiyo, wavamizi wale walitokwa na matabasamu waliposikia sauti hizo. Aliingia ndani ASP Lutonja akiwa amevaa nguo za kazi akionekana ni mwenye tabasamu pana, wale ambao walikuwa hawajui kabisa kuhusu upande wa pili wa afande huyu walionekana kutoamini kabisa kama angeweza kuwafanyia hivyo.
"Elius unajidai mjanja sana, huu mtandao ni mpana wewe umeona sasa" ASP Lutonja aliongwa na kisha alijongea hadi pale alipo Madevu ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti, alipishwa kwenye kiti hicho na kisha akaketi yeye.
"Napenda utambue hivi kila sehemu tuna vibaraka wetu ili kuhakikisha usalama wetu, maaskari wote waliokuwa wamejua ukweli wetu sasa ni hivi ni marehemu. Ujinga wa maaskari hao walikuwa ni kuwaeleza wenzao kuwa walikuwa wanaenda kumuambia mkuu wako Mwambe, wamemwambia na alipokuja kukuambia wewe nilikuwa nina taarifa tayari na nilitega sikio kusikiliza kile chote mlichokuwa mkikiongea. Sasa hii ndiyo zawadi yako na wewe, huyo Mwambe namuacha hana madhara kabisa sasa hivi" ASP Lutonja aliongea huku akitabasamu kwa dharau.
"Mwanaharamu mkubwa wewe" SSP Nkongo aliropoka akiwa hana uwezo wa kufanya chochote
"Ndiyo na uanaharamu wangu ndiyo leo nimekuja kuuonesha kwako, najua umeandika faili kuhusu uchunguzi wako. Lipo wapi?"
"Faili ninalo lakini siwezi kukupa hata ufanyeje"
"Alaaaaah! We nunda siyo, Manywele mpe demo kwanza" ASP Lutonja alipotoa kauli hiyo yule mwenye nywele nyingi aliyekuwa na silaha alimpiga risasi ya kichwa mtoto wake wa kiume mkubwa akaondokwa na uhai papo hapo.
"Noooooo! Fred my son" SSP Nkongo alishindwa kuvumilia akapaza sauti na machozi yakaanza kumtoka, mke wake naye ilikuwa ni hivyohivyo kutokana na uchungu wa kumpoteza mwana.
"Elius usilete ubishi kumbuka umebakiwa na mtoto mmoja tu yule pale ambaye haoni,leta faili hilo"
"Natoa! Natoa! Lipo kwenye gari"
"Mpe ufunguo Bwana Nyapara akalilete upesi sana"
Hakuleta ubishi alitoa ufunguo wa gari na kisha aliurusha mbele bado akiwa analia, Yule ambaye alikuwa amevaa nguo za kifungwa aliyesokota rasta aliuchukua na akatoka nje. Alirejea baada ya muda mfupi akiwa amebeba faili hilo ambalo lilikuwa limeambatanishwa na pingu, alimpa ASP Lutonja faili hilo.
"Anhaaaaah! Naona ulijiandaa kabisa kuniweka nguvuni hadi na pingu ulikuwa nazo, lakini umeshachelewa tayari ndugu. Faili ninalo mkononi"
"Faili unalo tayari naomba iache famili yangu bado nahitaji iendelee kuishi"
"Ngamia akiweza kupita kwenye tundu la sindano ndiyo suala hilo litawezekana, leo nataka ushuhudie kwa macho yako ile mikanda ya wazungu isiyohitajika nchini katika uhalisia. Madevu chukua silaha ya Nyapara umuangalie huyu firauni" ASP Lutonja alipoongea maneno hayo yule Nyapra mmoja aliyekuwa amemtuliza SSP Nkongo alimpa silaha Madevu, baada ya hapo wale manyapara wawili walimchukua mke wa SSP Nongo na kumlaza chini kinguvu.
Nguo zake zilichanwa mbele ya mume wake akiwa anashuhudia ambaye alitamani kuinamishwa kichwa chini lakini alilazimishwa kutazama, uchanwaji wa nguo na manyampara hao kulimwacha akiwa mtupu ndani ya muda mfupi tu. Mmoja alimshikilia na kisha mwingine alianza kumuinmgilia kinguvu katika njia zote mbili huku mume wake akishuhudiaa, aliporidhika alikuja kumkamata na kisha mwenzake akawa anamuingilia kinguvu vilevile hadi walipotosheka. Damu zilikuwa zimetapakaa kwenye eneo ambalo alikuwa akiingiliwa kutokana na kuingiliwa njia zisizo stahiki, alikuwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu aliyoyapata huku akiwa hana hata nguvu ya kusimama.
"Nkongo umeona mkanda wa X huo natumai umekuburudisha" ASP Lutonja aliongea kwa kejeli.
Lilikuwa ni tukio ambalo halikuwa likifaa kabisa kuangaliwa na macho ya SSP Nkongo, mke wake ambaye alikuwa akimpenda. Aliyekuwa akimpa hadhi kama ya malkia ndani ya majira hayo alikuwa amedhalilishwa vya kutosha, mwanamke ambaye alimpenda na kumuheshimu alimuona akiwa amefanywa kama kahaba ambaye alikuwa amevamiwa na wahuni. Jambo lenye kuumiza ambalo hajawawahi kufanyiwa kwenye maisha yake, lilikuwa ni hilo kuliko yote mazito ambayo aliwahi kuyapitia.
"Annaaaa!" Aliita jina la mke wake kwa uchungu sana lakini kelele zake hizo zilizua mengine kabisa, bastola ambayo ilikuwa ipo mikononi mwa Madevu ilikohoa baada ya ASP Lutonja kutoa ishara. Kichwa cha mke wake kilitobolewa kama ilivyofanya kwenye kichwa cha mtoto wake mkubwa Fred. Alilia sana huku akikumbuka jinsi ambavyo alikuwa akiishi na mke wake huyo, upendo wote alioneshewa na mke wake hapo ndiyo ulikuwa ukipita kama mkanda wa sinema kwenye kichwa chake. Alitamania hata tukio lile liwe halijatokea aweze kuwa na mke wake, lakini lilikuwa ni jambo ambalo haliwezekani kwani lilikuwa limetokea tayari. Alilia kama mtoto mdogo na kusababisha hadi James ambaye alikuwa amebaki peke yake naye alie kutokana na kilio cha baba yake, kilio hicho cha mtoto wake mmoja tu aliyekuwa amebakia kilimfanya geuze uso kumtazama mtoto huyo.
Kitendo cha kumuona tu mtoto wake akiwa ni mwenye kupapasa kilizidi kumtia uchungu,kujigonga kwa mtoto wake kwenye sehemu mbalimbali kulifanya aone kama alikuwa akijingonga yeye. Hakukuwa na msaada mwingine ambao ungeweza kumsaidia, kilio ndiyo ulikuwa msaada wake kwa muda huo aliokuwa amefikwa na makuu zaidi kwenye maisha yake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Vipi Nyapara mmeupenda na mzigo huo nini, mkiutaka ni juu yenu tu" ASP Lutonja aliongea maneno hayo huku akiwatazama wale wafungwa wenye vyeo gerezani.
Ilikuwa ni jambo la neema sana kwa Wanyapara hao na hawakutaka kupoteza muda, kwa kasi ya jabu walimuendea SSP Nkongo wakiwa a lengo moja tu ndani ya vichwa vyao. Ilikuwa ni kumuingili na si kitu kingine, walipomfikia walitaka kumkamata kwa nguvu na hapo walikutana na sekeseke jingine kabisa. SSP Nkongo hakuwa akitaka kabisa kufanyiwa kitu hicho, alikuwa yupo radhi afe lakini si kuingiliwa na wafungwa wale walio na uchu kutokana na kukaa gerezani. Mmojwapo alipomgusa tu alimzoa akanguka chini kisha akajifyatua na kusimama wima, wa pili alipomfuata alimuachia masumbwi ya maana yakampeleka chini. Alipotaka kumfuata kulekule chini alipokuwa ameanguka alipigwa risasi ya mgongo, bado hakutaka kukata taama kwa kupigwa risasi hiyo aliamua kujirusha na kumfuta hukohuko. Aliitwa shingo ya Nyapara na kumkaba kwa nguvu zake zote, wale waliokuwa wana silaha walikuwa wakifanya kazi ya kupiga risasi za mabega lakini mikono hiyo haikutoka . Nyapara alikuwa akitapatapa huku akirusha miguu kutokana na kukabwa huko, waliendelea kumpiga risasi mbalimbali kwenye viungo vyake ili aachie lakini ni kama vilikuwa si viungo vyake. Hakuachia kabisa hadi pale Nyapara aliposhiwa nguvu kabisa akawa haleti fujo kabisa, Nyapara mwingine alisogelea karibu akajaribu kumtoa mwenzake lakini alikutana na mikono imara zaidi ya chuma.
Kitendo cha Nyapara yule Marasta kusogea karibu kujaribu kumtoa mwenzake, wale wenye silaha wakaacha wote kutumia silaha zao. Hapo ndipo walipokuwa wamehalalisha kifo chake kwenye mikono ya SSP Nkongo ambaye alikuwa akitokwa damu sehemu mbalimbali, mwenzake akiwa anavutana naye ndiyo muda ambao Nyapara yule alikata roho akiwa yupo kwenye mikono ya adui yao. Mikono ilipokuja kulegea na kufanikiwa kumtoa, waliopoa mwili ambao haukuwa na uhai tofauti na kutarajia kuwa wangeopoa mwili wenye uhai. Hilo liliwatia hasira sana na wakamiminia risasi sehemu mbalimbali za mwili SSP Nkongo, mwili wake ulipoingiliwa na risasi hizo ulikuwa ukifanya kazi ya kuhaha kuhakikisha uhai hauondoki. Uhahaji huo wa kubaki na uhai haukufanikiwa kutokana na uhai kuwa na nguvu ya kutoka kuliko kubaki ndani ya mwili, SSP Nkongo aliaga dunia bila ya kutamka neno lolote na shingo yake iliangukia upande. Macho yake yalikuwa yakimtoka kuelekea eneo ambalo alikuwa amelala James, huo ndiyo ulikuwa mwisho wa Askari mzalendo ambaye aliondoka sambamba na watu wake muhimu wawili akimuacha mmoja hana msaada.
"Vipi ASP tummalize na huyu mtoto?" Madevu aliuliza
"Aaargh! Achana naye huyu, hajaona chochote na wala hajui kuhusu chochote kuhusu sisi. Tuondokeni haraka eneo hili, we Nyaparra beba mwenzio tutaenda kutengeneza kifo chake gerezani" ASP Lutonja aliongea na kisha alianza kupiga hatua kuelekea nje ya nyumba hiyo, wenzake walifuata nyuma kutoka nje.
****
Matukio yote yaliyokuwa yakitokea James hakuwa akiyaona kwa ufasaha kutokana na gesi ya sumu aliyokuwa amepulizwa kwenye macho yake. Gesi hiyo haikuwa imemuathiri sehemu kubwa ya macho yake kiasi cha kumfanya kutoona kabisa, alikuwa akiona maumbile ya watu pamoja na ukungu mwingi sana. Sauti zote zilizokuwa zikitoke alikuwa akizisikia barabara, aliweza kushuhudia maumbile ya watu hao yakifanya unyama pamoja na kelele nyingi ambazo zilikuwa zikitoka kwa wazazi wake. Nguo za rangi ya machungwa pamoja na sare za kazi alizovaa ASP Lutonja, aliziiona rangi yake lakini hakuweza kuwatambua wavaaji wake walikuwa ni kina nani, Kunyanyaswa na wale wavamizi napo kulinyima kabisa wasaa wa kuweza kusimama. Alikuwa akilia kwa uchungu katika muda ambao wavamizi hao walikuwa wakitenda unyama hadi wanaondoka, kelele za wazazi hadi zinatulia alikuwa akiendana nazo kwa kilio cha uchungu. Pamoja na kuwa bado alikuwa hajapevuka na alikuwa akielekea umri wa kupevuka, hakuwa na akili ya kitoto kiasi cha kutotambua kilichokuwa kikiendelea eneo hilo kilikuwa ni nini. Wavamizi walipotoa miguu yao na kutokomea kusikojulikana, tayari alikuwa amejua hakuwa na ndugu yeyote ambaye alikuwa amebakia hai.
Hilo lilimfanya aendelee kulia kimyakimya kutokana na sauti kumkauka kwa kulia muda mrefu, nguvu nazo kwenye mwili wake zilimuishia taratibu kila alipozidi kulia na mwishowe alipoteza fahamu na hakujua kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Alikuja kuamka katika majira ambayo hakuyajuakabisa, alipofungua macho yake aliona giza tu na hakuwa na uwezo wa kuona kabisa. Alipiga kelele kwa nguvu huku akiwaita wazazi wake, kelele hizo ziliambatana na sauti za kuhimizwa Msichna aende kumtuliza asifanye fujo. Akiwa hajui kinachoendelea alijikuta akilishikiliwa kwa nguvu sana, alihisi kukamatwa na mikono laini ya kike ambayo ilikuwa imemshinda nguvu alizonazo. Mikono hiyo ilipokuja kumuachia taratibu alipungukiwa nguvu na kisha aliiingiwa na usingizi wa ghafla ambao hakuutarajia kma uneweza kumpata.
****
Zilipita siku tatu ndani ya nchi nzima habari iliyokuwa imetawala ilikuwa ni kifo cha SSP Nkongo pamoja na mke wake ambaye liingiliwa kabla ya kuuliwa. Ilikuwa ni habari ya simanzi sana kwa watu waliokuwa wakimpenda afisa huyu wa jeshi la Magereza ambaye alikuwa amejizolea sifa lukuki, kifo chake hicho kilipelekea hata wale ambao walikuwa hawamjui kuanza kumfuatilia. Wengi walipobaini utendaji wake wa kazi pamoja na pongezi nyingi ambazo alikuwa amepatiwa na Mheshimiwa Rais walihuzunika sana, majira ya jioni ya siku hiyo habari zikiwa zimesambaa kuliibuka kwa msiba mwingine mzito sana ambao uliwafanya watu wabaki na hurum sana kwa kizazi cha Mzee Nkongo. Mama yake Mzazi SSP Nkongo naye aliaga dunia kwa shinikizo la damu ambalo lilichangiwa na kifo cha mtoto wake, ilikuwa ni misiba minne iliyokuwa ipo nyumbani kwa Mzee Nkongo Tanga.
Siku iliyofuata mazishi yaliyohudhuriwa na watu wengi sana yalifanyika kwenye Makaburi ya Bombo, watu waliokuwa wakitoka kwenye mikoa tofuti walikuja kuhudhuria kwenye mazishi hayo ya Afande Mzalendo. Viongozi mbalimbali wa kiserikali nao walikuwa wapo kwenye mazishi hayo kuifariji famili ya wafiwa ambayo ilikuwa imebaki Babu na Mjukuu tu. ambao walikuwa hawana muangalizi yeyote. Ilikuwa imepita miaka mingi sana Mzee Nkongo hakuwa ameenda nyumbani kwao, umri huo alikuwa ameshasahau ndugu zake wote waliokuwa wapo huko kwa Kagera kutokana kulowea Tanga tangu apangiwe ajira huko. Hivyo ndugu waliokuwa karibu yake walikuwa ni yeye, mjukuu wake pamoja na familia ya mkewe ambao walikuwa wenyeji wa mkoa huo.
Mazishi ya SSP Nkongo yalihudhuriwa hata wakuu mbalimbali wa majeshi nchini wakiongozwa na Amiri jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Marehemu wote wanne walipumzishwa kwenye nyumba zao za milele ndani ya siku hiyo, mazishi yalipokalimika watu wote walitawanyika na wachache wakaja kuifarijia familia ya Marehemu.
****
Siku ilishia hatimaye ikaingia siku ya pili na hadi ikaingia juma, nalo halikukaa na hatimaye likaja la pili yake hadi ukatimia mwenzi. Taratibu watanzania walianza kusahau kuhusu tukio hilo ambalo lilikuwa limemkuta kijana mdogo James ikimuacha akiwa hna wazazi, alikuwa akilelewa na babu yake Mzee Nkongo huku Inspekta Mwambe akiwa anakuja kumuona siku moja moja. Upofu ndiyo ulikuwa ni maisha yake kutokana na dawa aliyokuwa amewekewa na wavamizi wa nyumbani, unyonge ndiyo ulikuwa rafiki yake mkubwa ingawa alikuwa na rafiki mkubwa sana ambaye alikuwa akimchekesha kila siku. Ucheshi wa marehemu baba yake hata babu yake alikuwa nao na ndiyo huo alikuwa akiutumia kumchekesha lakini haikusaidia kitu katika kumuweka kuwa ni mwenye furaha. Bado aliendelea kuwa yu mwenye huzuni uliokuwa umezidishwa na kutokuwa na uwezo wa kuona ilihali alizaliwa akiwa anaona.
Ahadi za kumsaidia ambazo zilikuwa zimetolewa na viongozi wa juu wa kiserikali zikaungwa mkono na wananchi zilikuwa zimeyeyuka tayari, msaada wowote haukuja nyumbani hapo. Mzee Nkongo alizidi kuilaani serikali hiyo na akawa akiishi na Mjukuu kwa shida sana, pamoja na na shida hizo bado alimpenda sana James na alimona ni Elius wake wa pili baada ya kwanza kufariki. Alikuwa akihisi bado alikuwa ana huzuni kila akitazama hali ya Mjukuu wake ambaye ilikuwa ni yenye kusikitisha, alikuwa ni mwenye kupelekwa chooni na hata kufanyiwa huduma zingine muhimu katika maisha yake kutokana na kutojiweza. Mzee Nkongo aliendelea kutaabika naye na hakutaka kuona msaada wa yeyote zaidi ya Inspekta Mwambe ambaye alijitolea kuwasaidia tangu siku ya kwanza, wengine ambao walikuwa wakiahidi kumsaidia alikuwa akiwaona wanafiki. Hakuwa akiacha kuilaani serikali ambayo alikuwa ameifanyia kwa miaka mingi hadi anastaafu, ambayo pia mwanae aliitumikia kwa moyo wote hadi anafikwa umauti. Aliona kuwa hayo ndiyo yalikuwa malipo ya hiyo serikali katika kujituma kwake kwenye ajira, moyoni msemo wa fahila za punda ni mateke haukuwa ukimtoka kwa hayo aliyofanyiwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwaka mmoja baadaye ilikuwa ni pigo ingine kwa James katika maisha yake, Mzee Nkongo ambaye alikuwa msaada kwake naye hakukaa muda mrefu Mungu akamchukua akabaki akiwa peke yake. Taarifa za kifo cha Mzee Nkongo zilimfikia Inspekta Mwambe akiwa yu mgonjwa na hata alipokuja kupona na kwenda nyumbani kwa Mzee huyo, alipewa taarifa ya kucukuliwa James na ASP Lutonja ambaye alikuwa ameahidi kumlea. Hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya ambayo inasikitisha sana kwake, alimuonea huruma sana mtoto yule ambaye alikuwa ametelekezwa na ndugu wa mama yake baada ya kubaki yatima. Sasa alikuwa ameangukia kwenye mikono ya mtu ambaye alikuwa akihisi kabisa hakuwa mtu sahihi, aliumia sana lakini hakuwa na nguvu ya kuzuia hilo kwani hakuwa na nguvu ya kupinga hilo kutokana na kuwa mdogo kicheo na wala haikuwahi kujulikana kama alikuwa na urafiki mkubwa na Marehemu baba yake.
****
Maisha ndani ya nyumba ya ASP Lutonja yalianza kwa furaha kabisa, alianza kupata faraja kwa kuwa pmoja na mtu ambaye alikuwa akikaribiana naye rika. Malezi mazuri aliyokuwa nayo kwa Mke wa ASP Lutonja alianza kuona kama alikuwa akilelewa na mama yake, aliishia akiwa ni mwenye kuhudumiwa kwa kila kitu huku akipewa kila hitaji muhimu na rafiki wa Marehemu baba yake ambaye sauti yake hakuwa akiipenda kusikia. Kila akiisikia sauti yake alikuwa ni mwenye kukereka lakini upendo aliokuwa akipewa ulimuondolea kero yote ambayo alikuwa nayo kwa kusikia sauti hiyo, alipata raha ya maisha ile ambayo aliikosa kwa kundokewa na wazazi wake.
Upendo wa kinafiki aliokuwa akioneshwa na ASP Lutonja haukudumu kwa muda mrefu, muda huo hakujua kabisa kuwa alikuwa akisukiwa mpango wa kuweza kumuondoa ndani ya nyumba hiyo ili aonekane hafai. Jambo jingine alikuwa halitambua ni shinikizo la mama mwenye nyumba hiyo aliyekuwa akimpenda kwa dhati, huyo ndiyo chanzo cha yeye kuletwa ndani hapo. Pamoja na mwenye nyumba hiyo kudanganya vya kutosha kuwa alikuwa akiletewa msaada kipindi alichokuwa yupo kwa babu yake ili asiletwe hapo, hakuweza kushawishi kabisa kuzuia kuletwa hapo baada ya kufariki kwa Mzee Nkongo. Alikuwa akikereka kila anapomuona ndipo siku moja akamua kumfanyia hila, alikula njama na mfanyazi wa nyumba hiyo kumpakazia hila mbaya James.
Akiwa hana hili wala lile siku ya siku ulipotimia muda wa kulala akiwa ni mwenye kuongozwa kutokana na kutoona, alipelekwa chumbani kwa Jane mtoto wa kike pekee wa familia ya ASP Lutonja. Hakuwa akijua muundo wa vyumba ndani ya nyumba hiyo ulivyo yeye alipandishwa kitandani na kulala moja kwa moja katika kitanda kisicho chake, kutokana na kulala vibaya kwa Jane pia ambaye alikuw akichipukia yule Msaidizi wa kazi alitoa nguo zote na kisha akamvizia James akiwa tayari ameshalala kumtoa nguo pia. James alilala akijina yu huru kitandani alipozeoa kulala pasipo kujua mpango uliokuwa umesukwa, usingizi wake ulikuja kukatika baada ya kusikia kitu chenye ugumu kikitua kwenye mwili wake. Alipatwa na maumivu makali lakini hakuwa na wa kumsikiliza, bado aliendelea kushushiwa kipigo tu. Ugumu wa kitu ambacho kilikuwa kikitua mwilini mwake kwa nguvu, hakujua ulikuwa ni mkanda wa kijeshi ambao ulikuwa umeshikiliwa na ASP Lutonja.
"Mamaaaa!" Alilia kwa uchungu sana
"Baradhuri wewe umfuate huko kaburini kukuzaa kiumbe chenye laana kama wewe, yaani kukusaidia kote unadiriki kuja kumlala mwanangu wewe mtoto" Ilikuwa ni sauti ya Mke ASP Lutonja ikiambatana na kipigo alichokuwa kikishusha mume wake.
Masikini ya Mungu James hakuwa akiona na wala hakujua ni wapi akimbilie alipokuwa amekaa hapo kitandani, alipojaribu kusogea pembeni kutokana na kuumizwa sana na mkanda huo. Loh! Alianguka chini kama mzigo kutoka kwenye kitanda, huko kulimfanya apigwe kama mtu mzima na kuongezewa mateke, ASP Lutonja alimpiga bila hata ya kujali kuwa nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa hila aliyokuwa amempakazia
Nani ambaye angekuwa ni mtetezi kwenye siku hiyo ngumu ilihali wale waliokuwa wakiujua ukweli walikuwa wakitaka kumuona akiendelea kupata tabu, hakuna na msaada katika hali hiyo ya upofu ambao alikuwa nao. Kilio tu ndiyo ulikuwa msaada wake hakujua ni wapi pa kukimbilia, pande zote zilikuwa ni giza kwake na hakuona pa kwenda zaidi ya kulala chini hapo alipokuwa amelala bila ya kuwa na nguo huku akiendelea kupigwa kwa nguvu . Mkanda mgumu ambao alikuwa akipigwa nao ulianza kuleta athari kwenye mwili wake, haikupita muda alianza kusikia maumivu zadi kutokana na kuchanika sehemu mbalimbali za mwili wake. Bado ASP Lutonja hakuonesha dalili ya kusitisha kumpiga, alipokuwa akisogea uapnde ambao mkanda ulikuwa haufiki basi alionja teka la nguvu. Kipigo kizito cha mtu mzima kilidumu kwa muda mrefu na hakikuonekana dalili ya kutulia.
Baada ya muda mrefu wa maumivu ya sehemu mbalimbali za mwili wake, hatimaye James alipoteza fahamu akiwa bado anaendelea kupigwa. Aliendelea kupigwa hadi pale alipogeuka kama guni katikati ya kipigo ndipo mpigaji akajua kuwa alikuwa amesababisha mengine.
"Mungu wangu Baba jane hujaua kweli mtoto wa watu huyu?" Mke wa ASP Lutonja aliuliza kwa wasiwasi mkubwa, alipelekea mumewe asogee hadi karibu ya James na kumchunguza.
"Kazimia huyu mke wangu, hebu leteni nguo zake" ASP Lutonja alitoa amri baada ya kuto uhibitisho wa hali ya James.
Haraka sana nguo hizo zililetwa kwani zilikuwa zipo humohumo ndani, alimvalisha nguo hizo na kisha alichukua fimbo ambayo James alizoeleka kuitumia katika upofu wake. Alimnyanyua na hakutaka kabisa kusikiliza neno la mwingine, alipomuweka begani vizuri alimtazama mke wake.
Naenda kumtupa jalalani akiamka ajikute hukohuko, hatuwezi kukaa na mtoto firauni kama huyo" Aliongea na hakukuwa na mtu yeyote aliyepinga suala lile.
Alitoka naye hadi nje lilipo gari lake na kisha akamuweka sehemu ya mizigo, aliliondoa gari hilo kwa kasi sana akikata mitaa mbalimbali. Safari yake ilikuja kuishia kwenye eneo la kutupa uchafu ambayo lilikuwa lipo mbali kidogo na makazi ya watu, hapo alifungua sehemu ya kuwekea mizigo ya gari lake na akamtoa James halafu akamtupa kwenye eneo lenye uchafu mwingi sana. Alipohakikisha hakuwa ameonekana na mtu yeyote aliingia garini na kupotea kwenye eneo hilo, moyoni alishukuru sana kwa kuodokewa na kiumbe ambacho hakuwa akikitaka kukiona katika maisha yake. Aliona atakuwa huru sana na si kila siku kutazama sura ambayo alihisi ilikuwa imemgundua kuwa yeye ndiyo Mhusika mkuu wa mauaji, sasa aliona mke wake atakuwa ametulia na kuacha na tabia yake kukazania watoto ambao hawakuwazaa.
James alipokuja kuzinduka bado alijikuta akiwa yupo jalalani akiwa na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, aliijua kwa tabu aa kajaribu kupiga hatua kuelekea mahali ambapo hakuwa akipajua. Loh sallaleh! Upande ule ambao alikuwa akielekea kulikuwa na mteremko mkali sana ambao ulikuwa umejaa uchafu mwingi,kutokana na kutoona alijikuta akiporomoka huko yeye na fimbo yake. Alibiringita kwenye kifusi cha uchafu huku akilia kwa uchungu akitaja majina ya wazazi wake, alikuja kutua kwenye kitu kigumu sana ambacho hakukielewa kilikuwa ni nini. Maumivu yalimpta zaidi na kitu hicho kigumu alichokuwa ameangukia kilimpigiza karuka juu na katua upande wa pili akaendela kubiringita, hakuwa akiona alikuwa akielekea wapi ndani ya rundo hilo la uchafu zaidi ya kuvaana na kila aina uchafu ambao ulimbadilisha harufu na kunukia harufu inayotoka hapo.
Kubiringita huko hatimaye alikuja kuingia sehemu ambayo ailikuwa ina maji, alihisi kupelekewa na maji hayo yaliyokuwa na nguvu. Alipojaribu kujizuia hakuweza na hata ile fimbo aliyokuwa nao ilimtoka mkononi, alipiga kelele sana alipokuwa akipelekwa na maji hayo kwa nguvu lakini hakukuwa na aliyekuwa akimsikiliza. Ilikuwa ni kipindi ambacho mito ilikuwa imejaa kutokana na mvua zilizoanza kunyesha mikoani, ndiyo maana maji hayo yalikuwa na nguvu sana kutokana na kuwa mengi kupita kiasi. Alikuja kupelekekwa na maji hovyo na hatimaye alikuja kujigonga kwenye kitu kigumu kichwani, fahamu zilimtoka baada ya kujigonga kwenye hapo huku akianza kusikia kelele kwa mbali za watu.
****
Harakati za kumfuatilia James akiwa yupo nyumbani kwa mkuu ndiyo ziliendelea, alipopata uhakika alikuwa akipendwa sana na familia hiyo na alikuwa akionekana kama mmoja wa familia ile. Inspekta Mwambe aliamua kuacha kumfuatilia kwani aliona alikuwa yupo kwenye mikono salama, mara chache alizokuwa akikutana nao mjini wakiwa wapo pamoja naye na wakifurahia naye. Zilitosha kumpa uhakika alikuwa yupo mahali salama, kunawiri kwa James nako kulizidi kumdanganya akaaacha hata kumfuatilia. Muda alioacha kumfuatili ndiyo muda ambao Jmaes alikuwa akikaribia kukumbwa na dhahama, alipokuja kukumbwa na dhahama hakujua kabisa hadi pale alipokuja kusikia kwa majirani kuhusu kufukuzwa kwake.
Sababu ya kutaka kumuingilia binti wa pekee wa familia bado ilikuwa haingii akilini kake kutokana na hali aliyokuwa nayo, James huyu ambaye hata chooni alikuwa akipelekwa ni jambo ambalo haliingii akilini mwake kabisa. Siku hiyohiyo alianza kumtafuta asijue alikuwa ameenda wapi kutokana na wingi wa watu ndani ya jiji hili,, alihangika sana katika kumtafuta lakini hakupata hata fununu juu ya mahali ambapo James alikuwepo. Majukumu ya kazi ya siku nzima nayo yalimfanya hata azidi kupata tabu katika kuutmia muda wake vizuri, alipotoka kazini napo mazi ilikuwa ni hiyohiyo ya kumtafuta lakini hadi giza linaingia hakuwa amefanikiwa.
****
James alikuja kurejewa na fahamu zake kwa kuhisi ugumu uliokuwa umeukumba mgongo wake kutokana na sehemu aliyokuwa amelala, alipoinua kichwa chake na akajaribu kufungua macho yake huenda atabapata bahati ya kuona. Alikutana na giza zito kuashiria kuwa alikuwa bado yu katika upofu, akiwa katika hali hiyo alisikia sauti ya Mwanamama akiimba nyimbo zaa kikabila akiwa yupo umbali fupi kutoka hapo alipo. Kusikia sauti hiyo ngeni kulimfanya ahisi hakuwa kwenye mazingira salama, aliinuka kwa haraka sana lakini aliwahiwa kukamatwa kisha alisikia sauti ya Mzee ambayo ilimmshawishi kukaa chini. Alipokaa chini taratibu alianza kupapasa akiwa ni mwenye kutafuta kitu, hali hiyo iliwafanya wenyeji wake ambao walikuwa wnamtazama wasikitike. Walikuwa wameshajua kuwa huyo mtoto alikuwa ni kipofu, Mzee huyo kabisa ndiyo aliiingiwa na moyo wa huruma huku akimtazama jinsi alivyokuwa akihangika.
"Unatafuta nini?" Aliulizwa
"Fimbo yangu ipo wapi? Nitatembea vipi?" Aliuliza maswali mfululizo
"Mbona hukuwa na fimbo kabisa mwanangu" Mzee alimuambiwa
"Kwanza mbona siwajui nyinyi kina nani?"
"Sisi ni wasamriawema tu, tumekuokota hapo bondeni Darajani ulipelekwwa na maji ukajigonga kwenye ukingo wa daraja" Maneno hayo yalimfanya James aanze kulia baada ya kumbukumbu kumrudia
"Hapana usilie kwani kuna nini kimetokea"
"Sijui nimekosa nini jamani? Baba na Mama mnaniacha, nateseka hadi nasingiziwa kubaka. Kipofu kama mimi nitaanzaje wakati hata sioni hata kitu"
"Kijana umepatwa na nini?" Alipoulizwa swlai hilo ndiyo alipoanza kusimulia kila kitu juu ya kilichomtokea hadi inafika siku hiyo, Mzee huyo kila kitu kuhusu familia ya James alikikumbuka na hata sura ya kijana huyo ikamjia kwa mara ya mwsiho kumuona kwenye magazeti.
"Mungu wangu kumbe wewe ndiyo mtoto wa Nkongo yule aliyeuawa" Mwanamama aliyekuwa akipika alipayuka kwa nguvu.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa James kukaa na wazee hao kwenye nyumba yao iliyochoka, alilelelwa kama mtoto wa hapo akiwa mwenye kupewa upendo. Alijihisi amani moyoni mwake ingawa hakuwa kwenye mazingira yaliyokuwa mazuri. Alikuwa ni mwenye kufuatana na Mwanamama ambaye alitokea kuwa mlezi wake mkubwa kwenye shughuli mbalimbali, alimpenda Mmwanamama huyo kama mama yake kutokana na jinsi alivyokuwa akimpenda. Chakula alicholishwa na mikono ya Mwanamama huyo ingawa hakikuwa kizuri kwake aliona ni chenye kufaa kuliko kula kile kizuri kwenye mazingira hatarishi. Adabu aliyokuwa nayo taratibu alianza kupendwa na watu mbalimbali, uzuri wa sura ambao ulikuwa umepotea kutokana na wingi wa makovu nao ulirudi na kumfanya aonekane kijana mwenye kuvutia. Kipindi hicho alikuwa tayari ameshapevuka na akawa ni mwenye mvuto zaidi, upofu wake ukawa si sababu ya yeye kuanza kuvutia wasichana wa huko Uswahilini alipokuwa akielelewa. Pamoja na hyo yule Mwanamama bado alikuwa yu imara kumlinda, alimpenda kama mwanae.
****
Mwangaza katika maisha ya James ulianza kuonekana kwa hatua ndogo kabisa, kufikia hatua ya kuwa mwenye kujihisi na amani ndiyo ulikuwa hatua ya awali ya mwangaza kwenye maisha ya James. Hatua ya pili ilikuja kuonekana ilikuwa ni baada ya majuma kadhaa, siku akiwa yupo pamoja na Yule mwanamama kwenye biashara yake pikipiki aina ya boxer iliegeshwa kando. Alishuka mtu mzima ambaye alisogea hadi kwenye kibanda cha matunda iliyokuwa ni biashara yao, alikuwa ni mnadhifu ambaye alionekana kabisa alikuwa na nia ya dhati ya kununua matunda.
"Matikiti bei gani? Haaaah! James?" Aliuliza huyo mtu kuhusu matikiti maji lakini alishtuliwa na kumuona James.
"We nani?" James aliuliza aliposikia jina lake likiitwa.
"Anko Mwambe mimi" Aliongea mtu huyo ambaye hakuwa mwingine ila ni Inspekta Mwambe.
"Baba Mwambe" James alimtamka kisha akasimama akiwa na lengo la kumkimbilia Inspekta Mwambe asijue ni wapi alipo.
"James tulia kwanza utaumia, Anko hivi huyu unafahamiana naye kivipi? Mwanamama yule aliuliza huku akimshika James mkono.
Ilibidi Inspekta Mwambe aeleze na kisha james naye akaeleza, hapo ndipo aliporuhusiwa kwenda kwake. Baada ya hapo Yule Mwanamam alifunga kibanda chake na kisha aliongozana na Inspekta Mwambe hadi nyumbani anapoishi, huko walikutana na mume wake ambaye walimueleza kila kitu. Ilikuwa ni katika siku ambayo walikuwa wakikubali kutenganishwa na James waliyekuwa wamemzoea lakini hawakutaka kumuacha kirahisi, walihitajia kujua kuhusu usalama wake kutokana na mazingira aliyopelekwa akateseka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni zamu ya Inspetka Mwambe kuwaelewa uhakika wa usalama wake, katika muda huu ndipo alipotumia wasaa kumueleza kuwa nyumba yao waliyokuwa wakiishi tayari imeuzwa na watu wasiojulikana huku tuhuma nyingi zikienda kwenye familia ya mama yake mzazi, aliwaleza pia uwepo wa nyumba moja ambayo ilikuwa imebakia. Hii ilikuwa ni ile nyumba ya kule shamba ambayo Marehemu SSP Nkongo alikuwa akiitumia kupanga mikakati yake. Hapo wote walikuja kubaini kuwa baba yake kabla hajafikwa na umauti akiwa njiani kuufuta huo umauti, alikuwa tayari maeshampa taarifa ya uwepo wa nyumba ile kitahadahari. Yeye ndiye aliyeaminiwa akaambiwa kukitokea la kutokea basi ushahidi upo kule na funguo ya kule alielekezwa mahali ilipo. Inspekta Mwambe alitumia wasaa nuo kuwaeleza ile ndiyo nyumba pekee iliyobaki na haijulikani na yeyote.
Pamoja na maelezo hayo bado hawakutaka kumuachia James kirahisi nmna hiyo, iliwabidi waongozane hadi huko shamba kwenda kuishuhudia nyumba hiyo. Huko walifika na kuiona nyummba hiyo ya kisasa ambayo ilikuwa imesalimika. Hapo waliridhia kumuachia James lakini walipewa ombi. Waliombwa wamtunze hapohapo watalipwa chochote na humo watakuwa wanaishi, hilo ombi lilipita. Kuanzia siku hiyo wakaanza kuishi ndani ya nyumba hiyo yenye kila kitu wakimtunza James, uswahilinmi walipasahau kabisa na hapo ndiyo yakawa makazi yao.
Majuma kadhaa baadaye tatizo lile la kutoona iliwabidi kwenda kwa Daktari, gharama zote zilisimamiwa na Inspekta Mwambe. uchunguzi wa kitabibu ulionesha tatizo hilo lilikuwa likibika kabisa na huo ndiyo ukawa mwanzo wa furaha kwanza, miezi kadhaaa mbele James alitibiwa tatizo lake la kuona. Alifurahi sana kurudi kwenye ulimwengo waliokuwa wakiona kwa mara ya pili, malezi yote aliyokuwa akipewa na wale waliomuokota yalikuwa yamefikia tamati lakini hakuruhusu waondoke na hao aliwaheshimu kama wazazi wake wa hiyari.
Inspekta Mwambe alikuwa akija kuwaona kila siku akiwa na nguo za kiraia na walikuwa wakikaa naye kwa furaha sana, siku moja aliamua kuja na nguo zake za kazi na ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kuvaa nguo hizo James akiwa yu anaona. Siku hiyo maelewano hayakuwepo kabisa. Ulizuka mtafaruku isieleweke chanzo kilikuwa ni nini, hawakuelewana kabisa na hadi alipooondoka. Alipokuja siku inayofuata akiwa na nguo za kraia walielewana vizuri tu na hakukuwa na mkwaruzano. Hili ilimfanya aanze kumchunguza kwa ukaribu ilitokana na nini, alipogundua chanzo ilikuwa ni vazi lake ilibidi apelekwe kwa mataalamu wa Saikolojia ndipo hapo walipobaini kuwa alikuwa akikumbuka tukio la kuuawa kwa wazazi wake na kaka yake.
Tiba ya ushauri kutoka kwa mtaalam huyo wa Saikolojia aliipata na hatimaye alirudi kwenye hali ya kawaida ambayo ilisaidia hata asiwe na hasira kila anapoiona nguo ya kazi ya Mlezi wake mkuu. furaha iliendelea huku ASP Lutonja akiwa hajui lolote kwa mtoto wa mwenzake ambaye alikuwa amemfanyia hila akampiga na kumfukuza kwake. Mwaka uliofuata James alianzishwa kidato cha kwanza katika shule ya bweni , ilikuwa ni furaha kwake kwa kurudi kwenye mazinmgira ya kielimu tangu alipoikacha shue akiwa darasa la saba. Aliendekeza nguvu zake katika usomaji na alikuwa ni mwenye bidii huku akikumbuka kuwa alikuwa akihitajika kuyajenga maisha yake mwenyewe, tabia ya baba yake ya ucheshi ambayo alikuwa ameirithi ndiyo illirudi akiwa yupo ndani ya shule.
Ucheshi wake huo ulimfanya kutokea kuwa kipenzi cha watu ndani ya shue hiyo, si wasichana wala wavulana ndani ya shule wote walikuwa wakipenda kukaa karibu naye kutokana na ucheshi aliyokuwa nao. Moyo wake wa kusaidia mwanafunzi mwenzake yeyote atakayepatwa na matatizo nao ulimfanya azidi kupendwa, shule nzima jina lake ilikuwa midomoni mwa watu akiwa tu kidato cha kwanza. Upande wa walimu napo alitokea kujizolea umaarufu mkubwa sana akawa akipendwa na kila mwalimu, utiifu wake ndiyo ilikuwa chanzo cha kupendwa na walimu hao ndani ya shule aliyokuwa akisoma. Mwaka unaofuata wa kidato cha pili ulikuwa ni mwaka ambao ulitosha kabisa kushawishi walimua na hawa wanafunzi kumpatia uongozi James, uchaguzi mkuu wa serikali ya wanafunzi ndani ya shule hiyo ulipofanyia. Alipata uongozi wa kawaida na hapo ndipo alipozidi kujizolea umaarufu, bado hakuacha bidii yake ya masomo pamoja na umaarufu huo aliokuaw aamejizolea shuleni.
Alikuwa amebeba sifa ambazo alikuwa nazo marehemu baba yake kipindi akiwa shule, ubond ndiyo kitu pekee ambacho hakuwa amebeba kwenye sifa alizokuwa nazo baba yake. Jina la James lilikuwa ni mithili ya mate kwenye vinywa vya wanafunzi kwa jinsi lilivyokuwa limekaa kwenye vinywa vyao, pamoja na kuwa ni mwenye madaraka makubwa sana ndani ya shule aliyokuwa akisoma. Bado hakuwa mtu mwenye kujikweza sana, alijona yu mwanafunzi kama wanafunzi wengine. Mwaka wa pili uliisha akiwa ni mwenye sifa kedekede ndani ya shule yao, ulipoingia mwaka wa tatu akiwa yu kidato cha tatu uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ulifanyika kwa mara nyingine tena. Shinikizo kubwa la wanafunzi ndani ya shule hiyo lilimfanya aweze kugombea nafasi ya uongozi kwa mara nyingine, safari hii alitaka kuchukua nafasi ileile lakini shinikizo la watu lilipelekea agombee rais wa serikali ya wanafunzi.
Hakuwa na mpinzani hata kwenye nafasi hiyo na hatimaye alipita bila upinzani mubwa, akawa ni rais wa kwanza wa wanafunzi kutoke kwenye shule hiyo akiwa yu ngazi ya kawaida(o-level). Ilizoeleka wanafunzi wa shule hiyo wenye nafasi hiyo walikuwa wakitoka kwenye daraja za juu kielimu(o-level), hakika yeye ndiye aliyevunja rekodi hata kwenye uongozi wake kwa kuweza kuwaongoza wale waliokuwa wapo daraja za juu kielimu na hata daraja moja naye bila kupindisha chochote. Demokrasi ndiyo ilikuwa imetawala katika uongozi wake, ndiyo maana alikuwa ni kiepnzi cha watu sana. Hakwenda kinyume na miiko ya uongozi wake na alikuwa ni msikivu sana wa wanafunzi wengine, sifa zake zilikuwa ni zilezile ambazo zilikuwa zimempa jina kbwa katika shule hiyo.
Suala la wasichana lilikuwa ni urafiki wake wa kawaida kutokana na malengo aliyokuwa amejiwekea, alikuwa ni mwenye kuongoza kwenye masomo mbalimbali darasani hivyo hakutaka ashuke kidaraja kutokana na kuendekeza wasichana. Wapo wengi sana waliokuwa wakimpenda lakini hakulegeza msimamo wake, hata wasichana wengine walipokataliwa na kumzushia kutokuwa sawa kimwili bado hakuweza kuharibikiwa na heshima yake. Yote kutokana na kuwa kipenzi cha watu, yeyote ambaye angezusha uzushi kwake basi alikuwa na aibu ambayo ilikuwa ikimkumba yeye na hata kujitia matatizo. Bado aliendelea kuwavutia wengine wengi na hata waliokuwa wamemzidi vidato lakini waliishia kapa, miezi nayo ikakatika hatimaye mwaka huo ukaisha ukaingia mwaka mwingine.
Likizo ya mwisho wa mwaka ilipoisha mwaka mwingine ulifuata katika kipindi cha mwaka wa mwisho wa elimu ya daraja la kawaida, mwake huo nao alikuwa akiishi kwa misingi aliyokuwa amejiwekea hapo shule na hadi akahitimu kidato cha nne katika shule hiyo. Baada ya kuhitimu maisha ya nyumbani ndiyo yalifuata na akawa ni mwingi wa kukaa ndani sana, hakuwa mtu mwenye marafiki kutokana na kupoteza muda mwingi akiwa shule. Pia uwepo wa nyumba aliyokuwa akiishi eno la shamba, ulifanya awe na urafiki mkubwa na Mwambe ambaye alikuwa ni na cheo cha ASP(Mrakibu msaidizi). Yeye ndiye alikuwa akija kutoka naye na kutembea naye katika sehemu mbalimbali za katikati ya jiji zenye kuvutia, huyo ndiye aliyekuwa rafiki yake mkuwa sana.
Alipokosekana alikuwa ni mwenye kutoka na kwenda mwenyewe mjini katika sehemu ya kutuliza mawazo, alirejea nyumbani akiwa ametuliza akili yake vya kutosha huko mjini na alijumuika na wazazi wake wa hiyari ambao walikuwa wamekuwa na mionekano ya wenye nazo na si namna ile ambayo walikuwa wakiishi uswahilini. Miezi ilisogea na hatimaye matokeo ya kidato cha nne yakatoka akwa ni aliyefaulu kwa daraja la kwanza, muda wa kujiunga na kidato cha tano hakutaka kurudi tena kwenye shule ile bali alijiunga na shule ya sekondari ya Tambaza na akawa anakaa katikati ya jiji. Alisoma kwa miaka miwili na hatimaye alihitmu na alipangiwa kujiunga na jesi la kujenga taifa kambi ya Mgambo Kabuku jijini Tanga.
Huko ndipo alipoenda kukutana na Wilfred ambaye alikuja kuwa rafiki yake mkubwa, tabia ileile aliyokuwa nayo ndiyo ilimfanya we kipenzi cha watu ndani ya kambi hiyo. Si afande wala kuruti ambaye hakuwa akipenda kuwa naye. Kipindi hicho tayari alikuwa akijua kila kitu kuhusu Philipo Lutonja ambaye alikuwa ni Mrakibu mwandamizi wa jeshi la magereza(SSP), uchunguzi uliofanywa na ASP Mwambe kuhusu kifo cha baba yake alikuja kubaini kuwa huyo ndiye alikuwa mhusika mkuu wa mauaji ya wazazi wake. Hakuwa na la kufanya tena zaidi ya kuliacha suala hilo kama lilivyo, upana wa mtandao ambao ulikuwa ukihusika na kila kitu ulimfanya abaki na kidonda moyo lakini si kutafuta tiba.
Ndani ya kambi hiyo ndipo alipokuja kumuona msichna ambaye alikuwa akimfananisha hakujua alikuwa kamuona wapi, alidhani alikuwa tu kamfananisha na mtu. Hivyo aliacha kabisa kufuatilia suala hilo la kutaka kumjua kindani, aliendelea na mafunzo yake ya miezi mitatu ndani ya kambini. Uhalisi wa msichana huyo alikuja kuujua siku ambayo alijitaja mwenyewe bila kuulizwa lolote, hakika alikuwa ni Jane Philipo Lutonja. Msichana ambaye aliambiwa alimuingilia chumbani katika kipindi ambacho alikuwa yupo kwenye ulimwengo wa vipofu, siku hiyo ndiyo alijeruhiwa na mtu ambaye anamtaja hapo na kisha kutupwa Jalalani. Ubaya aliofanyiwa na familia hiyo ndiyo ulirudi kwenye kichwa chake, aliwahi kudhalilika kiasi cha kupigwa hana nguo mbele yake akiwa yupo ndani ya nyumba yao. Hakutaka kukaa eneo hilo alipokumbuka hayo, aliona alikuwa hahitajiki kabisa kuongea na mtoto muuaji ambaye alimuweka yatima.
Alienda kukaa huko eneo tulivu akiwa analia ndipo Wilfred akamfuata na kuamua kumsimulia kila kitu kuhusu maisha yake, siri ambayo hakuwahi kumsimulia yeyote yule zaidi ya watu wake wa karibu.
"Dah! Pole sana aisee, inamaana yule demu ndiyo chanzo cha kutekeseka kwako" Wilfred alimuambia
"Ndiyo Wil yani bila yule na baba yake sasa hivi ningekuwa nipo wazazi wangu wote na nisingekuwa nimepitia magumu niliyopitia" Alijibu
"Pole sana mtu wangu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yaani mwanangu inauma sana hivi kipofu kubaka ataweza wapi, ikiwa kuona penyewe haoni"
"Man mpotezee kama vipi na kaa mbali naye"
"Yaani mana nitaanza kumpotezea lakini najua ni suala gumu sana kutokana na yeye kunifuata kila muda"
"Si unajua kanasa kwako tayari ndiyo yupo hivyo, ila mwanangu kupitia hali fulani ya maisha kuna sababu zake. Hata haya yanayotokea ukiwa hapa kambini yasingetokea ikiwa hiko kipindi ulichopitia hukukipita, ona ni sehemu ya maisha tu"
"Najua hilo Wil ila ngumu sana, hebu fikiri wewe kusikia kilio cha wazazi wako kipindi wanakufa tena mama yako abakwe ndiyo afe. Halafu mtu mwenyewe ni huyo ambaye anakuweka kwake na kukutesa"
"Naelewa mtu wangu hebu chukulia kama halijatoke ukabiliane na wakati wako wa kimaisha uliobakia duniani"
"Poa mtu wangu, wewe ni zaidi ya ndugu"
"Hamna noma twendo kombania sasa hivi si unasikia filimbi hiyo, maafande wamerudi kwenye kikao"
Wote walinyanyuka na kwenda kukaa kwenye kombania yao katika kukaa mstari maarufu kama kufoleni, kutokana na kutotimia kwenye foleni hiyo walikumbana na adhabu ya kukunja ngumi chini. Walikaa namna hiyo hadi walipotimia wote ndiyo utaratibu mwingine ukafuata wakiwa hapo kwenye Kombania, saa nne kamili waliruhusiwa kwenda kulala kujiandaa na siku mpya. Uchovu wa siku nzima walilala usingizi mzito, saa kumi na moja alfajiri walikuja kuamshwa wote ulikuwa ni muda wa kujiandaa kwenda shamba. Mujibu wa ratibu ilikuwa ni kupanga mistari na kuhesabiwa idadi na ilipotimu saa kumi na mbili wote walielekea shambani, njia ya kuelekea shambani wengi walikuwa wakitembea sambamba na James kutokana na kuzoea vituko ambavyo alikuwa navyo. Siku hii ilikuwa ni afadhali kidogo kutokana na kutokuwa na watu wa kombania nyingine wakiwa wapo njiani. Hii ilimuwezesha kutoiona sura ya Jane hadi wanaingia shamba na kufanya kazi ambazo zilikuwa zimewaweka huko, majira ya saa nne walipokuwa wakinywa chai ndipo alipomuona na alipotaka kumfuata Wilfred alimuwahi na kusoge naye pembeni. Aliongea kwa muda mfupi na kisha alirudi pale alipo James, aliketi na aliendelea akunywa chai akiwa yupo kimya.
"Vipi umemuambiaje naona kageuza kaondoka?" Alimuuliza
"Mtu wangu unafikiri kuna kumficha tena yule, nimemuambia hutaki kukaa karibu naye tu kasepa" Wilfred aliongea
"Safi sana aisee, tumalizie turudi tukapige kazi"
Waliendelea kunywa chai ambayo ilikuwa ikiwapa nguvu ya kuingia shambani kwa mara ya pili, walipomaliza tu kunywa walisogea kando kwani muda ulikuwa bado na waliamua kuongea mambo yao mengine yaliyokuwa yakiwahusu wao. Hawakujalia kabisa Jane alikuwa ameumia namna gani kwa maneno ambayo alikuwa ameambiwa na Wilfred, ilikuwa ni kawaida tu kwa James kutokana na jinsi alivyokuwa akimchukia Jane.
****
Upande wa Jane ilikuwa ni maumivu makubwa kuambiwa maaneno yale na Wilfred, aliona kama alikuwa akiambiwa uongo lakini alipomtazama Mhusika alikuwa hana habari naye ndiyo hapo akajua kama ilikuwa ni ukweli. Moyo wake tayari ulikuwa umeshapenda kwa kijana huyo, hakuwa akijua kuwa kijana huyo ndiye yule ambaye alikuwa akiishi ndani ya nyumba yao miaka mingi iliyopita. Wala hakujali kuwa siku ambayo hakuwa ameingiliwa ila kutokana na ukali wa baba yake ilibidi tu akae kimya tu kulifanya suala hilo lionekane kweli, alipelekea mtu ambaye likuwa ameunasa moyo wake ndiyo ateseke akiwa kwenye hali ya upofu na hatimaye kwenda kutupwa jalalani.
Laiti angeliyajua hayo wala asingejileta karibu yake katika muda huo ambao alikuwa akichukiwa, aliona ni mwenye kuonewa na muda huo akiwa ameshika kikombe chake cha chai baada ya kumaliza kunywa chai. Machozi yalikuwa yakimlanga na hata marafiki zake wa karibu walipooona hali hiyo ilibadi wamuulize, hakutaka kuwaficha aliwaeleza kila kitu hadi wenyewe wakashangaa kabisa kwani haikuwahi kutokea hiyo. Kutokana na urafiki aliokuwa amejengeana nao akiwa yupo humo ndani ya kambi, aliwaomba wamsaidie nao walikubali ombi hilo.
Muda wa kurudi kambini ulipowadia wote kwa pamoja walirudi wakiwa makundi tofauti, muda huu ndiyo rafiki yake mmoja wa karibu alipotumia wasaa wa kuongea na James na kumueleza kuhusuhali hali halisi aliyo nayo rafiki yake. Alitumia kila aina ya ushawishi ya kuweza kumfanya James akubali kuongea naye lakini ilishindikana, walipozidi kumuambia hivyo neno la mwisho ambalo lilitoka kinywani mwa James ndiyo lilimfanya akose la kuongea.
"Namchukia!" James alitamka neno hulo akimuacha msichana huyo akiwa ameingiwa na mshangao, hakuujali mshangao huo yeye alikaza mwendo na kumfuata Wilfred ambaye alikuwa ametanguliwa mbele.
****
Siku zilisogea wakiwa wapo ndani ya kambi na Jane alibaki akiumia mwenyewe ndani ya moyo wake, muda kujiandaa na gwaride la mwisho hatimaye ulifika. Kipindi hicho ndipo Jane liweza kupitisha siku pasipo kumuona James kutokana na yeye kutokuwepo kwenye mazeozi ya gwaride, alikuwa akifanya kazi bustanini katika muda wote wa asubuhi hadi mchana. Aliweza kumuona kwa mbali akiwa na kundi la watu wakiongea na kufurahia mambo mbalimbali, lakini hakuweza kutia mguu na kusogea karibu yake kuongea naye kwa jinsi alivyokuwa na hofu naye. Aliedelea kuvumilia hali hiyo akiwa hapo kambini kuhofia kumkera James na hatimaye yakafika kwa wakubwa wa kambi. Sheria ya kambi ilikuwa ikikataza kuwa na mahusiano laiti ikujulikana hatua kali zinachukuliwa, hilo aliogopa sana kuweza kujiharibia na hatimaye kukosa cheti chake na kupoteza tu muda wa kuwa hapo kambini kisa mapenzi.
Siku ya kuhitimu mafunzo kwenye mahafali hayo ndiyo ilikuwa siku ambayo wote walitembelewa na wazazi wao, siku hii SSP Lutonja pia alikuwa yupo ndani ya kambi hii akiangalia jinsi vijana walivyokuwa wakipiga gwaride. Siku hiyo James ndiye liyekuwa kiongozi wa gadi zote zilizopo uwanjani na alitendea haki nafasi aliyokuwa amepewa, alikuwa kivutia kikubwa sana kwa wahudhuriaji wa shereha hiyo. Gwaride lilipoisha pamoja na taratibu zingine za kawaida, ulifuata muda wa kujikusanya pamoja na wazazi na wageni mbalimbali. Muda huu ndipo James alipopokea pongezi kutoka kwa wazazi mbalimbali kutokana na uwezo ambao alikuwa ameuonesha, SSP Lutonja naye alijikuta akimpongeza huku akiwa hamtambui kabisa kuwa huyo ndiye alikuwa ameharibu maisha yake katika kipindi cha miaka kdhaa nyuma. James aliupokea mkono huo wa pongezi lakini ana hasira kubwa sana moyoni mwake, alipoombwa kujumuika na familia hiyo iliyomuharibia maisha yake. Aligoma na kutoa udhuru wa uongo ili asikae nayo karibu tu na kisha alienda kwa wazazi wake wa hiyari ambao walikuja kumtebelea baada ya kumaliza mafunzo.
Siku liyofuata baada ya mafunzo kila Mhitimu alikabdhiwa cheti chake pamoja na posho yake, baada ya hapo wote waliruhusiwa kuondoka wakitumia magari mbalimbali ambayo yalikuwa aymekuja kukaa nje ya kambi hiyo. Kila mmoja alipanda gari ambalo lilikuwa likimfikicha huko alipokuwa akiishi, siku hiyo ndiyo siku ambayo moyo wa Jane ulimuuma kwa kuondoka ndani ya kambi hiyo liliyokuwa ni eneo rahisi sana kuonana na mwanaume aliyekuwa akimpenda.
Muda wa kukaa nyumbani kusubiria majina ya kujiunga na chuo ndiyo ulifuata kwa James yeye alieendelea kufurahia kukaa akiwa na familia yake na akimtembelea Mtu muhimu katika amsiha yake ASP Mwambe. Tayari muda huo hakuwa akimuita anko kama ilivyokuwa zamani, alibadili jina kabisa na kumuita baba kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye maisha yake. Alikuwa akimuheshimu kama baba yake na hata mke wake alikuwa akimuita mama yake, ASP Mwambe alikuwa na mtoto wa kike ambaye alimuona kama dada yake lakini maono hayo yalikuja kubadilika hapo awali kutokana mazoea yaliyokuwa yamejengeka baina yao. Binti huyu alikuwa akiitwa Sara, katika mazoea yaliyokuwa yapo baina yao wote wawili walijikuta wakipendana. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa James kuingia kwenye mapenzi, alifanya mapenzi hayo kwa siri akiwa yupo na binti huyo wa baba yake wa kumlea. Ulikuwa ni uhusiano uliojaa mapenzi ya dhati baina yao wawili, walianza kwa kukutana kwa siri na hatimaye wakajumuika katika sehemu mbalimbali kwa matembezi wakiwa wawili. ASP Mwambe wala hakuona uajabu kwa jinsi walivyokuwa wakitoka pamoja, yeye aliona ni mazoea ya kawaida ambayo walikuwa nayo tangu muda mrefu. Hakujua mazoea hayo tayari yalikuwa yamepiga hatua na kujenga kurasa mwingine baina ya wawili hao, wote wawili walikuwa wakingoja majibu ya chuo ingawa Sara alikuwa ametangulia mwaka mmoja kumaliza kidato cha sita.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment