Simulizi : Askari Jela
Sehemu Ya Nne (4)
Walifuatana kama kumbikumbi waliyokuwa wakitafuta sehemu ya kuanzisha kichuguu kila waendapo, walikuwa wakipendezana kwa jinsi wote walivyokuwa wana mvuto. Kila mmoja alijiona ni mwenye bahati kwa kuweza kumpata mwenzake, jambo hili lilifanya wawe ni wenye furaha muda wote. Hitaji la mioyo yao ndiyo lilisababisha wawe pamoja, haya yalikuwa ni mapenzi ambayo James hatakaa ayasahau kwenye maisha yake kwa jinsi yalivyomfsnya ajione yu kiumbe tofauti. Alizidi kuwa na furaha kutokana uwepo wa mwanamke huyu, hakujiona ni mwenye mapungufu katika maisha yake kila akifikiria alikuwa akipendwa na mwanamke mmoja mrembo miongoni mwa warembo. Mapenzi yao yalishamiri katika kipindi chote walichokuwa wakisubiri majina ya chuo, hata yalipotoka bado yaliendelea kushamiri ingawa walikuwa wamepangiwa vyuo tofauti ndani ya jiji la Dar es salaam.
Umbali hauleti athari yeyote kwenye mapenzi ya kweli na waliokua na malengo makubwa, hii ilijidhihirisha kutokana na kupangiwa vyuo tofauti ndani ya jiji la Dar es salaam. James alipangiwa chuo kikuu cha Dar es salaam huku Sara akipangiwa chuo cha usimamizi wa fedha IFM. Waliendelea kusoma kwa bidii na kila mwisho wa wiki walikuwa pamoja, walitembeleana sehemu mbalimbali za kupumzika wakiwa pamoja kila walipokuwa mapumzikoni. Mawasiliano baina yao nayo hayakufa kabisa kila walipokuwa mbali, haikupita muda wa siku nzima pasipo kuwasiliana zaidi ya mara moja kutokana na kila mmoja alivyokuwa akimjali mwenzake. Hii ndiyo ilikuwa nguzo la penzi lao na kulifanya lidumu, marafiki wa karibu wa kila mmoja ambao walikuwa wakisoma nao walikuwa wakijua kuhusu uhusiano wao. Kila mmoja alimuonesha rafiki yake ni jinsi gani ambavyo alikuwa akijiona ni wa fahari zaidi kuweza kuwa naye kimahusiano, marafiki wa karibu wa kila mmoja walikuwa wakiitambua vyema sura ya shemeji yao ambaye alikuwa akiuchengua moyo wa mwenzao.
Kuonesheana huku picha kulikuja kuibuka kwa athari kubwa kipindi hicho wakiwa wapo mbalimbali, mwanzo wa atahri hizo ulianza katika chuo cha IFM ndani ya kozi ambayo alikuwa akiichukua Sara. Picha hizo zilikuwa zipo kwenye simu ya marafiki zake ziliweza kujulikana na watu wa pembeni ndani ya chuo hicho, wengi walisifia kuweza kumpata mvulana huyo. Wengine walivutika kutokana na utanashati wake, lakini mmoja aliumia alipobaini hilo hata alipoweza kuiona iicha ya wawili wakiwa pamoja kupitia marafiki wale wapendao kusambaza mambo. Utanashati wa James uligeuka mada ndani ya chuo hicho miongoni mwa wanafunzi wa kike waliokuwa wakipenda kufuatilia watu, huku ndipo kulipelekea kumfikia Jane ambaye alikuwa akisoma masomo hayohayo kujua. Usiri wa taarifa hiyo katika kipindi cha wali ulimfanya asiweze mujua chochote kilichokuwa kinaendelea, hakuwa na mazoea na Sara ndiyo maana ilipelekea asijue kinachoendelea kwa muda mrefu hadi pale zilipoanza kusambaa.
Jane kutokana na kuwa ni mtoto wa mzazi ambaye alikuwa na uwezo wa juu kifedha, majigambo na majivuno yalikuwa hayamuishi. Hasa alipoanza kusumbuliwa na wavulana hapo chuoni kuliko wanafunzi wengine, ndiyo akawa anajiona mwenye hadhi ya kipekee kabisa. Hili lilisababisha amdharau Sara na hata iwe ngumu kusalimiana naye, ndiyo maana mwanzoni kabisa aliukosa uhondo wa kufahamu kuhusu hili. Mazoea waliyonayo baadhi ya marafiki zake ndiyo yalifanya ajue kuhusu Mvulana ambaye alikuwa akimpa hadhi ya kipekee Sara, sifa lukuki alizokuwa akimwagiwa juu ya mvulana huyo alitamani kabisa kumuona akiamini alikuwa hana hadhi ya kusifiwa hivyo kutokana na dharau alizonao kwa Msichana mwenzake. Siku alipokuja kuiona picha ya James akiwa pamoja wamekumbatiana na Sara tena ikiwa imepigwa kwa ufundi wa hali ya hali ya juu, ndiyo alipoanza kumchukia zaidi kutokana na kumpenda mwanaume tangu alipomuona katika mafunzo ya JKT. Hakujua alipo huyo mwanaume zaidi ya kujua alipo mpenzi wake, kundi la pamoja la Whatsapp la darasa lao ndiyo lilizidi kabisa kumuumiza kutokana na jinsi ambavyo Sara alikuwa akipenda kumtuma mpenzi akiwa naye karibu katika picha mbalimbali. Alijikuta akiumia sa kila anapopakua picha hizo na kuangalia, macho yake yalipokutana na picha hizo alikuwa kizifuta. Ilipotumwa picha ya James akiwa peke yake ndiyo alikuwa akiipakua na kuitia kwenye simu, moyoni alikuwa amejenga adhma ya kumtafuta James kwa nguvu zote aweze kuonana naye hakujali yale yaliyokuwa yametokea jeshini baina yao.
Alidodosa awezavyo na hatimaye akajua mahali ambapo James alikuwa akisoma, alijiona alikuwa ameanza kupata mwangaza wa kumpata lakini alipofikiri ukubwa wa chuo hicho pamoja na wingi wa wanafunzi. Aliingiwa na ugumu wa kuweza kumpata kutokana na kutojua alikuwa akisoma masomo gani, mtu peke ambaye alikuwa akijua hayo alikuwa ni Sara. Huyu ambaye alikuwa akimdharau kila siku, kumuuliza hilo suala ilikuwa ni ngumu sana kutokana na huyu mhusika tayari alikuwa ameshajenga chuki naye. Hata kama angekuwa hana chuki naye angeanzia wapi kumuuliza, alitambua ni jinsi gani wanawake walivyokuwa wana wivu wakipenda. Alihofia wivu huo ungepelekea hata awe katika matatizo ikiwa suala hlo litafika kwa baba yake, hofu ya kuchafua jina la baba yake ambalo lilikuwa limekua kwa kasi ndiyo ilikuwa ipo ndani ya moyo wake. Mtoto wa mkubwa wa magereza kuingilia penzi la mtu ingekuwa ndiyo habari ambayo ingebeba vichwa vya magazeti mbalimbali, hakuna ambaye hakumtambua kuwa alikuwa ni mtoto wa mkubwa huyo ambaye alikuwa ameshajizolea umaarufu jijini.
Kulinda heshima ya baba yake alikujali sana lakini kutafuta penzi napo hakuacha kupajali, hii ilifanya awe ni mwenda chuo kikuu cha Dar es salaama mara kwa mara. Aliamini ipo siku angeweza kumtia machoni, ukubwa wa chuo pamoja na wingi wa wanafunzi ulimkatisha tamaa hata ashindwe. Hakujua alikuwa akikaa sehemu gani jambo jingine ambalo lilimpa ugumu katika kumfuata, alikuwa ni mwenye tabia ya kuja ndani ya chuo kikuu hicho hata katika kipindi cha kati ya wiki lakini hakufanikiwa kumpata. Aliendelea kuwa na tabia hiyo karibu mwezi lakini mwisho wake alikata tamaa kumuona James kwa njia hiyo, aliona njia iliyobaki ilikuwa ni kuwatumia marafiki wa Sara ambao walikuwa ni watu wake wa karibu. Alijaribu kutumia mbinu hiyo kuweza kupata namba ya simu ya James lakini hilo nalo alishindwa, wivu aliokuwa nao mwenye mpenzi ulikuwa mwingi sana kutokana na sifa ambazo alikuwa amemwagiwa kila walipoiona sura yake. Hilo lilisababisha hata Jane akose namba hiyo kutokana na hofu ya mwenye mali kuporwa, hivyo hakugawa namba kwa watu wengi. Waliokuwa na namba hiyo walikuwa ni marafiki wa ksribu wsara. Ambao aliwadharau kipindi kwa kirefu kutokana na familia aliyokuwa akitokea.
Taratibu alijikuta akianza kumsalimia Sara bila mwenyewe kutaka ili aweze kuwa karibu naye, alikuwa akinyamaziwa mara nyingi sana alini bado hakuchoka kumsalimia. Alipokea dharau kama alivyokuwa akifanya dharau lakini hakukata tamaa, lengo ilikuwa ni kupata mawasiliano ya James hata kukutana naye. Wasichana hao walimtenga nao kutokana na tabia za kike ambazo walikuwa wameumbwa nazo, asili ya baadhi ya wenye jinsi ya kike kuweka visirani katika mioyo yao ndiyo ilisababisha hata ashindwe kukaa karibu nao. Alikata taama na hata akawa ni mwingi wa kuwafuatilia bila ya sababu yeyote, dharau zake ambazo alikuwa akizifanya aliziona hazina maana kabisa. Alijuta kuishi maisha ya kiumaarufu kisa kulewa pesa za baba yake, aliona laiti kama angekuwa na maisha ya kawaida ya kujichanganya na watu kama ilivyokuwa kwa Sara. Angekuwa ameshapata hata namba ya James na kuweza kukutana naye,dhumuni la moyoni mwake la kumpata James kwa namna yeyote ile ndiyo lilifanya hata awe mwenye kufikiria kumpindua mwanamke mwenzake kwa namna yeyote.
****
Maisha ya James ndani ya chuo kikuu Dar es salaam akiwa ni mkazi wa hostel za Mabibo Ubungo Kibangu, yalikuwa na furaha sana kila kukicha. Alikuwa amepata rafiki mpya kabisa ambaye alikuwa akisoma naye chuo hicho, wote walikuwa wakisoma masomo tofauti. Alikuwa ameingia kwenye urafiki na Norbert Kaila mwanafunzi wa chuo kikuu hicho anayechukulia masuala ya uandishi wa habari. Huyo ndiye alikuwa rafiki yake ambaye walikuwa wakipendana, ndiye pia rafiki pekee ambaye alikuwa na maelewano mazuri na mpenzi wake. James alimpenda sana rafiki huyu ambaye alikuwa ni mkware wa wanawake, hakumuhofia kabisa kuweza kumpindua kwa mpenzi kwa kutokana na heshima aliyokuwa akimpa shemeji yake. Matembezi aliyokuwa akiyafanya James basi mpenzi wake au Norbert alikuwa yupo,hakika walipendezana sana kwakuwa wote wawili walikuwa ni watanashati na wenye mvuto.
James alikuwa akiishi na rafiki yake huyo katika chumba kimoja ambapo muda mwingine ilimlazaimu kulala nje, yote ni kutokana na uingizwaji wanawake tofauti na rafiki yake huyo. Hakuwahi kumuambia neno lolote baya kuhusu tabia yake hiyo kutokana na yeye kuwa anapishwa kila akija Sara awe naye. Pamoja na kubadili wasichana namna hiyo James alikuwa akitambua wazi rafiki yake huyo alikuwa na mwanamke ambaye alikuwa masomoni nje ya nchi, mwanamke huyo ndiye ambaye alikuwa akimpenda kwa dhati. Aliishia kuziona picha za mwanamke huyo ambaye aliambiwa anaitwa Norene, aliendelea kuishi naye huku akivumilia kila kitu kuhusu tabia ambaye alikuwa nayo Norbert asiyepitiwa na mwanamke mrembo akakaa bila ya kumfuata. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yao wakiwa wapo chumbani kwao, alikuwa ameshamsahau kabisa Wilfred ambaye alikuwa ameamua kujiunga na jeshi la polisi baada ya kumaliza mafunzo ya jeshi la kujenga taifa.
****
Inavyojulikana kuwa mtafutaji hatoki mikono mitupu hata siku moja, ndiyo ilijidhihirisha katika siku moja ya mwisho wa wiki amapo Sara alikuwa yupo pamoja na rafiki yake wa karibu wakiwa wanatoka na kuelekea kwenye matembezi yao. Siku hiyo walikuwa na miadi ya kukutana na James pamoja na Norbert, walitoka pamoja majira ya saa tano asubuhi kwenda hadi jirani na hostel za kina James. Waliwakuta wakiwa tayari wamejiandaa na walikuwa wakisubiri ujio wao, siku hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza ya Norbert kuweza kumuona rafiki yake Sara na baada ya kutambulishwa tayari alikuwa ameingiwa na tamaa naye. Walipochukua usafiri na kuondoka huko walipokuwa wakielekea tayari mtafutaji ambaye alikuwa na tumaini la kutotoka mikono kapa alikuwa amewaona, Jane alikuwa amemfuatilia Sara tangu anatoka kwenye hostel alizokuwa akiishia hadi anafika hapo na kukutana na James.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona na James akiwa yupo mvulana mtanashati kama yeye, aliamua kuwafutilia akiwa amekodi teksi hadi walipofika kwenye ufukwe wa Coco. Hapo aliwashuhudia wakikumbatiana na wakitembea kwa upendo katika muda wote waliokuwa wakielekea kwenye eneo la kunywea vinywaji kwenye ufukwe huo. Vitendo vyote ambavyo vilikuwa vikifanywa nao vilikuwa vikimuumiza kila alipokuwa akiviona. Ilifika muda akiwa amekaa mbali na eneo hilo alikuwa akilia sana kila alipowaona, walipokuwa wakicheka pamoja huku wakilaliana kiupendo yeye alijiona alikuwa akitobolewa kwenye moyo wake. Kila kitendo kilichokuwa kikifanyika hapo kilimuumiza zaidi na hatimaye alishindwa kustahimili akaondoka, alitumia usafiri kama aliyokuwa amekuja huku njiani akiwa haishi kulia kutokana jinsi alivyokuwa akimpenda James.
****
"Yaani shem huyo mwenzako sijui umemlisha nini?" Rafiki wa Sara aliuliza huku akiwa amekaa pembeni ya Norbert.
"Unajua inabidi niulize shem kamlisha nini Jem maana kamkaa kinywani kila muda utafikiri mate" Norbert naye alitia maneno wote wakacheka
"Heeeh! kumbe wote nilijua huku" Rafiki yake Sara mshangao ulimtoka
"Ukisikia nyota zenye kuendana ndiyo hizi ndiyo maana tunapendana,Gilda shosti upo hapo?" Sara aliinggilia naye
"Sina usemi kwenu nyinyi kumbikumbi" Gilda alisema
"Kumbikumbi huwa wawiliwawili tu, hapa kuna wengine wanaotakiwa kusogezana karibu tu" Norbert aliropoka hukua akimbania jicho James kiutani, kicheko kilimkuta rafiki yake huyo ambaye alikuwa ameelewa maana ya fumbo hilo.
"Shem nawe usiongee mafumbo, nimekuelewa kabisa unachokisema" Sara aliongea
"Halafu shem huyo rafiki yako hajatulia" Gilda aliongea huku akicheka
"Sasa ninarukaruka au namna gani?" Norbert alitia masihara
"Kutulia ni jukumu la maji ya mtungini yanyweke wewe" James naye aliropoka
"Kumbe na wewe ndiyo zakoeh!" Sara alikuja juu
"Situlii kwako tu kuhakikisha unafurahi kwenye kila siku ya maisha yako" James alichombeza huku akimshika kidevu mpenziwe
"Loh! Wivu mwingi" Gilda aliweka jicho la kumsuta alipongea maneno hayo.
"Akaa we! Mwenye mali hulinda chake bibi" Sara
Waliendelea kufurahi siku hiyo huku wakiongea mambo mabalimbali, ilikuwa ni katika siku ambayo pia Norbert aliyekuwa mcheshi kama James aliendekeza tabia yake ileile ya kupenda wasichana. Wapendanao walipotoka kwenda faragha yeye alitumia wasaaa huo kumchembeza Gilda aliyekuwa wamekuja kwa mwaliko wa shoga yake, hadi wapendanao hao wanarudi tayari alikuwa ameshamzidi mrembo kwa maneno yake hadi akakosa usemi wa kuongea. Utani uliendelea kati yao wakiwa wapo hapo mezani, Gilda alianza taratibu kuwa karibu na Norbert na hata wakawa wanatania matani ambayo yalikuwa ni tofauti na walivyokuwa hawajabaki wawili. Mazoea hayo yalifanya James amkate jicho kwani alikuwa ameshatambua rafiki yake huyo, Norbert alirudisha jicho hilo kwa kumnyanyulia nyusi moja juu. Hiyo ilikuwa ni ishara tosha kuwa alikuwa tayari ameshaanza kumuingiza kwenye anga zake, hakika alikuwa akimtambua vyema huyo rafiki yake. Moyoni alibakia na mshangao kwa muda mfupi ambao alikuwa ameutumia kuweza kumshawishi, hakika alimuona alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na kizizi. Kutokana kuwa na mazoea ya kiheshima hadi kuwa na mazoea kama walikuwa na ukaribu ndani ya muda mfupi, hakika alimvulia kofia Norbert akamuona ni kiumbe wa ajabu sana. Hakuwahi kuona akitumia muda mfupi kumpata mwanamke na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza, waliendelea kuifurahia siku hiyo ya mwisho wa wiki lakini bado mshangao wake haukuwa umetoka kichwani mwake.
"Jamanieh! Kama vipi leo twendeni klabu tukafurahia siku hii" Norbert alitoa wazo"
"Enhee! Shem umeongea hapo twendeni jamani tukitoka hapa" Sara naye alidakia
"Mtu na shema wake akili zinafanana, haya limepita hilo sijui kwa shem hapo" James aliongea huku akimtazam Gilda
"Sina neno kabisa" Gilda aliridhia
"Raha iliyoje tunaingia kama jozi za viatu vile" Norbert aliropoka
"Huyu naye muone" Gilda aliongea huku akimpiga singi Norbert
Majira ya jua kutua wote walinyanyuka kwenye viti vyao na kuchukua usafiri, wakiwa katika muundo wa wawiliwawili walipanda usafiri ambao uliwapeleka moja kwa moja hadi kwenye klabu maarufu jijini Dar es salaam. Walifanikiwa kufika na wote waliingia ndani ya klabu ya muziki wakiwa ni wenye hamu sana ya kuucheza, muda huo muziki ulikuwa bado haujachangamka kutokana na kutokuwa muda wake wa kuchangamka. Wakiwa wanasubiri muda wa kuchangamka muziki huo walitumia kukaa chini na kuongea mambo mbalimbali. Muda wa kuucheza muziki huo ulipofika waliingia kati ya kuucheza wakiwa wawili wawili, uchangamfu ndiyo uliingia kwenye akili zao kwenye kipindi chote walichokuwa wakiucheza muziki huo wa ujana. Wakiwa kwenye kundi la watu walikuwa wakiucheza huku wakiwa na furaha tele, James alikuwa yu karibu na Sara wakiucheza muziki na Norbert alikuwa yu karibu ya Gilda. Hakika walipendeza kutokana na walivyoendana na jinsi walivyokuwa wakicheza kiufundi zaidi, wote waliujua kuucheza ingawa wengine walikuwa wakionekana hawakuwa wachezaji muziki.
Usiku mnene uliwakuta wakicheza muziki huku wakipumzika kwa vipindi chache,fujo zilipoanza kutawala kwenye muziki taratiou walijitoa na wakakaa pembeni wakiendelea kuongea. Muda ulipoanza kuyoyoma zaidi hatimaye walinyanyuka kwenye makochi maalum ya ndani ya klabu hiyo na wakaondoka. Wakiwa wawili vilevile waliondoka na kuelekea katika sehemu moja ya kuumzika, kinamna ya ajabu tu James alikuwa akimshngaa Norbert kwa jinsi alivyokuwa hafai kwa wanawake. Alikuwa bado haamini kama alikuwa ameweza kuongozana naye hadi kwenye nyumba ya kupumzikia, ahata alipochukua chumba na Sarah bado alikuwa anaona kama ulikua mchezo wa kuigiza. Kumuona rafiki yake huyo alikuwa ameingia chumba kimoja na Gilda, hakika hakutarajia ndani ya kipindi kifupi cha muda tangu waonane.
Asubuhi ya siku iliyofuata wote walikutana tayari wakiwa wametoka kulegeza uimara ya vitanda vilivyopo katika nyumba hiyo ya kupumzikia. Siku hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupumzika na walikuwa hawataki kwenda sehemu yeyote ile, wanaume hao wawili waliwasindikiza wanwake wao hadi kwenye hostel zao. Walipowafikisha ndiyo ikawa mara ya kwanza kwa James pamoja na Norbert kuonekana kwenye kundi la wasichana waliokuwa wakiishi hostel, siku hiyo ilikuwa ni usumbufu kwao kwani walisalimiana na wasichna tofauti ambao walikuwa wakiwachangamkia hadi wasichna wao waliingiwa na wivu. Nao kutotaka kuwaudhi waliondoka kwa haraka,kuondoka eneo hilo tayari Norbert alikuwa ameshaanza kutamani baadhi ya wasichana warembo aliowaona.
"Mwanangu huku kuna mashori balaa" Norbert alimuambia James baada ya kushuka kwenye kituo cha daladala Ubungo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Dah! We mtu mwisho kabisa ushatamani na kule" James aliongea huku akianza kucheka
"We unafikiri nani asitamani watoto micharuko wale, yaani kuingia tu walivyotupapatikia"
"Mtu wangu hivi lini utatulia na msichna mmoja?"
"Muda wa kugeuka jua kuzama mashariki labda"
"Haya haya ni maisha yako siwezi kukuhukumu kwakuwa mimi mwenye sina ukamilifu kwenye ya kwangu"
"Yaani ndiyo nakukubali hapo tu mwanangu, ndiyo maana hata wewe sikukulaumu kuwa na mmoja huna sababu ya kuwa kama nilivyokuwa hivi"
"Halafu kila siku neno lako ni hilo tu ila huniambii una sababu gani iliyokufanya uwe hivyo"
"Mwanangu ni stori ndefu sana ila napenda ujue hata mimi nilikuwa na msichana mmoja kama ulivyo wewe na nilimpenda sana"
"Sasa si unipe habari mtu wangu yaani mimi wako wa damu pia unanificha, ilikuwaje hadi ukakutana naye huyo msichana na kipi kimekufanya uwe namna hiyo" Maneno hayo walipokuwa wanayaongea tayari walikuwa amefika kwenye eneo la Ubungo maziwa jirani na ilipo mitambo ya umeme nchini.
Norbert alimtazaa rafiki yake na kisha alieleeza, "Nilikuwa ni kijana mmoja nisiyejua hata ujanja kwenye masuala haya, yote yalianza nikiwa kidato cha tatu nilipokuja kumpata msichana ambaye aliushika moyo wangu sana. Nakumbuka nilikuwa na kawaida sana ya kutoroka kwenye shule ya bweni niliyokuwa ninasoma na kuingia mtaani kwenda kujilia vitu vidogo kutokana na kukinaishwa na mlo mmoja wa bweni, kutoroka kwangu huku ndiyo ilikuwa sababu ya kuweza kukutana na msichana huyu. Ingawa nilikutana naye katika mazingira ambayo yalikuwa si mazuri bado haikuwa sababu kwa sisi kuja kushindwa kuanzisha pendo katika siku za mbeleni, alikuwa ni msichana ambaye alikuwa amenizidi kiumri kidogo. Siku ya kwanza kukutana naye ilikuwa ni kama kawaida yangu ya utoro katika mwisho wa wiki nipo mitaani. Siku hiyo majira ya jioni nikiwa naelekea shuleni upande wa nyuma wa ukuta ndipo nilipoweza kumshuhudia mtu akiwa ameanguka barabrani akiwa aangaliwa hali yake na Mwanamke mzee, nilitaka niwapuuzie lakini nafsi ilisita na kusogea karibu na eneo hilo. Upungufu wa mwangaza majira ya jioni haukuweza kunifanya nishindwe kumuona msichana huyu ambaye alikuwa ana majeraha kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake. Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kumuuliza yule Mwanmke mzee kuuhusu hali ya huyo na sababu zake, kutokana na kuaanza kumuuliza kiheshima haikumuwia vigumu kwa Mwanamke huyo kuniambia alikuwa amemuona eneo hilo akiwa ameanguka. Aliniomba nimsaidie kumbeba niende naye nyumbani kwake nami sikuona sababu ya kukataa nilifanya kama alivyotaka, nilimbeba na nikaelekea hadi huko alipokuwa akiishi kwenye nyumba ambayo ilikuwa imechakaa. Nilielekezwa kwa kumuweka binti huyo na mimi nikamuweka, alianza kupewa huduma nami nilikaa eneo hilo hadi inafika majira ya saa mbili. Chakula nilipewa nikala hapohapo na niliaga nikarudi shule nikiwa nimemuacha akiwa bado hajarejewa na fahamu, siku hiyo nilikuta wenzangu wakiwa wapo madarasani wanajisomea lakini nilipitiliza moja kwa moja hadi bwenini nikaenda kulala kutokana na kuchoka. Oyaa Jem gari hilo mtu wangu mbona huangalii hata mbele yako" Norbeet alisimulia na kisha alisitisha baada ya kuona gari likiwa linakuja mbele, James alikuwa akimsikiliza huku akiwa anamtazama pasipo kuangalia mbele.
"Dah! Mtu wangu nimenogewa endelea basi kunipa mkasa"
"Utoro kama kawaida nilikuwa nikiufanya lakini siku hizi nilipunguza kwenda mitaani na nilikuwa nakuja kwenye nyumba hii niliyomleta yule binti, nilimkuta akiwa bado ni mgonjwa lakini sikuwa nikichoka kuja kumuona. Hadi alipokuja kupatwa na nafuu na akaambiwa na Yule Mwanamke ambaye tayari nilikuwa anamuita mama juu ya mimi, alinishukuru sana na hapo ndipo ukaanza urafiki baina yetu. Alipokuja kupona kabisa niliweza kujua alikuwa ni mmoja wa wasichna warembo ambao walikuwa wamekosa matunzo, mioyo yetu taratibu ilianza kuzungumza na hatimaye siku moja nikaja kuingia kweny pendo lake. Sikuwahi kupenda kama nilivyopenda hapa nakuambia mtu wangu, Mwanakombo alikuwa ni kila kitu kwangu kama ningekuwa ni Askari basi huyu angekuwa ni Kamanda wangu. Mambo yote ya kitandani nilikuwa chekechea lakini nilikuja kupata shahada kabisa. Nilifurahi kuwa ndani ya penzi lake lakini sikuja kudumu kabisa mtu wangu, lilikuja kusambaratika kutokana na ujio wa mdada mmoja katika shule yetu kumleta mwanafunzi mpya. Huyu dada ambaye nilimuona kama jinamizi kwenye penzi letu alikuwa akiitwa Ester, alikwa ni sawa na mimi kiumri kimtazammo lakini alikuwa ameyaanza maisha mapema na alikuwa na usafiri wa maana. Huyu dada naye alikuja kunitamani lakini kutokana na kunogewa na Mwanakombo mtoto wa Kitanga nilipiga chini sikutaka mahusiano naye. Hapo ndiyo mwanzo wa matatizo ulipoanza, sikuwa nafikiria kama kabisa angekuja kufanya hivyo. Alipokuja kujua kuwa nina mahusiano na Mwanakombo alipanga mpango mbaya sana wa kuweza kumkomesha, alikuja siku akiwa na lengo la kumuambia ana kwa ana aniache. Siku hiyo alipokuja kumuona huyo Mwanakombo amuambie aliondoka bila ya kuaga, siku hiyo nilipokuwa nikiwatazama wote wawili niliweza kujua kuwa alikuwa wakifanana sana. Siku hiyo pia niliweza kujua kuwa huyo Ester alikuwa ni ndugu wa damu wa Mwanakombo, nilisimuliwa kila kitu juu ya undugu wao na jinsi walivyotengana. Haikuchukua muda mrefu tangu nifahamu hilo kipenzi changu aliuawana mhusika akawa ni Ester. Tangu siku hiyo Mwanamke alipokuwa chnazo cha kumkosa mpenzi wangu, nilianza kulipiza kwa kuwabadili tu kama nguo sikuwa na mapenzi nao. Rafiki yangu ambaye tulikuwa tukisoma naye shule moja ambaye anaitwa John kwa sasa yupo mafunzoni jeshi la polisi alinishauri lakini sikubadilika, hata huyo Ester mwenye nilikuja kumuweka katika orodha ya niliowachezea. Hivyo mtu wangu hii ndiyo sababu ya kuwa na wasichana wengi ingawa yupo mmoja Norene ninayempenda kwa dhati" Norbert alihitimisha kusimulia na muda huo wakiwa wamefika kwenye lango la kuingia hostel.
"Dah! Pole mtu wangu"
"Usijali jamaa ndiyo maisha haya ila hawa viumbe waache watakoma"
"Il sijapendelea unavyofanya mtu wangu"
"Tuiache hii habari"
Wote waliingia kwenye jengo lililokuwa na chumba chao ndani yake, waliingia kwenye chumba na walipumzika kutokana na shughuli ya usiku uliopita.
****
Kujua makazi ya James ilikuwa ni ushindi mkubwa sana kwake na aliamua kutopoteza nafasi hiyo, Jane alitoka nyumbani kwao majira ya jioni akiwa ameaga alikuwa anarudi Hosteli lakini haikuwa hivyo. Alikuwa na safari nyingine ya kuunganisha ndiyo aweze kupita na kwenda hostel, alipitia moja kwa moja hosteli za Mabibo ambapo alikuwa amepanga kwenda. Akiwa ameamua liwalo na liwe aliingia hadi ndani ya uzio wa hosteli hiyo, ukubwa wa hostel hizo ulimfanya yeye kutosonga mbele zaidi ya kuuliza wenyeji wa hapo. Aliamua kumtafuta Mlinzi na alimuuliza kuhusu mtu aliyekuwa akimtafuta, kutokana na James kuzungumza na watu wa aina tofauti hata wafanyakazi wa ndani ya jengo hilo. Haikumuwia vigumu Jane kuambiwa alikuwa anamjua huyo aliyekuwa akimfahamu. Hiyo ndiyo ilikuwa bahati yake baada ya kuhangaika kwa muda mrefu na hatimaye alikuwa ameweza kupata kile alichokuwa akikitafuta, alielekezwa moja kwa moja jengo alilokuwa anapatikana na chumba chake.
Alimshukuru san Mlinzi huyo na moja kwa moja alipiga hatua kwa madaha akiwa yu ndani ya mavazi yaliyokuwa yakimpendeza, alielekea ndani ya jengo aliloelekezwa na kisha alienda kugonga kwenye chumba ambacho alitajiwa na Mlinzi h. Mlango ulifunguliwa na alikutana na mtu mwingine tofauti na aliyekuwa amemkusudia hadi kufunga safari na kufika hapo, alikutana na Norbert ambaye alikuwa yupo kifua wazi kavaa nguo ya mazoezi akiwa na taulo begani.
"Karibu" Alikaribishwa
"Asante, mambo" Aliiitikia ukaribisho na akasabahi
"Poa tu, nikusaidie nini mrembo?"
"Samahani nahisi sijakosea nilivyoelekezwa, James anaishi hapa?"
"Haaah! Usiulize mashuzi kwenye shibe ya kunde mrembo, ndiyo anaishi ila una bahati mbaya sana"
"(Alicheka kwa sekunde kadhaa) Kwanini?"
"Ametoka muda si mrefu amepigiwa simu kuna jambo la muhimu ameitwa na mzazi wake"
"Hee! Jamani, kwahiyo atarudi?"
"Ndiyo imetoka hiyo kesho tena atapitiliza moja kwa moja chuo"
"(akionekana mwenye unyonge) Sawa huu mguu ulikuwa wake, wacha niende hivyo"
"Sasa si ungeukata tu uuache hapahapa akija nitampatia"
"(Akacheka tena) Mmmh! Mcheshi sana wewe kama James, wacha niende sijui unaweza kunipatia namba yake"
"Dakoka sifuri tu ninarudi" Norbert alipongea hivyo aliingia ndani ya chumba na alipotoka alikuwa na simu, alimpa akachukua namba hizo na kisha alizihifadhi kwenye simu yake.
"Asante mkaka wacha niende"
"Aaaaaah! Dadaeh! Vibaya hivyo sasa"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Jamani kwanini?"
"Yaani unakuja na kuondoka bila ya kujuana kweli, hivi akija na wewe ukamkosa kwenye simu nimuambie nani sasa"
"Ooooh! Sorry nina haraka ndiyo maana hata nimesahau, mwambie Jane alikuja"
"Wapo wengi sana anaowafahamu wana majina hayo nimuambie Jane yupi?"
"Mwambie Jane wa mgambo Tanga au Jane Lutonja" Alipotaja jina lake hakutaka kubaki hapo kwani aliyekuwa amemlenga hakuwepo, kuondoka ndiyo ulikuwa uamuzi na hakuwa na jingine la ziada.
****
Muda wa chakula cha usiku James alikuwa yupo meza moja na ASP Mwambe wakiwa wanakula chakula, jambo ambalo alikuwa ameitiwa tayari walikuwa amezungumza. Alikuwa pembeni ya Mke wa ASP Mwambe ambaye ni mama mzazi wa Sara, wote walikuwa wanakula chakula kwa furaha lakini furaha za wote zilikuwa ila ya Jmaes iltumbukia nyongo baada ya simu yake kuita. Kutokana na kutoona umuhimu wa kuipokea simu hiyo kando aliipokea huku akiwa ameshika kijiko cha chakula, aliisikia sauti nyororo ikimsabahi.
"Safi nani mwenzangu......Jane yupi najuana na wengi......nani kakupa namba yangu........Ok sasa sikia, iwe mwanzo na mwisho wa kunipigia simu sihitaji hata kuongea na wewe" James aliongea kwa upole, alipojua kuwa aliyekuwa akimpigia simu alikuwa ni Jnae alibadilika na alikata simu kisha akaizima.
"Vipi mwanangu mbona hivi?" Mama Saraha aliuliza lakini hakujibiwa na badala yake alimuona James akiinamisha kichwa chini
"James si umeulizwa au siku hizi na wewe ushaanza tabia ya kuficha mabo" ASP Mwambe aliingilia.
"Baba wacha niwaambie tu, huyu aliyepiga simu ni Jane lutonja sijui ananitafutia nini yaani waliyonifanyia kwao hawajatosheka tu" Alilalamika
"James kama ni huyo mimi nikiwa ni baba yako mlenzi nakushauri kaaaa naye mbali kabisa, SSP Lutonja akijua una mawasiliano tu na binti yake ni kero. Wangapi nimewashuhudia wapo gerezani kisa huyo binti, najua wewe ni kijana wa kiume ila hapo jali maisha yako" ASP Mwambe aliongea
"Sawa baba" Alitii
Hamu yote ya kula chakula ilikuwa imemuisha kabisa na aliinuka kwenye kiti na kuingia chumbani, aliwaacha walezi wake hao wakiwa wanamshangaa lakini hawakuamuambia kitu kitu chochote hadi pale alipoingia ndani. Uliposikika mlango wa chumbani kwake ukifungwa ndipo mume na mke hao walitazamana, walikaa kwa muda mfupi wakitazamana hivyo hivyo bila ya kuongea chochote. Walipochoka kutazamana kila mmoja alirudisha macho kwenye sahani yake ya chakula na wakaendelea kula, ukimya ulitawala kwa muda mfupi na sauti na vijiko vikigonga sahani kipindi wanakula ndiyo ilisikika.
"Baba Sara" Mama Sara aliuvunja ukimya huo.
"Ndiyo mke wangu" ASP Mwambe aliitikia
"James inabidi uwe mshauri wake mzuri sana la si hivyo tutampoteza huyu"
"Sitoruhusu hilo lipotee nampenda kama mwanangu wa kumzaa ndiyo maana nipo naye kwa miaka yote hii"
"Hata mimi pia, sina mtoto wa kiume lakini kwa ujio wake kwenye familia hii najihisi nina mtoto wa kiume"
"Tutamlinda mke wangu usijali"
Asubuhi ya siku iliyofuata James aliamka mapema na alipelekwa na Baba yake mlezi hadi chuoni, aliendelea na masomo kama kawaida ile namba akawa ameifungia kabisa. Siku hiyo nayo iliisha na kisha siku mpya ikafuata, Norbert alikuwa ameshaambiwa kila kitu juu ya Jane na kuwahi kuishi ndani ya nyumba yao huku akifichwa baadhi ya vitu ikiwemo uhusika wa baba yake Jane. Yeye naye aliunga mkono hilo suala na akitumia nafasi hiyo kumsaidia James. Alimua kumuambia ukweli huku akimtajia kila kitu juu ya asili ya James, Norbert alifanya tofauti na alivyofanya Wilfred alipokuwa jeshini. Alimua kumtuhumu kwa jinsi alivyochangia James kuharibikiwa na maisha kipindi akiwa na upofu, huo ulikuwa ni mwiba mchungu sana kwa Jane na hakuthubutu kabisa kuendelea kumfuata James kwani nafsi yake ilikuwa imemsuata tayari kwa hatia aliyokuwa ameifanya.
Kukaa kimya ilihali hakuwa ameingiliwa ukweli na James ilikuwa na hatia kubwa iliyohalalisha kupigwa kwake, kumbukumbu za jambo hilo zilimuumiza sana hasa akikumbuka alimshuhudia akipigwa uchi hadi ngozi yake ikachanika. Hakuwa na namna ya kujitetea kabisa kutokana kulitazama suala hilo likiwa linatokea hadi bila kutoa utetezi wowote, hofu dhidi ya baba yake ndiyo ilimfanya hata ashindwe kuongea chochote. Alipokuwa akitendewa jambo hilo tayari alikuwa ameanza kupata viashiria ya ukubwa ndani ya mwili wake, hakuwa mtoto hadi aseme kuwa alikuwa hajui kama maeneo yake yalikuwa hayajaguswa. Mwenyewe alianza kuacha kumfuatilia na huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuwa ni mwenye kuumia, masomo alikuwa akiendelea nayo na aliweza hata kuwa na mwanaume mwingine lakini bado hakuweza kumsahau James. Alikuwa na lengo lile la kuwa naye, upendo wa kweli kwa mtu aliyekuwa hana haja naye ndiyo ulikuwa unamsumbua sana. Uzuri ule aliokuwa akiuona ni silaha na ni sababu tosha ya kuwa na jeuri, hakuona sababu yeyote ya kuendelea kuwa nao ikiwa aliyekuwa akimthamini hana haja naye.
Jane huyu alibadilika kuwa ni binti mkimya muda wote aliyekuwa yupo kwa ajili ya masomo tu, mwanaume aliyekuwa naye alikuwa akikidhi haja ya mwili wake tu na si kuwa naye kimaisha. Hii ilifanya abadili wanaume kila kukicha akiona alikuwa amechoka kuwa na mwanaume mmoja, hakuona haja ya kujithamini ilihali hatahminiwi na yule aliyekuwa akimthamini. Hitaji la mwili lilipokuwa likimsumbua basi ilikuwa ni kwa mwanume yeyote yule, atakayeleta jeuri kwenye uhusiano wake kisa alikuwa amelala naye alikuwa akiishia kuachana naye. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake hadi anahitimu katika chuo hicho kwa kusoma miaka mitatu, siku ya mahafali alisherekea na familia yake huku akishuhudhia jinsi Sara Alivyokuwa yupo karibu na James. Siku hiyo pia aliweza kushuhudia familia nzima ya ASP Mwambe ambaye alikuwa akimJua ikiwa ipo karibu na James, siku hiyo ndipo alipoweza kutambua kuwa huyo aliyekuwa amemchukua mwanaume wa maisha yake alikuwa ni mtoto wa Afisa wa Magereza kama ilivyokuwa yeye.
James baada ya kumaliza masomo yake ya chuo mwaka huo aliohitimu mpenzi wake, aliamua kwenda kujiunga na jeshi la magereza kwa maamuzi yake mwenyewe. Aliingia kwenye mafunzo ya jeshi hilo, Jane naye alipopata habari kuwa James alikuwa amejiunga na jeshi la magereza naye aliamua kujiunga nalo. Walikutana kwenye mafunzo lakini hali ilikuwa ni ileile hakukuwa na maelewano kati yao, hadi muda wa mafunzo unaisha na wote kuajiriwa katika sehemu tofauti ndani ya jeshi hilo. Jane bado alikuwa na nia ileile ya kumpata James, kutimiza nia hiyo aliongea na baba yake ambaye alikuwa ni Kamishna msaidizi tayari. Akitumia hila aliweza kufanikisha kuhamishwa James katika ofisi gereza ambalo alikuwa akifanya kazi jijini Dar es salaam. Bado hakuwa ameweza kumshawishi James kuwa naye pamoja na kuwa yupo naye ndani ya ofisi moja. Ofisi ambayo alikuwa akiogopwa kutokana na kuwa ni binti wa afisa wa juu wa jeshi hilo, alikuwa ameona alikuwa ameweza kutimiza hila yake kumbe ndiyo kwanza alikuwa ameweza kufanikisha kuwa karibu kwa Sara na James ambao walikuwa maeneo tofauti ya ajira.
Wapenzi waliokuwa wametenganishwa na majukumu ya kazi sasa walikuwa wapo pamoja, hiyo ilikuwa ni hatua nzuri kwao lakini pia ilikuwa ni mbaya sana kwa Kwa Inspekta msaidizi Jane. Alikuwa ameanza kujuta kuweza kumuhamisha Inspekta msaidizi James ambaye alikuwa akitambulika kwa jina la Nkongo kuja jijini tena. Aliona ni bora hata angebaki hukohuko kuliko kuendelea kuwa kwenye ofisi moja naye akiwa hajatimiza kile ambacho alikuwa akitaka kitimie, uhasama wa James kwake bado ulikuwa ukiendelea na hakukuwa na hatua yeyote ya kuja kuongea naye na hata kufikia kuwa naye karibu. James alikuwa ni kipenzi cha watu ndani ya ofisi hiyo kutokana na kujiheshimu na pia kuwa mcheshi, alikuwa akiongea na kila mtu lakini si Jane ambaye alikuwa yupo kwenye orodha ya watu aliokuwa akiwachukia ndani ya dunia hii.
Kipindi hiko ndiyo alikuwa amepalilia kabisa mahusiano ya James na Sara, yalifikia hatua baba mzazi wa Sara ambaye alikuwa Mrakibu wa jeshi la magereza kwa wakati huo kujua. SP Mwambe alishangazwa sana na uhusiano huo lakini kutokana na wote kuwa wanapendana na yeye anawapenda, aliamua kuubariki uhusiano wao. Mama Sara naye hivyohivyo aliamua kuubariki uhusiano huo, sasa wakawa wapo huru kabisa na uhusiano na siyo wa kujibana kama ilivyokuwa awali. Mwezi mmoja baadaye katika shereha ya kuzaliwa James ambayo ilihudhuriwa na maaskari wenzake wengi, alimvisha pete ya uchumba Sara na hilo lilizidi kuwa pigo kubwa kwa Jane. Aliumia sana na hata ufanisi wa kazi ukapungua kabisa akawa si makini kabisa katika ufanyaji wa kazi kama ilivyokuwa hapo awali, hii ilikuja kusababisha hata baba yake alitambue hilo na alipojua binti yake alikuwa ni mwenye msongo wa mawazo bila ya kujua sababu yeyote. Aliamua kufanya mipango aende kujiendeleza kielimu zaidi nje ya nchi akiamini hio litaweza kumuokoa, Jane hakuwa na jinsi naye alikubali safari hiyo ili kwenda kutuliza akili yake huko na si kukaa na kuzidi kuumia akiwa yupo kazini.
Kipndi hicho kilikua tayari Kamishna msaidizi Lutonja alikuwa ameshatambua juu ya James kuwa ni mtoto wa aliyekuwa rafiki yake, aliamua kumuacha tu kwani aliona hakuwa na madhara ya yeyote. Hakuona haja ya kumuua mtu ambaye alikuwa anamuona hana hatari kwenye maisha yake,aliendelea na maisha yake akiwa bado yupo kwenye kikundi haramu tofauti na kile cha awali ambacho kilisambaratika baada ya umakini kurudi kwenye vyombo vyua dola. Uhaini na ujambazi aliokuwa ameufanya hakuwa ameuacha kabisa katika kipindi chote. Alikuwa akiendelea na uhaini huo kwa namna tofauti ya kuuza magendo. Alitokea kuwa Afisa mwenye fedha sana tofauti na mshahara wake, hilo liliweka mawswali ambayo mwenyewe baadaye aliyajua kuyazima kwa kujieleza alikuwa amewekeza kwenye shughli zingine tangu akiwa yupo kijana kabisa. Maswali ya mali zake yaliishia hapo na akawa akipata heshima yake kutokana na kuwa afisa mkubwa, hakika aliishi kwa raha sana pamoja na familia yake.
****
Maisha ya uchumba kati ya James na Sara yalidumu kwa muda mrefu hadi walipokaa na kuamua waweze kufanya mipango ya ndoa, walilifikisha suala hilo kwa wazazi nao waliliafikia bila ya pingamizi lolote. Wakishirikiana na wale wazazi wa hiyari wa James ambao walimuokota, walianza kufanya maandalizi taratibu. Taarifa zote za maandalizi ya ndoa hiyo tayari yalikuwa yamejulikana kazini kwa James na Sara, marafiki wa pande zote mbili walikuwa wakishirikiana nao bega kwa bga katika kufanya maaandalizi. Norbert, Wilfred ambaye alikuwa ni mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi. Walikuwa ni marafki wakubwa wa upande wa James, Gilda pamoja na marafiki wengine nao walisimama upande wa Sara.
Wote walikuwa wakiwatakia la heri kwenye maandlizi yao hayo ya ndoa, walijitoa katika kila kitu ilimradi shughuli hiyo ikamilike. Siku zilisogea na hatimaye siku ya harusi ikafika Jane akiwa yupo nje ya nchi kimasomo, hakuwa na taarifa yeyote juu ya kilichokuwa kikiendelea nchini. James na Sara kwa mara ya kwanza kwenye maisha yao walifikia ndoto ambayo walikuwa wakiisubiri kwa siku nyingi sana, siku waliyokuwa wapo mbele ya Mchungaji ambaye alifungisha ndoa yao walikuwa hawaamini kama wangeweza kufikia siku hiyo. Maisha ya uchumba kwa muda mrefu hatimaye walikuja kuwa kwenye hatua ya kuwa mwili mmoja, mbele ya Mcnungaji wote walikiri kutaka kuwa kwenye ndoa na mwenzake bila hata kusita. Lilipoulizwa pingamizi halikuwepo na hiyo ndiyo ikawa tikiti ya wao kuwa mwili mmoja, hatimaye walifanikiwa kuwa mume na mke na pete za ndoa wakavishana. Waliweka sahihi kwenye cheti chao cha ndoa, nderemo na vifijo zilitawala baada ya kufunga ndoa hiyo na sasa wakawa wa halali kwa Muumba wao. Sherehe kubwa ilifuata baadaye kwenye ukumbi mmoja maarufu jijini Dar es salaam, ndugu na marafiki pamoja na jamaa walihudhuria sherehe hiyo wakitoa pongezi zao. Wale wanafunzi waliokuwa wakisoma nao chuo kimoja ambao walitambua jinsi walivyokuwa wakipendana, waliwapa hongera kwa kufikiaa hatua hiyo kwa kutoa zawadi mbalimbali.
Zawadi nyingi kwenye sherehe zilitoka ikiwemo nyumba ya kisasa waliyokuwa wamekabidhiwa na SP Mwambe, wengi walikunywa na kufurahi ndani ya sherehe hiyo na hata muda wa kuisha kwa sherehe ulipofika. Walitamani iendelee lakini wakati ulikuwa haurudi nyuma, fungate ya mahaursi ilipangwa kwenye hoteli ya kifahari iliyopo visiwani Zanzibar. James na Sara kwa pamoja wakiwa wapo kwenye likizo walisaifri kwenda visiwani humo, ujio wao tayari ulikuwa umeshajulikana na kwa pamoja walipelekwa hadi hotelini hapo. Walikula fungate yao katika hoteli hiyo huku wakiwa ni wenye kujiona viumbe waliozaliwa upya, huduma zote muhimu ndani ya hoteli tayari zilikuwa zimegharamiwa katika kipindi chote walichokuwepo hotelini hapo.
Fungate ilipoisha katika muda ambao likizo zao zilikuwa zikikaribia kuisha, walirudi kwa pamoja jijini Dar es salaam. Waliamua kuweka makazi yao katika nyumba waliyokuwa wamepewa na SP Mwambe kama zawadi kwa kufunga ndoa. Maisha ya ndoa waliyaanza katika nyumba yao hiyo mpya ambayo ilikuwa ina kila kitu ndani yake, ndugu na jamaa walikuwa hawaishi kuja kuwatembelea hapo nyumbani kwao katika siku ambazo walikuwa wapo mapumzikoni. Hatimaye likizo waliyokuwa wamepewa kila mmoja iliisha na wote walirejea kazini, maisha ya ndoa yalikuwa ni matamu sana kwao hawakuwahi kuuona uchungu wake tangu walipoyaanza. Kila mmoja alikuwa akiitambua thamani ya mwenzake ndiyo siri ya kuwa na furaha katika ndoa yao, pia kila mmoja aliona alikuwa amepata mwenza sahihi kwenye maisha yake ndiyo maana waliianza ndoa yao kwa furaha sana. Kila muda walikuwa wakitamani kuwa karibu lakini majukumu ya kikazi yalikuwa yakiwafanya wawe mbalimbali, yalipoisha majukumu walikuwa pamoja katika muda wote. Kinai ya kuwa karibu na mwenzake haikusikika kwenye ndoa yao kwa jinsi walivyokuwa wakipendana, maisha yalizida kuwa mazuri wakiwa ameunganisha na kuwa mwili mmoja na hata mafanikio yao walikuwa wakichangia pamoja. Ndani ya ndoa hiyo kutokana a kuwa mmunganiko uliokuwa unajali maisha yao ya baadaye, waliweza kujenga nyumba ya pili kwa ushirikiano wao na pia walinunua magari mawili ambayo wote walikuwa wakiyatumia kwa ajili ya usafiri.
Bado hawakuwasahau wazazi katika kila siku ndani ya maisha yao kwani ndiyo walikuwa ni nguzo kwao, walienda kuwaona kila inapopatikana wasaa wa kufanya hivyo kutokana na upendo waliokuwa nao kwao. Wazazi wa hiyari wa James ambao walikuwa wakiishi shamba katika kipindi hiki tayari walikuwa wamezeeka, umri ulikuwa umewatupa mkono zaidi, wao utani mkubwa kwa wanandoa hawa ilikuwa ni kupatikana kwa mtoto tu ili wamuone wakiwa na mvi zao kichwani. Walikuwa wakifurahia sana kila wanapotembelewa na wapendanao, dua zote njema walizokuwa wakizijua wao waliwaombea ili wazidi kuwa na ndoa imara na itakayodumu kwa muda mrefu. Maisha marefu pia walizidi kuwaombea wanandoa hao ambao walikuwa wakiyafurahisha macho yao kila wanapowaona, walitamani hata waendelee kuishi milelele ili waionje furaha ya ndoa.
Haikupita miezi mingi sana kiasi cha kutahadharisha upunguaji wa mwaka, ndani ya mwaka huohuo Muumba aliiwaona katika maombi yao waliyokuwa wakitaka yatimie kila siku. Kujibiwa kwa ombi hilo walilokuwa wakiliomba kila siku na kuzidisha juhudi ya kulipata, ilizidisha furaha ndani ya ndoa yao. Mtoto ndiyo ombi ambalo walikuwa wakiliomba kila siku katika maisha yao pamoja na maombi mengine, hili lilijibiwa kwa Sara kunasa ujauzito katika kipindi hiko. Mapenzi baina yao yalizidi katika kipindi hiko ambacho James tayari alikuwa na cheo cha Inspekta ndani ya jeshi la Magereza, Sara alizidisha kudeka kila alipokuwa yupo karibu na mume wake katika kipindi hiko cha ujauzito. Habari ya ujauzito aliyokuwa nao Sara ilifika kwa kila mtu wa karibu na hata ofisini kwa kila mmoja, hongera nyingi ndiyo walizipokea kutokana na kuishi vizuri sana na watu.
Kipindi hiki ndiyo Jane alirejea kutoka nje ya nchi alipokuwa yupo kimasomo, alifikia nyumbani kwao ambapo alipokelewa vizuri sana kutokana na jinsi walivyomkumbuka kwa kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu . Alipumzika nyumbanni kwao akiwa hana hili wala lile juu ya ndoa aliyofunga James, moyoni bado hakuwa amemsahau alikuwa akimkumbuka na bado nia ya kuwa naye kimaisha ilikuwa ipo. Alipokuwa masomoni aliweza kutuliza akili yake kutokana na msongo wa mawazo, lakini hakuweza kuufanya moyo wake usiwe na hitaji la kuwa na James. Hilo ndiyo jambo ambalo alilishindwa kutokana na moyo kuwa na ushawishi mkubwa kulikoa akili katika mwili wake, alikuwa ameshakataa kuolewa na wanaume wengi na alikuwa akifikiria tu kuolewa na James. Hakuwa akijua bahati haikuwa yake kabisa na alikuwa akiwaza yasiyowezekana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliporejea kazini alipandishwa cheo na kuwa Inspekta kamili na siku aliyokuwa akiripoti ofisini watu wote walikuwa wakitambua ujio wake, James akiwa mmojawapo na katika muda huo alikuwa yupo juu yake kicheo kutokana na kutangulia kupandishwa cheo. Alikaa pamoja na wafanyakazi wengine ndani ya ofisi hiyo katika kumpokea, muda smbao walionana ana kwa ana James hakuwa na chuki ile aliyokuwa nayo hapo awali. Alipopewa heshima yake kama mkubwa yake aliipokea, alipopewa mkono naye aliupokea na ikawa kwa mara ya pili wanashikana viganja kabla ya kuwahi kufanya hivyo wakiwa pamoja mafunzo ya JKT. Kupokea mkono wa James ilikuwa ni faraja kutosha kwa Jane hadi akajikuta akiutazama mkono huo akihisi haukuwa wenyewe, kitendo cha kutazama kiganjani mwake alipokuwa ameshikana. Aliweza kuuona mkono wa kushoto wa James ukiwa na pete ya rangi ya dhahabu iliyokuwa ya duara, hii ilikuwa ni pete ya ndoa hata bila ya mtu kuambiwa ilikuwa inajulikana tu.
Aliuhisi moyo wake kama ulikuwa ukipasuka alipoiona bangili hiyo ndogo ya kidoleni ambayo ni sehemu ya pingu ambayo hufungwa maisha, wazo la kumkosa James lilimjia kichwani mwake lakini hakutaka kuliamini kabisa. Aliona ni kama utani vile kila akilifikiria wazo hilo, alijikaza kiafande na akaweza hata kumaliza kusalimiana na Inspekta mwenzake na kisha akahamia kwa maaskari wengine wa hapo Gerezani. Aliwasalimia mmoja baada ya mwingine huku akili yake ikiwa ipo kwenye pete ya ndoa aliyoiona, alipomaliza kuwasilimia wote aliingia kwenye ofisi yake nyingine ambayo ilikuwa ni eneo moja na ilipo ofisi ya Inspekta James. Alikaa kitini na akili yote ikawa ipo bado kwa mwanaume yule ambaye alikuwa akimuhitaji kwa kila hali kwenye maisha yake na sasa alikuwa amemkosa. Akiwa yu ndani ya mawazo rafiki yake kipenzi aliingia ofisni kwake, kutokana na kuwa alikuwa amemzidi cheo alipewa heshima yake. Alimruhusu kuketi kwenye kiti naye aliketi huku akitabsamu kudhihirisha urembo aliokuwa nao, Jane alibaki akimtazama rafiki yake huyo ambaye alikuwa amemjia ofisini hapo akionekana alikuwa na jambo.
"Shosti nikupongeze Ulaya imekupenda kwakweli" Alipongezwa
"Asante shosti niambie naona una jambo huo ujio wako si kawaida" Alimuambia
"Shosti umekosa vingi sana kwenda masomoni"
"Enhee! Wacha wee, kwanza nipe habari za hapa tangu nilipoondoka"
"Yapo! Mengi sana kikubwa ni Afande Nkongo kaoa"
"Unasema!"
"Ndiyo hivyo shosti yaani bonge la sherehe ofisi nzima tulikuwepo kasoro wewe tu" Maneno hayo yalikuwa ni yenye kumchoma sana lakini ilibidi ajiweke kwenye hali ya kawaida ingawa huyo shoga yake alikuwa akijua vizuri kama alikuwa akimpenda James
"Shosti ndiyo hivyo umeshawahiwa tayari tena ni yule Mdada wa TRA uliyesoma naye chuo"
"Sara!"
"Enhee! Kama ulikuwepo vile ni huyohuyo aliyekuwahi" Aliposikia hayo ndiyo aliweka kabisa mikono usoni mwake
"Shosti usihuzunike wanaume hawajaisha nilikuwa nakutaarifu tu, sasa hivi Afande James ni baba kijacho"
"Sawa" Unyonge ulimuingia ingawa alijilazimisha kutabasamu na kisha aliendelea na kuongea na rafiki yake huyo, hakukaa sana alinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje.
Inspketa Jane ndipo uchungu uipomshika na hata chozi likamdondoka kwa kuwahiwa kila kitu, muda huo wa kazi alijikuta akilia kwa sauti ya chini iliyokuwa imembatanishwa na kwikwi. Alilia sana na hata kilio kikamchoka na hakuona maana ya kulia ikiwa ilikuwa haimrudishi tena James kwenye mikono yake. Aliamua ajikaze na kutimiza wajibu wake uliokuwa umemuweka ndani ya ofisi hiyo, muda wa mapumziko mafupi ulipofika alienda kupata kifungua kinywa. Eneo la kupata kifungua kinywa alimuona Inspekta James akiwa amekaa na baadhi ya maofisa wakipata kifungua kinywa kwa pamoja, aliamua kujumuika nao huku macho yame yakiwa hayaishi kuitazama pete ya ndoa iliokuwa ipo kidoleni.
Ucheshi alikuwa nao mwanaume ampendaye ulikuwa ukimchekesha pia lakini kicheko hicho kilikuwa kikiyeyuka kila aitazamapo pete ile ya ndoa iliyopo kidoleni, kifungua kinywa chake alikimaliza lakini alijikuta akishindwa kukaa hapo mezani pamoja naye na aliinuka na kuondoka. Alirejea ofisini akiwa ni mwenye majonzi sana kwa kupoteza muda sana na akose alichokuwa akikitaka, muda wa mapumziko ulipoisha aliendelea na majukumu ya ofisni kama ilivyo kawaida. Ulipofika muda wa kutoka aliamua kuondoka akiwa ni wa kwanza kutoka ndani ya ofisi hiyo, alimuacha Inspekta James akiwa yupo ofisini kwake hajatoka. Safari yake baadaya kutoka ofisni hapo ilikuja kuishia kwenye jengo la mamlaka ya Mapato jirani kabisa na Stesheni, hapo alitafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari na alishuka huku akiacha macho ya watu yakishangaa jinsi msichana mrembo kama yeye aliyevaa vazi la jeshi la magereza lenye nyota. Hakujali macho ya watu kwani aliamini cheo alichokuwa ncho ndiyo kiliwafanya wabaki hivyo, aliingia ndani ya jengo la TRA na kisha alienda hadi mapokezi na kumuulizia aliyekuwa akimtafuta.
Umaarufu aliokuwa nao Sara ndani ya ofisi hizo haikumuwwia vigumu kuweza kumpata, alielekezwa hadi ilipo ofisi yake. Akiwa ni mwenye mwendo wa kimadaha alipiga hatua kuelea huko ofisini, alipofika alimkuta Sara akiwa ndiyo anakusanya vitu muhimu atoke ofisini. Alipomuona moyo ulizidi kupata maumivu lakini alijikaza na kisha akaguna alipokuwa yupo mlangoni, mguno huo ulimfanya Sara ambaye alikuwa ameanza kunenepa kutokana ujauzito kugeuka. Inspekta Jane aliachia tabasamu huku akimtazama mwenzake ambaye alikuwa amefanikiwa kupata anachokitaka, alipokewa na tabasamu pia kutoka kwa Sara ambaye alikuwa hana chuki ile aliyokuwa nayo chuo. Yote aliyokuwa akifanyiwa chuoni na Inspekta Jane alikuwa ameshayasahau tayari, Sara alijikuta akienda kumkumbatia kutokana na kutoonana kwa muda mrefu sana.
"Jamani ni wewe kweli au naona ndiyvyo sivyo" Sara aliongea kwa furaha
"Ndiyo mimi huyohuyo hakuna mwingine" Inspekta Jane aliongea huku akilazimisha tabasamu.
"Nyota hizo begani hapo si mchezo kama shemeji wako"
"Kawaida tu mwanamke kujituma unaipata hii, kama wewe tu ulivyo ndani ya ofisi hii"
"Nikupe hongera shosti wangu kwa hilo, haya nilisikia ulikuwa Ulaya umerudi lini?"
"Yaani hivi unavyoniona ndiyo naingia kazini kwa siku ya kwanza"
"Kumekupenda sana huko Ulaya"
"Halafu nyinyi mna tabia mbaya sana, yaani mmenivizia nimeondoka ndiyo mkafanya harusi yenu"
"Shosti sasa hapo sina kosa maana ulitutoroka wewe mwenyewe, yaani harusi ya Afande wako mwenyewe umeingia mitini"
"Ila hongera sana, Baba kijacho na Mama Kijacho"
"Asante shosti, wewe vipi mwenzetu lini tunakula pilau na sisi"
"Mwenzangu yaani hata mpango sina sasa hivi"
"Shosti usiseme hivyo umri unakimbia huu"
"yote mipango ya Mungu, nilikuja mara moja kukuona wacha nikukimbie mida hii nahitaji niwahi nyumbani nina ishu muhimu"
"Haya shosti, namba yako kwanza basi"
Walibadilishana namba za simu na waliagana, Inspekta Jane ndiyo alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya ofisi hiyo na kuondoka. Sara alifuata baada ya kufunga ofisi yake akiwa na furaha sana kwa kutembelewa na aliyekuwa hapatani naye akiwa chuo, alifurahi sana kuweza kuongea naye. Aliamini kabisa zile zilikuwa ni akili za kitoto tu kipindi wapo masomoni na sasa zilikuwa zimewaondoka, kinyongo alichokuwa nacho kipindi kile kilikuwa kimemuisha. Hakujua kabisa kuwa huyo aliyekuja hapo alikuwa ana kinyongo bado kisa Mwanaume aliyekuwa naye, hakujua kabisa huyo alikuja kumsalimia lakini si kwa nia ya urafiki.
Siku hiyo ilipita na siku nyingine ikafuata hatimaye nayo ikakatika na hata juma nalo likafutika, Inspekta Jane alikuwa tayari ana mawasiliano na mke wa Afande mwenzake. Urafiki wa kinafiki tayari alikuwa ameuanzisha tangu alipoenda siku ile ofisini kwenda kuhakikisha kama kweli alikuwa mjamzito. Mazoea yalienda na hatimaye iikafikia hatua akakaribishwa nyumbani kwa Afande mwenzake, napo alipazoea na hata alipomkuta Afande huyo alikuwa akimchangamkia ingawa alikuwa akijua alikuwa hahitaji uchangamfu ule aliokuwa nao. Sara akiwa hajui chochote kilichokuwa kimetokea kwenye maisha ya nyuma ya Mume wake alikuwa ni mwenye kuona walikuwa ni wana maelewano mazuri, Inspekta James naye alijua kulificha hilo suala na hakutaka mke wake awe na chuki na mtu mwingine. Aliweza kumficha na hata wakwe zake walipojua kuhusu hilo bado mke wake hakuwa akijua chochote kile, jinsi mke wake alivyokuwa akimpenda aliona kutakuwa na mtafaruku mkubwa sana ikiwa itajulikana. Alikuwa akijulikana aliwahi kupata na upofu lakini hakuwa akijulikana aliwahi kunyanyaswa na hata kutupwa jalalani, yote yalibaki siri yake ingawa hakutakiwa kukaa na siri kwa mke wake.
Chuki aliyokuwa nayo kwa Inspekta Jane bado alikuwa nayo na haijaisha hata kidogo, moyo wake ulikuwa unagoma kabisa kuwa na ukaribu na mtoto wa adui yake ambaye aliwaua wazazi wakena kumtia upofu. Kugoma kwa moyo ndiyo kulimfanya hata asihitaji kuwa karibu na binti huyo, hakutaka kuulazimisha moyo kwani alikuwa akijua wazi kufanya hivyo ni kujidanganya. Aliamua kuendana na moyo jinsi ulivyokuwa ukitaka na si alivyokuwa akitaka yeye. Kila alipoiona sura yake alikuwa akikumbuka jinsi alivyopigwa nyumbani huku akifokewa, kumbukumbu ya tukio hio ilimkumbusha na jinsi alivyokuwa akisikia sauti za wazazi wake siku ambayo waliuawa. Kutokana na kumbukumbu hizo kiukweli kabisa hakutaka kabisa kuiona sura ya Inspekt Jane, uwepo wa ajira nao ulimfanya awe anamuona kila siku.
****
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa Inspekta Jane kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda alikuwa akijaribu kumsahau Inspekta James lakini ilishindikana. Alianzisha hata uhusiano na mwanaume aliyekuwa na mvuto kama Inspekta James lakini bado alishindwa kumsahau, hii ilifanya hata aweze kuachana na mawanume huyo kwa ugomvi mkubwa san. Ugomvi huo ulitokana na yeye kutaja jina la 'James' akiwa yupo kunapo kati ya raha na mwanaume huyo, mtafaruku huo uliotokea kwenye chumba cha hoteli ulikuwa ukielekea kumuumiza na laiti kama angekuwa si Asakri basi angeumia vibaya. Siku hiyo aliondoka kwenye chumba hicho cha hoteli akiwa ametumia mafunzo yake ya kijeshi kumjeruhi huyo Mwanaume wake aliyeingiwa na wivu akataka kumpiga. Tangu siku hiyo aliona hana haja ya kuudanganya moyo wake ikiwa alikuwa akilikumbuka jina la aliyekuwa akimpenda akiwa yupo na mwingine.
Jina la James lilikuwa limemkaa kichwani na hata kinywani na hakuwa na namna ya kulisahau kabisa,hitaji la kuwa la kuwa na Inspekta James lilikuwa limezidi upande wote na akaona alikuwa akimhuhitaji zaidi. Taratibu hitaji hili lilikuja kumfanya ajihisi na wivu kila akimuona Inspekta James akiwa yupo na mkewe, aliona kama alikuwa akidhulumiwa na mwanamke mwenzake ambaye alikuwa na haki. Jambo hili llimfanya aitie vituko ndoa hiyo kila mara lakini kutokana uimara wa wapendao nao hao, waliweza kuvikabilia vituko vyote. Inspekta Jane hakuchoka aliendelea na harakati za kuifanya ndoa hiyo isidumu kabisa, yote alishindwa kwani alikutana Mwanamke ambaye alikuwa na moyo thabiti katika kumpenda mume wake. Alifikia hata hatua ya kuwatuma wanawake waje nyumbani kwa Inspekta Jame wakijifanya ni mahawara zake walikuwa hawahudumiwi, yote alishindwa kabisa kwani kila walichokuwa akiambiwa aliamini ni uongo kabisa. Walipozidi kuja mara kwa mara ndiyo aliamini walikuwa wakitumwa, upendo na kuaminiana ndiyo ilikuwa silaha ya ndoa hii ndiyo Inspekta Jane alishindwa kuishambulia hadi iyumbe.
Alipoona alikuwa hawezi kumuweka Inspekta James kwenye himaya aliamua kuvuruga kila kitu, alikuwa yupo radhi amkose na mke wake pia amkose kuliko kumuona akimuumiza moyo wake. Hii ilimfanya apange mpango wa kutaka kumuangamiza Inspekta James akiona roho yake itatulia ikiwa ataondoka kwenye uso wa dunia hii, alianza kuutekeleza mpango kwa kutaka kumuwekewa sumu mara mbili alipokuwa akija nyumbani kwake lakini jaribio hilo lilishindikana. Muumba alikuwa yupo na wanandoa hawa ndiyo maana hata majaribio hayo yalishindikana, alijairbu tena kumuwekea kwenye kinywaji sumu alipojumuika nao kwenye matembezi. Siku hiyo alifanikiwa kumuwekea sumu lakini bahati mbaya kinywaji hicho kilimwagika kabla hata hakijatumiwa na Inspekta James. Bado hakuchoka na aliamua kuumiza kichwa kwa mra nyingine, alitafuta mbinu nyingine ya kumuua Inspekta James na hatimaye akaona jaribu bahati yake kwa siku ya mwisho. Alijiapiza akishindwa kwa mbinu hiyo basi hatojaribu mbinu nyingine tena, ukatili aliokuwa nao baba yake naye tayari ulikuwa umeshavamia moyo wake.
Siku ya siku ambayo alikuwa amedhamiria kumuua Inspekta James kwa mbinu nyingine kabisa, ilikuwa ni siku ambayo Mama yake mzazi alikuwa akija kumuona kazini ili amuage kwani alikuwa akisafiri ghafla. Pia ilikuwa ni siku ambayo Sara akiwa pamoja na Mama yake walikuwa wametoka kuwachukua wakwe wa hiyari wa kule shamba walikuwa wakija nao mjini, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Sara hivyo walikuwa wakija kuhudhuria sherehe ambayo ingefanyika hapo baadaye nyumbani kwa Inspekta James. Majira ya kufanya hila ilipokaribia ilikuwa ni muda ambao Inspekta Jame alikuwa akitoka ofisini mara moja, Insekta Jane alikuwa amelitambua hilo na tayari alikuwa ameharibu breki ya gari.
Inspekta Jame alitoka hadi ndani nje na akaingia ya gari lake na alipoingia aliliwasha, alipotoka kuondoka alikumbuka alikuwa amesahau kitu muhimu ofisini kwake. Kutokana na haraka aliyokuwa nayo aliacha gari ikiwa inawaka na kisha alikimbia ndani ili awahi aje kuendelea na safari. Muda ambao anatoka kulikuwa na mahabusu waliokuwa wakishushwa kwenye gari baada ya kutoka mahakamani, kitendo cha kuacha ufunguo namna ile kilikuwa kimeonwa na Askari mmoja bandia aliyekuwa amechomekwa kumuokoa Mhalifu mwenyewe aliyekuwa anatoka mahakamani. Walitazama kila upande na kwa kasi ya ajabu yule Askari bandia aliwashambulia Maasakari halisi na kisha alikimbia pamoja na Mahabusu ndani ya gari ya Inspekta James, waliliondoa kwa kasi sana huku wakiacha risasi zikituia juu ya bati la gari hilo. Lango muda huo lilikuwa lipo wazi na walilivuka sasa wakawa wanakaribia barabarani, ilimbidi Yule Mhalifu aliyekuwa akiliendesha gari hilo akanyage breki kupunguza mwendo. Hawakujua kama gari hilo lilikuwa limeshaharibiwa breki, loh! alipokanyaga breki ilikuwa hakuna hata ya kupapasia. Mhalifu huyo alijikuta akikanyaga breki hata kasahau kuangalia mbele kwa jinsi alivyochanganyikiwa, mwenzake ambaye alijifanya Asakri alikuja kumgusa kumfanya aangalie mbele alikuwa tayari ameshachelewa. Alikutana uso kwa uso na gari aina ya toyota landcruiser, kishindo cha kugongana kilifanya hata magari hayo yayumbe na kulivamia gari jingine ambalo lilikuwa likipita kwa kasi likitokea njia iliyokuwa ikielekea nje ya mji. Ilikuwa ni ajali ya magari matatu ambayo iliwacha midomo wazi wote waliokuwa hapo karibu kutokana na jinsi magari hayo yalitoa kishindo.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maaskari magereza ambao walikuwa wakiwafukuza wale Wahalifu kwa risasi waliwasili hapo wakaikuta gari ya mkuu wao ikiwa haitazamiki kwa jinsi ilivyoharbika, pia walizishuhudia gari zingine mbili ambapo moja ilikuwa ikijulikana wazi kwao. Wote walipigwa mshangao na hata walibaki wakiwa wamezubaa kwa sekunde kadhaa, walikuja kushutuliwa na kelele za Inspekta James ambaye alikuwa ameyaona magari hayo.
"Saraaaa!" Inspekta Jame alipiga kelele kwa nguvu huku akiliendea gari dogo moja lililokuwa limepondeka kutokana na ajali hiyo.
Loh! Aliliona gari la mke wake ambalo alilitambua kupitia bati la namba za usajili, Inspekta James siku hiyo alichanganyikiwa kabisa. Makelele yalimtoka kama mwendawazimu huku akilisogelea gari la Sara ambalo alilizunguka, kupondeka kwa gari hilo ndani aliona taswira ya kimiminika chekundu jambo ambalo lilifanya ndiyo azidi kuchanganyikiwa hata akajaribu kuvuta kuvuta mabati hayo yaliyokuwa yakipondeka. Ugumu wa mabati ulikuwa si kuvutika na mikono ya mwanadamu, hivyo Inspekta James alionekana ni mwenye kucheza tu na si kufanya chochote. Alipokuwa akipiga makelele hayo alisikia sauti ya makelele mengine kabisa, makelele hayo yalimfanya anyamaze kwa ghafla na aangalie kule ambapo kelele hizo zilikuwa zikitoke. Aliweza kumuona Inspekta Jane naye akilia akiwa amesimama kwenye landsruiser ambaye ilikuwa imepatwa na ajali hiyo, aliisikia sauti yake akilalalamika kwa kutaja jina la mama yake. Aliganda kwa sekunde kadhaa akimtazama hadi plae akili yake ilipokaa sawa na kurudisha macho kwenye gari la mke wake. Inspekta James naye alijikuta akilia kwa uchungu sana hadi maaskari wa chini yake wakaja kumkamata na kumshikilia kiuimara zaidi, muda huo tayari kikosi cha uokoaji cha jeshi la magereza pamoja na jeshi la polisi kilikuwa kimewasili.
Kazi ya utoaji miili kwenye magari ilikuwa ni ngumu sana kutokana na jinsi yalivyokuwa yamepondekza magari yote, kutokana na magari hayo kuwa katika kasi kipindi yanagongana. Inspekta James akiwa ametulizwa chini kwa nguvu sana aliweza kushuhudia ndani ya gari lake kukitolewa miili ya wale waliokuwa wameiba gari lake na kujaribu kutoroka. Hao ndiyo walikuwa chanzo cha ajali na kila alipowatazama mmojawapo alikuwa amevaa sare kama zake, loh! Alianza kuliona vazi ambalo alikuwa amevaa lilikuwa limefanya mauaji hayo. Saikolojia yake ilikuwa tayari imevurugika kama alivyokuwa akiziona sare hizo kipindi cha nyuma, alipowatazama wale maaskari waliomshikilia aliona kama alikuwa ameshikiliwa na wauaji vile. Vazi la pili la kifungwa aliliona ni mojawapo ya vazi ambalo lilikuwa likihusika na tukio hilo baada ya kuliona kupitia mwili wa Yule Mahabusu ambaye alikuwa anatoroka. Alianza kupiga kelele huku akituhumu lakini hakuachiwa kutokana na kuonekana alikuwa amechanganyikiwa, akiwa kwenye kupiga kelele huko ambako kulichnganyika na kilioo. Aliweza kushuhudia pia gari ya mke wake ikikatwa mabati na kisha mwili wa kwanza ukatolewa ukiwa hauna uhai.
Hakika alimuona Sara akiwa ameumia sehemu mbalimbali za mwilini, mwili wake ulikuwa haujengi taswira nzuri kutokana na kujaa damu sehemu mbalimbali. Inspekta James alilia zaidi akimtazama mke wake aliyekuwa na ujauzito akifunikwa na shuke jeupe, aljaribu kufurukuta kwenye kundi la Askari waliokuwa wamemshikilia lakini hakufua dafu. Uokoaji uliendelea na hata aliishuhudia miili mingine mitatu ambayo ilikuwa ikitambulika kwenye macho yake ikitolewa, alizidi kuchnganyikiwa aliipoiona miili ya wazazi wake wa hiyari pamoja na Mama mkwe wake ikifunikwa na shuka pia. Kilio kilimtoka hadi nguvu zikaanza kumuishia, akiwa yupo kwenye hali hiyo alijikuta akishtuka baada ya kusikia makelele mengine ya mtu ambaye alikuwa amechnganyikiwa.
"Uwiiiii! Nimemuua Mama yanguuuuu!" Sauti ya Inspekta Jane akiwa akiwa ameshikiliwa alipouona mwili wa mama yake nayo ilipaa hadi ikafika mwenye masikio yake, hasira zilimpanda aliposikia kauli hiyo na akaona kabisa ajali hiyo ilikuwa ikihusika na mikono ya Inspekta Jane.
Kutokana na kuwa mwenye kuishiwa nguvu Maaskari waliokuwa wamemshikilia walilegeza mikono, walipokuja kutahamaki Inspekta James alikuwa tayari ameshawachomoka ghafla. Walimuona akitoka mbio huku akielekea kwenye eneo ambalo alikuwepo Inspekta Jane aliyekuwa amevaa mavazi kama yake, alipomkaribia alirusha ngumi ya nguvu sana lakini mkono wake uliwahi kudakwa na Maasakri wengine waliokuwa wapo pembeni ambao walimuwahi. Hapo alishikiliwa na watu wengi zaidi kuliko awali kutokana na kuonekana alikuwa amechnganyikiwa, kundi kubwa la Maaskari waliokuwa wamemshikilia walikuwa wakijaribu kumrudisha nyuma kutoka kwenye eneo hilo. Inspekta James alipoona hakuwa amepata wasaa wa kuweza kumtia adabu mbaya wake aliishia kupayuka na kumtuhumu kwa kile alichokuwa akikifanya, alikuwa akiwapa faida watu waliokuwa wamekuja kushuhudia tukio hilo la ajali.
"James nisamehe mimi sikujua kabisa, kukupenda ndiyo chanzo cha haya. Niliona bora tukose wote kukuua wewe kumbe natafuta matatizo mengine zaidi" Inspekta Jane aliropoka huku akipiga kelele kwa nguvu sana, haikupita muda alipoteza fahamu na maaskari waliokuwa wamemshukilia walimpeleka kwenye eneo la huduma ya kwanza.
Hali ilikuwa tete kwa Inspekta James pia kutokana na kuusikia ukweli, shinikizo la damu ambalo halijawahi kumsumbua kwa mara ya kwanza lilimsumbua na alipoteza faamu akiwa yu mwenye hali mbaya sana. Alianza kupatiwa huduma ya kwanza na maaskari wenzake lakini hali ilizidi kuwa tete kila walipokuwa wakihakiki vipimo vya shinikizo la damu, lilikuwa likishuka kila muda waliokuwa wakihangaika naye kumpatia huduma ya kwanza. Hali hii ilifanya gari la wagonjwa liitwe upesi na yeye kukimbizwa hospitalini ili kuokoa maisha yake. Zoezi la kutoa mili ndani ya magari yote baada ya kukamilika, gari la kuchukua miili hiyo liliibeba kwa jili ya kwenda kuhifadhiwa. Baada ya gari hilo kuondoka mabaki ya magari yaliondolewa eneo lote na babrabra ilisafishwa, gari lenye kubeba magari yaliyopatwa na ajali lilifika hapo. Magari yote matatu yalibebwa kwa kifaa maalum na kuwekwa kwenye gari hilo, yaliondolewa eneo hilo na barabara ikabaki ikiwa ni yenye mabaki madogo ya vioo.
****
Taarifa za kutokea kwa vifo hivyo zilimfikia SP Mwambe akiwa yupo ofisini kwake, ilikuwa ni siku ambayo alilia kama mtoto mdogo alipoipata taarifa hiyo akiwa ofisini. Kazi zote hazikufanyika kabisa na hata usafiri wake mwenyewe alishindwa kuuendesha, siku hiyo alishikiliwa na kupelekwa hadi hospitalini ambako miili ya awapendao ilikuwa imehifadhiwa. Akiwa ni mwenye kuongozana na kijana wa chini yake kicheo aliweza kupelekwa kuona miili hiyo, kilio kilizidia baada ya kuiona miili yote. Hakuwahi kuwaza kama ipo siku watu hao awapendao watakuja kuondoka ndani ya dunia hii na kumuacha peke yake akiwa hana ndugu yeyote. Mke wake na mtoto wake wa pekee wote walikuwa wamefarikia siku moja, ni pigo ambalo hajawahi kulipata kwenye maisha yake yote ambayo aliyapitia. Pigo la kwanza kulipata kwenye maisha yake ilikuwa ni kufiwa na mtoto wa kiume aliyefariki akiwa bado mchanga kabisa, alipopta mtoto wa kike katika uzao wa pili moyo wake ulitulia na upendo aliuweka kwa mwanae. Sasa mtoto wake huyo pekee ndiyo alikuwa amemuacha bila hata kusema hata kwaheri, utuzima wake aliokuwa nao siku hii alilia kama mtoto mdogo
Hali ilikuwa ni hiyohivyo kwa Kamishna Msaidizi Philipo Lutonja alipopokea taarifa za kifo cha mke wake, alilia sana kwa kumpoteza Mwanamke ambaye alikuwa akimpenda sana. Mwanamke ambaye alihangaisha moyo wake kumpata na hata akasaidiwa na rafiki yake Marehemu SSP Nkongo katika kumpata, sasa hakuwepo naye kabisa ndani ya dunia hii. Upweke tu ulikuwa ukiuvaa moyo wake pindi alipokuwa akiondoka mbali naye, alikuwa akitamani arejee hata alipokuwa yupo safarini kutokana na kutamani kuwa naye kila dakika. Sasa alikuwa ameondoka kiumjumla na hatarejea tena, hakutarajia kabisa jambo kama hilo kama litaweza kuja kumpata. Kilio chake naye kilipelekea kupoteza fahamu kama Inspekta James kutokana shinikizo la damu kupanda, siku nzima hakuamka alikuwa yupo mahututi kitandani. Matabibu walikuwa wakihangaika katika kuyaokoa maisha yake, alipokuja kuzinduka kutoka kwenye kuzimia huko alikuwa hawezi hata kutembea. Msiba tayari ulikuwa umewekwa na yeye alikuwa yu kwenye kiti cha magurudumu katika muuda wote aliokuwa yupo msibani, alikuwa ni mkimya ana asiyetaka kuongea na mtu yeyote. Huduma zote muhimu alikuw akifanyiwa kutokana na mshtuko huo aliokuwa amepata, hakuwa na tofauti kabisa na Mlemavu. Binti yake aliyekuwa amesababisha tukio hilo alikuwa tayari amerukwa na akili, alikuwa amefungwa kamba ndani ya chumba komoja cha nyumba hiyo huku akifanyiwa huduma zote kama ilivyo Baba yake. Mtoto wake mkubwa ndiyo aliongoza kila kitu kutokana na ndiye mtu pekee ambaye angeweza kusimamia, hakukuwa na mwingine ambaye alikuwa anajiweza ndani ya nyumba hiyo isipokuwa yeye tu.
****
Inspekta James alipokuja kurejewa na fahamu hakuwa na tofauti kabisa na mtu ambaye alikuwa amerukwa na akili, alikuwa akihudumiwa kila kitu katika kipindi chote cha msiba. Tofauti yake hakuwa mtu mwenye fujo yeye alikuwa kimya tu huku akiongea maneno ambayo yalikuwa hayana maana katika muda wote, alikuwa haishi kulitaja jina la mke wake. Hali hiyo ndiyo ilizidi kumuumiza SP Mwambe, mtu pekee wa karibu aliyekuwa amebakia alikuwa ni huyo ambaye amerukwa na akili. Wazee aliokuwa amesaidiana katika malezi ya Inspekta James nao walikuwa wapo kwenye vyumba vya kuhifadhi miili wakisubiria kwenda kupumzishwa kwenye nyumba zao za milele. Hatimaye siku ambayo ilikuwa imepangwa kuipumzisha miili ya marehemu wanne walioaga dunia ndani ya siku moja ilitimia, huu ulikuwa ni msiba wa pili kwa James kufiwa na watu wake wa karibu wenye idadi kama hiyo tangu walipoanza wazazi wake na Bibi yake. Muda wa kuaga miili hiyo kabla ya maziko James aliletwa akiwa ameshikiliwa kutokana na kurukwa na akili, marafiki zake wa karibu walikuwa akimuonea huruma sana kutokana na hali hiyo ambayo walikuwa nayo. Alifanikiwa kuuaga mwili wa mke huku akicheka kama ilikuwa habari ya kufurahisha kutokana na kurukwa na akili, miili mingine aliiaga kinamna hiyohiyo na kisha aliondolewa na taratibu zingine zikafuata. Mazishi ya miili yote minne yalifanyika jijini Dar es salaama kwenye Makaburi ya KInondoni, watu wengi waliokuwa wameguswa na tukio hilo walihudhuria huku wakimshudia Inspekta James alivyo.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa nyumbani kwa Kamishna Msaidizi Lutonja mazishi yalifanyika siku inayofuata baada ya kufanywa mazishi ya watu wa karibu wa SP Mwambe, watu wengi nao waliokuwa wameguswa na hali ambayo ilikuwa imempata Afisa huyo wa jeshi la Magereza walihudhuria kwa wingi. Ulikuwa ni msiba mkubwa lakini haukua umeuzidi ukubwa msiba ulifanyia siku iliyopita, wanahabari waliokuwa wakisaka habari kwa udi na uvumba kama ilivyokuwa kwenye msiba uliopita, walifurika kwa wingi sana kwenye msiba huo. Mazishi yalifanyika kwenye makaburi yaleyale yaliyofanyika mazishi siku iliyopita, Mume wa marehemu alishuhudiwa akiwa yu kwenye kiti cha magurudumu kutokana na kupatwa na hali mbaya kwa kifo cha mke wake. Watoto wote wa marehemu walikuwa wapo eneo hilo la maziko, Inspekta Jane waliweza kumuona akiwa yupo kwenye mikono ya maaskari imara wa jeshi hilo kutokana na kurukwa na akili. Wengi waliomuona walimulaani sana kutokana na kusababisha kifo cha mama yake mzazi, hawakujali hali ya kuchnganyikiwa ambayo ilikuwa imemkumba wao waliangusha laana zao pasipo kuzitamka waziwazi kutokana na kuingiwa na hasira. Binti kusababisha kifo cha mama yake kisa kutaka kumpoteza Mwanamke aliyekuwa hana mapenzi naye, ilikuwa ni jambo ambalo waliona alikuwa si kiumbe wa kawaida. Wengi walimuhukumu huku wakisahau hakuwa ni malaika bali alikuwa mwanadamu kama wao, alikuwa anakosea kama wanavyokosea wao. Maneno ya wanahabari wa magazetini yalikuwa tayari yamewapa sumu, hiyo ilikuwa ni habari ambayo ilitawala jiji zima na hata picha zake zilikuwa zimeshasambaa kwenye magazeti mbalimbaoli. Hakuna ambaye alikuwa haijui sura yake kutoka na jinsi magazeti yalivyoichapisha, wengi waliitambua vyema sura hiyo na haikuwapa shida kuanza kumnyoooshea vidole huku wakimuongelea vibaya. Pamoja na kurukwa huko na akili bado hawakumuonea huruma kabisa, wao waliendelea kumfanya mada katika eneo hilo la msiba hadi mazishini.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment