Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

KAHABA YUAN LIANG - 2

 









    Simulizi : Kahaba Yuan Liang

    Sehemu Ya Pili (2)





    …………………………………



    Ikulu; Chumba cha siri



           Waziri mkuu Januari Sasamba, pembeni yake alisimama waziri wa ulinzi, nyuma yao walisimama wapelelezi wawili waliotegemewa na nchi ya Goshani, Kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini. Bila shaka kuna ujumbe muhimu walimletea raisi Jonsoni Mtemvu, bila kujua siri nzito aliyoificha moyoni mwake, alionywa, akisema, atauawa, alipaswa kumwambia mtu mmoja tu wa kupeleka pesa, pesa nyingi sana ambazo zilizidi bajeti ya nchi…



    “,Mkuu, tumefanikiwa kupata msaada, usiku wa leo tunategemea kupata wapelelezi wa kimataifa kutoka Tanzania, the super three soldiers, kama ulivyonipatia maelekezo awali ……”,Januari Sasamba aliongea, akimtazama raisi aliyekuwa ameketi kitandani, uso haukuwa na tabasamu, alikosa furaha, Januari Sasamba alitambua jambo hilo, uso wa rafiki yake aliutambua nyakati zote za furaha na huzuni, tangu wakiwa masomoni, chuo kikuu cha Goshani.



    “,Vipi mkuu uko sawa kweli? “,Jonsoni Mtemvu aliuliza.



    “,Hayuko sawa, ugonjwa wa shingo bila shaka unamuumiza! “,waziri wa ulinzi, Saidi Mbeku aliongea.



    “,Msijali niko sawa, hakikisheni mnawapokea vizuri na kushirikiana nao kwenye kazi ili mtuhumiwa apatikane na diski ipatikane, mnaweza kwenda! lakini waziri Januari Sasamba naomba ubaki mahali hapa ……”,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Sawa mkuu, saluti! “,saluti zilipigwa, waziri wa ulinzi akatoka nje, akifuatiwa na kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini, waziri Januari Sasamba akabaki ndani ya chumba cha siri.



    …………………………………



    “,Tunapata wapi bilioni kumi?, zinahitajika kesho saa tano usiku, na wewe ndiye unapaswa kuzipeleka hakuna mwingine, ili kuikomboa diski, anasema tusipopeleka pesa, au tukaenda na polisi, ataweka wazi kila kitu, atatuuwa ……”,Jonsoni Mtemvu aliongea, akiwa amechanganyikiwa.



    “,Pesa zote hizo zinaenda wapi?, bajeti tu ya nchi bilioni moja,nani anahitaji? “,akiwa amejawa na mshangao, Januari Sasamba aliuliza.



    .



    “Mwanamke yule mwizi kanipigia nusu saa iliyopita,amesema atatupatia taarifa mahali pa kupeleka pesa ,japo hatuna pesa hizo, ni nyingi sana! “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Ngoja nikwambie, pesa za bandia zipo,mzigo tayali umeingia, tutatumia kumpekea na kumnasa! “,Januari Sasamba aliongea.



    “,Hapo sawa, itakua rahisi kumkamata, kama atakua hajakamatwa na wapelelezi kutoka Tanzania, naomba uwapatie ushirikiano wakifika, kazi njema, tutazidi kuwasiliana, “raisi Jonsoni Mtemvu aliongea, kisha akamruhusu Januari Sasamba kuondoka.



    …………………………………



    01:20pm, Goshani



           Helikopta yenye chapa ya Tanzania, ilitua makao makuu ya jeshi nchini Goshani, makamanda watatu walishuka, usoni walivaa miwani ya rangi nyeusi, chini walivaa suti nyeusi, miguuni walivaa viatu vyeupe, walifanana kwa kila kitu.



    “,Karibuni sana, karibuni sana Goshani! “,waziri wa ulinzi,Saidi Mbeku  aliongea, akawasalimu wageni wake, “,Asante sana, tumekaribia! “,Kendrick, kamanda namba moja alijibu kwa niaba ya wenzake,kisha waziri akawaongoza mpaka kwenye difenda za polisi, wakapakiwa, wakapelekwa hotelini.



    Costa;Goshani



         Difenda ya polisi ilisimama pembeni na hoteli, “High Classic Hotel “,ilisomeka, mabegi yao yakashushwa kwa msaada wa askari,moja kwa moja mpaka kwenye vyumba vitatu vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili ya wapelelezi kutoka Tanzania. “,Funguo zenu hizi hapa, mmoja atalala namba 20,mwingine 21 na watatu atatumia chumba namba 22,karibuni sana, tutaonana kesho asubuhi, salutii …”,Waziri wa ulinzi Saidi Mbeku aliongea, akakabidhi funguo kwa kamanda Kendrick, wakapigiana saluti, kisha akatoweka yeye pamoja na msafara wake.



    “,Karibuni sana,kila huduma mtaikuta ndani ya vyumba vyenu, chakula na kila kitu kwa ajili yenu kimeshalipiwa, mkiwa na tatizo tupigieni kupitia simu za mezani ndani ya vyumba vyenu, “muhudumu wa hoteli,alitoa maelekezo, huku akiwaongoza askari wa tatu wa kundi la the super three soldiers, kuelekea kwenye vyumba vyao.



    “,Hiki ni chumba namba ishirini, kinachofuata ni namba ishirini na moja, cha mwisho ni ishirini na mbili …”,muhudumu yule wa kike aliongea, alivutia kwa kila kitu, hakuchosha kutazamwa na kamanda Kendrick pamoja na kamanda Philipo.



    “,Asante, tumekuelewa! vipi nikiwa na shida binafsi na wewe nakupataje? “,Kamanda Kendrick alijikuta ameropoka, kilicho ndani ya moyo wake.



    “,Naitwa Ansie, napatikana vyumba vya wahudumu ghorofa ya mwisho, namba zangu ni zero saba ……”,muhudumu alimjibu Kamanda Kendrick,huku akibetua betua midomo yake, akiyarembua macho yake.



    “,Bwanaaaeee,hebu ingia ndani uko, umalaya wako mpaka nchi za watu! “,Kamanda Catherine aliona wivu, siku zote alimnyemelea kamanda Kendrick bila mafanikio, kazi zilimbana, alishindwa kuwa muwazi kuelezea hisia zake kwa Kendrick, aliamua kuvumilia,aliapa kusema ukweli siku moja.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Muone sura, wivu tu unakusumbua, “Kamanda Kendrick aliongea, huku muhudumu wa hoteli aliyejitambulisha kwa jina la Ansie akiondoka zake, huku makalio yake yakipepesuka huku na kule.



    “,Nikuonee wivu wewe, kwa pesa gani uliyonayo, mwanaume pesa bwanaa, “,Catherine aliongea,vidole vyake viwili alivichezesha hewani,mkono wake wa kushoto ulishika kiunoni.



    “,Hahahaaa “,kamanda Kendrick pamoja na



     kamanda Philipo walicheka, kisha wakaingia ndani ya vyumba vyao.



    …………………………………



    Chumba namba 22:



           Kamanda Catherine aliingia, akafunga mlango wake kwa ndani,”Duuuh walijuaje hawa, napenda sana chumba chenye gym ya kufanyia mazoezi,”akiwa amesimama alitabasamu, baada ya kuona chumba cha gym pembeni kabisa na mlango wake, akakifungua akakitazama, akazidi kutabasamu,akakifunga,akatembea kuelekea upande wa pili wa chumba, uso kwa uso na friji ya vinywaji, akaifungua,hakua mlevi, alifurahia juisi ya matunda, haikuwemo, akasonya, akachukua maji ya baridi kukata kiu.



    “,Washenzi kweli, wanafikiri sote walevi, nikiwa mlevi na kazi yangu hii, ata teke ntapiga kweli? “,kamanda Catherine aliongea, akanyanyua chupa ya maji, akanywa, sekunde tu, chupa ilikua tupu.



    Akavua suti yake ya bei ghari, akavaa nguo za kulalia, akajitupa kitandani, akauchapa usingizi …



    …………………………………



    Chumba namba 21:



              Kamanda Kendrick alikuwa bize akinywa bia, alipenda sana pombe licha ya kuonywa mara kadhaa na rafiki zake, lakini alishindwa kuacha tabia hii ambayo muda mwingine ilirudisha nyuma ufanisi wake wa kazi.



    Alifurahi sana kusogezewa vinywaji karibu yake, friji ilijaa pombe kuliko maji na juisi. Dakika tano tu tangu aingie chumbani,chupa tupu tatu za bia aina ya Safari, zilitelekezwa pembeni.



    Dakika kumi baadae alikuwa amekunywa bia sita, akatosheka, akajitupa kitandani, tai yake ilikuwa shingoni, suti yake ilikuwa mwilini, viatu vyake vilikuwa mwilini …



    …………………………………



    Chumba namba 20;



         Kendrick, the super three soldier namba moja, kiongozi mkuu wa kundi, alingia ndani ya chumba chake, kilikuwa na mwonekano mzuri sana, akaangaza huku na kule, akatabasamu, alifurahi sana kuona chumba cha kufanyia mazoezi (gym room).



    “,Walijipanga sana, wamedhamiria kutuandaa vizuri, tutajitoa kuwasaidia, wametupokea vizuri sana …”, Aliongea, akakikagua chumba chake vizuri, akapanga vifaa vyake vizuri, akavua suti yake,akavaa nguo za kulalia na kujipumzisha kitandani, huku akitafakari namna ya kuianza kazi yake jua litakapochomoza.



    …………………………………



    Huwei; Costa, Goshani



            Harakati ziliendelea kama kawaida katika mji mdogo wa Huwei, kaskazini mwa jiji la Costa nchini Goshani, watu wa eneo hili hawakuwa na muda wa kulala,asubuhi, mchana na usiku harakati ziliendelea, biashara haramu ndizo zilipelekea mji huu kukua kwa kasi.



    “,Dada unaenda wapi, lipia  pesa kabla hatujakuchafua sasa hivi, kama unaishi ndani ya jengo hili, onesha funguo za chumba ……”,pande la baba liliongea, lilikuwa na urefu wa futi saba, kifuani lilijazia, kwa kukadiria mtu huyu alikuwa na uzito wa takribani kilo mia moja.



    “,Ninaishi chumba namba therathini, sina historia ya kutembea na funguo, “Yuan Liang aliongea kwa kujiamini, bila wasiwasi wowote.



    “,Kama huna funguo, toa pesa, “jibaba lile liliongea, mikononi na kila sehemu ya mwili wake ilijaa tatoo na michoro ya kila aina.



    “,King of Huwei, Mfalme wa Huwei) “,Yuan Liang alisoma maandishi kwenye mkono wa kushoto wa jibaba lile lililokuwa limesimama mlangoni, akacheka kwa kejeli, akatoa dola kumi mfukoni,mara mbili zaidi ya pesa za kiingilio cha club ya muziki, ghorofa ya pili, akamrushia.



    “,Acha dharau we mwanamke, ntakutwanga ngumi sasa hivi ……”,jibaba lile liliongea, huku likiokota pesa lilizorushiwa, Yuan Liang akasonya tena kwa dharau, akaingia ndani.



    “,Unanisonya eee? tutaona utapita wapi wakati wa kurudi! “,jibaba lile liliongea, likaendelea na shughuli zake.



    ………………………………



    Casabranka Casino;



          Yuan Liang aliingia ndani ya club ya muziki, watu walibanjuka kwa staili mbalimbali, wengine walicheza nusu utupu huku wakirushiwa pesa na wanaume wenye pesa zao.



    Yuan Liang akajisogeza kaunta, aka agiza kinywaji, dakika mbili mbele, pombe kali aina ya konyagi ilisogezwa mbele yake, akaifungua, aka agiza maji pamoja na glasi,dakika moja mbele akaletewa glasi pamoja na chupa ya maji, maji ya Kilimanjaro kutoka nchini Tanzania.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akachanganya kwenye glasi, akaanza kunywa, huku midume na watu wenye pesa zao wakimtamani, wengine walikuwa makapuku, wengine walikuwa na pesa zao.



    “,Samahani dada tunaweza kukaa pamoja, “pedeshee mmoja mwenye kitambi kikubwa aliongea, kichwani alikuwa na kipara, hakuwa mfupi sana wala mrefu sana, alikuwa na kimo cha wastani.



    “,Usiwe na shaka! “,Yuan Liang aliongea, akiyalegeza macho yake yaliyojaa huba.



    “,Sijui dada unaitwa nani? “,mwanaume yule aliuliza, huku akiusogeza mkono wake kupapasa paja la Yuan Liang ambalo lilibaki wazi akiwa amekaa kwenye kiti.



    “,Usiongee sana sema una shilingi ngapi,? kama una dola mia mbili, utaonja penzi la mwanamke chotara wa kichina “,Yuan Liang aliongea.



    “,Nitakupatia dola mia tano, kwa saa moja tu! “,mwanaume yule aliongea, akafungua briefcase, noti nyingi zilipangwa zikapangika, Yuan Liang aliziona, akatikisa kichwa, akaashiria kukubali.



    “,Sisi kila kitu tunafanyia kwenye vyoo vyetu, twende huko! “,mwanaume yule aliongea, akanyanyuka, akaongozana na Yuan Liang.



    …………………………………



    Yuan Liang alifika katika vyoo vya kasino la Casablanca, akiwa ameongozana na pedeshee mwenye uchu wa mapenzi, kila mmoja alikuwa na mipango yake kichwani.



    “,Nikirekodi filamu ya ngono na mwanamke huyu, nitauza sana, nitapata pesa nyingi “,Mwanaume yule aliongea peke yake ndani ya nafsi yake, akaufungua mlango wa choo, akawa wa kwanza kuingia, Yuan Liang akafuatia, wakafunga mlango kwa ndani.



    “,Namuua kwa dakika moja, napitia dirishani, narukia ghorofa ya juu mpaka chumbani kwangu, natoweka na pesa zake, nahama hoteli hii, anakosa penzi na pesa vyote kwa pamoja! “,Yuan Liang aliongea, huku akikichunguza chumba cha choo, ghafla akashtuka, machale yakamcheza.



    Aliiona kamera ya tofauti sana, ikiwa juu imefungwa mithili ya taa, akaitambua, akatabasamu, akachukua miwani yake, akaivaa, akabonyeza batani katika miwani yake,miwani iliyounganishwa na kifaa kidogo katika kisigino cha kiatu chake kilichofanya kazi ya kukata mawasiliano ya simu na kifaa chochote kile cha mawasiliano ,kama kompyuta na Kamera.



    Pedeshee yule akatabasamu,akaweka begi la pesa pembeni, akaanza kutoa mavazi yake, akabaki na nguo yake ya ndani, Yuan Liang akacheza na hisia za mwanaume yule, Yuan Liang akavua kimini chake, akavua brauzi yake, akabaki akiwa na matiti yake yaliyomsimama vilivyo, akamsogelea pedeshee yule, wakakumbatiana, wakaanza kunyonyana ndimi, Yuan Liang alipoona hisia za mwanaume yule zilimepanda, akachomoa kisu kidogo alipokuwa amekificha katikati ya kiatu chake, akamfunga mdomo ghafla huku akiwa amempiga kabali, pedeshee alishindwa kujitetea, alirusha miguu huku na kule, akachomwa kisu cha mgongoni, ndani ya sekunde kumi tu, roho ya pedeshee yule ikaacha mwili …



    Yuan Liang akajifuta damu kwa kutumia suti za pedeshee yule,chumba cha choo kilitapakaa damu kila kona, akavaa harakaharaka, akachukua  briefcase ya pesa, akajaribu kufungua dirisha likakubali, akapenya kwenye nondo, akaruka serekasi,akatua ghorofa ya tatu, akatokezea mbele ya chumba chake, akaangaza huku na kule hakuona mtu, akaingia ndani ya chumba chake ……



    …………………………………



    Costa; Goshani, 7;50am



             Kamanda Kendrick alikuwa amemaliza kupiga mazoezi,alikuwa na dakika kumi tangu akurupuke usingizini, akaelekea bafuni, akaoga, akamaliza, akachukua suti yake, akaivaa mwilini, suti nyukundu tofauti na aliyokuwa amevaa usiku uliopita, akachukua bastola yake, akapachika magazine,akachukua kisu chake kidogo kilicho chongoka kama msumeno,silaha zake akaziweka katikati ya koti lake,tayali alikuwa amekamilika,akatoka nje.



    Uso kwa uso akakutana na kamanda Catherine,utazani walijiandaa kwa pamoja,mtu mmoja tu alikuwa amekosekana,kamanda Philipo.



    “,Uko shapu kamanda,mzima lakini?”,kamanda Kendrick aliongea.



    “,Mimi mzima,sjui wewe?”,kamanda Catherine aliongea,wakapigiana saluti.



    “,Niko poa, ngoja tumuamshe huyu mvivu! “,kamanda Kendrick aliongea, akaanza kugonga mlango wa kamanda Philipo, aligonga kwa takribani dakika tano bila mafanikio, akausukuma, ukafunguka, wote wakaingia ndani huku bastola zikiwa mikononi, Kendrick pamoja na Catherine, waliingiwa na hofu kwa kugonga mlango wa kamanda Philipo kwa muda mrefu bila mafanikio …



    “,What, nini hiki shiit! “,kamanda Kendrick aliongea, macho yake yalikutana na chupa sita za bia zikiwa zimesambaa sakafuni.



    “,Yaani nilijua tu, tangu jana nilipo ona friji iliyojaa bia, nilijua lazima ndugu yetu tumpotezee, hahahaa ……”,kamanda Catherine alicheka sana, akimcheka kamanda Philipo aliyekuwa amelala na viatu baada ya kuzidiwa na pombe, wote kwa pamoja walirudisha bastola zao mahala pake, kamanda Kendrick akimhurumia rafiki yake kwa ulevi uliozidi kipimo, huku Catherine akicheka, alishindwa kujizuia.



    Huwei;Masaa sita nyuma



                Yuan Liang alifika ndani ya chumba chake,alihema kwa kasi sana, tayali alikuwa ametekeleza mauaji, akafungasha kila kitu cha kwake,akavua kimini chake, akavaa suruali nyeusi ya jinzi, akachomoa kifaa kidogo cha kwenye kiatu chake, kifaa maalumu cha kukata mawasiliano, akakipachika kwenye kiatu kingine chekundu, kisha akakivaa, tayali mizigo yake ilikuwa sawa, akatoka ndani ya chumba chake, akafunga, akashuka ghorofani akiwa na haraka sana …



    “,Funguo zako hizi hapa, nashukuru sana “,Yuan Liang aliongea, alikutana na mzee aliyempokea, mzee ambaye alipenda ujana pasipo kawaida.



    “,Sawa mrembo,lakini mbona mapema sana? “,mzee yule alipokea funguo, akamtwika swali Yuan Liang.



    “,Mind your own business (jali shughuli zako) “,Yuan Liang alijibu kwa jeuli, mzee yule akakasirika.



    “,Fuck you son of bitch …”,mzee yule alifoka, akamtukana Yuan Liang kwa kizungu, akamshika makalio yake, alimtukana na kumdharau.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Puuuuuu ……”,Yuan Liang aliacha mabegi yake, akaruka mateke mawili, yakampata usoni mzee yule, kishindo kikasikika, akaanguka mita kadhaa eneo la mapokezi,uso wake ukavimba. “,Unanitukana mi malaya unanijua vizuri, pumbavu wewe, jitu zima ovyoo! “,Yuan Liang alimkejeli mzee yule, watu walianza kukusanyika katika mlango wa mapokezi kushuhudia, Yuan Liang akatoka haraka, akapanda pikipiki yake, akatoweka eneo lile la Casabranka Kasino.



    …………………………………



    Chumba namba 25;



             Mitambo yao ilizima ghafla,mara tu kijana wao alipotaka kuanza mchezo mchafu wa ngono na kumrekodi,machale yakawacheza,walichunguza mitambo yao, hawakuona tatizo, mitambo yao ilikuwa sawa kabisa.



    “,Nenda kachunguze nini kimetokea, hakikisha mwanamke yule hagundui kama alitaka kurekodiwa mkanda wa ngono “,bilionea Xavery, raia wa Italiano aliongea, akamtuma kijana wake aliyekuwa akiongoza mitambo ya kurekodia filamu chafu za ngono.



    “,Sawa bosi, ngoja nikaangalie nani anataka kutuharibia kazi yetu, video zingine tumerekodi vizuri isipokuwa hii ambayo imezingua tu kabla hatujaanza ……”,kijana yule aliongea, akatoweka chumba namba ishirini na tano.



    “,Vipi dogo mbona mapepe sana, “jibaba aliyehusika kulinda mlango wa kasino aliongea, huku akimtazama kwa macho yaliyojaa udadisi kijana yule aliyehusika na kurekodi filamu za ngono.



    “,Kazi ilitaka kuanza, kamera ikazima ghafla, hatujui nini tatizo, nd’o naenda kukagua bro …”,kijana yule aliongea, jibaba lile la mlango wa Casino likampisha, akaingia ndani ya ukumbi wa muziki.



    …………………………………



    Kijana yule aliyekuwa na sura halisi ya Kiafrika, huku rasta ndefu zikining’inia vizuri katika mgongo wake, alipenya katikati ya watu waliokuwa wanacheza mziki bila wasiwasi wowote,wanawake waliokosa heshima kwa wazazi wao, walikua uchi wa mnyama wakicheza na kurushiwa pesa na mapedeshee wenye pesa zao, walirekodiwa kwa ajili ya video zao kuuzwa kila kona ya dunia,shughuli mbalimbali za kuuza silaha pamoja na madawa ya kulevya ziliendelea ndani ya Kasino.



    Alifanikiwa kuvuka makundi ya watu waliocheza muziki, akakunja kulia, akakunja kushoto, “TOILETS “,kibao kilisomeka,akaingia, moja kwa moja mpaka kwenye vyumba walivyotumia kurekodia filamu zao.



    Akakagua choo kimoja baada ya kingine, “Puuuuu! “,alidondoka mweleka, aliteleza kwenye damu baada ya kufungua choo kimoja, mwenzao alikuwa ameuawa kikatili.



    “,Yalaaaaa! ,wameuwaa, amekufaaa! “,alipiga kelele, akatoka akikimbia, suti yake ilikuwa imetapakaa damu baada ya kudondoka,watu wote ndani ya kasino waliacha shughuli zao, walikimbia kuziokoa nafsi zao.



    “,Mbona unakimbia dogo, nini kimetokea?,damu hizo zimetoka wapi? “,jibaba lile la mlango wa kasino liliongea, huku likiwapisha raia waliotoka ndani ya kasino kwa fujo kuyaokoa maisha yao.



    “,Wamemuua Bensoni, wamemuua! “,kijana yule aliyehusika na kurekodi filamu za ngono aliongea.



    “,Unasemaje?? nenda kamwambie bosi haraka sana …”, mlinzi yule wa kasino aliongea, sura yake ilitisha,kutokana na mwili mkubwa aliokuwa nao.Alipomaliza kuongea, kijana yule alitimua mbio kuelekea kwa bosi wake, bilionea Xavery aliyemiliki jengo lote la Casabranka,pamoja na biashara zote ndani ya jengo hili, kasino la muziki lilibaki tupu, isipokuwa wafanyakazi wa kasino hili.



    …………………………………



    Wafanyakazi wa kasino pamoja na hoteli ya Casabranka walikaa kikao,walitaka kujua ninani alihusika na mauaji.



    “,Kuna mdada alisema anakaa chumba namba therathini, ni chotara wa kichina, anaongea kiswahili bila tatizo lolote, alinipita mlangoni kwa jeuri, sikumuona wakati wa kutoka, bila shaka ndiye muhusika …”,jibaba la mlango wa kasino la muziki aliongea.



    “,Huyo ndiyo anakaa chumba namba therathini, nilimpokea jana tu, lakini amekabidhi funguo nusu saa baada ya mauaji, akanipiga na mateke akaondoka, sina shaka, huyo ndiye ameua! “,mzee aliyependa ujana aliongea, akitoa maelekezo kwa bosi wake Xavery.



    “,Muuaji apatikane haraka sana,sina shida na pesa wala mauaji aliyoyafanya, nataka aungane na sisi kwenye kundi letu, mbinu alizotumia zitatufaa sana, anafaa kwa shughuli zetu, akipatikana nitawalipa pesa nyingi kama zawadi ya kumtafuta …”,bilionea Xaviery aliongea, vijana wake wakamuelewa.



    …………………………………



    Mexic;



                Yuan Liang aliendesha pikipiki yake,ndani ya nusu saa tu, alifika katika  makazi mapya, alipaki pikipiki yake ndani ya hoteli ya hadhi ya chini,hoteli zote kubwa eneo la Mexic,kilomita tano kutoka mji wa Huwei zilikuwa zimejaa.



    “,Shilingi elfu kumi tu chumba! “,mama mmoja umri wa miaka arobaini alimpokea Yuan Liang, akamkaribisha katika nyumba yake ya kulalia wageni.



    “,Umeme upo?, napata mahali pa kuhifadhia pikipiki yangu? “,Yuan Liang aliuliza maswali mawili kwa wakati mmoja.



    “,Vyote vinapatikana, usjali mwanangu! “,mwanamke yule alimpatia maelekezo Yuan Liang, Yuan Liang akalipia shilingi elfu hamsini, akapaki pikipiki yake mahali alipoelekezwa, kisha yeye akelekea ndani kupatiwa chumba cha kupumzika, ikiwa yapata majira ya saa kumi usiku.



    …………………………………



    Costa; Goshani, 8;00am



            Kamanda Kendrick alimuamsha kamanda Philipo,kamanda Philipo akakurupuka usingizini, mwili ukiwa umejaa uchovu.



    “,Amka wewe twende kazini, muda wa kazi sasa hivi! “,kamanda Kendrick aliongea.



    “,Nimechoka sanaa, niacheni ninawe uso, nisafishe kinywa changu,kisha nioge! “,kamanda Philipo alijitetea,huku akijinyosha na kupiga miayo.



    “Muda umeisha, hakuna kuoga hapa, nawa tuondoke! “,kamanda Kendrick alimjibu kamanda Philipo.



    “,Unalala sana kama mwanamke,siwezi nikaolewa na mwanaume mlevi,anayelala sana kama wewe,”kamanda Catherine alimtania kamanda Philipo.



    “,Hahahaaa”,wote walicheka sana,kamanda Philipo akanawa uso,akapiga mswaki,akiwa na suti yake aliyolala nayo tangu jana,wakatoka kuelekea Ikulu kuonana na raisi wa nchi ya Goshani,tayali kwa ajili ya kuanza kazi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    …………………………………



    Ikulu; Chumba cha siri 9;20am



              “,Naitwa kamanda Kendrick, kiongozi wa kundi, huyu anaitwa kamanda Philipo, na huyu anaitwa kamanda Catherine “,kamanda Kendrick aliwatambulisha wenzake mbele ya raisi Jonsoni Mtemvu, akiwa amelala kitandani.



    “,Karibuni sana, nazani kila kitu kuhusu kazi mlishapatiwa maelekezo, tutatoa ushirikiano wowote mtakapohitaji, msisite kunijulisha “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Sawa mheshimiwa,sisi tunaomba tupate askari wa kutuongoza, tufike hoteli aliyokuwa akiishi mgeni wako, kisha tufike hoteli mliyokutana, mwisho tuonane na walinzi wako waliokuwa zamu kukulinda “,kamanda Kendrick aliongea.



    “,Sawa vijana, Kamanda Gupta! “,raisi Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Nipo mkuu “kamanda Gupta aliitika, akasimama.



    “,Kamanda Yasini! “,raisi Jonsoni Mtemvu aliita tena.



    “,Nipo mkuu, “kamanda Yasini aliitika.



    “,Waongozeni askari hawa wapelelezi, wapatieni ushirikiano kila hatua “,Jonsoni Mtemvu aliongea.



    “,Sawa mkuu “,wakaitikia, wakaanza kutoka nje, wakiwa pamoja na kundi zima la the super three soldiers.





    Green pick hotel; 10;02



             Difenda mbili za polisi zilifunga breki kwa mara nyingine tena, katika hoteli ya green pick. Kamanda Kendrick akiwa ameongozana na kundi lake, mara baada ya kutoka ikulu kuonana na raisi Jonsoni Mtemvu, walianza kazi haraka sana kwa kufika maeneno muhimu kwa ajili ya kufanikisha upelelezi wao.



    “,tumefika et ee, “



    “,yes afande, tumefika …”,



    “,Hapa ndipo mheshimiwa aliwasiliana na mgeni wake kwa simu? “,



    “,Ndio afande, ni hapa! “,



    “,Sawa,tupelekeni kwenye chumba alichokuwa anaishi mgeni huyo …”,



    “,Usjali afande, tufuateni …”,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kundi la the super three soldiers, pamoja na kamanda Gupta na mwenzake kamanda Yasini. Wote wakashuka kwenye difenda yao ya mbele, wakaelekea ndani ya hoteli, kamanda Gupta pamoja na kamanda Yasini walitangulia mbele, kamanda Kendrick, Catherine pamoja na kamanda Philipo wakawafuata kwa nyuma.



    Wakafika mapokezi, wakajitambulisha, wakaonesha vitambulisho kama kawaida, kisha wakaanza safari kuelekea chumba namba kumi na tano.



    “,Muhudumu, umesema mgeni huyu alikua anaitwa nani? “,



    “,Yweon Lee, “



    “,raia wa nchi gani? “,



    “,Japan, “



    “,ana umri gani? na alikaa hotelini kwa siku ngapi …”,



    “,kuhusu umri,sifahamu! lakini amekaa hapa kwa wiki mbili …” ,



    “,Kwa nini usijue taarifa muhimu kama hizo, majambazi wanatumia sana vyumba vya wageni kama hivi, watakuja kufanya mauji ya kikatili siku moja, anyway tuyache hayo! kazi njema …”,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kamanda Kendrick pamoja na muhudumu wa mapokezi, katika hoteli ya Green pick. Wote wakiwa wanapanda juu ghorofani  kuelekea chumba namba kumi na tano, wakafika mbele ya mlango, akamuacha muhudumu aendelee na majukumu yake, wenyewe wakafungua chumba na kuingia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakachunguza kila kona,kamanda Philipo akapiga picha muonekano wa chumba,kamanda Catherine akafungua dirisha la vioo, akachungulia nje, akaona alama za viatu na makucha katika ukuta, machale yakamcheza.



    “,Kendrick …”,



    “,yes afande “



    “,njoeni muone hapa …”,



    Askari wote, Gupta, Yasini, Philipo pamoja na Kendrick wakasogea ukutani.



    “,mnaona nyayo za miguu, unaona makucha, harafu dirisha limelegea tofauti na madirisha ya vyumba vile, maua kule chini yamekanyagwa kanyagwa”,kamanda Catherine aliongea.



    “,Ndio afande, tumeona “,askari wote walijibu.



    “,ok, pigeni mahesabu ya kijasusi, mnafikiria nini katika vichwa vyenu …?”,kamanda Catherine akauliza tena.



    “,mtu wa chumba hiki, hakua anatumia njia halali kuingia chumbani mwake, kuna baadhi ya siku alipitia dirishani “,kamanda   Kendrick alijibu.



    “,Exactly,fikra zangu zinaniambia mtu aliyekuwa anaishi katika chumba hiki si wa kawaida, kuna siku aliruka kwa serekasi kutoka kwenye maua yale, akakanyaga hapa ukutani kwa miguu au makucha ya mikono kama unavyo ona, kisha akaingia ndani, “kamanda Catherine alipiga mahesabu ya kipelelezi,wote wakakubaliana na mawazo yake.



    “,Kweli we ni hatari mama, sijawahi juta kukufahamu, ngoja tuendelee na upelelezi, tutajua tu …”,Kendrick aliongea.



    “,kweli kabisa, “Philipo akaitikia.



    “,Maana haiwezekani dirisha hili liwe wazi, mengine yawe yamefungwa tena hoteli kubwa kama hii, “Catherine aliongea kwa mara nyingine tena.



    “,Tuliwambia wasi ingize mteja katika chumba hiki wala kubadili chochote ndani ya chumba hiki,nazani ndio maana hawajafunga dirisha hili…”,Gupta na Yasini,askari wapelelezi wa nchi ya Goshani waliongea.



    “,Ndio maana nikasema,dirisha hili lina tatizo,siku zote lilikuwa lina achwa wazi,ndiyo maana mtu wa chumba hiki aliondoka kwa haraka akasahau kufunga dirisha kwani ni mazoea yake,anyway,tuondokeni katika hoteli ya pili…”,Catherine aliongea,akafunga dirisha,wote wakatoka nje,wakafunga mlango wa chumba wakashuka ghorofani.



    …………………………………



    “,Samahani muhudumu,wakati chumba mnampatia mwanamke huyo,dirisha lilikuwa bovu?”,



    “,Hapana mheshimiwa,lilikua zima kabisa…”,



    “,Mbona limelegea,halifungi vizuri…”,



    “,Mmmh,kuhusu hilo sifahamu,kwasababu tulikatazwa kuingia mpaka uchunguzi ukamilike,kwahiyo hatujui chochote,lakini lilikua zima kabisa…”,



    “,Vipi kuhusu nyayo za viatu ukutani,karibu na dirisha la chumba namba kumi na tano,kulikoni?”,



    “,kama nilivyo kwambia awali,hatujui chochote kile,kama kuna nyayo za viatu ukutani,chumba hakikua hivyo awali…”,



    “,Ok thank you,sasa naanza kupata mwanga,tuondokeni,muhudumu asante ,na kazi njema,mnaweza kusafisha chumba na kumpatia mteja mwingine…”,



    “,Sawa mkuu,karibuni tena…”,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kamanda Kendrick pamoja na muhudumu wa hoteli,kwa mara nyingine tena.Mazungumzo yakamalizika,askari wote wakatoka nje ya hoteli,wakatoweka walikokufamu wao.



    …………………………………



    Serena hoteli;



            “Hiki ndicho chumba namba ishirini, kama mnavyo kiona, tangu tukio litokee hatujakifanyia hata usafi, tuliambiwa tusikanyage humu mpaka uchunguzi utakapo kamilika …”,meneja mkuu wa hoteli ya Serena, mheshimiwa Vandmir Gomez aliongea, suti nyeusi, tai nyeusi pamoja na viatu vyeusi viliupendezesha mwili wake,kila kona alipopita aliitwa kwa jina la bosi Gomez, jina sahihi kabisa ambalo liliendana na mavazi yake ya kifahari pamoja na pesa nyingi alizokuwa nazo, takribani dola za kimarekani bilioni moja, pesa ambazo zilipelekea atajwe katika jarida la Forbes Afrika mwaka 2017 ,kama tajiri pekee kijana barani Afrika mwenye umri wa miaka ishirini na tano tu.



    “,Usjali mheshimiwa, kuanzia leo kila kitu kitakua sawa …”,kamanda Catherine aliitikia, huku akitembea kuelekea bafuni, akawaacha makamanda wenzake wakifanya uchunguzi chumbani,huku kamanda Philipo akiwa bize kuchukua picha ambazo zingewasaidia baadae kwenye uchunguzi.



    “,nyote njoeni huku, asibaki hata mmoja …”,kamanda Catherine alikuta nondo imekunjwa,dirisha limekatwa, huku akiangalia kipande cha kioo kilichokatwa na kutelekezwa.



    “,Kuna nini tena? “,Philipo na wenzake waliuliza.



    “,Hapo ndipo mtuhumiwa alitorokea baada ya kumjeruhi mheshimiwa raisi,…”,bosi Gomez, meneja wa hoteli ya Serena aliongea.



    “,bila shaka, hata mimi nimeona, kamanda Kendrick na wenzako, naomba mchungulie dirishani harafu mniambie mmeona nini! “,kamanda Catherine aliongea, kamanda Philipo akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea, akawa wa kwanza kuchungulia dirishani, akafuta kendrick, kisha Gupta na Yasini wakamalizia.



    “,mneona nini? “,kamanda Catherine aliuliza swali kama kawaida yake.



    “,makucha na viatu, “walijibu.



    “,tayali tumeshamjua muuaji, aliyekuwa amepanga katika chumba namba kumi na tano kule Green pick, ndiye alimshambulia raisi …”,Catherine aliongea, huku akichunguza vioo vilivyokatwa dirishani, mtuhumiwa akapita.



    “,tena ni muuaji hatari sana, hiki ni kisu kigumu kuliko vyote duniani, kinaitwa the magic knife, kisu cha maajabu, kilitengenezwa nchini Marekani mwaka 1935,kilitumika katika vita ya pili ya dunia na kuua mamilioni ya watu, kina uwezo wa kukata chuma pamoja na vioo vigumu, kwani kina madini ya almasi ndani yake ……”,kamanda Catherine alionesha utalaamu wake katika upelelezi,wote wakimsikiliza kwa makini, huku kamanda Kendrick akitikisa kichwa, akikubaliana na maelezo ya kamanda Catherine, mpelelezi mtata wa kike, kutoka katika kundi la the super three soldiers la nchini Tanzania.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,tuondokeni, twendeni mahabusu tukaonane na walinzi wa mheshimiwa raisi, kisha tuhitimishe uchunguzi wetu, tukamkamate mtuhumiwa, maana sizani kama ni vigumu kumpata …”,kamanda Kendrick aliongea,wakatoka nje,wote wakamfuata,wakaaga uongozi wa hoteli, wakatoweka haraka sana katika hoteli ya Serena.



    …………………………………







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog