Search This Blog

Thursday 27 October 2022

ANGA LA WASHENZI (1) - 1















    IMEANDIKWA NA : STEVE MOLLEL



    *********************************************************************************



    Simulizi : Anga La Washenzi (1)

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Mvua ilikuwa inanyesha sana. Hali ya hewa ilikuwa baridi ikiambatana na upepo wa wastani. Watu wengi hawakwenda kazini, na hata wanafunzi pia wakitega shule kwa kisingizio cha barabara kufurika maji.

    .

    .

    .

    Pengine watu hawa walikuwa na hoja kutokana na miundombinu dhaifu ya jiji la Dar es Salaam ambayo haiwezi kurandana na mikikimikiki ya mvua. Ila kwa mwanaume Jonathan Mchau, hilo halikuwa na mashiko kamili kwani yeye alikuwa ofisini akiendelea na kazi zake kama ilivyo ada.

    .

    .

    .

    Ni ndani ya chumba kidogo kinachopatikana maeneo ya mwenge. Kwenye kuta za chumba hicho kulikuwa kumetundikwa picha kadhaa za kuchorwa kwa mikono. Picha hizi zilikuwa zimeundwa kimafumbo lakini pia zikibeba utajiri wa tamaduni za Afrika kwa ujumla.

    .

    .

    .

    Kama ungelipata nafasi ya kutembelea hapo basi ungepatwa na kamshangao kidogo kutazama picha hizo zilizofumwa na rangi mbalimbali za kuvutia kiasi kwamba ukasahau kuwa eneo hilo limepakana na barabara yenye makelele lukuki ya magari. Na hata kuta za jengo hilo zina nyufa kadhaa.

    .

    .

    .

    Mwanaume huyu ajulikanaye kwa jina la Jonathan, joh, ama Jona kama wamuitavyo watu wa karibu, alikuwa ni mwanaume mweusi mtulivu mwenye mwili wa kujaa, macho makubwa mabovu yasaidiwayo na vioo vya miwani, nywele ndefu kichwani na ndevu alizozichonga umbo la 'o'.

    .

    .

    .

    Hakuwa mtanashati sana, pengine kwasababu alikuwa kazini na kazi yake aihitaji unadhifu wa hali juu ilhali unacheza na rangi. Ila alikuwa mtulivu sana, na macho yake yaliganda kwenye karatasi aichorayo kwa umakini wa hali ya juu.

    .

    .

    .

    Alikuwa ndani ya ulimwengu wa peke yake asijali kabisa yanayoendelea nje ya karatasi. Unaweza kudhani mwanaume huyu hakuwa anajua kama kuna mvua ilikuwa inanyesha. Umaanani huu kupita kiasi ukamfanya asifahamu kama kuna mgeni ameingia eneo lake na kusimama kwa sekunde kadhaa.

    .

    .

    .

    Akashtuliwa, "Hello!"

    .

    .

    .

    Akatazama na kumkuta mwanamke fulani mrembo, mrefu mwenye rangi maji ya kunde. Alikuwa amevalia sweta rangi ya kijivu iliyofunika blauzi yake nyeupe, pamoja na suruali ya jeans iliyobana vema umbo lake la figa. Miguuni alivalia raba nyekundu.

    .

    .

    .

    Nywele na masikio yake alikuwa ameyaziba kwa kofia kubwa jeusi la soksi. Mgongoni alikuwa amebebelea begi kubwa jeusi, haya ya kuhifadhia tarakilishi mpakato. Uso wake ulikuwa mfupi na mpole. Macho yake yalikuwa ya wastani ila makali. Mdomo wake mdogo alioupaka rangi ya kahawia ulichanua kwa tabasamu.

    .

    .

    .

    "Samahani kwa kukutoa kazini," akasema mwanamke kwa sauti ya kumlaghai nyoka.

    .

    .

    "Usijali," akadakia Jonathan, "karibu sana." Akaacha kazi akasimama kumlaki mgeni.

    "Ahsante. Hapa ndiyo kwa Joh?"

    "Yes, ndiyo hapa."

    "Na wewe ndiye Joh mwenyewe?"

    "Ndio, ni mimi."

    "Ook, nimeagizwa na Beatrice Shauri kuulizia mzigo wake."

    "Bite?"

    "Ndio!"

    .

    .

    .

    Jonathan akatabasamu. Akafuata mfuko mmoja mkubwa mweupe wa rambo, ndani yake ulikuwa na kitu cha umbo la mstatili, akaunyanyua na kumkabidhi mgeni.

    .

    .

    .

    "Unaweza ukatazama."

    .

    .

    .

    Mgeni akatazama mzigo huo kisha akaurudisha ndani ya mfuko.

    .

    .

    .

    "Ahsante sana. Unamdai?"

    "Hapana."

    "So naweza nikaondoka nao?"

    "Hapana." Jonathan akatikisa kichwa. "Siwezi nikakupatia maana sijapata ridhaa ya mmiliki."

    "Bite ni dada yangu."

    "Taarifa hiyo haijitoshelezi kukupa mzigo wake, dada. Hakunipa agizo hilo."

    .

    .

    .

    Mwanamke yule akaguna na kubinua mdomo. Akapandisha mabega na kuzungusha macho.

    .

    .

    .

    "Ok," akasema kwa kupitia puani kisha akaenda zake. Ila punde anarejea tena.

    "Kaka mbona unakuwa si mwelewa lakini?" Alilalama. Macho yake yalikuwa yamelegea, mdomo wake ukitepeta.

    "Nimekwambia Bite ni dada yangu, ameniagiza. Simu yangu imezima chaji unajua umeme unavyosumbua siku hizi, ningempigia uongee naye!"

    .

    .

    .

    Joh alipigwa na bumbuwazi. Kuna kitu alikikokotoa kichwani.

    .

    .

    .

    "Dada," akaita. "Siwezi nikakupa kazi ya mtu. Na hii ni kwasababu sikupewa agizo hilo. Ni swala la uaminifu tu. Sikufahamu, siwezi kukuamini namna hiyo."

    .

    .

    .

    "Basi ntakuongezea pesa mara mbili ya aliyokulipa Bite," akasema mwanamke huyo kwa kujiamini. Hapo sasa ndiyo Jonathan akapata wasiwasi zaidi. Kwanini mwanamke huyu anataka mzigo huu kiasi hiki?

    .

    .

    .

    Aliona haja kubwa ya mwanamke huyo ndani ya macho yake. Alikuwa anataka ule mzigo kwa hali na mali.

    "Sema basi," mwanamke akasisitiza. Uso wake ulikuwa umekunjana. Alitazama majira ya saa yake kana kwamba mwanafunzi aliyechelewa zamu ya mwalimu mnoko.

    "Unataka shilingi ngapi?" Akauliza.

    "Sitaki pesa yako," Jonathan akajibu na kuongezea: "Naomba uende, dada."

    .

    .

    .

    Mwanamke akashusha pumzi ndefu. Akavua begi lake na kuzamisha mkono wake wa kuume ndani. Jonathan akapata shaka. Alitazama mkono huo vema. Alidhani huenda ukatoa silaha.

    .

    .

    .

    Kabla mkono huo haujatoka ndani ya begi, sauti ya wanaume ikasikika. Jonathan na mgeni wake wakatazama sauti hiyo inapotokea. Mlangoni wakawaona wanaume wawili waliovalia makoti marefu meusi ya kuwakinga na mvua.

    .

    .

    .

    Wanaume hawa walikuwa warefu na weusi. Mmoja alikuwa na mustachi mnene, mwingine kidevu na mashavu yake yakiwa hayana harara za ndevu. Miili yao ilikuwa imejaa wakitembea kikakamavu.

    .

    .

    .

    Haikuchukua muda mrefu Jonathan akagundua wanaume hao walikuwa ni wana usalama. Kwa namna walivyokuwa wanaongea, kutembea na muonekano wao pia ulisadifu hiyo dhana.

    .

    .

    .

    Alirudisha macho yake kwa yule mwanamke, akaona mwanamke huyo akifunga begi lake na huku mkononi akiwa mtupu. Mwanamke akamtazama Jonathan kwa jicho baya kisha akaondoka zake akisonya.

    .

    .

    .

    Jonathan alimsindikiza mwanamke huyo mpaka alipotoka mlangoni, kisha akahamishia macho yake kwa wageni wapya.

    .

    .

    .

    "Karibuni."

    "Ahsante," aliitikia mwanamume mmoja kisha kwa pamoja wakamsalimu Jonathan.

    "We ni Jonathan Mchau?" Aliuliza mwanaume mwenye mustachi. Sauti yake ilikuwa ya madaraka. Walikuwa wanamtazama Jonathan kana kwamba wanamfananisha na mtu waliyemuona kitambo.

    "Ndiye mimi," Jonathan akajibu.

    .

    .

    .

    Leo ilikuwa ni siku ya tofauti sana kwa Jonathan. Ugeni wa pili sasa huu unamtembelea. Kazi iliyomfanya asijali hali ya hewa akaja ofisini, ilikuwa imesimama. 'Karoho' kalikuwa kanamuuma. Aliona anapoteza muda.

    .

    .

    .

    "Tuna maongezi kidogo na wewe," akasema mwanaume mwenye mustachi. Yeye ndiye alikuwa muongeaji mkubwa mwenzake akiwa kimya.

    "Karibuni," Jonathan akasema akinyooshea mikono yake ndani.

    "Tunaweza tukafanyia hayo maongezi kwenye gari?"

    "Kwenye gari!" Jonathan alistaajabu. "Ni maongezi gani hayo? Na nyie ni wakina nani? - hamjajitambulisha."

    "Sisi ni polisi." Wanaume wale wageni wakaonyeshea vitambulisho vyao. "Hivyo usijali."

    "Sijali, ila ningependekeza tufanyie hayo maongezi hapa hapa ofisini kwangu," Jonathan alisema akiketi kitako.

    Wanaume wale wawili wakatazamana kisha muongeaji akasema:

    "Sawa."

    .

    .

    .

    Wakavuta viti vilivyoko kando, walionyeshewa na Jonathan, wakaketi.

    .

    .

    .

    "Jonathan, sisi sio wakaaji sana. Kwa majina naitwa inspekta Norbet Mlanje na huyu mwenzangu ni inspekta Nombo tumetokea kituo kikuu, central."

    "Karibuni inspekta."

    "Ahsante kwa mara nyingine. Nadhani mpaka hapo utakuwa ushajua tumekuja kufanya nini."

    "Sijajua," Jona akasema akitikisa kichwa.

    "Sawa, si mbaya tukaliweka wazi," akasema Inspekta Norbet akikuna ndevu. "Kama tulivyosema hapo awali, tumetoka central, na tumeagizwa kuja hapa kwa ajili ya kukuomba kurejea kundini. Mkuu anakuhitaji sana."

    .

    .

    .

    Jona akatabasamu.

    .

    .

    .

    "Siwezi kurudi," akajibu kwa ufupi na kisha akasimama. "Nina kazi nyingi zinaningoja. Mnaweza mkanipa nafasi?"

    .

    .

    .

    Inspekta wakatazamana alafu wakanyanyuka kishingo upande.

    .

    .

    .

    "Jona," inspekta Norbet aliita. "Taifa lako linakuhitaji kwa sasa. Nadhani ni wakati wa wewe kuacha ukaidi na kusikiza wito huu."

    "Inspekta Norbet," Jona akaita. "Sihitaji kazi yenu, naomba umwambie mkuu hilo. Tena umsisitizie. Sihitaji kazi yenu hata kidogo."

    .

    .

    .

    Inspekta wakatazamana kwa macho ya paka.

    .

    .

    .

    "Sawa, ila utakapobadili mawazo yako usisite kututaarifu."

    .

    .

    .

    Jonathan hakujibu, inspekta wakaondoka. Walifika mlangoni Norbet akamtazama tena Joh kana kwamba mama aliyekata tamaa juu ya mwanaye. Kisha wakatokomea.

    .

    .

    .

    Jonathan alitafakari kwa dakika mbili, akaketi kuendelea na kazi yake aliyokuwa anaifanya hapo awali. Ila kwa sasa akili yake haikuwa imetulia. Mawazo yalimpoka atensheni. Alimfikiria yule mwanamke, alafu pia na wale inspekta. Alijikuta anakosea kutenda kazi kila mara.

    .

    .

    .

    Mwishowe aliacha, akasimama na kwenda nje kutazama madhari, pengine angechangamsha akiliye. Alitazama namna mvua inavyokita ardhi, barabara ilivyolowana. Alitazama jinsi matairi ya magari yanavyotapanya maji barabarani.

    .

    .

    .

    Alitazama anga lilivyojibana na kuwa jeusi. Namna palivyokuwa tulivu usidhanie kama hapo ni Dar, tena majira hayo.

    .

    .

    .

    Akiwa anarandisha macho yake mithili ya mtalii mbugani Serengeti, kuna kitu alikiona kikamvutia. Mara ya kwanza alikipuuzia, na hata ya pili pia. Mara hii ya tatu akaamua kukitilia maanani. Ilikuwa ni gari kubwa, Range Rover Sport nyeusi, lililosimama hatua ishirini na tano za mtu mzima toka kwenye banda lake.

    .

    .

    .

    Taa za nyuma za gari hilo zilikuwa zinawaka. Gari lilikuwa linachemka, ungeliona hilo kwa wepesi kwa kutazama bomba lake la kutolea moshi. Pleti namba ya Kenya. Vioo vyake vilikuwa vyeusi, hivyo hata kama ungekuwa karibu usingeona walio ndani.

    .

    .

    .

    Jona alilitazama gari hilo akijiuliza maswali mepesi kichwani. Lipo hapo tangu muda gani? Linafanya nini hapo? Mbona haliondoki? Linamsubiri nani ama nini ilhali mabanda yamefungwa? Mara gari hilo linatiwa moto na kuondoka. Jona analisindikiza likiyoyoma kisha anarudi zake ndani kuendelea na kazi. Angalau akili yake ilikuwa freshi.

    .

    .

    .

    Alidumu kazini mpaka majira ya jioni akiwa ameisogeza sana kazi yake. Alifunga banda kwenye majira ya saa kumi na mbili, akapanda bodaboda mpaka kwenye baa moja isiyo na jina, maeneo ya karibu na makazi yake, Mbezi beach GOIG. Hapo akatulia akiwa ameagizia Alvaro baridi.

    .

    .

    .

    Watu walikuwa wachache, bila shaka sababu ya hali ya hewa. Jona alijitenga mbali na watu, akiketi kwenye meza pweke. Macho yake yalikuwa yanachambua mazingira huku mdomo wake ukipiga mafundo kadhaa ya kinywaji.

    .

    .

    .

    Taratibu akiwa hapo, anamezwa na tafakuri na taswira mithili ya ndoto. Haikuchukua muda mwingi kuhamishwa toka kwenye fahamu zake mpaka ulimwengu huo mwingine.

    .

    .

    .

    Hii ndiyo sababu mwanaume Jona hapendi kuketi pasipo shughuli. Kila anapokuwa huru, akili yake humkumbusha yaliyopita. Na yaliyopita si mema. Humuumiza. Humtonesha kidonda sugu kisichotaka kupona.

    .

    .

    .

    Anajiona kwenye nyumba kubwa inayoungua moto. Anavuja jasho jingi akitoa macho huku na kule. Anaita jina lisilosikika. Anazunguka huku na kule. Mbao za paa zinaanguka. Hewa inakuwa nzito ndani ya nyumba anashindwa kuhema. Macho yake yanamwaga machozi. Anajikuta anaishiwa nguvu akikohoa kwa pupa.

    .

    .

    .

    Haraka anatoka ndani. Anatembea hatua kadhaa kuacha kibaraza, mara anaanguka chini. Anajitahidi sana kuhema. Jasho bado linaendelea kummiminika. Punde fahamu zinaacha mwili wake, anazirai.

    .

    .

    .

    “Kaka!” kwa mbali sauti ya kike ilipenya kwenye ngoma ya masikio ya Jona.

    “Kakaa!” sauti hiyo ikajirudia, mara hii kwanguvu ikiambatana na kupigwa kwa meza. Jona akashtuka. Mbele yake alikuwa amesimama mhudumu, mwanamke mtu mzima mwenye uweupe mwekundu wa kujichubua.

    .

    .

    .
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ***

    ***

    ***

    “Vipi, kaka kuna tatizo?” Mwanamke aliuliza. Alikuwa amevalia suruali ya jeans na tisheti nyeupe ya bia ya Serengeti. Mkono wake wa kuume alikuwa ameshikilia sahani ndefu ya plastiki iliyobebelea kinywaji cha Balimi.

    .

    .

    .

    “Hamna tatizo dada,” Jona alijibu akipangusa uso. Alinyanyua kinywaji chake akapiga mafundo mawili. Mwanamke alimtazama kwa mashaka. Ni wazi alikuwa anastaajabu kutingwa kule kwa mwanaume huyo.

    .

    .

    .

    “Samahani,” akasema. “Nilitaka kujua kama utahitaji chochote toka jikoni.”

    “Ooh, kuna chakula gani?” Jona akauliza akiketi vema kitini.

    “Nyama ya kukaanga, rosti, ndizi, chips na ugali.”

    .

    .

    .

    Jona akatazama saa yake ya mkononi. Muda ulikuwa umeenda, na pia alihisi uchovu. Aliona ni vema akabeba chakula moja kwa moja aende nacho nyumbani, hivyo akaagizia na kungoja.

    .

    .

    .

    Baada ya muda mfupi, chakula kikaletwa, akalipia na kuondoka.

    Toka hapo bar mpaka nyumbani kwake si mbali. Mwendo wa wastani ungekufikisha kwa takribani dakika kumi. Kama ukikazana unaweza kuchukua hata dakika tano tu. Ila Jona hakuwa na haraka na nyumbani. Hakuwa na cha kuwahi, labda kama kungekuwa kuna mvua ingemkimbiza. .

    .

    .

    Mvua ilikuwa imekata, manyunyu tu ndiyo yalikuwa yanashuka. Nyumbani hakukuwa na mtu wa kumngojea, anaishi peke yake. Miguu yake ilitembea taratibu akitazama chini. Alipokaribia nyumbani kwake, akaona kuna gari limesimama kwa mbele, shaka likampata.

    Alisimama upesi, akalichambua gari hilo. Alisogea kidogo apate kuliona vema. Mara akagundua ni lile lile aliloliona kule kazini likiwa limesimama, na kisha kuondoka.

    .

    .

    .

    Lilikuwa ni Range Rover Sport, pleti namba yake ya Kenya.

    Jona akajikuta anapata maswali. Akiwa hapo anaendelea kutazama, akamuona mwanamke mmoja akitokea gizani, akapanda ndani ya gari hilo upesi. Mavazi ya mwanamke huyo yalimfanya Jona aamini ndiye yule mwanamke aliyemtembelea kazini akidai mzigo wa Beatrice.

    .

    .

    .

    Ina mana amenifuata nyumbani? Alijiuliza. Kumbe ndiye yeye aliyekuwa ndani ya gari hilo kule nje ya mabanda!

    .

    .

    .

    Hakutoka hapo alipokuwa amejibanza. Macho yake yaliendelea kutazama gari akingojea liondoke. Aliminya mfuko wa chakula, akasonya.

    .

    .

    “Chakula kinapoa.”

    .

    .

    Punde anamuona mwanaume mmoja mrefu akiwa kando na gari. Hakujua ametokea wapi. Mwanaume huyo aliegeza mikono yake dirishani mwa gari akasimama hapo kwa muda kidogo. Bila shaka alikuwa anaongea jambo na mtu ama watu waliomo ndani ya gari. .

    .

    .

    Alitazama huku na kule, akapanda kwenye chombo wakaondoka. Jona alisindikiza hilo gari mpaka lilipoyoyoma kisha akatoka alipokuwa na kuenenda nyumbani kwake. .

    .

    .

    Ilikuwa ni nyumba ya wastani, sebule na vyumba viwili, yenye uzio mfupi wa tofali na geti dogo jeusi. Ilikuwa kimya na tulivu sana, pia ilikuwa giza. .

    .

    .

    Jona alikula kisha akaelekea chumbani kwake pasipo kupoteza muda. Kilikuwa ni chumba kipana kidogo, kitanda kikubwa na kabati moja kubwa la nguo lenye kioo kipana. Pembezoni mwa kabati hilo kulikuwa kuna kitu kikubwa chenye pembe nne kikiwa kimefunikwa na shuka la kijivu.

    Jona alioga, kisha akafungua kabati lake na kitoa kisanduku fulani cha mbao, kidogo kwa umbo. Alikifungua, ndani yake kulikuwa kuna brashi kadhaa za kuchorea, mirija kadhaa ya rangi na penseli za mikaa, charcoal pencils.

    .

    .

    .

    Alikiweka kisanduku hicho juu ya stuli aliyosogeza karibu na kitu kilichofunikwa na shuka, kisha akalibandua shuka hilo. Kumbe hapo kulikuwa kuna makaratasi lukuki meupe marefu, mahususi kwa ajili ya kuchorea.

    .

    .

    .

    Karatasi ya kwanza kabisa ilikuwa ina picha ya mwanamke mrembo mwenye nywele za rasta. Jona aliitazama picha hiyo kwa sekunde kadhaa akifikiria jambo.

    .

    .

    .

    Mwanamke alikuwa anatabasamu, macho yake yaliangaza. Jona naye akajikuta anatabasamu, ila macho yake yakiwa mekundu.

    .

    .

    .

    Alifungua picha nyingine, picha ya mtoto wa kiume mwenye makadirio ya miaka mitatu.

    .

    .

    .

    Alitazama picha hiyo kwa sekunde kadhaa kabla hajaigeuza na kukutana na karatasi mpya isiyo na mchoro wowote. Hapo akaanza kuchora kwa kutumia penseli.

    .

    .

    .

    Hakutazamia popote pale isipokuwa alirejea kichwani mwake. Alichora picha ya mwanamke, yule aliyekuja kumtembelea ofisini akidai mzigo wa Beatrice. Alimchora mwanamke huyo hivyo hivyo kama anavyoonekana kuanzia kichwani mpaka kifuani asisahau hata vazi.

    .

    .

    .

    Alipomaliza aliketi kando, akitazama picha hiyo kwa umakini. Alijiuliza maswali kadhaa lakini hakuyapatia majibu. Alitamani Beatrice angekuwepo karibu ili amuulize, au basi angekuwa na simu ampigie.

    Mwishowe anaamua kuipuuzia, anafuata jokofu sebuleni na kutoa chupa kubwa ya whisky anayoanza kuigida akielekea chumbani. Alikunywa chupa yote, kisha akalala.

    .

    .

    .

    Hawezi kulala pasipo kufanya hivi. Hujaza jokofu lake mara kwa mara kwa vileo vikali, kwa kazi moja tu, kumsaidia alale.

    .

    .

    .

    Asipokunywa, usingizi huwa mrefu kupitiliza. Ataamka na kushtuka kila mara. Hatapata amani.

    Amekuwa akifanya hivi kwa takribani miaka mitatu sasa. Tangu pale alipoacha kazi yake ya uaskari, akiwa inspekta mwadilifu. .

    .

    .

    Ni miaka hiyo ya nyuma, mwanaume huyu alikuwa na furaha akitenda kazi yake kiufanisi. Alisuluhisha kesi kedekede zilizoonekana ngumu na zisizowezekana mbele ya macho ya wengine. Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumaliza makundi ya majambazi yaliyokuwa yameweka makazi yake ndani ya jiji la Dar es salaam.

    .

    .

    .

    Alifahamika kwa jina la Joh 'the knife', moto wa kuuotea mbali. Mwanaume mwenye mateke mazito, ngumi za kasi na matumizi mazuri ya silaha, haswa kisu. Hata kivuli chake kilikuwa kinaogopesha.

    .

    .

    .

    Simulizi hiyo ya kupendeza ilikuja kuhitimishwa muda mfupi baada ya baba yake mzazi alipofariki akiwa kazini, kituo cha polisi. Babaye alikuwa ni miongoni mwa maafisa polisi waliouawa kwenye mashambulizi ya majambazi vituoni vya polisi kwa dhumuni la kupoka silaha.

    .

    .

    .

    Ilikuwa bado miezi mitatu tu mzee huyo astaafu, adha hiyo ya kifo ikamkumba. Jambo hili lilimuuma sana Jona, akaapa kutafuta wahusika wote na kuwatia nguvuni. Ilimgharimu mwezi tu kufanikisha adhma hiyo. Alipomaliza akaamua kuacha kazi papo hapo.

    Maamuzi haya hakushawishiwa na yeyote yule isipokuwa akili yake. Alirudisha kila kitu cha jeshi akiandika barua ya kushindwa kuendelea na majukumu. Barua hiyo haikueleza sababu, bali tu hitaji.

    .

    .

    .

    Kiuhalisia, Jona alisononeshwa sana na namna jeshi la polisi lilivyomhudumia na kumjali marehemu baba yake. Aliona anastahili zaidi ya kile alichopewa na jeshi hilo. Alilipigania sana, alilitendea kazi kwa uadilifu na kwa uaminifu. Heshima aliyopata, haikuwa hata theluthi ya yale aliyotenda.

    .

    .

    "Nami nikifa nitatendwa hivi hivi," alikuwa anasema Jona.

    "Kama wameshindwa kumthamini baba yangu aliyewatumikia miaka nenda rudi, vipi kwangu? Familia yangu itaachwaje?"

    .

    .

    .

    Aliona kazi hiyo haimfai. Aliamua ahamishie nguvu zake kufanya mambo mengine yatakayomletea faida zaidi, ambayo ni kujihusisha na biashara. Kuwepo ndani ya jeshi la polisi kulikuwa kunamkumbusha baba yake na kifo chake. Mara kadhaa alijikuta anajiuliza endapo angekuwa katika nafasi ya baba yake, familia yake ingebakije, ingeishije? Upuuzi.

    .

    .

    .

    Alitaka kupumzisha akili yake na purukushani. Alikuwa na ndoto za kufanya biashara, atengeneze faida kisha aende mbali kabisa, ulimwengu mwingine ambapo hakutakuwa na simu za kuitwa ofisini wala kazi za kutumikishwa. Atakuwa na familia yake tu, karibu kabisa na maji ya bahari, visiwa, samaki, moto na miti.

    Ila matarajio hayo yote yanakatwa ghafla kana kwamba kibatari mbele ya kimbunga. Familia yake inauawa kwenye moto mkali ulioteketeza nyumba. Biashara yake ya kusafirisha korosho nje ya nchi inakufa, mtaji unakata. .

    .

    .

    Mambo haya yanatukia kwa haraka sana. Yanamwacha Jona katika fikirishi kali maisha yake yakigeuka juu chini, chini juu. Ni ndani ya muda mfupi anapoteza mihimili yake ya maisha. Anageuka kuwa fukara, na ombaomba.

    .

    .

    .

    Katika kipindi hicho cha ukata mnene, jeshi la polisi likatupa ndoana kwa Jona kumtaka arejee kazini kabla hajafa kibudu.

    .

    .

    .

    Lakini, ingawa Jona hakuwa na mbele wala nyuma, akakataa kata kata, wakati huo hana hata uhakika wa chakula mezani.

    Lakini je nani aliyapanga mambo haya yote kwa Jona? Yalitukia tu? .

    .

    .

    Taarifa ya kikosi cha zimamoto na uokoaji, ilisema nyumba iliungua kwa hitilafu za umeme. Sababu ambayo haikukuna kabisa kichwa cha Jona kwani aliamini aliweka makazi yake katika usalama kwa kufunga vifaa vya kuzima umeme punde tu hitilafu inapobainika.

    .

    .

    .

    Isitoshe, kama ukimuuliza leo hii kwanini biashara yake, iliyoanza kuchanua, ilikufa hatakupa jibu la kueleweka. Hajui. Ni ndani ya juma moja tu, mtandao wake wa biashara ukakata huko Vietnam, mizigo yake ikazuiliwa bandarini na kugubikwa na urasimu mkubwa.

    .

    .

    .

    Kama haikuwa kipaji chake cha kuchora, hakujua maisha yake yangeenda wapi. Angalau alipata chakula na hata nauli za kumsogeza toka eneo moja kwenda lingine. Japokuwa pesa ilikuwa finyu!

    Sasa kivipi mtu huyu atalala pasipo kilevi? Kwake, haikuwezekana. Alishuka chini kama embe lidondokavyo mtini. Alikuwa kama bado yu kwenye bumbuwazi. .

    .

    .

    Ikiwa ni kwenye komo la usiku, majira ya saa kumi na moja, gari nyeusi Mark X, inasogea mbele kidogo ya geti la Jona na kusimama. Anashuka mwanamke mmoja mrefu aliyevalia kimini kifupi cheusi na viatu vyenye kisigino kirefu.

    .

    .

    .

    Mwanamke huyo alikuwa na nywele nyingi alizozikusanya na kuzibana kwa kamba nyekundu, uso wake mnene ulikuwa una miwani ya macho yenye fremu nzito.

    .

    .

    .

    Aliegemea gari akitazama nyumba ya Jona. Punde akamwona mwanaume huyo akifungua mlango na kutoka ndani.

    Ilikuwa rahisi kwake kumuona Jona kuliko Jona kumuona kwani yeye alikuwa gizani wakati Jona akiwa kwenye mwanga.

    .

    .

    .

    Jona alifika getini ndiyo akajua kuna mtu yupo kando. Alishtuka, lakini hakumpa faida hiyo mgeni. Alisogea kwa kujiamini akasimama akimtazama mwanamke aliyekuwa hapo.

    .

    .

    .

    "Wewe nani?" Aliuliza pasipo salamu. Macho yake yalikuwa mekundu. Alikunja ndita.

    "Habari yako?" Mwanamke akasalimu kwa sauti tamu.

    "Nzuri," Jona akajibu.

    "Samahani kwa kukusumbua, Jona. Najua huu ndio muda pekee wa kukupata maana umekuwa ukishughulika na kubanwa kwa siku nzima. Kwa jina naitwa Nade, ni mtumishi wa Mheshimiwa Eliakim Mtaja, nimekuja kukufikishia wito wake binafsi kwako. Anakuhitaji.

    "Ananihitaji kivipi?" Akauliza Jona.

    "Nadhani ingekuwa vizuri ukaongea naye, sina majibu ya kukuridhisha. Naweza nikakupeleka?"

    "Hapana, huwezi."

    "Jona, sasa mheshimiwa atakupataje?"

    "Sijui."

    "Una simu?"

    "Hapana."

    .

    .

    .

    Mwanamke alifungua gari mlango wa nyuma akatoa Nokia xperia nyeusi akamkabidhi Jona.

    .

    .

    .

    "Ina kila kitu. Bila shaka mtawasiliana kwa kutumia hiyo."

    Jona akapandisha kichwa juu.

    "Sawa," alijibu kiufupi.

    "Naweza nikakupeleka job?" Mwanamke aliuliza.

    "Hapana," akajibu Jona. "Nashukuru."



    Jona alifika kazini akiwa tayari amechoka. Amechoshwa na mawazo. Hakushika kazi yoyote akitafakari kwa dakika kadhaa. Alitoa kiti ndani akakiweka nje alipoketi kutazama mazingira.







    Hii ndiyo ilikuwa desturi yake. Kila anapokumbana na jambo analohitaji kulifikiria vema, basi hutafuta mahala tofauti atakapopata hewa safi na kumtoa kwenye mazingira ya mazoea.







    Bado mazingira yalikuwa ya giza, giza la asubuhi. Magari yalikuwa yanakatiza barabarani mara kwa mara watu wakienda makazini. Fremu za maduka zilikuwa zinafunguliwa, sauti za milango ya bati zikasikika huku na kule.







    Lakini yote hayo hayakutosha kumuondoa Jona fikirani. Alijikuta anasonya kisha akachomoa simu mfukoni, ile aliyokabidhiwa na mwanamke aliyenadi kuagizwa na bwana Eliakimu Mtaja.







    Akaifungua na kuzama mtandaoni. Akaperuzi vichwa vya habari vya magazeti apate kujua kinachoendelea nchini na duniani kwa ujumla.







    Kwa muda mrefu sana hakufanya hilo zoezi. Alijiweka mbali na ulimwengu kabisa, si kwasababu ya kutokuwa na simu bali kwasababu ya kutotaka bughdha za ulimwengu. Aliuchoka, akataka mapumziko.







    Ila kwa sasa, kwa namna mambo yalivyokuwa yanatukia, aliona kuna haja ya kupitia na kufahamu mambo kadhaa. Pengine anaweza pata jambo muhimu la kumpa mwongozo.







    Alipitia vichwa vya magazeti nane. Miongoni mwao kichwa kimoja kikamgonga kichwa na kumpa hamu ya kutaka kujua zaidi. Kichwa hiki kilijirudia kwenye magazeti matano. Kilikuwa kinahusu mauaji ya mfanyabiashara ndani ya jiji la Dar es salaam.







    “Mfanyabiashara auawa na majambazi.”

    “Mfanyabiashara, almaarufu Bite wa China, auawa kwa risasi na watu wasiojulikana.”

    “Majambazi wamvamia na kumuua Bite!”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Kusaka undani zaidi wa taarifa hiyo, Jona akazama tena mtandaoni. Akaperuzi blogu kadhaa zilizojaribu kuelezea tukio hilo, hatimaye akakata kiu yake ya habari.







    Kwa msaada wa picha za mlengwa na taarifaze, aligundua kumbe aliyeuawa ni Beatrice Shauri! Hili likamshtua.







    Si muda mrefu sana nyuma mwanamke huyo alionana na Jona akamkabidhi kazi ya kufanya aliyoahidi kumlipa pesa nzuri. Bado Jona alikuwa anamkumbuka vizuri mwanamke huyo kwa tabasamu na sauti tamu.







    Alikumbuka hadi nguo alizokuja nazo siku hiyo alipoingia naye kwenye mahusiano ya kibiashara. Alikuwa amevalia suruali ya jinsi ya kubana na topu ya pinki. Nywele zake zilikuwa fupi, amezikata na kuzirepea vema.







    Ameuawa!?







    Jona aliacha shughuli zake akaufuata ule mzigo wa Beatrice Shauri, akautazama kwa kina. Ni kana kwamba kuna kitu alikuwa anatafuta. Japokuwa kazi hiyo aliifanya yeye mwenyewe kwa mikono yake, ila hakuwa amepata wasaa wa kuiperuzi.







    Mzigo huo ulikuwa mkubwa. Picha kubwa ya kuchorwa kwa mkono ambayo kama ungeitazama vibaya, basi ungesema imechukuliwa na kamera, tena yenye uwezo wa hali ya juu.







    Ilikuwa ni picha ya kisiwa kilichozingirwa na maji ya bahari. Kisiwa hicho kilikuwa cha kijani. Kilivutia machoni. Ukitazama vizuri pia hapo hapo pichani utaona ndege wekundu na weupe, upande wa kusini mwa kisiwa, wakiwa wanaruka pamoja.







    Kulikuwa kuna vialama na viashiria vingi pichani. Jona alishindwa kuving’amua. Kwa mara ya kwanza, wakati anavichora, hakuvijali ila kwa sasa anapata mushkeli na kuumiza kichwa.







    “Kwanini hii picha inatafutwa?” alijiuliza. Alitafakari kwa sekunde tano kabla hajaamua jambo kichwani:

    “Ni lazima itakuwa na mahusiano na kifo cha Bite.”







    Akaketi kitini akiendelea kutafakari na picha ipo mkononi. Akili yake ilimwambia kabisa wale watu aliowaona jana usiku nyumbani kwake watakuwa wanahusika na kifo cha Bite kwa namna moja ama nyingine.







    Lakini je sababu itakuwa ni hii picha? akaitazama tena.







    Maswali hayo yalikuwa magumu na majibu yake yalihitaji jitihada. Kama kuna siku mwanaume huyu alitamani kurudia kazi yake ya upelelezi basi ni hii. Alitamani kujua zaidi kuhusu Beatrice na ile picha.







    Alikuja kuondolewa kwenye lindi hilo la mawazo na mlio mkali wa simu. Alikuwa ni Mh. Eliakimu Mtaja. Pasipo kufikiria mara mbili, Jona akapokea na kuitweka sikioni.







    “Naongea na Johnathan Mchau?” Sauti kavu iliuliza.

    “Ndiye mimi.”

    “Kijana, naomba tukutane, nina shida nawe. Nimekutafuta kwa muda mrefu sana.”







    Jona hakuona tabu, akakubali wakapanga miadi. Bwana Eliakimu alimsisitizia na kumwomba sana asije akakosa.







    “Nakutegemea sana,” alisema kisha akakata simu.







    Ilikuwa ni saa moja sasa ya asubuhi. Mwanga wa jua ulishatawala na kuangaza. Haikupita muda mrefu, akaja mwanaume mmoja mfupi rangi maji ya kunde. Macho yake makubwa, ndevu lukuki kwenye taya.







    Mwanaume huyu anaitwa Jumanne. Ni mfanyakazi mshirika na Jona ndani ya banda moja. Ni maarufu sana kwa uchoraji, haswa michoro ya tingatinga.







    “Afadhali umekuja,” Jona akasema baada ya salamu. “Kuna mahali nataka kwenda mara moja!”







    Akaaga na kuondoka na mzigo wa Bite alioupitishia kwenye makazi yake. Baada ya nusu saa akawa ndani ya nyumba kubwa ya kuvutia. Mlinzi alimkaribisha na kumuelekeza mahali pa kukaa punde alipojitambulisha. Ilikuwa ni eneo dogo lililopo kwenye bustani, lina viti na paa dogo la kigae.







    Muda si mrefu akatoka mwanaume mnene, mfupi, mweusi mwenye panki. Alikuwa amevalia tisheti nyeupe iliyobinuliwa na kitambi chake kikubwa, bukta na viatu vyepesi.







    Akatazama kushoto na kulia kabla hajaenda kukutana na Jona bustanini. Walisalimiana na kujuliana hali kisha wakaelekea kwenye kiini cha mkutano.







    “Jona, nina shida kubwa, na nimeambiwa wewe ndiye unayeweza kun’saidia. Ni muda mrefu sasa nimeliripoti polisi, lakini naona hamna kitu. Kama bahati tu, afisa mmoja akanambia nikutafute japokuwa alikuwa hana namna yoyote ya kukupata. Alichokuwa anakijua kuhusu wewe ni makazi yako tu, napo hakuwa na uhakika sana.”







    Eliakimu akaweka kituo. Jona alikuwa anamsikiliza kwa umakini mkubwa.







    “Ila naamini yote yatakuwa historia sasa maana nimeshakupata,” Eliakimu akaendelea kunena.

    “Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu mke wangu apotee. Nimemtafuta maeneo yote ninayoyajua, sijampata. Kwao na kwa marafiki zake! Napata mashaka sana juu ya hili. Nahofia usalama na uzima wake.







    Jona, naomba unisaidie kumpata mke wangu. Nipo radhi kwa gharama yoyote ile ilimradi tu apatikane. Hata kama ameuawa, basi nijue na nani amehusika.”

    “Mzee,” Jona akaita. “Sidhani kama ninafaa kufanya hiyo kazi. Sipo tayari kwa sasa.”







    Uzuri bwana Eliakimu alishataarifiwa mapema juu ya ukaidi wa Jona. Mwanaume huyu alikuwa mgumu na mwenye msimamo mkali. Ilikuwa inahitaji roho ya nanga kumbadili fikra na mwenendo.







    “Jona, nimekuomba hili kama mume anayemhitaji mke wake, baba anayemtafuta mama wa watoto wake. Si kwamba nakupa kazi, la hasha! Tafadhali naomba unisaidie.







    Nipo radhi kukusaidia kwa namna yoyote ile. Nina mtandao mpana, ninafahamiana na watu lukuki wakubwa. Bila shaka itaweza kukurahisishia kazi.”







    Uso wa bwana Eliakimu ulikuwa umenyong’onyea. Usingeweza kuamini kama mtu huyu, waziri wa Habari na michezo, angewahi kuja kuomba kitu kwa mtu wa kawaida kiasi hiki.







    Watu hawa walikuwa wamezoa kutoa amri na maagizo na kisha jambo hutendeka. Ila kwa leo ilikuwa kinyume, alikuwa anaomba, tena kwa unyenyekevu.







    “Mheshimiwa,” Jona akaita. “Hili jambo si la kukurupukia kabisa, linanihitaji niwe mtulivu.







    Ningeomba unipatie usiku huu nilitafakari, nitakupa majibu.”







    Bwana Eliakimu hakupendezwa sana na hilo jibu. Aliona kama vile Jona ametumia njia ya kistaarabu kukataa ombi lake. Ila hakuwa na namna, alipiga konde, akaamini.







    “Sawa,” akasema kishingo upande. Jona akanyanyuka na kumpatia mkono wa kwaheri, akahepa zake.







    Baada ya robo saa akawa ameshafika kazini. Alimkuta Jumanne akiwa ameketi anabofya kioo cha simu yake kubwa isiyo na jina.







    “Vipi, kila kitu kipo sawa?” aliuliza.

    “Shwari tu,” Jumanne akajibu na kuongezea: “Kuna mgeni alikuja kukuulizia. Yani ile we umetoka tu, akaingia.”

    “Nani?” akauliza Jona akiwa anaketi.







    Kwa mujibu wa maelezo ya Jumanne, Jona alipata picha halisi. Mgeni huyo alikuwa ni yule dada aliyekuwa anataka mzigo wa Bite.







    “Bonge la ndinga mwanangu alikuja nalo, nikasema yees leo si ndo’ leo!” alisema Jumanne akitabasamu meno yote nje.

    “Ulivyomwambia sipo akasemaje?” Jona alipeleleza.

    “Akaniuliza vipi nyumbani kwako, nikamjibu haupo home.”







    Jona akawa kimya akitafakari. Tabasamu la Jumanne lilififia akiuliza:

    “Vipi mzee, kuna usalama?”







    Jona hakutaka kumpa mashaka Jumanne. Alilazimisha tabasamu usoni akapachika kiganja begani mwa mwenzake.







    “Kila kitu kipo sawa, J. Huna haja ya kuhofia.”

    “Haya bana, ila huyo manzi ni mkali! Nifanyiefanyie basi na mie mwenzako ning’aze.”

    “Sina hata namba yake. Hatujuani.”

    “We si ndo’ zako hizo. Wazungu wewe, hadi na wabongo wewe. Sijui mie hawanioni?”







    Kidogo Jona akapumzisha akili yake alipokuwa ananena na Jumanne. Walitabasamu na kucheka. Na siku ilikuwa hivyo mpaka jioni walipofunga wakiwa wameingiza USD 900 toka kwa watalii fulani wa kiamerika.







    Kama kawaida Jona akapitia bar aliipoketi kwa masaa mawili akinywa Alvaro baridi. Hapa ni mahala pake mahususi pa kupunguzia muda wa kwenda kuwa mpweke nyumbani.







    Alipomaliza akajikusanya na kuelekea nyumbani akitembea ado ado. Kichwani alikuwa na fikra mbalimbali zilizokuwa zinakatiza kwa awamu.







    Alifika nyumbani, akashika geti. Ajabu likafunguka pasipo kungoja funguo. Moyo wa Jona ukakita, akili yake ilimkimbiza haraka kwenye usalama wa mzigo wa Bite.







    Milango yote ilikuwa wazi. Kulikuwa kuna chapa za viatu sakafuni, na mazingira yalikuwa shaghalabaghala kuonyesha upekuzi ulitendeka.



    Moja kwa moja akaenda kwanza chumbani kwake karibia na eneo la kabati, akafunua zulia na kukutana na kamlango kadogo alikokafungua na kuzama chini.



    Ilikuwa ni handaki. Tena kubwa tu kutosha kabisa sebule na chumba kimoja. Humo kulikuwa kama stoo kwa kujazwa vitu kadha wa kadha.



    Jona akawasha taa apate kuona, kisha kama mtu anayejua anachofanya, akanyookea kwenye kona ya handaki.



    Akakuta picha ya Bite. Ilikuwa imefunikwa na kitambaa kikubwa ikiwa imetulia kabisa kama ilivyowekwa.



    Jona akashusha pumzi ndefu kwanza. Alijihisi amepata amani ya moyo. Alijikuta mpaka anatabasamu mwenyewe.



    Aliifunika tena picha kwa kitambaa na kuirejesha palepale alipoiweka. Alipaona hapo ni salama sasa. Mahali anapopaamini panaweza kumhifadhia jambo lake nyeti.



    Bila shaka wavamizi hawakuwa wanajua kama ndani ya nyumba hiyo kuna handaki. Kiufupi, hawakuwa wanajua lolote kuhusiana na nyumba hiyo.



    Walidhani ni ya kawaida kama zingine, ujinga ambao uliwagharimu. Walimchukulia Jona kiuwepesi, hawakumpa haswa uzito anaostahili.



    Nyumba hii japokuwa i ndogo kwa juu ya ardhi, yani kwenye macho ya kawaida ya binadamu, kiuhalisia ilikuwa kubwa sana kutokana na mambo kadha wa kadha yaliyowekwa katika muundo wa siri.



    Ukiachana na handaki ambalo nalo lina sebule na chumba, kuta za nyumba hii zina milango nyuma ya makabati ya vyombo na nguo.

    Huwezi ukalifahamu hili kama hujafundwa. Ukisogeza makabati haya pembeni, unakuta milango ya vyumba vidogo vidogo sana ambavyo vinatunza nyaraka na vifaa vya siri.



    Chumba kilichopo nyuma ya kabati la jikoni, kilikuwa kina nyaraka na makabrasha yake muhimu. Pia vitu vingine ambavyo hakutaka kuvipoteza, mathalan vifaa alivyokuwa anachezea marehemu mtoto wake. Na hata pia vile alivyokuwa anavipenda mkewe.



    Kwahiyo ndani ungekuta mipira ya kuchezea, midoli, marashi mbalimbali, nguo, viatu na kadhalika.



    Chumba cha siri kilichojificha nyuma ya kabati lake la nguo la chumbani, kilikuwa kina silaha tu, na si kingine cha ziada.



    Silaha hizi zilipachikwa ukutani zikipangiliwa vema. Zilikuwa ni silaha moto na baridi. Bunduki aina kadha wa kadha, mapanga, visu, mashoka, nondo, jambia na kadhalika.



    Ila silaha ya kisu ikiwa imetamalaki kuliko zingine. Kulikuwa kuna visu takribani mia moja! Vya kila aina. Vyenye mipini ya kila rangi na muundo wake.



    Hii ndiyo silaha Jona anaipenda. Silaha anayoimudu vema. Silaha ambayo hakuweza kwenda vitani pasipo kurandana nayo.



    Jona akishika kisu, ni hatari kuliko akishika bunduki.

    Kinachomfanya apende silaha ni sababu mbili. Mosi, hufanya kazi pasipo kukoma. Hakuna kusema imeishiwa kama utumiapo bunduki na risasi.



    Pili, aliona ndiyo silaha isababishayo maumivu anayoyataka kwa adui. Maumivu ya taratibu. Maumivu makali. Risasi humuondoa mtu haraka. Kuna watu hawastahili kifo cha haraka, aliamini.



    Alitoka kwenye handaki akarejeshea vitu kama vilivyokaa, akaenda kuketi sebuleni.



    Baada ya kupata picha hiyo sasa alikuwa ametua hofu. Lakini akajitwika mawazo zaidi. Mawazo ambayo aliona yanahitaji ufumbuzi wa haraka.



    Alichomoa chupa ya kileo ndani ya jokofu, akamiminia kwenye glasi na kuanza kunywa taratibu akikokotoa mambo kichwani.



    Alipomaliza kinywaji kwenye glasi, akabebelea chupa mkononi na kuanza kurandaranda ndani ya nyumba.



    Alitazama na kuchambua nyayo za viatu alizozikuta. Alienda nje ya jengo napo akatazama chini. Akaenda pia nje ya uzio.



    Akagundua nyumba yake ilivamiwa na watu watatu: mmoja alikuwa mwanamke, mwingine mwanaume. Wa tatu hakujua jinsia yake, yeye alikuwa dereva.



    Alijua hilo kwa kutazama alama za viatu vilivyotoka kwenye gari.

    Upande wa kulia wa gari, viatu vya kike vilitokea, ila kwa nyuma, si kwa dereva, kama ilivyokuwa kwa viatu vya kiume upande wa kushoto wa gari.



    Na viatu hivyo vikarudi na kuingia garini kwa mtindo uleule uliotokea. Gari ikarudishwa nyuma na kutimka. Ndiyo maana ikawa rahisi kwa Jona kujua kuwa dereva hakushuka.



    Kama gari lingeenda mbele lisirudi lilipotokea, ingemuwia vigumu kujua kuhusu mambo ya dereva, na watu waliotokea nyuma.



    Zaidi akagundua ni aina gani ya gari ilikuja hapo. Si nyingine bali ni ile ile Range Rover Sport. Aling'amua kwa ufananisho wa alama za matairi.



    Akarudi zake ndani akifunga milango yote. Akaoga na kujilaza kitandani. Hata hakula.

    Akiwa anangoja usingizi umchukue kwa msaada wa kileo alichopiga, akafanya maamuzi. Aliona ana haja ya kurudi kazini.



    Aliona ana hitaji la kufanya jitihada za kuutafuta ukweli uliojificha na kugubika swala la hil la picha na kifo cha Bite.



    Lakini pia kumsaidia bwana Eliakimu Mtaja, kumwepusha na hadha ya kuwa kama yeye, asiye na mtu anayempenda, maana uchungu wake anaujua.



    Lakini kabla hajaanza kuchambua kivipi atayafanyia kazi hayo mambo, usingizi ukampokonya fahamu. Alijikuta asubuhi ya saa kumi na moja.



    Kila yanapofika majira haya usingizi kwake hukata hivyo huamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na siku mpya.



    Alihisi njaa sana, ilimbidi atengeneze na kunywa chai, kitu ambacho si kawaida yake.



    Alipika chai na mayai. Kulikuwa kuna ubaridi wa mvua siku hiyo, kwahiyo alitaka apate joto.



    Akiwa anakunywa chai, mvua ikaanza kunyesha, tena kubwa haswa. Kwahiyo hata alipomaliza ikambidi angojee kidogo kuona kama itapungua.



    Alitazama nje akitumia dirisha la jikoni. Alikagua mazingira ya nyumba kwa macho kama mtu ambaye alikosa cha kufanya.



    Mvua ilikuwa inamiminika. Na baridi lilikuwa linaongezeka. Alistaajabu ni kwa namna gani ataenda kazini. Alitamani mvua ile ingemkutia akiwa kazini kama ilivyokuwa hapo juzi, lakini haikuwezekana.



    Alirudi zake kitandani akajilaza kwa malengo atafakari sasa alichokiachia njiani jana usiku. Alijifunika shuka na kuangaza darini.

    Hakukaa muda usingizi ukambeba tena. Hali ya hewa ilimshinikiza. Shuka alilojifunika ukijumlisha na hali ya baridi iliyozuka, hakuweza kujisaidia.



    Akalala. Ila usingizi tofauti na ule anaolala kila usiku, usingizi wa kushinikizwa na pombe. Usingizi huu ulikuwa halisi. Usingizi anaoukwepa kila uchwao kwani huwa unamletea matatizo, majinamizi ya kale.



    Alidumu kwa takribani dakika kama ishirini usingizini. Mara akaanza kupata njozi. Alijiona akiwa kwenye uwanja wa vita anapambana na watu waliovalia sare za jeshi. Ila hakujua jeshi la wapi.



    Watu hawa walikuwa wengi, ila yeye akiwa peke yake. Hakuwa na silaha, alitumia mikono na miguu yake tu. Aliopambana nao walikuwa na bunduki. Lakini akifanikiwa kuwamudu vema.



    Alizikwepa risasi. Aliwavunja na kuwatengua maadui pasipo huruma. Alikuwa kila anapommaliza mmoja, anakazana kwenda mbele zaidi kwa kukimbia.



    Baada ya muda, akiendekea kupambana kwa juhudi na kusogea mbele, akaona kijumba fulani kidogo, cha mbao chumba ghorofa mbili, umbali wa kama kilomita mbili.



    Kijumba hicho kilikuwa kimekaa kwenye mwinuko ulitosha kuona vema kwa chini. Yani kule ambapo yeye na hao watu wengine wanaparangana.



    Kwenye sakafu ya ghorofa hiyo, Jona aliona watatu. Hakuwa na uwezo wa kuwaona vizuri, lakini alijua mmoja atakuwa mkewe na mwingine mwanaye.



    Alizidi kupambana na kujongea. Kila aliposogea akatupa macho kwenye lile jengo. Punde akaona vizuri. Alikuwa sahihi. Mkewe na mwanaye walikuwepo hapo.



    Walikuwa wamefungwa kamba mikono na miguu wakifungwa pia na vinywa. Mwanamke alikuwa amepiga magoti, mtoto akiwa amesimama.



    Pembezoni yao alikuwa amesimama mwanajeshi mrefu aliyekuwa amebebelea bunduki ndogo, amewanyooshea mwanamke na mtoto waliofungwa.



    Basi Jona akazidi kuchanganyikiwa. Alipambana maradufu. Alizidi kujongea na kujongea. Alipokaribia jengo akasikia sauti kuu inapaza:

    "Simama hapo hapo, la sivyo nawateketeza hawa washenzi wako!" Akatii. Alisimama na kusalimu amri. Alipigishwa magoti kwa lazima akinyooshewa midomo ya bunduki.

    Macho yake yalitazama familia yake kwa uchungu. Yalivuja machozi. Alitamani kugeuka malaika akawaokoe lakini hakuweza.



    Alijitahidi kuwa mpole awanusuru.

    Mara giza likagubika asione jambo kabisa. Hakujua limetokea wapi. Punde tu, akasikia milio miwili ya risasi.

    Pah! - Pah!



    Akashtuka toka usingizini akihema kwanguvu. Alikunja ndita. Macho aliyatoa. Alimeza mate akitafakari. Mara akashtushwa na mlio wa simu iliyoita kandokando yake.



    Akaichukua na kuitazama. Alikuwa Mh. Eliakimu Mtaja. Akapokea na kuiweka simu sikioni. "Nakuja mheshimiwa!" Akasema na kujinyanyua.



    Mvua ilikuwa imepungua, manyunyu tu ndiyo yalikuwa yanarasha. Bado baridi lilikuwa linapuliza tena kwa kiasi kikubwa.



    Jona akavaa koti refu jeusi kisha akatoka. Alitumia usafiri wa daladala kwasababu ya mvua. Baada ya lisaa moja akawa amefika nyumbani kwa Mh. Waziri Eliakimu Mtaja. Alipokelewa wakafanyia maongezi ndani ya nyumba.



    "Nipo tayari kufanya kazi. Ila kwa masharti kadhaa," akasema Jona. "Naomba niyasikie," Mh. Eliakimu akatega sikio asikie vema.

    "Nataka nifanye kazi hii kwa namna nijuavyo, pasipo kuingiliwa na yeyote yule. Nitakusanya taarifa, nitazichambua, nitazifanyia hariri na kuchukua hatua.

    Sitahusika na jeshi la polisi, wala sitashirikiana nao. Nitafanya kazi kwa weledi wa siri mkubwa. Na ningependa iwe hivyo mpaka mwisho.



    Lakini zaidi, naomba ushirikiano ulio kamili." Jona akaweka kituo.



    Mheshimiwa akashusha pumzi ndefu, akajibu:

    "Sawa, nimekuelewa na nimeridhia." Lakini akapendekeza.

    "Najua kuna muda utakuwa unanihitaji, aidha nikupe baadhi ya taarifa ama nikusaidie kufanya jambo fulani litakalokusaidia.

    Sasa si kila muda nakuwa na fursa, nakuwa nabanwa na kutingwa na mambo mengi tena muhimu. Hivyo basi, kuna mtu ningependekeza uwe naye karibu. Anajua karibia kila kitu kunihusu.



    Atakusaidia sana kwenye kufanya kazi yako." Aliposema hayo akaita: "Hey!" Mara tokea ndani akaja mwanamke mrefu aliyevalia sketi ya kaki ya kumbana. Topu nyeusi iliyofunikwa na koti jeusi la kifungo kimoja.



    Mwanamke huyu hakuwa mgeni mbele ya macho ya Jona. Alimtambua upesi kuwa ndiye yule aliyekuja nyumbani kwake na kumpatia wito wa Mheshimiwa.



    Anaitwa Nade.



    Uso wake mpana. Nywele zake nyingi anazozibana. Na miwani ya macho yenye fremu nzito nyeusi, vilimtambulisha upesi.

    Alitambulishwa kwa Jona kama mlinzi binafsi wa Mheshimiwa. Jambo hilo likamshtua kidogo Jona. Hakulitarajia.



    Mwanamke huyu hakuonekana kama mlinzi. Alikuwa mrembo sana kuwa mlinzi. Aidha kazi ya ukarani ofisini, au mapokezi hotelini ndizo ambazo ungezifikiria punde ungemwona.



    Jona alijiuliza ni nini kilichofanya mwanamke huyo apewe kazi kubwa kiasi hicho. Hiyo ikawa mojawapo ya sababu ya kukubali kufanya naye kazi.



    Alitamani kumuona akiwa kazini. Alitamani kuona nini kipo nyuma ya ulimbwende wa mwanamke huyo kikamfanya aaminike.



    Alitaka kukosoa mawazo aliyoanza kuyajenga kichwani. "Sawa, nitafanya naye kazi," akajibu.



    Mheshimiwa akatabasamu. "Hautajutia uamuzi wako," akasema.

    .



    Cha kwanza alichokifanya Jona ni kuulizia taarifa zote za mtandaoni kumhusu mke wa Mheshimiwa. Alitaka kujua majina na akaunti zake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asiwe na bahati, Mheshimiwa akawa hajui lolote kuhusu hayo. Cha kufanya Jona akaomba jina kamili kisha akaendelea na mengine ambayo aliona yangeweza kumsaidia kwenye kazi. "Waweza nijuza anapendelea nini? Kwenda wapi? Kufanya nini?" "Anapenda sana kuogelea. Alikuwa anaenda kuogelea kila mwisho wa juma. Pia, ni mtu wa lakshari sana."

    "Unaweza ukamuelezea ni mtu wa aina gani kwa ujumla?"

    "Yah! Muongeaji, mchangamfu, anayependa starehe na kujishughulisha pia."

    "Na vipi kuhusu mavazi?"

    "Aaahm ... kwa kifupi anapenda kwenda na wakati."

    "Kabila lake?"

    "Mnyaturu."

    "Naomba unipatie picha yake." Mheshimiwa akaelekea chumbani na kutoka na albamu ya picha, akamkabidhi Jona. Jona akatazama na kuchagua picha tano. "Naweza nikaenda nazo zote hizi?"

    "Bila shaka," akajibu Mheshimiwa.

    "Ana ndugu yeyote hapa Dar?"

    "Ndio. Shangazi yake anaishi Kimara suka, nyumba namba 102. Na pia mama mdogo yake anaishi Kinondoni, kama nakumbuka vema, ni nyumba namba 52. Ghorofa moja rangi nyeupe.

    Hao ndiyo ninaowafahamu kwa hapa Dar."

    "Kwao ni wapi?"

    "Arusha; Mianzini."

    "Asante sana," Jona akasimama. "Nadhani nimepata pa kuanzia hii safari." Wakapeana mikono na Mheshimiwa. "Vipi hautahitaji fedha kufanikisha hili?" Mheshimiwa aliuliza.

    "Usijali nitakutaarifu punde nitakapokuwa nahitaji msaada," akasema Jona.



    Ila kabla hajaondoka, Mheshimiwa akamuita na kumwambia: "Nahitaji kumpata huyo mwanamke, si kingine. Mtafute na umlete hapa. Usihangaike na mengine kumhusu.

    Bila shaka tumeelewana." Jona akaitikia kwa kupandisha na kushusha kichwa chini. Ila uso wake ulikuwa na mashaka.



    Kauli ya Mheshimiwa ilimpatia maswali kadhaa. Alijiuliza nini kipo nyuma ya angalizo hilo.

    Alitoka ndani ya nyumba, akaenda kufuata daladala. Bado hali ya hewa ilikuwa ya manyunyu na baridi pia. Hivyo koti lake lilikuwa na faida.



    Alienda kazini akamkuta Jumanne ameketi akifanya kazi fulani kwa mkono. Akamsalimu kisha naye akaketi.



    Akatoa simu na kuzama mtandaoni. Akatafuta jina la mke wa Mheshimiwa ndani ya mtandao wa Facebook. "Mariam Jullian," akaandika hivyo na kusaka. Yakaja majibu mengi mno. Watu kutoka maeneo mbalimbali, ndani ya nje ya nchi.



    Ikamchukua muda kumpata aliyekuwa anamuhitaji akitumia mfanano wa picha za mtandaoni na zile alizokuwa nazo.



    Akapekua taarifa za mlengwa wake huyo lakini pia picha na matukio.

    Picha ya mwisho kurushwa mtandaoni humo ilikuwa ni jana yake tu. Hilo jambo likamshangaza Jona. Kumbe mwanamke huyu alikuwa hai, tena mwenye furaha.



    Akaipakua picha hiyo aitazame vizuri. Akaikagua mazingira akagundua ni ya hoteli. Alihangaika kujua ni hoteli gani na ipo wapi, ila ndani ya picha ile hakufanikiwa.

    Akarudi tena mtandaoni na kupekuwa. Akapakua tena picha mbili nyuma ya ile picha ya mwanzo, zote aliona zinarandana mazingira.



    Akaanza kuzikagua kwa undani. Katika hizo picha akafanikiwa kumuona mwanamapokezi wa hotel kwa mbali. Ni wazi zilipigwa malangoni mwa hoteli.



    Alikuwa ni mwanaume aliyevalia shati jeupe na tai ya mistari mistari. Alikuwa amezingirwa na meza kubwa inayong'aa.



    Mbele yake kulikuwa kuna tarakilishi nyeusi isiyo na chogo.



    Kwenye picha moja, mfanyakazi huyo alikuwa amefunikwa nusu ya kifua na tarakilishi, ila ya pili kidogo alikuwa wazi. Hiyo Jona ikamfaa.



    Akaivuta kwa ndani akilenga kifua cha mfanyakazi huyo. Alipokipata kwa karibu akapata kujua jina la hoteli.



    Lilikuwa limeandikwa juu kidogo ya mfuko pamoja na chapa yake.



    Ilimchukua umakini Jona kung'amua hilo kwani kuvuta picha kwa ndani kunaharibu ubora wa picha kimuonekano.



    Alimuaga Jumanne akaondoka akiahidi kurejea. Akaenda nyumbani kwake alipobadili nguo na kuchukua vitu kadhaa.



    Baada ya muda mfupi akawa ameshafika mbele ya hoteli anayoitaka. Akazama ndani mpaka mapokezi.



    Bahati akamkuta mwanampokezi yule aliyemuoma pichani, ila alikuwa njiani akitaka kuondoka baada ya kumuachia mwenzake zamu. "Samahani kidogo," akasema Jona akimsimamisha mlengwa wake. Akachoropoa kitambulisho cha polisi ndani ya koti na kuonyeshea.

    Kilikuwa kitambulisho feki, ila kwa macho ya raia wa kawaida asingeweza kugundua abadani.

    Hii ilikuwa ni mojawapo tu ya nyaraka feki alizonazo Jona. Ndani ya ghala lake, anazo nyaraka feki lukuki, kwa kazi lukuki kama mwenyewe asemavyo.



    Baada ya kutoka jeshini aliona anahitaji nyaraka hizo ili mambo fulani yaende, nyakati fulani. "Naitwa Inspekta Maganga. Kuna taarifa nazihitaji kutoka kwako." Mfanyakazi yule wa hotel akaonyesha hofu. Bila shaka hakuzoea madhila za polisi. Aligeuza shingo akamtazama mwenzake aliyemuachia zamu kwa macho ya maulizo. Alikuwa mwanamke mrembo mweupe ndani ya sare. "Karibu, inspekta," kisha akasema. Wakasogea karibu na kaunta. Wafanyakazi wa hoteli wakajitambulisha.



    Inspekta akatoa simu na kumuonyeshea mlengwa wake picha ile ya mke wa Mheshimiwa aliyoipiga karibu na malango. "Nahitaji taarifa za huyu mtu. Alikuja hapa jana majira ya saa nne asubuhi." Haikuwa ngumu kwa mfanyakazi yule wa hoteli kumng'amua mgeni huyo. Picha ilimsaidia kurejesha kumbukumbu haraka.



    Akaendeea tarakilishi na kupekua taarifa za wageni ndani ya muda husika. Punde tu akazipata. "Anaitwa Salome Gerald. Alikuwa ameongozana na mwanaume, kwa jina Mushi Gadi," akasema mhojiwa.

    "Ina maana wameshaondoka tayari?" Jona akauliza.

    "Ndiyo, wameondoka asubuhi na mapema leo hii."

    "Wametokea wapi? Na wanaelekea wapi?"

    "Wametokea Arusha, wanaelekea Iringa," mhojiwa akasoma taarifa za wageni ndani ya tarakilishi.

    "Walikuja na usafiri?"

    "Sijajua. Pengine tungetazama videos za cctv." Mchakato huo ukawachukua kama nusu saa, Jona akawa amepata kila anachokitaka. Akaaga na kuondoka.



    Akiwa ndani ya daladala akaendelea kupekua mtandaoni juu ya mke wa mheshimiwa.

    Miongoni mwa picha, akamuona mwanaume fulani aliyemtilia shaka. Mwanaume huyu alikuwa amefanana na yule aliyemuona kwenye video hotelini akiwa ameongozana na mke wa mheshimiwa.



    Akapakua picha hiyo na kuitunza. Akapakua pia na nyingine iliyoonyesha gari aliloliona pia kwenye video ya hotelini.



    Japokuwa picha hizi zilikuwa za muda mrefu nyuma, zilikuwa na manufaa. Zilimfanya Jona apate mwanga kidogo wa jambo lake.



    Aligundua mke wa mheshimiwa alikuwa ana mahusiano na yule mwanaume kwa muda mrefu. Akagundua pia Arusha ndipo mahali wanapokuwa mara nyingi.



    Zaidi akapata jina alitumialo mwanaume huyo. Japokuwa halikuwa halisi ila angalau litamsaidia mbali na lile feki alilotumia kujisajilia hotelini.



    Mwanaume huyu alikuwa anajiita Black Nyokaa mtandaoni. Alilijua hilo kwa kutazama picha moja ya mke wa mheshimiwa aliyomwalika mwanaume huyo.



    Basi Jona akazama tena kwenye profaili ya jamaa huyo apekue. Bahati isiwe kwake, hakukuta jambo la maana.



    Hata picha haikuwepo, bali jina tu na akaunti tupu..

    Alisonya akazima simu. Akaacha sasa kichwa chake kitafakari mambo aliyotoka kuyaona.



    Alitafakari mambo hayo nusura apitilizwe na gari. Alikurupuka akashuka na kukwea gari lingine akayookea moja kwa moja kwenye msiba wa Bite.



    Akiwa njiani alinunua kofia aliyoivaa kufunika uso wake usitambulike.

    Alifika eneoni akakuta magari na watu wengi, ilikuwa ni siku ya kuaga kabla mwili haujasafirishwa kwenda nyumbani mkoa wa Morogoro.



    Makazi ya Bite yalikuwa makubwa na ya kuvutia. Nyumba yenye uzio mzito mpana. Geti refu jeusi likiwa wazi kukaribisha waombolezaji.



    Jona alitafuta eneo akaketi kwanza asome namna mambo yanavyoenda.



    Lengo lake hapo lilikuwa ni kutafuta lolote jambo litakalomsaidia kwenye ung'amuzi wake juu ya kinachoendelea kumhusu Bite.



    Alijua hatoweza kutoka hapo msibani mtupu, anaweza kupata mwanga angalau akajua nini chanzo cha mauaji ya Bite na kama kina mahusiano na ule mzigo wake alionao.



    Penye wengi hapakosi jambo, walisema waswahili. Jona aliamini hilo na ndiyo maana yupo hapa.



    Alitazamatazama huku na kule, na hatimaye akapata eneo lililokuwa kijiwe cha stori. Walikuwa wamejikusanya wanaume kadhaa hapo wakiteta.



    Akajisogeza taratibu mpaka hapo. Akaketi akitega vema sikio.



    Kwa muda mfupi aliokuwa hapo akagundua Bite alikuwa anamiliki kampuni ya magari. Kampuni hii haikuwa na muda mrefu tangu ianzishwe, na mtu aliyeshirikiana naye kuianzisha alishakufa.





    Akiwa hapo bado anaendelea kuskiza, akamuona mwanamke fulani ndani ya hijabu. Alimtazama vema mwanamke huyu akamgundua ni yule anayemfuatilia - mwanamke aliyekuwa anataka mzigo wa Bite.



    Haraka Jona akanyanyuka na kuhakikisha macho yake hayabanduki toka kwa mwanamke huyo, kila alipoenda ma kuongea na watu akawa anamtazama.



    Haikuchukua muda mrefu akamuona huyo mwanamke akiwa anaongea na mwanaume fulani aliyekuwa amempa mgongo.



    Mwanaume huyo alikuwa mrefu mwenye mwili wa kujengeka. Kichwa chake hakikuwa na nywele ila mwingi wa ndevu.



    Jona alimtazama kwa umakini huyo mwanaume, kichwa chake kikamwambia mwanaume huyo ndiye yule aliyemuona siku ile nje ya nyumba yake wakiwa na Range Rover Sport nyeusi.



    Alipata hamu ya kujua hawa watu zaidi, malengo yao haswa ni nini na ni wakina nani. Alihakikisha hawatoi kwenye mboni ya macho yake.





    Aliwaweka kwenye uangalizi mpaka mwisho gari lililobebelea jeneza likiondoka. Watu hao wakajipaki kwenye gari lalo, Range Rover na kuhepa.



    Jona akakodi pikipiki na kuanza kulifuatilia gari hilo kwa nyuma akilipa umbali kidogo.



    Alilifuatilia mpaka maeneo fulani hivi ya Kawe gari hilo lilipoacha njia kuu ya lami na kushika ya vumbi.



    Likatembea kwa dakika nane. Hapo sasa dereva kwa urahisi akajua anafuatiliwa. Alikuwa ni yule mwanaume pande la mtu akishikilia usukani.



    Akamtazama mwenzake, mwanamke aliyeketi kushoto kwake, akamwambia: "Tumepata mkia."



    Mwanamke akatazama nyuma, akaona pikipiki. Alijitahidi kuing'amua sura ya Jona lakini akashindwa, kofia ilimkinga.



    Alisonya kisha akauliza; "Ni nani huyu?" Hakukuwa na mwenye majibu. Ila walijua tu hawapo salama, na ni lazima jambo lifanyike.



    Dereva akadaka njia zingine za kuchepukia, ndani ya muda mfupi wakatokea baharini, wakasimamisha gari.



    Jona naye akasimamisha pikipiki na kuwatazama. Mpaka hapo alikuwa amehisi huenda akawa ameshtukiwa.



    Alijifanya anatazama maji ya bahari kwa muda kidogo kisha akakwea tena pikipiki na kupotea.



    Pande lile la mtu na mwanamke aliyeongozana naye wakamtazama mpaka alipoyoyoma. Walishindwa kujua nini haswa lengo la huyo mtu, ambaye ni Jona sasa.



    Walikaa hapo eneo la bahari kwa muda wa dakika kumi kusoma mambo. Walipojihisi wapo salama, wakaondoka zao, lakini wakiwa waangalifu sana.



    Walisogeza chombo mpaka kwenye nyumba namba 89. Nyumba kubwa yenye uzio mrefu. Wakazama ndani na geti kufungwa nyuma yao.



    Walijua sasa wapo salama. Waliketi sebuleni wakajadili kuhusu pikipiki ile iliyokuwa inawafuata. "Kuna haja ya kumfikishia taarifa, mkuu?" Akauliza pande la mtu ambaye ndani ya maongezi haya jina lake lilijiweka wazi, Kinoo.



    Na la mwanamke lilikuwa Miranda. "Hapana, ni mapema sana," alijibu Miranda akiliza mifupa ya vidole vyake. Macho yake yalionyesha yupo mbali kifikra.

    "Tunahitaji kujua kwanza ni nani anayetufuatilia na anahitaji nini," akaendelea kueleza Miranda. "Endapo tukimwambia mkuu kwa taarifa hizi robo robo, hatatuelewa, atatuona wazembe." Kukawa kimya kidogo. "Shida ni kwamba tuna maadui wengi, ni ngumu kubashiri," alisema Miranda. "Ni kweli," akaitikia Kinoo. "Ila tuna jukumu la kujua ni adui gani ameanza kunyoosha mkono tusije tukawaamsha wengine usingizini." Miranda akaitikia kwa kutikisa kichwa. Alinyanyuka akaendea chupa ya kinywaji, wiski, akaiweka mezani pamoja na glasi mbili. "Sasa yule mshenzi ameshaenda, nini sasa kinafuata?" Akauliza Kinoo akijinyoosha kuiteka glas ajipatie kinywaji. "Hali inakuwa ngumu zaidi," akajibu Miranda. Alimimina kinywaji akanywa kwanza fundo moja kupoza koo. "Nani kammaliza Bite? Unajua hilo swali linanitatiza sana," alisema Miranda akimtazama Kinoo. "Na kamuua kwasababu gani? Amekufa kabla hajatusaidia kupata ile picha na kutufafanulia." "Picha si ipo kwa yule mchoraji?!" Akasema Kinoo. "Umeipata?" "Hapana, ila angalau tuna uhakika ipo." Miranda akanywa fundo mbili. "Hata nguvu za kuitafuta hiyo picha zinaniisha," akasema akitikisa kichwa. "Hapana!" Kinoo akawaka. "Mimi naamini yule mchoraji atakuwa anajua jambo. Sema wewe ndiyo unazingua?" "Mimi?" "Ndio!" "Kivipi nazingua?" "Unamremba sana yule boya, tunajikuta watakatifu sana yani."

    "Kwani wewe ulikuwa unatakaje, Kinoo? Tutengeneze kesi zingine? ... Si kila kitu chaendeshwa na mdomo wa risasi!" "Sasa kwa hiyo system tutapatia wapi hiyo picha? Tumekagua nyumba nzima hamna kitu! Ukimwomba akupe, hata kwa fedha, hataki! Sasa?" Miranda akashusha pumzi ndefu. Akanywa tena mafundo mawili. "Tujaribu tena," akashauri. "Unajua nini Kinoo, tatizo ni kwamba nataka kuepuka vyombo vya habari kabisa.

    Nataka tufanye mambo haya kwa siri, tumalize kwa siri. Unajua mwenyewe namna gani hii ishu ilivyo ngumu." "Una maanisha nini?" "Endapo hili jambo la huyu mchoraji likivuma, basi wale wabaya wetu watalifahamu, watajua kuna jambo na watalifuatilia.



    Huoni kama hapo itakuwa nongwa? Wakifuatilia wakajua ni kuhusu picha, basi watatusumbua zaidi. Watataka kujua kilicho kwenye picha.



    Kama waliweza kummaliza Bite kuficha siri, vipi wakisikia kuna jambo litakalovujisha neno?" Kukawa kimya. Kinoo alimalizia kinywaji chake glasini kisha akalaza mgongo kitini. "Miranda," akaita. "Mimi bana nakuachia hili jambo mwenyewe. Wewe utakavyoona, sawa. Utantaarifu." "Usijali," alisema Miranda kisha akanyanyuka. "Leo hatuendi?" Aliuliza. "Wapi?" Kinoo akatoa macho. "Nawe acha uoga, unadhani ni wapi?" Akaangua kicheko. "Ni klabu tu hapo!" "Siendi," Kinoo akajibu na kuongezea: "Hivi wewe hujachoka enh? Siku nzima msibani na bado unataka kwenda klabu! We kiboko."

    Miranda akatabasamu. Akanyanyua chupa kubwa ya wiski na kumiminia mdomoni. "Tena usinikumbushe huo msiba wa kis*nge. Nimekaa hapo kutwa nzima na wala sijapata chochote. Nimepoteza muda tu!" Kinoo akatabasamu. Akanyanyuka na kujinyoosha. "Maisha ndivyo yalivyo. Si kila mara wapata, la hasha! Kuna muda wakosa na kuna muda wapata. Cha msingi ni kutokata tamaa. Tuendelee kupambana." "Ila roho inaniuma sana, Kinoo," akasema Miranda akipiga kifua chake ngumi. "Kwanini?" "Kila mara tunazidiwa hatua, kwanini? Ina maana sisi ni wajinga na wazembe kiasi gani?" "Hapana, Miranda. Kila mbwa ana siku yake. Kuna siku wataingia kwenye anga letu. Anga la washenzi. Hakika watajuta!" Kinoo aliposema hivyo akapiga mihayo. Miranda alitabasamu na kumtaka aende akapumzike. "Usiku tuna kazi ya kufanya, bila shaka unakumbuka," akasema Miranda. "Tena?" "Ndio, kwani iliisha?" "Poa, mida!" Kinoo akatoka ndani, Miranda akaingia chumbani.



    Kinoo akaelekea nyuma ya nyumba ambapo kulikuwa kuna chumba kikubwa kilichojitenga ambacho kilifungwa na mlango wa bati.



    Akafungua mlango huo kwa kutumia funguo aliyoitwaa dirishani. Akatoa pikipiki moja matata, Ducati Monster nyekundu modeli ya 2016 aliyotia moto na kuhepa nayo.



    Alivalia kofia ngumu na uso wake ukazibwa na kioo cheusi cha kofia hivyo ikawa ngumu kumng'amua uso.

    Lakini Jona alimjua mwanaume huyo upesi. Alikuwa amejibanza kwenye jengo moja karibu sana na jengo alimotoka huyo mwanaume, yaani Kinoo.



    Lakini pia na nguo alizovaa Kinoo zilimfanya Jona, mwanaume mwenye macho mabovu ndani ya miwani, amkumbuke na kumtambua kwa usahihi.



    Alimtazama Kinoo anavyoyoyoma, kisha akaurudisha uso wake getini mwa jengo. Akatazama kwa muda pasipo kuona jambo.



    Akaamua kuondoka, ila akiapa kurudi na kufanyia jengo hilo upelelezi zaidi. Alitaka kujua uhusiano wa hao watu na kifo cha Bite,na picha pia.



    Ilimradi sasa alishajua makazi yao, kwake hii ni hatua muhimu kuelekea kupata majibu yake. Hivyo hakupoteza muda.



    Akajirudisha nyumbani asiende kazini. Alikoga na kula kisha akapumzika kidogo kabla ya kuanza kuchora picha kadhaa kwenyw makaratasi yake marefu.



    Leo hii hakuchorea chumbani, bali sebuleni. Alijivika earphone masikioni akisikiza muziki laini huku akitenda.



    Macho yalitazama katatasi, mkono wake ukienda kwa ustadi. Alikuwa anarejelea kwenye kumbukumbu zake, na baada ya muda picha ya mtu sasa ikaonekana vizuri.



    Alikuwa ni mwanaume mrefu mwenye mwili mpana. Alikuwa amevalia shati lililobana mwili. Kichwa chake hakikuwa na nywele, ila ndevu lukuki. Alikuwa ni Kinoo! Hata mtoto mdogo angekueleza hivyo kwa kutazama tu mara moja.

    Kama haitoshi, akachora pia na picha ya Bite vilevile kama alivyoichora awali. Alipomaliza akaketi na kuanza kuitazama picha hiyo kwa umakini kama fumbo.

    Hakudumu hapo muda mrefu, simu ikamshtua. Akaichomoa mfukoni na kutazama. Ulikuwa ni ujumbe toka kwa Nade.



    Kabla hajaujibu ujumbe huo, akajiuliza ni namba ngapi zilizotunzwa ndani ya simu hiyo. Ni mara ya pili sasa amekuwa akiona majina yanatokea katika njia ya kumrahisishia kufahamu.



    Ina maana namba hizo zilitunzwa kwa ajili ya matumizi yake? Ndio, akili yake ikamjibu.



    Ile simu alikuwa ameandaliwa, na hata watu wa kuwasiliana naye walishaainishwa. Alitumia muda wake kuperuzi majina yaliyotunzwa simuni, akayakuta manne tu.

    1. Mh. Eliakimu Mtaja

    2. Mama Mdogo (Kinondoni)

    3. Nade

    4. Shangazi (Kimara)



    Ikamshangaza kidogo. Alipewa simu hiyo akiwa hamjui yeyote kati ya hao, labda tu Mheshimiwa.

    Ina maana watu hao waliwekwa simuni kabla hata hajaipokea? - Hadi Mama Mdogo na Shangazi wa mke wa mheshimiwa!



    Alipuuzia maswali hayo akauendea ujumbe wa Nade na kuufungua. "Habari?" Ujumbe uliuliza. "Njema," Jona akajibu. Hata salio lilikuwa kedekede kwenye simu. "Kuna kitu umepata?" Ujumbe ukaingia. "Ndio," Jona akaandika, ila kabla hajajibu akasita. Akaufuta ujumbe huo na kuuandika mwingine. "Hapana, bado." "Kweli?" "Ndio." Kimya kidogo. "Haya sawa. Naomba unishirikishe utakapopata jambo. Hata kama kidogo. Sawa?" "Sawa." Jona akaweka simu chini. Alistaajabishwa na namna alivyoulizwa kuhusu upelelezi wake ndani ya masaa machache tu.

    Alijiuliza ni hofu ama hamu iliyosukuma maswali hayo.

    Hakutaka kuumiza kichwa chake zaidi. Alifunga zile picha alizokuwa amechora kisha akazipeleka chumbani.



    Baadae kwenye majira ya usiku akiwa yupo kitandani, na tayari amejishindilia kilevi, akazama kwenye mtandao wa Facebook na kuanza kuperuzi akaunti ya mke wa mheshimiwa.



    Akafungua akaunti yake upesi akiipa jina la Giovanni Lacatte. Akaweka taarifa bandia akijinadi anaishi Italia na anahusika na mitindo mavazi.



    Akarusha picha kadhaa za wanawake wanamitindo. Baada ya hapo akadukua akaunti mifumo na mara punde akawa ana wafuasi wengi waliomfuata.



    Wafuasi laki tatu! Wafuasi hawa wote walikuwa feki. Ila usingeweza kutambua mpaka uanze kuwatazama.



    Alikuwa ni mtu mmoja tu aliyezidishwa mara elfu!



    Jona alipoona kila kitu kipo sawa, akamuomba urafiki Mariam Jullian, mke wa Mheshimiwa.



    Haikupita muda mrefu, kabla hajaanza kusinzia, ombi lake likakubaliwa. Akiwa amefungua jicho moja, akamtumia Mariam ujumbe.



    Waliwasiliana wakitumia lugha ya kiingereza wakijuliana hali. Jona akamlaghai amempemda na angependa kumtumia kutangazia mavazi yake.



    Jambo hilo likamvutia sana Mariam. Akaingia mkenge akitaka kufanya kazi hiyo. Ila alishikwa tahadhari, akauliza kama kutakuwa kuna malipo yoyote anayotakiwa kufanya.



    Jona akamtoa shaka. Lakini pia kutengeneza mazingira ya 'kiprofesheno' hakutaka kuzoeana ghafla na 'mteja' wake, akamwambia atamtafuta tena siku za usoni.

    Mariam akiwa mwenye furaha, akaridhia na kuaga.



    Jona alikuwa sasa anasinzia mno. Akaiweka simu kando na kulala. Dakika tano kupita, akashtuka. Alisikia sauti ya mlango wa geti.



    Akakurupuka na kusimamisha masikio.

    .

    .

    .

    Hakusikia kitu. Akaamua kunyanyuka na kwenda mpaka jikoni alipochungulia nje. Hakuona jambo.



    Hakuridhika, akatoka nje. Aliangaza kila pande ya nyumba, hamna kitu. Sasa ni nini? Akajiuliza.



    Alitulia hapo nje kwa dakika kama tano kama atasikia ama kuona jambo lolote. Hola! Akaamua kujirejesha kitandani na kujilaza.



    Haya sasa ni mawenge, si bure. Aliongea na nafsi yake.

    Kabla hajalala akawaza kuhusu mambo yake anayoyafanyia kazi. Alikumbuka yale yote aliyoyatenda, akagundua siku ilikuwa ndefu sana.



    Ndani ya siku hiyo yalitukia mengi. Aliwaza nini kitajiri siku inayofuata. Akiwa dimbwini mwa fikra, usingizi ukambeba sasa pasipo taarifa. -- Ndani ya usiku huo huo. Majira ya saa tisa usiku, pembezoni mwa klabu ya usiku ya Masai.



    Nje ya uzio ilikuwa imepaki Range Rover sport, ile wanayoitumia Miranda na Kinoo. Gari hiyo ilikuwa imezimwa na haikuwa na mtu ndani yake.



    Muda kidogo mbele, Miranda anatoka ndani ya klabu. Alikuwa amevalia gauni fupi jeusi linalobana mwili. Viatu virefu vyekundu.



    Nywele zake ndefu za bandia alikuwa amezichana na kuzilazia pembeni. Kwenye mkono wake wa kushoto alikuwa ana kapochi kadogo chekundu. Wa kulia ana funguo ya gari.



    Alitazama kushoto na kulia kisha akaminya funguo, gari ikalia na kuwaka taa. Akafungua mlango na kuzama ndani.



    Alichoropoa simu ndani ya kipochi, akatuma ujumbe kwa Kinoo.

    "Fanya fasta, usiuweke usiku."

    .

    .

    Ndani ya muda mfupi, ujumbe ukaingia kumjibu;

    .

    .

    "Poa najitahidi. Tunaelewana bei."

    .

    .

    Haikupita muda mrefu, kama dakika tano, Kinoo akatoka naye ndani ya klabu akiwa ameongozana na mwanamke mweupe mrefu mwembamba.



    Alikuwa amenyoa upande mmoja, upande mwingine akiwa na nywele ndefu rangi ya bluu. Alitoga kila sikio mara tano na kuvisha hereni.



    Alivalia sidiria nyekundu na sketi fupi ya kuchanua rangi ya pinki aliyofananisha na mkoba wake aliouweka begani.



    Alikuwa na uso mwembamba usiovutia, ila aliupamba ukawa angalau. Akiwa ameshikwa kiuno na Kinoo, wakaelekea kwenye gari na kupanda, gari likaondoka.



    Usingejiumiza kichwa kujua mwanamke huyu alikuwa anajiuza, yani malaya ama tuseme changudoa.

    .

    .http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hukunambia kama mtakuwa wawili!" Alisema malaya akimtazama Miranda aliyekuwa anaendesha gari. "Unajua mkiwa wawili bei yake ni tofauti."

    .

    .

    "Nipo peke yangu tu," akasema Kinoo. "Huyo ahusiki na mambo yetu."

    .

    .

    Malaya akaitikia kwa kutikisa kichwa akibinua mdomo. Akachoropoa sigara kwenye mkoba.

    .

    .

    "Unataka ufanye nini?" Kinoo aliwahi kumuuliza. Hakungoja jibu, akammarufuku: "Ah! Ah! Huwezi ukavuta sigara humu. Rudisha!"

    .

    .

    Malaya akarudisha sigara akibinua mdomo.

    .

    . "Isiwe kesi."

    .

    .

    .

    Baada ya muda kidogo wa safari, Miranda akawashusha maeneo ya Kijitonyama Sayansi mbele ya nyumba ndogo yenye uzio.

    Wakateta kidogo na Kinoo.

    .

    .

    "Hakikisha kila kitu kinaenda sawa," alisema Miranda akikaza macho. "Si kila kitu unacho?"

    .

    .

    "Ndio, kila kitu kipo," akajibu Kinoo.

    .

    .

    "Sasa usije ukanogewa ukasahau kazi." "Haiwezi ikatokea. Kama lini?"

    .

    .

    "Poa. Kesho! Kama kuna lolote, utanchek kwa phone."

    .

    .

    "Usikonde."

    .

    .

    "Enjoy!"

    .

    .

    Gari likahepa. Kinoo akatazama kushoto na kulia. Kulikuwa kimya hamna mtu. Akazama na malaya ndani baada ya kufungua geti.



    Wakaekea moja kwa moja ndani ya chumba, milango ikifungwa. Wakapata maji na kujilaza kitandani kwa ajili ya kupeana raha.



    Walifanya tendo kwa muda wa lisaa. Kila mtu akawa hoi na mwenye kuhitaji kupumzika.

    Mwanamke akalala usingizi mzito akiwa tayari ameshapokea chake na kukiweka begini. Ila Kinoo alijitahidi sana kuepuka hilo swahibu. Akakaza macho.



    Alijua fika akilala itakula kwake. Hawa malaya huwa wanaondoka majira ya saa kumi na moja asubuhi na sasa ilikuwa saa kumi na madakika yake.



    Alipohakikisha mwanamke amelala vizuri, akatoka kitandani na kwenda kabatini.



    Kulikuwa kuna makabati mawili moja lilikaa karibu na kitanda na lingine karibu na mlango. Lililo karibu na mlango lilikuwa la ukubwa wa kati lenye milango miwili.



    Ila lililokaribu na kitanda lilikuwa kubwa na pana. Milango mitatu na kioo kikubwa. Lilikuwa ni la nguo.



    Kinoo alifuata hili la mlangoni akapenyeza mkono wake kwa nyuma, akatoka na ufunguo. Akalifungua kabati.

    Lilikuwa limegawanyika katika vipengele vitano. Cha kwanza kilikuwa kina vitu vilivyokuwa vimefunikwa na makaratasi magumu meusi.



    Vingine vilikuwa vina umbo la mstatili, vingine pembe tatu na hata zisizoeleweka.

    Kwenye makaratasi kulikuwa kuna maandishi madogo ya lugha ya kirusi. Maandishi hayakuwa mengi, yaliandikwa na kupigiwa mstari.



    Kipengele cha pili cha kabati kilikuwa kina matambara ya rangi mbalimbali. Hakikuonekana kama kina zaidi ya hapo, labda kama kingepekuliwa.



    Cha tatu kilikuwa kina kitambaa kimoja kikubwa cheusi pamoja na chupa moja kubwa ya plastiki yenye kifuniko kama cha pafyumu.



    Cha nne hakikuwa na kitu. Kitupu. Vichengachenga tu vya tembe za vidonge ndivyo vilizagaa.



    Cha tano kilikuwa kina chupa tatu za kioo. Chupa moja ilikuwa na shingo nyembamba, umbo la pembe tatu na kalio flat.

    Chupa nyingine ilikuwa na umbo la mstatili na shingo nyembamba kama ile ya kwanza. Na ya tatu vilevile kama hii ya pili.



    Zote zilikuwa zina vifuniko vya vyupa.



    Chupa hizi zilikuwa zimebandikwa vikaratasi vya rangi visivyo na maneno. Chupa ya kwanza ilikuwa na karatasi ya rangi ya nyeupe. Ya pili rangi ya chungwa. Na ya tatu rangi nyekundu.



    Lakini kile kilichomo ndani ya chupa zote hizi, kilikuwa cheupe kama maji. Kwa macho usingeona utofauti.



    Kinoo alinyanyua chupa moja baada ya moja, akaitikisa na kuitazama. Baada ya hapo akachukua kitambaa kilichopo kwenye kipengele cha tatu.

    Akafungua chupa yenye kikaratasi chekundu na kumiminia kwenye kitambaa kimiminika kidogo kilichomo ndani.



    Akarudisha chupa na kufunga kabati. Akazima taa na kwenda kitandani. "Hicho kitambaa cha nini?" Akashtuka kusikia hilo swali. Kumbe mwanamke alikuwa macho na alimuona.



    Hakuwa sasa na cha kueleza wala muda wa kupoteza, akamdaka mwanamke na kumziba mdomo na pua kwa kitambaa.



    Mwanamke akatapatapa kutafuta hewa. Alijaribu kujichoropoa, lakini hakufanikiwa abadani. Hakuweza kupambana na nguvu za mwanaume Kinoo.



    Baada ya dakika tatu akawa kimya tuli akiwa amefumba macho. Kinoo akammwagia pembeni. "Shenzi!" Akasonya. Alirudisha kitambaa kabatini na kulifunga. Akaunyanyua mwili wa malaya yule na kuupeleka kwenye chumba fulani kidogo alipoulaza chini kisha akatoka.



    Chumba hichi kilikuwa cheupe kisafi. Hakikuwa na kitu chochote kile. Kilikuwa kina dirisha dogo lililokuwa juu kabisa.



    Kinoo alirejea akiwa amebebelea kamera yenye miguu mirefu mitatu. Akaisimamisha na kuiwasha, akaielekezea kwa mwanamke yule chini.



    Alipoona inamchukua vema, akatoka na kwenda zake chumbani alipozima taa na kujifunika shuka akalala.



    Asubuhi, kwenye majira ya saa nne, akaamshwa na honi kali huko nje. Akakurupuka. Macho yake yalikuwa mekundu kwa kulewa usingizi.



    Alijinyanyua akaenda nje. Alijua atakuwa Miranda, na kweli. Akafungua geti Miranda akaingia ndani.

    "Vipi? Kila kitu kipo shwari?" Aliuliza Miranda wakitembea kuelekea ndani ya sebule.

    .

    .

    "Kila kitu kipo poa. Nimefanya kama maagizo yanavyosema," akaeleza Kinoo.

    .

    .

    "Enhe, ikawaje?" Miranda akauliza kwa shauku. Walishafika sasa sebuleni wakaketi kwenye sofa.

    .

    .

    "Sijatazama imekuaje. Unajua nilikuwa nimechoka sana. Hapa unavyoniona ndiyo umeniamsha wewe. Nimelala saa kumi na mbili kasoro!" Miranda akanyanyuka.

    .

    .

    "Twende ukanionyeshe," akaamuru. Akaongozana na Kinoo mpaka kwenye kile chumba kutazama.



    Walifungua wakapokelewa na harufu kali. Walikunja nyuso wakaziba pua.

    .

    . "Imefanya kazi." Alisema Miranda akitikisa kichwa. Sauti yake haikusikika vema kwasababu ya kujiziba.



    Mbele yao kulikuwa kuna kitu cheusi kisichoeleweka. Ni palepale alipowekwa yule malaya masaa kadhaa nyuma, sasa hivi palikuwa pana chembechembe nyeusi nyingi mno.



    Huwezi ukadhani kama binadamu alikuwa hivyo. Ni ngumu kuamini.



    Chembechembe hizo zilikuwa zinatoa harufu mithili ya pafyumu kali iliyooza ama kuchacha. Harufu hiyo ilikuwa nyepesi na kali kiasi cha kukutoa machozi ukiivuta mara mbili tu.



    Kinoo aliitwaa kamera wakatoka ndani ya chumba kwenda sebuleni. Wakaketi, Miranda akaanza kutazama nini kilichotukia.

    Kinoo alijitahidi kutazama, ila usingizi ulimmeza ndani ya muda mfupi. Hakuweza kudumu kuendelea kukodoa.

    Alikuwa na usingizi mzito. Aliachama mdomo wakati Miranda akifuatilia video kwa umakini. Mara nyingine akiipeleka mbele ama kuirudisha nyuma asipitwe na mambo muhimu.



    Alipomaliza kuitazama akajikuta anatabasamu.

    .

    .

    "Kinoo, hii ni kabambe!" Akasema akitikisa kichwa. "Imechukua dakika kumi tu, mwili wote umebadilika na kusahaulika! Hakika mkuu ataifurahia."

    .

    .

    Kimya.

    Alitazama akamuona Kinoo amelala. Akasonya akisimama. Akaaga kana kwamba Kinoo anamsikia kisha akaenda zake.



    Alijiweka kwenye gari akarudi kwenye makazi yake, Kawe. Alikuwa amebebelea kamera aliyokuwa anaitumia kutazamia video.



    Alipoingia ndani akanyanyua simu ya mezani akatia namba na kupiga.

    .

    .

    .

    "Hello, I've got good news to tell!" (Helo, nimepata taarifa nzuri za kuongelea)

    .

    .

    Alisema kisha akatabasamu.

    .

    .

    "Yes, it's about the chemical. The red one's proved its worth." (Ndio, ni kuhusu kemikali. Nyekundu imethibithisha thamani yake.)

    .

    .

    "Really. I am going to write a report about it. Expect my email at night." (Kweli. Naenda kuiandikia taarifa. Tegemea barua pepe yangu usiku.)

    .

    .

    "Ok, later then." (Sawa, baadae basi.)

    .

    .

    .

    Akakata simu kisha akashusha pumzi ndefu. Akaenda chumbani akiacha kila kitu sebuleni. Hakukaa muda mrefu chumbani akarejea akiwa amevalia bukta nyeusi na blauzi nyeupe.

    Akaangaza mezani, hakuona kamera. Moyo ukamlipuka! Hakukaa vizuri akaona mlango wa sebuleni upo wazi. Akili ikamtonya, nimevamiwa!



    Haraka akakimbia kufuata meza ya kulia chakula, chiniye akanyofoa bunduki ndogo.

    Macho yake yakaanza kuambaa ambaa huku masikio yake yakifanya kazi ya kushurutisha sauti ya kila kitu.



    Taratibu alikuwa anaufuta mlango wa sebule kwa tahadhari ya kiwango cha juu.

    .

    Aliufungua kwa mguu wake wa kushoto akanyooshea bunduki nje, mara mkono wake ukapigwa teke, bunduki ikaponyoka mkono na kurukia mbali.

    Alikuwa ni mwanaume mrefu aliyevalia suti na kinyago cheusi cha fuvu la kichwa cha binadamu. Mkono wake wa kushoto alikuwa ameshikilia kamera, ile aliyoweka Miranda mezani, huku akiwa hana silaha yoyote.

    Kwa tahadhari aliweka kamera chini kisha akajipanga kwa ajili ya pambano, Miranda pia. Wakakunja ngumi kila mmoja akimvizia mwenzake awe wa kwanza kufungua mchezo.



    Miranda aliitazama kamera kiwizi. Alikokotoa na umbali wa silaha yake ilipo. Aliwaza namna gani ya kufanya avipate vyote kwa pamoja. Adui yake alikuwa anawaza namna gani ya kufanya apate mwanya wa kuhepa na kamera.



    Hilo ndilo lilikuwa lengo lake, kamera tu! Hakuwa na haja na kingine chochote. Alijua fika kamera ile itakuwa na jambo muhimu, jambo ambalo litakuwa na soko huko anapotaka kuipeleka.



    Ila je, mkono wa mwanamke Miranda, utamruhusu?



    Akapima zogo kwa kurusha ngumi, Miranda akakwepa na kutupa yake, ikapanguliwa. Akatupa tena nyingine na nyingine, zote zikapanguliwa na mwanaume mvamizi kisha kukawa tena kimya. Wakitegeana.



    Mara hii Miranda hakungoja tena kwa muda, akarusha mateke mfululizo. Alijitupa hewani na kufungua nyonga zake. Mvamizi akajituma kukwepa kwa ustadi, kisha akautafuta mwanya na kumpatia Miranda teke la mgongoni lililomtupia chini.

    Miranda akanyanyuka upesi. Akakunja ngumi na kumjongea mvamizi. Alishajua sasa anapambana na mtu wa aina gani, mtu mtaalamu mwenye uwezo, hivyo ilibidi awe mwangalifu zaidi.



    Hakurusha ngumi wala teke, akangoja. Mvamizi akautuma mwili kwa ngumi mbili, kisha teke, ngumi tatu na teke la kujifungua, vyote Miranda akakwepa kana kwamba alikuwa na miadi navyo.



    Mvamizi aliporusha teke la kujikusanya, Miranda akaona sasa fursa ya kushambulia, upesi akainama kukwepa na kuufyeka mguu uliokuwa umemsimamisha mvamizi. Mvamizi akadondoka chini. Ila upesi akajifyatua na mikono yake akasimama.



    Akanguruma kwa hasira. Alikuwa amechukia. Pasipo kujua huo ukawa mtaji wa mafanikio kwa Miranda.

    Alitupa ngumi na mateke kwa fujo. Miranda akakwepa kwa kasi. Takribani ngumi na mateke ishirini yakavuka yakipita pembeni ya masikio ya mwanamke huyo aliyekuwa mwepesi kuepusha kichwa chake, wakati huo kichwani akitafakari namna ya kushambulia.

    Muda ulipowadia, mvamizi akajaa kwenye rada. Alirusha teke la mguu wake wa kushoto, Miranda akalidaka kwa mikono yake miwili. Mvamizi akataka kutuma teke la kulia kwa kutumia balansi ya mguu wa kushoto ulioshikwa na Miranda, akaula wa chuya.



    Akiwa hewani amejifyatua, Miranda akamsukuma, alafu kufumba na kufumbua akajituma hewani na kumpa teke kali alilolituma kwa nguvu zake zote, mwanaume akajikuta yupo chini akiugulia maumivu makali.



    Haraka Miranda akachumpa samasoti kuifuata bunduki. Akaiokota na kumnyooshea mvamizi, ajabu mvamizi naye alikuwa tayari ameshainyaka kamera na kuitia mkononi. “Ukifyatua tu, naiachia ipasuke! Ni wewe ndiye utakuwa na hasara ikiharibika.” Mvamizi akatishia. Alikuwa amenyoosha mkono wake wa kushoto akiishikilia kamera kwa kidole kimoja.



    Miranda akatulia kwanza akifikiria cha kwanza. Hakuharakisha kufyatua risasi, maana aliona anaweza akakosa anachokipigania japokuwa uwezekano ulikuwa mdogo. “Weka bunduki chini!” Mvamizi akaamuru. “Nimesema weka bunduki chini kabla sijaitupa kamera!” akarudia akitishia kwa kuchezesha kamera kidoleni. Miranda akamwomba asifanye hivyo kwani anatii agizo.



    Taratibu akainama akijifanya anataka weka silaha chini, ila akilini mwake alikuwa amepanga jambo.

    Kabla hajapata mwanya wa kulifanya, honi ikaita huko nje ya uzio! Wote wakatazama getini upesi kana kwamba wataona kitu.

    Mvamizi akajua sasa usalama wake unazidi kuwa finyu ya wembamba wa nyufa, na alitakiwa afanye jambo upesi kujing’amua. Hakuwa na budi bali kuituma kamera. Uhai wake ulikuwa muhimu kuliko kanda ya kifaa hicho.



    Akairushia mbali ya kulia mwa Miranda. Upande wa mkono ule ule ambao mwanamke huyo alikuwa amebebelea bunduki. Haraka Miranda akaikimbilia na kuinyaka mithili ya kipa mashuhuri. Mpaka chini akadondoka nayo akijigeuzia mgongo.

    Kurusha macho kwa mvamizi, akastaajabu kumuona yupo hewani anavuka ukuta! Akarusha risasi tatu haraka. Ila hazikufanikiwa, mvamizi akatua upande wa pili akakimbia.



    Punde, loki ya geti dogo ikavunjwa kwa teke kali akaingia Kinoo akiwa amebebelea bunduki ndogo. Aliangaza macho yake huku na huko, akamuona Miranda chini akiwa na kamera na bunduki. Haraka akamfuata. “Vipi, kuna nini?” “Ninyanyue twende ndani,” Miranda akasema akikunja sura kwa hisia za maumivu.



    Kinoo akambeba na kwenda naye ndani, akamuweka kwenye kochi. Miranda akamueleza yale yote yaliyotukia. “Miranda, si salama tena kukaa hapa,” alisema Kinoo akitikisa kichwa. “Kama wameshapajua, basi hili halitakuwa tukio la mwisho!” “Kinoo,” Miranda akaita. “Unadhani walikuwa hawajui hapo kabla kama naishi hapa?” “Ndio! Mbona hayakutukia haya?” “Hapana, mimi siamini.” Miranda akabinua mdomo. “Walikuwa wanajua, ila hawakuwa na sababu.” “Umemsahau yule jamaa aliyekuwa anatufuatilia kwenye bodaboda?” Kinoo akakumbushia akinyooshea kidole hewa. “Huoni kama haya matukio yanafuatana? Yule aliyekuwa kwenye boda ndiye huyu ambaye amekuja kutuvamia. Na itakuwa siku ile alijua haya makazi. Yani hatukufanikiwa kumpoteza maboya,” Kinoo akafafanua.



    Miranda akakaa kimya kwanza akitafakari. Alimuomba Kinoo amletee kinywaji, Kinoo akatii kwa kumletea chupa moja kubwa ya mvinyo. Mwanamke akaidaka na kuanza kuinywa kama samaki.

    Alipopumzika, akasema: “Kinoo, hawa watu wanatupanda kichwani. Kitu kinachonipa presha ni kwamba wanapataje taarifa, ina maanisha wanatufuatilia. Tena kwa ukaribu.



    Huyu mvamizi amejuaje kama nina kamera. Kuja kwake hapa ilikuwa ni sababu ya kamera tu, ndiyo maana alipoikwapua, alikuwa anahangaika kuondoka.



    Ina maana alituona tukitoka na yule mwanamke kule klabu? Ina maana aliniona nikitoka na kamera kule kwako?



    Hivi umeshajiuliza haya maswali?" "Nilikuambia mapema, Miranda. Tunahitaji kumwambia mkuu. Si mpaka maji yakomee shingoni," akasema Kinoo. "Sijakataa kumwambia mkuu, Kinoo. Ila basi tuwe na maelezo ya kueleweka. Anyway, leo nitamwambia yaliyotukia. Bila shaka tunahitaji ulinzi zaidi." "Utamwambia saa ngapi?" "Nikimtumia mrejesho wa zile kemikali." "Inabidi tujiandae." "Na nini?" "Kazi! Unajua tukituma taarifa kama hiyo kazi huja." "Hujazoea tu kazi, Kinoo?" Kinoo akatabasamu. "N'taachaje kuzoea sasa," akasema. Naye akachukua chupa ya mvinyo na kugida. .

    .

    .

    .

    *** .

    .

    .

    .

    Isingekuwa simu kuita, Jona asingeshtuka na kutoa macho yake kwenye kibao kikavu alichokuwa anapaka rangi.



    Alikunja ndita akikodoa macho ndani ya miwani yake. Aliikwapua simu na kuitazama. Nade!

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akasonya na kuiweka simu pembeni kisha akaendelea na kazi zake kama kawaida.



    Simu ikaendelea kuita na kuita. Aliipuzia akaendelea na kazi zake kama kawaida.



    Siku hiyo alikuwa ametingwa na kazi na tangu asubuhi na hakuwa na muda wa kupumzika. Alikuwa na kazi kama tatu hivi, kama si za kuzimaliza basi za kuzifikisha mahala fulani.

    Kazi hizo zilikuwa ni za michoro ya kawaida, michoro ambayo anaweza kuifanya, kama ingelikuwa ni ya tingatinga basi Jumanne angelimsaidia.



    Sasa ilikuwa ni majira ya saa sita mchana na ni kazi moja tu ndiyo alikuwa ameshaichorea ramani.



    Siku yake ilikuwa imebanwa kiasi kwamba hata simu hakushika, wala hakutaka kuishika.



    Jumbe kadhaa zilikuwa zimeingia, za kawaida na za mtandao wa Facebook ila hakupata wasaa wa kuzisoma.



    Ilipofika majira ya saa nane mchana, akiwa hata hajala, mgeni akaingia ndani ya fremu yake. Ila haraka akadakwa na Jumanne.

    Alikuwa ni mwanamke. Jona alijua hilo kwa sauti kwani hakuwa na muda wa kutazama.



    Ila punde akiendelea kusikia sauti hiyo ikiendelea kuongea na Jumanne, akaing'amua si ngeni.



    Akatazama, akamuona Nade. Alistaajabu amepajuaje hapo. Aliacha shughuli yake akamtazama mwanamke huyo aliyekuwa amevalia taiti ya zambarau na tisheti nyeusi.



    Miguuni alikuwa amevalia raba nyeusi na kama kawaida alikuwa amevalia miwani yenye fremu kubwa nyeusi, nywele zake ndefu zikiwa zimelala.

    .

    .

    .

    "Habari, Jona!" Akasalimu. Jona akashusha kwanza pumzi ndefu. .

    .

    "Njema, karibu,"

    .

    .

    "Ni mgeni wako?" Jumanne akauliza.

    .

    .

    "Ndio, wa kwangu," Jona akajibu upesi.

    .

    .

    "Duh! Haya bana. Acha mie mtazamaji nikae kando." Jumanne akatania, Jona akatabasamu. Alienda zake banda lingine na kumwacha Nade na Jona peke yao.

    .

    .

    "Karibu."

    .

    .

    "Ahsante, samahani kwa usumbufu Jona."

    .

    .

    "Pasipo samahani."

    "Nilijaribu sana kukutafuta kwa simu lakini haukuwa unapokea, ndiyo maana nikaja hapa."

    .

    .

    "Umepajuaje hapa?"

    .

    .

    Nade akatabasamu. .

    .

    "Ni mtafuta cha uvunguni tu," akajibu akiminya macho yake kana kwamba anakonyeza.

    .

    .

    "Enhe, kuna kipya?"Jona akauliza. Uso wake haukuwa na tembe ya masikhara. Hakutaka kupoteza muda kwa kazi alizonazo.



    Nade akaguna.

    .

    .

    "Sina. Nimekuja kutafuta hilo jipya kwako." Jona akatikisa kichwa. Akiwa ameshika brashi yake ya rangi akaendelea kuchora kwa sekunde ishirini kana kwamba hana mgeni.



    Alikuwa anafikiria jambo kichwani. Japokuwa macho yake yalikuwa juu ya ubao, akili yake ilikuwa inahangaika.

    .

    .

    Akaita:

    .

    .

    "Nade!" pasipo kung'oa macho yake kwenye kibao.

    .

    .

    "Abee!" Nade akaitika.

    .

    .

    "Kuna kitu wewe na Mheshimiwa mnanificha."

    .

    .

    Nade akanyamaza kwanza asiwahi kujibu.

    .

    .

    "Kitu gani, Jona?"

    .

    .

    "Mnajua wewe na mheshimiwa. Ni kipi hicho?"

    .

    .

    "Mbona hamna!"

    .

    .

    "Una uhakika na usemalo?"

    .

    .

    "Ndio. Nina uhakika."

    .

    .

    "Ni nini kinawasumbua hivi? Ni kitu gani hamtaki nijue?"

    .

    .

    "Hamna kitu, Jona. Kwanini unawaza hivyo?"

    .

    .

    "Kwanini unanifuatilia hivyo?"

    .

    .

    "Nakuf ... kivipi?"

    .

    .

    "Nade, embu tuache kufanyana watoto. Kuna jambo kati yako na mheshimiwa." Jona akaacha kuchora, akamtazama Nade machoni.

    .

    .

    "Kuna jambo mnanificha. Kuna jambo mnaepuka nisilijue. Ni bora mkaniambia mapema. "



    Nade akawa kimya akimtazama Jona. Mara akanyanyuka.

    .

    .

    "Naona leo haupo kwenye mood. Naomba niende." Jona akatikisa kichwa kisha akaendelea na kazi yake ya kuchora.

    "Nitakapokigundua mtakuwa mmechelewa."

    .

    .

    Nade asiseme jambo, akatoka ndani. Akaenda kwenye gari, Toyota Harrier, nyeusi alipojiweka na kufunga mlango.



    Ndani ya gari alikuwa mwenyewe. Alijilaza kwenye kiti kabla hajatoa simu yake mfukoni na kupiga.



    Punde ikapokelewa.

    .

    .

    "Mkuu, tunapoelekea kitumbua hiki kitaingia mchanga."

    .

    .

    .

    ***



    Fanzhèng wo yào ta si!" (Nataka afe kwa njia yoyote ile!) Mwanaume mezani akasisitizia.



    Mwanaume ndani ya suti akaitikia tena kwa kutikisa kichwa.

    .

    .

    .

    "Shì de xiansheng!" (Ndio, mkuu!)

    .

    .

    .

    Haraka akatoka ndani ya chumba akiwa haamini kama ametoka na pumzi yake. Alihema kwanguvu jasho likimchuruza.

    .

    .

    .

    ENDELEA…

    .

    .

    .

    Aliendea gari lake akajiweka na kutoka ndani ya eneo hilo mpaka kwenye bangaloo iliyokuwa umbali wa kama kilomita tatu toka kwenye yale makazi alipofikishia taarifa.



    Huko akakutana na wenzake wanne ambao alijumuika nao kwenye kunywa ulabu na kuvuta shisha iliyopo katikati ikiwa imezungukwa na kochi kubwa rangi nyekundu lililokuwa limejikunja kutengeneza umbo la ‘c’. Mwanaume mmoja alikuwa mwenye asili ya Uchina; nywele nyeusi, macho madogo na umbo dogo pia, alikuwa anajulikana kwa jina la Lee. Alikuwa mchangamfu na akiongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kasoro tu lafudhi.

    Wengine watatu walikuwa weusi ila wenye maumbo makubwa. Mmoja aliyekuwa amenyoa panki, pia akiwa na ndevu za duara, alikuwa anaitwa Mombo. Macho yake yalikuwa makubwa na sauti yake nzito.



    Mwingine alikuwa ana nywele hafifu kichwani, vichengachenga vya ndevu vya hapa na pale kidevuni. Mdomo wake ulikuwa mpana, sauti yake ikikwaruza kana kwamba amekula chokaa. Jina lake Devi.



    Wa mwisho yeye hakuwa na ndevu bali afro kubwa nyeusi ti! Alikuwa mwembamba mwenye macho mekundu malegevu. Mdomo wake mkavu mweusi kama kunguru. Aliitwa Nigaa. Alikuwa ndiye anayeshikilia bomba la shisha mara nyingi kuliko wenzake.

    Walipeana salamu kwa kugusanisha mabega yao kabla mwanaume huyu aliyevalia suti nyeusi kuketi na kuanza kuwapasha wenzake habari namna mambo yalivyotukia. Kwenye haya maongezi, alitambulishwa kwa jina la Bigo.

    .

    .

    “Una kazi nyepesi sana, Bigo,” akasema Devi na sauti yake inayotesa masikio. “Yani unahangaika na mchoraji?! Raha iliyoje. Si unammaliza ndani ya sekunde moja tu!”

    Wenzake wakamuunga mkono.

    .

    .

    “Yani kama ungeuawa kwasababu ya kushindwa kumuua mchoraji, kingekuwa ni kifo cha kizembe sana. Au una mpango wa kwenda mbinguni, Bigo?” Alisema Nigaa. Lee akaangua kicheko kikali wakati wenzake wakiishia kutabasamu.



    Mchina huyu ungeweza kumdhania kama mtu mpole wa pendo, na asiye na tatizo na watu. Mkarimu, mtulivu na mwenye kupenda kufurahi. Ila kiuhalisia, hayo yote yangekuwa uongo kupitiliza.



    Mwanaume huyu mwenye asili ya huko mashariki ya mbali mwa dunia, alikuwa ni miongoni mwa watu wauaji wakubwa kabisa kupata kutokea duniani. Alikuwa mkatili na mwenye upungufu wa huruma mwilini pindi awapo eneo la kazi.



    Si tu kwa hapa Tanzania, bali hata huko kwao Uchina. Alishaua watu wengi kiasi kwamba hakumbuki tena idadi. Anaweza akamuua mtu lisaa limoja nyuma kisha akasahau hata uso wake!



    Miaka ishirini na mitano huko nyuma, mchina huyu aliokotwa akiwa mdogo kabisa katikati ya jiji la Hongkong akiwa anazurura, hana makazi. Akalelewa katika familia ya Wu akichangamana na wenzake ambao nao pia waliokotwa ama kutekwa maeneo mbalimbali ya Uchina.

    Takribani walikuwa mia mbili, wavulana kwa wasichana. Walihudumiwa vema kwa chakula na sehemu za kupumzikia. Ila walikuwa wanapewa mafunzo ya kupambana, mafunzo ya kufa ama kupona.



    Walifundishwa namna ya kuua, na wakapandikiziwa roho mbaya ya unyama. Walifundwa kutokujali wala kutokuwa na rafiki. Ilipogundulikana mtoto mmoja ana urafiki na mwingine, basi alijaribiwa kwa kupewa pambano apambane na mwenzake mpaka pale kifo kitakapo watenganisha.



    Japokuwa walikula na kulala mahali pazuri, mazoezi haya yaliwafanya wawe wapweke kwa muda mwingi. Kutokuwa na furaha, wala amani. Ila kwa upande wa familia ya Wu, hiyo ilikuwa sherehe kubwa.

    Lengo lao lilikuwa linatimia. Walifanikiwa kuwaandaa watoto waliokuja kurithi mikoba ya wauaji waliosambaa ulimwenguni kote wakifanya hili ama lile kwa manufaa ya familia ya Wu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Miongoni mwa watoto mia mbili, ni watoto thelathini tu ndiyo ambao walifanikiwa kukua na kuungana na jeshi, wengine wakienda na maji! Miongoni mwa watoto hao waliofanikiwa, alikuwa ni huyu Lee Sun. Mtambo wa mauti wa familia ya Wu.



    Kabla hata hajaenda kwenye uwanja wa mapambano, huko ‘duniani’, alikuwa tayari ameshanyofoa uhai wa binadamu kumi na tano. Wote wakiwa watoto wenzake ndani ya mafunzo.



    Kazi yake ya kwanza ilikuwa ndani ya jiji la Hongkong, baadaye Bangkok, Thailand na kisha Rabat, Morocco. Kote huko akifanya kazi moja tu, kuua pasipo mjadala. Alikuwa anakabidhiwa picha ya mlengwa na makazi yake, kisha yeye anaenda kumaliza kazi.

    Baada ya mafanikio ya shughuli zake hizo, ndipo akahamishiwa Dar es salaam kuipa nguvu makao yao mapya yaliyoanza kumea ndani ya Afrika ya mashariki.

    .

    .

    .

    "Si kwamba nimeshindwa kumuua, ila majira ya kumuua. Unadhani ningemmaliza pale mgahawani polisi alipokuwapo ingekuaje?” aliuliza Bigo, kisha akaendeleza soga: “Hata tuseme ningemmaliza na polisi pia, huoni kama ingekuwa msala mkubwa – kuchoma utambi mapema hivyo?”

    .

    .

    Lee akatikisa kichwa.

    .

    .

    “Ndiyo maana umeachwa hai la sivyo ungeshakuwa historia sasa, Bigo. Ila ndani ya siku hizo mbili hakikisha unamaliza hiyo kazi. Kama utakwama, usisite kututaarifu. Twaweza kutoa msaada.”

    .

    .

    “Msijali,” Bigo akasema akitikisa kichwa. “Ni kazi ya mkono mmoja tu, sidhani kama nahitaji mkono mwingine wa ziada.”

    .

    .

    .

    ***

    .

    .

    .

    Kwa mujibu wa saa ya mkononi ya Jona, ilikuwa ni saa moja na dakika nane jioni. Kwa kiasi kikubwa alikuwa amesogeza kazi zake ‘lukuki’ na sasa alikuwa akifunga ajirudishe nyumbani kwa ajili ya mapumziko.



    Jumanne alikuwa tayari ameshaondoka, hivyo alikuwa mwenyewe. Kwenye mkono wake wa kuume alikuwa amebebelea mfuko mweupe wa Rambo wenye chapa nyekundu, ndani ukiwa umejazwa na baadhi ya vitu.



    Alipanda bodaboda, kama ilivyo kawaida yake mara kwa mara, akaenda moja kwa moja mpaka kwenye bar karibu na makazi yake alipojiweka na kuagiza kinywaji laini kisicho na kilevi.



    Akiwa anangojea kinywaji, alichomoa simu yake mfukoni akaitazama. Kulikuwa kuna ujumbe kwenye mtandao wa Facebook toka kwa mwanamke fulani ambaye hakumtambua kwa haraka.

    Mwanamke huyo alikuwa anampa salamu akiambatanisha na vimdoli vitatu vinavyotabasamu.

    Kabla hajamjibu mwanamke huyo, akaenda kutembelea kwanza ‘profile’ yake. Kwa mujibu wa maelezo aliyoyakuta huko, mwanamke huyu alikuwa ni raia wa Afrika ya kusini. Mjasiriamali anayejihusisha na mauzo ya nguo akimiliki maduka kadhaa ndani ya jiji la Pretoria.



    Hakufanikiwa kuona uso wake kwakuwa hakuwa ametuma picha yake hata moja, bali bidhaa zake anazoziuza. Kilichomfanya akajua kuwa ni mwanamke ni jina la mtu huyo na uchaguzi wa jinsia aliouteua kwenye ‘setting’ yake, ‘Female’. Akamjibu salamu yake kwa ufupi, kisha akaacha aone ni nini kitatokea. Punde kinywaji nacho kikaja akakinyaka na kuanza kunywa. Akaagiza pia na chakula ale hapo hapo ili amalize kila kitu kabla hajaenda zake nyumbani ambapo alilenga atajipumzisha moja kwa moja kutokana na uchovu aliokuwa nao.



    Alikula na kunywa akisahau kabisa kuhusu simu. Alipomaliza akalipia chakula na kwenda zake nyumbani. Alioga kisha akaendea jokofu kuchomoa chupa kubwa ya kilevi na kuketi kitandani.

    Hakuwa na mawazo mazito kichwani, alijitahidi kujipuuzisha. Alikunywa kileo chake taratibu macho yake yakiwanda wanda ndani ya nyumba yake pweke.



    Haikupita muda mrefu, simu yake ikaita. Alikuwa ni mheshimiwa. Alisita kupokea akijiuliza. Ila akaamua kukata shauri na kuiweka sikioni.

    .

    .

    “Kesho, majira ya saa tano asubuhi naomba tuonane nyumbani kwangu,” sauti ya mheshimiwa ilinguruma. Kabla Jona hajaongea, simu ikakata.

    Jona akajikuta anatabasamu akitikisa kichwa chake. Akanywa mafundo matatu, kisha akajilaza kitandani.

    .

    .

    “Mheshimiwa, bila shaka bado hatujafahamiana vizuri,” aliongea mwenyewe. “Tumeshayavulia nguo haya maji, hatuna budi kuyakoga.”

    .

    .

    Kama maneno hayo angeliyasikia bwana Eliakimu Mtaja, basi bila shaka angezidi kuchochea hofu.

    Kwa muda huu tu, akiwa ndani ya sebule yake mkononi akiwa amebebelea glasi yenye kiywaji chekundu, alikuwa tayari amepaliwa na mashaka.



    Mkono wake uliobebelea kinywaji ulikuwa unatetemeka. Alikuwa ameubinua mdomowe kama upinde wa mshale. Uso wake ulikuwa mweusi, macho yake yakizama ndani ya fikira.



    Pembeni yake alikuwa ameketi Nade akiwa amekunja nne, mapaja yake meupe yakiachwa wazi na kimini cheusi alichokuwa amevaa. Naye mkononi alikuwa amebebelea glasi kubwa ya kinywaji.



    Mazingira yalikuwa tulivu.

    Watu hawa wawili walikuwa wametekwa na mawazo. Walikuwa kimya ila sura zikiwa nzito. Kwa muda kidogo, tendo lililokuwa linafanyika ni kupeleka tu glasi ya kinywaji mdomoni kabla Nade hajauvunja ukimya kwa kuuliza:

    .

    .

    “Kwahiyo sasa? – Kuna haja ya kummaliza?”

    .

    .

    Mheshimiwa akashusha pumzi ndefu. Akanywa kwanza fundo moja.

    .

    .

    “Hapana, Nade. Si haraka kiasi hiko.”

    .

    .

    “Vipi sasa kama akiligundua ya chini ya zulia? Huoni tutakuwa tumeshachelewa?” Nade akauliza.

    .

    .

    “Hapana,” mheshimiwa akajibu akitikisa kichwa. “Jona ni mtu mdogo sana kumhofia. Ataenda kush’taki wapi?”

    “Mheshimiwa, ishu si wapi atashtakia, ila mambo yetu ya siri yataanza kuwa wazi. Inaweza ikakamata atensheni ya watu na mwishowe chombo kikaenda mrama. Tone moja la chumvi laweza kuharibu chakula.”

    .

    .

    Mheshimiwa akanywa kwanza kinywaji. Fundo moja tena.

    “Ila Nade, tukimmaliza sasa hivi, hatutampata Mariam. Tutampatia wapi yule mwanamke mzandiki? Mimi namhofia sana Mariam kuliko Jona. Mariam anajua vyetu vingi vya uvunguni.

    Kadiri anavyoendelea kuwa mbali ya mikono yetu, ndivyo mambo yanavyozidi kuchacha. Mariam anajua mikataba, nyaraka, mipango, watu na mpaka washirika wangu.



    Huko alipo hatujui anafanya nini, na yupo na nani. Nilitamani sana kumuagiza Jona ammalize mwanamke huyu pindi tu atakapomuona, ila niliona litazalisha maswali kichwani mwake.

    Nakosa usingizi kumuwaza mwanamke huyu. Sina raha kabisa! Lengo langu la kwanza ni kumpata huyu mwanamke. Kuhusu Jona, sijali. Nataka tu kumtumia kwasababu najua ana uwezo wa kumpata huyo mwanamke.



    Punde tu akapompata, ummalize upesi kabla hajaanza fyoko fyoko yoyote!”

    .

    .

    “Mheshimiwa,” Nade akaita. “N’tajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu, ila inabidi sasa niwe namfuatilia Jona kwa siri maana naona hatakuwa na mpango wa kunishirikisha kwenye mambo yake tangu aone namfuatilia kupitiliza.”

    .

    .

    “Hakikisha haumtoi machoni mwako, sawa?”

    .

    .

    “Bila shaka.”

    .

    .

    Dakika tano mbele, mlango unagongwa. Mheshimiwa anatabasamu kidogo, ana habari na ujio huu. Anampa Nade ishara ya kichwa, Nade ananyanyuka na kuuendea mlango.

    Mgeni alikuwa Miranda. Alikuwa amevalia koti dogo jeusi la ngozi, suruali ya jeans ya kumbana na viatu rangi ya kahawia vyenye visigino virefu.



    “Karibu sana, Miranda,” Nade alisema kwa bashasha la tabasamu, akiutanua mlango zaidi na kunyooshea mkono wake ndani.



    “Ahsante, nimekaribia. Mnaendeleaje?”



    “Tupo poa. Kitambo kweli umetususa!”



    “Sema tumesusana, Nade. Hata nanyi mmekaa kimya kama maji ya mtungini.”



    “Bila shaka kuna jambo kubwa limekuleta!”



    Miranda akatabasamu pasipo majibu. Aliketi akamtazama mheshimiwa, wakapeana salamu.



    “Najua umeshatambua nini kimenileta mheshimiwa.”



    “Hapana. Pengine unikumbushe si unajua mambo mengi, Miranda.”



    “Ni kuhusu ile ishu tuliyojadili siku ile kule Mango garden.”



    “Hivi tuliongelea kitu gaaa …” Mheshimiwa alikuna kichwa kwa kidole akijaribu kukumbuka pasipo mafanikio. Alimtazama Miranda, Miranda akampa ishara ya macho kwa kumtazama Nade. Basi Mheshimiwa akamtoa Nade sebuleni kwa ishara ya kumtikisia kichwa.



    Sasa wakawa wamebakia wenyewe sebuleni.



    “Ni kuhusu yale madawa tuliyokuwa tumeyagiza toka Uswizi.”



    “Oooh! Sasa nimekumbuka!” Mheshimiwa akaliza vidole vyake. “Enhee vipi kwani mzigo umeshakamilika?”



    “Ndio, upo tayari kabisa na umeshapakiwa kwenye makontena kwa ajili ya usafirishaji.”



    “Makontena? – mmepanga kutumia njia ya maji?”



    “Ndio. Ndiyo njia ya kubeba mzigo mingi zaidi.”



    “Ni sawa, pia ndiyo salama zaidi ukilinganisha na njia ya anga. Kwahiyo jumla kuna makontena mangapi?”



    “Hamsini na mbili.”



    “Ni mengi mno. Haiwezekani yakasafirishwa yote kwa siku moja.”



    “Una mpango gani, mheshimiwa?”



    “Kuna mwanya wa kusafirisha manne tu kwa sasa, na ni juma lijalo. Mnaweza mkafanya hivyo?”



    Miranda akasita kwanza kujibu apate kutafakari.



    “Siwezi nikatoa jibu la moja kwa moja mheshimiwa, kama unavyojua ni lazima nipeleke taarifa hizi kwa mkuu wa kitengo kisha yeye ndiyo anipe maagizo.”



    “Basi mtaarifu hivyo. Juma lijalo kuna mpango wa kuleta kontena ishirini zilizobebelea vifaa vya kujengea uwanja wa kisasa kama ule wa taifa. Kama unavyojua vifaa hivi havitozwi kodi, na hata upekuzi wake unakuwa hafifu kwakuwa ni vya serikali.”



    “Ni kweli mheshimiwa. Ila vipi na kuhusu hiyo mzigo mingine itakayokuwa imebakia? – nayo inabidi ije kwa namna yoyote ile ili kukamilisha pakeji nzima.”



    Mheshimiwa akafichama mdomo wake kwa kiganja akitafakari. Aliangazia mianya anayoweza kuenenda afanikishe zoezi hilo. Wazo likamjia.



    “Ok, tutafanya hivi. Kadhaa zitabebwa kama nilivyokuambia – kwa kutumia makontena ya vifaa vya uwanja wa mpira. Na hayo mengine, yote, tutapitishia kwa kutumia mgongo wa shirika la madawa nchini.



    Tutafanya kama malighafi za kutengenezea madawa ya kutulizia maumivu na nusu kaputi. Unaonaje?”



    Miranda akatikisa kichwa kuafki.



    “Ni sawa, ila napata shaka kidogo.”



    “Gani hilo?”



    “Kuhusu usalama wa hiyo mizigo na pia ka …”



    “Miranda, hilo ni jukumu langu. Nimeshawahi kuwaangusha?”



    “Hapana, mheshimiwa.”



    “Basi unaweza kwenda kumfikishia taarifa mkuu wako. Mashaka yangu yapo kwenye muda wa shirika la madawa maana bado sijaongea na mtu wa huko nikajua. Ila … n’tawataarifu kesho I think.”



    “Sawa. Ada?”



    “Miranda, sasa mnaniangusha. Ndiyo tumeanza kufanya hii kazi leo kiasi cha kutokujua ada?”



    “Hapana, mheshimiwa. Kusema ukweli kwa sasa hali yetu imetetereka kiuchumi haswa baada ya sera za mambo ya nje za baadhi ya nchi kubadilika. Tuwiane radhi mheshimiwa na utuzingatie.”



    “Nenda, nitaongea na mkuu wako.”



    Miranda akanyanyuka na kwenda. Mheshimiwa akamuita Nade aliyekuja sebuleni upesi na kuketi.



    “Sorry kwa kukutoa hapa, Nade.”



    “Usijali, mheshimiwa. I understand.”



    “Thanks. Sasa kuna kazi imeibuka hapa na inabidi ifanywe haraka. Kesho, asubuhi na mapema, nitakuagiza kwenda kuonana na Maxwell Ndoja. Unamkumbuka?”



    “Ndio.”



    “Kuna mambo machache nataka umfikishie mdomo kwa mdomo. Hak…”



    “Hakikisha hamtumii simu, mtandao wala njia yoyote itakayoacha ushahidi!” Nade alimalizia kauli ya Mheshimiwa.



    Mheshimiwa akajikuta anatabasamu.



    “Sitakuambia tena hayo maneno kumbe umeyashika kiasi hicho. Anyway, baada ya Ndoja itabidi uonane pia na Nassoro Mauje.”



    Baada ya kusema hayo, akafunguka kumwambia Nade mambo gani ya kwenda kujadiliana na hao watu. Alipomaliza akafungia mjadala kwa kusema:



    “Kuwa makini. Hakikisha unatumia kila njia kuhakikisha hili jambo linafanikiwa, sina haja ya kukueleza ni kiasi gani cha pesa tutakivuna endapo dili hii ikitiki, unajua mwenyewe.”



    “Ndio,” Nade akajibu kwa kutikisa kichwa.





    ***





    Saa 04:35 asubuhi, ndani ya nyumba ya marehemu Bite.





    Sebuleni kuna watu watano, wanne wageni machoni, mmoja bwana Kinoo. Katika hao wanne ambao ni wageni mbele ya mboni, mmoja alikuwa mwanaume mzee kuliko wote akiwa amevalia suti rangi ya nyekundu na tai nyeusi yenye vidotidoti vyeupe. Aitwa Brokoli.



    Mwingine alikuwa mwanaume mwenye makamo ya miaka thelathini mpaka na tano. Alikuwa mweusi mwenye kichwa cha duara, uso mtulivu na macho ya kistaarabu. Alivalia ‘body’ nyeusi na suruali ya jeans. Aitwa Mudy.



    Wengine wawili walikuwa mapacha wa kike, Sara na Sasha. Wasichana warembo warefu wenye nywele nyekundu, macho makali makubwa na ‘lips’ pana nyekundu.



    Sara alikuwa amevalia gauni jeupe lenye madoa madoa ya maua, Sasha akivalia blauzi ya kijani na suruali pana nyeusi inayobana juu na kumwaga chini. Kwa makadirio, warembo hawa wana miaka isiyozidi ishirini na nane, wala kupungua ishirini na tano.



    Mzee Brokoli ndiye aliyekuwa anaongoza kikao hichi ambacho kiliita wajumbe wanaohusika na kampuni ya magari ya marehemu Bite. Lengo lilikuwa ni kujadili mustakabali wa kampuni hiyo lakini pia kumwongelea marehemu Bite kwa ujumla.



    Kwenye meza ya kioo, hapo sebuleni, palikuwa pamejazwa vinywaji vilaini; sharubati takribani tatu; ya embe, pasheni na machungwa zikiwa zimetapakazwa kwenye glasi kubwa tano kulingana na idadi ya wajumbe.



    Watu hawa walikuwa tayari wameshaanza kikao, na walikuwa katikati ya maongezi ambayo yalikuwa yanapokelewa kwa umakini na utulivu mkubwa.



    Brokoli alikuwa ananguruma.



    “Hatuelewi nini chanzo cha mauaji haya. Mpaka sasa polisi hawajampata wala kumshikilia mtuhumiwa yeyote yule, inashangaza kwakweli lakini pia inatia hofu. Inatuweka kwenye njia panda kujua kama mauaji haya yanahusiana na kampuni ama la!



    Lakini kampuni inabidi iendelee. Si kwamba kifo cha Bite basi ndiyo kiwe kifo cha kampuni. Ni mapema sana kuamua hivyo. Ila kama nilivyosema hapo awali, ni lazima sasa kampuni hii ibadilike. Tufanye mambo mengine mbali na haya mambo ya magari.”



    Hoja hii ikachukua muda kujadiliwa. Muda wote huo Kinoo alikuwa kimya kwani hili halikuwa linamhusu. Yeye alihudhuria hichi kikao kama mdau tu wa mbali, mwakilishi wa kampuni moja mteja wa kampuni ya magari ya Bite.



    Hapa kikaoni yeye alikuwepo kwa lengo la kupata taarifa tu, kama kutakuwa kuna mpya, kumhusu Bite. Pengine akapata jambo likamjuza aliyehusika na kifo cha mwanamke huyo.



    Hilo lilikuwa muhimu sana kwao. Kumjua aliyehusika na mauaji kungewafanya wachukue hatua kujilinda na kufuatilia kwanini mwanamke huyo ambaye alikuwa amebebelea siri kubwa, siri ya mafanikio, akapata kadhia kama hiyo.



    Basi hitaji lake hili likamvuta mpaka ukingoni mwa kikao hichi, ambapo huko kuna kauli ya Mudy ilimshtua na kumfanya afikirishe zaidi akili yake.



    “Kuna taarifa niliiwasilisha kwa mpelelezi wa kesi hii ya Bite, ni muda mrefu sasa, nikitegemea ingesaidia kwa namna moja kubwa kumpata muuaji. Ila ajabu haikufuatiliwa, ikapuuzwa!



    Hata pale nilipokuwa nampigia simu mpelelezi na kumkumbushia, sikuwa Napata majibu ya maana. Kwakweli nikakata tamaa.”



    Kiu ya Kinoo ikakua. Alitaka kujua zaidi kuhusu taarifa hiyo, basi akawahi kuuliza:



    “Ni taarifa gani hiyo?”



    “Sidhani kama kuna haja ya kujadili tena mambo hayo!” Brokoli akaingilia kati. “Hayo yameshapita, na hata tukiyateta hapa hayatabadili chochote. Tuendelee na mengine.”



    “Mkuu Brokoli, huoni tukilitilia mkazo linaweza kuleta angalau haki kwa dada yetu aliyeuawa kinyama?” Mudy akauliza.



    Brokoli akamkazia macho na ndita. Akamuuliza:



    “Mudy, wewe ni nani kwenye kampuni?”



    “Accountant,” Mudy akajibu akitazama chini.



    “Na mimi ni nani?”



    “Mkurugenzi.”



    “Basi sina haja ya kuongea tena. Tugange yajayo, si ya nyuma. Ina maana kuna kitu haukuelewa huko nyuma tulivyokuwa tunaongea?”



    “Nilielewa, mkuu. Samahani.”



    Kikao kikaendelea na kukoma punde fupi. Watu wakanyanyuka na kuondoka zao.



    Lakini kifuani mwa Kinoo mulikuwa mna jambo. Jambo mtambuka kumhusu Brokoli. Alimtazama mzee huyo katika namna ya pekee, namna ya tofauti na alivyokuwa anamtazama mwanzoni.



    Aliridhia na akili yake mzee huyu anahitaji kufanyiwa upembuzi zaidi, tena wa kina. Kuna jambo analijua kuhusu Bite.



    Kwanza, alitaka kujua kwanini alikuwa anasimamia sana hoja yake ya kubadili biashara, akikataa abadani kuendelea na biashara ya magari. Pili, kwanini hakutaka kugusia swala la taarifa ya Mudy juu ya Bite, ilhali mwanzoni alisema amefadhaishwa na ukimya wa polisi.



    Aliamini kabisa endapo akiyapata majibu ya maswali hayo, basi hatotoka mtupu. Kuna kitu atapata, muhimu, chenye faida.



    Taratibu akiwa ndani ya gari lake akatazama uelekeo wa gari la Mudy ambalo ndani yake lilikuwa pia limewabebelea Sara na Sasha. Gari hilo lilipotoka ndani ya eneo la nyumba, Kinoo akatia moto injini na kulifuatilia taratibu.



    Alikuwa yupo ndani ya Range Rover sport wanayoitumia kwenye kazi zao.



    Lengo lake lilikuwa ni kujua makazi ya Mudy, kwani watamuhitaji mtu huyo muda si mrefu. Kama taarifa yake ilipuuzwa na Brokoli, basi wao walikuwa wanaitaka. Tena kwa udi na uvumba!



    “Pole sana, Mudy, ndiyo boss huyo!” alisema Sara akitikisa kichwa na kutabasamu. Mudy akasonya. Alikuwa anatazama mbele aelekeapo. Mkono wake wa kushoto akiwa ameketi Sara, na Sasha amekaa nyuma peke yake. Ni ndani ya Rav4 nyeupe.



    Mudy akatikisa kichwa na kutahamaki:



    “Mpumbavu kweli yule. Sasa alikuwa analalamika nini kuhusu polisi kama hataki tuchangie mawazo?”



    Sara na Sasha wakaangua kicheko.



    “Sasa na hivi Bite amefariki, yule mzee si ndo’ atatupelekesha mpaka basi!” Sasha akapayuka.



    “Nakwambia!” Sara akadakia. “Tutapelekwa kama gari bovu maana mzee yule hataki kushauriwa wala nini!”



    “Tatizo mkoloni sana!” Mudy akaunga mkono hoja. “Sijui ametuitia nini kwenye hicho kikao chake kama kila kitu tayari ana majibu nacho. Si angetutumia tu ujumbe!”



    “Kwakweli. Lakini Mudy, ulikuwa na taarifa gani kuhusu Bite? Mbona hujawahi hata kun’tonya siku zote hizo?” Sara aliuliza.



    “Tatizo mambo mengi,” Mudy akajibu. “Huwezi kuamini nilikuwa nimesahau kabisa mpaka pale niliposikia tena kuhusu Bite pale kwenye kikao.”



    “Tuambie basi nasi tujue,” Sasha akashupaza masikio, Mudy akatabasamu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mnapenda sana umbea na nyie.”



    “Tuambie bana, Mudy,” Sara naye akashadadia. “We hujui umbea kwa mwanamke ni sunna!”



    Kabla Mudy hajasema neno, hamaki dereva bodaboda akakatiza upesi mbele yake! Alijitahidi kukwepa bodaboda kwa kupeleka gari kando ambapo napo huko kulikuwa kuna gari iliyokuwa inakuja nyuma kwa kasi, hivyo akaishia kubamizwa ubavuni na kusababisha tafrani barabarani!



    Sara na Sasha walipiga kelele kali za hofu. Mudy alifanikiwa kulimudu gari akilipakia pembezoni mwa barabara.



    “Shit!” Akalaani akisaga meno. Dereva bodaboda alitokomea asionekane wapi alipoelekea. Hakuna hata aliyenakili pleti namba yake.



    “Ahsante, Mungu!” Sara alisema akihema kwanguvu. Vifua vyao vilikuwa vinapwita kwa hofu pana. Sasha yeye alikuwa ameishiwa nguvu kabisa.



    Hawakuamini kama wametoka salama katika sekeseke hilo. Walikuwa wazima wa afya ila shepu ya mbele ya gari ikiwa imeharibika kiasi.



    Punde alitokea dereva wa gari lile lililoparamiwa wakati Mudy anamkwepa bodaboda. Akaongea na Mudy kwa muda mchache kabla Mudy hajatoleshwa pesa, noti nyekundu kadhaa, dereva huyo akaondoka zake.



    Hwakuhitaji trafiki polisi, waliona ni vema wakamalizana wenyewe.



    “Pole sana, Mudy. Sasa?” Sara aliuliza.



    “Siku yangu ishaharibika. Sina pesa yoyote hapa, yote nimetoa sababu ya yule bodaboda fala!”



    “Pole sana, Mudy. Ila bora una uhai, hayo mengine ni ziada tu, na yanatafutwa.” Sasha alimfariji. Mudy akashusha pumzi ndefu.



    “Tatizo gari yenyewe ilikuwa ina mafuta kiduchu, nilikuwa nimepanga nipitie sheli hapo mbele nitie mafuta, sasa pesa imeshaenda … anyway, nyie pandeni tu daladala muende, mie n’tajua cha kufanya.”



    Sara na Sasha wakaondoka zao. Mudy akasema na yake kifuani: kweli wanawake si wa kuwategemea kwenye shida, hapa ningekuwa na wash’kaji zangu chap tatizo lingekuwa limeisha.



    Akiwa hapo bado hajajua cha kufanya, mara Range Rover sport inatokea na kupaki kandokando yake, Kinoo anashuka na kumsalimu. Anamjulia hali na anapendekeza kumsaidia.



    “Pole sana, ndiyo mambo ya barabarani hayo. Sasa inabidi uipeleke gereji ifanyiwe matengenezo.”



    Mudy akaomba apelekwe kwanza ATM apate kutoa pesa kwa ajili ya mahitaji yake. Kinoo akambeba kumpeleka huko. Safari ikasindikizwa na soga ambazo Kinoo alikuwa amelenga kupatia majibu maswali yake.



    “Nyumbani ni mbali sana?”



    “Kiasi, naishi Mbweni.”



    “Mmh … ni mbali!”



    “Basi mie kwakuwa nimeshapazoea, naona si mbali sana. Ila kila mtu ninapomwambia naishi Mbweni husema ni mbali.”



    Kinoo akatabasamu pasipo kuonyesha meno.



    “In fact, ni mbali … Ila inabidi upunguze mawazo usije ukapata maswahibu mengine barabarani, Mudy. Mambo kama yale hutokea tu.”



    Mudy hakuelewa, kabla hajapata mwanya wa kunena, Kinoo akaendelea kujazia nyama simulizi yake.



    “Kiukweli Brokoli hakutakiwa kukukrash namna ile, alifanya makosa. Sikupendezwa naye kabisa. Na naanza kupata mashaka kama tutawezana naye kwenye biashara.”

    Mudy akaguna na kutikisa kichwa pasipo kutia neno.



    “Kama kuna watu ambao wamezaliwa kwa ajili ya biashara duniani, Bite alikuwa mmojawao. Mwanamke yule alikuwa smart sana. Anajua kuongea, kupanga na kusimamia. Alikuwa mhimili mkubwa wa kampuni yenu. Pengo lake gumu kulijaza.”



    “Ni kweli,” Mudy akaunga mkono hoja. “Zaidi ya yote alikuwa anaishi vizuri sana na wafanyakazi wake, kila mtu alikuwa anampenda. Kifo chake kilitushtua mno. Ametuacha kwenye mikono migumu.”



    “Kwakweli. Ni jukumu letu kuhakikisha angalau kifo chake kinaheshimiwa kwa kupata haki na kuwatia nguvuni wauaji.”



    “Kivipi sasa na wakati polisi na mkurugenzi hawaeleweki? Naona kama Bite ameenda na hamna lolote litakalokuja kufanyika.”



    “Wewe unataka iwe hivyo?”



    “Hapana, ila sina la kufanya sasa.”



    “La kufanya halikosekani Mudy. Mimi pia sitaki iwe hivyo kama wewe, sasa watu wawili ni wachache kufanya jambo?”



    Mudy akasita kujibu.



    “Ulisema ni Barclays?” Kinoo aliuliza. Mbele yao umbali mfupi kulikuwa kuna ATM ya Barclays. Yalikuwa ni maeneo ya Sinza, Kijiweni.



    “Yah! Ni Barclays,” Mudy akalipuka kujibu. Gari likatafuta mahali pa kuegeshwa, akashuka na kwenda kwenye ATM kutoa pesa. Kinoo akampeleka tena sheli alipochukua mafuta kwa kutumia kidumu kisha akamrejesha mpaka kwenye gari lake.



    Wakaagana, Kinoo akahepa zake wakipeana miadi ya kukutana karibuni wapate kutazamia namna gani ya kujadili na kufufua kesi ya Bite. Walibadilishana namba za simu kwa ajili ya mawasiliano zaidi.





    ***





    Majira ya saa nane mchana, maeneo ya Mwenge.





    Kwa kiasi kikubwa sasa Jona alikuwa amesogeza kazi zake zilizokuwa zimemtinga. Mgongo ulikuwa unamuuma kwasababu ya kuukunja kwa muda mrefu. Alijinyanyua akaunyoosha akipiga mihayo.



    Alimtazama Jumanne aliyekuwa amelala kitini, akamshtua na kumuuliza:



    “Vipi, hatwendi kula?”



    Jumanne akatikisa kichwa na kufumba macho yake mazito mekundu.



    “Unaendekeza usingizi enh?”



    “Hamna … sina njaa.”



    “Njaa unayo sema usingizi kwako ndiyo bora zaidi. Haya mimi naenda.”



    Jumanne akatikisa kichwa akiwa amefumba macho yake.



    “Sasa ukiwa umelala, utaona wateja kweli Jumanne?”



    “Nikisikia tu miguu, naamka,” Jumanne akajibu akiwa bado amefumba macho. Jona akatikisa kichwa na kwenda zake kwa mama K wa mgahawani.



    Kama kawaida aliketi na kutoa simu yake wakati anangojea chakula na kuanza kuiperuzi. Alizama mtandaoni Facebook, akakuta jumbe tano, nne toka kwa mwanamke yule wa Afrika ya kusini.



    Alikuwa anamjulia hali na pia amemtumia picha kadhaa za bidhaa zake, nguo na mikoba akiulizia kuhusu mrejesho wa fasheni. Jona akampuuzia. Akaenda moja kwa moja kwenye ujumbe mmoja uliosalia, ulikuwa pia wa mtu mgeni – mwanaume mmoja toka Uarabuni.



    Nayo akapuuzia.



    Hakuona kama kuna la maana huko mtandaoni. Akakagua akaunti ya Mariam – mke wa mheshimiwa, hakupata jambo. Basi akaamua kuacha simu na kufikiri mambo yake mengine.



    Chakula kikaja, akala taratibu. Alimfikiria Nade kidogo, akaachana naye. Alimfikiria Mheshimiwa, hapo akakumbuka kwamba ana miadi naye siku hiyo. La haula! Alikuwa amesahau kabisa.



    Alitazama saa yake mkononi. Aliwaza ni muda gani anaweza akaenda kumuona Mheshimiwa, akaona kuna haja ya kumuuliza. Akanyanyua simu na kumpigia. Simu ikaita pasipo majibu.



    Alirudia kwa mara nne lakini hakukuwa na mabadiliko. Akapata mkanganyiko.



    “Pengine akikuta missed calls zangu atan’tafuta,” alihitimisha kwa kusema hivyo kabla hajaweka simu chini, akamalizia chakula.



    Akalipia na kutoka ndani.



    Akiwa hana hili wala lile akashika barabara kufuata njia mbili kubwa za lami apate kuvuka na kwenda ofisini. Alivuka njia ya kwanza. Akiisogelea ya pili, kuna gari moja ndogo Mark 2 nyeusi, ikahamia upande wa pili wa barabara.



    Upande huu ndiyo ambao Jona alikuwepo akiangaza avuke barabara.



    Baada ya kuona kuna mwanya wa magari, Jona akashusha miguu yake juu ya lami na kupiga hatua za haraka haraka avuke salama.



    Ajabu ile Mark 2, upesi nayo ikahama upande, ila sasa ikiwa imeongeza kasi maradufu! Mlio wake mkali uliokuwa unanguruma ulimshtua Jona, akarusha macho yake kutazama.



    Hatua kama tano tu mbele yake, gari hilo, Mark 2, lilikuwa linakuja kwa kasi kubwa. Kwa mahesabu tu ya haraka ni kwamba asingeweza kumaliza barabara kwa kasi ya hatua zake.



    Haraka aliwaza. Akarusha hatua zake kukimbia, ila napo hakuweza kumaliza kuvuka, gari lilikuwa tayari limeshamfikia karibu mno kumpindua na kumvunjavunja.



    Hapo sasa ikabidia atumie ujuzi wake kujiokoa maisha. Kwa kutumia mguu wake mmoja akajirusha juu, kufumba na kufumbua, mgongo wake ukatua kwenye bodi la gari, akabiringita mara mbili kabla hajamwagikia kando gari likipita!



    Alitua akiweka mkono wa kulia chini, mguu wa kushoto ukinyookea nyuma na wa kulia ukiwa umejisimika kwa kuukunja.



    Ilikuwa ni ajabu! Walioshuhudia tukio hilo waliachwa kwenye bumbuwazi. Walichozoea kukiona kwenye tamthilia walikiona mbele ya macho yao, tena kamera zikiwa hazipo.



    Upesi alisimama kana kwamba hakuna lililotokea, akatafuta miwani yake aliyoiona kando na kuiokota. Ilikuwa imevunjika kioo kimoja na fremu zake zikiwa legelege. Akaikunja na kuiweka mfukoni, akaenda zake ofisini.



    Watu walikuwa wanamtazama, wengine wakidhani pengine ameumia pasipo yeye mwenyewe kujua. Aliwaambia yu salama akizidisha hatua apotee hapo.



    “Upo sawa, Jona?” Jumanne alimpokea kwa maswali.



    “Nipo sawa, usijali J,” Jona akajibu akiketi kitako kwenye kiti. Akachomoa miwani yake mfukoni na kuitazama.



    Jumanne alikuwa anamkagua kwa kumuangaza huku na kule kama ataambulia kuona jeraha. Macho yake yalionyesha bado yupo kwenye bumbuwazi la kutoamini kilichotokea.



    Kabla Jona hajaanza kuwaza kuhusu lile gari, alikuwa anawaza kuhusu miwani yake kwanza. Alijua fika yeye pasipo miwani ni nusura kipofu. Miwani yake ndiyo macho yake, sasa itakuwaje pasipo nayo?



    Ataweza pambana kwenye hii vita akiwa haoni? Alijikuta anajiuliza.





    Hakutaka kukaa tena hapo kazini, akaondoka zake. Bila shaka safari hii ilikuwa ni kwenda kutafuta miwani ya macho.



    Kwa muda kidogo ni kama kichwa chake kilikuwa kimechina. Hakutaka kukifikirisha zaidi. Alikua anatazamia tu ni wapi atapata miwani nzuri kwa ajili ya macho yake mabovu.



    Alikuwa anahitaji miwani haraka iwezekanavyo alafu ndiyo mengine yafuatie. Akanyookea duka moja la mwarabu mzee katikati ya jiji, Kariakoo.



    Ilikuwa ni ajabu kwa namna alivyoliteua duka hilo ingali alikuwa mhafifu wa kuona. Aliposhuka tu kwenye gari alijikuta mwili wake ukielekea uelekeo huo ambao haukuwa mgeni kwake.



    Ni wazi huko nyuma alishawahi kuja kwenye duka hili kununua miwani.



    Muuzaji wake alikuwa mzee wa kiindi mwenye ndevu nyingi rangi ya kahawia na baghalasia nyeupe ya nyavunyavu akivalia kanzu fupi rangi ya maziwa, pamoja na viatu vya wazi.



    “Umewezaje kufika hapa pasi na miwani?” muuzaji alimuuliza akiinamisha mgongo wake na kunyoosha mkono kutwaa miwani fulani iliyokuwa imekingwa na zingine, ikipakana na kioo.



    “Naenda kwa hisia kama jongoo!” Jona akatania, wakacheka. Alikabidhiwa miwani akaijaribisha kwa kujivesha.



    Alikuwa anaona sawia! Bahati kwake alikuwa anajua vipimo vya macho yake na hata aina ya miwani anayotakiwa kuivaa hivyo hakujisumbua wala kumsumbua muuzaji.



    Akailipia, ila kabla hajaondoka muuzaji akateka kidogo muda wake. Alikuwa mjawa wa simulizi mwenye maneno mengi japokuwa Kiswahili kilikuwa kinamtatiza hapa na pale.



    Wakati Jona anapiga soga na muuzaji huyo, alikuwa anaangaza angaza huku na kule akifurahia uwezo wake wa kuona uliorejea.



    Akiwa anaangaza angaza huko, akamuona mtu fulani aliyemtilia shaka. Alikuwa ni mwanamke mrefu aliyekuwa amevalia blauzi nyeupe, suruali nyeusi ya kumbana na viatu vyenye kisigino msawazo.



    Hakufanikiwa kuona sura ya mwanamke huyu, ila aliamini kabisa alikuwa anamtazama yeye kwani aliukwepesha uso wake upesi punde tu alipotazama upande alipo – upande wa mashariki.



    Alikuwa amevalia nywele ndefu feki ambazo ziliziba shepu ya kichwa chake na masikio. Pengine Jona angeviona hivyo vitu vingemsaidia kumng’amua mwanamke huyo.



    Ni nani? Jona akajiuliza. Alipata tu hamu ya kuona sura ya mwanamke japo haikuwa kubwa. Hakuwa na mashaka kiasi cha kumfanya achukue hatua nzito.



    “Nilisahau kukupatia risiti bwana Jona,” muuzaji alimgutua, akamtazama.



    “Ahsante,” alijibu upesi akiikwapua risiti kisha akarudisha macho yake kwa yule mwanamke.



    Hakumuona! Alikuwa amepotea.



    Alitazama huku na huko lakini hakufanikiwa kumpata. Aliamua kupuuzia, akaaga na kwenda zake kujipaki kwenye gari. Akiwa sasa njiani akaanza kudadavua tukio lile la gari mark 2 kutaka kumgonga.



    Akili yake yote iliamini tukio lile lilikuwa la kupangwa na si bahati mbaya, lakini ni nani analifanya? Nani yupo nyuma ya tukio hilo? Kwanini anataka kumfanyia hivyo?



    Aliamini watakuwa ni wale watu waliokuwa wanamfuatilia mpaka nyumbani kwake, yani Miranda na Kinoo, japokuwa shaka lake lilikuwa sehemu moja – mbona hawakutumia gari lao, Range Rover sport?



    Ila hiyo ilikuwa sababu ndogo sana kutia dosari kwenye ubashiri wake. Pengine gari limebadilishwa kuvunja ushahidi, ama basi wana magari mengi. Akili yake iliwaza.



    “Nitajua leo,” akajikuta anafanya maamuzi.



    Aliona sasa ni wasaa wa kukutana na adui yake uso kwa uso, macho kwa macho. Akashuka na kukwea gari jingine lililompeleka mpaka maeneo ya Kawe alipoteka bodaboda na kwenda moja kwa moja mpaka getini mwa makazi ya Miranda.



    Akagonga geti mara tatu.



    Mlinzi akafungua na kumtazama. Alikuwa ni mwanaume mrefu mweusi aliyekuwa amevalia sare zenye rangi nyekundu na nyeusi, pamoja na kofia iliyochoka, mkononi akibebelea kirungu.



    Mwanaume huyu mlinzi alikuwa mgeni maeneo haya, bila shaka kama si jana yake basi ni juzi ndiyo aliwasili.



    “Naweza nikakusaidia?” mlinzi aliuliza kwa sauti ya amri.



    “Naomba kuonana na mwenye nyumba.”



    “Una miadi naye?”



    “Hapana. Ni dharura tu, kuna jambo muhimu nataka kuongea naye.”



    “Kama hauna miadi naye siwezi kukuruhusu.”



    “Nimekwambia ni dha …”



    “Nimekusikia, na bila shaka nawe umenisikia. Siwezi nikakuruhusu kama hauna miadi!” mlinzi akasema akitoa macho yake mekundu.



    Jona akasonya. Sasa alilazimishwa kufanya kitu ambacho hakikuwapo kwenye mipango kwakua hakuwa tayari kuona muda wake alioutumia kuja hapo unaenda bure.



    Alidaka kichwa cha mlinzi kwa kutumia mkono wake wa kuume, akakizungushia upande wa kisogo na kukikita, mlinzi akazirai. Akamsukumia ndani kabla hajaingia na kufunga mlango mdogo wa geti.



    Akagonga sasa mlango wa sebuleni na kusubiria majibu.



    Miranda alikuwa chumbani ila aliisikia hodi hiyo. Kabla hajanyanyuka kwenda kuipokea, akafungua dirisha la chumbani na kutazama nje.



    Chumba chake kilikuwa kimekaa mahali ambapo alikuwa na uwezo wa kutazama na kuona kibarazani.



    Akamuona Jona.



    Alishangazwa haswa. Amepajuaje hapa? Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kuja kichwani. Hodi iliita tena, akanyanyuka na kwenda sebuleni.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog