Search This Blog

Thursday 27 October 2022

ANGA LA WASHENZI (2) - 1

 











    IMEANDIKWA NA : STEVE MOLLEL



    *********************************************************************************



    Simulizi : Anga La Washenzi (2)

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    ILIPOISHIA



    Alipomaliza kula akalipia na kunyookea ubalozi wa China. Humo ndani hakumkuta balozi bali msaidizi wake. Wakateta kwa lisaa limoja kabla Jona hajatoka ndani ya jengo hilo.



    Kitendo cha kutoka tu, ikachukua dakika mbili, Sheng akaarifiwa juu ya ujio wa Jona. Na shuku zake zote alizozileta ubalozini!



    ENDELEA



    Sheng akaweka simu yake chini kisha akashusha pumzi ndefu akiwaza. Akawasha sigara yake kubwa na kuinyonya akijizungusha na kiti kwenda huku na kule.



    Jona ... Jona ... Jona ... kichwa chake kiliimba hili jina. Inawezekanaje mwanaume mmoja akamwangaisha na kumkosesha amani kiasi hiki? Mtu mmoja? Chawa mmoja kwenye nywele?



    Hapana! Akang'ata sigara yake na kuitafuna kwa hasira. Huu ulikuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu! Na hauvumiliki. Kabla hajanyanyua simu yake kupiga, mara ikaita, akapokea.



    Walikuwa ni vijana wake waliopo Nairobi wakimuuliza kama kuna haja ya kuendelea na zoezi lao la kummaliza bwana Kamau Githeri ama waachane naye kwa sasa.



    Akawaamuru warudi nyumbani kwanza. Hali si shwari. Lazima bwana Kamau atakuwa analindwa kwa hali ya juu, na macho ya wanausalama yatakuwa kwake muda mwingi tangu tishio hilo.



    Aliposema hayo, akawataka vijana warudi nyumbani, kuna kazi ya kufanya. Tena warudi upesi mara moja!



    Akaweka simu chini na kutumbukiza mikono mfukoni. Akafuata dirisha kubwa lililopo ofisini mwake alafu akatazama nje akitafakari.



    Baada ya kama dakika kumi na tano, akampigia simu mhasibu na kumuagiza atenge shilingi milioni mia moja kwa ajili ya oparesheni kabambe. Majira ya jioni kabla hawajafunga ofisi kuondoka, ahakikishe pesa hiyo inafika ofisini kwake pasipo kukosa.



    **



    "Hodi!"



    Ilibishwa mara moja na kuitikiwa. Ni ndani ya nyumba ndogo ya wastani ipatikanayo maeneo ya Kimara, Dar es salaam.



    Kwa kuitazama tu, nyumba hii ilikuwa na takribani vyumba vitatu. Na kama kuna cha zaidi basi ni jiko, choo na bafu. Jona alipekua kwa macho ya haraka akingoja afunguliwe mlango.



    Mazingira ya hapo hayakuwa tulivu sana. Si kwasababu ya kelele toka ndani, lah! Bali toka kwa majirani. Uzio kuzunguka nyumba hiyo ulikuwa umejengwa ndani ya muda mfupi. Na kwa Jona alidhani pengine ni sababu ya makelele hayo ayasikiayo, mwenye nyumba alikuwa anataka kujitenga kidogo na muingiliano mkubwa ndani ya eneo hili.



    "Karibu," alisema mwanamke mmoja mnene mweupe aliyevalia dira akikatisha uchambuzi wa Jona kichwani. Mwanamke huyu kwa makadirio ya Jona alikuwa na miaka 45 - 50. Na ndiye shangazi yake Miriam.



    "Ahsante." Jona akaingia ndani wakasalimiana.



    "Nimemkuta Miriam?"



    "Ndio, yupo anaoga. Baada ya muda mfupi atakuwa hapa."



    "Ahsante. Nitangoja."



    "Unatumia kinywaji gani?"



    "Maji yanatosha.'



    Mwenyeji akamletea Jona maji ya kunywa na kisha akaketi.



    "Wewe ndiye Jona?"



    "Ndio, ni mimi."



    "Naomba umsaidie mwanangu, tafadhali. Naomba sana baba. Hana amani wala raha. Amedhoofu mno. Wale washenzi wamemchakaza haswa!"



    "Amekuambia nini kuhusu hao watekaji wake?"



    "Mengi tu, nadhani atakueleza mwenyewe kwa undani. Ana taarifa za kutosha kabisa zitakazowasaidia kuwatia nguvuni."



    Jona akamiminia maji kwenye glasi na kunywa mafundo matatu akipeleka macho yake hapa na pale. Ndani ya muda mfupi akagundua mama huyo ni mjane kwa kuona picha za mumewe zikiwa zimetundikwa ukutani na maandishi ya kumtakia kheri huko aliko.



    Zaidi akafahamu mama huyu ajihusisha na shughuli za utengenezanaji bidhaa kwa mikono baada ya kuona vyeti kadhaa za maonyesho na tuzo za utambulisho pia toka SIDO.



    "Ulikuwa unayafahamu mahusiano kati ya Miriam na huyo mwanaume aliyemteka?" Jona akauliza.



    Shangazi akanyamaza kwanza kidogo. Kuna kitu kilimkaba kuropoka. Alikodoa macho yake na kuyafumba, akang'ata lips.



    "Kusema ukweli nilikuwa nayafahamu, japo sikuyaridhia kwakuwa Miriam alikuwa tayari ndani ya ndoa. Japo aliniletea mashtaka kadhaa toka kwa mumewe, sikuona haja ya kumshauri aachane naye, sisi ni wakristo, ndoa ni moja tu."



    "Huyo mwanaume ashawahi kuja hapa? Mnajuana?"



    "Hajawahi kufika hapa japo namjua kwa sura."



    "Ulimwonea wapi?"



    "Kwenye simu ya Miriam."



    "Miriam alivyopotea ulikuwa unafahamu alipo?"



    "Nilikuwa najua yupo Arusha lakini sikujua haswa ni wapi."



    "Kwanini Miriam ameamua kuja kwako baada ya kutoka Arusha na si kwenda kwa maa mdogo wake aishiye Kinondoni?"



    Kabla shangazi hajajibu hili, Miriam akafika. Alitabasamu kumwona Jona, tabasamu la matumaini. Akamsalimu na kumkaribisha. Shangazi akawapisha.



    Pasipo kuchelewa wakaanza maongezi yao. Miriam kwa hisia sana akaeleza namna alivyokuwa anatendewa mpaka alivyojinasua. Akamweleza Jona nini Nyokaa anafanya na wapi anapatikana.



    Habari hizo zikamtosheleza Jona. Sasa akapata wapi pa kuanzia kumuwinda Nyokaa. Kufanikisha hilo, Miriam akamuahidi kumuunga mkono kwa asilimia zote, lakini pia hakusita kumpatia tahadhari.



    "Kuwa makini, si watu wazuri kabisa. Hawaoni shida yoyote kumuua mtu kisha wakamnyofoa viungo vyake na kwenda kuviuza."



    Hili kwa Jona lilikuwa jipya. Hakujua kama Nyokaa, mbali na biashara ya madini, anafanya pia na biashara ya viungo vya binadamu akivisafirisha kwenda Afrika ya kusini.



    Kwasababu hii basi, amekuwa akiteka nyara watu na kuwahifadhi baada ya muda kisha akiwaua na kwenda kuuza viungo vyao kama vile: figo, maini na moyo.



    Hata hapo wanapoongea na Miriam, kulikuwa kuna watu huko waliotekwa na wengine wakiwa watoto.



    Hili likamgusa Jona katika namna ya kipekee.



    "Sasa unahitaji kwenda rehab, Miriam," Jona akashauri.



    "Nataka, lakini nahofia sana usalama wangu. Hata hapa ninapokaa, Nyokaa anapafahamu, anaweza akatuma watu waje kunimaliza."



    Jona akajaribu kumtoa hofu kwa kumwambia atamuweka chini ya ulinzi kwa wakati wote huo atakaokaa hapo lakini bado kwa Miriam hilo halikutosha kabisa.



    Hakuna mtu aliyekua anamwamini anaweza kumlinda isipokuwa Jona mwenyewe.



    "Usijali, nitakuwa nakuja kukutembelea na tutakuwa tunawasilana mara kwa mara, sawa?"



    "Sawa."



    Kwa namna Miriam alivyoitikia ilikuwa ni kama anataka kumridhisha Jona. Hata Jona naye alilitambua hilo. Hakupuuzia yale maelezo aliyoyasema Miriam juu ya usalama wake lakini aliona kwa hatua hiyo itakuwa njema huku akitafuta namna bora zaidi.



    Akamuaga Miriam anaenda zake. Alikuwa amechoka mno kwa siku hiyo, aliona ni kheri aende nyumbani kupumzika.



    Lakini kabla ya kunyookea huko akaenda kituo cha polisi cha karibu na kutoa taarifa juu ya Miriam akitaka mwanamke huyo pamoja pia na makazi yake yatazamwe kwa jicho la kipekee kwani wapo hatarini.



    Alipokamilisha zoezi lake hilo akajiweka kwenye daladala kurudi nyumbani.



    Akiwa njiani akatathmini kazi yote aliyofanya kwa siku hiyo. Haikuwa mbaya, akajivunia. Kila kesi iliyokuwa mikononi mwake ilikuwa imefikia pazuri na ufumbuzi wake unaonekana.



    Akafika nyumbani na kumkuta Marwa akiwa ameketi sebuleni.



    "Pole kwa upweke."



    "Nilikuwa na mke wangu, sikuwa mpweke."

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mke wako?"



    "Ndio."



    Marwa akaonyeshe tarakilishi yake mezani. Jona akacheka.



    "Msalimie mkeo, mwambie shemeji anamsalimu."



    "Na wewe pia, msalimu wa kwako aliyeko ndani ya jokofu," Marwa akatania. Jona akacheka tena, akamwambia mwanaume huyo ni namna gani hawezi kulala mpaka atie kinywaji mdomoni.



    Kichwa chake kimekuwa kikifikiria sana familia yake, haswa wakati wa usiku.



    "Huoni sasa ni muda wa wewe kutafuta mtu mwingine?" Marwa akauliza. Jona akamtazama mwanaume huyo na kumkubushia yale maelezo aliyompatia yeye kipindi kile.



    Akimpata huyo mwingine, atamuweka hatarini. Alafu kwa sasa yu bize hatokuwa radhi kusumbuliwa na 'calls' na jumbe za mara kwa mara.



    "Unajua wanawake muda mwingine wana matatizo. Unaweza ukawa unafuatilia kesi nyeti sana, pengine raisi ameuawa, lakini yeye akakutumia ujumbe ukiwa kazini 'ina maana raisi ni muhimu kuliko mimi?'"



    Wakacheka. Jona akaendea jokofu na kutoa kinywaji, akatafuta na glasi akaviwek mezani. Akawambia Marwa kuwa amechoka sana lakini hataweza kulala pasipo kinywaji.



    "Nikuwekee kidogo?"



    "Hapana!"



    "Najua imekupelekesha sana asubuhi ya leo. Wewe si mlevi."



    "Umejuaje?"



    "Hakuna swali ninaloulizwa sana kama hilo. 'Umejuaje?'," Jona akatabasamu na kuongezea: "Anyways, hauna sura ya pombe. Niambie kama nadanganya."



    Wakaendelea kuteta kidogo, na jambo la maana walilozungumza kabla Jona hajapitiwa na usingizi wa kilevi, ni kesho yake waende kuwatembelea wazazi wake Marwa.



    Jona alikuwa anataka kuona antidote wanayoitumia. Pengine anaweza kuifutia ufumbuzi.



    Marwa akajikuta anapata moyoni. Alitokea kumuamini sana Jona. Aliamini mwanaume huyo atalipatia swala lake ufumbuzi japo hakujua ni kwa namna gani.



    Hii inaitwa imani.



    Alimtazama Jona akiwa amelala kwenye kiti, akamnyanyua na kumbeba kisha akaenda kumlaza kitandani. Akamfunika na shuka jepesi.



    **



    Saa mbili asubuhi.



    "Jona, hili ni kushangaza kabisa!" Alipayuka Kamanda. "Leo punde nilipofika tu ofisini, nimepokea ujumbe toka kwa mtu nisiyemjua akijiita 'msamaria mwema'. Taarifa zake zimeniogopesha sana, na zaidi zimenifanya nikatafakari kwa kina ni nani mtu huyo na kama ujumbe alionitumia unaweza kuwa kweli."



    Kamanda akabofya tarakilishi yake wakati Jona 'aliyekula' suti akimtazama kwa umakini. Kidogo Kamanda akamkabidhi Jona tarakilishi yake apate kusoma ujumbe huo.



    Jona akaupitia kwa wepesi kisha akamtazama Kamanda.



    "Umeupata ujumbe huu mwenyewe?" Akauliza.



    "Sijajua. Ila huyu mtu amejuaje akaunti yangu ya barua pepe?"



    Kabla Jona hajajibu, simu ya mezani ya Kamanda ikaita. Akainyofoa kwenye kitako chake na kuiweka sikioni. Alikuwa ni Kamanda mkuu. Naye amepata ujumbe kama alioupata Kamanda kwenye akaunti yake.



    Wakateta kwa dakika kadhaa. Kisha,



    "Sawa mkuu," Kamanda akamalizia simu yake na kuirejesha kwenye kitako chake alafu akalaza mwili kitini.



    "Jona," Kamanda akaita. "Sheng Li ana kesi nzito ya kujibu. Hizi tuhuma si nyepesi hata kidogo. Muite kituoni na hii kesi utaibeba wewe."



    Kisha akamtazama Jona kwa macho ya pole, yenye kiini cha msisitizo.



    "Anza upelelezi mara moja!"





    Sasa tunda lilikuwa limekwiva. Kifuani Jona akatabasamu akiona sasa muda wa kumuingia Sheng kwa miguu yote umeshawasili.



    Alikuwa analingoja hili kwa muda.



    Akanyanyuka akibeba jukumu hilo na kurudi ofisini kwake alipotulia na kumpigia simu Marwa. Akamwambia njia yake imezaa matunda. Wamepata kile walichokuwa wanakitaka!



    "Sasa mji wa Roma unaanza kuanguka. Kwa ushahidi tulio nao Sheng haweza kututoka abadani!" Jona akatilia muhuri.



    Baada ya lisaa limoja akatoka ofisini, akiongozana na wenzake wawili, wakaelekea kwenye ofisi ya Sheng. Huko wakamkuta mwanaume huyo akiwa ana kikao kifupi na wafanyakazi wake wawili wenye asili ya China.



    Akapewa taarifa ana ugeni toka polisi. Alipotazama kwenye kamera, akajikuta anatabasamu baada ya kumwona Jona!



    Tabasamu lake hili halikuwa la furaha, bali kifo. Hasira na chuki. Alitetemeka kwa hasira na hata kikao chake hakuweza tena kuendelea nacho, akakivunja mara moja akihaidi watakifanya tena pale atakapotoa taarifa.



    Jona akaingia ofisini.



    "Bwana Sheng, naitwa inspekta Jonathan toka makao makuu, polisi," Jona akaonyeshea kitambulisho chake kisha akaelezea dhumuni la ujio wake kumtaarifu Sheng kuwa yupo chini ya upelelezi maalum kwa kuhusishwa na tuhuma kadhaa za mauaji, biashara za magendo, vilevile umiliki haramu wa jeshi.



    Jona akamtajia orodha ya viongozi anaotuhumiwa kuwaua hapa nchini na nchi jirani, Kenya. Akamtajia 'kambi zake za jeshi' iliyopo hapo makaoni na Nairobi na biashara zake anazofanya.



    Sheng akabadilika rangi kuwa mwekundu. Lakini akamudu kutabasamu na kumtazama Jona kwa utararibu. Akamuuliza:



    "Mbona sielewi unachokiongelea inspekta?"



    "Unaelewa kila kitu," Jona akasema kwa hakika. "Kila nilichokieleza hapo kina uthibitisho na ushahidi. N jambo la muda sasa uovu kukaa wazi. Hakuns linalodumu milele, Sheng!"



    Sheng akashindwa kuzuia hasira zake, akakunja sura sasa. Moyo wake uligeuka kuwa barafu. Mikono yake ilitetemeka akiwaza kama ana haja ya kutoa bunduki yake kwenye droo awamalize polisi hawa mara moja alafu awazike kwenye himaya yake.



    Lakini hapana! Kwa kufanya hivyo ataharibu zaidi. Mpaka polisi hao wamefika hapo ni wazi huko makaoni kuna taarifa zao. Endapo akiwaua, atawakaribisha nzi zaidi kwenye kidonda ambacho anaweza kukificha.



    Leo Sheng akawa amejifunza somo moja muhimu sana. Si kila mahali wapaswa kutumia bunduki. Pale mbu anapotoa juu ya korodani, ndipo unapoelewa kwamba si kila jambo husuluhishwa kwa nguvu.



    Akairudishia vizuri droo yake yenye bunduki alafu akatabasamu.



    "Ni tuhuma," akasema kwa lafudhi yake ya ki-Mandarin. "Sishangazwi na tuhuma hizo, najua mimi ni mfanyabiashara mkubwa siwezi kukosa maadui wa kuniharibia."



    Akaonya.



    "Endapo tuhuma hizi zitakapobainika ni za uongo basi wanasheria wangu watahakikisha serikali inanilipa fedha nyingi sana kama fidia ya kunisumbua ... na utambue kabisa, Jona. Hili litahatarisha uhusiano uliojengwa kwa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Na sina haja ya kukuelezea ni kwa namna gani mnavyonufaika na uhusiano huu, kila mwananchi anajua."



    "Lakini si kila mwanachi anajua mnayoyatenda," Jona akamkatiza. "Hawajui pia mnavyonufaika katika haya."



    Akanyanyuka na kumtaka Sheng afike kituo kikuu cha polisi kesho yake asubuhi na mapema. Kushindwa kufanya hivyo kutamuweka matatani vilevile kutaweka bayana asubuhi na mapema kuwa tuhuma zake ni za kweli.



    Aliposema hayo Jona akaaga na kwenda zake. Sheng akabaki akisaga meno. Alishindwa hata kuongea. Moyo wake ulikuwa unamuenda kasi. Jona alimfanya ajione ni mtoto mdogo asiye na kitu, mdhaifu na hana akili!



    Hakuwahi kudhalilishwa kiasi hiki. Akalalama kifuani. Haikuwahi kutoka hata siku moja.



    Alinyanyuka akaendea jokofu akafungua na kutoa maji makubwa, akanywa yote kana kwamba alikuwa na kiu cha karne!



    Alitaka kupooza hasira zake. Alihisi kifua kinawaka moto. Baada ya hapo, angalau akijihisi ana unafuu, akarejea kitini, akawaza namna ya kufanya.



    Ilimbidi awe mwangalifu sasa. Hata kama anataka kumwangamiza Jona basi afanye hilo kwa pole, kwa ustadi, mikono yake isinuke damu kualika nzi.



    **



    "Mlitumwa na nani kwenda kumvamia Marwa?" Aliuliza Jona akiwatazama wanaume wawili mbele yake. Wanaume hawa mmojawao alikuwa ni dereva, na mwingine akihusika moja kwa moja kwenye tendo la utekaji wa Marwa. Walikuwa wamevalia suruali zao za vitambaa huku vifua vikiwa wazi, mikono na miguu imefungiwa vitini.



    "Hatukutumwa na yeyote yule!" Dereva akaropoka. "Tumeshasema tulikuwa tunamdai kwa muda mrefu, tulikuwa tunataka pesa yetu!"



    "Pesa gani?" Jona akauliza.



    "Ya biashara. Alitudhulumu!" Dereva akaendelea kuropoka. Jona akatabasamu kisha akawasogelea karibu.



    "Nimeshaambiwa ninyi ni wabishi. Hampo tayari kusema lolote. Mmefunzwa kukaa kimya, mmefunzwa kupambana na mateso, lakini mimi pia mimefunzwa kutesa. Ebu tuone nani mshindi."



    Jona akatumia robo saa tu, akapata kila anachokihitaji. Wanaume wale hawakuweza kustahimili mateso aliyowapa wakaweka bayana kila jambo kwamba walitumwa na Sheng kumchukua Marwa wampeleke akajibu mashtaka yake.



    Jona akataka maelezo zaidi kutoka kwao, ni wapi Sheng anapozikia wafanyakazi punde anapowaua? Hapa watumishi hao wakaleta tena ka ubishi, Jona akarejea zoezi lake la kuwabana pumzi akiwapiga nyundo za mbavu!



    Hawakustahimili, wakalegea. Wakaeleza. Maelezo yote hayo Jona akayaandika na kumfikishia Kamanda.



    "Hakikisha kesho atakapofika hapa, unamtia ndani kisha unaenda fanya msako kwenye himaya yake nzima. Utakapokuta miili hiyo ardhini utakuwa ushahidi mzuri sana. Itasaidia ku 'finalise'," Kamanda akapendekeza.



    "Sawa, mkuu, nitalifanyia kazi!" Jona akalibeba hilo kisha akatoka zake nje ya ofisi.



    **



    Majira ya jioni ya saa kumi na mbili.



    "Wèishéme bùshì ta?" (Kwanini sio yeye?) Sauti iliuliza nyuma ya mlango.



    "Wo genben bù xihuan ta," (Simpendi kabisa,) sauti nyingine ikajibu. "Wo suoyào de zhishì siwáng!" (Ninachokitaka afe tu!)



    Kukawa kimya kidogo.



    "Nàme ni you shé me jìhuà?" (Kwahiyo nini umepanga?)



    "Wo xiang qieduàn ta yilài de shou," (nataka kukata mkono anaoutegemea,) kisha akaongezea, "Ni huì bang wo ma?" (Utanisaidia?)



    "Wo huì bangzhù," (Nitasaidia,) mwingine akajibu.



    "Názhe ta. Ni huì zài jiudiàn de àn bian kàn dào ta." (Chukua hii. Utamwona kwenye fukwe ya hotel.)



    Baada ya muda wa dakika tano, ndani ya ofisi ya Sheng akatoka mchina aliyebebelea mkoba mkubwa mweusi. Akapanda Range rover modeli ya zamani, rangi ya grey, akaelekea Sea View hotel.



    Baada ya mwendo wa dakika kadhaa akawasili, akaingia hotelini na asichukue muda mrefu akatoka akiwa na mikono mitupu. Akazama ndani ya gari na kupiga simu.



    "Ta yijing shou dàole. Dàn zhè hái bùgòu!" (Amepokea. Lakini amesema haitoshi.)



    "Ta xiang yào duoshao?" (Anahitaji kiasi gani?) Sauti ikauliza simuni.



    "Ba jiàgé fan bèi nàme gàosù ni zenme xiang!" (Ongezea mara mbili alafu sema unatakaje!) Mtumishi akajibu.



    "Méiguanxì!" (Sawa!) Sauti ikamjibu simuni.



    Baada ya kuteta huko na kukubaliana, mtumishi akawasha chombo chake na kutimka. Sheng akatabasamu akiwa ofisini. Sasa mambo yalienda kama alivyotarajia.



    Akajilaza kwenye kiti na kunyanyua simu kumpigia mhasibu, akamwambia amletee tena milioni mia moja. Alipoirudisha simu mezani, akatabasamu tena. Hakika hakutegemea kama siku hiyo ingeisha vizuri.



    **



    Bado mpaka saa moja usiku ...



    "Tuondoke, muda umewadia," akasema Jona akimtazama Marwa. Walikuwa wameketi ndani ya sebule ndogo ya kawaida lakini ikiwa imepambwa kwa usafi wa hali wa juu.



    "Hatumngojei baba?" Marwa akauliza.



    "Muda umeenda, Tutakuja siku nyingine," Jona akashauri na mara kidogo akatokea mama mtu mzima, makadirio miaka sitini kasoro kidogo. Alikuwa mwembamba mwenye nywele za mvi, lakini akiwa mwenye nguvu na uchangamfu.



    Akaketi kitini.



    "Naona baba amechelewa sana leo," akasema. "Sijui atakuwa amepitia wapi!"



    "Usijali, mama," Marwa akamtoa hofu. "Tutakuja siku nyingine kumwona. Kwa sasa tunaomba tukukimbie."



    "Mbona mnawahi hivyo na mmekuja muda si mrefu?" Mama akashangaa. "Kaeni mumngoje kidogo. Nadhani ndani ya muda mchache, atawasili."



    "Kuna mahali tunatakiwa kupitia mama," Jona akaeleza. "Tungekaa mpaka usiku mzito."



    Mama hakuwa na budi, akawatakia safari njema lakini kabla hawajaondoka akahitaji aongee kidogo na Marwa. Jona akatangulia kwenda nje.



    "Vipi? Mbona unaondoka haujatupatia dawa?" Mama aliuliza, na kuongezea. "Unajua imebakia kiasi kidogo sana!"



    Akafungua fundo lake la kanga na kutoa kachupa kadogo kumwonyeshea.



    "Unaona?"



    Ndani ya kachupa hako kulikuwa na kama katone hivi ka maji ambacho kukaona ilihitaji umakini wa hali ya juu.



    "Nimeona, mama," Marwa akasema kwa upole. "Nitakuletea tu."



    "Kaburini?" Mama akastaajabu. "Unadhani haka katatuweka hai mpaka lini, Marwa?"



    Marwa hakuwa na la kusema, akatazama chini.



    "Kuna shida gani, Marwa? Naomba uniambie. Dawa imeisha?"



    "Hapana."



    "Sasa nini shida? Niambie mwanangu."



    Marwa akajikuta macho yake yanakuwa mekundu. Sauti ya mama yake ilikuwa inatafuna moyo wake. Alitamani kumwambia hayupo tena kule apatapo dawa lakini alihofia. Angeweza kumuua mamaye kwa presha.



    Akamtia tu moyo ampe kitambo kidogo, atakuwa ameshaleta dawa hapo nyumbani.



    "Kama kuna shida tuambie," Mama akamwambia akimshika bega. "Sisi ni wazazi wako, hauna mtu mwingine wa kumwaminini."



    "Hakuna shida mama," Marwa akakazana. Alikaza uso wake usionyeshe majonzi. Akamkumbatia mama yake na kumuaga. Lakini alipogeuka tu chozi likamshuka haraka. Moyo wake ulikuwa unamuuma. Alikuwa anashuhudia wazazi wake wakifa mbele ya macho yake.



    Alienda kukutana na Jona wakaenda zao. Hakusema jambo mpaka wanafika nyumbani.



    "Marwa, it's going to be ok!" Jona akamfariji. "Tutapata antidote tu."



    Marwa akajikuta anadondosha chozi. Akamtazama Jona na kumwambia shida si kuipata, bali muda. Antidote aliyoiona inawatosha kwa usiku huo wa leo tu. Kesho yake hawatakuwa na cha kutia mdomoni, wataanza kuteseka mno.



    "Kwa umri wao ilibidi wawe wamepumzika, si kupitia shida hizi," alisema Marwa kwa uchungu.



    Jona akamtazama kwa huruma. Baada ya mafikirio kidogo, akamuuliza:



    "Unajua antidote hiyo ilipo?"



    "Kivipi?"



    "Unafahamu mahali wanapoihifadhi antidote hiyo kule kwa Sheng?"



    "Hapana," Marwa akajibu akitikisa kichwa. "Lakini nafahamu ilipo maabara."



    "Si mbaya," Jona akateta. "Basi jiandae saa tano tunaenda huko!"



    "Wapi?" Marwa akatahamaki kwa woga.



    "Ilipo antidote!" Jona akafafanua. Na asingoje maelezo zaidi, akaenda zake chumbani. Marwa akabaki anamtazama kwa mshangao.



    **



    Baada ya kunyata kidogo,



    "Upande huu!" Marwa akaelekeza kwa sauti ya chini. Alikuwa amevalia nguo nyeusi na kinyago usoni. Na Jona pia.



    Walikuwa tayari wameshazama kwenye ngome ya Sheng katika majira haya ya saa sita usiku. Lengo lao likiwa moja, kwenda kuinyaka antidote ndani ya maabara.



    Wakatembea tena kwa utaratibu wakichukua kila tahadhari, walipokaribia maabara, wakamwona mwanaume mmoja aliyebebelea bunduki kubwa ndefu mkononi. Jona akaitambua ni SMG.



    Mwanaume huyo alikuwa ni mlinzi. Alikuwa ameketi kwenye kibaraza cha jengo la maabara akichokonoa meno yake kwa kijiti.



    Jona akampanga Marwa.



    "Utatoka na kunyata kuelekea upande huu," akamwonyeshea upande wa kushoto. "Lazima atakutazama na aidha anaweza kukuita. Lakini kabla hajafanya kitu, atakuwa tayari yupo mikononi mwangu."



    Marwa hakupewa muda wa kufikiri, Jona akaanza kutekeleza mpango. Haraka akanyanyuka na kutembea upesi kuelekea upande wa kulia, lakini akifanya hayo miguu yake haikutoa sauti hata kidogo.



    Basi muda mchache, mlinzi akamwona Marwa akikatiza, haraka akanyanyuka na kuishikilia vema silaha yake. Akapaza sauti:



    "Wewe nani?"



    Marwa akasimama na kumtazama.



    "Mimi? Mimi naitwa Marwa!"



    "Marwa?" Mlinzi akatahamaki. Hakuwa analijua jina hilo katika orodha ya walinzi. Akamtaka Marwa anyooshe mikono juu na kupiga magoti.



    "Sina tatizo na wewe," Marwa akasema akishuka chini. "Mwenye tatizo ni huyo aliyepo nyuma yako."



    Haraka mlinzi akageuza shingo kutazama. Mara shingo hiyo ikadakwa na kuendelezewa safari. Akadondoka chini kama mbuyu.



    Wakamficha, kisha chap wakaufuata mlango mzito wa maabara. Ulikuwa ni mlango wa chuma wenye kitasa kipana. Wakajaribu kuufungua pasipo mafanikio.



    "Jona, inabidi tukachukue funguo!"



    "Wapi?"



    "Stoo. Kule wanapozihifadhi."



    "Hatuna muda huo Marwa. Mlinzi mwingine anaweza kutokea akagundua uwepo wetu. Na endapo akirusha risasi moja tu, atakuwa keshatibua mambo."



    "Sasa tunafanyaje?"



    Jona akavua mkanda wake na kuchomoa kichuma cha kushikilia vitundu mkandani. Akakipinda kichuma hicho kwa mdomo, akitumia sekunde kadhaa kama ishirini, alafu akakidumbukiza hicho kichuma ndani ya kitasa.



    Akapeleka mkono kushoto na kulia, mara mlango ukalia - kat! Wakajaribu kuufungua. Hola! Mlango haukufunguka.



    "Shit!" Jona akalaani.



    Akakirepea tena kile kichuma kwa kukibadili muundo wake, alafu akajaribu tena. Mlango ukalia tena - kat! usifunguke.



    "Jona, tunapoteza muda. Twende kule," Marwa akashauri.



    "Hapana, Marwa," Jona akatikisa kichwa. "Mlango huu umelokiwa mara tatu, utafunguka tu ... ngoja uone ..."



    Jona akachokonoa tena kitasa, mlango ukalia tena - kat! Na mara hii walipougusa ukatii amri! Wakazama ndani.



    Maabara ilikuwa kubwa. Wakitumia kurunzi kuangaza, wakaanza kupekua upesi upesi. Wakachukua dakika nyingi humo. Baadae ndipo wakaona chumba kidogo ndani ya maabara kikiwa kimeandikwa antidote mlangoni.



    Jona akafanya ufundi kufungua kitasa kisha wakazama humo ndani, baada ya muda kidogo wakatoka Jona akiwa amebebelea flask - chupa ya kioo yenye mdomo mwembamba chini ikiwa imejitanua mithili ya pembe tatu. Ndani ya chupa hiyo kulikuwa na kimiminika mithili ya maji.



    Kwa haraka wakajongea kuufuata mlango wa maabara, lakini kabla hawajaufikia, Marwa akajikwaa. Mguu wake ulidumbukia ndani ya vifereji vidogo vya kutolea uchafu, akajikuta yu chini kwa kukosa namna ya kujiokoa!



    Kabla hawajafanya jambo, ndani ya muda mfupi, wakasikia chupa kadhaa nazo zikidondoka na kusababisha kelele!



    Mara huko nje, sauti nzito ikauliza:



    "Nani huyo?"



    Alikuwa ni mjibaba wa miraba minne, mkononi akiwa ameshikilia bunduki ndogo.



    Mwili wake mpana kama gogo ulikuwa umesitiriwa na nguo nyeusi. Chini ana buti kubwa rangi ya kaki. Kichwa chake kinameremeta kwa kukosa nywele. Na mdomo wake ukiwa umefunikwa na mustachi mzito wenye afya tele.



    Jibaba hilo likalalama.



    "Yani hawa panya sasa naona wananipanda kichwani!"



    Likapiga hatua nzito kuufuata mlango lakini kabla hajaugusa, akauliza:



    "Isak yupo wapi?" Akitazama huku na kule kisha akalalama;



    "Hawa panya watamaliza vitu vyote humu ndani. Experiment gani hizo za kila siku kutumia panya!"



    Akasonya.



    "Hakuna mnyama namchukia ka --"



    Akashtuka kuona mlango una upenyo. Asiamini macho yake akausukuma kwa kidole, mara ukafunguka na kuachama. Akapata wasiwasi. Akashikilia vema bunduki yake na kuzamisha mkono ndani, akabofya switch, taa zikawaka!



    Akaangaza akinyooshea bunduki yake huko. Kwa mbali akona chupa kadhaa zikiwa zimepasuka. Akapiga hatua kusonga.



    Pembeni ya chupa hizo zilizopasuka, kwa chini ya meza za sementi zilizokuwa zimejengwa humo, alikuwa amelala Marwa.



    Alikuwa ameubana mdomo wake kwa nguvu akijitahidi kutulia lakini alikuwa anasikia maumivu makali sana. Chupa zile zilizoanguka zilimrushia kemikali usoni na alikuwa anahisi kuungua!



    **



    Yule mtu wa miraba akafika eneo hilo lililopasukia chupa, akaangaza akisukuma sukuma vyupa kwa buti lake jeusi akiwa amebinua mdomo. Akatazama kushoto na kulia. Akasonya lakini kabla hajapoga hatua akauona mguu wa Marwa. Akashtuka kana kwamba ameona nyoka kwenye majani.



    Akaamuru upesi Marwa atoke kwa uhai wake kabla hajamwaga ubongo.



    Kwa uoga Marwa akaanza kujisogeza akiomba asiuawe. Akatoka akiwa ameshikilia uso wake alioukunja kwa kuhisi maumivu makali.



    "Wewe nani?" Akauliza mtu mnene. Bwana, hakukaa sawa akala jiwe la kichwa!



    Si jiwe unalolijua wewe bali ngumi. Akadondokea chini kama kiroba cha tani. Kuangaza akamwona mwanaume akiwa amesimama mbele yake hatua kadhaa.



    Akaguna kwa kebehi. Akatazamia bunduki yake, akatahamaki Marwa ameshaikomba na kuijaza kiganjani.



    Akacheka. Akapangusa eneo alilopigwa kisha akasimama!



    Kwa mtu wa kawaida kwa ile ngumi aliyopewa, asingeamka abadani. Kwa unafuu angezirai, ila kawaida ni kufa tu.



    "Najua hamuwezi nipiga risasi!" Jamaa akagamba. "Mkipiga risasi mtashtua jengo zima hili, na ndani ya sekunde tu mtageuzwa bucha. Kama nyie ni wanaume kweli, kunja!" Akatapa akitoa macho yake makubwa mithili ya bundi.



    Kwakweli alikuwa anaogopesha. Mwili wake ulijawa na misuli na kwa kumtazama tu ungetambua amekomaa haswa. Nguo zilikuwa zimembana.



    Jona akamtaka Marwa ashushe bunduki, na asogee kando. Wakatengeneza ka uwanja kadogo kwa ajili ya pambano.



    "Utatambua kwanini nilipewa jina la Baba!" Akatapa jamaa akijitambulisha. Akanyoosha shingo yake kisha mabega, ka!-ka!-ka! Akanyoosha vidole ka!-ka!-ka!



    Alafu kama fuso akamfuata Jona. Akatupa mawe ya maana. Ngumi nzito haswa. Jona akazikwepa akisogea nyuma na pembeni.



    Baba akaendelea kurusha ngumi za mfululizo, mwishowe Jona katika kukwepa miwani yake ikadondoka chini. Kosa! Akala ngumi tatu zenye uzito wa tani! Akadondoka chini akiachama kwa maumivu makali! Kinyago kilipasuka. Akavuja damu mdomoni na puani kidogo.



    Baba akatabasamu kiushindi.



    "Amka!"



    Jona akapapasapapasa chini kuitafuta miwani yake, Baba akaisukumizia kando kwa mguu, kisha akamnyanyua Jona kama unyoya na kumsogeza karibu na uso wake.



    "We ni mtoto kwangu. Mimi ni Baba! Mimi ni nani?"



    Jona alikuwa anona maruweruwe kana kwamba mtu anayetazama akiwa chini ya maji ama ameingiliwa na maji machoni. Alikuwa anahangaika kuona lakini hakufanikiwa. Macho nayo yalikuwa yanamvuta.



    Baba akamrusha kwa juu alafu akamtwanga ngumi! Akabidukabiduka hewani kabla hajadondokea chini kama mzigo!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Tih!



    Akahisi mwili mzima umevunjika. Akagugumia kwa maumivu akijikusanya. Mdomoni alikuwa anamwaga damu.



    "Amka!" Baba akasema kwa kejeli akimtazama Jona. Haraka na kwa ukimya, Marwa akatambaa kuifuata miwani ya Jona. Haikuwa mbali sana na yeye. Alipoikamata mkononi akaificha alafu akamwita Baba.



    "Hey!"



    Baba akageuka kumtazama.



    Marwa bado alikuwa anagugulia maumivu ya kemikali, jicho lake moja akiwa amelifunga. Akamkebehi Baba kwa makusudi. Baba akakasirika na kumfuata. Marwa kwa kulenga, akairusha miwani juu ya mwili wa Jona.



    Jona akapapasa na kuikamata. Akaivaa.



    Baba akamnyanyua Marwa juu kama alivyofanya kwa Jona. Lakini kabla hajafanya kitu, akaguswa begani. Kugeuka likawa kaburi lake. Akapokea ngumi nzito ya shavu, akapepesuka.



    Asikae vema, Jona akampatia dabo bundle za teke. Akapepesuka akijakakamua kwa hali na mali asianguke chini.



    Jona akaamua sasa kumpatia KATAUTI - Mateke mawili yanayoyofyatuliwa baada ya kiumbe kupaa hewani kwa namna ya mzungusho. Baba akashindwa kustahimili! Akadondoka chini kama tembo.



    Jona akamuwahi Marwa kumjulia hali.



    "Upo ok?"



    "Yah! Am ok!" Marwa akajibu bado akiwa ameficha jicho lake moja.



    "Sure?" (Hakika?) Jona akasisitiza.



    "Yah! Niko ok!" Marwa akajibu lakini hali aliyomo ikimsaliti. Baadhi ya sehemu zake za uso zilikuwa zimeanza kubadili rangi, Jona aliliona hilo na akapata hofu.



    Kabla hajasema kitu, Marwa akamshtua Baba anakuja. Jona akasaga meno na kumwambia:



    "Ningoje hapa twende nyumbani."



    Bwana we! Kama kuna kosa aliwahi kufanya Baba tangu azaliwe, lilikuwa ni hili. Kuamka tena. Na hatokuja kulisahau kosa hili maisha yake yote.



    Kwa kasi ya ajabu, Jona alimrushia ngumi zisizo na idadi. Akajitahidi kupangua mbili tatu lakini baadae akashindwa. Jona alikuwa haraka mno. Kasi yake ilikuwa ya ajabu!



    Mpaka Jona anamaliza, Baba akajikuta hawezi kusogeza kiungo chochote cha mwili. Akadondoka kama mbuyu asiamke tena!



    Jona na Marwa wakatoka ndani ya maabara wakiwa wamebebelea antidote waliyoifuata. Wakatembea kwa tahadhari mpaka ukutani, wakaambaa na ukuta huo kwenda mbele, kidogo wakasikia sauti za watu wakiwa wanateta.



    Jona akaangaza, akaona watu wakikatiza. Akamuagiza Marwa amngoje kidogo, akasonga na kuchungulia, akawaona wanaume kama kumi kwa idadi. Wote walikuwa weusi. Walikuwa wanatoa maboksi toka chumba fulani hivi na kuyaweka nje.



    Kidogo, Jona akamwona mwanaume mwenye asili ya kichina akija hapo. Akafungua maboksi kadhaa na kuyatazama alafu akashika kiuno akiwatazama wanaume waliokuwa wanaendelea kuyaleta.



    Hawakuchukua muda mrefu, wakasitisha zoezi. Mchina akayahesabu maboksi yale alafu akapiga simu. Ndani ya muda mfupi, gari aina ya Van jeusi likaja hapo maboksi yakaanza kupakiwa.



    Kabla zoezi hilo halijakamilika, mara mlio wa tahadhari ukaita kwanguvu kuhabarisha hali si salama. Wanaume wale wakatazamana, kisha haraka wakaacha kupakia maboksi na kusambaa kila eneo.



    Baada ya muda mfupi wakagundua maabara ilikuwa imekwapuliwa, mlinzi mmoja amefariki na mwingine yu hoi hajiwezi.



    Kufuatilia nyayo za viatu na matone ya damu wakafika mpaka pale Jona alipokuwa anawachungulia. Wakagundua wameshatokomea.



    Taarifa zikamfikia Sheng. Akiwa amevalia 'casual' akafika eneo la tukio na kushuhudia kila kitu. Akang'ata meno kwa hasira. Kwa akili yake yote akaamini ni Marwa wakishirikiana na Jona ndiyo wamefanya hayo.



    Mosi, Marwa hawezi kupigana kuwaangusha wanaume wale, hivyo alimhitaji Jona. Pili, Jona hakuwa anajua mazingira hayo, hivyo alimhitaji Marwa.



    Walikuwa wanaisaka antidote. Si kwasababu nyigine bali kuwapelekea wazazi wa Marwa.



    Sheng akaagiza wazazi wa Marwa waangamizwe kabla ya jua la kesho halijazama. Na kuhusu Jona, awachiwe yeye anajua dawa yake.



    **



    "Inabidi twende hospitali," alisema Jona akimtazama Marwa kwa muda mfupi kabla hajarudishia macho yake mbele waendako.



    Walikuwa ndani ya gari Jona akishikilia usukani.



    "Nitakuwa poa tu usijali," Marwa akasema akiwa amelaza kichwa kitini.



    "Hapana, lazima twende hospitali! That is chemical!"



    Marwa hata kuongea hakuweza. Alikuwa anasikia maumivu makali. Alihisi kuna michanga na changarawe jichoni huku upande huo wa uso ukiwa unawaka moto.



    Wakashika barabara ya kwenda hospitali, wakasonga nayo kwa kwa dakika kadhaa, kabla ya kukata kona kwa mbele kuingia hospitalini, Jona akatazama sight mirror. Akakunja ndita na kusema:



    "Nahisi tunafuatwa!"



    Marwa akakodoa jicho lake moja lililozima ila ghafla akaliminya kwa kuhisi maumivu. Ni kama vile alipigwa na shoka kichwani.



    **





    Wakakata kona kuzama ndani ya hospitali, na lile gari ambalo Jona alikuwa analishuku likanyoosha na barabara. Wakatambua kumbe ilikuwa hofu yao tu, hakuna anayewafuata. Ndani ya muda mfupi wakaonana na daktari na kisha kujieleza.



    Marwa akaafanyiwa uchunguzi na ikabainika ameathirika na kemikali, mishipa midogo midogo ndani ya macho imeathirika na hivyo jicho lake hilo linaweza kuwa kipofu kabisa ama kufifia uwezo wake wa kuona.



    "Kama msingeliwahi zaidi basi lingepasuka ama kulika kabisa akawa chongo," alieleza daktari. Jona akapata shaka kwa Marwa kuwa na hali kama ya kwake.



    Baada ya muda mfupi wakaruhusiwa kutoka hospitalini wakiwa wamepatiwa dawa ya kutia jichoni na kupaka usoni.



    Kwa maumivu aliyokuwa nayo na 'ka ahueni' alikokapata baada ya kufanyiwa dawa, Marwa akalala akimwacha Jona peke yake anaendesha gari.



    Waliwasili nyumbani, Jona akamsaidia Marwa kushuka ndani ya gari na kumpeleka mpaka chumbani akapumzike alafu yeye akajirudisha sebuleni kana kwamba ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni wakati muda ulikuwa umeshaenda.



    Kwa sasa ilikuwa inaelekea saa tisa na nusu usiku.



    Alifungua jokofu atoe kinywaji, akatahamaki hakukuwa na kitu. Vilikuwa vimekwisha. Akalaani vikali. Vimeishaje hata hakutambua? Akaketi kitini akiwa amekangangikiwa na akijilaumu kwa kutotambua hilo mapema.



    Uzembe wa aina gani.



    Mwili wake ulikuwa unamuuma kwa zoezi alilotoka kufanya ndani ya himaya ya Sheng. Na kichwani pia alikuwa ana mawazo. Alihitaji kinywaji apate kulala.



    Awe anakunywa taratibu huku akiichambua siku yake nzima mpaka anapotelea usingizini. Kwa kufanya hivi huwa kunamsaidia kesho aamkapo ajue ni nini cha kufanya.



    Akakaa hapo kochini kwa muda mrefu sana. Macho yalikuwa meupe na yenye nguvu lakini mwilo ukowa hoi. Hata akajilaumu kwanini hakuteka vidonge vya usingizi kule hospitali.



    Alibadili kila mkao kitini mwishowe akaenda kitandani kujilaza. Muda mfupi akapitiwa na usingizi. Alipolala hapo kwa muda mfupi akakurupuka baada ya kuota ndoto mbaya.



    Huwa hivi kila alalapo pasi na kinywaji. Anaota familia yake. Anakumbuka siku aliyowaona wakiteketea ndani ya nyumba yao iliyogeuzwa tanuru.



    Akatazama saa, saa kumi na moja! Hata hivyo akashukuru ndoto hiyo kwa kumwamsha ndani ya muda. Akajiandaa kwenda kazini.



    Hakutaka kumsumbua Marwa, alijua amechoka sana na kitambo kifupi tu amelala. Akamtazama tu kwa kumkagua na macho yake alafu akaondoka.



    Lakini alipokuwa huko ofisini, bado akajihisi mchovu mno. Hakuweza kufanya kazi yake vema. Mwili ulikuwa mzito, alihisi pia kichwa kimeongezeka ukubwa anahangaika kukimudu.



    Haikutakiwa awe hivyo siku hiyo. Siku hiyo ilikuwa muhimu mno kwani Sheng alikuwa anafika kituoni kwa ajili ya mahojiano na pia atazamie kama kuna haja ya kumtia ndani.



    Alitakiwa awe mwenye nguvu, mwenye hari, lakini haikuwa hivyo.



    Akatazama saa yake. Akamuwaza kidogo Sheng na kile walichokifanya jana. Akajikuta anagutuka! Macho yalimtoka kwa kukumbuka jambo. Akabamiza meza.



    Shabash! Wazazi wake Marwa!



    Haraka akatoka ofisini, akajipakia ndani ya gari na kutimka haraka. Alijilaumu sana kwa uzembe alioufanya. Kivipi aliwasahau wazazi hao?



    Bayana hawatakuwa salama kwani Sheng atakuwa ameshagundua kwamba wameiba antidote. Moyoni akawa anasali akute kila jambo jema.



    Kwa kasi kubwa akaendesha gari akili yake ikiwa bize. Alipowasili, akakimbilia ndani na kuangaza. Hakukuta mtu sebuleni. Akaita, napo kimya.



    Akaenda chumbani. Akajikuta uchungu unamkaba baada ya kuona maiti mbili kitandani!



    Wazazi wake Marwa walikuwa wameshauwa. Walididimiziwa risasi kwenye mapaji yao ya uso.



    Jona akashindwa kuzuia machozi. Akaishiwa nguvu kabisa. Aliketi kitandani akishikilia kichwa chake kwa manung'uniko na lawama. Kazi yote waliyoifanya ilikuwa bure. Tena ikiwagharimu mara mbili yake.



    Kwa muda kidogo akawa hajui cha kufanya. Alihisi kichwa kimeacha kufanya kazi. Hana hisia wala wazo lolote.



    Hakufahamu ni kwasababu gani, ila baada ya muda, akajikuta anamkumbuka mkewe. Alijihisi mtupu. Mpweke rohoni. Alikumbuka tabasamu lake na namna alivyokuwa anamkumbatia kila arudipo kazini. Akimbebeleza alale na akimsihi aamke.



    Pengine alikuwa anahisi anakosa hayo mambo kwa kipindi kama hiki kigumu. Haikuwa la kuficha, muda huu alikuwa anamhitaji sana mke wake kuliko kipindi kingine chochote.



    Akiwa kama mtu asiyejitambua wala kuonyesha kujali akalala hapo na maiti hizo mbili.



    Alikuja kushtuliwa na kurejeshwa fahamuni baada ya ujumbe kuingia ndani ya simu yake. Simu ilitetemeka mfukoni, akaichomoa na kuitazama. Ilikuwa ni ujumbe toka kwa Marwa.



    'Naomba unisaidie kuwapelekea wazee antidote'



    Jona akatikisa kichwa chake kwa masikitiko. Akaamka na kuidumbukiza simu mfukoni kisha akaendea gari na kujipakia.



    Akiwa njiani, simu ikaita. Kamanda.



    "Upo wapi na unajua leo Sheng anakuja kituoni?" Kamanda alifoka.



    "Nipo njiani, mkuu," Jona akajibu alafu akakata simu.



    Muda mfupi akawa ameshafika na mbele yake, ndani ya ofisi, yupo mwanaume mchina. Mfanyabiashara mkubwa nchini, bwana Sheng tayari kwa ajili ya mahojiano.



    Lakini Jona hakuwa sawa. Asingeweza kufanya kazi yake inavyotakiwa. Akamwomba radhi Sheng na kumtaka aje siku nyingine atakayompa taarifa kwani kuna dharura.



    Sheng akatabasamu, kisha akamuuliza:



    "Unaenda msibani?"



    Jona akamtazama kwa jicho kali. Alitamani amrukie mwanaume huyo na kumnyofoa macho kisha ayatafune. Lakini akadumisha hari yake.



    "Ndio, naenda msibani," akajibu. "Bila shaka unaufahamu mi wa nani."



    Sheng akatabasamu tena kisha akasema:



    "Mlichofanya jana haikuwa good move. It was one of the most stupid step."



    Jona akamtazama Sheng kwa kitambo kidogo kabla hajamsogelea mwanaume huyo na kumtazama machoni.



    "Siku yako ipo karibuni. Nitakuvunjavunja kwa mkono wangu. Utalipa kila tone la damu ulilolimwaga."



    "Siku yangu!" Sheng akacheka. Akatikisa kichwa chake na kupepea kwa kidole. "Yako ndiyo ipo karibuni kuliko udhanivyo. Siku hiyo nitaimark kwenye kalenda na kuisherehekea kila mwaka."



    "Sheng," Jona akaita. "Mimi ni mfupa mgumu, wewe fisi huniwezi. Umeniwinda mara ngapi nikakurudishia maiti zako?"



    "Mara hii haitakuwa kama hapo mwanzo," Sheng akajitapa. "Hilo nakuahidi."



    Alafu akanyanyuka na kwenda zake Jona akimtazama kwa macho batili. Alifikiria kumsweka mwanaume huyo ndani mpaka atakapomaliza mchakato wa msiba, akaona hamna haja hiyo. Hajafikia hatua ya kumwogopa kiasi hiko!



    **



    Baada ya siku mbili.



    Walikuwa wameyapa mgongo makaburi wakitembea kuondoka zao. Walikuwa wamevalia nguo nyeusi juu mpaka chini. Nyuso zao zikipambwa na miwani, Jona ya macho na Marwa ya jua.



    Uso wa Marwa kwa upande wa kushoto ulikuwa mwekundu na hakuweza kustahimili jua, akauelekezea chini. Mikono yao ilikuwa ndani ya makoti marefu waliyoyavaa.



    Anga lilikuwa jeusi kiasi, jua kwa wastani, na kulikuwa kuna kila ishara ilkionyesha mvua ilinyesha muda kidogo hapo nyuma.



    Walipoyaacha makaburi kwa urefu mdogo wakielekea barabarani, simu ya Jona ikaita ndani ya koti. Akaichomoa na kuitazama, ilikuwa namba mpya. Akapokea na kuiweka sikioni.



    "Unahitajika kituoni. Haraka," sauti ilisema simuni kisha simu ikakata.



    Jona hakujua nini maana ya ujumbe huo na hakutaka kujishughulisha nao sana. Wakaendea usafiri wa daladala na kujipakia. Leo hawakuwa na gari kwani alilirudisha kituoni.



    Wakiwa humo ndani ya daladala, muda mchache mbele, ndipo Jona akaukumbuka ujumbe ule aliopewa kwenye simu baada ya kusikia taarifa redioni kuwa Kamanda wa polisi mkoa, ameuawa na watu wasiojulikana, usiku wa kuamkia leo!



    Akashangazwa sana na habari hizo. Akamtaka Marwa aelekee nyumbani, watakutana baadae. Akaenda moja kwa moja kituoni.



    ***





    Huko inspekta Jona akapata maelezo kuwa Kamanda aliuawa usiku na mtu aliyefika nyumbani kwake na mojawapo ya gari iliyopo kituoni.



    Jona akatahamaki. Kwa maelezo hayo maana yake Kamanda aliuawa na polisi? Alitaka taarifa zaidi lakini hakuna aliyempatia. Ilionekana kila mtu ana taarifa nusu nusu, na hakuna mwenye uhakika.



    Akiwa amekaa ofisini kwake akitafakari, akakumbuka hata maneno ya Sheng. Je ndiye kammaliza? Hapana. Mbona Sheng alisema atammaliza yeye na si Kamanda?



    Au hiyo ndiyo mojawapo ya njia ya kumtafuta? Akawaza sana. Akatamani apatiwe hii nafasi ya kufuatilia hili tukio. Akakaa humo ofisini mpaka majira fulani walipotoka kwenda kuonana na kamanda mkuu wa polisi. Alikuja kuwatembelea.



    "Wewe ndiyo Jona?" Kamanda mkuu akamuuliza kana kwamba hamjui. Akampatia mkono.



    "Ndiyo, ni mimi, afande," Jona akajibu kwa ukakamavu.



    "Oooh! Nilikuwa nikipata taarifa zako toka kwa bwana Chisanza."



    Bwana Chisanza ndilo jina la Kamanda aliyefariki dunia.



    "Alikuwa anakubali kazi zako. Ameondoka ametuachia pengo kubwa sana." Kamanda mkuu aliendelea kuongea na Jona. Akamshika bega lake la kulia alafu akaenda kwa mtu mwingine afuataye kwenye mstari walioupanga kumpokea mkuu huyo.



    Baada ya kusalimiana na kila mmoja, wakapata kuwa na kikao kidogo ndani ya kituo kikuu.



    "Hili jambo si la kuvumilika kabisa kabisa!" Alibweka Kamanda Mkuu. "Haiwezekani tukaenda kwa namna hii, lazima jambo lifanyike tena haraka iwezekanavyo, mambo yakae hadharani upesi ili wananchi wasipoteze imani kwa jeshi lao."



    Akanywa maji kupooza koo alafu akaendelea kunguruma.



    "Isipite wiki moja ... isipite wiki moja huyu muuaji hajakamatwa! Haiwezekani RPC auawe alafu hili jambo likachukuliwa wepesi wepesi tu. It is a serious issue. Na watu wote, nchi nzima wajue hilo. This is a serious issue."



    Baada ya maongezi hayo Kamanda Mkuu akapendekeza Jona apatiwe kesi hiyo mikononi mwake. Akamsihi aitendee haki, na ndani ya muda mfupi awe ameshaonyesha matunda.



    Kwa moyo mkunjufu, Jona akabeba jukumu hilo.



    **



    Aliyapekua mazingira yote ya ndani baada ya kufanya mahojiano na wanafamilia, mahojiano ambayo hayakuwa na matunda mengi kwake.



    Kwa ufupi akagundua muuaji alifika na gari na kulipaki nje, akazama ndani kwa kuruka ukuta kisha akamuua mlinzi kwa kumnyonga, na kutulia hapo kwa muda kidogo kabla hajarahisishiwa kazi kwa Kamanda kutoka nje akiongea na simu.



    Kamanda alikuwa anaongea na nani kwa muda huo? Na kwanini alitoka nje?



    Kwa haraka Jona akaelezwa na kumbukumbu yake kuwa ni yeye ndiye alikuwa anateta na Kamanda kwa muda huo. Kuhakikisha akatazama 'call log' kwenye simu yake. Na kuhusu kutoka nje, ni Kamanda alimweleza hivyo baada ya kuona mtandao unasumbuwa awapo ndani.



    Kwahiyo basi kwa upesi na wepesi kabisa, muuaji akamaliza tukio lake kwa kumpiga Kamanda risasi tatu za kichwani alafu akatumia tena ukuta na kuyeya.



    Sehemu za ukuta alizotumia kuingia na kutoka nazo zililuwa zimechafuka. Na kwa nje ya uzio alipokuwa anatua, aliacha alama za viatu.



    Mwanaume wa makamo, kwa mujibu wa ukubwa wa kiatu, na ni mwanaume mzito, kwa mujibu wa kutitia kwa nyayo za viatu ardhini.



    Ubaya hakuna aliyekuwa anajua kimo wala mjazo wake wa mwili kwani mtu ambaye angeweza kuwa shuhuda, yani mlinzi, aliuawa na wanafamilia wengine walikuwa ndani wakati wa tendo.



    Yani mwanaume mmoja tu alifanya haya, Jona aliwaza akiwa anatazama nyayo za viatu. Akapata wazo. Akapiga picha nyayo hizo na kuondoka zake kwenda kwa majirani kuuliza uliza kama kuna shuhuda yeyote aliyeona jambo.



    Lakini akawaza akiwa njiani. Mwanaume huyo muuaji alikuwa anategemea kumuua Kamanda hapo nje au ilitokea kama bahati ya mtende?



    **



    Alitazama viatu vya wale wanaume aliowakamata kule kwa Marwa akivilinganisha na picha yake ya nyayo za viatu alizozipiga nyumbani kwa Kamanda, akagundua vyafanana.



    Hapo Jona akapata kutengeneza picha yake kichwani kwamba mtu huyo alikuwa pia amevalia suti na kinyago usoni kama wafanyavyo wafuasi wa Sheng pindi watakapo kufanya tukio.



    Sasa angalau akawa amepata pa kuanzia. Sheng atakuwa anahusika na mauaji haya lakini kwanini amuue Kamanda?



    Simu ikaita na namba ngeni. Akapokea.



    "Halo ... ndio, ni mwenyewe ..."



    Simu ikakata. Huenda ni salio. Jona akaamua kuipigia namba hiyo na kuendelea kumskiza.



    " ... usijali, enhe ulikuwa unasema ... ndio ... una uhakika? ... ndio mida ya usiku ... sawa, nashukuru kwa taarifa."



    Mtu huyo aliyekuwa anaongea naye alijitambulisha kwa jina la Deo. Alikuwa ni mwanaume mwenye sauti nzito aliyejinasibu kuwa shahidi wa tukio. Ametumia namba ambazo Jona aliziacha kwa majirani kwa maelezo kuwa wakipata cha kumshirikisha basi wasisite kumtafuta.



    Bwana Deo akamwambia Jona kuwa alishuhudia gari la watu waliofanya tukio. Na alipolielezea gari hilo lipoje, Jona akajikuta anashangaa kwa kufananisha taarifa hizo na gari walilokuwa wanalitumia yeye na Marwa hapa karibuni.



    Habari hizi zikamshtua. Akataka kuonana na bwana Deo lakini mwanaume huyo akamwambia hana muda huo. Amejitolea tu kama msamaria mwema.



    Jona akashusha pumzi ndefu ya uchovu.



    **



    "Karibu," Jona alimwonyeshea Marwa chupa kubwa whisky akiiweka mezani.



    "Hapana, nashukuru," Marwa akamjibu akitabasamu kwa mbali. Jicho lake la kushoto lilikuwa limefunikwa na pamba na plasta. Walikuwa 'wamejiachia' sebuleni wakipigiwa muziki laini kandokando.



    "Poleni kwa msiba, wanasafirisha?" Marwa akauliza.



    "Nadhani," Jona akajibu akitazama chupa yake ya kileo. "Wataupeleka Morogoro."



    Kukawa kimya kidogo Jona akimiminia kinywaji kwenye glasi.



    "Vipi mmebaini chochote?"



    "Yah! .. " Jona akajibu pasi na uhakika ndani yake. "Kiasi chake. Natumai mengi yatakuja kwa mujibu wa muda."



    Kisha hawakuongea kwa muda mrefu kidogo Marwa akiwa anachezea simu na Jona akiwa anakunywa kinywaji chake.



    "Hii kesi inaonyesha dalili ya kuwa controversial sana," Jona akauvunja ukimya. Alikuwa ameshakata nusu chupa ya kileo chake. "Lakini nitaimaliza tu," akajihakikishia. "Nitashinda."



    Alikuwa kana kwamba anajiongelesha mwenyewe. Marwa alimuitikia kwa tabasamu tu na kupiga kimya. Pengine kwasababu hakujua nini Jona anamaanisha.



    Jona hakufunguka kwa undani.



    **



    "Unahitajika ofisini kwa Kamanda," alisema afande fulani mwanamke aliyechungulia mlangoni mwa ofisi ya Jona baada ya kugonga mara tatu.



    Jona asijiulize sana, akanyanyuka na kwenda huko alipokutana na kaimu Kamanda, ambaye kwa sasa tunaweza kusema yeye ndiye aliyekuwa katika nafasi ya marehemu Kamanda japokuwa bado hakuapishwa na kutangazwa.



    Lakini hakuwa mwenyewe, ofisini pia alikuwapo mwanaume mzungu aliyevalia suti rangi ya grey. Nywele zake zilikuwa za gold 'blonde'. Lips ya juu ya mdomowe ilifunikwa na mustachi, macho yake yakifanana na ya paka.



    Jona akaketi na kutambulishwa, yule mzungu alikwa anaitwa Elliot Parker. Ni mpelelezi mashuhuri toka kwenye shirika la viwango vya juu duniani kwenye maswala ya ujasusi na upelelezi.



    Akaambiwa kuanzia muda huo kesi ya mauaji ya Kamanda itakuwa mikononi mwa mzungu huyo, Elliot Parker. Ampatie ushirikiano wote.



    "Utamweleza ulipofikia na kila kitu ulichokipata huko," Kamanda akatoa agizo. Jona akiwa amepigwa na butwaa akauliza:



    "Kamanda, kwani kuna shida gani imetokea mpaka kufikia hatua ya kumpatia kesi mpelelezi wa kigeni?"



    "Kwasababu mojawapo ya mtuhumiwa ama watuhumiwa ni watu toka jeshi letu la polisi," Kamanda akajibu. "Hivyo kufanya kazi hii kwa ufanisi zaidi, pasipo na aina yoyote ya upendeleo ama kupindisha mambo, tulihitaji mtu toka nje."



    Jona akahisi hapa kuna jambo halipo sawa.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni nani huyo mtuhumiwa toka jeshi la polisi? Mbona upelelezi wake mfupi umeonyesha tofauti? Alijiuliza maswali haya kichwani kwa haraka. Ila hakuwa na namna zaidi ya kufuata agizo alilopewa na mkuu wake.



    Hakuwa katika nafasi ya kupinga agizo bali kutekeleza agizo. Akaongea na Elliot Parker mpaka alipofikia na kisha akisindikizana naye akampeleka mpaka nyumbani kwa marehemu Kamanda.



    Elliot Parker akitumia vifaa vyake vya kitaalamu akachukua ushahidi kwa 'kuscan' eneo ambalo mtuhumiwa alilishika wakati anaingilia na kutokea ndani kwa lengo la kupata alama za dole gumba.



    Alipomaliza hilo akatumia "magnifying glass' kupekulia njia na nyayo za mtuhumiwa. Akaandika taarifa na kisha wakaondoka na Jona kurudi kituoni.



    **



    "Marwa, things are not ok. Nasense kuna mchezo unafanyila nyuma ya mgongo wangu," alisema Jona akiwa ameshikilia kichwa chake amejilaza kitini.



    "Ni kuhusu ile kesi?" Marwa akauliza baada ya kuvuta juisi ndani ya glasi kwa mrija wake mwembamba. Mezani kulikuwa kuna dumu la lita tano likiwa limesheheni juisi ya embe. Kila mtu alikuwa na glasi yake ya juisi ila ya Jona haikuwa imepungua hata kidogo tangu ijazwe.



    Mrija ulikuwa unaeleaelea juu ukikosa mteja.



    "Yah ni kuhusu hiyo kesi," Jona akajibu. Macho yalionyesha yupo mbali kifkra. "Sielewi kuna nini hapa kati, lakini ..." Jona akatikisa kichwa. "Mambo hayapo sawa kabisa kabisa."



    "Nini shida haswa?" Marwa akauliza akimtazama Jona na chongo lake.



    "Nimefanya uchunguzi, na kwa clue ndogo niliyoipata, muuaji ni miongoni mwa watu wa Sheng kwa mujibu wa sare za viatu. Lakini ajabu ni kwamba, baadae shahidi anakuja kunambia gari aliloliona likiwa limebeba watuhumiwa ndilo lile tulilotumia hapa karibuni.



    Kama haitoshi, Kamanda naye ananiambia mmoja wa watuhumiwa ni mtu toka jeshi la polisi, nastaajabu amejuaje kama mmoja wa watuhumiwa ni polisi na huku hajafanya uchunguzi, mpaka anafikia hatua ya kumleta mtu mgeni? Na alafu ilikuaje watuhumiwa hao wa mauaji wakapata gari ambalo lipo kituoni?

    "

    Marwa akaguna. Akaweka glasi chini na kukiri kuna jambo.



    "Hapo inabidi uwe makini sana, Jona," akashauri. "Mi nakusihi kitu kimoja, usimwachie huyo mgeni akafanya upelelezi peke yake. Kula naye sahani moja. Unajua kwanini nakuambia hivyo?"



    Marwa akaweka kituo kisha akaendelea:



    "Hapo lolote linaweza kutokea. Sasa lazima na wewe uwe na nafasi ya kujihami. Uwe na maelezo yenye mantiki ya kukuweka salama na kulimaliza hili."



    Ujumbe huu ukapenya kwenye masikio ya Jona. Kweli ulikuwa na mashiko. Aliona ana haja ya kujua kila kitu kitakachoendelea kwenye kesi hiyo. Na si tu kujua, bali awe amemtangulia bwana Elliot Parker kwenye harakati zake.



    Ajue alichokiona mzungu huyo, alichokisikia, alichokiandika na kukisoma.



    Baada ya hapo, angalau Jona akapata unafuu wa mawazo. Akanyanyua juisi na kuigida mapafu kadhaa. Sasa kichwani mwake alikuwa anafikiria namna gani atahakikisha anamweka bwana Elliot Parker mgongoni mwake.



    Mara simu ikaita, akaitazama, alikuwa ni Miriam

    .

    "Hallo ... yes, habari yako? ... safi tu. Unaendeleaje? ... niko poa, nihabarishe ... saa hii? ... serious? ..."



    Jona akatazama saa yake ya mkononi, saa moja usiku.



    " ... ok, nakuja. Nipe dakika chache."



    Akakata simu na kumtazama Marwa.



    "Nadhani nimepata kazi ya dharura."



    **



    "Yupo wapi?" Lilikuwa swali la kwanza Jona kuuliza baada ya kuingia ndani mwa Shangazi yake Miriam. Alitumia kama nusu saa kufika hapo. Miriam, aliyekuwa ana uso wa hofu na macho mekundu, alimpokea na kumkumbatia kwanguvu. Hakuamini kama Jona angefika.



    "Ahsante sana kwa kuja, Jona," alisema kwa toni ya uoga. "Naogopa, naogopa!"



    "Usijali," Jona akamtoa hofu. "Yupo wapi?" Akarudia tena swali lake. Miriam akamwonyeshea mlango wa chumba kwa kidole, Jona akakimbilia huko kutazama akimwacha Miriam sebuleni.



    Baada ya muda mfupi akarejea.



    "It is not that serious," Jona alisema akiketi kochini. "Itakuwa ni Malaria tu si kingine."



    "Kweli?" Miriam akauliza akitoa macho.



    "Yah its true."



    "Tumpeleke basi hospitali!"



    "Hapana. Hamna haja hiyo. She is not in that critical situation, Miriam."



    "Kweli? Mimi niliogopa sana," akasema Miriam kisha akajilazimisha kutabasamu.



    "Ndo' ulikuwa ukiishi hivi na wanao?" Jona akauliza. Miriam akatabasamu kabla hajajibu.



    "Mimi muoga sana. Eliakimu ndiyo alikuwa akisumbuka nao sana kipindi wanaumwa. Mimi mmh mmh mwoga sana."



    "Hujawamiss watoto wako?"



    "Nimewamiss mno. Ila naona ni kheri kwao wakawa na mimi mbali kwa muda huu. Natumai huko kwa shangazi yao wanaishi vema japo kuna muda huwa nawakumbuka sana!"



    "Pole mama. "



    "Vipi kuhusu wewe?"



    "Mimi sina familia."



    "Haiwezekani. Serious?"



    "Ndio. Walifariki kwenye ajali ya moto miaka miwili iliyopita."



    "Oh my God. Pole sana," alisema Miriam akimtazama Jona kwa sura ya huruma. Jona hakutaka kuendelea na simulizi hizo, huwa zinamuumiza sana pindi anapozikumbuka, akabadili mada kwa kumtaka Miriam amwonyeshe jokofu lao apate kutengeneza dawa ya mgonjwa.



    "Dawa?" Miriam akatahamaki. "Hamna dawa kwenye friji."



    "Najua haipo, ndiyo maana nataka kutengeneza," Jona akamjibu na kuongezea: "Nikiona vilivyomo nitajua cha kufanya. Usiku huu haitakiwi aachwe hivi hivi."



    Wakaongozana mpaka jikoni, ndani ya jokofu Jona akatoa tunda moja la chenza na kulikata robo kipande kisha akakichemsha. Maji yake akampatia Miriam ampatie shangazi anywe.



    "Akimaliza atalala vema."



    Baada ya muda mfupi Miriam akarejea na kikombe kitupu. Akamwambia Jona tayari Shangazi amemaliza.



    "Una uhakika itamsaidia?"



    "Asilimia zote. Ndani ya kinywaji alichokunywa kuna unmodified natural quinine, itamsaidia."



    Miriam akamkumbatia tena Jona.



    "Nashukuru sana."



    "Nadhani napaswa kwenda sasa," Jona akasema akijipapasa mifuko.



    **



    Ngo! Ngo! Ngo!



    "Ingia," Jona alirusu hodi akitazama mlangoni. Akamwona bwana Elliot Parker akiingia ndani, amevalia suti nyeusi na kwenye mkono wake wa kushoto amebebelea mkoba wa kahawia.



    Wakasilimiana, Elliot akaketi na kueleza dhamira ya ujio wake. Yupo pale kwa ajili ya kumuuliza Jona maswali kadhaa juu ya kesi ya mauaji ya Kamanda.



    Jona hakuona shida, akamkarimu kwa mikono yote. Akamuahidi bwana Elliot atampatia ushirikiano wote autakao.



    Elliot Parker akafungua mkoba wake na kutoa karatasi kadhaa. Akazitazama kwa zamu alafu moja akaiweka mezani na zingine akazirudisha mkobani.



    Akaitazama tena ile karatasi aliyoiweka mezani alafu akaanza kumuuliza Jona maswali.



    "Do you know the last person Chisanza communicated with?" (Unamjua mtu wa mwisho aliyewasiliana na Chisanza?)



    "No, I dont," (Hapana, simjui,) Jona akajibu kwa kujiamini.



    "Are you sure?" (Una uhakika?)



    "Yes, I am." (Ndio, nina uhakika.)



    "The last person was you," (mtu wa mwisho alikuwa wewe,) akasema Elliot Parker. "And it happened a few minutes before Chisanza was killed. Anything to say about that?" (Na ilitokea muda mfupi kabla Chisanza hajauawa. Chochote cha kusema kuhusu hilo?)



    "I dont know anything about that," (sijui lolote kuhusu hilo,) alisema Jona. "I only contacted him about the case he gave me to deal with." (Niliwasiliana naye kuhusu kesi tu aliyonipa nihangaike nayo.)



    "But you know that his house troubles them with network, right? And one has to go out to talk clearly?" (Lakini unajua nyumba yao inawasumbua mtandao, sio? Na mtu inambidi aende nje aongee vizuri?)



    "Yes, I do." (Ndio, najua.)



    Elliot Parker akaandika karatasini. Alafu akamuuliza Jona kuhusu gari linalosadikika kutumiwa na wauaji. Lini ilikuwa mara yake ya mwisho kulitumia na kama kuna mtu yeyote anayemjua ameshawahi kutumia gari hilo tangu lije kituoni.



    Jona akaeleza hakuna aliyekuwa analitumia isipokuwa yeye tu ila kwenye shughuli zake za kazi. Baada ya maelezo hayo, bwana Elliot Parker akapaki vitu vyake na kuaga.



    Akamwacha Jona akiwa na maswali kichwani. Hakuelewa kinachoendelea.



    Ndani ya muda mfupi, wakaja polisi watatu, wakamuweka chini ya ulinzi. Akatiwa pingu mikononi.



    Alikuwa ni mtuhumiwa namba moja wa mauaji.



    Akatiwa lupango akichangamana na wahalifu wengine humo. Akaenda ukutani kabisa akaketi na kushika kichwa asiamini. Alidhani pengine ni ndoto, akafikicha macho yake lakini bado mambo yalikuwa yaleyale.



    Alikuwa lupango.



    Wamemchongea njia. Wamemzamisha mtegoni. Yale yote yalikuwa yamepangwa atiwe ndani. Ndivyo akili yake ilivyoamini.



    Wakatumia gari alilolitumia. Wakaua muda alioutumia.



    Kila kitu kilikuwa kimeshapangwa. Walimsoma. Walimfuatilia. Wakamzamisha!



    Kwa mara ya kwanza Jona alikuwa ametanguliwa mbele. Alifanywa mjinga. Alilambishwa mchanga. Kwa mara ya kwanza alizidiwa akili!



    Akawaza hii kesi yake itakwendaje. Je, wamejipanga kumsingizia sababu gani amemuua Kamanda? Akakosa jibu. Alihisi moyo wake umenyauka. Alihisi uchungu mno hata akashindwa kuzuia chozi lisimtoke.



    Alikuwa amefanya makosa kurudi jeshini. Hakutakiwa kurudi tena huku. Kaburi lake sasa limechimbwa na wanataka wamfukie kabisa.



    "Afande Devi," Jona akapaza sauti. "Naomba nifanyie mpango niongee na ndugu zangu." Alikuwa kifua wazi ana suruali pekee, miguuni peku. Mkono alikuwa ameutoa nje ya nondo za lupango akimwonyeshea polisi aliyekuwa anakatiza koridoni.



    "Jona," polisi huyo akashangaa. Akatazama pembeni alafu akarudisha macho yake kwa Jona. "Mwanangu, itakuwa msala. Si unajua ishu yako ilivyo hot."



    "Nifanyie bana Devi. Humu leo mimi kesho wewe. Hamna hata mtu anayejua kama nipo humu. Nifanyie msada," Jona aliteta kwa huruma.



    Afande Devi akaguna. Alikuwa ni mwanaume mwembamba asiyezidi miaka ishirini na tano. Alitazama kushoto na kulia kwake alafu akasema:



    "Acha nikajaribu. Ukiona sijarudi, ujue sijafanikiwa."



    "Nashukuru."



    Jona akakaa hapo akishikilia vyuma huku akimngojea afande Devi. Akawa anachungulia mara kwa mara akisimamisha masikio yake asikie kila jambo.



    Ikapita dakika kumi.



    Robo saa.



    Nusu saa.



    Lisaa limoja.



    Jona akakata tamaa. Akarudi ukutani na kuketi. Akainamisha uso wake chini.



    "Oya Jona!" Mara akasikia sauti ya chini ikimwita. Hataka akanyanyua uso wake kutazama. Alikuwa ni afande Devi. Haraka akanyanyuka na kwenda langoni.



    "Sikia. Vitu vyako sijaviona kabisa yani, sijui vimefichwa wapi havipo pale pa siku zote. Sasa kama vipi wewe tumia simu yangu. Umeshika namba kichwani?"



    "Ndio," Jona akawahi kujibu. Afande Devi akampatia simu yake kwa tahadhari alafu akawa anaigiza kuzungukazunguka maeneo hayo.



    Jona akampigia Marwa na kumpasha habari juu ya kilichotokea. Lakini akamwonya asije akakanyaga pale kituoni. Alihofia Sheng na kundi lake wanaweza wakam 'trace' na kummaliza.



    "Usijali, mi ntakuja," alisema Jona. "Nadhani unajua kila kitu hapo nyumbani. Ukihitaji akiba ya pesa utaikuta chumbani mwangu kabatini.



    Lakini naomba unifanyie kazi moja usiku huu. Naomba utafute kila unachokijua kuhusu mtu anayeitwa Elliot Parker. Ni mpelelezi toka shirika kubwa la ujasusi na upelelezi duniani."



    Akakata simu na kumkabidhi afande Devi.



    "Ahsante sana," akashukuru. Afande Devi akaenda zake.



    **



    Jioni ya saa kumi na moja: Makaoni.



    Akiwa amesindikizwa na wanaume wawili, mikono na miguu ikiwa imetiwa kwenye vitanzi vya pingu, akaingizwa ndani ya ofisi na kuagizwa aketi.



    Ofisini alimkuta Kamanda mkuu akiwa amejaa kwenye 'sofa' lake. Amekusanya viganja vyake viwili na kuviwekea kidevu kwa juu. Akamtazama Jona kana kwamba uwanja wa bao. Kisha kwa ishara, akawataka wale wasindikizaji waende nje. Wakatii agizo.



    Kwa muda wakatazamana na Jona kabla hajavuta pumzi ndefu na kuishusha.



    "Nilikuamini Jona kukupa nafasi hii, kukupa kesi hii. Ulikuwa ni mfano wa kuiga kwa uhodari na uchapaji wako wa kazi. Ufanisi na utendaji wako ulikupatia sifa kedekede, ukavuna imani za watu. Kwanini ukayafanya haya?"



    "Sihusiki Kamanda kwa lolote lile," Jona akajibu. "Sijatia mkono wangu kumwangamiza RPC. Na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo hapa karibuni."



    "Una maanisha nini kusema hapa karibuni?" Akauliza Kamada mkuu. "Ina maana ulikuwa umedhamiria kufanya hivyo hapo baadae?"



    "Hakuna anayejua ya baadae, Mkuu. Yote ni vitendawili. Lakini kwakuwa tunaongelea ya sasa na yaliyokwishatokea, basi mimi sijahusika kwa namna yoyote ile. Sijajua kwanini nachezewa mchezo huu!"



    "Mchezo?" Akauliza Kamanda kwa kebehi. "Unauona huu ni mchezo? Wake up Jona, this is reality. Unaenda kuozea jela. It is better ukawa muwazi nijue nakusaidiaje."



    "Mkuu," Jona akaita. "Kama kuwa muwazi ni kudanganya, basi sitaweza kamwe. Nasimamia kwenye ukweli siku zote. Sihusiki na haya mauaji."



    Kamanda mkuu akashusha pumzi. Akamtazama Jona kea sura ya huruma.



    "Ushahidi wote upo against you. Kila kitu kinanyooshea kidole kwako. Mpaka finger print inasema ni wewe. Utabishana na ukweli mpaka lini? ... anyways." Kamanda mkuu akalaza mgongo wake kwenye kiti.



    "Naweza nikakusaidia, ila kubali kwanza ukweli huu. Kubali haya mashtaka alafu mengine niachie mimi. Nitajua namna ya kuyamaliza. Sawa?"



    Jona akamtazama Kamanda mkuu kwa macho ya kitabe. Akatikisa kichwa chake mara tatu kisha akasema:



    "Kamwe sitakubali kitu ambacho sijafanya. It will never ever happen. Nawashauri msingoje kabisa."



    "Ok," Kamanda akasema akikunja uso. "Wacha tuone, muuaji wewe."



    **



    Saa mbili usiku ...





    "Jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa, bwana Chisanza, ambaye aliuawa kwa risasi usiku wa kuamkia jana maeneo ya nyumbani kwake, Mbezi: Goba.



    Kwa taarifa zaidi tuungane na ripota wetu Jack Chiwelu."



    "Tumesikitishwa sana sana sana ... " alinguruma Kamanda mkuu wa polisi akiwa amezingirwa na vinasa sauti vya kila aina ya chombo cha habari hapa nchini. "Baada ya kufanya upelelezi yakinifu, tena tukishirikiana na vyombo vya kipelezi toka nje ya nchi kwa ufanisi zaidi, na kugundua kuwa mwenzetu mmoja, afahamikaye kama inspekta Jonathan Mchau, amekidhi viwango vyote vya kuwa mtuhumiwa namba moja wa kesi hii. Akitumia ujuzi wake aliofundishwa na jeshi kutekeleza mauaji kinyume kabisa na kazi yake."



    Picha ya Jona ikarushwa hewani.



    "Sababu yake ya kutenda mauaji hayo bado haijajulikana. Linafanyiwa uchunguzi na punde utakapokamilika basi tutawajulisha na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani sheria ifuate mkondo wake.



    Na kwasababu basi sheria ni msumeno, itakata kila inapotakiwa. Na hili liwe onyo kwa maaskari wote nchini kuwa kofia zao za uaskari haziwafanyi wao kutenda wanachokitaka bali kufuata, kulinda na kutekeleza sheria tu!"



    "Nikiripoti toka hapa makaoni, mimi ni Jack Chiwelu, Mambosasa TV."



    Sheng akacheka kwanguvu sana. Hakika alikiona alichokuwa anakitaka. Alipata pia alichokuwa anakitaka. Usiku huu kwake ukawa mwanana kabisa kuliko zote alizowahi kuzipitia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akanyanyua glasi yake ya mvinyo na kupiga 'cheers' na Elliot Parker aliyekuwa amekaa pembeni yake. Mbuyu ulikuwa umedondoshwa pasipo jasho.



    "Congratulations, mr," (hongera, bwana,) Sheng alimwambia Elliot kisha wakanywa mafundo ya vinywaji.



    "But the work is not yet done," (Lakini kazi bado haijaisha,) Elliot akasisitizia. "We have to sink him into the jail as soon as possible." (Inabidi tumzamishe jela haraka iwezekanavyo.)



    **



    Wakati wote wakiwa wamelala ndani ya lupango, yeye alikuwa macho. Si kwasababu ya mbu na kunguni waliokuwa wanasumbua bali mawazo kichwani mwake. Alikuwa anahisi maumivu kwa kuonewa.



    Haki kuna muda dunia haipo 'fair'. Si kila anayetupiwa lupango ama jela basi mikono yake ina hatia.



    Leo hakuwa na pombe ya kumsaidia kulala. Leo hakuwa na Marwa wa kupiga naye soga. Leo alikuwa mwenyewe. Si akiegemea kochi bali ukuta.



    Usiku wa aina yake.





    Saa tisa jioni, Ramada hotel.



    Vx nyeusi iliingia na kupaki, ndaniye wakatoka Boka na Miranda walioshikana mikono kuingia ndani ya hoteli. Wakapata chakula na kujikuta wamejilaza kwenye vitanda vyembamba karibu na swimming pool.



    Walikuwa hapo kurefresh akili zao baada ya kupitia magumu kadhaa hapo nyuma. Boka akifiwa na mumewe wakati Miranda akiwa kwenye kiti-moto baada ya mauaji hayo.



    Lakini hatimaye yote yamepita. Yote yamekuwa kheri sasa. Ulikuwa wakati wa kukaa tena pamoja na kuangazia yajayo, tena katika namna ya pekee kabisa haswa baada ya kuachwa na nafasi sasa ya kujivinjari pasipo woga.



    Hakukuwa na mtu wa kuwanyima kumeza mate tena.



    "Unapenda sana kuja hapa?" Aliuliza Miranda ndani ya bikini. Umbo lake lilikuwa linaonekana vema na pengine kukushawishi ukamwona Boka hakufanya makosa kabisa kuwa 'zezeta' hapa.



    Alikuwa anavutia hasa. Kwa rangi yake, uso mpaka na umbo. Na hata namna alivyokuwa anaongea, alivutia kusikilizwa.



    "Pametulia sana hapa kuliko kwengine, haswa nyakati za siku za wiki. Ukija hapa you get a real refreshment," alieleza Boka aliyejivunia kuwa na mwanamke mrembo pembeni yake.



    Miranda akadaka glasi juu ya kameza kadogo pembeni ya kitanda, akanyonya mafundo mawili kabla hajalaza kichwa chake na kuuliza:



    "So nini plan yako kwa sasa?"



    Boka akatabasamu kwa mbali. Akageuza mwili wake na kumtazama Miranda.



    "Kukuoa," akajibu kwa ufupi.



    "Are you serious?" Miranda akaigiza kustaajabu.



    "Why not, nipo serious."



    Miranda akanyamaza kidogo akiwaza kichwani. Kwa wanawake wengine hii ilikuwa ni 'a million dollar chance'. Sio tu kwenye swala la kuolewa kama kila mwanamke ambavyo angependa kuwa na mume na familia yake, la hasha, bali kuolewa na mtu mwenye nafasi serikalini.



    Mtu mzito mwenye pesa. Haikuwa jambo dogo hata kidogo. Lilikuwa ni jambo la kutetemesha mwili na kuukimbiza moyo upesi haswa ukifikiria zile 'shopping' za Dubai, safari za China na Afrika ya kusini.



    Lakini kwa Miranda, hili halikuwahi kuwa lengo. Kuolewa. Achilia mbali kuolewa na Boka. Mwanaume huyu hajawahi kumvutia hata chembe. Hamsisimui. Alikuwa hapo kwa ajili ya kufanikisha malengo yake tu.



    Hapa akamkumbuka mke wa Boka.



    Japokuwa alikuwa ni adui kwenye 'mishe' zake, lakini kwa njia moja ama nyingine alikuwa anamhitaji. Kumtuliza mumewe asifikirie maswala ya kumuoa.



    Sasa mke huyo amefariki. Boka atakuwa mwepesi kutafuta mwanamke mwingine na hata kumuoa.



    Sasa nini maana yake hii? Inabidi kazi itendeke haraka iwezekanavyo kabla ya mambo haya ya kuoana. Aliwaza Miranda.



    Akanyanyua tena glasi ya juisi na kupeleka mrija mdomoni akiwa amejilaza. Akanywa mafundo mawili mepesi akichambua cha kunena.



    "Nadhani unajua cha kufanya, mheshimiwa. It is obvious baba yangu hatokukubalia kama hutomfanyia kazi yake."



    "Najua!" Boka akadakia. "Si nimeshamkubalia?"



    "Kazi moja!" Miranda akajistaajabisha. "You have to show wewe ni mtu anayeweza kumuamini na kumtegemea. Unajua hawa wazungu ni ngumu sana kumwamini mtu, lakini akishakuamini tu basi."



    "Kwahiyo unanishauri nini?"



    "Mpe sababu ya kukuamini. Tena si moja, kadhaa."



    "Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu. Ila vinataka muda. Huoni nitakawia kukuoa?"



    "Kwanini wahofu kuhusu hilo swala? Wadhani kuna mtu atakuja niiba au?" Miranda aliuliza kwa mishebeduo ya kike. "Mimi ni wako tu. Wala usiwe na papara. Hata kwa muda huo utakaokuwa unafanya mambo yako, mimi nitakuwa pembeni yako. Kuna shida?"



    Japo Boka hakujibu, alionekana kuafiki alichoambiwa. Hakuwa na usemi.



    "Vipi ile safari ya Afrika kusini?" Miranda akauliza. "Umeischedule lini?"



    "I think nitaenda huko wiki ijayo Jumatatu."



    Alivyojibu hivyo ni kana kwamba Jumatatu hiyo ilikuwa mbali. Siku hiyo ilikuwa ni Alhamis, kwahiyo Jumatatu ilikuwa ni hatua tatu tu kuifikia. Miranda akatabasamu. Hili halikuwa jibu baya kwake kabisa. Lilimaanisha ajiandae.



    Lakini kama haitoshi, Boka akamwambia anataka kumkabidhi biashara ya mkewe aiendeshe. Kampuni ile ya vipodozi na urembo, iliyosambaa Afrika mashariki, iwe chini yake.



    Swala hili likawa mtambuka kwa Miranda. Hakutaka kuingia kichwakichwa hapa. Alihofia kilichomkuta Mke wake Boka. Lakini pia kujianika kwa maadui zake.



    "Huoni tunapaswa kungoja kwanza kesi ya mkeo iishe?" Akauliza.



    Kichwani kwake akiwaza mpaka kesi hiyo ikiisha, Jona atakuwa amemsaidia ku 'clear' maadui zake hawa akawa salama.



    Hakujua Jona kwa wakati huo alikuwa rumande. Na kesi imesharudishiwa mikononi mwa inspekta Geof, ambaye hafahamu yale aliyokuwa anayafahamu Jona.



    Hata kidogo!



    **



    Baada ya mahojiano yake ya muda mfupi kulingana na muda aliopewa na daktari, inspekta Geof alisafisha koo lake na kusimama akimtazama mwanamke aliyejilaza kitandani.



    Mwanamke huyu alikuwa ni shoga yake marehemu mkewe Boka.



    Alikuwa anapata wakati mgumu sana kuongea. Mwili wake ulijawa na majeraha makubwa. Na maumivu aliyokuwa anayapata hayakuwa yanamithilika. Kama si sindano za kupunguza maumivu alizokuwa anadungwa, angekuwa analia muda wote.



    Ukimtazama ungemuonea huruma. Na kama ungekuwa na moyo mdogo basi isingekuwa ajabu ukajaza machozi machoni.



    Hii likazidi kumfanya inspekta Geof aone kuna haja ya kumtafuta mtu aliyehusika na hili kwa nguvu zote. Awajibishwe kwa mujibu wa kile alichokitenda.



    Akashusha pumzi ndefu. Mkono wake wa kuume ulikuwa umeshikilia notebook na kalamu.



    "Ahsante sana. Ugua pole. Nitakuja kukuona tena karibuni."



    Akatoka ndani ya hospitali na kuonana na daktari, kisha akaenda zake kwenye gari lake na kutulia humo kwa dakika kadhaa. Akapitia yale maelezo aliyopewa.



    Yote yakamjengea mantiki kumbe mauaji yale ya mkewe mheshimiwa yalikuwa ni kisa cha kimapenzi. Yalikuwa yamesukumwa na wivu wa mapenzi.



    Akatikisa kichwa chake kisha akazungushia duara kwa jina la Miranda kwenye notebook, na kuandika kando: 'the primary target'.



    **



    "Nilikuambia usije," Jona alilalama akiwa amekunja sura. Mikono yake ilikuwa imebana nondo za lupango kwanguvu kana kwamba anataka kuzing'oa.



    Alimtazama Marwa kwa macho makali. Lakini Marwa aliyekuwa amebebelea mfuko mweusi wa rambo, amesimama mbele yake, alikuwa akimtazama kwa huruma.



    "Lakini nitawezaje kukaa nyumbani kwa amani na wewe upo humu?" Marwa aliuliza.



    "Ni hatari, Marwa," Jona akamjibu akilalama. "Unadhani nakutania ninavyokuambia hivyo?"



    "Kama ni hatari basi tuwe wote. Siwezi nikakaa nyumbani na sijui huku unaendeleaje. Unataka nije nisikie wamekuua na kukuzika pasipo kukuona? Nitakaaje nyumbani nikila na kunywa huku sijui kama tumbo lako limepata kitu? Chakula kitashuka? Kama ni hatari na kuniua, basi waniue! Nimeshapoteza wazazi wangu, sina cha kupoteza tena. Na wewe upo ndani, ntajificha milele?



    Ukifa nitapata nguvu ya kulia na wakati ukiwa hai nilishindwa hata kunyoosha mkono kukusaidia? ... siwezi Jona."



    Marwa akafungua mfuko wake. Ndaniye kulikuwa kuna hotpot la wastani na chupa ya maji. Akampatia Jona ale.



    Ni kama vile alikuwa anajua mwanaume huyo hakula tangu alipowekwa humo ndani.



    "Wamekuruhusu kuja humu?" Jona aliuliza.



    "Hapana," Marwa akajibu. "Hawakuniruhusu, nikakaa hapo nje siku nzima mpaka askari fulani akaniita na kuniuliza kama nina shida yoyote. Nilipomweleza nimekuja kukuona wewe, akanisadia. Lakini ameniambia nifanye upesi."



    "Askari gani huyo?" Jona akauliza akila. Marwa akampatia maelezo yaliyomfanya Jona kutambua ni Afande Devi.



    Baada ya muda mfupi, akampatia Marwa vyombo aende zake upesi.



    "Kuwa makini sana," akamsisitizia. Marwa akapokea vyombo na kabla hajaenda, akamkumbushia Jona jambo.



    "Nilitafuta kuhusu Elliot Parker."



    "Ukapata nini?" Jona akawahi kuuliza kufupisha maongezi.



    "Nimetafuta kote lakini sijaona hilo jina kama ni mpelelezi wa aidha FBI, CIA, au INTERPOL."



    "Nilijua tu!" Jona akajisemea. "Sasa nenda. Fanya upesi! Kuwa makini sana."



    **



    "Ni nani yule?" Aliuliza koplo Massawe akimtazama Marwa anaishia. Kaunta alikuwa ameketi afande Devi akiwa anapekua daftari kubwa.



    "Ni kijana flani hivi," Afande Devi akajibu akifanya jitihada za kukatisha maongezi hayo kwa kufunguafungua daftari kujifanya yupo 'bize'.



    "Kijana gani na alikuja hapa kufanya nini?" Koplo Massawe akasisitizia. Alimtazama afande Devi kwa macho ya mashaka. Na kabla afande Devi hajajibu, akasema:



    "Unajua tumekatazwa kumruhusu yoyote kumletea chakula yule jamaa. Kwanini ukamruhusu aende huko na mimi nilimzuia?" Massawe akafoka.



    "Sikujua," afande Devi akajitetea. "Nilimkuta hapo nje kwa muda mrefu. Nikamuuliza akasema haja yake. Nikaona si vibaya ku-"



    "Usirudie tena!" Massawe akamkatiza. "Sawa?"



    "Sawa afande!"



    **



    Baada ya muda kidogo koplo Massawe akaondoka zake na kumwacha afande Devi peke yake. Devi asipoteze muda akaenda kumwona Jona rumande na kumwonya kuhusu watu wanaomtembelea.



    "Hawataki upatiwe chakula, Jona. Utakapoona nimewazuia wageni wako jua nimekosa namna ya kuwaruhusu."



    Jona akafadhaishwa sana na hili. Kwanini wanamfanyia hivyo? Nini lilikuwa kosa lake ndani ya jeshi? - uweledi wake?



    "Usijali," afande Devi akamtoa mashaka. "Nitakuwa nakusaidia kadiri ya uwezo wangu. Nitakapokuwa napata muda ntakuwa nakupenyezea hata kidogo. Lakini kwa siri sana."



    "Ahsante sana Devi," Jona akachonga. "Ila nakuomba uachane na hivi vitu. Wewe bado kijana mdogo na ndiyo kwanza umeanza kazi mwaka huu. Hili linaweza kukugharimu."



    "Wala usijali, Jona," Devi akamtoa mashaka. "Wewe ni miongoni mwa watu wachache sana walionipokea vema hapa kituoni wakaniheshimu japokuwa ni mdogo kwao kiumri na kicheo. Hustahili haya. Naamini hauna roho hiyo. Mimi nitakusaidia kadiri ya uwezo wangu."



    Afande Devi hakukaa sana hapo, akaenda zake kurudi anapotakiwa kuwapo. Alihofia koplo Massawe anaweza akarudi asimkute ikawa taabu.



    **



    Kamanda mkuu akiwa anaongozana na maaskari wengine wawili, mmoja akiwa amevalia kiraia, wakakomea langoni mwa rumande ya Jona. Kamanda akamtazama Jona kwa jicho la huruma kisha akadaka vyuma vya lango.



    Jona alikuwa amekaa mbali ukutani.



    Kamanda akatikisa kichwa kwa masikitiko. Kwa ishara, akamtaka mwanaume Jona ajongee karibu naye. Jona akatii. Akamsogelea mkuu wake huyo na kumtazama machoni.



    "Jona," Kamanda akaita. "Kwanini umekubali kuteseka kiasi hiki? Fanya yaishe. Niruhusu nikusaidie. Haustahili kabisa kuwapo humu ndani."



    Jona akamtazama Kamanda kwa sekunde kadhaa kisha akamjibu akiwa anang'ata meno.



    "Anayestahili kuwepo humu ndani ni wewe pamoja na wenzako. Nitakapofanikiwa kutoka humu, basi jua ni wewe ndiye utakayeingia."



    Kamanda mkuu akatabasamu.



    "Shida yako ipo hapo, Jona. Unashupaza sana shingo. Unajua kisa cha chui na chungu? ... chui alizamia kijijini kwa watu akiwa anatafuta chakula kwa ajili ya wanae. Hakutaka kumla mtu kabisa bali apekue majikoni aone kama atapata chochote kitu.



    Huko akafanikiwa kusikia harufu nzuri kabisa ya chakula toka kwenye chungu kidogo. Kuonja ... alah! Kilikuwa kitamu sana. Akaona kinafaa kupelekea watoto wake porini.



    Lakini si bahati, chui akazamisha kichwa chake ndani ya chungu hicho hata akashindwa kukitoa. Akahangaika huku na huko kujinasua asifanikiwe mpaka wanakijiji wakamsikia. Wakajaa kumzunguka.



    Walitaka sana kumsaidia, lakini silka ya chui iliwaogopesha kufanya hivyo. Je, Kucha zake zingewaacha salama? Walihofia. Na je wakishatoa hiko chungu kichwani, meno yake hayatawararua?"



    Kamanda akaweka kituo. Akameza mate na kumwambia Jona.



    "Badili hulka yako, uruhusu kusaidiwa. Kushupaza kwako shingo hakutakupelekea popote zaidi ya shimo la tewa."



    Jona akasaga meno.



    "Kama ungelibadili hulka yako kwanza, nisingelikuwepo humu ndani," akasema kwa kujiamini, kisha akaita, "Kamanda, kwa makusudi ulitengeneza kidonda kwasababu una dawa mkononi Sawa dawa yako yaweza kuponya lakini vipi maumivu niliyoyapata? Na je kovu utakaloniachia?"



    Akahitimisha.



    "Silambi mkono unaoniadhibu. Tena pasipo na hatia. Si kwamba ni kiburi, la hasha! Bali itanifanya niwe na hatia. Kamanda, acha nitapambana mpaka tone la mwisho."



    Kamanda mkuu akabinua mdomo wake kisha akamtazama mmoja wa watu alioongozana nao kuja hapo, yule aliyevalia kiraia. Akamuuliza:



    "Mmempa chakula enh?"



    "Hapana, mkuu. Hajala," mwanaume huyo akajitetea akitikisa kichwa.



    Kamanda akamtazama Jona kisha akarudisha macho yake kwa yule mwanaume aliyemuuliza. Akampatia maagizo.



    "Hakikisha hali kwa siku zote anazokaa humu ndani!"



    "Ndio, mkuu!" Akajibu mwanaume huyu kwa ukakamavu.



    **



    Asubuhi ...



    Mlango ulipofunguka, alitoka inspekta Geof akiwa amebebelea notebook yake mkononi. Nyuma yake alikuwapo mwanadada Miranda akimsindikiza.



    Wakasimama kibarazani, Inspekta akampatia Miranda mkono wa kheri kisha akamkumbusha hatakiwi kuondoka nje ya mji mpaka pale upelelezi utakapokamilika, na kesho atakuja tena kumwona.



    Aliposema hayo, inspekta akaondoka zake Miranda akimtazama mpaka anatoka nje ya geti. Akarudi sebuleni na kuketi akikuna kichwa chake kwa mawazo. Nywele zilikuwa timtim, na mwili wake ndani ya dira angavu ulikuwa unahangaika kuweka kila mkao.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliwaza. Hakuona kama una upenyo wa kuchomoka katika kesi hii. Kama upo basi ni kama ule wa tundu la sindano. Mambo yamekuwa magumu zaidi. Kwa dalili za wazi, inspekta alionekana kudhamiria kumtia ndani.



    Mawazo yake yakaenda mbali. Akamuwazia Jona. Kwanini kesi hii amepewa mtu mwingine mbali na yeye? Aliamini Jona ni mwerevu kung'amua muuaji na si huyu Geof ambaye macho yake yanakomea juu ya zulia.



    Akawaza afanyaje? Mawazo yake yote yakamuelekezea msaada wa pekee ni Jona. Akanyanyua simu na kupiga. Hakuwa anafahamu kuwa Jona yupo nyuma ya vyuma.



    Simu ikaita pasipo mafanikio. Akaamua kumpigia Kinoo amshirikishe habari zake kwa mara ya kwanza. Hata akisikia amekamatwa basi asije akastaajabu na aje kumtembelea rumande.



    Simu ikaita mara mbili kabla ya kupokelewa. Kulikuwa na makelele kuonyesha Kinoo alikuwa mjini kwenye pilika za magari na watu. Miranda asijali hilo, akatimiza adhma yake ya kumhabarisha Kinoo.



    "Sidhani kama kesho akija ataniachia huru. Maswali yake yote nilikuwa nababaika kujibu. Najiona kabisa nikitenga shingo kwa mchinjaji."



    "Sasa tunafanyaje?" Kinoo akauliza.



    "Tumtafute Jona. Naamini anaweza akanisaidia!"



    "Jona? Yule polisi?"



    "Ndio! Alikuwa ndiye mpelelezi wa hii kesi, ila wamembadilisha!"



    "Miranda, kwani hujasikia habari za Jona?"



    "Zipi?



    Kinoo akamhabarisha Miranda kwamba Jona amekamatwa anatuhumiwa kumuua RPC hivyo asitegemee kumsikia tena.



    Miranda akachanganyikiwa. Tumbo likamvuruga. Alikata simu akaiweka kando na kulaza kichwa chake kwenye kiti.



    Jona amekamatwa? Jona amemuua RPC? Maswali haya yakazunguka kichwani. Akajikuta anatikisa kichwa chake kama mwehu.



    Hapana.



    Hakuamini hata chembe.



    Akanyanyuka upesi na kwenda ndani.



    **



    "Jona, naamini hujaua," Miranda alisema kwa sauti ya chini akimtazama Jona kwa macho ya huruma. "You have been framed. Na ubaya si tu inakuumiza wewe bali hata na sisi. I need you out. Things are not the same."



    Macho ya Miranda yalibadilika rangi na kuwa mekundu.



    Jona alikuwa amesimama akishikilia nondo kwa mkono wake wa kuume akitazama chini. Sijui alikuwa anawaza nini. Ila ungemtazama ungeona moyo wake unaungua. Kifuani alikuwa ana moto mkali.



    Alikuwa anasikia maumivu aliyoyaonyesha kwa kung'ata meno yake.



    "Jona, Miranda akaita. "We have to do something. Usikae ukaridhika na hii hali. Najua you are innocent."



    "Nitafanya nini Miranda nikiwa humu rumande nimebanwa na vyuma?" Jona akauliza. Macho yake yalikuwa mekundu. "Nimedhamiria kweli kufanya kitu, lakini nafanyaje na nipo humu ndani?"



    Kabla Miranda hajasema kitu, afande Devi aliwasili eneoni akiwa amebebelea chakula kwenye mfuko. Akamkabidhi Jona.



    Akamtazama machoni.



    Akamtazama na Miranda kisha akarudisha macho yake kwa Jona.



    "Kula upesi!" Akasema kwa kunong'oneza kisha akaenda zake.



    **



    "Umempatia?" lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa koplo Massawe.



    "Ndio, nimempa," akajibu afande Devi. Uso wake alikuwa ameukunja. Macho yake yalionyesha mawazo. Aliketi akafungua daftari kubwa la hapo kaunta akaigiza kulitazama ila kiuhalisia alikuwa mbali sana kimawazo.



    Ndani ya muda mfupi, Miranda akafika hapo kaunta akiwa anatembea kwa madaha. Mwanamke huyo aka 'sign out' na kuwaaga.



    Massawe akanyanyua simu na kupiga.



    "Ndio, ameshakula kile chakula ... sawa, mkuu.





    Massawe aliongea akimtazama Miranda anayeyoyoma. Punde akakata simu akiwa anasikia sauti ya kicheko.



    Sasa alikuwa ameshakamilisha kazi yake. Anachongoja ni malipo tu toka katika mkono mchafu!! Akatabasamu alafu akamuagiza afande Devi aende ndani kuhakiki kama kweli Jona amekula na kumaliza kile chakula walichompatia.



    Afande Devi akatii amri. Upesi akaenda huko na baada ya muda mfupi akarejea akiwa ameshikilia mfuko wa nailoni mkononi.



    "Amekula ... amemamaliza!"



    "Una uhakika?" Massawe akahakiki. Alikwapua mfuko wa nailoni toka mikononi mwa Devi na kuupekua kama kuna mabaki.



    "Ndio, nina uhakika," Devi akajibu akitazama chini. Akaendea daftari kubwa la mapokezi, akaketi na kuanza kulipekua.



    Macho yake yalionyesha yupo mbali kimawazo. Hata daftari hilo hakuwa analipekua bali analifungua tu kuigiza.



    Hakudumu hapo muda, akalifunga daftari na kwenda zake kantini. Si kwamba alikuwa na njaa. Alienda kutafuta amani.



    **



    "Una uhakika?" Akauliza Kamanda mkuu. Macho yake yalikuwa na mabaki ya furaha katika hali hii ya kushangazwa.



    Alikuwa amevalia tisheti jepesi jeupe na suruali ya traki rangi ya bluu. Mbele yake, kiti kinachotazamana, alikuwa ameketi mwanaume mchina, Sheng, akiwa ndani ya shati jeupe, tai na suruali nyeusi ya kitambaa.



    Katikati yao kulikuwa kuna meza ndogo ya kioo. Juu yake kulikuwa na chupa kubwa ya wiski yenye mfumo wa kipekee ikiwa inafanana na viglasi vyake kwa kando.



    Viglasi hivyo vilikuwa vimejaa pomoni lakini havikuwa vimeguswa hata kidogo. Soga za hapa na pale zilikuwa zimenoga zikiyaweka makoo yao bize.



    "Uhakika kabisa," akajibu Sheng. Lafudhi yake ya kimandarin haikukoma kuonyesha asili yake. "Yani hatutohangaika hata kidogo, utakuja nambia menyewe."



    Basi Kamanda mkuu akacheka.



    "Yani mimi nilikuwa nimepanga kumpa mateso ya kila aina mpaka alainike. Unajua kijana yule ni mgumu sana?" Akauliza Kamanda mkuu kiretorikali. "Mgumu sana! Sasa nilikuwa nafikiria nimuingize kwenye tanuri gani asichomoke."



    Akacheka kidogo kama mtu anayeumwa kifua.



    "Kumbe kuna njia nyepesi bana."



    "Yes!" Sheng akatikisa kichwa. "Nakupa siku mbili tu, utaona matokeo yake."



    Kukawa kimya kidogo wote wakiwa na matabasamu usoni. Sasa wakapata wasaa wa kutia kinywaji mdomoni na kunywa fundo moja moja.



    "Lakini kuna jambo takuomba," alisema Sheng akiweka glas yake mezani.



    "Karibu, nakusikiliza," Kamanda akamkarimu akimtazama kwa macho ya umakini.



    "Naomba, ufanye kila ujhualo. Huyu mtu asitoke ndani kabisa! He stopped most of my things when he was out. Sitaki kabisa arudi uraiani!"



    Kamanda akatabasamu. Na kabla hajajibu akanywa kwanza fundo moja la wiski kisha akanguruma kupooza koo linaloungua.



    "Yani kuhusu hilo?" Akatikisa kichwa. "Usijali kabisa. Ondoa kila aina ya shaka. Nitahakikisha anabakia nyuma ya vyuma maisha yake yote. Na hata itakaposhindikana, basi atoke akiwa mfu."



    Sheng akakunwa sana na hilo jibu. Akanywa kwa pupa kimiminika kilichobakia kisha akabamiza kiglas mezani.



    "Ntashukuru sana. Now I can spend my night peacefully!"



    "Kabisa yani, ondoa hofu. Namfahamu vema yule kijana. Nafahamu uwezo wake vizuri sana. Akitoka mule ndani kwa njia yoyote ile, vitanda vyetu vitageuka kuwa jehanamu. Siwezi kabisa nikaliruhusu hilo."



    Bas mara Sheng akaingiza mkono wake mfukoni kana kwamba anatafuta kitu. Akaingiza kushoto kisha kulia. Akatoa pochi yake na kuitazama. Ilikuwa imesheheni fedha. Haikuwa na uwezo wa kufungwa. Kamanda akaitazama pochi hiyo akiimezea na kinywaji chake.



    Mara Sheng akamuuliza:



    "Unahitaji fedha yoyote ile?"



    Kamanda hakujibu, akabaki anajichekesha. Sheng akaiweka pochi yake mezani na kumsogezea Kamanda.



    "Ya soda hiyo."



    **



    "Mara yako ya mwisho kuonana naye ilikuwa lini?" Aliuliza Geof aliyejiveka suti matata ya kisasa rangi kahawia. Macho yake ya kazi yalikuwa yanamwangazoa Boka machoni.



    "Ni muda mrefu sasa sijaonana naye!" Boka akadanganya. Hapa walikuwa wanamwongelea Miranda na kwa akili zake tayari alifahamu wapi inspekta huyu anapoelekea na yeye hakuwa radhi kabisa kudhalilika.



    Kubainika kuwa mkewe alikufa kutoka na mahusiano na 'mchepuko' hakikuwa kitu anachotaka kimtokee hata kidogo.



    Ni fedheha. Aibu.



    Alishapata picha namna gani magazeti yatakavyomsakama na kumchora mbele za watu. Haswa magazeti ya udaku!!



    Hili kwake lilikuwa ni jinamizi alilokuwa anajitahidi kuliokoka. Japokuwa bado hakujua ni kwa namna gani jambo hilo lilivyo na kina kirefu.



    Hakuwaza ni kwa namna gani hili swala la Miranda kuhusika na kifo cha mkewe linaweza kuwa kweli, bali namna ambavyo atabaki salama kulinda heshima yake kwanza.



    Japo pia hakutaka Miranda ahusike na hili. Kwanza, hakuwa anaamini kama Miranda atakuwa ametia mkono kwenye mauaji ya mkewe.



    Kwake Miranda ni msichana mrembo asiye na makuu. Msichana ambaye hata kushika kijiko ama uma vizuri hawezi, sembuse kuua. Hakujua alikuwa anajidanganya.



    Mwanamke huyo alikuwa ni mafia haswa!!



    "Lakini mnawasiliana, sio?" Inspekta aliuliza ncha ya peni ikitoboa karatasi.



    "Ndio, tunawasiliana lakini ..." Boka akazimbazimba. " ... sio sana ..."



    "Unajua kama alikuwa anawasiliana na mkeo?" Inspekta akatupa swali jingine.



    "Sifahamu," Boka akajibu upesi. Inspekta akamtazama kwa muda kidogo machoni.



    "Mheshimiwa, huyu binti alikuwa ni mfanyakazi wa mkeo, ilikuwaje ukawa na mawasiliano naye ya karibu?"



    "Si karibu kihivyo," Boka akajitetea. "Unajua Miranda ni mwanamke mchangamfu sana na mwepesi kuzoea mtu. Mke wangu alinikutanisha naye, akanizoea!"



    "Mkeo akakupatia na namba yake?"



    "Ha ... hapana...! Niliipata namba yake sababu za kikazi, maana ndiyo alikuwa kaimu kwa company."



    "Na ukawa unakutana naye pasipo mkeo kujua."



    "Hapana. Unajua mke wangu ana wivu sana. Anapenda sana kuumba mambo ambayo hayapo! Mahusiano kati yangu na Miranda yalikuwa ni ya kikazi tu, si vinginevyo."



    "Kwa mujibu wa maelezo ya shuhuda namba moja wa ajali, rafiki yake mkeo aliyelazwa hospitali, amesema mkeo alishuhudia jumbe kadhaa za mapenzi kwenye simu yako toka kwa huyo mwanamke. Ni kweli?"



    "Kwenye simu yangu? - mimi? Mmmh mmh sidhani! ... chukua hata wewe utazame kama utaona!"



    Inspekta hakuuliza tena jambo, akanyanyuka na kuaga aende zake. Akamhusia mheshimiwa asitoke nje ya mkoa ama kukaa mbali na makazi yake kwa muda wote huu wa upelelezi.



    Akaenda akiwa sasa kichwani ameshamuongea mheshimiwa kama mtuhumiwa namba mbili wa mauaji. Maelezo yake yanayojikanganya na yale aliyoyatoa Miranda yalimtia hatiani.



    Pengine walishirikiana na Miranda kutimiza mauaji waishi pasipo na shida, inpekta Geof aliwaza.



    **



    "Mi -- mi -- skuona haja ya ..." Miranda aliongelea puani. Alikuwa ameibinyia simu sikioni, yupo sebuleni akitazama kwa macho ya kukanganyikwa.



    "Nisamehe, sikujua kama yangekuwa makubwa kiasi hiki. Kweli tulikuwa na ugomvi, but nilichukulia simple tu," Miranda aliruruma. Alisimama akashika kiuno chake akienda huku na huko. Mara akikuna nywele na kuminyaminya lips zake.



    "I am sorry nimekuingiza kwenye a big mess ... ndio, tulishawahi kukutana ... yes ... laki ... eeenh ... I didnt do it! Yeye ndo' alikuwa anatak ..."



    Simu ikakata.



    Miranda akaketi chini akishusha pumzi ndefu.



    "Bila Jona hapa naenda ndani huku najiona," akajisemea mwenyewe kama chizi.



    Hakuwa na amani. Tumbo lilikuwa linamkoroga. Mwili mzima anauhisi umekuwa dhaifu.



    **



    "Yes, Miranda," BC alinguruma baada ya kuchomoa simu yake mfukoni na kuiweka sikioni. Alikuwa ndani ya Mlimani City malls ndani ya duka la simu kama kawaida akiwa amenawiri na kupendeza hali iliyomfanya aonekane kijana zaidi kinyume kabisa na namba za umri wake.



    Alikuwa ametinga kaunda suti ya bluu. Kifuani amechomeka ua dogo jekundu spesheli. Chini miguu akiihifadhi ndani ya kiatu madhubuti cha ngozi.



    "What problem?" (Shida gani?) BC akauliza akiangazaangaza simu. Mara kidogo akaacha zoezi zima na kuisikiliza simu yake kwa umakini zaidi. Punde akatoka nje ya duka akiwa amekunja ndita.



    "That is real serious shit!" (Hilo ni jambo kubwa kweli!)



    Akatulia kidogo akiskiza. Kisha akasema kwa sauti ya agizo.



    "Let's meet immediately and see what we can do!" (Tukutane mara moja tutazame nini tunaweza fanya!)



    Akaskiza tena. Kisha akahitimisha.



    "It is either we get the door or make it by ourselves" (Ni aidha tuupate mlango ama tuutengeneze wenyewe!)



    ***



    Akakata simu na kuirejesha mfukoni. Hamu ya kuendelea na 'shopping' ilikata. Akatoka kufuata gari lake akakwea na kuhepa.



    **



    "Upo sawa mzee?" Aliuliza mahabusu mmoja akimtazama Jona kwa macho ya wasi.



    Jona alikuwa amelala chini akiwa ameshika kichwa kwa kuhisi maumivu makali. Pua yake ilikuwa inachuruza damu. Macho yake hayakuwa yanaona vema ingawa alivalia miwani.



    Alikuwa anajihisi mdhaifu mwili mzima. Haswa kwenye maungio ya mwili. Mishipa ya damu ilikuwa inamvuta, na kwa wakati huohuo akihisi baridi kali!!



    Wenzake, wanne, waliokuwepo ndani wakawa wanamtazama kwa hofu. Walikuwa wameshamtambua kama mtu asiyelala nyakati za usiku, ila hii ya leo ilikuwa mpya. Walihofu huenda amezidiwa. Haikuwa hali ya kawaida!



    Alikuwa ananguruma na kugugumia kwa maumivu. Mwili unamtoka jasho jingi, alafu bado anajikunyata!!



    "Muite afande," mmoja akashauri. Yule aliyekuwa karibu na langoni akapaza sauti kuita afande afande kuna mtu kazidiwa. Ndani ya muda mfupi afande fulani akafika hapo na kumtazama Jona.



    Akashtuka! Haraka akaenda kaunta na kumpasha habari koplo Massawe aliyekuwa ameketi hapo.



    "Afande, kuna mtu kazidiwa mahabusu. Tufanye namna!"



    "Nani huyo?"



    "Jona!"



    "Jona?"



    "Ndio. Anatokwa na damu puani. Anamiminika jasho."



    Massawe akaguna na kufikiri kidogo. Akachomoa simu yake na kupiga. Baada ya muda mfupi ikapokelewa. Akaelezea hilo jambo la Jona.



    "Aanh ... sawa, mkuu. Hamna shida."



    Massawe akakata na kisha akaketi.



    "Achana naye!" Akamwambia yule afande aliyekuja kumpasha.



    "Unasema?" Afande akashangaa.



    "Nimesema achana naye. Hujasikia nini hapo?" Massawe akapandisha sauti. "Achana naye atarejea kwenye hali yake mwenyewe!"



    Afande yule mpasha habari akanyamaza na duku lake kifuani. Na hii ndiyo moja ya shida ya jeshi. Pale mkubwa wako anapoamuru jambo huna nafasi ya kulikosoa zaidi ya kulifuata tu. Hata kama waliona halipo sahihi!



    Na kwa afande huyu alifanikiwa kulimeza duku lake akaendelea na mengine kwani alifundishwa kufanya hivi huko mafunzoni. Hata 'mkubwa' akikuagiza usukume jengo mpaka lianguke, huulizi kama inawezekana, bali unaweka mikono yako ukutani na kupoteza nguvu yako bure!



    Lengo kulazimisha tu utii ustawi ndani yako. Lakini pengine pia, kwa kujua ama kutokujua, huchochea hisia za uoga na unyenyekevu zoba.



    "Afandeee!" Sauti za mahabusu iliendelea kuita. "Mtu amezidiwa huku jamani!"



    Massawe kama vile hakusikia hayo akaendelea na kazi zake, afande mwingine akiwa anamtazama kwa kuibiaibia, alitumai pengine Massawe angeguswa hivi karibuni.



    Lakini alikosea. Massawe alitia pamba masikioni. Hakuwa anasikia wala kujali.



    **



    "Amekufa?" Aliuliza mwanaume aliyekuwa amesimama langoni. Macho yake yalikuwa yanamtazama Jona akiwa ametulia tuli hachezi wala hatikisiki!!



    Haraka akatoka langoni na kusogea karibu kuwakuta wenzake waliokuwa wanamtazama Jona kwa macho ya maulizo.



    "Amekufa nini?"



    "Sijui! Mbona ametulia hivi?"



    "Huyu atakuwa amekufa!" Akauliza mmoja kisha akaweka kiganja chake shavuni mwa Jona. "Wa baridi kweli!"



    Mwingine akaweka sikio kifuani, "bado mzima!" Akalipuka. "Nasikia mapigo yake ya moyo kwa mbali sana!"



    "Atakuwa kazirai nini?"



    "Labda. Unajua mwili wa binadamu ukishindwa kuhimili maumivu, unapoteza fahamu!"



    "Sasa tunafanyaje?"



    "Unadhani tutafanya nini hapa? Wenzake wenyewe wamemsusa!"



    "Wenzake gani?"



    "Si hao mapolisi wenzake!"



    "Huyu ni polisi?"



    "Ndo maana yake. Inasemekana ndo kamuua RPC. Sasa naona wenzake kama vile wamemshit! Si unajua ile? ... wanamkomoa flani hivi!"



    "Duh! Noma kweli mwanangu. Ila akifia humu itakuwa soo."



    "Hamna soo wala nini. Mbuzi atakuwa kafia kwa muuza supu!"



    Maongezi haya yote Jona alikuwa anayasikia kwa mbali sana ... mbali sana ...



    Kwa mbali sauti hizi zilivuma masikioni mwake katika mfumo wa mwangwi kana kwamba zinatokea ndani ya chungu ama pango kubwa. Hakuweza hata kutambua nani aliyekuwa anaongea hapa au pale japo alikuwa anawafahamu wote waliopo mule rumande.



    Alitamani kutikisa mwili wake lakini hakuwa anaweza hata kidogo. Mwili ulikuwa mzito mno! Kichwani alikuwa anasikia kana kwamba sauti ya panga ama jembe likiwa limekita kwenye mwamba mgumu!



    ... Kaaaaaangggg' ... kaaaaaanggggggg'



    Hakujua nini kinaendelea ndani ya mwili wake. Alifahamu fika tatizo litakuwa kile chakula alichokula. Ila hakutambua hii ilikuwa sumu gani. Na lengo lake mwilini lilikuwa ni nini.



    Mbona bado yupo hai? Lakini akalitilia mashaka hili. Pengine amekufa na yeye bado hajalitambua. Kama hawezi kusogeza kiungo chochote cha mwili, ni nini huko kama si kufa sasa?



    "Naaammmuuuuoooonnnnaaaa ...." alisikia sauti kwa mbali ikinong'ona kwa kujivuta. Neno moja alilisikia likiwa refu mno. Sauti hii akaitambua kuwa ya kipekee tofauti na zile alizokuwa anazisikia hapo awali.



    Lakini bado fahamu zake hazikuweza kumjuza ni ya nani haswa! Akakodoa macho, lakini alikuwa anaona kizakiza cha kina cha maji. Watu awaona kama vivuli kwenye kioo.



    "Kwwwwiiiiiiiissssshhhaaaaaa haaaabaaaarrriiii yaaaakkkeeee!!" Aliendelea kusikia kwa mbali. "Haaaaaaappppoooo haaaattaaatuusuuumbuuaaa tenaaa. Yeyyyyeee ndooo atttaatussumbuaa sisssiiii!"



    Kikafuatia kicheko. Haa haaaa haa haaaa haa!



    **



    "You are on time!" (Upo ndani ya muda!) Alisema BC akitazama saa yake mkononi. Alishafika nyumbani kwake, ameketi kibarazani penye viti na meza vya kupumzikia. Hakuwa amebadili nguo. Hakuingia hata ndani tokea amefika, zaidi ya kuketi hapo kumngoja mwanamke huyu,



    Miranda. Ambaye alifika hapo akiwa amevalia jeans ya bluu na tisheti jeusi.



    Uso wake haukuwa na furaha.



    Alivuta kiti akaketi kisha pasipo kupoteza muda akaendea kilichomleta hapo.



    "As I told you earlier. What should we do now?" (Kama nilivyokuambia hapo mapema. Nini tufanye sasa?)



    "It is simple. We want him out, right?" (Ni rahisi. Tunamtaka atoke, sio?)



    "Yes, we do! But do you think it will be that easy? He is charged of murder. Murder of a big man!" (Ndio, tunataka! Lakini unadhani itakuwa rahisi? Anashikiliwa kwa mauaji. Mauaji ya mtu mkubwa!)



    "Maybe we should try to bail him out. Even if it may cost much!" (Pengine tungejaribu kumtoa kwa dhamana. Japo inaweza kugharimu mno!)



    "What if that way won't work?" (Vipi kama njia hiyo haitafanikiwa?)



    "Then we'll try the other one." (Basi tutajaribu nyingine.)



    Miranda akachipua tabasamu. Lakini BC akampatia tahadhari.



    "That other way will only be possible if Jona complies with my conditions." (Hiyo njia nyingine itawezekana kama tu Jona atakubaliana na vigezo vyangu."



    **



    Majira ya asubuhi ... kama saa nne hivi.





    Kwa mbali kidogo Marwa anatazama kwenye lango la kituo kikuu akiwa amesimama na mfuko wake wa nailoni wenye chakula.



    Alikuwa amevalia suruali pana ya kitambaa na shati lililokunjamana kwa uhaba wa pasi.



    Akiwa anatazama huko akamwona afande Devi akitoka akiwa anaongozana na mwanamke fulani hivi, wakasimama langoni, na mara wakamtazama kwa pamoja, afande akamnyooshea kidole.



    Punde mwanamke huyo akaanza kuchukua hatua kumfuata Marwa. Alipomfikia akamsalimu na kujitambulisha kama rafiki yake Jona. Yupo hapo kumtembelea na kumjulia hali.



    Naye Marwa akajitambulisha kama ndugu na mkazi mmoja na Jona.



    Lakini haikuchukua muda mrefu, Miranda akatambua Marwa hakuwa sawa. Macho yake yalikuwa mekundu, pia hakuonyesha yupo 'comfortable' kuongea naye.



    Pengine alikuwa anamshuku anaweza akawa si mtu mzuri, akawaza. Kumwondoa hofu Marwa, Miranda akajipambanua kwa undani namna anavyoielewa kesi ile ya Jona kama ilivyopandikizwa mahususi kumteketeza, na mtuhumiwa wake mkubwa akiwa ni Sheng.



    Ils hakusita kuonyesha imani yake.



    "Naamini Jona atayashinda yote haya."



    Hapa Marwa akashindwa kubana hisia zake. Machozi yakamminika.



    Akasema:



    "Hata atakapoyashinda haya hatakuwa Jona wa awali."



    "Una maanisha nini?" Miranda akawahi kumuuliza.



    "Tayari wameshamtilia virus mwilini!" Marwa akajibu machozi yakibubujika. "Hataweza kudumu muda mrefu, labda tu awe anapewa antidote! ... Antidote ambayo anayo Sheng pekee!"



    Miranda akakaukiwa na mate mdomoni.



    "Umejuaje wamemtilia virus? Na kwanini wafanye hivyo?" Akauliza kwa kinywa chake kikavu.





    Marwa akafuta kwanza chozi lake alafu akamwambia alijua hilo punde tu alipomwona Jona. Hali yake aliyokuwa anaipitia ilikuwa ndiyo ileile ambayo wazazi wake waliipitia kwasababu ya kutiliwa virus.



    "Atapata shida sana," akasema Marwa akijaribu kukumbuka namna wazazi wake walivyokuwa wanahanya. "Namwonea huruma. Na Sheng atamgeuza mtumwa!"



    "Kivipi?" Miranda akawahi kuuliza.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Marwa akaeleza namna gani Sheng hutumia silaha hiyo ya virusi kumteka mtu akimfanya mtumwa wa antidote. Endapo unataka unafuu dhidi ya maumivu makali unayojisikia basi atakupatia antidote lakini kwa mabadilishano na kazi yake anayotaka utende.



    Miranda akapatwa na woga. Hata akaishiwa na nguvu. Akamtaka Marwa waende kantini wakaketi na kuongea zaidi.



    Wakaagiza chakula na kuendeleza soga. Miranda akamsikiliza vema Marwa akijieleza. Naye akaja kujinasibu kuwa yu mpangoni kumsaidia Jona atoke ndani, japo hajajua ni kwa namna gani.



    "Afande wameniambia hawezi kupata dhamana hata kidogo, wala nisijisumbue popote pale. Nawaza namna ya kumng'amua mule."



    "Dada yangu," Marwa akaita. "Naomba tu utafute namna yoyote. Na hata kama ukihitaji msaada toka kwangu, nipo radhi kukusaidia kadiri ya uwezo wangu wote ... Jona atapata shida sana mule ndani. Watamtesa haswa kwa wale virus kwa maana hata antidote tuliyonayo haitoshi hata zaidi ya siku nne!"



    Miranda akakuna kichwa chake kwa ukucha. Alikuwa anawaza. Alisonya kisha akatoa simu yake mfukoni na 'kuchonga' na BC. Akampasha habari namna alivyogonga mwamba kuhusu mambo ya dhamana.



    "Ok, but it should be as fast as possible!" (Sawa, lakini inabidi iwe haraka iwezekanavyo!)



    Miranda akakata simu kisha akamuaga Marwa, aenda zake. Wakabadilishana namba mwanamke huyo akayeya akionekana kuwa na haraka.



    Punde kidogo, Marwa akiwa bado yu kantini, akapokea ujumbe toka kwa Miranda.



    'Ukifika home, nishtue!'



    Akaujibu ujumbe huo kisha akarejesha simu mfukoni. Hata hakula. Hakuwa na hamu hiyo akitazama chakula alichomletea Jona hakikuguswa.



    Alikuwa anawaza ni muda gani Jona atarejewa na fahamu apate kumpa chakula. Alikuwa radhi kungoja hapo mpaka usiku alimradi lengo lake litimie.



    **



    "Kaka, naweza nikatoa vyombo?" Sauti ilimshtua toka usingizini. Marwa akafikicha macho yake na kumtazama mhudumu, mwanamke mwembamba mweupe. Kisha akiwa na wenge lake la usingizi, akatazama mezani. Bado kulikuwa na chakula alichoagiza lisaa nyuma.



    Akatikisa kichwa.



    "Chukua tu, dada, hamna shida."



    Mhudumu akakusanya chombo na kwenda nacho. Marwa alipotaka kugeuza shingo kumtazama mhudumu huyo ndipo alipogundua shingo yake ilikuwa inauma!



    Alikuwa amelalia kiti kwa muda mrefu. Shingo ilikuwa inamvuta kana kwamba amevunjika.



    Akiwa anahangaika nayo, mara akamwona afande Devi akiwa anaingia kantini. Akajikuta anataka kujua hali ya Jona. Lakini kabla hajafanya lolote lile, afande Devi akamwona mwanaume huyo, bila hiyana, akamjongea karibu.



    "Bado upo?" Akaigiza kushangaa.



    "Bado nipo, mkuu," Marwa akateta kinyonge akijitengenezea kitini. "Nitaenda wapi na sijampatia chakula ndugu yangu?"



    Afande Devi akatikisa kichwa. Mara akanyoosha mkono wake kumuita mhudumu, upesi akaja hapo na kumwagiza amletee soda.



    "Natamani sana kukusaidia ndugu yangu, sema nashindwa," alijieleza afande Devi. "Nakuonea huruma sana. Namwonea huruma pia na Jona, yupo kwenye shida kubwa sana kwakweli."



    Marwa akainamisha kichwa chake chini. Akakizuia na mkono kutengeneza tama.



    "Atateseka sana," akasema Marwa kwa masikitiko kisha akauliza: "Unaweza kumsaidia akapata dawa?"



    "Dawa ya nini?" Afande Devi akauliza akipokea soda yake toka kwa mhudumu.



    "Hamuoni anaumwa?" Marwa akastaajabu. Afande Devi akanywa kinywaji chake fundo moja alafu akatikisa kichwa.



    "Ninavyokuambia siwezi kumsaidia unadhani nakutania?" Akaifunika soda yake na kizibo isijazwe inzi. "Kwanza Jona haumwi magonjwa ya hospitali. Shida ni moja tu. Akitaka kupata unafuu inabidi akiri kutenda lile tukio."



    "Hata kama hajafanya!" Marwa akatahamaki.



    "Ni kwa uhai wake lakini!" Afande Devi akamsabahi akikodoa macho. "Kufa na huku bado hajahusika ama kuishi kipi bora?" Akauliza Devi.



    Marwa hakuwa na jibu, akakaa kimya. Devi akanywa mafundo kadhaa ya soda mpaka kuifikisha karibu na kikomo.



    "Anyway, lete chakula hicho nitampatia. Wewe nenda kapumzike. Siku nzima upo hapa."



    "Sure?" Marwa akahakiki.



    "Yeah. Leta tu wala usijali," afande Devi akamtoa mashaka. Marwa akamkabidhi chakula.



    "Nakuomba umpatie ndugu yangu. Nakuomba sana!" Marwa akasisitiza.



    **



    Jioni ya saa moja ...



    'Nimefika nyumbani' Marwa alituma ujumbe kwa Miranda kama mwanamke huyo alivyomtaka.



    Lakini kiuhalisia hakuwa bado amefika nyumbani bali karibia na maeneo ya nyumbani. Alikuwa amesimama dukani akinunua baadhi ya mahitaji yake, mojawapo likiwa hilo la vocha lililomwezesha kutuma ujumbe.



    Muda si mrefu, Miranda akampigia simu. Akapokea na kuipachika sikioni.



    "Ndio, nimefika ... kesho? Mida ya saa ngapi na wapi? Ooh! Unapafahamu? ... basi nakutumia ujumbe kukuelekeza ... sawa, n'tajitahidi!"



    Simu ilipokata alimalizia kuchukua vitu vyake hapo dukani, mkate na majani ya chai, alafu akashika zake barabara kwendelea na safari.



    Lakini kuna mtu alikuwa anamtazama!! Kuna mtu alikuwa anamfuatilia. Mwanaume huyu alikuwa amevalia kapelo nyeusi, shati jeusi na suruali ya jeans. Alikuwa ameweka mikono yake mfukoni.



    Kila Marwa alipokuwa anasogea, akasogea naye na mpaka akahakikisha Marwa aingiapo. Kazi yake ikawa imekomea hapo.



    **



    'Nimeshapaona mkuu.' ujumbe ulitumwa toka kwenye simu ndogo aina ya Samsung.



    'Safi, sasa ngoja mpaka ntakapokupa agizo' ujumbe ukaingia kwenye simu hiyo.



    'Sawa' ujumbe ukajibiwa.



    **



    Kwa dirishani moshi wa sigara ulikuwa unafuka. Kama ungelikuwa kwa nje ungeweza dhani kwa ndani kuna kitu fulani kimeshika moto.



    BC alikuwa anavuta sigara yake kubwa kwa fujo. Hufanya hivi akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake. Pembeni alikuwa ameketi Miranda akipooza koo lake na kinywaji ghali, John Walker.



    Kulikuwa kuna ukimya hapa. Kama vile shetani alikatiza. Kwa muda kidogo kila mmoja alikuwa akishughulisha mdomo wake.



    "What if we kill the inspector?" (Vipi kama tukimuua inspekta?) Aliuliza BC akiwa amefunikwa na moshi wa sigara. Uso wake alikuwa ameugeuzia dirishani.



    "No!' Miranda akatikisa kichwa. "You know what. Getting Jona out is our no-escape plan. Not only because Jona will save my ass, but will keep Sheng too obstracted to be comfortable. Without Jona, Sheng can even swallow us. We need him out, for me for us!" (Unajua nini. Kumtoa Jona ni mpango wetu usioepukika. Sio tu kwasababu Jona atanisaidia, lakini atamzuiza sana Sheng asiwe huru. Bila Jona, Sheng anaweza hata akatumeza. Tunamhitaji atoke, kwa ajili yangu, kwa ajili yetu!) Miranda alinguruma.



    "But Jona will be police no more!" (Lakini Jona hatakuwa polisi tena!) BC akatahadhari.



    "It doesn't matter!" (Haijalishi!) Miranda akatema cheche. "Jona will make Sheng pay for all he has gone through in whatever way!" (Jona atamfanya Sheng alipe kwa yote anayoyapitia kwa njia yoyote ile!)



    Miranda akasafisha koo na kuongezea:



    "This is the best chance to get Jona in our side!" (Hii ni nafasi yetu kubwa kumpata Jona kwenye upande wetu!)





    **



    BC akasafisha koo lake. Hakuwa anajua mengi kumhusu Jona ukilinganisha na Miranda. Miranda akachukua fursa hiyo kumweleza BC juu ya uwezo wa Jona.



    Ni mwanaume wa shoka. Mwanaume ngangari, mtu wa kazi!! Endapo wakimpata mwanaume huyo basi wasijali kabisa kuhusu ulinzi na usalama. Na wala Sheng hatakuwa tena mtu wa kumhofia.



    "Let's get the best out of this. It is obvious Jona's lost all of his interest in Police army. To him, they are now traitors and cruel organ." (Tufaidike na hili. Ni wazi Jona ameshapoteza hamu yake yote ndani ya jeshi la polisi. Kwake, sasa ni wasailiti na wakatili.)



    Maelezo haya kwa namna fulani yakagonga kichwa cha BC. Alitokea kuvutiwa nayo. Akampa Miranda kazi ya kuhakikisha hilo linatokea. Yaani kumshawishi Jona aingie upande wao.



    Hapo Miranda akakumbuka na agizo la Kinoo juu ya wale wanawake wawili: Sarah na Sasha. Akataka kumweleza BC lakini akaona huo si muda sahihi.



    Wacha kwanza wapambane na hili lililopo mezani. Hili lililo kubwa. Hayo mengine yatafuata baadae. Hata hakumtonya BC juu ya hali ya Jona kule gerezani kuwa yu hoi na ameshapandikiziwa virusi.



    Alihofia BC anaweza akabadili mawazo. Aidha akamchukulia Jona anaweza kuwa mzigo badala ya msaada kwao.



    "So what way we gonna use?" (Sasa njia gani tutatumia?) Akauliza Miranda. Aliona wameshakubaliana wanataka kumtoa Jona. Kitu pekee kilichobaki ni namna tu.



    BC akavut sigara kwa dakika kama mbili pasipo kusema kitu. Alipoweka sigara yake chini akabinua mdomo wake mkavu alafu akajitengenezea vema kumtazama Miranda.



    "We need plan in this," (tunahitaji mpango kwenye hili,) akanza kutambulisha wazo lake. Miranda akamuazima masikio yote.



    "We have to force him out. You know we can't do it while he's in the police station. It is better if we get the chance to have him in the truck!" (Inabidi tulazimishe atoke nje. Unajua hatuwezi akiwa ndani ya kituo cha polisi. Ni bora kama tukipata nafasi akiwa ndani ya gari!)



    Mpango wa BC hapa ulikuwa ni kumchomoa Jona toka garini kwa kuliteka gari hilo ama kulipindua, aidha likiwa linatoka mahakamani ama kwenda!!



    Lakini kwa Miranda alikuwa ana wazo jingine. Hili la BC aliliona ni gumu kutekelezeka kwa minajili kwamba polisi watampeleka Jona mahakamani pindi tu atakapokiri kama kweli alihusika na tukio la mauaji ya RPC kitu ambacho Jona hatakifanya abadani.



    Japo wanatumia virusi kumlazimisha afanye hivyo, Miranda aliamini Jona atakuwa mgumu kuridhia.



    Sasa wafanye nini?



    Akili yake ikawa hii: wamchomoe Jona akiwa hapo hapo kituoni!!



    "Serious??" BC akatahamaki. Lakini kabla hajamkatisha mwanamke huyo, akampatia nafasi kwanza amweleze.



    Miranda akafunguka kuwa anahitaji 'tiny gas containers' kwa gharama yoyote ile. Atahitaji kama kumi hivi na ndani ziwe zijazwe na Fluothane, Neothyl pamoja na Penthrane'.



    Kwa kutumia watu wawili atakaoongozana nao, basi atakamilisha zoezi la kumtoa Jona ndani ya rumande!!



    "Are you sure??" BC alikuwa na wasiwasi. Kupata gesi hizo haikuwa shida hata kidogo, lakini utendaji ulimstaajabisha.



    Hakutaka kumkatisha tamaa Miranda. Japo hakuelewa namba mpango huu utakavyotekelezwa, akaamua kumwamini na kumpatia nafasi. Ila akampa tahadhari.



    "You have to be very careful!" (Inabidi uwe makini sana!)



    "I know to keep my ass safe!" (Najua kujiweka salama!) Miranda akajibu kwa kujiamini.



    Kwa asilimia zote alikuwa anaamini mpango wake utatimia!!



    **



    Usiku wa saa tatu...



    "Naomba utupatie faragha," Miranda aliongea akimtazama Sarah. Ilikuwa ni punde kidogo tu baada ya kusalimiana na Kinoo na kujuliana hali. Sarah akanyanyuka na kuwapisha kwa kwenda nje lakini hakuwa anapenda kitu hichi hata kidogo.



    Alikunja sura yake, akabinua mdomo na kutembea kwa kasi kuelekea huko nje. Mimba nayo ilikuwa inachangia. Aliona anasumbuliwa, na aidha Miranda hakuwa anajali hali aliyomo.



    Kinoo akamtazama Sarah akiishia akijaribu kuhisi alichonacho mwanamke huyo kifuani. Alijua wazi Sarah alikuwa amekwazika na hakupenda kitu hicho kitokee.



    Alikuwa anampenda Sarah. Na mimba yake tumboni ilimfanya amjali maradufu.



    "Kwani tusingeweza kuongea akiwapo hapa?" Kinoo akauliza.



    "Kama nani?" Miranda akajibu kwa swali, kisha akaongezea: "mahusiano baina yako na yeye hayahusiani hata kidogo na kazi yetu!"



    "Ndiyo maana nikakusihi uwaingize!" Kinoo akatema cheche. "Tutaendelea kumtoa hivi kila tukiwa tunaongea mpaka lini? Anajihisi vibaya."



    "Kinoo," Miranda akaita. "Unadhani sijali? I do care but it takes time. Be patient. Kuna kazi tunatakiwa kuifanya hapa, tuweke nguvu zetu zote hapo, punde itakapokamilika, mambo yote haya yatakuwa mepesi kama kumsukuma mlevi!"



    Kinoo akatikisa kichwa akishushia pumzi puani. Akajaribu kutuliza moyo wake.



    "Kazi gani hiyo?" Akauliza.



    "Kumtorosha Jona kituoni!" Miranda akamjibu kana kwamba ni kazi ya kumuua mbu.



    Kinoo akashangazwa. Ulikuwa ni mpango hatari huo. Yani sawa na kwenda kucheza na domo la mamba!!



    Miranda akamtuliza.



    "Inawezekana. Na kama kila kitu kikifanyika poa, tutatumia dakika tano tu kukamilisha zoezi hilo pasipo kumwaga tone lolote la damu!"



    Kisha mwanamke huyo akatiririka kumwelezea Kinoo namna gani watafanikisha zoezi lao. Kinoo akasikiliza kwa umakini.



    **



    "Siku nyingine usinilete huku, uje mwenyewe!" Sarah alifoka akimtazama Kinoo kwa jicho la vita. Walikuwa ndani ya gari wakirudi nyumbani baada ya kumalizana na Miranda. Kinoo alikuwa ameshikilia usukani asionyeshe kukwaza na kauli ya 'mkewe'.



    "Haitojirudia tena, usijali."



    "Mara ya ngapi hii?" Akabweka Sarah. "Ya pili! Nikija mwanitoa nje. Wanileta huku ili un'toe nje?"



    "Ila nilikuambia ubakie nyumbani ukakataa," Kinoo akajitetea akiwa anatazama barabara.



    "Kwahiyo ndiyo maana ukaamua kuja kunikomoa, sio?" Miranda akatema cheche. "Wewe ulitarajia uniache nyumbani na nani? Nikae peke yangu nimekuwa mchawi na unajua kabisa hali yangu?"



    "Nisamehe, Sarah," Kinoo akaamua kukatisha maongezi. "Halitajirudia tena nimekuahidi."



    Lakini hilo halikuwa jepesi kwa Sarah. Na si tu Sarah, bali kwa wanawake. Kuna muda unaweza jikuta unahitaji 'earphones' kwani wakianza kuongea hawatakupa hata mapumziko ukanywa maji!



    Kinoo hakujua ni muda gani Sarah aliacha kuongea. Alihamishia akili yake yote barabarani. Na akiwaza kazi ambayo ipo mbele yao.



    Aliporudi fahamuni kuwa yupo na mtu pembeni yake, tayari mazingira yalikuwa kimya. Angalau akahema. Akamwambia sasa Sarah kuwa kuna kazo wanatakiwa kuifanya hapo mbeleni japo hakumuweka wazi ni ipi hiyo.



    Sarah akapuuzia. Alikuwa analipiza kile Kinoo alimfanyia kwa kumnyamazia wakati anaongea hapo nyuma. Kinoo naye akalitambua hilo, hakuangaika naye.



    "Naomba tupitie kwa Sasha," baada ya dakika mbili Sarah akanena.



    "Kufanya nini huko saa hii?" Kinoo akauliza.



    "Nataka nikalale huko leo. Sina hamu kabisa ya kuwa na wewe."



    "Eh!" Kinoo akaguna.



    Hakutaka kusema jambo akaamua kutimiza agizo la mpenzi wake huyo kuepusha maneno. Lakini bado alikuwa amekosea. Sarah akawaza pengine Kinoo alikuwa amemchoka.



    Yani amemwambia akalale kwa dada yake alafu anakubali pasipo hata kubisha? Akavuta mdomo mpaka wanawasili. Walipofika ndipo akatoa ya moyoni.



    "Naona umefurahi mimi kuja huku!"



    Kinoo akatikisa kichwa asiseme jambo. Aliona angeongea angesababisha vingine ambavyo hakuvitarajia. Akaongoza njia mpaka getini, akagonga na wakakaa kungoja.



    Ndani ya muda mfupi geti likafunguliwa na akatoka mwanamke mmoja mtu mzima. Wakamsalimu na kumwambia haja yao, kumwona Sasha.



    "Mbona amehama hapa siku nyingi!" Mwanamke huyo akawaeleza. Sarah akastaajabu. Inawezekanaje dada yake akahama hapo makazi yao ya muda mrefu pasipo kumwambia??



    Lakini pia atakuwa ameenda wapi na ilhali pesa hakuwa nayo? Hakupata majibu.



    "Amehamia wapi?" Sarah akauliza. Yule mwanamke akamwambia hafahamu. Kitu pekee anachojua ni kwamba mwanamke huyo amehama.



    "Ahsante sana," Kinoo akashukuru na kumtaka Sarah warejee kwenye usafiri waondoke zao.



    Lakini wakiwa wapo njiani, Sarah hakuwa na amani. Alikuwa anamuwaza pacha wake. Alihisi atakuwa shidani. Alikosa kabisa furaha.



    "Usijali, ni mtu mzima yule. Hawezi akawa amepotea," Kinoo akamtoa hofu.



    Angalau hili swala likawaleta pamoja baada ya kuhitilafiana hapa nyuma.



    "Mara yake ya mwisho kuonana naye alinambia hayuko vizuri kifedha. Hata nikamtoa nauli. Leo naambiwa amehama. Inashangaza!" Sarah aliongea kwa hisia.



    "Au kafukuzwa kodi?" Kinoo akauliza. Lakini kabla Sarah hajajibu, Kinoo akapuuza wazo lake hilo. "Ila haiwezekani! Si angekuja pale nyumbani??"



    Sarah akabaki kimya. Punde akatafuta simu yake na kumpigia dada yake. Sijui alikuwa anawaza nini akachelewa kufanya hilo. Aliweka simu sikioni kusikilizia, baada ya ukimya wa sekunde kadhaa, sauti ikamwambia anayempigia hapatikani!



    Akajaribu kama mara nne, yote majibu yakiwa hayohayo, HAPATIKANI!! Sarah akazidi kujawa na hofu.



    Mpaka wanafika nyumbani alikuwa kimya. Ila kheri alipokuwa anaingia ndani, simu yake ikaita. Kutazama alikuwa ni Sasha! Mwanamke huyo alimtafuta baada ya kukuta taarifa ya kutafutwa punde baada ya kuwasha simu yake.



    "Hallow!"



    "Hey nambie sis!"



    "Mambo?"



    "Poa. Unaendeleaje dear?"



    "Safi tu. Upo wapi?"



    "Mie? Ntakuwa wapi pengine zaidi ya nyumbani saa hii?



    "Nyumbani?"



    "Ndio. Nipo kwa bi Mwenda hapa."



    Bi Mwenda alikuwa ni yule mwanamke aliyewafungulia geti Sarah na Kinoo walipoenda kumtembelea Sasha kule makazini.



    "Sasha," Sarah akaita. "Kwanini unaniongopea?"



    "Nakuongopea? Kivipi dear?"



    "Umehamia wapi?"



    Kidogo kukawa kimya.



    "Najua umehama. Nambie umehamia wapi?"



    "Sarah, yah nimehama. It's a long story. Ntakutafuta tuongee."



    Simu ikakata. Sarah akaachwa na bumbuwazi. Akajaribu tena kupiga akaambiwa haipatikani!!



    Sasha ana nini?? Akajiuliza akiduwaa.



    **



    Usiku mzima alikuwa analia kwa maumivu makali! Mifupa ilikuwa inamuuma mwili mzima. Kichwa bado kinagonga na pua inamimina damu!!



    Kila alipotaka kusogeza kiungo chake cha mwili, akaishia kulalama na kushindwa. Haki mateso yalikuwa makali mno. Hakuwahi kujihisi mdhaifu kiasi hiki tangu azaliwe.



    Hakuwahi kuhisi maumivu makali kiasi hiki tangu atambulishwe duniani. Haya yalikuwa kiboko!! Ni kama vile alikuwa amevunjwavunjwa mwili mzima kisha akadumbukizwa kwenye bwawa la barafu akae humo kwa masaa!



    Hakuwa anahisi chochote kwa ngozi yake. Kichwa kilikuwa hakigongi tena bali kinampigia kelele kali! Ushawahi kusikia paka akikwarua bati? Ndivyo Jona alivyokuwa anasikia makelele sikioni!!



    Meno yalikuwa yanamuuma. Jasho lilimwagika.



    Wenzake hawakuwa na la kumsaidia zaidi ya kumtazama tu kwa huruma. Japo hawakuwa wanajua nini Jona anahisi mwilini, walimwona anateseka sana.



    "Jooonnnaaaa!" Sauti kwa mbali ilimfikia masikioni. Kama kawaida sauti hii alikuwa anaisikia kwa mbali sana. Kwa taratibu sana.



    Alitamani ajue sauti hii ni ya nani ila hakuweza. Maumivu alikuwa anayasikia. Kelele sikioni iliyokuwa inamuumiza, ilimnyima nafasi hiyo.



    Langoni alikuwa amesimama Kamanda mkuu. Alikuwa yu ndani ya sare yake ya jeshi iliyokuwa imechafuka kwa urembo na vyeo. Macho yake yalikuwa yanamtazama Jona aliyekuwa amelala chini.



    Kidogo akaungana na vijana wawili waliokuwa wamevalia kiraia. Walikuwa ni maaskari pia. Miongoni mwa vijana hao alikuwa ni yule 'jamaa' aliyemfuatiliw Marwa kuyafahamu makazi yake.



    Wote wakamtazama Jona kwa muda mchache kabla Kamanda mkuu hajaagiza wamlete ofisini kwake ana maongezi naye.



    **



    "Jona!" Kamanda akaita akimtazama Jona kitini. Jona alikuwa amekaa hapo akiendelea kuchuruza damu puani. Alikuwa ameketi kana kwamba mgonjwa wa utindio wa ubongo. Alikuwa ameng'ata meno, amekunja ndita, mabega ameyapandisha juu. Macho amefumba kusikilizia maumivu pomoni anayosikia.



    Kwa mbali sauti ya Kamanda ikamfikia:



    "Jona, utaendelea na mateso haya mpaka lini? Kubali yaishe. Si kila mara utaibuka kuwa mshindi! ... naweza nikakusaidia. Nipatie nafasi."



    Jona hakuwa na uwezo wa kujibu. Aliendelea kukaa vilevile kana kwamba hajasikia kitu.



    "Ukifanya mchezo utafia rumande kwa ubishi wako!" Kamanda akatishia. "Sasa chagua moja nikakutupie huko uendelee na maumivu yako ama nikusaidie upate unafuu??"



    Japo Jona hakuwa na uwezo wa kupambana, na alikuwa anasikia maumivu yasiyo na mithili, akafungua macho na kumtazama Kamanda. Macho yake yalikuwa mekundu mno!



    Alimtazama Kamanda kwa macho ya umauti. Macho ya kisasi!!



    Akiwa anahisi maumivu ya kufa, akanyoosha mkono wake akitaka kumkamata Kamanda. Ila haukufika, akashindwa kustahimili maumivu.



    "Unajifanya mgumu eenh?" Kamanda akamuuliza akibinua mdomo wake. Akagonga meza mara mbili.



    Puh! Puh!



    **



    Mlango wa ofisi ukafunguliwa, wakatoka vijana wawili wa Kamanda wakiwa wamembelelea Jona. Kwa upesi wakayoyoma naye wakielekea rumande kwenda kumtupia huko.



    Mlango wa ofisi ulipofunga, Kamanda akanyaka simu yake na kupiga.



    "Bado ni mgumu. Nadhani tuangalie namna ya pili sasa," Kamanda alisema kwa hakika.



    "Hapana," sauti ikavuma simuni. "Ngoja tutazame na kesho kama bado ataendelea kuvumilia. Virus hao wanatafuna kila siku inavyokwenda. Hataweza kuvumilia zaidi ya kesho. Na itapendeza zaidi kama yule rafiki yake atamletea antidote!"



    "Kivipi?" Kamanda akauliza.



    "Hao virus ambao wapo mwilini mwake hawaondolewi na antidote waliyonayo. Endapo atakampopatia, basi ataharibu mambo zaidi. Atapata maumivu maradufu!!"



    Kamanda akaridhika na hayo maelezo. Akakata simu.



    **



    "Nipo tayari kwa kila kitu," alisema Marwa akimtazama Miranda. Walikuwa wapo ndani ya nyumba ya Jona majira haya ya mchana. Miranda alifika hapo muda si mrefu hapo nyuma akiwa katika harakati zake za kuwezesha zoezi la kumtoa Jona kituoni.



    "Sawasawa!" Miranda akatikisa kichwa. "Hili zoezi inabidi lifanyike kesho kwa namna yoyote. Wewe kazi yako ni ndogo sana. Kule kituoni wameshakuzoea sasa kuwa unaleta chakula mara kwa mara.



    Sasa kesho yake nitakupatia hotpot la chakula ulipeleke huko. Utakapofika, utafanya njia zozote ulifungue pale kaunta, kwa muda wa sekunde kumi tu. Kisha ukifanikiwa kulipeleka kwa Jona, umtahadharishe asile.



    Ataliweka wazi kwa dakika moja, inatosha. Mengine mimi na Kinoo tutamalizana nayo."



    "Sawa, hamna shida," Marwa akapokea maelekezo. Kisha pasipo kupoteza muda akamwambia Miranda kuwa anataka kwenda kituoni kumpelekea chakula Jona.



    Na pia vilevile antidote!!



    "Hamna shida, naweza kukuwahisha," Miranda akamkarimu. Wakanyanyuka toka sebuleni na kwenda nje walipodumbukia ndani ya Range Rover sport nyeupe na kutimka.



    **

    Kwa kasi waliyoitumia hawakuchukua muda kuwasili, Marwa akashuka garini na kwendaze kituoni baada ya kuagana na Miranda aliyesema anaenda kushughulikia na kuweka mambo sawa.



    Marwa akaingia mapokezi na kukutana na afande Devi aliyempokea kwa ukarimu na kumjulia hali.



    "Nimekuja kumletea chakula jamaa 'angu," alisema Marwa kisha akafungua chakula na kukionyesha.



    "Najua umekuja sababu hiyo," alisema afande Devi pasipo kutazama chakula hicho. Ni kheri akuwapo koplo Massawe, basi akamruhusu akamwone mtu wake upesi huko rumande.



    Chap Marwa akafika huko na kumkuta Jona akiwa amejilaza hoi. Akamuita mara tatu akisaidiwa na mahabusu wengine. Jona akaamka na akiwa hajiwezi kwa lolote, wenziwe wakamburuta kusogea langoni.



    Kwa namna ambavyo Marwa alimwona Jona, akashindwa kuzuia machozi machoni mwake. Jona alikuwa amepungua. Ni mdhaifu. Hana afya wala havutii kumtazama.



    Si Jona yule umjuaye.



    "Jona," Marwa akaita. "Kula angalau." Akambembelezea chakula. Jona akatamani sana kumjibu lakini hakuwa anaweza.



    Alimtazama Marwa akamwona kwa mbali. Alitabasamu kumpa matumaini lakini Marwa akaishia kulia.



    "Nitashinda," Jona alisema kwa sauti ya chini. "Usijali, Marwa."



    Akala tonge mbili tatu, akashindwa kuendelea. Alilalama anasikia kichefuchefu, na kadiri anavyotafuna anasikia kichwa kinamuuma maradufu!!



    Japo ni kweli alitamani kula, tumbo lilikuwa tupu, hakuweza abadani!



    "Nimekulete antidote!" Marwa alimwambia kwa macho ya furaha. Alikuwa amemshikilia na mkono wake kumzuia aketi.



    Kabla Jona hajasema kitu, Marwa akatazama kushoto na kulia alafu akachonoa kichupa kidogo mfukoni, akamtaka Jona afungue mdomo.



    Akamminia chote kisha akamruhusu ajilaze chini.



    "Utakuwa sawa," Marwa aliamini.



    Jona akalala asiseme kitu. Muda si mrefu akakata fahamu kabisa!! Hakuwa anasikia, kuona wala kuhisi chochote.



    Maumivu yalizidi mwilini mpaka fahamu ikashindwa kustahimili. Marwa asiwe anajua hilo, akamtazama Jona kwa sekunde kadhaa. Na hata alipoona kimya akatambua mwanaume huyo atakuwa katika hatua za kuwa sawa. Hivyo hana haja ya kuhofu.



    Akamuaga Jona na kisha kwenda zake.



    **



    "Afandeee!" Sauti ikavuma ndani ya rumande. Si kwamba kulikuwa kimya, bali sauti hii ilikuwa kubwa kupita kiasi.



    "Afandee, kuna mtu anakufa huku!" Alipaza sauti jamaa mmoja aliye ndani ya chumba kimoja na Jona.



    Jona alikuwa anatoa damu masikioni, puani, mdomoni na machoni kama machozi!! Hakuwa anatikisika hata kidogo. Hakuonyesha dalili zozote za uhai.



    Hata mwili wake ulikuwa wa baridi kana kwamba ametoka kwenye jokofu!!



    Haraka afande Devi aliwasilia akamtazama Jona. Mahali alipokuwa amelaza kichwa chake palikuwa pametapakaa damu.



    Hata afande huyu akashtushwa sana na hili. Upesi akamweleza na kumsisitiza Massawe akamwambia mkuu wa kituo kuwa wanatakiwa kuchukua hatua upesi la sivyo mtu atawafia rumande iwe tabu!



    Taarifa zikafika kwa OCD, ila ikawa bure. Jona hakuruhusiwa kutoka kituoni kwa namna yoyote ile labda awe mfu tu!!



    "Nenda kaendelee na kazi yako. Kama kufa mwache afie humo. Alivyomuua RPC alidhani atastarehe??" Alisema OCD akiwa anachokonoa meno yake kwa toothpick.



    **



    "Ewaah ... naona ameshapatiwa ile antidote!" Alisema Kamanda mkuu akitabasamu na simu.



    "Yes ... he is in critical situation ... hawezi akafa? ... ooh sawa. Hamna shida nitafanya hivyo."



    Kamanda akakata simu kisha akacheka. Alipewa maagizo ya kuyatimiza.



    **



    "Naomba uningoje hapa," alisema Sarah kwa sauti ya kuamuru. Macho yake yalimtazama Kinoo kabla hajabanduka toka kwenye kiti cha gari na kwendaze ndani ya jengo maeneo ya Msasani.



    Kinoo akamtazama mwanamke huyo akizamia humo aliposema anaenda kukutana na dada yake, Sasha, kama walivyopeana maelekezo.



    Akawaza kidogo akijiuliza maswali kadhaa. Sasha alikuwa anafanya nini katika hilo jengo maeneo ya Msasani na kwanini Sarah hakutaka kuongozana naye kwenda humo.



    Kwani Sasha si shemeji yake??



    Hakuwaza wala kujihangaisha sana kwani alidhani pengine Sarah anataka tu kulipiza kisasi kwa vile anavyomfanyia akiwa anaongea na Miranda akimtaka atoke nje.



    Akajikuta anatabasamu na kupuuza. Kosa ambalo hakutakiwa kulifanya hata kidogo.



    Kwenye ulimwengu wa kijasusi, hakuna kitu kidogo hata siku moja. Kila tendo laweza kugeuka na kuwa sumu kali ys kumshusha tembo ndani ya sekunde kadhaa tu!!



    Kusogezea muda wake wa kungoja, akawasha redio na kulaza kiti, akajilaza.



    **







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog