Search This Blog

Friday 28 October 2022

JINI MWEUPE - 3

 









    Simulizi : Jini Mweupe

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Ofisi ya Ukombozi; 9;00am



           Kamanda Catherine, kiongozi mkuu wa idara ya mawasiliano na teknolojia, katika kundi lake la wapelelezi watatu, maarufu kama the super three soldiers, alikuwa amechanganyikiwa, taarifa aliyoipokea kwa mfumo wa barua pepe ya ofisi yao, pamoja na radio na televisheni zilizidi kumchanganya kupita maelezo. Alijizungusha kwenye kiti chake, ndani ya ofisi yao maarufu kama ofisi ya Ukombozi, kabla ya kuelekea kituoni itakapofika saa sita mchana, kwenda kujua nini kinaendelea …



    “,We have to go, tunapaswa kwenda,gaidi aliyeuawa alisema ukweli mtupu, tungemuhoji kabla hajafa tungejua mambo mengi zaidi, lakini ndo hivyo, they have killed him, wamemuua, hakijaharibika kitu, tukienda Gano, tutapata mahali pa kuanzia, tujue alipotoka Gano alielekea wapi tena, na kwanini anaua? Mauaji ya kufanana, sio bure, kuna kitu! “,kamanda Catherine, akiwa peke yake ofisini, ilikuwa kawaida yake kuwahi kazini siku zote, aliongea, akatafakari, akanyenyua simu yake, akampigia kamanda Kendrick, mkuu wake wa kazi …



    “,Yes kamanda, mzima? “,kamanda Kendrick aliongea, baada ya kupokea simu.



    “,Mimi mzima, vipi umefuatilia habari zilizopamba mtaani, Donald Mbeto ameshafanya yake nchini Gano, taifa letu linatutaka kwende haraka sana kisiwa cha Gano tukamtafute muuaji wetu, serikali ya Gano na wenyewe wametutumia ujumbe twende tukawasaidie uchunguzi wa mauaji yaliyofanyika! “,kamanda Catherine alieleza kwa kirefu zaidi.



    “,Nimeshapata taarifa hizo, ndiyo taarifa ambazo zimenichelewesha kufika ofisini mpaka sasa hivi, lakini tayali nimeshapata majibu, namna ya kumpata Donald Mbeto, nakuja sasa hivi ofisini, mpatie taarifa kamanda Philipo tukutane hapo ofisini, ndani ya nusu saa ijayo, “kamanda Kendrick aliongea.



    “,Sawa bosi, “kamanda Catherine aliongea, akakata simu, kisha akabonyeza tena simu yake, akaitafuta namba ya simu ya kamanda Philipo, akaipata, akapiga, kisha akaisogeza simu yake sikioni.



    “,Haloo Cathe,umesikia kuhusu Donald Mbeto huko Gano, yani huko ni kilio na kusaga meno kama jehanamu vile, niko njiani nakuja ofisini, tujue nini cha kufanya! kamanda Kendrick ameshafika ofisini? “,



    “,Yani simu hii ni kwa ajili ya huyu mshenzi,tumekubaliana tukutane hapa ndani ya nusu saa ijayo, kamanda Kendrick hajafika ofisini, lakini yuko njiani anakuja, usichelewe, usinywe bia yoyote, najua vizuri matatizo yako, usipo nisikiliza, utakwamisha kila kitu ……”,



    “,Hahahaa, sawa, nakuja, siwezi kulewa,nitalewa mpaka Donald Mbeto, huyu jini mweupe awe katika mikono yetu, “



    Yalikuwa ni maongezi ya simu kati ya kamanda Philipo, pamoja na Kamanda Catherine, kisha simu zilikatwa.



    Ofisi ya ukombozi; 10:02



    Kikao kifupi kiliendelea, kamanda Kendrick aliongoza majadiriano, kila mmoja alichangia maoni yake, akatoa mbinu mbalimbali za kumkamata Donald Mbeto.



    “,Kabla hatujafika mbali, kamanda Kendrick, hebu tueleze! nilipokupigia ulinambia kuna mbinu ambayo umeipata, hebu tuelezee na sisi tuitambue kama mbinu hiyo inafaa au haifai! “,kamanda Catherine aliongea,wenzake wakimsikiliza kwa makini.



    “,Usjali kuhusu hilo, vipi kuhusu ujumbe kutoka Gano,unasemaje, hebu tuusome halafu nitawaeleza mbinu hiyo ya kumkamata huyu Mwanaharamu. “,kamanda Kendrick aliongea, akijizungusha kwenye kiti chake huku na kule,wenzake wakimsikiliza kwa umakini wa hali ya juu.



    “,Mauaji yametokea tena kwa mara ya pili sasa, mauaji yanayofanana, kila tukio muuaji katumia sumu, sumu ambayo imetumika kwenye mauji huko nchini kwenu Tanzania, Ufilipino na nchi kadhaa za Afrika, Asia na Ulaya, tunahitaji msaada wenu, mje mara moja kushirikiana na vijana wetu kumsaka adui huyu! “,kamanda Catherine alimaliza kuusoma ujumbe wa barua pepe kutoka nchini Gano, akainua kichwa chake,wote watatu wakatazamana.



    “,Haya sasa, nazani umesikia, tueleze hiyo mbinu kisha tuanze kazi haraka sana…”,kamanda Philipo alichangia mawazo yake.



    “,Ok! kabla ya kuelekea nchini Gano, tunapaswa kulifumbua fumbo la kifo cha gaidi mshirika wa Donald Mbeto, gaidi aliyeuawa mahabusu, tukifanikiwa! lazima tujue mahali alipojificha Donald Mbeto, hata tukienda Gano, yatatokea kama yaliyotokea Ufilipino. “,kamanda Kendrick aliongea kwa hisia kali,wote wakatikisa vichwa vyao,bila shaka walikubaliana na mawazo yake.



    “,Kweli kabisa, kama vile ulikua kichwani mwangu,hata mimi niliwaza hivyo hivyo! mimi ninaona tukamuhoji vizuri askari aliyekuwa zamu, maana mpaka sasa hatujamuhoji kwa kipigo, lazima atasema ukweli,kuna kitu anajua tu yule, maana usiku wakati tunamuhoji hakujiamini hata kidogo “,kamanda Catherine aliongea,akanyenyuka kwenye kiti chake.



    “,Twendeni, twendeni kituoni haraka sana, tusipoteze muda, nazani tayali tumefikia muafaka! ,askari yule ahojiwe kwa kipigo, kama siyo yeye muuaji basi nitalipa kila kitu kwa ajili yake”,kamanda Kendrick aliongea, na yeye akanyenyuka kwenye kiti, akaweka tai yake vizuri,akajiandaa kwa ajili ya kutoka nje ya ofisi ya ukombozi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Philipo alichukua kompyuta ya ofisi, akaiweka kwenye begi lake, akanyenyuka kwenye kiti,kamanda Kendrick akatoka nje, kamanda Catherine akafuatia, kisha kamanda Philipo akafuata, akasimama nje ya mlango wa ofisi yao, akabonyeza bonyeza mashine pembeni ya mlango,akaingiza nywila (neno siri), mlango ukajiloki. Wakatoweka, wakaelekea kituoni.



    …………………………………



    Makao makuu ya polisi; 11:02



             Kamanda Catherine alikuwa amesimama, mkononi alikuwa ameshika plaizi,kamanda Philipo alikuwa amesimama pembeni ya Catherine, mkononi mwake alishika bakola, fimbo kubwa ya chuma isiyo katika, kamanda Kendrick yeye alikuwa amechuchumaa,mkononi alishika mjeledi, akamtazama askari wa zamu aliyelala chini kama mzigo, akiwa amefungwa mikono na miguu.



    “,Ukweli wako ndiyo utakuweka huru, jana tulikuhoji kwa upole, ukazani tunatania, hatujawahi kutania kazini hata siku moja, ndiyo maana tunategemewa na taifa letu, tuko hapa kwa ajili yako! “,kamanda Kendrick aliongea, kamanda Catherine akachuchumaa, akasogeza plaizi yake kwenye masikio ya askari yule, akayabana kwa nguvu bila huruma.



    “,yalaaaa! nakufa…a …”,kelele za uchungu zilisikika,askari yule alilia kama mtoto,damu ilichuruzika katika sikio lake,alitamani ajikune lakini hakuweza, mikono yake ilifungwa kwa pingu za chuma.



    “,Kufaaa! si hautaki kusema ukweli? “,kamanda Catherine alifoka.



    “,Sisemi, nasema sihusiki na chochote! “,askari yule aliongea kwa jeuli.



    “,Pyaaa! pyaaa! “,



    “,Yalaaaa! mama…aa”,



    Sauti za bakola zilisikika, kamanda Philipo alimchapa bakola mbili askari yule kwenye unyayo wa miguu yake,unyayo ukaacha mistali miwili iliyovuja damu,askari yule akaikunja na kuinyosha miguu yake, alitamani kujikuna lakini hakuweza.



    “,Nitasema, nitasema! msiniuee ……!”,askari yule alipiga kelele,maumivu yalimzidi nguvu, mwili wake ukashindwa kustahimili mateso ya kipigo ambacho nd’o kwanza kilikua kinaanza.



    “,Sema! semaa kabla sijakuchalaza na mjeledi wangu! “,kamanda Kendrick alifoka, akiwa amenyenyua mkono wake wa kulia juu, akijiandaa kumtandika nao askari yule.



    “,Nitasema mkuu, msinipigee! “,askari yule mamluki alililia, akaomba msamaha,alikuwa tayali kusema ukweli, wote wakaweka silaha zao za mateso pembeni, wakakaa tayali kwa ajili ya kumsikiliza.



    “,Haya tueleze, nani aliua? “,kamanda Philipo aliuliza swali.



    “,Mimi ndiye niliye muua gaidi yule, nilipewa sumu na kundi la D47 niweze kummaliza, kwa muda mrefu nashirikiana nao, nawapatia habari za upelelezi kisha wananipatia pesa, ndiyo maana imekua vigumu hata kumkamata Donald Mbeto”,askari yule aliongea, akaeleza kila kitu, hasira zikampanda kamanda Catherine, akamsogelea askari yule, akamkaba shingoni..



    “,Muachee, utamuua! Catherine utamuuaaa! “,kamanda Kendrick aliongea kwa taharuki, akiwa anafanya kazi ya ziada kutoa mkono wa Catherine katika shingo ya askari yule, huku kamanda Philipo akishirikiana naye kufanya shughuli hiyo.



    “,Haiwezekani kila siku tuhangaike kumsaka mtuhumiwa kumbe mchawi tunaye ndani,stupid comrade! hautufai katika jeshi letu, lazima sheria ichukue mkondo wake …”,kamanda Catherine alifoka,huku akiiweka vizuri suti yake, baada ya mkono wake kufanikiwa kutolewa na makamanda wenzake katika shingo ya askari yule msaliti.



    “,Sawa! tumesikia,makazi ya D47 yako wapi?  ,Donald Mbeto na yeye tunampata wapi?”,kamanda Kendrick aliuliza swali jingine,akimtazama askari yule msaliti,akijaribu kuinyosha shingo yake bila mafanikio,alimanusura kamanda Catherine amtoe koromeo.



    “,D47 wanapatikana katikati ya Bahari ya hindi,wana meli yao kubwa aneo hilo,hata Donald Mbeto hurudi eneo hilo kila anapomaliza kutekeleza tukio,huenda kupumzika kabla ya kupewa kazi nyingine…,ni hayo tu nayofahamu bosi!”,askari yule aliongea,kamanda Catherine akachana shati la askari yule,akamgeuza,uso ukalamba vumbi,mgongo wake ukabaki wazi,”D47 namba mia moja,”kamanda Philipo aliongea,alisoma chata kubwa iliyozungushiwa duara katika mgongo wa askari yule.Askari yule hakuwa mamluki tu,bali alikuwa mwanachama halisi wa D47.



    “,Ndio maana Tanzania hatuendelei,China watu kama hawa wanapigwa risasi mbele ya umma…”,kamanda Kendrick aliongea,akaanza kutoka mahabusu,wenzake wakamfuata.



    “,Mahabusu yake iongezewe ulinzi, asiingie wala kutoka mtu yoyote, kamanda Petro andaa helikopta ya kivita! tunapaswa kuelekea nchini Gano, kisha tutaelekea moja kwa moja katikati ya bahari ……” ,kamanda Kendrick alitoa maagizo,kisha wote watatu wakaelekea stoo ya silaha (Amala),wakachukua silaha zote zilizowafaa kwenye mapambano,visu, bastola, kamba, saa zao za kipelelezi pamoja na miwani ya mionzi mikali.



    ………………………………



    01:20



          Helikopta ya jeshi iliacha ardhi ya Dar es salaam Tanzania, siku ya ijumaa, saa saba mchana, ilipaa futi sitini kwenda juu, ikaelekea mashariki mwa mji wa Dar es salaam, katikati ya bahari.Askari wa the super three soldiers wote walivalia mavazi maalumu meusi, rangi ya shaba, yasiyo pitisha risasi(bullet proof), machoni walivaa miwani ya mionzi, mkono wa kushoto walivaa saa zao za kipelelezi kwa ajili ya mawasiliano.



    “,Kaa tayali kwa misheni, kushindwa ni dhambi, tuna dakika kumi za kufika eneo la tukio nchini Gano, tuna saa moja la kutekeleza misheni na kumpata Donald Mbeto, tunaelewana? “,kamanda Kendrick aliongea, akauliza swali askari wake.



    “,Ndiyo afande, tumeelewana! “,wote waliitikia,walikubaliana na maelekezo kutoka kwa mkuu wa kikundi, kamanda Kendrick, safari ikaendelea, helikopta ikaendelea kukata mawimbi.



    Gano:02:02pm



           Pilikapilika ziliendelea katika hospitali ya jiji la Gano,watu waliingia kuchukua miili ya ndugu zao,waliopoteza maisha kwa sumu hospitalini hapo,waandishi wa habari hawakuchoka, waliendelea kutimiza majukumu ya kuchukua taarifa mbalimbali kama kawaida yao. Polisi waliendelea kufanya uchunguzi wao, wakiongozwa na kamanda wao mkuu wa upelelezi kisiwani Gano.



    “,Jiandaeni kupokea wapelelezi kutoka Tanzania, watafanya uchunguzi kwa dakika kumi tu, kisha tutaongozana nao kwenye misheni katikati ya bahari …”,kamanda mkuu wa upelelezi kisiwa cha Gano aliongea,vijana wake ishirini wakapanga mstali, uwanja wa hospitali ya Gano,macho yao yalitazama anga, kaskazini, mashariki na magharibi.Kila mmoja akisimama wima kwa ushupavu, kupokea askari watatu wenye sifa kubwa dunia nzima, kwa upelelezi wao wa kishujaa.



    “,Simama wima, heshima toa! “,kamanda yule alitoa amri, helikopta ilipita katika anga la hospitali kwa spidi ya ajabu,ikapigiwa saluti za heshima, ikakunja kona ,kaskazini, kisha ikarudi tena magharibi, ikapunguza kasi, ikaanza kushuka chini iweze kutua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “,Makamanda wakishuka, piga saluti za heshima, kisha tutawaongoza mpaka eneo la tukio …”,kamanda yule aliongea kwa sauti kubwa, kisha akavuta pumzi ndefu. Macho yake yakiitazama helikopta kubwa ya kijeshi yenye chapa ya Tanzania, ikitua na kutimua vumbi zito eneo lote la uwanja wa hospitali ya Gano.



    “,Ndiyo afande, tumesikia, tuko tayali kutekeleza amri mkuu! “,sauti ilisikika, vijana waliopanga mistali miwili iliyonyooka waliitikia amri ya kiongozi wao, wakajiweka sawa, wakasimama wima bila kutikisika.



    …………………………………



    Helikopta ya jeshi la Tanzania ilitembea kilomita takribani ishirini,ikafika anga la kisiwa cha Gano,ikaanza kushuka taratibu, futi hamsini, arobaini, therathini, mpaka ishirini, ikaanza kufuata ramani mpaka mahali pa tukio, hospitali ya jiji la Gano, kisiwa kinachopatikana bahari ya hindi, jirani kabisa na nchi ya Tanzania.



    “,Tumefika, hakuna muda wa kupoteza, kila mtu atimize majukumu yake …”,kamanda Kendrick aliongea,akawakumbusha tena askari wenzake.



    “,Ndiyo afande! “,waliitikia, helikopta ikazunguka eneo la hospitali,ikakata kona, kisha ikatua katika uwanja wa hospitali, wakashuka wakitembea harakaharaka,huku wakipigiwa saluti za heshima, kisha askari wenyeji wakawaongoza mpaka eneo la tukio.



    “,Eneo lenyewe ndiyo hili, kama unavyoliona, aliingia kupitia choo hiki, akatoa mfuniko wa dali,akapita ndani kwa ndani mpaka chumba cha madawa, akaweka sumu kwenye madawa yote ya kimiminika, hivyo basi yoyote yule aliyetumia dawa hizo asubuhi ya leo aliweza kufa, mpaka sasa wamefariki dunia wananchi elfu tatu! “,kamanda mkuu wa upelelezi nchini Gano alitoa maelezo ya upelelezi wa awali,kamanda Kendrick akatikisa kichwa, akakagua choo chini na juu, kisha akatoka nje, akaangaza huku na kule.



    “,Hiyo karatasi vipi?”,kamanda Kendrick aliuliza swali, akasogea ukutani, mahali kulipokuwa na karatasi yenye wino mwekundu.



    “,Hiyo ndo karatasi iliyotuongezea taharuki, imeandikwa Jini mweupe, maandishi ya damu …!”,kamanda yule aliendelea kutoa maelezo yake.



    “,Sawa nilishapata jibu, huyu ni Donald Mbeto, hakuna mwingine, tuachieni kazi hii, tunaenda kuifanyia kazi, tukihitaji msaada tutawajulisha! “,kamanda Kendrick aliongea,aliona kazi hiyo aifanye yeye mwenyewe pamoja na vijana wake alio wazoea,ombi lake likakubaliwa, askari wa nchini Gano wakapiga saluti, wakaanza kutoka nje,waandishi wa habari wakitimiza majukumu yao kupiga picha na kurekodi kila tukio.



    “,Kwa niaba ya waziri wa ulinzi, tunawatakia safari njema na misheni njema, tulitamani sana kuongozana na nyinyi maana tuna hasira na huyu muuaji, kwa msaada wowote msisite kutufahamisha …”,kamanda mkuu wa upelelezi kisiwani Gano aliongea,wakapigiana saluti, the super three soldiers wakaingia ndani ya helikopta,baada ya dakika tano, helikopta ilikua futi sitini juu angani, ikaanza kuelekea kaskazini, kukiacha kisiwa cha Gano, kuelekea katikati ya bahari, kutekeleza misheni ngumu kuliko zote katika maisha yao ya kipelelezi, achilia mbali oparesheni ya kumsaka muuaji hatari Yuan Liang nchini Gano mwaka mmoja uliopita, hii ya Donald Mbeto iliwaumiza kichwa kila siku.



    …………………………………



    Mbezi, Dar es salaam :2:00



                Magaidi wa D47 kanda ya Dar es salaam, walikuwa wameketi kikao cha dharula, wakibadilishana mawazo,askari wa serikali,aliyewapatia taarifa kutoka serikalini na kufanikisha shughuli zao mbalimbali alikua hapatikani kwa simu tofauti na siku zote,tangu usiku wa saa nane walimtafuta wajue nini kinaendelea serikalini, lakini hakupatikana, simu yake haikuwa hewani kabisa, kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo hofu ilizidi kutanda.



    “,Hapa kuna kitu,sio kawaida yake kabisa,mimi nashauri twendeni kituoni,mmoja aingie mpaka kituoni,kama kuna lolote baya limemkuta,tumsaidie,bila hivyo kila kitu kitaharibika…”,gaidi D47 namba sitini aliongea,wenzake watatu wakiwa makini kumsikiliza.



    “,kweli kabisa,yule ana siri nyingi kama mwenzetu,akiwa pabaya hata sisi tuko pabaya,tuchukue silaha,mmoja ajifanye ameenda kushtaki,apeleleze kisha atuletee taarifa nje tujue mwenzetu yuko salama,au kagundulika,”gaidi D47 namba ishirini aliongea,wote wakanyenyuka,wakasogelea stoo yao ya silaha,wakachukua bunduki zao,mikanda ya risasi,wakatoka kwenye nyumba yao ya kifahari,wakaingia kwenye BMW nyeusi,wakatoweka katika makazi yao haraka sana kwa kasi ya ajabu.



    …………………………………



    Bahari ya Hindi:



            Burudani ziliendelea katikati ya bahari,kila mmoja aliyekuwa katika meli ya D47paraquaat aliburudika kwa starehe aliyohitaji,wengine walikunywa pombe,wengine walijidunga madawa ya kokeini,huku wengine wakizini,kila mmoja alifanya starehe aliyohitaji kufurahia ushindi wa Donald Mbeto,alifanikiwa kukamilisha kazi aliyotumwa na bosi kwa mataifa yote matano aliyotumwa kuua kwa sumu,akaitikisa dunia,jina lake likaenea duniani kote.



    “,Danger!danger!our kingdom is in danger!dange!danger!”,(Hatari!hatari!ufalme wetu uko hatarini!hatari!hatari!)



    Sauti ya hatari ilisikika,ikapenya katika masikio ya kila gaidi,kifaa maalumu kilitoa taarifa ya hatari, katika kila chumba,pamoja na kumbi za starehe ndani ya meli, magaidi wakaanza kukimbia huku na kule, kila mmoja alitambua jambo la kufanya anaposikia kengele hii, anaacha shughuli zake, anaenda kupanga mstali katika uwanja wa mazoezi.



    “,Kuna ndege imeonekana katika rada zetu, kuna ndege kubwa inasogea eneo letu, kutokea mashariki, bila shaka nchini Gano, mahali Donald Mbeto alipotekeleza mauaji muda mfupi uliopita, meli yetu itazama baharini, futi kumi kwenda chini kama nyambizi, lakini lolote linaweza kutokea, jiandaeni! “,bilionea wa kihindi, Paresh Kumar, aliongea kwa kiswahili,alikuwa na miaka  mingi pwani hii ya waswahili,alikifahamu kiswahili vizuri sana, baada ya kutoa amri kila gaidi alikimbilia eneo lake, kutimiza majukumu yake,waliamini helikopta hiyo ilikuja ukanda wao kwa vita na wala sio kitu kingine, walikua sahihi kabisa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bahari ya hindi; 2;40pm



     Donald Mbeto alikuwa amezungukwa na wanawake sita wa kizungu,hakuna aliyekuwa na akili zake,kila mmoja alikuwa amelewa chakali, akiwa uchi wa mnyama,chupa za pombe ya ya kizungu, “queen elizabeth”,zilizagaa kila kona ya chumba hiki chenye mwonekano wa kifahari zaidi, godoro la plastiki lillilojaa hewa ndani lilikuwa kitandani, Donald Mbeto alicheza mchezo mchafu na mwanamke mmoja baada ya mwingine, wanawake ambao walitekwa kutoka nchi mbalimbali za dunia, kumbukumbu zao zikafutwa kwa kutumia kompyuta, wakatumikishwa bila kujitambua, huku wakiingiziwa madawa ya kulevya mwilini ili kudumaza akili zao, wakatumika katika kila kazi, uzinzi, kusafirisha madawa(drugs)  pamoja na kuua.



    “,Ngo! ngo! ngo hodiii! “,licha ya kengele ya hatari kupigwa kwenye chumba cha Donald Mbeto hakuweza kusikia, ikabidi atumwe mtu kumgongea, maana alitegemewa sana kwenye kazi mbalimbali, mawazo yake siku zote yalileta matokeo chanya kwenye kazi za D47.



    “,Donald! Donald! kuna hatariii …!”,gaidi mwenye cheo cha chini sana aliita, akaongea kwa sauti kubwaa! .



    “,Kwichi, kwichii, kwichiii ………”,sauti ilisikika, sauti ambayo haikua ya Donald Mbeto, bali kelele za kitanda kilichokuwa kimezidiwa nguvu, gaidi yule hakuendelea kuita tena,alirudi kwa unyonge, kumpatia jibu mtu aliyemtuma, maana hakua na njia nyingine ya kufanya.



    “,Bosi! amelewa sana, nasikia sauti za walevi ndani ya chumba, nimeita sana hakuna aliyenijali …”,gaidi D47 namba arobaini na mbili aliongea, Paresh Kumar akakasirika, ujumbe alioupokea ulikuwa kinyume na matarajio yake.



    “,Ina maana mpaka sasa bado yuko chumbani na wanawake zake? “,bilionea wa kihindi, mmiliki wa kundi la kigaidi la D47 ,Paresh Kumar ,aliuliza swali kwa mshangao.



    “,Ndio bosi! “,gaidi yule aliitikia kinyonge, kwa heshima iliyojaa uoga mwingi ndani yake.



    Paresh Kumar alinyenyuka ofisini kwake,akatembea kwa haraka,kuelekea katika chumba cha kijana wake machachali, aliyemtegemea kwa kila jambo, mzee wa miaka sitini bwana Donald Mbeto.



    “,Paaaaa! “,alipiga kitasa na bastola kikaachia, akaingia ndani, uso kwa uso na wanawake sita wakivunja amri ya sita na kizee wa miaka sitini, mwenye damu mbichi kama kijana wa miaka ishirini tu, bilionea Paresh Kumar hakushtuka,hakuona cha ajabu chochote kile.



    “,boosi, ninini tatizo, mbonaaaa umekujaa mbioo?,”Donald Mbeto akiwa uchi wa mnyama, alijitoa mikononi mwa wanawake wale wa kizungu, akasogelea mavazi yake, akaanza kuvaa nguo moja baada ya nyingine, huku akimuuliza maswali bosi wake.



    “,Kengele ya hatari imepigwa, haujasikia! nimetuma watu kukuita haujasikia!, kuna tatizo kubwa, tena kubwa kabisaa! “,Paresh Kumar aliongea, mikono yake ikizungusha bastola yake kwenye kidole chake cha kati, mkono wa kulia.



    “,Tatizo gani hilo bosi?, na nyie malaya, ondokeni hapa, mnasubili nini? “,pombe zilimuishia Donald Mbeto,akauliza swali kwa mshangao, sura yake akaikunja kwa hasira, akawafukuza wanawake aliokuwa anakula nao raha, kwani walikuwa bado wanasubili kuendelea na starehe zao.



    “,Kuna ndege ya kivita inakuja kwenye ukanda wetu baharini,bila shaka imekuja kwa ubaya. “,Paresh Kumar aliongea.



    “,Unasemaje bosi? “,Donald  Mbeto aliongea kwa mshangao.



    “,Ndiyo, twende ukaone …!”,Paresh Kumar aliongea, akaweka bastola yake kwenye koti lake,akaongozana na bosi wake, mpaka chumba cha mawasiliano na teknolojia katika kundi la D47.



    “,Banard! “,



    “,Yes bosi! “,



    “,Vipi,bado ndege hiyo inakuja eneo tulilopo…”,



    ” „Ndio bosi,kama unavyo ona,”



    “,Hawa ni watu wabaya kwetu,Donald nazani umeona ndege hiyo ?”,



    “,Ndio bosi,waambie makepteni wazamishe meli kwenda chini kama nyambizi,tusionekane kwenye uso wa bahari,wakifika kwenye anga zetu tuwashambulie kwa makombola…”,



    “,Kweli kabisa Donald,hiyo ndiyo mipango yangu,tayali meli yetu imezama kama nyambizi,nenda kashirikiane na askari wa makombola,wapatia maelekezo,ndege ikifika usawa wa bahari yetu tulipue ndege yao,”



    “,Sawa bosi!”,



    Donald Mbeto aliitikia amri ya bosi wake,akatoka chumba cha mawasiliano,akamuacha Benard akiendelea na majukumu yake,kufuatilia mitambo ya ulinzi katika meli yao yenye uwezo wa kujigeuza kama ndege au nyambizi.



    “,Unazani watatumia dakika ngapi hawa washenzi mpaka kufika hapa?”,Paresh Kumar alimuuliza Benard,mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika kundi la D47.



    “,Dakika kumi zijazo,watakua katika anga letu…”,Benard aliongea.



    “,Ok sawa,ngoja nikawapange vijana wangu,hii ndege tuishambulie,isivuke anga letu.……”,Paresh Kumar aliongea,akaondoka zake.



    …………………………………



    2;00pm



            Kamanda Philipo alichukua kompyuta yake, akabonyeza kitufe,akafanya utundu wake, alibonyeza huku na kule, akapata alichokihitaji.



    “,Tumefika, meli yao inatakiwa iwe mahali hapa, lakini mbona hatuioni ,iko wapi? “,kamanda Philipo aliongea kwa mshangao, wote wakashangaa.



    “,Ina maana tumefika! “,kamanda Catherine aliuliza kwa mshangao.



    “,Ndio Cathe, tumefika, meli inaonekana iko hapa lakini hatuioni, nikisachi mtandao uneonesha hiyo meli ya Paraquat iko hapa ……!”,kamanda Philipo alitoa maelezo.



    “,Nimekumbuka kitu, kepteni! Kepteni! ondoa ndege yetu mahali hapa, meli yao inauwezo wa kujigeuza kama nyambizi, kama wametuona bila shakaa wametutega watushambulie ……”,kamanda Kendrick aliongea.



    “,Unasemaje?? “,wote waliuliza kwa mshangao, wote wakamgeukia kamanda Kendrick, walitaka afafanue vizuri kile alichozungumza.



    “,Puuuuuuu, puuuuu …”,



    “,Tumeshambuliwa, luka baharini …!”,



    “,Puuuuuuh puuuuuh!



    “,Nakufaaa…a……”,..



    Ghafla mripuko ulisikika,kabla hata kamanda Kendrick hajamaliza kuongea,helikopta ya the super three soldiers ilipasuka vipande vipande,kelele za kilio zilisikika ,kila mmoja aliipigania roho yake.



    …………………………………



    Makao makuu ya polisi; 4;02pm



             BMW ilipaki pembeni ya barabara, gaidi D47 namba sitini alishuka, akavuka barabara,akazisogelea ofisi za kituo cha polisi.



    “,Tukusaidie nini kijana! “,askari wa zamu mapokezi aliuliza.



    “,Nataka kuonana na polisi aliyekuwa zamu jana, kuna kesi niliandikisha kwake jana? “,gaidi D47 namba sitini aliongea..



    “,Yule mshenzi, msaliti wa serikali yetu, yuko mahabusu, hawezi kushirikiana na wauaji, niambie kesi hiyo inaitwaje, niangalie faili lake kabatini …”,askari wa zamu aliongea. Hakujibiwa,tayali alipata alichohitaji, gaidi alitoka nje haraka sana, aliona ulinzi ulikuwa dhaifu, akawajulisha wenzake.



    “,Twendeni,shambulia washenzi wote, asipone hata mbwa mmoja, mwenzetu yuko mahabusu, anapaswa kuuawa, kasema siri zetu …”,D47 namba sitini aliongea kwa hasira, akachukua bunduki, akavaa mkanda wa risasi begani, wenzake wakafanya vivyo hivyo, kila mmoja alichukua bunduki yake pamoja na mkanda begani, wakavuka barabara bila kuogopa kitu chochote kile, wakatembea kikomando kusogelea kituo cha polisi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Makao makuu ya polisi:



          Shambulio la kushtukiza lilipelekea askari wengi kupoteza maisha,magaidi wanne wa D47 walikuwa moto wa kuotea mbali, walifyatua risasi kama mashine, wakaua askari wote waliowasogelea kizembe,hawakuogopa chochote kile, walijiamini na kuendelea kushambulia huku wakiingia ndani kabisa ya kituo cha polisi.



    “,Mmoja aingie mahabusu, akamilishe kazi kisha tutoweke eneo hili,sisi tuko hapa nje tunadumisha ulinzi”,sauti ilisikika, gaidi D47 namba sitini alitoa amri,magaidi wawili wakaelekea mahabusu, huku wakisafisha njia kwa kuwafyekelea mbali askari ambao walikutana nao.



    “,Paaaaa, paaaaa! “,risasi mbili zilisikika, walimfyatulia risasi askari aliyekuwa gaidi mwenzao na kutoa siri zao, wakamuua, kisha wakarudi haraka sana.



    “,Tuondoke! tuondokee! “,



    “,Tubadirishe nguo, tuvae nguo zao, tutatoroka kwa urahisi, “



    “,Vipi kuhusu gari letu? “,



    “,Haina haja, tutaliacha palepale, tuchukue moja kati ya magari yao, itakua rahisi hata kupita barabarani ……”,



    “,Sawa mkuu …”,



    Magaidi wa D47 walijadiriana, wakakubaliana, wakawavua askari watano waliowaua, wakavaa sare zao za polisi, wakatoka nje haraka sana, wakajipakia katika difenda ya polisi yenye king’ora juu, wakatoweka eneo hilo, wakiwa wameua askari takribani ishirini, askari wengine haijulikani walikuwa wapi.



    …………………………………



    Nusu saa iliyopita;



            Donald Mbeto aliwaongoza magaidi wenzake, kitengo cha makombola,wote walikuwa makini kuitazama helikopta ya jeshi, helikopta ambayo ilitokea kisiwani Gano, ikafika katika ukanda wao,ikaonekana vizuri kupitia kompyuta na sattelite zao.



    “,Ni watanzania, washambulieni haraka sana, hawa ni watu hatari sana kwetu …!”,Donald Mbeto alitoa amri,magaidi wenzake wakabonyeza vitufe vya makombola, makombola mawili yakafyatuka baharini, moja likaipiga helikopta kwenye mkia, ikapepesuka na kupoteza mwelekeo, kombola la pili likaipiga kwenye kichwa na kuisambaratisha vipande vipande.



    “,Yeeeeeee!,wamekwishaa “,



    Magaidi wote walipiga kelele za shangwe, wakiongozwa na Donald Mbeto,aliyejiita jini mweupe kutokana na mnvi nyingi zilizomtapakaa kidevuni na kichwani,siku zote alitekeleza matukio hatari sana ya mauji, na kijifananisha kama jini asiye onekana, alijiamini na kujikubali kuliko kiumbe yoyote yule.



    “,Hapa kazi imekwisha, ngoja nikale zangu kuku bwanaaa wewe, wametukatishia starehe zetu hawa maboya, wakamsalimie shetani kuzimu ……”,Donald Mbeto alitukana,akaondoka zake, uso wake ulijaa tabasamu licha ya sura yake yenye mikunjo kwa mbali,kutokana na kula chumvi nyingi sana.



    …………………………………



    Kamanda Kendrick alitoa amri,vijana wake wajitupe kwenye maji, helikopta yao ililipuliwa kwenye mkia, ikaanza kuzunguka zunguka, rubani akashindwa kuiongoza, ikalipuliwa tena, kichwa kikasambaratika, wote watatu wakaruka, isipokuwa rubani aliyepasuka na kuchanika vipande vipande, akalia kwa uchungu na kufa palepale.



    Kila mmoja alijitupa kwenye maji na kuangukia upande wake, walikua wamepoteana,hawakuangukia sehemu moja.



    “,Kendrick! Kendrick! Philipo mko wapi? “,Catherine aliita,mikono yake akiitupa nyuma na mbele kuogelea, uso wake ulijaa huzuni, macho yake yakadondosha chozi, kelele alizozisikia kipindi ndege inalipuliwa zilimchanganya, hakujua nani amekufa, hakujua kama wenzake walifanikiwa kuluka, kila mmoja alijitupa kwenye maji bila kutambua kama mwenzake aliluka na kujiokoa.



    “,Kendrick don’t die please, usife kabla sijakuambia ukweli wa moyo wangu! “,Catherine aliendelea kuogelea kama samaki, huku akiongea maneno ya huzuni moyoni mwake, alizani kamanda Kendrick pamoja na kamanda Philipo walikuwa wamepoteza maisha, kumbe sivyo.



    …………………………………



    Kisiwa cha Comoro; 4;20pm



             Mtumbwi ulisogea mpaka ufukweni, mvuvi mwenye umri wa miaka hamsini alishangazwa na binadamu aliyemuokota baharini, akiwa amepoteza fahamu, akamkandamiza tumboni,akatapika takribani lita tatu za maji, akaendelea kumkandamiza tumboni, akatapika maji, macho yake yalifumba, pumzi yake ilikua kwa mbali sana, akamnyenyua mpaka kwenye kibanda chake cha makuti, kilomita moja kutoka baharini, samaki aliziacha palepale.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Babaa! huyu ni nani?, halafu mbona ana sura ya kitanzania, au ni mwenzetu? “,binti mrembo, mweupe, mwenye macho meupe ya duara, aliongea, akimshanga mwanaume aliyevutia, akiwa amevaa mavazi ya ajabu sana, usoni akiwa na miwani, mkononi alivaa saa ya dhahabu.



    “,Nimemuokota akiwa anahangaika kuogelea, nilipofika tu mahali alipokuwa, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu, nikamchukua na mtumbwi wangu mpaka mahali hapa! kabla ya yote, kachukue samaki ,nimeziacha kwenye mtumbwi, halafu njoo nazo, tuchemshe mgeni ale atakapopata fahamu …”,mzee yule aliongea, akamlaza kamanda Kendrick kwenye magome ya miti, apigwe na upepo, chini ya mti. Akimsubili aweze kuamka, awasimulie yaliyomkuta.



    …………………………………



    Kisiwa cha Mafia;



          Boti ya Mv Mafia ikiwa na abiria hamsini, ilitia nanga katika bandari ya mjini Mafia, abiria walijaa taharuki, mabaharia nao walijaa taharuki,mavazi aliyoyavaa mtu waliyemuokota katikati ya bahari akinywa maji na kuhangaika kujiokoa yalizidi kuwachanganya,abiria walishuka kwenye meli, walikuwa wamefika mwisho wa safari, akabaki nahodha na mabaharia wakimpatia huduma ya kwanza kamanda Philipo,alitema maji mengi takribani lita tano.



    “,Watokea wapi yahee,watoka Unguja au Pemba,wewe raia wa wapi?”,kamanda Philipo aliyafumbua macho yake,uso kwa uso na watu wanne wenye sare nyeupe zilizofanana,begani zilifanana na sare za polisi.



    “,Nyie polisi wa wapi?”,kamanda Philipo aliuliza.



    “,Hahaaaa,kachanganyikiwa huyu,lakini atakua mtanzania wa bara,anaongea kiswahili…!”,walicheka sana,kamanda Philipo alishindwa kujibu alichoulizwa,wakamuona kama amepagawa,wakaendelea kumpatia huduma ya kwanza ili akili yake irudi katika hali yake ya kawaida.



    …………………………………



    “,Hapo hapo ulipo we malaya,ukijitikisa tunakumaliza……!”,kamanda Catherine aliangukia mikononi mwa magaidi takribani ishirini wa kisomali, walimzunguka na spidi boti, huku wakimtaka ajisalimishe.



    “,Nyie ni wakina nani? “,kamanda Catherine aliuliza, mikono yake ikiwa imekamatwa na magaidi kwa nguvu, wakamtupia ndani,katika boti zao.



    “,Alshabaab! huuu ni ukanda wetu wa Afrika mashariki, yoyote anayekatiza eneo hili ni mali yetu …!”,gaidi moja lenye rasta ndefu zilizosokotana liliongea, Catherine akashtuka, akaanza kuwaangaza kwa umakini, akitafuta mbinu ya kujiokoa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Mkamateni, mfungeni pingu, tuondokee naye! “,gaidi yule alitoa amri, magaidi wawili wakamsogelea kamanda Catherine, hapo ndipo walikipata cha mtema kuni, wakajuta kumsogelea, aliluka mateke mawili hewani, yakawapiga usoni magaidi wale, wakadondokea ndani ya maji, akachomoa bomu dogo,akachomoa pini akalitupa ndani ya boti,akajitupa ndani ya maji kama samaki.



    “,Puuuuuu! puuuuu! “,mlipuko ulisikika, boti moja ya magaidi ikalipuka,kiongozi wao aliunguzwa na mlipuko, akafa palepale pamoja na vijana wake wawili, magaidi wengine wakashindwa kuendelea kumtafuta Catherine, wakasogeza boti zao karibu, wakiwa hawaamini kilichotokea, bosi wao alikuwa amekufa palepale, machozi yakawatoka kwa uchungu,shambulio la sekunde moja tu kutoka kwa Catherine liliwachanganya sana na kuharibu kila kitu katika kundi lao.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog