Search This Blog

Monday 24 October 2022

SIRI ILIYOTESA MAISHA YANGU - 4

 













    Simulizi : Siri Iliyotesa Maisha Yangu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Ulikuwa ni usiku wa manane Caroline akiwa usingizini, aligutuka na kitu kilichokuwa kikichimba ardhi jirani kabisa na mahali alipolala! Alinyanyuka haraka na kukaa, alishangaa kukuta aliyekuwa akichimba chini ni Harry.

    “Vipi tena?

    “Natafuta njia ya sisi kuondoka hapa! Nimeona huu mpango unafaa!”

    “Mpango gani?”

    “Nitachimba hapa ukutani  kisha tutatoka hadi nje  na kutambaa hadi  tulipoiacha ndege na kuondoka zetu, nina uhakika hawatakuwa na uwezo wa kuitungua ndege yetu, ninajua nitakavyoendesha na hawatawahi kabla hatujaondoka!”

    “Harry watasikia wakati ikinguruma!”

    “Wewe usijali nitakuonyesha jinsi ya kufanya kazi hiyo niachie mimi!”

    Aliendelea kuchimba  akisaidiwa na Caroline   lakini hawakufanikiwa kuutoboa ukuta  siku hiyo kwa  sababu hakuwa na vitendea kazi nzuri,  Harry alitumia kipande cha mti alichokikuta ndani ya kibanda hicho wakati nyumba ilikuwa na ukuta mnene, kulipokucha aliacha lakini usiku ulipoingia aliendelea na kazi yake. Kwa siku mbili alifanya kazi hiyo wakisaidiana na Caroline, siku ya tatu walifanikiwa kuutoboa ukuta ilikuwa ni kati kati ya usiku watu wote wakiwa wamelala.

    “Sasa?”

    “Ni wakati wa kuondoka lakini wewe baki kwanza nikaangalie hali huko nje, nitarudi kukushtua!”

    “Sawa darling!”

    Caroline  kwa kupitia tundu la ukutani alimshuhudia Harry akitambaa kwa tumbo na kupotelea gizani, alikaa kimya akimsubiri Harry arudi  na alimwombea kwa Mungu afike   kwenye ndege na kurudi  salama ili wapate kuondoka,  alitaka kuondoka Vietnam hakutaka kufika mahali pale.

    Kwa saa nzima hakumwona Harry akirejea, alianza kuingiwa na wasiwasi kuwa pengine alikuwa amekamatwa. Baadaye alishtuka aliposikia ndege ikiunguruma kwa kasi ya ajabu! Kisha zilifuata kelele za watu wengi wakikimbia kuelekea uwanjani, Caroline hakuyaamini masikio yake alipoisikia ndege ikiunguruma mawinguni alishindwa kuelewa kama kweli ilikuwa ikiondoka au la!

    Kwa kupitia katika tundu lilelile alitoka nje bila hata woga  na kukimbia kuelekea uwanjani, hakwenda hata hatua kumi mbele yake akawa ameingia mikononi mwa walinzi watatu wa Kivietnam, walianza kumshambulia na kurejeshwa moja kwa moja katika kibanda cha mahabusu na kumfungia, walinzi walipoliona shimo ukutani walielewa kilichotokea lakini walishindwa kuelewa ni kwanini Harry aliamua kutoroka peke yake  akimwacha Caroline mahali pale.

    Carolne alilia hadi asubuhi, hakutaka kuamini kama kweli Harry alikuwa amemtoroka na kumwacha mikononi mwa Wavietnam! Huo ulikuwa uuaji, alijilaumu kwa kila kitu alichokifanya ni kweli alikuwa meyaharibu maisha yake  mwenyewe, aligundua  Harry hakuwa na mapenzi ya dhati, alikwenda kwake kuharibu maisha tu na si kingine, alijuta na kuendelea kulia, hakujua ni kitu gani kingempata  kutoka kwa Wavietnam kwa kosa la kutoroka kwa Harry.

    Mwanga wa jua ulipoingia ndani ya nyumba yake  asubuhi kitu cha kwanza alichokigundua ndani ya nyumba ni kipande  kichafu cha karatasi kilichokuwa juu ya udongo,  kilikuwa na maandishi juu yake, alikichukua na kukinyoosha  taratibu!  Ulikuwa ni mwandiko wa Harry, ingawa uliandikwa vibaya, ilivyoonekana  maandishi  yaliandikwa kizani.

     Caroline nasikitika kwa yote yaliyotokea najua   Wavietnam watakuua, lakini  hicho ndicho nilichokitaka na ndiyo maana nikakuleta  hapo,  nilichohitaji ni ndege na tayari nimeipata na ina wateja  wanaoisubiri nchini Kenya  na baada ya hapo nitaendelea na maisha yangu bora na ya starehe,  nyumbani Tanzania ambako nitaitimiza ndoto yangu ya kuwa Rais! Pole sana kwa mateso utakayoyapata na kwa kukuharibia maisha yako!

    Caroline hakuweza kuimalizia barua hiyo, alianguka chini na kuanza kulia machozi, mara ghafla mlango ulifunguliwa wakaingia wanaume wawili na kuanza kumburuza hadi nje ambako alibebwa juu juu hadi mahali kwenye uwazi na kuanza kufungwa kwenye mti! Alijua huo ndio mwisho wake alilia akiomba angalau muujiza utokee! Alimkumbuka Dk. Ian na wema wake.

    Je nini kitaendelea? Harry atafanikiwa kufika  na ndege yake Kenya wakati msako mkali unaendelea? Je nini kitampata Caroline huko Vietnam?

                            Fuatilia wiki ijayo













    “Paaa!Tchaaa!Tchaaa!”

    “Mungu wangu weee!”

    Ilikuwa ni mijeledi iliyotua katika mwili wa Caroline, akipigwa na wanajeshi wa Kievetnam ili aseme mahali alikokimbilia Harry! Caroline alilia akiwaeleza wazi hakuwa na jibu la swali hilo, lakini hakuna aliyeelewa, alizidi kuchapwa na Wavietnam  bila huruma! Yalikuwa mateso makubwa mno kwake, damu zilimtoka karibu mwili mzima, alilia akimlaumu Harry kwa uamuzi wake wa kumteka na kumtelekeza porini mikononi mwa wauaji! Kwa hakika alikuwa amemharibia maisha yake yote, moyoni alijuta kumwacha Dk. Ian kwa ajili ya mtu ambaye hakumpenda hata kidogo, aliulaumu moyo wake na hakuwa tayari kumsamehe Harry tena milele.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kama hawataniua hapa ni lazima nimuue Harry siku moja, amerejea tena katika  orodha ya watu niliotaka kuwaua! Nilishamfuta lakini sasa amerudi! Kitendo alichonifanyia sitakisahau maishani mwangu! Labda nife lakini nikipona…..atakuja kujuta ni kwanini amenifanyia hivi!” Alisema Caroline huku akilia, Wavietnam wale hawakuelewa alichokisema walizidi kumshushia mvua ya mijeledi wakitaka asema ukweli ambao hakuujua hata kidogo!

    Mpaka saa moja jioni aliendelea kufungwa kwenye mti huo akichapwa! Karibu masaa yote alichapwa ni muda mfupi sana aliopumzishwa, kwa hakika alijua kifo chake kilikuwa kimefika! Aliikumbuka Tanzania na aliwakumbuka sana wazazi wake, alisikitika kufia katika nchi ambayo hata maiti yake  wasingeiona, aliamini  wangeendelea kujua alikuwa hai sehemu fulani wakati tayari alishakufa muda mrefu, mawazo hayo yalifanya machozi yazidi kumtoka zaidi.

    Baadaye alichoka na kulegea kiasi cha shingo yake kuangukia pembeni, walipoona hivyo Wavietnam  walijua angekufa na kwa amri ya mkuu wa kambi walimfungua na kwenda kumtupa tena katika kibanda ambacho yeye na Harry waliwekwa rumande mwanzo! Alilala sakafuni huku damu zikiendelea kumtoka, hakuwa na mtu mwingine wa kumlaumu zaidi ya Harry kwa mateso yote aliyoyapata, alitamani hata kukutana na Dk Ian tena na kumwomba msamaha ingawa alijua alikuwa mtu hatari!

    “Labda anaweza kunipa msamaha, kama nikimlilia  na kumwangukia miguuni na kumwambia rubani aliyenipa aliniteka na kunileta porini! Kwa hali niliyonayo nafikiri anaweza kuamini!”

    Aliwaza Caroline lakini hakuwa na uhakika  kama alichokiwaza kingeweza kumsaidia,  aliona bora  kukutana na Dk. Ian kuliko kuendelea kuwa mikononi mwa Wavietnam waliomtesa  kiasi hicho kwa sababu ya kitu ambacho hakukielewa kabisa! Kwa hakika hakuelewa mahali alikokuwa Harry lakini alilazimishwa aseme.

    Aliachwa alale chini bila kujigeuza  akiwa katika maumivu makali hadi asubuhi alipozinduliwa usingizini na mzee wa Kivietnam, alimkumbuka mzee huyo, ndiye aliyewatibu yeye na Harry walipopatwa na matatizo mara ya kwanza. Alimnyanyua na kumkalisha kitako, kisha  akachukua ndoo  ya maji iliyokuwa  karibu yake, akamwaga   dawa nyeusi  ndani yake kisha akaanza kumwogesha nayo mwilini! Alipomaliza alimlaza juu ya majani ya mgomba yaliyotandikwa chini!

    Hakusema naye kitu chochote sababu walikuwa hawaelewani lugha!  Baada ya kumaliza mzee huyo aliondoka lakini alirudi tena mchana na jioni kufanya kitu hichohicho na kiliendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu, Caroline alishangaa kuona akirejea katika hali yake ya zamani! Vidonda vyake vilianza kupona na mwili wake kupata nguvu, matumaini ya kupona yalirejea, katika muda wiki nzima alikuwa amepona kabisa ingawa mwili wake bado ulikuwa na makovu mengi makubwa! Hata siku moja hakuruhusiwa kutoka nje ya kibanda! Alikuwa ni kama Simba ndani ya kijumba chake, alipewa chakula mara moja tu kwa siku na watu wawili walimlinda mchana na  wengine wawili walimlinda usiku! Alikuwa katika mateso makali,  alimtupia lawama Harry, hakutegemea angetenda kitendo cha kinyama kiasi hicho!

                       **********

    Ilikuwa ni usiku wa manane akiwa amelala usingizi ndani ya kibanda chake, ilikuwa ni siku ya tano tangu apate nafuu, aliamshwa usingizini na kelele za vyuma vya mlango wa kuingilia katika kibanda hicho vilivyokuwa  vikifunguliwa, alishtuka kwa sababu hata siku moja hakuwahi kuamshwa usiku kiasi hicho! Hali ilikuwa kimya kupita kiasi, hata ndege hawakulia, hiyo iliashiria ulikuwa ni usiku wa saa nane ama saa tisa hivi! Alitetemeka mwili mzima.

    Aliingia  askari akiwa  na tochi mkononi na kumulika mahali alipolala  Caroline, akamshika mkono na kuanza kumburuza kwenda nje bila kusema neno lolote, huko nje aliungana na mwenzake wote wawili walimbeba juu juu kwenda naye upande wa pili wa kambi! Alijaribu kupiga kelele lakini alizibwa na mkono kwa kiganja cha mkono wa mmoja wa walinzi hao wa Kivietnam kuifanya sauti yake isifike mbali.

    Alitupwa chini katikati ya vichaka viwili na  askari mmoja alimshika mikono na mwingine kwa kutumia miguu yake akamgandamiza miguu! Caroline alijua kilichotaka kutokea!  Ni kitu ambacho alikiogopa sana maishani mwake,  aliamini walitaka kumbaka! Ghafla askari aliyemgandamiza mguu kwa kutumia mkono wake wa kushoto aliivua nguo yake ya ndani na kuichana  kisha akalishika gauni lake na kulifunua akiliacha limfunike usoni na kuziacha sehemu zake za siri wazi.

    “Mungu wangu! Eh Mungu wangu nisaidie! Wananiua!” Caroline hakuwa na mtu  mwingine wa kumlilia, isipokuwa Mungu peke yake kwa maumivu  makali yaliyompata akifanyiwa kitendo hicho cha kikatili, yalikuwa ni maumivu yasiyoelezeka! Alilia lakini walinzi hao hawakusikiliza, alipomaliza mmoja alimwachia mwenzke wakiwa wamebadilishana, ilifanyika shughuli ya masaa mawili  ndipo wakamrejesha  tena katika kibanda chake saa 11 alfajiri, akilia machozi, alikuwa amebakwa! Kilikuwa kilio kingine kwake na alitamani kufa kuliko kuishi.

    Vitendo hivyo havikukomea siku moja, viliendelea  kumtokea Caroline karibu kila baada ya siku moja,  akawa mtumwa wa mapenzi!  Ilikuwa ndiyo njia pekee ya maaskari wa Vietnam kujifurahisha,  hawakuwa na wasichana katika kambi yao, mimba yake ilizidi kukua lakini hawakujali, kila siku walimtendea unyama huo! Kwa miezi karibu mitano aliendelea kufanyiwa hivyo.

    Baadaye aligundua kuwa sehemu zake za siri zilikuwa vikivuja majimaji machafu yenye harufu mbaya, aligundua tayari alishapata gonjwa la zinaa! Hakujua hata alilipata kwa nani maana wanaume wengi  waliomwngilia kwa nguvu walikuwa wengi! Hakuna mwanaume hata mmoja aliyejali kuugua kwake kila siku waliendelea kumfanyia, alikuwa ni kama mateka asiye na kimbilio. 

                          ***************

    ”Wewe  malaya kwanini umeniambukiza ugonjwa wa zinaa?” Askari mmoja alimuuliza kwa lugha yao.

    “Mimi?”

    “Ndiyo, kwani nani?”

    “Sio mimi  afane ni nyie mlioniambukiza ugonjwa huu na hatimaye umesambaa kwenu wote, mimi sikuja hapa na ugonjwa  wowote! Vitendo vyenu  vya kikatili ndivyo vimenipa matatizo haya, tafadhali nitafutieni  tiba!” Alisema Caroline katika sauti ya kukata tamaa!

    “Unajibu jeuri siyo?”

    “Hapana siyo hivyo afande!”

    “ Leo nitakufundisha adabu!”

    Kilichofuata baada ya hapo kilikuwa ni kipigo tu si kutoka kwa askari huyo peke yake bali  aliendelea kupata vipigo kutoka kwa kila askari aliyembaka kwa madai  kuwa aliwaambukiza ugonjwa wa zinaa! Kitu ambacho Caroline alikuwa na uhakika kabisa hakukifanya, alijitahidi kujieleza kwao lakini hawakujali walichofanya ni kumpiga kila siku. Ni askari mmoja tu ambaye hakudiriki kumpiga,  Caroline alishangaa ni  kwanini! Mara nyingi askari huyo alikuwepo kujaribu kuwazuia wenzake wasifanye hivyo.

    “Caroline!” Mlinzi wa usiku alimwita  katikati ya usiku, alikuwa ni mlinzi  mpole ambaye hakumpiga kati ya wote waliombaka.

    “Naam afande!” Alijibu  Caroline kwa Kivietnam kutoka kwenye kibanda chake.

    “Kwanza pole sana kwa yanayokupata!”

    “Ahsante, nashukuru wewe hujanipiga!”

    “Unajua kwanini sijakungusa?”

    “Hapana!”

    “Ni mimi niliyekuambukiza  ugonjwa Caroline,  kwa sababu hiyo nimepanga mpango  kamambe wa kukutorosha, nimeongea na  askari mwenzangu   wa kambi yetu ya Kahtar! Atakuwa anatusubiri porini usiku wa leo, nitakukabidhi kwake nae atakupeleka kwa mwingine katika kambi ya Zentilio huyo atakusogeza mbele zaidi ambako utakabidhiwa kwa mwingine atakayekufikisha hadi barabarani, huko utapanda basi litakalokufikisha Phnom ambako utatafuta njia yoyote ya kuishi, ukibaki hapa nina hakika utakufa!

    “Nitaweza kweli kusafiri umbali wote huo na hii hali yangu ya ujauzito?  Kwani jumla  zitakuwa ni kama kilometa ngapi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kilometa  105!”

    “Sidhani kama nitaweza jina lako ni nani kweli?”

    “Hung!”

    “Hung hakuna utaratibu mwingine wa kusafiri?”

    “Sina na ninaomba utoke haraka ili tuondoke ni bahati leo nalinda peke yangu, nimekuonea huruma sana Caroline, nipo tayari kufa  ili nikuokoe”

    “Kweli?”

    “Ndio naomba utoke tuondoke!”

    Tumbo la Caroline lilikuwa kubwa mno, alikuwa mzito kufanya karibu kila kitu, alijikongoja taratibu  na kusimama wima kisha akatoka hadi nje, kila upande  wa kambi ulitawaliwa na giza nene! Hung hakutaka kutumia tochi kwa kuogopa kuonekana, alimwambia wainame na kunyata  taratibu hadi nje ya ngome kwa kupitia chooni! Hakuna mtu aliyemwona!

    “Caroline itabidi ujitahidi sana kutembea sababu ni lazima nihakikishe asubuhi nimerudi hapa!”

    “Nitajitahidi ingawa mimba inanipa uzito!” Aliitikia Caroline ingawa alijua wazi asingeweza, alikuwa tayari kufia mahali popote mbele ya safari lakini si kusubiri kifo chake katika kijumba cha mahabusu!

    Walitembea kwa karibu masaa manne wakipita katikati ya  pori na milima, wakipishana na wanyama wakali, mahali aliposhindwa kupita Caroline hasa katika mito, Hung alimbeba mgongoni na kumvusha, Caroline alichoka lakini alijitahidi kadri ya uwezo wake hakuwa na namna nyingine yoyote ya kujiokoa, saa nzima baadaye akiwa hoi walifika eneo la wazi katikati ya pori na kukaa chini, hata Hung alionekana kuwa amechoka hoi bin taaban.

    Muda mfupi  tu baadaye alitokea mtu aliyevaa nguo nyeusi mwili mzima na kwenda hadi mahali walipokaa Caroline na Hung na kuwasalimia katika lugha ya Kivietnam wote wakaitikia, Caroline alikuwa tayari kalala chini, maumivu ya mgongo na tumbo yalimsumbua kupita kiasi!

    “Xun, huyu ni Caroline ndiye niliyekueleza habari zake katika simu ya upepo naomba umsaidie kufika Zentilio, tafadhali fanya hivyo kwa heshima iliyopo kati yangu mimi na wewe na Mungu atakusaidia!”

    “Sawa nitafanya hivyo bosi!” Alijibu Xun kijana mrefu mwembamba huku akimnyanyua Caroline aliyekuwa akilalamika maumivu ya tumbo ili asimame wima waondoke!

    “Siwezi! Siwezi!” Alilalamika Caroline.

    “Hapana Caroline ni lazima ujitahidi tu,   ni lazima  Xun ufanye jambo hili usiku  na asubuhi awepo hapa!” Hung alisema.

    “Sawa Hung! Nashukuru kwa msaada wako lakini sijui kama nitafika nina wasiwasi nitafia njiani! Tumbo linaniuma mno!”

    “Hapana utafika!” Alijibu Hung na kuingiza mkono  wake mfukoni akatoa noti moja ya dola mia na kumkabidhi.

    “Ahsante!”

    “Hiyo itakusaidia  huko unakokwenda,  nimeitunza kwa muda mrefu, najua mjini utaibadilisha na kuitumia kutibiwa hospitali! sawa?”

    “Sawa!Mungu akubariki!”

    Caroline akawa ameingia mikononi mwa mwanajeshi mwingine, aliyekuwa na nguvu mpya! Yeye  akiwa na nguvu ileile  na zaidi ya hayo aliumwa tumbo kupita kiasi! Alimshuhudia Hung akiondoka, pamoja na kuwa alimbaka na kumsababishia ugonjwa alimshukuru kwa kuokoa maisha yake, machozi yalimtoka kutengana na mtu ambaye kwa hakika asingemwona tena maishani, hakuwa na uhakika wa kufika safari waliyokuwa wakienda.

                              ***************

    Walitembea  umbali wa kama kilometa saba porini, tumbo liliongezeka maumivu mara mbili zaidi, lilimnyonga sana sehemu za chini ya kitovu chake na liliuma na kuachia! Lilipoachia alitembea lakini lilipoanza aliinama kwa maumivu yaliyompata, nguvu zilianza kumwishia miguuni na  kumfanya ashindwe kutembea akiwa amenyooka.

    “Kaza mwendo!” Alisema Xun akiwa ameshika mkono,    alionekana kumvuta zaidi kuliko kumwongoza.

    “Siwezi kuendelea!” Alisema Caroline akiwa amefumba macho sababu ya maumivu.

    “Jikaze tu!”

    “Kwa kweli siwezi! Kusonga zaidi ya hapa!”

    Baada ya kusema maneno hayo tu, Caroline alianguka chini akiwa ameshika tumbo lake, alikuwa katika maumivu makali kupita kiasi,  Xun alijaribu kumbembeleza ili anyanyuke waendelee safari yao lakini haikuwezekana! Caroline aligoma kabisa.

    “Nikichelewa kurudi  nitapoteza maisha yangu,  tafadhali nyanyuka tuondoke!” Xun aliendelea kumbembeleza Caroline lakini bado aligoma.

    “Siwezi kuendelea nakushukuru sana kwa kunifikisha hapa! Wewe unaweza kurudi Mungu atanisaidia kwa njia anayofahamu mwenyewe, ahsante kwa msaada wako, rudi kambini usije kupatwa na matatizo!”

    Xun alikaa pale kwa karibu saa nzima na kushindwa kuvumilia  zaidi, ingawa alimuonea huruma sana Caroline alilazimika kuondoka  na kumwacha eneo hilo kurudi kambini! Muda mfupi tu baada ya  Xun kuondoka mfuko wa mtoto ulipasuka na maji  mengi pamoja na damu yakamwagika! Kichwa cha mtoto kilikuwa mlangoni! Caroline alikuwa akijifungua peke yake porini! Tena kabla ya wakati,   safari ndefu aliyotembea ilimsababishia uchungu.

    **************

    Mkuu wa  Mafia  katika  Cambodia, Meja Jenerali Chang Lou, alipata taarifa za ndege iliyotua porini na kulazimika  yeye na  wanajeshi kama ishirini kwenda kwenye kambi ya Wavietnam porini,  walipoongea  na mkuu wa kambi  hiyo  alikiri kuwa kweli ndege hiyo ilitua hapo lakini  baadaye Rubani alitoroka nayo  akimwacha mke wake. Mkuu wa  majeshi aliomba kuonana na Caroline,  walipomwaangalia katika kibanda chake asubuhi hiyo hawakumkuta! Askari aliyekuwa  zamu usiku  wa siku hiyo, Hung alikamatwa na kuwekwa rumande kwa kumtorosha Caroline!

    Palepale bila kupoteza muda mbwa wa  jeshi   hodari wa kunusa  harufu waliachiwa na kuingizwa ndani ya banda alilofungiwa  Caroline  kabla ya kutoroka ili   kunusa harufu yake na  baada ya hapo walianza kukimbia porini wakiifuata njia aliyopitishwa Caroline, pua zao zikiwa chini wakiifuata harufu! Maaskari walikimbia mbio nyuma yao wakiwafuata, kilometa 98 mbele mbwa walisimama kwenye uwanja wa wazi  mahali ambapo Caroline na Hung walipumzika kabla hajakabidhiwa kwa Xun!  Mahali hapo walilia kwa  sauti ya juu kisha wakazidi kusonga mbele, kulikuwa kama kilometa tano tu mbele wafike eneo alilokuwa amelala Caroline huku kichwa cha mtoto wake kikichungulia.

    Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/











    Akiwa peke yake porini na kwa nguvu zake zote Caroline alijitahidi, kusukuma hadi mtoto akatoka na kuanguka kwenye mchanga! Hakuwa na nguvu kabisa mwilini mwake, alilala chali akihema kwa nguvu, alionekana kama kupoteza kumbukumbu ya kitu kilichokuwa kimetokea, baada aliposikia sauti ya kitoto kikilia alikumbuka kilichotokea, hakuwa na maumivu tena.

    Alinyanyuka na kukaa mikono yake yote miwili ikiwa nyuma yake ikisaidia asirudi tena ardhini! Alimwangalia mtoto wake kwa macho ya huruma, alikuwa mtoto mdogo mno, akilinganishwa na watoto wachanga, aliowahi kuwaona kwa makadirio yake mtoto huyo hakuwa hata na kilo mbili! Aliamii yote hayo ilitokea sababu ya mtoto hhuyo kuzaliwa kabla ya wakati wake! Alikuwa mtoto wa kiume, roho ilimuuma sana sababu kwa hali aliyokuwa nayo mtoto wake alijua asingeishi, alihitaji msaada mkubwa sana wa hospitali huduma ambayo kwa mahali alipokuwa asingeweza kuipata!

    “Mtoto wa Harry huyu! Kaniachia mtoto kanikimbia, siji nitafika nae vipi nyumbani na hapa nilipo ni porini!Ah lakini Mungu anajua, asingeweza kunipa mtoto bila kunipa njia ya kujiokoa  nae na kwa sababu ya mtoto huyu nina uhakika wa kuokoka sasa!” Aliwaza Caroline.

    Alimnyanyua mtoto kutoka ardhini na kumbeba miononi mwake, alijisikia ……….na kumwekea mtoto ziwa mdomoni, alifurahi kuona mtoto akinyonya! Mpaka wakati huo kitovu kilikuwa bado hakijakatwa na hakuelewa kingekatika vipi, yeye na mtoto wake bado waliunganishwa na kitu kama utumbo uliotokea ndani mwake!

    Muda mfupi baadaye alijisikia kuumwa na tumbo tena ghafla alijisikia kitu kama uchungu kikimrudia kilimuuma tumbo lake.

    ‘Isije kuwa nina watoto wawili!” Aliwaza Caroline uchungu ulizidi kuongezeka zaidi na zaidi, alikaa vizuri akijianda kuona kitu kilichotokea, lakini badala ya mtoto kutoka kilitoka kipande cha nyama na kuanguka chini, kikifuatiwa na damu nyingi, baada tu ya kipande hicho kutoka tumbo lilitulia tuli.

    “Nafikiri hili ndilo huitwa placenta au kondo la nyuma!”Aliwaza Caroline huku akiangalia bonge hilo la nyama.

    Lilikuwa bado limeungana na mtoto wake na hakujua ni kwa jinsi gani angelitenganisha na mtoto wake, sababu hakuwa na utalaamu wowote ule wa kuifanay kazi hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kujifungua, katika maisha yake hakuwahi kumwona mtu akizaa

    “Sijui nitalikata vipi?” Aliwaza

    Alisimama wima akiwa na mtoto wake mikononi! Kondo la nyuma likining’inia, sababu ya uzito wake aliona kama lilikuwa likimuumiza mtoto wake, alilinyanyua nalo akalibeba mkononi mwake, aliangaza macho yake huku na kule na kuona alikuwa katikati ya pori, hakujua wapi kulikuwa mashariki, magharibi, kaskazini wala kusini! Kila upande ulifanana na mwingine! Lilikuwa ni pori lenye vichaka na miti mirefu hakuamini kama kulikosa wanyama wakali.

    Hapakuwa na dalili yoyote ya maisha ya binadamu katika pori hilo, ni milio ya ndege tu iliyosikika kila upande! Caroline alishindwa aelekee wapi kutoka hapo, ulikuwa ni wajibu wake kujiokoa.

    “Ni lazima nisongee mbele! Siwezi kukisubiri  kifo changu na mwanangu hapa!”Aliwaza Caroline na palepale aliamua kukatisha mkono wake wa kuume na kuanza kuchonga kuelekea porini zaidi, mtoto wake alizidikulia na aliendelea kumbembeleza huku akitembea katikati ya vichaka vyenye miiba mingi, alipozitupa fikra zake hadi nyumbani Tanzania aliwaona wazazi wake kimawazo, aliwaonea huruma sana pale ambapo wangepata taarifa za kifo chake! Alimwona mama yake akilia machozi huku akiliita jina lake.

    “Mungu nisaidie ili siku moja niweze kufika nyumbani Tanzania na kuonana na wazazi wangu!” Aliwaza Caroline.

    Kwa siku nzima alitembea porini akila matunda aliyoyaona katika miti! Hakukutana na mtu wala kuona njia za waenda kwa mguu! Hali iliyoonyesha hapakuwepo watu katika pori hilo, tayari alishaanza kukutana na wanyama kama Tembo, Twiga na Sokwe, kila alipowaona alijificha katika nyasi mpaka walipopita ndipo aliendelea! Alihofia Simba an Chui, ambao kwa hakika kama angekutana nao yeye na mtoto wake wangekuwa chakula chao! Alimwomba Mungu amuepushe na balaa hilo.

    Jua lilikuwa kali mno na liliwachoma ipasavyo yeye na mtoto wake, hakuwa na nguo yoyote ya kumfunika mtoto jambo lililomlazimisha avue gauni lake na kumvalisha, yeye akabaki hivyo hivyo na kuendelea kutembea, hakuona aibu sababu hapakuwa na mtu yoyote wa kumwona porini.

    Sababu ya kuunguzwa na jua mtoto alizidi kulia, Caroline alishindwa afanye kitu gani na alipomwekea titi mtoto hakunyonya tena, majira ya saa 9 akiwa tayari amekwishatembea kilomita 45 katikati ya pori mtoto wake alinyamaza kulia, akiamini alikuwa amepitiwa usingiz, kunyamaza huko kulimfanya aondokewe na wasiwasi wa kuliwa na wanyama! Akaongeza bidii ya kutembea zaidi kwenda mahali kusikojulikana akiamini ni lazima angefika mahali Fulani walipoishi watu, hata kama ingechukua wiki tatu za kutembea.

    Mpaka saa 12 jioni bado mtoto wake alikuwa hajalia! Wala kujitingisha, Caroline alishtuka na kumwangalia mtoto wake, aliangua kilio alipokuta tayari mtoto wake amekwishakauka mikononi mwake! Alikuwa amekufa! Alikaa chini na kuanza kulia kwa uchungu, hakuamini mpaka alipoweka sikio lake kifuani kwa mtoto kutousikia moyo ukipiga ndipo akaamini kweli mtoto wake hakuwepo tena duniani!

    Hakuwa na la kufanya zaidi ya kuuzika mwili wa mtoto wake, bila kuchelewa ingawa mwili wake haukuwa na nguvu nyingi alivunja tawi la mti na kulitumia kuchimba ardhini! Ingawa alikuwa peke yake aliamua kuuzika mwili wa mtoto wake ambaye alikuwa bado hajampata hata jina kwa heshima zote za kibinadamu.

    Sababu ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha udongo ulikuwa laini na kwa kutumia mti tu alifanikiwa kuchimba shimo dogo lenye urefu wa Cm………………kwenda chini na kuweka mwili wa mtoto wake ndani kabla ya kufukia alipiga magoti …………….machozi yalikuwa yakimtoka, wakati wote wa zoezi hilo! Alikuwa na uchungu mkubwa mno kumpoteza mtoto wake ambaye pamoja na ukatili ambao Harry alimfanyia alimwachia kama ukumbusho!?Baada ya kusali Caroline alinyanyuka na kusimama wima kabisa, akiliangalia kaburi dogo la mtoto wake, roho ilizidi kumuuma na alijua mtoto wake alikuwa ametangulia na yeye angemfuata baada ya muda si mrefu! Alijua na yeye angekufa katika masaa machache tu yaliyomfuata! Hakuwa na uhakika wa kutoka katika pori hilo akiwa salama na hata kama angetoka bado aliamini asingeweza kuukimbia mkono wa Dk. Ian ni lazima siku moja angeuawa kikatili! Bado alimlaumu Harry kwa yote hayo zaidi ya yote yeye mwenyewe kwa kuukubalia moyo wake kwa kila alichomweleza!?”Safari inaendelea, ni lazima nisonge mbele, mtoto nimepoteza lakini jukumu langu la kujiokoa bado lipo palepale!”Aliwaza Caroline na kuanza kutembea taratibu, kwa hatua tatu mbele alisimama, akageuka na kuliangalia tena kaburi la mwanae! Machozi yakamtoka.

    Alizidi kusonga mbele kwa masaa kama mawili giza likaanza kuingia, hakuwa na mahali pakulala zaidi ya kupanda katika mti mkubwa wa mkuyu uliokuwa jirani yake, kabla hajapanda aliwaza nyoka! Alikumbuka picha katika kitabu kimoja alichosoma akiwa mtoto ilimwonyesha mtu akipanda mti juu ya mti huo kulikuwa na nyoka mkubwa na chini ya mti alikuwepo Simba! Mtu huyo alitakiwa kuchagua ni wapi aende!

    “Na mimi yasije kunipata hayo hayo!” Aliwaza Caroline lakini hakusita alikuwa kama mtu aliyekwishakata tamaa ya maisha, aliuparamia mti huo na kupanda hadi juu yake bila kupata tatizo lolote!?”Nitalala hapa hadi asubuhi, kisha safari inaendelea!” Aliendelea na mawazo kichwani mwake huku akijigeuza ili asianguke, mwili wake wote ulikuwa umechoka, alilivua tena gauni lake na kujifunga kwenye mti ili asidondoke akisinzia.

                 ************

    “Wu! Wu! Wu!”

    “Uwiiiiiii! Uwiiiiii! Uwiiiii!” Mbwa walilia wakinusa chini, maaskari walipoangalia vizuri ardhini waliona damu ikiwa imemwagika katika majani, walishindwa kuelewa ni kitu gani kilitokea eneo hilo !Wote waliangaliana bila kuelewa cha kufanya!

    “Sasa hii damu ni ya nini?”

    “Labda amejifungua maana niliambiwa alikuwa na mimba kubwa!”

    “Kweli eh?”

    “Inawezekana kabisa!”

    “Basi kama amejifungua hayupo mbali na mahali hapa msako uendelee!”Maaskari waliendelea na maongezi yo, ilikujua mwelekeo wa mahali alipokwenda Caroline baada  ya kutoka hapo waliwategemea mbwa wao ambao bado waliendelea kunusa ardhini wakilia, kuashiria walikuwa wamekosa kitu walichokuwa wakikitafuta.

    Kutoka hapo mbwa walikata kushoto na kuzidi kuelekea porini, askari wakiwafuata nyuma huku wakikimbia mbio, kila mmoja wao alionekana kuwa amechoka, hilo liliwatia hasira zaidi maaskari hao.

    “Na tukimkatama sijui kitatokea nini, katusumbua sana huyu mwanamke!”

    “Sasa hivi tutamkamata, inavyoonekana hayupo mbali na mahali hapa!” Walizidi kuongea wakiwafuata mbwa wao nyuma, walishangaa kuona masaa yakizidi kusonga mbele bila kumpata, walikwenda kama kilometa……….ndipo mbwa wao waliposimama tena na kuanza kulia, huku wakifukua ardhini! Maaskari wote walishangaa kuona mbwa wakitoa maiti ya mtoto katika udongo!

    “Aisee kweli kajifungua mtoto kafariki na akazika hapa tena ni masaa machache tu yaliyopita si mnauona udongo ulivyo?”

    “Ndiyo!”

    “Achaneni na hicho kiumbe tuwasikilize mbwa nina imani hayupo mbali na maeneo haya!”

    Wote waliendelea kuwafuata mbwa wao nyuma, waliokimbia bila kuchoka, ardhi ya sehemu hiyo ilikuwa ya udongo wa mfinyanzi kila mahali walipokanyanga palionyesha alama za miguu na walipochunguza mbele yao pia waliona alama za miguu ardhini, kila mtu akawa na uhakika ilikuwa ni miguu ya Caroline.

    “basi kazi imekwisha kwa alama hizi tutampata sasa hivi!”

    “Tena kakanyaga humu si muda mrefu!”

    Waliendelea kuwafuata mbwa na alama za miguu hadi giza likaingia ikabidi wawe wakitumia tochi, walizifuata nyayo hizo hadi zikapotelea chini ya mti mkubwa wa mkuyu! Waliangalia huku na kule kuona kama ziliendelea lakini hawakuona mahali popote hata mbwa wao walishindwa kuendelea zaidi.

    “Nafikiri kapanda humu mtini!”

    “Inawezekana!” Walijibishana wao kwa wao na kisha kuanza kumulika kwa tochi zao mtini wakiangalia.

    “Yupo humu humu tu!”

                   ***********

    Muda mfupi tu baada ya kupanda mtini kwa ajili ya kulala macho ya Caroline yaliona moto ukiwa jirani tu na maeneo hayo, alichojifunza katika historia ni kuwa mahali popote palipowaka moto kulikuwa na binadamu! Moto huo ulitokea kama kilometa tano tu kutoka eneo hilo, ingawa aliogopa sana kuingia tena mikononi mwa Wavietnam alijikuta akipatwa na ushujaa ambao hata yeye hakuutegemea na kushuka haraka mtini na kuanza kutembea akiufuta moto huo! Alipita katika vichake taratibu sababu ya kiza, badala ya mita mia tano kama alizotegemea alijikuta akitembea kama kilometa mbili ndio akaufikia moto huo.

    Uliwaka chini ya miti mine mikubwa ambayo juu yake kulijengwa kibanda! Alionekana kuishi mtu maeneo hayo na aliishi peke yake, Caroline bila kuogopa alianza kupiga kelele kwa kiingereza akimwita mwenye nyumba hiyo lakini bado hali ilikuwa kimya kabisa, muda mfupi baadaye alishangaa kuona kitu kikilipuka alishindwa kuelewa kama kitu hicho kilikuwa binadamu au la!

    Badala ya Caroline kukimbia alibaki amesimama eneo hilo, bila kujua cha kufanya, mwili wake wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu, badala ya kitu hicho  kukimbia hali ikawa kimya kabisa, dakika kama ishirini hivi baadaye alisikia nyasi zikitingishika nyuma yake, alijua ni mnyama mkali lakini hakuwa hivyo alikuwa ni binadamu akitembea kuelekea mahali aliposimama Caroline.

    “Wewe nani?” Aliuliza kwa lugha ya Kiingereza mzee huyo mwenye ndevu nyingi nyeupe na mgongo wake ulikuwa umepinda, kabisa na alikuwa amenyoosha upinde wake tayari kuachia mshale!

    “Tafadhali usiniue sina matatizo yoyote, nahitaji msaada!”

    “Nimekuuliza wewe ni nani? Na unatafuta kitu gani hapa?”

    “Tafadhali naomab ushushe mshale wako chini ili nikueleze!”

    “Sema kwanza wewe ni Interpol?”

    “Hapana mimi siyo polisi ninaitwa Caroline, ninakimbia kuokoa maisha yangu, wanataka kuniua!” Alisema Caroline na alipomaliza tu sentensi hiyo mzee …………..upinde na kushusha mshale chini, akamsogelea karibu na wote wawili wakakaa chini, Caroline alimsimulia kila kitu kilichotokea katika maisha yake, tangu kifafa hadi Dk.Ian na alivyokutana tena na Harry!

    “Mjukuu wangu kwanini ulimwamini tena?”

    “Ni shetani tu aliniingia babu!”

    “Ninamfahamu vizuri Dk. Ian baba yaek Smith niliwahi kufanya naye biashara!”

    “Ulifikaje hapa porini babu?”

    “Ni habari ndefu sana ila niliua watu wengi sana nikiwa na gaidi la Kimataifa Carlos na hivi sasa dunia inanitafuta hakuna mtu yeyote anayejua niko hapa, ninaishi hapa peke yangu kwa miaka ishirini na sita!”

    “Sawa babu utanisaidiaje mimi kufika nyumbani?”

    “Kwanza kabisa naomba nikueleze wazi kuwa hivi sasa ni lazima ……………….! Ninawafahamu mafia sababu nimefanya nao kazi, ninajua wapo njiani wanakuja na watafika hadi hapa! Kifupi hutakiwi kabisa kukaa hapa!”

    “Sasa nitafanya kitu gani?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Subiri hapohapo nije!”Alisema mzee huyo na kuondoak aliporudi baada ya kama dakika tano hivi alimchukua Caroline na kumzungusha nyuma ya nyumba yake kulikokuwa na mti mkubwa sana, upana wa mti huo usingeweza kupungua mita……………….ulionekana kuwa miongoni mwa miti mingi ya zamani, alishangaa kumwona mzee huyo akibandua sehemu Fulani katika mti ndani yake ikaoneana sehemu kubwa iliyowazi.

    “Mjukuu wangu ingia hapa, utajificha nitakuhudumia kila kitu ukiwa humo, mpaka nitakapoona hali ni nzuri kukusaidia!”

    “Sawa babu!”Aliitikia Caroline na gome la mti lilirudishwa mahali pake, ndani kikawa kiza.

    Dakika tatu tu baada ya kumfungia Caroline ndani ya mti nyumba ya mzee…………….ilivamiwa na kundi la mbwa, walimwangusha chini na kuanza kumng’ata! Sekunde chache baadaye wakaingia askari wenye bunduki na kuwaamuru mbwa wamwachie mzee huyo.

    “Tueleze yule msichana yupo wapi?”

    “Ngojeni kwanza, msinipige subirini kwanza!” Alijibu mzee huyo.

    Caroline aliyasikia maneno hayo kutoka ndani ya mti na kujua ni lazima mzee……………….angewaonyesha mahali alipokuwa! Alijua mwisho wake umefika, alilia kwa chungu, hakuwa tayari kurudi tena kwa Wavietnam kupitia katika ufa wa mti alishuhudia mzee……………akipigwa kupita kiasi tena bila huruma, mbwa wao waliendelea kumng’ata bila huruma!?”Yaani kweli huyu mzee hatasema?”Alijiuliza Caroline bila kupata jibu alipofikiria kutoka ili akimbie alishindwa sababu mbwa wangemwona na kumkamata!

    Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo













    Wazazi mikononi mwa kifo

    B

    aadae taarifa za kutoroka ?kwa mke wa Dk. Ian, ?Caroline kadiri  tena pamoja na ndege aliyonunuliwa ambayo thamani yake ilikuwa zaidi ya dola milioni mia mbili, zilianza kutangazwa karibu na vyombo vyote vya habari duniani! Hiyo ikimaanisha redio, magazeti, televisheni hadi ndani ya mtandao wa intaneti! Karibu kila binadamu alilielewa jambo hilo ingawa hawakuelewa kitu chochote juu ya msako ulioendelea kimya kimya, Mafia hawakutaka kutangaza juu ya msako huo, walitaka kutumia mtandao wao kuwakamata Caroline na Harry kirahisi.

    Taarifa zilipowafikia wazazi wa Caroline, mama yake Dk. Cynthia na baba yake Profesa Kadiri walichanganyikiwa, walishindwa kuelewa nini kilichompata mtoto wao mpaka kufikia uamuzi wa kutoroka, walimfahamu vizuri Caroline, hakuwa mtu wa kuchukua maamuzi ya haraka haraka bila kufikiria! Waliamini haukuwa uamuzi wa Caroline, walichohisi wao  ni kwamba alitekwa na kupelekwa mahali kusikojulikana. Walihofia maisha ya mtoto wao, walijua pengine alikuwa marehemu kwa wakati huo! Mama yake alilia mno siku alipoiona sura ya mwanae akitangazwa katika luninga kuwa alikuwa ametoroka.

    Walikaa kwa wiki tatu wakisubiri Dk. Ian awapigie simu na kuwataarifu juu ya kilichotokea lakini hakufanya hivyo na walipopiga wao na kutaja majina yao waliambiwa Dk. Ian hakuwepo Canada wakati huo alikuwa safarini Miami kufuatilia ndege yake iliyopotea, kila siku walipopiga simu walijibiwa hivyo! Hilo ndilo lilizidisha wasiwasi zaidi ya maradufu, walishindwa kuelewa ni kwanini Dk. Ian hakufanya hivyo!

     Baadae fikra zao zilianza kuwafanya wafikiri  labda nae alikuwa pamoja na  Caroline ndani ya ndege lakini  kwa mujibu wa habari zilizoendelea kutangazwa katika vyombo vya habari  Dk. Ian hakujajwa mahali popote, hilo walilifuta na uamuzi uliowaijia vichwani mwao ambao waliouona wa busara ulikuwa ni kusafiri hadi Canada kwenda kuujua ukweli kutoka mdomoni mwa mkwe wao Dk. Ian.

    Hawakuhisi hata kidogo kuwa ni hasira ndiyo ilimfanya Dk Ian asiwapigie simu wala kuwatumia  ujumbe wowote  kuwataarifu juu ya yaliyompata mtoto wao! Dk. Ian alimchukia kila mtu kuanzia Caroline mpaka wazazi wake, alichokuwa amefanyiwa kilikuwa kitu kibaya sana, tayari kilishamrudisha kwenye kazi ya Mafia ambayo aliiacha muda mrefu, alikuwa tayari kumuua mtu yeyote au kufanya jambo lolote ili mradi  ampate Caroline!

    “Inabidi twende huko Canada, nafikiri mkwe wetu atakuwa na jibu zuri la maswali yetu!” Profesa Kadiri alimwambia mke wake.

    “Unafikiri ni sawa tukisafiri wote?”

    “Sioni ubaya wowote!”

    “Gharama je?”

    “Usijali tutatumia pesa tuliyonayo katika akaunti yetu, ni vyema tukasafiri wote wawili!”

    “Sawa basi, hakuna tatizo nitaomba ruhusa kazini, nafikiri wataniruhusu maana hata wasiponiruhusu kazi hazifanyiki!”

    “Utawezaje kufanya kazi wakati mwanao yupo wenye matatizo makubwa kiasi hicho?”

    Maandalizi ya safari yalianza kufanyika, walichukua pesa katika akaunti yao na kukata tiketi mbili za ndege kwenda na kurudi Canada katika shirika la ndege la Uingereza, British Airways! Ndege za shirika hilo zilianzia safari yake Nairobi nchini Kenya, hivyo baada ya kukamilisha taratibu zote kwa sababu wao waliishi Arusha walisafiri moja kwa moja hadi Nairobi ambako walipanda ndege na kuondoka kwenda zao Canada, hawakuwa na furaha hata kidogo na safari hiyo! Tofauti na safari nyingine zote walizokwisha safiri pamoja  kwenda nchi za nje, njia nzima Dk. Cynthia alilia akimlilia mwanae! Hakuwa na uhakika wa kumkuta nchini Canada na hakujua kama alikuwa hai au amekufa.

    Walitua uwanja wa ndege wa Ottawa nchini Canada saa kumi na mbili jioni, walikuwa wamesafiri karibu masaa kumi na nane njiani sababu ndege waliyopanda ilikuwa na mizunguko mingi na ilitua katika nchi  za  Dubai, Sweden, Norway, Denmark ndiyo ikaingia Canada! Kila mtu alikuwa amechoka sana wakati wanatua katika uwanja huo, hapakuwa na mtu wa kuwapokea uwanjani na kila kitu kilikuwa kigeni kwao! Ilikuwa ni siku ya kwanza kwao kuingia katika nchi hiyo kwani kila mara Caroline alipowaalika kwenda kumtembelea walikataa!

    Kwa taarifa walizokuwa nazo Dk. Ian alikuwa mtu maarufu sana katika nchi hiyo, hawakutegemea ingekuwa  kazi ngumu  kwao kumpata, walichokifanya kwa haraka baada ya kutoka nje ya uwanja ni kumwita dereva teksi aliyekuwa jirani akiita abiria na kumuuliza kama anamfahamu Dk. Ian.

    “Yeah! I know him!” (Ndiyo namfahamu!)

    “Can you take us to his resdential pallace?” (Unaweza kutupeleka nyumbani kwake?)

    “That’s very easy to do!” (Hilo ni jambo rahisi sana kufanya!)

    “How much are we going to pay you?” (Tutakulipa shilingi ngapi?)Mama yake Caroline aliuliza ili kujiepusha na migogoro ya abiria na madereva teksi kama ambay hutokea  nchini Tanzania.

    “We normally charge five dollars!” (Kwa kawaida tunatoza dola tano!)

    “I think we can afford that!” (Nafikiri tunaweza kumudu!)

    “Then let’s go!” (Basi twendeni!) Alisema dereva na kuwafungulia milango wote wakaingia.

    Safari ilianza kutoka uwanja wa ndege wa Ottawa kuelekea nyumbani kwa Dk. Ian,  giza lilikuwa bado halijaingia hivyo Profesa Kadiri aliweza kuiona vizuri mandhari ya jiji hilo maarufu duniani, alishangaa kuona majengo marefu kuliko hata aliyoyaona nchini Uingereza alikokwenda  masomoni! Pamoja na giza kuanza kutanda bado watu walikuwa wengi mitaani na karibu watu wote aliowaona walikuwa ni wazungu, mara chache sana aliwaona watu weusi! Mke wake wala hakuangalia nje wakati wote gari likipita uso wake aliulaza kwenye miguu ya mumewe na kuendelea kulia kwa uchungu, alikuwa na mawazo mengi sana juu ya mwanae.

    Gari liliuacha mji na kuanza kwenda  nje katika maeneo yaliyokuwa na miti mingi, alishindwa kulifananisha jiji hilo na jiji la Dar es Salaam ambalo halikuwa na  miti kabisa! Aliwasifu watu wa Canada kwa kutunza mazingira yao, kila sehemu aliyoiona ilikuwa  kijani na ilivutia macho kuangalia.

    “Where are you from?”(Nyinyi ni watu wa wapi?) Dereva aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu.

    “We are from Tanzania!” (Tunatoka Tanzania!)

    “Tanzania?” aliuliza dereva kwa mshangao.

    “Yes, heard of it?” (Ndiyo, umewahi kuisikia?)

    “Yeah! Yeah! Yeah! It is the most peaceful country in Africa, isn’t it? “( Ndiyo! Ndiyo! Ndiyo! Ni nchi yenye amani zaidi katika Afrika, au siyo?)

    “You are right!” (Sawa sawa!)

    “How are you related to Dk. Ian?” (Nyie mna uhusiano gani na Dk. Ian?)

    “He is our son in law!” ( Amemuoa binti yetu!)

    “So you mean the girl   who escaped with his jet, you daughter?” (Kwa hiyo mna maana yule binti aliyetoroka na ndege  yake ni binti yenu?) aliuliza dereva kwa mshangao, macho yake yalionyesha hofu kubwa.

    “Ofcourse she is!” (Ndiyo ni binti yetu!)

    “Are you not afraid of him? At the moment  Dr. Ian is not a good person! He has killed more than  ten workers within his pallace since his wife escaped! I’m sure you wont leave  his home safely” (Hammuogopi? Kwa sasa hivi Dk. Ian siyo mzuri, ameua zaidi ya wafanyakazi kumi ndani ya makazi yake tangu mke wake atoroke, nina uhakika hamtaondoka salama!)

    “No! We’re sure he wont do us any harm!” (Hapana, tuna uhakika hawezi kutudhuru sisi!)  alijibu Profesa Kadiri kwa uhakika, haikuwa rahisi kwake kufikiria kuwa Dk. Ian angeweza kuwafanyia mambo aliyosema dereva  huyo.

    “Please take my words!” (Tafadhali  aminini ninachokisema!) aliongeza dereva lakini hawakutaka kumuelewa walimwomba aongeze mwendo ili wafike upesi, dereva aliwatiii wateja wake na mbele kidogo gari lilikata kulia kuelekea kwenye lango kubwa ambalo mbele yake kulikuwa na bango lenye maandishi Dk. Ian Smith Resdential Pallace.

    “ Here we are!” (Tumefika!) alisema dereva na kupiga honi lakini kabla lango halijafunguliwa walitoka maaskari watatu na kulizunguka gari  mmoja wao akimuhoji dereva aeleze alikuwa  mgeni wa nani, alijitambulisha kwao na kuwaeleza kuwa aliwabeba wageni wa Dk. Ian! Aliposema hivyo tu lango lilifunguliwa, gari likaingia  na watu wote waliokuwemo ndani ya gari wakaandika majina yao katika kitabu na kutia saini! Profesa Kadiri na mke wake walishangazwa na utaratibu huo. Kabla maaskari hawajaliruhusu gari  mmoja wao alipiga simu ndani ya nyumba ya Dk. Ian .

    “Who are they?” (Ni akina nani?) ilikuwa sauti nzito ya Dk Ian.

    “Profesa Kadiri and Dr. Cynthia, they have claimed to be your Inlaws do you know them?” (Ni Profesa Kadiri na Dk. Cynthia wanadai wao ni wakwe zako! Unawafahamu?)

    “Yes! They have come for their deaths! Rope them immediately and take them to the torture room! I don’t want to see them, they will undergo pains until their daughter Caroline is found, understood?” (Ndiyo, wamevifuata vifo vyao! Wafungeni kamba haraka na muwapeleke kwenye chumba cha mateso, sitaki kuwaona watateseka mpaka siku mtoto wao atakapopatikana! Umenielewa?)

    “Yes, Sir!” (Ndiyo Bwana!)http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva wa teksi aliruhusiwa kuondoka na hapo hapo bila kuchelewa Profesa Kadiri na mke wake waliwekwa chini ya ulinzi na kufungwa kamba mikono na miguu, wakabebwa na kwenda kutupwa kwenye chumba cha mateso, watu wengi waliopelekwa huko hawakurudi salama.

    “Please don’t treat us badly, we’re his inlaws!” (Tafadhali  msitutende vibaya, sisi ni wakwe zake!) mama yake Caroline alisema huku akilia lakini hakuna aliyejali, yeye na mume wake wote walikuwa mgongoni mwa maaskari wenye nguvu wakipelekwa kwenye chumba cha mateso.

    ***************************

    Harry na Jet

    Ulikuwa ni mpango kamambe uliyopangwa kufanyika bila makosa, kwa utundu wake Harry aliichokonoa ndege ikiwa angani ili isiweze kunaswa na rada za nchi mbalimbali duniani,  alijua alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na hakutaka kupatikana, ilikuwa ni lazima afike nchini Kenya ambako angeiuza ndege hiyo kwa dolla za kimarekani milioni mia moja na themanini na tisa, huo ndio ungekuwa mwisho wa umaskini wake! Angekuwa tajiri tangu siku hiyo na si ajabu ndoto yake ya kuwa Rais ingetimia! Kwa mafuta yaliyokuwemo   ndani ya  tenki la ndege alikuwa na uhakika wa kufika mpaka Nairobi bila kutua mahali popote safari ambayo ingemchukua si zaidi ya masaa sita akiruka kwa mwendo wa kasi angani!

    Alijua wazi kabisa kuwa alimwacha Caroline katika mateso makali kupita kiasi, alijua angekufa lakini hakuumia moyoni kwani alichokitaka yeye ni pesa na alikuwa ameipata. Kilichompeleka nyumbani kwa Dk. Ian kutafuta kazi  hakikuwa ajira bali kuiba ndege hiyo, hakutegemea hata kidogo kukutana na Caroline pale! Hiyo ilikuwa ni bahati mbaya sana kwake, hakuwa na mapenzi na Caroline tangu shuleni isingewezekana ampende ukubwani, hicho ndicho alichoamini Harry!

    “Ni bahati mbaya sana kwake! Halikuwa lengo langu hata kidogo kumfanyia yaliyotokea, lakini pia nisingeweza kusafiri naye kwenda kuiuza ndege hii ingekuwa hatari zaidi!”

    Kabla hata ya kwenda nyumbani kwa Dk. Ian kutafuta kazi ya urubani Harry alishalipwa asilimia tano ya pesa zote kama tangulizo na sehemu ya pesa iliyobaki angemaliziwa baada ya kuifikisha ndege hiyo! Hivyo ilikuwa ni lazima kazi hiyo ikamilike na aliwafahamu vizuri wateja wake! Hawakuwa watu wema hata kidogo, walikuwa wauaji waliomiliki mtandao ulioitwa Al-qaeda  ambao matawi yao yalisambaa sehemu mbalimbali duniani, walioihitaji ndege hiyo walikuwa na tawi lao nchini  Sudan katika jiji la Khartoum  ndiyo waliomiliki kiwanda cha madawa kilicholipuliwa na Marekani. Hata kama angejaribu kuwakimbia na hiyo asilimia tano ni lazima wangempata! Woga juu ya watu hao ndizo zilimfanya ashindwe kubadili nia yake pamoja na kuwepo kwa vipindi alivyomuonea huruma Caroline wakiwa Miami.

    “I’m so sorry for Caroline, I know she is innocent! But I have put her into troubles!” (Namsikitikia sana Caroline, najua hana hatia na nimemuweka katika matatizo makubwa!) aliwaza Harry.

    Masaa saba tangu aruke toka Vietnam Harry alitua  na ndege yake kaskazini mwa Kenya karibu kabisa na  mpaka wa nchi hiyo na Sudan, ulikuwa ni usiku wa manane! Baada ya kutua katika kiwanja cha muda kilichojengwa tayari kwa kazi hiyo Harry aliteremka kwenye ndege na kulakiwa na wazee wa nane wenye ndevu nyingi, alipowaangalia aligundua walikuwa Waarabu, wawili kati yao aliwafahamu! Ndiyo alioongea nao nchini Marekani juu ya mpango huo. Walimkumbatia na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya, baadae walimtambulisha kwa wazee  wengine ambao  pia walimshika mkono wa pongezi, kulikuwa na vijana wengine wawili wao walikuwa Waafrika kama yeye, aliambiwa walikuwa ni marubani waliotegemea kuirusha ndege  hiyo kwenda Ujerumani kwa ajili ya kubadilishwa ili isitambulike.

    Makabidhiano ya ndege hiyo yalichukua kama dakika ishirini tu, gari la mafuta ya ndege lililokuwa uwanjani hapo liliijaza ndege ya mafuta tayari kwa safari, marubani waliaga na kuingia ndani ya ndege! Harry alishuhudia ndege ikiacha ardhi taratibu na yeye alipakiwa ndani ya moja ya magari yaliyokuwepo uwanjani hapo tayari kwa safari ya kwenda Khartoum ambako malipo yangemaliziwa.

    “Hivi kweli watanilipa hawa? Sijaingizwa mjini kweli?” alijiuliza Harry wakati magari yakichukua kasi.

    ********************************

    Akiwa ndani ya mti Caroline aliendelea kushuhudia askari wakimsulubu mzee Nelson Peace, babu aliyejitolea kumsaidia, askari walizidi kumshinikiza aeleze ukweli wa mahali alipojificha! Kwa kipigo alichokipata mzee huyo, Caroline alikosa uhakika kama asingewaonyesha mahali alipokuwa. Roho yake ilimuuma sana kujua alikuwa ameingia tena mikononi mwa Wavietnam  kitu ambacho hakutaka kabisa kitokee, pamoja na kipigo chote kilichotolewa bado mzee huyo hakudiriki kuyaonyesha maficho ya Caroline!

    Kitendo kilichokuwa kikitokea kilimkumbusha enzi za watoto wake walipocheza mchezo wa kujificha ulioitwa kombolela! Alikumbuka kitu kimoja walichoamini watoto kuwa ukiuma meno huku umejificha mtu aliyekutafuta asingekuona, pamoja na kuwa mtu mzima Caroline alilazimika kuuma meno yake akiamini asingeonekana.

    Mbwa walizidi kubweka wakiuzunguka mti aliojificha na waligalagala hadi chini kwa kilio, alielewa wazi walikuwa wakiwaonyesha ishara maaskari kuwa mtu waliyekuwa wakimtafuta alikuwa ndani ya mti huo! Maaskari walisogea hadi eneo hilo na kuanza kuuzunguka mti huku wakimburuza mzee Nelson chini ili awaonyeshe mahali alipokuwa Caroline lakini hakusema! Waliangalia juu ya mti lakini hawakumuona, mbwa nao walizidi kubweka wakiuzunguka mti huo mkubwa.

    “Show us the girl, you goddamn  oldman or else you are dead!” (Tuonyeshe huyo msichana aliyekuwa mzee vinginevyo tunakuua!) walizidi kumpiga mzee huyo, Caroline alitetemeka kupita kiasi na alihisi mkojo ukimpenya! Kwa kipigo alichopewa mzee huyo alijua kama yeye wangemkamata wangemuua kabisa. Mawazo yake yalimrudisha kwa baba na mama yake, alisikitika kufa akiwa mbali nao.

    Je, nini kitaendelea? Harry atalipwa? Caroline atakamatwa? Wazazi wa Caroline watapatwa na nini? Wiki ijayo.











    A

    liendelea kujificha ndani ?ya tundu lililokuwemo ?ndani ya mti, lakini kwa kuchungulia kupitia katika upenyo uliokuwepo kati ya gome la mlango na mti wenyewe alishuhudia mzee Nelson Peace akiendelea kupokea kipigo kutoka kwa maaskari wa Kivietnam, tena wakati huo hata mbwa walikuwa wakimshambulia kwa kumuuma na meno yao makali yenye ncha,  tayari walishaacha kubweka kuuzunguka mti!

    Pamoja na mateso yote aliyoyapata mzee Nelson  hakudiriki kutaja mahali alipomficha Caroline! Alionekana kuwa mtu aliyekuwa tayari kufa yeye lakini si kuonyesha mahali alipokuwa binti huyo! Caroline alimshukuru Mungu kwa jambo hilo ingawa hakuwa na uhakika kama lingedumu kwa muda mrefu.

    Dakika kumi na tano baadae mzee alikuwa hoi bin taabani kwa kipigo na  maaskari wale walianza kumvuta kuelekea porini, Caroline alijua walimpeleka huko kumuua,  hapakuwa na kitu kingine  ambacho wangeweza kufamnyia, alijisikia huruma sana moyoni mwake kwa sababu alijua mzee huyo aliutoa uhai ili kuokoa maisha ya msichana asiyemfahamu! Machozi ya uchungu yalimtoka Caroline.

    Baada ya maaskari kuondoka wakimvuta hali ilikuwa kimya kabisa, Caroline aliendelea kujificha ndani ya mti huo hadi jioni giza lilipoanza kuingia, tayari ulikuwa usiku mwingine! Kadri masaa yalivyozidi kusogea  ndivyo giza lilivyozidi kuongezeka na lilikuwa  kubwa zaidi ndani ya tundu alilojificha! Hali ilimtisha lakini alishindwa kufikiria kutoka ndani ya tundu kwa kuogopa kukamatwa, hakutaka kabisa kurudi tena mikononi mwa Wavietnam.

    Mpaka majira ya kama saa tisa za usiku hivi, ingawa hakuwa na uhakika sana Caroline alikuwa bado yu ndani ya tundu, alikuwa  hajapata hata lepe moja la usingizi, alikuwa bado yu katika maumivu aliyoyapata wakati wa kujifungua na uchovu wa safari ndefu ya kutembea kwa miguu. Kichwani mwake kulijaa mawazo mengi juu ya namna gani angeweza hatimae kufika Tanzania! Hiyo ndiyo nchi aliyoiota katika mawazo yake, aliamini kama ingetokea akafika Tanzania  maisha yake yangebadilika! Alipowafikiria baba na mama yake ndiyo alizidi kuitamani Tanzania.

    Pamoja na tamaa ya Tanzania, wazo moja tu lilimsumbua kichwani mwake, wazo la mauaji. Ilikuwa ni lazima awaue watu wote waliomfanyia ubaya katika maisha yake, hasa  Harry! Alimchukia mwanaume huyo kupita kiasi, hakutaka hata kusikia jina lake! Aliamini ni yeye aliyeyaharibu maisha yake baada ya kuwa ametulia na Dk. Ian, ni yeye aliyemfanya awe mtu wa kusakwa na Mafia dunia nzima!  na alijua kama siku moja angejikuta mikononi mwa  mtu huyo adhabu yake isingekuwa nyingine zaidi ya kifo! Kwanini afe sababu ya makosa yaliyofanywa na Harry? Hilo ndilo swali lililomsumbua kichwani mwake.

    “Naomba tu nisiingie mikononi mwake kabla sijalipiza kisasi, ni lazima niwaue Harry na wenzake ndipo Dk. Ian aniue!  Ndiyo nastahili kifo kwa mabaya niliyomfanyia, lakini asiniue kabla sijatimiza kazi yangu!” Aliwaza Caroline akiwa ndani ya mti, orodha ya majina ya watu aliotakiwa kuwaua alimwijia kichwani mwake!

    “Harry, Richard, Reginald na Dickson  ni lazima wafe, walichangia sana kuharibu maisha yangu, lakini Harry atakuwa wa mwisho! Kama nitafika Tanzania nitajificha hadi nimalize kwanza kuwaua wenzake ndipo nitammalizia yeye na baada ya kifo chake sitakuwa na haja ya kuishi zaidi!” Aliwaza Caroline, alikuwa amekataa tamaa  ya maisha kabisa hasa alipoufikiria umbali uliokuwepo kati ya mahali alipokuwa na nchi aliyotaka kwenda akiwa hana hata senti moja mfukoni!

    Ghafla wadudu kama panya wakubwa walianza kudondoka kutoka eneo lililokuwa juu yake  na kuanza kutafuna nyama za  vidoleni mwake,  hao ndiyo walimfanya aanze kufikiria kutoka ndani ya tundu, asingeweza kuyavumilia mateso aliyokuwa akiyapata.

    Alivumilia kwa muda lakini baadae alishindwa na kuamua kukiondoa kipande cha gome kilichofunika tundu hilo na kuruka hadi nje ambako alipambana na giza nene kupita kiasi!  Akiwa amesimama nje alisikia miungurumo ya manyama wakali kama Simba, hao ndiyo waliongeza hofu yake zaidi, aliogopa sana kifo cha  kuliwa na wanyama, alikuwa tayari kufa kifo kingine chochote lakini si kifo cha kutafunwa hadi mwisho!

    Hakuwa na mahali pengine pa kujificha zaidi ya kuingia ndani ya kijumba cha mzee Nelson! Alinyata taratibu na kuusogelea mlango wa nyumba hiyo, ulikuwa wazi na ndani yake pia hapakuwa na mwanga wowote ule! Akiwa ndani alipapasa kitanda na kuona mahali kilipokuwa akalala juu yake. Baadae alikumbuka kuwa hakufunga mlango na kurudi tena hadi mlangoni, ulikuwa na mlango wa miti uliotengenezwa vizuri, hakujua jinsi ya kuufungua kwa sababu haukuwa na komeo, ikabidi  aurudishie tu mahala pake na kurudi tena kitandani ambako alijilaza na kuendelea na mawazo  juu ya Tanzania na kilichokuwa mbele yake!

    Masaa mawili baadae alisikia kitu kikijivuta nje! Alijua  ni nyoka mkubwa kupita kiasi, alinyanyuka na kukimbia hadi mlangoni ambako aliushika mlango na kuugandamiza ili usifunguke, kitu hicho kilizidi kujivuta kuelekea mlangoni, Caroline alizidi kuingiwa na hofu na kuzidi kuusukuma mlango zaidi, kitu hicho kilipoufikia mlango kilitulia na baadae alisikia mlango ukigongwa taratibu! Kitendo hicho kilimfanya ahisi aliyekuwa nje alikuwa ni binadamu kwani mnyama asingeweza kugonga namna hiyo!

    “Sijui ni nani? Au ndio wale maaskari  wamerudi tena?” Alijiuliza Caroline huku akitetemeka mwili mzima! Na kadri mlango ulivyozidi kugongwa ndivyo hofu yake ilivyozidi kupanda.

    “Who is there?” (Nani anagonga?) Hatimaye alijikuta akiuliza baada ya mlango kuwa umegongwa sana lakini bila sauti yoyote kusikika!

    “Me?”( Mimi)

    “You? Who and what are you?” (Wewe ni nani?)

    “It is me Nel!” (Ni mimi Nelson)

    Kauli hiyo ilimfanya aikumbuke sauti ya  mzee Nelson Peace, pamoja na kuitambua bado hakufungua mlango mara moja, hakuamini kama  mzee huyo alikuwa peke yake, alihofia watu walimtanguliza ili agonge na wamkamate.

    “Lakini wamejuaje kuwa nipo humu?” Aliwaza Caroline huku macho yake yakichungulia nje, ingawa hali ilikuwa ya giza hakuona mtu yeyote aliyesimama wima zaidi ya aliyeonekana kulala chini, aliufungua mlango na kukuta kweli aliyekuwa amelala chini ni mzee Nelson.

    “I’m sorry Nelson!” (Nisamehe Nelson)

    “For ...wh..at?” (Kwa kosa gani?)

    “For causing you all these troubles!” (Kwa kukusababishia matatizo yote haya!)

    “Mention not, I was rea..dy to sacri..fice my li..fe for ..you!” (Usijali, niliku..wa tayari kupo......teza maisha yangu sab.....abu ...yako!) Alisema mzee huyo kwa shida kubwa.

    “Won’t they come back?” (Hawatarudi kweli?) Caroline aliuliza kwa hofu, aliwaogopa sana wavietnam.

    “I’m not sure,  I guess they wont! They know I’m dead!” (Sina uhakika, nahisi hawawezi kurudi wanajua nimekufa!)

    “Sure?” (Kweli?)

    “Yeah!” Aliitika mzee Nelson.

    Alimbeba na kwenda kumlaza kitandani, baada ya kuwekwa kitandani  mzee Nelson alimweleza Caroline jinsi hali yake ilivyokuwa mbaya na kiasi gani hakuwa na matumaini ya kupona, mwili wake ulikuwa umeharibiwa vibaya mno kwa kipigo na kwa sababu hiyo alimruhusu asubuhi ya siku iliyofuata Caroline aendelee na safari yake amwache yeye afe peke yake kwani kifo ndio alichokihitaji na alimwelekeza njia ya kupita hadi kuingia mjini Penh! Kwa mtu mwingine ushauri huo ungeweza kuwa mzuri  na wa busara lakini kwa Caroline alionekana tofauti kidogo.

    “Siwezi kukuacha hapa porini, umenisaidia sana mzee Nelson ni lazima nami niwe tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako, kama maaskari watakuja basi acha waje na lolote litokee lakini siwezi kukuacha  ufe peke yako” Alisema Caroline na aligundua tiba ya kumsaidia mzee huyo ilikuwa ni kumkanda na maji ya moto.

    Alimuuliza kama alikuwa na kiberiti sehemu yoyote ndani ya nyumba ili apate kuwasha moto na kuchemsha maji ya kumkanda, jibu alilolipata hakulitegemea!Hapakuwa na keberiti  ndani ya nyumba yake, moto ulipatikana kwa kupekecha vijiti viwili! Katika maisha yake Caroline hakuwahi kufanya  jambo hilo hata mara moja na hakuja kama angeweza!

    Alikumbuka kusoma upatikanaji huo wa moto katika historia tena akiwa shule ya msingi! Hakuwa na njia nyingine ya kupata moto zaidi ya hiyo na lengo lake lilikuwa kumsaidia mzee Nelson, aliulizia mahali vipande vya mti vilipokuwa na kuonyeshwa, akavichukua na kuviweka chini, akavuta nyasi kutoka darini mwa kibanda hicho na kuzivunjavunja kisha akaziweka sambamba na vijiti na kuanza  kupekecha,  ilikuwa kazi ngumu na alifanya kwa karibu masaa mawili ndipo moto ukapatikana, mikono yake ikiwa imechanika vibaya!

    Caroline alifurahi kupita kiasi na alichofanya ni kuzidi kupuliza nyasi ili moto usizime, huku akiongeza nyasi zaidi! Aliongeza kuni na moto ukawa mkubwa! Akausogeza katikati ya mafiga matatu yaliyokuwa pembeni na kuchukua chungu kilichokuwa pembeni na kukijaza maji akakikalisha juu ya mafiga hayo, alizidi kuchochea kuni katika moto na haukupita muda mrefu maji yalichemka, tayari ilishagonga saa kumi na mbili asubuhi mwanga ulishaanza kuonekana nje ya kibanda.

    Bila kuchelewa maji yakiwa bado ya moto alichukua kipande cha nguo cha mzee Nelson na kukidumbukiza  ndani ya maji hayo kisha kukitoa na  kumkanda nacho! Aliendelea kufanya hivyo kwa karibu saa nzima huku Mzee huyo akilalamikia maumivu  aliyokuwa akiyapata lakini Caroline hakuacha kwani ndiyo tiba pekee aliyokuwa nayo!  Baadae alimwacha.

    Kazi hiyo ilifanyika kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku tatu mfululizo hali ya mzee Nelson ikaanza kuwa nzuri! Akawa na uwezo hata wa kukaa na kusimama mwenyewe  bila msaada wa mtu! Mpaka wakati huo hapakuwa na mtu  wala askari aliyejitokeza  eneo hilo kumsaka Caroline.

    Siku ya tano mzee huyo tayari alikuwana uwezo wa kutoka hadi nje, maji ya moto yenye chumvi aliyokandwa na Caroline kila siku yalimsaidia! Kwa siku zote hizo waliishi pamoja wakila matunda yaliyokuwa ndani ya kibanda hicho, siku ya sita mzee Nelson alitembea pake yake hadi porini na kurudi na majani mengi ya kijani na kumkabidhi Caroline akimwomba ayachemshe, Caroline alifanya hivyo na maji ya mazito ya kijani yalipatikana baada ya kuchemshwa! Mzee huyo akawa anakunywa maji hayo kila siku asubuhi  na jioni, wiki moja baadae alikuwa mzima  wa afya! Tatizo pekee lililomsumbua likawa ni makovu na vidonda mwilini.

    **************

    “Caroline!” Ilikuwa ni alfajiri na mapema mzee Nelson alipoliita jina hilo, Caroline alikuwa  bado yu usingizini.

    “Naam babu! Aliitika baada ya kuitwa kama mara tatu hivi.

    “Nakushukuru kwa wema wako wote, umeokoa maisha yangu!”

    “Wewe ndiye umeniokoa zaidi, bila wewe ningekuwa tayari nimekwishakamatwa na tayari ningekuwa marehemu, ulikuwa ni wajibu wangu mimi kukusaidia sababu nilikusababishia matatizo makubwa sana!”

    “Usijali, ninachotaka kukuuliza ni kuwa, ni kitu gani unachotaka nikusaidie  kwa sasa?”

    “Nataka kufika kwetu Tanzania!”

    “Lakini ujue Mafia wanakusaka na siyo rahisi kuwakwepa mjukuu wangu!”

    “Lolote litakalotokea njiani  ni sawa babu lakini ni lazima nirudi nyumbani!”

    Mzee Nelson  alisikiliza kwa muda huku akimwangalia Caroline usoni, alielewa ni  jinsi gani msichana huyo alikuwa jasiri na asiyeogopa, hakutegemea msichana mdogo kama huyo kuwa shujaa kiasi hicho wakati alikuwa akitafutwa na watu hatari, Mafia. Kwa hakika alijua asingefika alikokuwa akienda! Asingefika Tanzania! Sehemu fulani njiani ni lazima angekamatwa na kuuawa, roho ilimuuma sana mzee huyo kwani alitokea kumpenda sana Caroline kama mjukuu wake.

    “Kwanini wewe na mimi tusihame pamoja  kwenda sehemu nyingine humu humu porini  mpaka hali itulie? Miaka mitano baadae hakuna mtu atakayekuwa anakutafuta, hapo ndipo utaweza kujitokeza.”

    “ Miaka mitano? Hapana babu, nashukuru kwa msaada wako lakini niache tu niendelee  na safari yako na ningependa kesho nisonge mbele!”

    “Kweli?”

    “Ndiyo, ninachokuomba wewe  ni kunipeleka mjini huko mbele nitajua mwenyewe cha kufanya, si unaweza kumpeleka kwa farasi wako?”

    “Ndiyo!”

    “Basi usiwe na wasiwasi, nipeleke kesho!”

    “Lakini utakuwa usiku maana mimi huwa siingii mjini mchana!”

    “Hakuna matatizo tukikaribia tu uniache, nitaingia mwenyewe! Kwani ni umbali gani kutoka hapa?”

    “Siyo mbali sana!”

    *****************

    Siku iliyofuata saa mbili usiku waliondoka porini kuelekea mjini Penh wakitumia farasi ya mzee Nelson aliyeitwa Gaze, Caroline alikuwa amekaa nyuma na mzee Nelson akiwa amemkumbatia! Ulikuwa usiku wa kiza kinene lakini bado mzee huyo alimpeleka farasi kwa kasi ya ajabu!  Alikuwa na uzoefu na njia, kulikuwa na baridi kali  kupita kiasi usiku huo, meno ya Caroline yaligongana.

    Tofauti na aliyosema mzee Nelson kuwa mjini palikuwa karibu, walisafiri kwa karibu masaa matatu  katikati ya pori bila kufika, wakipishana na wanyama wakali  wa kutisha. Caroline alichoka kukaa mgongoni kwa farasi.

    “Bado tu!”

    “Bado kidogo!” Alijibu mzee Nelson huku akicheka, ilivyoonyesha kulikuwa bado kuna umbali  mkubwa sana lakini hakutaka  kumvunja moyo Caroline, masaa mawili baadae taa zilianza kuonekana kwa mbali, hiyo ikaashiria walikuwa wakiingia mjini! Walikuwa wamesafiri kwa masaa saba porini! Mbele kidogo kama kilometa kumi farasi alianza kupunguza mwendo taratibu na hatimae alisimama na mbele chini ya mti mkubwa!

    “Mjukuu wangu Caroline mimi kama nilivyosema huwa siingii mjini, nina miaka zaidi ya ishirini porini ninajua siku yoyote  nikikanyaga mjini nitakamatwa, hivyo msaada wangu unaishia hapa! Nakutakia safari njema mjukuu wangu, nimefurahi sana kuishi nawe kwa siku hizi chache, ni matumaini yangu utarudi tena siku nyingine!” Alisema mzee Nelson, uso wake ulionyesha huzuni kubwa.

    ‘Sawa babu, ahsante kwa kila kitu , kwani utakuwa unaishi hapo hapo?”

    “Hapana, nitahama, siwezi kuishi pale tena, nitatokomea ndani  ya pori zaidi!”

    “Sasa mwisho wako utakuwa kitu gani maishani?”

    “Kufia porini tu siwezi hata siku moja kujitokeza, nitauawa!”

    Walikumbatiana na kuagana, roho ilimuuma sana mzee Nelson kwa sababu alielewa Caroline asingefika  alipokuwa akienda, ni lazima angekufa! Alibaki amesimama eneo hilo kwa muda mrefu akishuhudia Caroline akiishia gizani.

    “Caroline!” Mzee Nelson alimwita, moyoni alikuwa akisikia huruma zaidi.

    “Naam babu!”

    “Tafadhali sana rudi, huko unakokwenda kuna matatizo makubwa mjukuu wangu!”

    “Usijali babu, Mungu atanisaidia ni lazima nifike nyumbani  nionane na wazazi wangu na nina kazi ya kufanya!” Alijibu Caroline na kuzidi kutokomea gizani kuelekea mjini.

    ******************

    Jua la siku hiyo lilipojitokeza tayari alikuwa katika mji wa Penh ulikuwa ni mji mdogo lakini wenye watu wengi  kuliko Dar es Salaam, kila mtu alionekana kutembea kwa kasi ya ajabu kuelekea kazini, watu wa mji huo walitumia punda zaidi kama usafiri wao na walivaa kofia kubwa za mikeka vichwani mwao! Kwao ulikuwa ni kama mtindo, hata wanawake pia walivaa hivyo.

    Kila mtu aliyepita karibu yake  alimshangaa Caroline alionekana ni mtu tofauti kabisa  na wakazi wa eneo hilo!  Rangi ya ngozi yake na hata ufupi wa nywele zake uliwashangaza wengi. Alishinda akizunguka huku  na kule katika mji huo hadi usiku ukaingia, hakuwa na mahala pa kulala, na pia njaa ilimsumbua  kupita kiasi, siku hiyo alilala katika veranda na hakula kitu chochote. Aliishi hivyo kwa siku mbili, siku ya tatu alishindwa ikabidi aingie katika hoteli moja kuomba msaada.

    Mama mwenye hoteli hiyo alikuwa mzungu mzee  na aliongea kiingereza cha kimarekani, Caroline alimfuata na kumuuliza shida yake ya njaa, mama huyo hakuuliza  maswali mengi  ila aliagiza apewe chakula, wakati akila chakula hicho Caroline aligundua mama huyo alikuwa akimwangalia sana, alishindwa kuelewa ni kwa sababu gani alifanya hivyo ila aliomba Mungu asijemgundua kuwa ndiye aliyekuwa akitafutwa na Mafia!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘You are so beautiful, what’s your name my granddaughter?” (Wewe ni mzuri sana jina lako nani mjukuu wangu?)

    “Marione, thank you for your kindness! (Naitwa Marione, ahsante kwa wema wako!) Caroline alimdanganya jina, hakutaka kabisa kulitumia jina lake halisi, aliamini jina hilo pamoja na sura yake vilikuwa almasi kwa wakati huo.

    Baada ya hapo mama huyo alimdadisi Caroline mambo mengi juu ya mahali alikotokea na alikuwa nchini humo kufanya kitu  gani, alizidi kumdanganya kuwa mume wake na yeye  walikuwa wawindaji na walikwenda wote kufanya kazi hiyo katika misitu ya  Cambodia  lakini bahati mbaya mume wake alikufa kwa kukanyagwa na tembo!”

    “Kwa hiyo mimi nimetembea kutoka porini hadi hapa!’

    “Mungu wangu pole sana!’

    “Ahsante bibi!”

    “Ukitoka hapa utakwenda wapi?”

    “Sina pa kwenda!”

    Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Suzanne alikubali kumpa Caroline kazi ya kuhudumia katika hoteli yake, siku iliyofuata alimpeleka dukani na kumnunulia nguo nzuri zaidi, alipendeza na kuvutia! Akaanza kuishi katika hotelihiyo pamoja na wasichana wengine waliyofanya kazi za kuhudumia na kupika.  Kwa Caroline hiyo ilikuwa bahati kubwa, aliamini kwa utaratibu huo huo angefika Tanzania kwa wazazi na hatimae kulipa kisasi kwa watu waliomfanyia mabaya!

    ****************

    Siku yake ya kwanza kazini ni wavulana watatu wa kimarekani ndiyo aliowahudumia, yeye ndiye aliyepanga kuhudumia wateja ambao hawakuielewa lugha ya kivietnam! Kila alipowapelekea huduma wavulana hao walinong’onezana kitu, hakuelewa walikuwa wakiongea nini juu yake, lakini alijua wazi walimteta yeye! Walipomaliza  kula chakula  mmojawao alimwita.

    “Your name is?” (Jina lako ni nani?)

    “I’m Marione!” (Naitwa  Marione)

    “You are beautiful Marione, can we talk privately?”

    “No I’m busy! Thanks for your complements” (Hapana nina kazi nyingi sana! Ila nashukuru sana kwa sifa zako)

    “What about tomorrow?” (Vipi kesho?)

    “I’m not sure either?” (Sina uhakika pia).

    Walishamtilia mashaka tayari, ni jina tu ndilo lilikuwa tofauti lakini sura ilikuwa ili ile! Kama ni yeye walikuwa na uhakika wa kupata zawadi kubwa sana kutoka kwa Dk. Ian! Hicho ndicho walichonong’onezana vijana hao kabla ya kumwita Caroline! Walipanga kujaribu kumtaka urafiki ili tu wapate picha yake nakuituma Canada, kama angethibitishwa kuwa ndiye yeye basi wamkamate na kumsafirisha.

    “Ningependa sana kupiga picha na wewe?”

    “Mimi?”

    “Hapana, sipendi kupiga picha!” Caroline alikataa lakini kwa mama mwenye mgahawa hilo halikuwa na kizuizi sababu mteja alikuwa mfalme! Caroline alilazimishwa kufanya hivyo, ingawa hakutaka  ilibidi akubali na picha ikapigwa.

    Walipotoka hotelini hapo vijana hao bila kuchelewa walikwenda kwenye kompyuta na kuzituma picha hizo kwa Dk. Ian huko huko Canada kwa nje ya barua pepe, jibu lilifuata dakika chache baadae lilikuwa:

    “ She is the one, once you bring her here,  you are rich!” (Ni yeye mara mkimfikisha  hapa nyie matajiri!) Alisoma barua pepe hiyo, vijana hao walichanganyakiwa  walichanganyikwa kupita kiasi, ilikuwa ni lazima wamfikishe Caroline, Canada haraka iwezekanavyo hawakutaka kutumia nguvu!

    “Njia pekee ni kujifanya unamtaka kimapenzi, ipo siku atakubali na siku tutakayotoka nae kwenda popote kustarehe ndiyo siku tutakayomlewesha kwa madawa na kumsafirisha hadi Canada au?”

    “Sawa kabisa, hiyo ndiyo njia sahihi!” Wote waliitikia.

    Je, nini kitampata Caroline? Je, kweli atafika Tanzania? Wiki ijayo.













    “Lakini  lazima tufahamu ni kiasi gani Dk. Ian atatulipa, tusijejikuta tukifanya kazi halafu malipo yakawa kidogo, kumbukeni kumsafirisha kutoka hapa hadi Canada ni lazima tutumie ndege ya kukodi hivyo ni vyema tufahamu ni kiasi gani tutalipwa ili tupange bajeti yetu vizuri!”

    “Kwa hiyo?” Aliuliza mmoja wao.

    “Inabidi tumpigie simu Dk. Ian  kuuliza juu ya jambo hili!”

    “Tufanye lini?”

    “Leo hii hii, hakuna sababu ya kuchelewa!”

    Baada ya maongezi yao wote walitoka haraka na kwenda moja kwa moja hadi mjini kwenye kituo cha kupigia simu ambako walitafuta namba  ya Dk. Ian katika vitabu vya  simu na kufanikiwa kuipata! Hawakutaka kupoteza muda, waliipiga moja kwa moja bila kusita.

    “Hallow, Dr. Ian’s office can I help you? (Hallo hapa ni ofisi ya Dk. Ian, naweza kukusaidia?)

    “Can I speak to Dr. Ian himself?” ( Je, naweza kuongea na Dk. Ian mwenyewe?)

    “Can I know your name and the place you are calling from sir?” (Naweza kujua jina lako na unapiga simu kutoka wapi bwana?)

    “My name is O’brien, calling from Cambodia!” ( Ninaitwa O’brien napiga kutoka Cambodia)

    “Hold on.. (Subiri), ilisema sauti hiyo na baadae sauti nzito ilisikika.

    “Hallow, Dr. Ian speaking!” (Dk. Ian anaongea!)

    “Naitwa O’brien mmoja wa watu uliowasiliana nao kwa barua pepe juu ya Caroline! Unakumbuka?”

    “Ndiyo nakumbuka sasa kwanini hamjafika  naye hapa?”

    “Ni kwa sababu hatujafahamu ni kiasi gani utatulipa kwa kazi hiyo hatari!”

    “Unataka ulipwe kiasi gani?”

    “Chochote lakini kiwe kiasi kikubwa!”

    “ Sawa, nitawalipa dola millioni mbili”

    “Hakika?”

    “Huwa sidanganyi”

    “Tumemaliza, tupe wiki mbili au tatu Calorine atakuwa  mikononi mwako”

    “Kupitia akaunti gani ya benki niwalipe tangulizo la dola laki tano?”

    “Namba 01J200601293, benki ya Uingereza tawi la Trivial”

    Baada ya maongezi hayo simu ikakatwa, Kennedy aliruka juu na kushangilia, wenzake wote walimfuata kutaka kujua alichoongea na Dk. Ian, aliwasimulia kila kitu na alipofika mwisho wa maelezo yake wote walikumbatiana kwa pamoja na kujikuta wakitamka neno “Kwa heri unga na kwa heri madawa!” Kwa pesa waliokuwa wameahidiwa walikuwa na uhakika wa kuacha biashara ya unga na bado wakaendelea kuishi.

    Saa moja na nusu baadae walipiga simu ofisi za benki ya Uingereza na kuuliza kama kweli pesa iliingia. Hawakuamini masikio yao walipopewa jibu kuwa dola 500,000 tayari zilishaingia katika akaunti yao, kazi pekee iliyokuwa mbele yao ni kumteka Caroline na kumfikisha Canada ndipo wangemaliziwa sehemu ya pesa iliyobaki.

    “Kazi hii ni rahisi mno kama tulivyopanga jana, tunachotakiwa kufanya ni kucheza karata yetu vizuri bila kugundulika,  hatakiwi kabisa kuelewa kuwa sisi tumeshafahamu! Cha kufanya hapa wewe Kennedy kwa sura yako ilivyo nzuri tunakupa kazi ya kumfuatilia huyu mtoto, hakikisha  unajenga nae urafiki wa ghafla na awe mpenzi wako! Akikubali tu kuwa na wewe na kuwa anatoka naye  kwenda sehemu mbalimbali usiku au hata mchana  itakuwa rahisi sana sisi kumteka na kumpeleka hadi Canada kwa ndege ya kukodi!”

    “Lakini jambo hili haliwezi kuwa la haraka kiasi hicho, linahitaji muda zaidi!”

    “Ndiyo maana tumempa Dk. Ian wiki mbili, wewe fanya usanii wote uuwezao hakikisha mtoto anakubali!”

    “Ok, nitajaribu lakini itabidi mnikabidhi fungu la kutosha  kutanua naye ili  iwe rahisi  kumuingiza kingi”

    “Hiyo haina shida, kwa kuanzia kamata kwanza dola mia tano!” Nicky kiongozi wa kundi hilo alimkabidhi Kennedy pesa, kwa  kitendo hicho operesheni ya kumteka Caroline ilikuwa imeanzishwa rasmi!

    “Hatuhitaji kumsafirisha kwa ndege, ya nini gharama yote hiyo? Huyu ni wa kumlewesha madawa tu kisha tunatafuta cheti cha daktari kuwa ni mgonjwa wetu tunamsafirisha kumrudisha nyumbani Canada kutoka hapa Cambodia, basi! Hiyo itapunguza gharama kidogo, ndege ya kukodi itatugharimu pesa nyingi tutapunguza pesa zetu bure!” alisema O’brien kijana mdogo kuliko katika kundi lao lililoitwa Three some squad”

    Lilikuwa ni kundi la vijana wenye vipaji vya kuimba na kupiga muziki walisafiri sehemu mbalimbali duniani wakifanya maonyesho lakini mara nyingi  walisafiri  sana kati ya Pakstan na Cambodia!  Kwa kofia ya  uanamuziki walifanya biashara ya madawa ya kulevya bila kugundulika. Kennedy ndiye kijana pekee aliyekuwa na damu mchanganyiko wa Mwafrika na Mzungu katika kundi hilo, O’brien na Nicky walikuwa  Wazungu! Mchanganyiko wa rangi ulimfanya Kennedy kumvutia karibu kila msichana aliyemwona kwa kumtumia yeye walijua ni lazima tu Caroline angenasa!

    *************

    Jioni ya siku hiyo walikuwa ndani ya mgahawa wa mama Suzane ambao Caroline alifanya kazi, walikaa kwenye meza ya pembeni kabisa na muda mfupi msichana mfupi aliwafuata ili awahudumie walimkataa na kuomba waitiwe  Marione, jina ambalo Caroline alilitumia.

    “Sorry, don’t lake it badly and accept our demand! (Samahani, usituelewe vibaya na tafadhali kubali  takwa letu!)

    “Worry not, let me call her for you, a customer is always a king!” (Msiwe na wasiwasi acheni  niwaitie, mteja siku zote ni mfalme) Mhudumu alisema huku akiondoka na dakika mbili tu baadae Caroline alionekana akitembea kuelekea mezani,  alipofika aliwasalimia watu wote  kwa kuwashika mikono, wote walimwangalia kwa macho ya tamaa! Kwao tayari  Caroline alikuwa pesa! Uhai wake ulikuwa  mali lakini yeye  hakulifahamu hilo.

    “Why are you looking at me like that?” (Kwanini mnaniangalia namna hiyo?) Macho yao yalimtisha Caroline ilibidi aulize.

    “Uzuri wako! Wewe ni mzuri sana! Ni mwanamke wa kiafrika haswa! Tena hakuna mwingine kama wewe katika Cambodia!

    Badala ya kusema kitu chochote Caroline alitabasamu aliyachukulia maneno hayo kama utani, ilikuwa ni miaka mingi sana tangu aambiwe ni mzuri kwa mara ya mwisho! Mtu pekee aliyemwambia  hivyo hakuwa mwingine bali Dk. Ian! Kipindi hicho alikuwa msichana mrembo kweli kweli, kwa hali aliyokuwa nayo mahali pale aliamini aliyoambiwa yalikuwa utani.

    “What can I serve you?” (Niwahudumie nini?)

    “What do you have for dinner?” (Una chakula gani cha usiku?)

    Hapo Caroline hakujibu kitu chochote kwa sababu hakuwa na uzoefu wa vyakula vilivyouzwa mahali pale ndiyo kwanza alikuwa na siku mbili tu! Alichofanya ni kuchukua karatasi yenye orodha ya vyakula vyote na kuwakabidhi wateja wake ili wachague wenyewe, walipomaliza  aliondoka kupeleka oda yao jikoni.

    “Mnaonaje?” O’brien aliwauliza wenzake baada ya Caroline kuondoka!

    “Itakuwa kazi ngumu kidogo!”

    “Nyie niachieni mimi, si fungu ninalo mfukoni?” Kennedy alisema.

    “Ndiyo!”

    “Basi punguzeni wasiwasi!”

    ********

    Caroline hakurudi tena mpaka wakati analeta chakula mezani kwao na alisaidia kuwanawisha mikono na wote wakaanza kula, hawakutaka aondoke eneo hilo ili awe karibu nao walijaribu kufanya kilichowezekana ili awazoee, baada ya chakula Kennedy alichomoa noti ya dola mia katika pochi yake na kumkabidhi Caroline akalipe kaunta!

    Alipoondoka tu  mezani  Kennedy  na wenzake waondoka mezani mbio kwenda nje kabla hawajarudishiwa chenji! Nje  waliingia ndani ya teksi na kuondoka zao! Caroline aliporudi macho yake yalipambana na meza tupu! Alishindwa kuelewa walikuwa wapi, hakuwaona wakielekea bafuni! Mawazo yake yalimfanya afikiri walikuwa wamesahau chenji yao, alifungua mlango na kuanza kukimbia kwenda nje akiwatafuta lakini hakuwaona  ndipo  akarudi hadi ndani ambako alizikabidhi  pesa hizo kwa mama mwenye hoteli  na kumweleza kilichotokea.

    “I have their business card here!” (Ninayo kadi yao ya biashara hapa) alisema mama huyo, akaichukua kadi na  kunyanyua simu iliyokuwa mezani na kuanza kuponyeza namba ya simu aliyoiona katika kadi ya vijana wa The Three some!

    “Hallow Ken speaking!” ( Haloo Ken anaongea!)

    “Yeah, this  is mom, you forgot you change!” (Ndio, mimi ni mama! Mmesahau chenji yenu hapa!)

    “We did’nt forget, we meant it to be keep change for the girl who served us!” (Hatukusahau tulimaanisha msichana aliyetuhudumia aichukue kama zawadi yake!)

    “Thanks!” ( Ahsanteni) alimaliza mama na  kukata simu kisha akamgeukia Caroline huku akitabasamu.

    “Kumbe hawakusahau, ilikuwa zawadi yako!”

    “Oh Mungu wangu, pesa zote hiyo?”

    “Ndiyo! Hapa  hii ni  kawaida lakini chukua hizi dola hamsini na mimi nibakie na dola ishirini au?”

    “Hakuna shida mama!” aliitikia Caroline.

    Kipato cha siku hiyo kilimfanya aamini kuwa kama angeendelea kufanya kazi angeweza kupata nauli ya kumrudisha nyumbani kwao Tanzania, katika muda wa siku mbili alizofanya kazi katika hoteli hiyo alishaweka akiba ya dola tisini na nne, hiyo ilimaanisha kama angefanya kazi wiki mbili angeweza kupata hata nauli na kuendelea na safari yake!

    “Mimi hata nikifika Bombay  tu inatosha nitakuwa nimesogea mbele, nitakuwa nazidi kuikimbia mikono ya Dk. Ian zaidi, nina hakika asilimia mia mpaka sasa hajui kama nipo hapa!” Aliwaza Caroline.

    Asubuhi ya siku iliyofuata vijana hao walikuja tena hotelini kufungua vinywa vyao wakati wa kuondoka walimwachia Caroline chenji ya dola 20,  waliendelea hivyo kila siku, Kennedy alikuwa karibu sana na Caroline lakini bila kumweleza kitu chochote kuhusu mapenzi! Alishangazwa sana na hali hiyo, kwani alichojua ilikuwa si kawaida ya mwanaume kutoa msaada bila kuomba mapenzi.

    “Why are you doing all these to me?” (Kwanini mnanifanyia yote haya?) Kadri wema ulivyozidi  Caroline alishindwa kuvumilia na kujikuta akiuliza.

    “I love you and I know you’re in problems!” (Nakupenda na ninajua upo katika matatizo)

    “Who told you about my problems?” (Nani alikwambia juu ya matatizo yangu?)

    “Mom told me!” (Mama aliniambia) Kennedy alijibu na kumfanya Caroline ashangae ni kwanini mama alikuwa akitangaza siri zake! Lakini pamoja na hayo alijisifu kwa kumwambia uongo vinginevyo kama angesema ukweli siri yake yote ingekuwa nje na angekuwa katika hatari ya kukamatwa!

    “I loved my husband so much!He was my everthing and he died a bad death, infront of my eyes!” (Nilimpenda sana mume wangu na alikuwa ni kila kitu kwangu na alikufa kifo kibaya  mbele yangu!) Caroline aliongea huku akijifanya kulia ili kumficha Kennedy ukweli, alijua wazi hakuna kitu kingine ambacho kijana  huyo aliambiwa zaidi ya kuwa yeye na mume wake walikuwa wawindaji porini na mumewe alikufa kwa kukanyagwa na Tembo! Huo ndiyo uongo aliomwambia mama Suzane! Hakujua hata kidogo kuwa mtu aliyekuwa akiongea nae alifahamu kila kitu kuhusu yeye na alikuwa katika mpango mkali wa kumteka.

    “Don’t worry Marione I will help you!” (Usiwe na shaka Marione nitakusaidia)

    “Thank you, what is your name?” ( Ahsante, jina lako wewe ni nani?)

    “My name is Kennedy,  I would like you to call me Ken....This is O’brien and the one at the corner is Nicky…guys this is Marione, my friend!” (Jina langu ni Kennedy ila ningependa uniite Ken.....huyu ni O’brien na yule pale kwenye kona ni Nicky..... jamani huyu ni  rafiki yangu Marione!)  Kennedy alimtambulisha Caroline kwa rafiki zake, kila walipomwita Marione alijisikia furaha kwani aligundua hakuna mtu aliyemtambua.

    “Thank you so much for being good people to me!” (Asanteni sana kwa kuwa watu wema kwangu!) Alisema Caroline.

    Kwa siku nyingine tatu Caroline alizidi kuwaona vijana wale wakienda hotelini kula chakula na utaratibu wa Kennedy uliendelea kuwa ule ule wa kuwacha chenji ya dola 10 hadi 20 kila siku! Bila hata kutegemea Caroline alijikuta akivutiwa na Kennedy kupita kiasi,  macho yake yalianza kumwangalia Kennedy  kwa mtazamo tofauti, alianza kuuona uzuri wa sura yake! Hakutaka kwenda zaidi ya pale lakini alishindwa, alijaribu kwa njia zake zote asiende mahali moyo wake ulipotaka kwenda lakini  pia ilishindikana, Kennedy alizidi kuuteka moyo wake siku hadi siku.

    “Lakini nilishaapa siwezi kumpenda mwanaume tena maishani mwangu, eh Mungu nisaidie!” Alijisemea mwenye kichwani mwake  Caroline, alionekana kuzidiwa. Alijichukia kupita kiasi kwa tabia yake yakupenda ghafla.

    Wema  aliofanyiwa na Kennedy ulimteka kabisa, akamwona ndiye binadamu pekee mwenye moyo wa huruma aliyekutana nae katika Cambodia, moyo wake haukushtukia kitu chochote kibaya kutoka kwa Kennedy, alimwamini kupita kiasi bila kujua kilichokuwa kikiendelea kati ya Kennedy na Dk. Ian!

    “Ni huyu ndiye atanisaidia kurudi nyumbani Tanzania kwa wazazi wangu!” Hayo ndiyo yalikuwa mawazo yake.

    Kila mtu hotelini alianza kuhisi kulikuwa na kitu kilichoendelea kati ya Marione na Kennedy, hata mama mwenye hoteli alilielewa jambo hili na hakuwa na kipingamizi kwa sababu njia hiyo ilimletea wateja wengi, wasichana wote waliofanya kazi katika hoteli yake walikuwa na sura za kuvutia wateja! Kwa kufuata wasichana hawa hoteli yake iliuza chakula kingi sana kwa siku. Wakati mwingine aliwaruhusu wasichana hata kwenda kulala na wateja, hiyo ndiyo ilikuwa sifa ya mama Suzane. Hilo hata Kennedy na wenzake walishalisikia.

    “Mama ninaomba leo nimchukue Marione twende nae ukumbini akaone ninavyopiga muziki, maana yeye kila siku analala! Hachoki?” Kennedy alimwambia mama Suzane, Caroline akiwa amesimama kando yake baada ya chakula, ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu ya jioni na muda mfupi baadae alitegemea kwenda ukumbini kwenye hoteli ya kitalii ya  Triangle, ilikuwa hoteli maarufu sana katika Cambodia wakati huo..

    “Mimi sina kipingamizi na pia sina wasiwasi na wewe hata kidogo! Nyie mkielewana  inatosha ili mradi tu umrudishe mapema na salama!”

    “Hilo halina wasiwasi hata kidogo mama!”

    “Basi sawa! Au Marione unasemaje?”

    “Sawa tu mama, acha leo na mimi nikafurahie kidogo maisha!” Tayari alishaanza kuisahau tabu yake.

    “Basi nitakuja kumchukua saa tatu usiku!”

    “Sawa tu Kennedy!”

    Alipoondoka hapo Kennedy aliwaeleza wenzake juu ya mpango aliopanga na Caroline au Marione kama walivyomuita,  wote walikubaliana siku hiyo wasifanye kitu chochote kibaya ili  azidi kuwaamini zaidi, isitoshe mipango ilikuwa haijaandaliwa vizuri! Kweli siku hiyo Kennedy alimchukua Caroline na kwenda naye hadi ukumbini ambako walicheza muziki pamoja,  alimrudisha salama salimini  saa saba ya usiku! Kwa kitendo hicho  imani ya Caroline kwa Kennedy ilizidi kuongezeka taratibu,  katika muda wa wiki moja tu akawa hasikii wala haambiwi kwa Kennedy!  Lakini pamoja na hali hiyo bado hakuwa tayari kueleza ukweli kuhusu maisha yake!

    ***********************

    Siku tatu baadae mipango ya  kumteka Caroline na kumpeleka Canada iliandaliwa, cheti cha daktari kuonyesha kuwa alikuwa mgonjwa kiliandaliwa, dawa za usingizi ziliwekwa tayari na ujanja ulifanyika tiketi ya ndege ikakatwa bila hati ya kusafiria ya Caroline kuonyeshwa, pesa iliongea.

    Dk. Ian alitaarifiwa  kila kitu juu ya ujio wa Caroline na alikaa mkao wa kula akimsubiri kwa hamu, aliwaambia vijana wake wapunguze mateso kwa Profesa Kadiri na mkewe Cynthia kwa sababu mtoto wao alishapatikana, wazazi wa Caroline walikuwa katika hali mbaya nchini Canada ingawa yeye Caroline hakuwa na habari juu ya jambo hilo aliendelea kuamini walikuwa nchini Tanzania na alikuwa na hamu kubwa ya kuwaona.

    Kwa upande wake Dk. Ian kila kitu kilikuwa tayari kisubiri ujio wa Caroline, kila kitu kilikuwa tayari, shimo la kaburi lake lilishaandaliwa! Bunduki yake ilishajazwa risasi ishirini zikimsubiri Caroline afike!  Zote zilitegemewa kuusambaza mwili wake tena kwa mkono wa Dk.Ian mwenyewe.

    *************

    “Marione when are you off duty?” (Marione unapumzika lini kazi?)

    ‘Me?” (Mimi!)

    “Yeah,”(Ndiyo!)

    “Every Saturday!” (Kila Jumamosi!)

    “Do you like skiing?” (Unapenda kuteleza kwenye barafu?)

    “Very much, but have never tried it!” ( Sana lakini sijawahi kujaribu)

    “Why can’t you come with us to the virginia mountans where we shall be going for skiing next Saturday?” (Kwanini tusiende na sisi kwenye milima ya Virginia ambako tutakwenda kuteleza kwenye barafu?)

    “I would love to!” (Ningependa kwenda!)

    “No  problem you come with us!” (Hakuna tatizo tutakwenda wote)

    “But speak to mom first!” (Lakini ongea na mama kwanza!)

    Kennedy alipoongea na mama Suzane hapakuwa na kipingamizi chochote, Caroline alibaki kuisubiri siku ya Jumamosi kwa hamu kubwa! Tangu siku hiyo ya Alhamisi  siku zilikwenda taratibu  kupita kiasi, alitaka  hiyo ifike upesi ili aende na kustarehe na Kennedy kwenye barafu! Hakuelewa kitu chochote kilichoendelea, tayari alishaanza kuingia katika mapenzi na Kennedy, kuna wakati hata yeye mwenyewe alijishangaa ni kwanini ilikuwa rahisi  kwake kumwamimini mtu kiasi hicho!

    *********

    Ndege ilitegemewa kuruka kutoka   uwanja wa ndege wa Penh kuelekea Canada  saa tisa na nusu alasiri, kila kitu kilishawekwa tayari, aliyekuwa akisubiriwa ni Caroline peke yake! Ilipogonga  saa saba na nusu  honi ya gari ililia mbele ya nyumba  waliyoishi wafanyakazi wa mama Suzane, asubuhi ya siku hiyo Caroline alijiandaa tayari kwa safari ya kwenda milimani.

    “Marionneeeeeee!” Aliita msichana aliyekuwa nje!

    “Yees!”

    “Ken is here!’ (Keni amefika!)

    “I’m coming!” (Ninakuja!) aliongea huku akikimbia kushuka ngazi, hakutaka kumchelewesha Kennedy! Hakutaka kuonekana mtu asiyepangilia muda wake.

    “What should I bring you when I come back!” (Nikuletee nini nikirudi!) Caroline alimuuliza mfanyakazi mwenzake aliyekuwa nje.

    “Flowers” (Maua!), jina la msichana huyo aliitwa Flora na alipenda  maua kama lilivyokuwa jina lake, hasa ya rangi nyekundu.

    “I will do that!” Caroline alionekana mwenye furaha kupita kiasi, alionekana kama mtu  aliyeishi Cambodia kwa miaka kumi, wakati alikuwa na wiki moja na siku chache tu! Wasichana wenzake walimwonea wivu kupata mvulana mzuri kama Kennedy aliyempa maraha yote yaliyohitajika! Caroline aliteremka mpaka mahali lilipoegeshwa gari la Kennedy! Siku hiyo tofauti na siku nyingine zote aliachiwa kiti cha mbele ambacho mara zote alikikalia Nicky! Kennedy alikuwa akiendesha, Caroline aliiona hiyo kama heshima kubwa kwake, aliwasalimia wote na kukaa kitini, akafunga mlango na baadae mkanda, gari likaondoka.

    “Thank you for treating me like a queen!” (Ahsante kwa kunifanya Malkia) gari ilianza kuondoka kwa mwendo wa taratibu, Caroline alitoa mkono na kumpungia  Flora, aliyesimama nje akimwangalia kwa jicho la husuda!

    “See you later!” (Tutaonana baadae!) Alisema Caroline wakati gari likiondoka.

    “How are you today Caroli….aahgh! Marione!” (Unajisikiaje leo Carol…..aahgh! Marione?) Kennedy aligundua alilofanya  lilikuwa kosa kubwa, hata alipojaribu kurekebisha tayari alishachelewa, aliuona uso wa Caroline ukipauka ghafla, alionekana kama mtu aliyepokea habari za kifo..

    “Mh!” Caroline aliguna lakini hakusema kitu chochote, kilichoendelea kichwani mwake ni msululu wa maswali juu ya namna gani Kennedy alilifahamu jina lake halisi wakati yeye alishajitabulisha kama Marione! Wakati akiwaza hayo, gari likiwa limetembea  umbali wa kama kilometa tano hivi, alishutukia akiguswa na vitu kama midomo ya chupa katika kila upande wa shingo yake, aligeuka ili aone ni kitu gani kilimgusa macho yake yalikutana na mdomo wa miwili ya bastola.

    “Tulia hivyo hivyo wala usifanye vurugu, vinginevyo utakufa!” Zilikuwa sauti za  Nicky na  O’brien.

    “Ha! Kennedy vipi tena?”

    “Tulia usifanye fujo, kunguni we! Unadhani wema wote uliofanyiwa ulikuwa wa bure?”

    Caroline alibaki mdomo wazi kwake ilikuwa kama ndoto!

    “Kwa hiyo mnakwenda kunibaka?”

    “Akubake nani? Hii ni safari ya kwenda Canada kwa mumeo!”

    Mwili wote wa Caroline ulikufa ganzi, alitamani ardhi ipasuke aingie ndani yake.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog