Search This Blog

Monday 24 October 2022

FEDHEHA - 1

 http://pseudepigraphas.blogspot.com/2019/12/fedheha.html

    IMEANDIKWA NA : AHMED MNIACHI



    *********************************************************************************





    Simulizi : Fedheha

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    MAUAJI



    James Makabi alishangazwa na kitendo cha mtu mwenye kofia kubwa ya pama kumfuatilia kwa namna ya kuvizia. Mwanzo hakuwa na wazo lolote juu yake lakini akashangazwa na kitendo cha kiumbe huyo mrefu kupita kila anapopita. Wasiwasi ulianza kumuingia baada ya kugundua kuwa jamaa huyo alikuwa makini na hakutaka kabisa James agundue kuwa anafuatwa. Kila alipogeuka nyuma James alimshuhudia yule mtu akijifanya aidha kununua bidhaa, kuongea na simu au hata kujikuna pale alipokosa kisingizio cha haraka.

    Akaamua kubadili njia na kufuata barabara inayoelekea mtaa wa Kongo. Baada ya kutembea dakika kadhaa bila kumuona yule mtu akaamini kuwa alikuwa na wasiwasi wa bure. Akaamua kupita kichochoro kidogo ambacho kinatokea mtaa wa Lindi.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jua lilikuwa limepoteza ukali pia nuru yake ilianza kufifia, likafanya rangi ya kaa la moto, rangi ile ikaambukiza hata vidimbwi vidogo kwani navyo vilibadilika na kuwa na rangi hiyo. James akapiga hatua zaidi huku akielekea kituo cha daladala kilichoko mtaa wa Lindi.

    Akasimama pale kwa muda akisubiri gari linaloelekea Kiwalani. Akiwa ameegemea nguzo ya jengo moja ambayo kwa upande mwingine iliegemezwa meza ya kuuzia magazeti mara akaliona gari lenye ufito wa kijani ubavuni. Akaungana na abiria wengine ambao walikuwa wanatimua mbio bila shaka ikiwa ni kwa lengo la kuwahi sehemu ya kuketi.

    Akiwa miongoni mwa abiria waliokosa siti akashika bomba la juu ambalo watu wote waliosimama walikuwa wamelishika.

    “Oyaa, kaka mkubwa mwenye shati jeupe hapo geuka upande wa pili,”alipiga kelele konda huku akimnyooshea kidole James ambaye hakusita kugeuka. Alipogeuka ndipo alipopatwa na mshtuko wa mwaka! Yule mtu ambaye dakika kadhaa zilizopita alikuwa anamkimbia alikuwa amekaa siti ya nyuma kabisa akisoma gazeti.

    Kwa kasi ya aina yake James akajitoa kwenye msitu wa watu na kushuka kwenye gari.

    “Hawa wengine wezi tu,” alilalamika mmoja wa abiria ambaye alionekana kukerwa na kitendo cha James huku akiungwa mkono na abiria kadhaa, ambao walirusha maneno mawili matatu ya kashfa.

    “Abiria jikagueni kama kila mmoja simu yake ipo.” Aliongeza konda

    “Aaa, amechemsha huyo naona anatafuta sehemu nyingine.....” Mjadala ukaendelea zaidi ya hapo kama kawaida ya mijadala ambayo huibuka kwenye daladala.

    Akatembea haraka haraka akielekea mtaa wa Kipata, mara kwa mara alikuwa anageuka nyuma kuangalia kama bado anafuatwa na yule mtu mwenye kofia ya pama, hakumuona. Hilo la kutomuona bado halikuweza kumuondolea hofu na wasiwasi aliokuwa nao. Lakini nini hasa kilimfanya aingiwe na hofu? Ghafla alijiuliza swali ambalo lilimfanya asitishe mbio zake hizo. Kama gerezani alishaachiwa kwa msamaha wa Rais, haiwezekani aingiwe na hofu wakati hana kosa, akapiga moyo konde na kutafuta kituo kingine cha daladala.

    Alijidanganya, alijidanganya sana kwani mawazo juu ya mtu yule mwenye kofia ya pama yaliendelea kumtesa. Kwanini anaviziwa? Lazima kuna jambo si la kawaida! Ni jambo gani? Alijikuta akipata wakati mgumu kwa maswali yasiyo na majibu. Huku akiendelea kutafakari akajikuta akikabiliana na giza ambalo lilishatanda maeneo mbalimbali ya jiji.

    Baada ya kutembea kwa muda mrefu huku akiwa hana uelekeo maalum aliamua kurejea tena eneo la Suwata lililoko mtaa wa Lindi ili apande gari linaloelekea Kiwalani. Akafika eneo hilo na kukuta kukiwa na abiria wachache jambo lililomshangaza. Akatoa simu yake aina ya siemens na kuangalia muda, “Khaa!” Akashtuka baada ya kukuta kuwa ni saa nne kasorobo.

    “Bila shaka Tamasha atakuwa amechoka kunisubiri, labda ajue nilipouficha funguo,” alijikuta akiwaza kabla hajaingia kwenye daladala.

    Akaileta tena kichwani picha ya mtu yule mwenye kofia ya pama. Ni mtu mrefu, mpana kiasi mwenye kutembea kwa umadhubuti, hata mwili wake ulionesha kuwa ni mtu madhubuti. Uso wake ambao hata akiwa mbali haukustahimili kuficha weusi ulikuwa umezungukwa na sharubu zilizofuatiwa na ndevu zilizopunguzwa kwa ustadi. Wakati ule anamfuata James na hata pale alipokuwa anasoma gazeti bado hakudiriki kubandua mawani yake nyeusi.

    Akiwa kwenye siti ya nyuma kabisa ya gari hakuacha kuikagua kila siti kwa macho, pia kila abiria aliyeingia alihakikisha kuwa anamuona. Akaridhika baada ya konda kujitoma ndani ya gari huku akifunga mlango. Gari likaondoka huku akiwa ameondokewa kabisa na hofu ya mtu yule mrefu mwenye kofia ya pama. Akajikuta akirudiwa na furaha yake ambayo ilipotezwa na mtu yule mkakamavu.

    Saa nne na robo (4.15) daladala likasimama maeneo ya Kijiwe samli. James akateremka huku akijilaumu kwa kuchelewa nyumbani kwa sababu za kipuuzi. Alijiona mjinga baada ya kuona amemuogopa mtu kwa kuhisi anamfuatilia. Hata kama angekuwa anamfuatilia bado alijiona kutokuwa na sababu ya kumuogopa kwani hata macho yalihukumu kuwa yule ni mtu mkwasi. Mavazi yake peke yake yangeweza kuwa mtaji wake wa biashara ndogondogo. Yule mtu alikuwa amevaa suti ya kijivu ambayo ni ya gharama kubwa. James aliwahi kuona suti kama hiyo ikiuzwa kwenye duka fulani mitaa ya samora kwa bei ambayo ni mara nne ya kiwango cha juu cha mshahara wa mwalimu. James akajikuta akijilaumu maradufu kwa kitendo cha kumuogopa mtu yule.

    “Wakati mwingine woga unaweza kukufanya uipige ngwara bahati bila kutarajia”, aliwaza huku akijihisi kuipiga teke bahati.

    Akajishangaa mwenyewe baada ya kutanabahi kuwa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ameanza kuingiwa na woga. Kwanini amejikuta anamuogopa mtu ambaye hamfahamu? Mbona alipokuwa gerezani alikutana na watu wakorofi na wabaya sana lakini hakuwahofia na mara chache alipambana nao kitu kilichomjengea heshima na kuogopwa ndani ya gereza.

    Hakuwahi kuogopa kwenye maisha yake kama alivyoogopa ile siku aliyosimama mbele ya jaji kwa kosa la kusababisha ajali ambayo iliua makumi ya watu. Aliikumbuka vema siku hiyo kwani alikuwa anaendesha basi la abiria lililokuwa linatoka Dar es salaam likielekea Handeni huko Tanga. Hakukusudia kusababisha ajali hiyo na wala halikuwa kosa lake, kosa lilikuwa la muheshimiwa waziri wa Nchi, umaskini na majanga ambaye alikuwa anaendesha mwenyewe badala ya dereva wake tena akiwa amelewa chakari. Kesi iliposikilizwa waziri akashinda! Ni kawaida kwa nchi za kiafrika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yamepita........

    Akatembea taratibu akiupita ukumbi maarufu wa starehe unaojulikana kama Koyanga. Akaelekea mbele kidogo huku akisindikizwa na muziki nzito uliokuwa unasikika kutoka kwenye ukumbi huo wa starehe. Akakatisha kwenye kichochoro kidogo ambacho kilikuwa kinatenganisha baa ya Koyanga na nyumba iliyopakana na ukumbi huo.

    Baada ya kumaliza kile kichochoro akatembea hatua kama kumi, akaibukia mtaa mwingine na baada ya kuangalia upande wa kulia aliweza kuiona nyumba yake. Ilikuwa kama hatua thelathini za mtu mrefu kufika kwake. Mwenyewe hakuiita nyumba, alipenda kuita banda. Ilikuwa na chumba kimoja na sebule tu, wakati anakaribia kukamilisha chumba cha pili ndio akapatwa na balaa la kukamatwa baada ya ajali hiyo ya gari.

    Kwa mbali aliweza kuiona taa ya nje ikiwaka, akafurahi baada ya kubaini kuwa Tamasha atakuwa ameziona funguo pale zilipo. Akaufanya mwendo wake kuwa madhubuti zaidi huku akijisikia furaha moyoni. “Ndiyo maana nampenda huyu binti ana akili sana,” aliwaza James huku akihisi kama umbali wa nyumbani kwake umeongezeka kutokana na shauku ya kuonana na Tamasha. Alimpenda.

    Tofauti na matarajio yake, Tamasha alikuwa nje akihangaika na mapishi. Hakuna kizuizi kilichozuia macho ya James kuona jinsi kuku mkubwa aliyenona alivyojaa kwenye sufuria akiandaliwa. Hili likamshangaza kiasi kwani ndani hakuacha hata shilingi mia, kama si kuogopa kuonekana mtu aliyekosa ustaarabu angeuliza,

    “umempata wapi huyu kuku!?” Hakuuliza, alimpenda na kumuamini Tamasha. Alifahamu wazi kuwa lazima ataelezwa wapi alikompata kuku yule wa kienyeji katika wakati huu ambao wakazi wengi wa jiji la Dar es salaam wanakula miguu, utumbo na vichwa vya kuku.

    “Waooooh, karibu mpenzi,” Tamasha alimlaki mpenzi wake kwa furaha.

    “Oh, Ahsante dear, yaani ndo unaanza kupika saa hizi si ungepumzika tu!”

    “Ningeweza kupumzika kama si huyo mjomba aliyeko ndani, kuku kaja naye mwenyewe........” James akamkatisha kwa swali la haraka.

    “Mjomba! Mjomba gani?”

    “Haraka ya nini mpenzi, we ndiye unaetakiwa kunitambulisha kwake. Si uingie ndani ukamuone kakaa muda mrefu sana anakusubiri.”

    Moyo wake ukapiga mlipuko wa hofu, akasahau kuwa walikuwa hawajasalimiana na Tamasha, hakujali kusalimiana kwani akili yake yote ilikuwa huko ndani kwa mtu aliyejitambulisha kama mjomba. Haraka haraka akajitoma sebuleni ili kumuona mjombake aliyekuja na kuku wa kienyeji.

    “Paah.” Moyo wake ulilipuka baada ya kumuona mtu mkakamavu mwenye kofia ya pama akiwa amekaa kwenye kochi kama nyumbani kwake.

    “Ooh! Karibu sana bwana James Makabi!” Aliongea yule mtu kwa sauti ya ujivuni.

    Alijikuta akishindwa kuongea lolote na kukaa kwenye kiti kilichoelekeana naye. Yule mtu akasimama na kumsogelea James kisha akampa mkono.

    Kwa moyo uliojaa hofu James akaupokea mkono ule,

    Jambo jingine!

    Ulikuwa mkono mgumu uliojaa ukakamavu kwelikweli.

    “Habari yako bwana James,” alisalimia mtu yule mkakamavu mwenye kofia ya pama.

    “Aah! Salama mjomba,” alilazimisha tabasamu baada ya kumuona Tamasha anaingia ndani, hakutaka mpenzi wake atambue walakini uliopo.

    Akaitumia fursa hiyo kuusanifu mwili wa yule jamaa kwa haraka.

    “Dear, naomba uende hapo Koyanga ukachukue soda kwa ajili ya mjomba.......”akakohoa kidogo kisha akaendelea

    “......muulize kwanza atakunywa soda gani?”

    “Aah, mjomba alishakataa soda, tena kakataa hata chakula kasema hata nikiandaa yeye hatakula kwani amekuja kwa ajili ya mazungumzo tu!” Alimaliza Tamasha.





    “Ok, basi hakijaharibika kitu.”

    “Mi naondoka, hiyo mboga nitakuja kumaliza kutengeneza asubuhi.”

    “Leo hulali hapa?”

    “Leo ngumu dear si nilishakuambia nataka nimsindikize shangazi stendi kesho anaenda Mwanza?”

    “Oh, nilisahau dear.”

    “Kwa heri mjomba.”

    “Ahsante wasalimie nyumbani.”

    Baada ya Tamasha kuondoka yule mtu mrefu aliyevaa kofia ya pama akamgeukia James.

    “Naitwa Mjomba Masharubu..........”



    * * *

    JOHN OSCAR alitembea taratibu kuelekea ofisi ya mhariri mkuu wa gazeti la MUUNGWANA. Alikuwa ni kijana mwenye kimo na mwili wa wastani. Alivaa shati jeupe, suruali nyeusi na viatu vyeusi ambavyo vilikuwa vimeng’arishwa vema kwa dawa. Alikuwa na mwaka mmoja tu kwenye fani ya uandishi wa habari, hii ilikuwa ni baada ya kuachishwa kazi jeshi la polisi ambako alitumikia kwa miaka mitano na kisha kutimuliwa kazi baada ya kutokea kashfa ya kutoroka mahabusu kwenye kituo alichokuwa anafanyia kazi. Hakuhusika na utorokaji huo na wala hakuwa kazini siku ya tukio, lakini msamiati wa dhana ya uwajibikaji ukamfanya yeye pamoja na askari wenzie wa kituo hicho kufukuzwa kazi bila kujali walikuwa kazini au vinginevyo. Panga hilo liliwakuta askari wa vyeo vya chini.

    Kufukuzwa kwake haukuwa mwisho wa maisha, ndipo akaamua kujiunga na chuo kimoja kinachotoa kozi za jioni za uandishi wa habari. Baada ya kumaliza kozi yake kwa ngazi ya stashahada ndipo akapata ajira ya muda kwenye gazeti hilo ambalo halikuwa na umaarufu mkubwa. Alikuwa mchapakazi nzuri kiasi ambacho alipendwa na mhariri mkuu wa gazeti hilo huku akichukiwa na baadhi ya waandishi ambao waliona wanaanza kupokwa umaarufu na heshima zao. Hata hivyo zilikuwa ni chuki ndogo na za chinichini ambazo hakuzitilia maanani.

    “Habari Jesca!” Alisalimia huku akiingia ofisi ya mhariri mkuu.

    “He, kaka John mbona juu juu! Hata hutulii tukasalimiana vizuri?” Alisikika Jesca.

    Hakujibu badala yake aliingia ndani moja kwa moja.

    Ofisi ya mhariri mkuu ilikuwa ndogo yenye mandhari ya kuvutia. Ndani kulikuwa na viti vinne kimoja ndani ya mkunjo wa meza ya nusu duara ambacho alikaa mhariri mkuu, kimoja kilikuwa mbele kabisa karibu na meza huku viwili vikiwa nyuma kama hatua tatu kutoka kile kilichotangulia.Pembeni kulikuwa na kabati kubwa la chuma lenye rangi ya fedha lililosheheni vitabu vya aina mbalimbali. Ukutani kulikuwa na kalenda mpya ambayo ilikuwa na picha za viongozi mbalimbali wa chama na serikali. Kama zilivyo ofisi nyingi za wahariri hii nayo ilikuwa na ngamizi ya kisasa aina ya Hp Compaq yenye sikrini bapa huku kukiwa na kicharazio cha rangi ya fedha ‘keyboard’http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    John alilakiwa na ubaridi mkali uliotokana na kiyoyozi ambacho kiliwekwa namba ya juu kulingana na afya ya mhariri huyo ambaye hupendelea hali hiyo ya hewa. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuitwa na mhariri mkuu. Haikuwa mara ya kwanza kuingia ofisi hiyo, alikuwa anaingia mara kwa mara siku ambazo nafasi hiyo hukaimiwa na mhariri mkuu msaidizi ndugu Gideon Masatu ambaye alipenda sana kumtumia John kwenye kazi nyingi. Akamsalimia mkuu wake huyo wa kazi kabla ya kukaa kiti kimoja cha nyuma miongoni mwa viti vile viwili.

    “Oh, karibu ndugu John, keti hapo mbele usiwe na wasiwasi,” aliongea ndugu Kasim Jamali mhariri mkuu kwa sauti iliyojaa uchangamfu.

    “Ahsante mzee, shikamoo.”

    “Marahaba, tafadhali keti.”

    “Ahsante.”

    Akaketi na kumkazia macho mkuu wake wa kazi.

    Mzee Kasim alikuwa na kimo cha wastani ingawa unene ulimfanya aonekana kuwa mfupi. Kichwa chake kilikuwa kimesheheni nywele nyingi ambazo zilikuwa na mvi kiasi. Alikuwa anakaribia miaka sitini na mitano lakini bado alikuwa na afya madhubuti tofauti na wazee wa hirimu yake.

    Alikuwa amevaa kaunda suti nyeusi ambayo ilimkaa vema na kumfanya avutie.

    John, aliendelea kukaa kwa utulivu huku akisubiri alichoitiwa kwa shauku kubwa. Mhariri aliinua kichwa chake na kumkazia macho John. Kabla ya kuongea chochote akavuta saraka lililokuwa kwenye meza yake, akatoa kalamu na karatasi kisha akaanza kuongea bila kuandika chochote.

    “Ndugu John Oscar, ninayo furaha kubwa kukufahamisha kuwa ofisi yetu imekuchagua kwenda kwenye mkutano wa chama tawala cha MMD utakaofanyika makao makuu yake yaliyoko Magomeni.” Akatulia kidogo kisha akaendelea “… Hii ni nafasi kubwa na ya kipekee ambayo umepewa kutokana na umahiri wako katika fani hii pia ukiwa na sifa ya ziada ya kuwa mpigapicha nzuri. Nimekuita hapa kutokana na unyeti wa shuguli yenyewe na kile unachotakiwa kukifanya.” Akatulia na kumeza mate kabla ya kundelea tena.

    “… Kitu cha kwanza kuwa mwangalifu sana na aina ya picha utakazopiga, hakikisha unapata picha za maeneo yenye watu wengi na yasiyo na mianya. Tunapopiga picha za chama tawala hatutakiwi kuonesha nafasi zilizo wazi, hii ni kinyume kwa picha za vyama vya upinzani ambazo unatakiwa kupiga picha maeneo yenye mianya na watu wachache, hii hutuongezea heshima mbele ya serikali.” Akatulia tena na kumkazia macho John.

    “Nafikiri umenielewa.”

    “Sawa mkuu nimekuelewa.”

    “Hicho kipengere cha namna ya kupiga picha za chama tawala ndicho nilichokuitia, maagizo mengine utapewa na ndugu Masatu.”

    Akainuka kwenye kiti na kupeana mikono na mkuu wake wa kazi kabla hajaondoka ofisini humo.

    Akafungua mlango na kuingia kwenye chumba kidogo cha katibu muhutasi.

    “Sorry Jesca unajua nilikuwa na hofu ya kufukuzwa kazi ndiyo maana sikukusalimia vizuri wakati naingia.”

    “ha ha ha ha!” Akacheka kwa nguvu Jesca ukiwa ni ujanja wa kulazimisha jino lake la dhahabu lionekane. Alifanikiwa, maana Macho ya John yalitua kwenye jino hilo lenye mng’ao wa kipekee.

    “Vipi kulikuwa na usalama huko ndani?” Aliuliza Jesca.

    “Aaah, ni mambo ya kawaida tu, ni kuhusu mkutano mkuu wa MMD mwezi ujao.”

    “Hongera, nasikia kuna posho nzuri kule.”

    “Inatolewa na ofisi?”

    “Ofisi inatoa, pia chama nacho kinatoa chochote kwa vyombo vya habari ambavyo ni rafiki wa chama.”

    “Vyombo vya habari rafiki wa chama!!” Alistaajabu huku akiondoka eneo hilo.

    *****

    II



    “..... Huna sababu ya kuniogopa mimi ni mtu mwema, tena mwema sana kwako!” Aliongea Mjomba Masharubu kwa sauti nzito lakini yenye utulivu mkubwa huku akilazimisha upole ambao hakuwa nao.

    “Pamoja na wema wako kitendo cha kunifuata kwa kunivizia kimenipa hofu sana, pia nimeshangaa kwa jinsi ulivyoweza kupafahamu nyumbani kwangu na hata jina langu wakati mimi ndio mara ya kwanza nakuona!” Kwa sauti nzito Mjomba akacheka kidogo na kumkazia macho James.

    “Usiwe kama mtoto James, sio kila unayemfahamu anakufahamu na sio kila anayekufahamu unamfahamu, kuna watu wanaweza kukufahamu zaidi ya unavyojifahamu!” Akatulia tena na kufuta uso wake kwa kitambaa hku akibandika sigara mdomoni mwake kabla hajatoa kiberiti kidogo cha gesi.

    Pamoja na kauli hiyo nzuri ya kusisimua bado hakufanikiwa kuondoa mshangao katika nafsi ya James. Hapo kabla alimuogopa sana Mjomba, lakini muda huo akajikuta akiwa na shauku ya kutaka kujua mengi kuhusu mtu huyo pamoja na huo wema wake ambao amejisifu kuwa nao.

    “ James, Mimi nafahamu kuwa wewe ni dereva nzuri sana na umetoka gerezani hivi karibuni, kwa msamaha wa Rais kwani kifungo chako kilikuwa ni miaka mitano…..” akakohoa kidogo na kuvuta sigara yake funda tatu kwa utulivu mkubwa zaidi kama anayetafakari neno la kuongea kasha akaendelea,“..... Kutoka kwa msamaha wa Rais si jambo rahisi kama unavyofikiria ni lazima ufanyiwe mipango, mimi ndiye niliyekufanyia mpango mpaka ukapewa msamaha wa Rais.” Akatulia kidogo na kumpa nafasi ya kutafakari ujumbe huo mpya kabla ya kuendelea. Akainua macho na kumtazama Mjomba Masharubu usoni. Akakumbuka kitu! Alimuona siku ya kufunguliwa kwake lakini hakumtilia maanani, Mjomba hakuonesha dalili yoyote ya kuhusika kwake na msamaha huo.

    “Nafikiri unafahamu kuwa mambo ya hapa mjini ni kusaidiana, hivyo nami pia nimekuja kwako naomba msaada wako.”

    “Msaada upi ambao unahitaji kutoka kwangu?” Aliuliza James huku akiwa amepungukiwa na hofu iliyomtawala muda mfupi uliopita.

    “Kuna kijikazi kidogo nataka unisaidie, hata hivyo kutakuwa na bakhshishi nitakupa.”

    “Nafikiri ni bora unitajie hiyo kazi ili kupunguza dukuduku langu.”

    “Usijali ni kazi ndogo sana, ukishamaliza hiyo kazi kuna bakshishi ya nyumba, gari, shamba na pesa taslimu milioni mia mbili na hamsini”

    Akatumbua macho na kumtazama Mjomba Masharubu kwa mshangao huku nafsi yake ikiwa njia panda kama amuamini mtu huyo au vinginevyo.

    “Mia mbili hamsini milioni?” Aliuliza akitaka uhakika wa alichokisikia.

    “Usijali ni pesa ndogo sana hiyo, fedha ninazo hata nikitoa hicho kiasi ni kama sijapunguza chochote.”

    “Kazi gani?” Aliuliza tena James.

    “Utaifanya?”

    “Kwa kiasi hicho niko tayari kufanya kazi yoyote isipokuwa ushoga.”

    “Ha ha ha haaaaaaa..” Kwa mara ya kwanza tabasamu likachanua katika uso wa Mjomba Masharubu.

    “Unataka kuijua kazi yenyewe?”

    “Bila shaka, nawe unafahamu hilo”

    “Ok, kwanza chukua namba yangu ya simu ili ukikamilisha hiyo kazi uweze kunitafuta kwa ajili ya malipo yako,”

    “Poa, ngoja niisevu kwenye simu yangu.”



    * * *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ndani ya ukumbi wa KBT viongozi na wajumbe mbalimbali wa chama tawala MMD walikuwa wamekusanyika tayari kwa tukio maarufu ambalo linajulikana kama NATANGAZA NIA. Tukio hili hufanyika baada ya Katibu mkuu wa chama kupokea majina ya wanachama wote wenye nia ya kugombea uraisi. Hutajwa jina moja moja kisha mgombea hupewa nafasi ya kuthibitisha kwa mdomo kuwa ni kweli ameamua kuwania nafasi ya kugombea uraisi kupitia chama hicho, pia hupewa nafasi ya kuzungumza mawili matatu kwa wanachama wao, baada ya hapo huzinduliwa kampeni kwa wagombea ambao hupita mkoa hadi mkoa wakitafuta kuungwa mkono na wajumbe wa mkutano mkuu kwenye hatua ya mwisho .

    Ukumbi ulikuwa umepambwa kwa bendera za chama zenye rangi nyeupe na nyekundu huku katikati ya bendera kukiwa na alama ya msumeno. Nyimbo mbalimbali za kukisifu chama ziliimbwa, wanachama walionekana kuwa na furaha sana huku wakiwa wameficha hofu nzito katika nyoyo zao kwa kutojua nani atachukua hatamu ya kuongoza nchi na chama. waliita utaratibu huu kuwa mbio za kupokezana vijiti. Ni utaratibu ambao ulileta hofu kubwa kwani kila mmoja alikuwa na chaguo lake huku wengine wakitarajia vyeo iwapo Yule waliyempenda angebahatika kupata uongozi.

    Mijadala ya hapa na pale iliendelea huku kila mwananchi akijaribu kueleza hisia zake za nani anatamani awe mgombea wa chama hicho kikubwa chenye nguvu. Kuna wale ambao hawakuwa na makundi wao walikuwa wasikilizaji tu, hawa kwa kiasi kikubwa walikuwa ni wale wanaoangalia utendaji bora wa mtu atakayeteuliwa. Pamoja na mijadala hiyo yote hakuna aliyekuwa na uhakika nani na nani watagombea kutokana na usiri mkubwa uliogubika zoezi hilo. Yako baadhi ya majina ambayo yalitajwa tajwa lakini bado uhakika ulikuwa mdogo.

    Ghafla, lango kuu likafunguliwa



    Ghafla, lango kuu likafunguliwa msafara wa viongozi waandamizi wa chama na serikali ukaanza kuingia. Ulinzi mkali ulikuwa umeongozana na msafara huo. Nyimbo za chama zikaanza kuimbwa shangwe na vigeregere vikahanikiza ukumbi, mayowe na mbinja vikachukua nafasi yake. Mwanamuziki maarufu wa bendi ya chama Alex Kilaza akaanza kutumbuiza nyimbo mbali mbali na kuwafanya wanachama walipuke kwa nderemo na vifijo.

    Baada ya muda kelele zikapungua na watu wakaanza kukaa kwenye nafasi zao. Zikaanza hotuba mbalimbali za viongozi wastaafu wa chama na serikali, nyingi zikisifu kukua kwa uchumi na kuondoka kwa umaskini bila kusahau mikakati ya muhula unaokuja pindi kitakapoingia madarakani,baada ya hapo ikafuata nafasi ya Katibu mkuu kusoma majina ya watu walioweka nia ya kugombea uraisi.

    “MMD hoyeeee, Ushindi upooooo, Wapinzani kwishaaaa.”

    “Kwishaaa, kwisha kabisa chinjia baharini….” Walijibu wajumbe kwa maneno ambayo yalionekana kama yanaimeza demokrasia.

    “Ndugu wanachama, mashabiki, wakereketwa na wafurukutwa; MMD hoyeee!”

    “Hoyeeeeeeeee.” Sauti iliyochanganyika na mbinja ilirindima ukumbini.

    Akaanza kwa kuwasalimu kama ilivyo ada kisha akaongea maneno kadhaa ya kujitapa kisiasa, baada ya hapo ukafika wakati ambao wengi walikuwa wanausubiri kwa hamu kubwa.

    “............. Na sasa ni ule muda muafaka ambao tulikuwa tunausubiri kwa hamu kubwa.” Makofi, vigeregere na mbinja vikaongezeka, ukumbi ukahanikizwa kwa mbinje na mayowe.

    Baada ya kutulia katibu akaendelea. “......... waliojitokeza kuwania nafasi hiyo safari hii ni watano.” Ukumbi ukarindima tena kwa kelele na vifijo.

    “wa kwanza ni Bw.Gideon Kulindwa.” Makofi na vigelegele vikatawala tena kisha kukawa kimya. Tunamuomba asimame na kuthibitisha nia yake huku akiisindikiza kwa maneno mawili matatu, dakika tano tafadhali......” Baada ya kuzungumza na kupigiwa makofi kama yule wa kwanza wakafuata wengine watatu nao hawakuwa na tofauti kubwa na yule aliyetangulia.

    “....... Watano na wa mwisho ni Mheshimiwa Oscar Ole Nunga.” Hapo ukumbi ukalipuka kwa vifijo na nderemo. Ukumbi ukachangamka zaidi kuliko wakati wowote. Tabasamu likaonekana wazi katika wajihi wa mheshimiwa Ole Nunga. Hata pale alipomaliza kuongea bado shamra shamra ziliendelea. Shamra shamra hazikuishia hapo bali hata majumbani nako kulikuwa na shamrashamra kwani watu wengi walikuwa na imani na mheshimiwa huyo. Wengi walikuwa kando ya viredio vyao wakisikiliza mkutano huo ambao ulikuwa unarushwa moja kwa moja na kituo cha redio cha Taifa na baadhi vya watu binafsi na vile vya chama.

    Mkutano ukafungwa watu wakatawanyika ili kuwapa nafasi wagombea hao kuanza kampeni kabla ya kupatikana mmoja ambaye atakiwakilisha chama kwenye nafasi ya mgombea urais.



    * * *

    Akiwa amevaa fulana maalum nyeupe iliyokuwa na maandishi ya njano kifuani ikimtambulisha kuwa mwandishi wa gazeti la Muungwana, John Oscar aliamua kutoka ndani ya ukumbi ili apate picha za viongozi watakapokuwa kwenye msafara wa kuondoka. Aliamua kuifanya picha hiyo kuwa ya mwisho, akatembea hadi kituo cha mafuta ambacho hakikuwa mbali sana na eneo la mkutano.

    “Habari yako dada,” alimsalimia dada ambaye alikuwa amesimama karibu na kisima cha mafuta ya taa kikiwa na ubao mkubwa ulioandikwa KEROSENE.

    “Nzuri nikusaidie nini kaka.”

    “Kuna gari hilo hapo,” huku akinyoosha kidole kwenye gari bovu “naomba kukaa hapo juu nataka kupiga picha magari ya viongozi yatakapokuwa yanatoka mkutanoni.”

    “Ongea na meneja wetu hapo ndani!”

    Akatembea hadi kwenye ofisi ya kituo kile cha mafuta, ndani kulikuwa na kijana ambaye alikuwa anafuatilia mkutano kupitia runinga ndogo.

    “Habari mkuu,” alisalimia.

    “Salama kaka, karibu.”

    “Ahsante.”

    “Naitwa John Oscar,” huku akichomoa kitambulisho “ni mwandishi wa gazeti la muungwana.

    “Oh, karibu bwana John sijui nikusaidie nini?”

    “Nilikuwa naomba kukaa juu boneti ya hilo gari mbovu hapo nje nataka kuchukua picha za viongozi watakapokuwa wanatoka ukumbini.”

    “Aaaah, ni hilo tu! Unajua umenitisha sana?”

    “Kwa nini?”

    “Nilifikiri umekuja kunihoji juu ya skendo za uchakachuaji mafuta.”

    “Ha ha ha ha haaaa, kwani nanyi huwa manachakachua?”

    “Hapana, nilikuwa na hofu tu ya jina langu kuamkia gazetini siku inayofuata.”

    Wote wakaangua kicheko kisha John akaelekea kwenye lile gari bovu.

    Akiwa na kamera ya kisasa kabisa yenye mfumo wa dijitali aina ya NIKON D4, Kamera yenye uwezo mkubwa wa kigrafikali wa ‘megapikseli 16’ John Oscar alitulia juu ya boneti ya gari lile huku akiyaona mazingira aliyoyahitaji kwa usahihi mkubwa.



    * * *



    Upande wa pili wa barabara kulikuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa na jukumu maalum. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka licha ya kuwa na kipoza joto ndani ya gari. Moyo wake ulikuwa unapiga kwa nguvu hasa pale alipokuwa anasikia mlipuko wa shangwe kutoka kwenye ukumbi wa KBT. Mara kwa mara aliinua mkono wake wa kushoto na kuangalia muda. Wakati mwingine ilikuwa inamchukua sekunde thelathini tu kuuinua tena mkono huo na kutizama muda. Kuna wakati alijihisi hata kubanwa na haja ndogo. Kadri muda ulivyokuwa unazidi kuyoyoma ndivyo alivyozidi kutawaliwa na hofu.

    Ghafla, akasikia mlipuko mkubwa wa vifijo na nderemo. Mwili wake ukasisimka, damu ikachemka na kumfanya ahisi joto kali. Bila kujijua shati lake lilikuwa limelowa jasho kama mtu aliyemwagiwa maji.

    “Gari, nyumba, shamba na pesa taslimu, potelea mbali....” Aliwaza kwenye nafsi yake akijipa moyo wa kukabiliana na tukio lolote lile. Binafsi alichukulia tukio hilo kama nafasi yake ya mwisho katika maisha, akose ajutie au apate afurahie. Hakuona kama ana cha kupoteza kwani maisha yenyewe kila siku yalizidi kuwa magumu. Bei za vitu zilikuwa zinapanda siku hadi siku.

    “M.W.R...,M.W.R...M.W...” James Makabi aliyarudia rudia maneno ya windo lake. Aliyakariri maneno hayo kwani ndiyo maelekezo aliyoyapata kutoka kwa Mjomba Masharubu. Maneno ya Mjomba yakajirudia kichwani. Hakuelewa kabisa kirefu cha neno M.W.R, hakuambiwa kama kuna namba zingine baada ya maandishi hayo.

    “Kuwa makini sana, gari unalotakiwa kuligonga ni lile lenye nambari M.W.R baada ya hapo potea kabisa”



    Waaaaa...! Moyo wake ulitoa mlipuko pale aliposikia kwa mbali sauti iliyokuwa inasema mkutano umefungwa. Hakujali kama windo lake ni kiongozi au mwanachama wa kawaida, muhimu kwake ilikuwa ni kuhakikisha anakamilisha kazi aliyotumwa. Kwa upande mwingine aliwaza kuwa kama windo lake ni mwanasiasa basi hakuna kilichoharibika. Aliwachukia wanasiasa, alihisi kuwa ndio waliosababisha awe hapo alipo.

    Asingeweza kusahau jinsi alivyofaulu masomo ya darasa la saba lakini akakosa fursa ya kuendelea kutokana na serikali kuwazuia wakulima kuuza mazao yao wenyewe kule wanakotaka, badala yake serikali iliweka utaratibu wa kuwakopa wakulima kupitia vyama vya ushirika, kisha baada ya kuuza mazao yao kokote walikouza wakapanga nini wamlipe, ilimuuma sana kwani serikali ilikuwa haijushugulishi kwa namna yoyote kuwasaidia wakulima wakati wa maandalizi ya mashamba yao, badala yake waliwaingilia na kuwafanyia ukatili mkubwa ukifika muda wa mavuno. Jambo baya zaidi serikali ikathubutu hata kuweka askari wenye silaha za kivita barabarani ili kuwazuia watu kuuza mazao yao kwa utaratibu wanaoutaka kana kwamba walitoa msaada wa pembejeo. Bado wimbo wa kilimo kwanza ulikuwa mtaji wao wakati wa kuomba kura, aibu!

    Akakumbuka vema jinsi baba yake alivyoathiriwa na mfumo huo wa kikatili, kwani ufuta wake ulikopwa jambo lililosababisha akose fedha ya kumsomesha mwanawe. Baada ya baba yake kushindwa kumsomesha ndipo alipoamua kuja kujifunza ufundi magari hatimaye udereva.

    Mawazo hayo yalipokuwa yanapita kichwani akajikuta akipandwa na hasira na kuwa na dhamira ya dhati ya kutekeleza kazi yake si kwa sababu ya malipo atakayopewa tu bali pia kulipiza kisasi kwa mateso makali anayoyapata. Hofu ilikuwa imemtoka sasa. Alianza kuwaona watu wakiwa wanatawanyika, kisha magari ya viongozi ambayo yalifuata baada ya kutangulia msafara wa pikipiki na magari ya watu wa kawaida. Hapo akakumbuka vema maagizo ya Mjomba Masharubu.

    Hakuwa mbali sana na jengo la mikutano la chama cha MMD lililopo magomeni mwembe chai. Akapatwa na mshtuko baada ya kuliona windo lake kwa mbali. Aliwasha gari kisha akakaa tayari kwa tukio. Akaliondoa gari kwa kasi huku akiwa hajali kitendo cha askari wa usalama barabarani kusimama katikati ya barabara ile ya vumbi ambayo ilikuwa inaingia barabara ya morogoro, askari yule alikuwa ameliona gari lile lilivyokuwa linakuja kasi akajaribu kulizuia kwa kupunga mkono. Uhai mtamu, askari akajirusha kutoka barabarani na kujikuta akipiga mwereka mkubwa. Tahamaki, alikuwa kwenye mtaro akiwa tayari ameshavunjika mguu huku akikosa uhakika kama kiuno chake ni kizima.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mungu wangu....!” Alisikika askari wa kike ambaye alikuwa kando ya barabara huku akiwa amepigwa na bumbuwazi kwa tukio lile la ghafla.

    Buuuuuuuu! Kilisikika kishindo kizito ambacho kilifuatiwa na milio ya risasi. Gari aina ya Toyota Landcruiser yenye namba M.W.R likaacha barabara na kuingia kwenye mtaro huku kioo cha mbele kikipasuka na kutawanyika kabisa. Nissan Patrol iliondoka kwa kasi ya ajabu kisha likaiacha barabara ya morogoro na kufuata ile ya Kawawa. Kasi ilikuwa kubwa na ya kutisha hata magari mengine yalilazimika kukaa pembeni. Gari la polisi Deffender110 lilikuwa linaifuata ile Nissan kwa kasi. Dereva wa Nissan alionekana kuwa hodari zaidi kuliko polisi.

    Ghafla, akaliona gari lingine la polisi likija kutoka mbele yake.

    “Oh, Jesus...” alijisemea kwa sauti ndogo baada ya kugundua nyuma anafuatwa na mbele pia si shwari. Akazidi kuongeza kasi ya gari yake kwa kukanyaga kiongeza mwendo. Sasa ilikuwa ni kama anayetaka kuligonga lile gari la polisi. Kwa kasi aliyokuwa nayo alifahamu wazi kuwa baada ya tukio hilo hakuna kingine zaidi ya kifo, tena kifo kibaya ambacho hata sura haitajulikana. Kwa haraka akaangalia upande wa kulia na kushoto, akaziona nyumba za Kigogo bondeni ambazo zilikuwa zinaonekana kana kwamba zimejengwa shimoni.

    “Ni uamuzi sahihi!” Alijisemea kwa sauti ndogo huku akiuacha upande wake wa barabara na kufuata upande wa kulia. Almanusura asababishe ajali ya gari pale daladala ambalo lilikuwa linakuja kasi lilipofunga breki ya ghafla baada ya kuliona gari lile. Hakujali kitakachotokea akalipeleka gari upande wa kulia na kufuata mporomoko unaolekea nyumba za Kigogo.





    Gari likaserereka kuelekea kule bondeni, likagonga kwenye kitu kigumu likapinduka matairi yakawa juu bodi ikawa chini. Likaanza kuporomoka kwa mtindo wa pia.

    Dakika chache baadae gari likajipiga kwenye kiwambaza cha nyumba moja ambayo ilikuwa inauzwa pombe za kienyeji, ukasikika mlipuko mkubwa, gari likaanza kuwaka moto. Tafrani ikawa kubwa kila mtu akihaha kuyaokoa maisha yake, wako ambao pombe zilikuwa zimewakolea na walitembea kwa kuyumba lakini tukio hilo liliwarudishia fahamu zao na kujikuta wakitimua mbio za mashindano.

    Moto ulikuwa mkubwa na moshi wenye kutia hofu ukatanda eneo lote. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilazimika kuyakimbia majumba yao kutokana na kishindo hicho ambacho kila mmoja alikitafsiri kwa namna yake.

    Dakika chache baadae helikopta ya polisi ilitua ikiwa na viongozi waandamizi wa jeshi hilo. Kama ilivyo ada watu walianza kurudi eneo la tukio, taarifa zilisambaa eneo hilo ni gari ambalo limesababisha ajali ya gari la makamu wa Rais dakika chache zilizopita. Pale lilipolipuka kulikuwa na miili ya watu watatu ambao walikuwa wameungua vibaya. Ilikuwa ni vigumu kumfahamu yeyote kwani waliungua na kuwa weusi kama mkaa.

    Katika kundi la watu wale alikuwepo yule mtu mrefu ambaye alijitambulisha kwa James Makabi kama Mjomba Masharubu. Kama alivyokuwa siku ya kwanza leo hii pia alikuwa ametinga suti ya bei mbaya na kofia yake ya pama. Tofauti na watu wengine yeye alikuwa anaangalia tukio hili kwa tabasamu na furaha. Ni tabasamu ambalo alilificha ndani ya moyo wake, hata furaha yake aliificha pia, ikafunikwa vema na huzuni na mshtuko wa bandia. Alichokihitaji kilikuwa kimekamilika kama filamu fulani ya kusisimua. Kazi yake ilikuwa imekamlika kwa urahisi zaidi kuliko alivyopanga.

    “Kwisha!” Alinong’ona kwa sauti ambayo ni yeye mwenyewe tu ndiye aliyeisikia kisha akaliacha kundi lile la watu na kutokomea alikokujua mwenyewe.



    * * *



    John Oscar alishtuka baada ya kuliona Nissan Patrol lililokuwa linaelekea barabarani kwa kasi. Hisia kali za uaskari zilichukua nafasi yake lakini akajikuta akikumbuka kuwa alishafukuzwa siku nyingi hivyo hakuwa na haja ya kuingilia jambo hilo, yeye sasa ni mwandishi hivyo ni jukumu lake kushuhudia kitakachotokea ili aweze kuripoti kwa ufasaha hasa katika zama hizi ambazo habari ni biashara. Akakumbuka usemi maarufu kuwa bara nyingi habari mbaya ndio habari nzuri kwa mwandishi.

    Alitegemea kushuhudia ajali ya kawaida lakini haikuwa hivyo, alichokiona ni utaalamu mkubwa wa mauaji ya kukusudia ambao hakuwahi hata kuufikiria hapo kabla. Sambamba na ile ajali mbaya ya kukusudia alishuhudia muheshimiwa Ole Nunga akirushwa juu na kutupwa chini huku kwa masikio yake ya uaskari akisikia kitu kama mlipuko wa bastola ambao kwa kiasi fulani ulifunikwa na kishindo cha ajali ile. Kilichomshtua sio mlipuko wa bastola bali aina ya mlipuko aliousikia, Haukuwa mlipuko wa kawaida wa bastola. Kama sio milipuko miwili kwa pamoja basi ni aina ya bastola au silaha ambayo hapa nchini haifahamiki

    Mikono yake iliendelea kutetemeka na kuifanya kamera nayo kucheza cheza, akajikuta bila kujijua akipiga picha ovyo ovyo. Mambo yalikuwa yanafanyika kwa haraka sana kiasi cha kushtukia ndani ya muda mfupi ile Nissan patrol ikiwa imepotea machoni pake. Ghafla akajikuta akirejewa na akili zake za kawaida na kutambua kuwa yuko kazini. Alishuka haraka juu ya boneti ya lile gari bovu na kukimbilia eneo la tukio baada ya kuona watu wakianza kuzingira eneo lile. Aliwahi kuchukua mapema picha za marehemu Ole Nunga kabla polisi hawajawahi eneo la tukio na kuwazuia waandishi wa habari.

    Hakuishia hapo akakodi pikipiki ambayo ilimuwahisha pia eneo ambalo gari la muuaji lilikuwa limeelekea. Hapo akakutana na utata mwingine wa aina yake lile gari nalo lilikuwa limepata ajali, kulikuwa na maiti tatu zote zikiwa zimeungua vibaya.

    Zaidi ya vimo vyao kwani maiti moja ilionekana kuwa ya mtu mrefu kuliko hizi mbili zilizosalia hakuna kingine kilichoweza kumfanya yeyote kubaini maiti hizo.

    Baada ya maiti hizo kuondolewa ndipo akatanabahi kuwa fulana aliyovaa ilikuwa imeloa kutokana na jasho. Akapiga picha chache za mwisho kabla ya kuwahoji watu wawili watatu aliowakuta eneo la tukio ambao hawakutofautiana sana maelezo yao.



    III



    Ilikuwa Jumatatu ya aina yake, gumzo kubwa likiwa mauaji ya makamu wa Rais. Kila kona ya jiji mjadala ulikuwa huo, halikuwa jambo la kawaida kusikia mauaji ya mwanasiasa mkubwa kama huyo katika nchi yenye sifa ya amani na utulivu. Magazeti yote ya siku hiyo yalihanikizwa na habari hizo, hata magazeti ya michezo nayo yalikuwa na habari hiyo.

    Inspekta Tunu Nzowa wa kituo cha Magomeni alikuwa amejifungia ofisini kwake akiwa na rundo la magazeti mpaka yale ya michezo ambayo kwa kawaida hakupenda kuyasoma. Alikuwa ametoa agizo kwa Koplo Peter Mkwabi kumkusanyia magazeti yote ya siku hiyo. Aliyapitia magazeti yote kwa haraka haraka huku akiwa amekata tamaa ya kupata habari yoyote ambayo itamwongoza kwenye upelelezi wa tukio lile. Lakini alipofika kwenye gazeti la MUUNGWANA akagandisha macho yake hapo. Picha kubwa iliyopamba ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ilimfanya awe makini na gazeti hilo. Ilikuwa ni picha yenyewe hasa ambayo aliihitaji kwa wakati huo. Chini kulikuwa na maelezo kuwa habari na picha zaidi ziko ukurasa wa ndani.

    Akaliweka kando lile gazeti ili akili yake ipate kutulia kwanza ndipo asome vizuri kwani alikuwa hajawahi kushugulikia kesi ambayo ilikuwa nzito kama hiyo. Kwa upande mwingine alishangazwa na uamuzi wa haraka uliofanyika wa kukabidhiwa yeye jukumu hilo. Hakutaka kulifikiria sana hilo kutokana na kanuni za utii wanazofundishwa. Kengele ya simu yake ya mezani ikamtoa kwenye lindi la mawazo. Akanyanyua kiwiko cha simu na kusikiliza amri kutoka upande wa pili kwani namba alizoziona zilimjulisha kuwa anaongea na mkuu wake wa kazi.

    “Ndiyo afande.” Alijibu baada ya kusikia alichoambiwa.

    “Nimeamua kushirikiana na Koplo peter Mkwabi na kachero sajenti Dadi Kasweyaga wa kituo cha Buguruni.”

    Akasikiliza tena kilichoongelewa na mkuu huyo wa kazi kisha akajibu, “Hapana afande nimepitia rekodi za askari wengi nimeona kuwa hawa ndio watakaonifaa.”

    “Ahsante.” Alijibu kisha akarudisha kiwiko cha simu sehemu yake.

    Akashusha pumzi na kuitazama simu ile ya mezani kwa hasira, hakuhitaji kuongea na yeyote muda huo. Alihitaji kupitia gazeti lile kwa umakini mkubwa.

    “Tukio la jana tu leo hata sijafanya chochote naanza kuulizwa maendeleo ya kazi, upuuzi!” Aliongea kwa sauti ndogo kisha akamalizia kwa kusonya akionesha kukerwa na simu ya kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam.

    Kwa utulivu na umakini wa hali ya juu akaanza kufunua kurasa za gazeti la MUUNGWANA, ni kana kwamba gazeti hilo liliamua kuwa toleo maalum la mauaji ya Makamu wa Rais . Kulikuwa na picha mbalimbali za marehemu Ole Nunga kuanzia akiwa ukumbini mpaka wakati ule ajali inatokea.

    Kiasi fulani alishangazwa na umakini wa hali ya juu wa mwandishi au waandishi wa gazeti lile kwa jinsi walivyochukua picha na kutoa maelezo ya tukio zima kana kwamba walikuwa na fununu ya nini kitakachotokea.

    ‘…….. Wakati viongozi wanatoka ukumbini ndipo gari hilo jipya kabisa aina ya Nissan Patrol jeupe ambalo halijasajiliwa lilipojitokeza ghafla na kusababisha ajali hiyo ambayo ni wazi kuwa ilikusudiwa.’ Ilisomeka sehemu ya gazeti hilo.

    ***



    IV



    Kachero Inspekta Tunu Nzowa aliwasili katika viunga vya ofisi ya gazeti la Muungwana vilivyoko maeneo ya Ubungo Maziwa akiwa na wasaidizi wake Koplo Peter Mkwabi na Sajenti Dadi Kasweyaga.Akatembea taratibu hadi kwenye banda dogo la mlinzi ambaye alikuwa amevaa sare za rangi ya dhambarau.

    “Habari yako kijana!”

    “Nzuri shikamoo afande!” alijibu kijana yule kutoka kampuni ya KK Security.

    Inspekta hakujali kuitikia ile salamu badala yake akauliza moja kwa moja.

    “Naweza kuonana na Mhariri?”

    “Bila shaka, we nenda tu hapo lango kuu utaona kidirisha kimeandikwa mapokezi, hapo utaelekezwa uende wapi.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok.” Alijibu kwa mkato na kuondoka huku akifuatiwa kwa karibu na sajenti Dadi Kasweyaga. Koplo Peter alibaki kwenye gari akiwa ameegemea usukani.

    “Habari yako binti.” Alisalimia Inspekta Tunu ambaye alikuwa ameibana kofia yake kwapani na kuruhusu kuonekana nywele zake ambazo zilianza kupigiwa hodi na mvi.

    “Salama shikamoo.”

    “Marahaba, naweza kuonana na mhariri?”

    “Ndiyo, fuata hii Korido chumba cha mwisho kabisa utaona maandishi mlangoni MHARIRI MTENDAJI”

    Kachero Dadi kasweyaga ambaye tofauti na wenzake alikuwa amevaa nguo za kiraia akakaa kwenye moja ya viti vya mapokezi ambavyo vilikuwa vimepangwa pale kwenye korido huku akimsindikiza bosi wake kwa macho.

    “Karibu sana.” Mzee Kasim mhariri mkuu wa gazeti la Muungwana alimkaribisha Inspekta Tunu.

    “Ahsante mzee, bila shaka wewe ndio mhariri mkuu wa hili gazeti”

    “Ndiyo afande, tafadhali keti nikusikilize.” Aliongea Mzee Kasim kwa sauti yenye furaha.

    “Naitwa Inspekta Tunu Nzowa,” alijitambulisha huku akitoa kitambulisho chake.

    “Hakuna haja ya kitambulisho afande kwani tumeshakutana mara kadhaa ingawa hapa ofisini ni mara yako ya kwanza kufika.”

    Inspekta akakaa vizuri kwenye kiti na kumuelekea Mhariri.

    “Habari yako Ndugu Kasim!”

    “Ah tunashukuru Mungu habari ni nzuri!”

    “Sawa, bila shaka una taarifa juu ya mauaji ya makamu wa rais bwana Ole Nunga.”

    “Ndiyo, tuna taarifa hizo pengine sisi ndiyo ambao tumeiripoti vizuri zaidi habari hiyo.”

    “Na ndio sababu ya kuja hapa, kwani nimezisoma kwa kina kabisa taarifa hizi kupitia gazeti lenu.”

    “Sijui ni kwa vipi tunaweza kukusaidia afande.”

    “Vizuri, kuna chochote ambacho hakijaelezwa kwenye taarifa yenu?”

    “Ndiyo kuna mambo kadhaa ambayo yanatakiwa kupangiliwa ipasavyo kisha tutayaweka kwenye toleo linalofuata, kwani wakati ile taarifa inatoka tayari gazeti lilikuwa limekamilika likisubiri kuingia mtamboni”

    “Vizuri,moja nahitaji kuonana na mwandishi au waandishi ambao mliwatuma kwenye mkutano mkuu wa chama, pili nahitaji taarifa hiyo hata kama haijapangiliwa vizuri yaani naihitaji kama ilivyo tatu naomba kukufahamisha rasmi kuwa nazuia kuendelea kutolewa taarifa hii katika gazeti lako kwani inaweza kuleta usumbufu katika upelelezi wetu.” Akatulia na kumkazia macho mzee Kasim.





    “Ok, Mwandishi aliyefanya kazi hii ni mmoja tu na ameomba muda wa kuifanya kazi yake kwa utulivu akiwa nyumbani kwake, ameahidi kutuletea taarifa hiyo saa moja na nusu usiku kabla gazeti halijaenda mtamboni anaitwa John Oscar, Sijui kama utahitaji aje kwako au wewe ndio utaenda nyumbani kwake?”

    “Kutokana na mazingira jinsi yalivyo nahitaji kuonana naye nyumbani kwake.”

    “Anaishi kariakoo, mtaa wa Muheza karibu kabisa na makutano ya Muhonda nyumba namba 716.”

    “Ok Nashukuru kwa maelezo yako.” Wakapeana mikono kisha akainuka na kuondoka mle Ofisini.

    Safari ya kuelekea nyumbani kwa John ikaanza.



    “Nafikiri huyu kijana anaweza kutusaidia” alianzisha maongezi Inspekta huku akimkazia macho Kachero Dadi Kasweyaga.

    “Ni kweli afande lakini nahisi tunatakiwa kuwa makini sana.”

    “Umakini unatakiwa kwenye kazi yoyote, Sijui ni umakini gani unauzungumzia hapa?” Aliuliza huku akimkazia macho makali.

    “Huyu Mwandishi anaonekana kuwa muhimu sana na hawa wauaji wanaweza kuwa watu hatari hivyo lazima watamuua ili kupoteza ushahidi kama hatutamuweka chini ya uangalizi maalumu.”

    “Wazo zuri ambalo sikulifikiria kabla, nitajadiliana naye ili awe kwenye maficho hadi pale tutakapokamilisha uchunguzi.”



    ***

    Safari yao ikawafikisha makutano ya Muhonda na Muheza.

    “Ninyi mtanisubiri hapa nje wakati mimi nitakapokuwa nahojiana na jamaa huko ndani.”

    “Kwanini tusiingie wote afande” aliuliza kachero.

    “Nataka awe anajibu kwa utulivu kwani anaweza kubabaika atakapojikuta anakabiliana na maafande wawili.”

    “Huyo si mtuhumiwa afande hivyo hawezi kuwa na wasiwasi wa kuhojiwa tena kubwa zaidi ni mwandishi.” Alisikika kachero Dadi huku akiwa na shauku kubwa ya kwenda kumsaili huyo mtu.



    Wakati Inspekta anapiga hatua kuelekea ndani mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita. Aliitazama simu ile akaona ni namba ya Kamishna wa polisi wa makosa ya jinai muheshimiwa Kigoda Kanjowe.

    “Eeh, nakupata afande”

    “Kazi inaendelea vizuri, na hivi ninavyozungumza niko nyumbani kwa John Oscar Mwandishi wa gazeti la Muungwana nafikiri atatusaidia sana kurahisisha kazi yetu kwani anazo taarifa za kutosha juu ya tukio lile.”

    Akasikia mtu anashusha pumzi upande wa pili wa simu kisha simu ikakatwa.

    Kabla hajasonga mbele mara simu yake ikaanza kuita tena.

    “Ndiyo afande kuna tatizo?”

    “Unaweza kunielekeza hiyo nyumba iko wapi?”

    “Ndiyo.” Alijibu Inspekta huku akionesha wazi kukerwa na usumbufu huo wa mkuu wake wa kazi.

    “Huyu afande Kigoda ni msumbufu sana.”

    “Anasemaje?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Anataka kujua eneo iliko nyumba ya huyu mwandishi.”

    “Anahitaji nini wakati hii kazi tumeshakabidhiwa?”

    “Ah! Ni usumbufu tu.”

    Wakati anataka kupiga hatua tena mara simu yake ikaita kwa mara nyingine.

    “Hallow afande kuna nini tena?”

    “Hili swala ni nyeti sana na linahitaji usiri mkubwa naomba uwaruhusu hao uliongozana nao halafu ubaki peke yako na usionane nae mpaka nifike hapo.”

    “Kwa nini afande.”

    “Ni upelelezi nyeti ambao hautakiwa kufikiwa na kila sikio hivyo waruhusu hao halafu unisubiri baada ya dakika chache nitakuwa hapo na usiwaeleze kuwa mimi nitakuja hapo kwani sitaki yeyote abaini kuwa nachunguza haya mauaji.”

    Akawaruhusu wale vijana wawili akaamua kumsubiri Kamishna. Baada ya kupita nusu saa akaamua kupiga simu.

    “Eeeh afande mbona kimya?”

    “Basi...ah... samahani kwa usumbufu nenda uhojiane naye nitakukuta hapo kabla hujaondoka.”

    Inspekta alikunja uso kwa hasira baada ya kupata majibu hayo kutoka kwa mkuu wake, kama si nidhamu za kiaskari angeweza hata kumtukana.



    Nyumba namba 76 ilikuwa ni miongoni mwa nyumba chache ambazo hazikuwa na hadhi ya kuendelea kuwepo eneo la kariakoo. Kilichosababisha nyumba hiyo kupangishwa kwa bei kubwa ni kutokana na ubora wa eneo lakini si nyumba. Bati zake zilikuwa zimechakaa na kuwa nyekundu kutokana na kutu. Bila shaka kipindi cha mvua nyumba hiyo ilikuwa miongoni mwa nyumba zilizoleta kero kwa wapangaji kutokana na kuvuja.

    Akagonga mlango kama mara tatu ndipo akasikia mtu akimkaribisha.

    Mzee ambaye umri ulikuwa unampungia mkono ndiye aliyefungua mlango. Ingawa umri wa Inspekta Tunu ulikuwa umeenda kiasi cha kubakiza miaka mitano tu kustaafu kazi lakini kwa huyu mzee alikuwa sawa kabisa na mjukuu wake.

    “Shikamoo mzee!”

    “Marahaba, bila shaka unamuhitaji huyu John.”

    “Umejuaje?”

    “Leo amekuwa na wageni wengi sana tena huyu aliyemtembelea mara ya mwisho hata hajatoka huko ndani.”

    “Wageni wa aina gani?”

    “Wa mwisho ni askari kama wewe, karibu sana babu, yuko chumba cha uani huko.” Yule babu alimaliza kwa kicheko kikubwa. Inspekta alimkazia macho yule babu ambaye aliendelea kucheka akagundua kuwa akili zake zimeanza kurudi kwenye utoto kutokana na uzee.

    Akatembea kwa ukakamavu huku akivipita vyumba kadhaa ambavyo wapangaji walikuwa wanasikiliza Redio au kutazama runinga.

    Yule babu aliendelea kucheka hadi Inspekta alipoibukia uani. Uani kulikuwa na vyumba viwili ambavyo vilikuwa vimefungwa. Huku mlango ambao ulionesha kubeba vyumba viwili na sebule ukiwa wazi.

    Chumba hiki kilikuwa kimya, hazikusikika sauti za muziki kama vyumba vingine. Alipofika mlangoni akagonga mlango taratibu lakini hakuitikiwa. Akashangaa baada ya kulakiwa na ukimya huo.

    “Labda kenda kuoga.” Lilipita wazo lililkomfanya agande mlangoni lakini bado ukimya ulichukua zaidi ya muda wa kuoga.

    Akasukuma mlango na kuingia ndani, kwanza alishtushwa na harufu nzito. Ilikuwa ni harufu ambayo hukutana nayo mara kadhaa kwenye matukio ingawa ilikuwa imepita siku nyingi kabla ya kukabiliana na hali hiyo. DAMU! Mbona mapema? Alijiuliza huku akisonga mbele kwa tahadhali. Vitu vilikuwa vimetawanywa ovyo pale sebuleni. Karatasi zilikuwa zimetawanywa huku na huko. Hisia kali za hatari zikaendelea kumtawala kadri alivyokuwa anasonga mbele, kwanza akaangalia upande wa kulia mlango wa chumba ulikuwa umefungwa, alipoangalia ule wa kushoto ulikuwa umefunguliwa kidogo huku ukiacha nafasi kama ya mtu anayechungulia nje.

    Akasukuma ule mlango na kujitoma chumbani, kama hisia zake zilivyomtuma kwanza alianza kuona mchirizi wa damu akatembeza macho kwa haraka huku nywele zikimsisimka, mwili wa mtu ambaye alidhania kuwa ni John Oscar ulikuwa umelala chali huku ukiwa na jeraha baya la risasi upande wa kushoto. Moyo wa Inspekta ulikuwa unapiga kwa kasi kwani alihisi kuwa muuaji hayuko mbali kwani damu ilikuwa ni mbichi mno. Haraka haraka akainua Radio call yake, hakuwahi! Mkono wenye nguvu ulimshukia kichwani kwa pigo kali. Inspekta akalegea na kuanguka pale kwenye dimbwi la damu akapoteza fahamu. Kwa utulivu mkubwa muuaji akaondoka huku akikatisha pale kwenye korido bila wasiwasi.

    Hakuwa muuaji wa kawaida!



    ***

    Watu waliojawa na maswali walikuwa wameizunguka nyumba ile namba 716 wakati maiti zinatolewa ndani. Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam alikuwa miongoni mwa askari waliokuwepo eneo la tukio. Miongoni mwa watu walionekana kuwa na mawazo Mazito alikuwa Kachero Dadi Kasweyaga, Saa moja na nusu iliyopita alikuwa anaongea na Inspekta Tunu Nzowa lakini kwa sasa alikuwa nusu kuzimu.

    Pamoja na kutawaliwa na mawazo mengi ya kutatanisha bado aliendelea kuandika hili na lile, moyoni mwake alikuwa na kitu kizito ambacho alikuwa anawaza lakini akawa na hofu ya kukigusa. Alianza kufikiria upya kuhusu simu iliyopigwa na Kamishna maalum wa makosa ya jinai Kigoda Kanjowe, kwanini baada ya maongezi na mkuu huyo wao wakaambiwa waondoke na mwisho wa yote ni shambulizi kwa In spekta ambalo bila shaka lilikuwa ni kusudio la kumuua? Kuna nini kinaendelea juu ya sakata la kifo cha muheshimiwa makamu wa Rais? Maswali hayo yaliendelea kumtesa kachero huyo ambaye alikuwa na cheo kidogo.



    *****



    V

    Luteni Taisamo Alitazama kwa furaha jinsi watu walivyokuwa wanaburudika kwa muziki mtamu katika baa ile ya MASAWE NIGHT PARK iliyoko maeneo ya Vingunguti, kwake kilikuwa ni kichekesho kizuri kwani wengi walikuwa wanacheza bila kufuata utaratibu kutokana na vinywaji kuwakolea vichwani.Furaha yake ilikatika alipokumbuka kuwa ile ilikuwa tarehe 30 mwezi wa saba ambapo alitakiwa kulipa kodi ya nyumba. Akainuka pale kwenye kiti tayari kwa kuondoka.

    “Mbona unaondoka kaka si uliagiza mchemsho?” Sauti ya kike ikamzindua na kumfanya atahayari.

    “Nilitaka kununua sigara hapo nje.” Alijitetea.

    “Mbona hata hapa zipo?”

    “Aah, Kumbe, nilikuwa sifahamu basi nipe kwanza huo mchemsho pesa yako hii hapa.” Akamkabidhi noti ya shilingi elfu kumi.

    “Sigara gani unahitaji?”

    “We lete mchemsho tu nilitaka kununua sigara ili kuvuta muda.” Aliendelea kujitetea kwani hakuwa mvutaji.

    Wakati analetewa mchemsho mara simu yake ya kiganjani ikaanza kuita.

    “Hallow zero zero one fifty (00150) ni wewe?”

    “Ndiyo nani mwenzangu.” Alijibu kwa mshtuko kidogo kwani kutajwa kwa namba kulimaanisha kuwa kuna kazi muhimu anatakiwa kuifanya.

    “Rose hapa, uko wapi?”

    “Rose!?”

    “Ndiyo sitaki maswali zaidi, that’s my code name Liutenant, nisikilize kwa makini tafadhali. Uko wapi?” Ilikuwa ni sauti ya kike lakini iliyojaa amri.





    “Vingunguti, MASAWE NIGHT PARK.”

    “Kaa hapo hapo usiondoke hadi utakapopewa maagizo mengine.”

    Rose lilikuwa jina geni kwake kikazi na hakutaka kuhoji zaidi kama alivyoonywa kwani alijua wazi kuwa hilo si jina halisi. Tayari aliishiwa na hamu ya kula kutokana na shauku ya kujua alichoitiwa. Hisia zake zilimtuma kuwa huenda kuna safari ya Sudan kusini chini ya vikosi vya umoja wa mataifa kwenda kulinda amani au kutuliza machafuko.

    Dakika arobaini na tano zilikatika bila kupokea maagizo yoyote, mara simu yake ikaanza kuita tena.

    “Hallow.”

    “One fifty, toka hapo ulipo nenda upande wa barabara ndogo inayoungana na barabara ya Nyerere.”

    Bila kuhoji huku moyo ukienda kasi akainuka pale kwenye kiti na kuongoza kule alikoelekezwa. Kilichomshangaza hapa ni kuwa kama ni kuitwa kwenda kulinda amani basi huu ulikuwa utaratibu mpya. Alijua wazi kuwa kuna jambo zito anatakiwa kufanya. Bado ulikuwa ni utaratibu wa kushangaza mno kwake kwani hajawahi kuusikia.

    “Hata huagi?” Sauti ya msichana aliyemletea mchemsho haikuyafikia masikio yake wakati anaondoka kwa staili hiyo ya aina yake.

    Luteni Taisamo kijana mwenye urefu wa wastani, mwili uliojengeka kimazoezi, mweusi lakini mwenye wajihi wa kuvutia kutokana na mng’ao wa weusi wake. Suruali yake ya jeans ya bluu na viatu vyeusi vya ngozi vilimkaa vema, fulana yake nyeusi ambayo ilikuwa na maandishi ya kichina ilimfanya ilimfanya azidi kuvutia katika macho ya yeyote anayemtazama.

    “Yes, tunakuona one fifty. Simama hapohapo ulipo.” Mpaka hapo alikuwa na maswali mengi kichwani mwake kwani alikuwa hajawahi kuitwa na mkuu wake wa kazi kwa namna ya kustaajabisha kama hiyo. Pia huyo Rose kama alivyojitambulisha alikuwa mpya.

    “Haraka ingia kwenye Benz jeupe unaloliona mbele yako.” Hapo alisita kidogo kwani alihisi kuwa huenda anakifuata kifo mwenyewe, lakini akili yake ilikataa haraka sana kwani toka aingizwe kwenye kitengo cha Interejensia ndani ya jeshi(CMI) alikuwa hajawahi kufanya kazi yoyote ya hatari ambayo inaingilia maslahi na heshima za watu ambayo ingeweza kumfanya aandamwe kiasi kile.

    Akafuata lile Benzi, ndani hakuwepo yule mwanamke aliyekuwa anaongea naye kwenye simu.Hakushangaa kwani si jambo la ajabu kwa watu wa aina hiyo kuwasiliana na mtu ambaye hakuoni huku na yeye akipokea maelezo kutoka sehemu nyingine.

    Ndani ya gari kulikuwa na dereva ambaye pia hakumfahamu. Kwa macho ya haraka mno aliweza kubaini kuwa yule dereva si askari. Wakasalimiana kisha gari likaondoka kwa kasi likifuata barabara ya Nyerere kuelekea Tazara,lilipofika makutano ya Nyerere na Mandela likaacha barabara ya nyerere na kufuata ile ya Mandela. Mpaka kufikia hapo Taisamo aliamua kuacha kuendelea kuwaza, aliamua kutulia ili akili yake ikae vizuri kukabiliana na lililoko mbele yake. Hakutaka kumuuliza swali lolote yule dereva ingawa alishangaa kumuona akiwa hana dalili yoyote ya uaskari. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kumtambua hata askari ambaye ana miezi mitatu kazini.

    Waliongea mambo ya kawaida tu huku yule dereva akishindwa kugusia lolote kuhusu safari yao.

    “Jamaa akiniachia mpaka kesho ‘nitainjoi’ sana na huu mkoko.” Alisikika dereva na kumfanya Taisamo azidi kupigwa na mshangao.

    “Ina maana huwa hakuachii siku zote.” Alijifanya kama anayefahamu kuhusu gari hilo.

    “Thubutu, we unamjua vizuri yule mzee? Vile Vikorona na Korola atakuachieni muende mutakako na mafuta atakuongezeeni lakini hii Benzi sijui ni kwanini huwa anaitumia mara mojamoja, tena leo ajabu kunituma mimi na hii benzi.”

    Maelezo hayo yalimfanya Taisamo afahamu kuwa aliyemchukua hafahamu lolote. Pia hakutaka kuhoji na kumjua huyo anayemuita ni nani. Aliifahamu vema michezo ya watu wa Intelijensia, ni watu ambao mara nyingine hata wao wenyewe hawaaminiani.



    ***



    Gari lilisimama mbele ya majengo ya Wizara ya ulinzi.

    “Sasa kaka mkubwa ee, mzee aliniambia nikuache hapa, bila shaka mwenyewe unaelewa zaidi wacha mimi nitanue kidogo maana nikichelewa kidogo tu anaweza kuniambia nirudishe gari nyumbani” Maelezo hayo yaliliendeleza mshangao wa Taisamo ambaye alifahamu kwa taratibu za kazi huwa wanafanya kazi kwa UNIT, yaani kunakuwa na mgawanyo maalum wa vikundi ndani ya wapelelezi vikundi hivyo hufanya kazi kwa kushirikiana na ikitokea kazi huwa kuna UNIT maalum inapewa kazi hiyo na si mtu mmoja mmoja kama ambavyo alianza kuhisi Taisamo kuwa inataka kutokea kwake.

    Alisimama palepale aliposhushwa akaendelea kusubiri maagizo mengine kutoka kwa Rose. Dakika ilikatika mara akafuatwa na mlinzi aliyekuwa upande ule wa lango kuu la kuingilia ndani.

    “Habari yako.” Alisalimia mlinzi aliyekuwa analinda jengo lile.

    “Nzuri, samahani bwana kuna mtu ameniambia tuonane maeneo haya hivyo nasubiri simu yake.”

    “Ahaa! We ndo mgeni wa mzee, panda ghorofa ya mwisho kabisa fuata hiyo korido chumba cha mwisho upande wa kushoto gonga mara tatu.” Taisamo alimsikiliza yule mlinzi huku akifahamu wazi kuwa haongei na mlinzi wa kawaida. Dalili za ukachero za mtu huyo zisingeweza kujificha katika mboni kali za Taisamo. Uso uliojaa mishuguliko na ujanja wa kujifanya mtu wa kawaida.

    Akafanya kama alivyoelekezwa, kutokana na shauku aliyokuwa nayo alilazimika kupanda harakaharaka ngazi za jengo lile lenye ghorofa tano huku akisahau kabisa kama kuna lift ambayo ingemrahisishia zoezi lake.

    Akainua mkono wake wa kushoto na kutazama saa yake.

    “Saa nne nusu, anahitaji nini huyu Mwaikambo?” Alijiuliza huku akili yake ikimtuma kuwa anaitwa na mkuu wake wa UNIT mwenye cheo cha Meja. Hata hivyo alitatanishwa na staili iliyotumika ili kualikwa kwenye wito huo kwani Meja Mwaikambo alikuwa na namba zote za wale anaowaongoza kwenye UNIT yake, hakuwa na haja ya kumtumia mtu wa kati anayejiita Rose. Alipoufikia ule mlango akagonga mara tatu kama alivyoelekezwa.

    Simu yake ya mkononi ikaanza kuita tena.

    “Hallow.”

    “Hallow one fifty Rose hapa, fungua mlango uingie ndani.”

    Kidogo alianza kuhisi hasira baada ya kuona anapelekwapelekwa na mtu asiyemfahamu .Hakuwa mgeni sana na jengo hilo alishawahi kufika mara kadhaa lakini aliishia huko chini ambako nje ya kulikuwa na ofisi nyingine ya ziada ya Meja Mwaikambo; hakuwahi kufika ofisi za juu na wala hakujua nini kinaendelea zaidi ya kufahamu kuwa huko juu ndiko iliko ofisi ya waziri wa wizara husika na baadhi ya wakuu wakiwemo makatibu.

    Jengo hili lilikuwa na mambo mengi zaidi ya kiusalama yaliyokuwa yanaendelea bila kufahamika. Hapa ulifanyika uchujaji wa mambo na kupelekwa kwenye kitengo husika, sio kila kitu kilichogunduliwa na wapelelezi wa polisi CID kilikuwa ndani ya uwezo au majukumu yao, pia hata wale wa usalama wa taifa na wale majasusi wa kijeshi hawakuwa na uwezo wa kutekeleza kila jukumu. Hapa ulifanyika ubadilishanaji mkubwa wa taarifa kwa maslahi ya Taifa. Kila jambo lilipelekwa kwenye kitengo husika.

    Jengo hili ambalo lilizungukwa na majengo kadhaa ikiwa ni pamoja na benki ya wananchi na majengo kadhaa ya kampuni ya simu, lilikuwa na urefu wa kutosha kiasi kwamba kwa yeyote ambaye angepanda huko juu angeweza kufaidi mandhari nzuri ya bahari ya hindi.

    Akafungua mlango kama alivyoelekezwa na kuingia ndani, hakuamini macho yake, alipatwa na mshtuko kidogo na kisha akatoa heshima ya kijeshi kwa kupiga saluti. Macho yake yalitua kwa maafisa wale wawili wa juu kabisa katika ngazi za utawala ndani ya jeshi. Huyu mmoja alimfahamu zaidi kwani licha ya kuwa mkuu wake wa kazi pia aliwahi kuwa mwalimu wake alipokua anachukua mafunzo maalum ya usalama katika chuo maalum cha kijeshi ambacho kiko Dar es salaam lakini wengi hawakitambui.

    Zaidi ya kumuona kwenye runinga na picha alikuwa hajawahi kukutana na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Jenerali Othman Nalinga.Aliyatuliza macho kwa mzee yule kisha akayarudisha kwa mnadhimu mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Robert Ruhumbika.

    Hakuwahi kufikiria kuwa siku moja angeitwa na maafisa wale wazito, pia alishangaa kwani hata Meja Mwaikambo hakuwajibika moja kwa moja kwa wakuu hao na badala yake alipokea amri kutoka kwa Luteni kanali, Kanali na mara mojamoja sana kutoka kwa Brigedia Jenerari. Hakuna hata jambo moja ambalo alilifikiria katika kichwa chake ambalo linaweza kuwafanya wakuu wale wamuite moja kwa moja kwani mara nyingi aliwajibika kwa Meja ambaye pia alikuwa ni mkuu wa UNIT yao ambayo ilijulikana kwa jina la snake.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog