Search This Blog

Monday 24 October 2022

SIRI ILIYOTESA MAISHA YANGU - 5

 













    Simulizi : Siri Iliyotesa Maisha Yangu

    Sehemu Ya Tano (5)





    W

    aliingia Khartoum ?Sudani saa 12:30 ?asubuhi, wote wakiwa wamechoka kupita kiasi. Harry hakuwa na uhakika kama Waarabu aliokuwa nao ndani ya gari wangemlipa pesa zote walizomuahidi kwa malipo ya ndege  aliyoiiba kwa Dk. Ian na kumwacha Caroline katika matatizo makubwa.

    Alichowaza wakati huo kilikuwa pesa hakukumbuka hata kidogo kuwa alimwachia Caroline  kazi ngumu kwa kitendo alichokifanya, aliamini mikononi mwa Wavietnam asingetoka salama! Ni lazima wangemuua baada ya yeye kutoroka, kwa upande mwingine moyo wake ulimuuma sana  kusababisha  kifo cha mwanamke aliyempenda!

    Alijua wazi ni kiasi gani Caroline alimpenda kwa dhati, lakini kwa ugumu wa moyo aliokuwa nao Harry aliyaweka mawazo hayo pembeni na kufikiria pesa ambazo alikuwa na uhakika baada ya kuzipata ni lazima angechukua madaraka ya nchi  jirani ya  Jamhuri ya Sokomoni, aliutamani sana Uraisi wa nchi hiyo na kwa kutumia pesa ambayo angelipwa baada ya biashara haramu aliyoifanya  ingekuwa  kwake kushinda katika uchaguzi wa Vyama vingi uliotegemewa kufanyika  nchini humo miezi tisa mbele.

    Gari  lao lilisimama mbele ya jengo la ghorofa nne lililojengwa kwa vioo karibu kila mahali! Watu wengi walionekana kuingia na kutoka ndani ya jengo hilo, wazee wenye ndevu nyingi aliokuwa nao walishuka garini na kumwonyesha ishara kwamba naye alitakiwa kushuka, bila kuchelewa wala kusita Harry alianza kuwafuata wazee hao kwa nyuma, walipandisha jengo hilo hadi ghorofa ya nne na kila mahali walikopita kulikuwa na ulinzi mkali.

    Lango la ghorofa ya nne lilifunguliwa na walinzi wawili wenye miraba minne na wote walikuwa na bunduki mikononi mwao,hali hiyo ilimtia hofu sana Harry! Kwa mara ya kwanza alihisi kutetemeka na kichwani mwake mawazo ya kudhulumiwa yalianza kumwingia, kwa mahali alipokuwa hata kama wazee wale wangeamua kumuua hakuna mtu angefahamu. Mawazo hayo yalimfanya asite kidogo kuingia ndani lakini baadaye aliupa moyo konde na kuingia huku akitembea kwa unyonge.

    Walikwenda moja kwa moja hadi ndani kabisa ya jengo hilo, walivuka milango mitatu iliyokuwa na walinzi wa sampuli kama aliyoikuta kwenye lango la kwanza na kila mlinzi alikuwa na bunduki aina ya SMG, hali ya hatari ilitanda kila mahali na hakuna neno lolote lililoongewa zaidi ya “Asalam Aleykum!”.

    Waliingia  moja kwa moja ndani ya  chumba kidogo kilichoandikwa “Comference Room” na humo waliwakuta wazee wengine watano wenye ndevu nyingi kama walivyokuwa aliongozana nao, ilivyoonekana kufuga ndevu ulikuwa utamaduni wao!Wote waliketi kuizunguka meza kubwa iliyokuwemo ndani ya chumba hicho, wazee wale waliendelea kuongea katika lugha ambayo Harry hakuilewa lakini alihisi kilikuwa ni Kiarabu, aliingiwa na wasiwasi zaidi kuona hashirikishwi katika maongezi hayo.

    Mara ghafla milango miwili iliyokuwa nyuma ya chumba hicho ilifunguliwa wakaingia  wanaume wawili wenye misuli wakiwa wameshika bunduki mikononi mwao, alipowaona Harry alihisi  mkojo ukimpenya sababu ya woga, kwa hakika hakuamini kama eneo hilo lingekuwa na usalama kwake! Alianza kujilaumu ndani ya nafsi yake kwa kitendo cha kuwaamini wazee hao na  kuwapa ndege kabla ya malipo.

                 ***********

    Gari lilikuwa likizidi kwenda kwa kasi, Kennedy akiwa kwenye usukani na  bastola za O’brien na Nicky zilikuwa bado zimemlenga Caroline shingoni huku akiamriwa kutulia, kila kitu kilichotokea ndani ya gari kwake kilionekana ni kama ndoto ambayo baada ya muda mfupi angetoka ndani yake. Hakuwa tayari kuamini  kuwa alikuwa ametekwa, kwa mara nyingine tena aliulaumu moyo wake kwa kumuamini Kennedy.

    “Kennedy nimekosa nini na mnanipeleka wapi?”

    “Kwa mumeo!”

    “Mama yangu weeee!Kweli mnanipeleka kwa Dk. Ian? Hivi mnajua atakachonifanya? Ataniua tena kwa kifo kibaya sana!”

    “Sisi hiyo hatujali hata kidogo, kitu tunachoangalia ni maslahi! Maisha yako hivi sasa ni mali kubwa, kitendo cha sisi kukufikisha kwa mumeo ni kwaheri umasikini!” Alisema Kennedy lakini maongezi yote yalifanyika katika lugha ya Kiingereza.

    “Jamani msinipeleke, nihurumieni! Ni heri mniue nyinyi lakini si kunifikisha kwa Dk. Ian!”

    “Si ni mumeo lakini?”

    “Alikuwa mume wangu na kwa niliyomfanyia nina uhakika ataniua vibaya mno!” Caroline alizidi kujieleza lakini hakuna aliyeonekana kumjali, bastola zilizidi kumlenga na mbele kama kilometa ishirini gari lilipunguza mwendo na kuegesha pembeni.

    “Nicky hebu maliza hiyo  kazi, muda wa ndege umekaribia!” Kennedy alimgeukia Nicky na kumwambia baada ya gari kusimama huku akimkabidhi kiboksi kidogo alichokuwa nacho mkononi.

    “Sawa bosi!”

    Kitendo bila kuchelewa Nicky alikifungua hicho na kutoa bomba la sindano pamoja na kichupa kingine kidogo, Caroline alishuhudia kila kitu kilichoendelea huku akitetemeka na alipoangalia vizuri juu ya kichupa ambacho Nicky alikuwa akinyonya majimaji yaliyokuwa ndani yake kwa sindano, aliyaona maandishi yaliyoandikwa Pethedine! Aliijua dawa hiyo, miaka ya nyuma aliwahi kuumia mguu na daktari aliitumia kumchoma ili alale usingizi.

    Alielewa walichotaka kufanya, walitaka kumchoma dawa ya usingizi ili alale na wamsafirishe kwa urahisi, alianza kupiga kelele akiomba wasimchome dawa hiyo lakini baadaye  alipofikiria vizuri aliamua kutulia na kuruhusu wamchome, hata akina Kennedy walishangazwa na utulivu huo na kuangaliana machoni.

    “Ok! Get the stuff into my vein immediately!”(Nichomeni  hiyo dawa kwenye mshipa haraka!) Alisema Caroline, alitaka achomwe dawa  na alale ili kama  atafikishwa kwa Dk. Ian na kuuawa basi afe akiwa usingizini, hakuwa tayari kukutana na Dk. Ian macho kwa macho.

    Dawa hiyo ilichomwa kwenye mshipa na mchomaji akiwa Nicky, muda mfupi kabla hajalala alipata nafasi ya kuyafikiria mambo yaliyotokea maisha mwake, alijiona ni mwenye mkosi lakini mara nyingi alijitupia lawama mwenyewe kwa kutochukua maamuzi yaliyo sahihi!  Alipowafikiria baba na mama yake roho ilimuuma zaidi, alitamani kuwa nao tena wao walikuwa wazazi wake wasingemtupa hata kama angekuwa  na matatizo makubwa kiasi gani.

    “Nakufa bila kuwaona baba na mama yang.....!” Kabla hajaikamilisha sentensi hiyo usingizi mzito ulimpitia, hakujua kitu chochote kilichoendelea baada ya hapo.

    Kennedy na wenzake walisubiri kwa muda wa dakika ishirini ili alale vizuri ndipo wakaligeuza gari lao na kuanza kuliendesha kwa kasi kurudi mjini Penh ambako walichukua barabara ya  Hilbag  iliyoelekea uwanja wa ndege wa jiji hilo uliokuwa umbali wa kama kilometa ishirini kutoka mjini. Walitumia kama dakika tano tu kufika uwanjani ambako waliliegesha gari lao katika sehemu maalumu ya maegesho.

    Kabla hawajashuka  kwenye gari Kennedy alifungua  droo  iliyokuwa kushoto kwake na kutoa tiketi zao zote pamoja na cheti kilichoonyesha kuwa Caroline alikuwa mwanafunzi mgonjwa aliyekuwa akisafirishwa kutoka Vietnam kwenda  Ottawa nchini Canada ambako familia yake iliishi, ulikuwa ni uongo waliopanga ili kufanikisha mpango wao wa kumfikisha Caroline mikononi mwa Dk. Ian.

    “Psiiiiiiiiiii!” Kennedy alimwita mfanyakazi mmoja wa uwanja wa ndege aliyekwenda mbio mpaka mahali alipokuwa amesimama.

    “ Nikusaidie nini mzee?”

    “Tunahitaji machela, tuna mgonjwa ambaye tunasafiri naye kwenda Canada!”

    “Sawa subiri kidogo nije!” Alisema mfanyakazi huyo na kuondoka, aliporejea dakika moja baadaye alikuwa na machela waliyokuwa wakiisukuma yeye na wenzake wawili.

    “Yuko wapi mgonjwa?”?“Yupo ndani ya gari!”

    Vijana hao walisaidiana na O’brien pamoja na Nicky kumshusha Caroline kwenye gari na kumweka juu ya machela! Alikuwa hoi hajitambui bila kuelewa chochote kilichoendelea, alilala usingizi mzito mno  ambao haukumpa hata nafasi ya kuota ndoto moja. Baada ya kuteremshwa alipakiwa kwenye machela na walipoangalia saa zao waligundua zilikuwa zimesalia dakika thelathini tu ndege iruke, kifupi walikuwa wamechelewa hivyo zilihitajika juhudi za ziada ili kuwahi ndege.

    “Mgonjwa wenu ana matatizo gani?”

    “Alianguka ghafla juzi kama kinavyoonyesha hicho cheti madaktari wanasema amepatwa na Kiharusi!” Kennedy alidanganya lakini haikuwa rahisi kugundua sababu cheti kilionyesha hivyo.

    “Poleni sana!”

    “Ahsante!”

    Hawakupata usumbufu wowote ndani ya uwanja na hivyo kufanikiwa kuiwahi ndege, kila mahali walikopita watu waliwapa pole kwa mgonjwa waliyekuwa naye, waligongesha mikono mara kwa mara kujipongeza kwa jinsi kazi hiyo ilivyokuwa rahisi! Hawakuwa na kitu kingine walichokiwaza kichwani mwao zaidi ya pesa, kwa hakika waliamini  tayari umasikini walikuwa  wamepishana nao njia.

    Ndani ya ndege Caroline aliwekwa kwenye kiti cha katikati ambacho kililazwa kabisa na kuwa kama kitanda, pembeni yake mkono wa kushoto alikaa O’brien   kulia alikaa Kennedy na Nicky alikaa kiti cha mbele ya Caroline.

    Muda mfupi baadaye ndege iliiacha ardhi ya Vietnam lakini dakika mbili tu ikiwa angani rubani na Injinia waligundua kasoro fulani katika injini, kulikuwa na mlio usio wa kawaida! Wote waliangaliana machoni wakifikiria juu ya nini cha kufanya, ghafla ndege ilianza kupunguza nguvu na taratibu ikaanza kushuka ardhini, rubani alifanikiwa kuipeleka hadi chini bila matatizo yoyote na kuigesha vizuri.

    Hapakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya matengenezo yaliyochukua muda wa kama masaa matatu na nusu  ndipo ndege iliporuhusiwa kuruka tena,  safari hiyo ilikuwa haiendi moja kwa moja Canada, ndege ilikuwa  na ratiba ya kupita katika miji ya Stockholm nchini Sweden, Copenhagen  nchini Denmark ndipo itue nchini Canada katika jiji la Ottawa, hiyo ilikuwa ni safari ya masaa  sita kwa sababu  mzunguko  mrefu na mwendo wa ndege hiyo haukuwa wa kasi.

    Dawa ya Pethedine aliyochomwa Caroline humpa mtu usingizi kwa masaa sita jambo ambalo Kennedy na wanzake hawakulielewa vizuri, waliamini baada ya kumchoma angelala mpaka wanatua  nchini Canada, lakini  kitendo cha ndege kuharibika na kutua  kwa mara ya pili  uwanjani kufanyiwa matengenezo kilikula sehemu ya masaa hayo. Wakiwa katika uwanja wa ndege wa Sweden, Caroline alifumbua macho yake! Alipoangaza huku na kule aligundua alikuwa ndani ya ndege, alipotupa macho yake kushoto na kulia aliwaona O’brien na Kennedy wakiwa taabani usingizini. Hakumwona  Nicky tu kati yao na hakujua mahali alikokuwa.

    Alipotupa macho yake dirishani aligundua ndege ilikuwa nchi kavu sababu aliona ndege nyingine pamoja na majengo, kwake huo ulikuwa wakati muafaka wa kutoroka! Mambo mawili yalimfanya ashindwe kuchukua uamuzi huo haraka. Kwanza, hakujua mahali Nicky alikokuwa si ajabu kama angenyanyuka lazima angeonekana.

    Pili, hakujua walikuwa katika uwanja gani! Pengine walikuwa nchini Canada na kushuka kwake labda kungemtia mikononi mwa Dk. Ian jambo ambalo hakutaka kabisa litokee.Aliamua kutulia na muda mfupi baadaye alisikia sauti ya kike ikitangaza kuwa ndege ingeruka  katika muda wa dakika tano kutoka katika uwanja wa Copenhagen kuelekea Ottawa nchini Canada.

    “Ha! Kumbe tulikuwa Dernmark?” Aliwaza Caroline.

    Alijua wazi uwanja  wa ndege uliofuata ndiko alikokuwa akisubiriwa kwa hamu na kifo chake, alizidi kuogopa kwa hakika hakuwa tayari kuingia tena mikononi mwa Dk. Ian lakini alishindwa ni kwa njia gani angeweza kumwepuka. Kabla  ndege haijaanza kusogea mbele Caroline alitupa macho yake  kwenye kiti cha mbele na kumwona Nicky naye akiwa amelala fofofo, tena yeye hadi udelele ulimdondoka mdomoni!

    “Mungu wangu hii ndiyo nafasi pekee ya kuokoa maisha yangu!” Aliwaza Caroline na bila kusita aliufungua mkanda uliomfunga kwenye kiti, alipousikiliza vizuri  mwili wake aligundua nguvu za kutosha zilikuwepo kumwezesha kurotoka, alinyanyuka taratibu na kusimama  wima! Si Nicky, Kennedy wala O’brien aliyeshtukia hatua hiyo. Lakini ghafla Kennedy alijitingisha na kujigeuza, kuona hivyo Caroline alirudi kwa kasi  akajitupa   kwenye kiti na kuendelea kujifanya hana fahamu! Kwa jicho lake la pembeni alimshuhudia Kennedy akimwangalia kwa mshangao, alikuwa ameusikia mlio wa kiti wakati Caroline akijitupa.

    Ili kuhakikisha kuwa kweli Caroline alikuwa bado  yu usingizini  Kennedy aliingiza mkono  kwenye mfuko  wa shati lake na kutoa pini yenye ncha kali, aliizamisha moja kwa moja kwenye paja lake la kulia ili kuona kama angeshtuka, macho yote mawili yakiwa yamemwangalia Caroline usoni ili kuona kama angekunja uso wake jambo ambalo lingemaanisha ni yeye aliyejitupa kitini.

              *****************

    Harry alimshuhudia mzee mmoja akiwaamuru jambo wanaume wenye nguvu walioingia ndani ya chumba hicho, mwanzoni alifikiri wanaamrishwa kumuua lakini alishangaa baadaye mmoja wa wazee  hao alipomkabidhi kwa wanaume  hao wenye nguvu ili   wampeleke kwenye jengo la benki ya watu wa Sudan   kuchukua pesa yake!  Waliamriwa kumpa ulinzi uliotakiwa.

    “Au ulitaka tukulipe kwa utaratibu gani?”

    “Kwani hamuwezi kuniingizia hizo pesa kwenye akaunti yangu iliyoko katika benki ya Standard Bank  ya Uingereza ambayo ina tawi katika kila nchi? Mkiniwekea katika akaunti yangu ninaweza kuzichukua pesa hizo hata nikiwa    katika Jamhuri ya Sokomoni ambako nina kazi ya kufanya!” Alisema Harry.

    “Hiyo ni rahisi sana, maana kutembea na pesa  nyingi katika nchi isiyokuwa na amani kama hii ni hatari!”Alisema mzee mwingine na Harry akaandikiwa hundi ya jumla ya dola za Kimarekani Milioni.................

    Ilikuwa furaha mno kwake na hata wakati akitembea kwenda benki alikuwa akiimba wimbo wa mafanikio moyoni mwake, hata mara moja hakumfikiria Caroline ingawa alijua kwa wakati huo alikuwa katika matatizo makubwa sana na pengine tayari alikuwa mfu.

    “Tayari nimeshakuwa Rais wa Sokomoni!”

    Sokomoni ilikuwa ni nchi ndogo jirani kabisa na Tanzania, ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu wasiozidi milioni tano! Ilikuwa ni Jamhuri  ya kwanza katika Afrika kuamua kuanzisha mfumo wa vyama vingi, Raia wa nchi hizo mbili walikuwa na mahusiano makubwa  sana kulikuwa na watu wengi waliokuwa na ndugu pande zote mbili za nchi hizo, lilikuwa si jambo la ajabu kukuta shangazi anaishi  Sokomoni na baba anaishi Tanzania.

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Harry, alikuwa na uraia pande zote mbili kwani  bibi  yake mzaa mama na mama zake wengine wadogo waliishi katika Jamhuri hiyo na mara nyingi hata yeye mwenyewe alikwenda huko na kutambulika kama raia. Kwa pesa nyingi aliyopata alitaka kuutumia  upenyo huo kuukwaa Urais wa  Sokomoni kupitia chama chochote cha siasa kilichokuwa katika Upinzani akiwa katika umri mdogo.

    Baada tu ya kukabidhiwa hundi yake alisindikizwa hadi mjini ambako aliiweka hundi hiyo katika akaunti yake na siku hiyo hiyo alipanda ndege iliyompeleka moja kwa moja hadi nchini Sokomoni ambako alikuta vuguvugu la uchaguzi limepamba moto.

    Watu wa kwanza aliwafuata akitaka kujiunga na chama chao kwa lengo la kuwa Mfadhili na hatimaye kugombea  walikuwa  wenye chama cha CKMW au Chama cha Kutetea Maslahi ya wananchi.

    Je, nini kitatokea? Harry atafanikiwa kuwa Rais? Na je ndani ya ndege nini kitampata Caroline? Na je wazazi wake atakutana nao? Fuatilia wiki ijayo.













    S

    indano aliyochomwa ?mwilini mwake ?ilimsababishia Caroline maumivu makali kupita kiasi, Kennedy  alikuwa ametumia nguvu nyingi sana kuizamisha sindano hiyo pajani mwake lakini  pamoja na maumivu yote hayo Caroline hakudiriki kujitingisha, aliyafahamu madhara ya kufanya hivyo!

    Alibana pumzi kwa nguvu zote, hakukaza macho hata kidogo na wala hakuonyesha mshtuko wowote usoni mwake! Hata yeye mwenyewe alishindwa kuelewa  ni vipi aliweza kuyahimili maumivu makali kama hayo, aliamini kweli kwa binadamu wakati wa shida hupata nguvu za ziada.

    Kwa kitendo hicho Kennedy aliridhika kabisa kuwa Caroline alikuwa bado yu usingizini, hakutaka kupoteza muda zaidi aliangusha kichwa chake kwenye kiti na dakika chache baadaye alikuwa akikoroma!

    “Kalala!” Aliwaza Caroline

    Dakika chache tu baadaye ndege ilikuwa angani ikiitafuta nchi ya Dernmark,  Caroline alikuwa bado amefumba macho yake akiendelea  kujifanya hana fahamu! Hakutaka kufumbua macho mapema kwa kuogopa kugundulika, mawazo yake yote yalikuwa ni kwa jinsi gani angeweza kujiokoa kutoka mikononi mwa kifo kilichokuwa mbele yake.

    Katika masaa machache yaliyokuwa mbele yake alitakiwa kuwa maiti hilo hata yeye alilifahamu na hakuwa tayari kufa kirahisi, watu pekee waliokuwa na uwezo wa kuzuia asiokoke ni waliokuwa pembeni yake na aliyekuwa amekaa kiti cha mbele yaani Kennedy, O’brien na Nicky! Hao ndio waliokuwa wakimpeleka kwa Dk. Ian ambako yeye alikufananisha na machinjioni.

    “Lakini pengine Dk. Ian anaweza kunionea huruma hasa nikimwambia kuwa Harry aliniteka na kwenda kunitelekeza Vietnam!” Aliwaza Caroline lakini alishindwa kuelewa ni kwa jinsi gani angeweza kumshawishi Dk. Ian mpaka ayaamini maneno yake.

    “Hiyo ni sawa na kucheza kamari! Siwezi kufanya hivyo akikataa si nitakufa? Siwezi kujipeleka mwenyewe kufuata kifo changu, ni lazima nijaribu kujiokoa kwanza ikishindikana basi!” Aliendelea kuwaza  Caroline.

    Ndege iliendelea kukatiza mawinguni katika anga ya Sweden ikielekea Dernmark ambako abiria walishatangaziwa kuwa ingetua  katika muda wa masaa mawili yaliyokuwa mbele yao, abiria walishachoshwa na safari na walitamani kufika Canada haraka.

    “Tukifika Copenhagen kama watakuwa bado wamelala   nitashuka hapohapo na kuondoka zangu!” Aliwaza Caroline na alitamani sana hali hiyo itokee, kwa hakika hakutaka kabisa kukutana uso kwa uso na Dk. Ian! Aliufahamu ukatili wake na alikuwa na hakika angeuawa.

              ******************http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mpaka zikiwa zimesalia dakika ishirini ndege itue  katika uwanja wa ndege wa Copenhagen Kennedy, O’brien na Nicky walikuwa bado wako usingizini na Caroline alikuwa akiwaangalia kupitia kwenye  kona ya macho yake yote mawili! Hakutaka kufumbua macho kwa kuogopa kugundulika, alizidi kumwomba Mungu watu hao waendelee kulala ili  ndege ikitua tu katika uwanja wa Copenhagen achoropoke na kutoroka.

    “Ndege inakaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Copenhagen, abiria wote tunaombwa kufunga mikanda yenu tayari kwa kutua!” Ilisikika sauti ya kike ikiongea kutoka katika spika zilizokuwa pembeni mwa viti vya abiria. Ni sauti hiyo iliyowafanya Kennedy na wenzake kuzinduka kutoka usingizini na walipoamka tu wote walimtupia macho Caroline mahali alipolala! Aliona kila kilichoendelea na alilaumu ni kwanini waliamka. Caroline alishuhudia wakifunga mikanda yao vizuri tayari kwa kutua, roho ilimuuma sana na matumaini ya kunusurika na kifo yalizidi kupungua, baada ya kufunga mikanda yao alitegemea wangesinzia tena lakini haikuwa hivyo walikuwa macho mpaka wakati ndege inatua katika uwanja wa Copenhagen ambako waliendelea kuongea mengi kuhusu malipo ya pesa nyingi iliyokuwa mbele yao kama wangefanikiwa kumfikisha Caroline mikononi mwa Dk. Ian.

    “Ah! tutakuwa matajiri sasa!” Kennedy aliwaambia wenzake

    “Si bado yupo usingizini lakini?” Nicky aliuliza.

    “Ndiyo hawezi kuamka sasa hivi ile dawa ni  kali sana!”

    “Kwa kweli tumecheza mchezo mkali sana, hakuna mtu anayeweza kushtukia dili hili!”

    “Hata shetani mwenyewe hawezi kuelewa!”

    “Masikini msichana wa watu anakwenda kufa!” Kennedy alisema huku akimshika shavu Caroline.

    “Sasa sisi tufanye nini wakati tunahitaji pesa?”

    Kila kitu  ambacho Kennedy na wenzake waliongea  Caroline alikisikia na kuzidi kutishika zaidi,  alihisi mwili kutetemeka, alikiogopa sana kifo kilichokuwa mbele yake! Alijua asingeweza kusamehewa kwani Dk. Ian aliipenda sana ndege yake. Caroline alijutia   ujinga wake wa kutekwa kimapenzi kirahisi, alijilaumu kwa kushindwa kutofautisha mapenzi ya kweli na ya uongo.

    “Dalili za kwamba Harry hakunipenda niliziona tangu mwanzo tukiwa Arusha, aliponikataa kwa sababu tu nilikuwa na kifafa! Sasa sijui ni kitu gani kilichonifanya nimwamini  kwa mara ya pili na kumwacha mtu aliyeniponyesha ugonjwa uliofanya Harry aniache na kuyabadilisha kabisa maisha yangu! Kwa kweli sitamsamehe Harry maishani mwangu na ni lazima nimtafute kokote aliko duniani ili nimwonyeshe kuwa alichokifanya si kitu kizuri, labda nife lakini kama nikiwa hai na nikafanikiwa kufika huko Tanzania au hata Sokomoni ni lazima nimuue tena kwa mkono wangu mwenyewe na si yeye tu na wenzake wote waliochangia kuniumiza katika maisha yangu ni lazima waende kaburini” Aliendelea kuwaza Caroline.

    Mpaka ndege inaondoka Copenhagen kuelekea mwisho wa safari yao nchini Canada, nchi ambayo Caroline hakutaka kabisa kufika, Kennedy na wenzake walikuwa bado hawajalala usingizi maongezi yao yalikuwa juu ya pesa tu, hakuna kitu walichotamani kama kufika Canada na kumkabidhi Caroline mikononi mwa Dk. Ian.

    Dakika thelathini  na tano baadaye ndege ikiwa angani Caroline kupitia katika pembe ya jicho lake la kushoto aliweza kukiona kichwa cha  Kennedy kikiyumba upande mmoja hadi mwingine na  muda mfupi baadaye  alitulia, jambo lililoonyesha tayari alikuwa usingizini kwa mara nyingine! Kwa kutumia jicho lake la upande wa kulia alimwona O’brien naye akicheza mchezo wa aina hiyo hiyo na dakika chache baadaye naye alitulia.

    Caroline alishindwa kuelewa watu hawa walikuwa ni wa aina gani waliopenda usingizi kuliko kitu kingine chochote, alitamani kuwa na uwanja mwingine wa ndege  kutua kabla ya kuingia Ottawa lakini haikuwa hivyo,  nchi iliyokuwa mbele yao ilikuwa ni Canada peke yake na huo ndio ungekuwa mwisho wa safari ni katika mji huo ndiko kifo chake kilikokuwa, alitamani kufanya lolote asifike kabisa katika mji huo! Ilikuwa ni afadhali aruke kupitia dirishani na aanguke ardhini na kupasuka kuliko kuingia mikononi mwa Dk. Ian.

    “Nitafanya nini mimi? Nitafanya nini kujiokoa? Yaani kweli niingie mikononi mwa Dk. Ian? Haiwezekani! Ni lazima nifanye jambo” Caroline aliwaza na kujiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu.

    “Ndege ya shirika la ndege la British Airways ndiyo unayosafiri nayo kutoka Vietnam kwenda Canada! Ni shirika la uhakika na salama, kila mara unapofikiria kusafiri  tumia shirika hili ni raha na salama.Ndege yetu inategemewa kutua katika uwanja wa ndege wa Ottawa katika muda wa saa moja ijayo na huo ndio utakuwa mwisho wa safari yetu, pelekeni sifa ya shirika letu popote muendako  na mabaya yetu tuelezeni sisi!” Iliendelea kusema sauti ya msichana aliyekuwa akiongea na kipaza sauti, alitumia Kiingereza, Kiswidishi na Kifaransa. Safari hii Kennedy na wenzake hawakuzinduliwa na sauti hiyo, waliendelea kulala fofofo.

    “Ha! Bado saa moja tu! Ee Mungu nisaidie!” Caroline alijikuta akitamka.

                         *************

    “Chukua hii!”

    “Ni nini?”

    “Chukua tu itakusaidia, mimi ilishanisaidia mara nyingi sana nilipoingia katika matatizo!”

    “Ni nini lakini?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni sumu ambayo ukimgusa nayo mtu kwenye ngozi yake hutumia dakika kumi kupenya katika ngozi na kwenda kwenye damu! Ambacho hufuata baada ya hapo ni mtu kukauka na kufa katika muda wa dakika ishirini! unachotakiwa kufanya ni kunawa mikono katika muda wa sekunde thelathini baada ya kuigusa kama hukufanya hivyo hata wewe mwenyewe unaweza kufa!”

    Caroline aliipokea dawa hiyo iliyokuwa katika muundo wa unga mweusi na kuifunga katika  kipande cha karatasi ya  nailoni, alishauriwa  na mzee huyo aishonee katika pindo lake la gauni hivyo ndivyo alivyofanya, alifurahi kuipata na alipanga kuitumia kukamilisha lengo lake la kuwaua watu wote waliomfanyia unyama maishani.

    “Wa kwanza kumuua na sumu hii atakuwa Harry!” Aliwaza baada ya kumaliza kuishonea katika pindo la gauni lake.

    Hayo yalikuwa maongezi yaliyofanyika kati ya mzee Nelson  na Caroline porini, usiku  kabla hawajaondoka kwa farasi kuelekea mjini Penh!  Kwa sababu hakuuona  umuhimu wa sumu hiyo kabla ya kufika Tanzania au Sokomoni, Caroline alijikuta amesahau kama alikuwa nayo. Lakini akiwa katika mawazo mengi  ya namna gani angeweza kujiokoa  ikiwa ni dakika  kama arobaini na tano kabla ya ndege kutua  katika uwanja wa Ottawa, aliikumbuka sumu hiyo.

    Akiwa Penh kwenye mgahawa wa bibi Suzanne alinunua gauni jingine  akawa na magauni mawili aliyobadilisha mara kwa mara lakini bahati nzuri siku aliyotekwa alivaa  gauni alilotoka nalo porini hivyo sumu ilikuwa katika pindo la gauni lake.

    “Yes!Yes!Yes!Yes! Nakushukuru sana mzee Nelson, kweli umeokoa maisha yangu! Ni lazima niitumie sumu hii kutoroka, ni lazima hawa wajinga wafe kabla ndege haijatua!”

    Alipowaangalia  Kennedy na O’brien   aligundua   walikuwa   usingizini na  aliposikiliza vizuri katika viti vya mbele alimsikia Nicky akikoroma akajua naye alikuwa akiota ndoto zao za utajiri! Huo kwake   ulikuwa ndio wakati  muafaka wa kutekeleza alichotaka kukifanya. Kwa utaalam wa hali ya juu alijikunja nakushika gauni lake kwa chini na kuanza kulipapasa katika pindo lake.

    Haikumchukua muda mrefu akawa tayari ameshaligusa fundo la mahali sumu yake ilipofichwa, alizichana nyuzi zote na kukitoa kifuko cha nailoni kilichokuwemo, akiwa amelala hivyo hivyo alikifungua na kuchukua kiasi kidogo cha sumu na kukimwaga katika kiganja chake, sumu iliyobaki aliifunga vizuri na kuiweka pembeni mwake.

    Kwa mkono wake wa kulia alichukua sumu iliyokuwa katika kiganja chake, akaunyosha mkono wake na  kumpaka Kennedy shingoni, hakushtuka wala kujitingisha, aliamini kwa huyo kazi ilishakamilika! Bila kusita wala kuchelewa alichukua sumu nyingine na kumpaka O’brien usoni! Kwa huyo naye alijua kazi imekamilika akawa amebaki Nicky aliyekuwa kiti cha mbele kwa huyo ilimlazimu asimame taratibu bila kutingisha kitu chochote na kumpaka begani, alifanya mambo yote hayo bila kushtukiwa na abiria waliokuwemo ndani ya ndege.

    Kwa maelekezo aliyopewa alitakiwa  kunawa mikono yake katika muda wa sekunde thelathini tofauti na hapo hata yeye sumu hiyo ingemuua! Baada ya kukamilisha kazi ya kuwagusa kilichofuata mbele yake kilikuwa ni kunawa,  hakuwa na maji lakini kwa alivyofahamu ndani ya ndege kulikuwa na bafu na maji ya kutosha. Alichofanya ni kunyata taratibu na kumruka Kennedy akaingia kwenye korido na kuanza kutembea kwenda bafuni ambako alisukuma mlango na kukuta umefungwa, ilivyoonekana kulikuwa na mtu mwingine ndani ya choo hicho akijisaidia.

    “Ngo!Ngo!Ngo!” Caroline alianza kugonga mlangoni ili afunguliwe.

    “Pra...ttaata....pra....ttaatta,pra...ttaata!” Hiyo ndiyo sauti aliyoisikia kutoka ndani ya choo hicho, hakuhitaji muda mrefu kuelewa kuwa kulikuwa na mtu akiharisha vibaya sana ndani ya choo hicho.

    “Please open the door for me!”(Tafadhali nifungulie mlango!) Caroline alisema kwa sauti lakini mtu aliyekuwa ndani hakusikia, aliendelea na shughuli yake kama ilivyopangwa.

    Alishindwa kuelewa ni kipi afanye, zilibaki sekunde  chache sana kabla sumu haijamdhuru yeye mwenyewe! Tayari alishaanza kusikika kizunguzungu, hakuwa na la kufanya zaidi ya kuuparamia mlango wa choo cha wanaume, hakuona aibu kwani alitaka kuokoa maisha yake! Lakini alikuta nao pia  umefungwa jambo lililoashiria ndani  ya choo hicho kulikuwa na mtu. Caroline alichanganyikiwa  na kushindwa kuelewa ni wapi angepata maji ya kunawa kwani bila hivyo hata yeye angekufa.?Je nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.













    H

    arry alifika nchini ?Sokomoni akitokea Tan?zania na katika muda mfupi alioishi nchini humo alijipatia umaarufu mkubwa na kufahamika na karibu kila mtu wakubwa kwa wadogo, kilichomfanya ajulikane sana ni kitendo chake cha kutumia pesa nyingi kukifadhili   chama kikuu  cha upinzani nchini Sokomoni, Chama cha kutetea maslahi ya wananchi (CKMW)

    Alitumia pesa nyingi sana kukiimarisha chama hicho na  kuisaidia jamii ya watu wa Sokomoni iliyokuwa masikini, aliwapatia vijana wengi ajira na mikopo ya mitaji ili wajiajiri wenyewe. Ni hilo ndilo lilimpa umaarufu mkubwa katika nchi hiyo iliyokuwa chini ya Utawala wa chama kimoja tangu kupata uhuru wake mwaka 1972 kutoka kwa wakoloni katika mapinduzi yaliyoongozwa na Rais wa Kwanza wa nchi hiyo,Gabriel ambaye baadaye alifuatiwa na Rais wa pili wa nchi hiyo Derrick aliyeingia madarakani kwa kuipindua Serikali ya Rais Gabriel ambaye awali  ndiye alimnyang’anya  Derrick mke wake Kabula.

    Rais aliyekuwa madarakani kwa wakati huo, Pedro Kinasho aliiongoza nchi hiyo chini ya chama cha SPMD, kwa hakika katika kipindi hicho chama  hicho kilishapoteza umaarufu  na chama cha CKMW ndicho kilikuwa kikitamba nchini humo. Mwaka huo ndio ulikuwa mwaka wa kwanza kwa nchi ya Sokomoni kushiriki uchaguzi wa vyama vingi.

    Kwa sababu lengo la Harry lilikuwa ni  kutumia pesa aliyokuwa nayo  ili aingie madarakani, alijichomeka katika chama hicho kama mfadhili lakini lengo lake likiwa  ni baadaye kushika  uongozi wa  chama hicho na kugombea Urais, alikuwa kijana mdogo mno lakini kwa sababu alikuwa na pesa watu wengi ndani ya chama hicho walimwamini katika muda mfupi na kumtaka hata aongoze chama chao.

    “Lengo langu si kuongoza chama wala nchi hii ninataka kusaidia tu!” alisema Harry kila alipohojiwa na waandishi wa habari.

    Harry hakutaka kuionyesha nia yake waziwazi  lakini miezi michache baadaye alijikuta akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho na kukubali mara moja ni kipindi hicho ndio alimwaga pesa zaidi katika chama, chama chake kikapata umaarufu kupita kiasi, watu wengi walikihama chama Tawala na kujiunga na chama chake! Ilikuwepo kila dalili kuwa chama cha  CKMW kingeshinda na kuingia Ikulu na hiyo ingemfanya Harry kutimiza lengo lake la kuwa Rais!

    Hata mara moja Harry hakuwahi kumfikiria Caroline na mambo aliyomfanyia, kwanza alikuwa na uhakika Caroline alikuwa marehemu! Asingeweza kutoka mikononi mwa Wavietnam salama.

    “Acha afe ni jambo la kawaida wakati mwingine kuua ili uingie Ikulu tena ni afadhali mimi nimeua mtu mmoja tu! Vipi wanaua mamia ya watu kama inavyotokea huko  Bosnia na nchi nyingine?” Aliwaza Harry, mpaka wakati huo alikuwa na uhakika asilimia mia moja ni yeye ndiye angekuwa Rais wa nne wa nchi ya  Sokomoni na alihakikisha hilo linawezekana kwa kutembea kila pembe ya nchi ya Sokomoni akipiga kampeni na kumwaga misaada mbalimbali kwa wapiga kura, pamoja na umri wake kuwa mdogo wananchi wa Sokomoni walimwamini na kuahidi kumpa nchi.

                 **************

    Kizunguzungu kilizidi kumbana Caroline akiwa amesimama nje ya vyoo ndani ya ndege hiyo, ilikuwa tayari ni sekunde ya  ishirini na tano tangu aiguse sumu aliyoitumia kuwapaka O’brien na wenzake! Kwa mujibu wa mzee Nelson aliyempa sumu hiyo kama asingenawa katika muda wa sekunde thelathini hata yeye angekwenda na maji! Milango yote ya  chooni ilikuwa imefungwa na ndani yake ilisikika milio kama ya pikipiki ndogo aina ya Vespa ambazo hupatikana sana Zanzibar,   hapakuwa na dalili yoyote ya watu hao kufungua milango ya vyoo ili Caroline anawe, kwa hakika alijua kifo chake kimefika. Alijitemea mate mikononi ili anawe lakini hayakutosha na alipoiangalia saa yake ya mkononi tayari ilikuwa ikikimbilia sekunde ya ishirini na  tisa.

    “Siwezi! Siwezi kufa naona hivihivi!” Alijisemea kwa sauti ya chini Caroline.

    Bila aibu yoyote Caroline alichuchumaa, akalegeza sketi yake na kuishusha chini kwa kasi ya ajabu na aliishusha pamoja na nguo yake ya ndani, alikuwa amepata jibu la tatizo lake kama vile maji yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye mpira wa maji uliotoboka ndivyo mkojo wake ulivyomtoka, aliutumia mkojo wake mwenyewe kunawa tena kwenye veranda ya ndege.Hakuona aibu wala kuwa na hofu yoyote moyoni mwake.

    Wafanyakazi wa ndani ya ndege walikishuhudia kitendo alichokifanya na kwa haraka walitembea hadi sehemu aliyokuwa amechuchumaa na kuanza kumhoji maswali, alionekana kutokuwa na jibu la kuwaridhisha lakini kwa sababu alikuwa mteja hawakuwa na jambo la kumfanya.

    “My bladder was full, I had nothing to do except this!”(Mfuko wangu wa mkojo ulikuwa umejaa na sikuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya hii!) aliwajibu wafanyakazi hao huku akitabasamu.

    Kwa jinsi wafanyakazi wa ndege hiyo walivyoambiwa juu ya Caroline, alikuwa mgonjwa aliyekuwa akisafirishwa kwenda nyumbani kwao Canada, kwa sababu hiyo hawakushangazwa sana na kitendo alichokifanya walifikiri yote yaliyotokea yalikuwa ni sababu ya ugonjwa wake,hawakukasirishwa sana na kitendo hicho na badala yake walimsaidia na kumrudisha hadi kitini ambako alikaa na kujifanya amelala.

    Kutoka mahali alipolala hakusikia sauti wala kelele yoyote ya mhemo wala mkoromo kutoka mdomoni wala puani mwa O’brien na Kennedy aliolala katikati yao, hiyo ilimwonyesha kabisa kuwa tayari walishakata roho! Aliponyoosha mikono yake yote miwili  kujaribu kuwagusa, alishangazwa na jinsi miili yao ilivyokuwa migumu, ilikuwa ni kama ubao. Bila kutegemea alijikuta akinyanyuka na kuketi, akamfunua Kennedy na kumwangalia, mwili wake ulishabadilika rangi na kuwa kama mkaa. Alishangazwa na jinsi sumu hiyo ilivyofanya kazi, katika muda mfupi tayari ilishaua.

    “Mh! Hii sumu si mchezo! Sijui aliitengeneza kwa kutumia nini?” Aliwaza Caroline,   aliwapekua Kennedy na O’brien mifukoni na kuwakuta wakiwa na jumla ya Dola laki mbili  na nusu za Kimarekani zote alizichukua na kuzizamisha katika nguo yake ya ndani, alifurahi kuzipata pesa hizo na aliamini ni lazima zingemfikisha Tanzania ambako msako wake wa mauaji ungeendelea, alikuwa amepania kuua, kuwaua watu wote waliomfanyia mabaya zaidi sana alitamani kumuua Harry.

    Dakika chache baadaye sauti ya msichana akitangaza kuwa ndege ingetua kwenye uwanja wa ndege wa Ottawa katika muda wa dakika kumi na tano ilisikika, msichana huyo aliwataka watu kukaa vitini, kunyoosha viti vyao na kufunga mikanda yao vizuri kabla ndege haijatua, ili kuepuka viti vya akina Kennedy kurekebishwa na wafanyakazi wa ndege jambo ambalo lingefanya igundulike kuwa walikuwa wamekufa, Caroline aliifanya kazi hiyo mwenyewe na kuwafunika vizuri kwa kofia zao usoni kama vile walikuwa usingizini. Kwa sababu ya kukakamaa hawakuweza kukaa vizuri.

    “Can I help you?”(Nikusaidie?) mmoja wafanyakazi wa ndege alimuuliza Caroline.

    “Thanks! I appriciate.......”(Ahsante! Ninakushukuru......!)

    “Why is he so stiff?”(Kwanini amekakamaa kiasi hiki?) Mfanyakazi wa ndege aliuliza akitaka kumgusa O’brien.

    “No!No!No!No! dont disturb, let him enjoy his sleep!”(Hapana! Hapana! Usimsumbue! Mwache afaidi usingizi  wake) alisema Caroline kwa sauti ya juu, mfanyakazi huyo alionekana kushangazwa na mabadiliko aliyokuwa nayo Caroline aliyepakiwa ndani ya ndege akiwa hajitambui kabisa.

    “How are you doing at the moment?”(Unajisikiaje sasa hivi?)

    “Very fine!”(Najisikia vizuri!)

    “You were so sick when the brought you!”(Ulikuwa unaumwa sana walivyokuleta!) Aliuliza mfanyakazi wakati akiondoka kuelekea kwenye kiti chake na dakika kumi baadaye ndege ilikuwa ikiserereka ardhini kwenye uwanja wa Ottawa.

    Moyo wa Caroline ulidunda! Alijisikia hofu kubwa kupita kiasi, alijua kwa hakika nje ya uwanja alikuwepo Dk. Ian akimsubiri kwa ajili ya kumuua, ilikuwa ni lazima afanye chochote kilichowezekana lakini asiingie mikononi mwa mzee huyo mwenye roho mbaya.Tayari alishawaua Kennedy na wenzake hivyo kilichokuwa mbele yake ni kutoroka tu.

    Alikuwa mtu wa kwanza kufika  mlangoni ndege iliposimama na kutulia, alifanya  kila kitu kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha kuwa hagunduliki na hakuna mfanyakazi yeyote wa ndege aliyemwona wakati akitembea kuelekea mlangoni.Mlango ulipofunguliwa alikuwa mtu wa kwanza kuziteremka ngazi kutoka ndani ya ndege hiyo abiria wengine wengi walifuata nyuma yake. Alijua wazi muda si mrefu angekuwa akitafutwa hivyo ilikuwa ni lazima apotee kabla mambo hayajaharibika.

    Ingawa hakujua ni mlango gani angepitia lakini  hakuwa tayari kupitia mlango wa kawaida wa abiria ambako ni lazima angekutana ana kwa ana na Dk. Ian na huo ndio ungekuwa mwisho  wa maisha yake.

    “Pesa ni sabuni ya roho! Kwa pesa hii niliyonayo lazima nitatoka uwanjani bila kujulikana!” Alijipa moyo Caroline.

    Baada tu ya kuteremka aliizunguka ndege na kuanza kukimbia akiwa ameinama kuelekea upande wa pili wa kiwanja kulikokuwa na majengo makubwa yaliyojengwa kwa mabati,  hakujisikia mgeni sana kuwa nchini Canada,  nchi hiyo ilikuwa ni kama nyumbani kwa sababu aliishi hapo muda mrefu enzi za mapenzi yake na Dk. Ian. Pamoja na hayo yote bado mwili wake  ulitetemeka kwa hofu kubwa aliyokuwa nayo moyoni mwake.Alijua nje ya uwanja huo kulikuwa na mtu aliyekuwa na hamu kubwa ya kumuua kama kisasi kwa mabaya aliyomfanyia..

    “wo!wo!wo!” Zilikuwa ni sauti za kundi   la Mbwa  kama watano hivi waliokuwa wakibweka huku wakimkimbiza  Caroline, nyuma yao alikuwepo askari mwenye bunduki! Mbio hizo zilimfikisha kwenye uzio   wa senyenge uliokuwa mwisho wa kiwanja hicho, hapakuwa na sehemu zaidi ya kwenda! Mbwa walipomfikia walimvamia na kumwangusha chini, walianza kumuuma kwa meno mpaka askari alipofika na kuwaamuru waache.

    “Who are you?”(Wewe ni nani?)

    “Marione!” Alidanganya.

    “Why are you running? Are you a crack dealer?”(Kwanini unakimbia? Wewe ni muuza madawa ya kulevya?)

    “No!No! Not at all!”(Hapana! Hapana!)

    “Then why are running?”(Sasa kwanini unakimbia?)

    “Listen, can you save my life?”(Sikiliza, unaweza kuokoa maisha yangu?)

    “It depends!”(Inategemea!)http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “What if I give you ten  thousands USD? Will you let go of me?”(Vipi kama nikikupa dola elfu kumi utaniachia niondoke?)

    “Definately!”(bila shaka!)

    Bila kusita wala kupoteza muda Caroline alilipandisha gauni lake na kuingiza mikono yake ndani ya nguo ya ndani na kulichomoa bulungutu  la noti alilokuwa nalo na kuhesabu  dola elfu kumi, akamkabidhi askari huyo! Meno yote thelathini na mbili ya askari yalionekana, ilikuwa furaha kubwa mno kwake,  kuingia kazini na kutoka na dola elfu kumi?ni jambo ambalo hakulitegemea  kabisa siku hiyo.

    “Then show me the way out of the Airport without being noticed!”(Nionyeshe njia ya kutoka nje ya uwanja wa ndege bila kugundulika!)

    “Come with me!”(Nifuate!) Aliamuru askari na Caroline alianza kumfuata kwa nyuma, mbwa wote walikuwa kimya hakuna hata mmoja aliyediriki kubweka.

    “Mtu wa hatari yuko ndani ya uwanja! Tayari amekwishaua watu watatu kwa sumu, maaskari kaeni chonjo! Mtu huyu ni mwanamke, ni hatari na inaaminika anaua kwa kutumia sumu ya kukausha mwili!” Ilikuwa ni sauti kutoka katika spika zilizokuwepo uwanjani hapo, ilisikika wakiwa wametembea kama hatua ishirini hivi mbele,  bahati nzuri kwa sababu ya kubabaika na pesa alizopewa askari hakuisikia sauti hiyo lakini Caroline alijua muda si mrefu angesikia na mambo yangebadilika.

    Alijikunja na kulishika pindo la gauni lake, akaanza kulipapasa taratibu mpaka alipofikia sehemu alipoizamisha  sumu yake, aliingiza vidole viwili katika sehemu aliyoifumua na kuivuta karatasi ilimofungwa sumu hiyo, aliifungua taratibu na kuchukua kiasi kidogo  kwa kutumia vidole viwili, gumba na cha shahada baada ya kumaliza alikiingiza  kikaratasi ilimofungwa sumu ndani ya pindo la gauni lake.

    Sauti ya spika ziliendelea kutangaza  juu ya mtu aliyekuwa akitafutwa, Caroline alishindwa kuelewa ni kwanini askari huyo hakusikia, bila kusita wakati wakitembea alimsogelea na kumwekea mkono wake begani, hapohapo akampaka sumu.

    “Let me empty my bladder!”(acha nikojoe kwanza!)

    “No problem just go on!”(Hakuna tatizo endelea!)

    Caroline alitembea kwenda pembeni ambako alichuchumaa na kuanza kukojoa huku akiutumia mkojo wake mwenyewe kuinawa sumu aliyoigusa kwa mikono yake, alipomaliza alinyanyuka na kuendelea kumfuata askari.

    “Is it very far from here?”(Ni mbali sana kutoka hapa?)

    “No! we’re ab...out  to be the...re!” (Hapana tumekaribia kufika!) alisema askari na  sekunde chache baadaye alianguka chini kama mzigo na kutulia tuli! Kuona hivyo mbwa walianza kubweka kwa nguvu, alipogeuka kuangalia nyuma kundi kubwa la watu waliovaa mavazi  ya rangi nyeusi lilikuwa likija mbio kuelekea eneo alilokuwa, alipotaka kukimbia mbwa mmoja alimrukia na kuliuma gauni lake.

    Je, nini kitatokea? Je, Caroline atafanikiwa kuondoka uwanja wa ndege au ataingia mikononi mwa Dk. Ian? Fuatilia wiki ijayo!















    I

    likuwa ni ndani ya uwanja ?wa ndege wa Ottawa, tayari ?ilishatimu saa 2:30 ya usiku, Caroline alikuwa akijaribu kujiondoa mdomoni mwa mbwa walioling’ata gauni lake, walikuwa ni mbwa wanene na wenye nguvu kiasi kwamba ilikuwa kazi ngumu kuling’oa gauni lake katikati ya meno yao! Mbwa wengine walikuwa wakibweka na kundi kubwa la watu ambalo baadaye aligundua walikuwa ni maaskari lilizidi kumkaribia na hatimaye kumfikia.

    Maaskari waliwaamuru mbwa waache kumshambulia Caroline na walitii amri hiyo, mwili wake wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu! Kukamatwa kwake kulimaanisha kuingia mikononi mwa Dk. Ian na hilo lilimaanisha kifo chake na kama si kuingia mikononi mwa Dk. Ian angeingia mikononi mwa sheria kwa kosa la kuwaua O’brien na wenzake  na kama ingethibitika alitenda kosa hilo kwa sheria ya Canada ilivyokuwa angehukumiwa kifo kwa kuchomwa sindano ya sumu.

    Mawazo hayo yalimfanya aumie sana moyoni mwake, hakutaka kufa kabla hajalipiza kisasi kwa Harry na wenzake na hakutaka kufa kabla ya kuwaona wazazi wake, hakuwa na fikra hata kidogo kuwa baba na mama yake walikuwa katika mji huohuo tena ndani ya mateso makali, waliteswa kila siku na Dk. Ian kama kisasi kwa kitendo alichofanya mtoto wao.

    “Haiwezekani  ni lazima nijiokoe!”Aliwaza Caroline wakati akinyanyuliwa ardhini na mmoja wa maaskari na kuanza kupigwa kwa kirungu kichwani,  alipasuka juu ya jicho na kuanza kuvuja damu!

    “Who are you?”(Wewe nani?)

    “Me?”(Mimi?)

    “Yeah! who do you think is the shit am I speaking to?”(Ndiyo! Wewe unafikiri ni kinyesi gani ninayeongea naye?) Aliuliza askari kwa ukali.

    “I’m Marione!”(Mimi ni Marione!)

    “Why are you running?”(Kwanini unakimbia?)

    “They want to kill me! I beg you to save my life and I will pay you any amount of money if you won’t let me out of the airport through the front exit”(Wanataka kuniua, naomba muokoe maisha yangu! Nitawalipa kiasi chochote cha pesa kama tu hamtanipitisha mlango wa mbele wakati wa kutoka ndani ya uwanja!)Caroline aliongea huku mkono wake tayari ukiwa umeshika noti kumi za dola mia mia! Ilikuwa si rahisi kukumbuka ni muda gani alizitoa sehemu alipozificha! Alikuwa ameamua kutumia pesa kujiokoa.

    Jeshi la polisi nchini Canada katika kipindi hicho lilikuwa katika wakati mgumu, ni wiki hiyo hiyo wanajeshi wa jeshi hilo pamoja na wale wa zimamoto walikuwa wamegoma kufanya kazi sababu ya maslahi kidogo, wachache walikuwa kazini na hao walikuwa tayari kwa lolote ili mradi wameonyeshwa pesa, waliruhusu hata wafanyabiashara wa madawa ya kulevya kupita katika uwanja huo kama tu walipewa pesa!

    Kitendo cha Caroline kuwatajia pesa kilikuwa ni faraja kubwa kwao, walipoona noti za dola mia mia mikononi mwake, walihisi mate yakiwadondoka! Tangu asubuhi ya siku hiyo walikuwa hawajapata rushwa ya aina yoyote, mmoja wao alizidaka pesa hizo kwa mkono wake wa kulia na kumwamuru Caroline asimame.

    “Give us some more!”(Tupe zaidi ya hizi!)

    “How much?”(Kiasi gani?)

    “Ten thousand U$D!”(Dola elfu kumi!)

    “That’s a lot!”(Hizo ni nyingi sana!)

    “Then come with us!”(Basi tufuate!)

    “No! I’m not ready!”(Hapana! Sipo tayari!) Alijibu Caroline,  hakuwa tayari kupitishwa mlango wa mbele ambako kwa uhakika alijua Dk. Ian alikuwa akimsubiri tayari kwa kumuua, mpaka wakati huo alikuwa na uhakika kila kitu alichokifanya ndani ya ndege kilishajulikana na alishangaa ni kwanini maaskari hao walikuwa hawajagundua kilichotokea pamoja na vipaza sauti kuendelea kupita kelele na yeye mwenyewe Caroline kuvisikia.

    Bila kuchelewa wala kusita alidumbukiza mkono wake ndani ya chupi alimoficha pesa zake, hakutaka kuzitoa zote,  alijua maaskari wangeingiwa na tamaa baada ya kuziona na hata kumnyang’anya. Kwa utaalam wa ajabu  huku akitumia mkono mmoja kama vile mtu aliyekuwa akijikuna ngozi yake ya ndani, Caroline alihesabu noti moja moja mpaka zikatimia  nane kisha akazivuta na kuzitoa nje.

    “This is the only money I have! Please help me out of the Airport through the rear gate!”(Hiki ndiyo kiasi pekee cha pesa nilichonacho! Tafadhali nisaidieni nitoke nje ya uwanja kupitia mlango wa nyuma!)

    Hizo nazo askari alizidaka na wote walionekana kuridhishwa, walianza kutembea naye upande wa pili kulipokuwa na giza nene ambako walimweleza kulikuwa na mlango wa nyuma, vipaza sauti vilizidi kupiga kelele vikitoa taarifa juu ya mwanamke muuaji aliyekuwemo ndani ya uwanja,  yeye alisikia kila kitu lakini maaskari walionekana kutotilia maanani maneno hayo.Mbele kidogo  wazo liliingia kichwani mwa Caroline.

    “I have to be  very smart, I’m not supposed  to leave   any mark  or foot steps behind me!”(Lazima niwe makini sana, sitakiwi kuacha alama yoyote nyuma yangu!) Aliwaza Caroline na ni dakika hiyo hiyo wazo la kuwaua maaskari wote waliokuwa wakimsindikiza lilimwijia, alijua hao  ndio wangekuwa chanzo cha yeye kukamatwa baada ya kugundua ndiye aliyekuwa akitafutwa.

    Aliinama na kuligusa pindo la gauni lake mahali alimoficha kipaketi chenye sumu aliyopea na mzee Nelson porini, yeye aliita sumu hiyo sumu ya ukombozi ingawa iliondoa maisha ya watu katika kujiokoa kwake! Tayari  kwa kutumia sumu hiyo alishauwa watu wanne na alijua mbele yake ilikuwa ni lazima aue watu wengi zaidi ikiwa ni pamoja na Harry, Richard, Reginald, Dickson na Leonard Katunzi, huyu alikuwa mwandishi wa habari aliyemwandika yeye magazetini kuwa alikuwa na kifafa! Alitaka kumuua sababu alimuaibisha sana.

    Wakati ameinama maaskari waliokuwa naye walibaki kumshangaa bila kujua alichokuwa akifanya, haikumchukua hata sekunde tano kuitoa sumu hiyo kwenye pindo na kuishika mkononi, kwa sababu ya giza hakuna askari aliyegundua alichokuwa akifanya, akachukua kiasi kidogo cha unga huo na kuushika katika mkono wake wa kulia.

    “Hawa nao zamu yao imefika, si walengwa lakini inabidi wafe ili wasikwamishe mipango yangu, nikiwaacha hai hawa lazima watatoboa siri na nitashindwa kuondoka Canada!” Aliwaza Caroline roho na akili yake ilishaharibika, hakuwa binadamu wa kawaida tena! Kwa wakati huo kwake kuua kilikuwa kitu kidogo sana   ili mradi  anaokoa maisha yake, hata yeye mwenyewe alijishangaa! Katika maisha yake hakuwahi  kuwaza  kitu kama kuua mtu.

    “I have a bad thirsty can I have some water?” (nina kiu mbaya sana, naweza kupata maji kidogo?)

    “We have watertapes everywhere, one of the tapes is right behind you!”(Kuna mabomba kila mahali uwanjani moja ya mabomba hayo liko nyuma yako!) mmoja wa maaskari hao alimwambia Caroline.

    Tayari walishalifikia  kwenye geti la kutoka nje ya uwanja kupitia mlango wa nyuma,   Caroline pesa zake zilikuwa zimemsaidia! Alichofanya ni kuanza kuwaaga maaskari hao kwa kuwapa mkono wake wa kulia uliopakwa sumu, alihakikisha anamgusa kila askari na sumu hiyo, alipomaliza aliwahi haraka  sana kwenye bomba la maji lililokuwa nyuma yake na kunawa vizuri kisha akarudi mpaka mahali waliposimama maaskari  na kuanza kuongea nao huku akiwashukuru kwa wema waliomtendea.

    Alibaki nao kwa dakika kumi,  halikuwa lengo lake kubaki eneo hilo lakini alitaka kuhakikisha sumu imefanya kazi  miilini mwao ndio aondoke na kama ingeshindwa  ingebidi awapake tena kwa mtindo huohuo wa kuagana.Zilipotimia kama dakika kumi hivi, alishangaa kumwona mmoja wa maaskari hao akiyumba na baadaye kuanguka chini haikuchukua muda mrefu akafuatiwa na mwenzake na kila aliyeanguka chini hakusema kitu chochote alibaki kimya akitupa miguu yake huku na kule, jumla ya maaskari saba walikuwa wamelala chini hiyo ikifanya idadi ya watu  aliowaua kufikia kumi na moja.

    Mbwa walianza kubweka tena, Caroline hakutaka kupoteza muda zaidi katika eneo hilo alichofanya ni  kukimbia haraka kutoka nje ya  ngome ya uwanja, mbwa walimfuata  kwa nyuma lakini kabla hawajamfikia tayari alishafunga  lango na kujisikia yuko salama. Aliangalia macho yake huku na kule  kuona kama kulikuwa na mtu yeyote mwenye kusababisha hatari lakini  macho yake hayakukutana na kitu chochote cha aina hiyo.

    Alikichukua kipakiti chake na kukirudisha kwenye pindo la nguo yake, alikisukuma na kukiingiza ndani zaidi ili kisipotee, wazo la kurudi ndani na kuzichukua pesa alizowapa maaskari lilimwijia kichwani lakini aliogopa kufanya hivyo.

    “Naweza kurudi nikapambana na matatizo bure!” Aliwaza Caroline.

    Alichofanya ni kuanza kukimbia kuelekea mbele ya uwanja, ilimchukua kama dakika mbili tu akawa ameshajichanganya katikati ya makundi ya watu waliokuwepo uwanjani hapo bila kugundulika! Alifanya kila kitu kwa uangalifu, alielewa wazi msako dhidi yake ulikuwa ukiendelea. Alijificha nyuma ya nguzo kubwa ya jengo la uwanja akihakikisha asingeonekana, macho yake yalielekezwa kwenye lango kubwa la kutokea uwanjani.

    Haikuwa kazi ngumu kwa macho yake kumgundua Dk. Ian, mwili wake wote ulitetemeka na alihisi mkojo ukimpenya, alimwogopa sana mtu huyo kwake ilikuwa ni bora kukutana na shetani ana kwa ana kuliko kukutana na Dk. Ian! Aliamini kifo chake kilikuwa mikononi mwa mwanaume huyo aliyewahi kuwa mume wake lakini yeye mwenyewe ndiye akayaharibu mambo baada ya kudanganywa na  Harry, mwanaume aliyejifanya kumpenda.

    Kwa harakaharaka alirudi kinyumenyume na kujificha nyuma ya mgahawa mkubwa wa McDonald uliokuwepo uwanjani hapo, alisimama eneo lenye giza akiwa na uhakika kwa asilimia mia moja kuwa asingeweza kuonekana, akiwa hapo aliweza kumwona Dk. Ian akiwa ameshika mikono yake kichwani akishuhudia machela tatu zikitolewa ndani ya uwanja huo,  maiti  za  kina O’brien na wenzake zilikuwa zikitolewa  nje ya uwanja.

    Kila mtu aliyekuwepo uwanjani hapo alionekana kushangaa kupita kiasi, Caroline aliisikia sauti ya Dk. Ian kutoka sehemu aliyojificha ikifoka, mzee huyo aliahidi ni lazima  ampate Caroline! Watu wengi hawakumwelewa. Caroline alisikia kila kitu na kuzidi kuingiwa na hofu.

    “A serial killer is within the Airport, she is a woman! Tall, black and beautiful, she has already killed for men! If you suspect any person with  the same features please notify the police immediately!”(Muuaji anayeua watu mfululizo yupo ndani ya uwanja, ni mwanamke, mrefu, mweusi na mzuri, tayari amekwishaua wanaume wanne! Kama ukimhisi mtu yeyote mwenye sifa kama hizo tafadhali julisha polisi haraka!) Sauti ya kipaza sauti iliendelea kusikika.

    Kila mtu uwanjani hapo alionekana mwenye hofu, polisi walipita huku na kule wakijaribu kumtafuta mwanamke mwenye sifa zilizotajwa! Kuona hivyo Caroline aligundua eneo alilokuwa halikuwa na usalama, alikimbia kwa haraka akiwa ameinama hadi eneo yalipoegeshwa magari yaliyoonekana kama ya kukodi. Alilisogelea moja lililokuwa na dereva ndani yake na kufungua mlango.

    “Yes madame! Need a ride?”(Ndiyo mama! Unahitaji usafiri?)

    “Yes!”(Ndiyo!)

    “Where should I take to?”(Nikupeleke wapi?)

    “City centre!”(Jijini katikati!)

    “Three U$D!”(Dola tatu!)

    “No problem! If you drive fast and pass through the rat-rat routes I will pay you more!”(Hakuna matatizo na kama ukiendesha kwa kasi kupitia njia za panya nitakulipa pesa zaidi!) Alisema Caroline, kwa hofu aliyokuwa nayo mwili wake ulikuwa ukitetemeka! Dereva alimwangalia na kuonyesha mshangao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva alikuwa miongoni mwa watu waliolisikia tangazo la mwanamke aliyekuwa akitafutwa ndani ya uwanja wa ndege, muonekano wa Caroline ulimtia hofu kubwa, aliingiwa na wasiwasi kuwa  huenda mwanamke aliyekuwa akitafutwa ndiye alikuwa ndani ya gari lake!

    Hofu kubwa ilimpata na alihisi hata yeye angekuwa miongoni mwa watu ambao wangeuawa. Kwa kupitia kona ya jicho lake la kushoto aliweza kumchunguza Caroline  kwa makini na   bila shaka  yoyote alijua ni yeye! Alishindwa kuelewa ni nini kingempata, jasho jingi lilimtoka kiasi cha kulowanisha shati alilovaa, mapigo yake ya moyo yalienda kasi kuliko kawaida.

    Mbele kidogo  walifika darajani, lilikuwa daraja  kubwa ambalo chini yake ilipita treni ya umeme iliyokwenda kwa kasi, bila kutegemea Caroline alimwona dereva akifungua mlango wa gari  lililokuwa  likitembea kwa mwendo wa kasi,  aliruka na kuachia usukani, gari lilianza kuacha njia! Caroline alijaribu kwa uzoefu wake wote kuzuia gari lisianguke lakini iliendelea kuserereka na kubinuka likijigonga kwenye vyuma vya pembeni mwa daraja! Mara ghafla tairi ya mbele ilipasuka, gari likarushwa juu na kuanza kuanza kudumbukia  chini kulikokuwa na reli, lilipotua chini lilikuwa katikati ya reli na treni  la umeme lilikuwa  hatua chache kutoka mahali lilipokuwa gari.

    “Mamaaaaaaaaaaaaaaaaaa!” Caroline alilia tena kwa kiswahili akijua mwisho wake ulikuwa umefika, mwisho bila kulipiza kisasi.

    Je, nini kitatokea? Fuatilia wiki ijayo.













    D

    k. Colins Wiliamson ?hakuwa mtu maarufu ?masikioni mwa watu wengi wa Jiji la Ottawa, Canada. Hiyo ilitokana na ukweli kwamba juu ya utajiri wake lakini alitumia muda wake mwingi katika mashamba yake yaliyokuwa katika misitu ya Great jambo lililofanya aonekane mara chache sana katika maeneo ya mjini ambapo alikuwa anamiliki kiwanda cha maua na huko msituni alikuwa na kiwanda cha kuchana mbao.

    Akiwa ni mtu mzima mwenye nywele na ndevu nyeupe, Dk. Wiliamson alikuwa ni mtu mwenye msimamo sana na maisha yake tangu alipomaliza kesi yake iliyomfanya apoteze eneo kubwa la shamba lake. Hilo lilikuwa ni jambo kubwa lililomfanya awe na uchungu sana kitendo kilichomfanya atumie muda mwingi kuwaza na kupangilia upya maisha yake baada ya nusu ya utajiri wake kuporwa kwa hila.

    Ni mkulima ambaye alikuwa akitegemewa sana kutokana na misitu anayomiliki kutoa mbao kwa wingi ambazo zilihitajika kwa shughuli mbalimbali. Shamba kubwa na ambalo nusu yake iliporwa ni lile lililokuwa katika misitu ya ziwa la Great ambalo liko ndani ya mji wa Ottawa mpakani na Marekani hasa katika mji wa New York. Mbali na shamba hilo la miti karibu na ziwa hilo, pia alikuwa na mashamba mengine ya aina hiyo kando ya maziwa maarufu ya Winnipeg na Galgary.

    Biashara zake za mbao alizifanya pia katika nchi jirani za Marekani na Mexico na hivyo kuingiza kipato kikubwa ambacho ndicho kilichomwezesha kununua  kiwanda cha kuchana mbao ambacho alikitumia vilivyo na hivyo kuzidi kujitajirisha.

    Mzee Wiliamson alikuwa na mke na watoto wanne ambao wawili kati yao walihamishia maisha yao Marekani na waliobaki ambao ni watoto wa kike wawili alikuwa akiishi nao hapo hapo kwake.

    Shamba lake lilikatwa kinguvu baada ya kushindwa kesi! Karibu nusu nzima ya shamba hilo ilimegwa na Dk. Ian ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa baada ya kufanya hila na kufoji hati kadhaa za mashamba hayo na kisha kudai kwamba eneo la shamba ni mali yake. Ijapokuwa hilo jambo lilifanyika miaka mingi iliyopita, lakini hivi karibuni ndiyo kesi ilipatiwa ufumbuzi mahakamani huku yeye akiwa ameshindwa.

    Kwa jinsi Dk. Ian na Mzee Williamson walivyokuwa wameshibana, haikuwa rahisi kufikiri kwamba kulikuwa na chembe za usaliti. Ni jambo lililoanza kama mzaha hivi na hata Dk. Williamson hakulipa uzito. Lakini baadae alipokuja kushtuka, haki za shamba lake zilikuwa zimepindwa na mmiliki halali wa nusu ya shamba akawa ni Dk. Ian ambaye ni rafiki yake.

    Tukio hili lilimshangaza na kumchanganya sana, hasa alipogundua kwamba alikuwa amechelewa sana kwani Dk. Ian alikuwa amejiandaa vya kutosha kwa suala lile kiasi kwamba hata alipojaribu kwenda mahakamani kudai haki hiyo, alikuta amekwama na Dk. Ian ndiye aliyeonekana kuwa mwenye haki!

    Kutokea hapo Dk. Ian na Mzee Williamson hawakuwahi kuonana! Sio kwa kuwa huyu yuko mbali na yule yuko mbali, ila ni kutokana na kiwango cha chuki ambacho kilizaliwa baina yao na kuota mizizi kwa haraka kama moto kwenye majani makavu.

    Kupoteza haki zake kilikuwa ni kitendo kilichomuuma mno, na alijilaumu sana kwenye nafsi yake kwa kumuamini sana Dk. Ian kiasi cha kumpa siri zake ambazo alizitumia katika kumnyang’anya eneo la shamba lake. Na katika chuki hizohizo iliwahi kutokea siku ambapo Dk. Ian alimpigia simu Dk. Williamson na kumwonya kwamba kama ataendelea na jambo lolote la kumfanya adai eneo la shamba, basi atalia na Mungu wake. Japokuwa haya yalikuwa ni maneno ambayo angeweza kuyapeleka mahakamani, lakini alisita. Kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu aliamini kwamba kitendo hicho kitalipwa na Mungu siku moja.

    * * * * * * * * * * * * *

    Pengine ulikuwa ni wasaa wa mwisho kwa maisha ya Caroline. Kwa jinsi alivyochanganyikiwa kutokana na kupinduka na gari na jinsi treni la umeme lilivyokuwa likikaribia kwa kasi ya upepo, Caroline hakujua afanye nini ili kujinasua.

    Alijilaumu sana kwa kukikaribisha kifo bila kulipiza kisasi. Ni kwa kudra za Mungu tu alijishtukia akijipinda na kuruka kando kama mwanasarakasi na treni ya umeme ikapita kwa kasi ileile na kumpita kwa nusu sentimita tu kichwani pake!

    Baada ya treni kupita, Caroline akabaki ameduwaa akiangalia kama ambaye haamini kwamba tayari yuko salama. Aliangalia huku na huko kwa matumaini mapya kwamba ametoka kwenye aneo moja na amefika kwenye eneo jingine ambalo linaweza kuwa na usalama kwake.

    Lakini Caroline hakuwa mjinga, alifahamu fika kwamba vyombo vya usalama vya Canada viko ‘fasti’ sana katika kushughulikia matukio ya ajali, kwa maana hiyo alijua kwa vyovyote vile, akizubaa kwa dakika chache mahali hapo, kuna uwezekano mkubwa wa kukutwa na magari ya polisi ambayo yatafika kwenye eneo hilo na hivyo kumtia mbaroni. Hakupenda kukamatwa kirahisi namna hiyo. Kukamatwa kwake kulimaanisha mashaka makubwa kwenye maisha yake. Na aliogopa sana kumaliza maisha yake kwenye sindano ya sumu atakayochomwa baada ya hukumu ya kifo kufuatia mauaji ya watu ambayo ameyafanya.

    Alitaka kuinuka ili kukimbia, lakini akapata maumivu makali sana kwenye mguu wake wa kushoto. Alipouangalia, aligundua kwamba ulikuwa ukivuja damu nyingi na alipojaribu kuusogeza, upande wa goti ulionyesha kwamba umevunjika. Maumivu hayo yalimfanya alpige kelele za maumivu makali.

    Lakini bado alikumbuka kwamba anahitajika kuondoka eneo hilo haraka iwezekanavyo kwa vile hapo sio mahala salama kwa yeye kubaki kutokana na tabia za polisi wa Ottawa.

    Alijikongoja na kuanza kujiburuta akielekea msituni. Pamoja na kuwa alilazimika kujivuta, lakini alipata maumivu makali sana yaliyomfanya aanze kuutilia mashaka mguu wake kwamba inawezekana ukawa umekufa kabisa kiasi cha kukatwa. Hakujua huko anakokimbilia ni wapi na hakujua ni nani ambaye anaweza kumsaidia kuhusu mguu wake. Mara nyingine alilazimika kutambaa kwa umbali mrefu na mara nyingine aliinuka na kutembea kwa taabu sana akisaidia huku akishika miti.

    Maeneo yote aliyokuwa akikatiza kwenye msitu huo, hapakuwa na dalili zozote za kuwapo mtu au nyumba. Jambo hili alilifurahia baada ya kukumbuka kwamba nchi nzima ya Canada itakuwa imeshapata habari za kusakwa kwake na yeyote atakayeonana naye ni rahisi kumtambua na kumripoti. Kutokana na hali aliyonayo, asingewqeza kujitoa mikononi mwa polisi au hata ya hao ambao watamkamata. Zaidi ya mguu, maumivu yalikuwa karibu kila mahali mwilini mwake.

    Ilifika mahali ambapo mguu ulishindwa kabisa kuendelea kujisukuma kiasi akajikuta akijiegesha kando ya mti huku akilia. Kama kusingekuwa na maumivu makali kama yale, basi angepotiwa na usingizi kutokana na uchovu lakini haikuwezekana. Maumivu yalifunika kila kitu.

    Mara akashtukia amesimamiwa na mtu, akageuka kwa ghafla huku akionyesha dhahiri kiwango kikubwa cha mshtuko.

    “Who are you?” (We nani) yule mtu alimuuliza. Alikuwa ni mtu mzima mwenye sura ya ukarimu na ucheshi. Kabla hajajibu Caroline alimtazama kama anayemsoma huku moyo ukimdunda kwamba huyu ni nani na anajua nini kuhusu kusakwa kwake.

    “Me?… Why do you want to know my name?” (Mimi.. Kwa nini unataka kujua jina langu?)” Alijibu.

    “I’m the owner of this farm and I must know who are you and what are you doing here!” (Mimi ndio mwenye shamba hili, na lazima nijue wewe ni nani na unafanya nini hapa?)

    Caroline alishindwa kujibu haraka haraka. Alishindwa kujibu kutokana na sababu nyingi ambazo alikuwa nazo. Siku zote hakuwa tayari kumtajia jina mtu ambaye hamjui. Ingawaje alikuwa na maumivu makali sana katika mguu wake uliovunjika, lakini aliweza kuongea.

    “Listen my daughter, am Mr. Williamson, who is the owner of the farm. So explain yourself carefully and am will help you if you wish” (Sikiliza binti, mimi naitwa Mzee Williamson, ni mwenye shamba hili, jieleze vizuri kama una shida ninaweza kukusaidia), yule mzee alisema kwa sauti ya huruma.

    Caroline akajikuta akivutiwa na sura ya uaminifu ya mzee Wiliamson na maneno yake yenye dalili za hekima.

    “Excuse me, can you cure me before I axplain to you each and everything accured?” (Samahani unaweza kunisaidia dawa kabla sijakueleza yote yanayonisibu?) Caroline alilazimika kuomba hasa kutokana na maumivu makali aliyokuwa anaendelea kuyasikia. Mzee Williamson alimwinua na kumwongoza kutembea naye kuelekea kwenye nyumba yake. Alipofika huko alimweka kwenye nyumba yake ya shamba ambayo haikuwa na mtu mwingine yoyote. Alitengeneza maji ya moto na kuanza kumwosha ile sehemu ambayo ilikuwa ikivuja damu na baadae kumpaka dawa maalum kuzuia damu isiendelee kutoka.

    Alipomaliza yote hayo alimletea chakula ambacho Caroline alikula kwa kasi kutokana na njaa aliyokuwa nayo. Alipomaliza kunywa maji, Mzee Williamson akawa yuko jirani yake.

    “What happened?” (Nini kilikupata?) Mzee Williamson alionyesha hamu kubwa ya kutaka kujua kilichoendelea. Ni hapo ambapo Caroline aliamua kumweleza kila kitu bila kumficha, mambo yote makubwa katika maisha yake, kusakwa ili auawe na Dk. Ian pamoja na msako ambao unaendelea dhidi yake. Katika mazungumzo yote hayo, kikubwa kilichomshtua mzee Williamson ni pale alipotambua kwamba huyu aliwahi kuwa mke wa Dk. Ian ambaye yeye ni adui yake namba moja.

    “You said were Dk. Ian’s wife?” (Unasema ulikuwa ni mke wa Dk. Ian?) Yule mzee aliuliza baada ya Caroline kumaliza maelezo yake huku akionekana wazi kushtushwa?

    “Exactly, do you know him?” (Ndiyo, kwani unamfahamu?)

    “I’m not sure. There’s someone with the same name who confused me tha I put him to be my number one enemy in my life. He snatched my farm from the case which…” (Sina hakika. Yupo mtu mwenye jina kama hilo ambaye amenichanganya sana kwenye akili yangu na mpaka sasa nimemfanya kuwa adui namba moja katika maisha yangu. Mtu huyo alinidhulumu shamba langu katika kesi iliyo…)

    “He Snatched your farm? I’m talking about Dk. Ian who won the some alike case few days before we atarted these problems” (Alikudhulumu shamba? Dk. Ian ninayemzungumza mimi alishinda kesi kama hiyo siku chache kabla hatujaingia kwenye matatizo haya.”

    “Yes, it’s him. He is my biggest enemy that I can’t forgive him till the day I die!” (ndio, ni yeye huyo, yule ni adui yangu mkubwa na siwezi kumsamehe mpaka siku ya kufa.)

    “Why” (Kwa nini).

    “He made a very bad matter for me, he snatched my farm. Fist he was my best friend that I couldn’t think that he would do such a thing to me. But he did. He left me in tears for my rights he destroyed in the court” (Amenifanyia ushenzi mkubwa, alinipora shamba langu. Huyu mtu alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana na hata siku moja sikutegemea kama ana mawazo ya kutaka kunidhulumu eneo la shamba langu, na ndivyo alivyofanya kwa kweli. Amefanya hivyo na ameniacha mimi nikiwa nalilia haki zangu ambazo amezipinda mahakamani).

    Caroline akashangaa sana kusikia habari hizo. Pamoja na kujua uovu mkubwa wa Dk. Ian, lakini hakuwa amefikiria kwamba angeweza hata kujiingiza kwenye mambo ya kudhulumu wakulima.

    Mzee Wiliamson alimhakikishia Caroline kwamba yeye binafsi atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba anaokoka na balaa lile na kurudi nyumbani kwao Tanzania kwa vile yeye na Dk. Ian ni maadui na kwa sababu anamsaka ili amuue, basi yeye yuko tayari kumsaidia ili asipatikane.

    Kwa karibu mwezi mzima Caroline alikuwa hapo nyumbani kwa Mzee Williamson akitibiwa mguu wake na daktari wa mzee huyo ambaye karibu kila mara alikuwa akija kuhakikisha kwamba hali yake inakuwa nzuri. Baada ya kipindi hicho, Caroline alipata nafuu kubwa na aliweza hata kutembea mwenyewe bila msaada wa mtu yoyote au kuonekana na mtu kwamba aliwahi kuumia.

    Ni hapo ambapo Mzee Williamson alimpa mipango yake ya jinsi atakavyofanya mpaka kumwezesha kutoroka kwenye nchi hiyo.

    “I will bring to you a plastic surgery on specialist, he will make for you more than five faces that will help you in escaping. Without them you will be in trouble wherever you are seen. When we are ready will the faces you will leave for airport and fly to your homeland, it’s alright?” (Nitakuletea mtu ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza sura za bandia, kwa hiyo atakutengenezea sura za bandia zaidi ya tano na utazitumia hizo kutorokea. Kwa jinsi ulivyo, sura yako ikionekana mahali popote itakuwa ni balaa kwa sababu ni lazima watakukamata. Tukishatengeneza sura hizo, utaondoka moja kwa moja kwenda uwanja wa ndege na utaingia kwenye ndege na kuondoka kwenda nyumbani kwenu, sawa?)

    “It’s alright and thank you very much Mr. Williamson” (Sawa na ninashukuru sana mzee Williamson).

    Siku iliyofuata mzee mmoja wa Kijapan aitwae Sumo alifika hapo nyumbani na vifaa vyake na kufanya kazi hiyo. Ndani ya siku chache zikawa zimeshatengenezwa sura sita za bandia.

    Tiketi ya ndege ikakatwa haraka haraka na siku moja baadae, Caroline akiwa na sura mojawapo ya bandia alifanikiwa kuingia kwenye ndege bila kutambulika huku kwenye moja ya mizigo yake kukiwa na sura nyingine tano za bandia kwa akiba!

    Wakati anatafuta kiti chake akae, alishangaa sana kuona seti moja ya viti vitatu imekaliwa na kijana ambaye alimfahamu pamoja na mwanamke wa kizungu. Si tu kumfahamu, alishtuka sana alipogundua kwamba yule kijana alikuwa ni Dickson! Dickson ambaye zamani aliwahi kumbaka msituni baada ya kumnywesha madawa ya kulevya. Alijikuta akisimama na kumtazama kijana huyu huku akionyesha wazi kuduwaa. Akaamua kuketi kwenye viti hivyo.

    Dikson aliwahi kumchangamkia kwa kumsalimia pamoja na yule mwanamke wa kizungu. Dickson alipotambua kwamba anazungumza na Mtanzania mwenzake alifurahi sana. Dickson baada ya tukio lile alikuwa ametoroka nje ya nchi na hapo ndipo alikuwa akirudi nyumbani pamoja na mke wa kizungu.

    Alipoyakumbuka matukio aliyofanyiwa na Dickson, Caroline hasira zikampanda. Moyoni mwake akaapa kwamba mwanaume huyu masaa machache yajayo atakuwa ameingia kwenye orodha ya walio katika mpango wa kuuawa ambapo wengine ni Harry, Richard, Reginald, na Leonard Katunzi. Kwa kiwango ambacho alikuwa amefanyiwa ukatili na Dickson, hakuona haja yoyote ya kumsamehe.

    Wakiwa wamekaa pamoja, walikuwa wakizungumza mambo mengi mbalimbali kuhusu biashara huku Caroline akijitambulisha kwa jina bandia la Vicky akiwa ni mfanyabiashara. Maskini Dickson, alizugwa na sura ya bandia aliyokuwa ameivaa Caroline. Laiti kama angelijua kwamba anayezungumza naye pale ndiye Caroline, nadhani angeruka kwenye ndege!!

    Dickson alivutiwa vilivyo na uzuri wa ‘Vicky’ (Caroline) akamwambia kwa kiswahili ili mke wake asisikie kwamba watakapofika nyumbani, ni lazima wawasiliane ili waongee zaidi, kitu ambacho Caroline alikikubali.

    “Huu ndio wakati wangu, mwingine nimeshampata, ni lazima nimuue haraka iwezekanavyo”, aliwaza. Lakini wazo lingine lilimjia haraka, kwamba hawezi kumuua mtu huyo kwenye ndege. Akafikiria mbinu nyingine.

    * * * * * * * *

    Dunia nzima zilisambazwa habari kwamba msichana muuaji aitwae Marion au Caroline anatafutwa kutokana na mauaji makubwa ambayo ameyafanya kwa nyakati tofauti. Matangazo hayo yalikuwa yakirushwa kupitia televisheni, magazeti, redio na mitandao ya Internet. Mpaka humo ndani ya ndege abiria wote walikuwa na habari ya kusakwa kwa mwanamke huyo mdunguaji.

    Wakati dunia ikiwa kwenye msako mkubwa hivyo pamoja na polisi wa Kimataifa wa Interpol Dk. Ian naye alikuwa akiumiza kichwa chake kwamba ni vipi atamtia mikononi mwake Caroline.

    Je Caroline atafanikiwa kumuuua Dickson na ataweza kufika Tanzania salama? Usikose toleo lijalo.





    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/









    Wote wawili waliishi ndani ya chumba kidogo chenye hewa finyu, hapakuwa na kitanda wala mahali pa kukaa na kila siku sakafu ilimwagiwa chumvi iliyokula miguu  na makalio yao, walikula mara moja tu kwa siku, wazazi wa Caroline Dr Cynthia na profesa Kadiri walikuwa katika mateso makali mno! Hakuna mtu aliyeelewa juu ya kuwepo kwao ndani ya himaya ya Dr Ian hata balozi wa Tanzania nchini humo hakulielewa jambo hilo.

     Mara kwa mara walimwomba Dr Ian awaachie huru  kwa sababu hawakuwa na hatia, lakini mzee huyo katili hakuwajali, alizidi kuongeza mateso  kadri siku zilivyokwenda! Aliamini hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kumfanya Caroline arudi, kitendo chake cha kutoroka uwanja wa ndege na kuwaacha O’brien na wenzake wakiwa maiti kilimwongezea hasira zaidi, usiku na mchana kundi lake la mafia  lilikuwa katika msako mkali wa kimya kimya wakimtafuta Caroline  lakini hawakufanikiwa.

    Kila mtu aliamini Caroline au Marione kama pasipoti yake ilivyojieleza alikuwa bado yu ndani ya  nchi ya Canada, makachero waliigeuza nchi hiyo ‘njendani’  lakini hawakufanikiwa kumpata. Kila mtu alizidi kuchanganyikiwa!Viwanja  vyote vya ndege nchini humo vililindwa, watu  walipekuliwa ipasavyo mipakani na katika bandari zote!

    Njia zote za kutoka nje ya Canada ziliwekwa chini ya ulinzi mkali, Caroline akisakwa kwa udi na uvumba! Hakuna aliyejua kuwa tayari Caroline alishaondoka nchini humo kwa msaada wa Dr Wiliamson adui mkubwa wa Dr Ian na alikuwa njiani kuelekea Tanzania akitumia pasipoti yenye jina la Vicky na sura ya bandia iliyomfanya aonekane msichana mrembo..

    Ni kutopatikana kwa Caroline ndiko kulikomfanya Dr Ian aongeze mateso zaidi kwa wazazi wake alizidi kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliyefahamu kuwa  watu hao walikuwa ndani ya ngome yake, isipokuwa wafanyakazi wake! Siku zote  Profesa Kadiri na mkewe walikaa ndani   ya mahabusu na hawakuonekana na watu kabisa!

    Walikonda  vibaya na miili yao ilijaa  vidonda   sababu ya chumvi nyingi iliyomwagwa ndani ya chumba kidogo cha mahabusu walichofungiwa! Hawakuwa na uhakika kama wangetoka salama katika himaya hiyo! Maisha yao yalikuwa mikononi mwa Dr Ian, alikuwa na uwezo hata wa kuwaua mbali kama angetaka kufanya hivyo kila siku walimwomba Mungu awanusuru na janga walilokuwa ndani yake.

                   *************

    “Can we meet in Dar?”(Tunaweza kukutana Dar es Salaam?) aliongea Caroline  na maneno hayo yalimfanya mke wa Dickson ashituke na kugeuka kuwaangalia, kwa muda mrefu walikuwa wameongea kwa kiswahili bila yeye kuelewa kilichokuwa kikiongelewa.

    “Tafadhali Vicky usiongee kwa Kiingereza mke wangu ana wivu sana, utaleta matatizo  tumia tu kiswahili, unajua  huyu mwanamke nilimwoa sababu nilitaka kupata kibali cha kuishi Uingereza, vinginevyo nisingemwoa kabisa! Si unamwona alivyo mzee? Ninahitaji kijana kama wewe awe mke wangu au siyo?”

    “Sawa tu basi tukutane  Dar es Salaam!”

    “Hamna shida!” Alijibu Dickson huku akimwangalia Caroline kwa macho ya mshangao sana!

    “Vipi mbona unanishangaa kiasi hicho?”Caroline alijikuta akiuliza, macho ya Dickson yaliashiria wasiwasi fulani, akaanza kuhisi labda alishagundulika.

    “Hapana, ni sauti yako ndio iliyonishangaza!”

    “Ikoje Dickson?”

    “Ni ya mtu ninayemfahamu kabisa, ingawa sina uhakika nilimwona wapi, kwani mimi na wewe tumewahi kukutana mahali labda?”

    “Hapana sura yako ni ngeni kabisa machoni mwangu, kwani kabla ya kwenda Uingereza uliishi wapi?”?“Tanzania?”

    ‘Mji gani?”

    “Dar es Salaam!”

    “Mimi sijawahi kabisa kuishi Dar es Salaam!” Caroline alidanganya.

    Mke wa Dickson tayari alishalala usingizi tena na  tayari ndege ilikuwa ikielekea uwanja wa  ndege wa Dar es Salaam,  ilishatimu saa tisa na nusu ya alasiri! Hata Dickson pia alikuwa akiyumbisha  kichwa chake kwa usingizi, Caroline alikuwa macho akiwa na karatasi ndogo mkononi alikuwa akiisoma kilichoandikwa juu yake.

    “Dickson..... Reginald....... Harry........... Leonard ! Hawa wote ni lazima wafe tena kwa mkono wangu, nasikitika nimeua watu wengi sana maishani mwangu lakini sikuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kufanya hivyo!” Aliwaza Caroline!

    Ndege ilitua uwanja wa ndege wa Dar es Salaam saa kumi kasoro dakika kumi na tano na watu walianza kushuka  mmoja baada ya mwingine taratibu, Caroline alikuwa nyuma ya Dickson na  mke wake alikuwa mbele!

    Walipofika chini walianza kutembea taratibu kuelekea kwenye lango la kutokea, kichwani mwake Caroline alifikiria yaliyotokea uwanja wa ndege wa Ottawa, alihofia kukamatwa tena lakini kwa sura aliyokuwa nayo na jina alilotumia aliamini hakuna mtu angemgundua hata kama kungekuwa maaskari! Nje  ya uwanja waliagana, mke wa Dickson akionyesha chuki ya waziwazi kwa Caroline!

    “Tutafikia hoteli Landmark! Njoo pale hotelini saa moja na nusu jioni tuongee vizuri sawa?”

    “Sawa lakini kuna kitu kimoja nataka uelewe!”

    “Kitu gani hicho?”

    “Nakupenda sana Dickson, sijui kwanini nimetokea kukupenda ghafla kiasi hiki!”

    “Hata mimi pia!”

    Aliuacha uwanja wa ndege  akiamini   kazi iliyokuwa mbele yake ilikuwa imeanza kutekelezwa! Aliiita kazi hiyo Operesheni Lipa Kisasi au OLK! Watu wote waliomfanyia mabaya ilikuwa ni lazima wafe na wa mwisho kufa ilikuwa ni lazima awe Harry! Ingawa  hakufahamu  ni wapi alikokuwa kwa wakati huo lakini ilikuwa ni lazima afe! Kwa ubaya aliomfanyia hakukistahili   msamaha! Ni yeye aliyemsababishia yote yaliyotokea, ni yeye Harry aliyestahili kulaumiwa kwa vifo vya watu wote waliouawa kwa mkono wa Caroline.

    “Sikumaanishwa kuwa muuaji, ni Harry aliyesababisha yote haya ni lazima afe, damu yake ni halali yangu!” Aliwaza Caroline.

     Alikuwa ndani ya gari aina ya Mark II lililofanya kazi ya kubeba abiria kutoka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam  hadi mjini!  Teksi hiyo ilimkumbusha  ajali mbaya iliyotokea uwanja wa ndege wa Ottawa akijaribu kutoroka baada ya dereva kuruka.

    “Ni lazima alikufa! Kwa jinsi alivyoruka haiwezekani hata kidogo akawa salama!”

    “Nani dada?”  dereva aliuliza, Caroline alikuwa ameongea kwa sauti kubwa  bila kufahamu! 

    “Hapana nimepitiwa tu!”

    “Haiwezekani lazima kuna jambo linakutatiza!”

    “Babu  achana nayo hayo hayakuhusu!”

    “Siyo hivyo siku hizi kuna matatizo mengi duniani, si unaalewa mambo ya magaidi na mauaji yanayotokea, isijekuwa na wewe umepatwa na matatizo  ya aina hiyohiyo”

    “Mh!” Caroline aliguna hiyo ilimwonyesha wazi kuwa hata katika Tanzania taarifa zake zilishafika na alitakiwa kuwa mwangalifu sana!

    “Tunaelekea wapi?”

    “Hoteli New Africa! Ni shilingi ngapi?”

    “Elfu tano tu mwanangu!” Alijibu dereva aliyekuwa na umri sawa kabisa na babu yake na Caroline.

    “Ok!”

    Gari ilizidi kutiwa moto   mbele kidogo waliingia katikati ya jiji la Dar es Salaam maeneo ya Posta, Caroline aliona kitu  kwenye moja ya kuta  za nyumba! Moyo wake ulishtuka, ilikuwa ni picha yake kubwa ikiwa imebandikwa ukutani na juu yake yaliandikwa maneno “Most wanted” Reward 25m U$D! Aliikumbuka picha hiyo, ilikuwa ni picha aliyopigwa na Dr Ian kwa ajili ya hati yake ya kusafiria, alielewa lazima picha hiyo ilitolewa na mume wake wa zamani ili aweze kukamatwa kirahisi.

    “Simama!” alimwamuru dereva na dereva alisimama haraka bila kusita, Caroline aliruka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye picha hiyo! Aliiangalia kwa muda na kuyasoma maelezo yake, jina  lake  lilitajwa kabisa akiitwa muuaji namba moja aliyekuwa akitafutwa dunia nzima! “Serial  killer!” Hivyo ndivyo alivyotajwa katika tangazo hilo.

    Mwili wote wa Caroline ulilowa jasho na akaanza kutetemeka, kama hivyo ndivyo ilivyotangazwa dunia nzima basi hakuwa na mahali pa kukimbilia! Alibaki amesimama mbele ya tangazo hilo akihisi mwili wake ulikuwa umekufa ganzi!

    “Binti twende! Tunazidi kuchelewa, nitakuchaji gharama za kusubiri!”Alisema dereva akionyesha hali ya kuwa na wasiwasi, Caroline alitembea taratibu kurudi kwenye gari na kuingia ndani yake.

    “Mbona umeonyesha kushtuka sana, unafahamu huyo dada hatari nini?”

    “Hapana!”

    “Wanasema aliwahi kuishi hapa miaka ya nyuma akisoma sekondari ya Jangwani,lakini mimi simfahamu!” alisema mzee huyo, Caroline alipoyasoma macho  ya mzee huyo alijifunza kitu fulani!  Alihisi hali ya hatari! Mzee huyo alikuwa akimkazia sana macho shingoni mwake.

    “Binti mbona umevaa sura ya bandia?”Mzee huyo alimuuliza akionyesha mshangao

    “Hapana siyo sura ya bandia babu!”

    “Ah! Acha bwana huwezi kunidanganya mimi, nimepigana vita vya pili vya dunia sisi ndio wakongwe!”

    “”Masikini mzee huyu nae afe???”Alijiuliza Caroline kichwani mwake, hilo ndilo jambo pekee lililokuwa likimfuata mzee huyo, alikuwa hatari kubwa  kama tu angetoa taarifa yoyote juu yake! Hakupenda kumuua lakini alilazimika kufanya hivyo ili kujiokoa! Alikuwa ameponzwa na mdomo wake.

    Hapohapo alianza kujipapasa kwenye pindo la nguo yake na kuigusa sumu yake mahali ilipofichwa, lakini hakutaka kuichukua mara moja! Walipofika hotelini, Caroline alishuka haraka na kuingia hotelini akiwa na mizigo yake!

    “Binti hujanilipa!”

    “Subiri kidogo baba narudi muda si mrefu!”Alisema  Caroline akiingia ndani ambako aliweka mizigo yake chini sehemu ya mapokezi na kwenda baa ambako alinunua chupa ya maji  kisha kuinama na kukitoa kikaratasi chenye sumu katika gauni na kukishika vizuri mkononi, akakifungua na kuimwaga sumu kiasi  kiganjani mwake na kujipaka katika vidole vyake vya mkono wa kulia.

    Kwa haraka alikwenda hadi mahali ilipokuwa mizigo yake na kufungua pochi yake akatoa noti ya shilingi elfu kumi, iliyohitajika  kwa malipo ilikuwa shilingi elfu tano lakini  Caroline hakuwa na muda wa kutafuta chenji! Alichotaka kufanya wakati huo ni kumuua dereva wa teksi ili yeye awe salama.

    Alitembea haraka  hadi nje, akiwa ameishika noti mkono wa kulia pamoja na maji, alimkabidhi dereva noti kisha akampa mkono wake wa kulia  ili waagane, mkono huo ndio ulikuwa na sumu!  Wakiwa wameshikana alimwangalia mzee huyo kwa macho ya huruma   kwani alijua nae alikuwa njiani kuelekea jehamanu!

    Dereva aliondoka, mbele kama nusu kilometa hivi akiwa katika msongamano mrefu ya magari kuelekea kituo cha polisi cha kati alikokuwa akielekea ili  kutoa taarifa juu ya mwanamke wa ajabu aliyembeba ndani  katika gari lake, alianza kusikia kizunguzungu na baadaye mwili mzima ulianza kukakamaa  na macho yakageukia juu!

    Magari yakawa hayasogei mbele na kusababisha msongamano  mrefu  zaidi, madereva wa daladala walipoangalia vizuri baada ya kuona magari hayasogei kwa zaidi ya nusu saa, walimgundua mzee huyo akiwa  amekufa ndani ya gari lake.

    Walilisukuma gari  na kuliweka pembeni   na magari yakaendelea na safari zake, simu ilipigwa polisi na mwili wa mzee huyo ukaja kuchukuliwa kupelekwa hospitali   ya rufaa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, taarifa ilipotoka saa moja baadaye ilionyesha mzee huyo alikufa kwa sumu  ya Thiodane kali inayopenya katika ngozi.

    Sumu hiyo ilitambuliwa kuwa ndiyo iliyoua watu wengi nchini Canada! Wasiwasi kuwa muuaji aliyekuwa akisakwa dunia nzima alikuwa ameingia Tanzania ulitanda! Usalama uliimarishwa na msako mkali zaidi ulianzishwa, Caroline aliyaona yote hayo kupitia kwenye televisheni na kuingiwa na hofu kubwa zaidi, aligundua kuwa ilikuwa ni lazima abadili sura yake kabla hajakamatwa lakini asingeweza kufanya hivyo kabla hajakutana na Dickson.

    Hakuwa tena katika hoteli New Africa  kama alivyopanga, baada ya  dereva wa teksi kuondoka  akijua mbele angekufa  aliamua kubadili hoteli na kuhamia hoteli ya Livingstone iliyokuwa ilala, huko alichukua chumba  ghorofa ya juu kabisa na kujificha.

                            **********

    Saa moja na nusu jioni alipiga simu katika hoteli ya Landmark  walikofikia  Dickson na mkewe, simu hiyo ilipokelewa na msichana wa mapokezi.

    “Nikusaidie?”

    “Naomba kuongea na mgeni aitwaye Dickson!”

    “Naweza kufahamu nani anaongea?”

    “Mwambie naitwa Vicky!”

    “Subiri!”

    Dakika moja tu baadaye tayari Caroline na Dickson walikuwa katika maongezi yao, swali la kwanza  alilouliza Dickson baada ya kupokea simu ni kama Vicky alikuwa tayari, sura ya bandia iliyotengenezwa na mzee wa Kijapan, Sumo ilimchanganya akili Dickson, hakuwahi kukutana na msichana mzuri kiasi kile! Hata sekunde moja hakuwahi kuwaza kuwa mtu aliyekuwa  anapanga kuonana naye ndiye alikuwa muuaji wake!

    “Nakuja!”

    “Nipo Livingstone namba 11 usichelewe!”

    “Nipe dakika tano tu!”

    “Ok!”

    Dakika sita baadaye gari ilisimama moja yahoteli ya Livingstone, ilikuwa ni Landcruiser  Vx ambayo Dickson alikodi kwenye hoteli  ya Landmark ili aendeshe mwenyewe! Alimkuta Caroline akimsubiri nje.

    “Twenzetu!”

    “Ahsante!”Alijibu Caroline huku akipanda garini.

    “Tunaelekea wapi sasa?”

    “Bahari beach panafaa zaidi hakuna watu wengi, lakini mkeo umemuaga vipi?”

    “Achana naye wanawake wa kizungu hawana maana!”

    Kasi ambayo gari ilikwenda nayo haikuwa ya kawaida kwani katika muda wa dakika ishirini tayari walishafika kwenye hoteli hiyo iliyoko ufukweni mwa bahari ya Hindi na kushuka, walitembea wakiwa wameshikana mkono kwa mkono kuelekea pembeni mwa hoteli hiyo na kuketi ufukweni.

    “Utakunywa kitu gani?”

    “Nitakunywa maji!”

    “Chakula?”

    “Sasa hivi hapana!”

    Alipopita mhudumu Dickson alimwita na kumwagiza chupa mbili za maji, yalipoletewa wote waliendelea kunywa taratibu, kwa Caroline huo ndio ulikuwa wakati muafaka wa kufanya mauaji ya kulipiza kisasi aliyoyapanga, mambo ambayo Dickson alimfanyia yalikuwa mabaya mno, kila alipofikiria kitendo cha kubakwa na kufungiwa  ndani ya gunia, kisha kugonjwa na gari! Moyo wake ulizidi kushikwa na hasira kwa maoni yake Dickson hakustahili kuishi.

    Muda mfupi baadaye wakiongea Dickson alijikuta akimkumbatia Caroline na kuanza kupiga mabusu mengi akionyesha upendo wake, Caroline aliuona huo ndio ulikuwa  mwanya wa kulifanya alilotaka kulifanya, alipenyeza mkono wake hadi kwenye pindo la gauni na kuitoa karatasi yenye sumu, sumu iliyokuwa imebaki ilikuwa ni kidogo sana na aliamua kuimalizia kwa Dickson! Aliimwaga yote   kiganjani kisha kuipaka  shingoni mwake Dickson bila yeye kufahamu.

    “Niachie ninywe maji kwanza!”Alisema baada ya kukamilisha kazi hiyo, Dickson alimwachia  na Caroline  akaichukua chupa ya maji na kuanza kunywa baadaye alinawa mikono yake yote na kuwa safi, waliendelea na maongezi  Caroline akisubiri matokeo ya sumu.

    “Nasikia kizunguzungu! Nasikia kizunguzungu!”Alianza kulalamika Dickson sekunde chache baadaye.

    Kuona hivyo Caroline aliivua sura yake ya bandia na kubaki na sura yake halisi, alitaka Dickson aelewe kuwa ni yeye aliyefanya kitendo hicho.

    “Hukukosea uliposema sauti  yangu ilifanana na ya Caroline,  mimi ni Caroline! Ninakuua kulipiza kisasi kwa  ulivyonifanyia!”

    “Mungu wangu Caroline ni wewe?”

    “Ni mimi!”

    “Nisame……!” Dickson hakumalizia sentensi yake akaanguka chini na kukauka, Caroline aliichukua sura yake  ya bandia na kuitupa pembeni mwa mwili wa Dickson,  kisha akachukua ufunguo wa gari na kukimbia  moja kwa moja  hadi nje ambako alilichukua gari walilokwenda nalo na kukimbia hadi hotelini ambako aliliegesha na kushuka mbio akielekea hotelini.

    “Vipi binti wewe ni mpangaji hapa?” Mlinzi alimzuia asiingie hotelini!

    “Ndiyo!”

    “Upo chumba namba ngapi?”

    “Namba 11!”

    “Mbona sura ya mwenye chumba siyo hii? Mimi namfahamu vizuri mwenye chumba hicho!”

    Ikatokea hali ya kutoelewana, ilikuwa ni lazima Caroline aingie chumbani na kubadilisha sura,  alitamani kuwa na sumu yake ili ammalize pia mlinzi huyo lakini hakuwa nayo.

    Mambo yamezidi kuchachamaa kwa Caroline, hivi kweli atafanikiwa kuikamilisha kazi yake ya kulipiza kisasi bila kukamatwa? Fuatilia wiki ijayo











    D

    akika tatu tu baada ya ?Caroline kuondoka   ?ufukwe wa Hoteli ya Bahari Beach na kuingia ndani ya gari aina ya Landcruiser walilokwenda nalo na  kuondoka  akiwa tayari amekwishampeleka Dickson kuzimu, kijana aliyehudumia vinywaji alifika  kwenye meza yao  kuona kama kuna  vinywaji  vilivyohitajika zaidi, alishangazwa na ukimya alioukuta na alipoangalia vizuri alimwona mtu akiwa amelala  mchangani! Moyo wa mhudumu huyo ulishtuka ghafla ikabidi asogee karibu zaidi ili kufahamu kilichotokea.

    Mwanaume alikuwa amelala chini  huku macho na ulimi vikiwa umetoka nje! Alionekana mwenye sura ya kutisha, mhudumu huyo alipiga kelele akiita watu wamsaidie, dakika mbili tu baadaye   walinzi wa hoteli hiyo kutoka kampuni ya Omega Security walifika kutaka kujua kilichotokea.

    “Nini tena?”

    “Mtu kafa!”

    “Kafa? Yupo wapi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapo chini!”Alisema kijana huyo na walinzi  kwa kutumia tochi zao walimulika ardhini katika eneo alilokuwa amelala Dickson! Hakuwa mtu tena, jina lake lilishabadilika na kuwa maiti! Mwili wake ulikuwa mweusi kama mkaa na mgumu kama ubao! Kilikuwa kifo cha kushangaza kila mtu alibaki mdomo wazi.

    “Mh! Sijawahi kuona kifo cha kutisha kama hiki!”

    “Hata mimi!”

    “Imekuwaje lakini?”

    “Yaani  ni jambo la kushangaza sana,   mimi  ndiye niliwaletea vinywaji kisha nikaondoka ili  kuwapa nafasi waongee vizuri, niliporudi kutaka kujua kama walihitaji huduma zaidi ndio nikakutana na hali hii!”

    “Ina maana walikuwa wawili!?”

    “Ndiyo walikuwa pamoja na msichana mmoja mrembo hivi!”

    “Yuko wapi?”

    “Yeye sijamkuta!”

    “Basi yeye atakuwa anafahamu chanzo cha kifo cha huyo bwana!”

    “Inawezekana kabisa!”

    Walishauriana kwa muda  na  kufikia uamuzi wa kupiga simu polisi kuwataarifu juu ya tukio hilo, hazikupita hata  dakika kumi  tangu taarifa  ipelekwe, gari la doria likawa limekwishafika hotelini hapo likiwa na maaskari wasiopungua sita wote wakiwa na bunduki aina ya SMG mikononi mwao, wawili kati yao walivaa kiraia!

    “Vipi kuna matatizo gani hapa?”

    “Mtu kafariki dunia!”

    “Kwa sababu gani?Alikuwa  anaumwa?”

    “Hapana! Nafiiri kanyweshwa sumu!”

    “Umejuaje?”?”Mwili wake umebadilika na kuwa mweusi  kama mkaa na mwanamke aliyekuja naye ametoroka!”

    Mwenye hoteli hiyo alieleza kila kitu kwa askari kisha kuwachukua hadi mahali mwili wa Dickson ulipolala! Maaskari walishangazwa na jinsi mwili ulivyokuwa mweusi na walipomulika pembeni mwa mwili huo walikiona kitu ambacho wafanyakazi wa hoteli pamoja na walinzi hawakukigundua mapema.

    “Kha! Hii si sura ya bandia?”Alisema mmoja wa maaskari hao baada ya kukiokota kitu alichokiona ardhini.

    “Hebu!”  Askari mwingine aliomba na alipopewa  aliivaa usoni sura hiyo.

    “Ehee! Alifanana hivi hivi!”

    “Huyu lazima ni yule mwanamke anayetafutwa!”

    Maaskari walianza kuulizia kwa wafanyakazi  wa hoteli hiyo jinsi mwanamke huyo alivyokuwa, alivaa vipi na mwili wake ulikuwa  na  ukubwa wa saizi gani,  walikuwa na uhakika asilimia sabini kuwa mwanamke aliyefanya mauaji hayo ndiye Serial Killer.

    “Huyu ni yule yule! Mimi niliiona ile maiti ya dereva teksi, ilikuwa na hali hiihii, inabidi  watu wawe makini sana, huyu muuaji kwa hakika kaingia  Tanzania na  ni lazima akamatwe!”Alisema askari mmoja na kisha kupiga simu makao makuu  ya Polisi kutoa taarifa juu ya tukio hilo aliongea na ASP, Selemani Mvungi Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi!

    “Chukueni hiyo maiti muipeleke Muhimbili haraka sana! Na kijana aliyewahudumia  vinywaji mchukueni ili asaidie polisi, ongeeni   na walinzi kuona kama wanaikumbuka namba ya gari walilokuja nalo!”

    “Sawa afande!”

    Baada ya maongezi hayo simu ilikatwa na hapo hapo kama amri ya jeshi ilivyo askari walimwita mlinzi aliyekuwa nje wakati gari linaingia na  kuanza kumhoji!”

    “Ulikuwepo?”

    “Ndiyo!”

    “Unaweza kukumbuka namba za gari?”

    “Ya mwishoni ni 9 na huku mwanzo kuna 47, kuna herufi moja hapa kati siikumbuki vizuri!”

    “Ina rangi gani?”

    “Nyeupe!”

    “Ina maandishi mengine yoyote mbavuni?”

    “Ndiyo!”

    “Imeandikwa hoteli Landmark Ltd!”

    “Ahaaa! Basi inawezekana ni gari  la  hoteli hiyo  lililokuwa limekodishwa! Kuna magari ya kukodisha na kuendesha mwenyewe  pale”Mmoja wa maaskari aliyekuwa akichukua maelezo alisema na baaadye kumgeukia kijana aliyewahudumia.

    “Wewe ukimwona huyo mwanamke unaweza kumfahamu?”

    “Kwanini nisimfahamu wakati nimemwona kwa macho yangu?”

    “Wewe utaongozana na sisi kituoni, unahitajika ili uisaidie polisi kidogo!”

    “Kazi  yangu je?” Aliuliza kijana huyo kwa mshangao, aliielewa maana ya kuisaidia polisi.

    “Hiyo utafanya baadaye!”

    Maiti ilipakiwa ndani ya gari la polisi na gari liliondoka kuelekea hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, tayari ilishatimu saa nne na nusu ya usiku! Ilipopokelewa madaktari walishangazwa na hali  ambayo maiti ilikuwa nayo!

    “Jamani hivi huu ni ugonjwa gani? Kuna maiti nyingine niliipokea mchana nayo ilikuwa hivi hivi! Hivi hii si Gangrene kweli?” Aliuliza daktari akimaanisha ugonjwa wa kuoza na kuharibika sehemu ya mwili sababu ya mishipa ya damu kushindwa kupeleka damu katika eneo husika.

    “Hapana! Hii ni sumu Dk! Tena sumu kali sana!”

     Daktari wa zamu  aliandika katika karatasi na kuthibitisha kifo na  kuwaagiza maaskari waipeleke maiti ya Dickson chumba cha maiti haraka iwezekanavyo ili ihifadhiwe kwa ajili ya uchunguzi siku iliyofuata.

    Gari la polisi likiwa na kijana huyo liliondoka  hospitali na kwenda moja kwa moja hadi hoteli ya Landmark ambako liliegeshwa   kwenye maegesho   yaliyokuwa mbele  ya hoteli hiyo na maaskari walishuka na kutembea hadi mapokezi.

    “Binti hujambo?”

    “Sija...mbo shikamo...moo!”

    “Mimi naitwa Herman, wewe mwenzangu unaitwa nani?” Askari alijaribu kumzoea msichana huyo ili kumwondolea hofu.

    “Naitwa...twa....twa.... Bupe!”Aliongea msichana huyo kwa sauti ya kukatikakatika ingawa kwa  pozi.

    “Sasa dada Bupe, sisi nduguzo tunashida!”

    “Shida ga....gani?Niwasaidie? Ka…ka….ka...kaka zangu?” Aliuliza msichana huyo kwa sauti ya kukatikakatika!

    “Sisi ni makachero wa polisi, tunauliza kama hapa kwenu mna Landcruiser nyeupe ambayo namba zake zinaanzia na 47 na kumalizia na 9?”

    Bupe aliinamisha kichwa kwa muda wa kama sekunde tatu akifikiria, alikuwa akivuta kumbukumbu zake kuona kama kweli kulikuwa na gari la aina hiyo.

    “Hebu subirini kidogo nije!”Alisema msichana huyo huku akimshuka kwenye kitu kirefu alichokalia na kuanza kutembea hadi kwenye korido, aliingia ndani ya chumba kilichokuwa nje tu ya ofisi yake mlangoni kiliandikwa Meneja! Wakati akitembea nyuma yake aliacha gumzo kwa jinsi msichana huyo alivyoumbika!Alikuwa mwembamba mrefu na mwenye mguu uliojaa vizuri! Kila alipotembea nyuma yake alitingishika kama vile kitu kitadondoka!

    “Mzee Kapinga!”Alimwita mzee aliyekaa nyuma ya meza kubwa yenye kung’aa, alikuwa na upara  huyo ndiye alikuwa Meneja wa hoteli.

    “Naam binti!”

    “Kuna maaskari wanaiulizia ile Landcruiser yetu nyeupe, hivi iko wapi?”

    “Maaskari wanaiulizia?”

    “Ndiyo!”

    “Wapo wapi?”

    “Mapokezi!”

    “Iliondoka na yule mpangaji mwenye mke mzungu ambaye yupo chumba namba 210!Asije kuwa kapata ajali au kaenda kuitumia  gari yetu kwenye shughuli ya ujambazi, maana tangu atoke ile saa moja hajarudi au karudi?”

    “Bado! Ha...ta...ta...hata mimi nashangaa”

    “Hebu waite hao maaskari waingie hapa ndani niongee nao!”?”Sa….sa….sa….sawa bosi!”

    Bupe alisema na kutoka nje ya ofisi ya Meneja alichofanya  akiwa nje ni kumwita askari aliyekuwa amesimama mbele ya kaunta kwa mkono, askari wawili walimfuata hadi mlangoni.

    “Meneja anawaita!”

    “Yupo wapi?”

    “Humu ndani!”

    Maaskari wawili waliingia ndani ya ofisi ya Meneja na kuanza kuongea naye,   hawakuona sababu ya kuficha kitu chochote, walieleza kila kitu kilichotokea bayana!?“Gari yenu imetumika kufanya mauaji! Kuna mwanamume alikwenda nayo Bahari Beach akiwa na mwanamke, huyo mwanaume  amekufa na tunafikiri amekufa kwa kunyweshwa sumu! Tunahisi huyo mwanamke aliyemuua ndiye anayetafutwa sana duniani hivi sasa!”

    “Mh! Ina maana yule mpangaji wetu kutoka Uingereza amekufa! Haiwezekani, huyo ndiye alikodi hilo gari jioni!”

    “Gari alilokodi lina namba 47 mwanzoni na kuishia na 9!  Kama ni hivyo basi   kafariki kwa kunyweshwa sumu!”?“Hebu subiri kwanza!”Meneja alisema na kunyanyua simu  iliyokuwa mezani kwake na kupiga chumba alikopanga Dickson na mke wake, aliitikiwa na sauti ya kike iliyoongea Kiingereza kizuri, alifahamu wazi  mwanamke huyo ndiye alikuwa mke wa Dickson.

    “Can I speak to your husband?” (naweza kuongea na mumeo?)

    “He is not back yet! I don’t know what happened to him, he left  at 7:30 promising to be back at around 8:30!”(Hajarudi bado sijui kimempata kitu gani, aliondoka saa 1:30 akiahidi kurudi saa 8:30!) Alisema mama huyo kwa wasiwasi.

    “Tafadhali usimwambie kitu chochote!”Maaskari walimtahadharisha.

    “Ok! Thanks I just wanted to say hi!”(Haya asante, nilitaka tu kumsalimia!) alisema Meneja na simu ikakatwa.

    “Kwa hiyo gari lilikodiwa siyo?”

    “Ndiyo, lakini mara ya mwisho kama nusu saa iliyopita kuna mtu kanipigia simu na kuniambia lipo hoteli ya Livingstone limeegeshwa nje! Nyie mnasema mmeliacha bahari Beach?”

    “Hapana! Inavyodaiwa huyo mwanamke aliondoka nalo baada ya kufanya mauaji, hebu acha sisi twende kwanza huko Livingstone hoteli! Tukaangalie si ajabu huyo mwanamke amepanga hapo!”

    “Ok! Nijulisheni mkimkamata ili nije nichukue gari letu!”

    “Lakini gari hata likipatikana huwezi kulichukua  leo, itachukua muda kidogo!”

    Gari la polisi liliondoka hotelini Landmark kuelekea hoteli ya Livingstone kwa kasi ya ajabu! Bunduki za maaskari zikiwa tayari mikononi kwa lolote, ulikuwa ni msako wa kumsaka mwanamke muuaji aliyekuwa akisakwa na dunia nzima! Ilikuwa ni lazima akamatwe, askari waliamini kama wangemkamta wao ndiyo wangechukua zawadi ya dola 30 zilizokuwa zimetolewa kwa yeyote ambaye angesaidia kukamatwa kwa mwanamke huyo.

    “Watatupa kweli?”

    “Ndiyo, kwanini wasitupe wakati sisi ndiyo tumemkamata?”

    “Wewe unalifahamu vizuri jeshi letu lakini? Watasema sisi ni waajiriwa hatuhitaji zawadi! Angekuwa mtu mwingine wangempa”

    Maaskari waliendelea kuongea gari ikielekea hoteli ya Livingstone alikopanga Caroline.

              *********************

    Bado kulikuwa na mvurugano mkubwa katika  lango la kuingilia hotelini Livingstone, mzee wa Kikuria aliyekuwa mlinzi kwenye hoteli hiyo hakuwa tayari hata kidogo kumruhusu Caroline aingie ndani hakuamini kama alikuwa mteja wao, sura yake ilikuwa tofauti na ya msichana aliyechukua chumba! Kitendo cha Caroline kuivua sura ya bandia na kusahau kuivaa tena akiwa ufukweni baada ya kumuua Dickson ndicho kilisababisha yote hayo.

    Alichodai  mzee huyo ni kwamba, alimfahamu mteja wa chumba namba 11! Hofu ilizidi kumwingia Caroline,  alijua wazi sura yake ilikuwa mali mtu yeyote ambaye angewezeshwa kukamatwa angekuwa tajiri tangu siku hiyo!  Alishangaa ni kwanini mpaka wakati huo  mlinzi huyo wa Kikuria alikuwa  bado hajaigundua sura yake,  Caroline alijitahidi kuongea  huku sura yake ikiwa imeinamishwa ili kuuficha uso wake, hakuwa na uhakika na maisha yake  alijua wakati wowote mambo yangemharibikia.

    “Haiwezekani binti!Nyie ndio watu hatari unaweza kuingia ndani ya chumba cha  mtu halafu vitu vikapotea mimi nikafungwa bure!”

    “Siyo hivyo mzee mimi ndiye niliyepanga katika chumba hicho labda hukuniangalia vizuri  wakati naingia!”

    “Usinifanye mjinga,  uzee wangu upo kwenye meno lakini siyo macho,  meno yote nimepoteza lakini binti macho ninayo na ninaona kuliko wewe, wewe hapa hujawahi kufika!”

    “Basi mzee nisaidie!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haiwezekani!Nimesema haiwezekani!”Mzee huyo aliongea kwa sauti ya juu  kiasi kwamba walinzi na baadhi ya wapita njia walianza kusimama ili kusikiliza kilichokuwa kikiendelea, hofu ya caroline ilizidi kuongezeka, kwa hofu ya kugundulika,  alijikuta akifikia uamuzi wa kuivua tisheti yake na kuiweka kichwani akiacha matiti yake yamefunikwa na sidiria peke yake. Mlinzi alimwona kama mtu aliyetaka kuchanganyikiwa, hakuelewa maana ya kitendo hicho.

    “Mzee nisaidie basi!”

    “Bwana ondoka hapa mimi nimekwishasema haiwezekani kukuruhusu uingie ndani  ya hoteli!”

    Kwa mara ya kwanza Caroline alijisikia kusinyaa mwili,  nguvu zilimwishia alijua  alikuwa amefikia kifo chake bila kuikamilisha operesheni yake ya kuwaua wabaya wake wote. Aliumia kuwaacha Reginald,Leonard, Richard na Harry! 

    “Hivi kweli nife bila kumuua Harry? Hapana haiwezekani, ni heri wengine wote wabaki lakini Harry afe!”

    ***************

    Wakati hayo yakiendelea kwenye lango la kuingilia  hoteli ya Livingstone, gari la polisi lilizidi kukaribia! Maaskari walikuwa na hamu kubwa ya kumkamata Caroline, kwa sababu kuu mbili! Ya kwanza ni kumwona mwanamke aliyesumbua dunia na ya pili  ni kupata kitita cha dola milioni thelathini! Waliamini huo ndio ungekuwa mwisho wa umasikini wao!





    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog