Search This Blog

Monday 24 October 2022

SIRI ILIYOTESA MAISHA YANGU - 2

 

    Simulizi : Siri Iliyotesa Maisha Yangu

    Sehemu Ya Pili (2)





     “Alipozinduka  alitoka jukwaani mbio akiwafuta wavulana  alioongozana ukumbuni pamoja na Mariam  na  kama sikosei  vijana hao wanaitwa Richard na Dickson! Hivi unavyotuona tunamsubiri Mariam hapa ili aje achukue zawadi yake ya gari sababu wakati anatajwa alikuwa ameshaondoka!”

    Kwa maelezo aliyopewa alijua mwanae hakuwa hai wakati huo,   ilikuwa si rahisi kwa Caroline  aliyekwishajaribu kujiua siku za nyuma kustahimili aibu hiyo.

    “Lakini kwanini walinidanganya? Ni lazima huyo Mariam anajua mtoto wangu alipo!” Aliwaza shangazi yake Caroline wakati akitoka nje.

    Hali tayari ilishaashiria tatizo na hakuwa na njia nyingine ya kumpata mtoto wake zaidi ya kutoa taarifa polisi, hivyo alipofika nje aliingia ndani ya gari na kwenda moja kwa moja hadi kituo cha polisi kati ambako alitoa taarifa juu ya kupotea kwa Caroline.

    Ni humohumo kituoni  ambamo aliliona gazeti la Niambie la siku hiyo likiwa na picha kubwa ya msichana akiwa amelala  chali jukwaani huku mdomo wake ukiwa wazi na  umejaa   mapovu! Ilikuwa ni picha ya Caroline na juu yake yaliandikwa maandishi makubwa:kifafa chamuumbua mrembo Habari hiyo iliandikwa na mwandishi aitwaye Leonard Katunzi,mwandishi maarufu jijini Dar es Salaam.

    Maneno hayo yalimfanya shangazi yake alie machozi ndani ya kituo,moyo wake ulimuuma sana kwani ilikuwa ni aibu kubwa mno kwa mtoto wake na alijua tayari gazeti hilo lilishafika Arusha na wazazi wake Caroline walikuwa wamelisoma na si ajabu walikuwa njiani kuja Dar es Salaam.

    Kwa habari hiyo gazetini shangazi aliona dunia nzima   ilikuwa ikifahamu  Caroline alikuwa na kifafa na   kama alikuwa hajafa basi  alikuwa kati mpango wa kujitoa uhai! Ilikuwa si rahisi  kwa Caroline kuliona gazeti hilo na kuendelea kuwa hai.

    “Kuna msichana mmoja atakuwa anafahamu mahali mtoto wangu alipo maana  yeye ndiye alikuja jana nyumbani kwangu kumchukua!”

    “Kweli? Basi huyo ndiye tuanze nae katika upepelezi wetu   yupo wapi?”

    “Kuna sehemu anasubiriwa ili apewa zawadi yake ya ushindi wa Miss Bongo  amepewa ushindi  baada ya mwanangu kupatwa na  matatizo!” Alisema shangazi ingawa hakuwa tayari kuyataja matatizo yaliyompata Caroline.

    “Wapi wanapotoa hiyo zawadi!”

    “Ofisini kwa muaandaji wa Miss Bongo!”

    “Haya basi twendeni hukohuko tukamsubiri!”

    Waliingia ndani ya gari la  shangazi huyo na wote waliondoka kuelekea ofisini kwa muaandaji mtaa wa Aggrey Kariakoo, dakika  tano  baada ya kuwasili ofisini kwa muandaaji, Mariam   aliteremka ndani ya teksi nyeupe akiwa na miwani mnyeusi usoni tabasamu lilitawala mdomoni mwake hasa baada ya kuliona benzi limeegeshwa pembeni.

    “Nimeuaga umasikini!” Aliwaza Mariam.

    Wasichana wote  walimshangilia  Mariam wakimwita Miss Bongo, wapiga picha walipiga picha  nyingi zisizo  kwa ajili ya magazeti yao lakini kabla Mariam hajaufikia mlango wa kuingia ofisini maaskari kanzu watatu walimfuata kwa nyuma na kumsimamisha.

    “Dada upo chini ya ulinzi halali wa polisi!”

    “Nimefanya nini?”

    “Utaelezwa  kituoni!”

    Wasichana wote, waandishi na hata muaandaaji walishangazwa   na hatua hiyo! Mariam alipigwa pingu mikononi na kupakiwa ndani ya gari la shangazi yake Caroline na safari ya kwenda kituoni ilianza.

    Warembo pamoja na muandaaji walifuata nyuma ndani ya gari jingine hadi kituoni  ambako Mariam alitoa maelezo na baadaye kusukumiwa mahabusu! Katika maelezo yake aliwataja Richard na Dickson kama watu waliokuwa naye na  ilitolewa amri nao wasakwe.

                **************

    Pamoja na kujifanya akilia machozi ya geresha Dickson alifahamu kilichotokea, alikuwa amemuua bila hatia yoyote msichana mrembo Caroline baada ya kumpulizia madawa ya usingizi na  kumwingilia kimapenzi bila ridhaa yake! Alijua muda si mrefu sana angesakwa na kutiwa mbaroni jambo ambalo kwa hakika hakuwa tayari hata kidogo kupambana nalo! Dickson hakuwa tayari kukaa gerezani.

    “Itabidi nitoroke nitakwenda London mpaka  tatizo hili limalizike!” Aliwaza Dickson na alitaka kuukamilisha mpango huo mapema  iwezekanavyo.

    Aligundua  mahali alipouweka mwili wa Caroline ndani ya gunia palikuwa wazi na karibu sana na mjini! Hakutaka mwili  huo uonekane kwa sababu ungeweza kupimwa na kuonyesha alama zake za vidole na angesakwa kokote ambako angekimbilia na kurejeshwa Tanzania.

    “Ni lazima nilihamishe gunia  leo hii hii ikiwezekana nilifunge na jiwe na kulizamisha majini!” Aliwaza Dickson, Richard alishangazwa na ukimya aliokuwa nao rafiki yake siku hiyo ilikuwa si kawaida yake.

    “Richard ngoja  nifike nyumbani kidogo!” Alisema Dickson akisimama wima.

    “Usichelewe basi kurudi mshkaji si unajua tena tatizo lililotupata na mimi nakutegemea wewe?”

    “Hakuna noma mshkaji nitarudi baada ya muda mfupi  nakwenda kubadili nguo  tu!”

    “Sawa basi!”

    Dickson alitoka nje ya hoteli na kuingia ndani ya gari lake  badala ya kwenda nyumbani aliliendesha gari lake kwa kasi kuelekea  mahali alikolitupa gunia lililokuwa na mwili wa Caroline.

    Mita kumi kabla hajafika karibu kabisa na mahali gunia lilipokuwa akiendesha gari katikati ya vichaka alianza kusikia sauti ya msichana akilia na kuomba msaada.

    “Nisaidieni nakufa! Nisaidieni nakufa! Ndugu unayepita na gari tafafhali nisaidie!” Ilisema sauti ya msichana aliyelia.

    Sauti hiyo haikuwa ngeni masikioni mwa Dickson, alijua wazi ilikuwa ni sauti ya Caroline! Moyo wake ulipiga kwa nguvu na kuruka pigo moja kama Caroline alikuwa hai basi uwezekano wa yeye kuwa katika matatizo na hata kunyongwa ulikuwa mkubwa zaidi.

    “Au nimesikia vibaya?”Alijiuliza mwenyewe Dickson na kuzidi kusogea  karibu zaidi  alishangaa kuliona gunia lilirukaruka na kujinyonga nyonga huku sauti ya msichana ikilia kutoka ndani yake.

    “Nisaidie ndugu yangu, nisaidie dada au kaka yangu uliyekuja na gari, nimetupwa hapa na kijana anayeitwa Dickson alinibaka halafu akaja kunitupa hapa ili nife!” Aliendelea kusema Caroline ndani ya gunia bila kufahamu mtu aliyekuwa akimwomba msaada alikuwa Dickson.

    Maneno hayo yalimwonyesha Dickson wazi kuwa kama Caroline angepona basi lazima angetaja kila kitu kilichotokea na yeye angekuwa katika matatizo makubwa.

    “Ha! Kumbe afadhali nimeamua kurudi huku upo hai? Kwa maneno unayoyasema Caroline hustahili kuishi kabisa ni lazima ufe, utaniletea matatizo makubwa!”

    “Dickson kumbe ni wewe?”

    “Ndiyo ni mimi na ninakuua ili kukunyamazisha milele!”

    “Tafadhali usiniue Dickson, sitasema kitu chochote nisamehe Dickson!”Alisema Caroline kutoka ndani ya gunia.

    “Hapana ni lazima ufe!” Alisema Dickson na kuingia ndani ya gari lake na kuanza kulirudisha kinyumenyume! Lengo lake likiwa ni kuligonga gunia  hilo  na  gari mara nyingi mpaka Caroline afe ndio alibebe  kwenda kulitupa baharini!

    “Dickson tafadhali usiniue kaka yangu sitasema kitu chochote!” Aliendelea kuomba Caroline.

    Dickson hakusikiliza maneno hayo alizidi kuijaza gari yake moto kabla ya kuiruhusu kutoka na kwenda kuligonga gunia, hata Caroline aliugundua  alitakiwa kuuawa kwa mtindo gani, aliona ni heri angekufa  akiwa usingizini kuliko aina ya kifo alichotakiwa  kupambana nacho, alisikia gari likipigwa  moto na alizidi kulia akimwomba Dickson abadili msimamo.

    “Lazima ufe!” Alisema Dickson kwa sauti ya juu, akili yake ilishabadilika hakuwa binadamu tena bali mnyama.

    Je nini kitampata Caroline? Dickson atakamatwa? Fuatilia wiki ijayo!











    B

    aada ya Mariam Hassan ?kutiwa mahabusu ?msako mkali ulianza kuwasaka Richard na Dickson, magari yaliyojaza maaskari yaliondoka makao makuu ya jeshi la polisi kuelekea hoteli ya Sunshine alikofikia Richard! Walifika  na kujitambulisha mapokezi na kupelekewa moja kwa moja hadi chumbani kwa Richard!

    “Ngo!Ngo!Ngo!”Mlango uligongwa na koplo Kapesa akiwa na bunduki yake mkononi.

    “Nani wewe?” Richard aliuliza kutoka ndani.

    “Ni mimi aliitikia mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo aliyeitwa Naomi.

    Richard aliifahamu sauti hiyo na  hofu yake  ikapungua, alikwenda kwenda moja kwa moja na kufungua mlango wa chumba, Naomi aliingia ndani akiongozana na maaskari watatu wenye bunduki mikononi, Richard alitetemeka mwili mzima kwa hofu alishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka maaskari waje chumbani kwake.

    Alijaribu kulihusisha tukio hilo na  kupotea kwa Caroline, lakini alishindwa kupata uhakika.

    “Caroline atakuwa kafa au kapatwa na matatizo?” Aliwaza Richard kichwani mwake  bila kupata majibu wakati mmoja wa maaskari   akitoa pingu kiunoni kwake na kuanza kumsogelea Richard tayari kwa kumfunga!

    “Upo chini ya ulinzi halali wa jeshi la polisi na tafadhali sana usijaribu kufanya fujo vinginevyo nguvu ya jeshi itatumika!”

    “Sawa lakini kosa langu  hasa ni lipi napenda kufahamu!”

    “Unahusishwa na kupotea kwa msichana Caroline jana, maelezo hayo yanatosha mengine zaidi utaelezwa kituoni!” Alijibu askari.

    Pingu ziliizunguka   mikono ya Richard kwa  nyuma na kwa nguvu akatolewa chumbani na kupelekwa  moja kwa moja kwenye gari  la polisi  liliondoka kwa kasi kwenda kituoni ambako Richard alihojiwa na kutoa maelezo yake juu ya kupotea kwa Caroline  waliyekuwa naye siku moja kabla na alieleza kila kitu.

    “Nilimwacha ukumbini  jana baada ya kuanguka kifafa mbele za watu! Nilikasirika kwa sababu Caroline hakunieleza tangu mwanzo kuwa alikuwa mgonjwa wa kifafa!”

    “Alitokaje ukumbini?”

    “Kwa kweli sifahamu!”

    “Lakini si wewe ndiye ulikwenda naye?”

    “Ndiyo lakini....!”

    “Lakini nini?”

    “Hilo ndilo kosa langu afande kwani Caroline amepatwa nini? Amekufa?” Aliuliza Richard kwa mshangao.

    “Hata sisi hatujui!”

    “Tafadhali niambieni ukweli, bado nampenda sana Caroline nilifanya makosa makubwa  kumwacha ukumbini jana, rafiki yangu alinishinikiza kufanya hivyo! Nampenda  Caroline!”

    “Mpaka sasa hatufahamu kilichompata ila hajaonekana tangu jana kuna habari zinadai atakuwa amejiua au amebakwa na wahuni, shangazi yake ndiye ametoa taarifa hapa na tayari tumemekwisha mkamata mwenzako mmoja!”

    “Nani! Dickson?”
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana ni msichana, anaitwa Mariam Hassan, huyo Dickson bado tunamsaka ila kuna msamaria mwema ametupigia simu kuwa  katika pori la Msata huko Kibaha kuna gunia limetupwa na ndani yake kuna msichana analia, askari wetu wameondoka sasa hivi kwenda huko!”

    “Unafikiri msichana ndani ya gunia hilo atakuwa ni Caroline au?”

    “Kwa kweli sina uhakika sana!” Alijibu askari huyo aliyeonekana kumjali sana Richard.

    “We afande hebu muingize huyo rafiki yako mahabusu si umekwishamaliza kuchukua maelezo yake?” Mkuu wa kituo aliuamuru askari aliyekuwa akiongea na Richard.

    “Ndiyo afande!”

    “Sasa maongezi mengi ya  kazi gani?”

    “Nilikuwa najibu maswali yake fulani fulani!”

    “We hebu fungua mkanda bwana, vua viatu na hiyo saa yako!” Mkuu wa kituo alimwamuru Richard na alipomaliza alianza kumvuta mwenyewe kumpeleka mahabusu.

    “Una nini kingine kwenye hiyo kaptura yako?”

    “Sina kitu mkuu!”

    “Haya ingia humo ndani uongee na rafiki zako upesi!”

    “Sawa lakini naomba mnisaidie basi kumpigia simu baba yangu Arusha namba zake ni mbili,tatu....!” Kabla hajamaliza alizabwa kibao usoni na kuingia mwenyewe mahabusu.

    “Nani apige simu! Sisi? Hiyo si kazi yetu ingia Sheratoni ukale piza!” Alisema mkuu wa Kituo.

    Richard alitembea kinyonge na kuingia ndani ya mahabusu, kabla  ya mwili wake wote haujaishia ndani alisikia sauti ikimwita kwa nyuma na alipogeuka alimwona Mariam akichungulia kutoka mahabusu ya wanawake iliyokuwa upande wa  pili. Macho yake yalikuwa yamevimba na yalikuwa  mekundu kupita kiasi sababu ya kulia, ilionekana  alikuwa amelia sana kabla.

    Huo nido ukawa mwanzo wa Richard kuingia mahabusu!   alilia kwa  sababu alijua  hana hatia na  alimpenda mno Caroline asingeweza kumdhuru! Kosa pekee alilojilaumu kwa kulifanya ni kumwacha Caroline ukumbini peke yake hata hivyo alimlaumu Dickson kwa kosa hilo, ndiye aliyemshawishi kumwacha baada ya kumcheka akidai hapakuwa na sababu ya yeye kuwa na uhusiano na mwanamke mwenye kifafa.

    Mpaka wakati huo hakufahamu  ni wapi   rafiki yake Dickson alikokuwa lakini alielewa ni lazima   angekamatwa na kuungana naye mahabusu, hilo kwa Richard halikuwa suala kubwa, kilichomsumbua zaidi akilini mwake ni Caroline! alimwomba Mungu Caroline apatikane.

                ************

    Magazeti ya siku hiyo yaliandika habari juu ya kuvurugika kwa shindano la Miss Bongo baada ya mrembo aliyeshinda kuanguka kifafa ukumbini na hatimaye kupotea,  na  aliyechanguliwa baada ya mshindi kuonekana ana kifafa,  pamoja na mpenzi wa msichana aliyepotea walikuwa wakiisaidia polisi kufuatia kupotea kwa mrembo huyo!

    Habari za kupotea kwa Caroline na kukamatwa kwa Mariam zilitangazwa  pia katika redio mbalimbali na wazazi wa Caroline walizisikia habari hizo wakiwa nyumbani kwao Arusha  walichanganyikiwa kiasi cha kutosha na kulazimika kusafiri kwa haraka kwenda Dar es Salaam ili  kujua  kwa undani kilichotokea! Shangazi yake Caroline aliogopa kuwajulisha kwa simu kwa hofu ya kulaumiwa kufuatia kitendo chake cha kumruhusu Caroline kuondoka nyumbani kwenda kushiriki mashindano ya urembo, hapakuwa na njia ya kuwaeleza kuwa Caroline alidanganya na akaeleweka.

    Mama yake Caroline alilia njia nzima hadi wanaingia Dar es Salaam siku hiyo  saa mbili ya usiku.

               *****************

    Reginald Simon alikuwa kijana wa Kitanzania, mtanashati pengine kuliko wavulana wote katika jijini Dar es Salaam. Hali hii ilitokana na pato la kazi nzuri aliyoifanya kama Afisa Mali Asili mkoa wa Pwani! Kilichomwezesha kuipata nafasi hiyo katika umri mdogo si kingine bali ni Elimu nzuri aliyokuwa nayo katika mambo ya misitu  aliyoipata nchini Urusi ambako alisoma kwa miaka kumi!

    Katika umri wa miaka thelathini tu Reginald alimiliki nyumba  mbili za kifahari jijini Dar es Salaam na moja kubwa mjini Kibaha. Pia alimiliki gari nzuri aina ya Surf New Model!  Lililomfanya aonekana mwenye uwezo mkubwa zaidi.

    Pamoja na vitu vyote hivyo Reginald alikuwa bachela! Hakutaka kuoa na aliishi peke  akidai mwanamke aliyestahili kuwa mke wake   alikuwa bado hajazaliwa! Ni tabia yake hii iliyowafanya wasichana wengi kuchanganyikiwa kimapenzi juu yake na kujipitishapitisha  ili awaone lakini hawakupata kitu chochote, pesa na uzuri wa sura yake uliwatia kiwewe!

    Pamoja na kufanya kazi  mkoani Pwani Reginald   aliishi Mikocheni jijini Dar es Salaam, alilazimika kusafiri kila siku kwa gari asubuhi kwenda  kazini kibaha na kurudi Dar es Salaam ni siku za Jumamosi pekee yake ndizo alibaki kibaha. Sababu ya kubaki ilikuwa ni kujishughulisha na shughuli za uwindaji alizozifanya  katika pori  la Msata Kibaha! Alipenda sana kuwinda hilo ndilo jambo alilolifanya katika siku za mwisho wa wiki.

                 **************

    Ilikuwa ni siku ya Jumamosi majira ya saa nne, Reginald alikuwa akipita katikati ya pori huku akimvuta swala aliyemuua kumpeleka  mahali alikokusanya wanyama aliowaua siku hiyo, hiyo ilitokea baada ya kuishiwa  na risasi katika bunduki yake! Mara ghafla aliona kitu kama gunia likiwa limetupwa chini, tairi za gari zilikuwa zikionekena pembeni mwa gunia hilo.

    “Labda ni wafanyabiashara wa mkaa wamesahau mkaa wao hapa!” Aliwaza Reginald lakini baadaye alishtuka alipoona gunia hilo likichezacheza na ilifuata sauti ya msichana akilia  kutoka ndani ya gunia hilo, moyo wake ulipiga harakaharaka  ikabidi atoke mbio  kwenda kujificha katika kichaka kilichokuwa jirani na eneo hilo huku moyo wake ukidunda kwa nguvu.

    Alishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka msichana akawekwa ndani ya gunia na kutupwa eneo hilo.

    “Ingekuwa ni sauti ya  mwanaume ningeweza kufikiri  labda ni dereva teksi alitekwa na na majambazi wakaja kumtupa hapa ili afe lakini kwa msichana  sielewi kilichotokea lakini hapa ni lazima kuna tatizo tena tatizo kubwa!” Alizidi kuwaza  Reginald.

    Upande mmoja wa moyo wake uliposikia msichana   akizidi kulia na  kuomba msaada ulisikia huruma na kujikuta akitamani kutoka ndani ya kichaka kwenda kumfungulia   lakini alisita  kufanya hivyo kwa sababu hakujua waliomtupa walikuwa umbali gani kutoka eneo hilo na isitoshe alijua wazi kwa kufanya hivyo alama za vidole vyake zingeweza kubaki   kwenye gunia na baadaye kumponza, mawazo hayo yalimfanya azidi kuvuta subira!

    “Lakini acha kwanza nijulishe polisi juu ya suala hili, nafanya hivyo  kama msamaria mwema!” Alisema na kisha akaichomoa simu yake iliyokuwa kiunoni na kuanza kupiga namba 999 ili kuwajulisha polisi juu ya tukio  alilolishuhudia.

    Simu hiyo ilipokelewa na askari wa doria ndani ya gari la polisi aina ya gofu naye bila kuchelewa alipiga simu ya upepo kituoni kutoa taarifa hiyo. Kipindi taarifa inafika kituoni ndio askari walikuwa wamerejea  kutoka hotelini kumkamata Richard!

    “Nendeni haraka huko porini na mfuate maelezo hayo hayo  aliyowapeni huyo msamaria mwema  wahini ili muokoe maisha ya huyo msichana, inawezekana ndiye tunayemtafuta!” Mkuu wa kituo alisema.

    “Sawa afande!” Walijibu maaskari na kutoka nje ambako waliingia ndani ya gari aina ya Rangerover la polisi,  ni gari pekee ndilo lilitumika katika masuala ya haraka ya polisi.

    Kasi ambayo gari liliondoka nayo kituoni ilimshangaza kila mtu aliyekuwepo na  baadhi ya   walifikiri ni gari la mashindano!

    “Watafika kweli hawa?” Mkuu wa kituo alimuuliza askari aliyekuwa akipita karibu yake.

    “Watafika  tu afande wala usiwe na wasiwasi!” Vumbi lilitimka kituoni  na kuwaacha watu hawaonani.

              **************

    Saa nzima baadaye Reginald akiwa amejificha kichakani alishuhudia gari likija taratibu na kuegeshwa pembeni mwa gunia hilo, aliteremka kijana mmoja mrefu na   mtanashati   na kulisogelea gunia hilo! Reginald alianza kusikia tena sauti ya msichana ndani ya gunia akiomba msaada kwa kijana huyo huku akitaja jina la mtu aliyemtupa pale kuwa ni Dickson.

    “Ha! Kumbe wewe ni Dickson?”

    “Ndiyo! Lazima nikuue ili kukunyamazisha milele!” Alisema kijana huyo na msichana ndani ya gunia alianza kumbembeleza kijana huyo asimuue kwa ahadi  ya kutosema kuwa alimbaka lakini kijana huyo alizidi kusisitiza kuwa angemuua  atake asitake. Reginald aliyasikia maongezi yao yote na kujua kilichokuwa kikiendelea.

    “Ha! Kumbe huyu kijana  anataka kumuua msichana aliyeko ndani ya gunia! Haiwezekani lazima nifanye kitu fulani kumuokoa msichana huyu!  Lakini  huyu kijana anaweza kuwa na bunduki na akanimaliza! Laiti bunduki yangu ingekuwa  bado ina risasi ningemuua kutoka hapa hapa kichakani!” Alisema Reginald kwa masikitiko. Alihofu kijana huyo    angeweza kumuua!

    “Lazima nikuue kwa kukugonga na gari, nikusagesage kabisa malaya wewe!” Alisema kijana huyo na dakika mbili baadaye aliingia ndani ya gari lake na kuanza kurudi kinyumenyume  hatua kama kumi alisimama na kuanza kulijaza gari lake moto  ili akienda mbele aligonge gunia alilokuwemo msichana huyo kwa nguvu.

    Reginald alizidi kusikia sauti ya msichana akibembeleza asiuliwe lakini kijana huyo hakusikia kitu wala hakuona huruma, Reginald alishindwa kuelewa ni kosa gani msichana huyo alifanya mpaka kustahili kifo cha kutisha kiasi hicho!

    Reginald alijishika kichwani kwa woga alipoona gari likiondoka kwa kasi ya ajabu na kuligonga gunia hilo mpaka likaruka mbele!  Msichana ndani ya gunia alitoa kilio mara moja tu na kunyama kimya!

    Bila huruma kijana ndani ya gari alianza kulirudisha   kinyumenyume tena ili aligonge kwa mara ya pili ni hapo ndipo Reginald aliposhindwa kuvumilia,   hakuwa tayari kuona binadamu akiuawa kikatili namna hiyo mbele ya macho yake.

    Kabla gari halijaenda mbele kuligonga gunia tena Reginald alijikuta akichomoka  kichakani mbio akiwa na bunduki yake isiyo na risasi hata moja mkononi mwake, alikuwa amemlenga Dickson ndani ya gari.

    “Mikono juu! Nasema mikono juu!” Reginald alitishia kwani suala la bunduki kukosa risasi lilikuwa siri yake.

    “Mungu wangu! Wewe nani tena?” Reginald aliuliza kila mara.

    “Utanifahamu  baadaye lakini kwa sasa nasema nyosha mikono yako juu!” Aliendelea kusema Reginald ingawa alijua wazi bunduki yake haikuwa na risasi.

    “Hapa bora nife kabisa kuliko kukamatwa  ni heri kifo cha risasi kuliko hicho kifo kilichopo mbele yangu!” Alijisemea moyoni mwake Dickson na ghafla kama risasi alichomoka ndani ya gari lake na kuanza kukimbia kuelekea porini, Reginald hakuwa  na muda wa kumfukuza kwa nyuma, alimshukuru Mungu kwa kilichotokea.

    Hakutaka kupoteza muda wake, palepale alilisogelea gunia hilo na kuanza kulifungua, hakuamini macho yake alipokutana na sura ya Caroline  msichana aliyesifika kwa uzuri katika jiji la Dar es Salaam, hata yeye binafsi alimfahamu.

    “Caroline!”

    “Na..a..m!” Aliitika Caroline kwa shida, damu nyingi zilikuwa zikimtoka na  mkono na mguu mmoja ulikuwa umevunjika kiasi cha mifupa kuchungulia nje.

    “Lakini nini kimetokea Caroline?”

    “Wana....ta...ka kuni..ua!”

    “Akina nani?” Reginald aliuliza tena lakini hakujibiwa swali hilo, caroline alikaa kimya huku damu ikimtoka puani na mdomoni, gari lilimgonga vibaya, Reginald alilia machozi kwa uchungu kuona msichana mzuri kama huyo anakufa  mkononi mwake lakini  hakuwa na uwezo wa kuokoa maisha  ya binti huyo mzuri!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla alisikia muungurumo wa gari nyuma yake na alipogeuza shingo   gari   aina ya Rangerover lililoandikwa maneno “POLISI” ubavuni lilikuwa likiendeshwa kuelekea mahali alipokuwa kabla halijaegeshwa vizuri, maaskari zaidi ya kumi walikuwa ndani yake waliruka na kutua ardhini huku bunduki zao zikiwa zimemlenga Reginald.

    “Hapohapo ulipo mshenzi mkubwa wewe! Kwanini unaua kikatili kiasi hiki?” Alisema mmoja wa maaskari hao na Reginald alishangaa kuona anaitwa mshenzi, alijikuta akisimama wima  bunduki yake likiwa mkononi.

    “Jamani mimi sio muuaji aliyefanya mauaji haya  kakimbia....!” Kunyanyuka kwa Reginald akiwa na bunduki mkononi kuliwafanya maaskari walifikiri alitaka kuwashambulia  kwa bunduki yake! Kitendo bila kuchelewa askari mmoja alimimina risasi tano mwilini mwa Reginald  palepale akaanguka chini huku   damu zikiruka kutoka mwilini mwake kama bomba.

    “”Si..o....ye...ye!”” Caroline alisema kwa shida lengo lake likiwa ni kuwaeleza maaskari kuwa aliyetaka kumuua hakuwa  Reginald lakini alikuwa amechelewa, tayari Reginald alikuwa chini akitupatupa miguu hewani.

    Miili yote miwili ilibebwa na kuwekwa ndani ya gari la polisi na liliondoka kwa kasi kuelekea hospitali ya Tumbi Kibaha kwa lengo la kujaribu kuokoa maisha ya Caroline, kwa upande wa Reginald maaskari wote walikuwa na uhakika   alishafariki dunia!

    Je watu hawa wataokolewa? Nini kinaendelea katika simulizi hii ya kusikitisha?

                     Fuatilia wiki ijayo.











    T

    ayari wazazi wa Caroline ?walikuwa jijini Dar es Sa?laam tena upanga  nyumbani kwa shangazi yake na Caroline, walikuwa katika mjadala mzito juu ya kilichotokea.

     “Nilishindwa  kuwapeni taarifa  juu ya jambo hili!”alisema shangazi

    “Kwanini sasa?” profesa Kadili aliuliza swali jingine.

    “Kwa sababu nilifanya makosa kumruhusu Caroline kutoka nyumbani katika tarehe  za hatari!”

    “Usijali sana dada kwa hiyo hivi sasa yupo wapi?”

    “Bado hajapatikana polisi wanaendelea kumtafuta na haijulikani alipo!”

    “Kwani baada ya kuzinduka kutoka katika kifafa alikwenda wapi?”

    “Taarifa nilizozipata na ambazo hata polisi wanazo,alikimbia kwenda nje kuwafuata wavulana wawili na msichana mmoja waliokwenda nae ukumbini!”

    “Kwanini hao wavulana na huyo msichana wasikamatwe na kuhojiwa?”

    “Tayari wawili kati yao wamekwisha kamatwa na wapo rumande!”

    “Wanasema nini juu ya Caroline?”

    “Wamekana kuondoka naye ukumbini huku wakilia! Mvulana mmoja ndiye bado hajakamatwa lakini  polisi  bado wanaendelea na msako!”

    “Kwa akili ya Caroline ilivyo nina uhakika kabisa atakuwa tayari ameshajiua! Siyo kitu  rahisi kwake  kuanguka mbele za watu wengi  halafu aendelee kuwa hai si mnakumbuka aliyofanya Arusha!”

    “Usiseme hivyo baba Caroline! Mtoto atakuwa hai tu!” alisema mama yake Caroline.

    Baada ya maongezi hayo Kimya kikubwa kilipita katikati yao ni kwikwi za kilio tu zilizosikika, ilikuwa ni siku ya huzuni kubwa sana katika maisha ya Dk. Cynthia na mumewe Profesa John Kadiri ambao kwao  Caroline alikuwa  mtoto  pekee  na hawakuwa na tegemeo  la kupata  mtoto mwingine.

    Caroline alikuwa kila kitu kwake ukimuondoa kaka yake   waliyechangia nae mama, Dennis ambaye kwa wakati huo alikuwa mfanyabiashara mkoani Dodoma! Kwa sababu hiyo Cynthia hakuwa tayari kimwili na kiroho kumpoteza Caroline sababu tu ya ugonjwa wa kifafa! Aliendelea kulia akilitaja jina la mtoto wake!

    Ukimya uliokuwepo  ulikatishwa ghafla na mlio wa simu iliyokuwa mezani, shangazi alinyanyuka haraka na  kwenda kuipokea simu hiyo!

    “Hallow!.....ndiyo!...... nani anaongea? Ha! Kweli?…..yupo wapi?” Aliendelea kuongea  shangazi katika simu.

    Maongezi yake pamoja na kuwa  profesa Kadiri na mkewe Cynthia  hawakuyasikia  bado walielewa kilichoongelewa kutokana na majibu aliyoyatoa shangazi! Sura yake ilijaa tabasamu lililopotea muda mfupi  kabla simu haijakatika!

    “Ha!Kweli? Hali yake ikoje? ….atapona?….tunakuja sasa hivi nipo na wazazi wake hapa nyumbani kwangu!”

    Tayari Dk. Cynthia na mumewe walikuwa wima kabisa wakimsubiri shangazi amalize kuongea, mabadiliko ya sura yake na machozi yaliyomtoka yalionyesha kulikuwa na tatizo kubwa lililotokea!

    “Vipi dada?” Profesa John Kadiri aliuliza.

    “Twende hospitali ya jeshi Caroline amepatikana lakini hali yake ni mbaya sana!”

    “Nini kimempata?”

    “Sikuelezwa  vizuri nyie twendeni tu!”

    Walitoka nje na kuingia ndani ya gari na safari ya kwenda hospitali ya jeshi ilianza mara moja! Hospitali ya jeshi ilikuwa umbali wa kama kilometa mbili kutoka upanga  alipoishi shangazi lakini sababu barabara  kuwa ya lami iliwachukua kiasi cha kama dakika tano tu kufika na kuegesha gari lao na  wote watatu walishuka na kuanza kutembea kuelekea mapokezi.

    “Jamani tunamuulizia ndugu yetu!”

    “Dada hata salamu?”

    “Samahani ndugu yangu vichwa vyetu vimeingiliwa na mdudu, utanisamehe  kwa kutokuwa mstaarabu!”

    “Hakuna tatizo dada hapa kwetu ndio hivyo tunapokea watu wenye matatizo mbalimbali! Sijui mgonjwa wako ni nani?”

    “Anaitwa Caroline John Kadiri!”

    Shangazi alipotaja tu jina hilo nesi alionyesha mshtuko wa ajabu! Jambo lililowafanya shangazi, Dk. Cynthia na mumewe kushindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea kabla hawajafika hospitali!’

    “Vipi amefariki?” Dk.Cyanthia alijikuta akiuliza bila kutegemea.

    “Hapana lakini hali yake si nzuri, amekimbizwa chumba cha upasuaji!”

    “Kwani nini kilimpata?”

    “Alitekwa na kijana mmoja aliyempeleka porini akiwa amefungwa ndani ya gunia!”

    “Mungu wangu kijana gani huyo?”

    ‘Kakamatwa na kapigwa risasi kama tano hivi na maaskari kwenye mguu wake wa kulia alipoletwa hapa maaskari wakifikiri amekwisha kufa lakini  daktari alipompima aligundua alikuwa bado anahema! Hivyo wote wapo chumba cha upasuaji wakifanyiwa operesheni!”

    “Sasa sisi tufanye nini dada yangu?”

    “Nyie kaeni pale kwenye benchi msubiri mpaka watoke chumba cha upasuaji!”

    “Sawa!” Alijibu Dk. Cynthia huku akijifuta machozi na kwenda kwenye benchi ya kukaa! Walikaa hapo kwa dakika kama kumi tu roho zikiwa haziwapi na wote waliondoka na kuanza kutembea kuelekea chumba cha upasuaji huko walikaa katika benchi lililokuwa nje ya chumba hicho muhimu na kuanza kusubiri Caroline.

                *****************

    Kazi ya kumshona  sehemu alizopasuka na kuiweka sawa mifupa ya Caroline iliyovunjika vibaya, haikuwa ndogo, iliwachukua madaktari muda wa masaa mawili tu kuikamilisha huku chupa za damu  na  maji  zikiendelea kuingia katika mishipa yake, baada ya kazi hizo kukamilika Caroline alifungwa P.O.P  mkononi na mguuni, zikiacha sehemu zilizokuwa na vidonda peke yake kuwa wazi!  Kwa jinsi kazi hiyo ilivyofanyika kwa uangalifu matumaini ya Caroline kupona yalikuwa makubwa sana.

    “Dk. Cynthia vipi mbona upo hapa umetoka lini Arusha?” Lilikuwa swali kutoka kwa  Kepteni Slyvester Lukonge daktari bingwa wa upasuaji wa jeshi! Yeye na Dk. Cynthia walisoma pamoja chuo kikuu.

    “Mtoto wangu yuko huko  ndani anafanyiwa upasuaji!”

    “Mtoto wako? Ni yupi maana  maana hii operating Theater yetu ina vyumba vitano! Sasa sijui yuko chumba gani”

    “Anaitwa Caroline!”

    “Ahaaa! Kumbe Caroline ni mtoto wako?”

    “Ndiyo mtoto wangu wa kwanza na pekee tuliye naye! Huyu hapa ni mume wangu anaitwa Profesa John Kadiri”

    Dk. Lukonge  alishikana mkono na profesa  Kadiri wakisalimiana, baada ya salamu Dk. Lukonge aliwapa pole

    “Ni mimi na Dk. Kepteni Gindu  Sweya ndio tumemfanyia operesheni hiyo!”

    “Atapona lakini?”

    “Atapona ila aliumia sana  kwani amepata compound fracture katika mguu  na mkono wake wa kushoto   pia amevunjika mbavu tatu za ubavu wa kushoto! Inavyoonekana kuna watu walimpiga na vitu vizito baada ya kumbaka.

    “Alibakwa?”

    “Ndiyo kwa sababu kuna mbegu za kiume zimeoneana katika sehemu zake za siri!”

    Jibu hilo la daktari lilimfanya hata profesa Kadiri alie machozi! Profesa John Kadiri alipandwa na hasira kupita kiasi na alimwonea huruma mtoto wake kwani hata kama angepona kulikuwa na uwezekano mkubwa  aliambukizwa Ukimwi na wabakaji hao.

    Maongezi yao hayakuendelea zaidi kwani muda mfupi baadaye lango la chumba cha upasuaji  lilifunguliwa na machela mbili zikatoka zikiwa zimeongozana! Waliagana na daktari na kuanza kuzifuata machela hizo kwa nyuma, mbele mita kama hamsini moja ilisimama  kwenye wodi iliyoandikwa maneno Male WD 1, ilikuwa wodi ya wanaume na  ukafunguliwa  machela ikaingizwa ndani.

    Hawakusimama hapo waliamua kuifuata machela nyingine iliyoongoza hadi kwenye wodi iliyaondikwa Female wd 2 maneno ya kiingereza yaliyamaanisha ilikuwa ni wodi ya wanawake namba mbili, machela iliingizwa ndani ya wodi na wao waliifuata.

    “Jamani saa za kuona wagonjwa sio hizi, yaani usiku   huu mnataka kuona wagonjwa?Hebu tufuate taratibu za hospitali!”

    “Sawa binti lakini tulitaka tu kumchungulia mtoto wetu mara moja!”Dk. cynthia alisema.

    “Hapana mama haturuhusiwi kufanya hivyo  njooni  kesho asubuhi!”

    Dk. Cynthia hakutaka kubisha alifungua mkoba wake na kutoa kitambulisho  akamkabishi muuguzi huyo ili akisome, alitupa macho yake juu ya kitambulisho hicho kisha  akanyanyua uso na kumwangalia tena Dk. Cynthia usoni! Hakusema kitu zaidi ya kuwaruhusu wamwangalie  mgonjwa mara moja.

    “Fanyeni haraka kabla muuguzi mkuu hajafika itaniletea matatizo mimi!”

    Walitembea kwa harakaharaka hadi kwenye kitanda alicholazwa Caroline na kumwangalia kila mtu kati yao alisikitika kiasi cha kutosha! Ilikuwa si rahisi hata kidogo kuamini aliyelala kitandani pale alikuwa mtoto wao Caroline, uso wake ulikuwa umevimba na ulijaa bendeji nyingi zenye rangi nyekundu, mkono na mguu wake ulifungwa mhogo wa POP na alionekana kuhema kwa shida  hakuwa na fahamu yoyote sababu ya madawa ya usingizi aliyopewa chumba cha upasuaji.

    “Kwa hali niliyoiona mtoto wetu atapona lakini najiuliza ni kwanini walitaka kumuua? Je ni sababu ya kuugua kifafa tu? Na kwanini sasa walimbaka mwanangu kabla ya kumfanyia ukatili huu?” Alisema Dk, Cynthia  wakitembea kwenda nje ya wodi.

    “Haiwezekani ni lazima mtu aliyefanya ukatili huu afe! Hawezi kumfanyia mwanangu kitendo hiki halafu  yeye akandelee kuishi!” Aliwaza profesa Kadiri.

    Walipotika wodini walichukua gari lao na kuondoka kuelekea nyumbani, usikuw wa siku hiyo hakuna aliyepata usingizi kati yao walikesha wakiongea na kupanga kitu cha kufanya ili haki itendeke.

    “Ni lazima sheria ichukue mkondo wake, ni lazima watu hawa wafungwe kabisa!”Alisema Dk. Cynthia kwa hasira.

    Wakati Dk. Cynthia akiwaza juu ya sheria kuchukua mkondo wake, ndani ya kichwa cha mumewe iliendelea mipango ya mauaji na katikati ya usiku alimtoa dada yake nje na wakapanga kitu cha kufanya.

    “Tutamtafuta mtu na atamuua hapo hapo kitandani alipolala, jambazi mkubwa yule!”

    “Tutamuua na nini?” Shangazi aliuliza.

    “Nitatumia dawa fulani! Wewe hiyo niachie mimi, cha msingi apatikane nesi wa kufanya hilo jambo!” Profesa Kadiri aliongea akionyesha hasira yake yote.

                ******************

    Jioni ya siku hiyo Shangazi na profesa  Kadiri walikuwa ndani ya hoteli ya  Starlight wakiwa wamejificha pembeni kabisa mwa ukumbi wa hoteli hiyo, walikuwa hapo kumsubiri mtu mmoja muhimu waliyeamini angesaidia kuikamlisha azima yao! Hawakutaka kumshirikisha Dk. Cynthia  katika mpango huo.

    Aliyekuwa akisubiriwa alikuwa mmoja wa wauguzi katika wodi aliyolazwa Reginald, waliomba kuonana naye baada ya kazi ili awasaidie katika mpango mzima wa kumuua Reginald kabla hajazinduka usingizini!

    Mpaka wakati huo  waliamini ni Reginald aliyemteka Caroline na kumpeleka porini baada ya kumbaka! Ni habari hiyo ndiyo iliyotolewa na jeshi la polisi na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari . Pamoja na habari hiyo watu wengi waliomfahamu Reginald walishindwa kuziamini  yaliyosemwa na kitendo cha gari la Reginald kukutwa eneo la tukio kilizidisha hali ya wasiwasi kamakweli Reginald  alifanya unyama huo  lakini hapakuwa na njia ya kumsaidia kwani siku zote mbambwa na ngozi ndiye mwizi! Wengi walisubiri Reginald na Caroline wazinduke  wao ndio wangeeleza ukweli.

    Mamia ya watu walifurika nje ya lango la  kuingilia  katika hospitali ya jeshi wakitaka kuhakikisha habari  za Caroline kama zilikuwa kweli, watu mbalimbali waliomfahamu Reginald na walimwona kabla ya habari  ya tukio hilo  walilia na kulalamika  wakida Reginald alionewa lakini hilo halikuubadilisha ukweli, Reginald alibaki amelala kitandani akiwa amefungwa pingu pembeni mwa kitanda chake alihesabika jambazi na muuaji.

    “Tumekuita dada!” Profesa John Kadiri aliyaanzisha maongezi baada ya muuguzi waliyekuwa wakimsubiri kuwasili.

    “Ndiyo  nawasikilizeni!”

    “Umefanya kazi ya uuguzi kwa miaka mingapi mama?”

    “Mimi?”

    “Ndiyo!”

    “Huu ni mwaka wa kumi na moja!”

    “Una nyumba?”

    “Hapana!”

    “Umeolewa?”

    “Hapana!”

    “Mshahara wako ni shilingi ngapi?”

    “Elfu arobaini na tano!”

    “Aisee! Hebu nieleze vizuri kuhusu maisha yako!”

    Nesi  alishtuka kidogo lakini baada ya profesa John Kadiri na shangazi kujitambulisha ni ndugu wa mgonjwa Reginald   aliwaamini na kuwaeleza kila kitu katika maisha yake kuwa alizaliwa familia masikini na ni kwa mshahara mdogo alioupata katika hospitali ya jeshi aliwatunza wazazi wake.

    “Sasa sisi tunazo pesa nyingi  tunazotaka kukupa lakini utusaidie kukamilisha kazi moja tu wodini kwako!”

    “Kazi gani?”

    “Utusadiie kumchoma mgonwja  wetu dawa hii  katika mshipa ili apate nafuu upesi  sawa?” alisema profesa John Kadiri akimwonyesha muuguzi kichupa kidogo cha dawa alichokuwa nacho mkononi.

    “Ni dawa gani hiyo?”

    “Inaitwa Kristapeni!”

    “Hebu niione!” Aliomba kichupa kidogo alichokuwa nacho Profesa John Kadiri mkononi, alipopewa alikiangalia kwa  kama dakika moja nzima bila kujibu kitu! Taa zilizokuwepo zilimsaidia kuyaona maandishi  ya  Benzathin cyrstalline penicilline yaliyoandikwa kwenye kichupa hicho yakimaanisha ilikuwa dawa aina ya Kristapeni!

    “Mh! Crystapen gani hii nyekundu?”

    “Huo ndio muundo wake nilinunua Japan!”

    “Sawa nitawasaidia kumchoma lakini kesho  sababu naanza zamu ya usiku  lakini mtanipa shilingi ngapi?”

    “ Tutakupa shilingi milioni mbili!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Milioni mbili kwa kazi hii ya kumchoma mgonjwa sindano tu? Aliuliza muuguzi huyo mama wa watoto watatu kwa mshangao mkubwa alichotegemea yeye ilikuwa ni shilingi elfu tano.

    Mpaka wakati huo alikuwa bado hajawalipia watoto wake watatu ada za shule na alikuwa katika hatihati ya kufukuzwa katika  chumba alichoishi sababu kodi yake  kufikia mwisho!  Hivyo jambo lililokuwa likielezwa hapo lilikuwa  neema kubwa sana kwake wala hakutaka kujiuliza mara mbili ndiyo akubali kufanya alichoambiwa!

    “Kama ni hii dawa ya Crystapen tu nitamchoma sasa hayo malipo itakuwaje?”

    “Tutakupa hapahapa milioni moja halafu ukiikamilisha hiyo kazi tutakupatia akiba yako, sawa?”

    “Sawa nipeni basi mie niondoke!”

    Shangazi alifungua mkoba wake na kuchukua burungutu la   shilingi milioni moja na kumkabidhi nesi huyo na alizipokea huku akitetemeka mwili wake macho yake hayakuamini  kilichotokea, ilikuwa ni  mara ya kwanza katika maisha yake kukutana na kiasi kikubwa namna hiyo cha pesa!

    Baada ya kuzipokea pesa hizo nesi alikinusa kichupa na kukuta kikinukia manukato mazuri na  aligeuza macho yake   kumwangalia shangazi usoni.

    “Usishangae ni manukato katika mikono yangu hayo!”

    “Sawa nilikuwa najiuliza ni Kristapeni gani  inayonukia hivi?”

    Waliagana na wote kuondoka kurejea makwao walipofika nyumbani Profesa John Kadiri na shangazi hawakumweleza Dk. Cynthia juu ya kilichotokea  hotelini walimkuta ndani akiendelea kuwaza juu ya mtoto wake  ambaye hata siku hiyo pia hakurejewa na fahamu zake kiasi cha kuanza kuhisi aliumia  ubongo wake.

    “Jamani mlikuwa wapi?” Dk. Cynthia aliuliza.

    “Tulikwenda kuonana na mkuu wa polisi ili  jambazi apelekwe mahakamani baada tu ya kurejewa na  fahamu zake!”

    “Sawa mimi nimefikiri sana juu ya Caroline kutopatwa na fahamu zake leo, hii si kawaida  kabisa na nimepanga kumtafuta Dk.  Lukonge ili nimshauri ampige  picha ya CT Scan kuona kama ubongo wake haukuumia au nyie mnaonaje?”

    ‘Ni sawa  utakachosema wewe ni  sawa kwani ni mtaalam unaelewa!”

    Walikubaliana juu ya jambo hilo   hawakudiriki kumweleza juu ya mpango   wa mauaji waliokuwa  wamepanga kwani  walikuwa na uhakika angeupinga!

                  ****************

    Dawa waliyompa muuguzi haikuwa Crystapen kama walivyomweleza!! Bali dawa ya thiodan iliyojazwa ndani ya kichupa cha Kristapen! Profesa  Kadiri alikuwa amedhamiria  kumuua  Reginald akiamini  ni yeye ndiye alimteka, kumbaka na hatimaye kujaribu kumuua mtoto wake mpendwa Caroline!

    Asubuhi kulipokucha alichofanya muuguzi ni kwenda shuleni kwa watoto wake na kulipia ada  zote kisha akaondoka kwenda  nyumbani kwa  mama mwenye nyumba  na kulipa kodi ya mwaka mzima hata mama mwenye nyumba siku hiyo alishangaa.

    “Mama Edina leo umepata wapi pesa?”

    “Mambo ya bingo hayo mama!”Alisema kwa utani.

    Saa mbili kamili ya usiku alikuwa tayari kazini kwake na wauguzi waliokuwa wakimaliza zamu ya jioni walimpitishwa wadini kumkabidhi ripoti ya wodi nzima, walipofika katika kitanda cha Reginald walisimama kidogo

    “Huyu mgonjwa anaendelea vizuri fahamu zake tayari zimerejea, huyu hapa ni askari anamlinda si unajua matatizo yake?”

    “Ndiyo!”

    “Ila ana sindano nyingine ya Pethedine saa tatu   alilalamika maumivu na daktari akamwandikia sindano mbili moja tumeshamchoma bado hiyo ya saa tatu!”

    “Sawa!” Aliitikia mama Edina huku moyo wake ukifurahia, aliuona muda wa kuichoma sindano hiyo ndiyo wa kuikamilisha kazi yake.

    “Ha! Mwenzetu mbona leo meno yote thelathini na mbili nje?” Aliuliza mmoja wa waugui baada ya kushangazwa na furaha ya mama Edina usoni!

            ********************

    Gari lilikuwa likikimbia kwa kasi ya ajabu kuelekea katika mpaka wa Namanga, ilikuwa gari aina ya Peugeot yenye abiria saba ndani yake na miongoni mwa abiria hao alikuwemo Dickson, moyo wake ulikuwa ukipiga kwa kasi ya ajabu, alihofia kukamatwa wakati wowote, alikuwa akisafiri kuelekea Kenya ambako alitegemea kuunganisha  kwa ndege kwenda Uingereza kuikimbia kesi iliyokuwa nyuma yake, alikuwa na uhakika lazima Caroline angekufa kwa jinsi alivyomgonga  kwa nguvu na gari lake.

    “Atakuwa amekufa na hii itakuwa kesi ya mauaji!” Aliwaza Dickson na hakuwa na jambo jingine la kufanya zaidi ya kutoroka! Hakuwa na uhakika wa kuvuka mpaka kwani alijua taarifa na hata picha zake tayari zilikuwa mpakani! Kabla ya kufika mpakani alishuka na kupita njia za vichochorini hadi upande wa Kenya ambako alipanda magari mengi ya kwenda Nairobi. Moyo wake ukatulia.

               *******************

    Saa mbili na dakika hamsini na tano hivi  zikiwa zimesalia kama dakika tano tu kufikia saa tatu kamili muuguzi alinyanyuka kitini na kuchukua dawa tayari kwa kwenda kumchoma  Reginald sindano, badala ya kuchukua chupa ya Pethedine dawa ya maumivu aliyokuwa ameandikiwa,   alichukua kichupa cha dawa aliyopewa na kuanza kutembea nacho kwenda kitandani  ambako alimkuta askari amelala fofofo! Reginald alikuwa macho lakini katika maumivu makali sana!?“Pole sana!”

    “Ahsante naomba basi unichome ile sindano ya saa zile! Iliondoa kabisa maumivu yangu!” Alisema Reginald akiomba achomwe  sindano ya Pethedine!

    “Ndiyo  nimekuja kukuchoma hebu geukia ukutani!” Aliamuru nesi hakutaka Reginald aione chupa ya dawa aliyokuwa nayo!

    “ Kwani unanichoma matakoni mbona wenzako walinichoma kwenye mshipa?” Aliuliza Reginald.

    “We geuka tu!”Nesi alisema huku akitetemeka.

    Je nini kitatokea? Reginald atakufa? Nini kitampata Caroline? Fuatilia wiki ijayo.







    M

    uuguzi aliendelea ?kusimama na bomba ?lake la sindano mkononi, Reginald naye aliendelea kumwangalia kwa mshangao, aliushangaa utaratibu uliotaka kutumika kumchoma sindano, alijua kama angechomwa kwenye msuli ingechelewa kufanya kazi! Alitaka achomwe kwenye mshipa kama walivyofanya wauguzi wengine ili maumivu yake yapungue upesi. Fahamu zake zilirejea kwa kasi ya ajabu kuliko ilivyotegemewa, maumivu aliyoyapata baada ya kukatwa mguu wake uliomiminiwa risasi ndiyo yaliyomsumbua zaidi.

    “Sista mbona wenzako walinichoma kwenye mshipa lakini?”

    “Usinifundishe kazi, dawa hii inaweza hata kuchomwa    matakoni tafadhali geuka upesi mimi nifanye kazi yangu!”

    Reginald alipomwangalia muuguzi mkononi alishangaa kumwona akitetemeka kama mtu mwenye wasiwasi mwingine, alishindwa kuelewa ni kwanini muuguzi alikuwa na hali hiyo na  alihisi pengine hakuwa muuguzi mzoefu ambaye angeweza   kumsababishia ulemavu! 

    “Tafadhali geuka nikuchome sindano!”

    “No! No! No! Huwezi kunichoma matakoni  ni vyema unichome kama walivyonichoma wenzako!”

    “Wewe unanifundisha kazi siyo?”

    “Siyo hivyo sista lakini sitaki kuchomwa sindano matakoni nasema sitaki!” Reginald alisema kwa sauti ya juu.

    Askari alisikia kelele hizo na kuzinduka usingizini kwa hofu kubwa ambayo muuguzi alikuwa moyoni kuamka kwa askari kulimshtua muuguzi sana kwa haraka aliichukua sindano yake na  kuondoka nayo kurudi   ofisini kwake, mzozo  na Reginald alijua ungeweza kumletea matatizo makubwa  na hata kusababisha siri yake  igundulike.

    Alipofika wodini alilitupa bomba la sindano katika ndoo ya uchafu na kuchukua dawa halisi ya Pethedine aliyotakiwa  kumchoma nayo Reginald na kwenda hadi kitandani ambako aliichoma katika mshipa kama ilivyokuwa imeagizwa, Reginald alifurahi na  hakuchukua muda mrefu   akalala usingizi.

            *********************

    Huku akitetemekea mwili mzima aliketi kitini akijaribu kufikiria angemjibu nini Profesa Kadiri   amba ye tayari  alishapokea pesa yake ili akamlishie kazi  ya kumdunga sindano Reginald.

    “Kwani watajuaje kama sikumchoma?”Aliwaza muuguzi

    Baadaye wazo  jingine lilimwijia kichwani na kujikuta akitaka kujua,  kama kweli dawa aliyopewa na profesa Kadiri ilikuwa Kristapeni! Kichupa cha dawa hiyo kilikuwa bado kipo mezani kwake, alikichukua na kukifungua kisha akaminina dawa  iliyokuwa imebaki ndani yake kwenye   kiganja mkononi mwake.

    “Naifahamu ladha ya Kristapeni hebu ngoja niionje!”Alisema na baadaye kulamba dawa hiyo kwa ulimi wake! Alishangazwa na harufu hiyo na baadaye  kugundua ilikuwa ni harufu aliyoifahamu kabisa.

    “Mh! Hii  ni harufu ya nini mbona kama naifahamu?” Aliwaza muuguzi huyo lakini  dakika kumi baadaye wakati bado anawaza juu ya jambo hilo alishtuka macho yake yalipoanza kupatwa na kizunguzungu, ni hapo ndipo alipogundua alikuwa amelamba sumu  na kufahamu ilikuwa ni sumu ya  thiodani!

    Alinyanyuka na kutembea hadi kwenye karo la maji na kuanza kunywa maji kutoka kwenye bomba kisha akakiingiza kidole chake hadi kooni, haikuchukua muda akaanza  kutapika, pamoja na hayo yote bado kizunguzungu kilizidi kuongezeka.

    Ghafla alianguka chini na kuzirai, askari aliyekuwa akimlinda Reginald alimwona muuguzi akianguka na kunyanyuka kukimbia ofisini, alimkuta chini akitoa povu  bila kuchelewa alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa wagonjwa, badala ya wagonjwa peke yao kuja hata wauguzi wa wodi nyingine walifika na  kumkuta tayari muuguzi huyo ameshafariki dunia!

    Kifo cha muuguzi huyo kilizua kitendawili lakini uchunguzi ulipofanyika iligundulika   alikunywa sumu aina ya thiodani na kichupa chenye dawa hiyo kilikutwa wodini. Watu wote waliamini muuguzi huyo alijiua lakini sababu ya kufanya hivyo haikujulikana.

    Profesa Kadiri aliposikia jambo hilo alishangaa ni kwanini alikufa muuguzi badala ya Reginald! Alikwenda kitandani kwa Reginald kumsalimia  na kujifanya hafahamu kitu chochote, mdomoni alicheka lakini ndani ya moyo wake alijawa na hasira, bado alitaka Reginald afe kwa unyama alioamini alimfanyia mtoto wake.

              ******************

    Kila siku Reginald alilia akiomba Mungu awafunulie  watu    ni kiasi gani hakuwa na hatia,  mtu pekee wa kumuokoa katika kesi iliyokuwa ikimkabili ambayo ingepelekea hata anyongwe alikuwa ni Caroline! Ni yeye peke yake aliyeelewa kilichotokea na  ni yeye peke yake aliyekuwa na uwezo wa kumtoa Reginald hatiani!

    Taarifa alizozipata kutoka wodini kwa Caroline zilieleza kuwa  hali yake iliendelea kuwa mbaya siku hadi siku na matumaini ya kupona yalikuwa kidogo, hiyo ilimfanya apoteze  kabisa matumaini ya kutoka gerezani alijua mwisho wake  ulikuwa kunyongwa.

    Kwa mbili mfululizo tangu aingie hospitali hali ya Caroline ilikuwa mbaya hakuwa na fahamu kabisa! Lakini Reginald alipata nafuu na  kupelekwa moja kwa moja mahakamani ambako alisomewa mashtaka la kubaka na kujaribu kuua! Alikana mashtaka yote   na kupelekwa moja kwa moja mahabusu katika gereza la Segerea, kila siku alilia na alijiona mwenye bahati mbaya aliyeponzwa na usamaria wake!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ningejua hata nisingejaribu kumwokoa  huyo msichana! Maisha yangu yameharibika sababu yake!”Aliwaza Reginald kila siku lakini alishindwa kumlaumu Caroline moja kwa moja.

    Hali yake ilipozidi kuwa mbaya Iligundulika baadaye kumbe gari  lilimgonga  kichwani   na kukipasua kwa ndani na kuharibu sehemu  upande mmoja wa ubongo wake, majibu hayo yalipopatikana ililazimu arudishwe tena chumba cha upasuaji ambako alifanyiwa operesheni kuondoa damu iliyoganda na kuungandamiza ubongo wake! Profesa Kadiri na mkewe walizidi kupoteza matumaini yao juu ya mtoto wao kila siku kwao ilikuwa ni kilio tupu.

    “There was a brain damage on one of the  her brain hemespheres involving the medulla oblongata,  even the hearing and speech centres are damaged!(Upande mmoja wa ubongo umeharibiwa vibaya pamoja na medulla oblongata  hata vituo vinavyohusika na kuongea na kusikia pia vimeharibika) alisema Dk. Slyvester Lukonge baada ya operesheni alipoongea na  Dk. Cynthia na profesa Kadiri juu ya hali ya mtoto wao!

    “So Caroline wont hear or speak for life?(Kwa hiyo Caroline hataweza kusikia wala kuongea milele?) Profesa Kadiri aliuliza.

    “I’m afraid that is what is going to happen!(Nina wasiwasi hicho ndicho kitakachotokea)

    “Oh my God!”(Oh mungu wangu) alipiga kelele Dk Cynthia  huku akilia, roho ilimuuma sana alipomfikiria mtoto wake pekee akiwa kiziwi na  kipofu! Alishindwa kuelewa ni kitu gani kingefanyika kumsaidia Caroline, alikuwa daktari lakini alikosa kitu cha kufanya.

    “Kweli atapona mtoto wangu?” Profesa Kadiri alimuuliza daktari.

    “Kupona atapona ila wasiwasi wangu mimi ni kuongea na kusikia na ninafikiri itachukua muda mrefu kidogo kurejewa na fahamu!”

    “Sure?(Kweli?)

    “She is gonna be in a comatous state for a longtime!”(Atakuwa bila fahamu kwa kipindi kirefu)

                  ****************

    Maneno ya Dk.  yalikuwa kweli  tupu kwani Caroline alikaa hospitali kwa muda wa miaka miwili  bila fahamu, kitu pekee alichofanya akiwa kitandani  ni kila kati ya  tarehe 26-28  kupatwa na kifafa  na hiyo ndiyo iliyofanya hali yake izidi kuwa mbaya zaidi.

    Katika miaka yote hiyo miwili Reginald aliendelea kusota mahabusu, maisha yake yote yalishaharibika mipango yake yote   maishani ilishavurugika,kila kitu chake kilishahamia gerezani Segerea!  Taarifa kuwa Caroline kuwa katika hali kutojitambua ilimsikisha sana na ilimkatisha tamaa kwani  yeye ndiye mtu aliyemtegemea kueleza ukweli  bila Caroline  alijua angehukumiwa kunyongwa kwa mauaji  ambayo hakuyafanya,jambo hilo lilimuumiza  sana moyo wake ukizingatia.

    Kila baada ya mwezi mmoja Reginald alifikishwa mahakamani kwa kesi ya kubaka na kujaribu kufanya mauaji, pamoja na kukanusha bado kesi ilionekana kumuelemea na wengi walihisi angehukumiwa, kwa kesi ya kubaka na hukumu yake ilikuwa ni kufungwa maisha!

    Ndugu zake wote walishakata tamaa kabisa ingawa walikuwa na uhakika  mtoto wao hakutenda kosa hilo hawakuwa na njia ya kumsaidia,  walishafanya   mpango yote ili wamtoe gerezani lakini ilishindikikana, nyundo aliyoshindilia profesa Kadiri ilikuwa nzima! Yeye alitaka Reginald anyongwe au kufungwa maisha ndio roho yake ingefurahi.

                  **************

    “Mama ni heri uniruhusu nijiue kuliko kuhukumiwa kifungo cha maisha au kunyongwa kwa kosa ambalo kwa hakika sikulifanya! Sikumfanyia kitendo chochote kibaya Caroline mama, nilikuwa nikimuokoa kutoka kwa kijana aliyetaka kumuua kwa kumgonga na gari!” Reginald alimwambia mama yake siku moja alipomtembelea gerezani.

    “Hapana mwanangu usiseme maneno hayo!”

    “Siyo hivyo mama siwezi kunyongwa bila kosa naomba mkiniletea chakula  kesho niwekeeni kichupa cha dawa ya kunguni katikati ya ugali ili nife!Nataka kufa mama nimeteseka kwa muda mrefu sana!”

    “Siwezi kufanya hivyo mwanangu kama Mungu anachukua maisha yako acha ayachukue lakini hata siku moja siwezi kukuua  ni mimi niliyekuzaa!”

    Reginald alikuwa mtoto pekee wa bibi Magreth Lyimo, mwalimu wa shule ya msingi mstaafu! Alikuwa ndiye mtoto wake wa kwanza na ndiye alikuwa tegemeo lake! Mume wake alifariki miaka mingi kabla na kumwachia watoto watatu, Reginald aliyekuwa mtoto wa kwanza wakati huo akiwa darasa la saba, Judith na mdogo wao wa mwisho Neria.

    Mama yake alimsomesha Reginald kwa pesa za mshahara  wa ualimu na biashara ndogondogo hadi akamaliza chuo kikuu! Watoto wake wengine, Judith na Neria walipata mimba kabla ya  kuolewa na kuzaa nyumbani, waliishi  na watoto wao  nyumbani na hawakuwa na kazi.

    Hivyo tegemeo pekee la mama huyo lilikuwa ni Reginald! Kutiwa kwake mahabusu kulimfanya mama huyo akonde kwa mawazo, maisha yake yalibadilika na kuwa mabaya kupita kiasi, alianza hata kulala na njaa jambo alilolisahau kwa muda mrefu.

    Alilazimika kuuza nyumba zote za Reginald ili kuigharimia kesi, lakini bado hazikutosha, akatumia  pesa zote zilizokuwa katika benki nazo zikamalizika bila kesi kwisha ikabidi auze na nyumba ambayo Reginald alimnunulia na kwenda kupanga katika chumba kimoja eneo la Buguruni na binti zake. Alimpenda mno Reginald   alikuwa tayari kufanya lolote kumsaidia na siku zote aliamini mtoto wake hakufanya ukatili huo!

    “Reginald! Hawezi kuua, hii ni njama!” Hayo ndiyo yalikuwa maneno yake kila siku.

              ****************

    Kilikuwa ni kikao kingine kati ya madaktari, profesa John Kadiri na mkewe Dk. Cynthia. Madaktari wakijaribu kuwaelewesha wazazi ni kwanini mtoto wao alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wote huo!

    “Your daughter brain is damaged severely on top of that there is a  wave  of electric impulses  being discharged from the traumatized brain and make muscles contract between  26th up to 28th of every month, up this moment  we dont know why is this happening!  It makes her  condition worse, we have used a lot of anticonvulsives but  still no improvement!”(Ubongo wa binti yenu umeharibiwa vibaya sana na zaidi ya hayo kuna wimbi la umeme mwingine unatolewa katika ubongo ulioharibiwa kila tarehe 26-28 ya kila mwezi na kufanya misuli kukakamaa, tumeshindwa kuelewa hii ni kwanini? Tumempatia dawa za kuzuia degedege lakini hazisaidia!) daktari  alisema huku akimwangalia Dk. Cynthia usoni.

    “Is your daughter Epileptic?”(Mtoto wako ana kifafa?)

    “Yes she is!”(Ndiyo!)

    “Oh my God! Why didn’t you give us that history from the beginning?”(Oh Mungu wangu kwanini haukutupa historia hiyo kutoka mwanzo?)

    “We are sorry!”(Tusameheni sana!)

    “Kwa hiyo ni lazima tubadilishe dawa?”

    “Itakuwa vizuri sana!”

    “Tutamweka kwenye Amylobarbitone,pamoja na Niazepam nafikiri zitamsaidia!

    “Fanya lolote daktari maisha ya mtoto wetu yapo mikononi mwako!”

    Caroline alianzishiwa dawa hizo na alipozitumia kwa siku mbili tu hali yake ilianza kubadilika na kuwa nzuri, wiki mbili baadye alizinduka kutoka katika hali ya kupoteza fahamu, kila mtu alifurahi lakini hakuwa na uwezo wa kusema chochote, alikuwa ni kama bubu na hakuwa na kumbukumbu yoyote juu ya maisha yake  ya nyuma wala hakuelewa kuwa alilala kitandani hapo kwa miaka miwili na miezi mitatu!

    “Hii hali niliitegemea kabisa!” Daktari alisema.

    “ Kwa hiyo hataongea tena?”

    “Hapana inawezekana akaongea baadaye lakini mpaka afundishwe kuongea, hivi sasa huyu ni kama mtoto itabidi afundishwe kufanya kila kitu, ubongo wake umefuta kumbukumbu zake zote!”Alisema daktari lakini kwa profesa Kadiri na Cynthia   ilikuwa furaha kubwa kuona mtoto wao akiwa hai tena, hawakujali alikuwa bubu, kipofu wala kiziwi walichotaka ni Caroline tu.

    Taarifa za kuzinduka kwa Caroline usingizini zilimfikia Reginald mahabusu, alifurahi kupita kiasi kwani alijua ni yeye pekee ndiye angeweza kumtoa gerezani   sheria ya Tanzania  haikuwa na uwezo wa kumtendea haki kwani haikuwa na uwezo wa kupeleleza kesi hiyo na kuugundua ukweli.

    Furaha yake ilipotea alipoambiwa kuwa pamoja na kuwa kuzinduka Caroline hakuwa na uwezo wa kuongea neno lolote na hakuwa na kumbukumbu yoyote juu ya maisha ya nyuma! Ubongo wake uliumia sana na kupoteza kumbukumbu zake zote.

    Ilikuwa imebaki miezi miwili tu hukumu yake  ya kesi ya kubaka itolewe na ilionekana wazi angefungwa maisha sababu ushahidi wa cheti cha daktari uliokuwepo ulionyesha kweli Caroline alibakwa, ingawa cheti hakikuonyesha mbegu zilikuwa za nani.

    “Watanzania wengi sana wamefungwa kwa makosa ya kubaka bila hatia! Ee Mungu wangu mpe Caroline kumbukumbu zake ili aniokoe katika janga hili!” Alisema Reginald katika maombi yake kwa Mungu aliyoyafanya usiku kucha!

    Miezi miwili baadaye:

    “Kesi ya kubaka namba 204 ya mwaka huu mshtakiwa ni Reginald Lyimo tafadhali simama!”

    Ilikuwa ni sauti ya hakimu iliyosikiwa na mamia ya watu waliofurika ndani na nje ya  mahakama kusikiliza hukumu ya Reginald kila mtu alijua Reginald angehukumiwa kifungo cha maisha kwa kesi hiyo, Reginald alisimama kizimbani akiwa na pingu mikononi.

    Baada ya  Hakimu kusema maneno hayo  aliendelea kusoma maelezo ya kesi hiyo tangu  ianze, Reginald alisimama kizimbani  akilia machozi, alipowaangalia mama na dada zake  nao pia walikuwa wakilia machozi ya uchungu, Reginald aliomba Mungu  mambo  yawe ndoto.

    “Una la kujitetea kabla sijakuhukumu?”

    “Ndiyo Hakimu!”

    “Haya jitetee!”

    “Unayemwona hapo pembeni akilia ni mama yangu na wale wawili ni dada zangu nihurumie Hakimu  kwani wote wananitegemea mimi isitoshe mimi sikumbaka Caroline, nilikuwa nikimuokoa kutoka kwa mtu aliyetaka kumuua kwa kumgonga  kwa  gari ila ni vigumu kuthibitisha kama Caroline mwenyewe angekuwepo hapa angesema ukweli!”

    Hakimu alikuwa akimwangalia Reginald kwa jicho la hasira, alimwona muuaji na mbakaji na wala hakuyatilia maanani maneno yake.

    “Nooooooo! Mheshimiwa Hakimu hapanaaa! Haiwezekani!” Ilikuwa ni sauti ya msichana ikiongea kutoka kwenye lango la kuingilia mahakamani, msichana mmoja alikuwa akiingia mahakamani akiwa ameshikwa na watu wawili! Watu wote mahakamani waligeuka kumwangalia msichana huyo, alikuwa na bendeji nyingi usoni na alitembea kwa magongo.

    Je nini kitaendelea? Nani  kaingia mahakamani? Je, Reginald alinusuruka na adhabu ya kifungo cha maisha? Fuatilia wiki ijayo !













    Sehemu ya 9

    No!No!No! Haiwezekani mheshimiwa jaji huo utakuwa uonevu na ni heri fahamu zimenirudia mngeua mtu asiye na hatia!”Alisema msichana huyo akizidi kutembea kwenda katikati ya ukumbi wa Mahakama!

    Watu wote waligeuka kuangalia nyuma alikokuwa akitokea, kwa mbali wengi hawakumfahamu na hata Reginald mwenyewe hakumtambua mara moja kuwa msichana huyo alikuwa Caroline.

    Alimpomfikia Reginald, Caroline alimwita kwa jina na Reginald alipoangalia kwa makini macho yake yalitua moja kwa moja usoni kwa msichana  huyo na ingawa uso wake ulikuwa umefungwa na bendeji nyingi aliweza kumtambua.

    “Oh! Caroline ni wewe?”Aliuliza Reginald bila kuyaamini macho yake.

    “Ni mimi Reginald nimekuja kukusaidia baada ya kusikia mateso yako nimekuja kusema ukweli sababu najua wanataka kukuua kwa kosa ambalo hukulifanya! Caroline alisema kwa sauti, baba yake aliyekuwepo mahakamani alishangazwa sana na hali hiyo, alishindwa kuelewa, Caroline alitoka vipi hospitali ingawa alikuwa na uhakika fahamu zilishamrejea.

    “Nisaidie caroline wanataka kunihukumu kifo eti nilikubaka na kukupeleka porini kwa lengo la kukuua! Eti kweli nilifanya hivyo Caroline?”

    “Sio kweli! Bila wewe mimi ningekuwa marehemu!”

    Mahakama yote ilikuwa kimya hakimu alijua wazi kuwa Caroline alivunja utaratibu wa mahakama lakini alilazimika kunyamaza kwa sababu mguso alioupata kutokana na maneno ya caroline.

    Wote wawili walikumbatiana na kupigana mabusu mfululizo usoni, yote hiyo ilikuwa ni furaha walionekana  kama wapenzi, ingawa katika maisha yao hawakuwahi kuishi pamoja kwa hata masaa matatu.

    Jaji aliwaacha wafanye walichotaka kwa sababu alijua kesi ilikuwa imefika mwisho wake, asingeweza kumfunga Reginald wakati mtu aliyedaiwa kufanyiwa unyama alikuwa akimtetea, alishangazwa sana na kilichotokea na hakutegemea caroline angeweza kufika mahakamani siku hiyo, ulikuwa ni kama muujiza.

    “Mheshimiwa Jaji!” Caroline aliita.

    “Naitwa Caroline! Mimi ninayediwa kubakwa katika kesi hii lakini ukweli wa mambo ninao mimi! Mheshimiwa Jaji Reginald hakunibaka wala si yeye aliyenipeleka porini bali ni Dickson yeye na mpenzi wangu Richard pamoja na msichana aitwaye Mariam Hassan waliniacha kwenye mashindano ya Miss Bongo ambako kwa bahati mbaya niliangu………!”

    Alishindwa kumalizia sentensi yake kwa kuogopa kutaja kilichomuangusha mbele za watu lakini alieleza kila kitu kilichotokea na watu wote walikaa kimya wakimsikiliza yeye watu wengi akiwemo hakima walipigwa na butwaa na kushangazwa na habari alizozieleza Caroline, wengi walibadilisha misimamo yao na mtazamo waliokuwa nao juu ya Reginald.

    Hata baba yake Caroline mzee John Kadiri naye alijisikia mkosaji ndani ya nafsi yake kwa ktiendo chake cha kutaka kumuua kwa sindano ya sumu kitandani wakati si yeye aliyemfanyia unyama mtoto wake, alimwonea huruma sana Reginald kwani aliteseka gerezani bure.

    “Mheshimiwa hakimu Reginald hana hatia hata kidogo na ningekushauri umwachie huru na kama kuna uwezekano Dickson asakwe huyo ndiye aliyenifanyia unyama mimi, huyu Reginald ni msamaraia mwema aliyeokoa maisha yangu!” Alimaliza Caroline.

    Minong’ono ya chinichini ilisikka mahakamani, Carolne alikuwa amefanya kazi yake ya kumuokoa Reginald kutoka katika mikono ya kifo tena zikiwa ni dakika chache kabla ya hukumu! Kila mtu alimwona Reginald ni mtu mwenye bahati kubwa maishani mwake na kama caroline asingefika  mahakamani siku hiyo ni lazima angehukumiwa kifo!

    “Kwa sababu ya maelezo ya msichana huyo sina sababu ya kumhukumu kijana huyu na kulirudisha suala hili polisi ili Dickson asakwe kwa udi na uvumba na kufikishwa mbele ya sheria tangu sasa Reginald upo huru!”

    Reginald hakuyaamini macho wala masikio yake na alijikuta akilia machozi ya furaha na alimsogelea caroline walikumbatiana tena, mama na dada zake nao waliungana pamoja nao na kukumbatiana! Siku za huzini ilibadilika kuwa siku ya furaha kubwa kwao! Hakuna aliyekuwa tayari kuamini hatimaye Reginald alikuwa huru.

    “Pole sana Reginald kwa yaliyokupata hii  yote ni kwa sababu mimi sikuwepo, kuelezea ukweli huu!” caroline  alisema wakati yeye na Reginald wakitoka nje ya mahakama ambako walialikwa na ndugu jamaa na marafiki wengi kwa furaha kubwa! Nje ya uwanja wa mahakama palibadilika na kuwa sehemu ya chereko na nderemo kufuatia hukumu hiyo.

    “Pole sana kijana nafikiri utanisamehe hata mimi sikujua kwani si wewe uliyemfanyia ukatili mwanangu, nitaandaa sherehe jioni ili tuongee vizuri zaidi nafikiri utahudhuria!”

    “Sina kinyongo mzee hata mimi nitapenda kukutana na  wewe!”

    Waliondoka mahakamani ndani ya magari yao kuelekea majumbani, Reginald aliondoka na mama pamoja na dada zake ndani ya gari la mmoja wa ndugu zake caroline, caroline aliondoka na baba yake, kwa teksi waliyokodi na jioni ya siku hiyo familia zote zilikutana katika hoteli ya continental ambako baba yake caroline pamoja na shangazi yake walifanya hafla walimwomba msamaha Reginald kwa yaliyotomtokea kwa sababu ya binti yao, caroline alimwonea huruma sana Reginald kwa yaliyompta, hasa kitendo cha kupoteza mguu kwa ajili yake alipopigwa risasi  na polisi porini akijaribu kumwokoa.

    Wakati wa sherehe hiyoiliyohudhuriwa pia na marafiki wengi Reginald na caroline waliongea mambo mengi kuhusu maisha yao Reginald alijaribu kumshawishi caroline kuwa yaliyotokea akubali kuwa mpenzi wake na ikiwezekana awe mke wake kabisa kwa sababu alipoteza mguu wake akijaribu kumuokoa.

    Pamoja na kuujua ukweli caroline alikataa katakata alikuwa tayari kufanya jambo lolote kufidia lakini si kuwa na uhusiano kimapenzi na mwanaume yeyote yule duniani! Aliwachukia wanaume kwani walimsababishia matatizo makubwa na kumliza mara nyingi, aliuahidi moyo wake kutokuwa na uhusiano wa mwanaume kimapenzi.

    “Haiwezekani Reginald ndio uliniokoa na ninashukuru sana uliniokoa lakini siwezi hata siku moja kuwa na uhusiano na mwanaume kimapenzi kwani wanaume wameniumiza mara nyingi sana!”

    “kwanini?”

    “Basi tu!”Alijibu caroline bado hakuwa tayari kuivujisha siri yake ya kifafa.

    “Tafadhali fikiria suala hili mara mbili na ukumbuke mimi nimeharibu maisha yangu kwa sababu yako hata kama wengine walikuumiza mimi nitakupa furaha!” alisema Reginald akimshika caroline began.

    “Kwani nilikumwambia baba yangu akulipe fidia itakuwa vibaya?”

    “Sitaki kitu kingine zaidi yako caroline!”

    “Hiyo haiwezekani kabisa Reginald, siwapendi wanaume na ningeomba tuongee mambo mengine vinginevyo itakuwa bai tena!” Alisema caroline akionyesha kuchukizwa na suala hilo na mawazo yake yalipompeleka kwa Richard, Harry na Dickson chuki yake dhidi ya wanaume iliongezeka maradufu!

    “Wanaume ! Wanaume ni wanyama sana sitaki hata kuwasikia!”Alisema kwa sauti caroline.

    “Kwanini?”

    “Basi tu!”

    Usiku wa manane shereha ilikwisha na waliachana kurejea majumbani mwao usiku wa siku hiyo katika usingizi caroline aliota ndoto akitembea na Reginald ufukweni wakiwa wamekumbatiana na kupigana mabusu lakini ghafla alitokea msichana mwingine na Reginald alimwacha caroline akilia na kuondoka na msichana huyo!

    “Hii ndoto gani tena? Huyu naye ni wale wale tu!” aliwaza caroline huku akitetemeka kwa hofu!?



    Baada ya hapo waliendelea kuonana mara kwa mara na miezi michache baadaye Reginald alirudishwa kazini baada ya kutengenezewa mguu mzuri wa bandia ambao haikuwa rahisi hata kidogo kugundua alikuwa na kilema, aliendesha gari kama kawaida! Kituo chake cha kazi kilibadilishwa na kuhamishiwa jijini Dar es Salaam.

    Hivyo walionana karibu kila siku na uhusiano wao ulizidi kukomaa kila siku iliyokwenda kwa Mungu! Lakini bado kifafa kiliendelea kumsumbua kila ilipofika tarehe yake ilikuwa ni lazima aanguke, kwa kuogopa aibu wazazi wake waliamua kumtafutia chuo nje ya nchi ingawa alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam.





    Caroline alijiunga na chuo kikuu cha Ottawa, siku ya kuiaga Tanzania alisindikizwa uwanja wa ndege na wazazi wake pamoja na Reginald wote wawli walilia wakati wakiagana, ilikuwa si rahisi kuamini walikuwa wakitenganishwa na elimu!

    Alikuwa akienda nchini Canada  kwa masom ya miaka mitatu katika Sayansi ya kompyuta na baada ya hapo alitegemea kuongeza elimu ya utawala hivyo alitegemewa kuishi nchini Canada kwa miaka isiyopungua minne!

    Alishukuru kuondoka Tanzania kwani kama angebaki hata kwa mwezi mmoja lazima angekuwa hatarini, uzalendo ulishaanza kumshinda juu ya Reginald siku zote kijana huyo hakukata tamaa kumshawishi akubali kuwa mpenzi wake!

    “Nakwenda Reginald nakushuruku sana kwa kampani yako!”

    “Usinisahau caroline bado nakupenda na nitakupenda siku zote!”

    “Ahsante Reginald!”

    Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa Reginald na ilimchukua muda mrefu kuyaona maisha yakiwa kawaida bila caroline.





    Mwaka wa kwanza ulipita caroline akiwa Canada masomoni, na mawasiliano kati yao hayakukatika, waliandikiana barua pepe karibu kila siku na katika kila barua aliyoandika   reginadl hakuchoka kumweleza caroline wazi kuwa penzi lake lilikuwa bado motomoto na alimwomba ajitunze ili kama uwezekano ungekuwepo siku moja wafunge ndoa!?Uvumilivu wa Reginald hatimaye ulianza kumfanya caroline aliamini penzi lake, lakini kitu kimoja alikionea aibu nacho ni siri ya kifafa, jambo hilo lilimfanya  aogope kukubali ingawa alijisikia hoi katika mapenzi.

    Akiwa mwaka wa pili rafiki yake mmoja waliyelala naye chumba kimoja raia wa Uingereza, Careen aliligundua tatizo lake na kuamua kumtafutia msaada.

    “Ninamjua daktari ambaye amewatibu watu wengi sana hapa Canada, hata bibi yangu alikuwa na tatizo hili lakini hivi asa ni mzima!”

    Kweli?”

    “Ndiyo ukitaka nitakupeleka kwake!”

    Siku mbili baadaye msichana huyo alimpeleka caroline kwa daktari mmoja bingwa wa magonjwa ya akili na ubongo ambaye alimpa caroline dawa za kutumia miezi sita, baada ya matumizi ya miezi sita hali yake ilibadilika akawa anapitisha hata mwezi mzima bila kuanguka kifafa.

    Caroline alishangazwa na mabadiliko hayo ya afya yake akawa mtu wa furaha kubwa katika maisha yake kwani hakuwahi kutegemea katika maisha yake kuwa siku moja angepitisha hata mwezi mmoja bila kuanguka kifafa! Mabadiliko hayo yalimfanya aongeze bidii ya kuzitumia dawa hizo, hatimaye akawa anapitisha hata miezi mitatu bila kuanguka.

    “Thanks you Careen!”(Ahsante Careen!) alimshukuru rafiki yake baada ya mwaka mzima kupita bila kuanguka.

    Daktari alimwambia wazi kuwa katika maisha yake alitakiwa kunywa dawa hizo kila siku kwani kuacha kutumia dawea hizoiliyoitwa Centribarbitone, kwa siku saba kungemfanya siku ya nane aanguke tena!

    Alipomaliza masomo yake baada ya miaka minane alikumbuka kununua dawa ya kutosha kuja nazo Tanzania.

    Reginald alimtafutia kazi katika kampuni ya kompyuta ya network Africa, ambako aliajiriwa kama mtaalamu wa kompyuta na mkufunzi wa chuo kilichomilikiwa na shirika hilo! Uhusiano wake na Reginald ulizidi kukua na kukomaa! Caroline hakuwa na kipingamizi tena juu ya Reginald na kujikuta akifua mikononi mwake akawa mpenzi wake!

    “Usihofu caroline mimi sitakuumiza maishani mwako!”

    “Naamini Reginald nimekufanyia uchunguzi kweli unanipenda Reginald na ahsante sana kwa uaminifu wako!”

    “Nashauri tufunge ndoa caroline au unaonaje?”

    “Sina kipingamizi!”

    “Kweli?”?”Ndiyo!”





    Taarifa zilitolewa kwa wazazi wa pande zote mbili na mipango ya harusi ilifanywa kwa muda wa mwaka mzima, yalikuwa maandalizi mazito lengo likiwa ni kufanya harusi ambayo ingelitingisha jiji la Dar es Salaam.

    Mpaka wakati huo Reginald hakuelewa kitu chochote kuhusu kifafa cha mchumba wake na wala hakufahamu nini kilichomfanya awachukie wanaume kiasi hicho, caroline pia hakuwa tayari kutoboa siri hiyo.

    Siku nane kabla ya harusi yao caroline aligundua kuwa dawa zake zilikuwa zimekwisha alipiga simu  kwa daktari wake Canada akiomba atumiwe haraka iwezekanavyo maana bila dawa hizo lazima angeanguka siku ya harusi.

    “Harusi yetu itakuwa nzuri sana Reginald au siyo?”

    “Sana! Maaandalizi yake ni  ya nguvu!”Waliongea wakipita madukani kutafuta baadhi ya vitu kwa ajili ya harusi yao, ghafla walipokaribia kufika kwenye dula la SH Amon, waliona kundi la watu wamekusanyika ikabidi nao pia wasogee karibu kabisa ili kuona ni kitu gani kilitokea.

    “Kuna nini?”Reginald alimuuliza kijana mmoja.

    “Fika mwenyewe uone braza ni aibu !Kwini kafanya noma anatembea mtaani wakati anajua wazi mambo yake si safi!”

    “Kivipi?”

    “Fika uone mwenyewe braza!” Reginald na caroline walipenya katikati ya watu kwenda hadi mbele ili kuona ni kitu gani kilichokuwepo, walishangaa kukuta msichana mzuri akiwa amelala chini mapovu yakimtoka mdomoni.

    “Masikini msichana mzuri ana kifafa!” Reginald aliongea kwa sauti.

    Katika maisha yake ingawa caroline alikuwa na ugonjwa huo hakuwahi kumwona mtu aliyeanguka kifafa! Lilikuwa ni jambo la kusikitisha sana msichana mzuri alirusha mikono yake huku na kule akiuma meno yake, caroline aliogopa kuangalia na kuanza kumvuta Reginald ili waondoke.

    “Twende!”

    “Acha niangalie bwana!”

    “Sitaki tuondoke!”

    Reginald hakubisha sana walianza kuondoka pamoja kwenda dukani SH Amon kununua mavazi ya harusi pamoja na vipodozi.

    “Reginald  nikuulize swali?”

    “Uliza!”

    “Hivi ikitokea mpenzi wako akiwa na ugonjwa huu unaoweza kufanya kitu gani?”

    “Ha! Kifafa mimi mwanamke mwenye kifafa wa kazi gani!”

    Maneno hayo yalikuwa mkuki kwa caroline na alimwaga machozi mengi kupita kiasi, aliumia kugundua kuwa hata Reginald ipo siku angekuja kumwacha.

    “Mbona unalia?”

    “Ah!Ah! Ah! Ah! Basi tu!”

    “Basi tu nini?”

    Caroline hakujibu mawazo yalikuwe kwenye vidonge vyake alishindwa kuelewa kama vingewahi kabla ya siku saba!”

    “Kama dawa hizi hazitafika sijua nitafanya kitu gani? Nitaanguka siku  ya harusi!”Aliwaza caroline.

    Zikiwa zimebaki siku mbili alipopiga simu aliambiwa na daktari wake kuwa dawa zilitumwa siku nne kabla kutoka Canada alishangaa ni kwanini zilikuwa hazijafika mpaka siku hiyo!?Je nini kitaendelea? Dawa zitawahi? Fuatilia wiki ijayo

















    Siku mbili kabla ya harusi yao  ilikuwa  ni hekaheka tupu nyumbani kwa shangazi yake na Caroline Upanga, kila mtu alikuwa na furaha na maandalizi yalikuwa yakienda vizuri, wazazi wa Caroline walikuwepo jijini Dar es Salaam kwa wiki nzima kutoka Arusha kwa ajili ya  kuishuhudia harusi ya  mtoto wao pekee.

     Kilichowashangaza wengi siku tatu za mwisho  walionekana watu wasio na furaha kabisa  tofauti na  walivyotegemewa kuwa, jambo hilo liliwafanya watu wengi  kujiuliza maswali mengi.

    “Labda hawakutaka mtoto wao aolewe na mlemavu kama Reginald!”

    “Sasa hata kama hawakutaka watafanya nini wakati mtoto wao kampenda mlemavu? Isitoshe  nasikia Reginald alipigwa risasi  na kuvunjwa mfupa akimwokoa huyuhuyu Caroline alipotaka kuuawa  na jambazi porini  sasa wanataka aolewe na nani zaidi yake au upendo gani uzidi hapo?” yalikuwa ni maongezi ya baadhi ya majirani walioielewa vizuri historia ya Caroline na Reginald.

    Wazazi wa Caroline hawakuonekana na furaha hata kidogo pamoja na kuwa mtoto wao pekee alikuwa akiolewa!  Ni kweli hawakuwa na furaha na sababu ya jambo hilo haikuwa nyingine bali ni  hofu ya aibu  ambayo ingewapata baada ya  mtoto wao kuanguka kanisani wakati wa kufunga ndoa, hilo ndilo walilolitegemea baada ya Caroline kuwaeleza kuwa dawa zake zilikuwa zimekwisha.

    Walishindwa kuelewa nini kingefanyika kuzuia jambo hilo lisitokee walichanganyikiwa na matumaini yao yote yalikuwa ni kwa  mzigo wa dawa aliokuwa umetumwa na Dk. Ian, daktari wa   wa Caroline kutoka Canada,waliamini bila dawa hiyo Caroline angeanguka na ingekuwa aibu, hilo ndilo lililowatia hofu zaidi.

    Si peke yao waliokuwa na hofu hiyo, Caroline ndio aligubikwa na wasiwasi zaidi yao,hakuelewa ni kitu gani angefanya ili kujiepusha aibu iliyokuwa mbele yake!  Suluhu peke yake ilikuwa ni dawa lakini alishindwa kuelewa zilikwama wapi! Kadri masaa yalivyozidi kujivuta kwa kasi ndivyo wasiwasi wake ulivyozidi kupanda alihisi angepatwa na presha na kufa! Alikuwa tayari kwa hilo lakini si kuanguka kanisani mbele ya Reginald kwa kifafa.

    “Mama kwanini msimwambie mama yake na Reginald  tuahirishe harusi hii?”

    “Tumejaribu hivyo, yeye alikuwa tayari kukubali lakini wajomba zake na Reginald walikataa kabisa wakidai wametumia pesa nyingi sana kujiandaa na  hawana muda wa kusubiri!”

    “Mliwaeleza ni kwanini mlikuwa mkiahirisha harusi?”

    “Ndiyo!”

    “Mlisemaje?”

    “Kuwa utakuwa katika hedhi!”

    “Ah! Mama hiyo tu  haitoshi ungewaambia nina ugonjwa mkubwa!”

    “Sasa tufanya nini?”

    “Kwa kweli kama dawa hazitafika  mimi sitakwenda kanisani kufunga ndoa hiyo kesho kutwa!”

    Suala la kifafa lilichukua furaha yote yake na ya wazazi wake yote,  walinyong’onyea kiasi cha kila mtu kugundua kulikuwa na tatizo mioyoni mwao ni shangazi yake  Caroline peke yake ndiye aliyejitahidi kuchangamka ili kuondoa aibu hiyo.

    Waalikwa wote walishajiandaa kwa ajili ya harusi   na gharama kubwa zilishatumika  hivyo haikuwa rahisi   kuihairisha, kila mtu alishapania  Reginald   aliona masaa yakienda taratibu kupita kiasi, kila mara   alimpigia Caroline simu na kuiongelea siku ya ndoa yao! Alionyesha furaha kubwa isiyo kifani lakini alishangazwa na hali ya kupotea kwa uchangamfu wa Caroline kadri siku ya ndoa yao ilivyozidi kukaribia!

    “Caroline una tatizo nini?”

    “Mimi?”

    “Wewe ndiyo kwani naongea na nani?”

    “Sina tatizo lolote!”

    “Sasa kwanini uko hivyo?”

    “Basi tu ndoa inanitia hofu!” Caroline alijitahidi kadri ya uwezo wake kutomwonyesha Reginald kuwa alikuwa na tatizo lililomsumbua moyoni mwake, hakutaka kabisa aelewe kuwa alikuwa na kifafa! Hiyo ilikuwa ni siri ya kufa nayo moyoni mwake.

                 **************

    Yakiwa yamebaki masaa ishirni na nne ili ndoa yao ifungwe   Reginald alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu na  mtu huyo hakutaka kabisa  kutaja jina lake,alidai yeye na Caroline walisoma shule moja mjini Arusha! Alichokisema katika simu hiyo kilimtia Reginald simanzi kubwa moyoni mwake na hakikuwa kitu rahisi kwake kukiamini.

    “Kaka Reginald pole sana!”

    “Kwanini?Maandalizi ya harusi?”

    “Hapana pole kwa sababu unaoa kifafa!”

    “Ninaoa kifafa? Una maana gani kusema hivyo kwanza wewe ni nani?”

    “Hakuna haja ya kunijua jina ila nataka tu kukueleza kuwa Caroline ni mgonjwa wa kifafa na huanguka kati ya tarehe 26na 28 ya kila mwezi! Mimi nilisoma  na ni kifafa ndicho kilichomfanya aachwe na mpenzi wake wa kwanza, Harry alipoanguka siku ya sikukuu yake ya kuzaliwa na nimesikia pia aliachwa na Richard kijana aliyeko gerezani  alipoanguka siku ya Miss Bongo! Wewe kweli hujui? Au unapenda kifafa? Basi oa!” Baada ya maneno hayo tu simu ilikatika.

    Reginald hakuridhika na maneno hayo kwani katika maisha yake hakuwahi hata mara moja kumwona Caroline ameanguka kifafa! Na hata hiyo tarehe 26  na 28 alikuwa naye lakini hakuanguka.

     Alichukua kalamu na karatasi na kuanza  kunakili namba hizo kwenye karatasi,  bila kuchelewa  aliipiga tena namba hiyo kwa kutumia simu yake ya mkononi lakini haikupokelewa wala kuingia,aliendelea kuipiga kwa muda mrefu lakini jibu liliendelea kuwa hilo hilo kuwa ilikuwa haipatikani!

     Reginald alishindwa kuelewa asimame wapi, upande mmoja wa akili yake ulimwambia adharau lakini mwingine ulitaka ahakikishe! Alitaka kufahamu zaidi juu ya habari hiyo, ni kweli maneno hayo yalimuumiza sana moyo wake, hakuna kitu alichokiogopa maishani mwake kama ugonjwa wa kifafa na Ukoma!

    Kumbukumbu zilimiminika   kichwani akajikuta akiikumbuka siku yeye na Caroline walipomwona msichana aliyeanguka kifafa maeneo ya posta jijini! Alilikumbuka swali la Caroline akimuuliza kama ingetokea msichana wake  akawa na kifafa angefanya kitu gani.

    “Alibadilika sana nilipomjibu kuwa siwezi kuwa na msichana mwenye kifafa! Na alilia  machozi, tangu jibu hilo alikosa raha kabisa nafikiri suala hili lina ukweli fulani ndani yake,si vyema kulipuuzia ni lazima nikamuulize Caroline upesi na kama ni kweli nitaachana naye leo hii hii! Sitajali gharama kubwa kiasi gani itapatikana!”Aliwaza Reginald.

    Aliondoka kuelekea nyumbani kwa shangazi yake na Caroline upanga lakini kabla ya kufika aliamua kupita nyumbani kwao ambako alimweleza mama yake juu ya taarifa  ya simu aliyoipokea.

    Mama yake hakusikitika  wala kushtushwa na habari hiyo, ilionekana si ngeni kwake.

    “Mh! Reginald wewe ndio umesikia leo mwanangu?”

    ‘Ndiyo mama!”

    “Mbona sisi tunafahamu na tulifikiri hata wewe unaelewa!”

    “Hapana mama sasa kwanini hamkuniambia?”

    “Tulifikiri unalifahamu jambo hilo!”

    “Kama ni hivyo hakuna ndoa mama!  Hebu ngoja niende kwanza nyumbani kwao nikamuulize Caroline mwenyewe!”Alisema Reginald na kutoka nje ambako aliingia ndani ya gari lake na kuanza kuendesha kwa kasi kuelekea Upanga.

    Alipofika alishangazwa na umati mkubwa alioukuta mahali pale! Kulikuwa na shamshashara ya kila namna, aliwaona kama walikuwa wakipoteza muda wao  kuimba na kuchambua mchele wakati hapakuwa na ndoa tena.

    Alipobisha hodi mlango ulifunguliwa na  shangazi yake Caroline, aliingia hadi  sebuleni ambako aliwakuta baba na mama yake Caroline na kuwaamkia, alishangazwa na muonekano wa nyuso zao! Walionekana kama wakosaji na macho yao yalijaa aibu!

    Baada ya salamu alipelekwa moja kwa moja hadi chumbani  kwa Caroline, kitu cha kwanza alichogundua Caroline baada ya kumwona  Reginald ni wekundu wa macho na  alijua kulikuwa na tatizo, hakuwahi kumwona Reginald katika sura hiyo tangu amfahamu!

    “Reginald vipi?”

    “Vipi nini? Kwanini umeamua kunitia hasara kiasi hiki Caroline?”

    “Hasara gani? Reginald mbona sikuelewi?”

    “Ulijua kabisa una kifafa na hukuniambia kwanini lakini?”

    Sentensi hiyo iliufanya moyo  wa Caroline kufa ganzi, alishindwa kuelewa ni nani hasa aliyemwambia Reginald juu ya habari ya siri hiyo, aliinamisha uso wake kwa aibu na kuanza kulia machozi, hakusema kitu mpaka dakika kumi baadaye  Reginald alipotaka kufahamu ukweli.

    “Caro tafadhali niambie ukweli kumbuka harusi ni kesho! Je kweli una kifafa?”

    Caroline alifikiria kumwambia Reginald ukweli lakini alishindwa kufanya hivyo sababu  alijua kufanya hivyo kungemaanisha kuachwa na mwanaume kwa mara ya tatu maishani mwake sababu ya ugonjwa, alimpenda sana Reginald na hakutaka kutengana naye!

    Alibubujikwa na machozi mengi na kilio chake kilifika hadi sebuleni, mama na shangazi yake  walikwenda hadi chumbani kutaka kujua kilichotokea.

    “Vipi tena watoto mbona mnalia?”

    “Mama!”

    “Naam!”

    “Samahani naomba mtupe nafasi tuna maongezi kidogo!”Reginald alitamka akimwambia mama yake Caroline na  bila kugoma mama aliyaheshimu maamuzi yao na wote wawili walitoka nje kutoa nafasi kwa  watoto kuongea juu ya suala walilokuwa nalo!

    “Caroline tafadhali nieleze ukweli juu ya jambo hili nahitaji kufahamu!”

    “Watu hawapendi mimi na wewe tuoane Reginald!Kweli  umeamua kuwasikiliza!”

    “Ina maana ni uongo?”

    “Ndiyo!Mimi sina kifafa Reginald ni maneno ya watu, ingekuwa hivyo katika muda wote huo si ningeshaanguka?”

    Reginald alikaa kimya na kutafakari kwa muda wa kama dakika tano, hatimaye alifikia uamuzi wa kuyaona maneno yote aliyoyasikia kuwa ni majungu ya watu wasiopenda yeye aoe msichana mzuri kama Caroline!

    Alimkumbatia  na kumwomba msamaha, alimpiga mabusu usoni na Caroline aliyajibu huku akitabasamu! Kwa Reginald yakawa yamekwisha lakini kichwani kwa Caroline yaliendelea kumsumbua kwa sababu alijua wazi alikuwa na ugonjwa huo na hakuwa na dawa ya kuzuia kifafa kisimtokee siku iliyofuata ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho kuishi bila dawa za kuzuia asianguke. Ndani ya moyo wake bado aliujua ukweli kuwa  bila dawa ni lazima angeaibika tu!

     Mpaka jioni ya siku  ya Ijumaa bado mzigo wake wa dawa ulikuwa haujafika, ilibidi apige tena simu Canada kwa daktari wake kumuulizia mahali dawa zilipokuwa, safari hii alimweleza  kitu kilichotarajiwa kutokea bila kumficha  kuwa hakutaka   mchumba wake afahamu kuwa alikuwa mgonjwa!

    “Once he knows that I have got epilepsy, he wont marry me doctor please help me?”(Kama akijua tu nina kifafa hatanioa, tafadhali daktari nisaidie)

    “So?”(Sasa?)

    “Serve my life doctor!”(Okoa maisha yangu daktari) alisema Caroline huku akilia katika simu alijua msaada pekee alikuwa ni Dk. Ian.

    “It takes 14 hours flying from  Ottawa to Dar es Saalam will I be there before your wedding!”(Huchukua masaa 14 kuruka  kwa ndege kutoka hapa Ottawa hadi Dar es Salaam nitawahi kabla ya harusi yako?)http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yes sir!”(Ndiyo bwana!)

    “Will you pay for my tickets?”(Utalipia tiketi zangu?)

    “Sure!Just make me escape this shame!”(Hakika, niepushe tu na aibu hii)

    “I will be there tomorrow around 10:30, because I will be leaving  tonight!(Nitakuwa hapa kesho kwani nitaondoka leo usiku!)

    “Thank you I will appreciate you!’(Ahsante, nitashukuru sana daktari)

    Jibu hilo  lilimrudisha matumaini Caroline   moyo wake ulitulia kiasi cha kutosha na hata alipowapa wazazi wake taarifa hiyo  kila mmoja alirejewa na furaha yake na pilikapilika za maandalizi ya mwisho ya harusi ziliendelea.

    Baadaye alipata taarifa kuwa   ndege  aliyotumia Dk.Ian kusafirishia dawa zake kutoak Canada ilipata matatizo ya kiufundi ikiwa angani na kulipuka! Iliua abiria wote 241 waliokuwa katika ndege hiyo.

     Caroline alisikitika sana lakini kitu alichomsikitisha zaidi kilikuwa ni dawa yake, hata hivyo ahadi  kuwa daktari angefika siku iliyofuata ilimfanya ajisikie vizuri.

    “Bila daktari kuja nilikuwa naaibika!” Alimwambia mama yake.

               *****************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog