Search This Blog

Friday, 28 October 2022

ASKARI JELA - 5

 









    Simulizi : Askari Jela

    Sehemu Ya Tano (5)





    Maisha ya Inspekta James baada ya mazishi yalikuwa ni wa kuwekwa ndani akilelewa kama mtoto, SP mwambe alikuwa ameajiri wafanyakazi waliokuwa wakimuhudumia kwa gharama kubwa. Alikuwa akiendelea kumfanyia mipango ya kumpata Daktari ambaye angeweza kumpatia tiba, alihangika kwenye hospitali tofauti kila alipopata muda ilmradi tu James aweze kupona na arudi kwenye hali ya kawaida. Hakufanikiwa katika kipindi hicho alichokuwa akihangaika lakini hakukata tamaa naye, upendo aliokuwa naye kwa kijana huyo ambaye alikuwa akimheshimu kama baba yake mzazi. Ulimfanya asichoke kumuhudumia wala kutafuata matabibu tofauti, alikuwa akifanya kazi na kila muda wa kupumzika alikuwa akihangaika naye. Baada ya kuona tiba za hospitalini zilikuwa zikishindikana, alidiriki hata kwenda kwa waganga wa kienyeji ilimradi mwanae wa kumlea aweze kuwa sawa. Waganga wa kienyeji ambao hawakuwa wakiweza kulitibu tatizo hilo nao walijua kuila pesa kwa kumdanganya mambo mbalimbali, alijikuta akimaliza pesa kwa waganga na hatimaye akajikatia tamsa. Marafiki wakubwa wa Inspekta James ambao ni Norbert Kaila pamoja na ASP Wilfred nao hawakuchoka kabisa kuja kumuona rafiki yao, walikuwa wakimtia moyo sana SP MWambe juu ya hali ambayo alikuwa nayo kijana wake. Hawa nao walifanya hata asichoke kumlea kijana wake, alikuwa nao bega kwa bega pale ambapo panahitajika msaada wowote ule kutoka kwao. Nao walisaidia katika kumtafutia wataalamu mbalimbali,wote walikuwa wakihitajia kumuona rafiki yao akirudiwa na hali ya kawaida.



    ****



    Upande wa Inspekta Jane hali ilikuwa ni mbaya zaidi hadi ikafikia hatua ya kufungwa kamba, alishawahi kutoroka zaidi ya mara moja akiwa yu katika hali ya kurukwa na akili. Pia alishajaribu kufanya jaribio la kujiua baada ya kushika kisu pindi alipovamia jikoni, alikuwa akitunzwa kwa jicho la umakini sana. Baba yake naye alikuwa amepewa mapumziko kutokna na hali ambayo alikuwa nayo huku akiendelea na matibabu, wote wawili walikuwa ni watu wenye kuhudumiwa kila muda. Mtu pekee ambaye alikuwa akiweza kwenda kuendelea na majukumu alikuwa ni mtoto mkubwa familia hiyo, ilikuwa ni familia ambayo ilitawaliwa na ukimya mkubwa sana kutokana na huzuni ambayo walikuwa wanayo. Furaha ile ambayo ilikuwa ipo hapo awali ilitoweka kabisa, ukimya ndiyo ulikuwepo katika kipindi chote. Ulipita mwaka hali ikiwa ni hiyohiyo huku Mzee Lutonja akiwa ameanza kutembea lakini kwa shida sana, Binti naye ukichaa ndiyo ulikuwa umemkomaa kabisa. Hawakuweza kukaa naye hapo ndani ya nyumba hiyo kwa balaa alilokuwa akilileta, ilibidi apelekwe kwenye hospitali maalum ya kutunza watu wenye ulemavu wa akili.







    Ndani ya mwaka huo mpya SP Mwambe aliweza kupandishwa cheo akawa Mrakibu mwandamizi wa jeshi la magereza(SSP), mwaka huohuo pia ikiwa imetimia mwaka mmoja tangu Inspekta James arukwe na akili. Norbert alipendekeza apelekwe barani Ulaya ambapo kulikuwa kulikuwa na mtaalamu ambaye angemtibu, gharama zake zilikuwa kubwa lakini kutokana na wote kumuhitaji aweze kupona walichanga na kikapatikana kiasi ambacho kilisaidia kusamfirsha hadi huko. Alikaa huko kwa nusu mwaka akiwa ameongozana na Norbert, hatimaye aliweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida taratibu. Alipopona kabisa aliruhusiwa kurudi nyumbani Tanzania akiwa na rafiki ambaye alimpa shukrani kubwa sana, uwanja wa ndege alipokewa na watu wake wa karibu na kisha alipelekwa hadi nyumbani kwa Baba yake mlezi. Ilikuwa ni siku ambayo ilikuwa ya furaha sana kupona kwake, jioni ya siku hiyo walifanya tafrija fupi katika kumkaribisha tena kwa mara nyingine nyumbani. Tafrija ambayo bado Inspekta James aliona mapungufu yaliyokuwa yapo, hakuwa amezoea kufurahia ndani ya nyumba hiyo ila uwepo wa Sara na Mama yake. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza na alijitahidi sana kuikabili hali hiyo ingawa ilikuwa ni jambo ambalo gumu sana kwake, watu wachache wa karibu waliokuwa wana faraja kwa kupona kwake ndiyo walihudhuria tafrija hiyo. Inspekta James aliweza kuwaona Maafisa wenzake wakiwa wapo kwenye nguo za kiraia ndani ya tafrija hiyo, wale waliokuwa wapo karibu na Marehemu Sara nao aliwaona pia. Faraja iliingia ndani ya moyo wake kwa kuwaona wakiwa wamefurahi kwa yeye kupona, alijumuika nao kwa pamoja katika kuifurahia siku hiyo.

    "Kikubwa ni kumshukuru Mungu kwani yeye ndiyo kila kitu ndani ya dunia hii, bila yeye nisingeweza kurudi katika uzima huu. Kaniacha na kidonda kikubwa sana lakini sipaswi kuilaumu kazi yake. Watu niliowapenda kawachukua kwa awamu lakini bado ninapswa kumshukuru kwani ameweza kunifanya niwe na pumzi hadi muda huu, amenilinda panapo hatari. Napaswa ni mshukuru. Pia nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nikimsahau Baba hapa, Norbert na Wifred kwa kuchngia niweze kurudi katika hali ya kawaida. Hakika bil ya juhudi zao hawa nisingeweza kuwa mzima hadi leo hii, napenda nitamke kuwa ninawapenda sana" Inspekta James aliongea katika tafrija hiyo alipopewa nafasi ya kusema chochote, makofi yalipigwa baada ya kumaliza kutoa machache na kisha watu wakaendelea kufurahia.

    Siku iliyofuata habari kubwa iliyokuwa imetawala magazeti ilikuwa ni kupona kwa Inspekta James, kila gazeti lilikuwa na habari hiyo ingawa aikueleweka walikuwa wameipata vipi kutokana na jambo hilo kuwa ni siri kwa watu wa karibu waliokuwa wakitambua ujio wake nchini akitokea Ulaya. Siku iliyofuata ilikuwa ni muda wa kumiminika kwa watu ndani ya nyumba ya SSP Mwambe kuja kumuona huku waandishi wakitaka kumuona, hakuna ambaye alikuwa hajasahau tukio lilimkuta na wengi wao walikuja kumpa pole hapo nyumbani. Usumbufu wa wanahabari ulizidi na hatimaye wakaamua kuwazuia ili James aweze kupumzika kabla hajaripoti ofisini, hakuna ambaye alikuwa akimtakia mema hakufurahishwa na habari hii ya kurudi kwake katika hali ya kawaida. Siku zilisogea hatimaye alikuja kuripoti kazini baada ya kuwa nje kwa muda mrefu sana, ilikuwa ni kipindi ambacho kulikuwa na utawala wa Rais mpya nchini Tanzania ambaye alikuwa akiitwa Zuber Ameir. Kipindi hiki ndipo James alipobadilika na kuwa si yule wa awali hata marafiki aliyokuwa nao hapo ofisni walianza kumuogopa. Kumbukumbu ya kifo cha mke wake ndiyo ilimfanya awe hivyo, kila alipokua akivaa vazi lake la ofisini alijikuta akiwa anajichukia yeye mwenyewe akilitazama kwenye kioo. Alipoyaona mavazi ya wenzake ndiyo kabisa hakukuwa kuna maelewano, alikuwa akijaribu kujibu maongezi yao walipokuwa kikazi tu. Ucheshi wake aliokuwa nao hapo awali uliondoka kabisa, sura yenye hasira katika kila muda akiwa yupo ofisni ndiyo ilimtawala. Ule uzuri wake wa sura ulipotea kabisa kutokana na kuwa mwenye kukunja sura muda wote, alikuwa si Afande yule muelewa ambaye alikuwa amezoeleka na wafungwa kama ilivyokuwa hapo awali.



    Kitendo cha kifo cha wazazi wake, mke wake na wale wote aliokuwa akiwapenda kusababishwa na nguo kama zake za kazi pamoja na nguo za wafungwa. Alianza kuwachukia wafungwa wote waliokuwa wapo humo ndani pamoja na maaskari wenzake,kazi alikuwa akizitekeleza kama kawaida lakini hakuwa na maelewano na Askari yeyote aliyekuwa yupo kwenye sare za kazi. Jambo hili lilikuwa tayari limeshagundulika kwa SSP Mwambe lakini alishindwa pa kuanzia kwenda naye hospitali kutokana na hali hiyo. Kipindi hiki ndipo marafiki zake wa karibu walipogombana kutokana na tuhuma ambayo alikuwa amebebeshwa mmoja, Norbert na Wilfred walikosana baada ya kuchapishwa tuhuma dhidi ya Wilfred. Taaluma ya uandishi aliyokuwa nayo Norbert ndiyo ilisababisha waweze kufarikiana, Inspekta James alikuwa akiongea nao kwa pamoja na hata alipojaribu kusuluhisha ilishindikana.

    Muda baada ya kazi katika kipindi cha kuwa mwenye kuwa na sura ya huzuni kila wakati, alikuwa akiutumia katika kucheza ngumi na mazoezi ya viungo. Hakuwahi kuwaza kuwa na Msichna yeyote yule katika maisha yake baada ya kuondokwa na mke wake, nyumbani kwake aliongeza vifaa vingi vya mazoezi. Hakuwa mtembeai kabisa kila alipokuwa nje ya kazi, yeye alikuwa ameelekeza nguvu katika mazoezi kila siku. Mwili wake ulijengeka na kuwa mkakamvu zaidi na wenye kukaa kimazoezi zaidi, alikuwa ni mwenye kifua kipana. Kimo kirefu ambacho alikuwa amerithi kutoka kwa baba yake kilimfanya azidi kuonekana ni mwenye mwili mkubwa, maisha yalikuwa yakiendelea huku wafungwa ndani ya gereza wakiwa wamembatiza jina la Mnoko kutokana na kutokuwa na huruma nao. Kila ilipotokea fujo yeye ndiyo alikuwa akiingia ndani ya gereza hayo ikiwa wafungwa watukutu watawazidi nguvu maaskari, aliogopwa sana ndani ya gereza kutokana na ukatili aliokuwa akiufanya katika kupiga wafungwa waliokuwa watukutu.



    ****

    Ndani ya kipindi hiki ndiyo Mzee Lutonja alipona kabisa na alirejea tena kazini, kama kawaida vyombo vya habari viliitoa habari hiyo ya kurejea kwake kazini baada ya kupona. Nyumbani nwaandishi walikuwa hawaishi kuja kumuhoji katika kipindi cha mwanzo alichokuwa na faya njema kabisa, aliendelea na kazi kama kawaida lakini hakuweza kuacha tabia yake . Kuisahau tabia yake ya uhaini ilikuwa ni ngumu sana, ni sawa na nyani kulisahau pori, aliunda kikundi kipya kabisa akachana na kikundi ambacho kilikuwa kipo chini ya Mtandao ambacho alikuwepo baada ya kujitoa kwenye genge la Ibrahim aliyekuwa na cheo cha Luteni Jenerali tayari na alikuwa ni mnadhimu mkuu wa majeshi. Uuuzaji wa unga ndiyo ilikuwa biashara yake kubwa ambayo ilimuingiza pesa na akawa ni mwenye pesa nyingi kuliko awali, kipindi hicho tayari alikuwa ameshaanza kujenga chuki ka Inspekta James akimuona yeye ndiyo chanzo cha kufa kwa mke wake. Aliamini bila ya yeye kumfanyia matesomakubwa binti yake, mambo hayo yasingetokea kabisa. Alikuwa kila siku ya maisha yake akitafuta sababu ya kuweza kumuondoa kazini, alitaka amchafue ndani ya nchi hii kwa watu waliokuwa wakimuonea huruma baada ya kukutwa na matukio ya kusikitisha

    Tuhuma za kwanza dhidi ya Inspekta James ilikuwa ni juu ya unyanyasasi wafungwa, tuhuma hiyo ilitupilia mbali kabisa na mkuu wa jeshi la magereza baada ya kuulizwa wafungwa wanyonge gerezani. Wengi wa wafungwa wanyonge walikuwa wakisema alikuwa amewafanya waishi kwa amani, walikuwa hawaonewi kabisa kutokana na uwepo wake ndani ya gereza. Hii ilifanya tuhuma hiyo isiwe na nguvu kabisa, aliendelea kutafuta nafasi nyingine ya kuweza kumuharibia kazi kijana mabaye hakuwa na hatia yeyote ile kwake.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ****

    Mwaka miwili baadaye James alikiacha cheo cha Ukaguzi na hatimaye akawa Mrakibu msaidizi wa jeshi la magereza (ASP), kipindi hiko ndipo kulitokea mauaji ya mkuu wa majeshi nchini Jenerali Kulika. Tuhuma zote zilishushwa kwa Professa kijana Moses Gawaza, mwezi mmoja baadaye ilikuja kujulikana kuwa tuhuma hiyo alisingiziwa na wale wote waliokuwa wakihusika walijulikana. Kipindi hiki ndipo alipotambua rafiki yake kipenzi ambaye alidai alikuwa akipakaziwa habari na Norbert aliingizwa gerezani, alikuwa ni Wilfred ambaye alikuwa na cheo cha ukamishna tayari katika jeshi la polisi. Kuanzia siku ambayo alivaa vazi la Wafungwa ndiyo ulikuwa mwisho wake wa kuwa na urafiki naye. Hakuwa akimchukulia kama rafki yake na hata pale lilipofanyika kosa kubwa na yeye akihusika basi kipigo kilikuwa kinamhusu. Ndani ya mwaka huo ndiyo gereza jipya la wafungwa wenye makosa mazito lilifunguliwa, Maaskari wote watukutu waliamishiwa kwenye gereza hilo huku ASP James ambaye alizoeleka kuitwa ASP Nkongo akibaki gerezani hapo. Alibaki na wafungwa wenye akosa ya kawaida sana, wao nao walipokuwa wakileta ubishi walikuwa wakpewa kipigo kizito. Tabia hii ya kupiga wafungwa ndipo Kamishna Lutonja alipokuja kupata njia ya kuweza kumpakazia jambo.

    Aliletwa gerezani mfungwa mtukutu mmojawapo gerezani hapo, Mfungw huyo ilikuwa n imtego ambao ulikuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufikia lengo lake. Mfungwa huyo alifanya utukutu akiwa yupo gerezani, taarifa zilipomfikia ASP Nkongo alimpa kipigo kizito sana ambacho kilipelekea alazwe hospitali. Akiwa yupo huko hospitali tayari Tabibu ya jeshi hilo alikuwa ameshakula hongo, alimmaliza kabisa na hapo ikawa ni tuhum nzito ambayo haikueleweka ilisambaa vipi uraiani. Magazeti mbalimali yaliandika habari ile huku mengi yakisema alikuwa ameonewa, rekodi za gerezani zilikuwa zikionesha alikuwa ni mtuhumiwa wa wizi ambaye alikuwa yupo Mahabusu. Kukuzwa mambo kwa habari hiyo na magazeti zilifika hadi kwa Kamishna Jenerali wa jeshi la Magereza, huyo aliagiza uchunguzi ufanyke na kisha ASP Nkongo akaitwa na kuhojiwa. Tuhuma ilionekana kuwa nzito ambayo ilimuelemea kabisa, makamishna walikuwa kama wameambizana kwa jinsi walivyokuwa wakishusha shutuma juu ya kulichafua jeshi la Magereza. Aliyekuwa akimtetea alikuwa ni Kamishna msaidizi mwandamizi Mwambe, huyu ndiye alisimama peke yake katika kumtetea ili asiharibikiwe na kibarua. Utetezi wake uliokuwa na mshiko ulisikilizwaa na hatimaye uchunguzi kwa mara ya pili katika mwili wa Mfungwa ukafanyika, kilichosabaisha kifo chake kilionekana kilikuwa ni kitu kingine kabisa baada ya uchunguzi huo kumalizika. Ilionekana alikuwa amekabwa na kuuliwa akiwa amelazwa, tuhuma hiyo ndipo ilipohamia kwa kuitwa Daktari aliyekuwa akimtibu kuja toka maelezo yake siku inayofuata. Siku ya kutoa ushahidi wake Dakati huyo alikutwa akiwa amefariki nyumbani, hapo kulionekana na kulikuwa na mchezo mchafu uliokuwa ukihusika na ASP Nkongo hakuonekana na hatia yeyote ile. Ili kuepusha maneno zaidi ya wanahabari ilibidi ahamishiwe Gereza jipya ya Nyumba giza kuwafuata Maasakri watukutu waliotangulia.

    Baaada ya uhamisho huo kufanyika ulipita mwaka mmoja ndipo Mzee Mwambe akapandishwa cheo na Mheshimiwa Rais kuwa Kamishna kamili, aliteuliwa kuwa mkuu wa gereza la Nyumba ya giza akichukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa gereza hilo ambaye alifikia umri wa kustaafu. Alipewa muda wa kujiandaa na maisha kuianza safari yake ya kwenda kuripoti eneo jipya la kazi ambalo kulikuwa na Mwanae wa kumlea, katika kupandishwa huko ndipo mkuu wa magereza alistaafu na nafasi yake ikachukuliwa na Mzee Lutonja aliyekuwa Kamishna baada ya kupandishwa cheo na kuwa Kamishna Jenerali. Uteuzi huo hakuupenda kabisa Kamishna Mwambe lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuukubali, hakuwa na mamlaka ya kuingilia uteuzi wa Amiri jeshi mkuu. Muda wa kuripoti kwenye eneo jipya la kazi ulipotimia alichukuliwa na helikopta maalum kutokana na gereza hilo kutokuwa na njia nyingine ya kuweza kuingia, siku hiyo akiwa kwenye vazi lake la ofisini alipokelewa na Maafisa wa jesi hilo katika kituo kipya cha kazi. Ilikuwa ni siku ya furaha kuweza kuungana na mwanae mlezi, walipoonana furaha ilizidi hata wakakumbatina kutokana na kukaa muda mrefu bila kuonana. Kamishna Mwambe aliyaanza maisha mapya ndani ya ofisi yake mpya na akatokea kuheshimiwa sana na vijana wa chini, upendo aliokuwa nao na pia kukaa na watu tofauti ndani ya gereza hilo. Kulimfanya ajichukulie heshima hiyo, maaskari wote walifurahi sana kumpata kiongozi kama yeye ambaye alikuwa akikaa nao kama marafiki baada ya muda wa kazi, huko alianza maisha mapya akiwa hana cha kupoteza alichokiacha huko uraiani. Mtu wake muhimu alikuwa yupo ndani ya gereza hilo tu, aliyekubai maisha hayo na aliona ni afadhali hata aendelee kuishi hukohuko miaka yote.

    Kipindi hiko ndipo alipopokea lawama juu ya ukimya aliokuwa nao ASP Nkongo, ukaribu wake na kuelewana naye kuliwafanya wengi walalamikie juu ya tabia yake. Kutoongea na mtu ndiyo tabia ambayo ilikuwa ikiwakera sana maofisa wenzake, walimuona mwanzoni alikuwa na maringo lakini kuwa na hasira kulikuja kuwaaminisha hakukuwa na maringo yeyote yale kwenye nafsi yake. Wapo waliojaribu kukaa naye karibu katika kipindi cha kazi lakini walishindwa, wapo wale waliojaribu kuongea naye katika kipindi cha mazoezi wote wakiwa wana nguo za kiraia na walifanikiwa kuelewana naye. Walipoleta urafiki huo kipindi cha kazi wakiwa na sare waliambulia kutoleelewana, wapo waliodhani alikuwa akivuta bangi kutokana na tabia hiyo aliyokuwa nayo. Ila haikuwahi kuonekana akiivuta hiyo bangi jambo ambalo walishindwa kumtuhumu hivyo, walipoleta malalamiko hayo kwa Kamishna Mwambe alikuwa akiwaambia kila kitu kina sababu yake. Aliwaomba sana wamzoee huyo kwani hakupenda kuwa hivyo, kauli hiyo iliwafanya mwanzo wahisi alikuwa na ugonjwa wa akili. Habari zilipomfikia Kamishna alikanusha kabisa na akasema alikuwa na akili timamu kabisa na hakuwa kama hivyo wanavyodhani, hiyo iliwafanya wamuache ASP Nkongo kama alivyo na wakamzoea kama walivyoambiwa na mtu huyo ambaye alikuwa akielewana naye. Walikuwa wakiongea naye muda wa mazoezi tu katika kipindi wote wakiwa na nguo za kiraia, ingawa hakuwa na ucheshi kabisa.



    Hamu ya kutaka kujua kile ambacho kilisababisha akawa hivyo ndiyo walikuwa nayo, walikuwa wakimsumbua sana Kamishna Mwambe juu ya kuwaeleza karibu kila siku. Hii ilipelekea nyakati hiyo ya mapumziko aamue kuwaeleza kisa cha yote hadi akawa akitoa sharti na kutojua mwenyewe kama wanajua habari zake







    WAKATI ULIOPO



    "Sasa jamani najua mmesikia yote kuhusu kisa cha James, niambieni sasa ingekuwa ni wewe ungekuwa kwenye hali gani" Kamishna Mwambe aliuliza



    "Kwakweli mkuu hata mimi ningekuwa kenye hali hiyo" Mmojawapo alijibu

    "Yaani wazazi wako wauliwe uishi katika upofu kwa muda mrefu, unakuja kuwa na furaha lakini mwingine anakuja kuiharibu furaha hiyo" Kamishna Mwambe aliongezea

    "Kwakweli mkuu inamuma sana" Afisa mmoja wa kike aliongea huku machozi yakimtoka

    "Ndiyo mtambue sababu ya yeye kuwa hivi Nkongo wote wawili kuanzia baba na mwana si wananunaji wa hivyo" Aliwaambia

    "Jana hapa alipotabasamu nilimuona ni mwenye sura isiyo na ukatili hata kidogo,kwakweli namsikitikia sana"

    "Ndiyo ujue hakuna kiumbe aliyezaliwa na ukatili au roho ya kutokuwa na huruma, chanzo cha yote ni wanadamu" Aliwapa somo

    "Mkuu tumekuelewa"

    "Sasa ikiwa mnataka kuongea naye basi na tuwe na urafiki naye"

    "James ukitaka kuongea naye zingatia yafuatayo utaweza kuwa rafiki yake mkubwa sana, usije ukavaa sare za kazi kipindi unaenda kuongea na maongezi yenu yawe baada ya kazi. Nguo za kazi hizi za rangi ya brown akiziona nakumbuka matukio ya kifo cha mke wake na pia cha wazazi wake, waliosababusha haya wote walikuwa wamevaa nguo za aina hiyo pamoja na za wafungwa" Alimuambia

    "Sawa mkuu"

    "Ohoooo! Naona mitambo imekaa sawa kaeni angalieni mbele kuna mpira anaweza kuja muda wowote" Kamishna Mwambe aliongea baa baada ya mitambo ya televisheni kurudi tangu ilipoaktika, haikupita muda mrefu ASP Nkongo aliingia na kuja kuketi jirani na Baba yake mlezi.

    "Naona leo leo umekuja kwa mara ya pili kuja kuangalia mpira huku" Kamishna alimuambia huku akimtazama

    "Kuangalia mpira ndani muda mwingine kunaboa sana" ASP Nkongo alijibu huku akishangaa jinsi maofisa wenzake walivyokuwa wamekaa karibu na mkuu wao.

    "James" Afisa mmoja aliita na kupelekea atazamwe usoni,kutazamwa huko kulimpelekea amsifie kwa muonekano wake akiwa kwenye mavazi ya kiraia.

    Wengine nao walisifia hivyohivyo na kisha wakawa wanaangaia mpira huku wakiongea naye, ASP Nkongo ndani ya siku hiyo alishangaa sana kuona hadi maofisa wa kike wakiwa wanaangalia mpira. Mazungumzo kila muda ambao mpira ulikuwa ukibadilika muelekeo wake ndiyo yalitawala, waliokuwa wanajua mpira kiundani walikuwa wakitoa maelezo yao ambayo yalizusha mjadala huku mpira ukiwa unaendelea. Mechi ya siku hiyo iliyokuwa ikioneshwa kwenye luninga ilikuwa ikiwahusu mahasimu wakubwa wa timu ambayo anaishabikia ASP Nkongo, alikua akiiombea sana hiyo timu ambayo alikuwa akiishababikia iweze kufungwa. Kila muda timu pinzani ilikosa goli kwenye lango la mahasimu wa timu anayoishabikia alikuwa akiona walikuwa wamefanya uzembe mkubwa sana, haikupita muda mrefu mahasimu aliokuwa akiwachukia walishambuliwa sana na hatimaye wakafungwa. ASP Nkongo aliruka juu kwa nguvu huku akishangilia, alipokaa chini alimkata jicho Kamishna Mwambe alivyokuwa ametulia kimya kwani timu iliyofungwa ilikuwa ni timu ambayo anaipenda. Maafisa wote nao walimtazama jinsi alivyotulia kimya huku wengine kwa wakicheka, ama kweli kuangalia mira na hasimu wako tabu tupu.

    "Leo siku yenu Baba lazima mlale" Alimuambia Baba yake mlezi ambaye alikuwa amekaa kimya tu.

    "Haya mjanja wewe" Kamishna Mwambe hatimaye aliongea na wote walicheka kwa nguvu sana.



    ****



    "Jamani huyu James msimuone hivihivi tu kapitia mengi sana hebu fikiria ungekuwa wewe ungefanyaje hapo?" Kamishna Wilfred ambaye alikuwa akiwasimulia kile ambacho anakijua kuhusu ASP Nkongo aliwauliza.

    "Yaani tumehangaika naye sana alikuwa ni chizi kabisa bila ya mimi na Kaila pamoja na Mzee Mwambe asingekuwa hivi leo" Aliendelea kuwaambia alipoona wamekaa kimya.

    "Yaani siku ya kwanza kuingia gerezani nilidhani mshkaji yupo atanisevu niende vizuri na life ya huku, siku nikajiona nina urafiki na Afande Nkongo si nikaleta fujo. Aisee jamaa alinipiga marungu na mabuti juu hadi nikatoka nundu yaani sitasahau, hapo ndipo nilipojua kuwa huyu si mtu. Mwanzo nilimchukia pia kama mnavyomchukia nyinyi lakini baadaye Mzee Mwambe nilipata bahati ya kuongea naye ndiyo akaniambia chanzo cha yeye kuwa hivyo, jamani yule ukijifanya ujuaji ukiwa umevaa haya manguo yetu au za maafande utaumia. Waliwaua wazazi wake na pia waliosababisha mke wake akafariki walikuwa wamevaa nguo za aina hii hii, kuziona hizo nguo jua anaona kama ndiyo anatazamana na wauaji wake" Aliwaambiahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ebwanaeh! Sasa nimekupata vizuri kabisa,jamaa kapitia mengi kweli hadi kuwa kipofu" Mmoja alidakia

    "Yaani yule pale nahisi roho yake itatulia mpaka huyo mbaya wake aingie kaburini" Aliwaambia

    "Hivi huyu mkuu wa magereza na mambo aliyoyafanya mbona hakamatwi yaani?" Mmoja aliuliza

    "Hivi utaanzia wapi kumkamata na mtandao mpana aliokuwa nao, mara ya mwisho nikiwa kazini nilikuwa najua mzee alikuwa nauza unga yule lakini mtandao ni mpana aliokuwepo" Aliwaambia

    "Ama kweli hii nchi mwenye kauli si mwenzako, nimekuwa muuaji lakini anayenituma ndiyo kanifanyia fitina hadi nimeingia ndani mwaka wa nane huu"

    "Yaani ndiyo hivyo ila huyu Mkuu wa magereza hana muda mrefu ndani ya uraia kwa mfumo huu wa uongozi" Kamishna Wilfred aliwaambia

    "Sasa kaweza kuishi miaka yote hiyo hawajamuweza"

    "Majamaa sasa hivi kuna viumbe vitatu ni hatari sana, kuna Norbert Kaila nilijua mwandishi wa habari tu lakini ni mpelelezi. Kamishna John Faustin naye ni jasusi, kuna Professa Moses Gawaza naye ni mpelelezi. Hawa watu wameisambaratisha timu yetu hadi mimi nipo humu ndani" Aliwaambia huku akipiga muayo halafua akamalizia, "oyaa wacha tulale aisee kazi ya kesho si mchezo tukichelwa kulala imekula kwetu"

    Kila mmoja alijilaza kwenye kitanda chake kutokana na muda kuwa umekwenda, uchovu waliokuwa nao kwa siku nzima baada ya kupasua sana miamba. Uliwafanya waupate usingizi ndani ya muda mfupi, kulianza kusikika mikoromo kwa baadhi yao baada ya kuchotwa na usingizi.



    ****



    Utaratibu ulikuwa ni kama kawaida ndani ya gereza hili kila ikitimia muda wa alfajiri, wafungwa wote walikuwa macho na walikuwa wameshajiandaa. Wote walielekea maenno yao ya kazi wakiwa wanasimamiwa na Maaskari waliokuwa zamu, muda huu ASP Nkongo naye alikuwa yu macho na tayari alikuwa yupo maeneo ya juu ya gereza hilo kwenye nyumba yake akijiandaa kutoka nje na kuingia kazini. Muda mfupi baadaye alitoka huku akitembea kwa mwendo wa taratibu akiwa amevaa sare zake nadhifu, mkononi alikuwa na mkoba muhimu, aliingia kwenye ofisi yake na akautua mkoba huo na kisha alitoka huku akikunja mikono ya sare yake. Alishuka moja kwa moja chini ya ardhi kama ilivyokuwa kawaida yake na kupitia katika ofisi mbalimbali. Siku hii kidogo maofisa waliokuwa wapo chini yake walimfurahisha sana, hakumfokea mtu yeyote kwenye eneo lake la kazi. Aliporidhika na utaratibu ulivyokuwa ukienda alirudi ofisini kwake mara moja, kawaida ya gereza hili ilikuwa maofisa wanaingia kazini mapema sana tofauti na ilivyozoeleka kwenye magereza mengine. Hii ilitokana na wote kuwa na makazi ndani ya eneo hilohilo, walikuwa wakiwahi kutoka kuliko magereza mengine lakini masaa ya kazi yalikuwa ni yaleyale. Maofisa wa ngazi za chini kabisa wale ambao walikuwa hawashughuliki na sehemu hizo za ofisni ndiyo walikuwa wakifanya kazi kizamu. Walikuwa na siku nzima ya zamu ya kusimamia wafungwa na kisha siku inayofuata walikuwa walipumzika na wengine walichukua zamu. Huo ndiyo ulikuwa utaratibu wao kila siku kwa maafande wa kawaida. Maafande hao wa kawaida ndiyo waliyokuwa wakipendwa sana na ASP Nkongo ufanisi wao wa kazi, hao walikuwa hawana muda wa kuzembea katika eneo la kazi tofauti na wale wengine ambao walikuwa wapo maofisini.



    *****



    Majira ya muda wa kifungua kinywa baada ya Kamishna Mwambe kumaliza kupata kifungua kinywa chake alikuwa akitoka na kurudi ofisini kwake, akiwa yu njiani alikutana na Teddy ambaye alimpatia heshima yake. Aliipokea heshima hiyo huku akimtazama kwa tabasamu, Teddy hakutaka kujibaraguza aliamua kujieleza juu ya kuhitaji maongezi naye. Aliweka wazi kabisa alikuwa na maongezi naye ambayo yalikuwa si ya kiofisi, Kamishna Mwambe kwakuwa alikuwa akipenda sana kusikiliza maaskari wa chini yake aliamua kutafuta mahali palipokuwa patulivu akaketi naye chini na kusikiliza hiyo shida yake.

    "Ndiyo binti" Alimuitikia

    "Mkuu najua wewe ni kama baba yangu hivyo sitoona haya kukuambia kuhusu hili suala kwani ninahitaji sana msaada wako" Teddy aliongea

    "Wewe ni kama mwanangu upo huru kuongea nakusikiliza, hata ukiniita Baba ni sawa"

    "Mkuu kwa muda mrefu nimekuwa ninateseka kisa James, nimejaribu kila niwezalo lakini nimeshindwa hata kukaa kuongea naye. Nahitaji kuwa na mume mkuu na nahitaji kuwa familia, mwanaume peke nimuonaye ni yeye tu sina mwingine lakini ndiyo siyo muelewa. Naamini wewe anakuheshimu kama baba nimeamua kukufikishia hili kwako"

    "Je unampenda kwa dhati kabisa?"

    "Ninampenda kwa dhati"

    "Ok nimekusikia najua na yeye ni muda wa kupata mke pia nitaongea naye ila nitakupa masharti ukiongea naye jaribu kuyazingatia"

    "Sawa"

    "Unaweza kwenda binti suala hili limefika kwangu tayari nitajua namna ya kukusaidia" Kamishna Mwambe alipotoa ruhusa hiyo kwa Teddy aliondoka na kurejea eneo lake la kazi kwa haraka, alimuacha Mzee huyo akiyatafakari maneno hayo. Haikuwa mara ya kwanza kusikia tetesi juu ya binti huyu kumtaka ASP Nkongo, zilikuwa ni tetesi ambazo hakuwa na uhakika nazo na sasa alikuwa amejiwekea uhakika nao. Hakutaka kukaa eneo hilo kwa muda mrefu aliamua kuelekea ofisini kwake moja kwa moja.



    ****



    Baada ya muda wa kufanya kazi kuisha ndani ya ofisi zao kila mmoja alirejea kwenye makazi yake, muda huu ndiyo muda ambao Kamishna Mwambe aliutumia kujongea hadi nyumbani kwa ASP Nkongo. Kutokana na kupazoea na pia kuuzoea utaratibu wa kijana wake wa kumlea, alijua ndani ya muda huo alikuwa akifanya nini humo ndani. Hakutaka kubisha hodi alipitiliza moja kwa moja hadi ndani, alipoingia ndani ya sebule ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa ina samani kadhaa ikiwa na idadi kubwa ya vyuma vya kunyanyua vikiwa vimezagaa jirani na meza ya sebuleni. Jambo hilo halimkushngaza kabisa alikuwa tayari ameshamzoea Mwanae huyo tabia yake, alipongia alienda kuketi kwenye kochi mojawapo na kisha akatulia kwa sekunde kadha halafu akapaza sauti kumuita. ASP Nkongo alitokea akiwa amevaa kaptula huku akiwa kifua wazi, kutokana na kuitambua sauti ya mlezi alienda kuketi hadi jirani yake kwani alishatambua alikuwa na jambo ndiyo maana kamuita.

    "James mwanangu unajua miaka inakimbia hii sana, kamwe haitorudi nyuma" Alimuambia

    "Natammbua hilo Baba"

    "Sasa basi napenda uanze kuijenga familia kwa mara nyingine mwanangu, hivi unataka uondoke duniani hapa hata uzao hujaacha kweli"

    "Baba tatizo mazingira"

    "Mazingira yana nini mwanangu, yaani hadi nakuja kutamkiwa na binti ameamua kuweka haya zote pembeni anataka uwe mume wake" Maneno hayo yalipotoka ASP Nkongo alikaa kimya akawa amekosa la kuongea.

    "Si kama nakulazimisha mwanangu hebu fikiria kuhusu hilo, Teddy yule binti ambaye huwa unamjibu kiukali ni msichana ambaye anakupenda sana. Hivi ushawahi kuona mwanamke akitoka huko na kuja kumtamkia mzazi wa kiume wa fulani anampenda"

    "Hapana sijawahi kuona"

    "Sasa jiulize ni kwanini yeye kaja kunitamkie kuwa anakupenda, maana yake kashindwa kuvumilia kabisa"

    "Lakini"

    "Hakuna cha lakini hebu niambie yule binti unamuona vipi?"

    "Ni msichna mrembo sana na mwenye mvuto"

    "Saa ule urembo wake na mvuto wake wote jiulize wangapi wanamtaka lakini kaja kwako, James usifikiri humu ndani hakuna anayemtaka yule"

    "Sawa nimekuelewa"

    "Siyo unielewe tu hebu tafuta namna ya kuweza kuwa pamoja naye yule, unahitajiwa ukiwa hivi bado upo ujanani fikira ukija kuwa kama mimi na bado hutaki kuoa itakuwaje. James najua ulimpenda Sara tena sana lakini naomba ukubali ameshakwenda tayari muda mrefu, usiishi kama mimi niliyechoka wewe bado unahitaji Mwanamke kuliko kitu kingine chochote" Kamishna Mwambe aliongea huku machozi yakiwa yanamlenga, hali hiyo ilimfanya ASP Nkongo ainamishe uso wake chini mwenyewe hakutaka kumuangalia.

    "Mimi sina cha kupoteza James nimeshakuwa mtu mzima kuona sioni umuhimu lakini katika umri kama wako niliona umuhimu wake. Najua una uchungu umefiwa na kiumbe kilichokuwa kipo bado tumboni, hebu fikiria mimi nilifiwa na mtoto tena nikiwa nimemuona jinsi alivyochukua sura yangu lakini sikukata taama nikampata ambaye alikuwa mke wako" Maneno hayo yalimchoma sana Jmes hadi chozi likawa linakaribia kumtoka.

    "Baba nimekuelewa nipo tayari kuoa kwa mara nyigine"

    "Sasa huo ndiyo uanaume James, Mkuu Nkongo ameondoka na kuacha alama yake duniani basi na wewe uache ya kwako. Upo tayari kumuoa je ni nani? Maana si lazima unaweza kuchagua mwngine"

    "Teddy ndiye atakayekuwa mtu pekee anayenifaa, hata kama nikichagua mwingine nitaleta matatizo kama ya mwanzo. Nilikuwa simuhitaji Jane nafikiri matokeo yake umeyaona nimepoteza familia. Sipo tayari litokee hili ikiwa najua kuna ambaye ataumia nikichukua mwingine"

    Baada ya hapo Kamishna Mwambe alianza kumpa somo kijana wake juu ya maisha yake kwani aliona bado alikuwa akimkumbka tu mke wake. Alitumia muda huo kuongea naye kirefu zaidi huku akimuusia mambo mbalimbali, alikuwa akitaka aingie kwenye njia iliyo sahihi na si kufuata pasipo sahihi aje kupotea. Huyu kijana kuwa naye aliona kama alikuwa na mtoto wa kumzaa, hakutaka kumpoteza kinamna yeyote ie. Alikuwa akimlinda sana na hata zilipoibuka chuki dhidi yake alikuwa akimkingia kfua, upendo wote aliokuwa ameupoteza kwenye ajali ya gari la binti yake. Aliuhamishia kwa kijana wake wa kumlea ambaye alikuwa na kidonda kimoja naye katika ajali hiyo, kutokana na uzito wake aliokuwa akipewa na ASP Nkongo haikuchukua muda kuweza kukubaliwa maneno yake. Heshima aliyokuwa akipewa ilikuwa ni kubwa kutokana na mchango aliyonao katika maisha yake, hakutaka kumuangusha kwa kitu chochote kama yeye ambavyo hakuwahi kumuangusha. Mambo mengi ambayo alikuwa amefanyiwa yalikuwa hayalipiki, njia ambayo ingeweza kumuhisi kidogo alikuwa akirudisha fadhila ya yale aliyofanyiwa ilikuwa ni heshima na utiifu tu kwa Mlezi wake.





    _______________TIRIRIKA NAYO

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Teddy Andrew au wengi walivyokuwa wamemzoea kumuita kwa jina la Modo Teddy kutokana na wembamb wake aliyokuwa nao, jina hilo lilikuja kupotea baada ya kuupata mwili uliyokuwa na mvuto zaidi hata ya huo uwembamba aliyokuwa nao. Binti huyu alikuwa ni mmoja kati ya mabinti wapole, alikuwa ni mtoto wa pekee kwa tajiri Andrew ambaye alikuwa akisifika sana jijini Arusha. Alilelewa na kukulia katika maisha ya raha na wala hakuwahi kuijua shida, elimu yake aliisoma kwenye shule ya kimataifa kuanzia yu mtoto hadi anaingia sekondari. Alikuwa ni mwenye kipawa cha akili katika masomo yake, haikuwahi kutokea akashuka kimasomo kipindi akiwa yupo shule. Hii ilimfanya Mzee Andrew ambaye ajivunie kuwa na binti kama yeye na kumuongoza katika msingi wa kufuata katika masomo, baba yake alikuwa ni tajiri ambaye alikuwa akitilia mkazo suala lake la kujielimisha na pia alifuatilia kwa kina masomo yake. Teddy alifanikiwa kumaliza kidato cha sita katika shule ya kimataifa hapahapa nchini, kumaliza kwake shule nchini Tanzania hakukuweza kumkwepesha kutoingia kwenye mafunzo ya JKT kutokana na ulazima wake. Mzee wake alilipinga sana suala hilo kutokana na kumlea mwanae katika maisha ya kudekeza, lakini hakuweza kufua dafu mbele ya mfumo ambao ulikuwa umewekwa. Ilikuwa ni akose nafasi ya kujiunga na chuo kikuu au aingie jeshini aende chuoni, ilimbidi tu akubali tu aingie jeshini huko akiwa anamuonea huruma sana kutokana na kasumba mbaya ambayo ilikuwa imesambzwa dhidi ya jeshi. Kutoruhusiwa kwa mawasiliano ndani ya kambi muda wa mafunzo kulizidi kumtia hofu lakini aliamua kuwa na subira moyoni, mawasiliano alipokuja kuyapata na mwanae ilikuwa ni muda ambao alikuwa akitakiwa kwenda kufanya maombi ya chuo katikati ya mafunzo hayo.

    Mzee Andrew alipoweza kutuliza hofu aliyonayo baada ya kupata taarifa Binti yake alikuwa yupo mzima wa afya kabisa, muda wa mafunzo ulipoisha ndipo alipoweza kuja kumuona Binti yake katika siku ya Mahafali alivyopungua mwili. Ndipo siku hiyo alipofanikiwa kuja kuyaona mazingira ya kambi aliyokuwa akiishi, yalikuwa ni mazingira ambayo yalikuwa si ya kilelemama ambayo yalifanya ashangae kwa binti yake kuweza kuishi maisha kama hayo wakati alikuwa amezoea sana kudeka. Hatimaye siku inayofuata alirudi ndani ya jiji la Arusha na akayaanza maisha baada ya kutoka jeshini, katika muda huu ndipo alipoachiwa huru sana na Baba yake kutokana na kuwa amekua mtu mzima. Kipindi hicho ndipo Teedy alikuwa yupo katika mahusiano mazito sana na kijana wa hadhi ya kawaida ambaye alikuwa amekutana naye jeshini, walikuwa wapo ndani ya penzi la siri sana. Walikuwa wakipanga muda vizuri na kukutana na watu wa kawaida na kufurahi sana, alitokea kumuamini sana huyo kijana. Ilikuwa ni mara ya kwanza kujiingiza kwenye mahusiano ya mapenzi hivyo alijitoa mzima kabisa kwenye mahusiano hayo, mahusiano hayo ambayo yalikuja kujulikana na baba yake aliyapinga kwa nguvu zote lakini Teddy hakutaka kabisa kuyaacha na aliendelea nayo. Baba yake hakutaka kushindana naye kwa jinsi alivyokuwa akimpenda ilimbidi akae kimya tu, hakutaka alete matatizo mengine kisa kulazimisha.

    Muda wa mahusiano hayo haukufika hata mbali na Teddy alijikuta akijuta ndani ya maisha yake, ilikuwa katika muda ambao majina ya chuo yalikuwa yametoka na alikuwa akisubiri siku zisogee aweze kujiunga na chuo. Kipindi hicho ndipo alipogundua kuwa alikuwa amependa mtoto wa Mhalifu mkubwa sana jijini Arsuha ambaye aliambiwa ni mfanyabiashara wa kawaida, mambo yalikuja kujulikana siku ambapo alikuja kujulikana kuhusu utajiri wa baba yake na huyo Mhalifu. Alitekwa nyara na kushinikizwa mzazi wake alete pesa, Mzazi wake alipoleta jeuri tu Teddy alijikuta akibakwa na mtu ambaye alikuwa akimuona ni atakuja kuwa mkwe wake huku akishirikiana na Mwanae. Msako baadaye uliendeshwa na hatimaye watu hao wawili Baa na Mwana walikuja kuvamiwa kwenye maficho yao, walipojaribu kutoroka waliishia kuuacha uhai wao. Askari wa jeshi la polisi ambao walikuwa makini zaidi waliwashambulia, kuanzia siku hiyo Tedy alibadilika na kuwa mnyongea na asiye na furaha. Chuo ulipotimia muda hakikuendeka kabisa, aliathirika kisaikolojia kwa kitu alichofanyiwa na Mtu ambaye alimpenda sana. Hali yake ilitishia kabisa wazazi wake na kuona alikuwa akielekea kuchanganyikiwa, chuo hakukitaka tena na akawa ni wa kukaa ndani. Baba yake alipojaribu kumtafutia kazi nyingine za kufanya kutokana na ushawishi wake wa kifedha, aliishia kuzikataa na hakukuwa na wa kumlazimisha. Kipindi hiko mawazo yalipomzidi ndipo alipoamua kubadili maisha na kuwa ni wa kwenda mazoezini, alifanya mazoezi ili kupunguza mawazo lakini haikusaidai kitu. Ufanyaji huu mazoezi ndipo ulipopelekea akaingia kwenye uchezaji wa ngumi, suala hilo halikumfurahisha Baba yake lakini hakuwa na uwezo wa kulipinga. Aliamua kukubaliana na matakwa ya binti yake na si kushindana naye, Teddy kuanzia hapo aligeuka kuwa mwanamke ambaye alikuwa akijua vizuri sana kuitumia mikono yake katika kupigana ingawa mwili wake haukuwa mkomavu kutokana na kufanya mazoezi kwa muongozo wa walimu.



    Maisha ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu yalimfanya baba yake kutoyafurahia kabisa, alikuwa akitamani awe masomoni au awe kwenye shughuli ambayo ingemuingizia kipato. Alipoona hakuwa na uelekeo wa kufanya vile anavyotaka ilimbidi amuulize juu ya akitakacho, siku hiyo ndipo Mzee Andrew aliingiwa na mshangao mwingine baada ya binti yake kulichagua jeshi la wananchi. Hakutaka kupingana naye alijaribu kumtafutia nafasi lakini kwa bahati mbaya nafasi hazikuwa zimetoka, kulikuwa na nafasi ndani ya jeshi la Magereza ambalo pia alikubali tu kujiunga nalo hivyohivyo kutokana na kulipenda pia. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo kwa binti wa kitajiri kuingia ndani ya jeshi la magereza, baada ya mafunzo mafupi aliweza kupata kazi kwenye Gereza moja ambalo lilikuwa lipo Arusha. Alipatiwa nyumba na wazazi wake na pia sehemu ya kampuni kubwa ambayo wazazi wake walikuwa wakiiimiliki, aliendesha maisha yake peke yake na hakutaka kuwa mwenza. Teddy akiwa na cheo cha RSM naye alikuwa ni mmoja wa maaskari wa kike ambao walikuwa wakorofi, alikuwa akiogopeka na wafungwa. Alikuwa ni rafiki mzuri sana wa maaskari wenzake lakini alikuwa ni adui mkubwa wa wafungwa, ujeuri wowote utakaofanywa na wafungwa alikuwa akimpa dhabu kubwa na hata kipigo kizito. Ukorofi huo aliokuwa nao ulimfanya awe anashughulika na wafungwa wale ambao walikuwa na makosa makubwa gerezani, huko alikuwa akiingia na rungu au muda mwingine alikuwa akiingia bila ya rungu. Hatari yake ilikuwa ni ileile kutokana na kuwa mjuzi sana katika mapigano, aliweza kuwa kipenzi cha wafungwa wanyonge ndani ya gereza. Utukutu wake ulikuja kumfanya ahamishiwe kwenye gereza la Nyumba ya giza akiambatana na maaskari wengine watukutu, Baba yake alihuzunika kuwa mbali na binti yake lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuridhia tu na ile kampuni ambayo alikuwa amempa akamsaidia usimamizi.

    Alipokuja ndani ya gereza hili na kukutana na marafiki wapya waliokuwa watukutu kama yeye, alianza kujihisi yupo kwenye dunia ya watu kama yeye. Huko ndipo aliporejewa na furaha kwa mara nyingine na akanawiri kuliko awali, haikupita muda mrefu aliweza kumshuhudia afande mpya mtanashati asiyecheka na watu akiwasili ndani ya gereza hilo. Huyo ndiyo Afande ambaye alifanikiwa kuuteka moyo wake kwa mara ya pili tangu alipojeruhiwa, alijitahidi kila awezavyo kumpata lakini alishindwa. Hakuwa mwingine ila ni ASP Nkongo ambaye alikuwa mwenye sura ya hasira muda wote, aliposhindwa kumpata kwa kipindi kirefu cha muda ndipo alipoweza kumuomba msaada Mkuu wake ambaye alikuwa akielewana naye.



    ****

    ASO Nkongo baada ya kuondoka baba yake mlezi tangu amalize kufanya naye mazungumzo, moyoni mwake alikuwa tayari amekiri kuwa mke wake alikuwa tayari amekwenda na hatorejea tena. Aliamua tu kuweza kuwa na mahusiano na binti huyo ambaye alikuwa akimpenda, alipoyatazama mzingira ya nyumba yake aliyokuwa akiishi aliona kabisa yalikuwa yakimshawishi aweze kumuongeza ndani humo. Kutokuwa sawa kwa baadhi ya vitu kutokana na kutojali kwake aliona akifaa awe na mwenza ambaye atamuongoza kuweza kuwa na maisha mengine, mfumo wa maisha aliyokuwa akiufuata aliona ulikuwa ukihitaji kubadilika na kuingia katika mfumo mwingine lakini hakuwa akiweza kuubadili mfumo huo akiwa anaishi maisha ya upweke ndani ya Nyumbani yake. Uwepo wa ubavu wa kushoto ndiyo kitu pekee ambacho kingeweza kumbadilisha katika aliyokuwa akiishi, utaratibu aliokuwa amejiwekea ndani ya eneo hilo akiwa yupo peke yake ulikuwa ni utaratibu mgummu kwa yeye mwenyewe kuubadili pasipo kuwepo kwa mwingine. Siku zote mwanadamu hubadili mfumo wa maisha mabo alikuwa ameuzoea kutokana uwepo wa mwingine katika mazingira anayoishi, uwepo wa mtu mwingine hufanya atoke kwenye mazingira ya upweke na kuingia mazingira ya namna nyingine. Hapa ndipo ule mfumo wa maisha aliokuwa ameuzoea kipindi yu mpweke hubadilika, ASP Nkongo naye alionekana alikuwa akimuhitaji Teddy kuweza kubadilisha yake kutokana na kuingiwa na maneno ya baba yake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majira yale ya kuangalia mpira kutokana na kipindi hiko na michuano ya Klabu bingwa ya dunia yalifka, siku hiyo kwa mara ya kwanza Teedy aliletwa humo ndani ya Bwalo la maofisa ambao walikuwa wamemzidi cheo. Kwa mara ya kwanza aliweza kumuona ASP Nkongo akiwa ni mwenye tabasamu na si kununa kama alivyozea, hakika siku hiyo ilikuwa ni faraja kwake hasa alipokaribishwa kukaa jirani naye muda wa kuangalia luninga. Yote hiyo ilikuwa ni mipango ya Kamishna Mwambe aliyokuwa ameifanya. Wengi waliokuwa wapo humo ndani walibaki na maswali kwa Askari mwenye cheo cha kwaida kuweza kuingia humo ndani, walishindwa kuendelea kujiuliza maswali zaidi baada ya kujua alikuwa amekaribishwa na mkuu wao. Waliendelea kuangalia mpira huku wale walengwa wawili wakiwa wameingiwa na ukimya baada ya kukutana kwa mara ya kwanza, Teddy alikuwa yu mwingi wa kumuangalia usoni ASP Nkongo katika muda ambao alikuwa akiongea na kucheka na wenzake. Alipotazamwa yeye jamo la kwanza kulikimbilia ilikuwa ni kuangalia pembeni kutokana na kuingiwa na aibu kubwa , muda kadri ulivyoenda walijikuta wakiongea maneno machache wenyewe. Kamishna Mwambe alipoona wameanza kuongea wawili alizuga mwenye udhuru akatoka nje, aliporejea hakukaa sehemu aliyokuwa amekaa awali na alienda kuketi kwenye kiti kingine kabisa. Mpira uliendelea kuangaliwa huku ASP Nkongo na Teddy wakiwa wanaongea kwa pamoja, ilifika muda wote wawili wakawa na furaha kutokana na mioyo yao kuwa tayari ilikuwa imeanza kuzungumza. Muda wa mapumziko ya mechi waliyokuwa wakiitazama ndipo walipoazama kabisa kwenye mazungumzo huku wakicheka, wengi waliokuwa wakiangalia mpira pamoja nao walibaki wakishngaa lakini walikaa kimya kutokana ilikuwa ni habari ambayo haikuwa ikiwahusu.



    Mazungumzo waliyokuwa wakiyaendeleza yalipopiga hatua nzuri hatimaye walikaa karibu na kupunguza sauti wakawa wanaongea yao ya moyoni, kicheko kilichokuwa kipo mara ya kwanza kilipungua na hatimaye wakawa wanaongea bila ya kuwepo kicheko hicho na sauti ya chini sana. Muda wa kipindi cha pili katika mechi mbayo walikuwa wakiingalia ulipoanza, ASP Nkongo alirudisha macho yake kwenye luninga lakini hakuacha kuongea na Teddy kutoka na walikuwa wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo. Alikuwa akitupia jicho luninga huku akiongea na Teddy ambaye alikuwa amesogea karibu zaidi kutokana na mazungumzo kuwa yao kibinafsi, kufikia hatua hiyo na jinsi walivyokuwa wamekaa hakuna ambaye hakuwa akijua kuwa watu hao walikuwa na zaidi ya ukaribu mioyoni mwao. Tayari maofisa wengine walikuwa wameshajua kinachoendelea ingawa walikaa kimya kutokana na kuwa yalikuwa hayawahusu, waliwaachia wahusika na nafsi zao wayatawale mazungumzo yao. Hatimaye dakika tisini zikatimia na maafisa mmoja baada ya mmoja alitoka humo ndani ya Bwalo na kurejea kwenye nyumba zao, muda mfupi baadaye ndani ya Bwalo hilo walibaki wawili tu waliyokuwa wamezama kwenye maongezi yaliyojaa ukaribu zaidi.

    "Mkuu kwakweli sikutarajia kama upo hivi" Teddy walipokuwa amebaki wawili

    "No niite James tu hilo jina sitaki kulisikia nje ya ofisi" ASP Nkongo alikataa kuitwa jina hilo

    "Ok"

    "Sasa nafikiri hakuna ambacho hujanielewa hapo Teddy"

    "Nimekuelewa James nipe juda kwanza siwezi kukupa jibu kwa haraka"

    "Lini jamani wanadamu siku kuziona ni bahati je unatarajia kesho utaniona?"

    "No usiseme hivyo James"

    "Ndiyo ukweli hiyo"

    "Kuwa mwenye kusubiri nafikiri sitokuweka sana nitakuwa jibu lako"

    "Ok nimekuelewa"

    "Sasa?!"

    "Tutoke muda umeenda huu" ASP Nkongo aliongea huku akinyanyuka na kumpa mkono Teddy amuinue, tabasamu lilimtoka binti huyo aliponyooshewa mkono naye kwa madaha alimpa kiganja chake akamuinua.

    Walitoka wakiwa wameshikana mikono kwa namna ya upendo huku Askari ambaye alikuwa akihusika na kuzima taa humo Bwaloni akiiingia, walitembea kufuata njia ambayo ilikuwa ikienda eneo ambalo kulikuwa na nyumba za maaskari wa jeshi hilo pamoja na wafanyakazi wa mzabuni. Ilikuwa ni siku ya kwanza kwa wote wawili kuongozana pamoja, kila mmoja alijisikia ni kiumbe tofauti kwa kufutana na mwenzake. Waliongozana kwa pamoja hadi walipofika kwenye eneo ambalo lilikuwa likitenganisha njia, hapo walisimama na wakabaki wameshikana viganja vya mikono yao huku wakitazamana.

    "Sasa?!" Teddy aliuliza

    "Kesho kama vipi?" ASP Nkongo alimwambie hukua akitaka kuitoa mikono yake lakini Teddy hakuwa tayari.

    "Ngoja nikusindikize" ASP Nkongo aliamua kuongea na kisha akaanza kuongozana naye kuelekea kwenye eneo ambalo alikuwa akiishi, wote walienda hadi kwenye nyumba ya wastani ambayo ilikuwa imejengwa kisasa zaidi. Walipofika hapo bado walikuwa walikuwa wameshikana vignja vya mkono, ASP Nkongo alimpeleka hadi mlangoni kabisa.

    "Nikutakie usiku mwema" Alimuambiwa huku akimtazama usoni, katika namna ya kiajabu aliuachia mkono wake na hapo kukatokea jambo ambalo hakutarajia kama litatokea.

    Teddy baada ya kuachiwa kiganja cha mkono alijivuta mbele kwa nguvu, alitulizaa papi za midomo yake kwenye papi za musomo ya ASP Nkongo. Wote kwa pamoja alijikuta wakiwa wameingiwa kwenye hali nyingine kabisa, walidumu kwenye tendo hilo kwa muda mfupi na walipoachiana na walikumbatiana kila mmoja akiwa na hisia kwa mwenzake.

    "Nakupenda sana James nipo tayari kuwa nawe" Hatimaye Teddy alihalalisha mwanzo wa ukurasa mwingie kwake.



    Maisha ya mapya kati ya wale waliyokuwa wamepitia kwenye chungu kipindi cha nyuma yalichipuka kwa kasi kubwa , mtu wa knzwa kuyajua mahusiano hayo alikuwa yule ambaye alipelekea wakawa pamoja. Teddy alikuwa akijua kabisa kuishi naye mpenzi wake, alifuata kile ambacho aliambiwa na Kamishna Mwambe kilikuwa kikimkera ASP Nkongo. Hii ilifanya waishi kwa furaha na hata utaribu wa maisha ya ASP Nkongo ukaanza kubadilika, nyumbani kwake kukawa mahali palipokuwa pana usafi wa kipekee. Uhusiano huu ulianza kwa kujulikana na maofisa wa juu ambao waliwaona kwa siku ya kwanza pamoja na marafiki wa Teddy waliokuwa wakijua kila kitu. Taratibu ulianza kujulikana kwa baadhi ya maaskari wa chini na hatimaye Maafande wote wakawa wanatambua, kufikia kipindi hiko wote waili walijumuika kwa pamoja mazoezini. Wote wawilikwa kuwa pamoja walijiona ni viumbe ambao walikuwa wamezaliwa upya, walifuatana kama kumbikumbi katika kila sehemu walipokuwa wakielekea.







    Haikukaa muda mrefu sana hatimaye Teddy alihamisha makazi yake kabisa nyumbani kwa ASP Nkongo, huko walianza kuishi kama mume na mke. Utaribu mzima wa maisha ya ASP Nkongo ndiyo ulibadilika kabisa, kuishi na mwanamke ambaye alikuwa akimuelewa jinsi alivyo kulimfanya awe James yule ambaye alikuwa ni mcheshi sana katika kipindi cha nyuma. Hatimaye alianza kujijengea marafiki wengi sana kutokana na maofisa hao nao kujua jinsi ya kukaa naye na kuongea naye, muda mfupi tangu aweze kuwa na marafiki wengi alitokea kuwa kipenzi cha maofisa wengi kutokana na ucheshi aliokwua ameupoteza kurudi. Pamoja na hayo bado alikuwa hapendi kabisa maelewano na Askari aliyekuwa yupo ndani ya vazi la kazi, hii ilifanya Tedy kutovaa kabisa vazi hilo akiwa yupo naye ndani na muda wa kwenda kazni alikuwa akimuacha atangulie ndipo na yeye huvaa na kutoka. Huo ndiyo ulikuwa mfumo wa maisha yao na Teedy akawa kila siku akitaka hali hiyo iondokane ili aweze kuishi naye kiuhuru zaidi, suala hili aliamua kulifikisha kwa Mkwe wake ambaye aliahidi kulishughulikia. Suala hili pia lilikuwa limeshagunduliwa na baadhi ya maaskari ambao waliahidi pia kulishughulikia ili mwenzao arudi kwenye hali ya kawaida, haikupita muda mrefu sana tangu kuambiwa hatimaye maofisa wote waliungana na mkuu wa gereza wakamuita mtaalamu wa Saikolojia. ASP Nkongo aliposikia kuhusu ujio wa mtu huyo mwanzoni alionekana kutotaka suala hilo, Tedy alitumia ushawishi wake na hatimaye alikubali. Tiba alianza kupewa huku Teddy akiwa yupo karibu naye, kutoka na utaalamu wa mtu ambaye walikuwa wamemuajiri alianza kuridi katika hali yake ya kawaida. Taratibu aliona si kila aliyekuwa akivaa vazi kama lake alikuwa ni mtuhumiwa wa mauaji ya aliowapenda, hatua hiyo ilifikia pazuri sana na hata akwa anakaa na wenzake wakiwa wamevaa mavazi ya kazi. Tiba iliendelea na hata akwa anawaona wafungwa wengine waliokuwa ndani ya gereza hilo si wwaliosababisha awe hana furaha katika maisha yake, hatua ya mwisho ya tiba hiyo ilipokamilika alikuwa ni kiumbe mpya kabisa si yule ambaye alikuwa na ukatili. Hapo ndipo mapenzi baina yake na Teddy yalipizidi kuliko hata awali,pia ndiyo alizidi kuwa kipenzi cha Maaskari wote ndani ya gereza si wakubwa wala wadogo kutokana na kuwa mtu mwenye kupenda kuongea na atu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    James wa zamami mwenye ucheshi aliamka kwa mara nyingine hakuna ambaye alikuwa akimfahamu vizuri hakujua hilo, hata Kamishna Wilfred ambaye alikuwa yupo gerezani alifahamu kuhusu hilo. Pia wafungwa nao waliokuwa wakimuona katili walifahamu kuhusu hilo, alianza kukubalika miongoni mwa wafungwa kutokana na tabia yake. Ilifika kipindi alikuwa akienda kuka pamoja na wafungwa walipokuwa wapo kwenye mapumziko baada ya kupata chakula na kuongea nao, hii ilifanya wafungwa waliyokuwa wakimchukia wampende na hata kuongea nao kwa urafiki. Kutokana na tabia yake hiyo jeuri miongoni mwa wafungwa ikapungua, alikuwa akijua kuongea nao na kuwafanya wawe watiifu wakubwa kwa Maaskari waliokuwa wakiwasimamia. Kuongea kwake pia kulikuwa ni kwa maasakri waliokuwa na vyeo vya chini ambao walikuwa hawaonani naye mara kwa mara kutokana na mfumo wa utaritibu wa maisha wa hapo gerezani, ASP Nkongo alikuja kuwa askari ambaye alikuwa amevunja rekodi kwenye gereza hilo kwa kukaa sehemu moja na maasakari wa chini yake. Alidiriki hata kuingia kwenye bwalo lao la chakula na kukaa nao, muda mwingine alikuwa akila chakula ambacho walikuwa wakila wao. Aliongea nao kama alikuwa akiongea na mtu mwingine wa karibu naye, kutokana na tabia yake hiyo jina lake lilikaa vinywani mwa wengi sana kila wakati alikuwa akizungumziwa.

    Sifa zake za kulibadili gereza hilo hatimaye zilivuma nje ya gereza na akawa mwenye kujizolea heshima kubwa, vyombo vya habari vilikua vikitaja habari zake kila kukicha na hata ikafikia wanahabari wakafungga safari hadi ndani ya gereza hilo kuja kujionea hali halisi ilivyo. Hakupokea sifa nzuri kutoka kwa Kamishna jenerali Lutonja kutokana chuki ambayo alikuwa nayo, alipokea sifa hata kwa Rais Zuber Ameir ambaye alikuwa akilitembelea gereza hilo. Wafungwa wale waliyokuwa watukutu walikuwa watiifu sana kutokana na kujua namna ya kuishi nao, kwenye maonesho ikiwa sherehe itaandaliwa ndani ya gereza hilo wafungwa walitumika pia kuonesha ujuzi mbalimbali walikuwa nao.

    Mwezi mmoja baadaye hatimaye ASP Nkongo alimvalisha pete ya uchumba Teedy katika sherehe ambayo ilihudhuria na maskari watupu waliokuwa wapo gerezani humo, siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwake na mpenzi wake kutokana kufikia hatua nyingine kabisa ya uhusiano wao. Baraka zote walizipata kutoka kwa Kamishna Mwambe na pia wenzao waliwatakia maisha mema, baada ya kuisha kwa sherehe hiyo lilipita juma moja hatimaye Mzee Andrew akiwa na mke wake walikuja hapo gerezani kumuona binti yao. Siku hiyo nao walizidi kuwa na furaha kumuona binti yao alikuwa amerejewa na hali ya furaha ambayo aliikosa kwa kipindi kirefu, walikaribisha nyumbani kwa ASP Nkongo ambaye alikuwa ni mkwe wao mtarajiwa.

    "Lakini sijapenda mlivyovishana pete kiwizi namna hiyo" Mzee Andrew aliongea wakiwa wamekaa pamoja sebuleni.

    "Umeona Baba Teddy hawa watoto walivyo waone vile" Mama Teddy nay alidakia

    "Dady na Mummy jamani" Teddy alilalamika

    "Jamani nini naona siku hizi umemisi sana kudeka kama ilivyokuwa tabia yako" Mzee Andrew aliongea huku akitabasamu.

    "Haaah! Kumbe na ukubwa huo unadeka" ASP Nkongo naye aliongea huku akiweka uso wa mshangao.

    "Yaani huyu kwa kudeka ndiyo menyewe kabisa" Mzee Andrew alidakia

    "Daddy si nimeacha nimekua mimi" Teddy alionga huku akiziba uso wake.

    "Haya wanangu sisi tunasubiri pilau tule na wajukuu tuwaone lini sasa" Mama Teddy aliuliza

    "Tunafanya mipango hivyo Mungu akitujalia hatutamaliza mwaka huu tayari kila kitu" ASP Nkongo alijibu

    "Sisi pamoja nanyi kwenye kila hatua yenu, James asante sana" Mze Andrew alisema

    "Asante ya nini Baba?" ASP Nkongo aliuliza

    "Umeweza kunirudishia Teddy wangu yule ambaye alipotea miaka iliyopita sina budi nikushukuru" Aliambiwa



    Baba na Mama sina budi niwashukuru nyinyi kwani mmeweza kunipatia Teddy ambaye amenirudisha James yule ambaye nilipotea" ASP Nkongo aliongea huku akiuzungusha mkono wake begani kwa Teddy ambaye alimlalia kwenye bega lake.



    Wazazi hao hawakutaka kukaa muda mrefu kutokana na majukumu waliyokuwa nayo, ilipofika majira ya alasiri Helikopta ambayo iliwaleta hapo awali ilirudi tena na kuwachukua. Waliondoka wakiwa ni wenye furaha kubwa sana kwa kumuona binti yao akiwa yupo kwenye furaha, moyoni walikuwa wakishukuru ana ujio wa James kwenye maisha ya binti yao ambayo yalikuwa yamepoteza dira kutokana na kuathiriwa na maumivu aliyoyapitia kwenye maisha yake.



    Hazikupita siku nyingi rafiki yake James kipenzi ambaye walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu alifika naye kuja kuwaona, ilikuwa ni furaha sana kwa kuweza kuonana na Norbert kwa mara nyingine akiwa nimwenye furaha. Siku huyo walijikumbusha kipindi cha nyuma cha maisha yao walichokuwa wamepitia, ucheshi baina yao uliokuwa umepotea kwa kipindi kirefu cha muda ulirejea tena.







    "Mzee hongera kwa kuopoa humuhumu" Norbert alimpongeza wakiwa wanaongea wawili baada ya kupishwa na Teddy.

    "Asante aisee, vipi wewe huko bado hujaoa?" ASP Nkongo alizipokea pongezi na kisha akauliza.

    "Bdo niponipo aisee"

    "Aaah! Come on unangoja nini?"

    "Bado haijafikia muda muafaka ingawa tayari nina familia"

    "Norbert aisee umri unaenda huo na Norene una mtoto naye na unaishi naye, hebu muweka ndani"

    "Nipo kwenye mpango huo si unajua kila kitu mipango"

    "Aisee najua kwa mtindo huo ile tabia yako hutaacha kabisa"

    "(Norbert akacheka) Aisee wewe yaani hujasahau"

    "Akusahau nani we jamaa unapenda sketi balaa kama ndiyo zinakupa pumzi duniani"

    "Nitapunguza jamaa si unaona umri unakimbia huu"

    "Siyo upunguze uache kabisa na uwe mtu mpya kabisa"

    "Poa poa aisee nataka niwe kama wewe sasa hivi"

    "Ujibadili rangi uwe mweusi kama mimi au vipi?"

    "(Akacheka) Aise James hubadiliki wewe, vipi Wil anaendeleaje?"

    "Yupo poa sasa hivi ila anajuta kwa njia aliyopitia hadi anaacha familia na kuwa gerezani"

    "Keshachelewa tayari sasa, hatoliona jua la uraiani milele"

    Marafiki hao waliopotezana muda mrefu waliweka mazungimzo wakiwa wapo nyumbani, ASP Nkongo alikuwa hajaenda kazini siku hiyo na alikuwa akimpokea mgeni wake huyo. Si yeye tu hata Teddy naye hakuwa ameingia kazini, muda mfupi baadaye Teddy alirejea baada ya kuonga mambo yao mengine. Waliifurahia hiyo siku wakiwa pamoja. majira ya mchana Norbert aliwaaga na kuondoka baada ya kusalimia na Kamishna Mwambe.



    ****

    Hakuna kibaya ambacho hakina mwisho duniani, si kwa ubaya tu kila jambo lina mwisho wake. Ikiwa umebaki mwezi mmoja tu ASP Nkongo na Teddy wapate likizo kwa ajili ya kukamilisha shughuli ya kufunga pingu za maisha, ubaya wa Kamishna Jenerali wa magereza ulifahamika kwa wanausalama wa siri wa EASA na hapo huo ndiyo ukawa mwanzo wa kusakwa. Mambo yalipomzidi kombo alijaribu kutoroka lakini alishindwa kutokana na umakini wa wanausalama hao, alipoona hivyo aliamua kupamba nao kwa silaha aweze kutoroka. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa yeye kupigwa risasi na kufariki dunia, baada ya kifo chake ndiyo mabaya yake yote yalijulikana aliyokuwa akiyafanya. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa mtu kama yeye, habari hiyo ilifika kwa James akiwa yupo kazini. Hakuifurahia wala kuhuzunika kwa taarifa jiyo aliposikia, alishindwa kuifurahia taarifa hiyo kutokana yeye alikuwa na mwanadamu kifo kilikuwa kinamuhsu na pia alishindwa kuhuzunika kutokana na huyo aliyeuawa alikuwa ni mbaya wake. Alikuwa akimchukia sana lakini baada ya kifo chake hicho chuki yake iliisha papo hapo, hakuona sababu ya kuendelea kumchukia. Mazishi ya Kamishna Jenerali wa magereza yalifanyika kwenye makaburi ya Kinondoni na yalihudhuriwa na Kamishns Mwambe tu yeye hakuuhudhuria kabisa. Juma chache baadaye walisahau kabisa na hatimaye siku zilisonga, hatimaye muda wa likizo ulifika na wote wawili wakaenda likizo ambako walikuwa wakienda kukamilisha taratibu zote za ndoa.

    Walipotoka ndani ya gereza hilo kwa mara ya kwanza wakiwa na nguo za kiraia, walieleka jijini Arusha moja kwa moja nyumbani kwa Mzee Andrew. Walipokewa kwa mapokezi makubwa sana kutokana na ujio wao kuwepo taarifa zake kwa tajiri huyo, hiyo ilikuwa siku ya kwanza kwa ASP Nkongo kuweza kufika nyumbani kwa wakwe zake ambao walikuwa matajiri kupitiliza. Furaha aliyokuwa nayo haikuwa ikielezeka kabisa kutokana na jinsi alivyokubalika ukweni, alikaa hapo ukweni kwa siku kadhaa na kisha aliondoka kwenda kwenye nyumba ya mchumba wake ambako walifanya makazi kwa kipindi chote walichokuwa wapo jijini hapo. Hazikupita siku nyingi sherehe za awali zilianza katika kipindi hicho pia Kamishna Mwambe alikuwa ameomba likizo kwa ajili ya kusimamia shughuli hizo. Baada ya majuma mawili tangu shereha za awali kukamilika siku ya harusi iliwadia, ilikuwa ni mara ya pili kwa ASP Nkongo kufikia hatua hiyo na mara ya kwanza kwa Teddy. Hatimaye ndoa ilipita kanisani baada ya wote kuridhia na kutokuwepo pingamizi, shereha kubwa ilifuatia katika ukumbi uliokuwa mali ya Mzee Andrew. Wale wote walikuwa watu wa karibu wa pande zote walikuwa amefika ndani ya sherehe hiyo kubwa ambayo ilikuwa imehudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka na ushawishi aliyonao Mzee Andrew kama mmoja matajiri nchini. Kamishna Mwambe alijikuta akitokwa machozi ndani ya sherehe hiyo kutokana furaha ambayo ilipitiliza, hata alipopewa kipaza sauti aongee aliishia kutoa shukrani kwa Mkwe wake kutokana na kumfanya kijana wake kurudi katika hali ya kawaida.



    "Sina mengi ya kuongea napenda niwatakie kila la heri kwenye maisha yao, mkwe wangu wangu Teddy napenda niseme asante sana kwa kumfanya James kuwa mpya" Kamishna Mwambe aliongea huku akijifuta machozi ya furaha ambayo yalikuwa yakimtiririka huku shangwe zikisikika, baada ya hapo Mzee Andrew naye alishika kipaza sauti kuongea machache.

    "Narudia tena kusema neno lile ambalo niliwahi kukuambia, James asante sana kwa kunirudishia Teddy wangu aliyepotea bila wewe asingekuwa hivi. Sijutii uamuzi wangu wa kukukabidhi jumla Teddy wangu ikiwa umemrudisha, nashindwa hata nikupe zawadi gani kwa hilo kijana wangu. Teddy mwanangu kila la heri mheshimu na umpende Mumeo " Mzee Andrew aliongea na shangwe zikafuata baada ya kumaliza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sherehe kubwa ilipoisha fungate ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwenye hoteli ya Singita ndiyo ilifuata, maharusi waliondoka kuelekea huko hotelini usiku huo huo kwa kutmia ndege ya kukodi ambayo walikuwa wameandaliwa. Walikaa huko kwa muda waliotakiwa kukaa na hatimaye walirejea Arusha tena, walikaa jijini hapo kwa siku kadhaa na hatimaye walirejea kazini baada ya muda wao wa likizo kuanza kuyoyoma. Gerezani napo kulikuwa na shangwe kubwa walipowasili, waliandaliwa sherehe fupi ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia. Waliyaanza maisha ya ndoa wakiwa huku wakiendelea na kibarua chao, Askari jhela aliyepitia mazito aliishi maisha yenye furaha na mke wake wakaanzisha familia.



    MWISHO!!





0 comments:

Post a Comment

Blog