Search This Blog

Thursday, 27 October 2022

AFANDE ANAHUSIKA - 4

 







    Simulizi : Afande Anahusika

    Sehemu Ya Nne (4)





    Swali la Inspekta lilimuelekea Afande Marsha moja kwa moja na kujikuta badala ya kumjibu mkuu wake akabaki akimshangaa, kisha ndio akakumbuka kujibu kuwa hafahamu kama amejulikana na muuaji ama lah!

    “Umeniambia kuwa amekwambia amekuona sehemu ya tukio la kifo cha Loren badala ya kuniona mimi, sasa tambua kwamba aekujua na ili tuhakikishe hilo, ngoja tufanye kitu, twende sehemu,” akamshika mkono kma vile anamburuta na kuongozana nae kuelekea nje kwenye gari moja kati ya gari za Polisi zilizokuwa nje na kumuita dereva waondoke.

    Walikwenda hadi Sinza na kupaki sehemu ya mbali kidogo na nyumbani kwa kina Loren na kuongea na Mwana

    “Marsha wakati ukiingia humu ndani kwa kina Loren, ulimkuta ndugu yake wa kiume aitwae Chidy?”

    “Hapana hakuwepo Chidy na kiukweli tu sikumuulizia, ok hapo una ona kuna watu wamekusanyika, hiyo ni ishara ya kwamba mazishi hayana muda mrefu, kwani maiti yao mmeihifadhi wapi?”

    “Mwananyamala,”

    “Uchunguzi umeisha kamilika?”

    “Ndio asubuhi hii inapaswa kwenda kuchukua majibu hayo,”

    “Hebu kabla ya kwenda huko tuingie mle ndani, nitaomba wewe ubaki kwenye gari ili tu kufuatilia kila ambacho kitakuwa kikiendelea hapa wakati mimi nikiingia ndani, sawa Marsha?”

    “Sawa Mkuu!” Inspekta akashuka na kuelekea ndani ya nyumba ile yenye msiba na kufika kuwasalimia kwanza aliowakuta nje na kisha akawaulizia alipo amam wa Marehemu. Walimuelekeza na kwenda kumpa pole kisha akawaomba watu faragha kwa dakika zisizozidi tano.

    Wakatoka wote na kuwaacha wao tu wawili, kisha hapo ndio mahojiano yakaanza, alimpa pole tena kwa mara ya pili kisha akamuuliza ni wapi walipouona mwili wa marehemu? Mama akajibu kwamba mwili ulionekana maeneo ya jirani tu pale.

    “Mama wewe ulienda kuushuhudia?”

    “Baba yangu wee… hata nilipata nguvu basi? Lakini nilishuhudia tu mavazi yale aliyotoka akiwa amevaa, ndio ambayo niliyaona na kumtambua mwanangu,” mama akaanza kulia, Inspekta akampoza na kumuhakikishia tu kwamba watampata muuaji siku chache zijazo.

    Naweza kumuona wapi Chidy?Maana hapo nje hata sijamuona?”

    “Mwanangu, Sijui mimi nina balaa gani? Chidy nae katoweka tangu jana usiku hata kabla ya mwili wa ndugu yake kuonekana,”

    “Mama unasema?” Inspekta alipata mshangao mkubwa sana kufanya mama azidi kuangusha kilio.

    “Ndio hivyo mwanangu, Sijui nae kimempata kipi!” alitoka anaenda wapi?” alitoka hapa akisema anaenda Polisi kuonana na Inspekta mmoja ambae pia anampelekea funguo yake,”

    “Alikwambia funguo hiyo aliipata wapi?”

    “Ndio, alisema amepewa na jamaa yake na huyo askari ambae amemwambia amuwahishie kabla hajatoka kazini,”

    “Sasa alikwambia ilikuwaje akampa yeye,”

    “Kama ulikuwepo mwanangu, name nilimuuliza hivyo akajibu kwamba huyo amtu anasema aliwaona pamoja ana ndio akaomba msaada huo, baada ya hapo akaondoka,”

    “Alipoondoka hapo ndio hajarudi hadi sasa?”

    “Ndio baba yangu, Sijui yupo wapi? Yeye hiyo sio kawaida yake, ni heri hata Loren ambae huwa anapitisha hata wiki mbili, lakini Chidy wala sio kawaida yake,”

    “Basi mama acha mimi niende, nafikiri huu ni muda sasa wa kwenda kuruhusu maiti ya Loren ije nyumbani kwa mazishi huku nasi tukiendelea na taratibu zingine, pole sana mama yangu,” akanyanyuka na kutoka akiwa hajielewi, moja kwa moja hadi nje na kuwaaga wale aliowakuta pale kisha akaelekea garini.

    Alipoingia tu ndani ya gari akakkumbatia kichwachake kwa mikono yake na kusema

    “Ah! Kwanini lakini?”

    “Vipi Inspekta?”

    “Dah!Kwanza hebu nieleze usalama hapa ni vipi?” alisema huku akimkata jicho Marsha.

    “Usalama upo vizuri tu ila hapa kuna mtu ninamuhofia, yulee alievaa T sheti na Pocket, amekuwa akingea na simu tangu uingie, pia amesogea hadi hapa ilipo gari, nikamwambia dereva atoke na kujidai anafunga mlango.”

    “Ili ajue kuwa hakuna mtu si ndio?”

    “Yah! Nilitaka kumuona ni lipi lengo lake, dereva huyo akaondoka na kuelekea dukani, huku nyuma huyo jamaa akaja na kusogea kabisa jirani na gari na kulizunguka huku akiongea na simu,” alimeza mate na kumalizia

    “Kisha akarudi huko akiwa amemaliza kuongea na simu yake hadi tena wewe ulipotoka nje nae ndio akaanza kuongea tena na simu,”

    “Anhaa!Kwa picha hilo ulilolisema wewe, ina maana sasa tambua kwamba sasa hivi tutaanza kufuatiliwa, wanajipanga hao, piga ua!”

    “Dah! Hapo Inspekta umenifungua akili sasa,” Marsha akawa kama alieshituliwa.

    “Tuwe makini tangu sasa, Dereva zidisha umakini wako muda huu, tunaelekea moja kwa moja Mwananyamala hospitali,” wakati akiwa anatoa maelekezo hayo, simu ya Marsha ikaita, ajabu wote wakamtazama Marsha, nae akama mtu alieiogopa simu ile, akaitazama tu hadi Inspekta akamuuliza vipi?

    “Hii namba ni ya simu ya mezani, halafu ni ngeni kwangu!” wakawa kama wameshangaa hivi.

    Simu ile iliendelea tu kuita kwa fujo vilevile. Inspekta akamwambia pokea, Marsha akapokea kwa hofu kidogo, aliepiga ndio aliesalimia na kumuuliza Inspekta imekuwaje simu inaita kwa muda mrefu vile?

    Akajitetetea kwamba alikuwa yupo mbali na simu hiyo.





    Inspekta akamwambia kwa ishara kuwa iwapo aa wasiwai na simu ile basi aweke ‘Loud Speaker’ ili wamsikie wote, nae kwa kuwa tayari alikuwa na hofu, akaweka hiyo sauti ya nje.

    Aliepiga alikuwa ni dakatari wazamu wa hospitali ya Mwananyamala, aliesimamia uchunguzi wa kifo cha Loren, na sasa alitaka kujua kuhusu kuiruhusu maiti ichukuliwe na ndugu wa marehemu ama bado kuna shida nyingine?

    Inspekta Kalindimya akamwambia huku akipunga mikono kwamba hapana, asiruhusu kabisa maiti kutoka, nae akamjibu hivyo na kumwambia wawaambie ndugu wa marehemu wasubiri kwa nusu saa nyingine.

    Daktari akakata simu na wao wakaanza kuondoka maeneo ya Sinza na kuelekea hospitali ya Wilaya ya Kinondoni, Mwananyamala huku akiwa makini kuangalia kama wanafuatiliwa, kuna wakati alifanya makusudi na kumwambia dereva akatishe kulia ama akushoto tofauti kabisa na waendako.

    Alifanya hivyo maksudi ilimradi tu kujua kama wanafuatiliwa na kidudud mtu chochote, lakini akaona kama hawafuatwi, wakaelekea moja kwa moja Mwananyamala Hospitali na huku akimuhadithia Marsha yaliyojiri mle ndani.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Marsha alishangaa mno, hakuweza kuamini kile alichokisikia, na kuuliza kwa mara nyingine

    “Ina maana hata na Chidy nae ametoweka? Kuna siri gani hapo kati?”

    “Ndio hapo sasa!” wakawa tayari wamewasili kwenye geti la hospitali na Inspekta akamwambia dereva yeye anashuka na Marsha atangulie moja kwa moja kwa daktari huyo kwa ajili ya kuchukua majibu.

    Alidhamiria kujua ni nani anae wafuatilia na kama bado anaedelea, ndio maana akashuka pale, lakini hakugundua lolote, taratibu akaendelea kusogea na kutoa simu na kumpigia Marsha.

    Alimwambia amchukue daktari na kuelekea nae Murtuary watamkuta huko kwa ajili ya kuukagua mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho kabla hawajaukabidhi kwa nduguze kwa ajili ya mazishi.

    Akajivuta taratibu hadi kwenye jingo la kuhifadhia maiti na kuwaona kwa mbali makundi makundi kadhaa ya watu yakiwa yamesimama kwa kujitenga, lakini ilionekana dhahiri kwamba kuna jambo wanasubiri.

    Hilo sio lililompeleka pale, lakini alijaribu tu kutafuta sura anayoijua ili aweze angalau kumsogelea na kupiga nae story ili kuvuta muda, lakini hakumuona pia muda.

    Alitazama saa tena na kuona kama muda unazidi kwenda, akaamua kusogea kabisa mlangoni kwa Mhudumu wa maiti na kumsalimia, akiwa anamuuliza amsaidie nini, ndio kwa mbali akawaona Daktari akiwa ameongozana na Marsha wakisogea eneo hilo.

    Alijitokeza nje baada ya kuona simu yake ikiita na kisha akanyoosha mkono kwa Marsha aliekuwa akimpigia na kurudi ndani.

    Waliwasili na kuungana nae huku wakiwa wamesimama, daktari huyo hakuwa mgeni kwa Inspekta na wala Inspekta hakuwa mgeni kwenye macho ya Inspekta, walikuwa wakitambuana maana walikuwa wameisha fanya kazi nyingi sana.

    Baada ya salamu na kujuliana hali, Marsha alimwambia mkuu wake kuwa daktari ameisha mkabidhi ripoti ya uchunguzi wao na inaonesha tu kwamba marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani na kisha akakabwa shingoni na kisha akachomwa na kitu chenye ncha kali.

    “Doh!Daktari hakuna sumu iliyohusika pia?”

    ‘Hapana hatujaona athari yoyote ya sumu bali tulichokiona ni hicho tu tulichokiandika Inspekta,” alijibu daktari kwa kujiamini huku akijitikisa pale aliposimama.

    “Ok! Naweza kuiona maiti sasa hivi?” alimuuliza huku akimtazama, daktari akasema sawa, na kumuita muhudumu aliekuwemo mle na kumtaka kuwaongoza kwa maiti ile.walifika na kuvutiwa droo yenye maiti ile na kuiona.

    Muhudumu alisogea nyuma kidogo na kurejea na Gloves kama pea nne tofauti na kuwapa wote, wakazivaa ila tu daktari ambae alikuwa tayari mikononi ana gloves zake.

    Waliifunua na hawakushughulishwa sana na sura, kitu cha kwanza walichokihitaji ni pale kilipoingia kisu, walipoiona sehemu hiyo, wakatazamana Inspekta Kalindimya na Afande Marsha kisha akasema Inspekta kwamba tundu la kisu inaonesha kuwa safari hii hakikutumika kisu kidogo kama vile ambavyo vimekuwa vikitumika awali.

    “Ndio hata name hilo nimeliona, inaonekana ameamua muuaji kubadili mbinu,”

    “Ok! Tuapaswa kuongeza nguvu ya kumsaka huyu muuaji,” aliongea Inspekta akisogea nyuma ishara ya kuonesha ameridhika juu ya kile alichokuwa akikihitaji sasa amekiona, Marsha akamwambia muhudumu awape tu watu wenye maiti ile.

    Daktari akawaambia kuwa wakati wakifanya uchunguzi wamegundua kuwa sehemu ya sikio ya marehemu ilikatwa kidogo na kuwekewa dawa ya kukata damu, inspekta akaiomba tena maiti aione sehemu hiyo.

    Ikavutwa tena maiti na kufunuliwa toka kwenye mfuko wake maalum wa kuhifadhia maiti na hata kabla hawajaenda mbali zaidi, Inspekta akashtuka na kuguna kwa nguvu,

    “Ah! Huyu ni Chidy bhana, japo simjui Loren lakini huyu ni Chidy Marsha,” alisema huku akizidi kumtazama vizuri, Marsha nae akamsogelea zaidi na kumuweka sawa uso ukimtazama yeye.

    “Of Cuz ni kweli, kwani Chidy na Loren ni watu wawili tofauti?”

    “Yaah! Hao ni ndugu wawili tofauti,” alisema huku akivuta zipu kumfunika marehemu pasina tena hata kuliangalia hilo sikio lililokatwa.

    “Lakini mimi Sijui Chidy ni yupi na Loren ni yupi,” alijitetea Marsha







    “Loren ni mtu aliepotea awali na Chidy ni nduguye aliepotea jana tu baada ya kuleta funguo kituoni,” alifafanua Inspekta Kalindimya

    “Shit! Huyu ndio alieleta funguo, hilo mimi mbona nalijua?”

    “Sasa alieleta funguo kwako, sio tunaemtaka sisi, maana huyo ndio mtu alieleta simu pia kwangu, alikuwa ni kiungo kwetu,”

    “Kwa hiyo alieuawa ni huyo alieleta funguo, si ndio mkuu?” alihoji Marsha akimtazama mkuu wake kwa umakini mkubwa.

    “Ndio! Sasa inaonekana kabisa kuwa tumerudi nyuma Marsha,”

    “Tena ni zaidi ya hata pale tulipokuwepo, kama huyu ni Chidy, ina maana Loren yu hai, iweje nguo zake avae ndugu yake?” wakamuaga daktari na kuondoka haraka eneo lile kurejea nyumbani kwa kina Loren.

    Njiani walijadiliana sana. Inakuwaje tena mauaji yahamie kwa mtu huyu mwingine ambae hahusiki? Tena ilionesha dhahiri kwamba Chidy alikuwa akimpenda sana mdogo wake maana aikuwa akiumizwa sana na kutokuonekana kwa mdogo wake.

    Huenda kuna siri kubwa hapa kati juu ya familia hii, ni kwanini Loren tu? Sasa hadi nguo? Dah!

    “Kwani wakati ametoka kwako kukuletea funguo alikuwa na mavazi ya aina gani?” alihoji Inspekta.

    “Alikuwa amevaa Tsheti moja nyeusi na Jeanz ya bluu, hakuwa na mavazi hayo tuliyo yaona,” alijibu Marsha.

    Safari hii tena waliingia wote hadi kwa mama wa marehemu na kumwambia muda sio mrefu maiti itawasili pale nyumbani, lakini wana maswali machache.

    “Mama unasema ulimuona Loren wakati wakiubeba mwili wake kuingiza kwenye gari, alikuwa amevaaje?” swali hilo ndio lilikuwa la kwanza na mama kataja nguo zile zile ambazo amekutwa nazo marehemu huko hospitali.

    “Je wakati akiwa ameondoka hapa alikuwa maevaaje?”

    “Hivyo hivyo ndio alikuwa amevaa,” wakaona kama vile wamemaliza maswali yao, sasa ndio wakampasulia kuwa wana imani kwamba maiti illiyo patikana pale sio ya Loren

    “Ni ya nani?” mama aliekuwa akilia kwa taratibu, sasa akanyamaza na hata kabla hajaelezwa ni maiti ya nani, akaingia dada mmoja akilia kwa sauti ya huzuni sana, mkononi alikuwa ameshika simu ndogo, inaonesha kama simu hiyo ndio ilimpa taarifa hiyo na kumtaja Chidy huku akimsogelea mama Loren

    “Mama eeeh, kaka yangu mimi… Mama ni kaka Chidy ndio amefariki,” mama hakusema kitu wala hakujibu lolote, palepale akaanguka kimgongo mgongo na kuzimia.

    Kwa haraka tu Inspekta akamwambia Yule aliekuwa akilia kwamba wamnyanyue na kumpeleka sehemu yenye hewa zaidi na kumpepea. Dakika chache mbele akazinduka na kuanza kulia kwa kelele zaidi ya awali.

    Inspekta na Marsha wao wakatoka wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, wakiwa garini sasa walithibitisha kuwa muuaji huyo amejipanga.

    “Ujue huyu mtu habahatishi, huenda kuna mtihani alipewa Chidi na kushindwa kuutimiza sasa ndio hatma imekuwa hii, hawa wauaji ni watu wabaya sana,” aliongea Inspekta, dereva akamuuliza ni wapi wanaelekea? Marsha akamwambia waende moja kwa moja kituoni.

    Wote walikuwa kimya tu garini, Inspekta akaanza kujumlisha vile vifo na matukio jinsi yanavyotokea, alishindwa kabisa kupata picha ya matukio hayo.

    “MwanaHamisi alianza, akafuatia MwanaHeri na sasa Chidy, mbona nahisi kama Loren anahusika kwa asilimia mia moja bila kupepesa?” aliwaza Inspekta na wakati huo Marsha nae alifikiri

    “Huyu Inspekta nae amenichanganya sana, amemjuaje Chidy na kumgundua mapema mno wakati amemuona mara moja tu kama mimi? Ama ni kweli huyu mtu anahusika? Mbona nakuwa njia panda?Sasa kama kweli anahusika ni lini tutafanikiwa kumtia nguvuni?”

    Wakiwa katikati ya mawazo, dereva alisimamisha gari na kuwajulisha kuwa wamefika, lakini hakukuwa na hata mmoja ambae alimsikia, wote walikuwa mbali, akamgusa Marsha na kumwambia wamefika.

    Marsha alivyoshtuka ikawa na sababu ya Inspekta nae kuamka toka kwenye mawazo aliyokuwa nayo. Wakashuka na kuelekea ofisini, hawakukaa sana wakaagana kila mmoja kisema anaenda kupumzika wakati huo Inspekta akiwa wa kwanza kuondoka.

    Aliwasili nyumbani kwake na kwenda kujitupia kitandani, akakumbuka kuwa bado hajaoga, akaenda kuoga na kula kabisa, safari hii aliagiza chakula kupitia mmoja wa wale askari walinzi waliokuwepo pale.

    “Tunapaswa kuwa makini mno na maagizo tunayopokea, kosa moja magoli milioni, acha tu nitii sheria bila shuruti, nimuagize msosi jamaa nikaoge mimi, hadi nikimaliza nae atakuwa ameisha rejea,” aliwaza hivyo na kweli akatimiza.

    Akiwa mezani anakula, akachukua tena diary yake na kuanza kupitia tena siri za zile namba na kujumlisha na majina ya wahanga wa vifo vile. Hakuweza kuambua chochote. Bado ilikuwa ni mtihani kwake, akajikuta amechoka na kutokana na usingizi wa usiku uliopita aliokuwa kororkoroni, akalala mezani.

    Alishtuka usiku mnene na kuhamia kitandani kwake kulala. Wakati nae akiwa hivyo, Marsha nae alikuwa yupo macho akihangaika kufumbua fumbo lile la vifo, yeye kwa upande wake alikata tamaa mapema juu ya utafiti wa zile namba, kilichotokea ni kuanza kufuatilia nyendo za Inspekta kupitia namba yake iliyopo makao makuu ya Polisi.







    Ikapita wiki mzima pasina tukio lolote kubwa kutokea, siku moja wakiwa Inspekta Kalindimya na Afande Marsha wameketi sehemu moja wakipata kinywaji baada ya kutoka nyumbani kwa kina Loren, simu ya Inspekta ikaita.

    Inspekta akaiacha ikaita hadi ikakata na hata Marsha hakujua ni kwanini amefanya vile mkuu wake wa kazi. Ilipokata tu akamtaka Marsha anyanyuke na kuelekea nje

    “Twende Mwananyamala tukazihakiki zile Call box kama bado zipo salama, sina imani maana huyu mpumbavu anaendelea kucheza nasi tu huku wala hatumuoni kama ambavyo tulipaswa kuwa tunamuona,”

    “Lakini sasa mbona hujapokea hiyo simu mkuu? Huenda ana habari muhimu huyo,”

    “Marsha, ni mapema mno kwa wewe kulaumu, ni kwa vile bado hujakomaa katika kazi hii, kuna wakati unapaswa kufanya hivi ili mambo mengine yaende sawa, najua kwa sasa hutonielewa, ila tu siku chache mbele utajua,” wakiwa wanatoka nje ya hoteli hiyo, Marsha akaomba aoneshwe tu maana yake.

    Kwanza pale ni hotel na simu huyu jamaa anapopiga tanmbua kabisa kwamba ina tukio, ndio maana nimekwambia tuondoke,” kauli zile tata ndio zikazidi kumchanganya Marsha na kujiuliza tena ina maana ni kweli afande anahusika? Mbona anakwepa kuwasiliana na muuaji na ikiwa ni yeye ndio aiepiga?

    “Kifupi sasa hata name imani yangu kwa afande inazidi kupungua kama mvua inavyo pungua kiangazi,” aliwaza Marsha na kunyamaza huku akiingia ndani ya gari kwa upande wa abiria.

    Safari ikaanza kuelekea maeneo ya Mwananyamala, maana namba ile iliyotumika sasa ilikuwa ni ile ya Hospitali, sehemu ambayo Inspekta alitegemea kwamba jamaa akiingia tu yeye atajua lakini sasa hadi anapiga simu yeye huku hajui hata kidogo, akahisi kuna walakini.

    Walifika hadi kwenye Call box ya kwanza ya Maeneo ya Kwa mama Zacharia, walikuta mfumo mzima upo lakini haukuwa salama, Camera ilikuwepo, ila sehemu ndogo sana ya kipande cha waya hakikuwepo, waya ambao ulitumika kama antenna ya kurusha picha, ndio ulikatwa.

    Akaichukua Camera yake ikiwa haina kazi tena, kwa hasira akafyonya na kutoka kurejea garini ambapo alimkuta Marsha na kumuonesha, Marsha kwa kuwa nae sasa hakuwa na imani na Bosi wake, alimtazama tu na kujishangaza kidogo tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamini kabisa anachokifanya Afande sasa ni hadaa tu, kwani hawawezi kufanikiwa lolote iwapo tu Inspekta ataendelea kufanya mambo ya ulaghai kwa jeshi.

    “Hali ndio hiyo, sasa hebu twende A kisha tumalizie Hospitali, huenda huko tukapata pata,”

    “Inspekta, mimi sidhani kama tuna haja ya kwenda huko kote, maana ni kama tu tunakwenda kupoteza muda,” aliongea kama mtu aliekerwa na jambo hilo.

    “Marsha? Kwanini unasema hivyo?”

    “Inspekta mimi nahisi kuna mchezo tu unafanyika hapa huku tukipiga Mark time, tunaonekana tukifanya kazi lakini kumbe hakuna tunacho kifanya,”

    “KIVIPI Marsha? Hebu nielezee vizuri,”

    "Nina wasiwasi kuwa kuna usaliti kati yetu, maana kila tunapopiga hatua, tunajikuta tumerudi nyuma, hivyo miki binafsi sina imani na sisi wenyewe,"

    "Ni nani unahisi anafanya usaliti?"

    “Siwezi kujua bali ni mtu wetu tu wa karibu, inavunja sana moyo hali hii,"

    "Marsha kwakanuni za kijeshi hupaswi kukata tamaa na unapaswa kupambana mwanzo mwisho, hadi utakapomtia mikononi adui yako, usioneshe udhaifu wako kwa wenzako bali onyesha ujasiri wako kwa wenzako," alimtia moyo na kuwasha gari kuelekea Mwananyamala A.

    Huko napo kulikuwa na Call box nyingine ambayo waliitegesha Camera na mic ndogo. Walitegemea angalau vyenyewe watavikuta vikiwa salama, lakini wala haikuwa hivyo.

    walikuta uharibifu ukiwa umefanyika kwa kiwango kilekile cha Call box ile ya kwa mama Zacharia. Marsha alitaka kuzungumza kitu lakini akahisi atamkwaza mkuu wake wa kazi, akanyamaza hadi walipofika Mwananyamala hospitali.

    Inspekta akashuka tena peke yake na kwenda kufanya yake. akarudi akiwa na hasira hadi garini na kujitupia huku akilaumu kuwa ni hatari sanaa.

    Akageuka Marsha na kumuuliza vipi? nae akajibu hali ni ileile tu haina tofauti na vile za kule.

    "kwani Inspekta ulihisi kutakuwa na utofauti wowote kati ya hizo Call box?" swali likuwa ni la kebehi na hata Inspekta alielewa hivyo lakini wala hakuonesha kupanic balia lisema kwa hali iliokuwepo pale alitegemea itakuwa hivyo.

    Akawasha gari na kuondoka wakiwa wameelewana waelekee moja kwa moja kituoni kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya mipango mengine.

    Marsha alidhamiria kumchunguza zaidi bosi wake...

    "huenda mara ile ya kwanza nilikurupuka kama alivyosema mkuu, sasa napaswa kufuatilia kila step yake anayopiga, hakika mimi sasa nita deal nae tu!" aliwaza hadi wakiwa wamekaribia kituoni.

    Walishuka na kuelekea ofisini, wakiwa wameketi tu, Marsha akanyanyuka na kuelekea nje ambapo alielekea nje ya ofic yao na kuingia kwenye ofisi ya watu wa mahusiano na habari, akawaomba mawasiliano ya nambaya Inspekta.

    Mkuu wa zamu akampa na kuipitia, hakuona namba yeyote tofauti na zile ambazo zilipigwa wakiwa pamoja. aliporidhika hapo akachomoka na kuelekea ofisini kwa RPC ambapo huko napo akamkuta akiwa na RCO.

    Walipomuona wakamuuliza vipi? kuna mpya gani? Akawaeleza kila kitu juu ya hisia zake kwa Inspekta

    "Halafu wewe Afande ni mwenda wazimu eti? We si ndio ulimtetea na kusema hahusiki? Sasa imekuwaje?" RPC alimuhoji kwa mshangao.

    "Hapana sasa nimegundua kupitia baadhi makosa anayofanya kama hayo niliyo yaeleza kwenu,"

    "Ujue mimi sikuelewi, sasa unachotaka ni nini?"

    "Nataka nimchunguze yeye wakati akiendesha kesi hiihii, hivyo ningependa mimi nijiweke pembeni ili nipate wakati mzuri zaidi wa kumchunguza Inspekta," wakatazamana RPC na RCO na kukubaliana kuwa swala lake ni la msingi sana.

    "Wazo lako zuri sana unataka tufanyejesasa? Hebu kuwa miwazi," alisema RCO huku akitegemea Marsha kutoa wazo lake.

    "Naomba nikabidhi jukumu hili kwa Inspekta ambae nashauri asaidiane na Afande Jitu ambae nae asijue kama nawachunguza," alimaliza Marsha na wao wakajadiliana kidogo kabla ya kukubaliana kuwa anachosema Marsha ni sahihi, wakamwambia aende kumkabidhi faili hilo na amwambie Jitu juu ya mabadiliko hayo pia Inspekta nae amjulishe.

    Akasimama na kupiga saluti kisha akatoka na kuwaacha wakiwa wanajadiliana juu ya kile ambacho amewaeleza.

    "Kamanda, kwanini tufanye kazi na mtu ambae ana tuhumiwa kuhusika na kesi anayoisimamia? Huoni kuwa tunakuwa tunaleta tatizo lingine?" aliuliza RPC.

    "Ujue kwamba Kati ya vijana wanao aminika kwa kitengo changu, basi yeye ni namba moja na namba mbili wake sijamuona, ninaamini kabisa anahusishwa tu, hebu tumuache afanye kazi wakati huohuo Marsha atatujibu,"

    wakakubaliana hivyo na kutoka wakiagana kwa ahadi ya kuendelea kuwasiliana.





    Marsha alipotoka pale moja kwa moja akaelekea kwa Inspekta Jitu na kumkuta akiwa ameketi peke yake akifunua makabrasha yake, alimsalimu na kumpa taarifa toka ngazi za juu, alipotaka kujua ni kwa sababu gani yeye amejitoa? Marsha akajibu kwamba

    “Inspekta hata sielewi niseme nini, bado mimi sina imani na mtu miongoni mwetu,”

    “Kwamba tunasalitiwa?”

    “Ndio Jitu, naona kabisa kuna wakati mambo yanakuwa mazuri lakini ikifikia tu sehemu za kuelekea mwishoni mambo yanaharibika na kuparaganyika kabisa, yaani nachoka kabisa,”

    “Sasa ukisikia upelelezi ndio huo, ingekuwa ukifika tu unamaliza, huo sasa sio upelelezi huo ni ukamataji, na hiyo ni hatua ya mwisho na pia amini tu kuwa tuataifikia,”

    “Sio kwa mwendo huu Inspekta,”

    “Afande kwa nidhamu za jeshi unafanya makosa sana kukata tamaa, hupaswi kukatishwa tamaa na jambo lolote, songa mbele hadi dakika ya mwisho,” alimpa moyo Marsha bila kujua kuwa mwenzie ana duku duku sana na Inspekta Kalindimya.

    “Hebu niambie ni nani ambae unamshuku,”

    “Siwezi kubashiri wala kufanya utabiri lakini tambua kuwa kwa njia ya kutazama tu mwelekeo sina imani na Inspekta Kalindimya,”

    “Kwanini labda?” alimuuliza huku akikunja faili lake na kumtazama kwa umakini zaidi ya ule wa awali.

    Marsha akamueleza juu ya tukio lililotokea Mwananyamala tangu mwanzo

    “Yaani nilikaa kimya tu kwa kuwa ni bosi wangu na hata tulipokuwa tumekosa pale sehemu ya kwanza, Inspekta akawasha gari na kuelekea A kwenye Call box nyingine na kukuta mazingira yaleyale na kumalizia ile ya mwisho iliopo maeneo ya Hospitali.” Jitu alikuwa akimsikiliza tu

    “Kote hali ilikuwa ni sawa, hakuna sehemu yoyote ambayo Camera zilikutwa salama, kote zilikutwa zikiwa zimeharibiwa lakini zimeachwa, ila sehemu moja ambayo aliitumia mhalifu kutupigia tukiwa nae, na hakupokea, hapo Mic hazikukutwa kabisa,”

    “Sasa Marsha huoni kuwa ungekuwa nae karibu zaidi ungeweza kumpatia kiulaini zaidi?”

    “No! Mkiwa nyinyi ndio mnawajibika mimi nitawafuatilia kwa ukaribu na lakini pia nitakuwa na chanzo kingine cha habari,” akatabasamu

    “We mwendawazimu kweli, yaani unigeuze mimi kama mic yako ili upaze sauti?” nae akacheka.

    “Nataka nikutumie, maana wewe unaweza kuona pia point muhimu za kumtia hatiani, mi hakika sina imani nae kabisa na sasa hivi naenda IT room kuwasiliana nao, wamfungulie kila kitu kwenye simu yake na ikiwezekana wamuingizie Data,”

    “Ok! Fanyeni hivi, nyie mawasiliano yake yote yapitie humu kwanza…”

    “Tayari hilo mbona? Yaani imebaki tu utekelezaji best,” alimaliza Marsha huku akisimama na kujiandaa kutoka.

    Inspekta akaingia na wote wakasimama na kumpa saloot kisha akawasemesjha kwa kuanza na Marsha

    “Nimesikia umebadilishiwa kazi? Amenipigia simu RCO muda huu, vipi lakini kuna usalama ama kuna tatizo?” alimuuliza huku akimtazama, nae akajichekesha na kujibu ni salama.

    “Basi sawa, umeisha mkabidhi kila kitu?”

    “Ndio nilikuwa nampa hapa Mkuu!”

    “Sawa, ulikuwa unatoka?”

    “Ndio mkuu, natoka sasa nafikiri ni hadi baadae,”

    “Ok! Sasa we unaweza kwenda, name nataka kuongea kidogo na Jitu hapa,”



    Hapo ndio Marsha alikuwa akipataka, alitamani sana kujua ni nani aliepiga simu nje ya Yule mtu ambae Inspekta hakupokea. Akaelekea moja kwa moja kwa watu wa IT kujua kama anaweza kumtambua mtu huyo.

    Inspekta alipoketi akamwambia Jitu kuwa yeye alikuwa ni nyuma ya wakati, akamueleza baadhi ya matukio muhimu na kumtaka aseme nae wanajipanga vipi? Jitu akajitetea kuwa apewe muda.

    Lakini hata hivyo wakapanga siku ifuatayo asubuhi waende nyumbani kwa kina Loren kwa ajili ya uchunguzi zaidi hasa ukizingatia kwamba hawajarudi tangu waliyo ondoka siku ya msiba na hawajarejea tena.

    “Inspekta Jitu nashauri wewe uebnde peke yako ili kujua kama unafuatiliwa ama lah, maan inatambulika fika kwamba mimi najulikana,”

    “Umelenga nini kusema hivyo?”

    “Nataka nijue chanzo cha kuvuja upelelezi wetu, ni mtu wa ndani ya nyumba ile ama kuna chanzo kingine? Sasa wewe uende na kuingia bila kukaa muda mrefu, hapo tutajua, ama unasemaje?” Jitu akafikiria kwanza.

    Nae alipata kama wakati wa kujiuliza, ni vipi akatae kwenda yeye Inspekta ambae anajulikana na anataka aende yeye mgeni? Tayari Alisha jengewa shaka ya kutokumuamini Inspekta Kalindimya, Marsha alimuathiri kisaikolojia.

    “Inspekta kwa kuwa wewe tayari unajulikana kuwa ni nani, ni kwanini usiende na kutoa nafasi ya kuwatisha, kwani ni lazima wajiulize na hapo ndio watakurupuka,”

    “Huenda hujanielewa, ninachotaka mimi ni kupata chanzo cha kujulikana kwetu, Marsha tayari wamemuona japo wamehisi ni askari, ila walijuwa ni kama labda wa zamu tu, maana mtuhumiwa alipiga simu kunieleza juu ya kukosekana kwangu, kwenye tukio la mauaji ya kaka yake Loren,” alieleza kwa urefu.

    Ilionekana kama Jitu ameelewa lakini alikuwa na swali ambalo pia alishindwa kuliuliza, alitaka kumchana mkuu wake, lakini akaogopa na kumuuliza ni nani alimuuliza swali hilo?

    Akajibu ni mtuhumiwa na hapo Jitu akatikisa kichwa na kusema…



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Nimekuelewa Inspekta, lakini kwa maelezo tofauti mliyonipa, inapaswa kujipanga hasa kabla ya kukurupuka na kuna mambo inapaswa tujue sisi binafsi tu na yeyote asijue tofauti nasi,"

    "Na hiyo ndio huwa ni kawaida ya kazi hii ya upelelezi Jitu," alimaliza na kuaga kwamba wataonana siku ifuatayo asubuhi na mapema wakutane hapo.

    Inspekta akatoka na Jitu akabaki ndani peke yake na kumtaarifu Marsha juu ya uwpo wa safari ya kuelekea nyumbani kwa kina Loren asubuhi ya siku ifuatayo, kisha akampa na mipango yote ilivyo huku akimsisitiza kuwa makini.

    *********-



    Walifika nyumbani jwa kina Loren na kukaribishwa vizuri tu lakini ikiwa nyumba ni yenye simanzi sana, kila mmoja alionekana ni mtu mwenye huzuni mno, siku iliyopita walikuwa wamepanga aingie Inspekta Jitu peke yake, lakini kwa ushauri wa Jitu wakaingia wote.

    Waliketi kwenye viti vya ofisini 'Office Chairs' ambavyo vilikuwa uwani sehemu ya wazi na kutaka kuonana na mama yake marehemu, wakaambiwa yupo ndani amelala kwani hali yake sio mujarrab.

    Hali yake tangu kifo cha Chidy, ilipoteza mwelekeo na kuwa ni ya mashaka matupu, mara kichwa kinamuuma wakati mwingine anahisi presha, hiyo ndio ikawa ni hali yake.

    Sasa ikalazimu wafanye mahojiano na dada wa marehemu na kumswalika maswali mengi ya kutosha, lakini majibu yake yalionesha kutokujua lolote juu ya kifo cha ndugu yake.

    Nusu saa tu iliwatosha kuendelea kuwepo ndani ya nyumba ile, hivyo wakati inatimu saa tano asubuhi, nao wakawa wanatoka kuelekea ofisini kwao wakiwa hawajaambulia chochote.

    Wakatoka na kuendelea na shughuli zao mbalimbali wakiwa pamoja garini huku waki discuss juu ya mauaji hayo na muuaji ni nani. Kila walipokuwa wakifikiri na kujitahidi kumtafuta lakini wala hawakufanikiwa kupata walau fununu.

    Walirudi ofisini nakuendelea na uchunguzi wa kwenye faili lakini hawakuambulia lolote, walitamani tu siku iishe tu ili warudi majumbani mwao wakapumzike na kujipanga upya.

    Saa 10 jioni ilipotimu, afande akawa ni mtu wa kwanza kusimama ili kuelekea nyumbani huku akifuatiwa na Jitu ambae alitaka lift, wakatoka wakiwa wameisha funga ofisi na kuelekea nje ilipo gari.

    Kitendo cha kuingia garini tu, simu ya Inspekta ikaita. Gari ilikuwa iendeshwe na Jitu kwani ndio alikuwa na funguo ya gari na tayari alikuwa ameingia upande wa dereva, Inspekta akamzuia kuwasha kwanza.

    "Jamaa tena huyo," akasema huku akimuonesha simu, kisha akatoa headfones na kuvaa sikio moja na upande mwingine akampa Jitu ndio akapokea simu kwa utulivu mkubwa.

    Mpigaji alipopokelewa simu yake akaongea bila papara na kumpa hongera Inspekta kwa kuwatembelea siku hiyo, Inspekta akamwambia anaona kabisa kwamba wala hana jipya kwa siku ile.

    Jitu akashangaa na kujiuliza tena imekuwaje? Mpigaji nae upande wa pili akacheka kwa sauti ya juu baada ya kauli ile ya Inspekta na kusema kwamba yeye hakosi jipya,

    "Inspekta kila.ukiona simu yangu, ujue kuna kitu kipya," si inspekta Kalindimya wala Jitu walio ijibu kauli hiyo, wote walikuwa kimya wakimsikiliza kidume akitamba.

    "Muda mchacheujao, mwandishi wa habari na mfanya biashara mjasiriamali nitachukua pesa yake ili tu kukuonesha kuwa ninaiweza kazi na kwa kuwa hutaki kunielewa ninapokwambia kwamba achana na kazi hii nawe hutaki, sasa utawaponza wengi," aliongea kwa kujitapa.

    "Kwa hiyo kwa sababu mimi nimekataa kujiondoa kwenye kazi hii ndio unaua raia wasio na hatia?" aliuliza Inspekta kwa kebehi.

    "Hakuna hasira hapo, kwa kuwa wewe ni jeuri acha tu tuucheze mchezo wetu hadi dakika ya mwisho mmoja wetu atakaeruhusu kushindwa ndio mchezo utakuwa umeishia hapo,"

    "Sawa kabisa, unaonaje tu tuumalize mchezo leoleo?"

    "Hapana!leo ni siku ya game, tucheze game yetu na Mwana, hahahaa!" alimaliza kauli yake kwa cheko kubwa, cheko iliyomkera mno Jitu na kutaka kuongea kitu lakini Inspekta akamzuia.

    "Unajua mwanaume wa kweli haogopi kukutana na kidume mwenzie? Sasa wewe itakuwaje uogope kukutana nami uso kwa uso na hatimae unaenda kupambana na mabinti tu? Maana mimi nina hakika kabisa kuwa wewe unaua mabinti tu," aliongea Ispekta kwa nia ya kumpandisha jazba na ajikute ameropokwa tu maneno, lakini wala haikuwa hivyo, jamaa akaendelea kuongea bila jazba.

    "Inspekta tanbua kwamba kwa huyu meembo Mwana mimi wala sina nia nae mbaya, ni vile tu nahitaji pesa kwa ajili ya rambirambi ya mazishi ya Chidy bae aliuawa masikini ya Mungu bila kosa,"

    "Unajua kuwa unanipotezea muda tu bure?"

    " Ila wewe huoni unavyojaribu kuingilia kazi za watu ambazo hazikuhusu kope wala jicho? Na ole wako uendelee kunifuatilia,"

    "Ndugu huwezi kulitisha jeshi la Polisi eti lishindwe kufanya kaziyake inavyo stahili kwa sababu yako..."

    "Afande unajua sana kuongea, ila nilipiga simu kukutaarifu tu kuwa leo sina nia mbaya na Mwana ila akileta ubishi nitamjeruhi, kwani huyu kwenye idadi yangu ya watu wa kuwaua yeye hayupo..."

    "Sasa umeniambia ili iweje?" awamu hii Jitu ndio aliuliza akiwa na jazba, alitamani mno kama vile angekuwa anamuona mtu huyo.





    "Nimekwambia ili uwepo maeneo ya tukio ambalo nitalifanya maeneo ya Mwananyamala Studio, njoo ushuhudie tukio langu live leo hapo itakapo timu saa tatu usiku, mi nitakuwa Kigamboni, kwaheri!" Simu ikakatwa na kuwacha maafande wakitazamana na kushusha pumzi kwa nguvu.

    Jitu alikuwa ni mtu wa kwanza kutoa ile earfone sikioni mwake na kumuuliza Inspekta

    "Hivi huyu jamaa anaweza kuwa yupo seriuos kiasi hicho juu ya haya aliyo yasema?"

    "Yap!Huyu jamaa wala hatanii.lakini ujue kuwa kwasasa nahisi kuijua sauti yake?"

    "Sasa mkuu hapo tunafanyeje?" alihoji Jitu huku akijiweka vizuri kwenye siti yake.

    "Hatuna cha kufanya kwa sasa maana ni kama ulivyosikia tu hapo kwenye maongezi yake kuwa tukio litakuwa Studio, sasa jiulize hii studio inawaandishi wa habari wangapi?" aliuliza Inspekta na Jitu akajibuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Dah! Nahisi sasa kuishiwa mbinu, huyu jamaa ni hatari sana," hupaswi kukata tamaa, sasa ni saa 11 jioni, muda aliousema yeye unakaribia, fanya mpango wa kuomba askari kituoni pamoja na usafiri, nataka uwapange eneo lote tajwa, acha nami niwake hadi Kigamboni,"

    "Sasa unaenda kufanya nini huko na mtu humjui na pia Kigamboni ni kubwa?" Jitu aliuliza kwa mshangao.

    "Huzijui tricks zao hawa? huenda tukio likatokea huko Kigamboni na halafu akawa ametupanga sisi huku Kinondoni," alijibu kifupi tu lakini wakawa wameelewana.

    "Ok! Nimekuelewa Mkuu, acha nami nianze kujipanga tangu sasa, nafikiri tutawasiliana kila baada ya muda," wakaagana na kila mmoja akashika kazi yake huku Jitu akirudi kituoni na Inspekta Kalindimya akielekea Kigamboni.

    **********



    Marsha alikuwa akisikiliza mawasiliano yote ya Inspekta, mara tu baada ya kujua kwamba wameachana kati ya Inspekta Kalindimya na Jitu, yeye akajitokeza na kumvaa Jitu aliekuwa akiongea na baadhi ya askari.

    Alimsalimu na kumtaka faragha kidogo waongee. Jitu alisogea na kumsikiliza

    "Jitu kwa ukweli nimefuatilia maongezi yenu yote kwenye simu, nimezidi kupata uhakika kuwa sijakosea kuwa na mashaka na Inspekta Kalindimya juu ya kuhusika na vifo vya watu hawa,"

    "Kwanini Marsha?"

    "Maongezi yake yananishawishi niamini hivyo,"

    "Lakini mbona ameongea kawaida tu Marsha?"

    "Huenda wewe haukuwa makini ndio sababu, ulikuwa busy sana na kusikiliza anachojibu mtuhumiwa na sio anachokiongea Inspekta,"

    "Yawezekana, hebu nieleze kile ulichokisikia na kukushawishi uamini hivyo,"

    "Pale alipomwambia kuwa muuaji wa wanawake, yule jamaa wala hakubisha na Inspekta akazidi kunishtua baada ya kumwambia kuwa wakutane na kumaloza game."

    Sasa Marsha hili kweli si ni game? japo upande wetu ndio tunatakiwa tushinde game hii, bado hoja yako haina mashiko," Jitu sasa alimchana live.

    "Ok! nisikilize na hii nyingine... unakumbuka amemwambia mtuhumiwa kuwa ni muuaji wa wanawake?"

    "Ndio nakumbuka,"

    "Sasa kama muuaji si yeye huyo mtuhumiwa, ni nani sasa aliemuua Chidi?je ina maana Inspekta anamfahamu? na kama hamfahamu iweje amkatalie yule mtuhumiwa hata kabla ya yeye mwenyewe kukataa?" hapo sasa akawa ameongea point ambayo hata Jitu aliona ina mashiko.

    Akamwambia kuwa hapo sasa ndio pa kuanzia upelelezi wake na kwa upande wake amuachie yeye, wakaagana huku kila mtu akichukua muda wake kwa ajili ya kazi zake.

    **********



    Inspekta Kalindimya akaelekea moja kwa moja Kigamboni, bahati yake ilikuwa ni njema kwani wakati anafika Ferry akaikuta Pantoni ikiwa haijajaa hivyo alipata nafasi ya kuvuka kwa haraka.

    Kituo kilikuwa ni Kituo cha polisi, hapo ndio ilikuwa ni sehemu muafaka kwake kwenda ili kuweza kuweka guide ili ikitokea kitu chochote kama vile kuhitaji msaada ama tatizo lingine basi apate msaada kwa wakati muafaka.

    Hivyo akakutana na mkuu wa kituo aliekuwa nje akimshindikiza mtu aliekuwa amesimaa nae akimpa maelezo fulani, ndio akasogea na baada ya salamu ndio akampa taarifa za Kiitelejensia.

    "Afande inasadikiwa kwamba kuna tukio huenda likatokea huku sijui una habari?" alimuuliza mkuu wa kituo.

    "Hapana mimi sina habari," akamtazama Inspekta kwa mshangao.

    "Ohoo!sawa, kifupi ni kuwa kuna mtu mmoja anaehusika na yale mauaji mawili yaliyotokea Kinondoni, amepiga simu yupo huku,"

    "What? Unasemaje Inspekta?" Mkuu wa kituo aliuliza kwa mshangao utasema yeye ndio kaambiwa atauawa.

    "Naam! Na hiyo ndio sababu imenifanya niwe hapa muda huu,"

    "Hilo nalo hata nami nilihisi tu, ujaji wako wewe huku bila taarifa nilijua tu kuna jambo... kwanza ahsante kwa taarifa," baada tu ya taarifa ile akanyanyua simu na kumpigia simu mtu fulani.

    Alimwambia awapange askari wake takriban mji mzima,

    "Hakikisha umewasambaza kila sehemu, sawa?" kisha akakata simu na kuanza kuzunguka hapa na pale.

    Dakika moja tu mbele yao ikarudi gari moja ya Polisi aina ya Diffender ikiwa nyuma na mbele yake kukiwa na RAV 4 nyeupe hadi pale kituoni.

    Kwa mbali Inspekta akaiona pikipiki aina ya Boxer ikipita kwa mwendo wa kasi sana na mtu aliekuwahajavaa kitu chochote cha usalama mwilini lakini kasi yake ilikuwa ni kubwa mno.







    Wazo lake akalielekeza kwamba itakuwa mtu huyo anaiwahi Pantoni, kwani muda ulikuwa umekwenda sana, hilo ndio wazo ambalo alilipa nafasi ya kwanza.

    kwenye gari ile ya RAV 4 alishuka dada mmoja mnene hivi mweupe alikuwa na umbo zuri hasa la kike, alionekana nimrembo tena mwenye pesa zake.

    Kwa mwendo wa kawaida tu alielekea pale waliposimama wao na kuwasalimia kisha akamshukuru Mkuu wa kituo cha Polisi Kigamboni na kumwambia kuwa biashara imeshindikana.

    "Kwa hiyo itakuwaje sasa?" aliuliza mkuu wa kituo

    "Nafikiri nitakujulisha tena itakapokuwa tayari," alimjibu huku akiwaaga na kuondoka huku Mkuu akimkaribisha tena.

    Wakati yeye akiondoka simu yake ikaita, akaanza kuongea na huku upande wa pili, Inspekta akamuuliza mkuu wa kituo kwamba usalama umeimarishwa?

    "Inspekta hapa huyo muuaji akigusa tu amekamatwa, tayari nimeweka ulinzi wa kutosha mji mzima na vitongoji vyake, pia watu wetu huku, yaani raia ni washiriki sana wa ile program yetu ya Ulinzi shirikishi,"

    "Dah!hongereni sana, hivyo mkuu unanihakikishia tu kuwa sasa naweza kwenda?"

    "Yap!we unaweza kwenda tu wala usihofu Inspekta," wakashikana mikono kuagana huku wakianza kutembea taratibu kuelekea barabarani sehemu ambapo sasa alionekana yule kwanamke alkiongea na simu.

    Inspekta hakupenda kuongozana na yule mwanamke na hata muonekano wake kwa OCS - yaani mkuu wa kituo, ulimfanya Inspekta kujiuliza mwenyewe kuna nini?

    Akamuomba msamaha OCS na kumuuliza juu ya yule dada ambae sasa alikuwa tayari ameingia ndani ya gari na kuliwasha kwa ajili ya kuondoka.

    "Samahani Mkuu, huyo dada amekuja akiwa aneongozana na gari ya Polisi na kuja hadi hapa kukwambia kuwa biashara imeshindikana, kwani kuna biashara gani kati ya yeye na jeshi la Polisi?" alihoji.

    OCS huku akimshika begani kwa kujiamini kabisa akasema

    "Inspekta, kama raia wote wangefuata sheria ya fedha, kama huyu dada alivyo, basi amini matukio makubwa ya pesa yasingekuwepo abadan,"

    "Kwanini unasema hivyo mkuu?"

    "Huyu dada ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa Jijini, japo biashara hufanyika huko bara, lakini mara zote mizigo hununua huku Kigamboni. Lakini kwa kuwa huja na pesa nyingi basi hufika hapa kuomba ulinzi, huchukua mzigo wake na kurudi nao hadi nyumbani akiwa salama chini ya ulinzi wa jeshi letu adhimu," alieleza kwa kirefu OCS na Inspekta akamuelewa na kuhoji tena

    "Dah!heri yake anajua kuzitumia haki zake, ila tofauti na biashara ana kazi gani nyingine? maana katika mazingira ya kawaida ni vigumu mno kwa mfanyabiashara asie na elimu kuzijua haki hizo,"

    "Hahahaa kwanini unasema hivyo Inspekta?"

    "Ni kwa sababu wafanya biashara wengi wanafanya kazi zao kimazoea tu, hawajui kama muda unabadilika, sasa hilo ndio waliosoma wanajua, ndio maana nimeuliza nikiamini atakuwa amepita tu shule huyu," wakacheka taratibu, OCS akasema

    "Eeh ni kwli Inspekta, mwanadada huyu ni msomi, ana masters ya MASS Com., yupo kwenye kampuni fulani ya habari..." kabla OCS hajamaliza kuongea, Inspekta kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, akamkatisha maongezi kwa kumshika mkono na kumuuliza anakaa wapi.

    "Huyu dada atakuwa anaishi maeneo ya Kinondoni, ila sijajua ni Kinondoni..." kama mshale bila kujiuliza akachomoka Inspekta

    "Haa! Mkuu..." kitendo bila kuchelewa akakimbilia gari yake na huku akimwambia OCS kwamba huyo ndio mwanamke wanae muwinda hao wauwaji.

    OCS akashtuka na kupatwa na mshangao kwa ghafla, Inspekta akaingia garini haraka na kuliwasha kisha akaligeuza kwa kasi na kuondoka akiacha baadhi ya watu waliopo pale wabaki na mshangao.

    Alitaka kuwahi kumuepusha bi dada huyo kutokana na kifo ambacho kiliweza kuzuilika, aliamini inawezekana kabisa.

    OCS nae akili ikamuijia, nae palepale akawaamrisha askari wake waende Ferry kumuwahi Inspekta

    "Yule dada mliekuja nae anatakiwa hapa sasa hivi," alitoa maelezo bila kuwaambia ni kwanini na amefanya nini? bali alitoa tu amri kwamba apelekwe hapo.

    Askari walewale waliomshindikiza sehemu ya biashara sasa ndio wakawa wanachomoka tena kumfuata, gari hii sasa iliondoka mbio zaidi hata ile ya Inspekta.

    Inspekta alikimbiza sana gari, lakini muda waliokuwa wameachana ulikuwa ni mkubwa sana ambao ina maanisha kwamba ni lazima dada yule atakuwa amefika mbali mno.

    Hadi anafika kivukoni, hakuweza kuiona gari hiyo ila kwa mbali aliiona kama vile ipo kwenye foleni, akaona sasa huenda ataiwahi.

    Lakini dhahiri baada ya kupiga hesabu zake, akaona kwamba hatoweza kumuwahi tena, iwapo ataendwlea kumfuatilia kwa gari, alitamani wawe wawili garini, lakini ndio hivyo... alikuwa peke yake garini.

    Alitamani kuiacha gari yake iliaiwahi ile gari ya yule dada, lakini hilo pia ikawa haiwezekani, ingekuwa ni sawa na kuzuia wengine wasipite, sasa akalazimika kutafuta mchepuko.

    Upande ule aliokuwa akipita yeye kuelekea Kivukoni, nafasi ilikuwa ni haba sana, haikuwezekana kabisa kupaki gari maana kulikuwa na majani marefu na vichaka vidogo vidogo maalum kwa ajili ya kupendezesha eneo hilo.





    Hivyo upande huo ukawa haumfai yeye, akalazimika kuangalia upande wa pili, hapo sasa akachepuka pembeni, lakini kutokana na wembamba wa barabara alilazimika kusubiri sana gari za upande wa pili zilizotoka ndani ya kivuko zipite.

    Hapo muda ulizidi kulika na bi dada alizidi kusogea mbele. alipokuja kupata nafasi ya kuchepuka, akakutana na tatizo lingine, ni wapi apaki gari hiyo?

    Alikwenda umbali mrefu kidogo hadi karibu na majengo ya TanRoads kwa ajili ya kivuko na kutaka kupaki hapo, alizuiliwa lakini akalindwa na kitambulisho chake.

    Akashuka na kuanza kuelekea huko ilipo kuwa ile gari ya bi dada huyo. alikuwa mbiombio, gari takriban kumi bila kuliona, akajiuliza je huenda ameiacha nyuma? Akarudi kwa nyuma kidogo ili kuitazama kama ameivuka, lakini hakuiona.

    Uamuzi aliouchukua ni kuendelea kuangalia gari za mbele na iwapo ikatokea akaikosa, basi akaepalepale getini kusubiri hadi itakapomfikia gari hiyo ya huyo dada.

    Alipozimaliza gari zilizopo kwenye Mnyororo, aliona kundi.la watu likiruhusiwa kuingia kwenye pantoni, kutokana na kuwa na kigiza kilichokuwepo pale alihangaika sana kuiona gari.

    wakati ikipiga honi kuanza kuondoka, Panton inageuka upande kidogo kukata kona ili kuipata Angle yake vizuri, hapo ndio aliweza kuiona gari hiyo aina ya RAV 4.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akasogea mbele zaidi ili awahi hata kujirusha kwenye maji na kuingia kwa njia ya kuogelea, lakini akazuiliwa na askari wakiokuwepo pale, akatoa na kitambulisho lakini awamu hii hakikumsaidia.

    Waliendelea kumshikilia tu na kumzuia wakimwambia kuwa kina cha maji pale nibkirefu sana hivyo wao hawana ruhusa ya kumruhusu mtu yeyote.

    Rasmi akawa amechelewa, akaiona ilee... inapotea machoni mwake, akakasirika na kupiga ngumi kwenye paja lake na kujishika kiuno akiwa hajui la kufanya.

    Alishtuliwa na askari wawili waliofika pale na kumpigia saluti na kumuuliza kama amefanikiwa kumuona. Akawataka wajitambulishe kwanza, hawakubisha, wakajitambulisha.

    Baada ya kuwatambua akawapa maelezo kifupi tu na kuwataka warudi lindoni kwao yeye anavuka, wakageuza na kurejea kituoni huku yeye akianza kurejea ilipo gari kwa ajili ya maandalizi ya kuvuka.

    Akiwa garini akatoa simu na kumpigia Jitu, alipoipokea tu hata kabla ya salamu, akamuuliza alipo, nae akamjibu kuwa yupo Mwananyamala

    “Usalama upoje huko hadi muda huu?”

    “Nimesimama imara Mkuu, hapa nawazungukia kila sehemu ili kujua ni nini kinaendelea, kwani nimewasambaza sehemu zote kuzunguka Studio na maeneo ya Jirani,”

    “Safi sana, sasa hapo ulipo wewe ondoka muda huuhuu, elekea Ferry, lakini pitia njia hii ya Salender Bridge, maana Yule mwandishi nimepotezana nae,” alipo ongea hivyo Inspekta, moyo wake ukapiga mshindo na kumuuliza amemuona kwani?

    “Yap! Nimemuona lakini bahati mbaya tumepotezana kabla ya kuingia kwenye Pantoni, yeye alitangulia kabla yangu na mimi nikawa nimechelewa kumfikia hadi Pantoni inaondoka,”

    “Ok! Sasa tunafanyeje?” aliuliza Jitu kwa mshawasha.

    “Nenda kwenye barabara hiyo kama nilivyokueleza, kwani kama hana ratiba nyingine itakuwa ni lazima atakuwa anarudi kwake na hivyo ni lazima apite njia hii kwa kuwa anaishi kinondoni,”

    “Kinondoni ipi anaishi Mkuu?”

    “OCS wa Kigamboni amenieleza kuwa anaishi Kinondoni lakini hajui ni Kinondoni ipi, suala la msingi ni kumsimamaisha tu yeye pindi ukiiona hiyo RAV 4 nyeupe, ni new model, ina tairi za Sports,” baada ya maelezo hayo tu wakakata simu ili kila mmoja aweze kuwahi majukumu yake.

    Ilifika Pantoni nyingine na Inspekta akaingia, akiwa ndani ya Pantoni, inspekta Jitu akampigia simu na kumwambia kwamba kuna milio ya risasi imesikika maeneo ya inondoni Makaburini na hilo eneo yeye alikuwa tayari amelipita.

    “Kwa hiyo sasa Inspekta…”

    “Mkuu hapa tayari mimi nimeisha geuza, narejea huko kwenye milio hiyo huenda ndio mtu tumtakae,” alijibu Jitu huku akigeuza gari.

    “Sawa Jitu wewe rudi eneo la tukio haraka, mimi pia nipo njiani kuja hukohuko sasa hivi,” Jitu akapindua gari na kugeuza kwa mwendo wa kasi kuelekea maeneo ya Kinondoni Makaburini.

    Dakika 10 mbele Jitu akampigia simu Inspekta Kalindimya na kumwambia kuwa yeye yupo Mwananyamala hospitali, afike muda uleule bila kukosa, hakutoa kabisa nafasi ya kuulizwa zaidi akakata simu.

    Inspekta ambae nae muda huo alikuwa tayari ameisha toka ndani ya Pantoni, akanyoosha moja kwa moja kuelekea huko Hospitali kama alivyotakiwa. Alipita maeneo hayo ya makaburini kuangalia kama kuna chochote totauti, hakuona.

    Moja kwa moja hadi getini, akaingiza gari na kuipaki pembeni na kushuka, pale jirani na alipopaki yeye aliikuta gari moja ya Polisi aina ya Pick up ikiwa na Streacher, akasimama na kutazama ndani.

    Alikuwepo dereva peke yake akiwa ameegemea sterling, alionekana amechoka sana, nae hakutaka kumsumbua, maana anaijua kazi yao ilivyo. Alipotazama mbele kidogo akaiona gari ya Jitu ikiwa kwa pembeni kidogo.

    Huyo ndio mtu aliekuwa akimuhitaji, akaisogelea gari ile na alipoikaribia tu, Jitu aliekuwa mbali kidogo akamsemesha na kumsogelea.





    Alipomkaribia akamjulia hali kisha akataka kumueleza yaliyotokea,Inspekta hakutaka kujua yote kwanza, alichotaka kujua ni kwanini wapo pale.

    “Tupo hapa kwa sababu MwanaMtama Abdul, yupo hapa,”

    “Mwanamtama?Ndio nani huyo MwanaMtama?”

    “Ndio huyo Mfanyabiashara ulienipa maelekezo yake,”

    “Mh! Yupo katika hali gani?Mzima ama amekufa? Hebu nielezee hilo kwanza,”

    “Ndio maana nilikwambia uje huku ili tulizungumzie jambo hilo kwa kituo,”

    “Sawa,” akajibu kifupi tu huku wakielekea kwenye gari la Inspekta Kalindimya na kuingia ndani ya gari hiyo.

    Walipoingia na kufunga milango, Inspekta akaiwasha gari na kuiweka Silence ili waweze kula kipupwe wakati wakiongea, maana ilionekana Inspekta alikuwa na hamu kubwa mno ya kutaka kujua.

    Jitu akautumia muda huo kumueleza kwa kirefu kabisa Inspekta kilichojiri.

    Baada ya kuongea nawe pale na kuniamuru nigeuze gari kurejea maeneo ya Kinondoni Makaburini, nakaribia makaburi pale, nikaona kuna kikundi cha watu, sikutaka kuwapita burebure, nikasimama na kushuka kuwafuata, maana hata name nilisikia milio ya risasi.

    Mara tu baada ya kuwasalimia pale pembeni nilimuona mlinzi mtu ambae nilimtambua kuwa ni mlinzi wa eneo lile kutokana na sare zake za kazi alizovaa, huyo ndio nikamuita pembeni na kumuuliza kuna nini kilichotokea.

    Mlinzi huyo ambae hakuwa akijua anaongea na nani, akanijibu kuwa mida ile akiwa lindoni kwake, yeye analind pale jirani kuna jengo la vioo kama utakuwa na kumbukumbu nzuri Inspekta,”

    “Sawa kabisa, linataka kuwa na usawa wa geti la kwanza kutokea mashariki,”

    “Haswaa! Ndio hapo huyo mlinzi alikuwa akilinda,”

    “Ok unaweza kuendelea,” alimtaka aendelee, maana tayari eneo alilielewa.

    “Sawa, basi anasema wakati akiwa anzunguka zunguka akasikia sauti ya risasi kwa nyuma kidogo ya eneo lao, na baada ya sekunde chache ikampita kasi sana gari ndogo aina ya RAV 4 Nyeupe huku nyuma ikifuatiwa na pikipiki aina ya Boxer.” Hapo akanyamaza kidogo na kumeza mate kisha akaendelea

    “Gari ile ilikwenda na kusimama mbali kidogo na eneo hilo la tukio na kisha wakati yeye akiwa hajajua ni nii afanye mlango ukafunguliwa na aliekuwa ndani ya gari akavutwa chini na aliemvuta ndio akaingia garini na kuondoka na gari hiyo kwa kasi sana,”

    “Aaaah!Kwa hiyo wewe ukawapigia kwa huko mbele waizuie?” sasa alikuwa ana shauku ya kutaka kujua.

    “Hapana mkuu, mimi wakati nafika hicho kitendo kimeisha tokea dakika kadhaa ziklizopita, hivyo hapa anakueleza tu maelezo toka kwa Yule mlinzi,”

    “Dah huyo Mlinzi nae boya kweli, we unaona mtu unaibiwa halafu una bunduki unashindwa kutoa msaada, haina maana sasa ya kuwa ni mlinzi, maana ya kuwa mlinzi ni kumlinda mtu na mali zake,” alijikuta akiongea vitu ahata visivyokuwepo, Jitu akamwambia kuwa asingeweza kufanya hivyo kwani pale yeye alikuwa lindoni na asingeweza kuondoka kwenda kushambulia huko na kuacha lindo likiwa wazi.

    “Na hivi wanatumia bunduki zenyewe za kizamani, mtu unalinda mali zina thamani ya mabilioni unatumia bunduki ya mwaka 30, inaweka risasi moja tu chemba, pumbavu! Hebu Jitu Endelea hao tuachane nao.”

    “Umeona eenh? Basi huyo mlinzi akiwa hajui ni ni afanye, ile RAV 4 ikatokomea mbele na kufuatiwa na pikipiki huku Yule mwanamke akiwa amebaki pale chini bila kutikisika, kiasi yeye kwa huko mbali alipokuwa, alijua itakuwa wamemuua.

    Akamuita mwenzie anaelinda upande wa pili na kumwambia amsaidie kulinda pande zote ili yeye aende akatoe msaada kwa Yule mtu pasina kujua kama yu hai ama ni maiti, basi mwenzie akamruhusu na yeye akaenda mbio, lakini akiwa hatua kadhaa kabla hajamfikia, ikatokea Bajaj na kusimama jirani na Yule mtu ambae sasa Yule Mlinzi aliweza kumuona kuwa ni mwanamke, aliekuwa akivuja damu maeneo mengi ya mwili wake.

    Akiwa ameshuka Yule dereva wa Bajaj, Mlinzi nae alikuwa sasa amefika, simu ya Yule mtu pale chini ikaita, Yule dereva wa Bajaj akaiokota tena bila hata ya woga na kupokea…”

    “Yule mlinzi nae anamtazama tu?” aliuliza Inspekta kwa mshangao.

    “Ndio, sasa unafikiri Inspekta masomo yetu sisi na wao yanalingana? Yaani ingewezekana tungeyafuta kabisa mambo haya ya walinzi wa…” kabla hajamaliza, simu yake ikaita, akamuomba samahani mkuu wake wa kazi ili apokee, nae akamuitikia kwa kichwa kukubali, Jitu akaipokea na baada ya mzungumzaji kuongea maneno machache, Jitu akasema

    “Ok! Tunakuja sasa hivi, maana wala hatupo mbali!” alipokata tu simu, akamwambia mkuu wake wa kazi kuwa huyo aliepiga ni daktari na anahitaji kuwaona, tena muda huohuo.

    “Kwa hiyo story yetu ndio imeishia hapo kwa sasa, acha tukamsikilize kwanza daktari, huenda kukawa na la maana zaidi ya hayo tuyajuayo,” aliongezea Inspekta na kutoka garini, huku Jitu akifuatia, wakafunga na kuelekea mbele zilipo ofisi za daktari.

    Waliwasili na kukuta mle ndani kuna mtu mwingine akiwa na majonzi, daktari aliwakaribisha na kumuomba Yule mtu awapishe kidogo, akatoka na kuwaacha wao wakikaa.





    Daktari aliwakaribisha na kuanza kuwapa maelezo, hakuhitaji kufahamishana, maana wamekuwa wakionana mara kwa mara. Katika maelezo aliyowapa, aliwaambia kuwa baada ya uchunguzi wa awali, kuna kitu amegundua.

    Wameona kupitia vifaa vyao ikiwepo CT Scan kwamba Mfupa wa bega umevunjika na hivyo atahitaji operesheni kubwa zaidi ambayo inaweza kufanyika hospitali kubwa zaidi ya ile ya kwao.

    “Hivyo tangu sasa ninamuandikia barua ya rufaa na dakika chache zijazo tutamuondoa hapa kumpeleka Muhimbili,” alimaliza maelezo yake ambayo yalikuwa ni mafupi tu na hakukuwa na maoni zaidi ya kukubaliana na maamuzi ya daktari.

    Inspekta Kalindimya na Jitu wakatoka nje ikiwa ni saa tano usiku, Inspekta akamwambia Jitu afanye mpango wa kupeleka ulinzi sehemu atakayokuwepo mgonjwa wao.

    Wakaagana kila mmoja akiwa ameingia kwenye gari yake kwa ahadi ya kukutana siku ifuatayo, hawakukumbuka tena kumalizia story yao.

    **********



    Siku ya pili asubuhi, wakati Inspekta akiwa amefika ofisini kwake, akamkuta tayari Jitu akiwa amewasili, lakini alikuwa nje ya ofisi akiongea na simu, Inspekta akamfuata hukohuko alipokuwa na kusimama mbali nae kidogo.

    Alipomaliza kuongea na simu, kila mmoja akafuata mwenzie huku wakiwa na shauku ya kukutana, wakasimama penuni mwa ukuta wa jengo la Polisi na kuanza kuongea mawili matatu.

    Wakiwa wanapiga soga, kuna kitu Jitu alitaka kukisema, lakini alipotaka tu kukitamka simu ya Inspekta Kalindimya ikaita, namba aliitazama na kuijua kuwa ni katika namba zilezile za usumbufu, akaipokea na kuweka ‘Loud Speaker’ ili Jitu nae asikie kinacho zungumzwa.

    “Hellow Inspekta,” sauti tayari waliijua kwani muonekano tu wa zile namba, ilikuwa ikijulisha kabisa kuwa ni mtu yuleyule anaepiga tena.

    “Sema,” alijibu kifupi huku akirekodi mazungumzo hayo

    “Kama nilivyokueleza jana mapema, mimi binafsi Sikuwa na mpango wa kumhuru MwanaMtama, lakini kiherehere chake kikamponza, na ana bahati sana kwamba alipata dhamana kwa niliekuwa nae, lah sivyo nae ningempoteza tu Yule kuku wa mayai,” aliongea kwa sauti ya kujiamini sana, Jitu akamuuliza kwa hiyo anasemaje

    “Nimekupigia simu kukujulisha kuwa hii sasa ni last Warning, onyo la mwisho, achana na kesi yangu hii, wewe huiwezi, hata DCI anaweza kuishindwa kesi hii ikimfikia, achana nayo haraka nimesema,” alitoa sauti ya kuamrisha, Inspekta akacheka kwa dharau na kusema

    “Yaani hicho ndio kimekufanya unipigie simu?”

    “Ndi Inspekta lakini nafanya hivi leo kwa faida ya MwanaJuma,” simu ikakatwa hapohapo na kuwaacha maafande wakiwa hawajui cha kufanya, hasa Inspekta Kalindimya ambae alionekana kama amechanganywa ghafla na maneno hayo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakaanza kutafakari, Jitu akamuuliza mwenzie huyo MwanaJuma ni nani?

    “Hata namjua basi Jitu?Simjui huyo mtu ni nani!”

    “Sasa kwanini atishie kwa mtu usiemjua?”

    “Hapo sasa name ndio ninaposhangaa, yaani hii kazi hadi ikaishe, tunapaswa kuchukua na likizo dah!” alijibu Inspekta na Jitu akamwambia mwenzie waende ofisini na kukaa kujadili.

    Vichwa viliwauma wote, Inspekta alichukua File la kesi ile na kuanza kulipitia upya huku Jitu akiwa ameshika visu vilivyopatikana kwenye mauaji na kulinganisha alama za vidole yaani Finger prints toka kwenye Computer iliokuwepo kwenye ofisi yao.

    “Ujue muuaji ni mmoja tu Inspekta, na hata sipati pisha kwanini alikishika kisu vibaya kabla ya kuvaa gloves,”

    “Inaonekana vipi kwani?”

    “Njoo uone na tujadili hapa, huenda tukaokoteza kitu hapa cha maana," alijibu Inspekta huku akikunja file lake na kumsogelea mwenzie.

    Aliona nae alama za vidole zilionekana chini kwenye mpini huku sehemu ya juu ikiwa haionekani kwani gloves ilificha muonekano wake.

    "Sidhani kama kuna cha kutusaidia hapo, ila tu mimi nina swali moja kwako, hivi kwa MwanaMtama napo kilikutwa kisu?"

    "Hapana mkuu huko hapakuwa na kisu, lakini unakumbuka nilikueleza kwamba gari yake nayo ile RAV 4 nayo ilitekwa?"

    "Yap nakumbuka vema, ehee nayo vipi?"jana usiku nilipigiwa simu na kujulishwa na askari ambao niliwaweka kumlinda MwanaMtama kuwa wameletewa funguo na mtu akisema jina lake ni Loren alikuwa ameazima gari yako na amesema ikifika tu nipewe mimi," alitoa maelezo marefu Inspekta.

    "He!mbona sijakuelewa? Yaani mtu kaleta funguo ya gari yangu halafu upewe wewe?"

    "Na ndio kilichofanyika hicho, nikapewa hiyo funguo leo asubuhi, lakini mimi sikuamini kama kuna mtu ulimuachia gari na alete kwangu,"

    "Dah huyu mtu sijui ananitakia nini?Kwa hiyo umegundua nini kupitia funguo hiyo?"

    "Ajabu sasa baada ya kuingia ndani tu kumuona MwanaMeka, hakuwa kwenye hali nzuri ya mahojiano lakini nikataka tu kumsalimu kwanza, niliingia nikiwa bado nina funguo ile mkononi, Mwana alipoiona tu kwa sauti ndogo akasema ile ni funguo ya gari yake,"

    "Duh! kama movie vile, ikawaje?" nikamwambia atulie kwanza hali ikiwa vizuri tutampa funguo yake, kisha nikakaa kwa sekunde kadhaa nikatoka," Alimaliza huku akimwambia akaja ofisini na ndio walipokutana nje nae akiwa amefika.







    "Sasa hiyo gari yenyewe ipo wapi?" aliuliza kwa msisitizo

    “Ndio pale nilitaka kukueleza ila ukapigiwa simu, hiyo gari nimepigiwa simu imeonekana maeneo ya Mwana Nyamala Kisiwani, na muda huu hapa itakuwa imeisha anza kuvutwa na Clain kuletwa hapa,”

    “Ok! Umeagiza iletwe hapa au ipelekwe kule Kilwa Road?” alihoji Inspekta.

    “Hapana nimewaambia wailete tu huku ili tuweze kufanya uchunguzi kwa uhuru zaidi,” alijibu Inspekta huku akichukua simu yake na kumwambia Inspekta kuwa anampigia simu afande aliempa kazi hiyo.

    “Ndio, mmefika wapi?” aliuliza na kisha akashangaa

    “Ha! Sasa mimi ningeotaje? Mbona hukunijulisha mapema?”

    “Sawa tunakuja!” akakata simu na kumwambia mkuu wake kuwa vijana wameisha fika kitambo sana ila walikuwa hawajawajulisha kama wapo nje tayari.

    “Ohoo!Kwa hiyo wapo nje na gari yenyewe?” aliendelea kuuliza Inspekta.

    “Ndio, na ninaona twende tuakaione,” akajibu Jitu huku akitoka nje kuelekea huko ilipo gari. Waliikuta gari ileile ambayo Inspekta aliiona kwa mara ya kwanza huko Kigamboni na kumwambia Jitu kuwa ni gari hiyo aliyokuwa ameihisi.

    Jitu akatoa funguo kimya kimya na kufungua mlango, kupitia mlango huohuo mmoja wote wakasimama na kuangalia ndani kuona kama kuna lolote ambalo wanaweza kuliona.

    “Inspekta Jitu, huyo aliefanya ukaguzi wa awali, yupo wapi?” Jitu akageuka nyuma na kumuita askari mmoja alliekuwa amesimam na karatasi mkononi na aliposogea tu akamuuliza vipi? Mbona hajawapa amaeekezo yoyote ya huko walipotoka?Akadai kuwa alikuwa akisubiri waangalie kidogo.

    “Ok! Hebu tueleze huko imekuwaje?” aliamua tu Inspekta kuyafupisha maana ilikuwa inataka kuwa ni habari ndefu na lawama , ndio akaamua kufupisha kwa kumuuliza walichokiona huko.

    Nae hakutaka tena kuhangaika, bali alichukua jalada alilo lifungua na kumkabidhi afande Jitu ambae alilifunua kidogo huku Inspekta akizidi kulizunguka lile gari kwa ajili ya ukaguzi.

    Alipomaliza tu kuizunguka akamrudia Jitu na kumwambia vipi kuna jipya gani? Akamwambia kwamba amegundua kwamba kua namba imeonekana mle kwenye kisu pia na kimeambanishwa mlemle pia.

    Inspekta akamwambia waende ofisini wakaketi chini kwa utulivu ili wapiti vizuri, hapo tayari walikuwa wame hemkwa vibaya kutokana na kuonekana mle kuna mambo nyeti.

    Wakaelekea moja kwa moja ofisinikwao na kuingia kwenye meza ya Inspekta ndio wakaketi na kuanza kulisoma lile faili, Inspekta akiwa ameketi na Jitu amesimama kwa pembeni yake wakisoma na kujadiliana.

    “Umeona kuwa muhusika ni yuleyule tu?”

    “Hilo linajulikana Jitu, sasa hebu tujaribu kuangalia kitu kipya, muite Yule kijana umuulize kama alikumbuka kuchukua alama za vidole kwenye sterling ya gari,”

    “Dah! Kweli, ndio maana ukawa ni Inspekta, nimekubali mkuu, sikuweza kufikiri hata sekunde 0 juu ya jambo hilo,” akajibu huku akitoa simu na kumpigia afande huyo ambae aliitika na kusema anakuja muda ule ule.

    Alipofika tu wakaanza kumshambulia na maswali mfululizo huku akijitahidi kuyajibu kwa uthibitisho na hata kwenye swali lile la kuchukua alama za vidole.

    “Ndio mkuu, wakati unanipigia simu nikakumbuka kuwaita watu wa alama za vidole na waliahidi hadi kufikia mchana huu watakuwa wamekamilisha uchunguzi,” alijibu akiwa amekakamaa, wakamruhusu aende kuendelea na majukumu mengine.

    “Angalia kitu hiki afande Jitu,” Inspekta akamwambia mwenzie huku akimuonesha kwa kidole sehemu ya maelezo yaliyo andikwa na Yule askari walie mruhusu aondoke, ile sehemu iliandikwa kuwa

    Kuna namba imekutwa kwenye kisu chenye mpini wa rangi na namba hiyo inasomeka kama 68262. Walizamisha akili na macho yao hapo kwenye namba hiyo kwa takriban dakika kadhaa, lakini kile kilikuwa ni kizungumkuti, suala la namba kwao kilikuwa ni kama mtihani.

    Hawakuweza kulifumbua fumbo hilo, lakini kidogo Inspekta aliweza kugundua kitu, kitu chenyewe ni kwamba walio uawa wote ni kina Mwana na katika matukio yote matatu yaliyo tokea ya mauaji na kutekwa, yamewahusisha kina Mwana.

    “Na halafu, miiili yote ya waliouawa, yaani kina Mwana wawili, namba zao za mwishozote zimeishia na 74, Sijui muuaji ana maanisha nini!” alihoji huku akimtazama Jitu.

    “Halafu matukio mengi anayafanyia Mwana Nyamala,” aliongeza Inspekta.

    “Duh! Hilo ni fumbo afande,” aliongea Jitu akistaajabu utundu na umahiri wa mkuu wake wa kazi wa kufuatilia vitu ambavyo yeye aliviona kama ni vidogo vidogo sana.

    “Kweli hilo ni fumbo, tena zito sana lakini ni sisi ndio tunaopaswa kulifumbua, tunafanyeje sasa?” Jitu tayari alikuwa ameanza kuondoka pale alipokuwa amesimama awali na kwenda maeneo ya dirishani kuangalia mandhari ya nje.

    Swali lile likambadili mwelekeo na kujikuta akigeuka na kumwambia mkuu wake kwamba, waende chumba cha uchunguzi wa alama za vidole ili kuchukua majibu, huenda yatawapa mwanga.

    Wakatoka kwa kuongozana moja kwa moja hadi ghorofa ya pili ndio ilipo ofisi hiyo, walikuta majibu yapo tayari. Alie yapokea ni Inspekta, akayatazama na kuguna, kisha akamuangalia Jitu, wakakutanisha macho…







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog