Sehemu Ya Nne (4)
Robo saa ilitosha kuwafikisha katika eneo la tukio,walikutana na mlundo wa watu walio kuwa mazingira yale,huku nyuso zao zikionekana kuwa ni zenye mahamaniko makubwa, bila shaka ni kutokana na namna macho yao yalivyo shuhudia miili isiyo kuwa na uhai ya binadamu wenzao namna ilivyo uwawa kinyama. Kilanga na timu yake walishuka kwa mbwembwe katika tenga la polisi huku macho ya watu yakiwazonga, Walisogea mahala maiti ya koplo kidogori Ilipo lala huku kichwa chake kikiwa kimepasuliwa vibaya na kufanya jeraha kubwa kudhihirika,damu zilionekana kumtapakaa mwili mzima,sentimita chache kulikuwa na bunduki ya SMG iliyokuwa imetelekezwa kihasara., Kutoka mahala bunduki ilitelekezwa kulikuwa na fuko la Rambo lililokuwa limelowa kwa damu huku ndani yake kukiwa na kichwa cha mtu!. hali ilitisha!. Kilanga na Babra waliendelea kutizama na kudadafua mazingira yale katika bongo zao., “Ispekta Kilanga” Babra aliita kwa wahaka akiwa makini kutizama kifaa kidogo kilicho kuwa chini hatua chache kutoka mahala ilipo lala maiti ya koplo kidogori,. “ganda la risasi” alisema Babra akimwonyenyea Kilanga kile kifaa chenye rangi ya shaba, “Hii risasi bila shaka ilitumiwa na huyu askari kukabiliana na muuwaji,..lakini!.. sasa ilikuwaje..mpaka muuwaji akamshinda”? alisema kilanga “Kwanini unaseama muuwaji? pengine si muuwaji ila ni wauwaji” hawezi kuwa muuwaji mmoja akashindana na watu wawili tena wenye bunduki akawashinda ispekta” “Kisio lako ni sahihi Babra lakini hawa wauwaji inawezekana wakawa wanabunduki”. “Sina uhakika ispekta kilanga, kwasababu maiti ya huyu askari inaonekana imepondwa pondwa kichwa mpaka kufa, na si kifo cha risasi, sina uhakika wa asilimia mia kama wauwaji wana siraha,na hata kama wanazo silaha basi katika tukio hili hawakuzitumia.” “Ona hii tena Babra” alisema kilanga akiwa makini zaidi, “damu ispekta!.” Babra alisema huku akitizama damu iliyokuwa imekauka sentimita sabini kutoka kichwa cha mtu kilipokuwa kimetelekezwa, Kilanga alitizama kwa makini umbali kutoka kichwa cha mtu kilipokuwa akalinganisha kutoka umbali maiti ya koplo kidogori ilipolala akang’amua kitu.sura yake ikajaa muonekano wa viulizo kibao, “Taarifa zinaonyesha kila muuwaji anapofanya mauwaji anaondoka na kichwa cha mtu! Iweje hiki hajaondoka nacho!!. Kuna kitu hapa.” Kilanga aliwaza akilini, Alitoka hapo na kuingia ndani kuliko kuwa kunasadikika kulikuwa na mwili wa mzee mwana Malunde, walikuta mwili wa mwana malunde usio kuwa na kichwa ukiwa umelala bila uhai huku vitu vya kiganga vikiwa shabarabaghala mule ndani,. “Humu ndani kulikuwa na mvutano wa makabiliano baina ya muuwaji na marehemu” alisema kilanga huku akipachika sigara mdomoni na kuiwasha kwa kiberiti cha gesi kisha akavuta mkupuo mmoja na kutoa moshi mwembamba kupitia mdomoni na puani,. Babra alitikisa kichwa kukubaliana na kisio la Kilanga huku jasho la pua likijidhihirisha usoni mwake,. “Mpaka sasa sijajua yule askari kule nje ilikuwaje hadi akafika eneo hili kabla ya kukutana na umauti?” alisema Babra huku akipangusa jasho usoni mwake kwa kiganja chake cha mkono wa kushoto,. “Fanya mahojiano na familia ya huyu askari pengine tunaweza kupata lolote”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alisema Kilanga. “Afande yule ni askari anae tokea katika out post ya railway station” askari waliye ongazana nae alisema,. “Vizuri sana”, kilanga alisema kwa wahka “sasa ni wewe ndiye utakae fuatilia huko kituoni kwake na uje na taarifa zinazo husu uwepo wake eneo hili akiwa na silaha” alisema Kilanga huku macho yake yakiendelea kusaili maiti ya yule mganga wa kienyeji udadisi ukiongezeka mara dufu zaidi kwa kila dakika iliyo pita wasaa ule,. Aliingiza mkono mfukoni na kutoa kamera ndogo ya Samsung kisha akapiga picha kadhaa maiti ya mwanamalunde, Wakati huo huo kulikuwa na vilio tofauti vilivyo sindikizwa na maneno lukuki yenye kuwataja wapendwa wao na kufanya mchanganyiko ule wa sauti kuwa makelele,. ilikuwa ni familia ya marehemu mzee malunde na ile ya koplo kidogori, Babra alisogea mahala ambako mke wa koplo kidogori alikuwa akibugujikwa na machozi, kisha akatoa kitambaa katika mkoba wake na kumpa mke wa marehemu koplo kidogori kwa kujifutia machozi yaliyo kuwa yakimmiminika kwa kasi,alikuwa ni mwanamke mnene aliyeshiba kwelikweli, Utulivu ukapita baina ya Babra na mke wa marehemu koplo kidogori kabla ya kuanza kufanya mahojiano,. Dakika nne badae mahojiano yalianza kufanyika baina yao,hapo kwa kila sentesi aliyo izungumza mke wa koplo kidogori iliibua hisia hatari kwa Babra mapigo yake ya moyo yalienda kasi mpaka ujasiri wa kiaskari ukapotea, akaogopa na nguvu zikamwishia,.***************** ****************
Ray alikuwa katika usingizi mzito katika sofa alilo kuwa amejilaza huku mguu wake uliokuwa na bandeji kubwa pajani ukiwa umelazwa kihasara hasara pale sofani,. Pembeni katika sofa dogo, alikaa Richard aliyekuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, wasiwasi ulimwenea moyoni mwake, leso yake iliyo kuwa mkononi mwake ililowa kwa jasho la viganjani,.mwanaume mwingine aliyekuwa amesimama pembeni ya mahala alipo lala Ray alikuwa akivuta dawa katika kichupa kidogo kwa kutumia sindano iliyo kuwa imeunganishwa na bomba lake,.aliingiza ujazo aliona unatosha kisha akaminya kidogo,. matone ya dawa yaliruka kwa kasi, kisha akainama akielekeza ile sindano katika paja la Ray, taratibu alimdunga sindano ile na kuhakikisha ameingiza dawa yote iliyokuwa katika bomba la sindano,.kisha akachukua pamba iliyo lowanishwa na dawa maalumu ya kuzui damu na kuipachika mahala pale alipo mdunga sindano,. “hii itapunguza maumivu aliyo nayo kwa muda kadhaa ni bahati hakuna madhala katika mfupa wa mguu wake,.imekuwa bahati kwake hiyo risasi ilipenya katika nyama na kutokea upande wa pili wa mguu,. haikubaki mwilini mwake” Alisema dokta yule aiyekuwa ikimtibia Ray huku akiweka sawa miwani yake midogo ya macho iliyo pendezesha muonekano wake,. Richard alishusha pumzi ndefu kifua chake kikipanda na kushuka pindi alipo vuta pumzi kwa ndani na kuzitoa nje,mikono yake ikiwa kiunoni,.alisogea karibu na mahala alipo simama yule dokta akaingiza mkono mfukoni na kutoa burungutu la pesa kisha pasina kuhesabu wala kuzungumza akamkabidhi yule dokta,. “thanks mr small fish, well done” alisema kwa kimombo yule daktari huku akizipokea zile pesa na kuzitumbukiza katika mfuko wake wa koti la suti., “nitakuja tena jioni kumcheki” aliendelea kusema yule dokta,. Richard hakutia neno,. Ikawa anakusanya vifaa vyake vya kitabibu na kuvipachika katika mkoba wenye ukubwa wa wastani kisha taratibu akauendea mlango na kutokomea nje,. Richard alibaki amesimama mahala pale macho yake yakiwa kwa Ray,.huruma iliyo changanyikana na hofu iligubika ndani ya moyo wake, alimtizama Ray vile alivyo fumba kope za macho yake akiwa katika usingizi mzito wa dawa za usingizi alizo pewa, kumbukumbu za maisha ya nyuma zilipenya katika ubongo wake,.alikumbuka miaka mingi iliyopita namna walivyo kutana na mtu huyo wakiwa watoto wadogo wa miaka kumi.,****************
APRIL. 6 .1994 /KIGALI RWANDA, Ilikuwa ni usiku wa saa tano na nusu,Zilisikika sauti nyingi za vilio kila kona ya mtaa katika jiji la Kigali nchini Rwanda, Vishindo vya sauti za mabomu na risasi ziliugubika mji wa Kigali, ukimya uliokuwa umezoeleka hasa nyakati za usiku katika mji wa kigali siku hii ulipotea,miale mikubwa ya mioto ilitanda katika anga, moshi mzito ulifuka, nyumba za watu zilichomwa kwa moto! vilio na mayowe ya maumivu yalisikika kila mahali, watu waliuwana! Damu za watu wasio na hatia zilimwagika!, wanawake walibakwa kabla ya kuuwawa kwa panga, watoto walichomwa moto katika nyumba,.wakati wanaume walikatwa vichwa mala moja kwa upanga,. Yote haya yalitokea Ikiwa ni punde baada ya usiku huo vyombo vya habari kutangaza mauwaji ya rais Juvenal Habyarimana, Matokeo ya siasa za kikabila sasa zikaanza kuonekana,. Watu walichinjana kama kuku,watusi waliuwawa mithili ya nzige dhidi ya wanamgambo wa kihutu{interahamwe} kutoka chama cha MRND. Wao waliita opalesheni safisha Mende, Watusi walikuwa mende mbele ya wahutu, Kigali iligeuka machinjio ya watu, makelele yalilindima masikioni mwa wakazi walio kuwa wamejifungia milango kwa makomeo imara miyoni mwao wakitetemeka kwa mashaka makubwa,. watoto walijificha uvunguni,. hali ilikuwa tete! Laiti kama watu wangejua kitendo cha kujifungia majumbani mwao ni hatari zaidi kwa maisha yao katu wasinge endelea kukaa katika majumba yao wakiwa wamejifungia kwa ndani kwa makufuri mazito,wakiiamini milango yao kuwa ngoa ya kuwatenganisha na madhalimu wauwaji,. Sebastiani na mkewe Sophia walikuwa wakifanya maombi makubwa, waliamini yesu ndiye mwenye kuweza kubadilisha hali ile ya machafuko,na hata kuweza kuikinga nyumba yao dhidi ya kiama kile,. mtoto wao mdogo wa pekee Richard,. alikuwa amejikunyata uvunguni akitetemeka kwa hofu,. Sauti za mayowe za watoto wenziwe waliokuwa wakilia kwa kuomba msaada kutoka nyumba za jirani zilizidi kujenga hofu kubwa kwa Richard,. Magdalena mtumishi wa ndani ya nyumba ya Sebastiani pia alikuwa kajificha katika sinki la jikoni moyo ukimdunda kwa hofu mithili ya ngoma za kihehe,. Kadri muda ulivyo jongea ndivyo Sauti za Wanamgambo wa interahamwe zilivyozidi kukaribia nyumba ya Sebastiani,. Waliimba nyimbo za kuhamasisha oparesheni safisha mende!.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment