Simulizi : Jini Mweupe
Sehemu Ya Tano (5)
…………………………………
Milio ya risasi ikamkulupua usingizini kamanda Kendrick,akavaa suruali, akachukua bastola yake, akafungua mlango taratibu, huku akijiuliza maswali mengi, hakujua amefikaje katika chumba hiki cha wageni, chumba ambacho alipaswa kulala kamanda Catherine.
“,Jitokeze kabla sijawaua wazazi wako, moja, mbili tatu ……”,gaidi lile lilianza kuhesabu, Kendrick hakuwa tayali kuwapoteza ndugu zake, akajibanza ukutani, uso kwa uso na kamanda Catherine akiwa amelala chini.
“,Chuchumaa chini, watakuona, vipi tunafanyaje hapa?,nimefikilia mbinu ya kutumia nimeshindwa”,Catherine alimuuliza Kendrick.
“,Bunduki yako umeweka sailensa(silent mode )?”,Kendrick aliuliza.
“,Ndiyo, nimeweka …”,Catherine alijibu.
“,Piga kule mlangoni, wakiwa bize kuangaza mlangoni risasi hizo, tutaruka na kuwashambulia ,kwanza wako bize wanamuhudumia mwenzao, amefanya nini?……”,Kendrick aliuliza.
“,Nimempiga risasi kwenye dudu lake, alitaka kumubaka mdogo wako, “Catherine aliongea.
“,Sita, saba, nikifika kumi nauwa familia yako yote, nane, “gaidi aliendelea kuhesabu, akatoa onyo, akaendelea tena kuhesabu, Catherine na Kendrick wakasitisha mazungumzo yao, Catherine akapiga bastola kwenye mlango wa kutokea ndani ya nyumba, wote wakageuka, wakautazama.
“,Vuuuup, kwaaacha……”,Kendrick aliluka mateke mawili yaliyosindikizwa na ngumi, akamtandika ngumi gaidi D47 namba sitini ,mateke mawili yakawapata magaidi wawili waliokuwa wanampatia huduma mwenzao, wote wakagagaa. Catherine akawanyoshea bastola, akawateka, Kendrick na yeye akawanyoshea bastola yake.
“,Paaaa! “,alipiga risasi chini, magaidi yakarudisha mikono yao, yalitaka kuzichuka bastola zao zilizodondoka mita kadhaa na mahali yalipodondokea.
“,Mmejileta wenyewe, tulikuwa tumepanga leo tuwasake kona zote za mji huu wa makonda, karibuni sana nyumbani kwangu, “Kendrick aliongea, mkono wake wa kulia ulishika bastola, mkono wake mwingine alikuwa akiwafungua kamba wazazi wake, ghafla mlango ukafunguliwa, kamanda Philipo alikuwa amefika.
“,Ewalaaa! asante sana Mungu, leo sitalala kama maiti ,jana nimechoka sana sababu yenu, kazi ya leo imeisha asubuhi tu, sasa mtakipata cha mtema kuni! “,Kamanda Philipo aliongea, akayafunga kamba magaidi haya manne, huku Jackline akiyapiga teke kwa hasira na kuyatemea mate.
“,Asante wifi, umeyaokoa maisha yangu! “,Catherine alilia kwa furaha akamkumbatia Catherine.
“,Usjali wifi yangu, ni kazi yangu …”,Catherine alijibu.
“,Huyu ndiyo mkwe sasa, Kendrick unajua kuchagua ……”,mzee Steward na mke wake waliongea, wote wakamkumbatia Catherine, walishuhudia ushujaa wake, Kendrick yeye alikuwa amepigwa na butwaa, hakujua chochote kile, Catherine akakonyezana macho na kamanda Philipo, kamanda Philipo alifahamu kila kitu, wote wakatabasamu.
“,Saluti afandee! “,askari watano wenye virungu waliingia ndani, wakapiga saluti.
“,Salutiii, chukueni washenzi hawa, pakieni kwenye karandinga, mpaka chumba cha mateso, tutafika huko kufanya nao mahojiano, “Kendrick aliongea.
“Sawa mkuu, tumefika na kukagua gari lao, tumekuta maiti ya askari wetu anayelinda geti lako, “,askari wale waliendelea kuripoti.
“,Kwahyo wameuaa?”,aliuliza kwa hasira.
“,Ndiyo bosi,maiti iko kwenye gari lao”askari wale waliitikia.
“,Andika kwenye faili, jana wameua watu ishirini na moja, wakateketeza na kituo chetu, huyu ni mtu wa ishirini na mbili, toa taarifa kwa waziri pamoja na vyombo vya habari wapate taarifa hii ……”,Kendrick aliongea.
“,Sawa mkuu, salutii …”,vijana wale waliitikia, wakapiga saluti, wakawabeba msobemsobe magaidi wanne wa D47,wakaondoka nao.
…………………………………
“,Kabla ya yote,usiku mmelala pamoja, sisi kama wazazi tumeshuhudia, kulingana na mila yetu ya , tunapaswa kuwafungisha ndoa na kuwapatia baraka zote, tukiwa tunasubili ndoa rasmi, tucheze ngoma na kuburudika, “mama yake Kendrick aliongea, Catherine akatabasamu, Philipo akatabasamu, Kendrick akatabasamu japo kwa shingo upande.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Mama mimi sikulala naye chumba kimoja, sasa sijui nitamlisha nini! “,Kendrick aliongea, hofu ya majukumu ilimuandama moyoni.Isitoshe hakutambua chochote kile, Philipo na Catherine wakiwa wanachekelea kwa furaha, sio Philipo tu, Jackline alikuwa anafurahi kwa kile ambacho kilikuwa kinafanyika.
“,umelala naye hujalala naye sisi haituhusu, mpatie mkono mwenzako! “,mama Kendrick aliongea, alichoka kusubili mkwe kila siku,akiishia kuambulia ahadi zisizotimia kutoka kwa mtoto wake, leo alimkamatisha.
Catherine akamshika mkono Kendrick, akafunga na kanga mikono yao, akaongea maneno ya kimila, akatoa baraka zake zote yeye na mume wake, wote wakapiga kelele za shangwe. Mama Kendrick akapiga meza kama ngoma, mdundiko ukapigwa, Catherine akacheza, Phipo akacheza, wote uvumilivu ukawashinda, wakaanza kucheza ngoma kwa furaha.
Mtoni Kijichi :08:40am
Nyumba ya Kendrick ilijawa na furaha tele, kila mmoja alicheza kadiri alivyoweza, walisahau kabisa kuwa ilikuwa ni muda wa kazi, burudani iliwafanya wasahau kila kitu, walisahau majukumu mazito yaliyokuwa mbele yao.
“,Kendrick! saa tatu kasoro! “,Catherine aliitazama saa yake, akashtuka sana, muda ulikuwa unazidi kwenda mbele, walikuwa hawajafika ofisini.
“,What!twendeni,bila shaka wanatusubili…”,Philipo aliongea,kila mtu akachukua kilicho chake,Kendrick akaenda kuvaa suti yake nyeusi,wote wakaondoka kuelekea kazini
“,Oooh sitaki kuoa, ooh sijajipanga, utajipanga mpaka lini, utaoa kwa lazima ,mimi ndiyo mama Kendrick ……”,yalikuwa maneno ya mama Kendrick, akiwa amebaki nyumbani, yeye, mume wake pamoja na mwanae wa kike.
“,Kweli kabisa, lakini mimi bado nawafikilia wale majambazi, mimi naona kaka abadilishe kazi, kazi yake ni ya hatari watakuja kufa siku moja! “,Jacline aliongea.
“,Sasa askari wote wakiacha kazi, nani atakulinda?, acha watimize majukumu yao, kila mmoja atakufa, hakuna mtu yoyote atakayeishi milele …”,baba yake Kendrick, mzee Steward aliongea, binti yake akakaa kimya.
“,Haya sasa, mwanangu na mkwe wangu wote askari, nikiguswa tu na majirani,cha moto watakiona! “,mama yake Kendrick aliongea,licha ya kula chumvi nyingi, tabia za uswahilini alikua bado anazo. Waswahili husema ng’ombe hazeeki maini.
“,Sawa mke wangu, ngoja mi nijiandaee,nikazulule mtaani, maana muda mrefu sijaona magari, “mzee Steward aliongea.
“,weweee naye, tabia zako hujaziacha tu,bila shaka umekumbuka wanawake zako,haya kila laheri, uwasalimie wake wenza ……!”,mama Kendrick alizungumza.
“,Mama Kendrick, maneno gani unazungumza mbele ya binti yako, unamfundisha nini huyu mtoto! ……”,baba Kendrick aliongea, hasira zilimjaa usoni, sura yake ikakunjamana.
” ,Wewe naye hutaniwii! nilikua nimekukumbuka mume wangu, nisamehe bure …”,mama Kendrick aliongea, mzee Steward akaelekea chumbani, Jacline akacheka, utani wa wazazi wake ulimfurahisha sana.
………………………………
Chumba cha mateso :
Kendrick, Catherine pamoja na Philipo, walifika chumba cha mateso, chumba ambacho kilipatikana katika gereza kuu la Segerea.Ulinzi uliimarishwa, kila aliyeingia na kutoka, alikaguliwa kwa mashine maalumu ya umeme,hakuna aliyeruhusiwa kuingia na silaha isipokuwa kwa kibali maalumu.
“,You are not allowed to get in, unless you put down your guns ……”,(Hamruhusiwi kuingia ndani, mpaka tu mtakapo weka bunduki zenu chini …).
Mashine ya ukaguzi pembeni ya mlango iliongea kwa sauti, Kendrick, Catherine pamoja na Philipo, wote walikuwa na bastola katika miili yao, Kendrick alikuwa ameipachika kwenye kiatu chake, Philipo alikuwa ameipachika katika koti la suti yake, Catherine alikuwa ameipachika katikati ya mkanda wake.
“,Haina jinsi, milango hii ni ya umeme, msipo weka silaha zenu, milango haitafunguka ……”,askari magereza aliyekuwa anawaongoza aliongea, wote wakachomoa bastola zao, wakampatia mmoja kati ya askari magereza, akazihifadhi kisha wakarudi tena, mashine ikawakagua, walikuwa hawana silaha, mlango ukafunguka, wakaingia ndani, askari mkuu wa magereza alikuwa mbele akiongoza msafara, Kendrick alifuatia, kisha Catherine pamoja na Philipo walifata kwa nyuma.
“,Hawa ndiyo walifanya shambulio la kigaidi, wakateketeza kituo chenu? “,askari magereza aliuliza.
“,Ndio mkuu, tunapaswa kuwahoji tujue Donald Mbeto yuko wapi kwa sasa, ikiwezekana wafanye mawasiliano nao, tukawakamate! “,Catherine aliongea.
“,Magaidi wana roho ngumu, huwa hawasemi kirahisi namna hiyo, mmejipangaje? “,askari magereza aliongea.
“,Watasema tu, twende ukaone! “,kamanda Philipo aliongea, askari magereza aliwaamini sana vijana hawa, siku zote kazi yao ilikua ya uhakika.
Wakatembea korido ndefu, wakapita gereza la kwanza lililojaa wafungwa takribani elfu moja, wakiwa wamelaliana kama ndizi,baada ya dakika tano wakalivuka gereza hili, wakakata kona mkono wa kulia, wakakata kushoto, uso kwa uso na chumba kikubwa kilichozungushiwa nyavu kila kona. Mlangoni kilifungwa na kufuli kubwa la kilo tano, ndani ya chumba hiki kulikuwa na viti vitano, viti ambavyo vilikuwa maalumu kwa ajili ya kutoa mateso pamoja na kunyonga.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Karibuni sana, naona mmefurahi sana, lakini tambueni kuwa, wenzetu wakitambua jambo hili, watakuja kutukomboa ……”,chuma cha pua aliongea, alikuwa na roho ngumu sana, nyeti zake zilikuwa zimefungwa bandeji,haja ndogo alitumia mpira maalumu, lakini hakukoma, aliendelea kuwa katili kama kawaida.Mara tu baada ya kundi la the super three soldiers kuingia ndani ya chumba walichokuwa wamefungwa, aliwakaribisha kwa kejeli.
“,Hahaaaaa, mmekuja na malaya humu ndani! “,magaidi wote watatu walicheka, wakamkejeli Catherine. Catherine akataka kuwasogelea awatandike makonde, Kendrick akamzuia.
“,Nilitaka wote mtumie mipira kukojoa kama mwenzenu, muda mfupi ujao mtalia machozi, chekeni mara ya mwisho! “,Catherine alifoka, ngumi yake alikuwa ameikunja, akachomoa sindano za kibanio chake cha nywele, akajiandaa kutoa mateso wakati utakapofika.
Kendrick alijua nini cha kufanya,akasogelea meza yenye batani nyekundu,akafika, akakaa juu yake. Catherine pamoja na Philipo wakasimama katikati ya magaidi wanne.
“,Mnaweza kutwambia uwezo wa meli yenu ya D47paraquaat ……?”,Kendrick aliuliza swali la kwanza.
“,Hahaaaaa!,kirahisi rahisi hivyo, hata ufanye nini, kuingia ndani ya meli yetu hutaweza dunia yote imeshindwa, sembuse wewe sisimizi mdogo tu ……”,Chuma cha pua alicheka sana, akaongea kwa kejeli, akawaponza wenzake.
“,Yalaaa…aaaa, yalaa…aaa …”,Kendrick alibonyeza batani nyekundu iliyokuwa mezani, kelele za magaidi zikasikika, walipigwa na shoti ya umeme kutoka kwenye viti vya chuma walivyokalia, jasho likawatoka kama maji kwa sekunde moja tu. Baada ya dakika mbili Kendrick akabonyeza tena, shoti ikakata, zingezidi dakika mbili basi angewaua kabisa magaidi hawa.
“,Hehee…ee, bola utuue tu …”,chuma cha pua alicheka tena, Kendrick akakasilika, akabonyeza tena mtambo wa shoti ya umeme.
“,Yaaala…aa, uwiiii…ii! “,,yalipiga kelele, yakalia kwa uchungu.Catherine akayachoma na sindano zake mgongoni, kila mmoja, yakaugulia maumivu.
“,Hatusemi, tuueni tuu! “,yaligoma kutaja, Catherine akapataa wazo, akawaita pembeni wenzake,akawaeleza wazo lake.
“,Sikilizeni, tuyapatie nafasi yawasiliane na wenzao,sisi tujifanye wajinga,yatumie simu yetu kuwasiliana ,kisha tutaunganisha simu yetu pamoja na kompyuta tutajua imepigwa kutoka wapi,hawa wana roho ya paka hawawezi kusema.’ ,Catherine aliongea wenzake wakamuelewa.
“,Kwahiyo mnasema wenzenu wakipata taarifa watakuja kuwakomboa……?”,Catherine aliuliza.
“,Ndiyo,sasa hivi mnajifanya wajanja kwa vile hawana taarifa,Donald Mbeto atawaua nyoteee…”,magaidi haya manne yalijitamba na kuchimba mkwala.
“,Sasa sisi tunataka tuwapige mbele yenu hao mnaowategemea,simu inaletwa,muwapigie,waambieni mmekamatwa,waje wawaokoe……” Kendrick aliongea, yakatikisa kichwa, yakakonyezana.Dakika mbili tu, askari magereza alileta simu, akawakabidhi,chuma cha pua akafunguliwa mkono mmoja, akapatiwa simu,simu ilikuwa imewekwa raudi spika.Akabonyeza namba alizozifahamu yeye, akapiga.
“,Vipi imekuaje, mbona kimya? “,upande wa pili wa simu ulipokea.
“,Njoeni mtuokoe, tumekamatwa,tumebahatisha simu tuwapatie taarifa, “Chuma cha pua aliongea.
“,Hao mbwa wanajiamini nini, ndani ya nusu saa ijayo vijana watakuja kuwakomboa, “upande wa pili wa simu uliongea, simu ikakatwa, Philipo akachukua kompyuta yake, akaunganisha na simu ambayo imetumika,akabonyeza bonyeza, kisha akatoa jibu.
“,simu imepigwa kutoka katika ndege yao, iko futi sitini angani, tayali nimedukua (hack) mifumo yao ya mawasiliano,tuwafuateni huko huko,nyie maboya mmefeli ,hawatatambua mahali mlipo tena……”,Philipo aliongea,akatoka nje,yeye na wenzake,wakaondoka zao.
“,Shiit,roho yangu ilisita,sijui ilikuaje mpaka tukaingia mtegoni…”,magaidi walibaki wanalalamika,hakuna akiyewasikia,chumba chao kilifungwa kwa kufuli kubwa,huku wao wakiwa wamefungwa katika viti maalumu,miguu na mikono.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, katika kundi la D47,alipokea taarifa iliyomshitua sana,baada ya sekunde tu simu ikakatwa, ghafla mifumo yote ya mawasiliano ikazima.
“,Banard kuna nini?, “mmoja wa magaidi alimuuliza Bernard, mkuu na mtaalamu wa mitambo ya mawasiliano katika meli ya magaidi wa D47.
“,Wenzetu wanne ,kitengo cha Dar es salaam, Tanzania wamekamatwa! inatakiwa wakombolewe kabla hawajauawa, lakini ghafla simu imekatwa,nilipojaribu kutafuta mahali ilipotokea, mifumo yote imezima ……”,Benard aliongea.
“,Ina maana mifumo yetu ya ulinzi imedukuliwa? “,mmoja kati ya magaidi, chumba cha mawasiliano aliuliza.
“,Itakua hivyo, kampatie taarifa bosi haraka sana! “,Benard aliongea, akajaribu kurekebisha mitambo ikagoma, kompyuta zote zilikuwa zimezima. Ndani ya dakika tano tu, bilionea Paresh Kumar alifika katika ofisi hii, akiwa ameongozana na Donald Mbeto.
“,Bosi nimepokea taarifa, wenzetu wa Dar es salaam wamekamatwa! nilipojaribu kutaka kujua eneo walilopo, kompyuta zote zikazima, mifumo yetu imedukuliwa, ndiyo narekebisha, mpaka turudi hewani, saa moja litakua limepita tayali! “,Benard alitoa maelezo kwa bosi wake.
“,Sawa, weka mambo sawa, kisha fanya utundu wako tujue eneo walilopo,tutume vijana waende kuwakomboa! “,Paresh Kumar aliongea, Benard akatikisa kichwa, aliyaelewa maelekezo aliyopewa, akaanza kutekeleza kama alivyoelekezwa. Paresh Kumar akaondoka zake, akiwa pamoja na rafiki yake kipenzi, kijana wake wa kazi, jini mweupe au Donald Mbeto.
…………………………………
Kamanda Kendrick, Catherine, pamoja na Philipo walikuwa katika mavazi yaleyale ya kazi,usoni walivalia miwani yao ya mionzi,bastola zao zilikuwa kiunoni. Helikopta ya kivita iliiacha ardhi ya jiji la Dar es salaam saa tano kamili asubuhi, siku ya jumamosi.
“,ndege yao iko futi sitini juu,upande wa kaskazini,tunapaswa kuingia ndani ya ndege yao kabla mifumo yao ya mawasiliano haijawa activated ndani ya saa moja!”,kamanda Philipo alitoa maelekezo,akaeleweka,rubani akaendelea kutimiza majukumu yake.Makamanda watatu walijiandaa,walikuwa tayali kwa lolote lile,Catherine alikuwa bize akichukua silaha za kumfaa,silaha moja baada nyingine,katika sanduku kubwa ambalo walilipakia katika ndege,silaha za kila aina,silaha kubwa na ndogo.
“,Mabomu haya yatanifaa,visu hivi vitanifaa kufyeka shingo zao,bunduki kubwaa sitaki,bastola yangu inanitosha……”,Catherine aliongea,alikuwa amekamilika.
“,Mimi sichukui chochote kile,kisu changu,bastola yangu,pamoja na miwani yetu ya mionzi inatosha,……”,Kendrick aliongea,akatazama saa yake,ilikua saa tano na dakika kumi na tano,walikuwa wamekalibia,mahali ndege ya magaidi ilipoweka kambi angani.
“,Haloo,haloo ovaa,usawa wa ndege,usawa wa ndege mnatupata ovaa!”,simu ya mkonga ilisikika,upande wa pili wa simu uliongea.
“,tunawapata,tunawapata ovaa!”,rubani alizungumza.
“,Mmekalibia,angalieni mbele yenu,kazi ianze mara moja…”,kitengo cha mawasiliano cha jeshi walifatilia kila hatua za ndege yao,hawakutaka ishambuliwe kwa mara nyingine tena.Wakampatia maelekezo rubani wa ndege yao,kisha simu ikakatwa.
“,Tumefika,nazani ndiyo ndege hiyo kubwa mnayoiona mbelee yenuu……”,rubani aliongea,huku akishangaa,hakuwahi kuona ndege kubwa na ya ajabu kiasi kile.
“,Whaaat!ndege nzuri sana na kubwaa,Kendrick,tusitumie milipuko yoyote,tunapaswa kuilinda iwe salama,tukishinda vita hii,ndege itaifishwe iwe mali ya serikali ……”,Catherine aliongea, alishangazwa na ndege iliyonekana mbele yao.
“,Kweli kabisa, wazo zuri sana, ina maana hii ndiyo ilitushambulia? “,Philipo aliongea, akauliza swali, macho yake yalitazama mita mia mbili mbele yake, helikopta yao ikasogea karibu kabisa na ndege hii, ili wapate nafasi ya kuikamata kwa mikono sehemu yoyote ile, waweze kuingia ndani.
“,Ndiyo hii, kazi ianze mara moja! “,Kendrick aliongea kwa kifupi, akakamata bawa la ndege ya maadui wakapanda juu yake, alilikamatilia bawa kwa nguvu, akishindana na upepo mkali. Wenzake wakafanya kama yeye, wote wakakamatilia bawa la ndege ya magaidi wakaanza kuisogelea taratibu, upepo mkali ukivuma, lakini walikua imara, hawakutikisika, miwani ya mionzi ilifanya kazi yake ipasavyo, ikawakinga na upepo mkali machoni.
“,tumia emergency exit! kioo hicho hapo mbele, kisogeze chini juu, tuingie wote haraka sana kabla upepo haujaingia ndani ya ndege na kutuzidi nguvu …”,kamanda Philipo alitoa maelekezo,Kamanda Kendrick akafanya kama alivyoelekezwa, dirisha likafunguka, akaingia ndani, Catherine akafuatia, Philipo akawa wa mwisho, akarudisha kioo cha dirisha mahala pake, wote wakatokea ndani ya chumba cha choo.Huku ndege ikitikisika kwa sekunde kadhaa kisha ikarudi mahala pake.
…………………………………
“,Mbona ndege imetikisika kiasi hiki, ina maana kuna sehemu ya ndege yetu iko wazii, au tumevamiwa? “,rubani wa ndege hii ya magaidi alizungumza, machale yakamcheza,akamtuma msaidizi wake,kepteni ambaye alifanya kazi ya kuongoza ndege hii inaposafiri kama meli baharini, alikuwa na wasiwasi uliopitiliza.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Mwambie bosi,walinzi wakague kila sehemu, ulinzi uimalishwe, kila mtu achukue pozisheni yake,dirisha la dharula bila shaka lilikuwa wazi”rubani wa magaidi aliongea.
“,Sawa, hata mimi nimewaza jambo hilo! “,kepteni wa magaidi aliongea, akatoka chumba cha kuongoza ndege hii ya D47paraquaat, akaondoka zake.
…………………………………
“,bosi, bosi! “,kepteni alifika katika ofisi ya Paresh Kumar, bosi akashtuka, alikuwa ananyonyana ndimi na wanawake zake wa kizungu, wakakurupuka, walishtukizwa.
“,Mbona unaingia ofisi ya bosi wako bila taarifa, kuna tatizo gani? “,Paresh Kumar alifoka kwa hasira.
“,Bosi, dirisha la dharula lilifunguliwa muda mfupi uliopita, kisha likafungwa tena, hatujui kama aliyefanya hivyo ni mtu wetu au adui yetu, nimetumwa kuleta ripoti, ulinzi unapaswa kuimalishwa “,kepteni aliongea,maneno yakapenya vizuri katika kichwa chake, akawasukumia mbali wanawake zake, akafunga vifungo vya shati lake, akaondoka zake, akawaacha wanawake zake wa kizungu wakiwa na hasira, mmoja alikuwa na sindilia, mwingne alikuwa amebaki na bikini yake, ofisi ya Paresh Kumar ilikua zaidi ya kasino,uovu mwingi ulifanyika masaa yote. Akatoka nje ya ofisi yake, uso kwa uso na Donald Mbeto.
“,Kila mtu achukue pozisheni yake, hakikisheni aliyeingia ndani ya ngome yetu hatoki salama, maraisi wao waliowatuma, watajuta!!nitafanya mauaji mpaka nikabidhiwe migodi ninayohitaji, haiwezekani waingie madarakani kwa msaada wangu harafu waninyime ninachohitaji, walizani pesa zangu za kampeni ninawapa bure, kijani wangu utaendelea kufanya mauaji mpaka niseme basi, haya ondoka mara moja,kafanye kama nilivyokuagiza! “,Donald Mbeto alipokea maelezo kutoka kwa bosi wake, akaanza kazi, bosi wake alikuwa amekasirika, kengele ya hatari ikapigwa.
“,danger! danger! everyone should take his position (hatari! hatari!, kila mtu achukue nafasi yake…) ,Donald Mbeto maarufu kama jini mweupe alipiga kelele, magaidi wakakimbia huku na kule, kila mmoja akikamata silaha inayomfaa kwa mapambano.
Catherine, Kendrick pamoja na Philipo, walichungulia kupitia matundu madogo, katikati ya mlango, hawakuona mtu yoyote yule,Wote wakiwa na miwani yao ya mionzi mikali yenye lenzi, wakakitazama kitasa cha mlango kwa sekunde mbili, kitasa kikayeyushwa na mionzi mikali kutoka kwenye miwani, kitasa kikayeyuka,mlango ukafunguka. Wakatoka nje, uso kwa uso na bunduki nane, kulia na kushoto, mbele yao, kote kulikuwa na bunduki, waliwekwa chini ya ulinzi na magaidi waliovalia suti za bluu, zenye nembo ya D47.
“,Tumewakamata! hahaaa, tuwapeleke kwa bosi! “,magaidi yale yalicheka, the super three soldiers hawakuongea kitu chochote kile, walizitazama bunduki walizowekewa kichwani, sekunde mbili tu, bunduki za magaidi wale zilipigwa na mionzi kutoka kwenye miwani, bunduki zikayeyuka,zikawa kama uji.
“,What! nini hiki, maajabu haya! “,magaidi wale walishangaa,kitendo cha bunduki zao kuyeyuka kiliwashangaza sana, wakasahau kama walikuwa wamewaweka watu chini ya ulinzi.
“,Vuuuup, vuuuup, vuuup …”,Kendrick alipiga ngumi tatu, zikawapata magaidi watatu kichwani,wakadondoka chini, Catherine akaluka mateke mawili, magaidi wawili wakandoka chini, wakabaki wawili, wakiwa wamesimama, walikuwa hawajielewi, kitendo cha bunduki zao kuyeyuka mbele yao walikiona cha ajabu sana, wakawa kama vichaa, wakataka kukimbia, Kamanda Philipo alichomoa visu viwili, akavirusha, vikawapata mguuni, wakadondoka chini.
“,Yala…aaa, mmetuumiza washenzii nyie ……”,magaidi yale yalitukana,lakini haikubadirisha kitu chochote kile, Kendrick, Catherine pamoja na Philipo walichomoa bastola zao wakayanyoshea magaidi yale.
“„Nyote ingieni humo chooni haraka sana, nasema ingieeni! “,Kendrick aliyakalipia, magaidi sita yakiwa yameweka mikono kichwani yakaingia, kamanda Philipo akayaburuta magaidi ambayo yalichomwa na visu mguuni, yalikuw hayawezi kutembea, wote wakawekwa chooni.
“,Catherine akachomoa bomu lake dogo, akachomoa pini, akalitupilia ndani ya chumba cha choo.
“,Puuuuuu, puuuuuu! “,mlipuko ukasikika, ndege ikatikisika tena, kisha ikarudi katika hali yake ya kawaida, Kendrick na wenzake walilukia upande wa pili, wakalala chini, hawakujeluhiwa popote pale.
“,Umefanya nini, tulikubaliana vipi? situlisema hakuna kutumia milipuko …”,Kendrick alilamika.
“,Haina jinsi, hiyo ndiyo mbinu ya kuwaua kwa urahisi, muda mfupi ujao, wote watafika eneo hili, utaona watakavyo kufa,”Catherine aliongea, akachomoa mabomu yake mawili madogo, akayaseti yalipuke ndani ya dakika tano, wote wakatembea harakaharaka, mpaka mahali kulipokuwa na magari pamoja na ndege za kivita nyingi sana.
“,Waooooh! “,Philipo hakusita kuonesha furaha yake,alitazama ndege,magari pamoja na vifalu vya kivita,ghafla kundi kubwa la magaidi lilisikika,wakija mahali kuliposikika mlipuko,Catherine na kundi lake wakaingia chini ya magari,wakajificha,hawakuonekana,magaidi yakapita bila kukagua kona zote,lilikuwa kundi la magaidi takribani mia moja.
“,Hawa wehu,wametuchokoza,wameua wenzetu,mimi ndiye Donald Mbeto mwenyewe,nasema hivi,hawatoki salama mahali hapa……”,Donald Mbeto aliongea,alikuwa hana silaha yoyote ile mkononi,tofauti na wenzake ambao kila mmoja alikuwa ameshika bunduki yake.Alizigeuza geuza maiti za wenzao,moshi ukiwa unaishia na kubaki kweupe,mlipuko huu haukuhalibu ndege hii,bali iliwasambaratisha vipande vipande magaidi nane.
“,Kuna mabomu!kuna mtego”,Donald Mbeto aliongea,akaluka serekasi,akatua upande wa pili,akalala chini.
“,Puuuuu,puuuuu,puuuu,”mlipuko ulisikika tena,mabomu ambayo Catherine aliyatega,akayaweka chini ya maiti,yalililipuka,magaidi mia moja ambao waliongozwa na Donald Mbeto walijeruhiwa vibaya sana,wengine wakafa palepale.Isipokuwa Donald Mbeto ambaye hakujeruhiwa mahali popote pale.Akanyenyuka ,vijana wake walikuwa wameumia vibaya,wengine walivunjika shingo,miguu na wengine walikatika viuno.
“,Huo ni uzembe katika kazi,hunifaaii……”,Donald Mbeto aliongea,akammalizia gaidi mwenzake ambaye alivunjika miguu yote miwili,lakini alikuwa bado mzima,akilia na kuhitaji msaada.
“,Twendeni,twendeni tukaone,watakua wamekufa!,huo mlipuko sio wa kawaida…”,Philipo alitoa wazo lake.
“,Hapana,tusiende,wenzao najua watasogea tena,tusubili kidogo…”,Kendrick akakataa,akatoa sababu,wote wakakubaliana naye.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Jitokezeni,mbona mnajificha,kama nyie ni mashujaa kweli jitokezeni!”,sauti ilisikika,Donald Mbeto alipiga kelele,akafoka kwa hasira.
“,Hajafa,unamsikia anavyotukana,muda ukifika tutajitokeza,asiwe na shaka……”,Catherine alizungumza,mkono wake wa kulia alikuwa ameshika bastola mkono wa kushoto ulishika mabomu mawili.Aliona ndio silaha pekee ya kuua watu wengi kwa muda mfupi tu.
Ghafla sauti za watu kukimbia zilisikika,wote wakageuza shingo zao,wakatazama mahali sauti za vishindo zilikuwa zinatokea,jeshi kubwa lilikiongozwa na mwanaume wa kihindi lilisogea mahali mlipuko ulikuwa umetokea,mikononi walishika bunduki zao,walijiamini sana.
“,Kendrick tunafanya nini!”,Catherine aliomba ushauri kwa Kendrick,huku akifikilia mbinu ya kufanya.
“,Wote hawajui mahali tulipo,pembeni yetu kuna ndege nyingi kubwa,ndege zenye makombola,tukipanda ndege moja,shambulio moja tu tunawatekeza woteee!”,kamanda Philipo alitoa mawazo yake.
“,Wazo zuri sana,lakini vipi kuhusu mtuhumiwa wetu,tunapaswa kuondoka na Donald Mbeto kutoka mahali hapa,lazima akaonje joto la jiwe,asife kirahisi tu,anapaswa kufa kama alivyotesa raia wasio na hatia…”,Kendrick aliongea.
“,Nimewapata hilo niachieni mimi,pandeni ndani ya ndege,lakini msifanye chochote mpaka niwajulishe……”,Catherine alizungumza,kamanda Kendrick aliangalia kushoto na kulia,hakuna aliyewaona,akaingia ndani ya ndege ya kivita,kamanda Philipo akafuatia,wakasubili amri kutoka kwa Catherine,Catherine alipita chini ya magari,hakuonekana,jeshi la magaidi liliendelea kusogea mahali mlipuko ulikuwa umesikika,akarusha mabomu mawili,katikati ya miguu ya magaidi,kisha akarudi ,akipenyeza chini ya uvungu wa mataili ya gari pamoja na ndege.
“,Ukisikia mlipuko,washeni ndege,watakua bize na kujihami,nyie mtatumia upenyo huo kuwasogelea na kuwashambulia,hakikisheni mtu yoyote hapati upenyo kusogelea eneo hili,akaingia ndani ya vifaru,mtakua mmekwisha…”,Catherine aliongea.
“,Puuuu,puuu,puuuu,”mlipuko ukasikika,magaidi wengi wakafyekelewa mbali,bilionea Paresh Kumar alikufa palepale,magaidi wengine walizitupa silaha zao,wakalala chini kuepuka mlipuko huu,Kendrick akatumia mwanya huu,akawasha helikopta kubwa ya kivita,kamanda Philipo akachomoa makombola,yakatokeza pembe zote,mbele makombola mawili,nyuma makombola mawili,wakaanza kupaa hewani,ndani ya ndege hii kubwa yenye vioo kwa juu,kiasi kwamba anga lote lilionekana,ndege ya magaidi ikitaka kujigeuza umbo la meli,vioo ambavyo vimeifunika ndege vinajifunua,mabawa yanarudi kwa ndani.
Kendrick alipaa,hakutaka kupaa juu zaidi,angegonga vioo ,upepo ukaingia ndani ya ndege kubwa ya magaidi,akahatarisha maisha yao,alipofika usawa wa kufanya mashambulizi,futi kumi kwenda juu,akaisogeza helikopta eneo la magaidi,akafyatua makombola mawili,yakatekeza kundi lotee.
“,Bosiiiiiii ,bosiiii!”,Donald Mbeto alishuhudia kitendo cha bosi wake kushambuliwa,akakimbia mpaka eneo la tukio,kila kiungo cha bosi wake kilikuwa mahali pake,akakasirika.
Catherine alitabasamu,ushindi ulikuwa umekalibia,akaanza kusogea taratibu,kwa mara ya kwanza alikutana uso kwa uso na Donald Mbeto.Catherine alitazama juu,Kendrick alikuwa ameelekeza makombola kwa Donald Mbeto,alitaka kummalizia palepale.
“,Hapana,usimuue,nataka nimvunje miguu,mimi mwenyewe!”,Catherine aliongea kwa sauti,akawakataza wasimuue,kisha akakunja ngumi,Donald Mbeto akazifunga rasta zake nyeupe,akajikuna kidevu chake,akakunja ngumi.
11:40am
Donald Mbeto alimtazama Catherine juu mpaka chini,akamtazama usoni, kisha akaitazama miguu yake,alikuwa anafikilia mbinu ya kumshambulia, aivunje miguu yake. Donald Mbeto aliluka mateke mawili hewani, Catherine akazuia mateke yote kwa mikono yake,hajakaa sawa alipigwa ngwala akadondoka chini, Donald Mbeto akaluka hewani, akarudi chini kwa kasi akiwa amekunja kifuti cha mkono wake, akafika juu ya mguu wa Catherine, akaupiga na kifuti.
“,Kachwaaaaa!!, “mguu wa Catherine uliitikia.
“,Yalaa…aa! “,Catherine alipiga kelele, akajigeuza upande wa pili, akampiga Donald Mbeto na teke usoni, akadondokea upande wa pili, damu zikimvuja mapuani.
“,Shiiit! amemuumiza, atamuua, tushuke chini
……”,Kendrick akiwa juu ya helikopta, aliona kila kitu kilichokuwa kinaendelea,hisia za mapenzi zikamsumbua, alikuwa na hofu ya kumpoteza Catherine.
“,Usiwe na hofu, naona sasa mapenzi yameshakuingia, umeshapenda tayali ,usjali Catherine ni komandoo……”,kamanda Philipo alimuondoa shaka Kendrick.
“,Hapana, mwanamke ni mwanamke siku zote, isitoshe mtu anayepambana naye ni hatari sana,ameshamtemgua mguu ……”,kamanda Kendrick aliongea.
Catherine alijaribu kusimama,alishindwa,mguu wake wa kushoto ulikuwa na maumivu makali, aliteguliwa, alimanusura avunjwe mguu, akajaribu kusimama tena, akadondoka chini, mguu wake ulimuuma sana, alikuwa hananguvu kabisa.
“,Lazima ufe,huwezi kutoka salama, huwezi kumuuwa bosi wangu halafu uwe salama,mimi ndiyo jini mweupe,shujaa wa dunia”Donald Mbeto aliongea, akazishika rasta zake nyeup, akazifunga vizuri, akajikuna kidevu chake, akaanza kumsogelea Catherine aweze kummalizia.
Catherine alimuona Donald Mbeto akimsogelea, alimuangalia usoni, akayatazama macho yake kwa makini, akazitambua hisia zake, alikuwa anakuja kumshambulia, Catherine akajiandaa, japo alishindwa kusimama, lakini alijiamini, Donald Mbeto alipofika mahali Catherine alipokuwa, aliluka tena juu, akashuka chini kwa kasi na pigo lile lile, alitaka kuvunja mguu mwingine wa Catherine, Catherine alinyanyuka juu kama mzuka, akaluka hewani,mkononi alishika kisu chake, wote wakakutana hewani, alilipangua teke la Donald Mbeto akamsindikiza na visu viwili, alichoma visu viwili Donald Mbeto miguu yote ,kulia na kushoto,haikutosha, akampiga na teke, akadondokea mita kadhaa kama mzigo. Donald Mbeto akalia kwa uchungu,hakuwa na uwezo wa kusimama tena.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“,Haya sasa, wote viwete! “,Catherine aliongea,akatazama helikopta juu yake, akawanyoshea mkono Kendrick na Philipo, wakaishusha helikopta,Kendrick akachomoa pingu, akamfunga Donald Mbeto, wakamnyenyua na kumuweka kwenye helikopta,Kendrick akaipaisha juu, ikapasua vioo vya ndege kubwa ya magaidi hawa,ikatokomea hewani.
“,Bado kuna magaidi, wamejificha, lipua ndege yoteee! “,Kendrick aliongea,kamanda Philipo akafanya kama alivyoelekezwa, akaruhusu makombola mawili, yakaipiga ndege, ikapepesuka, ikapoteza mwelekeo, akaipiga tena na makombola mengine mawili, ikalipuka na kuungua moto, Kendrick akageuza helikopta, akaanza kurudi kusini,kisha akakunja tena kona, akaelekea mashariki, akaanza kuishusha chini helikopta, futi arobaini mpaka therathini,akaanza kurudi Dar es salaam,Tanzania
…………………………………
Chumba cha mateso :2:20
Magaidi wanne walisubili waweze kukombolewa,muda ukazidi kwenda, hakuna chochote kile kiliweza kutokea.
“,Tujikomboe sisi wenyewe, bila hivyo tutakufa, kifo chetu ni kunyongwa, hakuna hukumu nyingine tofauti na hiyo ambayo tunaweza kupewa …”,chuma cha pua aliongea.
“,Kweli kabisa, lakini gereza hili lina ulinzi mkali, hatuwezi kutoka kirahisi kama unavyofikilia ……”,gaidi D47 namba sitini aliongea.
“,Ngoja niwaoneshe,askari atakaye tuletea chakula, akitufungua tu mahali hapa,mimi naan.……”,chuma cha pua kabla hajamaliza kuongea,Catherine, Kendrick pamoja na Philipo walitokeza, Kendrick alikuwa anamburuta mtu hatari sana ambaye hawakutegemea kama angeweza kukamatwa.
“,Donald, wamekukamata! “,magaidi walishangaa, wakanyongonyea,nguvu zikawaishia.
“,Mliyekuwa mnategemea atakuja kuwakomboa huyu hapa, huu ndiyo mwisho wenu, chombo chenu tumekilipua,hakuna aliyetoka mzima zaidi ya huyu mtuhumiwa wetu, tunataka afe mbele ya raia ……”,Catherine aliongea, akiwa anatembea kwa kuchechemea, akamnyenyua Donald Mbeto, akamkalisha kwenye kiti cha mateso kilichokuwa wazi, wakamfunga mikono na miguu.
“,Hapa hamuwezi kutoroka kamwe! hata mfanye nini hamtaweza, subilini hukumu yenu ya kunyongwa hapohapo kwenye viti vyenu ……”,Kendrick aliongea,akamshika mkono Catherine, akambusu, akamsaidia kutoka ndani ya chumba cha mateso, walikuwa wamekamilisha kazi, kama ilivyotakiwa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa za kukamatwa kwa Donald Mbeto zikasambaa duniani kote,waandishi wa habari kutoka mataifa mbalimbali duniani walifika nchini Tanzania, walitaka kufanya mahojiano na Donald Mbeto, wampige picha na kuitambua sura yake,hawakutaka kupitwa na taarifa za mtu huyu,lakini ulinzi ulikuwa mkali,wengi walizuiliwa,vyombo vya habari kutoka Tanzania vikaifanya kazi hiyo.Huku hukumu ya magaidi hawa watano ikisubiliwa kwa hamu na watu wote duniani.
…MWISHO…………………
The super three soldiers walizawadiwa tuzo za heshima, kutoka mataifa yote ambayo Donald Mbeto maarufu kama jini mweupe alitekeleza mauaji ya sumu, Kendrick na Catherine wakafunga ndoa, huku kamanda philipo akiwa Mc wa ndoa yao.…
0 comments:
Post a Comment