Search This Blog

Monday 24 October 2022

NI ZAMU YAKO KUFA - 5

 









    Simulizi : Ni Zamu Yako Kufa

    Sehemu Ya Tano (5)





    Ndiyo! jambo moja Jacob Matata alikuwa amekosea. Hakuwa anajua kuwa nyumba aliyokuwa akiiendea ilikuwa na mitambo maalumu ya ulinzi. Mitambo hiyo ilikuwa na uwezo wa kumwona yeyote aliyekuwa eneo la kuzunguka jengo hilo kwa umbali wa mita thelathini. Hivyo Jacob alionekana tangu akiwa ananyatia kusogelea jengo hilo. Max, ambaye jina la siri katika operesheni hii alijulikana kama ‘bosi mwenye ndevu nyeupe’, alipewa taarifa juu ya ugeni huu. Walinzi waliokuwa katika mitambo ya kuangalia usalama kuzunguka jengo hilo hawakuweza kumtambua Jacob Matata. Hii ilisababishwa na sura ya bandia aliyokuwa amevaa.

    Ni wanausalama wengi ambao walikuwa wamewahi kuwekea shaka jumba hili. Hii iliwafanya mara kwa mara kutaka kuingia katika jumba hili, lakini mara nyingi juhudi zao ziliwafikisha mikononi mwa Max na kuzawadiwa kifo.

    Ilikuwa ni mara ya kwanza kuonekana mtu akitaka kuingia kwenye jengo hili katika mtindo aliotaka kuutumia Jacob, hivyo Max alipopewa juu ya taarifa hiyo alitaka kumwona mtu mwenyewe.

    Jinsi mtu huyo alivyokuwa akifanya mambo yake mpaka kuwaua wale mbwa kule nyuma ya ukuta, ilikuwa ni ujumbe tosha kwa akili ya Max kuamini kuwa aliyekuwa amekuja kuwatembelea hakuwa mwingine ila mpelelezi Jacob Matata. Alishindwa kujua kama ashukuru kwa kitendo cha Jacob kujileta au alaani. Lakini ukweli ulikuwa wazi moyoni kwake kuwa Jacob ndiye mpelelezi pekee ambaye alikuwa amemtoa jasho mpaka wakati huu.

    Tangu apewe agizo la kuwamaliza wapelelezi wote ambao wangetia mguu katika mji wa Arusha, Max alikuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Utaalamu na uchu wa fedha walizokuwa wameahidiwa uliwafanya watu wake wafanye kazi kwa kasi na bidii ya ajabu. Hakuwa akichelewa kupata taarifa za kuwasili kwa mpelelezi yeyote ndani ya mji wa Arusha. Wapelelezi toka Kenya,Uganda, Rwanda, Burundi na nchi nyingine za ukanda huu ni baadhi ya watu ambao tayari walikuwa wamemalizwa na kundi hili la Max.

    Mtu mmoja tu ndiye aliyekuwa akimzuia asikabidhi kazi, naye ni Jacob Matata. Tangu aingie Arusha imekuwa ni patashika tu.

    Wakati huu alipomwona Jacob anakuja Max alijiwa na maamuzi mawili. Moja ni kumkaribisha Jacob na pili ni kumkamata Merina.

    Merina kwa muda mrefu amekuwa akijulikana kama ‘malaika mweusi’ katika kundi hilo. Jina hili lilitokana na sifa za Merina. Alikuwa ni msichana katili na aliyeonekana kuwa mwema sana. Ni kwa sifa hizo Max alikuwa na hakika kuwa akimweka msichana huyu ili afanikishe kumnasa Jacob angefanikiwa. Kwani alishasikia kuwa Jacob alikuwa ni dhaifu mno kwa viumbe hawa wa kike.

    Na kweli mpaka siku za hivi karibuni, Merina alikuwa amefanikiwa kumwadaa Jacob Mtata kwa kujifanya kuwa ana machungu juu ya mauaji ya baba yake. Muda wote ambao Merina amekuwa na Jacob, amekuwa akitoa taarifa zote juu ya mwenendo na mipango ya Jacob Matata. Hata hivyo jambo moja lilikuwa likimshinda dada huyu juu ya Jacob Matata ni juu ya tabia ya mpelelezi huyo kutokuwa anatabirika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa Merina, Jacob alionekana kama mtu asiyetabirika na asiyekamatika kwa urahisi.

    Max alianza kutilia shaka utendaji wa ‘malaika mweusi’ yaani Merina. Hii ni kutokana na sehemu alizokuwa akiwaambia kuwa wangempata Jacob kukuta mara nyingi kuwa Jacob hakuwepo sehemu hizo.

    Hivyo kitendo cha kuona Jacob ameshafika kwenye himaya yake, Max aliamini kuwa malaika mweusi kwa sehemu alikuwa ameshindwa kazi yake.

    Kutimiza alichotaka kufanya wakati huu ikambidi Max aende kwenye chumba ambacho Jacob aliweza kumsikia wakati akiongea na Merina. Max aliongea kwa sauti makusudi akijua kabisa kuwa Jacob alikuwa akimsikia pale dirishani. Wakati akiongea hivyo tayari alikuwa ameshaandaa vijana wa kwenda kumpokea Merina, na wakati huo huo kwenda kumpokea Jacob pale nyuma ya nyumba.

    Alikuwa anamjua vizuri Jacob na Merina. Hakuna hata mmoja kati ya hao aliyeitaji kufanyiwa mchezo. Hivyo ulinzi na umakini mkubwa uliwekwa wakati watu hao wakitarajiwa kukamatwa.



    * * *



    Merina hakuwa amejiandaa kwa hilo. Hakutarajia kumkuta Jacob akiwa katika eneo kama hilo. Hivyo alishindwa kuuficha mshangao wake pale alipomkuta Jacob akiwa ndani ya chumba hicho huku wote wakiwa mateka. Walikuwa ni mateka kwa makosa tofauti.

    Mzee mwenye kipara alikuwa ni mmoja wa wauaji katili wa kundi hili la Max. Ndiye aliyeonekana kuongoza ulinzi katika chumba hiki ambacho Jacob na Merina walikuwa ni mateka.

    Jacob alinyang’anywa kila kitu alichokuwa nacho. Kisha akaamuliwa kukaa kwenye kiti fulani pembeni kabisa mwa chumba hicho. Jacob hakushindwa kutambua kuwa kiti hicho kilikuwa cha umeme maalumu kwa ajili ya kutesea watu. Lakini pamoja na kutambua hilo alitii na kwenda kukaa. Alipokaa tu kiti hicho kilitoa vitu kama mikono na kumshika kwa nguvu kiasi hakuwa na uwezo hata wa kutingisha miguu.

    “Hivi Max ndiyo unafanya nini…” Kabla Merina hajamaliza kauli yake alitulizwa kwa kofi kali toka kwa mzee mwenye kipara ambaye sasa alionekana dhahili kuwa alikuwa hana utani. Kuona amechapwa kofi, Merina alikuja juu na kuruka karate tatu mfulizo ambazo zote mzee mwenye kipara aliziona na kutoa kipigo ambacho kilimwacha Merina akiwa hoi bin taabani.

    Jacob alijikuta akimwusudu sana mzee mwenye kipara kwa jinsi alivyopanga na kuachia lile pigo, ilionyesha kuwa hakuwa wa kawaida katika fani. Alitamani wapewe uwanja lakini alijua hilo lisingeruhusiwa. Hakuwa na hakika kama angekuja pata nafasi ya kufanya hilo.

    “Jacob nasikitika kuwa leo ndio utakuwa mwisho wako. Hakuna cha kuweza kukufanya utoke salama katika mkono wangu. Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitakumaliza pasipo angalau kukupa ya kwenda kusimulia huko kuzimu unakoenda. Jaji Gordon tulimmaliza pasipo kujua sisi ni nani, hivyo itakuwa vizuri ukitujua na kwenda kuwajulisha huko waliko marehemu wote. Nitakueleza ili ukawaeleze sisi ni nani na tunafanya nini.

    Kwa kifupi sisi ndiyo waafrika tulio na mawazo ya kutaka kutumia mali tilizojaaliwa na mungu kuwa nazo hapa Afrika. Japo Umma wote na nchi zetu zinajaribu kutangaza suala la usawa ili hali ikijulikana wazi kuwa usawa si rahisi kufikiwa kwa sababu watu hatulingani kamwe”. Max aliruhusu mate kupita kisha akaendelea

    “Hatulingani kwa maana ya mitazamo na njia za kuweza kufanikiwa…. ...Wengine wanataka kuvuja jasho sana ili kufanikiwa, ili hali wengine hawako tayari……… ..Nasikitika kukuambia kuwa sitakuwa na mengi ya kukueleza na naamini kuwa hii ni siku ya mwisho kwa mimi kuonana na wewe kwani hutaliona jua la kesho” Aliongea hayo huku Jacob na wengine chumbani humo wakiwa wamenyamaza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tofauti na mawazo ya Max, Jacob alikuwa amezama katika kufikiri namna ya kuweza kujikwamua toka katika kitanzi hicho cha mauti.

    “Lazima uelewe Jacob kuwa sasa ni wakati wa watu wanaotaka maendeleo kuchukua nafasi zao. Tulifanya makusudi mazima kuvumisha taarifa kuwa kuna silaha za kibaolojia zimeingizwa katika nchi hii ili kufanyiwa majaribio. Tulijua fika kuwa wakuu mbali mbali wa nchi za ukanda huu wangetuma wapelelezi ili kuja kuchunguza juu ya hilo. Hakukuwa na sababu yoyote iliyotufanya tumuue jaji Mark Gordn na wale wagonjwa katika hospitali ya mkoa. Lengo hasa la kufanya hivyo ilikuwa ni kuwavuta ninyi wapelelezi mmiminike hapa Arusha, ambapo tumeandaa kundi hatari kabisa la kuwamaliza.

    Mpaka sasa tumeshafanikiwa kumaliza wapelelezi wote waliokuwa wametumwa na nchi zao kuja kufanya upelelezi juu ya uvumi ulioonezwa na sisi. Kifo chako na mpelelezi mwingine toka Kenya kitakuwa kimehitimisha kazi yetu kwa awamu ya kwanza….” Max alitaka kuendelea lakini alikatizwa na swali la Jacob.

    “ Najua kuwa hutafanikiwa kuniangamiza mimi, lakini kama ukifanikiwa nini itakuwa awamu ya pili? Jacob aliuliza huku sasa akianza kusikia maumivu kutokana na mbano ambao alikuwa akiupata toka kile kiti cha umeme alichokuwa amekalia.

    “ acha ujinga Jacob Matata, swali lako linaonyesha dhahiri ni jinsi gani huna uhakika wa kutoka hapa salama. Hivyo kabla sijajibu swali lako, napenda kukuhakikishia kuwa hutatoka hapa salama, kwani hakuna aliyewahi kuingia katika mikono yangu akatoka akiwa hai. Kwa vile umeomba kujua nini tutafanya sisiti kukueleza kuwa kesho mimi na kundi langu tutakuwa miongoni mwa watu matajiri katika nchi hii. Tutalipwa kitita cha pesa nyingi kwa kazi ya kufanikiwa kuwahadaa na kuwamaliza wapelelezi wa hadhi na ngazi yako katika ukanda huu. Nina hakika itawachukua muda mrefu wakuu wa idara za usalama wa nchi hizi kufikiria juu ya nini cha kufanya baada ya vifo vyenu.

    Pili, ni kuwa, waajili wetu watatupa kazi ya kuanza kuchukua mali mbalimbali katika ukanda huu. Bila shaka kwa kuanzia tutaanza na kwenye madini ya tanzanite kule Mererani. Kwa kifupi itakuwa ni burudani na raha tupu. Wakati huo hakutakuwa na mtu wa kutuzuia, maana watu kama wewe tumeshafanikiwa kuwamaliza” Alipofika hapo alitoa kicheko fulani cha kutisha sana.

    Kiti alichokuwa amekalia Jacob kiliendelea kumbana kiasi kuwa sasa akawa anapumua kwa shida, huku akiendelea kufikiri ni namna gani anaweza kujitoa mikononi mwa hao jamaa. Inaaminika kuwa akili za Jacob huongeza kasi ya kufikiri na usahihi kila anapokuwa katika wakati mgumu kama huu.

    “Wewe kwa vile umejaribu sana katika kuvuruga mipango yetu, kama ni kufa ni lazima utakufa huku ukituacha sisi tukielekea katika ngazi ya umilionea” Alipomaliza kusema hivyo, Max alisimama toka kwenye kiti alichokuwa amekaa. Alitoa bastola yake katika mfuko wa koti lake jeusi. Alienda kwenye kona moja, kisha akatoa ishara fulani kwa vibaraka wake waliokuwa hapo. Wote wakachukua nafasi zao chumbani humo.

    Merina alikuwa wa kwanza kujua nini kilikuwa kinaenda kufanyika. “Washenzi, mnatuua bila kosa lolote la msingi. Lakini lazima mjue kuwa arobaini yenu ipo na haiko mbali sana. Nasikitika kuupoteza muda wangu mwingi kwa kuwapa taarifa juu ya Jacob, ningejua ningemleta na kumpeleka kote mlikokuwa” Merina alisema maneno hayo kwa uchungu baada ya kutambua kuwa watu hao hawakuwa wa kutumikiwa. Kisha akageuza kichwa chake na kumwangalia Jacob Matata ambaye alionekana kutokuwa na uwezo tena kutokana na mateso aliyokuwa akiyapata kwenye kile kiti.

    “Jacob, naomba unisamahe na tafadhali utakapokutana na baba usimwambie juu ya hili nililomtendea. Najua huna kosa na kwa hivyo utaweza kukutana na baba huko aliko, nina makosa kwa hiyo nikifa sitakwenda kuishi sehemu ambayo ninyi wenye haki mtakuwa mnaishi milele…” Merina alisema maneno hayo kwa uchungu sana huku akimtazama Jacob.

    Jacob hakuyasikia maneno yote ya Merina! Tayari alikuwa ameshapoteza fahamu. Kiti alichokuwa ameamuriwa kukikalia kilikuwa maalumu kwa ajili ya mateso. Mara kikaliwapo huanza kumbana aliyekikalia mpaka kinamwua, ili mtu atoke salama juu ya kiti hicho ilibidi mtu azime swichi inayopeleka umeme kwenye hicho kiti. Hali hii ndiyo ilimtokea mpelelezi Jacob Matata, kwani mara baada ya kuwa amekaa kwenye hicho kiti alianza kubanwa taratibu mpaka wakati huu akajikuta amepoteza fahamu. Hakuwa amesikia maneno ya Merina.

    Max na kundi lake walikuwa tayari kuwamaliza mateka wao hao. Mzee wenye kipara alikuwa ameamuriwa kummaliza Merina ili hali Jacob angemalizwa na risasi za bastola ya Max.

    Chumba kilikuwa kimya kabisa huku Merina ambaye wakati huu alikuwa na fahamu zake kama kawaida, alikuwa akisubiri risasi kupenya kichwa chake. Hakuwa na namna ya kujiokoa.

    Wakati chumba kikiwa kimejaa hali ya mauaji na wauaji wakiwa tayari, ghafula kukatokea kishindo kikubwa na chumba chote kikawa kimejaa moshi mwingi. Kwa kasi ya ajabu Max alijirusha huku akimiminia risasi pale alipokuwa Jacob. Mzee mwenye kipara naye alijirusha kwa stahili ile ya Max, lakini yeye risasi zake zilimiminika pale alipokuwa amekaa Merina.





    Lakini si Max wala mzee mwenye kipara aliyefanikiwa lengo lake. Si Jacob wala Merina aliyepatwa na risasi za wauaji hao.

    Mtu mmoja tu ndiye aliyekuwa amefanikisha mahesabu yake, kwani kwa wakati mmoja alifanikiwa kufanya mambo matatu. Sekunde ya kwanza alipiga teke mlango wa chumba walichokuwa wakina Jacob. Sekunde ya pili aliitumia kupasua bomu la machozi alilokuwa nalo huku akirukia pale alipokuwa Jacob na kumkumba wote wakaanguka chini. Wakati ametua chini alijiviringisha na kwenda kukikumba kiti cha Merina nacho pia kikaanguka chini. Hivyo wakati Max na yule mzee mwenye kipara wanawahi kumimina risasi pale alipokuwa Jacob na Merina walikuwa tayari wameshachelewa kwani Jeti Maroo alikuwa ameshawawahi.

    Max hakuwa na uhakika kuwa risasi zake zilifanikiwa kumwingia Jacob Matata. lakini hakuwa na muda wa kuhakiki hilo. Kilichoshangaza ni namna mtu aliyeingia alivyofanikiwa kuingia ndani ya jumba hilo bila mwenyewe kuwa na taarifa. Hivyo kwa kutumia njia zake za siri alifanikiwa kutoka nje. Lengo lake ilikuwa ni kuwahi kutoka ili awaamuru na kuwaongoza vijana wake waliokuwa nje katika kuwamaliza wote waliokuwa ndani. Lakini wazo hilo lilipotea mara tu alipofika nje. Hakuwakuta vijana wake, bali maiti zao zikiwa zimetapaa kila sehemu. Kilichomshitua zaidi ni kule kugundua kuwa idadi kubwa ya walinzi hao hawakuwa wameuawa kwa risasi. Hii ilimwonyesha kuwa aliyekuja kumwokoa Jacob hakuwa mtu wa ka .

    Hiyo ilikuwa kazi ya Jeti Maroo. Na kwa hakika si mzee wa kawaida katika mchezo huu. Huyu ndiye yule mzee dereva aliyempokea Jacob Matata wakati anafika Arusha. Huyu ndiye yule aliyekuwa amepewa kazi ya kumsaidia Jacob Matata pindi akihitaji msaada. Kazi hii alipewa na mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi Bi. Anita.

    Jacob hakuwa anamjua vizuri mzee huyu. Hili pia lilifanya kutopenda kumshirikisha katika mipango yake mingi. Lakini mzee huyu ni miongoni mwa wapelelezi wa siri sana wa Ofisi Fukuzi. Kazi zake amekuwa akifanya katika mazingira ya kutoeleweka na yeyote zaidi ya mkurugenzi wa ofisi hiyo ya upelelezi.

    Mzee huyu alikuwa na utaalamu wa juu katika judo na kareti, pia alikuwa na uwezo wa kutumia silaha ya aina yoyote. Hii ndiyo iliyomfanya mkurugenzi wa Ofisi Fukuzi Bi. Anita amchague mzee huyo kumsaidia Jacob katika kazi hiyo.

    Pamoja na Jacob kuonyesha hali ya kutokuwa tayari kushirikiana naye, lakini Jeti Maroo hakukata tamaa na wala hakuacha hata hatua moja ya Jacob. Alikuwa akienda naye kila alipokuwa akienda. Alifanya yote hayo bila Jacob mwenyewe kujua.

    Ni katika kufuatilia huko ndipo alipofanikiwa kuongozana na Jacob kwa siri mpaka kwenye jumba hili la Max. Jumba ambalo Jeti alikuja gundua kuwa lilikuwa limesheeni sayansi na teknolojia ya juu. Kwani tangu pale Jacob alipotekwa nyara, yeye alianza harakati za kuhakikisha kuwa anamwokoa.

    Kazi ya kukifikia katika chumba walichokuwa wamewekwa Jacob na Merina haikuwa rahisi. Alikutana na vikwazo ambavyo kama si utaalamu na jitihada binafsi basi na yeye angekuwa katika chumba kile akisubiri risasi ipenye maungo yake. Ilimlazimu kutumia ujuzi wa judo na kareti ili kuweza kuwashinda vijana wa Max bila ya kushitukiwa na yeyote.

    Alimwona Max wakati akizama kwenye njia yake ya siri lakini hakupata nafasi ya kumfanya lolote. Jeti Maroo alimfungua Jacob ambaye hata hivyo hakuwa anajua lolota lililokuwa likiendelea kwani alikuwa bado amezirahi. Kama kawaida yake Jeti Maroo, tabasamu lilikuwa usoni.



    Max alipoona kazi iliyokuwa imefanywa na Jeti Maroo, hakuchelewa kujua nini kifanyike. Alimwamuru mzee mwenye kipara aandae gari la kuondoka nalo, kisha yeye akisaidiwa na vijana waliokuwa nao kwenye chumba walichokuwa wakitaka kuwaua Jacob na Merina waliingia kwenye chumba cha siri cha Max. Max alikuwa na hakika kuwa wangewahi kutoka kabla huyo mtu aliyekuja kuwaokoa Merina na Jacob hajatoka. Hata hivyo aliona ni hatari kuondoka hapo kama asingezichukua taarifa zake za siri zilizokuwa ndani ya chumba hicho cha siri.



    * * *

    Tangu walipokuwa wamefanikiwa kutoka katika jumba la Max, Jeti Maroo alikuwa na wasiwasi na hali ya Jacob Matata. Lakini wasiwasi huo haukuzidi ule aliokuwa nao msichana Merina. Alijiona ni msaliti na alihitaji msamaha wa Jacob Matata haraka iwezekanavyo. Hapa walikuwa nyumbani kwa Jeti Maroo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutokana na shughuli zake za siri kubwa, ofisi ya upelelezi Ofisi Fukuzi ilikuwa imempangishia nyumba karibuni kila mkoa nchini. Hii ndiyo ile nyumba ambayo Jacob na Merina walilala siku moja.

    Kabla hawajaondoka kwenye lile jumba la Max, walijaribu kuchunguza na kutafuta lolote ambalo walihisi lingeweza kuwasaidia. Hawakufanikiwa kupata lolote. Ndipo walipoanza safari ya kuja hapo nyumbani kwa huyo mzee Jeti

    “Inaonekana ule umeme kwenye kiti ulimuumiza sana…!!!! Mzee Jeti Maroo alisema huku akimwangalia Merina.

    “Kile kiti ni hatari, tena nashukuru kwa vile tu Jacob ni mtu wa mazoezi. Hakuna mtu ameshawahi kukaa kwenye kile kiti muda mrefu hivi na akawa bado anamatumaini ya kuishi. Kile kiti hutoa roho za watu vibaya sana” Merina alisema huku kiganja cha mkono wake kikiwa kinapita juu ya uso wa Jacob katika staili ya kuufuta.

    “Unaonaje kama tukitafuta daktari ili aje kumuhudumia? Merina alisema kwa sauti iliyoweka bayana huruma aliyokuwa nayo. Kabla mzee Jeti hajajibu, wote walishangaa pale waliposikia sauti ikijibu “Hamna haja ya kwenda”. Ilikuwa ni sauti ya Jacob. Merina aliruka kwa furaha.

    Jacob Matata alisimama na kujioonya kidogo. Kisha kama aneyeota alishangaa kidogo. Mzee Jeti Maroo alitoa huduma zote ambazo zilihitajika kwa Jacob.



    Saa sita usiku ilipokuwa inagonga, wote walikuwa kimya sebuleni. Jacob ndiye aliyekuwa wa kwanza kuongea, “nimekuwa nje ya ulimwengu kwa muda. Sijui ni namna gani nimeweza kutoka katika kile kinywa cha mauti? Ningependa nijue” Alisema huku akimtazama mzee Jeti Maroo.

    Hapo Mzee Jeti Maroo akachukua fursa kumwelezea Jacob kila kitu mpaka akafanikiwa kuwokoa katika mikono ya Max na Mzee mwenye kipara. Jacob alishukuru kwa hilo, akavuta pumzi ndefu kisha akamgeukia Merina. Macho yao yalipokutana safari hii hayakuwa yale waliyokuwa wamezoea kutazamana. Macho ya Jacob yalionyesha dhahili kuwa alikuwa kazini.

    “Merina ni wakati wako sasa wa kuweza kutuambia pande zote mbili za wewe. Sina haja ya kujua wewe ni nani maana hilo nalijua, ila sasa napenda kujua ukweli kuhusu wewe na kundi hili” Jacob alisema huku sauti yake ikiwa ngumu kiasi cha kumwogopesha Merina. Merina alitabasamu, kisha alianza kueleza moja baada ya jingine. “………..kwa kifupi ni kuwa walikuwa wamefanikiwa kuniajili kama mpiganaji upande wao. Ila mimi sikuajiliwa na huyu Max, mimi niliajiliwa na raia mmoja wa Canada aitwaye Allan Hilton. Huyu ndiye hasa aliye nyuma ya kila jambo linalofanyika hapa Arusha na kundi hili….” Hayo yalikuwa ni baadhi ya maelezo ya mwisho ya Merina.

    “Kwani lengo hasa la huyu mzungu Allan Hilton kuwatuma hawa watu hapa nchini ni nini hasa? Jacob Matata aliuliza kwa sauti ya kutafakari sana.

    “ Mimi alipokuja kuniajiri alisema kuwa alitaka nimsaidie kazi ya kuchukua mali hapa nchini. Lengo hasa ilikuwa ni kuiba kiwango kikubwa cha madini katika machimbo ya mererani. Nilipofika hapa nchini nilielezwa kuwa Max ndiye angekuwa kiongozi wa shughuli zote ambazo ningetakiwa kufanya nikiwa hapa. Sikuwa na shaka kwa kuwa nilijua kazi yenyewe ingekuwa ni uhalifu wa kawaida tu.

    Nilianza kupatwa na wasiwasi kufuatia kifo cha baba. Nilipokuja gundua kuwa kundi hili ndilo lilomuua baba niliapa kuwa ipo siku ningelipiza kisasi. Bado nilikuwa na hamu ya kupata pesa nilizokuwa nimeahidiwa kama mshahara kwa kazi ambayo ningepangiwa hapa.

    Siku chache zilizopita, tuliitwa na Max na akatuambia kuwa amepokea maagizo toka kwa bosi kuwa tulitakiwa kuwamaliza wapelelezi wote mashuhuri katika ukanda huu. Kazi hiyo tuliianza mara moja, huku wewe ukiwa ni miongoni mwa walengwa. Mpaka sasa tumeshafanikiwa kuwamaliza wapelelezi wote waliokuja hapa Arusha kufuatia taarifa za kuingia na kuwepo kwa silaha za hatari kwa njia zisizo sahihi. Taarifa hizo ni za uongo na zenye lengo la kuwavuta ninyi wapelelezi mje ili muuawe.

    Wewe pekee ndiye unayelisumbua kundi hilo mpaka sasa. Kama ungeuawa jana basi leo kulikuwa na kikao na huyo mzungu ambapo angetupangia kazi nyingine ambayo bila shaka ingekuwa ni kwenda kwenye machimbo ya tanzanite kule mererani kwa ajili ya kufanya uporaji mkubwa.

    Ila kwa sasa nachoweza kusema ni kuwa, naomba unisamehe kwa yote yaliyopita, kuanzia sasa nitakuwa upande wenu na upande wa baba yangu asilimia mia moja” Merina alisema hayo huku macho yake yakiwa yameelekezwa kwenye saa ya ukutani.

    “Mbona unaangalia saa ya ukutani, kuna nini? Jacob aliuliza

    “Muda huu ndiyo ilikuwa imepangwa kuwa kundi lote lingekutana kwenye nyumba fulani ya mmoja wetu ili tuweze kuongea na huyo bosi. Bosi huyo inasemekana alifika hapa tangu juzi, na alikuwa na hakika kuwa kufikia jana tungekuwa tumemaliza kazi ya kuwamaliza wapelelezi wote. Kwa sasa zimebakia dakika kadhaa kabla mkutano huo haujaanza, labda wawe wamehailisha” Merina alisema hayo huku akiwaangalia Jacob na Jeti Maroo kwa zamu.

    Jacob alimchunguza Merina na kutambua kuwa sasa alikuwa akiongea ukweli. Tofauti na siku kadhaa zilizopita ambapo alikuwa akimtilia mashaka.

    “Hebu kabla hatujaendele mbele zaidi ningependa kujua maana na watu wenye majina haya; Malaika wa giza, bosi mwenye ndevu nyeupe na mtakatifu wa kuzimu” Jacob aliuliza hayo huku akiwa anasimama na kuliendea jokofu la vinywaji baridi lilokuwa sebuleni hapo.

    Kidogo Merina alionekana kushangazwa na jinsi Jacob alivyoweza kuyajua majina hayo. Kwake majina hayo aliyafahamu yote lakini hakutegemea kama Jacob angeweza kuyajua kwa siku chache tu alizokuwa amekaa Arusha. Hapo akajikuta anamnyooshea Jacob mikono kimoyomoyo.

    “Mtakatifu wa kuzimu ni jina alilopewa Max, yule aliyetaka kutumaliza. Bosi mwenye ndevu nyeupe ndiyo yule Mzungu Mr. Allan Hilton. Malaika wa giza ni jina nililopewa mimi. Majina haya yalitolewa kulingana na sifa za mtu. Bila shaka nimejibu swali lako? Merina alimalizia kwa swali, huku Jacob akiwa anakaa mara baada ya kuwa amechukua bitter lemon moja toka jokofuni.

    “haya malaika wa giza nimekupata, sasa nadhani ni vema tuakaenda kwenye hicho kikao ili tuweze kuona kama twaweza kuwapata hawa jamaa. Na ili kwenda huko inabidi tuwe tumejiandaa kikamilifu na twende tukiwa kamili, kwani na wao watakuwa wakifanya mambo yao chini ya ulinzi mkali sana hivi sasa” Jacob alisema huku akimwangalia mzee Jeti Mroo ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mzee jeti, una silaha na vifaa vya kututosha katika vita hii iliyoko mbele yetu? Jacob alihoji





    “Usihofu, hapa nina vifaa vya kuweza kutosha wanajeshi hamsini wa kimarekani. Nadhani hapo unaweza kujua ni jinsi gani sina uhaba wa vitu kama hivyo” Alisema Jeti Miroo katika ali ya kujigamba.

    “Basi nadhani tutumie muda huu kuchagua vitendea kazi ambavyo tutaenda navyo huko” Alisema Jacob Matata huku akivuta pumzi ndefu, bila shaka kuashiria kuwa kazi ilikuwa inaenda kuanza ama kumalizika. Tayari ilikuwa inakimbilia saa saba na dakika saba za usiku.

    * * *

    Usiku huo huo ambao mpelelezi Jacob Matata, Jeti Maroo, na msichana Merina walikuwa wanajiandaa kwenda sehemu ambayo ilipangwa kuwe na mkutano wa kundi hatari la Max, upande mwingine nao ulikuwa na yake. Mzungu Allan Hilton na Max walikuwa wamezama katika mazungumzo ya mipango na mikakati mizito.

    Walikuwa ndani ya nyumba moja iliyo katikati kabisa ya mji wa Arusha. Nyumba hii ilikuwa imewekewa ulinzi wa kutosha.

    Max alishaona hatari na makali ya mpelelezi Jacob Matata, kwa hivyo aliakikisha kuwa ulinzi unaimalishwa kila sehemu waliyokuwa.

    Siku moja kabla, ujio wa huyu mzungu – Allan Hilton ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu. Lakini kwa mambo ambayo yalikuwa yamefanywa na Jacob Matata yalitia dosari ujio huo wa Allan Hilton.

    Ilivyokuwa ni kwamba Allan angekuja huku Jacob Matata tayari akiwa ni marehemu. Mauti ya mpelelezi Jacob Matata yangehitimisha kazi ya awamu ya kwanza ambayo kundi hili lilikuwa limepewa na Allan Hilton. Kuja kwa Allan kungemaanisha wapiganaji wa kundi hili kupata malipo yao kwa kazi ya kwanza. Lakini mtu mmoja tu alikuwa kikwazo.

    “Kuna mtu mmoja tu ambaye amefanya kazi yetu kuingia dosari. Huyu ni mpelelezi toka hapa hapa Tanzania. Tumekuwa katika harakati za kummaliza lakini hatujafanikiwa. Nathubutu kukiri kuwa mtu huyu si wa kawaida kwani mara nyingi amekuwa akifanikiwa kukwepa mitego yetu.

    Lakini isiwe tatizo, kwa vile Merina atakuwa amechukuliwa na Jacob, na Merina anajua kuwa tutakuwa na kikao usiku huu, basi twaweza kuwa na nafasi nyingine ya kummaliza Jacob Matata.

    Tayari nimeshatuma vijana wa kutosha kwenda kule tulikokuwa tumepanga kufanyia kikao chetu. Nina hakika kuwa Jacob atakuwa ameshajiandaa kuja pale kwa lengo la kutupata. Hapo ndipo atakutana na kiama yake. Kwa maana hiyo naomba tuahilishe mambo na mipango mingine, ili kesho tuifanye huku tukijua kuwa hakuna wa kutuzuia. Kitendo cha huyu Jacob kuwa hai ni hatari sana kwa kazi yoyote ile tanayodhamiria kuifanya” Max alitoa maelezo hayo huku ndani yake akiwa amejawa na hasira iliyochanganyika na aibu.

    Allan Hilton hakuwa na namna ila kukubaliana na ushauri wa Max. Hivyo ikaamuliwa kuwa kila kitu kisimamishwe mpaka hapo watakapokuwa wamefanikiwa kumwua Jacob Matata.



    * * *http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kama nilivyokuwa nimesema hali inaonyesha kuwa wameshajiandaa kutupokea, ona ulinzi ulivyoimarishwa…” Jacob alisema toka sehemu waliyokuwa wamejificha ili kuweza kuona hali ilivyokuwa kwenye nyumba ambayo waliamini kuwa mkutano ulikuwa ukifanyika.

    Tayari kwa msaada mkubwa wa Merina walikuwa wameshafanikiwa kujipenyeza na na kuwa hatua chache toka lilipokuwa jumba hilo. Jumba ambalo Merina aliwaelekeza kuwa ndimo ambamo mkutano baina ya kundi na Allan Hilton ungefanyika lilikuwa kubwa na la aina yake. Kulikuwa na ukuta mkubwa kuzunguka eneo lote la nyumba hiyo, huku kukiwa na geti moja tu la kuweza kupenya ukuta huo.

    Walinzi aliowaona Jacob kwa nje tu, ilitosha kumthibitishiaa kuwa watu hao walikuwa wamejiandaa kutokana na silaha na vifaa walivyokuwa wamesheheni.

    Baada ya kuangalia kwa kitambo Jacob alipata wazo; “angalieni, miye nitapanda juu ya mti ule ili niweze kuona hali ilivyo ndani ya ukuta huu” Jacob alisema huku akiwaacha Merina na Jeti Maroo wakiwa wanajiweka sawa ili kumlinda pindi akiwa anapanda mti alienda mpaka ulipokuwa ule mti.

    Alikuwa na utaalamu wa kupanda miti, hivyo alifika juu ya Mti bila hata ya huo Mti kutoa ukelele ambao ungewashitua walinzi walokuwa macho kama Paka mwenye njaa.

    Alipokuwa juu aliweza kuiona sehemu ya ndani kuzunguka jumba hilo vizuri sana. Aliweza kuwaona walinzi wakiwa wameenea kila sehemu. Akiwa bado anaangalia, alisikia mtu akikohoa chini alikokuwa amewaacha Jeti Maroo na Merina. Alidhani ni ishara toka kwa wenzie, hivyo alipoangalia chini macho yake yalikutana na kitu kingine tofauti na wale aliotarajia kuwaona hapo chini. Mdomo wa bastola aina ya KAHR K9 ya kiingereza ulikuwa sambamba na uso wake, huku uso wa mtu aliyekuwa ameshikiria bastola hiyo ukiwa umefunikwa kwa ile stahili ya kininja. Jacob hakuishia hapo, aliangalia pale alipokuwa amewaacha Jeti Maroo na Merina hakukuwa na mtu. Hapo akili yake ikamwambia kuwa mambo yameiva.

    Kabla hajafanya lolote alitupia macho ndani ya jumba hilo, hapo mwili wote ulimsisimka pale alipowaona Jeti Maroo na Merina wakiwa wanaongozwa kuingia ndani chini ya ulinzi mkali.

    Tabasamu lililokuwa usoni mwa mpelelezi Jacob Matata lilimshangaza jamaa aliyekuwa chini akimsubiri. Pamoja na kuwa alikuwa akitazamana na mdomo wa bastola hatari ya KAHR K9, lakini hakutaka kuonyesha hali ya kubabaika. Alifanya hivyo makusudi kwani alijua fika kuwa hilo lingemweka mtekaji wake katika wakati mgumu.

    “Sasa mbona umebaki kushikilia bastola tu, ua hujui matumizi yake, maana kama ningekuwa mimi tayari ningekuwa nimeshausarambatisha ubongo wa mtu kwa risasi tamu” Jacob alisema hayo huku akiwa anamwangalia mtekaji wake. Jamaa hakuonekana kutikiswa wala kubabaishwa na maneno ya Jacob. Kwa ishara tu, alimwashiria Jacob ashuke toka juu ya mti.

    Wakati anashuka Jacob alitumia fursa hiyo kuangalia saa yake na kubaini kuwa tayari ilikuwa ametimia saa nane na nusu usiku. Jacob alijua kuwa kuruhusu achukuliwe na huyu jamaa ingekuwa ni kufa kikondoo. Alijua fika kuwa ni rahisi kujiokoa toka kwenye mikono ya huyu jamaa mmoja, kuliko kwenda kufanya hivyo ndani ya jumba lililokuwa limejaa kila dalili ya ubaya na unyama kwa watu kama yeye.

    Hivyo akawa anashuka kwa mahesabu makubwa sana, huku akitafuta kosa lolote toka kwa adui wake. Jamaa aliyekuwa ametumwa kuja kumchukua Jacob hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa ni komandoo kamili. Hivyo mahesabu yaliyokuwa yakipigwa na Jacob wakati akishuka alikuwa akiyabaini kwa haraka zaidi. Hata wakati Jacob anafika chini huku akiwa amejiandaa kimapambano tayari huyu jamaa alishatambua hilo. Ila hakutaka kumwonyesha Jacob kuwa alikuwa ni mwerevu wa saizi yake.

    Jamaa huyu haikuwa mara yake ya kwanza kuzisikia sifa za Jacob Matata. Alikuwa ameshazisikia sehemu nyingi ambazo amewahi kufanya kazi kama hizo katika bara la Afrika. Hivyo leo alipoambiwa kuwa alitakiwa kuja hapo kumchukua Jacob aliona kama ni bahati kwake. Ni bahati kwa vile mara nyingi aliamini kuwa mengi yaliyokuwa yakinenwa kuhusu Jacob yalikuwa ni uongo mtupu. Alitaka ajaribu kiwango!

    “Weka mikono yako juu, kawaida huwa natoa onyo mara moja tu, usijaribu kufanya hila yoyote ile ambayo itatibua tabia yangu ya kutoa roho za watu kama wewe” Jamaa alionya mara tu Jacob alipokuwa amefika chini. Jacob alitii na kuweka mikono juu kama alivyokuwa ameamuriwa. Macho yake yalikuwa yakiangalia kila kiungo cha huyo jamaa. Alikuwa akitafuta mpenyo tu ili afanye vitu vyake.

    Hamu ya kutaka kupimana ubavu na Jacob ilimwongezeka huyo jamaa. Hivyo kwa makusudi akafanya kosa ambalo alijua kwa kiwango cha mpelelezi kama Jacob asingesita kulitumia ili kujaribu kujiokoa. Jamaa huyo alishusha bastola yake na kuifutika kiunoni, kisha akatoa vyuma kama pingu na kumsogelea Jacob Matata.

    Jacob alipoona hivyo aliona kuwa huo ndiyo ulikuwa mwanya wa yeye kujiokoa. Hakujua kuwa jamaa alifanya hivyo makusudi ili waingie katika kuonyeshana ujuzi. Jamaa alipomfikia Jacob alifanya kama aliyetaka kumfunga. Hapo ndipo Jacob alibadilika ghafula na kuwa mtu mwingine kabisa. Aliruka pembeni na kuachia mateke mawili ya kasi sana. Kwa vile jamaa alitegemea Jacob angefanya hivyo, alikuwa ameshajiandaa. Hivyo aliyakwepa mateke yote na kuruka juu kama nyani.

    Tayari eneo hilo likawa limeshageuka uwanja wa mapambano. Kila mmoja akawa amejipanga. Jacob alipoangalia namna jamaa alivyokuwa amejipanga, mara moja akatambua kuwa alikuwa anapambana na mtu ambaye ni komandoo kama yeye. Hivyo ushindi hapo ulitegemea ujanja kwani utaalamu walikuwa sawa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jamaa alirusha mapigo mawili katika mtindo wa judo, Jacob alifanikiwa kukwepa moja, moja lilimwingia. Wakati anajiweka sawa jamaa alikuja hewani kwa mtindo wa mwewe kuchukua kifaranga, alipotaka kuachia kipigo kwa Jacob alikutana na hewa tu, kwani tayari Jacob alikuwa ameshahama na kunesea upande mwingine. Hapo hapo Jacob alijikunjua kwa mateke mawili ya kasi mno yote yakampata jamaa. Jamaa huyo alitoa mguno ulioashiria kuwa kipigo hicho kilimwingia. Pamoja na hayo hakuchelewa zaidi kwani Jacob alijikuta tu kitu kizito kinatua shingoni kwake na kumpeleka chini. Alipotua chini ndipo alipotambua kuwa lilikuwa ni teke lililopigwa kiufundi. Ilibidi atumie nguvu za ziada kutoka pale alipokuwa ameangukia kwani tayari jamaa alikuwa hewani na alikuwa akishuka kwa pigo fulani ambalo Jacob alibaini kuwa kama lingempata basi angewafuata marehemu wengine waliotangulia. Hivyo alijiviringisha kwa kasi ya kimbunga na kusimama pembeni huku akisubiri jamaa atue pale chini. Jamaa kuona hivyo hakutua kizembe, alitua kwa sarakasi ya kifundi zaidi ambayo ilimwacha Jacob mdomo wazi.

    Jacob alijifanya kama anainama vile jamaa akajisogeza, Jacob akaachia ngumi tatu za kasi sana, wakati jamaa akielekea chini kufuatia ngumi hizo kumpata barabara, Jacob alimsindikiza kwa mateke mawili ambayo aliyapiga kwa ule mtindo wa kininja. Jamaa alitua chini huku akiugulia kwa maumivu. Jacob hakutaka kumpa nafasi kabisa, alimfuata kwa hadhali na kasi. Alijifanya kama anataka kumnyanyua jamaa akarusha teke moja kulenga paji la uso wa Jacob, Jacob akaliona na kumpa kareti mbili za shingo zilizompata sawasawa. Jamaa akalegea!





    MWISHO







0 comments:

Post a Comment

Blog