Search This Blog

Friday, 28 October 2022

JINI MWEUPE - 4

 









    Simulizi : Jini Mweupe

    Sehemu Ya Nne (4)





    Kisiwa cha Comoro :



         Kendrick aliyafumbua macho yake,akapapasa mikono yake huku na kule, akashika magome ya miti, akashtuka, akanyenyuka na kuketi, uso kwa uso na mzee mwenye umri sawa na marehemu baba yake, alipoyageuza macho yake upande wa pili, pembeni na mzee yule, alikutanisha macho yake na msichana mweupe,akiwa amevalia magome ya miti yaliyozuia sehemu zake za siri pamoja na matiti yake, macho yake yakashindwa kuvumilia,kope zake zikayaachia uhuru macho yake, yakatazama uzuri wa msichana huyu juu mpaka chini, akatabasamu, akamshukuru Mungu kwa uumbaji wake wa ajabu.



    “,Hapa ni wapi?,nyie ni akina nani? “,Kendrick aliuliza, akasimama, akaangaza huku na kule, aliona nyumba moja ya makuti iliyozungukwa na minazi mingi.



    “,Huu ni ufukwe wa kisiwa cha Komoro! “,mzee yule alimjibu Kendrick, akazidi kumpatia maswali mengi kichwani mwake yasiyokuwa na majibu.



    “,Nimefikaje hapa? “,Kendrick aliuliza tena.



    “,Nilikuokota baharini ukiogelea katikati ya bahari,nilikua navua samaki, nikasogeza mtumbwi wangu karibu nawe, ulikuwa umeishiwa nguvu, ukapoteza fahamu, kabla hujazama nilikuokoa na kukuweka katika mtumbwi wangu, nikakuleta mpaka hapa, naitwa mzee Fedinand, huyu ni binti yangu, anaitwa Upendo ………”,mzee yule alimaliza kumwelezea Kendrick, akajitambulisha, akamtambulisha na binti yake wa kike, wote wakatabasamu, walifurahi sana kukutana na mswahili mwenzao kwa takribani miaka kumi sasa, wakiishi peke yao ufukweni, wakivua samaki, kula matunda na kuwinda wanyama.



    “,Kabla sijajitambulisha,kwanini mko hapa, makazi haya yanaonekana yako mbali na binadamu, hamuogopi kuishi peke yenu?, hamuogopi maharamia, vipi kuhusu wanyama wakali, hamuwaogopi? “,Kendrick aliongea kwa mshangao, macho yake yakiangaza umbali wa mita kadhaa mbele yake, akaona bahari, kushoto aliona msitu mkubwa wa minazi, akageuza shingo yake mkono wa kulia, aliona minazi mingi sana, nyuma yake vivyo hivyo, kulikuwa na msitu mkubwa wa minazi, akapigwa na butwaa!



    “,Huyu ni binti yangu, ana miaka ishirini na mbili kwa sasa, akiwa na miaka kumi na mbili, tulisafiri naye kwenda Zanzibar kwa mapumziko  mafupi, tukapata ajari na Mv Spice,tulifanikiwa kuwahi maboya mimi na mwanangu, nikaogelea naye, nikiwa nimemshika ipasavyo mpaka tukafika hapa, tumeishi naye mpaka leo hii, sijawahi kuona binadamu yoyote, leo ndio nimekuona wewe eneo hili ……”,mzee yule alitoa maelezo marefu, kamanda Kendrick akamuangalia machoni, macho ya mzee yule yalisema ukweli, hayakudanganya chochote kile, Kendrick akamuamini mzee yule.



    “,Naitwa kamanda Kendrick, askari mkuu wa kikundi cha upelelezi cha the super three soldiers kutoka Tanzania, tukiwa katika majukumu yetu, ndege yetu ililipuliwa na maharamia, mpaka sasa sijui wenzangu wako hai au wamekufa! “,kamanda Kendrick alijitambulisha,mzee Fedinand na binti yake wakatazamana, kisha wakamtazama tena Kendrick.



    “,Mzee, haukuona mtu yoyote eneo hilo la bahari tofauti na mimi? “,Kendrick aliuliza tena.



    “,Hapana, sikuona chochote kile! “,mzee yule aliongea, binti yake akanyenyuka, akaenda ndani ya kibanda cha makuti, akarejea tena, mkononi alishika samaki waliochomwa,wakiwa wamefungwa vizuri kwenye majani ya miti, akasogea karibu na Kendrick, akapiga magoti kwa heshima, akamnawisha, akampatia samaki, akaanza kula.



    “,Sasa itakuaje?, natamani sana mwanangu kurudi Tanzania, nazani nyumbani mke wangu na watoto wanne wanazani tumeshapoteza maisha, isitoshe kwa sasa wamekua, natamani sana kuwaona! “,mzee yule aliongea kwa hisia kali, akadondosha chozi, binti yake na yeye uvumilivu ulimshinda,akamfuta machozi baba yake, huku na yeye chozi likimtiririka.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Msijali ondoeni shaka, mko mikono salama, mshukuruni Mungu kuwalinda kwa miaka kumi,kama mko salama mpaka leo hii, basi hamtapatwa na kitu chochote kile katika mikono yangu ……”,Kendrick aliongea, akitafuna samaki wazima wazima, njaa aliyokuwa nayo haikuwa ya kawaida, akamaliza kutafuna samaki watano, akatosheka, akanawa, akaifutafuta saa yake, akaiwasha, ilikua imezima baada ya kuingiliwa na maji, ikawaka kwa mara nyingine tena, akatabasamu, ghafla tabasamu lake likatoweka, saa yake iliwaka taa mbili tu za kijani badala ya tatu,akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu, mmoja kati yao hakuwa salama.



    …………………………………



    Kisiwa cha Mafia :



            Kamanda Philipo alikasirika, kicheko cha kejeli kutoka kwa watu waliomsaidia ndicho kilichomkasilisha,akajitoa mikononi mwao kwa nguvu, akasimama.



    “,Asanteni kwa msaada wenu, niacheni niondokee! “,kamanda Philipo aliongea, akaondoka zake, nahodha na mabaharia waliokuwa wanamuhudumia wakabaki midomo wazi,wakaachana naye,wakaendelea na shughuli zao, huku wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.



    “,Mimi niliwambia, ameshakua kichaa, kupona kifo baharini lazima uwe na kiwewe, ona sasa, yuko kama mwendawazimu! “,mmoja kati ya mabaharia wa mv Mafia aliongea, wote wakiwa makini kumsikiliza.



    “,Kweli kabisa, lakini asikuumize kichwa, achana naye, cha muhimu tumeshampatia msaada! “,baharia mwingine alizungumza, akatoa mawazo yake, wote wakaelekea kwenye majukumu yao.



    “,Mungu wangu wee! wote saa zao hazifanyi kazi,taa hata moja ya kwao  haiwaki, yes! imewaka, yes nyingine labda itawaka bado moja! “,Philipo aliongea kama kichaa, akiwa bize kuitazama saa yake mara tu baada ya kuiwasha, akaandika ujumbe kwa kupitia saa, akaituma, ili ajue wenzake wako mahali gani.



    “,Anyone online! Comrade Philipo, available in Mafia ……”,(Yoyote yule aliyeko hewani!, kamanda Philipo napatikana Mafia …”,)



    Alituma ujumbe kupitia saa yake, saa iliyounganishwa na saa za wenzake, akasimama kusubili majibu,wapita njia wakimshangaa kwa mavazi yake, mavazi ambayo yalikuwa maalumu kwa ajili ya kutekeleza misheni ambayo haikufanikiwa, misheni ya kuivamia meli ya D47.



    …………………………………



    “,Help me! Help me! nisaidieniii, nisaidieenii! “,kamanda Catherine alipiga kelele kuomba msaada, mikono yake ilichoka kuogelea, muda wowote angeweza kuzama,boti kubwa ikaanza kumsogelea, “Bakhresa “, ilisomeka, akaitambua, ilikua boti ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Zanzibar, mabaharia wawili wakajitupa ndani ya maji, wakampatia msaada, akaponea chupuchupu kufa maji.



    “,kulikoni kamanda, imekuaje? “,mabaharia wale walimuuliza swali Catherine, walimtambua, alikua maarufu sana jijini Dar es salaam yeye pamoja na kundi lake.



    “,Ndege yetu ilipata hitilafu, ikaanguka baharini, asanteni kwa msaada wenu! “,Catherine aliongea, akashukuru, akaiwasha saa yake, ajue kama wenzake wako hai au wamekufa, akatoa tabasamu zuri sana, saa iliwaka taa tatu za kijani,makamanda wote walikuwa wazima.



    “,Wenzako wako wapi, tuambie mlipoangukia tukawatafute, nyie ndio mnailinda nchi yetu, bila nyie sisi sio kitu! “,mabaharia wawili waliongea, huku abiria wakitikisa vichwa, walikubaliana na wazo hili, wakasubili majibu kutoka kwa Catherine.



    “,Msiwe na hofu, wote tayali ni wazima, asanteni kwa upendo wenu …”,Catherine aliongea,wakakubaliana naye, boti ikaendelea na safari ya kuelekea Dar es salaam Tanzania.



    “,Anyone online! Philipo available in Mafia …”,(Yoyote yule aliyeko hewani!, Philipo anapatikana Mafia …),meseji iliingia kwenye saa maalumu ya Catherine, akaisoma, akaandika ujumbe kujibu ujumbe ulioingia katika saa yake.



    “,Anyone online! Catherine is on the way to Dar es salaam, via mv Bakhresa …”,(Yoyote yule aliyeko hewani, Catherine yuko njiani anaelekea Dar es salaam Tanzania, kwa kutumia mv Bakhresa) “,alimaliza kuandika ujumbe mfupi, akatuma.



    ………………………………



    Kisiwa cha Comoro :



          Mzee Fedinand aliongoza njia, binti yake Upendo akafuatia, wakaongoza njia, kumtembeza Kendrick katika maeneo mbalimbali ya kisiwa hiki. Kendrick aliwaza mbali sana, alikua na hasira ya misheni kuharibika, isitoshe mwenzao mmoja saa yake ya mawasiliano haikuwa hewani.



    Ghafla ujumbe ukaingia, alikuwa ni Philipo, akausoma, Philipo alikuwa katika kisiwa cha Mafia, hofu ikazidi kumtanda, mtu aliyempenda, Catherine hakuwa hewani,ghafla taa nyingine ya saa yake ikawaka, taa zikawa tatu, wote walikua hai, ujumbe mwingine ukaingia katika saa yake, akaufungua, akausoma, Catherine alikua njiani anaelekea Tanzania, akafikiria, akajua nini cha kufanya, akaandika ujumbe.



    “,Kendrick is online, aim available in Comoro islands, Catherine just go to take helikopter, then come back to pick us ……”,(Kendrick yuko hewani, napatikana katika visiwa vya Komoro, Catherine nenda kachukue helikopta, kisha uje kutuchukua …”,)Kendrick alimaliza kuandika ujumbe, akautuma, moyo wake ukawa na amani.



    “,Hapa ndipo tunachukua minazi kwa ajili ya kutumia nyumbani. “,mzee Fedinand aliongea.



    “,Unasema? “,Kendrick hakuelewa, mawazo yake yalikua mbali, akauliza tena.



    “,Inaonekana hauko sawa, kuna tatizo lolote? “,mzee Fedinand aliuliza swali kwa Kendrick.



    “,Nilikua nashughulikia usafiri, muda wowote helikopta itakuja kutuchukua, kwa sasa niko ok kabisaa “,Kendrick aliongea, tabasamu zikaipamba sura ya mzee Fedinand pamoja na binti yake, wakamkumbatia Kendrick kwa furaha, hawakuamini kama muda mfupi ujao wangerejea tena Dar es salaam, baada ya kuishi miaka kumi katika kisiwa cha Komoro, Upendo akiwa binti mdogo, mpaka akawa mtu mzima.



    Makao makuu ya polisi :



           Catherine alichanganyikiwa, kituo cha polisi kitengo cha upelelezi kilikuwa kimevurugika, maiti nyingi zilitapakaa kila kona,watu wa huduma ya kwanza wakitimiza wajibu wao kubeba maiti na kuzipelekea mochwali, Catherine nguvu zilimuishia, akadondoka chini, akapiga magoti, alikuwa anatazama moja ya maiti iliypopigwa risasi nyingi sana tumboni, machozi yakamchuruzika kama maji bombani.



    “,D47 inatoshaa! nasema inatoshaa! mwisho wenu umekalibia,mmetuzidi ujanja lakini hamtatuzidi ujanja milele ……!Catherine alizungumza kwa uchungu, akaguswa begani, akageuka.



    “,Imekuaje! mlikuwa wapi mpaka tunaaibika kiasi hiki, shambulio hili limetuaibisha, lakini nimeshajua wakina nani wamefanya hivi…!”,kamanda Catherine alifoka kwa hasira, jasho jembamba likimtoka, mikono yake ilitetemeka, waziri wa ulinzi akaogopa,alizitambua hasira za Catherine.



    “,Askari wote leo wako bize na ulinzi,raisi ameingia bara, ana ziara huko kila mkoa,ndio maana ilikua rahisi kutekeleza shambulio hili,magaidi wameondoka na gari letu pamoja na sare za vijana wetu! “,waziri wa ulinzi aliongea,akajikuna kichwani, akaweka miwani yake vizuri, kisha akajiandaa kuzungumza kitu.



    “,wenzako wako wapi?, imekuaje ?,ndege yenu ilipotea kwenye rada zetu, tumeitafuta bila mafanikio, nikataka kutuma vijana waje kuwatafuta, ghafla nikapewa taarifa umerejea, nilikua njiani nakuja hapa, ghafla ndio tumekutana, hebu nieleze!! “,waziri wa ulinzi aliongea.



    “,Tulishambuliwa na magaidi, wengine nimewaponyoka,kundi limesambaratika, kila mtu yuko eneo lake, Philipo yuko Mafia, Kendrick yuko Komoro ,naomba muheshimiwa fanya jambo kwa ajili yao, tuma helikopta ikawachukue, ulinzi haujakaa vizuri kwa sasa ……” Catherine alitoa maelezo mafupi, akijifuta machozi kwa kutumia kitambaa chake.



    “,ok nafanya hivyo,helikopta itaenda kuwachukua nusu. saa kuanzia sasa, kabla jua halijazama, unachotakiwa kufanya, chunguza undani wa tukio hili, kisha nitumie taarifa ofisini kwangu …”,waziri wa ulinzi alizungumza, Catherine akatikisa kichwa, akapiga saluti,waziri akapanda kwenye gari lake, akaondoka zake,waandishi wa habari wakijitahidi kufanya mahojiano naye bila mafanikio, alikataa kuzungumzia chochote kile kuhusu tukio hili la kuvamiwa kwa kituo cha polisi kitengo cha upelelezi.



    …………………………………



    Helikopta ndogo yenye uwezo wa kubeba abiria sita, iliacha ardhi ya jeshi la anga,Dar es salaam,Tanzania, rubani wa helikopta alitimiza majukumu aliyoelekezwa,alipaswa kuwachukua makamanda wawili wa kitengo cha upelelezi, mmoja akiwa katika kisiwa cha Mafia, mwingine akiwa kisiwa cha Komoro.



    “,Usawa wa kisiwa, usawa wa kisiwa,unanipataa ovaaa! “,rubani wa helikopta alizungumza kupitia simu yake kubwa ya mkonga.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Halooo, halooo! ,oooh shiit! watakua hawana mawasiliano ya simu, hawapatikani hewani,”,aliendelea kuzungumza, akabonyeza tena simu yake ya mkonga, akaiunganisha na saa za kijeshi, saa za upelelezi.



    “,Haloo, halooo, niko Mafia, mko wapi ovaaa? “,aliuliza, akasubili jibu. Akiwa katika anga, usawa wa kisiwa cha Mafia.



    “,Niko Mafia, sogea bandarini, utaniona …”,sauti ilisikika upande wa pili.



    “,Nashuka sasa hivi,hakuna kupoteza hata sekunde, nimepewa nusu saa tu ya kuwachukua! “,rubani wa helikopta aliongea, akakata mawasiliano, akaiweka simu yake kwenye mifuko ya suti yake ya kijeshi. Baada ya dakika tano tu, alianza kuishusha ndege bandarini, ikatua juu ya meli moja, kamanda Philipo akaiona, akasogea karibu na meli hiyo, akaingia, moja kwa moja mpaka usawa wa helikopta, akapanda na kutokomea, wavuvi, mabaharia na abiria waliokuwa eneo hili la bandari wakabaki midomo wazi, wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.



    “,tunaelekea Komoro, kumchukua Kendrick, kisha tutarudi tena Dar es salaam Tanzania …”,rubani yule aliongea, helikopta ikipaa juu futi sitini, ikakunja kona na kuelekea upande wa kusini,bahari ya hindi.



    …………………………………



    6;02pm



          Kamanda Kendrick alisubili helikopta kwa hamu sana, alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kufika Dar es salaam,taarifa za kituo chao cha polisi kushambuliwa, askari wakauawa kinyama zilimshtua na kumsikitisha sana.



    “,Mbona hauna raha, nini tatizo Kendrick?, japo ni masaa kumi tu tumeweza kukutana, lakini nimetokea kukuzoea, unaonekana kijana mwenye huruma na hekima, sipendi uwe na majonzi ……”,mtoto wa mzee Fedinand aliongea, akamsogelea Kendrick, akakaa pembeni yake.



    “,Kuna taarifa mbaya kutoka serikalini, lakini usjali ni majukumu tu ya kikazi ……”,Kendrick aliongea, hakutaka kueleza kile ambacho kilikua kinamsumbua, akaficha,hakupaswa kumwamini mtu yoyote katika shughuli za kiserikali na kuziweka wazi.



    “,Papapapapapapapa! …”,muungurumo wa helikopta ulisikika, helikopta ndogo yenye rangi za kijeshi ilipita mita kadhaa usawa wa eneo lao, Kendrick akatazama juu, akaitambua ndege hii, ilikuwa helikopta ya Tanzania, akamshika mkono msichana wa mzee Fedinand.



    “,Twendeni wamekuja kutuchukua,baba, babaa, njoo twendee! “,Kendrick aliita, mzee Fedinand akatoka nje ya kibanda, mwilini akiwa amevaa magome ya miti, kwa miaka kumi sasa walitumia magome ya miti kama mavazi, nguo walizopotea nazo miaka kumi iliyopita walizivaa mpaka zikaisha. Hawakupata zingine, wakaamua watumie magome ya miti kusitiri miili yao.



    “,Philipo,!”,Kendrick aliita.



    “,Yes afande!”,philipo aliitikia,akamsogelea rafiki yake,wakakumbatiana.



    “,Hao ni wa kina nani,wanajua kiswahili?”,Philipo aliuliza.



    “,Yes wanajua,salimiana nao,mambo mengine tutazungumza baadae!”,Kendrick aliongea,akamsogelea mzee ambaye alikuwa amesimama sambamba na binti yake.



    “,Shikamoo mzee!”,Philipo alisalimia,akampatia mkono wa kulia,wakashikana kama salamu ya heshima.



    “,Marhaba!”,mzee yule aliitikia.



    “,Habari yako dada!”,alisalimia tena.



    “,Salama,asanteni sana kuja kutu……”,kabla Upendo hajamalizia kuongea, sauti ilisikika,sauti iliyomshitua na kumfanya ageuke haraka.



    “,Kamanda,tuondokeni!nilipewa nusu saa tu,nikichelewa nitaadhibiwa!”,rubani wa helikopta aliongea,Kendrick na Philipo wakamuelewa,walizitambua vizuri sana sheria za.kijeshi,wakajipakia ndani ya helikopta,helikopta ikapaa na kutokomea angani.



    …………………………………



    Bahari ya Hindi :6:30



             Mkuu wa kikundi cha magaidi wa D47,bilionea Paresh Kumar, alipata taarifa kutoka Tanzania,zilizidi kumfurahisha, akawa na furaha zilizopitiliza, tofauti na siku zote.



    “,Wale walikuwa askari wa Tanzania hatari wanaotutafuta kila siku, hasa Donald Mbeto ndiye muhusika mkuu,ndugu zetu kutoka Dar es salaam ndio wamenipatia taarifa hizi,wamemuua D47 namba mia moja, maana aligundulika kushirikiana na sisi, akapewa adhabu kama askari na kusema siri zetu zote, wameshambulia kituo cha polisi, wameua askari wote, ni shangwe na nderemo kwetu sisi, tunachopaswa kufanya ni kuwa makini, lazima watarudi kututafuta!! “,bilionea Paresh Kumar aliongea,mguu wake mmoja alikunja nne, kushoto aliketi mrembo wa kihindi, kulia aliketi mrembo wa kichina, wote walimpapasa na kumshika shika mwilini, alipenda sana wanawake, aliwateka kutoka pembe zote za dunia, akafuta kumbukumbu zao kichwani, wakamtumikia katika kundi lake katika shughuli mbalimbali.



    “,Kwa kuwa wameshajua eneo tulilopo,meli yetu ipae angani kama ndege, usawa wa mawingu, watahangaika kututafuta mpaka wanazeeka! “,Paresh Kumar alitoa amri, vijana wake wakaluka juu kwa shangwe, burudani zikaendelea, mziki ukapigwa, kila mtu akaendelea na starehe yake aliyoipenda, kufurahia ushindi, meli yao ikajigeuza, bawa likachomoza upande wa kulia, bawa lingine likachomoza upande wa kushoto, ikaanza kupaa hewani, ikaiacha bahari, haikuwa meli ya paraquat tena, bali ndege kubwa yenye uwezo wa ajabu.Makombola ya nyukilia yakachomoza kila upande wa ndege hii, kwa ajili ya ulinzi.



    Ofisi ya ukombozi: 7:00



           Catherine alianza upelelezi,aweze kuwapata washirika wa D47 waliofanya shambulio,akiwa anatafakari, akapata jibu, akaondoka haraka sana, kutoka katika kituo cha polisi kilichoshambuliwa, mpaka katika ofisi yao ya ukombozi, ndani ya jengo la China plaza, Kariakoo.



    “,This bastard kahusika! picha zake zisambazwe kila kona, tukimpata huyu, tutafahamu mengi ……”,Catherine aliongea, alimkumbuka raia wa kisomali waliyegongana vikumbo siku moja iliyopita,kijana aliyejaribu kufungua ofisi yao bila mafanikio na kuambulia kupigwa picha alipokosea neno siri la kufungulia mlango, Catherine akamkimbiza bila mafanikio, alitaka kumuhoji ajue nini alichotaka katika ofisi yao.



    “,Work done, kazi imekwisha,ngoja nikapige picha na eneo la tukio,ni attach kwenye picha yake,kisha nitume kwa waziri,vyombo vya habari viripoti taarifa hii…”,Catherine aliongea,akiitazama sura ya gaidi aliyetaka kuingia ndani ya ofisi yao siku moja iliyopita,akiwa ndani ya suti nyeusi,akiwa ameyavua mavazi yake ya kazi,akatoka nje ya ofisi ya ukombozi,akatokomea.



    …………………………………



    7:10pm



           Kendrick na Philipo walitaka kushushiwa katika eneo la tukio,mahali ambao kitengo chao cha cha upelelezi kilipatikana,kabla ya kushambuliwa,rubani wa helikopta akafanya hivyo,akashusha helikopta,ikatua ardhini na kuikanyaga ardhi ya Dar es salaam kwa mara nyingine tena,Kendrick akashuka,mkono wake wa kulia ulimshika Upendo,mtoto wa mzee Fedinand,Philipo akashuka,akiwa ameongozana na mzee Fedinand,uso kwa uso wakakutana na maiki nyingi za waandishi wa habari,wakitaka kuzungumza nao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “,Naripoti kutoka ITV the super brand Afrika mashariki,naitwa Abdalah Said Abdulah,wewe kama mkuu wa kitengo hiki,unaweza kutueleza chochote kuhusu shambulio hili……”,mwandishi wa habari aliuliza,mwilini alivaa suti nyeusi iliyofiti mwili wake ipasavyo.



    “,Sijui chochote,ndiyo narejea baada ya helikopta yetu kupotea baharini,tukiwa katika majukumu yetu,lakini naahidi, tutawakamata watu hawa ndani masaa ishirini na nne yajayo!”,Kendrick aliongea,mwandishi wa habari akimtazama Upendo kuanzia chini hadi juu,alishangazwa sana na mavazi yake.



    “,Huyu naye umemtoa wapi?, amevaa mavazi tofauti na asili ya mtanzania,”mwandishi aliendelea kuhoji.



    “,Huyu anaitwa Upendo,baba yake anaitwa mzee Fedinad,walipotea na meli ya mv spice miaka kumi iliyopita,walifanikiwa kupona kifo cha maji,baada ya kuogelea mpaka pwani ya kisiwa cha Komoro, eneo lisilo na watu,wakaishi huko wakila matunda na samaki,wameniokoa mimi leo hii,pengine bila wao nisingekuwa hai,popote walipo ndugu zao,wafike nyumbani kwangu,mtoni kijichi,wakiulizia kamanda Kendrick,watafikishwa mpaka mlangoni…”,kamanda Kendrick alitoa maelezo,akamshika mkono Upendo,wakasogea kabisa eneo la tukio.



    “,Sasa,unaweza,ukaa……”,mwandishi yule alitaka kuendelea kuhoji,Kendrick alichoka mahojiano,akaondoka zake,akafika eneo la tukio,akatazama kila kona,damu zilikuwa zimeganda na kutapakaa eneo lote.



    “,Kendrick uko salama,na huyu ni nani?”,Catherine alifika,akauliza swali.



    “,Nitakueleza kila kitu,endelea kuchukua taarifa za upelelezi wa mwanzo,sisi tunaelekea nyumbani na kamanda Philipo,baada ya upelelezi,mpatie waziri majibu taarifa za upelelezi kama sheria zinavyosema, kisha fika haraka nyumbani kwangu,tuzungumze suala hili.”Kendrick aliongea,akatoa maelezo mafupi,wakaongozana na Philipo,pamoja na mzee Fedinand,wakapanda gari ya polisi, wakatokomea.



    …………………………………



    Kendrick aliishi nyumba moja na mama yake mzazi,kaka zake wawili walipoteza maishi kwa mshituko, waliposikia taarifa za meli ya mv spice kuzama, meli ikiwa imembeba baba yao ambaye alikuwa ni tegemeo kubwa katika familia yao,mama yao alichanganyikiwa,akaugua ugonjwa wa akili kutokana na kupata pigo kubwa kwa wakati mmoja, mme wake na mtoto wake wa mwisho, walipoteza maisha kwa ajari ya meli, watoto wake wakafa kwa mshituko wa moyo,mara baada ya kupokea taarifa za kifo cha baba yao, pamoja na mdogo wao.



    Kendrick akiwa kidato cha nne, aliamua kumpeleka mama yake hospitali kuu ya vichaa mkoani Dodoma, hospitali ya Mirembe. Akatibiwa, huku Kendrick akijiunga na jeshi la kujenga taifa, akamaliza mafunzo ya miezi sita, akajiunga na jeshi la polisi, kutokana na utendaji wake, akapandishwa cheo kila kukicha, huku mama yake akipona ugonjwa wake wa akili, akamrudisha nyumbani, wakaishi tena pamoja.Kendrick alifikili baba yake, pamoja na mdogo wake walikuwa wamepoteza maisha katika ajali ya mv spice,kumbe sivyo, Mungu aliwakutanisha tena pamoja.



    “,Baba Josephat! “,mama yake Kendrick alipigwa na butwaa,hakuwahi kuisahau sura ya mume wake hata siku moja, aliitambua vizuri sana,alipigwa na butwaa baada ya Kendrick kurudi nyumbani na wageni,mmoja kati ya wageni akiwa ni mume wake wa ndoa.



    “,Mamaaa Josephat, ni wewe?,nyumba yetu imebadilika! “,mzee Fedinand aliita kwa mshango, akamkimbilia mke wake, wakakumbatiana.



    “,Mbona sielewiii, ina maana, wewe ndiye baba yangu ……?”,Kendrick aliuliza swali kwa mshangao, chozi la furaha likaanza kumtoka.



    “,Ndiyo kendrick, huyu ndiye baba yako,sijui umemtoa wapi? “,mama yake Kendrick aliongea, machozi yakimtiririka.



    “,Mama Josephat, huyu ndiye mtoto wetu wa mwisho Jacline, huyu ndiye nilisafiri naye kwenda Zanzibar,”mzee Fedinand aliongea.



    “,Mamaaa! “,Upendo aliita.



    “,Mwanangu! “,mama Kendrick aliitika.



    “,Mamaaaa! “,Upendo akaita tena.



    “,Jamani mwananguuu …”,mama Kendrick akaita  tena, akamkimbilia mwanae, wakakumbatiana, kila mmoja akiona kama ndoto.



    “,Kendrick mwanangu, najua unajiuliza maswali mengi, mimi sio Fedinand, naitwa Steward, siwezi kukwambia ukweli katika hali kama ambayo umetukata nayo kule, tulikuwa hatujui wewe ni mtu mwema au mbaya kwetu, ndiyo maana nilikuficha majina yetu halisi, na huyo siyo Upendo, bali ni mdogo wako Jacline, wahenga walisema usimtendee mema binadamu unayemfahamu peke yake, leo hii nimekuokoa baharini, kumbe namuokoa mtoto wangu, Mungu katumia njia ya ajabu kutukutanisha. “,mzee Fedinand alitoa maelezo marefu, kumbe jina lake sio Fedinand, alidanganya,jina lake halisi aliitwa Steward, Kendrick akamsogelea baba yake na kumkumbatia, furaha ikazaliwa upya katika familia ya kamanda Kendrick.



    Kamanda Philipo alijifuta chozi ambalo lilikuwa linamdondoka, alishuhudia kila kitu,Catherine alikuwa amesimama mlangoni, alikuwa tayali ameshafika muda mrefu, akajikuta anasimama mlangoni kama sanamu, alishindwa kuendelea mbele, nguvu zilimuishia, historia ya kustaajabisha aliyoisikia ilimchanganya sana, hakuamini kama Kendrick alipitia mkasa wa kutisha kiasi hicho, hakuwahi kumweleza hata siku moja, alikua msiri sana.



    “,Catherine! umefika, kumbe uko hapa, karibu ndani, nilitaka nikueleze kuhusu kukutana na watu hawa,tujue namna ya kuwasaidia kuwapata ndugu zao, lakini kumbe tayali wameshafika nyumbani! “,Kendrick aliongea kwa furaha, Catherine akatabasamu, akasogea sebureni, akakaa kwenye sofa.



    “„Josephat na Yohana wako wapi?  ,au wameshaoa, wako na familia zao? “,mzee Steward, baba yake Kendrick aliuliza, mama yake Kendrick akanyongonyea, tabasamu ikatoweka usoni mwake, vivyo hivyo kwa Kendrick, akapoteza furaha kabisa, akapiga moyo konde, akajikaza kiume na kuongea ukweli.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Kwa sasa ni marehemu, tuliwazika siku moja tu baada ya kupokea taarifa za meli kuzama na abiria wote kupoteza maisha, walipatwa na mshituko, wakafa palepale, mama naye akachanganyikiwa, lakini namshukuru Mungu, mama alipatiwa matibabu, kwa sasa ni mzima ……”,Kendrick aliongea,baba yake akadondosha chozi, haikusaidia chochote kile,watoto wake walikuwa tayali wameshapoteza maisha, wasingerudi tena.



    “,Wapumzikee kwa amani wanangu! “,mzee Steward alizungumza, mke wake akamkumbatia, akambembeleza, akajikaza kiume, akajaribu kuificha huzuni yake lakini hakuweza, machozi yake yaliendelea kutoka, alihuzunika sana kuwapoteza watoto wake.



    Mbezi :8:02



             Magaidi wa D47,kanda ya Dar es salaam, walikuwa wameketi katika nyumba yao ya kifahari,chupa za bia zilikua mezani, walikunywa mpaka wakatapika,walikamilisha kazi kama walivyopanga, bosi wao akafurahishwa zaidi na kitendo hicho, akamuingizia kila mtu dola elfu moja kwenye akaunti yake. Akawapatia kazi nyingine kubwa, kuhakikisha wanawaua maaskari watatu wanaolifuatilia kundi lao.



    “,Kesho asubuhi na mapema tunaanza kazi, hawa watu lazima tuwauee, tusipo waua sisi, watatuua! “,D47 namba sitini alizungumza, wenzake watatu wakiwa. pembeni yake,kila mmoja alikuwa ameshika chupa ya bia mkononi.



    “,Kweli kabisa,mimi nina plani,nina mipango ambayo itaifanya kazi hii kuwa rahisi kabisa……”,gaidi mwembamba,mrefu,mweupe,alizungumza,akawatazama wenzake usoni.Wote wakaweka bia zao,wakatulia kusikiliza mbinu hiyo,walikuwa na shauku ya kupata pesa nyingi kama wakifanikiwa kuwaua wapelelezi watatu hatari wa kundi la the super three soldiers.



    “,Mbinu gani hiyo chuma cha puaa?”,gaidi mwingine aliuliza,mweusi,mfupi,kichwani alikua na kipara.



    “,Tuteke familia zao,hasa ya kiongozi wao wa kundi,lazima watajileta wenyewe,wote watatu,kutaka kuwakomboa,sisi tutaacha eneo hili likiwa limetegwa mabomu,wakifika eneo hili kukomboa ndugu zao,tunalilipua,wanakufa woteeee!”,gaidi yule aliyejulikana kwa jina la chuma cha pua aliongea,licha ya wembamba pamoja na urefu wake,alikuwa amekomaa kama chuma,ngumi yake ilikuwa na uwezo wa kupasua matofauli kumi ya bloko,aliwahi kumuua gaidi mwenzake,allimpiga na kichwa chake,akampasua fuvu la kichwa,wote wakiwa mazoezini,wakamubatiza jina hilo,mwili wake ulikomaa kwelikweli.



    ” ,Yeeeeeeh!,”waligonga chupa zao kwa furaha,walikubaliana na plani ya mwenzao,kilichobakia ni utekelezaji,wakanywa bia kwa fujo, wakalewa chakali,usingizi ukawachukua,wakalaliana kama mizigo,wakiwa hawajitambui.



    …………………………………



    Ofisi ya Ukombozi:9:00pm



    Makamanda watatu walikutana tena,mara baada ya kutoka nyumbani kwa kamanda Kendrick.Kila mmoja aliketi katika kiti chake,ndani ya ofisi ya ukombozi.



    “,Catherine nipe ripoti!”,Kendrick aliongea,akijizungusha zungusha kwenye kiti chake.



    “,Kila kitu kiko sawa,picha za mmoja kati ya magaidi anayetuhumiwa kuhusika na shambulio,zimefika katika vyombo vya habari,kesho asubuhi taarifa zitaenea na kutangazwa kila kona.”,Catherine alimaliza kutoa ripoti yake.



    “,Ok sawa,sasa nazani mnafahamu magaidi walipo,mahali tuliposhambuliwa,walitugundua mapema,meli yao ikajibadirisha kama nyambizi,ikawa rahisi kutushambulia,hivyo basi,kabla ya mapambano tuelewe,meli yao ni ulinzi tosha kwao,ina uwezo kujigeuza katika maumbo mbalimbali,ikawa kama meli,nyambizi au hata ndege ,ikapaa angani kama ndege zingine!”,Kendrick alitoa maelezo mafupi.



    “,Sasa Kendrick ,tunafanya nini hapa? ,tutumie mbinu gani?”,Catherine aliuliza.



    “,Nafahamu nini cha kufanya,nikipata uhakika wa eneo walilopo,iwe baharini au angani,nitaweza kudukua(kuhack) mifumo yote ya mawasiliano kwenye chombo chao,itakua rahisi kuwavamia,hawatatuona wakati wa kukivamia chombo chao.



    “,Sawa,naona tukiwakamata hawa magaidi walioko Dar es salaam,watatusaidia kujua wenzao wako wapi,itakua rahisi kufanya udukuzi!”,Catherine aliongea.



    “,Wazo zuri,tukutane hapa saa kumi na mbili asubuhi,tuanze kazi,kila mmoja awe makini kujilinda,kila tunapopiga hatua,maadui zetu wako nyuma,zingatieni suala hili……”,Kendrick alizungumza.



    “,Sawa afandee!”,wote waliitikia,wakapigiana saluti za heshima,kila mmoja akatoka nje, kuelekea nyumbani kwake kupumzika..



    …………………………………



    Hisia za kimapenzi ziliusumbua moyo wake, kadri siku zilivyozidi kwenda, Kendrick hakuonesha hisia zozote za mapenzi juu yake,uvumilivu ukamshinda kabisa, moyo wake ulichoka kuteseka na mapenzi,akafikiria, akapata wazo, wazo aliliona sahihi.…



    “,Kendrick,nimepoteza funguo za nyumba yangu, sijui hata nafanya nini, hotelini siyo salama, siwezi kulala kabisa ……”,Catherine alidanganya, akiwa pembeni ya gari lake, sura yake ilikuwa siliasi, haikuonesha hata chembe ya uongo, alijiamini kwa yale aliyoyazungumza.



    “,Kwa nini usije kulala nyumbani kwangu, kuna vyumba vya kutosha, kesho tutatafuta funguo zako au kuchongesha zinginee! “,Kendrick aliongea.



    “,Hapo utakua umenisaidia saanaa, lakini ujue sasa hivi familia yako imeongezeka, mzee wako, mama yako pamoja na mdogo wako, hawawezi kukufikilia vibaya,wakafikili umeleta mwanamke ndani? “,Catherine alifurahi plani yake kufanikiwa kama alivyo panga,akajifanya kama hakupanga jambo hilo, akaendelea kuuliza maswali ya uchokozi.



    “,Hapana,wewe ni rafiki yangu,tunafanya kazi pamoja, hawezi kuwaza chochote kile, japo mama yangu kila siku ananiuliza kuhusu suala la kuoa, mimi bado sijawa tayali, nitamlisha nini mie? “,Kendrick alimjibu Catherine, uso wake ukaachia tabasamu kwa mbali. .



    “,Hahaaa, “wote wakacheka, wakajipakia kwenye magari yao, nje ya jengo la ofisi ya ukombozi, wakatokomea, kamanda Philipo alikuwa tayali ameshaondoka zake dakika takribani kumi zilizopita.



    …………………………………



    Mtoni Kijichi :



           Catherine na Kendrick walifika nyumbani, mama yake Kendrick, baba yake, pamoja na mdogo wake Jacline walikuwa tayali wamelala.



    “,Tutaonana kesho,kalale chumba cha wageni, pita korido hii, chumba cha kwanza mkono wa kushoto! “,Kendrick aliongea, baada ya kumaliza kula, yeye pamoja na Catherine.Kendrick alinyanyuka, akataka kwenda kuchukua maji ya kunywa kwenye friji.



    “,Sawa nimekuelewa, mbona unasimama, unaenda wapi? “,Catherine aliuliza.



    “,Naenda kunywa maji “,Kendrick alijibu.



    “,Subili nikuletee! “,Catherine aliongea, akanyanyuka kwenye sofa, akaisogelea friji, akachukua chupa ya maji ndani ya friji, akamimina kwenye grasi. Akageuka nyuma, Kendrick alikuwa anasinzia sinzia, usingizi ulikuwa unamzidi nguvu, hakutambua chochote kile kilichokuwa kinaendelea, catherine akaingiza mkono ndani ya koti lake la suti, akachukua kidonge cha usingizi, vidonge ambavyo walivitumia katika oparesheni mbalimbali za kijeshi. Baada ya kuweka kidonge kile ndani ya maji, akatikisa vizuri kiweze kuyeyuka, kisha akampelekea Kendrick.



    “,Kendrick, Kendrick! “,Catherine aliita.



    “,Yeeees, nanambiee! “,Aliitika kwa kigugumizi, usingizi ulimzidi nguvu, isitoshe alichoka sana, tangu asubuhi alizunguka huku na kule bila kupumzika.



    “,Kunywa maji, haya hapa! “,Catherine aliongea, Kendrick akachukua glasi ya maji, akanywa maji yote,akaweka glasi mezani, ndani ya sekunde mbili tu, akalala fofo.



    “,Hahaaa, leo unalala na mimi, kila siku nikigusia suala la mapenzi unaona kama natania, sasa leo tunalala wote, kesho wakitukuta, lazima tufunge ndoa ya mkeka, unasema huoi askari kama wewe, sasa utaoa kwa lazima…”,Catherine alisahau vita kubwa mbele yao kwa muda mfupi tu, hisia za mapenzi zilikuwa zimemtawala, akamnyenyua Kendrick, akampeleka katika chumba cha wageni, chumba ambacho alielekezwa akalale, wote wakalala huko.



    Mtoni kijichi :7:30am



          Magaidi wanne wa kundi la D47,walipaki gari nyeusi aina Toyota Hallier, pembeni, nje ya jumba la kamanda Kendrick, jumba ambalo lilizungushiwa geti kubwa.



    “,Hapa ndipo nyumbani kwake,waliotuelekeza hawajadanganya, kama unavyo ona, kuna askari getini, anatimiza majukumu yake ya ulinzi



    ……”,gaidi D47 alioongea.



    “,’Nazani mwenyewe ameshaelekea ofisini,chuma cha pua, toka kaongee na mlinzi, fanya lolote tuweze kuingia ndani! “,gaidi D47 aliendelea kuongea.



    “,Sawa bosi”,chuma cha pua aliitikia, akatoka nje, akalisogelea geti,mpaka mahali alipokuwa amesimama mlinzi.



    “,Karibu muheshimiwa, sijui nikusaidie nini? “,askari mwenye kirungu mkononi aliuliza,akamkaribisha kwa heshima zote gaidi, kutokana na suti nyeusi ya heshima aliyokuwa amevaa.



    “,Nina mazungumzo na bosi wako, tulisoma naye, ni muda mrefu hatujaonana, naomba kuzungumza naye…”,gaidi aliyejulikana kwa jina la chuma cha pua aliongea,askari yule akaonekana kuyaamini maneno ya mgeni huyu.



    “,Japo bosi hayupo, ameshaenda kazini, unaitwa nani? “,askari yule aliuliza swali tena,huku akidanganya kuwa Kendrick hayupo, alielekezwa kusema hivyo kwa mtu yoyote asiyemfahamu.



    “,Acha maswali yako kijana, au nimpigie simu uongee naye, utamwaga unga sasa hivi …”,chuma cha pua aliongea, akaingiza mikono yake mfukoni, akatoa simu, akajifanya kama anataka kupiga, askari yule akaanza kutetemeka kwa hofu.



    “,basi baba! basii, yaishee, ingia ndani ,lakini bosi hayupo……,”askari yule aliongea,akadanganya, hakuna aliyemsikiliza, akafungua mlango, chuma cha pua aliangalia kulia, akaangalia tena kushoto, hakuona mtu yoyote yule, alimpiga kabali askari yule, akaivunja shingo yake, ulimi wa askari yule ukatokeza kwa nje, akafa palepale. Chuma cha pua akambeba, akamuweka kwenye buti la gari,walitaka mauaji yafanyike kimya kimya, asigundue mtu yoyote yule, baada ya kumfyekelea mbali, magaidi wote watatu wakatoka ndani ya gari, wakaingia ndani ya jengo la kamanda Kendrick, wakafunga geti kwa ndani, asije akaingia mtu yoyote yuke, akaharibu mipango yao.



    “,Kaka yuko wapi?”,Jacline aliuliza,akiwa anaandaa chai mezani.



    “,Yuko na wifi yako,nimeona viatu vya kike mlangoni tofauti na vyangu wala vyako,leo amechelewa kwenda kazini,muache apumzikee…”,mama yake Kendrick aliongea,huku akitabasamu.



    “,Jana walikula naye,nilichungulia sebureni,ni yule msichana wanayefanya naye kazi,ni mrembo kwakweli,nilipomtambua nikarudi kulala…”,baba yake Kendrick,mzee Steward aliongea.



    “,Hahaaaa……”,wote wakacheka,wakaendelea kunywa chai.



    “,Hapo hapo mlipo,asijitikise mtu yoyote,mkijitikisa tunawaua!……”,sauti ya kutisha ilisikika,walipogeuza shingo zao,wakatazama mlangoni,uso kwa uso na wanaume wanne wenye bastola mkononi,usoni walivaa miwani rangi nyeusi,rangi ambayo ilifanana na suti zao pamoja na mabuti yao meusi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “,Nyie ni wakina nani?mnataka nini?”,mama yake Kendrick aliuliza swali.



    “,paaaaaaa!”,alichapwa kibao,akadondokea upande wa pili wa sofa.



    “,Mamaaaaaaa!”,Jacline alipiga kelele,hasira za mama yake kupigwa mbele yake zikampanda,akakosa cha kufanya.



    “,Kelele malaya wewe!”,Jackline alifokewa.Akazidi kukasirika.



    “,Malaya mwenyewe!”,Jackline hakuogopa chochote kile,akawatukana magaidi.wale,akamtemea makohozi usoni,gaidi ambaye alikuwa amemchapa kibao mama yake,huku akimwita Jackline malaya.



    “,Tunakubaka sote wanne sasa hivi,mbele ya baba yako,pamoja na mama yako,halafu tuone sisi na wewe nani malaya……”,chuma cha pua alizungumza,wakamfunga kamba mama yake Kendrick mkononi na miguuni,wakamfunga na baba yake.Wakajiandaa kumubaka Jackline,chuma.cha pua alianza kuifungua zipu yake.



    …………………………………



    Kamanda Catherine alikuwa amechoka sana,alilala na mtu aliyempenda kwa mara ya kwanza, lakini hakufanya naye chochote kile, alitaka kutimiza malengo yake, Kendrick aweze kufungishwa ndoa ya mkeka pamoja naye, watakapokutwa wamelala pamoja asubuhi. Usingizi hauna ndugu, alilala fofofo tofauti na siku zote, Kendrick ndiyo kabisaa, dawa ya usingizi aliyopatiwa usiku uliopita, iliendelea kutimiza majukumu yake, akauchapa usingizi bila hata kushtuka.



    Ghafla Catherine alikurupuka usingizi, mapigo ya moyo wake yalienda kasi sana,akageuka upande wa pili, akamgusa gusa Kendrick begani, hakushtuka! alikuwa bado amelala. Catherine akaitazama saa yake ya kijeshi, “8:00am”,saa yake ilisomeka.



    “,Saa mbili kamilii! “,aliongea peke yake kwa mshangao, akachukua viatu vyake, akavaa suti yake, akaziweka vizuri nywele zake, kwa mbali akasikia vitisho sebureni, akasikiliza kwa makini, mapigo ya moyo wake yakapiga kwa kasi sana,walikuwa wamevamiwa, akasogea kitandani, akampiga piga Kendrick aweze kushtuka,Kendrick hakushtuka, aliendelea kukoroma kama kawaida.



    “,Kendrick, Kendrick, tumevamiwa, najuta mimi! amka tukapambane! “,Catherine aliita, bila mafanikio,hakua na budi kuubeba mzigo yeye mwenyewe, bila hivyo chochote kile kingeweza kutokea, wazazi wa Kendrick wasije wakauawa, akalaumiwa,akakosa mume pamoja na kuharibu kazi yake.



    “,Kakaa, nabakwaa, kaka nabakwaaa, njooo unisaidiee ……”,Jackline alipiga kelele,kelele zikapenya katika matundu mawili ya masikio ya Catherine, akakasirika.



    “,Hahaaahaaa, hakuna atakayekuja kukusaidia, hahaa……”,magaidi yale yalizungumza, yakacheka kwa kejeli, Catherine akazidi kukasirika,alisikia kila kitu.



    “,nimelala kwa Kendrick, najua uko ofisini, njoo, tumevamiwa …”,Catherine alituma ujumbe kwa kamanda Philipo kupitia saa yake iliyotumika kama simu,akapiga mahesabu namna ya kuwavamia magaidi, awashambulie kabla hawajafanya ubakaji. Akafungua mlango taratibu, akachungulia,akamuona jambazi aliyegongana naye uso kwa uso, alimtambua vizuri sana.



    “,Wamejileta wenyewe, watakufa, “Catherine aliongea, akaifunga bastola yake mfumo wa sauti, akalala chini, hakuweza kuonekana, sofa zilimzuia. Chuma cha pua akachomoa uume wake uliosimama kwa njaa kali, bila aibu akamsogelea Jacline.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Yalaaaaaa ……”,uume wa chuma cha pua ulisambaratika, damu zikaruka, akapiga kelele za uchungu, hawakutambua risasi imetokea wapi. Wakaanza kupiga hovyo risasi, kwenye sofa, ukutani, dirishani, milangoni, walikuwa kama wamechanganyikiwa.



    “,Mtafuteni tumuue! jitokeze kabla hatujaua familia yako ……”,kiongozi wa kundi hili aliongea, alikuwa D47 namba sitini, bastola yake aliinyosha kuelekea juu, akafyatua risasi, zikapiga juu ya dali.



    “,Nasema jitokeze tutawauaa wazazi wako! “,gaidi alitoa amri kwa mara nyingine tena.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog